Watu 4 wafariki kwa ajili ya “Mafuta ya Upako”

mafuta

Jumla ya watu wanne wamefariki Jumapili nchini Ghana, walipokuwa wakikanyagana kwenye huduma ya “Mafuta ya Upako” katika kanisa la Synagogue Church of All Nations lililoanzishwa na Mtume TB Joshua wa Nigeria.

Msemaji wa polisi wa Mkoa wa Greater Accra kamanda Freeman Tetteh alisema wengine 15 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Mr Tetteh alisema waliokufa walikuwa wanawake watatu na mtu mmoja lakini umri haukujulikana.

Kufuatia vifo vya watu hao “polisi wameshauri viongozi wa kanisa kuacha usambazaji wa mafuta ya upako,” alisema.

Baadhi ya viongozi wa makanisa wamelaani jinsi anavyoendesha ibada zake, wakati wengine wamehoji historia yake kama mkristo.

Hata hivyo Mtume Joshua, amekanusha madai hayo kwamba hayana msingi na ni wivu kwa watu wanaotishiwa na mafanikio yake.

Africareview

 

Advertisements

91 thoughts on “Watu 4 wafariki kwa ajili ya “Mafuta ya Upako”

 1. Ndugu zangu mambo yote yapo wazi ,kinacho wasumbua watumishi wengi wa tz ni kuwa na imani za kusitasita neno lina sema mwenye haki ataishi kwa imani yake lakini akisitasita sin haja naye (yaani mungu hana haja naye).Kumbuka wote walio fanikiwa kihuduma kiwango chao cha imani kimekuwa juu sana na ndio maana unaona wanafanya mambo makubwa kupita vile wengi wanavyo fikiri Soma zekaria 7:11-13 .Kuhusu kubariki mifugo mazao na vingine vilivyo tajwa vimeandikwa ndani ya bibblia soma kumbukumbu 7:12-15 tusiwe wavivu wa kusoma biblia yatupasa kumtukuza mungu na siyo shetani ya kwamba yeye anaweza kufanya mambo makubwa kuliko mungu aliye hai ,kumbuka yesu amesema lolote mlioombalo kwa jina langu na baba yangu wa mbinguni atalifanya soma yohana 14:11-14.Hapo tafuta nini maana ya lolote sisi shida yetu tumempa mipaka mungu ya kufanya wakati yeye hana mipika.Tuliamini neno lamungu.

 2. Ulimi ni kiunngo kidogo lakini maangamizi yake ni makubwa tusiwe wepesi wakutamka jambo pasipo kukaachini na kumuuliza MUNGU juu ya jambohilo unaweza kuona ktk maisha yako haufanikiwi kimwili na kiroho pia /kihuduma kumbe umejaa kiburi na dharau kwa watumishi wa MUNGU kumbuka wakati wa MUSA baada ya kuoa mwanamke mkushi nini? kilitokea wakati ELISHA alipo paa wewe mwenye upaa kumbuka nini kilitokea TUSIWE WEPESI WA KUTAMKIA JAMBO AU KU COMMENT UBAYA KWA MTUMISHI WAMUNGU NASHANGAAAAAAAAA SA NAAAAAAAAAAAAAA UJAZO WAROHO MTAKATIFU KWA WATU WALEO TUMEJAZWA NA ROHO MTAKATIFU ILA TUNA WASEMA VIBAYA WATUMISHI WA MUNGU NA KUPANDIKIZA CHUKI KATI YA NDUGU NA NDUGU TAZAMA MATENDOYAKO KAMA YANA FANANA NA UJOZO WAROHO MTAKATIFU HALISI KUTOKA KWA MUNGU

 3. vip kuhusu waliokufa kwenye kukimbilia upako? maandiko gani yanadhibitisha hili?
  Roho mt. akishuka mahali watu waweza kufa? comment zenu nzuri lakini jibu maswali yangu.

 4. KUOKOKA NI KUTUBU KUUNGAMA KUJUTA DHAMBI ZAKO ULIZOFANYA KWA MAWAZO MANENO MATENDO NA KWA NJIA YOYOTE.KWA KUMAANISHA KUZIACHA KABISA.

 5. Wapendwa, Mungu atusaidie kujua na kuona yaliyo ya kweli na afungue macho na mioyo yetu tupate kuwajua watumishi wa Mungu na kuwaheshimu, nawashukuru wachangiaji wote kwa muda wenu hasa mlioweza kuitetea kweli ya Neno la Mungu pamoja na kujadili changamoto za kanisa letu, tusimame Imara katika Imani hata Bwana ajapo.

  Tunaomba radhi kwa maoni ambayo hatukuruhusu, ni kutokana na lugha kali zilizotumika na hata tulizoruhusu tumejaribu kupunguza makali ya maneno kwa watumishi wa Mungu.

  Ndugu Conrad/Cleopatra, nikupongeze kwa juhudi yako kubwa….kuna maoni unasema hukuyaona hapa ya ndugu Orbi, yamehamishwa kwenye mada husika.

  Tafadhali fungua hapa utaona maswali yako na majibu ya Orbi
  https://strictlygospel.wordpress.com/2011/01/14/tanzania-inasumbuliwa-na-malango/#comment-24792

  MJADALA HUU UNAFUNGWA, HATUTARUHUSU maoni mengine kutokana na mjadala huu. Kama mlivyoweza kujibu mada hii kwa ushirikiano, karibuni pia kwenye mada zingine za kuujenga mwili wa Kristo.

  Mungu aturehemu.

 6. ndugu Mkandya usibishane sana na huyo Obi…………..kuna comment zinazomchallenge hataki kuzitoa..mfano alizungumzia kuwa mafundisho ya “malango na mzaliwa wa kwanza kuwa ni ya upotofu” nami nikamuuliza aonyeshe ni kivipi..maana mafundisho hayo nilipata kuyasikia yakifundishwa kwa ufasaha&kibiblia sana na mwl mwakasege….nikamuuliza je anataka kutuambia kuwa mwl si mtumishi wa kweli kutoka kwa Bwana?nadhani anaogopa kujibu maana anaogopa watu wote kumpiga na mawe kama walivyoogopa mafarisayo kupigwa na watu kama wangesema Yohana mbatizaji si mtumishi wa Mungu.

  hata kama hii msg hataitoa ujumbe huu utakuwa umemfikia na ataelewa kuwa anahitaji kukaa chini na kujifunza zaidi biblia na si kukariri.

  mbarikiwe sana

 7. Ck Lwembe 04/06/2013 at 1:45 PM mfano wako wa daktari sijui unamaanisha daktari professional au wa miti shamba??ukienda kwa daktari ambaye ni professional hakuna hizo scenario mbili ulizozitaja maana daktari professional (hata kama hajaokoka) akiwa kazini hawezi kuacha kuhudumia wagonjwa ili kuangalia mpira au kufanya maombi…nasikitika sijawahi kuona let alone kusikia kitu kama hicho kikitokea katika maisha yangu.

  Pia hiyo nadharia ya kusema wachezaji wa mpira wanatoka katika hali ya kawaida kwenda kwenye anxiety na kazi yao haimpi utukufu Mungu nadhani ufanye utafiti na kusoma&kuongea na professional footballers ndipo utakapoelewa kuwa ni kazi kama kazi nyingine na kila kinachowapata wao hata wewe na mimi kinatupa tukiwa kazini. Je unadhani madaktari,maseremala,wachungaji,engineers, etc etc hawana hizo anxiety&stress kila siku kwenye kazi zao??watu makanisani hawagombani hadi kufukuzana??au hujasoma biblia iliposema muwe na hasira lakini msitende dhambi!!

  Unasema kuna watu amejitumbukiza kwenye pipa kujichoma kwa ajili ya mpira?sasa ukianza kutoa mifano ya individual ili ku-generalize kuwa mchezo wa mpira ni dhambi je utasemaje kuhusu baadhi wachungaji ambao wamekamatwa live wakizini..je utatuambia kuwa kazi ya uchungaji haimpi Mungu utukufu sababu tumewashuhudia baadhi yao wakizini?

  ndugu Ck Lwembe cjui kanisa unalosali na mafundisho unayoyasikiliza lakini ushauri wangu kwako ni muhimu sana kufanya bidii katika kupata ufahamu.

  ubarikiwe sana

  conrad

 8. Mkandya…..

  unasema niseme ni nini ambacho TB Joshua alitabiri Hakikutokea….? Kweli unashangaza…..Ok…… mnitakujibu…..mungu wa TB Joshua..alimtuma atabiri juu ya mechi ya mpira ikatokea…. na Sangoma wengi wa South Africa walifanya hivyo….Pweza pia alifanya hivyo…..wacheza kamari wengi walicheza kamari nani atashinda mechi hiyo….wakala dau…..anyway……na mungu wa Tb akafanya hivyo…! Sawa na pweza……sawa na sangoma……sawa na wacheza kamari wa Casino…..! hUWEZI kulinganisha Mungu na akina sangoma…..! That is not my GOD……! Please that is not my God…….that is not God of the Bible……that is not God of prophets like Jeremiah…….Ezekiel……and great prophets of the Bible…….

  Hivi kutabiri kitu kikatokea ina maana wewe ni nabii wa Mungu….? Hebu jibu swali hili……halafu nikupe Maandiko…..!!!!!

  Huyu ni “mungu” wa Nabii joshua anaacha Nigeria inaenda shimoni na kujulikana ulimwenguni wote kwa grand corruption akaona ampe unabii wa mpira…..! POLENI SANA

  UBARIKIWE…

 9. Haya, kwamba sasa nanyi mnajua kuwa nabii wenu hana sehemu katika Maandiko, hiyo ni hatua nzuri mliyoipiga. Na kuhusu swali lenu la kuoneshwa nabii wa kweli leo hii, pia mmejibiwa kwamba HAKUNA, na kama mnaye mnayemuona ni wa kweli, basi tuonesheni tu Huduma yake ilipotabiriwa nasi tumfuate. Lakini siwategemei mje na chochote, kwani mtawezaje kumjua nabii wa kweli huku hata hao wa uongo mmeshindwa kuwabaini?

  Na kuhusu michezo haswa utabiri wake na uhusiano wake na wokovu, ni kwamba michezo inaacha kuwa michezo pale inapochukua ‘roho’!

  Mara nyingi michezo inapokuwa katika ile innocent stage, wachezaji na mashabiki wao hukutana kwa ajili ya burudani tu, ndipo timu zingeshindana katika upendo. Lakini kadiri ushabiki unavyozidi, yaani ile ‘roho’ inapojipenyeza katika mioyo ya watu, pole pole ule ‘upendo’ hubadilika na kuzaliwa “ANXIETY” (Anxiety kwa tafsiri nyepesi ni hali ya wasiwasi, dukuduku au hamu); sasa, ushindi huwa ni muhimu kuliko mchezo wenyewe!

  Transition ya kutoka katika ule mchezo unaotawaliwa na ‘upendo’ kwenda katika mchezo unaotawaliwa na ‘anxiety’, ni VERY SMOOTH; mambo yote huonekana ni yale yale, upendo ukitawala, michezo ikiwaleta karibu zaidi, marafiki wengi zaidi, nk. ile hekima ya kibinadamu! Hata tempo ya ile ‘anxiety’ inapopandishwa kwa jino moja, usingeweza kugundua, sasa kumezaliwa umuhimu wa kumpata mchezaji fulani kutoka sehemu nyingine ili muweze kuwa timu yenye kushinda (wale wachezaji wenu mlioanza nao sasa hawafai tena)!

  Kwa kadiri ile ‘anxiety’ inavyopandishwa, nanyi hujitahidi kuituliza kwa mipango mipya, bali hayo yote hufikia mahali ikawa hamna uwezo wa kufanya lolote kuituliza, yaani ile “Amani ya Mungu, ipitayo akili zote,” yenye kuwahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu, huwa ilikwisha kuondolewa mioyoni mwenu siku nyingi na badala yake kupandikizwa ‘anxiety’! Anxiety ni roho kutoka kuzimu!!!

  Kwa vile huko mlipokuwa wachanga mlilelewa katika Kristo, basi mnapofika mahali mkashindwa kuituliza hiyo ‘anxiety’, basi ninyi humtafuta nabii awatabirie kama ambavyo wapagani humtafuta pweza au kakakuona au mtambuzi au msoma nyota!!! Basi akiwepo nabii wa jinsi hiyo (wa mfano wa Balaam), huyo huwapeleka katika maji marefu zaidi ya hiyo ‘anxiety, maana sasa mnalo tegemeo, Mungu amewaletea nabii!

  Najaribu kumwazia Kristo, kuwa alichapwa viboko na kuvalishwa taji la miiba, akabebeshwa msalaba mzito, akasulubiwa, akachomwa mkuki, nk ili mimi nipate kujua ManU itashinda!!! Ninawakumbuka mitume walivyoadhibiwa na kuuawa pamoja na wakristo walioyatoa maisha yao wakisimama na Neno la Mungu, kwamba hayo yote yalifanyika ili kukidhi dukuduku langu la mpira wa miguu, kwamba Mungu aliwapitisha hao wote katika hali hizo, kwa ajili ya jambo hilo!!!! Kwamba hayo makelele ya “Waaaaaaah!” ninayoyasikia saa nane za usiku katika “mikesha” ya mpira huwa ni kwa utukufu wa Mungu, wanae wanapofurahia kutazama unabii unavyotimia!

  Hata yule aliyejitumbukiza katika pipa la mafuta yanayochemka huko Shinyanga, akafa, baada ya timu yake kushindwa, ilikuwa ni kwa utukufu wa Mungu!!! Hao wacheza mpira wanaotoboa masikio na kuvaa hereni na kusuka nywele vyote ni kwa utukufu wa Mungu pia!!

  Hata hawa waliokufa kwa kukanyagwa wakigombea “Mafuta ya Upako”, hayo yanayouzwa kwa wenye pesa, na hapo nabii mwenye kumrudishia Mungu utukufu, alipoamua kuwasaidia masikini kwa kuwapa bure, wakaishia kukanyagana mpaka kuuana, yote ni kwa utukufu wa Mungu!

  Ni kweli, yote hayo ni kwa utukufu wa “mungu” wa kizazi hiki kiovu pamoja na manabii wake!!!

 10. Ha ha ha a!
  Orbi sina hakika kama unajua vema aina ya watu unaoongea nao katika huu uwanja. Unatumia nguvu nyingi sana na kuandika makala ndefu zilizojaa ” pet issues”. Nilitegemea wewe kwa kupata kwako nafasi ya kuwa Marekani na kwingine ulikofika ungekuwa ni mwenye kunena vitu vyenye kushikika.

  Hauna tofauti na mtu anayepanda kwenye mti na kisha anaanza kuukata huku aikuwa ungali juu yake.
  Wewe ni sehemu ya kanisa, umefanya nini kulisaidia kanisa? mimi sijaona mchango wako kwa kanisa. Na kama hujafanya chochote mamlaka ya kulilaumu kanisa unayatoa wapi? Unapolilaumu kanisa ambalo wewe ni sehemu yake ni sawa na kukata mti huku umepanda juu yake.

  Mungu hahitaji watu wawili ili afanye jambo. Wewe je umetumia masaa mangapi kuomba ili unachokiita kuswagwa kwa waumni kusiendelee?

  Hata kwenye makala yako hakuna chochote cha maana zaidi ya kulaumu tu kwa kurasa ndefu. Hakuna ‘substance katika makala zako nyingi Orbi , hakuna. Sikuoni kama wewe ni part ya kutatua unaloliita tatizo.

  Unasema unabii hauwezi kuwa unabii ati kwa sababu na pweza alitabiri!! Wewe ni mtu wa ajabu kweli, hujasoma kuhusu yule binti mwenye pepo wa utambuzi alivyokuwa anawatambua akina Paul kuwa wao ni watumishi wa Mungu aliyehai,kwani alikuwa anasema uongo? Hatuachi kuuamini unabii uliotimia just kwa sababu na mganga fulani au kiumbe mwingine nae alisema vivyo hivyo, hicho si kipimo cha unabii wa kweli

  Kipimo cha unabii si nani kasema, bali ni kutimia kwa lililosemwa na huyo nabii.

  Nasikitika kusema kwamba kuna makala zako nyingi akisoma mkristo mchanga ndo atapotea kabisa.

  Huwezi kujibu swala alilosema Meryn la kuonyesha nabii wa kweli kwa sababu kuna kitu ambacho hujataka kusema ambacho kiko moyoni mwako kwamba wewe unaamini kuwa leo hakuna manabii.
  Ndio maana badala ya kujibu hilo swala fupi unaongea maneno mengiiiii!

  Hakuna unabii ambao hutolewa kama mtu fulani atakavyo( au kama wewe Orbii utakavyo). Kwa matakwa yako wewe ungependa Tb Joshua atabiri habari za Boko haram, lakini kwa sababu unabii huwa hautoki kama mtu fulani atakavyo,yeye ametabiri habari ya mpira na ndege kuanguka.

  Halaf unachanganya vitu viwili isivyo lazima. Umasikini wa Afrika na suala la Afrika kuwa na manabii si vitu vinavyohusiana. Bila shaka bado uko Marekani Orbi, sasa nikuulize kuwa umeenda kufanya nini huko na kukimbia bara lako la Afrika? Come back home!!!!

  Elewa jambo moja,manabii wana viwango. Kuna viwango vya kimataifa, kitaifa, kikanisa, na individual level”. Huwezi ukaanza tu kuwa nabii wa kimataifa kwa mfano, kama hujapitia hivi viwango vingine ili uzoezwe kutumiwa. Si kila nabii aliweza kusimama mbele ya mfalme na kutoa unabii, hicho kilikuwa ni kiwango cha juu sana.

  Orbi fanya jambo moja; sema dhambi ya TB Joshua, sema ni jambo gani alitabiri halikutimia. Kama lipo ndo tujenge hoja hapo. Siyo hizo blablaa unazosema.

 11. asheri unasema “Ninavyofahamu mimi ni kuwa kutoka enzi za Agano la Kale mpaka Agano Jipya, michezo ilikuwepo na hata mashindano nayo yalikuwepo, lakini hatuna mahali popote ambapo manabii walitabiri kuwa timu/kundi fulani litashinda au litashidwa”..hv nikuulize je kuombea/kubariki ufugaji wa kuku, uuzaji mchicha, vitunguu, kuuza duka, biashara ya daladala, kutengeneza batiki, etc etc ni halali kibiblia? je kuna sehemu yoyote kwenye biblia ilipoandikwa neno kwa neno kuwa mitume walifanya haya mambo?je mambo yote wanayoyaombea watumishi wa Mungu yote yameandikwa neno kwa neno katika biblia?unaelewa maana ya Bwana Yesu aliposema akiwajalia Roho Mtakatifu atawafundisha yote na mtafanya zaidi ya haya??

  ni muhimu kusoma bible kwa kuelewa na kuomba ufahamu wa Roho Mtakatifu na si kukariri.

  Mbarikiwe wote

  Conrad

 12. Unaonaje Conrad, kwamba una mgonjwa aliye mahututi, labda ni mwanao, nawe umefanya jitihada zote kumuwahisha kwa daktari. Ulipofika hapo ukaambiwa, usubiri kidogo; kwamba
  1. Daktari yuko katika chumba cha maombi, ili Mungu amuongoze katika kuwahudumia.
  Au
  2. Daktari anamalizia kuangalia mechi ya ManU atakuja sasa hivi!

  Basi ikague dhamira yako katika majibu hayo mawili!

