Ninaomba mpenyo kwenye maisha yangu

maombi-

Naitwa mama Naomi, Naomba muungane nami katika kumuomba Mungu juu ya mambo yafuatayo;
1. Mungu anipe kazi tena nzuri – wazazi wangu wanaishi katika mazingira magumu sana ninapenda niwabariki kwa kuwatunza pia kuwajengea nyumba lakini sina kabisa fedha. pia ninahitaji kumpeleka mtoto shule lakini hatuna kitu.Mungu amenibarikia elimu nimetafuta kazi tangu 2011 hadi leo sijapata
2. Mama yangu anaumwa muda mrefu sasa ninaomba uponyaji kwake lakini pia wazazi wangu wote na ndugu zangu hawajaokoka nahitaji waokoke
3. Mtoto wetu ni mkubwa sasa umri wa kusoma shule lakini hajapata mwenzake, amekuwa akituomba tumnunulie mdogo wake wa kiume tunaomba Mungu atubariki katika hilo
4. Mume wangu ni mtafutaji sana lakini si mtu wa kufanikiwa, ana miaka mitano sasa anaanzisha miradi tofauti mara duka, kilimo nk lakini vyote vinakufa .

Tunampenda Mungu na kumheshimu.

–Salome

Ndugu mwanamaombi, popote ulipo, chukua nafasi ya kuomba kwa ajili ya dada Salome, tamka kitu juu yake ili Mungu afungue milango kwenye maisha yake.

Advertisements

9 thoughts on “Ninaomba mpenyo kwenye maisha yangu

 1. Pole sana mpendwa mi naomba kukusHauli kuwa pamoja na kuwa umemwomba sana Mungu hebu pokea na Roho ya utoaji toa sana vitu vyako kwa Mungu hiyo nikanuni haikwpeki ukifanya hinyo mambo yako yatabadilika sana.

 2. Mpendwa Mama Naomi,

  SAMAHANI, MIMI SIJAKUOMBEA ILI UPATE KAZI, NIMEKUOMBEA UPEWE HEKIMA!

  Nimepita hapa na kuyaona Mahangaiko yako, kwa kweli unashida, naweza kuhisi unavyojisikia. Uhitaji ni “UGONJWA” mbaya sana, shetani huutumia mwanya kama huo kuwa mtego wake wa kwanza kabisa katika kuwaangusha watoto wa Mungu; NAKUTAKA UWE MACHO!

  Ukipitia habari ya Ayubu ambayo ni ya kweli kabisa, na ni mfano halisi wa kipekee juu ya msiba huu wa ‘Uhitaji’, shetani kitu chake cha kwanza alichofanya ni kumwambia Mungu kuwa “Ayubu, ni lazima aonekane kuwa ni mcha Mungu, maana wewe (Mungu) umemzingira kila mahali” kwa Msemo rahisi, Shetani alimaanisha tu kwamba ‘Ayubu ni mcha Mungu kwa sababu anakila Kitu cha ki mwili!’

  Na Mungu katika kumthibitishia shetani kwamba, ‘Kuwa na kila kitu’ cha kimwili si sababu ya watoto wa Mungu kudumu katika ‘Ufalme wa Mungu’ ambao ni “Amani, haki na Furaha katika Roho mtakatifu” maana mambo hayo ndiyo husababisha Ibaada halisi moyoni mwa mwamini; shetani aliruhusiwa amjaribu Ayubu, ndipo shetani alianza kwa KUMUONDOLEA NA KUMKWAMISHA AYUBU KWAKILA KITU cha kimwili alichokuwa nacho na alichokihitaji, kimoja baada ya kimoja alimnyang’anya!

  Si hivyo tu, pia rafikize Ayubu na mkewe, “walimwacha” kwa maana ya kwamba, hawakumtia moyo! Walimvunja moyo, na kumhukumu kuwa ni mwovu, walimuona Ayubu si CHOCHOTE kwa Mungu na kwa wanadamu, maana, mawazo ya wanadamu, ni juu ya Mali na huwatanguliza Mbele Matajiri! Kwa Mtazamo huo huo, rafikize na mkewe walijaribu kuingiza Akilini mwa Ayubu wazo kuwa Mungu amemwacha ndiyo maana ‘KAMNYAMALIA KIMYA!’

