Kaldinali akosoa msimamo wa Obama kuhusu ushoga

Cardinal John Njue addresses a mass at Buruburu Catholic Church in 2008. The Catholic Church has criticised US President Obama stand on gay rights June 28, 2013. FILE

Kardinali John Njue alikosoa msimamo wa Marekani kuhusu kusimamia haki za mashoga tarehe 28 Juni 2013. Kaldinali huyo kutoka nchini Kenya alisema “”Hebu yeye (Obama) asahau, asahau na kusahau. Sidhani kama Mungu alifanya makosa alipomuumba Adamu na Eva na kuwaambia nini la kufanya” alisema Kardinali Njue katika Shrine Consolota mjini Nairobi Ijumaa.

Alisema hatuhitaji kupata mafunzo kutoka jamii “iliyoharibika”

Alhamis iliyopita, Rais Obama alisema mashoga kuthaminiwa kama watu wengine chini ya sheria ya Afrika. Licha ya kwamba ushoga ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi katika bara hili.

“Maoni yangu ya msingi ni kwamba bila ya kujali rangi, bila kujali dini, bila kujali jinsia, bila kujali hisia za kimapenzi, linapokuja sheria, watu wanapaswa kutendewa kwa usawa,” Raisi Obama alisema alipokuwa Senegal.

Suzane Onyango

Advertisements

6 thoughts on “Kaldinali akosoa msimamo wa Obama kuhusu ushoga

 1. Kaka Lwembe CK,

  Mara zote hupitia kwa makini sana Michango yako. Lakini nikiri wazi kwamba, katika hii SG site, nimejifunza mengi sana kutokana na michango ya wapendwa wengi waliomo humu ukiwemo wewe. Nimejifunza, kufundishika, kukumbushika, kutahadharika, kuambilika, kuonyeka nk. Nilipoitazama ile Hekima Ya Kweli Itokayo Kwa Mungu kupitia vyanzo mbali mbali katika biblia;
  Nimegundua kuwa “NABISHANA”kibinadamu, tena kama Binadamu wa kawaida tu!

  Nilipoisoma ile Walawi, Kwa polepole nikaisoma kama hivi, Walawi 20:13, “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa…..”
  na nilipooanisha na ile1kor. 2:6 inasema hivi:-

  6Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika.7Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri,tena iliyofichika kwa wanadamu, ambayo Mungu aliikusudia kabla ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. 8Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati zetu aliyeelewa jambo hili. Kwamaana kama wangelielewa, wasingemsulibisha Bwana wa utukufu. 9Lakini ni kama ilivyoandikwa:
  “Lile jambo ambalo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, wala halikuingia moyoni lile Mungu alilowaandalia wale wampendao.”
  10Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa njia ya Roho Wake.
  Roho huchunguza kila kitu, hata mambo yandani sana ya Mungu. 11Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 12Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho yule atokaye kwa Mungu, ili tuwezekuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure. 13Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa wale watu wa kiroho. 14Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni. 15Mtu wa kiroho hutambua mambo yote, lakini yeye mwenyewe
  hatambuliwi na mtu ye yote. 16“Kwa maana ni nani aliyejua nia ya Bwana ili apate kumfundisha?”
  Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

  Kwa Neno hili la Mungu, nakubaliana nawe MR. Lwembe CK, kuwa, huwezi kuchanganyaSiasa za Kidunia na Neno la Mungu, mwenyehekima alisema,“YA KAISARI MPE KAISARI, NA YA MUNGU MPE MNGU” fulu stopu! Obama kwa vyovyote vile yeye ni Kaisari, kwa hili, yeye ndiye amekuwa mwenye akili sana, maana amesimama vizuri katika zamu yake. Mimi tayari aliniona kuwa naelekea “Ujingani” maana nimechimba shimo kasha siwezi kutoka mwenyewe! Lo! CK asante kwa “kunitupia ile kamba” haraka, kwani, nisinge kufa kwa Baridi tu, bali njaa na kiu vyote vilikuwa vyangu! Kwakweli nilijaribu kudandia “Fuso” kwa mbele! Umeiona ile hatari ambayo ingenipata kama usingenionya kwa kusema “Mabinza nimeuona UBINADAMU wako”?!

