Rasimu ya Katiba, Mchungaji Mtikila kufungua kesi

Mtikila

Akinukuliwa na vyombo mbali mbali vya habari, Mchungaji Christopher Mtikila ambaye pia ni kingozi wa chama cha upinzani Democratic Party amesema kwenda mahakama ya kimataifa kufungua kesi kuhusu rasimu ya katiba kutoitambua Tanganyika. Mpendwa, Je umeipitia Rasimu ya Katiba mpya, Je una maoni gani? Ikiwa bado hujaisoma tafadhali isome

Toleo la Rasimu ya Katiba limechapishwa kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa kifungu cha 18(5) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, kwa madhumuni ya kuwepo kwa wananchi kusoma na kutoa maoni zaidi kwa Tume kuhusu maudhui yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.

Dar es Salaam, JOSEPH S. WARIOBA,
3 Juni, 2013 Mwenyekiti wa Tume

 gonga hapa

10 thoughts on “Rasimu ya Katiba, Mchungaji Mtikila kufungua kesi

  1. Asante ndugu Milinga na hasa kwenye suala la majina ya rais wa tanganyika na znz uko sahihi kama yakibadilika na kuwaita labda magavana…hii itapunguza ku-undermine hadhi ya huyo rais wa muungano na pia kuwafanya hao marais wa tz na znz kutokujiona ni zaidi kimamlaka…mfano rais wa tanganyika kutokana na ukubwa wa nchi yake ni lazima atajiona ni rais mwenye mamlaka makubwa sana ndani ya huo muungano hata kushinda rais wa huo muungano!.na mara nyingi huu ndio mtazamo wa viongozi wa kisiasa wa nchi maskini..!!

    ….pia umegusia suala la mgawanyo wa vyeo kwa kuzingatia utaifa…sasa sijui unalionaje hili suala katika hiyo serikali ya muungano?je hao mawaziri wa muungano watachaguliwa kwa kuangalia uwiano au kuangalia weledi wa mtu??maana hata huyo rais wa Muungano naona itakuwa ni vuta ni kuvute kila upande ukitaka atoke huku..hii itakwenda hadi kwa wafanyakazi wa wizara husika ya Muungano ndio kila upande utadai mfano wizara ya ulinzi kama ina wafanyakazi mia nne then mia mbili wawe wa-tanganyika na mia mbili wawe wa-znz bila hata kujali competence yao katika kazi..!..na hizi ndizo fikra za kimaskini ambazo zimetufanya tuwe tegemezi kwa miaka mingi!

    Mfumo unaoutaka wa serikal tatu ni mzuri lakini sio applicable kwa tz ya sasa wala ya miaka hata 20 toka sasa..bado tupo na uelewa mdogo sana na tunaangalia vitu kama u-znz na u-tanganyika, udini, ukabila, ukanda,etc katika mambo mengi sana ambayo yanapaswa kutumia utaalam…mpaka tutakapoondoka katika hii thinking level ndio tufikirie kuwa na mgawanyo huo…si umeona mwenyewe watu wanatoana roho kwa suala dogo tu la nani anaruhusa ya kuchinja nyama..hv kwel uhai wa mtu una thamani ya chini hadi kufikia kuuana kwa ajili ya ubishi wa nani anafaa kuchinja nyama??…kuua albino ili kuwa tajiri?..nikasikia pia kuna bibi sijui ametishia kugeuza mafuta ya huko mtwara kuwa maji na serikal ikamwogopa…!! huu ndio uelewa wa wengi so kuleta jambo lenye kuhitaji uelewa mpana na focus kwa hali ilivyo sasa ni kuleta vurugu tunayoweza kushindwa kuidhibiti..!.

    Binafsi kwa maelezo yako siogopi mfumo wa serikal tatu ila hofu yangu kubwa ni kwa watu ambao unataka huo mfumo utumike kwao. Nchi inahitaj overhaul kubwa sana ya mindset kabla ya kuleta huu mfumo maana kwa uelewa uliopo ni ngumu sana. Ni vile tu baba wa Taifa alikosea kidogo angeweza kufanya serikal moja toka mwanzoni ingekuwa solution nzuri na rahisi. Vipi hoja kuhusu kila nchi kujitenga kama serikali moja haiwezekani huoni kuwa ina manufaa sana kiuchumi???

    conrad

  2. Mpendwa Conrad,

    Nimefurahishwa na comments zako kuhusu mada hii.