 13. Conrad……

  Hivi nani amesema tunachukia unabii…? Tunapomkataa Nabii huyu wa Nigeria? Nadhani unasoma Biblia…..nadhani unajua Major na minor prophets walichoaandika na walipotumwa kwa Israel ili kutoa Unabii……..angalia hao manabii walisema nini.Leo kanisa liko under threat…..ulimwenguni mwote na hasa kanisa la nyumbani kwake Nigeria……halafu Mungu anamtuma Nabii atabiri juu ya mpira wa miguu…..!

  Halafu unaposema Mbona wachungaji wanaombea…..kuwatabiria…..Je wachungaji ndio kipimo cha Biblia…….kama wanaita mafisadi kufungua makanisa….kuzindua kanda…….Bila kukemea maovu…..kwa nguvu zao zote……hiyo ndio model ya Mungu….?

  Katika Israel kulitokea manabii wa uongo kila wakati wakisema Bwana kasema hivi ….mara kasema lile……Je sembuse leo…….Please soma Biblia kitabu chote ……kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo……ndipo uone utendaji wa Mungu……sio kusoma Biblia vipande vipande halafu unasema watu wanapotea kwa kukosa maarifa…….

  UBARIKIWE

  Naomba ubarikiwe….

 14. mnaochukia unabii kuhusu mpira wa miguu kweli mnatafakari vizuri maandiko??hv kwa ufahamu wenu mnafikiri mpira wa miguu ni mchezo tu usio na maana?hv mnajua kuwa mpira ni ajira ya watu kama vile madokta, maserelamala,engineers,etc na kuna watu wa Bwana huko ambao wamepakwa mafuta na wanafunga na kuomba Bwana awasaidie kucheza vizuri&kushinda kwenye hiyo kazi zao kama vile wewe na mimi tunapoamka asubuhi na kuomba Bwana atutangulie kwenye kazi zetu!! Na kupitia kipato wanachopata kwenye hiyo kazi yao kuna ambao wanatoa fungu la kumi, kueneza injili, kutunza yatima,maskini, etc zaidi ya baadhi ya wapendwa wasiotaka kufanya kazi.

  Yes Mungu yupo busy kufuatilia wacheza mpira maana Yeye anajishughulisha sana na mambo ya watoto wake…na wao ni sehemu ya hilo Kanisa maana Kanisa ni mwili wa Kristo na si jengo!!.Mungu wetu ni wa rehema na habagui professional za watu kama tunavyowaza ndio maana enzi za ujenzi wa sanduku la agano aliwapaka mafuta maserelama wakafanya kazi kwa ustadi usiopimika.

  …Mbona wachungaji wanasimama na kuwaombea madaktari,wafanyabiashara,etc na kuwatabiria&kuwabarikia…Je si sahihi kwao kufanya katika professional nyingine kama za mchezaji mpira. Hakika mnapotea kwa kutoyajua maandiko na Bwana atusaidie sana!!

  Conrad

 15. Maryn……..

  Ama kweli…….hivi nil lazima atajwe Nabii wa Kweli ili Nabii Joshua aonekana ni uongo…? Ndio Maandiko yanasema hivyo…..? Je Kutoka Kitabu Cha Malaki kuja Kitabu cha Mathew (Mathayo) Mbona kulikuwa kimya Kabisa hadi kipindi cha Yohana Mbatizaji utasemaje….? Hakukuwa na sauti yoyote ya Nabii……utaelezaje maana kulikua kimya kabisa mpaka sauti ya aliye nyikani iliposikika…..! Si afadhali Mungu awe kimya ili tumtafute kuliko kutuletea nabii za simba na yanga…? Tukadhani zimetoka kwa Bwana…? yaani Mungu ameona la maana sana kutuletea utabiri wa mpira…..? kitu ambacho hata pweza alifanya…au kuanguka kwa ndege wakati maelfu wanakufa kwa ukimwi na majanga mabli mbali mbali…… Please Maryn be serious…inaingia hiyo kwenye ufahamu wako wa kiroho…..?……Ni lazima awepo Nabii wa Kweli ili Wauongo aonekane……Mbona hamzielezeii hizi Nabii zake za Kiipuzi kama zinampa Mungu Utukufu ama vipi…….?

  Halafu ulaya ni wapi na wapi na nabii wa kweli…?……ndio Biblia yako inavyokufundisha jinsi ya kuwafahamu manabii wa Kweli angalia ulaya kinafanyika nini…….halafu ni ulaya ipi unayoizungumzia……? Maana ulaya ndio inayoongoza kwa upagani hivi sasa……Umewahi kufika uingereza……Germany…..Sweden……au na kuona idadi ya makanisa inavyofungwa….? au unasoma kwenye magazeti……..? Hujiulizi kwa nini tunalazimishwa ushoga……..Kanisa la ulaya lilishatekwa na liberal theologians na secularism……limebaki la Amerika lina uhai lakini likichechemea kwani secular humanism na pluralism inalifunga kanisa la usa taratibu.. ……..na Wakristo wa Marekani wenye macho ya kiroho wanamlilia Mungu kwa uamsho…….
  Nadhani Maryn wewe na wenye msimamo kama wako ndio mnaoswaga kwenda Israel kubatizwa Mto Jordan mkidhani mtaongeza lolote katika maisha yenu ya kumjua Yesu…….! Au kukimbilia Nigeria kuutafuta Upako……!Mnaanza Kuongeza rituals za kuhiji…….na kufanya maziara…….mahali penye miujiza na kuacha mambo muhimu ya Wakovu……..Kuna wenzio waliisha andika kuwa Nabii Joshua ni Tunu tuliyopewa Waafrika na Mungu……! yaani Mungu atupe Nabii Joshua kama Tunu na zawadi…………na kuiacha Afrika katika lindi la upofu na umaskini……giza na kuwa na hofu ya Freemansons kila kukicha! Kila siku viongozi wetu wanaondoka kwenda kutafuta wafadhili Ulaya……Wakati tuna johari na tunu toka kwa “mungu” ya nabii Joshua…….! .Please task your spiritual muscles to grow into mind of Christ……acheni kunywa maziwa ya kiroho…… tena yaliochacha toka kwa manabii kama TB Joshua…….Kanisa la Tanzania litabakia linazunguka jangwani…..! Mara hofu ya Freemanson….kuanzia kwenye sindano ya kushonea…..nepi za mtoto……magari…wasanii…….mvua…..jua…..kila kitu ni Freemansons kama sio upofu wa kiroho ni nini basi?

  Hii inaonyesha wazi jinsi ya wengi wetu tulivyofungwa hata kwenye ufahamu wa Kiroho……! Na mtu akiisha kufunga kwenye ufahamu wa Kiroho ameisha kufunga kila kitu………..hata akili ya kawaida itaacha kufanya kazi…..angalia alipokuja Babu wa Loliondo makanisa ndio yaliongoza yalivyopungua waumini…..kwenda kunywa Kikombe…..sasa kama makanisani watafanya hivi unategemea nini kwa wasiomcha Mungu…….ungelitegemea Kanisa la Mungu na kuongoza na kuwaonya watu……lakini wengi ndani ya kanisa ni vipofu…..sasa watamuongoza nani……Walionyesha mfano halisi kwenda Loliondo……na viongozi wa serikali wakafuata…….wameonyesha mfano mzuri kwenda Nigeria kutafuta upako …….na Lowasa na viongozi wengine wa serikali wakafuata……?

  Mara nyingi katika historia Kanisa huwa lina set standard na jamii inafuata…..Kanisa la Tanzania limeset standard na tunaiona…..ni kupgopa ushirikina kila kukicha…..sio Nuru tena inayowaka……angalia tunawaita akina nani kufungua matamasha…….tunawaita akina nani kuzindua album……tunawaita akina nani kuchangia ujenzi wa makanisa……..ni wale wale wanaipekeka Tanzania shimoni………..

  Mungu na aturehemu na kutusaidia…..

  UBARIKIWE…..

 16. naona mjadala unaendelea lakini wanaompinga mtumishi wa Mungu tbjoshua wameshindwa kabisa kumtaja kwa jina nabii yeyote (hata mmoja) waliyemthibitisha (kwa ufahamu wao na labda kibiblia) kuwa ni nabii wa Mungu hapa duniani na kubakia kuzungukazunguka. Je tutakapowatajia humu majina ya manabii wengine tunaowaona huku ulaya watawakubali??

  maryn

 17. mkandya 03/06/2013 at 7:28 PM ufahamu kuwa Mungu tunayemuabudu ni yeye yule yule hajabadilika wa agano la Kale ndiye yule wa Agano jipya. Huu uongo wa kusema hili jambo lilikuwa ni la agano la kale na si sahihi kwa agano jipya biblia inakataa.

  Yes Roho Mtakatifu anakaa ndani yako na kukumbusha hata kabla hujatenda dhambi lakini hakulazimishi kutokutenda dhambi. The moment unatenda dhambi uwepo wake unaondoka na nafsi yako itajua dhahiri kuwa ameondoka japokuwa watu kwa nje wanaweza wakakuona bado ni mpendwa mwenzao.

  Unataka kujua uwepo wa Bwana unakuwaje?unakumbuka Bwana Yesu kuna mahali alikuwa anafundisha na biblia inasema uweza wa Bwana ulikuwepo apate kuponya…kuna mahali pia bible inasema petro alifundisha kwa ujasiri na udhihirisho wa nguvu za roho mtakatifu maana roho wa Bwana alikuwepo…!.somo la kujua uwepo wa Bwana na namna ya kuingia uweponi mwake ni pana na nikipata nafasi nitaeleza ila ujue tu kuwa uwepo wa Bwana ni dhahiri na upo kwa wenye kuutafuta japo si wapendwa wote wanatembea katika uwepo wa Bwana mara zote.

  Joe

 18. Asheri,

  Asante mno kwa mchango wako……nadhani watu wengi hapa inabidi wasome tena ni nini Manabii wa Mungu walifanya hasa kuuleta ujumbe wa Mungu kwa njia ya unabii katika Agano la Kale na wasingethubutu kabisa hata kuandika kumtetea huyu Nabii Joshua……Nadhani wengi hapa hawajui kabisa akina Yeremia, Isaya, Ezekiel na wengineo kwa nini waliandika vitabu vyao…au walitoa unabii wao Israel ilipokuwa wapi na kwa nini! Laiti wangelijua kazi ya Nabii ni ipi wasingempapatikia huyu nabii mfu wa leo asemaye mara leo hii timu itashinda…mara ndege itaanguka…mara rais huyu atakufa…..halafu huyo “mungu” wake akakaa kimya wakati Kanisa likipita katika dhiki Nigeria…..

  Inawezekana huyo mungu yuko busy kufuatilizia ligi ya mpira…na labda anasubiri kombe la dunia au zile za nchi za Afrika zicheze halafu anawatuma wanabii wake kama Nabii Joshua watoe unabii……..amesahau kabisa Kanisa lina muhitaji….! That is not God of the Bible…..! Labda mungu huyu ni yule ambaye Kocha wa Bayern Munich Ottmar Hitzfeld alisema mwaka 1999 kama nakumbuka vizuri, timu yake iliposhindwa na Man United licha ya kucheza mpira mzuri akasema ” the god of football is a cruel god” hajali umecheza vizuri akitaka ushinde utashinda na akitaka ushindwe utashindwa……!

  Jamani wapendwa msivutiwe tu na sensationalism…..emotionalism…..wingi wa watu mkadhani ndio kazi ya Roho Mtakatifu…..! Au ndio upako…..! Upako wa Kweli unamheshimu Mungu……..! Roho mtakatifu hafanyi kazi huku akiyakanyaga maandiko yake…….akinyaga hata kazi za kinabii alizofanya huko nyuma……

  Mbarikiwe…..

 19. Wapendwa,

  Kuna hoja imezungumzwa kuwa hivi mtu kutabiri kuwa timu fulani itashinda ni dhambi? na kama suala hilo halimpi Mungu utukufu?

  Kwa mtizamo wangu, mtu akitabiri kuwa timu fulani itafungwa au itashinda si dhambi, ila kinachoweza kuwa tatizo ni nini kilichoko nyuma ya huo utabiri. Kuhusu hoja ya kuwa mtu akitabiri kuwa timu fulani itafungwa au itashinda kama linampa Mungu utukufu au la, hili nalo linaweza kuwa na majibu tofauti, lakini tunachopaswa kuangalia ni nini lengo la unabii huo.

  Unabii ni tamko analolitoa mtu kwa jambo litakalotokea. Unabii wa Mungu siku zote huwa na malengo fulani. Mungu akisema jambo fulani litatokea anakuwa na makusudi. Mara nyingi unabii ulikuwa ukiwaonya wanadamu kuhusu uovu wao, ukiwaelekeza watubu na kama hawatubu nini kitatokea kutokana na ukaidi wao. Vilevile, unabii huja kwa ajili ya kuwajulisha wahusika jambo fulani litakalotokea ili wachukue hatua fulani, inaweza kuwa hatari fulani inayowakabili, jambo fulani wanalotakiwa kulifanya n.k.

  Ninavyofahamu mimi ni kuwa kutoka enzi za Agano la Kale mpaka Agano Jipya, michezo ilikuwepo na hata mashindano nayo yalikuwepo, lakini hatuna mahali popote ambapo manabii walitabiri kuwa timu/kundi fulani litashinda au litashidwa. Kama hilo lilikuwepo, neno lingetuambia. Vilevile, toka zamani walikuwepo watawala ambao walikuwa wanakufa, naamini pia ajali zilikuwepo, lakini tunaona kuwa unabii ulikuwa ukitolewa kama mfalme atakufa au tukio fulani litatokea na unabii haukuishia kutoa taarifa tu, bali ulielekeza pia nini kitafuata au nini kifanyike. Hatuoni mahali ambapo unabii ulitolewa kuwa mfalme au mtawala fulani atakufa bila kuwa na sababu/au jambo fulani litakalofuata lisilohusiana na jambo la Kimungu.

  Katika 2Petro 1:20, 21 inasema watu wanapotoa unabii hunena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

  Naomba tutafakari yafuatayo:
  Je unabii wa kuwa timu fulani itashinda au timu fulani itashindwa unakuwa na makusudi gani? Sawa, Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu ametuambia kuwa timu x itashinda ili iweje? (then what?). Je ni ili tufurahi au?Tukishafurahi halafu inakuwaje? Je kuna kusudi lolote la Mungu katika kutuambia kuwa timu fulani itashinda hata tuseme kuwa Mungu amepewa utukufu?

  Mungu awabariki!

 20. Joe onyesha mahali ambapo biblia inasema kuwa vile vitambaa Paul mtume aliongozwa na Roho mt. ndipo akaangaza kuvitumia.

  Halaf utuonyeshe pia kuwa kutumia ‘maji’ si kitu kinachotoka kwa Roho mt.

  Naona ninyi mnataka watu wafanye huduma kama ambavyo ninyi mnafikiri au kwa style tu ambayo iliwahi kufanyika kwenye biblia, au kama ambavyo ninyi mmezoea.

  Ni rahisi kudhani kuwa hiyo ya Paul kuponya kwa vitambaa ilikuwa kitu rahisi kukiamini kwa sababu unakiona tu kimeandikwa kwenye biblia leo. Lakini elewa Kilileta shida vilevile kwa wakristo wasiojua sana uwezo wa Mungu hivihivi kama mnavyopata shida kuamini ninyi.

  Joe picha uliyonayo kuhusu uwepo wa Mungu ni ya agano la kale. Leo anayekushawishi kutubu dhambi ni Roho tena mtakatifu ambaye yuko ndani yako tayari. Mungu unayesema usiingie uweponi mwake bila kuwa umetubu kwanza, anakaa ndani yako. Kwa hiyo ukitenda dhambi usisubiri ukitaka kuingia kwenye uwepo wake (sijui ni wapi huko) ndipo utubu/ujitakase,bali fanya hivyo mara tu unapojua kuwa umetenda dhambi, maana hapohapo ulipo uko kwenye uwepo wake.

 21. Mpendwa Joe (03/06/2013 at 4:06 PM)

  Nakushukuru tena kwa mchango wako. Hata hivyo naomba nikusahihishe kidogo, Kwa mujibu wa Matendo 5, Anania na Safira hawakufa wakati wakienda kutoa sadaka, Biblia inasema kuwa waliuza kiwanja na kisha Anania akapeleka sehemu ya fedha miguuni pa Mitume akidai kuwa alicholeta ni thamani yote ya kiwanja. Kutokana na hatua hiyo, Petro alimweleza Anania makosa yake na ndipo akaanguka na kufa. Mkewe Safira alikuja baadaye akiwa hajui kama mumewe ameshakufa na ameshazikwa. Petro akamuuliza kama fedha iliyoletwa ni thamani yote ya kiwanja, akasema ndiyo, ndipo naye akaambiwa uovu wake na kisha akafariki. Hivyo watu wote walijua sababu watu hao kufa na wala haikuwa kimya kimya.

  Ufafanuzi huo haumaanishi kuwa kila anayepata adhabu kutokana na makosa yake, basi watu wote watajulishwa.

  Hata hivyo, habari ya kuwa watu wamekufa walipokuwa wakikanyagana kwenye huduma ya “Mafuta ya Upako” inatufanya tutafakari ili kujua nini kinaendelea. Hata hivyo nakiri kuwa hatuwezi kuwa na majibu kama watu hao walikufa kwasababu ya uovu fulani, ingawa siwezi kukubaliana na baadhi ya hoja kuwa labda ndiyo njia ambayo Mungu aliamua kuwachukua hao watumishi wake kama hakuna tatizo lolote.

  Kutokana na kutafakari tukio hilo, ndipo inatubidi kuangalia kile kilichokuwa kikifanyika hapo. Jibu tunalolipata ni kuwa ilikuwa ni huduma ya mafuta ya upako, ndipo nikajiuliza yale maswali kadhaa katika mchango wangu uliopita kuhusu mafuta ya upako. Naamini kuwa bado tunayo hoja ya kujadili kuhusu matumizi ya mafuta ya upako na vitu vingine kwenye huduma. Binafsi nakubaliana kuwa mafuta, maji, vitambaa na vinginevyo vinaweza kutumika katika kufanyika kwa muujiza fulani, lakini vitu hivyo hutumika kwa mazingira maalum na hatupaswi kuvifanya kuwa utaratibu, ndiyo maana katika mchango wangu wa (02/06/2013 at 12:45 AM) nilizungumzia suala zima la mtu kuchota maji na kuyapeleka kiwandani (kusindika) ambapo huwekwa kwenye chupa maalum na kuziweka lebo (nembo au hati miliki) halafu maji hayo yakaanza kusambazwa kama maji ya upako (anointing water).

 22. Orbi unatakiwa tu ujue jambo moja pia kwamba unapoandika kitu kwa jamii ya waamini kama hivi,kuna watu wenye kufikiri, wanamsikia na kumwelewa Mungu, wamejifunza na akili zao ziko timamu. Kwa hiyo kujua tu hivyo kukufanye ulete hoja yako ukiwa na unyenyekevu ndani yako,wala si makufuru.

  Sikia ulichokisema hapa ”kwa kifupi kanisa la Bwana kwa wenye macho ya Kiroho wanajua linapita kipindi kigumu…..Ngano na magugu vimekaa sambamba mno kwa sasa hivi”

  Je, unadhani ni wewe tu ndiye unaelewa kuwa kanisa la kristo linapita kwenye wakati mgumu?

