KUTOA ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato.

sadaka+zaka

Wana SG, mafundisho ya kutoa zaka kila upatapo kipato ni SAHIHI, sio mafundisho potofu hata kidogo. Naomba ninukuu maandiko ambayo tunayafahamu sote kisha nitayafafanua. “Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi“. – Mwanzo 28:22. Hebu ongezea na andiko hili “Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili”. – LUKA 11:42 (SUV msisitizo added).

Utoaji wa Zaka/Fungu la kumi/Sehemu ya kumi ni jambo lilikuwepo hata kabla na baada ya sheria. Yakobo anasemakatika kila utakalonipa hakika ………. Bwana Yesu anawaambia mafarisayo wasiache kutoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga. Swali ni kwamba ni wakati gani mboga mboga hizi zinapatikana? Je si wakati wa kuzivuna? Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa kila atoae zaka yampasa kuleta ZAKA KAMILI ( Malaki 3:10). Logical thinking rahisi ni zipi, kuleta zaka kamili kwa mtu wa kawaida ambaye uwekaji wa kumbu kumbu sio kivile? Hivi Mungu huagiza wanawe na kisha kuweka ugumu wa kuyatekeleza. ukikaa na zka muda mrefu hakuna uwezekano wa kusahau, na ukisahau itakuwa umetoa zaka kamili? Kwa nini mambo yasiwe rahisi kwa kutoa kila unapopata? Hebu chukulia mfanyakazi akae na zaka kisha baada ya mwaka ndipo atoe, Je, ataweza kutoa mapato ya 120% (yaani 10% mara miezi 12)?

Ninajua tunakubaliana kuwa kutoa Zaka ni wajibu wa kila mwamini. Sasa frequency (mara ngapi kwa kipindi gani) isiwe issue. Huenda mpendwa Milinga unatatizwa na andiko lifuatalo; nanukuu “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka”.  – KUMB 14:22. Kama ndiyo andiko hili, basi naomba uangalie tafasiri zingine zinasema nini kuhusu maongeo. Hebu angalia ya KJV – neno maongeo limetafsiri ni “increase”, yaani ongezeko. Hawa ndugu zetu walikuwa na aina mbali mbali za Zaka katika kitu kimoja. Wote tunajua kuwa zaka zinatolewa nyumbani mwa Bwana lakini hebu ona hii “Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;”. – KUMB 14:28(SUV – msisitizo added). Agizo hapa ni kuiweka zaka ndani ya malango yako sio nyumbani mwa Bwana!!!

Pia kuhusu ile zaka ya kila mwaka inawezekana walikuwa wanavuna mara moja kwa mwaka. Ona tafasiri hii  “You shall tithe all the yield of your seed, which comes forth from the field year by year”. – Deut 14: 22 – RSV. Hivyo mavuno ya shamba ni tofauti na mambo ya msharaha au faida katika biashara ambayo mpendwa anapata mapato kila mwezi, wiki n.k. Nimalizie kwa kusema, Zaka ya kila mwaka iliyoonyeshwa hapo juu, ilikuwa inatolewa nyumbani mwa Bwana lakini inaliwa na mtoaji pamoja na mlawi. Swali ni hili Je, Zaka unazotoa huwa unakula mwenyewe? Zaka ya kila baada ya miaka mitatu ilikuwa inatolewa na kuwekwa malangoni ili mlawi, mjane, watima na mgeni wakiiona waweze kuchangamkia (Soma mwenyewe KUMB 14:22-29 uthibitishe).

Ninaona kuwa nimejibu hoja hii na kuthibitisha kuwa kutoa zaka kila unapopata mapato ni mafundisho sahihi na inawezekana pia nimekuongezea na aina nyingine ya Zaka.

Keep on digging.

Mathew.
Advertisements

176 thoughts on “KUTOA ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato.

 1. Barikiwa sana mjoli Steve Sungura. Umefanya kazi iliyo njema kabisa. Kumbe Mungu ana watu hapa Tanzania wanaoweza kufundisha Gospel of the Grace of God with such fullness of grace? Kusema kweli mimi nimejifunza sana. Comment zako zimenigusa sana. Nikatamani hata nikufahamu binafsi ili niweze kufanya ushirika na wewe. Kufanya fellowship na wewe. Natamani nitapata kibali.

  Mungu ni mwema sana, asante sana SG; kwa kutoa nafasi ya kujadili namna hii. Hii maada imeenda kwa kurasa za word document 301. Ni kitabu cha kutosha kabisa. Nashauri m-compile jinsi ilivyo na ikiwezekana ifanywe kuwa kitabu cha kujifunzia kwa mwili wa Kristo.

  Amina Haleluya!

 2. Swala la utoaji ni swala jema sana.Lakini kwakua ilisumbua watumishi wa MUNGU kipindi kile kwa kusisitiza mambo ya DINI Mungu akakasirika akazikataa dini zao zote na nyimbo,vinanda na sikukuu zao.Sababu ninini?Hata sasa hivi fuatilia uone jinsi Dini na Madhehebu wanavyo sumbuka sana katika kutetea dini! Dini mnazo zitetea Mungu amekwisha zikataa! Amosi 5:21

  Badala ya kufundisha neon la uzima watu wamjue BWANA mnafundisha atoe zaka na sadaka mbalimbali.Ndio maana wanatoa lakini hawabarikiwi na wengine hata bado wamefungwa na yule muovu katika maisha yao.TOA UTABARIKIWA WEWE ACHA UTAPELI.Mfundishe waumini wenu njia ya BWANA wamjue wamtumikie.Mtu ameokolewa badala afundishwe neno.Anafundishwa kutoa iliabarikiwe.Wengi wamekua wakihama makanisa yenu sababu ya unafiki huohuo.Wanatoa hawabarikiwi,wakienda kwenye makanisa ambayo yanamafunuo katika kumtumikia BWANA.Wanafundishwa utumishi,wanatumika kwa moyo na MUNGU anafungua Baraka kwenye Nyanja mbalimbali za kimaisha.

  VIONGOZI VIPOFU MNAPOTEZA KONDOO WA BWANA MTAWALIPIA DAMU GANI????????
  Maana mnawafundisha kutoa zaka lakini sabato takatifu hamwafundishi mkidai imepitwa na wakati ni aganolakale.Kwani zaka ni agano!?
  Yesu aliwalaumu mafalisayo hivyohivyo. Mathayo 23:23 Wanatoa zaka weeee wakati mioyoni mwao wanatafuta kumuua Yesu.Ndio ninyi mnawalazimisha watu watoe matokeo yake wanatoa ilimuwapende au waonekane kama wanatoa.Mwisho wake hawabarikiwi sawasawa na maneno mnayo nadi.

  Waumini wenu wanatenda dhambi,kuikemea dhambi hiyo mnashindwa kwanini? Kwasababu mkiikemea watu hao watahama waende hukooooo…ambako hawatakemewa.
  NINYI MNACHOJALI NI KUJITAJIRISHA..MKIKUTANA KWENYE VIKAO MNAANZA KUJINADI”Namshukuru Bwana nyumba yangu imebarikiwa ninawaumini elfu tatu kati ya hao nina watumishi wa serkali elfu moja wenye mishahara ya maana pamoja na wafanya biashara za kwenda nje ya nchi mia sita”.

  WEWE MTUMISHI WA BWANA IWAPO HAUNA UHAKIKA NA MUNGU UNAYE MUHUBIRI BADALA YAKE MWAZO YAKO YOTE UMEYAWEKA KWENYE MISHAHARA YA WATU JE,UTAWEZA KUKEMEA DHAMBI?

  JIFUNZENI KWA NABII ELIYA AD2”The pool of Sloam Church”amefundisha watu kumjua Mungu wao na neno la Uzima,matokeo yake watu wanamtumikia MUNGU kwa moyo wa kupenda.

  Sio kila mara unawafundisha watu kutoa,mara uchumi na mkristo,mara wokovu wa kimaskini!Hizo ni mbwembwe tu!WAUMINI WAKO BADO WAMEFUNGWA NA MATESO YA SHETANI..KUOMBA MUNGU AKUPE MAFUNUO JINSI YA KUSAIDIA HAO WATU UNATUMIA MANENO YA UJANJA UJANJA ILIUJITAJIRISHE WEWE MWENYEWE.
  NARUDIA MANENO YA BWANA KWA KINYWA CHA AMOSI 5:21”Sipendezwi na makutano yenu ya dini”…japokua mnanitolea sadaka.msitari 22.

 3. Mate wangu Milinga

  Kwakua ni wewe Kaka yangu Kiroho na umekuja hapa baada ya muda mrefu na ni mara ya kwanza una show up hapa, na-respond kwa ajili yako na labda mgeni mwingine maana nilishamaliza hapa/uku, unless itokezee haja nzito tena ya kurespond kwa waliokua tuna engage nao. Nimesoma comments zako nimecheka na kubarikiwa kweli, manake umenikumbusha Misri kisha wanileta Canaan. Labda kwakua umelianzisha, niwabariki kabisa wapendwa hapa kwa kuongezea shuhuda ILI WAMTUKUZE YESU KWA KAZI YAKE NJEMA YA KUSAIDIA WANADAMU WAMJUE MUNGU WA KWELI. Toka miaka iyo niko full devil, wewe full Bwana, kisha na mimi later full Jesus, ilikua ni wewe na wenzako mkiwa wanafunzi mliookoka na mko fire mwanzo mwisho, mnaendesha ibada zenu, nikaja kuwachungulia/joke ‘’ninyi walokole msio na akili ,mnakaa kupigia-piga kelele na kusumbua watu’’, mlipokua mnafanya ibada zenu baada ya prep time, saa tano kasoro usiku nje, nyuma ya darasa la form 3b na juu 4b, chini ya mti ule, ‘’NIKANASWA NA UJINGA WENU’’ NA NIKAOKOKA.

  Nakumbuka, Hukuamini kua naweza acha kuruka majoka, dadaz, ngumi nje nje, vurugu,migomo ya shule kuvunja mali ya shule na kuzinyuka na vilanja, kuvunja stoo za misosi na kuchukua sukari, kuingia madeal ma walinzi jikoni na kunivushia nyama, maziwa, soap, wakitakaa, usiku nawavizia na kuwanyuka mitama na wenzangu kiisha tunateka portion ya chakula chenu wote, kudanganya mie mgonjwa ili nipate special menyu ya wagonjwa, kulala bwenini na kula ganja, fegi, darasani siji, kukacha tests, kuibia mitihani, kuchapa ela za Wanafunzi wenzangu wakitoa likizo( una bahati sana sikuzikomba zako), nilikua nakomba mpaka soksi mpya mpya, nk.

  Ilikuchukua ka muda kujua kweli Seleli amemaanisha au fix za town , kisha ukaanza kuamini na ghafla ukanipenda sana, ukanilea sana na wenzako lakini wewe ndio ulikua Kaka yangu wa kiroho kunilea. Kuna siku mlikua na maombi ya kufunga, mkanikomalia nifunge na mimi mara ya kwanza, tukawa tunaenda maombi pale shule ya Furaha Tbr, nilitaka kuzimia chumbani mule, njaa kali, siku ya kwanza ya kuacha msosi na kukomaa kama ninyi wazee wa kazi wa siku nyingi! Tumetoka mbali na asante kwa Bwana kwa ninyi kunilea, nakumbuka ulikua so close na moto wako ule wa kupaa-paa anytime, ukishukiwa hahahahah…Baada ya kuokoka that night, hamkujuaga tu, niliendelea nanyi but kwa siri naenda kwa Mama Mary RC- nilimpenda sana Mama yetu na nilikua mtumishi wa altare na unajua dini yetu ina hadhi duniani, kuicha haraka niliona si ‘sawa’, nikawa pia kwa siri nakata kiu kidogo kwa majoka then nakuja kwenu, NDIPO HATIMAYE akaja Mze Kapama usiku na akina Abel- GOSPEL CAMPAIGN-HUIMA, kwa hall ya shule, NIKAOKOKA TENA-nikawa Born Again AGAIN- if you like, and from that time on todate, MIMI NI MTU MWINGINE KTK BWANA, Aiiiiiiiiiimen.

  Sasa kuhusu Mijadala humu, trend ya ushiriki wangu uko ktk shape hizi:

  Kwanza, kwakweli nakuhakikishia kua si rahisi kwa ninayojua au yanayonisadia kukua kiroho na kumtumikia Mungu vema, nikachanganya mada wala Maandiko, unless unithibitishie hapa kua nimefanya ivyo na kama naweza fundisha Neno nje ya usahihi wake-as God wants/intended. Show me wapi na kwa lipi nimefanya ivyo, kisha substantiate, otherwise nitaona ulisema tu by the way mate.

  Pili napenda sana kujikita ktk Neno hasa mwanzo wa mijadala/mada/issue na wakati topic ina burn up, ili kumaliza maneno mengi ya by the way, so ninge-appreciate sana, nawe ukinipinga, leta Neno kwa kuri-site au hata kulitamka! Si lazima kulikariri kama lilivyo-sura na mstari

  Tatu, napenda kuongelea mambo kama Mwalimu aliyesomea Masomo jamii sio physics! Kwahiyo, kama mada ni ‘’Nguvu ya Damu ya Yesu’’, ni LAZIMA NA NI UALIMU MAKINI NA WENYE TIJA KUONGELEA KWANZA DAMU IN GENERAL TOKA AK-ZILE ZA WANYAMA kisha kirahisi kabisa napoendelea, naunga kwa ulaini Damu ya Yesu LEO-kama uko kunaitwa ni kutoka nje ya mada, kuongelea vitu vingi au nje ya context, basi NITARAJIE KUTOBADILIKA maana mwanafunzi abaki mwanafunzi, Mwl siko zote Mwl, mwana Fizikia vivyo ivyo na upako wake na Mwana lugha/jamii na upako wake na PIA MWANA KIPAJI CHAKE abaki nacho maana hatufanani yale tuliyojaliwa na Bwana ktk huduma. Pia elewa tu kirahisi kua wakati mwingine kwa AINA ya mada na NAMNA watu wanavyouliza main na minor issues, KUONGELEA VITU VINGI kama vile unakwenda mbali na ile iliyo kwa table kisha kurudi, ni kitu cha kawaida kabisa ktk mijadala moto moto, sitarajii navyo kufahamu na tunavyofahamiana , ushangae icho, utakua ni mate wangu au your God given fire/capacities nazozifahamu mimi, zimekua corrupted.

  Nne, nitamjibu/engage na Mtu KWA NAMNA ANAVYOKUJA! Kama alivyosema Paul-ninakua ktk hali zote kwa namna zote kuwapata wote or in this case..kufit situation zote. Ajaye kwa ‘fujo’, ‘upako’ huo upo, kwa utulivu, nipo sana, kiroho-roho-utapata pia, kiakili au na yale yote tuliyojaliwa kila mtu ya kimwili mazuri-yapo sana , akija kwa mastory ya mjini, wewe wajua mimi nitakua Mwl wake kwelikweli na akija on serious note-Biblically, Hoja, na nia ya kusaidiana then we will talk very lovely, powerfully and Godly lakini pia niseme kama Paul tena, akija kwa kudhani yeye ni bora zaidi, NITAMTHIBITISHIA NA MIMI NI BORA KWELI KWELI BILA KUMUNG’UNYA MANENO KWAMBA BWANA AMENIKUBALI NA NINA NEEMA TELE SI MCHEZO for his glory, Amen.

  Tano, napenda pia kutumia maarifa na vifaa vingine vya kufahamu na kufafamua mambo kama uzoefu, shuhuda, story, Akili, Maarifa ya kawaida, ILI MRADI ZIKO KTK CONTEXT NA SI KINYUME NA NENO.

  Baada ya kusema hayo, naangalia kwa ufupi uliyosema, Nataka kua constructively limited kwa my comments kwa zako ili nisirudie mada hii ambayo kimsingi ilisha kwisha, sema wewe tu mchelewaji ndio una hamu nayo, ikilazimu basi tuendeleze majadiliano.!!!!!!!!!!!!!!

  Kwamba maelezo ya Sungura sikubaliani nayo! NI KWELI kwa baadhi na mengine tunakubaliana. Pia yako maelezo mengine yangu amekubali pia kama yeye nilivyokubali yake. Yale tuliyotofautiana, itabaki ivyo maana msingi wake ni kutoa KWA HIARI ya mpaka KUJISIKIA na mimi ni kutoa HIARI ya KUAMUA bila kutoa nafasi ya uhuru sana au mpaka nafsi yangu itake sana maana nitashindwa mengi na mengine nitapuuzia kwa kua nature yangu kama Mwanadamu ambayo ndio nature yako wewe mate wangu, naijua inapokuja swala la noti zetu kuguswa. So statement yako kua sijakubali ya Sungura, SI kweli, SEMA baadhi. My advice: take your time kusoma comments za kutosha kama si zote , yaelekea kwa statement yako iyo, yako uliyosoma kweli na mengine ume rocket out tu mate.

  Na pia kuhusu Zaka, mimi nitatoa kwa kuamua mwenyewe kwa furaha yangu na kujipangia kua kila 1 kati ya 10 natoa kama my own way ya kuji-discipline kwa mali na mapato yangu yawe na agenda ya kimbingu na hiyo ni mbali na sadaka na machangizo mengine, lakini Sungura hatoa iyo bali anato sadaka tu, kwa ivyo, tutabaki tumetofautiana kwa namna iyo, mradi yeye wala mimi, hatulazimishwi kutoa icho tunachotoa na ivyo tulivyojipangia kutoa, umenipata sasa kaka? it is so clear and simple na nimeshangaa mtu wa aina yako, umeshindwa kuona na kua-appreciate my stand tamu na njema ivyo mbele za Bwana, sitakungoja maana msimamo wako kuhusu Zaka uko wazi sasa-Sungura/Lwembe/Amin namba 2 au wewe no. 1 kama mleta mada, wao 2,3,4, hence nita jia-appreciate mwenyewe kama Daudi alivyojitia moyo mwenyewe bila kuchelewa au kungoja wapendwa waguswe.

  Kwamba CK Lwembe na Sungura, wameitendea haki mada, ni sentence ya kishabiki zaidi kuliko facts. Ungekua muhalisia, si tu Seleli bali hata ungesoma comments za wengine, mfano yuko dada alitoa maandiko 56 kuhusu Utoaji generally na ya zaka pia yuko Mkaka alitoa ushuhuda binafsi kuhusu RM kumwambia kuhusu Kutoa, hayo na mengine mengi yangu,bado ungeona haki nyingine tuliyotenda kwa mada utaoji wa Watu wa Mungu. MATE wangu HUSIANGUSHE bwanaa, SOMA KABLA UJAKIMBILIA HAPA KUSEMA KITU, KIWANGO CHAKO NI CONVINCING, namna gani Kaka!!!!!!. I would love you mate kua fair hakimu not kuwatumia wao kusemea chako, ni bora useme tu moja kwa moja wewe pia ktk Utoaji na hasa Zaka, uko wapi na una shida au huna!

  Kwamba wameleta maandiko yenye mantiki na hoja! Yes or No! am sorry kwa mengine, sijaona hoja wala matumizi ya Neno kihalali na ktk hekima yote!- 2Tim.2:15c na Wakol.3:16. Nakuchalenji, angalia HOJA, MAELEZO, FAFANUZI NA MAANDIKO yangu kisha sema KWA HOJA kupinga yangu kimantiki then nitaona kama kweli una jambo la kunikosoa la nguvu hasa.

  Nitapenda fundisho si tu la ZAKA bali Utoaji wote na wowote na ktk yote, nitatoa kwa sharia ya rohoni ambayo kwangu si kwamba inanipa excuses bali kwa kua sasa naelewa zaidi, napenda na kupendwa zaidi, nitafanya zaidi utoaji na mengine.

  Kua hakuna aliyebarikiwa TZ kwa kutoa Zaka!!!!!!!!!!! Mate wangu, kwa hili, UMEKURUPUKA! How can you have the BEYOND REASONS OF DOUBTS, A CONFIRMED AND AFFIRMED spiritual research among the whole land Tz BODY OF CHRIST na kisha Watu waka-cooperate kutoa taarifa zao za fedha jinsi wanavyotoa na kisha kukuambia kua wamekwama na kwamba Mungu hakuwahi na hajawahi kuwabariki kwa utoji wao wa zaka hata kwa misingi ya Ibrahimu ? Milinga Juma Venerando my class mate, kwa ili umekuja kiinjilist/fire-fire one way no balance or simile, zaidi na si kimantiki. Kwakua tulisha maliza mada hii, nisiindelee sana otherwise ningekua na maswali kwa statement yako hii kukuthibitishia umekurupuka, labda nitayahamishia kule topic nyingine ya ‘’kama au kuna adhabu kutoa au kuacha toa kikumi, kama mwanya utatokea.

  Thanks brother and nina sign off tena kwa uku kwa ajili yako, ukipenda kunirudisha uku, unakaribishwa na nitakuja HAKIKA.

  Press on.

 4. Mpendwa Edwin Seleli my school mate,

  Kwanza naomba radhi kwamba sikuwa hewani kwa muda wa zaidi ya miezi 3 kutokana na kukatika kwa network ya internet hapa Kigoma nilipo. Sikuweza kufuatilia mijadala mingi hapa.Mada hii sikuweza kushiriki kabisa.

  Kwa kuwa mtandao umrudi sasa hapa nilipo, ninaweza sasa kushiriki mada zote.

  Mada hii nimeisoma sana na nimeweza kupitia hoja za wapendwa wengi. Hata hivyo nakiri kwamba Edwin Seleli namfaham tangu tukiwa Sekondari, nafahamu ongea yake, nafahamu swanglishi yake na anavyoipenda kila mara hata kwenye mijadala ya kiroho au mitaani yeye anapenda.

  Kwa wasiomfahamu Edwin ni kwamba kabla hajokoka pale Tabora alikuwa mtoto wa town sana na alipoenda Dar akasoma shule ya watoto wa mjini ndipo kabisa akawa mtoto wa Bongo.

  Katika mada hii Seleli umeeleza mambo mengi sana ingawa kwa kuchanganya mada nyingi kwa wakati mmoja. Hata hivyo inaoenesha kwamba bado maelezo na ufafanuzi wa hoja alioufanya Bwa. Sungura ni kama wewe hujaukubali.

  Nimependa sana Bw CK Lwembe na Mpendwa Sungura wanavyoelewa maandiko na hoja zao zenye mantiki. Katika mada hii ya Zaka hakika wameifanyiwa haki mada husika. Nami bila ajizi naungana nao kabisa kwamba somo la utoaji wa ZAKA limepotoshwa sana miaka nenda miaka rudi.

  Nadhani ni wakati mwafaka watumishi wa Mungu waliopo katika utumishi na hata wale wanaotarajiwa kuwa Mapasta kama Masanja Mkandamizaji, basi watarejea kwenye kweli hasa linapokuja swala la ZAKA.

  Edwin Seleli na wapendwa wengine ambao bado mwalipenda fundisho la Zaka nawaomba mtafakari upya. Soma tena maelezo ya Bwa. Sungura hasa yale ya mwanzoni kisha ubadilishe ufundishaji wako kuhusu ZAKA.

  Namalizia kwa kusema , “KAMWE HAKUNA MPENDWA WA KANISA LA KIROHO AU LA KILOKOLE HAPA TANZANIA ALIYEWAHI KUBARIKIWA KIFEDHA AU KIUCHUMI HADI AKAWA MILIONEA AU BILIONEA KWA SABABU TU YEYE ALITOA ZAKA KANISANI KILA MWEZI AU KILA MWAKA KAMA YUPO NAOMBA JINA LAKE”

 5. Naam Seleli;
  Nafikiri umekubaliana sasa na kauli/ushauri wangu wa kukubali kutokukubaliana ambao mara ya kwanza uliona ni kama wazo ambalo halina maana.

  Kiukweli nilijua kuwa hakuna namna unaweza kuthibitisha kuwa kwa mujibu wa agano jipya kila mkristo anapaswa kulipa zaka. Hakuna aliyewahi kuthibitisha hilo katika wote ambao husema mkristo anawajibika kulipa zaka. Na hiyo ni kwa sababu ni kweli kabisa kuwa mkristo hawajibiki kulipa zaka. Lakini mtu akiona kuwa kulipa zaka ndio njia inayomfaa yeye kumtolea Mungu,basi akazane kufanya hivyo kama anafanya kwa moyo wa kupenda. Si kama ambavyo leo iko katika makanisa mengi yanayoitwa ya kiroho,mpaka inafika hatua majina ya wasiotoa zaka kubandikwa ubaoni.

  Kwa hiyo suala la muhimu linalotakiwa ni mtu KUMTOLEA Mungu toleo analoona kuwa litaugusa moyo wa Mungu. Hivyo, kuna mwingine anaweza akaamua kutoa nusu ya mshahara wake, mwingine akaamua kutoa 20% ya mshahara wake, na mwingine hata mshahara wote. Limradi imefanyika kwa moyo wa kupenda.

  Juu ya mambo hayo hakuna sheria yoyote. Hiyo ndio maana ya kila mtu kufanya kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa kulazimishwa, na kuambiwa usipotoa kitu fulani umelaaniwa. Huko ndiko kumtolea Mungu kwa moyo wa kupaenda.

  Ni kweli kwa mujibu wa kanuni ya kibaiolojia, kila binadamu huwa ni lazima ayafanye hayo ambayo unasema hayakuandikwa kwenye biblia kuhusu Yesu.
  Lakini kwa mujibu wa kanuni ya utoaji si lazima kila anayetoa atoe kwa njia ya zaka ndipo ahesabiwe kuwa ameugusa moyo wa Mungu.
  Yenyewe inataka kila atoae kwa ajili ya kuugusa moyo wa Mungu anatakiwa tu atoe kwa moyo wa kupenda.

  Ni vema ukakumbuka kuwa katika huu mjadala mrefu kitu ambacho nimekionesha na kukisema kuwa ni tatizo si kule mtu/mkristo kutoa 10%(zaka) ya mapato yake, bali ni kule kulazimisha kuwa kila mtu/ mkristo anatakiwa kutoa zaka ya mapato yake ndipo aendelee kutoa matoleo mengine,kwamba asipofanya hivyo ati ametenda dhambi, au amemwibia Mungu.

  Si lazima kila mtu atoe kama Ibrahim baba yetu wa imani, au kama Kolnelio,bali kuna namna nyingi tu za kumtolea Mungu ambazo hugusa moyo wa Mungu zinapofanywa kwa moyo wa kupenda.

  Kitu kingine cha kuelewa ni kwamba zaka ilikuwa ‘so specific’ katika utoaji wake na matumizi yake kiasi kwamba si rahisi hao wa kanisa la kwanza (unaodhani kuwa yawezekana katika matoleo waliyotoa na zaka ilikuwemo) wawe waliitoa bila kuwa identified. Maana kumbuka zaka ilikuwa inatolewa hekaluni palipokuwepo na kuhani mkuu mara moja kwa mwaka, wala haikuwa inatolewa kwenye masinagogi.

  Na zaka ilikuwa miongoni mwa zile sheria zaidi ya mia sita,ikiwemo tohara. Ambazo ndio ule mzigo ambao Petro anauita kongwa lililowashinda wao akina Petro,pamoja na baba zao pia, ambalo mitume waliona si vema likatwishwa watu wanaomwamini kristo,yaani Kanisa.(Acts 15:10 Now then, why do you try to test God by putting on the necks of Gentiles a yoke that neither we nor our ancestors have been able to bear?
  Kongwa(sheria ya Musa) hili ni waliookoka wenye asili ya mafarisayo ndio walitaka kanisa wabebeshwe,lakini ashukuriwe Mungu maana mitume waliliona hilo, wakakataa.
  (Acts 15: 5 Then some of the believers who belonged to the party of the Pharisees stood up and said, “The Gentiles must be circumcised and required to keep the law of Moses.”)

  Kwa hiyo Seleli kama wewe umeona ili kujinidhamu vizuri kwa ajili ya Mungu kwa habari ya mapato yako kuna ulazima wa kujifunga kwenye mfumo wa zaka, basi fanya hivyo kwa bidii zote,na wala mimi sikwambii neno lolote, maana si dhambi.

  Mimi simtolei Mungu kwa njia hiyo ya mfumo wa zaka, bali nimeamua kumtolea kwa njia ya sadaka, machangizo, misaada, n.k, nawe usiniambie neno lolote, maana hivyo ndivyo nilivyokusudia mimi moyoni mwangu, maana si dhambi.

  Muktadha uliousema, unakufaa wewe na wale wanaoona kuwa bila kujifunga kwenye zaka hawawezi kujinidhamu kumtolea Mungu. Hii ni njia inayowafaa watu wasioujua vema uhuru ulio katika neema ya Mwana wa Mungu. Watu ambao wangetamani utumwa kuliko uhuru,maana uhuru kwao ni mzigo,kwa sababu uhuru unawataka wajipangie wao kwa moyo wa kupenda ni kitu gani wanachojisikia mioyoni mwao kitapendeza kumtolea Mungu wao.

  Kumtolea Mungu kwa njia niliyoianisha ndiko hasa kunakoonesha kuwa wakristo/kanisa haliko chini ya sheria ya torati, bali liko chini ya sheria ya roho wa uzima iliyo katika kristo Yesu, ambayo imeliweka kanisa mbali na sheria ya dhambi na mauti nalo liko huru kwelikweli.

  Seleli, si wajibu kila mkristo kumtolea Mungu kwa njia ya zaka!

  Bless u!

 6. Sungura, NINAHITIMISHA MADA HII KWA UPANDE WANGU

  Baada ya muda wa kutosha wa kuelimishana, kukosoana, kuhojiana, kukataliana, kukubaliana, Kuchallenjiana, kupingana tikitiki, hatimaye namaliza michango yangu kwa kufanya summary ya comments zanga na nyongeza kiasi kama ifuatatavyo.

  Najua kwa hakika mojowapo ya tabia kuu za Mungu, ni Utoaji ivyo sisi kwa wana wake, ni vema na haki si tu kua na tabia iyo bali kuifundisha, tetea, ambukiza

  Naamini na kwa kweli najua kabisa kwa dhati kua Biblia imesema, kutoa ni kwa kadri ya kila mtu alivyokusudia moyoni mwake, si kwa lazima

  Nafahamu kwa hiari inayotokana au kusukumwa na moyo wa kujiachia mbele za Bwana nafsi na yale tuliyonayo, na tafakari ya kweli jinsi Mungu anavyotupigania na kutushindia mengi, ndio moyo na akili aliyokua nayo Ibrahimu baada ya kushinda vita ile, ikapelekea kujaa shukrani kwa Bwana Mungu hata kutoa zaka ya kwanza kabisa ktk Bible kabla ya sheria au utaratibu wa wazi toka kwa Mungu ulioandikwa kuhusu kutoa Zaka.

  Ningependa maisha yangu yawe kwa mfano huo wa Ibrahimu kua, nitambuapo kua bila Mungu mimi si kitu na kua kuishi kwangu ni Bwana, yote niliyonayo, nitakayopata ni kwa neema yake, basi ufahamu huo unipelekee kwa raha, furaha, uhuru, hiari, maamuzi ya dhati ya moyo wangu, kujipangia mwenywe kua kila nipatapo, ninatoa 1 kwa mambo ya Mungu( Utumishi hemani kwangu, kwa Mlawi wangu wa leo, wahitaji nk kisha yaliyobaki 9 nakula. Nisipenda kua aina ya mkristo ambaye nakula kila kitu mwenyewe, ninaona huo ni ubinafsi uliopita mipaka. Hata kama Mchungaji wangu ni Mengi au Bakresa, sitoi kwa kanisa au kwake binafsi kwakua ni yeye ni mhitaji au maskini bali natimiza takwa la Neno ili nibarikiwe, yeye ndio ataamua afanye nini na toleo langu hata kama ni tone tu ktk bahari yake ya mafanikio binafsi.

  Sidhani kama ni vema kwa Mkristo anayeishi kama mtoto wa kiroho wa Baba yake kanisani, mwenye kuhusika kwa moyo na mwili shughuli na maono ya Baba yake anayemlea kiroho kisha mwana huyo awe na tabia ya kutoa KWANZA matoleo mbalimbali namely Zaka, Malimbuko, Changizo, Sadaka nyingine ziwazo zote, NJE ya kanisa lake, Mchungaji wake wala hasiwe na mzigo na kipao mbele kwa pale nyumbani. Pia naamini si hekima, kua Mkristo huyo akawa anatoa tu kwa wahitaji kanisani kwake bila kwanza kutoa kwa mambo ya jumla ya familia yao hapo kanisani kwa maana ndogo tu kua, kanisa kama familia, lazima litakua na utaratibu wa kuwasaidia wahitaji ndani humo kama wajane, yatima, wapendwa wenye mapito mazito. Ni hekima na busara kuishi kanisani kama kondoo wa baraka, mtu wa utaratibu, kutozua shari na tafrani, kutokua na mambo ya kwako-kwako kivyako-vyako. Jambo lolote likifanyika nje ya utaratiubu HALALI NA WA BARAKA TENA ULIOWEKWA NA WATU WA MUNGU MAKINI WENYE HEKIMA, RM, BIBLE MOYONI,hata kama ni jambo zuri lililotendwa bado halina baraka kwa maana hatukuitiwa fujo ndani ya kanisa/Ushirika mmoja.

  Ningependa kua Mtoaji hata aliyepitiliza au crazy if not sacrificial mfano kutoa hata 20%, 30%, 50%…. na hata Isack kwa kua KUTOA ni moja ya tabia KUU au KUBWA za Mungu ukisoma Biblia toka AK hado AJ ambapo utimilifu wake ni alipoMTOA Mwanae wa PEKEE wakati tungali tu dhambini wala hatuna habari lakini Yeye anawaza KUTOA ili tupone. Kwa mantiki hii, ningependa kua Mkristo ambaye kwa kauli ya mahubiri na mafundishao yangu kuhusu KUTOA ktk blog hii na uko na kule yawe ni yale chanya yanayo hamasisha,tia moyo, sukumwa kwa maarifa sahihi ya Neno kuwatia shime watu wa Mungu KUTOA na si vinginevyo maana najua hatari ya nature ya mwanadamu hasa nafsi zetu, zinapopewa nafasi ndogo kufanya vitu kujifurahisha, nature zetu hupitiliza na kusahau kabisa kuweka kipao mbele kwa vya Mungu. Ni heri mimi nihesabikie mbele za Bwana kua nimesema na kutenda ktk namna ambayo, haitoi mwanya kwa nafsi/nature zetu kupata mwanya kusumbua ya rohoni yanapostawi, naamini nikiwa mfundishaji wa namna hii, Bwana Mungu atanihesabia haki na kuniwekea marks zangu kua ninatenda jambo linalofurahisha moyo wake na lenye tija ktk kazi ya Bwana kwa Mwili wa Kristo

  Naamini kua Mathayo.23 kama ilivyo Mathayo 12 au injili yoyote ambapo tunakuta imeandikwa live kabisa kua Yesu anazungumza na Makutano na Wanafunzi wake, kisha anawa-address in particular, kundi fulani say Mafarisayo, Sadukayo, Waandishi, Wakuu wa dini, Watoza ushuru, wenye dhambi, Wacha Mungu, Watakatifu wa zamani nk, au anaongea na Makutano lakini haijaandikwa live kua anaongea na Wanafunzi wake, simple common senses can conclude accurately kua WANAFUNZI WAKE HASA WALE TENASHARA, WALIKUA NAYE KILA MARA hence kila kilichoongelewa, kina sehemu kwao pia hata kama hawakutajwa, na wakitajwa kabisa live, hapo tena ndio haswaa, linawahusu na wao pia.

  MANENO YA YESU MWENYEWE(which kwa hadhi ya Yesu, his Words/Msg should be for all generations past, present, future), si salama sana kuyachambua/kuchuja kua hili langu, lile la Mafariayo nk. Najua kwa hakika hata kama kweli aliwa-address makundi kadhaa ktk speech zake, Yesu hakumaanisha hao tu wahusike na Neno lake bali na wafuasi/Wanafuzni wake wote.Iliwapasa wadake yapi yakufanya toka hayo aliyoaddress some people in particular.Kunyambua kua ili ni la wale, na si lazima liwe letu leo, uhuru huo tunao hasa tuyachunguzapo maandiko yanaonyesha maneno na matendo ya wanadamu wenzetu akina Paul, Petro, tuna uhuru mkubwa kwao maana wao ni kama sisi tu, hakuna tofauti hata kidogo( Yak.5:17) but Yesu ni issue nyeti/nyingine. Kwa mantiki izo, ndio maana bado leo nitatoa zaka kwa mfano wa Ibrahimu na hata kwa kutumia Mathayo iyo 23 kwa kua nitafanya ya adili kwanza kama aliyosisitiza Bwana kisha siyaachi na yale mengine! why? Kwa kua nimesema juu kua, hata kama aliwa-address makundi kadhaa, Maneno yake Bwana, bado nasi yanatudai kupitia aliyowasema wengine KAMA VILE YALE ALIYOSEMA KUTUHUSU SISI, YANAVYO WAFAA/DAI/HUSIKA NA WENGINE NJE YA SISI wanafunzi/tenashara/Wana wa Mungu/Marafiki zake.

  Kwakweli nina amini kabisa kua yako mambo hayakuandikwa ktk Bible live yet ni KWELI TUPU. Lakini tunatambua kua hayo yasiyoandikwa ni KWELI TUPU kwa njia ya kutumia KWELI NYINGINE za NENO hilo hilo, ingawa pia kwa tafakari ya Akili zilizobarikiwa za mwili huu huu, pia ung’amuaji wa mambo ya kweli uwezekana pia. Mfano kwa kua imeandikwa ..’’alifanyika MWILI akakaa kwetu, then kwa mwili wake lazima alichoka,alilala, alishangaa, alililamika, aliona njaa/kiu, alilia, alikasirika sana/chukizwa, alihuzunika, alifurahi, ALIOGA,PIGA CHAFYA, MIAYO nk

  Kwa mantiki iyo juu, naamini kwa kweli kua ktk wale wanawake waliokua wanatoa substance zao kusapoti kazi ya Bwana, makusanyo ya matoleo/changizo mbalimbali zilizokua zinafanywa makanisani kusapoti kazi ya Paul, kuwasaidia wahitaji makanisa mengine, sadaka zilizokua zinaletwa miguuni pa Mitume, wapo wapendwa waliotoa malimbuko, zaka, sadaka za upendo nk maana haikuwahi kukatazwa kua kua wakitoa kwa mtindo huo ni dhambi!!!!!!!! Naamini wako waliotoa Zaka kwa moyo wa hiari, furaha na maamuzi yao binafsi kama Ibrahimu na hata walitoa Isack!-zaidi ya zaka ya 10%! Na kwakua waaumini wengi wa kanisa la Kwanza, wamekua na background ya AK na kwa kua hakuna andiko hata moja la LIVE au la indirect linazuia Zaka kwa mantiki ya Utoaji wa zaka wa aina ya Ibrahimu, na kwa kua kawaida watu wakisha kuokoka, ile furaha na raha ya kua ndani ya Bwana, uwaongezea thamani, kicho, heshima, kuwajibikia kwa mchecheto wa raha mambo ya Mungu na kazi yake-ktk mood iyo, mpendwa hufanyaga mambo mengi makubwa, thus, sioni kama mtu/wapendwa wale kujiwekea-this time-si kwa sheria ya mwili but kwa hiari na raha au tusema sheria ya rohoni kua anatakua anatoa zaka, sidhani kua ilikua ni issue kubwa saaana kama ilivyothihirishwa ktk mijadala yenu humu.

  Kwa mantiki iyo, siamini hata kidogo kua , walipookoka tu, kati ya vitu walivyowahi-wahi kuviacha na kupumua mpumuo mkubwa kua lo! afadhari tumeooka sasa, tunachana na hili na lile, zaka ni moja wapo!

  Hatimaye, ninaamini kua kumuhesimu Bwana kwa mali zetu, kujiwekea hazina mbinguni, wapeni watu vitu, heri kutoa kuliko kupokea, yote hayo yana namna nyingi za kuyatekeleza ila binafsi yangu, kujipangia pia kua niji-dicipline na nafsi/mali isiniendeshe/kunitawala, niithibiti vema kabisa ili niweze muheshimu Bwana kwa mali zangu, basi kutoa 1 ya kila kumi yangu to fit hayo maandiko kwa baraka zangu mwenyewe, ni staili ya maisha ya uchaji njema sana.

  Naona kua hitimisho langu hili, lina tija kwa maisha ya Kiroho ya MTU BINAFSI NA KIKANISA na nila mkristo mwema mwenye kutaka sana kazi ya Bwana kanisani kwake, kwa watu na nje ya kanisa, isonge mbele lakini pia linadhihirisha hamu ya mwana wa Mungu anayejizoeza maisha ya utaua kwa maneno na matendo eg ya utoaji sana kama Baba yake wa Mbinguni alivyo, hence, hitimisho lolote lisilo na muktadha huu wangu, naliona nila kinafsi zaidi kuliko mbingu .

  Press on.

 7. Seleli unaposema kuwa comments zangu zimejaa kasoro, ni kwa sababu unataka ziwe kama wewe unavyodhani zilitakiwa kuwa.

  Hakuna kasoro yoyote kwenye comments zangu kama ipo niambie tu nifafanue ili kujua zaidi nilimaanisha nini.

  Ha ha ha a…
  Kuna kitu umeichekesha, nilidhani kweli nilikosea katika kukiandika, lakini kumbe nilikuwa sawa kabisa,ila ni matatizo yako tu ya kukielewa. Na ni kule kusema kuwa Mungu hakuamuru walawi wapewe zaka sababu ya kutumikia madhabahu.

  Ni rahisi sana nilichokisema,kiangalie tu kwa makini;
  Kwamba kama Mungu angeamuru walawi wamtumikie madhabahuni au hemani au hekaluni lakini na urithi wa ardhi wapewe, basi kusingekuwa na sababu ya wao kupewa zaka kuwa urithi wao kwa ajili ya utumishi wao kwa Mungu. Yaani kama wangekuwa na ardhi au ruhusa ya kufanya shuguli zingine za kujipatia kipato, basi Mungu asingewapa zaka lakini utumishi wa hemani wangeendelea nao kama kawa.

  Kwa hiyo hawakupewa zaka kwa sababu walikuwa wanatumikia hemani,bali kwa sababu huo utumishi wa hemani uliwekewa sharti la kwamba mtu(mlawi) akiutumikia haruhusiwi kuwa na ardhi au kufanya shuguli nyingine. Simple..
  Wala hakuna uongo wowote nilioongea!!!!

  Halafu unamaanisha nini unaposema kuwa ili nihalarishe kula kila kitu mimi?

  Je, unamaanisha kuwa asiyetoa zaka anakula kila kitu yeye, zaka na sadaka au michango kipi huwa kikubwa zaidi kwa mtu anayejua maana ya utoaji?
  Dont try to judge wahat u are not sure of brother!

  Sioni aibu kukwambia kuwa ufahamu wako juu ya suala la zaka umefungwa, hutambui Seleli. Ndio maana unadhani kutoa zaka ni kuacha ubinafsi, lakini huoni kuwa anayetoa sadaka ndio hana ubinafsi kabisa.
  Ndio maana huwa nakuuliza kuwa zaka huwa zaka wakati gani; Je ni wakati nikitoa 10% ya, au ni wakati nikiandika kwenye bahasha kuwa hii ni 10% ya?
  Vipi kama mshahara wangu ni 10000, nami nikaweka kwenye kapu la sadaka shilingi 7000, nitahesabikaje nimetoa zaka pia? Think about it sir!

  Nakunukuu hapa:
  ” KILA MSHAHARA/KIPATO CHANGU, NIMEAMUA KWA KUPENDA, RAHA,FURAHA,HIARI, NAFURAHI SANA KUTOA ZAKA?”

  Good Seleli, that is you. Then usitake kila mtu awe kama wewe, aamue kama wewe, wengine wameamua kumtolea Mungu kwa namna nyingine, na wako confortable.

  Na hapa nakunukuu;
  ”Kutoa Zaka mahali unapolelewa kiroho ni hekima njema kwa mantiki ile ile ya kuwajali/kuwa support walawi, kuthamini vipawa ivyo Bwana alivyotupa-Hesabu.18:6-7, kusukuma kazi na maono ya nyumbani kwako. Hili lafaa sana na kama ni man-made then elewa sasa kua si kila mada-made ni evil! Ziko nyingi ktk Bible eg Paul na wanae au Musa na watu wake.”

  Huu nao unaweza ukawa ni ushauri mzuri Seleli, but dont make it a doctrine!
  Mtu anaweza kuamua kumtolea Mungu mahali asiposali pia, still it is biblical!

  Ukitaka unaweza kunijibu hili; Kwa nini zaka huwa mnaandika majina na kupewa lisiti lakini sadaka hamuandiki?

  Unadhani kuwa sijaiva na unataka kuniivisha, unaimba zilipendwa brother, nilishatoka kwenye huo upofu, and I’m aware of what am talking about.

  Wewe tuendelee tu, lakini utatoka hapa umeelewa hata kama hautakiri kuwa umeelewa!

 8. Sungura,

  Nilipokuuliza unipe maandiko ya kuthibitisha LIVE kua Bwana Yesu pia alioga, kupiga chafya, miayo, unajua kwa hakika sikua na nia ya kujadili ilo bali kukutafakarisha kua, yako mambo yatabaki kua ni kweli kabisa kwa kutumia both common senses and Biblical truths namely maandiko ambayo hayasemi live baadhi ya yet yanamajibu ya yale yasiyoandikwa mfano: Mfano kutoka kwa maandiko yanayosema LIVE baadhi ya facts kamaYesu kulia, alifanyika mwili na akaa kwetu, kujisikia kiu nk, kutokana na hayo hayo, tutapata mengine ambayo hayajaandikwa LIVE! Mfano ndio hayo ya kuoga, kuchoka, kupiga chafya nk.

  Usisahau kua kwanini nikakuuliza ivyo! ni kwa kua ktk swala la zaka, wewe umekataa kila hoja yangu kwakua tu sijakuonyesha andiko live kuhusu Zaka! Ingawa tumesema sana kuhusu Zaka kutolewa kabla ya sheria-Mwz.14:1-20 na Ibrahimu na Yesu kusemelea Zaka-Mathayo.23:23. Kwa kiasi kikubwa, umekubali kutoa Zaka kwa mfano wa Ibrahimu lakini bado ingawa umekubali, comment zako nyingi ulizitoa, zilijaa kasoro-kasoro, negative-negatives, kubatizaji majina mbalimbali mabaya toleo hili, ndio maana nimeshindwa kuulewa hasa moyo wako clear uko wapi/ukoje ktk toleo hilo na in fact, hata kama nilioonekana nimekuelewa, bado sikukuamini, why? Kauli zako ni ushuhuda. Utata umezidi sana kuliko soluhisho la fundisho/msimamo wako, ulipokana waziwazi kua maneno ya Yesu ktk Mathayo iyo, NI NONE OF YOUR BUSINESS!!!!!!!!!!!!!!!

  Hukuweza kabisa kujibu nilipokupa changamoto hii ambayo umeikimbia kama hujaiona kua ktk Mathayo.23 mstari wa 1-anaongea na Wanafunzi wake na Makutano, kisha mistari hii-4,5,6,7,13,14,15,16,17,18,19,20, 21,22,23,24,25,26,27,28,29,30,31,32,34,35, wakati anaongea na wote, anawa-address Mafaridayo na Waandishi kisha mistari hii 8,9,10,11,12,36,37 anawa-address Wanafunzi na bila shaka Makutano. Unawezaje kutenga Mistari aliyowa-address kundi moja, isiwe na maana/mantik/kitu cha kufanya/kutilia maanani kwa kundi jingine? Ndio maana nikakuuliza/kukutafakarisha kua kwa mtindo huo, utaleta conflicts kubwa sana kwa maneno ya Yesu mengine kama utachambua ivi kisa unakwepe Zaka!

  Nikakuuliza maneno ya Yesu ktk sehemu nyingine na nikatoa mfano wa Mathayo 12 utafanyaje wewe! Kwakua hapo Bwana pia ameongea na audience yote but pia akiwa anaongea, akawa-ddress baadhi ya makundi! UNATENGAJE MANENO YA YESU KWA KUNDI MOJA, YASIWE NA ISSUE YA KUFANYA KWA KUNDI JINGINE? U SEE JINSI KUKIMBIA KWAKO ZAKA KUNAVYOLETA VURUGU NYINGI KTK YALE MENGI ALIYOWAHI SEMA YESU MWENYEWE? Heri wanadamu wenzetu akina Paul, Petro, Musa, hawana shida tukichambua kua kwa hili, walikua wao kama wao na kwa kile, ni la Bwana kwa vizazi vyote, kwa wanadamu hawa, Bible inakubali na mifano ni mingi ya wao kwa wao wakisemana na hata Yesu akiwasema pia kua lile lilikua la fulani kwa sababu zile eg Musa.

  Tatizo unadhani unajua kila kitu na nikikuuliza swali, badala ya kujibu, unashangaa! Nakwambia tena kua aidha jibu au nielewe umeshindwa au unaweza ila jibu lake unajua litakupa utata mkubwa kama si majibu mengi ya yale umekataa kwa muda,Unajua unachokifanya kwa kukataa kujibu!!!!!!Umedharau kwa nini nimekuuliza sababu ya Mungu kuamuru Walawi wapewe zaka!

  Angalia jibu lako hili lisivyojitosheleza au limeacha jambo/au kusema uwongo!!!!!!!: ‘’Mungu aliamuru walawi wapewe zaka SI KWA SABABU WALIKUA WANAMTUMIKIA MADHABAHUNI, bali ni kwa sababu aliamuru wasiwe na urithi, na ndipo akasema zaka ndo iwe urithi wao.

  Angalia Mungu anasemaje ktk Hesabu.18: mistari hii….2 Na ndugu zako nao, kabila ya Lawi, kabila ya baba yako, uwalete karibu pamoja nawe, ili waungwe nawe, na kukuhudumia; bali wewe na wanao pamoja nawe mtakuwa mbele ya hema ya ushahidi. 6 Nami, tazama, nimewatwaa ndugu zenu Walawi miongoni mwa wana wa Israeli; kwenu ninyi watu hao ni kipawa alichopewa Bwana, waufanye utumishi wa hema ya kukutania. 20 Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. 21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania. 23 Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. 24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote. 26 27 Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu. 31 Nanyi mtakula hayo kila mahali, ninyi na watu wa nyumbani mwenu; kwa kuwa ni thawabu yenu badala ya utumishi wenu katika hema ya kukutania.

  Mungu anasema amewapa Zaka kwa kua hawatakua na urithi na PIA KAMA THAWABU AU BADALA YA UTUMISHI WA HEMANI-mistari ya 6, 31 iko wazi hapo juu….Wewe unasema ni sababu ya kutokua na Urithi tu ndio ilipelekea wapewe Zaka! U cannot outsmart God Sungura. Najua umeongea uwongo nusu kama si ukweli nusu hapo ili tu kupata hoja kwamba kama Walawi wetu leo wako safi kimaisha na ukatoa mfano kua kama Bill Gates ni Pastor wako, then uhalalishe kutoroka au kula kila kitu wewe! Niliwahi kukuliza, tunapoongelea Utoaji eg Zaka, ktk mambo ya imani yetu, tunazingatia ile mantiki ya Kutoa ina maana/baraka gani kwa Bwana au status za mtu tunayetoa kwakwe au kwa huduma yake?

  Lazima kuupinga ubinafsi hata kama madhara yakitokea yanamhusu muhusika. Kuunyuka usisambazwe na kuaminiwa , nayo ni huduma njema. Kama hukua hapa kuwazuia watu kutoa zaka, why umekua na maneno na majina mengi negative against it? Umesahau siyo?

  Kama sitoi kwa mujibu wa Ibrahimu-(hiari), manake ninakabwa kutoa kanisani kwangu! A u sure 100%? Si ndio notions kama izi zilinileta kwa mahojiano haya! You make Zaka thing at our churches full of problems, unspiritual and if we don’t know the Word/Bible!

  Kama kwa mujibu wa Utoaji zaka kama Ibrahimu ili linawezekana eg mshahara laki moja then mwezi huu, nikaamua kutoa 10%, mwezi ujao nikatoa 25%, na mwezi unaofuatia nikaamua sitoi zaka nikatoa sadaka tu, kwa nini hili lisiwezekane? Namely- KILA MSHAHARA/KIPATO CHANGU, NIMEAMUA KWA KUPENDA, RAHA,FURAHA,HIARI, NAFURAHI SANA KUTOA ZAKA?

  Kutoa Zaka mahali unapolelewa kiroho ni hekima njema kwa mantiki ile ile ya kuwajali/kuwa support walawi, kuthamini vipawa ivyo Bwana alivyotupa-Hesabu.18:6-7, kusukuma kazi na maono ya nyumbani kwako. Hili lafaa sana na kama ni man-made then elewa sasa kua si kila mada-made ni evil! Ziko nyingi ktk Bible eg Paul na wanae au Musa na watu wake.

  Kwamba je Melkizedeki ndo alikuwa kuhani wa mahali Ibrahim alikuwa anaabudu/anasali?
  JIBU: ni swali kua wakati wa zaka ya Ibrahimu kwa Melkizedeki, kulikuwepo hema ya kukutanikia ambayo kwayo, wangehitajika watu kuishi wakitenda kazi humo? Na sasa je baada ya ibrahimu, kama hema ilikuja na shughuli zikatakiwa ziwemo na kufanywa umo na kwa kua yaliyopita yalikua kivuli, leo pia tunayo hema, kwa nini tusizisapoti kwa matoleo mbalimbali, Zaka ikiwa the best kwa ya hapo home kwako kiroho/hemani?

  Bado hujaiva ktk swala la zaka Sungura! Utaiva tu, tuendelee kusaidiana/kuhojiana.

  Press on.

 9. Seleli, u can judge however it pleases your emotions!
  Unajua kwa nini habari za Yesu kuoga hazikuwekwa kwenye biblia? Ni kwa sababu hazikuwa na umuhimu wowote katika lile lengo ambalo yaliyoandikwa yaliandikwa kwalo.

  Kwa nini nipoteze kujadili jambo ambalo halina umuhimu wowote katika yale ambayo Mungu anataka nijue na kutende!!!?

  Lile ambalo halikuandikwa kwa sababu halikuwa na umuhimu wowote wa kuandikwa, wewe kama unadhani kuwa lilikuwa la muhimu basi liongeze kwenye kopi yako ya biblia.

  Na kama aliyeaandika yaliyoandikwa kwenye biblia aliliacha hilo huku akijua kuwa lilikuwa la muhimu kiasi hicho,basi mimi atakaponiuliza nitamwambia sikulifanya au nililifanya kwa hiari yangu/kwa kuamua mimi kufanya,kwa sababu hakuniambia nifanye ambayo hajayaandika bali nifanye yale aliyoyaandika. Sawa brother?

  Biblia imesema wazi habari za akina Barnaba, Anania na Safira kuuza viwanja vyao na kisha kutoa kilichopatikana miguuni pa mitume, hata haikusema kuwa walikitolea zaka kwanza ndo wakakipeleka kwa mitume. Biblia siyo kitabu kijinga kiache kuonesha suala linalodhaniwa ni la lazima kiasi hicho.

  Na nafikiri nimekupa mfano wa ‘acceptable assumptions’.
  Siku moja nilimuuliza rafiki yangu mwingereza alipokuwa Tanzania kuwa ‘unailinganishaje Tanzania na Uingereza’? akanijibu ‘huwezi kulinganisha’. Nilipomwuliza kwa nini akasema ni kwa sababu hakuna hata kitu kimoja kinachoelekeana ili tufanye ulinganifu.

  Una mawazo ya ajabu sana Seleli, ivi huelewi kweli kwa nini Mungu aliamuru walawi wapewe zaka, huijui sababu ya Mungu kufanya hivyo? (siyo swali la kujibu).

  Narudia, kuwa Mungu aliamuru walawi wapewe zaka si kwa sababu walikuwa wanamtumikia madhabahuni, bali ni kwa sababu aliamuru wasiwe na urithi, na ndipo akasema zaka ndo iwe urithi wao.

  Kwa mantiki hiyo, kama Mungu asingeamuru kuwa walawi hawatakiwi kuwa na ardhi ina maana wasingepewa zaka lakini kutumikia madhabahu wangeendelea.

  Swali ni je wanatumikia madhabahu leo wameamriwa wasiwe na urithi ( wasifanye kazi nyingine)? Jibu ni hapana. If so then, what tithe obligation for?

  Kitu kingine cha ajabu umekisema sana ni mtu kukuza ubinafsi na kutanguliza mambo yake. Ok, ivi unadhani kama kuna mtu wa hivyo wewe inakuhusu nini? maana madhara ya kutomtanguliza kwake Mungu mbele yakitokea yatamhusu yeye.

  Nilisema kinachoitwa zaka si aina ya kilichotolewa, bali mfumo wa/njia ya kilivyotolewa. Hivyo basi kama lengo la zaka ni kumheshimu Mungu kwa mali zetu, hata sadaka, zawadi (kama Kolnelio alivyotoa),changizo n.k huko kote ni kumheshimu Mungu, maana bado kilichotolewa ni mali. Yaani hakiwi mali kwa sababu kimetolewa kwa njia ya zaka, bali kwa sababu kimetolewa, tena kwa moyo wa kupenda.

  Seleli usijaribu kutaka kuwaaminisha watu kuwa nilikuwa hapa kuwazuia watu kutoa zaka. Tangu mwanzo kabisa nilisema kuwa kama ni kutoa si mwisho wa mwezi tu ikiwezekana hata kila siku, kama ni kutoa si 10% tu ikiwezekana hata 100%.Lakini nikasema kuna zaka kwa mujibu wa Ibrahim na zaka kwa mujibu wa Musa. Kwa mujibu wa Ibrahim zaka ilikuwa ni hiari, kwa mujibu wa Musa zaka ilikuwa ni lazima.

  Kwa hiyo nasisitiza hata sasa, kuwa anayetoa kwa mujibu wa Musa huyo anataka laana,na wengi wanayo. Maana wengi leo makanisani wanatoa( tena si kutoa ni kulipa) zaka kwa lazima,asipolipa ataulizwa, ndio maana wanaandikwa majina na kupewa kadi na lisiti, lakini sadaka haina lisiti maana yenyewe ni hiari.

  Ndio maana wewe nilikukatalia kuwa hutoi zaka kwa mujibu wa Ibrahim kama ulivyojaribu kusema. Kanisani kwenu lazima ukilipa huwa unapewa lisiti na una namba/kadi ya zaka kabisa.(labda kama umehama TAG brother).

  Let me break it down even more: Kutoa kwa mujibu wa Ibrahim maana yake ni kwamba kama mshahara wangu ni laki moja, mwezi huu naweza nikaamua kutoa 10%, mwezi ujao nikatoa 25%, na mwezi unaofuatia nikaamua sitoi zaka nikatoa sadaka tu. Tena sihitaji hata kuandika jina kwenye bahasha. Namwandikia nani ,kwa nini, na ili iweje?

  Man made doctrine nyingine katika zaka ni hiyo uligogusia ktk paragrafu yako ya mwisho ukinilaumu, kuwa lazima utoe zaka mahali unaposali.
  Hebu jijibu moyoni mwako swali hili, kwamba je Melkizedeki ndo alikuwa kuhani wa mahali Ibrahim alikuwa anaabudu/anasali?
  Na niliuliza tena swali hili kwamba ‘ what if my pastor is Bill Gates’? anahitaji zaka yako?

  Huko ndiko kuiva vema kwangu!

 10. Sungura,

  Kwa AINA na NAMNA ya mjadala huu ulivyokwenda( labda kwa mijadala mingine), kuacha/kukataa kujibu maswali unayoulizwa, kuna maana hizi:

  ( a) Huna majibu ya uhakika yasiyoacha shaka

  (b) Uko weak kuya-face maana unajua nguvu yake

  (c) KiMaandiko, huna nukuu unayoweza tumia mana unajua utazua maswali mazito mengine

  (d) Pia ni aibu kwako kukimbia maswali kwa sababu ambazo unaona tu kua huyu Mtu alitakiwa akiri tu kua hajui, basi yaishe au asaidiwe kuliko kujidai anajua au kusingizia kua maswali hayana umuhimu!

  Kwa nini nimeshikilia kukuuliza swali la, ‘’Je BWANA Yesu alioga, kupiga chafya na miayo? na kama ni ndiyo, unipe maandiko! Sababu ni:

  Moja: Uling’ang’ana sana kua hakuna hata andiko moja( la live ulimaanisha) ktk Agno Jipya linalosema tutoe Zaka.Niliku-evaluate nikakuona kua unadhani namna pekee ya kujua kitu fulani kilifanyika ni kukikuta live ktk andiko na mtu akijenga hoja ya msingi kabisa tokana na maandiko ya INDIRECT(yasiyo ya live), hutaki na unadai ni assumptions tu ilihali zina mashiko ya nguvu ambayo kuzikana ni ngumu maana si rahisi kupata hoja mbadala wa kuzipiku

  Pili: Najua kua jibu la maswali yangu unge/umesema ni Ndio ivyo nilitaka uniambie umejuaje kua ni ndio ili njia uliyotumia uone ukweli kua ndio ambayo nimetumia mimi kusema naamini ktk matoleo yote yaliyotolewa wakati wa kusapoti huduma ya Paul na kuleta kanisani, hata kama hakuna andiko la live( kama vile lisivyo kuwepo la Bwana kuoga/kupiga chafya/ miayo ingawa tunaamini/ jua /assume/ dhani kwa uhakika aliyafanya hayo), then wako waliotoa pia zaka maana hakikua kitu geni kwao na walijua na kuishi baadhi ya Torati na walijua nia ya Mungu kwanini zaka itolewe in the past kwa Watu waliotenda kazi yake hemani, vivyo ivyo kwa wanaotenda kazi Kanisa la kwanza ndani kanisani na nje uko kwa evengelism

  Kama kuna watu wanafanyaga maombi ni sahihi kukisia au KUAMINI kuwa na kufunga pia kulifanyika AU kama binadamu aliishi ni wazi alikua anavuta hewa na kama watu wa Kanisa la Kwanza walitokea na bado wakaendelea kuishi baadhi ya torati(mifano nilishatoa-reje post yangu), basi ni wazi walitoa matoleo ya aina nyingi, Zaka ikiwemo. Ni rahisi unapongelea Utoaji kwa aina ya watu wale, Zaka ilikuwepo! Ukitaka andiko live, nami nitakuomba pia la Yesu Live, kuoga/chafya/miayo!!!!!!!!! au la kukataza kutoa Zaka Agano Jipya.

  Umesema, ‘’wewe kwa kuyachunguza maandiko, umeshajiridhisha kuwa zaka leo si toleo kama ilivyokuwa wakati wa torati’’ Ni sawa but Ibrahimu kabla ya torati, mbona alitoa?

  Je vipi kuhusu Kumuheshimu Bwana kwa mali zetu na mtu akajiwekea personal discipline ya kutenga 1 kati ya 10? Na vipi kumpenda Mungu kwa roho,nafsi, akili,nguvu zangu zote ikanipelekea kuchukulia zaka kama njia bora sana ya kuhakisha Mungu kwanza, mengine baadaye?

  Hata kama hakuna anayewajibika kwa mwenziwe ila kusaidiana ni muhimu, ndio maana ya fellowship. Kama mtu anaenda mbali na kukuza sana ubinafsi na kuacha ya Mungu kwanza, huyo Mtu anashida na haachwi hivi hivi.

  Kwakua umesema ivi leo, ‘’Anayetaka kutoa zaka yeye atoe tu kwa utashi wake mwenyewe kama ilivyo kwa matoeo mengine’ = basi umeiva vema sasa maana siku za mwanzo na kati hapo, si tu uliweka wazi wewe hutoi bali pia ulivunja moyo wanayoitoa na ukaibeza sana kwa matamshi mengi ya kebehi na dharau

  Mabishano yasiyo na maana ni yale tu ya kuendelea kung’ang’ania kuwaondoa watu ktk kutoa na kuwaaminisha mambo dhaifu kua zaka si lazima, haipo Leo, kuitoa ni kua chini ya laana, ni kodi, chanzo cha umasikini au unaweza kuitoa kisha unakula wewe mwenyewe, si lazima umpe kuhani au kuipeleka kusaidia mambo ya ukuhanini mwako hapo unapolelewa kiroho. Lakini pia, kuliko hayo mafundisho ya uwongo yaendelee humu, NI LAZIMA KUYABISHA/PINGA mpaka yatakapokoma kuja na kufa kabisa, amin, amin nawaambia, hakika yatapingwa kila dk mpaka kusiwepo makao yake katikati ya Wanadamu.

  Asante Sungura,
  Press on.

 11. Samahani Seleli,

  Suala la kama Yesu alioga au kupiga chafya haliwezi kulinganishwa hata siku moja na ku-assume kuwa kama kuna sadaka au changizo lilifanyika basi na zaka ilitolewa. Ndio maana sintakaa hata siku moja nilijibie hata kama utaniuliza mara elfu moja, maana liko ‘so obvious’.

  Kama kuna sehemu yalifanyika maombi ni sahihi kukisia kuwa na kufunga pia kulifanyika.
  Na kama unaongelea kuhusu binadamu kuishi, huhitaji kukisia kama alikuwa anavuta hewa, bali unatakiwa kujua kuwa alikuwa anavuta hewa.

  Lakini si sawa hata kidogo kukisia kuwa kama kuna changizo lilifanyika mahali basi na zaka ilitolewa. Maana hakuna kanuni yoyote inayosema kuwa kufanyika kwa changizo basi lazima na zaka itolewe.

  Unajua nini Seleli?, tumeongea sana na tutajikuta tunarudia yaleyale. Na mwisho wa yote kila mtu ana uhuru wa kuchagua kusimama na analodhani litamfaa. Maana hatuwajibiki kila mmoja kwa mwenzake, bali kila mtu anawajibika kwa Mungu na kwa maish ayake mwenyewe.

  Mimi kwa kuchunguza kwangu maandiko nimeshajiridhisha kuwa zaka leo si toleo kama ilivyokuwa wakati wa torati, na hakuna laana yoyote kwa mkristo kutotoa zaka kama ilivyokuwa laana wakati wa torati ( kwa mujibu wa Malaki 3).

  Anayetaka kutoa zaka yeye atoe tu kwa utashi wake mwenyewe kama ilivyo kwa matoeo mengine.

  Kwa hiyo ukiona sijibu maswali kama ulivyotaka niyajibu si kwa sababu umenibana, ila ni kwa sababu sioni umuhimu wa kufanya hivyo zaidi ya kuendeleza mabishano yasiyo na maana.

  Asante Seleli!

 12. Sungura,

  Unafahamu wazi kua issues zako unazo leta, nina deal nazo vema sana, huwezi kataa hilo, hence Utakapo dhani uko unamaanisha kujadili jambo ili mpaka mwisho kwa kujibu hoja/maswali na si kuandika tu as if hakuna ulichoulizwa, then nitakujibu! in the meantime, ninakuona unafanya utani na sidhani kama napaswa kucheza na wewe mwenye utani! Unajua kwa nini haujibu maswali nayokubana nayo, wafahamu kabisa why! Ni mpaka unijibu kuonyesha yako ni sawia la sivyo unabaki na madeni mengi humu.

  Wewe unaongea sana kuhusu-kuassume! Lakini nilishakuambia na kukupa maswali/mifano kua ziko assumptions(kuamini kua mambo fulani ni sawa/yalifanyika), kuzikataa ni ngumu sana maana zina ukweli. Labda nirudie aka, Aya naomba andiko kua Yesu alioga, chafya na kupiga miayo?

  Press on

 13. Seleli maneno mengiiiii lakini ya pupa tu kwa sehemu kubwa.

  Kwa kifupi ni kwamba katika kuainisha kwako suala uliloliita ”from commmon position to special position” iliyo katika agano jipya, hakuna hata sehemu moja ya andiko la agano jipya ilipokupa -support kuwa kuna mahali zaka ilitolewa kwa mitume.

  Zaidi sana umefanya kama kawaida yako ilivyo, ya kufanya ‘assumption’. Kwamba una-assume katika hizo sadaka walizotoa watu kama akina Barnabas na zaka iikuwemo. Lakini biblia haisemi kuwa walitoa na zaka pia, bali waliuza walivyouza na pesa yake wakaileta kwa mitume. Na wala mitume hawakuletewa hiyo pesa ili waitumie wao, bali ili wawagawie wahitaji. Na ndio maana hapakuwepo na mhitaji kati yao (si kati yao mitume),bali ni kati yao waumini wote. Leo wahitaji hiyo zaka hata ikiwa mamilioni huwa hawaigusi.

  Wainjilisti wenyewe hiyo zaka hata huwa hawaigusi, nikakwambia ndio maana wameamua kuacha uinjilisti na kuwa wachungaji ili nao wajipatie zaka.

  Ninavyokuona kukomalia zaka kwako leo ni kwa ajili ya kuwatunza watumishi. Kuwatunza ni suala sahihi na lenye kukubalika kabisa,lakini ninachokushangaa ni kule kulazimisha kuwa ni lazima watunzwe kwa zaka,wakati iko wazi kabisa kuwa mitume walitunzwa kwa sadaka wala hakuna panapoonesha kuwa walipewa zaka.

  Hakuna hata andiko linaloonesha kuwa watu wa mataifa kama wakorintho, waefeso, wakolosai, wailipi n.k walifundishwa kutoa zaka. Maana hawa hawakuwa wayahudi, hawakujua huo utaratibu wa zaka.

  Kama zaka ni kwa ajili ya kuwatunza wachungaji, wahat if my pastor is Bilgates?

  Halafu kitu kingine unachomiss rafiki yangu ni kutojua mfumo wa agano jipya ulianza lini kutumika. Kitu ambacho umeking’ang’ania kwenye Mt 23:23 ni kitu kidogo sana kupotezea muda. Yesu alisema hakuja kuitangua au kuikomesha torati, bali kuitimiza au kuitenda.
  Maisha yake yote Yesu alikuwa anakwenda kwenye sinagogi na hekaluni pamoja na wanafunzi wake. Aliitimiza torati siku alipoangikwa msalabani,na siku amefufuka mfumo wa agano jipya ndo ukaanza kutumika. Tangu hapo huwaoni akina Petro wanaingia kwenye sinagogi tena.

  Yesu hakuwahi kufanya kazi kwa mfumo wa agano jipya. Kwa hiyo kilicho kwenye hiyo Mt.23:23 kinahusu sheria ya Musa tipically, ndio maana hukioni kwa mitume walipoanza kazi.

 14. Sungura,

  Kuhusu Mt 23:23

  Pongezi zako kwangu kua ninanatoa kwa mujibu wa sheria ya torati ni utani uliokwepa jambo nilikuuliza hukujibu! Nalirudia kwamba, kwakua ulisema Mathayo.23:23 haikuhusu na kwamba yale Yesu aliwaambia Mafarisayo na Waandishi ni utoaji sawa na Malaki.3:8, nikakuuliza, kwa hiyo unataka sema YESU alifundisha sheria ifuatwe? Ndipo nika-imply meaning kwamba kama Yesu ktk swala la zaka, alifundisha sheria iendelee kufuatwa na ukweli kua sura hiyo hiyo 23:1 maandiko yanaanza kwa kusema..Yesu anaongea na makutano na Wanafunzi wake akisema, basi mimi nikitoa kwa msingi huo kuna tatizo gani maana umesema Yesu aliback up sheria iendelee na nikasema hatuna jinsi ya kujitoa kwa kua mstari wa kwanza, audience ni makutano, wanafunzi, Mafarisayo na Masadukayo.
  Sasa kwa kua hukujibu, sasa jibu kwamba, kwa kua umesema ktk Mathayo.23, alifundisha utoaji sawa na Malaki.3:8 YESU ALIBACK UP SHERIA IENDELEEE ? na mimi nikitoa zaka kwa mantiki hiyo ya Yesu si sungura au Paul, kuna shida gani?

  Kwamba umenionyesha ktk Mt.23:23 kitu kidogo tu ulichonitahadharisha kuwa si rahisi mimi kukiona ktk hiyo mistari’ nacho ni wanafunzi wasifanye yale wanayofanya mafarisayo na ukadhani VERY WRONGLY mpaka nimecheka na ku-doubt uwezo wako wa kung’amua baadhi ya Kweli za Neno, kua Yesu alimaanisha Wanafunzi wasitoe zaka za mnaa, jira na bizari -ambayo ndio matendo Yesu alimaanisha kuyakataza Wanafunzi kuyatenda! Jesus Christ! is this your understanding? Ndicho kitu ulidhnai ni very spesheli siwezi kukiona wakati ni ALL TOGETHER WRONG? Shame upon u brother, bora hata usingesema kwa kujidai na kujiinua kuna umeona kitu spesheli ambacho mie si rahisi kukiona! Yaani hata siamini na majigambo yote ndio unaleta uwongo huu! Nisikie sasa ili uwelewa kuanzia leo vema kabisa.

  Ukisoma sura nzima hiyo na hata kweli za Neno la Mungu ktk yale aliyosema YESU maeneo mengine kwa watu kadhaa-( Yakupasa kuelewa siku zote kabla huja-conclude jambo/point toka kifungu fulani, kumbuka/pitia vifungu vingine maana yako maandiko yanajitafsiri yenyewe papo kwa papo au kwa kutumia vifungu vingine kuangalia fungu unaloshughulika nalo). Aliyosema Yesu ktk iyo Math.23, unapata hoja moja tu mahususi na ndio hiyo alimaanisha alipowaambia, WASIFANYE KWA MFANO WA MATENDO YA WAANDISHI NA MAFARISAYO, ongeza pia WAKUU WA DINI, MASADUKAYO nk. Hoja yenyewe ni ‘’YESU SIKU ZOTE ALIPINGA UNAFIKI WA HAO JAMAA, basi as simple as that. Tuangalie baadhi ya mistari ya sura hiyo ili ku-establish kwa usahihi nachofundisha kwa ili.

  Kwamba hii Mathayo.23:23,Umesema wewe haikuhusu, na najua kisa kuna zaka hapo ambayo umeitoroka maisha yako yote! sasa tuangalie baadhi ya mistari ili ku-establish kama hoja yako inasimama au la-TAFADHARI zingatia maelezo ya ziada baada ya kila mstari au JIBU MASWALI YAKE NITAKAYOIBUA WAKATI NAORODHESHA IYO MISTARI NA KUDADAVUA SOME tips from them.

  1 Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema: Notice: Audience hapa ni Makutano na Wanafunzi

  2 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa: 3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Notice: Yesu anawa-recommend kua jamaa wale wana serious authority( Musa doctrines or Word of God via Musa at that time hence yapo watakayotuambia shurti tuyashike na kuyatenda as said by Jesus

  Swali: Unadhani ktk yale waliyosema/fundisha jamaa wale na ukizingatia walikua wajuzi wa KWELI ZA Mungu ktk Agano la Kale, je, Kutoa Zaka hawakuisemelea/fundisha/waambia watu watende/wafanye?

  Mistari hii mingine yote…4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. 5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; 6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, 7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. Notice: 13 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie. 14 [Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.15 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe. 16 Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga. 17 Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu? 18 Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. 19 Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka? 20 Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.

  Na hii….21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake. 22 Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake. 23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. 24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. 25 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi. 26 Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. 27 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. 28 Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi. 29 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 30 na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. 31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. 32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. 33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? 34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

  Notice: Mistari yote hiyo, basically, Anaonyesha unafiki wao na kufanya mambo kwa show off, kuridhisha nafsi zao

  Swali: (a) Unadhani wakati Yesu anawa-address jamaa wale moja kwa moja na kushambulia mambo yao kadhaa hayo, audience nyingine ya Makutano na Wanafunzi, walikua hawapati msg ya kufanya toka yale aliyosema Bwana kwa Watu wale?

  (b) Ikiwa baadhi ya mambo hapo juu yatafanywa kwa kicho, uhalali, pendo la KiMungu na utaratibu unaofaa, kuna shida gani? Maana alichokataa Yesu hapo ni kufanya kwa show off au kugeuza ya kwanza kua ya pili na ya pili ya kwanza! Lakini kama ya kwanza yanabaki ya kwanza na ya pili ya baki ya pili na yote yakafanyika kwa utaratibu huo, wapi shida ya kutoa zaka? Wapi kujiondoa kua hamuhusiki na maneno haya ya Yesu?

  Na hii mistari …..8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. 9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. 11 Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. 12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa. 36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki. 37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

  Swali: (a) Yesu anawaambia nani hapo, Makutano na Wanafunzi tu au Mafarisayo na Waandishi tu au Wote?

  (b) Kama ni kwa Wote, kwa nini ktk mstari wa 23 tuseme hatuhusiki?

  (c) Kama ni kwa Wanafuzi tu, wataelewaje hayo kua yao bila kuangalia/zingatia yale aliyosema ya kwanza?

  Umesema kitu kingine hiki cha ajabu, ‘’Hakuna sehemu kwenye hiyo mistari panapoonesha kuwa mafarisayo walikuwa wanawaambia watu watoe zaka’’

  Jibu: I think brother, at this point, kwa kua nimesha-engage na wewe ktk mahojiano kwa muda sasa, I would wish to encourage/challenge you plz to raise the standards on some issues and kindly activate your good thinking capacity and natural IQ, may u be a little bit anointed and full of Spirit, Word and healthy brain/mind thinker Mister Sungura! Pia baadhi ya Maneno ya Mungu hutaelewa kwa kuchukua sura/mstari mmoja tu. Ni kweli ktk mistari iyo hatuoni Mafarisayo wakifundisha utoaji wa zaka lakini wewe unafahamu kua Mafarisayo na jamaa zao ndio walikua wanakalia kiti cha Musa na walikua ndio waalimu wa kiti/doctrine/maneno ya Mungu kwa Musa ktk Agano la Kale. Kati ya yaliyo uko, Utoaji zaka umo kama Neno la Mungu aliyehai-Sura za Hesabu.18 na Walawi.27, ivyo ni wazi walifundisha hayo sana na kusimamia yote ya Musa.

  Nilikuuliza kama Mathayo 12 inakuhusu, hukujibu badala yake ukaniambia tena kua hujui nilimaanisha yanakuhusuje maana kuna mengi yamesemwa ndani yake.

  Maelezo: Nimekuuliza swali hili kwa maana na huwa sikurupuki hata siku moja, nilishakuambia siku nyingi na u better be very carefull napouliza maswali na ukaamua kujibu ndio maana wengi wenu, hukimbia maana kuyajibu pia bila kua na anointing ya uhakika ya ufahamu, nikikujitia aibu zaidi. Sasa kutokana na yanayojili ktk Mat.23, nimeona nikufunue zaidi kwa kukuliza swali toka ktk andiko hilo pia, wewe jibu swali lake then tutaendelea au mara moja utaNIONA nakupeleka wapi!

  Swali: Niambie yapi ktk hayo yaliyosemwa yanakuhusu, ni yako wewe kama mfuasi wa Yesu leo?

  Press on.

 15. Sungura,

  Hi issue ya Mungu kua detailed and particular kwamba sikukupata kabisa mantiki yako, isinipotezee energy. Narudia kua hukuandika kichina au kimongolia mimi nishidwe kuelewa! such clear or by the way thing in this topic yet true, nisielewe! Naelewa vitu vingine vyenye kilo sembuse ako!

  Mwanzoni ulisema hiki..’’ Seleli sijui wewe Mungu unamwona ni kitu cha namna gani mpaka useme maneno haya, ”Tofauti iyo ktk kuchukulia mambo katika ugumu/uzito, je utaondoa ukweli kua mwisho wa siku, swala ni moja tu hapa yaani KUTOA tu?, ukasema, ”Ufahamu wako kabisa unakutuma kuwa Mungu anachotaka ni kutoa tu, very pathetic, ndipo ukasema, Sikia rafiki yangu, Mungu yuko so particular and very detailed. Siyo kutoa tu kama unavyodhani. Anajali nini unatoa, kwa nini unatoa, na unakitoaje. Kama ingekuwa suala ni kutoa tu, basi Anania na Safira wasingekufa kwa mali ambayo ilikuwa ya kwao wenyewe na walikuwa na uhuru wa kuamua watoe ngapi’’.

  Nilikujibu ivi..’’sasa Mungu kua detailed and particular ndio nifanyeje?, inanizuia kua Mtoaji kama Yeye, mwisho wa siku si nikutoa tu as simple as that!’’Halafu ukabisha kua sijui sijakuelewa au sijui nikusome tena, mara sijui mantiki yako nimeikosa na nimeingia chaka kama ni paper ya mtihani!na hata ukakana kabisa kua uliposema Mungu ni detailed and particular haukua unaongelea Utoaji ilihali immediately baada ya kusema statement yako ile, ulitoa mfano wa Anania na Safira!!ati uliongelea habari ya Mungu kujali unatoa nini, unakitoaje, na unakitoa kwa nani (particular & detailed), na mimi nikaja kuongelea kwamba Mungu ana tabia ya kutoa/ kutoa ni tabia ya Mungu.

  Wewe ni mwanafunzi wa ajabu kweli! Ukiongelea Mungu kujali unatoa nini, kwa namna gani na kwa nani, What does mere common senses can tell about the matter basically being talked about? ni Ubatizo au Kujazwa Roho? Sasa kwa mrejesho huu- kwa uliyosema na niliyosema, nani mbabaishaji na hana umakini ktk ku-keep the flow ya ideas /track ya tumetoka, tuko na tunaelekea wapi ktk mada hii? Mind you, si mara ya kwanza wewe kuchanganya mambo, kusahau uliyosema wakati ushahidi upo, mfano topic ya kuvunja laana, uliniruka kua ktk swali lako ulilouliza watu, mimi nili-zoom tu into it, sikutakiwa kuhusika, ukasahau kua ulialika wote wajibu(mimi ni kati wote pia-so it was justfied kulinyuka swali lako vilivyo)!!!!! Try to be makini kama unavyohubiri wengine.

  Umenukuu-‘’Waefeso.4:11-12’’-kuwatoa kua Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu kisha ukatazamisha kua,’’ hapo hajataja ‘makuhani’ maana wote Tuliookoka tuna common position ya kua ni Makuhani na ukasema basi wote tupewe zaka!!!!!!!!

  Jibu: Ni kitu cha ajabu Mkristo kua na ufahamu huu kwamba wakristo wote wapewe zaka. Uungaji wa kweli za Biblia kwa namna hii, umepotoka ingawa ni kweli tuna common position kua wote tu-makuhani. Tuelewe CP ziko nyingi si tu Makuhani. Mungu toka mwanzo amejidhihiirisha ni Mungu wa utaratibu, Ingawa anatuokoa wote kisha anatujaza wote Roho yule yule lakini anatuita/tutenga tofauti tofauti ktk majukumu yake-Mdo.13:1-3 na ni hayo majukumu yanatutuhamisha toka kwenye common positions( wote tuko Saved, Spirit filled, Makuhani, Chidren of God, loved same nk) to particular positions( Wachungaji, Mitume, Waalimu nk). No wonder hata mwanzo unamkuta Musa Vs. wana Israeli, Eliya Vs. Elisha, Manabii, Wafalme na Waamuzi Vs. WanaIsraeli despite wote ni Wana Israeli, Watu/Wana wa Mungu, wote wameitwa toka Misri au sisi toka duniani/ dhambini nk.

  Kwa izo particular positions/functions ambazo ni Mungu mwenyewe kabisa ameziweka, wale from common positions, wata-submit chini ya wale ktk particular statuses, no wonder unakuta tabia/utaratibu kama huu-Mdo.4:33-37 wa wengine kuwa chini ya/kupeleka vitu/sadaka kwa Mitume! Kwanini wafanye ivyo? si wangezitafuna/tumia tu kwakua hata wao kimsingi ni Wana wa Mungu na ni makuhani pia na tena ni potential candidates kutengwa to particular positions pia anytime-Mdo.1:15-26? na tena Bwana hajaacha kutoa ‘’wengine’’ kua…! Kwaivyo, from common positions(Makuhani, Wana wa Mungu, Friends of Jesus, slaves/servant of the Lord, Holy Spirit filled believers-Mdo.1:8, 2:1-4, saved Christians(all appointed for salvation via Christ-Waebrania.5:9 nk), to particular grades, Mungu ana wa-treat hao katika statutes spesheli ndio maana hata wamesemelewa kwa hadhi/unyeti kama huu- Wafilipi.2:18-30, Waebrania.13:17, 1Wathesalonike.5:12-13-Kwamba tuwaheshimu sana na kuwatambua walio juu yetu, wanaotuongoza, watulishao mambo ya rohoni na kwa ajili ya kazi na huduma zao kwetu na kwa Bwana-ingawa in the first place, tuna common statuses.

  Kwa mantiki hiyo juu, Hili lisisahaulike always kua Agano Kale ni kivuli picha yenyewe ni Agani Jipya-Waebrania.10:1-Mungu aliwaambia Wana Israeli kua Zaka amewapa Walawi kwakua hawana urithi kama wengine(ardhi) na hasa kilichokua cha kiroho/moyoni mwa Mungu ni kwamba alifanya ivyo KAMA MALIPO/ZAWADI KWA UTUMISHI WA HEKALUNI ULIOHITAJIKA WAO WATENGWE( shift from common position-Wana wa Israeli) to, in this case, a particular status then-Makuhani- KWA AJILI YA ULE UTUMISHI hemani-Hesabu.18:20-24,31

  Kwa maana iyo, ni kweli Mungu anaonyesha wazi kuwatenga watu toka kati yetu( common positions) na kuwapeleka/wapa particular positions( Agano la Kale-Walawi tu ndio kua Makuhani pia wakawepo Manabii, Wafalme,Waamuzi na (Agano Jipya- Mitume, Manabii, Waalimu, Wainjilist, Wachungaji nk-1Kor.12:27-29,Waefeso.4:11-12 na utengaji huu uliambatana na special privileges/rights ambazo walipewa pia, ZAKA ikiwa mojawapo. Kivuli cha Agano la kale, picha yake ni Agano Jipya kama ilivyoandikwa-Waebrania.10:1 hence, hakuna tatizo tukiwapa/tukiwatunza Watumishi wetu wa hema ya kukutanikia( in the correct sense of permanence of their availability in there to do the Work for God and us).

  Kwa ivyo ni aibu kubwa na kwa kweli ni kituko na ubinafsi uliovuka mipaka, Mkristo Kusema kua wote tupewe zaka au tuzile kwanza kama alivyodai Amin Yeremiah pia, bila kujali/kua na uelewa wa common Vs. particular positions(functions) ambazo Mungu mwenyewe na Mitume wanajua na bila kuelewa mantiki ya moyo wa Mungu kwanza kua kwa nini alitenga Watu toka katikati yetu ili wadumu ktk Kazi moja na kutokua na mambo mengi yakiwasumbua uku na kule na ivyo kuharibu utulivu wao ktk Utumishi.I real regret Sungura kua hutapewa zaka wewe unless u move toka common to particular position in TODAYS NEW TESTAMENT’S concepts na bahati mbaya sana hu-move kwa kuamua mwenyewe, ni mpaka Yeye akutoe kua….

  Kwamba aliwatoa wengine kua…ati hakutaja Makuhani hapo! hiyo statement yako imenishangaza kweli. Kwa hiyo kama hakutaja makuhani hapo, ehe Unataka sema nini hasa chenye mashiko? The opposite or other point should more powerful and makes sense than yours. This is the one na ya kupendeza kua wakati wote alitufanya tu Makuhani(moja wapo ya common positions), iko level nyingine ya kuwatwaa/kuwatenga BAADHI(Wengine) toka/ wenye common positions na kuwafanya wawe na particular ranks/grace ndio hao sasa Mitume, Waalimu, Manabii,Wainjilist, Wachungaji.Au kama unapenda nikuwambie ivi- WOTE NI MAKUHANI lakini SI WOTE watakua Mitume, Wainjilist, Waalimu,Manabii, Wachungaji-zingatia a key action word ktk hii 1Kor.12:28 ina a more serious divine word kwamba aliwa-APPOINT (=which tells a lot kwamba ni maamuzi Yake mahususi kwa ajili ya kazi mahususi)

  Katika haya maandiko niliyokupa ya 1Wakorintho 9:1-15 na Luka.10:7-ni kweli hakuna neno live hili ‘zaka’ ktk maandiko hayo ila sadaka nyingine but Unajua ndio wakati mwingine najiulizaga why Sungura uko na ujasiri sana kuwaambia wengine hawako makini lakini hua nikikukagua ktk baadhi ya vitu(si vyote to be fair na mie hua sina kunyanzi na wivu mbaya wa kujidai kutoona Kipaji/ huduma/ karama/uwezo na umaridadi Mungu aliompa Mtu na kumu-appreciate kazi yake njema kwa furaha yake na utukufu kwa Baba), najiuliza, where is smartness of this Sungura! Kwa maandiko hayo, nilidhani utawaza kwa uelewa mkubwa( a bit thinking big yet Biblical/Spiritual) na kuamini ivi mimi niaminivyo ndivyo ilivyo.

  Tunajua wanafunzi wengi wa kanisa la kwanza walikua bado wana-observe BAADHI ya mafundisho ya Musa 1Wakor.14:34(notice: ‘’baadhi’’ = which also partly clarifies kua si kila kitu ktk torati hakifai leo au kama mnavyoita ni laana- ni kutoelewa tu nini hasa Paul alimaanisha kwa kusema tumekombolewa na/toka laana ya Torati-Paul tunayemjua -kamwe asingeweza ita NENO LA MUNGU ALIYE HAI KUA NI LAANA! Never in hell or heaven, hata Yesu alisema hakuja kuitangua Torati na Manabii bali kuitimiliza hata akasema hakuna yodi wala dot- moja itaondolewa hata yote yatimie- Mathayo.5:17- yaliyonenwa na manabii kuhusu Yeye na kuwahusu wengine na vingine e.g. kuangamizwa kwa Nchi na iliyosema torati kuhusu Yeye na mengine yasiyovuruga yale atayakokuja kusemwa na Yeye mara atakapokuja kutokea waziwazi.Ndio maana siku za nyuma ktk mjadala hapa nimekua natumia statment hii kua’’ziko KWELI ktk torati zinahama na kutumika kama zilivyo as long as hazipingani na KWELI nyingine alizokuja funuo Yesu na Rm via Wanafuzi na mifano iko mingi mno ktk Neno ya kweli izo kuhama na kutumika aidha kama nukuu au hata kujengea msingi na kuendesha mambo wakati wa Kanisa la Kwanza-Agano Jipya, lakini bado wewe, Amin, Lwembe mlishindwa kabisa kuelewa such very simple truth.

  Kwa msingi huo kua Wanafunzi wa Kanisa la Kwanza wametokea ktk backgrounds ya Torati na hata baadhi ya kweli za Agano la Kale zilinukuliwa kuhuisha/kuback up kweli za Agano Jipya na pia zilitumika kuamua au kuendesha mambo-Mfano Paul analazimika kumtahiri Timothy ili kumfanya afiti kati ya waliotahiriwa-Mdo.16:1-5 ingawa Paul huyo huyo kwa mazingira mengine alikataa sana baadhi ya mambo ya Wayahudi wenziwe na Torati hata kumkemea Mkubwa wake(Petero) hadharani na kumwandika live kua alichemka na akamchana live kwa kua alijitenga na wasiotahiriwa kwa kuwaogopa waliotahiliwa-Gal.2:11-19 na aliponda kua ishu muhimu siyo kutahiriwa mwilini au la bali moyoni na kwamba ktk Bwana hakuna cha myunani wala mtumwa, bwana au myahudi-Gal.3:26-28.

  Na kwakua ni Yesu ndiye aliyesema kua Mafarisayo na Waandishi wanaa kwa kiti cha Musa ivyo watuambiayo kuyashika, hayo tuyatende nga si ktk mfano wa watendavyo-Mathayo.23:1-3, basi nina amini haya yafuatayo yalitendeka/tokea. Kama unakataa, ni sawa ila leta hoja nzito pia ziwe za Ki-maandiko-live au indirectly au kiufunuo, assumptions zenye mashiko au kimantiki kuweza kumuonyesha mtu jambo fulani kua ni dhahiri ndilo kama vile hakuna maandiko live kua Yesu aliogoa,kupiga chafya au miayo lakini ni wazi kwa kua kuna maandiko ya alikuja ktk mwili basi ni kudhani/ assume/ chukulia/amini kua aliooga,chafya,miayo ni dhahiri kabisa.

  (a) Wote Yesu na Wanafunzi, walikua –supported na Wanafunzi wao kifedha na kihali ili huduma zao zisonge mbele hata kama si lazima kumuona Yesu live anapokea sadaka, michango, zaka nk maana angeweza fanya ivyo mtunza fedha wa huduma yake Mr.Yuda.

  (b) Wengi wa Wanafunzi wa Yesu, Mitume, Makutano nk, walikua na Agano la kale kama Neno na Muongozo kwao wa Mungu maana kipindi icho ndio kwanza Agano jipya linajiunda/tengenezwa kwa maneno na matendo ya Yesu kisha Wanafunzi baadaye

  (c) Ivyo si ajabu kua Kati wa Matoleo Watu waliokua na background za Agano la Kale walitoa, zilikuwepo pia zaka, malimbuko. Na bila shaka kati ya michango( sadaka za changizo) kusapoti umishenari wa Paul, wapo wapendwa waliomtolea Bwana kwa ajili ya changizo izo kwa mfumo wa malimbuko, Zaka na pia wapo walioleta fedha au vitu kama sisi mpaka leo kwetu Geita, unaweza toa fedha live kama unazo au ukaleta mazao au mfungo akapigwa mnada, pesa ikapatikana, Jengo la Kanisa likajengwa au mchungaji akapata posho au crusade ikafanyika.

  (d) Kama hoja ni kua, hakuna andiko live kwamba waliosapoti huduma ya Yesu au Mitume walitoa Zaka basi pia hakuna andiko live kua Yesu au wanafunzi waliwahi kusema, Zaka kutoa ni mwiko au kama mnavyoita kila kitu ndani ya AK ati ni kua chini ya laana au waliwahi fundisha kua Utoaji wa zaka au hata malimbuko ni fundisho potofu na wala hakukuweko tangazo kua wale wote mnaotoa machangizo ktk makanisa mbalimbali, msitoe zaka

  (e) Kwa furaha na hiari na si kama sheria, wapo wengi walitoa zaka na matoleo mengine kama Ibrahimu, wakimshukuru Bwana kwa mambo mbalimbali ktk ibada zao huko makanisani

  (f) Naamini kuamini hayo (a-e) yaliyotokea kwa hoja zangu toka mwanzo kule juu, ni rahisi zaidi na ina mashiko ya nguvu sana kuliko kuamini kua kamwe hayakutokea.

  Kwamba ‘suala la zaka limesababisha wainjilisti wengi waache huduma ya uinjilisti na kuamua kuwa wachungaji’’, so what? Je hatuna waliosalia ambao hawajapiga goti kwa baali? Kwakua wapo waliocha LAKINI amini amini nakuambia, wako wengi sana wanaochapa injili hata leo, plz find them ili uwafurahie hao kuliko wale waliovuruga.

  Katika hii-Luka 8:2-3 kuhusu Walio sapoti huduma ya Bwana na team yake, umeshikilia kua support iyo ilikua ni sadaka tu.Mimi nilisema ni izo plus na aina nyingine za matoleo, walikua huru kufanya ivyo maana hawakuwahi kukuatazwa na hata ivyo, walifanya kwa upendo na hiari ivyo yote yangewezekana. Uking’ang’aniza kua ni sadaka tu, nitakuuliza una uhakika gani wa 100% ilikua ni strictly sadaka tu na kwamba utoaji mwingine kamwe wale wanawake na wengine hawakuutoa? Ni rahisi kwa anayefikiri kwa akili njema kuamini/kuchukulia/conclude kimashiko kua matoleo mbalimbali yaliweza fanyika na watu hawa kuliko kuamini ni toleo la aina moja tu.

  Nitakuletea pia responses zangu kuhusu responses zako kwa ile Mathayo.23:23

  Press on.

 16. Siyi kuna kitu ambacho mnakikosea kifikra katika suala zima la zaka.
  Mtu asiyetoa zaka lakini anatoa sadaka za kawaida, machangizo na misaada mbalimbali kuwasaidia wahitaji, iweje umseme kwamba amekuwa mwaminifu kwa mambo mengine yoote ya kiroho kasoro pesa/mali zake?

  Kwani hicho alichotoa(sadaka, machangizo, misaada kwa wahitaji n.k) ni mawe si pesa au ni hewa si mali?

  Kwa mtu mwenye uwezo sahihi wa fikra bila shaka alitambua kuwa tulichokuwa tunavutana hapa si kinachotolewa, bali ni ule mfumo wa kukitoa (The how of doing/ giving it).

  Unapoongelea kitu kinaitwa 10% na kingine kinaitwa sadaka, na kingine kinaitwa changizo n.k, hayo majina tofauti hayawi tofauti kwa sababu ya kinachochotolewa bali ni kwa sababu ya kinavyotolewa hicho kinachotolewa. Maana mwisho wa yote kikishawekwa kwenye kikapu chote kitaitwa matoleo, lakini kikirudi kwenye msingi wa jinsi kinavyotolewa kingine kitaitwa zaka, kingine sadaka na kingine changizo.

  Kinachoitwa zaka chenyewe kwa mujibu wa kanuni yake kinatakiwa kuwa 10% ya, na kama mtu ameweka 8% au 20% ya, basi hicho kimekuwa si zaka tena.

  Kwa hiyo ninachosimamia mimi katika hii mada ni kwamba hiyo kanuni ya 10% ambayo inasema mtu hakutakiwa kutoa pungufu au kuizidisha kutoka katika mapato yake, leo haipo.
  Kilichopo leo ni kutoa, tena kwa moyo wa kupenda. Ukiamua kutoa 100% sawa, 5% sawa, 19% sawa,10% sawa n.k. Maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.

  Asiyetaka kutoa huyo haujui si ukristo tu, bali hata ubinadamu. Dunia nzima hata waovu nao hufanya matendo ya huruma ya kuwasidia wengine, hata kama hawamchi Mungu, sembuse wanaomjua Mungu.

  Siyi bila shaka umenipata ndugu yagu!

  Asante.

 17. Sungura,
  Mjadala huu niliamua kuwa nasoma tu kinachoendelea bila ya kukoment chochote baada ya kuona mwelekeo wake
  Naona unachanganya mambo hapa. Mafarisayo walifanya mambo ya torati gani? Kutoa zaka ni torati gani hiyo? Ni torati ya Mungu au ya Musa? Hivi mtu anaweza kuwa mwaminifu katika mambo mengine yooote ya kiroho isipokuwa pesa/mali halafu bado akaendelea kuitwa mwaminifu?

 18. kuhusu Mt 23:23:

  Kwanza nakupongeza kwa kukubali kuwa unatoa kwa mujibu wa sheria ya torati, maana ulikuwa umeukataa sana huo ukweli.

  Ngoja nikuoneshe kitu kidogo tu ambacho nilikutahadharisha wakati ule kuwa si rahisi wewe ukakiona ktk hiyo mistari.

  Katika Mt 23;1 Yesu aliwaambia makutano na wanafunzi kwamba wafanye wanayoambiwa na mafarisaya,lakini wasifanye yale wanayofanya mafarisayo.

  Kati mstari wa 23 Yesu anawaambia mafarisayo kwa habari ya wao kutoa zaka ya mnanaa na bizari.

  Kwa kuwa Yesu aliwaambia wanafunzi wafanye wanachoambiwa kufanya na mafarisayo, lakini wasifanye walichokuwa wanaanya mafarisayo, kwa hiyo zaka ya mnanaa,jira na bizari wanafunzi hawakutakiwa kuitoa maana hicho ndicho kilikuwa kinafanywa na mafarisayo, lakini mambo ya haki,rehema,na uaminifu/imani amabayo mafarisayo walikuwa hawawezi kuyafanya bali walikuwa tu wanawahimiza watu wengine kuyafanya, hayo ndiyo wanafunzi walitakiwa kufanya.

  Kwa hiyo hapo Yesu hakuwa anawaambia wanafunzi watoe zaka za mnanaa, bali mafarisayo ndio alikuwa anawaambia waendelee kutoa. Na akawataka mafarisayo wafanye na mambo ya haki,rehema, na uaminifu ambayo Yesu na wanafunzi wake ndio mambo walikuwa wanatenda.
  Hakuna sehemu kwenye hiyo mistari panapoonesha kuwa mafarisayo walikuwa wanawaambia watu watoe zaka ya mnanaa, bali wao (mafarisayo ndio walikuwa wanatoa hiyo zaka( hicho ndicho walikuwa wanatenda), na Yesu anakataza sisi kutenda wanachotenda wao.
  Alikuwa anawapa ole mafarisayo kwa kuweza kuwa makini kufanya mambo madogomadogo sana yasiyo ya muhimusana, na kuacha mambo makubwa yaliyo ya muhimu zaidi.
  ( SIJUI KAMA UMEELEWA)

  Ukaniluliza kama Mathayo 12 inanihusu. Sijui ulimaanisha kunihusuje, maana kunamengi yamesemwa ndani yake.
  Lakini niuonehse tu kitu kimoja katika hiyo sura kiwa na-summary:

  Kwanza elewa Yesu alikuja kuitimiliza au kuitenda torati ya Musa ndipo akishamaliza hiyo kazi aleta agano jipya. Yaani aliiishi kwanza torati ta kutimiza masharti yake ndipo akafuzu kuwa initiator wa agano jipya, ambalo linakomesha utawala wa torati ya Musa.

  Ndio maana aliweza hata kuwaambia wafuasi wake kufanya yale ya torati ya Musa ambayo mafarisayo waliwaambia wafanye.

  Ndiposa katika hiyo Mathayo 12:20 anasema (A bruised reed he will not break,
  and a smoldering wick he will not snuff out,till he has brought justice through to victory).( Hii mistari ni sawa na inayosema hakuja juitangua torati)

  Which means once he has attained that victory he will break that reed and snuff out that smoldering wick.

  Huo ushindi tayari alishaupata ( yaani kufa na kufufuka kwake), kwa hiyo utendaji wa sheria ya Musa ulishakoma, haulihusu tena kanisa kuuishi leo.

  Kitu kingine hiki hapa ulisema ”Ati maelezo yako kwamba Mungu yuko detailed and particular haujaipata kabisa mantiki’’ mmmmh! Ni kichina icho/kile? Huyu vipi jamani, mbona kujidai kwiiiiingi kwa mambo peanut?!”

  Ukweli ni kwamba hukukielewa hicho kipengele na matokeo yake ukaingia chaka. Mimi niliongelea habari ya Mungu kujali unatoa nini, unakitoaje, na unakitoa kwa nani (particular & detailed)
  Wewe ukaja kuongelea kwamba Mungu ana tabia ya kutoa/ kutoa ni tabia ya Mungu.

  Sasa huoni kuwa hukuwa umelewa kilichokuwa nakiongelea ukalipuka kivyako?!

  Karibu

 19. Seleli:
  Naanza kwa kukunukuu ; ”Waefeso.4:11-12-Aliwatoa wengine kua Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu kwa ajili ya kuwajenga Watakatifu na kazi ya huduma ili kuujenga Mwili wa Kristo”

  Iasema alitoa wengine kuwa Mitume,…… (Kumbuka hapo hajataja makuhani).
  Neno ‘wengine’ hapa linamaanisha si wote wameteuliwa kuwa katika hizo huduma zilizotajwa, wala halimaanishi kuwa kama mtu si mtume basi ni nabii, au mchungaji. Bila shaka unajua kuwa wote wliozaliwa mara ya pili ni makuhani ikiwemo mimi na wewe,ambapo Yesu ni kuhani mkuu.

  Kwa hiyo hao waliotolewa kuwa mitume au walimu na wale ambao siyo mitume wala wainjilisti wote wana common position inayoitwa ukuhani, yaani kwamba wote ni makuhani wa Mungu. Kwa maana hiyo wote wanasifa ya kupewa zaka kwa mujibu wa kanuni ya zaka kwamba ni ya kuhani ( mlawi).

  Yote uliyosema katika 1Wakorintho 9:1-14 ni ya kweli,lakini hakuna sehemu imesema kuwa hiyo gharama ya kwenda vitani ni zaka, kwamba hiyo zabibu ya shamba ni zaka, kwamba hayo maziwa ya kundi ni zaka, kwamba hiyo nafaka inayopulwa ni zaka, kwamba hivyo vya mwilini ni zaka, kwamba hivyo vya hekaluni au madhabahuni ni zaka. Wala ule ujira wa mtenda kazi haikusema kuwa ni zaka, maana alichokuwa anasema Yesu hapo ni kuwaambia wanafunzi kwamba wakiingia kwenye nyumba kuhubiri wasikatae kula kama watapewa chakula.Zaka haikuwa inatolewa kwenye nyumba za watu bali hekaluni.
  Ndio maana katika kanisa la kwanza hatusomi popote kwamba injili ilipelekwa kwa zaka,bali kwa sadaka na machangizo.

  Na kwa tarifa yako hili suala la zaka limesababisha wainjilisti wengi waache huduma ya uinjilisti na kuamua kuwa wachungaji ili wawe na mamlaka juu ya zaka ( ili wawe salama kimapato). Hii ni kwa sababu, waliposubiri wachungaji wawagawie sehemu ya zaka ili nao waweze kujikimu kwa ajili ya kufanya mikutano sehemu mbalimbali,wachungaji hawakuwapa huo mgao.
  Na matokeo ya wainjilisti kuwa wachungaji ni shetani kujitawala katika jamii, mfano mzuri ni kwenu Mwanza (Geita) ambako mauaji ya albino na vikongwe yamezidi kushika kasi.

  Hakuna mikutano ya injili leo, maana wainjilisti badala ya kuwa nje wote wameamua kurudi ndani hekaluni ili nao wajipatie zaka. Na kuwa mwinjilist pekee aliyeshikilia huduma yake ya uinjilist tangu ujana hadi uzee wake (Moses Kulola) na yeye ameondoka tuna kazi kubwa ya kufanya katika hii nchi.

  Haya yote ni matokeo ya kung’ang’ani sheria ya zaka ambayo kimsingi leo hai-apply.

  Huna aibu Seleli kusema kuwa Yesu alitumia zaka wakati akiwa hapa duniani. Nani angempa hiyo zaka huyu aliyeonekana adui wa torati? Mafarisayo wangewezaje kufanya kufuru hiyo ya kumpa Yesu zaka iliyotolewa hekaluni?

  Umenukuu Luka 8:2-3 kujaribu ku-justify kuwa Yesu alitumia zaka. Ona kinachosemwa kwenye hiyo mistari.

  Luk 8:2-3 (English Standard Version);2 and also some women who had been healed of evil spirits and infirmities: Mary, called Magdalene, from whom seven demons had gone out, 3 and Joanna, the wife of Chuza, Herod’s household manager, and Susanna, and many others, who provided for them[a] out of their means.
  Was that Tithe? Hizi zilikuwa sadaka na michango tu ya kum-support Yesu wala hazikuwa zaka.

  P.T.O

 20. Amini Yeremiah Mgulumu,

  Sorry for tumbo, asante Bwana amekuponya. Laptop yako ina technical problems au ni demonic? Kama ni technical, tuwasiliane na kama ni attack, you know what to do, yaani fanya juu chini, I/WE NEED YOU HERE FULLY MPAKA KIELEWEKA HAPA KATI YA WALE WA KUJIACHIA/KUMUACHIA YOTE BWANA vs. WATOROKAJI WA ZAKA NA BILA SHAKA NA MATOLEO MENGINE –tusidanganye hapa, ukishaanza faulu moja ya kulinda nafsi yako ile na inywe kwanza, huzaliwa na mengine mengi mabovu sana.

  Asante kwa kukiri kua hujaona Maswali/hoja 17 hata kidogo, SASA ONA! Nangoja! Na nitakukumbusha bwana mkubwa, hamna shida, mie mdogo wako wa ukweli.

  Mh! ati mie umeniita kuwa ni kijana mkaidi badala ya msikivu! Mimi! aaa bwanaa! Kaka naona unataka kuyatibua mambo! muulize Sungura! aya nyie nichokozeni tu. Lakini hata ivyo Kaka yangu, serious speaking, niwasikilize nyie kwa kitu gani? Hiki cha kunikataza/na kuharibu wengine humu KUTOMTOLEA MUNGU jamani? hamuoni mtatumiwa kama Petro au? Mi mmniache, nitatoa tu Zaka tena napenda kujiadabisha ivyo kua nikipata tu, 1 ya Bwana, 9 nakula, mbona ni training nzuri sana ya kuua ubinafsi na kumkumbuka Muumba? Nyie mbona mnakimbia vitu vizuri?

  Hii claim kua..’’ Mshereheshaji(yaani mfafanuzi wa andiko) anajilinganisha na maandiko yenyewe yanavyojieleza’’ na kisha wasema..’’Pole sana mdogo wangu.’’
  JIBU: Sitaki pole yako, naifuta na isiwepo makao yake ktk Nchi, halafu yako maandiko kweli hayahitaji kufafanuliwa na yapo yanataka ufafanuizi, Mfano:’’Akupigaye la Kulia, mpe na la kushoto! Sasa je si unaona unapaswa kuwabariki Wafafanuzi/Washereheshaji kama hauna wivu mbaya?

  Ati unarudia kusema bila haya ‘’ Utoaji wa zaka kwa WAKRISTO ni POTOVU’’ na mara hii umeongeza gia nzito/mbaya kweli hii..’’ kua kutoa Zaka ni fundisho la kuzimu lenye nia tu ya kuwajaza baadhi ya watu mtumbo yao na wengine wakijazwa hofu’’
  JIBU: Yajibu maswali yangu 17, utakua umejibu wasiwasi wako huo wa uwongo na kufuta kauli yako mbovu iyo ya kutetea choyo na ubinafsi.