    Pamoja na hayo nadhani umehitimisha kwa kauli kwamba ungependelea tuwe na Serikali mbili kwa sababu za kisiasa. Hii inaonesha kwamba kama mapendekezo ya Tume ya Katiba ya Serikali tatu yatapita na wewe ukaombwa ukaipigie kura Rasmu hiyo utapiga kura ya HAPANA.

    Lakinni nikushauri tu kwamba nchi mbili au zaidi zinapoungana bila kujali ukubwa wa kijiografia wa nchi hizo lazima nchi hizo asilia zitabakia kuwepo na kitakachofanyika ni kuzaliwa taasisi imara kikatiba na kisheria zitakazosimamia muungano huo.

    Muungano wa nchi zozote unaweza kufananishwa na MUME na MKE wanaoungana kwenye NDOA.

    Kabla ya kuungana kwenye ndoa, kila mmoja wao anakuwa huru kabisa na anaweza kutumia majina yake halisi kwa shughuli zake za kila siku. Lakini akishafunga NDOA, lazima anabadilisha baadhi (siyo yote) ya taratibu na sheria alizokuwa nazo kabla ya ndoa.

    Mara nyingi au Wakati mwingine mwanamke na mwanaume hulazimika kubadilisha hata majina yao na kuitwa kwa mfano MR & MRS MILINGA. Kwa hiyo inapotokea mimi nashughulikia mambo yangu binafsi nitatumia jina langu binafsi lakini inapotokea kushughulikia maswala ya NDOA yetu lazima nitatumia MR & MRS MILINGA.

    Kwa mataifa kama Tanganyika na Zanzibar yaliyoungana lazima yote kwa pamoja yakubali kupoteza asili zao mbele ya macho ya dunia. Kwa hiyo ili kupoteza asili yao mbele ya dunia lazima kuwepo taasisi ikiwemo Rais wa Muungano anayetambulika kimataifa.

    Hawa marais wa Zanziba na Tanganyika kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba Mpya hawatatambulika kama marais mbele ya dunia. Yaani hawatakuwa na uwakilishi wa kimataifa katika umoja wa mataifa (UN). Huu utabaki ni utaratibu wa ndani ya nchi tu (internal arrangement) ambapo wao kama marais wa maeneo yao watashughulikia maswala ya maeneo yao.

    Conrad, kwa mfano Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa sasa anaitwa HUSSEIN ALLI HASSAN MWINYI. Wizara hii inaongozwa na Mzanzibar. Kwa muungano unaofuata Katiba huu ni unyanyasaji kwa watu wa Tanganyika kwani hakuna mtu wa Tanganyika anayeruhusiwa kwenda kuwa waziri upande wa Zanzibar.

    Makosa kama haya ya kuruhusu Wazanziba wapatiwe viti vya uwaziri katika mambo yasiyohusu Muungano litaisha tu kama tuna Serikali TATU. Mbona watu wa bara hawaruhusiwi kugombea uongozi wowote upande wa Zanzibar?

    Kuna hoja nyingine umesema kwamba USA ina mazingira tofauti na TZ. Ni kweli lakini kumbuka nilikuwa nakupa mifano tu duniani kama ulivyoniomba nikupe mifano ya nchi zenye marais zaidi ya wawili.

    Nimetumia mifano ya USA kwa sababu watu wengi husahau kwamba lile ni taifa lenye marais wengi waitwao magavana (Governors) ambao wanatawala nchi zao za asili (states) katika maeneo yao. Ikumbukwe kwamba hawa marais wa majimbo ya marekani hawawezi kuvuma nje ya mipaka ya marekani kwa sababu wao kikatiba hawaiwakilishi USA kama marais mbele ya dunia. Kwa mfumo wa USA Rais mmoja mtendaji ndiye anayekuwa Amiri Jeshi Mkuu, Ndiye anayetia saini mikataba yote ya kimataifa, ndiye sura halisi ya taifa au DOLA ya USA.

