Kukemea Mapepo

biblia

Bwana Yesu Asifiwe, je inawezekana watumishi wa Mungu kukemea mapepo na kuyapeleka kuzimu? naomba mnisaidie nani ana mamlaka ya kupeleka mapepo kuzimu na kwa mujibu wa maandiko yapi? Ahsanteni

–Andrew

Advertisements

39 thoughts on “Kukemea Mapepo

 1. Simon,

  Kuna wakati unapong’ang’nia sana Mungu akupe huduma au kipawa fulani, basi Mungu hukupatia hilo jambo, si ktk Mapenzi yake makamilifu, bali ktk Permissive Will; na hapo ndipo kuna kujitesa na kuihangaikia saaana huduma ikue, hata ikiwa ni ya kutoa mapepo! Huduma zinakuwa mithili ya uganga wa kienyeji!!!

  Tofauti na jinsi hiyo ni yale Mapenzi Makamilifu ya Mungu, huduma inayozaliwa kutoka hayo haina mambo ya kujitesa, huwa ni kuyatimiza Mapenzi ya Mungu ambayo hutanguliwa na Mungu mwenyewe! Imani huyakamilisha yote!

  Gbu!

 2. Nawapongeza wapendwa wote kwa michango yenu yenye kufikirisha na kuturudisha kwenye neno.
  Habari za wagerasi zinafikirisha pia, hivi ni kweli Yesu alikubariana na matakwa yao yote? Mbona mwishoni neno ‘na kumbe!’ limetumika. Hii maana yake ilitokea kinyume na matarajio ya mapepo.
  Hivi mbona wapendwa wenzetu wamegeuka wasemaji wa mapepo kwa mgongo wa neno, wakidai wao wanajua mipaka ya utendaji kazi wa Mungu.
  Wajitafakari upya
  Mungu wa Mbinguni na azidi kutubariki sote. Amina.

 3. kuna watu wana mfano wa utaua lakini wanazikana nguvu zake, wana nadharia nyingi sana, lakini si utendaji, ukipata mtu wa karibu anayeteswa na majini unaweza kuelewa, tunapowabeza wanaojitesa kwa kufunga na maombi kutafuta nguvu za Mungu ili kufanya huduma hizi, tujaribu kujiuliza kama kwa hizo nadharia nzuri tunazotiririsha tumeshawasaidia wangapi watoke kwenye vifungo kama hivyo. Jamani huduma si mchezo na si kirahisi tu kila mtu anaweza kukemea pepo wakamtii, jaribu kujiuliza je wewe umewahi kufanya huduma hiyo, maana ni ahadi kwa waaminio usiishie kubeza tu,kwa nadharia nyingi wakati kiuhalisia dhambi inakugaragaza kila siku.

 4. Natakujua njisi yakujikinga na mapepo, majini, mizimu yasinikaribie wala kunigusa kabisa

 5. Asante sana ndugu Lwembe.
  binafsi mm si mshabiki wa mambo na cna kawaida ya kukurupuka kwenye jambo lolote hasa likiwa la kiroho.
  najua utasema kuwa habari za yule tajiri na lazaro ni mfano na hakuna kitu kama hicho kwa sasa
  soma kwa kutafakari Zaburi 9:17,16:10 harafu rejea Luka 16:23-31 mimi baada ya kusoma hizo shuhuda hasa za kuzimu kwenye mateso nilirudi nikayapitia haya maandiko na nimeona ya kuwa hakuna jambo lililo nje ya maandiko kwani wasimamizi wa mateso hayo ni mapepo yakiongozwa na lusifa na pia kwenye baadhi ya shuhuda hizo nimeona lusifa akigawa majukumu kwa baadhi ya mapepo nayo huondoka kuelekea nchi kufanya uharibifu kwa watu hasa watumishi wa Mungu Nikwambie tu kuwa kuzimu kupo na ndiyo makao makuu ya mapepo yote na pia kumbuka kuna trilions ya mapepe kwa hiyo unapo yakemea kadhaa na kuyaseta kuzimu au kuyateketeza haina maana umeyamaliza na bado yapo mengi tu hapahapa dunian na mengine kuzimu.
  Hebu tafuta mda uzisome hizi shuhuda na hakuna upako wowote utakao kutoa ktk uwepo wa Mungu na RM

 6. Ndg Harrison,

  Kwanza asante kwa ushirika!
  Kuhusu Mapepo, umenifurahisha saana!

  Vitabu na rejea ulizozitoa ni jambo zuri na vinapanua mawazo, haswa ukiwa ndani ya wigo wa Maandiko, maana ni hatari sana iwapo utayaendea hayo bila kujifunga Nanga, kwani mara nyingi vitabu kama hivyo huwa vina anointing, kama ilivyo Biblia! Sikutishi, bali napenda kwamba, ukiisha yasoma hayo uyalete katika Maandiko ili uone kama yanakubaliana?

  Nasema hivyo kwa sababu hakuna ufunuo au maono au matukio yanayoweza kuyazidi Maandiko! Maandiko yanayo ndani yake mambo yoote, kutoka Mwanzo wa dunia hii tunayoishi mpaka mwisho wake, hakuna jambo jipya hapa katikati ambalo halimo humo.

  Iwapo utakuwa umejipeleka katika mawazo ya kwamba mapepo yanafungiwa kuzimu na kuchomwa moto yakateketea, ukajiaminisha katika hili, ni hatari kidogo maana utayaamini yasiyo halisi at the expense of the Truth which should’ve set you FREE, instead, knowledge hiyo ambayo si halisi becomes your prison cell!

  Hebu wazia jambo hili, kwamba tunayo mamlaka ya kuyateketeza mapepo na kuyafungia kuzimu; basi kwamba twafahamu pia kuwa mapepo hayazaliani, Je, tukiwa katika ufahamu huu, tukachangamkia kuyachoma moto na kuyafungia kuzimu, unaonaje, Bwana Yesu atakaporudi, si atatukuta tuko Shwaaari baada ya kuyatight mapepo yooote!!!! Je, linawezekana jambo hili, kama haliwezekani, ni kwanini?

  Gbu!

 7. SHALOM!!
  Kazi za mapepo,kazi za kichawi na hasa zile za kulishambulia kanisa zinatoka kuzimu kwa maana huko chini mikutano mikubwa ya kichawi ya mapepo kuhusu kuharibu kazi ya Bwana hufanywa kuzi ktk utafiti nilioufanya nimegundua kuzimu iko mara mbili
  1)Ni ulimwengu wa roho unaomwezesha mchawi kupata nguvu ya kuja kufanya uovu duniani. na kuna baadhi ya wachawi hupokea task zao moja kwa moja toka kwa lusifa.wanauelezea ulimwengu huu ni ule wenye nuru ingawa sio ya jua na majumba magari maduka nk kwa kifupi kuna mishemishe kama duniani tu na malango yake yote yapo ktk maji yaani bahari,maziwa mito n.k huu nilipata kuujua kupitia vitabu vya shuhuda vya waliokuwa wachawi na ss wameokoka kwa hiyo hawana hofu ya kufichua siri za shetani hivi ni baadhi ya vitabu MAISHA YANGU KUZIMU,NCHI YA WACHAWI,CHUO KIKUU CHA WACHAWI,MADHABAHU ZA KUZIMU N.K
  2)Huu ni ule wenye mateso kwa roho za watu walio kufa duniani huu inasemekana ni wenye giza lisilo mfano na huu hauna nuru ni giza tu nuru.

  Nuru inayoweza kupatikana hapa ni ile ya mioto inayowatesa watu daily
  huu nimeujua kupitia shuhuda mbalimbali za watu waliowahi kuzuru kuzimu na mbinguni na kuonyeshwa hali halisi ya kanisa la leo duniani
  baadhi yao ni A DIVINE REVELATIONS OF HELL. MARRY K. BAXTER mMarekani,ANGELICA ZAMBLANO 1st experience of heaven and hell and 2nd experience of heaven and hell. muEQUADOR,ushuhuda wa RODOLFO ACEVEDO juu ya mbinguni kuzimu na hali ya kanisa la leo mDominika na nyinginezo nyiingi.
  ktk hizi shuhuda niliweza kuona jinsi vikao vya mapepo juu ya namna ya kuvuruga na kuharibu na kuua watu duniani na kisha kupeleka roho zao kuzimu kwenye mateso ya umilele na wakisha maliza vikao vyao hutoka ma ardhi hujifungua na wao hutoka kuelekea duniani kisha hujifunga tena wengine huwa na mikuki mikononi
  ndiposa tunasema ingawa haikuandikwa kwenye biblia mahali popote yesu alipoyapeleka mapepo kuzimu lkn bado ulisema tukiwa naye tutafanya kazi hata zaidi ya alizofanya yeye kwa nn tusiwarudishe mapepo yalipotoka?

  Mi naomba muzitafute hizo shuhuda mtandaoni pia mkiweza tafuteni hvyo vitabu na baada ya kuzisoma rudini sasa tuijadili hii mada
  mubarike!! HARRISON

 8. HALELUYA watu wa SG.
  Kwa kweli Lwembe ni mmoja katika watu ambao huwa napenda kusoma coment zao lkn hapa umeniangusha kidogo eti unashanga wainjilist kukemea na kuziteketeza pepo kwa MOTO naomba ukasome ktk 2waf 1;10 na kuendelea
  nikwambie tu we nyoosha njia zako na Mungu yaani we kuwa tu mtu wa Mungu kama ELIYA na utashusha moto kutoka mbinguni na kuyatekeza mapepo na falme zao
  Bwana Yesu alisema tutafanya kazi kubwa zaidi ya alizozifanya yeye tatizo liko wapi Lwembe? mbona maandiko yapo wazi? au ulitaka mpaka Yesu aseme “nawapeleka kuzimu” ndo ujue kuwa hilo jambo lipo? sura ya mwisho na mstari wa mwisho wa injili ya yohana inasema
  NA KUNA NA MAMBO MENGINE ALIYOYAFANYA YESU TUKISEMA TUANDIKE MOJA MOJA HATA ULIMWENGU HAUTATOSHA KUHIFADHI VITABU VYAKE.
  Ni hayo tu jamani mubarikiwe.

 9. Mwisho katika kuimalizia ile tafakari, kuna matukio kama ya yule Mgerasi na lile jeshi la mapepo, maelezo ya tukio hilo mengi yamekwisha kuelezwa katika michango iliyopita. Hata hivyo maelezo ya mwisho ya Mjoli Haule, hayana nguvu ya hoja inayoweza kulisimamisha Fundisho hilo la Kanisa “kuyafungia mapepo kuzimu” kama anavyodai.

  Maelezo yake ya mwisho yanakiri kwamba Ufunguo wa Kuzimu anao Kristo, na pia amekiri kwamba Mamlaka yana mipaka, ngoja nimnukuu kidogo:
  ““Maana mwenye funguo (mamlaka) ya kufunga na kufungua kuzimu ni Yesu Kristo.
  Wale mapepo ya Gerasi yalimsii Bwana Yesu asiwafunge kuzimu
  Hizi falme na mamlaka zina mipaka wanayo miliki na kutawala
  Jeshi la pepo wa wagerasi walimsiii Yesu asiwafunge nje ya mipaka yao””

  Basi kwa kadiri ya maelezo haya na nukuu zake, vyote vinaongelea mapepo kuendelea kuzagaa duniani baada ya kutolewa kwa hao watu! Maelezo kama, “”Hata hivyo bado pamoja na kumuomba Bwana Yesu haya mapepo kuwaingia nguruwe bado wale Mapepo walikwenda baharini (falme na mamlaka) yaani kuzimu ndani ya mipaka yao”” ni nyongeza juu ya Neno la Mungu ambazo ni Mapokeo yawezayo kukutia hasara pindi nawe unavyoendelea kuyafundisha na kuwaaminisha uongo, wachanga wamjiao Kristo, kama Kuzimu iko ndani ya mipaka yao, nao wakaenda huko; basi lile ombi lao kuwa “asiwafunge kuzimu” lina maana gani? Ukiyavuka Maandiko lazima utaishia katika kujichanganya tu!!

  Ufunuo 6:8 “Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye…”
  Kuhusu hili unasema, “Hizi roho ktk kitabu ufunuo zinazungumzwa kuwa zilikuwepo /zipo /zinakuja na zote zinatoka kuzimu.” Kwa kiwango fulani ninakubaliana nawe katika jambo hili, kwamba hizo ni roho, pia zilikuwepo/zipo na zinakuja.

  Kwamba zilikuwepo, hilo ni kweli, maana Roho Mtakatifu aliliweka wazi jambo hilo katika 1Yoh 4:3 “…Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.” Basi tunapoizungumzia roho ya mpinga Kristo, twapaswa kuwa katika ufahamu kamili wa lini roho huyo alianza kutenda kazi. Tunapaswa kujua lini Shetani alikuwa ni “Mpinga Kristo”! Mpinga Kristo lazima aje kumpinga Kristo! Ndiposa, udhihirisho wa roho huyo tungeuona katika Yuda, yule shetani aliyechaguliwa na Kristo mwenyewe nao kuwa pamoja Kanisani!!! Kristo hakumpeleka Yuda kuzimu kumfungia ili asiiharibu huduma yake! Tena tunamuona Yuda akiendelea na huduma yake, akiiba sadaka nk, lakini hakutimuliwa akafungiwe huko kuzimu, Injili ingeparaganyika! Ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kuyaangalia Mapenzi ya Mungu kwa kina.