  Kupita kwenye wakati mgumu haina maana kanisa la Tanzania halijui linakoelekea, ndio maana nilikushangaa sana kusema hayo maneno. Na kama wewe ni sehemu ya kanisa halafu unasema halijui au liko utumwani basi wewe mwenyewe hujui unakoelekea.

  Ati kwa sababu tu ya watumishi kama yule wa Sloam ndo tuseme kanisa limepotea njia? hata kidogo!!

  Na suala la ngano na magugu kukaa pamoja ni la enzi na enzi, na Kristo alisema viacheni vikue pamoja. Magugu hayawezi kuizuia ngano kuwa ngano, zaidi sana yataizonga tu. Hakuna cha kushangaza katika hilo.

  Hapo juu umemwambia Cleopatra kuwa hakuna tofauti ya wewe muumini na mchungaji, bali kristo kagawa tu vipawa. Hata mimi naona uko sahihi.

  Lakini baadae umejipinga mwenyewe na kunipa mashaka kuwa majigambo yako ya kunena maneno makuu ya kuwashutumu watumishi wa Mungu ambao unadhani wameiacha njia hayana chembe za kutosha za umakini na uangalifu. Ona ulichokuja kusema baadae ”.na shetani katoka katika viti vya waumini kaingia mimbarini”

  Well, mimbarini ni mahali wanapokaa au kusimama wachumgaji, manabii, walimu n.k. Kwa hiyo unachomaanisha hapa ni kwamba ni kawaida shetani kukaa kwa waumini (sijui kama makao ya shetani ni kwa waumini anyway), lakini si kawaida kukaa kwa wachungaji, ndo maana unashangaa kuona leo hata kwao anakaa. Maana yake ni kwamba wewe si sawa na mchungaji wako kama ulivyosema kuwa wote mko sawa.

  Orbi umeniambia kuwa ulichomwambia Cleopatra hata mimi kinanitosha. Lakini mimi hata sioni kama Cleopatra mwenyewe kinamtosha ulichosema.

  Kwa upande wangu hakuna ”substance” ya maana sana ktk kile ulichosema zaidi ya lawana kwa watu fulani usiowakubali na kulilaumu kanisa la Tanzania.

  Usishambulie watu Orbi lete ”facts” ili tuchambue!!!!!

 23. Kuna mchango wa ndg Orbi niliokuwa ninausoma, GHAFLA umetoweka!!!

  Nimerefresh zaidi ya mara kumi, lakini sijafanikiwa, ulikuwa unafuata baada ya ule wa ndg Conrad!

  Mapepo kwenye mtandao??!!!! Hahahahahaha… msikemee wapendwa labda ni mambo ya kiufundi tu!!!

 24. Hivi wapendwa, mnajua kuwa Injili hupofua? Kama inavyomfungua macho mwenye kuamini, vivyo humpofusha macho asiyeamini!

  Lakini kwa habari ya akina Anania na Safira, wapendwa mnapojaribu kulileta tukio hilo katika ufananisho na hawa waliofariki wakikanyagana, inasikitisha sana kwamba mtakuwa mmeamua kujitoa ufahamu kabisa na kurudi katika ibada za sanamu! Pia na ile mifano mingine mnayotaka kuilazimisha ihalalishe vifo hivyo, bado si sahihi kwa maana vifo vyote hivyo vinayo maelezo yake (kama ambavyo ndg Asheri amevirejea kwa ufasaha), kwanini viliwafika hao waliofikwa, na ndiyo sababu nasi tumeweza kujifunza; yaani vifo hivyo kabla havijatokea taarifa zake zilitolewa!

  Maandiko yanasema, “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia WATUMISHI WAKE MANABII siri yake.” Amos 3:7 (msisitizo ni wangu). Hivi Joe, unaelewa sawa sawa Mungu anachokisema hapo? Hebu irudie kauli yako hii kisha uilinganishe na hicho anachokisema Mungu. Unasema:
  “Hivyo ndugu mimi na wewe hatuwezi kujua hakika kama hawa watu waliokufa wakikanyagana walikuwa waovu ama la maana biblia imetukataza kuhukumu ila siku ya mwisho atakaporudi mwenye kuhukumu mwenyewe hakika tutajua.”
  Nina wasi wasi kama kweli unafahamu, maana kwa maelezo yako hayo ni dhahiri kuwa unaenenda kwa hisia, macho yako yangali yamefumbwa kwa nguvu ya ibada za sanamu! Hivi siku akija Kristo, wewe kuyajua yaliyotokea leo hii itakusaidia nini? Mungu anasema atatujulisha kabla hayajatokea, sasa wewe kutufundisha tofauti maana yake nini? Ndg yangu usijitafutie matatizo na Mungu, LIAMINI hilo Andiko la Amos ili likufungue macho yako ya kiroho! Ukifunguka ndipo nawe utakuwa na uwezo wa kuuliza kama sisi ili upate maelezo hayo yaliyotolewa kabla watu hao hawajafa ili Mungu apate kutukuzwa! Usijaribu kujitengenezea hali ya kuendelea katika uongo, haitakusaidia kitu, sana sana utaishia kulia na kusaga meno tu, maana unapouendeleza uongo kwa kutafutiza mistari ya Biblia ni sawa nawe kuungana na nabii wako katika huduma mnayoifanya ya kuwapoteza watu pamoja na hao waliokufa! Hao wamekanyagana kaka kawaida ya stampade, wakiyagombea mafuta, ambayo wanaamini wakiyapata, maisha yao yatabadilika! Hata maji yake ya upako, mbona huwa yanauzwa!!

  Lakini ili mradi Mungu hakulizungumzia tukio hilo kabla halijatokea, yaani hakumjulisha nabii wake kuhusu jambo hilo, kuendelea kushikamana na nabii huyo ni upofu unaouzidi wa popo, maana nabii wako SI MTUMISHI wake Mungu, ndio maana hakuelezwa!!!

  Ukihitaji ushahidi zaidi ya huu, basi tusubiri ADHABU na si HUKUMU kama unavyosema, maana Hukumu huambatana na Neno, ukilikataa umekwisha kuhukumiwa, nalo Neno lenye kuhukumu, ndilo hilo katika Amos 3:7!

 25. Mkandya,

  Nadhani maelezo niliyompa dadangu Cleopatra yanakutosha na wewe pia …..nipe tu mwelekeo wako kanisa la Tanzania linaelekea wapi……nasubiri…

 26. Cleopatra…..

  Naona kwako mchungaji wako ni mtu muhumu sana……! Lakini Yesu hakufundisha hivyo, wote ni mwili wa Kristo…bali kila mtu amempatia huduma yake…..Mchungaji wangu katika kanisa nalo abudu hana hati miliki na Imani yangu….! Imani yangu imejengwa katika maneno ya Mungu…..! Narudia Maneno ya Mungu tu…! Siku ya hukumu sitatoa references za Mchungaji wangu……wala za Nabii Joshua…bali nilisimama vipi katika kumuishia Kristo na Neno lake….Sitaulizwa Kwa nini hukukubali unabii wa Nabii Joshua kuwa Nchi fulani itashinda mpira wa miguu….. Ila naona hati miliki yako ya imani imeshikwa na Manabii na mitume kama TB Joshua…….jambo hilo ni kinyume na Maandiko.

  Nakuuliza tena unahitaji Maandiko gani kukuonyesha huduma hiyo ni Potofu……? Nabii zake zinasema kwa sauti kubwa mno huyo ni kuliko kile anachokiri kwenye kinywa chake……Kumbuka hata shetani anakiri na kwa kutetemeka….Je itakuwaje watumishi wake……Biblia inasema watumishi hao hujigeuza mfano wa NURU….hata kuwapoteza Wateule…..Je utapotezaje wateule usipozungumza Lugha ya Kiroho…..! Usipofanya Miujiza….! Usipowapaka mafuta……!

  Unasema unajua Tanzania inakwenda wapi……Hebu tueleze hata Kiroho basi Tanzania inamwelekeo upi…? Maana Kiuchumi huna haja ya kumuleza mtu…..facts zinasema kwa sauti kubwa sana….!Labda uwe umefumba macho……ya mwilini na ya kiroho pia……. Kila kukicha tunapitishia michango kwa “watumishi” wakitaka tuwasaidie kwenda Nigeria kuchukua Upako…..? Je huo ndio mwelekeo unaozungumza…. kiroho..? Hebu tueleze maelfu ya Watanzania waliokua wakimiminika Kwenye Kikombe cha Babu Loliondo……! Nadhani kwa mtazamo wako ni dalili ya Kukua Kiroho…..! Hebu tueleze maelfu wanavyofurika kwenda kujifunza “malango”na Mzaliwa wa Kwanza” ….!Hebu tueleze maelfu na maelfu wakihama kanisa hadi kanisa…ili kuona Misukule tu! Nadhani kwako ni dalili ya kukua Kiroho…au ni dalili Njema hiyo……… Hebu tueleze maelfu na maelfu waliongia na hofu na pia upumbavu wa kuamini Freemasons…..Hebu nieleze juu mafundisho mwitu ya kutoka Pool of Siloam yanavyovuta mamia ya waumini wakiamini Shetani ameuawa na Nabii Eliya……

  Umesema kabisa…”watu kama ninyi mnajua Kanisa linakwenda wapi” Eleza basi ili tuifuate hiyo njia ambayo Kanisa la Mungu linaelekea…..lakini kama ndio Nigeria kuchukua mafuta ya UPAKO……basi tumekwisha………na kunyenyekea kwa huyo Nabii kijijini kwake…..Bwana na apitishie mbali ukengeufu huo……

  Labda nikipata nafasi nitakueleza maana Kanisa kuwemo utumwa Babeli……si mara moja wala mara mbili Kanisa la Mungu kuacha njia ya Neno la Mungu na kufuata mafunuo na mafundisho ya binadamu……Sijui kama unajua historia ya Kanisa la Mungu kwa kipindi chake chote toka Matendo ya Mitume hadi leo……kwa kifupi kanisa la Bwana kwa wenye macho ya Kiroho wanajua linapita kipindi kigumu…..Ngano na magugu vimekaa sambamba mno kwa sasa hivi…….na shetani katoka katika viti vya waumini kaingia mimbarini……na kama Bwana hataleta uamsho…unajua tutakwenda wapi……

  Ubarikiwe.

 27. mkandya nakujibu ifuatavyo:

  -Ivi katika agano jipya sisi (waamini) ndio tunaoponya wagonjwa?
  Sisi (waamini) tumepewa mamlaka ya kuponya wagonjwa kwa Jina la Yesu.

  -Ivi mtume Paul kuponya watu kwa vitambaa ilikuwa ya kibiblia?
  Ndio ilikuwa kibiblia maana alifanya vile kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na kutumia Jina la Yesu kwenye vitambaa.

  -Ivi Yusuf mwana wa Yakobo kuwatabiria mnyweshaji na muokaji wa mfame Farao ilikuwa inampa Mungu utukufu na kujenga mwili wa kristo wa wakati huo?
  Ndio ilikuwa inampa Mungu utukufu maana iliwezesha Mungu wa Israel kujulikana kuwa ni Mungu mkuu&uhakika kuliko miungu yote ya wakati ule na ndio maana Farao alimwita kumtafsiria ndoto yake baada ya watabiri wa miungu mingine kushindwa na hivyo Mungu wa Israel akapewa heshima ya kuwa mtawala kupitia Yusuph.

  -Hebu niambie Joel, unawezaje kupata utakaso nje ya uwepo wa Mungu au anayeweza kutakasa nje ya uwepo wa Mungu ni nani huyo?
  Unapata utakaso kwa toba ya kweli kupitia Bwana Yesu. Bwana Mungu ni Mungu mwenye utaratibu thabiti (protocol) ndio maana hata kwenye ujenzi wa sanduku la Agano alitoa instructions na sanduku halikujengwajengwa tu. Ndio maana alipokuwa anataka kukutana na wana wa Israel aliwaagiza wajitakase kabla maana akishuka na uwepo wake ni Mtakatifu sana.
  Uwepo wa Mungu hushuka na kukaa mahali palipo patakatifu sana ndio maana unaweza kuwa umeokoka na uwepo wa Mungu ukawa haupo na wewe na ndio unaweza sikia mtu aliyeokoka/mtumishi anazini/mwizi,etc. Haruni hakupata ukoma alipomteta Musa maana uwepo wa Mungu ulimfunika ila Mariam aliyemteta Musa aliupata ukoma.

  Joe

 28. Asheri 03/06/2013 at 11:18 AM naam umesoma vizuri kwenye biblia jinsi watu walivyokufa kwenye uwepo wa Mungu. Sasa nadhani unaelewa kuwa anania na safira walikufa sababu ya uovu wao na hii imeandikwa na kufunuliwa ili tuelewe na kuwa mfano kwetu. LAKINI pia ujue kuwa kwa nje (na kwa watu) tukio la kufa kwao lilionekana kama wamekufa wakati wakienda kutoa sadaka. Hii sababu ya kufa kwao imefunuliwa na Roho Mtakatifu kutuonya sisi kuwa waangalifu tunaposogea kwenye uwepo wa Mungu.

  Hivyo ndugu mimi na wewe hatuwezi kujua hakika kama hawa watu waliokufa wakikanyagana walikuwa waovu ama la maana biblia imetukataza kuhukumu ila siku ya mwisho atakaporudi mwenye kuhukumu mwenyewe hakika tutajua. Pia hatuwezi kujua kama ndio style ambayo Mungu ameamua kuitumia maana kama ulivyoona kwenye biblia Mungu alikuwa anawapiga wanadamu waliotenda uovu kwa style mbalimbali waliposogea kwenye uwepo wake.

  So ndugu kama maandiko yasemavyo mahali penye uwepo wa Mungu ni pa hatari sana kama ukienda bila kujitakasa ndio maana Mungu akaweka utaratibu wa toba kabla ya kupakaribia maana hata kama mtumishi atakuwa amepakwa mafuta kama Kuhani Eli hataweza kuzuia adhabu kutoka kwa Bwana labda iwe kwa rehema zake BWANA peke yake.

  Joe

 29. hivi kweli mtumishi akitabiri kuwa timu fulani itashinda ni dhambi?unauliza Mungu anatukuzwa katika utabiri huo?ni kwanini asitukuzwe?je si Mungu aliyeruhusu twende kwake kuuliza mambo ya watoto wake?au tunataka waganga wa kienyeji ndio wawe wanatuambia mambo yatakayotokea kama tulivyozoea?maana kanisa la leo tumeamua kumwachia shetani mambo mengi sana ayafanye na kuona si mambo yanayotakiwa kufanywa na watu wa Mungu wakati Mungu kupitia kwa Bwana Yesu ametupa mamlaka kubwa sana ya kutawala kila kitu katika dunia hii.

  Kwanini tumefikia hatua ya kumwogopa shetani na kuyaacha mambo mengi ambayo kuyajua&kufanya ni haki&mamlaka yetu. Hebu tuamke wapendwa.

 30. Binafsi nilimeskia huyu nabii tbjoshua kwa muda sasa lakini sikuwahi kufuatilia sana huduma yake hadi nilipoona huu mjadala ndipo nikaamua kuangalia mafundisho yake kwa siku kama tatu sasa. Nimemsikiliza sana na kwa umakini na sijaona anaponena kinyume na maandiko matakatifu ya kwenye Biblia. Na hakika si sahihi kumfananisha na babu wa loliondo au kibwetere maana hao kwa kuwasikiliza tu maneno yao mengi hayakuwa biblical.

  Kujua kama ni nabii wa kweli au si wa kweli siwezi kutolea jibu. Ila ninachokijua ni kuwa kama biblia inavyosema endapo huduma(nabii) anatoka kwa Bwana basi na huduma yake haitakufa. Hata waliopinga huduma ya Bwana Yesu kuna maandiko walisema kuwa ikiwa inatoka kwa Mungu basi itadumu. Tumeona pia hata hapa tz na uganda (kibwetere) huduma zilizokuwa kinyume na neno la Mungu zilikufa. Hivyo tusubiri, tuombe na tuone maana Mungu tunayemwabudu ni Mungu aliye hai hivyo kama huduma ya tbjoshua si ya kutoka kwake itakufa lakini kama ni ya kwake hakika itaendelea.

  Pia kwa uzoefu wangu wa muda mrefu kwenye wokovu nimeona watumishi wote walioanza huduma zao walizopewa na Bwana walipingwa sana tena sana na kuitwa majina ya kila namna. Hivi leo mnavyoona watumishi wakubwa kama mzee kulolwa, mwl mwakasege, askofu gamanywa, kakobe, etc etc walipoanza huduma zao kwa sisi tuliobahatika kuwaona mwanzoni waliitwa kila majina mabaya na hata kutengwa. LAKINI Mungu amesimama nao hadi hii leo ndio watu wengi wanawakubali sasa japo pia kuna baadhi wanaendelea kuwapinga.

  Pia hili suala la kupingwa halijaanza leo hata agano la kale&jipya huduma zilipingwa sana tena kuzidi (ukisoma biblia utaona vizuri). Katika habari ya kujua viongozi/rais ajaye hili suala lipo clear ni toka zamani za kuhani samweli ambapo Mungu alimjulisha mfalme (rais) ajaye wakati mfalme sauli bado anatawala. Hata hapa tz kuna watumishi wa Mungu ambao niliwahi kukutana nao zamani na wakanieleza habari za marais wanaokuja wa tz kwa majina na ikatokea.

  Mimi nadhani tusubiri na tutaujua ukweli maana hakika kama ni kutoka kwa Mungu hakuna wa kuzuia huduma yake na kama ni kutoka kwa mwanadamu/shetani itakufa.

  John

 31. Ndugu Joel umeuliza maswali mengi, lakini ngoja mimi nikujibu hivi:
  -Ivi katika agano jipya sisi (waamini) ndio tunaoponya wagonjwa?
  -Ivi mtume Paul kuponya watu kwa vitambaa ilikuwa ya kibiblia?
  -Ivi Yusuf mwana wa Yakobo kuwatabiria mnyweshaji na muokaji wa mfame Farao ilikuwa inampa Mungu utukufu na kujenga mwili wa kristo wa wakati huo?

  Halafu umemwambia Asheri hivi;Tena uwe na tahadhari sana unapokwenda kwenye uwepo wa Mungu ukiwa hujajitakasa maana Mungu ni mtakatifu sana na penye uwepo wake ni mahali pa kutisha sana kama hauko safi”

  Hebu niambie Joel, unawezaje kupata utakaso nje ya uwepo wa Mungu au anayeweza kutakasa nje ya uwepo wa Mungu ni nani huyo?
  Fikiri tena kama unaelewa maana ya uwepo wa Mungu Joel!.
  —————————————————————
  Orbi hujanijibu hata swali moja. Sawa. Acha nikwambie jambo moja kwamba usitake Cleopatra akulaani kwa kumsema vibaya TB Joshua,ila fanya hivi: Jilaani wewe mwenyewe kwa kumwambia Mungu manaeno haya kwamba ”Mungu naomba mapigo yanipate kuotkana na maneno niliyomnenea TB Joshua, kama kweli anakutumikia wewe”. Au mwandikie TB Joshua mwenyewe hayo maneno unayomnenea.

  Lakini pia nimegundua kuwa wewe mwenyewe Orbi kumbe kifikra umeshachoka tofauti na nilivyokuwa nakutazamia. Hebu ona ulivyosema hapa; ”Na ndio maana Tanzania kama nchi haijui inaenda wapi……kila mtumishi anafanya aonavyo vyema machoni mwake…….! Kanisa limeingia utumwani Babeli…”

  Labda wewe pamoja na mafisadi wa hii nchi ndo hamjui Tanzania inaenda wapi, lakini mimi na watu wenye mtazamo kama wa kwangu tunajua hii nchi inakwenda wapi!

