Je Mafundisho haya ni potofu?

false

Wapendwa,

Miongoni mwetu kuna wapendwa ambao ni wavivu wa kusoma maandiko na vitabu na mitandao ya kutosha kuwapa elimu pana. Wengi wetu si tu kwamba hata Biblia hatusomi bali hata vitabu vya waandishi mahiri na wazuri hatusomi.

Tunapaswa kuelewa kwamba mafundisho yafuatayo ni potofu ukubali au ukate:

1. Mafundisho kuhusu NYOTA ZILIZOIBWA
2. Mafundisho kuhusu kutoa ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato
3. Mafundisho ya kukataza wanawake kuvaa nguo za suruali ili hali zinafunika uchi na mwili wao kwa usahihi zaidi kuliko hata siketi na gauni,
4. Mafundisho kuhusu kuwazuia Watumishi wa Mungu wasioe
5. Mafundisho kuhusu SABATO kwamba ni sku ya Jumamosi na mtu asiyeacha kufanya kazi siku hiyo eti anakuwa mtenda dhambi
7. Mafundisho ya Kupaka watu MAFUTA eti ndio UPAKO hadi wengine huitwa wazee wa UPAKO,
8. Mafundisho ya kuhimiza UTAJIRI kwa masharti ya kutoa kwanza SADAKA kwamba ndipo utatajirikka badala ya kuhimiza watu kujiendeleza kiujuzi, kielimu na kufanya KAZI ili kupata utajiri.
9. Mafundisho ya kuzuia wanawake wasiwe viongozi wa kanisa, au wasiruhusiwe kufundisha,
10. Mafundisho ya kuzuia wanawake kufanya kazi zenye kipato kwa misingi ya dini au mafundisho,
11. Mafundisho ya Malango……, Mzaliwa wa kwanza…., mafundisho ya kufanya jambo fulani ndipo upate kitu fulani kwa Mungu,Na mengine mengi kama hayo.

Wapendwa Yote hayo mimi nayaweka kuwa ni mafundisho yenye utata sana na bila kujizungusha naomba niseme kwamba ni POTOFU.

Kama kanisani kwako mafundisho kama hayo bado yapo, na yanasisitizwa kila siku, tafakari upya kisha chukua hatua.

–Mr. Milinga

Advertisements

43 thoughts on “Je Mafundisho haya ni potofu?

 1. Ambokile Gwakisa,

  Mbona umekuwa mwepesi sana wa kutema cheche za laana kana kwamba wewe peke yako ndo kanisa? Wewe mwenyewe huonekani kuyaelewa sawasawa mambo yaliyo kwenye orodha ya mtoa mada!

  Laana isiyo haki haimfiki mtu, jaribu kuchambua hayo mambo ili tuone uelewa wako ulivyo juu yake, siyo kutema tu cheche za laana isiyo na sababu!

 2. Shida Ipo Kwako Wala Sio Mafundisho Tena Inawezekana Ktk Mambo Ya Mungu Ni Mjinga Na Mpumbavu Kiasi Cha Kutosha Ndo Maana Hata Hekima Punje Ya Mungu Kwako Ni Kitendawili,ila Tu Cha Kukutadhalisha Ni Kwamba Usiwe Mwepesi Wa Kuhukumu Kuwa Kitu Fulani Ni Potofu Kama Ukijui Au Kama Ujafunuliwa Na Mungu,kwani Inawezekana Biblia Huielewi,cha Mwisho Nikwambie Kwamba Usipo Rekebisha Mtazamo Wako Mwisho Wako Ni Jehanam Na Utakumbuka Haya Nilio Kuandikia Labda Uwe Umekusudia Kumtumikia Shetani Tena Usipo Badilika Maisha Yako Si Marefu Na Hii Itakuwa Ishara Kwako Na Kwa Wale Wenye Mtazamo Kama Wa Kwako,kabla Ujasema Chochote Muulize Mungu,mulize Mungu Maana Ya Suruali Na Sababu Ya Kuvaliwa Na Wanawake,pia Mulize Mungu Maana Ya Neno Malango Na Kwanini Lipo Kwenye Biblia Na Mjaribu Huyo Mungu Wako Halafu Uje Useme Ulicho Sema Uwezi Ukapeleka Wana Wa Mungu Kuzimu Kwa Njia Hiyo Hapo Umegonga Mwamba Yesu Yupo Makini Kwa Kaoisa Lake,tena Sijakuwekea Vifungu Kwani Kwako Ni Upuzi Kimekujaa Kiburi Cha Uzima.

 3. lazima uwelewe dhana nzima nini maana ya kitu potofu mafundisho yako hujafafanua, fafanua jenga hoja za kutosha

 4. Milinga Mtoto wa village!

  Hongera kwa kuja tena na kusoma kila nukta michango hapa, maana ulipopotea, ulitukatia hamu kuendelea kudeal na hoja zako sana maana Mtu washusha zigo pwaaa kama Mafarisayo kisha waende New-Zealand kula ‘’ngoko’’, sie tunabaki kumenyeka wenyewe na zigo ilo ambalo hata kwa kidole chako huligusi.
  Hata ivyo tulijitia moyo kulisogeza zigo, so far tumemaliza HOJA zako on Zaka, Nyota pia nilideal na hoja no. 3,9,10 kwa mpigo kama moja chini ya kichwa cha somo nilikiita ..’’Makatazo dhidi ya Wanawake ktk Biblia’’…Tafuta humo blog subject inaitwa… ‘’Mafundisho kuhusu wanawake yanatafsiriwa vibaya!!……kuna kazi nyingi za Wapendwa umo… na ilo somo langu kwa hoja 3 at per, kazi unayo maana comments ni 137… a good friendly adhabu, uyasome yote hayo.ili utubu vema mambo ya kuroka kambi bila taarifa, karibu uko. Hoja zilizobaki, labda ututie moyo tena maana Mchungaji aliponyukwa na kondoo wakasepa! Kurudi ni neema aisee.

  Press on.

 5. Wapendwa,

  Nimepitia michango ya wapendwa wote. Hata ya Edwin Seleli mtoto wa town nimeipitia neno kwa neno pamoja na kwamba ameandika mambo mengi sana.

  Siyo kwamba niko mafichoni, wala siyo kwamba nimetoa hoja na kukimbia mitini, la hasha bado nipo na ninaendelea kujifunza sana. Yaani nimejifunza mambo mengi na ninaendelea kufuatilia michango ya wapendwa.

  Hata hivyo, napendelea kuona mpendwa anayechukua angalau mada moja tu akaichambua kama alivyofanya kaka Lwembe na kaka Edwin Seleli kwenye mada ihusuyo NYOTA KUIBIWA au kaka Sungura alivyochambua mada ya ZAKA.

  Mimi nimeleta mada zenye changamoto tu kwa sasa makanisani ili wapendwa tujadili ukweli au upotofu. Sina haja ya kuja na msururu wa maandiko kuthibitisha upotofu huo ila kwa mpendwa mwenye upeo mkubwa anaweza akaleta uchambuzi wa mada angalu moja tu akatueleza yeye anavyoielewa.

  Mada inaendelea, na mjadala unaendelea.

 6. wapendwa kichwa hapo juu kinajieleza chenyewe,ni kwamba anatakakujua kama hayo mafundisho ni potofu au la?.kiukweli ni hekima ya MUNGU tu kuyapambanua hayo yote.sio sahihi kusema mafundisho hayo ni potofu,jua kwamba MUNGU hulituma NENO Kwa wakati na kwa watu wake na ndio tunayaita MAFUNUO, hili kuponya watu wake.BARIKIWA NA BWANA.

 7. Jamani hizi ni siku mbaya kila mtu na asome maandiko huku akimuomba roho Mtakatifu mfafanulie ilie aweze kukaa katika nuru ya Bwana maana ss tafasiri za binadamu zimekuwa nyingi sana

 8. Bwana Yesu asifiwe,

  Inatakiwa watu wajue lengo ya maombi. Nadhani maombi ina preventive and curative purpose. Tukiwa kwa upande moja tu tunapoteza ingine…

  Mubarikiwe.

 9. Shalom!
  Tunapaswa kujua kwa lazima au kwa hiari kwamba “mtumishi aliyeitwa na Mungu anaweza kuwa sauti ya Mungu kwa watu”, Lakini si kila mtumishi wa Mungu ni sauti ya Mungu kwa ajili yako…….

