Hatima yako ya Milele

destiny

Wote tunafahamu ya kuwa ipo siku moja maisha yetu hapa duniani yatafikia kikomo na baada ya hapo tutaingia katika umilele. Wanadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo kama Mungu alivyo Roho sisi nasi ni roho, tunazo nafsi na tunaishi katika miili hii ya nyama na damu. Ndio maana mtu anapoaga dunia tunasema “mwili wake…” maana mwenyewe ameshaondoka.

Neno la Mungu liko wazi kabisa kuwa kila mmoja wetu ataishi milele katika sehemu mojawapo ya hizi mbili, Mbinguni kwa Mungu au Jehanamu kwenye moto wa mateso alioandaliwa Ibilisi na malaika zake, huo ndio ukweli wenyewe na hakuna awezaye kuukwepa. Mungu hakukusudia mwanadamu aende Jehanamu, ila kama mtu akichagua kwenda huko Mungu hatamzuia maana Yeye ametupa uhuru wa kuchagua kumtii au kutokumtii. Ila ameweka wazi matokeo ya uchaguzi wetu, tukimtii tutaokolewa na kwenda mbinguni, tusipomtii tutapotea, tutahukumiwa na kwenda jehanamu kwenye mateso ya milele.

Wakati tungali hai hapa duniani yatupasa tufahamu haya mambo manne muhimu na kufanya uamuzi wa dhati:

1.       Sote tumemkosea Mungu na dhambi zetu zimetutenganisha na Mungu. Neno la Mungu linasema:

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”; – Warumi 3:23 SUV

2.      Mungu anaichukia dhambi kwani imetuletea mauti  na kuharibu ushirika tuliokuwa nao na Mungu

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” –Warumi 6:23 SUV

3.      Mungu anatupenda upeo, ndio maana akamtuma Mwana Wake wa Pekee aje azichukue dhambi zetu na kutupatanisha na Mungu kwa njia ya kifo chake pale msalabani

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” – Yohana 3:16 SUV

4.      Sasa kwa kuwa umeshafahamu haya yote una wajibu wa kuamua ama kumkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi wako au kukataa kufanya hivyo, nakusihi umkiri Kristo kama bado hujafanya hivyo.

Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia“. –Yohana 3:18,36 SUV

Baada ya kusoma maneno haya huwezi kudai hukuufahamu ukweli huu, nakushauri umgeukie Mungu kwa kumwamini na kumkiri Bwana Yesu kama hujafanya hivyo, tafadhali nakusihi usipuuzie wala usiahirishe jambo hili muhimu…saa ya wokovu ni sasa…hatima yako ya milele inategemea uamuzi wako . Usiudharau upendo na wema wa Mungu kwani ipo siku atakapouhukumu ulimwengu wote, utasemaje utakaposimama mbele zake ukijua ulidharau wito wake kwako? Usitegemee kuombewa msamaha na wengine ukishaaga dunia, hayo ni mapokeo ya kidini yasiyo na msingi kwenye Neno la Mungu. Neno la Mungu linasema hivi:

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu“; – Waebrania 9:27 SUV

Baada ya kifo kinachofuata ni hukumu, siyo kuombewa ili uokolewe. Wakati wa kuokolewa ni sasa ungali hai hapa duniani, Neno linasema hivi:

Mstari wa 9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. – Warumi” 10:8-10 SUV

 Mungu awabariki,

Patrick
 
Advertisements

8 thoughts on “Hatima yako ya Milele

 1. Ndg Harrison,

  Sote tumshukuru Bwana aliyetukirimia Wokovu wake, akatupatia na wasaa wa kulitafakari Neno lake.

  Ubarikiwe nawe pia!!!

 2. LWEMBE
  Mungu akubariki sana kwa kweli umeyaondoa mashaka yangu yote.

 3. Siyi na Lenda,
  Kwanza nataka niwaeleleze jambo moja kuu na la msingi katika mada hii ambalo naona mmelikosa kabisa; mada hii ni ya kiinjilisti na si ya kiMafundisho!

  Kwahiyo ninategemea kwamba sasa “Mtamkiri Yesu kwa vinywa vyenu” ili mpate kuvushwa kutoka “mwilini” na kuingizwa “rohoni”!

  Kuhusu Daniel 12:1, haya ni mambo yanayohusiana na Israeli, yaani hao watu wa Danieli, wakati huo Kanisa litakuwa limekwisha ondolewa uwanjani, ni wakati wa Dhiki Kuu! Katika shida hizo , watajumuika na wote walioikataa ofa hiyo aliyowaletea upya ndg Patrick, ili muikimbie hiyo aibu na kudharauliwa milele!!