    Hata Tanzania tukitaka marais wa Zanziba na Tanganyika tunaweza tukawaita WAKUU WA MAJIMBO badala ya Rais ILI KUONDOA UKAKASI masikioni mwa wasikiao na kuanza kuchanganyikiwa kwa kutoelewa Rais ni yupi sasa. Au mkubwa ni yupi (Protocal problems). Badala ya kumuita Rais wa Bara au Tanzania Bara, tumwite GAVANA WA TANGANYIKA. Na yule wa Zanziba tumwite GAVANA WA ZANZIBA. Au tunaweza tukawaita Waziri Mkuu wa Zanziba na Waziri Mkuu wa Tanganyika. Hawa wakawa Mawaziri Wakuu watendaji wa Serikali katika maeneo ya nchi zao tu.

    Mimi nadhani watu wengi wanachanganywa na cheo hiki cha RAIS. Kwamba kwa nini nchi iwe na MARAISI WATATU?

    Lakini kama tukiwa na RAIS mmoja anayesimamia DOLA KUU ya Muungano na wale wa nchi washirika wakaitwa kwa vyeo vingine kama nilivyosema hapo juu, basi nadhani watu wengi hawatapata ukakasi wa mlolongo wa marais watatu.

    Hata hivyo ikumbukwe kwamba mfumo wa Serikali Mbili siyo mfumo mzuri duniani kwa nchi mbili zilizoungana. Kwa mfano jaribu kuwaza kama KENYA, UGANDA, TANZANIA, RWANDA na BURUNDI zikiungana, je tutakuwa na serikali ngapi? Hapa lazima tutakuwa na Rais Mmoja wa Muungano (Sovereign State President) na pia kila nchi itabakia kuwa na Rais wa nchi yake anayeshughulikia maswala ya nchi yake ya Kenya, Uganda, nk.

    UBARIKIWE.

  3. Mr. Milinga 17/06/2013 at 6:31 PM nimekuelewa na ninashukuru….ila mifano uliyotoa ya nchi kama usa haiendani na hali halisi ya wa-tz.!

    huko u.s.a ulipozungumizia kuwa kuna marais wengi ni kuwa hilo taifa lina strong institutions na si watu binafsi..ndio maana majina ya hao maraisi wa majimbo huyasikii yakivuma maana kazi nyingi za gov zinafanywa na institutions!.tz kila kitu ni rais hakuna na hatujajenga mfumo wa institutions kufanya kazi..rais ndio anategemea awaambie watu wachimbe vyoo (wanavyotumia wenyewe),wapeleke watoto wao shule,wachimbe mitaro ya makazi yao,etc etc. Ndio maana hata wewe Mr. Milinga leo hii unaweza kuwa rais wa marekani na isiyumbe maana institutions ndio zinafanya asilimia kubwa ya kazi za urais.

    Nchi yetu tz uelewa wa watu bado ni wa chini…kuleta serikal yenye marais watatu ni vurugu kubwa sana kuanzia matumizi, msururu wa magari ya viongozi wenye utiriri wa motorcades, etc…hao ma-governor wa states ni watu wa kawaida sana tunapishana nao madukani na hawana misafara ya magari..sasa hv tz rais ni mmoja lakini folen ya kumsubiri apite inasimamisha shughul za watu zaidi ya masaa matatu..je itakuwaje tutakapokuwa na marais hao wote&mawaziri wakuu??..

