Malezi ya Mtoto – Mithali 22:6

 watoto

“Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.”

Kumlea mtoto maana yake ni nini ?

Ni kumtunza na kumfundisha/kumuelimisha mpaka afikie mahali pa kujitegemea mwenyewe.

Ni kumtunza na kumfundisha kwa vitendo na maneno mpaka awe mzima, kiakili na kiutu kiasi cha kuweza kuendelea mwenyewe bila ya kukutegemea.

Njia ipasayo kumlea mtoto ni ipi?

Ni njia ile nzuri yenye maadili mema yanayokubaliwa na Neno la Mungu pamoja na jamii unayoishi katikati yake.

 

Mwenendo wenu ni fundisho kubwa kabisa mbele ya mtoto wenu. Njia ipasayo kumlea mtoto ni kuketi na mtoto na kumshauri maadili mema ya maisha (Kumb 6:7). Ni kumwelekeza kwenye mambo matakatifu, kabla hajaharibiwa na walimwengu.

Kwa mfano:-

Pale Nyumbani: Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hataatakapokuwa mzee.

– Ibada za nyumbani kwa wazazi pamoja na mtoto/watoto ni kitu muhimu sana.

– Mazungumzo yenu yanayohusu watu wengine, majirani, watumishi wenzako nk.

– Mnavyojibizana na mkeo/mumeo mbele ya watoto na hata sura yako ya kila siku mbele za watoto.

– Unavyowaelekeza watoto wako kuhusu maadili mazuri kwa waliomzidi umri.

– Adabu na heshima mezani mkiwa peke yenu na watoto au mbele ya wageni.

– Ikiwa wewe ni omba omba kila wakati hata watoto wako watakua hivyo.

Mahudhurio ya ibada: Mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

– Unatarajia mtoto atachukua fundisho gani ukibaki nyumbani wakati wa ibada?

– Unatarajia mtoto atajifunza nini kama kila siku unachelewa ibada na kuwahi kutoka au kukaa nje ya kanisa saa ya mahubiri?

– Unatarajia mtoto atajifunza nini kama huchukui Biblia wala kitabu cha nyimbo unapoenda ibadani?

– Unatarajia kuelewekaje unapowaacha watoto nyuma wakati unapokwenda kuhudhuria vipindi mbali mbali vya ibada?

Tunapokuwa ibadani: Mlee mtoto katika njia ipasayo, naye hataiacha hata akiwa mzee.

– Usimwache mtoto acheze cheze na kutembea hovyo wakati wa ibada huku akipiga makelele.

– Sio vema wakati wa utoaji wa sadaka kumpa mtoto senti 20 au 50 wakati unazo pesa zaidi ya hizo. Au kukaa tu bila kutoa sadaka wakati unapofika wa kutoa sadaka.

– Sio vizuri kupiga usingizi wakati ibada inaendelea. Au kutafuna pipi au “gum“ na kuchafua kanisa.

Kumbuka unayomfundisha mwanao kwa vitendo, yaweza kuwa picha nzuri au mbaya ambayo kwake itakuwa vigumu sana kuisahau au kuiacha hata atakapokuwa mzee!!!

Kwa nini?

Mzazi ni mwalimu wa kwanza kabisa kwa mtoto. Hivyo kila utakalomfundisha mwanao:-

– Atalizingatia na kulishika siku zote za maisha yake. Mfano: kama unapenda nyimbo za “dance“ au za kidunia yeye naye atazipenda hizo.

– Yale anayoyaona kwako anajifunza na kuyatendea kazi. Kwa mfano, kusema uongo, kuahidi bila kutimiza ahadi, kutukana nk

– Ukifanya kazi au kuishi katika hali ya uvivu usishangae mtoto wako akiwa mvivu.

– Ukiwa na bidii au ulegevu katika mambo ya Mungu, mtoto wako atakuwa hivyo.

– Ukiwa na hali ya usengenyaji na kuwadharau wengine mtoto wako atayaiga hayo.

– Kama una kiburi na majivuno au hali ya kutokumtii mumeo au kumpenda mkeo mtoto atajifunza hali hiyo.

– Kama una hali ya kutokuwa na ibada za nyumbani na uvivu wa kushiriki vipindi kanisani, mtoto atayaiga hayo.

– Kama unashabikia ya dunia na kuweka kando mambo ya kiroho mtoto atakuwa hivyo.

Hivyo mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

TUWE VIELELELEZO VIZURI KWA WATOTO WETU NAO WATAKUA HIVYO.

Mchungaji Marandu

Advertisements

2 thoughts on “Malezi ya Mtoto – Mithali 22:6

  1. Asante sana mchungaji marandu, hakika hili ni darasa la kweli hasa kwangu mimi ambaye nimeanza maisha ya kulea miaka miachache iliyopita, kuna mengine nilikuwa nayafanya kama ulivyoyataja lakni baada ya kusoma mafundisho yako, nimejifunza mengi pia ya kufanyia kazi, pengine niulize swali mwenye jibu anisaidie wapendwa , kama ikitokea mnaishi familia lakini mzazi mmoja anampenda Mungu yahani ameokoka , na mzazi mwingine anampenda Mungu lakini anafanya mambo yake kidunia yahani hajaokoka , Sasa mzazi aliyeokoka anaweka nyimbo za kuhabudu na kusifu na mtoto , anamsomea mtoto neno la Mungu kabla ya kulala na wanaomba, kesho yake unafanya hivyo ukitoka kidogo unaporudi unakuta mwenzako ameweka miziki ya NDOMBOLO YA SORO, wako wanacheza na mtoto kama vile hawana akili nzuri. je ktk hili nifanyeje? maana ukweli ni kwamba nyumbani mwangu kuna amani, upendo, utu wema , utulivu lakini ktk hili ndicho kikwazo kinaniuma , na 1 wakolintho 7:13 inasema kuwa Na mwanamke ambaye ana mme asiyeamini, na mme yule anakubali kukaa naye asimuache mumewe, ninampenda sana mwenzangu kwa moyo wangu wote , Kwa vile neno linasema kuwa kadhalika ninyi wake , watiini waume zenu , kusudi ikiwa wako wasioliamini Neno wavutwe na mwenendo wa wake zao pasipo lile neno Ipetro 3:1, nimekuwa nikijitadi sana kufanya hili , hilo tu la ndombolo ya soro ndilo linanikwaza, ninaomba msaada wenu. Mbarikiwe sana wapendwa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s