 10. Hello SG,
  Napenda nami nichangie ktk hoja izi maana naona mtumishi huyu mtoa hoja alisha kwenda kwa muda JUU, atatukuta tunaendelea kula gombo hapa barabara kabisa pasi na shaka yoyote. Ninapenda sana nani baraka kwangu( to be always sincere) kuchangia/ kuongea nikiwa mimi halisi, free, relaxed, peace, social, straight and little very serious kwakua pretedence hunishinda mie.Maoni yangu ni kwa njia aidha za moja kwa moja na fupi yaani‘’tit for tat’’ and ‘’Ki-summary-summary’’ au pia kujadili kitu/kuchambua jambo Ki-Biblia, Kimaisha, Akili, Ufahamu huu huu wa kawaida pia Common senses ambazo husaidia kung’amua mambo, nyenzo za kupata maarifa/taarifa ambazo Bwana alitoa kwa Wanadamu wote, hauhitaji shule kubwa sana ya Chuo. Nitatumia pia Mahojiano nk na kwa kufanya ivyo, nina nia kabisa ya kuongea mambo mengi au machache ktk kitu/hoja moja ili kuleta tafakari nyingi ambazo mwisho wa siku zitatusaidia aidha kujijibu wenyewe au kutazamisha jibu lilipo au hoja gani ya kuchukua na kuiishi iyo.Nitakua nanukuu ya Milinga kisha nachangia yangu, leo naanza na hoja yake ya kwanza.
  Milinga:’’Mafundisho kuhusu NYOTA ZILIZOIBWA’’
  Maoni:Perfect statement kabisa na si tu ni potofu bali pia ni uhuni na dhambi kutapeli watu innocent labda wale wanaofuata-fuata mkumbo na fasheni za mbwembwe za utumishi wa kileo. Embu fikiri very seriously fact hii uone/u-feel watu wanavyotuchezea akili. Tunatoka nyumbani kwetu twaja ibadani sunday au seminar uliyotualika kwa matangazo mengi sana kama kuuza bidhaa vile, twajua twaja kusikia toka mbinguni Mungu anasemaje/ anatupozaje/anatutiaje moyo/ atuonyaje/tunasongaje mbele kwenye huduma iliyokwama au inayopata changamoto ya kuendelea, tufanyaje kupata mpenyo au karama hazitendi kazi ipasavyo, tufanyeje watu ktk mitaa yetu au ktk ukoo hawaookoki kirahisi pamoja na kuwashuhudia na kuishi kati yao kwa kiroho chote full cha Bible na cha man-made e.g kunyenyekea mpaka kuongea taratiibu na ku-create sura ya kulegea/ya upole na mororo hata kutembea mwendo wa pole, tufanyeje mchumba katuacha/katupiga chini wakati tulisha ji-commit mambo mengi naye na moyo tulishaufungua kwa ajili yake tu, ndugu wa mume wangu aliyefariki wanata ninyanganya mali zangu kwa jina langu, alizoniachia mpenzi wangu kabla hajafa, watoto wanafukuzwa shule karo kubwa sasa, kiwanja cha kanisa kinataka kununuliwa kwa utapeli/dhuluma na ubabe ili wajenge msikiti ilihali tulifunga na kuomba siku 40 Mungu akatupa kupitia Rashidi mjahidina kabisa aliyeamua kwa nia safi na kwa procedures zote kutuuzia na tulishamalizana nae kwa taratibu zote sema tu ukoo/jamaa na jumuiya ya waislamu wenziwe wameshikilia bango kua ni kufuru kuuza kiwanja kwa ‘makafiri’ ivyo Rashidi kaamuriwa arudishe ela yetu na kisha kukiuza kwa muislam, kuhubiri Injili kunazuiliwa na wapendwa kadhaa wamewekwa rumande,mume mkorofi mpiga mke anakuja kanisani analia lakini akifika geti la church anajitia moyo kufuta machozi maskini, au mke tukutu mdharau mume mwenye maneno kama filimbi uwanja wa taifa mechi kati ya Yanga na Simba na anakufanyia ivyo akiwa na confidence over 500% kwakua anajua wote ni wana wa Mungu na kama mume bora wa KiBiblia na wa mbinguni, kamwe hutaleta mwali mwingine na wala never on earth utakuja mduda ngumi moja tu ndogo na laini angalau mara moja kwa mwaka mzima, kazi tunazo lakini kipato kidogo na mahitaji ya michango mtaani pale, ktk familia, ukoo, kanisani ni mingi na bado kodi ya chumba, kibanda, nyumba, kioski, genge, hujalipa wala fuel ya mwezi hujatenga ela yake, magari yetu yamepata ajali na spare parts bei mauaji, umelipia kiwanja million 10 kisha unagundua umetapeliwa kwakua unashangaa mnajikuta wamiliki mko 3 na wote mna hati kabisa toka serikalini, Nchi inakwenda kama shamba la Bibi, kila mtu anachota tu na hatimaye akina mama wanajifungulia vibarazani na kulala chini kisa hakuna vitanda, wakati mwingine twaja na mizigo, challenges, confusions/ michubuko, michano kuraruliwa na makwazo ya wanadamu tuliyokutana nao week nzima shuleni, vyuoni, hudumani, biasharani, majirani,kanisani,ofisini, kati ya ndugu na jamaa wa karibu, umesikia Mungu amekuita ktk utumishi na umeshakwenda uko remote area Mtwara na tayari umechapa Injili lakini ni mwaka sasa Mkeo aliyekulia Mijini na Majijini amekataa kuku-join ktk huduma uko village, hataki kuacha saloon za Dar, umeomba na kufunga mpaka basi na ndio kwanza anafungua saloon yake Ilala mitaa ya kati,
  Yaani tuna mambo yote hayo tumebeba na tuna jua kwa hakika Bwana usema na kanisa lake, twaja ili Bwana aseme kupitia madhabahu na weye kiumbe pale uliyerehemiwa tu na kua trusted na Mungu kusimama mbele yetu kutuongoza/lisha mana safi, halafu ati una-take advantage ku-coin somo/fundisho liendane na hali halisi ati nyota zetu zimepigwa kabari/roba au vibaka wa ulimwengu wa roho waliiba! Zipi nyota zenyewe izo kwanza? Mbona Mitume na Manabii hawakuwahi kua na ‘’ze nyota kuibiwa doctrine’’? So wewe unayeleta karne hii ilo dude ndio spesheli mpendwa mwenye Roho, ops! I mean roho sana na una pata vitu vikali direct toka kiti cha enzi nini? nondo ambazo huwezi au eti si lazima uzikute ktk Bible! Yaani mpaka inatia hasira because mnenaji anajua kabisa kati ya wasikilizaji wake, si watoto wadogo kiroho au watu wa dini, anafahamu kwa hakika sisi hatutaki longolongo kwakua tumelishwa/tunajilisha Neno( sound doctrine) la msingi la Mitume na Manabii wa KWELI na above all, tumefurikishwa Roho Mtakatifu wa Mungu, Roho ya Mola mwenyewe inayotusimamia na kutuongoza ktk kweli yote hata kutunong’oneza na kutung’amulisha kujua kati ya madude na madudu Vs. KWELI ya Neno still bado mtu anasimama confidently kufundisha hayo? Nakwambia kwa wana wa Mungu aina yetu, hatumkawizi, ni haraka sana tunamshusha chini ya altar au tuna mzimia mic au tunamtumia kikaratasi pale juu kua akatishe mahubiri muda umekwisha au akishuka baada ya kuachilia madude yake, tunapo mpokea mic yeye akiwa amekaa chini pale anapumzika na kunywa maji, tuna-crush alichosema MBELE YAKE ili si tu kanisa lipone na yeye mwenyewe apone mara 3 na next time akikaribishwa mahala, kabla hajatiririka madude hayo tena, He/She will think twice.