  Haraka za kupata majibu ama kufunguliwa katika uhitaji wa aina yoyote ile ni hamu na tamaa ya kila Mwanadamu, maana huo ni Ubinadamu! Tunashuka moyo na kujiona si chochote mbele ya wenye “nazo” Hatuheshimiki na hatufikiriki kuwa tuna mawazo na ushauri mzuri, kwakuwa hatuna ‘Kitu’ cha ki mwili! Kweli ki mwili mambo huwa hivyo, lakini wewe mwana wa “Kiroho” hayakuhusu yote hayo, sasa, usivunjike moyo kwa ajili hiyo!

  Dadada yangu, kwakuwa naamini kuwa unayajua maandiko, kwa ajili hiyo sioni haja ya kunukuu mistari toka Biblia (ila ukinitaka kufanya hivyo nitakunukulia), Katika swala hili la “MTU KUWA NA KAZI YA KUFANYA” SI JAMBO LA KUMUOMBA MUNGU! Ni jambo ambalo Mtu ameumbwa nalo, kwa hiyo huwezi kuomba kitu ambacho tayari unacho! Wewe na Familia yako kazi mnayo, na hakuna andiko linalosema watu waombewe kupata kazi, ndiyo maana sijakuombea upate Kazi! Mama Naomi dada, unaweza kunishangaa kidogo, kwa nini nimefanya hivyo, si kwamba nina roho mbaya kiasi cha kukuonea wivu ukifanikiwa, ama ukipata kazi ile unayoamini ndiyo kazi!

  Tumeshauriwa kuwa, jambo lolote likitutatiza, tuyaangalie maandiko! Yesu alipoulizwa katika hoja ya mtu kuwa na wake wengi, alijibu hivi “….lakini mwanzo haikuwa hivyo…mke mmoja mme mmoja…”Hebu tuone katika swala la mtu kuwa na kazi ya kufanya mwanzo ilikuwaje? Na wote tunajua kuwa mwanzo wa Maisha ya mwanadamu ni katika Bustani ya huko Edeni. Biblia inasema katika kitabu cha mwanzo 2:15 kuwa, “15BWANA Mungu akamchukua huyo mtu akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza”. Tunachokiona hapo ni kwamba mtu aliumbwa na kazi yake tayari ilikuwepo! Tatizo letu, ambalo naliona na wewe Salome unalo ni ‘kupata kazi ya aina Fulani’ lakini kiukweli, wewe hapo ulipo unayo kazi, ambayo ndiyo sababu ya riziki yako ya kila siku! Sambamba na hilo hebu soma ule mstari wa 16 unasomeka hivi, “16BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu akamwambia, ‘‘Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani.”

  Hebu jiulize, tangu 2011 hadi unailete shida yako hiyo mbele za Mungu, hujapata kula hata siku moja? Jua unakula kwakuwa una “Itunza Bustani” ya aina Fulani ambayo katika macho ya ufahamu wako imefichwa! Neno la Mungu linasema, “…Asiyefanya kazi asile..” Sasa, jiulize tena, kwanini unakula nawe unasema, hufanyi kazi? Huoni kuwa, kama unakula na hufanyi kazi unavunja Neno la kweli la Mungu?

  Mimi naamini huvunji Neno la Mungu katika hilo la kula, kwasababu, wewe unayo kazi Fulani, maana kula kunaambatana na kazi Fulani ambayo Mungu alikupa, lakini si “kazi Fulani uitakayo!” Kula kunambatana na Kazi, na vyote hivyo Mungu amemuumba Mtu navyo, hupaswi kuyasumbukia kiasi hicho cha kulia mbele za Mungu, kazi ni kama chakula kipo kwa ajiri yetu, wala sisi hatujaumbwa kwa ajiri ya kazi na kula; Bali vyakula na kzi viliumbwa kwa ajili yetu! Kwa hiyo kazi unayo ndiyo maana unakula; Yesu alithibitisha kwa kusema kula wala kuvaa kusiwasumbue, hata Selemani na fahari yake yote, hajapata kuvaa kama, maua ya kondeni yanavyopendezeshwa kwa mavazi ya ajabu, wala Ndege wa angani hawajapata kukosa kula licha ya kwamba wao hawana Shambba (Hawafanyi kazi) tena hawana Ghara (Hawana maarifa / si wabunifu). Sembuse wewe Mwana wa Mungu mwenye mamlaka JITAMKIE NENO MWENYEWE KWA IMANI ITAKUWA TU!

