Napenda Kumpokea Bwana Yesu, lakini ni muislamu!

YesuniMungu

Bwana Yesu asifiwe, Mimi nataka kuokoka lakini muislam, nataka kumpokea Bwana Yesu katika maisha yangu sitajali kuhusu ndugu na wazazi wangu, Huu ni uamuzi wangu mimi.

Naombeni ushauri maana sijui pa kuanzia na muniombee niweze kuyashinda majaribu katika maisha yangu.

AI

Advertisements

20 thoughts on “Napenda Kumpokea Bwana Yesu, lakini ni muislamu!

 1. UMECHAGUA FUNGU JEMA
  TAFUTA WATU WALIO OKOKA UUNGANE NAO KWA SAFARI YA KWENDA MBINGUNI

 2. Hongera mpendwa kwa uamuzi wako mzuri wa kuchagua njia iliyo sahihi muombe Mungu kwa bidii zote naimani majaribu yote utayashinda,ubarikiwe sana.

 3. NENDA KANISA LA WALOKOLE LILILOKARIBU NAWE HARAKA WALA USISIKILIZE USHAURI WA MTU YEYOTE ASIYEOKOKA YESU YUPO NAWE SAIV

 4. Mungu akubariki tembelea kanisa la Wokovu liloko karibu nawe .Neema ya Mungu Itakuwa nawe

 5. SERIKALI ZETU, JAMII ZETU, NDUGU ZETU, FAMILIA ZETU, DINI ZETU PAMOJA NA MARAFIKI ZETU WANAOTUZUNGUKA…..Ni vikwazo vigumu mno kwa watu wengi wanaotaka kuyakabidhi maisha yao kwa bwana yesu!!. lakini wanaweza kukabili vikwazo hivyo kwa kuiambia jamii yote hiyo inayowazunguka hivi: NIMEKUTANA NA BWANA YESU KATIKA MAISHA YANGU YA ROHONI,AKANISISITIZA KUWA NIITAFAKARI NJIA YANGU NINAYOITUMAINI,KWA KUJIFUNZA ZAIDI NENO LA MUNGU KATIKA BIBLIA. Baada ya hapo,ili kusudi lako la rohoni liweze kuwa dhahili kwao,basi endelea kuwapa ushuhuda wako huo kadili wanapokuhoji,huku ukiwa muwazi kwa kila mtu ambaye ni kikwazo kwako…huku ukiendelea kumuomba Mungu kila wakati pamoja na kumuita na kumkaribisha bwana yesu akae ndani ya fikra zako,mawazo yako na rohoni mwako.Katika wakati huo,kujifunza neno la Mungu ni muhimu sana tena inakupasa ujifunze kwa biidii zote lakini ni lazima kupata msaada kutoka kwa waalimu mbalimbali wa neno la Mungu pamoja na kukuza mitazamo yako kutoka kwa wakristo mbalimbali kwa mfano kushiriki kimawazo katika blog za kikristo kama hii.Pia ni lazima uanze kujitenga na njia usioipenda huku ukiipenda njia ya biblia kwa kulisoma neno la Mungu pamoja na kujifunza kwa biidii yako yote kwa kuwa neno la Mungu ndilo silaha pekee ya kuzishinda hila za shetani,yaani KUUJUA UKWELI WA MAMBO.Wakikuuliza “shekhe mbona waisoma sana biblia na kujifunza sana mambo yake,wataka kuwa mkristo nini?….wajibu kwa busara hivi: NAJARIBU KUJIFUNZA KILE BWANA YESU ALICHONISISITIZA KUWA NIITAFAKARI NJIA YANGU NINAYOITUMAINI KWA KUJIFUNZA ZAIDI NENO LA MUNGU KATIKA BIBLIA.Istoshe ushindi wa jambo hili la kujifunza neno la Mungu na kulifuata katika biblia kwa biidii yako yote ni mwepesi mno kwa kuwa kama ni kweli sio ruhusa kwa muislamu kujifunza mambo ya biblia mbona Mashekhe, Maimamu na vijana wengi wa kiislamu wanaisoma na kuijua kwa kiasi kikubwa biblia!!