  Tutateda ivyo kwa ‘mtumishi’ wa ivyo na bado inakua kiroho safi tu na kama unadhani si sawa, basi angalia kama unaweza mzidi ukiroho rafiki na kaka yetu yetu mpenzi huyu aliyefanya ivi Yoh.2:11-17, Mat.21:12-13!!!! Ingawa specific context ni watu kugeuza nyumba ya Baba yake pango la wanyang’anyi nonetheless, general context does serve the purpose hapa pia kua SOME watumishi wa ivi leo na hayo wayafanyayo ni sawa tu na kugeuza madhabahu kijiwe cha kuchonga channels za kuleta watu na kuwavuna. Pia nampenda rafiki huyu kwa ukali na hasira zake takatifu dhidi ya watu wanaochezea kanisa, aliposema si tu mwanadamu lakini hata kiumbe toka mbinguni akiwachanganya tu wana wa Mungu au watu kuwafundisha Injili nyingine basi na alaaniwe Wagal.1:6-10.Watu wengine kwa jinsi walivyopitilizia utani kwa maisha yetu ya kwenda kwa Baba, some of us hatuhitaji kua kiroho kudeal nao! Unashituka ee! Ask Master kwa nini hakuanza kuwaombea au sijui kutumia yale mambo yetu yale tunapendaga ya ‘mpendwa plz tumia hekima eee’’alipokua ana-deal na wale waliopitiliza uhuni pale hekaluni lakini alitengeneza kikoto/fimbo na kuwanyuka huku akihakikisha njiwa wanatambaa na kupaa wakiimba pambio kuelekea wawinguni na mbuzi, kondoo, ng’ombe waki-dance kwa raha zao kuelekea mabondeni malishoni bila kusahau machenza na chungwa zikitambaa usawa wa chini kuwabariki watoto bila shaka waliokua wanarukia 1,2,3 na hata pesa zilizosambaa chini baada ya kubinua meza cha ‘burea de change’’ dealers wale, zikasaidia bajeti zao watu walikuwepo ktk tafrani ile.
  Mambo ya sijui nyota zimeibiwa, sijui tufanyiwe maombi spesheli ili kuzi-win back au sijui kuna vitu havijakaa sawa ivyo inatupasa kumsikiliza nabii na mtume fulani kisha atufanyie maombi spesheli ku-settle ishu kadhaa ambazo baada ya kuookoka, hua zinabaki au hazikukamilikaga zote, yote mafundisho ovyo kama hayo, yanatupiliwa mbali na Neno la Mungu lililo wazi kabisa mfano Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake” Ukichunguza kwa makini maandiko haya utangundua kwamba mtu anapookolewa kwanza “ROHO YAKE HUZALIWA UPYA” na kisha “HUTOLEWA” kwa 100% kutoka katika ufalme wa shetani (kama vile wana wa Israeli walivyotolewa Misri) na “HUINGIZWA” kwa 100% katika ufalme wa Mungu (kama vile wana wa Israel walivyokuwa chini ya utawala wa Mungu walipokuwa wakiiendea nchi ya ahadi)!Ktk 1 Yohana 5:19 “Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu (sisi tuliookoka); na dunia yote pia (wote ambao hawajaokoka) hukaa katika yule mwovu”. Sisi tu wa Mungu na kwa maana hiyo tu chini ya baraka na wasio na Yesu wao hukaa ktk yule mwovu kwa maana hiyo wako chini ya laana na madude yake yote e.g mambo ya nyota, unajimu wa majini, elimu dunia, nguvu za giza na wanga, roho za uharibufu na mafundisho ya mashetani na kuzimu nk!
  Yesu alisema mtaijua Kweli nayo Kweli itawaweka huru Yoh.8:32. Unajua wapendwa kujua Kweli= Neno au from Neno, ni raha, ulinzi na confidence tamu sana, mtu atakuja na maneno yake, mbwembwe nyiiiingi, vurugu kweli, matangazo weee,kelele, tambo nyingi, show off sana, we na Kweli yako ndani moyoni umejazaa, aaa huna presha, ana piga hadithi na longolongo zake hapo madhabuhuni au redioni or ktk Tv then una choice aidha kumsikiliza, au kumwacha uende kwenye shughuli za maana nyingine au ukiwa jasiri kama wengine siye bila aibu wala kusitasita maana na yeye hakua na soni na alikua na uthubutu huo na kama yuko kanisani kwako/ kwenu, simple tu! no maombi ya kukemea apigwe ganzi, no so called hekima inayocheleweshaga mambo sometimes bali unamshusha chini au zima mic au crush akiwa palepaple au andika kinote na mtume Mze/ shemasi kumuwekea pale mezani akiwa juu kua amalize in 2 minutes muda kwisha, kuna other internal church activities/ announcements/arrangements.
  Kweli nyingine ni hii..2Wakor.5:17-‘’Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama yamekua mapya’’. Sasa ako kanyota kalikoibiwa ka nini kukataka tena? Uko kalikokwenda si safi tu maana sasa ni mambo mapya na kila kitu chema tunapewa. Presha ya nini kujshughulisha na kuleta manyota yaliyofutwa na kuanzishiwa maisha mapya? Why kutafuta/kuunda na kukomalia ‘’fruitless UnBiblical spiritual home works izi’’? Si unaona tu ni uhuni wa madhabuhuni tu wa BAADHI ya wanadamu kuunda mambo ili kupata noti za kuishi mjini na kusaidia family na koo zao kisha kununua magari ya hammer, mashamba na plots Dar, Moro, Arusha, Mpanda, Iringa, Mbeya,Mwanza na pia kudaka vitalu vya kuwinda tembo wetu na na mashimo ya dhahabu na tanzanite tu!
  Nitaendelea na hoja ya 2 mpaka mwisho kuchangia
  Press on kunoana chuma kwa chuma,Amen.
  Edwin Seleli

 11. Asante sana Ndg Lwembe,

  Wanaotufuata wanaelimishwa. Ndio maana mazungumzo yetu ni ya maana sana. Ndugu Milinga ajitokeze ao abaki mafichoni, neno la Mungu litaishi milele. Unaposoma, usipendelee kusikia kama unavyopenda, lakini pima kuelewa kinachoandikwa. Naona ni jambo ndogo tu bado hatujaelewana. Kwanza nadhani wewe si Mchungaji(na kam sivyo samahani) kwani wengi ktk wachungaji hawafike kutusoma. Wangelifika na kudaka, makanisa yangelikuwa safi. Mimi vilevile si Mchungaji na ile ni hakika kabisa. Sasa wakati nilipotaja Wachungaji, Mitume, na Wainjilisti na nikatia kiendelesho, wewe uliwazia mambo yakuomba haihusu kila mukristo. Na kweli kam Mchungaji anajidai ya kwamba yeye pekee ndiye anaeweza kuomba na kukemea Ibilisi asiibe nyota, hapo ni upotofu, Atakuwa ametia karama za Roho Mtakatifu mfukoni mwake. Hili ni jambo linalokuhusu wewe, linalonihusu mim na Wakristo wengine waliookoka. Si hapa tunatoa injili kwenye hii blog? Ina maana tuko wainjilisti, si ndio? Yeyote anaetusoma anaona kam mim na wewe tumepatana kwa mafasiriyo ya nyota. Na mim nimeyapana kufwatana na ginsi inasikilikana ktk ulumwengu wa roho na vile Biblia inavyosema.

  Neno linalobaki ni hili: Wewe Unasema uzaifu wa imani ya mwanaadamu ndiyo tu tatizo, Ibilisi ni kam hayupo tena ao hana nguvu fulani, na mim ninasema Ibilisi yupo tangu zamani na leo angali, naye ni mwizi, myanganyi, mwongo na mushtaka.

  Kwa maslahi yako Ibilisi hana namna ya kuiba Neno Mungu aliloachilia ndani ya Mukristo. Basi tusiendelee kuomba msaada kwake Mungu? Na kama kuna kuchelewa kwa upande wa mwanaadamu kwani yeye ni zaifu, mpaka akaibwa, mim ninaamini Mungu hana kuchelewa, tuombe Mungu, ile nyota itarudi tu. Tazama, Lazaro aliekuwa tayari kaburini, it was too late for us, lakini Yesu akamtoa huko huko.

  Nakubaliana na wewe kam Ibilisi hawezi kuiba nyota kama Imani iko strong. Sasa nina swali :kuna mtu ambaye si zaifu, ao kuna mtakatifu ndani ya wanaadamu?
  Na mwizi anapoiba hafwatilie pahali ambapo kuna uzaifu? Ao mlinzi amesinzia, ao nyumba yaifungwe vizuri, …. mwizi anapata njia. Na inapoonekana ni upi uzaifu mwizi alirahishiwa, kunatiliwa mkazo mpaka mwizi labda atafute njama nyingine.

  Kama tukirudia kwenye Edeni, ni Hawa aliyeenda kumtafuta Shetani? Si Shetani aliejipanga sawasawa kama mwizi akifwatilia tu pale Mungu alietia neno? Na pale unaposema eti kam Mungu ameachilia baraka hakuna ginsi Shetani aipokonye, si hapo ndipo vilevile Shetani anapoenda ili azichukue akipitilia ku uzaifu fulani? Ao atashindwa, ao atafaulu. Na wewe nakuona tu ukiangalia kwenye ameshindwa, right Imani yako iko juu, lakini isikuzuie kufanya angalisho. Kama anashindwa ni amina, lakini akifaulu, maombi yatatumika. Shetani hana haja ya kujisumbua na binadaamu ambae hana Neno la Mungu lililoachiliwa moyoni mwake. Pale ndipo hatuelewane. Wewe unataka sema kama Mungu ana watu wake na Shetani anabaki na wengine. Kuna vita, Shetani bado kuachilia mpaka anapotupwa motoni. Na kama sivyo kama watumishi wa Mungu hawapo na wa Shetani hawapo vile vile.

  Tena ukasema kuna wenye wamekwisha kuwa n’gambo, pale n’gambo ni wapi? Una uhakika wako mwishoni? Je wote si tungali njiani, na imetupasa kupiga vita vizuri?

  Kuhusu maombi, hata Petro pamoja na upako aliyokuwa nayo, wakati alipoingizwa katika kifungo, Biblia inasema kam, kanisa lote walimuombea, si ndio?

  Kuhusu Shetani kutatiza wakristo, Paulo ana jambo la kuzungumza: “2 Wakorintho 12:7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi”
  Hii si inatuonyesha kam Paulo alitatizwa na Ibilisi? Kama alishindana, ina maana aliendelea kupiga vita kwa kuomba na kwa mwisho akatamka ya kwamba amepiga vita vizuri na mwisho amepata taji. Si vita yake ilidumu? Ndio maana katika uinjilisti wake aliweka mbele neno kupendana, kuchukuliana na kuombeana.

  Kuhusu uzima wa milele uhakika inakuwa ile siku mtu anapata wokovu, lakini Shetani atakuwa akinguruma kama Simba akitafuta ammezaye. Atakayeshinda atafika n’gambo. Na iwepo atashindwa kiisha aendelea kujifariji kama yeye iko n’gambo hataomba na atakataa kuombewa na hapo atajikuta ndani ya meno ya ule simba mubaya.

  Ok, nafikiri ndugu yangu, sisi wawili tumetosheka, kama kuna maswali ya wengine tutasema tena.

  Mim naona hivi:
  -Sitakuhukumu kama unakataa kuombea mtu mukristo ao wewe kuombewa ukilenga una Neno la Mungu na Shetani hawezi kukujongelea ao kujongelea mukristo mwenzako. Nimeona hiyo ni msimamo wako.
  -Mim nitajiombea, nitahitaji maombi ya wengine wakristo wanaookoka, tupendane na tuchukuliane kwani safari ni ndefu tena ya hatari.

