Si Mke mwema tu, hata mchumba bora hupatikana kwa Bwana!!

mke

Habari SG,

Jamani kuna shuhuda nyingine si tu zinasisimua/leta raha rohoni mara tu uzisikiapo lakini pia zinakua challenge/ somo kabisa la kutendea kazi na ku-share mara moja ili kusaidia/kubariki na wengine. Pia zinafanya hata mtu unashangaa na kupenda jinsi gani Wapendwa wanapoamua kutembea na Mungu na kumtumikia inavyopelekea Bwana naye kufurahi kua na mambo yao toka hatua za mwanzo kabisa.

Kila mmoja wetu anajua kua Bible inaongea sana jinsi ya kupata Mke kuliko Mume na maandiko maarufu ni kama-‘’Mithali18:22-‘’Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana’’ na Mithali.31:10-’’Mke mwema( Kiswahili imetumia neno moja tu .’’Mwema’’ lakini Kiingerea ktk Bible mbalimbali imetumia maneno mengi yenye nguvu ya ajabu na kushangaza kujua kumbe Mwanamke mtarajiwa kua Mke ni kitu kizuri na cha ajabu sana hasa aliyetoka kwa Bwana.Maneno yaliyotumika ni kama.’’ wife of noble character’’, ‘’capable’’, ‘’intelligent’’ ‘’virtuous woman’’, ‘a competent wife’’, ‘’worthy woman’’), ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Tena Biblia ya King James na New King James ndizo zimetumia neno ‘’Virtuous woman’’( notice: Ni woman!) na maana ya neno ‘’Virtuous’’ ni ‘’good’’, ‘’moral’’, ‘’ethical’’, ‘’upright’’, ‘’honourable’’, ‘’excellent’’, ‘’pure’’, ‘’worthy’’, ‘’honest’, ‘’righteous’’, ‘’exemplary’’, ‘’squeaky clean’’, ’’blameless’’, ’’praiseworthy’’, ‘’incorruptible’’, ’’high-principled’’), pia Mwanzo.24:1-67. Katika Agano Jipya, tunakutana na neno kuchumbia au Mchumba wazi wazi ktk Luka.2:5 ingawa hatuambiwi Joseph alimpataje mdada Mary. Kwakua ni ivyo kwamba Bible imeongolea sana kupata Mke mwema ambaye anapatikana tu kwa Bwana, mchumba bora je anayepelekea mke mwema, tunampataje? kwa kizazi chetu cha leo Agano jipya ambapo hatuchanguliwi Wachumba/Wake zetu na na wapendwa, Viongozi wa Kanisa. Wazazi kama zamani,tunafanyeje kua salama? Karinu soma ushuhuda mfupi ufuatao bila shaka kuna jambo Bwana atasema nasi.

USHUHUDA: Ni kijana mwenye bidii ya kazi ya Bwana na mpenda mambo ya kanisa, maongozi na mipangilio ya Wachungaji wake.Amekaa kanisani muda wa miaka kumi toka aokoke na imefika wakati sasa anataka kuachana na ukapera.Katika kukaa kwakwe kanisani na kushiriki mambo mengi,amefahamiana na wadada wengi kwa sababu iyo toka aanze kuwaza kuoa uku akiendelea na maombi na huduma, binti sayuni mmoja anaitwa Magret akawa anakuja-kuja sana ktk akili na nafsi yake na taratiibu akaanza urafiki wa kawaida lakini yeye anajua anacholenga. Akaendelea na maombi na huduma na shughuli za kanisani kama kawaida. Siku ya siku akasema, yatosha maombi na sasa ni wakati wa kwenda kumtamkia mdada uyo. Akiwa njiani kwenda na hata alishamwambia mdada mhusika kua wakutane mahala ‘’kuna ishu moja anataka kumtaharifu’’, ghafla moyoni akasikia mdada mwingine kashuka/kaingia na sauti hapo hapo inasema naye moyoni..’’ Magret hatakua mkeo bali Anna’’. Da! Kijana akashangaa kweli, akadhani ni mawazo au devo! Akavuta hatua kuendelea kidogo ghafla tena sauti ile ile.. ’’ Magret hatakua mkeo bali Anna’’.Kitu cha ajabu kingine ni kwamba, wakati sauti inasema naye, hapohapo akasikia love( falling in love) hamna mfano kwa Anna! Anasema hajawahi penda ivyo ghafla ingawa pia wanafahamiana naye Anna kwa miaka ktk huduma ya watoto ( Sunday school). Kijana akageuza kurudi kanisa kuingia chumba cha maombi na kumuuliza Mungu imekuaje? Wala hakusikia tena sauti bali ni growing love na peace ambayo hana jinsi ya kutoisikia/hisi-imejaa na inakua..Aliamua kwenda nyumbani na kupumzika. Anapoamka tu kwenda kanisani, ni love na amani ya ajabu inawaka ndani juu ya Anna and no more to Magret, lo! akajaribu kufanya maombi Bwana amsaidie kujua ni kweli ni Anna na love and peace anayosikia ni Yake Bwana au kibinadamu? ( ingawa kwa dalili zote. Alijua ni Mungu anafanya jambo ila kibinadamu akawa anasitasita tu. Aliporudi nyumbani, kilichotokea kilimshangaza kuliko kawaida..ghafla simu yake inalia…kuangalia kuna msg imetoka kwa binti sayuni Anna ikisema’’’Asante Yesu kwa kunipa Mkaka Mzuri mtumishi wako’’, alipoisoma hakuamini!!!!!!! akiibeba simu yake moja kwa moja mpaka kwa shemasi na kumwambia story nzima na ile sms. Shemasi hakua hata na muda wa kupoteza, akata shauri lile na leo hii Anna ndiye na Magret siye-atangoja wake.