    Tutengeneze mfumo wa kutegemea institutions kuendesha nchi, wananchi wenzetu wapate kuwa na uelewa wa kutenganisha mambo ya siasa na kufanya kazi then ndio tunaweza kufikiri kuwa na utiriri wa viongozi. Angalia sasa hv ni kama hakuna kazi zinazofocus future ya nchi maana kila mtu amekuwa anafanya siasa na kufikiri ni nani atakuja kuwa rais..ma-prof vyuoni, wakurugenz, madaktar, etc etc wote wameweka focus kwenye siasa tofauti na nchi ulizotolea mfano ambapo watu walioko kwenye institutions wanafocus mambo ya nchi na si siasa!

    mfumo wa serikal moja ungefaa sana ila kwasababu za kisiasa basi serikal mbili

  4. Mpendwa Conrad,

    Asante kwa changamoto yako kwangu uliyohoji kwamba nikueleze sababu nzito za kiuchumi ambazo zitapatikana kwa kuwa na marais watatu.

    Ukweli ni kwamba Mfumo wa marais 3 unapaswa kuusoma (study) vizuri. Tukiwa na marais watatu maana yake ni kwamba marais wawili yaani yule wa Zanzibar na yule wa Bara hawatatambulika kimataifa kama marais katika ngazi za kimataifa. Rais mmoja tu ndiye atakayetambulika kimataifa, kijeshi, sarafu na katika mikataba yote ya kimataifa. Marais wa nchi washirika hawatakuwa na nguvu yoyote kimataifa.

    Kusema ukweli mimi ningependekeza tena kwamba Rais wa Tanzania Bara awe na makao makuu yake mjini DODOMA yaani IKULU ya Tanzania Bara iwe na makao yake makuu Dodoma. Mawaziri wote wa Tanzania Bara Wizara zao zote ziwe Dodoma na Ile ya Muungano ndiyo iendelee kuwa na IKULU yake Dar wakati ile ya Zanzibar ikiendelea kuwa na makao yake Makuu Unguja.

    Upande wa hoja yako uliyotaka nikueleze sababu nzito za kiuchumi zitakazopatikana kwa kuwa na marais 3 ni kama ifuatavyo:

    1. Mawaziri wa Bara watajishughulisha na Maendeleo ya Bara tu badala ya kama ilivyo kwa sasa Waziri mmoja anaweza kupewa wizara wakati yeye ni Mzanzibar na hawi na uchungu na watu wa Bara.

    2. Kwa mujibu wa Rasmu ya Katiba Mpya Rais wa Tanzania Bara au wa Zanzibar atakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yahusuyo eneo lake kiuchumi, atakuwa na uwezo wa kutafuta vyanzo vya mapato vya serikali yake kutoka nje na ndani ya nchi yake.

    3. Serikali itakuwa na Mawaziri wachache tofauti na ilivyo sasa wapo zaidi ya 300, lakini kwa rasmu ya Katiba Mpya naamini wabunge hawatazidi 120 kwa upande wa bara na Zanzibar hawatazidi wabunge 60. Hii yote itapunguza matumizi ya Serikali na kuongeza uchumi kukua.

    4. Kwa mujibu wa Rasmu ya katiba Mpya ya 2013, Marais wote 3 watakuwa wanalazimika kukaa pamoja kama baraza la Usalama la Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano hatajiamulia maswala yoyote kitaifa au kimataifa bila kuwashirikisha marais wa nchi washirika, ikiwemo mikataba ya kimataifa. Kwa hiyo Rais wa jamhuri ya Muungano hataweza kutia saini mikataba ya hovyo isiyokuwa na tija upande mmoja wa Muungano. Hii itaondoa utamaduni wa kutia saini mikataba ya kinyonyaji inayonyonya rasilimali za Taifa na kuleta umaskini nchini. Hili litawezekana tu kama tuna marais 3 ambao wanashirikishwa kwanza kuhusu maamuzi yoyte yanayoathiri wananchi wa pande zote.

    KUHUSU HOJA YA MIFANO YA MATAIFA YENYE MARAIS 3 DUNIANI.

    Ukweli ni kwamba kuna mifumo mingi ya muungano wa nchi huru duniani kama ilivyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zilizoungana mwaka 1964. Hizi zilikuwa nchi huru kabisa baada ya kupata uhuru wao.

    Utakumbuka muungano wa nchi za kisoviet ya Urusi iliyosambaratika miaka ya 90. Muungano ule ulikuwa wa kila nchi kuwa na Rais wake lakini chini ya Rais Mtendaji mmoja wa Umoja huo.