  1 Thesalonike 4:16 ni Neno la faraja wanalopewa Kanisa, hao “waliomkiri Yesu kwa vinywa vyao” likiwaonesha hali nzima ya Tumaini lao katika Kristo!

  Maswali uliyoyauliza, hayana majibu yanayoyazidi Maandiko uliyoyanukuu. Tatizo ninaloliona kwako, ni hapo unapojaribu kuyapima mambo haya katika kipimo cha Mafundisho uliyoyazoea na hivyo kuishia katika mkanganyiko.

  Jambo kubwa kwenu ninaloliona likiwatatiza ni hali ya Mtu anapokufa, Je nini humtokea? Chimbuko la shida mliyonayo ambayo ndiyo inayowapelekea kulitilia shaka Neno la Mungu, inatokana na Fundisho lenu hili, mlilo likokotoa kutoka Mwanzo 2:7, 
“AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI; MTU AKAWA NAFSI HAI.”
  Ndipo ninyi kifungu hicho mmekitengenezea fundisho hili:
  MAVUMBI+ ROHO = NAFSI HAI (MWANZO 2:7)
CHEMBE CHEMBE ZA ARDHI – PUMZI = MWILI ULIOKUFA

  Mkiwa katika fundisho kama hili, ni dhahiri kwamba msingi wenu wa “ukristo” utakuwa umejengewa kutokea hapo Mwa 2:7 katika tafsiri hiyo mliyojitafsiria na sasa Injili inapoendelea mbele, ikiyafunua mambo ya “rohoni”, kwenu ninyi inakuwa ni vigumu kuyakamata hayo, maana mmjengwa juu ya msingi wa “mwilini” nayo Injili ikiwa imebadilika na kuwa ya “Rohoni”!

  Huyo Adamu unayemuona hapo katika Mwa 2:7, huyo unayeambiwa kuwa “Mtu akawa Nafsi Hai” hapa ndipo anapoanzia kuwa “mwili”, huyu ndiye aliye endelea hata akapewa Torati, ambayo imedumu mpaka ujio wa Kristo, hapo alipomkomboa na kumrudisha katika ile hali yake ya asili, akiwa ni “roho”, ile aliyofanana na Mungu, pale alipoumbwa, Mwa 1:26. Maana Mungu ni Roho (Yoh 4:24) huko ndiko kufanana kwao! Ndipo kurudishwa huko kunaitwa, “KUZALIWA MARA YA PILI”!!!

  Basi iwapo utafika katika kulielewa jambo hili vizuri, itakuwa rahisi kwako kuvielewa hivyo vifungu vingine vya Agano Jipya, hivyo vya rohoni, hata ukavileta pamoja na vifungu vya Agano la Kale “rohoni” ili kuikamilisha Injili.

  Kwa mfano ile Dan 12:2 inaposema, “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka”, kwa kadiri ya fundisho lenu, ninyi jambo hilo hulitazama katika msingi wa zege mlioujenga kwa kuokoteza Maandiko bila Roho, mkilikazia Fundisho lenu hilo kwa kile kifungu cha Mhu 9:5 “…lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.” Basi ninyi mmelichukua jambo hilo linaloongelewa hapo, linalohusu mambo ya mwilini, ambayo kwayo twapaswa kuyatimiza ya hapa duniani, na sasa wakati wetu wa kuyafanya hayo ukiwa umekwisha hapa duniani, ninyi mumelikazia hilo kinyume na muktadha wake, mkalifanya hilo kuwa ndiyo mwisho wa mkristo hadi hapo katika siku ya kufufuliwa hiyo miili tena!

  Basi hata mngeweza kuwaza kikawaida tu cha mwilini, kuwa hilo kumbukumbu lao limesahaulika wapi, duniani au mbinguni? Ni dhahiri kuwa limesahaulika duniani, maana hawapo tena hapa, hatuwezi kuwaita watufanyie lolote lile! Lakini huo si mwisho wao, roho zao huendelea kuwepo katika hayo makazi waliyotayarishiwa kwa ajili hiyo, KUSUBIRI ufufuo wa miili, kulingana na hatma yao katika siku umauti ulipowafika, kwamba walikuwa wamechagua upande upi, walimkiri Kristo kuwa ni Bwana, na sasa awachukue katika makazi aliyowatayarishia, au walimkebehi wakamtaka Baraba, yale mafundisho yao!!?

  Na kama mtajilazimisha kubaki katika mafundisho yenu, Je, mnasemaje kuhusu kifungu hiki cha Maandiko katika 1The 4:13-14, haswa huo mstari wa 14? “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14-Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, VIVYO HIVYO NA HAO WALIOLALA KATIKA YESU, MUNGU ATAWALETA PAMOJA NAYE.” Basi ungeyaonishaje mambo haya ya hao waliolala mavumbini kuamka na hao waliolala katika Yesu, Mungu kuwaleta pamoja na Yesu?