  Achilia mbali kwamba kanisa haliwezi kuingia kwenye utumwa wa Babel maana Babel yenyewe unayoisema haipo leo, lakini hata kama kungekuwa na utumwa wa namna yoyote kanisa lisingeweza kuingia utumwani, labda kama umesahau kuwa kanisa ni nini, na liko na nani ndani yake.
  Au labda sijajua kanisa unaloliongelea wewe ni lipi!!!!!

 32. Mpendwa Joe (02/06/2013 at 1:21 PM)
  Shalomu,

  Nakushukuru kwa kuniuliza swali kuhusu Anania na mkewe, Wana wa Eli na Huduma ya Paulo.

  Katika Matedo 5 tunasoma habari ya Anania na Mkewe Safira jinsi walivyokufa kutokana na kutenda dhambi ya kumdanganya Roho Mtakatifu. Watu hao walikufa kwa ajili ya uovu wao ambapo Mungu aliamua kuwaondoa. Hapo kusingekuwa na jambo lingine ambalo lingetokea.

  Katika 1Samweli sura ya 2 mpaka sura ya 4 tunasoma habari mbalimbali ikiwemo habari ya Eli na wanawe. Eli alikuwa kuhani na wanawe pia, lakini watoto wale walikuwa waovu, soma sura ya 2 utaona uovu wao ikiwemo kula nyama ya dhabihu kinyume cha utaratibu pamoja na kulala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania (uzinzi kwenye hema ya Mungu). Kutokana na uovu huo, Mungu alimwambia Eli kuwa atautaka mkono wake, na pia hatakuwepo mzee katika ukoo wake pamoja na mapigo mengine. Hivyo hao nao walikufa kwa ajili ya mapigo, hivyo kusingekuwa na kitu kingine ambacho kingetokea.

  Watoto wa Eli walikufa vitani baada ya Sanduku la Agano kupelekwa huko wakati taifa lilikuwa limefanya uovu, wao walitegemea Sanduku la Agano na siyo Mungu, ndiyo maana Israeli walipigwa na Sanduku la Agano likatekwa na Wafilisti, watoto wa Eli hawakufa kwa sababu ya kushikilia Sanduku lisianguke, hiyo ni habari nyingine. Kwa maana wao walikuwa walawi, wangelishika Sanduku la Agano wasingepigwa. Walikufa kutokana na taifa kushindwa vita, LAKINI kubwa zaidi ilikuwa ni mapigo kutokana na kile ambacho Mungu alikisema kutokana na uovu wao.

  Katika maandiko yote uliyoniuliza, watu hao walikufa kwa ajili ya uovu, hivyo Mungu mwenyewe aliamua kuwakatilia mbali kama sehemu ya adhabu. Hata wale wanaolala au kuumwa (hawawezi) kutokana na Meza ya Bwana ni kwa vile wanakwenda kinyume na neno la Mungu. Tukirudi kwenye habari hii, hatukuambiwa kuwa hao ndugu walikufa kutokana na uovu wao. Kama habari ingesema hivyo, mimi nisingezungumzia habari ya watu kufa. Naomba kama unalifahamu vizuri tukio hilo utujulishe.

  Nilichokisema mimi ni kutokana na habari kueleza kuwa walikufa “walipokuwa wakikanyagana kwenye huduma ya “Mafuta ya Upako”. Habari yenyewe inatuashiria kuwa kilichofanya wafe ni KUKANYAGANA WAKIGOMBEA MAFUTA YA UPAKO. Hapo ndipo tunapopaswa kujiuliza, kuna nini kwenye hayo mafuta mpaka watu wafe? Hivi upako unapatikana kwenye mafuta? je upako ni nini hasa? Je ni wapi katika neno la Mungu tulipoagizwa kugombea mafuta ili tupate upako? Nachelea tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukiabudu sanamu za mafuta badala ya kumtafuta Mungu kwa mujibu wa neno lake.

  Kuhusu huduma ya Paulo, mimi sikujadili huduma ya Paulo, lakini kama ulivyoniuliza, jibu langu ni kuwa Paulo alikuwa Mtume akimtumikia Mungu aliye hai, hivyo asingeweza kumtumikia MUNGU bila kuongozwa na Roho Mtakatifu.

  Mungu akubariki ndugu yangu Joe.

  Bwana Wetu Yesu Kristo ANAKUJA!

 33. DU MR ORBI UMENIFURAHISHA KWA SEHEMU NA KWA MANENO YAKO
  NDUGU WAPENDWA SANA NA BWANA WETU YESU KRISTO NYAKATI TULIZO NAZO NI NYAKATI ZA KUOMBOA WAKATI. WAPENZI KUMBUKEN MAANDIKON MAANDIKO YANANENAVYO KUWA NYAKATI ZA MWISHO KUTAKUWA NANYAKATI ZA HATARI NILIPOKUWA FORM 3 FARAKI YANGU ALNIAMBIA KUHUSU HUYU NABII AKASEMA ANAFANYA MIUJIZA BALAA ILA MIMI KWA UMAKINI NILIULIZA VP MAHUBIRI YAKE YANASEMAJE, WATU WENGI KWA SASA WANAPENDA INJIRI ZA MAFANIKIO KWA KUOMBEWA, NI KUJIFUNZA MAFANIKIO SI KOSA LAKN KILA SKU NI INJIRI HIYO HIYO, NI LAZIMA PIA TUTAZAMA NA UPONYAJI WA ROHO MAANA ROHO NDIYO HASA YESU ALIYO IJIA PIA TUTAMBUE KUWA MWILI HAUJA KOMBOLEWA ROHO NDIYO INAYO KOMBOLEWA NDIYO MAANA ROHO NA MWILI VINASHINDANA SIKU ZOTE. MWILI UNGEKUWA UMEKOMBOLEWA USINGE SHINDANA NA ROHO. TUWE MAKINI NA KILA MTU ANAYE TUJIA NA KUSEMA YEYE NI NABII LAKN. TUZIJARIBU HIZO ROHO JE ZIMETOKANA NA KRISTO TUSPO KUWA MAKIN UTABAK KUMSIFU NABII FULAN NA WATU WATENDA KWAKE KUCHUA UPAKO WAKATI YESU YUPO NA ROHO MTAKATIFU YUPO ATOAYE UPAKO. TUISINIE MAKUU KILA MTU ATENDE KAZI ALIYO ITIWA KULINGANA NA KIASI CHA IMANI YAKE USITAKE. KWA VILE FULANI ANAFANYA MIUJIZA HV NA WATU WENGI WAPO AKNISA LAKE BASI NA MIMI NIFANYE VILE HUKO NDIKO KUNIA MAKUU TENDA JINSI MUNGU ALIVYO KUJALIA NA S KWA MAJIVUNO BALI KWA UNYENYEKEVU UKIMHESABU MWENZIO NI BORA KULIKO NAFSI YAKO WAFILIP 2:1-5. TUWE MACHO NA MAMBO USIJE TUKADANGANYWA NA MAFUNDISHO YA MASHETANI SOMA KWA UMAKIN NENO HILI 2TIM 3:1-9.
  PIA TUTAMBUE KUWA KILA MKRISTO ALIYE MWAMINI YESU NA KUTUBU DHAMBI NA KUZIACHA ANA MAMLAKA YAKRISTO MAANA BIBLIA IMESEMA NA ISHARA HIZ ZITAAMBATANA WAAMINIO KWA JINA LANGU WATATOA PEPO………… MARKO 16:16-18

  JAMANI WAPENDWA JE KUNA FAIDA GAN KUWA NA WAUMINI WENG NA WANGALI KATIKA DHAMBI INGAWA N I MATAJIRI WA KIMWALI NI VYEMA MAMBO HAYA YAENDA SAMBAMBA ILI NA ROHO NAYO IPATE UZIMA WA MILELE

  UJIFUNZE KWELI NA KUWA MACHO YA ROHO ILI TUSIJE TUKADANGANYWA

 34. orbi 02/06/2013 at 7:40 AM mtaje basi huyo mchungaji wako kwa jina ili nasi tupate kumjadili hapa?usijifiche kwa jina la mchungaji Yesu!

  ww na wengine ambao ni wachanga kiroho ndio mnaosema unabii wake ni wa kutaka kukuza jina lake lakini hakuna hata chembe ya mahubiri yake utakayoyasikia yakijirudishia utukufu zaidi ya kumtukuza Bwana Yesu. Nenda kasome kwenye biblia agano la kale uone jinsi manabii walivyo heshimika zaidi wao (kwa majina yao) ndipo utaelewa maana ya lile neno la mkiheshimu Yesu na Baba wa mbinguni atawaheshimu ulimwenguni mbele za watu.

  Kuwazuia boko haramu??ha ha una uhakika gani kama si uwepo wake na watumishi wengine nchini kwake usingekuwa umewafanya hao boko haramu kuwa tayari wameshaipindua serikali?mbona mchungaji wako hajaweza kuzuia mauaji ya albino tz,mabomu makanisani,umaskini,magonjwa,etc?

  wel lete hiyo mistari/link yenye ushahidi inayoonyesha kuwa nabii tbjoshua kuwa si wa Bwana na si kuishia kusema sijui ulishamjadili. Pia siwezi kukulaani hata chembe maana (huna ushahidi halisi wa kimaandiko) kutomkubali kwako hata kuwe kuanzia asubuh hadi usiku, jan hadi dec HAKUWEZI kumwondolea huduma ya unabii aliopewa na Bwana maana hata Bwana Yesu enzi zake walimkataa bila kuwa na ushahidi halisia.

  cleopatra

 35. Kwa majibu yako CK Lwembe inaonesha kuwa kwa sasa humu duniani hakuna nabii yoyote wa Bwana. Kazi kweli kweli

  Conrad

 36. Haya mahubiri ya maji ya upako na mafuta ya upako yanahitaji umakini,sio kukubali kila kitu “eti kisa” kuna mfano wake ktk Bilblia,hata Biblia yenyewe inaonya kua shetani anaweza kujifanya malaika na “akahubiri injili”,watu waache ushabiki wao kwa wahubiri na wautafute ukweli maana hata aliepona kwa babu wa loliondo anaamini kua yule babu alikua na Roho Mtakatifu,tuache ushabiki na tuyachunguze maandiko,”peaple may condition themselves to believe frauds”

 37. Asheri 02/06/2013 at 12:45 AM unasemaje juu ya kina anania na safira walivyokufa wakati wakienda kutoa sadaka?je huduma ya paulo haikuongozwa na roho Mtakatifu?

  au unasemaje wale watoto wa kuhani Eli waliokufa wakijaribu kusaidia sanduku la Bwana lisianguke?je hakukuwa na uwepo wa Bwana kipindi wanafanya hivyo?je baba yao hakuwa kuhani mkubwa asiweze kuwafufua?

  Huduma ya Mungu pia mara nyingine huleta kifo kama ukienda bila kujitakasa mbele zake. Soma maandiko kuna ambao wamekuwa wamelala&hawawezi baada ya kupokea sakramenti bila kujitakasa. Tena uwe na tahadhari sana unapokwenda kwenye uwepo wa Mungu ukiwa hujajitakasa maana Mungu ni mtakatifu sana na penye uwepo wake ni mahali pa kutisha sana kama hauko safi. Jaribu kusoma agano la kale uone wana wa Israel walivyokuwa wanakufa walipokuwa wanakwenda mbele za Bwana bila kujitakasa na mara nyingi iliwabidi wajitakase hata siku tatu kabla ya kukutana na Mungu.

  Joe

 38. Dadangu Cleopatra,

  Unamjua Mchungaji wangu…..? Ni yule Mchungaji wa KWELI….naomba urudie kitabu kizima cha Yohana utamwona……! Na akitenda miujiza yake utaiiona ….wala sio hi ya kukanyagana kwa kugombea mafuta ya upako…….au kama ile miujiza ya mizizi ya Mzee wa Loliondo…..!na wengine kanisa linakua kwa wingi wa “misukule” inayorudishwa toka kuzimu kuliko hata waliookolea toka dhambini!

  Na Si mara moja wala mara mbili wala mara tatu Yesu Mchungaji wa Kweli ameonya kuhusu manabii uchwara watakaokuja kwa jina lake……! Mara leo mpira….mara kesho huyu atakua rais……mara raisi yule atakufa…..mara ndege itaanguka…..wakati kanisa la Mungu nyumbani kwake Nigeria linateketezwa na Boko Haram hata hajui aanzie wapi kutabiri na kuonya kuwa Boko Haram watatokea wapi…..! Maana roho ya deception iliyoko ndani yake si tofauti sana na ile ya Boko Haram……lengo lao kubwa ni kuondoa macho ya Kumuona Kristo!

  Unasema nitumie Maandiko kuhusu TB JOSHUA (Nadhani huko awali wengi nikiwemo na mimi tumeandika mno kuhusu “nabii” huyu) Omba strictly Gospel wakuletee ule mjadala….

  Lakini dadangu Cleopatra unataka ushahidi gani zaidi licha ya upuuzi wa Nabii zake ambazo hazina harufu hata chembe chembe za kuujenga Mwili wa Kristo! wala Kukua Kiroho….au kufanya watu wamjue na kumuishia Kristo isipokuwa kulitangaza jina nabii huyu chini ya Kivuli cha Kristo……na kuvuta makundi ya wakristo wachanga toka ulimwenguni kote kwenda kuhiji kwenye “Sinagogi” lake Nigeria……..Angalia watumishi wa Mungu waliodumaa kiroho Tanzania wakihaha kutafuta michango kwenda kupata “upako” wa kuzimu toka kwa Nabii huyu……..na wakirudi hakuna cha upako……wala chochote……bali zinabakia sarakasi za mimbarini na kelele nyingi na mafundisho mengi yaliyojaa ukengeufu………Kwa wengine utasikia malango……mara mzaliwa wa kwanza…..! wengine Wokovu sio kitu bali Power…….wengine tohara ya moyo…….wengine shetani aliisha uuawa na Nabii Eliya……na kwa wengine toka asubuhi hadi jioni ni mafanikio……. mafanikio mafanikio…….. tu yaani wanajaribu kula sahani moja na ulimwengu….!na takatataka nyingi za mafundisho chungu nzima toka kuzimu………..Na ndio maana Tanzania kama nchi haijui inaenda wapi……kila mtumishi anafanya aonavyo vyema machoni wake…….! Kanisa limeingia utumwani Babeli…..

  Hivyo dadangu Cleopatra nahitimisha kwa kusema hivi: hakika Sinagogi la Tb Joshua ni Sinagogi la Shetani……narudia tena…… Kwa Herufi kubwa ….KWA HAKIKA SINAGOGI LA TB JOSHUA NI SINAGOGI LA SHETANI ( ukitaka rarua mavazi yako kwa uchungu na unilaani na kunitupia mawe……au uniombee mapigo ya Bwana yanipate…ambayo na hakika hayatanipata na .niko tayari kufa kwa kusema hivyo kama ikibidi na hata kujitetea mbele ya kiti cha hukumu kwa msimamo huu….. !Kwani hilo ndilo Bwana aliloniitia) …..kwa mwenye macho ya Rohoni….. nabii zinazotolewa na nabii huyu hazimpi KABISA Kristo utukufu……..kwangu mimi naamini kabisa hili ndilo ambalo limetamkwa katika ufunuo 2: 9 na 3:9…….Maana kwa sasa tuko katika kipindi cha Kanisa……ambalo limeoshwa limetakaswa likimsubiri BWANA HARUSI…….na sio kipindi cha Sinagogi…..!

  MUNGU NA AKUBARIKI….

 39. Shalomu,

  Wapendwa, nimesoma michango mbalimbali katika habari hii, nami nimeona nichangie kidogo. Habari yenyewe inasema watu walikufa kwa KUKANYAGANA kwenye HUDUMA ya MAFUTA ya UPAKO. Kwa mtizamo wangu, hili lenyewe pekee yake (kama kweli limetokea) ni jambo linalotupasa tulitafakari. Swali la kujiuliza ni je hiyo huduma ya UPAKO wa MAFUTA ni kwa ajili ya kuleta nini? Mimi nafahamu kuwa huduma ya Mungu huleta uzima na siyo KIFO (labda mtu anisaidie).

  Huduma yoyote ya Kimungu hufanyika kwa utendaji wa Roho Mtakatifu, kwa hiyo tuseme kuwa Roho Mtakatifu alikuwa akiwahudumia watu lakini kwa BAHATI mbaya wakafa wakati wakiigombea huduma ya huyo Roho Mtakatifu? Ni ukweli ulio wazi kuwa zamani za Biblia kulikuwa na mikusanyiko mingi na Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa akifuatwa na makusanyiko makubwa, lakini hatuna mahali kwenye Biblia panapoonyesha kuwa kuna siku Yesu alisababisha watu wakafa kutokana na msongamano wa watu.

  Tukio linalofahamika la mtu kufa wakati wa huduma ya Roho Mtakatifu inaendelea ni siku Paulo alikuwa akifundisha na kijana mmoja aliyekuwa amekaa ukutani kuanguka akatokwa na roho. Hata hivyo ninaamini jambo lile lilikuwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu ndiyo maana kijana yule alifufuliwa. Je hao watu waliokufa wakati wa huduma ya mafuta walifufuka? Kama walikufa na kuzikwa, je suala hilo lina utukufu kwa Mungu? OK labda tukubaliane kuwa Mungu anatukuzwa inaposemwa kuwa WATU WANNE WALIKUFA KWA KUKANYAGANA WAKATI WAKIGOMBEA HUDUMA YA KIMUNGU. Mimi siamini kuwa jambo hili linampa Mungu utukufu, ila nikisaidiwa ninaweza kuamini.

  Jambo la pili ni matumizi ya hayo mafuta au maji ya upako. Si kwamba siamini juu ya vitu hivyo, la naamini, lakini ninachokizungumza hapa ni matumizi yake. Siku moja ndugu yangu mmoja akanishuhudia jinsi alivyofurahi baada ya kufanikiwa kupata maji ya upako kutoka kwa TB Joshua. Alinionyesha hiyo chupa, nikaiangalia na kumrudishia, kweli alikuwa na furaha sana kwa kuwa sasa anayo maji ya upako.

  Nililiwaza sana jambo hilo na kuliwianisha na maandiko, lakini sikupata usahihi wake. Nimemuona TB Joshua siku akihudumu kwa kutumia hayo maji ya upako, mfano kuna siku alikuwa akiwanywesha hayo maji akiwaambia wenye shida wafungue vinywa naye akawapulizia midomoni na kisha wanapona. Kuna siku nilimuona akiwamwagia wagonjwa mwilini wakapona. Nikirudi kwenye maji, yale maji yamefungwa kwenye chupa vizuri (kiwandani) tena kwa mfumo wa kisasa kabisa. Hii ina maana kuwa TB Joshua huyachukua hayo maji, sijui anayachota mto gani, anayaombea na kisha kuyapeleka kiwandani ili yakasindikwe na kuwekwa kwenye zile chupa. Inawezekana ikawa ni kiwanda chake au cha mtu mwingine, lakini cha msingi ni kuwa hupitia mchakato wa kiwandani. Yakisha sindikwa ndipo sasa husambazwa kwa ajili ya matumizi. Wapendwa hebu tusaidiane, hili nalo ni la kibiblia? Je watu wanapotumia hayo maji, humpa Utukufu Mungu au hayo maji au TB Joshua? Hivi watu wanapohangaika kuyatafuta hayo maji na kuyahifadhi wakiyatumia siku kwa siku huku na mengine wameyaweka akiba, ni suala la kiroho? Je ndivyo tulivyomjifunza Kristo?

