Je ni rahisi kutafuta amani na watu wote?

waebrania

Biblia inasema: “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao” – Waebrania 12:14.

Kwa tafsiri ingine, inasema, kuwa na salama. Wapendwa, tunapotazama ulimwengu huu, iwe katika makanisa, siasa, mitaani, … dunia nzima, amani salama imekosekana. Nimeona Biblia imeleta changamoto, wala haikusema « tutafute kupendwa na watu wote ! »

Tusaidiane : Ni mifano ipi ipatikanayo katika Biblia ambayo tunaweza timiza ili amani tuipate? Ninapotazama, naona watu wengi wanatafuta wapendwe na wanapokosa upendo wanapata majeraha makubwa. Naamini mchango wako itasaidia watu wengi.

Na Mungu wa Mbinguni akubariki.

Ziragora Alphonse

Advertisements

16 thoughts on “Je ni rahisi kutafuta amani na watu wote?

 1. Utakatifu ndiyo ticket pekee. pekee pekee ya kutuwezesha kuingia mbinguni
  utakatifu una uwanja mpana sana kuishi maisha matakatifu si lele mama ila kwa msaada wa Roho mtakatifu tunaweza “haleluyaa”
  tukumbuke Bwana alisema mpende adui yako na muombee anayekuudhi hii sidhani kama ina utofauti na ile ya hebr.12;14
  Utakuwa na utakatifu gani ikiwa hauna amani na watu? kumbe kumbe kule kuwa na amani na kila mtu ndipo kwa sehemu kuna zaa utakatiifuu
  ni hayo tu kwa leo ndugu zangu
  Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iendelee kuwa pamoja nanyi
  aamen.

 2. Niseme tu kuwa neno la Mungu halibadiliki,mbingu na nchi zitapita lkn neno la Mungu ladumu milele
  MUNGU amesema tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakaemuona MUNGU asipokuwa nao. tukitazama kwa makini hapa kuna vitu viwili vya msingi ktk safari y mbinguni
  1)amani
  2)utakatifu
  amani ni kitu cha muhimu sana ktk maisha ya mwanadamu haijalishi ameokoka au la amani inapokoseka ni rahisi mtu kuchukua hatua itakayomuangamiza kiroho, mf. kuua,kujiua n.k
  na Mungu kwa kulitambua hilo ili sisi tusiwe sababu ya wengine kuangamia.! na ingawa pia alifahamu kwetu sisi kama wanadamu ni ngumu kuwa na amani na kila mtu ndiposa anatuagiza tutafute kwa BIDII kwa maana ktk hali ya kawaida haiwezekani ww uwe na amani na kila mtu. hii inawezekana kwa kujishusha au kujidhili
  Yesu alisema ajikwezaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa na kama inashindakana sana tufunge na kuomba kwani Bwana Yesu alisema mengine hayawezekani ila kwa kufunga na kuomba
  2)utakatifu ndiyo tiketi pekee ya kut

 3. Amina kubwa.

  Ndugu Lwembe, umenibariki sana tena ngambo zote kabisa. Na wewe Mungu akubariki. Ninafurahia tena ushujaa wako ktk mtandao huu. Kweli unasoma, ninasadiki. Maarifa pamoja na uwepo wa Roho Mtakatifu sherti yeyote aliyeokoka avitafute kwa bidii. Hii blog ni Hekalu kubwa sana. Nafikiri kila mtu aliye na swali atapata jibu ndani ya SG.

  Haleluya!!!!!!

  God bless you.

 4. Ni kweli kwamba kwa asili, binadamu hutafuta kupendwa! Nasi mara nyingi tunapozungumzia upendo, huwa kwa namna fulani ya siri, tumeliweka sharti la kupendwa kwanza, ndipo tuurejeshe huo upendo kwa hao tunaogusana nao katika maisha. Huu ndio upendo unaotawala katika maisha yetu ya kawaida. Kwahiyo akitokea mtu ambaye ataanza kwa kutotuonesha upendo, basi atajibiwa kwa kiburi kinachowiana na hali aliyokuja nayo! Nao Upendo ukiwa ndiyo tafsiri ya Amani, basi amani hukosekana katika mazingira ya namna hiyo

  Seleli ameionesha mifano hai mingi sana yenye kuujaribu Upendo kwa mkristo, na akaionesha pia njia ya kuyajibu majaribu hayo ili ubaki katika kuwa na hiyo “Amani na watu wote.” Yaani ukitumia akili ulizopewa na Mungu, reasoning na logic ili kukabiliana na majaribu hayo yenye maudhui ya kuiondoa amani. Lakini kuna wakati ambapo unaweza kukanyagwa kidole, basi kwa ule uchungu, wengi waliokuwa katika pose ya amani na watu wote, nimewahi kuwaona wakilipuka kuliko maelezo, pozi yote ikitoweka kama tochi iliyozimwa, “bahati yako nimeokoka!”