  Baada ya Yuda kumaliza kazi yake aliondoka kwa kujinyonga, na ndipo roho ile iliyokuwa juu yake ikarudi kanisani tena, hiyo anayoizungumzia Yohana. Nayo alama (symbol) ya kurudi kwake na ministry yake ndiyo hiyo tunayooneshwa katika kitabu cha ufunuo hapo katika Ufu 6: 1-8. Huyo roho aliporudi,Ufu 6;1-2, alikuja na mafundisho yenye sura ya kiungu na mwonekano wa utakatifu, kama unavyomuona huyo farasi mweupe, akiwakilisha utakatifu; lakini mafundisho hayo yalikuwa ni yenye kufisha! Mitume walipambana vikali na mafundisho hayo, ukizisoma nyaraka zao utayaona hayo, ule upako wa “Simba”! Sasa si kwamba mpambano huo uliishia katika nyakati hizo za nyaraka, la hasha, yule roho angali anaendelea, nao mitume kupitia Kanisa, kwa zile nyaraka wangali wanapambana naye, huyo mpanda farasi mweupe! Huyu ndiye msimamizi wa mafundisho yote potofu, kama haya ya kuwafungia pepo kuzimu!!!

  Mbele katika nyakati roho huyu aliyejivika “utakatifu” alijibadili na kuwa farasi mwekundu, ule umwagaji wa damu isiyo na hatia, huyo alianza kulazimisha mafundisho yake potofu yafuatwe kwa nguvu, na hivyo mauaji ya Watakatifu yakashamiri. Lakini Mungu badala ya kuyafungia mapepo hayo kuzimu, yeye aliwapa kanisa upako wa “Ndama”, yule mnyama wa sadaka, ili kuyapitia hayo yote!

  Mafundisho ya uongo yakaendelea, yakiambatana na mauaji. Mauaji yalipoa baada ya mafundisho hayo kutawala, na ndipo biashara ya injili ikashika kasi chini ya yule mpanda farasi mweusi, ambaye ni roho yule yule! Unazijua zile “Hati za sadaka za dhambi” ambazo kanisa la Katoliki lilikuwa linawauzia waumini wake ili wafutiwe dhambi zao za miezi kadhaa kulingana na pochi unalokata? Hao hupatiwa “Hati ya Indulgence”, au unaujua ule uwezo liliojipachika wa kuwafutia watu dhambi zao (absolution)! Unaona, Mungu hajalipeleka Katoliki kuzimu akalifungie huko ili liache kuwadanganya watu, badala yake aliwainua akina Martin Luther kuyaondoa mafundisho hayo kwa Watakatifu wake, ule upako wa “Sura ya mtu”!!!

  Kimbembe kiko huku mwisho, hapa sasa tunao mchanganyiko kamili. Ukiichukua rangi nyeupe, ukaichanganya na nyekundu na nyeusi utapata hiyo kijivu!!! Huyu mpanda farasi wa mwisho anaitwa “Mauti”! yaani mafundisho yaliyotapakaa leo hii ni mauti ya moja kwa moja!! Lah…! Na kuzimu anafuatana na huyo “Mauti”!!! Upako wa “Tai” ndio ulio juu ya Kanisa ili kupambana na huyo Mauti na jeshi lake la Kuzimu! Upako wa “Tai” ni wa kinabii, nalo Neno la Mungu huenda kwa nabii. Basi huo ndio umuhimu wa kung’ang’ana na Neno la Mungu; Kanisa limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, Kanisa kwa Upako huo linarudi kikamilifu katika Msingi liliojengewa juu, NENO!

  “Kuzimu” anafuatana na huyo “Mauti”, hiki ndicho Biblia inachosema! Sasa huyo anayesema anayafungia mapepo kuzimu, jamani, huyo si ni lazima awe ni mbabaishaji!!! Huyo anatuondoa kwa makusudi katika tafakari ya kweli na kutupeleka huko porini kutuzubaisha!

  Kama Maandiko yanatuambia kuwa huyo “Mauti” wamefuatana na “Kuzimu” nasi twafahamu kwamba Kuzimu ilikuwa imefungwa mpaka hapo katika Ufunuo 9:1-2 huyo nyota anapopewa kulifungua, “…Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.” Huu ndio wakati ambapo kuzimu inafunguliwa!!!

  Basi, kwa uzoefu wa uongo, ni kwamba ukweli hutangulia ndipo uongo hufuata nyuma kuwaondoa watu katika kweli. Ndiposa, tunapozisikia kelele za kuyafungia mapepo kuzimu zikishamiri, ni wakati muafaka wa kuyatazama mambo hayo vizuri, huenda lile Shimo LIMEKWISHA KUFUNGULIWA!! Hebu ikagueni hali ya dunia, serikali zooote zimeoza, rushwa imetawala sehemu zoote. Njaa ghasia na fujo vimekuwa ni vitu vya kawaida. Makanisa ambayo ndiyo yanayopaswa kuwa kimbilio, sasa ni mapango ya wezi na uchafu wa kila aina; mapepo ya ushoga yamelivamia kanisa na kulishinda, sasa hivi yametapakaa mpaka katika makanisa ya Kipentekoste! Itazame Marekani, nchi iliyozaliwa kwa uhuru wa kuabudu, sasa ndiye kinara wa ushoga! Kanisa Katoliki lina kesi chungumzima za ulawiti wa watoto kwa watu wazima, badala ya kuwaadhibu wahusika linawahamisha kutoka hapo walipogundulika na kuwapeleka kwingineko wakaendelee na mambo yao! Mapepo yameteka kila kitu na yanaendelea, halafu wanatudanganya eti wameyafungia Kuzimu!!!

  Angalia mfumuko wa manabii wasio na ujumbe wowote ule isipokuwa mazingaombwe ya dini chini ya Upako wa Ulaghai uliosambaa dunia nzima, wakiziteka nafsi za watu waliolikataa Neno la Mungu Halisi, sasa wakigeuzwa kuwa ni wale “wenye mfano wa utauuwa”, wakiunganishwa katika jeshi hilo bila kujua!!!

  Wapendwa, BAKINI KATIKA WIGO WA MAANDIKO ndipo mtakuwa salama, hayo madude si mchezo, yana ujuzi na uzoefu wa mambo hayo ya ulaghai, kubalini muwe “washamba” wa Neno la Mungu, libebeni hilo mioyoni mwenu ili lizifichue hila za yule muovu!

  Mjoli Haule, Bwana akuzidishe katika tafakari na yote yenye kumtukuza yeye, kwa kadiri tunavyoendelea kujifunza.

  Mbarikiwe nyoote, kwa kuusoma mkeka huu!!!

 10. Katika kuendelea na ile tafakari aliyoileta mjoli Haule, hebu tuvitazame kwa pamoja vifungu vya Maandiko alivyovileta ili kuithibitisha hoja ya Mamlaka ya kuwafungia pepo kuzimu.

  Luka 10:9 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”
  Tumepewa amri ya kuwakanyaga nyoka na nge na nguvu zote za adui. Kama nimeilelewa vizuri amri hii, kwa upande mmoja inaniambia kuwa watakuwepo nyoka na nge, na pia nguvu za adui zitakuwepo kutenda kazi, hivyo Kanisa limepewa uwezo wa kuvikanyaga vyote, na halitadhurika. Halikupewa amri ya kuviondosha visiwepo kwa kuvifungia kokote kule hata kukiwa ni kuzimu!

  Mt 18:18 “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.”
  Kifungu hiki kinauzungumzia Ufalme wa mbinguni, ule Kanisa lililopewa Ufunguo wake. Na hivyo Kanisa linathibitishiwa kuhusu mkristo asiyeonyeka katika nyendo zake zilizo kinyume na maadili ya kikristo, na huyo, kanisa likifikia kumtupa huko nje ya Ufalme, basi huyo hana namna tena ya kurudi ndani, maana mbinguni pia wamelithibitisha hilo! Hata huyo akiwa ni pepo, basi anaishia kutupwa nje ya Ufalme na si kufungiwa kuzimu!

  Yeremia 1:9-10 “Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; -angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.”
  Pia,
  Yeremia 51:20-21 “Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake”

  Unabii huu unaihusu Israeli, wale wa mwilini, kwa kadiri utakavyouhusisha unabii huu na kanisa, jambo hilo lingekuonesha kwa uwazi kabisa kuwa suala la kuwafungia mapepo kuzimu ni jambo ambalo halipo kwa kanisa! Israeli hiyo hapo, ingali inapambana na “mataifa”; bali wako ndani ya nchi yao ya ahadi! Nalo Kanisa lapaswa kuwa katika nchi yao ya ahadi wakiwakanyaga nyoka na nge na kuzishinda nguvu zote za adui, amani ikiendelea kudumu ndani ya mipaka yao!!! Haya ndiyo mambo yanayopaswa kuendelea mpaka Bwana mwenyewe atakapokuja kuyamaliza!!!

  Pia dhana ya kwamba, “Kanisa limepewa Funguo ZA mbinguni kwa Uchache 1.jina la YESU, 2.DAMU YA YESU, NGUVU YA ROHO MTAKATIFU”, hii ni dhana inayoshawishi kwa namna fulani, lakini ni ujuzi wa maneno usio na tija. ‘Jina la Yesu na Damu ya Yesu na Nguvu ya Roho Mtakatifu’ mambo yote haya ni sehemu ya Injili, nayo Injili ni package inayopaswa kuliwa yote bila kusaza chochote ili mlaji apate manufaa kamili ya jambo hilo, ikiwa ni pamoja UFUNUO wa mipaka ya Mamlaka ya utawala aliopewa katika hiyo nchi aliyokirimiwa aitawale! Basi wewe umepewa kuitawala nchi, imekuaje tena unataka kuitawala na Kuzimu?

  Kuhusu, “Mara nyingi utawasikia wapendwa wakisema huyu ndugu amefunguliwa.” Iwapo tutayapeleka mawazo yetu kuwa hao tunaowasema “wamefunguliwa” kwamba walikuwa wamefungwa kuzimu, jambo hilo litazidi kutupeleka mbali na Injili ya Kweli. Kufunguliwa kwetu kuko kama hivi Maandiko yanavyotushuhudia:
  Efe 2:1-2 “-Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; -ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi.”
  Hakuna kufunguliwa kwetu kunakoizidi jinsi hii tunayooneshwa!

  Ngoja nikatizie hapa ili nisiwachoshe sana, kisha nimalizie fungu la mwisho la tafakari aliyoileta mjoli wa Bwana, Haule.

  Mbarikiwe!

 11. Mjoli Haule,
  Ninaandika kuthibitisha kututimilia lile ombi lako, “Naomba tena mnipe nafasi ktk mioyo yenu nami nichangie kwa sehemu
kwa kadri ya ufahamu wangu ktk maandiko(neno)”, basi binafsi katika kuipokea tafakari uliyoileta, kulingana na mada iliyopo na yanayojitokeza, yafuatayo ni majumuisho ya tafakari hiyo kadiri nilivyojaribu kuirudisha katika Maandiko ili kuupata UHAKIKA wa mambo hayo.

  Kuhusu ombi lako la kutaka tafakari yetu izame katika ukiroho zaidi, bado ninaamini kwamba michango yote iliyotolewa ilijikita kiroho zaidi kuliko kimwili. Maana mambo yote tunayohubiriwa na kufundishwa katika Agano Jipya ni ya KIROHO katika UJUMLA wake, nayo hufikiwa kwa IMANI tu! Bali ninafahamu pia kuwa udhihirisho wa hayo mambo ya kiroho, hayo hujidhihirisha katika mwili. Je, ni nani kati yetu anayejua kwa uhakika kinachofanyika hapo tunapowawekea mikono wagonjwa na viwete nk na kisha hao kupata uponyaji? Ni nani anayejua kwa uhakika kinachomtokea pepo hapo tunapoyakemea? Jibu rahisi na la KWELI, ni kwamba hakuna ajuaye, Bali sisi huyatenda hayo kwa Imani kulingana na Neno tulilolipokea, Neno la Kristo! Ujuzi wowote ule ulio nje ya hilo Neno, ni UBATILI!!!

  Pia, ni kweli kuwa Ufunguo ni mamlaka. Monita wa darasa anayo mamlaka ya kumtoa nje ya darasa mwanafunzi mtukutu asiyetaka kutii maelekezo anayopewa. Sasa mwanao akirudi nyumbani kuwa amefukuzwa shule na monita wa darasa lao, nawe mzazi ukalipokea jambo hilo na kuanza kumtafutia shule nyingine mwanao, bila shaka jambo hilo litadhihirisha kuwa mzazi wewe hujui chochote kuhusu shule na hivyo hata mamlaka zilivyogawiwa katika utawala wa shule huzijui!!

  Kanisa limepewa FUNGUO za Ufalme wa mbinguni, ndio hiyo Habari Njema. Mk 16:15/6 : -Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Hii ndiyo mamlaka waliyopewa Kanisa, kuwafungulia watu lango la mbinguni waingie, wooote watakaoipokea Habari Njema hiyo, watakaoikataa basi, hao watabaki huko nje kama wale waliobaki katika siku ya Nuhu! Mamlaka aliyopewa Nuhu ni ya kuwaingiza viumbe ndani ya safina, gharika ilpofika, wale waliobaki nje walimlilia awafungulie waingie, kwa huruma ya Nuhu angeweza kuwafungulia, lakini mamlaka ya kulifunga na kulifungua hilo lililofungwa, hayakuwa kwake!

  Mitume waliijua mipaka ya mamlaka waliyopewa, tofauti na wahubiri wa leo ambao wanataka kujitwalia mamlaka wasiyopewa. Kristo anatuambia, “Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu” Ufu 1:18, hivi, kwanini hajazungumzia Funguo za mbingu kwamba pia anazo? Yeye ni Mkamilifu katika kila jambo, ndipo hawezi kuzungumzia mamlaka aliyoikabidhi kwa Kanisa kwamba yeye tena anayo, itakuwa ni kuchanganyikiwa, au kutokuheshimu maamuzi yake mwenyewe! Vivyo kanisa kuyarukia Mamlaka aliyoamua yabaki kwake yeye mwenyewe Kristo, ni utovu wa nidhamu!