…kwanini kwako uogope kutishwa kana kwamba ni kosa la jinai?? Hapo nafikiri ni parahisi lakini panahitaji ujasiri wako mwenyewe, Wao wakiisoma biblia kwa lengo la kutafuta makosa ili waikosoe basi tumia nafasi hiyo na wewe ya kuisoma biblia ili kuiamini,kuijua vyema na kuikumbatia vyema kuwa ni neno la Mungu lenye kuleta wokovu kwako.TUMIA NAFASI HIYO KWA KUJIPIJISHA HATUA NA KUJIJENGA ZAIDI KATIKA BIBLIA NENO LA MUNGU. Kumbuka ndugu ya kuwa katika hili, usiogope bali ni lazima uwe na maamuzi yako binafsi pamoja na biidii yako ya rohoni ambayo Mungu mwenyewe atakua akikuona na kukusaidia hatua kwa hatua kukufundisha na kukuonyesha mambo yake makuu yaliyositirika kwa wateule wake….hivyo kamwe usikatishwe tamaa na mtu yeyote.Yeye kupitia nabii isaya alitangaza hivi: NIITE NAMI NITAKUITIKIA,NAMI NITAKUONYESHA MAMBO MAKUBWA MAGUMU USIYOYAJUA.(Yeremia 33:3).Nisisitize jambo la msingi tena ya kwamba ni lazima uwe na maamuzi yako ya rohoni wewe mwenyewe kwa sababu siku ya mwisho mbele za Mungu hakutakuwa na mambo ya kusingiziana bali kila mtu atauchukua mzigo wake wa dhambi yeye mwenyewe kama atakua ameshindwa kupita katika njia sahihi za wokovu wa Mungu eti kwa sababu ya kuogopa MAKATAZO NA VITISHO VYA WATU!!!….Muite bwana yesu ambaye ni dhihilisho la Mungu asieonekana kwetu,nae akiisikia sauti yako ya kweli kutoka rohoni mwako isioogopa makatazo na vitisho vya wanaadamu,basi nae atakusikia na kuja kwako ili kukufumbua macho na kukuonyesha njia ya kumfuata.Kumbuka ya kwamba katika biblia,Yule mwombaji kipofu,alikuwa ameketi kando ya njia kama wewe,nae aliposikia ya kwamba ni Yesu mnazareti anaepita, alianza kupaza sauti yake na kusema “mwana wa daudi yesu unirehemu….biblia inasema “NA WENGI WAKAMKEMEA ILI ANYAMAZE LAKINI ALIZIDI KUPAZA SAUTI “MWANA WA DAUDI UNIREHEMU!!!….YESU AKASIMAMA,AKASEMA,MUITENI….Wakamuita yule kipofu na kumwambia jipe moyo,inuka anakuita,yule kipofu akatupa vazi lake,akaruka,akamuendea yesu,Yesu akamjibu unataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia mwalimu wangu nataka ,NIPATE KUONA’.Yesu akamwambia enenda zako IMANI YAKO IMEKUPONYA….Mara akapata kuona “AKAMFUATA NJIANI.!!!!.Soma(marko 10:46-52)…Kwa hiyo, Pasipo kuogopa makatazo ya wanaadamu ni jukumu lako wewe kumuita bwana yesu kwa roho na imani yako yote mbele zake ili na yeye aisikie sauti yako ya imani ya kweli kutoka moyoni mwako, apate KUYAFUMBUA MACHO YAKO NA KUKUONYESHA NJIA. Kama kipofu yule asieona wala kuwa na uwezo wa kujitetea kwa lolote alipata ujasiri wa kutoyaogopa makatazo na vitisho vya watu….je, wewe sio zaidi??!!….”TAZAMA NASIMAMA MLANGONI NABISHA,MTU AKIISIKIA SAUTI YANGU NA KUUFUNGUA MLANGO,NITAINGIA KWAKE NAMI NITAKULA PAMOJA NAYE NAYE PAMOJA NAMI.(ufunuo wa yoh3:20).Utakapo fikia hatua hizi katika bidii yako,wataanza kukuzoea na kukuita mzee wa kuyachunguza maandiko kama shekhe ponda au dada/mama wa kufuatilia maandiko….jambo litakalokupa urahisi wa kwenda kanisani na kubatizwa na kuwa mkristo rasmi.Lakini kama ni kweli lengo lako ni kutoka gizani basi usiruhusu kutumia miezi zaidi ya minne kukamilisha kusudi lako bali ni miezi miwili mpaka mitatu au haraka iwezekanavyo kwa kuwa hakuna haja ya kumuhofu zaidi mwanadamu kwa kuwa huo ni wito kutoka kwa Mungu mwenyewe…kazi ya miezi hiyo michache haswa ni kujijengea mazingira ya ufahamu zaidi katika makusudi ya njia halisi unayoipenda huku ukiachia njia dhaifu ya upande ule usioupenda.MWISHO WA MAWAZO YANGU.