  Bali ndg Patrick, amesisitiza kuwa amani hiyo itafutwe katika utauwa!!

  Nikiirejea mifano aliyoitoa Seleli, hiyo aliyokuletea kutoka katika Biblia kama ulivyoihitaji, limekuwa ni jambo zuri kwamba mifano hiyo imeikata kiu yako, na kwamba kwa hiyo mifano sasa utakuwa umepata nguvu mpya katika duru za kukutafuta huko kuwa na amani na watu wote bila kusahau utauwa!

  Ninalotaka kuongeza kidogo, katika kulikamilisha jambo hili, haswa suala la “utauwa” linapojitokeza juu zaidi, kuwa ndilo kiongozi wa utafutaji huo wa kuwa na amani na watu wote, basi namna ya utafutaji huo, kwa kiwango fulani huhitaji uangalifu wa juu. Kwa maana ni rahisi sana kujikuta katika kutafuta kwetu kuwa na amani hiyo, tukaishia katika unafiki. Hebu na tuutazame mfano huu aliotuwekea Mungu, ili kwamba siku tutakapofika katika kulitafakari jambo hili la “kutafuta kuwa na amani na watu” tuwe na mifano yote ili kujifunza kwetu kuwe kamili, Gal 2:11-14,
  “Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu. Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa. Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao. Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?”

  Ndipo kutoka vifungu hivi vya Maandiko, jambo hili linajisistiza zaidi katika ujasiri unaotokana na huko kuwa na amani na watu wote, kwamba si tu kwa watu wasio wa kusanyiko letu la Kikristo, bali hata ndani ya makusanyiko yetu, hapo tunapouona upotofu basi twapaswa kurejeshana katika upendo uliojikita katika huko kutafuta kuwa na amani na watu wote, pamoja na hao wa kwetu, ambao ni wa thamani kubwa sana kutokana na Damu iliyowanunua!!

  Basi hayo yawezekana vipi? Siri ya utauwa ndiyo inayoyashikilia mambo haya! Nguvu ya kukitafuta chochote kile, kwa mkristo, huzaliwa katika imani. Kwa imani sisi hupokea hayo tuyatafutayo. Yaani shauku ya kukipata chochote kile, hujengeka katika msingi wa kuwa tumekwisha kukipokea kwa imani, Ebr 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Ndipo Kristo ametuachia Amani yake, ametupatia sisi hiyo amani yake! Yn 14:27
  “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.” Basi ni katika udhahiri huu, kwamba hiyo Amani ya Kristo inayotuzingira, hiyo ndiyo yenye kutuwezesha kuwapenda hata adui zetu. Nayo Amani hiyo hutuwezesha kuyatawala mazingira yetu pamoja na watuzungukao, maana kwa Amani hiyo Upendo hutafsirika kwetu hata sisi kuwa waraka! Ninaamini kwamba mitume wote ni kielelezo kamili cha kufikiwa kikamilifu kwa jambo hili la huko kutafuta kuwa na amani na watu wote katika mipaka ya utauwa, wakiidhihirisha hiyo Amani ya Kristo waliyoipokea!!

  Ubarikiwe, Muinjilisti Ziragora kwa changamoto!