  Jambo la mwisho ni suala la kutabiri kuwa timu fulani itashinda au itashindwa, Je tukubaliane kuwa Roho Mtakatifu alihusika kuiambia dunia kuwa timu fulani itashinda na nyingine itashindwa? OK, tufanye ndivyo ilivyokuwa, je ni kwa kusudi gani? Tuseme Mungu anatukuzwa katika utabiri huo? Kulingana na Maandiko, huduma nyingi za agano Jipya ikiwemo na unabii hulenga katika kuujenga mwili wa Kristo, je ni mwili gani unajengwa kwa kanisa kuambiwa kuwa timu fulani itashinda?

  Nawaombeni tutafakari zaidi, tunaweza kujifunza na pia kuona alama na hatari ambazo zinaweza kutusaidia kufungau macho na kuelewa.

  Mungu awabariki!

  Maran Atha.

 40. Nakumbuka zamani waliwahi kumsema Pastor Benny Hinn kuwa huduma yake si ya kweli. Lakini miaka imepita now anazaidi ya miaka 40 kwenye huduma ya kazi ya Bwana na anazidi kuhubiri injili kwa kufika hata nchi za kiarabu (miisho ya dunia) ambapo injili haikuwahi kufika na watu wanaokoka na kumrudia Mungu.

  Ukiangalia mara nyingi watu wanaopinga huduma za watumishi wanaofanya kazi ya kueneza injili ulimwenguni bila kuwa na ushahidi wa kweli utakuta hakika wachungaji wao wanaowaamini hawajaweza hata kufikisha injili ya Kristo ndani ya wilaya walizomo Tanzania let alone Tanzania nzima kama nchi.

  Pia ni muhimu sana kwa mtu uliyeokoka kuwa na exposure ya kiroho&kimwili kwa kusoma sana neno la Mungu na kutembelea sehemu mbalimbali duniani kuona watumishi wa Mungu wanavyofanya kazi kuliko kujificha katika ideology ya mchungaji wako. Nadhani kwa waliosafiri duniani na kuona kazi ya Bwana inavyokwenda wataelewa. Ila taratibu taratibu tutaeleweshana maana mwanzoni mwa wokovu nchini tz ukiwa na utajiri hata kidogo ulioneka si wa kiroho na ulitakiwa uwe maskini kama Lazaro.

  Joe

 41. orbi 01/06/2013 at 12:07 AM hivi mchungaji wako mbona hafufui wafu?kuponya viwete&vilema?ana imani kweli?..maana imeandikwa hivi vyote vitafanywa na wenye imani!!

  hivi si wakati toka enzi za mitume watu walikufa hata katika mikono ya mitume/manabii?je hii ni mara ya kwanza?mbona hatuoni wakina safira&anania wakirudishiwa uhai na mtume paulo?Je ni wapi kwenye biblia walipokataza kutabiri (kutoa unabii) wa matokeo ya mpira?au hata kutazama mpira ni mambo ya ushetani?je Mungu hakutupa mamlaka ya kutawala vyote duniani?

  nadhani ungejaribu kujibu swali liloulizwa hapo juu je kwa mtazamo wako nabii wa kweli kwa jina leo hii hapa duniani ni nani?na utupe mistari yenye kuonyesha anachokisema na kufanya nabii tbjoshua ambacho kibiblia kipo kinyume na neno la Mungu. Usipojibu kwa evidence basi hutakuwa tofauti na mafarisayo ambao baada ya kushindwa kumshitaki Bwana Yesu kwa evidence waliishia kusema amefanya hivi amefanya vile bila kuwa na ushahidi.

  Biblia inasema siku za mwisho watu wa Mungu watachukiwa&kushitakiwa kila mahali watakopokwenda na watakalofanya..wapendwa tujihadhari sana maana ni siku za mwisho na walokinyume na Bwana wapo kutushitaki kwa mashtaka yasiyo na ukweli&evidence…tukaze mwendo

  cleopatra

 42. Kihistoria nafahamu kwamba kutoka Malaki mpaka Yohana Mbatizaji ilipata miaka 400! Yaani akina Mkandya, iwapo mngeishi katika kipindi hicho cha hapo katikati baada ya nabii Malaki kuondoka na kabla ya Yohana, na mkawa na swali kama hili mlilo nalo leo hii, “Kwamba kwako nabii wa kweli leo ni yupi?” Ninaamini Shetani angewafanyia sherehe kubwa sana, angalijigeuza awe malaika wa nuru kama anavyowafanyia leo hii na angewapeni manabii wa “njaa yenu”; kila mmoja kwa kadiri ya tamaa yake!

  Unajua mkristo anapouliza “nabii wa kweli ni yupi?” Swali hili katika namna yoyote ile, huonesha kuwa mkristo huyo anahitaji msaada! Anahitaji kukalishwa chini na kufundishwa, kufundishwa kulitazama Neno la Mungu, ili awe ni mwenye kulirejea hilo katika mambo yote anayokutana nayo katika maisha yake, badala ya kuyategemea mambo ya mtaani au dini na shawishi zake!

  Hebu kitazame kisa cha yule mwanamke Msamaria pale kisimani, Yoh 4:7-30. Huyu alikuwa ni mwanamke wa kawaida tu wa mtaani, tena aliyeachwa na waume watano, hata huyu wa sita aliye naye si mumewe! Hakuwa na sifa yoyote ile ya utakatifu, lakini licha ya hali yake hiyo ya kiroho, alikuwa trained katika kuliangalia Neno la Mungu. Ndipo lile Neno lilipojidhihirisha mbele yake, she couldn’t miss It! “Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.” Kanisa halijui hata kama kuna nabii ajaye, achilia mbali kuwajua hata hawa marundo waliojitokeza wanatokea wapi!!!

  Huyo hapo mwanamke wa mtaani anayajua mambo hayo lakini makuhani wake hawajui chochote kuhusu hilo, mindset zao zimeelekezwa mbali sana na Neno la Mungu katika taratibu zao, kama ilivyo tena leo hii! Wakristo wanajipokelea tu kila ajiitae nabii ili mradi kawatabiria jambo linalowafurahisha! Angalia yaliyowakuta wenzenu, Mdo 5:36-37 “Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye… Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki…” Zigeuzeni nia zenu, rudini katika Maandiko kuyatafuta mambo ya Mungu, mtapona!

 43. Bwana unlitaka wawapake mafuta ili warejeshewe uhai,kwani TB Joshua ndiye aliyewaondolea uhai wao?
  Kila mtu ana namna yake ya kuondoka katika mwili. Nani anajua, labda siku yao ilikuwa imefika.

  Hilo si tukio la kwanza mtu kufa katika harakati za ibada, mimi namfahamu mchungaji mmoja aliondoka akiwa madhabahuni anahubiri.

  Halaf ndg. Orbi tatizo ni nini; watu kufa kwenye hilo kusanyiko au matumizi ya mafuta, au TB Joshua kutokuwa nabii wa kweli?

  Mimi huwa nasema mara kwa mara hata leo nasema kwako Orbi kuwa alipokuja Maboya anatumia kwa namna isiyo ya kawaida, watanzania walisema anatumia nguv za kuzimu, akaja Kakobe naye akitumiwa na Mungu isivyo kawaida wakasema anatumia uchawi wa kinaijeria na wengine wengi.
  Lakini sasa hivi hakuna hata mmoja anayeendelea kuwasema hao watumishi baada ya kuona kuwa si kuzimu wala Naijeria wanaowatumia hao watu, bali ni Jehova. Lakini sijaona hao watu wakisimama hadharani kutubu dhambi za kuwanenea vibaya hao watumishi.

  Otrbi wewe kwa kusoma makala zako mbalimbali unasound kama mtu mwenye uelewa mzuri wa Mungu, elewa kuwa haya maneno mnayopenda kuyasema juu ya watumishi wa Mungu mtayatolea hesabu. Ikiwa aliyempa upanga wake Sauli ili auangukie umuue, Daudi hakumwacha kuishi alimwambia kuwa alimgusa masihi wa Bwana, pamoja na kwamba Sauli alikuwa amekataliwa na Bwana.

  Nahisi kama watu wengi tunahukumu mambo ambayo hata kama ni ya kweli si saizi yetu kuyahukumu.

  Orbi kuna ubaya gani kutabiri matokeo ya mpira?
  Ulitaka afanye nini juu ya Boko haram? Kwani wakati Rwanda wamnamalizana Mungu hakuwa na mtu wa kumpa unabii ili atoe tahadhari?

  Tuonyesheni basi nabii wa kweli leo, mbona mnakwepa?!!!

 44. Mkandya…..Kwa nini hawakuwapaka mafuta hao marehemu na kuwarejeshea uhai ili “bwana” wa Nabii Joshua ajipatie utukufu…? Je kuna utukufu gani unaopatikana kwa hili tukio….? Sitaki kuandika mengi leo, kwani huko nyuma tulimuweka bayana kwa mapana na marefu “nabii” huyu Mnaijeria kwa kutumia Maandiko na nini kinachotokea ndani hilo Sinagogi lake….Lakini kizazi cha leo si kinataka Ishara…? Basi sasa kinaanza kupata ishara kamili kutoka kwa huyu “nabii Mnaijeria” Ameweza kumpa “mungu” wake utukufu kwa kutabiri kombe la nchi za kiafrika…..ambaye hata pweza alifanya…..na wanajimu na wasoma nyota wengi walifanya…….. Wakati Boko Haram inamaliza nchi yake kwa kulipua makanisa…….!Sasa Je Yatatimizwaje basi Maandiko yasemayo “YUMKINI KUWAPOTEZA HATA WATEULE” Wasipotokea “manabii” na “mitume” kama hawa katika zama za leo……….! Kweli Yesu alisema wazi……KAMA SIKU HIZO ZISINGALIFUPISHWA……na maadam hazijafupishwa…..tutaona mengi tusiyoyatarajia………

 45. Mama K, mimi napingana na wewe katika baadhi ya mitazamo yako. Sikia, hata kama umeokaka na umejazwa na Roho, usipochimba choo kipindupindu chaweza kuuondoa pamoja na huo upako ulio nao.

  Jiulize kwa nini Yohana mbatizaji alikufa akiwa kijana wala hakuwa ameshiba siku?

  Halaf hebu fuatilia kifo cha Elisha kilikuwaje?

  Point siyo mafuta, ni kukosa utaratibu ndiko kulikosababisha hao watu wafe. Hawakufa kwa sababu wamepakwa mafuta, bali ni kwa sababu ya kukanyagwa, suala ambalo ni la kiutaratibu tu wa kibinadamu.

  ANmina!

 46. Lenda kuna swali aliulizwa ndugu Lwembe hapo juu, sijui wewe kama unaweza kulijibu. Kwamba kwako nabii wa kweli leo ni yupi?

  Umewataja manabii kama Yermia, Isaya, Ezekiel n.k.
  Kwa mtazamo wa kwako na hata baadhi ya watu ni kwamba hao ndo walikuwa manabii wa kuaminika. Lakini unapaswa kujiuliza neno hili kuwa kama wewe ungeeishi katika nyakati za hao manabii ungeweza kuwaamini na unabii wao?

  Jibu lake ukitaka kulijua angalia kama watu wote waliwakubali hao manabii. Kumbuka wakati Yeremia anafuatwa na wana wa Israel wakitaka akawape unabii toka kwa Bwana, nae akawauliza kama Bwana akisema wataamini na kukubali, wakasema wataamini. Lakini mawazoni mwao walitaka unabii utoke ukiwaambia wakimbilie Misri. Yeremia aliwatolea unabii akisema kuwa Bwana asema watakaokimbilia Misri wataangamia kwa Upanga. Kwa hiyo ikawa kinyume na matakwa yao, wakamsakama Yeremia.

  Msidhani kuwa ilikuwa ni rahisi kuwaamini akina Isaya wakati ule, ilikuwa ni ngumu kama ilivyo tu leo. Kwa hiyo ninyi manaaona kila nabii aliyepo leo siyo wa kweli hata kama mgeishi wakati wa Yeremia na Isaya msingewaamini.

  Manabii wa uongo hawajaanza leo, hata wakati wa akina Isaya walikuwepo, lakini bado watu wenye kumwelewa na kumwamini Mungu walitambua kuwa akina Yeremia walikuwa ni manabii wa Mungu. Na wale wasioamini kama ninyi waliwaonea shaka kama ninyi mnavyoonea shaka kila nabii,wakati hata tukiwauliza mtuoneshe nabii ambaye ni wa Mungu leo hamwezi.

  Ni kweli manabii wa uongo wapo kama ambavyo manabii wa kweli wapo.

  Ukiwa huna hakika i bora kunyaza, maana si ujinga!

 47. EZEKIEL 13:17

  “NA WEWE, MWANADAMU, KAZA USO WAKO JUU YA BINTI ZA WATU WAKO, WATABIRIO KWA AKILI ZAO WENYEWE; UKATABIRI JUU YAO.”

  EZEKIELI 13: 18

  “USEME BWANA MUNGU WANGU ASEMA HIVI; OLE WAO WANAWAKE WALE WASHONAO HIRIZI KATIKA VIUNGO VYOTE VYA MIKONO, WAWEKAO LESO JUU YA VICHWA VYA KILA KIMO, ILI WAWINDE ROHO ZA WATU; JE! MTAZIWINDA ROHO ZA WATU WANGU, NA KUZIHIFADHI HAI ROHO ZENU WENYEWE?”

  EZEKIEL 13:21

  “ NA LESO ZENU NAZO NITAZIRARUA, NA KUWAOKOA WATU WANGU KATIKA MIKONO YENU TENA KUWINDWA; NANYI MTAJUA YA KUWA MIMI NDIMI BWANA.”

  MATHAYO 24:24

  “KWA MAANA WATATOKEA MAKRISTO WA UONGO, NA MANABII WA UONGO, NAO WATATOA ISHARA KUBWA NA MAAJABU,WAPATE KUWAPOTEZA YAMKINI HATA WALIO WATEULE”

  MATENDO YA MITUME 8:10

  “WOTE WAKAMSIKILIZA TANGU MDOGO HATA MKUBWA, WAKISEMA, MTU HUYU NI UWEZA WA MUNGU, ULE MKUU.”

  ISAYA 8:20

  “NA WAENENDE KWA SHERIA NA USHUHUDA; IKIWA HAWASEMI SAWASAWA NA NENO HILI, BILA SHAKA KWAO HAO HAPANA ASUBUHI.”

  EZEKIEL 13:10 ( EZEKIEL 13:1-70

  “KWA SABABU HIYO, KWA SABABU WAMEWASHAWISHI WATU WANGU, WAKISEMA AMANI; WALA HAPANA AMANI; NA MTU MMOJA AJENGAPO UKUTA, TAZAMA, WAUPAKA CHOKAA ISIYOKOROGWA VEMA”

  YEREMIA 23:14

  “KATIKA MANABII WA YERUSALEMU NIMEONA NIMEONA NENO LINALOCHUKIZA SANA; HUFANYA ZINAA; HUENENDA KATIKA MANENO YA UONGO, HUTIA NGUVU MIKONO YA WATENDAO MAOVU, HATA IKAWA HAPANA MTU AREJEAYE NA KUUACHA UOVU WAKE; WOTE WAMEKUWA KAMA SODOMA KWANGU, NA WENYEJI WAKE KAMA GOMORA”

  UFUNUO WA YOHANA 16:13

  “NIKAONA ROHO TATU ZA ZA UCHAFU ZILIZOFANANA NA VYURA, ZIKITOKA KATIKA KINYWA CHA YULE JOKA NA KATIKA KINYWA CHA YULE MNYAMA, NA KATIKA KINYWA CHA YULE NABII WA UONGO.”

 48. Oh my goodness, yaani huwa ikifika kwenye ishu kama hizi ndipo utajua kuna idadi kubwa ya wakristo wana ufahamu wa kuwatosha kwenda tu kanisani na kurudi nyumbani.

  Kwanza nawapa pole mnaohangaika na Lwembe, bila shaka hammfahamu vizuri uwezo wake wa kujenga hoja. Kuna issue za kubwabwaja nae lakini si issue kama hii. Kwa issue kama hii lazima uwe unamjua vizuri Lwembe.

  Watu mnasikitishwa na vifo vya hao wapendwa wakati mnajua kabisa kuwa kufa ni faida na kuishi ni kristo? Mtu mwingine ati kasema roho hizo zimepotea, duh pole!

  Mbarikiwe.

 49. Kwa kaka John Paul, naomba uniruhusu nijibu kama nilivyoelewa maswali yako,
  1 . swali namba moja umeuliza kama aliyekufa kipindi cha nabii Elisha alikufa peke yake au na wengine , Jibu ni kwamba alikufa peke yake kwa mjibu wa 2 Wafalme 7:2 ,20, Basi yule akida , ambaye mfalme alikuwa akimtegemea mkono wake , akamjibu yule mtu wa Mungu akasema , tazama kama Bwana angefanya madirisha mbinguni je jambo hili lingewezekana? akamwambia kuwa wewe utaona kwa macho lakini hutakula, 21 inasema Ikampata hivyohivyo kwa kuwa watu wakamkanyaga langoni akafa. hii inaonyesha aliyekufa ni yule aliyeambiwa kuwa atapata cha moto kwa sababu ya kutohamini kwake. Kumbuka kuwa Eliya na Elisha ni watumishi wa Mungu ambao walikuwa hawakopeshi Pia napenda tukosoane kidogo ktk hili ni kwamba umeandika nabii Eliya lakini tukio hili lilifanyika kupitia nabii Elisha siyo Eliya.
  2 Umeuliza kuwa kama watu wako ktk mahubiri mahali ambapo hakuna choo wanaweza kupata kipindupindu?
  Jibu kama wako sehemu linapohubiriwa neno kweli na nguvu ya Mungu iko pale ndugu yangu kipindupindu haitapata nafasi , kama wako pale wanamusikia Mungu wa kweli na wanaabudu ktk Roh na kweli nakwambia kipindupindu kitajifumba kinywa, Hebu tuangalie ukweli huu kupitia Marko 8: 1-4,9.Ktk siku zile kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, akawaita wanafunzi wake akawaambia , nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu watu wamekaa nami wala hawana kitu cha kula.4 wanafunzi wake wakamwambia je Ataweza wapi mtu kuwashibisha mikate hapa nyikani?Kumbuka pale walikuwa nyikani na kwa vyovyote wapo watu waliotaka kwenda haja ndogo na kubwa hata kama walikuwa hawajala kwa mda wa siku tatu, lakini hakuna ilipoandikwa kuwa watu wale walidhulika kwa kipindupindu maana nahamini kabisa hata siku zile kipindupindu kilikuwepo kama safura ilivyokuwepo Luka 14:2 inasema Na tazama , mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura.. Tukirudi nyikani kama watu wako sehemu linapohubiriwa neno Mungu atafunga hizo haja ndogo na kubwa ,hili watu wamsikilize yeye badala ya kuangaika kwenda haja ndogo au kubwa. Kumbuka Mungu anaweza kufunga na kufungua pia Isaya 22:22.ndiyo sababu nikasema kama watu wale wako mahali linapohubiriwa neno kweli na uweza wa Mungu uko mahali pale , Mungu atawasaidia wasidhulike kwa lolote hata kama wataenda haja kubwa mara mia kila mtu hawawezi kupata hicho kipindupindu.kama alivyowasaidia wale elfu nne waliokuwa nyikani wasikipate atawasaida na wengine maana ni yeye yule yule jana na leo na hata milele Waebrania 13:8 maana atuoni mahali watu wanalia kipindupindu ktk biblia hatuoni watu wakilia na kipindupindu ktk habari hii walipokuwa nyikani.na ninahamini kabisa kwamba nyikani hapakuwa na choo.
  3 Umeuliza kwa habari ya watu wanaopata hajari wakiwa ktk kuimba kwaya au kupeleka injiri , ndugu yangu ukiwa jemedari waYesu na asikari wa Yesu wakati mwingine unakumbana na mambo ya kijemedari, kumbuka Yohana 10:10 inasema mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuaribu, hapa huyu mwizi ni shetani na Yesu alikuja hili tuwe na uzima kisha tuwe nao tele. inabidi tujitahidi kusimama ktk maandiko ya ulinzi na tutumie damu ya Yesu kila wakati ktk maisha yetu kwa ajiri yetu na wapendwa wetu , hili shetani akija kuiba na kuvunja na kuharibu atukute tumo ndani ya safina ya damu ya Yesu.
  4umeuliza je kama watu wale kama walikufa kweli walitakiwa kuishi hadi lini,?Jibu. mimi nasema kama wale watu walikufa kweli walitakiwa kuishi siku nyingi maana imeandikwa kuwa kwa siku nyingi nitakushibisha zaburi 91:16. Mungu anapenda sana kutushibisha kwa siku nyingi angalia pia 1 Nyakati 29:12 , neno linasema kuwa Daudi akafa mwenye umri mwema , ameshiba siku na Mali, (John Paul na wanaosoma ujumbe huu mshibe siku, muishi umri mwema na mkawe na mali kwa jina la Yesu.) Maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwelu watoto wake.tusimame ktk neno lake maana tunachohamini ndicho kinachotokea , tunachokikiri ndicho tunachokipata. Ubarikiwe Ninakupenda na ninawapenda wana SG wote..