  Na Mungu wa Mbinguni atubariki sote.

  Amina.

 12. Ndg Ziragora,
  Ubarikiwe ndg yangu!
  Labda niseme kwamba nimeyaona malalamiko yako, na kwamba kwa sehemu yawezekana hujafika katika kina cha jambo hili la “nyota” licha ya tafsiri nzuri uliyoileta. Mimi nimefurahi pia kuwa angalau suala hili la “nyota kuibiwa”, umelipeleleza hadi huko Edeni, huo ni msingi mzuri wa kuanzia ili kupata ufahamu wa jambo hili, maana mambo yoote, huko Mwanzo ndiko yanakoanzia; ndipo Maandiko yanapongelea “kuibiwa hilo Neno”, basi utajua kwa uhakika ni nini kinachotokea badala ya kuyachukua maneno katika maana yake kimsamiati, halafu ukajifunga nayo miguu huko mbele, kisha ukashindwa kuendelea!

  Kule Edeni, nyoka alipomvizia Hawa, alijua kwa uhakika anachokifanya ni nini, yaani aliijua Sheria ya Mungu ihusuyo kuliamini Neno lake, ile IMANI; kwamba Mungu hamvumilii yeyote anayelitilia shaka Neno lake! Kwahiyo, kwa kadiri utakavyoyarudia mazungumzo yao, baina ya nyoka na Hawa, utaona kwamba, lengo la nyoka lilikuwa ni kumfikisha Hawa katika hali ya kulitilia shaka neno moja tu la Mungu. Naye akaipokea hoja ya nyoka, kwa sekunde tu, na lile shaka lililozaliwa hapo, likalipuka kuwa dhambi, uharibifu na kifo! Haya yaliwatokea baada ya kuipokea injili mpya ya nyoka juu ya Neno la Mungu lililotangulia, wakawa na ule mchanganyiko unaoleta kifo! Mtazame Petro, shaka ilipomuingia, Mt 14:29-31 “Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?”

  Huo ndio mpango wa Ibilisi, ndg Ziragora, kukutia SHAKA! Basi ule mpango wa zamani wa nyoka wa kule Bustani ya Edeni, umekuwa ni wenye mafanikio makubwa kwa miaka 6000, naye amekuwa mtaalamu katika kupanda mbegu ya mashaka mioyoni mwa watu. Alijifunza muda mrefu uliopita kwamba hakuwa na haja ya kukabiliana na Biblia nzima; anachohitaji kufanya ni kumleta mwathirika wake katika kulitilia shaka neno moja tu. Kisha SHAKA hilo, hufunguliwa mlango wazi na kuenea kutoka Mwanzo hadi Ufunuo!! Huo ndio ukweli wa mambo, naye angali anaendelea na jambo hilo kwa Injili hata leo, hapo wahubiri wenye Upako wa Siku za Mwisho, wanapoyafundisha kama hayo ya kuibiwa nyota wakiwaondoa watu katika kulitazama Neno la Mungu ambalo ndilo “Nyota” yao, na kisha kuwapeleka huko “gizani” walikowawashia vikoroboi!!!

  Hata utakapoyarudia Maandiko katika Marko 4:15, ninaamini kuwa sasa utaelewa, huyo Shetani katika KULIONDOA hilo Neno, alifanya nini; ALIPANDA MBEGU YA SHAKA!!! Ni ‘shaka’ pekee iwezayo kuliondoa Neno la Mungu mioyoni mwetu, ile Imani, nasi tukaishia katika mikono ya “warudisha nyota”!!! Tena twapaswa kufahamu kwamba, mwizi huondoka na hicho alichokiiba, Je Shetani aweza kuondoka na Neno la Mungu akakaa nalo hata leo alazimishwe kulirudisha? HAWEZI, litamuua, Neno hurudi kwake Mungu, zile Baraka!!!

  Kwa mfano, mhubiri anapokazana kulifundisha kusanyiko lake likiri kwamba, “Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye (Yesu) kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu” 1 Yohana 1:10; jambo hili hudhihirisha kwamba amevamia kazi, maana ujumbe huo ni wa kiinjilisti huko nje, kwani hao walioko kusanyikoni hapo, ni lazima watakuwa ni hao walio ondolewa dhambi zao hapo walipoisikia Injili hiyo 1Yn 1:10 na kuiamini na kisha kubatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo ili kuziondoa hizo dhambi unazozirejea katika hiyo 1Yohana 1:10!!! Nalo kundi hili linao ukiri mwingine: 1Yoh 3:9 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri…” Unaona ndg yangu? Tumekwisha livuka Jangwa, tuko katika Nchi Mpya! Bali nafahamu pia wako wale waliovuka kuingia Nchi Mpya, lakini walirudi tena huko ng’ambo kwenye mafundisho yao ya “kuibiana nyota” na kuzirejeza, kwa hiyari yao, naye Joshua aliwaruhusu kurudi huko kusiko na Ufufuo, kama ambavyo nayaona makundi makubwa yakirejea huko kwenye mizimu!!!

  Pia sijajua kinachokusumbua kuhusu Kum 28:14 ni nini. Basi kama kwa upeo wako Ibilisi hafunikiki, na huo uhakika unao nipa kwamba yupo pale pale, Imani i wapi basi? Au Kristo aliwafia hao manabii na mitume na wainjilisti nk ili hao ndio wasishindwe na Shetani, hata wazivunje kazi zake ili mdhaifu mimi nipate kuishi chini yao kwa ulinzi?? Au huko ndiko kufunga na kufungua mnakokurejea katika Maandiko katika namna ya kuyafungia makusanyiko yenu yasiufikie UHURU wa Neno? Nabii au mtume wa kweli atawapa kusanyiko lake silaha ya kupambana na Shetani, Neno la Mungu, na si kuwatisha na kuwaweka nyuma yake ili wabaki hapo maisha yao yoote wakimuogopa Shetani asiwaibie nyota zao, kama mnavyofanya ninyi!! Shetani hana “Nyota” za kutapika, acheni vichekesho, Shetani ammeze Mungu?!!!

  Halafu, wee Milinga, utakuja fukiwa huko chimbo, tinga tinga linapita huku juu, toka huko chimbo, njoo umjibu Ziragora, si unaona, eti Mungu kamezwa na Shetani!!!

  Mbarikiwe nyote, kwa kadiri tunavyoendelea kujifunza, maana Injili si lele mama!

 13. @Alphonse Ziragora,Mungu akubariki kwa maelezo yako yaani umenibariki na ninakubaliana na wewe.

 14. Naam Sungura, ni kweli, niko salama, nawe naona u salama pia, ashukuriwe Bwana atutiaye nguvu!

  Nikilirejea swali lako, naona SG wametufungulia thread ihusuyo jambo hilo, kwahiyo ninaamini kule kutakuwa na maelezo ya kutosha kukidhi haja yako kuhusu hilo.

  Bali kwa suala la, ”Kwa mfano: mhubiri anayewasimika wanawake kuwa wachungaji…”, jambo hili ukilitazama katika mkondo wa historia ya kanisa, itakuwa rahisi kuliona kwamba, Kanisa halijawahi kuwa na “mchungaji” mwanamke wala nabii wa kuliongoza kusanyiko (ukimuacha “nabii” wa Wasabato, mama Ellen White au akina Phoebe Palmer), kwani Msingi walioujenga mitume ulikuwa ni imara, maana ulijengwa kulingana na mfumo halisi na asili wa maumbile, sambamba na mapenzi ya Mungu, ule ufunuo!

  Hata Katoliki walipoikalia nafasi ya wao kuwa ndio “Kanisa”, waliendelea katika mfumo huo, ingawa wao walimchagua “Bikira Maria” wakimuweka katika nafasi ya “Muombezi”, kiroho, bali kwa jambo la kuwaweka wanawake kuwa mapadiri au maparoko, hilo hawakulifanya. Na hata Uamsho ulipoanza, katika maana ya “Reformers”, kutoka kwa Luther hadi tunapoifikia Pentekoste, hapo 1906, hakujawahi kuwako na wachungaji wanawake!

  Wanawake waanzilishi katika pilika za uchungaji walikuwa ni wake za wachungaji! Basi hata huu mfumuko wa wanawake wachungaji katika Upentekoste, na madhehebu mengine, umeshika kasi katika miaka ya themanini hapo wanaume viongozi walipo compromise Neno la Mungu, na hao wanaume wakaishia kujiaminisha kuwa Mungu amewatuma wanawake nao kuhubiri Injili, huko ndiko kuwasimika nilikokuongelea!

  Hilo ndivyo lilivyo katika urahisi huo, ndg yangu Sungura!