  Umejiamini ivi..’’HAKUNA KUTOA ZAKA KWA WAKRISTO KWANI MAFUNDISHO YAKINI YA YESU YANASEMA IFUATAVYO:
  1. Ampaye nabii atapata thawabu ya nabii.
  2.Yeyote ampaye ngaa kikombe kimoja mmojawapo wa wadogo hawa amenipa mimi. 3.Wapeni watu vitu nanyi mtapewa kipimo cha kushindiliwa na kusukwa sukwa.
  4. Apandaye haba atavuna haba na apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu
  JIBU: Je Nikimpa ZAKA nabii au mmoja wapo wa wadogo hawa au Watu na kuipanda sana kwa ukarimu, sita vuna? Kuna shida gani|?

  Press on.

 21. Sungura,

  Nina haja kweli ya kuchukua nguvu nyingi kusemea ulichomsemelea Dorica kwamba alimanisha nani! Mimi pia niliiona comment yake na kwa kua hakusema moja moja nani hasa ana maanisha, nikaicha tu ikae ivyo basi maaana hakukua na haja ya kumtolea ufafanuzi kwakua hakusema nani ‘anatusi. Sasa kwa kua umemsemelea moyo wake bila shaka unajua umetumia njia gani kufahamu kua hakumaanisha wewe ila Watu wengine( in this case/ your case-mimi nimo kwa hao watu), ngoja nisema haya

  Umenikumbusha mbali! Tulipokua watoto, tukipishana jambo eg ktk michezo au kazi nyumbani, mkosaji mdogo wetu wa mwisho, anaanza kulia halafu sharply and speedily anakimbia kwa Mama kushitaki! Kwa jinsi mkosaji anavyo lia, Mama alikua anatuadhibu sana sisi wengine ambao tulikua hatulii haraka lakini maskini wa Mungu kumbe tulikua hatuna hatia ila tatizo dogo hakimwagika tu kulia na akawahi kwa Mama, hakuna neema tena ya kusikilizwa sisi wakubwa zake, ni mboko tu basi! Ilikua inatughadhabisha vibaya sana,sana kabisa. Tulichofanya, tukaamua liwalo na liwe, ivyo kila akitoka kutushitaki na tunalazwa fimbo, tukirudi tu kucheza au kupalia, tunamdunda sana na sisi kukata kiu ya hasira na uwongo wake wa kutusakizia mambo mengi kumbe uwongo na yeye ndio haswaaaa alipaswa kutandikwa kila mara na kisha tukishamdunda, tunamzuia hakuna kwenda kwa Mama, atalia hapoo shambani weeee mpaka ataochoka na kutu join kulima/palizi.

  Sina uhakika kama Dorica amekusoma toka mwanzo wa mjadala huu! Je umekua Mwaminifu kumwambia kua ni mimi niliyeanza kukushitua kua unaropoka vingi hata kutumia statement kua unafyatuka tu? je umemwambia kua ni wewe ndiye umeita watu humu si mim tu kua hawajui, ni majuha ndio watasoma michango yao, wapumbavu kwa mfano ule wa Nyerere speech? sijui kama amekusoma upolifurahia badala ya kurekebisha Seleli kudhaniwa ana malaria na ana hitaji ambulance na pia kua ana effects za degedege alipokua mtoto? Sijui kama amepata muda wa kusoma unavyowakazania wenzio maneno ya kuwashusha kua hawako makini mpaka nikaanza kukuonyesha kua niko makini?-sijui kama amekusoma kudharirisha utumishi wetu Kanisani kua tuko ktk kongwa, laana na kwamba kutoa zaka ni kulipa kodi tu? sijui kama amekusoma ulipokua unaongeza na unafurahia mambo yakiongezwa chumvi sana na kuleta kashfa kuhusu hali ya Makanisani kwamba tunalazimishwa kutoa zaka( makanisa kabisa ya Roho Mt ati watu wanashurutishwa)! Hapo sijataja ya kuitwa kichwa ngumu,teeneger, nina upuuzi nk

  Ni kweli kabisa kulingana na michango na kauli zako kuhusu wewe binafsi, Zaka na Watumishi Makanisani, umeonyesha tabia ya kiburi, uchoyo, nafsi kutawala badala ya uradhi kwa mambo ya Mungu, moyo wa kutojali kazi ya Bwana na mambo ya Ufalme yasimame kwanza, ni kweli umejiinua, ni kweli ni mapinduzi ya kidevo kanisani kwako kwa jinsi ulivyo semelea namna ile na Watumishi wa Makanisa, ni kweli kua kinyume na mtembeo wa kanisani kwako au mtazamo wako kiujumla ni kuunda vikundi-vikundi vya migomo dhidi ya kanisa na mipangilio ya kanisani kwako au mwili wa Kristo hasa ikigusa vinoti vyako, ni kweli kabisa wewe u critizer mbaya,mshari na mhuumizaji mioyo, shughuli( injili) na maono ( mfano kuita zaka ambayo watu tunatoa kwa amani kabisa kua ni kongwa la laana na chanzo cha umaskini Kanisani na kwamba wasipewe Makuhani-Mtumishi akiyetengwa/tolewa kwa ajili yako Kanisani kwako. Kama hayo yote si tabia na moyo uliounyesha hapa kulingana na yale umesema mengi humu, kanusha sasa kwa ujasiri na Bwana anakuona kisha futa kauli zote zilizonifanya mie nikuone u mtu wa namna iyo na ukiri kua uliteleza baadhi ya maneno au ulizidisha chuki na dharau dhidi ya tolea la zaka na sisi tunatoa kwa furaha, umetuharibu baadhi. USIPOKANUSHA KUA HIZO SI TABIA ZAKO NA KUFUTA KAULI ZAKO BAADHI KUHUSU UTOAJI HUSUSANI ZAKA, BASI NI TABIA ZAKO NA NDIVYO ULIVYO.

  Nilikua nimekarika kweli kweli kiinjilist wakati najibu juu hapo, sasa nimefika kwa hili, kweli nimecheka sana, hahahahah…nipe no yako ya simu! am serious ninavunjika mbavu sana hapa..! da! nimecheka kweli Sungura, umerudia tena hii..’’ wewe nakujua kupata pressure ni rahisi kwa sababu ni mnene na mwenye kitambi kikubwa na gym huendi sana, So be careful brother!’’ daaaa! Nimecheka sana mie jamani, ila kuna kakitu hapo umeniambia ka ukweli kiana! Mh! will work on it.

  Hili swali lako hili…’’Kama sadaka na michango hiyo imetosha kuwatunza watumishi na kufanya yote ambayo kanisa linatakiwa kufanya kimapato, ni lazima tena tutoe na zaka, ya kazi gani? JIBU: Kama sadaka na michango haitoshi kwakua wanatoaga kwa staili ile yako ya mpaka wajisikieeeeee, wagusweeeeeee wakati mambo yao binafsi, hawangoji wajisikieeee, kwanini Wasifundishwe kwa ukakamavu mkubwa umuhimu wa kutoa zaka kwa ajili ya Kazi ya BWANA na umakusudi wa kujali toleo ilo na si kama sadaka na michango mingine ya mpaka wagusweeee, wakitoa, sawa, wasipotoa, sawa tu?

  Karibu sana kwa hayo majibu umesema yatokanayo na Mt 23:23

  Asante pia.

 22. Nilipoona post ya Erica mara moja niliifungua, nikakuta ina maneno machache tu.
  Lakini nilishtuka niliposoma anasema kuwa kuna watu wana matusi ya kilokole humu. Ndipo nikajiuliza nani katukana?
  Niliposoma koment ya Seleli kwangu nikajionea mwenyewe.
  Ok, thank you so very much Seleli kwa hayo yote uliyoniita.

  Ngoja ninukuu baadhi ya maneno hayo ” We si utakua na matatizo mengi sana ya kiroho namely kiburi, uchoyo, nafsi kutawala,kujiinua, mapinduzi ya kidevo kanisani kwako, kuunda vikundi-vikundi vya migomo dhidi ya kanisa na mipangilio ya kanisani kwako hasa ikigusa vinoti vyako, critizer mbaya, mshari na mhuumizaji mioyo, shughuli( injili) na maono ya Mtumishi akiyetengwa/tolewa kwa ajili yako Kanisani kwako hapo”

  Nyingine hii hapa: ”Yaani kama kuna ‘anointing’(ofcoz ya kidevo au pori) ya kufyatuka na kuropoka, wewe hamna tena Tz and East Africa aiseee!”

  Na hii nayo: ” nimecheka sana na hapo hapo kusikitika unavyotema cheche out of satanic porridge!”

  Ukichunguza kwenye hizi kufuru chache za Seleli utagundua nimeitwa shetani au mwenye upako wa shetani mara kadhaa. Anayesema hizo kufuru ni mkristo akimwambia mkristo mwenzake, just kwa sababu wamepishana na kutofautiana juu ya suala la utoaji wa zaka.

  Sijui huyu mwenye kutamka hayo anajua kuwa kuna siku atatoa hesabu ya hayo maneno,kwa sababu ni miongoni mwa maneno yasiyo maana.

  Lkini Seleli hujakomea hapo tu, leo umejidhihirisha zaidi kuwa umefura kwa hasira kiasi kwamba tungekuwa tunaonana ana kwa ana kama bubgeni, ungerusha hata ngumi. Maana naona jinsi gani unatamani kunipiga kabisa kwa jinsi ninavyokukera na msimamo wangu.

  Kumbuka hasira hukaa kifuaani pa mpumbavu Seleli. Na ukumbuke hasira husababisha pressure na wewe nakujua kupata pressure ni rahisi kwa sababu ni mnene na mwenye kitambi kikubwa, na gym huendi sana. So be careful brother!

  Na kwa nini umkasirikie mtu ambaye si wewe uliyemfia msalabani, na si wewe ambaye hataki kukutolea ambacho unadhani anatakiwa kutoa?

  Na nilikwambia kwamba kwa kuwa umekuja hapa kwa nia ya kushindana, basi usisubiri SG wakutangaze mshindi, bali jitangaze mwenyewe. Ulisemasema maneno hapo, lakini si unaona mwishowe umeamua kukubalianana na ushauri wangu, umeamua kujitangaza mshindi. Ona hapa:
  ”Muulize Amini, Lwembe, Kaswahili kwanini walihemea puani kwa swali hili kisha wakanipisha njia Askari wa Bwana mie nikapita mshindi! Aya mfupa umewashinda hayena, ostabeyi pusi ataweza?”

  Wewe hauna tofauti na mtu mmoja alikuwa anaitwa Suli kwenye biblia aliyewatesa na kuwaua wafuasi wa kristo akidhani kwa kufnya hivyo alikuwa anamtumikia Mungu. Likuja kujikuta anapiga teke mchokoo.

  Seleli hujui unachokiongea juu ya zaka zaidi ya kuonesha ukakamavu tu kwa sababu unajua unatetea mapokeo ambayo idadi kubwa ya wakristo hasa wapentekoste wanayatii kwa uoga na vitisho. Unapigana bila kuwa umejiuliza vema kama unachokipigania ni halali kwa muktadha wa unavyokipigania.

  Na hai-click kwenye akili yako hata kidogo kwamba kitu ambacho umekuwa ukikifanya miaka yote na hata wazee waliotutangulia wamekuwa wakikifanya miaka na miaka, ati leo mtu mmoja anaitwa Sungura, aje aseme kuwa hakiko sahihi,no way, haiwezekani!

  It took Jesus himself to change Saul, since Saul believed to be serving God out of persecuting the church.

  Sikulaumu brother kwa chochote unachokifanya hapa,si kosa lako. Najua wewe unajua kuwa unachosimamia ndo kiko sahihi kuliko ninachosimamia mimi. Lakini ukweli ni kwamba si hivyo unavyowaza!

  Ni vema ukajua hii mantiki iliyo katika hili swali: Je wachungaji wale ambao wanatakiwa kutunzwa na kanisa, wanahitaji zaka au wanahitaji fedha ili waishi?

  Jibu langu binafsi kwa hilo swali ni kwamba wanahitaji fedha ili waishi.
  Tukitoa sadaka na tukafanya machangizo yakaweza kuwatosha hawa watumishi, tunakuwa tumeshatimiza lile ambalo tunawiwa kufanya kwa ajili yao.
  (yaani kuwatunza)

  Kama sadaka na michango hiyo imetosha kuwatunza watumishi na kufanya yote ambayo kanisa linatakiwa kufanya kimapato, ni lazima tena tutoe na zaka, ya kazi gani?

  Seli baada ya kusema haya, baadae nakwenda kujibu mswali yako,hasa yatokanayo na Mt 23;23

  Asante!

 23. Mpendwa Seleli,marahaba.
  Nikuombe radhi kwa sababu ya kutopatikana kwenye mjadala kwa muda mrefu,hii ilisababishwa na mambo kadhaa yaliyonitokea,nimekuwa nauguza tumbo kwa karibu siku 9 hivi,pia laptop yangu imekuwa na matatizo na hata hapa niandikapo nipo kwenye internet cafe kama nilivyofanya jana.Na unafahamu jinsi isivyo huru kujadili issues kwenye migahawa hii.
  Pia nikiri wazi kuwa sijajibu hayo maswali yako 17 ambayo nina hakika sijawahi kuyaona tangu nianze kujadili hoja hii.
  Lakini nimecheka sana na staili yako ya kufuata ushauri wangu,unaonekana kuwa kijana mkaidi badala ya msikivu tabia ambayo haiwaasi wana wa Mungu ambao ni ndugu wa Bwana Yesu.
  Nimeshangazwa na ung’ang’anizi wako wa kuweka post ndeeefu ukijieleza kuhusiana na unachofahamu na unajaribu kujilinganisha nami ambaye nilikuwa napost maandiko mazima kama yalivyo kwenye biblia.Hii inashangaza kuwa Mshereheshaji(yaani mfafanuzi wa andiko) anajilinganisha na maandiko yenyewe yanavyojieleza.Pole sana mdogo wangu.
  Hata hivyo napenda kusisitiza kuwa fundisho la utoaji wa zaka kwa WAKRISTO ni POTOVU na la kuzimu lenye nia tu ya kuwajaza baadhi ya watu mtumbo yao na wengine wakijazwa hofu..
  Hili linathibitishwa na maandiko ambayo nimeyapost hapa na hata yale uliyoyapost wewe ukiyageuza tu yakufurahishe wewe. Kimsingi HAKUNA KUTOA ZAKA KWA WAKRISTO KWANI MAFUNDISHO YAKINI YA YESU YANASEMA IFUATAVYO:
  1. Ampaye nabii atapata thawabu ya nabii.
  2.Yeyote ampaye ngaa kikombe kimoja mmojawapo wa wadogo hawa amenipa mimi.
  3.Wapeni watu vitu nanyi mtapewa kipimo cha kushindiliwa na kusukwa sukwa.
  4. Apandaye haba atavuna haba na apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu

 24. Kuna watu wana matusi ya “kilokole” humu hivi kujishusha na kukubali kujifunza ni ngumu namna gani? Mungu aturehemu!

 25. Salaam ndugu mpendwa Amini Yeremia Mgulumu, Shikamoo Kaka, Ama baada ya salamu,mimi mzima, hofu na mashaka MENGI MNO ni kwako maana mh! kambi uliichafua kweli na haukuzoa!tumeteseka kweli bora umerudi.

  Mpendwa Kaka yangu Mkubwa, ulikua wapi kwani ni mwezi sasa! Ningekua mimi ndio mkubwa na wewe mdogo, ningekuadhibu, vibaya sana, tatizo, uliruhusiwa wewe kuanza kutokea duniani, inabidi niwe mpole na kukubali matokeo kua mkubwa ni mkubwa tu, nifanye nini sasa! sina jinsi.

  Sasa mkuu, napenda kabla ya yote, nikukumbushe kua humu ndani tena juu tu hapo si mbali, nilikutengenezea summary ya maswali 17 toka yale ya kwanza 21. Yameachama tu hapo yanakungoja! Hii ni katika jitihada ya kukuwajibisha uzoe takataka ulizochafua kwazo kambi hii ya Waebrania. TAFADHARI, usije hapa Kaka baada ya mwezi kwa kujikausha ivi kama vile hakuna uchafu kambini ulioutapakaza,plz zoa kisha tuimbe pambia kwa amani.

  Kuiita zaka ni FUNDISHO POTOFU bila hoja za kweli na zenye kuthibitika kote Agano la Kale na Jipya ni bure. Kwani mimi nikikuambia wewe Kaka yangu kua uko female wewe, je inakufanya uwe lady kweli?

  Ni ukweli kua ni baraka kua na Ujuzi wa kutengeneza maneno mengi ALIMRADI yana kilo hasa, ndio maana unagwaya kujibu hoja 17! Hii habari ya kulia-lia kua post ni ndefu, nitakuitia Lwembe, akwambie Isaya ina 66 books! Plz acha ayo, tulishatoa stage izo za kitoto, chapa kazi, soma! Iwe fupi, ndefu, kati, soma, Unakumbuka Post yako ya kwanza uliponiuliza maswali 8 na iliyofuata ulipokua una copy maandiko ya Zaka kama yalivyo na kuyapwaaa mazima-mazima? Mbona nilikula yote! Umesahau eee! Acha kulia halafu Mkubwa akilia-lia aibuuuuu! mie mdogo je! Soma on the spot, soma home usiku, soma week-end! Yaani nikufundishe na mbinu za usomaji jamani!
  Kuhusu kulishwa matago mwitu, majibu ni wewe jibu maswali yangu 17, statement yako hii itakua settled tikitiki.

  Maana ya zaka, acha kukomplicatiiiii, google mara moja, references nyingi ziko hapo na waalimu uko na kule duniani wamesemaje na pia vitabu wameandika watu uko google. Hizo references ulizonipa hazita-differ sana kimantiki na ki-normal practice ya nini Zaka na utoaji wake, hence zihitaji kuzisoma! Za nini kwanza wakati najua basic! Pia nilishakujibu hili ktk maswali yangu 17, go there! si unaona ulivyo vurugu wewe? hufanyi kazi humu. Jibu hoja izo, haya madude yako, yatakwisha

  Nadhani ninyi sasa ndio mvunje ukuta wa itikadi BINAFSI/NAFSI na kua na Kingdom mentality

  Hii ni janja tu.. ‘’palipo na wingi wa meneno kuna UOVU’’. Je Unapenda kua mpembuzi yakinifu kidogo? Aya je hili haliwezekani?..’’palipo na uchache wa maneno kuna uovu pia? Au hata kuna ushallow wa mambo? Kaka bwanaa, acha uvivu, fanya kazi hapa.

  Unanifurahishaga kweli na confidence zako izi pori za kuacha kazi na kuanza ushauri! Embu ona kujipa kazi izi za by the way…’’ ati niwe msikiaji mzuri na siyo msemaji mkubwa. JIBU: Nina ufuta ushauri wako wa uvivu huo na kukutaka jibu hoja 17 ya mambo uliyosababisha humu, ukimaliza hapo, nitakusikiliza.

  Na hii sala yako..’’Mungu akusaidie kupokea ufahamu ulio juu ya mapokeo ya kidhehebu uliyonayo.’’, naifuta kabisa maana ina roho nyuma ya kunitoa ktk Utoaji ambao ni tabia moja wapo kuu za Mungu.

  Usinidanganye kua ni mafundisho ya kidhehebu wakati nakula na kushare gombo sana hapa tena kwa usahihi kuliko hata wewe unayedaka part one tu kua ‘zaka unaitoa na kuila mwenywe’’ na unasahau conclusion na intro ya andiko husika! Na kisha maandiko mengine yanasemaje! Wewe kweli unajua Neno kwa mapana yake au pale ulikutapo, unafia hapo hapo?

  Hii tamu hii..’’NAKUPENDA SANA MDOGO WANGU, nami pia KUBWA LANGU.

  Press on

 26. Sungura,

  Sina la kukusaidia mimi ktk ili! Mmh! ya kweli hayo Sungura au wajipa moyo mtupu! Hapana! msaada upo na umeshatolewa na utaendelea kutolewa, maamuzi ya kuuchukua au la, ni yako! Mfano: Nilikuambia ktk post zangu za mwanzo kabisa na kurudia tena baadae kua ukishasema unampenda Mungu kwa jinsi ulivyo vyote na vile ulivyo navyo, hubaki na kitu cha kung’angania kama chako tu na nafsi yako choyo ya kuutafuta kwanza ufalme wa Dar kisha wa JUU badaye! Utatoa si tu 10% bali 30%,40%, 50%,30% 1OO% mpaka wewe mwenyewe au Isack! Unauona msaada mkubwa sana wa kiroho huo! Si upone tu Sungura! sasa ukikataa msaada na ukasimama kwa meza ukilia, mimi sijasaidiwa, ati nyumbai hakuna msaada, unatakiwa mboko/kudundwa wewe!

  Kuiita zaka laana, kodi, chanzo cha umaskini kanisani, kongwa, sihiitaji kuelewa zaidi ulimaanisha nini, maana hayo tu maneno mabovu dhidi ya utoaji Zaka, yanatosha kwa uovu wake, itakua ni kukosa akili na kazi ya kufanya kusubiri radio ya Philips ichezeshe CD ya digitali.

  Kuhusu kuhani huyu-Hebrews 4:14 kwamba Huyu ndiye kuhani wako ambaye Bwana amekupa na hahitaji zaka, ni kweli nami ni wangu na Yeye kama Yeye hahitaji Zaka LAKINI angalia mwongozo wake hapa- amesema ivi:

  Waefeso.4:11-12-Aliwatoa wengine kua Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu kwa ajili ya kuwajenga Watakatifu na kazi ya huduma ili kuujenga Mwili wa Kristo. Kwa kua ndivyo hivyo, Roho wake akavuvia akili na ufahamu wa Paul kuweza tafakari haya-1Wakorinto.9:1-14-mstari 7= ‘’ni askari gani aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe’’, ‘’nani apandaye shamba la mizabibu asile matunda yake?’’, ‘’Nani achungae kundi asinywe maziwa yake?’’, Mstari 9=’’Usimfunge kinywa ng’ombe apulapo nafaka’’, mstari 11= ‘’sisi tumewapandia vya rohoni, je kuvuna vyenu vya mwilini ni neno kubwa?’’, mstari 13= ‘’hamjui ya kua wale wazifanyao kazi za hekaluni hula ktk vitu vya hekalu’’ na ‘’wale waihudumiayo madhabahu hua na fungu lao ktk vitu vya madhabahu?’’, Mstari 14= ‘’Na Bwana vivyo ameamuru wale waihubirio injili wapate riziki kwa iyo injili’’ na
  Kisha akasema ivi ktk Luka.10:7, ’’maana mtenda kazi anastahili ujira wake’
  Sasa, wakati Yeye Mkuu hana haja ya Zaka kwakua yuko Juu tayari ingawa naamini kwa mfano/ukweli huu Luka.8:2-3, aliziihitaji sana tu aliopokua hapa chini, bado ameaMURU(hakuna kubembeleza akina Sungura na Amin wakorofi/watesaji na wasio baraka kwa hao Bwana Mwenyewe aliowatenga(e.g. Mchungaji) kwa ajili yao), wale, wanywe na kushiba toka MATOLEO yote( Zaka moja wapo) za akina WATESAJI NA VURUGU MECHI PIA WAGOMESHAJI UTOAJI KANISANI.Halafu nakupa msaada mkubwa na maridadi kabisa wa kiroho namna hii, unasema siwezi kukusaidia mie! We si utakua na matatizo mengi sana ya kiroho namely kiburi, uchoyo, nafsi kutawala,kujiinua, mapinduzi ya kidevo kanisani kwako, kuunda vikundi-vikundi vya migomo dhidi ya kanisa na mipangilio ya kanisani kwako hasa ikigusa vinoti vyako, critizer mbaya, mshari na mhuumizaji mioyo, shughuli( injili) na maono ya Mtumishi akiyetengwa/tolewa kwa ajili yako Kanisani kwako hapo. Nakuona Sungura pia na kaka yangu Mkubwa Amin, HAMKO SAWA ROHONI Brothers. U may appear fine hapa but kwa haya yaujazayo moyo uliotapika hapa, wewe hauko sawa na una shida kubwa ktk malezi ya kiroho na ujumla ya Ukristo wako chini ya mamlaka ya kiroho iliyowekwa juu yako hapo ulipo. Labda nikuulize ivi( let me see/sense/feel your heart kama nakosea, jibu swali hili: ‘’Sungura unampenda, kumuheshimu, kumthamini na kumtakia mema Mchungaji wako? How? Eehe! Hapo sasa! nakwambia nitakuONA tu mpaka ndani tokana na majibu yako! Hapo nitatembea ktk prophetic dimension, si zile zako za pekesure spirit! Aya jibu! Kaka Amin, pia jibu!

  Mimi ku-wish nimfahamu Mchungaji wako niongee naye pembeni kuhusu hali na tabia yako inahusianaje na kumtafuta na mke wako? Yaani kama kuna ‘anointing’(ofcoz ya kidevo au pori) ya kufyatuka na kuropoka, wewe hamna tena Tz and East Africa aiseee! Mimi nimsake wife wako? wa nini kwanza? Wakati nimeookoa mie maskini! mwe! nimecheka sana na hapo hapo kusikitika unavyotema cheche out of satanic porridge!

  Wajua ni mara 5 sasa unanikatalia kila nikisema natoa zaka ktk moyo na ufahamu wa Ibrahimu LAKINI hakuna hata mara moja umesema kwa nini unakataa! Stop jokes, do the job! Sana sana umesema ALITOA TOKA MALI SI YAKE! Hii ndio hoja ya kuniletea mimi? nitakufyatua na mimi! unanitia hasira kweli sasa! unauzi sana we mtu.

  Umesema kwa hiyo na mimi nasisitiza kutoa kwa kuwa nina rejea kwenye background ya torati? Na wewe umejibuje kwa hii ya Mt. 232:23? Si umetoka kusema kua hiyo ndio ya Malaki3:8? Kwa hiyo unasema YESU ALIFUNDISHA UTOAJI WA ZAKA UENDELEE KWA MUJIBU WA TORATI maana umesema hii Mathayo.23:23 ndio Malaki.3:8! Kwahiyo jibu langu ni ndio maana umesema kasema Mwenyewe kua tutoe kwa mujibu wa sheria! sasa je unataka nini cha zaidi? TOA SASA si kasema Master maana alikua anaongea na wote yaani jamaa wale na mstari wa 1 unasema na WANAFUNZI wake.
  Na hapa hapo tuanze ilo la Mathayo.23:23 nilikuhaidi moto wake baada ya wewe kusema wazi bila aibu wala tafakari ya kina na kicho kua HAYAKUHUSU ALIYOEMA YESU hapo.
  Maswali:
  (a) Unawezaje kujiondoa ikiwa Yesu anaongea na wote wale na wanafunzi?

  (b) Kwani hoja ya Yesu hapo ni kufanya ya rehema, imani, adili kisha kulipa Zaka au aina ya vitu vya kutoa? Yesu alikua anakomalia ulipaji wa mnanaa, jira na binzari hapo? ndio ilikua mantiki ya alichosema/taka wadake na kumeza watu wale na Wanafunzi? Huyu vipi ufahamu wake jamani? mnisadie humu duniani! khaa!

  (c) Mathayo.23:2-3= Yesu anawaambia Makutano na WANAFUNZI wake kua…’’ Mafarisayo na Masadukayo, wanakalia kiti cha Musa, KWAHIYO, YOYOTE (notice: ‘’yoyote’’ watakayo waambia MYASHIKE NA KUYATENDA lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende maana wao hunena lakini hawatendi. Kwakua ktk mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo, zaka imo, wakikuambia toa, unapaswa kutoa au la ilihali Yesu amesema wakituambia, tushike na kutenda? Ehe! Hapo sasa!

  (d) Mathayo.12:1-50 Maneno ya Yesu hapo yanakuhusu au la?

  Naachia hapo kwanza maana najua tu kwanza mpaka hapo sijui utalevel vipi uwongo na kiburi ulipo dare sema Maneno ya Bwana ktk Mathayo.23: 23 hayakuhusu! Unatisha sana kwa uasi wewe!

  Wewe jibu swali! YESU alioga/chafya/miayo? JIBU! Nakuona tu unavyozunga! JIBU! Full stop and perid! wacha maneno! Then utaniona kwa nini naamini Ibrahimu aliendelea kutoa zaka hata kwa mali zake tena kwa aina ya moyo wa mtu kama yule hata kama haikuandikwa live, nilikuambia assumptions nyingine zina nguvu sana, utapwaya wewe kuzikataa! Narudia, Je Yesu alioga/chafya/miayo? andiko? Ha ha ha h! cheza kweli wewe!jibu hapo na andiko! Muulize Amini, Lwembe, Kaswahili kwanini walihemea puani kwa swali hili kisha wakanipisha njia Askari wa Bwana mie nikapita mshindi! Aya mfupa umewashinda hayena, ostabeyi pusi ataweza? JIBU weweee, wacha masihara, tuko kazini hapa. Nitakaba kweli hii.

  Ati maelezo yako kwamba Mungu yuko detailed and particular haujaipata kabisa mantiki’’ mmmmh! Ni kichina icho/kile? Huyu vipi jamani, mbona kujidai kwiiiiingi kwa mambo peanut?!

  Unauliza..Tatizo ni nini mpaka Sadaka isitoshe kuwatunza Watumishi na wengine? JIBU: Muulize Mchungaji wako KAMA una mahusiano mazuri naye na wewe ni mwana kweli hapo/kwake na si jeuri na mtesaji wewe, am sure Pastor wako ATAKUAMBIA sincerely.( ila bwana nahisi kwa kukuambia muulize Pastor wako, unatoka jasho na kigugumizi eee! maana una madudu uko, kwa moyo huu niliouona hapa, mwe! Mungu akusaidie upone.
  Press on.

 27. Seleli ati nirudie kusoma comments zote, za kwako?!!! Give me a brake!

  Sihitaji msaada kwako maana huna cha kunisaidia katika hili Seleli, labda kwa mambo mengine kama yatakuwepo. Wewe ndo unahitaji msaada kuliko unavyodhani.

  Na bila shaka ulianza kujibu hoja zangu kabla ya kumaliza kusoma makala yangu yote.

  Ona ulichoniambia hapa:Usiwauzie kesi wengine kwa kusema ‘’ninyi hamuwezi toa majibu ya ‘yes or no’, hii case yako Kaka”

  Nilichokuwa najibu hiki hapa: ”na nadhani ndio maana umekua muoga sana kujibu swali hilo langu pamoja na wenzio wapinga zaka ktk mada hii, mmekwepa maana MMEONA moto hatari na mmoja alijaribu ndio kaharibu zaidi”

  Then niambie sasa unachosema nisiwauzie kesi wenzangu kutokana na hiyo nukuu.

  Kuna maneno yangu hapa umeyarudia rudia sana kuyanukuu ”Kuiita zaka laana, kodi, chanzo cha umaskini kanisani, kongwa ndio level kubwa ya majibu”

  Na nilimaanisha hichohicho nilichokisema kwenye hiyo tungo. Kama hujaelewa nilichomaanisha au kama unataka nithibitishe nilichokisema niambie tu.

  Unasema hujui kama niko mwaminifu kwa kuhani wangu! Unaweza kumuuliza kuhani wangu maana bila shaka unamjua.
  Huyu hapa (Hebrews 4:14 Therefore, since we have a great high priest who has ascended into heaven,[a] Jesus the Son of God, let us hold firmly to the faith we profess). Huyu ndiye kuhani wangu ambaye Bwana amenipa, na hahitaji zaka.

  Ona ulichosema hapa pia; ”I wish nimfahamu Mchungaji wako niongee naye pembeni kuhusu hali na tabia yako kwa ujumla je ni mshirika kweli WA UKWELI wa kanisani hapo ilo la pamoja au ni wale waishio makanisani kama wapitaji, mambo yakwende vema, yasiende ilimardi wao wameshiba, the rest, none of their business.”

  Hiki ndicho nilichosema kwamba ukiona maharage yanaanza kuibuka juu hizo ni dalili za kuiva. Umeshaanza kumtafuta mchungaji wangu, siku si nyingi utaanza kumtafuta na mke wangu, be careful!

  Wewe hutoi zaka kwa mujibu wa Ibrahim, wala usijidanganye. Lakini ni kweli unatoa kwa mujibu wa Mt.23:23, ambayo haina kabisa uhusiano na ile ya Ibrahim. Ndiyo maana jana nikakuuliza je unayafanya hayo ambayo Yesu aliwaambia mafarisayo wasiyaache? Yaangalie vizuri maana yako wazi kwenye hiyo mistari, pamoja na kwamba hukutaka kulijibu hilo swali,la kwamba huwa unatoa zaka ya hivyo vitu?

  Hiyo Mt. 232:23 ndiyo inayohusiana na Malaki 3, na ndiyo sheria yenyewe. Na ili ujue kuwa huwa hutoi kwa hiari kama ulivyojaribu kuichambua hiari hiyo kwa kuibugi kwenye makala yako kabla ya hii ninayojibu.
  Na ili ujue kuwa hiyo siyo hiari ni lazima, Israel walipoacha kuitoa Mungu alifunga madirisha, ikawa laana kwao. Kwa hiyo ulazima unakuja kwamba usipotoa, tena kama inavyotakiwa, unalaaniwa. Ili usilaaniwe hauna budi utoe, hapo hakuna hiari ni lazima.
  Unasema ni hiari wakati unaona makanisani jinsi watu wanavyoandamwa, wanaandikiwa risiti, wanaandikwa majina, wengine mpaka wanabandika majina ubaoni- Hiari ndo iko hivyo?
  Kama unadhani unatoa kama hiari jaribu siku moja toa pesa yote sadaka bila kutenga zaka yake, kama jina lako halitaweka ubaoni na wakati umetoa pesa yote kwa Bwana.
  Mbona hawawafuatilii wasiotoa sadaka? Jibu ni kwamba hawafanyi hivyo kwa sababu sadaka ndiyo wanayojua kuwa ni hiari. Likini siyo zaka.

  Umesema UNADHANI kuwa kanisa la kwanza katika machangizo yao walitoa na zaka kwa sababu walikuwa na background ya torati ya Musa. Kwa hiyo na wewe unasisitiza kutoa kwa kuwa unarejea kwenye background ya torati?

  Bahati mbaya sana kwako, maana biblia haijasema kuwa walitoa zaka, bali ni mawazo yako tu hayo. Na si kanisa lote walikuwa waebrania mpaka wawe na background ya torati. Wafikirie watu wa mataifa kama wakorintho, waefeso, n.k

  Yaani kama leo hii ilivyo ya muhimu zaka na wakati ule ingekuwa hivyo tusingekosa kuona angalao mara moja kwenye kanisa la kwanza majina ya wasiotoa (wakorofi kama mimi kama unavyoniita Seleli) yakibandikwa ubaoni. Lakni tunaona watu wanauza mali zao na kupeleka pesa wanayotaka wenyewe miguuni pa mitume, hatuoni wakiambiwa watoe zaka yake kwanza ndipo wapeleke kiasi wanachotaka miguuni pa mitume.

  Kama Sungura anaweza kusababisha kanisa liteseke kwa sababu hatoi zaka, basi kanisa ni shida kubwa aise.

  Kuhusu kusongesha kazi ya Mungu mbele, nilijua utakuja kama hivyo ulivyokuja. Nilijua utakuja kwa rejea za zaka ya wakati wa torati ya Musa ambayo kimsingi wewe unakana kuwa hutoi kwa mujibu huo. Au ukubali kuwa unatoa zaka kwa mujibu wa torati au ukubali ukweli kwamba mitume walifanya kazi ya Mungu kwa machangizo na sadaka wala si kwa zaka, zingekuwepo na zaka ingesema. Isingesubiri aje aseme Seleli.
  Maana kwa mujibu wa sheria ni kweli walawi ili wahudumie hekaluni ilibidi wapewa zaka maana hawakuwa na urithi ispokuwa hiyo zaka.

  Seleli unajua assumption yako ya Yesu kuoga na Ibrahim kutoa zaka toka mali yake mwenyewe hazina ‘correlation’, nakushangaa sana kuung’ang’ania.
  Biblia hata haijakuonesha sehemu nyingine yoyote alipokutana na Melkizedeki au kuhani mwingine yeyote. Usilazimishe kitu ambacho hakipo kwamba kipo,bora ulazimishe kitu ambacho hakipo kwamba hakipo.

  Maelezo yangu kwamba Mungu yuko detailed and particular haujaipata kabisa mantiki. Kama ingekuwa paper ningesema umeingia chaka mbaya, maana haikuhusu kabisa suala la Mungu kuwa mtoaji. Ukitaka unaweza kuisoma tena may be utaelewa.

  Kwa hiyo Seleli sasa hivi unadhani kuwa uko makini au umenikona?
  Mimi mbona sioni umenikona wapi!
  Nakingoja hicho cha Mt.23;23 ulichodai utanibana nacho.

  Ivi Seleli kwa nini unafikiria kuwa sadaka haiwezi kuwatunza wachungaji wetu kama wanahitaji kutunzwa, ikatosha na kuwasaidia wajane, yatima, na wahitaji wengine;in fact mpaka waimbaji? Tatizo ni nini mpaka isitoshe?

 28. Salaam ndugu mpendwa Edwin Seleli.
  Nashangazwa kuwa bado unaendelea kudhani kuwa ZAKA ni mojawapo ya matoleo ya kupeleka kwa mchungaji.Pia umetumia maneno mengi ya uongo kuwa hakuna mtu aliyethubutu kuita kuwa ZAKA ni FUNDISHO POTOFU.Mimi nimeliita hilo zaidi ya mara moja katika post zangu huko nyuma.Umedanganya tena kuwa hakuna mtu aliyetoa uthibitisho kuhusu nadharia ya upotofu wa fundisho la utoaji wa zaka kwa wakristo wakati unafahamu kuwa nimeshatoa post za kutosha kuthibitisha upotofu huo ambao unaondoa nadharia ya NEEMA YA KRISTO kwa kanisa.
  Kinachoonekana kwako ni ujuzi wa kutengeneza maneno mengi na post ndefu zinazojizungusha humo humo kutetea kisichoteteeka,kulinda kisicholindika na nafahamu kwa hakika kuwa wakristo sasa wameanza kuamka na kufahamu matango mwitu ambayo wamekuwa wakilishwa karne kwa karne.
  Katika mojawapo ya maelezo yako umetoa uthibitisho wa fundisho kuhusu zaka na mimi nakupa references ukazisome vizuri uelewe upotofu wa mafundisho hayo.
  Kama una bidii katika kujifunza nenda kasome KAMUSI YA BIBLIA iliyoandikwa na mtu anayeitwa Fleming katika maana ya neno ZAKA utaelewa,pia tafuta Britanica Encyclopaedia hapo utafahamu zaka imeanza kutolewa lini kwenye kanisa,kisha tafuta The american bible dictionary uone maana ya zaka kanisani halafu ulinganishe na maana ya zaka kibiblia.
  Kwa ujumla unachotaka tujifunze kuhusu uhalali wa fundisho la zaka kwenye kanisa ni kile kile tunachokijua,aya zile zile tunazozijua,nadharia ni ile ile tunayoijua isiyo na mashiko bali muendelezo wa mafundisho ya vitisho vya jehanamu kwa wasiotoa,kubarikiwa kwa watoaji n.k.
  Ni vizuri sasa uvunje ukuta wa itikadi usiokusaidia kwa lolote bali unaoendelea kujenga SILA kwenye moyo wako bila msaada wa Roho wa Mungu.
  Pia tambua kuwa palipo na wingi wa meneno kuna UOVU na hivyo jitahidi kuwa msikiaji mzuri na siyo msemaji mkubwa.
  Mungu akusaidie kupokea ufahamu ulio juu ya mapokeo ya kidhehebu uliyonayo.
  NAKUPENDA SANA MDOGO WANGU

 29. Sungura,

  Ni kweli tunaongelea Zaka lakini ni wazi itakua akili finyu, kufinya tafakari kubwa na kujipunja baadhi ya kweli, ikiwa tutaoongelea Temeke bila kusema Dar-es- Salaam ivyo ktk kujadili Wilaya iyo, kwa kukusudia au bila kukusudia, kwa kutaka au la, Dar itaguswa tena hata TZ zima, why? ziko facts nyingine kuhusu Temeke ambazo hazieleweki/hazitakua na mashiko/itakua kazi to make sense out of them kama Dar ambayo Temeke inalala na kuamka na tena Tz ambamo Dar inalala na kuamka ambayo pia ndani yake Temeke inalala na kuamka, havitaguswa. Hili nilifafanua/fundisha siku za mwanzo kwa kutumia mfano mwingine kua huwezi kuongelea somo la Damu ya Yesu leo, uka-make sense bila kusema kabla ya damu ya Yesu yaani damu za mafahari na viumbe wengine zilikuaje na zilifanya nini.Pia nilikuakbia sababu nyingine ya somo la Utoaji kwa ujumla kuletwa lilikuja ni kuitikia hitaji la mshiriki mmoja wa mjadala huu( rudia kusoma comments zote utamjua ni nani) aliyeomba Utoaji lifundishwe, sababu kuu izo 2 bado hutaki kuelewa na huelekei kuelewa, sasa mimi nikusaidije? Unao msimba mkubwa kwa kweli. Nitarudia sababu izi bila shaka kwa ufunuo mpya na wa aina nyingi mpaka utakapoelewa maana wengine shule ya msingi husoma miaka 10 na wengine miaka 7 ila msingi shurti wote wasome shule izo kabla ya kwenda sekondari.

  Sasa umesema Isaka alitolewa kama kafara, swali ni Kafara ni nini? si aina ya sadaka sema hii inakua ya kuteketezwa! Si unaona sasa wanione bure kuniambiana kichwa kigumu! nadhani hukupaswa kuropoka ivyo, kumbe wewe ndio una maneno ya kipagani kweli wala si mimi uliyenisemelea kwanza ndio maana kuna nyakati ukijaribu kunishauri au kunirekebisha, hua nacheka tu nasema, mwe! kuna watu duniani wana confidence za porini kweli!

  Usiwauzie kesi wengine kwa kusema ‘’ninyi hamuwezi toa majibu ya ‘yes or no’, hii case yako Kaka! uko na mimi hapa, kazi kazi tu, wengine waache! Wakija nitasalimimiana nao mara moja bila kuchelewa! hata ivyo wanayo yakwao pia makubwa bado kuyatubia! Kama unasema huoni ya kujibu na hujui kwa nini nakuona mliaji-liaji tu mwenye visingizio chunga nzima badala ya kuwajibika, basi nitakupa changamoto hii- fanya home yako, soma tulipoanza, mangapi nimekuuliza, ukayachoropoka, au nikipenda naweza kukutengenezea summary lakini onyesha nia kwanza, acha uvivu. Kama level hii kubwa isiyo kua na majibu ya ‘yes or no’ answers,( kitu ambacho ni ulongo tu lakini), kwani kuna majibu gani sasa? yako wapi hayo mengine zaidi ya miropoko tu na kejeli kwa utoaji hususani Zaka? Kuiita zaka laana, kodi, chanzo cha umaskini kanisani, kongwa ndio level kubwa ya majibu!? wewe unahtaji msaada tu wa Roho Mtakatifu akuponye maskini wa Mungu! hujijui una tatizo kubwa sana la ubinafsi, nafsi haijaanguka chini ikafa kwanza na pia huu mkristo mkorofi na mtesaji wa kazi ya BWANA wewe nahisi hadi hapo kanisani kwa mchungaji wako! Sidhani kabisa kua Sungura ivi ulivyo humu ktk swala la kutoa ati kanisa uko mtoto mzurii na mwaminifu kwa kuhani wako ambaye Bwana amekupa? Izi vurugu zako humU bila shaka ni mwanzo mwisho hata hapa unapolelewa! I wish nimfahamu Mchungaji wako niongee naye pembeni kuhusu hali na tabia yako kwa ujumla je ni mshirika kweli WA UKWELI wa kanisani hapo ilo la pamoja au ni wale waishio makanisani kama wapitaji, mambo yakwende vema, yasiende ilimardi wao wameshiba, the rest, none of their business.

  Hivi pia ndio naviita navyo ni visingizio kusema ivi…’’Sijataka tu tuingie ndani kwenye kuichambua hiyo zaka uliyong’ang’ania, kuiona masharti yake yalivyo na jinsi unavyoyavunja’ SWALI: Utataka lini? Unangoja nini? umezuiliwa na nani? au unaogopa nini? kama majibu kwa yote hayo ni none, aya twende kazi, ONGEA usisike ili tushikane vema. Kumbuka NA NARUDIA HAPA KWA UKAKAMAVU kua NINATOA ZAKA KWA MSINGI/MFANO wa ALIVYOFANYA IBRAHIMU-Mwz.14:1-20 kabla ya Sheria na NATOA ZAKA kwa mantiki ya dokezo la Yesu ktk Mathayo.23: 23 lakini pia kwa maandiko mengine ya ‘kumpenda Mungu kwa kila kitu changu’’ na ‘kumuheshimu Mungu kwa mali zangu’’ ivi unambanduaje Mtu hapo aliyeookoka na kujiachia kwa BWANA ivyo! Mbona rahisi tu tamu sana kutenda/kutoa ivyo? ivi wewe mwenzangu raha yako ya utoaji unaipatiaga wapi? Unamtoleaga nani wewe? wapi na kwenye manini? Wanashangaza hakika.

  Embu angalia capacity yako ingawa unajidai kila mara uko smart! Ati umesema,’’ zaka haikuwa toleo kwa ajili ya kufanyia uinjilisti na si toleo kwa ajili ya kazi ya Mungu kusonga mbele na kwamba Kazi ya Mungu inasongeshwa na sadaka pamoja na machangizo, na hata ukiwasoma mitume hivyo ndivyo walifanya’’. Sasa ngoja nikutest iyo capacity yako ya kufikiri vema imo au maneno tu ya bora liende!
  Maswali:
  (a) Wakati wa sheria, Zaka ilikua ni kwa ajili ya kuwa-sustain kimaisha Walawi waliokua wametengwa rasmi kwa kazi hekaluni na ivyo kutokua na ardhi( ishara ya kutojiangaisha kushughulikia maisha kama watu wengine bali kupata muda wa kujiweka sawa/kuangalia mambo ya huduma maalumu hema ya kukutanikia waliyotengwa kwayo bila kua na presha ya wale, wanywe wapi-Hesabu.18:1-32 na wakati wa Ibrahimu mwanzoni, aliitoa kwa kuhani Melkezedeki-Mwz.14:1-20 mfano wa Kuhani Yesu- Waebrania.7:1-28 na uwe na uhakika, Melkizedeki hakuitupa bali aliila na kuinywa vema sana. Sasa kwa kua Agano la Kale ni kivuli cha picha halisi ya Agano la Leo-Waebrania.10:1,na kwakua walitoa kwa Mungu kisha Walawi wakala ivyo ivyo Melkizedeki na ikahesabiwa kwa Ibrahimu na wana Israeli wamefanya vema, leo tukitoa kwa Walawi/Makuhani wetu kwa mantiki iyo iyo yaani wakastawi, wakatulia nyumbani kwa Bwana, wakala, wakashiba bila maangaiko,wakabaki na moyo, roho, akili moja tu ktk huduma, Je huduma ya Mungu haijasongeshwa mbele hapo? Je akienda kuhubiri kwa nauli ya zaka, Injili/huduma haijasonga mbele? Huyu vipi jamani! halafu unasema unawaza vema na uko makini na bila haya unaalika watu wakuchungulie/evaluate hoja zako! Huoni aibu hata kidogo! nikikuambia huna kitu au unapwaya kwa mengi kama nikiamua kukupima, utanikatalia bure tu lakini ukweli ndio kama huu juu, tayari hapo hamna kitu, ulidhani umetoa hoja nzito lakini kama navyokuambia kila siku, tusema yote kisha tuje ktk Neno na Roho Mtakatifu akivuvia akili fahamu zetu kuyanyambua mambo, ndipo utajua ni kweli nina kichwa kigumu kama ulivyonibatiza au nina Roho wa Mungu very active and moves amazingly in all members within using me for you, I mean u especially Sungura!!

  (b) Unadhani ipi ni rahisi kuwa na mashiko KiBiblia kati ya Zaka KAMWE haikutolewa au ilitolewa ktk machangizo na sadaka mbalimbali walizopewa Mitume kuchapa kazi ya Mungu isonge mbele? utoaji wa zaka yaani Mtu kutenga 1 ya kumi ya aliyokua nayo, haukutoka au vipi hasa ukizingatia wengi wa wana Kanisa, walikua na background ya Musa na torati-ziko baadhi ya kweli za torati- ziliendelea kutumiwa(zile nilisema zina hama moja kwa moja-mfano-1Wakorinto.14:34d)- Hili ni moja ya maswali viporo! Si unaona sasa, kukimbia kwako na kulia-lia na visingizio vya ati hakuna ya ‘yes or no’ here, sasa yanakurudia! Ni bora ungekua unamaliza kazi kiukakamavu tu ili mbele tunakwenda bila kurudi nyuma.

  (c) Na labda niparaphrase la (a) maana kufundisha mtu wa aina yako yataka moyo, neema, RM, skills/techiques nyingi mno na zipo tu zimejaa tu, relax. Unaelewa nini wewe kuhusu Kazi ya Bwana? Unadhani Kuhani wako akila na kunywa Matoleo yako( Zaka imo) kisha akafurahi na kupata raha yeye na famiia yake na kuchapa kazi, umefanya Kazi ya Bwana kwa kumlisha huyo au umefanya kazi ya serikali?

  Kama u-kodi wa zaka kwa msemo wako unakuja kwa kua Watu wanapewa namba na risiti-( ingawa nilishaeleza maana NJEMA SANA ya Taasisi kwa Kanisa kua na utaratibu thabiti na ulioenda shule kuhusu mambo ya fedha(fedha haiendeshwi/ kutunzwa kirohoroho-soma comments zangu za nyuma-ilikua very clearly clarified-wewe una tatizo la kumbukumbu kwa BAADHI ya mambo ya ufahamu, unasahau sana Sungura, yapi tulisema na sasa tunaendeleaje, siyo mara ya kwanza kusahau mambo ya msingi unayofafanuliwa! So, ili kuondoa huo u-kodi unausema, tukiondoa namba na risiti, UTATOA zaka maana vikwazo hamna tena! jibu utatoa?

  Ndiyo, nilishawahi jiuliza hili swali ”Why so much complications on tithe, and not on other forms of offerings?” na JIBU NIKAPATA HILI: because we have many undedicated members in the churches, the Sunguraz who would allow their selfishness to dominate their decisions to give at the expense of the church development and her activities advancement! Simple! Thus, transform or eliminate the Sunguraz on the face of the earth/church, then the World or Body of Christ will NO MORE suffocate in its dealings

  Walioniambia sieleweki ni wale wale tu na kama kweli wana hoja ya maana, wasema kwanza wanatoa zaka hawatoi na kwa nini? kisha waniambie kwa hoja ipi na kivipi sieleweki nami niwaulize yangu la sivyo nitajua ni wale wale tu! wana mateso kwa Kanisa na Watumishi wa humo kwa kujali yao na kubania walivyo navyo wakati huo huo wakitaka hawa ‘Walawi’ wahudumu ktk uwepo au udhihirisho mkubwa!

  Kuhusu Ibrahimu hatuoni mahali popote anatoa zaka mali yake mwenyewe? Mimi nimekupa kweli mafikirio yangu kua kama alitoa ya mali ya mapambano, sembuse mali yake mwenyewe! Na nilishawahi kukuambia siku za nyuma( case nyingine ya kusahau iyo) kua ziko fikra/assumption nyingine zina nguvu sana/zina mashiko KiBiblia na kiakili, kukataa ngumu! Mfano Yesu alioga/chafya-ingawa andiko live hamna lakini ni kweli alioga/chaya/kupiga miayo, sasa kwa mantiki iyo, Kama zaka baadae ktk sheria ilikuja fafanuliwa vile maana hasa ya kikumi na kama Ibrahimu alitoa kwa concept iyo iyo hata Yakobo kuhaidi tithe-concept iyo iyo toka kabla na wakati wa sheria inatembea na kama ule ndio ulikua moyo wa ibrahimu kuhusu Kutoa kwa Bwana iwe Isack-Kafara au Zaka, kwanini nisiseme kua pia alitoa zaka kwa mali yake ingawa haijaandikwa live kama vile hakuna live kuhusu miayo ya Yesu! Unanipata hapo? Aya, ngoja nione unavyoangaika kwa hili, nikuulize ivi, kwa kua umesisitiza sana( sijui una-agenda gani-itakua peupe soon tu) hatumuoni Ibrahimu anatoa zaka kwa mali yake mwenyewe, so Unataka sema/toa fundisho gani hapo? ehe! Nakusikiliza kwa makini sana!

  Umeshangaa ati namuona Mungu anachotaka ni kutoa tu.. NDIO kwa kua tunaongelea Utoaji na hasa ZAKA, tukiongelea mengine, huko nako utanikuta namsema Mungu wa hayo pia,YEYE NI YOTE KTK YOTE,hujui ilo? Sasa kama yuko detailes and so particular, nifanyeje mimi sasa? ndio anakuzulia usimuongelee in details kuhusu Yeye alivyo Mtoaji na kisha sisi twapaswa kua watoji too? We sijui unaongega nini sometimes! Unafyatuka tu pwaa!

  Hii ya Mathayo 23:23-24, umesema HAIKUHUSU! usijidai ati unajibu kwa level yangu! Yaani unavyojitapa na kama kweli ungekua thinker, ingependeza but on some issues, you poorly show up that boy! Mi nilitaka commitment iyo kujua kweli unamaanisha, sasa basi nitakujia kwa ilo nitakapowasili tena hapa vilivyo. Acha kujidai kwa kuniambia kua unajua nachotaka kusema! Wewe umekua nabii spesheli mpinga Zaka siyo? Halafu kisha unanigeuka na kunionya ati mie niache majigambo! Ona sasa! si yale yale! Ati unajua nachotaka kusema na ati wewe una jambo umeliona ambalo mie ni kavu! Sijaona! Mwe! izi confidence pori zenye 400% zinawaendesha puta-puta kweli.Aliyekuambia mie nina kitambi nani! nimekaba mpaka umenitafuta kunichungulia uko na kule mitandaoni eee? Aya na bado, na pia n kama ninacho, nitakubanaje! Aisee una ropoka kweli! yanakutoka eeee? Jiandae utayafyatua mengi kweli nikianza kukaba very soon! Huitaji kupiga debe wana SG kuamua, yaliyopo yanatutosha kuamuana, Nasema huna kitu kwa kua, siku za mwanzo uliwa grade wenzio hawana kitu na mie nilipoingia, ukani grade siko makini,nika kuthibitishia mpaka sasa kua ulikosea sana kunivamia kienyeji na pia kwa kua ulijidai sana mwanzoni, ukanivutia kukufutilia kujua kweli kuna vitu vikali na vyema KiMungu, Biblia, KiKanisa, KiUtumishi na KiAkili, sadly ndio nakuta kumbe una madudu mengiii na nimejua kumbe ilikua ni mbwembwe tu hence nimeendelea kukukona mwepesi na huna vitu kivileeee nilivyodhani kulinganisha na madoido yako na misifa kua unavyo
  Press on.

 30. Seleli amua wewe mwenyewe utanichukuliaje, kwa wepesi au kwa uzito au kwa vyovyote, I don’t care. Ninachojua ni kitu kimoja ninachokisema ni neno la Mungu wala sijakitunga. Kama wewe unaona matoleo yote yako sawa tu ki kanuni, basi ndio maana hatutaelewana kabisa.
  (Go gym brother to stimulate yo brain, may be u are being too big for rational reasoning- Just an advice).

  Unanishangaza sana kwamba tangu muda wote huo tumeongea hujang’amua hata msingi wetu wa kutofautiana. Unaponiuliza kwamba kama hayo si matoleo niseme yanaitwaje- so whata, nini cha msingi unachokitaka hapo?

  Nimekwambia tena na tena kwamba tunaongelea zaka. Hatuongelei malimbuko,wala sadaka, wala machangizo, wala misaada. Na kama tunaongelea zaka tunaongelea msingi na kanuni yake. Isaka alikuwa hatolewi zaka wala sadaka,bali alikuwa anatolewa kafara. Kwa hiyo hapa swala la Isaka wala hatukutakiwa kuliongelea, lakini wewe kwa sababu ya kichwa chako kuwa kigumu umelikokota mpaka hapa lisipohusika.

  Kuna nini abacho sijakujibu ambacho unalalamikia kuwa naleta visingizio? Hii si level ya mjadala wa ‘yes’ na ‘no’, kwa hiyo kama unategemea majibu sisisi utaendelea kulalamika sana kuwa nakwepa kujibu maswali yako. Labda kama itabidi kufanya hivyo ili kukufanya uelewe.

  Wenye akili timamu wanaofuatilia huu mjadala watagundua kuwa sijajikita kuongelea suala la utoaji kwa ujumla wake, bali naongelea kipengele cha zaka ambacho ndio hoja ya msingi. Na sijui kwa nini wewe unang’ang’ana sana kuongelea utoaji kwa ujumla. LET’S TALK TITHE! Ninaanza kuwa na wasiwasi kuwa inawezekana zaka ambayo umeng’ang’ania kuitoa huwa huitoi unavyotakiwa ndiyo maana unajificha sana kwenye utoaji wa jumla. Sijataka tu tuingie ndani kwenye kuichambua hiyo zaka uliyong’ang’ania, kuiona masharti yake yalivyo na jinsi unavyoyavunja.

  Kama unahamu sana ya kuongelea utoaji kwa ujumla ilete tu kama mada tutaiongea kwa mapana na marefu yake.

  Halafu zaka haikuwa toleo kwa ajili ya kufanyia uinjilisti kama unavyotaka kutuaminisha. Si toleo kwa ajili ya kazi ya Mungu kusonga mbele. Kazi ya Mungu inasongeshwa na sadaka pamoja na machangizo, na hata ukiwasoma mitume hivyo ndivyo walifanya.

  Wewe ndiye mwenye msimamo wa mapokeo, unaongozwa kwa hofu. Huwezi kujiruhusu kufahamu tofauti na ulivyopokeleshwa. Tangu ulipoambiwa habari za Kristo uliambiwa kuwa zaka ni lazima utoe, lakini usipotoa unamwibia Mungu, na kwamba utakuwa chini ya laana. Ndio maana huwezi hata kugundua kuwa huwa hauitoi zaka kwa Mujibu wa Ibrahim, ispokuwa kwa mujibu wa torati ya Musa. Nawe umeng’ang’ana kuwa unatoa kwa mujibu wa Ibrahim. Na mpaka unapewa na lisiti, unapewa na namba, ndio maana nikakwambia hiyo ni kodi sasa. Na huko siyo kutoa bali ni kulipa.

  Sijui sasa hapo unayetakiwa kunmwonesha kuwa umetoa ni Mungu au mwanadamu, maana Mungu hahitaji kukuandikia lisiti ndipo ajue umetoa. Na Yesu alisema toleo lako ni siri yako na Mungu,jirani yako hata hatakiwi kujua.

  Ivi Seleli ulishawahi kujiuliza hili swali ”Why so much complications on tithe, and not on other forms of offerings?”

  Si kwamba mimi sieleweki, wewe ndiye huelewi. Kwani kuna mtu mwingine ameniambia kuwa sieleweki,ispokuwa wewe ambaye huelewi? Wewe angalao kuna watu wamekwambia hueleweki.

  Wapi Ibrahim ulimwona anatoa zaka mali zake mwenyewe ili uithibatishe haya maneno yako ”JE SI MARA KUMI ALFU ANAWEZA TOA ZAKA KTK MALI ZAKE MWENYEWE?”?
  Unajaribu ku-assume kama kawida yako siyo? Ndipo sasa unatakiwa ujiulize sana kuwa kwa nini Ibrahim hatuoni mahali popote anatoa zaka mali yake mwenyewe?

  Seleli sijui wewe Mungu unamwona ni kitu cha namna gani mpaka useme maneno haya, ”Tofauti iyo ktk kuchukulia mambo katika ugumu/uzito, je utaondoa ukweli kua mwisho wa siku, swala ni moja tu hapa yaani KUTOA tu?”
  Ufahamu wako kabisa unakutuma kuwa Mungu anachotaka ni kutoa tu, very pathetic.

  Sikia rafiki yangu, Mungu yuko so particular and very detailed. Siyo kutoa tu kama unavyodhani. Anajali nini unatoa, kwa nini unatoa, na unakitoaje. Kama ingekuwa suala ni kutoa tu, basi Anania na Safira wasingekufa kwa mali ambayo ilikuwa ya kwao wenyewe na walikuwa na uhuru wa kuamua watoe ngapi.

  Seleli yote niliyoyasema katika mjadala huu tangu uanze mpaka hapa yalitosha kumfanya mchambuzi makini kujua msimamo wangu ni upi kuhusiana na hiyo Mathayo 23:23-24. Lakini kwa sababu wewe uko kivuvuzela zaidi acha nikunyambulishie kwa kiwango chako cha uelewa unachotaka( cha ndiyo/ hapana). JIBU NI KWAMBA HAINIHUSU.

  Na kwa kuwa wewe inakuhusu, je huwa unatoa zaka ya hivyo vitu?

  Karibu sana ulete huo moto unaosema tumeukwepa,maana umetanguliza mstari wa 1 wa hiyo Mt 23 ili kunitisha. Najua ulichokiona kwenye huo mstari unachotaka kuja nacho, lakini najua ambacho hujakiona kwa hiyo utakuja umetanguliza kitambi ukidhani unakuja kunibana.

  Kwa nini unatangulia sana kusema kuwa sina kitu,kwani wewe ndiye mwamuzi kati yetu? Acha kupiga mayowe Seleli, waachie wana SG wataona wenyewe.

  Karibu.

 31. Sungura,

  Nina wasi kama wewe si Mkristo mwololo wa kuongeleweshewa maneno ya kina na kweli tupu. Ukishakua na moyo kama wako wazi namna hii bila aibu kinyume na mambo ya kweli tupu ambayo sisi huyafanya kwa nia nzuri tu ili kazi ya Bwana isonge mbele na utumishi hapo nyumbani mwa Bwana uendelee, si rahisi Mtu wa aina yako kuchukuliwa kwa uzito unaostahili, una stahili wepesi, upewe uzito kwa lipi? Sema mwenyewe? Mtu anayetaka kujifunza anaonekana na mtu anayedhani misimamo yake binafsi ni sahihi hata kama ni nje ya NENO alimradi anaweza kuipa nafasi nafsi yake ishike hatamu, atakua na visingizio vingi.

  Nimekuambia kwa msingi wa Utoaji, kama umemtoa Isack, Zaka, Changizo, Sadaka za upendo za kawaida, msaada , haya yote ni MATOLEO! kwani yanaitwaje? Ila sasa yana maana gani, tolewaje, yanajumuisha nini ndipo tunapata tofauti za hapa na pale, lakini kimsingi YOTE NI MATOLEO, kama si matoleo, nipe jina lake!

  Mimi nadhani jibu hoja/maswali, hii habari ya kusema tu juu juu kua hakuna kitu wakati kuna vitu ambavyo unajua kwa nini unaogopa kujibu toka tumeanza, visingizio ungeviacha, vimekua vingi mpaka havina hata raha! Umepewa kazi,fanya na kama hakuna cha kufanya, onyesha kwa icho ulichopewa ni kweli hakina mashiko ya kufanywa, la sivyo yatakua ni maneno tu uliyotumia mara nyingi, kukimbia kuwajibika aidha kwa yale uliyosababisha/tamka au niliyoyaibua kutokana navyokuona unavyo jaribu kuharibu Utoaji humu-mara wakukubali hili mara kukataa, mara kusema hili sawa na kisha walitia kasoro, HUELEWEKI. Ndio yetu na iwe NDIO na hapana, HAPANA

  Sasa embu angalia! umesema mimi ni kipofu kutoona tofauti kati kutoa Zaka na Isack kwa Ibrahimu, kwamba kwa Isaka, Mungu aliwamwambia atoe na Zaka, Ibrahim aliamua mwenyewe)
  Maelezo: Mwisho wa siku vyote vilitolewa kwa Mungu, Isack kwa Mungu na hata Zaka kwa Mungu kupitia kuhani Melkizediki aliye mfano wa Yesu Kristo-Waebrania.7:1-22. Lazima uelewe kwamba, kwa yale mema alotenda Ibrahimu, Mungu alikua nyuma yake kuweka au kuanza kufunua mambo yake ndio maana RM kupitia Paul ktk iyo Ebrania 7, tunafunuliwa kile kitendo na mantiki ya Zaka kwa Melkizedeki mfano wa Kristo.

  Kwamba Ibrahimu alimtoa Isack baada ya kuambiwa na Mungu ila ya Zaka aliamua mwenyewe! unachojaribu kuharibu hapa ni kuingiza wazo kua Zaka ni mpaka mtu aamue na siyo kuona Neno linasemaje/walitendaje na kisha kutenda( unaleta kijanja yale yale mambo yako manyonge ya ukitoa sawa, ukiacha sawa tu, nimekumulika mapema kabisa hapo). Na jingine bovu sana umeharibu tayari ni kama una suggest Ibrahimu kumtoa Isack, yeye hakua na choice/utashi wa kufanya tofauti! Hii si tu ni udanganyifu bali pia ni ufinyu wa tafakari sahihi ya Neno.

  Ukweli ni kwamba, japokua Mungu alimuambia Ibrahimu( na huu ukweli si kitu kigeni wala hakuna haja ya kuukuzwa saaana kwa kua ndivyo Mungu ana-deal na sisi, ametuambia na sisi mengi ya kufanya ktk Biblia), LAKINI TUNA MAAMUZI KUKUBALI AU LA. Ndio maana baada ya Ibrahimu japo aliambiwa na Mungu, yet alichagua(alitii na) Kumtoa Isack, ivyo Mungu akamwambia ivi….Mwanzo.22:1-19 hasa mistari ya 12,15,16,17..Mungu anasema ‘’Sasa NIMEJUA wamcha Mungu wala HUKUNIZUILIA MWANAO, MWANA WAKO WA PEKEE(notice: interesting arrangement ya maneno hapo , Mungu anasisitiza admiration yake hapo…see this again..’’mwanao…mwana wako wa pekee’’-maana angeishia kwa ‘mwanao’’ ingetosha tu yet akaendelea kumimina moyo wake. Utoaji ule wa MAAMUZI YA DHATI ISIYORUDI NYUMA KAMWE, ilimgusa Mungu ikabidi ‘’Malaika akamwita tena mara ya PILI toka mbinguni kusema ( notice: hapo, anaitwa tena mara ya pili) kisha anasema maneno mazito haya.. ‘’KWA NAFSI YANGU NIMEAPA KWA KUA UMEFANYA JAMBO HILI NA HUKUNIZUILIA MWANAO, MWANA WAKO WA PEKEE! Kisha akasema..’’Kukubariki nitakubariki.

  Unaona hapo, nakurudisha kulekule kwenye misingi ya niliyoshiriki ktk mada hii kua ukishampenda Mungu kwa moyo, roho, akili, nguvu zako zote kama Ibrahimu, tunatenda zaidi ya hiari yaani pamoja na hirari lakini kuna KUSUDIO LA DHATI LA KUTENDA TU SI KUACHA AU sijui MPAKA KUJISIKIA! Kama ni kujisikia-sikia, unaweza elewea Ibrahimu Mze, mtoto wake wa pekee wa uzeeni kisha kuambiwa kumtoa na yeye KUKUBALI kumtoa, si kazi ndogo, ni zaidi ya hiari yaani ni hiki nachosema kila mara-kusudio la dhati la kutenda tu kwa BWANA na hakuna kutoa nafasi ya kuacha.

  Kwamba Ibrahimu alitoa Zaka si mali zake bali zile alizoteka! hii inanionyesha tatizo lile lile la kutorosha Mali Bwana alizokupa mwenyewe na pia nisema wazi kwa hili kua ndio maana mambo kama haya nashindwaga kuelewa unapokua unawaita wenzio hawawezi kuwaza vema wakati jambo kama hili, Kwa Akili ndogo tu umeshindwa kuwaz ivi: Kama Ibrahim anaweza kua na ufahamu wa rohoni kwa kumtukuza Mungu na kumshukuru kwa kutumia mali za mapambano ambayo yeye kwa kweli ndiye akiyeshiriki kuleta ushindi huo kwa kiasi kikubwa na ivyo anastahili kufurahia matunda ya vita, JE SI MARA KUMI ALFU ANAWEZA TOA ZAKA KTK MALI ZAKE MWENYEWE? Ukoje uwezo wako wa kung’amua na ku-think big unaosema unao lakini kila nikikupima ktk BAADHI( at least to be fair,sio zote) hoja na tafakari hasa zile nzito na zisizokua wazi zaidi, kweli unapwaya sana Sungura! sasa umeshindwaje kuwaza nilivyowaza hivo kama kweli uko smart upstairs achilia tu instairs( moyoni/rohoni?

  Umesema kua kutotofautisha Zaka na Sadaka ni kuchukulia mambo kwa wepesi! Tofauti iyo ktk kuchukulia mambo katika ugumu/uzito, je utaondoa ukweli kua mwisho wa siku, swala ni moja tu hapa yaani KUTOA tu? aya kama unaujasiri na unadhani kuna jambo kubwaaa sana, lete hiyo tofauti hapa halafu nitakuuliza swali hili moja tu, namely: So? Ivyo tu! ukishaelezea utadhani kuna kitu spesheli nitakuuliza tu, ‘ehe kwa iyo tutoe zaka na sadaka tusitoe? si unaona sasa huna kitu wewe cha kusema chenye kilo? Ndio maana kukuchukulia kivyepesi na maneno ya ivi ivi ni saizi yako kabisa, kwa wengine hamna shida. Labda ubadilike ktk mada nyingine, hii umefeli na wepesi ni halali kwako

  Kama kwa sentensi yako hi..’’ kusema kwangu kuwa zaka si lazima mtu atoe inamaanisha nimesema kuwa watu wasitoe sadaka’’, hukumaanisha kuvuruga watu wasitoe, aya weka hadharani tumalize hili, ulimaanisha nini? wasitoe sawa, watoe sawa? si ndio au? Fafanua nikukamate vema.

  Hii nilishasema mengi ya Yesu ktk Mathayo.23:23 kuzungumzia ZAKA, leo unanitaka ithibati ya hiyo kama ninayo! Nijibu kwanza swali langu la muda kuhusu hili andiko nililokuuliza kua Aliyosema Yesu hapo, UNAHUSIKA HAUHUSIKI? Kisha yaje mengine mengi maana unajua tu ukikosea jibu utakavyovuruga maandiko mengi Yesu alisema akiwa-address Makutano na wengine bila kutajwa wanafunzi ingawa Mathayo hii 23, angalia mstari wa 1, utakaa kimya ufikiri vizuri! na nadhani ndio maana umekua muoga sana kujibu swali hilo langu pamoja na wenzio wapinga zaka ktk mada hii, mmekwepa maana MMEONA moto hatari na mmoja alijaribu ndio kaharibu zaidi. Si unaona huna kitu! ndio maana kiboko ya mahojiano yote ni Neno a Mungu, linakata mashauri na kuamua case. Aya, kama unadhani unajua Neno wewe na Zaka hatupaswi kutoa leo maana siku za mwanzo ktk mjadala hii mliitia kua ni laana, jibu swali langu ilo juu la Mathayo. 23 kwanza.

  Basi nakungoja nione Mkristo sawa sawa anawazaje na kujibu hayo.

  Press on

 32. Seleli;
  Look at at you!!

  Sehemu kubwa ya mchango wako ni maneno ya kipagani tu ambayo mkristo yeyote mwenye kuwaza sawasawa hawezi kupoteza muda kuyajazia paragrafu. Japo pia comment yako ina typing errors nyingi.

  Nitajibu kitu tu ambacho angalao umeongea sense. Naanza kwa kukunukuu hapa chini.

  ”Upofu upi kuhusianisha Ibrahim kutoa zaka kwa Melkizedeki na Ibrahim kumtoa Isaka? Kwa iyo umechemka kujua inahusianaje? Si uulize usaidiewe? Tatizo unadhani wajua kumbe… kwani Isack na zaka si vyote VILITOELEWA kwa Mungu? yote si simply/basically ni Matoleo tu? au kingine kilipakuliwa na kingine kikamwagwa? Huyu vipi huyu jamani? ”

  Mkristo kipofu wewe,huuoni upofu wako? Wadhani kwamba kutoa zaka kwa Melkizedeki na kumtoa Isaka kwa Mungu viko sawa. Jiulize tu swali kwamba nani alimwambia Ibra atoe ile moja ya kumi ya nyara na nani alimwambia amtoe Isaka. Isaka alikuwa anatolewa kwa Mungu, kikumi kilitolewa kwa Melkizedeki. Au wewe biblia yako anakwambia kikumi kile kilitolewa kwa Mungu?

  Ibrahimu alimtoa Isaka kwa kuambiwa na Mungu (Mwa 22:2)

  Sehemu ya kumi kwa Melikizedeki Abram alitoa kwa kuamua mwenyewe (Mwa 14:20b). Na uelewe kitu kimoja kwamba Abram alitoa zaka ya vitu(nyara) ambavyo havikuwa vya kwake, bali vilikuwa nya wafalme wa Sodoma na Gomora. Na baada ya kutoa hiyo zaka Abram hakuchukua hata kitu kimoja ktk hizo nyara, na alipopewa alikataa katakata.

  Kwa hiyo Ibrahim hakuwahi kutoa zaka yoyote toka kwenye mali zake mwenyewe,kama wewe unajua aliwahi kutoa nioneshe tu nitafurahi.

  Na kama huelewi tofauti ya zaka na sadaka pamoja na kelele hizo zote basi unayachukua mambo kirahisi sana na kudhani kuwa vyote viko sawa.

  Na kama unadhani kusema kwangu kuwa zaka si lazima mtu atoe inamaanisha nimesema kuwa watu wasitoe sadaka pia, endelea kuamini hivyo.

  Unaposema zaka imesemwa na Yesu mwenyewe, onesha tu ithibati ya hiyo kama unayo.

  Hayo angalao ndiyo ye sense uliyoandika, mengine kama nilivyosema ni maneno ya vivi hivi hayafai kuwa ya mkristo anayewaza sawasawa.

 33. Sungura,

  Katika kuikana kwako zaka ili umbanie Mungu otwoo ulivyo nanvyo, umetukana/ibatiza mengi Zaka kama mara ni chanzo cha umaskini kanisani, ni laana, sasa ni kodi! Yaani unaangaika mpaka nacheka kweli tehe! nini hii yote Sungura? yaani kwa kweli kupitia wewe nimejua kwa nini Yesu alisema, ‘Mtu atakaye taka kuiponya nafsi yake, ataipoteza kwanza kisha aipate baadaye-Yaani ktk maisha yangu ya wokovu, nilikua sikudhani kuna ‘mpendwa’ too,3,4,5,6,…..tririons selfish kama wewe! mwe! yaani Mungu anataka only 1 kisha kula yote 9, yet na hako unakwangua kwa longo longo na janja nyingi?! ambazo hata ivyo so far nimeshazisaga tikitiki, hazinyanyuki tena na zikinyanyuliwa, zinazimwa chini haraka na hata nguvu yake ya mwanzoni si ya sasa, imepasuliwa na kuvujwa-vunjiliwa kwa kiasi kikubwa.

  Usinidanganye kua wewe ni Mkristo mwololo labda Mkristo wa ina nyingine,huwezi kua Mkristo safi halafu ukawa mtesaji wa kazi na Utumishi hapo kwakugoma kutoa, haiwezekani.

  Ni kweli Mambo ya Mungu si ya nguvu ya misuli, ni nguvu ya rohoni but niambie ukishakua na za rohoni izo zinajidhirishaje zimo? Si ktk kilive/kimwili? mfano kwa kuvunjilia mbali hoja na kila elimu ijiinuayo kinyume na Elimu ya Kristo kwa kua na Matumizi sahihi ya Neno na Akili kusimamisha ya Bwana na kushushu kuzimu ya devo na dogo dogo centre members wake, kwa hoja na maswali yanayotisha sana na kufanya wahusika kupumulia dirishani, bora mtu asilete za kuleta tu manake hakuna jiwe juu ya jiwe litasalia, ni kuvunjiliwa mbali na kuinyooonga/kaba kabaaari kali ya kona roho ya devo isupumue kamwe mpaka inyanyue tail up, chezea kweli wewe, hapa kazi kaaaazi tu, hakuna jingine, nikupasua miamba, kokoto, majiwe,mawe, michanga migumu na notorious changarawe.

  Ni kweli wakristo wote wa kweli, si kwa kuswaga ili ni kweli pia watakubali tena kwa kunyenyekea makemeo na makaripio mimi,mmoja wapo, wewe je?

  Upofu upi kuhusianisha Ibrahim kutoa zaka kwa Melkizedeki na Ibrahim kumtoa Isaka? Kwa iyo umechemka kujua inahusianaje? Si uulize usaidiewe? Tatizo unadhani wajua kumbe… kwani Isack na zaka si vyote VILITOELEWA kwa Mungu? yote si simply/basically ni Matoleo tu? au kingine kilipakuliwa na kingine kikamwagwa? Huyu vipi huyu jamani?

  Aya sasa yameanza kukutoka tu! kama kawa/zamani halafu unaniiga eti kuniambia ‘yatanitoka yote-mnaniiga- iga sana eee sasa! mara Lwembe kaanza nukta kwa nukta anointing, kisha wewe pia kwa hii na sasa mpaka ume CUT( at least unge copy,lo!) na ume-paste hii..’’yatakutoka yote/utaropa yote’’ halafu unakataa mie sijawa teacher wako! Mmh! wivu tu…angalia…ati umeuliza/umeniambia kidizaini Ivi..’’mie ni juha nisiyeweza kuelewa na ni kichwa ngumu?mwanzoni ulini value siko makini, teenager, ukasupport kua nina malaria and with dege-dege bebi effects, memory card swallower, mjinga,nina upuuzi,mie bebi nk, ayo hayatoshi, umeongeza leo kua labda mie juha na my head is stony siyo? Ha ha ha ha mwe! mtu mmoja matatizo yote hayo! Ni kweli kabisa au amesingiziwa/anazushiwaa tu na wanaombatiza/zushia ivyo wanajua why wanakazana kweli asiwachungulie humo ndani wanavyocheza netboli badala ya football? Aya,all thoso mibatizo recorded, to be used as references ktk cases, ila sasa ukinisaidia nijijue kweli nina matatizo hayo kwa kujibu viporo vyote-soma mwenyewe na kujibu mengine yaliyojiri todate, then nitajua kweli, I was sick with many magonjwa aisee, tatizo usipofanya ivyo, nani atabaki kua ndivyo alivyo na anayo yote yeye tena dabo-dabo?

  Ati nimeshindwa kutofautisha zaka na sadaka katika mjadala’’ Jibu: Si kweli maana nilifundisha uko nyuma kua zote simply ni matoleo, full stop! Sasa yanatolewaje, kwa namna gani na kwa nani nk, iyo ni ishu nyingine but basically yote ni matoleo tu, usibabaishe watu hapa ili utoroke naka zaka-si nshakuona tayari wewe tena-dk 1 ukiipata basi, uyooooo ushatimua na zaka mkononi ukale mwenyewe kama alivyokua kuambia bwana ganava gala…. na mwl wako mwingine-mze wa kukimbia maswali-tehe!

  Oo yes ni heri na bora KATIKATI YA WAJANJA NA WATORO WA ZAKA KAKA NYIE-mtu akijishuhudie na kujidhibitisha bila kumung’unya maneno, ukiita hayo ni majigamba na show off-ni sawa kabisa ili MPONE maana wengine inabidi waokolewe kama kwa moto

  Ati ‘’Sina mashiko ya kutosha kwenye biblia kui-justfy zaka leo, ndio maana hata ukijaribu umekuwa ukirudiarudia Mt 23;23-24’’ Swali: Unataka nirudie andiko lipi ndio ujue Zaka AJ imesemwa tena na Yesu mwenyewe? Nirudie rudie andiko la ‘ukinyukwa shavu hili, risite na jingine utatandikwe nalo pia’’? hapo ndio utajua naongolea zaka hapo? huyu vipi tena nauliza?

  Press on toa zaka Sungura or else fumba kinywa, usiharibu tunaotoa. Nitavunja vunjilia mbali kila kijinyanyuacho kinyume na utoaji wa aina zote na wowote, niko imara kabisa ktk ilo, alika hata majeshi mengine maana ya Lwembe, Amin, Kaswahili yamepwaya mbele ya askari wa Yesu, mie hapa! Sasa je?

 34. Hahahaa ..uwiii….chezea Seleli wewe!

  Sasa naona umeamua kurudi mwilini kabisa kwa majigambo yote, kwamba wewe ndo mwenye kusaga mawe na mifupa tikitiki, kwamba wewe ndiye umekuwa jiwe kuu la pembeni, walilolikataa waashi!!! Duh hongera sana kamanda.

  Lakini angalia maana utapiga ngumi ukuta rafiki yangu, unayajua matokeo yake. Kama ilivyo kwa mtu kupiga teke mchokoo huku akiwa peku.

  Angalia pia utadhani unamchana Sungura na Lwembe halafu utachanika mwenyewe. Maana nakuona sasa umekuja kimwili zaidi ukiwa umefura.

  Usipate shida rafiki yangu mambo ya Mungu si ya nguvu ya misuli, ni nguvu ya rohoni. Ndio maana nikakwambia kuwa kama wewe una nguvu ya rohoni tupige laana tu, kwa nini upate shida ya kuhangaika kuchana na kusaga tikitiki!

  Umesema nifumbe kinywa, mimi nimekifumbua, sasa unasemaje Seleli?

  Seleli utaropoka maneno yote, ukiweza au ukitaka tukana kabisa,kama SG watafumba macho ili kuipost comment yako, basi tutaisoma ili tukujue zaidi. Sema kabisa kwa herufi kubwa ikiwezekana kwamba Sungura anamtumikia Shetani! mbona umeisema kwa herufi ndogo?

  Maneno kama haya ya kwako huwa ni lazima yatoke pale kifutio kinapokutana na vumbi.

  Wewe si ulidhani kuwa wakristo wote ni wa kuswaga kwa makemeo na makaripio utadhani kuwa wewe ndo uliwaokoa au wote ni watoto wako, ndio maana umeamua kabisa ujiite wewe ndo jiwe kuu la pembeni. Ole wako, maana u jiwe kuu feki!

  Ulitakiwa uishi kizazi cha mafarisayo Seleli, hiki kizazi si size yako, usipoangalia utajikoki mpaka ulipuke.

  Ni upofu mkubwa sana kuhusisha Ibrahim kutoa zaka kwa Melkizedeki na Ibrahim kumtoa Isaka.
  Ivi wewe ni juha usiyeweza kuelewa? Hapa muda wote hatuongelei utoaji wa sadaka, ni wewe tu kichwa ngumu mwenye kudhani una akili nyingi sana ambaye umeshindwa kutofautisha zaka na sadaka katika mjadala.

  Lakini najua unafanya hivyo kwa sababu mbili:
  1. Unataka kujionesha jinsi wewe ulivyomtoaji mpaka kiasi cha kujikana ( Ni mafarisayo tu ndio walikuwa na hiyo tabia ya kupiga panda, nawe naona ni mmoja wao)
  2. Huna mashiko ya kutosha kwenye biblia kui-justfy zaka leo, ndio maana hata ukijaribu umekuwa ukirudiarudia Mt 23;23-24, ambayo nayo unaipa fafanuzi ya kulazimisha. Na baada ya hiyo unaongea tu assumption zako, kama ulivyosema hapa ”Nilidhani nyie Ni Watu wa rohoni kuyatambua na kudaka mambo kiroho kwamba, Maisha ya Utoaji ya Ibrahimu iwe Isack au zaka, Kiroho yanatuambia mambo haya:……..”

  Hahaaa, kumbe wewe hata huwezi kulaani, nilidhani na wewe unaweza toa laana, kumbe unategemea tu niwe nimelaaniwa kwa mujibu wa Malaki!!. Pole!!

  Sasa kwa taarifa yako hiyo laana iliyo kwa Malaki 3, kwangu mimi haipo kama ambavyo haikuwepo kwa Baba Ibrahim.
  Laana hiyo iko kwa mafarisayo origional na wewe ambaye umeamua kuwa farisayo kwa imani. Hiyo ndiyo laana ya torati yenyewe kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui! Huwezi itimizia matakwa yake leo.

  Infact hata huwa hutoi zaka ni kodi tu fulani ndiyo maana lazima upewe na lisiti,wewe na watoa risiti mkidhani kwamba uhai wenu wa kiroho kama mkristo uko katika zaka.

  Na ili ujue vema kwamba wewe una hasira ya kifarisayo, hata na kuzidi kidogo, ona haya maneno yanayotoka kwenye moyo uliojaa hila, kama ilivyokuwa mioyo ya mafarisayo na maswali yao ya hila kwa Yesu, japo walikwama kama ambavyo wewe umekwama. Ona maneno yako haya kwa Lwembe;
  ”Iyo Mathayo.23:23-24 uliyonukuu, inakuhusu au la ? au ilikua ya Mafarisayo tu? (ayaa!!! ha ha ha ha ha meeen…hapa unajua why ukishajibu tu, nimekumaliza kwingi hata kuleeee..unapajua sana- ha ha aha ha I can see it unahemea puani, tell Yusha aje na maji ya kunywa”

  Haya ni maneno kweli toka kwenye moyo na akili ya mkristo mature?

  Seleli au unaendaga tu kanisani kutoa zaka???

 35. Sungura/Lwembe,

  Navunja-vunja kila mfupa na jiwe, nakung’oa takataka kama ifuatavyo, nilisema naam nasema tena, kambi iliyochafuliwa nanyi, sharti mzoe kwa mikono yenu live.

  Sungura
  = mpaka hapo utakapoleta maana yako ya neno Hiari kwakua ulishawahi kuniuliza na nikatoa jibu safi, hukuwahi kusema lolote ivyo kauli yako kua mimi sijui neno hilo, ni uswahili wa yule jamaa yetu-maana hujasema lolote, ni chenga tu na maneno ya by the ways.

  Ati ‘’Huu ni mzaha mkubwa’’ Upi? angalia maelezo yangu juu na ruksa kunitaka uthibitisho wa utoaji wangu wa zaka kwa mantiki ya Ibrahimu na nia safi ya Yakobo-Kama utaki kunitaka uthibitisho, umeshaanza kunigwaya sana-ulizani mie cheap ee kama hao jamaa zako uliowavuruga siku nyingi! sasa hapa mwanzo mwisho, navunja vunja kila hila na kung’oa taka zote kisha napanda vya JUU na ukipandikiza mapandikizi, nayashukia kama mwewe kwa kifaranga, ni shwaaa! No more kifaranga on earth! Fanya mchezo kweli wewe, chezea wengine siyo Watu tunaomanisha kumtumikia Mungu na kutoa bila kujisaza na kweli siku tulipookoka, acha kabisa yaani we are deadly and gravely fallen in love with JESUS, kiasi kwamba hata confused Christians kama wewe, ukituchanganya,tunakuchana.

  Ati ‘’nimeshindwa kuelewa ‘applicability’ ya neno hiari’’=JIBU: The best applicability of it is doing it-GIVE-thas all! Come on stop tennis ball game!

  Ati, ‘’ningekuwa nimeelewa hiari wala tusingekuwa tunaendelea kutofautiana hapa’’ JIBU: Acha kelele za kutafuta huruma, hapa ni kazi, kazi tu, you just give and no more kutofautina AU la kama hutoi, usichafue watoaji, fumba kinywa wewe kiumbe, unamtumikia devo bila kujua AU ukipata uponyaji wa nafsi yako yenye ubinafsi na meteso mengi hapa mjini duniani mpaka ukatoa, usiichukue tena! maana ndicho umekua unafanya humu-mara kutoa ooh sijakataa, mara natoa zaka kwa hiari-kujisikiiiiiiiiiiya, mara sitoi kabisa, mara ni chanzo cha umaskini…u c! unatoa kisha unatwaa,yale yale ya another such very confused selfish Christian anaye tafsiri zaka ya kutoa kwa Mlawi, unajitolea weye kisha unaikula/ramba kwanza wewe ndio Mlawi baadaeeee…indeed beyond repair diseased Christians both you you.
  Kisha umeniita/omba ivi..’’Mtumishi wa Mungu Seleli, kwa kuwa tumekudhihirishia wazi kuwa sisi hatutoi zaka, tumeitoroka, na tumebania tushilingi twetu, fanya jambo moja nalo ni..Naomba utulaani!! JIBU: unaomba laana! Kwani huna? Hii je-Malaki.3:8-10 ya Mungu mwenyewe anasema, haikutoshi? Guess what! Si zaka tu ndio problem hapa, mpaka umeomba laana! Something very serious is not in pairs Sungura!

  Lwembe,

  Hamna jipya ulilosema hapa, yote tumeshayasema sana na kurudia rudia, ulikuwa wapi
  Aya umesema vema summary hii hapo chini:
  KABLA YA SHERIA

  1: Ibrahim: Mwa 14:18-20=Kimsingi hapa Ibrahim alitoa hilo fungu la kumi kwa imani. Baraka zilimtangulia Ibrahim, nalo fungu hilo limetolewa katika ushindi alioupata akizijibu fadhila hizo kwa matoleo hayo.
  2: Yakobo, Mwa 28:20-22=Yakobo atakuwa alikuwa anajua kuhusu fungu la kumi alilolitoa babu yake na tukio zima. Hali tete iliyomkabili, ilimlazimu kumtafuta Mungu kwa bidii, ndipo akaiweka nadhiri hiyo, kwa imani akiamini Mungu atamtendea na yeye kuitimiza nadhiri hiyo katika mapenzi ya kukirimiwa na Mungu mafanikio hayo anayoyategemea.

  WAKATI WA SHERIA:

  Taifa la Israeli, Hes 18:21-24
  Fungu la kumi linaamriwa kwa taifa la Israeli, hilo sasa ni amri kwa watu wa makabila hayo 11. Lakini baada muda kupita, wengine wakaanza kukacha kutoa fungu hilo la kumi, wengine wakileta pungufu kama akina Seleli na kelele nyingi za kumtolea Bwana, kumbe ni wezi tu! Walawi nao wakaanza mishe mishe ili wasife njaa, ndipo kemeo la hali hiyo likaja, Malaki 3:8-10

  NJIA PANDA YA WAKATI:

  Taifa la Israeli liko katika Utungu, Yohana Mbatizaji amekwisha yatayarisha mapito, na Taifa Jipya litayari kuzaliwa, Kanisa. Ndipo akilionya hilo taifa lenye Utungu, kwa kule kuicha kwao haki iwapasayo kulingana na nafasi waliyoikalia katika Programu ya Mungu, Mt 23:23-24“Onyo hili kama lilivyo hapo, linahusiana na Taifa la Israeli, Zaka yao ikiwa katika Sheria na si Nadhiri wala Imani!

  Tokana na summary yako hapo juu, nina maswali haya:
  (a) Wewe uko kundi gani?

  (b) Iyo Mathayo.23:23-24 uliyonukuu, inakuhusu au la ? au ilikua ya Mafarisayo tu? (ayaa!!! ha ha ha ha ha meeen…hapa unajua why ukishajibu tu, nimekumaliza kwingi hata kuleeee..unapajua sana- ha ha aha ha I can see it unahemea puani, tell Yusha aje na maji ya kunywa

  Ati, ‘’Kwa hiyo mtu anapotoa Zaka moja na kudai ameitoa kwa mantiki tatu- Imani, Nadhiri na Sheria, huyo ni muongo asiyejua hata anachokifanya!!! JIBU: soma mantiki yangu ya rohoni ktk ile nimetuma mwanzo, wacha kukurupuka, heri ungeuliza kwanza.

  Press on

 36. Sungura/Lwembe

  Nilidhani nyie Ni Watu wa rohoni kuyatambua na kudaka mambo kiroho kwamba, Maisha ya Utoaji ya Ibrahimu iwe Isack au zaka, Kiroho yanatuambia mambo haya:

  (a) Mtu aliyempenda Mungu kuliko matakwa yake binafsi-Mtoto wa pekee kumtoa sadaka ya kuteketezwa, ilihitaji upendo wa dhati kwa Mungu

  (b) Mtu aliyekua na shukrani kwa Mungu kwa maneno na Matendo-Kutoa zaka

  (c) Mtu aliyetambua kua bila Mungu yote aliyonayo, yasingewezekana ivyo kutojisaza kwa chochote iwe mali na maisha yake

  (d) Mtu ambaye kwa moyo wa furaha na kurithia(Uhiari), akitoa zaka hata kabla ya sharia

  Pia nilidhani, kwa kuona Yakobo anaahidi kutoa zaka, mngeona kitu hiki cha rohoni kua inapokuja kufanikiwa kwetu kokote kutakapokuja kutokea basi Mungu ataheshimiwa/kukumbukwa kwanza kisha mengine.

  Niliposema ninatoa zaka kwa mantiki ya Ibrahimu na Yakobo, nina maana izo juu za kiroho na Ukiwa mtu wa mwenye Moyo/Ukristo huo/Mtazamo huo, basi Kutoa na tena kutoa hata zaidi ya zaka, si jambo la kuleta maneno mengi na utaalamu toka effects za sembe duniani ambayo hata ivyo nayo mpaka mmeipata iyo sembe, bado ni MOLA huyo huyo kakujalieni ambaye leo hii, mwatimka mita nyingi na vishilingilingi vyenu.

  Baada ya kusema hayo, nitapitia posts zenu tena nifanye ile kazi maalumu na tamu ya kuvunja kila mfupa na jiwe!kila pando lisilopandwa na Baba sharti litang’olewa na kila mche Seleli atakauona umepinda, utavunja-vunja na kusagwa tikitiki

  Press on.

 37. Hahahaha….Seleli acha fiks!
  Eti, ““Kama kuendelea kutoa kwa Mungu like never before tena na zaka kwa mtindo/mantiki ya Ibrahimu, nia ya Yakobo na maneno ya Yesu”

  Ukweli wa Zaka huu hapa kama unaweza kukusaidia, ili kutoa kwako kuwe na tija:

  KABLA YA SHERIA:
  1: Ibrahim: Mwa 14:18-20
  “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”

  Kimsingi hapa Ibrahim alitoa hilo fungu la kumi kwa imani. Baraka zilimtangulia Ibrahim, nalo fungu hilo limetolewa katika ushindi alioupata akizijibu fadhila hizo kwa matoleo hayo.

  2: Yakobo, Mwa 28:20-22
  “Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

  Yakobo atakuwa alikuwa anajua kuhusu fungu la kumi alilolitoa babu yake na tukio zima. Hali tete iliyomkabili, ilimlazimu kumtafuta Mungu kwa bidii, ndipo akaiweka nadhiri hiyo, kwa imani akiamini Mungu atamtendea na yeye kuitimiza nadhiri hiyo katika mapenzi ya kukirimiwa na Mungu mafanikio hayo anayoyategemea.

  WAKATI WA SHERIA:
  Taifa la Israeli, Hes 18:21-24
  “Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania. Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa. Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.”

  Fungu la kumi linaamriwa kwa taifa la Israeli, hilo sasa ni amri kwa watu wa makabila hayo 11. Lakini baada muda kupita, wengine wakaanza kukacha kutoa fungu hilo la kumi, wengine wakileta pungufu kama akina Seleli na kelele nyingi za kumtolea Bwana, kumbe ni wezi tu! Walawi nao wakaanza mishe mishe ili wasife njaa, ndipo kemeo la hali hiyo likaja, Malaki 3:8-10
  “…Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

  NJIA PANDA YA WAKATI:
  Taifa la Israeli liko katika Utungu, Yohana Mbatizaji amekwisha yatayarisha mapito, na Taifa Jipya litayari kuzaliwa, Kanisa. Ndipo akilionya hilo taifa lenye Utungu, kwa kule kuicha kwao haki iwapasayo kulingana na nafasi waliyoikalia katika Programu ya Mungu, Mt 23:23-24
  “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.”

  Onyo hili kama lilivyo hapo, linahusiana na Taifa la Israeli, Zaka yao ikiwa katika Sheria na si Nadhiri wala Imani!

  Kwa hiyo mtu anapotoa Zaka moja na kudai ameitoa kwa mitindo mitatu, Imani, Nadhiri na Sheria, huyo ni muongo asiyejua hata anachokifanya!!!

  Gbu my mischievous brother!!

 38. Hahaaaaaa……Seleli!!

  Kwamba unatoa zaka kwa mujibu wa Ibrahim na Yakobo!!
  Huu ni mzaha mkubwa. Hata sihitaji kukutaka uthibitishe hilo maana tangau mwanzo umeshindwa kuelewa ‘applicability’ ya neno hiari. Ungekuwa umeelewa hiyo wala tusingekuwa tunaendelea kutofautiana hapa

  Mtumishi wa Mungu Seleli, kwa kuwa tumekudhihirishia wazi kuwa sisi hatutoi zaka, tumeitoroka, na tumebania tushilingi twetu, fanya jambo moja:

  Naomba utulaani!!

 39. Sungura,

  Hatimaye na wewe kwa kua umefanya utani muda mrefu, zigo la yale uliyofukia in Summary litafuata baada ya ya hii . U may wish kukaa kimya kama Mguluma Amini-maana summary /maswali yake bado hayajafanya lolote-( namngoja Lwembe pia atachomokaje kisha naye apewe lake la mwisho zigo tamu ila full of pin hatari, ngoja kabla ya Summary, nivunje mifupa ya hii by the ways yako kwa last post comments zako kwa yangu

  Kukabana ili ulete/nukuu Neno la Mungu yaani taarifa ya kile maandiko yanasema na kumaanisha, SI kuimba ngonjera wala ujinga kama uliropoka tena bali ni KUTAKA KILA MTU AWAJIBIKE KWA MATENDO NA MANENO YAKE NA TUKISHA JADII WEEE SASA HATIMAYE NI KUJIKITA KTK HOJA, KUJIBU MASWALI NA KUKATA MANENO NA MAHOJIANO KWA NENO LA MUNGU AMBALO NI FINAL SAY-kukataa kuliona hilo, ni prematurity and lack of professionalism/skills in debates both secular and in this case Spiritual, Unajua siku za mwanzoni ulivyokua na maneno ya kujidai kua uko makini, nili-expect special things and capacities toka kwako, hata ulipowaita wenzio hamnazo, kudhani hawana kitu, mimi nilikua nakuchora tu na sema huyu, hajui but ATAJUA VERY SOON AND WILL NEVER MAKE SUCH MISTAKE AGAIN IN HIS LIFE. Huwezi mvamia mtu ghafla bila kua na simile, calculations, step kwa step, ndizo confidence zile pori naziita ingawa wewe izo hunaga saaaana kiviiile kama wenzio beyond repair on some/many issues namely Amin, Lwembe na Siyi

  Umeniropokea ivi…’’umeamua kuyakataa maarifa na kukumbatia ujinga! JIBU: Kama kuendelea kutoa kwa Mungu like never before tena na zaka kwa mtindo/mantiki ya Ibrahimu, nia ya Yakobo na maneno ya Yesu, kwamba ni ujinga kung’anganana na hilo-hakika huo ni ujinga unaolipa hapa chini na JUU kule-Nitaendekea na the opposite yake ni ujinga hatari na kuzimu kabisa kama siyo wa nafsi/ubinafsi.

  Ati Mnenisaidia sasa naandika maneno machache’’ = SI kweli, inategemea mtu amekujaje/ amenivamiaje na anaongea nini ya major lakini umo umo anaibua mengine ya by the way, VYOTE LAZIMI VING’OLEWE au VIGUSWE by nukta kwa nukta caterpillar anointing illa kambi iliyochafuliwa kwa muda isafikshike na wahusika wote wazoe madude yao. Na kama kuna uhitaji, yapo nazalisha mie pia mengi-ni sawa tu maana niko kazini na lazima kieleweke tu kati ya nuru na giza, kubania ela na mali kustarehesha nafsi zenu mbovu badala ya kujiachia na kuachia bila kusaza kwa BWANA kwakua tunaishi na kuupata uhai wetu, kutoka kwakwe na hatuna haja kuleta akili mbaya( ziko nzuri) za sembe hata kumpigia Mungu na mambo yake na Watumishi wake mahesabu na kuwabajitiaaa weee-ukristo mchafu sana huo wenye mateso mengi kwa kanisa,kazi na Walawi wetu wa leo

  Ati nayoandika bado yana wingi wa magalasa, kuliko mengi yenye upungufu wa turufu’’mmmh! Maneno tu hayo..PROVE IT HERE KWA KUJIBU YOTE NILIYKUULIZA, am ready, you to show/prove me a failure and fool-aya nimekupa ruksa siku nyingi—si unionyesha wapi magalasha/utupu? Wapi nimekosea? Si uonyeshe una nini hasa wewe maana yote umeshayasema mpaka ya zaka kua ni chanzo cha umaskini eti ni laana mara eti unatoa pale tu utajisikia, mara utatoa kwa wahitaji kwanza kisha Mlawi na mambo ya umalawini hapo, huna mpango, sasa wewe mzima kweli wewe rohoni?

  Umedauti nilivyosema kua zaka inatumika kupeleka injili na ukaema ivi..’’,utadhani ninazo takwimu za mapato na matumizi ya zaka iliyopeleka injili!Swali: Kwa kutokua na data, ina maanisha mbali na matoleo mengine, ZAKA hazitumiki ka hilo pia? We vipi, unaongea vitu gani sasa?

  Unaona izi stori zako tena..’’Ni hiari yako bwana kung’ang’ana na hayo,lakini usiseme kuwa hatukukuambia.Unajisemea tu lolote alimradi usikike. JIBU: Sasa kwani mmeniambia nini cha maana zaidi ya ubinafsi? Ni kweli naongea si tu nisikike bali pia kusomeka na kisha, walio wabinafsi na choyo mpaka kwa Bwana na mambo yake, waache mara moja. Bahati mbaya na wewe/ninyi mnaongea ili msikike mkiambukiza watu kujali sana yao kwanza na Mungu baadaye, huduma ya kuzimu mia asimilia kabisa

  Hapa umeibia tu’’’Petro anawaambia wenzake kuwa tusiwatwike mataifa kongwa ambalo hata baba zetu liliwashinda-soma iyo story nzima hapo, kwa nini umekimbilia kuchomeka zaka kinamna? We kweli muongo sana yaani bado unakazana kutoroka zaka! Hata iyo statement…’’Baba zetu liliwashinda’’..wewe kama msomaji wa Bible ungeweza pata clue hasa kongwa lililo maanishw a ni lipi hapo ila ulivyo na shida myoni, haraka umechomekea zaka!!!!!!!! We kweli kiboko! Yaani unakwepesha kweli tuhela twako utwooo eee! Halafu twenyewe sijui sh ngapi maana nilishawaambia kuna mabilionaire wa dola wanatoa zaka, malimbuko, changizo na sadaka nyinge like crazy kumbe clever, wewe je na tushilingi twe tu?

  Press on

 40. Seleli;
  Hizi ngonjera waimbie wajinga wenye kusubiri kupewa taarifa ya kile maandiko yanasema na kumaanisha, si wale wenye kuzifuata taarifa hizo wenyewe kwenye maandiko.

  Pamoja na kwamba umeamua kuyakataa maarifa na kukumbatia ujinga, ambao kwa kweli si juu yetu sisi kuung’oa kichwani mwako, lakini angalao tumekusaidia hata kuweza kujitahidi kuandika angalao maneno machache japokuwa bado yana wingi wa magalasa, kuliko mengi yenye upungufu wa turufu.

  Ooh zaka inatumika kupeleka injili,utadhani unazo takwimu za mapato na matumizi ya zaka iliyopeleka injili!

  Ni hiari yako bwana kung’ang’ana na hayo,lakini usiseme kuwa hatukukuambia.

  Unajisemea tu lolote alimradi usikike.

  Petro anawaambia wenzake kuwa tusiwatwike mataifa kongwa ambalo hata baba zetu liliwashinda.

  Lakini naona mmataifa Seleli yeye ameamua kuliokoteza hilo kongwa lililowashinda baba zao akina Petro na kuamua kuliweka begani mwake.

  Hilo endelea kujitwika wewe Seleli, na watoto wako na wale wote wenye kusubiri kupelekewa taarifa za nini maandiko yanasema.

  Amina.

 41. Sungura,

  Yatakutoka yote yaujazayo moyo nakwambia kwa hapa na haujaanza leo! This time naona una kwenda advanced stage namely kuimba taarabu( baadhi ya mijineno ya Pwani inayohitaji kufutwa haraka duniani humu, kusiwepo makao yake tena ktk wanadamu wenye Mungu na wasio na Mungu

  Acha kuzunguka na kuongea mengi, KWA NINI USIJIBU MASWALI/HOJA/ISSUE NILIKUULIZA ZA NYUMA NA HATA KUWASAIDIA WAVURAGAJI WENZIO WA MAMBO YA KANISA NA UTUMISHI? Kumbe una muda ndio maana unanza kuwajibia na wenzio? Si ulisema hutaki kupoteza muda wewe au? Kwa nini muda huo wako ‘’finyu’’-(ujanja tu anyway), usiutumie kufanya ya maana hapa? Maana wajua wazi umeharibu humu BAADHI ya mambo.

  Nia ya Kristo ISINGEKUONGOZA KUVUNJA MOYO UTOAJI, KUONA NA KUKUBALI ZAKA KWA UHIARI LAKINI HAPO HAPO KUVURUGA UMUHIMU WAKE LEO, KUKATAA Mathayo 23:23 Maneno ya Yesu Mwenyewe kuhusu Zaka kisa kua hakutuambia sisi, unaweza kua na nia ya Kristo wewe na hapo hapo ukapinga/drop aliyosema? UNAMDANGANYA NANI KABISA on serious note Sungura? Na unawezaje kua na nia ya Kristo wewe Mkristo wa aina yako mwenye vurugu nyini, siasa na usumbufu kanisani? Unawezaje kua na nia ya Kristo uku ukidharau kwa mantiki za michango yako kazi, utumishi na tunayofanya kusuku kazi ya Bwana na kusupport Watumishi kwa matoleo yetu na Zaka ikiwemo? Mimi na wewe na ni nani at least ana NIA ya Kristo? Na ni at least hasumbuliwi na nafsi na ubinafsi? JIBU LIKO WAZI HAPA KWA MICHANGO YETU.

  Najua unasikia aibu maana nimeweka hadharani ubovu na bahati mbaya kufuta BAADHI ya uliyoandika hamuwezi, sasa imebaki toba tu,ifanyeni hata kikubwa-kubwa nyumbani, si lazima hapa.
  Usilete tena ujanja wa kusema nimewa-stop kusema! Mmh! Mantiki ya statement yangu unaijua sana tu! Nina maana acheni mbwembwe nyingine bali JIBUNI MASWALI/HOJA NA KAMA MNAOGOPA AU HAMTAKI SEMENI then mkipenda tumalize mada kwa hitimisho safi au ala basi tuendelee kufundishana mpaka tuelewane, niko pamoja nanyi kwa huduma hii tuliyoitiwa ingawa kwa mada hii ya Utoaji eg Zaka, mneharibu kweli si tu Mada-maarifa lakini kuvuruga mioyo ya utoaji na shughuli za Kanisa, Watumikoa humo tuliyopewa na Bwana na Injili maana ni gharam injili kuhubiriwa, Nitawarudisha kila sekunde kwa mstari ikiwa mtatoa hoja za kubania vehela na vimali vyenu

  Aya, fanya kazi-soma viporo vya nyuma, acha taarabu na mijineno Sungura, ukikimbia, Summary yako basi iko haja ya kukukabidhi ili utubu vema.

  Press on

 42. Ni juha tu au maamuma ndo anaweza dhani kuwa kinachotoka ndani ya Seleli kinatoka katika nia ya kristo.

  Ulitakiwa uishi enzi za mafarisayo na masadukayo Seleli, siyo kwenye hiki kizazi cha waliokombolewa.

  Unatuambia (Lwembe im particular) kwamba hili masuala ya kukushauri tuache.. – ukasema ”STOP IT”.

  Seleli who do you think you are anyway?
  What are you gonna do us if we won’t stop it?

  After all, tunajaribu kukusaidia tu maana hata hujitambui.

  By the way, hakuna aliyekulazimisha Kuliacha hilo nira, wewe endelea nalo tu pamoja na watoto wako nao uwaambie wasiliache. Halafu kaa ukisubiri ile pongezi toka kwa malaika unayoingojea ya mtoaji shujaa kuliko Kolonelio

  Bahati mbaya sana kwako ni kwamba Kolonelio mwenyewe hakupongezwa kwa sababu ya kutoa zaka, bali sadaka.

  Mind you, hauna mamlaka ya kutu-stop kusema tuonacho ni vema kusema.

  Sasa sijui utatufanyaje maana hatujastop kukwambia.

 43. Lwembe,

  NASEMA KIFUPI KWA SASA, NIMEPITIA POST YAKO, NAKUAMBIA on very serious note kama NIILIVYOMWAMBIA AMINI JEREMIAH MGULUMU….acha utani! wakati wa utani, matusi, ujanja, ukwepaji,ufunikaji, UMEKWISHA…umejibu kiujumla sana NILIYOKUKABA!!!!!!!!!!-unajua kwa hakika kwa nini UYAGUSI…na kwakua umeleta utani wa Yeremiah wa kutochapa kazi hapa, nitakusaidia kukuletea summary ya hayo marefu ili nikupe nafasi ya pili ya kuoyesha/kuthibitisha kama kweli unajua, una Neno wewe na una ufahamu wa kweli wa Mbinguni kunisaidia mie au mimi nifanye ivyo kisha wewe uwe zero. Am serious and honest, hakuna ulichoandika, ni atmosphere tu na umebaki almost kutukana na kufoka bila sababu-najua kwa nini unahemea puani! Nitakusadia kukuletea summary ili ukiacha record inabaki hapa kua ulishindwa tikitiki.