 6. HONGERA KWA KUIKUBALI SAUTI YA MUNGU MAANA SI WEWE ULIYEMCHAGUA BWANA YESU BALI YEYE NDIYE ALIYEKUCHAGUA WEWE. HAKIKA MUNGU AKUBARIKI NA NI MAOMBI YANGU KWAMBA MUNGU AKUPELEKE MAHALI SAHIHI PA KUMWABUDU YEYE KATIKA ROHO NA KWELI. HONGERA KWA USHINDI NA KARIBU NDANI YA KIZAZI CHA NNE UJIFUNZE NENO NAWE UTAPATA UFAHAMU NA KWA HAKIKA UTAUFURAHIA WOKOVU WA KWELI!

 7. Hongera sana kwa uamuzi sahihi uliamua. Hakika Bwana Yesu ndiye njia ya kweli hivyo usiogope fanya tekeleza uamuzi huo sasa. Mungu akubariki na akusaidie.

 8. karibu ndg, hayo ni maisha yako hayaangalii ndugu wala wazazi kwani kila mmoja atahukumiwa kwa namna yake wakati wako ni sasa mpokee yesu katika maisha yako, mizigo yote uliyonayo itakuwa miepesi

 9. naomba mumsaidie kuwasiliana na mwinjilist peter rashidi aweze kumsaidia kwqa mujibu wa elimu ya dini yas kiisalamu contact for peter rashidi ni 0688432950-0754538017-0715538070

 10. Hongera sana umechagua fungu lililo jema, Mungu wetu akutie nguvu katika safari hii nzuri ambayo Mungu ameianzisha maishani mwako!

 11. OPEN UP TO YOUR LORD IS NOCKING AT YOUR HEART DOOR,THEN AFTER ACCEPTING HIM IT IS ALL ABOUT STANDING FIRM AND MOVING FORWARD, IF YOU WILL NEED SUPORT FROM YOUR FELLOW MUSLIM REPENTED TO GLORIOUS JESUS I HAVE SOME FEW AND IF YOU WILL LOVE TO GET TESTIMONOIES FROM THEIR EXPERIENCE WITH JESUS MIDST OF THEIR FAMILIES.

 12. Bwana Yesu apewe sifa wana wa Mungu. Napenda kukutia Moyo ndugu unayetaka kumpokea Bwana Yesu. Kwanza kabisa nikupe hongera kwa kuwa msikivu kwa wito wa Bwana Yesu na kuwa wokovu ndio njia hasaaaa ambayo watu wote yafaa waifuate bila kujali dini na madhehebu yao.

  Usiogope kwanza Bwana Yesu si mkristo bali Yeye ndiye mwanzo wako na mwisho wako wewe, alikuja duniani kwa ajili ya kila mtu ukiwemo na wewe. hivyo uamuzi wa kumgeukia Bwana Yesu kimsingi ni kwamba unarudi nyumbani baada ya kupotea njia na kutangatanga weeeee!! sasa unarudi nyumbani. ubarikiwe.

 13. kiri na kuamini kwamba Bwana YESU Ni Mwokozi wa maisha yako…

  fanya maombi na soma Biblia kwa spidi kali katika vitabu vya Mathayo, Marko, Luka na Yohana..tafuta kusanyiko linalomuamini Yesu Kama ni Bwana na Mwokozi wa ulimwengu alikufa na kufufuka katika wafu,,hafu uungane nao ujifunze zaidi.

  Hongera na Bwana YESU Asifiwe kwa kukuwezesha kufanya uamuzi bora kabisa wa kuokoka..karibu kwa Yesu..

 14. Ndg AZ,
  Kwa kuwa umeshaamua kutokujali ndg na wazazi (ambao bila shaka nao ni waislamu), basi chukua hatua ya VITENDO kwa kwenda katika kanisa lililo karibu nawe WANAPOUKUBALI na WANAFUNDISHA HABARI ZA WOKOVU wa Yesu Kristo. Ukifika pale mtafute mchungaji au muhudumu, umweleze UAMUZI wako naye, kwa hakika, ATAKUSAIDIA!

  Inawezekana kusali SALA YA TOBA, kwa imani, katika mtandao hata hapa hapa SG lakini ni VEMA ikifanyika mbele ya mashahidi, wakuone nao uwaone uwatambue ndg zako nao wakupokee!
  Hongera!

 15. Bwana asifiwe
  Amina ndugu Kaka ama Dada njia ile unapenda kumufata Bwana wetu YESU ndio NJIA ,KWELI NA UZIMA akuna njina ingine apa jni ya jua watu wanapasha kuokolewa nalo ila njina la YESU . tafuta kanisa enye iko karibu nawe ya Kiroho Mutumishi atakusaidia kwa kukuwa mukristu .

  UBARIKIWE NDUGU

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s