 15. Ndugu Lwembe,
  Ubarikiwe, na ukipenda Mungu atakuwezesha.
  Nawaza mpendwa, ungelitumia njia nyingine ku support hii hoja no1 ya Milinga bila kuvamia maondiko yangu, kuyageuza ao kuyasoma vibaya. Ku hii topic sijawai kuwa kwa upande wa Milinga. Ni kweli simchukie, nampenda sana kama binaadamu aneestahili heshima. Sione mahala umetaja niliposema Milinga ana haki. Na iwepo atakuwa hata na nusu ya haki ktk point ingine sitasitasita kuwa kwa upande wake kwani hapa hatutumie ushabik, tupane neno halisi. Ninachoona pia ni kama umepinga Milinga kwenye point yake ya 9 inayohusu kuzuia wanawake wasiwe viongozi wa makanisa….bila kumpa andiko.
  Nafikiri ungetumia hikima ungeliniuliza nikupashe zaidi namna gani neno la Mungu, ambalo ni baraka(nafikiri hautakanusha) inawezaibwa , ni nani anayeweza kuliiba na ni nani anaeweza kuibwa. Bila Shaka utakuwa kwa upande wangu nikisema Mungu yeye hawezi ibwa na Ibilisi.Lakini hapa hatuzungumzie Mungu kwani hana uzaifu yoyote. Ao unafikiri wakristo tunaishi ndani ya dunia ambamo Ibilisi hayupo ? Bibilia inasema wazi kama » Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye(Yesu) kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu :1 Yohana 1:10) »
  Hoja ya Milinga ina tamko tatu kubwa : « nyota », « kuibwa » na « upotofu »
  1. Kwanza nilipana msimamo wangu kam mafundisho hayo si upotofu.
  2. Nikafasiri maana ya nyota. Nashangaa kwa nini unaumwa kwa sababu nilifasiri ile neno. Wala wewe ulitaka liendelee fichwa kusudi wewe na Milinga muendelee na msimamo wenu unaojaa utata. Nikaonyesha moja kwa moja ktk Biblia kam nyota ile ni Neno la Mungu ,maana yakeYesu Kristo, na bila shaka ni Baraka kwani Baraka ziko tu palepale. Nafikiri mpaka pale, mpendwa, hakuna utata fulani.
  3. Labda haukusikia namna gani ile neno inawezaibwa japo hio nilifasiri ya kutosha. Hatutachoka, ebu upewe mafasiriyo zaidi. Ninaanza nikikuonya kam usidai unasoma mingi wakati unashindwa kusoma na kusikia ukarasa moja tu.
  Usikamate mukristo kama ni mtu aliefika mbinguni tayari, ambae hapigane tena na Ibilisi, ambae hakutane na miiba na michongoma, ambae hana tena kuinuka na kushuka, ….
  Nilisema waziwazi kam anaeiba Neno ao Nyota ni Ibilisi, kwa nini haukushika ile ? Na nikasema aniiba namna gani; Ni wakati anapopoteza mwanaadamu akiwanyanganya ile Neno. Labda ungeliuliza mafasiriyo zaidi na maandiko mengi kama hauelewe namna gani Ibilisi anaiba Neno la Mungu ambalo mwanaadamu aliloshika moyoni.
  Mambo ilianza hapo Eden. Adamu alipewa Neno la uzima lakini Ibilisi alipofika kalibeba na akatia neno tofauti :”Mwanzo 2:16-17: Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”
  Ibilisi alipofika akasema:”Mwanzo3: 4 -5: Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
  kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

  Utasubutu mpendwa kusema kwa mtandao huu kam Baraka waliokuwa nazo Adamu na Hawa kabla shetani kuwanyanganya neno la uzima ndizo waliendelea kuwa nazo kiisha Ibilisi kuwavamia?Ao kama neno la Mungu halikuwa mioyoni mwao? Huone kama Hawa alilitamka kama Mungu alivyolisema?

  Wewe unasema kam mtu anajipotosha mwenyewe, ni mojawapo wa maneno ya Biblia, lakini je muanzilishi si Shetani? Nawaza hautakuwa kwa upande wa Shetani ili naye umtetee!

  Shahiri ni nyingi kabisa, hatutakawa pale,nikupe ingine moja tu :
  « Marko 4 : 15 Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. »

  Nani awezae panda mbegu moyoni mwa mtu isipokuwa Mungu ? Nafikiri umeona kamaShetani aweza kuiba Neno. Na kama ulisikia connection ya neno na nyota,sione tena fasi utakapopotelea.
  Wakati unapotaja Kum28 :14, unawaza umefunika Ibilisi ? Nakuhakikisha Ibilisi yupo pale pale. Ndio maana Mungu akaleta manabii, mitume, wainjilistiili,…. wavunje njama za mwovu, wamunyanganye nyota anazoiba usiku kama mchana. Hapa ndipo uamzi iko :wala utabaki ktk kutofahamu,nyota yako iibwe ao utapata maarifa na utaomba Mungu pamoja na kuombewa na watumishi wa Mungu ili nyota yako Ibilisi ayitapike.Watumishi wa Mungu wana uwezo ya kufunga na kufungua.Kwanini wasifungue kilichofungwa na Shetani ? Ao unakuwa shabik wa Shetani kiwango umtetee tusimguse. Upende,usipende atatapika nyota za wakristo wanaotaka kwani Mungu hashurtishe mtu yeyote katika chaguo lake.
  Anyway,kam wewe bado kusikia,naamina wengine wamesikia. Si kwa bure Neno la Mungu linasema « tuombeane », Mungu anajua kam tuko vitani.
  God bless you.

 16. Hey Lwembe rafiki yangu, najua uko salama.

  Kwa sehemu kubwa mchango wako ni mzuri tu na mawazo yako uliyotuwasilishia katika huu mchango nayaheshimu. Kuna kipengele tu kimoja kidogo sana nahitaji unifafanulie, nakunukuu:

  ” Kwa mfano: mhubiri anayewasimika wanawake kuwa wachungaji…..”

  Ulimaanisha mhubiri haruhusiwi kumsimika mwanamke kuwa mchungaji au mwanamke haruhusiwi kuwa mchungaji?

  Ni hapo tu ndugu yangu!!!

 17. Ndg Alphonse Ziragora,

  Maelezo yako yamenichanganya kidogo. Mr. Milinga anasema, “Mafundisho kuhusu NYOTA ZILIZOIBWA” ni POTOFU; wewe unasema SI POTOFU, lakini maelezo yako yanaonesha kuwa unakubaliana na Mr. Milinga!! Hilo ndilo linanishangaza! Mimi nilitegemea kwamba wewe utakuja na Maandiko yanayoshuhudia watu kuibiwa nyota katika Biblia, lakini badala yake umekuja na maelezo na rejea za Maandiko ambazo zinazungumzia “nyota”

  Kwanza unatuambia kuwa, ““Nyota zilizoibwa” inamaanisha “, nyota iliopotea ao baraka zilizofungwa.”” Kwahiyo, kulingana na kauli yako, Nyota ni Baraka! Ndipo kwa fundisho lenu Baraka zinaweza kuibiwa!

  Basi na tuyaangalie Maandiko ili tuyahakiki hayo mnayotufundisha. Awali ya yote, ili mtu aibiwe chochote kile ni lazima awenacho kitu hicho kwanza. Basi hata kuhusu Baraka, ndivyo ilivyo pia.

  Kulingana na Maandiko twafahamu kwamba Baraka zote zatokana na Mungu, ule uwepo wake katika kulitimiza Neno lake alilokupa, hiyo ndiyo tafsiri rahisi ya Baraka na jinsi yake kama tunavyoweza kuiona hapa katika Kum 28:1-15. Nitanukuu kiasi:
  “Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.”

  Basi, kwa Maandiko hayo, twaweza kusema kwa uhakika kuwa Mungu alikwisha kuzitamka Baraka juu yetu, bali, ili Baraka hizo zitutimilie ni LAZIMA tuwe katika mkao wa kuitii Sauti ya BWANA, Mungu wetu. Sasa sijui suala la kuibiwa Baraka linatoka wapi? Huyo mwizi awezaye kumuiba Mungu, ni nani huyo? Huu ndio UPOTOFU anaousema Milinga kuhusu jambo hili la “Nyota Kuibiwa”!!!

  Uwepo wa Bwana unaomzunguka mkristo, ndio hiyo “Nyota” au “Baraka”; nao uwepo huo hudumu kwa mkristo huyo mpaka hapo yeye mwenyewe, kwa hiari yake atakapokengeuka “katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia” (Kum 28:14). Hapa ndipo mkristo hujiondoa mwenyewe Uweponi mwa Mungu na Baraka zake, mkristo huiacha “Nyota” yake kama wale Mamajusi walivyoiacha “Nyota” iliyowaongoza kwa kushawishika na umaarufu wa Yerusalemu, ule Mji Mkuu wa dini, wakadhani hapo ndipo alipo Mungu; kama nasi tunavyoshawishiwa na wahubiri wa “Nyota” hata tumejiondoa Uweponi mwa Mungu kuwafuata hao na sasa wanatuzungusha jangwani huko ziliko laana na mahangaiko yake!

  Basi jueni wazi kuwa Mungu ni Neno lake katika Ukamilifu wake. Na kwa mkristo, Injili waliyoihubiri mitume ndiyo PEKEE yenye uwezo wa kukuweka hapo Uweponi mwa Bwana kikamilifu kwa siku ya leo, nawe unapoisikiliza sauti yake, yaani unapoitii, ndipo Baraka hizo zitakutimilia. Kama ni kazi zako za mikono, hizo zitabarikiwa, na chchote ukifanyacho! Yusufu kule Misri ni mfano halisi wa jambo hilo. Wachawi wote wa Misri hawakuweza “kumwibia nyota” yake!!!