 5. Asante sana Mr EDWIN,
  Umetupatia mifano mingi na nilidhania unayo kufwatana na somo lako hapo juu sana. Nimeona mifano miwili: Yesu analipa ushuru, na ile ilikuwa kutafuta amani na watoza ushuru. Na Timotheo akaitika kutahiliwa kimwili ili atafute amani angaloa baba yake wa imani alihubiri kam kutahiriwa kwa kweli ni rohoni . Hiyo mifano sikuiwazia, na umeniongezea mingi sana pamoja na wale wengine waliokusoma. Mungu akubariki sana.
  Samahani kwa ile neno pressing on niliyoitumia. Sikuitumia kama jina lako, wala sikujua kam wewe ni kwa jina maarufu press on, wala si wewe nilikuwa naambia. Ukitazama vizuri nilitaka sawa vile umefafanua pale juu, kumwambia mpendwa Nickson, kulingana na idea yake nzuri asonge mbele ikiwezekana atuletee mifano. Na amina kubwa kama wewe mpendwa umeleta mifano. Mim nilipendekeza mifano, kwa sababu kwa mfano ni rahisi sana kuambia mtu awe na amani na watu wote kuliko kumuonyesha namana gani ataweza na aliyeweza hapo zamani alifanya jambo lipi.
  Kufuatana na hii mifano, kabisa naona zaidi kam kuna asilimiya kubwa mifano ingine ipatikane. Nimeona jambo lingine linaloleta ukosefu wa amani ni kukwazana. Hivi naona Yesu alikataa kukwaza watoza ushuru na Timotheo alikataa kukwaza waliokuwa wakiishi naye.

  Asante sana tena Mr Edwin.

 6. Alphonse Ziragora

  Sujui kwa nini nimekawia kujibu ombi lako uliloniomba kwa uzuri namna hii muda sasa umepita kwa kusema’’’Nakusihi, utusaidie jamani Mfano au Mifano ktk Biblia ambapo tunaona waliotutangulia walifanya kitendo au matendo gani ili wawe na amani na watu wote au mtu fulani?Pole sana nimekawia, naona nilichukuliwa na mijadala mizuri ya Hoja nyingine motomoto, nikasahu kuchungulia sehemu nyingine/masomo mengine.

  Kuna dhana kadhaa zinazotoa maana/mantiki ya kutafuta amani na Watu nazo ni kusababisha/kuleta upendo/upendano, maelewano, upatano, utulivu, maingiliano,urafiki, kuondoa ugomvi, kusigana, utata, kuepusha shari, makwazo nk, Vilevile ni kuamua kua muungwana, mstaarabu. Kutokana na hayo, kuna hii mifano nayokumbuka haraka ktk Agano Jipya ya Yesu mwenyewe na Paul

  Mathayo.17:24-27-Wapokeaji wa ushuru wa hekalu wanamjia Petero na kumuuliza(kumbana) kwa swali , ‘’Je Mwalimu wenu anatoa Kodi ya Hekalu? Soma habari iyo mwishowe Yesu anasema, ILI TUSIWAKWAZE/TUSIWE KWAZO, anamwambia mvuvi Peter akamuopoe samaki wa kwanza, mdomoni atakua na pesa, kisha akalipe kodi ya Bwana na yeye.

  Mdo.16:1-3 Hapa Timotheo inabidi atahiriwe sababu hakua myahudi original na kwa kua ktk eneo lile wayahudi(waliokua washikilia kweli msimamo wa kutahiriwa) walikua wengi.

  Changamoto ya kufikiri na kufanya assignement ni hii! Maeneo mengine Paul mwenyewe alikua hodari kupinga Watu wakishaamini kipindi kile( kuokoka ), si lazima watahiriwe( kimwili-tendo la sheria) bali muhimu ni tohara ya rohoni. Sasa kwa nini hapa aliamua kumtahiri Brother Timothy? Jibu: Bila shaka kwa ajili ya kutafuta amani( angalia maana zake juu), kwa kua ni ivyo, je kule ambako alipinga kulikua hakuna haja ya kutafuta amani na Watu? Zawadi yako iyo Kaka Alphonse.

  Press on( notice: Umenichekesha/umenibariki kuniita ktk post yako ‘’Press on’’! iyo ni sahihi yangu ya kipendwa, kiswahili chake ni ‘’Songa/Chuchumilia Mbele’’..Jina langu liko Juu pale kabla ya Post brother..hahahaha! ubarikiwe Mr. Press on no. 2.

 7. Amina, na ubarikiwe Mr Nickson Mabena.
  Pressing on, waweza kutuletea mfano ao mifano ktk Biblia ambapo tunaona waliotutangulia walifanya kitendo ao matenda gani ili wawe na amani na watu wote ao mtu fulani?
  Nakusihi, utusaidie jamani!

  Asante.

