Mafundisho kuhusu wanawake yanatafsiriwa vibaya!!

lwakatare

Mafundisho ya kuwazuia Wanawake wasiwe Viongozi na Wasifundishe YALISHA ONGELEWA KWA KIREFU SANA nyakati za nyuma na kuamsha hisia nyingi. Maandiko ya 1Timetheo 2:11-13 yamekuwa yakitumiwa kimakosa na Watumishi wengi kama reference ya kuwanyima Wanawake Utumishi katika Uongozi na Kufundisha. Lakini niseme kuwa Watumishi hao wanayatumia maandiko hayo bila kuzingatia kanuni za kusoma na kupata tafsiri sahihi ya Maandiko.

Kwa mfano ukisoma maandiko haya utaona kuwa yanawataka Wanawake Wazee WAFUNDISHE. Naomba ninukuu “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji ….., bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili,…….” 1Tito 2:3-4. (SUV – msisitizo added). Tafsiri zingine kwenye mistari hii zinasema ” The aged women ……… teachers of good things that they may teach young women….” (KJV), “Bid the older women …….. they are to teach what is good and so train the young women…..” (RSV). Hapa mtu anaweza kujiuliza mbona hili agizo linatofautiana na ile lililopo kwenye Timetheo lakini maagizo yote mawili yanayotoka kwa mtu mmoja – Mtume Paulo? Hebu tuangalie tafsiri zingine kuhusiana na Maandiko ya 1Timetheo 2:11-13

9 Similarly also nashim (women) should adorn themselves with respectable ………………., 10 But with what is proper for nashim professing,…………. 11 Let the isha (wife) learn in silence in all submission. 12 I do not allow an isha (wife) either to have teaching authority over or to have hishtaltut (domination, taking control) over [her] man, but to be in silence. 13 For Adam was formed rishonah (first), then Chavah. (Orthodox Jewish Bible – Msisitizo added).

Ni dhahiri kuwa kuna maneno mawili ambayo yametumiwa kum-adress, mtu huyu mwenye jinsia ya kike. Neno la kwanza ni NASHIM (yaani Mwanamke) na neno la pili ni ISHA (yaani Mke). Kwa kifupi ukiusoma vizuri mstari wa 11 hadi 13 unazungumzia mahusiano ya Mme na Mke. Kwa hiyo kulifanya agizo hilo li-apply kwa Kanisa /Jamii sio sahihi na linazua maswali kama mwanamke kazuiwa kufundisha wapi, kutawala wapi? n.k. Pia jambo jingine ambalo ni la msingi kwa wapendwa kulielewa ni jinsi mstari wa 11 ulivyoanza; unasema – SIMPI …… ni nani huyo ambaye hatoi ruhusa? Je, hili ni agizo la Bwana kwa kila mtu? Hapana, lugha yake ingekuwa ni tofauti.

–Mathew.

Advertisements

186 thoughts on “Mafundisho kuhusu wanawake yanatafsiriwa vibaya!!

 1. Ndugu Siyi,

  Ni wewe ambaye hujanielewa. Utakapoeleza kwa nini wewe ni muongo kiasi kile nilichikuonyesha wakati wa kuthamathisha mjadala au wakati utakapotubu, hayo maswali yote RM atakujibu. Kwanza kabla ya kuuliza nani alieumbwa kwa ajili ya mwengine unatakiwa ufahamu kuumbwa kwa ajili ya …. inasema nini. Hali kadhalika kuwa msaidizi wa… Hivi nakuona ungali una maswali yanayo majibu kwani RM alikukimbia ukiwa muongo. Jamaniiii huko jela hakuna mzaha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Mungu akuwezeshe ili ujirekebishe.

 2. Ziragora,
  Najua hujanielewa na hutanielewa kwa maana nakuuliza hata maswali lakini hutaki kujibu. Siku ile nilikuulizeni kuwa,
  Ni nani kati ya mwanaume na mwanamke aliyeumbwa kwa ajili ya mwenzake ???? Jibu mpaka leo sijaliona. Leo nakuongezea swali la ziada linalosema,
  Ni nini maana ya Hawa kuumbwa kama msaidizi kwa Adamu?
  Najua unakwepa lakini ukweli wa mambo unaujua fika. Pole sana.

 3. Lwembe,

  Kweli mjadala haupo. Kuandika siyo kusema mjadala upo. Kuendelea kwa mjadala siyo kurudilia uliyoyasema zamani. Kuna alama zinazothibitisha kuisha kwa mjadala;

  1. Katika makala yako ya 25/03/2014 at 9:57 PM , unasema Seleli na wenzie(unamaanisha wengi), hujue hata kama ni wangapi katika unayoita mjadala. Baadaye umefika taja jina langu nyuma sana tena kwa hofu pasipo kunukuu niliyoyasema. Pia ukasema wachanga watamuona kuwa sahihi katika Neno la Mungu. Upungufu wako unakusahaulisha kama Kristo hakuja kwa wale maandishi na mafarisayo ambao walijidai kuwa wema.
  2. Unayoandika yote hamna jambo jipya. Unataka upate jibu gani? Nenda kasome uliyopewa zamani. Ndio maana ya kukuwekea tu ile ya zamani kwani najua unapenda utumie hila ili uhalalishe upungufu wako.
  3. Tulipomalizia ni hiyo nafasi unapohofia tu wakati wewe na Siyi mulijinasisha kirahisi katika uongo, baba ya waongo akiwa Ibilisi. Nikiwaona kuwa wa dhamani nilijaribu kuwadisconnect kutoka huyo Ibilisi lakini mulimpenda sana. Ukitazama vizuri utaona hoja zangu ziliishia hapo, kwa kuwa nuru na giza havichangane.
  4. Nilimfwata sana Ndugu Milinga, anayo upako wa RM. Muendelee naye pengine atawasaidia kumuacha Ibilisi. Na kama naye hafaulu, Yesu mwenyewe ataendea washughulikia.
  5. Muko sahihi kabisa mnapokosa hoja kamili na kurudilia maanguko kwani RM hawezi waangazia mkiwa kwa upande wa Ibilisi.
  6. Lwembe, ulijaribu kutubu baadae ukarudia na kusema haukutubu, huyo ni Ibilisi ambaye ana operate ndani yako. Jaribu utubu kweli uone kama RM hatakuinulia hoja zisizo na hila. Hapa tulipo, usisahau,ni kanisani ambapo imetupasa kuepuka hila na uongo wote. Fikirini muongo anaeingia madhabahuni na kuanza kukemea wanawake!!! Hivi utasikiwa kweli?
  Kwa mwisho niliwaambia mapema kama sina la kuwaambia tena isipokua kuwashawishi “kutubu na kuokoka.”

  Lwembe, Mungu anakupenda, anachochukia ni ule msimamo wako wa kupendelea kuwa rafiki ya Ibilisi ukitumia uongo na hila.

  Mungu aendelee kuwatembelea.

 4. Ndugu Siyi,

  Acha kuzusha mambo ambayo huwezi. Unafikiri hiyo pole yako itaondoa uongo wako? Ulipobandikiwa hizo hoja ni kwamba hizo ndizo zilithamatisha kiukweli majadiliano ya Ziragora na Siyi, hapo ukihusika na uongo iliokupeleka upande wa Ibilisi. Sasa kweli kama ukiomba utasikiwa na yule tu. Mwaka inawezapita pengine na makosa fulani lakini dhambi kuipona ni kutubu.

  Nadhani umedaka na utajirekebisha.

 5. Milinga,
  Maswali ya tarehe 08/03/14
  Naona hapa uliweka wazi kwa kila mmoja. Mimi ngoja nianze kwa kuchokoza mambo na nina imani wengine watakuja na nondo zaidi.

  Swali 1
  Mungu ni Mwanaume au ni mwanamke? Kwa nini ?
  Jibu
  Mungu ni mwanaume. Kwa sababu amejifunua kwetu kama mwanaume.

  Swali 2
  Malaika Mbinguni ni wanawake au ni wanaume?
  Jibu
  Nao wamekuwa wakifunuliwa kwetu kama wanaume. Majina yao ni ya kiume. Na kwa mujibu wa Biblia, wanaonekana kama viumbe wasio na jinsia japo wanaweza kujitokeza/kujifunua kwa jinsia mojawapo kati ya hizi mbili zilizopo. Kama wewe unaafahamu zaidi, tufahamishe na wenzako rafiki.

  Swali 3
  Shetani ni mwanaume au ni mwanamke?
  Jibu
  Ana umbile na sifa kama walizo nazo malaika wengine.
  Nakusubiri kwa majibu ya maswali yangu ya siku ile hapo juu..
  Karibu kwa mchango wako pia

 6. Milinga,
  Haya ni majibu ya maswali yako ya tarehe 3/3/14. Umenishangaa na unafikiri nimelogwa na kufundishwa mafundisho potofu. Unadhani mimi kabla ya kukomenti kinyume na mawazo yako, unafikiri sikusoma maana ya kuhani, kazi za kuhani na ukuhani anaouzungumzia Petro katika agano jipya. Yote hayo nayaelewa vizuri kaka. Na kabla sijakujibu, naomba nikwambie kuwa, mwanamke kuwa chini ya mwanaume, haina maana kuwa yuko inferior. Mwanamume na mwanamke, wako sawa mbele ya msalaba wa Kristo. Hakuna aliye najisi zaidi ya mwingine. Wote ni wadhambi na wanahitaji rehema za Mungu kwa ajili ya wokovu wao. Hoja ya mwanamume kuwa mtawala ni hoja ya kimajukumu tu, ambayo Mungu alidesign tangu mwanzo kabla ya dhambi. Pamoja na kwamba Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke, Mungu aliwapa majukumu tofauti. Mmoja kuwa mtawala-mwanamume na mwingine kuwa mtawaliwa-mwanamke. Ukiisoma vizuri ukailewa vyema dhana hii, haitakusumbua tena kaka.
  Sasa najibu maswali yako ya siku ile tena kwa ufupi kabisa.
  Swali 1
  Je, mwanamke anaruhusiwa kuwa mwalimu wa watoto kanisani kwenu?
  Jibu
  Anaruhusiwa sana. Na siyo kanisani kwetu tu. Ningefurahi kama ungesema hivi, Mwanamke anaruhusiwa kufundisha watoto kwa mujibu wa Biblia? Nasema hivyo kwa sababu, huenda kuna mambo mengine yanayofanyika hata kanisani kwetu ambayo ni unbiblical. Nimesema huenda!!! Kwa hiyo mimi binafsi sivuti mtu awe msabato wa jmosi. Navuta mtu awe mfuasi halisi wa Biblia peke yake- yaani Mungu. Wanawake Biblia imewaruhusu kuwafundisha watoto nyumbani na kanisani, naam hata wanawake wenzao. Ushahidi upo ndaniya Biblia-utafute
  Swali 2
  Je, mwanamke anaruhusiwa kuwa mwalimu wa Shule ya Msingi au Sec?
  Jibu
  Ndiyo anaruhusiwa kwa sababu, wanafunzi wote walio shule ya msingi na sekondari, bado ni watoto. Wanahitaji malezi ya mama kwa kiasi kikubwa. Kwa hiyo nikiona mwanamke anafundisha watoto wa shule ya msingi na sekondari, mimi sipati shida yoyote kimaandiko.

  Swali 3
  Je, Mwanamke anaruhusiwa kuwa Mkufunzi wa Chuo Kikuu?
  Jibu
  Anaruhusiwa kama atakaowafundisha ni wawanwake tu. Kama kuna wanaume ndani yake, haruhusiwi hata kidogo. Najua unashangaa sana kwa hili. Sawa, lakini huo ndio ukweli wa Biblia kama kweli tumeamua Biblia ituambie kila kitu. Watu wanaosoma chuo kikuu, ni watu wazima, hivyo mwanamke hana mamlaka ya kuwafundisha, kuwaonya, kuwakemea, na kuwarudi watu wazima ambao ni wanaume labda kama ni wanawake tu, tena mwalimu huyo ni lazima awe mama wa umri mkubwa zaidi ya hao wanawake wanaofundishwa

  Swali 4
  Je, Mwanamke anaruhusiwa kuwa Daktari wa magonjwa?
  Jibu
  Kwa mawazo yangu mimi, anaruhusiwa kuwa daktari wa magonjwa. Na atapaswa kutibu watoto na wanawake wenzake tu. Hatawatibu wanaume wakubwa. Wao watatibiwa na wanaume wenzao. Najua maelezo haya ni magumu sana kueleweka. Hata mimi Siyi huwa natibiwa na akina mama ninapougua. Nahudumiwa na manesi akina dada. Lakini tukirudi kuiangalia Biblia, hivi kweli hii ni sahihi mwanamke mkubwa kumtibu mwanamume mkubwa? Nakumbuka kisa kimoja ndani ya Biblia ambacho wanawake waliwahudumia akina baba kwa kuwapa chakula na malazi. Sina uhakika kama huduma hizo naweza kuzilinganisha na matiababu. LAkini uelewa wangu ni kwamba, mwanamke, akimhudumia kwa maana ya kumtibu mwanamume, ni kumpa mwanamke mamlaka ya kumfundisha, kumuonya na kumkemea mwanamume huyo, maana kuna maradhi mengine huwapata wanaume kwa sababu ya ufedhuli wao. Na Biblia haimruhusu mwanamke kumkanya, kumuonya au kumfundisha mwanamume. Huu ndiyo uelewa wangu. Nasubiri kama mna uelewa tofauti ili nami nijifunze kwenu pia.

  Swali 5
  Je, Mwanamke anaruhusiwa kuwa Mkulima wa mashamba?
  Jibu
  Hapana. Kazi ya kulima ni kazi ya mwanamume. Mwanamke anaweza kuifanya kama atakuwa anamsaidia mumuewe tu au kama atakuwa ni mjane.

  Swali 6
  Je, mwanamke anaruhusiwa kuendesha ndege au treni au Meli?
  Jibu
  Hapana. Hizo ni kazi za wanaume japo kwa sasa kuna wanawake wanaofanya kazi hizo. Kibiblia binafsi sijaona aya inayowaunga mkono kufanya hizo kazi zao. Labda kama wewe/na wengine mnazo aya hizo tusaidiane.

  Swali 7
  Je, Mwanamke anaruhusiwa kusoma shule ya awali mpaka Chuo Kikuu?
  Jibu
  Nafikiri anaruhusiwa endapo tu majukumu yake atakayoyapata baada ya kisomo chake, yasiwe ni majukumu ya kuwaongoza wanaume-kuwa juu ya wanaume kimamlaka. Kibiblia siyo sahihi.

  Swali 8
  Je, unadhani ni sawa Mwanamke kwenda kusali kanisani?
  Jibu
  Ni sawa na anapaswa kwenda kusali lakini akajifunze kwa utulivu na unyenyekevu ndani ya kanisa. Hatapaswa kufundisha/kuwahubiri wanaume. Na kama atakuwa nabii, sharti afunike kichwa kabla ya kutoa unabii tena siyo mbele ya halaiki.
  Swali 9
  Je, mwanamke anaruhusiwa kuwa mfanya biashara?
  Jibu
  Ndiyo. Kuna wanawake wengi ndani ya Biblia waliokuwa wafanyabiashara wa biashara ndogondogo. Sidhani kama ni sahihi kuwa ma-wholesales!! Biashara ndogondogo ni lukusa kwao.
  Milinga, najua uhalisia wa maisha yetu ya sasa, wengi tumekuwa tukiutumia udhaifu na hali halisi tulionayo sasa kutaka kuilazimisha ikubaliane na neon la Mungu. Neno la Mungu litabaki kuwa ni neno la Mungu. Nakusubiri nikuone na mwitiko wako na kama utakuwa na uelewa tofauti, leta tujifunze sote.
  Karibu sana

 7. Ziragora,
  Pole rafiki kwa kutonielewa. Jaribu kufuatilia mahojiano yangu na watu wengine juu ya mada hii huenda utaelewa baadaye.
  Nakuombea tu.
  Ubarikiwe pia

 8. Seleli na wenzio,

  Ukisikia mapumba, haya yenu wewe na wenzio ndio tops!
  Mnapindisha Neno la Mungu, halafu mnataka kukimbia; tumesimamisha jua na mwezi mpaka tuwanyooshe huo mpindo! Eti oh, huu mjadala ulikwisha; mbona ninyi ndio wachangiaji wa mwisho, tena ni jana tu, sasa mmechangiaje mjadala uliomalizika? Tunayajua maroho ya dini yalivyo maoga, ndio maana mmeshikwa makoo msiukimbize uongo wenu, tulieni hapo mpaka tukafukuze hako ka nanihii ka uongo kanako waongoza!

  Kwanza, mmerefusha mjadala kwa makusudi, mkijaribu kupandikiza roho ya ukaidi ndani ya watakatifu walionunuliwa kwa Damu ya thamani sana, sijajua hili mmelifanya kwa ujinga au kwamba ninyi ni mamluki!?

  Maelezo yenu mmeyatengeneza ktk namna ambayo mchanga anayewasoma ni rahisi sana kuwaamini na kuyapokea kama ni Neno la Mungu, jambo ambalo si kweli! Hebu uangalieni uongo wenu ninyi wenyewe,
  “” Swala hili la Wanawake na Huduma au nafasi yao Kanisani tumelishasema sana hapa leo comments zimefika 170, tumeshusha shule hatari sana na za ukweli kiakili, busara, hekima, common senses, kimaandiko kama yalivyo na zaidi sana Ki Neno Hai as per RM.””
  Halafu juu ya msingi wa maelezo haya, ndio mmeleta hizi shule:
  “” Kama Paul anasema wazi SIMPI mwanamke ruhusu, kama anasema kabisa hapo naongea MIMI si Bwana, kama anasema kabisa naongea kwa jinsi ya kibinadamu, sasa hapo unahitaji akili gani spesheli kuelewa kua ni Paul apo kabisa wala si Mungu wala Roho Mtakatifu ? we vipi mbona vepa tu Kaka unatwanga apa kuhusu Wanawake na huduma?””

  Hii ni HILA kamili ya udanganyifu mnayoifanya ambayo haina tofauti na alichokifanya Nyoka kwa Hawa!!!! Hebu wewe mwenyewe jaribu kulitazama hili unalolifanya, hapo Biblia inapaosema “Simpi ruhusa mwanamke…”, wewe unasema huyo alikuwa ni Paulo akiongea kama yeye na si Neno la Mungu, kwahiyo panda mimbarani dada yangu utuongoze ktk hiyo Nchi mpya, hiyo injili; je, hili linatofauti gani la alilolifanya nyoka? Ni jambo lilelile; Simpi maana yake usile!!!! Nawe unapolifanya si agizo kwa kanisa maana yake unamwambia huyo mwanamke kula, Hautakufa!

  Haya, kuhusu hilo la “Simpi ruhusa mwanamke…” mnalokazana kulipinda, mkiongopa kwamba mtume Paulo, huyo aliyewekwa na Kristo awe mhubiri na mtume, na mwalimu wa Mataifa, bila ya aibu mnamuongopea kuwa alisema kwamba ‘hapa ni mimi wala si Bwana’, hiki hapa Injili inachokisema ktk kutufundisha jinsi ya wokovu:
  1Tim 2: “8 Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. … 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. 13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.”

  Kuna mahali popote hapo ambapo mtume Paulo anasema kwamba “Hapa ni mimi wala si Bwana”???? Kwanini muongeze lisilokuwepo??? Muongezaji yuko mmoja tu tunayemfahamu!!!! Jamani tena hata sababu ya kwanini haruhusiwi mmepewa, msichokielewa ni nini? Au mnadhani kwamba Eva kabla ya kudanganywa alikuwa galasa? She had all the understanding just like mwanamke wa leo aliyejazwa RM; Free will haiondoki kwa RM, bali kumsikiliza RM ndio kunakoleta tofauti kwa leo ktk kipimo cha dhambi inayotunyemelea, ndio maana mwanamke anarudishwa awe chini ya mwanaume, haya ndiyo mapenzi ya Mungu!!!

  Haya, ushahidi wa pili wa mwanamke kutokuruhusiwa, huu hapa tena:
  1Kor 11: 34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 35Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. … 37 Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. 38Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.”

  If you guys are not quickened you will NEVER understand It! Mmerudi kule Edeni ktk position ya Hawa alipoamua kumsikiliza Nyoka badala ya kubaki ktk wigo wa Neno la Mungu, nanyi mmeyapokea maarifa mapya mliyopewa na huyo roho wa dini. Na hamuilewi hata nafasi yenu wala umuhimu wake, ndipo mnajionea sawa tu! Lakini Mungu alitenganisha toka alipotuumba, tazama mnachoambiwa hapa:
  1Kor 11:3 “3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.”

  Kuna mwanamke kuwa kichwa ktk maelezo hayo? Au ninyi ni kwa RM yupi, na mliyempata wapi, hata mnamfanya mwanamke kuwa kichwa cha kanisa? Acheni mizaha yenu hiyo!! Ndio maana unaniambia sina hata aibu kwa jinsi nilivyoling’ang’ania andiko hilo ambalo wewe na wenzio, kama kaka yako Ziragora aliyepoteza mwelekeo wa Injili na sasa anatembea na pingu akijaribu kulifunga Neno la Mungu, mmeng’ang’ana bila ufahamu kwamba kifungu hicho mtume Paulo alisema hayo ni yeye na si Bwana; hivi ninyi mko alright kweli? How can you be sooo blind in this sweet Gospel light that’s being shed to lighten your path? Hivi huwa mnachukua wasaa wa kusoma mkijifunza kutoka Biblia zenu au ni watu wa kukopi mafundisho ya walimu wenu halafu mnakuja na daftari zenu mnatutiririshia mavepa yenu ya ukweli!??

  Mnaniletea mifano ya Agano la Kale ili muendelee nayo huku, basi mlisemaje kuwa mlijazwa RM huku mkijirejesha huko nyuma, wakati hayo yote yaliyofanyika huko yalikuwa na kazi ya kutuleta kwa Kristo, basi mlifikaje kwa Kristo ilhali mngali kwenye Torati? Nyie ni akina nani haswa? Mnatokea wapi, Siloamu??? Huko ndiko wako watu waliopinda hata hawajali Biblia inasema nini, wao humsikilizaga nabii wao tu, nawaona nanyi ni sampuli hiyo hiyo!!!

  Ama kweli, “being religious without having an understanding of the Word of God” is your beat!!!

 9. Seleli,

  Kwa kiasi fulani umenishangaza sana nilipoyasoma haya maelezo yako, ingawa sikupenda kuamini kwamba ufahamu wako umegoteshewa hapo, lakini sina budi kukubali kwamba kiwango chako cha ufahamu kiko chini saana, yaani spiritually you are not quickened! Tazama unachosema: Eti,
  “”Suala la ktk Biblia kuna Maneno na Matendo ya Mungu, Wanadamu na devo ni wazi na tumesha jadili na kukuelimisha sana, sema kuna wakati unakuaga kama Wasabato dini mfu kurefusha mambo weeee, kuzuga na kuzungusha weeee, mambo siiiimpoo ila unayapindua pindua ili tu kuingiza fix zako za mfumo dume mfu unGodly one.””

  Kwa upole, ukiwa ni ndg yangu, ninakuhakikishia kuwa mtazamo wako huu uliopindishwa, ndio kiini cha wewe kupotea na kurudishwa gizani ulimotolewa, ndio maana umeshindwa kuyaelewa Maandiko ktk ukamilifu wake zaidi ya kujiridhisha kwa hako kamfuko ka rambo kaliko jaa ufahamu hybrid, wakati wenzako wanabeba magunia ya Neno la Mungu, lile pure breed, pedigree!

  Kwamba ‘ktk Biblia kuna Maneno ya na Matendo ya Mungu, Wanadamu na devo’ inadhihirisha jinsi madude ya dini yalivyokuseti, yaani na ujanja ujanja wako wote wa kusoma huko Tabora zilikokuwa the best of schools, kweli, how can u be soooo low ktk understanding hata umeshindwa ku comprehend Biblia ni nini, na unaishia ktk pumba kama hizi za mtu aliyesoma shule za Tapa!!!

  Kuna tofauti kubwa sana, kama Mbingu na Kuzimu kati ya statement mbili hizi, hebu chukua wasaa uzitafakari.
  1. Ktk Biblia kuna Maneno na Matendo ya Mungu, Wanadamu na devo.
  2. Biblia ni Neno la Mungu kuhusu Matendo ya Mungu, Wanadamu na devo.

  To be honest, umewapoteza wachanga wengi sana ktk kuwafundisha kwako jambo hili, umeifisha ndani yao nguvu ya Injili, ile mbegu, wamebaki hawana mbele wala nyuma kuhusu Injili, kipi ni Neno la Mungu na kipi ni neno la binadamu au mila kama mnavyo yaita mafundisho ya Paulo!

  Haya hebu niambie hapa napo inakuwaje, mtume Paulo anaposema, 1Kor 11:1
  “Nifuateni mimi kama ninavyo mfuata Kristo”!

  Tumfuate ktk mila zao? Au hayo nayo ni mambo yake tu, sisi tuendelee na yetu, tumfuate Seleli kama anavyomfuata nanihii!!!!

  Kupotea ni rahisi sana haswa unapojifanya unaijua njia usiyoijua!

  ….. nitaendelea ili nikuoneshe jinsi ulivyo chini ktk ufahamu, labda itakusaidia kuzinduka ktk usingizi wa pono uliolazwa na madude ya dini, ujiweke sawa na Neno la Mungu, ili usije nawe ukaanza kuita, “Mzee Yesu! naomba umtume huyo Lwembe aniletee maji nibatizwe kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili dhambi zangu ziondelewe nami nihamie huko mliko!!!!!

 10. Ndio kaka yangu Siyi,

  Mimi sina hoja kabisa kwani mjadala imeisha. Hoja nyuma ya mjadala ni mzaa. Ndio maana naweka ile ya zamani. Sikupenda kucheza na matope kama wewe unayerudisha swali zilizojibiwa zamani. Sioni hata kwa nini ucheke! Au ulipenda tu jitoa muhanga ndani ya upungufu.

  Mungu akubariki.

 11. Ziragora,
  Unachekesha kweli. Hii ni ishsra ya kuishiwa/kuzidiwa hoja. Huna hoja kaka. Umetuletea pachiko la mwaka jana, je, hivi pachiko linajibu hata maswali niliyokuulizeni siku ile hapo juu baada ya Milinga kuuliza?? Waweza kuyajibu hayo maswali kaka???
  Na nitakuongzea swali lingine la tafakari, Je, kati ya Adamu na Hawa, ni nani aliyeumbwa kwa ajili ya mwingine? Unafikiri ina maana gani hiyo kuumbwa kwa ajili ya …?
  Au nitekenye zaidi akili yako, hebu nieleze ni nini maana ya msaidizi?
  Ubarikiwe

 12. Wapendwa wote wana SG,

  Bwana Yesu Asifiwe!

  Nimependa, kwa wote waliofika nyuma, niwawekee haya maneno machache ya zamani. Kwa kuyasoma mtaona inayoendelea ni kurudi nyuma bila faida yoyote. Na kwa sasa sijaona anaeinua hoja ambayo haina jibu huko nyuma.

  Sasa kila yeyote ambaye ana hoja, asome kwanza, kiiisha ainuwe hoja yake akinukuu mahala kunakoandikwa hoja ya mwengine kwa kuonyesha upungufu au akimusupport. Lakini unapokurupuka tu , itakuwa vigumu ku connect hoja zipatikanazo ndani ya huu mjadala ambao kiukweli uliisha. Anyway, tuko huru sote, ndio maana tunaitika kuendelea:

  “Alphonse ziragora 12/09/2013 at 5:15 PM

  Ndugu yangu Siyi,

  Nashukuru kwa kuniandikia, na Mungu akubariki. Ni vizuri sana kujadili Neno la Mungu. Ninachoona sana ktk mijadala kam hii, ni vigumu kuona inaisha watu wakikubali ukweli. Lakini Mijadala ina aina mbalimbali. Kuna yenye inaisha pasipo conclusion na ingine, zaidi ile ya kuomba shauri, inaisha vizuri kuliko. Lakini yote inasaidia watu hata wao pasipo kukiri. Ndugu Siyi ulikuwa tayari umekubali mambo mawili: vazi na waandishi. Lakini naona jambo la waandishi tena linazuka.
  Nitapima kukujibu:

  1)SINA DENI YAKO YA MAJIBU. Labda haukusoma vizuri au ulitarajia nikujibu namna unavyopenda. Na kam una haja ya elimu zaidi, leta suala yako.
  2)MAMBO YA ADAMU NA HAWA/KUKANDAMIZWA KWA MWANAMKE/UTAWALA WA MWANAUME/KUTAMANI MWANAMKE:
  Juu ya Adamu na Hawa sina maelezo mengine, Biblia pekee inasema. Unataka mim niseme pahali pa Biblia kam wewe unayo desturi? Au kam hujue na unataka ufahamu zaidi ya Biblia kwa nini huulize RM? Hata wewe nakuona ukisema “Biblia haiseme” wakati unapoongea juu ya mwanamke kuletwa auwawe yeye pekee pasipo aliyehusika naye dhambi. Kwa nini haukujibu na uhakika? Ni kwani Biblia haikujibu, full stop.
  Kam unakubali kam Debora alipewa utawala na Mungu, kwa nini asiwape wengine? Unasema Ni Mungu pekee aliyempa bali yaikutoka ktk uchaguzi wa wanadamu. Unamaanisha ku ngambo ya wanaume, ndipo mtu anajipatia yeye pekee madaraka kanisani, ao kuchaguliwa?
  Tangu mbele ni Mungu mhusika kwa kuchagua ni nani atakaemtumikia. Iwe wazi, kam ni Mwanamke atainuliwa, kama ni mwanaume sawa. Mungu wetu ni Yule Yule jana, leo na hata milele. Hakuna hata siku moja ataitika mtu a mu dictate eti chagua mwanaume na umuwache mwanamke. Kam atawafanya wanaume wawe wengi, haya! Kama atawafanya wanawake wawe wengi, haya!

  Lile neno la Yesu kuhusu tamaa ya mwanaume kwa mwanamuke lilingana na moja kati ya zile amri kumi za Mungu. Na alipenda aonyeshe kam dhambi si kitenda tu kam jinsi torati iliazibu lakini hata kuwaza, kupangilia, … vibaya yote ni dhambi. Lakini ndugu, naona kam una nia ya kuongeza kidogo kwa ile Yesu alisema, nawaza ungeliizusha nafasi nyingine labda. Kwa nini unataka uwe wa kiroho kuliko Yesu? Akisema, usiongeze.

  3) KUPUZI UJUMBE WA WAMAMA:
  Ile unayoleta ni tafsiri yako tu. Ndugu yangu, kuwa na mashaka na kupuzi si neno moja. Imeandikwa kama wale mitume “walipuzi”. Si tena pengine unasema tuheshimu maneno ya Biblia? Sasa kwa nini kila ujapo, ni tafsiri tu ? Unataka fundisha watu kam hakuna neno kamilifu ndani ya Biblia kam Ndugu Siyi hajatafsiri? Biblia ni neno la Mungu ; lina uhakika kuliko maneno yako yote.

  4) KAMA MIMI BINAFSI NILIWAI ONA NDANI YA BIBLIA WANAWAKE WENGINE KAM HILDA, MIRIAMU NK, MUNGU AKIWACHAGUA KUWA WACHUNGAJI, ASKOFU, …. KANISANI:
  Ktk agano jipya, Biblia inatuelezea tu mambo yaliyofanyika mda kitambo, just wakati mitume walipokuwa hai. Haiseme kama Mungu hawezi tena kuleta mwanamke kama Debora. Sasa hapa nikitia akili zangu, sitafahamu. Ukweli unabaki pale pale : Mungu akipenda atamuweka kwani angeliapa kutoweka mwanamke atawale wanaume, isingeliwezekana atiye Debora kutawala Israeli yote. Jambo muhimu ni kwamba tutawatambua kwa matendo. Atakapokuwa mwanamke, kama matendo yake hayafae utawala wake utavunjika, mwanaume hali kadhalika. Nafikiri ndugu yangu, uwe na bidii, katika kuyatazama yaliyo kweli : « Kwa upande wangu, nikisoma Biblia naona kam Mungu aliweka wanawake wachache sana. Ninaona hata leo, si ndani ya kanisa tu, bali ktk domains zingine, naona tu watawala wanawake ni wachache licha yu kuwa wengi kwa idadi ktk dunia. Ile tu inaweza nisukuma kusema kam watabaki wachache(Kwani Mungu habadiliki). Lakini hii ni kwa maoni yangu, Mungu akiwa na siri yote. »
  5) HAWA WANAWAKE WA CHEO :
  Ni kweli tafsiri zote si sawa. Nazo tena ni watu wanazifanya kufwatana na lugha mbalimbali. Na unaelewa jinsi ni nyingi kabisa. Lakini jambo la kuzingatia ni ile neno « CHEO ». Na ile ndio nilisisitiza sana nikisema, Mungu anainua anaetaka kuinua. Ina maana nimeona Mungu anampa « CHEO » anaemtaka. Ile conclusion niliitia kwani niliona fasi nyingine tafsiri zinachanganya kidogo, lakini pale kwenye cheo kunabaki. Na umbalimbali ya pale sina ruhusa ya kuongeza.

  6) PAULO/RM
  Ona, nimesema ile tangu mbele kam kuwa na RM yaimfanye mtu kulingana na Mungu. Mtu anayo udhaifu tu pamoja na kuwa na RM. Ndio maana kila mara inatubidi kuomba. RM yeye anatuombea lakini haombe kwa ajili yake mwenyewe. Mtu anabadilika, lakini RM sivyo. Ile shairi mbili ziko tofauti. Utofauti wake si udhaifu wa Mungu, ni wa Paulo kam mwanaadamu, tena nampenda sana kwani hajawai ficha udhaifu wake, wa mwili wala wa roho. Ni hii ukweli yake ya kutoficha ndio inamfanya awe miongoni mwa waandishi wa Biblia. Kuwa mkweli ndiyo ya maana. Kwani « mtajua kweli, na kweli itawaweka huru ». Haleluya !!!
  7) AMTEGEMEAYE MWANAADAMU ALAANIWE :
  Hapa unanishangaza kabisa labda kwa mara ya kwanza ukinifundisha hii shairi ya YEREMIA 17 :5 ambayo nilikutolea hapa sasa 09/09/2013 tena nikikuandikia wewe nikikuomba kutotegemea walimu, wachungaji, maaskofu, na hata mitume kwani wote ni wanaadamu.Tena ndipo unajibu kwayo. Labda hukusoma na ndio maana unaendelea kudai majibu fulani ambayo umekwishapata. Msimamo wangu uko pale, tena kwa mkazo. Labda kam umepunguza kuwategemea, basi Bwana apewe sifa.

  8) Kwa mwisho, ndugu yangu, tuchangiye shairi hizi :
  “1 Wakorintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; WALA HAPO SI MIMI, ILA BWANA; mke asiachane na mumewe;
  1 Wakorintho 7:12 Lakini watu WENGINE NAWAAMBIA MIMI, WALA SI BWANA, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.”

  “Warumi 7 :
  15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
  16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
  17 Basi sasa si mimi NAFSI YANGU ninayetenda hilo, bali ni ile DHAMBI IKAAYO NDANI YANGU
  18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya MWILI wangu, HALIKAI NENO JEMA; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
  19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
  20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, SI MIMI NAFSI YANGU NILITENDAYE, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
  21 BASI NIMEONA SHERIA HII, YA KUWA KWANGU MIMI NITAKAYE KUTENDA LILILO JEMA, LIPO LILILO BAYA.
  22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
  23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, INAPIGA VITA NA ILE SHERIA YA AKILI ZANGU, na kunifanya mateka ya ile SHERIA YA DHAMBI ILIYO KATIKA VIUNGO VYANGU.”

  Mungu akubariki, na karibu tena mara nyingine.”

  Mbarikiwe.

 13. Ziragora/ Seleli na wengine wenye mitazamo hafifu kama hiyo
  Siku ile nimeleta maswali ambayo nilidhani kuwa yatawafanya mfikiri kwa kiasi fulani. Lakini naona bado akili zenu zimefungwa. Nilitamani kuona majibu ya maswali hayo. LAkini kwa vile ni maswali yanayowabana kwenye mitazamo yenu, ndiyo maana hamkuyajibu na badala yake mmeleta porojo kubwa tu.
  Kama maswali yamewashinda kuyajibu, nawaomba mrejee kusoma mwanzo 1-5 ili mpate kuelewa .
  Sisi hatubahitidshi wala hatutumiii hisia wala mtizamo wa mazingira ya sasa. Tuko makini sana na mambo tunayoyasema kutoka ndani ya Biblia.

 14. Mpendwa Siyi,

  Kuwa muungwana ni mojawapo wa vigezo vya kuthibitisha mtu amekua. Kurudilia mambo tuliyoyaongelea mda mrefu bila kuleta jambo jipya ndani, mimi nayaona kama kucheza na matope. Ndiyo maana ninapaste mahala tuliporudilia tukijadili. Na kama itahitajika, wakati wowote utakapojiruhusu kurudikia kauli yako ya huko nyuma nitapastia tu jibu ulilolipata.

  Hii ndio ya hapa karibu:

  “Alphonse Ziragora 04/11/2013 at 2:27 PM

  Siyi,

  Mnapoendelea kujadili, ina maana mnataka copy-paste:

  Nakukumbusha tu jinsi nilikuambia tangu awali kama hudaiwi kitu chochote kingine ukiwa jela pamoja na waongo wote. Sina haja yoyote ya kuingia ktk mbingu unayotengeneza wewe mwenyewe, ambamo watakaoingia ni waongo maksusi kama wewe, na wenye kuimbaimba tu « Roho mtakatifu- Roho mtakafujo ». Kama hupendi lipa haka ya jela ambayo ni kuomba masamaha tu, baki humo humo pamoja na wote watakaokufwata humo, hapo ukiendelea lalamika na kuimbaimba, full stop. Wewe pekee hukuona kama rejea zako zilikuishia wakati ulibaki ukizungumza na Ndugu Seleli? Muongo anapokwisha shikwa hupungukiwa sana hadi atakapolipa gharama. Panya ikiwa imenaswa ndani ya mtego, harakati zake za kuchunguza kam mtego ingali hazina faida. Inabidi ibahatike itoke ndipo ijue kuchunguza.

  Asante.”

  Ubarikiwe.

 15. Siyi/Mjema/Lwembe/Yusha/ Mabinza na they like!

  Siyi, Acha maneno mepesi, eti wote wanaokizana na Neno la Mungu”, nani hao zaidi ya washika dini mfu, Imani kavu, Wasoma Maandiko si Neno, wenye roho zilizowakalia na kuwandamiza hata kuwaloga maisha yao ya imani na ibada za Wanadamu eg Ellen Black wala si Roho Mtakatifu, wenye ibada kame zisizo na uhai na ubichi wa uwepo wa Mungu bali ni taratibu za karne na karne nenda rudi?

  Swala hili la Wanawake na Huduma au nafasi yao Kanisani tumelishasema sana hapa leo comments zimefika 170, tumeshusha shule hatari sana na za ukweli kiakili, busara, hekima, common senses, kimaandiko kama yalivyo na zaidi sana Ki Neno Hai as per RM.

  Yote mnayokomalia wewe, Mjema, Lwembe, Mabinza kuhusu kuwa down play Wanawake mbele za Mungu ni marudia yale yale yanayochosha sana humu na majibu yake yako humu humu sema tu mnacheza tennis ball na kumualika kila Mtu mzima wa kucheza gozi kabisa aungane nanyi! Nyie chezeni mkichoka ndio tunanza gozi kubwa ika kwa sasa ni vema kuwachomekea pasi za hapa na pale kuwakuza na kuondoa utoto wa dini unawafanya kuona Mwanamke aliyejaa Roho kabisa kua kama kibatari ktk mambo ya Ufalme, nyie vipi?

  Rudieni comments zote nyuma, kila mnachouliza kiko uko na majibu yamejaa uko, acheni kupoteza muda hapa, kama hamna ufunuo mpya au wa kale yet umevuviwa, plz go home to drink water!!!!!!!!

  The Bottom line ni…MBELE ZA MUNGU, wote tunapotential sawa toka kwa Baba huyo huyo kufanya mambo yake ndio maana Wanaume hawakupewa RM dume na Wanawake RM jike, plz stop mambo yenu ya kitoto ktk argument kwa some very clear issues. Wote tunapendwa na Baba na tunatumiwa sawa sawa na mbele zake hakuna hii mambo yenu ya man-made ya grading Wanadamu to A and C. Yanapooneka ktk Bible mambo kama hayo ya grading up and down kama Paul anavyosema au generally Wanafunzi eg kuwahesabu Waume tu bila Wanawake, rest assured ni mambo a kibinadamu na mila si NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE.

  Huwezi sema Paul kusema simpi mwanamke ruhusa ku.. eti liwe ni NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE wakati apo kasema yeye kama Kiongozi ktk kundi la Bwana kuweka mambo sawa kwa wakatiu ule ktk hali iliyokuwepo pale kanisa! Ukikomalia ivyo kua ni Neno la Bwana kwa kiiiiiiiila kizazi, utakua ni Mtu mwenye both confusions ya dini, kiongozi wako wa kiroho alikukalia na maono plus mafuniko yake au kama vipi utakua na common sense zenye kuhitaji maombi spesheli ya kuvunja ujinga kubuhu.

  SISI SOTE NI WANA WA THAMANI MBELE ZAKE, wawe KE au ME, Wayahudi au gentiles, wametahiriwa, keketwa au bado, we are the same, stop such religious deadly politics.Amen

  Press on

 16. Lwembe,

  Da! kwa hoja hii kuhusu Wanawake ktk Imani na huduma, aise una bonge ya mapumba hamna tena mfano, mwe! huoni aibu kwa unayoyaandika yanakuchoresha ulivyo severely wrong mtazamo wako nyongo dhidi ya Wanawake waliojaa Roho Mtakatifu kama wewe Mwanaume!

  Hii topic kua muda mrefu ni ukweli tu wala usifosi kingi kwa kutengeneza mechanically hoja kua topic ktk kitabu cha Mwanzo ndio za muda mreeeefuuuuu. Mmmmmh! acha mambo yako, topic hi ya muda mrefu ni ya muda mrefu tu, over and out

  Hizi ni mastory ya town ya radio craaaaadiz efwe emeee…”’Siku zote nikisoma kwamba, “Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga” nilikuwa nashindwa kuelewa sawasawa, inakuwaje? Bali kwenye mjadala huu ndio nimelijua vizuri jambo hili, kumbe mtu anatangulia kwanza kuwa mjinga, na kwa hiyari yake anaendelea ktk ujinga, akiongozwa na huo ujinga!!!””…ungepumzika tu kuliko kupoteza muda na energy kuandika hii vepa bro

  Swala la ktk Biblia kuna Maneno na Matendo ya Mungu, Wanadamu na devo ni wazi na tumesha jadili na kukuelimisha sana, sema kuna wakati unakuaga kama Wasabato dini mfu kurefusha mambo weeee, kuzuga na kuzungusha weeee, mambo siiiimpoo ila unayapindua pindua ili tu kuingiza fix zako za mfumo dume mfu unGodly one.

  Kama Paul anasema wazi SIMPI mwanamke ruhusu, kama anasema kabisa hapo naongea MIMI si Bwana, kama anasema kabisa naongea kwa jinsi ya kibinadamu, sasa hapo unahitaji akili gani spesheli kuelewa kua ni Paul apo kabisa wala si Mungu wala Roho Mtakatifu ? we vipi mbona vepa tu Kaka unatwanga apa kuhusu Wanawake na huduma?

  Hi phrase yako ukiisoma kwa juu juu ni kama ya ya kirooooohooo, ni kama vile ya Mtu makiiiiini ktk Neno na anaongea jambo la kweliiiii kumbe ni a great display ya gross confusions ya extremism spirit ya dini au imani hai yet based on man-made formula fulani ivi as result pia ya influence ya kiongozi wa dini/maono/ministry anayemkalia mhusika…. look at this in the light of whole counsel of the living Word of God, you will realize my conclusion on this mess… ”’Kwa ujinga, wakristo wengi hudhani kwamba wakiisha kujazwa RM basi wana uhuru wa kufanya lolote moyo wake unalopenda kuhusu Injili, haswa kuhubiri, wakijaribu kuziruka taratibu zilizowekwa na RM huyo huyo wanayesema wamejazwa! Inashangaza saana, lakini RM ndiye ambaye hulisimamia na kuliongoza Kanisa, na huyo ndiye aliyekuwa ndani ya Paulo akiweka utaratibu huu kwa kanisa la Mataifa, sisi tusiomjua Mungu, na sasa tunaukataa, kwa ujinga tukiongozana Shimoni!!!

  Why nimesema iyo phrase above ni display ya extremism au effects ya kiongozi wa kiroho mwenye mlengo mmoja tu kama jongoo movements aliyewamezesha madude na kuwatawala washirika wake kama robots? ni kwa kua PAMOJA NA SISI KUA NA RM, haimaanisha ubinadamu wetu wafa, we are not robots or dead bodies when RM anatujaza na kutuongoza neither does it mean kua RM akiingia, hatuna choise wala will zetu kama Watu, we vipi wewe! Kwahiyo, no wonder ktk Neno, yes Paul amejazwa RM yet kuna nyakati anasema mambo humo akiwa very clear kua, ni Yeye si Bwana na ivyo si RM…mbona simple sana iyo kuelewa wewe? ndio maana nikasema phrase yako pale ni kama vile ina kitu kumbe vepa tu pia kama kawaida mwanzo mwisho waga una produce hayo.

  Sasa hapa umeongea nini sasa?……””Vipawa vya RM huongozwa na RM, na vipawa vya dini huongozwa na roho wa dini; jaribuni kuvipambanua vipawa mlivyo navyo, ni nani anayevisimamia, maana Vipawa havina majuto!!!!”’ ehe ulitaka kusema nini hasa? au ndio yalee ya kila linalokuja,pwaaa unalibwaga hapa! plz be selective at least.

  Hii nayo ni pumba tu, ”Usikubali kuwa “guinea pig” wa majaribio ya kukiuka taratibu alizoziweka Mungu; Buckle up (The Word), son of man! Those religious airbags will never work when you hit hell!, sasa umeongea nini apo?

  Aisee hii ni kweli kabisaa hiii..”Ujinga una gharama!!! LAKINI kama ujanja/uelewa ni kukomalia mbuyu ni Mti mgumu sana na kamwe hauwezi kua kuni, huo ni upumbavu wenye gharamu za ajabu na maumivu makubwa mno maana hata kama Mbuyu ni Mti mkubwa, ukinyukwa na greda, utapasuka vipande vidogo tu na kua kuni kwa hivyo ni ni kweli mbuyu ni Mti mgumu na mkubwa sana lakini bado unaweza kua kuni. Ni kweli tumejazwa na tuna RM lakini bado tunaweza na tu wanadamu sisi na tabia na matakwa yetu yako active tukisema au kuandika ktk nyaraka kama Paul, upo apo? we vipi bwanaaaa!

  Press on

 17. Milinga, Ziragora na wengine
  Wote wenye mitazamo kinzani na neno la Mungu…
  Shalom..
  Nimeona maswali ya kaka Milinga, hoja za Ziragora michango mizuri ya ndg Lwembe kwenye mada hii. Kimsingi, nyote nawaombea sana.
  Kabla sijajibu maswali ya Milinga, naomba atafakari kama siyo kuja na majibu ya maswali haya.
  1. Milinga, kwa vile tunajadili Biblia naomba nikuulize swali hili la kwanza; Je, unaijua ajira ya mwanamke tangu mwanzo wa kuumbwa kwake? Kama ni ajira zaidi ya moja, waweza kuitaja kwa mujibu wa Biblia? Halafu jaribu kuilinganisha ajira hiyo/hizo ndani ya Biblia na hali halisi ya sasa tuliyo nayo.
  2. Ni kweli ndani ya Biblia kuna manabii na waamuzi wanawake. Naomba unioneshe ni sehemu gani katika Biblia walifanya hizo kazi zao za kinabii mbele ya wanaume au kazi za uamuzi wakiwaamua wanaume? Walifanyeje kazi zao hizo? Naomba rejea za maandiko zinazoonesha utendaji wao wa kazi kama walivyooneshwa wanaume. Nitafurahi kujifunza kutoka kwako
  3. Sasa umemaliza kujibu swali la pili, jaribu tena kutondoa kwa kuangalia mazingira yaliyomfanya Mungu kuwaita wanawake kuwa manabii na waamuzi pamoja na kwamba wanaume walikuwepo. Au kwa nini Mungu aliwachagua wanawake? Nitafurahi kujifunza kutoka kwako pia.
  4. Unafikiri Yesu na mitume (kwa sababu agano jipya kwa wakati huo halikuwepo), walikosea kuwatumia wanaume tu kwenye majukumu hayo ya uongozi wa kanisa? Kwani wakati wao, wanawake hawakuwepo?
  5. Ulishawahi kuziangalia sababu za Paulo za “Simpi ruhusa mwanamke….” Ndani ya kanisa????? NI sababu za kiutamaduni, kimila au za kimazingira tu? Hebu sema kidogo hapa pia.
  Leo naomba nikupatie haya machache kwanza, ili utafakari na kuniletea majibu sahihi.
  Ubarikiwe na Bwana

 18. Ndugu Lwembe,

  Hutakiwe kushikwa na kigugumizi wakati unapoona wana wa nuru wakiongezeka. Je unataka wakufwate huko uliko kwa Ibilisi? Isipime pindisha Injili Lwembe. Hakikisha umetubu uongo wako. Hapa ni kanisani. Ndio maana utawaona tu wateule wa Bwana wakikany’aga hila za Lwembe. Kiukweli ni kwamba huleti jambo jipya. Rudilia tena ile makala yangu ya 07/03/2014.
  Asante.

 19. Mr. Milinga,

  Ngoja nijaribu kuyajibu kwa kiasi haya maswali ya jumla uliyoyaleta:

  1. Mungu ni Mwanaume au ni mwanamke? Kwa nini ?

  JIBU:
  Mungu ni Roho!
  Yh 4:24 ” Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” Basi jambo la kuwa mke au mume hilo ni la mwilini, ndio maaana linaongozana na swali jingine la “Kwa nini?” Hebu jitahidi, hama toka huko mwilini, panda huku juu Rohoni utayaona hayo!

  Mwa 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu … 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Umemuona mtu wa kwanza, alikuwa mwanaume na mwanamke huyo mtu; sasa usikimbilie akili yako ya viungo vya kike na vya kiume, huyu alikuwa ni roho mwenye masculine na feminine spirit, hivyo viungo walipewa baadaye walipofinyangwa na kutenganishwa, huko Mw 2:7/21-23!

  2. Malaika Mbinguni ni wanawake au ni wanaume?

  3. Shetani ni mwanaume au ni mwanamke?

  Maswali 2 na 3 nitayajibu pamoja kwa sababu yanashabihiana. Maelezo yaliyoko ktk Mk 12 kuanzia kifungu cha 18-25, yanaweza kukuonesha wenzako waliokuwapo siku hizo ambao nao walitatizika kama wewe kuhusu mambo ya jinsia au mwili na tamaa zake ktk ujumla, kwa wote walio mwilini!

  Kristo alipowatazama akawaona jinsi ambavyo kwa kung’ang’ana kwao mwilini, wanatamani kuendelea na mbinje zao mpaka mbinguni, akawasikitikia, hata kuwaambia, “Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?” Unauona umuhimu wa kuyafuatilia Maandiko ili kujua kwa usahihi yanachofundisha? Ukiyakurupukia ndio hivyo, UNAPOTEA!!! Oh, sijui Paulo alikuwa anafundisha mila, jamani, kwani Mungu ni kabila gani?? Acheni mizaha isiyokuwa na maana, mtapotea mchana kweupe!

  “25Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.”

  Hayo mambo yako Milinga hakuna mbinguni, bambo huko ni tuliiiiiii, la ukiona michosho, basi endelea na jeuri ya kuwasimamisha walimu wanawake!!

 20. Milinga,

  Twende pole pole brother!
  Kwanza mimi sijasema kwamba mwanamke haruhusiwi kupewa ukuhani. Pili ninavyofahamu ni kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumpa mwingine ukuhani isipokuwa Mungu tu, ila kama ninyi mnapeana ukuhani, well, nayo ni safi!!!!

  Halafu, Ukuhani na Uchungaji si sawa. Jaribu kuzitazama kazi za kuhani ktk Agano la Kale, kubwa ya yote ilikuwa ni kuhusiana na usimamizi au utoaji wa sadaka ya Dhambi kwa ajili ya kusanyiko lake, above all other rituals! Lakini baada ya Kristo kulitokea mabadiliko, baada ya Sheria kubadilika na ukuhani pia! Katika mabadiliko hayo ndio unaona wakristo waliojazwa RM wakipewa ukuhani, wake kwa waume, 1Petro2:9 ambayo maelezo yake yako wazi ukuhani huu ni zaidi ya ukuhani wa AK. Sasa kupewa ukuhani hakuyabadilishi maumbile yako bali kunakupa mamlaka zaidi ktk majukumu uliyopangiwa tangu asili!

  Mchungaji ni mtu anayechunga kusanyiko. Huyu si mnyapara wa kusanyiko! Ndani yake Mungu amemjalia kipawa cha upendo wa kulihurumia kusanyiko lake. Asipokuona kusanyikoni Milinga, kwa wiki mbili mfululizo, lazima ainuke kukutafuta kondoo wake, basi fikiria mke wa mtu akizunguka majumbani! Tena huyu, Mungu humjaza kipawa cha Imani, maana yeye husimama kati ya mbwa mwitu na kusanyiko kulilinda lisiraruliwe na adui. Basi kama uliambiwa mwanamke alidanganywa gubi gubi, hakushtuka hata chembe, akaumeza uongo wote akiamini kwamba ndio kweli, hili pekee halikuoneshi asili ya maumbile yake, kwamba anapaswa kumilikiwa? Au hujui kwamba ukamilifu wa mwanamke uko ndani ya mwanaume? Kwa akili yako, unadhani Nyoka angethubutu kumsimamisha Hawa ampige fix akiwa na mumewe? Nalo kanisa linaloliacha Neno la Mungu na kutembea pekee huwa ni target ya maroho ya dini!!!

  Najua utajidanganya kwa kukosa ufahamu kwamba mbona mwanamke naye amejazwa RM! Hilo ni sawa, lakini aliyemuumba ndiye anayeujua udhaifu aliomuumba nao, ndio anatuambia jinsi ya kuishi naye! Tena basi, hata huo unabii unaodhani unampa ruhusa ya kuwa mchungaji, kwa taratibu, hizo huduma nne huwa chini ya mchungaji; naye nabii anapokuwa na ujumbe, huwa haumwagwi tu kwa kusanyiko, bali unabii wake hupimwa kwanza na “wazee wa kanisa”!!! Au umeuzoea utaratibu tulionao leo hii ambao mtu akiwa na kipawa cha unabii tu anafungua kanisa lake!!!!

  Wazo lako kwamba kwa mwanamke kutokupewa nafasi ya uchungaji ni kubaguliwa, kwamba mtume Paulo ni mwenye imani kali sana (extremist) wa masculinity, kwa kule kutowapa nafasi wanawake; kwahiyo wewe na wenzio ndio mnajitoa muhanga kuwatetea, binafsi sikushauri uendelee na harakati hizo kwani haujui malaika atachokea wapi kukuvumilia, asije akakupiga upofu kama wale wa Sodoma na harakati zako zikaishia ukingoni pamoja nawe!!!

  Kuhusu ubaguzi, usijisumbue sana akili yako, jaribu kuchunguza, wanawake halisi, walio na genes za kike, wasiopandikizwa genes za kiume huko maabara, wanapenda saaana kutawaliwa; yachunguze Maandiko utaliona hilo, km Sara, si unamuona akimuita Ibrahimu mumewe ‘Bwana!’ Halafu, hebu jaribu kuitafuta picha ya Joyce Banda, rais wa Malawi alipokuwa akisalimiana na akina Kikwete, for once u’ll luv it, AMEPIGA MAGOTI, a character befitting a Christian woman!!!!

  Maswali hayo mengine ulimuuliza Siyi, nimemuona amerudi, kabla ya kukujibu, atakuwa anajaribu kuangalia kwanza, kwanini Hawa alidanganywa siku ya Sabato!? Whyyyyyyyyy not on Sunday?????

 21. Ndg Ziragora,

  Naona unasumbuka na kauli zako, zinakufanya uwe unaongea bila dira!

  Usinishambulie mimi, wewe gombana na Injili, humo ndimo imeandikwa “Simpi ruhusa mwanamke…”; kama unasema huyo ni Paulo, hilo ni jema, basi kubali pia kwamba hilo ni sehemu ya Injili, ndio maana limo humo kwa ruhusa ya Mungu, ie kama unaamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu; la kama umechagua ujinga, ukakuongoza kuamini kuwa ndani ya Biblia kuna mafundisho ya mila, maneno ya Shetani na ya watu na upuuzi mwingine, kama huo wa “udhaifu wa Paulo” unaoung’ang’ania kwa kukosa uelewa wa anachokufundisha, basi nawe ongeza neno lako ujumuike na hao wengine, kama moyo wako unavyopenda, “” Nampa nafasi mwanamke””!!!! Kundi la kuipokea ‘injili’ yako mbona ni kubwa sana!

  BALI wenye mapenzi na Injili ya Kweli, hawataipokea hiyo, kwa maana wanafahamu fika kwamba Mungu ataihukumu dunia sawasawa na Injili aliyoihubiri mtume Paulo na si injili uchwara za akina Ziragora, zitakazowaishilizia kilio kwa ujinga!

  Mungu akusaidie, akupe na moyo wa kujifunza!

 22. Seleli,

  Kwanza kwa kusema “topic ni ya muda mreeeefuuuuu” ni dhahiri kuwa uko ktk wishes, mimi nadhani topic ya muda mreeeeeeefuuuuuuuuuuu…… ni Mwanzo 1:1, na bado tunaendelea nayo VERY FRESH, ya “leoleo”; ndivyo lilivyo Neno la Mungu, hakuna la muda mreeeefuuuu!!!!

  Siku zote nikisoma kwamba, “Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga” nilikuwa nashindwa kuelewa sawasawa, inakuwaje? Bali kwenye mjadala huu ndio nimelijua vizuri jambo hili, kumbe mtu anatangulia kwanza kuwa mjinga, na kwa hiyari yake anaendelea ktk ujinga, akiongozwa na huo ujinga!!!

  Sasa mjinga akikutana na mafumbo ya Mungu, ndio anaishia ktk upumbavu kama huu, kama unavyolihusisha Neno la Mungu kupitia mtume Paulo, hilo linalosema, “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume…”, bila hata ya aibu, kwa kejeli unasema eti mtume Paulo kwa kauli hiyo anawanyanyapaa wanawake!! Tena basi, inasikitisha zaidi hapo inapoonekana kwamba unao ufahamu kamili kwamba Mungu ndiye aliyeyanena hayo unayoyaita vepa, kupitia Paulo, kama kauli yako hii inavyojidhihirisha:
  “”Ila kuna Watu wana pumba umu, sijapata kuona na pia wapo bila aibu kabisa wanasapoti vepa izo! Huyu Mungu anayewanyanyapaa Wanawake zama za leo Agano Jipya ni wa Mtakuja Village Liwaleeeee si wa Mbinguni””

  Zab 92:5-6, inadhihirisha hali ya kiroho ya mkristo wa jinsi hii, “Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa. Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.”

  Kwa ujinga, wakristo wengi hudhani kwamba wakiisha kujazwa RM basi wana uhuru wa kufanya lolote moyo wake unalopenda kuhusu Injili, haswa kuhubiri, wakijaribu kuziruka taratibu zilizowekwa na RM huyo huyo wanayesema wamejazwa! Inashangaza saana, lakini RM ndiye ambaye hulisimamia na kuliongoza Kanisa, na huyo ndiye aliyekuwa ndani ya Paulo akiweka utaratibu huu kwa kanisa la Mataifa, sisi tusiomjua Mungu, na sasa tunaukataa, kwa ujinga tukiongozana Shimoni!!!

  Vipawa vya RM huongozwa na RM, na vipawa vya dini huongozwa na roho wa dini; jaribuni kuvipambanua vipawa mlivyo navyo, ni nani anayevisimamia, maana Vipawa havina majuto!!!!

  Usikubali kuwa “guinea pig” wa majaribio ya kukiuka taratibu alizoziweka Mungu; Buckle up (The Word), son of man! Those religious airbags will never work when you hit hell!

  Ujinga una gharama!!!

 23. Swali kwa wote waliowahi kuchangia mada hii huko nyuma na sasa hivi.

  Hebu niambieni,

  1. Mungu ni Mwanaume au ni mwanamke? Kwa nini ?

  2. Malaika Mbinguni ni wanawake au ni wanaume?

  3. Shetani ni mwanaume au ni mwanamke?

  Ukinipatia majibu ya maswali haya utakuwa umenisaidia saaaaaana.

  Milinga.

 24. Mzee CK Lwembe,

  Asante kwa maelezo mazuri yenye ufafanuzi wa kina wa hoja hii. Nimependa jinsi unavyojenga hoja yako. Ubarikiwe. sana. Mungu akuinue juu na uzidi kuwa na vipawa vya kuwaelekeza watumishi wa Mungu.

  Hata hivyo, umechekesha uliponukuu maandiko ya Paulo, ukanishangaa mimi niliposhangaa Bwana Siyi . Nakunukuu, ” Hivi ni Siyi anayekuchekesha kweli au ni mtume Paulo aliyesema “Simpi nafasi mwanamke…”? Usipende kujichekesha bila Maarifa, utaishia kilio!”

  Unajua wewe nimekuweka katika kundi la waumini wenye imani kali sana (extremist) wa masculinity. Unaamini sana kuwa Mungu anachunga kondoo wake kupitia wanaume tu at lakini anaweza kusema na kusanyiko lake kupitia mwanamke. Ajabu gani.

  Lwembe hivi unaelewa kwamba kazi ya ukuhani ambayo leo nyie mwaiita uchungaji haina tofauti na Unabii ambao wewe wasema mwanamke anaweza kuwa nabii lakini katu haruhusiwi kuwa Kuhani au Mchungaji.

  Yesu alipopaa alitoa vipawa akawapa wengine kuwa Mitume, Manabii, Wachungaji, Walimu na Wainjilisti. Je, wanawake ni wapi wamebaguliwa wasipewe moja ya vipawa hivyo vya RM ambaye hana ubaguzi wa kijinsia? Hivi RM anabagua anapotoa vipawa? Je, Mungu anabagua jinsia atoapo vipawa?

  Kipawa cha ukuhani au uchungaji kama wasemavyo wengi leo kinapokuja kwa mtu toka kwa Mungu kinabagua kwa sababu tu huyu ana via vya uzazi vya kike kwa hiyo kipawa kinamkwepa kwa sababu ana uke na wewe kinakuijia toka kwa Mungu kwa sababu una uume? Tofauti ya mke na mume ni nini kama siyo via vya uzazi tu?

  Hata hivyo maswali yangu mengi hukuyajibu. Naomba uyajibu.

 25. Amaa! mmelianzisha tena hili? TOPIC ya muda mreeeefuuuuu hii na kila maswali na mnayosema tena humu, in one way or full ways, yameshasemwa humu, hakuna jipya!

  Ila kuna Watu wana pumba umu, sijapata kuona na pia wapo bila aibu kabisa wanasapoti vepa izo! Huyu Mungu anayewanyanyapaa Wanawake zama za leo Agano Jipya ni wa Mtakuja Village Liwaleeeee si wa Mbinguni

  Paul au tamaduni kama zilionyesha kuwa-degrade Wanawake, ni wao kama Watu na izo customs za Viumbe na si Mungu Muumba

  Wajua kuna wakati mnakomalia hoja wakati hata akili yako ya dona tu inakuzomea ndani kwamba iloooo ilooo iloooo but unakaushia tu

  Come on guys, stop lowering down your God given status by discussing the minor things like Wanawake stop, Wanaume Juu-indeed that is an advanced communal foolishness

  Mwamamke kama Mwanaume wana RM mmoja, no way we can down play them and if we do like Paul, then we know that is human role/factor in the Bible which again si dhambi maana ni Mungu ameruhusu vyote viwe recorded ktk Kitabu namely human part, His Part and Devoz role-Ukibisha ilo, ni mbishi tu wa by the way and bora liende but without a stone on the table.

  Acheni fix Wanaume za wakati mnakunywa mtori, Mwanamke akishaokoka, ni habari nyingine kubwa sana kabisa JUU kama sisi

  Press on

 26. Lwembe,

  Simpi siyo shida. Acha chamsha uongo mbele ya Paulo. Yeye si kama wewe. Hahitaji uongo wako. Akiwa dhaifu kwa mwili anasema, ikiwa ni kwa roho anasema wazi. Anaposema yeye anatofautisha na wakati Mungu anamuagiza kusema. Hayo tuliyaongea sana ukaishia kwenye uongo tu!!! Hivi hujatosheka na uongo? Unataka uwe na uzito upi ndipo uuwache?

  Siku nyingi eee… Yes, naona tulipoamalizia kaka . Acha ni paste hiyo kauli yangu, pengine ndipo utakuwa na ujanja wa kuendelesha vizuru zaidi.

  “Alphonse ziragora 16/09/2013 at 9:55 AM

  Ndugu yangu Lwembe,

  Nakupenda sana na wala sitaki upotee. Sasa naona ukiendeleacheka baada ya kuwa umejifunga wewe pekee mikono na miguu.
  Kiri wazi udhaifu yako ndani ya mjadala huu, ufunguliwe, RM akuangazie. Na wakati utakapomaliza kiri, Neno la Mungu litafika kwa uwingi ndani yako. RM atakapotaka anitumie kwa ajili ya kukuelimisha zaidi juu ya Neno la Mungu na Maneno ya Mungu, hapo ukiisha mrudilia, nitakuwa tayari kwa kukuletea maelezo yake ktk mjadala mwengine ambao utaweka ukiomba msaada.

  Bwana Yesu akubariki.”

  Asante

 27. Milinga,

  Hivi ni Siyi anayekuchekesha kweli au ni mtume Paulo aliyesema “Simpi nafasi mwanamke…”? Usipende kujichekesha bila Maarifa, utaishia kilio!

  Kuhusu ukuhani, bado sote tunayo nafasi ya kuliangalia hilo vizuri ili tupate uelewa sahihi wa jambo hili kulingana na Maandiko yanavyotutaka. Kauli za Siyi na Mabinza zinaweza kwa kiasi zikawa zimejikanganya ktk kutamatisha kwao, lakini kimsingi, wamesimama ktk Fundisho halisi la Biblia.

  Hata nawe pia naona umejikanganya, hapo unapotuambia kuwa ktk Agano la Kale kulikuwa na makuhani wanawake, sidhani kama unakijua unachosema, maana kuhani na nabii ni vitu viwili tofauti ambavyo nakuona umevifanya ni kimoja!!! Kwa taarifa yako HAKUNA kuhani mwanamke ktk Torati! Unabii ni sawa, wako manabii wanawake, tena si huko tu bali mpaka ktk Agano Jipya wapo na wataendelea kuwapo kwa kadiri Mungu atakavyo waita kutumika ktk nafasi hizo.

  Nao unabii wanaopewa ktk Agano Jipya ni ule unaohusiana na makusanyiko yetu ambao wapaswa kuwa chini ya mchungaji. Nabii wa kusanyiko hupokea Neno linalolihusu kusanyiko specific ktk shida waliyonayo au maelekezo kutoka kwa Mungu kuhusu jambo lolote wanalokabiliana nalo, na pia shida za kusanyiko, Mungu hupelekewa kupitia huyo. Nabii sio mwalimu. Ualimu ni karama nyingine kabisa!

  Ukuhani wa Agano la Kale uko wazi sana, sijui ni kwanini umelikosa jambo hili. Nao ukuhani wa Agano Jipya anaopewa muaminio, ni ukuhani bora zaidi kuliko ule wa AK. Sasa unapojaribu kulileta jambo jipya ktk utendaji wa zamani, ni dhahiri kuwa utakuwa umechanganyikiwa kimaisha, maana wokovu wetu unadhihirika ktk maisha tunayoyaishi na si hadithi za dini!

  Paulo amefundisha wazi kuwa ukuhani umebadilika pamoja na sheria yake, basi ulipaswa utafute kuyajua hayo kwanza kabla hujaanza kufundisha vitu usivyovielewa! Tulia kidogo uyasikilize Maandiko yanachokuambia kaka!! Angalia vitimbi unavyotuletea, “”Aidha, Mariamu aliyemzaa Yesu naye anasemwa kuwa alikuwa kuhani na Nabii (Luka 1:46-55).”” Huku ndiko kuchanganyikiwa kimaisha ninakokusema, hayo Maandiko ndio yamekuambia kuwa Mariamu alikuwa kuhani?!!!!

  Jambo la usawa ktk Kristo hilo ni kweli, lakini usawa usiozingatia majukumu ni upotofu. Mungu siku zote ametuwekea majukumu, nako kuyatimiza majukumu hayo kama tulivyopangiwa ndiko kumheshimu huyo aliyetupangia hayo majukumu. Tazama jambo hili, kwamba Mungu aliposhuka bustanini, hakuwaita wote wawili ili kudhihirisha mtazamo wako uliopotoka, bali, “9 BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?” Sijui kama unaweza kudaka chochote hapo? Na mwisho Mungu anamwadhibu kwa kosa la kuisikiliza sauti ya mkewe, “17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale…”!!!

  Milinga, muwe makini kidogo, nyakati zimebadilika, Adamu wa kwanza aliyeanguka, sasa amekuwa fortified ktk Adamu wa Pili, hasikilizi tena sauti ya mkewe bali ya Sauti ya Mungu tu!!! Basi kama ambavyo Adamu alipoisikiliza sauti ya mkewe, kwa hiyari yake alikuwa ameamua kujitenga na Mungu ili aambatane na mkewe, ndivyo na mwaminio wa leo huyo wa mwilini, anavyoamua kuambatana na Mafundisho ya dini yake, akijitenga na Mungu, na kwa huyu wa leo, HAKUNA dhibihu baada ya kuvionja vipawa, halafu ukarudi nyuma ukaanza kufundisha madudu!!!

  Pia unapaswa ufahamu kwamba Agano Jipya lina mambo mapya, yasikilize kwa makini. Kichwa cha mwanamke ni mwanaume, haya ndiyo mambo mapya brother! Au nikija nyumbani kwako kisha nikamwita shemeji chemba na kuongea nae usiyoyasikia, utaridhika kweli? Labda uwe jigolo, vinginevyo lazima utawaka tu! Mwanamke sharti awe ktk hali ya kumilikiwa, kama hamlitaki hilo basi rudini kwenye upagani wenu, huko ambako waume mnatawaliwa na wake zenu!!!

  Otherwise karibu ktk Ukristo, where men are men and women are so happy abt it!!!

 28. @ kastori,

  Wapendwa wengi hawakijui hata wanachokiamini, Biblia yenyewe hawaiamini licha ya wao kudhania kuwa wanaiamini! Nao watu wa jinsi hii huwa wamegubikwa na ujinga wa dini, kwahiyo ni vigumu sana kwao kufika mahali mkajadiliana ktk Msingi endelevu uliojengeka juu ya Biblia kwani hawakawii kuyarejea mafundisho yao ambayo wao hudhania kuwa ndilo Neno la Mungu!!!

  @ Ziragora,

  Jambo la Hukumu halikwepeki ndg yangu almradi tunaongelea Neno ambalo ndilo lenye Kuhukumu! Kama Neno limesema “Simpi nafasi mwanamke…” wewe ukimpa nafasi mwanamke, umekwisha kuhukumiwa, linalobakia kwako ni kusubiri utekelezwaji wa adhabu ya Hukumu hiyo tu!

 29. Mpendwa, MJ, Siyi

  Unachekesha sana. Pamoja na kwamba mjadala huu ni wa siku nyingi nimeona si vyema mjadala ukaisha bila kusema jambo kutokana na mawazo yako ambayo yanapotosha kanisa la Kristo.

  Hivi unaposema kwamba mwanamke hakupewa mamlaka yoyote ya kikuhani na kwamba kumpa mwanamke mamlaka ya kikuhani ni UASI ULIOPITILIZA unaelewa unachokisema au umekariri tu? Nanukuu kauli yaako, ” Kuwaruhusu Wanawake kuwa wachungaji, walimu, manabii, watawala n.k. ndani ya kanisa la Mungu, ni UASI ULIOZIDI MIPAKA. Kama Mungu mwenyewe amekataa, sisi hatuna mamlaka ya kubadilisha amri hiyo”. mwisho wa kunukuu.

  Hivi Siyi wewe mbona unaonekana kuwa na elimu ya maandiko lakini hapa umejikwaa sana? Umepata wapi ujasiri huu. Nani amekuroga na kukufundisha mafundisho potofu kama hayo?

  Ukweli ni kwamba MWANAMKE na MWANAUME wako sawa mbele za Mungu. WOTE NI MAKUHANI. HIVI UNAJUA KAZI ZA KUHANI WA AGANO LA KALE? Je, katika Agano Jipya KUHANI ni nani? Hujui kwamba kila Mkristo ni Kuhani? Hujui kwamba katika Agano Jipya Kuhani Mkuu ni Kristo?

  Siyi na Mabinza, naona mumepotoka sana. Mwadhani mwanamke siyo Kuhani kwa mitazamo ya maandiko gani? Kama kuna andiko unadhani linakulinda kwenye hoja hii, tafakari tena.

  Katika Agano Jipya hatuna tena huduma za Makuhani kama ilivyokuwa zamani za Musa na Manabii.

  Hata hivyo, enzi za Musa pia walikuwepo manabii na Makuhani wengi tu wa kike. Kwa kuwataja wachache; alikuwepo Nabii miriam (Kut 15:20), Nabii Debora (Waamuzi 4:4), Nabii Hulda (2 Falme 22:14), Nabii Nowadia (Nehemia 6:14), yupo Nabii mwanamke aliyekuwa mke wa Nabii Isaya (Isaya 8:3), Nabii Elizabeth (Luka 1:41-45) Pia kulikuwepo Nabii Anna (Luka 2:36-38). Pia kulikuwepo manabii binti wanne wa Mwinjilist Filipo(Mdo 21:9). Aidha, Mariamu aliyemzaa Yesu naye anasemwa kuwa alikuwa kuhani na Nabii (Luka 1:46-55).

  Ukiacha maandiko ya Mtume Paulo aliyekazia zaidi kuwa mwanamke na mwanaume ni sawa katika Kristo (Gal 3:28), hata katika Agano la kale hakuna ushahidi wowote unaoonesha kwamba Mungu aliwakataza wanawake wasiwe makuhani wala manabii kama nilivyoeleza kwa kina orodha ya manabii wa kike hapo awali.

  Kusema kwamba wanawake hawajaruhusiwa kuwa MAKUHANI ni ushamba wa zamani kabisa ambao haupo hata katika maandiko. Ukisema wanawake hawaruhusiwi kuwa makuhani, unapaswa unieleze hao niliokuorodheshea walikuwa wanafanya nini kama siyo ukuhani na uchungaji.

  Hivi Nabii Debora hakuwa mwanamke? Kazi aliyoifanya ya kuwa mwamuzi wa Israeli haikuwa kutawala watu wote wanawake kwa wanaume? Je, kuna sehemu tunasoma kwamba alishindwa majukumu yake ya ukuhani wa Israeli kwa sababu alikuwa mwanamke?

  Siyi nakuomba unijibu maswali haya machache kisha tumalize mjadala huu:

  1. Je, mwanamke anaruhusiwa kuwa mwalimu wa watoto kanisani kwenu?

  2. Je, mwanamke anaruhusiwa kuwa mwalimu wa Shule ya Msingi au Sec?

  3. Je, Mwanamke anaruhusiwa kuwa Mkufunzi wa Chuo Kikuu?

  4. Je, Mwanamke anaruhusiwa kuwa Daktari wa magonjwa?

  5. Je, Mwanamke anaruhusiwa kuwa Mkulima wa mashamba?

  6. Je, mwanamke anaruhusiwa kuendesha ndege au treni au Meli?

  7. Je, Mwanamke anaruhusiwa kusoma shule ya awali mpaka Chuo Kikuu?

  8. Je, unadhani ni sawa Mwanamke kwenda kusali kanisani?

  9. Je, mwanamke anaruhusiwa kuwa mfanya biashara?

  Kama majibu yako ni “NDIYO” kwa kila swali, niambie kwa nini unadhani ukuhani pekee ndiyo kazi mwanamke amekatazwa na Mungu?

  Naomba majibu.

 30. Ewe mwanaume, usiwashambulie wanawake ukidhani wanaume wao ni watakatifu! Usihukumu ili nawe usihukumiwe! Hata kwa kuchanganya mambo ambayo hayafanani au kujifanya bora kuliko waliotangulia au kutia mkazo kwenye anguko pasipo kujali wokovu pengine inaweza kuwa upotofu!

 31. Neno la Mungu linameandikwa katika namna ambayo linahojika na hata kukataliwa na wenye akili,busara,hekima za kibinadamu na wanatheologia wa seminari. LAKINI kwa wajinga kila neno la Mungu ni amina. ukiona unakataa neno la Mungu kwa tafsiri pana za kibinadamu na kulikosoa neno, usipate shida jua wewe ni mpinga kristo kwani kristo ndiye neno. Kristo anasema walio wake wanaijua na kuisikia sauti yake (yaani Neno lake) ukiona unapinga Neno lake juwa wewe sio wake. Kristo anasema baba nakushukuru kwa kuwa mambo haya uliwanyima wenye hekima na akili ukawapa watoto wachanga( yaani wasio na akili,wasioweza kuhoji, kwao neno la mungu ni amina) jua kwamba si tu mhubiri mwanamke amepotoka ila hata wale wanao kaa na kuhubiriwa na huyo mwanamke wamepotoka pia, kwani jinsi kuhani alivyo ndivyo na watu wake walivyo. MWANAWAKE walileta anguko katika dunia na hata sasa wanaleta anguko kimya kimya na waziwazi.
  je ni fundisho gani linaloruhusu mwanamke siku ya harusi yake avae nguo mgongo wazi na kifua wazi tena madhabauni? hata mchungaji alipooa mkewe naye alivaa hivyo hivyo!

  kama kujichubua ni dhambi ya kumkosoa Mungu katika uumbaji wake je kupaka kucha rangi, kusuka rasta,kupaka wanja si hayo hayo? karibia wachungaji wote wamefumbwa katika hayo kwani wake zao ndio vinara wa kupendeza katika mwili je atawezaje kukemea wakati yeye ndio anatoa hele ya kufanya hayo yote?

  siku zimeisha mtoto wa Mungu baki jinsi Mungu alivyokuumba na kama tayari ulishapotoka sikia neno lake jutia ya nyuma na usonge mbele sawasawa na neno lake naye atakupokea kwa haraka sana ..ooko

 32. Siyi,

  Mnapoendelea kujadili, ina maana mnataka copy-paste:

  Nakukumbusha tu jinsi nilikuambia tangu awali kamba hudaiwi kitu chochote kingine ukiwa jela pamoja na waongo wote. Sina haja yoyote ya kuingia ktk mbingu unayotengeneza peke yako ambamo watakaoingia ni waongo maksusi kama wewe, na wenye kuimbaimba tu « Roho mtakatifu- Roho mtakafujo ». Kama hupendi lipa haka ya jela ambayo ni kuomba masamaha tu, baki humo humo pamoja na wote watakaokufwata humo, hapo ukiendelea kulalamika na kuimbaimba, full stop. Wewe peke hukuona kama rejea zako zilikuishia wakati ulibaki ukizungmza na Ndugu Seleli? Muongo anapokwisha shikwa hupungukiwa sana hadi atakapolipa gharama. Panya ikiwa imenaswa ndani ya mtego, harakati zake za kuchunguza kam mtego ingali hazina faida. Inabidi ibahatike itoke ndipo ijue kuchunguza.

  Asante.

 33. Ndugu Mabinza,

  Ninachoona kwako ni kwamba una tatizo la kutofautisha uongo na mtazamo/maoni/msimamo. Ndio maana unasema neno uoga na uongo kirahisi tu pasipo kufikiri. Kwa hivi itakuwa vigumu kwako kuhojiana na waliokua kiroho.

  Ungekuwa muungwana, kam ukidhani mjadala imeisha ukizubaa, ungetafuta namna ya ku post mjadala mwengine ambamo utatia kipengele kinachoifanana ( ikiwa SG itaikuali) kuliko kuzusha mambo yaliyomalizika. Wala usihudhunike kam ulikuwa kwa upande wa walioshindwa kwani hii ni kawaida kuwe wanaoshinda na wanaoshindwa. Kwani najua una uhakika kwamba simple copy-paste inajibu swali lako unaloletea Ndugu Seleli. Sasa nakuomba uheshimu hii mjadala na wana SG wote, usiwahesabu kuwa watoto wachanga, na usifikiri mjadala huu ni mchezo wa kitoto ambapo tutapotezea mda tuki copy-paste tu. Unapofahamu Neno la Mungu ni jipya kila siku, fahamu vile vile kam mijadala inaweza wekwa upya kam mwenye kuiweka anayo upako wa Mungu, wala hakuna atakaemzuiza kam Mungu ndie ameruhusu.

  Hata ukipeleleza mambo ya sheria utakuta mtu akishindwa kwenye kituo fulani cha sheria, hawezi leta tena ile ile mashtaka hapo hapo. Inambidi kulalamikia nafasi nyingine. Usipofahamu ile utakuwa umehakikisha ungali mchanga.

  Kwa mwisho, harakati zote za kuwarudisha watu nyuma, kwa kujipendeza tu, hazitafaulu. Au utajadili na wengine wapya ambao kwao hili jambo ni lipya.

  Asante

 34. Seleli,
  Hakuna mtu anayeleta mzaha kaka!! Nawe unashangaza tu!! Hakuna mzaha kwenye masuala ya wokovu. Acha kuchafua hewa kaka. Msingi wa maandiko uko bayana kabisa na wewe kipindi kile ulikiri kabisa kwa kinywa na maandishi yako kuwa, ni kweli Mungu hana upendeleo lakini ametugawia majukumu tofauti. Wanaume kuwa na mamlaka ndani ya kanisa na wanawake kukaa kimya!!Ukibisha, nitakukopia michango yako na tarehe ya michango hiyo na kuiweka hapa ili iwe ushahidi. Acha kuwa kinyonga kaka.
  Mungu akubariki Nshosha ng’ombe

 35. @Haule
  Muhtasari wa majibu
  Biblia kuanzia mwanzo hadi ufunuo, hairuhusu wanawake kuwa na mamlaka kwa wanaume, aidha kwa kuwafundisha, kuwatawala, kutoa unabii, nk. Majukumu ya kimamlaka ama kiutawala, Mungu aliyagawa kwa wanaume tu. Kuwaruhusu Wanawake kuwa wachungaji, walimu, manabii, watawala n.k. ndani ya kanisa la Mungu, ni UASI ULIOZIDI MIPAKA. Kama Mungu mwenyewe amekataa, sisi hatuna mamlaka ya kubadilisha amri hiyo. Tunasubiri Mungu mwenyewe aje abadili au awaite wanawake hao kama alivyowahi kufanya kwa baadhi tu ya wanawake wachache huko nyuma (agano la kale). Na Mungu alitoa sababu kwa nini alifanya hivyo. Baada ya hapo, tunaona Mungu aliendelea na msimamo wake huohuo wa mamlaka kwa wanaume tu hadi agano jipya.
  Nafikiri kaka Haule tulijadili sana masuala haya. Jaribu kurejea kwenye mijadala yote inayohusu huduma za wanawake ndani ya kanisa kwenye blog hii. Aidha, waweza kufuatilia michango yangu huko nilichangia nini kwa marefu na mapana kabisa. Huko utajifunza zaidi. Ubarikiwe na Bwana mjoli wa Kristo

 36. Haule,
  Binafsi nakushukueru sana kwa maswali yako tena. Ni ukweli usiopingika kwamba, maswali haya, yanaweza kuwa yalishajibiwa kwenye mijadala/michango huko juu. Pamoja na mitazamo yetu tofauti, ukweli wa Biblia wapendwa, utabaki palepale.

 37. Mabinza,
  Umejibu vyema sana mjoli wa Bwana. Ukiwaangalia watu wa leo kama akina Seleli, Ziragora, utawaoana kabisa kuwa, ni akina Petro kabla ya uongofu.Watu wa kutunisha misuli bila ya kujua wakifanyacho. Waache watunishe misuli yao, lakini sisi tunawaendea kwa jina la Bwana.
  Mwanamke hana mamlaka wala chembe ya kuwa na mamlaka ya kikuhani. Kama mna dhana zanamna hiyo vichwani mwenu, TOKEN BABEL.
  m-barikiwe

 38. Mjoli Haule,
  Ninaamini kuwa unafahamu kwamba Neno la Mungu ni Jipya kila leo, tunapata Ufunuo juu ya Ufunuo, kwa kadiri tunavyoshare, hata yakiwa ni magumu, lakini bado yanatuhusu!

  Pia bado kuna maswali mengi ambayo hayajajibiwa, mengine yameachwa kuulizwa baada ya kuona kwamba kuna wapendwa Hawaiamini Biblia ktk ujumla wake kuwa ni Neno la Mungu nk, kwahiyo kama unacho cha kushare, ni vizuri ukakileta kwa kuwa hatujawahi kuwa ktk mashindano kuhusu suala hili, labda kuishindania Kweli, na iwapo Seleli anasema walishinda, basi ni simanzi kiasi gani, ktk kambi ya Mungu, kwamba wamemshinda mtume Paulo!!!!