  Pamoja na sababu hiyo hapo, mimi niliona nikuombee upate “HEKIMA” ambayo Mtu hawi nayo isipokuwa awe na Ufahamu na Maarifa. Ndiyo maana shetani hufunga ama kuondoa Maarifa, ndiyo maana Neno linasema, “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” Sasa, bila kuwa na uwezo wa ‘UFAHAMU’ (understanding ability) huwezi kuwa na MAARIFA – ambao ndiyo nguvu ya kuendeshea Hekima (Knwoledge is power!), kwa hiyo ukiwa na Uwezo wa kufahamu mambo jumlisha na Maarifa ndipo unapata Hekima! (Understanding ability + Knwoledge = Wisedome) Kwa sababu, Maarifa ndiyo “Cement” kati ya Ufahamu na Hekima; Kwa maana hiyo, hakuna mwenye Hekina asiye na Fikra na maarifa! Umaarufu wa Selemani ulitokana na kuomba kwake HEKIMA, sote tunajua alivyokuwa ni mjuzi wa kubuni Biashara (Kazi) ambayo ilimfanya awe mkuu sana kiuchumi, si hivyo tu aliweza pia kuongoza visivyo vya kawaida! Pata Hekima ili ujue kubuni na kuifanya kazi itakayompendeza Mungu, ili aibariki nawe upate Furaha na mafanikio ya moyo wako!

  NAKUTAKIA AMANI YA BWANA MBAYO ULIMWENGU HUU PAMOJA NA FAHARI YAKE HAUWEZI KUKUPATIA!

 3. shalom! Usikate tamaa,nakuomba uchukue sadaka yoyote uipeleke mbele za Bwana kwa njia ya maombi ukisikia amani ya kuitoa sehemu yoyote toa ila uwe na uhakika kuwa amani utakayoipata iwe ni ya Kristo. usiache kuomba

 4. Ayubu alisema kuwa najua mtetezi wangu yu hai akisha kunijaribu nitatoka kama dhaabu, dada natamka neno hili ktk jina la Yesu , unakwenda kutoka kama dhaabu ktk mapito , bado Mungu atakijaza kinywa chako kicheko na midomo yako ataijaza shangwe, Ayubu 8:21, Mungu akomeshe siku za kuomboleza kwako Isaya 60:20. Mungu baba atakuvua gunia na atakuvika furaha Zaburi 30:11. Yuko anafanya jangwa lako hili liwe kama bustani ya Eden , anafanya nyika yako iwe kama bustani ya Bwana , Nasema hivi ndani yako itasikilikana furaha kushukru na sauti ya kuimba sawa na Isaya 51:3. dada usiogope Mungu yuko pamoja na wewe , usifadhaike yeye ni Mungu wako, atakutia nguvu , atakusaidia, naamu atakushika kwa mkono wa kuume wa haki yake Isaya 40:11. atakupa kila haja ya moyo wako Zaburi 20:4. ktk mambo hayo yote utashinda na zaidi ya kushinda ktk yeye aliyetupenda. Warumi 8:37. Yeye aliyemtoa mwanae wa pekee hatakosa kukulimia na wewe mambo yote unayohitaji. Warumi 8:32. Mungu ni mwaminifu na hawezi kufanya uhaminifu wake kuwa uongo. Hivyo ninakusihii endelea kuwa mwaminifu kwake pia , endelelea kuwa mwaminifu na wewe mbele zake. hakika utavuna kwa wakati wako usipochoka na kuzimia roho yako, Wgaratia 6:9.Kwani yako matumahini ya mti ya kuwa ukikatwa utachipua tena, wala machipukizi yake hayatakoma, ijapokuwa mizizi yake uchakaa mchangani, na shina lake hufa ktk udongo,lakini kwa harufu ya maji utachipuka na kutoa matawi kama mche. Ayubu 14:8-9 kwa hafuru ya maji utachipuka tena dada , dada harufu ya maji ni neno la Mungu endelea kulitamka na kufanya kile linachosema,tafuta maandiko yanayohusu mafanikio ya KiMungu pamoja na yanayofundisha kumtolea Mungu kwa uhaminifu, yatamke na kuyatamka na kuyatenda siyo kutamka tu, mimi nilikuwa nikiuza nyanya nilikuwa natembea na ndoo mbili na nusu za nyanya kichwani, kwa mwendo wa masaa matano kwenda sokoni kuziuza, nilikuwa nikipata shilling 2000 kwa week, lakini nilipoanza kusoma neno na kutafakari na kuhamini na kuliweka ktk matendo , hakika mti wangu mkavu ulianza kuchipuka , na kutoa matawi kama mche. leo hii nikikumbuka alikonitoa Mungu, nilivyo na usafiri wangu mwenyewe, nilivyo na cha kuwapa wahitaji hata kama siyo wote duniani, nilivyo na amani na furaha , nilivyo na kazi nzuri na malipo safi kabisa , nilivyo na mume mwema, na mtoto , nilivyo na nyumba na chakula cha kutosha , ni ushuuda wa ajabu, ninabaki kumtukuza na kumsifu na kubariki jina lake, na kuendelea kuhamini nguvu zilizo ktk neno lake, ndiyo maana ninaliheshimu neno lake na kulihamini kuliko kingine chochote ktk maisha yangu. . Haleluya. sifa na utukufu ni kwa Bwana atuchukuliaye mzigo siku kwa siku, aliyebadiri matanga yangu yakawa machezo, aliyenivua gunia akanivika furaha, aliyekomesha siku za kuomboleza kwangu.