 50. Oguda, ni kweli, huu ni mkesha!!
  Swali unaloniuliza ndg Oguda, nadhani ni sehemu ya mkesha huo! Kwa mfano nikisema Oguda ndiye nabii wa kweli, bado itanilazimu nithibitishe jambo hilo kwa Maandiko, ni wapi ilipoandikwa ministry yako? Au nikiwa sina uthibitisho huo, basi nije na blah blah za miujiza na mahubiri matamu na watu kuokoka, na watu kumpa maisha yao Bwana Yesu na maji ya upako na mambo mengine ya siasa za dini, ambayo hukubalika na jamii kirahisi na kupingika kirahisi pia, yaani ule mkesha!

  Lakini, mimi sizungumzii siasa za dini, ninamzungumzia Mungu, udhihirisho wake! Yaani unaposema kwamba Oguda ni nabii, maana yake unasema Mungu ametutembelea, naye anautumia mwili wa Oguda, ule alioukomboa! Ndio maana Kristo alisema yeye ni Mwana wa Adamu, yaani nabii, Mungu akiwa ndani yake! Sasa tusemeje, kwamba Mungu anaweza kututembelea bila ya taarifa? Hivi Rais anaweza akasafiri hadi Mwanza bila ya taarifa? Hiki ndicho ninachokiulizia, hiyo taarifa ya kututembelea kupitia TB Joshua, iko wapi? Maana Biblia inasema “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” It is that simple!!!

  Na iwapo ujio huo haujawekwa wazi kwa manabii wake, basi it is not in the programme, that’s the long and short of it, miujiza notwithstanding!!

  Lakini tatizo liko wapi? At least Oguda unafahamu, shida ni hapo unapo compromise the truth! Wewe unafahamu fika kuwa kanisa, lilipozitupa nje zile Huduma Tano, wao walimfungia nje Roho Mtakatifu, yule Mwalimu, wakambadili na taratibu zao.
  Lakini Mungu alilitayarishia Kanisa lake mambo yote; “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.” Unaona ndg Oguda, Mungu HAJAWAHI kusema jambo halafu lisiwe, Kama ameusema utaratibu huo kwa ajili ya kuwakamilisha watakatifu wake, huwezi wewe ukawakamilisha nje ya mpango huo, ukifanikiwa, basi nawe utakuwa ni Mungu!

  Matokeo ya kuenenda nje ya mpango wa Mungu ndiyo haya tunayoyaona, makundi makubwa ya wakristo walioiva nusu yakizunguka zunguka kama yatima, kutoka kwa nabii huyu kwenda kwa yule!

  Kusanyiko halina mwalimu wala nabii wala mchungaji wala mtume wala mwinjilisti; ambavyo kwa kadiri ya vipawa hivyo vitano, kwa pamoja huileta Huduma ya Kristo katika kusanyiko. Huo ndio mpango wa Mungu! Kinyume chake makanisa yetu yanajiendesha katika mifumo waliyoibuni Wakatoliki kuvibadili vipawa hivyo, vingine wameshindwa kuviigiza na mwishoni kubaki na wachungaji na wainjilisti na walimu wa shule za jumapili za watoto na mashuleni! Ndipo makusanyiko yetu HAYAWEZI KUKAMILISHWA katika imani!

  Ndio maana ninapouliza ni wapi nabii Joshua alitabiriwa kuinuliwa, wengi wananiona mzushi, au nina wivu au ni mtu ninayependa kuwakashifu watu; hao wote ni wakristo wanaodai kuongozwa na Roho Mtakatifu halafu hawajui lolote kuhusu jambo hilo kuwa katika Biblia zao mambo hayo yameahidiwa, kwa hiyo wanayo haki ya kuwakagua hao manabii na mitume ili kupata uhakika zaidi kabla ya kuwapokea!

  Nazo taratibu hizo zimefikia wakati wake wa kujaribiwa, hao hapo manabii, kwa maelfu, hata walikotokea hawajulikani, wameibuka tu, mitume na manabii; makanisa hayana uwezo wa kuhimili kishindo chake, waumini wanavutwa kama na sumaku! Hata ukimuuliza nabii mwenyewe, chimbuko lako ni nini, hajui, yeye anahubiri injili ya miujiza tu! Na wengi hudhania kuwa hao ni wapentekoste, kwa kule kujiwakilisha kwao, nayo makundi yetu yamekosa ufahamu kwa kule kutofundishwa mambo hayo makanisani kwetu. Lakini Upentekoste HAUKUSIMAMA kwa kusimamishwa nabii, huo mlipuko wa Azusa! Alikuwa ni mchungaji aliyesimama katika Neno na kuisubiri Ahadi! Na uwepo wa Mungu ulishuka na kurestore yaliyo haribiwa. Jamani, hamjui mnakotoka? Hivi kuna yeyote yule ambaye amewahi kumsikia mzee Moses Kulola akijiita mtume au nabii? Mmewahi kumsikia Oral Roberts akijiita mtume au nabii? Huyo mchungaji Seymour wa Azusa , huyo mwenye kuhusika na huo “mlipuko, mmewahi kusikia kuwa alibadili title? Mmezikagua confession zao? Hivi hawa manabii mkiwakusanya, je wote wako katika imani moja? Are they speaking the same thing? THEY ARE NOT! “…atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?” Labda ndg Oguda unaweza kumjibu Kristo swali lake!

  Mkristo anashindwa kuamini kwamba miujiza na vipawa si kigezo cha kutumwa na Mungu, kwa sababu Biblia yake si Yakini yake tena bali wale manabii na mitume na wachungaji na wainjilisti na walimu wake wa mshahara!

  Mungu akimsimamisha nabii, kuna mambo mawili yanayokutokea, upende usipende, ukimpokea nabii huyo, umeokoka na ukimkataa YOU ARE LOST! There is no drunk sober man position katika jambo hilo. Mambo ya sijui hajapata nafasi moyoni mwangu ni siasa za dini; Mungu hajapata nafasi moyoni mwako!? Yaani wale watu wa Ninawi wangesema Yona hajapata nafasi moyoni mwao, si wangekuwa wako chini ya bahari before they knew it!

  Basi ndg Oguda, ktk jambo hili, kweli ni ‘ngoma nzito’ (mpendwa Haule alisema, “mbombo ngafu”); nabii hawezi kukosa watu wa kumpokea, hata akiwa ni wa Uongo, ndipo mimi NINAKUBALI KUPOTEA kwa KUMKATAA nabii Joshua na nitabishana na Mungu mpaka anioneshe ni wapi alipoahidi ujio huo. Na hao waliompokea, nawatakia “Safari Njema” – BON VOYAGE!!

 51. Ktk hili nasema pengine tusimame ktk maandiko , na hili tujue habari hizi kamili wa kutusaidia ni Roh mtakatifu, imeandikwa ktk Yohana 14:26 kuwa atatufundisha na kutukumbusha yote , ndiyo maana anitwa msaidizi hili atusaidie ktk maeneo yale ambayo hatujui na tunapata tatizo kuyafahamu, yeye amebobea ktk kila neno na ana uweza wa kutupa ukweli wote. Tusome pia 1 Yohana 2:27 neno linasema Nayo mafuta yale mliyopata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha , hii aimaanishi kuwa hatuna haja ya wachungaji au hatuitaji mafundisho la hasha , inamaanisha kuwa kuna anayeweza kutupa msaada kutupa majibu ambayo mwanadamu yeyote hawezi kutupatia, Mfano wangu mwenyewe kuna mtumishi nilimuongelea na kaka yangu, kaka yangu ameokoka akaniambia kuwa kuwa makini sana na mafundisho yake alinishauri kuwa nimuombe Mungu anionyeshe ukweli,, nilifanyia ushauri ule kazi nikaingia maombi ya kufunga na kuomba , kweli baada ya week kama moja Mungu aliniletea yule mtumishi ktk ndoto usiku tuliyoongea mimi na yeye yalinipa jibu la swali langu . Mbarikiwe sana watu wa Mungu ninawapenda sana.

 52. Kuna faida gan kuhubiri uponyaji na huku roho inaangamia na kwenda jjehanamu Yesu kaja kuweka huru kila kifungo s cha magonjwa peke yake ila kifungo cha dhambi nk. kwa ushauri wangu tutamchambua Tb Joshua mbaka basi huyu atasema hili na huyu atasema hili lakin kikubwa cha ujadil watu waijue kweli ya Mungu Tu ili waweze kutambua huyu ni nabii wa uongo au ni nabii wa kweli hata Yesu alipo fanya miujiza mingi wasema anatoa pepo kwa kutumia mkuu wa pepo mathayo 12:24-37, Hivyo basi hatupaswi kumtazaa mtumishi wa Mungu kwa macho ya kibidamu udhania kumbe siye unaona ndiye kumbe siye cha msingi tutakiwa tusiamini kila roho inayo tujia bali tuzjaribu kama kweli zimetoka kwa Bwana na kwa kibnadamu chetu maana mambo ya roho hutambulikana ktk Roho, na si kwa kibidamu kwa ubinadamu tumefichwa mengi sana ila tukiwa na Roho atatufunulia mafumbo na siri zilizo jificha, ila tukitaft kwa ubidamu tuishia kukosoa huduma. wapenz katika Bwana nawasihi katika Roho kwamba tuwe makin nyakat hizi kila mtu asimama kwa miguu yake ili Bwana akapate kusema naye binafsi Ezekieli 2:1- kuna faida kuzunguza na Bwana. amina tuwe macho na kukesha kukitambua shetan yuko mawindoni akiwinda watu wa Mungu apate kuwaangamiza. watumishi uwaye yoyote songa katika hudum yako iwe kuhubiri basi hubiri kwa moyo iwe unabii kaa uweponi mwa Mungu ili upate ujumbe wa kulifaa kanisa na nchi pia kwa ujumla iwe mchungaji chunga kwa unyenyekevu kondoo uliwopewa na Bwana na kuzilea kwa kicho cha kristo. waombeni watumishi wa Mungu katika kuombea na kuakaa uweponi mwa Bwana utawajua zaidi kama kweli ni watumishi wa kristo ila tusikulupe na kuwanena vibaya kama hatuna uthibitisho katika neno na Roho mtakatifu akishuhudia ndani yetu.
  nimejifunza kupia mjadala huu
  AMANI YA KRISTO IWE PAMOJA NANYI NYOTE BARIKIWA

 53. Jina la BWANA lIBARIKIWE.kwa kweli nashukuru nimeingia katika mtandao huu sikutegemea, namshukuru Mungu kuwa kuna watu wanajuwa kuchambua Neno.Ninaona jinsi ndugu Lwembe na Grace walivyo na taadhari naunga mkono maoni yao na kwa kweli ukiwa mtu wa rohoni yanagusa/yanaonya kabisa yaani ROHO MT.anaonesha waziwazi jinsi ambavyo kanisa lisivyofanana na kanisa la kwanza(misingi ya manabii na mitume)hali ya sasa hivi inatisha sana kwa sisi tuliookoka zamani yaani 1990 kurudi nyuma.Kwanza jiulize ktk magazeti ya tanzania kulikuwa na matangazo ya waganga wa jadi wakitangaza wanatibu hiki na kile wengi sana.Je wamekwenda wapi? umesikia kuna mmoja ametokewa na YESU kuwa atubu na aende kanisani akatubu aombewe aokoke?hayo makundi ya makuhani wa majini au wenye kumsikiliza shetani na kuafikiana nae wako wapi?wamehama Tz wakaenda kenya?kuna mtu mmoja hivi mwanzo alikuwa kanisa fulani akatolewa kwa mgogoro fulani,tulipokutana siku moja akasema anafanya huduma za kinabii,..njoo uone hema langu watu wengi.. napuliza tuuu watu wanaanguka..alijigamba.na wa aina hiyo ni wengi sana kama anavosema Lwembe na Grace.- Kama MUNGU akituweka jiandaeni kuona mwisho wao na sio mwanzo.Lakini kwa hofu na sio kuwa tuwaseme-hatujaruhusiwa kuwanenea watumishi mabaya,ila tuzipime roho zilizo juu yao. tujiepushe nazo hata kama anafanya ishara kuu-tishika na utakatifu bila dhambi na sio ishara ya mtu.

 54. Well said CK Lwembe
  .Tunaishi nyakati za mwisho njaa,magonjwa,ujasusi,na shida za kila aina.Napenda kuonya mwili wa kristo tuwe makini sana na tusikimbilie manabii, manabii wengi wanajitokeza kila kukicha baadhi yao ni wa kweli na wengi sana ni wa uongo .kuna makanisa mengi sasa hivi yanatoa waumini wao kafara kwa shetani.Ndudu zangu tuwe makini sana na makisa yanayoweka miujiza mbele badala ya kufundisha neno na kuwapeleka watu kwa Yesu ( wokovu).Na utashangaa watu wanasafiri hadi Nigeria kwenda kuponywa,wakati kupona ni imani,unaweza kubaki Tanzania ukasimamia ahadi za Mungu za uponyaji na ukapona.Tuwe makini hizi nyakati tunazoishi watu wanaweza kuishia kutolewa kafara kwa shetani bila kujijua,neno linasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.Naomba makanisa yafundishe neno , watu wakijua neno watakuwa huru.
  Mbarikiwe sana wapendwa.

 55. Mtakesha saaana, hiyo ngoma ni ‘nzito’, lkn mnaweza kuimudu. songeni mbele wana wa Mungu.

  just come clean mr. Lwembe, nani kwako basi ni nabii wa kweli toka mlipuko wa Azuza, America???

  Tufundishe namna ya kumtambua nabii wa kweli sasa ili tsambamba, vinginevyo, ni assumptions tu km zilivyokuwa wkt wa Kristo.

  Tatizo nilionalo ni lilelile, la mwl kutaka kuwa mtume, ama , mch kutaka kuwa nabii, ndicho kinallitesa kns la Kristo leo hii. Kujitambua ndiyo tatizo kubwa miongoni mwetu, 1kor.12 yoote, utajitambua uko wapi. You can not claim kujua siri ya mtungi wkt kata ndiyo inayoijua na mbebaji wa mtungi. jua wewe umeitiwa nini kwenye mwili w Kristo.

  Good evening, mubarikiwe.

  Oguda

 56. Sam nakubaliana na wewe kuhusu mtumishi kupata nafasi ndani ya moyo wa mtu. Mimi huyo tbjoshua hajapata nafasi ndani yangu hivyo mwanzoni sikuwa na uhakika nae lakini baada ya kufuatilia sana,kumsikiliza na zaidi kupima/kutambua matendo ya huduma yake sina shaka na huduma Bwana aliyompa.

  Neno la Mungu linasema hata kama mtu akiwa nabii wa uongo mwisho wa siku tutamtambua kwa matendo yake. Na matendo ya tbjoshua ni yenye kumrudishia utukufu Bwana na si kujisifia/kujitukuza yeye binafsi, unyenyekevu wa hali ya juu kwa Roho Mtakatifu, watu kuokoka, watu wengi kusikia/kuhubiriwa habari/injili ya Yesu hadi miisho ya dunia (kwa njia ya tv,etc),kuponywa magonjwa na kufunguliwa kutoka vifungo vya giza, kuwapenda na kuwasaidia maskini,etc.
  Ukipima na kulinganisha na neno la Mungu hakika watumishi (hasa wa Tanzania) inawafaa kujifunza kwake hasa kwa hili la unyenyekevu kwa Roho Mtakatifu na kutojirudishia sifa/utukufu.

  Maria

 57. Ndg Sam,
  Labda nikushukuru kwa wazo lako hilo lenye changamoto! Unajua, ni kutoka katika “uchanga” ndipo watu hukua hata kufika katika “ukomavu” na hivyo kuwa na uwezo wa kujibu hoja straight na kuyatafsiri Maandiko inavyopasa!

  Ninajua nimekusikitisha kwa “uchanga” wangu, uniwie radhi! Lakini wewe umenifadhaisha zaidi katika “ukomavu” wako kiroho, na umahiri wako wa Maandiko, kwamba nilitegemea unipe “jibu straight” la swali dogo nililokuuliza; TB Joshua, ni nani katika Maandiko? Badala yake umeishia kuniteremshia masikitiko ya uchanga wangu ambayo hayajanisaidia sana katika jambo tunaloliongelea. Tena katika ukomavu wako, naona umenionesha umahiri katika kuzitafuta link za TB Joshua kuliko Maandiko, au hizo link ndilo Neno la Mungu?

  Mwisho labda niseme tu kuwa tumekutana sote “tusio na uwezo wa kujibu hoja straight na kutafsiri maandiko ni mdogo labda tu-wachanga kiroho au tunapotea kwa kutoyajua maandiko.”

  Basi, nakushauri tuendelee kujifunza kwa waliokomaa badala ya kujiingiza katika wishful thinking za ukomavu, ambazo zinatuingiza katika ngome za kiroho kwa hasara yetu wenyewe!