  Gbu!

 39. Seleli,
  Acha uoga!!!
  Inashangaza sana mtu anavyoweza kujifikisha katika kuuamini uongo wake! Hii statement yako,
  “”Bottom line ni hii statement niliwapa na hamjawahi vuka tuta hilo kua’’ Biblia ina taarifa ya maneno na matendo ya Mungu, Watu, Shetani na Wanyama. Unaposoma zingatia hayo ndipo utajua aliyosema Paul kuhusu Wanawake ni NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE PAST, PRESENT AND FUTURE au ni Maneno yake kama Mtu kwa mahali husika na wakati husika kwa kundi husika AKITATUA/WEKA UTARATIBU SPECIFIC kwa kundi hilo tu.””
  kwamba umerudi nayo tena, proves that ume lock ktk understanding! Kama Biblia SI Neno la Mungu pekee, basi umebaki na nini, kama si hadithi za abunuwasi?

  Niliwauliza, ni yapi kati ya aliyoyaandika Paul ni Scripture na yapi ni mafundisho ya mila na desturi kwa makundi aliyoyaandikia, hamjawahi kunipa jibu! Tena nikakuuliza Torati ni Mila na Desturi?

  Pia niliwaulizeni hivi, iwapo huyo asiyepewa ruhusa ya kufundisha ni mke (Isha), yaani kumfundisha mumewe, ndipo ninauliza, Je, mke huyo anaweza kuwafundisha na kuwatawala wanaume wengine? Ndipo mke huyo akiwa ni mchungaji, je, mumewe anaruhusiwa kuwa sehemu ya kusanyiko hilo?

  Haya ndiyo mambo madogo ya msingi unayopaswa kuyajibu bila stori ndefu, kama unayo mamlaka katika hilo!

  Gbu!

 40. Siyi,
  Nakukumbusha tu jinsi nilikuambia tangu awali kamba hudaiwi kitu chochote kingine ukiwa jela pamoja na wawongo wote. Sina haja yoyote ya kuingia ktk mbingu unayotengeneza peke yako ambamo watakaoingia ni wawongo maksusi kama wewe, na wenye kuimbaimba tu « Roho mtakatifu- Roho mtakafujo ». Kama hupendi lipa haki ya jela ambayo ni kuomba masamaha tu, baki humo humo pamoja na wote watakaokufwata humo, hapo ukiendelea kulalamika na kuimbaimba, full stop. Wewe peke hukuona kama rejea zako zilikuishia wakati ulibaki ukizungmza na Ndugu Seleli? Mwongo anapokwisha shikwa hupungukiwa sana hadi atakapolipa gharama. Panya ikiwa imenaswa ndani ya mtego, harakati zake za kuchunguza kam mtego ingali hazina faida. Inabidi ibahatike itoke ndipo ijue kuchunguza.
  Asante.

 41. Humphrey and Haule,

  Hii topic tumeijadili sana hapa hapa, ina comments 142 hadi sasa na KILA MLIOULIZA YAMESHAJIBIWA HUMU NA TENA ZAIDI, kama mtapata muda, pitieni zote.

  Lwembe and Siyi, Mnasikitisha tu maana mnajua tulijdili sana na mkashindwa kabisa kabisa kusimamisha hoja zeu dhidi ya zetu, mtanataka tena tuanze upya? Kama vipi semeni, nitakachofanya ni ku-copy juu na kuwa-pastia hapa maana mnaleta mzaha! Ukisha shindwa, umeshindwa, that is all.

  Bottom line ni hii statement niliwapa na hamjawahi vuka tuta hilo kua’’ Biblia ina taarifa ya maneno na matendo ya Mungu, Watu, Shetani na Wanyama. Unaposoma zingatia hayo ndipo utajua aliyosema Paul kuhusu Wanawake ni NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE PAST,PRESENT AND FUTURE au ni Maneno yake kama Mtu kwa mahali husika na wakati husika kwa kundi husika AKITATUA/WEKA UTARATIBU SPECIFIC kwa kundi hilo tu.

  Hamna hoja ninyi Siyi na Lwembe, tuliwashinda na tunashinda tena na tutaendelea kuwashinda, Mungu anawatumia Wanadamu Wote KE/ME.

  Press on

 42. Waajoli Siyi,Lwembe,Humphrery&SG
  Shalom
  Naomba kuwapa changamoto…

  1.Huduma tano ktk Kanisa ,Roho Mtakatifu amewapa wanaume peke yao au na wanawake pia

  2.Kama amewapa na wanawake ,Wapi wanastahili kuhudumu hizo huduma,

  3.kama kuna maandiko yoyote ktk agano jipya Mtume Paul anakataza Wanawake wasiwe Makuhani.

  4.Je ukuhani wa maandiko haya 1Petro2:9 ni kwa ajili ya wanaume tu.

  Baadaye Mungu akipenda tuuende kutazama Ukuhani na unabii baadaya ya hayo maswali manne.

  Basi itakuwa vema na itapendeza tukiwa na maelezo mafupi ya kina yenye kukolea munyu tufaidike wale wenye kusikia.

  Kristo; ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika

  Awabariki

  Amen

 43. Ziragora,
  Pole kwa ujasiri huo wa kutaka hadi kumsahihisha Mungu. Hicho ni kipaji kikubwa mno kutoka kwa yule jamaa. Be careful, utaishia kusiko!!

 44. Ziragora, Humphrey na Lwembe,
  Wengi wanafikiri kuwa, kuwa na RM ni kuyatafsiri maandiko visivyo. Yaani Rm anapomwingia mtu, anakuwa na uwezo wa kuisoma Biblia kinyumenyume. Kama Biblia imesema usizini, yeye huifasiri kuwa yuko huru tu kuzini maana alishaokoka for all. Hana hatia tena anayoweza kuifanya. Sijui kama kweli huyo ni RM!! Mimi nafikiri huyo huwa ni ROho Mtakafujo.
  Mungu amesema wanawake wasipewe fursa na hadhi ya ukuhani, mtu mwingine anakuwa mbishi tu ati Biblia haikumaanisha hivyo!! Ukimwuliza, ilimaanisha nini, anakwambia matakwa yake binafsi tena kwa kumsingizia Roho Mtakatifu eti kamfunulia!! Ajabu sana hii!! Watu wengi wa namna hii watapotea kwa kujifanya vichwa maji!!
  Salama yetu ya kupona siku zote, ni kutii kile Biblia inachokisema. Ukianza kuleta falsafa za darasani na reasonings za ajabuajabu kwa Mungu, YEYE atakutema nje!! Humphrey na Lwembe Bwana awabariki kwa uelewa huo safi na sahihi. Songeni mbele. Ziragora, tunapenda kwenda na wewe mbinguni. Lakini kwa ugumu wa moyo ulionao, tutakuacha rafiki usipoangalia. Mungu akusaidie. Sisi tumesema tu.

 45. Humphrey,

  Wokovu tumeupokea kutoka ndani ya Biblia, kama umepaona hapo mahali Biblia ilipokuambia “Simpi mwanamke ruhusa…”, ukilipokea jambo hilo ukaliamini moyoni mwako na kulikiri kwa kinywa chako, NDIO Wokovu wenyewe!!!!!!!!

  Vitabu vya Paulo ni sehemu ya Biblia, ukiviondoa, au ukiondoa chochote kile, basi na wokovu wako pia unaondoka na hicho ulichokiondoa!!!

  Gbu!

 46. hello guys,
  nilikua napata shida sana juu ya mamlaka ya mwanamke juu ya kuhubiri, mimi ninavyoelewa biblia haimpi mwanamke ruhusa kabisa na huo ndo msimamo wangu ingawa nikuliza kwa watumishi wengine wanasema huyo ni paulo alisema, swali langu ni je vitabu vya paulo havifai kwa kujifunzia, pili nini lengo la vitabu vyake, pia tunajifunza kupitia mifano iliyokuepo tangu enzi hadi leo.
  biblia inasema kila neno lenye pumzi ya Bwana linafaa kwa kujifunzia.
  naombeni na nyie mnisaidie!

 47. Ndugu yangu Siyi,

  Pole sana kaka !!!
  Naona kam wakati niliposema uko jela, ulidhani ni mchezo tu. Lakini ukijaribu fikiri kiroho utaona ungali unajiingiza zaidi humo. Kwa msimamo wa mwili na akili za kibinaadam unaona ile proverb ya huko vijijini inakusaidia; lakini ukiiconnect na Bible: Mwanzo 3: 9-13 …, utagundua kwa nini umebaki uchi na ni nani aliyebeba vazi lako; vile vile utaona maana na uzito wa kuwa uchi. Sasa ndugu yangu, utapata vazi lingine wapi? Na kumbuka uliingia jela ukiwa na vazi lako, sasa leo uko uchi!!!! Umeona tena jinsi wewe mweyewe umejipeleka pabaya zaidi? Dawa iko; ni kumrudilia Yesu Kristo. Sivyo utakuwa ukijinasisha kila mara kirahisi pasipo kufahamu. Ndio maana kabla ya kujadiliana imetupasa kuomba. Nafikiri unaona vema matunda ya maombi. Unapodhani umedhulumiwa kwa machambo, dawa si kujivua nguo!!! You must pray mpaka RM anakufunulia kweli ili uwe huru kwani “Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

  Yesu akusaidie my brother.

 48. Ndugu yangu Siyi,

  Pole sana kaka Siyi!!!
  Naona kam wakati niliposema uko jela, ulidhani ni mchezo tu. Lakini ukijaribu ingia kiroho utaona ungali unajiingiza zaidi humo. Kwa msimamo wa mwili na akili za kibinaadam unaona ile proverb ya huko vijijini inakusaidia; lakini ukiiconnect na Bible: Mwanzo 3: 9-13 …, utagundua kwa nini umebaki uchi na ni nani aliyebeba vazi lako; vile vile utaona maana na uzito wa kuwa uchi. Sasa ndugu yangu, utapata vazi lingine wapi? Na kumbuka uliingia jela ukiwa na vazi lako, sasa leo uko uchi!!!! Umeona tena jinsi wewe mweyewe umejipeleka pabaya zaidi? Dawa iko; ni kumrudilia Yesu Kristo. Sivyo utakuwa ukijinasisha kila mara kirahisi pasipo kufahamu. Ndio maana kabla ya kujadiliana imetupasa kuomba. Nafikiri unaona vema matunda ya maombi. Unapodhani umedhulumiwa kwa machambo, dawa si kujivua nguo!!! You must pray mpaka RM anakufunulia kweli ili uwe huru kwani “Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

  Yesu akusaidie my brother.

 49. Siyi,

  Kwakua lengo ni kuelimishana NENO la MUNGU basi ELIMIKA KUA MWANAMKE ALIEYOOKOKA, NI MTUMISHI WA MUNGU MWENYE KARAMA, VIPAWA, UPAKO, UWEZO KUTENDA YA BWANA KAMA WEWE NA MIMI MAANA NI RM HUTUPA WOTE. NI MAJUKUMU YA KUONGOZA TU KTK LEVEL KUBWA YA MAAMUZI YA MWISHIO NDIO KWA UPENDO, HATUTAMPA NAFASI IYO, ILA MENGINE YOTE , SAFI TU.

  So acha kutoa hoja very weak au kutoa points kama vile Wanawake ni zero kwa kila kitu, kama ulivyo wahi sema kua ni wadhaifu sana kwa maana ile chafu na mbaya na wala si ile aliyo maanisha Petro na nilikuelimisha sana kwa hilo( the idea of weaker comparing to a Male), bado ulibisha na kuchangia kuonyesha kama vile wao wako benet-benet na devo! we vipi bwanaa! ivyo,usiniaambie nina point- less wakati huna uwezo wa kuthibitisha ivyo na pia points zako izo unazosema ni poinfull maana ndio mantiki ya kumesema zangu pointless, ukizichunguza, ni kilio tu. Ukisema my point ni point less, nitahojiana nawe kukuthibitishia ni za nguvu mno na kama utaita iyo ni ushindani, nitasema sawa kwa kua ni mabishano ya hoja na mimi si wa kwanza, kama husomi Bible, shauri yako, ivyo nitafanya ushindani mzuri bila simile, kuvunya ya kidume kibaya na kusimamisha ya Mungu mwenye kuwapenda wote na kuwathamini na hata kuwatumia Wanawake, past,present and future barabara kabisa.

  BY THE WAY………

  Poleni sana uko kijijini kwenu, Nawahimiza, acheni kuogea mtoni, mtakwaa magonjwa ya ngozi, tumbo na pia kuwaambukiza wengine magonjwa aisee, maana mnaporudi kuoga uko uko, mtatapakaza ayo ‘’madude’’ brother. Plz have mercy on them.
  Mazingira ayo ndio yanawepelekea kuwaza na kutoa misemo chovu kama iyo ya Kuny’anganywa nguo uko mtoni.

  …… Mara aliyeoko juu mgoje chini( badala ya kumpandia uko uko),

  ……..Au Aliyekupa wewe kaninyima mimi( so what? Ehe, ok, umenyimwa sasa, so?),

  …….Au Ndoa ndoana( not necessary coz ndoa inaweza pia kua ndoo ya baraka),

  …….Au dunia mduara( halafu? aliyesema ni mstatiri nani? na kwani lazima wote tuduararike?, si kuna short cuts za uhakika tena si za kufoji bali za kimkakati kabisa)

  ……..Au ponda mali kufa kwaja( si lazima kuponda na kufa bali ni kula mema ya nchi na kushiba siku, namna gani hapa!

  And other misemo ya kilevi-levi ivi na kipepo almost kama si ya kivivu, kutakiana shari na mikosi na mablaa. Heri wewe na wana kijiji hao, wakajaza misemo ya Biblia na hiyo mingine ikaja baadaye au kwakweli ikafutika kabisa wala kusiwepo makao yake ktkt ya Wanadamu, Come on Siyi! Namna gani misemo ovyo kabisa hii ya ujima ule mbaya! Therefore, be informed that the crazy man will not take my nguo mtoni because naogea bafuni!

  Press on.

 50. Seleli,
  Msemo mmoja wa zamani huko kijijini kwetu unasema hivi: UKIWA UNAOGA MTONI, HALAFU KICHAA AKAJA AKACHUKUA NGUO ZAKO AKAANZA KUKIMBIA NAZO, WEWE ULIYE UCHI UKIANZA KUMKIMBIZA, NANI ATAONEKANA KICHAA ZAIDI YA MWINGINE KATI YA HAO WAWILI? Jibu la msemo huu, nalitumia na mimi hapa leo kwenye machambo yako haya kaka!!
  Naam, natambua kweli kuwa wewe ni bwana mkubwa, huenda kweli sina uelewa kama wako. Wewe uko juu sana ndg yangu!! Nasema hivyo kwa sababu, lengo na madhumuni ya sisi kuwa tunajadiliana hapa, si kupimana uelewa wala akili. Bali ni kuelimishana NENO la MUNGU tu.
  Msemo wa zamani huo, unatosha kujibu post yako kaka.
  Barikiwa sana

 51. Lwembe,

  Unajijua wewe ni cheap so nimeona nikujibu post yako kirahisi –rahisi tu` ila nitapitisha pia some points kukusadia.

  Uliniuliza maswali, na unajua nimeyanyuka yote vema sana mpaka huna tena jinsi, ukasingizia kua yamekua ya Hapana na Ndiyo answers ivyo ni vuguvugu! Ha ha ha, usinichekeshe Lwembe, huna jinsi na ulidhani maswali yako yako so brainy kumbe so cheap na nimeyaweza kweli! brother uko mwepesi mzee, kubali tu.

  Umesingizia hivi kwamba,’’Kuhusu Biblia ni Neno la nani? Naona ufahamu wetu UMEGOTA’’
  =Acha UWONGO! Umegota wako but wetu umeweza kukuelimisha kua Biblia ina taarifa iliyorekodiwa/andikwa kuhusu Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani, ushahidi wa kweli wa kimaandiko nimekupa mwingi mno, mkubwa kuliko wote tunautoa kwa role model wetu wa mwanzo mpaka mwisho yaani Yesu Kristo-Alisema, Musa aliwaambia muwaache wake zenu na kuwapa taraka LAKINI toka mwanzo haikua ivyo, maana yake toka mwanzo, NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE NI MTU KE/ME WAKAE PAMOJA na WATATENGANA KWA SABABU YA UASHERATI. Hapa Yesu alionyesha wazi wazi kua ruksa ile ilikua ni tendo na neno la mtu- Musa kama kiongozi wa Kiroho wa wakati ule na kwa mazingira yake/yale na aina ya watu wale( Yesu aliwasema kua jamaa walikua wana shingo ngumu), ivyo Musa kama Mtu aliafanya maamuzi ili mambo yaendeje, yaendeshweje. Ukweli huu una apply sana kwa Paul kwa makanisa aliyokua ameyazaa na anayaongoza. Sasa kama akili yako haielewi shule hii ya RM via me, umegota wewe hakika.

  Umesisitiza-“ALL Scriptures…” na kuniambia ati niacha mambo ya kitoto ya kukimbilia tafsiri zisizojitosheleza ili ni manipulate Neno la Mungu!!! na ukakazia God said ALL SCRIPTURE is His!

  In the first place, hakuna aliyesema Maandiko si ya Mungu(property)! You always go to West while we are far away at North-West! Nilichokuongezea ambacho your religious brain get hard time to get ni kua, wakati ni kweli All maandiko ni ya Bwana(afterall yawe ya nani tena, Siyi?), Yet ndani ya maandiko hayo, tumepewa taarifa ya maneno na metendo ya Shetani na Watu, Simple!

  Sasa ni akili kwa kichwani na rohoni, unaposoma kujua which ni ya Mungu-aliyosema Yeye na yale mengine e.g ya amerokodiwa tu mla mkate kama mimi na wewe au Yakobo anasema vizuri kwamba mwenzie Eliya alikua kama sisi tu ili kufunga ujinga wa watu kudhani, waliotutangulia, hawakua watu kwa kawaida, kumbe ni wanadamu tu wa kawaida ambao tunapewa taarifa ya mambo yao humo kama Yezeberi anamtishia Eliya, Paul anasema mimi naongea si Bwana au ninatamani wote msioe kama mimi au ya kusema nimendika barua hii kwa mkono wangu mwenyewe au Daudi akilalama ktk maombi ya toba baada ya kuzini na kuua au Ayubu akimkemea/fokea mkewe aliyekua ananamshauri amkufuru Mungu ili afe n.k.

  Umenitishia ivi..’’God will hold me responsible kwa vitu ambavyo havina tija’’= That must be ‘god’ and her headq is at Yombo Dovya! na si Mungu anayependa na kufurahia wana/Watu wake wakipata/wakiwa na knowledge maana alishakua kua concernd kwa kusema, ‘’Watu wake wanangamiZWA( not angaMIA) kwa kukosa Maarifa(knowledge)

  Kwamba,’’After all I could be giving myself over to some stupid spirit!= ni again hii mbwembwe zile zile za kudeploy big words/statements wakati hamna haja na si ya kweli bali ni mambo yako ya bora liende na blaah blaah tennis ball playing

  Ati, ‘’Mkiambiwa ninyi mnafanya kazi ya Mpinga Kristo, mnalalama, they are smart, intellectual, and you name it!’’, =Stop using big words/statements wakati essence zake, u got slender command on them.Kwa nature/uwezo wako limited, ili ueleweke kirahisi, would strongly advice, plz keep simple!

  Sometimes unafanyaga ni bora liende tu! look at this?=Ziragora, analeta mambo ya unafiki wa zile Fellowships, mama mkatoliki na baba mpentekoste’’…Sasa kama umechoka, si utulie tukuletee heavy stuff, ubarikiwe kuliko mablaah-blaah ayo!

  Uliuliza swali“”Kwamba Mungu alikubali kuchanganya Neno lake na mila?, nikakupa mifano ya maandiko kisha nikataka utumie common senses tu, huna haja ya ufunuo kwa haya ili uamue mwenyewe.”

  Kwanza najua kwakua wewe ni mtu wa mastory ya town ya Clouds efwe eme radio, mwenye blaah-blaah, hukuamini na jasho lilikutokea, nilipojibu swali lako hilo kwa maandiko 7 perfect kabisa yanayoonyesha mambo ya mila, desturi(tamaduni) zilizokuwepo kipindi icho ktk haya- Mathayo.15:26, Mathayo.14:21, Mdo.10:28-29, Galatia.2:7-18, Mdo.16:1-3, 1Wakor.7:17-24, Wagal.3:28.

  Kisha ukaamua case yako mwenyewe kwa kujimaliza ivi kusema,’’ Nukuu zote nilizokupa ni Torati’’.

  Swali:

  (a) Je wakataa ndani ya hayo maandiko, si mambo ya tamaduni(Mila na desturi)? Be clear nikumalize vema zaidi.

  (b) Au niiweke kwa mtindo huu, Je Wanawake kwenda na marashi kuupaka mwili wa Yesu kaburini au Yesu kusema, kwanini mnaliharifu Neno la Mungu kwa kufuata mapokeo yenu, je hakukua na mila na desturi hapo?

  (c) Je yote hayo si yamo umo ktk maandishi ya Maandiko? Kwa iyo, Je ndani ya Neno la MUNGU kuna mambo ya mila na desturi au la? Look at you! sijui unawazaje na IQ yako inactivate kwa capacity ipi on simple stuff to make cheap senses from topics/mada/points?

  Umesema,’’Paulo wala mitume hawana Mila wala Desturi za kipagani kama tunavyojidhania,hao wamezaliwa katika Torati, hiyo ndiyo Mila na Desturi yao’’= Aliyesema wana desturi za kipagani nani? be smart and keep the flow of ideas unapoongea! Lakini pia common senses zinaweza kutusaidia kutamka vitu vizuri ili kutojiaibisha kwa kuonekana, alimradi lolote likija, unafyatuka. At least fyatuka yes, yet connectively/relevantly!

  Hii claim yako..’’Ninatukuza zaidi “kunena kwa lugha” na kuombea wagonjwa’’,=yapaswa itoke kwa mpagani na si wewe usemaye umeokoka na una RM. Ziko nyakati mimi hukudhani wewe uko ktk imani potofu pia! Sorry for this but points zako, misisitizo yako kwa mengi but pia against or at the expense ya kuwa-degrade Wanawake waliookoka na wenye RM na Utumishi, Karama toka kwa RM huyo huyo, ni ushahidi na sababu ya mimi kukuwekea question mark!

  Kama iyo haitoshi, kuponda kwako mambo delicate ambayo generally are true Biblically and held by the Body of Christ with great weight, honor nayo ni ushahidi na sababu tosha ya mtu kukukwere. Make no mistake kwa swali langu nililoulizaga la ‘’asante-asante Yesu’ kwa intention njema kabisa ya kutaka kuangalia kwa upya yale tuyafanyayo ili kujua yametokana na KiBiblia au ni yetu tu ingawa si mabaya maana si kila man-made ni evil hence twaweza kuendelea kuyafanya/tumia kama ni yetu, then tu-establish na ku-accept the fact kua , wengine wanaweza fanya tofauti nasi na wakawa sahihi kwa kua si lazima wafanye kama sisi, that was the point ya ile mada, ila kama kawaida yako, ulitwist na umeendelea kunukuu kwa kutwist kufit in your crippled understanding ya mambo.I real have queries on the group you are in! will continue to search for this mysterious religious/faith faction of yours. I can see kuna ‘madude’ uko, hauko normal brother.

  Nilisema kufunika vichwa ilikua ni ushauri au maamuzi ya Kiongozi wa Kiroho kwa wana wake wa kiroho kwa namna ile aliona ni vema kuliendesha na kulisimamia kanisa la mahali pale na nyakati zile na kwa tamaduni walizoishi kwazo na wala si NENO LA MUNGU KWA KILA KIZAZI past,present and future. Si mara moja au mbili Paul kusema mambo kama ushauri au kuamua vitu vifanyweje kama kiongozi. Hicho nilichosema ni perfect knowledge, God’s understanding of the scriptures and correct diving of the Word. Kushindwa kuelewa this simple point, ni tatizo la ufahamu ambalo sina jinsi ya kukusaidia. Otherwise nikukuulize ivi, may be kutafunguka uko moyoni na upstairs kwako! JE WANAWAKE WOTE PAST,PRESENT AND FUTURE WASIPOFUNIKA VICHWA, WALIKWENDA/WATAKWENDA JEHANUM? JIBU hapo! Look at you!

  Ati ili mradi nimekamata vifungu vya Maandiko na kuanza kuzunguka navyo’’= Lwembe acha maneno ya kunywa chai! ni lazima Neno litumike na nakuhakikishia na wewe wajua, sijatumia andiko vibaya, bila uelewa wenye afya. Usinidangaye na wala usidanganye watu, wewe nawe toa vifungu vyako na vilete kwa usahihi ingawa bahati mbaya ni kua hata ukitumiaga maandiko na kufafanua, ni vichekesho na aibu. Hatujaaanza leo kukufahamu jinsi unavyo hitaji ku-raise standards. Utakagi tu kujitahidi na kukubali kua unapungua sana, uko kama Siyi in many occasions, tena kwa wewe, ni bora Siyi, weye una machache mno aisee yaliyo substances! Hua hueleweki na uko na blaah..blaah nyingi na empty presentations to be honest.

  I, ‘you’re pushing standards raising brother, presses on.

 52. Seleli,
  jambo la kwanza katika mjadala ni Kiongozi, yaani a common agreed reference point. Ambayo mimi nilidhani ni Biblia. Lakini kwa kadiri tunavyoendelea, nazidi kuona tofauti, na mwisho ndio nimejiridhisha kuwa mimi na wewe hatuioni Biblia katika jicho moja, na pia nimekuona ni mtu unayedhania unaiamini Biblia, lakini hauiamini!

  Wewe kwa kauli yako na mwenendo mzima wa mijadala mingi tu, unasema Biblia ina maeno ya Mungu na ya watu na ya Shetani, pacha wako Ziragora anatamatisha version yenu hiyo kuwa halafu kuna Neno la Mungu na maneno ya Mungu!

  Mimi ninaiona Biblia kuwa, maneno yote yaliyomo humo, ni ya Mungu! Yaani ni INSPIRED, that is to say, it has been written thru that extraordinary or supernatural divine influence vouchsafed to those who wrote the Holy Scriptures, rendering their writings infallible. ALL SCRIPTURE IS GIVEN BY INSIPIRATION OF GOD, not in the sense of their being works of genius or supernatural insight, but breathed into by God in such a sense that the writers were supernaturally guided to express exactly what God intended them to express as a revelation of His mind and will. There are no errors in the Bible as it came from God. And I do not say that they contain, but that they are, the Word of God. The gift of inspiration rendered the writers the organs of God for the infallible communication of His mind and will, in the very manner and words in which it was given. Hence, The Bible is The Word of The Living God in its entirety!

  Unaona Seleli, this is where we part company! Maana unaniambia kuwa Paulo alikuwa mtu kama wewe, kwahiyo he is subject to making mistakes, something which is pathetic to me! Ndio maana kwa kufika katika uelewa huu, ni vizuri kwamba ukiisha present your case, ukaiona imefikia katika hiyo ‘deep chasm’ inayotutenganisha, we can happily end it there!! Kwa mfano, wewe kwa kuongozwa na jinsi unavyoichukulia Biblia, unaamini kwamba mt. Paulo aliposema “Simpi ruhusa mwanamke…” alikuwa ana deal na mila na desturi (sijui za kabila gani), za sehemu hiyo kama yeye binafsi na si agizo la Mungu kwa kanisa lote la dunia. Lakini mimi ninaamini kwamba hilo ni Agizo Takatifu la Mungu kwa vizazi vyote, maana Biblia yenyewe imekwisha fungwa! Matokeo yake: Wewe ukipewa mamlaka utawasimika wanawake kufundisha, na mimi sintawasimika!!!

  Hata hivyo inatujenga sana hapo tunapozipata differing views, ambazo kwazo tunapata changamoto ya kuyahakiki hayo, na mwisho kuitumia vizuri fursa yetu ya kuchagua chochote kile na kufa nacho!

  Gbu, my brother!

 53. Siyi,
  Sometimes plz try to be serious! unaongeaga mbwembwe sana mfano ati tungesoma posts za Lwembe kwa kutulia, tusingechanganyikiwa! On serious note, kitu gani Lwembe ameandika toka tuanze debate hii ambacho kiko so huge mpaka kituchanganye! Very funny indeed.

  Hii claim/cry kua kua ninaandika mengi saaana, again ni mastory tu maana nilisha rule out kua kama hutaki au u mvivu kuchapa kazi hapa au huna techniques za kusoma e.g. kaa na soma yote at per au week-ends au when at home, then kaa pembeni. Afterall, kila mmoja wetu humu, si mara moja au mbili, amesha andika mengi na marefu lakini hutanisikia hata siku moja nalia-lia humu! mi nachapa kazi tu kwa kwenda mbele, andika yoyote kwa urefu wowote, nitatwaa upako wa ‘nukta kwa nukta’ na kumaliza kazi, niko kikazi zaidi mimi humu, sina mchezo!

  Umesema kua ‘’nina pointi kiduchuuu!’’, sijui nicheke au nilie! Some humans bwana ni very interesting! Kwa iyo wewe una points nyingi mno naza nguvu kweli ktk post zako eti ee? huoni aibu rafiki? Nakuchallenge, show me your very huge and many points na nionyeshe vyangu tuchache! Kichekesho kweli umenipa!

  Kwamba, ninarudia yaleyale ya miaka ya 47 na mengine hayana pointi kabisa’’ ni kweli nitarudia yale yale inapobidi na tena kutumia maandiko yale yale pale ninapoona kuna kujidai kuto kuona hayo yaliyokwisha pita na kama hamna point kabisa unavyodai, ni lazima huthibitishe, otherwise iyo na hii ya mwaka 47 ni again, clouds efwe eme mastory ya town!

  Umesema statement yangu hii ni hojaless namely..’’Ndani ya Bibliaa, kuna maneno ya Mungu, Watu na shetani!!

  Rejea post yangu, nilitoa maandiko mengi kabisa na Nilikuuliza swali kua Yezeberi anapotamka maneno ya kutishia uhai wa Eliya, Daudi anapo regret kutenda dhambi ile , Ayubu kulaani siku alioyozaliwa, pepo kusema ni legion, shetani kusema nimetoka kuzunguka, kisha kumpiga Ayubu na majipu,Paul kusema simpi, ninatamani, nimeandika barua hii kwa mkono wangu mwenyewe, sina amri ya Bwana ila ninatoa ushauri nk, je hayo maneno na matendo ni Mungu au ni Watu na Shetani? HUKUJIBU swali hili na unajua kwa nini umekimbia moto huo! Sasa kusema tu kirahisi kua nilichosema ni hoja-less bila kuthibitisha niliyoya-raise kua ni point less kwa wewe kujibu swali langu, unakua mwepesi sana ktk kuhojiana nami Nzala Siyi, kweli kabisa na wala sikuonei na sijidai bali ni ukweli tu kua nimekuzidia mno Siyi, hu mwepesi wewe kama Lwembe, hamna vitu vingi nyinyi vya mashiko na I think you know it, sema tu mtu kuamua kufa na tai yake kwa shingo. Kumbuka kujibu, Je yale ni maneno na matendo ya nani?

  Ukasema ati nikajichanganya kusema hayo yote, hayafanyi Biblia ikose nguvu ya Kuitwa Neno la Mungu’’, Nionyeshe nimejichanganya wapi! Mimi nimesema kua Bible ni Kitabu chenye rekodi ya Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani na kwa kuwepo taarifa za Watu na devo humo hakukifanyi KUA HAKINA MANENO NA MATENDO YA MUNGU ivyo kinabaki kua kitakatifu. Aya embu sema statement yako kupinga nilichosema ili nione ulivyo smart na usivyojichanganya na kua ktk statement yako, nithibitishie kua ndani ya Bible KAMWE hakuna taarifa/rekodi ya maneno na matendo ya Watu, Mungu na Shetani! Aya jibu/state now.

  Umeniuliza kua, maneno hayo ya watu na shetani yalitoka kwa nani wakati wa kuandikwa kwa Biblia?
  Jibu:Yalitoka kwa watu na shetani na habari ya hayo/zake izo, waandishi wakaandika aidha kwakua walikuwepo na waliona na kusikia live kama Wanafunzi wa Yesu waliondika taarifa za Yesu( Injili), au walisimuliwa mambo yote toka kwa wale waliokuwepo live na kisha kufanya utafiti kuyathibitisha na hatimaye kuyaandika- Mdo.1:1-3 na Injili ya Luka.1:1-4, au walifunuliwa na Mungu( RM) kuelewa/ kufahamu/kung’amua mambo na kisha kuyaandika mfano Yohana, Paul, Petro nk au walipewa/ingiziwa Neno moyoni la kusema mfano Manabii

  Mimi nilitoa hoja kwamba kutofautiana kwa baadhi ya waandishi wa Biblia kama akina Marko, Mathayo kuhusu lile vazi, mwingine kusema lilikua la zambarau na mwenzake kusema ni jekundu kua ni fact inayoonyesha kua japo walitumiwa na MUNGU lakini walikua ni wanadamu kamili ili kuondoa notion inayojengwa na michango yenu mibovu kua kwa kuwa walitumiwa na Mungu, mna-imply kama vile walikua super humans! Ivyo nilitaka kuendelea kuthibitisha bila kuacha shaka kua role ya kibinadamu ktk Maandishi ya Bible ipo na ushahidi ni kama ule juu ya baadhi ya matendo na maneno ya Watu yameelezwa wazi humo ktk Bible na sasa hata namna walivyowakilisha baadhi ya kweli za maisha ya YESU, walitofautiana na sababu za kutofautiana ni kama vile ukweli kua walikua wanadamu si malaika, walikaa maeneo tofauti, elimu yao tofauti, uwezo binafsi tofauti, uelewa wa mambo tofauti, ufunuo tofauti, walishi vipindi tofauti nk hata bila shaka utawala wa kidini na serikali walimo ishi nitofauti na hata waliowatumia kutoka kwao kupata habari za Yesu, walikua nao na uwezo tofauti kwa kutoa taarifa alizosaka mwandishi kama Luka.

  Hiyo ndio ilikua hoja yangu ya nguvu sana, cha ajabu unaniuliza swali hili..’’unafikiri tofauti hizo zilitokana na ubinadamu wao, mila/desturi, udhaiifu wa waandishi? Hivi wewe unaelewa kweli unafanya nini humu ktk mjadala au bora liende? Kwa swali lako ilo, jihukumu mwenyewe unauonaje uwepo wako kwa ujumla wa kufahamu mambo na kueleza?uko blessed greately kweli au so skiny?

  Kisha ukasema ati Seleli, mbona unachanganyikiwa kaka kwa mambo madogo? Mimi nichanganyikiwe mimi? aya jipime nayokuletea na unayotupia tu ilimradi, yapi ni ya pori?

  Halafu kwa kujiamini kabisa bila aibu unaniuliza ati, ‘’Kwa mfano, unaelewaje unaposoma Luka 1:1-4 na 2 Petro 1?’’. Kwani mimi nilisemaje kuhusu aandiko ilo la Luka na unadhani kuna nini hapo kwa 2Petro.1 spesheli connecting to what am saying? Kichekesho kweli wewe mwanzo mwisho.

  Na hii imeniacha nacheka vibaya ati..’’ Unapenda sana kunichokoza kwa maswali ili kufungua ufahamu wako’’, Mmh! sijapata kuona watu kama wewe na Lwembe wenye confidence pori za 400%! Jesus Christ help me! Kwahiyo una maswali ya kufungua ufahamu wangu? Ha ha ha ha ha, mwe! aisee, embu niishie hapo, sina mbavu.

  Lwembez post is next.

  Press on

 54. Siyi na Lwembe( hizo 3 paraz za mwanzo ni zenu wote kisha zinafuata ya kila mmoja)

  Nilikua sijajibu posts zenu za mwisho kwa yangu maana niliona nipuuze tu kwakua ni tabu mno uelewa wenu, ni masikitiko vitu muandikavyo lakini nikasema, well, watu wengine huelewa jambo ukilisema mara mia vile vile na pia kwa njia nyingine nyingi, ndio kisa cha kutoa muda wangu kusema nanyi tena leo.Natamani mgejua jinsi gani myaandikayo yanaonyesha mlivyo weupe sana ktk ufahamu na uelewa wa Neno la Mungu na hekima ya kujua application ya Neno kwa nyakati , majira na vizazi. Nitapitia baadhi ya yale mliosema kama ifuatavyo:

  Nataka nisema kwanza mapema kabisa, kwa hakika na nguvu nyingi kua kama mtakua mna-debate tuuuu bila at last, kutumia Neno la Mungu, basi ninyi ni watu wa blaah-blaah. Nisingetegemea Lwembe kusema kua ninazunguka na maandiko! Ninaku challenge-THIBITISHA WAPI NA ANDIKO GANI, SIJATUMIA KWA HALALI, USAHIHI NA NA HEKIMA YOTE YA MUNGU. Kamwe mimi sibaki ktk mastori tu na vitu vyepesi mnavyopenda tukae umo, naweza mambo yote anyway, namely mastory ya town clouds efwe eme radio, maneno ya kufurahisha baraza hili na hadithi za abunuwasi vitu ambavyo kwa kweli mnavyo navyo ‘upako’ kweli maana mwanzo mwisho ktk mada hii na nyingine, ndio kinachodhihirika zaidi kuliko substances! Kuna nyakati chache sana mmeongea vitu serious stuff for good brain/mind/spirit to pay attention but the rest, print your own posts and kisha jisomeeni wenyewe home jioni and ask yourselves very sincerely kama kuna weight humo au atmosphere!

  Therefore, inafika wakati, tunatoka uko na kwenda level ya mwisho yaani Matumizi ya one and final truth= Neno la Mungu. Kuona ukakasi ktk hili au kutoa kauli za kupuuza utumiaji wa Neno la Mungu, si tu ni proof ya lack of seriousness ya Mtu lakini pia ni kuonyesha aina gani ya Mtu unaye-engage naye ktk mahojiano na ivyo umu-treat kwa weight ipi. Linapotumika NENO kwa uhalali-2Timo.2:15d na likiwa ndani yetu ktk hekima yote-Col.3:16, basi Neno hili hukata mashauri/maneno, huamua kesi, kutoa muongozo,huonyesha njia, huelekeza hata akili, fahamu zetu zifikieje kusema hiki ni kile na kile ni hiki kwa ivyo, NITATUMIA MAANDIKO/NENO LA MUNGU SANA KABISA NA HATA KWA KURUDIA-RUDIA YALE YALE MAANA kwa mfano Yoh.3:16 ilipotokea, mpaka leo twaitumia kila mara.

  Press on.

 55. Ndugu Siyi,

  Unaweza lalamika uwezavyo, ni kawaida. Unapokuwa ndani, utalalamika tu, lakini kama hujalipa garama hutoki. Wewe mwenyewe ukajiweka ndani kupitia uwongo wako, sasa nikufanye je rafiki yangu? Nakulilia tu wala sikuchekelee. Tengeneza naye aliyekunasa bwana…. Mimi sina ujanja wa kunasa waongo kirahisi hivi ndugu yangu. Ukiona uko huru humo ndani utabaki humo tu. Na niliongozwa na RM kukuambia kam hudaiwe kitu chochote kingine wakati ungali jela. Lakini hata mwenye kuwa jela anaweza akapeleka mashtaka yake mahala pengine hapo akiwatumia watetezi. Ndio maana nikakwambia unaweza leta ingine mjadala. Lakini kam unakimbia kifungo kwenye mjadala huu nitakukuta wewe kule utakapoenda na nita copy-paste wongo wako(jambo rahisi kabisa), bila shaka utaingizwa tena ndani. Sasa makimbilio tu ni kwa Yesu; kiri na usamehewe. Na usifikiri nitabadili huu msimamo kwani malipo si mingi kwako. Lipa Bwana….Ulipotiwa jela niliyopost ilienda directly bila kungoja “your post is waiting for moderation”. Decision inapotoka kwa RM haizuizwe hata dakika moja.

  Bwana Yesu akuokoe Ndugu yangu Siyi.

 56. Ziragora,
  Ha ha ha ha ha !!! Unacheekesha sana mwanaume wewe!! Yaani unaitisha wito ilhali hujaeleweka!!!! Ha ha ha ha!!! Wewe ni wa aina yake kwa kweli!!! Sasa kama huyo aliyesema SIMPI….alikuwa Paulo na si Bwana, mbona alimrejea Bwana-torati? Mimi nitaendelea kukukaba shingo hadi ueleze ukweli hapa kwa kweli!!! Ha ha ha ha!! Maana nimeona unaleta utani kaka.
  Mimi siko jela, ndiyo maana niko huru kiasi hiki. Siongozwi na mafundisho ya kanisa wala policies za dunia. Naongozwa na mafundisho ya BIBLIA tu. Naamini katika Biblia pekee ndimo mna uzima maana ndimo ninamomkuta Kristo. Kama Biblia inanihimiza kusali jmosi kama siku ya saba-sabato- ibada kwa Mungu, nitafanya hivyo, maana huo ndio uhuru nilio nao.
  Ziragora, ukiwaonea aibu walimwengu, watakupeleka jehanamu kabisa. Shika NENO la MUNGU ili upone rafiki. Tofauti na hapo, utakomea kupiga zeze hapa SG, waimbaji ni wengine!!
  Ubarikiwe

 57. Ndugu yangu Lwembe,

  Nakupenda sana na wala sitaki upotee. Sasa naona ukiendeleacheka baada ya kuwa umejifunga wewe pekee mikono na miguu.
  Kiri wazi udhaifu yako ndani ya mjadala huu, ufunguliwe, RM akuangazie. Na wakati utakapomaliza kiri, Neno la Mungu litafika kwa uwingi ndani yako. RM atakapotaka anitumie kwa ajili ya kukuelimisha zaidi juu ya Neno la Mungu na Maneno ya Mungu, hapo ukiisha mrudilia, nitakuwa tayari kwa kukuletea maelezo yake ktk mjadala mwengine ambao utaweka ukiomba msaada.

  Bwana Yesu akubariki.

 58. Ndugu yangu Siyi,

  Kusemasha ukweli ni kwamba huna pa kukimbilia. Uko jela, hapo ukiishajinasisha wewe pekee kwa uwongo kadhaa ambao nimekuonyesha ktk hoja zangu zilizopita. Sasa wewe unataka urudi nyuma kwenye “SIMPI”. Ukiwa jela, uko. Unatakiwa lipa garama fulani. Si nyingi, ni kuamini Neno la Mungu jinsi lilivyo na kuacha tafsiri mbovu za wanaadamu. Maneno kam “SMPI”, “NI MIMI WALA SI BWANA”, “ASEMA BWNA” tumekwisha yajadili yakutosha. Kam hujarudilia ukweli wa Neno la Mungu, hutoki jela. Wakati ungali humo, hudaiwe mengine. Acha leta ingine hila ya sabato na juma pili, nk. Ukiwa umenaswa basi…. Najua utalalamika, lakini jela hutoki bila kulipa hiyo garama. Kumbuka: RM hazihakiwi. Wewe huone jinsi kwa siku chache umenasika kirahisi, unawaza ni nguvu zangu? Ni nguvu za RM. Halelua!!!
  Maneno ya Mungu na Neno la Mungu si jambo jipya. Biblia inaongea wazi. Ukipenda ufahamu leta mjadala ukiuliza msaada. Nasema:”Sitahamisha mjadala katika mjadala mwengine”. Inabidi ukiri kam kwa nguvu za RM umeelewa udhaifu yako katika mjadala huu, kiisha uombe msaada hapo ukianzisha mjadala mwengine.

  Asante ndugu yangu na RM akuwezeshe.

 59. Ziragora,
  Ha ha ha ha ha! Unaniambia, “…fanya hima ukengeuke, unabaki na hatua kidogo tu.”!!! Sawa kaka, lakini hebu niambie kwanza hiyo “siri ingine” unayonidokeza kwamba: “kuna tofauti kati ya NENO LA MUNGU na MANENO ya MUNGU.” Nipe hiyo siri ndg yangu!

  Ubarikiwe!

 60. Ziragora,
  HA ha ha ha, Kwimbilagulu, kumala amimbo!!! Ngoja nikuachie RM anene na wewe!! Maana umekuwa ukimsingizia RM kuwa anakuongoza kumbe unajitetea ufuate mitizamo na falsafa zako mwenyewe. Na ndivyo walivyo watu wengi leo. Wanajidai kusema RM ameionesha/ameniongoza kusema hivi…. kumbe watu hao wanatekeleza hisia, na mitazamo yao binafsi!!
  Nakuhurumia maana umeng’ang’ana na neno la Paulo SIMPI… Sasa ukiangalia katika vitabu vyote 14 vya Paulo, utakuta ametumia neno SIMPI…? Ukiangalia taratibu zote za kupata viongozi ktk makanisa ya Paulo, je alitumia neno SIMPI? Na hata kwenye kauli hiyo ya SIMPI, hebu angalia Sababu ya Paulo baada ya neno lake SIMPI…1Timothy 2:12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

  Angalia sababu ya Paulo ya kutompa mwanake ruhusa ya kufundisha…
  Sababu ya Kwanza:
  13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
  Sababu ya Pili:
  14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
  Sasa kama kweli unaongozwa na RM, unafikiri kauli hizi za Paulo zinatofautiana na zile za Mungu katika Mwanzo 3? Na kama ni desturi, je, desturi za Mungu na za Paulo zinatofautiana hapa? Sikia, nimekupa aya za Biblia lukuki ya namna hii toka agano la kale hadi jipya. But unaonekana kutoelewa!!
  Anyway, rafiki, Binafsi, siwezi kukulazimisha uisikie sauti ya Mungu ktk hili. Kazi yangu mimi ni kusema tu ile kweli. Halafu uchaguzi unabaki ni wa kwako mwenyewe.
  Na mimi nakuona unaisoma Biblia kama gazeti, ndio maana unapata NENO LA MUNGU na MANENO YA MUNGU ndani ya kitabu kimoja chenye vitabu 66!!! Kama siyo kuchanganyikwa ni nini rafiki? Bwana atusaidie sote ndg yangu. Sabato njema, maana lleo ni sabato. Hata kama unasali j2, inabidi ubadili mwelekeo wa kulifuata neno la Mungu na siyo maneno ya Mungu.
  Ubarikiwe mno

 61. Ndugu yangu Siyi,

  Bwana Yesu apewe sifa !

  Na wewe nikutayarishe nikupe jibu fupi.
  -Umekwishaona mtu anayedai deni bila kulifafanua? Kwa nini uchochee wongo?
  Ni jambo rahisi kufanya: Inaomba tu ku copy-paste deni lako nami nina copy-paste malipo. Kwa nini kuzoea ubishi tu pasipo mwisho?
  -Mimi simtegemee mwanadamu yeyote, na kama kuna hata chembechembe ya tamko langu inayohusu ile hoja yako uyi copy-paste katika jibu lako. Au ulichanganywa na masemi ya Ndugu yangu Lwembe kwa post yake ya 06/09/2013 kiisha ukaniandikia pasipo kuchunguza!!!
  Unaona jinsi unajiweka hadharani wewe pekee kirahisi tu?
  -Niliyeongelea alikuwepo nyuma ya Adamu, unaelewa? Ni Debora; utasema Mungu alipungukiwa? Lakini sikuone ukitembea mpaka pale. Umejidanganya tu kidogo, naamini utarekebisha. Na katika hoja hako ulisema Mwanamke atakuwa mtawala kanisani na mahala ingine kam Mungu atasema. Sasa anapotaka sema anakuomba shauri ? Basi piga magoti, uombe Mungu, naye atajitetea mahala ambapo unadhani mwanamke amewekwa kuwa kiongozi pasipo Mungu kutaka. Sasa Ndugu yangu, wewe unadhani kama Mungu alimaliza tayari kuongea na watu ? Utawala wote unapewa na Mungu. Usimtilie Mungu mipaka bwana….
  -Unajifanya professor ya ile unayoita « Fundamental Rules for Interpreting Scripture”. Je ile ndiyo imekuchanganya ukasahau ukweli? Rudilia aliekufunza akuelimishe zaidi. Wewe umesema unategemea Biblia lakini method ya kuisoma naona huitoshe kwa RM mwenyewe. Kwani hili neno” Fundamental Rules for Interpreting Scripture » hutaliona ndani ya Bible.

  Na RM akuwezeshe.

 62. Ndugu Lwembe,

  Bwana Yesu asifiwe sana !

  Ndugu yangu nashukuru sana kuona jinsi RM aneendelea kukutembelea. Yeyote aliyekusoma huko mwanzoni atawaza ni mwengine Lwembe. Haleluya!!!

  Nimekutayarisha kama nitakuwa mfupi kwa majibu. Inayobaki ni jambo ndogo tu, “KUTOFAUTISHA WONGO NA KWELI”. Mambo mengine, utazungukazunguka bila kujuwa uwanja uko wapi wala kujua unacheza mchezo gani.

  Nikakuongoza vema, lakini ukajifanya tu kipofu ndugu yangu. Nilikuomba uulize Paulo, unapuzi tu… Yeye ni mkweli wewe unamfanya mwongo, hapo ukidhani unamtetea!!!!

  Yesu, unayo kazi kufanya hapa tena, BWANA !!!

  Mpendwa, unawaza unampita yeye Paulo akili, ili umkosoe? “Yeye nasema, « ni mimi wala si Bwana”, wewe unasema “ni Bwana” !!! Hivi mpaka hapo hujaelewa kama unajiangusha wewe pekee ndani ya mtego? Sasa ukinaswa utaanzasema “Eh!! Mim Lwembe, Shetani ameniangusha.” Huone hatari kweli rafiki yangu Lwembe? Usininganiye pale ndugu yangu, fanya hima ukengeuke, unabaki na hatua kidogo tu. Nikuambie siri ingine: “kuna tofauti kati ya NENO LA MUNGU na MANENO ya MUNGU ».

  RM akusaidie.

 63. Ziragora,
  Ubarikiwe kwa kunirudia rafiki. Nami leo sitaki kuchelewesha mambo. Naenda moja kwa moja kwenye hoja zako.
  Kwanza, umedai huna deni ya majibu ya maswali yangu. Mimi naona kama unayo japo waikwepa. Mimi naona mara nyingine si lazima kujibu kila kitu. Hata hayo uliyoyajibu, yanatosha. Maana nimeyapitia yote na kuyapima kwa viwango vya Kibiblia na kuona kuwa mengi unayalazimisha yakubaliane na uhalisia wa maisha ya sasa ndani ya kanisa na nje ya kanisa pia. Ni hatari mno kama utaendelea kufanya hivyo rafiki.
  Pili, Nashukuru kama umekubaliana na Biblia kwa masuala ya utawala kama ilivyokuwa kwa akina Adamu na Hawa. Ubarikiwe maana umekiri kuwa, utawala ni kwa mwanaume na si vinginevyo japo huko mbele umejichanganya tena. Twende taratibu tukieleweshana tu. Mfumo wa Mungu kujipatia viongozi wa kiume tangu mwanzo, aliuweka YEYE. Tangua mwanzo, hakuna hata aya moja ndani ya Biblia inayosema kuwa mamlaka au urithi wa Baba ulipelekwa kwa mwanamke. Hadi kipindi cha Israel, wananume ndiyo waliokuwa warithi wa mamlaka pamoja na mali/rasilimali, isipokuwa kwa wanaume ambao hawakuwa na watoto wa kiume, Hesabu 27:6-11.
  Katika utawala, Mungu aliweka wanaume. Katika mamlaka ndani ya kanisa, Mungu aliweka wanaume. Makuhani wote walikuwa waanaume. Umesema kuwa natafsiri sana maandiko. Leo ngoja nikupatie na wewe aya hizo usome..
  Walawi 21: Pitia baadhiya sifa za Makuhani- Wanaume tu!! Zingatia; Biblia inapotumia neno WANA it means SONS!!
  1 Kisha Bwana akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake;
  2 isipokuwa ni kwa ajili ya jamaa yake wa karibu, kwa ajili ya mama yake, na kwa ajili baba yake, na kwa ajili ya mwanawe, na kwa ajili ya binti yake, na kwa ajili ya nduguye mwanamume;
  3 na kwa ajili ya umbu lake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo.
  4 Asijitie unajisi, ijapokuwa ni mkubwa katika watu wake, hata akajinajisi.
  5 Wasijifanyie upaa kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao.
  6 Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za Bwana kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.
  7 WASIMWOE mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake.
  8 Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi Bwana niwatakasaye ninyi ni mtakatifu.
  9 Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa moto.
  10 Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;
  11 wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;
  12 wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi Bwana.
  13 NAYE ATAMWOA MWANAMKE katika ubikira wake.
  14 ASITWAE MJANE, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.
  15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.
  16 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
  17 Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
  18 Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,
  19 au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,
  20 au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;
  21 mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za Bwana kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
  22 Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.
  23 Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye.
  24 Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.

  Sifa zingine za viongozi wenye mamlaka ndani ya Biblia
  Mdo 6:1-6,
  1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung’uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
  2 Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani.
  3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;
  4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.
  5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;
  6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.

  Sasa umeona kuna wanawake hapo??

  Daktari Luka alifahamu kuwa uongozi ulikuwa ni kwa wanaume tu Mdo 13:1-3,
  1 Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli.
  2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
  3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

  Mdo 14:23,
  23 Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini
  1Timoth 3:1-12
  1 NI NENO LA KUAMINIWA; MTU AKITAKA KAZI YA ASKOFU,
  2 BASI IMEMPASA ASKOFU AWE MTU ASIYELAUMIKA, MUME WA MKE MMOJA, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
  3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
  4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
  5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
  6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
  7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
  8 Vivyo hivyo mashemasi
  9 wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.
  10 Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.
  11 Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
  12 Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
  na Tito 1:5-9 )
  5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
  6 ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.
  7 Maana imempasa askofu
  8 bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;
  9 akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.

  Sasa Ziragora, baada ya kusoma aya hizo zote, umeona kuna mwanamke anazungumziwaa hapo kuwa naye alipaswa kuwa kiongozi? Jibu ni hakuna. Ndiyo maana nilikwambia kuwa, Mungu alikuwa na makusudi maalumu kufanya hivyo. Ilipobidi Mungu kusimamisha wanawake, ALITAMKA KWA KINYWA CHAKE. HE POINTED THEM. Na bado Mungu hata leo akitaka kusimamisha mwanamke, anaweza kufanya hivyo but, ni sharti apatikane mwanamke huyo kwa kinywa cha Bwana. Vinginenvyo, tunajustfy dhambi!!

  Tatu, KUPUZI UJUMBE WA WAMAMA: Naona napo umekataa majibu yangu eti nimetafsiri sana Biblia. Nina wasiwasi na kanuni uzitumiazo wakati wa kujifunza neno. Napendekeza utumie kanuni hizi ili uwe unaielewa Biblia unapoisoma na siyo kuchukua kiaya kimoja na kukidefine visivyo. Kanuni bora za usomaji wa Biblia;
  Fundamental Rules for Interpreting Scripture
  1. Pray before you start reading your Bible.
  2. Since Jesus spoke and the Bible writers wrote primarily for the people of their day, always consider the historical, geographical, and cultural setting of the passage you are studying.
  3. Always consider the context of the unit, chapter, and book when interpreting a text. The meaning of each verse must agree with the theme of the unit, chapter, and book, as well as the overall teaching of the Bible.
  4. When interpreting a passage or verse, make sure to study each sentence grammatically to get the correct meaning. Pay special attention to the verbs as they deal with actions.
  5. Make sure to get the meaning of each text as intended by the Bible writer or inspired speaker before making application. This is called bridge-building and is important in giving Bible studies.
  6. Difficult texts must be interpreted in the light of the clear teachings of the whole Bible. Therefore, study all that Scripture teaches on a given subject before coming to a conclusion on any single verse.
  7. The New Testament must be interpreted in the light of the Old Testament and vice versa. The Old Testament is promise and the New Testament is fulfillment. Both complement each other.
  8. For accuracy, use the best translations and, if at all possible, compare with the original text.
  Sasa, nilichokifanya kwenye hoja yako ya wanafunzi wa Yesu kupuuza maneno eti kwa vile yaliletwa na wanawake, ni hicho hapo. Sijatafsiri Biblia kwa mawazo yangu tu. Bali nilifuata kanuni hizi. Sasa sijui wewe unapong’ang’ana kuwa lilikuwa ni suala la stereotyping, umetumia kanuni gani?
  Nne, AMTEGEMEAYE MWANAADAMU ALAANIWE,
  Kimsingi, mimi sifuati mafundihso ya wachungaji, wazee wala mitume mamboleo. Nafuata mafundisho ya biblia tu.
  Kuhusu aya hizi za akujadiliana, jaribu kwanza kuziapply hizo fundamentals kwenye aya hizi ili uone kama hutazielewa bado. Ukishindwa kuzielewa, utazileta tena tuziangalie kwa pamoja. Hatuwezi kuchoka kwa kazi ya Bwana. Warumi 1:16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

  Bwana akubariki pia. Karibu kwa mara niyngine rafiki

 64. Ndg Ziragora,
  Asante kwa mawaidha!
  Unaniambia kuwa nawe unawaamini mitume, lakini maelezo yako yanaonesha tofauti kidogo, lakini ninaamini, utalifikia jambo hilo lililo jema!

  Pia ninakuona umekwama katika uelewa. Nimekuambia hivi hayo unayosema, “”“asema Bwana”, that’s clear.”” Ni mitume ndio waliokuambia kuwa “Asema Bwana” hiyo unayoiona clear! Kwahiyo mambo yote unayoyasoma katika Biblia, yanatoka katika vinywa vya hao mitume na manabii, pamoja na hayo unayodhani Kristo ameyanena moja kwa moja kwenye Biblia yako, yoote ni mitume ndio wanaokuambia kuwa “Yesu akasema”!!! Kama unajiona unamwamini sana Yesu na unamfuata, basi jua kuwa mitume wamefanya kazi vizuri sana, wamekuhadithia habari za Kristo mpaka umejiona ni “Bibi Arusi” wake kwa neno lao na si kwa neno la Kristo!!

  Jambo jingine nimekuambia kwamba mambo yote unayoyaona kama hayo ambayo Paulo anayokuambia “Hapa ni mimi, wala si Bwana” hayo ndiyo yanayo litimiza lile Neno waliloambiwa, Mt 18:18 “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Basi kama unayo macho, ndiyo hayo yaliyo wazi kabisa kwamba Mungu mbinguni ameyapitisha. Kama ni jambo la HIARI basi Mungu amelipitisha hivyo, litimizwe katika Hiari na si katika Sharti kama hilo la kuoa wanavyolitimiza Katoliki. Wala uongo wao hauibadili kweli ya Mungu, labda wewe mwenyewe uwe umejifikisha katika kuuamini uongo kama ninavyokuona unavyoupigia debe uongo wa Wakatoliki kuhusu jambo hilo, lakini Mungu amekwisha sema hayo ni mafundisho ya mashetani, basi unayo hiari ya kumuamini Mungu au kuwaamini Wakatoliki!

  Paulo anasema “Nifuateni mimi kama ninavyomfuata Kristo”, maana yake TUMFUATE yeye Paulo ndiyo TUTAMFIKIA KRISTO! kama amekuambia “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha” usiseme ati huyo ni Paulo kama yeye tu; utakuwa hujauelewa Mpangilio wa Injili, MFUATE yeye, usimruhusu mwanamke kufundisha kanisani, Mungu atakutupa huko nje kwa kumkaidi mtumishi wake mwaminifu! Wala usijaribu kumuingizia mawazo, eti alikuwa anazungumzia mila za Kiyahudi, huo ni uongo, umelipata wapi wewe neno hilo la mila za Wayahudi? Torati ya Mungu leo mnataka kuiondoa nguvu yake na kuifanya ni upagani?

  Hata hiyo 1Kor 7:10-12, sijui kinachokuhangaisha kuhusu hayo wanayofundishwa Kanisa ni nini, mbona kila kitu kiko wazi tu. Unaposema kuwa hilo ni neno la Paulo tu, ili iwe nini? Kwamba halina thawabu ukilitimiza? Au jambo hili analolifundisha Paulo, “ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache”, wewe kwa ile kanuni Yenu, ndio unatufundisha kwamba huyo ndugu aliye na mke wa jinsi hiyo, hata akimuacha si dhambi? Sema sawasawa unachofundisha ni nini, Ziragora??

  Kuhusu yule mwanamke mzinzi, niliyokueleza yanajitosheleza sana, kama utakuwa si mtu wa kupenda kupenyeza mawazo yako na kuwaongoza watu kulitilia shaka Neno la Mungu. Labda nikuuulize, hivi, wewe unafikiri kuwa unajua kuliko Kristo? katika tukio hilo Kristo alikuwepo, unafikiri alisahau kuwauliza wale washitaki wa yule mwanamke yu wapi mwanaume mliyemkamata naye? Au uliposoma ile Kum 22:22, je, umeliona humo sharti la adhabu kutolewa kuwa ni LAZIMA wote wawili waletwe? Bwana Torati ndio huyo hapo, pokea uliyopewa ndg yangu, usipende kuingiza ingiza vitu visivyokuwepo, mwisho mtapewa roho ya kuyaamini hayo mnayojipachikia, sijui mila, mara desturi, mara mwanamke alikuwa anakandamizwa; jamani ninyi mnamjua mwanamke kuliko huyo aliyemuumba, Mungu anamkandamiza mwanamke? Hivi hamnaga uoga enhe??

  Unatuambia, “”Lakini ya muhimu ni kwamba ingelikuwa torati ina nguvu kiwango iheshimike siku zote, huyu mwanamke hangeliponyoka hawa wanaume. Ndio maana imeandikwa”sisi hatupo tena chini ya laana ya sheria”.””
  Bali Ziragora utakuwa hujaelewa kilichotokea. Hao wote waliomleta yule mwanamke walistahili kupigwa mawe mpaka wafe kwa makosa yao! NGUVU ya Neno lililotoka katika kinywa cha Kristo hapo alipowaambia kuwa asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha mawe, iliwakamata wote wakajiona “utupu” mbele zake, huyo Neno, wakaondoka kwa aibu! Ebr 4:12-13 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, … hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”
  Umeelewa ndg yangu? Torati ina nguvu sana ndio maana ilipoletwa katika ukamilifu wake wale wanaume walikimbia! Usije ukaanza kufundisha tofauti, maana ndio kazi yenu, mkaanza kusameheana katika uzinzi, ukiulizwa, oh “”sisi hatupo tena chini ya laana ya sheria”, MMEKUFA!!

  Hiyo hali anayoizungumzia Paulo katika hiyo Rum 7, ni kweli huo mvutano upo, basi unapokutana na mvutano wa jinsihiyo, yule “mtu wa ndani”, huyo aliyezaliwa kwa Roho, huyo chakula chake ni Neno lote,”Bibi Arusi”, msikilize huyo zaidi, maana jambo hili limekwisha kuwekwa wazi kwako mapema ili uyajue hayo, yasikukamate kama mtu aliye usingizini! Huyo mtu wa ndani ndiye pekee awezaye kukuondoa katika mvutano huo maana nguvu yake yatokana na Mungu. Usije ukayachukua hayo anayokuonesha Paulo, ukayatengenezea kisingizio cha kujiaminisha mambo ya mwilini, utayarudia ya mwilini, utamuona Paulo katika udhaifu na kuamini kuwa alikuwa na udhaifu lakini ukitakiwa uuonesha udhaifu huo, hutaweza, hiyo nayo ni kesi nyingine! Bali muache yule mtu wa ndani akuongoze, Biblia yako itakuwa mpya, utaupata wepesi wa kuyainukia mambo ya Mungu kilaini saaana! Paulo akikuambia “NATAKA MJUE” unapokea hilo analotaka ujue, huanzishi mambo yenu yale, eti ‘oh ana shauri tu, si Amri ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu’, mbona Amri ya Nne hamuitimizi, si mnapenda Amri ninyi baada ya upendo kuwashinda!

  Ziragora ndg yangu, asante sana, nikushukuru kwa ushirikiano, na kama kuna jambo linalohitaji ufafanuzi zaidi, ni furaha yangu kulitimiza hilo,

  Ubarikiwe!

 65. Ndugu yangu Siyi,

  Nashukuru kwa kuniandikia, na Mungu akubariki. Ni vizuri sana kujadili Neno la Mungu. Ninachoona sana ktk mijadala kam hii, ni vigumu kuona inaisha watu wakikubali ukweli. Lakini Mijadala ina aina mbalimbali. Kuna yenye inaisha pasipo conclusion na ingine, zaidi ile ya kuomba shauri, inaisha vizuri kuliko. Lakini yote inasaidia watu hata wao pasipo kukiri. Ndugu Siyi ulikuwa tayari umekubali mambo mawili: vazi na waandishi. Lakini naona jambo la waandishi tena linazuka.
  Nitapima kukujibu:

  1)SINA DENI YAKO YA MAJIBU. Labda haukusoma vizuri au ulitarajia nikujibu namna unavyopenda. Na kam una haja ya elimu zaidi, leta suala yako.
  2)MAMBO YA ADAMU NA HAWA/KUKANDAMIZWA KWA MWANAMKE/UTAWALA WA MWANAUME/KUTAMANI MWANAMKE:
  Juu ya Adamu na Hawa sina maelezo mengine, Biblia pekee inasema. Unataka mim niseme pahali pa Biblia kam wewe unayo desturi? Au kam hujue na unataka ufahamu zaidi ya Biblia kwa nini huulize RM? Hata wewe nakuona ukisema “Biblia haiseme” wakati unapoongea juu ya mwanamke kuletwa auwawe yeye pekee pasipo aliyehusika naye dhambi. Kwa nini haukujibu na uhakika? Ni kwani Biblia haikujibu, full stop.
  Kam unakubali kam Debora alipewa utawala na Mungu, kwa nini asiwape wengine? Unasema Ni Mungu pekee aliyempa bali yaikutoka ktk uchaguzi wa wanadamu. Unamaanisha ku ngambo ya wanaume, ndipo mtu anajipatia yeye pekee madaraka kanisani, ao kuchaguliwa? Tangu mbele ni Mungu mhusika kwa kuchagua ni nani atakaemtumikia. Iwe wazi, kam ni Mwanamke atainuliwa, kama ni mwanaume sawa. Mungu wetu ni Yule Yule jana, leo na hata milele. Hakuna hata siku moja ataitika mtu a mu dictate eti chagua mwanaume na umuwache mwanamke. Kam atawafanya wanaume wawe wengi, haya! Kama atawafanya wanawake wawe wengi, haya!

  Lile neno la Yesu kuhusu tama ya mwanaume kwa mwanamuke lilingana na moja kati ya zile amri kumi za Mungu. Na alipenda aonyeshe kam dhambi si kitenda tu kam jinsi torati iliazibu lakini hata kuwaza, kupanga, … vibaya yote ni dhambi. Lakini ndugu, naona kam una nia ya kuongeza kidogo kwa ile Yesu alisema, nawaza ungeliizusha nafasi nyingine labda. Kwa nini unataka uwe wa kiroho kuliko Yesu? Akisema, usiongeze.

  3) KUPUZI UJUMBE WA WAMAMA:
  Ile unayoleta ni tafsiri yako tu. Ndugu yangu, kuwa na mashaka na kupuzi si neno moja. Imeandikwa kama wale mitume “walipuzi”. Si tena pengine unasema tuheshimu maneno ya Biblia? Sasa kwa nini kila ujapo, ni tafsiri tu ? Unataka fundisha watu kam hakuna neno kamilifu ndani ya Biblia kam Ndugu Siyi hajatafsiri? Biblia ni neno la Mungu ; lina uhakika kuliko maneno yako yote.

  4) KAMA MIMI BINAFSI NILIWAI ONA NDANI YA BIBLIA WANAWAKE WENGINE KAM HILDA, MIRIAMU NK, MUNGU AKIWACHAGUA KUWA WACHUNGAJI, ASKOFU, …. KANISANI:
  Ktk agano jipya, Biblia inatuelezea tu mambo yaliyofanyika mda kitambo, just wakati mitume walipokuwa hai. Haiseme kama Mungu hawezi tena kuleta mwanamke kama Debora. Sasa hapa nikitia akili zangu, sitafahamu. Ukweli unabaki pale pale : Mungu akipenda atamuweka kwani angeliapa kutoweka mwanamke atawale wanaume, isingeliwezekana atiye Debora kutawala Israeli yote. Jambo muhimu ni kwamba tutawatambua kwa matendo. Atakapokuwa mwanamke, kama matendo yake hayafae utawala wake utavunjika, mwanaume hali kadhalika. Nafikiri ndugu yangu, uwe na bidii, katika kuyatazama yaliyo kweli : « Kwa upande wangu, nikisoma Biblia naona kam Mungu aliweka wanawake wachache sana. Ninaona hata leo, si ndani ya kanisa tu, bali ktk domains zingine, naona tu watawala wanawake ni wachache licha yu kuwa wengi kwa idadi ktk dunia. Ile tu inaweza nisukuma kusema kam watabaki wachache(Kwani Mungu habadiliki). Lakini hii ni kwa maoni yangu, Mungu akiwa na Siri yote. »
  5) HAWA WANAWAKE WA CHEO :
  Ni kweli tafsiri zote si sawa. Nazo tena ni watu wanazifanya kufwatana na lugha mbalimbali. Na unaelewa jinsi ni nyingi kabisa. Lakini jambo la kuzingatia ni ile neno « CHEO ». Na ile ndio nilisisitiza sana nikisema, Mungu anainua anaetaka kuinua. Ina maana nimeona Mungu anampa « CHEO » anaemtaka. Ile conclusion niliitia kwani niliona fasi nyingine tafsiri zinachanganya kidogo, lakini pale kwenye cheo kunabaki. Na umbalimbali ya pale sina ruhusa ya kuongeza.

  6) PAULO/RM
  Ona, nimesema ile tangu mbele kam kuwa na RM yaimfanye mtu kulingana na Mungu. Mtu anayo udhaifu tu pamoja na kuwa na RM. Ndio maana kila mara inatubidi kuomba. RM yeye anatuombea lakini haombe kwa ajili yake mwenyewe. Mtu anabadilika, lakini RM sivyo. Ile shairi mbili ziko tofauti. Utofauti wake si udhaifu wa Mungu, ni wa Paulo kam mwanaadamu, tena nampenda sana kwani yajawai ficha udhaifu wake, wa mwili au wa roho. Ni hii ukweli yake ya kutoficha ndio inamfanya awe miongoni mwa waandishi wa Biblia. Kuwa mkweli ndiyo ya maana. Kwani « mtajua kweli, na kweli itawaweka huru ». Haleluya !!!
  7) AMTEGEMEAYE MWANAADAMU ALAANIWE :
  Hapa unanishangaza kabisa labda kwa mara ya kwanza ukinifundisha hii shairi ya YEREMIA 17 :5 ambayo nilikutolea hapa sasa 09/09/2013 tena nikikuandikia wewe nikikuomba kutotegemea walimu, wachungaji, maaskofu, na hata mitume kwani wote ni wanaadamu.Tena ndipo unajibu kwayo. Labda hukusoma na ndio maana unaendelea kudai majibu fulani ambayo umekwishapata. Msimamo wangu uko pale, tena kwa mkazo. Labda kam umepunguza kuwategemea, basi Bwana apewe sifa.

  8) Kwa mwisho, ndugu yangu, tuchangiye shairi hizi :
  “1 Wakorintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; WALA HAPO SI MIMI, ILA BWANA; mke asiachane na mumewe;
  1 Wakorintho 7:12 Lakini watu WENGINE NAWAAMBIA MIMI, WALA SI BWANA, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.”

  “Warumi 7 :
  15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
  16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
  17 Basi sasa si mimi NAFSI YANGU ninayetenda hilo, bali ni ile DHAMBI IKAAYO NDANI YANGU
  18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya MWILI wangu, HALIKAI NENO JEMA; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
  19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
  20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, SI MIMI NAFSI YANGU NILITENDAYE, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
  21 BASI NIMEONA SHERIA HII, YA KUWA KWANGU MIMI NITAKAYE KUTENDA LILILO JEMA, LIPO LILILO BAYA.
  22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
  23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, INAPIGA VITA NA ILE SHERIA YA AKILI ZANGU, na kunifanya mateka ya ile SHERIA YA DHAMBI ILIYO KATIKA VIUNGO VYANGU.”

  Mungu akubariki, na karibu tena mara nyingine.

 66. Ndugu yangu Lwembe,

  Bwana Yesu asifiwe sana!
  Nashukuru sana kuona unaniandikia. Ni neema kubwa kuona wapendwa wanajadili kwa wema. Tutakapokutana mjini moja , nitafurahi sana kukuona macho kwa macho.

  Nashukuru tena Mungu anaeufikisha hapa tulipo. Naamini RM ataendelea kutenda kazi yake.

  Kawaida hatushiriki mijadala kwa kucheza. Mjadala ni mojawapo wa watu kuonana hata mmoja akiwa mbali ya mwengine, haswa kuzungumza Neno la Mungu. It’s nice. Nilitaka kukujibu kwa fungo moja tu, lakini kwani hatukubaliana kwanza, naona ni vema niwe wazi zaidi. Ina maana univumilie basi niwe mrefu kidogo kwa majibu, na baadaye usiseme kuna yale ambayo sikujibu wakati ningelikuwa nimeyaweka kwenye fungo moja. Ina maana nakuomba kutokwazika ninaporudilia bila kutaka ambayo uliwai sikia siku nyingine:

  1)Asante kunihurumia nisijikatekate kama waislamu. Asante tena kuandika very cleary. Ndio maana nakupendaga…..

  2)Paulo/Petro/Waandishi wengine wa Biblia:
  -Mim ninawaamini 100% nawe unadai hiyo hiyo tu. Now where is the difference? “KILA MMOJA ANADHANI NI YEYE ANEYEAMINI HAWA WAANDISHI VIZURI KULIKO MWENGINE”.

  Mtu akiwa ndani ya Yesu haogopi sema ukweli. Sikiliza sasa niseme:

  -Mim kwa upande wangu naona kuamini mitume(na wala siseme kuwategemea) ni kuhakikisha waliyosema namna ipasavyo. Hawahitaji ushabik. Wanaposema “asema Bwana”, that’s clear. Lakini wanaposema “ingelikuwa heri, siwashurtishe, ni mimi wala si Bwana, …”, unapowaamini inatakiwa usigeuze maandiko yao, usiwatese Bwana….
  -“Nadhani, kam mtu” kwa upande wako unadai kam yale yote waliyoyasema , licha ya kuangazia wasomaji ili wasiyalinganishe na yale Mungu aliesema, ni bila shaka maneno ya Mungu. Hapo naona umewasemea wongo. Soma tena hapa na uone jinsi Paulo anachapa kazi sawasawa bila kujihusisha na majivuno:
  “1 Wakorintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; WALA HAPO SI MIMI, ILA BWANA; mke asiachane na mumewe;
  1 Wakorintho 7:12 Lakini watu WENGINE NAWAAMBIA MIMI, WALA SI BWANA, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.”
  Unafia nini na Paulo? mim namuona akiwa mkweli kabisa. Na hii ukweli kamilifu ndio ikafanya aandike ndani ya kitabu kitakatifu. Mahala anaposema “Wala si Bwana”, ukitia, “ni Bwana” unafikiri kile unachopata ni Biblia tena?
  3)Kwa ngambo ya wakayoliki, usiwasemee kwani wanapoulizwa wanadai wanaiga Mtume. Ukiwatazama utaona wana tatizo kam lako kwani moja kwa moja walidaka ile mtume aliyosema kam amri ya Mungu. Aliposema ni heri kuwa kam yeye, wakadaka kam Mungu alisema vile:”Ni Heri kutoowa”. Sasa wanataka wawe heri.
  4)Yule Mwanamke……
  Ni kweli WOTE WAWILI iliwapasa wafe kufwatana na torati(Kumbukumbu la Torati 22:22). Lakini wale wanaume hawakufanya vile. Biblia haikusema kama wakipata mmoja warizike na kuuwa ule. Wanaohusika ni wanani? Si wanaume? Lakini ya muhimu ni kwamba ingelikuwa torati ina nguvu kiwango iheshimike siku zote, huyu mwanamke hangeliponyoka hawa wanaume. Ndio maana imeandikwa”sisi hatupo tena chini ya laana ya sheria”.
  5) Bibi Arusi:
  Wewe unaleta huzuni. Ni vile tu, unapojitahidi kwa nguvu zako mwenyewe bila kuongozwa na RM utajinasisha kirahisi wewe mwenyewe. Kabla ya kusema hatuna akili katika post yako ya 07/09/2013 wakati niliposema kanisa ya Mungu inaitwa Bibi Arusi, na Ndugu Seleli kutonipinga, unarudi tena na rejea tofauti.
  Mpendwa, elewa kama tuna miili, nafsi na roho. Lakini Biblia inatuelewesha kam damu(nafsi) na nyama(mwili) hazirithi ufalme wa mbingu. Ndio maana Mungu ana haja ya roho. Lakini hii roho inapigana na nafsi na mwili. Tunavyo vyote. Basi uliza Paulo bwana, atakuelezea:
  “Warumi 7 :
  15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
  16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.
  17 Basi sasa si mimi NAFSI YANGU ninayetenda hilo, bali ni ile DHAMBI IKAAYO NDANI YANGU
  18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya MWILI wangu, HALIKAI NENO JEMA; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
  19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
  20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, SI MIMI NAFSI YANGU NILITENDAYE, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
  21 BASI NIMEONA SHERIA HII, YA KUWA KWANGU MIMI NITAKAYE KUTENDA LILILO JEMA, LIPO LILILO BAYA.
  22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani,
  23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, INAPIGA VITA NA ILE SHERIA YA AKILI ZANGU, na kunifanya mateka ya ile SHERIA YA DHAMBI ILIYO KATIKA VIUNGO VYANGU.”

  Nimalizie pale.

  Na Mungu akubariki.

 67. Ziragora,
  Imenibidi nirudi rafiki kwa ajili ya kukidhi haja ya moyo wako baada ya kutoridhika na maelelzo yangu ya kwenye link niliyokupa kwa kudai kuwa hukuielewa vizuri na hivyo kuonesha kana kwamba nimechoka kujibu au nimeishiwa hoja. Aidha umemchamba ndg Lwembe alipojaribu kukudosa kuhusu majibu ya hoja zangu za siku zilizopita ambazo hujajibu hadi sasa, lakini ukaonekana kumkemea na kumtaka anyamaze ili Siyi ajitetee mwenyewe!!! Nami bila ya kusita, ngoja niiache Biblia ijitetee yenyewe maana mimi Siyi, sina maelezo ya kukufanya uelewe isipokuwa maelezo ya Biblia yenyewe ndg yangu.
  Kwanza, umebisha kuwa, wanawake kutofundisha na kuwa na mamlaka ndani ya kanisani, ni mila tu ambazo watu wa zamani aghalabu wayahudi ndiyo waliokuwa na tabia hizo. Naomba nikujibu kwa maelezo yenye maswali ndani yake. Unaelewa maana ya Hawa kutolewa ubavuni tena baada ya ndume kuwa ilishaishi kwa muda tu ilikwishafanya na baadhi ya kazi ilizopewa na Mungu? Ziragora, unafahamu maana ya kutawala? Mungu alipomwambia Hawa kuwa atatawaliwa na Adamu nayo hii ilikuwa ni desturi? Na kama ni ndiyo ilikuwa ni desturi ya nani? Ya Adamu au ya Mungu? Nataka nikuache utafakari kidogo. Katika Yohana 8: 3-4, haina maana kwamba hizo zilikuwa ni mila kandamizi kwa wanawake. Biblia pale imenyamaza kuwa mwanaume alikuwa wapi muda ule au alikimbia kama ilivyo kawaida ya wanaume wazinifu wa siku hizi!! Biblia haisemmi kuwa mwanaume na yeye alikamatwa halafu akaachiwa kwa sababu ya desturi au mfumo dume!! Hasha!! Biblia iko kimya kwenye aya hii lakini ukiangalia kuanzia mwanzo, kwa wayahudi wa mwanzo-Israel wenyewe, dhambi kama hii iliaapply kwa wanawake na wanaume. Soma Mambo ya Walawi 20:1, Mithali 6:3, Katika agano jipya Yesu ni kweli kuwa hakusema kila amtazamaye mwanaume…. Bali alisema kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani… Lakini hili haliwahalalishii wanawake kutenda dhambi ya kutamani waume au wanaume kutamani wanaume wenzao eti lisiwe kosa/dhambi!! Hasha, dhambi iko palepale. Na suala la dhambi, (kuzini, kuiba, nk) halina cha madaraka wala mamlaka kwa wanaume na wanawake!!! Kwa hiyo dhambi ni dhambi na utawala ni utrawala tu. Biblia inaeleza kwa uwazi kuwa, suala la utawala wa Mwanaume kwa mwnamke halikuwa ni la kidesturi bali lilikuwa ni mpango wa Mungu tangu mwanzo hasa baada ya anguko la mwanadamu dhambini, mwanzo 3.
  Luka 24 : 9, wanawake hawa hawahusiani na mamlaka wala kufundisha ndani ya kanisa hata kidogo. Ukisoma kazi iliyowapeleka kaburini asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma(jumapili), ilikuwa ni kutimiza kile ambacho hawakukifanya siku ya sita (ijumaa) kwa sababu ya ufinyu wa muda maana sababto ilkuwa imeshaangia. Na hivyo ikawalazimu kupumzika kama ilivyokuwa imeamriwa. Kwa vile thenashara walikuwa wamekimbia wote wakati wa kuuwawa kwa Kristo siku hiyo ya sita, waliofanya jitihada za kuuhifadhi mwili wa Yesu walikuwa ni wanafunzi wa Yesu wa Kike, na miongoni mwao ni hao uliowataja. Maneno ya wanawake hao yalionekana kama upuzi si kwa sababu waliyoyaleta ni wanawake, bali ni kwa sababu ya uhaba wa imani juu ya ufufuo wa Yesu kwa kuzingatia walivyokuwa hawajaongoka. Kabla ya Yesu kuuawawa, waliamini kabisa kuwa Yesu asingefanyiwa hayo hadi kufa, ndiyo maana walipoona Yesu anakamatwa na kupigwa vile wasivyotarajia, walikimbia wote na hivyo kupoteza kabisa imani yao kwa huyo MWANAUME-YESU kuwa asingefufuka kabisa. Ndiyo maana ilikuwa ni ngumu kwao kuamini ufufuo wa Bwana wao na wala halikuwa suala la destu hapo kaka.
  Ukisema kuwa ilikuwa ni desturi tu basi hata Yesu tunayemwamini kuwa ni Mungu, ana desturi, basi itakuwa ni vyema tu tukiziamini na kuzifuta desturi hizo maana YEYE ni mfano na kielelezo chetu, ndiyo maana hadi mitume akina Paulo tunawaona wanamfuata kwa kuzifundisha desturi hizohizo.
  Pili, kuhusu Waamzi 4 : 4, hapa tunaona mwanamke akiwa kiongozi-mwamuzi wa Israel. Lakini ndg yangu Ziragora kama wewe ni msomaji mzuri wa Biblia, utakuwa ulishakutana na wanawake wengine wa namna hiyo mf Hilda, Miriamu nk, God aliwachagua mwenyewe. Makuhani na viongozi wengine wa dini walikuwepo, but God didn’t use these men to choose/select those women as national leaders/prophetesses. God Himself chose them. Mungu hajachoka kuchagua hadi leo. Akiwachagua wanawake leo, watanena tu na watakuwa na mamlaka pia. Lakini tofauti na hapo, yaani tunapowapigia kura sisi wenyewe na kujidai kuwa Mungu kawachagua, twatenda dhambi na kumsingizia Mungu kosa asilolitenda kamwe. Tumekuwa manabii na wapaka chokaa isiyokorogwa vyema—tukijipalia mikaa vichwani mwetu … Ezekieli 22:28 Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiona ubatili, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo Bwana hakusema neno 29 Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang’anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki. 30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. 31 Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.

  Mungu anasema tumepotoka sote, sasa ni wakati wa mimi na wewe kupajenga palipobomoka bomani-Hekaluni mwa Bwana. Simamia kweli ya Biblia na si vinginevyo rafiki.

  Tatu, kuhusu Matendo 13:50, mimi sijui unaisomaje Biblia yako ndg Ziragora. Huenda ni kwa sababu ya toleo la Biblia unayotumia. Hebu angalia tofauti iliyopo!! SUV= Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye CHEO NA WAKUU WA MJI, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao; na KJV = Acts 13:50 But the Jews stirred up the devout and honourable women, and the chief men of the city, and raised persecution against Paul and Barnabas, and expelled them out of their coasts.