  Na swali jepesi ni ili kwa anayesoma hapa na atakaye kuja soma baadaye mwakani-kumbukumbu si inabaki..swali ni KAMA UMEULIZWA JAMBO-SI UJIBU TU-unagwaya nini? na kama halina haja ya kujibiwa-si usema hoja ya kukataa kujibu-kwa nini wafoka bila kueleza wazi kwa nini haujibu?

  Na challenge ni hii, niambie umeniuliza nini wewe toka tuanze mjadala mimi nikaepa, kimbia, zunguka-zunguka, tukana, hemea juu kwa juu-TOA USHAIDI! Ndio maana NASEMA UNAJUA UNACHOFANYA KWA KUOGOPA KUJIBU MASWALI/HOJA/ISSUE/MAJIBU NILIYO RAISE-kuna vitu hatari kuliko umeviona!kama unabisha-viguse/jibu.

  Haya maswala ya kugeuka kua washauri wangu mara kuniambia nijishushe, ninyenyekee, siju nifanyeje..STOP IT! sihitaji na wala hamjastahili nyie kunishauri ivyo kwa matunguri mliosema humu kupinga na kuvunja moyo wa Utoaji kwa ajili ya maendeleo ya kanisa. Nasema tena, STOP USHAURI WENU PORI, FANYENI KAZI HAPA…mnanifanya niwaone kichekesho kujitia kua Washauri nasaha wakati mna madudu na madude mengi mliyoyasema humu kinyume na Zaka, Utoaji, Kanisa na Watumishi. Narudia, stop utani, JIBU MASWALI/angali MAJIBU YANGU-SEMA WAPI HUJAELEWA AU PINGA NIONE/NIJIFUNZE KAMA KUNA LOLOTE…Summary yako ya Maswali tu au majibu yangu tu basi yaja…itendee haki, mambo ya kunishauri, tupa uko forests, mnaleta ujanja hapa badala ya kuchapa kazi- Angalau na mimi nimechachamaa kidogo kwako na Amini, bado kiumbe mmoja naye summary yake lazima ainywe! Hamuwezi kuchafua kambi kisha mtegemee watu wazoe/wasafishe-U MUST DO THAT JOB BY YOUR OWN HANDS NA MIMI NDIO NIMEWEKWA KAMA MYAMPALA WENU NA KWAKWELI KAZI MNAYO-Kama takataka hazizolewi toka humu kanisani-kambi tena na nyinyi kwa mikono yenu, HAKIKA MNYAMPALA MNAYE IMARA KABISA, KABISA,KABISA..24/7 I am telling you.

  Press on.

 44. Seleli,
  Ninakushukuru kwa hizi 99 books!
  Jambo moja ambalo nina uhakika nalo ni kwamba umeongea ukweli unaoufahamu, na jinsi unavyoweza kulielewa jambo, kwa kadiri ya uwezo wako wa kiakili wa kuyapokea na kuyatafakari, na hapa nina uhakika kuwa umefikia ukomo wako!

  Uliniambia niyarudie niliyoyaandika, nimefanya hivyo, nayo maelezo niliyoyatoa yako sahihi na yamesimama katika urahisi wa kuyaelewa Maandiko kama yalivyokusudiwa yaeleweke! Halafu nikayarudia na uliyoyaandika, mara tatu, nikafika ktk kuelewa kwa uhakika kuwa HUJUI unachokisema! Maelezo yako mengi ni sentiments, na nikisema nikufuate katika huo mkorogo wa dini uliokukamata katika makucha yake, nina uhakika haitamsaidia yeyote yule wala wewe! Wewe unadhani ninatania, lakini Iam dead sincere ni makorokoro, siwezi kutania ktk Neno la Mungu!

  Mungu akikuambia “Usizitegemee akili zako”, halafu wewe ukajifanya unajua, eti ukasema “hajasema usizitumie”, hilo pekee laonesha kuwa hata hizo akili zenyewe huna, unawezaje kutumia kitu halafu usiwe unakitegemea hapo unapokitumia?! Ndio maana nilikuambia ‘kujua kwingi’ kunaweza kukutumbukiza katika uzezeta wa kiroho! Hebu kutazame huko “kutumia akili” kwako, sidhani kama kuna jambo linalodhihirisha udhaifu wa matumizi ya akili katika mambo ya Mungu kuliko maelezo yako! Ingawa unajiona ni mwenye “akili sana”, lakini maelezo yako yanaonesha tofauti, kama ujumbe uliodhahiri kama huo katika Mt 23:23, unaweza ukaunga’ang’aniza kwa Kanisa, basi akili yenyewe hiyo unayoipigia kelele iko wapi! Seleli una akili ya kawaida tu, ambayo ndani yake hakuna ‘Maarifa’, ndio maana unajifananisha na mt. Paulo; eti unadhani anaposema “Akili” ndiyo kama hiyo uliyonayo, kama nawe unayo akili kama hiyo anayoizungumzia Paulo, ungejibebeshaje zigo la Torati huku ukitangaza Neema? Una akili ya kawaida tu ya kukufikisha kanisani na kuyasikiliza mahubiri na kutii amri za kanisa, hilo lililokalia kiti cha Kristo, lakini huna uwezo wa kuyaelewa Maandiko kupitia utaji wa dini uliokufunika, imba mapambio tu!

  Hii inatokana na ukweli kwamba katika wakati fulani uliikataa Kweli ya Maandiko. Ukifikia kulikataa Neno lolote lile ktk Biblia, kwa kisingizio chochote kile, ukaanza kuligawa Neno, oh, huyu alikuwa ni Paulo tu, oh, huyu ni Petro tu, tumfuate nani sasa, Petro mwanafunzi au Yesu Mwalimu, nk, basi jua ya kwamba TAYARI umekamatwa na “a Deaf and Dumb” spirit, kwa kukiri kwako mwenyewe! Maana imeandikwa “Mtu hata ishi kwa mkate pekee, bali kwa KILA neno litokalo ktk kinywa cha Mungu”. Ninaamini hii ndiyo sababu watu wengi wa dini wamefungwa ufahamu wao, yaani wako katika ile hali ambayo mt Paulo amewaachilia nayo kwa Neno, akiwafungia nje kabisa, “mjinga na awe mjinga”, ila wao wanaendelea, wakijiona ni wenye akili sana na wamejazwa RM, bali ni “wajinga”; hao “wenye mfano wa utauwa…”; Unaweza kujikuta ktk hali mbaya kuliko ya yule Simon mchawi, huyu aliitafuta Rehema ya Mungu, lakini sisi tunaendelea tu!

  Najua ninapozungumzia kujazwa Roho Mtakatifu, wewe huamini kwamba ni huko kunena kwa lugha, bali mimi simaanishi hilo, maana kunena ni kipawa cha Roho Mtakatifu na si RM! RM hukuongoza kuliamini Neno la Mungu, tena huliweka wazi kwa kukufungua hizo akili zako unazozitegemea sana ili upate kuyaelewa na Maandiko (Lk 24:45 “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuyaelewa na Maandiko”)! Basi kwa kushindwa kwako kuyaelewa Maandiko YOOOOOOTE uliyoletewa ni ishara kwamba ungali ‘mkavu’, tena ni mkavu saaana! Ndio maana nakuambia kuwa kama hutajinyenyekeza, basi utabakia kuyazunguka Maandiko kama walivyoizunguka nyumba kule Sodoma wasiuone Mlango, ambao kwa leo ni Kristo ule ufunuo; “Juu ya Mwamba huu nitalijenga Kanisa…”; umeelewa Seleli! Mwamba ni Ufunuo wa Kristo ni nani!!! Unaona, hauwezi kuukwepa Ufunuo na ukabaki salama, lazima utakuwa mwathirika!!!

  Mwisho nataka nikuhakikishie kuwa “KRISTO NI MWISHO WA SHERIA” na si hadithi za dini, aidha ni mwisho wa Sheria au wewe si mkristo!

  Hivi, Kristo anaposema hakuja kuitangua Torati, au anaposema Ukuhani umebadilika huwa unaelewa nini? Au unapoambiwa kuwa Kristo ni Mwisho wa Sheria huwa unaelewa nini? Kwa mjadala huu nimeelewa kuwa hauelewi chochote kama walimu wako ambavyo hawakuelewa, maana kama ungekuwa unaelewa basi sifa ingewarudia walimu wako pia!!!

  Lkini Torati au Sheria, kwa mkristo ilikoma katika ujio wa Kristo, bali haikukoma kwa makundi ya Wafarisayo na Waandishi na Wasadukayo, maana hao hawakuipokea ile Injili, kwahiyo wanaendelea nayo kama ilivyotolewa na Musa. Hata Maandiko yanayomuonesha Kuhani Mkuu akijivua Ukuhani yalipaswa kukushuhudia hilo, ni kwavile tu ufahamu wako umefungwa, ndio maana umekuja na vitu vya ajabu kulihusu tukio hilo, ukithibitisha kunyang’anywa hata akili ya kawaida tu hiyo ambayo huwa unapigia kelele nyingi za “kuconnect” na sasa ukishindwa kabisa kuitambua Sheria inayomsimika na kumuongoza Kuhani, na jinsi INAVYOVUNJWA, halafu ukiambiwa kuwa akili zenyewe huna, unalalama na kung’ang’aniza kuja na makorokoro!

  Pia Kanisa maana yake ni hao walioitwa watoke katika taratibu hizo za Sheria na mizimu, nao wakiwa wamekwisha kutolewa huko, ndipo wanaketishwa huko Heavenly places in Christ Jesus, na kupewa jinsi mpya, hiyo SHERIA YA KIFALME,
  ambayo inaongozwa na Roho Mtakatifu ! Basi huyo Mkufunzi atakurudishaje nyuma uyatimize hayo aliyokutoa kwayo? Task your understanding!!! Wewe unadhani wale Wakristo waliwezaje kutoa mali zao ZOOTE, jambo lililomshinda yule Kijana Tajiri, ambalo hata wewe na kujisifu kwako huliwezi, kwanza ukibanwa na kanisa lenyewe utalikimbia, unadhani Wakristo wale waliwezaje? Kwa SHERIA YA KIFALME!!!!!!
  What is the “Dynamics” that is driving that mechanical giving that you are doing? Don’t let it be the Law? If your church is leading you into that abyss, then its fine, you can perish with it!
  Acha UJEURI, jinyenyekeze!!!

 45. Yeremiah Amin Mguluma,

  Summary ya yale Mambo/ Maswali tu sasa! Ndio tunamaliza-maliza ivyo Mjadala huu.

  MAMBO 17 YENYE MASWALI YENYE VIPENGERE KADHAA-mengine umeyazalisha wewe ktk kujadili hii mada, mengine nimeyaibua mimi ktk kusoma uliyoandika. Ni sharti uyajibu na kama hujibu, useme ni kwanini labda huwezi, huna uwezo, hujui jibu, hujaelewa ili ufafanuliwe au umekamatika vilivyo na huna hoja tena au pengine unajua moto wake ivyo unakimbia mita mia kutoyajibu maana unajua utaingia matatizoni kama vile kujijua ulikua huna la maana ktk mjadala huu, ulikwenda kinyume na mapenzi ya Mungu, umepotosha/danganya wengi, huna uwezo na hivyo itakua wazi kua unakataa tu kukubali na kubariki nguvu ya mwenzio ktk mjadala huu kua kwakweli imekusaga tikitiki na huna jinsi ya kusimamisha mafundisho yako kinyume na Utoaji(Zaka) Mambo yenyewe ni haya(Chagua kati ya Mauti na Uzima-Kujibu au Kutojibu vyote vitanipa conclusion moja nzito sana(I can’t wait to plate it here live and lively!)

  JAMBO LA KWANZA: Wewe unasemaje kuhusu hizI sababu zangu kwa nini leo tutoe Zaka? Nazo ni Ibrahimu anatoa KABLA ya Sheria-Mwa.14:18-20, Yakobo alihaidi kutoa zaka KABLA ya sheria-Mwanzo.28:10-22(notice: alihaidi-hapa cha muhimu ni moyo unaomrithia Bwana na kutaka kutoa zaka,Pia Mathayo.23:23-Yesu anasema….’Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache na tena Mathayo.23:1-3- Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake( Notice hapa anawaambia Wanafunzi na Watu wengine) akasema, ‘’Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi’-ZAKA bila shaka ilikua mojawapo la Mafundisho na ivyo hata kunukuu leo hili andiko ni sahihi kabisa-Malaki.3:8-10-‘’Leteni Zaka kamili/zote ghalani mwangu ili kuwemo chakula Nyumbani mwangu’’

  JAMBO LA PILI: Je huyu ‘’Farisayo’’ wetu wa leo akilifundisha swala la zaka kwa maana ya ile Yesu alisema kua wao wanakaa kwa kiti cha Musa ivyo wakifundisha, tutende hence kama mafundisho yao wakitumia maandiko ya AK kuhusu zaka BILA KUATHILI KWELI NYINGINE za Bible hasa za AJ , Je si sharti tushike na kutenda kwa kua ‘Musa Mkubwa’ amewasemelea/commentia ivyo kwetu sisi wanafunzi leo kua wayafundishayo tuyatende?

  JAMBO LA TATU: Ingawa Paul alifanya kazi kwa mikono yake mwenyewe- Mdo.18:1-3, kwa maana iyo leo Watumishi wakachape kazi zao wenyewe ili kupata sembe lakini kuna kweli nyingine hii ktk 1Wakorinto.9:1-15! Paul anayesema anajizuilia tu kama yeye iyo HAKI(notice hapa kua ni Haki YAKE) ya kuchuma vya mwilini kwakua aliwapandia vya rohoni na kua..BWANA ALIAMURU WAHUBIRIO INJILI WAISHI KWA INJILI NA WAHUDUMUO MADHABAHUNI, WALE VYA MADHABAHUNI. Pia Yeye mwenyewe Master alisema, ‘’Mtenda kazi anastaili ujira wake, alipowatuma wanafunzi ktk Luka.10:1-7, Sasa je kuna nongwa gani/kwa nini mnaleta maneno mabovu kuhusu Watumishi leo tukiwawezesha kwa Zaka na matoleo mengine nakwa mali zetu kama walivyomfanyia YESU-Luka.8:1-3 ili wakabaki na jambo moja tu ambalo kanisa la kwanza-Viongozi waliliona haraka mara moja na kujishitukia kisha kujirudi mapema, walipokua wanachukuliwa na ubize wa mambo mengine kwa kadri Kanisa lilivyokua linaongezeka-Mdo.6:2-3 ?

  JAMBO LA NNE: Tokana na andiko ili ulilonipa- Torati:14:21-29-Ninazingatia hasa mistari (23,27,29)= ‘’Usiache Kutoa Zaka’’ kisha mstari 23- ‘’Kula mbele za Bwana’’ halafu mwishoni mstari huo anasema ‘’ili ujifunze Kumcha Bwana daima’’ halafu anaendelea mstari 27 ‘’kutomwacha Mlawi’’ kisha mstari 29 anataja na wengine ‘’yatima, mjane nk kwa Zaka’’ na kisha bado mstari 29 anarudia tena ‘’Mlawi asiachwe’’( notice: mistari 27 na 29 inatumia/inasisistiza kwa maneno yale yale almost kuhusu ‘’’kumjali Mlawi’’ ivyo basi Kwangu mimi Zaka kutolewa ina connection na ‘’Kujifunza kumcha Mungu daima’’ kama alivyosema-that was the theme/msg! kwamba nani akula kwanza kati ya yeye aitoae au Mlawi na wengine kati yao-sioni kama ni hoja kwa andiko hilo na kuwekea uzito kuhusu ‘’kuila zaka yako mwenyewe na kuacha MISISITIZO KAMA IYO YA 27 na 29 KWA Mtu mmoja-Mlawi kusemelewa ivyo na hata kutoona kabisa neno kuu ili hapa-ILI UPATE KUJIFUNZA KUMCHA BWANA DAIMA, ni ukosefu wa ufahamu wa kudaka/ng’amua mambo ya msingi/uzito ktk Neno/andiko.! kwangu.Pia ukweli huo kwamba ktk sura moja Bwana ameongela Mtu mmoja-Mlawi kwa uzito huo, basi ukweli huu ukihamia kwetu leo maana AK ni Kivuli cha uhalisia Leo, Ivyo Kuwajali/Support kwa ZAKA na matoleo mengine kwa maisha na huduma zao kwetu na kwa Mungu hawa Watumishi wa leo waliotengwa/tolewa kwa ajili ya Utumishi PERMANET hapo hekaluni/jengoni Kanisani kama ilivyokua kwa Mlawi, ni sawa kabisa, Wewe wasemaje? Na Wapi nilikwepa ukweli wa andiko hili kama ulivyodai? na wapi sikulielewa andiko hili?

  JAMBO LA TANO: Nilitoa mfano kua yaliyosemwa pale ktk Andiko ilo Torati.14 ni sawa na Mtu kusema ivi ’’Usiache kwenda kanisani siku zote za maisha yako juma 3,4,5-j2 (alama ya koma), utakaa nyumbani ufurahi na kupumzika ili familia yako ipate uwepo wako pia, ili upate kujifunza kumcha Mungu daima’’- Sasa nikasema, Kutafsri hiyo statement kua amemaanisha ‘’nikae nyumbani na familia na nisiende kanisani, ndio kosa la uelewa ulofanya!!!!! Umechukua part hii ‘’Kula mbele za Bwana’’, ukaacha ‘’Usiache kuatoa Zaka’’ na ‘’Upate kujifunza kumcha Bwana daima’’ na kutomsahau Mlawi aliyesemwa 27 na 29 sura moja hiyo hiyo kuonyesha msisitizo!, Je nakusingizia kua umekosa ufahamu sahihi kwa ilo? Jitetee au nithibitishe mimi kua ndio nimekosa ulewa sawa kwa hili?

  JAMBO LA SITA: Pia nikashauri ni vema kua na Elimu ya Biblia lakini pia vyanzo vingine hence nikasema tafuta Bible commentaries, angalia ZINAHITIMISHA nini hasa Main issues hapo kwa andiko hilo. Je uliangalia commentaries na ukakuta hoja kuu hapo ni ‘’’kutoa zaka na kisha kuitafuna mwenyewe kwanza kama ulivyong’ang’ania iyo kweli moja tu? kwa nini hata kwa kusoma tu bila Bible commentaries, hukuona/umejizuia kuona msisitizo kwa Mtu mmoja(Mlawi) kuongelewa kwa uzito ktk sura iyo iyo?

  JAMBO LA SABA: Ulisema hakuna andiko hata moja linalosema kua ZAKA ni SADAKA/TOLEO linalopaswa kukabidhiwa kwa kuhani. Je huoni kua unashangaza na kudanganya ukizingatia andiko ilo ulilonipa mwenyewe na hili Hesabu.18:1-32(Zingatia mistari 2-4,8-15,18-20,21,23-31) nikakuongezea na hili Nehemia.10:37-38 ?

  JAMBO LA NANE: Je toka uanze mjadala mpaka sasa, unadhani umeshaonyesha kinaga-ubaga wapi ktk Agano Jipya wapi ZAKA ilifutwa?, sema hapa waziwazi na kwa hoja nzito ili kuthibiisha PASI NA KUACHA SHAKA kua kweli kuendelea kutoa Zaka leo ni tango mwitu kama ulivyodai ili tuache mara moja?

  JAMBO LA TISA: Ulisema unafuatila maendeleo ya ukuaji wa Kiroho cha Watu humu, kama una jukumu ilo sasa ilikuaje Ulitamka wazi humu bila aibu kua-’WEWE HUTOI ZAKA NA HUAMINI KTK TOLEO ILO KABISA’’? Ulivyojiinua kua una ujumbe kama wa Yeremiah wa kujenga kanisa la Kristo kisha unasema wazi wazi ivyo hutotoa Zaka( hata basi kwa msingi wa Ibrahimu-Hiari) na bila haya, unasema na kumtaja-taja sana Roho Mtakatifu!!!!!!!!! ivi kweli Kaka unatoa wapi confidence hii? Je nikisema hii ni ile 200% confidence pori ya Lwembe, ninawaonea?

  JAMBO LA KUMI: Nilikuuliza majibu niliyokupa ya Maswali yako 9 kuhusu zaka post yako ya kwanza ni sawa au la? Kama sawa kubali na kama si sawa, pinga/sema hapa wazi wazi na ushahidi/hoja nzito

  JAMBO LA KUMI NA MOJA: Ivi kweli on serious note, Lwembe amefundisha nini icho KINACHOFUNUA SIRI za Mungu? plz show it hapa waziwazi ili kuhalalisha baraka yako uliyompa la sivyo nitachukulia maneno yako ni ‘by the way tu i.e yale yakipendwa basi?

  JAMBO LA KUMI NA MBILI: Uliuliza kama nilisoma kuona Kwanini Ibrahim alimpa Mfalme na kuhani Melkizedeki na kama ni sahihi kutoa zaka mali isiyo yako?, nilijibu kua Niliona alitoa kwa sababu ya furaha na moyo wake wa kupenda kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyo kua upande wake wakati anamuokoa nduguye Lot na kwamba si sawa kutoa Zaka kwa vile vizivyo vyako, utakua mwizi kwanza in the first place! Wewe wasemaje? Au kwa swali lako ilo, una suggest Ibrahimu alitoa visivyo vyake? Sema kama ni ivyo nicheke kwanza kisha nikupe jibu!!!!!!!

  JAMBO LA KUMI NA TATU:Ulisema Yesu wakati wa huduma yake aliishi akifuata imani na mapokeo ya kiyahudi, na kua wanafunzi wake waliishi kama waumini wa dini ya kiyahudi na kufuata mapokeo ya kiyahudi. Sasa, Kwakua Wanafunzi wake walishi kwa kufuta mapokeo ya Wayahudi, je ndani ya mapokeo hayo ya kidini na desturi, Zaka ilikuwemo ama la? Na kama lilikua fundisho, je Wanafunzi walioishi kwa kufuata mapokeo hayo, walitoa Zaka au hawakutoa?

  JAMBO LA KUMI NA NNE: Ulitumia andiko la Matendo 2:44-45; 4:34-35 kusema kua hakukuweko na Utoaji wa 10% bali wa 100% na kwamba huko ndiko kuitimliza torati kulikofanywa na Yesu. Je, Nisaidie kujua, umefiakiaje conclusion iyo ya 100%? na How do you know ili kuifikia iyo 100% ya utoaji, hakuna walioleta 10% ilihali umesema mwenyewe waliishi wakifuata taratibu za mapokeo na kiyahudi?-Seriously tell me about it na kisha Umefikiaje conclusion kua Utoaji huo 100% ndio Kutimiliza Torati? Seriously tell me about it again

  JAMBO LA KUMI NA TANO Ulisema, maandiko yanatufundisha kuwa KUHANI WA KIKRISTO NI MKRISTO ALIYEKOMBOLEWA NA YESU na ya kuwa Uchungaji,Ualimu,Utume,Uinjilisti ama Unabii ni WIZARA/HUDUMA ZA KIKUHANI SI UKUHANI: Je si kweli Wizarani umo wamewekwa wengine kutenda na kutumika umo moja PERMANENTLY= kulihudumia Neno day and – Mdo.6:2,4? Sasa wanaishije/kulaje/lalaje/hudumuje bila/kama hawaishi? Na wataishije bila kua na kipato? Unawezaje kukana uspesheli wa Walawi/Wa Yuda wetu wa leo kupewa Zaka na kuwatunza ili watumike vema umo nyumbani mwa Bwana/Wizarani?

  JAMBO LA KUMI NA SITA Ulisema UTOAJI WA ZAKA KANISANI UMEANZA MWAKA 777 BAADA YA KRISTO TENA KWA AGIZO LA GAVANA CHALAGNE. Je, Tunaongozwa na Ukweli toka ktk Bible mfano Ibrahimu alivyofanya au Yesu alivyosema au Historia ya bwana mkubwa Gavana? Ukweli upi wa Utoaji Zaka ulianza? wa Gavana au toka zama za Ibrahimu? Kama ukweli ni kua toka Ibrahimu kulikua na Zaka, kuna haja gani ya kunukuu Gavana na maamuzi yake? Authority iko wapi, ktk Neno au bwana Gavana?-Religious/Churchish Historical books/facts?

  JAMBO LA KUMI NA SABA: Ulisema, haupingani na kumtolea Mungu na ati unatumia kanuni ya Yesu kumtolea Mungu isemeyo ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE: Je Unawezaje kutumia kanuni hii.. ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE nk wakati ulisema huna mpango wa kutoa (iwe kwa Hiari kama Ibrahimu au sheria basi)? Nini maana ya kumpenda MUNGU kwa moyo, roho,nguvu,akili? Je mali zako na kila ulichonacho kinahusika ktk maana ya kumpenda Mungu kwa kila kitu? na kama ni ivyo huoni kua na tabia ya kukumbuka kutenga 1 kwa ajili ya Mungu ni jambo jema la uchaji na kicho wala si laana na torati? yaani kati ya kumi, toa 1 tu kisha zile 9 zote kula utakavyo!

  Naongoja Majibu..

  Press on.

 46. Sungura,

  Unidanganye kua tulikua hatushindani! Tuwe wa kweli tu na ndio mambo kama haya siyapendi- yaku-pretend! Ivyo tulikua Tunashindana kwa Hoja kwa maana njema. Sitajitangaza MSHINDI, inatakupasa wewe uliyeshindwa ukubali kwanza kisha bila ajizi wala kumung’unya maneno, upesi sana nitamaliza mwenyewe au la basi tuendelee/tumalizie.Tuko ktk Mjadala na Mahojiano-KUSHINDANA KWA HOJA. Paul aliingia kila mara ktk masinagogi, imeandikwa, alikwenda KUHOJIANA NAO-yaani alitoka nyumbani kabisa na agenda moja-KWENDA DEBATE- Mdo.17:1-4, 16-17, Mdo.18:1-4(reasoning with them tena reasoning hardly with/against those ‘’much know wa dini! The same alifanya Appolo hapa-Mdo.18:28 and likely Bwana Mwenyewe hapa Luka.2:46-47 tena akiwa kijana mdogo tu kabla hajanza kuwakaba koo alipokua mkubwa akipita uko na kule na Neno/hoja moto na kila walipumuuliza/kumtega/ku-reason naye/ au wakaja na mijadala/ubishi wa nafsi na matakwa yao, walimtambua kweli kweli, walikubali wenyewe na kunyoosha mikono na kupinda miguu kukimbia(Notice hapa-kumbe Kukimbia hoja/maswali/issues/kuogopa kukamatika, hakujaanza leo, be so informed! so sishangai sana mki-copy/cut na ku-paste kukacha leo ktk mada hii. Kwa iyo ni kweli nimejaza hoja nyingi kichwani na moyoni za Kweli KiBiblia kuhusu kumpenda Baba kwa kila kitu bila kujisaza wala kuleta sokomoko za nafsi tesi na tata zisipotandikwa kibao, zitulie ili tutoe na tena tutoe na hata zaidi ya 10% mpaka Isaka atoke tu, hayo nimeyazaja haswaaaa!

  Ni pande 2 zenye Hoja zinashindana na kila upande ukiamini kua hoja yake ni sahihi na ukikazana kuuambia/kuuelimisha/kuuchallenge/kuukosoa upande wa pili:

  UPANDE WANGU MSIMAMO WAKE NI: Ni Kutoa Zaka ni namna bora ya kujifunza kicho ktk maisha yetu kwa kuyajali KWANZA au PIA YA BWANA KWA UPENDO, SHURKRANI NA FURAHA KABISA KAMA IBRAHIMU Mwanzo.14:1-20 NA KAMA ALIVYOSEMA YESU Mathayo.23:23 KUA TUYAFAYE YA FADHIRA BILA KUYAACHA NAYALE MENGINE(ZAKA), IVYO KWA HIARI YENYE MAAMUZI YA DHATI NA KUKUSUDIA(SIYO HIARI ILE MBOVU YA KUKUMBATIA UBINAFSI/NAFSI NA MATAKWA YAKE YANAYOATHIRI MATAKWA YA MUNGU- ILE HIARI YA NIFANYE SAWA, NISIFANYE YOTE SAFI TU) BALI NI HIARI YENYE KURITHIA NA KUFURAHIA NA KUTIA BIDII KUA KILA NIPATAPO 10, MOJA TU NATOA KWA MUNGU NA MAMBO YAKE HALAFU MIE NAKULA ZOTE 9. Upande huu WANGU ni mtamu sana, una kibali mbinguni na unatoa picha ya wale Wakristo walio wa baraka makanisani na mbele ya Watumishi wa Mungu wanaowalea kiroho, Wakristo wasiojisaza inapokuja swala la Mungu, wameiweza nafsi na mwili, wameipoteza nafsi ili waipate ikiwa imeshiba na yenye taji kubwa JUU.

  UPADE WENU SUNGURA, AMIN MGULUMA, KASWAHILI, LWEMBE NA WENGINE WALIOJIFICHA KWA PAZIA LA MALALAMIKO DHIDI YA MAMBO YA KAWAIDA KTK MIJADALA NA WANAOTAKA KUJIANDIKISHA KWENU, MSIMAMO WAKE NI: Kulingana na michango yenu yote humu ni ule wa KUGOMA KABISA KUTOA ZAKA au kutoa kwa masharti ya mpaka mjisikiiiiieee, mjigusisheeee, mgusishweeeeee, muhiari kwanzaaa kutoa au kuacha au muamue kutoa lakini kwa vurugu na bila utaratibu mfano kuanza kugawa/kutoa kwa maskini na Wajane au kali kuliko zote ni ile ya Amin Mguluma ya -kuanza kuiramba/tafuna Zaka mwenyewe kwanza! Kisha Kanisani pale unapolishwa, kwa huyo anayekuelea hapo ambaye atatoa hesabu kwa Mungu jinsi alivyowajibika juu ya maisha yako na Utumishi aliyotengwa kwa huo, hapo hamna habari nako, uyo awaleaye hamna habari naye wala kumfeel/kumheshimu na kutambua kazi yake. Upande wenu huu ni mchungu sana, hauna kibali mbinguni labda kwenye akili zenu na unatoa picha ya Wakristo walio teso kwa afya ya Kanisa na Watumishi wa humo nyuwani mwake, nila Watu ngaa wanasema wanampenda Mungu lakini ni maneno tu ukigusa mali zao ndipo wao halisi unawajua, wanatetea na kupigania nafsi na matakwa yake kwa visingizio vingi vya kisiasa kama vile Zaka ni laana, zaka ni wakati wa torati, zaka ilifutwa-wakati wakishindwa kabisa tikitiki kuonyesha wapi ilifutwa ktk Agano Jipya, mara zaka ni chanzo cha umaskini kanisani na maneno kama hayo ya ovyo toka kwa Watu wanajidai wanamjua Mungu sana, wanalijua Neno, ati wana ujumbe wa kama Nabii Yeremiah wa kuboa kisha kujenga kumbe wanabomo dabo-dabo!

  Iyo ya mwisho ulosema kua ‘’Utoto kufanywa na mtu mzima ni mzaha! ni kweli maana ndio iliyowapelekea kuuambia ovyo upande wangu uku upande wenu ukashangilia sana maneno au matusi kama vile siye tunahitaji ambulance, tuna effects za malaria, dege-dege,tuko teenager, hatuko makini, tumepungukiwa na uwezo wa kufiri nk lakini uzuri upande wangu ulioambiwa/ropokewa ivyo, uko na utu uzima sana ktk Mijadala na Mahojiano ivyo ukawa na balance/kifua cha ku-accomodate all, kuchukuliana na kuwapenda upande wa Ufanyao Utoto ktk kazi nzito hii.

  Sasa umenipiga stop nisikupe MKATE WAKO WA MTAMA! mwe! Umetoroka tena kama unavyotoroka Zaka? Mbona unakimbia na maneno ya counselling za ulongo kama Amini Jeremiah my Kaka wakati kazi hafanyi! nifanyeje sasa na zigo la viporo vyako liko tayari na limeniiva bara bara ili nikupakulie ulile haswaaa? Nafanyaje sasa maana mzigo wako Kaka ninao hapa? kwakua nilikua wa kwanza kudokeza mwanzoniii kisha ukaja kukazia kua tufike mwisho na ndio maana nimefanya summary kwa kila mmoja wenu ili janja za kuacha jiwe juu ya jiwe bila kubomolewa, zifike mwisho. Ngoja nitaona cha kufanya-HUTANIKIMBIA KAKA, utafanikiwa kukimbia Zaka kanisani kwako ila mimi kuniepa, si rahisi ni heri tulimalize tu hili jambo pamoja maana tumetoka nalo mbali.

  Press on.

 47. Seleli, kama unasubili kutangazwa mshindi hapa, basi unachelewa bure, jitangaze mwenyewe kuwa ni mshindi maana ulikuwa unashindana wewe mwenyewe peke yako. Sikuwa nafanya shindano la kidini hapa mimi.

  Hata usipoteze muda wako kuniandikia waraka, sintajisumbua kuusoma. Ukimpa mtu nafasi ya kujieleza ndipo utajua kuwa kichwa chake kimejazwa nini. Nilishajua kilichojaa kichwani mwako, hata sihitaji kupoteza muda zaidi.

  Nilishakwambia zaka toa, ikiwezekana si kutoka mshahara wako tu, bali hata mtu akikupa zawadi ya pipi nenda kaitolee zaka pia, mjoli mwaminifu wewe!

  Utoto kufanywa na mtu mzima ni mzaha!

  Asante!

 48. Kaka Yangu Yeremiah Mguluma Amin,

  Tunataka kumaliza Mjadala huu upesi si ndio? Mimi kuwaletea Wewe, Lwembe na nadhani machache ya Sungura-yanakuja-Mlioayacha wenyewe toka tumeanza(mengi ni serious questions ambayo yaliyonahitaj majibu, mengine ni statements kubwa-kubwa lakini zinapingana na points mnazosema tena baadae ktk post iyo iyo au nyingine kadri tulivyoendelea, HAYA HAYAWEZI KUACHWA BILA MAJIBU-na ili tuhitimishe vema, FANYA SEHEMU YAKO.PLZ NIKUOMBE ANGALAU NA WEWE UWE SERIOUS DAKIKA IZI ZA MWISHO BASI, KUA COMMITTED HAPA, acha ujanja-janja.

  Mfano: Umetamka humu kua Unamtolea Mungu kwa kanuni ya kumpenda Mungu kwa akili yako yote, nguvu, roho,moyo nk lakini pia ukasema wewe hutowagi zaka kamwe! Nikakuuliza swali hapo, unawezaje kuongea confidently kua huna mpango wa kutoa Zaka, yaani wee ukipata 10-Vyote unakula na hata ile 1 tu Mungu anataka pia nayo unameza kisha useme unampenda Mungu kwa kila kitu? Maswali na issues kama izo ziko nyingi halafu unataka kukimbia tumalize mada bila wewe kuwajibika? PLZ ACHA UTANI!

  Nimekuuliza mambo 21 humu kama summary yangu kwako tunapomaliza mjadala, jibu hayo wala hakuna kukimbia, wajibika. Na pia usinidangaye wala usidanganye Watu hapa kua nimetumia maandiko vibaya! Kwa nini unaleta utani ktk kazi nzito! Nionyeshe wapi nimekosea nitajua kweli kuliko kusema general statements za uwongo na uvivu. Narudia tena, Tumalize mjadala kama watu wenye Roho na Akili pia. Fanya kazi yak, Unaposua sua na kurukia vingine ndio unaprolong mambo. Wewe umeulizwa mambo yako au yangu, si ujibu tu, unaogopa au unakimbia nini? si una Neno wewe, si umesema huduma yako ni kubomo na kujenga, si unasema unajua Neno wewe, sasa kwa nini usikitendee haki kipawa/karama/huduma uliyonayo? Narudia plz acha utani, fanya kazi hapa. Mimi nimemaliza kwa upande wangu, bado wewe na ndio unatufanya tusimalize maana unakwepa na unachokikwepa toka tuanze na sasa summary hiyo ya MAMBO HAYO 21 yenye vijipengere NILIYOYAPIKA VEMA KABISA, UNAKIJUA SANA unakimbia!!!!!, sasa si bora useme tu hali tete then tuchukuliane na kila mtu amalize conclusion yake hapa! Seme tu ukweli kiungwana, nitaelewa!

  NB: Ukiendelea kugoma kujibu mzigo wako ulioukwepa toka tumeanza na yale uliyoyazalisha mwenyewe na niliyozalisha mie pia, NITAKUPA ALTERNATIVES NA CONCLUSION YANGU KUKIMBIA KWAKO PIA

  Press on Kaka, plz stop teasing, fanya kazi tunamalize vema.

 49. Seleli mpendwa wangu.
  Salaam
  Nawiwa kukuambia mambo machache sana kuhusu suala zima la imani na michango yako kama mkristo mwenye bidii katika kumjua Mungu lakini unayepungukiwa na maarifa ya kiMungu katika kulifahamu neno la Mungu na mafundisho ya madhehebu.
  Kwa kuzitazama post zako mwenyewe unaona jinsi ambavyo unatumia nguvu nyingi sana za akili zako kujaribu kupeleka ujumbe unaodhani kuwa ni wa Mungu ilhali ni mawazo ya kidhehebu na ubishi ulio nao ambao haukusaidii bali unakufanya udumae kiimani. Hebu zipitie hoja zako na kisha pitia michango ya wapendwa wengine uone jinsi ulivyotumia MAELFU YA MANENO kuelezea vitu ambavyo havina support ya neno la Mungu.Mahali pengine umetumia maandiko ukadhihirisha jinsi ulivyo na kongwa la mafundisho ya udhehebu.
  Tafakari kwa makini jambo hili acha ubishi usio na maana hautakusaidia wala hutaweza kuwasaidia wengine kumjua Mungu unayemuabudu.
  Ubarikiwe kwa kukubali ushauri wangu huu.

 50. Sungura,

  We are not done yet, your package is on the way!wewe naye umefukia mengi yangu kama Lwembe na Yeremia Mguluma, niliwaambia kila mara utafika wakati nitamtaka kila mhusika ajibu kama mimi kila mmoja mlivyonitaka na ku-raise issues nika-deal nayo kwa roho nyeupe. Mwisho wa Utoro wa Zaka mpaka kukwepa maswali/hoja/issues zangu UMEFIKA! Waraka ni mrefu kwa Lwembe kwa kua nakusanya yote aliyokwepa na reply zake alizonihusisha kama 3-so mwachie atasoma mwenyewe kama ni siku 2 atajua mwenyewe maana ni wake hasa na yeye alishakuambia acha kulila-lia kama bebi na alikufanyia counselling kwa kukuambia Kitabu cha Isaya kina vitabu 66! Umesahau ilo mara? Na Pia ya Yeremiah ni ndefu kwa kua naye ni mfunikaji wa mambo na pia ktk reply zake 2 kanitaka/taka kwa issues kadhaa, so wote hawa wana haki ya kupata responses zangu, nina haki ya kutaka responses zao ktk ya nyuma waliyoyaacha kijanja. Ninapokuandalia na wewe waraka wako kwa yale yote uliyofunikia maana HAKIKA MWISHO WA UJANJA umefika, utakaposoma na kujibu yote NDIPO nitajua kama uwezo wa kufikiri kwangu kweli umepotea au hii ni janja nyingine ya kulia-lia. We will be done mkifanya kwa UAMINIFU part yanu-ACHA WARAKA ZA WATU( Lwembe na Yeremiah) –ndio maana hua nina/nime-address MTU HUSIKA-kama ni ya wa Jumla, am smart, will use ‘’Wapendwa’’ or ‘’Ndugu Wote’’ au ‘Hellow Everybody’’. Hence, Kama ni ya Mtu, ukiingia uko, basi vumilia/furahia yote.

  Press on waiting your bread Kaka, hapa akimbii Mtu, ushaanza kutoroka kama tricks zako za kukacha Zaka-Jan-Dec, ati you think we are done! Who told you wajaki hutatenda haki kwingi-nilichukuliana nawe tu!

 51. Amin Mguluma Yeremiah,

  KAKA YANGU MKUBWA, UNAYO KAZI KUBWA SANA YA KUFANYA HUMU AMBAYO HUJAIFANYA.MWISHO WA KUFUNIKA MAMBO UMEFIKA-najishuhudia mwenyewe kua SIJAFUNIKA JAMBO LOLOTE MLILONITAKA NIJIBU/TOA MAELEZO AU FAFANUA, NIMEKUA MWAMINIFU KWA KILA STEP, SASA NI WAKATI WAKO KISHA NAKWENDA KWA MKWEPAJI/MFUNIKAJI MWINGINE-ANANIJUA SANA TU. Zingatia kila nukta hapa chini na UJIBU KILA CHEMBE ILI tuwe fair play.SIKIZA—hata kama hujibu au hutaki kujibu, Pia sema why kama nilivyofanya mie kwa baadhi ya issues chache sana-Kusema kwako why kunakufanya kua fair na pia kumuonyesha mwenzio ilo linalokufanya usijibu au kukaata kujibu lina mashiko kweli au janja-janja tu. Karibu sasa hapa chini ufanye kazi/huduma yako kwa uaminifu wote iyo uliyosema ya kubomoa mabaya na kisha kujenga Kanisa kwa mazuri.Najua Watu tunatofautiana, si rahisi nikufanye uwe mimi, hatuwezi katu tukawa sawa 100% lakini at least kwa yale basics tujitahidi kua nayo, ivyo mimi napenda sana ktk an art of writing kuzingatia/kua na ‘attention to details’, ‘being systematic and to follow up on each issue’’ to ensure relevance and ideas/topics flow/ connections-hii haimaanishi kua siwezi kosea ktk maandishi. Nimesoma reply zako 2 za ivi karibuni- jinsi unavyojibu sasa, nakuona kama unaibuka tu wakati unajua una KAZI KUBWA ya kufanya ambayo umeifukia, sasa umefika ule wakati nilisema kila wa mwisho wa kufukia kwa kua kuanzia sasa nitarejea kila nilichowaulizeni. Unakumbuka uliniuliza maswali 8 yafuatayo ktk post yako ya kwanza kujibu yangu ya somo la Utoaji generally namely….1. Zaka ni nini, 2. Inatolewaje kwa Mungu.3. Nani anastahili kutumia toleo la zaka.4. Zaka ni ya nini, 5. Je Yesu aliwahi kutoa zaka kama mkristo?, 6. Kanisa la kwanza walitoa zaka?, 7. Zaka imeanza kutolewa kanisani lini ?, 8. Kwa nini iwe ngumu leo kutoa zaka?, 9. Soma maandiko haya Torati 14:21-28, Hesabu 18:21-26, 20 Walawi 27:32 Maswali/mambo hayo uliyonitaka nijibu, yalijibiwa ivi nimechukua sehemu za majibu hayo/yale yaliyopita na pia nimeongezea inputs nyiingine ktk majibu yale ya kwanza tokana na comment nyingine nyingi nilizochangia humu toka mwanzo mpaka sasa

  MOJA: Nimesoma tayari maandiko haya kuhusu zaka-Torati 14:21-28, Hesabu 18:21-26, 20 Walawi 27:32 na mengine mengi.PILI: Zaka ni nini? ina maana kadhaa, kwanza- kwa maana ya kimaandishi, ni sehemu ya Kumi ya kitu, Biblia za Kiingereza e.g. NKJ inatumia maneno mawili namely ‘tenth’ pale kwa Yakobo alipoahidi na pia ‘tithe’ ktk Malaki na hayo ya juu ulionipa na hata wa Yesu. Maana ya wazi ya KiBiblia ni sehemu ya Kumi ya maongezeko iwe mazao. Maana ya Kiroho(tokana na uhiari na love kwa Baba yetu) ni sehemu ya Kumi ya Ulichonacho/ulichokipata/ twaa/pewa.TATU: Inatolewaje kwa Mungu? Kwa kua MUNGU hua haji live kuchukua basi anatwaa kupitia wanadamu kuichukua na kuitumia.NNE:Nani anastahili kutumia toleo la zaka? Kuhani wako kwa maana ya leo. Kuhani kuipokea na kuibariki kisha kuila na kufurahia maisha na huduma, ndio hapo Mungu anakula!!. Pia wahitaji wanaweza kupewa lakini si busara kumsahau au kumwacha Mlawi wako au kumfanya awe second then wahitaji first. Kilichoanza kwanza katika wakati Mungu anakuja na mawazo/mambo haya ni Mlawi kwanza kisha wanadamu wahitaji. In fact kwa macho ya Mungu, Mlawi ni mhitaji no. 1 kwa kua walikua hawana urithi wa mashiko kama wanadamu wengine, ukweli huu una apply hata leo kwakua Agano la Kale ni kivuli cha yajayo hivyo kutokua na uriti wa ardhi kipindi kile ni sawa na leo kutowaruhusu Watumishi wetu wa madhabuhuni kwa nia njema kabisa ya kitumishi na kiroho na upendo kwenda huku na kule kusaka noti, kulima, kuhudhuria mikutano serikalini na kusafir-safiri kikazi kwa kua ni Mchungaji hapo hapo ni Mkurugenzi wa gesi ya Mtwara Nchini, week 3 yuko Mtwara kushughulika na wana Mtwara, week 1 kanisani kupanda madhabahuni eti alete vitu kabisa toka JUU kwakua pia eti wakati yuko bize na wana Mtwara ktk vurugu zile, eti alipata muda wa kuomba na kumsikiliza Mungu Roho Mtakatifu kuhusu chukula cha kuleta altar.

  TANO: Zaka ni ya nini? Ni ili kuwemo chakula gharani na nyumbani mwake Mungu ili wakaamo/wahuduo humo, wale, wanywe na washibe tele kisha wachape kazi ya Mola. Pia ni kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji lakini kwa mpangilio/wazo la kwanza la Mungu alipokuja na mambo haya i.e. Mlawi first, no ujanja au twisting apo! SITA:Je Yesu aliwahi kutoa zaka kama Mkristo? Jibu: Kwa kua aliwahi kulipa kodi Mathayo.17:24-27 LABDA aliwahi kulipa ZAKA kwa maana ile ya pili ya matumizi ya Zaka yaani kusaidia Wahitaji. Besides, kwa kua Yeye aliishi kati yao kama ‘’Mlawi wao Mkuu’ -sasa Myuda Kuhuni Mkuu, alistahili kutunzwa ivyo HAKULIPA ZAKA bali WALIMLIPA YEYE zaka-yaani kwa ajili ya kumtunza pia ku-support huduma yake kwa mali zao-Luka.8:1-3. SABA: Kanisa la kwanza walitoa zaka? Kama Walimsikia Yesu akisema kua Mafarisayo na Masadukayo wana kaa kwa kiti cha Musa ivyo wayafundishayo tuyashike na kuyatenda na kwakua kati ya Kanisa la Kwanza, viongozi wao na members wengi walikua ni wanafunzi wa Mafarisayo na kwakua uwezakano wa Mitume kufundisha kupinga kutoa Zaka ingekua kinyume na tamko ya Bwana wao,then walitoa Zaka hakika hata kama haikuandikwa kama vile haikuandikwa Yesu alioga au la ingawa ni wazi alioga tena na sabuni na hata alijisugua kwa mawe kuondoa magacha miguuni maana alitumia sana kutembea huku akiwa amevaa viatu kama vya wa masai kidogo au sandals za wazi zile wanauuzaga machinga. NANE: Zaka imeanza kutolewa kanisani lini? Wakati ambao Neno kuhusu utoaji wake, lilipokuwepo au kuwekwa kwa wanadamu. TISA:Kwa nini iwe ngumu leo kutoa zaka? Kwa sababu ya mioyo ya choyo, ubinafsi, unyimivu,kiburi against Neno la Mungu, Kuutafuta kwanza ufalme wa Duniani na mambo yake halafu ya mbinguni ungoje kwanza, ufahamu ovyo wa Neno na mambo ya Mungu, kupoa kiroho, kukua na kukomaa vibaya kiroho, nature ya much know ya mwanadamu, influence ya Siasa, ukabila, majungu na kukosa nidhamu kanisani na dhidi ya Wapakwa mafuta wa Bwana wale wa kweli, kujiinua na madhara ya shibe ya sembe kupelekea watu kumsahau Mungu, utayari wa moyo kufa nk.
  JAMBO LA KWANZA: Nilikuuliza maswali majibu niliyokupa sawa au la? Kama sawa kubali na kama si sawa, pinga/sema hapa wazi wazi na ushahidi/hoja nzito

  Ati‘’ Lwembe Mungu akubariki kwa fundisho lako kuu linaloifunua siri kuu ya Mungu.
  Kwa bahati mbaya Seleli bado anapingana na neno la Mungu lililo hai kwa kung’ang’ania mafundisho ya dhehebu lake’’ = Kutiana moyo kwingine ni fix tupu Wandugu:
  JAMBO LA PILI: Ivi kweli on serious note, Lwembe amefundisha nini icho kinachofunua siri za Mungu? plz show it hapa waziwazi ili kuhalalisha baraka yako kwakwe ni kweli au ni by the way maneno tu ya kipendwa?

  Ati ‘’Ninafuatilia kuona maendeleo ya kukua kiroho kwa wote wanaopenda kumjua Mungu wa kweli’’ JAMBO LA TATU: Wewe unampenda Mungu kweli? una maendeleo ya kukua Kiroho kweli? ilikuaje Ulitamka wazi humu bila aibu kua ‘’MIMI SITOI ZAKA NA SIAMINI KAMA ZAKA KABISA’’: Wewe kweli ulivyojiinua kua una ujumbe kama wa Yeremiah wa kujenga kanisa la Kristo kisha unasema wazi wazi ivyo hutoa Zaka( hata kwa msingi wa Ibrahimu-Hiari) na bila haya, unasema na kumtaja-taja sana Roho Mtakatifu!!!!!!!!! ivi kweli Kaka unatoa wapi confidence hii? Je nikisema hii ni ile 200% confidence pori ya Lwembe, ninawaonea?

  Ati, Umemshangaa Siyi kwa kusema ‘’ZAKA KWA KANISA ni tango mwitu na kisha kujidai ivi..’’ Tafakari kauli yangu hii utanielewa sana’’ JAMBO LA NNE: Je toka uanze mjadala mpaka sasa, unadhani umeshaonyesha kinaga-ubaga wapi ktk Agano Jipya, ZAKA ilifutwa? Wapi/kivipi, sema hapa waziwazi na kwa hoja nzito ili kuthibiisha PASI NA KUACHA SHAKA kua kweli kuendelea kutoa Zaka leo ni tango mwitu fundisho ili tuache mara moja

  Uliwahi kutetea( by implications ) comments za Lwembe, Kaswahili na Sungura kuhusu Watumishi wa Makanisa, wakafanye kazi maana leo hawajanyimwa kua na urithi wa ardhi kama Walawi: JAMBO LA TANO: Ukizingatia jibu langu ktk swali lako la 4 kule juu hili-Nani anastahili kutumia toleo la zaka?na aliyosem Bwana hapa-Yohana.10:11-14, wewe wasemaje?

  Mliwahi kunukuu vema Biblia kua Paul alifanya kazi kwa mikono yake mwenyewe- Mdo.18:1-3, kwa maana iyo, leo Watumishi wakachape kazi zao wenywe ili kupata sembe: JAMBO LA SITA: Nilisema kua ktk 1Wakorinto.9:1-15! Paul anayesema ni haki yake kuchuma vya mwilini kwakua aliwapandia vya rohoni na kua..BWANA ALIAMURU WAHUBIRIO INJILI WAISHI KWA INJILI NA WAHUDUMUO MADHABAHUNI, WALE VYA MADHABAHUNI na Yeye mwenyewe Master alisema, ‘’Mtenda kazi anastaili ujira wake, alipowatuma wanafunzi ktk Luka.10:1-7, je kuna nongwa gani Watumishi leo tukiwawezesha kwa Zaka au mali zetu kama walivyomfanyia YESU-Luka.8:1-3 ili wakabaki na jambo moja tu ambalo kanisa la kwanza-Viongozi waliliona haraka mara moja na kujishitukia kisha kujirudi haraka, walipokua wanachukuliwa na ubize wa mambo mengine kwa kadri Kanisa lilivyokua linaongezeka-Mdo.6:2-3?

  Ulisema hakuna andiko hata moja linalosema kua ZAKA ni SADAKA/TOLEO linalopaswa kukabidhiwa kwa kuhani:JAMBO LA SABA: Nilijibu kwa kukuliza, KAMA YANENEVYO MAANDIKO, nithibitishie haya, Hua tunajuaje kua kunywa (sijasema ‘kulewa’) pombe, kuvuta sigara, bangi, madawa ni dhambi! na kwaba tunatumiaga nukuu zipi kuwaambia/shauri wapendwa wanao fanya kazi viwanda cha sigara, bia, vitengo vya afya ambao wanagawa condoms ili wa Tz wasife kwa kufanya ng’ono zembe nk? na kwamba, Tunafahamuje kwa hakika Yesu alioga, Kupiga chafya na miayo?

  Nilisema sababu ambazo naziona kua kwazo mimi/wengi wetu tumeridhika na tunafuraha kulipa/kutoa/kuleta zaka LEO sisi wa Agano Jipya, nazo ni: Zipo BAADHI ya kweli za Biblia zinahama moja kwa moja KAMA ZILIVYO toka kabla na baada ya sheria za Agano la Kale to Jipya AS LONG AS HAZIHARIBU KWELI ZA AGANO JIPYA- mfano tendo la imani la Ibrahimu mpaka leo limetuletea baraka, Yesu kutumia nukuu kadhaa za kale ktk mafundisho yake kama walivyofanya wanafunzi wake, mfano Paul, Stephano na Petro. Kwa ivyo, kuchukua ya Agano la kale kwa mantiki hii na kuyahamisha/ kuyafanya/ kuyatumia leo ni truly Biblical act and it is justified kabisa pasi na shaka yoyote, hence kama Ibrahimu alitoa zaka-Mwa.14:18-20 na Yakobo alihaidi kutoa zakaMwanzo.28:10-22(notice:alihaidi-hapa cha muhimu ni moyo unaomrithia Bwana na kutaka kutoa zaka na waliyafanya hayo kwa hiari kabla ya sheria, no wonder LEO NITATOKA ZAKA KWA KUHANI au kupeleka Nyumbani mwa Bwana( ambako ofcoz Kuhani na hao wakaao/tumikao humo, wapo).Pia Katika Mathayo.23:23 Yesu anasema-‘’Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache na tena KatikaMathayo.23:1-3-Imeandikwa-Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake( NOTICE NI WATU NA WANAFUNZI WAKE KABISA) akasema, ‘’Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi’-ZAKA lazima ilikua mojawapo la Mafundisho makubwa kabisa. Halafu, Kwa msingi huo hii andiko bado ili Malaki.3:8-10-‘’Leteni Zaka kamili/zote ghalani mwangu ili kuwemo chakula Nyumbani mwangu’’ linabana mpaka leo simply because halijawahi vunjwa kwa yale aloposema ktk Mathayo.23:23:
  JAMBO LA NANE: Wewe unasemaje kuhusu hizo sababu zangu kwa nini leo tutoe Zaka?

  Nilisema kama ktk moja ya point zake kwenye hotuba ya Mlimani-Mathayo 5:17-18 nia kwamba hakuja kutengua Torati bali kuitimiliza, mbingu na Nchi zitapita….- Hotuba nzima ni Mathayo sura zote za 5,6,7, na kwakua aliwaambia kua Mafarisayo wanakaa kwa kiti cha Musa na kwakua tumejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii ambao nao wamejenga juu ya Msingi Yesu-ambaye naye anasema hakuja kutengua msingi ule wa Torati bali KUUTIMILIZA(kwa namna ofcoz aliyoionyesha mwenyewe ktk hotuba nzima ile na si kama Watakavyo wa dini leo-hii muhimu sana ku-note icho) kwa kua aligusa moja baada ya jingine toka ya Kale na kusema ya Leo: JAMBO LA TISA: Je huyu ‘’Farisayo’’ wetu wa leo akilifundisha swala la zaka maana ya ile Yesu alisema , jamaa wanakaa kitu cha Musa, wakifundisha, tutende hence kama mafundisho yake tena akitumia maandiko ya AK ya zaka BILA KUATHILI KWELI NYINGINE za akina Musa wadogo( Mitume na Manabii) na Musa Mkubwa-Yesu, Je si sharti nishike na kutenda kwa kua Musa Mkubwa amewasemelea/commentia ivyo kwetu sisi wanafunzi leo kua wayafundishayo tuyatende?.

  Amin Yeremiah Mguluma,

  Maandiko Kuhusu Zaka uliyonipa kuyasoma na kutoridhika na uelewa wangu kwayo plus niliyokupa

  Torati:14:21-29-Ninazingatia hasa mistari (23,27,29)= Nilisema anaposema Usiache Kutoa Zaka kisha anasema ktk mstari 23- Kula mbele za Bwana halafu mwishoni mstari huo anasema ili ujifunze Kumcha Bwana daima halafu anaendelea kusema mstari 27 kutomwacha Mlawi kisha mstari 29 anataja na wengine na yatima, mjane nk kwa Zaka iliyosemwa juu pale isiachwe kutolewa na kisha bado mstari 29 anarudia tena kusema Mlawi asiachwe( tena mistari 27 na 29 inatumia/inasisistiza kwa maneno yale yale kuhusu kwa nini Mlawi wamjali-soma! Iyo inaonyesha nini? simply msisitizo na kwamba huyo Mtu bila shaka ni muhimu kweli kati kati yao! Ndio maana sura moja- mtu mmoja anasisitiziwa/wekewa uzito huo. JAMBO LA KUMI: Kwangu mimi Zaka kutolewa ina connection na Kujifunza kumcha Mungu daima kama alivyosema-that was the theme/msg! kwamba nani akula kwanza kati ya yeye aitoae au Mlawi na wengine kati yao-sioni kama ni hoja kwangu.Pia ukweli kwamba ktk sura moja Bwana ameongela Mtu mmoja-Mlawi kwa uzito huo, basi ukweli huu ukihamia kwetu leo kwa Watumishi waliotengwa/tolewa kwa ajili ya Utumishi PERMANET hapo hekaluni/jengoni Kanisani, ni sawa kabisa maana Bible says AK ni kivuli cha kweli halisi yaliyo/yatakayokuwepo AJ, wewe wasemaje? Wapi nilikosea au kukwepa ukweli wa maandiko kama ulivyosema?

  Nilitoa mfano kua yaliyosemwa pale juu ktk Andiko ilo ni sawa na Mtu kusema ivi ’’Usiache kwenda kanisani siku zote za maisha yako, juma 3,4,5-j2, utakaa nyumbani ufurahi na kupumzika ili familia yako ipate uwepo wako pia’ ili upate kujifunza kumcha Mungu daima’’-Kusema kua hapo amemaanisha nikae nyumbani na familia na nisiende kanisani, ndio kosa la uelewa ulofanya.JAMBO LA KUMI NA MOJA: Wewe unasemaje kwa ilo?
  Pia nikashauri ni vema kua na Elimu ya Biblia lakini pia vyanzo vingine hence nikasema tafuta Bible commentaries, angalia ZINAHITIMISHA nini hasa Main issues hapo kwa andiko hilo. JAMBO LA KUMI NA MBILI: Je uliangalia commentaries na ukakuta hoja kuu hapo ni kutoa zaka na kisha kuitafuna mwenyewe kwanza kama ulivyong’ang’ania iyo kweli moja tu? kwa nini hata kwa kusoma tu bila Bible commentaries, hukuona/umejizuia kuona msisitizo kwa Mtu mmoja kuongelewa kwa uzito ktk sura iyo iyo?

  Nikasema, ikiwa tunakuta Zaka kwa Mlawi kabla ya hapa-Kumbu.14, kulingana na Wataalamu wa dini/maandiko kukuzidi waliopanga vitabu ktk mpanglio uliyopo ktk Bible leo yaani unaiona uku Walawi.27:30-33 kisha Hesabu.18:20-32 then ndiyo Kumbu. 14 na kisha hata Nehemia.10:37-38 mbele uko.JAMBO LA KUMI NA TATU: Kwakua kanuni moja wapo ya kutafsiri maandiko ni kuangalia kweli nyingine za Maandiko, je kwa nini huoni Mlawi ana uzito wa pekee kwa kua ktk maandiko mengine yamesema kuhusu Yeye kupewa Zaka kuliko kuitafuna wewe mwenyewe au kuwapa yatima, Wajane nk? na kama Walawi ni Kabila lililotengwa kwa kazi maalumu ya Mungu hekaluni na kama Agano la Kale ni kivuli cha uhalisia leo, je Leo hatuna waliotengwa spesheli kwa kazi maalumu humo Jengoni kanisani na ili wakae kwa moyo mmoja uko ktk utumishi , tunawakataza kwa hekima, upendo na unyeti wa kazi ya kulihudumia Neno/Madhabuhi kwa ajili yetu-Mdo.6:2-4( angalia kwa macho matatu part ya mwisho ya mstari wa 2 na wa 4 mzima-una nguvu sana kwa point yangu hii ya huduma ya Neno ya kudumu jengoni au nje ulimwenguni but from the base-the church) kwa nini wasistahili zaka leo watu hawa kama vile zamani?

  Niliponukuu Mwanzo.14:1-20 kama andiko zuri sana na lenye nguvu kuonyesha Zaka mapema sana inatolewa tena kabla ya sheria(mtu na moyo wake wa kupenda na furaha kwa Bwana wake, anatoa kwa Mungu kupitia Kuhani Melkizedeki na ivyo hata leo tunaweza fanya ivyo kwa furaha kabisa na kufundisha ilo, uliropoka kua ni aibu kubwa kunukuu andiko hili kuhalalisha Ufundishaji Zaka tunaofundishwa na kufundisha wengine. Pia hili la Mathayo.23:23- uliruka na kusema Yesu aliwaambia ilo Mafarisayo na Waandishi implying kua halituhusu -JAMBO LA KUMI NA NNE: Je Ubaya, aibu na upotofu wa kunukuu maandiko hayo kufundishwa LEO ni upi Biblically? Pia ktk yale YOTE YESU aliyowaambia watu wengine( Mafarisayo, Masadukayo, Waandishi, Wakuu, Makutano) hayatuhusu? Hakuna tunayoweza/paswa kuyachukua na sisi Wanafunzi wake? Kama ni hapana, kwa nini? kama ni ndio yanatuhusu, kwa nini Zaka kwa andiko ilo lisiwe neno kwetu ivyo tutoe?

  Uliuliza kama nilisoma kuona Kwanini Ibrahim alimpa Mfalme na kuhani Melkizedeki na kama ni sahihi kutoa zaka mali isiyo yako?-JAMBO LA KUMI NA TANO: Niliona ni kwa sababu ya furaha na moyo wake wa kupenda kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyo kua upande wake wakati anamuokoa nduguye na kwamba kama ni sahihi kutoa Zaka mali isiyo yako, si sawa, utakua mwizi kwanza in the first place! Wewe wasemaje?

  Ulisema Yesu wakati wa huduma yake aliishi akifuata imani na mapokeo ya kiyahudi, na kua wanafunzi wake waliishi kama waumini wa dini ya kiyahudi na kufuata mapokeo ya kiyahudi.JAMBO LA KUMI NA SITA: Kwakua Wanafunzi wake walishi kwa kufuta mapokeo ya Wayahudi, je ndani ya mapokeo hayo ya kidini na desturi, Zaka ilikuwemo ama la? Na kama lilikua fundisho, je Wanafunzi walioishi kwa kufuata mapokeo hayo, walitoa hawakutoa?

  Ulitumia andiko la Matendo 2:44-45; 4:34-35 kusema kua hakukuweko na Utoaji wa 10% bali wa 100% na kwamba huko ndiko kuitimliza torati kulikofanywa na Yesu.JAMBO LA KUMI NA SABA: Nisaidie kujua, umefiakiaje conclusion iyo ya 100%? na How do you know ili kuifikia iyo 100% ya utoaji, hakuna walioleta 10%?-Seriously tell me about it na kisha Umefikiaje conclusion kua Utoaji huo 100% ndio Kutimiliza Torati? Seriously tell me about it again

  Ulisema, maandiko yanatufundisha kuwa KUHANI WA KIKRISTO NI MKRISTO ALIYEKOMBOLEWA NA YESU na ya kuwa Uchungaji,Ualimu,utume,uinjilisti ama unabii ni WIZARA/HUDUMA ZA KIKUHANI SI UKUHANI-JAMBO LA KUMI NA NANE: Je si kweli Wizarani umo wamewekwa wengine kutenda na kutumika umo moja kwa moja, kulihudumia Neno day and night? Unawezaje kukana uspesheli wa Walawi/Wa Yuda wetu wa leo kupewa Zaka na kuwatunza ili watumike vema umo nyumbani mwa Bwana?.

  Ulisema UTOAJI WA ZAKA KANISANI UMEANZA MWAKA 777 BAADA YA KRISTO TENA KWA AGIZO LA GAVANA CHALAGNE:JAMBO LA KUMI NA TISA: Tunaongozwa na Ukweli toka ktk Bible mfano Ibrahimu alivyofanya au Yesu alivyosema au Gavana? Ukweli upi wa Utoaji Zaka ulianza, wa Gavana au toka zama za Ibrahimu? Kama ukweli ni toka Ibrahimu kulikua na Zaka, kuna haja gani ya kunukuu Gavana na maamuzi yake? Authority iko wapi, ktk Neno au bwana Gavana?

  Ulisema, haupingani na kumtolea Mungu na ati unatumia kanuni ya Yesu kumtolea Mungu isemeyo ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE: JAMBO LA ISHIRINI: …Unawezaje kutumia kanuni hii.. ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE’ wakati ulisema huna mpango wa kutoa (iwe kwa Hiari kama Ibrahimu au sheria basi)? Nini maana ya kumpenda MUNGU kwa moyo, roho,nguvu,akili? Je mali zako na kila ulichonacho kinahusika ktk maana ya kumpenda Mungu kwa kila kitu? na kama ni ivyo huoni kua na tabia ya kukumbuka kutenga 1 kwa ajili ya Mungu ni jambo jema la uchaji na kicho wala si laana na torati? yaani kati ya kumi, toa 1 tu kisha zile 9 zote kula utakavyo!

  Ulisema,ZAKA HAZIKWENDA KWA MAKUHANI KAMA TUFANYAVYO SASA NA HAIKUWEPO HATA KWA WAYAHUDI WENYEWE NA HILI LINA UTHIBITISHO WA KUTOSHA KABISA KINYUME NA UNG’ANG’ANIZI WETU WA KULAZIMISHA MATOLEO-JAMBO LA ISHIRINI NA MOJA= Vipi maandiko uliyoyatoa wewe ayanyoneysha Zaka kwa Mlawi?

  Niishie hapo kwa sasa, ktk kuyapitia mengi uliyofunika au kujibu ovyo ovyo, nimekutumia ktk summary barabara mambo 21 yenye kipengele au vipengele/maswali madogo kadhaa, kukiwa na mengine uliyofunika(nitakagua TENA baadae kule tulipotoka kote) nitakupa mzigo/kiporo chako ili tumalize debate hii kila mmoja akiwa mwaminifu siyo janja-janja tu, hence jibu 21 issues izo, na kama unadhani kati ya mambo uloniuliza wewe, sijafanya chochote, sema ni yapi, mara moja nitashugulika bila kufunika kama wewe, Lwembe na Sungura ambaye ndiyo my next and final assignment, he will also get his kiporo right here, will right back for him. MWISHO ULE NILISEMA UTAFIKA KWA KILA MWANADAMU KTK DEBATE HII ALIYESHIRIKI KIFISADI, UMEFIKA! Ndipo tutahitimisha ivi punde kama mkitimiza masharti ya mahojiano ya kikumbwa (kutofunika mambo kivyepesi tu), sasa vigezo na mashati vitazingatiwa ili ku-end the debate rasmi.

  Press on.

 52. Let me be honest guys;

  ”Nina mashaka makubwa kama Seleli yuko sawa kwenye uwezo wake wa kufikiri”.

  Siyo siri sijapoteza dakika nyingi sana kusoma hii barua ndefu iliao upatu!

  Ingekuwa ni upotevu wa muda!!!

  I think we are done.

 53. Lwembe,

  Kuhusu Kutumbukiza somo la Utoaji na maelezo yangu ati kutoeleweka naongea nini ktk somo ilo, Plz be serious kidogo! nilishaweka sawa ili kua kwa CORRECT judgement yangu nilipokuja tu mara ya kwanza na kuwakuteni mkimenyana kuhusu Zaka kutoa au la LEO na request ya Mchangiajai mmoja Mr. Tumain Nelson aliyejitambulisha kua bado mchanga kiimani na akaomba live humu humu lifundishwe somo la Kutoa, NDIPO nalifanya huduma iyo-nikisema hua hamsomi KWANZA maoni na yaliyojiri NDIPO mtu uanze kuchangia, mnasema ni udhaifu kuwaambia ivyo wakati the real udhaifu na very boring kujadili pale mtu anapokukurupuka tu na kujitupia pale anapokuta jambo/ somo/ majadiliano yalipo bila ku-take trouble kusoma kwanza

  Au basi kwakua hamwezi kusoma yote labda mmechelewa mjadala umeshakwenda sana na comments ni mia na kidogo na ukweli kua Watu hawawezi wakawepo mtandaoni kila siku, then mtu akijitupia/akijiingiza, ajitupie na kuangukia mjadalani vema na si ovyo ovyo tu mradi amesema kitu.Embu tukatae semi/ msemo /dhana kua Waafrika/Wa Tz lazy kusoma mambo na ati ukitaka kumficha Mwafrika kitu cha thamani-mikataba ya kuramba gold mpaka tufe wote, kitie ktk Maandishi tena marefu!- ndio maana hata migodi wanauza kwa miaka 50 kisa Waziri mmoja hajasoma yale mabook makubwa ya Mikatabu wanayosign ktk Hotel London! Sasa kama nilishaweka sawa ivyo na nia,sababu na uwezo wa kuleta somo zima ktk Utoaji ulikuwepo, unaliletaje hapa tena ilihali tumeshakwenda masafa?

  Basi kama ni ivi then mambo 3 ni hakika, kwanza, hauko serious na kazi hapa-mi niko kazini/huduma hapa-ni mwanzo mwisho huduma tu Kaka, Pili, unapenda Utani sana na kuchekesha-which is good anyway, Tatu unapenda wakati tunakwenda Mwanza, tukifika Chalinze, turudi Tageta home kwangu hapa kuchukua vitumbua vya mchele na mikate ya blue band and tandibondi kisha tuanze tena to Mwanza via Chalinze-punishment ya abiria wa aina yako ni kukushusha Ubungo Mataa!!!!!! ili serious mind/spirits-Wasafiri wafike Mwanza on time! Kwamba sieleweki ktk Somo lile la Utoaji! Kwanza huo ni uwongo mtupu, kalisome tena, pili, nimeshasema ktk Mijadala, kama huonyeshi wapi mtu kakosea/haeleweki basi aidha huyo asemaye hayo ndio haeleweki plus plus au anajiweka/ana weka claim yake isiyokua substantiated with facts matatani kua cheaply treated kama si ku-suffer a public shame ya kua dismissed mara moja.

  Na ili jingine la wewe kua Mshauri Nasaha ati unasema tuwe wasikivu-nai treat kama simama-dede joke!!!!!! Huna qualities ktk debate hii kwa capacity yako, kusema/kushauri ilo-at least let us be fair brother Lwembe na ivi hiyo 200% confidence kujipachika vyeo eg wewe kua mshauri nasaha, mara moderator kuharmonise Seleli Vs. Sungura game/debate mara Kaka Yangu Yeremiah Mgulumu kua ati Mfundishaji hodari, Mjenga kanisa na hii kali ya mwaka ati Mwangalizi wa Kukua kwa Kiroho cha watu hapa, mwee!!!!! Mnambwembwe na promo! Lo! Utadhani kweli mko ivyo lakini sasa ukiambaa na maandishi/comments zenu ‘nukta kwa nukta anointing( severe yet friendly/ positively intended check ups), sadly many of them(not all, to be fair) hamna kitu, ni fix tupu kwa kweli!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kwamba na mimi nije na kula mlichokileta! Yaani mna full confidence yet fake mpaka nachoka!-Kipi on serious note zaidi ya wewe kucheza-cheza tennis ball humu na Yeremiah kushusha lecture safi ya Zaka Agano la Kale but akifelli kabisa, kabisa seriously kuonyesha wapi Agano Jipya imefutwa-nimesoma nukta kwa nukta maelezo yenu WOTE -mko hoi kweli, imewakaba ile mbaya/nzuri, hii pini ya Mathayo.23:23!

  Ati makorokoro yangu ya dini, nirudi nayo kwenye kigunia changu na ati nimevuka nayo mpaka uku Agano Jipya!=Mh! Andiko la kwanza la Mtu maarufu na mkuu sana ktk Imani yetu na hata ujio wa YESU ametoka umo yaani bwana Ibrahimu ktk Mwanzo.14:1-20 alitoa Zaka kabla ya sheria na tena Kiongozi Mkuu na final role model wetu YESU KRISTO ktk Mathayo.23:23 amesema kuhusu Zaka hapo(nitayarudia haya maandiko mpaka yawaingie kwa roho, nafsi, mwili(nafsi,akili-kwenye matatizo ya kutaka kukana kweli izo na kubania vishilingi/vipato vyenu), hayo yote yanathibitisha BILA KUACHA SHAKA Utoaji wa Zaka-Notice: Ni Mtu Mkuu KTK Imani yetu-Ibrahimu na Kiongozi Mkuu WA Imani yetu-Yesu-these heavy weight, mmoja ametenda na wa pili amemea zaka.Sasa nani ana uwezo wa kukana hayo kwa dhati na usahihi kama kweli mna Roho wa Mungu, mmeokoka na Bible ni final authority kwenu na ninyi ni wana wema kanisani kwenu chini ya Makuhani wenu uko? Nadhani dini MBAYA hasa( maana iko dini nzuri) na makorokoro unayosema Lwembe na niongoze na manyangalagata ni kukataa kweli izo za Wakuu Maarufu ktk imani yetu.

  Ati.’’Seleli na Sungura nyote wawili ni watu wa kutumia sana “akili na reasoning na resoning of reason, logic”=Lwembe, naomba tena uwe serious! Neno la Mungu ndio final, lina kata mashauri/maneno, tukishatumia/kunukuu Neno la Mungu KWA USAHIHI kujibu/fafanua jambo tena KWA USAHIHI(unless Mtu aonyeshe BILA kuacha shaka kua hakuna Usahihi), basi jambo ilo LIMEKWISHA/LIMESHAAMULIWA/SHAURI LIMEKATWA-hii ndio naita maturity and professionality hata sound spirituality ktk Mijadala ya Watu wakubwa kama sisi sote. Nilishakujibu mara 2 kuhusu wasiwasi wako wa kuikimbia Akili yako na kuacha kuitumia, sasa najibu tena mara ya 3 na nitajibu tena na tena ktk ili mara 4,5,10…. na uelewe na kukubali au prove me wrong(unless wewe una tennis ball humu).

  Nilisema,Biblia inadokeza kutozitegemea /lalia/egemea AKILI -Mithali.3:9- lakini haijasema KUTOZITUMIA! Pia nikasema tukiwa ndani ya Kristo, tu viumbe vipya(AKILI imo)-2Wakorinto.5:17, nikasema Paul mwenyewe anakimjibu Festus alipowekwa kiti moto na Wakuu wale, anasema ninaongea maneno ya AKILI na Kweli- Mdo. 26:25 ivyo ni sahihi kabisa kusema-maana amesema mwenyewe tayari – uyasomayo leo ya Paul ktk Matendo iyo 26 pale bila shaka na kwingine ktk nyaraka zake-iko wazi kwa anayesoma na Akili njema pia , ni/kuna maneno ya Akili pia. Bado nikasema, sisi ni mahekalu ya RM ivyo anakalia/anamiliki kila kitu na AKILI ikiwemo-1Wokorinto.6:19.

  Kwa iyo narudia, acheni uvivu hasa wewe na Kaka Amin Yeremiah Mguluma wa kufikiri/ kupembua/ kuchekecha/kutakafari mambo ya Mungu, acheni woga na maangalizo fake yasiyo na msingi maana tu ndani ya Yesu, tumebadilishwa, viungo vyote vya ndani na nje, vinavyoonekana na visivyoonekana, ni potential tools kuvitumia/kutumiwa. ACHENI KUTIA HOFU WATU ATI AKILI HATARI SANA bwanaa!!!!!!! Mmmh! KWANI SISI CHIMPANZEE! SISI NI WATU/WANADAMU.

  Na leo niongoze kweli nyingine izi nzito sana za maandiko Mdo.17:1-4, 16-17, Mdo. 18:1-4-hapa Paul ANAHOJIANA na Watu-debate kali-kama tunavyofanya hapa!-Kiingereza hapo ambacho ukikitumia wengine humu wana case nacho, ktk maandiko hayo inatumia neno..Paul REASONED with them! Si unaona hapo Kiingereza kimenisaidia kufafanua jambo nalo eleza!!!! Namna gani watu humu! Sasa ktk Ku-reason kitu-AKILI pia hutumika….ivyo ni sahihi kusema Tuyasomayo ktk Nyaraka za Paul-yapo ya Ufunuo moja kwa moja na yapo ya Akili-yaku-reason!

  Huo juu hapo ni ukweli mwepesi tu wala si kukufuru na wala haihitaji misismko ya Kipendwa ya Lwembe na Amini kwa kua tu hakuna ufahamu wa mambo, wapendwa hukeme-kemega mambo au kujitia kutahadharisha baadhi ya vitu kumbe walaaa hamna lolote la maana maana ukiyapima haya wanayo tahadharisha/ onya/kemea kwa Neno kama nilivyofanya hapo juu, yanaoneka wazi ni mihemko tu ya kipendwa tuliyozoega-maana tunaweza jadili jambo weee til mwakani lakini ikifika kutumia mamlaka ya mwisho-NENO la Mungu, basi mashauri yanakatwa/maneno yanakwisha na jambo/hoja hiyo inakwisha /imetendewa haki na Elimu na Maarifa yanakua yamekamilika kwa wasomaji na sisi Wana Mjadala.

  Kama mpaka hapa hujaelewa na mtarudia tena tahadhari zenu fake kuhusu Akili, basi nimeshajenga msingi hence kazi yangu itakua ndogo tu, ni copy na kuwapestia iki iki then kuwafafanulia zaidi au kuyaongea haya haya kwa namna nyingine-maana ziko njia nyingi za kufundisha Mtu anayejifanya haelewi wakati anapata mambo kabisa but wivu tu wa kukubali kua anapata vitu ndio una mkaba, so nitatumia njia kama mfano kuwaulizeni maswali au ku-test from Scriptures KWA yale tunayoweza tumia Akili tu kuelewa mbali nay ale ya Kufahamu kwa Ufunuo na Imani tu bila kuelewa kwa Akili-that will be my next simple job.

  Hili andiko ulilotumia la..Lk 10:21 na kushadidia kua mie nimefichwa mambo na umepewa weye kinda-hujalitendea haki- Biblia inadokeza ktk-2Timothy.2:15-‘’Kutumia kwa HALALI(usahihi/haki/kisawa-sawa/ inavyotakiwa/ kwa maarifa na ufahamu wa kweli wa/kwa Neno husika) Neno la Kweli’’ kwa iyo ni mpaka uthibitishe hapa wewe uliyepewa mambo ukoje/una hoja gani ili mimi nijue kweli nimefichwa, otherwise yale yale…this claim is dismissed angrily kwa kua claims zako na Amin Mguluma kama izi hanging, ni nyingi ktk mjadala huu, zinakera na kutupotezea muda.

  Kuhusu “kuubeba msalaba na hata ukatoa andiko hili zuri-Mt 10:38 mbali na haya Mathayo16:24-25 na Luka.9:23-24 niliyoyatoa mwanzoni wakati najibu claims fake/baseless za Sungura ati umesema…nimepitiliza na msalaba huo!!!!!! Unakataaje fact/truth iyo Kuhusu YESU mwenyewe kutu-task? Itoshe kusema tu kua soma Bible yako toka Mwanzo-Ufunuo, utakutana na kweli KUU MOJA…iko sehemu ya Mungu 100% Kufanya na iko pia 100% ya Mwanadamu kufanya-Mmoja kati yao hasipofanya sehemu yake-aka kaa tu hapo kama rirobot au tikitimaji, mwingine hafanyi! full stop and period and simple,right?

  Hata ili uokoke, hii KWELI ina-apply e.g. ATAKAYE AMINI NA KUBATIZWA ..ndiye ……MUNGU anafanya part yake namely kukuvuta kwa Yesu, kuachilia Roho wake kuku-convict madhambi yako, anakuletea Mhubiri au ana sababisha Mahubiri uyasikie hata kama yatatokea kwenye mti wa mpera uko porini wakati unachunga nguruwe HALAFU yatakayofuatia baada ya hapo, ni task yako si Mungu, ndiyo mantiki ya USIPO UBEBA MSALABA WAKO/USIPOIPOTEZA NAFSI YAKO/USIPOIKATALIA MAMBO YAKE-aina ya Udhibiti/U-hard training/usulubishaji-utesaji huo nilisema basi nafsi/ubinafsi/roho ya choyo na ubahili/kutojali ya JUU kwa kukimbilia/ kimbizana na ya dunia na anasa zake vitaku pelekesha mpaka kugomea hata 1 kati ya Kumi, yaani wewe uwe huru kwa raha zako kuramba 9 lakini kui-train hard bila huruma nafsi yako yenye ubinafsi basi 1 tu itengwe/iende kwa Bwana bdo nayo unatka kufyeka! What insubordination is that!

  Hata ili andiko ulilotumia Mt 11:28, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao ili kujibu hoja yangu ya kubeba msalaba/kuipoteza/sulubisha nafsi,pia ni kosa lile lile la kutumia andiko ISIVYO HALALI-out of context and hata connectivity kabisa- ivi Lwembe a u serious! Huoni aya my dear bro! unaibua-ibuka tu maandiko na kuyabandika vyovyote na kokote! Mwe! humu kuna kazi na Yesu ana viumbe adimu kwa kweli, amewaokoa dizani mbalimbali na nyingine ni kali ile mbaya,anajua Mwenyewe! mwe!nachekaje! ivi inakuaje umenukuu-nukuu ivi Lwembe!!!! tehe tehe!kha!

  Umenikana nilivyosema kua Wewe umesema WAZI WAZI KWA MAANDIKO HAYA..Mwanzo14:1-20 na Mathayo.23:23 kua Zaka inatambaa toka la Kale mpaka Jipya… na ati ninajikanganya- narudia tena kusema plz be serious Lwembe, acha utani!!!!!!! Ktk post yako ile ya kwanza ya ulipojidai kua moderator wetu humu(in fact a very boring moderation kwa kua ni less qualitative and awkwardly done), ulisema maneno baadhi ivi na zingatia nilipopigia mistari na kuyalaliza maneno-Italics-kumbuka aya ni maneno yako mwenyew..’’ Jambo linalojadiliwa hapa ni ZAKA na UTOAJI wake, Je, jambo hili linaendeshwa kulingana na muktadha wa Maandiko au NJE, wenye kusema linaendeshwa katika upotofu, HAWAKUSEMA kuwa ZAKA ISITOLEWE! Ndio maana wakaleta na zile nyakati tatu, kabla ya Sheria, wakati wa Sheria na wakati wa Kanisa, Tunaishi katika mifumo inayowakilisha utawala. Ili Mifumo iwe kamili, husimamiwa,unapokuwa chini ya Mfumo fulani, basi unakuwa na wajibu wa kuwatii wasimamizi wa Mfumo huo kimilifu ili undelee kufaidika na jumuiya hiyo kulingana na Mamlaka hiyo inayokutawala.Mifumo hiyo ikiwa ni makanisa yetu katika maana ya madhehebu, tunapaswa kuziheshimu Mamlaka zinazotutawala kama Maandiko yanavyotufundisha. Nazo Mamlaka hizi za kidini zinazotutawala, licha ya kwamba mifumo yao ni tofauti kabisa na hiyo ya KiBiblia, bado zinatutawala kwa Neno la Mungu, Mt 23:1-3 “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda …”Kwahiyo ni halali kwa Mamlaka hizo ambazo leo hii zimekaa ktk Kiti cha Kristo, zisikilizwe nasi wafuasi wake katika yote wanayo tuamuru, pamoja na ZAKA katika jinsi yoyote ile watakayoiamuru ikusanywe!

  Tokana na hayo yako baadhi ya uliyosema-nimechomo-chomoa vipande, si masentence yoote-ndipo nikasema UMESEMA WAZI WAZI kua no problem ktk Zaka na umeionyesha wewe inatambaa toka Mwanzo- Ufunuo yaani kabla ya Sheria, wakati wa Sheria na kisha Kanisa- Sasa UNAPINGAJE/kanaje ilo ILO? You are not serious man. Nawahimiza sawa hasa wewe na Amin na kwa mbaaali Sungura (Kaswahli yeye ni off the line/beyond repair kabisa) kua plz be smart kidogo, kujua mnatoka wapi,mnaenda wapi, mnaendaje uko, mmesema nini, yapi mlipaswa mkafunika au kama mlijibu, mlijibuje ili connect KILA MARA ukooo mnakokwenda, otherwise relevance yenu na connectivity ya ideas/flow yenu is too distorted and severely virused! Mfano ni hapo juu…aliyosema Lwembe, nikasema aliyosema sasa ana ruka! Indeed tennis ball engagement with this guy in this debate!

  Sasa a real case ya kujikanganya ni hii uliyosema wewe ivi.. ‘Hiyo Mwanzo niliyoinukuu haina uhusiano wowote na Mt 23:23 na kua Moja ni Shukurani iliyojiviringisha katika Upendo na nyingine ni Tozo lililojiviringisha ktk Utii wa Sheria!’’ Can you imagine that? IVI UNA HABARI HATA KWA COMMON SENSES HAPO UMESEMA YESU ALITETEA/ ENDORSE UTOAJI WA ZAKA KWA SHERIA coz ndiye aliyeyasema hayo ya Mathayo 23:23? Embu soma tena ulichoandika hapo between the line! Brother plz come on, raise the standards in debating!lo! nikisema tumieni Akili kwa kua ni baraka na kipawa chema, mnakemea-kemea,angalia sasa umesema nini hapa wakati tumeshasema na Biblia ilishasema kwanza kabla yetu wote kua ujio wa Bwana ulikua ni mwisho wa Sheria but hapa unasema maneno ya Yesu alisema Utoaji wa Zaka uendelee kwa/under same same sheria! Unashituka kua nimekuwekea maneno mdomoni! No way! Tumia tu simply akili au common senses(no need ya ufunuo hapo au kumsakizia RM)- soma ulichosema! Very suprising indeed, as a matter of fact, very destructively funny!!!!!!!!!

  Pia umesema ivi..’’Kwahiyo kama Zaka yako unaitoa kwa nguvu ya kifungu hiki cha Mt 23:23, ukilihalalisha hilo linalozungumziwa hapo kwamba ili mradi limezungumziwa katika Agano Jipya, basi linalihusu Kanisa, utakuwa umepotezwa njia’’ Sasa nikuulize swali ambalo nilimuuliza Mguluma Amin hajajibu mpaka sasa na nitamuuliza tena ktk majibu yangu kwa post zake 2 sasa ivi- KWA HIYO UNASEMA ALIYOSEMA YESU HAPO, SISI WANAFUNZI WAKE , HAYATUHUSU BALI ALIWAAMBIA MAFARISAYO TU? jibu ili hapa haraka kisha jiandae kweli kweli kwa yatakayojiri-nina hamu na weye/na jibu ilo!confirm fasta hapo plz!

  Umenicheka sana ivi..’hahahaa ati kwa kua nataka andiko live linalokomesha Zaka LEO au ilo andiko-Mt 23:23 na kuita mie jeuri na kunisikitikia kua nitakula hasara na kua sikusikii na umenilaumu kua nimetumia akili na logic zake’’- Kucheka ni njema, enjoy my brother, me too like it sana ila cheka penye mashiko otherwise ambulance ya Kaswahili na uswazi wake watatinga sasa ivi kukutwaa! Kwa nini kwa kua baada y akucheka, HAUJANIONYESHA KINAGA-UBAGA ANDIKO ILO LINALOKATAA ZAKA AGANO JIPYA ili tuache mara moja! Umecheka tu and then ukafanya faulu ile ile ya kubandua tu maandiko kokote na kuyabandika vyovyote bila kuzingatia 2Timoth.2:15! Ndio maana ukafanya kituko iki cha kuchukua andiko hili-Mdo 12:7 kuhusu kuvuka nyundo yaani swali ilo nililowauliza na kisha ukanogewa kubandua na kubandika jingine ili tena – Rum 10:2-3 na ukasisitiza ili neno nzuri kabisa tu..“Kwa maana KRISTO NI MWISHO WA SHERIA, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.” –

  Sasa, pale juu umesemaje? Kua Yesu ktk Mathayo.23:23 anasemelea/ridhia-maana alikubali pale waendelee kutoa zaka-kwa Sheria sasa unasema Yeye ni mwisho wa Sheria!!!!!! Nikikuambia raise the standards ktk debating skills/smartness, utakasirika? Nikisema cheka penye mashiko ili kukwepa very hungry and angry ambulance ya Mr .Uswazi, utasema nakukwaza? Umeona hapo juu ORIGINAL MKANGANYIKO WAKO? Be fair Lwembe at least for yourself, sema kweli, ivi unadhani napaswa kweli kukusikiliza kama ulivyonitaka kama mbwembwe zenyewe ndio izi? Unazo qualities/qualifications kweli? ndio maana cheo chako ulichokitwaa cha kua Moderator wetu ktk mjadala huu naona ni fix za mjini bro-yaani huna sifa kabisa! Wewe ndio haswaa Unatakiwa kua heavly moderated kama nilivyofanya apo juu, we bado sana Kaka kusema kweli.

  Kama kawaida yenu na Amin Mgulumu kua na, confidence pori za 200% and baseless kumtaja-taja RM bila hata haya ivi..’Ndio maana sisi tunahitaji kujazwa RM ili atuongoze kuyafikia hayo anayokuja nayo Paulo’’-Look at you! utadhani kweliiiii na kwamba uko seriosiiiiiiiiii, unaongea maneno ya Kirohooooo kama kweli uko ivyo! Mpendwa bwanaa!Ungekua umejaa ki kwelii, ungesema uliyosema against zaka LEO? Acheni mbwembwe Wandugu.

  Kisha unajidai vile vile kama kiroho-roho vile kumbe hamna lolote ulichekecha liliosemwa na Neno ktk kuangalia kweli zake nyingiiii ndani yake,ati umesema..’’hayo ambayo hakujifunza kwa Gamalieli (shule zenu za teolojia) bali kwa UFUNUO (huo mnaoudharau) kwa Bwana Yesu Kristo mwenyewe; Gal 1:11-12’’-Hakuna anayedharau Ufunuo wa Roho na wala asiwepo anayedharau matumizi ya Akili ya Mtu aliye na Roho kama Paulo huyo huyo Mdo.26:25- aliposema mwenyewe..’’ninasema maneno ya KWELI NA AKILI’’, ivyo kuna sehemu ya Ufunuo(toka juu kuja chini-au toka kwake kuja kwetu na KUNA AKILI/UELEWA/UFAHAMU toka/kupitia Sisi na vilivyomo- toka kwakwe huyo huyo Bwana wa vyote.Ivi sijui mnashida gani na swala la kutumia Akili! Are U humans? Au SAVED humans? and a u SAVED humans under/in with the Holy Spirit? Shida nini nyie?

  Ati unatisha ivi..’’Mimi Nitajuaje mambo hayo ya Mungu ambayo yako beyond akili?= Ni kweli yako beyond lakini mue mnaku wa kweli kama mie, kusema kweli/kukubali kweli! ukweli ni kwamba si yote ni beyond Akili-acheni ulongo! e.g ‘usizini’, ‘usiue’, ‘fanyeni kwanza haya ya fadhira bila kuacha na yale mengine(ya Zaka)- Mt.23:23, Wala msiche kukusanyika pamoja, furahi nasema tena furahini, ‘’Tafuteni KWANZA ufalme wa Mbinguni na Haki yake’’…, ‘’Haki yenu isipozidi ya Mafarisayo KAMWE hamtaingia Ufalme wa mbinguni’’ nk.. sasa mbona simple tu hapo?, clear kabisa yanaeleweka kwa AKILI hii hii ya sembe, hamna complications! Mnaleta Ulongo-ulongo tu na maneno yenu ya Kipendwa tuliyozoe ambayo mie nilishayapima na kuyaacha siku kadhaa, yale ya mishituko-mishituko, maangalizo-angalizo, mikwara-kwara,hofu-hofu, woga-woga, maonyo-maonyo,makeo makeo nk..yote hayo ni mema nani mazoea mazuri kua nayo IKIWA TU YANATUMIKA sahihi, si hii yenu ya kukariri na kubandika-bandua vitisho ovyo kabisa ati akili mbaya sana, hatari kweli utadhani ndani ya heads zenu mna ice cream na any time hua zinamelt kisha mnabaki na atmosphere tu! badala kumshukuru Mungu Baba kwa kutupa Akili njema tena yenye afya si ngonjwa na yenye upako wa Roho.

  Ati..’’Mkristo yeyote aliyejazwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu! Kuinukuu Mt 23:23 ili kuiendeleza Sheria kwa hao waliokombolewa kwa Damu ya thamani’’-Ndio yale yale maneno kama ya kiroho kilicho shiba kweli vile but ukiyapima/chambua/tazamisha ktk kweli nyingi au nyingine ktk Bible, unakuta ni mbwembwe baseless tu za Kipendwa! Unaona pia unarudia tena sick confidence 200% za kumtaja-taja RM bure maskini wa Mungu!-why mnamsakiziaga mambo ivi wala hana habari/hajawatumeni? Na tena hapa unaelekea kusema ALICHOKISEMA YESU ni YEYE aliendeleza Sheria, right? sasa confirm na hili tena kama kulee juu nilipokuuliza Nitangoja nione na hili-yaani I can imagine utakavyopotea ktk majibu yako! Tehe tehe! yaaani utoweka mbali hamna mfano, wewe tena, du! nakupata sana tu ha ha aha, utaselelekea mita mia hata utapaaa! Kazi kweli! nangoja kwa hamu kaka yangu Lwembe

  Kisha umesema kweli hii…’’Torati yote INAISHIA kwa Kristo! Zaka nayo iliyo sehemu ya hiyo Torati au Sheria, nayo pia inaishia hapo ndg yangu’’-nakubali kabisa SI TU KWAKUA UMESEMA VIZURI ILO BALI NENO KWANZA LILISHASEMA IVYO…lakini swali hapa ni..IPI ZAKA ISIYO KTK TORATI ISIYOISHIA ILIPOISHIA TORATI-umeelewa Kiswahili cha Kaswahili hapo? Aya nipe jibu-ha ha ha nimekukamata hapo LIVE! Nakuona tu unavyopumua Kaka, well, maliza upumuaji, toa jibu plz.

  Umenitaka tena niwe msikivu na niache kutumia Akili(sijui nitumie maji au hata Roho lakini sijui atanitumiaje bila kua na Akili-mnaona statements zenu kama vile zina kilo au kiroho kumbe fix tu) kisha ukasema unionyeshe yaani kunifundisha kitu barabara kabisa kuhusu kukoma kwa ukuhani na kisha kwa confidence zile zile 200% za pori/baseless bila hata haya ukafanya ile foul ya bandika-bandua Maandiko kwa kunipa ili-MT. 26:65 la Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, ukalinganisha na andiko hili-LAW 21:10-kuhani mkuu akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake” =Yaani unajua nasikia kunywa maji kwanza au sijui nipasukeje na kicheko, mwe! ha ha ha ha ha! Hapa nacheka kuna mashiko si kama yako ileee! SWALI dogo tu hapa na hoja yako hapa inakufa mara moja ni-ktk Akili ya kawaida kabisa(narudi kule kule maana tumezoea kumsingiziia/sakizia RM-ofcoz anayo sehemu yake kubwa ya kuyajua ya Mungu) but kwa hapa-Wazo kuu linazungumwa ktk maandiko hayo mawili ni sawa? Ile ‘asiyachane mavazi yake’ ktk Walawi ni sawa na ilo la ‘kuyachana’ alikofanya Kuhani ktk iyo Mathayo? Jamani! Wandugu! Lo!

  Tena kwa kujiamini ukasema ivi..’’Ukuhani wa Kilawi unaishia hapo alipouchukua Mwenyewe’’ ukimaanisha kwa yule jamaa kuchana mavazi yake then Yesu akatwaa Ukuhani, jamani! that means before this tukio, alikua bado si kuhani au hajatwaa Ukuhani!!!! Mwe!! Opsuuuuuu! nipumue kwanza maana mpaka inachosha! aisee, kama ufahamu wenyewe ndio huu wa Mtu(Moderator wetu) ktk hot debate hii, tumekula hasara, mapindizi ya Misri na yaje sana ivi, tupate mwingine!

  Mwisho ukatania ivi-si mbaya anyway inaleta u-lively ktk debate, I love it, ukauliza..’’Duh! Sungura utaweza kusoma kweli? Nilikuwa naendelea lakini kwa ajili yako naishia hapa!=JIBU: lo! asante kwa kuishia hapo maana kwa hakika toka ulikoanza na mpaka hapa, ukiondoa machache, mengine ni ni off! Unajua Lwembe, on serious note, sikuonei wala kuku-degrade! Embu nakuomba fanya ivi, print post yako kisha usiku maliza ratiba ya family hapo eg kula, sali na wanao na wife, kisha ukiwa bed, so relaxed with CD ya nyimbo za polepole a.k.a kuabudu then isome taratibu..U WILL AGREE WITH ME KAMA KWELI NA WEWE NI MSIKIVU NA UNATAMANI KU-raise the standards KTK DEBATE, HIYO PAPER UKIINZA TOKA A-Z, ni full of atmosphere sehemu kubwa my brother. Kama nasema ulongo au nakuonea, basi nionyeshe ktk reply yako wapi nakuonea!

  God bless u lovely friend, Moderator plus Professional Mshauri wetu hapa.

  Press on.

 54. Nami niwashukuru nyote: Nguluma, Seleli, Lwembe, Siyi na wote tulioshiriki mada hii. Ndio maana ya blogs kama hizi kuwepo kwa ajili yetu.

  Ninawabariki nyote.

 55. Amin Nguluma,
  Moyo unanisukuma kukushukuru pia. Nakutia moyo kaka uwe mberoya zaidi wa maandiko.
  barikiwa sana

 56. Siyi,
  Mimi nimekuelewa rafiki yangu, tatizo ni hawa wengine hawakufahamu!
  Mimi nimekuelewa tokea mwanzo ulipochangia kuwa haujui kinachoongelewa, na hata Zaka yenyewe hujui ni nini, na kwa kadiri unavyoendelea na maelezo yako, inaonesha pia kusanyiko lako walisahau kutengeneza fundisho la Zaka na hivyo wanaendelea nayo ile ya Sheria, ambapo Sheria ya Zaka kulingana na maelezo yako itakuwa ni Sheria ya Maadili, maana kama ingekuwa ni temporal law, basi ingeishia kwa Kristo! Unaona jinsi ambavyo mafundisho yenu yasivyo na mizizi katika Neno la Mungu?

  Jaribu kusoma mada na post za wachangiaji waliofuata wametoa maelezo mazuri sana na rejea za Maandiko kuhusu waliyoyasema. Chukua Biblia yako kisha wafuate nyuma, utaelewa kinachozungumziwa, ni ZAKA na si matoleo mengine, na wala hatuzungumzii nani anatoa zaidi au nani anakwepa, bali tunaitazama ZAKA ili kuubaini ukweli unaohusiana na utoaji wa Zaka, Je, ni amri ya kanisa au unaitoaje kama unatoa!!!?

  Seleli pia ameshindwa kukamata kinachozungumziwa, badala ya kuitazama mada yeye katumbukiza mambo ya utoaji na kung’ang’ana nayo hata maelezo yake yasingekuambia haswa ni nini anachokiongelea!!

  Jaribuni kuwa wasikivu!!!

 57. Mpendwa Siyi nashangaa jinsi ulivyoshikwa na hilo tango mwitu ZAKA KWA KANISA kiasi ambacho unadhani ni fundisho la Mungu.Hilo ni pokeo kama lile la ubatizo wa watoto wachanga kwenye baadhi ya makanisa yetu.Tafakari kauli yangu hii utanielewa sana na Mungu akubariki sana

 58. Siyi nimekuuliza swali jepesi ”hoja gani hiyo”?
  Hujalijibu halafu unaanza kuongea mambo ya kitoto. Hatuko kwenye hii blog kusemasema chochote wala kupoteza muda, hili ni kanisa la mfumo wake. Kwa hiyo mambo ya kitoto hapa si mahali pake.

  Kama unadhani wokovu si lazima basi achana nao wala usipoteze muda wako. Kama unadhani mambo ya Mungu si lazima,mbona unapoteza muda wako kuyafuatilia? achana nayo.

  Unataka tuendelee kufafanua neno ”lazima” mpaka saa ngapi? Kwani tunafundisha watoto wa kindergarten hapa? Kama hamtaki kuelewa si mkubali kuwa mjadala huu si size yenu.

  Ulishawahi kusoma mahali popote kwenye biblia kuwa kuna watu walileta zaka miguuni pa mitume? Au Anania na Safira walichokificha biblia yako inasema kilikuwa ni zaka?

  Quit babyish mindset!!

  Msidhani kuwa hatujui maana ya utoaji. Tunapoongelea zaka hatugusii maeneo mengine ya utoaji si kwa sababu hatuwezi kuyasemea,bali ni kwa sababu tumeamua kujikita kwenye hoja moja iliyo mezani.

  Ati Mitume walipoitikia wito kama huu, mali zao zote, walizifanya za shirika kwa ajili ya kazi ya Bwana!

  Siyi toa basi na wewe suruali zako miguuni pa mchungaji wako ili zifanywe za shirika kwa ajili ya kazi ya Bwana!
  Mbona unampa zaka tu ambayo ni kijisehemu kidogo sana cha mali ulizonazo kama kweli unataka vitu vyako viwe vya shirika kwa ajili ya kazi ya Bwana?

  Usidhani kuwa hii hoja nimeivamia brother, ninajua ninachokisema na wala sijakijua leo. Mada nisizozijua huwa sichangii zaidi ya kukomenti inapobidi.

  Wewe kama unadhani kila kilichoandikwa kwenye biblia kinakuhusu na unatakiwa kukifanya bila kujali majira na nyakati zake, basi fanya ili umuoneshe Mungu jinsi ulivyo mtii na mnyenyekevu!

  Siyi is that clear brother?

 59. Mrs. NYAKI,

  Sidhani kama ulilosema ni kweli, kama umepitia michango yote hapa, si mimi tu nayechanganya lugha labda ungekua mkweli ungesema..naongoza kuchanganya!!! Hata ivyo, shida nini, izi ni lugha tu za Wanadamu kwa matumizi yetu, kwa ivyo, be free kutumia . Pia hoja kama ipo, ipo tu, haiondolewi na lugha-hiki ulichokisema nacho ni ajabu tu! maana mbona mie nimeelewa hoja/points za wengine walipotumia au kuchanganya Kiingereza!

  Kwamba..’’MADA ZA WENZIO ZINAELEWEKA= maoni yangu ktk ili ni kua kama umesema ivyo, kuna tatizo somewhere! Kama mtu anasema Zaka ni chanzo cha umaskini Kanisani au anaweza akatoa au akaacha haisumbui au anaelekea kusema, anaweza fanya uko na kule na hapo kanisani/ukuhanini kwake, si haja sana kwa kua tu anajali yatima na wajane au kama mtu anaweza ona andiko kabisa la Zaka kabla ya sheria Mwanzo 14:1-20 na Mathayo.23:233 kisha akasema hiyo haituhusu leo au Yesu alikua anawaambia Mafarisayo tu sisi hatuna haja nayo, then UNASEMA MADA ZINAELEWEKA, basi nakuona ni wale wale tu watorokaji Utaoji kwa mbwembwe nyingii na ujanja wa kushibisha nafsi tu na kubania kwa ajili ya ‘Utafuteni kwanza Ufalme wa Dar-es Salaam kisha wa JUU baadae’’!!!!!!!!

  Ukitumia Kiingereza au basi kukusaidia kuulewa kama Kiingereza una case nacho, hata Kiyunani/Kiebrania wakati wa kufundisha/kujadili ili kuleta maana halisi ya mwanzo au msisitizo au vocabulary inayotakiwa kubebe uzito sawa wa mada/Neno/Wazo unaloshughulika nalo, ni kawaida kabisa ktk habari ya kutafuta na kushare maarifa, ivyo si kua wasio na point ndio wanakimbilia ivyo bali wenye point na wenye kukazana kuleta /weka peupe iyo/izo point. Si unaona na wewe hapa umekazan kweli kama mie kwa hili….kuna kakiingereza/Kakiswahili hapa-neno ‘’pointi’’ tena mixture yenyewe kama yangu vileee… ‘’WATU WASIO KUWA NA PONTI.-si unaona? Ni mambo ya kawada tu tena safi/matamu tu.

  Ninyi Wana Mahesabu mnasema ivi….’’ TUNAJUA KUWA HATA UKITOA KWA MWAKA ZAKA HAIWI 120% BALI INABAKI KUWA 10% TOFAUTI NI KUWA TU 10% YA MWAKA ITAKUWA KUBWA KULIKO 10% YA MWEZI’’..Hii ni kitu gani? Umesema nini hapo? Sasa sijui hapo uweke ktk Kiswahili kingine chepesi au Kiingereza maana nimetoka kapa kabisa dada! Na Kwa ulichosema hapo, Je wajionaje wewe ndugu yangu, unaelekea kukimbia au unapenda sana kutoa Zaka na matoleo mengine bila mijadala na maneno mengiiiii ya wenzio? Nitafurahi kujua msimamo wako kuhusu Zaka Leo au Jana ilI nisipate tabu bure kumbe uko side fulani halafu umetafuta tu pazia ya Kiingereza kujificha!!!!!!!!!!!

  Press on

 60. WEWE SELELII HATA KAMA UNA HOJA KUCHANGANYA KWAKO LUGHA KUNAKUFANYA UONEKANE HUNA HOJA, MADA ZA WENZIO ZINAELEWEKA ILA WEWE UNACHANGANYYA KIINGEREZA NA KISWAHILI NI MTINDO UNAOKIMBILIWA NA WATU WASIO KUWA NA PONTI.

  HALAFU MWANZISHA MADA SISI WANA MAHESABU TUNAJUA KUWA HATA UKITOA KWA MWAKA ZAKA HAIWI 120% BALI INABAKI KUWA 10% TOFAUTI NI KUWA TU 10% YA MWAKA ITAKUWA KUBWA KULIKO 10% YA MWEZI.

 61. Lwembe,
  Ha ha ha, Kwani kutoa zaka ni kisingizio cha kuipeleka mbele kazi ya Bwana? Ha ha ha!! Napenda kukwambia kuwa, siyo kisingizio ila ni jukumu mojawapo kwa wote wanaliitia jina la Bwana. Kama wewe hulioni kama ni jukumu, basi fanya matengenezo hapo, maana umepungua pakubwa!!!
  Kuhusu sheria, nashangaa rafiki yangu unazibeza weeeee!! Yaani na ujanja wako wooote, umeshindwa kutambua kuwa dunia na vyote viijazavyo viliumbwa kwa sheria ya Mungu, vinaitii hiyo sheria, na vitakuja kuondolewa kwa sheria iyohiyo?? Au hukusoma??
  Pole ndg yangu kama umegupikwa na sheria za muda(temporal laws)-zilizotuleta kwa Kristo tu. Nafikiri una kazi kubwa ya kujifunza torati!! Otherwise, utapotea tu, maana torati ni kioo…
  Ubarikiwe sana.

 62. Sungura,
  Una hoja nzuri kibinadamu zinazokubembeleza usitoe zaka. Kwa mtu asiye wa rohoni, yaani mwenye carnal mind tu, anakuelewa tu vizuri na huenda akaadopt msimamo wako huo.
  Umesema vyema kabisa zaka siyo ya lazima. Ni kweli. Na kwa Mungu siyo zaka tu, bali mambo yote kwa Mungu siyo ya lazima. Hata wokovu siyo wa lazima!! Mungu hana tabia ya kulazimisha mtu afanye anachokitaka.
  Hata kwa wasabato, kutoa zaka siyo lazima. Akina Siyi tunatoa tu kwa sababu ya kuitikia wito wake wa enendeni… Mitume walipoitikia wito kama huu, mali zao zote, walizifanya za shirika kwa ajili ya kazi ya Bwana. Hivyo kutoa zaka kwa kila pato ni suala la uongofu tu, maana hata kipindi cha mitume, wasiowaongofu walikuwepo – akina Anania na Safira.
  Hivyo basi, tunatoa ili kazi ya Bwana isonge mbele. Hili linaweza lisiwe na maana yoyote kwako, lakini kwa Mungu lina maana tena kubwa sana. Kuna baadhi ya watu ndani ya Biblia ambao kwa mara ya kwanza, walidhani kuwa Mungu hana maana yoyote, japo walikuja kujutia kwa mashaka na mawazo yao hayo potofu. Soma Mwanzo 22 na 26.
  Ubarikiwe sana mjoli

 63. Sungura,
  Siyi anasikia kizunguzungu! Ngoja akaangalie kwenye ‘Sheria za Maadili’ na zile Amri Kumi zilizoko ndani ya sanduku, zile ambazo ziko kwenye Hekalu la Mbinguni, ili apate mwanga zaidi kisha atakurudia!
  Hahahaha…..! Siyi acha mzaha, sema Wasabato Zaka yenu mnaikusanyaje, chini ya Laana ya Sheria au mnatoaga tu kwa kisingizio cha kuipeleka mbele kazi ya Mungu?!!!