 58. Ck Lwembe nasikitika uwezo wako wa kujibu hoja straight na kutafsiri maandiko ni mdogo labda u-mchanga kiroho au unapotea kwa kutoyajua maandiko.

  sam

 59. Waraka wa kwanza wa Yohana 4:2, jamani ukristu ni imani na si dhehebu,kanisa,sinagogi au mchungaji.Ukiamini katika Kristu ya kwamba ni mwana wa Mungu na kufuata amri zake, kamwe hautoweza kupotea,tujiulize yule mwethiopia aliyebatizwa akiwa njiani alienda kuhubiriwa na mchungaji,nabii au mtume gani? Roho wa Kristu (ambaye ndiye yeye) aliye ndani yako, atakuongoza katika kweli yote, naamini kabisa siku ya Bwana watanyakuliwa waumini na wachungaji wao wataachwa. Kristu alipotoa ule mfano magugu mathayo 13:24-30 alikuwa akionyesha wazi mbinu atakayoitumia kuwashughulikia wajiingizao katikati ya injili yake na kuipotosha ni kwamba atawaachilia wakue pamoja na ngano kwa kuwa iwapo angeliwang’oa wakati mavuno hayajakomaa angeliweza kuharibu na mavuno yake.(watumishi),Hatutohesabiwa kwa sababu ya manabii,mitume au wachungaji bali kwa sababu ya imani, Swala la mtumishi wa Mungu kuhofia vipawa vya Kiroho kama miujiza,uponyaji,unabii,uchungaji,uinjilisti..kosa hilo halina rehema!(huponi) ni kheri kuugua hata Ukimwi unaweza kupona kwa jina la Yesu! lakini swala kumkashifu Roho ni la kuangamia mwili na roho Jehanam, Kuna AMRI MOJA TU muhimu ambayo watu wa kristu wamepewa duniani nayo ni mpende Bwana Mungu wako na jirani yako yaani PENDANENI na sio HUKUMIANENI! muhukumu wa kanisa la Kristu ni Kristu na si watumishi.Wacha neno la Mungu limuhukumu mtu yaani iwapo ameenda kinyume nalo na si kuhukumu kwa hofu yetu juu ya kazi na miujiza ambayo nayo ni moja kati ya alama za utendaji kazi wa Mungu tangu kale.
  Uoga ni tunda la udhaifu wa kuwa na imani haba,ni njia kuu aitumiayo Shetani kuikwamisha kazi ya Mungu,Timotheo 2:14-15
  Mbarikiwe!

 60. @ Sara,
  Dada yangu umenifurahisha saana! Eti, “Au wewe mwenzetu ni ‘roho’”! Hahahaha…!
  Sara, sote tu ‘roho’ iwapo tumezaliwa kwa Roho (Yn 3:6)!!! Naye Roho wa Mungu anapotufunika, ndipo hutufunulia yaliyojificha! Naye Roho wa Mungu hapatikani nje ya Neno lake. Tazama hapa anachosema, Yn 6:63 “…maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Unaona dada Sara! lijaze Neno la Mungu ndani yako, hilo ndilo Roho tena Uzima! Basi lolote linalokujia, lipime kwanza hapo katika hilo Neno lililojaa humo moyoni mwako, usitumie akili, shetani anajua jinsi ya kuzichezesha akili zetu mpaka tumfuate!

  Basi, rudi katika Maandiko, itafute huduma hiyo ulipoahidiwa, usipoiona, basi endelea kuitazama ili kujionea ile Mt 24:24 inavyotimia, jinsi makundi yetu yanavyosombwa na Elnino za manabii, si huko tu hata wa hapa kwetu!

  Pia, unapaswa kufahamu kwamba Mungu alisema hao wamepakwa mafuta kwa ajili hiyo, kwahiyo usitegemee kuwakamata kirahisi kwa kuwasikiliza mahubiri yao, yanbariki saaana, ukiumwa unapona, biashara zinafanikiwa na mambo mengi mazuri tu, lakini mwishoni watakufikisha katika kulikana Neno la Mungu, japo nukta moja tu, bali hiyo inatosha wewe kutupwa nje ya wokovu! Duh, ni balaaa kiasi gani!

 61. @ Zoe,
  Unajua hayo unayonitaka nikuoneshe, sidhani kama ndiyo yatakayokupa ufahamu. Biblia inapokuambia kuwa Shetani hujigeuza awe kama malaika wa nuru, wewe hulichukuliaje jambo hilo? Kwamba ajapo kwako huyo aliyejigeuza atakuwa na yale mapembe wanayomchora? Mungu ametufundisha kulitazama Neno lake! Tunamtambua mtumishi wa Mungu kwa Neno la Mungu tu. Jambo la kwanza ndio hilo, tunataka kujua nafasi yake hiyo ya unabii iko wapi katika Maandiko ili tuitambue Huduma yake! Kristo hakutambuliwa kwa miujiza bali kwa Neno la Mungu alilolileta kupitia manabii wake, “Bikira atachukua mimba”, ikawa hivyo! Ni lazima mambo hayo yaoane, utabiri katika Neno na kudhihirika kwa jambo hilo, vinginevyo mtampokea Ibilisi kama wenzenu Wasabato!

  Lete udhihirisho wa Maandiko, TB Joshua, hiyo huduma yake ni nini na iwapi katika Maandiko? Ukiuleta udhihirisho huo, ndipo twaweza kwenda hatua inayofuata. Ni vizuri na ni salama tukikaa ndani ya Maandiko badala ya hisia zetu!

 62. @ Sam
  Ninakushukuru kwa kunipa link ya habari za Tb Joshua.

  Kwa bahati mbaya hukunielewa nilichokizungumzia. Mimi sikutaka kuzijua habari zake binafsi, ndio maana nilikuletea ule mfano wa Wayahudi na Yohana Mbatizaji. Nikakuambia kuwa wale Wayahudi walimfahamu Yohana kuwa ni mwana wa Zakaria, kuhani, lakini walitaka kujua yeye ni nani kulingana na Maandiko!! Tazama maswali yao wanayomuuliza Yohana KUHUSU HUDUMA YAKE, (sio, sijui wewe ni kabila gani?): “Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?” Yn 1:21-23. Nae Yohana jibu lake lilikuwa hivi: “Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.” Unaona, hakuanza kusema eti oh, mnanionea wivu nk. Yeye anajua anakotoka, hajakurupuka tu, bali amekuja kulingana na Neno la Mungu, nayo Huduma yake inalidhihirisha lile Neno lililonenwa, sasa likikamilishwa. Je, kuna jambo gumu gani nasi tunapomuuliza nabii wako?

  Nikiyarejea maswali yako, kwamba nimewahi au sijawahi kuiona mistari mingi inayoonesha huduma ya kinabii hadi nyakati hizi! Mistari niliyoiona kuhusu unabii, ni ile inayohusiana na vipawa katika makusanyiko yetu, kama 1Kor 12:4-11 na pia zile Huduma tano, katika Efe 4:11, vipawa ambavyo viko chini ya mchungaji wa kusanyiko (local church) hapo vinapo hudumu. Kusanyiko lolote lile linalodai kuwa linaongozwa na Roho Mtakatifu, linapaswa kuwa na vipawa hivyo pamoja na hizo Huduma.

  Lakini linaposhindikana jambo hilo, ndipo Mungu humsimamisha nabii kutoka uweponi Mwake; nje ya zile huduma tano zilizoshindwa na vile vipawa tisa vilivyofishwa, ndipo nabii huletwa kwa kazi ya kulirejesha Kanisa (lote la ulimwengu/dunia) lililopoteza mwelekeo na kusambaratikia vipawa na miujiza na kuipenda injili ya uongo kuliko ile Kweli, kanisa ambalo halina Kipimo tena cha kuwapimia manabii na mitume; Mungu ameahidi kumleta Elia kwa kazi hiyo kwa ajili ya Kanisa, ule mwili wa Kristo, Malaki 4:5 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya.” Huyu ndiye nabii ambaye Kanisa lapaswa kumtarajia, Je, ndg Sam, ndiye huyo TB Joshua? Na kama si huyo, je, ni nani basi? Suala kwamba Biblia imtaje kwa jina, ni la kimwili saana. Hakuna mahali katika Biblia ambapo tumeelekezwa kumfuata Mungu kupitia majina ya watu. Tumefundishwa kuzijaribu roho na si majina! Huo ndio Mwongozo tunaopaswa kuufuata, TUZIKAGUE ROHO, sio kupofushwa na miujiza!

  Pia kuna manabii wengine wawili, hawa hawalihusu Kanisa bali Israeli, Mungu ameahidi kuwapelekea hao katika Ufu 11. Kwahiyo, sidhani kama TB Joshua atakuwa ni kati ya hao, kwani mazingira hayaruhusu jambo hilo la yeye kuwa nabii kwa Israeli huku akiwahudumia Mataifa!

  Lakini, Kanisa, pia linayo ahadi ya manabii wasio na idadi katika Mt 24:24! Hapa ndio “akili mu kichwa!”

  Kuhusu huduma ya mchungaji wangu kuwa ametabiriwa katika Biblia? Mchungaji yeyote anayehusika na kusanyiko la Mungu ni lazima awe katika kiwango kile cha Efe 4, zile Huduma Tano. Naye mchungaji huyo atayafundisha yooote kama yalivyofundishwa na mitume, maana Kristo aliyaweka yote ndani ya mitume wake ili tuletewe, basi aliyewapokea mitume amempokea Kristo. Ndipo mchungaji huyo, atalileta kusanyiko hilo, kwa mafundisho hayo ya mitume, katika umoja wa Roho. “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote” Efe 4:4-6. Hata yakiwako makusanyiko milioni mia duniani, yakiwa chini ya wachungaji hawa, yataufikia huo umoja wa Roho na vyote hata kuwa mwili mmoja, maana fundisho lao ni moja! Haya ninayokueleza ndiyo niliyofundishwa na mchungaji wangu!

  Pia kuna wachungaji wa vyuo, hao kila mmoja huja na fundisho lake kulingana na chuo alichosomea. Kama ni Mkatoliki atakuhakikishia kuwa mwombezi ni Mariamu mama wa Mungu”, na kama ni Msabato atakuhakikishia kuwa nabii aliyetabiriwa ni “mama Ellen White”; nawe Sam, kuhusu mambo haya, ninakuona unayanawa maji kama Pilato, kuwa huoni kosa lao! Hiyo ndiyo Injili maarufu leo hii, inayo compromise Neno la Mungu! Sikiliza Sam, Mungu hapigwi fiksi, kama hiyo midude ya Katoliki sio Injili, basi kuyaonesha hayo hivyo ndiko kutakako wasaidia Wakatoliki wanaoweza kusaidika kuikimbia Hukumu inayokuja, kama ambavyo tunakuambia wewe nawe, kuwa mtazame vizuri huyo nabii wako!

  Swali la mwisho unaloniuliza, “”Naomba ujibu hoja “ni ujumbe upi huo kibiblia unaoweza kumdhihirisha mtumishi wa Bwana tbjoshua kuwa si nabii??”” Jibu ni kwamba, sijakataa kuwa huyo si nabii, bali sijausikia ujumbe wowote kutoka kwa TB Joshua unaomdhihirisha kuwa yeye ni nabii kutoka Uweponi mwa Bwana kulingana na Ahadi ya Mungu. Ndipo naweza kusema kwamba huyo ni nabii kulingana na Mt 24:24, lile kundi kubwa lisilo na idadi wala ujumbe, lililoibuka siku za leo ktk kila kona; labda mnioneshe huduma hiyo imesimama katika Andiko lipi na udhihirisho wake. Tuambieni, TB Joshua ni nani???

 63. MAMBO MENGINE HUONEKANA MEMA MACHONI PA MTU, KUMBE NI NJIA YA MAUTI! INAFAA NINI KUCHUKUA KIASI KIKUBWA CHA UTAJIRI WAKO ILI KUINUNUA HEKIMA WAKATI MAARIFA HUNA? ACHA NENO LA mUNGU LIKAE KWA WINGI NDANI YA WATOTO WA MUNGU!

  TB JOSHUA NI MTUMISHI WA MUNGU, ACHA AFUNGE MATITA MATITA YA MAGUGU TIYARI KWA MOTO, kAMA YEYE SI MBEGU, NAMSHAURI ASIACHE ILI NENO LA MUNGU LITIMIE NA IONEKANE KUWA MUNGU NI MKWELI KWA NENO LAKE!

 64. Bwana Yesu asifiwe, ni kweli roho mtakatifu ana njia mbali mbali ktk utendaji wake, mfano tukiangalia Yesu alimpaka kipofu tope, naaman akaambiwa akaoge mara 7 mto yordani, mwingine akaambiwa akanawe ktk birika la sloam, lkn tujue wapendwa lilikuwa agizo kwa wakt husika na walipotii walipona, maji ya mto yordani wengi nadhani wanaoga na kuogelea lkn kwa kuwa si agizo hayana nguvu ya uponyaji, leo basi tungechukua tope tuwapake vipofu wote wa watanzania kwa kuwa si agizo la roho mtakatif upofu wao hautaondoka, hivi vitu vya upako , sabuni,mafuta,tope la mto yordani, maji ya israel ,maji tusifanye ndio fundisho, tuliangalie neno tutapona roho na mwili

 65. CK lwembe umesema “TB Joshua yeye binafsi, bali ninaizungumzia “roho” inayohudumu katika kusanyiko hilo, kwamba roho hiyo si ile ya Kristo maana imeshindwa kujitambulisha huduma yake ndani ya Neno”. Mimi mbona namsikiliza huyu mtumishi na sijaona kama anahubiri nje ya neno la Kristo. Au wewe mwenzetu ni ‘roho’ basi utufunulie hapa hilo neno analohubiri lililo kinyume na neno la Mungu.

  Sara

 66. asante ndugu Lwembe.

  Mimi nadhani katika hoja ya uhakika wa mtumishi TBJOSHUA ungeleta hapa mambo unayoona anayafanya ambayo yapo kinyume na neno la Mungu ili kutusaidia kufahamu (kama hatukuyafahamu). Otherwise kumkataa tu ni sawa na kipindi cha Bwana Yesu ambapo hata ndugu zake wa damu hawakumwamini (Yoh7:5) na wengine wakasema sivyo anawadanganya makutano (Yoh7:12).

  So kama hautakuja na mambo anayofanya direct ya kuonyesha wapi TBjoshua yupo kinyume na neno la Mungu then hatutashangaa sana maana kama hata kwa Bwana Yesu walishindwa kuthibitisha direct si itakuwa zaidi kwa mtumishi mdogo kama tbjoshua.

  Zoe

 67. ndugu Ck Lwembe naona haupo straight kwenye kujibu maswali simple niliyokuuliza zaidi ya kuongea spiritual politiks ambazo si mahali pake.

  Kama unataka kujua TB Joshua ni nani unaweza angalia historia yake kwenye mtandao wake (www.scoan.org/about/prophet-tb-joshua/‎) maana mm binafsi sikuzaliwa nchi anayotoka hivyo siwezi kujua maisha yake binafsi zaidi ya kuchambua na kulipima neno la Mungu analohubiri na sijaona anapokwenda kinyume na biblia. Nachelea kufuatilia ukoo, familia, ndugu,etc anakotoka zaidi ya kufatilia kama neno li sawa na bible maana hata Bwana Yesu kuna waliohoji kama neno jema laweza kutoka nazareti alipozaliwa.

  Unasema “akiwa ni nabii, basi sharti huduma yake iwe imenenwa katika Maandiko. Iwapo hamna uwezo wa kuionesha huduma hiyo ilipotabiriwa katika Maandiko, basi jueni wazi kuwa mna matatizo!! ” labda nikuulize kwa kusoma kwako biblia hujawahi ona mistari mingi inayoonesha huduma ya kinabii hadi nyakati hizi?kama ndio basi nadhani utumie muda kusoma. Au labda ulitaka huduma yake itabiriwe kwa kumtaja jina lake?..je huduma ya mchungaji wa kanisa lako imetabiriwa kwa namna hii katika biblia?

  Si kila mtumishi lazima apate nafasi kwenye nafsi ya mtu na kutopata hiyo nafasi hakumuondolei utumishi huyo mtumishi. Binafsi kuna watumishi ambao Mungu hakuwapa nafasi ndani yangu lakini nina uhakika ni watumishi halisi kama inenwavyo kwenye biblia.

  Juu ya ukatoliki au usabato nimeshaeleza kuwa ukihubiri injili ya Yesu na kumwacha Mungu aliyehai ajitetee na kuwashuhudia wote ambao wanamhitaji hakutakuwa na haja ya kusimama na kufanya hukumu kazi ambayo hatukupewa..acha watu wachomwe mioyo na injili kama biblia isemavyo nao watajua njia sahihi ya kuifuata na si kutumia nguvu ya kusema dhehebu hili ama lile ndio sahihi.

  Naomba ujibu hoja “ni ujumbe upi huo kibiblia unaoweza kumdhihirisha mtumishi wa Bwana tbjoshua kuwa si nabii??pia labda utupe na mfano halisi ( kwa kumtaja jina) wa sasa kwa mtumishi yoyote yule unaemfahamu ambaye kwa uelewa wako anastahili kuitwa nabii”

  sam

 68. Ndg zangu, Sam na wengineo,

  Kwanza, niwashukuruni nyote kwa mawazo yenu mazuri mliyoyatoa, ninaamini yanawakilisha kile kilichomo mioyoni mwenu.

  Pili, tunapoyatafakari mambo ya Mungu, haswa katika nyakati hizi tulizomo, ni muhimu kwetu kutambua na kuamua tafakari yetu isimame katika Msingi upi, Msingi wa Neno la Mungu katika ukamilifu wake au Msingi wa kidhehebu (katika maana ya mafundisho yetu tuliyoyazoea)?

  Labda nijisemee hivi, mimi, Msingi ninaoupenda, na ambao nimejihakikishia kuwa hautetereki, ni NENO LA MUNGU kama lilivyofunuliwa katika BIBLIA. Hii ndiyo YAKINI yangu. Japo nikishindwa mahali fulani, bado nitaamka kuikabili Challenge ya Neno hilo, maana ninafahamu kuwa jambo hilo ni kati ya mimi na Mungu, naye Mungu amenitaka NITHUBUTU kulichukua Neno lake; ninaamini hilo ndilo linalompasa mkristo yeyote yule, KUTHUBUTU!

  Kuhusu kumsikiliza TB Joshua, binafsi nimemsikiliza sana, ili niweze kuwa katika nafasi ya kufanya uamuzi sahihi, ili akiwa ni nabii wa Mungu, basi nimpokee yeye na ujumbe aliokuja nao kwa ajili yangu kulingana na Ahadi ya Mungu ihusuyo ujio wake; la siyaoni hayo katika huduma hiyo, basi nabwaga manyanga! Mimi nafahamu kuwa Mungu alikwisha lifunga Neno lake ktk Biblia, ndipo yeyote anayekuja leo hii, haswa akiwa ni nabii, basi sharti huduma yake iwe imenenwa katika Maandiko. Iwapo hamna uwezo wa kuionesha huduma hiyo ilipotabiriwa katika Maandiko, basi jueni wazi kuwa mna matatizo!!

  Pia nimekusisitizia kuwa nabii ni kipawa ambacho mtu huzaliwa nacho, hakina majuto. Kwahiyo mimi sikusema kwamba TB Joshua si nabii, wala reference yangu ya Maandiko hailioneshi jambo hilo hivyo. Biblia ikisema watakuja “manabii”, tena watakuwa wapakwa mafuta, basi twapaswa kuamini hivyo, ndio maana unawaona akina TB Joshua wanatabiri mipira na vifo na siasa na kuwatabiria waumini wao kuhusu hili na lile! Pia kwa upako huo wanaihubiri Injili moto moto isiyo na mwelekeo wowote, pamoja na wokovu au kuongoka na uponyo na miujiza yake, kwa ajili ya kuwakusanya wote ambao majina yao hayamo katika kitabu cha uzima! Unaona, Mungu alisema hao ni wapakwa Mafuta, nawe elewa hivyo, hao si wa kuchezea, UTAPOTEA!! Sasa jambo hilo si la ajabu, Balaam alikuwa ni nabii, alitabiri mpaka kuzaliwa kwa Kristo, halafu alikuwa ni MCHAWI! Kwahiyo wa Uongo na wa Kweli, wote ni manabii, tofauti yao ni ile Mbegu iliyomo ndani yao, kama ndani yao kuna uzao wa Mungu (1Yoh 3:9-10), basi watanena na kufundisha jambo lile lile walilonena manabii wenzao na mitume maana huo ndio Msingi ambao Kanisa limejengwa juu yake. Kwahiyo ni vizuri uchukue wasaa kidogo, uirudishe huduma katika Maandiko, kama unaweza kuthubutu!