  Mapepo yanao ufahamu kamili wa mamlaka na mipaka yake, Mt 8:29 “Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” Labda niwaulize, hivi unapomkamata mtu aliye na uhuru wa kwenda akutakako, nawe ukamchukua na kumfungia, je si adhabu hiyo? Basi kama huyo aliye na Mamlaka ya Hukumu, alipokutana na hao waipasayo Hukumu na kisha wakaiongelea hiyo Hukumu, katika namna ya HAKI ya hiyo Hukumu, naye HAKI akaitimiza ile HAKI kwa kuwaridhia ombi lao lililo ndani ya Haki yao, basi iweje leo ninyi mnaodai kuongozwa na huyo HAKI muanze kutembeza UONEVU katika jina la HAKI?

  Kanisa lapaswa kujihadhari sana na mambo yanayojichomekeza katika Injili, mambo haya si bure, ni mikakati thabiti! Hebu itazameni vizuri kwa jicho la kiroho ile sala aliyotufundisha Kristo, Mt 6:9-10:
  “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”
  Ili sala hiyo iwe kamili ni lazima kwanza tujue ni Jina lipi tupasalo kulitukuza. Huo ndio mwanzo wa safari hiyo katika hiyo MAZE, ukikosea mlango wa kuingilia, basi hutafanikiwa kumfikia huyo Mungu! Jambo la pili ni Ufalme. Basi Ufalme huo tunaoutaka utujie, mamlaka ya ufalme huo yako kwa nani? Ufunguo alipewa Petro, ni lazima turudi tumtazame Petro ili atufungulie ule Mlango katika hiyo Maze ya Injili! Na la Tatu ni Mapenzi ya Mungu. Sisi hatuna mapenzi yetu ya kuyatimiza, bali tunayo Mapenzi ya Mungu tu katika maisha yetu ya Wokovu. Basi Mapenzi ya Mungu ya wapi leo hii? Mapenzi ya Mungu yako katika Neno lake lililo Hai, Biblia. Kama Mapenzi yake ni kwa Kanisa kuwekwa huru na shida ya mapepo, basi amelipa mamlaka ya kuwafukuza katika maeneo wasiyoyataka yawepo, ndani ya kusanyiko la watakatifu, pamoja na hao wanaoujia Utakatifu huo kupitia hiyo Habari Njema. Lifanyeni jambo hilo kama yalivyo Mapenzi ya Mungu, yadhihirisheni hivyo ili mpate kulitukuza Jina lake alilowapa katika Haki!

  Kuongeza chochote kile nje ya Mapenzi ya Mungu ni hasara! Ndio maana Patrick alisema mapepo hayo yenye kuijua Haki na HAKI mwenyewe, yatakuwa yanawang’ong’a kwani mnakuwa vichekesho hapo mnapoyapigia kelele zisizo na maana! Bali kwa imani iliyozaliwa kwa audience yenu pale mlipolizungumzia Neno la Mungu lihusulo uponyaji, Mungu hushuka kulitimiza Neno lake, hata jambo hilo kiroho lingekuwa, “Imani yako imekuponya” na si zile kelele zenye zaidi ya miaka 100, kila siku mnayafungia mapepo kuzimu, anayeyafungulia ni nani? Acheni Patrick awashangaeni!

  Kwa leo nikomee hapa, nivute pumzi kidogo, kisha nimalizie tafakari hii kwa kuyaendea hayo Maandiko mengine ya Ufunuo na Yeremia nk ili kulitazama zaidi jambo hili la kukemea mapepo na kuyafungia kuzimu!

  Mbarikiwe nyoote!

 12. Wapendwa,

  Kwa habari hii ya kutoa pepo ni vema tukafuata mfano na utangulizi uliowekwa na Bwana Yesu na Kanisa la mwanzo. Bwana Yesu alisema wazi pepo linakwenda wapi baada ya kumtoka mtu.

  24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, – Luka 11:24 SUV

  Sasa maneno haya ya Bwana Yesu tunayaoanisha vipi na kilichotokea pale katika ile nchi ya Wagerasi? Maana pepo Jeshi lilimtoka yule Mgerasi kuwaingia nguruwe na hatimaye kuwazamisha kwenye maji, nguruwe wakafa na mapepo yale bila shaka yakaelekea kutangatanga mahali pasipo maji kama Bwana Yesu alivyosema. Bado natafakari hilo, kuna mengi tunayoweza kujifunza katika hiyo habari ya Mgerasi aliyefunguliwa, mfano, pepo haliwezi kujiamulia tu kumwingia mtu au mnyama ila yanatafuta nafasi iwe ni kupewa ruhusa na Mungu, au kwa hila za ibilisi kupitia uongo wake, dhambi, maagano, n.k.

  Bwana Yesu hakutuambia tuyapeleke au tuyafungie mapepo kuzimu, na hata Mtume Paulo ambaye alipata mafunuo mengi na kupewa kujua mengi kuhusu utendaji wa ufalme wa giza hakuwahi kuliandikia Kanisa liyafungie mapepo kuzimu. Badala yake anatuambia hivi:

  11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
  12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. – Waefeso 6:11-12 SUV

  Sehemu nyingine tena alituandikia habari za “mfalme wa uweza wa anga” yaani ile roho itendayo kazi ndani ya wale wasiomjua Mungu (Waefeso 2:2) lakini hakusema tumfunge tumpeleke kuzimu ila leo hii kuna watu wanahangaika kumfunga mkuu wa anga kila kukicha, sasa hebu tujiulize hii imekaaje kaaje, mkuu wa anga tumfunge leo na kesho tena na kesho kutwa tena na tena na tena…yatupasa tujiulize, je huko kumfunga kwetu kunatekelezeka kweli? Mitume wala Kanisa la mwanzo hawakupoteza muda wakifanya hivyo na wala hakuna andiko linalotuagiza tumfunge mfalme au mkuu wa uweza wa anga ambaye pia ni roho ileile ya Mungu wa ulimwengu huu inayowapofusha watu wasiione nuru ya Injili wakaokolewa (2 Wakorintho 4:4)

  Baada ya kufufuka kwake Bwana Yesu aliwaagiza wanafunzi wake na sisi leo hii akisema hivi:

  21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. – Yohana 20:21 SUV

  Hivyo tutoe pepo kama Bwana Yesu alivyotoa, tusi-complicate mambo.

  Tunapotoa pepo tunatumia mamlaka yetu katika Kristo, hatuombi hivyo kutumia andiko la kuomba chochote hapo si mahali pake na kwa kuwa tu maneno “ombeni chochote” yametumika haina maana kwamba unaweza kujiombea tu chochote kile unachotaka, hapana, lazima hicho “chochote” utakachokiomba kiwe kinaendana na Neno.

  Tumepewa amri na mamlaka ya kulitumia Jina la Yesu kutoa pepo, hatumuombi Mungu alitoe pepo hapana sisi ndio tunalitoa pepo kwa mamlaka tuliyopewa na Bwana Yesu, kwani tunaye Roho Mtakatifu ndani yetu.

  Yatosha kufanya kama alivyofanya Bwana Yesu maana Yeye ndiye mfano wetu naye ameshatuagiza “toeni pepo”.

  Mbarikiwe,

  Patrick

 13. Shalom SG

  Kwa kweli namtukuza Mungu Baba wa Bwana yetu Yesu Kristo kwa kutubariki baraka zote za rohoni ktk Kristo Yesu kwa kutujalia kwa kadri ya utukufu wake.

  Nawashukuru wote ,
  Mfalme wa amani Kristo Yesu awabariki.

  Naomba tena nmnipe nafasi ktk mioyo yenu nami nichangie kwa sehemu
  kwa kadri ya ufahamu wangu ktk maandiko(neno).

  Nilikuwa na naomba tafakari yetu izame ndani zaidi.ktk hoja hii ya kukemea mapepo kwani vinavyoamabatana navyo ni vya kiroho zaidi au viko ktk kwa lugha ya rohoni(kimbingu)zaidi.

  Tunapoutazama ufunguo tuwe rohoni maana halisi kuwa ni mamlaka.(tutumie zaidi macho ya kiroho tunapotafari hii hoja)

  Mtume Yohana awe mfano kwetu
  Yuko ktk maono bado anaangalia vitu ktk hali ya kimwili kiasi yule malaika anapambanua hizo roho ktk maana halisi Ufu17

  mst.15
  Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha..

  mst.18
  “Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.”

  Kuzimu shurti tuitazame kuwa ni roho na tuone ktk macho/lugha ya kroho,maandiko ufu6:8 inasema MAUTI NA KUZIMU amepanda farasi

  hizi ni roho (falme na mamlaka)yaani( wanyama,mwanamke ,farasi,nzige nk)

  Hizi roho ktk kitabu ufunuo zinazungumzwa kuwa zilikuwepo /zipo /zinakuja na zote zinatoka kuzimu.

  Zina mipaka yake

  Sasa fikiria kwa uchache mst. LK 10:19,YER 1:9-10,YER 51:20-21,MT18:18,

  Yesu Kristo amaeinyang’anya hii roho mauti na kuzimu mamalaka juu ya Kanisahii(Wana wa Mungu) kwa kuishinda Ufu1:18

  Amechukua fungua ZA milango ya kuzimu maana ndani ya Kuzimu kuna Falme na wafalme.ziko nyingi kama tulivyo ona kwenye Ufu9 kwenye lile shimo la ABIZO.

  Kwa ushindi wa Bwana Yesu Malango ya kuzimu ayatalishinda kanisa,

  Kanisa limepewa Funguo ZA mbinguni kwa Uchache 1.jina la YESU,2.DAMU YA YESU,NGUVU YA ROHO MTAKATIFU.

  Kristo anasema nanyi kiniomba lolote kwa Jina langu hilo nitalifanyaMT14:13

  Mara nyingi utawasikia wapendwa wakise huyu ndugu amefunguliwa.

  kusema amefunguliwa inamaanisha alikuwa alifungwa.sasa kama tunaweza kuomba vilivyofungwa kwenye falme na maamlaka za giza vikafunguliwa.kwanini tushindwe kuvifunga.kwa Jina la YESU

  Maana mwenye funguo(mamlaka) ya kufunga na kufungu kuzimu ni Yesu Kristo

  Wale mapepo ya Gerasi yalimsii Bwana Yesu asiwafunge kuzimu

  Lk 8:31 “Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.

  Hizi falme na mamlaka zina mipaka wanayo miliki na kutawala

  Jeshi la pepo wa wagerasi walimsiii Yesu asiwafunge nje ya mipaka yao

  Mk 5.10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.

  Hata hivyo bado pamoja na kumuomba Bwana Yesu haya mapepo kuwaingia nguruwe bado wale Mapepo walikwenda baharini (falme na mamlaka)yaani kuzimu ndani ya mipaka yao.

  Tutafakari sana maandiko haya

  Ufu5:5.10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

  Efe2:2.6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;

  Efe 4.8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.

  Zab8:4-8

  Neno anatubariki baraka za rohoni kwa hili andiko
  “Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao”
  maana tulipokuwa hatuna wokovu tulipunguiwa na utukufu wa Mungu

  Mnisamehe kwa maandiko marefu

  Nitakuwa nje ya network kwa kitambo BWANA akipenda nitajumuika nanyi tena.

  Mungu wa Faraja atufariji na kutuokoa na kila neno baya na atuhifadhi ata ajapo kulitwaa Kanisa lake Utukufu una yeye miliele na milele

  Amen
  Barikiwa

  Mjoli Haule

 14. @ Patrick
  Asante kwa comment, na pia kwa jitihada ya kuelimisha kuhusu ukweli wa Maandiko, may the Lord richly bless you!

  @ Mjoli Haule
  Nimefurahi saaana kukuona tena ndugu yangu na mwenyeji wangu! Ninamshukuru Bwana kwa ajili yako, karibu sana, na Bwana akubariki!

  @ Wapendwa
  Changamoto za jambo hili la “Kuyafungia mapepo Kuzimu” ni nyingi, na zinahitaji tafakari iliyojikita katika uamuzi thabiti wa kumfuata ‘nani’, Maandiko au Mazoea?

  Basi tunaporudi katika tafakari ya michango iliyotolewa, na katika ile kiu ya kujifunza, mambo ya NZIGE yaliyojitokeza yameniongezea shauku ya kulitazama zaidi jambo hili ili kuupata ukweli wake, maana hayo yamenukuliwa kutoka katika Neno la Mungu ambalo tumepewa sisi tulijue hilo, wakati tungalipo hapa duniani!

  Kwa kadiri jambo hili la nzige linavyojitokeza katika Maandiko, mimi nimeliona linahusiana na “Mapigo”. Katika hali ya Anguko dunia iliyomo, nzige ni balaa! Wale nzige walioifunika Misri (Kut 10:14), hawa walikuja kwa Neno la Mungu na kulitimiza kusudi lake, walikuwa ni nzige wa asili, hawakuwa mapepo, Maandiko yanashuhudia hivyo. Pia tukumbuke ya kwamba mambo ya Agano la Kale, yule ‘Mwalimu’, yalikuwa ni ya kimwili zaidi, kwa watu wa kimwili.

  Nzige tunaowaona katika kitabu cha Ufunuo, hawa maelezo yao ni kama walivyoyatoa wapendwa Haule na Patrick, kama yalivyoandikwa. Hawa si nzige wa asili, hata mawindo yao si yale ya nzige wa asili. Tena nzige hawa ni sehemu ya vile vitasa au mapigo. Mapigo haya yanapokuja, huo utakuwa ni wakati ambao Injili ya kuokoa itakuwa imefungwa, hakuna anayeweza kuokoka tena katika wakati huo, licha ya mahubiri kuendelea na watu kujidhania kuwa wanaokoka na kujiridhisha hivyo, lakini Milango ya Neema itakuwa imekwisha kufungwa!!

