Waraka wa Roho Mtakatifu!

abel-o

Roho Mtakatifu anasema:

Nimekuwepo kabla ulimwengu kuumbwa, najua wakati uliopita, naelewa wakati uliopo najua na kushughulika na wakati ujao.

Nina alama ya hua, moto, fimbo, mafuta, maji, upepo na wingu lakini ni nafsi yenye hisia, mimi ni Mungu Roho.

Najua yaliyo katika moyo wa Mungu maana mimi ni sehemu ya ndani ya Mungu, mimi ni ndani ya Mungu, Mungu ndani ya Yesu na mimi ndani ya Yesu na naweza kuwa ndani ya mtu yeyote aaminiye na kunipokea.

Nimekuwa pamoja na wote waliomtumikia Mungu, niliwawezesha na walifanikiwa waliposikiliza ushauri wangu, niliwezesha kuzaliwa kwa Yesu na nikiwa ndani yake Aliweza kutimiza mapenzi ya Mungu yote, hata alipokufa alifufuka kwa nguvu na uweza wangu.

Mimi ni msaidizi na mwalimu wa kweli, hushauri mtu kusikia, kuamini na kupokea Neno.Huwezesha mtu kuzaliwa mara ya pili na akinipa nafasi hujaa ndani yake na kumwongoza katika njia za haki,na kumfanya akue, akomae na kuwa imara kiroho. Mimi ni nguvu itendayo kazi ndani ya mtu na naweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko uyaombayo au uyawazayo.

Kwa kazi yangu utafanyika imara katika utu wako wa ndani. Ukitaka kweli kuwa mtoto wa Mungu lazima ukubali kuongozwa nami, mimi ni ndani yako na huhisi maumivu yako wakati wa mateso na hukuombea kwa kuugua kusikowezwa kutamkwa.Mimi ni mpole na mnyenyekevu, ukinipa nafasi na usiponizima wewe na kila mtu utakayekutana naye ataona matokeo ya kuongozwa na mimi ambayo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.

Nitakuwezesha kuishi kwa mimi na kuenenda kwa mimi.

Ingawa mimi ni msaada wako mkuu lakini mara nyingi nakosa nafasi ya kukuongoza na kukushauri , ninatoa vipawa na karama ambazo mara nyingi hupingwa na kupigwa vita…

Ulimwengu unakusababishia dhiki, huzuni, fadhaa, majonzi na taabu za kila namna lakini mimi ni mfariji wako mkuu, faraja yangu kwako ni kuu kuliko faraja zingine zote.

Hata hivyo nitashinda, napenda kukufanya wewe kuwa mshindi, najua hila za adui na adui hawezi kusimama mbele yangu, ukiwa na mimi wewe ni tishio kwa adui na utashinda na zaidi ya kushinda…

Nipe nafasi nikuongoze kutimiza kusudi la Mungu maishani mwako, nikuongoze katika mapenzi ya Mungu baba yako, kwa msaada wangu utatenda makuu ili jina la Yesu lililotukuka sana litukuzwe maishani mwako.

Wako Roho Mtakatifu

Written by Pastor Abel Orgenes. 2010

Advertisements

3 thoughts on “Waraka wa Roho Mtakatifu!

  1. Shalom,
    Roho Mtakatifu nisamehee kwa kutokukutumia naomba utengeneze moyo wangu ili nawe MUNGU ROHO MTAKATIFU Upate Nafasi Ndani ya Moyo Wangu UNISAIDIE NA UNITUMIE KADRI UTAKAVYOPENDA NAOMBA RALAU KILA KITAKACHOJIINUA KUTOKUTIMIZA KUSUDI LA KIMUNGU KATIKA MAISHA YANGU………..AMIN

  2. Tazama mimi ni mjakazi wako na iwe kwangu kama ulivyosema . Luka 1:38. anitumie apendavyo na aniongoze ktk njia ipasayo, nimekuwa nikiimba sana wimbo wa Ninakuhitaji wa dada Grolia Murilo, ninabarikiwa sana na wimbo huu. Utusaidie Roho Mtakatifu, maana pasipo wewe sisi hatuwezi kufanya neno lolote. Yohana 15:5.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s