 64. Mpendwa Lwembe Mungu akubariki kwa fundisho lako kuu linaloifunua siri kuu ya Mungu.
  Kwa bahati mbaya Seleli bado anapingana na neno la Mungu lililo hai kwa kung’ang’ania mafundisho ya dhehebu lake.Simlaumu bali ninamshauri asome kwa makini post zote nilizotuma na ayasome maandiko kwa utulivu.Asome pia post ya Mwisho ya Lwembe kabla ya mchango wangu huu.
  Ninafuatilia kuona maendeleo ya kukua kiroho kwa wote wanaopenda kumjua Mungu wa kweli

 65. Sungura,
  Laiti ungekuwa kwenye akili/mawazo ya Mungu, kanuni zake, sheria zake, taratibu zake na pendo lake kuu, ungetii tu maana kuna wakati mwingine Mungu hutamwelewa na badala yake itakubidi kutii tu. Una hoja nzuri lakini sijui kama ni nzuri mbele za Mungu pia.

 66. Ok, kama kuhani mkuu sasa hivi katoka katika kabila la Yuda ambalo lina urithi (yaani halina katazo la Mungu la kuwa na ardhi) tofauti na kabila la Lawi ambalo Mungu alilikataza kuwa na ardhi, basi zaka inabaki kuwa hiari na wala si kutoka katika kipato cha mtoaji cha kila mwaka au mwezi au siku. Maana Ibrahim ambaye anasimama kama kielelezo hatumwoni akitoa zaka kutoka kwenye mali alizokuwa nazo, bali tunaona analifanya hilo kwenye eneo moja la kuteka nyara, na wala hatumwoni akifanya hivyo tena. Hata Yakobo mjukuu tunaona anamwahidi Mungu kuwa atamtolea zaka ikiwa ata..mfanikisha….

  Lakini zaka ya utaratibu wa Musa zaka haikuwa hiari au under a certain condition, ilibidi watoe kutoka kwenye kipato chao wala siyo kutoka kwenye nyara, au labda mpaka Mungu atakapowafanyia kitu fulani.

  Leo wewe kutoa zaka kwenye kila mshahara wako kwa mfano, kwamba na usipofanya hivyo ati ni dhambi, ni kutoa zaka sawasawa na wakati wa Musa (lazima) wala si sawasawa na wakati wa Ibrahim (hiari).

  Kuhusu zaka kuwa pesa, hilo labda hujaisoma tu sawasawa kanuni ya zaka ya wakati wa Musa ilivyokuwa inataka. Mojawapo ya matakwa yake ilikuwa ni kutoizidisha wala kuipunguza zaka yako, na kutokutoa pesa. Maana waliokuwa wanalazimika kuwauza mifugo wao ili waweze kusafiri kwa urahisi kufika Jerusalem (Hekaluni ) walilazimika kununua tena mifugo mara wanapofika Jerusalemu, wala hawakuruhusiwa kutoa hiyo pesa ati kwa sababu ndio thamani ya mifugo na mazao waliyokuwa wanakuja kutoa.

  Ni kwamba Mungu alitaka makuhani wapewe zaka kwa sababu walitoka katika kabila ambalo halikutakiwa kuwa na urithi wa ardhi, na hivyo zaka ndo ikawa urithi wao.

  Hebrews 7 does not talk about moral laws, it talks all about Tithe and Priesthood. So whatever the law changes it mentions, whatever regulations it mentions, they are all together Tithe and Priesthood related.

  Amesema kama ukuhani umebadilika, basi na sheria inabidi ibadilike. Kwa hilo badiliko la sheria linalosemwa si sheria ya jinsi ukuhani ulivyokuwa unatakiwa kupatikana, bali nisheria ya jinsi huyo kuhani anavyotakiwa kutendewa, ambapo moja ya alichotakiwa kutendewa na watu ni kupewa zaka kama urithi wake.

  Good, you got it right on regulations being set apart!

  Ufalme wa Mungu ni mfumo wa jinsi Mungu anavyofanya mambo yake katika utawala wake. Na sis kwa kuwa tumekubali kuingia katika huo mfumo ni lazima tufuata utendaji uliopo kwenye neno lake wa huo mfumo.

  Utawala ni upana wa eneo ambalo Mungu anaweza kudhihirisha mamlaka yake,
  amabayo kimsingi haina mipaka.

 67. @ Nguluma,
  Amina, brother!
  Tumshukuru Bwana zaidi atupaye moyo wa kujifunza Neno lake katika Upendo na Utii!

  Asante, na Bwana akubariki na akuzidishe katika tafakari ya Neno lake, ili tunapokutanika katika namna ya ulimwengu wa roho, basi kutoka katika pando la zao hilo la Tafakari, na tuliwakilishe hilo Tengo la “Zaka ya Tafakari ya Neno” tuliyoipata katika jitihada hiyo, tuilete mahali hapa, SG, alipopachagua Mungu, ili tuile sote, kusanyiko hili!!!

  Na Seleli naye awepo, ale pamoja nasi hicho tulichokileta, nayo makorokoro yake ya dini, arudi nayo kwenye kigunia chake, kwani hayo amevuka nayo huku yasikotakiwa! Hahaha…!

  Mbarikiwe nyote!

 68. Seleli na Sungura nyote wawili ni watu wa kutumia sana “akili na reasoning na resoning of reason, logic” na kwa kadiri ninavyoisoma michango yenu, sehemu kubwa imegubikwa na matumizi hayo ambayo nimewaonya mara nyingi kuwa Mungu hapendezwi! Angalia mnavyopasuana vichwa kwa maswali mnayoulizana? Hahahahaha.. mtafia jangwani bila majibu!

  Mungu ameyaficha majibu ya maswali yenu ya kitafiti yasiyo ongozwa na RM, Lk 10:21, “Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili (Seleli na Sungura); umewafunulia watoto wachanga (akina Lwembe); Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza”
  Ndio maana kila mnavyohangaika kuyajibu maswali hayo mnaishia kuyarudia matapishi ya Torati na kuendelea kuishi kwayo kama ninavyomuona Seleli! Mungu ameyaficha majibu yake ili mdhihirike, amenifunulia mimi Lwembe, mtoto niwezaye kujifunza! Ninyi ni mijitu mikubwa, kumbe mnakulaga mpaka kwa mama ntilie, na wengine mnakula kwenye mahoteli ya kisasa hayo ma mega churches, kumbe hamshibi nyumbani, loh, hahahahah…!

  Tazameni, mimi ni mtu NILIYEOKOLEWA, kwa hiyo it is natural for me to relax hapo ninapouzindukia ukweli huo! Ukinikuta ninajibidiisha kujiokoa, basi hata huyo aliyeniokoa atakuwa ananishangaa ktk bidii yangu hiyo, maana ni ishara ya kukosa shukurani, na hivyo atalazimika kunifanyia la ziada ili nizinduke kutoka athari ya kuangamia inayoendelea kunishikilia, lile jinamizi! Nimewaona mnajisifia “kuubeba msalaba wako”, huko kujisulubu, Mt 10:38, “Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.” Inasikitisha kwamba umepitiliza na msalaba huo, hukumuona Kristo pale Njia panda ya Wakati akikuita, Mt 11:28, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”Pole sana ndg yangu, akili nyingi bila Maarifa!

  Haya, Seleli katika kujikanganya kwako kuhusu Zaka unasema,
  ““”Mimi nimemuonyesha WAZI WAZI KWA MAANDIKO HAYA..Mwanzo14:1-20 na Mathayo.23:23 kua Zaka inatambaa toka la Kale mpaka Jipya… Amin Jeremiah hawezi najua kuvuka iyo nyundo, angalia toka ameanza kujibu mpaka sasa, haja-establish kwa hakika kua ZAKA agano Jipya ni a big No kwa kua labda Yesu au Wanafunzi (Mitume),walisema hapana kwa ilo””
  Huku ndiko kujikanganya ninakokusema. Hiyo Mwanzo unayoinukuu haina uhusiano wowote na na hayo yanayoonekana ktk Mt 23:23; Moja ni Shukurani iliyojiviringisha katika Upendo na nyingine ni Tozo lililojiviringisha ktk Utii wa Sheria! Ndipo unapojipachika katika hiyo Mt 23:23, sioni ni kwanini unakataa nawe kuitimiza sabato ya Kiyahudi kama Wasabato, ilhali umevuka nayo! Beba vizuri ‘nyundo’ yako hiyo!!

  Sikiliza Seleli, usiwe muoga wa kukabiliana na ukweli, na hivyo kutokuwa tayari kusikiliza chochote kile zaidi ya kuendelea katika wishful thinking ya mafundisho ya dini at the expense of your precious soul! Wewe mwenyewe unakubali kwamba Mungu anao utaratibu, nakunukuu: “”…BUT kwa utaratibu-Mungu wetu ni Mungu wa Utaratibu…”Basi inashangaza hapo unapokazana kuuvuruga Utaratibu wa Mungu kwa kulazimisha taratibu za kanisa lenu kuwa ndizo za Mungu! Kama ni Zaka, Mungu ndiye aliyeianzisha, na kama ni vyeo vya Ukuhani, pia ni Mungu ndiye aliyeviasisi. Kwahiyo ni muhimu kuwa msikivu katika maelekezo unayopewa ili uende naye sambamba, vinginevyo unaweza kuishia kumtolea Mungu nje ya utaratibu kama Kaini!!! Utashangaa siku ukifika huko mbinguni, kifua mbele, ukitegemea hazina iliyofurika kwa matoleo uliyokuwa ukiyatoa, lakini kadi lako linasoma ZERO, uliwapa kanisa lako na si Mungu!

  Kwahiyo kama Zaka yako unaitoa kwa nguvu ya kifungu hiki cha Mt 23:23, ukilihalalisha hilo linalozungumziwa hapo kwamba ili mradi limezungumziwa katika Agano Jipya, basi linalihusu Kanisa, utakuwa umepotezwa njia, huyo aliyekuongoza huko amekupeleka machinjioni! Zaka inayozungumziwa hapo inahusika na Sheria, ndipo usijidanganye kuwa eti utampiga fix Mungu kwa kumchomekea hiyo Zaka yako, bali unakuwa umejiunga na hilo kundi linalokumbushwa wajibu, pamoja na akina Siyi!

  Seleli, unataka uoneshwe kifungu ‘live’ kinachokomesha Zaka hiyo ya Mt 23:23; hahahaha! Inanilazimu nikucheke kidogo maana mara nyingi nimekuambia ujeuri wako utakutia hasara lakini husikii, umetumia akili na logic zake, na ukajihakikishia kuwa hapa “hawezi najua kuvuka iyo nyundo”! Hivi hujawahi kusoma pale makufuli na minyororo aliyofungiwa Petro ilipojifunguaga yenyewe (Mdo 12:7)? Haya, hii hapa ‘Nyundo” ya Kweli, tazama inavyokuvunja miguu, msikilize mt. Paulo anavyokusimanga na juhudi zako hizo za kumtolea Mungu, Rum 10:2-3:
  “Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.”
  Basi hiyo ndiyo hali yao wooote wanaojaribu kuivusha Sheria ili iendelee kuwaongoza huku ktk Agano Jipya, ile Nchi Mpya! Haya endelea kifungu cha 4:
  “Kwa maana KRISTO NI MWISHO WA SHERIA, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.”

  Umemuelewa anachokisema mt. Paulo? Au kwako haya ndiyo yale mambo magumu ya Paulo aliyoyasema mt. Petro?? Petro alipozungumzia kuhusu kumuelewa Paul, hakuwa anabahatisha, alikuwa anatoa tahadhari kwetu sisi watu wa Mataifa ambao Injili tunayoletewa ni “package inayojumuisha AK lililohai na Miisho yake kuingia ktk AJ, vyote ndani Fungu Moja linaloitwa Biblia! Ndio maana sisi tunahitaji kujazwa RM ili atuongoze kuyafikia hayo anayokuja nayo Paulo, hayo ambayo hakujifunza kwa Gamalieli (shule zenu za teolojia) bali kwa UFUNUO (huo mnaoudharau) kwa Bwana Yesu Kristo mwenyewe; Gal 1:11-12, “Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.” Hebu liwazie jambo hilo, kwamba wewe unayetumia akili utayajuaje mambo haya ya Mungu ambayo yako beyond akili???? No wonder mnajirudisha wenyewe kwenye Laana, kwa “raha zenu!!!” Zaka iliyoamriwa katika SHERIA, inakoma na SHERIA yake, HAIVUKI kuingia katika Agano Jipya, kwa Mkristo yeyote aliyejazwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu! Kuinukuu Mt 23:23 ili kuiendeleza Sheria kwa hao waliokombolewa kwa Damu ya thamani, ni kosa linalohitaji kutubiwa na yeyote anayefundisha hivyo!

  MWISHO wa jambo huashiria KIFO cha jambo hilo! Basi unapovusha mizoga, ni dhahiri kuwa unavusha pamoja nayo na mabalaa yoote yanayoambatana na mizoga hiyo, ndizo hizo laana zinazoambatana na Torati. Naye Mungu hawajibiki katika jambo ambalo amekwisha liweka wazi kwa wale ambao ni watiifu, na wenye usikivu! Kwahiyo unapojirudisha katika Laana uliyotolewa kwayo, kwa hiari yako ya kumpendezesha mtu fulani, ule Unafiki, jua kwamba hakuna Damu tena ya kukuokoa! Ni jambo gumu, lakini linapaswa kusemwa hivyo ili libakie kuwa ni Kweli ya Mungu!

  Mungu anapokuambia jambo hili nimelifikisha Mwisho wake, kama kweli unao utii, basi hata kama hujaelewa ni kivipi, unapaswa kuamini kwanza. Torati yote INAISHIA kwa Kristo! Zaka nayo iliyo sehemu ya hiyo Torati au Sheria, nayo pia inaishia hapo ndg yangu, uwe msikivu, acha kutumia akili! Nako kutumia akili tunakokuzungumzia hapa, ni ktk muktadha wa Maandiko na si katika Uzezeta. Hakuna zezeta atakayeuona ufalme wa Mungu kwa taarifa yako. Naye anayejiingiza katika kuyatafsiri Maandiko apendavyo yeye, huyo amejizezetesha mwenyewe, Zaka iliyoamriwa katika Sheria aidha ilikoma au Kristo hakuwa mwisho wa Sheria!

  Kristo ndiye Mwisho wa Sheria, maana yake ni uvikusanye vyooote vilivyo vya SHERIA, usiache hata kitu kimoja, usije ukawa kama Akani, hata kikikupendeza vipi machoni pako, au ukakiona ni chema, tena unaweza “kumtolea Mungu”, nawe ukajiingiza ktk mawazo kama ya mfalme Sauli, ISULUBISHE akili yako, vikusanye vyooote, vibebe njoo uvitue miguuni pa Kristo, Kisha yasikilize Maelekezo Mapya; Usivushe chochote kile!

  Labda nikuoneshe tena ndg yangu Seleli ni kivipi mambo hayo ya Ukuhani ule wa Kilawi yanakoma pamoja na SHERIA iliyouzaa na vyote vinavyoihusu, ukiyaelewa vizuri unaweza ukamuelimisha na mshikaji wako Siyi ili uiponye nafsi yake.

  Sote tunafahamu kwamba kuraruka kwa Pazia la Hekalu ilikuwa ni udhihirisho wa KIMWILI wa kumalizika kwa Huduma ya Ukuhani wa Kilawi. Ndg Nguluma amelielezea jambo hilo akatoa na Maandiko unaweza ukayasoma tena kwa wakati wako. Lakini mimi napenda niwarudishe nyuma kidogo ili mlione jambo hilo linavyotimia kiroho kwanza, ndipo kuraruka kwa Pazia kunaweza kuwa wazi zaidi kwetu ktk maana. Basi kama Maandiko yanavyotufundisha, Sheria yote iliishia kwa Kristo. Jambo hili linajidhihirisha zaidi kimwili na kiroho ktk Maandiko hapo Msimamizi wa Sheria hiyo anapojiondoa katika usimamizi huo kwa HIARI yake mwenyewe ili kuyapisha Maaandiko yatimie. Msimamizi wa Sheria ni Kuhani Mkuu, Sheria yooote katika ujumla wake, pamoja na Zaka yake, na Amri Kumi zake, na sabato na vyote. Sasa, iwapo msimamizi hayupo, sheria itakuwepo kweli? Hebu muwe wa kweli, Seleli na Siyi, Sheria bila Polisi ina nguvu? HAINA!!!

  Angalieni ninyi wenyewe jinsi Msimamizi wa Sheria alivyojivua Ukuhani, MT. 26:65:
  “Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake”

  Nayo Sheria ya Ukuhani inasema hivi, LAW 21:10:
  “Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake”

  Hapa ndipo Sheria na Torati yake vinapokomea! Hao hapo, Kuhani Mkuu akirirarua vazi lake mbele ya Kristo aliye Mwana wa Mungu, unafiki umemuongoza kumkiri Kristo na kuuvua Ukuhani alioushikilia kwa Sheria iliyo Halali na sasa akilazimika kuuvua maana huyo aliye zaidi ya huo Ukuhani amefika! Isingewezekana akaendelea katika Ukuhani ilhali KUHANI mwenyewe amekwisha kuja!

  Ukuhani wa Kilawi unaishia hapo alipouchukua Mwenyewe na kisha kutupa sisi tulioipokea Injili upande huu. Tena ili kuufikia Ukuhani huo, akatuwekea mitume, wachungaji, walimu, wainjilisti na manabii katika kila kusanyiko lake ili watukamilishe tuufikie Ukuhani huo tulioitiwa. Hiyo ndiyo New Order!!!!

  Pia Mlawi hakuwa na urithi, kwa hiyo yeyote anayepokea Zaka, halafu akawa na mradi wowote ule, shamba au duka au ameajiriwa au chochote kinachomuingizia kipato, huyu atakuwa amekosea, ni vizuri amtafute Mungu ili apate kuongozwa ktk Njia sahihi, yaani kama ni yule aliyeitiwa Huduma hiyo na Kristo mwenyewe, vinginevyo aitii roho inayomuongoza, maana pia inayo kazi inayoifanya!

  Sasa angalia pia Ukuhani wa Agano Jipya unapoishia, hapo nawe unaporirarua Vazi lako ulilovikwa, ukiipa nafasi Chuki, Tamaa ya mali, Uongo, … endelea kujaza mwenyewe, nk!!!

  Duh! Sungura utaweza kusoma kweli? Nilikuwa naendelea lakini kwa ajili yako naishia hapa!

  God bless u all, friends!

 69. Sungura,

  Sentensi hii ‘’’siwezi kuwaswaga wote mpaka Dar na hua natoa Zaka uko home kwa njia ya mifugo’’….. ilitakiwa kuweka neno ‘’MALIMBUKO’’ kwa wazaliwa wa kwanza.
  Je Biblia inasema kwamba uwauze hao ng’ombe halafu ukatoe hiyo pesa uliyowauza? JIBU: Biblia inasema/inaonyesha nitoe Zaka kama Ibrahimi ..Mwanzo.14:1-20 na muongozo wa YESU Mathayo.23:23 na kwa kua zaka ni tenth of ya Mapato/Mali yangu kwa hiyo Mali/Kipato nilicho nacho ni nini sasa? Ng’ombe siyo? Therefore, ninaweza hesabu ng’ombe kumi kati ya Mia-nikatoa au nikauza hao mia kisha pesa 10% nikatoani kitu kilekile au nikatoa Magunia Kumi kati ya Mia ya mahindi au nikauza Mia kisha ela sawa na magunia kumi nikatoa-Swala hapa ni Zaka kutoka toka kati ya income/mali/vitu vyangu,baaaaasiii! kwa pendo langu yet kwa maamuzi ya umuhimu wa kutoa na si kutorokea kwa uhiari ili mtu awe mjanja kutoa au kuacha kirahisi tu namna iyo.

  ‘’Kwa nini Mungu aliataka makuhani na walawi wapewe zaka? Ukijibu sahihi hili swali ndio jibu ya hicho ulichotaka nikuoneshe!’’ JIBU: Ukijibu kwa dhati kwa nini Ibrahimu alitoa Zaka au kile kilichomsukuma) then utalewa kwa nini nimekua nakuambia kwa nini HATA LEO ZAKA tunatoa na unatakiwa utoe.

  Ati Zaka haijawahi na haiwezi kua Pesa!!!!!!!!! SWALI: nini maana ya Zaka?

  ‘’Habari ya Waebrania 7: 12, 18.

  1. Which law must be changed also? Answer: Priesthood ownership as per Moses Law ie only Levi tribe . Change has happened since We have a new chief priest, Jesus Christ. He does not belongs to the family of Aaron, like Israel’s priests. What changed was the law about how people should worship (give honour to) God. That does not mean that the moral law had changed. The moral law means the law about what is good or bad. What God considers to be right and good is always right and good. That never changes.

  2.Which former regulation is set aside? Answer: The above reply connects remotely here too, in addition, Priesthood WAS through fleshly inheritance ie Arons line-the emphasis here is Priesthood by FRESHLY inheritance! this commandement/regulations is set aside- is weak system as for now we have the Priest not by freshly connections, He is made from Above, afterrall, He was from Judah Tribe! Thus, He is a Priest in the order/manner of Melchizedek- who was not a Livite yet a Priest

  Ati, nikisema ‘’Ufalme wa Mungu ni Utawala wa Mungu bado utaniuliza ‘Utawala wa Mungu ni nini? mwe! kwa iyo hujui ‘’Utawala wa Mungu ni nini’’?!!! au unanichezesha danadana tutoke kwa lengo la mimi kukukazania na kukukaba kotekote usitoroke na Zaka ili usiwe mwizi wewe as per Malaki:3:8-10-notice ni Mungu wa mbinguni amekuchana live kua wewe Mwizi-si mimi wala mchungaji wako. Aya ngoja tumalize kabisa kila janja yako- Kwanza, uliniuliza..’’Ufalme wa Mungu’’ ni nini? nikajibu thabiti kabisa Kimaandiko na kwa akili correctly ya sembe, hapo kwanza ULIKUBALI AU la? Kama la? Nipe maana yako sahihi kuliko yangu tuone! Naingoja na najua kama kawaida yako, utafunika na kuzusha mengine ya dana dana-karibu tutacheza vema tu, hamna shida, mimi tena Kaka , umesahau memory card rafiki yangu Kaswahili na Uswahili wake alivyooonyeshwa na nguvu nyingine nimezimeza! UTAWALA wa Mungu-ni Maongozi, Mamlaka na Utendaji wa Mungu Mbinguni na Duniani kwa viumbe vinavyoonekana na visivyoonekana, vyenye uhai na visivyo na uhai, period and full stop! Una kingine/jingine? Leta! Ila kumbuka..hatuongelei tu weeee ‘Ufalme wa Mungu’ mara ‘Utawala wa Mungu’’ weee viishie hapo! Mmh! so what!, hoja ni hii, nilisema na sasa nasema, kumbuka, Utawala/Ufalme huu una shughuli na sisi raia wake ivyo, tunatakiwa kuhusika nao kwa mali na hali na katika mali ndio hapo ZAKA utoe-ako usikapoteze Kaka akoo kapoint-niko makini apo..ehee! weweeee! Usikapelekesha weee mbali, ninakavuta tena haraka-kaja mara 7! Asante.

  Press on.

 70. Ok Seleli, kuna kitu hapa nakunukuu ” Kama nina ng’ombe 1000 nyumbani Geita hapa, nataka kwenda kuishi Dar na siwezi kuwaswaga wote mpaka Dar na hua natoa Zaka uko home kwa njia ya mifugo wazaliwa wa kwanza, nikiwauza na kisha nikatoa pesa thamani sawa na ng’ombe au mahindi magunia 5000, kuna shida hapo Zaka kua ktk form ya mane ? kuna dhambi? ipi?”

  -Je biblia inasema ufanye hivyo kama huu mfano wako au inasemaje kwamba uwauze hao ng’ombe halafu ukatoe hiyo pesa uliyowauza?
  -Je wazaliwa wa kwanza wa mifugo ndo walikuwa wanatolewa zaka?

  Kuna nukuu nyingine hapa:NISITOE KWAKE AU MAONO NA MZIGO ALIONAO! Kuna andiko ilo? Show me! We vipi!
  Unataka nikuoneshe!ok, jibu lake ni kwamba; kwa nini Mungu aliataka makuhani na walawi wapewe zaka? Ukijibu sahihi hili swali ndio jibu ya hicho ulichotaka nikuoneshe!

  Nakunukuu tena ”Umesema Zaka HAITAKIWA kua ni vitu vya kumtolea Bwana! Unaona sasa! wewe una matatizo bro ktk Utoaji”

  Hapa nilikuwa nakwambia kuwa zaka haiwezi kuwa kitu chochote, na kwamba pesa haiwezi, na haijawahi kuwa zaka. Nilichokosea hapo ni kosa la kawaida tu la kiuandishi, kama ambavyo wewe umesema ”HAITAKIWA” badala haitakiwi, lakini nilielewa unamaanisha nini.

  Kwa habari ya Waebrania 7, nilitaka uongelee zaidi kilichosemwa mtari wa 12 angalao na 18. ( 12 For when the priesthood is changed, the law must be changed also, 18 The former regulation is set aside because it was weak and useless 19 (for the law made nothing perfect), and a better hope is introduced, by which we draw near to God).
  Labda nirahisishe zaidi:
  1. Which law must be changed also?
  2.Which former regulation is set aside?

  Juu ya ufalme wa Mungu ukisema ni utawala wa Mungu bado nitakuuliza utawala wa Mungu ni nini?

 71. Sungura,

  Nami nilikujibu kwa vyepesi/Kiujumla sana but kwa Usahihi kabisa kuhusu ili ” The Kingdom of God?. Labda nirudie/niongeze/nifafanue, kwanza kupitia Neno(always kwenye Neno kwanza) then ukipenda kwa kutumia ufahamu/akili ya kawaida bila kuvuruga Neno.

  Kwa kutumia maneno ya Mungu haya…Luka.17:20-21-‘’Ufalme wa Mungu uko ndani mwenu’, Luka.9:2-akawatuma kuhubiri ‘’Ufalme wa Mbinguni’’ na kuponya wagonjwa’’, Mathayo.4:17-Yesu akaanza kuhubiri akisema, Tubuni maana ‘’Ufalme wa Mungu umekaribia’’ pia Mathayo.10:7- hubirini mkisema ‘Ufalme wa Mungu’’ umekaribia Therefore, kwa mantiki izo presented by the Word of God, UFALME WA MUNGU NI UTAWALA WA MUNGU.Importantly, Utawala huu haulei angani bali una matakwa yake yanayotakiwa yaingizwe/yatwaliwe/yasemelewe na kutekelezwa/kuchukuliwa na Wanadamu-ndo maana ya kuhuubiri Utawala huu kwa Watu kama alivyotaka Yesu. Kwa akili ya kawaida tu ya sembe, Unaposema ‘’Ufalme means kuna Mfalme aliyeoko au ana eneo analotawala/ongoza so mfano: Ufalme wa Nyerere au Mswati 11 ’’ simply means ‘Utawala wa Nyerere au Mswati 11’’ ktk eneo husika.

  Sasa, uki-connect na topic yetu ya Utoaji eg Zaka(usisahamu ilo maana ndiko nilisema Kuutafuta kwanza Ufalme wa Mungu kunahusisha pia Kujikana nafsi zetu na kisha kutoa eg Zaka ili kutimiza/ku-suppoert matakwa ya Ufalme huo, UKAKATAA!!!!!!!!-we wa ajabu sana-ndio ukaja na hili swali!). Ivyo Kama Ufalme(in fact niseme KWA KUA) Ufalme/Utawala huu una shughuli nyingi na sisi ni Raia wake basi, tunapaswa kuhakikisha matakwa yake yanasonga mbele na moja wapo ya njia za ku-push mambo ya Utawala huu wa BABA Mungu ni KUTOA zaka na zaidi ya zaka.

  Umesema huna shida ktk kutoa! Mmh! kweli? Nadhani shida unayo ktk Utoaji, usingeongea yote hayo Negative ktk Utaoji eg Zaka! Si bure! Huwezi chukua time na energy yote kuponda na ku-twist issue ya Utoaji na ukasema uko salama, usinidangaye hapa!

  Yes, Cha msingi ni kutoa kama mtu alivyokusudia moyoni mwake BUT kwa utaratibu-Mungu wetu ni Mungu wa Utaratibu na Kanisa –kama kweli wewe ni mtoto wa Kiroho Mtiifu na wa baraka kwa Mtu wa Mungu aliyewekwa kukusimamia weye Waebrania.13:17 na kama si mkorofi na kuvuruga watumishi wewe, basi Utafuata taratibu za Kanisa lako-kwa mantiki hii, huwezi ukawa Mkristo uliyetulia ukaacha nyumbani kwako ovyo, kutowajali wa nyumbani mwako kisha ukakimbilia kutoa eti nje uko kwa mhubiri na Mtume wa TV au yatima na masikini!, hayo yafanyike baadae BAADA ya hapo kwako/kwenu kwanza. Ukisema ili mradi tu unafanya/unatoa vyovyote kwa yeyote eti kwa kua moyo wako umejisia/umependa na hapo kwa kuhani kwako na shughuli zenu hazikwendi au hata kama zinakwenda but wewe kama Mtoto kweli, haushiriki chochote iyo ni kukosa Ufahamu wa nini maana ya kukaa chini ya maongozi, ni vurugu na ukorofi na ni Mkristo mwenye maudhi mengi kanisani na ASIYEKUA NA HEKIMA NA UTARATIBU hata kidogo, hafai!

  Tunaposema suppott kwa Wachungaji, si maanishi tu kumpa yeye TU bali ni pamoja na ivyo lakini pia kusaidia mambo ya kanisani kwako na maono yake, ni njia moja wapo ya mimi kua mshirika wa kweli na kusikia kuhusika na mambo ya home hapo na njia ya Mungu kunibariki pia napokunjua mkono na moyo Kutoa, heri kutoa kuliko kupokea Mdo 20:35. Hata kama Pastor wangu ni Bili Gates, Bible haijasema kua akifikia hapo, NISITOE KWAKE AU MAONO NA MZIGO ALIONAO! Kuna andiko ilo? Show me! We vipi!

  Zaka SIMPLY MEANS tenth of… na kwa mantiki ya Utoaji basi Kikumi cha yale niliyonayo/pewa/twaa iwe mazao, madini,mifugo, fedha vitu vingine kama vinafaa-si makapi, vilema na au vya by the way status but vyenye heshima na kicho kwa Bwana, NATOA, Kama nina ng’ombe 1000 nyumbani Geita hapa, nataka kwenda kuishi Dar na siwezi kuwaswaga wote mpaka Dar na hua natoa Zaka uko home kwa njia ya mifugo wazaliwa wa kwanza, nikiwauza na kisha nikatoa pesa thamani sawa na ng’ombe au mahindi magunia 5000, kuna shida hapo Zaka kua ktk form ya mane ? kuna dhambi? ipi? Namna gani hapa Sungura na ujanja wako unatwist-twist vitu vya ki-Sunday school hapa!!!!!!!!!!!!

  Umesema Zaka HAITAKIWA kua ni vitu vya kumtolea Bwana! Unaona sasa! wewe una matatizo bro ktk Utoaji!

  Umenipa ‘’Waebrania sura ya 7, hasa mstari wa 12-18 lakini nilishaga soma na nimesoma tena mistari yote.1-28 Sura nzima na nimejifunza/soma haya: Yesu Kristo ndio Kuhani wa Milele, Melkizedeki hakua wa ukoo wa Levi yet alipokea Titthe, Walawi ingawa walikua hawajatokea duniani na ambao walikua wanapokea Zaka, walitoa Zaka kupitia Ibrahimu kwa kua walikua wamo viunoni mwa Ibrahimu, Yesu kuhani wa Milele hakutokea ktk Levi ila Judah kwa sheria/matakwa ya Mungu kwa Mfano wa Melkizedeki ambae hakuna Mlawi yet Kuhani…nk, Aya unataka kusema nini? karibu.

  NOTICE: Kila swali unaloniuliza, najibu, wewe yangu unafunika! Time is coming soonest ambapo nitakuTAKA uyajibu YOTE kama ulinivyoniTAKA nifanye na nimekua mwaminifu ktk mjadala huu kufanya hayo

  Press on

 72. Seleli nimekuuliza kitu chepesi sana kwamba ”what is the kingdom of God?

  Je unataka kujua ni kiasi gani namtolea Mungu au kama unadhani nina shida na suala la utoaji, je shida yangu hiyo kama ipo kweli inakuhusuje wewe?
  Kama ambavyo kutoa kwako zaka hakunihusu mimi na watoto wangu, bali kunakuhusu wewe na wanao.

  Tunachotaka uelewe hapa ni kwamba usiwalazimishe watu kila wakipata mishahara yao ati ni lazima watoe zaka. Cha msingi ni kutoa kama mtu alivyokusudia moyoni mwake, kama ataamua atoe mshahara wake wote kwa watoto yatima,ni sawa. au kwa wajane ni sawa,au akiamua tu atoe sadaka kanisani ni sawa.

  Halafu usidhani kuwa wachungaji wote wanahitaji support ya washirika, tembea uone. Kuna sehemu zingine washirika wanahitaji support ya mchungaji. Kama wewe mchungaji wako anahitaji support mpe wala usiache,lakini usilazimishe kila mtu afanye hivyo. Yesu hakusema wapeni wachungaji vitu bali alisema wapeni watu vitu. Kama mchungaji naye anauhitaji tutampa maana naye ni mtu.

  Seleli unatakiwa kuelewa kuwa zaka haikuwa kitu chochote almradi ni moja ya kumi, hapana. Zaka haijawahi kuwa pesa si kwamba hapakuwa na pesa, bali ni kwa sababu Mungu hakuagiza zaka iwe pesa.

  Unaponijibu kwa swalai kama zaka haiwezi kuwa mojawapo ya vitu vya kumtolea jibu lake ni rahisi sana,haitakiwi kuwa!
  Sasa rudi unijibu la kwangu kwamba lini zaka imewahi kuwa pesa kiasi cha wewe leo kutoa pesa kama zaka?

  Nilikupa kitabu cha Waebrania sura ya 7, hasa mstari wa 12-18, soma uniambie umejifunza nini.

  Na kama unakubali kuwa zaka ni hiari basi usitake kila mtu akipata mshahara wake lazima atoe kikumi! Anaweza akaamua kutoa kwa namna nyingine.

 73. Sungura,

  Ulihitaji kung’amua tu mara moja si lazima nikufahamishe, ni wazi kwa mtiririko wa mawazo/ michango ya mtu hapa, unaelewa tu nia au mlengo wake mara moja Sungura mbona mie nimelewa siku nyingi mlengo wenu!

  Asante kwa offer yako hii kuwapa ‘support yako Watumishi au Kazi ya Bwana nilipo, aya sasa ndio maneno ya kuongea mtu wa rohoni na anayejenga Kanisa Ila nashauri, anza kwanza pale kwako, toa iyo support kwa kuhani, kanisa,programme zake hapo unapolelewa na kulishwa na kwa huyo atayewajibika mbele za Mungu kutoa hesabu ya maisha yako mbele za Mungu(ulezi wake kwako) kama Neno linavyowa-task gravely Waebrania.13:17 Makuhani wetu hawa wa leo ambao michango yenu imejaa kebehi a dharau dhidi yao mkitaka kufanya mnavyotaka Kanisani na si chini ya utaratibu ulioamriwa/wekwa kama Lwembe alivyo-note ingawa umepitiliza kama hukusoma point yake iyo

  Kwamba ‘’zaka haina faida kwa Kanisa bali inaongeza laana ya umasikini kwa sababu ni watu wachache sana wanaolibeba hilo kongwa kwa furaha’’ ndio sitakuelewa kabisa brother Sungura. Ati Zaka haina faida ktk Kanisa na shughuli za umo? A u serious or umezidi utani sasa na kebehi kwa Kanisa wewe? anayeibeba bila kua na furaha nani? Wewe na wenzako au sisi?

  Zaka si lazima SIJAPINGA na wala sisemi ZAKA si Hiari, nachopinga ni kuchukulia kwamba, kwakua Zaka si lazima, isimaanishe kua tusitilie maanani/uzito kutoa na ivyo kutorokea ktk ukweli huo.Ungeniuliza mimi, ningekuambia ivi, kwa kua ni KWELI TUPU KWA AGANO JIPYA, ZAKA na hata UTOAJI mwingine wowote si KWA SHERIA AU KULAZIMISHANA kwa maana sasa tunafanya wa UPENDO NA KWA MOYO basi ninatoa zaidi sasa Zaka na zaidi ya Zaka kuliko wakati mwingine maana palipo na upendo, furaha,moyo kuna raha ya kufanya mambo zaidi tena kila mara na zaidi ya vipimo vilivyozooleka

  Kama Kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu(mamo Yake, Matakwa yake) hausiani na kuyaacha yote na kuweka agenda ya mambo ya mbinguni mbele Mathayo.6:33 au kuyakimbilia ya mbinguni, kuyajali ya Mungu kwanza(eg Kutoa Zaka na mengine) kisha yetu, basi kweli AMUA/DHANI KWA UPYA kama kweli sijui manaa ya Ufalme(Serikali/Utawala na interests) wa Mungu.

  Yesu alisema ivi kuhusu kuisulubisha nafsi…Mathayo16:24-25 na Luka.9:23-24-maneno anayotumia Yesu mwenyewe hapo ni ‘’Kujikana mwenyewe’’, ‘’kuubeba msalaba wako’’ tena si siku moja bali.. ‘’kila siku’’. Na Yesu yuko very SPECIFIC kwa kusema..Mtu AKITAKA(Si kulazimishwa) KUNIFUTA basi AJI( sio nitamsaidia!!) bali yeye mwenyewe AJI/AI-kane nafsi yake( ndio suluba hiyo/ndio kusulubisha/kuitesa/itia adabu nafsi ivyo) kisha abebe(sio Mimi Yesu nitafanya ivyo) msalaba wake(notice neno MSALABA ktk Biblia ina maana ya Kusulubisha/mateso/kujikana/sadaka nzito nk) na kumfuta YEYE kila siku ( manake msalaba/kujikana/kutiisha nafsi/kuinyuka itulie/kuisalimisha kwa matakwa ya Yesu/ya mambo ya rohoni, kuitandika makofi ya mbele na nyuma mpaka itulie ni KILA SIKU. Kama hujaelewa mpaka hapo, nitumia maneno ya mchangiaji mwingine humu kwa mada hii ambayo najua aidha haukuusoma kabisa au ulisoma juu juu tu ukakimbia moto ule wa ushuhuda wake ndugu Shoo GAP kua, Watu wenye shida ya Utoaji watakua na matatizo makubwa kuliko haya za zaka.

  Ninalewa sana Maandiko haya kuhusu Zaka Kale na Jipya.. Mwanzo 14:1-20 na Mathayo.23:23 ndio maana napiga kelele(nahubiri/fundisha), je wewe waelewa maandiko hayo? Naomba usibadilishe MANTIKI kuu, ukachukua minor na uache ujanja, ninafuatilia kila nukta! SIJASEMA NIPE ANDIKO LINALOSEMA ZAKA MSITOE KWA LAZIMA-nilichowatakeni wewe na Yeremia na mwingine yoyote NIPENI ANDIKO LINALOSEMA WAZI WAZI ZAKA AGANO JIPYA STOP! Hapo sasa! msikwepe!maana mie nimewapa hayo kuonyesha hakuna stop.Kazi kwenu/kwako, nakungoja na nitakukumbusha iyo pini

  Nimedokeza kua si mapokeo ya ki dhehebu/dini/imani ni PEPO au evil, ni kutokuelewa tu. Yesu alipinga BAADHI ya mapokeo lakini ni ukweli pia aliishi kati ya na ndani ya BAADHI ya mapokeo , kama ni msomaji wa Bible hili halihitaji kutuchukuali muda, ivyo usinishange mie, si kwanza na kama mapokeo yananifanya na kunisaidia mie kuisulubisha nafsi, kujikana sana na kuubebea msalaba kila siku bila kujipa ahuheni, I am telling you, I like them and ni worth it, hayana shida kwa maani iyo hata kidogo AS LONG AS HAYAVURUGI MAANDIKO basi, simple tu namna iyo.
  Kwamba wapi zaka katika Biblia iliwahi kuwa dinari, shekeli, au shilingi? Kama papo nioneshe Seleli’’nani nakuuliza, Pesa haiwezi kua mojawapo ya vitu/mali za kumtolea Mungu? Huyo aliyeanzisha Zaka kuwa pesa, sina haja sana ya kumjua! Wa nini sasa kwanza? Kwani uanzishaji wake ULIVURUGA MAANDIKO KWA MANTIKI YA KUTOA KWA AJILI YA MUNGU NA SHUGHULI ZA MAMBO YA UFALME? Lini ilianza kua ivyo pia inanisaidia nini mimi leo? Si unaona tu unavyoangaika kutoroka Kaka!

  Ilo la pili lianzishe nami nitakufuta hamna shida Kaka.Amen.

  Press on.

 74. Kama hicho ndicho unachotamani ulitakiwa kuwa umeliweka wazi mapema Seleli, kuliko kuendelea kutusumbua na suala ambalo tumekupa majibu yaliyowazi.

  Kama kuna watumishi wa kweli wa Mungu au hata kama ni hapo kwenye kusanyaiko lenu wanauhitaji basi naomba unipe utaratibu ili niweze kuwapa ‘support yangu’ hilo wala halina tatizo.

  Hakuna faida yoyote ya maana ambayo zaka imeleta kwa kanisa zaidi ya kuongeza laana ya umasikini kwa sababu ni watu wachache sana wanaolibeba hilo kongwa kwa furaha.
  Na kama unataka kusaidia injili kuhubiriwa toa mali yako kama kanisa la kwanza walivyofanya kwa kuleta vitu vyao miguuni pa mitume.

  Kama unapinga hii sentensi kwamba ‘zaka si lazima’ inamaana unasema kuwa zaka ni lazima. Kwa hiyo umekubaliana na ukweli niliokwambia kuwa wewe hutoi zaka kwa hiari. Halafu Seleli kutoa zaka si kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu, vinginevyo hujui pia maana ya neno ”Ufalme wa Mungu”.

  Kwamba unaisulubu nafsi yako…,pole sana unafanya kazi ambayo tayari kristo kesha ifanya msalabani kwa ajili yetu. Yeye ndiye aliyesulubu nafsi yake kwa ajili yetu. Kazi yetu sisi ni kumfuata yeye. Hakuna anayeteswa na zaka zaidi ya wewe mwenyewe, mimi nimeshakwambia kabisa huwa hata sijisumbui kutoa hiyo kodi kama wewe unavyohangaika kutoa, na wala kutoa kwako hiyo kodi kusikufanye ujisifu hata kidogo. Unaipigia kelele sana kwa sababu ya kutokuelewa maandiko, ndio maana hutuelewi kabisa msimamo wetu, mpaka unauliza tuna matatizo gani. Pole!

  Kama uwezo wako wa kufikiri unakwambia kuwa ili kujua zaka leo si toleo la lazima unataka mpaka upate mahali katika agano jipya panasema zaka si lazima au panaposema zaka ikome kutolewa kwa lazima, basi sidhani kama muda wote huu tumekuwa tunajadili hii mada na mtu mwenye akili iiyokaa sawa juu ya haya mambo.
  Hebu soma Waebrania 7, hasa mtari wa 12-18. Labda kidogo inaweza kukusaidia kuelewa.

  Na baada ya kusoma paragrafu yako ya mwisho hapa ndipo nimetambua bayana kuwa tunahangaika na kupoteza muda na mtu ambaye kilichojaa kichwani mwake mapokeo ya ki dhehebu tu.

  ”Kuna swali niliwahi kukuuliza bila shaka, kwamba wapi zaka katika biblia iliwahi kuwa dinari, shekeli, au shilingi? Kama papo nioneshe Seleli. Na kama hapapo jiulize sana kwamba nani alianzisha zaka kuwa pesa, na lini ilianza kuwa hivyo”.

  Muda mwingi tumejadili kama zaka ni leo ni lazima kutoa au la, tulikuwa hatujajadili jinsi ilivyotakiwa kutolewa kwa mujibu wa sheria ya zaka. Kwa kuwa hatujakubaliana kwenye hili la kwanza, ngoja twende kwa la pili ili uone jinsi gani unachojivunia kukitoa hata hukitoi kwa utaratibu ulioamriwa.

 75. Amini Yeremiah Mguluma,

  Umesema Ati ’’Ujumbe wako ni kama‘’aliopewa nabii Yeremia kuambiwa kuwa atabomoa kuta na kuzijenga na hii ndiyo kazi yako kama mjenzi wa kanisa hai la kristo Yesu mwokozi wetu’’: Kaka yangu kweli nakwambia(tuongee kama Watu wanaokwenda mbinguni), HAUJENGI bali huna haribu sana mambo kanisani wewe!

  Umetamka wazi hapa bila aibu kua ‘’MIMI SITOI ZAKA NA SIAMINI KAMA ZAKA KABISA’’: Aibu kweli nakwambia! Ningekua mimi wewe nisingeongea tena baada ya kuropoko ivyo! Wewe ujiinuae kua una ujumbe kama wa Yeremiah wa kujenga kanisa la Kristo kisha unasema wazi wazi ivyo? na unasema na kumtaja-taja sana Roho Mtakatifu!!!!!!!!! ivi kweli Kaka unatoa wapi confidence hii ya kusema wazi hutoi Zaka(iwe kwa sheria au hiari in this case maana hujatenganisha) wakati Ibrahimu tunajua wote hapa kua alitoa tena kabla ya sheria na hapo hapo unasema unasimamia maandiko na unaongozwa na Roho wa Yesu?!!!!!! Jamani plz be serious/CONCERNED at least mara moja tu ndugu!!!!!!!

  Hapo juu umesema uliyosema na sasa unesema ivi..‘’Kwa hiyo sipingani na kumtolea Mungu na mimi ninatumia kanuni ya Yesu kumtolea Mungu isemeyo ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE’=Sasa Kaka yangu nikisema sikulewi au nikisema hauko na mtiririko A-Z au nikisema hausomi KWANZA ya wengine/yangu au hata YAKO KWANZA in this case, unang’aka! Umedhihirisha hapa na kwingine kwingi tu…Unawezaje kutumia kanuni hii.. ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE’ kisha ukatamka uliyosema juu pale kua huna mpango wa kutoa (iwe kwa Hiari kama Ibrahimu au sheria basi)? ivi unaelewa maana ya kumpenda MUNGU kwa kila ulichonacho? Yaani kweli Mungu akusaidie Kaka, seriously speaking.

  Angalia unavyomsingia Roho wa Bwana ivi‘’Kama Roho mtakatifu atanielekeza kuwa mshahara wangu WOTE WA MWEZI HUU NIUTUMIE KWA AJILI YA KUJENGA UFALME WAKE WALA SIJIULIZI MARA MBILI NINATEKELEZA ALICHOSEMA MWENYENAVYO AMBAYE NI MUNGU’’=SWALI: JE ROHO ANAWEZA KUKUELEKEZA NJE YA NENO? Na kama si ivyo je KAMA NENO limesema kitu WAZIWAZI eg (Mathayo.23:23/Mwanzo.14:1-20) halafu unangoja uelekezwe badala ya kutenda Neno, huoni Kaka una matatizo? Sema kweli, uko salama kweli au nafsi inakutesa Kaka?

  Iki bado nakiita ni kituko hiki..’’Hii kanuni ya 10% imeanza mwaka 777 kabla ya hapo haikuwepo na kama una uthibitisho kuwa ilikuwepo naomba ulete hapa uthibitisho’’JIBU: Na ya Ibrahimu Mwanzo 14:1-20 ilianza lini? Na iyo Mwaka 777 kuanza kwa 10%, naomba uthibitisho toka Bible? Jibu hapo, ukikwepa nitakuambia , hausomi kwanza na Kuelewa kabla ya kujibu kama ambavyo unafanya kwa kufunika maswali na hoja nyingi, mimi niko Mwaminifu at least kila mkinitaka kujibu, najibu au najitahidi kutoa maelezo, wewe, Sungura, si waaminifu ktk mjadala, hamuwajibiki ila mnapenda kuwawajibisha wengine, sina tabu na sitachoka kufanya huduma/kuwajibika au kuwajibishwa, nitafanya kazi mtakazonipa na nitakazoziibua mwenyewe, hamna shida mpendwa, hapa ni mwanzo mwisho for his glory,Amen.

  Mjenzi gani wa kanisa atasem ivi hadharani..‘’ZAKA HAZIKWENDA KWA MAKUHANI KAMA MFANYAVYO SASA HAIKUWEPO HATA KWA WAYAHUDI WENYEWE NA HILI LINA UTHIBITISHO WA KUTOSHA KABISA KINYUME NA UNG’ANG’ANIZI WENU WA KULAZIMISHA MATOLEO’’=nikikuambia unabomoa, utasema nakushutumu wakati nafsi/ubinafsi/moyo wako uko wazi hapa namna hii Kaka?!! si wewe uliyetoa maandiko ya Zaka mengi na moja wapo, yanasema wazi wazi kuhusu Mlawi walifanya kazi ya ukuhani? Na ukifananishia waliokua wanafanyan kazi za Ukuhani Hekaluni kipindi kile kwa maana Agano la Kale ni kivuli cha la Leo, sasa leo wale ni akina nani? Hilo hata Sunday school watoto wanajua, aibu kweli kua Kaka yangu na mkubwa wangu kama wewe unasumbuka na ako!!!!!!!! Du! Hata siamini kama ni wewe Kaka.

  Umenishangaza kuniambia ivi ..’’Nimeng’ang’ania maelezo ya Yesu kwenye Yesu alisema ‘Mathayo23:23 OLE wenu ….. KWA KUWA MNATOA ZAKA YA MNAA NAA…..???? Hapa inatulazimisha vipi kutoa zaka???? Je sisi ni WAANDISHI AMA MAFARISAYO?: Sasa kwanza ning’ang’ane na ya nani wa muhimu sana na nambari one ktk Imani yetu na Bible yote zaidi ya aliyosema Yesu? Pili, SWALI: Unataka kusema kua yale yote Yesu aliyowaambia Mafarisayo na Waandishi, sisi hayatuhusu au ni ili tu la zaka? YAANI HAPA NAKUTAKA UWE MWAMINIFU KAMA MIMI KUJIBU UNAYOULIZWA bila kulia-lia au kukwepa au kufunika na Sijui unachomokaje na swali hili Kaka yangu.

  Umenionya vizuri kwa kweli, sana tu ivi..’’Kamwe hii haiwezi kuwa njia nzuri kwako ya kujifunza hata kama UNAJUA MENGI KWA NAMNA GANI na kwamba Kuna wakati unapaswa kunyamaza na kujifunza kutoka kwa wenzako ili UJENGEKE VIZURI.JIBU: Naupokea ushauri mwema huu kwa kicho na moyo kama mtu anayependa kuongezeka kimo na kina ktk Bwana ila kama mie sijakusaidia basi wapo waliosema mengi humu kabla na baada yangu ambao sijui na sina uhakika kama kweli umnesoma maoni yao na kisha KUELEWA, nao ni Magret aliyetoa maandiko 54 kuhusu Utoaji in general na Zaka yakiwemo, Mathewe Maduhu, Nzala Siyi, Tumaini Nelson, Damas Nkenda, Shoo GAP, Je Umesoma kweli maoni, mafundisho na na shuhuda zao? Kwa kweli sidhani! Kwa iyo ulipaswa kama ni wakuelewa na wewe unalitekeleza ilo shauri ulikonipa sasa, hawa wangekua wamesha kusaidia Kaka yangu, tena wengine walisema kabla ya mimi. Kwaiyo ni rahisi kuona hapa kua ingawa ushauri wako ni mzuri lakini nguvu iliyoutoa siyo ya kicho ktk cha Bwana bali Kibinadamu tu kile si cha upako(mfano: kuzidiwa na hoja, kubanwa, wivu,kulazimisha watu wanyamaze bila kuwapa hoja au kujibu maswali, kutaka watu tumeze mambo ya binafsi na mateso ya nafsi zinazosumbuka na kushiba duniani ilhali mambo ya Mungu ya lale nk…na kwa kweli utaniona nina maneno mengi sana zaidi ya yaliyopita ikiwa kibidamu kisicho cha upako iki kikiendelea kumwaga mambo yake humu eti tumeze tu kimya-kimya bila kutapika)

  Press on.

 76. Sungura,

  Umeuliza nachotaka hasa ni nini? Narekebisha kua NACHOTAMANI ni kuwaona Watu wazima kiroho,Kiutumishi na Akili kama nyie mkisisitiza na kuhimiza mambo mema ya kusaidia Kanisa, Watumishi wa Mungu, Injili, Watu wa Mungu na agenda za KiMungu na si vinginevyo, siasa na ujuaji wa darasa za dini tu bila kubalance na kicho, unyenyekevu hapana Kanisani bali UWana wa Mungu watiifu, wenye lengo moja chini ya Kuhani wao basi, na kwa ilo nitasimamia mpaka the end and end and the end…..

  Umeuliza ambacho sijaelewa ni nini katika hii mada: Jibu: Ni kuwaona Watu wanajua baadhi ya mambo Makanisani yamekua yanafanyika ktk furaha, raha, uhiari, moyo na yanaleta faida nyingi kwa miaka ktk Ufalme wa Mungu na Agizo kuu lakini wanazuka Watu wa kizazi cha leo waKiroho lakini chenye mchanganyo wa ujuzi wa Elimu Dunia kuwavuruga watu na kanisa kwa kuwaingizia ideas ambazo kwa kweli kimsingi hata wasingewaingizia, bado Wana wa Mungu wanakwenda Mbinguni wala hawajafanya kosa la mauti au uhai yaani kuendea kinyume Neno la Mungu, sana sana aidha kwa kujua au kutokujua, wanasababisha usumbufu kanisani na kuchanganya Watumishi na mambo ya msingi Kanisani.

  Sina Nia ya kuwabadilisha wachangiaji wengine ambao wanasema zaka leo si lazima kutoa Ila nina nia THABITI NA HAITACHUJA WALA KUPUNGUA NGUVU ya kuwaambia kua ingawa statement yao yaonekeana ni ya Kiroho lakini yaujazayo moyo, humtoka mtu ivyo Wanasumbulia na nafsi, hazijafa bado tikitiki kwa Bwana, wanaendeshwa na ‘’Put Secod things First badala ya First Things First’’ Principle= Utafuteni KWANZA ufalme KISHA/NA MENGINE….

  Umesisitiza..‘’Wewe ndiye unayetakiwa kubadilika’’=Jibu: Mimi nilishabadilika mpaka kufikia level ya kujidhuru, sijali nafsi yangu inanisumbua au kunipigia kelele vipi, nitaisulubu tu, nitaikandamiza vibaya sana, nitaizaba makofi ya kufunika ya nguvu sana mfano naweza kopa ili mambo ya Mungu au kama mpendwa ana jambo, nimsaidie kisha nakinywea kikombe cha kulipa deni. Kama naweza hata kopa kununua gari, plot, nakwambia hua nakopo na nitakopa kama kuna jambo la KiMungu linanitaka sana na sina pesa wakati huo-Kwa moyo huu, Zaka si issue kwangu kama inavyowatesa nyie, sitoi Zaka tu , wakati mwingine ni zaidi ya Zaka(10%). Ninyi mnashida gani Wapendwa? Mbona mi naona raha tu na simple kufanya ivyo?

  Neno ”hiari” ulishaniuliza maana yake na nikatoa, sasa kwa kua hujasema maana yako wewe ili nione kama nimekosea au la, basi statement yako kua wenda sijui maana ya ilo neno inakua ‘by the way utterance’ hence it is dismissed!

  Umejiamini kwa kusema..‘’Ukweli ni kwamba wewe Seleli zaka huitoi kama sadaka ya hiari’’Jibu: Ninakusaheme bure.

  Lwembe alichosema tokea mwanzo wa debate hii na ghafla aliyosema mwishoni, ni vitu viwili tofauti na hata tone ya arguement zake, unazi-sense kama umakini wako uliosemaga unao unakusaidia, ktk mijadala unaweza si tu kuangalia/kusoma maandishi bali unawezapata radha/ aina moyo wa Mtu au software yake iko wapi hasa. Ivyo kwa kuzingatia ilo, USIMNUKUU Lwembe vibaya at your advantage kwa kua andiko lake la mwisho, limewaweka ktk task ya kukiri alichosema kua hampingi Zaka au mnapinga! Iyo naona umekwepa! Nakuona tu! acha ujanja wa sungura!

  Amin J- kwa kweli huyu Kaka yangu, hana jipya zaidi ya KUONGELEA KWA UZURI SANA ZAKA AGANO LA KALE LAKINI AMESHINDWA TIKITIKI KUONYESHA WAZIWAZI KUA KUNA MAHALA ZAKA ILIFIKA IKAFUTWA KTK AGANO JPYA. Mimi nimemuonyesha WAZI WAZI KWA MAANDIKO HAYA..Mwanzo14:1-20 na Mathayo.23:23 kua Zaka inatambaa toka la Kale mpaka Jipya…Amin Jeremiah hawezi najua kuvuka iyo nyundo, angalia toka ameanza kujibu mpaka sasa, haja-establish kwa hakika kua ZAKA agano Jipya ni a big No kwa kua labda Yesu au Wanafunzi (Mitume),walisema hapana kwa ilo, ataangaika wee na lecture zake lakini hapo hakatizi! Hence kumnukuu hapa kua amesema jambo la kunisaidia, si kweli bali ni cheap politics again za kufagililia bila base.

  Sidhani kama‘mapokeo/mazoea/ ya dini au dhehebu YOTE NI MABAYA AU PEPO! Ni kukosa ufahamu tu wa mambo.

  Ati umenitaka nivue au niendele kuishi ktk‘’kongwa!Jibu: Unasingizia tu, hamna kongwa wala kanga ya kuivua hapa bali nakataa vurugu zenu kanisani uko au hapa.

  Umeongea vema kiroho ivi..‘’kumwona Mungu akinielekeza kupanda palipo na udongo mzuri zaidi’’Jibu: Alishanionyesha ktk NENO lake, sitaki ufunuo zaidi ya huo na kwa mujibu wa Neno lake, Zaka na Matoleo mengine, udongo wake mzuri wa kuyapanda ni Kwa Kuhani wangu, Kanisa langu napolelewa, then Wahitaji kanisani hapo then nje uko-kwa mpangilio huo na si vinginevyo kama kuacha Kanisa langu napolishwa na kulelewa kisha nitoe kwa kanisa jingine, kwa mhubiri wa TV, kwa kusaidia Wahitaji Nje ya Kanisa uko, kwa kuacha ya madhabahu kwanza na kusaidia wengine na mambo kama hayo ya kukosa utaratibu na hekima ktk kukaa kwako/kwangu Kanisani

  Press on

 77. CK Lwembe Mungu akubariki sana kwa mchango wako,umewakilisha ile HEKIMA ya Kimungu ipaswayo kutenda kazi ndani yetu.
  Ninaamini umetoa mchango huo kwa moyo wa KUPENDA
  Amen

 78. Mpendwa Seleli
  Sitachoka kufunua chochote ambacho Mungu wa mbinguni atanipa kuliambia kanisa lake hata kama itakuwa halijaeleweka na watu wengi kwani ndio ujumbe aliopewa nabii Yeremia kuambiwa kuwa atabomoa kuta na kuzijenga,na hii ndiyo kazi yangu kama mjenzi wa kanisa hai la kristo Yesu mwokozi wetu.
  Hebu acha kuruka ruka na maandiko na tumia muda kuisoma habari husika kisha ndiyo uje na hoja ya kupingana nayo. Maandiko yanamuagizi Muisraeli kutoacha kutoa zaka ya fungu la kumi katika mapato yake mwaka baada ya mwaka na kisha anaagizwa kula zaka hiyo katika mahali alipopachagua Bwana Mungu wake ili ajifunze kumcha Bwana Mungu wake.
  Katika hoja yangu ya awali nilitoa tafsiri ya toleo hili zaka kuwa ni TENGO ambalo wana wa israeli walipaswa kuliweka kama akiba ya chakula wakati wa makusanyiko matakatifu ambayo lengo lake kuu lilikuwa ni kujifunza neno la Mungu.Na unafahamu kuwa walikuwa na makusanyiko makubwa matatu katika kila mwaka yaani siku ya kwanza ya mwezi wa Habibu kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya pasaka,Kisha siku ya vibanda ambayo walikumbuka jinsi walivyosafiri jangwani wakitokea utumwani katika nchi ya Misri na kisha siku kuu ya mavuno (Pentekoste) ambayo iliwakumbusha jinsi walivyopokea mavuno ya kwanza katika nchi ya ahadi mara baada ya kutoka utumwani Misri.
  Sasa makusanyiko yote haya yalihusisha kukaa mahali pamoja kwa zaidi ya siku nane wakijifunza torati,wakiimba zaburi na kujikumbusha mfundisho ya manabii kadhaa (Soma kitabu cha Ezra,habari za ujenzi wa hekalu wakati wa suleimani n.k)
  Ili kuweza kushiriki ibada hizi kwa uhuru walipaswa kuwa na chakula ambacho utaratibu ndio ulikuwa huu wa kutenga sehemu ya kumi ya mavuno ama mazao ya wanyama kwa ajili ya wajibu huo.
  Sasa kwa maelezo haya na mimi kama mwalimu wa kanisa hai la Yesu kristo nakutaka usome kwa utaratibu aya zile za Kumbu kumbu 14:21-26 ili uelewe maana ya maandiko. Vinginevyo utakuwa unajisifu bure kuwa una Roho akuongozae wakati ukweli unatumia akili zako.Roho mtakatifu hajipingi wala hajichanganyi mdogo wangu.Alilosema Mungu ndilo linathibitishwa na Roho mtakatifu,asikiaye na afahamu.
  Umetaka kujua kama mimi natoa ZAKA,JIBU RAHISI NI KUWA MIMI SITOI ZAKA NA SIAMINI KAMA ZAKA KABISA na Mungu ananibariki kila uchao.
  Unajinasibu kuwa umemruhusu Roho mtakatifu,lakini kwa anayesoma post zako anaona jinsi unavyomdhalilisha kwani hauonyeshi kama unasoma maandiko na kuyaelewa bali umelewa mafundisho ya dhehebu lako na unadhani huyo ndiye Roho mtakatifu. Kama ni mnyenyekevu kwa Mungu utaelewa ninachokisema hapa na tumia muda wako kujitafakari na kurekebisha. Si kila ulichofundishwa na ukakishika ni ufunuo wa Roho mtakatifu bali mengine ni MAN MADE.
  Na ili ufahamu kuwa hutumii ufunuo wa Roho mtakatifu unapoandika post zako hebu tafakari mojawapo ya post zako ” Wakristo waliojitoa asilimia zote kwa Bwana na kuacha hizi sarakazi za kukatalia/kubania vinoti na tushilingi twao.”
  Kwa post hii unaonyesha jinsi ambavyo hujui tofauti kati ya sadaka,dhabihu na Zaka.
  Zaka ni toleo lakini si dhabihu wala sadaka. Ni TENGO,Sadaka na dhabihu ni matoleo yaliyopaswa kukabidhiwa kwa makuhani yaani walawi kutoka ukoo wa Haruni ili ZISONGEZWE MBELE ZA MUNGU.Kamwe Zaka kama zaka haikusongezwa bali sehemu yake ndiyo iliyotolewa kama dhabihu ikaitwa SADAKA YA KUINULIWA.
  Kwa hiyo sipingani na kumtolea Mungu na mimi ninatumia kanuni ya Yesu kumtolea Mungu isemeyo ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE NA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE’
  Falsafa hii ndiyo iliyotumika wakati wa huduma ya kanisa la Kwanza pale Yerusalem ambapo watu walitoa vitu vyao vyote wakaviweka miguuni mwa mitume ili vitumike kwa utukufu wa Mungu.
  Mimi ninaamini kuwa vyote nilivyonavyo ikiwemo mashamba,nyumba n.k si vyangu ni vya Bwana na ninavitumia kwa ajili yake pale Roho mtakatifu anaponiongoza kufanya. Kama Roho mtakatifu atanielekeza kuwa mshahara wangu WOTE WA MWEZI HUU NIUTUMIE KWA AJILI YA KUJENGA UFALME WAKE WALA SIJIULIZI MARA MBILI NINATEKELEZA ALICHOSEMA MWENYENAVYO AMBAYE NI MUNGU.
  Mtume Petro anatufundisha pia kanuni hii ya kumtolea Mungu anapomuuliza Yesu kuwa WATAPATA NINI WAO AMBAO WAMEACHA VYOTE KWA AJILI YA YESU,Na ndipo Yesu anamjibu kuwa watalipwa MARA MIA SASA NA KISHA UZIMA WA MILELE. Kanuni ya Yesu kwenye utoaji ni 100% na si 10%
  Hii kanuni ya 10% imeanza mwaka 777 kabla ya hapo haikuwepo na kama una uthibitisho kuwa ilikuwepo naomba ulete hapa uthibitisho huo na si hisia zako mdogo wangu.
  Nataka nisisitize kuwa kanuni ya utoaji wa ZAKA KWENDA KWA MAKUHANI KAMA MFANYAVYO SASA HAIKUWEPO HATA KWA WAYAHUDI WENYEWE NA HILI LINA UTHIBITISHO WA KUTOSHA KABISA KINYUME NA UNG’ANG’ANIZI WENU WA KULAZIMISHA MATOLEO.
  Labda upate nafasi pia ya kusoma hoja yangu nilipochambua Mwanzo 14 na kisha ndipo uchekelee kuwa hapo SITOKI,Sitoki nini mdogo wangu???? mbona hoja ipo wazi tu.
  Unapong’ang’ania maelezo ya Yesu kwenye Mathayo23:23 bila kutafakari vizuri.Hivi Yesu alisema tunatoa zaka ya mnaa naa ama aliwaambia OLE wenu ….. KWA KUWA MNATOA ZAKA YA MNAA NAA…..???? Hapa inatulazimisha vipi kutoa zaka???? Je sisi ni WAANDISHI AMA MAFARISAYO????
  Kwamba eti baadhi ya hoja ninazokuja nazo huwa mmeshazijadili huu nao ni udhaifu mkubwa kwani mara zote ninapoingia kwenye mjadala kwanza natumia muda wa kutosha kupitia majadiliano yaliyopita ili kuona yale ninayojifunza kwanza na kisha ndiyo ninachukua muda kutoa maoni yangu kwa yale ambayo naona kuna ulazima wa kufanya hivyo.
  Tatizo ulilonalo mdogo wangu ni kuwa UNA MANENO MENGI SANA na kwa hiyo sidhani kama UNAPATA MUDA WA KUSIKILIZA AMA KUSOMA NA KUELEWA WENZAKO WANASEMAJE NA NDIYO MAANA UTAONA KUWA KARIBU 70% YA MJADALA HUU WEWE UMEKUWA UKIRUSHA MANENO KWA WATU WENGINE KAMA AKINA SUNGURA N.K.
  Kamwe hii haiwezi kuwa njia nzuri kwako ya kujifunza hata kama UNAJUA MENGI KWA NAMNA GANI.Kuna wakati unapaswa kunyamaza na kujifunza kutoka kwa wenzako ili UJENGEKE VIZURI.
  Kabla sijaendelea na mambo mengine niishie hapa kwa faida yetu sote.

 79. Ivi Seleli unachotaka hasa ni nini au ambacho hujaelewa ni nini katika hii mada?

  Au uliingia kwenye huu mjadala wa zaka ukiwa na imani kuwa wewe ndiye unayekwenda kuwabadilisha wachangiaji wengine ambao wanasema zaka leo si lazima kutoa?
  Lakini matokeo yake yamekuja kwamba wewe ndiye unayetakiwa kubadilika, na kwa vile hukuwa umetegemea hivyo basi hauko tayari kubadilika.

  Sasa hivi unajificha kwenye neno ”hiari” lakini ukweli ni kwamba au huelewi maana ya neno hiari katika suala la zaka au unaelewa lakini unajificha tu nyuma ya hili neno kujaribu kutuonesha kwamba unakubaliana na sisi kwamba zaka ni hiari.

  Ukweli ni kwamba wewe Seleli zaka huitoi kama sadaka ya hiari. Hutoi kwa mujibu wa Ibrahim wala Yakobo.

  Kuna maelezo mengi ya kukusaidia uelewe wadau wameyatoa hapa,yakiwemo ya Lwembe na Amin haya ya mwisho mwisho,lakini bado huoneshi kukubali huo ukweli, na ni kwa sababu ya mapokeo/mazoea/ dini (dhehebu) kiasi kwamba ukijaribu kufikiri kuwa siku moja upate hela fulani ati utoe tu sadaka ya kawaida bila kuitolea zaka na kupata ile stakabdhi ya zaka akili inakwambia nooooo!

  Kaka una hiari ya kuendelea na hilo kongwa hasa kama unaona linakusaidia, hakuna anayekulazimisha kulivua!

  Siku litakapokuchosha ulivue,na ndipo utakaposhangaa kuwa kulivua kwako hakutapunguza baraka yoyote zaidi itakuwa ni nafasi ya wewe kumwona Mungu akikuelekeza kupanda palipo na udongo mzuri zaidi, maana nimekuona unapenda kumtolea!!!!!

 80. Lwembe,

  Nimecheka sana kuhusu mama ntilie, NI KWELI NAKULA HUKO PIA TENA KWA AMANI TELE WALA SIJADANGANYA NA SOME OF THEM NI WAPENDWA WANA BIASHARA IYO, SO TUNAKWENDAGA KUWAUNGISHA! SI UNAONA HADI HAPO UMEKWISHA NYANG’ANYANG’A KAMA ILIVYO HOJA MFU YA Sungura kua ni roho ya umaskini kula uko, nayo kwisha habari yake-kumbe kukosa upembuzi yakinifu, unawamis-lead mbaya-kuna wapendwa/watu kupitia biashara iyo iyo sehemu kadhaa jijini, walikotega, leo hii maisha yao na mali walizonazo, hamtakaa mseme ovyo namna iyo, eti hawapiki dagaa kwakua kilo 20,000 labda dagaa za kuku! Mwe! You are very funny brother, ha ha aha ha, ni baraka tele kua na Watu kama nyie pia who can make us smile and burst in kicheko in the middle of hot debates like this, me too like making people break in kicheko, so I enjoy your talent too brother. Ila kweli umenishangaza, kumbe huna habari iyo kabisaaa, hujui dagaa ni mboga common sana kwa Mama Lishe! Aya bwana Kaka, asante kwa kutuburudisha humu ndani.

  Role yako uliyojipachika ya kua moderator, mara ya kwanza uliicheza bila utimilifu so sikua na haja ya kusema kitu lakini this time, umeongelea VEMA SANA tena wazi wazi kua Tutoe Zaka,unaweza sema ivyo LOUD AND CLEAR ILI Kaka Sungura, Yeremiah, Kaswahili, Mabinza, wakusikie? NA UMESEMA STATEMENT HII…kua KATI YAO(WALIO-DEBATE HII MADA), HAKUNA ALIYESEMA TUSITOE ZAKA! Aiseee! Kweli! umesoma comments zao zote toka mwanzo til now? Comments zao kwa hoja na zile za by the way? Kaka Mabinza/ Yeremia/Sungura/Kaswahili-ALICHOSEMA LWEMBE MNAKUBALI MKIZINGATIA MME-DEBATE NA KUSEMA NINI TOKA TUANZE MPAKA TUNAPOHITIMISHA SASA? PLZ CONFIRM

  Iyo maneno kua ZAKA ndio kichocheo cha utitiri wa Makanisa mengi ya Kipentekoste, well, some lakini not all na ndio hii lack of carefulness ktk statements alizotumia Sungura na Kaswahili zilizonikifu ile mbaya, ku-generalize kua uko Makanisani ni hali ngumu, ni ukatapilla tu kwenye zaka mwanzo mwisho, ni Wachungaji kula tu Zaka, wavivu!!! Ilo ulosema Lwembe sasa ivi ni kama tamko la Sungura juzi kati hapa ati Zaka ndio chanzo cha umaskini Makanisani! Nyinyi Watu mnafanana-fanana sometimes! Sasa plz usidhubutu Lwembe kurudi uko, tutakesha hapa bro I am telling you FIRMLY, Nitaendelea kuwathibitishia tena na tena kua tupo/yako Makanisa mengiiiii, sisi Waumini hatuna shida na kutoa na pia kwa raha zetu tunatoa ZaKa, Malimbuko na sadaka/matoleo mengine mengii, nyinyi tu ndio mlitaka kutuingizia foreign devilish if not faulty/selfish humanic idea ya kutatiza mambo au mioyo yetu, nakuambia wewe na wengine wote hapa na watakaokuja, KAMWE mambo binafsi kuyaleta ili kuharibu/kuambukiza maambukizi hatari mambo jamii(ya Kanisa/ Waumini wote kwa ujumla, HAYATAPITA HAPA BILA KUSHUGHULIKIWA!

  Mstake kutuchanganya hapa! Ooh mara Zaka imetolewa sana Agano la Kale, sasa Jipya nimelistop, ni laana kutoa kwakua tutakua chini ya sheria, mara ooooh kwa hiari tutoe tu, mara oooh zaka ndio chanzo cha umaskini Makanisani, mara ooh zaka tutoe wenyewe na tule siye eti ndio maandiko yanamaanisha ivyo na eti kwa kuzi/ji tolea wenyewe kisha kuzitafuna wenyewe, ati ndipo twajifunza kumuhofu Bwana, mara ooh hakuna aliyesema tusitoe, mara ooh tunapotosha maandiko kwa kusisitiza itolewe, mara ooh tutatoa tunapojisikia, mara ooh wanakula wachungaji tu, wenye shida hawapewi, mara ooh Wachungaji wa leo si Makuhani, mara ooh kila mtu ni kuhani, yaani mnavuruga mchana/usiku mpaka jioni!!!!!!!!! Unajiuliza ivi wanadamu woooote nyinyi mnavyoangaika ivi, nini hasa? Kutoroka na ivyo vihela na vimali vyenu siyo? Kumkacha BWANA NA KAZI YAKE NA WATU WAKE WATUMIKAO HAP0 TENA KWA AJILI YETU, MNAPAA NAZO ILI MJITOLEE NA KUZILA WENYEWE! Jesus Christ! shame on you people of God.

  Hata brother Nzala nae amewasaidia vema sana this time debate yote-usabato pembeni, kasema kama anavyoona Neno na Ufahamu wa jumla wa tabia ya Mungu ya Utoaji na Watu wa zamani walivyotoa vyote tu na hata amewazidi kwa mbali upeo wa kuona why tunahitaji leo tena si tu Zaka mbali zaidi yapo maana kazi ni kubwa, bado hamsikii? Ivi ninyi mnashida gani? By the way, ivi mna shilling ngazpi kwanza izo zinazogomba ivyo? mna migodi ninyi?njooni niwapeleke home Geita kwetu niwashangaze kuwaonyesha Wapendwa walivyo watoaji yet mali walizonazo, hutakaa mseme politics izi humu, au mna ng’ombe wangapi nyie au tu-mbuzi na tu-kondoo? Twendeni niwaonyeshe Wapendwa wanaleta ng’ombe wazima-wazima-tunayaita ‘’manzagamba’’-ile midume nyati ya ng’ombe yenye nundu zina-sing pambio kulia kushoto, yakitembea, hayo yanaswagwa kuletwa kanisani,ombewa, uzwa kisha tunafanya crudade ya hatari, Watu wananyakuliwa toka giza to nuruni, tu-mbuzi na tu-kondoo hata tukuku ndio kama kawaida. Huku kwenu Dar kuku wa kienyeji tu alfu 15-20, ndio maaana mnakua bahili kweli mpaka kwa Mungu na mambo yake-aisee ‘upako’’ wenu wa kubajeti ni hatari-mpaka mna-frustrate smooth working ya Taasisi ya Mungu-Kanisa kwa kutomtolea!!!!!! twendeni mle kuku mpaka mtubu kisha niwape zawadi ya kuku 10 kila mmoja lakini mkifika Dar tu, kila kuku 10 niliyowapa bure kabisa, mmoja, atolewe kama zaka, hamtaki ilo, kaeni na hao vifaranga wa huku alfu 20 mmoja!!!!!

  Kuhusu matumizi ya AKILI, hili nimeshalisemea sana na kwakua bado linashikiwa bango baya, ni lazima nilifundishe tena na tena na sitachoka mpaka liwakae/liwafumue fahamu zenu. Maelezo mengi kuhusu ili, rejea majibu yangu kwako ktk hoja ya ‘makatazo kwa wanawake’ na hata majibu yangu hapa hapa kwa Yeremiah. Uliyoyasema mengi nimeyasema mie, umerudia-rudia tu…nilikupa maandiko ya ‘’tukiwa ndani ya Kristo, tu viumbe vipya(akili imo), nikasema Paul mwenyewe anaongea na Mkuu na kumwambia anasema maneno ya Akili na Kweli-ivyo uyasomayo leo ktk Mdo 26 pale, ni maneno ya Akili pia na nikasema, SISI NI HEKALU YA RM ivyo anakalia kila kitu na Akili, kwa iyo narudia, acheni uvivu wa kufikiri/kupembua/kuchekecha/kutakafari mambo ya Mungu, acheni woga na maangalizo fake yasiyo na msingi maana tu ndani ya Yesu, tumebadilishwa, viungo vyote vya ndani na nje, vinaonekana na visivyoonekana, ni potential tools kuvitumia/kutumiwa. ACHENI KUTIA HOFU WATU ATI AKILI HATARI SANA bwanaa!!!!!!! Mmmh! KWANI SISI CHIMPANZEE! SISI NI WATU/WANADAMU-as a matter of fact hata chimpanzee ana akili nyingi tu na anazitumia vema, je si zaidi aliye na Yesu, tena yeye ni Mwanadamu-zaidi ya kima kubwa lao lile! Nyie vipi bwanaaa!

  Press on, acheni maneno wala siasa cha ccm/cdm Makanisan, ktk huduma na kwa Makuhani wetu wa leo waliotengwa/itwa kwa kazi maalumu ya hapo Ukuhanini

 81. Yeremiah Mgulumu,

  Sasa Kaka nikuache kwanza usome my comments hapo juu ziko mbili maana sijui ulikua wapi siku zote izi kaka , nikiongeza tena kwa hii yako ya sasa si tutakua hatuendi katika hitimisho kama ilivyokua nia ya washiriki kadhaa hapa! uwe una wahi basi tukiwa ktk mijadala hii, nakuomba soma comments zangu zote za sasa maana bado unahangaikia naza week ileeeee sasa hapo tunafika kweli, lini tutahitimisha bro wangu? comment za wakati uleee na izi mbili za leo zangu, zinaout weigh kwa kiasi kikubwa unayosema Kaka mbona sioni issue mpya?! well kukutendea haki, nimepitia hili lako la sasa ivi ndio maana nasema nikupe muda umalizane nacomment za juma 2 zimepita kisha usome na jana hapo then tuelewane tunamalizaje,aya kazi ni kwko

 82. Mpendwa Seleli
  Leo tena nimeonelea niendelee kushughulika na hoja zako ili kama ni wa kusikia sauti ya Mungu kweli kweli basi ufunguliwe kuyafahamu maandiko na maana yake.
  Inasikitisha kuwa bado unaendelea kujivika kongwa la kuwa WACHUNGAJI ndio makuhani wako kwa maana ya kuwa ndio makuhani wa AGANO JIPYA.Huu ni upotofu wa kimaandiko kabisa na unahitaji ukombozi wa kifikra. Hivi kuna andiko lolote linalounga mkono mtazamo huu ama umebobea kwenye kushika mafundisho ya MADHEHEBU yanayolazimisha matakwa ya kibinadamu na kuacha MAAGIZO NA MAELEKEZO YA MUNGU.
  Ili kukufundisha kuhusiana na UKUHANI WA KIKRISTO nilikupa maandiko kutoka Waraka wa kwanza wa mtume Petro2:2,5,9 unaofunua ni nani anayetambulika kama KUHANI WA AGANO JIPYA KUWA ni kila aliyeitwa kuwa MWANA WA MUNGU kwa maana ni huduma ya kila MKRISTO,kwani mara baada ya Bwana Yesu kukata roho pale msalabani PAZIA LA HEKALU LILIPASUKA VIPANDE VIWILI kuashiria kuwa sote tuliokombolewa kwa damu ya thamani ya Yesu tuna ruhusa ya KUKISOGELEA KITI CHA REHEMA CHA MUNGU KWA DAMU YA YESU ALIYE KUHANI WETU MKUU WA MFANO WA MELKIZEDEKI.
  Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
  Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
  Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
  Na kwa kuzingatia maneno haya ndipo mtume Paulo akiwaandikia barua yake ya pili kanisa la KORINTHO anafunua wajibu uliopandwa mioyoni kwa kila aliyezaliwa kwa ROHO kama ifuatavyo (2korintho 5:17-19)
  Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
  Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
  yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
  Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
  Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
  Kwa hiyo ni upotovu kumuita MCHUNGAJI kwa maana ya huduma yake ya kichungaji kuwa ndiye kuhani wetu bali yeye MCHUNGAJI ni kuhani pamoja nasi kwani sote tu makuhani chini ya KUHANI MKUU YESU KRISTO.
  Katika mchango wangu uliopita nilinukuu kutoka kitabu cha hesabu 18:21-26 na nikaeleza tafsiri ya kilichoitwa ZAKA ILIYOKABIDHIWA KWA MAKUHANI KUWA NI kitu kilichoitwa SADAKA YA KUINULIWA ambacho ilikuwa ni sehemu kutoka katika ile ZAKA NZIMA.Hii ndiyo iliyoitwa ZAKA na ambayo ilitambulika kama SADAKA YA KUINULIWA.Hebu tuyasome vizuri maandiko yale;
  Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.
  (Hesabu 18:24)
  Sasa ndugu yangu nakuona unapoteza utulivu na kushindwa kuelewa hata maandiko yanasemaje na unakukuruka kutetea kitu ambacho huna mafundisho ya kutosha wala uelewa.Unashupaza shingo kutetea mafundisho ya dhehebu lako ili mradi tu UONEKANE WA KIROHO.Hii ni hatari kubwa sana mpendwa Seleli.
  Seleli nalazimika kukuona hivyo kwani inaonekana hupendi kukutana na vitu usivyovipenda na kwa hiyo hupendi kufahamu udhaifu wako na pia nguvu ya mpinzani wako.Huu ni udhaifu unaotokana na jeraha la dhamira ambalo tiba yake ni kuufahamu ukweli na kweli yote ili uwe huru kweli kweli.
  Nimeshangaa kuwa hukupata nafasi ya kusoma vizuri habari ile ya Ibrahimu kumpa sehemu ya kumi mfalme wa Salemu aitwaye kuhani Melkizedeki.Ungelisoma ndipo ungelifahamu kwa nini nilikucheka.Umejaa ushabiki mdogo wangu.
  Nilieleza na hapa narudia kueleza kuwa IBRAHIMU HAKUTOA VYAKE KUMPA MELKIZEDEKI SEHEMU YA KUMI BALI ALITOA KATIKA MAREJESHO YA VILIVYOTEKWA NA MAADUI WA MFALME WA MOABU KUTOKA KWA MFALME WA MOABU NA WATU WAKE,KWA HIYO HAIKUWA ZAWADI KWAKE IBRAHIMU BALI YEYE ALIWAKOMBOA NA AKAKOMBOA MALI ZAO NA NDIPO SEHEMU YA KUMI ALIMPA MFALME MELKIZEDEKI BAADA YA MFALME MELKIZEDEKI KUTOA CHAKULA NA VINYWAJI NA BARAKA KWA IBRAHIMU NA JESHI LAKE LA UKOMBOZI.
  Sasa hebu uniambie jambo moja. Ikitokea mathalan mali ya jirani yako imeibiwa na wewe umefanikiwa kumkamata mwizi na mali zote za jirani alizoibiwa,utapeleka ZAKA KANISANI KWA MCHUNGAJI WAKO kutoka kwenye hizi mali za wizi ulizozikomboa ambazo unafahamu fika kuwa ni mali za jirani YAKO????
  Hebu isome mwenyewe ile habari na utafakari kisha uondoe unazi wa kidini na kidhehebu tunapojadili mambo ya kuzijenga roho zetu zipate kumtii kristo Yesu kwani hapa hatubishani bali tunafundishana na kuelekezana mpendwa.
  Umetaka nikuthibitishie kuwa Yesu pamoja na kuwa aliishi na kufuata desturi za dini ya kiyahudi hakuwahi kutoa ZAKA KAMA MKRISTO.
  Nadhani ni kwa spoon feeding pekee ndiye anayeweza kutoa hoja kama hiyo mpendwa wangu. Hebu soma vizuri vitabu vyote vya INJILI ambavyo ni vinne uone na ujifunze maisha ya Yesu na huduma yake.
  Ilikuwa ni desturi yake kwenda hekaluni na kwenye masinagogi na huko alipata nafasi ya kufundisha mbele za viongozi wa dini ya kiyahudi (Luka 4:16)
  ‘Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. ‘
  Lakini alitembea huku na huko akihubiri habari njema ya ufalme,mahali pengine alijitenga na wanafunzi wake (Wakristo wa kwanza) akawafundisha kwa kina ujumbe alioukusudia.
  ‘Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;
  wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.
  Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,
  Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza?
  Kwa hiyo hakuna shaka kwa wasomaji wa injili kufahamu kuwa Bwana Yesu wakati wa huduma yake alitenganisha utendaji wake wa huduma kama MWANA WA MUNGU na ubinadamu wake kama mtu wa kabila la YUDA aliye muumini wa dini ya kiyahudi na ndio maana alitahiriwa,alikombolewa kwa huwa wawili,alifuatana na wazazi wake kwenda kuhiji akiwa na miaka 12,alishiriki mijadala ya kidini ya kiyahudi n.k. Lakini kwa mamlaka yake kama Mwana wa Mungu na mwokozi wa ULIMWENGU,alitembea huku na kule akihubiri injili,aliwakusanya makutano na wakati mwingine wanafunzi wake akawafundisha habari njema ya UFALME WA MUNGU,alitenga muda wa maombi n.k.Hata mfumo wake wa kitaasisi alikuwa na MTUNZA FEDHA aliyeitwa YUDA ISKARIOTE ambaye hakuwa kutoka ukoo wa Lawi wala hakuwa kuhani.Alikuwa na wasaidizi watatu yaani Petro,Yohana na Yakobo ambao alishiriki nao mambo mazito tofauti na wanafunzi wengine na ndiyo maana utaona kuwa siku ya kuteswa kwake aliwashirikisha maombi ya mwisho.
  Kwa hiyo kwa msomaji mzuri wa maandiko hawezi kuuliza swali hilo labda kwa mtu aliyeathirika na mapokeo ya kidhehebu.
  Unataka napo nikuthibitishie kuwa wanafunzi wa Yesu hawakutoa ZAKA. Walitoaje?? kwenye kanisa lipo???? wao kama taasisi ndogo walikuwa wakitunzwa na watu mbali mbali na ndio maana Mwinjilisti Luka anaamua kutaja baadhi yao kuwa ni akina Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Kuza kuwa ndio waliokuwa na wajibu wa kumtunza Yesu kwa mali zao. Sasa sijui kwa sababu umezoea kusoma biblia kwa mtindo wa MISTARI YA MOYO na hivyo huna muda wa kusoma habari kwenye vitabu hivyo ama sijui ni nini lakini.
  Katika post iliyopita nilitoa mpaka maandiko ya jinsi kanisa la kwanza lilivyoendeshwa ikiwemo namna walivyotoa MALI ZAO ZOTE NA KUWAKABIDHI MITUME ILI VITUMIWE NA KANISA KWA MAANA YA KUNDI LILE LA WAAMINI WA KWANZA.Sijui unataka upewe ushahidi gani kuthibitisha tunachokisimamia. Ili pia ufahamu nadharia ya utoaji wa 100% hebu jiulize sababu ya Petro kumuuliza Yesu kuwa watapata nini wao waliotoa mali zao zote kwa ajili yake Yesu ambapo Yesu anamjibu kuwa WATAPATA MARA MIA SASA NA UZIMA WA MILELE.
  Kwa hiyo leo niishie hapa kwa kukutaka ujitahidi kusimama kwa miguu yako mwenyewe na kusoma maandiko kisha uyatafakari kwa kina badala ya kung’ang’ania mafundisho ya dhehebu lako ambayo sehumu fulani huwa ni UTASHI WA KIBINADAMU.
  Wakatabahu

 83. Sungura,

  Offer/Suggestion yako, this time so clear hili kua ’’tufikirie kuhitimisha sasa, imekubaliwa na namaliza kwa haya yangu kwa yale yako kama ifuatavyo:

  The ‘’Mama Ntilie thing’’, nilidhani ungechukulia kama Illustration kuback- up major point, in this case kwakua u missed that, niiseme tu kua ni KUJINYIMA/KUJIKATALIA NAFSI FOR KINGDOM’S sake, basi ivyo tu, u mean u missed that au unatania tu hapa!!!!!!!! By the way, nikuchallenge ufanye search on behaviour mbalimbali za some rich people, nadhani hujawaona SOME extremely rich people yet so simple hata kula maeneo yako na yangu, lala guest houses,safari ktk means ambayo watu wa kawaida hutumia, kwa iyo kula kwa mama lishe husiiponde hata chembe, watakushangaza wenye nazo lakini wako uko, halafu wewe husiye nazo ndio eti wajidaiiii Serena Hotel! Au mfano mdogo tu, umeshakutana na SOME rich Chaga? Lakini angalia life yao kama ni ya kujitutumua! Hence, kama vile si kweli kila alae kwa mama Ntilie anasumbuliwa na roho ya umaskini vile vile si kweli anaye-spend life ktk mambo makuu ndio yuko huru na amebarikiwa! Anaweza kua ana roho ya ufujaji, kujipenda kupitiliza, roho ya kutapanya ovyo tena kwa NAFSI yake lakini sasa mlete(mbip) kwenye kutoa kwa Bwana na hasa Zaka! U will see!

  Ati‘’Kwani madirisha hayajafunguka tu Seleli tangu umeanza kutoa?=JIBU: nami nina swali: Wewe una-define/elewaje madirisha ya Mbinguni kufunguka? Naona una tatizo hapo tena!!!!think about this, Kama Mtu anaweza kukaa miaka 4 hajui hospitali wala malaria despite mbu anao wahudumia kila iitwapo leo hata kama gari halijaja au nyumba na cheo, is that not zao la dirisha kufunguliwa? Kama Wanagu wanaweza kua wa kwanza darasani kila mtihani ingawa shule waliyopo si ya international au sijui academy na wengine kufaulu kuzidi hao wa-international, je ilo halitatoa maana ya dirisha kufunguliwa? Au kwako kujua kweli madirisha yamemfungukia Seleli ni mpaka awe na gari ya hammer, ale Sheraton ya zamani, ana simu kali, nyumba 10 Dar? Aya pick maana unayoona yafaa kwa dhana yako wewe.

  Kwamba ‘’ninaflow off ile mbaya na ili Lwembe asiendelee kunivunja mbavu kwa sababu ya comments zako, tufikirie kuhitimisha sasa’’= mmmh! Yale yale maneno rahisi! Kama uthibitishi huo uuoff flow basi hakika yeye asemaye ivyo ndiye na kashindwa hoja na kujibu maswali mazito, inabaki visingizio. Lwembe aendelee tu kukuchekesha maana hana jipya na kwa kweli kwa hoja/kihoja, brother hua hawezi zaidi ya ‘simba na yanga bila goli, ingawa mara chache husema mazito hasa pale anaporuka na wewe unapotoka nje kisha akikufuata uko kuvunja nguvu iyo, unaanza kulia uku unakimbila ndani na kumgeuka kua ametoa nje! Sungura bwana!

  Mwisho, umetoa kahekima aka ka kijanjaaa kweli..’’Kukubaliana na kutokukubaliana yote ni mema’’…mwe! nani kasema? Sungura siyo? Mimi nasema, TUKUBALIANE KUTOA ZAKA NA MATOLEO MENGINE YOTE KWA HIARI LAKINI PIA KWA KUAMUA KWA MAKUSUDI KABISA KAMA TUAMUAVYO MENGINE YA MAISHA HAYA KAZI YA BWANA ISONGE MBELE NA KWAMBA IZI SARAKASI ZA KUTOROKA ZAKA NA KUIKWEPA KAMA POLICE, TUACHE MARA MOJA

  Press on.

 84. Amin Yeremiah Mguluma,

  Maelezo yako mengine na majibu yangu ni kama ifuatavyo:

  Umetamka kua‘’Post yangu ilidhihirisha kuwa utoaji wa Zaka kwa mkristo ni fundisho potofu na si la kibiblia’’=BADO HUJASEMA LOLOTE KTK HILI clearly! Umejikuta tu unaleelezea sana tena vema kuhusu ZAKA Agano la Kale na hujasema sasa wapi ilikatwa na Bwana rasmi kua isimame maana si kupotoka kuendelea kuitoa hata kama ni kwa hiari na kwa moyo wa kupenda. SASA NDIO SEMA USIKIKE NA KUSOMEKA HAPA-nangoja/ twangoja.

  Umesisitiza ivi‘’ukweli wa kimaandiko kuwa mtoa zaka ndiye mla zaka’’ kwa iyo? na kama mtafsiri mzuri wa maandiko kama uli-imply kua ndivyo ulivyo na mimi siyo, unaweza jenga hoja/point kwa andiko moja tu hili ya nani anapaswa/haki ya kula zaka? Kweli nyingine za Mungu hatuzizangatii ili kuhitimisha bila ulemavu wa hitimisho? Au serious wewe ni classic Mtafsiri na Mtafiti wa maandiko? Mmh! unaweza elewa kwa nini ktk response ya kwanza nimesema, brother, sioni kitu ulichokazana kuandika! Think about this, Kwa hiyo message unayotaka mimi na Wasomaji wako tuondoke nayo ni kujitolea Zaka na kuitafuna sisi wenyewe! Confirm plz…. Du! Hii kali, Ajabu kabisa!

  Umesema‘’KUTOA ZAKA NA KUTUMIA MBELE ZA BWANA MUNGU NDICHO KUJIFUNZA KUMCHA BWANA MUNGU WAKO na si KUTOA ZAKA PEKEE’’=Unazitoa kwa nani? Kwako weye mwenyewe na kisha wala mwenyewe ndio iletelezee kujifunza kumcha Bwana daima? Ooh My God! Ndio kwa ufahamu wako wote, umeelewa ivyo? Jesus Christ! Sijui nikusaidieje ndugu yangu? Ndio maana nasema husomi wewe post and comments kabla hujaibuka au ukisoma, nimesema HAULEWI! Nililisemea vema hili, plz go back and soma pole pole, nilisisitiza…Hitimisho hili…’’Upate kujifunza kumcha Bwana daima, has nothing to do with wewe kujitolea zaka mwenyewe kisha kuitafuna mwenyewe! Come on brother, it is simply does not make sense! Ivi some wapendwa mnakugaje lakini? ndio uvivu wa kufikiri huu. Ivi kweli Mungu anakutegemea usomapo Neno lake, uibuke na akili iliyodaka ivyo ulivyosema? Jamani! kazi kweli ipo!. Besides, muhimu hapo ni kutoa Zaka na kuirarua Mwenyewe au ni ukweli kua Zaka zilitolewa? Which is important/an issue hapa kama ukifikiri/kutumia akili kidogo tu iyo mnayopiga vita uncessarily/UnBiblically?

  Umenishauri‘’Mruhusu Roho mtakatifu atende kazi ndani yako ili uwekwe huru kweli kweli’’= NILISHAMRUHUSU SANA NA NDIO HUYU ANANITUMIA KUKUSISITIZA BROTHER, ACHA SARAKASI ZA KUPIGA TEKE ZAKA KWA KUISHIBISHA NAFSI YAKO, KWANZA MUNGU KISHA MENGINE YAFUATE.Usimsemelee RM confidently ivyo wakati uyafanyayo ni kinyume, itakua ni mbwembwe tu za kipendwa ambazo nazijua sana, hua hazina base ukizichekecha kwa mambo ya msingi ya Neno na kutenda Neno, ivyo tu yanapeperuka kama upepo.

  Umejidai kua ‘Uilichokiandikia ni kitu umefanyia utafiti wa kutosha ikiwemo kupitia Bible comentaries’’=kafanye tena utafiti bado safari ndefu, kama utafiti wako umekupelekea wewe kutoroka Zaka, such research is fake and haina mashiko mbinguni na wala dunia walipo wanadamu, Kanisa na Watumishi wa Baba, wanaotaka sana Wakristo waliojitoa asilimia zote kwa Bwana na kuacha hizi sarakazi za kukatalia/kubania vinoti na tushilingi twao.

  Umeclaim ivi‘’unapojenga hoja zako hutaka kutuliza akili zako za kawaida’’-I wish ungekua msomaji kwanza wa mambo humu hoja husika na nyingine nyingi tu za baraka, kabla hujaibuka tu, tatizo lako la kupotea ktk mijadala kisha kurudi,makes all worse to your side, you are always late in here brother! Swala la matumizi ya akili nilisha mjibu Lwembe na hapa nalisisitiza kwa maandiko maana wapendwa tuache uvivu wa kufikiri tukiadhani tunatakiwa tu ku-spiritualize kila kitu au tusomapo Bible, tuwe kama ‘’marobots-kua hamna akili, fahamu, kuchekekecha, kutafakari, kuchambua, kuwaza deep nk tukidhani Ufunuo hujaga tu paap! pufuu kama kuangusha kitu! Yes, hata ukija ivyo, amini, amin nakuambia, tayari wewe kama MTU( unless uko robot wewe), yote uliyonayo, yanakua yametumika/nururishwa/huishwa/vuviwa/tumiwa. Kwa taaarifa yako katika ya yale Paul aliandika/sema unayosoma leo, yalitokana na Akili! nakuona unashituka! Tuache misisimko ya kukemea-kemea ovyo wapendwa, aya anasema mwenyewe ivi hapa- Mdo 26:25 ‘ninasema maneno ya ukweli na ya Akili( Kiingereza NKJ imetumia maneno ‘’words of truths and reason- ndani ya reasoning kuna akili, intellect, IQ, logic, thinking usages. Ishu ni kua ndani ya Mungu,moyo wote kwake kisha yote uliyonayo na Akili ikiwemo vinakua wonderful tools to use hence, wacha uvivu maana uyasomayo aliyosema Paul, kasema mwenyewe hapo, anaongea/aliongea maneno ya Akili! Kumbuka pia Mithali.3:9 imesema tusizitegemee Akili LAKINI HAIJASEMA TUSISITUMIE! Tena kwa context ya pale pale iyo Mithali, inaweza kua mbali sana na vile tumezoea kunukuu andiko ilo kuwazima Wapendwa kutokua Wapevu wa kufirikiri na kutafakari maneno ya Mungu. Halafu wewe mtu unasahauje kua Mtu ndani ya Kristo, yote yanakua mapya(akili safi imo kabisa ndio ile Paul CONDIDENTLY alimwambia Mkuu yule maneno ambayo leo unayasoma na tunasema ni ya Mungu na pia unasahau kabisa kua tukishaokoka,Roho Mtakatifu hukaa ndani yetu, sasa sijui Akili yako Haikaliwi? Jibu mwenyewe! All am saying kwako brother na Wapendwa wengine wenye tendency hii, STOP UVIVU WA KUFIKIRI, TUMIA AKILI PIA KWAKUA TU NDANI YA BWANA NA YOTE TULIYONAYO NI TOOLS NJEMA SANA KUYAENDEA MAMBO YAKE AS LONG AS HATUTOKI NJE YA MSTARI, nyie vipi wapendwa?!!!!!!!!

  Ati ‘’Tena mimi nimekupa maandiko ya kutosha kukuthibitishia kuhusu ninachokiamini na kukifahamu kuhusiana na UPOTOFU WA FUNDISHO LA UTOAJI WA ZAKA KWA WAKRISTO=Na mimi nimekupa maandiko haya mazito ambayo fanya ufanyanyo lakini mimi najua na nafsi yako inajua , hukatizi hapa..Mwanzo.14:1-20 Ibrahimi kwa kupenda /hiari/ /kujisikia/ kufurahia na more important to God na yeye..AKAAMUA kutoa ZAKA kabla ya sheria! Kwa iyo lecture zako zote zenye utata mwingi to be honest, za past, present, future, zinakua finished and dead kwa andiko hili maana unataka kutoroka kutoa zaka kwa kua wasema/hoja zako zote tata unaziegemeza kua ilikua ni sharia kutoa Zaka na hili Mathayo.23:23 Master mwenyewe anaongelea Zaka hapo WAZI WAZI au ile mnapenda, LIVE-LIVE na kamwe HAKATAZI ZAKA but wewe unakataza!!!!!! Lo! umetoa wapi ujasiri huo? nani mpotofu? Nani mtafsiri mbaya wa maandiko matakatifu? Nani ameshuka hadhi haswa? Nani anatumia akili vibaya?( maana kutumia akili vyema kuyajua mambo ya Mungu-Neno likiwemo, ni safi kabisa na baraka simply because Bwana Yesu hajaokoa pusi, boxes, empty tins au chimpanzee bali Wanadamu wenye akili na fahamu bora kabisa tena)

  Kwamba,‘’Lakini hufahamu kuwa kuwepo kwa mpangilio wa vitabu kwenye biblia si kuwa ndivyo ilivyoagizwa na Mungu bali ni utaratibu tu waliouweka wakusanyaji wa maandiko hayo ili kuleta mtiririko’’-ndio maana nikasema husomi vema post zote za wachangiaji humu kabla ya kuibuka, au ukisoma, unasoma za baadhi tu-mimi zikiwemo na bahati mbaya mengine bado, huelewi! Sometimes nijiangalia unavyojibu-mfano baada ya mimi kujibu maswali yako mengii yale, nakuona unakujaga na kunaanza tu hapo hapo unapokutia post na comments!!!!!!! hukuhitaji kulisema ili, tulishaligusia humu!!!!!!!

  Umekanusha,‘’Si kweli kuwa habari iliyoanza kuelezea ZAKA kwenye Mambo ya walawi 27:31-33 ndiyo yalikuwa maelekezo ya awali kabla ya yale ya kumbu kumbu la torati 14:21-28’= yapi yalikua na maelezo ya kwanza? Kitabu gani? Lakini pia kwa kuelewa sana ilo, inakusaidiaje wewe kutoroka/kugoma kutoa Zaka kanisani kwako? You see, ndio maana nilisema ktk response ya kwanza juu hapo kua, I am sorry brother, sikuona kitu ktk maelezo haya yote yako ya leo.

  Ume-claim kwa herufi kumbwa hivi’’HUU NI UPOTOFU MKUBWA WA KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU= ni kutia chumvi tu kusikokua na sababu, hamna upotofu wowote bali kuna UPOFU WA ROHONI WA WATU KUKATAA KUTOA KWA BWANA NA WATU WAKE NA UPORAJI UNASUKUMWA NA NAFSI ZA WANADAMU, KUYATWAA ISIVYOPASWA HATA YALE YAMPASAYO MOLA, NYUMBA YAKE, WAISHIMO NA KUTENDA HUDUMA HUMO NA WENGINE ILI

  Umesema, ‘’Ukweli ni kuwa Mambo ya walawi ni kitabu kuonyesha majukumu na wajibu wa kabila la Lawi, Kitabu cha kumbu kumbu la torati ni mtiririko wa sheria ambazo wana wa Israeli kwa ujumla wao kufuatana na makabila yao (Wakiwemo walawi) na kitabu cha hesabu kinatoa kumbu kumbu za matukio na maagizo mbali mbali wakati wote wa safari ya wana wa israel kuelekea kwenye nchi ya ahadi’’= kwa kutoa summary hii ambayo yeyote anawezaipata tu ktk google kirahisi kabisa kuhusu maudhui( central themes) ya vitabu vyote vya Bible, je umeweza onyesha kitabu gani kilianza kuandika kuhusu Zaka? kwa kua mie nimesema kwa kua naona Zaka ktk Walawi basi nayaona maelezo kuhusu zaka ktk mpangilio wa Bible tuliyonayo sasa yanaanzia hapo maana ndivyo ktk Bible vitabu vimepangwa ivyo lakini wewe ukasema ni upotofu wa kufasiri!!!!!!!! Ingawa pia sijakupata unapotumia neno kutafsiri maandiko(ukizingatia maana yake) na swala la kuelewa Kitabu gani kina aanza na kingine kilikuja baadaye.

  Lakini pia hata tukijua sana kitabu gani kilianza na kikafuata, ndio inaondoa ukweli kuhusu kumtolea Bwana Zaka kale na leo ni jambo la baraka? You see! Again sioni substance hapa kwa wewe kusema ivyo!

  Umesema‘’Ndiyo maana kwenye kitabu cha kumbu kumbu la Torati maelekezo kuhusiana na Zaka ni marefu na yamerudiwa mara nyingi kuanzia sura ya 12 mpaka ya 16 kuliko kwenye vitabu vingine’’= Kwa iyo?

  Press on

 85. Wapendwa,

  Kama nilivyosema hapo awali, nimejifunza mambo mengi sana katika mjadala huu! Pia ni vizuri kutokuyaacha hayo uliyojifunza ili yanapojitokeza huko mbele, basi ule ujuzi ulioupata ukusaidie katika mwenendo mzima wa kulishughulikia jambo hilo.

  Katika yanayozidi kujitokeza, moja kubwa nililoliona ni wapendwa kung’ang’ania jambo ambalo liko wazi kwa makusudi au kwa kutokuwa na uwezo wa kuelewa, au kwa kujilazimisha kutokuelewa kutokana na uoga wa kukubali makosa na hivyo kupiga hatua ikupasayo katika ukamilifu ambayo ingekufanya kuwa tofauti katika kusanyiko lako.

  Jambo linalojadiliwa hapa ni ZAKA na UTOAJI wake, Je, jambo hili linaendeshwa kulingana na muktadha wa Maandiko au NJE, na hivyo kulifanya jambo zima kuwa katika UPOTOFU kimafundisho? Michango ndivyo kama nyote mlivyoisoma, bali napenda kusema kwamba wengi niliowasoma, hao wenye kusema linaendeshwa katika upotofu, HAWAKUSEMA kuwa ZAKA ISITOLEWE! Ndio maana wakaleta na zile nyakati tatu, kabla ya Sheria, wakati wa Sheria na wakati wa Kanisa, wakiliweka wazi jambo hilo ili kuyabaini mapungufu na matokeo yake kiroho.

  Basi, nataka niseme kwamba, ni vizuri sote tukatambua kwamba, tunaishi katika Mifumo. Nayo Mfumo huwakilisha utawala. Ili Mifumo iwe kamili, husimamiwa. Ndiposa, unapokuwa chini ya Mfumo fulani, basi unakuwa na wajibu wa kuwatii wasimamizi wa Mfumo huo kimilifu ili undelee kufaidika na jumuiya hiyo kulingana na Mamlaka hiyo inayokutawala.

  Sasa, Mifumo hiyo ikiwa ni makanisa yetu, katika maana ya madhehebu, kama sote tunavyofahamu, taratibu zake za utawala zinatofautiana sana! Hiyo ni Kweli mojawapo ambayo hatupaswi kuifunika. Ndio kusema katika kutofautiana kwetu, tunapaswa kuziheshimu Mamlaka zinazotutawala kama Maandiko yanavyotufundisha. Nazo Mamlaka hizi za kidini zinazotutawala, licha ya kwamba mifumo yao ni tofauti kabisa na hiyo ya Kibiblia, bado zinatutawala kwa Neno la Mungu, Mt 23:1-3 “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda …”
  Kwahiyo ni halali kwa Mamlaka hizo ambazo leo hii zimekaa ktk Kiti cha Kristo, zisikilizwe nasi wafuasi wake katika yote wanayo tuamuru, pamoja na ZAKA katika jinsi yoyote ile watakayoiamuru ikusanywe! Katoliki nadhani wanakusanya mshahara wa wiki mbili katika mwaka, hicho ndicho kiwango chao cha ZAKA, wengine wameibadili wanaiita Ahadi nk. Nadhani katika wakabaji wa ZAKA, katika maana ya Fungu la Kumi, makanisa ya Kipentekoste katika maana ya vipawa, haswa haya mitume na manabii ndiyo yanaongoza, na hayana mchezo, laana zinatembea nje nje kwa wakwepaji!

  Pia jambo hili la ZAKA, katika makanisa ya Kipentekoste, limekuwa ndio kichocheo kikubwa cha mfumuko wa utitiri wa makanisa hayo, kwani kila pale yeyote yule ktk hao waumini wake, anapojitambua kuwa ana kipawa, haswa cha uponyaji, basi huwa hawachukui muda kabla hawajaanzisha “ministry” zao, na kukaa mkao wa kutajirika! Nimewaona wachangiaji wakizungumzia magari ya ‘hummer’; hayo ni kwa locals, bali wakali wenyewe wako mbali, wanashindana katika sophistications za jetplanes! Hilo ndilo ono lao wote, licha ya kujitambulisha na maskini wanapoanza. Wakianza kukubuhu huwa hawaonekani kirahisi tena kama pale mwanzo, mchujo ni mkali mpaka uwafikie kwa shida yako ya kuwaomba nauli! BALI inakubidi UTII! Hata nimewahi kumsikia mtume akitoa ahadi ya pesa kutokana na fungu la kumi analotegemea kulipata kutoka ktk mafao ya muumini wake anayetarajia kustaafu!!!