  Mapigo hayo yanaambatana na ujio wa HUKUMU, kwahiyo, nyakati hizo zitakuwa ni nyakati za michezo ya dini! Hebu litazame jambo hili: kwamba yule nyota aliyeanguka kutoka mbinguni na kisha KUPEWA ufunguo wa shimo la kuzimu, “Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. Nzige wakatoka katika ule moshi, …” (Ufu 9:2-3); basi nazidi kujiuliza hawa wahubiri wanaoyafungia mapepo kuzimu, funguo hizo wamezipata wapi? Maana tunasoma katika Mt 16:19 kuwa Kanisa limepewa funguo za ufalme wa mbinguni tu, ambazo linazinazitumia kufungiana nje mmoja kwa mwingine! Yaani kama ni Wasabato, basi wamewafungia nje madhehebu mengine yote yanayosali Jumapili, nao Wakatoliki waliwafungia nje Waprotestanti wote miaka mingi iliyopita, nk nk!

  Funguo za kuzimu anazo Kristo mwenyewe, “Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu” Ufu 1:18, ninaamini ndizo hizo anazopewa huyo nyota aifungue kuzimu! Hata hao malaika wanne waliofungwa kwenye huo mto Frati nao wanafunguliwa katika kipindi hicho, ndipo wanatoka na jeshi lao la wapanda farasi milioni mia mbili kwa kazi hiyo ya mapigo, sio kuokoa! Ndio maana tunasema yeyote anayefundisha kuyafungia mapepo kuzimu atakuwa hajaielewa vizuri Injili! Ili uweze kuufunga mlango wowote ule, unapaswa uwe nazo funguo kwanza, na hatuoni sehemu yoyote ile ambayo kanisa limekabidhiwa ufunguo wa kuzimu!!!

  Funguo za kuzimu alikuwa nazo Ibilisi huko nyuma ndio maana mawakala wake walikuwa na uwezo wakuingia na kutoka, hata tunamuona yule mwanamke mchawi wa Endor akimpandishia Sauli nabii Samweli. Lakini baada ya Kristo kuteremka huko akazinyang’anya hizo funguo, Efeso 4:8, kwahiyo, hiyo sehemu aliyoifunga hakuna anayeweza kufungua kumtoa wala kumuingiza yeyote yule, kule shimoni!

  Makazi ya mapepo na Ibilisi ni kuzimu katika maana ya dimension, ambako pia wafu wasio katika Kristo hupelekwa huko kufungiwa, katika sehemu husika kusubiri Hukumu inayojumuisha ziwa la moto!

  Basi Kanisa, wafungulieni watu Mbingu; acheni michezo ya kuigiza ya kuyafungia mapepo huko msiko kujua, maana mngekujua basi mngejua kuwa funguo za huko anazo nani!!! hata yule nyota alipewa kufungua tu na si kufunga kulingana na programu!!!

  Mbarikiwe nyoote!

 15. Haule, God bless you I can see the best spirit in you. That spirit which teach us of the Kingdom. Sorry for the language.

 16. Mpendwa Mjoli John Haule,

  Sasa nimekuelewa, naona umekuwa na haraka ya kujibu ile hoja yangu ya mwanzo na katika haraka hiyo umenipachikia maneno ambayo sijawahi kuyasema. Ngoja ninukuu ulivyodhania nimesema:

  “Niliandika haya maandiko kukupa changamoto ya uliyosema/unaendelea kusema kuwa mapepo hawapo kuzimu.” – John Haule

  Ni wapi mpendwa niliposema hivyo? Ukirudi nyuma utaona baada ya kunukuu Ufunuo 12:9 na 12 nimesema hivi:

  “9 Basi joka hilo kuu likatupwa nje, yule nyoka wa kale aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye watu wote ulimwenguni. Alitupwa chini ardhini, yeye pamoja na malaika wake. – Ufunuo 12:9 SNT

  Hapo tunaona alitupwa duniani yeye pamoja na malaika zake. Halafu tukiendelea kusoma mistari inayofuata tunakutana na maneno yafuatayo:

  12 Kwa hiyo furahini ninyi mbingu, na wote wakaao mbinguni! Bali ole wenu nchi na bahari maana shetani amekuja kwenu akiwa amejaa ghadhabu, kwa maana anajua kuwa muda wake ni mfupi!” – Ufunuo 12:12 SNT

  Hivyo basi tunaona wazi kuwa shetani wala mapepo hawakutupwa kuzimu bali duniani. Labda niongezee kuwa kuna wale malaika walio asi na wamefungwa kwenye giza hadi siku yao ya kuhukumiwa hao hawawezi kutoka huko kifungoni kuja duniani kamwe – Yuda 1:6

  Sijadai kuwa huko kuzimu hakuna mapepo, Maandiko yanasema wazi kuwa wapo wamefungwa bado na iyo sehemu walipofungwa hawawezi kutoka, ila iko siku hao mapepo waliofungwa watafunguliwa kwa amri ya Mungu mwenyewe, siyo ya mtu yeyote yule. Ninachosema mimi ni hiki, hatujaambiwa tuyapeleke mapepo kuzimu, wala tuyasage tikitiki, tumepewa amri na mamlaka ya kuyatoa, full stop!

  Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe…. – Mathayo 10:1 SUV.

  Kama nilivyomjibu Mpendwa Mabinza LS, pepo halitoki kwa sababu nyingine yoyote ila kwa sababu ya Uweza uliopo katika Jina La Yesu na haki aliyonayo mkemeaji ya kulitumia jina hilo na ikiwa pepo litatoka wakati mkemeaji hana mamlaka ya kulitumia Jina hilo, yaani ni mkengeufu basi tuna kila sababu ya kuzingatia Mathayo 7:22 kuwa huyo ni kati ya wale watakaokuja kusema siku ile “tulitoa pepo kwa Jina lako”, mtu wa aina hii kutoka kule kwa pepo kunamdanganya afurahie ajione yuko sawa mbele za Mungu kumbe sivyo ilivyo. Ndiyo maana Bwana Yesu aliwaambia wale 70 waliporudi, “msifurahi kwa kuwa mapepo yanawatii, bali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa Mbinguni”…na ndiyo maana pia akasema “mtawatambua kwa matunda yao”

  Sasa kwa habari za kivuli cha Petro kuponya wagonjwa pamoja na kuwa haikuwahi kuonekana kwenye maandiko hapo awali lengo lililokusudiwa lilifanikiwa: wagonjwa walipona. Sasa labda tujiulize, je wanafunzi walipewa amri na mamlaka ya kuponya wagonjwa? Jibu ni ndiyo na sote tunakubaliana na hilo. Swali lingine, je walipewa formula ya kuombea wagonjwa wapone? No, hapana wao na sisi leo tulichoamriwa ni kuponya wagonjwa, iwe kwa vivuli, vitambaa, viatu, karatasi, kupitia internet, au kwa mtindo wowote ule haikinzani na Maandiko mradi mamlaka na uweza wa Jina la Yesu vimetumika.

  Kwa habari za milango ya kuzimu kutolishinda Kanisa la Kristo, Maandiko yako wazi kuwa sisi tuliookolewa tumhamishwa toka ufalme wa giza, himaya ya iblisi hadi ufalme wa Mwana wa Pendo lake, ufalme wa Nuru. Hivyo kila mwanadamu leo hii yuko kwenye ufalme wa Mungu au wa Ibilisi. Wote wasiookolewa wako mautini, wako chini hukumu tayari ila wanapookoka wanaondolewa chini ya hukumu na mauti na kuingia Uzimani.

  Kwa maneno mengine kuzimu imewakamata tayari ila kwa kuwa bado wako hai wanayo nafasi ya kuokoka, ila wakifia kwenye hali hiyo basi ni wa kuzimu na jehanamu moja kwa moja. Sasa tunaposonga mbele kama Kanisa ambalo Kristo mwenyewe analijenga kuzimu haiwezi kutuzuia kuwanyakua waliofungwa chini ya kongwa la Ibilisi.

  Wapendwa, tujihadhari tusiende mbele ya mipaka ya Neno la Mungu kuna hatari yake. Kama alivyoelezea vizuri Mpendwa CK Lwembe, Mungu ni Mungu wa utaratibu, yaani pattern, na Bwana Yesu naye avivyo hivyo kwani alisema hajifanyii fanyi chochote kila bali anachomuona Baba anakifanya naye ndicho anachokifanya, yaani kwa maneno mengine anamsikiliza na kumtii Roho wa Mungu katika yote including kutoa pepo.

  Hivyo basi, kuyapeleka mapepo kuzimu na mambo mengine kama hayo ni kwenda mbele zaidi ya mipaka yetu Kimaandiko, ila pepo litatoka lakini kuzimu haliendi, likikuambiwa linarudi kuzimu linakudanganya tu ili kukuchota uendelee kwenda mbele zaidi ya mipaka yako Kimaandiko matokeo yake unakuta watu wanaleta “ujuzi” mpya waliougundua baada ya kujibishana na mapepo na kuufundisha kama vile ni kweli ya Neno la Mungu.

  Wapendwa naona niukunjie huu mkeka hapa nisiwachoshe, tuendelee kujifunza pamoja.

  Patrick

 17. Mpendwa Mabinza LS:

  Napenda kujibu hoja ulizoibua kama ifuatavyo:

  Kwa kifupi tu hoja zako ya 1 na ya 2, jibu lake rahisi sana tu: Mapepo yanatoka kwa sababu ya uweza uliopo katika Jina la Yesu na haki aliyonayo mkemeaji ya kulitumia Jina hilo. Full stop. Na pia hatumuombi Mungu ili mapepo yatoke tunayaamuru yatoke maana sisi tuliookoka tumepewa mamlaka ya kulitumia Jina la Yesu, Wana wa Skeva walijaribu bila kuwa mamlaka ya kulitumia Jina La Yesu, sote tunajua kilichotokea.

  Baada ya kusema hivyo nirudie kusema hivi: kuyaa mapepo, kuyapeleka kuzimu au kuyachoma moto hayo ni yetu sisi, maana hukumu yao bado. Kumbuka Neno linasema sisi katika siku ile ya hukumu ambyo bado haijafika (future tense) tuliookoka tutahukumu malaika bila shaka ni wale walioasi:

  3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? – 1 Wakorintho 6:3

  Tunapokemea mapepo kwa Jina la Yesu lazima yatoke na yanatoka, ila hayaendi kuzimu wala hayasagiki tikitiki wala hayaungui na keteketea, ila yanatoka na kama Bwana Yesu alivyosema yakitoka yanazungukazunguka sehemu kavu halafu yanarudi kuangalia yalikotoka kama yanaweza kurudi. Kama umewahi kushiriki huduma ya deliverance kwa muda utaigundua kweli hii, binafsi nimeshashiriki tukoa pepo sana tu na kuyapeleka kuzimu, kuyasaga, kuyachoma n.k na watu wakafunguliwa na baadaye nikashuhudia pepo limerudi na tatizo lilelile limemrudia yule mtu kwa nguvu zaidi, obviously pepo halikusagika tikitiki, halikuungua na kuteketea kwa moto na wala halikurudi kuzimu. Ikabidi kurudi kwenye maandiko na baada ya kuujua ukweli huo na kumfundisha yule mtu ukweli huo akawekwa huru baada ya session ile na kuendelea kuwa huru kabisa.

  Hitimisho langu ni hili: pamoja na kwamba tunayo mamlaka juu ya mapepo, mamlaka yetu ni kuyatoa tu, hiyo ya kuyahukumu siku yake bado na mapepo yanalitambua hilo na yanatambua vilevile ya kuwa tunapofanya hivyo tunadhihirisha tulivyo weupe kimaandiko. Kutoka lazima yatoke kwa Jina la Yesu limetumika ila hayarudi kukaa kuzimu. Hivyo basi shetani hajamtoa shetani hapo ila amesalimu amri mbele ya Jina la Yesu.

  Hoja yako ya 3 nitaiacha kama ilivyo na kushauri tu kuwa kila mmoja wetu anayemkiri Kristo kama Bwana na mwokozi wake anao wajibu wa kufunza Neno la Mungu na kulishika. Tunaye Roho Mt. hivyo tusibweteke kumezameza kila kitu mradi mtu fulani kasema au kafanya, kila mmoja wetu ayachunguze Maandiko kama wale Waberoya kuona kama mambo haya ndivyo yalivyo.

  Mbarikiwe wote.

  Patrick.

 18. Asante
  Mpendwa Patrick…

  soma tena nilichoandika ujanielewa hata sasa,
  Ingawa umeelewa kuwa hawa ni mapepo(ufu9) sio nzige wa kawaida kut10:14 na Mith30:21 umekubali kwa kuzunguka.

  Niliandika haya maandiko kukupa changamoto ya uliyosema/unaendelea kusema kuwa mapepo hawapo kuzimu.

  Maandiko yanaonyesha kuwa mapepo wapo kuzimu kufuatana na ufu9,Na nimekuelezea kuwa hata kama maandiko yanasema shetani na malaika zake wametupwa ktk nchi kwa andiko ilo la ufu9 tunapata ufahamu kuwa ni sehemu maalumu ktk ulimwengu wa roho,

  Hizi ni falme na mamlaka na ziko sehemu mbalimbali ktk nchi(ardhi) baharini/maziwa/mito/njia panda nk, Hizo zote ni kuzimu.

  ole ni kwa nchi na bahari ……

  Maandiko ya kut10:14 na mith 30:27 nimenukuu ili kuwa kielelezo cha tofauti ya nzige wa kawaida na wale wa Ufu9 na makandokando yao yote km nywele/mfalme nk ambao kuthibitisha kuwa mapepo wapo kuzimu na ndio kwao hasa wanakostahili kuwako.