  Kweli, iweni welevu kama Nyoka, lakini wapole kama Njiwa. ORBI naye anzidi kungongomelea misumari kwa watu wenyetabia za “Kibinadamu” anasema ni “hatari kwemba nyumbani mwa Mungu huku hutaki kuacha kumebeba furushi la upagani, mapokeo, na udini! ”

  Asante Lwembe, kweli Biblia imesema sawa, kuwa “MTU AMBAYE HANA ROHO WA MUNGU HAWEZI KUPOKEA MAMBO YATOKAYO KWA ROHO WA MUNGU, KWA KUWA NI UPUZI KWAKE, NAYE HAWEZI KUYAELEWA KWA SABABU HAYO YANAELEWEKA TU KWA JINSI YA ROHONI”

  Barikiweni wote!

 2. Brother Mabinza,
  Unajua, inafurahisha sana pale mifano inapokuwa halisi; Jambo hilo huongeza uelewa wa somo vizuri sana!

  Hebu tuiangalie ile tabia ya Ubinadamu, ngoja nikunukuu kuhusu yule jambazi Mabinza na rafikiye Lazaro:
  ““Na hata jirani yake au mtu mwingine aitwaye Lazaro atakapo sema ukweli wa sifa ya Mabinza kuwa, “Mabinza, wewe bwana UJAMBAZI wako umekuinua sana, naona una Gari sita sasa, ghorofa zuri upanga na una Hoteli ya Kisasa kabisa Mbezi Bichi, hongera sana Bwana! Nakuhakikishia kuwa, kitu atakachofanya Mabinza ni kufungua kesi ya Kukashifiwa na kuvunjiwa Heshi yake, lakini la pili atainua uadui mkubwa sana dhidi ya Lazaro; Tabia kama hiyo ndiyo Ubinadamu wenyewe.””

  Basi nimefurahi kuiona hiyo tabia ya Ubinadamu kwako, hapo unaponiambia kuwa “Kwanza niseme kuwa hukunielewa hata kidogo!” halafu unaniuliza, “ipo haki gani kumchukia badala ya kuuchukia ule ushoga wenyewe kama tabia mbaya yoyote?” Ndipo ninajiuliza, sikukuelewa katika lipi? Kama ni ushabiki ndio huu unaouendeleza, unajua imenilazimu nicheke saaana pale nilipoukumbuka ule usemi uliouleta katika mada ya “Nyota”, “become willing slaves to victory … if you get sucked in, it can be extremely difficult to think your way clear again” ambapo unasema, “…muumini hatoki humo kabisa na kwa hiari yake hutumia kila siraha kujilinda ili aendelee kuwa MTUMWA wa himani yake hiyo!” hivyo ndivyo ninavyokuona katika habari hii ya Ushoga!!!

  Roho Mt, kuhusu hali hiyo ya kutumika Utumwani huko ulikotekwa, anasema, 2The 2:11-12 “Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”

  Basi kabla hujawa “Sucked in completely”, ngoja nikutupie kamba ndugu yangu ili kama itakufaa, basi uikimbie hiyo ahadi ya Hukumu inayowasubiri hao wanaojifurahisha katika udhalimu huu wa Ushoga kwa kuwakingia vifua na kuufanya si jambo baya sana, kwamba linaweza kutubiwa kama dhambi nyingine nk!

  Kwanza, hebu jaribu kusoma tena kwa taratibu hiki kifungu: 1Fal 14:24 “Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.” Utaona, Mataifa ndio wenye tabia hiyo ya ushoga, nao Mungu aliwafukuza katika nchi na kuwapa nchi hiyo Israeli! Alipokwisha wafukuza hao mataifa, Israeli wakapewa hilo Neno kuwa asiwepo SHOGA kati yao!!! Sasa unapoambiwa “ASIWEPO” kati yenu, ninyi ambao mmezaliwa jangwani, je, ndio kusema mfukuziwe huko jangwani, ambako bila Mungu si mtakufa tu!? Hata unapomuangalia Asa, unapaswa ujue kuwa hao aliowafuza katika nchi yake, walikuwa ni wale masalia ya mataifa waliobaki na kuishi nao, maana Mungu alikwisha amuru kuwa Muisraeli shoga anapaswa kuuliwa, Law 20:13, “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.” Kwa hiyo hiyo Haki unayowatafutia mashoga, hiyo ndiyo tunataka utuoneshe katika Maandiko ni wapi ilipo! Kama tulikuwa na ushoga hapo tulipokuwa gizani, naye Mungu ametukirimia Neema ya wokovu na kutusamehe mambo hayo, basi iweje tena leo hii sisi tuliolipokea hilo Neno la Msamaha, na kuvionja vipawa, tuugeukie ushoga, huo ambao twapaswa kuuliwa kwa huo, na sasa tuufanye si jambo la “kumchukia shoga” bali tuuchukie ushoga! Ni uongo wa Ibilisi!!! Shoga anapaswa kuuawa, basi nikimchukia, nitakuwa nimeitimiza Haki ya Mungu, maana ni sawa na kumuua!!!

