Kuota unakimbizwa na nyoka

gm

Ni ujumbe kwako kwamba roho ya uongo inakunyemelea maana nyoka katika ulimwengu wa roho ni roho ya uongo na kumbuka shetani alivaa umbo la nyoka na kuwadanganya hata akina Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni wakatenda dhambi (Mwanzo 3:4) na katika Ufunuo 20:2 shetani anaitwa nyoka wa zamani yaani aliyewadanganya akina Adamu na Hawa. Hivyo ni kuwa makini sana na kuvunja roho hiyo kwa jina la YESU KRISTO na mpango huo wa kuzimu hautafanikiwa.

Na mfano mzuri ni mimi siku moja nikiwa kanisani tunaomba nilimwona nyoka anazunguka na kwa sababu nilikua sijajua kwamba hiyo ni roho ya uongo unanyemelea watu wa MUNGU hakika kesho yake ulizuka uongo mkubwa na kusababisha hadi baadhi ya viongozi wa kanisa kukosana na ndio ikawa mwanzo wa mimi kujua kwamba nyoka anamaanisha nini katika ulimwengu wa roho.

MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kuwa suluhisho pekee la yote haya na yote yanayowasumbua wanadamu ni YESU KRISTO na yeye mwenyewe katika Mathayo 11:28

–Gasper Madumla

Advertisements

7 thoughts on “Kuota unakimbizwa na nyoka

 1. shalom,naomba kujua nini maana ukiota unapaa au unaogelea kwenye bwawa au mto?

 2. nimejifunza mengi kutokana na ndoto nimefurahia mafundisho ila jamii iache kuamini maovu au ubaya juu ya ndoto bila kuwa na hofu ya mungu

 3. Watoto wa Mungu,

  Fikira za kuamini juu ya ndoto si jambo jipya au geni, ni jambo lilianza kutatiza vichwa vya watu zama za kale sana. Inakadiliwa kuwa katika mwaka wa 3100 BC watu walianza kujishughurisha sana na swala la ndoto na usingizi. Na katika karne ya 7BC, mwanafunzi wa kifalme aitwaye ASSURBANIPAL, alijishughurisha kwa bidii nyingi ili kujua ndoto ni nini , zintokeaje na hasa kama zina maana yeyote kwa binadamu, kwa mjibu wa imani na mafundisho ya Mesopotamia, Ssirya, Babeli na Misri, iliaminiwa kuwa ndoto ni MATOKEO YA ROHO KUHAMA TOKA KATIKA MWILI NA KUUENDEA ULIMWENGU WA KIUUNGU, AMBAKO HUWEZESHWA MWOTAJI KUWASILIANA NA WATU AMA KUPATIWA TAARIFA, MAELEKEZO, SIRI, MBINU ZA MAISHA YA USHINDI KATIKA VITA, KUONGEA NA WATU KWA MAMBO AMBAYO WASINGEWEZA KUYATAJA WAKIWA WANAONANA USO KWA USO NK!

  Inaaminiwa pia kwamba, mawasiliano yanayofanyika katika ndoto huwa ni kuambiana ukweli mtupu kati ya mwotaji na wale anaozungumza nao au kuwaona katika ndoto; mfano Mtu amemuua jirani yake, akiulizwa katika ndoto huwa hana uwezo wa kuficha siri ile, bali hueleza mwanzo mwisho ukweli wote juu yatukio husika na sababu zilizopelekea afanye tukio lile!

  Wa Babylon na Wassyria wamezigawa Ndoto katika makundi mawili moja, ni “ndoto njema/ nzuri” hizi hutokana na miungu wema na ya pili ni “ndoto mbaya/ ovu” hizi hutokana na miungu waovu (mashetani/ pepo wabaya), lakini ndoto zote zina maana moja tu ni “Kumtaarifu” muotaji. Wamisiri katika 2000 BC, wao walifikia mkataa kuwa Ndoto ni tukio maalumu kutoka kwa miungu,kwa ajiri ya utabiri na taarifa zisizo za kitabiri, wamisiri walitumia vitanda maalu vilivyojulikana kuwa ni vitanda vya ‘ ‘maono’ ili wapewe maono, mafunuo, furaha, maelekezo ama taarifa mhimu na miungu kupitia ndoto.

  Nadhalia juu ya ndoto na uotaji, zilifanya kuwa Elimu na wachawi, waganga na watu waliokuwa wakijulikana kuwa ni “wenye Hekma” Elimu ya sayansi ya ndoto huitwa ONEIROLOGY inasema kuwa; Ndoto ni swala la ‘KISAIKLOJIA’ hivyo wataalmu wa kale kama akina ARISTOTLE na wengine walikosea katika falsafa zao juu ya ndoto ni nini, Ndoto ni mkusanyiko wa matukio na vitendo ambavyo havihitajiki katika kuhifadhiwa na ubongo wa kutunza kumbukumbu, ni kitu au jambo mhimu lipaswalo kukumbukwa na mhusika ndilo hubakizwa katika ubongo wa kumbukumbu, vinginevyo ubongo unaweza kupata joto (overheat) na kusababisha madhara kwa mhusika, kwa hiyo mengine yote yasiyo mhimu huondolewa na kufutwa katika kumbukumbu kwa njia maalumu (kama wanyama wacheuavyo) hiyo ndiyo faida na kazi ya ndoto, wa ONEIROLOGISTS ndivyo wasemavyo!.