  Yesu alivyosema mapepo yakitoka mtu yanazunguka sehemu kavu, ipi sehemu kavu.?unaweza kunisaidia fundisho hapo.ufahamu wangu wa maandiko kwa sehemu nimekuonyesha sehemu ktk ulimwengu wa roho.

  Maandiko yatuaambia vita yetu sisi si ktk damu na nyama ni ktk ulimwengu wa roho juu ya falme na mamlaka na wakuu wa giza ili na majeshi ya mapepo wabaya ktk ulimwengu wa roho.

  Tunachopaswa ni kuwa na haki (kuvaa silaha)na ufahamu wa Neno la Mungu(YESU)ujuzi wa kweli naye yumo ndani yetu nasi ndani yake.Tuna mamlaka(funguo) juu ya nchi na juu ya Adui.

  Tunapofunga falme na mamlaka ni swala la ufahamu ktk ulimwengu wa roho,tuko na ufunguo.(muhuri/rakiri)kwa lile neno mbingu inathibitisha.

  wapendwa tunaye Roho Mtakatiu ndani yetu ni kiongozi hivi watu walipokuwa wamejipanga kwenye njia kuu ili waponwe na kivuli cha Petro,Nani aliwafundisha! au walisoma andiko gani alilosema Yesu. kuwa wakae njia kuu na kuwaelekeza kufanya hivyo.

  Tatizo tunapokea mambo mengi ya imani lakini hatuyatumii.

  Tuko na ujuzi mdogo namna hii kuhusu mapepo na kuzimu,

  kama kuna mpendwa humu aliwahi kuwa mtumishi wa shetani mf mganga wa kienyeji kabla Yesu ajamkomboa na kumweka huru atakuwa anashangaa kabisa.

  Yesu alipotuambia malango ya kuzimu hayatalishinda kanisa alkuwa anamaanisha kuwa huko ndiko makao makuu ya mashetani/mapepo na uchafu wote unaoitwa uchafu.

  Barikiwa

  Mjoli Haule

 19. Wapenda,
  Patrick G. Kamera, Apostle Emanuel na wengine,

  (1) Kama, kuyapeleka kuzimu, kuyachoma moto na au kuyasaga tikitiki ni kitendo kinafanywa Nje ya Neno la Mungu (kwa mana hiyo wanadanganya), na Mungu anasema kuwa, yeye hulichunguza Neno lake apate kulitimiza, na mahali pengine anasema anajibu maombi ambayo yatakuwa ndani ya mapenzi yake; Na kwakuwa, upo ushahidi wa wazi makanisani watu wakishuhudia kuwa mapepo waliyokuwa nayo yamewatoka, na wengine wanakuja na magari yao mapya, watoto wachanga mikononi mwao, wakileta sadaka za mapesa ili kutoa shukurani kwa Mungu kanisani, huku wakieleza wazi kuwa, yale mapepo yaliyokuwa yamefunga Baraka zao sasa hayapo tena, sasa wanafuraha tele, Je, hapo mnasemaje matokeo yaliyosababisha ushuhuda huo, ni matokeo ya uongo wa shetani?

  (2) Lakini pia, tunashuhudima moja kwa moja kupitia macho na masikio yetu katika tv, radioni, mikutano ya hazara na makanisani, watu wakifunguliwa kwa maombi kama hayo, ambayo kumbe si Neno la Mungu, Je, ni nguvu gani inayowaponya iwapo kuna andiko linasema “shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake?”

  (3) Patric G, umesema, nakuu, “…..tunaonyesha kuwa hata maandiko yenyewe hatuyajui. Kwa habari ya mapepo, Bwana Yesu aliagiza hivi:’’….TOENI PEPO….” Sasa hayo mengine ya kuyapeleka kuzimu, kuyachoma moto, kuyasaga tikitiki n.k. ni ya kwetu sisi….”

  Kwakuwa mnatuongopea na kutupoteza kwa kutuaminisha uongo, mmetudanganya kwa Muda mrefu na hamtaki kuacha kutuongopea! Wala hamuombi msamaha kwa Mungu mnayezidi kumpotoshea Neno lake, ingawa sina haki ya kumsemea, maana yeye atajua la kuwafanya watumishi waongo, ila mimi nasemea kwa upande wetu; Kwa vile mwenye kuomba msamaha ndiye anayesamehewa, ninyi hamjatuomba msamaha kwakutuongopea kwa muda mrefu na kutuaminisha uongo; SAMAHANI, Je, sasa, tuwatendeje ndugu zetu?

 20. Nami nakubaliana nawe mpendwa, hakuna andiko linatuagiza kuwa tuyapeleke mapepo kuzimu japo tumeagizwa kuyakemea, na kuyatoa kwa neno la yesu krsto

 21. Amen Mtakatifu John,

  Nashukuru kwa changamoto uliyonipa, nimeipokea nikifuatisha mfano wa wale watu wa Berea ambao waliyachunguza maandiko kuona kama asemavyo Paulo ndivyo ilivyo.

  Tukirudi kwenye maandiko, cha kwanza kabisa tunaona kuwa wale nzige waliovamia Misri katika ule mfululizo wa mapigo ya Mungu dhidi ya Wamirsi ni tofauti kabisa na wale nzige wa Ufunuo.

  Tukiyaangalia Maandiko, ile sura nzima ya 10 ya Kutoka, utakubaliana nami kuwa wale nzige walikuwa ni nzige wadudu halisi kuanzia maumbo yao na tabia zao na siyo mapepo, walikula mimea tu hadi hapakuwa na mti, mmea wala jani lililosalia katika Misri yote (Kutoka 10:15) . Hawa nzige wa Misri hawakuwadhuru watu. Vilevile tunaona kuwa hawa nzige wa Misri waliletwa na upepo wa mashariki, walitanda juu ya nchi yote ya Misri wakaifunika na waliondolewa kwa upepo wa magharibi hadi kwenye bahari ya Shamu. Vilevile tukumbuke kuwa Mungu alisema kuwa hapajawahi kutokea nzige kama hao na hatakuja kuwepo nzige kama hao tena (Kutoka 10:14)

  Wale nzige wa Ufunuo 9, siyo nzige wa kawaida kuanzia maumbo yao, wana nyuso za wanadamu na nywele kama wanawake, wana dirii za chuma kifuani, meno kama simba, mikia kama nge n.k, kifupi wana sura za ajabu kabisa tofauti na wale wa Misri tena wana mfalme pia, na katika hilo umejipinga mwenyewe kwani umenukuu andiko la Methali lisemalo “nzige hawana mfalme”. Ni kweli nzige halisi hawana mfalme, ila hawa wa ufunuo ambao ni roho chafu wanaye mfallme Abadoni au Apolioni.

  Nzige wa Ufunuo wametokea kwenye moshi wa Shimoni kuzimu hawakuletwa na upepo wa mashariki kama wale wa Misri. Nzige wa ufunuo wamepewa mamlaka ya kuwauma watu (wasio na chapa ya Mungu) kama nge vile ila wameamriwa wasiiguse mimea wala kitu chochote kibichi (Ufunuo 9:4), Nzige wa ufunuo walipewa miezi mitano ya kuwatesa watu, nzige wa Misri hawakupewa muda specific.

  Baada ya kusema hayo yote tunarudi palepale kuwa hatujapewa mamlaka wala maagizo ya kupeleka mapepo kuzimu, haipo katika Maandiko hata tufanye text-proofing namna gani, Kimaandiko hatuwezi kuhalalisha mapokeo hayo. Angalia mifano yote ya mapepo waliofungwa kuzima nani anayewafungulia huko? Mungu mwenyewe aliyewafungia huko, na pia kuzimu walikofungiwa na kwa muda tu, nyumbani kwao kwa kudumu ni jehanamu, huko wanasubiria muda wao na wanajua unakuja.

  Maandiko yako wazi, Ibilisi na malaika zake wametupwa duniani, Neno linasema hivi:

  9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. – Ufunuo 12:9 SUV
  12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. – Ufunuo 12:12 SUV

  Isitoshe hakuna hata siku moja Bwana Yesu alipokemea mapepo na kuyaamuru yarudi kuzimu, kama kuna ambaye angeweza kufanya hivyo ni Yeye na hakufanya hivyo na tena alisema wazi pepo limtokapo mtu linazunguka zunguka sehemu kavu halafu linarudi kuangalia kama lilipotoka kuna nafasi…ilbilisi naye anazunguka zunguka kama alivyokiri alipokuja kujihudhurisha mbele za Mungu pamoja na wana wa Mungu.

  Nisiwachose kwa mkeka mreeeefuuu….nimalizie tu kwa kusisitiza kuwa kuyaamuru mapepo yaende kuzimu ni mapokeo yasiyo na msingi wa kimaandiko, tunapofanya hivyo sana sana tunayapa mapepo nafasi ya kutung’ong’a tu kwani tunayaonyesha kuwa hata maandiko yenyewe hatuyajui.
  Kwa habari ya mapepo, Bwana Yesu aliagiza hivi: “…TOENI PEPO…” sasa hayo mengine ya kuyapeleka kuzimu, kuyachoma moto, kuyasaga tikitiki n.k. ni ya kwetu sisi. Mbarikiwe.

  Patrick

 22. Bwana Yesu asifiwe SG,
  Kitambo sasa sikuwepo kwenye jukwaa,hongereni kwa ushindi ktk kushindania imani yetu ktk Kristo Yesu
  Namshukuru Bwana kwa kunipa tena muda wa kusoma na labda kuandika kwa sehemu sawa na ufahamu wangu ktk maandiko,
  Nianze kuchangia
  huu mjadala wa kukemea mapepo,
  Naomba ndugu Patrick Kamera labda nikupe changamoto za mistari ya maandiko,sawa na post yako ya 13/06/2013 at 12:08 PM kuwa…

  “Hivyo basi tunaona wazi kuwa shetani wala mapepo hawakutupwa kuzimu bali duniani. Labda niongezee kuwa kuna wale malaika walio asi na wamefungwa kwenye giza hadi siku yao ya kuhukumiwa hao hawawezi kutoka huko kifungoni kuja duniani kamwe – Yuda 1:6”

  Ukisoma ufu 9,tutakutana na Habari ya nzige waliofunguliwa toka kuzimu na kwa mujibu wa maandiko hawa sio nzige wa kawaida kulingana na maandiko ni mapepo ebu tuaangalie mist hii ifutayo

  “Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi(Mith 30:27)”

  “Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo. (kut10:14)”

  Tukiyarejea maandiko hawa nzige ni mapepo yaliyofungiwa kuzimu,kwanza yana mfalme abadoni (Ufu 9:11)pili maandiko yanasisitiza hakutakuwa na nzige kama hawa wa Kut 10:14

  Pepo kuzimu ndio kwao wanakopaswa kuwako Mpendwa Patrick na ni maandiko .

  Pia kuna walifungwa mto Frati(ufu9:14)
  Maandiko yameandika kuwa wametupwa duniani ndio Lakini ni maeneo maalumu ktk ulimwengu wa roho,kama bahari,mto,kuzimu nk.

  Watumishi wa Bwana wanapowafungia kuzimu mapepo ni maandiko na mamlaka ya kufanya wanayo ni maandiko(math18:18)kwani kuzimu ni sehemu sahihi kwao kufungwa,hata hapo Bwana atakapowafungua kwa kusudi kama tulivyoona kwenye Ufu 9, ile Nyota (Malaika)alipopewa mamlaka kuwafungua

  wale malaika wasiolinda enzi yao(Yuda6:1 a Mw6:2,2Pet2:4)maandiko yanasema wamefungwa vifungo vyo milele chini ya giza(shetani)mpaka ije hukumu .

  Mjoli Haule.

 23. Ndugu CK Lwembe,

  Nimependa uchambuzi wako ulivyozingatia ujumla na mtiririko wa Maandiko, nimejifunza kitu, ubarikiwe mtumishi wa Mungu.

  NImejifunza kuwa Mungu ni Mungu wa utaratibu siyo upole as such ila pattern, sijapata neno la Kiswahili linalofaa hapo. Musa alionyeshwa pattern ya kujenga hema ya kukutania na vyote vilivyomo, Nuhu alionyeshwa pattern ya safina, Bwana Yesu alisema anafanya kile tu anachomuona Baba yake anakifanya ikiwa ni pamoja na kutoa pepo, kwa maneno mengine anafuata utaratibu au pattern ya Mungu.

  Sasa tukumbuke kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka akiwa na mamlaka yote mbinguni na duniani na chini ya nchi pia alipowatokea wanafunzi wake alisema hivi::

  21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.” – Yohana 20:21 SNT – . Hebu tutafakari hilo kwanza

  Mzidi kubarikiwa,

  Patrick

 24. Wapendwa,
  Jambo hili la kuyakemea mapepo na kuyafungia kuzimu, ni la kufikirika zaidi kuliko uhalisi wake. Roho zinazoshughulika na mafunuo ni nyingi sana, ndio maana kanisa linatahadharishwa kuhusu jambo hilo likiambiwa LIZIPIME kwanza roho zote kabla ya kuzipokea! Kipimo cha kuzipimia roho hizo tulichopewa ni Biblia, yaani Maandiko, hayo ndiye Mungu! Hakuna mafunuo yanayoweza kuyazidi Maandiko. Jambo la kwanza tunalopaswa kujiuliza ni, Je, tumemjulia wapi Mungu, au Roho Mtakatifu au Kristo? Jibu la kweli lisilo na shaka ni, “Tumemjua Mungu kupitia Maandiko”!!! Huo ndio Msingi imara tunaopaswa kujengwa juu yake.

  Kwahiyo hata tunapoliendea jambo hili la kuyafungia mapepo kuzimu, tukiwa na shauku ya kuujua ukweli, basi ni lazima tumuulize Mungu, yaani turudi katika Maandiko tupate kuipima hiyo roho inayotufundisha mambo hayo ili tuone iwapo ni Roho ya Kristo au la.

