Pete ya Uchumba

uchumba1

Wana wa Mungu, Naomba kujua kuhusu pete ya uchumba Je, inatakiwa kumvalisha mchumba wako kanisani, nyumbani kwa wazazi wake, siku ya kutoa posa au kufanya surprise?

–Godfrey E. Kissui

Advertisements

19 thoughts on “Pete ya Uchumba

 1. Ndg Godfrey E. Kisui na wana kanisa wote la kielektronikali SGM, nawasalimu katika jina la Yesu! Kwa habari ya kuvalishana pete nionavyo mimi huwa inategemea huo uchumba ni wa kikristo ama wananchi wa kawaida (Dini zingine/wapagani). Na katika madhehebu ya Kikristo wamegawanyika ktk madhehebu ya kipentekoste, waprotestanti na RC. Kwa uzoefu wangu, wakristo wa RC na waprotestanti hawana ratiba ya kutangaza uchumba unapokuwepo isipokua ktk zile siku 21 kabla ya ndoa halisi. Kwa upande wa madhehebu mengi ya kipentekoste, baada ya kijana kumaliza taratibu za kuwaona wazazi wa binti na kulipa mahari huleta taarifa ktk uongozi wa kanisa na uchumba wao kutangazwa rasmi. Wakati wa kutangaza rasmi uchumba hio ndio huwa nafasi ya kuweza kumvalisha mchumba wake pete ya ndoa. Kwa desturi ya makanisa ya kipentekoste kumuona binti amevaa pete ya uchumba bila ya kanisa kujua ni jambo linaloweza kuleta maswali mengi sana na kutiliwa mashaka. Hatua ya kutangaza uchumba hua ni kwa ajili ya kuwalinda watarajiwa na kanisa kuwaombea ili makusudi yao ya kuoana yaweze kutimia. Ukinipa nafasi kushauri naona kuvalishana pete madhabahuni -kwenye altare ya Bwana ndio mahali sahihi kupita mahali pengine popote. Wazazi ama wawakilishi wao waje pia kanisani kushuhudia tukio hilo na wahusika waombewe kwa kuwekwa mikononi mwa Bwana ktk mahusiano yao hata watakapokamilika kwa kufunga ndoa yao. Mmebarikiwa! Elia Kisigila Pst. Mjoli wa wajoli wa Bwana.

 2. Mpendwa JOHN PAUL , amina kubwa tuimizane tu kwa safari yetu . ya kwenda kumulaki BWANA ARUSI mawinguni

  Siku moja Mungu atukutanishe ndugu

 3. Ndg Rova Olombi, Barikiwa na Bwana Mungu na tuzidi kuombeana katika safari hii ya Mbinguni.

  Tuendelee Kujifunza!

 4. Ndugu JOHN PAUL

  Kweli nimekusoma na tena nimekuelewa kwa makini sana . kufatana naupendo ya MUNGU.Nimeshukuru sana tena sana . Nika kumbuka vile ADAM ya kwanza alipotenda zambi katika shamba la EDENI akafijama . lakini kwa UPENDO kubwa ya MUNGU wetu akamutafuta na kuwapa mafazi . Ile inaonesha kabisa MUNGU ni mwenye REHEMA na MEHEMA ile mbili ni BABU ya masamaha .
  Ndio tusamehane kwa mambo yote sio ya kukumbuka tena MEZALI 16 : 2

  UBARIKIWE

 5. Ndg Rova Olombi,

  Neno la Mungu linasema ni lazima kumsamehe mtu aliyekukosea ili na Mungu aweze kukusamehe makosa yako. Hivyo kama mtu anakataa kusamehe basi naye anajiweka katika mazingira ya kukosa msamaha toka kwa Mungu.

  Sisi kama binadamu tuna makosa mengi na twahitaji kusameheana sisi kwa sisi ndipo na Mungu anasamehe makosa yetu. Tuweke MSAMAHA mbele, ututangulie!

 6. Bwana apewe sifa wapendwa!!
  Asante bw. Godfrey kwa kuleta hoja hiyo. Kwangu mimi nafikiri mara tu baada ya kuvuka hatua ya urafiki na kuingia kwenye uchumba ndipo yafaa kuvishana pete si tu kama ishara ya upendo bali ni kielelezo na utambulisho kwa watu wengine kuwa tayari mlango ya kupokea mchumba umefungwa. Tendo hilo laweza kufanyika kanisani au nyumbani au popote kutegemeana na makubaliano yenu.
  Wachangiaji wengi wameongelea sana kuvishwa pete kwa mwanamke/msichana. Je, hairuhusiwi au ni makosa mwanamume akivishwa pete ya uchumba? Naomba ufafanuzi ktk hili maana huwa najiuliza swali hili pasipo majibu.

 7. Kwa ndugu John Paul,
  Bwana asifiwe nimeshukuru sana kwa na ndiko yako ni kweli kabisa .Sasa kama vile unasema mutu ao mwenzio anakatala Musamaha pale tayari umekuwa UHURU kwa kukamata njia zingine ama kuolewa ao kuowa juu ya tamaa ya mwili . Je kuna njia mingi ya ndoa NDOA kufunjika kama vile ya Mutumishi BENNY HINN leo wamekuwa pamoja na mke wake .

  Kweli nimekufata Sawa Sawa asie kubali masamaha na Mungu anasema nini pale ?
  Ubarikiwe wote

 8. Kwa ndg Rova Olombi,

  Mimi nadhani mtu anapokwenda nje ya ndoa hapo anakuwa amehatarisha maisha yake ya kiroho. Ndiyo. Tunatakiwa kusamehe, lakini mtu akikataa kusamehe hata akiombwa msamaha, huyo anakuwa na maslahi yake binafsi. Pengine anakataa kusamehe ili naye alipize kisasi au hataki tu kuendelea ktk ndoa hiyo.