  Wote wanasayansi, wanafalsafa na wanadini hutofautiana katika kuamini na namna wanavyozungumzia juu ya ndoto, lakini wanadini na wataalamu wa ndoto wa kale wanakubaliana kwa namna fuani kuwa ndoto huweza kuwasilisha jambo la kiroho! Rekodi ya kale kabisa juu ya ndoto katika Biblia imetajwa katika kitabu cha Mwanzo 20:3 ambapo panasema hivi, “3Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua, yeye ni mke wa mtu.’’ Ndoto hii ya Abimeleki, ni ndoto isiyo na tafasiri toka kwa mtu mwingine, ipo kamili na ujumbe iliyoubeba ni wa moja kwa moja kama taarifa kwa mhusika. Ndoto nyingine ya kale maalufu isiyohitaji tafsiri ni ile Ndoto ya Yakobo inayopatikana katika Mwanzo 28:10-22, ijulikanayo kama ‘ndoto ya vitado vya ngazi’

  Mwotaji anaweza kuota ndoto akaweza kuikumbuka, lakini pia asiweze kuielewa hata kama ndoto ile inamhusu mwotaji, au hata iwapo ndoto ile ina ujumbe maalumu usio wa siri na labda pia inawahusu watu wengine. Mfano wa ndoto kama hiyo ni kama zile ndoto mbili za Yusufu aliyoota kuhusu miganda ya nduguze ikiinama mbele ya mganda wake, iliyorekodiwa katika mwanzo 37:5-8 na ile ya pili aliyoota juu ya jua, mwezi na nyota, inayotajwa katika mwanzo 37:9-11. Lakini pia mtu aweza kuota ndoto inayomhusu yeye mwenyewe tu, ikawa pia asijue tafsri yake, mfano wa ndoto ya namna hiyo ni kama ile waliyoota wale mnyweshaji na muokaji wa farao wa misri ambayo imetajwa katika mwnzo 40:5 nakuendelea.

  Iwe kwa vyoyote vile si hoja, ila cha msingi ni kuelewa iwapo ndoto husika inatoka kwa Mungu ama la. Ndoto, hutegemea sana mazingira, mila na desturi za mwotaji! Mfano, mwotataji hawezi kuota kitu kama nyoka iwapo nyoka hajawahi kusikia habari zake ama hata kumuona kwa macho. Lakini hatari kubwa kuliko zote zinazotajwa katika kuitafasiri ndoto, ni pale mtafasiri, anapobeba maana ya ndoto hiyo kwa mtazamo wake wa kihisia, kiakili, ki mazingira tu, na ama wa kilozi. Si kila kuota ama kumuona Nyoka pahala maalumu si lazima iwe ni alama ya ‘ushetani’. Mmisri ama mchina na ama mtu wa jamii fulani ya kihindi akiota ainafulani ya Nyoka, kwake ni ishara njema, tofauti na mlokole wa kitanzania akiota ama akiona hivyo, si shida kwake kuoanisha tukio lile na ushetani.

  Mapokeo huathili sana mienendo katika ubinadamu, katika jamii fulani Paka, Bundi ama Fisi ni ishara mbaya, ambapo katika jamii hiyohiyo Nyoka wa kijani na wale weupe ni ishara njema. Iko pia jamii, ambapo mwanajamii akiota kakutana na mwanamke asubuhi mara tu alipokuwa akitoka nyumbani kwake kuelekea shambani ama kokote kule, yeye huona hiyo ni ishara mbaya! Kwa maana hiyo, watafasiri wengi wa ndoto, huzitafasiri ndoto zile si kwa kuisikiliza sauti ya Mungu, kwakuwa wao wenyewe hawaijui sauti ya Mungu mwenyewe, aina ya ndoto, mazingira ya mwotaji, mahusiano ya kijamii na ujumbe wa ndoto ile kwa mhusika binafsi, ama kwa jamii kwa mjibu wa Neno la Mungu!

  Tukiitazama Biblia, tunaweza kuona kwamba, Ndoto ikija kutoka kwa Mungu, huja kwa Lugha na hata muonekano unaotambulishwa na Mungu mwenyewe, kwa; Tunaliona hilo tunapoitzama ndoto ya mfalme Nebkandreza, alipoota juu ya ile sanamu kuu ya kutisha. Mwotaji aliona dhahabu, fedha, chuma na udongo ambavyo kwa pamoja vimefanya sanamu kubwa, vilevile aliona jiwe na upepo, vyote hivyo alikuwa anavijua kwa jina na hata kwa uhalisia lakini maana ya ndoto na lugha iliyo wasilisha picha ile hakuijua, hadi alipokuja mtu wa Mungu, mtu yule mwenye kujua lugha iliyowakilishwa na picha ile!

  Kuota ndoto hakujalishi kama mhusika ni mcha mungu, bali cha mhimu ni ile ndoto, na ujumbe iliyobeba, kama kweli vinatoka kwa Mungu; Je utawezaje kujua kuwa hii ndoto inatoka kwa Mungu na huyu anayeitafasiri ni mtumishi wa Mungu wa kweli? Utagundua hivyo tu iwapo Roho wa Mungu amemiminwa kwako! Mdo 2:17 inasema,

  “17Katika siku za mwisho, asema Bwana,
  nitamimina Roho wangu juu ya wote
  wenye mwili.
  Wana wenu na binti zetu watatabiri,
  vijana wenu wataona maono
  na wazee wenu wataota ndoto.
  18Hata juu ya watumishi wangu
  nitamwaga Roho wangu,
  nao watatabiri”.

  “UFAHAMU NI CHEMBE YA UHAI!”

 4. Amina mtumishi wa Mungu nimebarikiwa sana na somo.MUNGU AKUTIE NGUVU KWENYE HUDUMA HI NA AKUPE ROHO YA UNYENYEKEVU.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s