Christina Shusho ashinda tuzo London!

Ambwene Mwamwaja akiwa na tuzo ya Christina Shusho mkononi, pembeni ni kijana Karabo Mongatane wa Afrika ya kusini ambaye amenyakua tuzo ya album ya mwaka kwa wapigaji wa Afro Jazz.

Mwimbaji nyota wa gospel nchini mwanamama Christina Shusho ametwaa tuzo ya mwimbaji wa mwaka kwa nchi za Afrika mashariki katika tuzo za Africa Gospel Music Awards zilizofanyika usiku wa kuamkia leo jumapili katika ukumbi wa The great hall chuo kikuu cha Queen Mary jijini London nchini Uingereza.

Shusho amepata tuzo hiyo katika kinyang’anyiro cha waimbaji wapatao tisa kutoka Kenya pamoja na Uganda huku Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na waimbaji wawili, Shusho pamoja na Martha Mwaipaja ambapo hii ni mara ya tatu kwa Shusho kuingizwa katika kinyang’anyiro hicho na hatimaye safari hii kura zimetosha ameondoka na tuzo ambayo imepokelewa kwa niaba yake na mkurugenzi wa GK Ambwene Mwamwaja.

Pamoja na Christina Shusho mwimbaji aliewika zaidi kwakuondoka na tuzo mbili kati ya tatu alizopendekezwa ni mwanamama Ntokozo Mbambo wa Nqubeko ambaye hata hivyo hakuhudhuria tuzo hizo ambazo zilikuwa na kasoro za kiufundi za hapa na pale huku mwimbaji kutoka DRC mwenye makazi yake nchini Uingereza bibie Dena Mwana aliweza kuwasimamisha watu kwa uhodari wake katika uimbaji. Kiujumla waimbaji kutoka Afrika magharibi, Ghana na Nigeria wameondoka na tuzo hizo zaidi ukilinganisha na waimbaji kutoka sehemu nyingine.

Gospel Kitaa

6 thoughts on “Christina Shusho ashinda tuzo London!

 1. Kutumia Muziki wa Live ni gharama sana kuanzia kuwa na vyombo, Wapigaji, mazoezi na gharama zingine katika kufanikisha mazoezi mpaka performance. Matumizi ya CD (Playback) yamekuwa pia na unafuu wake kwa maana ya Uhakika wa Kupiga wimbo hata kama wanamuziki hawapo, lakini pia ina simplify muda wa kukutana pamoja na kuepuka gharama zisizo na msingi na zile za Msingi kila inapohitajika perfomance. Muziki wa Live na playback vyote vina uzuri wake na Ubaya wake kama ambavyo nimeonesha hapo juu. Siku za hivi karibuni nimeona kuna kurejea upya kwa Wanamuziki Wa Injili katika Muziki wa Live ambao una radha yake sana ukiacha changamoto zake za hapa na pale. Pamoja na urejeo huu bado nimeona kuna mapungufu ya hapa na pale. Its either Wanamuziki Bado hawajajipanga rasmi katika kurejea kwao katika Muziki wa Live ama Aina ya wapigaji wanaotaka kupiga katika Standards zao wamekuwa adimu ama gharama pia. Producers wa Muziki kama Mtangoo kule Arusha, Bakunde na Man Water ambao wametengeneza kazi za Wanamuziki wengi wa Injili hapa Tanzania wamelazimisha Wanamuziki Wanaowapigia wanamuziki hawa kupiga aina ya Muziki ambao kwa namna moja umeshazoeleka kwenye Jamii.

 2. Dada Shusho Hongera ni Sawa

  Dada ata mimi na penda manyimbo zako enye inanipaka moyo kama vile UNIPE MACHO NIONE.
  SASA dada ujuwe wewe ni muhubiri ya NENO la MUNGU kupitiya ma nyimbo enye unazoimba .sio ya kukwenda kwenye mashindano ya dunia iyi uju wote awakuje na nia moja .pole sana endelea na nyimbo zako na kumutumikiya Mungu wetu.adui iko na njia mingi ya kutupima . Basi kama nimesema makosa munisameha wote wasomaji enye ilikuwa kwenye mafikiri yangu iyi

  Mubarikiwe wote

 3. Dada Shusho,
  Sifa zimurudilie Mwenyezi Mungu ambae amekuwezesha. Nasikia furaha nyingi mno kwa habari za kufaulu kwako..
  God bless you.

 4. Hongera sana dada Shusho. Napenda nyimbo zako Mungu azidi kukuinua zaidi kwa utukufu wake.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s