  Tatizo ninaloliona kwa wakristo wengi, ni kubabaishwa kwa sauti wanazozisikia, ziko sauti nyingi sana. Kuna sauti ya dhehebu lako, ambayo mara nyingi hujiwakilisha kama Sauti ya Mungu, halafu kuna Sauti ya Mungu mwenyewe, Biblia yako, halafu kuna sauti za wahubiri wa mafanikio na kurejesha nyota zilizoibiwa, wengine wanasafisha nyota, na wengine kuvunja laana, nk basi mwisho wa siku Sauti ya Mungu hufishwa kwa kelele za hizo sauti nyingine naye mkristo hujiondoa uweponi mwa Neno la Mungu na kwenda kuitumikia hiyo miungu mingine!

  Mmewaona “Waiba Nyota”? Ni wahubiri wote wasioihubiri Injili kamili kama walivyokabidhiwa mitume! Kwa mfano: mhubiri anayewasimika wanawake kuwa wachungaji, au anayewatafutia wakristo vifungu katika Biblia na kuwatisha ili waongeze matoleo apate kutimiza malengo yake ya kifedha, au mchungaji au askofu anayemiliki dhehebu, au mhubiri anayewadanganya watu kuwa wameibiwa nyota zao, msururu ni mrefu sana, bali ili uweze kuyajua hayo, ONDOKANA na UVIVU, chukua Biblia yako uyakague yote wanayokuhubiria, Mungu ni Mwaminifu, atakufunulia na kukupa kuielewa Sauti yake; “kondoo wangu waijua Sauti yangu”!!!

  Upako ulio juu ya wahubiri leo hii, unao uwezo wa kuyapandikiza mioyoni mwenu “mapungufu yoote, na tamaa zake” wanayokuhubirieni na yakakutimilieni. Jilindeni nafsi zenu, jivikeni Injili halisi iliyohubiriwa na mitume, ndipo mtakuwa salama na mta enjoy Uwepo Wake Kristo unaofungamana na Injili hiyo!

  Mbarikiwe.

 18. Naamini hamjambo wapendwa.

  Tuangalie ile point ya pili. Hatutachoka, Neno la Mungu liko kila siku lipya.

  Milinga alidai kam “Mafundisho kuhusu kutoa ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato” ni upotofu.

  Nafikiri hapa inatakiwa tumufwate vizuri neno kwa neno.

  Aliyoyasema wenda akayasikia yakihubiriwa mahala fulani na yale mafundisho yakamupotosha yeye. Baada ya pale akashika kam kila fundisho inayohusu ile topic ni upotofu.

  Ninapojaribu kumuelewa, naona kam hana tatizo yoyote kwa neno ZAKA. Hoja yake iko namna inatolewa ao namna ma Paster wanahubiri kuhusu ZAKA.

  Biblia ina msimamo tofauti juu ya zaka kufwatana na nyakati, na si kila andiko inayosema juu ya fungu la kumi ni zaka.

  Ibrahim alitoa fungu la kumi kwa Melkisedek kama shukran wakati alipokwisha kumusaidia kwa vita. Na Biblia inasema kam ni fungu ya kumi ya vyote, lakini haiseme jambo hilo kwa urefu kwani vyote ni neno gumu kuelewa wakati hakutoa ku shamba lake, viti vyake, na vingine vyote….

  Yakobo alitoa fungu la kumi kama nadhiri. Alipokimbia ndunguye Esau aliona maisha yake iko mashakani, alipoamka usingizini na akiisha ota ndoto, akasema,” Bwana ukinilinda, ninaenda salama na kurundi salama nitatoa fungu la kumi hapa hapa, na utakuwa Mungu Wangu.”

  Toka familia ya Lawi kuchaguliwa kumtumikia Mungu na kutokuwa na uriti, Mungu akaamuri ile familia (kabila) ihudumiwe kivifaa na wengine. Sadaka zilikuwa nyingi sana, na moja wapo ni zaka. Na ile zaka ilipewa limoja kwa myaka tatu, wala kwa mwaka moja, wala kwa myezi tatu, … Na kazi yake ni kulisha mulawi, mjane, yatima na mgeni anaekuwa malangoni mwa mtu wa Izraeli (muyahudi)

  Jambo lingine, utaona Biblia ikisema kam ni zaka la maongeo ao mazidio, hapana ya pato yote.
  “Kumbukumbu la Torati 26:12 Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;”
  ” Kumbukumbu la Torati14:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.”

  Katika agano jipya, mambo ya zaka hayipatikane “sana”. Yesu hakukataza kutoa zaka, lakini akaonya Mafarisayo waliyokuwa wakijihesabia haki kwa njia ya zaka.(Luka 11:42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.)

  Nataka niambie ndugu Milinga kam kutoa zaka si upotofu, lakini agano jipya haitie mkazo. Na kama ni jambo jema huko ku agano la kale hatutaweza litupilia kwani tunatumia union bible.

  Ningelikuelewa kama ungelisema kuna walimu wanaofundisha hili jambo bila kulielewa vizuri ao kwa faida yao wenyewe, wanazuia hata ile utoaji wanaohubiri wenyewe. Kwa mfano, zaka ya yote haijawai kutimizwa hata siku moja. Ile inatuma wakristo wanaogopa kutoa wasidaiwe wanadanganya Mungu. Tukumbuke kama dhambi ya Anania na Safira si kutotoa bali kudanganya Roho Mtakatifu wakitoa kidogo. Ebu sijue kama hata kutoa mingi kuliko Mungu ataikamate je.

  Hili neno lingelihubiriwa sawa ktk agano la kale, bila shaka wakristo wengi wangelitoa wakiwa na uhakika. Na kutia mkazo kwa zaka kuliko matoleo mengine ni process mbaya kwani kuna shukran, malimbuko, sadaka ya kawayida, ….
  Kwa mfano, mshahara wa mfanya kazi si maongeo yake. Nani mfanya kazi anaepokea kwa mwezi bila kulipa garama ya ile mwezi wakati anapotumika? Ukimudai fungu la kumi kwa mshahara yake yote na labda ile mshahara haitoshelee hata kulipa deni alio nayo kwa ile mwezi, utakuwa umemupeleka kuiba mwanadamu ukimpelekea Mungu, na ile ni dhambi kabisa. Biblia inasema kama ukitaka tao sadaka, na unakumbuka uko na tatizo na ndugu yako, acha ile sadaka utatue kwanza ile tatizo.

  Lakini kama kiisha mwezi ao myezi fulani, ao mwaka, mukristo akifanya account na kuona ana hakiba gani na kiisha anatosha zaka ktk ile hakiba, atatoa akiwa na uhakika kam hesabu yake Mungu anaikubali na hii itafanana na ile ya agani la kale, tukizingatia kama kuna mjane, yatima na mgenivilevile wanaodai kwa ile fungu la kumi.

  Lakini hii ya kila siku au juma ao mwezi ao upatapo, kutakuwa kusahau, kuiba watu ukimpelekea Mungu asiye hitaji hata moja, kuiba Mungu kama vile Malaki anasema, na kutojisikia amani hata kiisha kutoa kwani ingine mahubiri yanapopita utaona ungali mkosefu

  Kwa hii topic, nadhani ndungu Milinga umekuwa very agressif; rekebisha. Kutoa zaka haipotoshe mtu, lakini muinjilisti anaeogopesha watu anawazuia kutoa ao kama wakitoa wanabaki tu wakijihukumu. Ule kama iko tunamuonya.

  Asante hata hivi kwa ile changamoto, wenda watakaosoma maelekezo yote watajua wafanye nini.

  Na Mungu wa Mbinguni Awabariki.

 19. ejo mwe bandu fyo fiki yaan nyie watu ndo nn. ndugu zangu tumjue Mungu tusipotoshwe na haya

 20. Bwana Milinga usifikiri watu wamelala hata biblia husomi.swala la utoaji zaka soma malaki 3 kuanzia 7 hacha kupotosha watu tumia biblia Mungu hasije akakuhadhibu

 21. Bwana Yesu apewe sifa !!!

  Warumi 14:1 “yeye aliye dhaifu wa imani mkaribisheni msihukumu mawazo yake.

  Rumi 10:17 “Imani nyingine pasipo neno la kristo haidumu

  Wafilipi 1:27-28 ” ..lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyiopasa injili ya kristo ili nikija na kuwaona ninyi au nisipokuwepo niyasikie mambo yenu kama mnasimama imara katika roho moja kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya injili wala hamwogopi adui zenu kakika neno lololte kwani hao ni ishara madhubuti ya kupotea bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu huo utokao kwa Mungu.

  Kuanzia hiyo No 1-11 Milinga kasome

  Hesabu 24:7 ,Malaki 3:10 ,Waefeso 4:24 , 1 Timotheo 2:9-10 ,
  1 Wakorintho 7 : 25-38 , Mwanzo 2: 3 , Wakolosai 2:16 na
  1 Timotheo 2 :12
  Ubarikiwe kwani injili inatutaka kuyachunguza maandiko lakini omba Roho Mtakatifu akupe ufahamu na akuondolee giza ndani yako itakayoleta kuipinga kweli ya in jili

  Amen

 22. Emmanuel John;
  Unaonekana wewe ni msomi. Je ulishawahi kujiuliza kuwa hiyo Malaki 3 walikuwa wanaambiwa akina nani, kwa nini waliambiwa,hali ya kimazingira ilikuwaje wakati wanaambiwa, na je kuna sehemu nyingine kwenye biblia watu walishawahi kuambiwa hivyo?