  Tazama, sote Mungu ametupa akili. Kuna wakristo wengi ambao wanaamini ktk kutumia akili na logic yake, hilo ni jema sana. Lakini kuna jambo ambalo hawajalifahamu, kule kuigawa akili hiyo aliyokupa Mungu, ili sehemu kubwa ya akili hiyo uitenge kulipokea Neno la Mungu kikamilifu, Imani ipate kuzaliwa, na ile sehemu ndogo iliyobaki, kuiamuru iwajibike kwa hiyo kubwa. Sasa hili lawezekana pale utakapoamua kulisikiliza Neno la Mungu katika ukamilifu wake. Ndio kusema Akili inaweza kubadilishwa na kuwa Nia ya Kristo, yaani, The Brain can be converted to the Mind of Christ, naye mtu aliyefika kuwa ktk jinsi hii, huyu ndiye huwa ule Mwili wa Kristo (the Mystical Body of Christ). Au mtu huyo pia iwapo Mafundisho ya Dhehebu lake, hilo lililokaa katika Kiti cha Kristo, yataichukua ile sehemu kubwa ya akili yake na kuitawala, basi akili ya mtu huyo pia hubadilishwa na kuwa Nia ya Fundisho hilo, naye mtu huyo huwa Mwili wa hilo Dhehebu, ile roho ya dhehebu, naye ataendelea kupingana na Kweli ya Biblia all the way right into perdition!

  Hivyo basi, sote na tufahamu ya kwamba tunawajibika kuzitii NIA zetu kulingana na miili tuliyobadilishwa kuwa, yaani kutoka ile miili iliyokuwa ya Mizimu kulingana na NIA ya Mizimu ya kwenu, kuja katika Nia tuliyo sasa; kulingana na dhehebu lako, yaani jela uliyofungwa, twapaswa kumtii Bwana Jela kikamilifu bila ya manung’uniko ya sijui nakula kwa mama ntilie dagaa! Jamani, mamantilie gani anapika dagaa, hizo ambazo kilo moja ni shs 20,000/=!! Au dagaa za kuku? Basi haijalishi unakula nini na wapi, unatakiwa utoe ZAKA kulingana na ulivyoamriwa!

  Tena uongo kama huu wa kujitia unakula kwa mama ntilie, siku zake si nyingi sana, maana tunataka katiba ya Tanganyika itakapotengenezwa kipengele cha ZAKA kiongezwe kwa wakristo wote ili iwe inakatwa moja kwa moja katika mshahara baada tu ya kodi ya mapato na pia kwa wafanya biashara katika hesabu zao za mwaka na kuwasilishwa moja kwa moja kwa madhehebu husika!!!

  Nasi tunaorudi huko Mwanzo, na kuwa watumwa wa Kristo,lile Neno, kulingana furaha yetu katika ushindi tuliopata au tunaoutarajia kulingana na Neno la Bwana, iwapo nasi tutamwambia Bwana tunakutolea FUNGU hili la KUMI kutoka nyara ulizotubariki, kama alivyofanya baba yetu Ibrahimu, au tukamwambia, “Bwana, ukitushindia katika haya tuyaendeayo, kama kaka yetu Yakobo nasi twakuahidi KIKUMI katika yote!” Basi twapaswa kufahamu kwamba tumejitia katika majaribu, hivyo twapaswa kusimama imara ktk kuilinda Ahadi yetu hiyo hata kifo, maana nguvu zote za kuzimu huinuka kuhakikisha HAUITIMIZI Ahadi yako hiyo! Usikurupuke kumuahidi Mungu jambo lolote kwa akili zako au ushawishi wa dini, kaa chini, umuombe Mungu akuongoze katika hilo upendalo kulifanya, KUMTOLEA MUNGU FUNGU LA KUMI, ndipo kwa Imani uinuke na kuliahidi na kulitenda katika ukamilifu wake kama ulivyoliahidi, USIZIDISHE wala USIPUNGUZE kwa kisingizio chochote kile! Haleluyaaaa, Neno limetimia, Milango ya Kuzimu umeishinda katika Yeye akupaye Kushinda!!!

  TAYARISHA makapu na maghala ya kuhifadhia, BOMBA la BARAKA li tayari kukufungukia, endelea kumtukuza Bwana!!!

  Mbarikiwe nyoote, mliochangia na kulifungua jambo hili, maana Elimu zoote zimeletwa katika kipimo cha Neno la Mungu, ili Mungu mwenyewe apate kujitukuza ndani yetu sote tulioshiriki mjadala huu!

  Amen!!!!!!

 86. Amin Yeremiah Mguluma

  Unajua una maelezo mengi lakini hamna kitu, bora yawe na vitu brother!!!!! Sorry!!!!!!!!. Mr Sungura amependekeza kufikiria kuhitimisha mada hii ingawa pia niligusia ilo ktk michango yangu ya mwisho mwishoni ili tuweke wazi kila mtu hapa msimamo wake, nitafanya ivyo ivi karibuni lakini kabla ya hapo, kutokana na wewe kuibua mengi tena , nijibu tu kwa kifupi ili ukiendelea au tunapo hitimisha, nijue moja kwa moja uko wapi maana ni kama sikuelewi-elewi vile! because kwa upande mmoja, utaongelea kwa uzuri Utaoji wa Zaka zamani,upande wa pili, unaongela ni upotofu kufanya ivyo LEO BILA KUONYESHA TUMEPOTOKAJE MAKANISANI KWETU LEO, SISI WAUMINI TUNAOTOA ZAKA KWA HIARI NA KUPENDA INGAWA MLILIWEKA NA KUIJADILI KI-NEGATIVE ZAIDI KUONYESHA UKO NA KULE MAKANISANI NI KAMA TUNAPIGWA KABARI DIRECTLY AU INDIRECTY KUTOA ZAKA.

  MASWALI MAKUU YANGU KWAKO NI:

  MOJA:Wewe kama mtu wa Mungu wa dhati na unamtaja Roho Mtakatifu kua anakuongoza hata kunishauri mie( ushauri wa ajabu kweli maana angekua anakuongoza, ningeona tu hapa moyo wako), je unatoa zaka au hautoi kamwe LEO hii? Niko very interested ujibu hapo CLEARLY AND OPENLY

  PILI: Kama Zama izi hautoi kamwe kwa kua inasemekana ni FUNDISHO POTOFU yaani in effect tunaomtolea Mungu zaka leo, tumepotoka au tumemeza fundisho la uharibufu au ovu, wapi SPECIFICALLY Biblia imesema ivyo au indirectly na kua HAKIKA SISI LEO WANA WA Mungu tukifanya ivo ni uasi dhidi ya kweLi ya Maandiko au Neno la Mungu na kazi ya Kristo msalabani? Tell me very clearly then tutakua tunatamitisha hii mada soon

  Maelezo yako mengine yoote, kusema kweli nimeya-treat cheaply kwa kua nakuona kwanza hausomi michango inayotolewa humu hasa yangu na wengine walioongea kuhusu Zaka jana na leo safi(nitagusia why nakuona ivyo ktk response yangu ya ujumla kwa uliyosema ktk posy yako), pili unaibua vitu vingine ambavyo havina substance..mfano jijibu tu mwenyewe kwa nini mambo kuhusu wafalme au Waamuzi, hatuvikuti ktk sehemu ya kitabu cha ufunuo au mbele ya Mathayo? Unadhani waliopanga ivyo unawazidi shule ya Dini/theologia/Maandiko ? Wewe? we vipi bwanaa! Sasa unajengaje hoja dhaifu kuhusu kati ya Mambo ya Walawi na Kumbukumbua au Hesabu kuanza au kutoanza, kua na content hii au ile? Is that an issue hapa ktk hoja hii? Sasa kama content za vitabu ivyo ni izo ulizosema, so what? Inaondoa ukweli kua Zaka ni moja ya ingredients kubwa ktk Agano la Kale kuanzia kwa Musa na vitabu vingine hata Nehemiah? Hoja ktk meza ni Zaka kila mwezi au nipatapo kipato na kama Zaka ipo ktk Maandiko Kale na Leo na ivyo tutoe au la AU hoja ni kitabu hiki na kile kina haya na yale? Lo! plz don’t rush brother, jumping out so easily !!!!!!!!! Tafadhari jibu yale maswali 2 tu pale juu ili kuku-limit ktk lile haswaa tunalotaka kujua ufahamu/msimamo wako Hai and Biblically supported kati ya maswali meeengiii unayafukia kila ujibupo!
  Press on

 87. Seleli, Sungura, Lwembe, Kaswahili na wengine wote…
  Ha ha ha haa!! Unachekesha sana mjoli wa Bwana. Mimi nimekupata vizuri. Lakini ukisoma koments zangu toka juu, utanikuta nasisitiza kuwa Utoaji wa matoleo yote, ikiwemo ZAKA, ni mojawapo ya njia ya kuihubiri injili. Sasa kama ni mojawapo ya utimizaji wa agizo la Kristo la “Enendeni ulimwenguni kote mkihubiri injili….Math 28:19”, sidhani kama kuna excuse hapa ya kuanza kujustify kuwa kuna uhiari ama la!. Tukisema kutoa zaka ni hiari, ni sawa na kusema kuwa, kuihubiri injili nako ni hiari!! Maana matoleo ikiwemo zaka, hufanya kazi ya utume yaani kuwafikia watu hadi maeneo ya mbali sana tusikoweza kufika wengine.
  Kufanya kazi ya Mungu hakuna uhiriari hapo. Ni suala la kutii uishi, kataa ufe. Yona alijidai kuwa mtu wa hoja nzuri na nyingi sana, hadi akaamua kufa (kutupwa baharini) kisa anakimbia-kukataa kufanya kazi ya Mungu, bado Mungu alimtoa huko kilindini mwa bahari akiwa amenyoroka ile mbaya. Mungu akiamua kutuadhibu kwa kutokutoa zaka/matoleo eti tukijidadi kuwa ni hiari, aweza kutuadhibu papo hapo ama atakuja kutuadhibu baadaye tu, maana kazi yake imejengwa kwenye misingi ya tii uishi, asi ufe.
  Hata Paulo alilisisitiza hili suala la kutoa kuwa, ni lazima watu watoe ili kazi ya Bwana isonge mbele..
  Warumi 10:14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
  15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
  Bwana awabariki sana.

 88. Mpendwa Edwin Salaam
  Ninamshukuru Mno Mungu baba wa Bwana wetu Yesu kristo kwa namna atupavyo kushinda naam na zaidi ya kushinda
  Nimesoma tena majibu yako uliyotoa siku kadhaa nyuma kuhusiana na post yangu inayodhihirisha kuwa utoaji wa Zaka kwa mkristo ni fundisho potofu na si la kibiblia.
  Na kwa kudhihirisha hilo katika hatua ya awali umeonyesha dhahiri ambavyo unachuja ngamia na kumeza mbu kwa kuamua kwa dhahiri kukata mtiririko wa andiko ili upate unachokihitaji.
  Ukweli ni kuwa vyovyote ulivyonitambua ndiye mimi hasa na si mwingine hivyo ulichojibu ndicho ulivyonielewa.
  Katika hatua ya awali kabisa umetaka kuukwepa ukweli wa kimaandiko kuwa mtoa zaka ndiye mla zaka kwa kuzingatia maandiko haya yafuatayo;
  ‘Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
  Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima. ‘
  Unachopaswa ni kuwa KUTOA ZAKA NA KISHA KUTUMIA MBELE ZA BWANA MUNGU NDICHO KINACHOPELEKEA KUJIFUNZA KUMCHA BWANA MUNGU WAKO na si KUTOA ZAKA PEKEE.Kama umeelewa maudhui ya mistari hiyo ya Kumb 14:22-23. Kwa hiyo kufikia hapa umepoteza hadhi ya kutafsiri maandiko kama mwalimu wa neno la Mungu.
  Rafiki yangu acha kutumia hadaa kwenye tafsiri ya maandiko bali hebu mruhusu Roho mtakatifu atende kazi ndani yako ili uwekwe huru kweli kweli. Nilichokuandikia ni kitu nilichofanyia utafiti wa kutosha ikiwemo kupitia Bible comentaries kadhaa na kutafakari tafsiri zake.Kwa bahati mbaya unapojenga hoja zako hutaka kutuliza akili zako za kawaida na kuyapitia maandiko haya ambayo kwa hakika yapo wazi na hayajifichi.Tena mimi nimekupa maandiko ya kutosha kukuthibitishia kuhusu ninachokiamini na kukifahamu kuhusiana na UPOTOFU WA FUNDISHO LA UTOAJI WA ZAKA KWA WAKRISTO.
  Inasikitisha kuwa ingawa unajifanya mjuzi kuhusiana na biblia kwa kutaka nitafute vyanzo vingine vya kujifunza namna bora ya kuisoma biblia,lakini hufahamu kuwa kuwepo kwa mpangilio wa vitabu kwenye biblia si kuwa ndivyo ilivyoagizwa na Mungu bali ni utaratibu tu waliouweka wakusanyaji wa maandiko hayo ili kuleta mtiririko wenye kurahisisha usomaji na upataji wa habari kwenye kitabu hivyo. Si kweli kuwa habari iliyoanza kuelezea ZAKA kwenye Mambo ya walawi 27:31-33 ndiyo yalikuwa maelekezo ya awali kabla ya yale ya kumbu kumbu la torati 14:21-28. HUU NI UPOTOFU MKUBWA WA KUTAFSIRI MAANDIKO MATAKATIFU.
  Ukweli ni kuwa Mambo ya walawi ni kitabu kilichoandikwa maalum kuonyesha majukumu na wajibu wa kabila la Lawi kama ukoo wa Kikuhani na Kitabu cha kumbu kumbu la torati ni mtiririko wa sheria ambazo wana wa Israeli kwa ujumla wao kufuatana na makabila yao (Wakiwemo walawi) walipaswa kuzifuata. Wakati huo huo kitabu cha hesabu kinatoa kumbu kumbu za matukio na maagizo mbali mbali wakati wote wa safari ya wana wa israel kuelekea kwenye nchi ya ahadi.
  Ndiyo maana unaona kuwa kwenye kitabu cha kumbu kumbu la Torati maelekezo kuhusiana na Zaka ni marefu na yamerudiwa mara nyingi kuanzia sura ya 12 mpaka ya 16 kuliko kwenye vitabu vingine.

 89. Seleli maombi yako ya Mungu kutunyang’anya vingi tulivyonavyo il upewe wewe uliye na vichache hayatasikiwa. Zaidi sana wewe utanyang’wanywa vichache vyako tupewe sisi wenye vingi.

  Mawazo yako unayosema ya kula kwa mama ntilie huwa ni mawazo ambayo unayakuta kwa watu masikini tu, wala kwa tajiri huyakuti. Kula kwa mama ntilie siyo unyenyekevu ni umasikini tu wala usijifariji.

  Nilidhani wewe unayejisema ni mwaminifu wa kutoa zaka ulishatoka kwenye kula kwa mama ntilie, kumbe na wewe bado unaogelea humohumo walimo wakristo wengi!!! Kwani madirisha hayajafunguka tu Seleli tangu umeanza kutoa?

  Kusema kweli unaflow off ile mbaya. Na ili Lwembe asiendelee kunivunja mbavu kwa sababu ya comments zako tufikirie kuhitimisha sasa.

  Kukubaliana na kutokukubaliana yote ni mema.

 90. Lwembe,

  Mmmmmmm! maneno tu ayo lakini ukweli ni kwamba si wewe wala Sungura so far aliye kabiliana na hoja zangu barabara, Wengi mnakwepa kujibu maswaali yangu ingawa mie hakuna swali mnaloniuliza hata kama ni off au by the way, naloaacha aidha nalikakabili kama lilivyo au hata kuligusia tu kwa yale by the ways na napo-nukta kwa nukta clear your things, mnaibuka na mengine, Wacheni maneno hapa, toeni izo pesa na mali makanisanI kwenu, kwa kazi ya Bwana na Makuhani wenu, mambo ya Juu Yakwende BASI

  PRESS ON

 91. @ Seleli,
  Kaka, wamekutoa steam yote! Naona sasa unaflow off ile mbaya, tunajidundia tu!!!

  Kula pozi kidogo mpaka kaupako karudi!
  Kaka Siyi yeye nasubiri upako toka Sheria za Maadili zile naandikwa kwa kidole cha Mungu!!

  Chezea Sungura wewe!!!!!

 92. Lwembe na siyi, mapacha,

  Ati mnasema? ole wenu na nyinyi kama mnakataa kutoa zaka kwa hoja dhaifu na mfu, zisemeni hapa tuzikwangue vibaya/vizuri sana, mnataka kuleta mambo ya nafsi kwa ela ya Mungu na mali anazo wapa kwa muda tu Mungu Baba, kuzifurahia na kumtumikia nazo kwazo? mtanyanganywa enyi nyote nyie kisha tupwe wengine ambao when it come to God and things of the Kingdom, kulala njaa na kuvaa kawaida ili mambo ya JUU yakwenda si issue! kwani nikila kwa mama ntilie dagaa safi,kapilipili kidogo na kalimao kwa mbaaali escorted na kabamia na ugali sembe kwa alfu 2 badala ya alfu 3-5 kwa hotel halafu mwisho wa mwezi najikuta nimesave alfu 2 kwa kila mlo kwa kuiminya na kuitandika nafsi yangu kwa kipengele cha msosi tu hapo bado vocha, moderm ya internet,movies kununua cd na magari ya mikopo pia poloti za kule wapi kule naninhiii mabwepande, niambie hapo sijafanya kitu kwa Bwana nyumbani mwake, kwa Watumish wake na Watu wake?Kinachogomba hapa si ati kuna fundisho la kweli la Mungu wa mbinguni tumelikosana/tunakosea sana huko makanisani kwetu kuhusa zaka na sijui why zaka tu maana hata matoleo mengine yote yalianzia uko uko tu kwa Agano la KALE na tumehama nayo todate lakini eti Lwembe, Kaswahili, YeremIa, sijui na Mabinza na mwenyewe Sungura na Ivi na wewe Siyi au nakosea, ati wanasema ni laaana kutoa Zaka wakati ni kwa kupenda kwangu mwenyewe na kwa raha zangu na Bwana !!!!! jamani mwe!hapa hamna kingine bali nafsi selfish na tafuteni kwanza Ufalme wa Dunia spirit, hmna lolote

  Press on

 93. Ha ha ha haaa!! Lwembe, Umewaona eee!! Mimi nawachungulia tu kwanza, wamenyane weee!! But watambue kuwa, kweli ya Mungu huwa haishadidiwi na logic za watu. Huwa inasimama yenyewe tu. Hata kama watu watatafuta defending mechanisms, bado neno la Mungu litasimama palepale.
  Bwana autsaidie sote.

 94. Hahahahaha…!
  Kaswahili, ulidhani “Mfia Dini” ni Siyi tu, enhe? The debate has proved you wrong!

  “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote”; hamjaambiwa muwakanyage vidole wenzenu kwa viatu vyenu vya mchuchumio!! Amani itatoweka, oh hoo!

 95. Sungura,

  Nothing is to much here for me or any body who loves to give to God without human selfish nature influences! Only those who are still in the bondage of ‘Second things First’’ and are not freely enjoying the life of ‘’First things First’, will see/twist minor/clearer things to be hard just to blanket their own ego.

  Weledi wa kutosha nilionao mimi ni huu….. ninatoa zaka na matolea yote bila kujisaza wala kuwaza kwa msukumo wa kibinadamu kibaya wala si nia safi ya Ki- Mungu, eti kutafiti zaka kuwepo kabla na baada ya torati, kwanini? kwakua tu nampenda Mungu, Kazi na Watu wake basi, sitaki zaidi na nitampinga kila anayeleta zaidi au pungufu ya hapo kuninyima fursa iyo au kuwaingizia idea nyingine watu ili wachukulie mambo haya cheap tu, ufanye usifanye safi tu, kisa mpaka uguswe/ujisikie…-hatuenendi kwa kujisikia/hisia bali Neno linasemaje/limeonyesha nini.Kama unawaona ktk Bible wapo waliotoa kwa moyo wa kupenda, unangoja nini kutoa sasa? si utende Neno wewe! kama walitoa zaka kabla ya sheria na YESU mwenyewe akasemelea/gusia kwa namna ile, acha manenno yako cheap haya ya Sungura wa TZ, unangoja nini kutoa? Kujisikia eti! Na NENO lililokuonyesha/fundisha ivyo lina power gani ya kua final kwako ikiwa hisia/kujisikia/kuguswaaa ndio dira/activating/deciding factor ya utendaji wetu wote or atleast wa kila mara? We vipi ndugu! Unashindwa kudaka iyo halafu unasema/imply una weledi! unahitaji maombi si weledi in the first place, hali yako ni tete na too extreme.

  Kama utumwa wa dini ni kua na msimamo ule pale juu, basi nasema kama Yakobo, kua kuna dini safi/nzuri, yangu moja wapo ila yako mbovu kweli, haifai maana inaleta mambo ya Mungu na ya kibinadamu kibaya umo umo. Swala la kua na upendo wa Kristo ku-engage na mimi ktk debate hii,nimelithibitisha ilo sana zaidi yako hata wakati unapitiliza na meneno yako na majina uliyoniita kwanza na baadae. Mimi kusema kweli sipotezi muda, niko ktk huduma kabisa hapa kuhakikisha mambo ya Mungu, Kanisa., Watumishi ambayo tumekua nayo miaka tena yaliyo na uhai, si mafu, yenye kusukuma kazi ya Mungu mbele, hayo yasimame kisha kubomoa kila fikra na elimu ipingayo hayo, wewe ndio utajua kama unapoteza au uko ktk huduma pia na sijui ya nani( Bwana Yesu, bwana wewe au yule mwingine simtaji)

  Ati ‘Seleli ivi unaelewa maana ya neno kujisikia kufanya kitu fulani? JIBU: Naelewa kabisaa hakuna kiguma hapo na hasa kwa muktadha wa mada hii ni Ni kupenda/ kuridhia /kuhiari/kufurahia/kutaka PIA MUHIMU ZAIDI KWANGU..ni kuamua kutenda. Na mimi nikuulize swali ingawa haujibu maswali wewe! Ukiona jambo linakuhitaji/unajua kabisa linakuhitaji/ukataarifiwa kabisa kua unatakiwa/ unajua kabis bila nguvu yenu ya pamoja pale kanisai , mambo hayakwendi, utangoja UJISIKIE iyo yako? Ukijibu ivyo, utaelewa kwanini nimekomaa against iyo tabia/tendency kwa watu wa Mungu na tunajua inavyokwamisha mengi ya Mungu lakini yao,hayakwami wala hawangoji kujisikia yako -icho nacho hudaki na kisha unasema una weledi! Unashindwa kabisa kuona kwa kuzingatia hali halisi iliyopo ktk makanisa mengi, iyo kujisikiiiia/kungoja kuguswaaaa inavyo suffocate mengi-unakua kama hujui wakati unajua, sasa una weledi wewe au mbishi tu wa kawaida ku-back mambo yako binafsi yasiyo na faida kwa kanisa? Mimi nikiamua kupambana na iyo, una sema niko ktk kifungo cha dini! basi dini kama ni iyo, aisee na idumu sana na ni vema kua nayo na nitaishikilia kweli kweli.

  Sasa hili nalo nila kusema au ni yale yale tu? unakubali nini, unakataa nini?
  kwa hii hapa?..’’Elewa kuwa mfumo aliotoa nao Ibra ni tofauti kabisaaa kwa mbali na mfumo unaosisitizwa katika kitabu cha Malaki= bila shaka ndio, sasa ya nini tena hapa! Wewe si uchukue ya Ibra! Utachukua iyo? endelea nayo na ubarikiwe si tena maswali ya kabla na baada ya totari pale noti/account au Mali zako zikitakiwa kufanya jambo

  Na hii..’’Ndio maana humwoni Ibra mahali pengine akitoa zaka tofauti na hapo kwa Melkizedeki’’’ KWA HIYO? Tutoe mara moja tu eee? Si unaona sasa mambo yako! Ndio maana nimekuuliza pale juu, wewe hueleweki wakataa nini, wakubali nini maana hutasema ivi vema sana kuhusu Hiari halafu ghafla idea una inject! Na pia kumbe unaweza kua-assume pia siyo..kua hatumuoni akitoa tena ili utuangalisha wazo ilo uliwazalo kua sahihi ingawa si sahihi kwa hapa! Sasa mbona ulikua unanikataza kuassume/kutpa ideas sustancial? Again, unakataa nini , unakubaliga nini!

  Sasa unaleta kituko kingine hiki..’’Ngoja leo nimalizie na kitu kigumu kidogo; Zaka ndio chanzo mojawapo kikubwa cha umasikini uliopindukia kwa kanisa leo!!! Unaona sasa! ati unaweledi! Hili limetoka wapi? Nipe andiko? Nalingoja ilo andiko.! Sungura kaka wacha maneno, toa zaka, hacholopoki mtu hapa. Unaibuka na hili la kwenda mbali ya hoja, niking’oka na kuruka na wewe uko nje, unanikimbia na kunisema niko nje! Wewe! Stop mambo yako hayo kaka.

  Press on

 96. Sungura,

  Mistari niliyowapa hii ya Mwanzo. 14:1-20 na Mathayo. 23:23, inatosha sana, so usiniambie kua niliyowapa haitoshi wakati hujaweza na HUTAWEZA KUIPINGA KWA HOJA kuhusu zaka Agano la Kale na Jipya.Mwanzoni kulee ktk michango yenu(tatizo mnakosa kabisaaa ‘upako’ wa nukta kwa nukta), mlioonyesha /sema indirectly or directly kua hakuna andiko ktk Agano Jipya kuhusu Zaka wala uwezekano wa Zaka kua ilihama, bali iliishia kule kule ilikoanzia!

  Kwanini nimewapa akina google family? Kwanza, maandiko niliyowapa unayosema hayatoshi mpaka niwape hayo ya akina google, ni hayo hayo tu, hii Mathayo.23:23 ya google ndio iyo ya kwako hapo ktk printed copy ya Biblia yako na pia waliyosema jamaa wa au walirushia kwa google YALIYOSAHIHI kulingana na Bible ndio hayo hayo tu, sasa kwanini kama hamtamwamini Seleli, msiamini hata wenye akili nyingi za kusomea dini na Historia ya Kanisa na materials za ivyo? kwa ugumu wa mioyo, si angalau niwaandikie mruhusu kutoa taraka = kufundishwa na wengine kwa namna nyingine labda mtapona? Kwamba, nihakikishe nafanya check & balance kisha niamue! Aa bwanaa Sungura, nilishaamua siku nyingi mie, hii ‘taraka permit’’ application hapa, ni kwa ajili yenu tu wenye spesheli mind/mioyo. Kama wapo wanaokataa, ukakimblia uko, uku wako wanaokubali ambao wengine hawamjui Mungu bali ni degree tu za Dini ktk Vyuo yet wakaja na conclusion izo za kukubali Yesu hakukataza zaka bila shaka baada ya kufanya tafiti na kukubuhu ktk Elimu Dunia dini kuliko wewe, huoni hao wanakushitaki kaka? ni ushahidi/ ushuhuhuda mbele za Mwenyewe maana usisahu imeandikwa ..’’Haki yenu isipozidi…si tu hamtaingia bali pia KAMWE!…

  Umekana/jiaminisha kua..’’Hakuna falsafa mpya niliyoleta toka kwa hao uliowanukuu ambayo hatujaijadili tayari hapa’’ Jibu: Basi Nashauri(nashauri tu si lazima) kua tendeni kwa BIDII pia bila kuitegea sana ‘Hiari’ au ‘gusa/jisikia’ spirit kutoa zaka maana hao niliwaletea wameikubali sina uhakika kwa Roho bali kisomi sana, nadhani shule yao ya dini/maandiko.Historia ya Wana Israeli na mambo yao ya kuabudu na utoaji ni kubwa sana, inatisha, labda una insignificant dot moja tu ktk cv yako kuhusu elimu Dini/Maandiko as compared na wao/ CV zao, Plz wasikilize hao, mwache Seleli pendingii kwanza ila utashanga kukuta mwisho wa siku ni yale yale alokumbieni.

  Umenituma, nikamuulize aliyesema Zaka zina finance Kazi ya Mungu swali hili:’’Did Abraham or Jacob tithe to finance God’s work? Or did the first church tithe to finance God’s work or rather offered contributions by even some of them selling their own properties? JIBU: Wala simfuati kumuuliza, ni my size ili sema tu hunanionaga bado sijasoma Historia sijui ya Kanisa na bwana gavana Galange na eti Histori ya kuanza Utoaji wa Zaka kwa mfumo huu wa Yeremia Amini, so Abraham tithed and Jacob DID NOT in the first place RATHER PLEDGED-showed readiness to do it(notice: don’t make the same mistake about Jacob-why doing the same foul while already cleared? you c.. same syndrome-‘nukta kwa nukta anointing-less!!!!),they did so to show their love, appreciations, thanksgiving and dependency to God. By that time, SO CALLED WORK OF GOD IN AN UNIFIED STRUCTURES, WAS NOT YET INSTITUTED, nonetheless, notice here importantly, TITHE or willingfull heart to give is indisputable. Later when the Work of God indeed in a known protocol began to operate, then we see the financing fact stomed in, the same truth is holding water with us today hence tithing in this regards, is critically justified. As a matter of fact, bearing in mind the todays work of God’s needs being far huge compared to those days eg today the population is estimated to number almost 7 bil and I am afraid almost more than 3\4 got no JESUS in their life-going to hell should their breathing in and out job is made to cease, you can understand now why we need your 20,30,50…100 and now with this fact, 7bil yet 3\4 Jesus-less humans, Sungura and the like, bring your 150, 170….10000, say amen if you love them to be saved and get the ticket to see our father in heaven, say it now?waiting!!!!!!!!! sasa hapo kuna haja ya kumfuata yule jamaa uliniambia kumuuliza kweli?aa bwana!

  Mwisho umenipa task nyingine(da! wewe kwa kuni-assign haujambo but mi nafanya tu tasks zako kwa uaminifu kabisa, ngoja ije wewe, eti easily wasema hakuna cha kujibu!! mwe! kha!) Ati..’’niendelee na kufanya utafiti, nitaupata tu ukweli’’ JIBU: sifanyi utafiti kwa jambo lililo clear, ni sawa sawa kuniambia nitafiti suruali niliyoivaa kwa body yangu!!!!!!! Maombi spesheli yatahitjika kwa such person

  Press on but now, no more 10 but ni 150..170……10000! sasa je? Au hujaguswa/mpaka ujisikieeeee wakati ni kuona na kutenda mara moja kwa sababu ya fact/assumption hii ya almost ¾ ya 7 bil, no Jesus!-all on the way to hell FOR HE SAID,’I AM THE WAY, TRUTH AND THE LIGHT,NO ONE COMES TO FATHER (BE WITH GOD IN HEAVEN) EXCEPT THROUGH ME- JESUS ONLY.So paifull all those souls are in danger/risk of hell fire halafu bado mnabania vihela na vimali vyenu vya duniani tena tulivyopewa na Mwenyewe kwa muda kama mawakili/wawakilishi wake wa kumiliki na kutawala! Ee Mungu tusaidie au nipe ela na mali zote za Sungura, Kaswahili, Yeremiah, Lwembe, Milinga, wanyang’anye ee Bwana, nipe mie, nifanye vitu hatari for your glory my father amen, mi ni full kujiachia kwake ili mradi basically tu si kianasa sana- tunakula na kulala na shule na hospitali kwa my ukoo/family, yatosha, mengine kwa Bwana, sina haja kukaa nayo saaana/yooote wakati hata nikiyatoa tena ndio safi maana yote nitayakuta kwa data base ya JUU again for my own gain eternally.

  Press on.

 97. Seleli I think this topic was too much for you, I don’t see you comprehending anything to help you out of the ditch that you are in!!!!

  Kama uko na weledi wa kutosha ambao unaweza kukusaidia ukauona ukweli na nafsi yako ikaelewa hata kama hutakiri kwetu, basi soma tena hata tu mchango wa Lwembe hapo juu maana ame-paraphrase vizuri kile ambacho tumekuwa tukikijadili.

  Kimsingi ninavyokuaona ni kwamba ukweli wa maana na nafasi ya fungu la kumi leo kutokana na maelezo ambayo tumekupa umeuelewa. Ila utumwa wa dini umekushika kiasi kwamba wewe ili ujue umemtolea Mungu lazima neno ‘fungu la kumi’ liwepo katik utoaji wako. Ukweli kuna wakati nimekuwa nikiona kama napoteza muda kujadili na wewe hii mada, lakini basi tu nimevumilia kwa sababu ya upendo wa Mungu.

  Hebu ona ulivyosema hapa kwa mfano wakat unaninukuu mimi: ”… unakubali pia Ibrahimu alitoa KWA HIARI-mfano ulioutumia sana na wa kweli kabisa lakini hapo hapo unasahua KWA HIARI iyo iyo Ibra huyo huyo alitenga tenth of..! Was that sheria? Si unaona unavyomisi nukta-nukta flow na mpaka huna sahau ulisema nini/umetoka wapi na unakwendaje, Kaka Sungura bwanaa!”

  Seleli unaponiambia nimesahau kwa hiari hiyohiyo Ibra alitenga tenth of.., ala, kumbe ile hiari ambayo mimi nimeisema kwa kuirudiarudia ulidhani nilikuwa nasemea hiari ya Ibra kutoa nini kama siyo fungu la kumi kwa Melkizedeki!!!???
  Au kuna nini kingine ambacho unamuona Ibra akitoa kwa hiari( kwa kuamua mwenyewe) ?
  U mguna wa kuelewa logic katika sentensi Seleli.

  Seleli ivi unaelewa maana ya neno kujisikia kufanya kitu fulani? Hebu sema maana yake halafu tuone kama wewe huwa hujisikii.

  Siyo mimi Seleli, biblia yenyewe imesema wanaong’ang’ana kuwa chini ya sheria wako chini ya laana. Ni ukweli usiopingika, kuwa kwa maelezo yako hata ya hii comment yako ya mwisho, unatoa zaka kwa mfumo wa sheria ya torati ya Musa.
  Elewa kuwa mfumo aliotoa nao Ibra ni tofauti kabisaaa kwa mbali na mfumo unaosisitizwa katika kitabu cha Malaki.

  Ndio maana humwoni Ibra mahali pengine akitoa zaka tofauti na hapo kwa Melkizedeki. Seleli kama wewe ukipata elfu tano lazima uitolee zaka ndipo ufanye mambo mengine hiyo ni sheria ndugu yangu wala siyo hiari kama unavyodhani. Mbona unashindwa kutofautisha hivi vitu viwili wewe?(neno hiari kwako limekuwa lugha ngumu kweli japokuwa hata hujui kama hulielewi na ndo linakufanya u-miss point)

  Ngoja leo nimalizie na kitu kigumu kidogo; Zaka ndio chanzo mojawapo kikubwa cha umasikini uliopindukia kwa kanisa leo!!!

  Asante.

  .

 98. Sungura,

  Umesisitiza kua umesema tena na tena kwamba zaka ni toleo la hiari, na anayetaka kutoa ikiwezekana atoe kila siku, si kila mwezi tu au wiki = EXCELLENT!…nimependa iyo ya kila siku which can also symbolically means KUTOA KWA SABABU TUNAMPENDA NA HIARI BILA KUFUNGWA NA TIMINGS. Hapa tunakubaliana swadakta kabisa Sungura. Hata ivyo, si wewe umesema ni Biblia ilishasema wakati wa Daudi na tunavyomuona Ibrahimu kuhusu kutoa kwa Hiari na moyo wa kupenda, si kitu kigeni ulichosema, Ni Neno la Mungu si la Sungura ivyo huitaji nguvu kubwa kulisemelea ilo maana twalosoma ktk Biblia wazi wazi tu.

  Pia ukasema, asiyemtolea Mungu kwa njia ya zaka asihukumiwe kuwa anatenda dhambi, hakuna dhambi yoyote anayotenda. NI KWELI MAANA KWA MSINGI WA KUTOA KWA HIARI, YUKO SAWA ILA ASIZOEE TABIA IYO YA KUACHA ACHA KUTOA TU NA HIARI YAKE KUA CRONICALLY NGONJWA TU 24/7 MAANA HAIWI-ACTIVE ZINAPOGUSWA NOTI ZAKE KWA MAMBO YA MUNGU NA WENGINE BUT KWA YA KWAKE TU, lo! ni hatari! Hiari iyo ni so active 24hrs.

  Umesema, ‘ninakudanganya au sijui maana ya fungu la kumi, ila nachojua ni kumtolea Mungu basi’ du! Hii kali! Mi nakudanganya! We kweli afande bro! Nakana sijakudanganya maana najua Fungu la Kumi ni sehemu ya kumi ya…ingawa pia natarajia kuiona miaka ktk uhai wangu Bwana akinibarikia mno kisha nitatoa kwa hiari na kupenda na kwa kua hairi yangu si ngonjwa wala in-active hence, nitatoa zaidi ya sehemu ya kumi ya…namely sehemu ya ishirini, hamsini ya….nk!

  Umesema,’’ninaposema sitoi fungu la kumi kama sheria, maana yake ni kwamba naweza kupata laki tano nikaitoa yote kwenye mchango wa ujenzi wa kanisa bila kuwa nimeondoa ile hamasini elfu kuitoa kama zaka, hicho ndicho una maanisha Seleli?JIBU: Ndiyo, nitatoa kwanza Zaka kisha inayobaki nitatoa tena mengine kwa raha zangu kabisa kwa our dad up there, sina shida ya nafsi ktk hayo, mwenzio nilishadata kwa Bwana kuhusu kutoa na kuachilia kila kitu(at leat mengi) na NASEMA KWELI MBELE ZA BWANA NA MUNGU YUKO HAPA ANANIONA ILE SOFTWARE NILIYONAYO /ALONIPA/NILIYOAMUA KUA NAYO KUHUSU KUJITOA/KUTOA HATA KAMA SINA MILIONI!-maana sasa inabidi tuwe hai mbele za Bwana hapa si tu ilimradi kusema-sema na kujadili-jadili wee, na ajishuudie mtu kwa utukufu wa BWANA maana hata Yesu alijishuhudia na walipombana akawapa live kua kwanza yuko sahihi kusema kweli kujiuhusu maana ni kweli tu lakini pia hayuko mwenyewe bali Yeye aliyemtuma yuko naye naye anamshuhudia na walipokua wabishi sana , dini zimawajaa, akawamaliza kua kama yote hayo, hayawaingii basi wazifanyie TBS kazi zake, watagundua zinamshuhudia kuliko maelezo. Besides, kutenga tenth of… ilifanyika kabla ya sheria!!!!ivyo si sheria kwa mantiki iyo, ndio maana nakuombea ‘upako’ wangu wa nukta kwa nukta! yale ‘marefuu/mengii’ unayoyakemea! tehe! Why? Kwakua ulisha-establish so truly/strongly kua twatoa kwa hiari na unakubali pia Ibrahimu alitoa KWA HIARI-mfano ulioutumia sana na wa kweli kabisa lakini hapo hapo unasahua KWA HIARI iyo iyo Ibra huyo huyo alitenga tenth of..! Was that sheria? Si unaona unavyomisi nukta-nukta flow na mpaka huna sahau ulisema nini/umetoka wapi na unakwendaje, Kaka Sungura bwanaa!

  Kutafuta jina jingine nikitoa laki na nusu kwa mfano kama Zaka toka laki 5, ni sawa ndio maana niliwahi sema mwanzo kua kwa HIARI NA MOYO WA FURAHA, HAKUNA YALE MAMBO YAKO YA ati TUNATIWA KABARI/TULAZIMISHWA CHURCH UKO, wengine hatugomei/komei tu kwa fungu la 10 bali hata fungu la 20,30,40… na nadhani tayari jina ndio hilo hilo tu nimeshalipata, hamna haja ya ku- crake kusaka jingine nalo ni..’’fungu la…. ‘…Make it simple, isn’t it?

  Umeshauri, ‘’Mimi nafikiri badala ya hiyo bahasha kuiandika ‘fungu la kumi’ unaweza ukaandika ‘sadaka ya upendo kwa Bwana’ au fungu la thelathini.Mwitikio: Nakubali ya pili-fungu la 30 KWANZA kisha sadaka ya kawaida/nyingine ya upendo mfano ile tuitoayo kawaida ktk ibada au kusaidia wahitaji

  Kuhusu kumheshimu Bwana kwa mali zetu, ishu si kutenga sehemu ya mapato yetu kwa ajili yake ndo tuonekane kuwa tumemheshimu. Suala ni kumtolea,tena sadaka inayompendeza = THIS ONE, this time, from your own, IS BEAUTIFUL INDEED AND IT IS SWALLOWED IN WHOLE SALE, Nonetheless, kutenga kikumi still ni Biblical, from Ibrahimz times, ni ka-discipline katamu ako, usikaache kaenda zake, kadake and kisha nenda kengine e.g. 20,30…….

  Umetoa wazo hili..’’Na njia nzuri mojawapo ya kumtolea ni kuwakumbuka yatima,wajane, masikini, wageni, na wahitaji kwa ujumla. Huko ndiko mimi moyo wangu nimeuelekeza katika kumtolea kwangu Mungu=Again, excellent Spirit indeed Sungura mjanja wa Yesu wewe, umejishuhudia mwenyewe, ina nguvu sana iyo, mimi pia haswaaa ila equally or more KWANZA to Mlawi wangu leo na mambo yake na ya mahali pa Walawi wa LEO wahudumupo kufanya kazi kwa ajili ya Mungu na yetu kisha wengine wafuate…Hapa hutanitoa na hapa ni ruksa tutofautiane milele na tutakutana mbinguni Sungura uzuri wake, wewe anza nje uko na kaa uko weee kuhudumia wa uko-( in this case yoyote nje ya Mlawi wako ni wa uko as far as am concerned hata kama yuko church hapo au street), mimi nitaanza na ndani kwanza-Mlawi na kwa Walawi(Kanisani jengo) kisha nitakufuata uko na najua ktk date base ya JUU..kwa gea hii yangu ya dabo-dabo, hutanipata maana kushindani ktk kutenda wema nayo safi tu, haivurugi Bible.

  Umesema, ‘’Lakini kama huwa unatoa 75% kanisani na hilo kanisa likawa halina programe za kuwakumbuka yatima,wajane, masikini, na wahitaji, ispokuwa mapato hayo yote hula mchungaji na watoto wake,nakwambia ukweli Seleli, kwamba itakuwa kazi ngumu sana wewe kuiweka hiyo kumbukumbu =UNGEKUA HAPA NINGEKUPA SODA NA PIG MEAT(pork- au nayo kuiondoa duniani ni issue kwako Biblically!) kama hujafunga(ila sijui unafungaga kweli wewe na mamisimamo yako haya kwa zaka kua sheria maana kufunga kunaonekana na wengi ktk sheria ingawa Yesu alikua hana shida nayo).Balance iyo kati ya Walawi na Wahitaji hoping Walawi wanakua treated with urgency kama si weight, hapo umetema cheche, this time- salama kweli and it so lovable, Godly and CUTE POINT indeed-thank God kanisani kwetu na I hope mengi hasa yale yanayoendeshwa kitaasisi si baadhi ya ki-private/family project, hufanya hayo, kwa kuhani na kwa wahitaji.

  Umekubali ivi.’’wala mimi sijakataa’’ kum-support Pastor muhitaji, Safi tena Sungura ila tuwe na uhakika kweli wana uwezo, wasije kua wanaendesha magari na wamejenga nyumba kumbe kuna wapendwa waliguswa tu MARA MOJA but baada ya hayo, daily living eg kula, kulaa, kara za watoto, hospitali, bili ya umeme, maji, nk, ni mbinde na nyie wapendwa mkishaona magari/nyumba zao, basi mnawakaukia! Natamani tungekua na uzoefu unao fanana kuhusu maisha ya baadhi ya watumishi wa Mungu wa kweli ktk madhehebu ya kipentekoste (simelei dini/dhehebu nyingine), ktk mazingira yetu TZ si mastory za Ulaya-Ulaya na Yuesi-yuesi za Kaswahili, uone jinsi gani tunafanyaga kosa kuangalia mambo yao kwa nje na kuachaniza tukijua/assume mambo yao safi 24/7 hence, kuguswa tena, au ile yako..kujisiiikiiiiiya tena kutenda au ninayopenda sana-KUAMUA MARA MOJA bila kugoja-goja wee kuguswaaaaa/kujisikiaaaaaaaa,ilisha-stop.

  Nimependa hii assumption kwelikweli Sungura..’Na nafikiri Petro hata hakuitolea zaka alienda kuilipa kodi moja kwa moja hiyo shekel’’ Izi ndizo nasemaga substancial ideas/assumptions ambazo ni ngumu kuzikataa/zinabana, ndizo nilipokua nawaambia mara kadhaa, wewe na Kaswahili mnazikemea kua ni kimwili, ni assumptions tu(implying kama vile hazima maana)! Si mnaona mlivyokua wrong? Think about what you just thought! so stony, unakanaje ilo jiwe? Si mtu utapya tu ktk reasoning gift! Ila attention! tehe! nakuona tu unavyoandaa mazingira hapo! usikachukulie ako kama escape eee, ya kutotoa Zaka kwa hiari tehe!

  Nimecheka sana hii…’’Kutoelewa context ni sawa na mtu kusoma habari za kuzaliwa kwa Yesu, alafu anaanza kutuhubiria hivi: ‘biblia inasema atazaliwa,sujui mwaka gani, labda 2050 au mwaka 3000′ hahaha..lovely again! Ila sidhani kama sielewi maudhui mie! Kweli kabisaaa eti sielewi! Wakati maudhui kwa Ibrahimu tu yananitosha mie kutoa zaka,nikiyaacha hayo unayotaka kumaanisha ya time/circumstances/majira bound messages of God to people, hapo si unaona naelewa na nimecholopoka mita nyingi tu, hunipati kaka? ivyo sitamtahiri mwanangu siku ya 8 maana sihamishi si logos zote zinahama kama zilivyo ila napenda rhema bila kudharau kabisa logos lakini pia bila kufungwa sana nayo nikose uhuru wa rhema ingawa pia sipitilizi wakati napata/natambaa ki-rhema!du! hii nimesema ni mchanganyo maalumu yet baraka tu usipoukurupukia.

  Hii tena umenimaliza!!!!! ’’usijidanganye Seleli, wewe wala hutoi zaka kwa historia ya Ibrahim, bali unatoa zaka kwa historia ya torati ya Musa. Uko chini ya laana ya torati’’ Mwe! yamekua hayo tena! Tumeanza vizuriiii na tunakaribia kuhitimisha mada hii, ghafla umenigeuka! Umetema zile zako cheche mbayua tena! Umeharibu kweli! mie niko chini ya laana tena! Du! Hii kali! Sasa nijitetee au niiache tu maana maelezo yote toka tumeanza debate hii na my inputs zangu za leo na hata kuweka mioyo yetu peupe yale hasa tunayofanya na tunayopenda tuyafanye one day, yanatosha kumaliza claim yako hii iyo. Mimi NIMEBARIKWA, SIKO CHINI YA NGUVU YA UHARIBIFU ( ndio laana manake), lo!aisee Afande Sungura, hapo tena ulitaka kulitibua sema nimelimaliza kirahisi/kiungwana tu kwa kua ninalengo ktk post yangu ya mwisho leo, kumaliza my participation ktk mada hii.

  Press on

 99. Wapendwa,
  Kwanza niwapongezeni nyote kwa jitihada nzuri na wakati wenu mlioutoa katika kulijadili suala hili la Zaka, maana kwa hakika mambo mengi yamejitokeza ambayo kwa yeyote aliye na moyo wa kujifunza, ninaamini anaendelea kufunguka kwa kadiri wapendwa mnavyoyafungulia mabomba ya Baraka, mbarikiwe na Bwana!

  Tukirudi katika mada, mimi binafsi nimejifunza mengi sana katika mjadala huu. Ni kutokana na hayo niliyojifunza, ndipo napenda kuleta mrejesho ili walimu wangu mpate kuiona faida iliyopatikana kutoka hayo mliyoyafundisha!

  La kwanza nililojifunza ni kwamba wengi wenu hamko tayari kujifunza, maana kujifunza huchukua kumsikiliza mwenza na kuyatafakari anayoyasema.

  Katika kujifunza, yaani kutoka mtazamo wa Zaka, nimeliona jambo hili la Walawi kuwa ni kabila, pamoja na hayo majukumu waliyopewa. Ndipo nikajaribu kuwaza kwamba Israeli ingekuwa ni Tz, mpangilio wake ungekuwaje? Walawi wangesambazwa nchi yote, nayo Zaka inayokusanywa kitongoji cha Tegeta labda, basi ingewahudumia Walawi, yatima, wajane na wageni walioko hapo Tegeta kwanza. Kwa maana nyingine ni kwamba kusanyiko lililoko Tegeta lingekuwa ni sovereign. Sasa jambo hili ni kulingana na Torati. Sioni haja ya kuzirejea aina za Zaka, bali nazungumzia jinsi yake, chini ya mfumo wa utawala kwa kadiri ulivyosimikwa katika kuyasimamia mambo haya.

  Kwahiyo, shida inaanzia hapa kwa Kanisa. Hapo linapoyarejea haya waliyoamriwa Israeli na kuyaingiza katika mifumo yao, ambayo ni tofauti kabisa! Zaka si toleo la kawaida, ni toleo la kibiashara. Linakwenda na hesabu, nao Walawi ndio waliosimama badala ya Kristo, ndiposa, wajane, yatima na wageni walirehemiwa kupitia hao. Pia Zaka aliyoitaka Mungu katika Hekima yake ni fungu la kumi tu, kwahiyo kutoa zaidi na kujisifia ni Ufarisayo mamboleo!

  Torati iliambatana na matendo yaliyoratibiwa na Sheria. Kwahiyo kanisa linapoweka msisitizo wa aina yoyote ile, katika jambo hili la Zaka, likiyarejea Maandiko katika Torati, ile Sheria kama Malaki nk, jambo hilo lingelirudisha kusanyiko lote katika Sheria, ile Laana! Maana msingi wa matoleo yenu ya Zaka ungekuwa ni Torati, ndipo mngewajibika kuyatimiza yote yaipasayo Sheria, licha ya ukiri wenu wa wokovu na kujazwa Roho Mtakatifu! Neema ya Mungu hailazimishwi mtu, bali wampendao Mungu huipokea Neema hiyo kwa unyofu na kutulia hapo chini, miguuni pake, kama watoto wadogo ili wafunzwe!

  Nimemuona mchangiaji mmoja, katika kusisitiza hoja yake, akasema Zaka ilivushwa kutoka Agano la Kale kuja Jipya, bali ni vizuri tukumbushane kuwa ni hatari kukivusha chochote kinachohusiana na Sheria, maana kufanya hivyo ni kuikataa Neema hiyo iliyotutangazia kuwa Kristo ndiye mwisho wa Sheria, nayo Zaka iliyoambatana na Sheria yapaswa pia kuishia hapo. Tusichanganye mambo! Unajua, Agano ni Agano, ndipo unapoingia katika Agano lolote lile ni vizuri ukakaa katika mipaka ya Agano hilo. Basi ikiwa unadai kuwa ni mteja wa Agano

  Jambo jingine nililoliona, ni kwamba wachangiaji wengi hawako tayari kuisikiliza Biblia, wanapenda kuhalalisha mafundisho ya makanisa yao kuwa ndilo neno la Mungu. Hebu liangalieni upya swali la msingi sana aliloliuliza Sungura kuhusu utoaji wa Zaka katika kuhusiana na vipindi ili kuileta maana kamili ya jambo unalolifanya. Vipindi viko vitatu cha tatu hiki ndicho tulimo sasa swali ni kwamba tunatoa Zaka hiyo kulingana na kipindi gani? ninanukuu:
  “”1. Wakati wa Ibrahim (kabla ya torati ya Musa)

  2. Wakati wa torati ya Musa

  3. Wakati wa sasa (wakati wa kanisa)
  NAOMBA SIYI UNIAMBIE KWA MTAZAMO WAKO NI WAKATI UPI KATI YA HIZO MBILI ZA KWANZA KANISA LINAPASWA KUFUATA?””
  Haya hebu liangalieni jibu la Siyi:
  “Kipindi hichi cha tatu, Yesu ameagiza zaka ziendelee kutolewa ili kumaintain ule Upendo wetu kwa Mungu-yaani utii na kazi nyingine ya ZAKA, ikilenga kuhubiri habari njema ya ufalme wa Mungu (Sijui kwa makanisa ya j2).”

  Jibu hilo linadhihirisha kuwa aidha mchangiaji kajitumbukiza kwenye majadiliano bila ya kulielewa linalozungumziwa, au mafundisho aliyopewa kuhusu Zaka ni hafifu, kutokana na labda kwamba walimu wake pia ufahamu wao ni mdogo nk. Unajua mambo ya kutumia akili yaani “your own understanding”, katika mambo ya Mungu, huonekana kama si kitu sana, lakini ni hatari kuliko hatari yoyote ile unayoweza kuifikiria! Hebu wazia kwamba unarukia katika jiwe ili kuvuka kijito, nawe unapolikanyaga tu, ukashuka nalo hadi kuzimu! Maana umeongozana na walimu waliokudanganya kwa kuirejea Malaki, wakakutisha na kukufundisha kuleta fungu la kumi, halafu wakakwambia eti hata ukizidisha si neno, nawe ukawakubalia na kujirudisha katika Sheria ambayo kwayo HAKUNA ahesabiwaye Haki, ni balaa!

  Pia nimeona wachangiaji wengi hukirejea kifungu cha Luka 11:42 ili kuhalalisha Amri ya Zaka kuendelea katika Agano Jipya. Lakini iwapo utakitazama kifungu hicho ukiwa umejitoa katika kongwa la dini, utaona kwamba walielezwa mambo hao walikuwa ni Wafarisayo, sasa sidhani kwamba hao walikuwa ni Kanisa! Ndio kusema yeyote anayekirejea kifungu hicho katika namna ya kuyatii hayo huyo ni Mfarisayo!

  Hata pia nimemsoma mchangiaji mwingine akiyarejea maneno ya Yesu, Mt 23:1-3 “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda …” akilichomekea Andiko hili ili kuhalalisha kuendeleza TOZO la Zaka kulingana na Sheria (wengi nimewaona wakidhani kwamba Zaka katika Sheria ni matoleo ya upendo, jambo ambalo si kweli, walitoa kwa utii wa Sheria; nayo Sheria ndg yake ni Uvunjaji wake, ndio maana Malaki anawakaripia!). Kwa kutumia “akili yako” waweza kuona ni sahihi kulitumia Andiko hilo katika uelewa huo, Lakini ukweli ni kwamba inakubidi uwe mnyofu ili Mungu akuoeshe jinsi yake badala ya kujikurupukia tu nakujilazimisha kutoa Zaka katika mtindo wa Torati, wakati kumbe hapa ndipo ilipo njia panda ya wakati, Agano la Kale katika maana ya Torati NGUVU yake ikikomea hapa!

  Ndio kusema Kristo analigawa kusanyiko lake, kundi moja analirudisha katika Torati liendelee huko ili kuukamilisha unabii unaolihusu, ile Israeli, akiwaambia waendelee kuwasikiliza hao waliokalia kiti cha Musa; nadhani mchangiaji huyu siku hiyo katika roho alikuwepo hapo kati ya hao makutano kama ndg yangu Siyi; lakini kundi la pili, hilo dogo, ambalo ni Kanisa, hao huishi na kunawiri kwa Ufunuo, huyu hapa Petro hebu yatazameni hayo: Mdo 5:27-29 “Kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.” Huyu ni Kuhani Mkuu, huyo aketiye katika kiti cha Musa, sasa wasikilize hao walioambiwa wamsikilize huyo Kuhani Mkuu, “Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.”!!! Nguvu ya Torati kwa Kanisa imeishia hapa!!! Hauwezi kuvitenganisha Sheria na Torati kama akina Siyi wanavyojitahidi kwa kuzitegemea akili zao, pamoja na wote wenye kuirejea Torati kwa vipande, aidha unavuka unaingia katika Agano Jipya ambalo ndilo funga kazi, au unabaki katika Sheria kama Israeli, huenda nawe ukawa mrithi wa Ahadi yao ya kurejewa, au mbaya kuliko, unabaki unaning’inia hewani ambako hakuna Oxygen, kwa Israeli haupo na kwa Kanisa haupo!!!

  Pia nimewaona wachangiaji ambao wamejiridhisha kwa matakwa yao kwamba kuitimiliza Torati ni kuyavusha hayo ya Sheria na kuyaingiza katika Agano Jipya kwa namna ile ile ya Torati bali huku wakiyaita ni ya “rohoni” au “upendo! Angalia kifungu hiki na mnukuu Seleli:
  “Kwa msingi huo no.3, hii andiko bado ili Malaki.3:8-10-‘’Leteni Zaka kamili/zote ghalani mwangu ili kuwemo chakula Nyumbani mwangu’’ linalipa na linabana mpaka leo simply because kwanza, halijawahi vunjwa maana hakuja kutengua bali kutimiliza-kutimilizaje?…”

  Bali kutimilizwa kwa Torati si kuyavusha mambo ya Torati na kuyaleta huku katika Agano Jipya! Unapoambiwa kitu hiki kipya, huwa unaelewa nini? Ni lazima kitu hicho kiwe kipya kwa maana ya upya au huyo anayekwambia hayo awe muongo au hakijui anachosema! Kitu kikuu kuu hakiwezi kuwa kipya! Kinaweza kikawa kama kipya hapo kinapofanyiwa matengenezo, kama ambavyo akina Siyi na wengineo wanavyojaribu kuli furbish Agano hilo la kale ili liwe Jipya kwa kulichanganya na Jipya na hivyo kulizeesha hili Jipya!

  Wapendwa hebu tuzungumzieni ZAKA, msilete mambo ya sadaka na kuipigia makelele mengi!

  Nikilijibu swali la Sungura alilolikwepa Siyi kwa kutiririsha mambo ya “kumpenda sana Mungu” huku akiendelea kuivunja Amri yake ya Zaka hapo anapoitoa bila mpangilio ilihali anatoa fungu la kumi kulingana na Torati, akiona Torati inambana anajidai anatoa kama Ibrahimu (nadhani alikuwa hajui kuwa Ibrahimu alitoa fungu la kumi la nyara; nikimnukuu Shoo Gap: Biblia inatuambia Ibrahim alitoa zaka ya mateka, haizungumzi kuhusu utoaji wa zaka wa mali alizokuwa anamiliki/ amezalisha mwenyewe. Tuwe makini hapo), akidhani eti atamdanganya Mungu kujifanya anamtolea katika upendo! HAKUNA kitu kama hicho, Mungu anayajua yote pamoja na dini dini zetu!

  Nyie mnaojidai kumtolea Mungu Zaka kwa staili ya Abrahamu, mmemuona Melkizedeki alichofanya? Tena mnaweza kupatafuta popote pale alipokuwa akilitimiza Agizo la Mungu kuhusu kutoa Zaka? Au hata Yakobo, kuna mahali mnaweza kuliona hilo agizo? Hakuna mahali popote kwahiyo kutoa kwenu kunakomuhusisha Ibrahimu au Yakobo huku mkijua fika kuwa mnatoa Zaka zenu kulingana na Torati ni Unafiki wa hali ya juu! Tena naweza kusema Unafiki huo unauzidi hata ule wa Kaini! Angalia kauli ya Siyi hapa kuhusu utoaji hapo anapomfanya Kaini kuwa alikiuka utoaji, ““Pamoja na kwamba ulikuwa ni utaratibu wa muda, nina imani unafahamu kwa hao waliokuwa wakiukiuka utaratibu huo. Tukianza na Kaini na wengine wengi wenye tabia kama hizo waliofuata.”” Huu ndio uongo wa kidini utakaotugharimu wengi wetu. Mungu ni mwenye Haki, basi unapomuingizia uongo wako ili uwe wake inakuaje?

  Kaini hakukiuka utoaji wowote ule, Mwa 4:2-3 “…Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.” Je, wapendwa kuna ukiukwaji wowote ule hapo? Au je, Mungu hapokei mazao ya shamba, na kama hapokei, Je, mchicha ni nini? Unakuona kuzitegemea akili zenu kunako wapeleka? Kaini alitoa sadaka yake bila ufunuo, kama ambavyo maelfu ya wakristo wanaotoa Zaka leo hii bila ufunuo! Imani ni Ufunuo, kwa imani Abeli alimtolea Mungu sadaka iliyo bora! Ibrahimu alimtolea Mungu ile Zaka kwa imani, hakujikoki tu! Yakobo alimtolea Mungu pia hilo fungu lake la kumi kwa imani!

  Kwahiyo nanyi ndg zangu jipimeni wenyewe kwa Mungu kuhusu Imani hapo mtakapoisikia Sauti yake ikikuambieni kuhusu kumtolea Zaka, ili ahadi yenu isiwe kwa wanadamu bali kwa Mungu!!!

  Mbarikiwe nyoote!

 100. Hey hey hey Seleli, taratibu kaka!!!!

  Naona umeona mistari unayotupa wewe haitoshi hivyo umeamua kuhamia kwenye Google. Pole ndugu yangu,maana huko ulikohamia ndio kugumu zaidi, mimi hata sitaki kwenda na wewe maana ndo utachanganyikiwa kabisa.

  wewe kama umeamua kwenda nenda mwenyewe. Hakiksha tu unafanya check & balnce kwa kuangalia pande zote za hao wasomi, yaani wana-support na wanaopinga halafu wewe mwenyewe ndo utaamua kipi ni kipi!

  Hakuna falsafa mpya uliyoleta toka kwa hao uliowanukuu ambayo hatujaijadili tayari hapa.
  Kuna moja hapa ngoja niinukuu ”People are being taught today that tithing is “done away.” Does God show anywhere in Scripture – beginning in Genesis – that He has used any other system than tithing to finance His Work?”

  Nami nakutuma Seleli ukamuulize huyo aliyesema haya swali hili:
  Did Abraham or Jacob tithe to finance God’s work? Or did the first church tithe to finance God’s work or rather offered contributions by even some of them selling their own properties?

  Endelea kufanya utafiti Seleli, utaupata tu ukweli.

  Asante!

 101. Ndugu yangu Seleli, ni bora umesema ukweli kwamba umechukizwa na kauli yangu. Ndio maana nimerudia sana kukifafanua hicho kipengele (kutoa zaka kwa lazima) lakini bado umekuwa hunielewi, sasa najua ni kwa nini. Ila kumbuka nimesema tangu mwanzo na hata sasa nasema kwamba zaka ni toleo la hiari, na nikasema anayetaka kutoa ikiwezekana atoe kila siku,si kila mwezi tu au wiki. Lakini asiyemtolea Mungu kwa njia ya zaka asihukumiwe kuwa anatenda dhambi, hakuna dhambi yoyote anayotenda.

  Lakini kuna kitu hapa twende sawa, nakunukuu: ”Sikuwahi kutoa kama sheria na wala sitatoa kwa mujibu wa matakwa ya sheria kama unavyoshauri, lakini kwakua nina love kwa Baba, sijisazi na ndio maana si tu 10& bali kwa raha zangu mbele za Bwana hata 20%,30% na nimemuomba Mungu kabla sijafa au hajarudi Bwana, nijiwekee rekodi ( hazina) kwenye vitabu vya database mbinguni Ufunuo.20:11-12 Zaka ya 50%-75% and why not 100&?-tutaitafutia jina tu siyo shida kutoka maana ya Ki-maandishi ya Neno Zaka( yaani tenth of….).”

  Hapa Seleli kuna kitu unanidanganya au hujui maana ya fungu la kumi, ila unachojua wewe ni kumtolea Mungu basi.
  Unaposema hutoi fungu la kumi kama sheria, maana yake ni kwamba unaweza ukapata laki tano ukaitoa yote kwenye mchango wa ujenzi wa kanisa bila kuwa umeondoa ile hamasini elfu ukaitoa kama zaka, hicho ndicho una maanisha Seleli?

  Na kama unaweza ukapata laki tano ukaamua kutoa laki moja na nusu ukaiweka kwenye bahasha kisha ukaandika kwamba hili ni fungu la kumi,siyo kweli hilo halitakuwa fungu la kumi kwa kanuni ya biblia. Kwa hiyo tafuta jina jingine la kuliita hilo toleo kama ulivyosema.
  Mimi nafikiri badala ya hiyo bahasha kuiandika ‘fungu la kumi’ unaweza ukaandika ‘sadaka ya upendo kwa Bwana’ au fungu la thelathini. Na sadaka kama hiyo au fungu kama hilo halina kanuni kwenye biblia.
  Na kwa habari ya kujiwekea kumbukumbu kwenye data base za mbinguni na mimi nakutia moyo,come on, keep it up man!!

  Kuhusu kumheshimu Bwana kwa mali zetu, ishu si kutenga sehemu ya mapato yetu kwa ajili yake ndo tuonekane kuwa tumemheshimu. Suala ni kumtolea,tena sadaka inayompendeza. Na njia nzuri mojawapo ya kumtolea ni kuwakumbuka yatima,wajane, masikini, wageni, na wahitaji kwa ujumla. Huko ndiko mimi moyo wangu nimeuelekeza katika kumtolea kwangu Mungu.

  Na hata wewe nikwambie kitu kwa vile unataka kuweka kumbukumbu mbinguni,wakumbuke watu hao. Lakini kama huwa unatoa 75% kanisani na hilo kanisa likawa halina programe za kuwakumbuka yatima,wajane, masikini, na wahitaji, ispokuwa mapato hayo yote hula mchungaji na watoto wake,nakwambia ukweli Seleli, kwamba itakuwa kazi ngumu sana wewe kuiweka hiyo kumbukumbu.

  Seleli kama mchungaji wako anajimudu kimapato kutokana na labda biashara zake(tena nyie mko huko Geita migodini, anaweza akawa na mgodi wake),anaweza kuwa anafanya kazi ya taaluma yake ( kama hajaamua kuacha kazi,nk.) anahitaji saupport yako ya nini sasa? Lakini kama hajimudu na anahitaji support kwa nini msim-support, wala mimi sijakataa?
  Nilichosema ni kwamba hata kama hamtamtegemeza kwa hela zenu, bado Mungu atajua jinsi ya kumtunza.
  Kwani wakati Yesu anamwambia Petro akachukue shekel kutoka kwa samaki ili walipe kodi walikuwa wapi hao wanawake kumpa hiyo hela ya kodi?( Na nafikiri Petro hata hakuitolea zaka alienda kuilipa kodi moja kwa moja hiyo shekel).

  Seleli kama huelewi kuwa neno la Mungu lina nyakati zilizoamriwa, tutapigizana kelele sana hapa. Na huko ndiko tunakokuita kutokuelewa maudhui(context), yaani kuelewa kuwa hilo neno linakuhusuje wewe leo. Ni sawa na mtu kusoma habari za kuzaliwa kwa Yesu, alafu anaanza kutuhubiria hivi: ‘biblia inasema atazaliwa,sujui mwaka gani, labda 2050 au mwaka 3000’.
  Huyo mtu atakuwa amesoma neno la Mungu lakini hakuelewa nyakati zilizoamriwa za hicho kifungu.

  Kama tunachukua tu kilichoandikwa (logos) na kukiweka kwenye matendo, basi ukizaa mtoto wa kiume lazima ukamtahiri siku ya nane maana imeandikwa hivyo Seleli.

  Pole Seleli kwa shida unayoipata kwa kunitafakari bila kunimaliza, nakuaomba usinitafakari mimi bali kitafakari ninachokuandikia. Maana yawezekana ninaongea mambo ya rohoni wakati wewe uko mwilini, hautayatambua.

  Mwisho, usijidanganye Seleli, wewe wala hutoi zaka kwa historia ya Ibrahim, bali unatoa zaka kwa historia ya torati ya Musa. Uko chini ya laana ya torati.

  Asante.

 102. Yah, Sungura,
  Leo nimeandika mengi kidogo japo si sana. Jitahidi kunifuatilia ndg yangu….
  Nashukuru kwa kunijirejea rafiki yangu, pamoja na kwamba mimi nilikuwa nimeshakata tamaa kuwa Sungura haelewi somo la utoaji na huenda ana kashetani ndani yake kanakomsumbua ndiyo maana amefikia hatua hii ya hatari sana. (samahani Sungura kama u mwepesi wa hasira, kwa kusema kuwa una kashetani)!! Ninasema kwa nia njema sana rafiki yangu. Kila ninapoangalia ndani ya neno ya neno la Mungu, napata nguvu na msukumo fulani wa kufanya kile Mungu asemacho. Roho Mtakatifu yu anena nami sana kwa hili na mengine mengi yahusuyo injili.
  Kaswahili nilimwambia kuwa, kuna wakati mwingine, tunaweza tusimwelewe Mungu kwa undani sana kwa kila atuagizacho. Lakini maadamu ameagiza, ni vyema tukatii tu na kufuata maagizo hayo maadamu yameandikwa/yamefunuliwa kwetu kwa uchache huo.
  Nikubali kwamba, ni kweli kuna baadhi ya makanisa yanayofanya ujasiliamali kwa waumini wake. Viongozi wana magari ya kifahari sana ukilinganisha na hali za waumini, hitaji la watu wengine mahalia, wagonjwa, wajane, na wote wasiojiweza, unaona kabisa kuwa kama hii ndiyo dini, Mungu atusaidie tu. Kristo na Mitume kama vielelezo kwetu, hawakuishi maisha kama wanayoishi leo baadhi ya viongozi wetu wa dini kwenye baadhi ya makanisa yetu. Najua wengine wataanza kunishambulia kwa hojazao. Sina nia mbaya na kiongozi yoyote wa dini. Ila shida yangu ni kutuona hao viongozi hawatumikii kanisa, badala yake, wanatumikiwa na kuheshimiwa saaaaana kiasi cha nusura kuabudiwa. Mungu atusaidie tu, maana sisi sote tunahitaji rehema zake. Hakuna aliye mwema.
  Aidha, nikubaliane na wewe kaka Sungura kuwa, hata mimi nilikuelewa kuwa, HUPINGI kutoa ZAKA. Ila unatoa zaka pale unapojisikia/kuguswa tu-yaani pale unapoamua wewe. Ukata/Shida zikikuzonga kwa mwaka mzima(sikuombei hayo), ni dhahiri kuwa ZAKA hutakumbuka kabisaaa. Kwa mantiki hiyo, Mungu wako anakuwa ni Mungu wa wakati ukiwa na neema tu, pale unapopata changamoto, Mungu unamsahau!! Huenda usiwe hivyo, but najaribu kuogelea kwenye mawazo yako.
  Mimi ni msabato kaka. Msabato ninayeukulia wokovu kila siku. Na ninaomba Mungu anisaidie nifikie ukamilifu. Kama Msabato, ninaamini kuwa, kama jambo linaonekana kuandikwa ndani ya Biblia, na lina pumzi bado, hilo kwangu ni agizo tayari. Wengi nikifikia hapa, huwa ni ngumu sana kunielewa. Kuna sheria nyingi sana ambazo Mungu ametupa kuishi kwazo japo watu wanafahamu amri 10 tu na labda torati ya Musa iliyopitwa na wakati. Kwa sheria za Mungu, ninaamini kuwa, ninapojitahidi kutii zingine zote ila nikajikwaa katika moja au nikalegalega ktk moja,(kumbuka kulegalega huanzia moyoni-then hujihirisha ktk mwili), nitakuwa nimekosa juu ya yote-Yakobo 2:10. Hivyo nitakuwa mkosaji tu sawa na mdhambi yoyote. Kama kutoa ni agizo la Mungu, basi budi kutoa tu kwa kila nikipatacho.
  Nakubaliana na wewe kuwa ZAKA ni hiari kama ilivyo hiari kutii amri zingine. Mungu halazimishi watu kuzitii amri zake. Na kwa sababu ya wingi wa rehema zake, hata kwa hao tunaoziasi sheria zake, mara nyingine madhara hayatupati papohapo, ndiyo maana tunabweteka na kuanza kumchambua na kumhoji sana Mungu mambo ambayo hata Mmwanaye-Yesu aliyaagiza kuwa watu wasiyaache-luka 11:42.
  Natambua kuwa, ndani ya mjadala huu kaka Sungura, mada ya ZAKA iligusia vipindi hivyo vitatu. Na ukiangalia kipindi cha kwanza na pili, matoleo mengi yalilenga kuonesha upendo-utii wa watu hao kwa Mungu wao na makafara.
  Kipindi hichi cha tatu, Yesu ameagiza zaka ziendelee kutolewa ili kumaintain ule Upendo wetu kwa Mungu-yaani utii na kazi nyingine ya ZAKA, ikilenga kuhubiri habari njema ya ufalme wa Mungu(Sijui kwa makanisa ya j2). Lakini kwa wasabato, kwa uelewa wangu mfinyu wa jumla, ZAKA huwa na malengo hayo makuu na mengine mengi tu. Kwa hiyo, ninapoamua kutoa leo zaka, na kesho nisitoe, ni sawa na kusema kuwa, leo nimeamua kumpenda –kumtii Mungu na kufanya kazi ya ENENDENI ULIMWENGUNI KOTE MKAIHUBIRI INJILI… na kesho sijisikii kumpenda-kumtii na kufanya kazi yake- kwa maana ya kutotoa hizo ZAKA.
  Mwisho nijibu swali lako, sasa, kuwa kati ya hizo nyakati mbili za kwanza, kipengele tunachopaswa kukizingatia katika utoaji ni kile cha kuonesha upendo-utii wetu kwa Mungu tu. Habari za makafara leo hatuna. Yesu alishakuwa kafara kwa ajili yetu sote. Na kipengele cha sasa cha kutoa ZAKA, ni kwa ajili ya utume basi. Kumbuka neno utume ni dhana pana. Mf, kuwafikishia watu injili ikiwa ni pamoja na kuwatimizia mahitaji yao ya kimwili kama Yesu na mitume walivyofanya.
  Wakati Ibrahimu haikuwa lazima kutoa zaka kama ilivyo hivi leo. Maana Mungu hamshurutishi kumpenda, kumtii wala kumshukuru kiumbe aliyemuumba. Ametupa free will ya kuchagua kumpenda-kumtii au kumuasi. Kwa kipindi cha Musa, ilikuwa ni lazima kwa sababu ya sheria-torati ya Musa iliyotolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu. Kumbuka Israel kwa kipindi kile, walikuwa ni watu ambao walikuwa utumwani kwa muda mrefu, sheria na taratibu nyingi za Mungu, hawakuzijua kama ilivyokuwa kwa baba zao. Kimsingi walikuwa ni waasi. Ndiyo maana wakati Mungu anaaamua kuwakomboa utumwani, Mungu anamwagiza Musa kutengeneza sheria ndogondogo(by laws) zitakazowafanya waendane na maagizo ya Mungu ya tangu mwanzo(moral laws). Yesu alikuja kuzikomesha hizo taratibu/sheria za Musa, na akuturejesha kule mwanzo kabisa, kwenye utii usio wa lazima. Kwa leo mtu anapoamua kutoa zaka na halafu kesho akaacha, ni sawa na mtu anayeamka asubuhi akasali na kesho yake akiamka hasali na wala haimpi shida moyoni mwake. Huu ni umauti mkubwa wa kiroho walio nao watu wengi sana ndani ya makanisa yetu. Mungu atusaidie sote.
  Habari za mtoa ZAKA kutangazwa mbele ya kanisa na kuitwa mbele ya kanisa/umati wa watu ili aombewe, HUU NI UNAFIKI NA UFARISAYO WA HALI YA JUU SANA. WACHUNGAJI WANAOFANYA HIVYO, WANAHITAJI KUSAIDIWA SANA SANA. Utoaji wa zaka wa mtu ndani ya kanisa, haupaswi kufahamika kwa yeyote labda mhazini tu na viongozi wa juu kama kuna hitaji hilo. Pamoja na hawa watu wachache kujua, bado hubakia kuwa ni siri zao. Hawapaswi kabisa kutajataja kwa waumini wengine, zaidi ya kuwaombea tu wabarikiwe zaidi. Kwa wasabato kaka Sungura, habari za kutangazana Siyi katoa sh ngapi, hazipo. Na kama ukiiona sehemu yoyote, jua tu kuwa hao watakuwa wamekengeuka vya kutosha.

  Risiti hutolewa kama utaratibu tu wa kumhakikishia yule aliyetoa kuwa, kile alichokitoa, kilifika kwa ofisi ya mhazini kikiwa salama-chote. Utaratibu huu umekuja baada ya baadhi ya watu, wahazini ama mashemasi kutokuwa waaminifu katika ukusanyaji za matoleo ikiwemo na zaka. Utaratibu wa risiti hauna shida yoyote, ndio maana hutolewa kwa bahasha kama unavyotoa matoleo yako yakiwa ndani ya bahasha.
  Hakuna mtu mwingine anayeona, ni wewe tu na huyo aliyezipokea hizo pesa-mhazini. Kinyume na hapo, kaka, makosa makubwa mbele za Mungu. Ukimwona mchungaji anatangaza, watoa zaka au sadaka, jua anahitaji kusaidiwa sana tena kwa unyekekevu mkubwa sana badala ya kumlaumu.

  Hivyo kaka, Concept ya kutoa ZAKA na Sadaka kwa sasa, ni kuonesha uhusiano wetu mzuri na Mungu kwa kuifanya kazi yake hata sehemu za mbali tusikoweza kufika, ZAKA na SADAKA hufika huko. Nikushauri tu uendelee kutoa zaka na sadaka kwa mpangilio kadri Mungu anavyokubariki kwa kukupa uzima-uhai, afya, mali, famila, nk. Baraka hizo zote, zina makusudi kwa Mungu- makusudi hayo ni pamoja na kumfanyia kazi yake.
  Barikiwa sana. Tuko pamoja ndg yangu.

 103. Sungura, Kaswahili, Yeremiah,Mabinza,
  Na Wana SG wote

  Zingatia hili ina nguvu sana na hakuna mwenye hoja kuchomoka hapa, Mungu ana akili sana, alijua tu kuna watakaotaka ukwepaji.

  KWELI KUU KUHUSU ZAKA ZIKO NYINGI ktk Bible na hata kwa kutumia akili tu why tutoe eg Zaka LAKINI FUNGA KAZI YA DEBATE YOTE NI

  KUTOKA AGANO LA KALE…
  Mwanzo.14:1-20 Ibrahimi anatoa Zaka KABLA YA SHERIA-kwa hiari na moyo wa kupenda kwake

  KUTOKA AGANO JIPYA…..( hii nzuri kwa wanotafuta maandiko live-live)
  Mathayo.23:23 ‘’Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache’’

  Wote mliofuatilia mjadala huu, hakuna hata mmoja kati ya wa waliojadili, amekuaa na ujasiri kusema MOJA KWA MOJA kua kutoa zaka ni FUNDISHO POTOFU kama hoja halisi ya Milinga ilivyosema, na kama wapo waliosema, bado ktk kuchambua waliosema, hakuna hoja nzito( ni uzungushaji tu na kutafsri Maandiko ktk ufahamu wa ajabu tu, ila mimi na baadhi tumethibitisha kwa majadiliano na mahojiano mengi KWA HOJA( ziwe by Facts/Word/ Understandings/ Thinking/ Reasoning/Assumptions zenye kilo kuzikana wameshindwa kua KUTOA ZAKA SI FUNDISHO POTOFU HATA KIDOGO,

  KUMALIZA KAZI KABISA, WAFUATAO NI BAADHI YA WATAALAMU WA MAANDIKO-Nikitegemea kwa ule umakini wenu na kua watu wa substance kama mlivyosema mnao ingawa ktk debate hii yote…mm!, mngeshajua kunaa vyanzo vingine vya maarifa.Watafute ktk google, chukua Mathayo.23:23 kisha i..google maana yake, wanasema, yafutayo chini. Haya sasa kati yenu nani anasimama tena kupingana na hawa wataalamu maana tukiwaijia kwa ufunuo/Ufahamu/uvuvio Bwana anaachilia hapa spespeli, mnaruka ooh! ni assumptions tu, mawazo tu, aya twende kidini/kitaaluma zaidi, someni chini hapo na kama kuna mwenye Ujasiri na asema sasa kua Zaka ni fundisho potofu au tutoe au la!

  Some Bible Experts On Tithing

  Mathayo. 23:23

  What is Christ saying here? These people should have tithed; there was nothing wrong with that. The Expositor’s Bible Commentary, concerning this verse, says, “Jesus does not condemn scrupulous observance in these things.” Jesus instituted the tithing law and knew what it was intended to do for the ministry. He knew the purpose for it, even as we do now, but the Pharisees did not understand the spiritual intent. They knew to tithe, but did not understand the rest. John O. Reid

  In this denunciation of the Pharisees, Jesus does not condemn tithing – or even punctilious observance of it. Instead, He denounces their lack of justice, mercy, and faith! To the contrary, He supports tithing: “These you ought to have done [justice, mercy, and faith], without leaving the others [tithing] undone.”Richard T. Ritenbaugh

  People are being taught today that tithing is “done away.” Does God show anywhere in Scripture – beginning in Genesis – that He has used any other system than tithing to finance His Work? Jesus, the very Head of the church, had a golden opportunity to state emphatically that the tithing law had been changed, but He did no such thing. Instead, He said of carefully determining the amount of tithe, “This you ought not to have left undone.”John W. Ritenbaugh

  Jamani Wandugu, hama jinsi, toeni ZAKA, wacheni maneno!!!!!!!!!!!! NA NIKA NAWAONA, HAMNA TENA KAULI KINYUME NA HAYO JUU MAANA HATA MKISEMA, ITAKUA WAZI PEUPE WAPI/NANI ANAHITAJI MSAADA SASA WA MUNGU MWENYEWE MAANA SIYE WENGINE NDIO TUNA-SIGN-SING OFF IVYO UNLESS KUAKUA NA ULAZIMA SANA WA HARAKA KURUDI MARA MOJA.

  Press on.

 104. Sungura,

  Yataka moyo ulioshuka kuona kosa na kulikiri hata ‘kikubwa basi’’ ivyo sishangai wewe kuendelea kukataa kua ulizidisha chumvi sana maana kama mnaweza sema yote mliyosema dhidi ya Makanisa na Watumishi( Walawi wetu wa leo) kisa kutoa izo fedha zenu, basi ibaki tu ivyo kua hataki kuliona ilo. Kuna namna ya kusemana sisi kwa sisi lakini si katika kiwango cha kuonyesha kila kitu kimevurugika! Nikwambie kweli, nimeichukia sana kauli ya kua Watu makansani tunalazimishwa na hata ukini- challenge kua nisemelee tu Kanisa langu, ninyi mlitoa wapi ujasiri wa kuponda zaka ya makanisa yote/yetu? Si unaona matatizo yale yale, unatoka nje ya mada(unaibua jambo ghafla), tukikufuata uko uko, unakimbia kurudi ndani halafu unatugeuka kua tuko nje!

  Ni kweli kama ulivyosema, huwezi na hutanibadilisha kuniaminisha kwa hoja mfu kua Kutoa zaka ni fundisho potofu.Nimekua natoa na nitatoa tena na tena kwa furaha na moyo na hiari na hata kuwahamasiha wengine faida za kutoa sadaka zote tu mpaka Yesu arudi. Nikushauri usiiponde indirectly or directly, acha tutoe tu na kila utakapofanya huduma ya kuishusha, mie nimepakwa kuinyanyua sana kabisa. Sikuwahi kutoa kama sheria na wala sitatoa kwa mujibu wa matakwa ya sheria kama unavyoshauri, lakini kwakua nina love kwa Baba, sijisazi na ndio maana si tu 10& bali kwa raha zangu mbele za Bwana hata 20%,30% na nimemuomba Mungu kabla sijafa au hajarudi Bwana, nijiwekee rekodi ( hazina) kwenye vitabu vya database mbinguni Ufunuo.20:11-12 Zaka ya 50%-75% and why not 100&?-tutaitafutia jina tu siyo shida kutoka maana ya Ki-maandishi ya Neno Zaka( yaani tenth of….). Ni kweli Mungu si masikini mpaka atake msaada wangu lakini muulize Yeye atakuambia hua anapenda kushirikiana nasi na kukutengenezea mazingira ya kutubariki na pia kutufundisha kumuhofu Yeye tunapokua na Mind iyo ya kutenga sehemu ya yale atupayo kwa ajili ya mambo yake Yeye huyo huyo-Kumbu.14:23 soma part ya mwisho na Mithali.3:9-‘’Mheshimu Bwana kwa Mali zako- kwangu ZAKA ni mojawapo ya matoleo ya kuonyesha heshima sana kwa Mungu kwa nilivyonavyo, yaani kama nitajijengea tena kwa moyo wa kupenda kua kila nipatacho, Kikumi ni cha Bwana, yaani ni baraka kweli kua na hali/tabia iyo akilini na rohoni-Ni hali ya hewa ya kiroho chenye afya sana kama unataka mawazo yangu.

  Ni kweli Pastor hataniuliza kama sijatoa ila atachapa gombo bila kumung’unya maneno wala kubembeleza kiumbe yoyote, kukwangua tabia mbaya ya Washirika kujali nafsi zao tu kuliko mambo ya ufalme. Wanapaki Magari nje wakati wa ibada, wana plots Dar 3, wanachukua mikopo kwa bank kununua gari yet hawawezi kutoa Zaka eti mpaka wajisikieeeeee, mbovu sana tabia hii, imelitesa Kanisa, Watumishi- Watu kujisikia eti ndio watende hasa kwenye kugusa noti zao na bahati mbaya ‘Kujisikia spirit/tendency imeenda mpaka kwenye ushuhudiaji, kutembelea Wagonjwa, kufika ktk mkutano wa injili wa kanisa lake mshirika mwenyewe, mikesha, mifungo ndio usiseme, mpaka wajisikie na wafunge kuombea Nchi, Street neighbours wafunguliwe waookoke, kazi ipo wakati ilihali mambo yao binafsi, hamna kujisikia ni maamuzi tu haraka kweli, wanakukuruka hamna mfano na kuingia hata madeni na risks za hatari —-Ishindwe iyo roho kabisa, kabisa namaanisha, Amen. Na kama Mchungaji haitaji msaada wangu ili aishi, basi wewe ujasoma Bibilia na kama unaisoma, unafanya ivyo kipinzani au kidini zaidi( too much on the context part of the Bible-it is good but harmful if not carefully used) ivyo haudaki vitu. Yesu alikua Mungu lakini alihitaji support kwa huduma yake ya watu hawa wanaomfanyia ivi ! Luka.8:1-3-najua utaisaka Zaka hapo live-live, hutaiona but mi naona zaidi ya zaka hapo,tena ni Wanawake, Wow! great and God bless all women, sisi Wanaume Bwana akanyage kiburi na udume wetu mbovu mpaka una-contaminate kwenye Kumtolea Bwana na kuzungusha maneno tu mara hiari na mara ni fundisho potofu, mara ilikuaje kabla na baada ya torati,nini yote hii mambo ya mizungunguko! What for?

  Kuhusu kuwaambia Waumini, wasipotoa Zaka Wamelaaniwa, Wezi nk, Wachungaji/ Wahubiri wakisema/wakahubiri ivyo, wanakosa gani Sungura? au wanatoa kitabu cha Malaki.66:666 siyo! Je hili si Neno la Mungu..Malaki.3:8-10? Unakana siyo Neno lake? sema basi kama una ubavu na Mwenyewe akusikie? Na hili je Mathayo.23:23..’’Imewapasa kutenda hayo kwanza BILA KUYAACHA NA HAYO MENGINE-yapi? Soma hapo-Ni ya Zaka! Washirika wakitoa kwa hofu, shauri yao, ni wabishi, wagumu, wabinafsi, wagumu. Halafu unawahurumia wa nini wakati wao ndio wanaowafikisha Makuhani wao level hiyo! Na pia wakati Mungu mwenyewe tena kupitia nabii live, akawapasha live kua wamelaaniwa, ni Wezi, kwani hawakupata hofu ya kulaaniwa na Mungu na wakatoa? Sasa je, na kwani Mungu hakujua kwa kumtuma nabii wake kuwaambia maneno kama yale, wangepata hofu na wengine wangenuna kwakua ‘wametukanwa’ Wezi! Alijua yote na bado akaruhusu iyo ‘kristapeni full dozo’’ iwafyatukie Watu barabara, ivyo ivyo kavu-kavu, wapone, wasipone, wajae hofu au la, Daktari amemaliza kazi! unadhani Mungu alikua ana interest ya kubembeleza ktk andiko ilo kama wewe! Mimi ‘nikiraruliwa’ ivyo na Pastor wangu au mhubiri mgeni toka madhabuni, mbona napomoka kwa toba kama nimechemka mahala ktk Utoaji wangu in general na Zaka in specific, wewe una tatizo gani lakini Sungura, unajua nimekua nakutafakari sana sikumalizi! We mpendwa dizaini gani aisee?!lo!

  Kwamba Historia ya kuanza Zaka kwa mfumo wa leo ilianza mwaka 777 baada ya Kristo aliyosisitiza Yeremia Amini, inasaidia nini on serious note Sungura? let us be serious jamani kidogo na Mungu wetu na tujirudi ndugu zanguni mwe! ivi mimi nikitoa kwa Historia ya Ibrahimu na nisiposoma kamwe Historia ya Kanisa kujua Zaka ilianza sijui lini na yule bwana gavana aliyemsema Mr. Amin, nitapungukiwa na nini? ( by the way msiifanye History iyo ni kitu spesheli sana cha professionals few here maana naona nayo mnaishikia bango kweli wakati si deal yoyote, maana yako huko google yamejazana na hata post nzima ya Jeremiah -iko almost kama ilivyo ktk google hence, sina haja ya kusoma iyo ili nijue ndio nitoe na ifutikie mbali, iniache mie ninatoa kwa History ya Ibrahimu na Yesu ktk iyo Mathayo baaasi, simple tu na ninabarikiwa. Nitaisoma na kukutana na Mr.gavana kama ninataka kupata degree ya dini si ya rohoni ya mapenzi yangu na Mungu.

  Ubairikiwe Amen.

  Press on giving 10%, 20%, 30%…

 105. Ndugu yangu Siyi unanihuzunisha kweli!

  Ulivyomjibu Kaswajili imeonesha kuwa hata mimi hujanielewa japo umesema umenielewa. Nafikiri nimekuonesha kabisa namna yangu ya kumtolea Mungu. Kwa hiyo kule kukwambbia tu kwamba huwa namtolea Mungu inatosha kuua wazo kwamba tunapinga kumtolea Mungu.

  Tumeiweka wazi kwamba:
  1. Hakuna anayepinga kumtolea Mungu – mimi namtolea sana tu
  2. Hakuna anayesema kuwa mtu akiamua kutoa zaka anatenda dhambi.

  Lakini ieleweke wazi kwamba ZAKA mtu ni hiari yake kutoa. Kwamba leo akipata labda laki mbili akaamua kutoa elfu ishirini zaka amefanya vyema. Kesho kutwa tena akapata laki mbili akaamua kumlipia mtoto wake shule hiyo hela yote amefanya vema pia. Au nikapata hela nikaamua yote kuwapa wajane bila kuwa nimetoa 10% yake hakuna kosa lolote.

  Kama kuna jambo umeligundua katika huu mjadala ni kwamba wachangiaji wengi tumeweka wazi kuwa kuna vipindi vitatu vya utoaji wa zaka tunavyoviongelea.
  1. Wakati wa Ibrahim (kabla ya torti ya Musa)
  2. Wakati wa torati ya Musa
  3. Wakati wa sasa (wakati wa kanisa)

  Lakini wakati huu wa sasa zaka inatakiwa kutolewa kwa kufuata mojawapo ya hizo nyakati mbili za kwanza. NAOMBA SIYI UNIAMBIE KWA MTAZAMO WAKO NI WAKATI UPI KATI YA HIZO MBILI ZA KWANZA KANISA LINAPASWA KUFUATA?

  Wakati wa Ibrahim hawakutoa zaka kwa kila kitu wanachopata, bali walitoa walipotaka wenyewe.

  Wakati wa Torati ya Musa ilikuwa ni lazima utoe zaka ya kipato chako.

  Siyi sisi kwetu mtu akitoa sadaka(offering) hapewi stakabadhi, lakini anayetoa zaka anapewa, na tena anaambiwa apite mbele au asimame aombewe. Je na kwenu huwa inafanyika hivyo? unafikiri ni kwa nini iwe hivyo wakati unaweza ukakuta aliyetoa sadaka ametoa asilimia kubwa tu ya kipato chake? Je kufanya hivyo ni sawa?

  Twende pamoja Siyi!

 106. Seleli nini ambacho unanitaka nikiri kuwa niliteleza na kuzidisha chumvi? Hakuna kitu nilichoteleza wala kuzidisha chumvi, kwa hiyo hakuna kitu cha kukiri.

  Halafu unaposema huko makanisani hatuna hali mbaya kihivyo, nakushangaa. Kwani wewe ni mshirika wa makanisa yote Seleli, au makanisa yote huwa yanaripoti kwako kiasi cha wewe kujua kuwa hali si mbaya? Wewe semea tu kanisani kwako basi

  Ukweli utabaki kuwa ukweli kwamba zaka ni toleo la hiari kwa anayetaka kutoa. Lakini kama wewe unataka kuitoa kama sheria basi nakushauri ufanye hivyo kwa utimilifu kama sheria inavyotaka katika kutoa zaka, ikiwemo kutotoa zaka pungufu wala iliyozidi maana Mungu si masikini mpaka atake msaada kwako.

  Kumbuka pia kwamba mchungaji anayemjua Mungu hahitaji msaada wako ili aishi, wala hatakiwi kukuuliza kwa nini umeacha kutoa sadaka, kama utakuwa umeacha kutoa. Aliyemwita ndiye atakayekushugulikia wewe kama kweli anataka utoe ili yeye aishi. Walawi hawakuwauliza watu kwa nin hamtoi zaka. Walichokifanya walitoka madhabahuni na kutafuta mashamba, n ndipo aliyewaita alipowashugulikia watu(Soma habari za Nehemia)

  Tufuate ushauri wa Paulo kwamba kila mtu afanye kama alivyokusudia moyoni mwake. Kwamba wewe umekusudia kutoa 10% kama sheria,basi fanya hivyo. Na mwingine amekusudia kutoa zaka kama toleo la hiari basi nae afanye hivyo. Na mwingine amekusudia kutomtolea Mungu kwa njia ya zaka nae afanye hivyo, maana kumtolea Mungu si kwa njia ya zaka pekee.

  Narudia tena kusema kuwa kuna kitu hujanielewa tangu mwanzo wa michango yangu, hata sasa bado hujanielewa. Nakifafanua kwa mara ya mwisho, nakunukuu kwanza: …na pia MISIMAMO YAKO BINAFSI KUHUSU ZAKA imeleta shida-kipengele cha kua watu wanalazimishwa kanisani ulivyokiongolea( highlight sana)…:

  Neno kulazimisha hapa kwa Kiswahili kingine, ni kule kuwaambia waumini kuwa wasipotoa zaka watalaaniwa, wasipotoa zaka wanamwibia Mungu, wasipotoa zaka hawaendi mbinguni n.k. Hivyo kuwafanya waumini watoe zaka si kwa sababu wametaka bali kwa sababu ya hayo maneno ya hofu. Huko ndiko kuwalazimsha nilikosema.

  Seleli siko hapa kukubadilisha msimamo wako, wala wa mtu yeyote, ispokuwa niko hapa kusema ukweli ambao mimi nauona ndivyo ulivyo katika neno la Mungu. Ambaye naweza akaona kuwa kuna ukweli nimeusema ambao uko sawa na neno la Mungu huyo ndiye atakuwa mtu ambaye nimeandika haya yote kwa ajili yake.

  Nikushauri tena kitu kingine kwamba soma vizuri historia ya kanisa, ndipo utagundua mambo mengi,ikiwemo kama alivyokwambia Mabinza kuwa zaka kwa mfumo wa leo ilianza mwaka 777 baada ya kristo.

  Asante kwa muda wako!

 107. Amini Mguluma,

  Nimeitedea haki post yako kwa kuisoma yote na SIJAONA KWA UHAKIKA UMETHIBITISHA KUA KUTOA ZAKA LEO NI FUNDISHO POFOTU na kwa kweli utashanga kweli ukipitia majibu yangu kwako ktk post 2 natuma,soma zote ndio ujibu, usikurupuke plz. Ila pia post yako ya kwanza ilitoka kwa jina la Amin Yeremiah na hii Jina la juu hapo, natumai sijakosea, naongea na mtu huyo huyo. Najua Watu tunatofautiana, si rahisi nikufanye uwe mimi, hatuwezi katu tukawa sawa, ivyo mimi napenda sana ktk an art of writing kuzingatia/kua na ‘attention to details’, ‘being systematic and to follow up on each issue’’ to ensure relevance and ideas/topics connections kwaiyo jinsi ulivyojibu sasa, nakuona kama umeibuka tu! Napenda kujiridhisha kwanza, kama ni wewe ndiye uliyenitaka nijibu maswali 8 yafuatayo….1. Zaka ni nini, 2. Inatolewaje kwa Mungu.3. Nani anastahili kutumia toleo la zaka.4. Zaka ni ya nini, 5. Je Yesu aliwahi kutoa zaka kama mkristo?, 6. Kanisa la kwanza walitoa zaka?, 7. Zaka imeanzakutolewa kanisani lini ?, 8. Kwa nini iwe ngumu leo kutoa zaka? Kama ndiwe, je umepitia post yangu YOTE kwanza kabla ya kujibu ulivyojibu? Maswali hayo uliyonitaka nijibu, yamejibiwa kwa USAHIHI au la? Kama yamejibiwa sawa au yamekosewa, tafadhari tuwe sysyematic, sema kama sawa au uonyeshe majibu sahihi kama kuna kukosewa! Tuko ktk mjadala, ruska kukubali,kupinga, kukataa,kusahihisha na kubariki kwa ukweli/dhati na hoja tu. Ulileta issues nyingi ktk moja, ni vema ikawa cleared then tunakua tumetoka kwenye matawi mengiii taratibu tunateremka kwa shina moja tu. Nitangoja jibu lako ktk hayo kama utapenda nieendelee kuchangia mada/maswali yako.

  Hata hivyo niseme wazi kuwa umekwepa UKWELI WA KIMAANDIKO katika kusoma na kuelewa maandiko niliyokupa uyasome na kuyatafakari na kwamba Mafundisho ya ZAKA ni kwa andiko ili-Kumb 14:21-28. Sasa embu tuzingatie pamoja, ndani ya hili andiko kuna maneno kama haya kuhusu Zaka, nayo ni ‘’Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka’’Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ILI UPATE KUJIFUNZA KUMCHA BWANA MUNGU WAKO DAIMA ( tafadhari sana zingatia iyo statement ktk herufi kubwa na aliyosema kuhusu Kutoa Zaka pale juu). Ukishaambiwa utatoa Zaka ili upate kujifunza kumcha BWANA MUNGU WAKO DAIMA, HIYO INGETOSHA KUKUFAHAMISHA,INATOKA KWANZA KWA BWANA kisha inayobaki iyo ndio ale mbele za Bwana, kutafsri hapo kua anatoa Zaka ndiyo aile yeye, sit u ni kukosa mantiki nzima ya anachokisema bali pia ni kushindwa kuunganisha hasa ujumbe hapo nini! Alichokisema hapo ni sawa na ivi…’’Usiache kwenda kanisani(Zaka) siku zote za maisha yako Juma 3,4,5-j2, utakaa nyumbani ufurahi na kupumzika ili familia yako ipate uwepo wako pia’’-Kusema kua hapo amemaanisha nikae nyumbani na familia na nisiende kanisani, ndio kosa la uelewa ulofanya.Pia ni vema kua na Elimu ya Biblia na vyanzo vingine,tafuta Bible commentaries ZINAHITIMISHA nini kwa andiko/mstari huo , utajicheka uliyosema!!!!!!!!!We need to do our home works sometimes kabla ya kuibuka na kusema!!!!!!!

  Sasa ikiwa unakuta kwanza na Utoaji Zaka Unapinga nini? na pili ikiwa unamuona Mlawi ktk list ya Wala Zaka, kwa nini, kwa andiko hili, kwa kua hajaonekana mara moja kua ndio anapelekewa/chukua Zaka kwa ajili yake na kutoa mbele za Bwana, ndio ufanye issue?!Kuna haja ya msisitizo huo kweli? ina umuhimu gani kua nani anaanza kuchukua Zaka? Lakini kosa jingine KUBWA ulofanya ktk kutafsri vibaya andiko ilo ni kung’ang’ana maana uipate hapa hapa ktk andiko hili hili na unasahau kabisa, sheria ya Zaka zimetoka kabla ya hapa Kumbu 14. Alianzia kwanza Walawi 27:30-33 kisha Hesabu.18:20-32 then Kumbu na mbele uko hata wakati wa Nehemia 10:37-38.Sijakulewa msisitizo wako una tija gani ktk Hoja yako ILIYOKOSEWA SANA kua Zaka ni fundisho potofu kua mpaka hapo hatuoni Zaka anapewa nani na unasahau Neno linaji-support kwa kuangalia maandiko mengine kuhusu Zaka yalisemaje waziwazi tena ya kwanza kabla ya hili la Kumbu 14.Nadhani umeona wewe ndio umekosea si mimi! na Wala kamwe sijatafsiri tofauti ktk post yangu kwako. Kwa iyo statements zako izi..’’Biblia mpaka hapa haitaji ZAKA KUKABIDHIWA KWA KUHANI na kuwa mlaji wa zaka ni mtoaji, hazina mashiko, ukizingatia Maandiko ya kwanza kuhusu Zaka yalisemaje na kwa mfano niliokupa wa ‘Utaenda kanisani siku zote, utakaa nyumbani na familia…..’’

  Umesema, ‘Utoe elimu kwangu kuhusiana na Zaka kwa kupitia maandiko mengine yanayotoa tafsiri ya neno zaka’’ Ukasisitiza kua Makuhani walipaswa kutoa Zaka toka Zaka! Sasa hapa cha ajabu nini maana hata Makuhani(Wachungaji wetu leo) hata wakipewa Zaka leo na wao pia kwa kicho chao wanatoa kwenye iyo iyo. Ndivyo walivyoagizwa pia Wachungaji wa Kale.Nini cha ajabu hapa au unakataa nini na unakubali nini? hiki ulichosema, kinajibu vipi hoja yako isiyo sahihi kua Zaka ni mafundisho potofu? Nadhani unaona unavyoendelea kupwaya na hamna Elimu mpya hapa uliyonipa, zaidi naona unajichanganya-unakubali kila kitu na sijui unawezaje kuhitimsha claim yako kua Zaka ni doctrine potofu!!!!!!!!!!!!

  Ati Nunukuu Ibrahimu alipompa mfalme na kuhani Melkizedeki wa Salem kama fundisho la utoaji wa zaka kua ni aibu kweli kweli’’ =Sijakuelewa kabisa, aibu gani na iko wapi! Kama kuna andiko bora sana na lenye nguvu ya ajabu kuhusu Utoaji ZAKA na linalokata mzizi wa fitina kama kutoa ni sheria au la, kabla ya torati au la na kama tunatoa kwa lazima au hairi, ni hili sasa! Huna hata hoja chembe, unaweza kana uweli mzito wa maisha na tendo hili la Ibrahimu, NASEMA TENA HUWEZI KUKANA ZAKA HIYO KABLA HATA YA MUSA, utakua unaleta utani! Jaribu ni/tuone hoja zako izo-I real need to see/read it, go ahead.

  Umeuliza, ‘’si Zaka kama tunavyofundisha sisi ni matoleo ya mali ulizotolea jasho,ni zako na unamrudishia Mungu shukurani’’ Si si tunaofundisha bali Maandiko yanasema ivyo lakini pia yanaongeza zaidi, si tu lazima ukitolee jasho ndio uhalali waka uwepo wa kutoa bali ni MOYO WA HESHIMA NA SHUKRANI KWA MUNGU KWAMALI ZAKO, IWE UMETOA JASHO, UMEPEWA, UMEBARIKIWA NA MPENDWA, UMEOOKOTA BURUNGUTU AU DHAHABU , UMEPATA URITHI WA BURE nk vyote TUNAWEZA TOA ZAKO KWAKUA TUNAKUMUHESHIMU BWANA NA KWA MALI ZETU ZOTE NA TUNAJIFUNZ KUMTUMIKIA TUNAPOKUA NA IYO MIND/REMINDER YA KUTENGA TENTH KWA MUNGU kama ilivyoandikwa Kumbu.14:23 kipengele cha mwisho…’’ Ili upate kujifunza kumuhofu( heshimu/ Kumcha ) Mungu Milele’’( notice: NI MILELE) na nyundo nyingine hii inamaliza kazi vema kabisa- Mithali.3:9-‘’Muheshimu BWANA kwa mali zako na malimbuko ya maongezeko yako’’- kama kutoa Malimbuko ni ishara ya kumuheshimu Mungu vivyo ivyo na aina nyingine zote za Sadaka e.g. ZaKA, Changizo nk as long as zinakenda kufanya mambo meme kwa Mungu na Wanadamu, iyo tu , rahisi kabisa.

  Umeuliza kama nimesoma-‘’Kwanini Ibrahim alimpa mfalme na kuhani Melkizedeki ni za nani??? Sasa wewe bwana naona unataka nijaze vitu vingi, hili ni swali kweli kwa umaana wake? La nini? ili iweje jibu lake? Ndio uhalalishe nini sasa kua hakuna Kutoa zaka? Aaa jamani na mimi usivunje mbavu sasa! Cha msingi, Ibrahimu alitoa zaka, period!! Zaka imetoka imetoka over and out! Sasa ni za nini wakati unajua aliyepewa ni Mfalme na Kuhani, swali gaini ili tena!Tokea kwa maandiko hayo ya Ibrahimu kutoa Zaka, umeuliza-‘’Je ni sahihi kutoa zaka mali isiyo yako?’’ Jibu: Mtu anatoaje Zaka kwa mali isiyo yake? amekua mwizi?

  Ulisema umepasuka mbavu kuona nahalalisha Yesu aliwahi kutoa zaka kama MKRISTO’’ na wakati wa huduma yake aliishi akifuata imani na mapokeo ya kiyahudi, kwa hiyo hajawahi kutoa zaka kama MKRISTO na kua wanafunzi wake waliishi kama waumini wa dini ya kiyahudi na kufuata mapokeo ya kiyahudi= Kwanza ubarikiwe kwa kucheka, ni baraka sometime ktk hot debates kucheka na kufurahi, napenda sana iyo,hua sijibani-bani mimi pia nikifurahi, inafanya uhai hapa, kama vile kweli tuna-fellowship live siyo maandishi tu na kioo cha computer,so keep it up bro. Nikukosoe kua sikuhalalisha Bwana alitoa, nilitoa mawazo kwa hoja kadhaa na kusema nina aamini kama hakutoa basi walimtolea kama kuhani wao-yaani walitoa kwa ajili ya huduma yake-ruksa kukataa au kukubali ila kwa hoja pia sio sitaki-sitaki tu. Na mimi nikuulize haya Maswali: Kwanza:YESU KUHANI MKUU tumuache, sasa kwakua Wanafunzi wake walishi kwa kufuta mapokeo ya Wayahudi, je ndani ya mapokeo hayo ya kidini na desturi, Zaka ilikuawe ama la? Prove it. Mbili:Na kama lilikua fundisho, je Wanafunzi walioishi kwa kufuata mapokeo hayo, walitoa hawakutoa? TAFADHARI SANA UWE MWAMINIFU KUJIBU KAMA NAVYOYATENDEA HAKI MNAPONIWAJIBISHA KWA MASWALI YENU YOTE MNAYOULIZA NA ISSUES ZA BY THE WAYS. Ninakungoja ktk ili pia sawa na mengine.

  Umekwepa kusema Zaka kama moja ya matoleo kwa kuchukua andiko la Luka
  Matendo 2:44-45; 4:34-35 na ukahitimisha kua walitumia kanuni ya kutoa 100% na si 10% na huku ndiko kuitimliza torati kulikofanywa na Yesu.Kwa hiyo wanafunzi wa Yesu hawakutoa zaka kama WAKRISTO’’. Maswali:Kwanza nisaidie kujua, umefiakiaje conclusion iyo ya 100%? Pili: How do you know ili kuifikia iyo 100% ya utoaji, hakuna walioleta 10%?Seriously tell me about it. Tatu:Kisha Umefikiaje conclusion kua Utoaji huo 100% ndio Kutimiliza Torati? Seriously tell me about it again. Nne: Ukijibu swali la juu kua waliishi ktk mapokeo ya Kiyahudi, then utanisaidia kama kweli hawakutoa kama Wakristo ama la manaa sioni Kutoa Zaka kunaharibu vipi kua Mkristo. Tadhari unaona nasisitiza uaminifu na kutendea haki mijiadala kwa kujibu ulichouliza ili kuepusha kukimbia tu na sentence za jumla, izo kila mtu anaweza, haitatusaidia ktk hoja mezani kufukia mambo ikiwa kila mtu atafanya ivyo maana kila mtu anaweza kupuuza pia

  Maandiko yanatufundisha kuwa KUHANI WA KIKRISTO NI MKRISTO ALIYEKOMBOLEWA NA YESU na ya kuwa Uchungaji,Ualimu,utume,uinjilisti ama unabii ni WIZARA/HUDUMA ZA KIKUHANI SI UKUHANI= Sawa kabisa ulichosema lakini pia usisahau ktk izo zio Wizara, umo wamewekwa wengine kutenda na kutumika umo moja kwa moja, kulihudumia Neno day and night na hata wanalipotaka kuchukulia na shughuri nyinginee nyingii, Roho Mt akawasaidia kushituka mapema, wakajitenga kw aksuudi moja tu la ukuhani wa leo Mdo.6:2-3-soma kwa macho yote mstari wa 2. Kisha umesema mwenyewe nukuu ya Bible kua kati ya sisi Makuhani wote, Bwana alitoa wengine kua…..Hii ndio mantiki ya Mungu toka Agano la Kale wakati wa sheria na mpaka leo kuwajali hao wakaao umo na kutumika umo pia na si kuaachwa peke yako, kama ilivyokua kwa Mlawi kule, ndivyo ilivyo leo, usisahanu kanuni hii- Kale ilikua ni Kivuli, Leo Picha kamili.