  Bali wewe uliyeamua kuchukuliana nao, kama ambavyo Wasabato na makanisa mengine yanayokiri “kuongozwa na Roho Mt” yanavyofanya, kuwasimika kuwa maaskofu na wengine kuanzisha vitengo ndani ya makanisa yao vya kuwahudumia mashoga, yaani kanisa likiwa ni madhabahu ya Mungu, kisha unakuja hapo na “machukizo”, kama si mizaha ni nini? “…wakijifurahisha katika udhalimu” kwa Jina la Bwana!!!

  Shetani anashindwa kwa NENO tu, sio kwa siasa za dini!! Angalia alivyolivuta kanisa mpaka limekuwa sucked in kichwa kwanza!!

  Mungu hadhihakiwi kwa siasa uchwara na huruma za dini. Aliwaambia Israeli, Kum 25:17 “…katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.” Sauli aliingiwa na huruma za dini na siasa uchwara za Haki za Binadamu, akawaacha Amaleki kinyume na alivyoamriwa na Mungu, BWANA akaurarua ufalme mkononi mwake, na kumpa jirani yake, Daudi. Kwa sababu hukuitii sauti ya BWANA! 1 Sam 28:17-18.

  Hiyo ndiyo hasara ya kutokuitii Sauti ya Mungu! Kinaondolewa “Kiti” chako katika ule Ufalme wa mbinguni, nawe kwa ile “Nguvu ya Upotevu” uliyoletewa utaendelea katika dini na siasa zake kama hayo makanisa: askofu shoga, mchungaji mwanamke msagaji, mzee wa kanisa mzinzi, waimba kwaya wamevaa bikini nk!!! hata akili zikikurudia hutakuwa na namna ya kutoka; SUCKED IN!!!!

 3. Mpendwa, Lwembe ,,

  Kwanza niseme kuwa hukunielewa hata kidogo!
  Mimi siungi mkono ushoga wala sishabikii ushoga ndugu yasngu, ninachojaribu kusema hapa ni kwamba, Kiongozi wa Nchi Raia wote ni wake. inapofika katika swala la sheria. Haiwezekani Kiongozi atangaze kuwa kila atakaye muona Mtu aliye athirika na ushoga Muueni, kama upo utawala wa sheria uso ruhusu hilo!

  Katika nukuu ulizotoa ni kweli imeandikwa hivyo, lakini watu hao hawakuuawa, walifukuzwa ama kutengwa mbali na watu wasiokuwa mashoga. Lakini pia hukuniambia iwapo kuna haki ya kutubu ukiwa Shoga ama la. Kama ambavyo Mkoma alitengwa na alipotakasika alirudishwa kundini; Je, Shoga akitubu baada ya kusikizishwa Injili inakuwaje? Na ikiwa naye anayo nafasi ama haki ya kupata kibari cha msamaha mbele ya Mungu, ipo haki gani kumchukia badala ya kuuchukia ule ushoga wenyewe kama tabia mbaya yoyote?

  Kauli ya Obama nilivyomuelewa, yeye si kwamba anahamasisha ushoga na kwamba ana upenda sana ushoga kama ushoga, yeye anawapenda wale mashoga na anatamani sana wasiendelee kuwa mashoga, watubu, waache tabia ile na jamii iwachukulie kuwa ni watu sawa na watu wengine ila ni WADHAMBI TU!

  Vinginevyo, itakuwa sijaelewa Sababu ya Mungu, kumtaadhalisha Kaini juu ya Dhambi iliyokuwa mbele yake, ingawa Mungu pamoja na kuwa alijua kuwa Kaini ni lazima atanguka tu, lakini alitahadhalisha kwa nini?!

  Ziko dhambi ambazo ziliainishwa kuwa ni za kifo, lakini sjui kama mashoga nao waliuawa. Lwembe unachosema ni kama kuwa, kila shoga auawe tu, bila kujari iwapo wapo watakaopatwa na Neno na kutubu. Ni dhambi gani iliyonyekundu kama Bendera lakini Mungu yuko tayari kuifanya nyeupe kama Theruji?!

  Mimi nakoma hapo, nikitumaini utanirudia hivi punde ili nijifunze zaidi.