  SUV imetumia neno wanawake watauwa na haijabainisha hao wakuu wa mji kuwa walikuwa ni wanaume (chief men), lakini KJV yenyewe imeonesha wazi kabisa kuwa hao hawakuwa wanawake watauwa, bali walikuwa ni wanawake walioheshimiwa tu lakini WAKUU WA MIJI(chief men) walikuwa ni wanaume!!! Sasa ngoja nikuulize, wewe yaelekea lugha(ikiwemo ya Kiingereza, na (vibantus) siyo tatizo. Je, ni kweli kabisa hukuliona hilo Ziragora au ubishi tu? Na kwa upande wa wanawake waheshimiwa, kwani kwa wanaume kupewa mamlaka ya kuwatawala wanawake, ndiyo sababu ya kuwadharau wanawake? Hujasoma Biblia inatuambia wanawaume tunapswa kuwapenda sana wanawake? Je, kitu kinachopendwa, kinaweza kudharauliwa? Hebu tafakari pia na hapa.
  Nne, nakunukuu “1 Timotheo 2:12 SIMPI mwanamke ruhusa ya kufundisha…, “1 Wakorintho 14:34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa…,” Ziragora, ukisema kuwa Paulo alikengeuka kidogo katika usemi wake, una maanisha nini? Una maanisha kuwa Paulo hakuongozwa na Roho Mtakatifu wakati anaandika nyaraka(epistles) 14 hizi? Kimsingi Paulo alikuwa hapindishi chochote na alikuwa anafundisha kile Mungu alichokifundisha kwa akina Adamu na Hawa, Israel hadi kipindi cha Yesu. Ndiyo maana Paulo anaendelea kusimamia ukweli wa Biblia.
  Acha kufuata mawazo ya watu Ziragora. Mtegemee Mungu nawe utaishi rafiki; YEREMIA 17:5 BWANA ASEMA HIVI, AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU, AMFANYAYE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE NA MOYONI MWAKE AMEMWACHA BWANA.
  Mwisho, Biblia iko wazi sana ndg Ziragora. Ukiamua kuifuata, utakuwa u heri sana. Lakini ukiamua kutii HISIA na hali halisi ya sasa ukiufuatisha ulimwengu, basi utapotea na huo ulimwengu. Wito wangu kwako ni huu, Suala la kuwa na mamlaka na wanawake kufundisha kanisani, Mungu kaliweka vyema sana. Pamoja na mifumo ya 50 kwa 50 iliyopo sasa, bado Mungu hajabadilisha msimamo wake wa tangu mwanzo kwamba, Mwanaume ni mtawala sehemu zote. Tunasubiri hadi Mungu atakaposema au chagua wanawake kwa kinywa chake kama alivyofanya kipindi kilichopita. Lakini kwa sasa, Biblia inatuagiza kuwa wanaume ni wenye mamlaka yote ya kikuhani na kiutawala na si vinginevyo. .
  Bwana akubariki pia.

 68. Ndg Ziragora,

  Usijikatekate ndg yangu, usije ukawa kama wale wahindi waisilamu wanajikataga vibaya sana ili Mungu awaelewe!!

  Bado naona ungali unatatanika kuhusu maagizo ya Mungu katika Biblia, hayo yote unayoyasema kuwa ni Mungu alinena, ukweli ni kwamba ni hao akina Paulo ndio wanatuambia kuwa “Mungu anasema” au “Bwana Asema” kwahiyo ni lazima uwaamini hawa kikamilifu kwanza, ndio kwa neno lao nawe useme kuwa, “Bwana Asema”! Maana hawa si kwamba ni watu tu wa kawaida, hapana hao ni watu waliotakaswa katika kweli, Yn 17:19 “Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.” Basi wakiisha kutakasika katika hiyo kweli, ndio wanatuletea sisi pia hiyo kweli, ambayo nasi Kristo alituombea tayari, 20-“Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.” Unaona ndg yangu, ukiliamini neno la hao ndio unatakasika, ukianza kusema oh huyu ni mtu kama mimi, basi unabakia na uchafu wako na dini yako!

  Hii kweli ya Biblia ndio inaonyesha nguvu za Mungu, kwa nini Paulo asukumwe kusema tu “ingelikuwa heri watu wawe kama yeye” na wala hasemi kam ni amri kuwa sawa naye? Huone tofauti kati amri ya Mungu na neno la mtu? sasa kam huyu mtu aliitikiwa na Mungu aandike vile, sisi hatuna ruhusa ya kuondoa neno aliloandika.”
  Hauko mbali sana na ukweli, jaribu kulichukua hilo kuwa ni neno la Mungu, akijiwakilisha katika hali ya mtume husika ili wewe nawe uweze kulielewa hilo katika jinsi hiyo kama unavyolielewa, Je, kunatofauti ya maudhui? Hakuna! Lakini unapoendelea katika maelezo yako unasema,
  “Hata hivi kuna makanisa zinazofwata lile fundisho kam wa katoliki wanaosema kam kuwa padri au askofu au pope inafaa mtu awe bila kuowa!!!! Sasa hawa hawaseme kam wengine wanaoowa ni wenye dhambi. Vile vile hatuwezi sema kam wao wanakosea kwa kutoowa. Yote inatokana na KWELI ilio ktk Biblia, inayotuonyesha hii ni maisha ya mtume fulani na ile ni amri ya Mungu.”
  Hapa ndipo ninaliona tatizo. Kulichukua neno hilo analolisema Paulo, na kwa hila kulirahisi na kulifanya kuwa Sheria ya kutimizwa na wote wanaoitwa katika utumishi wa kanisa, huku ukilirahisisha kuwa si amri, ni sadistic play! Hiari inakoma kuwa hiari hapo inapokuwa Sharti la kufuatwa au Amri. Kanisa Katoliki halitoi hiari ya jambo hilo bali linalazimisha watumishi wake kutokuoa! 1Tim 4:1-3 inalisema jambo hili kuwa ni mafundisho ya mashetani, “…wakiwazuia watu wasioe”, basi sioni ni kwa kigezo gani unawahesabia kutokuwa na dhambi katika jambo lililowazi kiasi hiki!

  Kuhusu yule mwanamke mzinzi aliyeponywa kupigwa mawe mpaka afe kwa kosa la uzinzi, mimi nafikiri Maandiko yanajitosheleza katika maelezo yake. Mawazo ya kuuliza yu wapi yule mwanaume aliyekamatwa naye katika uzinzi huo, hayana mantiki kwa sababu Mungu anayehusika, hakulileta suala la mwanaume huyo, vinginevyo tutajiingiza katika assumptions za kila aina. Kwamfano, yawezekana kwamba yule mwanaume aliwazidi nguvu wafumanizi wake na akatimua mbio kuelekea ule mji wa kukimbilia (city of refuge), Hebroni, naye akiisha kungia katika mji huo hawaruhusiwi kumkamata (Joshua 21:13)! Tena wahubiri wengi hulichukulia tukio hili kuwa ndilo kigezo cha kuwasamehe wazinzi, lakini ni makosa kwa sababu Kristo hakumsamehe yule mwanamke, bali aliwaruhusu hao washiktaki wake waitimize Hukumu hiyo kulingana na Torati yao ambayo huwataka waliosafi, wasio na dhambi tu, ndio wanaostahili kuitimiza Hukumu hiyo, na kati yao hao hakuwepo aliye safi!

  Naye Kristo hakuja kuhukumu bali kuokoa, ndio maana akamwambia, “Wala mimi sikuhukumu”, akamruhusu aende zake na kumuonya asitende dhambi tena! Unaweza kuwaona pia wale waliomwita Kristo Beelzebub, hao aliwasamehe, lakini aliwaambia akija RM, kosa kama lile hawatasamehewa katika ulimwengu huu wala ujao; nao ujio wa Roho Mtakatifu tunauona katika siku ya Pentekoste, basi ni wangapi wetu kuanzia siku hiyo, ambao kwa kuyarahisi waliyoyafundisha mitume kwa uongozi wa RM, au kwa hila ya kuyapindisha mashauri yao, kama huko kuoa wanakozuiliwa hao mapadre wa Katoliki, tumejiingiza katika kumkufuru huyo RM? Hatari ni kubwa sana kuliko tunavyodhania!

  Na mwisho unaniambia,
  ““Nini anakuonyesha kam ktk agano jipya mwili hayipo? Ina maana hujue inayomfanya mtu (mwili, nafsi na roho)? Nani akakwambia kam kulibaki tu roho? Hiyo ni hila nyingine bwana!!!!!””
  Ziragora, usinichekeshe ndg yangu! Wewe, si ndiye uliyeniambia kuwa wewe ni “Bibi Arusi”, mara moja hii umesahau? Si uliniambia kuwa ninyi “Ni muungano wa Roho zilizookoka, na linaitwa Bibi Arusi.” Kwani sasa hivi mko wapi mbinguni au duniani? Au ulichukua tu nukuu na kuibandika hapa ili kunikomesha niache kuwabishia ninyi “mabibi arusi”?

  Unajua, umenichekesha sana, mpaka nikamkumbuka Nikodemu na “kuzaliwa mara ya pili” Yn 3:4 “… Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Lakini nadhani utakuwa hujayatafakari tu Maandiko vizuri, maana hivyo ndivyo yanavyotufundisha na kututimilia. Hebu kiangalie kifungu hiki, Yn3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Haya endelea hapa Yn 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” unaona, katika huo mwili uliozaliwa kwa mwili huwezi kumuabudu Mungu huku katika Agano Jipya! Ndio maana ni lazima uzaliwe mara ya pili kwa Roho nawe uwe roho ,ndio unaweza kumuelewa anachofundisha Paulo! Au umewahi kusoma popote pale katika Agano la Kale kuwa kuna mtu aliyewahi kuzaliwa mara ya pili?

  Tazama hapa kinachomtokea Mkristo halisi, 1Yn 3:9 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” Unaona ndg yangu, inamchukua Mungu, huyo ambaye ni Roho, kukuzaa mara ya pili, yaani anazaliwa huyo Ziragora wa roho, yule wa mwili anakuwa hana kazi zaidi ya kumbeba tu huyu wa roho, huyu ndiye anayeyaelewa mambo ya Mungu sawa sawa, ndio maana hawezi kutenda dhambi yaani kukufuru! Huyu ndiye anayezaliwa kupitia Injili ya Mitume, huyo ‘Bibi Arusi’, kwa sababu Injili hiyo ndiyo Mungu, hakuna injili nyingine inayoweza kumzaa huyo!!!

  Ubarikiwe sana ndg yangu, tumuombe Mungu kwa pamoja atuinulie zile Huduma Tano katika makusanyiko yetu, ili tupate kusogea mbele zaidi tukifikie kimo chake, Kristo!

 69. Ndugu Siyi,

  Ni kweli ktk mjadala huo sikuwa nawe. Hii haimaanishe kam sikuisoma. Wenda nimeisoma kwa msisitizo mdogo. Lakini nadhani hukuwa ukicheza hapo ukiingia ndani ya mijadala isiyo tofuti! Hivi ulifika hapa ongelea tena hapa. Kwenye blog hii nipo lakini sichange nafasi zote. Pengine nasoma tu. Basi huku ao kule tofauti ni kwamba kinachoongelewa kwa upande moja ni kanisa ya kilutheri/focus/hasa Adam-Hawa/ Paulo-Petro kidogo.
  Na iwepo maneno yamekukauka, basi utakuwa mkweli kutujulisha. Na itakuwa vizuri zaidi ukisema kama huna tena ya kujadili kirahisi isipokuwa kutuandikia kipekee kama ulivyopendelea kwa “mwisho”(tuseme hivo) wa ile mjadala mwingine. Hii ni busara kabisa. Lakini kwa kweli kuna mambo niliyosimamisha kipekee, tena nilikuwa nikijibu kwa suala zako. Kam umetosheka, ni amina. Si mimi tena nitaswali wakati nilipokujibu na kukuswali. Katika mjadaka ile hukunijibu na sikuwepo, najua ulijibu wengine kwa suala yao kulingana na namna walivyokufikishia hoja.

  Asante ndugu yangu Siyi, ubarikiwe.

 70. Ndg Lwembe,

  Nami nakushukuru pia .
  Nitajitahidi nijibu kwa hoja yako inayolingana na mazungumzo yetu. Ambayo niliandikia wengine nikiyarudilia nitakuwa nikipoteza muda kwani labda nao watafika na hoja nyingine. Niliyoandikia Siyi na wengine, licha ya kuwa umeyasoma, sitayajibu kwako.

  -Kama ninalalamika, elewa tu sikulalamikie kwani sihitaji chochote kwako kwa kunisaidia.
  -Kufundisha na kusikiwa ni mambo tofauti. Sasa acha kuzuia wengine kusikiliza. kama Yesu mwenyewe hakusikiwa na wote, mim ni nani ili nijikatekate Lwembe anisikie?
  -Niliyesema unatetea si Paulo, ni Mungu(Yesu Kristo). Paulo unaweza ukamtetee namna uwezavyo, lakini unapotetea Mungu, ndipo najiuliza kam yeye hana nguvu za kujitetea mwenyewe. Nakuona ukisema alinena na hakunena, je wewe unanena pahali pake?
  -Kulingana na hoja yako kam Mwanamke kufundisha ni dhambi, ile ni maoni yako. na ikiwa utajitaabisha kutengeneza dhambi utakosa uzitie wapi.
  -Unapokuwa kwa upande wa totari, nadhani unakosewa jambo fulani ao unacheza tu. Nilileta mfano wa jambo lililo ndani ya torati; ulisoma? labda niliudilie tu kwako. Kulingana na torati, mwanamke aliekuwa alikamatwa akifanya uwasherati aliletwa kwa Yesu ili naye aruhusu kam torati huyu mwanamke auwawe kwa mawe, lakini Yesu hakubali. min kawaida simpe mtu mifano mingi wakati ninapoona amapuzi bila sababu ilie moja niliyompa. Basi kam utazingatiya mambo yote ya torati(ambayo inafanya mila ya wayahudi) sijue kam utaweza. Hata hivi, ndugu yangu, kufwatana na jinsi wewe ni msomi wa Biblia, najua una uhakika hauheshimu torati. Unajifanya kam hujuwe kusudi labda mada isiishe.
  -Nini anakuonyesha kam ktk agano jipya mwili hayipo? Ina maana hujue inayomfanya mtu (mwili, nafsi na roho)? Nani akakwambia kam kulibaki tu roho? Hiyo ni hila nyingine bwana!!!!!

  Ubarikiwe sana.

 71. Seleli,
  Kama ‘memory lapse’ haijakukamata, basi utakumbuka nilikuambia kuwa utazunguka sana na Maandiko kama walivyoizunguka nyumba wasiuone mlango, nakuona bado uko katika zoezi hilo!

  Maswali yote uliyojaribu kuyajibu umeishia katika “NDIYO na HAPANA”!!!
  Nayo tafsiri ya kiroho ya majibu hayo ya “NDIYO na HAPANA” ki Maandiko ni “UVUGUVUGU”; hiyo ndiyo hali ya kanisa la leo, lenyewe ni “NDIYO na HAPANA”, mwanzo mwisho!!! Hii ndiyo ile “Mule Religion” niliyokuambia. Ukiwauliza, mwanamke anaruhusiwa kufundisha? Jibu lao Ndiyo na Hapana. Wakijitahidi, kama wamepinda sana, “hamna tabu, wakifundisha sawa, wasipofundisha yote sawa tu, ni mambo ya mila na desturi tu, tunabarikiwa tu namna zote”!!!

  Kuhusu Biblia ni Neno la nani? Naona ufahamu wenu UMEGOTA. Naona hata uwezo wa kulielewa swali hamnao, ndio maana mmekazana off ile mbaya! Yaani inaonesha siku zote mnapoambiwaga kuwa “Biblia ni Neno la Mungu”, huwaga mnaitikia vitu msivyovijua, ukimuuliza yule “mule”, who is your papa? Jibu “nwho, nwho!” Who is you mama? “nwho, nwho!” Sikilizeni: “ALL Scripture…” acha mambo ya kitoto ya kukimbilia tafsiri zisizojitosheleza ili u manipulate Neno la Mungu!!! God will hold you responsible kwa vitu ambavyo havina tija. After all you could be giving yourself over to some stupid spirit! But God said ALL SCRIPTURE is His! Hicho ndicho anachokisema Mungu, Maandiko yote ni ya Kwake!!! Ndio maana nimewaambieni kwa kuwa mmejazwa Roho Mtakatifu ninyi yatenganisheni basi, yapi ni “MAANDIKO YOTE” na yapi ni hayo mambo yenu ya kifo! Mkiambiwa ninyi mnafanya kazi ya Mpinga Kristo, mnalalama, mnadhani Mpinga Kristo ana pembe za nyati kichwani? Jaribu kumtazama aliyekufundisha hii injili unayoihubiri uone kama ana pembe, they are smart, intellectual, and you name it!

  Si umemuona Ziragora, analeta mambo ya unafiki wa zile Fellowships, mama mkatoliki na baba mpentekoste, tena baba mwenyewe ana mke tayari, kwahiyo watoto hao hulelewa kwa mama yao, ndipo mama yao huwatengea muda wa jioni wa kujifurasha na mambo ya baba yao, lakini asubuhi wote “Salaamu Maria, … utuombee”!

  Halafu angalia mnavyotiririka mpaka mnatia huruma! Eti,
  “”Kwamba Mungu alikubali kuchanganya Neno lake na mila, nitakupa mifano hii ya maandiko kisha amua case mwenyewe.”” Nukuu zote ulizozileta ni Torati, ndio maana nilikuambia unahitaji kufundishwa vizuri ili uweze kuufikia ukamilifu, ule Utakatifu! Rudi kwa mchungaji wako kamuulize kuhusu zile Huduma Tano, mkimuomba Mungu atawaleteeni ili ziwasaidie kuwaweka sawa kuliko hivi mnavyojikurupukia tu, ingawa Ziragora ndio hazitaki kabisa kwa hasara yake!

  Paulo wala mitume hawana Mila wala Desturi za kipagani kama mnavyojidhanisha kwa ile “namna Yenu”; hao wamezaliwa katika Torati, hiyo ndiyo Mila na Desturi yao, naye mwanamke akiwa ni sehemu ya jamii hiyo, aliiishia hiyo. Nayo Torati ndiyo inayotuleta kwa Kristo! Najua hujui chochote kuhusu hilo, zaidi yakuvisoma vifungu hivyo na kuishia hapo tu, ukikutukuza zaidi “kunena kwa lugha” na kuombea wagonjwa, lakini hilo si kosa lako, ni kosa la mfumo uliomo, huo ndio umbali unaoweza kukufikisha, zaidi ya hapo ni kiza kitupu!

  Najua utakuwa unalalama, lakini jikague kauli yako mpya, hii inayohusu mwanamke kujifunika kichwa:
  “”Mfano maagizo (ACTUALLY NI MASHAURI-soma hapo-alikua anashauri) kuhusu KUFUNIKA KICHWA KWA MWANAMKE asalipo au anapohutubu”” Unauona huo Mpindo wa Neno la Mungu unaowatengenezea wajinga? Neno hili hapa kama lilivyo:
  1Kor 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. 4-Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake. 5Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake” Jamani huo ni “USHAURI” kweli? Kwamba ANATAKA TUJUE ni ushauri au jinsi mpya ya kuenenda katika Imani yetu Mpya? Haya mambo Seleli, are the Deep Things of God, usiyavamie vamie tu, wakati hujui lolote! Sikutishi wala sijidai, bali huo ndio ukweli wa Neno la Mungu. Mwanamke anapaswa kufunika kichwa chake, anapokisogelea Kiti cha Rehema, Hilo ndilo Fundisho la Mitume! Naye mwanaume hapaswi kufunika kichwa chake. Umeyaona mabadiliko hayo? Si uliambiwa Ukuhani umebadilika, na Sheria pia (Ebr 7:12), tazama ilivyompasa mwanaume, yule Kuhani, yeye alipaswa AFUNIKE nywele zake! halafu unawaona maaskofu wako wanavyochemka, wanaendelea katika Ukuhani wa Kale wakizifunka nywele zao kwa yale makofia yao makubwa, wamepigwa chenga na Maandiko!!

  Sasa mwanamke afunike nywele zake na kitu gani, gunia au sufuria, au afunike na nini? Hapo ndipo kuna mtihani, wengine wamekurupuka na kuwafunga wanawake vitambaa kwa kukosa subira, wakaondoka na kujitungia mambo yao; wengine ndio ninyi akina Seleli na makundi yenu, mkasema ah, huo ni “ushauri tu” mkaishia “empty headed’! Lakini hilo ndilo agizo la Mungu kwa Kanisa lake Takatifu, mwanamke inampasa afunike kichwa chake! Afunike kwa kitu gani? Mstari wa 15 “Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.” Umeelewa Seleli? Sio mnawaachia tu wanawake zenu wananyoa nywele wanakuwa vipara wengine madenge hata kama si zile titi usingejua kuwa huyo ni mwanamke, Mungu anasema its an abomination!

  Itawachukua kulinyenyekea Neno la Mungu ili kuyaelewa haya na mengineyo mengi sana ambayo kwa kadiri ninavyowaona mnachomokaga tu kama mishale isiyo na mwelekeo, ili mradi mmekamata vifungu vya Maandiko na kuanza kuzunguka navyo kama pia!!!

  Gbu, my “vuguvugu” brother!

 72. Ndg. Ziragora,

  Kwanza nikushukuru kwa kutuandikia!
  Pili, sijakuelewa kabisa unachojaribu kukisema, achilia mbali kukifundisha!
  Na tatu, ninakuona umekuwa mtu wa malalamiko na kushawishi!

  Lakini hata hivyo, ngoja tuyaangalie tena haya uliyoyaleta.
  Ndg Siyi amekuuliza swali la moja kwa moja na akakuomba aya za Maandiko kuyathibitisha madai yako kwamba :
  “KUKATAZA WANAWAKE KUFUNDISHA KANISANI NI DESTURI”
  Badala ya kuonesha ni vifungu gani, umekuja na maelezo mengi yasiyo na rejea!! Pia amekuuliza:
  “Kwani Biblia imetafasiriwa kwa kufuata desturi za maeneo mbalimbali?”
  Inaonesha pia huna jibu!

  Ndipo tunapoendelea, napenda niliweke wazi jambo hili ambalo nawaona mnalirudia rudia sana, kwa kejeli, kwamba mnaniona ni mtu mwenye kujifanya namtetea Paulo: “Unayedhani kutetea hahitaji atetewe, naye amenyeyekea mpaka mauti, sasa kiburi ni ya nini?” Lakini ni kweli, eleweni hivyo, kwa sababu ili ufikie kumtetea yeyote yule, basi ni lazima kwanza uwe CONVINCED ktk jambo analolizungumzia, na kisha uwe CONCERNED, ndipo unapoweza kusimama naye, hivyo ndivyo ilivyo kwangu!! Ndio maana narudia kuwaambia, tena na tena, kuwa ninamuona Kristo ndani yake, huyo aliyepewa kumdhihirisha, kwa kuchaguliwa toka tumboni mwa mama yake!!!

  Unasema hivi, baada ya kushindwa kuthibitisha kwa Maandiko ni wapi desturi zinafundishwa katika Maandiko:
  “”Kwa mwisho naomba tuwe wazi: “Nikisema “wanawake wanaweza fundisha kanisani nimetenda dhambi?” Na kama ndivyo nimevunja sheria gani ya Mungu? Na wewe unayeseme nimetenda dhambi UMENIHUKUMU kwa bure tena umekuwa MWONGO na hapo una tatizo mbili. Ninataka tufafanue vizuri, tunazungmuzia dhambi ao kuitika/kukataa kumuiga Paulo katika mila yake.”

  JIBU: Kwa kuwapa wanawake nafasi ya kufundisha kanisani, utakuwa umejitenga na Mungu, kwa uchaguzi wako mwenyewe, yaani una DHAMBI! Pia unapaswa ufahamu kwamba katika Agano Jipya hakuna mambo ya Mwilini, ukiona unawaona ‘watu’ humo basi jua kuwa una matatizo makubwa sana, maana hili ndilo Agano la Mwisho ambalo kila mwaminio anapaswa kuwa sehemu yake, basi ukiwaona “watu”, jua kuwa uko NJE! Vinginevyo, dini zetu zinakuwa ndio vyombo vyetu vya usafiri kutupeleka huko Gizani; maana imeandikwa, 2Kor 5:16,
“Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.” Kama mnaweza kuelewa maana ya kifungu hiki, itawasaidia kuhamia rohoni, huko anakohudumu mt. Paulo, mkishindwa basi endeleeni mwilini, mtayapata ya mwilini, kwanza mnakuwa raia wema!

  Mwisho nikuambie nawe hivi, kwamba hizo unazosema Mila na Desturi za Paulo, utakuwa hujaelewa tu, huyo hana mila za kipagani kama unavyofikiri; Mila na Desturi alizo nazo ni Torati au ukipenda Sheria!!! Basi kama unaona Sheria hazifai kwa Mkristo, katika namna Yenu mnayoifundisha, hilo pekee laonesha kuwa ninyi hata Ukristo wenyewe hamuujui! Kwani huwezi kuufikia ukamilifu, huko kuwa Mkristo, bila ya Torati, hiyo ambayo ndiyo “inayokuleta kwa Kristo”, au umefikaje, umeingilia dirishani? Au hujaiona Torati ndani ya Injili?!!!

  Jipatanishe na hayo machache kwanza, ndipo tuendelee katika tafakari ya “Biblia, ni Neno la nani?” ili tufikie katika kimo cha Kristo, badala ya kuwa mumiani (vampires) tukivinyofoa viungo vya Kristo kama wanavyowafanya albino!!!

  Gbu!

 73. Ndugu Seleli, Lwembe, Yusha, Siyi , Sungura, Mabinza,

  I.Kwa wote,
  Naomba munisamehe kabisa kwani sipatikane weekend. Hii inanisukuma nichukue mda ili nisome posts zote zenu ndugu zangu, mulizopost during the weekend. Ndio maana nimeamua kuwaandikia kwa limoja.Hivi samahani vilevile kam mutakuta sikurudilia nukta kwa nukta yote muliyoandika.Nakamata tu essentiel.
  Kwa namna ya kupambana hapa kwenye blog,inategemea ;kila mtu anayo style yake. Kuonya kwa wema,nadhani kwa upande wangu , itasaidia wote, zaidi waliowachanga ambao nafikiri ni wengi wanaotusoma. Dada Janeth alijitokeza hapo juu kidogo akasimulia mambo ya fujo. Unajua wadada wengi hahaje kwenye mijadala kwani mara na mara wanashindwa kupambana kwa mtindo huu. Lakini labda tukibadili style watakuja. Na hii zaidi ndio ilokuwa lengo langu, kam kila mtu ajisikie free.
  Nilijitokeza mara nyingi wakati niliona ndugu Lwembe anaaga kirahisi pasipo kutujulisha kam amekengeuka ao la. Na kupitia andiko lake nikaona ana huzuni kwani alidhani ametatizwa ao amechoka kuambia wasiyosikia. Nilipoomba wenye kujadili waje na hoja fupi zinazojaa wema, nikamuona amejipa moyo. Samahani tena Lwembe kwa kuwa uliona niliweka posts 3 za kufwatana. Kweli nilifafanua kwamba ni kwa sababu nilikuwa nimeandikia mmoja pahali pa mwengine, na niliomba masamaha. Nafikiri ni wewe pekee ambae hukunisameye kwani umenifokea kam nimeandika mingi na bado nitaandika tena. Naomba utulivu kabisa, kwanini matusi tunapojadili neon la Mungu? Unayedhani kutetea hahitaji atetewe, naye amenyeyekea mpaka mauti, sasa kiburi ni ya nini?
  Baada ya Lwembe kuondoka, ndugu yangu Seleli akawa kam amepunguza speed.
  Sasa karibu tena kwa wote na tubarikiwe pamoja.
  Style yangu ni kutia focus kwa jambo halisi, tunalijadili na linaisha kwa wema. Na iwepo wamoja watakataa, tunajua Ibilisi angali ana operate, waliyookoka wataendelea kuwuombea. Na tusisahau ile, sharti tutie kwenye fungo moja maombi na mjadala kusudi tushinde mwovu.
  Nimesema kwa uwingi kam Shetani hafurahi kuwa ameandikwa ndani ya Biblia, lakini kwa upande mwengine anafurahi wakati anapopata watu wenye kumsaidia kujificha wakimtetea kama mambo yake mabaya hayapo ndani ya Bible, wakidai yote ni tamko ya Mungu. Hapo Ibilisi anajikuta na sifa zake kam huko kuzimu ambapo wanamuita Mungu. Mambo kam yale ya kusaidia Shetani hapo ukisema uko kwa upande wa Yesu mim nayapinga.
  Neno lingine nililoomba ni kuwacha ushabik na kuepuka kukataza mwengine kuamua ginsi anavyopenda akiwa amepata mpenyo wa Neno la Mungu.
  Kwa mwisho naomba tuwe wazi: “Nikisema “wanawake wanaweza fundisha kanisani nimetenda dhambi?” Na kama ndivyo nimevunja sheria gani ya Mungu? Na wewe unayeseme nimetenda dhambi UMENIHUKUMU kwa bure tena umekuwa MWONGO na hapo una tatizo mbili. Ninataka tufafanue vizuri, tunazungmuzia dhambi ao kuitika/kukataa kumuiga Paulo katika mila yake.
  Kujitokeza kwangu kwa mda kam huu wakati Ndugu Seleli amepost tayari mambo mengi isionekane nimekuzuia kumsoma vizuri na kujibu. Mim nimemsoma kabisa, niko kwa upande wake 100% kwa mafikara bali mim nina style yangu, naye ana yake. Baadhi ya suala ningelijubu amekwisha kujibu tena kwa urefu; isitoshe ameweka suala. Utakapo mjibu utakuwa tayari umenijibu; na Mungu wa mbiguni amubariki.

  II.Ndugu Siyi,
  Nimikusamehe kabisa. Nilikujua kama mwenye utaratibu na sikutaraiia unaweza jiingiza katika kosa kama lile. Basi na Mungu wa mbinguni akurehemu.
  Wewe ninakuandikia mingi kidogo kwani ulinisuali wa mwisho. Suala lako, ulipenda nikuonyesha mahala ambapo kunaonyesha kama” KUKATAZA WANAWAKE KUFUNDISHA KANISANI NI DESTURI” tunaipata wapi ktk Biblia.
  Ukitazama vizuri sizunguke kabisa. Jambo linaloleta tatizo zaidi ni kupeleka mshairi moja kwenye laboratory na kuanza kufanya analysis hapo ukisahau kam ni ile muungano wa maandiko yote inayoleta kitabu kuitwa Biblia. Anaesoma mshairi moja amepata elimu ndogo, anaesoma aya yote anaelemishwa zaidi, anaesoma kitabu kimoja anaelimshwa zaidi tena, na yeye anaesoma vitabu vyote vya Biblia anaelimishwa kuliko hawa wengine wote kam amedaka aliyoyasoma kwa UTUKUFU wa Mungu. Ndio maana wakati unapoona mshairi fulanu haitoshelee kuonyesha kam Biblia ina manage vizuri ulimwengu wote, endelea soma na hapo utapata nafasi nyingi inayoleta nuru yote licha ya kuwa ya mwisho haiangushi ya kwanza.
  Kwa mfano : Waebrania 12:14, NIV Bible “Make every effort to live in peace with all men and to be holy; without holiness no one will see the Lord ” , lakini ukisoma Warumi 12:18 utaona ikisema “If it is possible, as far as it depends on you, live at pace with everyone”. Angalia na tazama neno kubwa tofauti ni “if it is possible”. Kazi RM anayofanya ni kuonyesha yeye anayemtafuta, ni ipi adake ; ile inayoonyesha ukweli yote as the Bible manage the world.
  MAJIBU KWAKO :
  Kuna maandiko fulani yanayoonyesha kam mila ya ile wakati ilikuwa kudharau wanawake hata wakati walipokuwa na ujumbe halisi kutoka Mungu.Hii ilikuwa ni desturi tu wanaume waliorizika nayo kutoka torati. Kwa mfano :
  1)”Yohana 8: 3-4: Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
  Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.”
  Nataka ujiulize, huyu mwanamke alizini naye peke yake? Si mila ya ile wakati ilinyanyasa wanawake? Je umewayi sikia mitume wakiacha mila yao? Na hiyo mila haiandikwe ndani ya Biblia?
  2)« Luka 24 : 9 Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote.
  10 Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao;
  11 hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo.
  12 MANENO YAO YAKAONEKANA KUWA KAMA UPUZI KWAO, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hata kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia. »
  HAPA KWANZA,INAOMBA KUJIULIZA KWA NINI HABARI NJEMA WANAWAKE WALIYOPEWA NA MALAIKA WA MUNGU,HAWA MITUME WAYIFANYE KUWA UPUZI. HII SITATIZO YA MALAIKA BALI PROBLEM YA MILA WALIKUWA NAYO. NA MUNGU HAKUWAPIGA HAWA WANAUME KWANI MUNGU ANAJUA MILA IKO.
  3) « Waamzi 4 : 4 Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.
  5 Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
  6 Huyo akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu toka Kedesh-Naftali, akamwambia, Je! Bwana, Mungu wa Israeli, hakutoa amri, akisema, Enenda, ukawavute kwako, huko katika mlima wa Tabori, watu elfu kumi wa wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni?
  7 Nami nitakuvutia Sisera, amiri wa jeshi lake Yabini, hata mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako.
  8 Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi.
  9 Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana Bwana atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi. »
  HAPA UNAONA DEBORA AKIWA MUAMZI, WATU WOTE ALIWAAMURU, INA MAANA ALIKUWA NA MAMLAKA JUU YAO. TUNAONA HATA JEMADARI MKUBWA MWANAMUME BARAKA ANAOGOPA KWENDA VITANI PEKE YAKE KWANI SI YEYE ALIYEPEWA ILE UJUMBE. MUNGU ANAPOPENDA HESHIMISHA MWANAMKE, HAKUNA MTU ANAYEWEZA MZUIZA.
  JAMBO LINGINE DEBORA HAKUWA TU MUAMZI,ALIKUWA VILEVILE NABII. NA WAKATI ULE UNABII ULIKUWA NA SAMANI KUBWA NYUMBANI MWA MUNGU LAKINI NENO NITATAKA NIANGAZIE ZAIDI NI ULE UTAWALA ALIKUWA NAWO JUU YA ISRAELI YOTE.
  4) « Matendo ya Mitume 13:50 Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye CHEO NA WAKUU WA MJI, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. »
  HAPA BIBLIA INAWATAJA WANAWAKE WENYE CHEO TENA WAKUU WA MJI.KUWA MKUBWA WA MJI INA MAANA UNATAWALA, SI NDIO ?

  Sasa Paulo anaposema « Wanawake wasifundishe kanisani ,wanyenyekee mbele ya waume….»,ile haina tofauti na ile iliyoleta mitume kupuza injili waliyoletewa na wanawake. Na hii ni mila Kabisa.
  5)« 1 Timotheo 2:12 SIMPI mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. »
  Hili tamko « SIMPI » inaonyesha vilevile kam anatofautisha neno lake na lile halisi la Mungu.
  6) « 1 Wakorintho 14:34 Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo TORATI nayo »
  Huyu alieandika pale ku 1 Timotheo na 1 Wakorintho ni mtu mmoja, Paulo,mtumishi wa Mungu. Lakini kwa sababu ni mwanaadamu,amejikuta amegeuza masemi kidogo. Hii yote ina maana kwetu : « UTUKUFU NI WA MUNGU »
  Ndio maana imeandikwa « YEREMIA 17:5 BWANA ASEMA HIVI, AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU, AMFANYAYE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE NA MOYONI MWAKE AMEMWACHA BWANA »
  Katika shairi hizi ninazorudilia kwani wengine labda waliwai kuzileta tena, ukiyasoma kwa msimamo wa katafuta kufahamu, utaona viruzi tofauti kati ya tamko ao agizo la Mungu na mafundisho fulani ya watu. Hawa watu si wawongo na wanao RM . lakini UTUKUFU ni wa Mungu. Na hii maoni yao inayokuwa wazi kama ni yao kipekee ndio inaendelea angazia zaidi UKWELI iliyo ndani ya BIBLIA.
  Fikiria kama BIBLIA ingelikua kama Quran ambayo mashabik wayo wanadai kam ilishuka toka mbiguni na unapoisoma kidogo utaona neno « andika…. », utaona kam haina Ukweli kwani Mungu hawezi andika yeye pekee tena aseme na Muhammad aandike. Ndio maana inaonekana wazi kam hicho kitabu hakina neno la Mungu kwani hamna UKWELI.
  Hii shairi kidogo inaonyesha wazi kam “kukataza wanawake kufundisha” ni desturu tu na wala haihusu amri kutoka kwa Mungu.
  Ubarikiwe.

  II.Ndugu Seleli,
  Mim naona sina mengi ya kuongeza,isipokuwa kukushukuru kwa kurudia. Ulikua ukihitajika kama wengine wote. Jambo lakurudilia maandiko haina tatizo kwani hata ni mtu huyu mmoja anayerudilia anajitahidi aeleze kitofauti kwa manufaa ya wote ; na ile ndiyo umefanya ;God bless you.

  III. Ndugu Lwembe,
  Nakushukuru pia kwa bidii unayo. Saulo alikuwa nayo vilevile kabla aitwe Paulo,wala hakupoteza bidii yake hapo akiitumia kwa kazi ya Mungu.
  Nina neno ndogo kwako inayohusu suala yako :
  -Ukichanganyikiwa mwenyewe usidhani ni mwengine amekuchanganya. Sema ukweli tu.
  -Kila wakati Ndugu Siyi anapoelewana na wale ambao wana maoni tofauti, sijue kwa nini unafika ukikaripa. Sisemi kam amekwisha jipanga kwa upande mwengine lakini ana namna yake ya kufikiri. Mim namtazama akiacha mambo yote mengine inayozunguuka mada(kam vazi na uandishi wa Biblia) lakini angali akiswali juu ya mwanamke kufundisha. Kam itafika wakati aamue namna usiyopenda, umuwache.
  -Unasema wamenidanganya na una uhakika nimekuonya usiwategemee wachungaji na maaskofu kwani “ategemeaye mwanaadamu alaaniwe”,Bwana Mungu amesema. Nafikiri umeisoma pale juu kwa ile niliyoleta kwa Siyi. Lakini mpendwa, kumbuka wewe unasema kam nimekuonya usiwasikilize wachungaji. Hii inaonyesha kam husome vizuri yale wengine wanaoandika wakati wewe unayo bidii ya kuandika. Kwa upande mwengine hulete jibu kwa suala zetu, unafanya haraka kusuali na kunena unayotaka. Nafikiri hujachelewa,unawezaanza hata leo. Wachungaji na maaskofu, mim nilisema hata waheshimiwe,sivyo ? Sasa kuwasikiliza na kuwategemea ni mambo mawili tofauti. Ukimtegemea ina maana kwa bahati mbaya akienda jehenum nawe waenda. Lakini kumsikiliza haikuleti mara moja kufanya yote anayoyafanya.
  -Kwa mambo ingine, soma vizuri sasa aliyoandika ndugu Seleli ;naye namuona akitusihi kumsoma vizuri. Hapa sipendi nianze kukujibu tena wakati ninapoona Seleli alipoona nimechelewa alijibu kwa yote, tena kwa urefu. Kamata mda umjibu pasipo kukwepa.

  IV.NduguYusha
  Ubarikiwe na Mungu akuwezeshe kwa yale utakayotuletea. Nimekuona zaidi ukitutayarisha kwa yale utayoandika. Umepinga Ndugu Seleli name pia, basi tunasubiri.

  V. Ndugu Sungura, Ndugu Mabinza,
  Karibu tena. Au mmeacha mjadala ? Kila mmoja nilimsoma vizuri kabla sijaanza jadili, Sungura na Mabinza, ondoeni tule tu tofauti tudogo, kiisha mada imalizike.

  Asante ndugu zangu na Mungu wa mbinguni awabariki.

 74. Lwembe, Ziragora, Seleli na SG wote.
  Lwembe, nakushukuru bro kwa kuamua na wewe kuacha udini, udhehebu na kusimamia Biblia. Binafsi nimefurahishwa na misimamo yako ya ki-Biblia. Mungu akubariki kwa hoja nzuri katika mada hii. Nafikiri Seleli na wengine wangesoma vizuri na kwa kutulia mapachiko yako ya sasa, wasingeendelea kuchanganyikiwa!!
  Seleli
  Kimsingi unaandika mengi saaana lakini pointi kiduchuuu, unarudia yaleyale ya miaka ya 47 na mengine hayana pointi kabisa. Unang’ang’aniza pointless ziwe point!! Binafsi sitakuandikia mengi sana kama wewe. Nitadondoa baadhi tu ya yale uliyoyaleta.
  Kwanza, naona umeng’ang’ania hojaless yako kuwa, Ndani ya Bibliaa, kuna maneno ya Mungu, Watu na shetani!! Halafu ukajichanganya ukasema tena kuwa, pamoja na hayo yote, haiifanyi Biblia ikose nguvu ya Kuitwa Neno la Mungu. Swali kwako la tafakari, maneno hayo ya watu na shetani yalitoka kwa nani wakati wa kuandikwa kwa Biblia? Tafadhari naomba ujibu ukirejea kauli yako hii “Jezebeli alimtishia Nabii Eliya kua anamtenda kama alivyowafanyizia manabii wa baali’’, SWALI: Je hilo ni neno la Bwana na lina pumzi yake na huyo anayesema ndani ya mwanamke jeuri yule anayemtisha vikali sana Mtu wa MUNGU huyu, ni Roho wa Mungu?”

  Seleli, unafikiri kuonekana kutofautiana kwa baadhi ya waandishi wa Biblia kama akina Marko, mathayo, Luka, nk(kama ulivyonukuu) unafikiri tofauti hizo zilitokana na ubinadamu wao, mila/desturi zao au hisia zao? Kwa mf. 2 timoth 3:16, aliyeandika ALL SCRIPTURES na aliyeandika KILA ANDIKO…, unafikiri tofauti hizi zilitokana na nini? Hisia, mila/desturi au udhaiifu wa waandishi?
  Seleli, mbona unachanganyikiwa kaka kwa mambo madogo? Kwa mfano, unaelewaje unaposoma luka 1:1-4 na 2 Petro 1? Napenda sana kukuchokoza kwa amaswali ili kufungua ufahamu wako. Karibu sana.
  Ziragora,
  Nakusubiri kwa majibu ya maswali yangu!!
  Bwana awabariki sanaa

 75. Lwembe/Yusha

  Kwakua majibu yenu kwa post yangu kwa Siyi nimeona hamko serious hapa basi nami nawajibu pia kimastory-story/kinyepesi post zenu za recently hapa.. Ila nangoja msome tena ya SIYI na kisha ya Lwembe parts 2 kisha mseme sasa)

  Lwembe, Aaa tafadhari bwana, acha utani! nimepitia majibu yako, kweli Yusha angekua mkweli mbele za Bwana,angekuambia umejibu porojo. Let us be honest and fair, fanya ivi Yusha, soma kazi yangu ya kwanza kwa Siyi na vipande 2 kwa Lwembe then tell me the truth kama kuna kitu kweli hakijawa dealt with sawa sawa.Unajua nilishajua njia bora sana ya ku-engage na wewe Lwembe namely, the more you bring your cheap stuffs, the more I release heavy things true ones Kibiblia na kiakili na kwa jinsi hiyo, hata wewe ukisoma tu unayoandika/jibu kulinganisha na ninayokuletea, unajua tu wapi kuna substance, sema watu mnaonaga wivu tu na aibu kusema, ‘’brother, yeah man, I HAVE SEEN IT, sasa badala yake mnabaki tu vikaenda na vikarudi!!!!!!!!!!!!

  Yusha, pitia zote zangu kwa Siyi na kisha zangu 2 kwa Lwembe kisha sema. Uwe mtulivu tu, some tena na kisha niambie kwa dhati wapi hujaelewa. Kwa kusema kweli hata maswali/hoja ulizosema sasa za sijui Mitume walikua wanaume nk, umerudia yale yale ambayo nilishayajibu kwa kukukutumia post yako mwenyewe ambayo hukujibu na labda hukusoma ndio maana umesema vitu leo kama vile hajajaviongelea kabisaaa. SOMAGA KWANZA MAMBO HAPA MPAKA MWISHO NDIO ANDIKA, la sivyo, ukikurupuka tu na kubwaga chochote hapo, inaboa kweli maana unajiuliza huyu mtu ni mtani, Je kweli yuko commited na huduma hapa, au anacheza cheza tu, au anaota, au alisafiki kisha akaja kuibukia hapa kienyeji tu pwaaa, unajiuiza amesoma kweli au misisimko tu. Kusema kua ukiwa na porojo ndo unaandika sana, hilo neno sawa kabisa kwa Lwembe lakini never kwangu na kama kweli unabisha, NAKUPA TEST, NIONYESHE HAPA HATA POINT/HOJA/ISSUE KTK POSTS ZANGU kitu nimeandika porojo ambacho kwa akili ya kawaida, kiroho na Kibiblia, hakieleweki! Aya show me!

  Otherwise, sitaki kujisifu lakini ikibidi nitajisifu kama Paul. Embu soma materials zangu na zako au haswa Lwembe kisha linganisha, nani yuko serious hapa? nani analeta vitu hatari? nani analeta Biblia ktk hekima yote na mapana si kukariri na kufia ktk andiko moja bila kuangalia kweli nyingine? nani anafundisha mambo kwa urahisi na mbinu nyingi na sahihi kueleweka? nani ananukuu NENO kwa hakika na vya kutosha?( hesabu maandiko na maneno nayotumia na ya wewe au Lwembe- kukuthibitishia sina mchezo, ninakula na kumeza gombo acha kabisa na nina wajibika kwa dhati hapa si wewe kaoga na kenye visingizio na misisimko ya kipendwa ile ya bure bure! ati umeona kuna Hila! Mmmh! Mpendwa bwana, wacha utani, chapa kazi hapa. Kwa iyo kusema tu kirahisi kua nimeandika sana coz nina porojo wakati naachilia Biblia, na si tu kuachilia lakini kushare Neno kwa usahihi na hekima yote pia na mifano ya ufundishaji, ni utani.Bila kuthibitisha icho, sasa wewe ndio utakua na porojo, muongo, muoga na msema maneno tu ya ovyo, BILA KUTHIBITISHA ukisemacho, yatakua ni maneno ya by the way. Unajua ni rahisi tu mtu kukusoma kua umeona mawe hatari sana humu ktk posts zangu, tena mengine unamshanga Mungu Roho Mtakatifu na una gain sana knowledge ila wivu tu unawala na uchungu wa kukubali kua mnatakiwa kupandisha viwango. Kwaiyo, usinidangaye brother kwa maneno mepesi, kama unajiamini na kweli una Neno na maarifa sahihi kama navyojiamini mie, onesha hapa! Tumeruhusiwa kujionyesha kua tumekubaliwa na Bwana, tukilitumia Neno kwa halali, so onyesha una kitu, sema. Aya karibu uKatae au pinga hoja zangu kwa kutoa zako, Usikimbilie kusema tu ooh porojo, mara kuna hila ya shetani, mara ooh nafasi ya Wanawake ipo, mara ni elimu ile niko nayo ndio maana nafundisha hayo, itakua kama tuko chekechea. Kama kweli una jambo la KWELI NA SAHIHI kinyume na yangu, na useme sasa, mbona rahis tu! we si unakitu bwana, sema sasa! Unanidanganya kua huna muda wa kubishana! mmmh! Haya basi tuhojiane maan ni kiBiblia kabisa kuhojiana au nayo hujui! unakalia maneno mepesiiiii ooo huna muda wa kubisha! Si usema ukweli tu umeona msitu mnene huu mpendwa, Bwana ananitumia vya hatari na mimi najua hata kama hau-appreciate live hapa lakini moyoni, Roho Mtakatifu anakuambia, anachosema Seleli na kufundisha is right na simply correct, sema tu kile kiburi cha uzima na kukaririshwa mambo pia kujitia moyo cha uwongo, ndio unakalia kukataa tu wakati nakuona kabisa unagain kweli big knoweldege kupitia posts angu. Jifunzeni kua na moy wa mbinguni wa kubariki siyo wivu na roho mbaya ya kujikausha wakati mambo safi unapata.

  Aya soma tena kwa taratibu hata kwa siku 2 my fundisho kwa Siyi na nyie wote kisha vipande 2 vyangu kwa Lwembe kisha ingia uwanjani/sinagogini kwa mahojiano KAMA UNADHANI UNAKITU cha ukweli kabisa kiunyume na yangu na kama unaweza nithibitishe mie nimekosea LAKINI kwa maana ya Neno la Mungu ktk hekima na uhalali wote, karibu na usipokuja nitajua umekubali Roho wa Bwana yu juu yangu kwa nguvu nyingi ktk kukufundisha ya kweli kabisa, sema kukiri unasumbuia na nature tu ya kibinadamu kama lwembe, hana kitu na napewa vitu, anajikausha kama vipo wakati vipi sana, so heavy and sweet and lovely. Nitakungoja U SHOW UP KUTHIBITISHA ULIYONIAMBIA LASIVYO UWE POROJO NAMBA ONE AU UKO SHALLOW KIJANA-Kubali tu usaidiwe/tusaidiane

  Press on

 76. Lwembe,

  (Siyi,-baadhi ya mambo/hoja zenu zinafanana, ivyo nawe soma majibu yangu kwake

  Ziragora-Karibu usome tujifunze pamoja

  Lwembe, ktk majibu/post zako kwa Ziragola, ni wazi haumjibu yeye tu maana umetumia plural maeneo kadhaa na pia mambo unayo-raise sasa nimeshawahi kujadili sana na wewe, kwaivyo mimi kuamua kuwajibika hata ktk yale umemu-address Ziragola wakati ndani yake unaongea na wengi, ni halali kabisa. Lakini hata ivyo, hata kama ungekua hujamu-address yeye tu na ungekua makini kutumia singular nouns/pronouns tu na hata kugusa yale tu ya Ziragola(kitu ambacho kingekua kigumu kwa kua tayari mnayoongea na Ziragola, tuliyaongea sana mengine directly na mengine indirectly-soma posts nyingi za nyuma juu huko hapa hapa na kwa mada hii hii), bado kwa kua LENGO KUU HAPA NI KUFUNDISHANA/KUSAIDIANA, ni halali kabisa, kabisa mimi kuchip in hata kama hujaniandika jina langu mie mwanzo wa post yako. Kwa misingi iyo, nina pitia posts zako zote 3, yaani mbili kwa Ziragola na 1 kwa Siyi kama ifuatavyo:

  Umedai, “Maneno yote yaliyomo ndani ya Biblia, bila kuondoa chochote wala kuongeza, katika ujumla wake, ndiyo yanaifanya Biblia kuwa NENO la MUNGU, ambalo Neno hilo ndiye Kristo.

  JIBU: Ukweli huo haufuti ukweli mwingine pia kua wakati Mungu analileta Neno hili, alitumia Watu hai si maiti au wenye mtindio wa ubongo! Walikua na hisia, akili, udhaifu/uimara, mila, desturi, waliishi ktk jamii,mfumo wa maisha na siasa/tawala, mapendeleo(preferences) zao binafsi, tone tofauti ktk kusisitiza/sema mambo, Elimu na uwezo tofauti, vipaji na karama tofauti, yote hayo ya Mtu yamejidhihirisha wazi wazi ktk maandishi ya Biblia. nk. Lakini pia ktk kutoa fundisho na ujumbe kwa vizazi vijavyo, Mungu aliruhusu ziandikwe Historia tu za kawaida za maisha ya Watu mfano Wafalme mbalimbali waliotawala, mambo yao na vituko vyao. Hata ungesoma Historia ya kawaida tu ya darasani kwa habari ya Taifa ya Israel na tawala za dunia, bado ungekua na vitabu vya kawaida kabisa vilivyoandikwa mambo ya Watawala wa Nchi au jamii zile. Nachokazana kufundisha hapa ni kujaribu kuwaambia wapendwa kua jambo la kawaida halimaanishi kua si la kweli. Si lazima kutunga/kuzidisha chumvi/ku-over spiritualize mambo ili yawe au tujisikia nia ya Ki-MUNGU kwelikweli! Hapana! ni kosa! Jambo la kawaida bado linaweza kua la kweli tupu na likatusaidia kimwili na kiroho pia.

  Tusichukulie kwamba, kwa kua Kitabu Biblia kina maneno ya Mungu basi tukapaaa sana mawinguni na kujisahau kujua ukweli huo naojaribu sana kusema kwako Lwembe na niliyomwambia Siyi ktk post iliyotangulia na siku za nyuma nilimgusia ilo Yusha na Mabinza. Msijisikie kua mnapungukiwa au mnapunguza kitu ktk Neno la Mungu kwa kuelewa icho nachowaambieni, si kweli! si kweli kabisa! SI MALAIKA WALIONDIKA BIBLE WALA SI ROHO MT ALIYEKUA NA KIDOLE NA MKONO ANAANDIKA BALI NI ROHO ALIWATUMIA WATU NA PIA WATU HAO HAO, WAKATI WANAANDIKA YA MUNGU, UANADAMU WAO UKAWA DHAHILI UMO-hii kweli, kweli, kweli kabisa na wala kwa kujua ivyo, haituondoi ktk imani, wala si kufuru na wala dhambi na haiondoi ukweli kua ndani ya Bible kuna maneno na matendo ya Mungu yamerekodiwa humo.

  Ooh my Jesus Christ! nyie WapendwaJamani, eleweni mnapofundishwa mambo very simple na clear facts/truths zenye ushahidi mwingi ktk Biblia iyo iyo. Biblia wala Mungu hawana shida na ilo ndio maana wako fair and open kuweka hadharani kila kitu namna iyo ktk Bible, ninyi mnataka kusaidia nini sasa? kuweka ukiroho artificial ambao haupo na wala Mwenyewe hakuuweka kinanma ivyo? Biblia inapokua na kumbukumbu tu-simply ni kumbukumbu kama kumbukumbu nyingine tu kuhusu Watu mfano Mfalme mmoja labda Daudi kuchukua mke wa mtu na kuua mumewe! Hii ibaki tu ivyo ktk urahisi wake huo huo, basi au dola moja inapigana vita na nyingine, ni rahisi tu iyo kumbukumbu ya Historia ya Watu na tawala za dunia ndani ya Bible, very clear! Shida ni nini? mnataka kuongeza nini? ukiroho wa nini hapo? Tumeyapata leo kwa kua yaliandikwa kama kumbukumbu za kifalme/rekodi za Ikulu/kasri pale na yakakakusanya na kukubaliwa yawemo ktk Kitabu cha Maandiko na yawe kwa ajili ya kutufundisha sisi tulifikiliwa na miisho ya zamani hizi, as simple as that.! Tusichokonoe au kusaka dhahabu ambayo haipo! Ilishaweka hapo tu kirahis kua Rais mmoja amezini na akaua na wakaandika taarifa iyo na leo tunaisoma, ivyo tu.

  Umeuliza maswali haya, majibu ni kama ifuatavyo:

  SWALI:Je, hawa “watu wa kiroho”, ndio wanaotusimulia kuhusu Mungu na watu na Shetani, kwa jinsi wao wanavyowafahamu hao?

  JIBU: Ndio na hapana!
  Ndio, kwakua yako waliyoandika kwa kufahamu kupitia kuishi nyakati izo mfano waandishi wa Ikulu/Makasri ya wakati wa Wafalme au kusoma au kusimuliwa na Baba zao Historia ya MUNGU wao ndio maana unakuta sentence kama Mungu wa Baba zenu …. Au Mungu mwenyewe kuwaambia wawafundishe vizazi kwa vizazi vyao au wengine waliona live na kusikia ivyo wakaandika mfano mzuri ni injili zote maana walikuwepo, wakaona ,onja ,sikia shuhudia, shiriki na wengine waliwauliza wale waliokuwepo na kuona mfano Luka.1:1-4 na Mdo.1:1-3

  Hapana, kwa kua wengine walifunuliwa moja kwa moja kwa njia ya ndoto,maono, kusikia sauti live au ya moyoni, akili na ufahamu kuvuviwa/nururishwa/angaziwa ivyo wakang’amua, kuchambua mambo na kuyaandika ktk upeo wa KiMungu na maarifa makubwa( mfano mzuri ni Paul).Kwa iyo, walijua na kufahamu baadhi ya mambo ya Mungu si kwa kuona au kuambiwa bali kwa kufunuliwa/ kuonyeshwa/ kuvuviwa.

  SWALI:Hawa “watu wa kiroho”, walikuwa na uwezo wa kuyajua mawazo ya Mungu, na ya hao watu, na ya Shetani, na kisha wakayaandika kama yalivyo?

  JIBU: Ndio na hapana!
  Ndio, kwakuaYAPO BAADHI waliona,sikia, shuhudia ivyo kirahisi kabisa wakajua na kuandika/kutusimuliwa! Hakuna kuweka kiroho-roho hapo-kuspiritualize ili iwe ya KiMungu zaidi, hapana! yenyewe kama ilivyo ni kweli tupu na yatosha! Maana ni kweli waliyaona na kuyaonja au basi waliyaelewa sana ndio maana wanayasimulia/shuhudia! Simple. Ni kama leo unapowashuhudia Watu mtaani waokoke, why? Ni kwakua unajua na una ushuhuda na umeonja au umefahamu sana kwa hakika icho unachowaanbia/wasimulia kwa dhati wakisikie na kukikubali, simple!
  Hapana, kwa kua YAPO BAADHI, hawakuyaonja, ona, sikia live kibinadamu bali ni MPAKA walipoonyeshwa/ vuviwa/ wezeshwa/letewa/angaziwa/nururishwa na Mungu mwenyewe-mfano Manabii na Ufunuo, baadhi ya maneno ktk Nyaraka za Paul na wengine.

  SWALI:Kwa vile Biblia ni muungano wa vitabu vilivyoandikwa na watu wa kiroho, vikiongelea Mungu na watu na Shetani, kwanini kiitwe ‘Kitakatifu’ wakati humo ndani kuna mchanganyiko wa maneno ya Mungu na ya Shetani na ya watu? Au wote hao ni watakatifu?

  JIBU: Ni kitakatifu kwa kua kuna Maneno na Matendo ya Mungu Mtakatifu na Watu wacha Mungu, vile vile kuwepo kwa maneno na metendo ya Wanadamu na Shetani yaliyorekodiwa humo, haimaanishi SHETANI mwenyewe live aliandika humo au mwanadamu ktk uovu wako-roho ile aliandika humo bali bado ni Wanadamu wacha Mungu waliotoa repoti izo za Wanadamu wenzao waliofanya maovu na aliyofanya shetani. Kuwepo kwa taarifa za maovu ya Wanadamu na Shetani ndani ya Bible hakukifanyi kiwe kichafu/kisiwe kitakatifu.Mfano: Kuwepo kwa Watu kanisani wasiomcha Mungu e.g Wakorinto kuna zinaa ambayo hata nje haikuwako, au machafu/madhaifu ktk makanisa yale ktk ufunuo, bado hakukufanya Kanisa lisiwe takatifu au la KiMungu ndio maana pamoja na hayo, bado wanaitwa watakatifu au Kanisa takatifu la Mungu. Wewe kua na tongotongo haimaanishi si mtu tena au Baba yako mzazi kua mlevi ua mwanga haimaanishi si Mzazi tena, ivyo ivyo Biblia ni takatifu hata kama umo ndani kumerekodiwa mambo mabaya/machafu ya devo na Watu.

  SWALI:Kulingana na kauli yako(Ziragola), sasa ninaelewa kuwa Neno la Mungu ktk maana ya Biblia ni mchanganyiko wa maneno ya Mungu na ya watu na ya Shetani, je, ni sawa?

  JIBU: Sema ivi kwa usahihi kua….Ndani ya Biblia kumerekodiwa Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani au Biblia inaonyesha Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani au Biblia inasimulia Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani au Waandishi wa Biblia wamelezea Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani, simple, right? so changua statement unayoona inakufaa na haikuletei ukakasi au pepo-pepo ivi lakini UKWELI ni huo na wala haubadiliki na wala kuwekea ukiro-roho artificial kwa mambo ambao Mungu mwenyewe hajayaficha ktk hata maneno na matendo yake mwenyewe live, ni kukosa au kukata ufahamu/elimu tu kitu ambacho hakibadilishi elimu iyo bali huyo asiye na elimu hiyo achague kubadilika ktk uelewe wake au aache na kubaki na fikra mgando za kiroho na kimwili ktk kuyaelewa mambo ya Mungu na Maandiko.

  Umeuliza, Paul, anaposema ni yeye basi ni yeye.Ni fafanulie zaidi huo muktadha (context) wa kauli yako hiyo kulingana na Fundisho lako( Ziragola)

  JIBU: Ziragora atafafanua bila shaka kwa namna aliotaka uelewe but mimi nasema kwa ujumla hapa kua, hakuna kitu kigumu hapo usichoelewa, unless hutaki tu basi, tuache kuzungusha mambo unnecessarily. The idea hapo ni kua yako maneno na matendo ya Mtu ktk Bible mfano ndio huo Paul anasema, ni yeye si Bwana au ni Bwana sasa, rahisi tu namna iyo, hakuna context zaidi ya kuelewa kua ktk kuyasema ya MUNGU, ya Roho pia na yake amesema, baaasi, tena kwa yeye mwenyewe live kusema, ‘’hapa sina cha Bwana’’ ili MIMI nasema….mbona rahisi tu! context gani spesheli inayotakwa kuundwa au kuspiritualiziwa hapo! ndio hayo matatizo ya kukuza vitu na kuvipamba wakati Mungu mwenyewe kaviruhusu viwemo kama vilivyo lasivyo alikua na uwezo wa kuzuia na kuhakikisha kila dot ktk Bible inasema kama wale manabii kua ‘’Bwana asema… au ni ‘’Mimi MUNGU WA MAJESHI nasemaaaa…… nk. USILAZIMISHE MAMBO,MTAUNDA VITU VINGINE HATARI TOKA MAMBO MARAHISI KTK BIBLE.

  Lwembe, UMEULIZA MASWALI HAYA TENA, MAJIBU YAKE NI KAMA IFUATAVYO:

  SWALI:Vifungu ktk Maandiko, ambavyo vinasema dhahiri kuwa “Hapa ni mimi…” au vyenye maudhui ya jinsi hii, ambavyo umesema ni maneno ya watu, vinamuhusu nani haswa, na kwa manufaa gani?

  JIBU: Vinawahusu yeye aliyesema, wale aliokua anasema nao na sisi tunaosoma leo ila kwa sisi wa leo, tuna uhuru kwa kuangalia na kufahamu kisha kuchukua yale yanafaaa/tunaweza LEO na kuyaacha ya kwake maana ni yake kama Mtu na si amri kwa vizazi vyote.Imekubaliwa ivyo ktk Neno hilo hilo ilipoandikwa, Maneno ya Kristo yakae ndani yetu richly ktk HEKIMA YOTE- Wakolosai.3:16( notice: Neno ‘’hekima yote’ is the key, ni very critical ktk kufahamu Neno na kuamua mambo) na pia kuyatumia kwa halali/usahihi-2Timo.2:15c. Therefore, kwa hiari au la, tunaweza amua kua yanatufaa au la ivyo tunaweza chukua au kaacha yale ya kwake kwa watu wake na ambayo amesema live kua ni ya kwake na si ya BWANA, maana mpendwa wetu huyo ni mtu yule kama sisi, hana uspesheli wowote kua labda ni malaika au nusu Mtu na Mungu na hata ukitaka kumfanya awe si mwanadamu kama sisi, atakucheka na ktk maandiko atakusuta maana alishajiweka wazi hata kulia kua anakaa ktk dhambi na ana mwili wa mauti unamsumbua, akitakacho hakifanyi na kile akichukiacho ndicho anafanya- Rumi.7:5-25-notice mistari ya14-25! ni mwanadamu tu yule kama sisi( Yakobo.5:17-18, Mdo.10:25-26, Galatia.3:15)na wao wanalijua ilo na hawana shida kutambuliwa ivyo maana ndivyo walivyo HAKIKA-si malaika hao!

  SWALI:Vifungu ambavyo havina maelezo ya kwamba ni nani anayeelekeza, ni Bwana au ni mtume mwenyewe kwa akili yake, hivi mnaviweka katika fungu gani, la watu au la Mungu? Hivi pia vinamuhusu nani, na kwa manufaa gani?

  JIBU: Vya Ivyo vipo tunavichukua kama ni vya wote na bado vipo, hatutavichukua kama vya wote kwa karne zote. Kuna vifungu visivyokua vya live kwa Mtu kusema ni yeye bado vinakua si vya wote.Kinachoongonza kukata mashauri hapo ni kwa kutumia KWELI nyingine za Neno ilo ilo kama hizi za ‘’kulitumia Neno la Mungu kwa halali/usahihi’’ au ‘’kwa hekima yote’’. Mfano maagizo( ACTUALLY NI MASHAURI-soma hapo-alikua anashauri) kuhusu KUFUNIKA KICHWA KWA MWANAMKE asalipo au anapohutubu(Notice: Wanawake pia Wanahutubu = Kufundisha (Yusha/Lwembe/Siyi/Mabinza-mtaongea nini tena hapo! ingawa hawaruhusiwi mbele ya Kanisa but kwingine, ruksa maana wana huduma/karama pia na wametolewa pia na RM kwa kazi izo- mnaona umuhimu wa kitu nawaambieni kila siku cha kulielewa Neno ktk mapana yake yote na sio kufia pale unapoyakutia-mengine yanagomaga-mlidhani hawana huduma/karama au Rm hawezi watoa wao pia kua Waalimu nk = kufundisha-1Wokor.11:1-16.

  Ivyo, hata kukiwa hakuna sentence kama ‘MIMI’ nasema wanawake funikeni vichwa’’ bado hekima toka kuzijua kweli nyingine ktk NENO hilo hilo, itatufanya kujua na kuamua kua ilo si ‘’NENO LA ALFA NA OMEGA, MIMI NIKO AMBAYE NIKO kua kilaaaa mwanadama past,present future kama ni wakike, afunge vitambaa, asema Bwana wa Majeshiiiiiiiiiiiiiiiiiii’’. Tuna uhuru wa kuyachukua kama yanatufaa leo ingawa yaliwafaa wale na pia hata tukiyaacha bado si kosa la kutupwa jehanum au kutulisha hasara labda ati tunakosa manufaa mazito sana ya kiroho! si kweli na kwanza kwa leo, wala hayapo na hayana mashiko kama yalivyokua na mashiko kwao kipindi icho ktk tamaduni izo

  SWALI: Pia kizazi chetu, na hao wengine waliotutangulia, ni kwa kigezo gani tunazitumia nyaraka walizoandikiwa kundi la watu specific, kulingana na hali walizokuwa nazo na uhusiano wao na hao waliowaandikia?

  JIBU: Kigezo kikubwa ni kujua lipi ni NENO AU UJUMBE WA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE PAST, PRESENT AND FUTURE NA YAPI NI YA NYAKATI, TAMADUNI NA VIONGOZI WA KIROHO WA WAKATI HUO-mfano Musa aliwaruhusu kuwatimua kwa taraka wake zao-Marco.10:1-9 kwa sababu ya hali halisi yaani shingo ngumu ya wapendwa wale ivyo kama kiongozi akafanya maamuzi/maagizo ambayo Yesu alidokeza kua hayakua ni mpango wa Mungu original-yaani lile haswaaaa la VIZAZI VYOTE, ndio hayo pia na Paul alikataza,agiza au kushauri baadhi ya mambo yeye pia kama kiongozi-1Wakor.7:17

  SWALI:Kwa kuwa ninyi mnaongozwa na RM, mkiwa katika Kweli yote, ni kwanini mnasita kuyaondoa maneno ya watu na Shetani ndani ya Biblia ili tubaki na Maneno ya Mungu tu ambayo ndiyo yenye faida (Yn 17:17)?

  JIBU: Ni Mungu mwenyewe ameruhusu kila kitu kiwemo kwa uwazi kabisa wala hana shida ili kupitia vyote tu, matendo na maneno ya Mungu, Watu na Shetani tujifunze mazuri nakucha mabaya. Na pia kwa kutumia Akili yenye afya ni rahisi kuwaza kwa kina ivi kua hata kama angeamua kubakiza yake tu Mungu, bado angehitaji Mtu si maiti kuyaandika na kama huyo ambaye angeandika angekua Mtu, anayewaza yake pia, mwenye akili, hisia, taste/tone, likes, dislikes, wishes, tamaduni,mila na desturi, siasa na mfumo wa maisha ktk Nchi au tawala anakoishi, elimu, ujuzi, vipaji, BADO hayo yote yangejitokeza ktk uandishi wa ya Mungu tu.Mfano: 1Wakor.7:39-40 Paul anatumia maneno haya..’’ ndivyo ninavyoona MIMI, NAMI NADHANI ya kua MIMI nami nina Roho wa Mungu.Ili hayo yasitokee kamwe, basi ni maiti ndio ingefaa na Mungu wetu ni Emmunel-pamoja nasi tukiwa hai kutenda kazi zake na si tukiwa tumekufa.

  Umesema uwongo hapa wakati unamjibu Siyi na mnajipamoyo wa uwongo na kweli..’Biblia ni Neno la Mungu! Yaonekana ni jambo jepesi, lakini ugumu wake nadhani nawe umeuona, ndivyo Injili ilivyoletwa!!! JIBU: Biblia kua ni Kitabu chenye kumbukumbu ya maneno na matedo ya Mungu, Watu na Shetani ndani yake ni rahisi sana kuelewa na Injili haikuletwa kwa mtindo wako Lwembe au Siyo wa kulazimishia mambo/ukiroho fake ktk mambo ambayo Mungu mwenyewe ameruhusu yawe very simple and physically clear.

  Umempongeza Siyi kwa Hii nukuu aliyoileta, kutoka 2Tim 3:16 na kusema ndilo Neno la Mungu, mwenye uwezo wa kuelewa na afahamu kwamba huo ndio Msingi tunaojengewa sisi

  Mwitikio: Tafadhari soma maelezo yangu kwakwe Siyi kuhusu andiko hilo. Itoshe kusema ivi kua ni kila andiko LENYE …. Yes, ni kila andiko AU ni Maandiko yote lakini fungua macho uone ivi kua ni kweli, ni KILA au ni kweli ni MAANDIKO YOTE lakini YENYE pumzi ya Mungu…..( hujaona/daka kitu hapo?) AU nitoe mfano huu yaani lazima uelewe Lwembe tu,hakuna kushindwa au kujifanya hamulewi, sasa ni ufundishaji tu 24/7. Sasa, Jezebeli alimtishia Nabii Eliya kua anamtenda kama alivyowafanyizia manabii wa baali’’, SWALI: Je hilo ni neno la Bwana na lina pumzi yake na huyo anayesema ndani ya mwanamke jeuri yule anayemtisha vikali sana Mtu wa MUNGU huyu, ni Roho wa Mungu? na statement iyo imevuviwa na Bwana wa majeshi eti eeee? Ha ha ha ha. Mtanielewa tu shule hi in JESUS name na Roho Mtakatifu is upon me hugely and actively to bring senses in here for his own glory amen.It has been and shall it be in his mighty power,alleluyah.

  Umesema vema ivi, ‘’Kuamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu, si jambo dogo, hilo ndilo pekee linaloweza kukufanya ukae katika Fundisho la Mitume. Mwitikio: Hilo lakini lisimaanishe kua hatuna nafasi ya kutafakari na kujua yapi ni ya Mungu kwa vizazi na tamaduni zote, yapi ni ya Mtu-tuchague kuyachukua au la na yapi ya devo tuyatupilie mbali.

  Umesema veme ivi, ‘’Kauli ya Kristo kwamba “Mtu hataishi kwa mkate pekee bali kwa KILA Neno litokalo katika kinywa cha Mungu” kwako inakuwa halisi, maana unakijua’’. Mwitikio: Yesu mwenyewe wakati anachambua na kutafakari maneno yake au ya Baba yake, alionyesha wazi kua ktk Marco.10:1-9, Musa alisema na kutenda jambo ambalo halikua ktk original plan ya Mungu. Kwa kua sisi tunamfuta Yesu kama kielelezo alfa na omega, wengine wafuate nyuma ya hapo, basi tusomapo leo neno, NENO LA MUNGU kwa macho hayo ya kujua ya Mungu, Watu na devo ni yapi, ndipo hapo, tutapata mkate halisi huo wa VIZAZI VYOTE

  Umekosea sana hapa..’’Basi ukisema neno hili Mungu hahusiki nalo, unakuwa umepungukiwa’’. JIBU: Si kweli katu maana Yesu ktk Marco juu hapo, ameonyesha kua lile alilofanya Musa lilikua la wale kwa situation yao, leo hakuna kuwatimua wake zetu isipokua kwa sababu moja tu.Huwezi kusema leo wanawake wetu wakiacha kufunika vichwa, basi kuna kitu kikubwa sana,sana cha kiroho wanakosa au kanisa hilo la wanawake wa ivyo ati watatupwa jehanum wote mara moja maana Mungu hana mchezo, anataka vizazi vyote, wanawake wote kufunika vichwa-ha ha ha ha ha au ati tukilacha ilo la Paul, tumepungukiwa mambo ya kutisha sana ya Ki Mungu! mmh! mnavitisho kama vya kiroho vile lakini siku zote napopima na Kweli au hekima ya Neno na matumizi halali ya Neno, mnayosema/tishia, yanapwaya matisho au matashi yenu, yanakua ni ya ivi ivi tu

  Umemuuliza Ziragola kua ni wapi ambapo Maandiko yanasema Paulo alikuwa anasimika makanisa ya kimila? Au ni wapi ambapo Mungu alikubali kuchanganya Mila na Neno lake?

  JIBU:Hakuna hata mmoja humu aliyesema kua Paul alikua anasimika makanisa ya mila! Haya ni maneno yako yenye lengo la kupotosha ukweli na ufahamu ambao umekataa kuupokea! Ila kwamba makanisa yalipotokea, yalikua katika Nchi, Jamii yenye mila na desturi na kwamba hata hao wanadamu/Kanisa wana mila na desturi zao, na tena baadhi ziliendelea kuenziwa nje na ndani ya makanisa, ni kweli tupu

  Kwamba Mungu alikubali kuchanganya Neno lake na mila, nitakupa mifano hii ya maandiko kisha amua case mwenyewe.

  • Mathayo.15:26= Yesu anamwambia Mwanamke Mkananayo kua,si vyema chakula cha Watoto kuwapa Mbwa! Watoto maanake Wayahudi/Wateule na Mbwa manake wasiokua Wayahudi/ Mataifa/najisi machoni pa Wayahudi

  • Mathayo.14:21=Wale waliokula walikua wanaume alfu 5 mbali na Wanawake na Watoto

  • Mdo.10:28-29 = Ninyi mnajua kua si halali Mtu aliye myahudi ashikamane na mtu wa Taifa lingine wala kumuendea lakimi Mungu amenionya nisimuite mtu awaye yote mchafu wala najisi, kwa sababu hiyo nalikuja nilipoitwa wala nisikatae….

  • Galatia.2:7-18= Walipoona nimekabishiwa Injili ya wasiotahiriwa ….,nilishindana na Kefa uso kwa uso maana alikua akila na mataifa lakini alijitenga walipokuja waliotahiriwa

  • Mdo.16:1-3=Paul anaamua kumtahiri Timothy kwa sababu ya Wayahudi waliokua wengi ktk ule mji na walijua baba yake Timothy ni Myunani ivyo walikua hawatahiri( ni hajisi/si kamilifu machoni pa Wayahudi sasa kwa kua Paul alitaka kumchukua katika huduma na ili akubalike, akamtahiri!

  • 1Wakor.7:17-24= Mtu ameitwa hajatahiriwa, hana haja ya kutahiri na aliyeitwa akiwa ametahiriwa, hasijifanye hajatahiri, kutahiri au kuto kutahiriwa si kitu

  • Wagal.3:28=Hapana Myahudi wala Myunani, hapana mtumwa wala huru, mtu mke au mume maana ninyi nyote mmekua mmoja ktk Kristo Yesu

  Unaamuaje swali/case yako? Aya jimalize/jiponye mwenyewe kwa mifano iyo na mingine mingi tu muda haunitoshi

  Ulimaliza kwa kutoa onyo la uwongo hili linaloonyesha mtu asiyependa kujifunza hata akipewa vitu vitamu vipi bado anajidai haelewi na ana kua na wivu tu kukubalii na kumbariki Bwana kwa kazi njema ndani ya mwenziwe mfundishaji! Umesema jambo sio sahihi ambalo nimeshakufundisha na kufundisha mpaka basi lakini leo umerudia ati ‘’’Mnapolikaribia Neno la Mungu, msije kwa akili zenu!!!’’

  JIBU: Nitarudia hoja zangu nzito mpaka hutaelewa tu-Mdo.26:25 Paul anasema ninasema maneno ya KWELI NA AKILI-reason.Kwa iyo leo usomapo baadhi ya maandishi ya Paul, ni ya Roho ( Ufunuo wa moja kwa moja) na pia ni ya AKILI-kasema mwenywe! Angalia kwa mfano anavyotumia common senses au reasoning/Akili au opinions ya kawaida kwa kufundisha mambo mfano-1Wakor.11:14-‘Je hayo maumbile/nature/ukweli halisia haufundishi ya kwamba, mwanaume akiwa na nywele ndefu ni aibu? Kwa maneno mengine alitaka wa-think/reason kuangalia na kuzingatia facts za kawaida za maisha haya haya. Hata, Mdo.17:28 anakua na ufahamu/Akili ya kurefer/ anatumia maneno/fact za hata mwimba mshairi wa kawaida kusupport hoja zake, tena angalia pia akili hii anayotumia kufundisha taratibu za kunena vema kanisani, anatumia njia ya comparisons to make sense to the people-1Wakor.14:7-8 anasema ‘’hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti ikiwa ni filimbi,kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kinubi? Au baragumu ikitoa sauti isiyojulikana,nani atajifanya tayari kwa vita? Vivyo ivyo na nanyi msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo, litajulikanaje? Maana mtakua mkinena hewani tu’’’. Somo maeneo mengi ya nyaraka za Paul uone revelations nyingi sana lakini pia ziko nyingi sana reasonings, thinking big, thinking of the thinking itself ie logic, powerful common senses,active IQ, professionality, shule/usomi wake au hata msome Dr.Luka ktk Luka.1:1-4 anavyosema mwenyewe kua amefanya utafiti na kupata ufahamu/taarifa za kutosha kujiridhisha toka kwa wale walioshuudia na sasa akaamua kuandika kwa mpangilio/utaratibu habari za Yesu.

  Napenda nikuambie kua kusema hautumii Akili uyaijiapo Maneno au Mambo kwa ujumla tu ya Mungu IT DOES NOT MAKE YOU SPIRITUAL, the opposite is very true! and it only serves to bring about sluggishness against the increase in the attainment of knowledge of God.Be informed therefore kua Akili zetu na vyote tulivyo navyo nje na ndani ya miili yetu ni tools ktk kumuendea, kumtumikia na kumfahamu Yeye na maneno yake, Usidanganye watu hata kidogo kua tumjiapo Mungu na Maneno yake, tuwe mbumbumbu au akili za uji au vichwa empty no charge! si kweli kabisa na huna hoja.

  Najua nimefundisha vema mno na kwa ustadi mkubwa, wala sitasubiri unisemelea ilo, ninasema mara moja kama Paul, kwa iyo, kama unadhani hujaelewa jambo kwa dhati katika majibu na mafundisho yote niliyokuambia leo, karibu na pia ruksa kama unadhani una solid hoja kushinda zangu, karibu pinga/kataa na usema sasa nami nitakusikia na kukusoma kisha kufundisha tena kwa nguvu sana kwa utukufu wa Yesu Kristo na kwa furaha yangu pia mfundishaji, Amen.

  Press on.

 77. Seleli, Ziragora na Sungura,

  Mnajikanyaga sana! Kisa ni kwamba mmeifanya mioyo yenu kuwa migumu sana, mpaka you miss the fun of the Gospel! Rafiki zangu, tunazungumzia Bible Land! Yaani, ingieni humo katika hiyo Nchi, acheni kuleta hadithi za kanisani kwenu!!!

  Seleli, umerudi tena na maelezo yako mazuri sana, lakini ni ya mtu aliyeikosa issue, na akauziwa replica ya kichina! Kwa kadiri ya hiyo repilica uliyouziwa, huo ufahamu, maswali yako, pamoja na hitimisho lake, vyote viko sahihi, bali vinakupeleka porini!

  Kimsingi mimi nimekuelewa vizuri sana, yaani hiyo namna YENU, ambayo kwayo mnajifikisha katika ufahamu mlionao, unaowapa “hekima” ya kuligawa Neno la Mungu, kutoka humo mkiyatenganisha ‘Maagizo ya Watu’ na kuyahalalishia vipindi au mahali, au mkiyakabidhi upepo uyapeperushie mbali; bali huo ni ubatili!

  Ukweli usiobadilika ni kwamba, Biblia ina vitabu 66 ambavyo katika ujumla wake vinaitwa Maandiko Matakatifu. Tena hayo maneno mnayoyaona humo katika Biblia, Mungu ameyahakiki mara saba, tena isitoshe ameyachagua hayo yawemo humo kutoka katika mabilioni ya maneno kama anavyoshuhudia Yohana, 21:25 “Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.” Jambo hili pekee lilipaswa kuwaonesha kwamba humo ndani hakuna neno linalo elea ovyo ovyo, yote yamehakikiwa ndipo tukaletewa. Sijajua ninyi mnaposoma hiki kifungu huwa mnaelewa nini? 2Tim 3:16
  “ALL SCRIPTURE IS GIVEN BY INSPIRATION OF GOD, …”!!! Ni kipi kilicho kigumu kueleweka katika Andiko hili? Mnaitukuza sana akili mliyonayo, sasa inashindwaje kukamata such an open sentense? Hivi ukiambiwa nioneshe “Maandiko”, kwa akili uliyonayo, naona utaanza kuhangaika kuhighlight kila fungu linalosema “Bwana asema” ndani ya Biblia yako ndio umuoneshe huyo anayekuuliza, lakini unapaswa umkabidhi Biblia yako tu, basi, hiyo ndiyo Maandiko!

  Pia naona mmekazana sana kuyadesturisha Maandiko, ngoja nikunukuu:
  “”… ndani ya Bible kuna maneno/matendo ya Mungu, kujua kua baadhi ya makatazo dhidi ya Wanawake, yalikua ni kutokana na mila, desturi na maongozi ya Kiroho na kiimani ya viongozi Watu Wanaume walioshikilia baadhi ya mila na desturi na sheria za dini/Musa kwa ukali kabisa na wala si LAZIMA kwamba alikua ni Mungu aliyewaambia ivyo.” Si ajabu Siyi anasemaga tusisome Biblia kama gazeti, maana matokeo yake ni kama maelezo yako haya, ni akili za mtaani kabisa za mtu aliyetoroka shule!

  Lakini, Taifa limezaliwa jangwani, ni watu wawili tu katika kundi lote lililotoka Misri ndio waliosalia katika kundi hili jipya, hili ambalo limezaliwa katika Torati, ambayo ndio Mila na Desturi yao, basi utawaingiziaje mila na desturi zisizoeleweka? Paulo hana mila wala Desturi zaidi ya Torati, na wala hajawahi kusimika makanisa ya kimila, labda haya yenu mnayoyasimika siku hizi! Kwahiyo kisingizio cha mila na desturi ni upotoshaji wa makusudi wa kusudi la Mungu, kwa Fundisho lenu hilo.

  Unajua Seleli, nyie ma “Bibi Arusi” mnafurahisha sana, kumbe hata huyo aliyewachumbia hamumjui! Hebu ziangalie kauli zenu, Seleli: “Role model wetu katika wanadamu wote ktk Bible ni YESU si Paul wala Musa!” na ya Ziragoza: “Kanisa la Mungu halina askofu, mchungaji wala mwalimu. kwa lugha ingine Mchungaji ni Mmoja ambae ni Yesu Kristo. Ni muungano wa Roho zilizookoka, na linaitwa Bibi Arusi.” Halafu kuna sehemu Seleli katika kuisistiza kauli yako hiyo ukanukuu kwa furaha kabisa, 1Kor 11:1 “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo” na kusisitiza kwamba Paulo mwenyewe amesema tumfuate Kristo!!!

  Halafu unaniambia eti una akili sana, kwamba wewe si chimp, wala si robot au viazi! Hivi hapo ni kweli kwamba Paulo anatuambia tumfuate Kristo? Hata hiyo kazi unayofanya, huko uliko ajiriwa, vyeti vyako siyo vya kufoji kweli??? Mbona mambo yaliyo wazi kabisa mnashindwa kuyaelewa, kweli nyie ni ma ‘Bibi Arusi’ au ndio mnaendelea na forgeries tu? Hahahahah….! Acheni usanii!

  Mnachekesha sana hapo mnapokomaa kujifanya eti mnamjua sana Kristo; Seleli yeye anasema huyo ndiye ‘Role Model’ wake, na Ziragora naye, huyo ndiye ‘Mchungaji’ wake! Sasa nikiwauliza, Who is it that presented to you, that whom you call your Role Model? What if they lied to you? By whose words was your Role Model presented? I mean by whose craftiness was your Role Model’s image transformed into a reality till you believe that you know Him by His personality? Au mlitazama sana “Sinema za Yesu” hadi akili zenu zimepindia kwenye hizo scenes na sasa mnaposoma habari za Kristo mindset zenu zinawarudisha huko nanyi mnamuona na kujiona mmekutana naye na mnamfahamu kabisa, hata mnajisikia kwamba huyu Paulo atatueleza nini sisi!!

  Sikilizeni enyi ma “Bibi Arusi”, Yesu Kristo, huyo aliyewachumbia ni Neno la Mungu, hayo yooote mnayoyasoma humo katika Biblia, mpaka haya yaliyoandikwa, “uniletee koti langu”, ni Neno la Mungu!!! Mungu ndiye anayetusimulia sisi habari zote unazozisoma ndani ya Biblia, si za watu tu na Shetani, bali mpaka mawe, bahari, punda, samaki, merikebu mitumbwi, vyote unavyovisoma humo ndilo Neno lake lililoamriwa tupewe sisi kwa ajili ya kujifunza na kutuongoza! Kama unataka kusoma vitabu alivyoandika Musa, basi nenda huko Misri, kama vipo utavikuta huko, lakini unayoyasoma katika Biblia, AUTHOR ni Mungu katika SIMPLICITY!!!