  Hii ya mwisho kwangu ni kituko-‘’UTOAJI WA ZAKA KANISANI UMEANZA MWAKA 777 BAADA YA KRISTO TENA KWA AGIZO LA GAVANA CHALAGNE’’. Kwa hiyo? Huyu Gavana ndio ananifanya nitoe leo hapa Kwetu Geita? Mbona ninatoa siku nyingi kwa furaha na sijawahi msikia huyu jamaa yako brother ila nimemuona Ibrahimu na Wapendwa wengine ktk Bible wanapenda kutoa nikaiga hao! Kindly send my regards to the his Excellency governor Galagne, tell him HE MUST BE SAVED TO GET IN HEAVEN IF HE IS NOT AND AFTER BEING BORN AGAIN, HE CAN NOW GIVE THE TITHE OUT OF THE WILL WHICH MEANS NOT WELCOMING EXCUSES RATHER UREGENCY OF DOING IT OUT OF LOVE AND THE JOY OF HIS NEW LIFE IN CHRIST WHO GAVE EVERYTHING INCLUDING HIS OWN LIFE FOR HIM/ME AND YOU Yeremiah.Amen.

  Press on.

 108. Did you know…

  The percentage of income that Christians give to God’s work declined for 40+ year!
  While he was living, Larry Burkett of Crown Financial Ministries had estimated that only 5% of Christian gave 10% or more to the Lord.

  Barna Research reports that only 7% of Christians “tithe” (give 10% or more of their income to God’s work.
  90% of churches have no active plan to teach biblical financial or giving principles to their congregation.
  85% of pastors feel unequipped, uncomfortable and untrained to teach biblical financial and giving principles.
  In light of these statistics, here are some practical ways a church or ministry can use Scripture passages to teach and encourage God’s people in faithful Christian giving and joyful generosity:

  q Gen 14:19 (Abraham’s give of 10%)

  q Gen 28:20-22 (Jacob decision to give 10% to God)

  q Exod 35:4-29 (Moses and the people’s gifts to build the tabernacle)

  q Lev 27:30 (Tithe of everything is the Lord’s)

  q Lev 27:32 (Every tenth animal is the Lord’s)

  q Num 18:21 (Tithes support ministers of God)

  q Deut 12:5-7 (Tithes, special gifts, freewill offerings)

  q Deut 14:22-29 (Set aside a tenth to learn to revere God)

  q 2 Chr 31:2-12 (Hezekiah generosity & giving instructions)

  q Neh 10:35-37 (Nehemiah’s giving instructions)

  q Neh 12:43-47 (Faithful giving to God’s ministers)

  q Neh 13:11-13 (Nehemiah’s rebuke & the results)

  q Mal 3:7-12 (Holding back tithes & offerings is stealing from God)

  q Matt 23:23 (Jesus’ affirmation of tithing)

  q Luke 11:42 (Jesus’ affirmation of tithing)

  q I Kings 17:8-16 (Elijah and the starving widow)

  q Deut 8:18 (God gives people ability to produce wealth)

  q Prov 3:9-10 (Honor the Lord with your wealth & firstfruits)

  q Exod 36:3-6 (Moses restrains people from bringing offerings)

  q Mal 1:6-14 (Malachi’s rebuke for bringing bad offerings)

  q Hag 1:4-11 (Haggai’s giving challenge)

  q 1 Chr 29:2-9 (David’s generous gift & giving challenge)

  q 1 Chr 29:11-17 (Everything we have and gives comes from God)

  q Luke 6:38 (Give and God will see others give to you)

  q 2 Cor 8:2-21 (Rich generosity in the midst of extreme poverty)

  q 2 Cor 9:5-15 (God loves a cheerful giver)

  q Deut 28:12-13, 43-45 (Blessings & curses for obedience)

  q Ps 50:9-12 (God owns everything)

  q Prov 11:24-25 (Generosity is the pathway for more)

  q Prov 18:9 (Slackness in giving is the same as destroying things)

  q Prov 22:9 (Generous man will be blessed)

  q Prov 28:22 (Stingy man is eager to get rich, but gets poverty)

  q Prov 28:27 (Give and have enough, withhold and be cursed)

  q Matt 6:25-34 (Don’t worry, but seek first the kingdom of God)

  q Mark 12:41-44 (Rich people giving and the widow’s mite)

  q Deut 16:10 (Give in proportion to the blessings the Lord has given you)

  q Deut 16:16 (No man should appear before the Lord empty-handed)

  q Deut 16:17 (Each person should give in proportion to the way God has blessed them)

  q 1 Cor 16:2 (On the first day of each week, give according to God’s blessing)

  q 1 Tim 6:6-11 (Cautions about the materialism and the love of money)

  q 1 Tim 6:17-19 (Instructions to be generous and willing to share)

  q 1 Sam 30:24 (Those who stay with the supplies share with those on the front lines)

  q Matt 6:19-21 (Do not store up for yourselves treasure on earth – heart & treasure linked)

  q Heb 6:10 (God is not unfair, He will not forget the help you gave)

  q Isa 32:8 (Noble man makes noble plans)

  q Acts 2:44-45 (Believers had everything in common)

  q Acts 4:34-37 (No needy persons. Sale of lands and houses.)

  q Rom 12:13 (Share with God’s people who are in need)

  q Heb 13:16 (Don’t forget to do good and share with others)

  q I Jn 3:17 (Do you see brothers in need – help them)

  q Luke 18:22-25 (Rich man turns away from Jesus)

  q Gal 6:6 (Support financially those who teach you the Word of God)

  q Matt 25:35-40 (Helping the least of the brethren is helping Jesus)

  Acts 20:35 (It is more blessed to given than to receive)

  http://www.kluth.org/church/100generosity.htm

 109. Sungura,
  Kimsingi mimi nimekuelewa kwa hoja zako hizo. Ni hoja nzuri. Najaribu kumwangalia na kumjifunza Mungu kwa umakini mkubwa. Kuna sehemu zingine huwa simwelewi na hivyo nabaki kutii tu kama Ibrahimu, Isaka, Nuhu, Eliya, Henoko, Musa, Mitume nk. Kama Mungu ameagiza na kuna elements hadi kwenye agano jipya za kauli hiyo, acha nitii tu kwanza, maana UTII ndio msingi wa wokovu kwa wanadamu. Kwa vile tunampenda Mungu, sharti tutatii neno lake. Kwa vile sina nuru inayopingana na utoaji wa zaka kwa kila mapato yangu, acha tu nimtolee Mungu hiyo zaka na sadaka zingine maana hata uzima, chakula, hewa, kazi na baraka zingine anazonipa kila dakika, Mungu atanishangaa sana nikiwa na roho ya korosho-kutokuwa na shukrani kwake.
  Ngoja nimshukuru na kumwabudu Mungu kwa matoleo. Nikipata nuru mpya, nitakuijia kaka Sungura.

  Ubarikiwe

 110. Ninaheshimu mchango wa kila mmoja hapa.
  Baada ya kuyapitia majadiliano haya, ninaomba niweke mtizamo wangu binafsi wa Kujitoa kwa Mungu(ambapo zaka ni sehemu mojawapo ya somo hili la kujitoa kwa Kristo). Maelezo haya ni baada ya mafundisho yenye kujichanganya kuhusu kumtolea Mungu na hasa somo la zaka niliyokutana nayo. Roho wa Kristo alinipeleka shule hii na imekuwa ya faida sana kwangu. naomba niwashirikishe.

  Nilipompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu, nilimaanisha kujitoa kabisa mimi na kila nilicho nacho kwa Kristo (1Kor.6:19-20; Rum. 7:4; Rum. 14:7-8). Ni lazima pia tujue kuwa tumeumbwa, na kuokolewa na Kristo kwa ajili ya Kristo(Kol. 1:15-17). Ukishaokoka wewe sio mali yako mwenyewe tena. You belong to Jesus Christ 100%, NOT 10%, 30% or 99%. Kwa hiyo kila ulichonacho ni mali ya Kristo(HII NI HOJA YA MSINGI SANA). Yesu Kristo hakukataa kutoa zaka, wala msingi wa mafunzo yake haukuwa kuhimiza wala kuchukua muda na nguvu nyingi kufundisha kuhusu zaka, wala mitume hawakuhimiza sana kutoa zaka. Ukisoma Mt. 23:23 Yesu anawapa Mafarisayo ole, kwa kujihesabia haki kwa sababu ya kutoa zaka mpaka ya vitu vidogo kama viungo vya chakula, NA KUACHA MAMBO YA MSINGI ZAIDI YA SHERIA, anawaambia haya mambo ya msingi wapaswa kufanya bila kuacha yale ya kutoa zaka. Wafundishaji wa utoaji zaka wenyewe hawawezi kutoa zaka ya kila kitu mfano viungo vya chakula au mtu kakupa pipi mbili ukaanza kumumunya, hapo bila kutoa zaka. Kimahesabu 10% ni 10% ya kila kitu, kama ni swala kutimimiza torati ya zaka. Mt.5:20 Yesu anatuambia kwamba haki yetu isipozidi haki ya waandishi na mafarisayo (Yaani tutoe zaka zaidi ya hii ya Mafarisayo ya 10% ya viungo vya chakula) hatuwezi ingia kwenye ufalme wa Mungu.

  Wanaosimamia kwamba zaka ilikuwepo kabla ya Torati wako sahihi kabisa, lakini ni lazima tukumbuke kuwa mwanzo wa utoaji zaka alikuwa Ibrahim na alitoa kwa Melkizedeki, kuhani anayesimama kwa mfano wa Yesu Kristo. Biblia inatuambia Ibrahim alitoa zaka ya mateka, haizungunzi kuhusu utoaji wa zaka wa mali alizokuwa anamiliki/ amezalisha mwenyewe(Tuwe makini hapo). Lakini Ibrahim anakuwa rafiki wa Mungu kwa sababu ya KUJITOA KWA MUNGU KABISA KABISA 100%, binafsi ninakubali kuwa ndiye mtu aliyejua kumtolea Mungu kuliko wanadamu wote baada ya Yesu Kristo. Kwanza, alijitoa kwa kusudi la Mungu na akaiacha familia ya baba yake kwenda asikokujua, niambie hiyo ni kutoa zaka ya asilimia ngapi? Pili, alipomtoa Isaka awe sadaka ya kuteketeza, Isaka mtoto pekee wa ahadi, mtoto wa uzeeni, fanya mahesabu halafu uniambie hiyo ni zaka ya asilimia ngapi. Kumbuka, hakuwa namtoa kama Hanna alivyomtoa Samweli akae kanisani, alimtoa afe. kwa hiyo kama ni kabla ya Torati ni lazima uzungunze kujitoa 100% kama Ibrahim kama nasi tunatamani kuitwa wana wa Ibrahim.
  Nilipoaanza kufundishwa mtizamo huu, Roho Mtakatifu alinipeleka kwenye somo la Yesu juu ya mwana mpotevu (Luka. 15: 11 – 32). Hawa watoto waliishi na baba yao siku zote, kila kilicho baba ni chao na kila kilicho chao ni cha baba yao(hakukuwa na mpaka) soma mstari wa 31. Maisha ya ubinafsi yakamea ndani ya motto mdogo akataka kuwe na mpaka wa mali yake nay a familia, baba yake akamridhia na akampa. Kwa tafsiri na vipimo vya kidunia Yule mdogo alikuwa tajiri kuliko mkubwa, lakini kwa kipimo cha Ki-Mungu alikuwa ametengwa na familia ya Baba/ alikuwa amekufa(mstari wa 32). Biblia haituambii kuwa alifanya uovu mwingine, bali alikataa kumiliki pamoja na familia, vyote viwe vyao wote. Kanisa la kwanza liliishi maisha yah ii familia walikuwa na kila kitu shirika(Mdo.2:44-45). Yule kijana mkubwa aliyebaki hakufahamu utajiri aliokuwa nao kwa kukubali kuwa shirika na baba na familia kwa ujumla, ndio maana alighadhibika alipokuta ndugu yake kachinjiwa ndama aliyenona. Lakini Baba yake anamwambia “Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako”. Ukitaka kumiliki 90% mwenyewe hutakuwa tofauti na yule mwana mpotevu, lakini nia ya dhati ya Mungu ni tumiliki pamoja Naye, vya Mungu view vyetu na vyetu view vya Mungu. Mungu akikuambia nimekuja kuchukua mshahara wako wa mwezi huu wote, au lile gari lake alilokukabidhi, au nyumba hupaswi kuumia. Usiwe na roho ya kujipenda nafsi, choyo au unyimi, kumbuka Yesu ansema jilinde na choyo, uzima wa mtu haupo katika wingi wa mali alizo nazo.

  Nihitimishe kwa kusema, ukikuta Mkristo anakataa kutoa zaka au anabisha kutoa zaka ana shida kubwa kuliko anavyodhani, (ila sisi watumishi tuwe makini tusichanganye watu kuhusu utoaji wa zaka) ili kutimiza haki ya kuzidi waandishi na mafarisayo kila aliyezaliwa mara ya pili anapaswa kutoa zaidi ya 10%, hii itakusaidia ku- compensate vile vitu tusivyoweza kukokotoa zaka yake. YesuKumbuka Yesu anasema hazina yako iliko ndipo ulipo moyo wako, kama hazina(mali) yako haipo kwa Yesu yote, moyo wako hauwezi kamwe kuwa kwa Yesu. Tuendelee kujadili kwa namna ya kujenga kwani akuhimizae kujitoa kwa Mungu au kumtolea Mungu anataka uwe na uhusiano wa karibu sana na Yesu na uishi maisha ya barika.

 111. Kaswahili,
  Ha ha ha haa!! Popo au ndege!! Teh teh teh!!
  Haya bwana ubarikiwe kwa changamoto hizo… Kimsingi kuna sehemu za hoja zangu hukuzielewa. Huenda sikujieleza vizuri au wewe mwenyewe tu hukunielewa.
  Narudia kwa ufupi. Ninavyoamini mimi kaka, suala la kutoa, ni kanuni za mbingu. It is Biblical! Na kwa vile ni Biblical, Mungu ametuachia uhuru wa kufanya uamuzi wa kutoa ama la, kutii ama kuasi! Unapotoa, kuna baraka za Mungu-uzima wa milele. Usipotoa, kuna laana za Mungu-mauti ya milele. Kama suala la utoaji ni Biblical, na Biblia tunaamini kuwa ni neno la Mungu; Na Mungu aliagiza watu wamwabudu kwa matoleo pia; Je, kutoa zaka (kama mojawapo ya matoleo) bado kuna tatizo gani hadi tufikie hatua ya kumhoji Mungu?
  Mpaka hapa sidhani kama umenielewa Kaswahili!! Ngoja nitoe maelezo zaidi. Mwanadamu alipoanguka dhambini, Mungu alianzisha utaratibu funge wa matoleo. Utaratibu ambao, ulikuwa ni ya muda tu. Utaratibu ambao hata haukuondoa dhambi-yaani sadaka za kafara. Pamoja na kwamba ulikuwa ni utaratibu wa muda, nina imani unafahamu kwa hao waliokuwa wakiukiuka utaratibu huo. Tukianza na Kaini na wengine wengi wenye tabia kama hizo waliofuata. Tunajua vizuri historia zao.
  Mimi nina imani kuwa, kama Mungu aliagiza, mimi sina haki ya kumhoji Mungu ilhali mimi mwenyewe ni mali yake na hizo mali nazo ni zake pia. Ili nieleweke zaidi; Ngoja nikupe mfano kabisaa.
  Ibrahimu alipoambiwa atoke nchi ya Uru ya Ukaldayo aende asikokujua, Kaswahili na Sungura leo mngebisha kuwa huyu ni Mungu wa namna gani!! Mbona haeleweki?? Kwa watu wenye uwezo mzuri wa kufikiri kama Kaswahili, Sungura na wengine wengi hapa Sg, wangeendelea kuhoji na kumshangaa Ibrahimu mzee wa watu yu aenda sehemu asiyoijua!! Yumkini, wangesema kuwa mzee huyu anazeeka vibaya jamani!!!…
  Aidha, Ibrahimu alipojaribiwa kutoa matoleo kwa zawadi aliyokuwa amepewa na Mungu, yaani mwanawe, hakusita. Kumbuka aliisotea kwa muda gani? Je, kwani Ibrahimu hakuwa na fursa ya kukataa au kumhoji Mungu? Lakini kwa unyekekvu mkuu, Ibrahimu aliiskia sauti ya Mungu…
  Mfano mwingine, Isaka aliishi (mwanzo 26)nchi ya ….Njaa ilipoingia ktk nchi hiyo, watu walianza kuhamia nchi zingine zenye shibe-chakula. But Mungu anamkataza Isaka asiende huko kuliko na chakula. Mungu anamwambia akae ktk nchi hiyohiyo ya njaa, halafu anaahidi kumbariki hapohapo kwenye njaa… kwa watu wenye reasoning kubwa kama nyie, mngembishia Mungu na kusema haiwezekani, mbona wengine wanahama?
  Kwa ufupi kaka Kaswahili, ninasema hivi, Mungu anapoagiza kitu, mwanadamu hana haki ya kukigeuza na kukitafutia visingizio. Ni ukweli usiopingika kuwa, hadi tunaenda mbinguni, hatutakuwa tumemfahamu Mungu vya kutosha kiasi cha kuanza kumbishia kwa baadhi ya mambo kama haya ya utoaji wa zaka. Kwa sasa, kuna mambo ambayo Mungu anatutaka tufanye, nasi hatuna budi kuyafanya licha ya kutoyajua kiundani-maadamu yameandikwa ndani ya Biblia. Sharti tuwe kama akina Ibrahimu baba yetu wa Imani. Tukifika mbinguni, tutamhoji Mungu ana kwa ana.
  Kwa mfano nimeona unachanganya eti kuna sheria za mwilini na sheria za rohoni-Torati.
  Kimsingi Mungu ametupa neno na sheria zake ambazo zimejengwa kwenye upendo – Agape!! Mungu alipotoa maagizo au sheria, aliziandika ndani ya mioyo ya watu wake. Tangu mwanzo, kila mtu alifahamu kuwa, kuiba, kuzini, kuwa na sanamu nk ni dhambi. Ndiyo maana ukiangalia vizuri vizazi vya mwanzo kabla ya Waisrael pale mlimani Sinai(sheria 10 zinapotolewa na zilipodhihirishwa kwa maandishi tangible), vizazi hivyo viliishi kwa kufuata sheria hizo. Kila aliyezivunja, alionekana katenda dhambi. Hivyo sheria za Mungu ziko ndani ya mioyo ya watu wake hadi leo hii. Ndiyo maana tunaambiwa, utii wetu wa sheria za Mungu, sharti uanzie moyoni mwetu. Utoaji wa zaka, sadaka, kutoiba, kutozini nk, sharti kuanzie ndani ya mioyo ya watu, ndipo Mungu atatukuzwa.
  Mungu hatulazimishi kuzishika au kuzitii hizi sheria au neno. Kadhalika, Mungu hatulazimishi kutoa zaka wala sadaka. Kufanya matendo haya, yanapaswa kuongozwa na upendo wa Mungu ulio ndani yetu. Kwa maneno mengine, kwa vile Mungu tunampenda sana, tutakuwa tayari kufanya kila aagizalo bila kuona kuwa ni mzigo. Neno la Mungu kwetu, linahitaji UTII, utii usio wa shurti. Utii uliojengwa kwenye upendo. Ndiyo maana Mungu kwenye sheria zake ametanguliza neno UPENDO, then UTII(kushika amri zake ambako huja automatically kutoka kwenye msukumo wa ndani).
  Na kinyume cha UTII, ni uasi ambao nao chanzo chake, ni moyoni then hujidhihirisha kwa nje. Mtu anapoamua kutomtii Mungu kwa zaka, sadaka, au sheria zake tokea moyoni mwake, japo kimwili anaweza kujionesha kinyume, mbele za Mungu hana tofauti na muasi au mnafiki.
  Mwisho, laiti tungemfahamu Mungu vizuri ndg yangu Kaswahili, Sungura na wengine, tusingekuwa na wasiwasi juu ya miili yetu, mali zetu tulizo nazo ni mali ya Mungu. Hakuna kipimo kikubwa kinachodhihirisha upendo wetu na anachokiangali Mungu kwa karibu kama UTOAJI. Ni ngumu kueleweka kwa akili za kibindamu.
  Lakini nirejee kauli ya Yesu kuwa; “Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu” Luka 14:33
  Wito wa Paulo kwetu;
  1 Timotheo 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
  Waebrania 13:5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
  Barikiwa

 112. Sungura,

  Ni muhimu sana kama unajua wanasoma Watu wengi, basi yale ya msingi ya Makanisani, ya Ukweli na yamekua yanafanyika na kuleta faida kubwa ktk Huduma na Mambo ya kanisa kwa ujumla mfano Utoaji mbalimbali iwe malimbuko, changizo, Zaka, basi hayo ndio tuyajengee. Hatuwezi sema sincerely kwa kua topic ya mahojiano haya ni Potofu au hapana, ukashikilia bango kua ni fundisho potofu kufanya ivyo leo.Tokea lini Kumtolea Mungu past, present, future kukawa fundisho potofu?

  Ushahidi wa wanaosoma wengi ni Ndugu Nelsom Tumaini ambaye amejisema mwenyewe kua ni mchanga na ana mwaka mmoja tu ktk Imani, lakini ametatizika na namna unavyoongelea swala la Utoaji iwe Zaka au la( SABABU YA MIMI KULETA SOMO LA UTOAJI IN GENERAL is justified maana aliomba ivyo ktk comments zake) na pia MISIMAMO YAKO BINAFSI KUHUSU ZAKA imeleta shida-kipengele cha kua watu wanalazimishwa kanisani ulivyokiongolea( highlight sana) na hata ku-support comments kama za Mr. Kaswahili kuwasema Watumishi wote ni Makupe-including my and your Pastor in this case, badala ya kukazana kumsaidia akae sawa, umemtia moyo na maneno yake ambayo yanaonyesha aina ya Mkristo kanisani kwake na asivyo wa baraka kwa Mchungaji wake.UKIWA MUUNGWANA NA KAMA ULIVYOTAKA WENGINE WAWE HATA UKASHAURI TUWE NA USTAARABU WA KUKUBALI KWELI/HOJA KAMA MWENZIO AMESEMA VEMA( mimi nimeshakuonyesha mfano), kubali tu kua ktk maelezo yako, UMETELEZA. Ukiwa mnyenyekevu ukubali ilo. Haiwezekani mtu ana mwaka mmoja ktk Wokovu aone kuna ubinafsi zaidi wa wanadamu ktk kutetea kutotoa Zaka, wewe useme ulikua sawa! Si kweli na unapohalilisha ilo, hakika nitegemee kukupinga kabisa bila kuchelewa na kukuonyesha unakosea Sungura. Vi vema ukayashika unayoshauri wenzio, uyaishi na kudhihirisha maneno yako mwenyewe.Kubali uliteleza/kuzidisha chumvi, huko Makanisani hatuna hali mbaya kiivyo na kulikua hakuna sababu ya wewe kusemelea sana misimamo binafsi kama ndio Neno la Mungu au general conduct ya Wapendwa wakati wengine hatuna shida na tunapenda kutoa kila kitu ikibidi mradi tu mambo ya Mungu, Watumishi na Mahitaji ya Watu, yakwenda mbele, yasikwame na Mungu atukumbuke sana.

  Kwamba Kanisa lina hitaji nini kati ya fedha na Zaka, jibu ni vyote! Ni sawa sawa na kuuliza Kanisa lina hitaji maombi au maombezi! Lakini wakati Ibrahimu anatoa, jijibu mwenyewe kwa nini alitenganisha tenth ya…. Si angetoa tu? si vyote ni vitu tu au Wanyama tu au Fedha tu. Wakati Mungu anawaambia watenge tenth , wasimsahau Mlawi au Wahitaji, si wangetoa tu chcochote iwe fifth, fourth? Si sadaka tu ni sadaka? Si matoleo ni matoleo tu! Ukiniuliza mie nitakujibu Mungu ni Mungu wa UTARATIBU na PIA wanadamu wakiweka utaratibu( kutengenisha zaka na malimbuko na pia michango ya ujenzi,malimbuko kwa maana nzuri tu ( kumbukumbu, kukumbushana, wanapohitajika kuonyesha ushahidi ktk mabanks au serikalini au mashirika ya nje cash flow/income ya kanisa kabla hawajasaidiwa hapo kanisani au iyo Ministry ya kweli au reports ktk ngazi za juu ya kanisa, haina shida wala si dhambi.

  Mabinza nimeshajibu kila hoja, karibu usome na kama una neno au sikujibu anui kama ulivyonitaka, utasema. Maswali uliyokataa kuyajibu najua kwa nini-yanakukaba kwahiyo, nimeshapata jibu na ni sawa na umeelewa. Mengine au maelezo yangu kadhaa kama yanatoka nje ya mada, ni kwakua chanzo ni wewe, una raise issues ambazo hazina umuhinu sana lakini vilevile kuzi-clear once for all ili zisijitokeze sana, ninaona ni sawa ili hatimaye tunabaki au kukufanya ubaki kwa ya msingi ktt meza. Sitasita kufanya ivyo tena kama utanipeleka uko.

  Press on.

 113. Seleli sioni kitu cha msingi sana cha kukujibu. kwanza sehemu kubwa uetoka nje ya mada. Unatumia paragrafu ndefu kujitetea kutokana na mimi kukushauri upunguze kuchanganya changanya lugha, huo ulikuwa ushauri tu. Kama wewe unaona ni mtindo mzuri wa uandishi endelea nao.

  Suala la kushuka roho mt, na mambo ya ‘assumptions. sintayajibia chochote maana hapa hata hayahusiki kiasi cha sisi kupoteza muda kulijadili.

  Michango yetu inasomwa na watu wengi na wenye ufahamu wa kutosha, wao ndio wanaweza wakasema au wakaelewa nani anaeleweka na nani haeleweki kati ya mimi na wewe.

  Nafikiri kuna mambo mengine ya msingi umeulizwa na Mabinza unatakiwa kuyatolea majibu anuai.

  Unaposema unakubaliana na mimi kuwa kutoa ni hiari, kwa nini nikisema kuwa kutoa zaka ni hiari unaonekana kutonielewa Seleli? Au maana ya neno hiari ni nini hapo kama sio kusema ni kutoa ninachotaka mimi kutoa au nilichoguswa/jisikia moyoni mwangu kutoa. Si Paulo anasema kila mtu afanye kama alivyokusudia moyoni mwake. Mimi na wewe tukiwa na elfu kumi wote wewe ukakusudia kutoa shilingi 1000 na mimi shilingi 600, tatizo liko wapi, si ndivyo kila mmoja alivyokusudia?

  Lakini unatakiwa ujiulize sana kitu hiki kwamba,je kanisa linahitaji fedha au zaka kwa ajili ya mahitaji yake.

  Basi kama tunakubaliana kuwa kutoa ni hiari yaani mtu kutoa anachoona yeye ni sawa kutoa, kwa nini sasa tunatenganisha kwamba hii pesa ni zaka na hii pesa ni sadaka( labda ya shukurani), zote si ni pesa hizo , kwa nini mtu asitoe tu bila kutenganisha?

  Asante.

 114. Mr. siyi,salaam!

  Hapa nakunukuu comments zako kwa sungura:

  “…. Lakini inaonekana kuwa, wewe umeshikilia msimamo wako tu wa roho ya unyimivu. kutotoa zaka [na sadaka] mpaka uguswe”

  “Kimsingi, dini [tendo] iliyo bora mbele za Mungu siyo kile kitendo cha kutoa, bali ni ule msukumo kutoka moyoni mwa mtu. hicho ndicho Mungu huangalia”

  Katika aya ya kwanza unamshutumu sungura kwa kuendelea na msimamo wake wa kichoyo wa kutotoa zaka na sadaka ama mpaka aguswe.
  Aya ya pili umekiri kuwa dini iliyo bora mbele za mungu au cha msingi si kutoa, bali ni ule msukumo kutoka moyoni mwa mtu. hicho ndicho mungu huangalia. umesema vizuri sana hapa. na mimi niongezee kwa kumnukuu paulo anasema, hatanikiwa na imani ya kuhamisha milima. hata nikitoa mali zangu zote nikawapa maskini, na nikautoa mwili wangu niungue moto. kama sina upendo si kitu. kimsingi msukumo kutoka moyoni ambao ndo umesema ndo kitu cha msingi ktk utoaji hutokana na mguso ambao sungura anasimamia. ukiguswa moyoni unasikia msukumo moyoni. na huo msukumo wa moyoni hutoka ktk pendo. na pendo haliwezi kujuta. bali pendo hutabasamu. pendo halitembei pamoja na majuto. na aina hii ya utoaji ndiyo paulo ameisisitiza. na ndo sungura anaamini inatakiwa iwe hivyo. cha msingi kama ulivyosema ni msukumo kutoka moyoni. si msukumo kutoka ktk torati. msukumo utokao ktk torati,yaani sheria, ni msukumo wa nje. hautoki ndani moyoni. na mungu hafurahishwi na msukumo wa nje. lakini mr. siyi, nikiangalia aya ya kwanza nikiilinganisha na aya ya pili unaninishangaza! nashindwa kuelewa kama wewe ni popo au ni ndege! lakin pia kuna sehemu nyingine umesema, nakunukuu: makuhani hawa, yaani wachungaji wako full time kwenye huduma, na hawaruhusiwi kujishughulisha na kazi yoyote isipokuwa huduma hiyo tu. mwisho wa kunukuu. swali: nani aliwafanya kuwa full time kwenye huduma? pili, wapi imeandikwa wachungaji hawaruhusiwi kujishughulisha na kazi nyingine yoyote mbali ya huduma? unataka kusema wachungaji leo ndo wapo bize sana kumshinda paulo aliyezunguka sehemu huku na kule akipeleka injili na kupanda makanisa kibao, lakini pia akirudi kuyatembelea kuangalia maendeleo yake, na bado aliweza kutengeneza mahema na kuendeleza biznez yake hiyo?

 115. Mchungaji Mkenda mimi binafsi nashukuru kwa kujitokeza kwako katika mjadala huu.

  Kwa kuwa umesema zaka ilikuwepo hata kabla ya torati, na mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia zote. Lakini naomba tu unijibu hili swali langu dogo.

  Swali:
  Utoaji wa zaka kabla ya torati unatofauti na utoaji wa zaka wakati wa torati?

  Asante mchungaji.

 116. “42Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kutoa matoleo hayo, wala msisahau kufanya hayo mengine.”

  Bwana Yesu apewe sifa. Yesu aliwafundisha mitume kutoa zaka na sadaka na ktk mstari huo hapo juu anawaambia kwamba pamoja na kwamba wanatoa zaka lakini waanze na kutenda haki, upendo wa Mungu na hatimaye wasiache kumtolea Mungu zaka. Kwa mantiki hiyo Yesu hakutengua utoaji wa zaka hata kidogo pia ujue kuwa zaka ilikuwepo kabla ya Torati, ikawepo wakati wa torati, ikawepo wakati wa manabii na hatimaye Agano jipya. Nakumbuka Yesu/Mungu si kigeugeu, Mungu ni yule yule jana leo na milele, wanadamu ndio wanaotaka kumpangia mipaka ya kibinadamu. Kumbuka kati ya sadaka yenye ahadi nyuma yake ni Zaka, Malaki 3:10-12, soma uelewe kwa makini.

  TAHADHARI: Nawaomba tuache mawazo kwamba sisi watumishi tunataka zaka zenu/fedha zenu kwa ajili ya faida yetu sisi si kweli hata kidogo. Kama kanisa/huduma ina utaratibu sahihi na wana mcha na kumhofu Mungu suala la zaka au sadaka si siri ya Mchungaji peke yake. Au kama kuna mtu anataka kujua jinsi sisi wachungaji tunavyofanya matumizi halali awasiliane na mimi na akitaka aje ofiisini kwangu nitamsaidia.

  Asanteni sana, nitachangia tena wakati mwingine.

  Rev. Damasus F. Mkenda

 117. Mabinza brother,
  Nimeitendea haki makala yako na nimeisoma yote kabisa, karibu kwa mrejesho wangu huu.
  Umesema unataka kujua ukweli wa zaka katika nyakati zetu. SWALI: ukweli gani unaoujua wewe TUTOE ZAKA LEO AU IMEPITWA NA WAKATI?
  Umesema, Agano la Kale ni Kivuli( Biblia imesema actually) halafu wewe ukasema, kama kopi imeondoka na imekuja original, kipo ina makao? JIBU: Kopi kama kopi haina makao tena kama original ipo ila na kwa maisha ya kawaida, TUNAKUAGA NA ORIGINAL KWANZA then copy, kwa muktadha wa Biblia na Mpangilio wake, ajabu Kivuli kilianza kuja Live! Kusemea original! Ajabu ee! KWA HIYO SI AJABU KWA MSINGI HUU, HUYO HUYO ORIGINAL AKAWA ANA NUKUU SANA KOPI NA KISHA HATA KUTEKELEZA YOTE YALIYOSEMWA NA KOPI(MUSA NA MANABII), MENGINE AKIYATEKELEZA KAMA YALIVYO( kuzaliwa na kufa kwake) NA MENGINE KWA FASHION YAKE/ALIYOANZISHA YEYE ORIGINAL-maana kama original, ingawa alipaswa kutekeleza yale kopi iliyomsemelea( maana kopi yenyewe nayo haikusema-sema tu bali ilisemeshwa na Original mwingine wa SIKU NYINGI/MZE WA SIKU( NIKO AMBAYE NIKO), bado original aliyekuja, alikua na haki yake ya kuyaanzisha mengine mapya au kwa usahihi tusema-si mapya bali yale yale ila ktk upya-kwa kua alisema hata nukta moja ya kopi, haitapita mpaka yametekelezwa yote ya Kopi

  Umesema nikuonyeshe hiyo Zaka ipo wapi katika Agano jipya na kua haubishani bali unanataka tu uone basi’’ JIBU: Hutakaa uione live lakini ipo kwa msingi ule juu maana wakati hata kopi wa pili anaandaliwa( Musa), kulikua na kopi mwingine kabla yake aliyetoa Zaka bila kopi wa pili kuanza maisha..Mwanzo.14:1-20. Swali! Je sasa umeiona Zaka kwa misingi iyo ya Original alivyosema na kopi wa kwanza( Ibrahimu) alivyofanya kabla ya kopi wa pili( Musa) kuifanya iwe sheria? NIJIBU TAFADHARI.

  Umesema vema hapa.. ‘cha kaisari mpe kaisari na cha Mungu mpe Mungu’, tunajua cha Mungu ni Ibaada, kodi tunatoa serikalini na Ibaada tunafanya kwa Mungu! JIBU: Hakuna ibada isiyokua na matoleo na Zaka ni mojawapo ya matoeleo. Na kama Serikali inataka kodi kuendesha mambo, Serikali( Utawala/Ufalme) wa Mungu duniani, UNATAKA SANA BOTH NGUVU ZA ROHONI NA MWILINI(MALI,PESA,VITU) tena kuzidi Serikali za Wanadamu maana tuna kazi kubwa ya kuupiundua Ulimwengu wote kwa Mfalme/Rasi wa Kweli.

  Kuhusu ili andiko Lk. 11:42, umefafanua ivi-‘’Mafarisayo walitoa zaka kwa mjibu wa Torati haijaelezwa kama Yesu alisema waendelee kutoa ama la, walipuuza haki na upendo wa Mungu, na kutoa tu zaka za mbogamboga, ‘ILIWAPASA’ kutoa matoleo hayo, wala ‘WASISAHAU’ kufanya hayo mengine”- Sasa Mabinza , hapa umejijibu au hujajijibu? Mie naona umejijibu tayari. Iyo ‘’iliwapasa’’ usiende mbali saana kua kuna kitu spesheli Yesu aliongea hapo kwa kificho au fumbo!! wala haihitaji kutulia sana kujua ilo. Labda kwa kua umesema unataka ‘kujua’ tafsiri yangu ya kutaka kwako kuona tu basi, soma andiko ilo ilo sehemu nyingine-mfano- Mathayo.23:23 halafu niambie, unaona nini? au nisaidie tu kua ni sawa kirahis tu Mtu kukumba ..Ole wako wewe Mabinza, unakazana kweli kulipa Zaka wakati hujasamehe Mkeo, fanya kwanza AU ulitakiwa/paswa kwanza kushughulika na mapatano na wife kisha endelea na mengine hayo ya ibada-Zaka-si rahisi tu ivyo au? Umeelewa? Jibu tafadhari.

  Kuhusu kama Wanafunzi walitimiliza Haki au la kama nilivyokuuliza, umesema..’’ Biblia haisemi kuwa kutoa zaka ndiyo kunamfanya mtu kuwa katika haki, bali mwenye imani ndiye mwenye haki!- Sawa kabisa Mwenye Imani ndiye mwenye Haki.Sasa Maswali 3 na uwe mwaminifu kuyajibu. Kwanza: Haki hiyo aliyosemea Yesu ktk andiko ilo kama ukisoma context ya hapo ni Haki iyo ya Imani ulosema? Pili: Biblia inasemaje kuhusu Imani bila matendo? Tatu: Je waweza sema una Imani/Haki uliyopewa na BWANA kwanza kwa Neema-si kwa matendo ya sharia halafu BAADA ya imani/Haki yakufanywa Mwana, ukakaa bila kutenda eg Matoleo eg Zaka pia ukisema, ilimradi una Haki kwa Neema, huna haja ya kiutenda?

  Kuhusu Luka.6:38, umesema..’’Zaka haipewi Mtu yeyote tu. Zaka ilitolewa kwa Mungu kwa ajili ya kuendeleza Kazi yake!- Maswali 3 kwako brother…. Moja:Mungu anaichukuaje/tumiaje? Anakujaga live na kuila/tumia iyo?, Pili: Izo kazi za MUNGU zinazotakiwa kuendelezwa kwa zaka KAMA ULIVYOSEMA, zipo leo? Tatu: Kama zipo Zaka inatakiwa haitakiwi? Uwe mwaminifu tu Kaka Mabinza kujibu kila swali. Ukisahau nitakutia moyo kwa kukumbusha! Usijali, niko kwa kazi iyo hapa bro wangu.

  Swali langu nililokutaka unipe andiko nione live kama ulivyotaka nikupe la Zaka live, nilipokuuliza Kama Yesu alioga na kupiga chafya-nipe andiko, umejibu kwa kweli, to be honest, vizuri sana, sana kwa maelezo na maandiko haya-‘Yesu “alijaribiwa kama sisi pia alipoona njaa shetani akaja kumjaribu, wakati mashua inasukwa sukwa na upepo Bwana Yesu alikuwa amelala pia alizaliwa, alikuwa na mwili’’, kwa kutumia haya maandiko, ingawa hujahitimisha nione LIVE-sujui bahati mbaya au nitumie neno lako la ‘tekiniki’ na bila shaka ndio maana Mr. Kaswahili na Sungura na hata sasa Amini Yeremiah hajajibu/wamekwepa mita mia kujibu ilo, nawe umeniachia ni-conclude kua kwa mantiki iyo ya maandiko ulonia basi- Yesu alioga na alipiga chafya, ongeza miayo, kukaa, kusimama, kucheka,kulia, kukasirika, kuchukizwa, kuhuzunika nk-sasa izi ndio wenzio wanaziita ni assumptions/tafakari/ thinking tu bure wakati kwanza ni obvious, pili hazivurugi maandiko, tatu zina mashiko kweli kiasi kwamba mtu kuzipinga, kwakweli awe na capacity ya ajabu, otherwise, atakua weak tu, maana zina nguvu kweli na zimekamata/bana hasa. Ila unajua Mabinza, ingawa tumekubaliana ktk ili, HUKUNIPA ANDIKO WAZI WAZI BADO KUA ALIOGA/CHAFYA!usisahu ako, tehe! anyway, nadhani tumeshakubaliana kwa ilo, kwa iyo kigezo kua hakuna live-live ktk Bible..well, ni tahadhari njema sana kwa Mtu wa Mungu lakini pia haimaniishi sasa kila kitu ni kukataa tu,kugoma weeee

  Umesema…’’Tatizo ninaloliona kwako, unadhani ule “Mwili” ndiyo yule “Yesu” tunayemwabudu! Ule ulikuwa mwili tu kama mwili wangu na wako’’. Kwanza sina tatizo bro kabisaaaaa kwa haya ulosema na uelewa wa maandiko ktk Bible, pili, nifafanulie iyo sentence yako, umeniacha hoi kabisa! Una maanisha nini “Mwili” ndiyo yule “Yesu”? kwani siyo/hakua Yeye? aisee hi kali.

  Umesema‘’Kwakuwa Yesu ndiye Neno lenyewe, yeye ndiye aliyemwacha Musa katika ruhusa ya kuwaruhusu wanaume wawape Taraka wake zao’’ JIBU: SI KWELI HATA KIDOGO! Neno huyo huyo ndiye alisema…’’Musa aliwaruhusu taraka kwa sababu ya mioyo yenu migumu! Naomba usimsingizie Neno Mabinza

  Kusema ukweli, hutalitendea haki swali hili-embu rudia tu kwa amani kusoma majibu yako ulichoandika na swali langu hili -Swali:’’Yesu aliwaambia Wanafunzi wake ktk Mathayo.5:17-19 kua hakuja kuivunja Torati na manabii na ktk Mathayo.23:1-3 kua Waandishi na Mafarisayo wamekaa kwa kiti cha Musa, wayafundishayo Tuyashike na kuyatenda? UPI NI MSINGI WA KUKAMATA ILI TUSILAANIWE SI TU KWA KUFUNDISHA VIBAYA/TOFAUTI BALI HATA KWA KUTOTEKELEZA MATAKWA YAKE?

  Swali hili langu..’’Unadhani Mitume na Manabii wa Kanisa la kwanza, walisimama/jenga ktk Misngi upi? Ukajibu ni Yesu. Sawa kabisa lakini Yesu naye anasema alikuja timiliza ya nyuma pia, sasa Zaka ipo haipo? Maana Zaka ni ya nyuma uko tena ya nyuma kwelikweli kabla ya Musa!

  Swali langu hili tena—‘Kwakua Maagano yanapatana na ingawa huoni ktk Agano moja jambo ambalo linaonekana ktk Agano jingine, je inamaana kwa kutokuliona na wakati umesema yanapata, ni kweli halipo? Na halikufanyika? Umejibu vema sana ivi..’’Tukiangalia Agano la Kale tunauangalia mwili ambao Sheria yake ni matendo na maamrisho ya Torati kwa njia ya matendo ya kimwili. Na tunapoliangalia Agano jipya tunaiangalia Roho, ambayo Sheria yake ni Upendo uliojengwa kwa njia ya Imani!Kwa hiyo, Agano la kale hudhihirisha matendo yetu kwa kusimamiwa na sheria ya Mwilini, wakati Agano Jipya hudhihirisha matendo yetu kwa kusimamiwa na sheria ya Rohoni! Neno ni Roho, tena ni uzima! KWA MAELEZO HAYO MAZURI KAMA NINI, SISI LEO KTK SHERIA YA UPENDO NA UZIMA, TUKITOA ZAKA NA ZAIDI YA ZAKA ni sawa si sawa? Inapendeza, haipendezi? Ni muhimu si muhimu?

  Hakika ukisoma majibu/maelezo yangu yote na kisha Ukijibu Maswali yote Mapya tena kwa uaminifu-halita sahaulika hata swali moja maana nitakukumbusha kwa upendo, basi statement yako hii nzuri..”Ufahamu ni chembe ya uhai” ITATIMIZWA KWAKO, amen.

  Press on.

 118. Kaswahili,

  Angalia point yako hii( zingatia nimeifanyia kazi kweli iwe bora-kwa ilo nibariki tu mfano nime-edit kuondoa full stops kila sehemu, kukosekana kwa herufi kubwa kuna kostahili, kutumia panchuation marks sehemu stahili nk-si unajua unavyoandika wewe, yataka mtu mwenye moyo mpana wa kuwavumilia wenzie kama mie I think e.g. pamoja na uandishi wako wote huu na majina yote ulonibatiza na hata likiko humu la mwisho ktk machango huu la ‘Mtu wa Mirembe-uyo ni mie tu hamna mwingine-hahaha( Sungura-umeona lugha picha iyo kama ya uyanga-simba? na si unaona mie nimeelewa kirahiiiiisi, take my ‘anointing’ brother Sungura) lakini bado nimetoa sadaka ya kuedit maandishi yako very suffocationg indeed Mr. Kiswahili-Ops! Napenda Kiswa.. than Kaswa..sijui why! but I think nakwepa ‘Kaswahili’ kwakua naona uswahili so close kila uchangiapo-tehe!-hii ni ya kufurahisha table talks, hapo na wewe uwe na kifua Kaka, so take it easy! so hiki chako nilichoki-edit hiki- ni moja ya substance so nice nakuta kwa mara ya kwanza naposoma michango yako…Hii hapa‘Yesu anasema: Sikuja kuitangua Torati yaani sikuja kui-nullify au kuikejeli au kwa maana nyingine kuidhihaki au kuitweza kuwa haikuwa lolote wala chochote, bali kuitimiliza. Kwa maneno ya Kiingereza tunasema: To substantiate it au to uncover it to its reality au to bring it to its wholeness au to bring it to its tangibility. Ukiona kivuli pekee cha mtu bila kumwona mtu halisi mwenye kile kivuli yamkini kuna baadhi ya maswali hutoweza kuyajibu. Maswali kama: je, huyo mtu ni light skinned au black skinned? je, rangi yake ya macho yake ni ipi? I am telling you, I love it, Eeeeemen-sasa tatizo lako..sasa ivi utavuruga, ngoja niendelee kujipa moyo kupitia mpaka mwisho pamoja na suffocation iliyoko ktk /unavyoandika

  Umesema tena..’’Yesu alipomwambia Yohana Mbatizaji kuwa-yanipasa kutimiza haki yote. hiyo haki yote ni ipi? bila shaka Seleli atasema hiyo haki yote ni zaka. Seleli amekiri kuwa hajaona popote ktk agano jipya Yesu alitoa zaka. na mimi ndo nasema hizo ndo zinaitwa facts na si assumptions zake’’ Aya tayari kazi imeanza, si unaona umeshavuruga! Nilisema! Kaswahili na Uswahili wake bwanaa, kazi!!!! Ni kweli kabisa hakuna ilo andiko la ‘Naye alipoteremka toka Mlima Mzeituni, akachukua Zaka yake na kuipeleka kwa Kuhani Kayafa na kesho yake akachukua nyingine na kuwapa Maskini’.Ila nikiangalia maisha ya Yesu na wakati alipokua duniani, maneno aliyosema kuhusu Torati, aina ya Watu alikua anaishi kati yao, system za ibada na makanisa( sinagogi) yalikuwepo basi ni kweli nika Assume /dhani/fikiri au niiweke kiroho-roho-ninaamini hata kama hakutoa Yeye live, lakini pia HAKUIPINGA na pia WAKO WALIOMTOLEA YEYE KAMA KUHUNI MWENYE UTUMISHI ULIOHITAJI SUPPORT YA WANADAMU NA MALI/PESA NA VITU VINGINE VYAO. Wewe unasemaje? Assumption yangu hii ina mashiko haina? Pili imekwenda kinyume na kanuni za Neno au la? Aya nakutaka uwe mwaminifu pia kujibu kama vile mimi mki-raise issues nazoona as per my judgement kua ni issue( si lazima iwe sawa sawa na judgement ya Sungura), lazima najibu/tolea ufafanuzi nk kwa furaha ana amani tu.

  Umesema, ‘’eti nasisi tuthibitishe kwenye agano jipya ambapo maandiko yanasema Yesu hakutoa fungu la kumi! very weak!’’ mmmmmh! Acha utani na kuniiga! Eti Very weak! Usikimbie hapo haraka haraka! Nimekuona kabisaaa! Kuna msumari hapo, tafadhari uukabiri kwa uaminifu. Aya Jibu, JE KUNA ANDIKO LIMEWAAMBIENI LIVE IVI…’’Naye Yesu akasema, amini, amini nawaambieni, Matoleo yote mliyotoa wakati wa Musa kama Zaka, Malimbuko, Changizo, hayafai kitu maana Mimi mnionaye Ndiye, Musa aliwaandikia kutoa Zaka kwa kua mioyo yenu ilikua migumu, sasa Mwana amewake huru kweli kweli’’’ lipo ilo andiko? Kama halipo, nini kinakuongoza kusema hatutoi leo? Assumption au Sauti toka JUU? hehehehe! Yaani kama nakuona vile unavyohema/angaika, sijui unamochokaje hapo! Nakungoja sana na ukikwepa tu, nitakarudia-rudia tu somewhere-tehe! halafu utakacho-assume/amini, linganisha na changu pale juu then niambie, kipi kinalipa/mashiko! Yaani una kazi kweli hapa. Si bora tu tutoe na kusisitiza kutoa na kutia moyo kutoa kwa mambo ya Mungu na Watumishi uliowaita kupe kuliko kubana vishilingi ivyo vidogoooooo.!
  Umesema ivi ..‘’ktk luka 11:42 kuhusu hayo mengine. yes, hayo mengine inaweza kuwa ni torati ya Musa na zaka ikiwemo kama alivyosema Seleli. KUMBE SASA UMEELEWA AU? Na umetumia neno INAWEZEKANA( Assumption) NA ZAKA IKAWEMO! Kumbe unaweza fanya assumption yenye mashiko na ambayo haivurugi Neno siyo? Safi. Aisee uko kama Kondoo kama Mbuzi..Yesu kupitia Mchungaji wako uliyemuita kupe, anakazi kukuchunga mpaka ufike JUU Kaswahili

  Umeseme/tuchallenge/jichallenge ivi….’’Tujiulize, Yesu alikuwa ktk harmony na mafarisayo na wanasheria kuhusu mfumo wa imani yao kwa Mungu? na je, mafarisayo na wanasheria walikuwa ktk amani na Yesu? kama siyo, kwa nini? na kama nilivyofafanua kwa mifano hapo juu nikaonesha kwamba ikumbukwe Yesu hakuwa na uadui na torati, make atakuwaje na uadui na kuvuli chake, isipokuwa kama halisi imekuja kwa nini niendelee kuhangaika na kivuli chake? kama Yesu alijua mafarisayo na wanasheria hawaitaki halisi wanataka kuendelea kungangania kivuli chake’’ KWA HIYO KWA UFAHAMU HUU MZURI, KWA NINI TUSITIE MOYO SANA/KUFUNDISHA KWA UJASIRI UTOAJI WA AINA NYINGI TU NA ZAKA IKIWEMO? UNASEMAJE KWA HILI?

  Mwisho, umesema…’’Seleli alitegemea Yesu angewaambiaje? soma wagalatia 3:21-29 na wagalatia 3:1-14. Well done kwa maandiko hayo, so powerfull but ehe! Yanahusiaje na nilichosema maana naona umeni support nilichosema au? Embu show ume differ na mimi wapi kwa maandiko haya mazuri kabisa? Na kama unakubalina name, unakua muungwana tu kusema..NAKUBALIANA NAWE Seleli au hii point safi kama nilivyokuonyesha mfano.

  Press on.

 119. Sungura,
  Umenipa ushauri mzuri kupunguza Code mix/switch, asante ila tena usifanye kama ndio topic hapa kururudia-rudia! nitajitahidi ila isitufunge/isinifunge sana mpaka nikakosa raha. Ni sawa sawa na wewe nikumbie acha kabisa kutumia Kiingereza! Kwa nini sasa wakati Izi zote ni lugha tu wengi wanaelewa? ivyo ruksa kutumia tumia na wakati mwingine code swit/mix ina utamu wake, so take it easy, go to major issues on the table!!!!!! Ingekua Kiarabu hapo kweli ni issue kubwa.

  Natumia ‘’cha uyanga na usimba’’ kama lugha picha kuwakilisha dhana halisi, ili nalo una raise!!!!! We kweli umekua mlalamishi sasa, sijui unazidiwa na nini Kaka? kama kuwataja mbona nimewataja live tu-soma tena comment zangu nyingine! uwe unaelewa mambo madogo, kwa nini mambo madogo unafanya makuuubwa na halafu mambo MAKUBWA KWELI mfano KUTOA TOA ZAKA MPAKA UJISIKIE unafanya issue ndogo! Halafu ujuzi wako ktk Neno unakusaidieje Sungura, umesahau Yesu alipokua anatumia Mifano ya lugha picha/vifaa vya lugha ( Languahe devices) nyingi halafu Watu aidha wenyewe wanapata majibu, wakati mwingine anawafafanulia na wengine anawaacha ivyo ivyo solemba! Ivi una apply vipi wewe Bible Knowledge? si katika maisha ya rohoni na haya kawaida! Aaa bwana, usitake niandike weee kwa vitu vidogo kama ivyo, halafu sijui umesomea chemistry! Sasa mie kama nimesomea Kiswahili/English-Fasihi, unanifanyaje na Yesu kaniweka hapa kanisani akijua alinisomesha( wezesha) kusoma Kiswahili na Kingereza kwa upande wa Fasihi, mnanifanyaje,si ufurahi tu kua na ndugu wa aina yangu kama navyojitahidi kufurahi kua nawe ingawa kwa la zaka bado?

  Kutofautiana ni sawa na ni kweli ninatoa mawazo yangu, ndicho na wewe ufayacho humu, ni sawa katika majadiliano kusema facts, assumptions zenye mashiko na hazivurgi Kanuni za Neno, opinions, mitazamo na Biblical scriptures, mbona ya kawaida tu haya, kwa iyo, unaposema ni mawazo yangu ni sawa, wewe kama hunapinga, hamna shida, pinga tu ila leta ilo wazo/fact/assumption/Bible verser yako against mine, ivyo tu basi. Niliposema ‘Siasa’ kanisani, si kwakua unanipinga! Yaani kwa kweli Sungura naona sijui ukapumzike! Simply ni matumizi ya lugha tena kuwakilisha dhana ya mashindano kanisani kwenu uko si mema ktk kutekeleza maono ya Kanisa au Kuhani wako, mbona rahis iyo nayo. Usilalamike kua sioni mawazo yako ya msingi, soma comments zangu, nimekubaliana na Biblia kisha na wewe kua KUTOA NI HIARI, ILA NIMEONGEZEA PIA NI MUHIMU-kama ungetaka summary ya yoooote niliyosema umu maana Umuhimu huo ndio mmeushambulia mpaka inakua tutoe au tusitoe-kama yalivyo mojawapo ya maneno yako, ati ni sawa tu.

  Kuhusu kua ati‘’nalazimisha kuwa katika misaada ambayo Paulo ailipewa na kanisa ati na zaka ilikuwemo,’’. Nakanusha vikali, sijalamizimisha, ni muono wako-ulivyochukua na kutafsiri! Ni mawazo yangu, ruksa kuyapinga ila kwa hoja ya mashiko ya kiakili, kimaisha, kihuduma au KiBiblia, si tu kusema, haipo! Narudia tena ivi….NINAAMINI/( au nitumie ile usiyopenda-nina –Assume) kwa aina ya Utumishi wa Paul, Wito mkubwa aliokua nao, aina ya Watu aliokua anawalea-yaani wanajua Torati ivyo Zaka wanajua-haikua kitu kigeni, Paul mwenyewe kama Farisayo, bila shaka ktk matolea au kifupi Sadaka alizokusanya/kusanyiwa, na zaka zilikuwepo,Au ktk Wale waliokua wanapenda kutoa kwa ajili yake, naamini kuna wapendwa tena wengi tu na hata watu wa dini tu( akina Kornelio type), waliotoa na zako kwa huduma na maisha yake. Haya nipinge nione hoja/wazo lako na wewe kama lina kilo! Sema sasa hapana kimbia hiyo-Nangoja!

  Hili la mwisho ulosema, sijui umakini wako uko wapi au nawe ni una-utoto ndugu yangu, nilidhani ni mie tu kama usemavyo- umesema ivi’’ Roho mtakatifu alishuka mara moja tu, Unaposema alishuka tena na tena kana kwamba alikuwa anarudi mbinguni na kushuka tena siyo sawa. ‘’Labda kama ungesema aliwajaza tena na tena ningekubaliana na wewe’’ Sasa angalia nilichosema, nime-copy hapa-‘Aliposhuka toka siku ile ya pentekoste Mdo.2:1-4, alishuka tena na tena kwa wale wale na wengine wapya- Mdo.4:31. So, ni kweli tuna muhitaji tena na tena, kwa wapya kumpokea kwa upya na kwa ‘wazee’ kujazwa/kufurikishwa tena na tena na tena. Hiyo ya mwisho hukuiona ya ‘’Wazee’?! au ulinidaka pale kwa intro tu ili kufosi hoja yako mechanically?! Kama point yako haina nguvu, haina tu, aina jinsi Sungura.

  Press on

 120. Siyi nashukuru pia,
  Lakini kina kitu kimoja bado nashindwa kuelewa kwa nini sieleweki sawasawa. Si vizuri kujisifu, lakini niseme tu kwamba ‘I give a lot’. Huwa sipendi mwenye uhitaji apite mbele yangu halaf nisimpe, wakati nina nafasi ya kufanya hivyo. Nashangaa sana hata wewe unaponiambia nimeshikilia msimamo wangu wa roho ya unyimifu wa kutotoa zaka na sadaka.

  Ninachokataa ni kule kutoa zaka au 10% ya pato langu kama sheria,kwamba ukipata hele fulani ati ni lazima utoe 10% yake, na usipofanya hivyo ni dhambi.

  Lakini nashukuru umekuwa muwazi kuhusu jinsi utaratibu ulivyo kwenu wasabato.
  Kibiblia katika aganom jipya hakuna sharti la kwamba wanafanya huduma hawaruhusiwi kufanya na kitu kingine. Ndio maana Paulo alikuwa anafanya shughuli zingine za mikono.

  Si dhambi pia mtu kuamua kufanya huduma ya madhabahu tu. Lakini haina maana kuwa huyo mtu hana urithi mwingine. Anaweza kuwa na mashamba, mifugo , nyumba n.k ambavyo ni urithi toka kwa wazazi wake. Tofauti kabisa na utaratibu wa ukuhani wa wana wa Lawi,wao hawakuwa na hawakuruhusiwa kuwa na chochote zaidi ya zaka.

  Lakini Siyi, hata kama kuna madhehebu ambayo yana utaratibu wa kwamba watumishi wake lazima wawe full time kwenye huduma, sadaka za hiari zinatosha kabisa kuwafanya waishi. Zaka inaweza kuwa ndogo sana ukilinganisha na sadaka zingine za kawaida. Maana kama kuna utaratibu kwamba waishi kwa zaka tu bila kugusa sadaka,basi kwa watu wanaojua kutoa sadaka huwa ni nyingi zaidi kutoka kwenye kipato chao kuliko zaka.

  Unaposema ‘free will’ maana yake ni kwamba kufanya au kutofanya yote ni sawa, hakuna hatia. Lakini kama kitu ni lazima kifanyike hapo hakuna free will, kuna nafasi moja tu, au ukifanye uhesabiwe haki au usikifanye uhesabiwe dhambi.

  Kwa mfano hakuna uhuru kwenye kuzini, yenyewe ni ‘one way traffic’ kwamba ukiiba umetenda dhambi, kwa hiyo ‘option’ pekee iliyopo ili uende sawa na Mungu ni utoiba.

  Njia ya kumtolea Mungu si zaka pekee yake, ziko nyingi tu.
  Siyi kwani anayetoa zaka elfu 20 kutoka kwenye laki mbili na anayetoa sadaka elfu ishirini kutoka kwenye laki mbili tofauti ni nini mbele za Mungu.

  Asante Siyi!

 121. Sungura,
  Kimsingi nakushukuru rafiki kwa hoja zako nzuri(majibu yako). Nimejaribu kusoma na mawazo mengi ya watu kwenye mjadala huu, lakini inaonekana kuwa, wewe umeshikilia msimamo wako tu ya roho ya unyimifu. Kutotoa zaka (na sadaka), hadi uguswe kufanya hivyo.

  Kimsingi, dini(tendo) iliyobora mbele za Mungu siyo kile kitendo cha kutoa, bali ni ule msukumo wa kutenda kutoka moyoni mwa mtu. Hicho ndicho Mungu huangalia. Lakini ikumbukwe kwamba, Mungu ametoa sheria zake na kuziandika mioyoni mwa watu wake. Sheria zilizojengwa kwenye msingi wa upendo. Na katika huo upendo, sheria zote hutimilika-rumi 10:13.
  Nijuavyo mimi, kwetu bado kuna hao makuhani pamoja na kwamba, sisi sote ni ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa miliki ya Mungu 1 Petro 2:9 Makuhani hawa(wachungaji) wako full time kwenye huduma na hawaruhusiwi kujishughulisha na kazi yoyote isipokuwa huduma hiyo tu. Hivyo ni halali kutoa zaka hiyo kwa wasabato(huu ni uelewa wangu, labda kama sielewi vyema watu wengine-wasabato wanisaidie). Hivyo bwana Sungura, kama kwenu(kanisani) wachungaji wana lukusa ya kujiishughulisha na miradi mingine zaidi ya huduma, waweza (japo sidhani kama ni sahihi) kujenga hoja hizo.
  Hivyo, kutoa zaka, sadaka kwa wasabato, ni tendo la kuonesha upendo kwa Mungu(utii wa sheria bila shurti), maana Mungu ametupa free will ya kumwabudu. Kadhalika, tuna uhuru wa kumwabudu Mungu hata katika matoleo ya zaka na sadaka. Kutoa ni ibada.

  Ubarikiwe ndg yangu

 122. Sungura,

  Hapana ogopa kuassume, siyo Assumptions zote mbaya au hazifai, ili mradi ziko na agreement na Neno, hazivurugi kanuni za Neno, na pia zikipimika ktk facts za maisha ya kawaida, zikatiki, basi zafaa tu hamna shida. Nimekuuliza Yesu alioga/chafya-Jibu hapo! halafu nipe andiko! Ila kwa ishu ya akina Paul, kweli kuna haja ya kuchukua muda kwa hili Mr.Sungura? ina umuhimu huo kweli ktk discussion hii? What was my MAJOR point in a nomal judgment?NI KUWAACHA WENZIE KTK KAZI/AGREEMENT/JAMBO LILE KWALO WALILOSHIKA /KUBALIANA NA HATA KUONDOKA PAMOJA KWA ILO AU neno home? Yaani ktk msisitizo wangu wote wa mfano huo umechukua home na si kuacha kazi/jambo la pamoja? -Kama ni Jerusalme au Antiok, Judea, jamani si alikwenda to anapokaa/walipokua wanaishi, sasa kumbe alikwenda wapi? Uko Jesusalem alikua mkimbizi! Mbona iki kitu very simple au?

  Aisee! Unanitia majaribuni brother kuandika kwa urefu, ngoja nijizuie tu kwa kuandika ktk bullets. Kwa mazingira haya, labda nitumie neno la kiroho-roho kua nina amini( nikisema nina assume-unaona kama haina nyama sana wakati unaweza assume kitu safi tu alimradi hakivurugi ya msingi/kanuni za Neno).So nina amini, alipowaacha wenziwe, ofcoz alikwenda HOME si kwenye mti au godauni!.Embu pia angalia mlolongo huu wa Mr. Mark John ktk maandiko haya.

  • Mdo. 11:25-26= Barnaba anamtafuta Saul na kumleta Antiock

  • Mdo. 11:27-30=Wanakuja Manabii toka Yerusalem to Antiokia,mmoja wapo akatoa unabii kuhusu Njaa kuikumba Nchi

  • Mdo.11:29-30 Wanafunzi wakatuma msaada kwa ndugu wa Yudea

  • Mdo.11:30= Wakatuma pia kwa wazee kwa mkono wa Barnada na Saul

  • Mdo.12:1-2: Herod Mfalme akamchinja Yakobo na kumtia gerezani Petro

  • Mdo.12:3-10: Kanisa linamuombea sana Peter kisha Malaika anamuokoa na kumtoa gerezani, then Peter kama haamini vile but akafunguka na kuelewa kisha…. (Angalia andiko linalofuata kwa macho yote)

  • Mdo.12:12:Peter akaja ktk nyumba ya Mariamu mama yake Mark John

  • Mdo.13:1-3: Roho Mtakatifu anasema wamtengee Barnaba na Saul

  • Mdo.13:5:Pia walikua na John Mark kama msaidizi wao.Notice: Alikua msaidizi wao manake alikua muhimu kweli kwao na walimuhitaji kwelikweli

  • Mdo.13:13:Hapa sasa ndio John Mark akatibua mambo, imendikwa- John akaondoka kurudi Jerusalem( wapi sasa ndani ya Jerusalme, kwenye mti? Ofcoz Home kwao au kwake, sidhani kama alikua ana shinda kanisani saa zote

  • Mdo.15:36-38: Kunatokea ushindani kati ya Paul na Barnaba na Paul anasema waziwazi kabisa mstari wa 38 kua/tena imeandikwa Paul akasisitiza kua ‘’haifai kumchukua mtu ALIYEWAACHA NA HAKWENDA NAO KTK KAZI/HUDUMA!!!!!!!!!!!

  • Mdo.15:39-40: Wapendwa wakagawanyika seriously kwa kua Bibilia inasema contention( synonyms ya Contention ni dispute, disagreement, arguement, debate, strife, controversy) become so sharp that they parted from one another( si unaona wapendwa wanaojali mambo yao binafsi mpaka hata kuwaacha wenzao kazini, wanavyoweza leta shida ktk lengo Moja? Si unaona? Mpaka kusababisha Magiants wale wa Utumishi kushindana!

  Saa ujibu mwenyewe, kama Paul aliyekua naye anasema jamaa aliwaacha kwa kazi, kujenga hoja( na wewe naona ume assume pia-well done bro, kuwa inawezekana alienda home kwa sababu binafsi-well fine BUT aliwaacha kazini is the fact-ambacho unapenda iko wazi hapo na kwakua halikua jambo jema, Pau is not stupid kukasirikia jambo lile. Kwamba why Barnaba alimchukua? ungetoa jibu wewe maana hutaki kabisa watu wa-assume! Wakati kama nilivyosema strongly pale juu, assumptions nyingine si mbaya, ni karibu na kweli au ni kweli kabisa kama vile Yesu alioga na hakika alipiga chafya hata kama hakuna maandiko. Kwa iyo kwakua umeniuliza why Barnaba alimchukua basi naamini/na ili uanze kuzoea ku-assume si pepo, naacha kutumia-‘naamini’ na nasema nina assume alimchukua kwa kua toka mwanzo, Barnaba anaonekana ni mtu wa tabia ya reconcile mambo ktk Bible. Ndiye aliyemkingia kifua Paul alipotoka tu U-Saul ili kukubalika kanisani, no wonder huduma yake iyo iliendelea. Sasa huu ni ukweli ktk Bible na ningepaswa kusema moja kwa moja ila nimetumia nina assume kwa kua wewe unayependa so called facts hata katika maeneo ambayo yako obvious kujua kinacho na kilochoweza kutokea/endelea, unaweza uliza ..’Wapi pameandikwa kua alifanya ivyo kwa sababu ni huduma yake! Si mnaona mambo yenu? Halafu mtu akiandika sana ili kuweka so clear issues, oohhh! Unaandika sana! Sasa nifanyejie wakati una raise issues na unataka kujua au umenichallenge ili nitoe ufafanuzi?

  Ati Paul ndio aliyegeuka na kisha kumsifu yeye aliyewaacha job! Du! Pima mwenyewe situ ufunuo unakataa bali hata akili ya kawaida ile kabisaa ambayo hata haijafunguliwa/vuviwa itakucheka! Yaani Mtu (Paul) kakupa live kua aliwaacha kwa job mpaka wakawa na kudebate mbaya na brother Barnaba kisha useme( assume kua Paul ndio aligeuka! Assumption hii haina mashiko, na nakushauri basi , uache assumption naona huwezi fanya tangible and very strong assumptions ambazo kuzikana kazi kweli na unajua ilo bro kama vipi jaribu kukana zote nilizo share humu kwa hoja au assumptions nyingine strong zako, nitafurahi kujifunza pia.

  Nadhani inatosha, mambo mengine ya kuendelea kusema siko makini, niyache tu kwakua umakini haujifichagi,na kwakweli uwe huru sana, wala sijisikia vibaya ukinimbia ivyo hata kidogo, nadhani ninavyojibu ndio unawaza ivyo kumbe mie waaala nina amani na nina enjooooooy, I wish ungenifahamu, sina tabu kabisa kuitwa majina yote toka ya mwanzo mlioyoniita mpaka la mwisho la Brother Kaswahili kua mi wa Mirembe-soma comments zake.So be blessed all na plz don’t make excuses kua una wasiwasi sikuelew!mmmh! kuna kiarabu umu nisikuelewa!, hamna issue bro so huge from your side nishindwe kuilewa, umenisingizi tu jingine hilo na laiti ungejua kwa nini siku ya kwanza kabisa ulipojibu my UTOAJI IN GENERAL subject nilikuambia statement hii..’’Sungura Mtu kama amevaa Suruali na ukamwambia amevaa kaputura, nani ana tatizo kubwa? Unakumbuka? Kama ungevuta subiri ukatafakari iyo caution-ingekuoa na mengi-you know (well, ok you can assume) what I mean exactly. Notice: Nimekuuliza/na mimi nimeraise maswali mengi sana kwako, uwe mwaminifu kunijibu each kama mimi nisivyoacha kitu mkiniuliza au kuraise jambo. Aya nakusubiri kwa hamu kabla sijakuletea suggestion ya ku-conclude mada hili vema kabisa.

  Press on.

 123. Sungura,

  Ni kweli ni hiari na Idumu iyo na Hakuna aliyesema kua ni lazima kulipa Zaka. Hiki ki-notion cha KUA TUSITOE KWA LAZIMA jinsi kilivyokua over-highlighted ktk comments zenu nyingi na kikajengewa misingi mpaka kuwaona Watumishi kama Walaji tu na kupe( Refer Kaswahiz beyond repair comments), msomaji asiye makini/mchanga atatoka na ujumbe negative badala ya positive wa KUTOA iyo Zaka. Kwa nini mtu asiweke much msisitizo kwa UMUHIMU WA KUTOA KWA BWANA NA KAZI YAKE badala yake kila akichangia, hata kama atagusa Hiari na kuonekana anatoa bado atapollute tu at last or in the middle directly or indirectly! Nini iyo inayomsukuma mtu kujenga weee negative kama siyo roho nyingine kwa kujua au kutojua, ubinafsi, unyimivu,kutafuta kwanza ufalme wa Dunia at the expense of God’s Kingdom.

  Eti waga tunalazimishwa uko makanisani! ivi kweli mimi na pesa yangu, kuna kiumbe anaweza nilazimisha au ni kuweka mambo chumvi kutimiliza matakwa ya nafsi mbovu tu? Moyo kama mbaya mbaya tu ktk Utoaji, hakuna kulazimishwa wala nini-tena kwa mtu blessed and by grace thinker angejiuliza mpaka mlazimishwe kama kupo kweli uko kwenu-unadhani tatizo ni nini/nani? Walazimishaji au walazimishwaji? Think about that kisha jijibu mwenywe na nafsi yako kwa uaminifu mbele za Bwana. Ukiniuliza jibu, nitakuambia mara moja bila kuongoja Ufunuo nalo ni-kama kuna kulazimishwa, conclusion ya research iyo itakua- uko kulazimishwa ni udhihirisho wa even a deeper problem Kiroho kwa Washirika hao.Bwana Yesu aliwajibu wale kua Musa aliwaruhusu kuwaandikia taraka na kisha kuwatimua wake zao kwa SABABU YA MIOYO YENU MIGUMU/MIBOVU-so tatizo halikua kuingiza system mpya as such( taraka) na kutimua wake bali kitu kingine kabisaaa.Marco.10:4-5. Kumbe yawezekana Kanisa fulani likaweka system fulani tu yaku- follow up au kama reminder/kuwashitua tu wapendwa kipendwa-pendwa, kwa upendo sio kijeshi( hali mbaya ya ubabe na mabavu inayojengwa na commentz zenu), kwa kua tu Watu migomo Jan-Deb kanisani hapo na mambo hayakwendi na kama ni ivyo basi izo sytems(taraka)zidumu! Ooh Yes, si mnawagomea / vuruga/changanya akina Musa wenu.

  Labda nikuambie ukweli, hicho haswaa ndicho kimenifanya kuingia debate hii-icho kiinjection kua Watu wanalazimishwa as if hii ni ALL TZ/WORLD CHURCH problem. Kiinjection icho ni kama kidogo lakini imagine kiwafikie Waamuni wote makanisa yote au kukawa na washirika, Wazee wa Kanisa, Mashemasi wa ivyo, embu niambie hali ya kanisa capacity yake financially ya kufanya kazi? vipi na washirika wachanga ambao ndio kwanza wanaingia kanisani na ule moyo woooote mkubwa wa kuokoka na kupenda mambo yoote ya Mungu, ile hali bora kabisa tunayokuwaga nayo mara tu tunampomuonja Yesu kabla ya KUKOMAA NA KUPITILIZIA kama baadhi yenu humu, I hope tunavyoendelea na talks hapa, kama wewe ni mmoja wapo, huu ni muda wa kupona once for all, say amen.

  Msimamo wako uliosema peupe, ni mzuri kwa maana ya sadaka but umenishangaza kweli! kua waga hutengi Kikumi!!!!! Lakini tayari ulishasema kua unatoa Zaka in one of your comments, so uliposema unatowaga Zaka, unaitoaje? embu DEFINE ZAKA/TITHE?-Google tu hapo! Si ulisema unatoa ZAKA kwa hiari, zaka ipi ambayo si from ‘tenth of…. na kuendelea?..ajabu kabisa, una mambo mengi sana Sungura, ngoja niendelee kujifunza/kushangaa. Na kwamba unatoa Zaka kokote kule! Aisee! Imagine Washirika wote kanisani kwako/kwa kuhani wako/wenu, mna misimamo iyo, mnafanyaje maisha ya huyu Mtumishi? Family yake, vipi kuendesha seminar hapo? Wanao safisha msalato na mabenchi kanisani na walinzi Jan-Dec, wanaishije na wakati wanakufanyia wewe huduma? Vipi crusade itafanyikaje? Kwa sadaka tu za kawaida za kila mtu mpaka atakapojisikia? Ajabu kabisa, kabisa! Na labda fafanua, mpaka utakapojisikia maana yake ndio Hiari au feelings/emotions? Na Je tunaongozwa na Neno au mahisia yetu? Vipi kanisani hapa ikatokea wote au half hamjisikii tu kutoa chochote acha tu Zaka bali hata sadaka ya kila siku j2! Ni sawa Watu waje nyumbani wa Bwana mikono mitupu? Ivi ilo ni kanisa gani on serious note la Watu kujisikia ndio Watende hata ktk mambo ambayo Bible imewataka straight kutenda unajisikia hujisikii? Au hii kujisikia tunaiapply tu inapo gusa noti zetu siyo? Ajabu jamani, mwe! Kujisikia is the base! Na je ukiona Uhitaji kwa Kuhani/kanisa lako lakini hujisikii na ela au gunia la mahindi unalo, unafanyaje kuvuja Kujisikia ili utende tendo?

  Umesema’’Watumishi wanaosoma kitabu cha Malaki.3 kusema ”kama kuna mtu huwa hutoi zaka wewe ni mwizi, unamwibia Mungu”, hukubaliani nao- Kwani wamesoma kitabu cha nani icho? Ati umesema ‘’wakati huyo anayeambiwa hayo ametoa sadaka yake na na michango mingine, sasa Pastor atakujuaje? Unataka kusema anasoma majina mnapotoa mfano iyo sadaka ya kawaida/kila siku hua anawaona na kuchungulia kama Yesu? Au to be fair, ahubirije ilo andiko maana kweli siku zote watakuwepo waliotoa kwa namna ulivyosema? Sasa Pastor asemeje/ ahubirije jamani? awaandikishe majina na sadaka mnayotoa ili akisimama, awe careful kutowakwaza? Huyo Mchungaji kwa kweli ana kazi ktk uso wa Nchi. Kama ni mie , nitakwenda kimwili nanyi mpaka mtanitambua au nalizaini, huwezi kunisumbua wakati kila mtu anataka kwenda mbinguni,mwishowe nikose bure kama greatest Pastor Mr. Moses kwa maana ya Kanani-Hesabu.20:1-12

  Inaendelea……………………………

 124. Mtoto wa Mungu Seleli,

  Nimekuelewa vizuri, ila Maswali yako ni mengi, na ya ‘kitekniki’ na yenye ujuzi, labda kuchelewa naomba nikujibu hivi, ninachohitaji ni kujua ukweli wa zaka katika nyakati zetu. Nimeyapenda maulizo yako, nami nitayajibu kama ifuatavyo, ila yaliyojirudia nitayajibu kwa fungu moja. Umeuliza,

  SWALI: Je kivuli cha Zaka iliyoanza Agano la Kale ni kipi leo Agano jipya? Mfano: Ibrahimu Alitoa zaka Agano la kale, leo kivuli chake cha rohoni ni nini?

  Swali lako lingine linalofanana na hilo ni:-
  SWALI:
  (a) Ndani ya haki zote ambayo Yesu lisema twapaswa kuitimiza zaka imo haimo?

  JIBU: Maswali hayo mawili ndiyo niliyowauliza ninyi, tena unayarudisha kwangu? Nimeuliza kuwa, Zaka iliyotumika katikaTorati imesimama wapi katika Agano jipya? Wewe ndiye uliyepaswa kunijibu kuwa Mstari huu hapa, mabinza soma, imo! Lakini ukiniuliza mimi, aaa mkubwa, mimi sijui.
  Ni kweli kuwa Torati ni kivuli cha mambo ya Rohoni, tunajua kivuli ni ‘Kopi’ Je, ‘orijino’ ikiletwa ‘kopi’ itasimamia hoja tena? Orijino ndiye Yesu kwakuwa Biblia inasema yeye ndiye hilo Neno la Mungu. Kwakuwa ‘orijino’ ipo inapaswa hoja hiyo ya Zaka isimame pahala Fulani kwa uwazi, inapaswa tuione na katika hii ‘orijino’ Maana Biblia ni kamili. Kama ‘Orijino’alikuja kuitimiliza hiyo ‘Kopi’ na hakuifundisha hiyo zaka, labda sasa inapaswa tusiijadili, maana kumbe haipo, labda ilishia pale alipoacha kuifundisha! Sasa ili nielewe nionyesheni hiyo Zaka ipo wapi katika Agano jipya, mimi sibishani nataka tu niione, basi!

  Umeendelea kuuliza,
  SWALI: Umesema Yesu kwa majibu yake alikubaliana nayo lakini humuoni akioa Zaka, je kwakuwa humuoni ndiyo alikataa/hakutoa wakati unajua na andiko linaonyesha na unasema alikubaliana nalo?

  JIBU: Yesu ni Mungu, lakini kumbuka alipolipa kodi ilitajwa waziwazi, na ukiangalia katika Agano la kale, Neno linasema “samweli, hawakukukataa wewe, wamenikataa mimi, acha wapate huyo mfalme wamtakaye, naye atawatoza kodi…” unaona kitu kipo kote wazi wazi, pia imesemwa ‘cha kaisari mpe kaisari na cha Mungu mpe Mungu’, tunajua cha Mungu ni Ibaada, kodi tunatoa serikalini na Ibaada tunafanya kwa Mungu!

  Swali ulilouliza ni sawa na lile swali aliloulizwa Yesu na wale watu waliotaka kujua juu ya Sheria ya ndoa na Taraka. Yesu aliwajibu kuwa “Musa aliruhusu hilo kwa sababu ya kutofundishika kwenu (Shingo ngumu), lakini mwanzo haikuwa hivyo Mke mmoja kwa Mume mmoja”. Kuniuliza kuwa alikubali mbona nashangaa kutomuona akitoa, angalia andiko hilo!

  Umeniambia, “Umesema- licha ya kunukuliwa akimwambia Yohana mbatizaji kwamba, tunapaswa kuitekeleza haki yote”

  SWALI:
  (b)Naukimfuatilia Yesu kila aliposema kuhusu haki eg.Haki yenu isipozidi ya Mafarisayo, KAMWE HAMTAINGIA UFALME, unadhani kati ya haki hizo za mafarisayo ambazo Yesu alitu challenge nazo kuwazidi, ulipaji/utoaji wa zaka umo au la? Kwa maneno mengine walikuwa wanatoa hawatoi?

  JIBU: Mafarisayo walitoa zaka kwa mjibu wa Torati haijaelezwa kama Yesu alisema waendelee kutoa ama la! Ila Yesu katika Lk. 11:42, jibu analitoa mwenyewe kuwa, “Ole wao mafarisayo kwakuwa walipuuza haki na upendo wa Mungu, na kutoa tu zaka za mbogamboga. ‘ILIWAPASA’ kutoa matoleo hayo, wala ‘WASISAHAU’ kufanya hayo mengine”

  Ukitulia, utajua kuwa sentesi ‘ILIWAPASA’ inazungumzia ‘Pasti tensi’ (wakati uliopita). Na ‘MSISAHAU’ inazungumzia ‘Presenti contuasi tensi’ (kitenzi cha wakati unaoendelea) Sentesi hizo mbili zipo wazi na zinafafanua wazi kuwa kunajambo endelevu na kunajambo lililokoma kwa namna walivyokuwa wakilitekeleza halikupaswa kuendelea hivyo,yote yamo katika habari moja ileile, ingawa watendaji wake hawana habari juu ya kipi kidumishwe!

  Labda kama sentesi ingali sema hivi “42Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuza haki na upendo wa Mungu. ‘INAWAPASA’ (badala ya “ILIWAPASA”) kutoa matoleo hayo, wala ‘MSISAHAU’ kufanya hayo mengine.” Hapo ningejua kuwa mstari huo unazungumzia mambo mawili yanayotakiwa yaende sambamba wakati wote katika maisha yote ya Mkristo! Nipe tu mstari Seleli, ‘nipone’ wapi zaka Agano jipya linahimiza?

  UMEULIZA: Je mitume walitii Maneno ya Yesu kuhusu kuitimiliza haki yote au kutenda kuzidi haki za Mafarisayo?

  JIBU: Ndiyo, lakini si Mitume wote. Biblia inasema, “Kwakuamini mtu hupata haki”, na kuamini huko ni juu ya Neno la Mungu alilonena kwa wakati. Wale waliodumu katika kumwamini Yesu hao ndiyo walioitimiliza haki yote, lakini Biblia haisemi kuwa kutoa zaka ndiyo kunamfanya mtu kuwa katika haki, bali mwenye imani ndiye mwenye haki!

  Kuhusiana na hiyo ’Luka.6:38, umeiona inazungumzia vitu vya kupeana, nami nakubaliana na hilo, licha ya wewe pia kuona kuwa mstari huo hauzungumzii zaka, umezidi kuuliza hivi,

  SWALI:
  (a)Umejuaje ivyo vitu vya kupeana/kuwapa Watu hakuna Zaka?
  (b)Kwani ivyo vitu ni nini?
  (c)e zaka haiwezi kua kitu cha kupeana?

  JIBU: Swali (a) na (c) yanafanana, nakujibu kwa pamoj kuwa, vitu hivyo siyo Zaka, zaka iliagizwa itolewe kwa Mungu. Zaka haipewi Mtu yeyote tu. Zaka ilitolewa kwa Mungu kwa ajili ya kuendeleza Kazi yake!

  (b) Vitu hivyo ni matoleo na ama misaada na machangizo.

  Umeendelea kuninukuu, nilipotaka kujua iwapo Mitume nao waliwahi kutoa zaka wakati wakiwa na Yesu na hata baada ya Yesu kupaa mbinguni, umenijibu kwa kusema, “Nimeshakuuliza kama Mitume walitimiliza haki yote na chini hapa swali ni…” na ukaniuliza hivi,

  (a)Bwana Yesu aliwahi kuoga maji bafuni, Kupiga chafya na miayo? nipe andiko?

  b)Na kama unajua kwa HAKIKI alioga/chafya? nini icho kinakufanya/ au umefiaje (nadhani ulimaanisha ‘umefikiaje’) maamuzi hayo/kuchukua uelewa huo kua kwa hakika alioga na kuchafya hata kama ndani ya BIBLE hakipo live love (nadhani ulimaanisha ‘Live’) neno kwa neno?

  JIBU: Maswali yote yanafanana, najibu hivi, Biblia inasema, (Yesu) “alijaribiwa kama sisi. Neno linaendelea kusema, naye alipoona njaa shetani akaja kumjaribu, si hivyo tu Neno pia linasema, wakati mashua inasukwa sukwa na upepo Bwana Yesu alikuwa amelala na zaidi sana Neno linasema, alizaliwa, alikuwa na mwili, na alijaribiwa kama sisi….”

  Tatizo ninaloliona kwako, unadhani ule “Mwili” ndiyo yule “Yesu” tunayemwabudu! Ule ulikuwa mwili tu kama mwili wangu na wako, tabia na sifa za kimaumbile zilikuwa zile zile za Mtu, naam, ni Mtu aliyepata kuishi kama mwanadamu yeyote Yule! Kama yesu angalipungua katika sifa za maumbile, basi, matatizo mawili yangetokea na moja la tatu, moja, angekuwa KILEMA. Pili, shetani angechukua “Advanteji” kwamba , Mungu alimleta “Sadaka” asiye ‘Stahili’ na shetani kwa kushindwa kwake angetafuta visingizio, ambavyo vingeonekana ni kweli kwetu na kwa malaika! Na tatu, Mungu angeonekana si “Mwenye haki” ametumia hila katika vita vya kuziharibu kazi zake shetani; Ametumia ujaja kinyume na ahadi yake kuwa ni mkweli, ni wahaki na ni mwema! Kwa hiyo shetani angetumia hiyo kama “Nafasi” kwetu kwa kutuambia “ukweli” kuwa Yesu hakujaribiwa kama ninyi, maana hakuzaliwa kama ninyi, ndiyo maana alishinda majaribu, ninyi HAMUWEZI, nasi kwa kuliona hilo tungesema “Yesi” shetani mkweli, na hapo shetani angeshinda! Mungu kwa kuliona hilo akaja Mtu kweli, Adamu kama wa mwanza, ila Adamu huyu wa pili aliyashinda ‘Mauti’!

  Maswali yako mengine yametokana na mimi kusisitiza kuwa, Neno tulilo limesimama kwa misingi ya mitume na Manabii, ndipo ulipouliza kama ifuatavyo:-

  Swali:
  (a) Yesu aliwaambia Wanafunzi wake ktk Mathayo.5:17-19 kua hakuja kuivunja Torati na manabii na ktk Mathayo.23:1-3 kua Waandishi na Mafarisayo wamekaa kwa kiti cha Musa, wayafundishayo Tuyashike na kuyatenda? UPI NI MSINGI WA KUKAMATA ILI TUSILAANIWE SI TU KWA KUFUNDISHA VIBAYA/TOFAUTI BALI HATA KWA KUTOTEKELEZA MATAKWA YAKE?

  JIBU: Biblia nilikwisha kukwambia kuwa ni Toshelevu. Biblia ipo ikiwa Jawabu kwa wakati uliopita, uliopo na ujao. Biblia inasema Mungu ni wa mipango na Malengo, hivyo husimamia na kuzingatia “NYAKATI”, Biblia inasema na kwa utimilifu wa wakati Kristo alizaliwa. Kwa hiyo kila jambo liko kwa wakati wake kwa makusudi ya Mungu. Agano la kale ni kivuli cha Agano Jipya ambalo sheria zake ni za mwilini. Kwakuwa Yesu ndiye Neno lenyewe, yeye ndiye aliyemwacha Musa katika ruhusa ya kuwaruhusu wanaume wawape Taraka wake zao, lakini ndiye huyohuyo alikuja kuliweka sawa hilo kuwa, watu wasifanye hivyo kwakuwa mwanzo haikuwa hivyo, kwa nini? Kwa sababu wakati wa watu kulijurishwa jambo hilo ulikuwa umefika, mtu awe wa kiroho kama ilivyokusudiwa tangu mwanzo – Asife!

  Kuna makatazo mwanzo wa wakati fulani, lakini ikakubaliwa mwisho wa wakati fulani. Mwanzo iliruhusiwa kula Matunda, ukaja wakati ikaruhusiwa kula majani ya kondeni, ukafika wakati ikaruhusiwa kula aina fulani tu ya wanyama na hatimaye ukafika wakati, tunaambiwa tule vyote tena bila hata kuulizauliza!

  Pia kuna makubalio mwanzo wa wakati fulani na kuna makatazo mwisho wa wakati fulani. Mwanzo ilikubaliwa kutoa taraka lakini ikafika wakati ikakatazwa kutao taraka! . Hilo jambo Zaka, namna inavyotolewa, unaweza ukawa unilazimisha iwe, kumbe si wakati wake kuwa, ama unaweza kuliondoa kumbe si wakati wake kuondolewa. Ndiyo maana tuliangalie wote tuone linafanyika kimafunuo tu ama kiujuzijuzi wa kibinadamu tu! “LIPO NENO LA WAKATI; SI WAKATI WA KILA NENO!”

  (b) na unadhani Mitume na Manabii wa Kanisa la kwanza, walisimama/jenga ktk Misngi gani? wa kwao kwao, kivyao yao tu au kuna source? ipi?

  JIBU: Msingi ni Kristo Yesu.

  (c) iyo source itakua ni Yesu aliyesema hakuja kutengua Torati bali kuitimiliza ktk utimilizaji aliouonyesha mwenyewe ktk Mathayo sura zote za 5,6,7-Hotuba yote ya Mlimani akipangua kubaki/kutenda kwa motives na matakwa ya dini/imani/taratibu mfu bali kuzihuisha zile tu zisizopinga kweli alizokuja nazo/onyesha na kwamba jamaa wale(Mafarisayo) kuna vitu wanafundisha kwa kua wana kaa ktk kiti cha Musa au kuna source nyingine?

  JIBU: Chanzo cha kila Neno ni Mungu, Mungu ndiye Yesu na huyo Yesu ndiye Neno la Mungu. Ukamilifu wa hilo Neno la Mungu ni UPENDO, na Mungu ndiye PENDO! Lakini Neno la Mungu limesimama juu ya ‘NYAKATI’ kwa Imani. Biblia inasema “si Kazi yenu kuujua wakati ulio katika mamlaka ya Mungu.” Kwa hiyo upo wakati wa kusema, na wakunyamaza….!

  Nilipozungumzia ukamilifu wa Neno la Mungu, wewe ukaniuliza hivi,

  SWALI:Kwakua Maagano yanapatana na ingawa huoni ktk Agano moja jambo ambalo linaonekana ktk Agano jingine, je inamaana kwa kutokuliona na wakati umesema yanapata, ni kweli halipo? Na halikufanyika?

  JIBU: Ukweli ni kwamba, mtu akiomba kazi au labda akataka kujiunga na kozi fulani, katika barua yake ya Maombi, huambatanisha KIVULI cha cheti chake, lakini unapofika wakati wa usaili na au wakati wa kupewa ‘Rejistrasheni’ hapo ni wakati wa mwombaji kuleta cheti HALISI; Kwanini? Kuthibitisha uhalisi wa taarifa alizotoa awali, wakati wa maombi!

  Kristo alisema, nilikuja kuitimiliza sheria yangu, kulihakiki Neno langu na kulithibitisha. Kwa namna gani? Ni kwa kuja na Agano lenye Torati halisi. Tukiangalia Agano la Kale tunauangalia mwili ambao Sheria yake ni matendo na maamrisho ya Torati kwa njia ya matendo ya kimwili. Na tunapoliangalia Agano jipya tunaiangalia Roho, ambayo Sheria yake ni Upendo uliojengwa kwa njia ya Imani!

  Kwa hiyo, Agano la kale hudhihirisha matendo yetu kwa kusimamiwa na sheria ya Mwilini, wakati Agano Jipya hudhihirisha matendo yetu kwa kusimamiwa na sheria ya Rohoni! Neno ni Roho, tena ni uzima!

  ”Ufahamu ni chembe ya uhai”

 125. Wapendwa katika jina kuu la Yesu kristo mwokozi wetu.
  Salaamu
  Nimekuwa mpotevu katika mijadala hii kwa muda mrefu kiasi ambacho nimejikuta mgeni waktati mwingine.
  Mpendwa Seleli nimelazimika kujitokeza tena kushughulika na namna ulivyojaribu kujibu hoja nilizoleta kwakos wiki kadhaa zilizopita.
  Hata hivyo niseme wazi kuwa umekwepa UKWELI WA KIMAANDIKO katika kusoma na kuelewa maandiko niliyokupa uyasome na kuyatafakari.
  Ili kupata ukweli wa kile ninachokisema kuwa mafundisho ya ZAKA ni potofu napenda niyaweke hapa maandiko ya Kumb 14:21-28 ili tuone kama ulichokijibu kina ukweli wowote.
  ‘Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
  Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
  Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
  Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;
  ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;
  na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
  na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
  Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;
  na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo. ‘
  Biblia ni kitabu ambacho hakipingani na kina majibu yote ya imani. unaposoma mstari ule wa 22 ndipo unaona agizo la kutoa ZAKA YA FUNGU LA KUMI na kisha yanafuatia maelezo yanayomuagiza mtoaji NAWE UTAKULA MBELE ZA BWANA MUNGU WAKO,ZAKA YA ………..
  Biblia mpaka hapa haitaji ZAKA KUKABIDHIWA KWA KUHANI kama yalivyo matoleo ya Malimbuko ambayo yanamwagiza mtoaji asile mpaka kwanza apeleke mganda wa malimbuko kwa kuhani.
  Lakini maandiko yanaendelea kutupa hakikisho kuwa mlaji wa zaka ni mtoaji kwa kumpa maagizo namna ya kusafirisha toleo la zaka mpaka mahali ambapo Mungu amepachagua yaani kwenye kusanyiko na kisha linatoa maelezo ya matumizi ya fedha za zaka kuwa zifanyie nini ‘ Na zile fedha uzitumie kama itamanivyo roho yako………………………………’
  Maandiko yanaonyesha hata toleo la mwaka wa tatu la ZAKA litunzwe wapi na kwa nini.
  Sijui ni kwa nini umeamua kulitafsiri kinyume andiko hili dhahiri.
  Lakini labda nikupe pumzi kidogo na kisha nitoe elimu kwako kuhusiana na ZAka kwa kupitia maandiko mengine yanayotoa tafsiri ya neno zaka.
  ‘Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.
  ……………………………………….Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.
  ………………………………………………Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu.
  Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana. ‘
  (Hesabu 18:21,24,27-28)
  Maandiko niliyoyapost sasa hivi yanaonyesha kile ambacho makuhani walipaswa kupatiwa kama ZAKA yaani SADAKA YA KUINULIWA KUTOKA KWENYE ILE ZAKA.Na ndiyo maana ya maneno yale ya USIACHE KUTOA ZAKA YA FUNGU LA KUMI kama utatafakari vya kutosha ukiongozwa na Roho mtakatifu.
  Ndiyo maelezo yanayofafanua lile andiko la Mambo ya walawi 27:32 yasemayo
  ‘Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa Bwana. ‘
  KILA APITAYE CHINI YA FIMBO,Wakati gani??? ni katika eneo la mkusanyiko makuhani walichagua wenyewe sehemu ya ZAKA kutoka kwa wana wa israeli ili iwe sadaka ya kuinuliwa kama njia ya kubariki chakula kama tufanyavyo leo kwenye kuombea chakula.
  Umenukuu pia mafundisho ya utoaji wa Ibrahimu alipompa mfalme na kuhani Melkizedeki wa Salem kama fundisho la utoaji wa zaka. Ni aibu kweli kweli na uthibitisho kuwa hukuwahi kuisoma kwa makini habari hiyo. Na labda nikuzindue kidogo.
  Zaka kama mnavyofundisha ninyi ni matoleo ya mali ulizotolea jasho,ni zako na unamrudishia Mungu shukurani (Si ni ndivyo kaka)
  Lakin umewahi kujiuliza ama kusoma kuwa sehemu ya kumi ambayo Ibrahim alimpa mfalme na kuhani Melkizedeki ni za nani???
  Hebu soma kipande hiki cha maandiko utafakari upya:
  ‘Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.
  Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
  Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
  Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
  Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe.
  Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi,
  ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;
  isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao. ‘
  Ibrahim anamjibu mfalme Kedorloama kuwa ‘Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi,
  ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;
  isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao’
  Je ni sahihi kutoa zaka mali isiyo yako???
  Hata mfano wa ahadi ya Yakobo ya kumtole Mungu fungu la kumi haiwi amri kwani ilikuwa ni HIYARI YAKE YAKOBO MWENYEWE tena kwa sharti la kulindwa na kutunzwa na Mungu na kwa hiyo si lazima (kama zaka ni sadaka)
  Umejaribu kutumia mifano kadhaa kuhalalisha kuwa Yesu aliwahi kutoa zaka kama MKRISTO,nikapasuka mbavu kweli kweli.
  HIVI JAMANI YESU ALIWAHI KUWA MKRISTO???? Jibu ni hapana kwani yeye ndiye Kristo mwenyewe na wakati wa huduma yake aliishi akifuata imani na mapokeo ya kiyahudi,kwa hiyo hajawahi kutoa zaka kama MKRISTO.
  Hata wanafunzi wake waliishi kama waumini wa dini ya kiyahudi na kufuata mapokeo ya kiyahudi lakini lilipokuja suala la ukristo wao tunaona Mwinjilisti Luka akituambia maneno haya:
  ‘Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika,
  wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.
  Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
  wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.
  (Matendo 2:44-45;4:34-35)
  Kama kutoa hawa walitumia kanuni ya kutoa 100% na si 10% na huku ndiko kuitimliza torati kulikofanywa na Yesu.
  Kwa hiyo wanafunzi wa Yesu hawakutoa zaka kama WAKRISTO
  Hata hivyo bado kuna kitu cha kujifunza kwa ziada.
  Ni nani anastahili kupewa zaka kwa mujibu wa mafundisho ya waalimu wa zaka??
  Wachungaji,waalimu,wainjilisti,mitume ama manabii??? Kwamba wao ndio makuhani wa AGANO JIPYA???
  Je biblia inatuambia Makuhani wa agano jipya ni nani???
  (1Petro2:2,9)
  ‘Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ……………..Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ‘
  Mtume Paulo akitaka kulifafanua hili katika nyaraka zake anasema;
  ‘Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya………………………yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
  Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. ‘
  (2Korintho 5:17,19-20)
  Maandiko yanatufundisha kuwa KUHANI WA KIKRISTO NI MKRISTO ALIYEKOMBOLEWA NA YESU na ya kuwa Uchungaji,Ualimu,utume,uinjilisti ama unabii ni WIZARA/HUDUMA ZA KIKUHANI SI UKUHANI WENYWE NA NDIYO MAANA KWENYE WARAKA WA EFESO PAULO ANASEMA
  ‘Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
  kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; ‘
  Efeso 4:11-12
  Nadhani unaweza kuona ukweli wa kimaandiko kuhusiana na tafsiri hii na ile yako ambayo imeegemea mapokeo ya mafundisho kwenye madhehebu
  Kwa kukujulisha tu ni kuwa UTOAJI WA ZAKA KANISANI UMEANZA MWAKA 777 BAADA YA KRISTO TENA KWA AGIZO LA GAVANA CHALAGNE.

 126. Mtumishi wa Mungu Seleli Ubarikiwe kwa kunijibia maswali yangu aliyoniuliza Mtumishi wa Mungu Sungura!Binafsi nimepitia kila andiko ulilotoa na nimekupata vizuri sana then thnx kwa kuniongezea mistari abt Roho Mtakatifu.Ujuwe shida ipo palepale kwa badhi ya wapendwa kutotaka kukubali ukweli ambao ni Neno la Mungu!thn umejaribu kujibu hoja za kila mmoja kwa kutumia Neno la Mungu na cyo neno lako binafsi bt inakuwa ngumu kwa baadhi ya wapendwa!Hizi ndizo hasara za kuzoelea NENO LA MUNGU na kuona as if mtu flani hawezi nieleza kitu kipya!Tutapona kweli wapendwa kwa kiburi hiki?Mungu aturehemu kwakweli!coz mambo yako wazi sana na ukipitia kila andiko alilotoa Seleli lipo clear!Oooh! God Help these wapendwa Pliiiz! coz we are in da same Journey&we need all of us 2 rich U!hatuhitaji hata mmoja aishie njian!2nahitaji wote kumaliza safari salama JEHOVA.

 127. Seleli kitu kingine nikushauri ndugu yangu:

  Punguza mchanganyo wa Kiswahili na Kiingereza( code-mixing & code- switching). Fanya hivyo tu inapokuwa imelazimu.

  Pia kuna kitu unakisema sana mara kwa mara kwenye michango yako, cha uyanga na usimba. Mimi naona kama ni kielelezo cha unafiki fulani wa kuwasema watu fulani. Huo nao ni utoto katika ulimwengu wa midahalo.

  Ni bora ukasema tu kama unaona akina Sungura, Kaswahili na wengine ambao hawakubaliani na wewe, mawazo yao ndio unayoyaona ni ya kisiasa. Lakini wale ambao wanayakubali wanayaona kuwa ni ya msingi.

  Kuwa kama ulivyosema Paulo alikuwa (yaani bacjk and white)

  Na usiaribu kuwa unaongea hitimisho, mawazo yako siyo hitimisho la hoja hii Seleli, ni mawazo tu kama ya mtu mwingine. Yanaweza kuwa sahihi au siyo sahihi.

  Kuna vitu utavirudia na kuvirudia lakini ukweli utabaki palepale kuwa ni mawazo yako.

  Kwa mfano kulazimisha kuwa katika misaada ambayo Paulo ailipewa na kanisa ati na zaka ilikuwemo, milele yataendelea kuwa ni mawazo yako tu Seleli. Hilo suala haliko kwenye maandiko popote.

  Roho mtakatifu alishuka mara moja tu na yupo hapa mpaka kanisa litakapoondoka. Unaposema alishuka tena na tena kana kwamba alikuwa anarudi mbinguni na kushuka tena siyo sawa. Labda kama ungesema aliwajaza tena na tena ningekubaliana na wewe.

  Asante.

 128. Siyi upo rafiki yangu!!!

  Niende moja kwa moja kwenye pointi ya ulichoniuliza:
  1. Kwa ufafanuzi wa Kiswahili neno matoleo ni la jumla (inclusive) likiwa na maana kuwa zaka, malimbuko, sadaka, dhabihu vyote viko ndani yake. Kwa kiingereza nimeshindwa kulipata hilo neno matoleo linaitwaje.

  2. Aya ya Mathayo 23:23 naielewa kama ifuatavyo; kwamba Yesu anawaonya mafarisayo kwamba walikuwa makini sana kutoa zaka hata ya vitu vidogovidogo sana kama mchicha na bizari, lakini wakiwa wameshindwa kukumbuka mambo ya msingi ya sheria (torati) ambayo ni adili au haki, rehema na uaminifu. Hivyo anawaambia kuwa Iliwapasa kuyashika hayo mambo ya msingi na kuwa makini nayo kama ambavyo walikuwa makini katika utoaji wa zaka.

  Na Yesu aliwaambia kuwa waendelee kutoa zaka kwa sababu suala la uwepo wa makuhani (ambao ndiyo hasa msingi wa zaka kutolewa kama sheria) lilikuwa bado lipo. Kwamba walawi na makuhani ambao zaka ndio ilikuwa urithi wao walikuwa bado wanaendelea kutumika katika hekalu, hivyo lazima zaka ilitakiwa kuendelea kutolewa.

  3. Kwa suala la Mdo 5: 8 iko hivi;
  Utoaji huo ulikuwa wa hiari. Lakini kosa la Anania na Safira ni kule kudanganya thamani waliyouza kiwanja chao. e.g Kama wangesema kwamba kiwanja walikiuza kwa milioni moja na wakaamua kuleta laki nane, kusingekuwa na tatizo,lakini wa wanakubiana waseme kuwa wamekiuza kwa laki nane. Mstari wa 4 anasema ” While it remained, was it not your own? And after it was sold, was it not in your own control? Why have you conceived this thing in your heart?

  Huo utoaji uliofanyika katika kanisa la kwanza hapo ukisoma Mdo 3;32 -36 ulikuwa utoaji wa hiari.

  Asante

 129. Seleli hakuna kitu ambacho nimebadilika. Niliposoma unavyonipongeza kwa kubadilika ndipo nilipotambua kuwa hukuwa umenielewa toka mwanzo.

  Mimi tangu mwanzo nimesema zaka ni toleo la hiari, kwamba nikitaka kutoa natoa nisipotaka sitoi, nikasema tena kuwa si sheria kama ilivyokuwa wakati wa torati.

  Hebu ngoja labda nikupe msimamo wangu peupe kabisa ”MIMI HATASIKUMBUKI MARA YA MWISHO KUTOA TOLEO LINAITWA ZAKA ILIKUWA NI LINI”
  Yaani ni hivi, nikipata shilingi laki moja huwa sitengi ati elfu kumi ya zaka, bali kama nimejisikia kutoa elfu tano sadaka hiyo ndo nitatoa, kama nimejisikia kutoa elfu 30 sadaka hiyo ndo nitatoa, kama nimejisikia kuitoa yote sadaka hivyo ndivyo nitafanya.

  Nikijisikia kutoa mshahara wote kanisani au kwa watoto yatima/wajane au masikini au popote pale hivyo ndivyo nitafanya. Sifungwi na sheria yoyote. Kukiwa na changizo natoa kama nitakavyoguswa.

  Natamani ungekuwa hapa ana kwa ana nikwambie kwa sauti kuu kwamba, sikubaliani na watumishi wanaosoma kitabu cha Malaki tatu na kuanza kusema ”kama kuna mtu huwa hutoi zaka wewe ni mwizi, unamwibia Mungu”, wakati huyo anayeambiwa hayo ametoa sadaka yake na na michango mingine kama ilikuwepo. Halafu huyu mtu anasimama na kusema ”ukitoa sadaka peke yake haitoshi lazima utoe na zaka”. Yaani kama katika laki moja yangu nimetoa sadaka elfu 30 ati naambiwa haitoshi mpaka nitoe na 10% yake, yaani elfu kumi!!?

  Seleli nimekuwa na wasiwasi sana tangu mwanzo kuwa hatuelewani. Ndio maana nimeshangaa sana uliponisifu kuwa nimebadilika. Na hata unaponishukuru ati kwamba nimetubu pia nimeshangaa sana. Kukwambia kuwa hauko makini si dhambi mpaka nitubu. Na hata sasa nakwambia hivyo hivyo Seleli, maana tangu mwanzo nimesema zaka ni sadaka ya hiari (kwa maana ya kwamba mtu akitoa sawa asipotoa sawa pia). Si hiari kwa maana ya kwamba mtu lazima aitoe lakini asiitoe huku amenuna bali huku akitabasamu.

  Halafu Seleli ukiambiwakuwa kuna wakti unatumia ‘assumptions’ unaona kama unasemwa vibaya. Kuna kitu hapa umesema lakini unajua kabisa kuwa siyo ‘fact’ bali mawazo yako, na unataka tukiamini hivyo. Kusema kuwa baadae Mark alikuja kubadilika siyo sawa maana huwezi thibitisha hilo. Inawezekana Paul ndo alibadilika na kugundua kuwa Mark anafaa, kwa nini Barnabas alin’gang’ania kwenda na Mark, au Barnabas yeye alikuwa anapenda kuambatana na watu wabovu? Kumbuka pia Barnabas hakuwa mtu wa mchezo.

  Je kama Mark aliamua kurudi Jerusalem kwa sababu nzuri tu, ambayo yawezekana Paul hakuikubali tu kwa sababu zake binafsi? Kwani Mark alirudi Jerusalem kwenye kustarehe? Na kwa mbaya zaidi unasema alienda home, una uhakika kwao ilikuwa ni Jerusalem?. Nakunukuu ulivyosema;

  ” thank God, Mark baadae uko alikuja kubadilika(kukaa level, in this case ya hoja yetu hapa-aliacha maneno-maneno kanisani, mambo ya Simba naYanga ya vuta uku, vuta kule na kuingiza mawazo ya kuharibu badala ya kujenga) na Paul akamsifu..”

  Mimi tangu mwanzo wa hoja nimekuwa nikisema kwa nini zake ilitoka kuwa hiari hadi kuja kuwa sheria, lakini wewe naona bado unasisitiza andiko la Malaiki 3 kuwa asiyetoa ni mwizi.

  Japokuwa pia kwenye mchango wangu hapo juu nilionesha jinsi ambavyo ukuhani ulibadilika na hivyo sheria nayo haina budi kubadilika, lakini hoja hiyo umejifanya hujaiona na kuona tu mengine ambayo mengine hayakuwa ya muhimu sana kama hiyo hoja.

  Zaka siyo kipimo cha moyo wa utoaji kwa mtu anayempenda Mungu, bali sadaka ni kipimo kizuri kwa hilo. Ibrahim hakuonesha moyo wa utoaji kwa kutoa zaka bali kwa kutoa sadaka ya mwanae wa pekee. Kama zaka kingekuwa kipimo basi ingetosha Mungu kupima Ibrahim wakati anatoa zaka kwa Melkizeki.

  Tukiendelea kutoelewana,basi itafika mahali tukubaliane kutokukubaliana!

  Asante.