    Unafahamu pia Muungano wa nchi za Ulaya. Huu ni muungano ambao nchi zote za Ulaya zimeungana pamoja na zina Bendera yao ya Muungano yenye nyota 12 lakini kumbuka kila nchi inaendelea kuwa na Rais wake hadi sasa. Lakini wanakoelekea ni kuwa na Rais mmoja wa Ulaya kama ilivyo kwa USA.

    Unafahamu pia Muungano wa mataifa 50 ya Amerika au United States of Amerika yaani USA. Muungano huu unajumuisha nchi takribani 50 zilizoungana na kuamua kuwa na Rais mmoja Mtendaji wa muungano huo yaani Federal Republic President ambapo kuna taasisi imara sana zinazomsaidia kutawala taifa hilo kama vile CIA, FBI, Bunge la Congres, Ikulu ya Washington, Jeshi kubwa la kitaifa, nk. Ukweli ni kwamba muungano huu wa USA una marais wapatao 50 hivi wanaotawala States au Majimbo yao na Rais Mtendaji wa Muungano haruhusiwi kuingilia maamuzi yao labda kwa kukata rufani tu kwa mujibu wa Sheria. Muungano wa Marekani ni Muungano wa pekee duniani tena unatolewa mifano ya kila mara ila ni kwa sababu ni muungano ambao umekaa miaka mingi tangu ulipoasisiwa kwa karne nyingi zilizopita. Hata hivyo, Kila Jimbo au State ina Serikali yake, Rais wake, bunge lake, Sheria zake, na taratibu zake.

    Mpendwa, Conrad utakubaliana na mimi kwamba USA ni taifa lenye nguvu duniani kiuchumi, kijeshi, kifedha, kisiasa, nk. Hii si kwa sababu tu ni nchi yenye muungano wenye mfumo wa shirikisho ya nchi nyingi ambazo zinajiendesha kifedha na kisiasa tu bali pia ni nchi yenye kuwa na Serikali Kuu moja ambayo hutambulika kimataifa.

    Tanzania ikiwa na nchi mbili zilizoungana, Rais wa Bara ataendelea kuwa na majukumu ya kushughulikia maendeleo ya Bara kwa muda wake mwingi, kuliko ilivyo sasa hivi ambapo Rais wetu anakuwa bize muda mwingi na maswala ya kimataifa, ziara nyingi za nje na kujikuta hana muda wa kushughulikia maendeleo ya watu wake. Mwangalie Rais Kikwete kwa mfano, kuna maswala mengi humshinda kushughulikia haraka kwa sababu tu yeye anakuwa hayupo labda yuko nje ya nchi na anashindwa kutekeleza haraka kwakuwa yuko nje ya nchi mfano ni lile swala la kulipuka mabomu Arusha kanisa la RC na lile bomu lililolipukia mkutano wa CHADEMA tarehe 15/06/2013. Kikwete alishindwa kufika mara moja kutatua na kuwashughulikia wahusika.

    Marais wa Majimbo Amerika wako bize na maendeleo ya Majimbo yao ( busy with their States development) lakini marais wa Afrika utaona kwamba wako bize na ziara za nje tu wakila posho za safari na kujitafutia au kujikusanyia utajiri mkubwa badala ya utajiri wa watu wao.

    Lakini katika mfumo wa Serikali yenye marais watatu, lazima wale wawili wa nchi washirika watakuwa bize na maendeleo ya watu wao.

    Ni matumaini yangu kwamba, hapo tumeelewana mpendwa. Kama una maswali au maoni zaidi karibu tena.