  Na ukishapata maibu ya hapo ujiulize sasa kuwa wewe ni nani, unaishi nyakati gani kuhusiana na hilo suala, na linakuhusuje!
  Asante Emma.

 23. Millinga katoa msimamo wake yeye kama yeye.

  Lakini ningependa tu tukumbushane kuwa suala namba 1,2,3,5,6,7,8,10 na 11 kutoka katika hiyo orodha ya Millinga tulishazijadili sana tu hapa SG, kwa hiyo kuanza upya ni kupoteza muda wakati nakala zake unaweza ukazitafuta ukazipata.

  Ndugu yangu Lwembe sijaelewa kama uko serious uliponitaja kwenye orodha ya unaowataka watoe zaka, maana nimeona kama umemalizia na ka-utani fulani hivi.

  Lakini bila shaka unakumbuka msimamo wangu ni kwamba mimi moja ya kumi sitoi maana siyo lazima, na anayetoa namhimiza aendelee kutoa kama alivyokusudia moyoni mwake maana siyo dhambi kutoa fungu la kumi.

  Lakini yeyete(na wengi wako kwenye hili kundi) anayetoa zaka kwa hofu baada ya kusomewa Malaki 3 na kuambiwa kuwa yeye kama hatoi ni mwizi anayemwibia Mungu, basi ajue kuwa anapoteza muda na pesa yake. Ni bora hiyo pesa akawape masikini.

  Mantiki yake nyepesi ni kwamba zaka walipewa walawi ambao walikuwa makuhani, na ilibidi wapewe zake si kwa sababu ni makuhani bali kwa sababu hawakutakiwa kuwa na urithi wa ardhi. Na hawakuwa na ardhi si kwa sababu ardhi ilikosekana, bali ni kwa sababu Mungu alitaka wasiwe na ardhi ili wajihusishe tu na shughuli za hekalu na madhabahu.

  Sasa leo hii ukuhani hauko kwa Lawi, bali kwa Yuda(Simba wa kabila la Yuda) ambaye ana urithi wa ardhi, sasa zaka tunataka apewe ya nini? Na wanaokomaa kusema kuwa tunamwibia Mungu wanajua kabisa kuwa Mungu hahitaji dola wala shilingi ya Tz,na alitumia huo msemo wa kumwibia akimanisha kutokuwatunza walawi, ambao leo hata siyo makuhani tena.

  Halafu kwa ninyi watoa zaka kama kweli mnafanya kitu mnachokijua, hebu niambieni ni lini zaka iliwahi kuwa pesa! Kwamba ni wakati gani katika biblia watu (Israel)walikuwa wanatoa zaka ya pesa,shekeli,au dinari?

  Usifanye jambo kwa kutishwa na maneno ya watu:

  Chunguza biblia nukta kwa nukta, ndipo utagundua mwenyewe ama umedanganywa au umeambiwa ukweli!

  Ujinga juu ya Zaka umeongeza umasikini kwa wakristo.

 24. Dah kwa kweli umejitahidi kuandika ndugu milinga, Na pia ni vizuri kwa mawazo yako uko sahihi kabisa kwani kila mtu huwaza sawasawa na akili yake inavyomtuma
  sasa mm napenda niseme haya machache: Unajua ukisema mafundisho potofu maana yake ni tayari yamewapotosha na kuwapoteza watu wengi kwa vile ulivyoandika
  Sasa basi unaweza ukawa sahihi au wrong kwa hayo yote uliyoyaandika kwani Neno lolote au fundisho lolote linaloendana na Mungu huwa na Kifungu cha Neno la Mungu Pembeni sio maneno matupu kama ulivyoandika, kwani Kumbuka Biblia inasema ghadhabu ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu, lakini ghadhabu ya Mungu yenyewe Hutenda haki, Sasa pengine umeumizwa mahali ndo ukafikia kuandika huvyo? Nakushauri tumia Maandiko

  Pia Kuna vitu vingi sana ambavyo shetani kaiba, we soma Neno utaona, sasa tunapotaka kuvirudisha hapo usiite mafundisho potofu, kuna maarifa yamekosekkana hapo, Kwa nn watu wa Mungu wanaangamizwa? Neneo Limepungua sio potofu

  Pia Mafundisho ya kutoa zaka katika kila mapato yako ni lazima usipotoa biblia inakuita wewew ni Mwizi, penda usipende, ndo Hivyo yaani Malaki 3, Mm mwenyewe hapa napenda hata mwezi uishe haraka ili nikatoe fungu langu la kumi au zaka, Huyo Mchungaji asiyetaka kukufundisha wewe kutoa zaka anakutakia laana katika maisha yako be Care Ndg,
  Naomba niishie hapa kwa leo, Nimeeleweka,

  Emmanuel john

 25. Bwana Yesu asifiwe,

  Nadhani ndugu Milinga alitaka elewa mambo na hapo akatumia ujanja fulani wa kuhakikisha aliyotamka. It’s his method. So inabidi tumueleweshe point by point mambo aliyohakikisha. Na mafundisho ao ufunuo utoke ndani ya Bible. Milinga alitia mkazo juu ya upotofu wa mafundisho, akaepuka fundisha yaliyo kweli. Ina maana labda hana kweli na anapenda aipate kwenye blog hii. Ebu tumupe mafundisho zaidi, labda tutamuona tena akirudi kuyapinga.
  Kwa ujumla mim sione upotofu hata moja kwa ile ndungu Milinga uliotaja nikishika tu ginsi ulivyo andika. Kila topic ita depend upon muinjilisti analenga nini, ao aliitafsiri je. Kwa mfano: kuna tofauti kati ya zambi na kosa, tofauti pia kati ya tamko “moja wapo” na “yote”. Kama muinjislisti fulani amefunza watu kama “mzaliwa wa kwanza” ni “moja wapo” wa malango ya baraka ao laana, hajakosea; tofauti kabisa na ginsi angeliseme kama mzaliwa wa kwanza ndiye pekee anaeleta baraka, … Naona kama Milinga, pengine alijitia kwa upande wa mafikiri fulani, ndipo akaandika aliotaka. Na hakuna aliotaja isiyopatikana ndani ya Bible. Wapendwa, tujiulize kwa nini huyu ndungu alipinga maandiko bila kuelewesha yeye alitosha aliyoyasema wapi na zaidi akisema watu wengine hawasome vitabu. Yeye alisoma vitabu gani ili tumukubali? Mimi nitasema leo juu ya pont No 1, na ikiwezekana tuendelee, wenda Milinga atatosheka.

  1. “Nyota zilizoibwa” inamaanisha “, nyota iliopotea ao baraka zilizofungwa”. Sijue Ndugu Milinga kwa upande wako uliwayi kusikia je ile mafundisho, lakini mambo ya baraka kufungwa ni kibiblia kabisa. Baraka kufungwa inatokana na ginsi Ibilisi anavyoshika mateka watu, na akifaulu anabaki kuwa mushtaki mbele ya Mwenyezi Mungu.

  “Ufunuo wa Yohana 12:10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku”.

  “2 Petro 1:19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.”

  Nyota inapozuka mioyoni ni kwamba neno la unabii lililo imara zaidi liko mioyoni. Lakini Ibilisi anapoangusha mwanaadamu ndani ya dhambi, neno la unabii analiiba, na nyota inakimbia.

  Kwa kweli nyota ni Neno la Mungu, na bila ile hakuna baraka.

  “Ufunuo wa Yohana 22:16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.”

  Mimi nikifundisha juu ya nyota kuibwa, ni kusema Ibilisi anapokushika, anakubeba mbali ya uwepo wa Yesu Kristo, na neno ambayo ni Nyota ya asubui unaikosa.

  Ndugu Milinga, una swali?

  God bless you.

 26. Umenipa shaka sana kwa baadhi ya oanisho lako la mafundisho potofu,ila nikuambie sio yote ni potovu hebu jipange vizuri,mtumishi

 27. Asante sana Milinga, nimekupata sawasawa Hata bila mafafanuzi, lakini ni kweli inahitajika clarification kwa kiasi fulani ili kuonesha mtazamo wako katika mafundisho uliyoyaorodhesha. Kwa kuwa ni mengi mimi natoa mchango wa jumla bila kutaja fundisho mojamoja kama ifuatavyo;

  Madhara ya mafundisho huwa hayatokani na fundisho lenyewe hasa, isipokuwa inachangiwa na vitu mbalimbali. Kwanza ni nia ya mfundishaji na uelewa alionao katika neno la Mungu, ambao mara nyingi huathiriwa na misingi ya dini yake.

  Nikianza na nia ya mhubiri ni kwamba akitoa fundisho lolote kutoka katika nia ya kujipatia faida au umaarufu, watu wataona na kwa huyo mtumishi atakuwa amepotosha fundisho kwa application ambayo si sawa. Hivyo kabla ya kuhukumu fundisho, kwanza tumuangalie anayefundisha ili kujiridhisha na ule uaminifu wake (genuine in his speech). Mtu ambaye hana nia ya kujinufaisha huwa mwepesi kujifunza na kubadilisha fundisho lake (maana hakuna anayeanza na ujuzi).

