Upendo wa Mungu kwetu

jesuslovesu

Salamu kupitia jina la Yesu Kristo.

Wakati wote ninapotafakari kuhusu upendo wa Mungu juu ya maisha ya kila mmoja wetu, uwa nafikia kipindi machozi yanataka kunitoka (Yohana 3:16; Yohana 15:13; Warumi 8:32; Zaburi 84:11; Yeremia 29:11).

Ebu fikiri kuhusu uumbaji wa Mungu na jinsi alivyofanya kuhusu mwanadamu. Ebu kumbuka mwanadamu alivyomwacha Mungu na kuanza kutawaliwa na shetani. Ebu fikiri kuhusu wokovu mkuu unavyomrejeza mwanadamu katika hadhi ile aliyoumbiwa.

Adamu hakuumbwa katika magonjwa, umaskini, matatizo, shida, mahangaiko n.k. Hivyo basi haya yote si sehemu ya maisha yetu. Hata hivyo pamoja na ukweli huu bado wengi wetu wanaonekana kuendelea kuteseka katika mambo hayo. Je, nini hakiko mahali pake kisababishacho mtoto wa Mungu ashambuliwe na mambo hayo?

–Joseph Richard
Advertisements

7 thoughts on “Upendo wa Mungu kwetu

 1. libarikiwe jina la Bwana, kwa kazi munayo ifanya kwa ku ubiri injili kupitiya neti, Mungu awabariki.

 2. Asante sana kaka Joseph Richard, aliyetoa mada hii, asante waliochangia kaka Dan Mbisso,Dada Vai,Kaka John Paul na dada yetu Nshimimana Emmanuel toka Burudi. Mbarikiwe sana kwa michango yenu, Na mimi naongezea hapo kuwa tunapopitia ktk matatizo na magumu siyo mwisho , tukumbuke siku zote kuwa Mungu utenda kazi pamoja na wale wampendao kwa kuwapatia mema Warumi 8:28. pia tukumbuke siku zote na kutamka kama Paulo aliyesema ktk wafilipi 1:19a Kuwa maana ninajua kuwa haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu. Pia tuige mfano wa Daudi tunaona ktk 1 samweli 16 . anapakwa mafuta awe mfalme , lakini ukisoma sura zinazofuatia unaona alipitia ktk mambo magumu na mchungu, Saul alimuonea wivu akasema moyoni mwake nitamwoza binti yangu awe mtego kwake tena kwamba mkono wa wafilisiti uwe juu yake, Naye Sauli akawaambia watumishi wake akasema mwambie Daudi sitaki mahali yoyote hila nataka govi mia za wafilisiti, basi Saul alithani kumuangamiza Daudi kwa mkono wa wafilisiti, 1Samweli 18:21-30. Napenda sana Mungu alivyompigania Daudi ktk kila vita , Saul alimtaka alete govi mia lakini yeye alimletea mia mbili. neno linasema Daudi alitenda kwa busara ktk njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye. Hapa tunaona hata ktk mapito tukimtanguliza Mungu anakuwa pamoja nasi , na tutaibuka kidedea siku zote , atatupa kushinda siku zote. Daudi aliendelea kuteswa na Saul anawindwa kama mnyama , lakini mwisho alisimama ktk kiti na kuwa mfalme kama Mungu alivyokuwa amekusudia , tunasoma pia ktk 1 Nyakati 29:28, Kuwa Daudi akafa mwenye umri mwema , ameshiba siku na mali na heshima, Nataka tuangalie Mungu huyu wa Daudi , piga picha ktk hayo unayopitia na habari ya Daudi ikutie Moyo ujue kuwa Mungu huyu wa Daudi atakufanyia kama alivyofanya kwa Daudi.Kuna kipindi Roh mtakatifu aliniambia kuwa Mary ukitaka kuelewa vizuri kitabu cha zaburi soma kwanza kitabu cha 1 samweli. Pia nimependa huyu ndugu aliyesema kuwa marehemu shetani, nimefurahi sana , maana ni kweli kwa waliokoka na kuamini kuwa Yesu ni Bwana na mwokozi wetu, shetani ni marehemu maana tunahamini kuwa msalabani yote yalikwisha, na pia tunahamini kuwa mwana wa Mungu Yesu alithiilishwa hili azivunje kazi za ibilisi. 1 Yohana 3:8, Pia tunajua kuwa Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea Luka 19;10. Pia neno linasema kuwa kama unahamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu kuushinda ulimwengu ni lazima, imeandikwa kuwa mwenye kuushinda ulimwengu ni nani isipokuwa yule aaminiye ya kwamba Yesu ni mwana wa Mungu? 1Yohana 5:5.na neno linasema kuwa aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye ktk dunia 1Yohana 4:4. Haleluya magonjwa, umasikini, kushindwa, na yote anayoweza kunibambikia shetani hakuna kitakachofanikiwa ktk maisha yangu maana ninaamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, kila linalokumbana nalo kushinda ni lazima nishinde kwa sababu ya yule aliye ndani yangu ambaye ni mkuu sana kuliko aliyeko duniani. Ninawapenda sana mzidi kubarikiwa sana.