  5. Mr. Milinga 15/06/2013 at 1:25 PM hebu nitajie sababu nzito za kiuchumi zinazokufanya uamini kuwa maraisi watatu ndio watasaidia kuleta maendeleo ya tz maana maraisi wawili kwa mtazamo wako wameshindwa kuleta…labda nchi mmoja ikiwa na maraisi watatu akili ya nchi kukua kiuchumi ndio itaongezeka zaidi kuliko marais wawili walipo now….na labda uje na mfano dhahiri unaoonesha ni wapi duniani nchi moja iliyo na marais watatu imesaidika kukua kiuchumi…

    ..nakubali hoja ya kuwa na rais mmoja ukizingatia idadi ya watu wa znz ni nusu kama si robo ya idadi ya wakazi wa wilaya kama ilala dsm…so znz yote inaweza kuwa mkoa mdogo wa tz na serikali ikawa moja…!

    lakini kama serikali moja ikishindikana kwann hoja ya kuvunja muungano inaogopwa kujadiliwa?kwan tz bara kuna nini cha zaidi inachopata kiuchumi kutoka znz hadi iogope kusimama yenyewe?mafuta ambayo hayajulikana vizuri ama??je dunian kote nchi zilizoendelea zilitumia mafuta tu?how about bahari, madini, gesi, mbuga za wanyama, mito, maziwa, ardhi tele iliyopo tz bara vyote havitoshi kusimama kwa nchi?..labda ikibaki tz bara peke yake na muungano ukaja kwenye muungano wa nchi zote za afrika mashari itakuwa bora zaidi

    conrad

  6. Mimi Rasmu ya Katiba Mpya nimeisoma sura kwa sura na aya kwa aya na mstari kwa mstari. Baada ya kuisoma siku moja tu baada ya kuzinduliwa hadi sasa nimeshaimaliza yote.

    Kusema ukweli kama siyo mtu mwenye nia mbaya na nchi hii, Rasimu hiyo ina mambo mengi mazuri na ya kupendeza endapo tu itapitishwa ingawa Chama Cha Mapinduzi kina mashaka na kimeomba wanachama wake waisome na kusisitiza msimamo wa Serikali Mbili nadhani wana CCM tunapaswa kuwaza kwa undani sana kabla ya kukataa mapendekezo ya Serikali mbili.

    Kusema ukweli serikali mbili zitaendeleza mzozo kutoka pande zote mbili. Kama tunapenda muungano wa Zanziba na Tanganyika uendelee basi tujadiliane jinsi ya kuwa na Serikali Moja yenye nguvu.

    Kama serikali moja nayo tunaona haina nafasi, ujanja na busara kwa maoni yangu ni kuwa na Serikali TATU.

  7. Kwa mtu anayepinga serikali 3 ni mtu asiyejtambua wala kuelewa anachozungmza,sisi tunahitaji serikali na lazima hadhi ya Tanganyika irudi

  8. Tatizo la Watanzania wengi wanaongea hata kabla ya kufanya uchunguzi au utafiti wa hoja zao.

    Tuna watanzania wanaopenda kuonekana wanaongea tu. Sasa kama huyu askofu Luzoka ambaye dada Anna anatolea nukuu yake analalamikaaaa weee mpaka lini. Unapotoa tahadhari mbona hutoi mapendekezo ya kuepuka tahadhari hiyo. Wewe unapendekeza serikali ngapi? Au na wewe unaingia kwenye kundi la watu wasiotaka mabadiliko hata kama yangekuwa ya heri?

    Ukija kwenye hoja ya serikali tatu, wote wanaopinga mfumo wa serikali tatu hawana jipya kabisa. Wameshindwa kupendekeza serikali ya mfumo gani ya muungano ambayo wanaona itaendelea kuwepo miaka 100 ijayo bila ya malalamiko ya upande wowote.

    Ngoja nikupe matatizo yaliyopo leo kwa serikali mbili tulizonazo yaani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    A. Malalamiko ya upande wa Tanganyika ni haya yafuatayo, Watu wa bara wanalalamika kwamba:

    1. Wazanzibar wanabebwa sana na Serikali ya Muungano kwa kila jambo.
    2. Wazanzibar wana Rais wao, sisi bara hatuna Rais wetu.
    3. Wazanzibari wana bendera yao sisi Tanganyika hatuna Bendera yetu
    4. Watanganyika hatuna vitambulisho rasmi vya uraia wao Zanziba wanavyo vya kumtambulisha Mzanzibari mkaazi.
    5. Wazanzibari wanapewa uwaziri katika serikali ya Muungano lakini mtu wa Bara hawezi kupewa hata uenyekiti wa mtaa kule zanziba
    6. Wazanzibari wanaruhusiwa kuishi bara mahali popote na hata kugombea nafasi yoyote kisiasa, lakini watanganyika hawawezi kugombea nafasi yoyote Zanziba.

