Kuushinda Ulimwengu – I

kanisa

Shalom Wapendwa ninawasalimu katika jina lipitalo majina yote jina la YESU KRISTO!

Nimeona leo tushiriki kwa pamoja kuumega mkate huu. Nimshukuru Mungu aliyetuokoa toka huko utumwani kwa shetani haikuwa kazi rahisi kwani hatungeweza kujikomboa, lakini Mungu alituhurumia sisi maskini Kol 1:13-14 “Kwa maana alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwa, 14ambaye katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi” Wokovu huu tulioupata, ni ishara za huruma zake Mungu wetu na maandalizi yake yalianza kwa wale manabii wakisema kuhusu neema ambayo ingetujia mimi na wewe, na walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa, wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo ndani yao Roho wa Mungu alionyesha walipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata. Mitume walidhihirishiwa kwamba walikuwa hawajihudumii wao wenyewe, bali walihudumu kwa ajili yetu katika mambo hayo ambayo sasa yanahubiriwa kwetu kwa uweza wa nguvu za Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. (1Pet 1:10-12).

Mungu anatangazwa kuwa hashughulikii wokovu wa mtu binafsi tu dini, dhehebu, kanisa, wala sharika, bali kwa mataifa yote kwa kuanzia lile la Israeli hadi hapa kwetu Tanzania. Kwa Wakristo tukio kuu lililo msingi wa imani ni ufufuko wa Yesu, aliyetoka kaburini mzima na kuutwa utukufu kwa kuishinda mauti.

IMANI KTK SIKU ZA MWISHO

Wapendwa katika Kristo Yesu, kama ilivyotabiliwa katika siku za mwisho, kuna mambo Mengi yapo yakiendelea sasa. Japo hayo yapo kanisa linazidi kukosa nguvu ya Mungu katika Kristo. Yapo mengi sana sihitaji kuorodhesha kila mtu anaona kanisa jinsi tunavyoenenda. Neno linazungumza kuhusu kuushinda ulimwengu, maana usipo ushinda ulimwengu umekuwa mtumwa wa kisirisiri. Unaweza kushangaa sana kwa nini ninasema hivyo, ninachoamini mimi nafasi ya Mtu wa Mungu Duniani ni kumiliki pamoja na watakatifu wa Mungu Duniani, maana ni mapenzi ya Mungu, kwamba watoto wake, tuishi maisha mzuri, ya ushindi na mafanikio, ili tuweze kulitimiza kusudi la Mungu la kutufanywa vyombo vya ibada kumwabudu Mungu, kama kuna shida kidogo Huwezipata nafasi za Kufanya ibada kwa uhuru (hilo tunashuhudia sehemu zenye vita na machafuko). Nahum 1:9 “Mnawaza nini juu ya Bwana, kwa maana Bwana atayakomesha mateso ya watu wake, hayatainuka tena”  1Yohana 5:1-4 4 “Kwa maana, kila kitu kilichozaliwa na Mungu, huushinda ulimwengu, na huku ndiko kushinda, kuushindako ulimwengu, ni hiyo Imani yetu.”

Nikipitia Biblia yangu naona kila mahali palipotokea uasi kwa taifa teule la Israel, Mungu aliachilia maadui wawapige Israel. Hivyo ni shauri la kila Mkristo bila kujali kama dini yangu inasema nini, maana najua hata wewe wajua kwamba ziko dini/dhehebu ambazo zinakufanya uokoke akilini tu, yaani sehemu nyingine zinakuwa hazijaokoka pamoja na Moyo wako unakuwa haujampokea Kristo. Ndipo unapoweza wapata wale wanafiki wa imani, wanaoweza kwenda kanisani huku wakibeba fedha chafu za rushwa na EPA bila woga wana toa sadaka na wanatoka salama. IVI KWELI INAWEZEKANAJE??siwafukuzi bali imetupasa kujiuliza na kuwasaidia lakini sio sisi ku ‘‘bow down to them’’. KANISA NI MAHALI PA KUWAPA MUONGOZO WAKOSEFU BILA KUJALI ELIMU NA VYEO. Kumbuka habari za Anania na mkewe, NASIKIA KUSEMA KANISA LA LEO kuna kitu kimepungua,  maana kanisa la Rohoni huwezi ukatoa sadaka chafu ukatoka salama ATI NA ROHO MTAKATIFU YUPO.