  Nimewahi kukuambia huko nyuma, kwamba hapo alipowaambia mitume kwamba mtakalo lifunga/fungua duniani, na mbinguni litakuwa hivyo, nikawaambia kwamba yaliyofungwa na kufunguliwa yamo humo humo katika Biblia, nadhani hamkuelewa, bali ndivyo ilivyo, maana iwapo Mungu hakuyafunga hayo mnayodhania ni maneno tu ya watu, kama “uniletee koti langu”, basi yasingepita katika ule mchujo yalioupitia “MARA SABA”! Hiyo ndiyo ART ya MASTER ARTIST, it is so simple till great thinkers like Seleli and Ziragora miss IT!! God approved every word, every comma, every bit of all that you see in the Bible to be His Word by The Holy Spirit!

  Ukivitaka vitabu alivyoandika Paulo, nenda kwenye maktaba za Kifarisayo kama vipo utavikuta huko, kwanza mtumwa analo neno lake? Wote unaowaona katika Biblia hakuna hata mmoja aliyejikurupukia kuifanya kazi ya Mungu kama ninyi akina Seleli, wenzenu walikamatwa wakawa watumwa wa Kristo, tofauti na ninyi ambao ni watumwa wa makanisa yenu, kwahiyo hata utumishi wenu unalinda maslahi hayo! Lakini 2Petro 1:21 inasema wazi kuhusu Neno la Mungu, “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na RM” basi yote unayoyaona katika Biblia ni huo unabii, umeletwaje? Kama unavyouona humo! Umeelewa Seleli? Mitume wanakuhakikishia kwamba, hilo neno wanalokuletea na la kinabii, 2Pet 1:19 “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi” sasa wewe ndg yangu unaposema “hili fundisho lilikuwa la lile kanisa tu sisi halituhusu” unalo neno la unabii nawe hata ulikate hilo neno la Paulo?

  Kwanza ukiisha sema kuwa oh, huyu ni Paulo tu, au oh, huyu ni Petro tu, unakuwa umekwisha mnyofoa viungo huyo Bwana Arusi wenu, ndiyo maana ninawashangaa ma “Bibi Arusi” ninyi mnaomnyofoa viungo Bwana Arusi wenu! Bwana Arusi ni NENO, nawe unapolipokea LOOTE bila kunyofoa chochote ndipo mnapokuwa Mwili Mmoja, “…naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”!!! Vinginevyo umechumbiwa na huyo roho aliyelipindisha hilo Neno, hata ikiwa ni dhehebu lako!

  Hivi mlipokuwa wadogo hamjawahi kusimuliwa hadithi? Kama ni babayo anayekusimulia hajawahi kukuambia katika hiyo hadithi kuwa simba akamwambia nyati labda; basi ukiulizwa ni nani aliyekwambia mambo haya, utasema simba na nyati??

  Hebu ngoja niwatazame kama mnalo mlilolielewa, ikibidi nishuke chini zaidi!!

  Gbu, “pasua kichwa” friends!

 78. Edwin Seleli,hongera sana kwa jitihada zako tena naona unabidii kabisa,na ninafikiri kila mtu amekupata vizuri sana.to my side naona uko sahihi kabisa kutokana na elimu yako ambayo sijui inatokana na nani.walio wa Kristo hawana muda wa kubishana ila kuishi NENO(kupambana na dhambi)sababu ndiyo itamufanya mtu kuuridhi ufalme wa Yesu Kristo.
  Mtu aundapo porojo huwa anatiririka sana hasa akikutana na watu wenya akili zao na msimamo,yaani kutiririka kwako kuna nikumbusha majadiliano ya Yesu na shetani(eti imeandikwa)
  Ikiwa Yesu mwenye asili ya mbinguni katumika na mitume 12 na kati yao hakua mwanamke,na hao mitume hakuna siku waliwezaka funzwa na mwanamke;itakua je kwa mimi nilie ichukua asili ya Kristo?
  #Seleli tumeisha jua HILA za ibilisi kanisani.mwanamke atabaki tu mwanamke na nafasi yake kanisani ipo,kama wakina Dorcas na wengine wakati wa mitume.
  Goodbye brother!!!!!

 79. Siyi,
  Lwembe, kuna baadhi ya hoja zinakuhusu, Mabinza na Yusha pia mtatenda vyema sana kwa nafsi na utumish wenu mkisoma pia.
  Ziragola-Karibu kwa ajili ya kujengana, usome pia.
  Napenda kutoa responses zangu kwa posts zako, namely ile moja uliyotujumuisha na zile 2 specifically kwa Ziragola kama ifuatavyo: Tafadhari wengine tuko very serious kazini/hudumani hapa, hoja inaletwa, inakua-cleared na wote na upande mmoja ukitaka maelezo, majibu, upande wa pili utekeleze mara moja au la useme kwa nini hautekelezi. Naomba tuwe very commited lakini pia mkipenda mambo ya mastori ya town na ma-by ways, uko nako nimo! ya serious na kudeal na issues,nimo! ya kuweka peupe kati ya serious stuff na mambo mepesi ya wepesi nako naelea kama kawaida, uchaguzi ni wako/wenu which flavour mnapenda, niko ready kudance kotekote kati ya real football na soft tennis ball- kama nikufundishana kwa utulivu sawa na kama ni mahojiano mazito nayo sawa maana yamo ktk Bible, ni watu kutosoma Neno na kujua mambo mengi tu kabla ya kuamua KTK hekima yote SAHIHI kua kitu fulani ni mbaya au la. Na asikudanganye mtu, mahojiano ni mashindano ya pande 2 kila mmoja ukiwa na upande wake na ukijua ni wa kweli na ukitaka kuufanya mwingine uacha wa kwake BUT KWA HOJA NZITO SANA, uende upande mwingine. Mahojiano( mashindano ya hoja) yanaweza yakawa ya tija au ya kupoteza muda na kukuza ubishi usioongeza thamani-nadhani tuwe ktk kundi la kwenye tija. Na bado nasisitiza/weka sawa kua si kila ubishi ni mbaya, ule wenye kukazania KWELI IWE KWELI kwa UKWELI-safi na ile inayokomaa tu ili mradi ni simba na yanga-mbovu, inachwa mara moja na mhusika kwa kuamua yeye mwenyewe au la, anabishwa kwa hoja matata sana na barabara kabisa mpaka yeye ajione live kua hana kitu na anapoendelea ndio utupu utakua dhahiri kwakua hoja nyingine na majibu kwa hoja zake, yataendelea kumiminika na kuweka wazi utupu huo.

  Umesema..’’Kimsingi Biblia nzima ni neno Mungu, tena lote, maneno yote yaliyomo ndani yake, yanafaa kwa mafundisho’’. JIBU: Ndio kwa maana ya Mungu kuwatumia Watu kuandika rekodi mbalimbali ya Matendo, Maneno ya Mungu, Watu wenyewe na Shetani. Kukazania kua ni Neno la Mungu lote, isitishie watu kwa kuwaaminisha kua KILA kilichomo ni Mungu alisema LIVE toka Juu au kilitelemka! Hapana, SI YOTE maana mengine, waliokuwepo waliosikia na kuona ya Mungu, Watu( Historia za Wafalme) na Shetani na simply wakaandika kwa/ au uku wakiwa na uwezeshwaji wa Roho wa Mungu bila wao kupotea/kupoteza Uanadamu wao wakati wanafanya kazi iyo kama akili, Elimu, kutofautisha/kurepoti mambo tofauti(Mathayo anasema vazi lilikua la rangi Nyekundu-(scarlet robe) Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 lakini Marco atasema ni la rangi Zambaro-(purple).Marco.15:15-17 hasa mstari 17. ,pia hata kuwaza,kutafakari,kukumbuka,kuulizia/kutafiti habari husika kwa wahusika/mashahidi ( e.g. Luka.1:1-4, Mdo.1:1-3) ivyo ni Neno la Mungu lote lakini pia lenye sehemu ya Binadamu kubwa tu sana.

  Umenukuu hili-2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu na ukasema kua unaipenda zaidi KJV imetumia neno ALL-16 All scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness: JIBU: Ni kweli kwa UPANDE MMOJA kwa maana ile ya jumla nimedokeza juu LAKINI kwa UPANDE WA PILI, upo ukweli huu hapo nimesema= SEHEMU YA MTU KABISA,KABISA- Mifano iko mingi sana labda nitoe mipya mingine kama huu:2Wakor.12:2-3, Paul anasema anamjua Mtu mmoja ktk Bwana kama ktk mwili SIJUI au nje ya mwili SIJUI ila Mungu anajua.( Notice: Napenda utafakari ivi-Imeandikwa ‘’Kiila andiko lenye Pumzi ya Mungu ni Neno la Mungu, lakini ingawa umesema unapenda Kiingereza, maoni yangu Kiswahili imeseme VEMA sana ingawa mimi pia napenda sana Kiingereza. Kiswahili imesema, KILA ANDIKO…(pause kwanza) halafu LENYE PUMZI YA MUNGU! wow!great is Kiswahili in this case! Napata ufahamu kua, Maandiko ni mengi na yanaeleza mengi ya Wanadamu, Mungu na Shetani au to MAKE IT EFFECTIVE, yanaeleza mengi ya ALIYOSEMA/TENDA Mungu, Mtu na Shetani ivyo tuwe waangalifu kabla ya kunyanyuka na kitu na kusema ni cha Mungu straight kama Neno la kutekeleza kwa vizazi vyote.Pia Ayubu.3:1-26, anapolaani siku ya kuzawaliwa kwake na kuichakaza vibaya sana siku iyo,hapa simply mwanadamu amerekodiwa ktk Bible alivyokua analalamika wakati yuko ktk hard time-kama Rais( Mfalme) Hezekia.Isaya.38:2-3, as simple as that, ivyo tu, right? indeed very simple, right? hamna uspesheli wowote hapo wala ukiroho wa ajabu au maneno yale la kulia-lia Kimaombi ya Hezikia ni NENO LA MUNGU WA MAJESHI, ALFA NA OMEGA, HAKUNA! Msing’ang’anizage mambo hayapo!!! Kama yapo, yapo na hayahitaji sisi kukaza misuli na kushapa kuyasemelea au tetea na kama hayapo, hayapo tu basi, simple! Over and out!!!!!!!!!!

  Umesema.’’Biblia ni neno la Mungu. Biblia nzima, yafaa kwa mafundisho ya kuwatia adabu watu wamrudie Mungu’’JIBU: Ni kweli kwa maana ile ile ya jumla nilivyodokeza pale juu YAANI ufaaji huo wa Biblia kuwafundisha watu na kuwatia adabu ni kwa kua kuna ukweli ule ule tena kwamba ndani yake kuna MATENDO NA MANENO YA WATU-walipokosea na kupatia tunajifunza AU ya Shetani-alikosea moja kwa moja hence hatujifunzi kwake bali tunamkwepa na na yako ya Mungu, yote safi tunameza past, present and future na ni cross or above borders, cultures, political and an individual systems.

  Umesema, ‘’Mungu ameiandika Biblia kwa (kwa njia ya uvuvio wa RM) wakinukuua watu, shetani’’ JIBU: Ni kweli ILA wakati wanafanya iyo kazi, hawakua mochwari bodies walikua na akili, hisia,kuona, kutafakari, tamaduni, mila,elimu, maamuzi yao binafsi,utashi VYOTE KABISA active na hai sana tena hata madhaifu yao kama watu-si malaika wale walioandika Bible, tu ndio maana Mathayo na Marco watatofautiana kuhusu rangi ya vazi lile Mathayo.27:28 Vs. Marco Marco.15:17 au Paul atasema mwenyewe ktk maandiko kua hana amri ya Bwana ila anashauri tu jambo-1Wakor.7:6,12,25 au anaTAMANI tu kama yeye kua wanaume wote wawe kama yeye (kutooa)-mstari 7 au atasema Yeye kama yeye HATOI ruhusu kwa Mwanamke kusimama na kufundisha Kanisa-1Wakorinto.14:34 connect na 1Timo.2:11-12( kwa maana tu rahisi-wala hakuna ufunuo hapo maridadi na adimu vibaya sana kuwatisha-tisha watu bure au kutoa picha mbayaaaaa kuhusu wanawake!

  Hapo ni simple tu kua …kwa jamii ile na tamaduni zile-ni kinyume na maadili mwanamke kufundisha-( I mean unapofundisha kitu chochote cha kiroho au kimwili), kutakua na kuelimisha mambo, kuelekeza mambo, kukemea, fanya maamuzi, onya nk sasa yote hayo Mwanamke ayafanye mbele ya Kanisa wakiwepo waume za wengine/wake,kaka, wajomba zao na kwanini hata wachumba basi wa kiume wasiwepo! Hence, Mwanamke asingeweza fanya iyo huduma mbele ya halaika mchanganyiko kama ile ila kwingine, ruksa kabisa na Biblia inakubali kwa mantiki nyingi tu-pitia post zangu ktk mada hii hii, so ni ivyo Ivyo tu basi, hakuna ishu kubwa hapo wala kua Mwanamke ni nyoka au yuko karibu na kulaghaiwa na devo ile mbaya au ati ni kwa tafsri ngonjwa ile ya kusema ni wadhaifu kwa maana zetu mbovu wanaume tunazozitoa kwa sababu ya kuathiriwa na mila au mfumo dume tu na wala si kwa mantiki ile 1Petro.3:7 alimaanisha, ukisoma kwa makini pale na kutafuta kweli nyingine nyingi za Bible(nilishatoa somo kwa hilo andiko hapa na mada ya yule Mlutheri Mwanamke kua Askofu-rejea posts zangu-ndio maana nawatakeni sana SOMENI VITU HUMU KABLA HAMJASEMA, INATIA AIBU KUSEMA MAMBO WAKATI YALISHAFUNDISHWA KWA KINA NA INAOYESHA MTU SI COMMITTED, ANACHEZA-CHEZA TU HUMU BY THE WAY maana hawezi kamwe kua relevant and solid participant kama anaibuka tu na kukimbilia kuandika ktk mada inayoendelea (labla kama ni mpya) bila kujiridhisha/familiarize yaliyopo/pita kwanza. Pia Paul atajileza alivyodhaifu kua hajui kama ni alimuona mtu yule akiwa ndani au nje ya mwili-2Wakor.12:2-3 au kua dhambi inaishi ndani yake na kwamba yale anayoyachukuia na hapaswi kufanya, anafanya na yale anayotakiwa kufanya, hafanyi na kwamba anajililia nani atamuoka na mwili wa mauti-Rom.7:15,17-25, nk, ningeza kuandika na kuandika, mifano ni mingi mno ktk Bible.

  Kuhusu ‘’Mtu anapoandika kitabu akanukuu vitabu, kauli nk za waandishi au wasemaji wengine, kile kitabu hakitaitwa kwa jina la mwandishi huyo eti kwa sababu kuna maneno au nukuu za watu wengine? Hasha!! Kitabu kitajulikana kwa jina la yule mwandishi’’ JIBU: Usitafute point kirahisi namna hiyo kwa kulifanya jambo la kawaida kua kuuuuuubwa kiroho wakati ni iko very clear! Sahihi ni kusema WAANDISHI WA BIBLE NI WATU-si mmoja na waliotumiwa na Roho!simple and truly balanced fact. Tofauti na ufahamu huu, mtatupeleka kule kwa imani ya wana wa Hajiri kua kiliteremshwa live kile kinovel chao! Chetu HAKIKUTEREMSHWA LIVE NA WALA ROHO HANA VIDOLE NA MIKONO BALI NI WATU WALIANDIKA WAKIONGOZWA/HUSISHWA/VUVIWA/ELEKEZWA/PEWA NA Roho, LAKINI, hiyo haiondoi ukweli kua Uanadamu wao KAMILI kabisa upo ktk Bible iyo iyo na katika maandishi ya umo umo.

  Mungu ana makanisa yenye desturi tofautitofauti pamoja na kwamba yana tumia Biblia moja!! JIBU: Mungu ana kanisa MOJA tu ila majina ni mengi ya makundi ya Kanisa hilo sehemu mbalimbali duniani. Kwa maana iyo, desturi na mila zitakua tofauti tofauti kwa Kanisa ilo ilo moja na majina ya makundi ya Kanisa ilo eg madhehebu kwa kua ingawa Kanisa ni moja lakini watu hao ni wa mataifa, rangi, lugha mbalimbali-hili mbinguni na duniani linafahamika – Mdo.10:34-35, Mdo.17:23-28, Ufunuo.5:9 na 14:6. Yale yote NDANI YA BIBLE ya Mungu kwa vizazi VYOTE past,present, future( MAANA YAMO HUMO) SHARTI yaheshimiwe na wote na yako juu ya mila, desturi, mipaka, rangi, kabila na utaifa na watu na na yale yote NDANI YA BIBLE ya Wanadamu( MAANA YAMO KWA HAKIKA, hayatakua kwa vizazi vyote ivyo KAMWE SI lazima yafutwe na kila mila, desturi, Mataifa, kabila na Watu.

  Umeuliza ivi, ‘’Kwani Biblia imetafasiriwa kwa kufuata desturi za maeneo mbalimbali? JIBU: Walioandika, waliandika pia kwa kufuata/kua –influenced mbali na Roho but pia Mila na desturi na sisi tunaosoma na kuhubiri/kufundisha, twapwaswa kabisa, kabisa kuzingatia kua kuna mambo ya mila na desturi ktk Bible kabla ya kuwaambiwa watu hili ni Neno au message ya Mungu kwenu/kwa vizazi vyote, chukueni na tendeeeni kazi lazima.Mfano wa mambo ya mila ni distance iliyokuwepo ktk ya Wanaume na Wanawake hata ktk mikutano wasihesabiwe mpaka ya YESU mwenyewe, kufunga vitambaa vichwani, mwanamke akitokwa damu, mwenye ukoma ni najisi ivyo anatengwa/ jitenga , ubaguzi wa kitaifa na kikabila eg Wayahudi na Wasamalia/Mataifa( Yoh.4:1-26 story ya kisimani), Yesu kumjibu Mkananayo kua si vema chakula cha watoto kumpa DOG-Mathayo.15:26

  Press on(Una jambo hujaelewa/ pinga/ kataa/kubali kwa furaha na kutukuza utendaji wa Roho Mtakatifu juu yangu kama Yesu alivyosema wazi kua yuko juu yake-Luka.4:17-19 ivyo si kujidai/gamba bali ni madhara ya Watu kukariri au kukosa ufahamu wa Maneno ya Mungu ili kuweza amua/ona/hukumu mambo mbalimbali, basi yote sema na unakaribishwa.NB: Responses zinazokuja ni kwa Lwembe kwa hoja za Ziragora.

 80. Lwembe, Siyi, Yusha na Mabinza(ninalo neno/fundisho nanyi nzuri na la ukweli tupu)
  Ziragora- karibu kusoma hii pia.

  Lwembe, Katika majibu yako kwa Ziragora, mambo 2 yamenifanya nirudi hapa: kwanza, umesema unapenda sasa ujifunze zaidi namna YETU wapendwa, labda inaweza kuwa na nuru zaidi na hivyo kusaidia wengi wetu na Pili, baadhi ya hoja zako kuhusu ndani ya Biblia kuna maneno na matendo yaliyorekodiwa humo ya Mungu, Watu na Shetani, umegusia yale niliwahi kuchangia sana siku za kwanza na kati lakini jinsi ulivyosemelea ni kama hujaelewa au hunapinga tu bila hoja ya kueleweka. Sasa ni muhimu nikawajibika kama ifuatavyo ktk kazi hii ya kufundishana NENO LA UZIMA kwa Utukufu wa Mungu. Nitatumia njia nyingi za ufundishaji na natumaini utaelewa kama kweli una dhati ya kuelewa, lakini hata usipoelewa iwe kwa dhati au makusudi, BADO nitafurahi kueleza tena na tena labda kwa kurudia yale yale lakini kwa upako tofauti au kuongea mapya kwa mbinu nyingine bora za ufundishaji na kushare Neno ilimradi tu, kila jitihada nitaifanya kuhakikisha, ya KWELI( truth) na ya UKWELI HALISIA-hasa ule usiopingana na Neno/Kweli( fact), yanaeleweka na ya kawada tu, yasiyo ya hoja na akili/ufahamu sahihi wa mambo, yanakwisha kabisa nguvu yake. Ninaanza seminar/fundisho kisha nitaleta responses zangu kwa posts zenu Lwembe na Siyi.

  Fundisho
  Kuna uwezekano pengine mmeelewa concept lakini hamjaelewa au mmeshituliwa na kugha tu. Labda nilivyoanza siku za mwanzo kusema hili jambo kwa kutumia lugha hii, ‘’Biblia ina maneno na matendo ya Mungu, Shetani na Watu’’ pengine iliwashitua na mkaaona mpendwa Seleli kusema ivyo, ni kufuru kubwa! Ukweli ni kwamba hakuna kufuru yoyote na ni swala rahisi sana la kuamua kuelewa tu yaani kupata ufahamu, maana hata kama mtakataa ufahamu, bado kweli/fact, haibadiliki. Kwa mantiki iyo, sasa napenda niwaletee sentences zifuatazo! Tafadhari someni kwa utulivu wa rohoni na wa akili hii hii ya kawaida ambayo mnaikataa kua haifai kutumiwa wakati wa kujifunza, kutafakari NENO na mambo ya Mungu, kisha jibuni maswali 2 chini:
  (a) Biblia ni Kitabu chenye Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani

  (b) Biblia ina Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani

  (c) Ndani ya Kitabu cha Biblia kuna Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani

  (d) Biblia ni Kitabu kilichorekodi Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani

  (e) Biblia ni Kitabu chenye Maneno ya Mungu yenye kueleza Matendo na Maneno ya Watu na Shetani

  (f) Biblia ni Kitabu chenye Maneno na Matendo ya Mungu tu.( yaani kwamwe HAKUNA KATU taarifa/story za kweli/mambo ya waliyofanya na kutenda mazuri au mabaya ya Watu na Shetani humo Kitabuni)

  (g) Biblia ni Kitabu chenye Maneno na Matendo ya Mungu na Watu tu.

  (h) Biblia ni Kitabu chenye Maneno na Matendo ambayo Mungu aliwatumia Watu kuandika taarifa/story za kweli za Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani

  (i) Biblia ni Kitabu chenye Maneno na Matendo ya Mungu ambayo Mungu aliwatumia Watu kuandika Maneno na Matendo ya Mungu tu na wala hao Watu kamwe hawakuandika Maneno na Metendo ya Wanadamu na Shetani

  Maswali:
  MOJA: Ipi/zipi kati ya izo juu, mnadhani inawakilisha vema kile tunachojadili kuhusu Matendo na Maneno ndani ya Biblia
  PILI: Kama katika izo juu, hakuna yoyote inayowakilisha kwa usahihi kuhusu Maneno na Matendo ndani ya Biblia, taja yenu

  Kwa kuzingatia hayo juu, napenda kwa MAKUSUDI KABISA NA nia BORA HASWA ya kusaidiana mambo hapa, KUONGEZA au KUJIBU MASWALI YOTE ambayo Siyi ktk post yake hata yeye anajua hakuyatendea haki maana amejibu jumla-humla na kwakweli hakua serious! HUWEZI ACHA KITU/VITU VIMEKUA RAISED, VERY SERIOUS ONES ILI KU-CLEAR THINGS, HALAFU UKAKIMBIA-KIMBIA TU KTK MAJIBU. Tafadhari sana specifically Siyi na Lwembe na generally, yeyote anayesoma mada na mijadala hii, MUWE MNAJIBU HOJA.Na labda nisema ivi, kwakua nina uzoefu sana sasa ktk mijadala ya humu kua baadhi ya watu hawawi committed kudeal na issues, kuwajibika kwa dhati kushughulika na mambo ambayo upande wa pili umeweka mezani na kwa kua, kwa kukwepa kuwajibika ivyo, kunaleta usumbufu wa kurudia-rudia baadhi ya hoja/maswali na kwa kua, kwa kupuuza kujibu hoja, inaharibu kusudi zima la kufundishana, NITAPENDA KUKUBALI KWA MOYO USUMBUFU huo na KUHAKIKISHA KUA MASWALI HAYAKWEPEKI KAMWE- yatarudiwa na kukumbushwa kila mara uko tuendeko KAMA YATAPUUZWA MAANA NAJUA YAKIJIBIWA KWA DHATI, TUMEMALIZA TATIZO NA LABDA KUKWEPA KUYAKABILI, INA MAANISHA WAHUSIKA WANAJUA KWA NINI HAWATAKI KUYAJIBU-ni ishara kua wanaelewa ila tu sasa wanapenda mambo yasiyoisha just for funny-(which is good anyway to enjoy and laugh-I like it too) lakini pia ni kwa ubishi tu tena ule mbaya usio na tija/hoja/grounds. Lakini pia nimegundua kuuliza maswali/ku-raise hoja, ni njia imara sana kumumlika Mtu ili yeye mwenyewe na wasomaji wajue, anafanya makusudi na hana kitu na sasa basi tu ni mambo ya by the ways in the debates and sharings here, hence nitaidumisha kweli kweli hii ya maswali, inaweka wepesi wa mtu peupe na labda kwa njia hii, itatusaidia kupitisha fundisho na kuhitimisha vema.

  Mathayo:4:1-11=Yesu anaongozwa na Roho kwenda kujaribiwa, huyo anaerepotiwa kuongea na kutenda ktk mistari 3,5-6,8-9 ni SHETANI
  Yohana.8:1-11= Kafumwa ktk uzinzi, ktk mistari 11a, ni MTU(mwanamke) anajibu swali la Yesu
  1Wafalme.18:30-37= Eliya na manabii wa baali, Ni MTU huyo ( Eliya) amuomba Mungu ktk mistari iyo
  1Wafalme.19:2= Mfalme Ahab anamueleza mauji Eliya aliyofanya kwa mabaali, kisha mstari wa 2 ni MTU(Mwanamke Jezeberi) ana apa kumfanyizia Eliya
  2Samweli.11:1-17= Ni MTU( Daudi) huyu analala na mke wa Mtu, anamlengesha mume wa mtu afe vitani
  Mwanzo.20:1-13, 26:1-10 = Ni watu hawa, wanaulizwa kuhusu wake zao, wanasema ni dada zao.
  Ayubu.1:7,9-11, 2:2,4-5,7 =Huyu anaongea hapo na kumtandika Ayubu na majibu ni SHETANI .
  Luka.8:30= Anayesema hapo kua yeye ni Legion ni yule PEPO/SHETANI

  Marco.5:9bc,10,12-13abc=Yanayongea hapo kua yafukuziwe kwa nguruwe na yanayowaingia nguruwe na kuwapelekesha hadi baharini ni MAPEPO/SHETANI

  Mdo.16:17dc= Yule kiumbe wa uaguzi ndani ya Mjakazi yule aliyesema maneno yale ni PEPO/SHETANI

  Mdo.19:15-16 = Huyo aliyeongea na kuwaweza wana wa Skewa Myahudi Kuhani Mkuu- kuwapiga/rarua na wakakimbia uchi ni MAPEPO/SHETANI
  Hesabu.20:10= Huyo aliyekasirika sana hapo na kuwaita kondoo zake ni waasi ni MTU
  Yoshua.24:14-28 = Huyo anayeongea hapo na hao wanaongea hapo ni MTU/WATU

  KWA MSINGI HUO, YAFUATAYO NI MAHITIMISHO THABITI KABISA NA KWELI TUPU.
  • Biblia inaonyesha wazi matendo na maneno ya Mungu, Watu na Shetani

  • Tunaposoma Biblia, si kufuru hata kidogo kutafuta kujua na kuangalia lipi ni tendo na Neno la Mtu ,Mungu au shetani

  • Kwa kua kuna sehemu ya Watu ktk maandiko basi hao watu waliishi duniani kwenye mila na desturi na taratibu nyingine za kimaisha

  • Hivyo si ajabu na wala haipunguzi nguvu kua ndani ya Bible kuna maneno/matendo ya Mungu, kujua kua baadhi ya makatazo dhidi ya Wanawake, yalikua ni kutokana na mila, desturi na maongozi ya Kiroho na kiimani ya viongozi Watu Wanaume walioshikilia baadhi ya mila na desturi na sheria za dini/Musa kwa ukali kabisa na wala si LAZIMA kwamba alikua ni Mungu aliyewaambia ivyo.

  • Kwakua ni ivyo, basi baadhi ya waliyosema/kataza Watu( si Mungu), si LAZIMA tuyashikilie mpaka kufa kwa vizazi vyote past,present and future kama NENO LA MWENYEZI MUNGU LA MILELE kwa wakati na mila na jamii zote duniani bila kujali maeneo yao, culture zao.

  Mshangao: Ivi kweli mpaka hapo, kunaweza kukawa na yeyote ambaye HAJAELEWA katu? Kweli? kwa mtiririko wa fundisho kama hilo? Basi tutakua tuna tofauti kubwa sana ya masikitiko ktk habari ya uelewa kwenye fahamu/ akili za kawaida na za rohoni kwa mambo ya Mungu na Neno lake

  Naishia hapo kwa sasa, karibuni kwa jambo lolote ambalo hamjaelewa bado( KAMA KWELI KABISA LIPO). Kama mmeelewa fundisho hilo mbarikini Bwana na ivyo tutakua tumemaliza hoja hii kwa uzuri kabisa na kisha kuweni waungwana kwa kua-appreciate tu, wivu ule mbaya ni roho nyingine.

  Itafuata post ya majibu yangu kwa posts zenu Lwembe na Siyi( yale mambo yangu ya ‘nukta kwa nukta checking anointing’’ of your posts’’)

  Press on.

 81. Ziragora,

  Ninakushukuru mpendwa katika jitihada yako tunapoitafakari Biblia, ili kujua kwa uhakika ni neno la nani! tena naona na wewe sasa umekuwa mjuzi wa “kuandika mingi”, lakini nafikiri sasa unayo mingi ya kuandika!

  Kwa kadiri ya maelezo yako, naona ni yenye kujichanganya changanya kwa kiasi fulani. Kwamba nilipozungumzia “walimu”, nimekushangaa jinsi ulivyotaharuki, na kunionya kwamba nisiwasikilize hao. Huenda hapo ndipo lilipo chimbuko la tofauti zetu. Maana kama unaniambia nisiwategemee hao ambao Mungu amewatayarisha kwa kazi hiyo, ni nani basi atakayenifunza? Maana Biblia unayoniambia niitegemee hiyo ndiyo inayoniambia kuwa Mungu, “… alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu…” (EFE. 4:11-12)

  Sasa, utakamilishiwa wapi iwapo umewakataa wote aliokuletea Mungu? Hili pekee laonesha kwamba wewe huiamini Biblia! Maana ni nani awezaye kuyajua mawazo ya Mungu kama si Roho wake, huyo ambaye yu ndani ya huyo “mwalimu” ili ayafunue yote yaliyofichika?

  Unasema, “Kanisa la Mungu halina askofu, mchungaji wala mwalimu. kwa lugha ingine Mchungaji ni Mmoja ambae ni Yesu Kristo. Ni muungano wa Roho zilizookoka, na linaitwa Bibi Arusi.” Je hili jambo unalonifundisha, si kinyume na hiyo Efe 4:11-12? Kwanza utawezaje kuokokea rohoni ilihali mwili ungali kifungoni?

  Nataka nikwambie kwamba hili ni Fundisho la uongo litokanalo na “roho” zidanganyazo, hizo zenye kushawishi dhidi ya Neno la Mungu, kama unavyoiona kauli yako ilivyo kinyume na Neno la Mungu!!! Tena wamekudanganya kwamba Neno la Mungu halina Fundisho (Doctrine), kama unavyokiri hapa, “Lakini tunalojadili ni makanisa yanayoonekana kwa macho, ambayo yana doctrines, …” Bali Kanisa liwe la rohoni au hili linaloonekana kwa macho ya nyama, yote yapaswa kuwa na “Doctrine”; litazame Kanisa la Kwanza, hao walioingia siku ya Pentekoste, Mdo 2:42 “Wakawa wakidumu katika FUNDISHO LA MITUME …”!!! Unaona, wewe mwenyewe hapa unafundisha “doctrine” ya kulirahisisha Neno la Mungu kwa kuliondoa nguvu yake hapo unapolifanya liamulike kwa Desturi na Mila; “…sione vibaya mwanamke akifundisha. Hili jambo halinichanganye hata kidogo kwani si Amri, ni desturi tu.”!! Nimekuuliza, ni wapi ambapo Maandiko yanasema Paulo alikuwa anasimika makanisa ya kimila? Hujanijibu! Au ni wapi ambapo Mungu alikubali kuchanganya Mila na Neno lake? Vueni viatu vyenu Ziragora mnapolikaribia Neno la Mungu, msije kwa akili zenu!!!

  Hakuna Bibi Arusi nje ya Neno la Mungu; huo mchanganyiko wa Neno la Mungu na Mila na Desturi, hauna uwezo wa kumzaa Bibi Arusi, ni michezo ya kuigiza mnayoifanya! Ni Fundisho la Mitume pekee lenye uwezo wa kumzaa Bibi Arusi, lilimzaa wakati wa Kanisa la Kwanza, litamzaa na leo hii tena, na wakati wote mpaka Bwana atakapokuja!!!
  Ngoja niishie hapa kwa leo ili nisiandike mengi!

  Gbu!

 82. Siyi,

  Kwanza, nimefurahi sana ndg yangu, kwamba unakielewa unachokisema: Biblia ni Neno la Mungu! Yaonekana ni jambo jepesi, lakini ugumu wake nadhani nawe umeuona, ndivyo Injili ilivyoletwa!!! Hii nukuu uliyoileta, kutoka 2Tim 3:16,
“All scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness” ndilo Neno la Mungu, mwenye uwezo wa kuelewa na afahamu kwamba huo ndio Msingi tunaojengewa sisi ambao hatujawahi kuwa na manabii wala hatukumjua Mungu, nalo Neno hilo ni la Mitume, wamelileta kwetu kwa uvuvio wa Mungu ili nasi tuweze kupokea kama Wayahudi!

  Basi jambo la kuamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu, si jambo dogo, hilo ndilo pekee linaloweza kukufanya ukae katika Fundisho la Mitume, uonyeke na kufunzwa na kuongozwa katika Haki. Biblia yoote inapokuwa ndilo Neno la Mungu kwako, pia ile kauli ya Kristo kwamba “Mtu hataishi kwa mkate pekee bali kwa KILA Neno litokalo katika kinywa cha Mungu” kwako inakuwa halisi, maana unakijua “Kinywa cha Mungu” ni kipi, Manabii na Mitume!! Basi ukisema neno hili Mungu hahusiki nalo, unakuwa umepungukiwa, na aliyepungukiwa ana shida katika Imani!!!

  Gbu brother

 83. Ziragora,
  Kwanza, Nashukuru kwa kuniamndikia specifically kaka. Pili, niombe samahani kama umekwazwa na mimi kukichambua kiswahili chako!! Ni kweli kabisa hata mimi si mkamilifu katika yote, likiwemo na suala la lugha. Ni shida tupu ndg yangu. Ni ajabu kweli niliyoifanya ya kuona kibanzi cha Ziragora, nikasahau cha kwangu!! Nisamehe mno kama nimekuudhi kwa hilo. Tuendelee sasa.
  Suala la Biblia na maneno ya watu, shetani nk, nafikiri tumelimaliza kabisa na limeeleweka vyema sana. Shida yangu nakuona unatumia hisia sana Ziragora. Unasema huoni shida kuwaona wanawake wakiwa viongozi au wakihubiri ndani ya kanisa; Una aya za maandiko zinazounga mkono hoja ya utetezi wako huo? Kwa nini unasema ni masuala ya desturi tu za mahali husika? Kwani Biblia imetafasiriwa kwa kufuata desturi za maeneo mbalimbali?
  Sina maana kwamba nawakandamiza wanawake. Hasha. Nawapenda sana wanawake na kuwaheshimu pia. Najua mbele za Mungu, wanaume na wanawake ni sawa. Ninachozungumzia mimi, ni ule mgawanyo wa majukumu/mamlaka tu!! Kibiblia unavyoisoma wewe, majukumu ya mwanamke na mwanaume yako sawa? Naomba ulete dondoo za kimaandiko rafiki. Acha kuzunguka m-mbuyu!! Maongezi haya, yako kwa ajili ya kujifunza. Huenda kweli sina uelewa sahihi katika hili. Naomba unisaidie sasa ndg yangu.
  Wakatabahu!!

 84. Ndugu Siyi,

  Nimekuandikia specially first kwani ne vema nikuheshimu.
  Kwa upande mwengine nakujulisha kama hata siasa kimataifa imekataza kuzarau mtu ukilenga lugha yake, rangi yake au nchi yake. Sasa kam sisi tuliyookoka tunafanya mambo kam yale, je tutakuwa mfano gani kwa mataifa? Mada si kiswahili ya Tanzania(vijijini au mitaani), Kenya, Congo, Uganda, Burundi, au kwenye border hapo ukichanganya masemi mawili. Usifikiri literature unayoitumia is very nice. Lakini tunachukua mda tukuelewe, not as we want but as you wrote. Nadhani hii niliyizungumuzia tena, nikisema tuone tunaletaje majibu kwa wandugu zetu. Kuna neno lingini ndugu Siyi, neno “sorry” si nzito kusema kwa mukristo. Hapa hatupo kwenye uwanja wa mapambano, ni uwanja wa maongezi. Sasa kam husikii kwa nini uendelea andika? Nadhani ungeliniomba nirudilie niliyoandika hata ktk lugha ingine nyingi; bila shaka ningelisikia vizuri zaidi.

  Kwa andiko lingine, sileti kwani umepata ya kutosha. Shida ni kufikiria tafsiri pahali pa kulizingatia lile neno. Dawa si andiko lingine. Ikiwa ni vile muislamu anaetufwata atasema Biblia inajipinga yenyewe. Tunapoelewana kam Biblia yetu haikuanguka toka mbinguni, kama iliandikwa na watu na kama hata Shetani tunajua uwepo wake na hila zake kwani ameandikwa ndani ya Biblia, kam Shetani hahusike kwa uandishi wa Biblia, kam Shetani anatetemeka mbela ya Biblia, kweli this is not clear? Isitoshe, sisi sote tumeelewana kama waandishi wa Biblia ni wa Kiroho, na tukasema kama walisema kweli. Hii kweli ya Biblia ndio inaonyesha nguvu za Mungu. kwa nini Paulo asukumwe kusema tu “ingelikuwa heri watu wawe kama yeye” na wala hasemi kam ni amri kuwa sawa naye? Huone tofauti kati amri ya Mungu na neno la mtu? sasa kam huyu mtu aliitikiwa na Mungu aandike vile, sisi hatuna ruhusa ya kuondoa neno aliloandika. Hata hivi kuna makanisa zinazofwata lile fundisho kam wa katoliki wanaosema kam kuwa padri au askofu au pope inafaa mtu awe bila kuowa!!!! Sasa hawa hawaseme kam wengine wanaoowa ni wenye dhambi. Vile vile hatuwezi sema kam wao wanakosea kwa kutoowa. Yote inatokana na KWELI ilio ktk Biblia, inayotuonyesha hii ni maisha ya mtume fulani na ile ni amri ya Mungu. Na Biblia inasema “Mutajua kweli na kweli itawaweka huru”. Neno lote liitwalo amri kutoka Mwenyezi Mungu linapaswa tekelezwa na wote,

  Kanisa la Mungu halina askofu, mchungaji wala mwalimu. kwa lugha ingine Mchungaji ni Mmoja ambae ni Yesu Kristo. Ni muungano wa Roho zilizookoka, na linaitwa Bibi Arusi. Lakini tunalojadili ni makanisa yanayoonekana kwa macho, ambayo yana doctrines, na namna mbalimbali ya kuabudu katika kumuogopa Mungu.
  Kwa mfano, mim ninayeongea, nashiriki kanisa ambalo wanawake hawafundishe na wala si wachungaji. Lakini sijasikia hata siku moja Mchungaji akiwakataza kufundisha na kufwatana na Biblia sione kwa nini mwanamke asifundishe. Na ninaposhiriki kanisa lingine(nikiwa kwa mfano safarini), sione vibaya mwanamke akifundisha. Hili jambo halinichanganye hata kidogo kwani si Amri, ni desturi tu. Kushiriki kwangu ktk kanisa ya pahali haina uhusiano na kuwa ndani ya Bibi Arusi. Au Mchungaji wangu, hata angelifanya kosa, hili kosa halitingise uwepo wangu ktk Bibi Arusi. Biblia inasema “ategemeae mwanaadamu na alaaniwe”

  Nashukuru tena ndugu yangu, na Mungu wa Mbinguni akubariki.

 85. Ndg Ziragora,
  Kwanza nikushukuru kwa majibu, kwa kadri ya namna ulivyonijibu, asante sana.

  Kwamba Biblia imeandikwa na binadamu, hilo sioni kama lina leta shida sana, maana twafahamu kwamba hata Mungu alipomaliza kuumba, bado kulikuwa hakuna wa kuilima ardhi, na hivyo akamfinyanga Adamu na kumkabidhi kazi hiyo. Kwahiyo jambo la kuandika ninaamini liko katika maudhui hayo pia.

  Lakini tunaposema “ndani ya Biblia yamo maneno ya Mungu, ya watu na ya Shetani” si sawa na kusema “Biblia inaongea juu ya Mungu, Watu na Shetani”! Kwa maana kauli ya kwamba “ndani ya Biblia yamo maneno ya Mungu, watu na Shetani” ambayo ndiyo inayozungumziwa toka huko tulikoanza na mada hii, inatatanisha katika kufahamu kwa uhakika wazo lililoandikwa ni la nani, la Mungu au la mtu aliyeandika au la Shetani? Na pia halikubaliani na Msingi tuliojengewa ili kuweza kuipokea Biblia kama Neno la Mungu. Hebu utazame huo Msingi, 2Tim 3:16
  “All scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness”

  Kwahiyo iwapo mtu ataichukulia Biblia kuwa ina maneno ya Mungu, watu na Shetani, katika namna ya kwamba mawazo ya hao yamo humo, basi itambidi atenganishe kwanza kipi ni Scripture na kipi ni maneno ya huyo Shetani na watu, bali kifungu hicho kinasema MAANDIKO YOOOOTE, yameletwa kwa uvuvio wa Mungu! Kwahiyo licha ya kuonekana kibinadamu sana, twapaswa kuyapokea katika jinsi yalivyoletwa, maana twafahamu pia kuwa yako hivyo ili kuwakwaza wengine, lile jiwe la kujikwaa walilowekewa!

  Juu ya hayo bado tunao uhuru wa kulipokea kama Neno la Mungu katika ukamilifu wake au kulifanya tunavyotaka, yaani kulisulubisha tena, kama mwinjilisti

  kuyaamini haya tunayoyasoma ktika Biblia kwamba yanatokana na mtazamo wa mtu tu kama yeye, au ni Shetani ndiye aliyeyaleta au ni ya Mungu?

  Kwahiyo tunaposema maneno

 86. Wapendwa,
  Ziragora, Lwembe, Seleli
  Ziragora, nimefurahishwa sana na maelezo yako yakinifu “Siku nyingine nikasema si vema watu kutengeneza dhambi ambazo Mungu hakuweka kupitia amri. Pengine lile jambo usilolipenda utalifanya kuwa dhambi na lile unalolipenda licha ya kuwa ni dhambi kabisa utalihalalisha. Ndio maana ni vizuri sana kufwata kwa makini ile ambayo Biblia inaongea na wala si wachungaji, maaskofu pamoja na kuwaheshimu. Sijui ni Kiswahili cha kikenya. Uganda au kikongo… Ha ha ha ha!! But very sweet!!
  Kimsingi Biblia nzima ni neno Mungu, tena lote, maneno yote yaliyomo ndani yake, yanafaa kwa mafundisho.
  2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
  Naipenda zaidi KJV imetumia neno ALL; Just look;
  16 All scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness:
  Biblia ni neno la Mungu. Biblia nzima, yafaa kwa mafundisho ya kuwatia adabu watu wamrudie Mungu. Mungu ameiandika Biblia kwa (kwa njia ya uvuvio wa RM) kunukuu watu, shetani na hata mapepo ili kutufundisha sisi. Yote haya Mungu aliyafunua kwa watumishi wake manabii, ili sisi tuujue ubaya wa dhambi na shetani mwenyewe., tuujue ubaya wa kuwa na tabia mbaya au kutotii neno lake, lakini pia tuujue upendo wa Mungu kupitia maisha ya manabii wake, wahusika wengine ndani ya Biblia na hata kupitia Mwanaye Kristo Yesu. Haina maana kuwa, kwa vile kuna maneno ya shetani, watu nk yaliyonukuliwa na Mungu mwenyewe ndani ya Biblia, yanalihafifisha neno lake.
  Hivyo basi, kusema Biblia ina maneno ya watu na shetani, ni kuonesha udhaifu wa kufikiri tu. Nasema ni udhaifu wa kufikiri kwa sababu, kila tunachokifanya sisi binadamu kinachoonekana kuwa ni kizuri mbele za Mungu na wanadamu, tunafuata utaratibu na mfumo wa Mungu.Mf. Mtu anapoandika kitabu akanukuu vitabu, kauli nk za waandishi au wasemaji wengine, kile kitabu hakitaitwa kwa jina la mwandishi huyo eti kwa sababu kuna maneno au nukuu za watu wengine? Hasha!! Kitabu kitajulikana kwa jina la yule mwandishi na si vinginevyo labda aingie mkataba na wachapishaji!! Nukuu tunazozirejea kwenye maandishi/kazi za watu wengine, tunafanya hivyo kwa lengo la kuelimisha hicho tunachokikusudia watu wakielewe. Kadhalika Mungu naye alifanya vivyo hivyo kama mwasisi na mnukuzi wa kwanza katika maandishi na kauli za watu au mapepo. Mungu atusaidie wapendwa.
  Nirudi tena kwa kaka Ziragora;
  Nanukuu “Ni halali kabisa Mwanamke kufundisha na kuwa kiongozi kanisani. Lakini kama si desturi ya kanisa lingine kusiwe hukumu.”
  Kaka, naomba unieleze kama Mungu ana makanisa yenye desturi tofautitofauti pamoja na kwamba yana tumia Biblia moja!! Nitafurahi kujifunza kwako ukija na rejea za maandiko.
  M-barikiwe nyote wapendwa.

 87. Ndugu Seleli, Ndugu Siyi,

  Naamini hamjambo.

  Nafikiri Seleli umeona kam niliyoandikia Siyi ni ya kwako, sorry.
  Ndugu Siyi, Biblia inapata sifa katika ukweli wake, na ile ndiyo inaifanya kuwa takatifu. Bila shaka Mungu alipopenda kutuelezea uwepo wa Shetani ili tumuepuke alipana order iandikwe ndani ya Biblia. Ndio maana unamuona Shetani akitamkwa ktk Biblia. Kuwa ndani ya Biblia yaimpe Ibilisi nguvu. Hii ndio inapunguza nguvu zake. nafikiri huyu Ibilisi hapendezwe awe ameandikwa ktk Biblia kwani ndipo anapata kuhayarishwa. lakini ukweli ni kam ameandikwa ndani. Tungelimjua je hangeliandikwa ndani? Huone kam kuandikwa ndani kwake kunaleta ukweli zaidi ktk Biblia na hapo inapata Sifa kwani Ibilisi anayiogopa?

  Asante.

 88. Ndugu Siyi,

  Asante sana kwa namna unavyosema hapo juu. Kweli sisi sote tulisoma. Inategemea ni method ipi iliyotumiwa. Neno la Mungu ni tamu sana. linaporudiliwa lanaendelea kuwa lipya. Si uliona Ndugu yangu Lwembe alikuwa ameondoka. Hivi nimemrudisha. Na times anaporudi anapata maelezo yale yale labda kwa mafasiriyo tofauti. Na kwa mwisho itakuwa anaposhindwa sikia basi atabaki na mzigo wake. Anapoanza sema kama hatuelewane nafasi ndogo mim naendelea kumwambia karibu, pamoja na wengine wanao tatizo kam lake. Ninapotazama anayoyazungumza, naona anampenda Mungu. Lakini kwa ile hali ya kumpenda, anatafuta atumie ushabik. Hii inaleta kila mwanaadamu kujidanganya. Wakati unapopima kuongea kam Shetani ameandikwa ndani ya Bible, yeye anaona si vizuri licha ya kuwa hii ndiyo ukweli. Jambo kama lile linaletwa na ile ushabik anayo. Anasikia ile tamko inampeleka kuwaza kam imesemeka Shetani akachangia kuandika Biblia. Unajua ushabik ni jambo la hatari linaloleta mtu kuwaza ametetea na wala amebomoa. Sasa ndugu Lwembe atakapotusikia, anaacha ushabik na anaingilia kusoma Biblia tu ,si ndipo atakapo mjua Mungu ginsi alivyo ndani ya Biblia?
  Nirudilie tena:
  “Ni halali kabisa Mwanamke kufundisha na kuwa kiongozi kanisani. Lakini kama si desturi ya kanisa lingine kusiwe hukumu.”

  Mubarikiwe nyote munaotusoma

 89. Siyi,

  Kila kitu kipo hapa, hapa ktk mada hii uko juu, nilisema muda mrefu sana, tafadhahri mnasumbua sana,mnapokua hamsomi na kuibuka tu,! tafuteni/tumieni mbinu ya kusoma vitu viwe virefu, vyakati au vifupi, njia ziko nyingi na mkiamua mnaweza sana, maana mnasomaga vingi zaidi vya vya humu ( magazeti makala zote za mwana halisi/Rais mwema, novels, vitabu vya dini nk) na kupoteza muda kwa mengi mengine ktk maisha haya badala ya kutenga muda kusoma ya Mungu na mambo ya imani. Jaribuni kua serious na committed hapa. Nimesaidia tu mara moja kukujibu ivi shida yako, ilikua nisifanye maana nauchukia sana uvivi, kila kitu mmeshapewa bado mnauliza!!!!!!!! Nime-copy na ku-paste haya ya chini na modifications kidogo kisha nakutaka ujibu swali moja chini ili uwe umepata jibu lako. Angalia hapa kwanza.

  Ayubu.1:7,9-11, 2:2,4-5 =Huyu ni nani hapa anaongea wakati Mungu amemuuliza ametoka wapi?

  Luka.8:20= Na je wakati Yesu anataka kumuweka huru huyu jamaa, unakumbuka aliuliza nini? so yule aliyojibu ni Mungu eti eee? yale ni maneno ya Mungu Baba wa Mbinguni aliojibu yule kiumbe ndani ya yule Mtu?

  Marco.5:1-10=Na ‘’majamaa’’ yale yalipomuomba Yesu ayafukuzie kwa nguruwe, yale maombi ni maneno ya Roho Mt?
  Mdo.16:16-18= Yule kiumbe wa uaguzi ndani ya Mjakazi yule aliyesema maneno yale kwa Paul ni maneno ya Mungu yale?

  Mdo.19:13-16 = Wale mapepo waliowaweza wana wa Skewa Myahudi Kuhani Mkuu- hayo Matendo na Maneno ni ya Mungu?

  SWALI LAKO: Kwa vile Biblia ina maneno ya Mungu, watu na shetani, je, bado ina sifa ya kuitwa neno la Mungu?

  JIBU LANGU: Ni swali- Baada ya kujibu maswali ya hayo maandiko juu, wewe wasemaje kuhusu swali lako?

  Press on

 90. Ndugu Lwembe,

  Narudia kwani nafikiri sikuona vizuri suala 1, 2, 3 na 4. Naleta majibu na lengo la kuleta shauri wala si kuhojiana tena.
  Kabla nilete jibu, ningelipenda nikushawishi usiendelee kuleta picha yako ili uibandike wengine. Mim nimeandika mambo kazaa kwa hii mada lakini sijawai kusema juu ya walimu, wachungaji ao maaskofu. Lakini wewe unaponijibu unasema inategemea jinsi ulivyofundishwa nao na jinsi mim nilivyofundishwa na wengine wa upande wangu. Ndugu yangu, ndio maana unapendelea tafsiri na unatupilia mbali andiko halisi. Sikiliza, unapoendelea tembea nyuma yao utaendelea kutetea maslahi ya doctrines na wala kamwe hutatosha kitambaa kwenye macho. Kwani wao walitia sahihi kwenye mambo ya doctrine ya kanisa yao. Na ukizunguuka dunia mzima hutaona kanisa (jengo) lonalotembea 100% kwenye andiko. Hata lile la Paulo lilikuwa tofauti na lile la Petro. Hapa juu nilikuambia kam kwa mujibu wa Petro kuwa mukristo sherti utahiliwe kimwili, lakini katika makanisa ya Paulo sivyo. Nikuulize nani kati ya wale alitenda dhambi licha ya yale mambo kuandikwa ndani ya Biblia ? Sasa kwangu ni hivi : ya msingi ni kuamini Yesu Kristo kam ni mwana wa Mungu, aliekufa akafufuka ili tuokolewe. Ile utaipata kupitia mukristo yeyote aneyestahili na haihusu mchungaji wala askofu tu. Mafundisho halisi ingine utaipata ndani ya Biblia, na Biblia iko very clear.
  Kwa masuala yako:
  1.Je, hawa “watu wa kiroho”, ndio wanaotusimulia kuhusu Mungu na watu na Shetani, kwa jinsi wao wanavyowafahamu hao?
  Jibu: Hawa watu wanatoa ripoti. Kwa mfano, wanaposema walitembea toka Yerusalemu mpaka Damaski, wao wamesema, na nafasi kama zile hautamwona akilitaja jina la Mungu(Yesu), pengine wanashuhudia waliyoyaona(kwa mfano: Yesu akafufua Lazaro), pengine waliandika waliyoyafanya(mfano: walibatiza kwa jina la Yesu angalau si vile Yesu aliagiza), pengine waliandika maagizo ya Mungu ambayo Yesu naye alitamka pasipo kuyaandika(mfano: umpende jirani yako kam vile wewe mwenyewe), pengine waliandika ufunuo pekee hapo wakiwa sawa bila ufahamu wao(mfano: Ufunuo wa Yahana), pengine waliandika maagizo mengine wakisisitiza kam ni Roho Mtakatifu aliwaamuru. Kuongozwa na RM ni tofauti sana na kuamriwa na Yule RM. Anapoamriwa, ni kwamba amri inapewa watu na yeyoye atakayekeuka atakuwa ametenda dhambi. Siku nyingine nikasema si vema watu kutengeneza dhambi ambazo Mungu hakuweka kupitia amri. Pengine lile jambo usilolipenda utalifanya kuwa dhambi na lile unalolipenda licha ya kuwa ni dhambi kabisa utalihalalisha. Ndio maana ni vizuri sana kufwata kwa makini ile ambayo Biblia inaongea na wala si wachungaji, maaskofu pamoja na kuwaheshimu.
  2.Hawa “watu wa kiroho”, walikuwa na uwezo wa kuyajua mawazo ya Mungu, na ya hao watu, na ya Shetani, na kisha wakayaandika kama yalivyo?
  Jibu: Hawa watu waliandika waliyoyaona, waliyoyafanya na waliyoambiwa na Mungu kuyaandika kama mwenendo na kama amri(hapa fanya angalisho; kunapo amri kuna dhambi vilevile), na mengine kam informations itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Iko wazi kabisa, Musa hangelijua mambo yoye toka Mwanzo bila Mungu kumwambia. Fact ya kuambiliwa na Mungu haimpe Musa umungu kiwango aandike maneno Mungu aliemwambia tu. Ndio maana akasema na ginsi alipoishi na Lutu, na mengine kwa kiwango Fulani hayasaidie mtu kwa wokovu.
  3.Kwa vile Biblia ni muungano wa vitabu vilivyoandikwa na watu wa kiroho, vikiongelea Mungu na watu na Shetani, kwanini kiitwe ‘Kitakatifu’ wakati humo ndani kuna mchanganyiko wa maneno ya Mungu na ya Shetani na ya watu? Au wote hao ni watakatifu?
  Jibu: Sisi wakristo tuko tofauti sana na waislamu ambao wanakamata kitabu ginsi kilivyo kam kitakatifu(asiye muislamu asikiguse, kinapozeheka kizikwe na heshima, …). Unaposikia neno Biblia takatifu, tupa mafikara yako kwenye maneno matakatifu yaliyomo. Na yale ndio yakifanya kiwe kitakatifu. Usipime kuangalia mwenye aliandika. Hata lingelikuwa neno moja lililotamkwa na Mungu lina nguvu ya kufanya lile fungo lote liwe takatifu. Ndio maana Mungu akaangazia wote waliyoandika kusikuwe hata mmoja atakaesema Mungu alinena na wala hakunena. Lile ni fundisho kubwa linalokuambia na wewe usisubutu kusema mtume ao muandishi fulani aliripoti maneno ya Mungu wakati yeye pekee alikiri kam ni maneno yake. Kuwa maneno ya mwanaadamu yapatikane kwa namna inayoonekana vizuri ndani ya Biblia pasipo kutafutisha nayo ni moja wapo wa kafanya Biblia iseme kweli na igeuzwe takatifu licha ya kuwa na yale matamko ya waandishi yapo vilevile. Wangelikuwa wakorofi ktk maandiko yao kam Biblia haina samani yoyote. Mim nashukuru sana wote kam wa kina Paulo wanasema kweli eti hapa ni mim ninasema wala si Mungu. Haleluya!!!!

  4.Kulingana na kauli yako, sasa ninaelewa kuwa Neno la Mungu ktk maana ya Biblia ni mchanganyiko wa maneno ya Mungu na ya watu na ya Shetani, je, ni sawa?
  Jibu: Hii nimeigusia hapo juu, niirudilie kidogo. Ukiangalia pale ku mwanzo utaona vile vile Shetani alisema maneno Fulani akiambia Hawa na yakaandikwa sawasawa ndani ya Biblia. Hii inamaanisha kam tamko za Shetani nazo zipo ndani ya Biblia. Na pale ku agano jipya utaona ginsi waandishi wa Injili walisema namna Shetani (Yule joka) aliwai mwambiya Yesu. Yale yote ni matamshi ya Shetani. Ile iliandikwa na watu waliopewa habari na Mungu. Ukiona vizuri, Musa alieandika vile vitabu vya mwanzo hakuwepo wakati Shetani alipozungumza na Hawa. Vilevile, Shetani alipomjaribu Yesu nyikani, hakuwa mtu mwengine. Ile informations tunazozipata, ni Mungu pekee anaezitupatia kwa ufunuo kupitia muandishi. Iwe wazi kam Shetani hakuhusika kwa kuandika haya mambo. Hapo ndipo anapata shida kwani Mungu hangeliingilia kam sisi hatuna namna ya kumuepuka huyu Ibilisi.
  Kifupi ni kwamba mim sisikiye Biblia namna unavyoitaja hapa. Shika kam iliandikwa na watu wa kiroho, ambao hawawezi geuka Mungu, wenye walitii Mungu kiwango walitii yote Mungu aliwaambia waandike na wakawa waminifu kiwango na ile waliosema binafsi hawakuficha. Sasa, nakuomba usiwafanye manabii wa wongo wakati wao wanatupilia mbali lile jambo wakiwa wazi ndani ya yale walioandika yote.
  Labda ungelikuswali jambo moja : « umewai kupata ndani ya Biblia neno lililokuchanganya na haukuweza fahamu kama ni Mungu alilolitamka ao kuliagiza yeye pekee ? »
  Mambo ingine, unapotelea labda ndani ya hizo tafsiri ulizokiri umezipata kwa wachungaji. ACHANA NA ILE BWANA …. BWANA YESU ANAKUPENDA.

 91. Seleli,
  Kwa vile Biblia ina maneno ya Mungu, watu na shetani, je, bado ina sifa ya kuitwa neno la Mungu?

 92. Labda kama tunapenda kurudia-rudia mambo! Kuhusu ktk Biblia kume-rekodiwa humo Maneno na Matendo ya Mungu, Watu na Shetani, nilishatoa somo zima na refu sana hapa hapa mwanzoni kabisa kwa mifano ya maandiko yote haya mnayotumia sasa na kisha baadae nikatoa maandiko mengine mengi mnayorudia tena humu, na Lwembe alisoma yote kabisa na akashindwa kabisa kukataa kwa misingi ya hoja za kueleweka. Tafadharini niwahamasishe msome kwanza michango mingiiiii hapo juuu, yote mnayosema sasa yako uko kisha kama Lwembe hajaelewa kuhusu Mungu, Mtu au Shetani kutenda/kuongea ktk Bible na aseme sasa. Otherwise, kila kitu kipo hapa hapa mwanzo na kati tena na mifano ya akili na maarifa ya kawaida lakini ya nguvu sana kumuelewesha. Nadhani the best way, ni kukukopia na kukupastia or rather in effect, kukukatia kabisa na kukpastia

  Press on.

 93. Ndugu Lwembe,
  Salama ya Bwana Yesu Kristo iwe nawe.
  Nashukuru sana kwa namna unaongea, it’s clear.
  Niliposema unapendelea kusema Shetani ni kwamba niligundua kam ktk maandiko yako huko juu, yote ambayo mtu mwengine alikuwa akisema kam hayalingane na yale unayowazia ulikuwa ukilenga Shetani amemvamia. Uniruhusi nijumlishe na hili jambo la kusema utawabeba wapi. Kufwatana na masemi yako ku §1, naona bila shaka unasisitiza kam si Mungu pekee anaeongelewa ktk Biblia. Ni hii ndio wengi walikuambia huko juu, nami nikaendelea. Please, sijawai sema Shetani amechangia ktk uandishi wa Biblia!!!! Soma vizuri, “Biblia inaongea juu ya Mungu, Watu na Shetani, ni watu waliyoiandika, tena nikasema wa kiroho”. Nawe umekuwa mkweli unapokubali kam kuwa na RM kiasi gani hailete mwanaadamu kuwa Mungu. Ukatiya mashaka lakini ukilenga anawekwa katika ukweli yote ya Mungu. Nitasahihisha kidigo nikisema Mungu anamupa ukweli anapopenda, wala si mtu anayeshurtisha Mungu. Hii UKWELI ndiyo inamsukuma Paulo kunena yaliyo kweli:” 1 Wakorintho 7:8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo”, hapa haseme Mungu amemtuma anene na watu wakae sawa yeye alie bila kuowa. Na maandishi mengi yako wazi wakati mwanaadamu amesema yeye binafsi kama mwenye hekima ao akinena aliyotumwa kikwelikweli na Mwenyezi Mungu.

  Unaposema hiyo yote ndio inaunga biblia, Neno la Mungu, ni kweli. Inayobaki ni kuidaka ginsi ilivyo bila kuleta tafsiri mahala ambapo haihitajiki. Nadhani unajua jinsi repoti inafanywa ; iwezekane iwe ya kampuni moja na msimamizi moja. Lakini maneno yote itakayopatikana ndani ya ripoti haitoke ndani ya kinywa cha manager angalau ripoti yenyewe inahusu kampuni yake. Nadhani umepima fahamu vizuri Biblia iko je. The summary of the Bible is the Word of God na hii inatosha kwa wokovu, but point by point, ndipo utakuta mambo ya mwanaadamu wa kiroho. Kwa mfano mtume anaposema” Fulani, uniletee joho nililosahau”, ile ni fundisho lakini si Neno kutoka kinywani mwa Mungu. Na hii discussion haihusu the summary of Bible, inahusu points ambazo Mungu amekubali ziandikwe, lakini siyo funguo ya wokovu, na wala haihusu dhambi. Ona, dhambi inabaki dhambi popote, lakini haiwezikane nguo ziwe sawasawa duniani pote.

  Sijue nijibie je kwa swali zako kwani yana majubu yenyewe:
  a) Kuna agizo zipatikanazo ktk Biblia zinayohusu mila, utazikuta haswa ktk agano la kale, na wala wewe leo hauzifwate bila kujihesabia dhambi.
  b) Yeye aneyeandika(mfanya ripoti), mfalme, muongozi(Musa, Abraham, ….), Biblia inatuonyesha namna walivyotembea lakini mara na mara haituagize kutembea kam wao. Walikuwa wanaadamu na walitembea kwa kiwango kidogo fulani kinyume ya mapenzi ya Mungu.
  c) Nilikuambia, Shetani simtaki. Hakuandika Biblia, wote pamoja na mitume, tunajua kwa kiwango kidogo tu Shetani kupitia Maandiko matakatifu. Tena nikujulishe kam mim sina kweli yote. Yesu alipoulizwa alisema kama mkweli(mwema) ni Mungu tu, akijua kam yeye ni Mungu. This means that mitume nao hawana kweli yote. Kweli yote iko kwa Mungu na anaionyesha kupitia maagizo yake ambayo yako cleary written in the Bible.

  Mungu akubariki sana.

 94. Ziragora huyu Lwembe haeleweki kuhusu ubatizo tunamfuata Yesu, mitume walikosea.
  Good Bless u all

 95. Ndg Ziragora,

  Shalom!
  Unaniuliza, kwanini Shetani anakamata nafasi kubwa ndani ya ninayoyatamka!
  Sina uhakika na hilo unalolisema, lakini kwa jinsi ninavyoyasoma unayo yaandika
  yawezekana ukaniona hivyo, kutokana na msimamo wako kuhusu Maandiko. Lakini kuhusu Mungu na Shetani, mambo haya yanaambatana kuanzia Mwanzo 3 hadi Ufunuo 22:19 anapomalizia kwa onyo hili: “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mji mtakatifu…” Sijui ni kitabu gani ktk Biblia ambacho umesoma na Shetani hajatajwa humo au kuoneshwa kazi zake; au utakuwa ni uoga tu wa kukabiliana na ukweli wa Injili!

  Kuhusu suala la Maandiko, inategemea sana jinsi mwalimu wako alivyokufundisha. Kwa mfano mimi, mwalimu wangu alinifundisha kuwa “Maneno yote yaliyomo ndani ya Biblia, bila kuondoa chochote wala kuongeza, katika ujumla wake, ndiyo yanaifanya Biblia kuwa NENO la MUNGU, ambalo Neno hilo ndiye Kristo; ndio maana unaona tunatofautiana kidogo! Basi nikiiachilia hiyo jinsi niliyofundishwa, napenda sasa nijifunze zaidi namna yenu wapendwa, labda inaweza kuwa na Nuru zaidi na hivyo kutusaidia wengi wetu.

  Umeniuliza iwapo nakanusha au la, kwamba “Mtu awe amejazwa RM kiasi gani, hawezi geuka Mungu.” Hii ni kweli kabisa, hawezi geuka Mungu, ila atawekwa katika Kweli yote ya Mungu!

  Pia unasema, “Biblia ni muungano wa vitabu vilivyoandikwa na watu wa kiroho. Inaongea juu ya Mungu, watu na Shetani…” hebu nifafanulie zaidi kuhusu haya:
  1. Je, hawa “watu wa kiroho”, ndio wanaotusimulia kuhusu Mungu na watu na Shetani, kwa jinsi wao wanavyowafahamu hao?
  2. Hawa “watu wa kiroho”, walikuwa na uwezo wa kuyajua mawazo ya Mungu, na ya hao watu, na ya Shetani, na kisha wakayaandika kama yalivyo?
  3. Kwa vile Biblia ni muungano wa vitabu vilivyoandikwa na watu wa kiroho, vikiongelea Mungu na watu na Shetani, kwanini kiitwe ‘Kitakatifu’ wakati humo ndani kuna mchanganyiko wa maneno ya Mungu na ya Shetani na ya watu? Au wote hao ni watakatifu?
  4. Kulingana na kauli yako, sasa ninaelewa kuwa Neno la Mungu ktk maana ya Biblia ni mchanganyiko wa maneno ya Mungu na ya watu na ya Shetani, je, ni sawa?

  Halafu umeniambia, “Usipime kumsingizia mtume Paulo kwa kudai uko kwa upande wake. Anaposema ni yeye na wala hapana Mungu; full stop; don’t add.” Hapa nimekuelewa vizuri sana, ila nifafanulie zaidi huo muktadha (context) wa kauli yako hiyo kulingana na Fundisho lako:
  a) Vifungu ktk Maandiko, ambavyo vinasema dhahiri kuwa “Hapa ni mimi…” au vyenye maudhui ya jinsi hii, ambavyo umesema ni maneno ya watu, vinamuhusu nani haswa, na kwa manufaa gani?
  b) Vifungu ambavyo havina maelezo ya kwamba ni nani anayeelekeza, ni Bwana au ni mtume mwenyewe kwa akili yake, hivi mnaviweka katika fungu gani, la watu au la Mungu? Hivi pia vinamuhusu nani, na kwa manufaa gani?
  c) Pia kizazi chetu, na hao wengine waliotutangulia, ni kwa kigezo gani tunazitumia nyaraka walizoandikiwa kundi la watu specific, kulingana na hali walizokuwa nazo na uhusiano wao na hao waliowaandikia?
  d) Kwa kuwa ninyi mnaongozwa na RM, mkiwa katika Kweli yote, ni kwanini mnasita kuyaondoa maneno ya watu na Shetani ndani ya Biblia ili tubaki na Maneno ya Mungu tu ambayo ndiyo yenye faida (Yn 17:17)?

  Kuhusu ubatizo, umesema tuiache, lakini wewe mwenyewe umeshindwa kuiacha hapo unapoendelea kusema natumia akili zangu na, “Aibu ni kwamba unataka watu wote wafwate akili zako, utawafikisha wapi?” Labda niseme kwamba hata Mungu anafahamu kwamba watakuwepo watu watakaomuonea AIBU, kwahiyo kauli yako hii inadhihirisha kwamba unawaonea aibu mitume, hilo ni jambo la kawaida, pia sijapaona mahali popote pale nilipomwambia yeyote yule anifuate mimi, kwanza nitampeleka wapi, akipenda amfuate Petro na mitume, hao walio na Funguo za Ufame wa Mbinguni, au akishindwa, basi akufuate hata wewe!

  Gbu, brother!

 96. Ndugu Lwembe,

  Mpendwa kwa nini Shetani awe akikamata nafasi kubwa ndani ya yale unayoyatamka?
  Wewe unapendelea sana tafsiri kuliko maandiko, baada ya pale unaibandika kwa wengine. Ninaposema Paulo alikuwa wazi anaposema ni yeye anaandika na wala si amri kutoka Mwenyezi Mungu, wewe tayari umeona tafsiri yako tu kam Biblia imekuwa ya Mungu, watu na Shetani, what’s this?????

  Labda tuangazie wengine: Biblia ni muungano wa vitabu vilivyondikwa na watu wa kiroho. Inaongea juu ya Mungu, watu na Shetani, sivyo hatungelijua uwepo wa Shetani.

  Nilisema: “Mtu awe amejazwa RM kiwango gani, hawezi geuka Mungu”. Ndugu Lwembe umekanusha ile au la?

  Mambo ya kubatiza tuiache kwanza kwani haiko ndani ya mada. ilikuwa swali ya ndugu Siyi. Wewe lakini nakuona ukitumia akili zako kama ulivyosema kwa mwisho bila kuzingatia vizuri maandiko. Aibu ni kwamba unataka watu wote wafwate akili zako, utawafikisha wapi?

  Usipime kumsingizia mtume Paulo kwa kudai uko kwa upande wake. Anaposema ni yeye na wala hapana Mungu; full stop; don’t add. Kwako unaona kama yule ambae hapendi kuongeza, kwa akili zako, ameunganisha Mungu, Watu na Shetani. Akili nyingi zile bwana!!!

  Hapana kusahau:
  1)”Wanawake kutofundisha kanisani” si amri kutoka Mwenyezi Mungu.
  2) “Wanawake kutovaa suruali”, si amri kutoka Mwenyezi Mungu na haina msingi hata kidogo.

  Sasa usipime ingiza akili zako ndani ya Biblia, haitageuka. Na usipendelee kuandika mingi. Please, ogopa kuwa upset ,and be concise.

  God bess you.

 97. Janeth S.M

  ‘Fujo’ zipi tena dada? Fananua kidogoo nikupate, unisaidie na nikusaidie! Ndio maana ya fellowiship hii hapa! Uwe huru na wazi

  Ila uko juu sijui kama umepata muda wa kusoma zote, kuna fujo huko! Lo! labda ‘fujo’ unazo weza kua unamaanisha au unazoziona( nitangoja jibu/ufafanuzi wako), ni kwa sababu ya kupangua fujo MBAYA KULIKO kinyume nanyi WANAWAKE ambazo si Mungu aliyeamuru bali mfumo dume usiyo mtakatifu bali mtakaukandamizaji na kuwalazimisha nyie mu-operate below potentialities mlizowekewa na Yeye si wao. wakisahau kabisa kwamba Bwana ni mmoja tu kiukweliiii na sisi WOTE kabisa(wenye fujo original-Lwembe,Siyi na wenziwe) na (wenye fujo kusababishwa-Seleli), tu MABIBI ARUSI

  Mfano wa mengi ya wana original fujo waliyosema humu/uko juu(SOMA YOTE UKO YAFADHARI) ni kua nyie Wanawake( yaani wewe Janeth na Roho Mtakatifu wako tele na NENO full na mbinguni wamekuchangua) ati ROHO Mtakatifu hawezi kukufanya Mtume, Mwalimu, Mwinjilist, Nabii, Mchungaji hata wa watoto na wale wakao nyumbani mwako kuwaelekeza ktk kicho cha Mungu, huduma izo ni kwa wanaume tu!!!!!!!! au nyie mna udhafi sana-hatari-hatari tupu bila kujua kwa dhati na kina, udhaifu aliousema Petro hapo ni upu hasa lakini Wanaume wana original fujo humu, wakiongozwa na hisia zao za kimila/desturi/mazoea na kiume kibaya cha kivyao na kamwe si cha KiMungu, wakautafsiri udhaifu hapo kumaanisha mambo mabovu-bovu! Ingawa baadhi wamekwepa ilo, hawajasema wazi(wameogopa) lakini radha na hoja ya nyuma ya yale wamesema ktk michango yao, hujitaji ufunuo kujua hapo kuna shoti mbaya.

  Fujo mbovu kama izo, sharti zishugulikiwe kwa nguvu nyingi sana ili kamwe zisiamke tena na kila zikiamka, zitakandamizwa chini zaidi mpaka zisiwe na makazi katika ya Wanawadamu wote Ke/Me-MABIBI wote wa Arusi wa Bwana mmoja tu, Amen.

  Una swali/hoja, umeridhika , vyote na vyovyote, Karibu, mara moja nitafanya kazi. Press on.

 98. Lwembe,

  Amen kwa kuniaga ktk mada hii,ila unakaribishwa tena ukipenda, nitakaribia bila kusita hata chembe,ni pazuri sana hapa/mada hii. Basi pasi na shaka, kwa sasa nami nakuga kama ifuatavyo:

  Niliyoyaongea KWELI ninaamini na si kuamini tu bali NAJUA KWA HAKIKA KUA NDIO MOYO WA MUNGU JUU YA WANADAMU WOTE PARTICULARY WANAWAKE IN THIS CASE. Mungu ni wa wote na hana upendeleo wala hawezi degrade mwanadamu yeyote kwa mantiki ya race, gender, color nk. Chochote kitacho wanachukulia wanawake kwa maana ya negative always au in many cases, HICHO SI CHA MUNGU hata tone, ni hisia, personalities za Wanadamu Wanaume, maana Biblia imejaa Wanawake waliofanya mazito mazuri na pia sisi wenyewe ni mashahidi kua ktk maisha yetu ya Wokovu ktk makanisa, shuleni, vyuoni, WAKO WANAWAKE BORA SANA KIROHO KWA MBAALI KUZIDI WAUME ZAO,KAKA, WANAFUNZI WA KIUME-sasa huo uspeshality wa kiroho wa Mwanaume always uko wapi? Lazima tutambue kua mwisho wa siku, MWANADAMU NI MWANADAMU TU-awe Me/ke, rich,poor,mzungu, black or yellow if you like-WE ALL NEED God’s grace and destiny yetu kwa kweli haiko ktk kua Me bali kwa neema na kujitahidi kama vile ilivyo kwa Wanawake. Mungu kututenganisha toka mbinguni kimajukumu/nafasi/jinsia na taarifa kua wao Wanawake, walivyokua wa kwanza kudanganywa bustanini, isiwe chukuliwe/tusimuingizie Mungu hisia zetu(kosa kubwa wengi mmelifanya humu ktk mjadala) na tunadhani Mungu alikua anasend msg kwetu kua hao Viumbe ni hatari sana ivyo sharti tuwatiishe kweli kweli hapana mchezo kitu ambacho kwa kutumia jambo ambalo nimewafundisha sana humu…KULITUMIA NENO LA MUNGU KWA HALALI NA KUA NA NENO LA MUNGU KWA MAPANA NA HEKIMA YOTE, utakubaliana nami kua Neno la Mungu kwa vizazi vyote(phrase nyingine iyo usiisahau tunapomaliza hii mada pia) ni WOTE WAMETENDA DHAMBI NA KUPUNGUKIWA NA UTUKUFU WA MUNGU, IVYO WOTE KABISA-siyo akina Ke tu-wanamuhitaji Mungu kuwasaidia kuanzia zero to hero.

  Sijafika ukomo wa ufahamu ktk kufafanua na kunyambua hilo juu, nina vyovingi kwa neema, so pengine kufika kwako ukomo kutoa dhana ya kua Wanaume tu ndio kila kitu hakunihusu hata kidogo, bado ziko njia nyingi za ufundishaji nitatumia kuweka peupe hilo niliolosema juu kule na pia kusisitiza WANAWAKE NI WATUMISHI KAMA SISI NA WAKO WENGINE BORA KUZIDI HATA WANAUME NA ALIYEWAPA HAYO WALIYO NAYO IWE KARAMA, HUDUMA VIPAWA, HE MUS BE VERY SMART AND KNOWS WHAT HE DID. Kwa ivyo, ukipenda, tegemea kupata mengi toka kwangu si kwa maandiko yanayokataza Asifundishe tu-maana ilo wote tunakubaliana ni NDANI YA KANISA-haki ya Kiongozi wa Kiroho kuweka sawa mambo kama ilivyokua kwa Musa-Yesu alisema, bali pia nitakuonyesha mengi matamu nje na ndani ya kanisa ambayo wanawake wamefanya si lazima la kufundisha tu.

  Hii kitu umesema imenipata hii “Spiritual Amnesia” kupoteza kumbukumbu ya nilikotoka na Mada wala unakokwenda nayo’’,= umenisingizia tu maana kama kuna watu wanasahau floo, hawasomi mpaka mwisho kisha wajibu kwa USAHIHI, wanaweza mix vitu hapo hapo dk chache, umo sana na nimekuonyesha several times ulivyochanganya mambo

  Ati, umetoa ushahidi wa gonjwa ulosema hilo limenipata kwa hii-KUA NINAKUBALI KWA SHINGO UPANDE KUWA MWANAMKE ASIRUHUSIWE KUFUNDISHA!!!!’’ Jibu: Ni aibu kweli kama unaweza mzushia mtu gonjwa kubwa kama lile juu kisha ukatoa ushahidi weaka kama huu! Soma commentz zangu zote, utagundua kua mimi hushambulia mambo mabovu au kufundisha jambo, hatua kwa hatua na kujenga hoja taratibu tu mpaka mtaipata/itawakolea tu, hata kama hamsemi hadharani amen basi rohoni/privetely uko mtasema tu-Nilianza kwa kuwaambieni kua ktk Bible kuna God’s part na huma role, kisha nikasema Mungu kweli aliwatumia watu but hawakua dead bodies ivyo likely wakati wanasema/andika/hudumu , human factor lazima ionekane because they were humans in the first place anyway! ndipo nikaanza kushare insights on human role toka ktk maandiko yenye statements kama I wish, SI-mpi, SIna amri ya Bwana ila NAshauri na kisha nikaunganisha na point kuhusu Kudaka ‘’Neno/Ujumbe/Kitu cha KiMungu kwa Vizazi vyote’ kutoka maandiko ktk Bible yanayoonyesha kuna human role au Waandishi wametofautiina kueleza mambo hata nilitoa mfano wa Marco and Mathayo -Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 ..Wakamvua Yesu nguo na kumvika vazi JEKUNDU (scarlet robe) lakini Marco.15:15-17 hasa mstari 17..Wakamvika vazi la rangi ya ZAMBARAU(purple).Hapa waandishi ni wawili tofauti ila tukio lilelile lakini limesemwa tofauti ie rangi ya nguo zile, ingawa ulijibu kijanja ati vazi la kifalme so linaakisi rangi/mwanga tofauti-very funny! Coz hao walio andika walikua umbali gani mpaka mwanga huwachanganye ivyo? na kwani walikua na Master siku ile tu?/ was the vazi a one day experience? Je hawajawahi kuona other Kings in the robe/garments? na kisha pia tofauti iliyopo kati ya Yakobo na Paul kuhusu topic ya imani na matendo nk.

  Hayo yote juu yakanileta kukuonyesha kuwa ili kuelewa msg ya Mungu ndani ya Bible wakati mwingine, ni kusoma kwa macho 3-Kujua/kua attention kudaka lipi hapa Ni Mungu, Mtu au devo kabla uja-conclude jambo kua la Mungu ivyo MUST Wanadamu wote past,present and future, Wazingatie na ivyo kwa uelewa huo wote then ukusaidie/utusaidie kujua na kuanalyse vema kwa balance yenye hekima iliyojitosheleza kuhusu Maandiko ya kukataza Wanawake. Sasa shule yoooote hiyo juu ukisema nimepoteza kumbukumbu, nina gonjwa baya hilo ulosema limenipata basi twende wote kwa specialist na specimens zetu( kazi zetu zooote humu) then aliye na magonywa mengi kusema ukweli,si lile tu, itajulikana.

  Yes, amen, umetakia mema nipate DOUBLE PORTION, ila nilishakua nayo iyo na ndio hii kwayo nawakaba ile mbaya/nzuri(we mwenyewe unajua flavour yake) mambo yote manyonge yatakwisha nanasimika ya hekima yote ya Neno.

  Press on and was nice engaging with u, any time, 24/7-welcome bro,Amen.

 99. Ndg Ziragora,

  Ninaliona jambo moja kwako ambalo wakristo wengi wameaminishwa hivyo, kwamba ndani ya Biblia kuna maneno ya Watu, na ya Shetani, na ya Mungu! Ninafahamu kuwa hili ni jambo jepesi kupokelewa na yeyote yule ambaye Msingi aliojengewa ni dhaifu, na matokeo ya kulipokea jambo hilo ni KULIGAWA Neno la Mungu katika hayo MAFUNGU MATATU!!! Hii ndiyo kazi anayoifanya Ibilisi tangu Edeni. Ndipo kuanzia hapo unapolipokea jambo hilo, Injili hupoteza Nguvu yake, nawe kubakia kuwa mtumwa wa Dini!

  Na matokeo yake utakuwa unakimbia hiki na kile ukijificha katika vichaka vya tafsiri za dini. Biblia inapokwambia mwanamke hapaswi kufundisha, utajiridhisha kwa maelezo ya “mila na desturi”, eti mt Paulo alikuwa anarekebisha hilo! Sasa, hata nikiwauliza, Je, hao Wakorinto waliokuwa wanafundishwa hayo, ilikuwa ni kwa ajili ya wito gani, kuwa Wakristo au Paulo pia alikuwa ni mwalimu wa mila, kwamba alikuwa anajenga na makanisa ya kimila?? Mara oh, hapo Paulo anayasema hayo kama yeye! Basi huyo RM mnayesema anawaongoza yu wapi hata mnaanza kuwaona watu katika Biblia? Hamkusoma na kuelewa hapo aliposema simjui mtu kwa jinsi ya mwili tena, kwamba mambo aliyonayo Paulo ni ya ROHONI tu, hamkumuelewa? Mmerudi mwilini mlikotolewa?!!

  Sikiliza ndg yangu Ziragora, ukiisha igawa Injili, unakuwa umeivunja nguvu yake, maana umemkaribisha Shetani mtembee naye njia nzima, naye ndiye anakuwa Mshauri wako mpya, na si RM kama unavyowaza!!!

  Biblia yooote bila kuondoa hata nukta, wala kuongeza chochote kile, NDIYO INAITWA NENO LA MUNGU!!! Mambo yote unayoyasoma humo ni Mungu ndiye anayewahadithia watoto wake. Hivi Musa alikuwepo wakati wa uumbaji? Au Musa alikuwepo wakati wa Ibrahimu? Hao manabii na waliyoyaandika, waliwezaje kujua kuwa fulani anawaza hiki au kile? Ni nani awezaye kuyajua mawazo ya mtu na hata ya Shetani? Mungu amejishusha chini sana ili apate kuongea nasi ktk kiwango chetu! Ukilielewa hili ndipo Biblia yako inakuwa mpya! Zab 12:6,
  “Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.”

  Hivi mt. Paulo anaposema kuwa ametengwa tangu tumboni mwa mama yake ili kumdhihirisha Kristo, huwa mnaelewa nini? Hilo ni jambo kuu sana, kwamba huyo mnayemuona hapo si mtu wa kawaida, ni Kristo Mwenyewe, kama Mungu alivyokuwa ndani ya Kristo na ulimwengu wa dini haukumjua, na sasa Kristo yuko ndani ya mitume wake na ulimwengu wa dini tena haumjui licha ya kukiri kwao kuwa wao ni wakristo, bali hata Kristo mwenyewe hawamjui, kwa sababu Shetani amewafunika na Blanketi la Shaka, akawaambia humo yamo maneno ya Watu na ya Shetani na ya Mungu, wakameza na sasa hawajui lolote tena!

