Wakati ni sasa, Rekebisha njia zako!

kanisa

Ndugu wapendwa katika Bwana Shalom! Napenda leo tushirikiane somo fupi kidogo kwa nyakati tulizo nazo. 2tim 3:1-9,16 Roho Mtakatifu alimfunulia mtume Paulo kwa nyakati za mwisho kuwa kutakuwa na nyakati za hatari, ndizo tulizo kipindi hiki ikiwa sisi kama wasafiri na wapitaji ulimwenguni hatuna mji udumuo bali tunautazamia mji mpya Jerusalem. Nyakati tulizo nazo ni nyakati za kutisha na Bwana yu mlangoni, shetani akitambua kuwa amebakiza muda mchache anakomboa wakati nakuwameza wakristo wazuri, anapiga mbio kuharibu imani ya Kristo Yesu ili watu wengi wapotee zaidi katika udanganyifu wa dhambi.

Kumpenda Mungu hakupo, mioyo ya watu imelala, uamsho umepoa wapendwa wetu wanarudi nyuma wapendwa! na tuogope kusikia mwenzetu amepotea dhambini maana tu viungo vya Kristo, Bwana yu mlangoni dalili zinaonyesha siku ile iliyo kuu ya ghadhabu na ya kutisha Malaki 4 siku hiyo inawaka kama tanuru, jiweke tayari tujitakase na kuondoa maovu yote ndani yetu ikiwezekana Mungu atunusuru na siku uliyo kuu na ya maombolezo makuu wakati ni sasa na sio kesho rekebisha njia zako. Maana haujui ni siku ipi Bwana yuaja hujui lini ni mwisho wako.

Isije ikiwa kama wanawake kumi Mathayo 25 watano walikuwa wapumbavu kwa kutokuweka mafuta ya akiba basi nasi tujiwekee akiba ya matendo mema (wema hauozi ) wema ni akiba tusilale usingizi tukeshe katika sala.

Bwana yu karibu. mpendwa fikiria ulimwengu unavyo elekea na tambua hizi ni nyakati za hatari tazama jinsi roho ya mpinga Kristo ilivyo jiinua na inatenda kazi kwa siri 2 wathesalonike 2:1-13

Naomba Mungu Baba atie Roho ya hekima Na ufunuo katika kumjua yeye macho ya miyo yenu yatiwe nuru.

BARIKIWA SANA

–EV B Mwai

Advertisements

One thought on “Wakati ni sasa, Rekebisha njia zako!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s