 130. Tumaini Nelson,

  Aliposhuka toka siku ile ya pentekoste Mdo.2:1-4, alishuka tena na tena kwa wale wale na wengine wapya- Mdo.4:31. So ni kweli tuna muhitaji tena na tena, kwa wapya kumpokea kwa upya na kwa ‘wazee’ kujazwa/kufurikishwa tena na tena na tena kama alivyosema Tumaini Nelson-uko sahihi bwanaa Nelson, hujaharibu kitu hapo Biblically. Pia angalia hapa- Luka.24:45…Kiingereza NIV Bible inasema vema- ‘’Then he opened their minds so they could understand the Scriptures(Notice hapo connection kati ya Mind( ufahamu/akili) opened one na kuelewa maandiko).Embu angalia ‘Mind’ ni nini iyo ambayo BWANA Yesu aliifungua/ruhusu/wezesha kufahamu maandiko. Zifuatazo ni baadhi ya maana za ‘Mind’ from google (MOJA: The human consciousness that originates in the brain and is manifested especially in thought, perception, emotion, will, memory, and imagination, PILI: The principle of intelligence, TATU: the spirit of consciousness regarded as an aspect of reality.NNE:The faculty of thinking, reasoning, and applying knowledge: TANO: A person of great mental ability. Kwa iyo ni sawa kabisa kusema Yesu aliwezesha/fungua/vuvia/huisha akili, intelligence, mental ability, ubongo kujua/kuhisi/kufikiri/kufahamu/kutafakari jambo na kupata ukweli. Kama Yesu anaweza fanya ivyo katika Mind ya Mtu, Roho Mtakatifu anaweza pia sana kabisa na in fact ndio moja ya kazi yake spesheli kwa kanisa lake la leo, ni kwa huyo(RM) akishafungua Mind KiMungu ndio tunaweza ona Zaka ktk Agano Jipya na matoleo aliyokusanya /kusanyiwa Paulo kupitia hata maandiko indirect na si mpaka yale ya direct kama ya Mr.Kaswahili

  Kuna kweli nyingine hi kuhusu Roho kutujaza na kua naye in full kila mara kwa MOYO PONDEKA ili kufunulia kweli nyingi za Maandiko wether from direct-live live or indirect Maneno ya Mungu ( maana ukiwa na siasa kwa delicate life issues za uhai wa kiroho na kimwili wa kanisa au kuchezesha game ya Yanga na Simba church kwako-atakunyima mengi au yale ya juu-level nyingine. Mathayo.17:10-13 Imagine wanafunzi wanauliza swali kuhusu Ujio wa Eliya kua inapaswa aje kwanza, angalia majibu ya Yesu halafu kisha hao hao waliouliza, wanapata jibu-wana connect wenyewe kwenye jibu-why? MIND-yenye maana/mambo yote juu pale, ilifunguliwa/funguka by the power/ backing of Jesus/Holy Spirit.Pia Yohana.12:16 Wanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo lakini Yesu alipotukuzwa,WALIKUMBUKA kua mambo haya YALIANDIKWA kuhusu Yeye…KUKUMBUKA in this context ni zaidi ya kukumbuka tu simply but ni zaidi ya ilo yaani ni KUELEWA which is the function/product/work ya Mind but si normal mind tu rather ni ile ILIYOVUVIWA/HUISHWA/WEZESHWA, again by the power of the Holy Ghost. Ongeza na ni hii Mathayo.13:10-11 Yesu anasema wengine hawaelewi bali wao Wanafunzi WAMEPEWA KUJUA siri za Ufalme=kupewa ni kuwezeshwa pia na nani nawezesha? Roho Mtakatifu/Yesu.

  CONCLUSIVELY: Indeed we need Holy Spirit now like never before because sasa kuna watu makanisa ya leo wanavuruga KWELI basic za Mungu, Kanisa, Wapendwa na mpaka Watumishi wa Kweli wanaotulea, si kama zamani, kule zamaniiiiiii tulipookokaga, tulikua hatuna shida kuzitenda na kufurahi ila baada ya kukua na ‘’KUKOMAA KIROHO SANA’’, tunaleta maneno mengiiiiiiiiii kwa mambo so simple and lovable kumfanyia Mungu na sisi wenyewe.

  Press on.

 131. Sungura,

  Asante kwa pole yako. Usijari kwakua kila swali kila linalohitaji majibu toka kwangu, HAKIKA nitatoa bila shaka wala kusita au kupoteza hata nukta lakini sa far hakuna lililobaki na nimeshajibu yote na kama kuna anayekataa, aje na hoja anakataaje si tu ‘sitaki-sitaki’. Kwamba sitatoa majibu ya kuridhisha, inawezekana na ivyo wengine watasaidia ila kwa wewe na Kaswahili, nitajitahidi kuridhisha sana kabisa. Pia ingekua vema uniambie so far yapi ambayo sijakuridhisha! then nijibu mara moja, otherwise nitachukulia umependa tu utani au by the way words! Ushauri kua tuiseme mada na si kusemana, ni badiliko jema kabisa kwako na hongera kwa iyo toba/kujirudi na sasa we can talk maana walioacha mada na kusema personalities na hata ‘almost kutukana’ ana/wanajulikana wazi hapa! Ivyo nakubaliana nawe kama nilivyokuambia mwanzo, stick to issues not personalities. Ujuzi wa kuandika muhimu, ni kipaji toka kwa Baba na utaendelea kutumika mpaka mwisho-ndio maana ya facility hii, hatutumii mdomo bali maandishi. Afterall, kila mtu umu nilipokua napitia michango yenu yote kwanza na hata mada nyingine uko na kule, humu, kwa kweli mna ujuzi/ anointing hi hi ya kuandika sema viwango tunazidiana tu na ni kawaida kabisa.

  Points nyingine ulizoandika zote kwa leo ni za mtu tofauti kabisa na wa mwanzo niliyemkuta humo.Sasa ivi uko straight/clean kua Zaka ni sawa bila kuchanganya-changanya mara sawa la.Kwakua ulimesema toka mwanzo kua ni Hiari na ukatoa Ibrahimu kutoa zaka kama mfano bora( ingawa ulikosea kwa kusema hata Yakobo alitoa-nikakuitia kama ulivyosema-wakati mwanzo wa zaka anatuonyesha ule Moyo mzuri wa kupenda/kutaka kutoa zaka kwa yeye kuhaidi tu), basi hiari iyo kabla ya sheria ipo mpaka leo ndio maana siye wenzio hayo tunayajua kitambo na hakuna tunachomsazia Bwana

  Ni kweli Tunapofika Agano Jipya, ni mabadiliko (ofcoz needless to emphasis kwakua hata jina tu Agano la Kale Vs. Jipya tells simply the meaning/content/ shift) lakini zingatia ili mpaka atakaporudi Bwana kua mabadiliko wakati wetu wa Agano Jipya haimanisha kufa kwa KILA KITU KTK AGANO LA KALE( Kama nilivyojibu maswali ya Ndugu Amin Jeremiah, ukipenda pitia na kama utakua na swali, 24hrs karibu).Mfano wa vitu/kweli ambazo hazifi/zinahama moja kwa moja ni Zaka ( unaona tena hapo sasa-ilipeni/itoeni tu maana inakaba kweli toka Mwanzo) na pia kuhesabiwa haki kwa Kumwamini Mungu si matendo-ilianza kwa Ibrahimu. Hence, Yako yanayokufa kabisa( na ni mengi), yapo yanayoTIMILIZWA-yaani simply yanaendelee ila kwa fashion ya kama atakavyo/alivyoanzisha Mwenyewe( Yesu) baada ya -Soma Sura zote za Hotuba ya Mlimani Mathayo.5,6,7 aliposema ‘Sijaja kuvunja ila KUTIMILIZA-then see alisema nini kufafanua utimilizaji na pia angalia maisha yake kwa ujumla ktk Injili zote 4 alifanya nini kutimiliza torati-very clear and lovely to learn, ivyo tu basi.

  Umesema..’’sadaka na machangizo vinatosha, maana leo hata zaka zinapotolewa ki- matumizi huwa zinachanganywa na sadaka zingine’’= WHAT AGAIN ARE YOU TRYING TO SAY HAPA? Kua zinatosha ivyo tusitoe Zaka au tutoe zaka na sadaka na michango mingine lakini kuwe na system njema ya kutenganisha Zaka na hayo Matoleo mengine kwakua zinachanganyanywa umo? WHAT IS THIS AGAIN Mister? or una imply kua tutoe Zaka kifichoni? Au hicho kificho/uchanganyaji zote umo unaupenda na udumu? Kitu gani hasa hapo una-suggest na hujaki-articulate straight? COME UP CLEAR man. Na Kama una jaribu kusema kua mradi tunatoa na vyote vinaingia umo umo kuwepo zaka au hakuna vyote sawa tu, si mradi tunatoa tu na vimechanganywa umo umo tu na kua vinatosha ivyo ivyo!Mmh! embu fafanua then nitajua nisemeje hapa maana nahisi( sina uhakika- I may be wrong, its fine) kuna kitu hapo hatari cha kukishughulikia haraka sana!

  Umehitimisha ivi’’Hivyo kwa mujibu wa mabaliko hayo yaliyosemwa hapo juu, zaka ni toleo la hiari ambalo kwa anayetaka kutoa hata akitoa si tu kila mwezi na wiki bali hata kila siku haina shida = excellent now, indeed you have changed si kama nilivyokukuta and you are MORE blessed IF and WHEN you do it.

  Press on giving zaka na zaidI ya zaka coz una Uhiyari na Love kwa BABA ikiwepo, no Agano la Kale or Jipya wala kutafuta andiko live-live Agano la Jipya kama anavyolitafuta Kaswahili la zaka e.g. ‘’Amin Amin nawaambieni nyinyi msipotoa Zaka na Malimbuko kwa Makuhani na Ukuhani wa Leo, hakika hamtaingia ktk Ufalme wangu’’, eti akiliona ilo then ndio atoe Zaka wakati mpaka sasa hajanionyesha andiko gani Yesu alioga na kupiga chafya wakati kwa Hakika wote twajua alioga na kupiga chafya.Icho kinachomuongoza/mnunulisha Kaswahili kujua kwa hakika kua Yesu alioga/chafya bila kua na andiko la live-live ndicho kilichonimulikia kujua na pia maandiko niliyo-share ktk majibu yangu kwa Jeremiah indirectly or directly yana draw the line of conclusion truly bila kuharibu kweli za Bible iyo iyo on Zaka na matoleo mengine shifting from Old to New Agano.

  BLESSED BE THE NAME OF THE LORD.

  Edwin Seleli

 132. Salu Lujenje

  Nakubaliana nawewe kabisa kua ‘’’Kanisa haliwezi kwenda mbele bila michango tena ya hiari’’ and KATI YA MICHANGO HIYO( ambayo simply/ basically ni Sadaka tu au /Matoleo tu hayo), je ZAKA zimo hazimo? Zitolewe au zisitolewe ili Kanisa kama ulivyosema liende mbele? Napenda nifahamu moja kwa moja ufahamu/msimamo wako ktk hili ili nikufafanulie msingi wangu mtamu sana na mzito kweli kua nakubali kutoa Zaka leo Agano Jipya kwakua UKISHAMPENDA MUNGU, HUNAFANYA ZAIDI YA ZAKA namely kumtoa hata Isaka. Halafu sijakupata uliposema tutawakwaza Wapendwa! Ni kwa ukweli huo uliosema Kanisa haliwezi kwenda bila Michango au eti kutoa zaka ni sheria kama maelezo yako mengine huko chini yanavyoeeleke ku-suggest(sina uhakika ndio maana nimeomba ulewa/msimamo wako black and white pale juu na kwa ushahidi).Kwangu mie na hata ni tabia ya Yesu na wengine kama hakina Paul Vs. Petro Wagalatia.2:11-16-Paul anasema nilipoona Njia za Peter zimepind (hazijanyooka), NIKAMPINGA USO KWA USO-notice hawa ni Wandugu ktk Bwana na pillars wa kanisa but mmoja akaleta siasa kwa mambo ya msingi akijua kabisa anafanya mambo ya ovyo au Paul na Sila Vs. Barnaba na Marco J.- Mdo.15:36-41 wakati Marco John anavuruga kazi ya Bwana(maana alitoroka kazi just to go back home i.e. mvivu/mbinafsi-kujali hamu zake/mamboyake = kwenda home, akiwaacha wenzie ktk uwanja wa kazi/mapambano)-Mdo.13:13 then eti baadae ‘upako’ ukaja, akataka/kachukuliwa kwa huduma ndipo ‘walivyokabana na the serious black and white guy I like, kamanda Paul’- KJV Kingereza inatumia statement-‘when contention became so sharp’ yaani waliposhindana sana/kupingana sana/ kutokukubaliana sana then wakagawanyika, thank God, Mark baadae uko alikuja kubadilika(kukaa level, in this case ya hoja yetu hapa-aliacha maneno-maneno kanisani, mambo ya Simba naYanga ya vuta uku, vuta kule na kuingiza mawazo ya kuharibu badala ya kujenga) na Paul akamsifu Wakolosai.4:10, Filemoni.1:24.

  Therefore, inapokuja swala la kuongea ukweli, na unajua wajua ukweli na unajua kua wao pia wanajua sana au basically ukweli lakini kwa ukorofi/utundu/ubinafsi/shibe tu zinawasumbua, hakuna rehema hapo wala kutumia hekima waitakayo wa ina hiyo, heri wangekua hawajui chochote wala ujuzi wa kweli za Neno hawana, hapo rehema a hekima wangestahili, thus, kwa hao ishu ya kukwaza au kutokwaza, si jambo la kulea hata kidogo, halina tija wala credit JUU kwa extremity level ya kufanya kwa makusudi hayo wayafanyayo au at least waliokua wanayafanya maana naona kwa urahisi kabisa naposoma comments zinatoka sasa, vinara wa mambo hayo ya Simba na Yanga against Kanisa,Watumishi wa kweli wa Mungu na kazi ya Mungu nje na ndani ya makanisani yetu, wanavyokaa level kama Mark John bado kidogo ili watakaa tu level hapa hapa pia for His Glory Amen.

  Nimependa mshangao wako huu ‘’Zaka ziko za aina 15 katika Agano la kale (Torati-sheria ya Mungu kupitia Musa)) lakini zote hizi tumeacha tunangalia zaidi mshahara maana yake nini?’’ Nashauri, tuanze kufundisha izo na kuwatia moyo watu watoe na izo pia si kama sheria bali kwa Hiari na moyo wa kupenda( Wala hili la Hiari na Moyo wa kupenda tusilisisitize sana weee as if makanisani uko ni ‘Uhitla’ tu mwanzo mwisho-si kweli kabisa labda machache and after all, ivi kweli Mwanadamu akigoma kutoa ela yake, nani ana uwezo wa kumnyakua kama si Mungu tu! Ivyo basi wafundishaji/ wakumbashaji watafanya ivyo kwa moyo huo huo safi na nina ushahidi pia mwingi tu wa Watumishi wa MUNGU wamekua wanafaya Ufundishaji wa matoleo yote na Watu wa Mungu kwa raha zao, wanatoa hata sasa sadaka za aina nyingi kweli acha tu Zaka ambayo inasubua baadhi ya watu kwa sababu ya roho za ubinafsi/kujipenda wenyewe( nafsi) kupita kiasi!

  Umeshanga, Why mshahara unang’ang’aniwa?( ingawa mie ningesema-Why sie washirika tunang’ang’ania mshahara hatuuachilii kwa Bwana?), simply ni kwakua ndio kipato kikuu na cha uhakika cha watu wa mijini/jijini, kwetu hatuna shida kwakua tunatoa kuku, ng’ombe, magunia ya mazao, kama nina matuta 1000 ya mahindi, nahesabu 10pec yake ni ya kanisa au nimevuna karanga magunia 500, kikumi chake yote kanisani kwa raha zangu kabisa na Bwana wangu, sina tabu na nikifanikiwa kuuza na kushika ela ya magunia hayo hayo, bado kikumi au hata kiishirini,kithelathini, nitatoa tu kwa furaha na naimba pambio kisha narudi home nasikia raha, furaha na kama napaa-paa ivi mbinguni,nasikia uwepo na upenzi sana ndani ya Mungu nifanyapo hayo, wewe je? Unajisikiagaje kule ndani? Au waga/ulishafanyaga hayo? Nishuhudie kidogo nakungoja hapa.

  Swali lako hili ‘’suala la kilipa kwa mwezi limekujaje? Nakushauri, pitia michango yangu yote hapa iliyotangulia ktk hoja hii mwanzo mpaka mwisho bila kuchoka kwa kua unataka kuelewa. Naona kwa maswali yako mengine, hujasoma michango iliyotangulia yote au baadhi. Ukishapitia hapo, kama swali lako ilo halikujibiwa ukaridhika, karibu tena mpendwa uulize na utajibiwa pasi na shaka yoyote. Kunukuu maelezao ya Agano la Kale kua kutoa toa Zaka tena kamili ni mwizi, ni SAWA NA AMENI KWA HERUFI KUBWA. Tuache wizi. Na kwakua moja wapo ya amri 10 za Mungu ni Usiibe na ilitoka Kale si Jipya na ktk Jipya, hajawahi sema Ibeni au mnapozidiwa, piga saini uli upate cha juu, basi NI WIZI NA NIKUA MWIZI kutolipa Zaka-Ni Mungu amesema si mtu!!!!!!!!!!!! Inauma/udhi but ndio salama na Uzima tele kukemewa na Baba.

  Kuhusu wasiwasi wako kua tuna kazana na ustawi wa jamii na kuacha Utumishi, ikiwa ivyo ni mbaya sana! Kuacha utumishi! lo! Hata ivyo, tukifanya kwanza utumishi na kisha kustawisha jamii, very excellent indeed. Lakini pia ktk Neno kuna balance-Kutaka/kufanya sana huduma then UKASAHAU KABISA KUWAJALI( Ustawi wa jamii huo) WA KWENU, ni ubaya( Mungu hataki hata umtumikie maana akisha sema sisi ni wabaya kuliko wasio amini, manake we should go home na kulima tumbuku ikibidi! 1Timotheo 5:7-8

  Kuhusu Paulo kusema hajawahi kumlemea mtu hujishughulisha kwa kazi zake mwenyewe-hili nimesema sana ktk michango yangu-ndio maana nikasema, embu pata muda, pitia iyo lakini nisema kwa ufupi hapa, ni kweli alisema ivyo, na nikweli alipiga kazi na lakini ni kweli pia alisaidiwa sana kwa matoleo ya Wapendwa na naamini walikuwepo wapendwa kwa hiari na upendo kabisa tena wakijua aina ya utumishi mtamu, wa baraka, mzito na wenye mateso mengi wa kaka Paulo, walitoa zaka nzito bila shaka zaidi hata ya kikumi tu ndio maana ktk maandiko haya alisema hanajizuia haki yake ya kula/kulishwa na kusupportiwa na wane lakini halisema bayana kua ana HAKI iyo na kuweka moto zaidi, alisema ni Bwana aliamuru wanaohubiri Injili waishi kwa Injili-1Wakorinto.9:1-15.

  Kwa maneno mengine, kama alikua na haki iyo, bila shaka aliitumia mahala kwingine na wakati mwingine, ni ngumu kusema toka mwanzo mpaka mwisho kwa aina ya huduma ile, hakuwahi kamwe kula vya wanae-si kweli hata kidogo na hajawahi kuwepo mtumishi wa ivyo duniani, Yesu ni mfano pia wa kusaidiwa na kussapotiwa na ingawa alikua Mungu pia na yeye mwenywe alisema, mtenda kazi ANASTAHILI UJIRA-Luka.10:7. Ivyo hakuna hatari yoyote kwa Watumishi kuishi kwa kua-Supported na Wanao wa Kiroho. Kwanza kwangu mie ukiniuliza na kwa uzoefu wa mambo ya Watumishi, ni heri sana Mtumishi asapotiwe yote kabisa ili abaki na moja tu-LA MADHABAHUNI KWA AJILI yetu kuliko mara amesafiri eti yuko ziara ya Obama maana ni mwajiriwa wa Wizara ya Membe, mara ameitwa na Rais kwa tume ya Ukimwi maana ni Kiongozi wa jamii,mara aende Mkoani kulima ili kupata karo maana washirika kanisani mmegoma, hali ngumu kwakwe, watoto wanatimuliwa na mke ananza kuleta shida kwakua hatunzwi halafu atoke huko apande mimbari kulisha Neno-Kaomba na kusikia sauti ya Mungu saa ngapi? MIMI NATAMANI SIKU MOJA NIWE KAMA BILL GATES KISHA WACHUNGAJI WOTE WA KWELI WA WILAYANI NA MIKOANI, NITAWAJENGEA NYUMBA, NUNULIWA MAGARI 2, NITALIPA KARO ZA WANAO WALIOZALIWA NA WALIOTUMBONI(wanaokuja) mpaka za chuo kikuu, nitawanunuliwa plots 2 Dar na shamba la kutisha sana huko huko kwao ili 24hrs wao na Biblia na madhabahu tu na watu wa Mungu walishwe vema kabisa katika uwepo wa ajabu na utulivu wa mioyoni, nafsini na roho za Watumishi wetu.

  Umeuliza, Ni wapi kwenye agano jipya zaka na fungu la kumi vinapofundishwa? sisi hatufuati dini(Tourati) maana kama ndivyo baasi tufuate na mengine kama kutoa zaka zote 15 pamoja na kutawadha kabla kuingia ibadani maana torati ni ya mwilini zaidi na tuwapige wazinzi mawe, na mwanamke akiwa kwenye hedhi atengwe siku saba nk’’ Jibu: Tafadhari soma michango yangu yote kwanza bila kuchoka bila shaka kwa una nia ya dhati ya kuelewa na pia una uwezo wa kusoma vitu vikubwa, utaweza tu ivi vya hapa. Ni kweli hatufungwi na sheria na wala tukishaookoka hatuenendi kwa sheria bali MOYO, UPENDO,UPENZI, UHIARI, RAHA, FURAHA, UHURU ktk Roho ndio maana Ibrahimu alitoa zaka kwa msingi huo, Yakobo alihaidi kuitoa kwa msingi huo, yote haya yakifanyika KABLA YA SHERIA ivyo oeo, kwakua tuna mpenda sana huyu Yehova kuliko nafsi zetu na vimishahara na vihela na vimali vyetu na kwa kua tunapenda sana mambo yake na ufalme wake na watu wake aliowaita, basi HATUTASAZA KITU MBELE NA KWA AJILI YAKE NA KWA KWELI KWA AJILI YA FAIDA YETU PIA, sema amen brother?

  Nadhani brother, kwakua uliomba( Watu) ukisema tusaidie hapo( Maswali/hoja zako), nimesaidia kiasi kikubwa kabisa na kama utakua bado na swali/hoja/kukubali au kukataa, yote sawa na kwakweli uwe huru kabisa,karibu sana mpendwa.

  Press on.

 133. Tumaini kama wapendwa hawana Roho mt. ni akina nani sasa waliye nae?
  Maana tangu alipshuka siku ya pentekoste hajawahi kuondoka.

  Au wewe tu ndiye uko nae, wapendwa hawamruhusu…., ina maana wewe haumo miongoni mwa hao wapendwa ambao hawamruhusu au hawana Roho mt.

 134. Sungura,
  Seleli, Kaswahili na wengine my beloved ones!!!
  Oooh, Duuu, ha ha ha haaaa!! Angalieni, msimpatie nafasi shetani wapendwa. Kukosoana na kurekebishana kwa hoja za kimaandiko yaani kuhojiana, ndio msingi mzuri wa kujifunza neno la Mungu. Paulo ni mfano mzuri sana kwetu jinsi alivyohojiana na watu kwa hekima. Tuombe Mungu atuongezee hekima na busara.
  Nawafahamu sana SG kuwa si wapesi wa hasira. Vinginevyo wangekuwa walishawafire zamani!!! Tumshukuru Mungu kwa hilo.
  Nikushukuru ndg Sungura kwa hoja zako. Umesema zaka siyo ya lazima, ilhali ni mojawapo ya matoleo.
  Naomba nikuulize maswali ndg Sungura.
  1. Kuna tofauti kati ya matoleo na zaka?
  2. Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
  Unaelewaje aya hii kaka Sungura?

  3. Mdo 5: 8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.
  Je, huu nao ulikuwa ni utoaji wa lazima au hiari?

  Karibu ndg yangu…
  Barikiwa

 135. BILA ROHO MTAKATIFU HATUWEZI KUSOMA RAMANI COZ YEYE NDIYE MSAIDIZI WETU Mdo 1:8 inaeleza wazi kabisa.Tatizo siyo kwamba somo la ZAKA halieleweki bali wapendwa hawamruhusu au hawana ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye anayefungua fahamu ili kujua siri za MUNGU!1Kor2:9-16.So kunahaja wapendwa wakampokea au kujazwa ROHOMTAKATIFU ILI NENO LA MUNGU LIELEWEKE KILAINI!GOD BLESS U ALL.

 136. Seleli pole sana,maana naona una mambo mengi ya kutolea majibu, na kwa hakika najua hautaweza kutoa majibu ya kuridhisha.

  Ni vizuri tukawa wakweli(honest) tukaacha kutafuta ujuzi wa kuandika, matokeo yake tunajikuta tunasemana sisi badala ya kuisema mada.

  Edwin umesema sana kuwa mimi na akina Kaswahili ndo tumeiacha hoja iliyoko mezani. Lbda niseme hivi; katika kanuni ya mijadala siwezi kukubaliana na au kuikataa hoja bila kwanza kukubaliana katika uhalali wa hicho kinachojadiliwa.

  Ni lazima tukubaliane kwanza maana ya zaka, ilianza lini, kwa nini ilianzishwa (msingi wa kutoa zaka), ni toleo la hiari au sheria (lazima mtu atoe). Tukishamaliza hapo ndipo sasa tunajadili kama kutoa kwa wiki au kwa mwezi ni sahihi.

  Nilisema kwamba zaka ilianza kuonekana tangu kwa Ibrahim ikiwa ni toleo la hiari,kwamba mtu akitaka kutoa anatoa asipotaka kutoa hatoi na hafungwi na sheria yoyote.

  Lakini wakti wa Musa zaka ilitoka kuwa hiari ikawa sheria, kwamba mtu lazima atoe,asipotoa sheria inamtia hatiani. Na huo ndio wakati ambao hata Malaki ambaye kutoka kwake tunalipata lile andiko maarufu la utoaji wa zaka.(Malaki 3)

  Lakini sababu ya Mungu kuifanya zaka iwe sheria inajulikana, nayo ni uwepo wa wana wa Lawi ambao walitumikia ukuhani.

  Tunapofika kwenye agano jipya kuna mabadiliko makubwa sana ya kimfumo ambayo yalitokea. Kwanza agano linabadilika kutoka kuwa la kutendeka mwilini hadi kuwa la kutendeka rohoni, ukuhani nao pia unabadilika mabadiliko ambayo yanauondoa msingi wa zaka kuwa sheria ambao uliwekwa wakati wa Musa.

  Ona mwandishi wa kitabu cha waebrania anavyoyasema hayo mabadiliko.(ambaye inasadikika kuwa alikuwa na Paul)

  (Hebrews 7:11 Now if perfection had been attainable through the Levitical priesthood (for under it the people received the law), what further need would there have been for another priest to arise after the order of Melchizedek, rather than one named after the order of Aaron? 12 For when there is a change in the priesthood, there is necessarily a change in the law as well. 13 For the one of whom these things are spoken belonged to another tribe, from which no one has ever served at the altar. 14 For it is evident that our Lord was descended from Judah, and in connection with that tribe Moses said nothing about priests.)
  Seleli, pia niliposema hakuna ukuhani leo baadae nikasem ukuhani unatoka kwa Yuda, just nilimaanisha leo hakuna kuhani ambaye anatimiza majukumu ya kikuhani ktk hekalu la kimwili kama makuhani wa kabila la Lawi walivyofanya wakati ule. Maana wao walitimiza majukumu yao kimwili kabisa ndani ya hekalu, lakini leo katika utumishi Mungu anasema ametoa mitume, manabii…… ambao utumishi wao hauilazimu zaka iwe toleo la sheria(lazima), maana wao wanaruhusiwa hata katika shughuli zingine mbali na huduma ya injili. Zaidi sana sadaka na machangizo vinatosha, maana leo hata zaka zinapotolewa ki- matumizi huwa zinachanganywa na sadaka zingine

  Hivyo kwa mujibu wa mabaliko hayo yaliyosemwa hapo juu, zaka ni toleo la hiari ambalo kwa anayetaka kutoa hata akitoa si tu kila mwezi na wiki bali hata kila siku haina shida.

  Tuendelee

 137. Hapa wapendwa tutawakwaza watu lakini ukweli ni msumeno. Kanisa haliwezi kwenda mbele bila michango tena ya hiari soma mdo: 4:— pale mitume walipoamua kuuza mali zao iliwafanye kazi ya Mungu hata Anania na Safira wakakosea wakapingwa na roho wa bwana na kufa.

  Lakini ni kweli pia kuwa neno la Mungu linasema hatutahesabiwa haki kwa matendo ya sheria maana na zaka ziko za aina 15 katika agano la kale (Torati-sheria ya Mungu kupitia Musa)) lakini zote hizi tumeacha tunangalia zaidi mshahara maana yake nini?

  Zaka kuu wakati ule ilikuwa ni malimbuko yalikuwa yakitolewa kwa mwaka mara moja sasa suala la kilipa kwa mwezi limekujaje? kuna ushaidi kuwa makanisa mengine usipotoa unatengwa kwa maelezo kuwa umemuibia Mungu.wakichukulia maelezo ya agano la kale lilelile wasiwasi wangu ni kuwa tumeacha yale ya muhimu na kuangalia maisha na ustawi wa mali mwili na kanisa kama ajira na sio utumishi hata Paulo aliwahi kusema hajawahi kumlemea mtu hujishughulisha kwa kazi zake mwenyewe hili sio kwa wachungaji wetu wengi wao hutegemea wakristo watoe ili maisha yao na ya kanisa yendelee hii ni htari kwa ustawi wa mambo ya rohoni iwapo hatutakuwa mamcho!!

  Pia inge faa uanangalie msingi wa swali kabla hujaleta mistari kuwa zaka ni sheria na kama ni sheria je tunabarikiwa chini ya sheria maana neno la Mungu linasema hatutahesbiwa haki kwa sheria

  hebu tusaidie hapa Ni wapi kwenye agano jipya zaka na fungu la kumi vinapofundishwa? sisi hatufuati dini (Tourati) maana kama ndivyo baasi tufuate na mengine kama kutoa zaka zote 15 pamoja na kutawadha kabla kuingia ibadani maana torati ni ya mwilini zaidi na tuwapige wazinzi mawe, na mwanamke akiwa kwenye hedhi atengwe siku saba nk

  tusaidie hapo

  Sallu

 138. Mabinza,

  Umesena umefutilia mada kwa karibu na bado hujafunguka kuhusu zaka! Aya pole na karibu twende taratibu. Nitaanza na wewe kwa kukuuliza maswali.Aright brother, let me try this way ili ufunguke.

  Umesema-‘’Biblia inasema kuwa Torati ni kivuri cha mambo ya Rohoni’

  SWALI: Je kivuli cha Zaka iliyoanza Agano la Kale ni kipi leo Agano Jipya? Mfano: Ibrahimu Alitoa zaka Agano Kale, leo kivuli chake cha rohoni ni?

  Umenukuu andiko ili-‘’Lk. 11:42 naona inasema hivi, “42Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kutoa matoleo hayo, wala msisahau kufanya hayo mengine.” Kwa mstari huu naendelea kuelewa kwamba zaka ilitolewa kwa mjibu wa Torati, ambayo pia Yesu alipokuja alikubaliana nayo lakini sioni popote kama naye alitoa Zaka’’.

  SWALI:Umesema Yesu kwa majibu yake alikubaliana nayo lakini humuoni akitoa Zaka, je kwa kua humuoni ndio alikataa/hakutoa wakati unajua na andiko linaonyesha na umesema alikubaliana nalo?

  Umesema-‘’licha ya kunukuliwa akimwambia Yohana mbatizaji kwamba, “tunapaswa kuitekeleza haki yote”

  SWALI:

  (a)Ndani ya Haki yote ambayo Yesu alisema twapwaswa kuitimiliza, Zaka imo haimo?

  (b) Na ukimfuatilia Yesu kila aliposema kuhusu Haki e.g. Haki yenu isipozidi ya Mafarisayo, KAMWE HAMTAINGIA UFALME, unadhani kati ya haki izo za Mafarisayo ambazo Yesu alituchallenge kuwazidi, ulipaji/utoaji wa Zaka umo au la? kwa maneno mengine Mafarisayo walikua wanatoa hawatoi?

  Umesema-‘’Katika agano la jipya kiuwazi sijaona fundisho lolote linalo onyesha kama Mitume walipata kutoa zaka wakati wote walipokuwa na Yesu ama baadaye’’

  SWALI: Je mitume walitii Maneno ya Yesu kuhusu kuitimiliza haki yote au kutenda kuzidi haki za Mafarisayo?

  Umesema-‘’Luka.6:38. Iliyonukuliwa na mchangiaji mmoja, nayo haizungumzii Zaka! Inasema, “38Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.” Hapo napo hapana neno Zaka pale!’’

  SWALI:

  (a)Umejuaje ivyo vitu vya kupeana/kuwapa Watu hakuna Zaka?

  (b)Kwani ivyo vitu ni nini?

  (c)e zaka haiwezi kua kitu cha kupeana?

  Umeomba kuuliza ivi-‘’naomba kusaidiwa ni wapi kunasomeka kuwa Mitume walitoa Zaka wakati wa Yesu na baada ya yeye kupaa mbinguni?

  Jibu: Nimeshakuuliza kama Mitume walitimiliza haki yote na chini hapa swali ni

  SWALI:

  (a)Bwana Yesu aliwahi kuoga maji bafuni, Kupiga chafya na miayo? nipe andiko?

  (b)Na kama unajua kwa HAKIKI alioga/chafya? nini icho kinakufanya/ au umefiaje maamuzi hayo/kuchukua uelewa huo kua kwa hakika alioga na kuchafya hata kama ndani ya BIBLE hakipo live love neno kwa neno?

  Umesisitiza- ‘’tunasimama kwa misingi ya Mitume na Manabii, ambapo mitume wameonya kuwa “Sisi (mitume), malaika ama mtu mwingine akifundisha, mafundisho kinyume na haya tunayoyafundisha na alaaniwe!”

  SWALI:

  (a) Yesu aliwaambia Wanafunzi wake ktk Mathayo.5:17-19 kua hakuja kuivunja Torati na manabii na ktk Mathayo.23:1-3 kua Waandishi na Mafarisayo wamekaa kwa kiti cha Musa, wayafundishayo Tuyashike na kuyatenda? UPI NI MSINGI WA KUKAMATA ILI TUSILAANIWE SI TU KWA KUFUNDISHA VIBAYA/TOFAUTI BALI HATA KWA KUTOTEKELEZA MATAKWA YAKE?

  (b) na unadhani Mitume na Manabii wa Kanisa la kwanza, walisimama/jenga ktk Misngi gani? wa kwao kwao, kivyao yao tu au kuna source? ipi?

  (c) iyo source itakua ni Yesu aliyesema hakuja kutengua Torati bali kuitimiliza ktk utimilizaji aliouonyesha mwenyewe ktk Mathayo sura zote za 5,6,7-Hotuba yote ya Mlimani akipangua kubaki/kutenda kwa motives na matakwa ya dini/imani/taratibu mfu bali kuzihuisha zile tu zisizopinga kweli alizokuja nazo/onyesha na kwamba jamaa wale(Mafarisayo) kuna vitu wanafundisha kwa kua wana kaa ktk kiti cha Musa au kuna source nyingine?

  Umesema-‘’Neno la Mungu ni toshelevu, Agano la kale linapatana na Agano jipya, ni wapi katika mafundisho ya Mitume wana fundisha utoaji wa Zaka?’’

  SWALI: Kwakua Maagano yanapatana na ingawa huoni ktk Agano moja jambo ambalo linaonekana ktk Agano jingine, je inamaana kwa kutokuliona na wakati umesema yanapata, ni kweli halipo? Na halikufanyika?

  Umemaliza kwa msemo mzuri sana huu-“Ufahamu ni chembe ya uhai!” Ni kweli maana Mungu akishafahamika vema kua Yeye ndiye mwenye vyote na hata siye ni mali yake na kwamba hata ivi vishilingi tunavyomiliki ni vyake na kwamba kwakwe Yeye twaingia na kutoka na kwamba ukimuondoa Yeye ktk maisha, hakuna maana ya maisha haya na yajayo, basi hakuna tutakachobakiza bila kumpa au kupenda mambo yake na watu wake pia Watumishi wake mambo yao/yake yawe swadakta kabisa.Amen.

  TAFADHARI NIKUOMBE SANA KIRAFIKI NA KWA FAIDA YA KANISA HILI, TWENDE POLEPOLE /TARATIBU,HOJA KWA HOJA AU SWALI KWA JIBU/SWALI MAANA ZIKO AINA NYINGI ZA KUJIBU MFANO MZURI HATA YESU ALIJIBU SWALI KWA SWALI KISHA WALIPOJIIBU WENYEWE, WAKAWA WAMEPATA JIBU WENYEWE TU KIRAHIS NAMNA IYO. Tutumie usmart huo ndipo tusonge mbele. MIMI NIKO TAYARI KUJIBU MASWALI YAKO MENGINE, KARIBU KABISA SO NA WEWE PIA KARIBU NIJIBU YANGU man of God Mabinza.

  Press on.

  Edwin Seleli

 139. Jamani wapendwa Bwana Yesu apewe sifa,
  Hili swala la zaka kimsingi limeonekana kwenye torati, Ibrahimu hakutoa kwa sheria na wala haiwiani na torati maana torati inataka utoe kwa ukamilifu ndipo uexperience baraka za Mungu. Ibrahimu wakati anaenda vitani kumuokoa ndugu yake alikua ameshabarikiwa na Mungu, Pia hata wakati anamtolea Melkizedek Kuhani wa salemu sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokua navyo ni baada ya kubarikiwa na kuhani si kabla.

  Kumbukeni pia Bwana Yesu alipokuja alizaliwa ktk jamii ya kiyahudi ambayo ilikua inashika torati ya Musa so na Bwana Yesu aliishi kwa kuishika torati hiyohiyo tena kwa ukamilifu wote kuliko mwanadamu yeyote ndo maana akawa mwenye haki mbele ya Mungu. Ndo maana utaona mara kadhaa aliongea na mafarisayo akiwarudisha na kufanya reference kwenye sheria zao. Kumbukeni pia kipindi kile agano jipya lilikua bado so Yesu alifanya huduma yake ktk agano la kale au torati ndo maana ilikua rahisi hata mafarisayo kusema mbona hapo wanafunzi wako wamekiuka sheria? nk.

  Kumbukeni agano jipya sheria ya Mungu si torati au sheria ya Musa kama wengine mnavyoiita, kumbuka kwa sheria ya musa au torati utakatifu ulikua wa nje yaani uikamilishe torati kwa matendo, kwa agano jipya utakatifu ni kuanzia ndani kuja nje yaani inside-out. na kwa mtu anayesoma vizuri biblia utagundua japo tunaishi kwenye neema ila viwango vya utakatifu kwenye agano jipya ni tofauti na kule kwenye kale maana viko juu. sisi hatuna jino kwa jino, tuna kumpenda adui, uzinzi si kwa matendo tu nk nk.

  Kadhalika, kutoa zaka si sheria inayotubana sisi ila haina maana tusimtolee Mungu, ila ninachojua mimi mtu anayeielewa vizuri haki aipatayo mtu kwa kumwamini Bwana Yesu akakua katika neema na upendo kwa Bwana Yesu si tu atatoa 10% bali atatoa kwa MOYO WA KUPENDA hivyo si ajabu baadhi hutoa zaidi ya hiyo 10% mimi nawafahamu baadhi ya watu ambao wanatoa zaidi si kwamba wanakipato kikubwa no no no bali wanampenda sana Mungu kwani wana value kile allichofanya Bwana Yesu kufanyika mdhambi in our place, na haki yake was imputed to us we did not labor for!

  Mimi ninachojua ni kwamba kwa moyo wa kupenda mtolee Bwana Mungu wako.

  Kama unataka kuitimiza torati je waweza?? fikiri mara mbili!! Yeye Mungu kwenye Yer 31:31- anaona wanadamu hawawezi na wamekua wanaivunja sheria yake so akaona afanye mpango mwingine.

  Kristo aliposema alikuja kuitimiza torati hakua na maana alikuja kuipa nguvu au kuiongezea labda vipengele fulani ili iwe njema no no no kumbuka kwamba kwa historia ya torati hakuna mwanadamu ambaye alipata haki mbele ya Mungu kwa njia ya sheria maana ilimpasa mtu aziishi kwa ukamilifu sheria zote ndipo ahesabiwe haki. Ndo maana Daudi akasema laiti Mungu angehesabu makosa yetu nani angesimama?? maana hakukua na mwenye haki aliyepata haki kwa sheria. Hivyo basi Yesu alikuja akaiishi sheria yote bila kuikosa ndo maana biblia inasema aliishi bila kutenda dhambi akampendeza Mungu na wanadamu hivyo akahesabiwa kwake kuwa mwenye haki. HAPO NDIPO ALIPOITIMIZA SHERIA YOTE.

  Kilichofanyika ni kubadilisha yaani yeye akatupa haki yake akabeba uovu wetu ambao mshahara wake ni mauti, he died on our place. Wapendwa hakuna mtu awezaye kuishi kwa sheria. Yatupasa tuweke juhudi kuifahamu vizuri neema tuliyopewa

 140. Mabinza,
  umenukuu vema kwamba Torati maana yake ni sheria. na ni sheria iliyotekelezwa katika mwili. Tena kwamba Torati ilikuwa ni kivuli cha mambo halisi. palipo na kivuli lazima kuna kitu halisi nyuma ya kivuli. Yesu alikuja kuitimiliza torati maana yake alikuja kuleta ile halisi. kivuli ni kama tumaini. halisi ikishafika tumaini haliwi tena. torati ilitoka kwa Mungu. na Yesu alitoka kwa Mungu. ningemshangaa Yesu kama angesema torati is fallacy, yaani torati ni kitu cha kipuuzi tu. mwakilishi ni mtu anayesimama kwenye nafasi au mahali alipopaswa kusimama mtu fulani maalum. aliyewakilishwa akirejea bila shaka atamwambia mwakilishi wake-well done, sasa nimesharejea, enenda zako kwa amani, asante sana. ndiyo maana Yesu anasema: sikuja kuitangua torati. yaani sikuja kui-nullify, au kuikejeli, au kwa maana nyingine kuidhihaki, au kuitweza kuwa haikuwa lolote wala chochote. bali kuitimiliza. kwa maneno ya kiingereza tunasema: to substantiate it, au to uncover it to its reality, au to bring it to its wholeness, au to bring it to its tangibility. ukiona kivuli pekee cha mtu bila kumwona mtu halisi mwenye kile kivuli yamkini kuna baadhi ya maswali hutoweza kuyajibu. maswali kama: je, huyo mtu ni light skinned au black skinned? je, rangi yake ya macho yake ni ipi? n.k. katika kutengeneza sera na mipango ya maendeleo, serikali hutakiwa kuangalia mambo mengi. miongoni mwa hayo mambo ni kuzingatia wakati na maendeleo ya kiteknolojia ambapo dunia imefika. kwa hiyo mf. baada ya uongozi wa Nyerere kuondoka madarakani, baadhi ya sera na mipango ambayo serikali yake iliitumia na kufanikisha maendeleo Tanzania, haifai kitu katika huu uongozi wa kikwete kwa sababu ya wakati na dunia ilipofika leo kiteknolojia, kiuchumi,kijamii na kisiasa pia. kwa 7bu sera na mipango hiyo haiwezi kufaa kitu kwa kipindi hiki, kikwete aibeze na kusema huo ni upuuzi? la hasha, bali ataziambia hizo sera na mipango-thanks men! natambua mchango wenu wa dhati. pumzikeni kwa amani sasa. nshaingia mimi wa .com. lakini maendeleo yatakayopatikana ktk uongozi wangu yanamsingi wake kwenu. najua kuna mtu kutoka mirembe humu ataona loops kwenye mifano yangu hii na atataka kuitumia kujinyonga.

  Mabinza, Yesu alipomwambia Yohana Mbatizaji kuwa-yanipasa kutimiza haki yote. hiyo haki yote ni ipi? bila shaka Seleli atasema hiyo haki yote ni zaka. Seleli amekiri kuwa hajaona popote ktk agano jipya Yesu alitoa zaka. na mimi ndo nasema hizo ndo zinaitwa facts na si assumptions zake. eti nasisi tuthibitishe kwenye agano jipya ambapo maandiko yanasema Yesu hakutoa fungu la kumi! very weak! hata kipindi hicho, mafarisayo walifuata agano la kale. hawakumtambua achilia mbali kumkubali agano jipya, yaani Yesu. wayahudi hawaliamini achilia mbali kulifuata agano jipya hata leo. wayahudi hao hao ktk mashtaka yao dhidi ya Yesu wanasema mtu huyu amekuwa akiivunja na hata kuipotosha torati ya Musa. ktk luka 11:42 kuhusu hayo mengine. yes, hayo mengine inaweza kuwa ni torati ya Musa na zaka ikiwemo kama alivyosema Seleli.

  Tujiulize, Yesu alikuwa ktk harmony na mafarisayo na wanasheria kuhusu mfumo wa imani yao kwa Mungu? na je, mafarisayo na wanasheria walikuwa ktk amani na Yesu? kama siyo, kwa nini? na kama nilivyofafanua kwa mifano hapo juu nikaonesha kwamba ikumbukwe Yesu hakuwa na uadui na torati, make atakuwaje na uadui na kuvuli chake, isipokuwa kama halisi imekuja kwa nini niendelee kuhangaika na kivuli chake? kama Yesu alijua mafarisayo na wanasheria hawaitaki halisi wanataka kuendelea kungangania kivuli chake, Seleli alitegemea Yesu angewaambiaje? soma wagalatia 3:21-29 na wagalatia 3:1-14. asante.

 141. Tumaini Nelson,

  Amen mpendwa, asante kwa kunibariki, sifa na utukufu kwa Bwana. Wala usikubali mtu yoyote akubeze wala kukudharau humu. Unayo kweli na umeshaonja Yesu, mtu hakumbandui hapo hata aje na sarakasi za Mtakuja primary skuli au nafuka moshi au anasema yuko makini sana kumbe under serious talks, so cheap! Tena nakuambia ukweli, hasara tuliyonayo sie Wakristo wa zamani, hua tunadhani Mungu sharti atutumie sana sisi kuliko nyie wa juzi! Very wrong! Sasa imagine, just simple test! Mtu makini akisoma points zako na unavyojenga truths na kuiback up na akasoma ya nani huyuuu nani sijui Kiswahili or Kaswahili, nani utadhani ni matured sana? Jibu ni wazi! Si kua ndani ya Dini/Imani/wokovu muda mrefu ndio deal sana bali MOYO wako ukoje na Bwana, hapo ndio mwisho wa majadiliano. Hata hii zaka inayotuangaisha hapa ktk debate, ni moyo tu mbovu ingawa watu wana claim wanamjua sana Mungu eti na kumpeeeenda ile mbaya wakati kuachia tena tushilingi ili mambo yake BABA yao na Watu wake wasonge mbele, inakua nongwa. So chilly out brother, hapa hakiharibikia kitu na niko imara kabisa mwanzo mwisho, we endelea kubarikiwa tu unaposoma na mengine yakiwa magumu napokwangua rough surface, relax cz mwisho wa siku, aim ni super,amen.

  Press on

 142. Mr.Kaswahili,

  Uliponivamia mara ya kwanza wakati unajibu mchango wangu ktk mada hii nilipoaamua kuongelea Utoaji in general kugusia Zaka lightly, uliniambia siko makini na sina facts na substance, kua ungeniitia ambulance na kua labda nina celebral malaria na niliugua degedege nilipokua bebi. Sasa majibu yako ya sasa unanita mimi ni mwalimu wa wajinga na natetea Ulaji wangu! Najua hali yako ngumu kwa sasa ktk hoja na majadiliano(naona tu unavyojibu-so cheap maskini mpaka na-feel kwakweli kwamba, well, umeshajifunza and next time, utamvamia mtu haraka. Lo! ubarikiwe tu ila bwanaa najua yatakutoka tu mengi maana sikuachii mpaka umerudi kundi maana Bwana ana haja nawe kijana wa Yesu mwenye kuhitaji an ICU MASTER JESUS FIRST CLASS ON AIR IN AN HEAVENLY JUMBO JET OPERATION ambayo ataifanya through people na watu wenyewe ndio sie.

  Kwanza ili usiendelee kutenda dhambi bure, MIMI SI MCHUNGAJI,MZE WA KANISA,SHEMASI,KIONGOZI YOTOTE WA IDARA KUBWA NJE NA NDANI YA KANISA YA WALIOOKOKA BALI NI MSHIRIKA NA MTENDAJI WA HAPA NA PALE NAPOTUMWA NA KUAGIZWA NA VIONGOZI NA WATUMISHI WA MUNGU NJE NA NDANI YA KANISA LANGU. Aya si unaona mpaka hapo tu, unahitaji toba nzito brother maana mara nina celebral au nilishawahi nyukwa na degedega, mara rafika yako Sungura akakusaidia kufikiri kua nawinda Uchungaji mara mie mpuuzi,mtoto-toto na kua siko makini na sina facts na substance ktk debate na Ufundishaji hapa, sasa yote hayo baada ya kukuambia mie nani, si unaona mlivyonionea tu bure mie mkaka wa wa Yesu? Sasa unafanyaje na umeshanitenda hayo yote na hili la sasa kua mie teacher wa wajinga na jingine mie mlaji natetea mrija na kitumbua changu kumbe walaa sina kitubua wala bagia!. ILA WEWE NA SUNGURA NA YEYOTE HUMU ASIPOTHIBITISHA MIE NINA MALARIAL CELEBRAL DEGEDEGE HISTORY, MPUUZI, MTOTO,MWALIMU WA WAJINGA,NAIHITAJI AMBULANCE NA NALINDA ULAJI NA MIRIJA KWA HOJA MADHUBUTI NA KUZINGATIA NAYOWAULIZENI KILA MARA LAKINI UKIJIBU WEWE KASWAHILI, HAUGUSII HOJA NA MASWALI YANGU, UNA SWEEP TU, BASI, MWENYE MAGONJWA HAYO NA HISTORY IYO NA TABIA IZO, NA ASIYE NA FACTS/ SUBSTANCES ATAJULIKANA TU TUNAVYOENDELEA KUHOJIANA HAPA BARABARA KABISA

  Pili, ili tusipoteze lengo, katika majadiliano yote haya, Usisahau na nilisema nitalisisitiza hili mara kwa mara kila napohisi/soma na kuona aidha directly au indirectly kiumbe yeyote analeta janja za porini kanisani, kua UTOAJI NI MOJA YA TABIA KUU ZA MUNGU NA IVYO SISI KAMA WANA WAKE, TUNAPASWA KUA KAMA BABA, UNLESS NI WATOTO PORI AU HARAMU. KWAMBA MOYO UNAPOKUA NA LOVE KWA MUNGU, UHIARI UNAKUWEPO AUTOMATIC NA HENCE KUMTOLEA BABA IWE FUNGU LA KUMI,20,30,50 AU HATA ISAKA KABISA, SI ISSUE, NI VITU VINAFLOO TU SIMPLE NA KWA RAHA NAMNA IYO. THUS, HAKUTAKUWEPO NA AKILI MBOVU, SIASA UANAHARAKATI WALA UASASI ZISIZO ZA SERIKALI KANISANI KUANZA KUGOMESHA NA KU KUWAWAZISHA WATU OOH MSITOE ZAKA, MARA AGANO LA KALE AU JIPYA, MARA SILIONI KTK AGANO JIPYA YESU ANATOA NA KWAMBA UKIONA MKRISTO WA IVYO, BASI UNAJUA TU AMEOKAOKA YES, ANA DINI NA IMANI FINE BUT ANA FULL OF STUBBORN DISEASE IN HIS NOTORIOUS MOYO.

  Sasa embu tuyaangalie maneno/majibu yako kama yana kitu/umakini/facts/substance ulizodai unazo sana na wengine eti hatuna-hahaha! Watu bwana, mbwembwe nyingiii kazi zero!

  ‘’kuwa umeshindwa kuthibitisha nilichokutaka uthibitishe ktk agano jipya dhidi ya msimamo wako wa msisitizo spesheli [special insitence] wa zaka, nimekudharau kabisa’’
  JIBU: Wewe kunidharau haina shida yaani wala usipe tabu maana kwa kweli sidhani niko humu au niliingia ktk mada izi kusaka heshima ila nilikua na nia moja tu baada ya kupitia michango yenu nyote kabisa katika mada zote za Milinga ambazo so far tunazijadili, nia hiyo niliyonayo ambayo aidha nimeshaigusia ktk michango yangu au utaendelea tu kuing’amua kadri tunavyoendelea, nitaikamilisha hakika. Ati nimeshindwa kuthibitisha Zaka Agano Jipya!!!!!!!! unless utakua na matatizo mengi aisee, kwa kua nimekupa maandiko ya ‘’Yesu kutoivunja torati’’ ‘’kuyatenda hayo ya kwanza bila kuacha na mengine’’ na ‘’Mafarisayo wakaa kwa kiti cha Musa’’, na ‘’haki yetu isipozidi ya mafarisayo! Sasa ulitaka maandiko au uthibitisho gani zaidi ya huo? Au ukute kabisa neno kwa neno imeandikwa—‘’naye YESU akaenda katika sinagogi na kumpa zaka Farisayo Mkuu wa Misa’’, Si unaona ufahamu wako ulivyo sasa! ndio maana nikauliza, mbona unajua kwa hakika Yesu alioga lakini nkikuomba andiko hilo utanipa mpaka aje Bwana? Hapo nani ana substance na empy sentence btn you and me?

  Ati-‘’badala yake nakuja na assumptions’’-Assumption nyingineni ni tangible si vapour, ziko so Biblical na in alignment with Bibilcal truths-unless uziprove wrong kitu ambacho najua you are too weak to succefully do that pamoja na majingambo mengiii ya mwanzo kabla ya kufahamiana vema, assumption izo zina mashiko kweli kweli na zina bana hasa mpaka haupumui-nakuona tu naposoma reply zako unavyoangaika vibaya na una pa kwenda, kote kote naziba, hapana leta maneno ya street kanisani kwako hapo brorther, toa zaka iyo kwa kanisa lako hapo, shughuli ziendelee na Kuhani wako ale mara moja, ana ruksa iyo toka juu, wacha roho ya uchoyo, ubinafsi na madhara ya shibe ya dona kukufanya kumsahau Mungu eti kwa tushilingi twako peanut wakati wapendwa wana tithe dollars. U NEED TO CHANGE YOUR ALTITUDE IMMEDIEATELY kuhusiana na maisha yako ya utoaji

  Ati-‘’umetumia andiko kwenye agano jipya yesu aliposema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza, na andiko kuhusu criticism ya Yesu dhidi ya unafiki wa walimu wa sheria na mafarisayo ktk mathayo 23:23 na msisitizo wa yesu kuwa inawapasa kuyafanya hayo bila kuyaacha na hayo mengine kama kichaka chako cha kujihami’’Sasa ulitaka nitumie andiko lililoko wapi Quran? surat alihanjamina 45:23! Ooh yes, bora nijihami na kujifichia uko kabisa katika andiko ilo na mengine hapo juu.Halafu kumbe na wewe unalifahamu ilo andiko, kwa nini usilitumie kutoa Zaka leo? Unaona hapo sasa, si umekwisha! Sana sana nategemea ufyatue tena cheche ya lijineno, this time utaniita sijui Professor wa….kazi na kwako!

  Ati-‘’pia ktk mission ya paulo unataka kutulazimisha kuamini kuwa miongoni mwa matoleo na machangizo ku-support injili yaliyotolewa na waumini wa makanisa mbali mbali aliyoyafungua paulo eti miongoni mwake na zaka ilitolewa japo maandiko hayajabainisha wazi tu’’. Na wewe unajuaje Zaka haikuwemo kama moja wapo ya matoleo? Lakini Kipi kirahisi na haraka kuelewa kati ya haya! Kua kwa kua watu walitoa matoleo na walikua na ufahamu mkubwa kuhusu mambo ya zaka ivyo kuna uwezekano hata zaka zilitoka AU

  Walitoa tu nyingine zooote ila zakat u hawakutoa?

  Umesema mwisho kua nina blabla blah! Mhh!Ya kweli hayo? Mbona mweye blah bla yuko wazi tu hapa!

  Press on.

 143. Mabinza,

  Umesena umefutilia mada kwa karibu na bado hujafunguka kuhusu zaka! Aya pole na karibu twende taratibu. Nitaanza na wewe kwa kukuuliza maswali na pia kukuhimiza usome michango yangu yote kabisa kwanza halafu niijie tena kama hujafunguka au umefunguka na kuona hoja thabiti basi tu hutaki! maana baadhi ya maswali uliyouliza, nimeyajibu na mengine nimeyagusia vema kabisa, labda hukusoma michango yangu yote au umesoma lakini ndio ivyo tena, tatizo ni kubwa hapa/humu nalo ni ..moyo! Aright brother, let me try this way ili ufunguke. Soma sasa nyongeza yangu kidogo na Maswali kwakua ndio Majibu yako! Usipuuze kujibu kwa kua kila ukisema, itabidi turudi kwanza hapo ulipopaacha na nadhani wote humu tunapenda usmart ktk kufundishana/challenjiana/ulizana na hata kupingana. Sikushauri ufanye kama Kaswahili maana badala ya kujibu hoja au kukataa hoja kwa hoja, amezidiwa na kubaki kutukana tu( nadhani alifanya faulu kubwa toka mwanzo kuvamia ovyo ovyo)-nitakualika pia utasome majibu yangu kwake mara moja nikishamalizana nawe maana pia nitakayo mjibu, yanaweza pia saidia yako.

  Umesema-‘’Biblia inasema kuwa Torati ni kivuri cha mambo ya Rohoni’’
  SWALI: Je kivuli cha Zaka iliyoanza Agano la Kale ni kipi leo Agano Jipya? Mfano: Ibrahimu Alitoa zaka Agano Kale, leo kivuli chake cha rohoni ni?

  Umenukuu andiko ili-‘’Lk. 11:42 naona inasema hivi, “42Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kutoa matoleo hayo, wala msisahau kufanya hayo mengine.” Kwa mstari huu naendelea kuelewa kwamba zaka ilitolewa kwa mjibu wa Torati, ambayo pia Yesu alipokuja alikubaliana nayo lakini sioni popote kama naye alitoa Zaka’’.

  SWALI:Umesema Yesu kwa majibu yake alikubaliana nayo ( jambo ambalo Mr.Kaswahili anajifanya kipofu), lakini humuoni akitoa Zaka, je kwa kua humuoni ndio alikataa/hakutua wakati unajua na andiko linaonyesha na umesema alikubaliana nalo?

  Umesema-‘’licha ya kunukuliwa akimwambia Yohana mbatizaji kwamba, “tunapaswa kuitekeleza haki yote”

  SWALI: Ndani ya Haki yote ambayo Yesu alisema twapwaswa kuitimiliza, Zaka imo haimo? Na ukimfuatilia Yesu kila aliposema kuhusu Haki e.g. Haki yenu isipozidi ya Mafarisayo, KAMWE HAMTAINGI UFALME, unadhani kati ya haki izo za Mafarisayo ambazo Yesu alituchallenge kuwazidi, ulipaji/utoaji wa Zaka umo au la? kwa maneno mengine Mafarisayo walikua wanatoa hawatoi?

  Umesema-‘’Katika agano la jipya kiuwazi sijaona fundisho lolote linalo onyesha kama Mitume walipata kutoa zaka wakati wote walipokuwa na Yesu ama baadaye’’

  SWALI: Je mitume walitii Maneno ya Yesu kuhusu kuitimiliza haki yote au kutenda kuzidi haki za Mafarisayo?

  ‘’Luka.6:38. Iliyonukuliwa na mchangiaji mmoja, nayo haizungumzii Zaka! Inasema, “38Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.” Hapo napo hapana neno Zaka pale!’’

  SWALI: Umejuaje ivyo vitu vya kupeana/kuwapa Watu hakuna Zaka? Kwani ivyo vitu ni nini? je zaka haiwezi kua kitu cha kupeana?

  Umeoma na kuuliza ivi-‘’naomba kusaidiwa ni wapi kunasomeka kuwa Mitume walitoa Zaka wakati wa Yesu na baada ya yeye kupaa mbinguni?
  Jibu: Nimeshakuuliza kama Mitume walitimiliza haki yote na chini hapo swali ni

  SWALI: Bwana Yesu aliwahi kuoga maji bafuni? Kupiga chafya na miayo?

  Umesisitiza- ‘’tunasimama kwa misingi ya Mitume na Manabii, ambapo mitume wameonya kuwa “Sisi (mitume), malaika ama mtu mwingine akifundisha, mafundisho kinyume na haya tunayoyafundisha na alaaniwe!”

  SWALI: Kwa nini Yesu aliwaambia Wanafunzi wake ktk Mathayo.5:17-19 kua hakuja kuivunja Torati na manabii na ktk Mathayo.23:1-3 kua Waandishi na Mafarisayo wamekaa kwa kiti cha Musa, wayafundishayo Tuyashike na kuyatenda? UPI NI MSINGI WA KUKAMATA ILI TUSILAANIWE SI TU KWA KUFUNDISHA VIBAYA/TOFAUTI BALI HATA KWA KUTOTEKELEZA MATAKWA YAKE?

  Umesema-‘’Neno la Mungu ni toshelevu, Agano la kale linapatana na Agano jipya, ni wapi katika mafundisho ya Mitume wana fundisha utoaji wa Zaka?’’

  SWALI: Kwakua Maagano yanapatana na ingawa huoni ktk Agano moja jambo ambalo linaonekana ktk Agano jingine, je inamaana kwa kutokuliona na wakati umesema yanapata, ni kweli halipo? Na halikufanyika?

  Umemaliza kwa msemo mzuri sana huu-“Ufahamu ni chembe ya uhai!” Ni kweli maana Mungu akishafahamika vema kua Yeye ndiye mwenye vyote na hata siye ni mali yake na kwamba hata ivi vishilingi tunavyomiliki ni vyake na kwamba kwakwe Yeye twaingia na kutoka na kwamba ukimuondoa Yeye ktk maisha, hakuna maana ya maisha haya na yajayo, basi hakuna tutakachobakiza bila kumpa au kupenda mambo yake na watu wake pia Watumishi wake mambo yao/yake yawe swadakta kabisa.Amen.

  TAFADHARI SANA TWENDE POLEPOLE NA KWA UTARATIBU, HOJA KWA HOJA SWALI KWA SWALI AU JIBU ndipo tusonge mbele. MIMI NIKO TAYARI KUJIBU MASWALI YAKO YOTE HATA KAMA NI MIA, NITAYAMALIZA TU SO NA WEWE PIA NIJIBU YANGU.

  Press on.

 144. Na Uzuri tumepewa Roho mtakatifu ambaye ukiwa msikivu yeye ndiye msaada mkubwa ktk kila jambo.Vilevile nimebarikiwa kwa namna unavyoweza kutoa raman na Dira ya namna ya wapendwa wachanga kupita bila kupuuza coz umeona kondoo mchanga mimi nicje nikapotea.MUNGU AZIDI KUKUBARIKI KTK HUDUMA HI NA NAJUA MUNGU ANAPATA SIFA NA UTUKUFU KWA KUWA NA MAJEMBE KAWA WEWE SELELI.

 145. Mtumishi wa Mungu Edwin Seleli Mungu akubariki sana na aendelee kukupa roho ya unyenyekevu ktk huduma na amini utazidi kuvuka viwango vya juu kila cku itwapo.Nguvu ya roho wa Mungu ipo juu yako na inaonyesha ni jinsi gani unavyomsikiliza Roho Mtakatifu ambaye ndiyo msaada wetu!Wengi wanashindwa kufikia kiwango kama chako coz wanatumia akili zao za kibinadadu,uzoefu wao ktk neno thtswhy wanakengeuka coz ya kiburi na kuona as if watu kama Kina Tumaini hawawezi kuwa na jipya coz ya uchanga wao!Bt nimebarikiwa sana na unyenyekevu wako kiroho ambao huo ambao Mungu wetu tunayemwabudu anaangalia.Na wewe ni mtumishi unayependa kujifunza kila siku!Ckushangaa sana nilipo bezwa baada ya kuchangia coz kabla cjaokoka nilijua Kila anayesema ameokoka hawezi kuwa Muongo,mfitini,mwizi.Mzinzi,mwenyekukatisha tamaa n.k bt aftr being born again nilishanga sana kukutana nayo bt I thnk God coz niliendelea na safari ya wokovu na zaidi niligundua wa kuanaliwa c wanadamu bali ni Mungu pekee ambaye amenipa neema ya bure ya wokovu.

 146. Wapendwa,

  Mimi nimefuatilia kwa ukaribu wa kutosha mjadala huu juu ya swala hili la zaka, bado sijafunguka vya kutosha, ningali bado natatanika sana juu ya swala hili la zaka. Torati ni sheria iliyosimama kimwili, Biblia inasema kuwa Torati ni kivuri cha mambo ya Rohoni, na inaendelea kuweka wazi kuwa Bwana wetu kristo alikuja kuitimiliza kweli hiyo na kuifanya Torati kuwa ya Rohoni sawasawa na Neno la Mungu kusema, “Nitaiweka sheria yangu katika mioyo yao” nikisoma ile Lk. 11:42 naona inasema hivi, “42Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kutoa matoleo hayo, wala msisahau kufanya hayo mengine.” Kwa mstari huu naendelea kuelewa kwamba zaka ilitolewa kwa mjibu wa Torati, ambayo pia Yesu alipokuja alikubaliana nayo lakini sioni popote kama naye alitoa Zaka, licha ya kunukuliwa akimwambia Yohana mbatizaji kwamba, “tunapaswa kuitekeleza haki yote”!. Katika agano la jipya kiuwazi sijaona fundisho lolote linalo onyesha kama Mitume walipata kutoa zaka wakati wote walipokuwa na Yesu ama baadaye. Luka.6:38. Iliyonukuliwa na mchangiaji mmoja, nayo haizungumzii Zaka! Inasema, “38Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.” Hapo napo hapana neno Zaka pale!

  Naamini Biblia, napenda kujifunza, naomba kusaidiwa ni wapi kunasomeka kuwa Mitume walitoa Zaka wakati wa Yesu na baada ya yeye kupaa mbinguni? Mbili, ikiwa tunasimama kwa misingi ya Mitume na Manabii, ambapo mitume wameonya kuwa “Sisi (mitume), malaika ama mtu mwingine akifundisha, mafundisho kinyume na haya tunayoyafundisha na alaaniwe!” na kwakuwa Neno la Mungu ni toshelevu, Agano la kale linapatana na Agano jipya, ni wapi katika mafundisho ya Mitume wana fundisha utoaji wa Zaka?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 147. Mr. Seleli,

  Wajinga ndio waliwao. wewe si lazima ni mjinga. bali ni mwalimu wa wajinga. ninaamini unajua unachokifanya. utafanya kila mbinu, halali au chafu kutetea ulaji wako. ni kama mbinu zinatumiwa na chama cha mapinduzi na serikali yake dhidi ya wanaopigania ukombozi, yaani utu, ukweli, uwazi, haki na usawa. siku zote mwalimu wa wajinga sala zake ni wajinga wake wasielevuke. make wakielevuka tu, the deal is over! so ni kufa na kupona kitumbua kisiingie mchanga kama siyo kukosekana kabisa. kwa kuwa umeshindwa kuthibitisha nilichokutaka uthibitishe ktk agano jipya dhidi ya msimamo wako wa msisitizo spesheli [special insitence] wa zaka, nimekudharau kabisa. umeshindwa kuthibitisha badala yake unakuja na assumptions. umetumia andiko kwenye agano jipya yesu aliposema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza, na andiko kuhusu criticism ya Yesu dhidi ya unafiki wa walimu wa sheria na mafarisayo ktk mathayo 23:23 na msisitizo wa yesu kuwa inawapasa kuyafanya hayo bila kuyaacha na hayo mengine kama kichaka chako cha kujihami. pia ktk mission ya paulo unataka kutulazimisha kuamini kuwa miongoni mwa matoleo na machangizo ku-support injili yaliyotolewa na waumini wa makanisa mbali mbali aliyoyafungua paulo eti miongoni mwake na zaka ilitolewa japo maandiko hayajabainisha wazi tu. eti Yesu aliposema-bila kuyaacha na hayo mengine-eti ktk hayo mengine na zaka imo! eti biblia kutobainisha kuwa Yesu alitoa zaka, eti ni sawa tu na vile biblia haijasema pia mahali Yesu alikwenda kuoga! unafaa sana kuwa mwalimu wa wajinga. endelea bwana. na hapo una dili zuri kaka, maana wajinga wa kuwalaghai na blah blah ili wewe uendelee kula kuku kwa mrija wapo kibao!

 148. Kaswahili,
  Nimekulewa kuhusu jina lako sahihi Kaswahili Vs. Kiswahili tho if you ask me, would friendly still pick for you the second coz the first..ooh meen!see/read it again boy! tehe! ( take it easy). Umenipa hongera kwa michango yangu ya mwisho mwisho ku imetulia na eti nimejaribu kuwa articulate kuliko hapo mwanzo. Well, asante though TOKA MWANZO ILITULIA NA PIA KUTEGEMEA UNAMJIBU NANI NA KWA JINSI ALIVYOKUJA BILA KUCHUKUA TAHADHARI ANAVAMIAJE KILA MTU then ili ku-carpet the rough surface, you cruise it more u know, at least once, twice and to the extreme fourfold and so on and as a result, the outer layer which seems rough will go away since its dweling was not yet subjected to deep tests!!!!! Ume note pia ‘’swanglish’ zangu zimepungua! na kwamba ‘’drip ( bila shaka ya kuondoa yale magonjwa mlionibambikiza na yakabarkiwa na jamaa mmoja) ilinisaidia’, Well,my Swanglish ni njema sana kuliko kutukumia ‘mungu’ badala ya Mungu, ‘yesu’ badala ya Yesu, ‘agano jipya’ badala ya Agano Jipya and no paragrapha, many full stops all over na more political and mababu wa kale nukuu than the Bible back up in your writings. I hope to reduce swangilish, as sweet as it is for me, as you FIRST AND SPEEDILY do away your ‘’urgently need prayers’’ way of writings’’ brother Kiswahili( ops! I mean Kaswa….)

  Kwamba kama mimi na wenzangu mngejenga hoja zetu kwa kujibu ktk namna ya kuchanganua [analyse] maswali ya msingi yaliyoulizwa na bw. Jeremiah, yanayotoka ktk hoja ya msingi, ningefurahi sana. Kwanza, am sorry siko hapa kukufurahisha brother kwa kua kwa hakika kuna mengine ya Mungu haswaa nitasema, hutafurahi, so you have the choice kufurahi or kununa e.g. ZAKA ni muhimu kutoa hata leo, na mtu wa Mungu yeyote anaye kazana kuvunja moyo Utoaji in general na specific, ana aidha tatizo binafsi la kiroho au personal sickness against Wapakwa Mafuta walioa wa Kweli wa madhabahuni mfano kuwaonea wivu na kuwachafua eti wanakula kula tu vya watu na wavivu au ana ufinyu wa uelewa wa Neno ktk East-West, North- South dimension if you register what I am talking about, sasa hapo usipofurahi wakati nimesema kweli tupu na ushahidi wa aina ya hao watu umethihirika wazi wazi ktk hoja hii kwa michango yao mbalimbali, mimi ni haja ya kukufurahisha! Ili iweje kwanza? Halafu?. Pia huwezi jenga hoja nyingine kwa jinsi ZILIVYO KAA KAA NA NAMNA ZILIVYOVURUGWA/VURUGIKA kwa moja kwa moja kujibu maswali kama ulivyotaka, aina nyingine ya hoja, unaanzia kwenye msingi ndipo maswali hujiseti tu so simply, hili halihitaji mimi niandike sana tena mseme nina nina memory card nimemeza and in this case itakua active mpaka kwa vodole vya ku-type na kwamba m-card iyo inaonekana live kwenye kucha ikitokeza na kurudi ndani kila mara!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Maswali yako yote haya( angalia hata unavyoandika ni zaidi ya Swanglish problem maaana hujui ktk mambo ya Imani na Bible, huyu jamaa ‘’yesu’’, ‘’mungu’ ni wa kukumewa na kuwatowesha, si wetu) namely- ‘’yesu aliwahi kutoa zaka? ‘’au ktk injili zake ni wapi aliongelea zaka?’’, ‘’na je kanisa la kwanza walitoa zaka?’’, au ni mtume yupi kati ya mitume wa yesu ktk kanisa la kwanza aliyewahi kufundisha utoji wa zaka?’’. ‘’au kama kuna mahali popote ktk agano jipya biblia imesisitiza utoaji wa zaka kwa kanisa?’, Yote yameshajibiwa kwa response yangu kwa Amini Jeremiah, soma na kama una hoja for or against, naisubiri kwa hamu kubwa sana.

  Umesema ‘’Mr. upo tayari kutulia miguuni pangu na kujifunza endapo unaweza kujibu maswali haya kwa uthibitisho dhahiri and with articuracy. usianze kuruka huku na kule tena. la sivyo malaria itakuwa bado imo. bw. Seleli’’ At least your are coming down now, kwamba uko tayari kukaa miguuni kujifunza kwangu! Mmh! wonderful change of intention! Why? Umeona nini? ooh sorry, condition yako ni mpaka nijibu maswali! Well, let us think here , kama nisingejibu maswali, ungepata uhalali wa kutotoa na kuendelea kupinga zaka na kuvuruga watoaji wake si ndio? Aya another thought (we si umesema una penda facts bwana na substance au sio wewe?, aya tuendelee, let me see if kweli au mbwembwe tu)-Ok, sasa nimeshajibu maswali yako/ya Amini Jeremiah, je kama ukitaa kukubali kwa hoja zako dhaifu, si yanarudi yale yale tu?-ile roho itendendayo kazi ndani ya kugomea utoaji e.g zaka?

  Conclusively then, bora hata usisome majibu kwa kua ktk mambo ya imani, kama ndani kumeshaingia kitu ingine, hata kama angejibu Malaika Gabriel na Yesu kuchukua kidole chako na kukigusisha kwa ubavu wake, yet ungeibuka na mengine. Kama moyo wa Kutoa haupo, haupo tu, nenda semina zote, kaa kwa miguu na mabega ya manabii na mitumje wote, pat ash kumi tu au billion, hutakaa ubadilike kama hujaamua kupondeka ndani kwanza. Mambo yote yanaanza na wewe then ndio miguu ya akina Seleli( ingawa in this case na kwa nature yako hii, better find another teacher/brother and I strongly suggest to you Sungura and Lwembe, I will be there in that seminar as an observer ila ole wenu mnipe mic kwa nusu tu, you will see and conclude indeed I have eaten memory card from CHINA ya JUU and dozi probably haijanisaidia because ‘’verily, verily I say unto you, no stone of suffocating/diluting/polliuting/devilishly and humanly contaminating UTOAJI WA AINA ZOTE PAST,PRESENT,FURURE IN ALIGNMENT WITH JESUS TRUTHS AND OF OLD TESTMENT TRANSFERRED TRUTHS IN NON- VIOLATION OF JESUS’ ONES, shall be left unturned!)

  Umesema..’’Ninaamini ktk utoaji kabisa. wala sipo kinyume na kutoa mali zetu kwa ajili ya ufalme wa mungu. ni kweli kabisa mungu ndiye aliyetufundisha utoaji at the first take. alipomtoa mwanae wa pekee na kipenzi kwa ajili yetu tuliokuwa waasi na wakaidi mbele zake. na namna ya utoaji ambayo naamini kuwa ndo sawa ni ile ambayo paulo ameifundisha ktk 2wakor 9:6-8, iwapo mtu anataka utoaji wenye kuambatana na thawabu ya mungu’’. Wow! you are a good boy now aah! Nakuona unakaa vema sasa eee! Basi barikiwa na. FANYA IVYO NA UTAISHI, kelele na maneno mengine against major tabia hii ya Mungu wako huyu na madhabahu za Bwana na hao aliowawakamata watutumikie/wamtumikie, ukiendelea nayo, U WILL NEVER OUTSMART GOD, SANA SANA, UTAISHIA TU KUBAYA.

  Kwamba ‘’Sungura alichanganua vizuri kabisa kwa kuonesha zaka ilianzia wapi ktk agano la kale. akaonesha kwamba kwanza zaka kwa mara ya kwanza ktk agano la kale inaanza kutolewa na ibrahim na kisha yakobo kabla haijaja kuwa sheria baada ya waana wa israeli kurudi kutoka utumwani misri. makusudi ya mungu kuifanya zaka kuwa sheria sungura kayaeleza. na kwamba baada ya ule ukuhani kubadilika kuliondoa usheria ktk utoaji wa zaka, kaueleza pia’’. Maelezo yake yake yalikua mema, hamna jipya hapo, yamo ktk BIBLE-soma maandiko aliyotoa Amini Jeremiah, pia yako maandiko mengine kuhusu Zaka ingawa Yokobo hakuwahi kutoa in the first instance, alihaid!!!!!!! Na kama alijua Ibrahimu alitoa kabla ya sheria, why aingize mawazo ovyo ya kusema makanisani watu wametungiwa sheria wakati tunatoa kwa kupenda na hakuna aliyewahi shitakiwa au fungwa au tengwa kwa kutooa zaka kwa KANISA LA KWELI? au kuweka bahasha spesheli za zaka ili kutrack/ensure well record za finances for reporting kwa vikao vya ndani na nje ya Kanisa, kuombea grant nje au serikalini ili kufanya vitu vya maendeleo ya kimwili pia e.g. kusaidia hao mnaosema sana namely yatima, wajane, street children au kupata support/loan banks which would like to see kwanza ktk vitabu how stable income ya kanisa ilivyo kabla hawajaachilia grant au loan, halafu sytems izo za well financial management kwa waliokoka ambao zamani tulidharauliwa kua mambo yetu tunaendesha shaghalabaghala/kipendwapendwa tu, hamna professionality bali kiroho-roho tu 24/7, ndio mnaita/mnatafsiri kua ni sheria, kufuatiliana, kulazimishana! Such beyond control defects katika comphrehension ya mambo mema!

  Unaona jinsi gani mtu akisha ruhusu kuharibu moyo wake, hata kitu chema kabisa peee, kinakua devilish tu kwa akili yake! No wonder BWANA ALISEMA linda sana moyo wako, maana uko kuna sorce ya mambo mengi kama si yote-Mithali.4:23

  Kwamba ‘’Sungurs akasema kama kuna mtu anadai hili kusudi la mungu halikubadilika hata ktk ukuhani mpya atuoneshe ili kututhibitishia hili ktk agano jipya. Mwambie asome majibu yangu kwa Amini Jeremiah na kisha aje na issue yoyote kama hajaelewa au anapinga, will right there for him. Pia yeye anaweza onyesha kwanza wapi KUSUDI liliwahi badilika. Napenda kusoma iyo kwa macho yote mpaka na tochi then nitajibu haraka sana.

  Unalalamika kua..Kwa nini zaka iwe special offering namna hii kanisani’’ kwa nini kutotoa zaka ndiyo tu kunahubiriwa ndiko kumwibia mungu na si matoleo mengine?’’ Kwanza uspesheli aliunzisha Mungu mwenyewe eg imagine this…si kitu cha kawaida kabira zote kutoa tenth kuipa kabisa moja tu! thas great uspesheli isn’t it? Pili, mhubiri wa kwanza kuhubiri/ kuisemelea/kugusia iyo toka Gen-Agano Jipya si Watumishi leo ni Mungu mwenyewe mpaka kuwaita Watu wezi! Tatu, ili Watumishi wasiseme sana, TOA! SIMPLE AS THAT. Kama chakula hakipo gharani na nyumbani mwake Mungu watu njaaa, kazi zake Mola mwenyewe zinakwama lakini hapo hapo mnataka/manategemea mnapokunja kanisani, mkute mambo yote safi, hii si fair! Ni lazima Watumishi bila kumung’unya maneno au kubembeleza, wawachape na Neno tu, wawakemee na kurudia rudia mpaka mtakapoelewa/ lainika/guswa au kama vipi, mtoweke hapo na muhame church iyo maana nyie wakorofi na hamfai kukaa nyuwani mwake Bwana maana mpo hapo kama wapitaji, hamtaki kijiuhusisha na mambo ya nyumbani kwenu na wala hamna huruma na watu ambao mnataka sana wawajibike pale mnapokufa, kuzika, oa, mnaumwa,mnapotaka maombi, recommendation letters, referees, kuwachambulia Neno nk.kuendesha gari kuja nyumbani kwenu kukuona na watoto nk

  Eti unashangaa ivi-’’bahasha zenye majina ya mtoaji wa zaka na lisiti za zaka ni za nini kwenye baadhi ya makanisa? JIBU SOMA JUU NIMESHAKUPA- yaani kuokoka ni kua smart/professiona pia, kama una hisia kua unafuatiliwa, ni kwakua una matatizo ktk nafsi yako ktk utoaji, una taka kukacha au kuwepo na ka mpenyo ka kufanya utakavyo! Kama unatoaga na unapenda sana kutoa na unasikia ni tamu na raha sana kutoa kwa Baba na unafurahi kweli mambo ya Mungu, Kanisa na Wachunga wako yanapokwenda safi, kwanini uone bahasha na risit nuksi kanisani wakati wenzio wanahangaika na smartness tu ya utunzaji wa fedha? Mbona wengine tunaona safi tu, ishu nini hapa? personal or all the whole church matter? Jibu unalo. Lalini hata ivyo, kwani izo bahasha na risiti zikidumu ili zikusaidie kukukumbusha( a reminder tool wajibu wako kwa kanisa na Kuhani wako kama mwana wa hapo kwenu na hata maendeleo ya jumla ya kwenu hapo na wahitaji, unaona nongwa gani? Mbona Mungu amewakumbusha watu toka Gen-Agano Jipya? Cant you connect the two?

  Umeuliza-‘’Hivi kuna watu wangapi makanisani wanaoitimiza hii sheria sawasawa? yaani wanaotoa zaka sawasawa na kamili? je, unaweza ukaniambia namna hii zaka si kongwa kwa watu wengi makanisani? unaweza kuniambia namna hii watu wengi makanisani hawako guilt kwa kumwibia mungu, kwa kushindwa kutoa zaka sawasawa?’’ Wanaweza kua wengi au wachache au hawapo kabisa! Lakini iyo haindoi/halalishi wizi na uzembe kwa watu hao. Kama hawatoi zaka kamili ni simply vibaka hao! Ni kongwa kwa wale tu wasiotoa na wana-siasa kanisani na wale walio shiba kisha kuanza kumsahau/Kutomuheshimu Mungu kwa mali zao. Yes watakua guilt tu as long as hawatoi zaka kamili mpaka hapo watakapotubu na kuacha utani kanisani. Ni kweli kumbe unajua wanamuibia Mungu haswaaa na ogopa mwanadamu akifikia hatua ya kuiiibia hata mbingu siyo BOT au kambi la JWTZ kwenye ulinzi wa kutisha!

  Ati‘’Kwangu zaka ni sawa na matoleo mengine tu. ntatoa zaka yangu kama walivyotoa kina yakobo. kwamba-kwa kuwa bwana umenifanyia au umefanya hili nitakupa 10 percent au hata 20, au hata 50 Percent ya nilicho nacho. sifungwi kamwe ktk hili’’. Kwanza soma Biblia yako tena, Yakobo alionyesha KWANZA moyo wa kutoa kwa kuahidi kutoa tenth, uwe makini ktk usomaji wako wa Neno, be attentive to details! Yes Zaka ni aina moja wapo ya matoleo lakini ina kautaratibu wake ivyo si vyovyote tu utakavyo bali ni tenth of… so usitoe fifth or fourth of…unanzia tenth kupanda… na kama umesema hata 20,50 unaweza toa basi sasa unaanza kuelewa kua kukiwa na uhiyari na love, you can be crazy for Jesus/God to do like never before, hongera! Tunza hii roho/moyo/ufahamu wala usichafuliwa na akina Sungura na wenziwe, hatari! Ila hata kama wakichafua, tutateketeza kila uchafu mara moja kwa nguvu za hatari in Jesus name or his glory, amen.

  Umenipa kazi hii-‘’la unidhibitishie katika agano jipya kama nilikuta hapo juu, nipo tayari kutubu ukiweza kunithibitishia’’ Kwanza nikupe hongera unaendelea kua ‘’good boy’’ mpaka uko tayari kutubu in case… Ila pamoja na kwamba uko good boy, nakuhaidi, ukigeuka tu any time, nitakua tayari 24hrs kukurejesha! Au kuuacha upotee lakini baada ya mambo mengi mazito kuachiliwa hapa! Ili utubu or not, soma majibu yangu kwa Amini Yeremiah kisha ninakusubiri kwa hamu! Kama umetubu au umegoma nione namna gani kuandaa dawa/this time dozi ni kukutibu wewe, me no more degedege or celebral au upuuzi disease from its carrier! guess who is that!

  Umekiri ivi vema sana‘’Sina shida na utoaji kanisani na hata nje ya kanisa. naomba usinielewe vibaya. ni kweli pia kwamba watumikao madhabahuni wanahaki kula madhabahuni. wala sina shida na hilo’. Hongera na fanya ivyo uishi, ukichafuliwa na jamaa hapa, tutauvamia uchafu huo hamna mfano, sharti nuru na giza viwe separate!

  Hapa umeanza matatizo/ugonjwa tena..‘’lakini matoleo yanayotolewa madhabahuni, au na michango mingine kanisani si haki ya kuhani tu. mashemasi wangapi wanapewa fungu? wambaji wa sifa wanapewa fungu? wengine mpaka wanamaliza mazoezi wanakosa nauli ya kurudia makwao wanaanza kuwaombaomba wenzao. wajane na wazee wanakumbukwa? wasiojiweza makanisani wanasaidiwa? makanisa mangapi wanafanya hivyo? kunafungu linalotengwa kwa ajili ya kuwatembelea wagojwa mahospitalini, wafungwa magerezani na maskini mitaani ili kuwabariki na kuwaonesha upendo wa mungu kwao?’’. Wewe toa and nenda kwa amani home assured of smartness ya data base managers wa ya mbinguni to capture it(Rev.20:11-12). Hao wote wanasaidiwa inapowezekana nyinyi nyote mkitoa KAMILI na KWA UAMINIFU-sasa kama kati ya washirika 1000, watoaji hasa ni 40, unategemea nini? na tena kati hao, kambare ni 15, wengine wote dagaa, si unanielewa lugha iyo, aklili tu wala si ufunuo inakupa jibu!

  Usema ivi-‘’bwana yesu alionesha njia alipowaosha wanafunzi wake miguu’’. Una maana gani andiko ili kwa hoja mezani? Pia umesema philosofia nzuri tu izi( it is good to think hata kama tuko rohoni hasa utapokaanza/kuendelea kutoa vyote/yote bila siasa- ‘’mama hawezi kula kabla watoto wake hawajashiba. kuku huwachakulia watoto wake kwanza wale. hawezi kushiba kabla watoto wake hawajashiba. huwezi ukatarajia kuvuna bila kupanda, kupalilia, kumwagilia maji, na kutia mbolea. huwezi kutegemea kupata maziwa bila kwanza kumlisha sawasawa na kumtibu mbuzi. siwezi nikawa mchungaji wa kanisa, mimi niko njema wakati kuna washirika wangu wamechoka, na kwao habari njema si njema. siwezi nikawa mchungaji wa kanisa nikafundisha hesabu ya kutoa kabla ya kufundisha kwanza hesabu ya kujumlisha na kuzidisha’’. SASA SWALI: nionyeshe kanisa ambalo hali izo zote hazipo au wachungaji wake wamefanya the best na kanisa ilo lote , kila mtu mambo safi? Nipe mifano ya Tz, Ulaya unakopenda, nenda kwa brother wetu juzi alikuja hapa TZ na sehemu nyingine?nipe mifano toka kwa Dr. Young mwenye kanisa kubwa duniani au yale mengine makubwa ya ajabu ya Nigeria? NAKUHAKIKISHIA MPAKA YESU ANARUDI, SIKU ZOTE MASKINI MTAKUA NAO NA PIA WAHITAJI. Therefore, thinking yako iyo juu ni njema kweli but Biblically and in regards with Christinity History and churchish Practice/ experience, it is knocked out and rendered useless.
  Press on.

 149. TUMAINI NELSON
  Mpendwa Mtoto wa Mungu wa thamani sana Tumaini N, kwanza nimefurahi kusoma unasema waziwazi kua UMEOOKA! Great proclamation and confidence maana leo tuna baadhi ya Wapendwa ambao si tu hawajitambulishi waziwazi kua Yesu ni Master kwao lakini hata ukiwawahi hadharani mbele za wenzao ( shuleni/ vyuoni/ maofisi/ marafiki/ majirani/daladalani nk) na kuwasalimia kwa furaha kabisa na kwa sauti kubwa-‘Bwana Yesu asifiwe’, jinsi atakavyokwepa, itikia, badilika uso, toa sauti,ni kama anakuambia kwani lazima kusalimia kwa sauti au lazima salama ya kanisani hapa, Mungu atusaidie!. Bless u bother for not being ashmed of JESUS your Lord na Yeye mwenyewe anapenda sana iyo ya kukubaliwa/ kukiriwa/ kutambuliwa/ kutangazwa/kuinuliwa/ kutambulishwa/mfuasi wake kuji-identify naye hadharani- Luka.9:26, Marco.8:38. I love it na kwangu si kitu kidogo hasa kama ulivyosema wewe mwenyewe kua huu mchanga

  Pia ingawa umesema u mchanga lakini UMENISHANGAZA kweli kweli Tumaini N kwa baadhi ya maneno uliyosema ktk response yako nayo ni ‘’Tupeana hoja kwa hekima na busara bt si kuweka na mambo ya kubezana au kupondana!, NA ‘’Lengo kubwa nikuelimishana kwa kufuata maelekezo sahihi ya Neno la Mungu!Bila kuweka interest binafsi! NA ‘’Naamini Mungu humpenda mtu ambaye ni mnyenyekevu mbele zake’’ NA ‘’!Wapendwa ningebarikiwa sana kama mgetumia Lugha ambazo hata mtu ambaye hamjui Mungu anakuwa hatii shaka!’Coz kuna lugha ambazo zinatumika as if ni mipasho au kudharauliana na kama vile kujiona mmoja ni bora kuliko mwingine! NA ‘’Hivi Kwa maneno hayo Roho Mtatifu ambaye ndiye msaidizi wetu ktk kila jambo yupo? JESUS CHRIST my Lord and saviour! Na unasema wewe ni mchanga bado. What God given wisdom is this man of God Tumaini! UMENIGUSA, UMENICHALLENGE SANA, UMENIFUNDISHA MIMI KAKA YAKO, UMENIONYA VEMA SANA MIMI NDUGU YAKO KTK BWANA NA NIMEPATA KITU SAFI KTK ROHO YANGU, NIMEMEZA YOTE ULIYOSEMA NA WEWE UMEBARIKIWA NA GREAT IS AND SHALL IT BE YOUR WISDOM AND GROWTH IN JESUS,Amen.

  Tena pamoja na uchanga wako, katika mchango wako mwanzoni ktk mada hii, uliwahi sema ivi’’Somo la utowaji limekuwa mtihani kwa wakristo wengi na hii ni kwasabu waliyo wengi ni wachoyo!Huwezi ukawa mchoyo then ukategemea utapata baraka.Utowaji ni lazima( bila shaka ulikusudia kusema ni muhimu-naiona point yako nzuri tu kwa mtu mwelewa) kwa kila mwamini tukianzia zaka,malimbuko,dhabihu n.k.Cku zote wapendwa tumeshindwa kubarikiwa kwasababu ya roho ya uchoyo! Ukitaka kubarikiwa zingatia utoaji’’ Nataka nikwambie kwa nguvu nyingi sana kua kama huu ndio uchanga na udumu mpaka Master atakapokuja na usije KOMAA NA WALA KOKOMAZWA UKAONDOLEWA KTK UFAHAMU HUU, kamwe husiruhusu mtu yeyote hata kama ameokoka miaka 80, kukutoa ktk msingi na MOYO huo wala kukuingizia tafakari nyingine.Shikilia hapo hapo kisha utamuona Mungu kuliko wale wa miaka 6, 10, 30 ktk Bwana waliokomaa sana kupitilizia.

  Pia ktk mchango wako huo huo statemet ya mwisho ulishauri ivi-‘’Mtumishi nashauri somo ungefundisha SOMO LA UTOAJI KWA UJUMLA ili watu wasipitwe na baraka ambazo Mungu anazishusha’’. Najua kwa jina ‘Mtumishi’ ulimaanisha kati ya wale waliokua wanachangia wafanye iyo kazi, haikufanywa bahati mbaya sana na badala yake zikaingizwa siasa na janja za Kibinadamu, interests binafsi and personal resistances kuambukiza watu same rebellion against Neno la Mungu na wapakwa mafuta wale WA KWELI Watumishi wa Mungu Walawi wetu wa leo na hata pale wewe mwenyewe ulipochangia huu huu mchango na kugusia sadaka nyingine ( mimi nilielewa kirahisi kabisa kua ulikua una fanya attempt njema ya kuoyesha aina za sadaka ili kusisitiza hoja yako ya Utoaji ili kumtolea Mungu zote aliye yote ktk yote kwa maisha yetu), again bahati mbaya, baadhi ya wachangiaji, wakakudaka juu kwa juu na kuubeza mchango/nia safi ya moyo wako. Sasa mimi nilifanya kazi iyo-SOMO LA UTOAJI IN GENERAL AMBALO AMINI JEREMIA AMEONA IYO NIA YANGU THABITI NA YA MBINGUNI KABISA KWA NINI NICHUKUE MUDA KWA MAKUSUDI YA NGUVU KABISA AMBAYO BADO YAKO MADHUBUTI TENA TENA KULETA SOMO HILO, BILA SHAKA UMESOMA SOMO ILO NA KAMA BADO NA KWAKUA UNA MOYO HUU NA HATA IVYO ILIKUA NI KIU YAKO KUPATA SOMO ILO LOTE LA UTOAJI IN GENERAL, SOMA SASA IVI NA KWA KUA UMESEMA UNAJIFUNZA NENO KWA BIDII, UKIPENDA PRINT KABISA SOMO ILO, NUNUA FAILI YAKE, TITLE IT ‘SOMO LA UTOAJI’, THEN PIN THEM IN AND KISHA ENDELEA KUJAZA MASOMO HAYO YA UTOAJI NA MICHANGO MINGI HUMU UTAKAYO ONA INAKUFAA KUHUSU UTOAJI.WAWEZA PATA MAFAILI MENGINE KWA MASOMO MENGINE PIA NA BAADA YA MIAKA 3,5 YA WOKOVU WAKO, WEWE NI NA UTAKUA MTU HATARI SANA KTK MAMBO YA UFALME KWA UTUKUFU WAKE. NAHUHAKIKA KWA JINSI NAKUVYOKUONA KTK MANENO YAKO YANAYOWAKILISHA NDANI UKOJE/MOYO WAKO KUHUSU KUMPENDA MUNGU, UU IMARA SANA WEWE NA JINSI UFAHAMU WAKO ULIVYOFUNGUKA KUHUSU UHIARI NA LOVE YA KUMTOLEA MUNGU ULIYONAYO, UTAKUA NA UWEZO WA KUCHAMBUA KATI YA GUGU NA NGANO KTK MICHANGO YA WATU MBALIMBALI HUMU.

  Pia ulishauri, ‘’Ebu tusome neno la Mungu kwa kumruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutafsiri tusisome kama vile ni hadithi au gazeti’’ THIS IS POWERFUL STATEMENT AS FAR AS AM CONCERNED. Kwakua Yesu alisema hakuja kuitangua torati ila kuitimiliza na moja ya mambo ya Torati ni Utoaji mbalimbali eg ZAKA na kwakua Yesu mwenyewe ndio final role model etu ivyo tunafuta alivyoonyesha/sema namna anavyotimiliza Torati( karibu usome response yangu kwa Amini Yeremia kwa makini na kama utapenda, kukuibuka somo la aina iyo, ninaweza ongea kidogo kuhusu Yesu na kuitimiliza Torati e.g moja wapo kwa kusema ivi ktk Mathayo 23:23 na kwa kua alisema pia Mafarisayo na Masadukayo wana kaa ktk kiti cha Musa ivyo, wayafundishayo tuyashike na kuyatenda( which also simply meant kuyashika na kutenda wayafundishayo yale ambayo hayata athili Kweli za Yesu mwenyewe( always remember Yesu ni final role model) alizoleta aidha mpya au alizotimiliza/fashion to suits his from zile zilizokuwepo za Musa na kwa kua torati na manabii vyote utimilifu wake ni Yesu na kwa kua Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii ambao nao, hawana misingi yao kivyao bali Yesu ambaye naye pamoja na yake mengi mapya( ana haki hiy kama Kuhani Mkuu zaidi ya Musa) ila yako kadhaa aliyojenga kwa Musa THEN hakika kama ulivyoshauri, tukisoma Neno kwa kuongozwa na Roho kutafsiri, huyu Roho ambaye YESU AMEMSEMA HATANENA YA KWAKWE au KWA MAMLAKA YAKE MWENYEWE BALI ATATWAA YALIYO YAKE ( YESU)-wow! great, what a great protocol /order/system! Tunarudi kule kule kwa Msingi-Yohana.16:12-14), RM KAMWE HATAKUTAFSILIa KUA KUTOA MATOLEO e.g. ZAKA ni fundisho potofu au la kuzimu au la kibinadamu.If that happens, rest assured,it will not be the Holy Spirit, rather something else is operating!!!!!!!!!!!!

  Katika yote, I give you this thinking- MOYO UKISHA PENDA kitu/mtu bwanaa hata katika mambo ya kawaida ya maisha e.g. Wachumba, Wanandoa, Kula, Kusafiri, Kusoma I am telling u, hata kama kuna nini, ufafanya tu jambo kutimiliza love yako kwa kitu icho. Unajua kwa kufikiri ivi, unaweza fahamu kwa nini Ibrahimu alito zaka na Yakobo kuhaidi kutoa wakati kulikua hakuna references wazi wazi za mafundisho ya Mungu kuhusu mambo haya kwa wanadamu kama wakati wa MUSA ndiposa unaweza elewa kwa nini Mungu aliwahi sema, ataandika sheria mioyoni mwa watu na Paul alipokua akijibu hoja kuhusu watu walikuwepo kabla ya YESU AU KUSIKIA KUOKOKA WATAHUKUMIAWAJE, aligusia ndani ya waadamu, kuna KWELI tayari. Sasa kama naweza fall in love na mdada mzuri wa Bwana halafu bila hata kufundishwa, vitu tu vikajiseti moyoni kumfanyia mpenzi wangu huyo kwa raha zote na sacrifice za kutisha sana hazina mfano mwanzo mwsiho, je kwa Mungu ambaye baaada ya mbwembwe zote za duniani izi, hatimaye nitatoweka kisha nikutane naye uso kwa uso, si zaidi sana nikafanya kwakwe? Nadhani umebarikiwa mwana wa Mungu kwa tafakari yangu hii toka michango yako 2 ktk hoja izi za Mr. Milinga. Ubarikiwe tena na tena na dumu ktk Bwana na ikitokea unakuta Baba na Mama, Waalimu shuleni, Kaka na Dada Wakubwa home,Wachungaji, Wazee, Mashemasi kanisani nk ‘’wanagombana’’ ( a good fight I should hope at least) mbele ya Watoto, Wanafunzi class, washirika wachanga Sunday school lo! bahati mbaya kweli ila uzuri ni huu…Yohana.6:36 ‘’Wale wote alionipa Baba, nisiwapoteze…… Hence, kamwe hutapotezwa/potea hata kama siye akina kaka ‘’tumetumiwa/tumejitumia vibaya’’ NI SERIOUS ISSUE KWA BABA YAKE NA EXTREME ASSIGNMENT KWA ALIYETUMWA(YESU) NA BOSS WAKE MUNGU BABA), ku-make sure, kwa kweli haupotei/hatupotei. Na utajua ukipewa a VERY SERIOUS TASK NA BOSS WAKO NA WEWE MWENYWE HATA IVYO, IYO TASK UNAIPENDA VERY SERIOUSLY TOO,NO MATTER WHAT IT TAKES, YOU WILL DO ALL, IN AND OUT OF YOUR CAPACITY TO SEE IT THROUGH.

  Press on.

 150. Amini Jeremiah Shalom.

  Kaswahili( unaweza soma hapa kwa maswali yako yote lakini pia ninaandaa spesheli kwa ajili yako wewe baadae kwa yale ambayo sitayagusa hapa)

  Mr. Jeremiah Amin-I think kati ya wasomaji wote visible hapa so far kwa mada/hoja hii, umekua tofauti kidogo so nikupongeze kwa KUONA/KUDAKA kwa dhati( I felt it when reading your comments about my subject).Nakuhakikishia nilipoona vema kuzungumzia subject nzima ya UTOAJI kisha ZAKA kwa UCHACHE au KIRAHISI( NI MAKUSUDI PIA maana niliona ukisha maliza ng’ombe mzima, mkia si ishu sana ya kuangaika nayo), sikua mjinga hata kidogo wala mpuuzi, labda nina celebral malaria au nilipokua bebi nilinyukwa na degedge kama walivyodai watu wa Mungu hawa Sungura na Kiswahili. Sitasita kugusia msingi huu wa tabia mojawapo KUU SANA ya Mungu kila mara mbali na ile ya Utakatifu, KWA UJASIRI MWINGI maana msingi ukiachwa basi kila mtu atatawaliwa na akili mbaya (ziko nzuri)/janja/ujuaji/siasa zake tu sasa. Sifa na Utukufu kwa Bwana kwa yote uliyosema kuhusu mie na somo langu na namna nilivyolileta, bila uwezeshwaji wa Bwana na uvuvio wa Roho wake ingekua ngumu kuwakilisha nilivyofanya , once again in JESUS NAME, ALL THE CREDITS BACK TO HIM, Amen.

  Now, back to business brother, ume raise concerns namely ‘’umepatwa na mshituko mkubwa nilipoona kuwa nami nadhani mafundisho ya utoaji wa ZAKA ni kati ya mafundisho stahiki ya utoaji, pia ‘Hakuna hata aya moja ambayo umejaribu ama kuelezea kuwa ZAKA ni SADAKA/TOLEO linalopaswa kukabidhiwa kwa kuhani kama yanenavyo maandiko na ’’Na kama Zaka imewahi kuwa toleo la kupelekwa madhabahuni kwa Bwana katika wakati wowote ule’’. Jibu ni KWELI KABISA, HUTAKAA UPATE MAANDIKO hayo ‘live-live’ au neno kwa neno mfano- ‘’Amin, Amin nawaambeeni, yeyote asiyepeleka zaka kwa Kuhani/Mchungaji wake wa kweli, hakika hatauona ufalme wa Mungu’’ au ‘’Hakika nawaambieni enyi kizazi cha nyoka,toeni zaka zenu madhabahuni pa Bwana kila mpatapo kipato!!!!!! Sasa kama watu wa Mungu or in effect tuseme kama Wanae Baba wa Mbinguni, katika kile kicho cha ndani cha kumjua Bwana na kumpenda kwa dhati na Roho wa Mungu ndani yetu, hua tunawezaje kujua na kuzitendea kazi KWELI nyingine za Biblia hata kama hazikuandikwa wazi wazi? Hua tunafanyaje kwa mambo hayo? Sasa kwa swali hili inayolenga kujibu concerns zako NZURI pale juu, taratiiibu nisome hapa maelezo/hoja zangu kisha utafanya maamuzi kama kuna hoja umeridishwa au la halafu tuhitimishe aidha kwa kua na msimamo mmoja au miwili halafu ajabu yake, wote tubaki salama na kisha tukutane kwa Baba one day.

  Labda kabla sijaenda mbali, ili kuumba practical part ya swali langu pale juu, kwakua umesisitiza ktk concerns zako kupata ushahidi KAMA YANENEVYO MAANDIKO, nikuulize haya yafutayo:

  (a) Hua tunajuaje kua kunywa ( sijasema ‘kulewa’) pombe ni dhambi! vivid andiko? Angalia sijakurupuka kuuliza hili!

  (b) Hua tunajuaje kuvuta sigara, bangi,mihandarati ni dhambi! vivid andiko?

  (c) Tunaweza vipi kuwaambia wapendwa wanao fanya kazi viwanda cha sigara, bia, vitengo vya afya ambao wanagawa condoms ili wa Tz wasife kwa kufanya ng’ono zembe nk? Why tunawabanaga wao kama Wateule waache kazi izo ! vivid andiko?

  Namna ambazo mimi/wengi wetu tumeridhika kwazo kua kulipa/kutoa/kuleta zaka leo kwa sisi wa Agano Jipya ni sawa kama ilivyo vema kabisa kumpa Kuhani, ni izi zifutazo:

  MOSI: Zipo BAADHI ya kweli za Biblia zinahama moja kwa moja KAMA ZILIVYO toka kabla na baada ya sheria Agano la Kale to Jipya. Yesu ni kwanza kuzihamisha au kuzitumia na hata wanafunzi wake ktk occasions mbalimbali kwa mfano tendo la imani la Ibrahimu mpaka leo limetuletea baraka, Yesu kutumia nukuu kadhaa za kale ktk mafundisho yake kama walivyofanya wanafunzi wake, mfano Paul, Stephano na Petro. Kwa ivyo, kuchukua ya Agano la kale kwa mantiki hii na kuyahamisha/ kuyafanya/ kuyatumia leo ni truly Biblical act and it is justified kabisa pasi na shaka yoyote, hence kama Ibrahimu alitoa zaka- Mwa.14:18-20 na Yakobo alihaidi kutoa zakaMwanzo.28:10-22(notice:alihaidi-hapa cha muhimu ni moyo unaomrithia Bwana na kutaka kutoa zaka na waliyafanya hayo kwa hiari kabla ya sheria, no wonder LEO NITATOKA ZAKA KWA KUHANI au kupeleka Nyumbani mwa Bwana( ambako ofcoz Kuhani na hao wakaao/tumikao humo, wapo).

  PILI: Katika Mathayo.23:23 Yesu anasema-‘’Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Hapa at least ni wazi Yesu amegusa moja kwa moja issue ya zaka lakini comment yake ndio kwangu hoja ya msingi. Kwakua amegusia kulipa zaka izo na akasema, hayo imetupasa kuyafanya, ni rahisi kuamini kua katika kutaja aina za zaka, angeweza taja zote lakini kwa kuto zitaja zote haimaanisha amezifuta na ndipo sa kwa kusema waendelee kuyafanya, basi kutoa zaka todate is justified.

  TATU:KatikaMathayo.23:1-3-Imeandikwa-Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake( NOTICE NI WATU NA WANAFUNZI WAKE KABISA) akasema, ‘’Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi’’ Sasa nikuulize, Kati ya Mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo ambao wanakaa kwa kiti cha Musa which means wanachukua/refer Moses directives, Utoaji wa aina zote including zaka, umo? Can you imagine ni Yesu anasema Tuyashike na kuyatenda YOYOTE jamaa hawa wanao refer Musa, wanafundisha? And this is a big thought to chew..Ikiwa Yesu amewa-credit jamaa hao ambao aliwashughulikia kweli ktk mahubiri yake kua wanakaa kwa kiti cha Musa kwa maana yako mambo mbali na yale walioongezaga kwamba hayo tuyatende, why iwe tabu Mchungaji leo akinukuu ya KALE na kutufundisha ili tushike na kutenda? I would think if you ask me, many Wachungaji wetu wa leo (well, at least not all),ni more spiritual than Mafarisayo na Masudukayo kwakua si tu wanakaa kwa kiti cha Musa but cha Mitume na Manabii( ambao nao walikaa/tumia/refer Musa kama vile Yesu) na pia kiti cha Yesu na mwisho wa yote kiti cha Roho Mtakatifu ambao hao wote Yesu anasema ivi Mathayo.5:17-19 ‘’hakuja kuitangua Torati bali kuitimiliza! anahitimilizaje? Nimedokeza juu pale no. mosi kua zipo kweli za Agano la Kale, Yeye mwenyewe amezihamisha/ridhia ktk matendo na matamshi yake zinahama moja kwa moja, zaka moja wapo na ziko nyingine, amezileta leo kwa fashion nyingine (angalia hotuba yote ya mlimani Mathayo sura zote 3 za 5,6,7..angalia alivyofafanua mwenyewe nini maana ya kutimiliza au alisema nini kwa yale ya zamani na sasa akasema nini kwa sisi wa leo.

  NNE: Kwa msingi huo no.3, hii andiko bado ili Malaki.3:8-10-‘’Leteni Zaka kamili/zote ghalani mwangu ili kuwemo chakula Nyumbani mwangu’’ linalipa na linabana mpaka leo simply because kwanza, halijawahi vunjwa maana hakuja kutengua bali kutimiliza-kutimilizaje? Aligusia mwenyewe ktk Mathayo 23:23 na Hotuba yote ya Mlimani Matayo 5,6,7 na pili bado Farisayo, in our case Watumishi wanaotulea, kwa kua Wanakaa kwa kiti cha Musa kama ilivyo kwa mitume na manabii ambao nao walikaa kwa kiti icho bila kuathili kweli KUU nyingine alizowaletea Musa Mkuu-Yesu, huyu farisayo wetu wa leo akilifundisha naye pia BILA KUATHILI KWELI NYINGINE za akina Musa wadogo( Mitume na Manabii) na Musa Mkubwa-Yesu, sharti nishike na kutenda kwa kua Musa Mkubwa amewasemelea/commentia ivyo kwetu sisi wanafunzi.