  Kama nilivyousoma mchango wa dada Leva, jambo hili la kuyafungia mapepo kuzimu, amelijumuisha katika ile Ahadi ya Yn 14:12 “Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya…” Ni rahisi sana kuliamini jambo hili katika jinsi hii na hivyo kulipokea, kama ambavyo makundi yetu yameaminishwa, lakini tunapaswa kulipima kwanza! Basi, itatufaidia zaidi iwapo tutaitafakari Ahadi hii katika ujumla wa jambo zima la uhusiano wetu katika namna ya kuzitenda kazi hizo kulingana na Maandiko yanavyotufundisha.

  Musa alipolijenga Sanduku la Agano, hakuna chochote katika ujenzi huo ambacho yeye alitumia akili zake. Mambo yote alioneshwa, naye akayatimiza kama alivyoyaona. Mungu ndiye mjenzi na mbunifu wa kazi zake zote!

  Kristo alipokuwepo hapa duniani, yeye alikuwa ni kielelezo cha utendaji wa Mungu, akiyaweka wazi mambo mengi Makuu, zile Siri, ambazo amezifunga katika Neno lake, licha ya uwazi lilivyoandikwa.

  Basi tunapoichunguza Siri hii ya utendaji wa Kazi zake, hapo tunapoziendea hizo “Kubwa zaidi”, ni vizuri tukaziendea hizo katika Msingi aliotuwekea. Ukweli Mkuu wa jambo hili tunaweza kuuona katika Yn 15:19 hapo anatuambia kuwa, “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.” Kulingana na maelezo yake haya, ni dhahiri kwamba Baba yake ndiye aliyeyashughulikia yote yaliyojidhihirisha katika Kristo! Vivyo, Kanisa lapaswa kuyadhihirisha ayatendayo Kristo.

  Hilo lapaswa kuwa hivyo kwa Kanisa kutokana na ukweli huu unaojionesha katika Yn 14:19-20 “Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.” Hii ni mojawapo ya zile Siri ambazo Kanisa limefunuliwa, ambavyo linapofikia katika kiwango hicho cha kulitambua jambo hilo, basi ndipo hatua hii kwake pia ingekuwa dhahiri kama ilivyokuwa kwa Kristo. Kwahiyo utendaji wetu wote humdhihirisha roho aliye ndani yetu, huyo anayetuongoza katika kuzitenda hizo “kazi kubwa zaidi”. Lakini jambo hili la kuyafungia hayo mapepo kuzimu halionekani katika Maandiko!

  Ndg Patrick ametoa angalizo na maelezo mazuri sana kuhusiana na jambo hili. Kwa kadiri ya mbwembwe za wahubiri wetu wa leo, mbwembwe hizo hudhihirisha wazi kuwa azitendeye kazi hizo si Kristo aliye ndani yao bali wao wenyewe kwa vipawa walivyokirimiwa! Mungu huyaendesha mambo yote kwa utaratibu maalumu. Upo wakati ambapo yeye hukiachia kikombe kijae. Kwahiyo haiwezekani kwamba katika wakati huo ageuze nia! Huduma inayoendelea leo hii kwa Kanisa ni ile Huduma ya Kristo ihusuyo KUOKOA. Kuyafungia mapepo kuzimu ni Huduma ya HUKUMU ambayo muhula wake bado! Hebu liangalieni tukio la yule Mgerasi mwenye mapepo, laweza kuwafunulia jambo fulani, Mt 8:29 “Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” Aha, kumbe kuna mihula! Lk 8:31 “Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.” [“And they besought him that he would not command them to go out into the deep” KJV]. Nayo mapepo haya yanayozunguka duniani, yapo hapa hapa duniani yalikotupwa, ndiyo maana hakuwapeleka huko kifungoni (Shimoni), badala yake aliwaruhusu wawaingie nguruwe!!!

  Sasa, iwapo Kristo hakuyafungia mapepo na wala hajawahi kutupa neno la kuyafungia kuzimu mapepo, je, wahubiri wetu wanapata wapi ufunuo wa kuyaseta tikitiki mapepo na kuyachoma moto? Mimi nimewasikia mara nyingi wakiwa katika huko kukemea mapepo, ambavyo ni tofauti kabisa na Mafundisho ya Biblia. Leo hii utamsikia mtumishi akiyakemea mapepo kwa nguvu kubwa sana kuliko nguvu anayotumia kuihubiri Injili; yaani wao hupiga kelele kuliko mapepo! “Nashusha moto sasa, ninazifunga nguvu zote za giza, ninavikusanya vinyamkera vyoote na vibwengo na jini makata na marafiki zake wote, ninayaseta na ninayatupa yote kuzimu na kuyafungia huko katika Jina la Yesu!! Holy Spirit Fire, fire, fire, fire… x 666!” halafu utayasikia mapepo yakilia, “Naungua! Naungua…!” Watu wote hulipokea jambo hilo kwa furaha ya ushindi katika Kristo!!!

  Ukiyatazama mambo hayo ya kuyashushia moto mapepo, hatujapewa Ahadi hiyo tuitimize! Mitume wakati fulani walitaka kulifanya jambo hilo la kuwashushia moto wapinzani, Lk 9:54 “Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize…? Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]” kwahiyo bila shaka roho hiyo waliyokuwa nayo wanafunzi wake katika wakati huo, ndiyo iliyo ndani ya wahubiri wanao shusha mioto leo hii, wakitenda kazi nje ya programu!

  Otherwise kushusha moto katika programu ya Mungu kunahusiana na manabii wa uongo pale katika Ufu 13:13 “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.” Kwa ajili ya kuwaghiribu watu akili zao, basi yatazameni wenyewe mambo haya, isije ikawa yanatutimilia nasi hatujui!

  Kwahiyo mambo ya kuyafungia mapepo kuzimu ni Injili za uongo ambazo huwapumbaza watu na kuwafanya wasiwe na shauku ya kuisikiliza Injili ya Kweli ambayo ingezifunua dhambi zao na kuwashitaki katika dhamira zao pale mambo yao ya sirini yanapowekwa wazi kwa Injili ya kweli, ule Upanga ukatao kuwili, hata kuwaleta katika hali kama iliyowakuta wale mkutano waliowajalia akina Petro siku ya Pentekoste, walipochomwa mioyo yao, nao wakitafuta kuikimbia Hukumu inayowajia wakawauliza Petro na mitume wengine, “TUTENDEJE, NDUGU ZETU?”

  Hiyo ndio Injili iliyo Hai, inao Uzima iwapo nawe utaitii na kulichukua jibu la swali hilo pale Mdo 2:38 kama lile kundi siku ile, ili Mungu awajibike kwako na kuufungua ufahamu wako ili uyaelewe na Maandiko, uondokane na uteja wa wauza Injili!!!

  Bwana na atusaidie kuiona Kweli yake!

 25. @ Andrew…

  TANGAZO:

  HUTAKIWI KUPOTEZA MUDA WAKO KUKEMEA MAPEPO..

  UNAZO FUNGUO ZA KUFUNGA NA KUFUNGUA

  UNAYO MAMLAKA YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA

  UNAYO FIMBO INAYOCHIPUA

  UNALO JINA LA YESU

  NA SASA KIZAZI CHA NNE MUNGU MWENYEWE AMESHUKA KUJA KUWAANGAMIZA VIBAYA WABAYA WAKE WOTE WALIOHARIBU SHAMBA LAKE NA WALIOMUUA MWANAWE MPENDWA ALIPOTUMWA KUCHUKUA MATUNDA…

  MAHALI LILIPO KANISA (WEWE) NDIPO ALIPO MUNGU- SHEITWAAAANI HAWEZI KUSOGEA…

  SASA…TUMIA HEKIMA NA MAARIFA NA UFAHAMU WAKO KUOMNGEA NA MUNGU UKIWA UNAKISOGELEA KITI CHA NEEMA KUBWA UPATE MSAADA UNAOUHITAJI HATA WAKATI UNAMUOMBEA MTU ALIYE NA MAPEPO…TUMIA SILAHA HIZO HAPO JUU …..

  KAMA HUNA MAFUTA YA NEEMA KUBWA ISIYOZUILIWA NA KITU CHOCHOTE KUTENDA LLOLOTE BASI SOGEA MBELE ZA BWANA UKIUTENGENEZA MOYO WAKO KWA TOBA NA SHUKURANI KWA KUMAANISHA…ILI UPATIWE UJASIRI NA UHODARI KATIKA KAZI HIYO.. KUMBUKA VITA SI VYAKO NI VYA BWANA …

  AMEN

  Bezaleli DC

  Dr.Damian C.Mallya. DDS,MPH

  >________________________________ > From: Strictly Gospel >To: damiancosmas@yahoo.com >Sent: Sunday, 9 June 2013, 20:33 >Subject: [New post] Kukemea Mapepo > > > > WordPress.com >Strictly Gospel posted: ” Bwana Yesu Asifiwe, je inawezekana watumishi wa Mungu kukemea mapepo na kuyapeleka kuzimu? naomba mnisaidie nani ana mamlaka ya kupeleka mapepo kuzimu na kwa mujibu wa maandiko yapi? Ahsanteni

 26. Mpendwa Alex;

  Hitaji lako limekuwa la jumla sana, Sikujua hasa unamaanisha ‘Kumfahamu’ kwa namna gani, ila tu nimejitahidi kukutafutia walau Historia kwa Ufupi ya Huyu Mtu unayehitaji kumfahamu, kwakuwa Mtu huyu ni “Mzungu” habari zake pia zinapatikana kwa kizungu, lakini kama habari hizi si zile ulizomaanisha kuzipata, utanisamehe na uweke kwa ufafanuzi hitaji lako. sisemi kuwa za Kiswahili ama Lugha nyingine hazipo ila nilizobahatika kuzipata ni hizi za “Umombo” Sasa fuatilia umjue na pia nimekuwekea na Baadhi ya Mikutano yake ya kitumishi aliyopata kufanya wakati wa Uhai wake – Enjoy yourself !

  William Marrion Branham

  Biography:
  William Marrion Branham was born April 6, 1909, on a small farm near Berksville, KY. His parents were poor, did not attend church and made their living by farming and logging. During Branham’s early childhood, the family moved several times, finally settling in Jeffersonville, IN, where he attended public schools through eighth grade.

  Branham tells of being called by God to the ministry at the age of seven by a voice high up in a tree which said, “Do not drink or smoke or defile your body in any way, for when you get older I’ll have a work for you to do.” He reports being very terrified and bewildered. Nonetheless, he was not converted until the age of nineteen. At the age of twenty-four, he began preaching in a tent in his home town.

  Branham tells of two major things that happened during his first year of ministry. The first was a series of seven visions he received on Sunday morning in 1933 just before church. The first three visions showed the rise of Mussolini in Italy, the rise of Hitler in Germany, and the rise of communism. Next they showed a soon-coming rapid rise in technology, then a tragic falling of morality of women, the rise of a powerful but cruel woman in America, and finally the destruction of the United States. The second major event occurred on the Ohio River. Branham’s ministry had prospered, with many conversions, and he was in the process of baptizing about five hundred converts when at the seventeenth person a bright light or fire appeared over him and a voice spoke, “As John the Baptist foreran the first coming of Christ, your ministry shall forerun the second coming.” Approximately five thousand people were on the river banks observing. Many screamed; many fainted. A report of the incident was carried by UPI [the United Press International] all over the nation and Canada.

  During this period, Branham met and married Hope Brumback. The couple had two children, Sharon Rose and Billy Paul, Jr. Hope and Sharon died in 1937 when the Ohio River flooded. Branham later married Meda Broy, with whom he had three children: Rebekah, born in 1946; Sarah, 1951; and Joseph, 1955.

  Branham began his healing ministry after having a visit from an angel in May, 1946. St. Louis was the site of his first meeting, followed by the trips to Texas, Louisiana, Florida, California, and eventually all over the United States. Soon he was traveling extensively into Canada, Mexico, Europe, Africa, and India.

  As his ministry grew, Branham enlisted assistants such as Gordon Lindsay and Jack Moore. His popularity blossomed as Branham emerged as the undisputed founder-leader of the healing revival movement. Lindsay and Moore began a magazine called The Voice of Healing. The publication was designed to recount the activities of Branham’s meetings past and planned. Soon after the men began the publication, Branham announced he was retiring from the healing revival circuit. Although later, in 1948, Branham resumed his activities, The Voice of Healing was altered to cover meetings of many healing evangelists and not just Branham.

  By 1955, Branham’s teaching and preaching ministry came under severe attacks over doctrinal disagreement with the pentecostal denominations that had previously supported him. Also at this time, the IRS accused him of evasion of taxes on gifts he had been receiving, although he had not kept the money for himself. Eventually, the case was settled out of court. However, Branham continued his work despite the criticism until 1965, using a blend of preaching and healing services. In one year alone, he reported over a half-million conversions — thirty thousand in one meeting in Durban, South Africa. Thousands of supporters believed in his ability to heal, foretell the future, and even raise the dead.

  In December 1965, he was fatally injured in a car accident. He died on December 24, 1965, but was not buried until Easter of 1966, because his wife, who had also been in the accident, was unable to decide where to bury him.