  Ndio maana kuna wakati niliwaombeni mnioneshe kitabu japo kimoja, alichokiandika Mungu, au Yesu, au Roho Mtakatifu kwa mkono wake, lakini sijapata jibu mpaka leo kwa sababu HAKUNA! Mwili wa Mungu ni hao watu wake, hata pale anapowaambia mtakalolifunga/fungua duniani na mbinguni litafungwa/funguliwa, hilo pekee lilipaswa kutudhihirishia kuwa ni Mungu mwenyewe akiwa ndani yao, akijificha humo ulimwengu usimuone, bali Kanisa layajua hayo, sasa iweje leo hii tena mrudi na kusema huyo ni Paulo?! Injili imewashinda? Hata huko kulikana neno hilo mnakokufanya, Je, mtakuwa mnatenda kazi ya nani? ni kazi ya Ibilisi, maana Kutenda Kazi ya Mungu ni kuwapokea hao aliowatuma, sasa ukilikataa neno la Paulo ukamsingizia kuwa alikuwa anarekebisha mila, kwamba hata wewe mwenyewe dhamira yako inakushuhudia kuwa unasema uongo, maana Biblia haifundishi mila na desturi, bali Sheria ya Mungu, hata hao Israeli, Torati waliyopewa huko jangwani ndio utamaduni wao, tena ni mila na desturi, au hamlijui hilo? Kwahiyo unapolikataa neno lolote wanalofundisha mitume kwa kisingizio chochote kile, unajifungia nje wewe mwenyewe!

  Angalia mnavyoachwa njia panda katika mambo ya Mungu yaliyo rahisi kabisa, baada ya kuupokea uongo, na kuufanya uwaongoze, sasa Ubatizo unawachanganya kiasi hamjui hata mlichokifuata. Katika Mathayo 28:19 Kristo anawaagiza wanafunzi wake, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu”, basi hata kwa akili ya kawaida tu, ukiwa umejitoa kutoka lile Blanketi la Shetani, kwa agizo hilo, si ni wazi kwamba ungemuuliza Kristo kwamba tupe basi jina hilo ni lipi? Yaani kama haujaathirika kiufahamu! Halafu pia unapaswa kuwa katika akili zako timamu ili ujue utaratibu wa jambo na uwajibikaji wake kwa hilo jambo. Hao wanaopewa agizo hilo ni mitume na si mchungaji wako, wala si nabii wako wala si askofu wako nk. ile legacy, kwahiyo kujivika kongwa la kumsikiliza kiongozi wako ambaye hakuwepo siku hiyo kati ya hao waliopewa jukumu hilo ni zaidi ya UJINGA! Maana anayewajibika katika hilo ni hao mitume waliokuletea wewe Injili, sasa wewe umekupata wapi huko kujua kwingi, kuliko hao waliokuletea habari? Ulipaswa uwe msikivu ili Mungu awajibike kwako hapo unapowapokea hao aliowatuma!

  Unaiona michezo ya Shetani? Amekuchanganya kidogo tu, akakurudisha kulekule alikoigawa Injili, kisha akakuambia ukatae Ubatizo wanaoufundisha mitume, kwamba tumfuate nani, Yesu aliye Master na Role model wetu au Petro mwanafunzi? Basi hapo ndipo ulipokomea, Mlangoni, badala ya kuchoma ndani Shetani akakuongoza pembeni akakuingiza katika UTUMWA wa dini, nawe kazi uliyonayo ni kupandikiza mbegu za hitilafu, zikilitilia Shaka Neno la Mungu, yaani umebebeshwa kiroba cha mbegu hizo, na unaendelea kuzipanda kila kukicha!

  Kama ili kuwa mchawi ni lazima uwe initiated kulingana na utaratibu wao, je, Ukristo si zaidi? Uchawi unaigiza Ukristo! Basi ili kuwa Mkristo, utaratibu wa kuwa INITIATED ndio huu hapa Mk 16:15-16 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Ndipo unapaswa uwatazame hao waliotumwa ili upate kuyaelewa na hayo makuu wanayokuletea, usijaribu kuwatangulia mbele, Mungu atakuua kwa hakika! Kitabu cha Matendo ya Mitume ndicho kimebeba ushuhuda wa Utumishi wao chini ya Uongozi wa Roho Mtakatifu, Huyo hapo Petro akichapa Injili iliyojaa Nguvu za Mungu zenye kumkamata mwenye dhambi aliyekusudiwa Wokovu, Mdo 2:14-36 na katika kifungu cha 37 Maandiko yanasema, kuhusu hiyo Injili, “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?” Unaona? Hakuna anayengojea gari au nyumba ya ghorofa hapo, haya maziganza yaliyojaa leo hii, wao wanajua kosa lao linahitaji wafe! Sasa itazame NEEMA wanayotangaziwa, kifungu cha 38
  “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

  Unaona ndg yangu Ziragora, hiyo ndiyo Injili ya Kweli yenye Kuokoa. Unapaswa ujipime hapo, kama nawe ni hao “walioitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” au umeitwa na dhehebu lako? Pia HAKUNA hata mtu mmoja ndani ya Biblia aliyewahi kubatizwa kwa “Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”, ukimkuta humo nami nijulishe ili niitubie dhambi yangu pamoja na mitume niliowapokea, usipomuona yeyote yule, basi ndg yangu, mjini tunasemaga, “AKILI MU KICHWA!”

  Gbu, brother!

 100. Lwembe,

  Hongera kwa kuiga my nukta kwa nukta anointing,umeipenda eee? Umenisifu kua nina BIDII for ‘Mule Religion’,Jibu: sidhani kama ni kweli maana dini nayoitetea mie kua Wanawake pia wanaweza nani watumishi pia wanaweza kua na karama na huduma kama sisi, ni ya kibiblia pasi na shaka ila yenu ya kumsingizia/ kum-potray Paul as Mtu severely against females, mnambambikizia hisia na kutoelewa kwenu intent ya moyo wake na Akili yake kama kiongozi wao ki- kanisa/kiroho wakati anaandika kusolve issues zilizokuwepo on the ground

  Umetoa angalizo hili kua kuna..’’Mchanganyiko wa Neno la Mungu na hekima ya kibinadamu’’Jibu: Kujifunza Neno la Mungu kwa kuangalia/zingatia kua walioandika si malaika bali WATU kabisa kama mimi na wewe na kwamba japokua walitumiwa na RM but iyo haiondoi ukweli kua walikua ni Watu tena waliotofautiana hata ktk kuelezea baadhi ya mambo, si dhambi wala kufuru na swala la kuelewa tu basi.Kwa iyo unionapo mimi namuangalia Paul kama Paul au Yesu alipo muangalia Musa kama Musa na hata kusema ‘aliwandikia kuwafukuza wake zao kwa sababu ya shingo zao ngumu lakini toka mwanzo haikua mpango wa Mungu kufukuzana’’ sikosei lolote na kama ndio waiitwa iyo hekima ya kibinadamu basi ni njema kabisa maana iko sawa na Neno na wengine ktk Neno walifanyaje.

  Umesema vema hapa..’’Wana wa Mungu wamezaliwa kwa Roho wa Mungu, wanamjua Baba yao, tena wanaijua na sauti Yake! Aliponena kupitia mtumishi wake Paulo LAKINI kama una maana ili kua mwana wa Mungu wa ukweli ni kumeza tu usomapo Neno bila tafakari SAHIHI ili ujue KTK HEKIMA yote namna ya kutumia Maneno hayo, hiyo si sifa ya kua mwana bali ni ukosefu wa ufahamu tu na bila shaka Bwana asingependa kua na wana wasiofahmu vitu vya msingi maana anataka sana tuijue kweli na kisha kwa kuijua kweli( kulifahamu Neno ktk maarifa na hekima ya kutosha/yote), itatuweka huru( ufahamu ni chembe ya uhai anasema vema kabisa Mr. Mabinza)

  Hapa umetishia tu unnessarily kua..’’Nalo Neno la Mungu lina jinsi ya kutimia’, so kwa iyo ndo linatimia kwangu vibaya eti ee? chekesha kweli Lwembe,Neno linatimia kwangu vizuri, huoni navyokataa yenu mabovu au ya ufahamu wa upande mmoja wa Neno-chanzo cha uanzishwaji wa imani mbovu nyingi? Mtu anaibuka na mstari mmoja na anakomaa nao na kuanza doctrine!

  Umekosea kweli kusema/leta ulichoelewa vibaya ktk andiko hili, na ndio maana sitaacha kuwasisitizia, ni vema na usalama sana KUYAFAHAMU MANENO YA MUNGU KTK MAPANA YAKE KABLA YA ku-CONCLUDE jambo, ule mtindo wenu wa kukuta BAADHI ya mandiko yalipo na kufilia hapo, acheni, mtataabisha watu na sheria nyingi, mtawakataa watu wa thamani mbele za Bwana eg wanawake kwa uelewa mbovu wa Neno, kuibuka na mistari/sura bila kufanya home work ya kuliangalia Neno West-East, North and South,ni chanzo cha imani nyingi potofu. Embu nijifunze toka kwako andiko hili Gal. 1:11-12, uliloleta ila kwa muongozo wa maswali yangu kama ifuatavyo, je,

  (a) Injili iyo anayosema/ zungumzia Paul hapa, kwa uelewa wako, alimaanisha izo sentence 2 ulizozinyofoa na kunukuu hapa au simply he is one way/kuna hoja anajenga/anatoa explanation on call yake kwa ujumla ya kuhubiri na aina ya msg yake, alipewa na nani, alistruggle vipi mpaka kukubaliwa na wenziwe toka former mtesaji wa kanisa? zingatia Galati.1:1-10, kisha mistari uliyonyofoa ya 11-12 then endelea 13-24 kisha anaendelea/na wewe endelea til Gal.2:1-2. Nina uhakika ukisoma Neno hili kwa UPANA huu, utasikia aibu tu hata kama hutakiri hapa hadharani.

  (b) Unadhanije wewe, wakati anasema/andika ivyo, alikua ana-address situation on the ground e.g. upinzani na kusitasita kwa baadhi ya watu juu ya huduma/injili na mafundisho yake au simply writing down freely flowing revelational ideas/Msg and nothing on the ground as prevailing circumstances?

  Mpaka umeitafuta hii ‘Tumeitoa wapi ya asante asante?’’ tena ya miaka 2 almost iliyopita ktk mada nyingine kabisa kisha kuilazimishia hapa, tehe tehe… ok sasa natambua kwakweli Lwembe be honest, umeshindwa kukabili hoja zangu na kujibu kwa ufahamu mzuri maswali yangu, hali yako tete.

  Hili andiko-1Kor 14:34-35 nimeshalisemelea/fundisha lote mistari yote ya 1-40, kwa nini una kaa tu mistari hii hapa 34-35? Una personal gain najua! soma tena nilicho-analyse kwa majibu yangu kwa Yusha-ni vema kujifunza mambo ya kweli kuliko kugoma! Au niulize ivi, kwa nini hukuona KWANZA Paul alipokataza kunena lugha zaidi ya watu 3 au kuzuia kabisa unenaji kama hakuna mtafsiri ktk mistari ya mwanzo hii 26-30?…ukaona kwa haraka hii ya kukataza wanawake hapa-34-35? Si usema tu amen mpendwa kuna kitu umepata hapo au ndio yale yale ya kufa na tai? Ndio maana sitawaacha kuwabana sana kua ni usalama kujua Neno kwa UPANA wote, ni NI HEKIMA kuliko ya kwenu ya kukuta hapo yalipo na kupaki hapohapo, be carefully, maandiko mengine yanahitaji kutulia/ku-cross cheki na mengine, la sivyo mtapotsha watu wengi na kuunda doctrine nyingi.

  Umeunganisha andiko la juu na haya(jitihada za makusudi lakini mbovu kupata mwanya wa kumkandamiza Mwanamke – ukasema…’Torati yenyewe kwa sehemu hii hapa:
  Hes 30:3-8 na kisha ukaunga tena na hili kwa kusema ivi…’’Torati hiyo ilimekuwa fine tuned hapa-1Kor 11:3, kisha ukaendelea na hili..’’1Tim 2:12 -15.Jibu: Nimeshangaa sana kumbe wajua SASA kutumia torati wewe? si ulisema haurudi uko tena? uliyaita/kuita makorokoroni kwa Seleli wakati nilifundisha kua ziko kweli ktk Agano la Kale, ZINAHAMIA Agano J na nikasema kua nyingine zinahama KAMA ZILIVYO na hata nikawakataza kua muwe waangalifu kusema kila kitu Agano la Kale kukitumia/fanya/fuata/ ni Laana. Sasa umetumia andiko hili- Hes 30:3-8? Nikufanyeje? Umeuona ukweli sasa siyo?

  Lakini hata ivyo, maandiko mengine uliyotumia, nilishayatumia na kueleza kua ni kweli Paul aliweka katazo kwa wanawake kunena-Kufundisha NDANI ya Kanisa-nilichambua kwa kina kwa nini iwe ndani ya kanisa kwa kuangalia maneno yaliyotumika ktk 1Worinto.14 na 1Timo.2: kama ‘wanyenyekee’’, ‘wasiwatawale wanaume’- statements zinazoonyesha concern ya Paul ktk kuweka sawa mambo ndani ya Kanisa kwa kuzingatia Torati pia inasemaje-(kuhusu Mamlaka ya Wanaume juu ya Wanawake na pia mila na desturi walizo ishi kwamo, sijaona unachajaribu kufanya kwa kuyanukuu hapa etna, je ni kwamba unataka kusema, hakuna uhusika wa Paul kama Paul? Wakati nilishaonyesha ivyo kwa maneno kama Simpi/ I wish nk-rejea nilichoandika kuhusu mistari yote 40 ya 1Wakor.14, aliyosema Paul?mbona sijaona point hapa au ulikua unajifurahisha tu kwa kurudia rudia au raha ya kuniiga my nukta kwa nukta anointing?

  Umedanganya ivi kua…’’Wanawake wa makusanyiko hayo, wanalitii Agizo hili, kwa raha zao, na hivyo kudumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi, chapa ya wokovu wao’. Swali: Una hakika Wanawake wanafurahia kuwafanya wao zero kwa mambo mengi hata bila kuzingatia ilikua ni jambo la kufundisha tu NDANI ya kanisa?

  Hii bado nairudia kwakua ina nguvu sana na ni kweli kua, Role model wa MWISHO wetu katika wanadamu wote ktk Bible ni YESU si Paul wala Musa! Paul alishasema mwenyewe kua Tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo-ivyo Kristo hapo ndio focus/target siyo Paul na hata ivyo ktk Waefeso 5, alimaliza kabisa kusema MFUATENI MUNGU kama wana wapendwao! Final ni Bwana na hawa Paul, Petro, Yohana Mbatizaji na wengine wote, hawana shida kukubali kujua ilo, wewe tu una mambo yako ya kuwinda chance ku-harass Wanawake kwa kisingizio kua Mungu amekupa nafasi kuwapanda vichwa na mabega, wanyamaze kimya kote na popote! Kwa iyo kwa kua Yesu ni final, basi zingatia alikua na tabia/ mwelekeo/treatment gani kwa Wanawake, utatubu huo uanaume mbaya Lwembe. Ni vema ukazingatia ili unapoangalia Kanisa la Agano Jipya na Wanawake

  Umeshangaa kwa kuuliza swali la ajabu hili..’’Inawezekanaje mtu akawa na ujasiri wa kulihamisha Neno la Mungu kwa KULITOA katika wakati? Jibu: Nimeshasema na narudia tena kua Yesu ktk Marco 10:1-12 alihamisha Neno la Musa na kuweka lake-hayo ndio nasemaga ‘’Neno/Ujumbe/Kitu cha Ki- Mungu kwa vizazi vyote bila kujali sasa tamaduni na mila nk’’, aliposema MUSA(role model mdogo Asiye final )aliwaandikia/aliwaruhusu wafukuze na kuwapa taraka kwa sababu ya mioyo yao migumu (notice: Hapo ni Kiongozi wao wa Kiroho-Musa anasema/fanya maamuzi/weka utaratibu kusolve mambo-Kama Paul-(role model mdogo mwingine alivyofanya ktk makanisa aliyokua Baba) na si lazima waliyosema yawe kwa vizazi vyote past,present, future, LAKINI role model FINAL Yesu akasema, kua toka mwanzo haikua ivyo, maana hakuna kuachana-no taraka kabisa! Sasa nikuulize Swali: Unachukua la role model Final au wadogo? Mbona naona nafundisha vitu so simple bado hudaki, shida huelewi au kuna vitu umeshameza dhidhi ya Wanawake?

  Lile andiko la kumkana RM umetumia vibaya tu kunitisha, haukuzingatia kanuni hii ya matumizi ya Neno kwa usahihi..2Timoth.2:15c. Nataka nikuambie kua KULIFAHAMU NENO KTK HEKIMA YOTE NDIO MTAJI NA NINAPOJARIBU KUKUFUNDISHA ILO, UKASEMA NI KUMKUFURU RM au ulipotumia ile la Wagal. kua nimelaaniwa, unakosea sana na utakosa mengi, mimi nimebarikiwa nani mtumishi wa Mungu wa kweli na nina jitahidi kujaza Neno ndani yangu ktk balance zote, si zenu za kung’oka na kipande kimoja na kuwakataa watu(wanawake) ktk mambo mengine wakati walikatazwa wapi tu, Neno limesema wazi-lakini ninyi mnapitiliza na kudhani huo ndio uongozi barabara wa kua Mwanaume haswa wa kiroho kumbe ni ujinga na uonevu tu wa kibinadamu dhidi yao tu. Watu wangu wanaangaMIZWA kwa kukosa maarifa and in this case, Watu wangu wanaANGAMIZA wenzao(females) KWA KUKOSA MAARIFA-ie UFAHAMU/TAARIFA YA NENO LA MUNGU KTK HEKIMA NA MAPANA YAKE.

  Press on

 101. Siyi,

  Umesema, ‘’Ni kweli mtu anayesimamia neno, huonekana mshamba katika macho ya duniani- na kutoa andiko hili…1 korinth 1: 18 . Swali: Sasa wao wakiona neno la msalaba ni upuuzi, sisi inatufanyaje kua washamba? We vipi ndugu?

  M23 kuifuata kwa namna ya dini ndio shoti but kwa namna ya alivyoleleza Mkuu alivyo, iyo ndio safi, tatizo ndio liko hapo tu.

  Kwamba naweza kubaliana na wewe kuwa Paulo alipotema ngeli za neno, Foestus baada ya kuchomwa na injili ile alimwambia Paulo kaheuka!! Jibu: Ninakubaliana nawe kwa sehemu kua Injili fire-fire iliwatandika kweli wale wakuu but nilitaka uone pia mbali na Mafunuo na hekima toka juu lakini pia usomi ulimuwezesha akawa na uwezo wa kujieleza, kusuka nondo, ku-reason, argue, debate, thinking big, thinking of the thinking-logic, IQ, kua na active intelligency, smartness upstairs na ivyo vyote vya Paul ilikua ni tool hatari sana kwa kila aliyesimama mbele yake kumsikiliza/pinga/..ndicho kilitokea siku iyo Mdo. Sura yote ya 26 mpaka kufika Mstar wake wa 25 anajisema yeye mwenywe kua ninasema( kwa maneno yangu ni kama alisema-nashusha nondo) za kweli na AKILI-neno Akili kiingereza inatumia REASON-words of reason!Umeiona iyo? tamu sana-ndio maana nawabana hapana toroka kufikiri na kua na akili/uelewa, kua na ‘upako’ si excuse ya kufikiri, kutumia akili, bongo! Nyie vipi? naman gani hapa wapendwa nawaambia hili kila siku tena kwa ushahidi thabiti toka Neno!

  Umenishangaza kwa kunisisitizia vema ivi-Plz, heshimu wanawake, penda wanawake, jali wanawake, ILA HAPA umeropoka unless UJIBU SWALI AMBALO HII NI MARA YA 4 NAKUULIZA…..’’Umesema ivi..’’but do not let them to lead you into sin coz of their weaknesses!!. SWALI: HII WEAKNESS uliyokomalia ni ipi maana nimekuelimisha mantiki ya andko hilo..1Peter.3:7- ktk post 2, it appears huelewi due to either ulishakua na pre-concieved wrong ideas against Wanawake au faulty understanding on what coud probably that andiko mean! Jibu sasa nione unaelewaje ndio maana mwanzo kabisa niliwauliza’’Wanawake wana matatizo gani? Hamkujibu! Do u see I keep the flow ee! Nifyatuki fyatuki bora lije na liende!

  Nilikuuliza ivi..’’KILA MWANAMKE ATAKAYE VAA SURUALI KWA KUA umesema MUNGU AMEKATAA, ATAKWENDA JEHANUM? Ukajibu…Ndiyo ataenda jehanamu kweli asipotubu mapema
  My response: NA WEWE IN THIS CASE NI BEYOND REPAIR na iyo mbingu hakika ni private entity yako located at Chalinze, ivi huoni hata aya kujibu namna ambayo mtu akisoma anaku zero down? Ati kiiiiiila mwanamke duniani akivaa tu troza anatupwa jehanum akifa na troza lake bila kutubu! Sijui ninywe maji au uji nikapumzike kisha nikuteremkie kama rocket madude yako haya? Mwe! ha ha ha ha aibu kweli jamani! na mtu anajiamini kweli kujibu ati oo yes ni fire wote, kha! Kweli huna mungu wa aina yake.Sasa embu nikupige msasa kidogo uone ulivyo haribu
  Maswali:

  (a) Mashariki ya mbali na kati( wanavaa kanzu/magauni/mabaibui kama wafanyavyo waislamu kwetu, yapi ni mavazi ya kike na kiume in that case?
  (b) Troza ya kiume ndio dhambi au hata ya kike? Ha haha na hamu kuona utajibuje tena hili-nakuona kama kawaida utaingia mzima mzima tehe!
  (c) Aliyesema Suruali ni nguo za kiume nani? Biblia au Watu ndio wanadhani/chukulia ivyo? tehe! mwe! kazi unayo maana hapa ukijibu tu vyovyote kuna swaki tena, pini kali.
  (d) Je mwanamke kujisitiri kwa ubora zaidi viungo vya siri ktk sehemu hatarishi eg wanajeshi vitani, mazoezi ya michezo, mbu wanapokua wakali dhidi ya manesi hospitali usiku, fundi umeme anayepanda juu, cleaners ktk maofisi, wanaoishi Nchi za Ulaya na mabara mengine kwenye baridi za kufa mtu au kugandisha/kudhuru hata ngozi/misuli/viungo, uko kooote na hao wooooote wakivaa troza, wanatupwa jehanum eti eee? Ha ha ha yaani jamani its so funny to engage nawe ktk debate, yaani kama Lwembe vile ingawa Yusha mjanjaa weeee na Mabinza, wanaende kimahesabu, hawaingii wazima wazima pwaa kisha kuabika bwerereee kama wewe Siyi na …. Ha ha ha ah.

  (e) This is silly question lakini ngoja nikuulize tu…Mwanamke Mpendwa anayetaka kupanda Mlima Kilimanjoro, ili akwepe kutupwa jehanum, apande amevaa mpaka juu kule, suketi eti ee? troza no way au siyo?

  Niliuliza kimsingi kabisa ivi…’’JE KUTOKUVAA SURUALI KWA UELEWA WAKO WA MAMBO YA MUNGU, NENO LAKE KWA MAPANA YAKE NA MOYO/TABIA YA MUNGU BABA YAKO AND I HOPE NDIO BABA YANGU-ingawa sijui lini ulishafanywa Mwana, JE KATAZO ILO NI NENO LA NIKO AMBAYE NIKO KWA VIZAZI VYOTE PAST, PRESENT AND FUTURE REGARDLESS YA CULTURE, WETHER, AINA YA KAZI? Ukajibu bila haya ivi….Katazo hilo ni la Mungu mwenyewe ndio na ni la vizazi vyote. Mungu hajabadilika wala hajatangua chochote.

  My response: Nilikuuliza ivyo nikilnga uone/uwe na ufahamu mkuwab wa mambo nimeyauliza pale juu (a-e) lakini naona majibu yako, yanaonyesha wazi, umepita kapa, ngoja nisubiri ukatakavyo jibu ya juu then nione kuna haja kweli ya kudeal nawe ktk ili au tukubaliane tu kudance-dance wawili angalau ka muda kapite

  Post nyingine uliniambia ivi…ktk 1 korinth 14 nachanganya bado ile issue ya watu wote kunena kwa lugha ndani ya kanisa na kisha kuonekana kana kwamba wana mapepo’’Jibu: Unajua usipende kuonyesha confidence kubwa wakati vitu hamna! Sasa umenifundisha nini! Nilichokisema mie ndicho umesema! Kuweka utaratibu wakati wa kunena-ndipo hapo AKAKATAZA wasinene zaid ya 3…therefore ukatazaji huo ndio Utaratibu wenyewe huo ulfikiwa/wekwa kwa kukataza baadhi ya mambo. We ulitakiwa tu baada ya mimi kuwafundisheni mistari kwa mistari iyo ya 1Worinto 14, ungesema amen basi siyo tena confidence/mbwembewe za ovyo, I read don’t know unamisje vitu minor kisha kujidai kufundisha kitu ambacho tayari wewe mwenyewe ulisha kimisi ivyo unafundisha kitu from missing base/reference/ground-mambo hayaendi ivyo.

  Ulisema unakubaliana nami kabisa kuwa wanawake wanaweza KUFUNDISHA nje ya kanisa, kama vile kwenye miji ya watu, hospitalini, nk, sehemu ambazo si rasmi kwa ajili ya makuahani: JIBU: Asante kwa kuelewewa kua WANAWEZA NA WANA UWEZO/KARAMA/HUDUMA TENA RM alizowapa kabisaaa, ndio faida ya my nukta kwa nukta anointing-inanisaidia kumulika kila chembe, kukwangua yote ya ma-by the ways ili tubaki na balanced stuff mezani

  Pongezi zako kwa Mabinza, zikancell kwanza akisha jibu my response…so relax kwanza.
  Ni kweli umesema kua…’’WAKATI UMEFIKA SASA WA KUSIMAMA KWENYE NENO LA MUNGU PEKE YAKE BILA KUJALI MAPOKEO POTOFU YALIYOPO SASA NDANI YA KANISA’’…lakini muhimu zaidi, Wakati umefika naamu nao ULIKUWEPO na sasa UNAJIRUDIA(upo) ambapo SI TU TUTASIMAMA KTK NENO LA MUNGU peke yake bali pia ktk NENO LA MUNGU KWA USAHIHI SANA KWA KUZINGATIA MAPANA YAKE YOTE.

  Press on.

 102. Bwana Yesu asifiwe,
  Biblia isema « Warumi 15:14 Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana ».
  Kwa hivi naomba utulivu wakati tunapojadili. Mim sijue kam mtume Paulo na wengine mitume wa Yesu wangelijitokeza hapa,wangelitushangaa kiasi gani !!!!! Nafikiri hawahitaji tuwapiganie hata ktk maandiko.
  Naona wengine wetu wameanza give up ktk huzuni kabisa, and this is not interesting.
  Labda tungeliangalia kwa makini kam tunajibiaje wenzetu ao kam tunajitokeza nasi tupate vilevile elimu. Nafikiri hakuna hata mtu mmoja anaejitoshelea angalau awe amejazwa RM kwa uwingi.
  Ndugu Siyi hakukosea kabisa kam pengine ameitika kwa nusu maoni ya wengine. Hii inastahili.
  1) Naona Ndugu Yusha ana swali hapa juu. Nataka nilete maoni kulingana na hilo swali. Ulioandika Yusha inaonyesha wazi kam Paulo alisema DESTURI, na wala si AMRI ya kutoka Mwenyezi Mungu. Mambo ya desturi inaweza tekelezwa au la pasipo kuhusika na dhambi. Mtume Paulo iko wazi katika mafundisho yake. Ni sisi ambao hatumuelewi. Tujitahidi kabisa kumuelewa. Hakuwa kam hawa manabii wa wongo ambao wanadai Mungu alinena na wala hakunena. Utamuona Paulo akiandika akilenga his wish (1 Wakorintho 7:7-8 Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo) ; pengine ananena mambo ya desturi kama vile tunavyoongelea hapa ; pengine anatoa amri itokayo kwa Yesu (2 Wathesalonike 3:6 Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.)
  Hii ni shahiri kidogo tu, ya muhimu ni kuona kama Paulo alikuwa wazi kabisa.
  Kutokana na hii, wanawake wakifundisha ao kuwa viongozi haiyamaanisha kanisa lile limepotoka kwa kutenda dhambi.
  2) Nataka vilevile niongee na Siyi hivi :
  -Nakushukuru Siyi kwa kuwa umesema unapendelea kuwa kwa upande wa Mwenyezi Mungu na ya kuwa unatazamia masemi ya Biblia. Na nilipoyasoma shahiri ulizoleta kuhakikisha kam wanawake hawastahili kuvaa suruali, niliona kabisa you’re right. Lakini nilipojiswali kwa nini Yesu hakuvaa vile na hata neno suruali haitajwe ktk agano jipya, nimepata elimu zaidi. Niliposoma NIV Bible (ambayo ni moja wapo wa tafsiri kwa lugha ya kingereza zinazoaminika), niliona ile inayotajwa kuwa suruali kwa kiswahili ni UNDERGARMENTS or UNDERCLOVES or UNDERPANTS. Hivi nikatazama kwenye dictionaries kwa lugha mbalimbali nikaona kwamba inayoitwa suruali namna tunayoijua leo, ilikuwa kwa mwanzo feminine cloves. Ikanisukuma nione nguo gani makuhani walizozivaa, kwani hii inayotajwa kwa shahiri ulizozipana hazihusu nguo za kuonekana kwa inje. Ndipo nikagundua kwamba kanzu na joho zilikuwa ndizo nguo zilizotajwa zaidi. Hata kwa agano jipya ni zile zile tu. Na nikagundua kam wanawake walivaa vile vile kanzu. Zilishonwaje, Biblia haisemi. Soma shahiri hizi chache: Mwanzo 37:3, Kutoka 28:4, Yohana 19:23, Luka 6:29. Hizi shahiri zaonyesha nguo kamili za makuhani, nguo ambazo Yesu alivaa, nguo ambazo wengine walioishi wakati Yesu alipokuwa ndani ya mwili walivaa, na ginsi wanawake walilia wakionyesha kanzu ambazo Dorika alikuwa amewashonea.
  Hii yote inamaanisha kam kwa majina nguo za wanaume na wanawake hazitofautiane. Na kam si kwa majina in general, itakuwa namna zimeshonwa. Biblia haisemi kanzu za wanawake zilikuaje ukilinganisha na za wanaume, lakini kwa sababu imeandikwa mwanamke asivae nguo ya mwanamume, kulikua tofauti fulani. Hivi ijulikane kam mwanamke asivae nguo ya mumewe. “Sheria” haingelikuepo kam nguo ya mwanamke haina uhusiano kwa majina ao kufanana na ile ya mwanamume.

  -Kwa nini mitume walibatiza kwa Jina moja, Biblia haisemi. Kwa nini Paulo alijetenga na Petro, yale yote ni maswali. Lakini bila kuleta filozofia za kuumiza akili za watu, ni rahisi sana kuona kama ni ule udhaifu mitume walikuwa wakikiri kila wakati. Mtu kuwa na RM haimleti kulingana na Mungu ambaye ni yeye pekee hana udhaifu. Mwanaadamu ni dhaifu tu (1 Wakorintho 2:3 Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi.) Waliyofwata mambo ya historia ya kiteolojia wanasema kam ile wakati mitume waliobatiza kwa Jina la Yesu, wayahudi walikuwa wamefanya bidii ili wazimishe lile Jina la Yesu. Ikawabidi mitume walitumie sana hata ktk kubatiza ili wahakikishe kam Yesu ni Mungu. Lakini Bilia ilinyamaza.

  Samahani, nilijitahidi kuwa fupi ktk maandiko ili isomwe kwa urahisi. Kam kuna swali, karibu. Iwe imeongelewa ktk mjadala mwengine ao juu kidogo, inaporudi ni kwamba haikuisha, au imeisha bila kuelewana.

  God bless you.

 103. Mabinza,

  Pole kaka, umesema, Katikati nimekuchanganya! hutachanganyikiwa tena, tuanze polepole Mabinza, utaelewa tu ingawa ukichanganyikiwa, utakua UMEJICHANGANYA au kuna madude mengine YANAKUPELEKEA KUCHANGANYIKIWA lakini nakuhakikishia KAMWE..hoja/comments na Mafundisho yangu, kwa mwenye UELEWA, HATANGANYIKIWA- labda kama kuna yale mambo yale…yenu yale ya ‘desh..desh’’ ONLY..si unajua tena! Lembe atakuambia

  Sasa si unaona hii vurugu umeanza nayo ni baab kubwa, kunyanyuka na andiko hili-2Tim. 2:20 na kuliingiza hapa. Nashauri ivi…SOMA KWANZA SURA NZIMA HIYO KISHA ANGALIA SANA kuanzia mstari 19-21 Uone kama ulivyonukuu kwa kipengere hiki cha kukataza Wanawake kina-relate! NEVER! Umefanya kosa la kiufundi kaka- yale yale ya Yusha, Lwembe na Siyi-baadhi ya maandiko unapolikutia, basi unafilia hapo!

  Ni kweli Mwanamke alidanganywa na shetani! Lakini si ni kweli pia Mwanaume alidanganywa na Mwanamke?aliyekua anatakiwa amlinde/kumuongoza, so Nani mjinga zaidi? Lakini swali jingine, kwa Mwanamke kuanza kudanganywa, ina maana unataka kusema/kudhani Mwanaume hawezi anzwa kudanganywa na akadanganyika?

  Umetoa mfano mzuri sana wa… mwalimu aliyedanganyika atafundisha uongo! Mtu dhaifu, huwezi kumpa kazi ya Jeshi! LAKINI Mwl mzuri anaweza ZUSHIWA kua alidanganyika ili ubora wake usitambuliwe maana wale weak teachers wenyewe kabisa wanaona huyo Mwl huyu bora akija Skuli iyo, no job for them au wanafunzi watahamia wengi kwa kituo chake cha tuition.

  Mfano huu nao mzuri… Wa kila aina ya Chombo na kinatumika wapi, kisha ukasema ivi…,vivyo hivyo, mwanamke hupewa karama kwa kadri ya Roho anavyotaka kumtumia! Lakini kwakuwa lilosema asihubiri ni Neno la Mungu. JIBU: Kosa kubwa tena umefanya hapa! Haijasem Asihubiri bali asihubiri Kanisani..tena si kuhubiri as such..1Timotheo.2:11-12 imeweka vema—ni kwamba ASIFUNDISHE, wapi? bila shaka ukiunganisha na 1Wakor.14:34 -jibu ni KANISANI-yaani picha/mantiki ni hii- kwa tamaduni za wale kipindi kile na influence ya torati kipindi kile, Mwanamke kusimama mbele ya Wanaume kuwafundisha/ elekeza/onyesha njia nk, hakupaswa.

  Pia umesma ivi..’’Roho hawezi kujipinga ati atokee mwanamke adai kuwa ana Karama ya kuhutubu’’ JIBU: HAIJAANDIKWA kokote kua RM amekataa kuwapa Wanawake huduma/karama ya kuhutubu ila kilichoandikwa nai KUTOHUTUBU MBELE YA KANISA.

  Pia umesema, karama ni sawa kuwa nazo maana hazina majuto! Swali: Je Wanawake wakiwa nazo ndio majuto?

  Pia..’’Rais wa kike hawezi kuitwa Baba’’ Jibu: Ni kweli lakini kumbe BADO NI RAIS tu huyo Mwanamke!hata kama haitwi Baba! na kodi utalipa,ukikataa au mkaandama bila kibali chake/walio chini yake, MTAPIGWA TU na mimi nasema WAPIGENI tu, mtanyukwa enyi Wanaume kupita dola-hi mwambie kwa sauti Siyi, Lwembe na Yusha
  Hapa umebalansi vema kabisa…’Isifikiriwe kuwa, mbinguni kuna mfumo Dume, la hapana’…. Ndicho nachotakaga kufundisha kwa kutumia maneno kama ‘Neno la Mungu kwa vizazi vyote’’, kwa kuelewa ivi kua kwa Mungu hatimaye hakuna Ke/Me…unaweza fahamu kua misisitizo ktk Bible-Agano la K na J kuhusu kuweka gap kati ya Mwanamke toka Mwanaume, isikurupukiwe kikukariri bali kwa kuangalia/zingatia NENO/MOYO NA MUNGU KWA UPANA WAKE.

  Unadhani ktk majibu yangu umepata“Ufahamu KTK chembe yako ya uhai!”?
  Press on

 104. Yusha,
  Sasa wewe rafiki yangu, unaibukaje namna hii kimya-kimya badala ya kuchapa kazi kwanza? Yaani unajua kabisa kuna mambo unatakiwa kufanya halafu unamaliza kijanja ivi kwa kuanza maombi na kumtaka Mungu ju yangu!!!! Mpendwa na wewe bwana, hutaacha lini mambo yako haya ya misismko ile ya kipendwa mibaya ile ati oooh jamani, tumuoombeni! Mmh! nani mie! Au nyie! sasa maombi ya namna iyo ya nini hapa wakati tunachapa kazi mwanzo mwisho! Ni ivi, SIHITAJI MAOMBI WALA NINI, NATAKA UCHAPE KAZI/HUDUMA YA KUGAWA NENO KWA UHALALI—2Timothy.2:15c si kwa KUKARIRISHWA!! kwa ivo, maombi ayo weka pending kwanza, utapoteza time na energy, chapa kazi Kaka.

  Umeuliza tafsiri ya ..1wakorintho 14:33-34. Ulitakiwa uulize kwanza nani anafafanue kisha tasfiri na kama niivyo, umeishangaza kweli kumbe husomi posts humu wewe ziwe zako na wengine!!!!!!!!! nimeshajibu sana ilo. PLZ ILI USIONEKANA HAUKO SERIOSU KAZINI, UKIJA HUMU, FANYA HOME WORK YAKO KWANZA KWA KUSOMA YOTE KWA WOTE NDIPO SEMA KITU,LASIVYO UTAONEKA UNAKURUPUKA, UNSERIOUS GUY AND NOT COMMITTED KUSAIDIA MAMBO HAPA. Ila kwa mtu kama mie, sistachoka,nita-copy a ku-paste toka kwa yale nimeshare kwa wengine maana swali lako hili limenithibitishia hauko serious hapa, ukiibuka, unaibukia misisimko tu lakini kazi hufanyi, huyu mpendwa vipi!

  Nilichapa kazi barabara hii nikichukua sura nzima yote.(mistari 40) kama ifuatavyo(si ninajua wewe, Lwembe, Siyi, Mabinza, mna tatizo moja namely kufia ktk baadhi ya maandiko kama yalivyo na unapoyakutia pale pale!-yaani Neno la Mungu halijakaa ndani yenu ktk HEKIMA YOTE but kwa hekima robo na nusu may be.1Wakorintho.14:1–40 ( Tafadhari soma kwa makini maelezo ya ziada ktk mabano kwa kila mstari)

  Mstari wa 5= Imeandikwa, ‘Nataka’(Kiingereza inatumia neno turi hili-I WISH ninyi NYOTE..mnene kwa lugha’’(Notice: Ana ‘WISH’ tu kama MTU/Kiongozi wa Kiroho wao na pia ninyi ‘NYOTE’-hakuna cha Mme/Ke hapo.

  Mstari wa 6= Imeandikwa, Nikiwajia naongea kwa lugha, itawafaidia nini? isipokua nikinena kwa ufunuo, Elimu/Maarifa, Hotuba au Fundisho (Notice:anaanza kutoa dondoo hapa kuhusu tatizo analoliona Kanisani kwake hapo-atakapoendelea kuongea mistari inayofuata 7-13, unatambua mara moja ni lipi)

  Mistari wa 14,15,16-21: Anaendelea kugusia tatizo-kukosekana kwa utaratibu ktk kunena kwa Lugha na pia anaanza kudondoa nini cha kufanya-kuweka taratibu.

  Mistari ya 22-25: Anaendelea kusema athari za kukosekana utaratibu ktk unenaji lugha na kisha anasema kunena ni sahihi na ina faida yake-ishara kwa wasioamini lakini kwa utaratibu au kuwepo na kutafsiriwa ili mgeni(asiye amini naye afaidi/ajengwe/achallenjiwe njia zake mbaya, asije akawaona wote vichwa maji humo kanisani maana wote wanena kwa lugha mpya-haelewei!

  Mistari ya 26-33: Hapa sasa anaweka wazi utaratibu aliokua anaudokeza taratibu kwa mifano na hoja mbalimbali mistai iliyotangulia na pia kwa solutions izi alizotoa ktk mistari hii, inatoa picha wazi tatizo lililokuwepo kanisani pale na ivyo yeye kama Mchungaji/Mtumishi anayewasimamia wanae wa Kiroho, alipaswa kuwashauri cha kufanya( Notice: Mstari wa 27,28,29=Hata Wanaume hapa WAMEZUILIWA KUNENA! mpaka Paul kama kiongozi wao, anatoa maximum no. ya wangapi wanene(watoe unabii-yaani hata kama una Roho ndio anakuambia nena/amekufurikish-lakini kwa kua amesema max ni 3 na pia mstari wa 32 roho za Manabii huwatii Manabii, BASI KAA KIMYA kanisani-ivyo kukuza/kung’ang’ania tu ukweli kua WANAWAKE WALIKATAZWA- lakini bila kuona la juu yake la Wanaume/ Watu wote pia nao walikatazwa/wekewa utaratibu, kabla hajamalizia la Wanawake Mistari 34-35, ndicho nacho sema ni kukosa ufahamu wa Neno la Msingi KTK UPANA WAKE na kuondoka tu na kitu kimoja kukifanya ndio issue kubwa sana-cha Wanawake kunyamazishwa!!!)

  Mistari ya 34-35: Ndipo sasa anatoa utaratibu kwa Wanawake pia kua na wao wasinene mbele ya Kanisa.(Notice: Hajaanzia hapa, wapo waliokatazwa pia toka juu yaani makatazo kuhusu Unenaji lugha na sasa makatazo juu ya Unenaji (Kuhutubu).Kwa nini Wanawake wanyamaze na hawana ruksa kunena MBELE YA KANISA? Jibu anasema: Wanatakiwa wawe wanyenyekevu na kama pia SHERIA YA TORATI inavyosema-(Hapa utaelewa kwa nini ktk michango yangu- nimekua natumia phrase..’’Zipo kweli nyingine ZINAHAMA MOJA KWA MOJA toka Agano la Kale to Jipya’’ na kwamba kuongea tu kiujumla kua Agano la Kale, mambo yake yote kuyafuata ni kujiweka chini ya laana-SI KWELI-NI KUKOSA UFAHAMU TU WA NENO LA MUNGU KTK UPANA WAKE-natumia kwa makusudi sana iyo phrase -‘’NENO LA MUNGU KTK UPANA WAKE’’( nitaliongelea ili pia kuhusu kama kweli KILA NENO/KITU CHA AGANO LA KALE NI LEO KWETU ni zero plus,plus NA HATARI-laana!!!!!!!

  Na jibu jingine ni aibu kwa yeye kuongea Kanisani.Sasa zingatia hii-ukisoma tu ako…’ni aibu wao kunena kanisani’, huwezi pata hasa mantiki ni nini-inabidi uunganishe na ki-hinti ameshakisema mwenyewe hiki..’’wanapaswa kuwa wanyenyekevu! Lakini Wanyenyekevu tu basi, iishie hapo? Au ina connect na nini hasa? Kwa nini asisitizie Wanawake kutunza hiyo nidhamu/tabia njema ya kunyenyekea? kwani kuna tatizo gani mpaka Paul akazane kusema, wanapaswa kua wanyenyekevu kama TORATI PIA INAVYOSEMA?

  Ni kwamba, ukishaona neno KUNYENYEKEA linaambatanishwa na jinsia-(be submissive ie submit under/to someone), ilo likiunganishwa na KUWAKATAZA kunena Kanisani na Torati ikawa refered, ni mara moja unajua hapo Kanisani, kwa kua kuna Wanaume na ukizingatia mila na desturi zao wao kama wayahudi Kabla na hasa wakati wa Sheria kuhusu ranking system iliyokuwepo ktk ya Mme/Ke na ukweli kua yeye anenaye(kuhutubu/kufundisha lazima, in one way or the other, ATAELEKEZA, FUNDISHA,KEMEA(fokea),AMURU, FANYA MAAMUZI nk…isingekua ni hekima MWANAMKE kunena-akiyafanya yote hayo mbele za WANAUME ( Waume,Kaka,Wajomba zao, Wakuu wa Dini, Wasomi wa Sheria nk wako hapo chini wanamsikiliza mdada/Mmama amechachamaa moto!!!!!!!- DESTURI/MILA NA SHERIA ZA TORATI-zingekataa, Wasikilizaji wasingeruhusu au hata kuacha hudhuria ibada ya ivyo-Mwanamke Kunena.=Kumbuka tena ni swala la Mila na Desturi tu hapa Paulo alilokua anaweka sawa.Unganisha na mantiki hizi ktk maandiko haya: 1Timoth.2:11-12- hapa anaweka wazi zaidi kua Simpi ruhusa Mwanamke KUFUNDISHA!!!!!!! Na kama hajualewa kua Paul alikua anaweka sawa ktk ile-1Wakorinto. 14, mambo ya Mila, Desturi, Tamaduni za wakati ule pia kwa kuzingatia Sheria zilikuwaje wakati wa Torati ndio maana alikazana kweli kuwasisitizia wawe wanyenyekevu na wakajifunze kwa waume zao, kutovuruga Utaratibu wa Mamlaka ktk ya Mme/Ke, anamalizia kabisa hapa ktk iyo Timotheo kua…simpi ruhusa mwanamke kufundisha AU KUWA NA MAMLAKA juu ya Mwanaume-(Notice: hapo kua Unenaji uliyosemwa ktk Wakorinto pale ni Ufundishaji ambao umewekwa wazi ktk Timotheo hii na ivyo Mwanamke kusimama na kufundisha mbele za wanaume kwa kua ktk Ufundishaji atakemea, amuru mambo, pitisha maamuzi, panga vitu, pangua mambo, elekeza matters kwa/mbele za Wanaume, iyo haitakua picha nzuri na a healthy church practice-more acute case by then- ndani ya Kanisa ktk swala zima la kua Wanawake kufundishwa kua chini ya mamlaka.

  Na swali hili pia…2Petro 1:21, nilichapa kazi njema hivi….. Kwamba,’Watu hao waliandika/sema hilo neno wakiongozwa na RM’’, Sasa kuna haja ya kusisitiza ilo? Unakuza mambo tu unnecessarily! LAKINI nimewafundisheni Wewe, Lwembe, Siyi na sasa nitangeukia na Mabinza kua HAO hawakua matikitiki maji wala mochwari hao bali Watu na tofauti zao, mfano..Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 ..Wakamvua Yesu nguo na kumvika vazi JEKUNDU (scarlet robe) lakini Marco.15:15-17 hasa mstari 17..Wakamvika vazi la rangi ya ZAMBARAU (purple).Hapa waandishi ni wawili tofauti ila tukio lilelile lakini limesemwa tofauti ie rangi ya nguo zile. Swali: Kwakua waliongozwa na RM na RM ni smart, nani aliongoza watoe report tofauti ya nguo zile kwa tukio hilo? sijui utajibuje! Nimeshakukaba eee?!

  Na neno la Mungu kusema kiongozi wa kanisa lazima awe na mke moja;inamaanisha nini?kwa nini hawakusema awe na mke ao mume moja?JIBU: Soma post zangu kwa Lwembe na Siyi kuhusu kukubaliana kwangu na Neno kuhusu Wanaume kuongoza NDANI ya Kanisa na kwa mambo yetu ya imani eg hata ktk familia na pia angalizo/fundisho langu kua kwa nini ni NDANI ya kanisa tu.

  Aya nianze kukukumbusha na wewe viporo…nitakuandalia pia summary yako toka kwa baadhi ya mambo nimekuuliza umefunika au umepewe lift Lwembe ambaye naye ndio ivyo tena huyu brother, akibu ni matatizo mengi aongeza na ninampa vitu vingine, anachanganyikiwa-ni ngumu sana mimi kuacha jiwe juu ya jiwe ambalo sitalibomoa, OK EMBU NA WEWE KAZI MOYO NA FANYA KAZI/SWALI HILI…Ktk Karama/huduma RM anagawa kama amependavyo kwa KILA mtu au kama Yeye Mwenyewe alivyowatoa na ANAENDELEA kuwatoa maana wale wa mwanzo waliotolewa yaani Mitume, hawapo leo, Je kati ya hao wanaopewa vipawa vyote ivyo( karama/huduma), WANAWAKE WAMO? Yaani RM anawapaga au kwa kua ni WANAWAKE, hawapewi? Anza ako kwanza then nitakujia na mengine.
  Press on

 105. Watu wengine ni Mungu na maombi tu!!wanawake kutokufundisha Paul hakuikataza kwa kanisa la mahali tu,ila ilikua ni desturi ya makanisa yote ya watakatifu.basi naomba mtu1 kuleta tafsiri ya andiko hili 1wakorintho 14:33-34«kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko,bali wa amani;vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.34.wanawake na wanyamanze katika kanisa,…..»Pili eti mimi Paul nasema na si Mungu;je bilblia ni neno la Mungu ao la mtu(watu)? 2Petro 1:21«maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na roho mtakatifu»walimu wetu nini maana ya neno hili?Na neno la Mungu kusema kiongozi wa kanisa lazima awe na mke moja;inamaanisha nini?kwa nini hawakusema awe na mke ao mume moja?

 106. Seleli, ndg yangu,
  Mwisho napenda nikuage katika mada hii, tumeijadili na wewe kwa kireefu sana, ninaamini uliyoyaongea yote ndivyo unavyo yafahamu na unavyoamini, na huo ndio ukomo wako, nami pia niliyoyaongea ndivyo ninavyoyafahamu na kuamini na sitegemei kuendelea kupata chochote zaidi kutoka ktk Maandiko cha kuweza kushare nawe na ndg wengine kwa msingi wa vifungu hivi vinavyomkataza mwanamke asifundishe.

  Basi ktk suala hili la wanawake kufundisha, ili kukudhihirishia kuwa umefikia ukomo wa kutumia kwako akili, na kwa kadiri tutakavyoendelea uta burst zaidi na mwishowe hata hao mliokuwa pamoja ktk msimamo wa kuwaruhusu wanawake wafundishe, watashindwa kukuelewa, maana hawatajua umepatwa na nini! Bali mimi najua ulichopatwa, kinaitwa “Spiritual Amnesia” yaani umepoteza kumbukumbu, hujui ulikotoka na Mada wala unakokwenda nayo!

  Angalia ulivyowageuka nduguzo ukiwaacha huko porini mlikokuwa pamoja, kwenye hayo Mahepe! Ngoja nikinukuu hiki unachokisema, huku tunavyomaliza hii mada:

  “””Kumbuka tena ni swala la Mila na Desturi tu hapa Paulo alilokua anaweka sawa.Unganisha na mantiki hizi ktk maandiko haya: 1Timoth.2:11-12- hapa anaweka wazi zaidi kua Simpi ruhusa Mwanamke KUFUNDISHA!!!!!!! Na kama hajualewa kua Paul alikua anaweka sawa ktk ile-1Wakorinto. 14, mambo ya Mila, Desturi, Tamaduni za wakati ule pia kwa kuzingatia Sheria zilikuwaje wakati wa Torati ndio maana alikazana kweli kuwasisitizia wawe wanyenyekevu na wakajifunze kwa waume zao, kutovuruga Utaratibu wa Mamlaka ktk ya Mme/Ke, anamalizia kabisa hapa ktk iyo Timotheo kua…simpi ruhusa mwanamke kufundisha AU KUWA NA MAMLAKA juu ya Mwanaume-(Notice: hapo kua Unenaji uliyosemwa ktk Wakorinto pale ni Ufundishaji ambao umewekwa wazi ktk Timotheo hii na ivyo Mwanamke kusimama na kufundisha mbele za wanaume kwa kua ktk Ufundishaji atakemea, amuru mambo, pitisha maamuzi, panga vitu, pangua mambo, elekeza matters kwa/mbele za Wanaume, iyo haitakua picha nzuri na a healthy church practice-more acute case by then- ndani ya Kanisa ktk swala zima la kua Wanawake kufundishwa kua chini ya mamlaka.

  Hitimisho kwa sasa ni kwamba, Ukatazaji wa Wanawake huu ni pale tu Wanapofanya mambo yatakapowawekwa wao kua kama viongozi wa kuwaelekeza Watu wote na wanaume, lakini kama ilo halipo, basi Karama/Huduma/Vipawa ambavyo Roho Mtakatifu huwapo Wote, basi na wavitumie tu pasi na shaka, wata-adjust tu/adjustiwa tu pale inapokuja kua mbele za Wanaume tena KANISANI NA KTK FAMILIA TU.”””

  Jamani mmekiona hicho anachokisema Seleli?
  ANAKUBALI KWA SHINGO UPANDE KUWA MWANAMKE ASIRUHUSIWE KUFUNDISHA!!!!!!!
  Oh, Haleluyaaaaaa! Jina la Bwana libarikiwe! Utukufu na Sifa kwake aliyetukomboa kwa Damu yake ya thamani!
  “My father, my father, the chariot of Israel, and the horsemen Thereof”!!! Seleli, nawe umeliona “Koti la Paulo”analokutupia, lidake uondoke zako na DOUBLE PORTION, ukaihubiri Injili ya Kristo kama walivyoihubiri mitume, tena uwaanzie katika Msingi, Mdo 2:38!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Gbu & all!

 107. Seleli,
  Ninakusifu kwa jambo moja, UNA BIDII saaana!
  Mafundisho yako pia, katika bidii uliyonayo ni Super Hybrid, kutoka katika ile ‘Mule Religion’, ambayo ni mchanganyiko wa Neno la Mungu na hekima ya kibinadamu!

  Unajua, yule mnyama anayeitwa Mule, ni mchanganyiko wa punda na farasi, ametengenezwa na wanasayansi ktk maabara; ana kasi ya farasi na nguvu ya punda ya kubeba mizigo, ile BIDII, bali hakuwemo katika uumbaji wa asili; kwahiyo lile Neno la Mungu lisemalo kila mbegu na izae kwa jinsi yake haliwezi kumtimilia huyo Mule, kwahiyo hana uwezo wa kujizaa!!! Nayo Bidii yako, haiwezi kuwa tofauti na huyo mule, tena wanyama hao hawamjui baba yao wala mama yao, ndipo hata heshima yao haina baba wala mama, labda maabara walikozaliwa, hayo makanisa!!

  Bali wana wa Mungu wamezaliwa kwa Roho wa Mungu, wanamjua Baba yao, tena wanaijua na sauti Yake! Aliponena kupitia mtumishi wake Paulo, wao walimtambua, maana Roho aliyekuwa ndani ya Paulo akiyahudumu hayo, ndiye huyo aliyewazaa!

  Nalo Neno la Mungu lina jinsi ya kutimia isiyoelezeka wala kuonekana kirahisi hapo linapowatimilia wakusudiwa, kwa sababu ni la kinabii, nao unabii unatambulikaga baadae au awepo mtu wa kinabii wa kulikamata hilo linalotimia machoni pa wote waliofungwa wasiuone, kama Maandiko yanavyojidhihirisha ktk Lk 4:21, hapo Kristo anapourejea unabii alioutoa kupitia mtumishi wake Isaya mamia ya miaka huko nyuma, na sasa akiwathibitishia, “…Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Na pia Mdo 2:16, mtazame Petro anavyourejea unabii, “…Lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli…”, unaona, inamchukua mtu wa kinabii kuutambua ujumbe wa kinabii, ni ujumbe wa Rohoni kwa watu wa Rohoni, kuzidhihirisha nyakati!

  Ndipo napenda sote kwa pamoja tuyarejee hayo unayoyafundisha pamoja na wakufunzi wako, ili tujiridhishe iwapo Injili mnayoihubiri leo hii ndiyo hiyo waliyoihubiri akina Paulo, ikiwa ni hiyo basi ni jambo jema, la si hiyo, je, yawezekana Andiko hili la Gal 1:8-9 likawa linawatimilia pasi kujua? “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”!!! Maana haya yanapaswa yawatimilie watu, ili mradi yamenenwa hivyo na Mungu (au ni Paulo tu na kanisa lake!).

  Pia nataka tuziweke wazi hali za kiroho za wahubiri hawa wawili, Paulo kwa upande mmoja na Seleli kwa upande mwingine kwa ushuhuda wao wenyewe, kwamba Nguvu inayotenda kazi ndani yao asili yake ni ipi?

  Mt. PAULO, Gal 1:11-12:
  “Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.”
  Paulo anaendelea kututhibitishia utume wake hapo anapotuambia,
  “…Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake”

  Mwl wetu SELELI, kutoka nukuu za ushuhuda wake ktk mada ya ‘Tumeitoa wapi…”:
  “Wengi wetu ktk huduma na mimi nikiwemo…tunapowaombea watu kujazwa Roho Mt tunawaambiaga waseme ”asante Yesu”.. mara nyingi and kila mara huku tunachochea maombi na at last kunatokea ishara nyingi zinazoonyesha wapo waliojazwa mfano kunena kwa lugha.”
  (Masikini! hajui hata hiyo midude ilikotokea, anaipokea tu!) Sijaiona rejea ya ki Maandiko ya jambo hilo analowafundisha hao wanaomfuata, kwahiyo inaweza kuwa ni mambo ya yale maroho ya dini wanayoyatumikia, huenda nao walitengwa kwa ajili hiyo!!

  Haya, hebu na tuziangalie Huduma zao kwa kadiri ya Nguvu iliyo ndani yao:-

  MT. PAUL: 1Kor 14:34-35:
  “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.”

  Torati yenyewe kwa sehemu hii hapa:
  Hes 30:3-8
  “Tena mtu mke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aketi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake; babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika.
  Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na BWANA atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza. Tena kama amekwisha kuolewa na mume, wakati huo wa nadhiri zake, au wa neno hilo alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na mumewe akasikia, naye akamnyamazia siku hiyo aliyosikia neno hilo; ndipo nadhiri zake zitathibitika, na vile vifungo ambavyo ameifunga nafsi yake vitathibitika. Lakini kama mumewe akimkataza siku hiyo aliyolisikia; ndipo ataitangua nadhiri yake iliyo juu yake na neno alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na BWANA atamsamehe.“
  16 “Hizi ndizo amri, ambazo BWANA alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, ali nyumbani mwa babaye.”

  Halafu angalia Torati hiyo ilivyokuwa fine tuned hapa ktk AJ kwa ajili ya Kanisa la Mungu:1Kor 11:3
  “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, … “

  1Tim 2:12 -15
  “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.”

  MATOKEO KWA WALIOIPOKEA INJILI HII:
  Wanawake wa makusanyiko hayo wanalitii Agizo hili, kwa raha zao, na hivyo kudumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi, chapa ya wokovu wao, kwa ile Nguvu iliyojihifadhi ndani ya lile Neno litokalo ndani ya kile chombo cha udongo kilichotengwa kwa ajili ya kulidhihirisha jambo hilo, Mhubiri na Mhubiriwa!!!

  SELELI: 1Timo.2:12
  …Paul anasema. Simpi/ I do not give…ruhusa Mwanamke..ni yeye kama Paul ktk kanisa na situation iliyokuwepo, anafanya maamuzi kama kiongozi wa kanisa kusettle issues, kuweka system upon which mambo yafanyike kwa uzuri.Kuchukua hii kama ni criss-crossing Gen-Rev God’s everlasting Word ni influence mbaya ya dini/dhehebu la mhusika, ni stubborn personal software za wanaume na ni ufinyu wa kudaka hasa cha Mungu ni kipi na mtu ni kipi maana tumesha establish fact beyond critic kua Mungu alitumia Watu hai na si wa mochori! Ivyo walikua na hisia zao na muono wao pia tamaduni zao

  1Wakorinto.7:12
  …Lakini watu wengine nawaambia MIMI wala si Bwana….. Yeye mwenyewe Paul anasema wazi na live kua si Bwana ananena bali Yeye! Hence,Kuhamisha alichokisema hapa brother Po kiwe ni cutting across Heavenly God’s everlasting Word, simply ni ujinga tu na artificial kiroho!=ile kukomalia kua kila kitu ni Mungu ndani ya Bible na eti kwa kufanya ivyo ndio mtu anataka ifahamike kua hana mchezo na Neno la Mungu na heshima aliyo nayo kwa Bible ni nambari 1! mwe!

  Nyongeza ni kwamba, Role model wetu katika wanadamu wote ktk Bible ni YESU si Paul wala Musa! KAMA YESU ALIKUA SO POSITIVE, CARING and COOPERATIVE TO WOMEN needs/dignity(fanya survey and see Jesus and mwitikio wake kwa kila women aliyekutana naye) then example yake MUST be no. 1 to CUT( copy haitoshi) and Paste. Hii haimaanisha hata kidogo kua Kaka Paul did wrong, a big NO! He was simply as Kiongozi wa particular group, playing his role to settle the things in order. Besides, Angalia ktk Bible MUNGU ALIVYOTUMIA WANAWAKE TOKA AGANO ZEE NA JIPYA that by itself should tell somebody kua alichofanya Paul was specific and limited to him and his group and never to be taken as universal God’s commandment. Hence, kuliahamishia kama lilivyo kwetu leo ni UPOTOFU NA UJINGA.

  [Hii ndiyo inaitwa MAHEPE, ngoma ya mashetani, haijulikani inapoanzia wala inapoishia, it’s a ‘merry-go round’, and a savage one for that matter, because it sends you into spiritua death straight, in a one stop flight! Inawezekanaje mtu akawa na ujasiri wa kulihamisha Neno la Mungu kwa KULITOA katika wakati? Iwapo Mwana wa Mungu alijidhihirisha ndani ya mtume Paulo, je, Paulo hakuwa Mwili wa Kristo? au tunaimbaga tu mapambio kumbe hatujui chochote kuhusu Mungu! Duh kweli Mungu atusaidie!!!]

  MATOKEO KWA WALIOIPOKEA injili HII ya MAKOROKORO:
  Wanawake wa makusanyiko hayo nao wanautii Mpindo huu wa Neno, kwa raha zao, kwa hawa, Neno la Mungu limechanganyika na mila na desturi za sehemu zao, ile Hybrid, na hivyo hawa hudumu katika machafuko na hila na wivu, na fitina, pamoja na moyo wa tamaa, chapa ya kupotea kwao, kwa ile Nguvu iliyojihifadhi ndani ya ile injili itokayo ndani ya kile chombo cha udongo kilichotengwa kwa ajili ya kulidhihirisha jambo hilo la uovu, mhubiri na mhubiriwa!!! Maana injili hii haina Nguvu ya Wokovu ndani yake, bali ile nguvu ya uasi!

  Basi hapa sasa ndipo unaweza kuyaona makanisa mawili yakigawanyika kutokana na vifungu hivyo vichache tu vya Maandiko. Hayo hapo makanisa yako mawili, Esau na Yakobo, mtiti toka tumboni mwa mama yao, Biblia!

  Kanisa moja likivichukua vifungu hivyo kuwa ni Neno la Mungu linalowapa nguvu ya kuzitawala roho za udanganyifu na machafuko, ambazo zinatenda kazi vizazi vyoote, yaani nyakati zote mpaka siku ya ziwa la moto, zitakapoteketezwa pamoja na miili yote iliyokuwa ikitumika kuudhihirisha uasi huo, yale Malango ya Kuzimu, Kanisa hili linayashinda yote na kuendelea katika Ibada safi! Kanisa la pili ni hilo lililoipokea injili hiyo iliyopindishwa na hizo roho za udanganyifu na zenye kushawishi dhidi ya Neno la Mungu, nalo likiwa limetekwa na kupofushwa macho yake ya kiroho, hivyo hilo litaendelea katika ukomavu wa hayo, moja kwa moja mpaka mwisho wa dahari!

  Basi, katika haya mambo na ushindani wa Injili tunaouona, licha ya kwamba yaonekana ni mizaha, bali bado twapaswa kuwa makini kidogo, maana nyakati hizi tulizonazo ni ule wakati ambao tuliahidiwa Ujio wa Roho Mtakatifu kuhudumu. Sasa wakati huo ulianza siku ya Pentekoste hapo RM alipojichukulia vyombo vyake, wale mitume na kuanza kuhudumu. Naye Paulo aliongezwa katika hao kama tulivyousoma ushuhuda wake hapo juu, akimdhihirisha Kristo ndani yake. Ndipo unaposimama kupingana nao, ukiyavuruga hayo waliyoyahubiri, ukiyapoteza hayo makusanyiko uliyoyaongoza katika hiyo njia, jambo hilo linawakilisha kumkana RM ambako ni kumkufuru. Dhambi hii haina MSAMAHA, Mk 3:29 “… bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele”, sasa hebu linganisha jambo hili na ile Laana aliyoitamka Paulo kwa hao watakaofundisha injili tofauti, ni jambo lile lile, ukilaaniwa ndio basi tena, hakuna Injili ya kuwaokoa waliolaaniwa na Injili, nawe kama Kaini unaondoka Usoni pa Mungu, unaitafuta Nod yako (hata likiwa ni dhehebu lako) na kuendelea kuipindisha Injili huko!

  Gbu!

 108. Seleli,
  Ubarikiwe kwa maelezo yako ya majibu kwa Lwembe (na kidogo kwa Siyi). Pamoja na kugupikwa na utata mwingi wa maelezo yako brother, lakini napenda kuappreciate baadhi ya maelezo yako hayo.
  1. Ubarikiwe kwa kuwa tofauti na waj2 wengi wanaodai kuwa Agano la Kale lote halifai tena kwa mafundisho. Na ukiangalia kwa undani, kinachopigwa vita ni sheria/amri za Mungu. Wanasahahu kuwa sheria/amri za Mungu ndilo neno la Mungu-Biblia. Ubarikiwe hapa bro.
  2. 1 korinth 14, naona unachanganya bado ile issue ya watu wote kunena kwa lugha ndani ya kanisa na kisha kuonekana kana kwamba wana mapepo, badala yake Paulo anawapa utaratibu wa kunena kwa lugha. Na haina maana kwamba wanaume walikatazwa kunena, ila Paulo alikuwa anawapa tu utaratibu wa namna ya kunena kwa lugha ili kulijenga kanisa.
  3. Nikubaliane na wewe kabisa kuwa wanawake wanaweza kufundisha ndini. Jambo la msingi hapa ni wanaweza kufundisha wapi? Kanisani au nje ya kanisa na kwa watu gani? Kimsingi ndani ya kanisa, hawapaswi hata kidogo wala kwenye cruisade yoyote maalumu-jukwaani. Ila nje ya kanisa, kama vile kwenye miji ya watu, hospitalini, nk, sehemu ambazo si rasmi kwa ajili ya makuahani, wanaweza kufanya hivyo tena kwa wanawake wenzao na siyo kwa wanaume. Wakati wa mitume wanawake pia walikuwa na huduma. Mifano ipo mingi sana. Lakini hawakupaswa kusimama kwenye mimbari wala majukwaani wakizitumia karama zao hizo. Walizitumia sehemu maalumu ndiyo maana, hatuwaoni wanawake wakishughulikiwa kwa sababu ya injili kama walivyoshughulikiwa wanaume-mitume.

  riMabinza,
  Nimefurahishwa sana na mchango kwa kutumia mifanooo (mzee wa mifano) ha ha ha ha ha!! Hiyo ni Biblical kabisa mwanaume na kamanda wa Yesu. Enzila yene nsoga gete nyanda.
  Wajoli tuko pamoja??
  WAKATI UMEFIKA SASA WA KUSIMAMA KWENYE NENO LA MUNGU PEKE YAKE BILA KUJALI MAPOKEO POTOFU YALIYOPO SASANDANI YA KANISA
  Barikiweni

 109. Seleli,

  ulianza vizuri lakini katikati umenichanganya, hadi nafika mwisho sijajua kama unapita kulia ama kushoto! 2Tim. 2:20, inasema,
  “20Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.”

  Sidhani na siamini kuwa kwa vile mwanamke hutumiwa naye na Mungu, ndiyo kiwe kigezo cha ‘kuliondoa’ lile fundisho kuwa wanawake wasifundishe. sababu ya wao kutofundisha imeelezwa wazi kwamba, Mwanamke alidanganywa na shetani! Ukijua kuwa mwalimu anayeingia hapa Darasani, alidanganyika na kufuata mafundisho ya uongo, wakati alipokuwa kule chuoni, Mwanafunzi ajuaye maana ya kujifunza, hatakubali afundishwe na mwalimu yule, sababu ni moja tu kuwa, mwalimu yule atafundisha uongo! Mtu dhaifu, huwezi kumpa kazi ya Jeshi!

  Vyombo ni vyombo lakini kila chombo kwa matumizi yake. Chombo cha chuma huinjikwa jikoni lakini chombo cha mti, mfano mwiko, hutumika kuchanganya unga katika maji ya moto ili kufanya ugali uwe ugali, uji uwe uji n.k. Lakini katu, chanji au kibuyu huwezi kukiinjika jikoni ili upike chai ama chochote kile; Chungu chaweza kuinjikwa jikoni ili kupika kande za mahidi na zikaiva watu wakala, lakini chungu huwezi kukifanya kiwe kinu, utwange mahindi ili kupata unga watu wale, vivyo hivyo, mwanamke hupewa karama kwa kadri ya Roho anavyotaka kumtumia! Lakini kwakuwa lilosema asihubiri ni Neno la Mungu, basi Roho hawezi kujipinga ati atokee mwanamke adai kuwa ana Karama ya kuhutubu, karama ni sawa kuwa nazo maana hazina majuto!

  Ninachokiona hapa ni kama Siasa, eti haki sawa, ni kweli wote tunahaki sawa kwamba tu wanadamu, lakini heshima tofauti, Rais wa kike hawezi kuitwa Baba na wanaye kwa kigezo kuwa marais mara nyingi huwa wanaume, ataitwa mama na kupewa heshima ya umama. Chombo cha mbao ni kwa heshima kama mti, cha udongo kwa heshima kama udongo na cha chuma kwa heshima kama chuma! Hata hivyo, mfalme hutumia KIKOMBE CHA DHAHABU!

  Isifikiriwe kuwa, mbinguni kuna mfumo Dume, la hapana, Mbinguni hakuna jinsia. Iko HESHIMA tu basi! Watu wengi wa dini, hudhani kuwa, kila mwenye pesa ama umaarufu anafaa kuwa mchungaji, mwalimu ama mwinjilisti au kuwa Nabii ama mtume n.k. Ndipo wanapofikia kuanzisha makanisa na kufungisha ndoa ingawa wanajua kuwa wao ni wanawake. Sababu kubwa ni matokeo ya KULIKATAA NENO LA MUNGU na kuingiza “ifruensi” za ubinadamu na akili na mafundisho ya kimwili katika jamii husika. Neno la Mungu, hujitetea na kujisimamia lenyewe. ‘Ukilishika sanduku la Bwana kwa maelezo kuwa lisianguke, wakati wewe si mlawi unakufa palepale, haijarishi eti wewe ni mwanamme, mwanamke, myuda, mbenjamini, askofu, au mtume. Pale ni HESHIMA tu kwa mjibu wa Neno basi!’

  Kazi ya kulituza sanduku la Agano la Bwana ni jukumu la Lawi, vivyo hivyo kuhutubu hilo ni Jukumu la Kiume basi! Ukiondo lile Neno HAI na Kuongeza lile neno MFU kwa sababu yoyote ile nje ya Neno, mapigo lazima yaliandame Kanisa, ndipo utasikia “Tumekosea wapi Kanisa?”

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 110. Lwembe,

  Siyi- karibu na wewe ule Mkate hapa.
  Neno la Mungu HUKATA/HUAMUA MAMBO/ MASHAURI, IVYO NI VEMA NA HAKI WOTE HUMU, TUKAPUNGUZA mastory ya Radio Clouds efwe…eme na kujikita kwa Neno na Hekima njema za JUU na CHINI hence napolitumia ni vema na haki na tena napolitumia kwa halali-2Timo.2:15c, ina lipa na yenye nguvu sana so, hii habari yako kua nazunguka na maandiko kama nyumba Sodoma na sita uona mlango, ni stori zako zile zile za radio One Stereo na Kraaaaudis efwe eeeme! but base huna brother…yaani nikwambie ukweli kwa upendo? nakutafutaga sana unasemaga nini hasa jiwe kwa mambo mengi si yote, but ola! Why? What is the problem with you my brother? Kabla ya kupiga story, at least achilia basi pini kali angalau mwenzangu! Lo! Hakuna aliyeyagawa maandiko kwa maana mbaya-soma iyo 2Timo.2:15c..imeruhusu ivi.. rightly (correctly) DIVIDING the word of Truth! Si unaona ukitumia Neno, unavyomaliza kraaadis efwe eeem preacher..You! sasa niambie point yako itasimama tena? Nikisema uko cheap in bringing substances, unafoka! Ha ha ha ha!Kugawa Neno kwa usahihi ni Biblical, unakuza mambo kuleta hoja zako ambazo again, ni vapour brother, am sorry! right? kwa aina ya kazi yako humu, wewe kwako ilo andiko linasomeka ivi..Incorrectly dividing the Word of Truth!!!!!!!

  Ati sieleweki kwa hili..‘’Nimenukuu yawahusuyo wanawake ktk Agano la Kale na Jipya, badala ya kuyaacha Maandiko yenyewe yajishuhudie’’= sasa hapa umeongea nini Lwembe? Yaani nasikia kunywa maji mpendwa, mwe! Ati, nimewashawishi kuwa,
  ”Ukisoma Biblia kuna ukweli ulio wazi kua Wanawake wametumika na kutumiwa na Mungu sana kwa kufanya mengi mema hata kama madhaifu/mabaya yapo kama yalivyo mabaya tena makali kweli ya Wanaume”= Je unakataa ushawishi huu si kweli? ktk Biblia je si kweli Wanawake wametumika na Kutumiwa na Mungu sana kabisa? Je si kweli Wanaume wamefanya maovu makubwa na mengi kuzidi wanawake ktk Biblia? Yaani ndio maana nilisema, kadri unavyoendelea ku-debate, una shusha ‘P’ Kaka! capacity yako ni ndogo mno na hutaki kukubali nguvu ya mwenzio, kitaeleweka tu.

  Na hili dude ni ri nini hili ulosema.. ’’Ushawishi wangu unaonyesha udhaifu ulionao juu ya wanawake! Udhaifu wako wa kwanza ni UCHONGANISHI! Una udhaifu kama aliokuwa nao Adamu’’ == epsuuuuu! Ngoja nipumue!come on! hahaha! Unajua nakuona unavyopumulia machine bro eeee! Hali tete! Umeshindwa kabisa kupenyana hoja zangu bali sasa lolote liki-click, unafyatuka! Kwa hili ngoja nami ni-dance-dance na wewe tu sasa, hamna cha kukujibu maana vapour tupu! mwe! Kaka umekata net hamna tena! Tehe tehe!

  Umesema kuhusu status ya wanawake, ‘’wameanza kuruhusiwa kupiga kura mwaka 1920,kama umemuelewa Siyi’’== sasa dude hili tena la nini? kwa iyo Siyi kakupa hapo bonge la point eti eee? Ha ha ha yaani leo mbona mnanimvunja mbavu! Mwe! kwa hiyo na Roho Mtakatifu alianza kugawa karama, vipawa, huduma kwa Watu WOTE- wanaume na Wanawake- hapo status wote iko juu-1Wakorinto.12:4-11 mwaka afu na kenda yenye mbili with ziro siyo? Leo ni leo! Nitayajua mengi! Siyi unamuongezeaje mwenzio confusion Kaka? huyu ndugu ni wa kusaidiwa sana kisha afuate wewe Siyi, mh! ila na wewe, sijui tuanze na Siyi? Yaani kweli mnanipa hard time ya kuchangua nani yuko na urgency kungolewa toka madude kadhaa?

  Ila kwa hili kweli nisicheke, hakika Lwembe Mungu akusaidie ndugu ktk ufahamu, kuna shida nasema ilo kwa love in Christ!unashida ya ufahamu! Umesema kua kwa maandiko hayo..’’Waefeso.4:11-12 na 1Wakorinto.12:1-13 kwamba kwa nini sijasema hapa ni Paul anasema, hapa ni Mungu! JIBU: Sasa nikuulize, ktk Maandiko hayo, umeona directly au indirectly Paul anasema…NINA gawa karama mbalimbali kama NINAVYOpenda na NINAtoa wengine kua Mitume, Waalimu nk? kama alivyosema kwa haya? e.g. SIMPI- mwanamke ruhusa-1Timo.2:12 au kwa wana wali SINA Amri ya Bwana ila NINAtoa shauli LANGU-1Kor.7:25. Hapa napo si unaona ukitumia Neno/Maandiko, mashauri yanakwatwa? Utasimama tena kweli? kivipi kama sasa hutakua unaleta mchezo wa kombolea tujifiche, inuka, kaa!

  Hapo napo nimesikitikia understanding yako jamani! khaaa! Lakini nafurahi kwakua niliwahi mwambia Sungura aliposhituka kweli ule mzaha wako wa ‘666 asante’ wakati tunaanza debate na wewe, nikamjibu, ‘I know how to help you become so vividly empty ktk debate! Sungura see here now…akisoma hapa atanilewa sasa na huu ni mfano tosha. Ni Paulo mwenywe amesema ktk mstari wa 13 1Kor 12 kua inasema hakuna huyu myahudi, Myunani, Mtumwa au Aliye huru’’ sasa mimi nikasema( kwa mantiki hiyo bila kuvuruga maana ya mstari huu naongeza pia hakuna huyu mwanamke au mwanaume, amesoma hajasoma, anazo au maskini, mzungu au mwafrika, wa Dar au uko vijijini Babati, Ujiji KGM na Nyanzalaki Burundi), wewe Lwembe ukasema, nina udhaifu wa Adamu wa kupenda wanawake kuliko Neno la Mungu! acha nicheke kwanza ha ha ha ha! Mweeee! Aisee hapana! hii nafunga nayo mwaka! Mimi nina kula sahani moja na Adamu kwa ma-Ladies! Ha ha ha ha! Kweli ktk debate hii, nimekukaba Lwembe, tuseme kweli yaani vitu unavyolipua havina kope wala nyusi sembuse sikio! Na ukasema kwa mimi kuongezea maneno ya ufafanuzi yale ya hakuna Me/Ke, Msomi au Mjinga nk..NIMEONGEZEA NENO LA MUNGU! du! Nasikia sijui niache kwanza kuandika! Ivi level yako Lwembe kumbe ni this much poor! Am sorry for saying that, I didn’t know brother!

  Sasa let me just u know..put you on a little test aah! A u ready? Kuna hili andiko hapa.. Yohana.3:15-Mungu aliupenda ULIMWENGU….. fafanua? hasa neno ulimwengu- Hahaha nakuona tu unavyoanza kuhema, ready kufyatuka maana kwa swali ilo tayari nshakukaba tena na umekwisha-kama unabisha, jibu basi nione! Ila pia yale yale nawaambieni, kua Muwe MNATUMIA AKILI pia kuyaelewa ya Mungu, mnakataaga na kusema nyie ati mnapojifunza Neno, Akili isitumike!Sasa swali tu la Akili ni hili…hao Paul alowataja mstari huo wa 13- hakuna Wanaume na Wanawake? Mtu akisema ktk Yesu, hakuna Wa Tz au Wa-USA—kwa iyo hakuna Wanawake umo? Je ange/ningesema… Hakuna Wanaume, Wanawake, Vijana, Wazee, Wasichana, Wavulana wa KIYUNANI, GREEK nk…hapo je? Sasa ina tofauti gani na fafanuzi yangu? Ha ha ha, Leo Kaka nimekukaba zaidi kuliko siku nyingine, uko nyang’anyang’a tehe! tehe! si unaona nilivyotoa pini hii tena ulivyokwisha? Unasimamaje? Try it!

  Hapa umeleta utani sasa, Hili swali ni valid, jibu, wacha ulongo kusema halina jinsi ya kujibika Biblically bali sema UMECHEMKA KUJIBU, NI PINI MOTOO IYO kisha omba msaada! SWALI! Valid ni hili bado…’’wapi alipiga marufuku Mwanamke kutokua Mtume, Nabiii, Mwalimu nk wakati Yesu anasema aliwatoa wengine na wala hajasema aliwatoa WANAUME tu kua….?” Lete jibu hapo, unafunika! Mpaka ujibu, nitakukaba tu ktk comments nyingine mpaka ujibu au ukiacha na iujulikane, umeshindwa and next time utakua makini ku-engage na Mtu ktk debate!

  Pia hili swali bado ni valid, acha utani, jibu! Swali ili kua Kwa wanawake kutokuwepo ktk wale 12, nani kasema INA MAANA HAWANA HUDUMA IZO? au nisema, nani anasema RM hawezi wapa huduma izo? Jibu bwanaa wacha mambo ya kusema ati Wanawake kutumika kati yetu ni kujenga ufalme wa luciferi, haya ni mastori ya mjini ya kraaaadis efwe eeme! Jibu swali ilo au iyo pini moto nini? waijua eee?!.

  Umeshangaa mimi kusema ivi..’’Tunaweza fuata mifano mizuri ya Wanadamu wenzetu ya Kiroho au Kimwili’’ ati ukang’aka ivi….Mnaiona hiyo hila? Na kuuliza ivi..’’ Ni wapi ktk Maandiko mlipoambiwa muwafuate wanadamu wenzenu waliowatangulia ktk mambo ya kiroho na kimwili?
  Jibu: Unashangaza! Umetoka kukamaa kua hatuwezi mfahamu Yesu bila hao waliotujuza! Sasa swali lako la juu, ulikua unaumwa or? Sasa hao ni akina nani? Chimpanzee from Mbujimai Congo forest ya Mobuto Seseko na Ndezileee Kabilaa kule kwa wazee wa M23? Si ni watu hao au? akina Mitume na Manabii si humans hao au ni pusi? Pia ulivyo muongo hati hatuwezi wapiku kumjua Bwana! kwani kati ya Yesu na Mitume na Manabii ktk Agano Jipya, nani alianza kuwepo na kujitambulisha? Kwa ile Miaka 3 na nusu Yesu anapiga kazi hapa, alikua hajatambulikana? Na nani amekwambia kua kwa sisi Mataifa na hata baadhi ya wayahudi walikuja kujuzwa/kuhubiriwa na Mitume na HATA WATU WENGINE-maana Injili haikububiriwa na Mitume tu wakati wa wa mitume-be careful, baadae walipokwenda pande za Dunia na Injili, ati kwa kua kuna Mtu alitutambulisha Yesu, Kamwe tusimuanglie na kumfahamu YESU moja kwa moja mpaka tu lazimia MITUME au yeye huyo alinitambuisha kwa Yesu? Unaleta mambo ya kwenda kwa Yesu via Bikira safi mdada yule? Halafu nilisha kujibu na kila mara nakuambia Neno la Mungu hukata mashauri-ulishawahi leta hili swali nikalifyeka ivi…wakati ni kweli tunaweza iga mifano ya hao walitutangulia vema ktk imani lakini wao wenyewe wamesema ivi…( Lwembe baada ya kunukuu Neno kwa usahihi hapa, hutanyanyuka tena, Neno kiboka, mwanzo mwisho, ila maneno yetu, hayo yataendelea hasa yale yako ya kraaaadis efwe emee!jahazi mastori ya town.

  Angalia hapa.. 1Wakorinto.11:1-‘’Nifuateni mimi kama NAVYOMFUATA Kristo! sasa hapa nani Kingi hasa wa kufuatwa? The final one? Aya na hii…Waefeso.5:1 ‘Mfuateni Mungu kama Watoto wanaopendwa’- sasa hapa je si unaona Kamanda mwenyewe Po anakukana na kukurekebisha ufahamu hata humaanishaga nini siku zote? Ni kua watu wamfuate Mungu!tena notice: Hii Bible NKJ…kwa maandiko hayo 2 inatumia the same words…’be imitators! confirming the same concept ya kumuiga/Kumfuata/kufauta mfano wa Mungu/Kristo-Wafilipi.2:5

  Nikwambie kweli Lwembe? My brother WEWE HUNA AU UNA NENO CHACHE SANA na UFAHAMU WENYE UTATA MWINGI KUHUSU NENO NA UPANA WAKE KWA MAPANA YAKE ila kwa kweli hongera kwa ma- kraaaaadis FM-jahazi mastori ya town, aa mbona haujambo!

  Press on( nitamalizia post yako latest kabisa, don’t worry).Siyi..kaa standby maana umechafua na wewe kambi kwa hapa kisha kuleee kwa kiporo, sijasahau, wewe! eee!nilikuseti uingie site kisha nimalize, tehe! ur done boy, wait fire muriro very soon and pole in advance.

 111. Lwembe,

  Posts zako 2 za ivi karibuni, ile ya juzi ileee na hii latest nilikua sijazipitia, Karibu kwa niliyoitikia kwa yako ileee kama ifutavyo kisha nitaitikia ya latest

  Jitahidi iki kimoja tu kua unapoulizwa issues, Kindly, jielekeza kwenye hicho, maneno kua mie ni Mpinga Kristo mara sijui nimenyang’anywa hata kile kidogo nilichonacho, yanatoka wapi na ya nini? Mpinga Kristo ni statement kubwa sana kuitumia hapa against your own brother AMBAYE UNAJUA KWA HAKIKA SI MPINGA KRISTO! Inakua kama unazidisha utani au pia inaku- disqualify capacity yako ktk Kujadili mambo in connection with sound TAFAKARI/TAFAKURI) ya Neno. Well, wewe baki na maneno-neno, mimi ninatakukuba tu na hoja mwanzo mwisho kila napokujibu, mpaka ukae line clear au udhaifu wako uwe wazi zaidi na zaidi maana tayari tatizo lako ktk kuyafahamu maandiko ktk Roho na Akili njema kwa upana na usahihi wake, umejithihirisha si ktk mada hii-namna unavyo argue na ku-present your things lakini pia ktk mada nyingine nyini past, present and may be future. Seriously, tuangalie pamoja ulicho andika na kama nakuonea, sema ni wapi brother.