  Au hata nikikuuliza, Henoko alikwenda wapi? Au Elia, alikwenda wapi? Au Musa huyo aliyekufa na mwili wake kugombewa, ilikuwaje tena akaja pale mlimani ili hali Ufufuo bado?

  Au yule mwizi pale msalabani, Lk 23:43 “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” nasi sote twafahamu kuwa yule mwivi alikufa pale msalabani muda ule ule, ndipo kama Injili ni ya kuaminiwa, basi twapaswa kuamini hivyo kwamba alikwenda peponi, yule wa Mwa 1:26, na yule wa Mwa 2:7, huyo alikwenda kaburini huko ambako aliingia katika kutokujua lolote, maana huyo ni mavumbi!

  Basi ndugu zangu hebu jitahidini muufikie wakati, maana ninawaona ni kama mtu anayesafiri kwa punda, au hata ikiwa ni kwa ndege, ila ni katika wakati wa watu kwenda anga za juu zaidi, huko mwezini ambako huwezi kwenda kwa punda au hata aeroplane, haiwezi kustahimili mawimbi, ni nyakati za ROCKET, lile Neno kamili!

  Njooni na tafakari inayoendana na hali nzima ya Neno lililofungwa, Alfa hadi Omega, kuhusu hayo niliyowaonesha, halafu tuendelee kujifunza pamoja!

  Mbarikiwe nyoote!

 4. “NAYO MAVUMBI KUIRUDIA NCHI KAMA YALIVYOKUWA, NAYO ROHO KUMRUDIA MUNGU ALIYEITOA.” MHUBIRI 12:7
  “AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI; MTU AKAWA NAFSI HAI.” MWANZO 2:7

  MAVUMBI+ ROHO = NAFSI HAI (MWANZO 2:7)
  CHEMBE CHEMBE ZA ARDHI – PUMZI = MWILI ULIOKUFA

  “KWA KUWA UHAI WANGU UKALI MZIMA NDANI YANGU, NA ROHO YA MUNGU I KATIKA PUA YANGU” AYUBU 27:3

  “..ROHO ILE ITENDAYO DHAMBI ITAKUFA” EZEKIEL 18:4

  “HAO WAFU WALIOSALIA HAWAKUWA HAI, HATA ITIMIE ILE MIAKA ELFU.” UFUNUO 20:5

  WAFU WOTE WAMELALA HAWAJUI NENO LOLOTE, WALA KUHISI, WALA KUNUSA, WALA KUSIKIA WALA KUONA, WALA KUIMBA MPAKA YESU AJAPO.

  “KWA SABABU WALIO HAI WANAJUA YA KWAMBA WATAKUFA;LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE,,” MHUBIRI 9:5
  “..NAJUA YA KUWA ATAFUFUKA KATIKA UFUFUO SIKU YA MWISHO” YOHANA 11:24

  “SIO WAMSIFUO BWANA, WALA WOWOTE WASHUKAO KWENYE KIMYA;” ZABURI 115:17

  “KWA SABABU BWANA MWENYEWE ATASHUKA KUTOKA MBINGUNI, PAMOJA NA

  MWALIKO, NA SAUTI YA MALAIKA MKUU, NA PARAPANDA YA MUNGU; NAO

  WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, KISHA SI TULIO HAI,

  TULIOSALIA, TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO KATIKA MAWINGU , ILI

  TUMLAKI BWANA HEWANI; NA HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.
  1 WATHESALONIKE 4:16,17

 5. Hi kaka Patrick,
  Ubarikiwe kwa somo zuri lenye changamoto za tafakari nyingi. Binafsi limenibariki sana na baada ya kubarikiwa, nikawa na changamoto hizi kwa mujibu wa Biblia. Hebu nizipitie na wewe na wengine ili nami nieleweshwe vyema…
  Umesema kuwa, mtu anapokufa, hukumu- Waebrania 9:27. Hukumu ambayo ni ya milele(yaani anaenda mbinguni au jehanamu milele). Kwa mujibu wa maelezo shadidifu ya hoja hii ni sawa kabisa. Mimi naomba unisaidie hivi ni kweli mtu anapokufa, anaenda mbinguni au jehanamu ambako atakaa milele? Wewe na wengine, unazielewaje aya hizi?
  Daniel 12: 1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. 2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.

  1 thesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

  Yohana 5: 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.

  Yohana 6: 39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.

  Mdo 24: 15 Nina tumaini kwa Mungu, ambalo hata hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.

  Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.

