Isije Ikawa Umembeba Yona!

HadithiyaYona

Kwenye Biblia, katika Kitabu cha Yona, tunapata habari za watumishi wa ile Melikebu aliyopanda Yona, jinsi walivyohangaika baharini, wakatosa mizigo yao wakitafuta ufumbuzi wa namna ya kupita katika ile dhoruba lakini haikusaidia. Walipomtosa Yona Baharini DHORUBA ilitulia, wakafanikiwa kuendelea na safari yao.

Yawezekana unafanya kazi pamoja na mtu, au unashirikiana naye. Lakini mambo yamekuwa hayaendi. Kabla hujawa naye mambo yalikuwa sawa tu, lakini sasa DHORUBA ni kubwa. Unajaribu kuacha baadhi ya mambo/Majukumu ili muweze kujikita katika machache lakini bado haisadii. Kaa chini.

Omba Mungu akufunulie. Wale jamaa wa kwenye melikebu walipiga kura, ikamwangukia Yona. Yawezekana uliye naye hapo AMEKIMBIA KAZI YA MUNGU/WITO ama kwa kujua au kutokujua. Pengine alitakiwa achunge Kanisa au alitakiwa awe mahali fulani akiihubiri Injili. Utashangaa, mkigundua kusudi la Mungu lililo nyuma ya matatizo mnayopitia, amani itapatikana na SHUGHULI yako Itasimama Imara Tena!

Advertisements

5 thoughts on “Isije Ikawa Umembeba Yona!

 1. Rova! Unataka kumtosa mtoto wa Mungu baharini? Eh! Ni hatari sana kuwaza jambo kama hilo juu ya wana wa Mungu! Yona, alikuwa ni nabii! Nabii ni mbeba ujumbe na maono ya Mungu kwa watu wake. Hukumu zao huwaga Mungu mwenyewe anazishikilia.

  Ndiyo, alijaribu kumkimbia Mungu, kuikimbia kazi aliyotumwa kuifanya, akabadili njia na kuelekea Tarshishi badala ya Ninawi alikotumwa! Lakini kuna jambo hapo ambalo ni zaidi ya huko kukimbia. Mungu anapokutuma kazi fulani, Yeye Mwenyewe huwepo kuitimiza. Tena njia za kuitimiza huwa anazo Yeye na si nabii anayemtuma! Naye Mungu anatuambia kuwa kusudi lake ni lazima litimie. Kwahiyo ni kwa jinsi gani Yeye amepanga kusudi lake litimie, jambo hilo hujifunua kwa kadri anavyolikamilisha kusudi lake.

  Ndipo twafahamu sasa kuwa kukimbia kwa Yona kulikuwa ndani ya kusudi la Mungu, ili apate kujitukuza kwa hao wasioamini kwanza, na kisha awarejeshe wanae waliokuwa huko Ninawi!

  Pale ile merikebu ilipokamatwa katika tufani na usalama wa abiria wake na mizigo kuwa hatarini, nazo jitihada zao za kujiokoa zilipoonekana kushindwa, waliigeukia miungu yao kwa msaada, wapate KUOKOLEWA (Yona 1:5 “Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake …”). Lakini kila walivyoiomba miungu hiyo, hali ilizidi kuwa mbaya. Jibu la maombi yao kwa hiyo miungu yao lilikuwa ni kuongezeka kwa dhoruba!!! Lo! Walikuwa ni watu wenye kukata tamaa kiasi gani, matumaini ya kuishi yakitoweka machoni pao, miungu yao imejificha, dini zao hazikuwa na msaada wowote! Ndipo wakamkuta Yona amelala fofofo licha ya makelele ya maombi na sala za nguvu na mayowe na upepo na dhoruba zinazoipiga merikebu!

  WAKAMSHANGAA!!! He was the ODD person in the boat! Wakiwa katika butwaa, wakamkusanyikia hapo ili wajue kulikoni hata awe amelala fofofo katika kitim tim kile! Wakajiagua kuhusu balaa lililowakumba, hilo lililozifunga mbingu miungu yao isiwasikie, nayo kura ikamuangukia Yona! Ni yeye pekee ambaye alikuwa hajayapeleka maombi ya kuokolewa kwa Mungu wake, “Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.” Wakamhoji ili kumbaini, na alipomaliza kujitambulisha na kuwapa maelezo ya safari yake, yaani ile Injili ya wokovu; akiwaambia kuwa wokovu wenu uko katika KUMTII MUNGU wangu! Walisita kuyatii maagizo aliyowapa Yona, wakajaribu kujiokoa wenyewe kwa kanuni zao na “Sheria zao za Maadili” ya kibaharia, yaani dini zao; wakaongeza jitihada ili waifikie pwani, dhoruba ikawa kali zaidi kwa kadiri ya jitihada zao! Walipoona wameshindwa, wakamgeukia Yona na KUIPOKEA ile Injili, lile ONO; wakaiachilia miungu yao iliyoshindwa, “Basi wakamlilia BWANA, wakasema, Twakuomba, Ee BWANA, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, BWANA, umefanya kama ulivyopenda”; wakaitii ile SAUTI kutoka kwa Yona, wakamtosa baharini; KUKAWA SHWARI! Maandiko yanasema wapagani wale WAKAMUOGOPA Mungu wa Waebrania! “Ndipo wale watu wakamwogopa BWANA mno, wakamtolea BWANA sadaka, na kuweka nadhiri”, kama ambavyo wapagani wa leo na miungu yao, wangesimama na kumuogopa Mungu wetu katika Kristo, iwapo nasi tungesimama na Neno, nazo ishara tulizoahidiwa zinapofuatana nasi! Lakini badala yake tunajiunga na makundi ya kipuuzi ya mihadhara ya dini inayozalisha chuki na insecurity, kinyume na utukufu wa Mungu unaopaswa kutufunika.

