Tusijisumbue, Tuliamini Neno

biblia

6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. – Wafilipi 4:6-7 SUV

Neno la Mungu linatuambia hivi – tusijisumbue kwa jambo lolote – yaani tusiruhusu chochote kitufanye tuanze kusumbuka mioyoni mwetu tujikiulizauliza itakuwaje, tutafanyaje hadi kufikia hatua ya kukosa amani na kuruhusu hofu, mashaka, wasiwasi na woga viweke makao ndani yetu na kuanza kututesa. Tunalo Neno la Mungu, lililojaa ahadi zake kwetu na ahadi zake zote kwetu ni ndio na amina katika Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu.

Tunapaswa kuleta haja zetu zote mbele za Mungu kwa njia ya sala na maombi tukiwa na mioyo iliyojaa shukurani kwani tunazo ahadi nyingi za ukuu, wema na utayari wa Mungu wetu kukutana na mahitaji yetu. Tukumbuke ni neema ya Mungu tu inayotuwezesha kupokea vyote Mungu alivyo navyo kwa ajili yetu tunapoliamini Neno lake Yeye aliyemtoa Mwanae kwa ajili yetu hatakosa kutukirimia vyote pamoja naye. Wapendwa, lazima tufikie mahali tuliamini Neno la Mungu kuliko tunavyoyaamini mazingira yetu.

Tunapoleta haja zetu mbele zake kwa imani tukiwa na mioyo ya shukrani, kwanza kabisa amani yake ipitayo fahamu zetu itatuhifadhi mioyo yetu na nia zetu na hivyo itatuepusha na hali ya kuwa na wasiwasi na kukosa amani, Ndio maana unaweza kumuona mtu anayemjua na kumwamini Mungu wake anapitia mambo magumu sana lakini amejaa furaha na amani tele, hanung’uniki, halalamiki wala hatumii yale anayoyapitia kama kisingizio cha kutafuta huruma za wanadamu. Ameshakabidhi yote mikononi mwa Mungu na anaamini kabisa ya kuwa Mungu amemsikia na ufumbuzi upo tayari, kwani analiamini Neno la Mungu.

huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. . – 1 Petro 5:7 SUV

Wapendwa, badala ya kuendelea kuhangaika na fadhaa zetu sisi wenyewe, tuitikie wito na ahadi ya Mungu kwetu. Tumtwike Yeye fadhaa zetu zote, Yeye Muumba wa vyote, Mwenye ufahamu wote na hekima yote kwa upendo  anatukaribisha tumtwike fadhaa zetu zote. Tuuitikie mwaliko huu wa Mungu wetu leo, tusiupuuzie.

Leo hii ujapo mbele za Baba yako wa Mbinguni, kumbuka ya kuwa ameahidi kukutana na kila hitaji lako tena anajishughulisha sana kwa mambo yako. Amani yake ipitayo akili zote itakuhifadhi moyo wako na nia yako katika Kristo Yesu usiyumbishwe na mashaka, hofu au wasiwasi. Na moyo wako unapokuwa umefunikwa na amani ya Mungu basi ni rahisi kwako kuisikia sauti yake akikuongoza na kukuelekeza hatua za kuchukua kupata ufumbuzi katika yale yanayokukabili.

Mzidi kubarikiwa na Bwana Yesu,

Patrick

Advertisements

3 thoughts on “Tusijisumbue, Tuliamini Neno

  1. Nawashkuru wa2mish wa mungu kwa kaz ya bwana iende mbele il wa2 wajue kuwa mungu anaweza

  2. Asante sana mtumishi Bwana, kweli nimeona neno likifanya kazi ktk maisha yangu, na mada hii uliyozungumzia leo kuwa tusijisumbue kwa neno lolote bali ktk kila kitu kwa kusali na kuomba pamoja na kushukru haja zetu na zijulikane na Bwana, Ushuuda wa neno hili .kanisani kwetu tunalipia kipindi fulani kinachorushwa hewani kwenye radio , sasa watu huwa wanatoa kwa moyo hili kipindi kiendelee, kuna kipindi fulani tulikaa ktk kikao wakawa ikaonekana kuwa haikuwepo pesa kwa ajiri ya kulipia kipindi kile tena, wengi walitoa maoni ,wengine wakasema tuache kabisa tufute huduma hile, wengine wakasema wampigie simu anayehusika hili atukopeshe arushe kipindi tutamlipa pesa ikipatikana, wengine wakasema wataenda kuongea na mtu wanayejuana naye hili atusaidie, mimi nilikaa kimya mda wote, walipomaliza wote maoni yao ilionekana hakukuwa na muhafaka, ndipo nilisimama nikasema maandiko yanasemaje kuhusu hili? nikawaambia neno hili kuwa neno linasema tusijisumbue kwa neno lolote, na pia haja zetu na zijulikane na Mungu, na pia niliwapa neno Yeremia 33:3 kuwa anasema tumuite naye atatuitikia atatuonysha mambo makubwa magumu tusiyoyajua, nikasema kwa hiyo nionavyo mimi twende tukaombe na Mungu atafanya njia maana hii kazi ni yake na yeye ndiye tunataka apewe utukufu, wakasema sawa. Tukaenda tukaomba baada ya siku mbili zikaja taarifa kuwa kuna mtu alitoa pesa kwa ajiri ya kipindi kile , alilipia miezi mitatu. Bwana Asifiwe sana, tulishkru na kufurahi, na baada ya miezi mitatu tulikuwa na pesa ya kutosha ya kuendelea kulipia maana watu walikuwa wakitoa tusiowajua . Bwana Yesu asifiwe sana, hadi leo hii kipindi kinaendelea bila shida kabisa . Bwana asifiwe anayeliangalia neno lake akalitimiza.Mbarikiwe , ninawapenda.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s