    B: Malalamiko ya Wazanzibari ni haya yafuatayo. Wanalalamika kwamba:

    1. Serikali ya Muungano inawabana sana kiasi kwamba wanajiona kama vile bado wako chini ya ukoloni wa Tanganyika. Hawako huru.
    2. Hawana dola yao kamili na hivyo wanataka dola yao huru.
    3. Wanapoleta bidhaa upande wa bara wanatozwa ushuru na kodi wakati wameshalipia vyote hivyo wakiwa Zanziba
    4. Wamekataliwa na Serikali ya Muungano kujiunga na OIC (Organisation of Islamic Countries) kwamba wao walikuwa na nia njema ya kupata missaada toka jumuia hiyo ya kiislam duniani.
    5. Wazanzibar wananyimwa nafasi sawa katika maswala ya Muungano kama vile uwakilishi kwenye balozi zetu za nje, na kwenye ajira pia.
    6. Mgawanyo wa rasilimali za nchi haupo kwa usawa kwamba wao wanapata mgawo mdogo sana hasa kwenye misaada toka nje ya nchi, na rasilimali zote za humu nchini.
    7. Watanganyika ndio wanaojipendelea kwenye ngazi ya urais kiasi kwamba wazanzibar wameachwa bila kutoa Rais wa Muungano kwa muda mrefu wanaoongoza ni wa tanganyika tu. (Zanziba imewahi kutoa Rais wa muungano mara moja tu tangu muungano uasisiwe mwaka 1964).

    Kwa hiyo katika Muungano wenye malalamiko toka pande zote za nchi washirika kama hakuna katiba inayowaunganisha, mtaendelea kuwa na malalamiko yasiyoisha milele au muungano utavunjika siku moja.

    Kwa hiyo kuna njia mbili tu za kutatua mzozo kama huu wa nchi mbili huru zilizoungana Kama Tanganyika na Zanzibar:

    PENDEKEZO LA KWANZA KUWA NA MFUMO WA SERIKALI MOJA TU.
    Katika pendekezo kama hili la serikali moja ili kuepuka ugomvi na kusambaratika lazima pia kuwepo mgawanyo sawa wa madaraka kwamba kama awamu hii Rais ametoka upande mmoja basi awamu ijayo atoke upande mwingine wa muungano. Na hapo iwe hivyo kwenye kila swala la utawala kwa maana ya wizara zote na Idara na balozi za nje.

    Nilitegemea kwamba watoa maoni wengi wangependekeza tuwe na mfumo wa serikali moja yenye nguvu, Rais mmoja mwenye nguvu bara na visiwani, mawaziri wenye nguvu pande zote za bara na visiwani, taasisi zenye nguvu pande zote za muungano, nk. Tuwe na bendera moja, balozi mmoja wa nje, wimbo mmmoja wa taifa, nk nk. Lakini watu wanaogopa kutoa maoni hayo wanakimbilia tu tuendelee na serikali mbili. WHY? Kama kweli watu wanasema gharama ya kuendesha serikali TATU ni kubwa basi wapendekeze serikali moja tu maana ndiyo haitakuwa na gharama za utawala kama hii iliyopo ya serikali MBILI.

    PENDEKEZO LA PILI NI SERIKALI MBILI.
    Katika pendekezo kama hili, ambalo ndilo lililopo hadi sasa ni kwamba udhaifu wake ni mkubwa zaidi kwa sababu lazima kuna upande mmoja utashindwa kupata haki sawa mbele ya mwingine kama nilivyoeleza awali.

    Kwa hiyo kuendelea na mfumo huu wa serikali mbili itaendeleza malalamiko ambayo hayataisha milele.