  Pia hoja yangu kuhusu Ukatoliki na Usabato Masalia, yawezekana nawe ukawa ni sehemu ya Injili ile ambayo “si moto wala baridi” ile Injili vuguvugu, hiyo inayozalishwa vyuoni, lakini ndugu zangu, nabii anayetoka Uweponi mwa Bwana ni lazima aje na Neno litakalo yaondoa machafuko yaliyopo leo hii kuhusu Imani, 1Kor 14:33 “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani”! Nabii wa Mungu hawezi kutengeneza dhehebu lake, halafu awe kimya kuhusu nafsi zinazoangamia katika injili za uongo! Nimekutajia Ukatoliki na Usabato kwa sababu hao hawana tofauti na SCOAN, ndani yao hakuna Neno la wokovu, ni miujiza tu ya majengo mazuri na uongo na vipawa!

  Wingi wa watu katika huduma si kigezo cha uhalali wa mhudumu! Wengi wetu huvutwa katika huduma kwa kigezo hicho, lakini huo ni utoto tu. Na katika utoto huo, pale huduma wanayoipenda inapokosolewa kulingana na Maandiko, basi wengi wao hukimbilia kujihami kwa maneno kama “wivu” au “usihukumu” na visingizio vinginevyo katika uoga wao wa kusahihishwa. Hivi ndg zangu kuna Injili isiyo na Hukumu? Au ninyi mnaelewa nini hapa pazia la Injili linapofunuliwa, Mk 16:16-17 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”, je, hamuioni hiyo Hukumu inayoambatana na Injili? Palipo na Wokovu, pana Kuangamia pia!!!

  Pia ni vizuri ukafahamu kwamba mimi simzungumzii TB Joshua yeye binafsi, bali ninaizungumzia “roho” inayohudumu katika kusanyiko hilo, kwamba roho hiyo si ile ya Kristo maana imeshindwa kujitambulisha huduma yake ndani ya Neno. Yaani leo hii tunayo maswali kama waliyokuwa nayo wale Wayahudi kuhusu Yohana Mbatizaji, Yn 1:19 “Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?” Sasa, si kwamba walikuwa hawamjui, la, wanamjua ni mtoto wa kuhani, tena wa uzeeni, ila wanataka kujua Huduma hiyo ni ipi katika Ahadi ya Mungu? Sio mtu ajikurupukie tu, miujiza haijalishi, bali tunataka tujue TB Joshua ni nani? Kama kuna aliye na jibu hilo, binafsi nitafurahi sana kulipata!!

  Sam, Zoe na yeyote aliye na jibu, tafadhari msiniache njiani!

 69. George L. Chiwango 25/05/2013 at 1:10 PM soma biblia vizuri na kwa utulivu!

  Kuna wakina anania na safira waliokufa kwenye uwepo wa Roho Mtakatifu enzi za mtume paulo, etc etc. Kufa au kutokufa inategemea na hali ya kiroho pamoja na mazingira ya kimwili

  deo

 70. Ni kweli John Paul. Hiyo ndiyo maana yangu. Kwamba kwa kuwa kuupinga ukristo hakuna madhara yoyote, basi imekuwa ni fashion kuwapinga watumishi wa Mungu kama T. B. Joshua. Wewe uliona wapi sasa hivi mpaka kesi za kuchoma makanisa wanakamatwa wakristo na kubambikiziwa? Makanisa yakichomwa unaambiwa eti misikiti na makanisa yanachomwa. wakati si kweli. Kinachochomwa ni makanisa tu.

 71. Hii inaonyesha “SPIRITUAL BANKRUPTCY” waliyo nayo watu, ROHO MTAKATIFU ndiye anayepaka mafuta, HE IS THE ONE ANOINTING

 72. nadhani siku hizi roho ya wivu imewajaa watumishi maana kila mtumishi anaefanikiwa kuhubiri vizuri na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na watu wengi wakampenda basi baadhi wa watumishi wanaanza kumnenea mabaya.

  Lakini tujiulize, hivi kwani Bwana Yesu alipokuwa kwenye mikutano yake watu hawakujaa?au wale mitume enzi zake hatusomi kuwa walihubiri kwa nguvu hata watu wote wa mji wakastaajabu?

  Sasa ninyi watumishi mnaoona watumishi wengine wenye kuwa na watu wengi kuwa si wa Bwana basi kwanini wachungaji wenu mnaowaamini kuwa ndio wapakwa mafuta pekee wasihubiri kwa upako na kutikisa ulimwengu kama enzi za pentekoste??let say kwanini watumishi/wachungaji/wainjilisti wa tz wasiwe kama benny hinn, tbjoshua wakaenda huko nchi nyingine na kutikisa kwa upako wa kipentecoste?

  Tupunguze wivu na tuangalie zaidi neno la Bwana

  Joe

 73. asante ndugu CK Lwembe kwa maandishi yako na kuyachunguza maandiko!

  Mimi nimemsikiliza tbjoshua katika mahubiri mengi na jinsi anavyonena katika neno halisi la kwenye biblia pasipo kutumia maneno yake ya ziada…nadhani pia ungejaribu kumsikiliza ili yamkini kuna mambo anayoyahubiri yaliyokinyume na neno la Bwana uje nayo ukatujulishe.

  hiyo hoja yako ya “Anasemaje kuhusu Ukatoliki na Usabato Masalia,nk” naona haina umakini maana hakuna sehemu yoyote kwenye biblia inayotutaka tuzungumze juu ya ukatoliki na usabato masalia…sisi kibiblia hatujapewa jukumu la kuhukumu wengine wakati tungalipo duniani bali kuihubiri injili ya kristo tu!

  pia labda utueleza ni ujumbe upi huo kibiblia unaoweza kumdhihirisha mtumishi wa Bwana tbjoshua kuwa si nabii??pia labda utupe na mfano halisi ( kwa kumtaja jina) wa sasa kwa mtumishi yoyote yule unaemfahamu ambaye kwa uelewa wako anastahili kuitwa nabii..

  sam

 74. Kuhusu manabii na vipawa na miujiza yake, Biblia imetutahadharisha na kutuonya sana, kwamba tuwe macho, fake ni vingi sana! Nalo Kanisa halina udhuru wowote kuhusu jambo hilo, maana sioni liambiwe nini zaidi ya hayo!

  Pia tunapaswa kufahamu kwamba, wajapo hao manabii wa uongo, si kwamba eti watakuja wakifundisha mambo kama ya kiisilamu au kibudha, la hasha, hao watakuja wakiihubiri Injili. Tena Injili hiyo itafanana sana na ile ya Kweli, ndio maana Maandiko yanasema Injili hiyo itawasomba wengi saaana, YAMKINI wateule! Ni wateule tu ndio watakaopona kusombwa katika Injili hiyo ya ulaghai!
  “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.” (Mt 24:24-25)

  Wengi wetu, kutokana na pressure za maisha, Imani imetupungukia kwa kiasi fulani. Nao manabii hao walipojitokeza na kutuita, kwa ishara na miujiza yenye kukutatana na mahitaji na matamanio yetu, tulipowaitikia na kuwafuata, basi sehemu kubwa ya ile Imani tuliyobakiwa nayo, ile ambayo ingetufanya tuliamini Neno la Mungu na hilo kuwa ndiyo Yakini yetu, ilitutowekea, badala yake sasa tumewekewa “imani” ya miujiza na ishara inayoambatana na utukufu wa nabii katika jina la Yesu! Hatuna tena uwezo wa kuyatofautisha mambo hayo, ilimradi nabii alimtaja Yesu, kwetu sisi huyo ni mtumishi wa BWANA. Kipimo chetu ni ile miujiza na jina la Yesu kutajwa tajwa katika mahubiri na maombezi.

  Yale MAARIFA hatuna tena, Neno la Mungu, linalopaswa kujaa kwa wingi ndani yetu na kuwa kipimo cha kuwakagua hao watumishi, halimo. Kwahiyo hatuna kipimo cha kuzikagua huduma, nalo Neno la Mungu linatutimilia mchana kweupe, tukipotezwa!!!

  Nabii sio mwinjilisti wala mchungaji. Nabii humuwakilisha Mungu. Yeye huja na “BWANA ASEMA”; Likiwa ni Neno kutoka katika kinywa cha Mungu ambalo wachungaji na wainjilisti wanapaswa kuendelea nalo kuwapelekea watu. Kwahiyo nabii yeyote anayefundisha tofauti na watumishi waliomtangulia, hao ambao walikuwa na hiyo BWANA ASEMA, basi jambo hilo lingewakilisha kuchanganyikiwa kwa Mungu, suala ambalo HALIPO!!! Hakuna MAARIFA yanayozidi jinsi hii ya kuwabaini hao WAONGO, ndio maana wao huhakikisha wamekutoa katika katika Imani hiyo kwanza, kama alivyofanywa Hawa, kisha hukujaza madude yao ambayo HUKUTENGA kabisa na ile IMANI, ukabaki kuwa mtu wa dini, yakini yako ikiwa ni ile miujiza na mafundisho yao. Ndipo ungetoka kwa nabii huyu na kwenda kwa yule na kwa yule… katika safari yako ndefu ya kuzunguka jangwani!

  AMKENI, Upentekoste ndio kiwango cha mwisho cha Kanisa. Nao Upentekoste haukusimama kwa kuinuliwa nabii yeyote yule, bali kwa Kanisa kuitafuta nafasi yake katika Maandiko. Nacho kipawa cha nabii chapaswa kuweko katika makusanyiko yetu kulingana na zile huduma tano katika kiwango cha akina Agabo Mdo 21:10; kipawa hicho huwa kiko chini ya mchungaji wa kusanyiko!
  Lakini, manabii hawa unaowaona leo kwa wingi, waliochipua kama uyoga, si manabii kwamba wanalo Neno kutoka kwa Mungu, hawa wana vipawa tu, vya uponyaji na utambuzi nk kulingana na roho ya wakati hiyo yenye kulidhihirisha lile Neno la “makristo wa uongo”. Sasa hawa si akina Kristo yaani wakijiwakilisha kama Kristo, hapana, kristo maana yake ni “mpakwa mafuta. ” basi manabii wetu hawa wa leo ni “wapakwa mafuta wa uongo”. Je, kwa upako walionao, ni nani awezaye kuwakwepa au kuwakimbia au kuwakana? Ndio maana Biblia ilisema “yamkini wateule”!!!

  Mmeelewa enyi wafuasi wa TB Joshua? Baada ya hizo “ishara na miujiza” hebu litafuteni Neno alilowaletea kutoka katika Kiti cha Enzi, ni lipi? Anasemaje kuhusu Ukatoliki na Usabato Masalia nk? Ame compromise? Au anatembeza uinjilisti wa kawaida na miujiza na kuwatabiria hiki na kile ambavyo ninyi kwa kukosa kwenu Maarifa mnaona ndilo Neno la Mungu? Sijausikia Ujumbe wowote ule unaomdhihirisha kuwa yeye ni nabii, zaidi ya miujiza na utabiri mwingineo wa kawaida ya matukio, yaani vile vipawa, ambavyo havina majuto!

  Huduma hizi huongozwa na roho. Mara nyingi hao wanaotumiwa hufikishwa katika kiwango cha kuamini kuwa Roho wa Mungu ndiye anayewaongoza, maana kwao hao, Shetani alijigeuza kama malaika wa nuru, wakampokea, ndipo yale Maandiko katika 2Kor 11:13-15 yanatimia kulingana na kushamiri kwa huduma hizo;
  “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, …”

  Basi, Ishara na miujiza yote inayowachanganya, Mungu aliahidi kuwa itafuatana nanyi mkiliamini Neno lake. Kwahiyo jitahidini mrudi pale mlipoondokea kuifuata miujiza, mtamkuta Bwana wa Miujiza akiwasubiri hapo, wakati Neema ingalipo, ili muukimbie Uharibifu unaokuja. Mmewahi kusoma popote pale ambapo Kristo alikwenda msibani au kuzika? Au mmewahi kusoma kwamba alipokuwa akihudumu watu wakakanyagana wakafa? Au hamjasoma kuhusu yule kijana aliyeanguka kutoka ghorofani aliposinzia, akafa Mdo 20:9? Yachunguzeni Maandiko, Roho ya unabii ni Roho ya Kristo; “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele” Ebr 13:8!!!

  Mbarikiwe!!

 75. Najiuliza mambo kadhaa kuhusiana na suala hili:
  1. Hivi yule mlinzi, nyakati za Elia Mtishbi, aliyekanyagwa hadi kufa pale kipimo cha unga kilipouzwa kwa robo shekeli alikufa peke yake?
  2. Ikitokea kwenye mkutano wa Injili kisha kukawa hakuna vyoo wala usafi kwa ujumla, Je, watu hawawezi kupata kipindupindu?
  3. Kuna ajali nyingi hutokea wakati wa safari za wanakwaya au hata watu wakitoka au kwenda kwenye Injili. Je, hili likoje?
  4. Je, hao waliokufa hapo, kama ni kweli, walitakiwa waishi hadi lini?

 76. @ Kamau,

  Kwamba linapokuja suala la IMANI ya KWELI (kwa TB Joshua) watu ni mafundi sana wa KUPINGA lakini linapokuja suala la IMANI YA UONGO, mfano Uislam, wanakuwa KIMYA kuupinga!
  Je, Hivyo ndivyo unamaanisha?

 77. Labda pia tuzungumzie juu ya watu kufa wakiyagombania ati hayo ‘mafuta’ ama maji ya upako km nijuavyo mimi. Mtakumbuka, jinsi yule mama alivyohangaika kupenya hata kuligusa pindo lake nguo ya Bwn Yesu na kuupata uponyaji wake, je, vp wale waliohatarisha maisha yao kwa kumteremsha ndg yao ktk Sinagogi kupitia kupasua paa lake. Panapo mzoga ‘aliyenona’ ndipo Tai ‘wengi’ hukimbilia huko ili kupata minofu yake wakawa wazima, wakaishi ndg zangu. Sasa kwenye harakati za kusongamana hata km tukio hilio lilikuwako kiukweli, why put blames on man of God??? Km taratibu hazikuzingatiwa ni wazi ni lazma, madhara yatatokea.

  Hofu yangu ilikuwa ni kwenye hayo mnayosema, ati, Mafuta ya Upako, nikadhani YALIPOTUMIKA AMA KUTUMIWA, YALIWALETEA MADHARA. Hapo, sawa, tungalikuwa HOI.

  Mubarikiwe.

 78. Duuh, mtumishi wa Mungu, Mr. Kamau, umenichekesha kikweli, ‘observation’ yako kwa maoni y wapendwa ‘very critical’. Kiukweli kbs, wapendwa wengi ni kama Mungu wao mara zote hayupo na ameenda likizo, kiasi kwamba wakifanya vituz waganga wa jadi / kienyeji, na wengine kwa sura ya malaika wa nuru km ‘Mch’. Ambilikile Mwasapile (u remember him??). Hakuna ht mmoja km ulivyosema ashangaaye juu y waislam kutulipua, naam, tujipe poole ht kwa hilo.

  Sasa, ushangae km kweli Mkristo leo hii anaweza akahoji, na kukanusha ati matumizi ya mafuta si ya kibiblia!!?? Nadhani, turudi nyuma na tuangalie mafundisho yetu ya awali na ya msingi, mapokeo yetu ndg zangu yasitufanye tuwe na mila na desturi za kushambulia kila huduma ya R/M. hV huwa mi ninahoji, je, vp ikitokea mtumishi amemfungua mtu mdhaifu kwa kumchanganyia tope na mate, au, na kitu chochote kile, itakuwaje ktk kanisa laleo?? Eliya, alimfufua mtoto aliyekuwa amekufa kwa kumlalia juu, na ht Petro naye kadhalika, Je, ikitokea leo itakuwaje???

  Kusema kweli, sijawahi kuyaona mafuta ya upako ya SCOAN, bali maji ya upako, yaani, yaliyoombewa kwa jina lake Bwn Yesu.

  Mubarikiwe.

 79. ujasiri wa ‘wakristo’ ni kupinga kanisa tu, kwa waislamu hata pua hawasogezi. wanalipuliwa lakini kimya. hiyo ndiyo tofauti ya Imani ya kweli na uongo. Yesu wanampiinga lakini Wanaowalipua kila mtu kimya.

 80. Kipimo kikubwa cha kujua mafundisho sahihi ni kuangalia mhubiri anarudisha utukufu kwa nani?nimemuangalia sana huyu tbjoshua kwenye tv na kuona anavyorudisha utukufu kwa kila jambo kwa Bwana Yesu na hili jambo ni nadra sana siku hizi hata hapa tz hasa kwa wahubiri walio na waumini wengi.

  Sikatai anayo mapungufu yake kama binadamu lakini ni mnyenyekevu sana kwa Mungu ktk kila jambo analosema japokuwa angeweza kabisa kuwa na majivuno sababu ya kuwa na waumini wengi.

 81. Vai 21/05/2013 at 6:48 PM hebu tueleza madhara ya kusali kwenye sinagogi na si Kanisani? maana mimi nijuavyo hata Bwana Yesu injili kwa sehemu kubwa aliinena akiwa kwenye masinagogi. au hata hiyo ilikuwa si sahihi??

 82. nadhani watu mnaomsema vibaya nabii wa Bwana TB Joshua mngeangalia kwa makini huduma yake au kuwauliza watu waliokwenda na kuona kwa macho mambo ambayo Roho Mtakatifu anayafanya kabla ya kuongea.

  Nahofia ndugu zangu katika Bwana tuwe makini sana tunapokufuru na kunenea vibaya huduma na karama za Roho Mtakatifu pasipokuwa na uhakika maana dhambi zote mwanadamu atasamehewa ila si ile ya kumkufuru Roho Mtakatifu.

 83. huwa kuna maagano ya damu au makafara ambayo huwa yanafanywa kwa siri sana hasa kwenye hizo dini ambazo msingi wake, limbuko lake na chanzo chake sio vya KRISTO YESU bali ni vya uovu tu. halafu wana wa Mungu hilo sio KANISA bali ni SINAGOGI. Mungu atupe Neema YA KUFAHAMU

 84. Waliokufa KIROHO ni wengi zaidi, kwa maelfu kama si kwa mamilioni!!
  “Watu wangu wanangamizwa kwa kukosa MAARIFA”!!!!

 85. Mh! Ninayo mashaka makubwa sana na “source ya habari hii”.
  T.B. Joshua pamoja na huduma anayoiongoza ya SCOAN hajawahi kuhudumia watu kwa mafuta ya upako wala kugawa kwa watu kitu kinachoitwa mafuta ya upako.

  Inabidi tutafute ukweli wa tukio husika.

 86. je, upako huo unazidi ule wa sikuya pentekoste?
  sidhani! Mambo yamafuta na upako ni yakucunguzwa sana!!
  Huduma hiyo siyo ya kibiblia.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s