Kwakua Mke mwema anapatikana/anatoka kwa Bwana basi vivyo ivyo kwa nini isiwe hata Mume na pia mchumba?.Na kweli ingawa Magret,Anna, wote ni wadada wa nguvu ktk kanisa na utumishi lakini kujua hasa ni nani kati ya hao maana wote wana viwango tu kiimani na kikanisa/kiushirika,hakika Roho Mtakatifu inabidi ahusike, otherwise, it is confusions out of so many blessings maana wote wanafaaa na wanalipa maana wana mpenda Yesu na wako serious ktk utumishi na wokovu na wanakwenda mbinguni.

Press on,

Edwin Seleli

Advertisements

16 thoughts on “Si Mke mwema tu, hata mchumba bora hupatikana kwa Bwana!!

 1. Niwakumbushe vijana wetu wa kike na kiume,kuingia katika ndoa ni mpango wa Mungu juu yako.So your role here is to follow instruction,in order to archieve your goal in marriage.HAPPY HUSBAND,HAPPY WIFE.DON’T LOOK AT PHYSICAL APPEARANCE,FIND HOW SPIRITUAL LIFE IS.TRUE HUSBAND OR WOMAN COMES FROM GOD WHO SEARCHES HEARTS.

 2. amen ushuhuda huu umenipa nguvu a kuzidi kufuga na kuomba Mungu atimize mapenzi yake kwangu kwenye mahusiano baada ya misukosuko niliyonayo katika uchumba nilionao

 3. nami nimebarikiwa sana lakini nipo njia panda nilikuwa na mchumba lakini tumeachana bila sababu ya maana nahisi nilikurupuka namwomba mungu anisaidie nipate mume mwema maana naamini yupo bwana amwandaa kwa ajili yangu

 4. Ahsante!bila shaka hiyo sauti ya kwanza niliyoisikia haikutoka kwa Mungu kwasababu hao kina dada wawili(Loisi)walikuwa ni wakristo wa jina maana hawajaokoka.Wala hayakuwa mawazo yangu maana wala sikuwahi kuwawazia akilini mwangu.

 5. BWANA YESU ASIFIWE WATUMISHI WA MUNGU, MUNGU NI MWEMA, KAMA KWELI TUKIOMBA NA KUMTANGULIZA YEYE HAKIKA ANATENDA, TUSIVUNJIKE MIOYO PIA TUWE NA SUBIRA! MBARIKIWE SANA WAPENDWA

 6. Pastor Amosi Munkenyi,

  Ubarikiwe kwa kupata experience iyo ktk mahusiano na kutafuta mwenza na kukaa ktk ndoa sasa 15, wow, safi sana, na mdumu hata miaka na miaka mingine, aimen

  Ila swali dogo ili upate nafasi ya kufafanua..ulisikia sauti kua mchumba ni LOISI kisha baada ya kuomba Mungu akufafanulie ni LOISI yupi maana walikua 2-bila shaka unaowafahamu, Bwana akakuambia ni Rhoda atakua Mkeo na ndie hadi sasa, aliyesema nawe mara ya kwanza -ile sauti ulisikia kua ni Loisi, ni nani? pepo, Mungu au mawazo yaliyoiandama sana akili yako?

  Press on

 7. NI HAKIKA NA KWELI HATA MIMI ILITOKEA,SIKU MOJA NILISIKIA SAUTI INANIAMBIA MCHUMBA WAKO NI LOISI,NA WALIKUWEPO KINA LOISI WAWILI,IKABIDI NIMUULIZE MUNGU ANIFUNULIE NI YUPI SASA.WAKATI WA MAOMBI BWANA AKANIAMBIA RHODA ATAKUWA MKEO,HAPA SASA ILINILAZIMU NIZAME SANA KATIKA MAOMBI,HATIMAYE JIBU LIKAWA KWAMBA RHODA NDIYE MKE MWEMA NA HADI SASA TUMEDUMU KATIKA NDOA KWA MIAKA ZAIDI YA 15

 8. Nimefurahishwa sana na ushuhuda huo hapo juu,unafundisha sana,kila mtu anaye aliyepangiwa na Mungu ila tusibweteke tudumu katika maombi Bwana aweze kutufunulia wenye kuhitaji.

 9. Ushuhuda mzuri unatia moyo,Mungu azidi kututia nguvu ktk kutafuta aliye wa bwana.

 10. Nimebarikiwa sana na ushuhuda huu,kwani inanipa nguvu yakuzd kumuomba Mungu na mim anipe mume mwema. Kwan na mim nipo kwenye maombi hayo hayoo na mim nimechoka kudanganywa na vijana wa siku hiz naamin Mungu na mim atanipa tu wa kwangu.

 11. mimi nimeipenda sana hii. Mimi nilijaribu sana kama kujitafutia mwenyewe lakini. hai kutokea, kuna kipindi nilikua na mtumishi wa Mungu lakini, nilikua nikipata ndozo za ajabu ajabu nikajua huyu sio wangu. sasa hivi naendelea na maisha na najua Mungu atamleta aliye mwema kwa wakati wake mwenyewe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s