  PARTIAL LISTING OF WILLIAM BRANHAM MEETINGS AND APPEARANCES
  St. Louis, MO June 25, 1946
  Jonesboro, AR Summer, 1946
  Los Angeles, CA 1946
  Long Beach, CA 1946
  Santa Rosa, CA 1946
  Fresno, CA 1946
  Canada 1946
  Shreveport, LA June, 1947
  Jonesboro, AR June 1947
  Albertan, Canada August, 1947
  Saskatoon, Canada August, 1947
  Camden, AR Fall, 1947
  Phoenix, AZ November 23 – December 21, 1947
  Miami, FL January, 1948
  Phoenix, AZ March 4-5, 1948
  Pensacola, FL April, 1948
  Kansas City, KS April 13, 1948
  Tacoma, WA May 12-17, 1948
  Seattle, WA November, 1948
  Zion, IL July 1, 1949
  Minneapolis, MN July 11-16, 1949
  Dallas, TX October 28, 1949
  Jeffersonville, IN December 25, 1949 – January, 1950
  Louisville, KY January, 1950
  Houston, TX January 10-February 16, 1950
  Beaumont, TX February, 1950
  Jeffersonville, IN February 22, 1950
  Little Rock, AR February 27, 1950
  El Dorado, AR March, 1950
  Camden, AR March, 1950
  New York, NY April 5, 1950
  European Tour April-May, 1950
  Minneapolis, MN July, 1950
  Cleveland, OH August 8-27, 1950
  Minneapolis, MN 1951
  Jeffersonville, IN March 19, 1951
  Houston, TX March, 1951
  Phoenix, AZ April 13-15, 1951
  Los Angeles, CA May 2-18, 1951
  Ft. Wayne, IN July, 1951
  Toledo, OH July 17-22, 1951
  Zion, IL July 24-25, 1951
  Erie, PA July 27-31, 1951
  Jeffersonville, IN August 26, 1951
  New York, NY September 21 – October 1, 1951
  Johannesburg, South Africa October, 1951
  Durban, South Africa October, 1951
  Klerksdorp, South Africa October 14-16, 1951
  Kimberly, South Africa October 17-21, 1951
  Bloemfontein, South Africa October 24-28, 1951
  Capetown, South Africa October 29 – November 6, 1951
  Port Elizabeth, South Africa November 7-11, 1951
  Grahamstown, South Africa November 12-13, 1951
  East London, South Africa November 12-13, 1951
  Durban, South Africa November 21-25, 1951
  Salisbury, Rhodesia November 28-19, 1951
  Pretoria, South Africa December 2, 1951
  Johannesburg, South Africa December, 1951
  Jeffersonville, IN January 30 – February 25, 1952
  Phoenix, AZ April 13-15, 1952
  Hammond, IN July 13-20, 1952
  Chicago, IL August 9, 1952
  Battle Creek, MI August 16-18, 1952
  Jeffersonville, IN March 25 – April 5, 1953
  Jonesboro, AR May 6-12, 1953
  Connersville, IN June 6-14, 1953
  West Palm Beach, FL July 15, 1953
  Jeffersonville, IN July 19-29, 1953
  Chicago, IL August 29 – September 7, 1953
  Zion, IL September, 1953
  Owensboro, KY November 6-15, 1953
  Evansville, IN November 22, 1953
  West Palm Beach, FL November 29 – December 12, 1953
  Chicago, IL December 13, 1953
  Jeffersonville, IN January 3, 1954
  Woodriver, IL February 16-17, 1954
  Phoenix, AZ February 28 – March 7, 1954
  Columbus, OH March 14, 1954
  Chicago, IL March 20, 1954
  Louisville, KY March 29 – April 12, 1954
  Jeffersonville, KY May 9-15, 1954
  Chicago, IL July 14-25, 1954
  Washington, DC July, 1954
  Phoenix, AZ August 2-8, 1954
  Los Angeles, CA August 9-11, 1954
  Washington, DC August, 1954
  New York, NY August 24 – September 2, 1954
  Bombay, India September 19, 1954
  Jeffersonville, IN October 3-24, 1954
  Binghamton, NY December 3-7, 1954
  Jeffersonville, IN December 12 – January 9, 1955
  Chicago, IL January 10-23, 1955
  Phoenix, AZ February 20 – March 2, 1955
  Los Angeles, CA March 11-12, 1955
  Jeffersonville, IN April 3, 1955
  Chicago, IL April 5, 1955
  Jeffersonville, IN April 10, 1955
  Chicago, IL May 1, 1955
  Lausanne, Switzerland May, 1955
  Jeffersonville, IN May 19-22, 1955
  Macon, GA June 3-12, 1955
  Karsruhe, Germany July 18-21, 1955
  Shawano, WI July, 1955
  Jeffersonville, IN July 24-31, 1955
  Campbellsville, KY August 6-8, 1955
  Jeffersonville, IN September 11, 1955
  Chicago, IL October 2-9, 1955
  San Fernando, CA November 10-11, 14, 1955
  North Hollywood, CA November 13, 15-20, 1955
  Jeffersonville, IN January 1, 1956
  Chicago, IL January 4, 1956
  Jeffersonville, IN January 8-15, 1956
  Chicago, IL January 16, 1956
  Sturgis, MI January 20-22, 1956
  Owensboro, KY January 28-29, 1956
  Georgetown, IL February, 1956
  Minneapolis, MN February, 1956
  Sioux Falls, SD February 23-25, 1956
  Jeffersonville, IN March 5 – April 1, 1956
  Chicago, IL April 3-8, 1956
  Columbia, SC April 14-15, 1956
  Spindale, NC April 17, 1956
  Southern Pines, NC April 18-20, 1956
  Charlotte, NC April 25-29, 1956
  Jeffersonville, IN May 13 – June 10, 1956
  Indianapolis, IN June 13, 1956
  Jeffersonville, IN June 17, 1956
  Chicago, IL June 21, 1956
  Minneapolis, MN July, 1956
  Jeffersonville, IN July 15, 1956
  Shreveport, LA July 26-29, 1956
  Jeffersonville, IN August 5, 1956
  Prince Albert, Canada August 14-16, 1956
  Jeffersonville, IN August 26 – September 2, 1956
  Los Angeles, CA September 15, 1956
  Jeffersonville, IN September 16, 1956
  Chicago, IL September 30 – October 10, 1956
  Jeffersonville, IN November 25, 1956
  New York, NY December 6, 1956
  Brooklyn, NY December 7-9, 1956
  Parkersburg, WV December 15, 1956
  Jeffersonville, IN December 28-29, 1956
  Chicago, IL January 13, 1957
  Sturgis, MI January 14-15, 1957
  Jeffersonville, IN January 20, 1957
  Lima, OH January 26-27, 1957
  Phoenix, AZ February 23 – March 10, 1957
  Los Angeles, CA March, 1957
  Oakland, CA March 22-26, 1957
  Jeffersonville, IN April 7-21, 1957
  Saskatoon, Canada May 15-20, 1957
  Jeffersonville, IN June 2, 1957
  Indianapolis, IN June 11-14, 1957
  Jeffersonville, IN June 23, 1957
  Chicago, IL June 29 – July 7, 1957
  Tacoma, WA July 27-28, 1957
  Edmonton, Canada August 4-12, 1957
  Jeffersonville, IN August 15 – October 6, 1957
  Newark, NJ December, 1957
  Brooklyn, NY December 8-15, 1957
  Parkersburg, WV December 15, 1957
  Jeffersonville, IN December 28-29, 1957
  Los Angeles, CA 1958
  Prescott, AZ 1958
  Macon, GA 1958
  Charlotte, NC 1958
  Jeffersonville, IN January, 1958
  Chicago, IL January 5-12, 1958
  Waterloo, IA January 26 – February 2, 1958
  South Bend, IN February 7-8, 1958
  Terre Haute, IN February 14, 1958
  Chattanooga, TN February 25 – March 3, 1958
  Jeffersonville, IN March 9, 1958
  Harrisonburg, VA March 16, 1958
  Middletown, OH March 26-30, 1958
  Jeffersonville, IN April 6, 1958
  Burlington, VT April 8, 1958
  Spindale, NC April 27, 1958
  New York, NY May 1, 1958
  Hartford, CT May 3, 1958
  Burlington, CT May 8, 1958
  Pittsfield, MA May 10, 1958
  Everett, ME May 12, 1958
  Bangor, ME May, 1958
  Fairfield, ME May, 1958
  Concord, NH May 23, 1958
  New York, NY May 24-28, 1958
  Shreveport, LA June, 1958
  Dallas, TX June 9-13, 1958
  Greenville, SC June 17-22, 1958
  Southern Pines, NC June 24-25, 1958
  Jeffersonville, IN July 20 – December 28, 1958
  Tifton, GA January 8, 1959
  Jeffersonville, IN January 20-25, 1959
  Owensboro, KY January 29, 1959
  San Juan, Puerto Rico February 9-11, 1959
  Jeffersonville, IN March 1-19, 1959
  Cleveland, TN March 30-31, 1959
  Los Angeles, CA April 4-19, 1959
  San Jose, CA April 22-24, 1959
  Jeffersonville, IN April 26 – May 25, 1959
  Kentucky June, 1959
  Chicago, IL June 9-15, 1959
  Jeffersonville, IN June 25-28, 1959
  Cleveland, TN July 5-8, 1959
  Jeffersonville, IN July 11 – August 3, 1959
  Chatauqua, OH August 8-15, 1959
  Jeffersonville, IN August 23 – September 20, 1959
  Utica, IN October 1, 1959
  Clarkville, IN October 2-5, 1959
  Depauw, IN November, 1959
  Jeffersonville, IN November 8, 1959
  Tifton, GA November 9, 1959
  Jeffersonville, IN November 15, 1959
  San Jose, CA November 20-29, 1959
  Jeffersonville, IN December 16, 1959 – January 6, 1960
  Tifton, GA January 8-10, 1960
  Puerto Rico February 11, 1960
  Jeffersonville, IN February 21, 1960
  Phoenix, AZ February 28 – March 13, 1960
  Tulsa, OK March 28 – April 2, 1960
  Jeffersonville, IN April 17 – June 4, 1960
  Chatauqua, OH June 6-12, 1960
  Middletown, OH June 11, 1960
  Klamath Falls, OR July 8-17, 1960
  Lakeport, CA July 19-24, 1960
  Yakima, WA July 29-August 8, 1960
  Chicago, IL August 30, 1960
  Jeffersonville, IN September 11 – November 13, 1960
  Shreveport, LA November 19-27, 1960
  Jeffersonville, IN December 4, 1960 – January 12, 1961
  Shreveport, LA January 17, 1961
  Beaumont, TX January 18-24, 1961
  Phoenix, AZ January 29-31, 1961
  Tucson, AZ February 5, 1961
  Long Beach, CA February 13-19, 1961
  Tulare, CA February 24, 1961
  Visalia, Ca February 26, 1961
  Jeffersonville, IN March 5, 1961
  Richmond, CA March 8, 1961
  Los Angeles, CA March 12, 1961
  Middletown, OH March 15-19, 1961
  Jeffersonville, IN April 2, 1961
  Bloomington, IL April 9-16, 1961
  Chicago, IL April 23-30, 1961
  Grand Prairie, Canada May 15-17, 1961
  Dawson Creek, Canada May 20-22, 1961
  Jeffersonville, IN June 11 – August 6, 1961
  Tifton, GA August 8, 1961
  Jeffersonville, IN August 13 – December 31, 1961
  Phoenix, AZ January 17 – 21, 1962
  Tempe, AZ January 22, 1962
  Phoenix, AZ January 23-29, 1962
  Jeffersonville, IN February 4 – March 18, 1962
  Tifton, GA March 19, 1962
  Jeffersonville, IN April 1, 1962
  Cleveland, TN April 7-8, 1962
  Jeffersonville, IN April 22 – May 13, 1962
  Green Lake, WI May 18-19, 1962
  Chicago, IL May 20-21, 1962
  Jeffersonville, IN May 27, 1962
  Clarksville, IN May 31, 1962
  Jeffersonville, N June 1-3, 1962
  Southern Pines, NC June 7-10, 1962
  Columbia, SC June 11-12, 1962
  South Gate, CA June 20-24, 1962
  Santa Maria, CA June 27 – July 1, 1962
  Grass Valley, CA July 4-8, 1962
  Spokane, WA July 11-15, 1962
  Salem, OR July 18-22, 1962
  Port Alberni, Canada July 24-26, 1962
  Victoria, Canada July 27-29, 1962
  Jeffersonville, IN September 8 – November 4, 1962
  Elizabethtown, KY November 11, 1962
  Jeffersonville, IN November 11, 1962
  Shreveport, LA November 22-25, 1962
  Jeffersonville, IN December 9-31, 1962
  Sabino Canyon, AZ January, 1963
  Phoenix, AZ January 12-15, 1963
  Mesa, AZ January 16, 1963
  Tempe, AZ January 17, 1963
  Phoenix, AZ January 18-29, 1963
  Tucson, AZ January 21, 1963
  Phoenix, AZ January 22-27, 1963
  Tucson, AZ February 23-27, 1963
  Sunset Mountain, AZ February 28, 1963
  Houston, TX March 4, 1963
  Jeffersonville, IN March 17-24, 1963
  Albuquerque, NM April 12, 1963
  Sierra Vista, AZ April 21, 1963
  Phoenix, AZ April 28, 1963
  Tucson, AZ June 4-8, 1963
  Jeffersonville, IN June 23, 1963
  Hot Springs, AR June 26-28, 1963
  Jeffersonville, IN June 30 – July 28, 1963
  Chicago, IL July 31 – August 4, 1963
  Jeffersonville, IN August 18 – September 1, 1963
  Colorado October 24 1963
  Tucson, AZ October 28 – November 3, 1963
  Jeffersonville, IN November 10, 1963
  New York, NY November 12-17, 1963
  Campbellsville, KY November 18, 1963
  Jeffersonville, IN November 24, 1963
  Tucson, AZ November 27, 1963
  Shreveport, LA November 27 – December 1, 1963
  Phoenix, AZ December 14, 1963
  Tucson, AZ December 16, 1963
  Jeffersonville, IN December 22-29, 1963
  Sierra Vista, AZ January 12, 1964
  Phoenix, AZ January 19-26, 1964
  Bakersfield, CA February 5-9, 1964
  Tulare, CA February 12-16, 1964
  Dallas, TX March 11-15, 1964
  Beaumont, TX March 11-15, 1964
  Denham Springs, LA March 18-22, 1964
  Louisville, MS April 1-5, 1964
  Birmingham, AL April 9-12, 1964
  Tampa, FL April 15-19, 1964
  Tucson, AZ April 27, 1964
  Prescott, AZ May 31, 1964
  Jeffersonville, IN June 14-17, 1964
  Topeka, KS June 18-21, 1964
  Philadelphia, PA June 29, 1964
  Jeffersonville, IN July 5 – August 30, 1964
  Yuma, AZ December 5, 1964
  Phoenix, AZ December 12, 1964
  Tucson, AZ December 21, 1964
  Phoenix, AZ December 27, 1964
  Phoenix, AZ January 17-25, 1965
  Flagstaff, AZ February 6, 1965
  Jeffersonville, IN February 17-21, 1965
  Phoenix, AZ April 10, 1965
  Jeffersonville, IN April 18, 1965
  Los Angeles, CA April 24-29, 1965
  Johannesburg, Africa May 27, 1965
  Jeffersonville, IN July 11 – August 29, 1965
  Phoenix, AZ September 11, 1965
  Tucson, AZ September 19, 1965
  Prescott, AZ October 31, 1965
  Tucson, AZ November 21, 1965
  Shreveport, LA November 25-28, 1965
  Yuma, AZ December 4, 1965
  Rialto, CA December 5, 1965
  San Bernadino, CA December 6, 1965
  Covina, CA December 7, 1965
  Tucson, AZ December 12, 1965
  Amarillo, TX December 18-24, 1965