 3. Wapendwa Bwana Yesu asifiwe!
  Ninamshukuru Mungu aliemtumia ndugu Joseph kuleta mada hi maana ni muhimu sana katika maisha ya ukristo.
  Ukweli ni kwamba Mungu alimuumba mwanadamu akiwa na lengo zuli sana, yaani alitaka amuakilishe duniani. Alimuumba akiwa na umungu ndani yake wa kumiliki vyote vilivyomo dunuani. Kabla ya kumuumba, tukumbuke kwamba alimutialishiya kwanza vyote ili asipungukiwe cocote. Hayo yanamaanisha kwamba Adamu alikuwa tajiri. Kulikuwa mti wa uzima kana kwamba adamu alikuwa na afya tele. Lakini tukumbuke kuwa Mungu siyo wa vurugu yani kila kitu chake kimepangwa vizuri, diyo maana masharti …..siku utakula kwenye mti wa kujulisha mema na mabaya lazima utakufa… biblia inasema wazi kwamba Mungu Analinda sana neno lake ili alitimize. ( Yer.1:12) Sasa Adamu ameibiwa mamraka yote aliyekuwa amepewa na Muumba na hapo hapo akaanza kujishughurikia mwenyewe haraka alianza kutafuta mavazi mwenyewe. (Biblia haijasema kwamba alijitafutia na chakula, labda alikuwa hajawa na njaa, Mungu asingekuja mapema nja ingempiga na kuanza kutangatanga…!!!) Kwa nini sasa yamempata? Mtoto wa Mungu haishi kwa chakula tu, baali kwa neno lake Mungu (Mt. 4). Alipoibiwa maagizo ya Mungu adamu alipoteza uzima kabisaa na kizazozi chake chote mpaka alipo kuja Yesu Kristo kizazi ca mwanamke kama alivyo sema Mungu kule Edeni.
  Biblia inasema kwamba Mwana wa Mungu (Yesu Kristo) alikuja ili aziharibu kazi zote za shetani. Vipi aliweza kuziharibu sasa? Alimnyang’anya mamlaka yate pale msalabani, Nifuate vizuri ujuwe kwa njia gani amemyang’anya:
  SHETANI HAKUJIPA MAMLAKA? HATA YESU SHETANI ALIMWAMBIA KWAMBA AMEPEWA ( matayo 4:12) ALIPEWA NA ADAMU NAKUANZIA HAPO AKAANZA KUMTAWALA AKIMKANDAMIZA SANA YEYE NA KIZAZI CHAKE KWA UMASIKINI, UGONJWA, DHAMBI NA MAMBO YOTE MABAYA KAMA MNAVYO JUWA MPAKA KUWAWUWA NA KUZIWEHA RAHO ZAO JEREZANI. SASA MUNGU NI MWENYE HAKI HUKUMU ZAKE NI ZA HAKI KATIKA ULIMWENGU WETU NA ULIMWENGU WA ROHO, KWA HAYO KAMBA ANGEMSHAMBULIA SHETANI NA KUMYANGANYA MAMRAKA SHETANI NA KUMURUDISHIA ADAMU TIALI ANGEKUWA MBALI NA HAKI NA HAYO KWA MUNGU NI KAMA SUMU. iLIBIDI SASA MUNGU AANDAE NJIYA NYINGINE KATIKA HAKI NA KWELI KWANJIA AMBAYO SHETANI HAKUWEZA KUTAMBUWA. SHELIA MPYA ILITENGENEZEWA PALE PALE EDENI? MUNGU AKASEMA: KIZAZI CHA MAMA HUU KITAKUPONDA KICHWE…..MWANZO 3.
  MYAKA NENDA RUDI YESU KRISTO AKAZALIWA NA BIKIRA MARIAMU? KUMBUKA YESU SIYO MBEGU YA MTU? ASIRI YAKE NI YA MUNGU WAFILIPI 2, SHATENI AMEPEWA MAMRAKA JUU YA KIZAZI CHA ADAMU TU SASA YESU SIYO KIZAZI CHA ADAMU, NI KIZAZI CHA MUNGU KUPITIA MARIAMU? SHETANI HAKUJUWA SIRI HIYO ALIMUFANANISHA YESU NAYE AKANYAMANZA NA UTAONA MALA NYINGI YESU ALIJIITA MWANA WA ADAMU NA SHETANI AKAYAELEWA HIVYO MPAKA YESU ALIPO KUFA. KUMBUKA PETRO ALIMUITA KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI NA YESU AKAMUAMBIYA ASIWAMBIYE WATU UNAJUWA NI KWA NINI? HAKUTAKA KUFUNUWA SIRI AMEN! MAANA ANGEJUWA ASINGEMUUWA YESU.
  ALIPOMUUWA SASA SHELIA ILIMUSHIKA SHETANI KWA MANA ALIUWA MTU WA WENGINE SIYO WAKE KI ASIRI NDIPO AKANYANGANYIWA MAMRAKA YATE JUU YA WANADAMU MAANA AMEFANYA KOSA SANA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
  kUANZIYA HAPO YESU AMEKUWA HAKIMU SASA WA WANADAMU HEBRANIA 7:22-25 .
  sASA KWA NINI WATU WA MUNGU WANASUMBUKA? NI KWA SABABU HAWAJUWI HAKI YAWO KATIKA AGANO JIPYA YOTE YESU AMEYAMALIZA SASA NI MUDHAMINI WA KANISA. ( KWAWO WOTE WALIOZALIWA MALA YA 2) HALELUA!!! SOMA VIZURI WARAKA WA WAEFESO NA UTAFAKARI UTAONA SANA WEWE NI NANI NA HAKI YAKO NI IPI KTK KRISTO. NINOMBA ROHO WA MUNGU AKUFUNULIYE MENGI KATIKA JINA KUBWA LA YESU KRISTO.
  MUBARIKIWE WAPENDWA!!!!