  La pili ni uelewa wa anayefundisha. Hii inachangia sana katika kupotosha maandiko. Watu wanakwepa elimu ya Mungu kwa maana ya kwenda shule angalau secular, kwa madai ya kuongozwa na ‘roho’. Hii mentality imeleta shida kubwa sana katika kanisa. Wahubiri wanakuwa na nia nzuri lakini ujuzi wa kuyaelewa maandiko katika context yake wanashindwa. Hivyo wanaanza kudandia mafundisho wanayosikia kwa wengine kupitia wahubiri wakubwa bila kujua kwamba “udanganyifu wa mafundisho huvuta watu wengi kuliko ukweli wa mafundisho”

  Fundisho lolote la kweli lazima liwe wazi kwa kila mtu. Kuwaambia watu kwamba unachofundisha ni cha hali ya juu na kinahitaji mtu wa rohoni ndiye anaweza kuelewa, huko ni kuficha makucha ili kughiribu akili za watu wasio na ujuzi.

  Mwisho nasema, tusiwe na haraka kusema ni mafundisho potofu tu lakini twende mbali kidogo kwa kuwachunguza pia wasemao. Ishara ya kuwa mtu ni potofu ni nyingi lakini naeleza chache hapa;

  1. Watu hawa hudai kuwa wao wanongea na Mungu moja kwa moja kuliko wengine.
  2. Watu hawa hawana uwazi kwa washirika wao bali wanadai kutetemekewa na hawataki kuhojiwa kwa fundisho lolote.
  3. Akitokea mtu akahoji fundisha, kinachofuata ni vitisho vya kupatwa na mabaya.
  4. Hutumia maneno ya Biblia yanayohusu manabii na Bwana Yesu, wanayageuza na kujiweka wao wenyewe kana kwamba maandiko hayo yanawahusu wao.
  5. Zaidi ya yote hayo, wanawadharau watumishi wengine na kuwafundisha washirika wao kuwa wao ndio walioitwa tu.

  JohnR.

 28. Mtumish nisaide, kuhusu somo la mavazi yampasayo, mwanaume au mwanamke, mimi nilielewa suluali ni mw,ume!.

 29. Mr. Milinga umesema kweli japo hujataja maandiko gani yaliyoandika ila ni kweli kabisa list hiyo iko sahihi tena no 11. Hapo utatupata wengi labda niongeze na no 12. Ubatizo wa maji mengi na madogo na hapa kuna mafundisho mengi potofu. Wapendwa muache uvivu Someni biblia zenu mtapata majibu! kama hamkubaliani naye basi leteni nyie hizo reference kupinga aliyoandika.

 30. Nadhani ndg Milinga unataka kuipotosha jamii ya wakristo. mfn. je umetumia criteria gani kubainisha upotofu wa mafundisho hayo? si yote ni potofu. thibitisha kwa kuonyesha vigezo ktk BIBLIA. upotofu wa fundisho la zaka

 31. Kazi ya kulisha kondoo wa Yesu Kristo Bwana ni wito, kuelezea neno la Mungu kwa kutumia akili za kibinadamu na si Roho Mtakatifu, ambayo ni nafsi ya Mungu ndo yanatokea mambo ya kutojua kipi ni sahihi na kipi si sahihi mbele za Mungu, kumbuka kuwa sheria ya Bwana ni Kamilifu, haina udhaifu wowote kwa ulimwengu mzima, haiko kwenye utamaduni, ukabila, rangi, utaifa, mahara popote ulimwenguni imesitilika, Kumbuka kuwa unapofundisha neno la Mungu lazima lisitilike kila mahari ulimwenguni. Tutafute kuongozwa na Roho wa Mungu tunapotoa mafundisho ya Mungu, maana Roho Hufundisha na kutuongoza katika njia itupasayo! Ni si kuhukumu kwa kutumia akili, ndo maana inatokea kupingwa.

 32. Milinga, Sungura na Mkandya,

  Acheni kukwepa kutoa FUNGU LA KUMI!!

  Angalia Millinga ulipofikishwa na ukwepaji huo, umekuja na msururu usio na rejea ya Biblia hata moja! yaani umenyang’anywa vifungu vyooote umebaki debe tupu!!

  Katoe fungu la kumi, tena ulitume kwangu, halafu ndio urejeshewe ulivyoibiwa na Shetani, ile nyota yako iliyokuwa iking’aa!!!

  Chunga; usije ukawa “SUCKED IN”!!!

 33. Umeeleza maeneo mengi ya mafundisho ambayo umesema ni potofu je unayo reference yeyote katka Biblia kuhusu haya uliyoyasema? naomba unipatie tafadhali.

 34. Milinga umenena mwana wa Mungu, lakini bila shaka unafahamu kuwa utawashitua wengi kwa hoja yako hiyo na pengine utapingwa na wengi pia. Unachotakiwa kufanya ni anza kuelezea hoja moja moja kama ulivyoainisha hapo chini tena kimaandiko kabisa ili mtu anaposoma na maandiko yameoneshwa hapo unakua umepunguza idadi ya maswali ambayo pengine ungeulizwa.

  Nawasilisha

  Flano

 35. Mpendwa Milinga na SG wote,
  Kabla sijatoa maoni yangu kuhusu mambo uliyorodhesha kama Mafundisho potofu; naomba nitutofautishe kati ya Mafundisho na Ufunuo. Fundisho linaenda na Agizo la moja kwa moja katika Neno la Mungu wakati Ufunuo ni jambo mtumishi analolipata unaposoma Neno kwa ajili ya kutatua shida iliyopo kwa mtu, watu au jamii fulani. Katika orodha ilyotolewa, kwa uelewa wangu yafuatayo ni:

  A) Ufunuo:
  Nyota zilizoibiwa
  Watumishi wasioe
  Utajiri kwa kutoa Sadaka
  Kupaka watu mafuta
  Kuwazuia Wanawake wasifanye kazi
  Malango, Mzaliwa wa kwanza na kufanya jambo ili upate kitu

  B) Mafundisho:
  Kutoa Zaka
  Wanawake kuvaa suruali
  Sabato
  Wanawake wasiwe viongozi wa Kanisa

  Haitegemewi ufunuo fulani u-apply kwa kila mtu au jamii. Hivyo wanaotumia ufunuo ku-universalize (kuufanya utumike kwa kila mtu) wanaweza kuonekana wanaleta mafundisho potofu. Kuhusu Mafundisho; kwa ujumla naweza kueleza kuwa yapo Mafundisho/Maagizo ambayo ni endelevu na ambayo yana ukomo. Katika Mafundisho yenye ukomo, mtu anaweza kuyaona kuwa ni potofu ikiwa mhusika atataka kuendeleza, lakini si hivyo, kinachotakiwa ni uelewa wa kina na kutofautisha majira na nyakati.

  Niishie hapa kwa sasa,

  Keep on digging,
  Mathew.

 36. Praise Jesus!

  Naomba, ikiwa email address ya ndugu huyu aliyetoa changamoto hii inaweza patikana, ningetaka kuwasiliana naye bilateral kwa lengo la muhimu sana.

  Nitashukuru.

  Br. Shammy

 37. Kaka Milinga hao wanaofundisha wameona result ya mafundisho hayo kwa kutumia hiyo hiyo Biblia takatifu na sio kwa kusoma mstari mmoja bali mistari mingi, unaposema uamini kuibiwa nyota it means uamini kama kuna uchawi katika ulimwengu huu na kama hakuna uchawi it means shetani hayupo.na ndio maana biblia imesema vita vyenu si katika damu na nyama bali ni katika falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho hiyo ni Waefeso 6:10-16 sasa tujiulize nini kazi ya hayo mapepo na hao wakuu wa giza. Muombe Mungu wa kutumia Roho Mtakatifu uweze kutafakari hayo uliyoandika

 38. ndugu millinga unapo leta soma kama hili kuwa makini unaweza wewe ndo ukaleta upotofu wa mafundisho basi ni vyema kama umejua mafundisho hayo nipotofu ni vyema akaleta maelezo yanayo enda sambamba na Neno la Mungu kuliko kuhukumu na kuwaacha watu njia panda kwa kutoelewa kuwa ashike lipi na aache lipi hivyo ikiwa umeona hayo mafundisho leta mafundisho kwa soma ulilo litaja kwa Neno si kwa poroja ambazo hazitokani na Neno la Mungu

 39. No. 11 Mafundisho ya Malango……, Mzaliwa wa kwanza??????????? Mr. Milinga njoo na maandiko kwa kila kipengele ulichotaja.

 40. Ha ha ha haa!! Unachekesha kweli kaka Milinga. Labda ungeanza kutufundisha kwa nini unafikiri kuwa mafundisho hayo ni POTOFU? Maana wote wanaofundisha ayo, wanatumia Biblia. Sasa, hebu tumia Biblia na wewe kututhibitishia kuwa mafundisho hayo kweli ni POTOFU, badala ya kukomea kusema tu.
  Mimi ninavyojua, kuna baadhi ya mafundisho hayo uliyoyatoa, siyo potofu kabisa. Mf. Sabato (pumziko takatifu la ibada kwa Mungu siku nzima), hili siyo fundisho potofu hata kidogo. Kama unabisha, tafuta hata aya moja ndani ya Biblia, inayosema watu wapumzike lile pumziko takatifu siku nnyingine yoyote tofauti na jmosi. Ukilipata hilo, wewe lilete, nakuahidi zawadi ya milioni 1 live. Kazi kwako kaka.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s