Nyumba za kupanga na mazindiko

nyumba

Wewe ni mkristo, unaishi kwenye nyumba ya kupanga. Usiku unaamshwa na mwenye-nyumba wako kwamba amekuja mganga wa kienyeji ili azindike nyumba hiyo. Akasema wanaanzia ndani kisha watamalizia nje, kwa kuchimba vitu kwenye pembe ya nyumba!

Je, wewe kama Mkristo, utachukua hatua gani?

Advertisements

13 thoughts on “Nyumba za kupanga na mazindiko

 1. Ni vyema kua sehemu sahihi , kama ni Roho alinipangia niwe hapo itabidi ajitukuze kwa muda wake maana saa yake ya kujitwalia utukufu imefika.(tuongozwe na Roho).

 2. Sitokubali kufanyiwa kwenye chumba changu, Pia ntachukua hatua kumwomba MUNGU nakukemea kila aina nguvu za giza maana tumepewa mamlaka

 3. Nitaamka ila sitashirikiana nao wakati mganga anaendelea na kazi yake mi naendelea kuomba kubatilisha kazi ya hayo matambiko baadaye akishamaliza hiyo ni nafasi nzuri kwangu kama mkristo kuitumia kuongea na mwenye nyumba kuhusu Mungu wa kweli ili aweze kuokoka na kutoka kwenye giza hilo.

 4. Ok!
  Swali zuri sana hilo kwanza kabisa sitaruhusu kitu kama hicho kufanyika nyumbani kwangu hata kama nimepanga kwani kwa wakati huo mimi ndo ninayemiliki hiyo nyumba. Na kama atang’angania kufanya hivyo nitamkubalia ila nitamwambia aje siku nyingine. Ndipo nitapofanya maombi kuzungushia damu ya Yesu na Kwa kusimamia Neno asiwepo kwenu mtu mke au mume alogaye au….
  NATHANI KWA HILO HATATHUBUTU KUINGIA KWANI ATAKUTANA NA MWANAUME YESU MLANGONI NA WALA HATATIA MGUU NDANI
  Gloooooooooooooory!!!!!!!!

 5. Hivii, mwenye nyumba akikuuliza kuwa kwa nini unaogopa wakati wewe unamwamini Yesu, kiboko ya wachawi na kuwa mazindiko hayo siyo kwa ajili yako bali kwa ajili ya watu wenye nia mbaya na maisha yake na wala hakuwekei zindiko wewe, UTAMJIBUJE?

 6. Ningekuwa mimi, kwa kujua Kristo ndani yng ni mkuu kuliko mazindiko, ningewaambia waendelee na mambo yao wakimaliza waniage halafu napumzika kuwasubiri!

  Niliwaza jinsi ambavyo hakuna namna sumaku ya kufanya ikanasa mti au umeme ukapita kwenye mpira (rubber), vivyo hivyo hicho wanachofanya hapo ni kwa ajili yao. Nitasitisha mamlaka yake kwa muda nitakaokuwa hapo, na kwa kadri nitakavyokuwa karibu na Mungu, hakuwezi kuwa na madhara kwangu kama ambavyo umeme hauna madhara kwa kwa kitu cha mpira.

 7. Nyumba si ya kwako ni ya watu,wewe umepanga tu,unalipia kodi pango. Nyumba ambayo hata hujui ilijengwa lini na pesa zilizotumika kujenga zilipatikana wapi? Kwahiyo hata akija mwenye anataka kuzindika nyumba yake,wewe usibishane nae maana huenda hata pia wakati wa kujenga ilimwagika damu ya mtu kwanza kwenye msingi aliyoipa mizimu na miungu yake anayoiamini. Ikikupata hivyo,mimi nashauri…….kwanza mshukuru Mungu kwa kukujulisha SIRI YA NYUMBA kuwa ina maagano na miungu………then chukua hatua uhame,maana hata mkibishana na mwenye nyumba,ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Maana wewe utabomoa ufalme wa giza kwa jina la Yesu,then atakuja mwenye nyumba na waganga wake nao watajenga tena ufalme wao,jambo ambalo litapelekea mashindano hata kutokea katika mwili. Wakati mwingine unashindwa na kufeli maisha kwasababu umekaa katika nyumba yenye maagano na kuzimu,zimefukiwa vichwa na mambo mengine kama hayo,tena chini ya sakafu kabisa. CHUKUA HATUA,MAANA AKILI UNAZO.Haimaanishi kuwa ukiondoka wewe ni mwoga LA HASHA,bali kama umemhubiria mwenye nyumba INJILI halafu amekukataa,basi nia yako na nia yake haviendani. Kama ingekuwa umemhubiria INJILI halafu akaokoka au akaacha miungu yake basi utaendelea kukaa ktk nyumba,lakini kama amekukataa msiendelee kubishana,usije ukafungiwa nira nae.

  ________________________________

 8. Dah hatua nitakayochukuwa ni kufanya utaratibu wa kuhama tu hakuna njia nyingine kwani sisi wakristo hatuamini matambiko wala mazindiko matambiko na mazindiko nikutoa fungu lakumi tu kwa mungu wetu baasi

 9. Kama umeokoka na umo ndani ya Yesu neno linasema utashinda, mfukuze yeye na mchawi wake yahani mganga, waambie kwa jina la Yesu naharibu madawa yenu na mazindiko yenu yasifanye kazi na kila siraha itakayofanyika juu yangu na familia yangu na mahali hapa ninapokaa haitafanikiwa Isaya 54:17, usiposema ukweli ukawa na woga utakayeathilika na zile tunguli ni wewe unayekaa ndani ya nyumba hile, Kumbuka aliye ndani yako ni mkuu kuliko hao wachawi na waganga na matunguli yao. 1Yohana 4:4.wenzangu waliotangulia hapo juu wamesema vema kabisa kuwa unapokuwa umepanga mda hule uliolipia nyumba hile inakuwa chini yako asante wapendwa . Sheria mojawapo ya Imani ni kutamka unachokihamini na unachokijua Mtamkie huyo mwenye nyumba na mganga wake bila hofu wala woga wafukuze kabisa wakome . ikitokea akakwambia huame hama tafuta nyumba nyingine maana zipo nyingi asitutishie , na ukifanya hivyo utakuwa umemuheshimu Mungu na Mungu baba mwenye huruma
  atakusaidia mbele ya safari, imeandikwa imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Matendo 5:29 . Mtiini Mungu mpingeni shetani naye atawakimbia Yakobo 4:7.

 10. Kama mkristu ninayeamini siwezi kukubali kwa sababu kisheria ukipanga nyumba kama ndg. Stephano kwa muda uliolipia inakuwa chini yako. Hivyo, katika hilo lazima mpangaji uwe na msimamo.

 11. mimim siwezi kukubaki kukubali kuamshwa usiku na wala kuruhusu mganga aingie ndani kwangu kwa sababu ninapokuwa nimepanga nyumba kwa wakati huo ni mali yangu asubiri nihame

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s