 4. Nikikunukuu ndg Mabinza, kuhusu Ushoga na ushabiki wake, unasema, “Mimi nafikili ipo tofauti kati ya KUUKUBALI USHOGA na KUMKUBALI SHOGA!” halafu unatamatisha kwamba, “Lakini haitafaa kiongozi wa Nchi atakaposema kwa sauti kubwa kuwa mimi “SIWAPENDI WATU WAOVU” ila anaweza kusema kwa sauti kubwa na kwa kurudia rudia kuwa mimi “SIUPENDI UOVU”.

  Mawazo kama hayo ndiyo yanayotawala ulimwengu kwa sasa, na yanaendelea kupandikizwa katika mioyo ya watu ili wachukuliane na jambo hilo la ushoga kwa visingizio kama hivyo vyako, kinyume na Neno la Mungu!

  Lakini, swali unalopaswa kujiuliza kabla hujawafundisha watu kuchukuliana na Ushoga ni hili: “Je, Mungu huibadili nia yake?” iwapo umepata kibu kwamba ni “NDIYO”, basi unaweza kuendelea na mafundisho ya jinsi hiyo! Bali nia ya Mungu kuhusu mashoga unaweza kuitazama jinsi ilivyojidhihirisha ndani ya watawala kama Obama, ambapo katika siku hizo alikuwako mtawala somo wa Obama akiitwa Rehoboamu, 1Fal 14:24 “Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.” Hayo ndio mambo ya watawala na mashabiki wao walio nje ya mapenzi ya Bwana. Lakini mtazame Asa, 1Fal 15:11-12 “Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi. Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.” Mabinza unazijua “sanamu” za leo? Zinaitwa “Haki za Binadamu”!!! Lakini Mungu alikwisha agiza kuwa, “Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.” Kum 23:17; Nayo Israeli ndiyo iliyo mfano wa Kanisa! Sasa hebu tazama kile Roho anenacho katika siku ya leo kuhusu jambo hilo, 1Kor 6:9 “… Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti…”, basi sidhani kama kulishabikia jambo la jinsi hii kutakuacha salama!!!

  Hata hivyo kumlaumu sana Obama na watawala wenzake wa mataifa mengine, itakuwa si kutenda Haki, haswa kiongozi wa lawama hizo anapokuwa ni Kadinali wa Kikatoliki! Kwamba hao Obama anaowatetea, ni wangapi kati ya hao ambao ushoga wao unatokana na vitendo vya ulawiti walivyofanyiwa wakiwa watoto na makasisi wa Kikatoliki? Kadinali Njue alipaswa kwanza kuukosoa uongozi wa kanisa Katoliki kwa kuwalea makasisi wake wenye kujihusisha na vitendo hivyo! Katika siku za leo za utandawazi, yamejitokeza malalamiko ya miaka ya 1940s ya makasisi wa Kikatoliki waliolawitiwa na wenzao, hata baada ya kupeleka malalamiko, vinara wa mambo hayo hawakuchukuliwa hatua yoyote ile! Basi hebu niambie huko siku za giza ilikuwaje? Hata hapa Tz kuna kasisi alikamatwa akimlawiti kijana kwenye gari, nadhani ilikuwa katika maeneo ya chuo kikuuu!!!

  Basi kama kanisa limeukubali Ushoga, kama sote tulivyo mashahidi wa ndoa zinazofungwa makanisani za jinsia moja, au maaskofu mashoga wanaosimikwa kila kukicha; halafu unayo taasisi kubwa kama Katoliki ambayo viongozi wao wanashiriki kibubu kuzalisha mashoga, sasa watu wadogo kama akina Obama wanaweza kufanya nini zaidi ya kujiunga na injili hiyo mpya ya “Haki za Binadamu”??

  Kadinali anasema, “Hatuhitaji kupata mafunzo kutoka jamii iliyoharibika.” Lakini ukweli ni kwamba “walioiharibu jamii, na wanaoendelea kuiharibu jamii” ni kanisa, likiongozwa na kanisa Katoliki (angalia kesi walizonazo dunia nzima kuhusu ulawiti wa watoto na vijana na hata wao kwa wao!). Wanasiasa wanaendeleza matakwa ya kanisa, kwahiyo si wa kulaumiwa kihivyo!!

  Viongozi wa dini kama Kadinali Njue, wanajaribu kuficha ukweli hapo wanapojiosha kwa kuwashambulia wanasiasa ili kutupumbaza sisi maamuma wao!!