  Basi huko baharini walikomtosa, Mungu alimtayarisha samaki maalumu wa kumsafirisha Yona. Akiwa katika tumbo la yule samaki, Yona aliutafuta mwelekeo wa Hekalu la Suleiman, maana hilo liliibeba ile Ahadi ya kusikilizwa watakapolielekea kwa maombi, ule mfano wa Kristo, unaona, “Ombeni lolote kwa jina langu…”!!

  Ninawi ulikuwa ni mji wa wavuvi, naye mungu wao alikuwa ni nyangumi. Yule samaki alipofika pwani na kufungua kinywa chake, wavuvi wote walisimama na kupigwa butwaa na kisha kujitupa chini ili kuabudu, mungu wao amewatembelea!! Ndipo wakamuona Yona akitoka katika kinywa cha samaki huyo, mzima mwenye afya, tena aliye na ujumbe kutoka kwa Mungu aliyemtuma mungu wao amsafirishe! Wakaipokea INJILI, wakatubu na kuachana na miungu yao!!!

  Nayo Ishara ya Yona, katika Kristo, Mungu aliirejea tena katika kuukamilisha wokovu wetu.

  Basi mnapolitafakari jambo la kumtosa mwana wa Mungu aliye miongoni mwenu, labda kwa kuyumba kwa baraka zenu, hakikisheni kuwa yeye mwenyewe ndiye anayewapa ushauri huo wa kumtosa, ili kwenu nanyi kurejezwa kwa baraka hizo kuwe ushuhuda kama ilivyokuwa kwa wale wapagani!

 2. Excellent and powerful short and clear msg., bless u dabo-dabo,

  East-West thought!…..On one hand, kweli inawezekana amekacha kazi ya BWANA ivyo mbingu iko kinyume naye, On the other hand, inawezekana uliye naye hapo hajakacha kazi but simply ni agent tu wa devo hence katika maombi pia utafunuliwa kua jaamaa uyo( boss job, wa chini yako, house girl/boy, member ktk kwaya, mchungaji wako msaidizi, fellow mpendwa, fellowship member, ana serve master mwingine na ameji-commit uko ingawa kwa nje ni kama yuko kwetu/kwako ndio maana mambo yanakwama/breach/abort/hayakwendi/siri zavuja/ hali ya mbinde-mbinde hudumani nk. On the extreme hand, yawezekana uliyenaye hapo wala si satanic agent, na wala hachakacha huduma ya mbinguni bali ni mpendwa tu mzembe/mvivu/hasiye-prioritize mambo/maono ya kanisa/Mchungaji wake kwanza, aliye busy na kaizari tu, ana-lack of knowledge ndio maana anangamizwa na mambo ya Mungu na watu wake wanaangamizwa, yaani ameookoka but yupo yupo tu,,,anaweza kata mwezi hata kusema na one human kuhusu kuokoka au kukata week bila kusoma Neno kwakwe sawa tu ivyo mambo kwa ujumla yake binafsi, anapokaa, kanisani, kikundini-kanisani, hayakwendi kwa kua kiungo kimoja ktk body of Christ ni ”mnyooo” kabisa na tegezi kweli.

 3. Kweli wna ya Mungu iyi ndio NENO la MUNGU kama vile sisi wakristu apa Duniani tuko kama vile ndani ya chombo . kwa mufano dunia ni bahari Dhuruba ni matatizo ya jamaa ya rafiki ya mke ama mume na umaskini na utajiri na magonjwa na NK. ile inaleta Dhuruba ukikuwa na wasiliano na MUNGU wako utatupa YONA majini kwa IMANI. iyi ndio NENO ya kiroho na ndio Dhuruba itapowa ndani ya Maisha yetu.NENO iyi Mungu akupe macho ya Kiroho utahelewa kabisa

  Mungu awabariki

 4. Hii ni kweli kabisa. Naamini hapo wengi tunakosea hapo kwa kufikiri kila tatizo ni la KUKEMEA au KUFUNGA NA KUOMBA. Kuna mengine hayaishi hata kwa kufunga na kuomba. Matatizo mengine dawa yake ni KUSIKILIZA Mungu anataka uwe wapi!
  Hata kama Yona angekemea vipi, dhoruba ile isingekoma!
  Mungu atusaidie tuweze kuisikia sauti yake.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s