 8. Kuwa na amani na watu wote inawezekana kabisa, lakini kupendwa na watu wote ni HAIWEZEKANI. kwan hata Yesu mwenyewe hakupendwa na watu wote, na sisi tuliookoka lazima ulimwengu utatuchukia tu!!
  Kwa akili za kibinadamu inaonekana kama ni ngumu kidogo kuwa na amani na watu wote, ndiyo maana biblia inasema tutafute kwa BIDII, maana yake sio rahis hata kidogo… Lakin yote yawezekana kwake yeye aaminiye!!!
  Pendo lile lile la Mungu alilotupenda sisi, linakaa kwetu, maana Roho mtakatifu ameshalimimina ndani ya mioyo yetu. ( RUMI 5:5),
  kwa hiyo kama Roho wa Mungu anakaa kwetu basi ni rahisi sna kwetu kuwa na amani na watu wote, kwani moja ya tunda la Roho ni UPENDO, AMANI… Galatia 5:22.

 9. Patrick na Edwin,

  Mubarikiwe sana.
  Hapa kitabu cha Warumi kinalegeze kidogo. Lakini Kile cha Waebrania kinasisitiza kabisa, Tena kinasema kwa bidii. Asante kwa mazungumzo yenu. Mulitoa karibu jaribu zote ktk dunia hii. Baah… ni magumu!
  Tutiye basi mipaka kwa wandungu na wadada humo kanisani. Nayo inawezekana? Tukumbuke kam mada si kutafuta watupende, lakini sisi kuwapa amani hata wakati wao hawataki kutupatia ile amani.
  Kweli ni puzzle, lakini Partick si ulipima kutuelezea mambo pale kwa warumi? Asante. Na Edwin, si ulipumua ukisikia kam ni namna tuwezavyo? Kitu tunachotafuta ni kupata moja kwa moja katka Biblia, nani alieweza tafuta ile amani na watu hata namna anavyoweza.
  Naona jambo lingine: Kukimbia.
  Najua Edwin atasema, mpaka lini? Lakini hata once ikiwa mfano ndani ya Biblia, itatusaidia.
  Naamini kam Yesu hangelilazimishwa kukimbizwa mpaka Misri. Alizaliwa akiwa Mungu na nguvu zake zote. Angepiga vita na angelishindana. Lakini kwa mafikara yangu kidogo nadhani alitafuta ampe Herode amani, asimpige saa ile ile, aonyeshe upole wake. Nilitambuwa kam wengine hawakuipata kwani watoto waliuwawa. Inaonekana hata Yesu alifanya namna iwezekanavyo. Lakini nafikiri ni mfano.
  Jambo lingine ni kuachilia utukufu. Yesu alifanya ile, ili sisi tupate amani.
  Ni mtihani jameni, lakini tuendelee.

  God bless you.

 10. Patrick Kamera na Ziragora,

  lo! apfuuuuuu! ngoja nipumue mie kwa furaha! afadhari manake ingekua kazi sasa!..kumbe ni….”Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu”’ sawa kabisa. Jamani, kuna ndugu/majirani/marafiki/Wanafunzi/wafanya biashara/staff wenzetu, acheni tu…yaani unaookoka na kuookoka na kuookoka kisha unabaki tu sasa umeookoka, bado hakutakua na amani, atakutembelea home kwangu kisha anataka kwenda night club, aje nimfungulie mie kabisaaa!, atataka kuvuta cigar au kununua Tusker laga imlaghai hapooo home kwangu eti kisha sijampa ela mie na wala sipaswi kumtawala yeye ni mtu mzima, nikae na imani yangu na yeye ya kwake ila undugu ndio ubaki! Yaani ninyi nawaambia humu duniani kuna watu/ndugu wa damu ni wakorofi hujapata kuona na mpaka una ona dhahiri kweli YESU amenibadilisha ..yaani mwenyewe unajishuhudia live kwa uhakika kua kuna kitu kilifanyika siku ileee nilipookoka maana ni maudhi, kutiana majazba na kukasirishana mwanzo mwisho, mtu anafanya mambo ndani mwako nani ndugu yako na anajua kwa hakika imani yako haitaki mambo/ hali izo na bado anafanya! ukimgusa tu kidogo, anatishia kuvunja undugu! sasa kuna wakati unakumbuka yaaani ingekua kipindi kile kibovu cha kutokua na nuru na software hazijabadilishwa, ni mara moja ishu ndogo sana iyo kuimaliza, very speedily, you cleare it once and for all…maana mtu atawezaje kudharau kiasi icho? Ila wana-taka advantge kwakua wanajua tu sisi ni waungwana,si wepesi kuzipiga, tunaogopa/kumuheshimu Mungu nk…wanajuga sana tu hao.