  Ubarikiwe na Bwana

 6. Sawa kabisa Patrick,

  Pengine mtu atasema ngoja nitafute kwanza kisha nile maisha ndipo niamini! hatari kweli maana waweza kweli jitahidi au mambo kwako yakatiki tu kirahisi bila kukazana saaana, kisha kupata mali na wakati unajiandaa uanze kula, kunywa na kusherehekea, usiku huo huo aliyesababisha uwepo/utokezee dunia, kumbe akawa na ratiba nyingine kabisa( kukuondoa duniani bila hata consultations na wewe maana si lazima, hawajibiki kufanya ivyo -Luka.12:13-21

  Pengine mtu atatunza sana cheo kikubwa alicho nacho na kwamba ni kushusha status kuamini na kuanza mambo ya ibada-ibada na kwenda-kwenda kanisani kuimba na kucheza-cheza kama watoto! be informed kua walikuwepo wakuu sana ktk dunia hii waliovuma lakini walikua waamini/wachaji Mungu mpaka kua wenye mamlaka ktk Nchi ya ugeni-Mwanzo.41:37-46 na mwingine alikua Rais wa Nchi(Mfalme) lakini alikua mnyenyekevu kiasi kwamba wakati wa kumuadhimisha Bwana, hakujali status/personality yake, alicheza mbele ya watu, wakubwa mpaka kwa vijakazi hadi watunza/mtunza status na protocol ali-comment maneno fulani kumaanisha Mfalme awe makini kidogo maana anashusha hadhi lakini Rais alimjibu safi na barabara kabisa -2Sam.6:12-22, Pia Rais mwingine yeye alileta dharau baada ya kuingia Ikulu na kuutawala ulimwengu, akampuuza Mungu, ilibidi ageuzwe kua ngombe ale majani porini! no more baga,mishikaki,misambusa wala juice baridi hata ziara za kiserikali zote cancelled, akatafuna majani si wiki moja tu bali MIAKA 7-as per AP-Bible, ili akishakua na adabu ya kumgeukia Mungu ndipo arudi Ikulu-Daniel.4: 28-47

  Pengine mtu atasema yeye ni mrembo sana, viwango vyake vya uzuri ni zaidi ya kua mwamini Yesu, ni mrembo sana kudeal na mambo ya imani na kanisa la Kristo! Sikia rafiki, wako hata sasa na walikuwepo wadada warembo matata sana hujapata ona duniani!-ni warembo/ walimbwende mpaka jinsi wengine walivyowatatiza waume zao na wanadamu wanaume wengine ile hatari,walikua visura hasa mpakaMungu alikubali waandikiwe CV yao iyo hadharani bila kuchagua maneno ktk Neno lake, mmoja anaitwa Sara-Gen.12:10-20 na mwingine Rebeka Gen.24:15-16- na mwingine Esther-Esta.2:1-18 au kijana aweza dhani yeye ni Mkaka so handsome to associate na mambo ya imani, my friend, alikuwepo mkaka wa nguvu rohoni( Ki Mungu) mpaka mwili nje-ni mzuri wa hatari-1Sam.17:41-42

  Tunaweza weka orodha ndefu ya watu mashuhuri na matajiri katika jamii kama Yusufu wa Alimathaya au wasomi kama Paul na tabibu Luka au wenye kazi zao zenye ela nje nje yaani TRA wa siku izo kama -Mathayo, Zakayo,au basi na watu wa kawaida au masikini. Wote hao walifika mahali pa kutambua hakika bila kumwamini Yesu, hakuna njia nyingine ya kupona

  Yeye ni zaidi ya dini, dhehebu, taratibu za imani. Alipokuja alikuta dini zipi so hakuleta dini! Dini na madhehebu hayakuwahi kufa kwa ajili ya watu, Yeye alifanya ivyo, wala taasisi zetu za dini hazijawahi kuwapenda wanadamu kiasi kwamba zilikua tayari kufa na kufanyika fidia ya wanadamu, ila Yeye alipita hatua iyo na ndio maana anasema, hakuna upendo kama huu-wa mtu kuutoa uhai wake kwa akili ya mwingine/rafiki zake…Huyo ndie Yesu our loving and the most dear Master and saviour. He meant business alipokuja hapa chini na akijua kwa hakika atakwenda kuteswa mbaya msalabani ili tu mimi, sisi na wewe utakayekubali Injili hii, tupatikane mbinguni na si moto wa non-stop! Karibu kwake, uzuri wake Yeye hua hamkatai mtu kwa kipindi hiki cha neema, hata kama unadhani uko zaidi ya repair, atakushangaza na love yake inayopita mipaka, kanuni, calculations, utaratibu wa kawaida, mawazo ya watu na wasiwasi wa mtu. Come to Him and we who are already in Him, let us stick in and with Him forever, Amen.

  Press on,

  Edwin Seleli

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s