  Hii ni story brother Lwembe, kindly be serious-Makanisa yenye Wachungaji Wanawake haimanishi kua wana lazimika kupata mashoga!!! unatoa wapi maneno haya?..plz Talk substances my brother. By the way, Unaelewa kweli maana ya Mashoga? na Kanisaje in its proper strict Biblical sense? Ni lazima tu waibukie ktk ‘Makanisa’ yanayochungwa na Wa Kike? Mbona unaongea vitu vya ufahamu so low! Umetokewa na nini Kaka?

  Kuhusu BAADHI ya kweli kuvuka toka Agano la Kale kuja Jipya, umepinga lakini huna hoja, ni maneno tu ya Yanga na Simba. Kwanza epukeni kusema kila kitu cha Agano la Kale ni laana! Plz tafuteni lugha nyingine au angalieni kwa makini Paul anapo tumia neno Laana kwa ya AG, anakua anaongeleaga nini hasa-theme ya hoja yake ni nini, that very thing anachosema, si ku-rule out tuuu generally kua kila kitu was and is nul and void! Ivi you guys mnaongeaga nini? Unasema Kila NENO la MUNGU Agano la Kale ni zero? Yesu alisemaje ktk Mt.5:17-19? Au Paul anasemaje ktk hili hili andiko letu la kukataza Wanawake..1Wakorinto.14:33-35..angalia mstari 34…’’ Hawaruhusiwi kunena bali wawe wanyenyekevu KAMA VILE INENAVYO TORATI! Wow! so sweet point aah! Ukikataa iyo, si unaonekana tu simba- yanga thing wewe! sasa mifano kama iyo ya BAADHI ya kweli kuhama toka kule mpaka kwetu na tunaitumia leo na Yesu alitumia sana na zimejaa tele ktk Agano Jipya, tena nyingine zikihama KAMA ZILIVYO, Mungu wangu na Baba yangu, U don’t want me to pick on that topic! utakimbia Lwembe, ziko nyingi-nimekusudia kuitengenezea post yaake iyo fact nikipata muda au huu ubishi mbaya wa kusema kila kitu ktk AK ni laana, ukiendelea.

  Usikatae tu bila hoja, hili ni kweli tupu pia kua Ni kweli ndani ya Biblia kuna Maneno na Matendo ya Watu pia maana wamejisema wenyewe, wakati gani ni Bwana na wakati gani ni wao kama Watu wa Mungu vile vile AU wengine wa kawaida tu. Pia Watu wameandikwa na Waandishi wa Biblia yale waliyotenda/fanya. Mifano ni mingi kama- Jezeberi alipoapa kua atamteda Eliya kama alivyowafanya manabii wa baali-1Kings.19:1-2 , tunacho ambiwa shetani alichosema na kufanya ktk Ayubu.1:7,9-11,13-19 pia 2:2,4-5,7 au mapepo legion walivyomjibu Yesu- Marco.5:8-9, pepo wa uaguzi aliyesema maneno yale kwa Paul-Mdo.16:16-18 au wale mapepo waliowaweza wana wa Skewa Myahudi Kuhani Mkuu- Mdo.19:13-16 nk, UNASEMAJE? Hayo Matendo na Maneno ktk maandiko hayo, ni Mungu amesema au WATU na DEVO? Si mbaya wala kufuru kujua kua ktk Bible yako Maneno/Matendo ya Mungu na Wanadamu na hata shetani naye kaelezwa aliyosema/tenda. Wakati mwingine appreciate tu Lwembe unapofundishwa Elimu ya Neno la Mungu ktk Roho na hata Ufahamu/ Akili njema kabisa ya kawaida, kukataa tu bila kua na hoja ili mradi umepinga, haibadili ukweli kua hoja za mwenzio zimekuzidia mno Lwembe.

  Umeniuliza, Paul aliposema kua hapa ni ‘’Mimi si Bwana’’, tunai-apply kwa kila andiko maana huoni iyo statment yake ktk Andiko la kukataza Wanawake na umedauti labda sisi ni Waislamu kwa kua wanamkataga Paul! JIBU: Kwanza acha utani mbaya, sisi/mimi si Answari Suna wala Shiha nor Suni but Nimejazwa Roho, nimeookaka mimi kabisa, I have fallen in love with Jesus and the Bible, so drop hayo maneno ya mtaani kua sie ni Madina and Macca children!!!!!! Come on…una utani mbaya kweli wewe! Pili, Ongeza umakini wako ktk kusoma posts zangu, always nilishakuambia ili ukitoa hapa mchano na uonekane kua ..u did your home work seriously and uko committed kwa huduma hapa, SOMO KWANZA MPAKA MWISHO KISHA NDIO ANZA KUJIBU—Lakini leo naongeza ivi..SOMAGA POSTS KWA MOYO WA KUELEWA KWANZA SI KWA AJILI YA uyanga na usimba mbaya( uyanga na simba mzuri ktk debate, huo fine kabisa) but wako huu, hauna mashiko

  Hili andiko unapokutana na katazo kwa Wanawake ktk mistari ya 33-35 ya 1Wokorinto.14: limeanzia mistari ya 1-32 mpaka 37-40, mfano mdogo tu wa human aspect ktk Neno ni…angalia mstari wa 5’ anasema….I’ wish you all spoke with tongues = Hi ni ‘wish’ ya Baba wa Kiroho kwa Wanae-nothing to do with a Word of God hapo! It is a mere wish-an expression of good hearted Father kwa watoto yet he had an agenda to settle things on the ground! Things were not in order! Sura nzima yote iyo ukiisoma, unaona mambo 2 tu- BABA WA KIROHO AKI-DEAL NA ISSUES ZA WANAE- AKITOA USHAURI WAKE NA HAPO HAPO MAWAIDHA YENYE MAUDHUI YA NENO/AMRI ZA MUNGU-mstari 37-as simple as that. Ni kutumia Ufahamu wa Neno la Mungu KWA MAPANA YAKE(ninatumia phrase hii sana kwakua nimeona Lwembe na Yusha nk, mnatatizo la kukomaa na andiko moja tu tena na kubaki nalo pale pale ulipolikutia na kusahau Neno linaji-support and so kwa mantiki hii, ktk 1Timotheo.2:11-12-Anasema maneno yale yale almost kuhusu kukataza Wanawake kunena yeye kama yeye Kiongozi wao wa kiroho kwa situation iliyokuwepo a ktk aina ya mila na desturi za watu wale kuhusu MWANAMKE kusimama na kufundisha Kanisa na wanaume wamo-ni kama loe msikitini mwa waislamu-mila na desturi ndio hizi hizi zilikuwepo kipindi kile. Kwa iyo, kama huioni live iyo ‘Hapa ni MIMI’ si BWANA, unaiona indirectly ktk kujieleza kwake na pia unaiona live ktk iyo1Timotheo kwa kua ni katazo lilelile-NENO LA MUNGU-hubebena.

  Labda nirudie/ niongezee hiki kuonyesha why tunalazimika kuzingatia/kutafakari tunaposoma Maandiko ili kujua Wapi ni Neno la Mungu kwa vizazi vyote past, present, future bila kujali rangi, mipaka ya Nchi, Mila na Desturi na HILO TULICHUKUE na wapi ni Mtu wa kiroho alitoa tu ushauri au kuelezea mambo tu -SI LAZIMA hayo aliyoshauri/sema/fanya/elezea yawe ni NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE ivyo tuna uhuru wa kuchukua kama habari tu/taarifa ya yaliyojiri na pengine kujaribu kulifitisha kwa kuzingatia mila, desturi, taratibu zetu—maaana si Neno la Mungu wa vizazi vyote bali la Mtu/Watu au au kuacha/tupilia pending uko-hamna tabu kabisa na wala Mungu hana shida na iyo, ni wasiwasi wetu due to ignorance basi, ivyo tu. Sababu ni:

  (a)Ni pale tunapowakuta wao wenyewe wamesema, wanachosema si BWANA bali ni wao

  (b) Ni pale tunawakuta wao wenyewe wanamsema mwenzao kua tenda/sema aliyosema lakini si Mungu, mfano YESU-kusema Musa aliwaambia kuwatimua wake LAKINI toka mwanzo haikua ivyo-yaani toka mwanzo NENO/MPANGO/ELEKEZO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE halikua ivyo, ni ninyi tu na shingo ngumu zenu ndio maana KIONGOZI wenu wa Kiroho ilibidi awashauri ivyo/aamue case zeni ivyo! wow! naandika mpaka nasikia upako unashuka, alleluyah,aiiiiiiiimen..Marco 10:1-9. Unaweza elewa kwa nini pia natumia sana phrase ya ‘Kiongozi wa Kiroho wao ku-deal na issues za mahala kwa watu wake kwa wakati wake ktk tamaduni husika’’

  (c) Tunapokuta Waandishi ktk /wa Bible wanatofautiana ktk maneno ingawa lile jambo la msingi kuu, wamekubaliana-hili nalo linaendelea kuthibitisha kua hata kama walitumiwa na Roho Mtakatifu, hawakua mochwari dead bodies-bado walikua Watu wenye asili hii na kila mmoja na uwezo wake, ndio maana Mathayo atasema vazi lilikua la rangi Nyekundu-(scarlet robe) Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 lakini Marco atasema ni la rangi Zambaro-(purple).Marco.15:15-17 hasa mstari 17.

  Niliuliza je ktk hoja zenu kwa 1Wakorinto.14:33-35 mlizingatia muktadha? ukasema swali langu la kipagani! Ninaelewa kwa nini umebaki kufoka tu na almost kutukana badala ya kujibu jambo! Nakuhakikishai nikiuliza jambo ktk mijadala hii kwa mada yoyote-YOU BETTER BE CAREFULL KUJIBU AU CARELESS KUTOJIBU-ninakua nina maana kubwa kabisa kama nilivyoonyesha tayari –soma post yangu iliyotangulia, nilipochambua mistari yote ktk sura iyo.Nilitaka muone tatizo lenu la kukomalia/kalia baadhi ya maandiko/andiko na kulalalia hapo hapo ulipolikuta! Ukisoma sura yote, utagundua WOTE/WANAUME WALIKUA WA KWANZA kukatazwa kunena( unabii) zaidi ya 3-Wakawekewe hata limit ya wangapi watoe unabii-can u imagine that? Unabii! Ambao wengi wetu tunasemaga akisha kuja RM hakuna control! Ndio akaendelea na mpaka 33-35 kukataza sasa Wanawake kunena(kufundisha) this was my point I wanted you gusy to see-halafu unakimbilia kusema ni swali la kipagani!-nasema tena siku zote, ukiacha/mkiacha maswali yangu,mnajua why?Kuna moto au mko totally blind kuona nilichoona ambacho unfortunately napokazana mkione, mnafoka na kuropoka maneno kama upagani, ushoga, nimenyang’anywa na kidogo nilichonacho na kali ya yote mie mpinga Kristo! du! Ila pamoja na maneno haya yote, ndio yananipa upako acha kabisa, so nitaendelea kuachilia pini hatari mwanzo mwisho for his glory amen, kitaeleweka tu nani kweli ana Neno ktk hekima yote na nani aidha ana one side au off the way kabisa ktk kula/kuumega Mkate huu wa uzima.

  Pia hili la Tito 2:3-4, usimtetee tu Yusha bila sababu ya KWELI-mpendwa huyu naye ni mwoga tu ndio tatizo lake BWANA amsaidie-ana dhani kukaa kimya ndio hekima na utakatifu kumbe kwa hapa si mahali pake, hapa kikazi zaidi hapana kingine,mi nachapa kazi tu day and night hapa, kukaa kimya kwa mambo ya msingi kama haya, itahesabika kwakwe ni muoga, kaona moto na hawezi sogeza mguu au simply hajui na amechukua uamuzi wa busara kujifunza sasa. Hilo la Tito pia nilitaka muone kua kumbe Wanawake wanaweza FUNDISHA PIA-yaani wana Karama/huduma/uwezoa huo, Bwana anawapaka kwa ilo sema tu kutokana na tamaduni zao na Torati pia, WASINGEFUNDISHA KANISANI AMBAPO KUNA WANAUME WAMEKAA UMO-typical of misikitini leo maana Watu wale wa Mashariki mbali na kati, wanashabiana mengi ya mila na desturi na pia labda hili hamlijuai, ni kwamba Uislamu umeigiza mengi ya Kiyahudi-haya yote ya kuvua viatu, kutenga Wanawake, kuvaa kanzu, wanawake mabaibui/kujifunika, si yao ni yetu/ya wenzetu Jews! Hence, kwamba wanaweza fundisha-wana mafuta/karama/hudumaa kama sisi, ni dhahiri kabisa ndio maana kumsaidia Yusha, nikamuuliza RM anapogawa uwezo/karama/huduma anagawa kwa Wanaume tu? You see guys, ndicho nilitaka mkipate-lakini bado mnasingizia eti mie mbishi badala ya kusema amen, bless u brother Seleli, keep the fire/things flowing! Nyie Wapendwa bwana, wivu tu!ku-appreciate/bless/aknowledge ni tabia njema ya Mungu pia, si mawivu tu na mauchungu na kujikaushaaaa kama vile hubarikiwi/hupata vitu very sweet vya kiroho na Neno na hata Akili! roho iyo na ife in JESUS name kabisa. Sasa ukinuna/ jikausha/kataa kila kitu/goma kusema oo yes hapa nimepata kitu maridadi kabisa au kuachilia neno lolote la baraka kukubali kwa dhati kazi njema ya RM na karama/huduma zake ndani yetu, ndio ili iweje? Itaniondolea mafuta? Wakati ndio yamejaa tele na Neno mifupani limejaa na linaniwaka moto, siwezi tulia? Aya Kaka, endelea na kujikausha na mimi nachapa kazi 24/7, we sikilizia tu, isome namba mpendwa treni inapokata mbuga kwenda Nchi ya ahadi JUU uku nikimega mkate by his grace, amen.

  Niliuliza..wapi imeandikwa RM kamwe hatatoa karama/huduma ya Ufundishaji na Maongozi kwa kiumbe Mwanamke? Ukasema sina hata haya kuuliza ilo swali! Nadhani jibu langu la juu linatosha na pia nilitaka ujibu ili nikukabe! Kisha uwe umejijibu mwenyewe! una bahati nimekusaidia kwa kujibu pale juu, na post zilizotangulia kabla yah ii, this time umekua mjanja but husiejijua kua umefanya ujanja mzuri hapo( but in overall ni ujanja mbaya maana mnakwepa kazi-bado nitawatafuta tu, hakwepi mtu hapa akishakwepa duty yake, atakamatwa tu, heri yeye amalizae kazi yake salama, ataenda zake kwa amani)

  Sasa hiki ulichosema, kinaonyesha kiasi gani unahitaji kusoma tena na tena na tena post zangu na jinsi tulivyo na kazi ya kukusaidia, sitachoka kukusaidia kwa namna nyingi, haisumbui kutake time na wewe kaka ktk Bwana.Embu angalia ulichosema hiki with 400%- confidence- nimeongeza toka ile yenu ya zamani-200%!- Ati ni Mungu ndiye aliyesema “Simpi’’ ruhusa mwanamke…” Wakati Paul ndio anasema yeye Mwenyewe? Fafanuzi zangu juu zitakusadia kuweka sawa hili.

  Huu woga wako wa kujifunza haufai ati..’’Kama Neno hili si la Mungu basi acheni kuvitumia vitabu vyoote vya Paulo’’= Nakwambia ivi Paul angekuwepo leo angekucheka au kukudharau kua una misisimko tu ya kipendwa isiyo na base kwa kumsingizia! Ameshasema ni ‘yeye’ unamlazimishaje? Mbona sehemu nyingine anasema live kabisa kua hapa nasema MIMI wala sina Amri ya Bwana? 1Wakorinto.7:25? Na hapo unachomokaje? Ivi Lwembe a u serious huelewi shule hii toka nianze post nyingi kweli mpaka hii ya sasa?
  Mwisho umetaka sana nikuleze swali ulilouliza kuhusu Andiko la kukataza Wanawake- Ni matumaini yangu kama umesoma post zilizotangulia kwa moyo wa kuelewa, nilipochambua vema mistari yote ya andiko ilo na sasa hii, huna tena hoja.

  Press on in heaven yet while here, I press on in light sharing the Word mpaka utaelewa na kujengwa tu kisha kukubali publically au hata kikubwa-privately.Amen

 112. Seleli,
  Sijaropoka kusema kuwa baadhi ya wachangiaji, wanatumia HISIA tu. Na ni kweli mtu anayesimamia neno, huonekana mshamba katika macho ya duniani. 1 korinth 1: 18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Watu leo wanalilazimisha neno likubaliane na matakwa yao bila kujali Mungu anasemaje. Wameidhararu hekima ya Mungu… Hatari kweli.

  Ukiwaona watu wanashikilia sana M23 na kupuuza mengine, jua hao kuna tatizo ndani yao. M23 ni sehemu tu ya SHERIA/AMRI za Mungu. Neno lote ni AMRI/SHERIA za Mungu. Rejea kwenye post yangu ya mwishomwisho katika mjadala huu; https://strictlygospel.wordpress.com/2012/06/23/sababu-za-wakristo-kuabudu-jumapili/ nimejibu maswali ya mjoli mmoja wa Bwana huko. Watu wanaolitii na kulifuata neno(sheria/amri) la Mungu ndio huonekana kituko kwa walimwengu. Maana wasikilizaji ama wasomaji wengi, hutazama background belief ya msemaji!! Na kama hawaendani na hiyo belief, ndiyo utawaona wanajustfy yasiyojustifaika. Seleli, utakubaliana na mimi kuwa, Paulo alipotema ngeli za neno, Foestus baada ya kuchomwa na injili ile alimwambia Paulo kaheuka!! Soma historia zote za mitume, waliishiaje…na kwa nini ilikuwa hivyo kwao? Jibu utakuta ni ile kusema kweli tu. Kupiga kampeni halisi ya Kristo.
  Kadhalika, na mimi sikusema kuwa wanawake kutopewa mamlaka, ni namna fulani ya kuwakandamiza, kuwadharau, kuwabeza nk, la hasha. Tafadhari usichochee moto usiowaka. Uache tu. Wanawake ni viumbe wa thamani sana mbele za Mungu na Mungu anatambua sana huduma zao katika shamba lake. Ukirejea kwenye agano jipya utakutana na mifano ya wanawake ambao Mungu aliwatambua hadi akawa anawafufua kupitia mitume wake ili waendelee na huduma. Plz, heshimu wanawake, penda wanawake, jali wanawake, but do not let them to lead you into sin coz of their weaknesses!!.

  Majibu ya maswali yako.
  (a) KILA MWANAMKE ATAKAYE VAA SURUALI KWA KUA umesema MUNGU AMEKATAA, ATAKWENDA JEHANUM?
  Jibu
  Ndiyo ataenda jehanamu kweli asipotubu mapema, maana kinywa cha Bwana kimenena. Rejea majibu yangu kwa Sungura.

  (b) JE KUTOKUVAA SURUALI KWA UELEWA WAKO WA MAMBO YA MUNGU, NENO LAKE KWA MAPANA YAKE NA MOYO/TABIA YA MUNGU BABA YAKO AND I HOPE NDIO BABA YANGU-ingawa sijui lini ulishafanywa Mwana, JE KATAZO ILO NI NENO LA NIKO AMBAYE NIKO KWA VIZAZI VYOTE PAST, PRESENT AND FUTURE REGARDLESS YA CULTURE, WETHER, AINA YA KAZI nk, embu nijibu hayo kwanza nione kama kuna ulazima wa kuingia Msikitini wa Wayahudi kama Appolo na Paul ili KUHOJIANA.

  Jibu.
  Katazo hilo ni la Mungu mwenyewe ndio na ni la vizazi vyote. Mungu hajabadilika wala hajatangua chochote.

  Ubarikiwe bro.

  Lwembe,
  Ubarikiwe sana kwa mchango wako mzuri. Kimsingi umenibariki sana, na kuvunja mbavu kweli!!! Mambo uliyoyasema, ni Biblical kabisa kaka. Sina cha kuongezea maana ulichosema ndicho uelewa wangu pia. Ni kweli mojawapo ya kiashirio cha kutembea na Mungu bega kwa bega ktk neno lake ni kutii neno lake tu basi. Kama kuna mtu ana hoja tofauti ya Kibiblia, atusaidie, tutamshukuru sana kama atatuonesha kuwa tumepotoka.
  Ubarikiwe bro.

  Francis,
  Ubarikiwe na Bwana. Ingependeza zaidi kama ungewasaidia ndg hawa badala ya kuwaona wanalilazimisha neno kukubaliana na akili zao. Wasaidie tafadhari. Toa somo nyeti lenye kutangua mawazo hayo unayoyaona kuwa ni potofu. Bwana akutangulie unapofikiria kufanya hivyo.
  Mungu akubariki kaka.

 113. Seleli, nilipotuma ulemchango wangu wa mwisho ndio niauona huu wako mpya, lakini hata hivyo, naona ni vizuri nikujibu ili uwe na uhakika kwamba nimekielewa vizuri unachokisema!

  Kwanza kabisa, hapo ulipojiridhisha na kujiaminisha uongo kwamba ndani ya Biblia kuna maneno ya Mungu, ya watu na ya Shetani, huo ndio ulikuwa Ukomo wako wa kuelewa chochote kile kinachomhusu Mungu! Nayo maelezo yako yanadhihirisha jambo hilo moja kwa moja.

  Hebu tazama akili yako ilivyonasia kwenye tafsiri zako, ““Paul mwenyewe anasema MIMI wala SI BWANA na pia SIMPI ruhusa…. ni yeye kama Paulo anayetoa agizo/ushauri-1Wakorinto.7:12,25, 1Timo.2:11-12””
  Unajua watu wengine mnashangaza sana, Maandiko yamekuonya wazi kabisa kuhusu kulitafsiri Neno la Mungu kwa akili yako dhaifu, hiyo unayoidhania kuwa unayo saana, bali wenzako waliiona kuwa ni mavi, wewe umeng’ang’ana nayo!
  2Petro 1:21“Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na RM”
  Ndipo unaponijia na tafsiri zilizochoka kama hiyo, nazidi kukushangaa, yaani umeng’ang’ania kizibiti kwapani mpaka kwa Hakimu, kila aliye na akili timamu anakushangaa! Umeambiwa usitafsiri Neno la Mungu husikii, hebu nitafsirie na hili, “Bikira atachukua mimba”!

  Pia umekuja na maelezo mengi yasiyo na rejea. Torati ndiye Mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, sasa unapotaka kupandia mambo ya Musa ili uyafanye Fundisho, ndiyo unazidi kutokomea huko porini ulikojipeleka. Kwa taarifa yako Wayahudi walio ktk Sheria wanaendelea na vikaratasi vya talaka mpaka leo hii!!! Ni wakristo waliozaliwa mara ya pili tu ndio ambao wamerudishwa huko Mwanzo, na wanayafurahia maisha hayo. Maana hao ni subjects wa Agano Jipya, Nguvu inayowatala imeyafanya hayo kuwa laini. Subiri uwaone akina Seleli wenye kuigiza ukristo, hawa ndio vichekesho kabisa, eti huruhusiwi kumuacha mke mzinzi, labda muasherati, wakiyarejea Maandiko hayo na menginewe yanayohusu uasherati, kwa akili zao zilizokosa Maarifa! Ni wakristo wangapi leo hii wanaishi na wake wazinzi kwa kisingizio cha kwamba alivyoviunganisha Mungu mwanadamu asivitenganishe?

  “”Paul anaandika kwa kuangalia/zingatia tendo/neno la mwenziwe, anamsema mwenziwe Petro kwa kusema…’’nikampinga Kefa maana hakuenenda sawa…Wagalatia.2:10-11”” Kwahiyo na wewe Seleli unampinga Paulo, “Nampa mwanamke ruhusa…”, ndio maana Siyi anakuambia unachekesha!!!

  “”Petro naye anamsemelea mwenziwe Paul kua ‘’ndugu yetu Paul kapewa hekima na anasema/andika mambo magumu kuyaelewa-2Petro.3:15-16”” Paulo kapewa hekima na nani? Si unawaona wenye Ufahamu wa kiMungu wanavyowaonya ninyi wenye kuwarukia tu watu msiowajua, kisa nini, eti kanisani kwetu huwaga nafundisha semina! Mambo aliyoyaandika Paulo ni kwa Makanisa ya Watakatifu, brother, na sio biashara ya sokoni, ndio maana unatoka kapa!!!

  “”Ninyi msipokula mwili wa mwana wa Adamu na na kuinywa damu yake, hamnao huo uzima’’-Yoh.6:53”” Unajaribu kujenga hoja kwa msingi uliouzoea wa kutumia akili, wenzako waliotumia akili waliondoka, walimuona Kristo anawapeleka nje ya Torati, wakamuona anataka kuwafanya mavampire, kama nawe ninavyokuona kauli za Paulo zinavyokutoa nje ya kusanyiko la Watakatifu kwa kujifanya eti unatafakari! Hata unalolitafakari silioni, nakuona unapapukia tu mambo magumu aliyokuambi Petro, wewe unayafanya rahisi; wenzako mitume walipoambiwa maneno hayo ya kula nyama za watu, walitulia, mpaka wakaulizwa ninyi hamuondoki kama wenzenu akina Seleli wanaosikitikia wanawake kuzuiwa kufundisha? “Twende wapi ndg yetu Paulo, tukuache wewe uliyekabidhiwa Neno la Uzima utufundishe! “‘’Amini, Amini nawaambia, wapo wanaosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka wamemuona mwana wa adamu akija ktk ufalme wake-Matt.16:28” Ni kweli, mitume na wale 3000 hawakuonja mauti mpaka walipoingizwa katika Ufalme wa Mwana wa Adamu siku ya Pentekoste hapo walipompokea RM. Au nawe unajiunganishia mambo yako ya kawaida ya Injili Pori, kwamba mpaka leo wapo!!!

  Haya maelezo yako mengine unayoyafundisha kiufafanuzi zaidi wa kialimu, naona itakuwa vizuri nikiyaunganisha katika summary ya mafundisho yako yote, ili sote tufikie mahali ambapo tutaelewana vizuri kuhusu mambo tunayoyaongelea, tukiyatupilia mbali mashaka mashaka yetu!

  Gbu!

 114. Alphonse,
  Nakushukuru tu hata wewe kwa mawazo yako kaka. Kimsingi sina mawazo au fikra zangu mwenyewe katika kujadili haya. Natumia aya za Biblia kama inavyoelekeza yenyewe. Mimi napenda na najitahidi niwe upande wa Mungu. Najua hii itanilipa zaidi ya kuwaonea aibu binadamu wenzangu. Majibu ya maswali yako ya suruali au sketi kwa wanaume na wanawake, nimeyajibu kwa kaka Sungura hapo juu. Tafadhari karejee hapo.
  Kwa habari ya kubatiza kwa majina matatu, kweli kuna shida leo. Namshukuru Mungu naona na wewe umekiri kuwa unafuata kauli ya Mungu(Yesu) ktk hili-yaani kubatizwa kwa majina matatu. Hata mimi nafuata utaratibu huohuo. Na bado naendelea kujifunza kwa nini mitume walikiuka agizo la Bwana wao la kubatiza kwa majina matatu na badala yake wakabatiza kwa jina moja tu? Naendelea kujifunza/kuchimba changamoto hiyo. Kama una ufahamu mwingine mzuri zaidi, nitapenda kujifunza kwako pia.
  Karibu sana

 115. Sungura,
  Ubarikiwe kwa maswali. Nitajibu tu kwa kadri ya uelewa nilio nao ndani ya neno.
  1. Kwa hiyo Siyi unasemaje,suruali si sawa kwa wanawake?

  Jibu
  Baada ya anguko la Adamu na Hawa, Mungu anaonekana kuwavika ngozi ya kondoo. Biblia haisemi kuwa Mungu alimtengenezea Adamu Suruali ya ngozi na Hawa Sketi ya ngozi, isipokuwa inasema tu kuwa Mungu aliwavika ngozi.

  Lakini ukisoma Torati 22:5, utakuta Mungu anaonesha msimamo wake juu ya mavazi yamhusuyo mwanamke na mwanaume na kwamba hayapaswi kuwa interchangeably!! Ukisoma Biblia yako ya Kiswahili, neno suruali utalikuta limetumika kwa wanaume tu, Kutoka 28:42, 39:28, Walawi 6:10, 16:4, Ezekiel 44:18, Daniel 3:21 na 3:27. Biblia za Kiingereza, zimetumia undergament au breeches, yote yakiwa na maana ya kaputura au suruali-rejea kamusi yoyote ya Kiingereza. Mantiki tunayoipata hapa ni kwamba, mavazi ya suruali ni kwa wanaume tu na si vinginevyo.

  Na ukiangalia katika historia za makuhani ndani ya Biblia, huwezi kukuta vazi la kikuhani kuvaliwa na mwanamke. Mavazi ya wanawake, yalikuwa ya wanawake na ya wanaume ya wanaume tu. Ukiangalia historia za makanisa makubwa na makongwe duniani (Wasabato, Wakatholiki, Wapentekoste nk), huwezi kuona kama wanawake wa zamani walivaa mavazi ya kiume au wa kiume kuvaa ya kike.

  2. Kuna sehemu ambapo Mungu kasema mwanamke asivae suruali?

  Jibu
  Ndiyo, Rejea aya hizo hapo juu, Mungu kakataza kabisa na kusema kuwa, kukiuka taratibu zake za uvaaji kwa wanadamu alizozisema, ni machukizo mbele zake. Torati 22:5. Sasa nimekuonesha aya hizo, sijui kama hizi nazo ni HISIA. Anyway, kama ni hisia, utanitondolea ndg yangu ili na mimi nijifunze.

  3. Na unadhani kwamba kuna mtu anaweza kureason mpaka akapindisha kweli ya Mungu? ,hebu nioneshe huyo mtu na hiyo kweli ya Mungu iliyopindishwa ikapinda

  Jibu
  Ndiyo. Inawezekana kabisa mtu kufanya reasoning akakengeuka. Kwa mfano, unakijua vizuri kisa cha Kora? Hoja zake za kudai kuwa Israel yote walikuwa ni watakatifu kwa wakati ule kama Musa, Haruni na makuhani wengine!! Unakumbuka kaka Sungura? Kama hukumbuki, soma Heasabu 16 uone kilichokuwa kikidaiwa kama kiko tofauti na madai ya leo ya wanawake kuwa makuhani na kuvaa suruali… Mfano mwingine, unamkumbuka mtu maarufu sana ndani ya Biblia -Ayubu? Unakumbuka kuwa Ayubu alikuwa na dhambi ya kujihesabia haki? Kama hukumbuki, soma Sura ya 32 uone alichojichanganya huyo jamaa. Mifano ni mingi sana kaka, sitaimaliza.

  Nina imani mpaka hapa utakuwa umenipata vyema. Kama una uelewa tofauti, nitafurahi kujifunza kutoka kwako pia. Karibu sana.
  Ubarikiwe.

 116. Bwana Yesu asifiwe sana,

  Turudilie mjadala. Inasema “mafundisho kuhusu wanawake yanatafsiriwa vibaya!!”; Mathew akapost hiyo. Sasa ni ktk kanisa gani? Nadhani si ktk kanisa la Yesu iitwayo Bibi arusi ! Ile kanisa ni ya ajabu sana, inahusu roho za watu na hapana mwili yao.
  Wote wanaoendelea kuchangia nawashukuru sana, wanafunza wengi kufanya utafiti ktk Biblia. Aliye na masikio ya kiroho adake.
  Yesu akiishapaa mbinguni, mitume walibaki waki build makanisa ya pahali. Walitafsiri, walionya, walifundisha. Hapo hapo wakaanza doctrines. Na hizo doctrines zilianza pasipo wao kutaka kusudi Yesu aendelee fanya kazi yake kwa njia ya RM. Ile ya Paulo ikawa tofauti na ile ya Kefa. Kwa mfano ktk makanisa zilizoongozwa na Kefa(Petro) ilimubidi kila mukristo kutahiliwa kimwili. Ktk makanisa zilizoongonzwa na Paulo, ile haikuwa tatizo. Hawo hawo mitume wanadai ya kuwa wanapotaka kutenda mema, MABAYA yanawatangulia.
  Sasa nadhani haina maana kuzunguka bila mwisho kwenye neno isiyo na msingi kule kwenye Bibi arusi.
  Yeye Mathew, alisema “… yanatafsiriwa vibaya”, na Paulo alimtangulia akimuarifu eti naye anapotaka mema(kuanadika/kusema/kutenda/…) mabaya yanatangulia. Tutafute mpenyo kwa Yesu, yeye ambae hila haikuwai fika mdomoni mwake.
  Kwa hiyo tutafautishe maneno: dhambi na tafsiri mbaya. Je wanawake hawaruhusiwe kujazwa RM? Na wakifundisha vizuri watenda dhambi? Wala wanaofwata mafundisho yao watenda dhambi? Lakini kuko wale wanawake kama vile wanaume ambao hawaruhusiwe kufundisha; wale wasiookoka. Paulo akiwa ndani ya roho, alisema kiroho na aliwapenya wale wanawake wa yale makanisa aliyoandikia akaona hawastahili.
  Jambo lingine, tuangalie vema, tusianguke kwani toka zamani mpaka leo makanisa yametofautika lakini RM yeye ni mmoja.
  Sasa Mathew, aliona kwa wajibu wake tafsiri ni mbaya lakini hakusema kam ni dhambi. Si kila kitu kibaya ni dhambi. Tazama ilikuwa vibaya kwa wanafunzi wa Yesu kula pasipo kuosha mikono, lakini Yesu akaona hakuna tatizo. Na kwa wajibu wa makuhani, ilikuwa vile vile vibaya Yesu aongee na wenye dhambi. Yesu akaona ile ndio iliyo mleta.
  Lakini walipo mletea mwanamke aliezini, angalau ali muprotect, alimusamehe dhambi.
  This means that, kitu kibaya kinahusu zaidi yule anaeona ni kibaya, lakini dhambi inabaki ni dhambi. Siseme kam zambi si mbaya, lakini nataka sema kam kiitwacho kibaya chote si dhambi na dhambi inabaki mbaya popote except kwa Shetani.
  Nasema hivi, nami kam mwanaadamu:
  -Kanisa la pahali ambayo imeona kama wanawake wa ile kanisa hawastahili kufundisha halijakosea: msimamo huo si dhambi ikiwa ni RM aliyefunua, na siku litapata mwanamke anaestahili litabadili msimamo kwa maongozo tu ya RM.
  -Na lingine ambalo limeonyeshwa na ule ule RM kam kuna wanawake wanaojazwa RM, na yule RM amewapa ujumbe/huduma, watawaruhusu kufundisha na hata kuwa viongozi bila uhusiano yoyote na dhambi. Yeye anayeruhusi ao kukataza si mwanaadamu, lakini ni RM.

  Na wakati moja RM atakataza kwani angali akitayarisha na wakati mwengine ataruhusu kwani ameona chombo chake ni tayari. Bwana Yesu Asifwe!!!!!!

  Kwa mwisho, nataka kila mtu ajue kama kuna fasi nyingi Shetani anatutakia tuanguke dhambini. Isingelikuwa vema tuanze sisi pekee kutengeneza zingine dhambi. Tusipiganie uwepo wa zambi bwana…. Na ile amboyo ni zambi kama vile “kutopenda jirani”, si inakuwa vigumu kuipiganisha? Sasa kwa nini tujichanechane kwenye blog hii tukitafuta tuifanye aibu na dhambi mwanamke kufundisha? Ao asivae suruali? Pima tembea ktk nchi nyingine, au huko vijijini, utawakuta wamevaa sawasawa? Mungu hakudefine nguo. Aliepewa hiyo mamlaka ni mshonaji, awe ameokoka au la. Na nyakati vilevile zimepewa malaka. Hata tuwike, au tujichanechane tutaona tu hata hapo tulipo, mivalio imekwisha badilika mno.

  Thanks.

 117. Shalom wapenzi!!
  Kwa wote kwanza.
  Niwashukuru wapenzi kwa michango yenu mizuri na maswali yenu yenye hekima nyingi. Kimsingi, niseme tu kuwa si rahisi kwa mtu kutangaza waziwazi tena peupee kama hapa SG kuwa anapingana na sera ya wanawake kuwa viongozi ndani ya kanisa hata nje ya kanisa, hasa kwa kuzingatia nyakati zetu hizi tulizo nazo leo. Nasema si rahisi kwa sababu, hadi baadhi ya viongozi wa dini, huwa hawajibu maswali ya namna hii pamoja na kwamba wana nuru hiyo. Harakati za wanawake mnazifahamu wote. Kukusikia unazikandia harakati zao, baadhi yao(wasio na uelewa) kama alivyosema kaka Lwembe, watahakikisha kuwa wanakula na wewe sahani moja hadi tonge la mwisho. Swali la kujiuliza, je, tukae kimya kwa sababu ya hali halisi ya sasa? Au akina Siyi na Lwembe hatuelewi tu mambo haya wala hayana maana na dhana tunazokutana nazo ndani ya neno? Niwaombe tuache ushabiki wa kidini/dhehebu tujadili kwa kueleweshana tu hoja hii.
  Kwa wale walionifahamu tokea mwanzo, niliwahi kusema kuwa, sisimamii dini, dhehebu wala usabato. Nasimamia kweli ya Mungu tu basi. Na nimekuwa nikijitahidi kuanika waziwazi mbele za watu kile ninachokijua ili nami nisikie wao wanasemaje kuhusu hicho kwa mujibu wa Neno la Mungu. Kimsingi nimejifunza mengi na mengine yamekuwa na changamoto kubwa sana kwangu na ninaendelea kuyafanyia kazi. Kupinga hoja za wanawake kuwa viongozi ndani na nje ya kanisa, kimsingi huo ndio uelewa wangu wa neno. Wanawake hawapaswi kabisa kuwa na wadhifa huo. Kama kuna mtu anajua zaidi ya hapo, atufundishe vizuri na siyo kuingiza HISIA za kuogopa kuonekana wa ajabu mbele ya jamii. Mgogoro wa suala hili tete, ni cross-cutting!!! Kama Biblia ni neno la Mungu, basi tulitumie hilo kufundishana kama kuna uhalali ama la wa wanawake kuwa viongozi. Tuache mazoea yaliyopo. Tusaidiane wapendwa.
  Ninachojua ni hiki, Shetani anacheza sana na akili za watu. Tumwombe Mungu atupe nguvu yake(Holy Spirit) ili tutambue mambo. Dunia iko pabaya sana. Kuna mambo mengine sana tumeyashikilia na kuyapigia debe, na tusipobadilika, hakika yake ni tutapotea. Mungu atusaidie sote.
  Bwana awabariki sana

 118. Lwembe/Yusha/Mabinza/

  Tunamalizia kuhusu Wanawake kisha twende kwenye Kutumia Akili na Neno la Mungu.

  Huwa nawa-challenge msiwe wavivu wa kufikiri na kusingizia eti kutumia akili hatari sana, embu fikiri ivi, Wakati Paul anawaandikia ivyo 1Worinto.14:33-35 na 1Timothy.2:11-12 au anatamka hayo:

  (a) Je unadhani ON SERIOUS NOTE, Kukataza kwakwe Wanawake Kunena/Kufundisha, alikua ana maanisha ilo jambo liwe la kuzingatiwa kwa vizazi vyote, tamaduni zote na karne zote zijazo na kwa watakaookoka wote duniani?

  (b) Au Kati ya yale alisema mfano ‘’Makatazo kwa Wanawake’’ na aliyosema MENGINE kama vile…‘’Wokovu ktk mmoja tu Yesu Kristo’’, ‘’Haki kwa Imani si matendo, yapi mnadhani(hata kwa Akili tu-usikimbilie ufunuo kwanza), Paul alijua na hata leo angefufuka, angekuambia kwa hili nilimaanisha kwa pale kanisani na lile ni kwa vizazi vyote(cross cut)

  Press on.

 119. Yusha/Lwembe/Siyi/Mabinza/Amin

  Sungura unakaribishwa pia
  .
  Tuendelee kuchapa kazi hapa, Karibuni kwa uelimishaji kwa kujibu maswali yafutatayo. Naomba tuchape Kazi/Tufanye huduma hapa, hapana kulia-lia, kukwepa wala kuleta misisimko ya kipendwa kwa kuanza makemeo, maangalizo, sijui maonyo,ushauri na mbwembwe nyingine,yote tutapena BAADA ya Kazi/ huduma, hapa ni tuchape kazi mwanzo mwisho tu basi ili tufaidi wote.

  Ktk 1Wakorinto.14:33-35/ 1Timotheo.2:11-12 Haruhusiwi mwanamke kufundisha Kanisani. Nina maswali haya ya kutafakarisha ili mlete vitu LAKINI VYA UKWELI KWA MAPANA YA NENO NA HATA KWA KUTUMIA AKILI ZA KAWAIDA HIZI SAFI SANA TULIZOPEWA NA BABA-Kumbukeni siku zote sisi si boxes/chupa ya Fanta au chimpanzee!!!!!!!!!!!!!!!!!

  (a) Kwa iyo makanisa yote leo duniani ya Waliookoka na wana Roho Mtakatifu na Mungu anasema na kujidhiirisha yu kati yao ambamo pia kuna WANAWAKE AMBAO HAWAJAPIGWA MARUFUKU kufanya ya Bwana kuanzia ya madhabahuni mpaka ya uongozi, wanakwenda jehanum? Wamekosea sana, sana Neno? Je ninyi mna akili,Roho, Ufunuo, Ujuzi wa Neno sana kuliko wao duniani kote uko kwa Wana wa Mungu wote siyo? Confirm plz!

  (b) Kwa kuzingatia concern ya Paul wakati anaweka mambo sawa hasa kwa jamii ile ambayo Mwanamke kusimamana kufundisha Wanaume, Mila na Desturi zisinge ruhusu na wanadamu wale kwa jinsi walivyoshikilia mapokea na system za wakati wa sheria ambazo zilimweka Mwanamke chini sana, Je leo hii ktk jamii nyingine ambapo hakuna iyo concern kubwa ya Mwanamke shurti kua chini au wa nyumbani, mahali ambako duniani leo hii hata wanawake wamekwenda shule na wengine wataalamu wa maandiko na Neno na ivyo wameajiriwa kabisa ktk Vyuo vya Biblia-uko ambako akina Yusha/Lwembe/Siyi watakapo kwenda, watakaa chini ya Phd/MA na BA zao kama Wakufunzi wao/wenu, hao ktk jamii izo/izi za leo kwa namna iyo, wakifundisha kuna tatizo gani?

  (c)Kwakua pia aim ya Paul ilikua kuhakikisha anafundisha Wanawake kua watiifu/wanyenyekevu-kua chini ya mamlaka kama pia inenavyo torati na kwamba mwanamke asimtawale Mwanaume, Je ni sawa sawa kusema kua jamii ile ilikua na matatizo ya Wanawake kupenda kutawala na kua juu ya wanaume ivyo jitihada kubwa na za makusudi kila mara kufundisha na kukazia Wanawake chini na Wanaume juu?

  (d) Kama Jibu la juu ni ndio, je hakuna uwezekano jamii nyingine humu duniani zenye Wanawake ambao nature yao wala hawana agenda ya kuwapanda vichwa Wanaume wao ivyo hakuna haja ya mikazo ya kuwakata na kuwaweka chini siku zote?

  (e) Kama Jamii izo zipo, je wasipotekeleza agizo la Paul na wakawapa Wanawake kufundisha mbele ya Makanisa, ni dhambi? ipi?

  (f)Au Wanawake wa wakati na jamii ya Paul kama jibu la (C) ni ndio, inawakilisha wanawake wote past,present, future worldwide ivyo tuwadhibiti mwanzo-mwisho until Yesu aje?

  Press on( Ninawaletea swali jingine la kuhusu AKILI NA NENO LA MUNGU-maana nalo limejiri sana ktk mijadala hii, wengi wenu mkipinga kutumia Akili bali Roho tu, kwa swali ninaloleta tutajua kati ya mbivu na mbichi-Kweli na Ulongo.

 120. Pole sana Lwembe na Nzala kwa kulazimisha Biblia ikubaliane na akili zenu.

 121. Siyi,

  Unamaanisha nini kua hoja zimejengwa kwa HISIA? Ivi limekutoka tu au ume-cook kwanza ilo neno? Unajua haya mambo yakuongeaga big statements ktk mijadala halafu mkikabwa mnashindwa ku-clear the ground, wacha Kaka! why should you kill yourself easily before the brutarily injured buffalo Siyi?Kui-support Biblia haimfanyi Mtu kua mshamba- I can deadly debate on this if u like, will make your all points zero plus plus I am telling u! Who told you Mtu akishiba Neno na kulisimamia ati ndio anakua mwana Ujima nambari one? Namna magani hapa maneno yako! yanatia hasira mbaya, hapa ushanijaza pumzi, nasikia kupaaa mawinguni vibaya sana niziunguze hoja zako mfu kwa moto wa Bansen Bunner ya/wa JUU,wacha maneno mepesi!

  Aliyekuambia ukisimama na NENO unakua zuzu-zuzu, zezeta, zero-zero and local- local human nani? kama si unlearned street, badly demonised thoughts? KUISHI NA KUSIMAMIA NENO KUNALETA AKILI na UMARIDADI KOTE KOTE ROHONI NA MWILINI- tena nikwambie, Neno na Roho Mtakatifu ndani yetu (si dini ya Amri za M23 from Congo Mbujimai forests, TUNAFANYWA kua hatari kabisa mbele ya wenye kujaza Physics na amri za M23 uko nje. Ngoja uone Watu waliojaza Neno na kulisimamia walivyo smart:

  Mdo.18:24-28- Mr Appolo hapo, mstari wa 24 Kiingerea NKJ inasema HE WAS MIGHTY, IN SCRIPTURES, Mstari 26 akaingia game/debate Msikitini mmoja wa Wayahudi Efeso, aliwanyuka kwa hoja matata sana, akipangua hoja zao na kumaliza kazi kabisa mpaka mstari wa 28. Roho Mtakatifu anakubali CV yake iandikwe kitabuni humo Mdo kua ..Kiingereza yake nimependa…He VIGOROUSLY REFUTED the Jews PUBLICALLY-hapana sirini au kiheshimiwa bali unawashusha ‘P’ nje nje mwanzo mwisho mbele ya wote, akiwathibitishia TOKA MAANDIKO kua YESU ndiye Masihi

  Mdo. 26:1-32 Paul ameshitakiwa na Wayahudi halafu Mfalme Agrippa anafanya KOSA KUBWA SANA LA KIUFUNDI kumpa ruksa kamanda Po ajitetee! Paul Alitiririka public lecture ya hatari mpaka mstari wa 24 Mheshiwa Festus aliyekua barazani/Kikaoni pia, akafyatuka…..kwa maneno yangu ni sawa alisema…’’Paul umedata au? Kusoma kwako kwingi kumekufanya kichwani kumekata networks’’ Ndipo Paul akajibu kitu ambacho nimekua kila siku nawaambia wapendwa humu kwamba tukiokoka na kujazwa Roho, si uvivu wa kifikiri-(being ANOINTED IS NO EXCUSE FOR THINKING), sisi roboti,maboga, matikiti maji wala kabechi, TUNA ROHO NA TUNA AKILI SAFI…Mstari wa 25..Paul anamjibu Festus..MIMI SI KICHAA MHESHIMIWA LAKINI NAONGEA MANENO YA ‘KWELI’’ NA ‘AKILI’ na Kiingereza imetumia maneno ya/ with ‘reason’

  Sasa MWANAUME MWENYEWE ktk Luka.14:1-6 ,Yesu akijua Wazee wa kushika sheria wasivyo na Roho, Mstari 3 akataka kuponya mtu lakini akauliza kwanza, Je ni Sheria kuponya siku ya Sabato? Wale jamaa sijui walishitukia nini-Biblia inasema walikaa kimya!!!! Imagine Yesu anauliza swali sio Siyi anamuuliza Seleli- but jamana wakala ‘kobisi-mute( they must have been very smart kukaa kimya manake wanajua Mwanaume alivyo na akili za hatari plus Hekima/Mafunuo yasiyopimika. Mstari wa 4 Yesu anaona hakuna haja ya kupoteza muda, wakae tu kimya, Yeye ni kuchapa kazi tu mwanzo-mwisho-akamponya yule. Akaona amalize kabisa mzizi wa fitina ili kusije zuka tena zengwe, akawauliza swali mstari wa 5..nani hapa Punda au Maksai wake akiangukia shimoni, atamwacha kwa kua ni siku ya sabato? Ajabu yake wale jamaa kwa mara ya PILI, wama mute-mstari wa 6!!!!!!!! Wewee, bila shaka wanaujua moto wake. Notice: Kiingereza yangu NKJ naipenda, Yesu alipowauliza mara ya kwanza, Inasema mstari 4..they kept silent-walikaa kimya! Kama hawaelewi vile au wanaeelewa lakini ndio nani aanze sijui! Alipowauiza swali la pili mstari 5..imeandikwa they COULD NOT answer him…nimependa ivyo verb –COULD not—implies ability/capability and not will to act or not. KWA IYO NI SAWA NA KUSEMA..walishindwa kumjibu kwa maana ya walishindwa kupata hoja kinyume naye, walipigwa goli bila kipa maaana ni lile bao la pembeni ya goli juu kabisa kwenye kona na kwa kasi ya ajabu, hakuna kipa atadaka zaidi ya kuangali tu mpira utatiksa nyavu

  Nikisemelea la Yohana 8:1-12 Unajua washika sheria bila Roho walivyojidai much know kumvaa Yesu kienyeji na torati zao, wakajidai kuleta u-smartness wao hapo na maswali…mstari wa 6 naupendaga siku zote..jamaaa wanauliza na kuendelea kushoot swali labda na pofu or wether povu[-I don’t care-limemjaa kwa mudomo na matwi yule spokesman wao, Bwana akawa naye ame MUTE! Huku anaandika-andika chini kwa kidole. Walivyolikoleza sana, NDIPO usharp/usmart/uehekima/uakili wa Mtu mwenye Uungu- unavyoonekana, mstari wa 7..’’Yeye ambaye hana dhambi, awe wa kwanza kuua huyu mwanamke na jiwe! Dozi over and out, Daktari kamaliza kazi yake,mgonjwa achague kunywa na kutema, apone au afe! Kilichoendelea kila mtu alikumbuka madude aliyofanya hata yale ya kuamkia usiku iyo day ya kumswaga yule Lady maskini kwa Mwokozi.

  Labda niishie kwa hili la Mathayo.12:1-8, Wanafunzi wako na Kamanda Yesu aliyesema hata hana pahala pa kulaza Kichwa, a busy man of God, kumbe Wanafunzi njaa zina wauma sana na mbaya zaidi ilikua siku ya Sabato, wkwa kua walipita ktk shamba, wakaona tusife bure, wanavunja masuke ili kula, Biblia inasema mstari wa 2-Mafarisayo WAKAWAONA wanafanya KAZI-siku ya wana m23! Na kisha ku-mchallenge/shitaki/mlaumu Yesu kuhusu kitendo cha Wanafunzi kilicho kinyume na Sabato. Ndipo Mtu alijaa Neno na kulitetea, akawamaliza tikitiki- Mistari ya 3-8 na hasa ya mstari wa 8 unapiga mpaka pentagon ya dini na imani mbovu zote zenye bila Roho wa Uzima.

  Tafahari USIPUNGEZE HESHIMA NA THAMANI YA +IMPACTS KIROHO NA KIMWLI YA NENO LA MUNGU KTK MAISHA YA WALE WALIOAMINIO- so, no ushamba kwa maana zote bali ni umjini/umbinguni kwa maana zote njema kabisa.

  Swala la MAMLAKA NA UGAWANYAJI MAJUKUMU KATI YA ME/KE- SOMA POST YANGU KWA YUSHA NA LWEMBE juu-halina ubishi, usikuze maneo na kuunda hoja ambayo haina haja, ni sawa na kuuliza kama Kanisani waga kuna sala! Come on, it is obvious maana kanisani kwa kweli hakujawahi kua kijiwe cha kunywea ‘henkeni’. The issue ktk ilo ni kua Wakati Wanaume tumepewe Supremancy iyo isimaanishe na tusi behave na kuwa treat kama they are basically useless au extremely dangerous vessels! The Bible says they are delicate/weaker (notice: WeakER vessel-an idea of comparisons- with who/which? donkey, stone, pig meat? No ! with a Man, hence they are WEAKER not WORSE vessels –come on people, understand these cheap things aah!

  Suruali kwa wanawake ili nilianzie kwa kukuliza tu kwanza nijue una capacity ya uulewa kiasi gani ktk mambo haya ili nipime kama kuna haka kweli ya kudeal na jambo ili kwa mimi kupata serious challenge toka kwako au ni yale mambo yatu ya kadance hapa na pale. SWALI: (a) KILA MWANAMKE ATAKAYE VAA SURUALI KWA KUA umesema MUNGU AMEKATAA, ATAKWENDA JEHANUM? (b) JE KUTOKUVAA SURUALI KWA UELEWA WAKO WA MAMBO YA MUNGU, NENO LAKE KWA MAPANA YAKE NA MOYO/TABIA YA MUNGU BABA YAKO AND I HOPE NDIO BABA YANGU-ingawa sijui lini ulishafanywa Mwana, JE KATAZO ILO NI NENO LA NIKO AMBAYE NIKO KWA VIZAZI VYOTE PAST, PRESENT AND FUTURE REGARDLESS YA CULTURE, WETHER, AINA YA KAZI nk, embu nijibu hayo kwanza nione kama kuna ulazima wa kuingia Msikitini wa Wayahudi kama Appolo na Paul ili KUHOJIANA.

  Issue ya Kutumia REASONING/AKILI…nimeshajibu kwa kiasi kwa post hii na rejea post zangu 3 kwa Lwembe, Yusha na Amini ktk mada hii na ya Zaka…soma zote kisha lete hoja hapa ya kuni-challenge kupinga yale nimesema au kunionyesha wapi nimekosea prove me wrong or blesss me with a a big YES…only two choices in mijadala..hakuna netral, ingekua btn Cdm Vs. Ccm agenda, hapo kuna neutral but si kwa Neno la Mungu-ONE MUST BE TERRIBLY WRONG AND ANOTHER HUGELY CORRECTLY.

  Press on.

 122. Seleli nilikuambia huko nyuma kuwa utazunguka na Maandiko mpaka basi, kama walivyoizunguka nyumba Sodoma wasiuone Mlango!

  Pia nilikuambia kuwa ili mradi umeyagawa Maandiko, nao ufahamu juu yake unakuondoka pia! Angalia ulivyojikoroga, mpaka hueleweki hata unalolisema!!

  Haya, ngoja nikufuate huko porini uliko:
  Maelezo 1: Umenukuu yawahusuyo wanawake ktk Agano la Kale na Jipya, badala ya kuyaacha Maandiko yenyewe yajishuhudie, unatushawishi kuwa,
  ”Ukisoma Biblia kwa mantiki ya kumtazama kiumbe mwanamke na positive role yake kuhusu Mungu pamoja/katikati ya Wanadamu utapata ukweli ulio wazi kua Wanawake wametumika na kutumiwa na Mungu sana kwa kufanya mengi mema hata kama madhaifu/mabaya yapo kama yalivyo mabaya tena makali kweli ya Wanaume”
  Ushawishi wako unaonyesha udhaifu ulionao juu ya wanawake! Udhaifu wako wa kwanza ni UCHONGANISHI! Una udhaifu kama aliokuwa nao Adamu, yeye penzi kwa mkewe lilikuwa kubwa kiasi kwamba akamsikiliza akijua fika kuwa hilo ni KOSA, halafu alipotightiwa, akamchonganisha na Mungu!! Bali ktk siku hizo DAMU ilikuwa bado haijamwagika, leo hii kaka, wewe pamoja na hao wanaokusikiliza na kukusifia, … “mtakwenda mbinguni”!!!! Paulo na Wagalatia wake waliomsikiliza, walie tu!

  Pia kuhusu status ya wanawake, naona umekurupuka nayo tu bila ufahamu, kwa taarifa yako wanawake wameanza kuruhusiwa kupiga kura mwaka 1920, kama umemuelewa Siyi anachokuambia, unaweza ukajisaidia kuikimbia Hukumu! Kama kati ya mitume 12 hakuna mwanamke, basi tambua hivyo tu. Haya masuala ya sijui “Hakuna mwanamke mwenye akili angependa awe mtume…” hii ni dalili tosha kuwa umechanganyikiwa ki ufahamu! Hivi “uteuzi” unatoaga fursa kwa yeyote yule kupenda kuteuliwa kuwa kigezo cha kuteuliwa kwao? Labda nikukubalie kuwa Mwanamke mwenye AKILI hawezi kukubali kulifundisha Kanisa, hao wasiokuwa na akili ndio wanakwea tu mimbarani na kufuwafundisha wenzao wasio na akili pia, ambao wanaume waliomo katika makusanyiko hayo kwa kutumia akili ambazo hawana, walipoambiwa kuwa Kanisa ni Bibi Arusi wa Kristo, basi nao wamejihesabia kuwa ni “wanawake” tena wao ni vijana, ndipo hao wanawake wanaowafundisha, ni wale wazee, Tito 2:3-5 wanawake wazee wawe na mwenendo wa utakatifu, ili wawafunze, wawatie wanawake vijana akili…”!!! unayaona hayo makusanyiko yenu, kiroho ni makusanyiko ya wanawake!!!
  Na hilo ndilo Neno la Mungu kwa vizazi vyote vitakavyoipokea Injili kama ilivyohubiriwa na mitume, kwa Wagalatia kwanza, na kisha kwa Wanyamwezi na wengineo, VIZAZI VYOOOTE, mpaka Bwana atakapokuja!

  Maelezo 2: Ngoja niyanukuu maelezo yako:
  “Biblia inasema kua Yeye (Yesu) mwenyewe aliwatoa wengine kua Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu-Waefeso.4:11-12 na pia ktk 1Wakorinto.12:1-13-Inasema Roho Mtakatifu anagawa karama mbalimbali kwa KILA MMOJA kama apendavyo na kisha mstari 13 inasema hakuna huyu myahudi, Myunani, Mtumwa au Aliye huru( kwa mantiki hii bila kuvuruga maana ya mstari huu naongeza pia hakuna huyu mwanamke au mwanaume, amesoma hajasoma, anazo au maskini, mzungu au mwafrika, wa Dar au uko vijijini Babati, Ujiji KGM na Nyanzalaki Burundi) na hata Mdo.10:34-35-imeandikwa..Sasa natambua MUNGU HANA UPENDELEO ila ktk kila taifa YEYOTE akimcha, anakubaliwa!”

  Nikikuambia kuwa Seleli una udhaifu wa Adamu wa kupenda wanawake kuliko Neno la Mungu unakuwa mbishi! Angalia usivyokuwa na uoga na Neno la Mungu: “kwa mantiki hii bila kuvuruga maana ya mstari huu NAONGEZA pia hakuna huyu MWANAMKE au mwanaume, …”; wewe kweli umepitiliza! UMEAMBIWA USIONGEZE WALA USIPUNGUZE katika Neno la Mungu, ila wewe unaendelea tu, unao ubavu wa kustahimili mapigo ya Mungu, au unadhani ni hiyo michezo ya kanisa?!!! Halafu usivyokuwa hata na aibu, huko nyuma umekazana saaaaana kutufundisha kuwa, oh, Paulo kasema “hapa ni mimi…”, oh, hapa Paulo anasema “hapa ni Bwana” oh, hapa Paulo alikuwa anasimika kanisa lake, kwa hiyo huu ujumbe uliwahusu kanisa hilo tu na si dunia nzima; halafu hapa unapotaka kudandia gari la Paulo, eti, unajidai macho makavu kama yule Simon aliyetaka kununua kipawa cha Roho Mtakatifu, Unasema Biblia inasema kua Yeye (Yesu) mwenyewe…! Labda nikuulize, Biblia nayo inasemaga? Iliyasemea wapi hayo, na nani alikuwepo ilipoyasema hayo, na Yesu alikutana wapi na huyo Biblia hata amueleze hayo?? Acheni Unafiki! Hiki mnakikubali na kukiinua kama nNeno la Mungu na hiki mnakikataa, vyote kutoka chanzo hicho hicho, Biblia yooote ni Neno la Mungu, ndio maana ninawaambia viacheni vitabu vya Paulo msivitumie! Ni nani kati yenu ambaye ni Mgalatia au Muefeso au Mrumi au Mkorinto au ni Tito au ni Timotheo? Sasa mnanatumiaje jumbe hizo nanyi haziwahusu kizazi hiki? Mkiambiwa mmetolewa nje ya reli mnabisha!!!

  Angalia swali lako hili lisivyo na jinsi ya kulijibu kiBiblia, (a)Je Mungu kwa maana izo hapo juu, hawezi na wapi alipiga marufuku Mwanamke kutokua Mtume, Nabiii, Mwalimu nk wakati Yesu anasema aliwatoa wengine na wala hajasema aliwatoa WANAUME tu kua….?” Hivi unajua kusoma kweli wewe? Yaani ufahamu wako uko kamili kweli? Mwenye kuwachagua kwa kazi yake kawaacha, kawapa kazi nyingine, sasa wewe masikini unahangaika na nini? Marufuku umeiona halafu unajitoa akili unajifanya hujaiona!! Wale WATAKATIFU waliyaelewa hayo bila shida, tabu ni kwenu ninyi watu wa makanisa, wenye mfano wa utauwa!

  Angalia siasa zako za dini, utadhani uko bungeni! (b) Hamuoni kwamba kukazania kua, kwasababu tu ktk wale 12, Wanawake hawakuwemo wala kua Makuhani enzi zile kisha sisi wenyewe- tutafsiri kua ina maana Wanawake hawakuruhusiwa kua na huduma izo TOKA MBINGUNI, ni kukosa ufahamu wa kweli nyingine za Neno maana wakati mwingine kama si wote,”
  Jibu: Napenda kujibu swali la nyongeza la mhe. Mbunge wa Upinzani, kama ifuatavyo: kutokana na mh. Mbunge wa Upinzani kukiri kwamba ktk wale mitume 12, wanawake hawakuwemo, na wala hawajawahi kuwa Makuhani, kwa ushahidi wa Neno la Mungu, kwa kadiri ya Uchaguzi wa Mungu mwenyewe, basi kambi ya Upinzani kuwasimika wanawake katika nafasi hizo ni kuisahihisha Kazi ya Mungu, na ni utovu wa nidhamu unaodhihirisha kwamba nao wamepata na wanautumia Upako wa Lusifa katika kujenga himaya yao, yaani lile ‘kanisa’ jingine!

  Maelezo 3: Angalia unavyoendelea na ushawishi wako ili kuwatoa nje ya Ufalme wa Mungu hao watakao kusikiliza: “Kanisa limejengwa juu ya misingi ya Mitume na Manabii
Maoni/Swali: Kama watu wa Mungu, wa rohoni, tukumbuke kua tunaweza fuata mifano ya Wanadamu wenzetu walio tutangulia na kufanya vema ktk mambo ya kiroho hata ya kimwili”
  Mnaiona hiyo hila? Ni wapi ktk Maandiko mlipoambiwa muwafuate wanadamu wenzenu waliowatangulia ktk mambo ya kiroho na kimwili? Mtu akikusikia unavyompamba Yesu anaweza kudhani mnatoka naye kijiji kimoja. Kumbe huna lolote, mitume ndio waliokufahamisha kuhusu Kristo na sasa unajifanya unamjua kuliko wao! Huyo Kristo mwenyewe atakuwa anakuona mzushi tu, kama hao waliokuletea habari zake unajidai kuwapiku, basi wakuoneje, watakuwa wanakushangaa tu unavyojikoki!

  Hivi unajua kuwa lile vazi alilovishwa Kristo lilikuwa ni la Kifalme? Kaka, nikiyasoma hayo maelezo uliyoyatoa huo Wekundu na Zambarau, mimi hilo sijaliona kama lina tofauti sana, maana kwa maelezo hayo, basi nimejua kuwa vazi hilo lilikuwa ni Velvet, nayo reflection yake yaweza kukupa rangi hizo mbili kutegemeana na angle ulinayolitazamia! Mambo ya Kifalme hayo Seleli, gari kubwa!!!

  Huo Msingi wanaokuelekeza akina Petro na Paulo kuwa ni Yesu, kwa akili yako ya dini unadhani huyo ni Yesu yupi? Ni Yesu huyo wanayekuhubiria wao!!! Changamsha akili hiyo, acha kujichanganya, wasikilize uyaone hayo unayohubiriwa! Huo “msingi mdogo wa Paulo” umeutoa wapi? Unacho kitabu alichokiandika alipokuwa Mfarisayo, nasi utupatie kopi? Kama unazizungumzia Nyaraka zilizomo katka Biblia ndizo unaziita “msingi mdogo wa Paulo”, basi ndg yangu utakuwa si tu kwamba umepitiliza, bali ni FINITO, yaani we acha tu!!!

  Ngoja nikuache kwa Siyi, huenda yeye akafanikiwa kukurejeza, potelea mbali hata ukiwa Msabato, angalau mkimaliza ile Dhiki Kuu mnaweza kupona pamoja na yale makundi mengine, mkawa mnatufagilia zile barabara zetu za Dhahabu!

  Gbu!

 123. Yusha/Lwembe,( Siyi nawe karibu kuna baadhi ya niliyoandika yanakubalina na wewe ila ktk post yako mengine nitakujibu kivyako niyafyekeleee mbali porini mapema sana)

  Hili ni Angalizo lisilo na msingi kua ni kupotoka Ukisoma Bible kwa kuzingatia yapi ni Maneno/Matendo ya Watu, Mungu au Shetani. Kwa nini angalizo hilo ni kama la kiroho saaana kumbe hamna kitu? ni kwa sababu:(Tuangalie Neno lenyewe linatufundisha/onyesha nini-siku zote tuongee yote na hata kama Mtu(mimi, wewe na yeyote) atakua ameoneoneka kama aliyosema ni ya kiroho kweli lakini yalete yote kuyapimisha ktk Neno ndio utajua ni misisimko/mbwembwe tu au kweli kuna kitu cha KiMungu cha kudaka hapo)

  Paul mwenyewe anasema MIMI wala SI BWANA na pia SIMPI ruhusa…. ni yeye kama Paulo anayetoa agizo/ushauri-1Wakorinto.7:12,25, 1Timo.2:11-12

  Yesu mwenyewe final role model wetu anasema ‘MUSA aliwaambia ivyo …lakini toka MWANZO(MUNGU ALIVYO-PLAN /SEMA) HAIKUA IVYO i.e. NENO LA MUNGU la toka mwanzo kwa VIZAZI VYOTE SI LILE ALILOSEMA MUSA KWA/KUAMUA CASE ZENU ENYI WENYE SHINGO NGUMU-maana nyingine ni kua kutokana na ugumu/ukorofi/matatizo yaliyokuwepo/mliyokua nayo, mlifanya KIONGOZI WENU WA KIROHO kufanya maamuzi hayo-ya kuwaruhusu kuwatimua wake zenu na kuwapa taraka ILA Neno/plan ya Mungu-kitu cha KiMungu kwa vizazi vyote si ivyo- i.e.hakuna taraka!- Marco.10:2-9

  Paul anaandika kwa kuangalia/zingatia tendo/neno la mwenziwe, anamsema mwenziwe Petro kwa kusema…’’nikampinga Kefa maana hakuenenda sawa…..Wagalatia.2:10-11

  Petro naye anamsemelea mwenziwe Paul kua ‘’ndugu yetu Paul kapewa hekima na anasema/andika mambo magumu kuyaelewa-2Petro.3:15-16

  Hili andiko- 1Wakorintho.14:33–40 Lenye kuwakataza wanawake KUSIMAMA MBELE YA MAKANISA NA KUFUNDISHA ILI HALI HUMO NDANI KUNA WANAUME, tuliangalie ktk upana wake. Mlifanya haraka kunikimbia eti mie mbishi! Mimi nilileta maswali na kuwa challenge ili mpate wasaa wa kutulia na kuchambua mambo na kuligawa NENO vema kwa haki na usahihi-2Timotheo.2:15, katika hili tuko pamoja kwa asililmia kubwa sema tu tunatofautiana ktk mambo machache kadhaa kwa mantiki nitakayoelezea. Nifutilieni kwa makini ndugu Yusha na Lwembe na huyu wa juzi hapa Siyi.

  Ikumbukwe kua yapo Maneno ya Mungu utalewa hapo hapo kama yalivyo na ulipoyakutia mfano- Usiue, ‘Usizini’, ‘Enendeni Ulimwenguni kote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe’ Ila yako mengine mfano ya Yesu mwenyewe..’Ninyi msipokula mwili wa mwana wa Adamu na na kuinywa damu yake, hamnao huo uzima’’-Yoh.6:53 au ‘’Amini, Amini nawaambia, wapo wanaosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka wamemuona mwana wa adamu akija ktk ufalme wake-Matt.16:28, maandiko kama hayo na mengine kadhaa ya aina hii, YANALAZIMISHA KUWEPO NA TAFAKARI NA TAFITI YA NENO KWA KUVUKA MIPAKA YA PALE ULIPOYAKUTA-Kuepuka hatari ya kung’ang’ana na ilo moja tu ktk mahala hapo tu pamoja ulipolikutia, ukajikuta unasema vitu/sisitiza dhana ambazo yeye asomaye, anatambua mara moja kua kuna ufahamu mmoja tu ktk ilo na kunakukosekana kukubwa kwa ufahamu mwingine ili Mhusika atoke/adake kile haswa cha kukuishi kama Neno/Fundisho/Amri/Ujumbe wa Mungu kwa VIZAZI VYOTE kwa NYAKATI ZOTE KTK TAMADUNI ZOTE PAST,PRESENT, FUTURE.

  Kwa mantiki ya hapo juu, basi tuangalie baadhi ya mistari ya ili-1Wakorintho.14:33–40 ( Tafadhari soma kwa makini maelezo ya ziada ktk mabano kwa kila mstari)

  Mstari wa 5= Imeandikwa, ‘Nataka’(Kiingereza inatumia neno turi hili-I WISH ninyi NYOTE..mnene kwa lugha’’(Notice: Ana ‘WISH’ tu kama MTU/Kiongozi wa Kiroho wao na pia ninyi ‘NYOTE’-hakuna cha Mme/Ke hapo.

  Mstari wa 6= Imeandikwa, Nikiwajia naongea kwa lugha, itawafaidia nini? isipokua nikinena kwa ufunuo, Elimu/Maarifa, Hotuba au Fundisho (Notice:anaanza kutoa dondoo hapa kuhusu tatizo analoliona Kanisani kwake hapo-atakapoendelea kuongea mistari inayofuata 7-13, unatambua mara moja ni lipi)

  Mistari wa 14,15,16-21: Anaendelea kugusia tatizo-kukosekana kwa utaratibu ktk kunena kwa Lugha na pia anaanza kudondoa nini cha kufanya-kuweka taratibu.

  Mistari ya 22-25: Anaendelea kusema athari za kukosekana utaratibu ktk unenaji lugha na kisha anasema kunena ni sahihi na ina faida yake-ishara kwa wasioamini lakini kwa utaratibu au kuwepo na kutafsiriwa ili mgeni(asiye amini naye afaidi/ajengwe/achallenjiwe njia zake mbaya, asije akawaona wote vichwa maji humo kanisani maana wote wanena kwa lugha mpya-haelewei!

  Mistari ya 26-33: Hapa sasa anaweka wazi utaratibu aliokua anaudokeza taratibu kwa mifano na hoja mbalimbali mistai iliyotangulia na pia kwa solutions izi alizotoa ktk mistari hii, inatoa picha wazi tatizo lililokuwepo kanisani pale na ivyo yeye kama Mchungaji/Mtumishi anayewasimamia wanae wa Kiroho, alipaswa kuwashauri cha kufanya( Notice: Mstari wa 27,28,29=Hata Wanaume hapa WAMEZUILIWA KUNENA! mpaka Paul kama kiongozi wao, anatoa maximum no. ya wangapi wanene(watoe unabii-yaani hata kama una Roho ndio anakuambia nena/amekufurikish-lakini kwa kua amesema max ni 3 na pia mstari wa 32 roho za Manabii huwatii Manabii, BASI KAA KIMYA kanisani-ivyo kukuza/kung’ang’ania tu ukweli kua WANAWAKE WALIKATAZWA- lakini bila kuona la juu yake la Wanaume/ Watu wote pia nao walikatazwa/wekewa utaratibu, kabla hajamalizia la Wanawake Mistari 34-35, ndicho nacho sema ni kukosa ufahamu wa Neno la Msingi KTK UPANA WAKE na kuondoka tu na kitu kimoja kukifanya ndio issue kubwa sana-cha Wanawake kunyamazishwa!!!)

  Mistari ya 34-35: Ndipo sasa anatoa utaratibu kwa Wanawake pia kua na wao wasinene mbele ya Kanisa.(Notice: Hajaanzia hapa, wapo waliokatazwa pia toka juu yaani makatazo kuhusu Unenaji lugha na sasa makatazo juu ya Unenaji (Kuhutubu).Kwa nini Wanawake wanyamaze na hawana ruksa kunena MBELE YA KANISA? Jibu anasema: Wanatakiwa wawe wanyenyekevu na kama pia SHERIA YA TORATI inavyosema-(Hapa utaelewa kwa nini ktk michango yangu- nimekua natumia phrase..’’Zipo kweli nyingine ZINAHAMA MOJA KWA MOJA toka Agano la Kale to Jipya’’ na kwamba kuongea tu kiujumla kua Agano la Kale, mambo yake yote kuyafuata ni kujiweka chini ya laana-SI KWELI-NI KUKOSA UFAHAMU TU WA NENO LA MUNGU KTK UPANA WAKE-natumia kwa makusudi sana iyo phrase -‘’NENO LA MUNGU KTK UPANA WAKE’’( nitaliongelea ili pia kuhusu kama kweli KILA NENO/KITU CHA AGANO LA KALE NI LEO KWETU ni zero plus,plus NA HATARI-laana!!!!!!!

  Na jibu jingine ni aibu kwa yeye kuongea Kanisani.Sasa zingatia hii-ukisoma tu ako…’ni aibu wao kunena kanisani’, huwezi pata hasa mantiki ni nini-inabidi uunganishe na ki-hinti ameshakisema mwenyewe hiki..’’wanapaswa kuwa wanyenyekevu! Lakini Wanyenyekevu tu basi, iishie hapo? Au ina connect na nini hasa? Kwa nini asisitizie Wanawake kutunza hiyo nidhamu/tabia njema ya kunyenyekea? kwani kuna tatizo gani mpaka Paul akazane kusema, wanapaswa kua wanyenyekevu kama TORATI PIA INAVYOSEMA?

  Ni kwamba, ukishaona neno KUNYENYEKEA linaambatanishwa na jinsia-(be submissive ie submit under/to someone), ilo likiunganishwa na KUWAKATAZA kunena Kanisani na Torati ikawa refered, ni mara moja unajua hapo Kanisani, kwa kua kuna Wanaume na ukizingatia mila na desturi zao wao kama wayahudi Kabla na hasa wakati wa Sheria kuhusu ranking system iliyokuwepo ktk ya Mme/Ke na ukweli kua yeye anenaye(kuhutubu/kufundisha lazima, in one way or the other, ATAELEKEZA, FUNDISHA,KEMEA(fokea),AMURU, FANYA MAAMUZI nk…isingekua ni hekima MWANAMKE kunena-akiyafanya yote hayo mbele za WANAUME ( Waume,Kaka,Wajomba zao, Wakuu wa Dini, Wasomi wa Sheria nk wako hapo chini wanamsikiliza mdada/Mmama amechachamaa moto!!!!!!!- DESTURI/MILA NA SHERIA ZA TORATI-zingekataa, Wasikilizaji wasingeruhusu au hata kuacha hudhuria ibada ya ivyo-Mwanamke Kunena.=Kumbuka tena ni swala la Mila na Desturi tu hapa Paulo alilokua anaweka sawa.Unganisha na mantiki hizi ktk maandiko haya: 1Timoth.2:11-12- hapa anaweka wazi zaidi kua Simpi ruhusa Mwanamke KUFUNDISHA!!!!!!! Na kama hajualewa kua Paul alikua anaweka sawa ktk ile-1Wakorinto. 14, mambo ya Mila, Desturi, Tamaduni za wakati ule pia kwa kuzingatia Sheria zilikuwaje wakati wa Torati ndio maana alikazana kweli kuwasisitizia wawe wanyenyekevu na wakajifunze kwa waume zao, kutovuruga Utaratibu wa Mamlaka ktk ya Mme/Ke, anamalizia kabisa hapa ktk iyo Timotheo kua…simpi ruhusa mwanamke kufundisha AU KUWA NA MAMLAKA juu ya Mwanaume-(Notice: hapo kua Unenaji uliyosemwa ktk Wakorinto pale ni Ufundishaji ambao umewekwa wazi ktk Timotheo hii na ivyo Mwanamke kusimama na kufundisha mbele za wanaume kwa kua ktk Ufundishaji atakemea, amuru mambo, pitisha maamuzi, panga vitu, pangua mambo, elekeza matters kwa/mbele za Wanaume, iyo haitakua picha nzuri na a healthy church practice-more acute case by then- ndani ya Kanisa ktk swala zima la kua Wanawake kufundishwa kua chini ya mamlaka.

  Hitimisho kwa sasa ni kwamba, Ukatazaji wa Wanawake huu ni pale tu Wanapofanya mambo yatakapowawekwa wao kua kama viongozi wa kuwaelekeza Watu wote na wanaume, lakini kama ilo halipo, basi Karama/Huduma/Vipawa ambavyo Roho Mtakatifu huwapo Wote, basi na wavitumie tu pasi na shaka, wata-adjust tu/adjustiwa tu pale inapokuja kua mbele za Wanaume tena KANISANI NA KTK FAMILIA TU, nje uko habari ni nyingine, ndipo sa hata Mkuu wa Wilaya/Mkoa/ Rais wanaweza kua Wanawake na sisi bado tunakua chini yao, sasa je kwani tufanyeje? Hata JWTZ wako mpaka major general Wanawake-wanatoa amri na wanaume wajeshi rank ya chini, wana-salute ‘ndio afande’ kisha haraka kutekeleza, abishe kwakua yeye mwanaume, aone cha mtema kuni.

  Press on.

 124. Bwana Yesu asifiwe,

  Mim naona ndugu SIYI hayupo ndani ya mjadala huu. Anapana summary ya fikara zake tu. Soma vizuri, na utaona kuna yeye aliyeswali, na wengine kila moja ana msimamo wake. Ungelikuwa serious ungelionyesha tu kam uko upande upi. Au unasema wanawake hustahili au la / au wavae suruali au la. Nakuona lakini ukipima sema hawastahili vaa suruali: Je unafahamu suruali ilianza siku gani? na unafahamu ni nani aliivaa wa kwanza? Je Mungu gani akanena about suruali?
  Eleza ndugu yangu….

  Lakini Hum! kweli wanaadamu wamekuwa specialists kutengeneza dhambi ambayo Mungu hakufafanua. Je nani Mungu aendelee kutia amri zake ili dhambi ziongezeke?

  Kam Mungu hakunena, hakunena. Wananaje pahali pake? Tazama: Yesu akasema “….. wabatizeni kwa jina la baba, la mwana na la RM” ; Mitume siku fulani wakabatiza kwa Jina la Yesu. Je kuna dhambi hapo? Inaomba kujiweka ndani ya RM, utaelewa. Si hii nayo inaleta tatizo ndani ya makanisa? Ukiona pahali Mungu ananena HimSelf simamia pale. Ukiona ni mtu alinena, shika kam ni neno la mwanaadamu na endelea tafuta kam Mungu alisema nini. Na iwepo hakunema jambo lolote, do not create sins. Kwa nini wanaadamu hupenda kuwa wakali kuliko Mungu?

  God bless you.

 125. Kwa hiyo Siyi unasemaje,suruali si sawa kwa wanawake?

  Kuna sehemu ambapo Mungu kasema mwanamke asivae suruali?

  Haya tuonyeshe ili tujue wewe na sisi nani anakwenda kwa hisia.

  Na unadhani kwamba kuna mtu anaweza kureason mpaka akapindisha kweli ya Mungu? ,hebu nioneshe huyo mtu na hiyo kweli ya Mungu iliyopindishwa ikapinda.

 126. Shalo wajoli ie Seleli, Sungura, Lwembe, Yusha, Ziagroa na particulary Mathew
  Naona baadhi yenu mzunguka mbuyu tu!! Hoja zenu zimejengwa na kutawaliwa sana na HISIA. Halafu mnogopa kuitwa washamba (watu wasiowastaarabu hapa duniani) kuonekana mnaisupport Biblia kuwawekea wanawake mipaka ya kuwa na mamlaka kama Mungu alivyowafanya na badala yake, mnahukumu hata Mungu kuwa hakufanya vyema vyema!!!
  Mnachekesha kweli!!! Chagueni moja, kuchagua sera za Mungu(wanawake kuwa na mipaka ya kimamlaka) au Luciferian policy(50 kwa 50).
  Seleli nimeona umeenda zaidi hadi kwenye mavazi, napo unaonekana kuhalalisha suruali kwa wanawake??? Ha ha ha ha !!! Sometimes reasoning ni njema, but sometimes zina hatari sana mbele za Mungu, hasa reasoning zinazopindisha neno la Mungu ili kufit matakwa ya mwanadamu mdhambi

 127. Yusha/Lwembe

  Yusha, Nadhani uache woga na kuwadhania wenzio wabishi mpaka kunukuu maandiko VIBAYA ili mradi kutimiza haja ya kunisakizia mie Mjinga. Lakini hata ivyo, kuna ubishi wenye faida ikiwa unataka kuweka SAWA mambo ya kukaririshwa kidini Maandiko.Husisingizie kua unajitenga na wabishi, si kweli, acha kulia-lia bali soma hoja zangu kisha onyesha wapi nimekosea au wapi wewe ndio hujui. Kung’ang’ana kua Injili itabaki palepale ni matamshi ya husia tu lakini hakuna maarifa/ufahamu uliyojaa pande zote. SASA NIFUATE TARATIBU KTK FAFANUZI ZANGU IZI KISHA PATA UFAHAMU NA MENGINE, JIBU MASWALI UKISAIDIWA NA LWEMBE.

  Maelezo 1: Agano la Kale Wanawake wanaonekana kufanya makubwa ya kuwaongoza Watu hata kupanga/Kushiriki mikakati ya Ukombozi wa Taifa kwa kujitoa muhanga mfano Esta-4:16-17. Agano Jipya pia tunawaona wakifanya mambo mbalimbali hata kumhudumia Yesu na mali zao-Luka.8:1-3. Ukisoma Biblia kwa mantiki ya kumtazama kiumbe mwanamke na positive role yake kuhusu Mungu pamoja/katikati ya Wanadamu utapata ukweli ulio wazi kua Wanawake wametumika na kutumiwa na Mungu sana kwa kufanya mengi mema hata kama madhaifu/mabaya yapo kama yalivyo mabaya tena makali kweli ya Wanaume

  Swali: Kutowaona Wanawake kama Makuhani kule AK na kutowaona kati ya Mitume 12 uku AJ-( bila shaka hakuna Mwanamke mwenye akili angependa kua Mtume ili tu Lwembe na Yusha wawe hoja zenye ufahamu wa upande 1 wa shilling bila kua na mwingine, halafu uyo Mwanamke Mtume akaishia kua Yuda!!!!!-kwa ivo fact ya Mtu kua au kutokua Mtume isifanywe dili saaana bali cha Ki Mungu hasa ni Mwamini Bwana awe Mkristo wa Kweli), na hata wakati wanahesabu watu waliohudhuria/Kufaidi baadhi ya baraka ktk Mikutano ya Yesu, Waandishi Wanaume, hawakua wana taja orodha ya Wanawake na Watoto-Mathayo.14:21, Je unataka kusema kua ilo ndio NENO LA MUNGU KWA VIZAZI VYOTE-Ujumbe toka Kiti cha Enzi ambao Roho Mt alihukusudia haswaa wasomaji tung’oke nao?

  Maelezo 2: Biblia inasema kua Yeye( Yesu) mwenyewe aliwatoa wengine kua Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu-Waefeso.4:11-12 na pia ktk 1Wakorinto.12:1-13-Inasema Roho Mtakatifu anagawa karama mbalimbali kwa KILA MMOJA kama apendavyo na kisha mstari 13 inasema hakuna huyu myahudi, Myunani, Mtumwa au Aliye huru( kwa mantiki hii bila kuvuruga maana ya mstari huu naongeza pia hakuna huyu mwanamke au mwanaume, amesoma hajasoma, anazo au maskini, mzungu au mwafrika, wa Dar au uko vijijini Babati, Ujiji KGM na Nyanzalaki Burundi) na hata Mdo.10:34-35-imeandikwa..Sasa natambua MUNGU HANA UPENDELEO ila ktk kila taifa YEYOTE akimcha, anakubaliwa!

  Swali: (a)Je Mungu kwa maana izo hapo juu, hawezi na wapi alipiga marufuku Mwanamke kutokua Mtume, Nabiii, Mwalimu nk wakati Yesu anasema aliwatoa wengine na wala hajasema aliwatoa WANAUME tu kua….?