Madhara yatakayotokea badae siku zinakuja, ni matokeo ya kuingiza uharibifu mdogomdogo katika kanisa la Mungu. Watu wameshindwa kuchukua nafasi zao za imani majumbani mwetu, mahala pa kazi, kwenye biashara, shuleni, vyuoni, nk. Hivyo kujikuta tunakubaliana kwa hoja zitolewazo kutoka katika hekima za kibinadamu. Unaonaje rasimu ya KATIBA? Viongozi wetu wamejiandaaje kuhusu kanisa na watoto wa Mungu? Kuhamasisha washirika kuisoma rasimu ya katiba? je kanisa limemwomba Mungu kiasi cha kupata hekima kutoka kwa Mungu kwa habari ya Mambo yale ambayo Siyo au Ndiyo???

Barikiwa na Bwana

Nitaendelea———

Anthony

Advertisements

6 thoughts on “Kuushinda Ulimwengu – I

 1. “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.” 1 YOHANA 2:15,16

  Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. YOHANA 16:33

 2. Lenda, Shalom!
  Ni kweli, kuushinda kwetu ulimwengu ni kiroho! Pia ni kweli kwamba sisi si wa ulimwengu huu!

  Haya yote ni mambo halisi kabisa, kwamba hiyo vita yetu ya kuushinda ulimwengu, “… si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Basi utapiganaje hiyo vita ya kiroho nawe ukiwa ungali mwilini? Silaha zote zikupasazo kuwa nazo kwa ajili ya vita hiyo ni za kiroho, sasa itakuwaje kwa mtu aliyeyakataa mambo ya rohoni akang’ang’ana na ya mwilini halafu anataka kwenda kupigana vita ya kiroho, je, ataiona kweli mishale ya moto? Maana Shetani anakuja na mishale ya moto nayo yawezwa kuzimwa kwa ngao ya imani tu! Nayo imani huja kwa kulisikia Neno la Kristo ambalo ndilo hilo linalotufundisha kuwa, “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.”

  Sasa ukiwakuta hao wanaodai kuwa wanaushinda ulimwengu halafu unapowatazama unawaona wanaongozwa na nabii mwanamke na wachungaji wanawake, halafu wanakuaga kuwa wanakwenda vitani, unalionaje jambo hilo ndugu yangu Lenda? Vita si jambo la mchezo, hiyo ngao ya kujikinga na mishale ya moto huna, kweli utarudi salama kambini? Maana tunaambiwa, “…zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu”! Hayo majeshi ya pepo utayashindaje nawe ngao ya imani yenye uwezo wa kuizima hiyo mishale ya moto unayorushiwa huna! Umelikataa Neno liwezalo kukujengea Imani ya kweli, umeridhika na imani mbadala!!!

  Mungu kuhusu watu wa jinsi hiyo, hao wanaojikoki na kwenda katika vita wasiyoijua, anasema hao ni wajinga! 1Kor 14:37/8, ““Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.”

  Ndipo basi kwa watu hao wanaotaka kwenda huko vitani, wanapaswa wazuiwe hata kwa nguvu na kuwabakiza kambini ili waendelee na mafundisho ya UTAKASO ili kuiondoa hiyo orodha ya kimwili uliyoianisha katika mifumo ya maisha yao ambayo ndiyo iliyowajengea ujeuri na ukaidi hata wanataka kwenda kujinyonga huko katika uwanja wa mapambano, kwa kujitosa kabla hawajahitimu mafunzo!

  Basi, wakilitii hilo Neno watavikwa taji, kwa kujazwa Roho Mtakatifu, sasa ndipo wataweza kutoka na kuushinda ulimwengu, maana hao ni viumbe vipya, hao wamekuwa converted kutoka wale wa mwilini wenye mambo hayo uliyoyataja, na sasa ni wa kiroho waliovishwa silaha zote za Mungu, lile NENO!! Vinginevyo ni hadithi za Abunuwasi tu!!!

  Ubarikiwe!

 3. kushindana kwetu si juu ya katiba na vyeo siko kuushinda ulimwengu Biblia inakosema ni kuushinda kiroho, kuvua utu wa kale. Maana sisi si wa ulimwengu huu na kuyashinda mauti kwa njia ya kuvikwa haki ya kuishi milele.

  shinda haya ambayo ni ya ulimwengu:

  ulevi
  fitina
  husuda
  ufisadi
  Hasira
  uzushi
  faraka uchawi
  uvivu
  uadui
  wivu
  ulafi
  uzinzi
  usengenyaji
  tamaa za macho

  wana wa ufalme walioushinda ulimwengu wameyashinda hayo KRISTO akiwa mfano wetu maana amesema tuenende kama alivyoenenda.

  “Yesu akajibu, ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa wayahudi? Yohana 18:36

  mengi yatakuja katika sheria na taratibu na katiba ya kupinga neno. Muhimu uwe shahidi mwaminifu kama Yesu. Japo sheria Haikuona hatia juu yake alibebeshwa lawama.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s