Ushuhuda na Shukrani kwa Mungu kunijalia mtoto

mtoto

Wapendwa jina la Bwana libarikiwe! Ninaitwa Faith, ni takribani miaka 2 imepita sasa tangu nilipotuma maombi yangu juu ya Mtoto,

Kabla ya hapo niliharibikiwa na ujauzito mara 2, ndipo september 2011 mimi na Mume wangu tulimuomba Mungu atuonyeshe tatizo. Mungu ni mwaminifu, mmoja wa marafiki akatuelekeza kwa Dactari mmoja katika hospitali fulani hapa Arusha, tukaanza kuhudhuria kwa kufanya vipimo vingi, ambavyo vingine vilionyesha kuwa ningeweza kuwa na Saratani ya kizazi.

Mume wangu ni Daktari, kwa kuwa mimi sikutaka kuelewa maelezo ya majibu ya daktari basi mimi na Mume wangu tulitoka hospitali tukiwa hatuongei kwa kutofautiana imani kidogo (ukimya haukua na ugomvi). Siku iliyofuata mume wangu aliniita chumbani akajaribu kunichorea kabisa kwa maelezo ya kutosha ili nielewe hatari iliyokua inanikabili kutokana na majibu ya Daktari. Basi baada ya hapo nilimlilia Mungu kwa uchungu na kukataa kabisa yale majibu. Mwezi wa 10 mwaka 2011ule uvimbe uliokua kwenye kizazi ukatoka katika mfumo wa damu. Tukamtukuza Mungu kwa uponyaji, mwishoni mwa mwezi wa Decemba nikafanya vipimo vingine ambavyo vilionyesha kuwa nilikuwa na wingi wa sukari ktk mwili ambayo ingenipelekea kuugua kisukari na ndiyo iliyokua sababu ya kuharibika kwa mimba. Na pia vipimo vikaonyesha kuwa nisingeweza kuwa mjamzito kwa wakati ule na kwamba ningelitakiwa kuanza kumeza dawa za ugonjwa wa kisukari tarehe 17 mwezi February.

Moyo wangu uliinama kwa kiasi, nikakutana na mtumishi wa Mungu na bila kumwambia chochote aliniambia nipokee mtoto kwa jina la Yesu, nikaitika amina, wiki iliyofuata Nikakutana na mama mmoja mtumishi wa Mungu na nikamweleza mambo niliyokua nikipitia, Imani yake ilikua kuu sana, akaniambia, “Faith labda umebeba mapacha” kilikua kitu cha ajabu sana kwangu, wiki iliyofuata January 14 nikakutana na Mama mwingine wa imani, naye akaniambia Faith hauna tatizo la kubeba mimba, tatizo lako ni kutunza mtoto, naye akafanya maombi makali ya kumwombea mtoto katika tumbo, Siku iliyofuata nikaenda kumsalimu mama yangu mzazi (naye ni mtu wa imani) Akaniuliza kama nina habari njema, nikamweleza matatizo yote sawasawa na majibu ya Daktari, mama akaniambia hapana, wewe si mgonjwa una ujauzito wa mtoto wa kiume. Tarehe 17 Januari nikafanya vipimo na kugundua nilikua na ujauzito wa wiki 3.

Kutokana na hali ilivyokua, nilielekea hospitali ambapo vipimo vilionyesha kuwa mwili wangu haukuweza kuzalisha hormony za kumkuza mtoto, kwahiyo wakanipatia dawa mbadala ambazo nilikua nikizitumia. Ilipofika wiki zaidi ya 6, hormony zilikua zikishuka badala ya kupanda, ndipo Daktari akaniambia mtoto hataweza kukua ktk hali hiyo, nilirudi nyumbani nikiwa na huzuni sana. Nikajifungia chumbani kwangu nikimlilia MUNGU. Mungu akasema nami kwa lugha ambayo niliweza kuielewa akaniambia “MY MIRACLES ARE NOT THIRP PART but MY MIRACLES ARE COMPREHENSIVE” Ikiwa na maana kwamba muujiza wangu sio kama bima iliyo nusunusu ila umekamilika (bima kubwa). Ndipo nikajua kuwa Mtoto wangu ni Muujiza kutoka kwa Mungu na nikapata amani ya ajabu. Baada ya hapo mambo mengine mengi yalitokea lakini Mungu alitimiza Muujiza wake kwangu. Sasa nina mtoto wa kiume anayeitwa FarrellMiracle.

Jina la Bwana Libarikiwe.

Mungu awabariki kwa maombi yenu ktk hili.

Faith
Advertisements

8 thoughts on “Ushuhuda na Shukrani kwa Mungu kunijalia mtoto

  1. Hongera sana dada,bila shaka umefurahi Mungu alipokutendea hayo. Lakini kumbuka pia yakija magumu usijaribu hata mara moja kumuacha Mungu(Refer Ambwene Mwasongwe`s song MSULIWA IMANI)

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s