  (b) Hamuoni kwamba kukazania kua, kwasababu tu ktk wale 12, Wanawake hawakuwemo wala kua Makuhani enzi zile kisha sisi wenyewe- tutafsiri kua ina maana Wanawake hawakuruhusiwa kua na huduma izo TOKA MBINGUNI, ni kukosa ufahamu wa kweli nyingine za Neno maana wakati mwingine kama si wote, ili kuhitimisha na kuibuka na maana/ujumbe na kua na uhakika kua hii hasa ndio message iliyokusudiwa toka kiti cha Enzi kwa vizazi vyote,ni LAZIMA KUANGALIA KAMA NENO HILI LA MUNGU TOKA HAPA LINAKUBALIANA NA KWELI NYINGINE TOKA PANDE ZILE(zingatia/unganisha na Maelezo no. 1 na swali lake pale juu)

  Maelezo.3: Kanisa limejengwa juu ya misingi ya Mitume na Manabii
  Maoni/Swali: Kama watu wa Mungu, wa rohoni, tukumbuke kua tunaweza fuata mifano ya Wanadamu wenzetu walio tutangulia na kufanya vema ktk mambo ya kiroho hata ya kimwili, lakini inapokuja swala la kiroho, yote tuyafuatayo ya Mitume na Manabii yatapimwa kwa kumwangalia the ONE and the ONE ONLY, the ONCE and for ALL Kiongozi wa Imani Yetu, Mwanaume Yesu Kristo. Unaposoma Biblia nakukuta watu kama akina Enock, Eliya, Paul, Musa, ni rahisi kibindamu ku-admire mpaka kupitilizia na hata kwa uwongo wa shetani au ufahamu mdogo wa Mtu ktk mambo ya Mungu au madhara ya dini/imani yake, umfanya kudhani hao walikua special wanadamu(super- humans) ndio maana ziko imani nyingine huwaabudu na kutukuza Watu hata kuwapa madaraja ya Utakatifu na kuwaona wao hawakua wanadamu kama mimi na wewe.

  Roho Mtakatifu aliliona ilo na kumsukuma Yakobo kuandika ili kuvunja iyo mitazano/ mafikra/ madhanio tu ya kibinadamu ktk Yakobo.5:17-18—anaanza kwa kusema Eliya( ambaye ukisoma habari zake, unaweza jiona kua u zero wewe kama hujui Neno na nafasi yako mbele za Mungu), alikua Mtu( Mwanadamu) mwenye nature kama sisi ( hapa manake asitishwe mtu wala sisi wenyewe tusikuze mambo kwa kumuingizia mtu u-speciality ambao hata yeye mwenyewe angekuwepo leo, angewaitia moto toka JUU huwafyatue pia), ila tofauti ni ndogo tu, aliomba kwa BIDII! basi-hamna cha ajabu kingine! Sasa kwa kua hawa walikua ni Watu tu lakini ambao hawakuishi mbinguni bali hapa hapa ktk mila na desturi na taratibu, ndio maana yako mambo ktk Biblia iyo iyo wanatofautiana ktk kuyaelezea na kuyasema. Biblia inaposema waliyonena waliyoongozwa na RM, haimaanishi Mungu alitumia wehu/mento/tahahira bali Watu kamili waliokua tofauti na uthibitisho ndio huo kwamba, yako mambo wanatofautiana! Mfano, Jinsi Yakobo alivyoongelea Imani na kua na Matendo au Matajiri na Maskini ni tofauti kabisa na Paul

  Mfano mwingine ni-Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 ..Wakamvua Yesu nguo na kumvika vazi JEKUNDU (scarlet robe) lakini Marco.15:15-17 hasa mstari 17..Wakamvika vazi la rangi ya ZAMBARAU (purple).Hapa waandishi ni wawili tofauti ila tukio lilelile lakini limesemwa tofauti ie rangi ya nguo zile. Ndio maana si dhambi wala kufuru tunaposoma Biblia kufahamu kua kuna human role! Kua hao walikua ni Watu waliondika, si robot. Vivyo ivyo hawa waandishi waliandika pia habari za WATU WENGINE si malaika, jinsi walivyoenenda na MUNGU na huduma ya Bwana. Hata hao Watu ktk Biblia wamejisema wazi kua kuna mambo wamesema SI ya Bwana bali ya wao tu kama Watu lakini wa Mungu—mfano 1Wakorinto.7:12, 25 Paul anasema MIMI na wala si BWANA, nasema….. na pia… ‘’Kwa habari ya wanawali, SINA amri ya Bwana lakini NATOA shauri LANGU…Kwakua kuna tofuti izo, ndio maana Paul mwenyewe ameshauri Watu wamfuate yeye( mfano wake) KAMA anavyo mfuata Kristo-1Wakorinto.11:1-focus hapa si Paul bali yule aliyesema mwenyewe Paul kua naye anamfuta na kama iyo hakueleweka, basi hi ni wazi zaidi Waefeso.5:1-‘’Mfuateni Mungu( be imitators of God) kama Watoto wapendwao. Kwa mantiki ya nilichosema hapo, NDIO TUMEJENGWA JUU YA MSINGI WA MANABII NA MITUME LAKINI HAWA WNATOFAUTI ZAO NDIO MAANA WAO WENYEWE Paul na Petro, wanatuelekeza siku zote ktk maandishi yao, MSINGI MKUU WENYEWE-YESU KRISTO

  Ivyo nikimwangalia Msingi mdogo mfano Paul na kujua kwa hakika ktk Bible, iko sehemu ya mwanadamu maana wamejisema wenyewe kama nilivyosema juu pale, basi hata haya maswala ya Wanawake kupigwa marufuku kusimama kanisani na kufundisha, HALIWEZI KUA NI NENO LA YEYE NIKO AMBAYE NIKO NA KWAMBA VIZAZI VYOTE PAST,PRESENT AND FUTURE, WAWAZUIE WANAWAKE! ILO LILIOKUA NENO LA MAONGOZI LA MTUMISHI WA MUNGU WA MAHALI PAMOJA KWA NYAKATI ZILE. Na kwa kua MSINGI MKUU mwenyewe hakuwahi kuonyesha hali iyo ya kuwazuia Wanawake, tunachukua nani sasa ktk ya Msingi Mkuu na mdogo? Kumbuka pia Roho Mtakatifu ambaye angekuja baadae na ndiye huyo aliyewavuvia Wote waliokuwepo na kuja baadae wakasema/kuandika ya Bwana kisha pia yao ila kwa yale ya YESU, BWANA ALISEMA RM, HASINGE NENA YA KWAKE KIVYAKE BALI ATATWAA YALIYO YA YESU NA KUWAAMBIA-ivyo KAMWE HAIWEZI KUA NI ROHO MTAKATIFU ALIYEPIGA MARUFUKU WANAWAKE KUFUNDISHA MAANA YESU-uko ROHO ANAKOTAKIWA KUCHUKUA YA KUONGEA, HAKUWAHI KUFANYA ICHO, hence aliyesema ivyo ni MTU(PAUL) kama kiongozi wa Makanisa na wakati husika na hali iliyokuwepo wakati huo. Kuelewa ivyo si kukufuru Neno na wala haiondoi ukweli kua bado nimeooka na nina Roho wa BWANA na nampenda Mungu na bado haimanishi kua Biblia si Neno la Mungu—-Ni NENO la MUNGU in general terms lakini ni ukweli pia ndani humo kuna ya Mungu, binadamu. Kukataa ufahamu huu ni sawa sawa na kusema YESU kisha ROHO MT waliwakatalia mbali Wanawake kufundisha! ilihali ni Roho huyo huyo ndio anawapa karama na huduma mbalimbali KILA MMOJA-bila kujali jinsia, rangi, elimu, umri. Kwakweli kama mpaka hapo, hamjaelewa, mna tatizo kubwa la kukariri Neno badala ya KUTAFAKARI NA KUELEWA!

  Press on.

 128. Kwanza nimefunzwa kujiepusha na watu wabishi,kama wewe ni mubishi baki na ubishi wako,ila ukweli unabaki pale pale,na Injili haiwezi badilika kamwe,kama vile Mungu habadiliki.1wakorintho 13:33“…kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifum”makanisa yote ya watakatifu hawana viongozi ao walimu wakike;na kama kanisa lako lina viongozi wakike yaani si kanisa la watakatifu ila la watakafujo(shetani)pili Waefeso 2:20“Mmejengwa juu ya msingi(mafundisho) wa mitume na manabii,naye Kristo Yesu ndiye mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”katika fundi la mitume hakuna kwenye mwanamke alionekana akiwa mwalimu ao kiongozi wa kanisa,na manabii nao hapakuonekanake kuhani mwanamke,mwalimu mku Yesu hakukuwaka na mtume mwanamke.sasa wapendwa tujifunze kwa nani?hivi biblia kitabu cha nani? 2Petro 1:21“Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na RM”semina ikiundwa kwa ajili ya wamama,mama mwenzao hajakosea kuwafunza sababu inahusu wanawake,ila semina ikilenga kanisa lote na apewe mwanaume usukani.kwa mwisho 1Wakorintho 14:37-38“Mtu akijiona kuwa ni nabii ao mtu wa rohoni,na ayatambue hayo ninayowaandikia,ya kwamba ni maagizo ya Bwana.38Lakini mtu akiwa mjinga,na awe mjinga.”Amina.

 129. Seleli acha fix!
  Wewe ulikwisha kubali halafu unageuka unaanza mambo ya kutuzungusha! Kiboko ya Mpinga Kristo ni Neno la Mungu katika ukamilifu wake pekee! Sasa, kama wewe huyo Mpinga Kristo amekwisha kutoa kwenye reli, unategemea nini tena, si ni lazima aendelee kukutumia! Ishu ilikwisha malizika kwa heshima na taadhima ya Maandiko, umerudi tena na ubishi wako wa siasa za dini!

  Si mmekubali wanawake wawe wachungaji wenu, wasubirini na mashoga, nao sasa hivi wanaendelea kuyateka makanisa, si umemsikia Papa alivyolainishwa, sasa wanaelekea huko kwenu, halafu ndio utakijua tunachokuambia, na usidhani eti utakimbia, si rahisi, utakuwa umekwisha pigwa locki ya kiroho!

  Halafu unanisingizia kuwa eti kuwa mimi nakubali kuhamisha mambo ya Torati niyavushe yaje huku kwenye Nchi Mpya! Wee! Kwani mimi ni Mgalatia? Sithubutu hata kidogo! Bali mimi huirejea Torati hapo ninapokutana na watu wa dini kama wewe ili kuibanisha kweli kutoka kwa School Master, na ukibahatika basi ikulete kwa Kristo, ukiwa jeuri nakuacha ufe nayo kama Wagalatia wa leo akina Siyi na wewe unayependa sana kuyavusha vusha mambo yaliyokufa!

  Halafu wewe uliwahi kuniambia kuwa Biblia ina maneno ya watu, ukanionesha na sehemu ambazo mtume Paulo anasema “hapa ni mimi na si Bwana”; labda nikuulize, hiyo “hapa ni mimi …” huwaga mnaiunganisha katika kila kifungu mnachotaka kukipindua? Maana sijaiona hiyo katika hivyo vifungu vinavyomkataza mwanamke! Au na ninyi ni wale waisilamu mlio ktk ukristo msiomkubali Paulo, ila mnazuga tu?

  Hebu iangalie argument yako hapa ilivyo ya kipagani:
  “”1Wakorintho 14:33“–Vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu, 34wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusu kunena bali watii’’= Nauliza ivi, muktadha wa pale ktk maandiko hayo na ilo Paul alilokua analisimika/panda/sisitiza hapo, umelizingatia kua ni strictly swala la kufundisha tu basi? Nauliza tu nielimishe ndugu Mwalimu Yusha””

  Yusha atakuwa ameshindwa kukujibu, maana yeye kama mwalimu, ametambua kuwa uwezo wako wakuyaelewa hayo ni mdogo sana, utakuwa umeyarukia tu mambo yasiyo saizi yako, maana kuna gumu gani hapo la kueleweka hata uhitaji mwalimu? Akufundishe nini, kusoma? Au akufundishe ubishi???

  Halafu ukairukia “”Tito 2:3-4, “wanawake wazee wawe na mwenendo mzuri, ili WAWAFUNZE wanawake vijana jinsi ya kuishi na waume na watoto wao(yaani wawafunze kupitia mwenendo wao)na si kufundisha kanisa’’= sasa kama wanaweza WAFUNZA wenzao kwa mwenendo na kusema/kufundisha(acha ujanja hapo Yusha), kwa nini Wasifundishe kanisani mfano, tukawaandalia wanawake wote kisha wao wakawa Wakufunzi wa seminar iyo? halafu kama wanaweza toa Unabii yaani wanapewa na RM karama ya unabii, wapi imeandikwa RM kamwe hatatoa karama/huduma ya Ufundishaji na Maongozi kwa kiumbe Mwanamke? Yaani sijui unajibuje haya..nitakung’ang’ania mpaka ujibu haya na mengine humu na yanayokuja, hakimbii mtu hapa wala visingizio kua wewe si msemaji sana!!!!!!!!!””

  Halafu bila ya aibu eti unauliza, “wapi imeandikwa RM kamwe hatatoa karama/huduma ya Ufundishaji na Maongozi kwa kiumbe Mwanamke?” Jamani! Hivi wewe unaelewaga mambo nje ya mahubiri ya kanisani kwenu kweli? Vifungu vyote hivyo ulivyovinukuu kutoka ktk Maandiko hivyo ambavyo Yusha amekuongozea hiyo sala ya toba unayoiruka sasa hivi, kwani amevinukuu kutoka magazeti ya udaku? Ah, lakini hauiamini hata Biblia yenyewe, umeibanjua banjua sana!! Hii ndiyo hasara ya kulikataa Neno la Mungu, anakunyang’anya mpaka ‘kidogo’ ulichonacho, angalia ulivyobaki na dini! Mungu ndiye aliyesema “Simpi ruhusa mwanamke…” usijidanganye kwa siasa za dini, kama Neno hili si la Mungu basi acheni kuvitumia vitabu vyoote vya Paulo, na mtaendelea kuvinyofoa kimoja kimoja, kwa kadiri mnavyoyakataa Maandiko mpaka mtaurudia upagani mlikotolewa!

  Kuhusu andiko hilo linalomkataza mwanamke kufundisha nimewahi kuwaulizeni, kulingana na uelewa wenu mnaoufundisha, na hamjanipa jibu bado, hebu nieleze basi Seleli kuhusu jambo hili la msingi, hapo tulipoanzia, inakuwaje?
  Niliwaulizeni hivi, iwapo huyo asiyepewa ruhusa ya kufundisha ni mke (Isha), yaani kumfundisha mumewe, ndipo ninakuuliza nawe Seleli, Je, mke huyo anaweza kuwafundisha na kuwatawala wanaume wengine? Ndipo mke huyo akiwa ni mchungaji, je, mumewe anaruhusiwa kuwa sehemu ya kusanyiko hilo?

  “Press on”, but not in the way of Hades!!!

  God bless u!

 130. Bwana Yesu Asifiwe,

  Mim nadhani jambo utofauti katika makanisa halianzi leo. Hili jambo lilianza wakati ya mitume na makanisa yale ya kwanza. Ndio maana katika Ufunuo tunaona Yoana akiambiwa aseme kwa kila kanisa maneno fulani. Na ukiyatazama utakuta yale yote hayafanane kwani makanisa hayakufanana angalao yaliongozwa na mitume. Nimeona shujaa watatu ndani ya mjadala huu, Mr Lwembe, Mr Yushu na Mr Sungura. Samahani kama wewe sikukutaja hapa, Mungu anakutazama. Ninapoona namna maelezo iko kweli yote inategemea Bible. Nafikiri mnapoandika maoni yenu ni kwamba msaidie watu wengi waone mbali. Shida ni kwamba mazungumzo mengi yanaelekea maneno ambayo Paulo ao Petro, ao …. waliyoyasema. Mim naomba nielewe: Neno linasema anaetegemea mwanaadamu na alaaniwe. Na kule ku agano la kale kulikuepo amri kumi za Mungu ambazo zingali zinasimama imara, na pembeni kulikuwa amri nyingi sana za Musa ambazo sisi tusio wayahudi ni vigumu sana kuzifwatilia. Sasa Mutuambie kikweli na mutuonyeshe neno halisi ya Yesu Kristo akikataza Mwanamke kufundisha ao akimruhusu, hapo labda tutaelewa. Na si kwa bure nimewataja, ni kwa sababu nimeona ninyi nyote mumesimama kwenye andiko, na shida imekuwa tu ni tafsiri. Na mambo hii wakati yanapelekwa ktk mjadala mwengine wa kuvaa suruali ao la, tunaona tu ni the same discussion. Ndio maana naomba msaada kwa niaba ya wote ambao wanachanganyikiwa kam mim, tupate neno Mungu (Yesu Kristo) alilotamka, sivyo wamoja watakuwa wa Kefa na wengina wa Paulo na wengine wa waraka fulani, na wengine kwa waraka ingine. Bila mwangaza hili jambo litahusu mila ya pahali………….

  Na Mungu wetu awabariki

 131. Yusha na Lwembe,

  Niliwasoma comments zenu zote muda sasa toka tu zinapoingia, nilipozi tu kuto-respond nione kama kuna jipya au mtu mwingine awasaidie lakini hawajajitokeza, sasa nninapenda nianze kwa kusema haya kwanza kisha nitawaletea wote wa wawili sasa maana mna tatizo linalofanana, yale maswali ambayo nimekua nikimwahidi Lwembe muda sasa toka tuanze debate hii.

  Umefurahi ivi na hata mimi nilipokujibu kwa uaminifu maswali yako yote, si kwamba sikujua ulitaka nini, umesema..‘’majibu yenyewe yote ni negative yaani mwanamke hakuonekana kokote kwa hali ya uongozi wakati wa Yesu na wa kanisa la kale=Majibu ni positive kwa kua ni kweli hakuonekana lakini iyo haimaanishi kua Mungu andio AMETAMKA/THIBITISHA KUA HAWAJAWAHI NA HAWAFAI/HAWAWEZI KAMWE…linganisha na Agano la Kale role yao uko, utashangaa, unachokifanya wewe ni kujiaminisha ili kukidhi matakwa ya ukariri wa BAADHI ya maandiko kama yalivyo bila kulinganisha na kweli za maandiko mengine in the same-same BIBLE

  Umesema kweli kabisa ivi..‘’nilitaka kusema hivi kanisa linajengwa juu ya mafundisho(msingi) ya mitume na manabii na Yesu mwenyewe ndiyo jiwe kuu(mwalimi mkuu)’’ .Nyongeza ni kua Misingi iyo ya Mitume na Manabii yote chini ya MSINGI MKUU YESU, HAIJAWAHI NA WALA HAITAKA IWE NA AGENDA YA KUWAONA WANAWAKE KUA HAWAWEZI KUFUNDISHA! MSINGI MKUU YESU MWENYEWE HAUJAWAHI SEMA/HATA GUSIA ILO NA HATA NAMNA ALIVYOWA-TREAT WANAWAKE SI KAMA YUSHA NA LWEMBE LEO

  Umesema kweli ivi ‘’kila andiko lenye kuwa katika biblia ni pumzi ya Mungu na lifaa kwa mafundisho,kuwaonya na kuwaongoza watakatifu’’.Tahadhari ni kwamba, usije chukua andiko moja ukaapaa nalo bila kuangalia maandiko mengine

  Umetoa angalizo lisilo na msingi hili..‘’uonapo mtu anaanza eti hili kasema Paulo,hili ni Luka ect..juwa huyo kapotoka na ni mpinga Kristo’’JIBU: Tafadhari soma post yangu ndefu MPAKA MWISHO, USIKIMBILIE KUJIBU TU HARAKA, soma ukiwa umetulia niliyomjibu Lwembe mwanzoni ktk mada hii hii! Usingeshangaa au kutoa angalizo kama ili ambalo ni kama la kiroho vile kumbe hamna lolote! Ktk maelezo yangu, nilifundisha kua Paul mwenyewe anasema ‘’ hapa nasema MIMI wala si BWANA’’ na pia nikasema Yesu mwenyewe final role model wetu anasema ‘MUSA aliwaambia ivyo …lakini toKa MWANZO(MUNGU ALIVYOPLAN/SEMA) HAIKUA IVYO’’.. pia nikasema Paul anamsema mwenziwe Petro kwa kusema…’’nikampinga Kefa maana….. na Petro naye anamsema Paul kua ‘’ndugu yetu Paul kapewa hekima na anasema/andika mambo magumu kuyaelewa’’ mifano ktk Bible ya ivi, mingi tu…Sasa unasema nini bwana Yusha? Upotofu na upinga Kristo uko wapi hapa maana si mimi niliyeanza kusema! Si unaona wapendwa sometimes tunatamka statements kuuubwa kuonyesha kuna ukiroho kweli lakini ukizi-examine kwa kuangalia kweli NYINGI/NYINGINE za Neno (nasisitiza kweli NYINGI/NYINGINE maana nakuonan una tatizo la kukariri kweli moja na kupaa nayo brother), izo statements zinakwishilia mbali na makao yake kati ya Wanadamu duniani, hutoweka moja kwa moja

  Umesema kweli ivi..‘’ikiwa wakati katika Agano la kale hapakua kuhani mwanamke’’=SWALI: UKWELI HUO WA AGANO LA KALE ni kati ya zile ZINAZOHAMA MOJA KWA MOJA KUJA LEO AGANO JIPYA? Lwembe unakumbuka ktk michango yangu, niliwahi sema kwa umakini kwa kutumia neno BAADHI ya kweli za Agano la Kale zimahama kama zilivyo maana hazijawahi kusimamishwa..eg Zaka, ulikataa, sasa unamwambiaje Yusha amaehamisha ili(ingawa uhamishaji huu kwa hili si kati ya yale nilisema BAADHI ya kweli), kumbe Lwembe mnajua ilo la BAADHI ya kweli zinahama siyo? Oo yes maana ume-support kila alichosema Yusha! Sasa kwa nini nilipofundisha ilo, ulipinga? Kwa iyo unakubali kua sometimes unashiriki mijadal si kwa kuachilia vitu vitamu, vyenye faida bali ni ‘’u-Simba na u-Yanga bad game?( ingawa u-Simba na u-Yanga good game, safi sana and lovely maana unaibua mengi mema)

  Umesema kweli ivi..‘’Yesu mwenyewe hakuchaguaka mtume mwanamke na hakuna mwanamke aliyeweza kuliongoza kanisa’’..SWALI: Kwa iyo? unataka kusema(ku-assume-assumption ile mbaya now) kua kwa iyo kwa ilo YESU ALITOA MESSAGE indirectly kua Wanawake hawafai/hawa-qualify/hawawezi kutwaa majukumu hayo? Plz confirm,hapana kwepa hii pia.

  Umeuliza‘’kwa nini leo kuwe viongozi wa makanisa?: Jibu: KWA NINI WASIWEPO? TENA KWA NINI RM ASIWAPE KARAMA/HUDUMA IYO NDANI YAO? WEWE ALIYEKUAMBIA RM YUKO LIMITED TU KUTOA KARAMA/HUDUMA/MWITO KWA WANAUME TU NANI? PAUL? USIMSINGIZIE HATA KIDOGO

  Umesema vema ivi ‘’mwanamke kukatazwa kufundisha si sheria ya mtu ila ya kanisa la kwanza 1Wakorintho 14:33“–Vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”34wanawake na wanyamanze katika kanisa, maana hawana ruhusu kunena bali watii’’= Nauliza ivi, muktadha wa pale ktk maandiko hayo na ilo Paul alilokua analisimika/panda/sisitiza hapo, umelizingatia kua ni strictly swala la kufundisha tu basi? Nauliza tu nielimishe ndugu Mwalimu Yusha

  Umekua tena na ufahamu mwema kidogo hapa kabla hujavuruga kwa kusema‘’‘’wanawake wana weza towa unabii,kuimba ect na si kufundisha ao kuwa wazee wa kanisa’’ HALAFU ukatoa mwenyewe andiko hili..Tito 2:3-4,wanawake wazee wawe na mwenendo mzuri,ili WAWAFUNZE wanawake vijana jinsi ya kuishi na waume na watoto wao(yaani wawafunze kupitia mwenendo wao)na si kufundisha kanisa’’= sasa kama wanaweza WAFUNZA wenzao kwa mwenendo na kusema/kufundisha(acha ujanja hapo Yusha), kwa nini Wasifundishe kanisani mfano, tukawaandalia wanawake wote kisha wao wakawa Wakufunzi wa seminar iyo? halafu kama wanaweza toa Unabii yaani wanapewa na RM karama ya unabii, wapi imeandikwa RM kamwe hatatoa karama/huduma ya Ufundishaji na Maongozi kwa kiumbe Mwanamke? Yaani sijui unajibuje haya..nitakung’ang’ania mpaka ujibu haya na mengine humu na yanayokuja, hakimbii mtu hapa wala visingizio kua wewe si msemaji sana!!!!!!!!!

  Umechachamaa ivi…‘’yaani ni marufuku kwa mwanamke kufundisha ao kuwa kiongozi wa kanisa na si Paulo ila desturi ya makanisa yote ya watakatifu 1wakorintho 14:33’’=Kwa iyo makanisa yote leo duniani ya Waliookoka na wana Roho Mtakatifu na Mungu anasema na kujidhiirisha yu kati yao ambamo pia kuna WANAWAKE AMBAO HAWAJAPIGWA MARUFUKU kufanya ya Bwana kuanzia ya madhabahuni mpaka ya uongozi, wanakwenda jehanum? Wamekosea sana, sana Neno? Wewe una akili,Roho, Ufunuo, Mjuzi wa Neno sana kuliko wao duniani kote uko kwa Wana wa Mungu wote siyo? Confirm plz! Si unaona sasa Yusha unavyohitaji kukaa chini ktk seminar!

  Umesema kwa kujiamini kua‘’mpango wa Mungu ni mwanamke atii,mingo miliyo nayo ya kuwafanya wanawake wawe walimu na viongozi wa makanisa si mapenzi ya Mungu ila mupango wa ROMA ulio fanyaka 28/02/1999,ulio shiriki makinisa 1000 na viongozi wa serikali 3000’’= Nauliza ivi, una uhakika kua ndio mpango wa Mungu kwa WANAWAKE huo tu basi? Upi ni mpango wa Mungu ktk utendaji na huduma mbalimbali? Una uhakika kua Mungu wa Mbinuni KAMWE Hawezi mfanya MWANAMKE kua kiongozi? Umesoma kweli Biblia yako wewe toka Agano la Kale? Ukishajijibu rohoni hayo au jibu hapa hadharani kama kweli u jasiri wewe na mjadili mada wa dhati na mwaminifu then NATAMKA HAPA KUIFUTA KAULI YAKO ILIYOPUNGUA MASHIKO NA KUKUREKEBISHA KUA KUTII NI MPANGO WA MUNGU KWA WANADAMU WOTE-na kwa kweli si mpango( hilo ni neno kubwa) sema/tuseme tu simply kua ni maagizo ya Mungu kwa wote na kwamba Wanawake wamekua Viongozi au la..soma mwenyewe Bible kisha lete jibu hapa

  Umetishia/tia hofu kua ni‘’njama za ibili zimeisha julikana na walio wakiroho wanaona’’= Nakwambia ivi Yusha kama Kua kwako rohoni unakosema uko, kunakupelekea kuona kua Paul alikataza wanawake wote duniani PAST,PRESENT AND FUTURE mpaka Yesu aje na kwamba lile lilikua neno la mbingu mpaka nchi Mungu Baba wa Mbinguni alimtuma Paul kulisema na kwamba si neno zuri tu la kimaongozi toka kwa kiongozi wa kiroho imara kabisa wa MAHALI HUSIKA NA KIPINDI HUSIKA KWA MAONO NA MSISITIZO WA AINA YA MTU(KIONGOZI HUSIKA) KULINGANA NA MAONO, MZIGO WA KAZI YA MUNGU ALIOKUA NAO NA KULE ALIPOTAKA SANA KUUPELEKA/KUUTILMILIZA TENA KTK AINA FULANI YA TAMADUNI NA DESTURI YA ULIMWENGU WA WAKATI WAKE, basi kiroho chako icho kitakua kinahitaji seminar tu na uponyaji tele utaingia maana Mtaijua/mtaifahamu KWELI nayo itawaweka HURU( kua huru ni pamoja na kua na akili, uelewa,maarifa BALANCED ya NENO NA MAMBO YA MUNGU KISHA KUTENDA na si kukariri/ririshwa tu

  Umejilinda(kuandaa mazingira ya kukimbia/kutojibu maswali/kutowajibika hapa kwa kauli na matamko yako kwa kusema ivi‘’mimi si msemaji sana ila ninabaki na ukweli nilio nao’’=NASEMA ACHA WOGA, FUNGUKA MPENDWA, KAMA UNAJAMBO LA KUSAIDIA AU HATA KUCHANGANYA AU USILOJUA, UMEKARIRI TU, VYOTE MWAGA HADHARANI HAPA, TUTASAIDIANA, KUKOSOANA, KUPONGEZANA, KUKUBALIANA,KUTOKUKUBALIANA ILA KWA HOJA, KUCHEKA NA KUFURAHI MAANA SISI SI MAWE HUMU NA PIA HATA KUCHEKANA! So haitusadii sana kujua ati wewe si msemaji! So what? Hapa ni plat form ya kufellowship kwa uhuru wote, so relax na as long as umeshaingia hapa, basi ni msemaji pia, wale wasiojitokeza hadharani, hao kweli tunaweza dhani kua si wasemaji, but wewe Yusha! Aaa bwanaa, mbona unatiririka vema tu sema kasoro uliyonayo ni iyo tu ya kukariri baadhi ya Maandiko KAMA YALIVYO LIVE hasa kuhusu Kukatazwa Wanawake ktk Makanisa husika.Pia kabla ya kubaki na ukweli ulio nao HAKIKISHA kama ukweli huo unakubaliana na KWEI nyingine NYINGI ktk Neno kuhusu Wanawake na role yao ktk Huduma,Kanisa na generally moyo wa Mungu kwao, usichoropoke tu na kweli moja…uko ni kukariri au ni kua kama wale wenzetu wa siku moja tu ya kuabudu kama maandiko yasemavyo wakati kweli nyingine kama tusifungwe na siku, miezi nk, huzi/hawazizingatii, je wataka kua mmoja wa hao wasio na Roho wa Uhuru na maarifa bali dini na kukariri/kumeza BAADHI kama yalivyo?

  Nilihitimisha majibu yangu kwa kukuambia strongly ivi: ‘’Jua kamwe MOYO WA MBINGUNI NA WAKAO HUKO, HAWANA NA HAWAJAWAHI KUDHARAU WANAWAKE WALA PAUL HASILAUMIWE AU KUCHUKULIWA KUA ALIHALALISHA KUWA-TREAT SECOND HAND WANAWAKE KTK MAMBO YA MUNGU NA UTUMISHI-iyo itakua inavuruga kweli nyingi za Bible toka Agano la Kale na Mpya hata na tabia za MWENYEWE Master kuwalekea hawa viumbe safi’’..NAKUTAKA TENA ZINGATIA ILO TENA, LIPE NAFASI NA UTAONA JINSI BIBLIA INAVYOFUNUKA POLEPOLE VEMA SANA KTK UFAHAMU WAKO, UKIWAONA WANAWAKE WALIOKUA MASHUJAA, VYOMBO MARIDADI KABISA KTK KUTUMIWA NA MUNGU KWA MAMBO MAKUBWA SI TU UFUNDISHAJI.NA KAMA MUNGU ANAWEZA WATUMIA KWA KIWANGO ICHO NA KWA MAMBO HAYO MAKUBWA, KWANINI AKILI YAKO ISIKUBALI KUA PIA HATA KUFUNDISHA, WANAWEZA? NA JE UNADHANI PAUL ALIKUA HALIJUI ILO? BILA SHAKA ALILIFAHAMU KABISA LAKINI KWA NINI ALIKATAZA? BILA SHAKA UTAELEWA KUA NI SITUATIONAL EVENT NA SI CROSS-CUT PHENOMENON.Halafu

  Wapendwa ndio maana nawa-challenge msiwe wavivu wa kufikiri na kusingizia eti kutumia akili hatari sana, embu fikiri ivi, Unadhani Wakati Paul anawaandikia ivyo au anatamka hayo, alikua ana maanisha ilo jambo liwe la kuzingatiwa kwa vizazi vyote, tamaduni zote na karne zote zijazo na kwa watakaookoka wote duniani kama yale aliyosema kuhusu Wokovu ktk mmoja tu Yesu Kristo na haki kwa Imani si matendo? Jamani embu muwe thinkers kidogo Watu wa Mungu, sisi tumebarikiwa ndani mpaka nje, kila kiungo kinahuishwa, tumieni hata Akili izo mnazosema hazitumiki ktk Kutafakari Neno la Mungu na mambo ya Mbinguni na Uuungu na Wanadamu! Kwa tafakari iyo nimewapa, kati ya Makatazo dhidi ya Wanawake Vs. Wokovu ktk Yesu tu na Haki kwa Imani si Matendo ya sheria, lipi mnadhani kwa Akili tu-usikimbilie ufunuo kwanza, Paul alijua na hata leo angefufuka, angekuambia, hili ni la vizazi vyote(cross cut) na hili ni la mahala husika(situational)? Jibuni Tafadhari…yaani hata akili tu zenu hapo zinawambia jibu SAHIHI KABISA wala si pepo kawatumia hata kidogo.

  Press on.

 132. Amina, Yusha!
  “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” (UFU. 22:11)
  Aimeeen!!!!!

 133. @Ck Lwembe nami nashukuru kukutana na watu ambao bado wakingali katika msimamo wa neno la Mungu bila ya kuyabadirisha,Watu lazima wabadirike ila injili ya Yesu kristo haiwezi badirika,Pia namshukuru RM ambaye hutufunulia ila za ibilisi kanisani kila kuchwapo na kutufanya imara kila siku.Cha muhimu 1Yohana 4:1“Wapenzi,msiiamini kila roho,bali zijaribuni hizo,kwamba zimetokana na Mungu;kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”na tunawatambua na kwa matendo(tafsiri)zao,1Wathesalinike 5:21“Jaribuni mambo yote;lishikeni lililo jema”La hatari catholic hupangia madhehebu mengi,wawe na viongozi na walimu wanawake ila wao hawana padri mwanamke na hata kufundisha hawafundishi.Watoto wa Mungu tuwe kama watu wa beroya.

  May God protect you all with the temptations of evil.
  Amin.

 134. @ Seleli,
  Unaniambia, “Umeamuru ivi.. ‘’Seleli na Sungura acheni kujizungusha, rudini kwenye mada, mjibuni Yusha!” hahahaha…! Kwa kweli inanibidi nikupongeze kwa ujasiri wako wa kuyajibu maswali ya Yusha kwa UAMINIFU, hongera sana!

  Basi niseme kwamba, kulingana na majibu uliyoyatoa baada ya mjadala mreeefu sana ukikazana kuyapinga Maandiko na kuyatafsiri unavyojua wewe, na hivyo kuwapoteza mabinti za Mungu wengi tu, ambao wanakuamini kuwa unaongozwa na RM, kwamba huku mwisho umewageuka na kukaa sawa, ukiwaacha huko maporini ulikowapeleka kwa tafsiri zako; Basi Toba yako na imfikie Bwana, ili hao uliowapoteza, Rehema ya Mungu iwafunike waione na NJIA ya kurudia!

  Usiwasahau washikaji mliokuwa nao katika kuipindisha Injili, warejeze nao!

  @ Yusha
  Ninapenda kusimama nawe, katika kiwango ulichoyarejea Maandiko na kwa Imani ukasimama kwayo dhidi ya hila ya uharibifu yenye kujenga jinsi ya kulipuuzisha Neno la Mungu kwa makusudi ya kuwaondoa waaminio katika Hofu ya Mungu, Ubarikiwe sana!

  Katika namna ya ajabu Maandiko hututimilia bila sisi kujua. Hebu litazame tena jibu lako, hilo lililoambatana na shukurani ya majibu ya Seleli, uliweke katika kioo cha Neno la Mungu: 2Kor 5:16,
  “Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.”
  Ndipo inaonekana kwamba, katika ulimwengu wa Roho, huko tulikokuwa tunayaongelea haya mambo, roho zimetambuana!! Angalia jinsi ulivyotamatisha jambo hili kwa ushahidi wa majibu ya maswali yaliyotokana na Maandiko kulingana na mtiririko mzima wa majadiliano:
  “uonapo mtu anaanza eti hili kasema Paulo, hili ni Luka ect.. juwa huyo kapotoka na ni mpinga kristo.”!!! Basi Maandiko hayo katika 2Kor 5:16 leo hii yametimia machoni petu!!

  Mbarikiwe nyoote mlioufikia Ujuzi wa KWELI hii!!

 135. Ninashukuru sana kwa majibu niliyo pewa,na majibu yenyewe yote ni negative yaani mwanamke hakuonekana kokote kwa hali ya uongozi wakati wa Yesu na wa kanisa la kale.nilitaka kusema hivi kanisa linajengwa juu ya mafundisho(msingi) ya mitume na manabii na Yesu mwenyewe ndiyo jiwe kuu(mwalimi mkuu) Waefeso 2:20,kwa hiyo is must kanisa la kristo kujinga juu ya msingi huo.kila andiko lenye kuwa katika biblia ni pumzi ya Mungu na lifaa kwa mafundisho,kuwaonya na kuwaongoza watakatifu;uonapo mtu anaanza eti hili kasema Paulo,hili ni Luka ect..juwa huyo kapotoka na ni mpinga kristo.ikiwa wakati katika agano la kale hapakua kuhani mwanamke na Yesu mwenyewe hakuchaguaka mtume mwanamke na hakuna mwanamke aliyeweza kuliongoza kanisa,kwa nini leo kuwe viongozi wa makanisa?hayo wameyatoa wapi?kama sio makristo wa uongo?mwanamke kukatazwa kufundisha si sheria ya mtu ila ya kanisa la kwanza 1Wakorintho 14:33“–Vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”34wanawake na wanyamanze katika kanisa,maana hawana ruhusu kunena bali watii…wanawake wana weza towa unabii,kuimba ect na si kufundisha ao kuwa wazee wa kanisa.Tito 2:3-4,wanawake wazee wawe na mwenendo mzuri,ili wawafunze wali wanawake vijana jinsi ya kuishi na waume na watoto wao(yaani wawafunze kupitia mwenendo wao)na si kufundisha kanisa.yaani ni marufuku kwa mwanamke kufundisha ao kuwa kiongozi wa kanisa na si Paulo ila desturi ya makanisa yote ya watakatifu 1wakorintho 14:33.na mupango wa Mungu ni mwanamke atii,mingo miliyo nayo ya kuwafanya wanawake wawe walimu na viongozi wa makanisa si mapenzi ya Mungu ila mupango wa ROMA ulio fanyaka 28/02/1999,ulio shiriki makinisa 1000 na viongozi wa serikali 3000,njama za ibili zimeisha julikana na walio wakiroho wanaona.
  Mungu awabariki,mimi si msemaji sana ila ninabaki na ukweli nilio nao. Amina.

 136. Lwembe,

  Umeshauri/amuru ivi.. ‘’Seleli na Sungura acheni kujizungusha, rudini kwenye mada, mjibuni Yusha!

  JIBU: mmh! umetoa wapi huu ujasiri wa kuamuru wengine kurudi kwenye mada? U KNOW EXACTLY WHAT I MEAN! See tulishasema ktk mijadala, by the ways zipo tu as long as tunazi-clear then back to major issue tabled au haya ni maono mapya! Pia nimeshakujibu post yako kwa ‘zigo’ ilo kubwa…nukta kwa nukta, hakuna hoja/tashwishi/doubt yoyote niliyokwepa ivyo nimetende haki kwa post yako, wewe umetoa wapi ujasiri wakati hujasema kitu kwa yangu au ndio evalution aliyomaanisha Yusha kua mada inakwenda mwisho nini-(which is good) so kama umeelewa yaishe, kama bado yaanze-mind u, yawe bado kweli otherwise kupuuza kujibu kwa mantiki hii ni sawa-lakin hii isimaanishe/kutoa mwanya kwa ujanja wa kuacha maswali tu kiholela kukwepa kujijibu/kujibiwa/kuvunja nguvu ya hoja isiyo ya kweli(maana hoja nzuri/kitu kizuri lazima kiishi na kiwe appreciated).

  Press on

 137. Yusha,

  Umesema, ‘’I see maada karibu kwisha’’, ni kweli LAKINI UKWELI KABISA NI KWAMBA IMEKWISHA labda Lwembe asema jambo LA MSINGI baada ya kusoma michango mingi na ule ‘mzigo’ ie post kubwa niliyomtumia kujibu/clear kila nukta na chembe aliyo-raise. Namsubiri aseme ameridhika na kubarikiwa na kwamba hawezi penya tena msitu huo wa hoja kwa HOJA na si tu arimradi kasema kitu au akakokomaa and yet bado ukikomaa naye, anachuja au anaanza kufyatuka yoyote tu sasa e.g. ‘666 asante thing’, kwa ivyo, ngoja tusubiri kidogo

  INGAWA SIJAJUA NIA YAKO AMBAYO ITAKUA PEUPE TU VERY SOON IVYO KUSHUGHULIKIWA PIA but kwa iki kipande umesema vema sana..’’kuanzia kwa mitume hadi kwetu sote tunajifunza kwa Yesu Kristo na si kwa mtu yeyote“lazima tujifunze kwa Yesu”na Roho mtakatifu ndiye mwalimu’’, Ila tuweke balansi kua tunaweza jifunza hata kwa wengine mfano Paul, Peter, Ubrahimu, mimi, wewe lakini mwisho wa siku, wa mwisho ni mmoja tu, alfa and omega, wakati mengine yote ya wengine wote yanaposemwa/fanywa lazima YAMULIKIKE/YAMULIKWE/YANUNURISHWE KWA KUANGALIA /ZINGATIA MWENYEWE ALIFANYAJE/SEMAJE/ISHIJE/TENDAJE na ili kulenga kabisa mada ya mezani-ALIKUA NA TABIA GANI DHIDI YA WANAWAKE..huyo ndiye nilimwambia Lwembe point rahisi kabisa kuelewa kua ONCE AND FOR FINAL ROLE MODEL WETU NI MASTER MWENYEWE, full stop, period! Lakini hii haimanishi kua tukifanya KITU TOFAUTI NA ALIYOFANYA/SEMA-KWA MAANA NZURI-nasisitiza-kwa maana nzuri( hapa nabana kabisa kupata mpenyo wa kuingiza hoja weak), itakua dhambi au kufuru, as long as icho tukifanyacho ambacho Yeye hakufanya, hakivunji Neno, akivurugi kanuni za Mungu na uumbaji wake na jinsi anavyohusiana na Watu vizazi vyote, hakivurugi moyo wenyewe wa Yesu kuwaelekea Wanadamu wote( hapa naziba kotekote-hakuna kupumua hapo-kusaka mianya ya kuingiza mawazo yenye fikra dhaifu kihoja kudhani kwakua Yesu ni ONCE FOR ALL FINAL ROLE MODEL KAMA TULIVYOSEMA NA KWA KUA HAKUCHAGUA WANAWAKE KTK WALE 12, BASI NASI TUACHE/TUSIWATUMIE! Mwe! Mmh! too weak si ndio maana uko mbele TUNAMUONA YEYE MWENYEWE NA MOYO WAKE, MAHUSIANO YAKE, TABIA ZAKE KUWAELEKEA WANADAMU MUHIMU SANA HAWA CHINI YA JUA- THE WONDERFUL WOMEN). Kubadilisha KWELI NZITO HII AMBAYO NGUMU HASA KUIKANA, ni kuleta ufahamu wa kidini kwa kuhamisha MOJA KWA MOJA ALOSEMA PAUL KWA WANAWAKE on specifics yeye kama Kiongozi wa mahala kwa kipindi chake na kwa kusema hivyo, haimaanishi kuwadharau akina Paul atakaye elewa ivyo, ni mwenye makusudi tu, hamna lolote!

  Umeuliza Maswali mengi kidogo kama ifuatavyo na majibu yake simple ni kama ifuatavyo:

  SWALI: Wakati anachagua mitume12 mulikuaka wanawake kati yao?
  JIBU: Wanawake hawakuwamo

  SWALI:Ikiwa walikuepo ni akina nani?
  JINA: Hawakuwepo ivyo hakuna majina

  SWALI: Na ikiwa hawakuepo ni kwa nini?
  JIBU: Sijui maana Biblia nayo haijasema wala kuona iyo ni issue ya kimbingu kuuuuuubwaaaa kabisa kuisemelea ili isivuruge maandiko/kweli nyingine nyingi za MSINGi za Mungu na NENO lake kwetu sisi leo(zingatia aka eee..’’kweti sisi LEO’’- hakuna room ya dini kuingizwa hapa, naziba kotekote lakini kwa hoja si ilimradi-ukitaka kujua nguvu yake-ipinge kwa kuleta hoja nawe pia, tuone ipi ina mashiko)

  SWALI: Wakati RM kashuka(siku ya pentecost)Je kuliwezaka ibuka mitume wa kike(wanawake)?
  JIBU: Hawakuibuka maana Bible haionyeshi wazi wazi

  SWALI:Kama wapo nijulisheni.
  JIBU: Hawapo

  SWALI:Nipeni andiko linalo shuhudia safari moja ya injili ya mwanamke.
  JIBU: Halipo

  Haya baada ya kuyajibu maswali yako yote bila kuyakimbia/kuafunika, unadhani unataka sema/hitimisha nini kuhusu Wanawake kwenye Utumishi, Kanisani na Makatazo? JIBU PIA NAKUSUBIRI

  Pia umetoa andiko ili…Tito 2:3-5 wanawake wazee wawe na mwenendo wa utakatifu,ili wawafunze,wawatie wanawake vijana akili,na si ili walifunze kanisa. Nakuuliza kidogo kua ulikusudia kusema nini hasa kwa andiko ilo ukizingatia hoja mezani? Karibu ujibu hapo kwanza ndipo ramani iwe wazi
  SWALI: Ulipolitoa/share ulikusudia nini? what are you trying to say? SEMA HAPA WAZIWAZI ILI TUSHUGULIKE..plz naomba iyo tenda mara moja-sema wazi.

  Press on ukijua kamwe MOYO WA MBINGUNI NA WAKAO HUKO, HAWANA NA HAWAJAWAHI KUDHARAU WANAWAKE WALA PAUL HASILAUMIWE AU KUCHUKULIWA KUA ALIHALALISHA KUWA-TREAT SECOND HAND WANAWAKE KTK MAMBO YA MUNGU NA UTUMISHI-iyo itakua inavuruga kweli nyingi za Bible toka Agano la Kale na Mpya hata na tabia za MWENYEWE Maste kuwalekea hawa viumbe safi. Bila shaka kwa hitimisho ili, unaweza nusa(lwembe mjamja, alisha nusa ndio maana amechochea eti tujibu maswali yako), moto wake/hoja barabara zilivyo, ukijaribu kuleta mafundisho ya Mtu na dini yake kinyume na Misingi/KWELI nyingiiiii/zooooote za NENO

 138. Sungura,

  Uliniomba nikutafsirie paragraph moja hapa kwa Kiswahili,nimefanya ivyo chini hapo na nyongeza ya mambo mengine ili kuhitimisha all by the ways na tubaki/tumalizie hoja mezani, nadhani yote hapo chini yasichukue space sana ukizingatia hoja tuliyonayo ambayo mpaka sasa Lwembe ameshindwa kabisa kuchomoka/ hajajibu post yangu mpaka sasa ili nimalizie my participation ktk debate hii kuhusu makatazo dhidi ya Wanawake kwa kumletea maswali mazito kuhusu Wanawake na role yao ktk Bwana, ili kama kweli na ubavu wa hoja, ajibu na kisha tutajua yeye na Mungu nani yuko sawa kuhusu Wanawake na Kingdom yake Bwana ambao Lwembe anataka kanisani umo wakae tu kama boxes, wakiwa hawana vitu vya KiMungu.

  Uliomba nisaidie kuitafsiri comment yangu kwa Kiswahili ili unikujibu vema-da! unanipa kazi kweli, mimi maswali yangu,unafukia, kisa hamna cha kujibu-! Mh! nikuulize kitu kweli halafu useme sijauliza!!!!!!!!!!!! Mmmh! Sungura bwana uko kama jina lako Kaka, kweli majina bwana yana nguvu-tehe! Aya nimetafsri iyo uloniomba ivi……

  ORIGANL=’’You claims to be ‘Makini’ man are nt you?What are you waiting then? Until you show your ‘so called Biblical contextualization RIGHT HERE, will consider this as baseless claim. I can ensure you, I know the context part of the scriptures and also the Spiritual part ( rhema if you like-do u know it anyway? when context is thrown?), there is a time we stick on the context only but also we are not deadly religious believers! We can also, by the Holy Spirit, go to another dimension yet within the Word’s limits.”

  TAFSIRI=Unaj….(Kiswahili cha ‘claim’ si cha kirafiki sana,tafadhari jitafsirie ingawa najua ungekua wewe hapo, ungefyatuka tu/ungetema cheche tu zile alisema Lwembe kua mnililetwa kuniadhibu mie- tehe! Lwembe bwana na assumptions zenye hazina mashiko…kazi kweli)….kua mtu makini, si ndivyo? Unasubiri nini? Ni mpaka utakapodhihirisha iyo…’’Biblical contextualization’’ yako( hii tafsiri mwenyewe maana ndio wewe uliisema kwanza) hapa haswaa, nitachukulia ulilo niambia kama jambo lisilokua na msingi. Ninakuhakikishia, nafahamu muktadha wa maandiko na pia sehemu ya kiroho chake( yaani rhema kama unapenda-je waifahamu hata ivyo? kitu ambacho utupa nje/uvuka mazingatio ya muktadha? Uko wakati tutajikita katika muktadha tu lakini pia sisi si watu/waamini wa dini mfu! tunaweza, kwa msaada ya Roho Mtakatifu, kwenda ktk kiwango kingine lakini tukabaki ktk mipaka ya Neno’’..

  Najua u msaulifu wa vitu vingi Sungura hasa vyangu ingawa vyako ungependa sana kila mtu akumbuke na kuvisoma milele hata kama vina uu-mtu zaidi kuliko Kanisa au kirafiki niseme huna ile ‘anointing’ ya nukta kwa nukta. Nilikujibu ivyo juu hapo baada ya wewe kusema haya hapo chini kuhusu mie.Uliyosema/nidozi ni…’’

  ‘’Seleli I’m not worrying with but rather worrying about, you are paying heavy emphasis to pet and trivial issues.Are you a teenager in such debates like this,or you zoomed in on this discussion thinking that the only true answers are those analyzed by you?For your information Seleli if we were here to criticize ourselves I could have told you long time ago that most of your opinions are quite biblical concepts which lack biblical contextualization at large.And since you don’t know that you don’t know, you are just being religiously naive, and that’s why you think whatever u speak here is of biblical substance, thus it has to be esteemed by every one.

  Nathani ulisem hayo ya juu, ukiwa unajibu sehemu ya majibu yangu hii hapa’’Umenishauli ivi-‘’Na wewe Seleli usiwe mtu wa kulalamika sana na kuhamishwa kwenye hoja ili kuanza kujibu mashambulizi binafsi. Mambo mengine yapuuze ili uendelee kuchangia hoja ya msingi’’. HUJANISOMA TU ILA UTANIPATA TU TUNAVYOENDELEA HAPA, SO SINA HAJA YA KULALAMIKA! KWANINI KWANZA NILALAMIKE, KUNA KITU GANI CHA KULALAMIKA HAPA!!!! Aaa bwanaa Sungura, these things are cheap and common in talks, UME-INTERPRETE MY WAYS WRONGLY. NAHAKUHAKIKISHIA HAKUNA HATA MMOJA INCLUDING WEWE, ANAYEWEZA NITOA KWA HOJA-in the sense kunipoteza kabisaaaa! Never! NIKIONEKANA NIMETOKA, NINA SABABU NZURI TU KISHA NIKIRUDI, UKO NILIKOKWENDA NIMEMALIZA KAZI-ikubalike au ikataliwe lakini mioyoni/akilini mwao uko nilikokwenda temporarily, wanajua tu kilichofanyika na hatimaye tunaweza kutana uku niliporudi, then we can go on with sweet business-though anytime when business changes from sweetness to bitterness( Gods Word/Church Biblical) doctrine/Utumishi/Born Again’s all Together Cores kuvurugwa), ‘anointing’ ya kupaa kuligeukia ilo, iko tu unspeakably very ready, so usiwe na wasi hata kidogo,I know both tennis and footballs, don’t worry with me kabisa, help/advise others e.g. Kaswahili and well, sometimes yourself man-YOU KNOW WHAT EXACTLY I MEAN.

  Kisha ulijitetea na kuniambia..’’Have a look at what you corrected me here’’, I quote you:‘’Hii statement yako,’’Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako na Seleli yameshatoka kwenye hoja msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za ninyi kushambuliana kwa maneno’’ rekebisha isomeka ivi.. ’’Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako KWA Seleli yameshatoka kwenye hoja ya msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za WEWE( Lwembe) kushambuliA kwa maneno YASIYOKUA NA MASHIKO/HAYA- SUBSTANTIATE CLAIMS ZAKO(Lwembe) TO OUTSMART hoja za Seleli.

  Kisha ukanitaka iki= To’’Reread your statement to see if I were wrong grammatically semantically’’= JIBU: NILIKUREKEBISHA-zingati marekebisho yangu kila kila inputs nikitaka usinijumuishe mie na Lwembe ktk ilo ulosema bali liwe ni Lwembe analofanya/nifanyia mie! Ivyo tu yet u missed the point why niliingiza marekebisho hayo, ukajitetea kua ulikua sahihi semantically and grammatically!- kumbe mie nilikua na nala kwangu neno hapo- najitenga na inclusion yako kua mimi sifanyi kama anavyofanya Lwembe kama ulivyosema. Umeelewa na kuona sasa why nilikurekebisha? I easily hope so.

  Mwisho ni ya ‘’666 Asante asante’’, umesema nikusaidie maana naonekana nimeelewa alivyosema ivyo Lwembe. Ni kweli nimeelewa na hata nikakuambia wewe tu ndio mgeni ktk ilo, sikua na maana ya kusupport alichosema bali nilisema ivyo kwa kua hiyo ilikua ni moja wapo wa mada iliwahi kua discussed mwaka juzi forum nyingine ya SG ndio uko Lwembe akaingizanga mzaha huo-mada ilikuja kama swali tu likiwa na lengo la kuyapitia kwa upya yale tunayofanyaga kila mara kama ni Biblical au ni man-made yet mema tu maana si kila man-made jambo la kiroho ni pepo! Umeelewa sasa? ni ishu ya zamani and haina umuhimu kwa hapa basi tu Lwembe alichomekea baada ya kuzidiwa na hoja zangu kuhusu Mafundisho kuhusu Wanawake-si unajua mtu akibanwa, anafyatuka lolote! Naona ana copy na kupaste toka kwa jamaaa mmoja huku huku, hapa hapa!

  Press on.

 139. Lwembe pengine nikiri tu kwamba, inawezekana kweli sikukuelewa, na hata sasa sijakuelewa bado ulichokuwa unamwambia Seleli katika hii sentensi:

  ”.. ndipo ninapojua kuwa wewe ulifuatisha tu sala ya toba uliyoongozwa na pastor wako, kisha Mungu akakupa ‘roho mpya’ kwa huo uaminifu wako, ambayo kwayo ulinena zile “Asante Yesu” x 666, bali hukuirudisha nafsi yako katika Maandiko ili kujifunza zaidi upate kuvishwa ile Taji, yaani RM!”

  Lakini pia Seleli anaweza kunisaidia kujua ulikuwa unamaanisha nini, maana kaonesha kuwa ameelewa. Namnukuu pia ” Iyo 666 Lwembe alishaonywa mara kadhaa, hapa siyo mwanzo na wewe hujui imetokea wapi, mie najua na Lwembe anafahamu namaanisha nini hapa”

  Mimi sioni shida kukiri, ikiwa nili-misinterprete !!

  Asante!

 140. Samahani Seleli, naomba unisaidie kuitafsiri hii comment yako kwa Kiswahili ili nikujibu vema. Hii hapa

  ”Sungura,

  You claims to be ‘Makini’ man are nt you?What are you waiting then? Until you show your ‘so called Biblical contextualization RIGHT HERE,will consider this as baseless claim. I can ensure you, I know the context part of the scriptures and also the Spiritual part ( rhema if you like-do u know it anyway? when context is thrown?), there is a time we stick on the context only but also we are not deadly religious believers! We can also, by the Holy Spirit, go to another dimension yet within the Word’s limits.”

  Asante.

 141. Wapendwa, kumbe ndivyo mlivyo, mwenzenu akiondoka, nyuma yake mnaanza kumchonganisha! Sungura acha uchonganishi, ni wapi mimi nilisema Seleli amejazwa RM kwa hizo “Asante Yesu” x 666? Nakunukuu:
  “”Lwembe kakwambia kuwa ulijazwa Roho mt. kwa kusema asante Yesu x 666, nikamwambia siyo sawa kukuambia hivyo, maana kusema hivyo ni kufuru mbele za Mungu. Namba 666 wote tunaielewa maana yake ni nini, sasa kuihusisha na ujazo wa Roho mt. kwa mtu ni kuandika bila kuwa na kiasi.””

  Hili ndilo tatizo la kutumia akili, mara nyingi wanaotumia akili they get carried away by their sentiments, halafu wanaziunga kuwa its what God taught! Huu nimfano mzuri sana kama unaweza kujifunza, ulipokopy na kupaste nilichomwambia Seleli, ulikopi sawa sawa, bali mbele huko umekitafsiri kwa akili yako kama mnavyoyatafsiri maelezo ya mt Paulo kwa akili zenu! Angalia hiki ulichokopi na kupaste:
  “””…. kisha Mungu akakupa ‘roho mpya’ kwa huo uaminifu wako, ambayo kwayo ulinena zile “Asante Yesu” x 666,..”
  Je, haya maelezo ni sawa na huo uchonganishi unaoufanya, oblivious to my stated fact?

  Kama Seleli alijazwa RM kwa hizo “Asante Yesu”, na mt Paulo alijazwa nini? Unaziona akili zinapokwamia? Hazikawii kujilock! Mimi nimesema huyo alipewa ‘roho mpya’ nalo jambo hilo ni kulingana na Programu ya Wokovu, iwapo utazitambua hatua unazopitia. Maana si kwamba jambo la Wokovu limekurupuka tu, lilipangwa toka huko nyuma, unaanza kwa kutolewa hilo limoyo la jiwe, hilo lisilo amini kwamba Biblia ni Neno la Mungu, na kuwekewa moyo mpya wa nyama, kisha unapewa roho mpya, na mwisho ndipo unajazwa RM! Eze 36:26-27 “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.” Huo ndio utaratibu aliouweka Mungu, na kutabiriwa miaka 800 kabla ya Kristo, na unatimia katika ujio wa Kristo! RM siyo jambo la mzaha kama mnavyotaka kulifanya, RM ni Mungu ndani yako akikuongoza na si makelele yasiyoeleweka! Lah, kweli Mungu atusaidie!!!

  Halafu unalalamika bila kulitafiti jambo, hivi kama hulijui jambo kuna shida gani kuuliza, muulize Seleli hivi unairudia hiyo “Asante Yesu” mara ngapi mpaka ujazwe? Haiwezi kuzidi mara 666 maana hiyo ndiyo namba ya mwanadamu, kama unayo ‘understanding’! Rev 13:18 “…for it is the number of a man; and his number is Six hundred threescore and six.” Basi ni vizuri ukafahamu kwamba sikukosea katika kauli yangu, bali nilijua kwenu ninyi mliolikataa Neno la Mungu, naye akiwa amewafungia milango ya Ufunuo kwa kuthamini kwenu akili zenu, mtayaelewa haya katika kiwango hicho unachokilalamikia na kunichonganisha na wote wanao amini katika hizo “Asante Yesu” x 666, kuwa ndiko kujazwa RM, kulingana na mafundisho ya makanisa yao ambayo wao huamini kwamba ndilo Neno la Mungu!

  Nimewiwa kuliweka sawa hilo tu,
  Thanx, Sungura!

 142. Sungura,

  Mmh! aaa wapi kaka! Hotuba ya Nyerere hainuhusu kabisaa lakini acha nifurahi tu maana wakati Kaswahili aliponiambia/nikacheka sana kua ninaahitaji ambulance, unakumbuka ulishangilije? Tena ukakimenya na Kiingereza…’’there u are’-ukafurahi mwenyewe! Ukasindikizia kua nau nyemelea uPasteri! Sasa unataka kunizuia nisifurahi mie pia, mwe! au we afande mpendwa? Haha! Unaona sasa nakuona hapo unavyoshusha pumzi! Ulisahau kabisaa mshangiliaji wa kwanza ni wewe na mie nime..CUT na Kupaste yako.

  Lakini kaukweli Kanauma, kapo kwa kauli za Lwembe pamoja na mambo yake ya kudharau Wanawake kutotumiwa na MUNGU kanisani. Kilichonishangaza wakati mie nakuandikia hatukuwasilina naye, nafungua nione updates ktk pande hi, nakuta almost the same kakuambia, hapo upati msg kaka! si unaona hapo Hotuba ya Mkuu hainihusu! aaa bwana, tuvitu vingine utakubali na yanaisha, ukivi-raise, vinavutia nije! Halafu si unaona ulivyojibu kwa mfano wa Hotuba, umethibitisha Lwembe yuko sawa? Aya jihukumu mwenyewe. Alikuambia uchache wa maneno lazima uwe na kitu nani? Sa nyingine ni ushalo tu wa mambo basi, si kweli maneno mengi hayana point! Unaweza tiririka toka nukta mpaka mwisho ni upako full. Iyo 666 Lwembe alishaonywa mara kadhaa, hapa siyo mwanzo na wewe hujui imetokea wapi, mie najua na Lwembe anafahamu namaanisha nini hapa! Si sijamunga mkono na wewe si muonyaji wa kwanza kwa hili kwa Lwembe, muulize atakupa ushuuda, wewe tu ndio mgeni kwalo! Ila na wewe ndugu yangu, msahaulifu kweli, mwenzio nina upako wa nukta kwa nukta! Ooh! Umesahau kabisa kua ni wewe ulinikataza kutotaja majina kwa mafumbo, sasa ninanukuu live, umekuja na jingine! Mh! we kiboko brother! Umenichekesha kweli kua Kaswahili ameninyima usingizi! Haha Brother a u serious? Come on..that cheap brother on making senses here! No way. You too now knows your technical mistake! Remember my parable’’MTU AKIWA AMEVAA SURUALI, UKAMWAMBIA ANA KAPUTURA, NANI ANA TATIZO KUBWA? Ayaa jibu unalo!

  Hii nimeipenda…. ‘’Ukiona harage linakimbilia juu hizo ni dalili za kuiva’’ Haaha, Great idea! So who this harage linapanda? Lwembe? Ops! No..Exactly..You! (me exclusive completely). Sasa wimbo wako wa kila mara ..’uwe makini’…iyo weka pending kwanza, tupige kazi hapa, ngoja nisubiri Lwembe anachomokaje ktk majibu yangu kupinga mambo mambo yake ya dini dhidi ya Wanawake Jeshi kubwa la Bwana

  Press on.

 143. Edwin u mtu wa ajabu sana, mchangao wako hapa ulikuwa unamjibu Lwembe, lakini mbona jina la Sungura na Kaswahili hayaishi maandishini mwako? Wamekutibua sana eh, au ulidhani mawazo yako ni msahafu kwamba kila mtu atayashangilia tu na kuyapigia makofi?

  Kwanza wala mimi sipingani na wewe katika suala zima la nafasi ya mwanamke katika mwili wa kristo. Kinachonishangaza tu ni kwamba hauishi kunitaja. Unang’ang’aniza kuleta huku hoja za suala la zaka ambalo mimi na wewe ndo tumetofautiana kimtazamo.

  Lwembe kakwambia kuwa ulijazwa Roho mt. kwa kusema asante Yesu x 666, nikamwambia siyo sawa kukuambia hivyo,maana kusema hivyo ni kufuru mbele za Mungu. Namba 666 wote tunaielewa maana yake ni nini, sasa kuihusisha na ujazo wa Roho mt. kwa mtu ni kuandika bila kuwa na kiasi.

  Lakini Seleli hata hilo hujaliona umebaki kushangilia tu yale ambayo unadhani Lwembe alikuwa anampasha Sungura na Kaswahili. Umechelewa ndg yangu.
  Nakufananisha sasa na watu waliosemwa na Nyerere kwenye moja ya hotuba zake akiwaambia baadhi ya viongozi, kwamba katika utawala wake kwa kuwa yeye hakuwa malaika alifanya mambo mema na mengine ya kipumbavu. Cha ajabu wao wanaacha yale mema na kushangilia yale ya kipumbavu.

  Kuwa makini Seleli, usiwe kama hao viongozi tafadhali.
  Lakini pia ni ukweli usiopingika kuwa Kaswahili na Sungura wamekunyima usingizi kiasi kwamba ukipata mtu anajaribu kukusaidia kuwashambulia unapata ahueni ndio maana unashangilia sana.

  Hatushangilii wingi wa maneno, bali tunashangilia ukweli wa maudhui hata kama ni wa maneno machache.

  Ukiona harage linakimbilia juu hizo ni dalili za kuiva.

  Asante

 144. Ninashukuru sana kwa walimu wetu walio changia ili kujaribu kutuweka sawa na I see maada karibu kwisha;kuanzia kwa mitume hadi kwetu sote tunajifunza kwa Yesu Kristo na si kwa mtu yeyote“lazima tujifunze kwa Yesu”na Roho mtakatifu ndiye mwalimu.sasa ninaswali kwa walimu wetu;wakati anachugua mitume12 mulikuaka wanawake kati yao?ikiwa walikuepo ni akina nani?na ikiwa hawakuepo ni kwa nini?pili kisha RM kushuka(siku ya pentecost)Je kuliwezaka ibuka mitume wa kike(wanawake)?kama wapo nijulisheni.Tito 2:3-5 wanawake wazee wawe na mwenendo wa utakatifu,ili wawafunze,wawatie wanawake vijana akili,na si ili walifunze kanisa.kwa mwisho nipeni andiko linalo shuhudia safari moja ya injili ya mwanamke.Asanteni my God be with u all.

 145. Sungura,

  You claims to be ‘Makini’ man are nt you?What are you waiting then? Until you show your ‘so called Biblical contextualization RIGHT HERE,will consider this as baseless claim. I can ensure you, I know the context part of the scriptures and also the Spiritual part ( rhema if you like-do u know it anyway? when context is thrown?), there is a time we stick on the context only but also we are not deadly religious believers! We can also, by the Holy Spirit, go to another dimension yet within the Word’s limits.

  Press on,

 146. Lwembe

  Mbona unaga kwa heri wakati umeacha ‘’very suffocating dust brother? Is it fair for your readers? Hapana, ungoje hapo hapo kwanza ili tusaidiane kuondoa hii vumbi nzito. Be patient, usome kwanza clearance then aga kwa amani. Kwakua umemjibu vema kabisa Sungura kua Isaya ameandika vitabu 66( nimecheka kweli Lwembe na maneno yako brother) basi karibu usome probably 99 books below, unaweza soma ukiwa home usiku au week-end si lazima at per ili ku-eliminate completely mambo ya sijui ‘ndeeefu/ saaana syndrome !!!!!!!

  Usisahau kua tuko ktk hoja ya Makatazo dhidi ya Wanawake( Tafsiri mbaya ya Maandiko) na ninakutumia Maswali baada ya hii, ifike mahali tuache kuwapuuza Wanawake! on serious note mbele za Mungu tuko sawa and so it is with Utumishi, karama, huduma, RM anaweza mtumia au call ANY ktk Utumishi regardless of gender. Kwanza nijibu baadhi ya hoja zako ktk post zako 2 kwa mpigo kama ifuatavyo.

  Unasema’’uilitegemea ningekuonesha angalau kitabu kimoja ndani ya Biblia ambacho Mungu au Yesu alikiandika, lakini badala yake umenijia na stori kwamba eti Mungu alimwambia Musa ndio akaandika! Je, si ukweli zaidi kwamba Musa ndiye aliyeandika akituambia kuwa Mungu ndiye amemwambia ayaandike hayo!? Think hard man, use that logic!’’ This is the logic u neeed= Kama Musa ndiye anayetuambia kua ni Mungu alimwambia aandike na kwakua amesema yeye mwenyewe kua ni Mungu alimwambia aandike kwa iyo ingawa ni kweli aliandika Musa lakini maneno ni ya Yeye aliyemwambia aandike, right? I guess that is even thinking hardest. Kama maelezo yako juu pale umeyatumia ukidhani yana kilo za kutosha kupinga hoja yangu kua ktk Bible kuna human role/factor, basi umefail brother, uwe mkweli tu kwa kua katika Nyaraka za Paul, nilikupa andiko kua yeye mwenyewe Paul anasema ivi 1Wakorinto.7:12…Lakini watu wengine nawaambia MIMI wala SI Bwana.Ni ngumu kweli na wewe wajua kukataa iyo statement na bado ukikataa, wepesi wa hoja yako against mine, utakua dhahiri. Ivi, on serous note, how can you deny mhusika anasema, Ni YEYE wala si BWANA? Unawezaje kumuwekea maneno mdomoni? You like thinking? Are nt you? here it is..Kama Paul angekua in one town say Mwanza( Korinto)…akawaandikia barua iyo na kusema..SI BWANA BALI NI MIMI NAWAAMBIENI( ofcoz kama Baba yenu wa kiroho), kisha akaja Mbeya then akasikia Lwembe anahubiri Mwanzo uko kua Ni Mungu alisema yale alosema Paul mwenyewe kua ni Yeye anasema si Mungu, would Paul understand you? si atakufungia safari na kuja kukurarua live kanisa palepale-u know that he was a no nonsense man aah? Vitu wazi kama ivi, vibaki ivyo-ivyo, kuvipindisha/saidia eti viwe vya kiroho-roho eti ndio UKIROHO na KUMUOGOPA MUNGU ni uwongo mwepesi tu na ni Unnecessary –Over-spiritualization which does not make sense at all!

  Umesema ukiniuliza..‘’Yesu ndiye master( Notice: ni ‘M’aster, huyo wa ‘ma’ster ni wa wengine , I hope not yours too), nilionana naye wapi, nitakuletea hadithi ya sijui soma Luka, au Marko’-Kama nitakuthibitishia toka Watu waliona na kusikia live Maneno na Matendo ya Yesu na wakayarekodi au walipata habari kamili toka kwa walioona na kusikia, halafu nikaona umo ktk rekodi kua kuna watu waliposikia habari zake kwa kuambiwa na wale waliosikia na kuona na kisha wakaamini na kweli kukatokea mabadiliko na ishara za nje na ndani Mdo.2:1-4,14-41, Mdo.10:1-48 halafu wewe ukaziita izo sources kua zitakua hadithi wakati hata Historically tu, ni kweli kuna watu waliishi wanaoitwa akina Luka, Petro,Paul then utakua na shida kubwa, tena yenye kuhitaji msaada wa haraka

  ‘’ Ati nikifika mahali nikatatizika ktk Neno,’’ Ni kweli yako maandiko unaweza fika mahala ukatizika, let me test you by just this..Luka.9:27..’those who are standing here, will not taste death until they see the Kingdom’,did they not die those who stood there He referred too?for it is more than 2000years now since He said so, right! Lakini kusoma kuhusu Paul anasema ni MIMI na wala si BWANA anaongea, hakuna hata chembe ya mtatiziko hapo, unaunda tu artificially/ mechanically.

  ‘’ Ati Kukidhi mafundisho yenu dhaifu baada ya kutatizika!! This one is terminated as above.

  ‘’ Ati Nimemkiri Kristo na ninayoyakiri, sikurudisha nafsi yangu katika Maandiko ili kujifunza zaidi upate kuvishwa ile Taji, yaani RM!’’Kwanza the term/claim kurudisha nafsi, I treat it with less weight for it is a mere noise, pili ndio mara ya kwanza nasikia RM ni taji, thus, it is not Biblical and so this inconsiderately uttered claim is severely dismissed!

  ‘’Kwamba hakuna mtu yeyote aliyewahi kuandika Biblia, kwa maana ya vitabu viliyomo humo, isipokuwa kwa Roho Mtakatifu, huyo ndiye Mtunzi na Mwandishi na Mkusanyaji wa nyaraka hizo’’ Sounds somehow spiritual but subject to criss-crossings checks, will it stand?( be indeed spiritually balanced), Lets us see… Ni kweli RM ndiye ALIYEWATUMIA lakini hakutunga kitu! Yesu alisema, akija RM atachukua yaliyo yake( Yesu) na kutupasha habari, hana yake kivyake-vyake-Yoh.16:13-14 na kati ya vya Yesu ni yale yote aliyoongea na kutenda kati ya Watu ambao wengine waliyarekodi ndio leo Injili zile 4.Be carefull Lwembe na statements zako! RM hatungi vitu vipya, nasisitizo ilo kwakua ndio mojawapo ya chanzo cha mafunuo mengi ndoto nyingi za watu leo zinazovuruga maandiko na mbwembwe za kileo.Pia ingawa RM ndiye aliwatumia lakini walioshika karamu na makatasi/magombo STRICTLY ni WATU!-wala sembe na bamia kama kawaida, Unapoanza kuingiza notion kua Hawakuandika Watu, unatupeleka kwa jamaa zetu kua kilishushwa kama kilivyo, You got to be both spiritually carefull and mindfull when you boldy say huge things Lwembe.

  ‘’ Mpangilio ni staili aliyoiamua Roho Mtakatifu katika kuyaleta yote hayo yaliyomo’’ You see now! Be well informed kua izi aya, mistari hata mpangilio ni man-made good job of recent developments, zamani haikua ivyo-yalikua ni magombo yet bado ilikua ni Mungu na Neno lake. Be carefull again unaposema statement kubwa-kubwa!

  Ati ‘’Mungu ndiye anayekusimulia na kukufunza mambo yote hayo, pamoja na hayo unayosema ni maneno ya Shetani’’ Kwamba‘Mungu anayetusimulia kauli hizo za Shetani, vinginevyo ni nani aliyewahi kuongea na Shetani hata akayarekodi mazungumzo hayo?’’! Be carefull again, usifanye mechanical spiritualization! Spirituality kama ipo, ipo tu wala Mungu hajakutuma ui-create brother, God is very open, hana shida ikifahamika kua ni Watu wanaandika mambo yake, Don’t fight for God for nothing, He is not aware (at least interested) of your freely offered fight support. What is this thing ‘Mungu anatusimulia! Come on! Wakati Ayubu anashambuliwa alikua ni yeye, ivyo kuandika/au kusimulia mtu ikaandikwa yaliyoandikwa kuhusu yeye, ni yeye anasimulia si Mungu! ni yeye alipigwa na majipu, ni yeye kweli aiwahi ishi duniani, ni yeye alikua na mifugo na wife, ni yeye alimsikia Mungu akihojiana na devo na ni yeye alisikia majibu ya devo kwa Mungu…mambo yote hayo kweli yalimtokea huyu Mwanadamu mla asali, ngano kama mimi na wewe kisha akasimulia na yakaandikwa-usiingizie supernaturality hapo na wala kuujua ukweli huu kua ni Ayubu alifanyiwa hayo yote na akasimulia yeye si Mungu yakaandikwa, hakuondoi ukweli kua ni maneno ya Mungu lakini pia na ya kwake maana alilaani hata siku aliyotungwa mimba-ni yeye analaaani maana hali ilikua tete .

  Ati’mfalme Daudi angeweza kweli kuziandika habari zake za uzinzi?Ati ‘’Angezificha kama alivyotaka kuificha mimba ya mke wa askari wake! Kwa iyo Mungu aliziandika mwenyewe akazishusha chin siyo? Come on be serious! Na huyu anayejiweka wazi sana mambo yake ktk Zaburi ni nani? Daudi sifa yake moja ilikua ni toba kweli kweli na bila haya. Sioni Daudi kwa dhati na maisha yake jumla alivyokua kua alifichaga dhambi. Tofautisha an attempt ili awe free ku sin na Mrs. Uriah-kwa kumset Mr auwawe na kuficha dhambi!

  Umeniuliza kwa kunipa mfano kwakweli mzuri sana wa Bibi Kizee, Mkulima na Baba yangu anayenisimulia hadithi’’ hahaha..i love the parable man, Great idea, deserves apprecition! Ni kweli huwezi claim unajua Bibi Wizard na Mkulima kuliko Baba mwenye hadithi, so what now? What are you mistargetly trying to say? Any connection na tunayosema au unalichosema? I can see CLEARLY havita-connect ukizingatiia majibu yangu juu,any attempt will be mechanicall subject to failure-try it plz.

  Ati, ‘’Nikukuta statement “hili si Bwana, bali mimi…” usije ukapelekwa nje ya kambi na maroho ya dini kwa kukudhanisha kwamba Mungu hahusiki katika hilo!’’-REFER MAELEZO YANGU MWANZO pia….this is too much attention na exergeration kuhusu kupelekwa na maroho ya dini, hapa kazi kazi tu, hamna roho wala nini, ni kupiga kazi mezani Kaka, hoja kwa hoja, ukiwa mkweli, unakubali na kubariki mwenzio au la mbishi basi tupige kazi tu, ukweli, hoja strong zitakua clear pasi na shaka, hakuna kificho, na kama mtu hakubali live na kuchukua fundisho, hoja safi, atakubali secretely tu.

  Ati ‘’niwaze limefikaje hilo hata kuwamo humo katika Neno la Mungu? this is cheap! no supernatulity, read Historia ya kanisa,mambo ya Imani na maandiko-yalikusanywaje! DO YOUR HOME kuliko kuspiritulize irrationally.

  Kwamba, ‘’Maana maneno yote unayoyaona humo ndani, bila ya kuondoa hata nukta moja, kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo, hayo katika ujumla wake ndiyo yanayomfunua Kristo, katika Mwili na Roho, yule Neno; “Kabla ya Ibrahim, nalikuwepo”! Very true and so? Unataka kuunda hoja hapa kwamba kwa kua ni ukweli huo, then si Wanadamu walioandika bali alisimulia Mungu? halafu akandika nani, Malaika siyo? Baseless notion indeed.

  Hapa, Mfano huu pia mzuri kweli-‘Ukimchukua mbwa ukampasua, ukaitoa akili yake na kisha kumuwekea ya panya, ni lazima ata behave kama panya, maana ana akili ya panya! Ila UMEKOSEA SANA KUDHANI neno ‘’Mind’’ hapa= ‘MIND’ of CHRIST-ndio iyo ya mfano wako! Lo! hapa tena nimekucheka rafiki na ujanja wote, una fanya faulu mbovu kama iyo! Embu angalia kwa mantiki hii hii ya andiko ilo-maana neno Mind ktk Bible linatokea kwingi, soma Kiswahili Bible in this case imesema vema sana kuzidi English-namely ‘’Nia’’ ya Kristo siyo akili( tangible matter)ya panya au dog kwa parable yako. Ooh men..hapa umeniangusha bro.

  Ati ukiniuliza vifungu vingapi Paulo ambavyo hajasema kuwa haya ni “Bwana asema” ambavyo mnavitumia kwa uhakika bila kusema kuwa oh hapa alikuwa ni Paulo? Viko vingi, kama hajasema SPECIFICALLY kua ni yeye, tunatumia kama Bwana na kama amesema mwenyewe kua si Bwana, navyo twatumia ila kwa uhuru wa kutosha kabisa. Lakini vilevile mind you, hata kama vingine twavitumia ambavyo hajasema ni yeye,so tunachukua moja kwa moja kama ni Bwana, tunatumia pia ushauri wa Roho-embu appy iyo kwa andiko la ‘’akupigaye shavu moja,mpe la pili! Je tunalitekeleza kama lilivyo?

  Ati kama ni“Paulo tu” na mamlaka ya Kufunga na Kufungua, ati mnayoyabishia yamekwishafungwa tayari, hapa duniani na huko mbinguni’- Come on! Plz fanya home work kuangalia context ya andiko ‘Kufunga na kufungua duniani na mbinguni’’ na kisha point yako ya aliyosema Paul. Too irrelevant and mechanical integration of unconnected Biblical point’s brother.

  Ati’’akili yako hauwezi kuyapambanua mambo ya Mungu, hayo hueleweka kwa UFUNUO tu!’ True but not all the time mfano Usiue! U don’t need ufunuo or leteni Zaka kamili (waonyeshe hii Sungura na Kaswahili-tehe), hauitaji ufunuo hapo. Again, nakuona unapenda sana spiritualization eee! Ni kitu kizuri ila unapitiliza bro! hauko carefull, inakufanya unaibuka na dini mpya au doctrine ya kwako-kwako tu

  Ati’’basi Paulo yeye amepewa macho ya rohoni, anayaona hayo mapepo ya dini, naye anajua kuwa tukimfuate yeye anayetupeleka kwa Kristo, mapepo hayo yatakimbia!’’ wewe hauna macho ya rohoni? Halafu nani anatunza kanisa kati ya Paul na RM? Nani ana mandate iyo? hakuna mapepo Paul anayoyaona NI WEWE, yeye yuko peace tu maana anajua Kanisa( Him inclusive) yuko MWENYEWE!

  Ati’Sungura Kanijia na pose ya ‘Dr Luka’, sawa na kunituliza Seleli. Soma kuanzia juu ktk hoja hii hii, nilileta somo zima kwa kuunganisha hoja 3 at per za Milinga kuhusu Wanawake na uko nikaongea human role/factor ktk Bible na Luka nilimtaja kwa details sana kabla ya Sungura kuja na point iyo iyo tena, so hajanipoza bali labda alirudia point bila kusoma kwanza kwa MAKINI yaliyotangulia ili awe relevant na kuko-connect

  Ati its a useless move in the Gospel, God said Luka is a saint! So who is not saint? You? and if Luka is saint, was He an angel? And why is it that the Bible calls us too as saints and small gods? He was and will always be same human as me and you,nothing special or supernatural-usije ukaleta mambo ya dini yangu ya kale ya kua Watakatifu ni specified few humans na wanaishi uzunguni tu hapa bongo, none!

  Parable hii, great one, nimecheka mpaka basi uliyomuuliza Sungura’’-ukifunguka, una mambo ya ajabu sana mazuri machache na mengi ni na yale mengine yale…tehe!.. Umesema’’unaulizwa darasani ni nani ambaye ni mtu wa zamani kuliko wote duniani? unatoa jibu kuwa ni Adamu! ZERO! swali lile lile, nawe unajibu kuwa mtu wa kwanza ni Zinjanthropus! ZERO! Ni kweli akili ina weza kushindwa kujua kati ya Adam na Mr. Zinja, same applies kwa BAADHI ya Maandiko but si YOTE NA WAKATI WOTE e.g. nimeshatoa mfano..Usiue..au niongeze..’Asiye fanya kazi na Asile’’…sasa mbona simple tu, akili imelewa fasta tena sio akili kuvuviwa , in this case, akili hii hii ya matobolwa ya Tbr. I can see the same zeal-To over-spiritualize!

  Kwamba,’’Ndio maana haupaswi kuitegemea akili yako ikuongoze katika mambo ya Mungu’’ Ndio na Siyo, mfano ni angalia juu hapo.Ati ‘subiri Ufunuo! SI WAKATI WOTE, MENGINE YALISHAFUNULIA,SOMA TU, ACHA EXCUSES.

  Kuhusu ‘Kuwaheshimu Watumishi wa Mungu akina Paul’’ na kwamba kuwagusa ni soo coz kuna kufa haraka’’ Yeye hasingetishia ivi, kitisho/adhabu aliyosema ni Kuhubiri tofauti na Injili ya Kristo, mengine ya kumungalia yeye kama yeye, kama Yesu alivyomuagalia Musa kama Musa kwa kusema aliwaandikia kutoa taraka kwakua mioyo yenu migumu lakini Mungu akupanga ivyo toka mwanzo, si dhambi na ivyo hafi mtu hapa kwa kua hata ivyo yeye mwenyewe Paul hana shida mtu wa watu maana kajisema mwenyewe kua ni yeye na si Bwana kwa jambo lile, Don’t make brother Paul looks like the way you want him to be.

  Hii nimependa ulivyomsaidia Sungura maana anasumbua kidogo mambo ya msingi. Ukiwa ndani ya hoja mezani tena KiMsingi- mzito ( somo langu la ‘Utoaji’ in General na Zaka specific ni mfano unadumu), ana anataka ionekane iko nje, ukitetea msimamoo wako si kiubishi tu bali kwa ukweliii na ili kumuelewesha kirahisi, ukampa mifano kadhaa, anasema umetoka nje ya mada kabisaaa, wakati ni yeye anatoa nje wachangiaji wrongly lakini tu basi ukiamua umkubalie na kisha ukatoka naye nje uko uko alikokupeleka yeye in the first instance , analalama kisha kujipachika cheo cha mshauri nasaha wa mambo ya Kuandika! Check ktk Hoja ya Zaka uko, nimemjibu ivi ivi almost ulivyofanya na nashagaa kweli iki ulichomwambia kua’’Kuhusu hoja zinazojitokeza na kuonekana kana kwamba ziko nje ya mada, itakuwa ni ufinyu wako wa kuelewa misingi ya mijadala tu. Kwani katika maelezo yako iwapo litatokea jambo ambalo umelisimamisha kutetea hoja hiyo katika presentation ambayo ni manipulative, ndipo hilo huwekwa sawa ili kuuvunja msingi unaoujenga katika hoja hiyo, kaka! Haujawahi kusikiliza kesi, ambapo shahidi anaulizwa kuhusu uzinzi alioufanya miaka iliyopita, wakati kesi inayoendelea ni ya uhaini? Lengo huwa ni kumuondoa katika ushahidi kwa kuonesha kuwa huyo si mwaminifu’’ This is excellent parable and illustration Lwembe, hapa sincerely hata kama hatukubaliani mambo yako mengi eg hii hoja tunayoenda nayo ya kuwaona Wanawake hamna kitu kwa Mambo mazito ya Mungu, but what you challenged him is a stone!

