Masanja Mkandamizaji Kuhudumu Washington DC Jumapili hii

masanja1

Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara maalum, atahudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya kesho (Jumapili 07/07/2013)

Bwn. Mgaya ambaye pia hufahamika kama Mchungaji Mtarajiwa au Masanja Mkandamizaji Mungu amekuwa akimtumia katika mikutano mikubwa ya Injili Tanzania, atasimama madhabahuni Jumapili kwenye kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES katika ibada ya kawaida ya kila Jumapili ambayo hufanyika kuanzia saa saba kamili mchana mpaka saa tisa kamili alasiri (1:00pm – 3:00pm)

Anwani ni
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii itakuwa ni huduma ya kwanza nchini Marekani kwa Mtumishi huyu ambaye ni Mchungaji msaidizi katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka lililopo Kariakoo jimbo la Temeke jijini Dar Es Salaam likiongozwa na Askofu Bruno Mwakibolwa na ameshafanya huduma katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania. 

Bwn. Emmanuel Mgaya ambaye pia ni mchekeshaji maarufu kupitia vipindi vya runinga Tanzania, yuko Marekani kwa ziara maalum ya Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili linalofanyika leo Jumamosi (June 6, 2013)

Nyote mnakaribishwa

Advertisements

3 thoughts on “Masanja Mkandamizaji Kuhudumu Washington DC Jumapili hii

  1. Kaza buti mwanawane huo ni mwanzo mzuri tunaomba na wasanii wengine waige mfano wako najua watakua wanakupinga machoni moyoni wanakukubali.

  2. Mtumishi,

    Mimi ninakutakia mito ya baraka itiririke kila kona utakayopita hapo USA. Lakini usiishie kula bata tu za Marekani hebu jaribu pia kuangalia fursa za uchumi wako na taifa lako la Tanzania kama zinaweza kupatikana hapo marekani.

    Usitoke Marekani bila kupora chochote hasa mbinu nzuri za Uinjilisti, Mbinu za biashara kwa wasanii wenzio, Mbinu za mauzo ya CD zako na wasanii wote wa Tanzania, na jinsi gani unaweza kuwekeza miradi mikubwa hapo USA ili nchi yako na Kanisa lako kuweza kunufaika kiuchumi na kiroho.

    Nakutakia kazi njema na Mahubiri yenye upako mzito hapo kesho madhabahuni.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s