  Suala la ndoa ndiyo mtihani mkubwa zaidi katika maisha ya mwanadamu. Mtu anayekataa kumsamehe mwenzi wake huyo hataki tena kuwa pamoja naye. Na sidhani kama inawezekana kumlazimisha!

 9. Nami naungana na ndg Daniel Elisante lakini kwa hivi:
  Mambo ya pete ya uchumba yameshamiri sana katika siku zetu. Je, pete hii ya uchumba ni suala la Kikristo au ni la watu wote? Nini hasa ULAZIMA wa pete ya uchumba? Kwani haiwezekani tu kuwaita watu wa karibu, mkatambulishana kwamba mmeanza maisha ya matumaini ya kuja kuoana baadaye? Pete ya uchumba ina NGUVU yoyote ya kumshikilia/kumzuia mchumba asing’atuke na uchumba kuvunjika? Kama siyo, kwa nini basi pete ya uchumba?

 10. HAPA KWELI NAMI NAHITAJI MSAADA WAPENDWA. INANIPAGA CHANGAMOTO SANA. UPI NI MFUMO NA TARATIBU SAHIHI?

  ________________________________

 11. Mimi nadhani hayo ni mapokeo yaliyohalilishwa na binadamu. Kuvishana pete/kuwa na pete si ishara kamili ya upendo kwa mwenza wako. Watu wanapeana pete za uchumba baadaye tena wanavalishana kanisani, wakishaoana mume anaanza kutafuta wadada wengine, mke naye akigundua anajirusha na majamaa huko nje. Hapo pete ina maana gani tena. Cha muhimu kila mmoja atunze ahadi yake ya ndo. UZINZI uwe MWIKO. Vinginevyo watu wanatumia pete kufarijiana tu.

 12. BWANA ASIFIWE

  WANDUGU TAFAZARI SWALI ENYE TUKO NAONGELEA JUU YA PETE ,,,,NI YA MUIMO SANA MBELE YA MUNGU ,,,,,,,,SASA SWALI YANGU MIMI NAULIZA KAMA MUMEFANYA NDOA KISHA NDOA INAFUJIKA AMA BIBI ALIENDA INJE YA NDOA AMA bWANA ALIENDA INJE YA NDOA SASA BIBI AKAKAMATA PETE YAKE AKAKURUDISHIYA NYUMBANI NA KUTOKA ATA ATAKI KUSIKIYA MASAMAHA YAKO .ITAKUWA VIPI ?
  NA MUJUWE NDANI YA NDOA NDIO SHETANI ANAPIGANISHA SANA APA DUNIANI ,NDUGU MUNISAIDIYE NA SWALI IYO

  MUBARIKIWE

 13. Pete ya uchumba ni zawadi kwa mhusika pia ni isha ya kumkubali huyo unayemvalisha,tena hufanyika mbele ya wutu kudhihirisha kuwa umemkubali huyo unaye mvaalisha.Kama ewe ni mkristo ni vyema tendo hilo likafanyika kanisani ikiwa ni isha yakuwa Mungu amejibu maombi yako ya kukupatia mke mwema coz kuvalishana pete ya uchumba passway ya kuelekea ndoa. NI MTAZAMO WAANGU)

 14. Bwn apewe sifa ndg yangu Kissui G??? Ninadhani, ni vyema mambo haya yakafanyika mbele ya kadamnasi ya watu wa Mungu wengi, yaani, kanisani. Ni kweli waweza kulifanyia ktk faragha y nyumbani kwenu, lkn, hao weengi unaoshiriki nao mkate wa Bwn wakawa hawana hbr, na ht km ukiwafahamisha, ridhiko halitakidhika. Kanisa ndo watu wa kwenu, na ndg zako. Na pia, ni vyema, pete ya uchumba ikapata baraka za mikono ya mch wako madhabahuni, pmj, nanyi wachumba wawili kuwekewa mikono ya mch, na maombi y kanisa zima ili uchumba wenu uwe w amani na mafanikio, vinginevyo, kuna kushindwa katikati. Mungu akubariki. Oguda J.E.

 15. pete ya uchumba ni utambulisho kwa watu wote kuwa unategemea kuoana naye (mwanamke/mwanaume huyo). ni tangazo kwa watu wote; nyumbani au kanisani. siyo sapraizi. hata kidogo. ila taarifa ndo yaweza kuwa sapraizi, ila kuvalishana hufanywa mbele ya watu wa karibu kabisa wa pande zote mbili.

 16. Kimsingi,pete ya uchumba “engagement ring” inatakiwa ivalishwe pale mnapotangazia uchumba wenu iwe kanisani au hata nyumbani kutegemeana na wahusika.Bahati mbaya sana si wote wanaofungia ndoa zao kanisani.Kumbuka kuna ndoa za kimila,ndoa za kiserikali na za kidini.Pete ya uchumba ina maana kubwa hasa kwa wachumba si kitu cha kufanya tu ili kufurahishana.Ni moja ya zawadi unayompa binti kama ishara ya upendo wako kwake.Kama unakubaliana na mimi,je kuna haja gani ya kuonyeshea upendo wako mafichoni?

 17. Shallom
  Mimi nauliza kama basi mulifanya ndoa katika kanisa tatizo ika tokeya kwenye ndoa yenu. ama kama Bwana akaenda inje ya ndoa na bibi akakasirika na kukupa PETE ya ndoa amekurudishiya ata kama umemuomba masamaha aina zote na kusema kweli mbele ya Mke alakini apendi kusikiya na ndoa ikavujinga . mimi nauliza. pale utafanya nini na ninyi wote ni walokole .

  MAJIBU KWENU

  Mungu awabariki

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s