 5. Bwana Yesu apewe sifa, napenda kukupa hongera sana Dada Salome kwa kuendelea kumpenda Bwana Yesu japo unaona upepo mwingi katika maisha yako. Napenda tukumbuke kuwa neno la Mungu linatufundisha kuwa” BWANA NDIYE MCHUNGAJI SITAPUNGUKIWA NA KITU, ….. KATIKA MAJANI MABICHI HUNIONGOZA, KANDO YA MAJI YA UTULIVU HUNILAZA………… NIJAPOPITA KATI YA BONDE LA UVULI WA MAUTI SITAOGOPA MABAYA MAANA WEWE U PAMOJA NAMI.”

  wapendwa tabia za wachungaji wa wanyama ni kuhakikisha usalama wa wanyama wake wawapo malishoni, si hivyo tu bali kuhakikisha wanapata malisho safi ndo maana wachungaji wa wanyama huhama hama leo atalisha mbagala kesho ataona no ngoja nipeleke gongolamboto maana mbagala majani yamekauka. na gongolamboto yakipungua na kukauka usishangae ukakutana na kundi la mifugo pale mizani wanaswagwa kwenda kula malisho mazuri kibaha.

  Namaanisha kuwa Bwana Yesu ndiye mchungaji wetu hivyo hakika hatutapungukiwa kabisa, yeye ndiye ajuaye malisho yanayomfaa mtoto wangu SALOME yapo kibaha na si kimara, hivyo dada itakulazimu utembee hadi kibaha but ukifika pale lazima tu siku moja utarudi hapa strict kushuhudia maana hakika Bwana Yesu anayo majani mabichi kwa ajili yako. Japo unapita kwenye bonde la uvuli wa mauti linalofisha miradi na mpenyo hakika usiogope maana yeye aliye kweli na amini anasema YU PAMOJA NAWE, kwenye Isaya 43 anasema ujapopita kwenye maji mengi hutagharikishwa, na ujapopita kwenye miali ya moto hutateketea, yaani kweli mafuriko huenda yakatupata na miali ya moto ikakudondokea ila Yeye aliye Amini NA Kweli amesema HUTATEKETEA NA KUTAGHARIKISHWA.

  Dada nasema hivyo bse hata mimi nimepita kwenye failures nyingi hadi kutapeliwa zaidi ya milioni13 ambazo nilizitegemea sana kwenye biashara na sijapata hata sh1, nimetapeliwa kiwanja nilichokilipia 6mil by 2008 but wonderful Mungu amenipa nyumba modern mwezi uliopita yaani at zero cost yaani sijalipia hata shilingi moja.

  Wewe endelea kusimama kwenye neno lake, hakikisha kidogo upatacho unamkumbuka Mungu (zaka aka 10%) utaona ipo siku Suprise itakuzukia maana neno la Mungu kwenye Wakorinto linasema MUNGU HUMPA MBENGU MWENYE KUPANDA NA MKATE KUWA CHAKULA……..

  Jitie nguvu kwa Bwana, tutazidi kumsihi Bwana Yesu kwa ajili yako

  Flano

 6. Endelea kumuomba Mungu hipo siku njia zitafunguka. Ila ukifunga na kuomba kwa mda mrefu bila kupata jibu. Ujue kuna kitu ulichonacho au unacho kifanya kinacho zuia majibu kukufikia ukisha kitambua na kukiondoa utapata majibu ya mAombi yako hata sasa hivi.(chunguza toba yako kama iko sawa)

 7. usivunjike moyo, kwani Mungu yupo nawe katika hayo yote . Mpe Mungu wakati atatenda,atendalo ni kukutengeneza ili utakapobarikiwa usimsahau. naomba usitazame shida bali mtazame Mungu mana Yeye ndiye msaada wako wa karibu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s