  TANO: Hatimaye Hili andiko la 1Wakorinto.9:1-15 nalitumia hapa tena, kuonyesha uwezekano wa Paul kua alitunzwa/supportiwa na matoleo mbalimbali ya wapendwa/wanae wa Kiroho, zaka should be one of them logically hence si tu aliishi kwa kushona mahema miaka yote ukizingatia ukweli rahisi kabisa na wazi kuhusu aina ya huduma aliyokua nayo ya uku na kule ktk dunia ya wakati ule, thus, anasema ni haki yake ila alijizuilia tu( this should be mistaken kua ilikua ni kila siku na nyakati zote na kwa makanisa yote eti alijizuilia!!!-mistari 11,13-14 anasema kua kama ‘’amewapandia vya rohoni kwa nini asivune vya mwilini from them’’ na kwamba ‘’Bwana mwenyewe ameamuru, wanao hubiri Injili, waishi kwa iyo’ na pia ‘’wanaotumika madhabahuni, wanakula vya madhabahuni’’. Sasa kwamba aliziitisha yeye mwenyewe au waliguswa tu wakampelekea/kumbariki-this to me is not the stuff for serious mind! Cha msingi matoleo yalitoka-na kwa kua zaka ni moja ya matoleo na kwa kua watu hao walijua sana Musa directives na Manabii na kwakua Paul alisoma hapo Yesu aliposema kuna vitu Mafarisayo na jamaa zao wakifundisha tukamate na kushika na kwakua Paul alikua Farisayo wa Mafarisayo, unaweza ona kua HE DID NOT MAKE MISTAKE IN OTHER OCCASIONS!!!!!!!!!

  Nimejadili hapo juu nikilenga mambo haya: (a)ZAKA NI SAWA KUVUKA TOKA KALE KUJA LEO KAMA VILE KWA MATOLEO MENGINE KWA KUA MSINGI NI MOYO WA KUPENDA NA HIARI,(b) KUMPA KUHANI AU MTU/KIONGOZI WAKO WA KIROHO ZAKA NA MATOLEO MENGINE NI SAWA KABISA, (c)KUYAPELEKA UKO ANAKOFANYIA KAZI YA BWANA KAMA HUTAKI KUMPA YEYE LIVE INGAWA OFCOZ UTAMKUTA YEYE HUYO HUYO NAKO NI SAWA TU(hakwepeki huyu jamaa), (d) AKIAMUA KULA YEYE TU NI SAWA KWAKUA HAKI IYO INAHAMA KAMA ILIVYO TOKA KALE MPAKA JIPYA, (f) AKIAMUA KUIFANYIA SHUGHULI NYINGINE ZA MAENDELEO NA KIJAMII YANAYOLENGA MAMBO YA UFALME NAYO NI SAWA ILA ASIWEKEWA MASHARTI NA MADEGEDEGE KWA KUA FROM THE BEGINNING ANA IYO DIVINE RIGHT TOKA KWA MOLA MWENYEWE(g) KWAMBA KWELI NYINGINE ZA BIBLE HUTAZIPATA NENO KWA NENO LAKINI KWA KUJUA MAMBO MENGINE MENGI KTK BIBLE, NI RAHISI KUPATA CONCEPTS/JAMBO MOJA NA BADO LIKAWA KWELI KABISA WALA HALIATHILI KWELI NYINGINE ZA NDANI YA BIBLIA HUMO HUMO HATA KAMA HUWEZI LISITE LIVE-mfano jinsi unavyoweza jibu maswali niliyuliza mwanzoni kabisa juu pale.

  Sasa baada ya kusema hayo, ninapenda kujibu maswali yako so simply kama ifuatavyo:

  MOJA: Nimesoma tayari maandiko haya kuhusu zaka-Torati 14:21-28, Hesabu 18:21-26, 20 Walawi 27:32 na mengine mengi.

  PILI: Zaka ni nini? ina maana kadhaa, kwanza- kwa maana ya kimaandishi, ni sehemu ya Kumi ya kitu, Biblia za Kiingereza e.g. NKJ inatumia maneno mawili namely ‘tenth’ pale kwa Yakobo alipoahidi na pia ‘tithe’ ktk Malaki na hayo ya juu ulionipa na hata wa Yesu. Maana ya wazi ya KiBiblia ni sehemu ya Kumi ya maongezeko iwe mazao. Maana ya Kiroho ni sehemu ya Kumi ya Ulichonacho/ulichokipata/ twaa/pewa-hapa hausubili mpaka viongezeke( hakuna kukwepa, I kitu imekamata hapana mchezo!!!!!!!!) na mfano mzuri ni toleo la Ibrahimu ktk Mwanzo, baada ya Bwana kumpa ushindi, kwa furaha yake, aliamua kutoa zaka kwa vile alivyokua navyo na alivyo rejesha baada ya kumkomboa Lot.

  TATU: Inatolewaje kwa Mungu? Kwa kua MUNGU hua haji live kuchukua basi anatwaa kupitia wanadamu kuichukua na kuitumia.

  NNE:Nani anastahili kutumia toleo la zaka? Kuhani wako kwa maana ya leo. Kuhani kuipokea na kuibariki kisha kuila na kufurahia maisha na huduma, ndio hapo Mungu anakula!!!!!!!!!! Hii tamu sana kwa watu wa imani na wana kweli wa Mungu but wana siasa kanisani,watajuana na Mwenyewe. Pia wahitaji wanaweza kupewa lakini si busara kumsahau au kumwacha Mlawi wako au kumfanya awe second then wahitaji first. Kilichoanza kwanza katika wakati Mungu anakuja na mawazo/mambo haya ni Mlawi kwanza kisha wanadamu wahitaji. In fact kwa macho ya Mungu, Mlawi ni mhitaji no. 1 kwa kua walikua hawana urithi wa mashiko kama wanadamu wengine.

  TANO: Zaka ni ya nini? Ni ili kuwemo chakula gharani na nyumbani mwake Mungu ili wakaamo/wahuduo humo, wale, wanywe na washibe tele kisha wachape kazi ya Mola. Pia ni kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji lakini kwa mpangilio/wazo la kwanza la Mungu alipokuja na mambo haya i.e. Mlawi first, no ujanja hapo!

  SITA:Je Yesu aliwahi kutoa zaka kama Mkristo? Jibu langu ni ni maswali pia namely, Je YESU aliwahi kuoga kama Wakristo wengine? andiko? kuugua Malaria kama Wakristo? andiko? Lakini kwa kua aliwahi kulipa kodi Mathayo.17:24-27 LABDA aliwahi kulipa ZAKA kwa maana ile ya pili ya Zaka na matumizi yake yaani kusaidia wahitaji. Besides, kwa kua Yeye aliishi kati yao kama Mlawi Mkuu wao, HAKULIPA ZAKA bali WALIMLIPA YEYE zaka.

  SABA: Kanisa la kwanza walitoa zaka? Kama Walimsikia Yesu akisema kua Mafarisayo na Masadukayo wana kaa kwa kiti cha Musa ivyo wayafundishayo tuyashike na kuyatenda na kwakua kati ya Kanisa la Kwanza, viongozi wao na members wengi walikua ni wanafunzi wa Mafarisayo na kwakua uwezakano wa Mitume kufundisha kupinga kutoa Zaka ingekua kinyume na tamko ya Bwana wao,then walitoa Zaka hakika hata kama haikuandikwa kama vile haikuandikwa Yesu alioga au la ingawa ni wazi alioga tena na sabuni na hata alijisugua kwa mawe kuondoa magacha miguuni maana alitumia sana kutembea huku akiwa amevaa viatu kama vya wa masai kidogo au sandals za wazi zile wanauuzaga machinga.

  NANE: Zaka imeanza kutolewa kanisani lini? Wakati ambao Neno kuhusu utoaji wake, lilipokuwepo au kuwekwa kwa wanadamu

  TISA:Kwa nini iwe ngumu leo kutoa zaka? Kwa sababu ya mioyo ya choyo, ubinafsi, unyimivu,kiburi against Neno la Mungu, Kuutafuta kwanza ufalme wa Duniani na mambo yake halafu ya mbinguni ungoje kwanza, ufahamu ovyo wa Neno na mambo ya Mungu, kupoa kiroho, kukua na kukomaa vibaya kiroho, nature ya much know ya mwanadamu, influence ya Siasa, ukabila, majungu na kukosa nidhamu kanisani na dhidi ya Wapakwa mafuta wa Bwana wale wa kweli, kujiinua na madhara ya shibe ya sembe kupelekea watu kumsahau Mungu, utayari wa moyo kufa nk..U know sababu ni nyingi sana hamna mfano brother Yeremiah.

  Amani ya Mungu Baba iwe nanyi enyi nyote,

  Kama una swali au YEYOTE mwingine, ikiwa kuna jambo ktk presentation yangu, hujaelewa, mnakaribishwa na pia ruska kunipinga ila sema unapinga wapi halafu lete hoja maridadi kabisa, nitaziona na kusema kitu.

  Press on

 151. Kwakweli wapendwa nazidi kujifunza mambo mengi sana kupitia page hii na Labda niwaeleze mimi bado mchanga kiroho coz nilipata neema ya wokovu last year february!Ila nafanya juhudi sana ya kusoma neno la Mungu na kumruhusu da HOLYSPIRIT anifundishe zaidi!Bt hapa jambo linalonishangaza kuona wapendwa badala ya kupeana hoja kwa hekima na busara bt mnaweka na mambo ya kubezana au kupondana!

  Mimi nadhani dhana kubwa nikuelimishana kwa kufuata maelekezo sahihi ya neno la Mungu!Bila kuweka interest binafsi!Naamini Mungu humpenda mtu ambaye ni mnyenyekevu mbele zake!Wapendwa ningebarikiwa sana kama mgetumia Lugha ambazo hata mtu ambaye hamjui Mungu anakuwa hatii shaka!Coz kuna lugha ambazo zinatumika as if ni mipasho au kudharauliana na kama vile kujiona mmoja ni bora kuliko mwingine!Hivi Kwa maneno hayo Roho Mtatifu ambaye ndiye msaidizi wetu ktk kila jambo yupo?Anyway let me end here for a moment while am still watchin wht is goin on to wapendwa!coz I wanna learn more 4rm u guyz!GOD BLESS U ALL.

 152. Mr. SELELI,

  Kwanza naitwa Kaswahili na si Kiswahili. pili, hongera! michango yako ya mwisho mwisho umetulia na umejaribu kuwa articulate kuliko hapo mwanzo. make hata swanglish naona imepungua! hongera, naona drip ilikusaidia.

  Kama wewe na wenzio mngejenga hoja zenyu kwa kujibu ktk namna ya kuchanganua [analyse] maswali ya msingi yaliyoulizwa na bw. Jeremiah, yanayotoka ktk hoja ya msingi, ningefurahi sana. hasa haya mawili kwamba: je, yesu aliwahi kutoa zaka? au ktk injili zake ni wapi aliongelea zaka? na je, kanisa la kwanza walitoa zaka? na au, ni mtume yupi kati ya mitume wa yesu ktk kanisa la kwanza aliyewahi kufundisha utoji wa zaka? au kama kuna mahali popote ktk agano jipya biblia imesisitiza utoaji wa zaka kwa kanisa? mr., nipotayari kutulia miguuni pako na kujifunza endapo unaweza kujibu maswali haya kwa uthibitisho dhahiri and with articuracy. usianze kuruka huku na kule tena. la sivyo malaria itakuwa bado imo. bw. seleli, ninaamini ktk utoaji kabisa. wala sipo kinyume na kutoa mali zetu kwa ajili ya ufalme wa mungu. ni kweli kabisa mungu ndiye aliyetufundisha utoaji at the first take. alipomtoa mwanae wa pekee na kipenzi kwa ajili yetu tuliokuwa waasi na wakaidi mbele zake. na namna ya utoaji ambayo naamini kuwa ndo sawa ni ile ambayo paulo ameifundisha ktk 2wakor 9:6-8, iwapo mtu anataka utoaji wenye kuambatana na thawabu ya mungu. sungura alichanganua vizuri kabisa kwa kuonesha zaka ilianzia wapi ktk agano la kale. akaonesha kwamba kwanza zaka kwa mara ya kwanza ktk agano la kale inaanza kutolewa na ibrahim na kisha yakobo kabla haijaja kuwa sheria baada ya waana wa israeli kurudi kutoka utumwani misri. makusudi ya mungu kuifanya zaka kuwa sheria sungura kayaeleza. na kwamba baada ya ule ukuhani kubadilika kuliondoa usheria ktk utoaji wa zaka, kaueleza pia. afu akasema kama kuna mtu anadai hili kusudi la mungu halikubadilika hata ktk ukuhani mpya atuoneshe ili kututhibitishia hili ktk agano jipya. kwa nini zaka iwe special offering namna hii kanisani? kwa nini kutotoa zaka ndiyo tu kunahubiriwa ndiko kumwibia mungu na si matoleo mengine? bahasha zenye majina ya mtoaji wa zaka na lisiti za zaka ni za nini kwenye baadhi ya makanisa? hivi kuna watu wangapi makanisani wanaoitimiza hii sheria sawasawa? yaani wanaotoa zaka sawasawa na kamili? je, unaweza ukaniambia namna hii zaka si kongwa kwa watu wengi makanisani? unaweza kuniambia namna hii watu wengi makanisani hawako guilt kwa kumwibia mungu, kwa kushindwa kutoa zaka sawasawa? kwangu zaka ni sawa na matoleo mengine tu. ntatoa zaka yangu kama walivyotoa kina yakobo. kwamba-kwa kuwa bwana umenifanyia au umefanya hili nitakupa 10 percent au hata 20, au hata 50 Percent ya nilicho nacho. sifungwi kamwe ktk hili. la unidhibitishie katika agano jipya kama nilikuta hapo juu, nipo tayari kutubu ukiweza kunithibitishia. sina shida na utoaji kanisani na hata nje ya kanisa. naomba usinielewe vibaya. ni kweli pia kwamba watumikao madhabahuni wanahaki kula madhabahuni. wala sina shida na hilo. lakini matoleo yanayotolewa madhabahuni, au na michango mingine kanisani si haki ya kuhani tu. mashemasi wangapi wanapewa fungu? wambaji wa sifa wanapewa fungu? wengine mpaka wanamaliza mazoezi wanakosa nauli ya kurudia makwao wanaanza kuwaombaomba wenzao. wajane na wazee wanakumbukwa? wasiojiweza makanisani wanasaidiwa? makanisa mangapi wanafanya hivyo? kunafungu linalotengwa kwa ajili ya kuwatembelea wagojwa mahospitalini, wafungwa magerezani na maskini mitaani ili kuwabariki na kuwaonesha upendo wa mungu kwao? bwana yesu alionesha njia alipowaosha wanafunzi wake miguu. mama hawezi kula kabla watoto wake hawajashiba. kuku huwachakulia watoto wake kwanza wale. hawezi kushiba kabla watoto wake hawajashiba. huwezi ukatarajia kuvuna bila kupanda, kupalilia, kumwagilia maji, na kutia mbolea. huwezi kutegemea kupata maziwa bila kwanza kumlisha sawasawa na kumtibu mbuzi. siwezi nikawa mchungaji wa kanisa, mimi niko njema wakati kuna washirika wangu wamechoka, na kwao habari njema si njema. siwezi nikawa mchungaji wa kanisa nikafundisha hesabu ya kutoa kabla ya kufundisha kwanza hesabu ya kujumlisha na kuzidisha. asante.

 153. Kiswahili,

  Nimecheka kweli hii kitu..‘Ungeita Abulance fasta, …tehe tehe uko very funny brother, may be unanizidi! asante kwa kunipa raha, yaani seriously na Mungu ni shahidi, nimecheka mpaka basi,mwe! Ni mara ya kwanza toka nije duniani mimi kuambiwa aidha nina celebral malaria au wakati niko beby, niliugua degedege na kwamba wenda nimemeza memory kadi! Hahahah!umeyatoa wapi maneno haya mteule? Sasa kabla hujaniletea ambulance, let us see nani hasa anahihitaji ambulance hasa!

  ‘’Unayoongea yenyewe hayana subtance yoyote ktk hoja inayotakiwa kujadiliwa. unarukaruka tu kama mbayuwayu’’= Nimeongea Utoaji in general na kisha nikamalizia na Zaka kama moja wapo ya utoaji ili kuondoa hali zozote za ushawishi wa moja kwa moja au wa chini ya carpet ambao aidha kwa kujua au kutojua, baadhi ya michango yako, inaambukiza kitu mbaya kwa Wana wa Mungu kuhusu thamani walio nayo moyoni juu ya Watumishi wao/wa Mungu Makanisani. Pia kwa jinsi michango na mielekeo ya MISISITIZO yako ilivyokua,mimi kuweka nguvu nyingi ktk swala zima la Utoaji kama tabia ya Mungu in general ilikua ni lazima sana (maana nimesoma toka mwanzo comment zenu zote!). Hata kama mnasema hakuna anayepinga, lakini mwenye akili za ndani na nje, asomapo comments zenu, anaweza on/taste/sense hata tone ya maneno yenu na aina ya moyo/mkristo husika ktk swala la Utoaji na maisha yake hapo kanisani kwakwe na Watumishi wanaomlea (kama analelewa kweli maana wako Wakristo wa aina ya leo, wanaojichunga wenyewe au kwa TV za Wahubiri mbalimbali). Sasa je, Hapo hakuna substance kweli kama ulivyosema? JIBU NI SI KWELI-ni maneno tu rahisi ya kukataa jambo bila kua na hoja.

  ‘’Hoja inayojadiliwa hapa ni utoaji wa fungu la kumi au zaka makanisani leo na kwamba je, fungu la kumi ni hiari ya mtu kutoka moyoni mwake kama 2wakor inavyoelekeza au inabaki ni sheria pia ktk hili agano jipya?’’= Hii si hoja original bali ni haya ni maelezo nyongeza au dadavuvi ambayo imebidi myaongeze-kitu ambacho si kibaya na huwezi kwepa hiyo ktk kujadili jambo. Hoja original ya Milinga ilikua-‘’Mafundisho kuhusu kutoa ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato’’. Kilichopepelekea mpaka kuwaza Uhiari au Sheria ni interpretation zako/zenu toka Hoja hiyo-again kitu ambacho bado ni chema tu maana utadadavuaje bila kugusa baadhi ya mambo ili kujibu/kufafanua/kuchambua hoja original!

  ‘’Badala ya mtu kuja na facts kuhusu hoja iliyopo mezani, anakuja na maelezo mareeeefu ambayo hata hayajikiti kwenye hoja inayojadiliwa, ni umbayuwayu tu kuruka huku na kule aimlessly’’= Fact ziko wazi kwa mwenye kutaka kuelewa. Mtu anapokuambia Utaoji kama tabia kuu ya Mungu na kukupa mifano yake Mungu mwenyewe ktk Kutoa kisha Watu heavy wa Mungu ktk Bible waliotoa aina zote tu za matoleo ili kuimarisha moyo wa utoaji udumu na siasa za leo na ujuaji wa baadhi ya Wakristo zife, HIYO ni AIM kubwa sana yenye kibali hata JUU kwa Baba na ni FACT KUBWA SANA bwana Kiswahili. Kukataa ukweli huu na hata kupambana na ukweli mwingine wa kutoa Zaka ili nyumbani mwa Mungu kuwepo na chakula na Walioko umo wachape kazi kwa amani, kukataa kuona ukweli huo kua Utoaji wa aina zote unatapakaa toka Mwz-Ufunuo, huu sasa ni ZAIDI ya UMBAYUWAYU-sijui tuite ni nini sasa, well, labda U-kware! bila shaka unafahamu tabia zao kware wa vijijini kule kwetu/kwenu!

  ‘’Ulaya wachungaji ambao wewe unawaita makuhani wanalipwa mishahara na kanisa’’= Hapa nipe ufafanuzi, mimi leo Wachungaji KWELI nawaita Makuhani kwa maana ya Ki- Biblia hasa kwa kazi walizokua Wanafanya ktk Agano la Kale na wa leo wanazozifanya kwa form ya Agano Jipya, sasa wewe unawaitaje Kiswahili? Kwamba wa Ulaya wana lipwa mshahara, so what! Unakusudia kusema nini hapa? Tuanze kuwalipa Salary na si Posho tena na siye siyo? Mambo ya Ulaya-Ulaya sio? Na sijui ni Ulaya ipi unayomaanisha au uliyoenda? be specific halafu nikushangaze /nikubane kidogo au ndio mambo yale yale ya stori za mambo ya Ulaya za kijiweni brother! Labda a thought for you- umeshawahi jiuliza kwanini tunawalipa posho na si salary? Unaelewa maana ya malipo yakishachukua form ya neno Salary system au unadhani itakua ni mashahara tu basi na hakuna yaambatanayo?.

  Na umeshatafakari hata siku moja comment za Yesu kuhusu Mtumishi anayelipwa mshahara? embu kidogoo take time hapa halafu niambie unaelewa nini ktk connecting it na swala la moyo wa KWELI na TOTALLY kwa Huduma Yohana.10:11-14. Make no mistake about me/it-maana nakuona u mwepesi ku-twist serious stuff! I am not suggesting all the hired ( Salary system) are not commited but it is my interest uone na kwa kweli ujiulize, why would Jesus, once and for all final role model comment such?

  ‘’Wana aidha biznezi au kazi zao wenyewe’’= a u trying to say, huku mtu awe mchungaji na huku ni mfanyabiashara au ameajiriwa Serikalini/Umoja wa Mataifa nk? and you think this so sweet for all men and women of God to cut and paste? Confirm then will challenge/ask you badly Mr.Kiswahili.

  ‘’Hakuna ukupe na u-oya oya kama wa hawa wanaolowa suti nzima hadi wanatoa na tai jicho limewatoka na mishipa yote ya uso wakihubiri kwa nguvu zote’’= You see, Mkristo wa ivi, unaweza jua tatizo si Zaka tu,kuna more than that! Ndio maana nilidokeza kwa Mr. Sungura kua you guys you appear too stubbornly personal kwenye swala la Utoaji e.g. ZAKA than a church problem! At least to be fair, na kama kweli wewe ni mtu wa substances na facts kama ulivyo-imply kua ndivyo-kitu ambacho sadly sijakiona, ungewaheshimu walio honest kwa kutumia neno staha la kuwatenga na hao wengine wasio waaminifu e.g. SOME ya Watumishi…lakini sweeping statement kama izi agaist Watumishi wa MUNGU ambao in fact wangependa kuishi kama wewe tu lakini one day ghafla wakakamatwa/kitu kikashuka moyoni, wakaingizwa kazini na Mwenyewe na kuambiwa kuacha kila kitu na kumfuta/kumtumikia Master, hao wote kuwaita ni lazy, u-oya oya, kupe-KUNA TATIZO MY BROTHER KTK MOYO WAKO, U NEED JESUS URGENTLY! Kwamba wanahubiri kwa nguu zote! So ulitakaje kwani? Wahubiri ki-lazy! Namna gani hapa Kiswahili unaongea……!!!!!!!!

  ‘’Wakia-accuse watu wa Mungu kwa fungu la kumi= Hii statement ni so common sasa ktk comment zako na Sungura! Unajua mpaka nashawishika kutaka kujua nyie mko wapi wenzangu? Kanisa gani LA KWELI(note strictly the word ‘LA KWELI’) lina accuse watu? Labda nifafanulie- Mchungaji wako akinukuu andiko la Mungu mwenyewe aliposema , wewe usie leta FUNGU LA KUMI KAMILI NI MWIZI NA Yesu MWENYEWE ALIPOSEMA tufanye ya rehema kwanza BILA KUACHA NA YALE MENGINE, ni Pastor au NENO lime-accuse? Au demonstrate hapa, Pastor wako anapoongelea utoaji zaka kwa hiari na akanukuu maandiko hayo na mengine kwa subject iyo, ahubirije/afundisheje ili usijisikie kua accused au kumuona yeye bali Neno lililokuita wewe kibaka? Show it here! Otherwise, ninadhanie kama Sungura(kasha niambukiza tayari, unaona sasa madhara haya!), wewe ni aina ya wapendwa wanaotaka kusikia yale wanayotaka kusikia bali si Mungu anayotaka wao wayasikie au Mtumishi wa Mungu anavyoona ni uhai na salam kundi kuyasikia.

  ‘’Ufisadi umeshamiri mpaka makanisani’’= Makanisa yapi? yote? At least treat the honest with the sense of respect bwanaa, izi ndio maana naona ni siasa za Sungura na wewe, sijajua wengine humu.

  ‘’Watu wamegundua njia ya kuukata ktk maisha kwa kisingizio cha maono ya kumtumikia mungu,tunashuhudia wachungaji wanamiliki hummer na magari mengine ya kifahari na majumba makubwa ya kifahari ilihali bizinezi zao ni church tu’’= kwa upande mmoja nakubaliana na wewe-at least kwa hiili hauhitaji ambulances 2! Yes, wapo baadhi very unfaithful kabisa kabisa ila again ningekua mie wewe ktk kuisema point hi, ningekazana kukua na kuongeza umakini kwa vipimo vyenu(ofcoz all fake/weak and faulty self-esteem dictated scalig anyway), ningetumia maneno ‘wengine’’ au ‘’baadhi’ ya wachungaji… si wote! Tuna watu wa Mungu, so many, so many kwa kweli Wilayani, Tarafani, Mikoani huko na Miji mingine, great lovers of Jesus and deep faitfully in Utumishi, hawa wachache baadhi wa Mijini na Majijini walio haribu si picha ya Kanisa lote! Hii mambo ya samaki mmoja akioza wote kwisha ilitolewa wakati mababu wanakunywa wanzuki probably!

  ‘’Huku humohumo church kuna washirika maskini wa kutupwa! = hii nayo ni common sasa ktk michango yenu. Kanisa la KWELI haliwezi kuacha kuishi kama familia na kusaidiana. Lakini if you are real thinker/analysts, nitajie Kanisa moja tu DUNIANI very succssfull kwa vipimo vyako na Sungura hakusaidie aliye support ambulance yako ininyakue, ambalo Watumishi wanaishi ktk chumba kimoja na sebule na kutembea kwa mguu acha baiskeli-Kujinyima hasa na hatimaye washirika wa humo, hakuna maskini na wahitaji hasa? Au nitajie Kanisa very successful na mchungaji ana ndege 2 za halali, mpendwa mmoja kwa HIARI yake alimnunulia na kila mshirika aendeapo kanisani hupewa lunch na nauli ya tax then nionyeshe humu kua hakuna maskini? You see now, capacity yako na nani kwa kweli anahitaji situ land ambulances 2 but this time air-ambulance!
  ‘’Si bora mwl. nyerere ambaye hakuona fahari kujifaharisha wakati wananchi wake ni maskini wa kutupwa’’ = kwakweli abarikiwe Kiongozi wetu huyu, honestly I (used) love him so much na sijui kwakweli Mungu atusaidie kama tutakuja pata mwanadamu wa ivi ktk Nchi na bara hili. Nevertheless, pamoja na kujiminya kwakwe kule kuzuri na kwa level ile ya ajabu na njema sana, are we rich? Wewe hapo ni poor rich? Kwa iyo maskini na matajiri tutakua nao siku zote regardless si ndio? So then what is your point on this brother Kiswahili? You see! hamna kitu/mashiko.

  ‘’Nahisi na wewe ni walewale tu wasaka tonge kwa mgongo wa utumishi wa mungu, acheni uvivu’’- brother let me try this, Kazi ni nini? napohubiri, fundisha, fungisha ndoa, zika, ombea wagonjwa, tembekea washirika mahospitakini, misimbani, kaa ofisini masaa 7 nikafanya counselling, kuongoza maombi mkesha wote, wakati unaenda lala, mimi nirudi kesho kuandaa ibada ya J2, kusafiri uku na kule kuhubiri, kuhudhuria vikao vya Kikanisa, kuitwa na serikali ktk tume mbalimbali kuchangia na kutoa mada kuhusu maendeleo na matatizo ya kijamii nk, ni kazi si kazi? Uvivu uko wapi hapo maana hayo ndio wayafayayo Watu wa Mungu hapo kanisani kwako, naamu na makubwa zaidi ya hayo e.g. una koroma ktk usingizi na kula Jan-Den but Pastor wako anakuombeeni weye,kanisa lote, Nchi na kufunga kila mwezi siku 5! Halafu unasema waache uvivu! U need Jesus’ second touch brother and Holy Spirit friendly adjusting operation Mr.Kiswahili.

  ‘’Jifunzeni kwa paulo ili jina la mungu litukanwe bure-2wakor.3:7-9 wachungaji maslahi na wavivu leo wataweza hii? -Baadhi siyo yet Paul huyo huyo alisema haya, 1Wakorinto.9:1-15! Paul anayesema ni haki yake kuchuma vya mwilini kwakua aliwapandia vya rohoni, alikua ni maslahi Apostle? Swala la kujizuilia kutokula ni choice yake kama Paul lakini rule of the game, kasema yeye mwenyewe hapo hapo kua ni HAKI yao na zaidi sana, role model wetu si Paul kwa asilimia mia bali ni Yesu ambaye Paul anamnukuu/actually anam-interprete ktk andiko ilo ilo juu kua ..BWANA ALIAMURU WAHUBIRIO INJILI WAISHI KWA INJILI NA WAHUDUMUO MADHABAHUNI, WALE VYA MADHABAHUNI na Yeye mwenyewe Master alisema..Mtenda kazi anastaili ujira wake, alipowatuma wanafunzi Luka.10:1-7 kufanya moja wapo ya shughuli wazifanyazo wachungaji wako ambao wewe unawaita wavivu na wayafanyayo si kazi! You see jinsi gani uko mwepesi ktk mambo haya bro ignorantly ukidhani una kitu?

  Sasa bwana Kiswahili baada ya soma langu la Utoaji in general then kugusia Zaka in specific, later comments zenu na Sungura then my comments / response zangu kwa comments zenu, nadhani mmenionea tu bure kwakua kwa hakika sina celebral malaria wala sikuwahi kuugua degedege wakati nilipokua bebi na kwa kweli iyo ambulance mtaimsumbua bure tu driver wa watu maana sihiitaji ila kuna uwezekano, kinyume chake kikawa kweli kabisa! Wewe waonaje Mister? na msema ukweli ni mpenzi wa MUNGU!

  Press on.

 154. Mpendwa Selel Edwin,Salaam.
  Nimefurahishwa sana na mchango wako kuhusiana na somo lihusulo KUTOA ZAKA kila mwezi au upatapo kipato. Nimefurahi kwa sababu umefunua moyo wa Mungu,umefunua tabia ya Mungu na umedhihirisha kile kipimo cha ndani cha mwana wa Mungu yaani MKRISTO ANAYEMUAMINI YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WAKE ANAPASWA KUONEKANA KUWA NACHO.
  Ukweli upendo wa Mungu hudhihirishwa na utayari wake wa kutoa kwa ajili ya ndugu. Bwana Yesu anasema katika mahali fulani kuwa Aliyesamehewa sana hutoa zaidi bali aliyesamehewa kidogo hupenda kidogo,ndiposa mtume Paulo anatufundisha kuwa Apandaye haba huvuna haba na apandaye kwa ukarimu huvuna kwa ukarimu.
  Lakini nimepatwa na mshituko mkubwa nilipoona kuwa nawe unadhani mafundisho ya utoaji wa ZAKA ni kati ya mafundisho stahiki ya utoaji. Nimepitia andiko lako kwa makini na kugundua kuwa kwa asilimia 100% umefundisha kwa umakini na ushahidi mkubwa kuhusu nadharia na tabia ya utoaji kwa Mungu ukitumia kwa ukamilifu na uhakika maandiko uliyoyanukuu ku support comments zako.
  Hata hivyo hakuna hata aya moja ambayo umejaribu ama kuelezea kuwa ZAKA ni SADAKA/TOLEO linalopaswa kukabidhiwa kwa kuhani kama yanenavyo maandiko. Hili ni moja ya udhaifu mkubwa uliopo kwa waalimu wa toleo la ZAKA. Lakini naomba nikushauri kwa makini sana usome vizuri na kuyatafakari maandiko haya na kisha upitie andiko lako uone kama kuna mahali Zaka imewahi kuwa toleo la kupelekwa madhabahuni kwa Bwana katika wakati wowote ule.
  Hebu soma Kumbu kumbu la Torati 14:21-28,Hesabu 18:21-26,Walawi 27:32. Ninaamini utafahamu yafuatayo:
  1. Zaka ni nini
  2. Inatolewaje kwa Mungu.
  3. Nani anastahili kutumia toleo la zaka.
  4. Zaka ni ya nini
  5. Je Yesu aliwahi kutoa zaka kama mkristo?
  6. Kanisa la kwanza walitoa zaka?
  7. Zaka imeanzakutolewa kanisani lini ?
  8. Kwa nini iwe ngumu leo kutoa zaka?

  Ninadhani nimetoa mchango wangu wa awali na nitakuwa tayari kuhangia kwenye mada hii kwa utukufu wa Mungu aliye hai.
  Mungu akubariki sana

 155. Ndugu Sungura,

  Ndio maana nikasema nadhani umakini unaosema unao indirectly, utakua kwa mambo mengine, hapa umefeli brother. Unasema tunaongelea-‘Utoaji wa zaka katika mukdha wa kama leo kutoa zaka ni lazima au hiari’’ lakini hoja ya Milinga ambayo Mathew aliijibu na kwa hiyo mkaendelea na wengine ni ‘’Kutoa Zaka kila mwezi au kila upatapo kipato’’. Kama tunataka kujikita ktk kitu kimoja tu(jambo ambalo haliwezekani katika majadiliano kwa baadhi na namna ya mada fulani zilivyo na unaweza thibitisha ilo hata ktk michango yenu mingine ktk mada nyingine), basi tungekaa hapo. Mpaka umeingiza swala la hiari au la, na kuitafuta ilikuaje kabla na wakati wa sheria nk ni mambo ambayo imekubidi uyagusie ili kudadavua sawia maswala uliyotaka kuweka mezani, kwako iyo ilikua njia bora ya kusema hoja zako-Hii ni kawaida kabisa! Mimi kugusia Utoaji kwa ujumla na kisha kumalizia kirahisi Zaka kama aina mojawapo ya Utoaji ktk maisha yetu ya uchaji Mungu, nimefanya kilekile ulicho fanya, cha ajabu kipi?

  Naona tatizo moja tu ktk skills zako za kuhojiana au kujadili jambo Sungura-la ule mfano wa vipofu 4 walioambiwa waelezee kile wanachokipapasa( Tembo), mmoja alishikishwa sikio,mwingine mkonga,wa tatu guu na wa mwisho tumbo.Huyu wa tumbo kwa uwezo wake wote wa kusemelea tumbo hilo, atakapodhani maelezo yote kuhusu sehemu nyingine za Tembo yanapaswa kua kama tumbo, kuna tatizo kubwa sana kwa kipofu mshika/mpapasa tumbo!

  Kama hoja hasa kwa msisitizo wa michango yako ilikua ni swala la Hiari, basi mahojiano /majadiliano haya, yalishafika kikoma kitambo kwa kua situ tunakubaliana bali ni maandiko yanasema ivyo. Sasa mambo ya Wachungaji wanakula wenyewe na kuwaacha yatima, wajane, yamekujaje hapa kama kweli unataka kukaa ktk kitu kimoja?

  Na kama kweli dhati ya moyo wako ni kufundisha ilo la utoaji za zaka kwa hiari na unajua kwa hakika kazi na umuhimu wa zaka na matoleo mengine ktk kanisa la Mungu wakati ule na sasa kwa mujibu wa Neno, kwa nini uwe mtu wa kuingiza mambo ya siasa Sungura ktk mambo ya Mungu ambayo wala wachungaji hawahusiki ni Biblia yako/yangu inahusika.! Mbona naanza kuwaza kua hii mada umetenda personal zaidi kuliko kama inavyotakiwa iwe! Mtu akisoma comments zako toka mwanzo, unaona kuna tatizo binafsi zaidi kuliko kikanisa. Na sijui kanisa gani la kweli LINALAZIMISHA WATU-maana hilo umeliongolea kwa nguvu kweli! au kuna tatizo tena la kuelewa kati ya kanisa la kweli na madhehebu? KWELI KANISA LA KWELI, LENYE WATUMISHI WA KWELI WA MUNGU NA WAUMINI WA KWELI WANAOLIJUA NENO, KUTAKUA NA KULAZIMISHANA? Si kweli kabisa!

  Umesema, ‘’Hoja ya zaka tumeianzia kwa Ibrahim, hatujaianzia Agano jipya kama unavyodai Seleli’’-‘’Nani amesema hamjasema kua ilianzia Agano la Kale? Mbona unaleta claim nyingine tena ya ajabu Sungura?

  Umeniuliza ‘’Seleli nini tofauti ya hekalu na kanisa? una uhakika na ulichosema kwamba zamani lilikuwa hekalu na leo ni kanisa?’ Majibu ni- Maana za kimwili-yote ni majengo ambamo watu wa imani hukutana kufanya mambo ya ibada.Maana za Kihistoria ya Dini ya Hekalu-Jengo kubwa Jerusalem ambamo wayahudi na hata watu wengine kwa utaratibu uliowekwa, walikwenda kuabudu hapo na maana ya Kiroho-ni mwili wa Muumini. Kwa upande mwingine, ‘Kanisa’-maana ya kiroho- ni muumini mmoja aliyemwamini Bwana, au kusanyiko lao, na ya kimwili ni kama ya hekalu pale juu-jengo hao waumini wakusanyikapo kufanya ibada ya pamoja. Sasa niliposema zamani hekalu leo Kanisa-nililenga ya kimwili ili kuelezea zaidi shughuli zinazofanyika hapo na wafanyao humo na umuhimu wa Wakristo Kutoa iwe Zaka au toleo lolote lile ili Kazi ya Bwana kimwili hapo Jengoni na Kiroho ndani ya majengo yetu-Hekalu la RM, kusitatizike, ulikua hujaelewa nini sasa hapo au ni yale yale mambo yako Sungura ya kuingiza mambo yako binafsi ktk system njema kabisa ya Mungu Baba na sisi watu/watoto wake hatuna shida nayo na tunafurahi kwakweli kutoa tena aina zote za matoleo situ Zaka hii ambayo aidha mnapambana nayo au kuingizia watu mawazo mengine maana maneno huumba na kila imani yaja kwa kusikia, wakati kwa HIARI zetu tumekua tunatoa iwe mwisho wa mwezi, kati, mwanzoni, kwa week, siku, tunapobarikiwa na nina moyo wa kutoa, sifungwi tena na hekima izi za financial managements bad spirit’’

  Umesema..’’Kumbuka walawi lilikuwa ni kabila haikuwa huduma. Huduma ilikuwa ni ukuhani’’, Naona na wewe Sungura unapenda kama mimi kundika kwa urefu! Hukua na haja ya kurudia hii maana ktk mchango wangu nimetumia Walawi/Makuhani wala sijasema Mafarisayo/Makuhani! Nilijua tunaongea lugha moja bila shaka unge-connect tu simply.

  Umesema’’Leo hii tukiongelea ukuhani inabidi Wahudumu wa huo ukuhani waitwe Wayuda siyo Walawi tena. Mimi na wewe leo siyo Walawi ni Wayuda’’- Kwa iyo wewe ni kuhani siyo? Kwakua ni MYuda? Na mbona post yako uliponijibu ulisema ‘’leo hakuna Walawi wala Makuhani’’! umegueka au umeelewa sasa Sungura baada ya kusoma kwa utulivu maandiko niliyokupa haya 1Petro.2:9, 2Wakorinto.5:18-21? Kama bado sema!

  Umesema ‘’Paulo hakuwahi kusema kuwa watu wakusanye zaka apelekewe, zaidi sana alifanya kazi kwa mikono yake, wala hakumlemea mtu/kanisa’’- kwa upande mmoja ni sawa na nikatoa mistari hii 1-6,12 ya 1Wakorinto 9 Ila hapa hukujibu hoja yangu ivyo naisisitiza kua kama yeye mwenyewe alisema maneno haya yote-1Wakorinto.9:1-15 e.g.Mimi niliyewapandia vya rohoni je sina haki ya kuvuna vya vya mwilini au aliposema Bwana ameamuru wale wanahubiri Injili waishi kwa Injili au wale wanaohudumu madhabahuni wale vya madhabahuni, ni rahisi kwa meneno yake hayo kuamini kua kuna nyakati nyingi tu aliwafunisha na alihudumiwa pia na zaka za wanae kuliko kusema kua KAMWE HAKUWAHI-kama unavyojitahidi kuunda ilo wazo lisilokua na mashiko kwa kweli.

  Umeniuliza’ Ivi unajua sawasawa waliokuwa wanatakiwa kula zaka ni nani na nani? Mimi pia nikuulize, ni wakina nani Leo wanatakiwa kula zaka?

  Mwisho umeni-sorry na kusema nimeandika upuuzi na pia utoto mwingi! mmh! aa wapi Sungura! Mtu akibanwa bwana, yanamtoka kweli yauzayo moyo! Unajua katika yote uliyochangia kwa swala hili, nimejaribu sana kutafakari , shida yako ni nini hasa! mara Utoaji wa zaka unakubali, mara wanakula Wachungaji tu, mara hawapaswi kuishi kwa iyo kwa leo na sasa mara sisi leo ni Makuhani na ni Wayuda,mara kipindi kile ukasema- hakuna makuhani kabisa leo! Jamani, ivi shida nini? why all these mahangaiko? Ni personal problems au general church issue? nini moyo wako ktk swala zima la kutoa( na ndio maana niliona vema kusemelea Kutoa in general) ili kama kuna Watumishi wa Mungu na Wakristo humu, wamesoma BAADHI ya michango yako/yenu hatari, wajue tabia hii ya Kutoa(zaka ikiwa moja wapo) ni asili ya mwenyewe na kwa namna yoyote ile, kusiwepo na mtu katika yale atajayosema, ya kumuondoa mwana wa Mungu ktk tabia iyo kuu ya Mungu wetu-sioni haya kusisitiza ilo na Mwalimu mzuri will always go to the base kabla ya matofari!

  Lakini pia ktk debate skills ukiona mtu anaanza kuacha hoja ktk meza na ku-attack personalities mara huyu mtoto, yule mkubwa, kuacha kujibu alichoulizwa au kua challenged (niliona kuna mtu humu pia alikuchallenge uwe unajibu unachouulizwa), basi unafahamu maana yake nini na level ya huyu mtu ktk midhahalo na majadiliano ikoje e.g. ana capacity ya kuweza kuangalia upande wa pili SINCERELY na KUONA au ni mlengo mmoja ambao unaweza ukawa unamkosesha vitu vingi sana kwa kudhani kuna kila kitu uko kwakwe! Na kwa kweli najiuliza tu nani ni zaidi ya mtoto kati ya aliyetoa changamoto kua tusome kwa kua tunafanya mengine mengi yanayokula mida yetu sana na yeye ambaye ametamka ‘mijineno’ mithili ya kutukana?( ingawa si tusi perce) na sijui iyo ndio hekima kubwa zaidi ya mkubwa,mi sijui ila tuendelee kuelemishana na kisha kama umakini sina na mie mtoto, mtanisadia kukua-kua angalau na kupata umakini.

  Ukipenda kujibu hoja na comment zangu, ubarikiwe na kama huna muda kama ulivyodai(I doubt and I can prove it kwa maswali/hoja 2 tu kati ya nyingi nikikuuliza kama ungekua haukasiriki haraka na ‘kutema cheche’ bwana Sungura).Haya ya sijui utoto au ukubwa, weka bembeni na kama ulivyosema mwanzoni, izo ni longolongo kaka, kaa ktk issue on the table, mengine no tija, Amen?

  Otherwise, yooote tunaweza yatupa nje uko but la msingi ni hili…TUENDELEE KUTOA na KUTIA MOYO SANA,SANA KUMTOLEA BWANA KWA AINA ZOTE NA FREQUENCIES ZOZOTE ILI KUSAPOTI MAMBO YA KANISA, UFALME NA WATUMISHI BILA KULETA Siasa na juaji nyingiiii wakati watu wana raha, furaha, willingness ya kumtolea na tumekua tunafanya ivyo kwa amani kabisa pasi na shaka yoyote.

  Sungura,‘’Nahisi Seleli ananyemelea kuwa mchungaji’’. tahadhari watakaokuwa washirika wake’’= He! yamekua hayo tena! Mimi kuvizia uchungaji! Brother una mafundisho mengi kweli umu, kumbe uchungaji ni wa kuwinda na si kuitwa na Mwenyewe? Nonetheless, kwa wanadamu Waamini aina yako na jamaa yangu mmoja anaitwa Kiswahili ambaye nitaongea naye pia hapa na labda wako wengine ktk platform hii-nitaendelea kufahamu, Uchungaji wa kuwinda,kuvizia, kunyemelea na kwakweli hata kuitwa, siko tayari! Why? Muulize Mchungaji Musa ilikuaje aliambiwa kabisaaa live hiki na akaelewa swadakta-Hesabu.20:8 lakini kwanza akabwatuka kwa kuwaita ivi..Hesabu.20:10c halafu akafanya iki-Hesabu 20:9-11 na kisha ikamcost iki-Hesabu.20:12

  ‘’Kwamba wajiandae kukamliwa vya kutosha’’
  =We will see brother Sungura.

  ‘’Kwake washirika ni shamba la kuvuna na kula kuku kwa mrija’’= assumption too extreme to be true, right? so it is dismissed without much attention to it bro Sungura.

  ‘’Wengine kama wajane,yatima, waimbaji, nk. watajiua huko’’= above comments apply too here, ila pia huruma kama izo zifanyike baada ya yale ya kwanza.Alikuwepo mmoja kama wewe lakini majibu ya Master haya, Matt.26:6-9 yaliweka sawa akili na mawazo from sembe na si Roho bro.

  ‘’Comments za Seleli, maana zinawakilisha aina fulani ya wakristo ambao ni msiba kwa kanisa’’= mmh! Wakristo gani hao Sungura kama si maneno yako tu! aya sema,be free, tuko huru ktk platform hii! On the other hand, najaribu kufikiri Mchungaji mwenye washirika aina yako kama 5 tu ktk kundi la say 1000 na liwe kanisa la Wiyani au Tarafani, kwakweli, HE MUST BE VERY SURE KUA ALITWA aisee! Lo! maana Kondoo si Kondoo and Mbuzi si Mbuzi.Unajua kupitia wewe naendelea kufahamu jinsi gani Wachungaji wetu wanavyohitaji kutiwa moyo na pia kuombewa Mungu wangu, mwe! Can you imagine brother Sungura, Pastor wako akae ktk wito na nafasi yake Jan-Dec, years and years kuhahakisha aina yako muhumini wewe unafika mbinguni! Man, I telling you, Mungu awasaidie tu Servant hawa.

  Press on.

  Seleli

 156. There u are Kaswahili.
  Tena nahisi Seleli ananyemelea kuwa mchungaji . Nami natangulia kuwapa tahadhari watakaokuwa washirika wake kwamba wajiandae kukamliwa vya kutosha ili bwana mkubwa ale na kunywa. Maana kwake washirika ni shamba la kuvuna na kula kuku kwa mrija. Wengine kama wajane,yatima, waimbaji, nk. watajiua huko.

  Hata hivyo tujipongeze kwa kule tu kuweza kutoa muda kusoma comments za Seleli, maana zinawakilisha aina fulani ya wakristo ambao ni msiba kwa kanisa.

 157. Yaani ningekuwa nawe karibu EDWIN SELELI bila kusita ningeita Abulance fasta!

  Kama huna cerebral malaria, basi ushawahi kuugua degedege utotoni. fuatilia historia yako utotoni. make unaongea weee… utadhani umemeza memory card bwana! unayoongea yenyewe hayana subtance yoyote ktk hoja inayotakiwa kujadiliwa. unarukaruka tu kama mbayuwayu.

  Hoja inayojadiliwa hapa ni utoaji wa fungu la kumi au zaka makanisani leo. kwamba je, fungu la kumi ni hiari ya mtu kutoka moyoni mwake kama 2wakor inavyoelekeza au inabaki ni sheria pia ktk hili agano jipya?

  Hakuna anayepinga utoaji hapa, ieleweke. badala ya mtu kuja na facts kuhusu hoja iliyopo mezani, anakuja na maelezo mareeeefu ambayo hata hayajikiti kwenye hoja inayojadiliwa. ni umbayuwayu tu kuruka huku na kule aimlessly. bw. edwin, ulaya wachungaji ambao wewe unawaita makuhani wanalipwa mishahara na kanisa. yes, wanaweza kupewa nyumba na gari kwa ajili ya huduma, lakini pia wana aidha biznezi au kazi zao wenyewe. hakuna ukupe na u-oya oya kama wa hawa wanaolowa suti nzima hadi wanatoa na tai jicho limewatoka na mishipa yote ya uso wakihubiri kwa nguvu zote wakia-accuse watu wa mungu kwa fungu la kumi. ufisadi umeshamiri mpaka makanisani. watu wamegundua njia ya kuukata ktk maisha kwa kisingizio cha maono ya kumtumikia mungu. tunashuhudia wachungaji wanamiliki hummer na magari mengine ya kifahari na majumba makubwa ya kifahari ilihali bizinezi zao ni church tu, huku humohumo church kuna washirika maskini wa kutupwa! si bora mwl. nyerere ambaye hakuona fahari kujifaharisha wakati wananchi wake ni maskini wa kutupwa. nahisi na wewe ni walewale tu wasaka tonge kwa mgongo wa utumishi wa mungu. acheni uvivu. jifunzeni kwa paulo ili jina la mungu litukanwe bure. 2wakor.3:7-9 bibli yangu ya kiingereza inasomeka hivi: for you yourselves know how you ought to follow our example. we were not lezy when we were with you. we never accepted food from any one without paying for it. we worked and worked so we should not be a burden to any of you. we worked night and day. we had the right to ask you to help us. but we worked to take of ourselves so that we would be an example for you to follow. wachungaji maslahi na wavivu leo wataweza hii? tena utawasikia wengine wanawatolea uvivu washirika wao, eti: nayajua baadhi ya mkanisa hapa ambayo washirika wake wamewanunulia wachungaji wao vx na wamewajengea nyumba nzuri lakini hapa watu wagum wa kutoa ndiyo maana hambarikiwi.

  point moja ktk mchango wa bw.siyi nimeipenda ambayo ni ukweli kwamba, utoaji ni kielelezo cha upendo unapofanywa kwa hiari kutoka moyoni mwa mtu. awali hapo nyuma nilitangulia kusema, baada ya watu kujikita ktk hoja ya msingi kujibu hoja za kina sungura na maswali ya msingi yaliyowekwa mwanzoni kabisa amin jeremiah, hakuna mtu atayekuja na hoja zenye mantiki akajikita katk hoja ya msingi kujibu maswali ya amin jeremiah na kuweza ku-counteract hoja za sungura ambaye msimamo wake ni kwamba, utoaji wa zaka haupaswi kuwa ni sheria. bali itolewe kwa hiari na upendo wa moyo. ameanza ibrahim na yakobo akaonesha jinsi walivyomtolea mungu fungu la kumi kwa hiari. akaonesha lini zaka ilianza kuwa sheria na kusudi la mungu kufanya hivyo. na akaonesha baada ya ukuhani kubadilika hilo sharti halipo na halituhusu sisi leo hii. akasema kama kuna mtu anaweza ktk agano hili jipya kutuonesha ambapo yesu au hata mitume walipoongelea suala la fungu la kumi ktk matoleo na likasisitizwa kuwa ni sheria hakuna aliyefanya hivyo na hakuna anayeweza kufanya hivyo zaid ya blah blah za kimbayuwayu.

 158. Ndugu Seleli;

  Hatuongelei utoaji generally, bali tunaongelea utoaji wa zaka, na wenyewe ktika mukdha wa kama leo kutoa zaka ni lazim au hiari.

  Kulazimisha kuongelea utoaji kwa ujumla wake ni kupoteza muda wa kuandika maneno mengi ambayo yako nje ya mada. Hakuna anayekataa utoaji hapa kama unasoma hoja za wachangiaji kwa umakini.

  Halafu nikakwambia unaandika too much,make your points short, maana muda wa kukaa na kusoma makala ndefu wengine hatuna Seleli.

  Hoja ya zaka tumeianzia kwa Ibrahim, hatujaianzi agano jipya kama unavyodai Seleli. Kama na kwa Ibrahim ni karibu sana, mimi sioni zaka nyuma zaidi ya Ibrahim, labda nioneshe.

  Seleli nini tofauti ya hekalu na kanisa? una uhakika na ulichosema kwamba zamani lilikuwa hekalu na leo ni kanisa?

  Kumbuka walawi lilikuwa ni kabila haikuwa huduma. Huduma ilikuwa ni ukuhani. Na suala la zaka kama sheria iliwekwa kwa sababu huo ukoo haukuwa na urithi wa ardhi kwa agizo la Mungu (nimeyasema hayo).

  Leo hii tukiongelea ukuhani inabidi wahudumu wa huo ukuhani waitwe wayuda siyo walawi tena. Na wayuda walikuwa na urithi wa ardhi hivyo hawalazimiki kuishi kwa zaka kama walawi ambao hawakuwa na ardhi. Kwa mantiki hiyo suala la zaka kama sheria linakufa lenyewe. Maana kilichokuwa kinamkasirisha Mungu mpaka kuwaita watu wake wezi ni kutokuwatunza hao walawi, hivyo kusababisha wasimfanyie Mungu huduma hekaluni na Mungu alipokosa kufanyiwa huduma aliwapiga Israel. Mimi na wewe leo siyo walawi ni wayuda.

  Kwamba mtenda kazi anastahili ujira wake; sawa kabisa Seleli. Ndio maana Paul wakati mwingine alifanyiwa machangizo, lakini hakuwahi kusema kuwa watu wakusanye zaka apelekewe, zaidi sana alifanya kazi kwa mikono yake, wala hakumlemea mtu/kanisa.

  Seleli nikikwambia kuwa hauko makini unakasirishwa, lakini huo ndio ukweli. Tangu mwanzo mie nasema kuwa zaka ni sadaka ya hiari kama ilivyokuwa kwa Ibrahim, lakini naona hukuyasoma hayo nilipoyaandika.
  Maana ona unavyoniambia hapa, nakunukuu: ”Sasa kwakua Agano Jipya leo, mambo hufanyika kwa hiari, je mtu akiamua kwa upendo wake tu kutoa zaidi ya fungu la ten, kuna tabu? si hiari bwanaa? si love yake kwa Mungu? mbona ni simple logic iyo bwana Sungura? Hence, kama hiari ni bottom-line ktk utoaji wowote Agano Jipya then anything OUR OF HIARI is possible and justified, as simple as that, right?. Au kama 20, 30, 50 ni nongwa au inakuchanganya, basi na suggest kwako kua akitoa 20,30 then sema tu ametoa fungu la kumi mara 2, 3! Simple! Some wapendwa bwana, kazi kweli ”

  Unaona hicho kisentensi ulichomalizia ‘some wapendwa bwana, kazi kweli’ .
  Unaona mimi ni mtu mgumu kuelewa eh?. Wewe ndo mgumu kueleweka ndugu.
  Ona nilivyowahi kusema katika mchango wangu wa kuhusu zaka kuwa hiari, najinukuu: ”Kwa hiyo leo zaka ni kitu cha hiari kama wakati wa akina Ibrahim. Lakini utashangaa leo zaka imekuwa sheria kali kuliko hata wakati wa mafarisayo. ”

  Kwa habari za Kornelio nilikwambia hauko makini kwa sababu hoja iliyoko mezani si utoaji wa sadaka za kawaia bali utoaji wa zaka, na wewe ukanukuu habari ya mtu aliyetoa sadaka. Seleli usitake kufundisha kitu ambacho si mada tunayoongelea ( yaani utoaji kwa ujumla) ati kwa sababu tu unaona kuwa una facts za kutosha. Kama unataka tujadili hicho kilete kama hoja inayojitegemea.

  Seleli ona kitu unachoniambia hapa ” Sasa kama una concern zako kua nafaidi sana, ooh waimbaji , wajane,yatima hawapewi, kwani wewe ndio Mungu? can you out smart God? Alivyopangaga kua Makuhani/Walawi wazitafune kwa raha zao sadaka na zaka zote, kulikua hakuna hao humans unawaowaonea huruma sana? Ni huzuni iliyoje!

  Ivi unajua sawasawa waliokuwa wanatakiwa kula zaka ni nani na nani?
  Ivi unajua kuwa makuhani, waimbaji, walinzi, nk. wote waliokuwa wanatumika hekaluni walikuwa wanatakiwa kupata sehemu ya hiyo zaka? Na hao ndio walitengeneza kitu kinaitwa walawi.Kwa kiswahili kingine ni kwamba ukoo wa Lawi pekee ndio walitakiwa kufanya huduma za hekalu.

  Sorry for this Seleli:

  Seleli umeandika vitu vingi sana vya kipuuzi na visvyokuwa na hekima ndani yake. soma makal yako paragrafu ya mwisho kabisa utaona.
  Nimejizuia sana kukujibu sawasawa na huo upuuzi wako. Siko hapa kusoma makala zako ndefu ambazo sehemu kubwa zimejaa utoto japokuwa nahisi wewe si kijana mdogo.

  Wewe kama unaona kuandika makala ndefu iliyojaa pumba ni sifa, andika tu wanaopenda kusoma pumba kama wapo watapoteza huo muda. Kumbuka hoja hii ililetwa na Millinga ikiwa ndani ya ”…mafundisho potofu’….’, lakini SG kwa busara wakaamua kuitenga ili tusijichanganye katika kuijadili, lakini pamoja na hayo wewe unalazimsha kuichanganya bado. Halaf nikikwambia fupisha dondoo zako unaona huo ni upuuzi.

  Seleli ukiendelea kuandika makala ndefu zenye kutoka nje ya mada sintohangaika kukujibu, watakujibu wegine wenye muda ya kusoma hayo.

  Hata hapa umenifanya niandike sana!!!

  Asante

 159. Sungura,
  Mtu akiwa amevaa suruali na ukamwambia amevaa kaputura, nani atakua na tatizo?
  Kwanza nilidokeza toka mwanzo kua ktk maoni yangu, ninapenda kujenga msingi wa hoja zangu kwa kuonyesha tabia mojawapo ya Mungu ambayo ni Utoaji maana wanadamu wahusianapo na Mungu, huambiwa na huyo huyo Mungu aidha kwa maelekezo ya sheria iliyo andikwa mioyoni mwao au ya nje.Kujua kama tuyafanyanyo ni sawa au la, tunaanzia kwa Mwenyewe, overlooking the source of everything leads to confusions. Nigetegemea umakini wako(well,kama upo kweli kwa sababu nimepitia uliyo comment kujibu yangu but..mmmh!), ungekusaidia kuona mara moja KWELI MUNGU NI MTOAJI NA ANAITIKIA VIPI AU AMEHAIDI NINI KWA WATOAJI/UTOAJI-wa aina zote. Kushindwa kutoka na icho as one major theme ktk maoni yangu, kwangu ninaona tayari huo umakini wako may be uko ktk mambo mengine not in this mada ya Zaka specifically and Utoaji Generally.

  Kwamba nimeongelea mambo mengi wakati tunaongelea Utoaji wa Zaka! It is very funny people would wish to go for easy way and cheap stuff na kutojishughulisha na main issues ili nyingine zijiseti tu zenyewe. Kama mtu akiongelea tu damu ya Yesu na thamani/kazi yake ktk maisha yetu Agano jipya badala ya kuanzia ilikuaje kuhusu damu za wanyama na mapatanisho kipindi cha Agano la Kale, will it make sense? Ni rahisi watu wachache to make sense out of a lecture ONLY on the blood of JESUS today lakini wengi will make a lot when discussing LEO from JANA na during this process it is common mambo mengi kujitokeza, hence, kufanya iyo ni major concern, again tunarudi kule kule, ‘’kumwambia mvaa suruali kua amevaa kabutura parable/illustration!!!!!
  Kwamba leo hakuna Makuhani wala Walawi bali ni Mitume, Manabii, Waalimu, Waainjilist, Wachungaji! Hii ni sawasawa na kusema, leo hakuna Wanyama wala nyama bali kuna Simba, Chui,Fisi, Duma! Halafu ghafla tena unasema,Wanyama wala nyama ambao Simba ndio Mkuu wao leo wapo ila hawaonekani kwa macho! What is this! It is very disappointing on the level people can argue or table their thoughts! so awkward like this wakati wana-imply kua wao ni makini na eti wengine sio! Biblia inasema Agano la Kale ilikua na kivuli cha mambo yajayo/yaliyokua yaje later, yaani kwa maneno mengine, ilikua ni ‘negative’’ halafu ukiisafisha unapata ‘picha’ hasa-Wakolosai.2:17. Sasa kama zamani Mungu aliwatenga watu kwa kazi maalumu na kuwapa rights fulani na walitoka ktk specific tribe, leo hii Mungu huyo huyo anawatenga/waita watu pia kwa ajili ya kazi izo izo kwa namna ya leo! i.e. LEO ni JENGONI KANISANI ilihali JANA ilikua JENGONI-HEKALUNI.

  Majina yanaweza badilika from Walawi/Makuhani to Wachungaji, it was ‘negative’ then but leo ni picha yenyewe! Mbona hii ni rahisi kabisa kuelewa! Kwa mtu makini kama mnavyojidhania/dhaniwa, hili ulioni pia! Lakini basi ili kuridhisha watu wanaokariri mambo kama yalivyo, Biblia ktk 1Petro.2:9 inatuita kua sisi ni Ukuhani mtakatafi na pia kama ilivyokua zamani kazi za Makuhani ndivyo ilivyo leo kwetu, 2Wakorinto.5:18-21 inasema,tumepewa huduma ya upatanisho pia, therefore ni rahisi kabisa ku-conclude Biblically kua leo Walawi/ Makuhani tupo namely ni mimi na wewe na wengine in broader terms ( kama hujitambui, ilo ni tatizo jingine!) na in specific manner, kama ilivyokua Kale kua walitengwa hata kutokua/kujishughulisha kua na particular assets bali wakae kuhudumu Hekaluni, ivyo ivyo kati kati yetu ALL WE MAKUHANI NA WALAWI WA LEO, ikitokea mmoja wetu akawa commissioned na Kuhani Mkuu kua ni wa nyumbani mwake Bwana siku zote basi ni Mlawi haswaa. Na kwakua ni ivyo then kwanini hasipate haki ya kuhudumiwa? Si imeandikwa mtenda kazi amestaili ujira wake-Luka.10:7 na pia imeandikwa uzimzuilie nafaka maksai cow apulapo na kwamba nani anaendae vitani kwa gharama zake mwenyewe, nani apandaye mizabibu hasile matunda yake, au achungae mifugo hasinywe maziwa yake au kama wamewapandia vya rohoni, ni kitu cha ajabu kuvuna vya mwilini au wanaotumika madhabahuni si wana haki ya hushiriki matoleo ya madhabahu na kwamba Bwana ameamuru, wale wanaohubiri Injili, waishi kutokana na Injili-1Wakorinto.9:1-15. Ati Ukuhani wa leo hakuko Jengoni bali moyoni! Well, it is too sweet to be true na ni kama iko kiroho sana statement hii but practically, hamna kitu hapo! Let me test it/you…ehe! Niambie ukifiwa, unataka kuoa, kuombewa,kushiriki meza ya Bwana, kuendesha ibada, kuhubiri, kuonyesha upendo kwa ndugu, kutembelea wagonjwa, kumbariki Mtumishi anayekulea( au unajilealeaaa nini Sungura? yaani Baba, Mama, Shangazi, Kiranja, Kaka Mkubwa wa kiroho kwa miasha yako, wote hao ni wewe mwenyewe au siyo), kuzika, kubatiza, counselling ya ndoa inayotaka kuvunjika, uchumba unaokwenda mrama, aya yote yanafanyikaga wapi na nani uyafanya/ukufanyia? Ni rohoni/moyoni eti ee? Very funny indeed!

  Umesema Paul aliishi kwa kushona mahema! SI KWELI! Sema ivi, alifanya kazi nyingine, in this case ya tent making ili kupata kipato na anointed thinker mzuri, will say ili KUONGEZA KIPATO kuweza kusaidia wengine na huduma yake e.g. may be wakati wapendwa walipokua wagumu kutoa, kama ilivyo leo. Angekua anaishi kwa tent making tu, asingesema aliyosema hapo.-1Wakorinto.9:1-15. On the other hand, kwasababu ya aina ya wapendwa na prevailing situation, kuna nyakati kadhaa, alijizuilia haki iyo aliyoisemelea anayo ktk maandiko hayo, angalia mistari 1-6,12, nonetheless, studying about Paul na nature ya huduma zake ktk makanisa yote ya mataifa/maeneo kadhaa kwa dunia ya wakati ule, kujizuilia kutumia sadaka na matolea mengine, haikua the order of the day nor the rule of the game kwakwe. Lakini hata ivyo, simple common senses activation would help someone kuona kua kwa nature ya huduma ya Paulo e.g. safari zile, uzibe ule, wakati gani angeweza pata muda kukaa na kutengeneza mahema ili kuishi? Hey! Guy, come on, ingawa tuna Roho Mtakatifu but being anointed is no excuse for thinking and actually thinking big and fruitfully. Wewe mtu ni fire kwa gombo mwanzo-mwisho-24/hrs halafu wife/watoto wake hakuna record yake, ni gombo tu kwa kwenda mbele, lini na saa ngapi kila mara alikaa na kuanza kukomalia kusuka mahema?
  Umekataa kua Mtu akitoa 15, 20, 50 si zaka! Fine kwa maana ya religious understanding ya mambo ya Mungu kwakua base hapa ni sheria STRICTLY ilisema nini lakini hapo hapo tumesha-establish the truth kua Ibrahimu na Yakobo walitoa zaka kwa hiari. Sasa kwakua Agano Jipya leo, mambo hufanyika kwa hiari, je mtu akiamua kwa upendo wake tu kutoa zaidi ya fungu la ten, kuna tabu? si hiari bwanaa? si love yake kwa Mungu? mbona ni simple logic iyo bwana Sungura? Hence, kama hiari ni bottom-line ktk utoaji wowote Agano Jipya then anything OUR OF HIARI is possible and justified, as simple as that, right?. Au kama 20, 30, 50 ni nongwa au inakuchanganya, basi na suggest kwako kua akitoa 20,30 then sema tu ametoa fungu la kumi mara 2, 3! Simple! Some wapendwa bwana, kazi kweli.

  Kuhusu Kornelio, umesema sio Zaka aliyotoa! Kwani nani amesema ni Zaka? Unaweza pitia tena niliyosema wakati natoa mfano wa huyu kamanda? Where is so called umakini wako hapa man?

  Kwamba umesema tuache longolongo! sasa post yangu ya kwanza niliyofundisha kuhusu Utuoaji in general na zaka in specific na nguvu yake/yaani Utoaji ulisababisha nini kwa wapendwa pia mwitikio wa Mungu then comments zako ambazo kwakweli zina lack stones, na my reply zangu za sasa, who is indeed longo longo here? be honest!

  Kwamba Wachungaji tu wanakula Zaka! Sasa ulitaka ale nani, wewe au Kulumanzira asiye wa madhabahuni permanently? Refer nilichosema juu hapo Kimaandiko, kwani Wachungaji wanakula kwakua wameamua wao au wana ruksa toka JUU? we vipi Sungura mbona unaleta uanaharakati wa haki za binadamu ktk mambo ya Mungu na body of Christ? The Church is not Political/Asasai zisizo za Kiserikali entities kaka. Kama Wachungaji, Wainjilist, Waalimu, Manabii, Mitume, Mkristo, Mimi,tunafanya kazi ya Walawi/ Makuhani kwa form/fashion ya Agano Jipya na on specific permanence of duties ya altar Minister ni ruksa kuzila zaka na mambo yako tena huku ninanena kwa ndimi barabara kabisa. Sasa kama una concern zako kua nafaidi sana, ooh waimbaji , wajane,yatima hawapewi, kwani wewe ndio Mungu? can you out smart God? Alivyopangaga kua Makuhani/Walawi wazitafune kwa raha zao sadaka na zaka zote, kulikua hakuna hao humans unawaowaonea huruma sana? Well, wanaweza sadiwa if and when possible but si lazima kutoka kwa zaka. Namna gani hapa kulazimisha politics na human feelings/concerns, as good as they are yet contrary to the divine arrangements!

  Hakuna anayelazimisha kuishi nyakati za Malaki lakini pia equally important, hatuwezi kupuuza some truths zina hamu moja kwa moja toka KALE NA LEO AU ZIMAHAMA INDIRECTLY KATIKA FORM/FASHION NYINGINE YA KILEO. Kwamba katika post yako iliyotangulia unasema kutoa Zaka ni sawa ila iwe kwa hiari, sasa makelele yote ya nini Sungura na kutufanya tuandike wee kumbe unaelewa! Kama kwenu mnalazimishwa, mnamantatizo nyote but watu wa Rohoni, Watumishi, hawawezi lazimisha mtu kutoa matoleo yoyote, hapa naona umeongeza sukari kama si sukari guru. Labda pia utofautishe wakati Mchungaji wako anapokua jasiri kusema kweli, kufundisha kweli ya Neno kua asiye toa zaka, Bible imekuita ni mwizi equal to kibaka, akikomaa Pastor wako na kurarau tabia iyo chafu akiwa ndani ya Neno, usitafute janja ya kutoroka na kuanza kusema oooh! tunalazimishana, tukanwa! We pona tu ndugu. Kama ni kulazimishwa au kutukanwa mwizi-kama kweli kuambiwa/tajwa kwa jina lako /tabia yako ni tusi, basi si Pastor wako bali Mze wa siku ndio aliianzisha saga ilo na kama una ubavu, mgunie/mgomee Mola uone! Plz leave your Pastor alone, He/She is innocent, only doing the right thing kukuchana live ili mpone nyie Wapendwa wakorofi ktk Utoaji wa aina zote

  Hatimaye umeomba nifupishe comments zangu! Mwe! Jibu langu ni STOP UVIVU, soma! Mnaangalia mechi ya Brazili na Spain fainali za Kombe la Mabara zimepita dk 90, tathmilia na movies ktk series masaa 6, unasoma novel kubwa kuzidi Bible, Magazeti 4, unafuatilia British Premier mwanzo mwisho, unapiga mastory na wapendwa/staff wenzio masaa, umesoma rasimu ya Katiba yote, shuleni na Vyuoni mmekula books kubwa kubwa na hata papers mmeandika, unashindwa kusoma nusu page, page au pages 2 za majadiliano ya mambo ya Ufalme! Wacha uvivu Mtanzania!!!!!!!!!! Read,read.
  Press on.

 160. Seleli sioni kama uko makini.

  Umeandika comment ndeefu, halafu umechanganya mambo mengiiii, wakati hapa tunaongelea utoaji wa zaka.

  Lakini kuna mambo umesema acha nikujibu:

  Umesema habari za walawi na makuhani kama watu ambao wanapaswa waishi kwa zaka. Hii siyo kweli maana leo hakuna walawi wala makuhani, bali kuna mitume, manabii, wainjilisti , wachungaji na walimu. Na ukuhani uliopo leo ambao Yesu ni kuhani mkuu hautumiki katika hekalu la mawe bali liko rohoni,yaani moyoni mwako.

  Kama hizi huduma tano zinatakiwa kuishi kwa zaka, basi Paul asingeishi kwa kushona mahema.

  Umesema habari ya kutoa zaka ya 20% na 50%. Seleli hiyo siyo zaka ndugu yangu. Sheria ya zaka haikuruhusu mtu kupunguza wala kuongeza. Hiyo simply ni sadaka tu ya kawaida ambayo mwenye kuitoa hudhani ametoa zaka

  Umeongelea habari za Kornelio kuwa utoaji wake ulifanyika ukumbusho mbele za Mungu, ni kweli kabisa. Lkini hakutoa zaka bali sadaka tena kuwapa wahitaji. Na huo ndio unatakiwa kuwa msingi wa utoaji leo. (Acts 10:1. At Caesarea there was a man named Cornelius, a centurion in what was known as the Italian Regiment. 2 He and all his family were devout and God-fearing; he gave generously to those in need and prayed to God regularly. 4 Cornelius stared at him in fear. “What is it, Lord?” he asked.
  The angel answered, “Your prayers and gifts to the poor have come up as a memorial offering before God)

  Tuacheni longolongo wakristo wenzangu, huu ndio aina ya utoaji ambao tunatakiwa kuufanya leo, lazima tutabarikiwa.
  Sio kung’ang’ana na utoaji wa zaka ambazo huwa wanakula tu wachungaji huku wajane, yatima, wageni, wagonjwa, masikini wakiachwa bila kukumbukwa, halaf mtu anarudi nyumbani kifua mbele kuwa amemtolea Mungu.

  Makanisa mengi hata kuwakumbuka tu waimbaji leo kwa nauli ni kazi ngumu wakati karibu siku nne za wiki huwa wako madhabahuni wanamtumikia Mungu, halafu unasema zaka ni ya makuhani, wapi hao?.

  Tusijilazimishe kuishi nyakati za Malaki wakati hazituhusu leo, bali ni watu fulani waliamua kufanya kwa akili kuwabana wakristo watoe kwa lazima kwa kuwatisha kuwa wasipotoa zaka watakuwa wanamwibia Mungu.

  Seleli make your points short please!!!!

 161. Siyi ni wewe Siyi yuleyule ninayekufahamu au huyu ni mpya!!!
  Mbona unasema kama mtu mwingine tu asiyejua kujenga hoja?

  Kwa habari ya suala la sabato,hilo tulilijadili sana miezi miwili -mitatu iliyopita, kama bado linakusumbua basi ni kwa sababu umeamua kutokuelewa, hivyo endelea kufanya unavyoona wewe ni vyema.

  Juu ya utoaji umenishangaza sana Siyi vile ambavyo umekuwa ”partial” kuhusu msimamo wangu. Wewe unanishambulia kwa habari ya utoaji kwa jumla, wakati mjadala uko ndani zaidi, yaani tunaongelea zaka ambayo ni sehemu ya huo utoaji. Tuko deep tunajadili kwa nini zaka iwe sadaka ya lazima na si hiari???

  Mimi nimesema zaka tunaiona kuanzia kwa Ibrahim, wewe unasema kuanzia kwa Adamu, sijui kama unaweza kututhibitishia hilo.
  Hapa hatuongelei utoaji kwa ujumla wake,bali tunaongelea kipengele cha zaka ambayo bila shaka unaelewa ina kanuni zake za utoaji ambazo mtoaji hutakiwa kuzifuata.

  Mimi msimamo wangu ni kwamba zaka si sadaka ya lazima kama ambavyo wengi mnadai , bali ni sadaka ya hiari.

  Siyi umenukuu mistari mizuri sana ambayo kama ungeitafakari sawasawa maana yake, ungeelewa ninachokisema hapa.
  Nakunukuu:”2Wakorintho 9:7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”

  Sasa kama unajua si kwa huzuni wala kwa lazima, kwa nini leo zaka watu wanalazimishwa kuitoa, tena kwa kuandika majina na kupewa lisiti, mbona haiwi hivyo kwa sadaka zingine? Au ninyi wasabato kwenu mnafanyaje?

  Siyi naomba uje na hoja zenye mashiko, kama una cha kusema kuhusu zaka naomba uingie deep. Kama huna basi endekea tu kusoma hoja za wengine maana kwa kweli umekuja na hoja nyepesi sana.

  Lakini nahisi uliamua kuchangia kwa sababu niligusia suala la sabato. Kumbuka hilo hatulijadili hapa, nililigusia tu kama mfano.

  Asante.

 162. HOJA YA PILI YA MR.MILINGA NA MAONI YANGU

  Milinga:Mafundisho kuhusu kutoa ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato

  Maoni: Ni ajabu kweli kuona jinsi gani watu/wapendwa wanavyoweza kukazana kweli kutafuta mipenyo ili tu kutotoa fungu la kumi TENA KWA AJILI YA MAMBO YA MUNGU LAKINI KODI KWA SERIKALI AMBAYO NYINGINE ZINAKWENDA KUTUMIKA KWA UFISADI WA KILA AINA, HAWAKAZANI KUIKWEPA AU HATA KUICHUKIA BASI. Si kwamba ni ajabu tu lakini kwa kua Biblia inasema yaujazayo moyo ndio yanamtoka mtu yaani kwa maneno yangu, ile ‘software’ yenyewe kabisa ya mtu/mpendwa akiwa mwenyewe halisi, ile/yule ‘yeye’ haswaaa, hata akifanya pretedence awapo kati ya watu wa Mungu wenziwe, hua haifichiki ndipo sa unaona mtu kabisa anampenda Mungu na kufahamu tabia zake kuu, moja wapo kubwa sana mbali na ile ya Utakatifu ni hii ya utoaji, nevertheless, bado mtu au mtoto wa Mungu anakomaa kutafuta kamlango ka kuzibania noti zake izo tena chache kweli wakati wako wana wa Mungu wameshavuka pingu za mateso ya roho za ubinafsi na kujipenda nafsi wenyewe kuliko Mungu na sasa hawaongelei fungu la kumi kwa kua hayo ni mambo basics kwa faith beginners! bali wanaongelea fungu la 15,20,30 na wengine 50! Napenda kuchangia hoja hii kwa ku-estabish solid ground ya tabia hii ya Mungu ya Utoaji na mapenzi yake kwetu kwa ujumla kisha nita-conclude kwa nguvu nyingi sana in Jesus name kuhimiza na kutia moyo utoaji wa aina ZOTE na kwa frequencies ZOZOTE, ziwe short or long waves because we love Him and all what we have and mpaka sisi wenyewe ni mali yake, we got nothing we own for real on serious note!

  Katika Yoh.3:16 Mungu aliupenda Ulimwengu kisha AKAMTOA mwanae wa pekee. Yesu alisema ktk Yoh.15:13 hakuna love kubwa kama hii ya mtu KUUTOA uhai wake kwa ajli ya rafiki zake na Paul anamnukuu Bwana ktk Mdo.20:35 kua ni baraka zaidi au Heri (ni bora/furaha/yafaa/njema nk) KUTOA kuliko kupokea, hapa tabia njema ya kupenda kutoa/kujitolea inatiliwa maanani/mkazo kati ya wanadamu

  UTOAJI ulipelekea mpaka mtu ambaye hajaokoka akasikilizwa mbinguni na kumbukumbu ya utoaji wake ikawa smartly and correctly recorded na some ‘’Bill Gates tools users angels’ in heaven-Mdo.10:1-4. Si tu yeye bali wokovu uliwapata hata majirani, housemaids, marafiki, ndugu na jamaa zake..Mdo.10:24,44-48! can you imagine that for a second! Jinsi gani nguvu ya Utoaji ilivyo? Japokua ni plan ya Mungu toka hakujawekwa misingi ya dunia sisi tuokolewe lakini kwa hapa naona Bwana alifanya ‘emergency strategy’ ku-manifest iyo plan iliyokuwepo tu toka mwanzo.

  UTOAJI ulipelekea Mungu kujisikia raha mpaka ku-confirm na ku re-affirm commitment yake kuhakikisha Ibrahimu ana pata uzao mwingi ambamo humo humo Masiya angetokea pale alipomtoa mwanae wa pekee bila utani wala maigizo au danganya toto game, kumchinja kama sadaka ya kuteketezwa. Na kwakua Mungu huona mioyo, alijua dizani ya wapendwa kama Ibrahimu means business inapokuja swala la kumwamini na kumuishia Mola kwa kuachilia kila alichonacho kwakwe ivyo ilibidi Mungu aweke malaika mmoja awe on standby. Ndiposa aliponyanyua/nyoosha tu mkono wenye kisu kushusha kwa koo la innocent son Isack, rocketfully an angel on duty/guard akafanya hima kumwita mpendwa maridadi kabisa yule kwenye utoaji tena wa zaidi ya fungu la kumi…your own ONLY loving son,da! iyo kitu ikawa tamu sana mbele za Mungu, ikamshinda kuvumilia/kujikausha ndipo akatoa appreciations( inapendeza kuona kua Mungu ana-appreciate pia a well done job ya mtu,hapuuzi au kujifanya hai-feel!),moyo wake ukayatoa yalioujaza au yaliyobubujishwa na tendo la Utoaji la senior brother…Mwanzo.22:1-19 hasa mistari ya 12,15,16,17..Mungu anasema ‘’Sasa NIMEJUA wamcha Mungu wala HUKUNIZUILIA MWANAO, MWANA WAKO WA PEKEE( interesting arrangement ya maneno hapo , Mungu anasisitiza admiration yake hapo…see this again..’’mwanao…mwana wako wa pekee’’)

  Halafu inakua kama bado Mungu hakukata kiu sawa sawa(unajua utoaji ule ulimgusa/mshangaza sana) ivyo basi.. ‘’Malaika akamwita tena mara ya PILI toka mbinguni kusema ( unaona hapo, anaitwa tena) halafu Mungu anaona ili kukata kiu ya furaha yake na kuridhia/kuappreciate kazi njema/ tendo la Utoaji la brother, anasema maneno mazito haya.. ‘’KWA NAFSI YANGU NIMEAPA KWA KUA UMEFANYA JAMBO HILI NA HUKUNIZUILIA MWANAO, MWANA WAKO WA PEKEE! Kisha anafanya ile nilidokeza juu..Confirming na Affirming… anasema..’’Kukubaliki nitakubaliki na kukuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota na mchanga wa beach baharani. Ulishawahi fikiri vipi kama Ibrahimu angembania-bania Isack ingekuaje kuhusu Yesu kuja kutokea? Ofcoz angekujaga tu Mwokozi but kubania kwa Ibrahimu kungemkosesha yeye mwenyewe hadhi aliyonayo leo ktk mambo ya Imani na mbele za Mungu. Unaonaje/utajisikiaje wewe Rais Obama au JK akupeti-peti kwenye bega a kusema..’’aisee kwakweli sasa nimejua wewe ni rafiki yangu na unanipenda’’! mwe! Nakwambia hata kama sina pesa, ghafla BOT yote nitaona ni yangu saa iyo iyo! Sasa wandugu,why tunambania bania vinoti vyetu vya Tanzania na kuyaacha mambo ya kanisa kusota na watumishi wa Mungu/walawi wetu wa ukweli ku-sweat, wanalala njaa wakati mwingine, suti hawana, watoto wao skuli wanatimuliwa, wanakaa nyumba ya kupanga tena sebule na chumba,watoto wanalala sebuleni nk wakati nje hapo wapendwa wamebaki benzi, prado, terekta,katapilla,saloon, wana majumba Mbezi, Msasani, Bunju, Boko, Madale,Kitunda,Pugu halafu sadaka na fungu la kumi kufacilitate mambo ya ufalme na daily activities/uses ktk nyumba ya Bwana, tunakua kila mtu ni financial management experts! hata kama ulisomea kufundisha maigizo, nyimbo, ngonjera,mashairi, vyuma vya magari na tureni,siasa, idara za chama cha CCM na Chadema, human resources, kuchoma sindano ngombe na pusi or watu au kuchoma moto sodium kwa bansen burner kule lab lakini inapokuja swala la kutoa sadaka na mafungu ya kumi, suddenly tunakua Financial, Budgeting, Philosophy and critical thinking and argumentation experts!

  Kuna watu wanaompenda Mungu bila kujisaza mpaka wanatoa sadaka ya utakaso kwa familia zao kwa MAMBO YA KUFIKIRIKA! Can you imagine that? Mpendwa anavyompenda Mungu na kujua kila alichonacho si chake na kwakwe cha kwanza ni kumpendeza Mungu kwanza nasi kubania-bania mali, anatoa sadaka ya kutisha kwa kua-assume tu may be mmoja wa wana familia yake anaweza kua amemkosa Mungu-Ayubu.1:1-5 see mstari wa 5.. anatoa sadaka ya kuteketeza kwa KILA mtoto(alikua nao kumi), so kama ni kondoo au ng’ombe 10 wana uwawa kwa ajili yao just because yeye kudhani tu wenda ktk kuenenda kwao, watoto wakawa wameharibu somewhere- think about this once again-ng’ombe, kondoo au hata mbuzi 10 kuuwawa kila majira ya ibada baada ya feasting! Leo hapa Dar bei ya mbuzi/ng’ombe/kondoo mmoja ni sh ngapi? Halafu bado tunatafuta kutoroka na kuingia mitini kutotoa fungu la kumi kama moja wapo ya matoleo mengi tu ktk Bible?

  Pia kuna mpendwa hapa anampenda Mungu kiasi kwamba hata kama alipewa chance ya kutoroka kutoa, opportunity ambazo tunazisaka kweli mechanically na si God given lakini kaka Daudi hakuchangamkia iyo chance ya kuingia mitini bali aliamua kuweka akiba ya matolea yenye thamani zaidi ya fungu la kumi kwa ajili ya mwanae kuja kujenga nyumba ya Bwana- angalia madini na vito vya thamani vinatisha sana alivyoweka/toa huyu brother hapa-1Nyakati.29:2-5

  The fact that Abraham na Jacob gave tenth/tithe Gen.14:18-20, 28:22 before even specific Moses Laws or clear/popular prophets’ utterances, that by its self-cements the fact that, God loved from the past, when his people honour Him with their possessions-Proverbs.3:9

  Yesu mwenyewe ametia moyo swala zima la kua na moyo wa kutoa aliposema tutoe ili nasi tupewe kipimo cha kushindiliwa..Luka.6:38

  Nimeongelea Utoaji kwa ujumla ktk mifano hapo juu kuonyesha jinsi gani hii ni moja ya tabia kuu za Mungu na watu wake wanaomfuta kwa dhati. Na tunaposema utoaji, umo twakuta aina nyingi mifano zaka, malimbuko, changizo, sadaka za kuteketeza nk. Kwa kweli iyo hapo juu, jitihada yoyote ya kupangua /ku-adjust/ ku-harmonise /kubalance balance/kutwist focus ili watu wawe na second thought kuhusu kumtolea Mungu na hasa kwa maana hii ya zaka, ni msukumo wa kibinadamu zaidi kuliko Roho Mtakatifu na si moyo wa dhati wa kutaka kumpendeza Mungu kwa kufundisha jambo la kimbinguni la kikweliii. Pia jitihada izo zinatoa picha ya nature mbaya ya mwanadamu ambayo aidha viongozi wa mhusika kiroho au yeye mwenyewe hawajaishughulikia. Ni indicator ya madhara ya shibe kwa mtu kuanza kumsahau Mungu kwa ku-less prioritize mambo yake, ni roho ya ubinafsi na kujipenda/kujihurumia kupita kiasi.

  Mtu akimpenda Mungu, hajisazi, si tu fungu la Kumi hata Isack kabisa ambaye ni zaidi ya fungu la kumi, hatatoka tu maana kwakwe yeye twaishi na kuenenda na kupata uhai. Yaani hata kua na wazo la kua kutoa zaka kila mwezi ni upotofu! Ilo wazo on serious note, linatokana na nini au ni kitu gani kimeki-inspire icho kiwazo au kuzaa thinking/wazo ilo? Ni Roho Mtakatifu? The opposite can be very true!!!!!!!! Ukitaka kujua kua something is wrong, tujipime tu tulikuaje kabla ya kuzikamata noti? Uko nyuma? mbona tulitoa tu fresh tena kwa raha hata ubongo kama vile haukufanya kazi? leo imekuaje? Kumetokea nini? au ndio Roho anasema more clearer than the past days nini? eti eee? Mh! hamna lolote ni kiburi cha uzima/maisha ndicho kinatusumbua, heri tuwe kama zamani, vitoto vizuriiii vya Yesu kufanya na kutenda mambo yote ya Ufalme na kanisa, Mungu nisaidie mie kwanza na kisha wenzangu.

  KAMA kutoa KILA MWEZI fungu la kumi ndio kuna leta upotofu, kwangu hii ni minor issue, in fact this query is dismissed! Wajua kuna vitu so simple and minor ambavyo when are mechanically given huge weight to artificially make them sound voluminous and are made sweatingly climb the ladder, still their simplicity/lightness is vivid! Why monthly giving frequencies? Kwakua many members wa mijini na majijini wana income kupitia salary nazo hutoka mwisho wa mwezi, then logically it is easily and peacefully follows that kanisa kuweka utaratibu kwa upendo tu si kimabavu ili wawe wanatoa kila au mwisho wa mwezi, it is logical, right? kuna tabu gani hapo? Mbona wapo pia kuna members wengine ambao si wafanyakazi, wanatoa kila baada ya week, wengine siku? Kama kipato kinaingia kila week, mwisho wa mwezi, siku na mtu anaweza na anampenda Mungu wake na mambo ya kanisa/ufalme na Wachungaji wake wa KWELI( Walawi wa uhakika), si anatoa tu kwa raha na furaha zake!

  Mantiki nyingine ya kutoa kila mwezi ni kua kuna watu wengine hapo kanisani, wanahitaji kula,kulala, kusomesha watoto, kama staff wa kila siku kanisani namely walinzi, wafanya usafi wa mazingira, viti/benchi na vyoo vya kanisa ili ujapo kanisani , usianze kutukana live au moyoni ukutapo vyoo/viti vichafu mbaya, wahasibu wa kanisa, housemaids wa nyumba ya kuhani, sasa hawa wote wanatuhudumia/hudumia madhabahu na kanisa/jengo kwa ujumla, wale wapi? wanaendaje home? kodi je? Ingawa fungu la Kumi ni kwa Makuhani but kwa upendo wa baadhi ya watumishi na care zao, hasa pale washirika wanaompenda Mungu ambao hawatoi fungu la kumi bali la 15, 20, 50, basi baraka iyo hua extended kuhudumia wengine/mambo mengine pia. Isingekua kuna mahitaji ya kila siku/monthly ya mjengoni kanisani hapo na watumikao humo, well, mnaweza kukaa na fungu zenu za kumi toka jan na dec mkazitoa but hawa watumishi mtakua mmewatendea haki? Mungu alijua nyumba yake itakua na shughuli na washughulikaji ivyo anahimiza kuhakikisha iwe full kwa chakula(‘’chakula’…a symbolic language kumaanisha kuwepo na majibu ya mahitaji yake na wakaao/watumiko hapo kwa ajili yetu)-Malaki.3:10.

  Na sijui why kila mwezi iwe bonge la issue wakati wako wanapokea/ earn kila week na kutoa out of their willingness ? That is why nasema hapa hamna serious stuff for serious mind/spirit to discuss hence this case, is therefore once again dismissed mercilessly. Sana sana ni kibinadamu zaidi ndio kinachotusumbua tu wanadamu, hakuna Roho wala sincerity kua kuna kitu cha kiMungu VERY CRITICAL tunakosea/ kinamiss/tumepotoka! Mmh! kiko wapi? show us/ me here boldly! bring that substance here and we will discuss/chew it together to help/bless each other in love- which does not mean failing to speak straight to one another the truth/fact.

  Halafu embu pia tutumie common au spiritual senses/reasoning kidogo, why would God in the whole Bible, only here allows people to TEST Him ktk eneo hilo la kuleta zaka kamili uku akiwahaidi /akiwavutia/tia hamu kwa baraka za kutisha sana atakazoachia? Majibu ni hoja 3…kwanza anajua ‘much know nature’’ za wanadamu inapokuja swala la kuachilia mali/ fedha kwa Mungu( mambo ya imani kumpa/kutoa kwa Mungu aliyeko eti ndani ya Pastor/Kuhani wako na uyo kuhani azitafune izo noti kwa raha kabisa maana ana ruksa toka JUU kisha wewe uamini/ujue kwa hakika amekula Mungu halafu same same man of God wako mnakutana naye sokoni kununua bamia na sangara au na yeye anabamizwa kama wewe na ‘anopheles’ na ku-suffer badly malaria due to unfriendly parasites’ job in his body, iyo ‘much know nature’ ikishawaza ivyo kwakweli itakataa/kataza/wagomesha wanadamu wasitoe.

  Pili, Mungu anajali na yuko fair! hawezi ona Watumishi wake alio watwaa kati yetu kumtumikia kwa ajili yetu, wafe njaa, wasote usiku na mchana kuomba na kufunga wakati tuna koroma, walie na kung’ang’ana na Mungu kila mara kupata nguvu, upako na Neno la kusema ili tukija tukute/tujue kweli Bwana amesema, halafu watu hao hao wa thamani, wawe frustrated na tabia zetu mbovu za unyimivu na kubania vinoti na vishiringi mpaka wengine inapelekea wanajuta kwanini walikubali mwito na mbaya zaidi wengine wanachoka kabisa na kurudi village kulima kwakua hali ngumu, wapendwa stiff-necked wanakomoa, wamegoma kutoa zaka na hata sadaka nyingine. Thus, Bwana inabidi afanye attractions/divine tempting if you like ili wale wagumu nao wakunjue mioyo na mikono hatari iyo inayo bajeti kuzidi waliosomea class kabisaa mambo ya budgeting!

  Tatu, basi tu Mungu kama Baba, wakati mwingine pamoja na matatizo yetu e.g. ya kutotoa ili tubarikiwe, atalazimika kutusaidia tu ivyo ivyo. Unajua tena dad na watoto wake awapendae sana, so inabidi ‘kama alazimishie vile’ baraka, maana anazo nyingi lakini tunagoma kuzitwaa kwa kutoa, sasa naye anataka sana na ni raha yake kuwabariki wanae so inabdi tu sasa atushitue kidogo…’Hey! You guys/children, why are you too slow/hard, come on I have plenty in the store, give, give, give to my house or if you think I am making a joke (after all I never joke), well, test me/put me on test for this…give exact tithe then see/prove me wrong yaani if I will not do what I promised’’

  Conclusively, Kwakua Mungu mwenyewe ni Mtoaji number 1 na kwakua Watu wazito ktk Bible/imani yetu walitoa sana hata wengine mafungu ya kumi kwa vipato vyao na hata ktk kila maongezeko na vilevile Yesu mwenyewe kuhimiza moyo wa kutoa ( mafungu ya kumi yakiwemo- Matayo.23:23) na kwakua mtu akishampenda Mungu au mtu/kitu, atafanya zaidi hata ya utaratibu ili tu kukukamilisha kiu ya pendo lake kwakwe ampendaye( iwe kutoa au kutumika kila sec,saa,dk,day,week mwezi nk basi swala la kutoa zaka kila mwezi ni jema sana na ashukuriwe Mungu kwakua, wakati wengine wanaona frequencies za kila mwezi ni tabu, wengine walishatoka uko kwa beginners struggles to an advanced eagle! Ni utukufu hata utukufu, alisema, ‘’kazi nizifanyazo mie mtazifanya naam na kubwa kuliko izo( Utoaji wa zero to hero pia included hapa)

  .

  Nitaendelea na hoja ya 3 kuhusu ”wanawake kukatazwa mambo kadhaa, hapa nina interests binafsi pia kwakua when a woman is mistreated, nina tatizo kubwa na mwanaume yoyote wa aina iyo kuanzia Baba yangu mzazi, thank God ameookoka sasa. So kwa kua nilikua na background spesheli na my no more mom, expect me to be on the side of the women sana tena kwa raha na confidence zote kabisa na hoja maridhawa hasa.

  Press on,

 163. Sungura,
  Nakushukuru kwa text yako nzuri ambayo uliiandika kwa ufundi mkubwa. Ni nzuri maana hadi wajoli wa Bwana, wanakufagilia kuwa umevunja mzizi wa fitina. Pamoja na hayo yote, mimi ngoja nikueleze wapi umeimiss shabaha yenyewe.
  Kwanza, Suala la utoaji, ni kanuni ya Mungu. Ni sheria ya Mungu. Haikuanzia kwa Waisrael kama ulivyosema kaka/dada. Ilianza tangua enzi za uumbaji. Mungu alipoumba mbingu na vyote, vilikabidhiwa kwa vyote kwa Adamu isipokuwa kitu kimoja tu(mti wa ujuzi wa mema na mabaya). Unaweza kuwana tafakari ndefu kwa nini Mungu alimpa vitu vyote hivyo hivyo? Mungu ni upendo, alitaka kuwafundisha viumbe wake(wanadamu) kuwa, kutoa ni ishara ya upendo…
  Pili, baada ya mwanadamu kuanguka dhambini, upendo wa Mungu kwa mwanadamu haukuishia pale. Bado aliendelea kuwajulisha kuwa, utoaji ni tabia ya Mungu. Alimchukua kondoo akamchinja na kuwavika nguo nyingine… Ukisoma uzao wa Adamu, Kaini, Abel na wengine hadi kwa akina Ibrahimu na uzao wake, utoaji ulikuwa ulikuwa ni jambo la msingi na la kuonesha utii na upendo wao kwa Mungu. Hata kama wasingekuwepo makuhani(walawi), utoaji ni mpango wa Mungu tangumwanzo ndg yangu.
  Kipindi cha Yesu, naye aliendelea kussisitiza suala la utoaji, akisisitiza kuwa, utoaji huo sharti uanzie moyoni mwa mhusika. Luka 11:42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili. Mitume nao hawakubaki nyuma katika suala la utoaji. 2 Wakorintho 9:7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Kama wewe hutatoa kwa kisingizio cha hoja zako hizo, usidanganyike ndg yangu, utakuwa unamwibia Mungu na hautaenda mbinguni maana hakuna mwizi wala mchoyo atayeenda mbinguni.

  TATU, suala la sabato kuitunza kimwili na kiroho, mimi sijakuelewa. Nahisi na hapa napo, umemiss shabaha sana. Maana ukisema kusali jumamosi ni kutunza sabato kimwili, je, Mungu naye aliitunza sabato kimwili unaposoma mwanzo 2:1-1-3? 1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
  Je, hata Yesu naye aliitunza sabato kimwili unaposoma luka 4:16? 16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
  Je, mitume nao waliitunza sabato kimwili? Hebu soma Biblia yako vizuriili uelewe maana ya kuitunza sabato kimwili na kiroho. Hapa una shida ya uelewa kaka/dada. Jifunze kwanza maana ya kutunza sabato kimwili na kiroho ndipo utakuwa na ujasiri wa kusema hivyo ulivyosema hapo juu.
  Mwisho, nakupa shauri, ya kutoa zaka na sadaka na kuitunza sabato ya Mungu kama unavyotunza amri/sheria zingine kwa msukumo wa moyoni.
  Barikiwa sana.

 164. Nachelea hii mijadala humu ni ya watu wachanga sana kiroho na hata kifikra kwa walio wengi. Ndiyo maana nilisema, baada ya maswali ya msingi na yenye kufikirisha ya ndg. Amini Jeremiah, na hoja nzito na zenye kufikirisha pia za ndg. Sungura, kitachofuatia ni kitu kinaitwa “Religional conservatism and martyrism” yaani uhafidhina-dini na ufia dini. bw. siyi unacheka nini?! kicheko chako kinaonesha huna hoja zenye msingi na mantiki ili ku-counteract hoja za kina sungura na amini,ila kwa kuwa wewe ni mshika dini na mfia dini, hutaki hata kutia akili kuzitafakari hoja zao ili kutafuta kama kuna substance kwenye hoja zao. badala yake unataka ukajipange na wewe kuja kujibu mashambulizi. ok, kajipange bwana unaweza ukaja na hoja bora. ila ninachotegemea ni blah blah tu. hatushindani humu. hii ni mijadala yenye lengo la kusaidiana kiroho. ni kama lile baraza la lililokaa kule yerusaleemu ambalo lilihusisha wazee na mitume kuhusu mataifa wanaookoka yawapasa kufuata desturi za kiyahudi au la. matendo 15:1-20. sasa ndo maana nimesema baadhi ya watu humu ni wachanga kiroho na kifikra pia. make mtu anashindwa kuja na hoja zenye mashiko na au mantiki, badala yake analipuka na hoja nyepesi tu za kibishi na zilizojaa blah blah tu. badala ya kumshika yesu kama njia kweli na uzima, ili waijue kweli na hiyo kweli iwaweke huru kweli kweli, wameshika dini kweli kweli na imewapofusha. wameganda kwayo kama ruba huwatoi kamwe! walichokishika wamekishika. haijalishi wameshika jiwe wakaacha mkate wa uzima. watu kama kina nelson. sijui yeye kabarikiwa mwezangu kwa kuwa mwaminifu ktk zaka! make huwezi ukawasema watu hawabarikiwi kwa 7bu ya uchoyo wao kama wewe hufanyi vizr ktk eneo hilo. au wewe ni choka mbaya tu kama hao unaowa-accuse kwa uchoyo. mchango wako wewe unaonesha tu kuwa ulichokishika umekishika, hutaki kujua kabisa. uwe sahihi au la, haijalishi!

 165. Tumain asante kwa kutumia haki yako ya kuchangia mada. Lakini nasikitika sana kwamba watu tumeingia ndani sana kwenye hii mada halafu wewe unapapasa tu juujuu tena kwa hoja nyepesi.

  Wewe unaongelea tu utoaji, wenzio tunaongelea kinachotakiwa kutolewa na namna kinavyotolewa. Unatakiwa uje hapa utuchambulie kwa nini tutoe zaka leo.

  Mbaya zaidi unaongelea na mambo ya malimbuko na dhabihu. Malimbuko ni neno la kikulima na kifugaji (likimaanisha mazao ya kwanza). Leo hii sijui sadaka hiyo mfanyabiashara wa nguo, duka, catering nk,atayatoa wapi hayo mazao ya kwanza ya wanyama na mimea mpaka akayatoe sasdaka, kama siyo kulazimisha kuwa faida anayoanza kupata kwenye biashara yake ndio iwe malimbuko!!!

  Dhabihu unayoisema na yenyewe sijui ni ipi zaidi ya dhabihu ya sifa na shukurani na kuutoa mwili wako mwenyewe
  Lakini dhabihu kwa maana ya agano la kale ilikuwa ni sadaka ya kuteketezwa ambayo kwa msingi wa agano jipya sadaka hiyo ni kristo mweyewe kujitoa msalabani tena mara moja tu. Hakuna tena dhabihu ya wanyama kutolewa baada ya Yesu kujitoa dhabihu mwenyewe.

  Tumaini ninyi ndio wakristo mnaosoma tu biblia na kushindwa kutofautisha kuwa ziko tofauti nyingi kimfumo kati ya agano jipya na la kale. Hivyo kuyachukua mambo kwa ujumla bila uchambuzi wa kuelewa kuwa kuna tofauti ya nyakati,ni kitokuijua kazi alikuja kufanya Kristo.

  Unadhani kuna mkristo yeyote aliye serious ambaye anasoma biblia kama hadithi? zaidi sana kuna idadi kubwa ya wakristo kama wewe wenye kuisoma biblia kwa jicho la mapokeo na matokeo yake ni kung’ang’ania vitu ambavyo havipo kama wewe unavyotaka leo tutoe malimbuko, zaka na dhabihu ya wanyama.

  Tumaini unadhani kwamba hatutoi? la hasha, tunawapa sana watu, tena vitu vingi tu kuliko unavyodhani.

  Asante.

 166. Ubarikiwe mtumishi kwa huduma unayoitoa Mungu aendelee kukutia nguvu.Somo la utowaji limekuwa mtihani kwa wakristo wengi na hii ni kwasabu waliyo wengi ni wachoyo!Huwezi ukawa mchoyo then ukategemea utapata baraka.Utowaji ni lazaima kwa kila mwamini tukianzia zaka,malimbuko,dhabihu n.k.Cku zote wapendwa tumeshindwa kubarikiwa kwasababu yaho ya uchoyo!Thn bebu tusome neno la Mungu kwa kumruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutafsiri tusisome kama vile ni hadithi au gazeti!Ukitaka kubarikiwa zingatia utoaji.Mtumishi nashauri somo ungefundisha somo la utoaji kwa ujumla ili watu wasipitwe na Baraka ambazo Mungu anazishusha.

 167. Ndg.Amin Jeremiah ameuliza maswali ya msingi ya kufikirisha na yanayohitaji majibu anuai. Lakini Sungura amekata mzizi wa fitina. Ninachotegemea sasa ni mlipuko wa kitu kinaitwa relional consertism and martyrism.

 168. Ha ha ha haa ha ha!! Duuu!! Na wewe upo rafiki!! teh teh teh!! Nimefurahishwa sana na hoja zako ndiyo maana nimecheka sana. Ngoja nitakuijia na mimi kaka Sungura.

 169. Mathew asante kwa fafanuzi yako. Ila umeanzia kwa mjukuu Yakobo wakati zaka tuniona kuanzia kwa Ibrahim mwenyewe.

  Kuna mambo mambo ya msingi ya kuchunguza ktika utoaji wa zaka, mojawapo ni haya,kwamba Ibrahim hata Yakobo walitoa zaka kwa hiari. Lakini kufika mpaka kwa mafarisayo zaka haikuwa hiari tena bali sheria.

  Ni vema tukaelewa ni lini zaka ilitoka kuwa hiari mpaka kuwa sheria, na kwa nini ilifanywa kuwa sheria, na kwa nini sheria hiyo ilifunge kanisa leo. Pia tujue kwa nini kipindi chote cha kanisa la kwanza hatuoni mtume hata mmoja analiongelea hilo suala la zaka linaloonekana leo kuwa ni suala muhimu sana?

  -Tunajua zaka ilianza kuwa sheria baada ya wana wa Israel kutoka utumwani Misri.
  -Sababu iliyopelekea zaka kuwa sheria ni wana wa lawi ambao Mungu aliwataka wasiwe na urithi wa ardhi kati ya wale wana kumi na mbili wa Yakobo.
  Na Mungu alitaka wasiwe na ardhi ili wamtumikie madhabahuni. Lakini kwa kuwa na wao ni wanadamu mahitaji yao ya kila siku ilikuwa ni lazima yapatikane, ndipo Mungu akaamuru yale makabila 11 watoe sehemu ya kumi kwa ajili ya hili kabila moja.

  Tunajua hakuna mahali zaka imetajwa katika agano jipya ispokuwa kile kinachoongelewa kinafanyiwa rejea ya mfumo wa agano la kale, e.g hapo Yesu anapowaambia mafarisayo, na katika Ebrania 7:5

  Mafarisayo kuambiwa ”….bila kuyaacha hayo ya pili” Lakini tujiulize ya pili yapi? ni yale ya kutoa zaka za mnanaa na mboga. Kwa nini watu watoe mboga, nani alikuwa anakula hizi mbogamboga? bila shaka ni huyo farisayo ambaye ki- msingi alikuwa ni mlawi ambaye hakuwa na ardhi kama urithi.

  Je, Yesu kuwaambia mafarisayo ”bila kuyaacha hayo ya pili” alikuwa anatuambia na sisi kuwa tusiyaache? La hasha, nakataa. Mfumo wa agano ambalo mafarisayo walikuwa wanalitumikia ni tofauti kabisa na mfumo wa agano ambalo sisi tunalitumikia.

  Tofauti iko wapi?
  Tofauti ni kwamba kitu kilichopelekea kutoa zaka kuwe sheria kimsingi leo hakipo. Nacho ni uwepo wa walawi ambao walinyimwa kuwa na ardhi ili watumikie ukuhani,na hivyo Mungu kuamur zaka iwe njia pekee ya wao kupata mahitaji yao. Numbers 18:21
  As for the tribe of Levi, your relatives, I will compensate them for their service in the Tabernacle. Instead of an allotment of land, I will give them the tithes from the entire land of Israe (New Living Translation)

  Sharti la makuhani au watumishi wa madhabahu kutokutakiwa kuwa na ardhi leo halipo kwa sababu leo ukuhani hauko kwa Lawi tena bali kwa Yuda ambaye ana urithi wa ardhi( Yesu kama kuhani mkuu anatokea kabila la Yuda).
  Ndio maana leo mtu anaweza kuwa mchungaji au nabii huku anaendelea na biashara au kazi ya taaluma yake.

  Kwa hiyo leo zaka ni kitu cha hiari kama wakati wa akina Ibrahim. Lakini utashangaa leo zaka imekuwa sheria kali kuliko hata wakati wa mafarisayo. Na mimi naamini kama zaka inapaswa kuwa sheria ya lazima basi mtume Paul angeishi kwa zaka wala si kwa kushona mahema, maana alikuwa na makanisa mengi mno.
  KUNA MAMBO HUWA YANANISHANGAZA:
  -Huwa nashangaa sana ninapoona mtumishi fulani anaanza kusoma kitabu cha Malaki 3: na kuanza kuwaambia waumini wasiotoa zaka ni vibaka na wamelaaniwa, bila kujiuliza hilo andiko kimsingi walikuwa wanaambiwa waisrael ambao ndio walikuwa wanaishi chini ya huo mfumo.

  – Kwamba inawezekanaje mtu kuelewa kuwa leo hatupaswi kutunza sabato ktk mwili (Jumamos) lakini anashindwa kuelewa kuwa kutoa zaka si lazima!!!!

  – Kila siku huwa ninashangaa kuona kwamba ktk utoaji wa hii sadaka (zaka) ati mtu ni lazima aandike jina lake na apewe stakabadhi. Huwa najiuliza ambaye anatakiwa kuona hilo jina na kiasi mtu alichotoa ni nani na kwa nini, na ili iweje?

  Kusema kweli hakuna namna yoyote chini ya mfumo wa agano jipya tunaweza ku-justify kwamba zaka ni sheria ya lazima, hakuna namna!!!!

  Kilichopo ni watu kukumbatia mapokeo na kujawa na hofu ya kuambiwa kuwa usipotoa unalaaniwe.

  Kung’ang’ania hiyo sheria ni kujiweka chini ya laana ya torati, ndio maana leo wakristo wengi badala ya kubarikiwa kutokana na kutoa zaka,lakini wamelpigika na laana ya umasikini wa uchumi kwa sababu ni wachache sana wanaoupatia sawasawa utoaji wa zaka kiasi cha wao kubarikiwa.

  Anaetoa zaka atoe tu kama kutoa nadhiri kwa Mungu wala si kama sheria ya lazima, atabarikiwa!!!

 170. 1. Zaka ni nini???
  2. Yesu aliwahi kutoa zaka kama Mkristo???
  3. Kanisa la kwanza walitoa Zaka????
  4. Zaka ina kazi gani kwenye kanisa????
  5. Utaratibu wa kutoa zaka ni upi kwa mujibu wa maandiko matakatifu????
  Pengine leo niishie hapo kwa leo

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s