 5. Hamjambo wana SG,

  Mimi nafikili ipo tofauti kati ya KUUKUBALI USHOGA na KUMKUBALI SHOGA! Kimsingi Obama kama Kiongozi mkuu wa Nchi, wote ni wake, walioathirika na Ushoga na wasio Mashoga. Sisi tunaishi na Jamii iliyoharibika na kupotoka pia, kwa Maadili, kwa dawa za kulevya, Wizi, Unyanganyi, Ufuska, kwa kutotii sheria halali za nchi, wavunja katiba, wala rushwa, wafanya magendo nk. Lakina haitafaa kiongozi wa Nchi atakaposema kwa sauti kubwa kuwa mimi “SIWAPENDI WATU WAOVU” ila anaweza kusema kwa sauti kubwa na kwa kurudia rudia kuwa mimi “SIUPENDI UOVU”

  Kama Mungu asingempenda “Mdhami” kuja na kufa kwa yesu msalabani kusinge kuwa ni mhimu kutekelezwa na Mungu! Biblia inasema, “Kwajinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanaye wa Pekee!” Msimamo wa kuchukia Ubaya hakuthibitishwi kwa kuwachukia wabaya! Mfano mmoja wa wazi na mwepesi ni kuwa, Baba anaweza kuwa Mzinzi lakini hataki kabisa kumuuona Mkewe akizini, vivyo hivyo Mke wa mtu aweza kuwa fuska vya kutosha lakini hataki kuitwa hivyo wala kumuona mmewe akisogeleana mwanamke mwingine kimapenzi. Baba aweza kuwa Jambazi la kutumia silaha, lakini mtoto wake mdogo akijaribu kuchomoa shilling walau Mia moja tu, atampiga mpaka basi! Na hata jirani yake au mtu mwingine aitwaye Lazaro atakapo sema ukweli wa sifa ya Mabinza kuwa, “Mabinza, wewe bwana UJAMBAZI wako umekuinua sana, naona una Gari sita sasa, ghorofa zuri upanga na una Hoteli ya Kisasa kabisa Mbezi Bichi, hongera sana Bwana! Nakuhakikishia kuwa, kitu atakachofanya Mabinza ni kufungua kesi ya Kukashifiwa na kuvunjiwa Heshi yake, lakini la pili atainua uadui mkubwa sana dhidi ya Lazaro; Tabia kama hiyo ndiyo Ubinadamu wenyewe. Ubinadamu ni wa Mwanadamu, Mwanadamu hapendi kufanyiwa ubaya (hapendi ubaya) lakini anaishi na kuufanya ubaya bila kuujutia kama ambavyo angeudhika sana kama angefanyiwa yeye, katika hili Ubinadamu ni Ubinafsi!

  Lakini tunapozungumzia Kuuchukia uovu na kutoutenda kabisa, hatumaanishi kuwachukia waovu, hali hiyo ndiyo huitwa UTU, na hivyo ndivyo Mungu alipomuumba kiumbe wa Mfano wake alimwita, MTU! Biblia inasema katika kitabu cha Mw. 1: na akasema hivyo katika kitabu cha Mwanzo. Binadamu atendapo jambo ama tendo la HURUMA husemwa kafanya UTU, si kafanya ubinadamu! Wapo viongozi wengi wenye mioyo ya kibidamu na hawana utu hata kidogo, hujifanya kukemea uovu huku wao ndiyo vinala wa uovu, wanaingiza Dawa za kulevya kuwaangamiza masikini na wakati huo wanajifanya wacha Mungu na watetezi wa haki za Binadamu. Wanaiba na kupola lasirimali za mataifa yao na Kufanya Ujasusi dhidi ya nchi zao na watu wao, watu hawa huitwa na Biblia ni watu wa siku za mwisho katika kundi la watu “WASIOWAPENDA WAKWAO!” lakini hao ndiyo vinala wa kukemea uovu, na ndiyo watoa sadaka, mafungu ya kumi, sadaka za shukrani na misaada kw changizo mbalimbali za kidini!

  Kwakifupi, kwa kauli ya Obama juu ya kuwajari na kuwalinda mashoga dhidi ya utu na hakiza kisheria zinazo wahusu watu ama binadamu, mimi naona YUPO SAHIHI na hilo ni tendo la kiutu! La kama kahimiza watu kuwa mashoga na kwamba kuwa Shoga ni haki ya Msingi ya kibinadamu, huo nauona ni Ubinadamu, ambao kwa ujumla ni “UDHAMBI!”

  Asante Kaldinali John Njue, Mungu aendelee kukufunulia mapenzi na ukweli wa Neno lake..

 6. People have forgot the teaching of apostle, Paul talk in the book of Roman 1:26-27 about lust for the same sex, western nation should not pressure African country. We as God people need to follow God instructions

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s