  Restriction
  [Note: What follows is a description of the documents in this collection which are available for use at BGC Archives in Wheaton, Illinois, USA. The actual documents are not, in most cases, available online, only this description of them. Nor are they available for sale or rent.] Source:
  Source: Billy Graham Center

  *****

 27. Bwana Yesu asifiwe naomba kuuliza Je,kunaanaye mfahamu Nabii William Marrion Branham

 28. Ahsante. Ukisoma Luka 4:1-13, utaona Yesu hali amejaa Roho mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akajaribiwa na ibilisi. Ukisoma ule mstari wa 5 na wa 6 utaona kwamba shetani aliye mkuu wa ulimwengu anamwonyesha Yesu fahari ya milki yake na kumwambia kwamba atampa endapo Yesu atasujudu mbele yake. Tena anaonesha umiliki kwa kusema “Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo.” lakini Yesu kwa kuwa alikuwa anajua kwamba amekuja kwa kazi ya kumnyang’anya hiyo milki akamshinda kwa Neno kwa kumjibu, Imeandikwa, msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Hapo nilikuwa natoa ufafanuzi juu ya shetani kunyang’anywa utawala wa shetani mara baada ya Bwana Yesu kufa na kufufuka na ushindi wetu. Sasa nirudi kwenye swali ni kwamba ukisoma Luka 4:18-19, Inasema, Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta (upako) kuwahubiri maskini habari njema. (zingatia neno hili) “AMENITUMA KUWATANGAZIA, WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO” Na vipofu kupata kuona tena (zingatia hapa tena) “KUWAACHA HURU WALIOTESWA. Sasa ni kwamba wale mapepo baada ya kutoka kuzimu na kuja duniania kama tulivyoona awali waliwaweka watu wengi katika vifungo na mateso, Hivyo ukirejea maneno ya Yesu kwenye ufunuo 1:18 ni kwamba siyo funguo za kuzimu kama ilivyoandikwa, Bali ni funguo za kuwafungu “wafungwa” na kuwaweka huru ” walioteswa”. Yaani funguo za shida na matatizo yetu. Kwa kusema, “NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU. Mungu awabariki.

 29. @ Jeremiah Samwel:

  Je, kuzimu kupo wazi kiasi kwamba mapepo yana uhuru wa kwenda na kutoka huko? Uf. 1:18 inasema Yesu ndiyo ana funguo za Kuzimu; Sasa anazo za nini wakati kumbe kule kupo wazi, kiasi kwamba mipepo inajiendea na kurudi bila tatizo lolote wakati wote, au anasubiri watu wanaoyarudisha Kuzimu kwa kuyakemea, wakisha yamaliza hapa Duniani ndipo afunge Geti?

 30. Amina Bw. Patrick. Kwanza kabisa tujue shetani alitoka wapi? Rejea [Ezekiel 28:13-19, Ufun 12:7:9, Isaya 14:12. Neno “SHETANI” maana yake Adui, Mshindani, Mpinzani, yeye aletaye vizuizi. Baada ya kumfahamu shetani na alikotokea, sasa tujue kuzimu ni wapi? . Kuzimu ni shimo la kiza ambalo liko duniani, ambako ndiko shetani na malaika zake walitupwa kusubiri adhabu kwani alishahukumiwa. Shimo hilo halionekani kwa macho kwani liko rohoni, kutokana na asili ya shetani mwenyewe. Sasa kuzimu ndiyo makazi ya shetani na malaika zake, kuzimu yenyewe ikiwa hapahapa duniani ila katika ulimwengu wa roho. Ukisoma vizuri kitabu cha ufunua kuanzia sura ya 5 na ya 10 (zingatia sura ya 8 na ya 9) kwa msaada wa roho mtakatifu, utaona Ufu 8:1-6 Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo , akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi. Na wale malaika saba wenye baragumu wakajifanya tayari ili wazipige. Sasa ishara ya zile baragumu ni vipindi na nyakati tofautitofauti zilizotokea duniani. Ambapo utaona sasakuanzia mstari wa 7 na kuendelea kila malaika alipopuliza baragumu kuna tukio lilitokea duniani. Sasa baadhi yalishatokea zamani hata kabla ya Yesu kuja na sasa tupo katika tukio lingine, kwani pindi malaika anapoipiga ile baragumu tukio fulani linatokea duniani. Sasa ukisoma ile sura ya 9 utaona mstari wa 1 Malaika wa tano akaipiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Sasa ukiendelea kusoma hadi mstari wa 12, utaona sasa kuzimu inafunguliwa na viumbe wanatoka kuingia duniani, ndio pepo wachafu, au roho chafu, wakaruhusiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala mti wowote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. Wakapewa amri kwamba wasiwauwe bali wateswe miezi mitano. Sasa nifupishe kwa kusema ni kweli baada ya mwanadamu kuasi alipoteza umiliki na utawala wa dunia na shetani akamiliki. Lakini Yesu aliturudishia tena utawala huo na ndiyo maana akasema, “Nimepewa mamlaka yote mbingunh na duniani math 28: 18 nasisi tumezichukua chapa za Yesu. Galatia 6:17 na Yesu ni mfalme wa wafalme, nasi ndiyo wafalme na Yesu ni mfalme mkuu. Hivyo tuna amri na mamlaka juu ya pepo na kuwatiisha warudi kuzimu kwani ndiko kwenye utawala wao na siyo katika mazingira ya utawala ya mwanadamu. Mungu awabariki.

 31. Amen Ndugu Mwanyongo, uzidi kubarikiwa na Bwana Yesu!

  Ndugu Leva, ubarikiwe kwa kutukumbusha baadhi ahadi tulizonazo katika Kristo. Hizo ahadi zote ni kweli kabisa na tunapaswa kuzipokea, kuziamini na hata kuziidai katika maisha yetu.

  Pamoja na ukweli huo, hatuwezi kuziitia ama kuzidai ahadi hizo kwa masuala yaliyo kinyume na Neno la Mungu na mojawapo ni hilo la kuyapeleka mapepo kuzimu.

  Utakubaliana nami ya kuwa shetani tokea mwanzo anazungukazunguka duniani, alikuja bustanini Edeni akawarubuni Adamu na Eva – Mwanzo 3:1

  Kwenye kitabu cha Ayubu shetani alijihudhurisha mbele za Mungu pamoja na wana wa Mungu na alipoulizwa na Mungu ametokea wapi alijibu “kuzunguka huko na huko duniani” -Ayubu 1:7

  Tukumbuke kuwa Bwana Yesu alimwita shetani “mkuu wa ulimwengu huu”- Yohana 14:30

  Isitoshe Bwana Yesu alisema alimwona shetani akianguka toka mbinguni duniani kama umeme/ radi – Luka 10:18 (Radi/Umeme huipiga nchi siyo kuzimu)

  Yohana naye kaitka Ufunuo alionyeshwa vile vita mbinguni shetani alipoasi na matokeo yake:

  9 Basi joka hilo kuu likatupwa nje, yule nyoka wa kale aitwaye Ibilisi na Shetani, adanganyaye watu wote ulimwenguni. Alitupwa chini ardhini, yeye pamoja na malaika wake. – Ufunuo 12:9 SNT

  Hapo tunaona alitupwa duniani yeye pamoja na malaika zake. Halafu tukiendelea kusoma mistari inayofuata tunakutana na maneno yafuatayo:

  12 Kwa hiyo furahini ninyi mbingu, na wote wakaao mbinguni! Bali ole wenu nchi na bahari maana shetani amekuja kwenu akiwa amejaa ghadhabu, kwa maana anajua kuwa muda wake ni mfupi!” – Ufunuo 12:12 SNT

  Hivyo basi tunaona wazi kuwa shetani wala mapepo hawakutupwa kuzimu bali duniani. Labda niongezee kuwa kuna wale malaika walio asi na wamefungwa kwenye giza hadi siku yao ya kuhukumiwa hao hawawezi kutoka huko kifungoni kuja duniani kamwe – Yuda 1:6

  Kifupi hatuna msingi wa KImaandiko kutuelekeza kuyatuma mapepo kuzimu, Bwana Yesu hakufanya wala kufundisha hivyo, Mitume na wanafunzi wa mwanzo hawakufanya hivyo. Kwa hiyo basi sisi leo tukijaribu kuzilazimishia ahadi za Mungu ili kufanya hivyo ni kutokuligawanya Neno la Mungu kwa usahihi

  Tuendelee kujifunza Neno la Mungu pamoja.

 32. Ndio unaweza kuyapeka kuzimu kwa jina la yesu. Ukiomba neno lolote kwa jina la yesu nitalifanya, alafu amini amini nawaambia yeye aniaminie mimi kazi nizifanyazo atafanya NAAM NA KUBWA ZAIDI ATAFANYA kwa sababu mimi naenda kwa baba maana yake endelea wewe kutumia uweza wa jina la yesu. Kuna msitari kwe zaburi umeandikwa mbingu ni mbingu za bwana lakini nchi amewapa wanadamu. Sasa nchi hawajapewa mapepo lazima yakae kuzimu tu katika jina la yesu.

 33. shetani alitupwa wapi? na makao yake ni wapi? biblia inatuambia. je mamlaka tuliyo pewa yakoje je nikuyafunga mapepo na kuyaamulu yaende kuzimu je Yesu aliyamulu mapepo yaende kuzimu? shetani anazunguka wapi kuwatafuta watu wa Mungu? tafakari vyema mamlaka tuliyo pewa

 34. Wapendwa, kwa habari ya kutoa pepo tunayo mifano mingi kwenye Neno la Mungu, ni vizuri tukaizingatia hiyo badala ya kuongezea mafunuo yetu na mbwembwe za ziada kama hizo za kuamuru mapepo yaende kuzimu, kuyateketeza kwa moto, kuyasaga tikitiki n.k.

  Hakuna sehemu yoyote kwenye Neno la Mungu ambapo tunaona mapepo yanatolewa na kuamriwa yaende kuzimu. Bwana Yesu alisema hivi, mapepo yanapokemewa na kutolewa yanakwenda yakizunguka zunguka kwenye sehemu kavu yakitafuta mahali pa kuingia, halafu yanarudi kuangalia kama pale yalipotolewa kuna nafasi ili yaweze kuingia na kukaribisha na mengine pia. Habari kamili inapatikana hapa: Luka 11:14-26

  Swali, sasa kama Bwana Yesu mwenyewe alisema hivyo, kwanini hakuongezea kuwa tunapaswa kuyaamuru yaende kuzimu? Au kwanini yeye mwenyewe hakuwahi kufanya hivyo walau hata mara moja?

  Mfamo mwingine, Mtume Paulo alipokemea pepo wa uaguzi toka kwa yule binti hakuliamuru liende kuzimu, aliliamuru limtoke na ikawa hivyo. Habari kamili Matendo 16:16-18

  Tunachopaswa kufanya ni kutoa pepo kwa jina la Yesu na kuwafundisha watu mamlaka waliyonayo kupitia kwa Bwana Yesu juu ya nguvu zote za giza na hivyo hatuna sababu ya kuhofu chochote. Luka 10:19 inasema:

  19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

  Mbarikiwe

  Patrick

 35. Biblia inatuambia ibilisi baba wa uongo alishahukumiwa na alipohukumiwa aliomba adhabu yake iwe wakati wa kiama, ndipo akatupwa katika makao yake ambayo ni kwenye shimo linaitwa kuzimu. Hivyo ibilisi na mapepo makao yao ni kuzimu na mwanadamu anayemwamini Yesu kristo amepe wa amri na mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kila nguvu za shetani na hakuna cha kumdhuru na pia amepewa mamlaka ya kufunga na kufungua, hivyo mwenye mamlaka ya kuyarudisha mapepo kuzimu ni mtu yeyote anayemwamini Bwana Yesu kristo na kazi zake. Kwa kuwa kuzimu ndiyo makazi ya mapepo hivyo kuyatiisha yarudi huko na yasirudi tena duniani, kwa kuwa tunazo chapa zake Yesu. Amina

 36. sidhani kama tuna mamlaka ya kuwapeleka mapepo kuzimu. Ila tuna mamlaka ya kuwatoa/kuwafukuza tu kuwatoka watu. Sidhani kama wanaofukuza mapepo yaende kuzimu wana ushahidi wa kimaandiko.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s