  Sasa kutunza amani, ninafanyaga alternatives nyingi mfano…naondoka narudi late ni kulala tu in case aliyenitembelea home hapa ni Baba wakubwa au makaka wa kubwa wa ukoo, au nampotezea wanapotaka kufika kwangu uku Dar, au kwakweli nalazimika hata kusafiri tu hata hapo Moro ili nikiwambia nimesafiri iwe kweli si uwongo au wengine wadogo wadogo hawa, hao saizi yangu, ninawaka vibaya kuna kuwepo na adabu hapo, au wengine nawazui uko uko home town kwa kuwatumia msaada bila wao kuja kama naweza kwa wakati huo maana nawajua wakija ni majaribu kweli, ila wengine kama ni majirani, inabidi uwe mpole tu mfano anafungulia muziki taarabu full volume na ole wako ukamuombe/ukamrekebishe kwa hekima zote za mpaka kugeuza sura, ngozi ya uso ukaiweka ya upoleee, sauti taratitibuu iliyojaa ”upako”, si kuongea haraka haraka kama akina siye, bado uta-bounce na tena unaweza ambulia matuzi ambayo pia kama hujakaa sawa, waweza zidiwa wewe mmh na devo akaja ghafla, ukaliachia moja matata, ikawa mbaya sana kule ndani mwako, sasa sijui wakati mwingine uhamie pengine au ikivuka mipaka sijui umpele rumande! lakin nayo utahama mara ngapi, utafunga wengi mara ngapi?mwishowe watakutafutia majambzi , wakuwaishe kwenda kwa Baba!..jamani, mbona kazi duniani hapa!..ndio maana namwelewa Yesu alivyosema ktk Mathayo. 10..34 Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. 35 Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake. 36 Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.37 Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili. 39 Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.

  Press on making peace with everybody WHEN it is possible.

  Edwin Seleli

 11. Mpendwa Ziragora na wana SG wote,

  Neno la Mungu linasema hivi:

  Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote. – Warumi 12:18 SNT

  Warumi 12:1-21 sura nzima imejaa maelekezo ya jinsi tunavyoweza kuenenda ili tuwe na amani na wote na tumpendeze Mungu na kuwa na amani na watu wanaotuzunguka.

  Maandiko yametupa mwongozo huu ambao yapasa tuufuate kadiri tuwezavyo kwani pamoja na kutaka kwetu au kutafuta kwetu kuwa na amani na watu wote kuna mipaka yake. Sisi kama Kanisa la Kristo hatutakiwi kufanya suluhu yoyote na dhambi, wala ku-compromise Neno linavyosema ili mradi tu tuwe na amani.

  Katika kutaka kwetu kuwa na amani na watu wote tusisahau kuwa Neno pia linasema hivi:

  12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. – 2 Timotheo 3:12 SUV

  Hivyo tukishafanya yote tunayoweza kufanya ndani ya mipaka ya Neno la Mungu ili kuleta na kudumisha amani tumwachie Mungu mwenyewe. Daima tukumbuke ya kuwa imetupasa kumpendeza Mungu kuliko wanadamu.

  Tuendelee kujifunza pamoja,

  Blessings,

  Patrick

 12. Bwana Yesu asifiwe,

  Nafikiri neno la Mungu linaishi. Ina maana inawezekana kuwa na amani na watu wote. Mim naona shauri 1 na mfano 1

  I. Shauri: kuitika kutanguliza wengine:

  “Warumi 12: 9-10: Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
  Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;”
  Kwa mfano, una kipande moja kidigo cha mkate, wala hauwezi kigawa kwa vipande viwili. Hii somo linatuambia kam ni vema kakipatia mwenzako, wewe unabaki pasipo kula.

  II. Mfano wa jambo alilofanya baba yetu wa imani: Kuachilia

  “Mwanzo 13:8-9: Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.
  Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.”

  Tunaona kam Abramu kwa kutafuta amani na nduguye pamoja na wachungaji vile vile, aliachilia, hakuendelea kukwezana na nduguye. Alimwomba nduguye kuchagua ardhi nzuri, naye akatwaa ya kubaki.

  Mubarikiwe.

 13. Amani ya Kristo Yesu iwe nanyi,kabla sija leta mifano,je inawezekana mtu kuwa na amani au usalama na watu wote?

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s