 4. Labda mambo mengine ya kujiuliza hapa ni:

  Umasikini ni nini?
  Utajiri ni nini?
  Mtu anapataje utajiri?
  Neno la Mungu linasemaje kuhusu utajiri na umasikini?
  Yesu Kristo alileta nini Duniani?
  Je, Yesu alikuja kuleta na Utajiri?

  Hayo ni baadhi tu ya vipengere vinavyoweza kutusaidia kujadili suala hili ili tusijikute tunajadili pasipo msingi.

 5. Wapendwa wana wa Mungu namshukuru Mungu kwa ajili ya Joseph maana ameleta mada nzuri sana.
  Nikweli kabisa kwamba Mungu alipomuumba Adamu hakumuwekea matatizo yoyote wala laana, mauti, magonjwa hayakuwepo ndani ya bustani ya Edeni. Maana “KILA ALICHOKIFANYA MUNGU NATAZAMA KILIKUWA NI CHEMA SANA – MWANZO 1:31” Tunaona laana, mauti, magonjwa, mafarakano n.k. yalitokea baada tu ya Adamu kuliacha AGIZO/NENO la Mungu alilokuwa ameagizwa na Mungu. Pia kitu ambacho marehemu shetani aliiba kwa Adamu ni NAFSI HAI ya Mungu ambayo ilikuwa ndiyo imebeba HISIA ya Mungu, AKILI ya Mungu, HIARI ya Mungu/HIARI MOJA na MATAMANIO YA MOYO ya Mungu mwenyewe. Adamu aliibiwa NAFSI HAI ya Mungu na shetani, na akapewa nafsi mfu ambayo ni nafsi ya shetani iliyobeba mauti, laana, magonjwa,vilio, huzuni, mikosi, kuchukiwa, uchungu, dhambi, uovu na mambo mabaya yote yanayowapata watu na wanadamu. Pia baada ya Adamu kuacha AGIZO tunaona hakuna mahali popote ambapo tunaona TOBA YA KWELI ikifanyika hivyo laana,mauti, magonjwa, umasikini, ujinga n.k viliendelea kulitesa KANISA au WANA WAA MUNGU. kumbuka pia Adamu alikuwa akiliwakilisha KANISA hivyo basi si kwamba Adamu ndiye alianguka kwenye uovu bali KANISA ndilo lilianguka kwenye uovu na kujikuta linatembea kwenye mateso mengi na dhiki kubwa na ndiposa DINI NA MADHEHEBU yalianzishwa yakaiba nafasi ya KANISA yakajiita kuwa nayo ni makanisa. Pia kitu kingine kilichotokea baada ya anguko la ADAMU/KANISA marehemu shetani ndiye alikuwa anamiliki na kutawala juu ya uumbaji wote badala ya Adamu/ Kanisa kama Mungu alivyokuwa amekusudia tangu mwanzo. Hivyo KANISA/ADAMU akawa chini ya utawala wa mambo yote mabaya yaliyotengenezwa na Marehemu shetani. Pia marehemu shetani alibadilisha majira na nyakati za Mungu akatengeneza majira za uovu zinazoitwa siku za Jumatatu/Moonday – Jumapili/Sun day badala ya majira ya siku ya 1-7 “Mwanzo 1:1-31” na akatengeneza miezi ya January – Decemba badala ya mwezi ABIBU/NISANI – ADARI “ESTA 3:7″. Kwahiyo hapa tunaona wazi kabisa kuwa majira aliyokuwa ameitamka Mungu mwenyewe kwenye NENO/ KITABU CHA NENO ilifichwa na dunia na badala yake KANISA / WANA WA MUNGU tukawa tunatembea kwenye majira za uovu zilizobeba laana, mauti, magonjwa, umasikini, mateso ya kila aina bila sisi kujua. Lakini sasa tunamshukuru MUNGU WA ELIYA, MUNGU WA KANISA LA KWELI, MUNGU WA SILOAM, MUNGU WA KIZAZI CHA NNE AMBAYE NDIYE MUNGU WA KWELI AMETUFUNULIA WANA WA MUNGU SIRI HII KUBWA ” 1KORINTHO 2:6-10″ KUPITIA NABII WA KWELI ELIYA NA HIVI SASA KANISA TUMESHINDA,TUMEREJESHEWA NAFSI HAI YA MUNGU, HIVYO KANISA TUKO JUU YA MAGONJWA YOTE NA LAANA ZOTE ZIMEFUTWA JUU YAO WOTE WANAOLIAMINI NENO AMBALO MUNGU AMELIWEKA NDANI YA KINYWA CHA NABII ALIYEMWITA KATIKA JINA LA YESU.

 6. Mpendwa Joseph and wana SG wote,

  Nawaslimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo! Hata mimi kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari ni kwa nini mahangaiko na dhiki vimekuwa ni seheme u ya maisha ya watoto wa Mungu. Nimejifunza kuwa wakati mwingine Mungu huruhusu hayo yatupitie kwa makusudi yake yaliyo mema. Tunaona jinsi ambavyo Yakobo, baada ya kudanganya katika harakati za kupata ‘uzaliwa wa kwanza’ kutoka kwa kaka yake Esau (Mwanzo 27) alikimbilia kwa mjomba wake. Huko aliteseka kwa jumla ya miaka ishirini akifanya kazi katika boma la mjomba wake kabla ya kurudi Kaanani (Mwanzo 28-31). Tunaona jinsi baada ya hayo yote, Yakobo alikuwa ‘disciplined’ na ‘character’ yake kubadilika kabisa na kuwa mtumishi wa Mungu kama jinsi Mungu mwenyewe alivyomtengeneza. Yakobo akaanza kumtegemea Mungu na kumtukuza kwa kila jambo kuliko ilivyo kuwa awali (angalia alivyokuwa akisemezana na Labani alipokuwa akijaribu kukimbia- Mwanzo 31:38-42).

  Mfano mwingine ni ndugu yetu Yusufu ambaye ilibidi apate dhiki kwa miaka 13 kabla ya kuinuliwa na kuwasaidia ndugu zake na hatimaye kujenga taifa la Israel (Mwanzo 37, 39-47). Tazama pia maisha ya Ayubu ambaye alikuwa ‘mkamilifu na mwelekevu’ (Ayubu 1: 1) lakini Mungu aliruhusu dhiki impitie kwa muda.

  Jambo nililojifunza kwa watu hawa wote ni kwamba mateso na dhiki ni mambo ya mpito tu, na kama Mungu ameyaruhusu ni kwa ajili ya mapenzi yake mema kwetu (Warumi 8:28).

  Mungu awabariki sana!

  Daniel.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s