    PENDEKEZO LA TATU NI SERIKALI TATU:

    Kwenye pendekezo kama hili la serikali TATU, hata mimi naliunga mkono ikiwa swala la serikali moja litashindikana labda kwa wananchi wa upande mmoja. Serikali tatu itakuwa ndiyo suluhisho la kudumu la matatizo niliyoyataja hapo awali yanayolalamikiwa na watu wa pande zote.

    Kwa mfano, Waziri wa Kilimo wa Tanzania au Waziri wa Maji wa Tanzania kwa sasa hana mamlaka yoyote Zanzibar kwa sasa. Mawaziri hawa watabaki wanashughulikia maswala ya upande wa bara tu. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Tanzania Dr Shukuru Kawambwa hana la kufanya Zanziba mpaka aombe kibali kwa Waziri wa Elimu na Amali Zanziba. Kwa kuweka Serikali Tatu ndiyo kusema mawaziri wote wasiohusika na maswala ya Muungano watabaki upande wa serikali ya Bara chini ya Rais wao kama ilivyo Zanziba kila jambo linafanywa chini ya usimamizi wa Rais wa Zanziba.

    Mawaziri wa Muungano watabakia kuwa wafuatao na hawa ndio watashughulikia mambo yote ya Muungano:

    1. Waziri wa Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
    2. Waziri wa Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
    3. Waziri wa Mambo ya Ndani (Uraia na Uhamiaji);
    4. Waziri wa Fedha (Sarafu na Benki Kuu);
    5. Waziri wa Mambo ya Nje;
    6. Waziri wa Usajili wa Vyama vya Siasa; na
    7. Waziri wa Ushirikiano bara na Visiwani atakayeshughulika na Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na
    mambo ya Muungano.

    Kwa hiyo utaona kwamba tutakuwa na serikali ya Muungano yenye mawaziri kamili wasiozidi Saba pamoja na Manaibu wao kwa pamoja hawatazidi 15.

    Na kama serikali ya Tanganyika (au hata ukiita Tanzania Bara mimi sijali) katiba yake ikiweka ukomo wa mawaziri wasiozidi 17 kwa mfano na ile ya Zanziba nayo ikaweka ukomo wa mawaziri wasiozidi 13 pia kwa mfano ndiyo kusema serikali zote TATU zitakuwa na MAWAZIRI 45 tu. Tofauti na sasa ambapo serikali ya Muungano peke yake ina mawaziri zaidi ya 60 bila kuongeza wale wa Zanziba.

    Isitoshe serikali hii ya Muungano (ambayo ndani yake kuna ile ya Tanganyika yaani imejificha kwa ndani) litakalofanyika ni kuiagawa tu. Mawaziri waliokuwa wanashughulika na mambo yasiyokuwa ya Muungano kama vile Maji, Kilimo, Elimu, Utalii, Maliasili, Viwanda/Biashara, Miundombinu, Ardhi/Nyumba, nk wataondolewa kwenye baraza la mawaziri wa Muungano wawe na baraza lao na Rais wao kama ilivyo kwa Zanziba.

    Kwa hiyo watu wanaoshabikia serikali Mbili ni watu wasiochambua kwa undani na hawataki tu kuona mabadiliko.

    Mzee Mtikila na wenzake wasituletee matatizo watuache tupate Katiba Mpya ya Mwaka 2014 itakayofaa kwa miaka 100 ijayo. Mungu ibariki Zanzibar Mungu ibariki Tanzania Bara/Tanganyika.

  9. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mkoani Tabora Mhashamu Paulo Luzoka ameitahadharisha Tume ya mabadiliko ya katiba na jamii kwa ujumla juu ya rasimu ya katiba iliyotolewa hivi karibuni, kuhusiana na serikali tatu, kuwa iwe makini na mambo ambayo yanaweza kuleta kuvunjwa muungano na kuleta mgawanyiko.
    Askofu Luzoka amesema haoni sababu ya kuwepo na serikali tatu ikizingatiwa kuwepo kwa changamoto za uendeshaji, huku akidai kuwa, kwa namna moja ama nyingine, maadui wanaweza kutumia udhaifu wa kiongozi mmojawapo na kusababisha mgawanyiko, na machafuko.

Andika maoni yako