  ‘Ati mie nimewabehua watumishi wa Mungu Musa na Paulo, akiwafanya si lolote, yeye role model wake ni Yesu na kwamba nikadhibiwa na Mungu kwa kuniletea akina cha matusi Sungura na Kaswahili wakampagawisha’’ ’’umenichekesha kweli, usijari kwa kua ktk mijadala mizito ukibana vema sana mianya, mtu ana shindwa kupumua then anapitilizia! We wajua mimi ufurahi tu tena nachekaga mpaka machozi kuona mwana mdahalo mwenzangu anavyofyatuka baada ya kushindwa tikitiki kuchomoka ALIPOJIWEKA kisha ukamsindikizia kumuweka-Hahaha! Kamwe usini-misinterprete kua nalalama bali kila naponukuu, ni kujenga msingi tu wa hoja husika na pia burudani ktk debates, ningejiruhusu pia kufunguka, lo! si unajua nimeza memory card alisema/dhani Kaswahili tena alikosea si card, ni cards, na unajua sana nikiziachilia! Tehe! Ushauri wako huu kua Wa Emausi, kama nao wangekuwa ni wa vya matusi, Si wangeishia kulia na kusaga meno kwa mizaha kama yenu ya leo!!!’’ Wahusika hasa wamekusikia. Ila kama niliyokujibu mwanzoni, hakuna mzaha hata kidogo kuhusu ukweli kua Ktk Biblie kuna rekodi ya mambo ya Mungu, Watu na Shetani-Ni UKWELI mrahisi tu wala siyo kufuru, sema kama una matatizo ya uelewa uliyopitiliza.

  Ati tujitahidi kulielewa Neno la Mungu kuliko kujificha ktk vichaka vya dini! Umesema ivyo kwakua tunaongelea makatazo kuhusu Wanawake sasa KAMA KUTAKUWEPO NA MTU YOYOTE,KIKUNDI CHOCHOTE CHA IMANI KINACHOCHUKUA MOJA KWA MOJA ALIYOSEMA PAUL KAMA PAUL NA KAMA KIONGOZI WA KUNDI LA BWANA LA MAHALI FULANI KTK TAMADUNI HUSIKA, NA KUYAHAMISHIA KANISANI KWAKE ILI KUWAZIMA WANAWAKE KUTOFANYA YA MUNGU KWA UHURU, HAKIKA, HAKIKA, HAKIKA HAKIKA ICHO NDIO KICHAKA CHA DINI HASA.

  Kumbuka nilikuhaidi kukupa maswali ili kujua una tatizo gani na Wanawake kua watu wa Mungu kama sie Wanaume na Bwana kuwatumia? ujibipo ni/tutajua kama uko beyond repair na wewe au kuna tumaini, YANAKUJA,PLZ UWE MWANAMDAHALO MZURI KUJIBU SIYO KUKIMBIA AU KUACHA BILA MAELEZO HASWA. Soma kwanza 99 pages izi kisha maswali yanakusanya ‘’upako’-Lazima ifike mahali dini/imani yako/zetu ziache mambo ya dharau na mfumo dume mbovu usio wa baraka( kuna mfumo dume mwema) dhidi ya Watumishi wa Mungu wanawake Jeshi KUBWA,amen.

  Press on.

 147. Asante Lwembe,
  Hatuhitaji kupiga panda juu ya kile tulichoandika hapa,kwa kuwa wanaosoma michango yetu wanaufaham juu ya elimu ya Mungu,hivyo yatosha wao kuamua mioyoni mwao kuwa nani kasema ukweli na nani kahubiri mapokeo ya dini yake.

  Pia hili nisiliache wengine wakadhani ndivyo lilivyo,kwamba Mungu kamwita Luka ‘mtakatifu’. Lwembe ndio maana nakwambia nenda darasani ukasome haya mambo,lakini wewe unasema ufunuo unatosha.

  Ukiona majina kama Mathayo mtakatifu,Yohana mtakatifu, Luka mtakatifu n.k

  Hayo maneno mtakatifu yaliwekwa tu kidini na kanisa Rumi kama unavyoona leo kuna mtakatifu Augustine, mtakatifu Koretha,mtakatifu Cecilia, baadae utasikia saint Nyerere.

  Kwa hiyo kigezo cha ubora wa vitabu vya Luka ni maudhui yaliyo ndani yake,wala si umtakatifu aloitwa. Na Luka alikuwa medical dr.(tabibu), na hayo aliyoandika haukuwa ufunuo,bali alikunya data toka vyanzo vya kuaminika na kuzifanyia utafiti ili kujiridhisha kama mambo hayo yalikuwa kama yalivyosema yalikuwa.

  Tchao Lwembe

 148. Seleli I’m not worrying with but rather worrying about, you are paying heavy emphasis to pet and trivial issues.

  Are you a teenager in such debates like this,or you zoomed in on this discussion thinking that the only true answers are those analyzed by you?

  For your information Seleli if we were here to criticize ourselves I could have told you long time ago that most of your opinions are quite biblical concepts which lack biblical contextualization at large.

  And since you don’t know that you don’t know, you are just being religiously naive, and that’s why you think whatever u speak here is of biblical substance, thus it has to be esteemed by every one.

  Have a look at what you corrected me here, I quote you:
  Hii statement yako,’’Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako na Seleli yameshatoka kwenye hoja msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za ninyi kushambuliana kwa maneno’’ rekebisha isomeka ivi.. ’’Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako KWA Seleli yameshatoka kwenye hoja ya msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za WEWE( Lwembe) kushambuliA kwa maneno kushambuliA kwa maneno- YASIYOKUA NA MASHIKO/HAYA- SUBSTANTIATE CLAIMS ZAKO(Lwembe) TO OUTSMART hoja za Seleli.

  Reread my statement to see if I was wrong grammatically semantically!

  Thank you

 149. Sungura, acha kujiongelesha kama mtoto mdogo, ni wapi kwenye Biblia walisema msiandike saana? Mbona Isaya kaandika chapter 66 peke yake na Obadia hajalalamika!!

  Hivi mtu akikuambia kuwa ukifundisha tofauti na haya ninayoyafundisha na Ulaaniwe, je, hilo ni jambo jepesi? Elimu ni jambo zuri, kazitafutieni ajira elimu zenu, hata zikiwa ni za dini, lakini mnapoyasogelea mambo ya Mungu, ziwekeni kando elimu zenu za mtaani njooni mjifunze ile Elimu Kubwa yao.

  Sungura unatujia na pose ya ‘Dr Luka’, sawa, Seleli umemtuliza nayo, lakini its a useless move in the Gospel, God said Luka is a saint! Naye Mungu anawaheshimu zaidi watakatifu wake kuliko wasomi wenu. Kusoma sana sio kumjua Mungu, na wala Mungu hajawahi kuwategemea wasomi licha ya kwamba anawatumia, bali si kwa usomi wao ila kwa unyofu wao! Kwa mfano unaulizwa darasani ni nani ambaye ni mtu wa zamani kuliko wote duniani? Hapo ndio uko chuoni huko China, basi nakuona unatoa jibu kuwa ni Adamu! ZERO! Unalalamika lakini unafundishwa kuwa the oldest man ni ‘Zinjanthropus’, basi unalielewa hilo vizuri. Kisha unarudi Bongo na kujiunga na chuo chenu cha Biblia cha Jehova Witness, kwenye yale Majumba yenu ya kiFalme, kisha unaletewa swali lile lile, nawe unajibu kuwa mtu wa kwanza ni Zinjanthropus! ZERO! Unaona, zote ni elimu na zinatoa digrii, lakini zinatofautiana kiasi hicho!

  Ndio maana haupaswi kuitegemea akili yako ikuongoze katika mambo ya Mungu, subiri Ufunuo! Lk 24:45 “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.” Petro alijuaje kuwa Safira anawazingua? Itazame sifa kuu ya Neno, “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, … tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.” And the Word is Christ! Kwanini Safira alikufa? Ministry ilikuwa ime change, hawakujua maskini, walidhani ni ile Huduma ya Yesu Mnazareth, aliyekuwa anazomewa na kudhihakiwa, kumbe masikini mambo yalikuwa yamebadilika, yule Mwanakondoo amebadilika amekuwa Simba! Huduma ya mitume ni Huduma ya Roho Mtakatifu, hiyo ambayo waliambiwa kuwa ikija hiyo, ukiifanyia mzaha wowote ule, utaishia kuzimu na madigrii yako! Umeelewa kwanini Safira alianguka akafa?!

  Mtazame Abimeleki, Biblia ilisema alikuwa ni mtu wa haki, tena Ibrahim ndiye aliyemdanganya kuwa Sara ni dada yake, lakini Mungu anamwambia kuwa amekufa! Tena anamwambia akisha mrudisha mke wa mtumishi wake, amuoombe amuwekee mikono ndio atapona! Ndio maana tunawaonya kuhusu kuwarahisi watumishi wa Mungu, ni soo kali sana!

  Au Miriam dada yake Musa, kwa kule kuwa kwake nabii akajidhania kuwa anajua, kama ambavyo wengi leo hii kwa kunena kwao kwa lugha, sijui “Asante Yesu” x 666, nao walipolipuka katika mtiririko huo, basi wanajiona wanamjua Mungu kuliko akina Paulo, kama wale wengine nao wanaoutangaza “uongo wao wa udhaifu wa mtume Paulo”, ili kwa uongo huo wasile kitimoto! Ni hatari kuliko mnavyowazia, ukoma wa kiroho uko mlangoni kwenu msipokuwa makini!

  Kuhusu hoja zinazojitokeza na kuonekana kana kwamba ziko nje ya mada, itakuwa ni ufinyu wako wa kuelewa misingi ya mijadala tu. Kwani katika maelezo yako iwapo litatokea jambo ambalo umelisimamisha kutetea hoja hiyo katika presentation ambayo ni manipulative, ndipo hilo huwekwa sawa ili kuuvunja msingi unaoujenga katika hoja hiyo, kaka! Haujawahi kusikiliza kesi, ambapo shahidi anaulizwa kuhusu uzinzi alioufanya miaka iliyopita, wakati kesi inayoendelea ni ya uhaini? Lengo huwa ni kumuondoa katika ushahidi kwa kuonesha kuwa huyo si mwaminifu, sembuse mambo ya Mungu!

  Mwisho, kuhusu lugha, Hebu itazameni fact hii: kwamba Seleli ndiye aliyeanza kuwabehua watumishi wa Mungu Musa na Paulo, akiwafanya si lolote, yeye role model wake ni Yesu! Mungu definately hakufurahishwa, kwa hiyo akamletea cha matusi Sungura na Kaswahili wakampagawisha, ndipo kwa taharuki, mara anataka kuwapeleka polisi na kulalama kwingi! Ndio maana ninawataka muwe watchful, msidharau watu, mnaweza kuwa mnajibishana na Kristo aliyechange form, kama wale wanafunzi wake walioongozana naye kwenda Emausi, je, kama nao wangekuwa ni vya matusi? Si wangeishia kulia na kusaga meno kwa mizaha kama yenu ya leo!!!

  Katika kumalizia, ninawashukuru nyooote kwa ushirikiano mliouonesha kwa kadiri tulivyojadili jambo hili kwa upendo utupasao wakristo, mapungufu yetu ni mengi, bali tujitahidi yasituongoze ktk kulikwepa Neno la Mungu kwa kutuficha ktk vichaka vya dini!

  Asanteni na kwaherini!!

 150. Sungura,

  A simple logic can help you to know kua kama naandika sana pia naweza andika kidogo pale inapobidi( Notice: inapobidi), so relax, don’t make it a deal or topic, all are possible yet strictly inategemea what is on the table burning! Mfano Mtu ktk hoja moja, aki-raise hoja/maswali mengi, mengine ya msingi ambayo unajua yakijibiwa, yana-back up hoja mezani, yanazima/ziba kabisa mianya ya janja-janja au in one way or the other, yana-connect some concepts ktk Hoja iyo iyo ya msingi consequently, kuandika kwa urefu ktk situation iyo ni common thing. Hoja/Maswali mengine yanakua si ya msingi ila yanatumiwa na mhusika kama vile ni ya msingi kwelikweli na tena kila mara kuback up mambo yake wrong from the first instance, hayo nayo sharti yatoweshwe kwa hoja nyingi kabisa kiasi kwamba kabla hujasign off ktk hoja ilo/mambo yake hayo umuache, yeye mwenyewe moyoni au wasomaji, wanajua tu hapa, hamna kitu na huyu hana hoja! Hapana kumuacha haraka mtu anayetumia uwongo/dini/nafsi kusema au kupollute kweli! ‘Kweli’ si tu itasimama bali itasimamiwa isimame -hence kuandika sana/ kirefu ktk mazingira kama hayo, ni justified kabisa.

  Ngoja nitoe mfano: Ivi akitokea Mtu hapa akasema hakuna kuokoka duniani na akawa serious kabisa kupullute iyo kazi ya Yesu kwetu, lo! na kwamba mambo ya ROHO MTAKATIFU NI DINI TU! My Lord, my God, nakwambia nyie wengine wote ruksa, nendeni mkalale kwa amani but mimi na BWANA, tuacheni hapa kanisani SG blog.Niache tu maana hapa tayari nasikia kuchemka kisima cha ndani vizuri/vibaya sana na natamani kiumbe yeyote wa uwezo/dini yoyote alianzishe ilo as long as Bible ni base ya faith yake, thus again-kuandika sana ktk mazingira hayo, ni baraka safi. Besides, Mr. Milinga kaleta hoja11-sasa,approaches zetu kwazo tutatofautiana ktk kuchangia na ni baraka kua na varieties ya mambo hata ktk life ya kawaida uko na kule, so, mwingine atapenda kusema kitu kidogo tu, mwingine ata-appreciate tu, mwingine ataenda hatua mbele kidogo-akasema uzoefu wake ktk ilo na mwingine akaamua kuleta soma zima kabisa kwa jambo ilo, ivyo be patient with and get used with different capacities/gifts/talents/ decisions on choices/ preferences of people kama vile tunavyokuvumilia, wote hawawezi kua Sungura humu wala Seleli au Lwembe kama siyo Nzala, Kaswahili na Nelson T. However, kwa kusema ivyo, I am not entertaining Lwembez fashion, that is beyond discussion/repair na nina/kuna namna yake ya ku-engage naye-He is an easy brother to engage with, you only help me to accelerate, exposing his own emptiness-simple!

  Hii statement yako,’’Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako na Seleli yameshatoka kwenye hoja msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za ninyi kushambuliana kwa maneno’’ rekebisha isomeka ivi.. ’’Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako KWA Seleli yameshatoka kwenye hoja ya msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za WEWE( Lwembe) kushambuliA kwa maneno- YASIYOKUA NA MASHIKO/HAYA- SUBSTANTIATE CLAIMS ZAKO(Lwembe) TO OUTSMART hoja za Seleli.

  Umenishauli ivi-‘’Na wewe Seleli usiwe mtu wa kulalamika sana na kuhamishwa kwenye hoja ili kuanza kujibu mashambulizi binafsi. Mambo mengine yapuuze ili uendelee kuchangia hoja ya msingi’’. HUJANISOMA TU ILA UTANIPATA TU TUNAVYOENDELEA HAPA, SO SINA HAJA YA KULALAMIKA! KWANINI KWANZA NILALAMIKE, KUNA KITU GANI CHA KULALAMIKA HAPA!!!! Aaa bwanaa Sungura, these things are cheap and common in talks, UME-INTERPRETE MY WAYS WRONGLY. NAHAKUHAKIKISHIA HAKUNA HATA MMOJA INCLUDING WEWE, ANAYEWEZA NITOA KWA HOJA-in the sense kunipoteza kabisaaaa! Never! NIKIONEKANA NIMETOKA, NINA SABABU NZURI TU KISHA NIKIRUDI, UKO NILIKOKWENDA NIMEMALIZA KAZI-ikubalike au ikataliwe lakini mioyoni/akilini mwao uko nilikokwenda temporarily, wanajua tu kilichofanyika na hatimaye tunaweza kutana uku niliporudi, then we can go on with sweet business-though anytime when business changes from sweetness to bitterness( Gods Word/Church Biblical doctrine/Utumishi/Born Again’s all Together Cores kuvurugwa), ‘anointing’ ya kupaa kuligeukia ilo, iko tu unspeakably very ready, so usiwe na wasi hata kidogo,I know both tennis and footballs, don’t worry with me kabisa, help/advise others e.g. Kaswahili and well, sometimes yourself man-YOU KNOW WHAT EXACTLY I MEAN.

  The last statement yako’’Kumbukeni kuna kuamua kutokukubaliana pia juu ya hoja na kila mtu akaendelea kuamini na kufanya anavyoona yeye’’- ni sawa’ on side but on the other side ATTENTION! Kama tunatumia Bible moja hii hii lakini Strictly and only kwa principle hii- Roho Mmoja, Bwana Mmoja, Mungu Mmoja, Imani Moja,Ubatizo mmoja, na Mwili mmoja-1Wakorinto.12:13, Waefeso.4:4-6, room ya kila mtu aendelee na anavyoona inafaa is minimal au should be removed kabisa kama inang’angania basi na ivunjwe nguvu kwa nguvu nyingi sana.

  Press on.

 151. Dah, shida tu ni kwamba Lwembe na Seleli mnaandika sana!

  Mimi msimamo wangu katika mijadala kam hii ni kuwa mkweli na kusimamia ukweli, ka sababu mwisho wa yote mijadala ikiishi sisi ni ndugu. Ni sawa na timu ya mpira wakati wa mazoezi huwa wanagawanyika na kuanza kushindana lakini mwisho wa siku ni wao ni timu moja. Hivyo ni muhimu kwa kila mchezaji kuangalia asimuumize mwenzake maana kwa kufanya hivyo ataigharimu timu nzima akiwamo na yeye mwenyewe.

  Baada ya kusema hayo napenda kusema hivi;

  Nikuonavyo Lwembe u mzuri sana katika kuelezea mambo ya nadharia na kujua kutumia lugha za kejeli zenye kuonesha kuwa wewe unajua,lakini tukirudi kwenye uhalisia wa jambo husika maneno yako huwa hayana ‘substance’ ndani yake.(nasema haya si kwa sbabu hatukubaliani na wewe katika hoja hii)

  Ni vema tuwe na tabia ya kukubali pale mtu anapoonesha ukweli wa hoja iliyo mezani.

  Ukweli ni kwamba biblia ni kitabu chenye kumbukumbu ya matendo ya Mungu pia na ya wanadamu. Na kuwemo kwa kumbukumbu ya matendo ya wanadamu hakuipunguzii biblia sifa yake ya kuwa ni neno la Mungu. Hizo record za matendo ya wanadamu mazuri na mabaya yapo kwa ajili yetu kujifunza.

  Lwembe hukumbuki kabisa kwamba hata Paulo kuna sehemu anasema hapo ni mimi wala si Bwana wakati anawaandikia wakorintho?

  Mwandishi wa kitabu cha Luka na Matendo ya mitume ambaye ni Dr. Luka, wala hakuwa mwanafunzi wa Yesu na wala hasemi kuwa aliandika hayo kwa ufunuo wa Roho mt. bali alikusanya taarifa toka kwa waliyashuhudia hayo ndipo naye akapata cha kuandika. Lakini kwa sababu kilichoandikwa kiko sahihi leo kinafanya kazi maishani mwetu (Luka 1:1-4)

  Halafu si kweli kwamba kila kitu kinahitaji ufunuo, kuna vitu vinahitaji akili ya kawaida tu kuvielewa. Ni kujidanganya sana kudhani kwambi akili ambayo Mungu ametupa ati haina maana yoyote katika kumjua yeye. Kuna wakati Paulo anasema ataimba/ataomba kwa roho na kwa akili pia. Biblia imesema tubadilishwe nia zetu. Neno nia linaloongelewa hapa ni akili. Na kama unajua kuwa mtu akiokoka anakuwa na nia ya kristo kwa nini useme tena kuwa kwa akili hawezi kuyapambanua mambo ya Mungu?

  Halafu Lwembe ona unachomwambia Seleli hapa: ”…. kisha Mungu akakupa ‘roho mpya’ kwa huo uaminifu wako, ambayo kwayo ulinena zile “Asante Yesu” x 666,..” Haya si maneno ya kumwambia mkristo mwenzako Lwembe, unachokimaanisha kwa hiyo x 666 si kitu sahihi cha kumwambia mkristo mwenzio, ni tukano kwa mwili wa kristo. Tusiandike mpaka tukapitiliza!!!

  Lakini pia kuna swali la kipuuzi na kidhihaka umeniuliza ambalo hata siwezi poteza muda kukujibu. Hili hapa: ”Sungura, labda nikuulize kidogo …. nchi ya maziwa na asali”, kwamba mimi nilidhani ni “the land of plenty” au ni nchi ambamo wanawake wanaruhusiwa kufundisha na kuwatawala waume zao, yaani nchi ambayo inadumisha ‘haki sawa kwa wote’, halafu hata hizo haki zenyewe hazijawa defined, kwa lugha nyepesi, ‘Democracy’ ambayo it’s all sails without an anchor!; Yaani the carnal church??

  Siwezi kupoteza muda kujibu hiyo dhihaka Lwembe, sorry!

  Ukiangalia sehemu kubwa ya majibu yako na majibizano yako na Seleli yameshatoka kwenye hoja msingi na kuanza kujadili habari zingine au za akina Paulo mtume au za ninyi kushambuliana kwa maneno.

  Na wewe Seleli usiwe mtu wa kulalamika sana na kuhamishwa kwenye hoja ili kuanza kujibu mashambulizi binafsi. Mambo mengine yapuuze ili uendelee kuchangia hoja ya msingi.

  Kumbueni kuna kuamua kutokukubaliana pia juu ya hoja na kila mtu akaendelea kuamini na kufanya anavyoona yeye ni sawa. Maana mwisho wa yote iko siku tutajua kwa nin Roho mt. amekuwa akiwatumia wanawake na wakati kumbe hawatakiwi kuwafundisha wala kuwaongoza wanaume kwa namna yoyote. Maana kuna hata wanawake wameandika vitabu ambavyo vimewafundisha wanaume mambo makubwa.

  Mbarikiwe.

 152. Nimeyasoma maelezo uliyoyatoa yooote ndg yangu! Pia nimekielewa unachokisema katika ujumla wake ndio maana nili comment juu yake. Nayo majibu haya mapya uliyonipa juu ya hilo nililolizungumza, ni mazuri, na yanatoa maelezo mengi kuliko uliyoyaandika. Nimeipenda conclusion yako hii, “simple!!!!!!!!!!!!!!period!”

  Hata hivyo nilitegemea utanionesha angalau kitabu kimoja ndani ya Biblia ambacho Mungu au Yesu alikiandika, lakini badala yake umenijia na stori kwamba eti Mungu alimwambia Musa ndio akaandika! Je, si ukweli zaidi kwamba Musa ndiye aliyeandika akituambia kuwa Mungu ndiye amemwambia ayaandike hayo!? Think hard man, use that logic!

  Umeniambia kuwa Yesu ndiye master wako, lakini hata nikikuuliza kuwa wewe ulionana naye wapi mpaka akawa master wako, hadithi utakayoniletea ni hiyo hiyo ya sijui soma Luka, au Marko au Petro au waraka wa Paulo nk! halafu bila ya aibu ukifika mahali ukatatizika, kutokana mfumo uliouzoea, unawaruka na kuwabambika kuwa oh, huyo alikuwa ni paroko wa Wagalatia! Sasa, mbona hayo mengine aliyowambia hao hao Wagalatia mnayachukua na kufundisha watu wenu?! Kama si tabia ya unafiki ni nini basi? Ni katika unafiki huo ndio mna u dismember Mwili wa Kristo ili kukidhi mafundisho yenu dhaifu!!

  Unaponiambia kuwa wewe umemkiri Kristo na kwamba ndiye Master wako, na ninapoyasoma hayo unayoyakiri, ndipo ninapojua kuwa wewe ulifuatisha tu sala ya toba uliyoongozwa na pastor wako, kisha Mungu akakupa ‘roho mpya’ kwa huo uaminifu wako, ambayo kwayo ulinena zile “Asante Yesu” x 666, bali hukuirudisha nafsi yako katika Maandiko ili kujifunza zaidi upate kuvishwa ile Taji, yaani RM!

  Bali, napenda nikueleze kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuandika Biblia, kwa maana ya vitabu viliyomo humo, isipokuwa kwa Roho Mtakatifu, huyo ndiye Mtunzi na Mwandishi na Mkusanyaji wa nyaraka hizo. Ndipo kwa kadiri unavyovisoma, na maelezo yake yooote yalivyo, hiyo ndiyo staili aliyoiamua Roho Mtakatifu katika kuyaleta yote hayo yaliyomo. Mungu ndiye anayekusimulia na kukufunza mambo yote hayo, pamoja na hayo unayosema ni maneno ya Shetani, ni kwamba hujajua tu, Mungu ndiye anayetusimulia kauli hizo za Shetani, vinginevyo ni nani aliyewahi kuongea na Shetani hata akayarekodi mazungumzo hayo?! Hivi kwa mawazo yako, mfalme Daudi angeweza kuziandika habari zake za uzinzi? Angezificha kama alivyotaka kuificha mimba ya mke wa askari wake! Au nikuulize Seleli, ulipokuwa mdogo, hujawahi kusimuliwa hadithi? Basi katika hadithi hiyo, ilipofika baba au mama, anakwambia “basi bibi kizee yule akamuuliza mkulima, naye mkulima akawaza, bibi huyu ni mchawi nini?” basi unaweza kung’ang’ania kuwa unamjua bibi kizee huyo na huyo mkulima kwa hadithi hiyo kuliko huyo baba yako alioyajua mpaka mawazo yao?

  Kwahiyo unapokutana na maneno kama “hili si Bwana, bali mimi…” usije ukapelekwa nje ya kambi na maroho ya dini kwa kukudhanisha kwamba Mungu hahusiki katika hilo! Hebu wazia, limefikaje hilo hata kuwamo humo katika Neno la Mungu? Maana maneno yote unayoyaona humo ndani, bila ya kuondoa hata nukta moja, kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo, hayo katika ujumla wake ndiyo yanayomfunua Kristo, katika Mwili na Roho, yule Neno; “Kabla ya Ibrahim, nalikuwepo”!

  Mungu ni Roho, ndipo kwake yeye, kututumia sisi ni furaha yake, iwapo tutakuwa tayari kutumika, ule mwili. Mungu aliwatumia hao wote unaowajua ambao wewe wadhani walikuwa ni watu tu, ila walikuwa ni zaidi ya watu, supernatural! Roho wa Mungu akikufikia hauwezi ukawa kama ulivyokuwa hapo nyuma; mtume Yohana walimtumbukiza ndani ya pipa la mafuta yanayochemka, akatoka na ngozi nyororo kuliko umri wake, Petro aliwaomba watesi wake wamsulubishe kichwa chini, Paulo Mfarisayo, aliubwaga ufarisayo na umaarufu wake, na mafanikio ya kimwili ambayo angeyapata, vyote anasema akaviona ni mavi, akawa mtumwa wa Kristo wa hiari!

  Hebu iangalie hii Ahadi ya Kristo kwa Kanisa lake katika Mt 28:20, “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Kifungu hiki kingekuonesha ile siri iliyokuwa ikifanya kazi ndani yao, ile siri ya utauwa, kwamba hao unaowaona walikuwa ni makasha tu, au kwa usahihi zaidi hao ndio ule Mwili wa Kristo! 1Kor 2:16 , “For who hath known the mind of the Lord, that he may instruct him? But WE HAVE THE MIND OF CHRIST”, unamuona huyo Kristo unayesema umemkiri kuwa Bwana na Mwokozi wako? Ukimchukua mbwa ukampasua, ukaitoa akili yake na kisha kumuwekea ya panya, ni lazima ata behave kama panya, maana ana akili ya panya! Basi hiyo miili iliyonunuliwa kwa Damu ya thamani, ikiisha kuwekewa THE MIND of CHRIST, inakuwa ni nani? Amejificha Master wako kwa ulimwengu bali wao na waliofunuliwa siri hiyo, wanalijua hilo, ndio maana wanakuwekea Baraka katika hilo wanalokufundisha na Laana pia ukijifanya kuwa behua!!! Hiyo ndio sababu pekee inayotulazimu kuisikiliza vizuri Sauti ya Mungu, amejificha ndani ya hayo makasha!

  Wahubiri wengi wanapenda sana yale mamlaka ya kufunga na kufungua, lakini ni hao Mwili wa Kristo katika maana ya hiyo Mt 28:20 ambao wana hiyo mind of Christ, hao pekee ndiyo wenye mamlaka hayo kwani ni yeye Kristo ayatimizaye hayo ndani yao. Isaya 9:6 inasema “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake…” unauona huo Uweza wa Kifalme ulio juu ya mabega ya huyo mtoto mwanaume? Basi mabega si ni sehemu ya mwili wake, nao mwili huo wenye huo Uweza wa Kifalme, ndio hao akina Paulo na mitume wote, ndio maana ninakwambia Biblia ni Neno la Mungu in its entirety!

  Na hata nikikuuliza kutoka katika base ya argument yako, kuwa ni vifungu vingapi katika nyaraka za Paulo ambavyo hajasema kuwa haya ni “Bwana asema” ambavyo mnavitumia kwa uhakika bila kusema kuwa oh hapa alikuwa ni Paulo? Huu ndio unafiki ninaousema! Halafu hata ikiwa ni “Paulo tu”, basi kule Kufunga na Kufungua, ile mamlaka waliyopewa, iko wapi kama si hayo mnayoyabishia huku yakiwa yamekwishafungwa tayari, hapa duniani na huko mbinguni, siku ile yalipowekwa hapo ili Wagalatia ninyi wa leo mkutane nayo! Roho hazifi kaka, zinawashawishi mpaka mnazipa ruhusa kuwamiliki miili yenu!

  Ndio maana Mungu anasema, “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe”, maana kwa akili yako hauwezi kuyapambanua mambo ya Mungu, hayo hueleweka kwa UFUNUO tu! Basi Paulo anapotuambia sisi Wakorinto wa leo, zile roho zinazotunyemelea zitutawale, kwamba tumfuate yeye, tusiwe wabishi, yeye amepewa macho ya rohoni, anayaona hayo mapepo ya dini, naye anajua kuwa tukimfuate yeye anayetupeleka kwa Kristo, mapepo hayo yatakimbia! Lakini tukimbeza na ku sneak mbele yake kwa akili zetu na hizo logic, na tafsiri na kanuni zetu, basi tutaelewa nini? Mungu huufunga mlango wa Ufunuo usoni petu, ndio maana tunabaki tunayazunguka Maandiko kama walivyoizunguka nyumba wasiuone mlango kule Sodoma!

  Gbu my brother!

 153. Lwembe,

  Yapi ni wrong nayofundisha? SHOW/SUBSTANTIATE IT, Mbona mimi nakupa solid and tangible hoja ku-confirm nayosema? If you will not prove me wrong then you are badly triple wrong na kila utakachosema itakua sasa ni maneno ya by the way ya kuchangamsha baraza brother Lwembe. Sasa narudia tena kuhusu nilichokisema as a matter of fact, nina copy na ku-paste nilichosema maana naposoma response yako na maswali unayouliza , inakua kama hukusoma kama tough reader au umesoma kweli na umeelewa yet unapenda tu-fellowship Alright, here go below my brother.

  Nakumbusha kua tuko ktk hoja kuhusu ‘’Makatazo mbalimbali kwa Wanawake’’ katika Biblia na nilitoa maoni ktk page forum hii hii kwa kuko-combine hoja 3 kwa mpigo za Milinga namely
  HOJA NO. 3-Mafundisho ya kukataza wanawake kuvaa suruali ili hali zinafunika uchi na mwili wao kwa usahihi zaidi kuliko hata siketi na gauni.
  HOJA NO. 9-Mafundisho ya kuzuia wanawake wasiwe viongozi wa kanisa au wasiruhusiwe kufundisha
  HOJA NO. 10- Mafundisho ya kuzuia wanawake kufanya kazi zenye kipato kwa misingi ya dini au mafundisho
  Nilitoa maoni mengi sana, bila shaka umesoma mpaka mwisho, kama uliishia njiani, rudi tena soma. Kwa kifupi nikasema jambo hili chini ambalo limekuletea maswali na niseme tu kweli-NINAELEWA WHY UNAPATA SHIDA KUKUBALI UKWELI HUU CHINI UKIDHANI KWA KUFANYA IVYO UNAKUFURU AU VIPI KUMBE NENO LENYEWE LIMEJIWEKA WAZI NA WALA HALINA TATIZO KUJIWEKA HIVYO/KUA WAZI IVYO. NA MIMI KAMA MTU NILIYEOOKOKA NA NIMEJAZWA ROHO MTAKATIFU NA KWAKWELI NATAKA KWENDA MBINGUNI, NAJUA NINI MAANA YA KUKUFURU NA ADHABU YAKE, IVYO HAKUNA JINSI UNAWEZA NIDHANIA MIMI KUFANYA KOSA KAMA ILO.UNACHOJARIBU KUFANYA WEWE KATIKA WASIWASI WAKO NA HURUMA ZAKO IZI ZA KIBINADAMU AMBAZO KWA KWELI HAZINA MASHIKO, BORA UNIHURUMIE KWA MAMBO MENGINE YA MSINGI, NI KILE WANASEMA KU-CAST IN THE DOUBTS ON THE FACTS/TRUTHS TO CATCH SOME TO YOUR SIDE intentionally, ignorantly or innocently-as simple as that! AND GUESS WHICH SIDE OF YOURS IS THAT?= RELIGIOUS BOXES AS OPPOSED TO GOD OF ALL THE PEOPLE WHO LOVES AND TREAT THEM EQAULLY REGARDLESS OF THEIR GENDER, RACE, BACKGROUND,GEOGRAPHICAL LOCATIONS etc.

  Ukweli wenyewe ni huu niliosema kwa ujasiri kua makatazo dhidi ya wanawake kwa mambo kadhaa ktk Biblia yalikua sahihi kwa KANISA HUSIKA,ENEO HUSIKA NA KIONGOZI HUSIKA MWENYE MOYO NA WITO WA KWAKWE YEYE ALIOPEWA NA MUNGU NA KWA JINSI ANAVYOKAZANA YEYE KAMA YEYE KUTIMILIZA ILO ALILONALO TOKA KWA MUNGU KATIKA WAKATI HUSIKA YEYE NA KANISA ILO WALIPOKUWEPO KTK USO WA NCHI. Nilisema ivi: Katika Biblia ‘’Kuna Meneno na Matendo ya Mungu pia kuna Maneno na Matendo ya Wanadamu na hata kuna Maneno na Matendo ya shetani, VYOTE vimerekodia humo’’ ni kama inashitua lakini tulia kwanza na ukumbuke bado nimeookoka!nampenda Yesu na napenda/nakwenda mbinguni hence usifanye haraka kunikemea, utapoteza muda. Nilithibitisha ilo kwa hoja izi rahisi kabisa kuelewa kwa anayependa ofcoz kuelewa mambo mepesi tu haya.

  UTHIBITISHO KUA KUNA MANENO NA MATENDO YA MUNGU UMO KTK BIBLIA, UNATOKA UMO UMO KTK BIBLIA YENYEWE

  Biblia, Inasema na kuonyesha kua Wanadamu walikua na Yesu wakati yuko duniani ivyo wakamsikia na kumuona aliyotenda na kusema kisha wakayarekodi, wengine walipewa Neno/oteshwa ndoto za Mungu zenye Neno au ujumbe/wakaona maono yenye ujumbe wa Mungu/ wakatokewa na Malaika wa Mungu na wakapewa jumbe/ Neno la Mungu, walitwaliwa/ingizwa ktk ulimwengu wa Roho ( Mungu) na kisha kisikizishwa Maneno/Sauiti ya ujumbe wa Neno la Mungu wakaundika, waliingiliwa/jazwa na Roho ya/wa Mungu ambaye akasema ndani yao ujumbe au Neno la Mungu au akawapa/ akawahuisha/ akawanunulisha/ akawavuvia akili, ufahamu kujua mambo ya Mungu yaani akawafunulia Elimu na mambo ya Mungu kisha wakayaandika na ikadhihirika wanapoandika e.g. Paul, wengine walisikia moja kwa moja tena kwa masikio ya nyama Mungu alipoongea toka mbinguni au kichakani kinachowaka moto halafu wakaandika hayo waliyoyasikia live nk. Na wengine walisikia moja kwa mojo moyoni mwao Mungu akisema na wao wakasema yakaandikwa. Maandiko/vitabu vifutavyo ni ushahidi.

  A: Injili zote 4- Ni record ya maneno na matendo ya Yesu wakati yuko hapa duniani live- ni sawasawa na mtu kusafiri/kukua/kuishi na JK-kila anakachosema na kutenda, no question unasikia na kuona then una record kisha kesho Daily News au Mwanahalisi/Mawio Newspapers.

  B: Yeremia, Ezekieli, Daudi Isaya na manabii wote wakubwa kwa wadogo-walipewa/ingiziwa/sikia Neno la kusema ndio hayo yaliyorekodiwa katika vitabu vyao

  C: Maandishi ktk Biblia yamesema ivyo kua Maneno yaliyomo ndani ya Biblia ni maneno ya Mungu- 2Peter.1:19-21, 2Peter.3:15-16, Revelation.1:9-11, 2Timothy.3:14-17- Luke.1:1-4- Acts.1:1-3

  UTHIBITISHO KUA KUNA MANENO NA MATENDO YA MWANADAMU UMO KTK BIBLIA, UNATOKA UMO UMO KTK BIBLIA YENYEWE

  Biblia hiyo hiyo iliyosema yale juu, inasema/onyesha maneno na matendo ya Wanadamu..Maandiko/vitabu vifutavyo ni ushahidi.

  A:1Timo.2:12…Paul anasem..Simpi/ I do not give…ruhusa Mwanamke..ni yeye kama Paul ktk kanisa na situation iliyokuwepo, anafanya maamuzi kama kiongozi wa kanisa kusettle issues, kuweka system upon which mambo yafanyike kwa uzuri.Kuchukua hii kama ni criss-crossing Gen-Rev God’s everlasting Word ni influence mbaya ya dini/dhehebu la mhusika, ni stubborn personal software za wanaume na ni ufinyu wa kudaka hasa cha Mungu ni kipi na mtu ni kipi maana tumesha establish fact beyond critic kua Mungu alitumia Watu hai na si wa mochori! Ivyo walikua na hisia zao na muono wao pia tamadanu zao

  B: 1Wakorinto.7:12…Lakini watu wengine nawaambia MIMI wala si Bwana….. Yeye mwenyewe Paul anasema wazi na live kua si Bwana ananena bali Yeye! Hence,Kuhamisha alichokisema hapa brother Po kiwe ni cutting across Heavenly God’s everlasting Word, simply ni ujinga tu na artificial kiroho!=ile kukomalia kua kila kitu ni Mungu ndani ya Bible na eti kwa kufanya ivyo ndio mtu anataka ifahamike kua hana mchezo na Neno la Mungu na heshima aliyo nayo kwa Bible ni nambari 1! mwe!

  C:Marco.10:2-9-Yesu anasema Musa ALIWAANDIKIA KURUSU MEN KUTOA TARAKA kwa sababu ya mioyo yao korofi/migumu halafu anasema LAKINI…(sasa hii ndio ya Mungu)…TOKA ZAMANI haikua ivyo so no room ya taraka. Sasa kuhamisha hii specific instruction kwa particular place tena kwa specific wakorofi humans(kondoo wa Musa), mpaka akaruhusu sasa potelea kwa mbali afanyeje sasa bora wawatimue tu Wake zao, kuifanya kua iyo ndio Word of God kwa vizazi vyote, kuna shoti ya uelewa hapo

  D:Hesabu.20:7-12- Mungu alimwambia Musa kua AUAMBIE/auongelee mwamba mbele yao lakini yeye kwanza akawaita wao waasi halafu akasema Je TUWA tokezee maji kwa mwamba huu kisha AKAUPIGA! Hapa Neno na Tendo la Mungu na la Mwanadamu ni dhahiri

  E:Ayubu.3:1-12-Imeandikwa..na’ilaaniwe siku niliyozaliwa iwe na giza siku iyo na tasa,giza la mauti na liitafune,mwanga usiiangazie,isihesabiwe ktk hesabu za miezi, kwa nini sikufa iyo siku? kwa nini magoti yalinipokea nilipotoka tumboni na matiti yalikuwepo ya kunyonya maziwa? na hata Yeremia.20:14-15-ilaniwe siku niliyozaliwa wala isipate baraka na yule aliyepeleka habari haraka kua kaziliwa beby boy naye atandikwe na laana! Sasa haya ni maneno ya Mungu au simply Watu tu/Wanadamu hawa wametaitiwa na wanalalama basi! You see the human factor/role in the Bible is clear.

  UTHIBITISHO KUA KUNA MANENO NA MATENDO YA SHETANI UMO KTK BIBLIA, UNATOKA UMO UMO KTK BIBLIA YENYEWE
  Biblia hiyo hiyo iliyosema yale juu, inasema/onyesha maneno na matendo ya shetani..Maandiko/vitabu vifutavyo ni ushahidi.

  A :Ayubu.1:7,9-11, 2:2,4-5 –Hapa ni shetani anaongea ( maneno yake) alipohojiwa na Mungu na hapa ni matendo yake devo- Ayubu:1:15-19 na 2:7

  B:Marco.5:9-12 Hapa majeshi ya pepo- Legion yanaongea, hata yanaomba sehemu ya kufukuziwa pia kusihi yasipelekwa nje ya mji/Nchi
  Therefore, kwa msingi huo juu, makatazo na maelekezo juu ya mambo kadhaa kwa Wanawake e.g. kutokua viongozi, kutovaa mavazi fulani, kufunga vitambaa vichwani, ongeza na ya kileo ya kwetu mfano kutoruhusiwa kusoma sana, kua na kazi,kudrive magari,kua na urithi, kugombea nafasi kadhaa za social-economical positions n,k. mambo yafananayo na hayo,yalikua nia kwa ajili ya wahusika na mhusika na SI NENO LA MILELE TOKA MBINGUNI KWA WANADAMU WOTE VIZAZI VYOTE la sivyo THE ONE AND ONLY ONE GENESIS-REVELATION ROLE MODEL BWANA YESU(na si Paul, Musa au Eiya wala Petro au Yohana Mbatizaji) angelisemea! KAMA KWELI HAYA MAKATAZOA YALIKUA NI MAJOR ISSUE AND VERY CRITICAL, A LIFE AND DEATH IN HELL OR HEAVEN THING, hakika, hakika, hakika Yesu mwema angesema. Wala asingekua Paul ndio wa kulianzisha maana Yesu ana hekima na akili nyingi ktk malezi kuliko mwanadamu yoyote. Lakini pia Paulo amekuja baadae ktk huduma, walikuwepo senior wake kabla yake na hawakua na fundisho ilo kua la wote ktk makanisa yote kwa vizazi vyote kwa ulimwengu ule-hii nayo ni so strong stone kuonyesha wazi kua lilianzia kwa Paul na wanae watumishi na definitely liliishia kwa Paul-never to be transferred to us today!

  KAMA MPAKA HAPA LWEMBE AU YEYOTE HUMU WA AINA YAKO, HUJAELEWA KUHUSU WANAWAKE NI WATUMISHI NA THAMANI SAWA NA SISI MBELE ZA MUNGU, BASI IN MY NEXT REPLY UTAKAPO JIBU, NITAHOJI MASWALI KADHAA AMBAYO NITAPENDA UJAJIBU KISHA TATIZO ULILO/MLIO NALO/NAYO LITAKUA/YATAKUA PEUPE HADHARANI KABISA.

  Kwahiyo,swali lako hili-’’Basi kwa kutumia Akili, Reason, na Reasoning of Reason, Logic; ninakuambia hivi: statement yako hiyo si ya kweli, kwa sababu ndani ya Biblia hakuna maneno ya Mungu wala maneno ya Yesu! Labda unithibitishie vinginevyo!’’ limejibiwa na nyongeza nyingi kua yapo pia umo umo maneno na matendo ya Wanadamu na devo, all recorded in the same BOOK, simple!!!!!!!!!!!!!!period!

  Press on.

 154. Biblia hiyo hiyo iliyosema yale juu, inasema/onyesha maneno na matendo ya Wanadamu..Maandiko/vitabu vifutavyo ni ushahidi.

 155. Jambo ambalo nimeliona kwako Seleli, ni kwamba you are very sincere katika haya unayoyafundisha, lakini sincerely wrong!! Kwahiyo nimerudi kwa sababu you are my brother in Christ, and I love u!

  Nikikuunga mkono katika “Kutokuzitegemea akili zako, bali Kuzitumia”, ingawa sijafika katika kukuelewa sawa sawa ni kwa jinsi gani unaweza ukaitumia akili yako bila kuitegemea, lakini potelea kwa mbali, nairejea moja wapo ya zile statement zako 
  “NI KWELI TUPU KUA BIBLIA NI / INA MANENO NA MATENDO YA MUNGU YALIYOREKODIWA HUMO, na upande wa pili wa coin iyo iyo, BIBLIA INA MANENO NA MATENDO YA WANADAMU YALIYOANDIKWA HUMO.”

  Basi kwa kutumia Akili, Reason, na Reasoning of Reason, Logic; ninakuambia hivi: statement yako hiyo si ya kweli, kwa sababu ndani ya Biblia hakuna maneno ya Mungu wala maneno ya Yesu! Labda unithibitishie vinginevyo!

 156. Lwembe,

  ‘’Unajua inasikitisha sana unapomuona ndg yako anapanda ndege ya kwenda Mtwara kwa furaha ilhali safari yenu ilikuwa ni ya Mwanza!- Si kweli, acha maneno kwa kua kama ndugu huyo si mgonjwa medically au hajanyukwa na jini, akipanda ya Mtwara, hakika ana kwenda Mtwara! Wewe kama unadhani anapaswa kwenda Mwanza, then show him before he lands in Mtwara mistakenly, otherwise, the Mtwara going brother knows beyond query that, where is heading ndio destiny yake kwa HAKIKA, hence plz reserve your free offered unnecessary huruma, I hope wako wengi wanahihitaji uko brother.

  ‘’Amelikataa Neno la Mungu’’- unajua kama Mtu wa Mungu nilye na Yesu kama Bwana na Mwokozi, siwezi kulikataa Neno.Plz acheni maneno mepesi ktk hot debate bwanaa!

  ‘’Bible Yote, entirety ni Neno la Mungu’- NDIO lakini humo humo kumerekodia maneno, matendo hata vutuko vya wanadamu eg Daudi kumset Uria kupigwa mkuki/mshale afe kisha kujitwaliwa wife wake! Kituko kweli icho cha mpendwa David, nacho kimeandikwa umo umo kwenye maneno pure ya Mungu! mbona rahisi kabisa hii kuelewa?

  ‘’Kukuona kwamba umeshuka chini sana katika ufahamu’’= haya ndio yale maneno mepesi ya wenzio ktk comments mbalimbali ambayo kwa kweli ni kuyacha tu maana kama huthibitishi mtu ameshuka ufahamu au si makini au ana malaria, upuuzi, degedege disease History basi wayasemayo hayo, wanaweza ku ndio wenyewe haswa au victims indeed wa hayo madude.

  Umeshangaa mimi kwa ujasiri kabisa kusema ivi ktk Bible kuna ‘’MANENO NA MATENDO YA MUNGU YALIYOREKODIWA HUMO, na upande wa pili wa coin iyo iyo, BIBLIA INA MANENO NA MATENDO YA WANADAMU YALIYOANDIKWA HUMO’’ Sasa see jinsi mnavyoshangaza ktk debate skills zenu! Wewe mwenyewe umedokeza hiki-‘’Pia umo kuna- Maneno ya Shetani, maana hiyo ndiyo version kamili ya wote walioaminishwa hivyo!’. Sasa u see, kwa hiyo unataka kukataa ndani ya Bible maneno ya devo hayajerekodiwa? Huyu ni nani hapa anaongea wakati Mungu amemuuliza unatoka wapi?Ayubu.1:7,9-11, 2:2,4-5 Na je wakati Yesu anataka kutimua pepo kwa yule jamaa, unakumbuka aliuliza nini? so yule aliyojibu ni Mungu eti eee? yale ni maneno ya Mungu Baba wa Mbinguni? Marco.5:1-10. Na ‘’majamaa’’ yale yalipomuomba Yesu ayafukuzie kwa pigs, yale maombi ni maneno ya Roho Mtakatifu eti ee? Very sadly funny indeed Lwembe my brother.

  Hii ndio HASARA ya kutumia akili katika mambo ya Mungu!!! Hapa nitasema kidogo kwa ili kwakua imekua tatizo/ BASELESS COMMON EXCUSE kwa Wapendwa wengi sababu ya mapokea mabaya( yapo mazuri) kuhusu matumizi ya Akili. Kwanza Biblia inadokeza kutozitegemea /lalia/egemea akili na si KUTOZITUMIA-Mithali.3:9.Lakini part (a) ya verse iyo inaanza kwa kusema, ‘’Trust in the Lord with all your heart’’. Kwaiyo kuna connection/facts hizi 2, kwanza, akili ambayo ina-operate yenyewe bila kua na Mungu kwanza/kua dictated au kushikwa somewhere na Mungu, iyo ndio hatari lakini wakati imeshikwa/ambatanishwa/inahusiana na Mungu-ndio maana ya wakati mtu ame’Trust in the Lord with all his/her heart’, wow! great Akili shall that be, no wonder Paul anasema ivi CONFIDENTLY ktk Mdo 26:25 ‘ninasema maneno ya ukweli na ya Akili( Kiingereza NKJ imetumia maneno ‘’words of truths and reason- ndani ya reasoning kuna akili, intellect, IQ, logic, thinking usages. Ishu ni kua ndani ya Mungu,moyo wote kwake kisha yote uliyonayo na Akili ikiwemo vinakua wonderful tools to use hence, wacha uvivu Lwembe, think and think deeply coz you are connected with Master, He is in control of you except bad spirit interference ya dhehebu/dini yako ku-degrade Wanadamu mbele ya Mungu kisa wanawake! Simpy, you ensure all the time uko under His coverage ya Neno lake, Roho wake, terms zake, knowledge yake nk then use Akili tu. Besides, na hii je- 1Wokorinto.6:19- baada tu ya kuokoka, our bodies are the temple of the Holy Spirit, sasa wakati Holy Spirit ndiye Mkaazi rasmi but also final admin Officer ndani ya nyumba yake-Miili yetu ambayo ina akili pia,kwa nini tusizitumie/asizitumie vema sana akili izi? Kwa iyo being anointed is no excuse for thinking, you be as anointed as Mount Kilimanjaro, be filled by Holy Spirit like never before yet you can also think-a function of Akili usage.

  “Role model wetu katika wanadamu wote ktk Bible ni YESU si Paul wala Musa!” ni Cult Spell- usi- exaggerate Lwembe, hamna cult thing hapa, acha vitisho bro kwa kua wewe mwenyewe umenukuu hii..“Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo” 1Kor11:1 Sasa embu tumia Akili izo izo unazotaka zikae tu bila kutumiwa kutakafari mambo ya Mungu, here we go- Kama Paul amesema tumfuate yeye KAMA ANAVYOMFUTA KRISTO, who is real or final role model hapa? Aaa jamani lo! mbona very cheap mtu wa Mungu wewe ii kitu! Alternatively, ngoja nikubrainstorm kidogo kwa swali hili then u will get it right niliposema na bado nasema, wengine wanaweza kua role model but the real one, ni Master mwenyew. Mfano: Ukikuta labda Paul na Petro au Yakobo ktk writings zao kuelezea concept fulani ya Mungu au watu wa MUNGU wakawa wanapingana/hawakubalini, unachukua lipi? Wapi au nani utachukua as final? au pia hujui ilo kua Waandishi walikua ni wanadamu si MALAIKA kama nilivyosema hoja no 2 ktk post yangu wakati nina weka carpet kabla sijajibu hoja 3 za Milinga? Embu soma aliyosema Yakobo kuhusu kupata haki kwa matendo na aliyosema Paul au angalia aliyosema Yakobo kuhusu matajiri/maskini na imani vs Paul na swala zima la kua na imani kwa kila mtu….hapo unafanyaje? Nani role model? Yakobo, Paul au at last ni JIWE KUU LA PEMBENI? Halafu kama wao wenyewe e.g. Paul anasema ana role model wake anayemfuta, why unakua na care/huruma/hofu za ajabu kwa status ya Paulo wakati yeye kashakupa live anaye wake? Mbona una presha ya bure wakati rafiki yangu Paul waaala hana mpango na kwakweli atakushangaa that day kwa credit crossing line unazompa!

  ‘’Maana sioni reference point itakayotuongoza katika majadiliano na mtu ambaye haiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu= this one is cheap, therefore it is not given weight bro

  Naona its a waste of time and energy ku engage na mtu wa jinsi hiyo, kwa sababu itakuwa ni UNAFIKI!!!-You know precisely that as long as you bring a point Biblically BOTH ANGLELS balanced, there will be no wastage of time and energy at all. Failure to engage in such discussions (East-West, North-South many truths of the Bible is not only baseless excuse but also a little premature escape.

  ‘’May the Grace of God catch you before you HIT that pit! I refuse such ‘sembe’ motivated prayers because no pit toward which I am heading rather I am Hitting things against religious and badly sick people of God who would advocate Women degradation in the name of spirituality maintenance of which, the interpretation of their so called Biblical Spirituality as far as the women’s roles in God, is with fault in the first place and severely virused!

  ‘’Ciao!!- No brother, it should be Ciao Again!

  ‘’Over & Out’’- I encourage you that it should be Over and Out and IN….Don’t go away….welcome in brother.

  Press on

 157. Ndg yangu Seleli umenishangaza saana kwa haya uliyoyaandika!
  Unajua inasikitisha sana unapomuona ndg yako anapanda ndege ya kwenda Mtwara kwa furaha ilhali safari yenu ilikuwa ni ya Mwanza!

  Kwa ufahamu nilionao ni kwamba hali kama yako humpata mtu ambaye amelikataa Neno la Mungu katika wakati fulani katika maisha yake na hajawahi kujirudi bali anaendelea kusonga mbele!

  Ili kulidhihirisha jambo hili, ninapick statement zako mbili, ambazo kwa ushahidi kulingana na Biblia, kwangu mimi ambaye ninaiamini kuwa Yooote, in its entirety ni Neno la Mungu, zinanitosha kufikia kukuona kwamba umeshuka chini sana katika ufahamu:

  A: “NI KWELI TUPU KUA BIBLIA NI / INA MANENO NA MATENDO YA MUNGU YALIYOREKODIWA HUMO, na upande wa pili wa coin iyo iyo, BIBLIA INA MANENO NA MATENDO YA WANADAMU YALIYOANDIKWA HUMO.”

  Nadhani umesahau kuwa humo yamo pia maneno ya Shetani, maana hiyo ndiyo version kamili ya wote walioaminishwa hivyo! Hii ndio HASARA ya kutumia akili katika mambo ya Mungu!!!

  B: “Role model wetu katika wanadamu wote ktk Bible ni YESU si Paul wala Musa!”

  Ili mtu afike katika KUAMINI kwamba yaliyomo ndani ya Biblia si Neno la Mungu pekee, hatua yake ya kwanza, hapo anapokuwa initiated into that Cult Spell, huwa anatenganishiwa viungo vya Mwili wa Kristo, vinabanguliwa na kufanywa independent, na kuanzia hapo, they are gone, down into that pit!!!

  Huyo mt Paul, ambaye Mungu alimchagua awe mwalimu wetu, ambaye wewe unamuona “SI ROLE MODEL” ya kukufaa wewe uliye mjuzi wa Maandiko, uliyejazwa Roho Mtakatifu mpaka anafurika, akikuinua katika hayo majigambo; lakini mtume Paulo anatuambia Kanisa, hao wenye kumthamini kama ROLE MODEL yao, anasema, “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo” 1Kor11:1 Huu ndio ukweli wa Injili, mwenye kuupenda ujinga na aendelee katika ujinga wake, lakini katika siku hiyo ya Hukumu, gharama ya ujinga huo wa kujitakia italipwa kwa kipimo cha haya ambayo leo unayaona si Role model, lakini Mungu ameyachagua hayo yawe ndiyo Role model katika kuhukumu! Rum 2:16 “…katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”

  Unajua kinachomfika muumini wa kimwili? Kama ambavyo Adamu alijitenga na Neno la Mungu ili aambatane na mkewe, ndivyo muumini wa kawaida anavyojitenga na Neno la Mungu ili aambatane na mafundisho ya dhehebu lake! Bali hakuna tena Damu kwa ajili yake huyo anayejitenga leo hii!!!

  Kwahiyo huku kujiongelesha kwako mambo haya, it closes the chapter, maana sioni reference point itakayotuongoza katika majadiliano na mtu ambaye haiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu, naona its a waste of time and energy ku engage na mtu wa jinsi hiyo, kwa sababu itakuwa ni UNAFIKI!!!

  Thank you so much, my onetime brother, may the Grace of God catch you before you HIT that pit!

  Ciao!!,

  Over & Out!

 158. Sungura, labda nikuulize kidogo, maana yawezekana kweli nikawa silijui jambo hili la “nchi ya maziwa na asali”, kwamba mimi nilidhani ni “the land of plenty” au ni nchi ambamo wanawake wanaruhusiwa kufundisha na kuwatawala waume zao, yaani nchi ambayo inadumisha ‘haki sawa kwa wote’, halafu hata hizo haki zenyewe hazijawa defined, kwa lugha nyepesi, ‘Democracy’ ambayo it’s all sails without an anchor!; Yaani the carnal church??

  Boy, the true Church of God is anchored in Christ, the Word! And she is sold “lock, stock and barrel” to It! Tunafuata kinachofundishwa na Biblia sio what some back slid pastor is teaching!

  Kuhusu Petro, unaweza ukadhani kuwa Petro aliwaonya waamini huko nyuma tu, lakini maonyo hayo yako valid hata leo hii, hauwaoni watu wanavyopotea kwa kujaribu kuyafafanua au kuyatafsiri mafundisho yake kwa kutumia akili? Kama Paulo alipewa hayo kwa ufunuo, sioni ni kwa jinsi gani mtu asiyekuwa na ufunuo atayaelewa hayo!

  Sijajua kwa uhakika mindset yako imeelekezwa upande gani haswa, hapo unaposema, “… ni kwa sababu yalikuwa yako kiwango cha juu sana cha kisomi na maarifa.” Kwamba unautukuza usomi wa Paulo, kuwa ndicho kigezo Mungu alichokitumia kumchagua? Bali mimi ninaamini kuwa Paulo alipelekwa shule bora zaidi na alipewa uwezo wa kuyaelewa yaliyofundishwa huko ili atakapogeuka kuifundisha Injili, basi ijengeke juu ya msingi wa mitume, hiyo Injili mpya aliyofunuliwa, na manabii, hayo aliyojifunza huko katika Ufarisayo! Pia aweze kukuhubiri na wewe Sungura, the intellectual person wa leo! Hiyo ndiyo sababu pekee mimi na wewe tumepelekwa shule kusoma, ili tuweze kuipata Injili, ule uzima wa milele, ndani ya Biblia aliyotutayarishia kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa na si mitaani! Efe 1:4 “…kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu…”

  Wanawake ni mabinti wa Mungu, tena anawapenda sana! kwahiyo Mungu kuwatumia walio wake, kuna ajabu gani Sungura? Pia nadhani unajua kuwa hao waliumbwa ili wawe wasaidizi wetu wanaume, umeiona Hekima ya Mungu?

  Hapa naona unasema nimeacha ile Yoeli 2:28-29, hapana sikuicha, itakuwa kichwa chako kilipata moto baada ya kupagawishana na Seleli, lakini ngoja niyanukuu tena niliyoyaandika:

  “”Kuhusu Yoeli 2:28-29, ninaamini jambo hilo lilitimia katika siku ya Pentekoste, kama Petro alivyoyarejea Maandiko kwa RM! Kwahiyo kama ndg yangu Sungura unataka ufafanuzi wowote ule kuhusu jambo hilo, ninakushauri uchangamshe akili, badala ya kuendelea kuwa mtumwa wa mawazo ya maprofesa wa dini, rudi katika Maandiko utaupata ufafanuzi ulio fresh from the Throne! Jambo lililotokea siku hiyo ndio UFAFANUZI wa Maandiko hayo kaka!!! Umezoea theory tu? Inapokuja vitendo unachemka!

  Kwani ktk siku ile ya Pentekoste, kulikuwa hakuna wanawake pale juu? Walikuwepo tele, mpaka “Mariamu mama wa Mungu” alikuwepo pale juu, na walijazwa RM katika kipimo kile kile walichojazwa wanaume waliokuwepo! Ila hauwaoni wakiinuka kufundisha kwa sababu wamejazwa RM!!! Hiyo ndiyo sababu pekee ambayo inamfanya mwanamke asiinuke kuyavunja Maandiko, huko Kujazwa RM!!! Mwanamke aliyeupitia Ubatizo wa RM hawezi kuinuka kufundisha, maana huyo Roho aliye ndani yake ndiye huyo aliyeyaandika hayo yanayomkataza! Kazi ya RM ni kuviongoza vipawa vyake kufanya kazi katika utaratibu alioupanga na kuvitoa!!!””

  Karibu ndg yangu Sungura katika “nchi ya Maziwa na Asali”!!!

 159. Lwembe ukisema kuwa sisi tumepumbazika hiyo hainipi shida, nilishazizoea hizo kauli zako.

  Lajini uko palepale kwamba watu wengi hawaelewi lugha ya picha ambayo biblia imetumia. Uliza wangapi wanajua maana ya nchi ya maziwa na asali. Hata wewe mwenyewe sina hakika kama unajua sawasawa.

  Petro mwenyewe aliwaonya waamini kwamba wawe makini na mafundisho ya Paul. Si kwa sababu yalikuwa potofu au yalikuwa magumu au si kwa sababu hao waumini hawakuwa na Roho mt, bali ni kwa sababu yalikuwa yako kiwango cha juu sana cha kisomi na maarifa.

  Halafu jiulize hili swali la kawaida, kwamba kwa nini Mungu anawatumia wanawake wanaomtumikia?

  Lakini hata hivyo mbona umeongelea tu Wagalatia3:27-28, halafu ukaacha kitabu cha Yoel 2:28-29?
  Asante Lwembe.

 160. WANAWAKE NA MAKATAZO KTK BIBLIA

  HOJA NO. 3-Mafundisho ya kukataza wanawake kuvaa suruali ili hali zinafunika uchi na mwili wao kwa usahihi zaidi kuliko hata siketi na gauni.

  HOJA NO. 9-Mafundisho ya kuzuia wanawake wasiwe viongozi wa kanisa au wasiruhusiwe kufundisha

  HOJA NO. 10- Mafundisho ya kuzuia wanawake kufanya kazi zenye kipato kwa misingi ya dini au mafundisho

  MAONI: Kabla ya kwenda mbali, ninapenda niwahamasishe KWA MOYO WANGU WOTE NA RAHA NAFSINI, NAWASHAWISHI ENYI VIUMBE WOTE WANAWAKE, MSOME HII MAKALA. Naanza kwa kuweka ‘kapeti nyekundu’’ kwanza kama ifuatavyo kisha hoja 3 kwa mpigo hapo juu zitajiseti tu zenyewe!

  Kwanza, Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vyenye Maneno ya Mungu kwakua Mungu aliwatumia Watu ili Maneno yake yapite/yaandikwe: 2Peter.1:19-21- PETER SAYS HUMANS SPOKE FROM GOD AS THEY WERE CARRIED ALONG BY THE HOLY SPIRIT-carried by Holy Spirit’- Hence what they spoke is the Word of God), 2Peter.3:15-16-PETER SAYS WHAT PAUL WROTE, WAS FROM GOD GIVEN WISDOM (an understanding/revelations as inspired/released by God to someone)- Hence what He wrote is the Word of God, Revelation.1:9-11-JOHN SAYS THAT HE WAS IN THE SPIRIT AND HE HEARD LOUD VOICE TELLING HIM TO WRITE TO 7 CHURCHES-Hence what He heard and wrote is the Word of God, 2Timothy.3:14-17-All SCRIPTURE IS GOD-BREATHED)-Hence all scriptures in the Bible is God’s life/breath/word-Luke.1:1-4-LUKE WRITES A CAREFULLY INVISTIGATED AN ACCOUNT OF JESUS FROM THE EYEWITHNESSES AND SERVANTS OF THE WORD-Hence what He wrote from those who heard/saw Jesus (what He did and say) must be the Word of God because Jesus is God, Acts.1:1-3-LUKE WROTE ALL ABOUT JESUS DEEDS/WORDS-Hence because He wrote what Jesus did/said, what is contained is the Word of God

  Pili, Kwakua waliotumiwa kuandika/kusema/kutamka Maneno ya Mungu ktk Biblia hawakua Malaika( WAKAMILIFU KWA KILA KITU) bali Wanadamu na ingawa walikua Wanadamu lakini pia hawakua ‘marobots’, ‘mabox’, ‘madoli ya plastics,’ ‘matikiti maji’ basi ni ukweli ulio wazi kua ndani ya Biblia iyo iyo yenye Maneno ya Mungu, kuna sehemu ya Mwanadamu( In fact an active human factor/role).Kukataa ukweli huu basi bila kujua au kwa kujua,mhusika anasema Mungu alitumia wanadamu walioko ‘mochwari’. Sasa kwakua Mungu hushirikiana/huwatumia Wanadamu walio hai wakiwa na akili,nafsi,roho,moyo,mwili,hisia,utashi,tamaduni(mila na desturi) pia wanaoishi ktk jamii,mfumo fulani wa Siasa na Serikali, waliosoma elimu za fani mbalimbali na elimu izo zikawajaa vema, wanaoishi na kukuzwa/kulia katika kanuni fulani ndani ya familia na koo zao, na kwamba wana asili zao kama watu/wanadamu binafsi yaani ‘’particular software’ zao walizozaliwa/umbwa nazo( that unique part of each person hata kama ni mapacha wa yai moja yet ni tofauti na ushahidi ni kidole gumba au shape ya sikio kwa ndani vinavochukuliwaga alama ili kutofautisha mwanadamu mmoja na mwingine), tena walioshi sehemu na nyakati tofauti, basi ktk Biblia kutakua na TOFAUTI PIA KATIKA NAMNA YA KUYABEBA/SEMA/ITIKIA /TAMKA/SIMAMIA MAMBO AU MANENO YA MUNGU NA WATU WAKE.

  Tatu, Kwa hoja mbili hapo juu, basi nina ujasiri wote kusema ktk Biblia kuna Maneno ya Mungu na Mambo ( maneno, matendo) ya Wanadamu kama Watu wala si ya Mungu na wala si yeye aliyewavuvia/wafanya wayafanye/seme bali walifanya/sema kwa utashi wao kama binadamu ingawa yote ya Mungu na Watu, vimerekodiwa humo ktk Book moja linaitwa Bible kwa ajili yetu sisi tuliyofikiriwa na miisho ya nyakati-1Wakorinto.10:11.Kwa nguvu sana tunaweza conclude hivi na bado tukawa salama kimahusiano yetu na Mungu na Roho Mtakatifu( in fact hata YEYE/WAO wanajua ilo but presha/misismko/mihemko yetu tu sometimes inatupelekaga puta) kua upande mmoja wa shilingi, NI KWELI TUPU KUA BIBLIA NI / INA MANENO NA MATENDO YA MUNGU YALIYOREKODIWA HUMO, na upande wa pili wa coin iyo iyo, BIBLIA INA MANENO NA MATENDO YA WANADAMU YALIYOANDIKWA HUMO.

  Nne, Mifano ya active role/factor ya Mwanadamu ktk Biblia yenye Maneno ya Mungu ni kama ifuatavyo: Hapa nakusudia ku-establish more hoja no. 2 juu hapo kuonyesha uanadamu ambao si Mungu alihusika bali wao wenyewe ivyo kuchukulia kila kitu ktk Bible kua ni Neno la Mungu ni tatizo la ufahamu tu na kukaririshwa toka zamani maana tulikua tunameza tu na kwamba mtu akielimishwa, atapata ufahamu/uelewa na kama hatakataa na kukomalia aliyomeza siku za zamani then na adumu ivyo ivyo na tutakutana kwa Baba JUU.
  A:1 Timo.2:12…Paul anasem..Simpi/ I do not give…ruhusa Mwanamke..ni yeye kama Paul ktk kanisa na situation iliyokuwepo, anafanya maamuzi kama kiongozi wa kanisa kusettle issues, kuweka system upon which mambo yafanyike kwa uzuri.Kuchukua hii kama a criss-crossing Gen-Rev God’s everlasting Word ni influence mbaya ya dini/dhehebu la mhusika, ni stubborn personal software za wanaume na ni ufinyu wa kudaka hasa cha Mungu ni kipi na mtu ni kipi maana tumesha establish fact beyond critic kua Mungu alitumia Watu hai na si wa mochori!
  B: 1Wakorinto.7:12…Lakini watu wengine nawaambia MIMI wala si Bwana….. Yeye mwenyewe kamanda Po anapangua/chana wazi na live kua si Bwana ananena bali Yeye! Hence,Kuhamisha alichokisema hapa brother Po kiwe ni cutting across Heavenly God’s everlasting Word, simply ni ujinga tu na artificial kiroho!=ile kukomalia kua kila kitu ni Mungu ndani ya Bible na eti kwa kufanya ivyo ndio mtu anataka ifahamike kua hana mchezo na Neno la Mungu na heshima aliyo nayo kwa Bible ni nambari 1! mwe! mmh! hamna lolote, lack of understanding tu!
  C:Marco.10:2-9-Yesu anasema Musa ALIWAANDIKIA KURUSU MEN KUTOA TARAKA kwa sababu ya mioyo yao korofi/migumu halafu anasema LAKINI…(sasa hii ndio ya Mungu)…TOKA ZAMANI haikua ivyo so no room ya taraka. Sasa kuhamisha hii specific instruction kwa particular place tena kwa specific wakorofi humans(kondoo wa Musa), mpaka akaruhusu sasa potelea kwa mbali, wawatimue tu Wake zao na kuleta akina mwali wapya, kuifanya kua iyo ndio Word of God kwa vizazi vyote, kuna shoti ya uelewa hapo.
  D: Hesabu.20:7-12- Mungu alimwambia Musa kua AUAMBIE/auongelee mwamba mbele yao lakini yeye kwanza akawaita wao waasi halafu akasema Je TUWA tokezee maji kwa mwamba huu kisha AKAUPIGA! Hapa Neno na Tendo la Mungu na la Mwanadamu ni dhahiri but reccorded in the same, same Holy Book.
  E: Ayubu.3:1-12-Imeandikwa..na ‘’ilaaniwe siku niliyozaliwa,iwe na giza siku iyo na tasa,giza la mauti na liitafune,mwanga usiiangazie,isihesabiwe ktk hesabu za miezi, kwa nini sikufa iyo siku? kwa nini magoti yalinipokea nilipotoka tumboni na matiti yalikuwepo ya kunyonya maziwa? na hata Yeremia.20:14-15-ilaniwe siku niliyozaliwa wala isipate baraka na yule aliyepeleka habari haraka kua kaziliwa beby boy naye atandikwe na laana! Sasa haya ni maneno ya Mungu au simply Watu tu/Wanadamu hawa wametaitiwa basi! You see the human factor/role in the Bible is clear.

  Kwa iyo ni sahihi kabisa Tunaposoma Biblia, kua na ufahamu wa mambo mengi kama nilivyoorodhesha ktk hoja no. 2 ambayo na kuya-summary yote ni sawa na kusema, ktk Biblia kuna 1.MANENO NA MATENDO YA MUNGU, 2. MANENO NA MATENDO YA WANADAMU na vyote ivyo vime rekodiwa humo humo. Kwa maana iyo Yesu alikua sahihi kusema/kumuangalia Musa kama Musa alipojibu kua aliwaandikiwa/elelekeza watu kutoa taraka kwa sababu ya ugumu ya mioyo yao lakini si Mungu alisema ivyo au ilo jambo (neno la Musa) halikua nina la Mungu ndio maana ya Yesu kusema ..TOKA MWANZO HAIKUA IVYO! Kwa msingi huu muhimu sana, sasa nina-respond hoja tatu za Milinga..No. 3,9,10 kirahisi kabisa na hata nikiachia hapa, mwenye ufahamu amesha nidaka haraka/kitambo, kama ifuatavyo:

  HOJA NO. 3-Mafundisho ya kukataza wanawake kuvaa suruali ili hali zinafunika uchi na mwili wao kwa usahihi zaidi kuliko hata siketi na gauni.
  MWITIKIO: Ni Fundisho la KWELI kwa kanisa lile na kwa wakati ule na kwa situation ya wakati ule, mahala pale.Paul kama kiongozi wa kanisa na Baba, alikua anaweka utaratibu particularly kwa kanisa husika ndio maana hatuna ushahidi kua alisambaza barua/doctrine/directive hi ya kukataza ‘matroza wearing’ kwa ladies kwa makanisa mengine. Ingekua kweli amepewa ilo kama ni once for all the Neno la Mungu kwa vizazi vyote, He was such smart man kiroho na kiakili hence would have ensured this ina cut across kwa wana wake wote wa kiroho ktk makanisa yote ktk ulimwengu ule. Besides, at least hata Kanisa MAMA Jerusalemu, wangeli-back hii Paul’s spiritual administrative decision iwe kwa wote but they did not! Ukweli huu una clear hata mambo yale mengine aliyosema/agiza/shauri/elekeza ya kufuga nywele ndefu kwa wanaume or kunyoa, kufunikwa vichwa kwa wanawake na mambo yanayofanana na hayo. Kulihamishia fundisho/elekezo ili particular la brother Po kama lilivyo kwetu leo sisi ni UPOTOFU na kwa kweli ni UJINGA-which means, elimu inatakiwa ipite, watu waelimishwe, then easy like that, watakaa line clear.

  HOJA NO. 9-Mafundisho ya kuzuia wanawake wasiwe viongozi wa kanisa au wasiruhusiwe kufundisha.
  MWITIKIO: The above jibu lina appy perfectly hapa, Nyongeza ni kwamba, Role model wetu katika wanadamu wote ktk Bible ni YESU si Paul wala Musa! KAMA YESU ALIKUA SO POSITIVE, CARING and COOPERATIVE TO WOMEN needs/dignity(fanya survey and see Jesus and mwitikio wake kwa kila women aliyekutana naye) then example yake MUST be no. 1 to CUT( copy haitoshi) and Paste. Hii haimaanisha hata kidogo kua Kaka Paul did wrong, a big NO! He was simply as Kiongozi wa particular group, playing his role to settle the things in order. Besides, Angalia ktk Bible MUNGU ALIVYOTUMIA WANAWAKE TOKA AGANO ZEE NA JIPYA that by itself should tell somebody kua alichofanya Paul was specific and limited to him and his group and never to be taken as universal God’s commandment. Hence, kuliahamishia kama lilivyo kwetu leo ni UPOTOFU NA UJINGA.

  HOJA NO. 10- Mafundisho ya kuzuia wanawake kufanya kazi zenye kipato kwa misingi ya dini au mafundisho.
  MWITIKIO:The above majibu yana-apply hapa, nyongeza ni kwamba hasiye fanya kazi, asile, ili-cover wote lasivyo angekua specific pia kama nilivyosema mwanzoni ktk hoja no. 2 kua ‘software’ za watu e.g. kama wanaume zitawaendesha/sukuma kufanya maamuzi dhidi ya Wanawake na kutafuta uhalali Ki-Mungu lakini ukweli kwamba maamuzi/matamko/maneno/makatazo hayo yametoka kwa mla dona tu, Mtu mwanaume mkorofi huyu, utabaki ivyo, hence, kuwakataza wasifanye kazi, ongeza hata wasisome sana, kufanya biashara zizonalipa sana, situ ni UPOTOFU NA UUJNINGA bali pia ni WOGA NA UBINAFSI WA WANAUME. Embu na tupone sie wanaume in Jesus name, amen.

  Amani ya Kristo iwe nanyi enyi nyote,

  Press on,

  Edwin Seleli

 161. Naam Sungura,
  Binafsi sioni shida yoyote katika Andiko lolote lile, bali nawaoneni ninyi ndio mnaohangaika na tafsiri zenu.

  Lugha pia katika mambo ya Mungu sio tatizo, ikibidi Mungu mwenyewe hushuka ili kuyatafsiri hayo anayoyasema, angalia kilichofanyika siku ya Pentekoste au pale nyumbani kwa Kornelio, au alivyomkalisha Paulo kumfunza, kuna mtu iliyemtoka mishipa ya shingo kutafsiri hayo?!

  Unaniambia, “biblia inaposema neno ”nchi ya maziwa na asali” mtu wa tabora lazima ataanza kuona asali kichwani mwake, na mmasai na msukuma lazima wataanza kuona maziwa vichwani mwao maana wanadamu huwa tunafikiri kwa picha.” Kwa upande wangu kauli kama hizi zako, ninaamini ndizo zinazo wapumbaza zaidi ninyi wenyewe kuliko hao wasukuma au wanyamwezi kama unavyodhania. Hebu nikuulize, mtu akisema, “maisha ni matamu sana!” wewe huwa unayapima katika utamu gani, wa asali au chumvi?

  Kuhusu kujifunza wajibu/kazi ya RM kwa mwamini, hilo ni kweli, maana wengi wetu hatujui kazi yake sawa sawa. Wengine hudhani kazi ya RM ni kunena kwa lugha au kukupa ndoto, au kukupa msisimuko fulani nk. lakini kazi ya RM ni kukufunulia Neno la Mungu, akikuweka katika kweli yote, akikuonesha wabishi waliopo na watakaokuja, ndio maana kwa RM, mt. Paulo anatamatisha kuhusu wabishi, hao watakao kuwepo leo hii kuyabishia aliyoyafundisha katika kuweka Msingi wa Kanisa, kwa kuwaambia kwamba “mtu akitaka kuwa mjinga na awe mjinga”!

  Kuhusu Yoeli 2:28-29, ninaamini jambo hilo lilitimia katika siku ya Pentekoste, kama Petro alivyoyarejea Maandiko kwa RM! Kwahiyo kama ndg yangu Sungura unataka ufafanuzi wowote ule kuhusu jambo hilo, ninakushauri uchangamshe akili, badala ya kuendelea kuwa mtumwa wa mawazo ya maprofesa wa dini, rudi katika Maandiko utaupata ufafanuzi ulio fresh from the Throne! Jambo lililotokea siku hiyo ndio UFAFANUZI wa Maandiko hayo kaka!!! Umezoea theory tu? Inapokuja vitendo unachemka!

  Kwani ktk siku ile ya Pentekoste, kulikuwa hakuna wanawake pale juu? Walikuwepo tele, mpaka “Mariamu mama wa Mungu” alikuwepo pale juu, na walijazwa RM katika kipimo kile kile walichojazwa wanaume waliokuwepo! Ila hauwaoni wakiinuka kufundisha kwa sababu wamejazwa RM!!! Hiyo ndiyo sababu pekee ambayo inamfanya mwanamke asiinuke kuyavunja Maandiko, huko Kujazwa RM!!! Mwanamke aliyeupitia Ubatizo wa RM hawezi kuinuka kufundisha, maana huyo Roho aliye ndani yake ndiye huyo aliyeyaandika hayo yanayomkataza! Kazi ya RM ni kuviongoza vipawa vyake kufanya kazi katika utaratibu alioupanga na kuvitoa!!!

  Na kuhusu Wagalatia 3:27:28, Ili uvielewe vizuri vifungu hivi vya Maandiko, itakulazimu kwanza uende na hiyo order, yaani huko kubatizwa katika Kristo, na kumvaa Kristo. Basi kubatizwa katika Kristo ni nini, na hata huko kumvaa? Kristo ni Neno la Mungu, nalo Neno linalomfunua Kristo ni kutoka Mwa 1:1 hadi Ufunuo 22:21. Ndipo ukikwama popote pale, au ukajiwekea tafsiri zako, huyo anakuwa si Yeye, unakuwa umebatizwa na kumvaa kristo wa kuchorwa ukutani au ubaoni huko chuo! Basi hebu kagua ni makristo wangapi wa kuchora waliovaliwa leo hii wakila pose ya Kristo?

  Halafu jitahidi uwe unajibu maswali unayoulizwa

  God bless u brother!

 162. Lwembe ndugu yangu,
  Kinacholeta shida siyo kilichoandikwa katika hayo maandiko yenye kutatiza. Bali ni ile lugha iliyotumika na jinsi sisi tunavyoielewa.

  Kumbuka jambo moja kwamba lugha ya asili ya biblia siyo Kiswahili, siyo Kiingereza,na wala si Kigiriki. Kwa hiyo ili kuelewa hasa nini kilimaanishwa ni lazima uangalie kwenye lugha ya asili.

  Mfano; biblia inaposema neno ”nchi ya maziwa na asali” mtu wa tabora lazima ataanza kuona asali kichwani mwake, na mmasai na msukuma lazima wataanza kuona maziwa vichwani mwao maana wanadamu huwa tunafikiri kwa picha.

  Lakini wayahudi walijua kuwa kunachoongelewa hapo hakikuwa maziwa na asali. Ndio maana wapelelzi waliporudi hawakurudi na chupa za maziwa wala asali, bali walirudi na zabibu na makomamanga, wapi na wapi.

  Lakini leo waswahili wanaendelea kusema Kanaan ilikuwa imejaa maziwa na asali, tukiwaambia kuwa hapakuwa na wingi wa ng’ombe wala mizinga ya nyuki huko wanasema tunakana kile biblia imeandika.

  Lugha ya biblia imejaa lugha ya picha (metaphors), lazima tu mtu ujue jinsi ya kuzitafsiri, la sivyo utafundisha watu magumashi.

  Halaf naona kuna haja ya kujifunza wajibu/kazi ya Roho mtakatifu kwa mwamini. Maana kama mtu anaweza akafikiri kwamba ni kazi ya Roho mtakatifu kumjulisha neno mwanamke linapokuwa limetumika mahali fulani kwenye biblia linamaanisha aliyeolewa, bikra, mjane, aliyeolewa, nk, basi ni dalili nzuri ya kuwa mtu huyo hajui wajibu wake na wa Roho mt. kuhusu neno la Mungu lililoandikwa.

  Tufanye zoezi moja Lwembe, fafanua hii mistari :

  Yoel 2:28-29“Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

  Wagalatia 3:27-28. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

  Ziragora,asante kwa mchango wako.

  Nafurahia kusoma hoja zako Lwembe.

 163. Unajua, ndg yangu Sungura, nimekuwa nikiyatafakari uliyoyaandika, lakini kila ninapojaribu kukujibu, natatizika kidogo, maana nashindwa kuifikia hiyo “school of thought” inayokutawala, ili kwa uhakika nikujibu katika kiwango chako. Yaani nikikijua chuo ulichosomea, kama ni vyuo vya SDA au Kiluteri au Kikatoliki, nk basi ningemperuzi mkufunzi wako kisha nikakupa majibu yaliyorahisi kueleweka kwako. Maana tatizo kubwa la Theolojia, ni kwamba huwa inawa brainwash wateja wake into conformity and subserviency to the views of the founders of the relevant doctrines that they uphold, the Bible notwithstanding!
  Hata hivyo ngoja nijaribu generally.

  Kulingana na “Kanuni zenu za Kutafsiri Maandiko” unasema kuwa, “… neno mwanamke kwa mfano, ni neno la jumla (inclusive) ambalo ndani yake kuna msichana, binti, mwanamke asiyeolewa, mwanamke aliyeolewa, mwanamwali (bikira)”, bali mimi nafahamu kuwa neno hili “mwanamke”, ni neno la kawaida linaloeleweka hivyo hata na mtu asiyewahi kwenda shule, ila ninyi katika kujikweza kwenu, ndio mnayalazimisha hata yaliyo dhahiri kuwa ya chuo!
  Pia kuhusu huko kusomea Theologia unakofikiri kutakuleta katika kuyaelewa Maandiko, nikionacho kwenu ni kinyume chake, vyuo vimewapeleka mbali zaidi na Neno la Mungu kuliko hapo mlipotoka kwenda huko vyuoni! Yaani mnaishia kuwa VIPOFU, nanyi hamjui! Hebu utazame upofu uliopigwa kwa Theolojia yako katika hili ulilolirejea. Kifua mbele unakandia wasiovithamini hivyo vyuo vyenu: “Wao akina Mabinza huona hata kwenda chuo kujifunza haya mambo ni kupoteza muda, maana wao huwa wanasema Roho mtakatifu atosha…” Nataka nikuambie kuwa, Roho Mtakatifu pekee ndiye mwenye kutosha katika kufundisha lolote lile linalomhusu Yeye. Yeye ndiye Mwalimu Bora kwa yoote yamhusuyo Mungu. Mtume Paulo alifundishwa na mwalimu bora katika nchi katika mambo ya Torati na Ufarisayo, anaitwa Gamaliel, bali Roho Mtakatifu ilimbidi amchukue kando na kumfunza upya Neno libebalo Uzima.

  Unaendelea, “… Lakini hawakumbuki hata manabii enzi za akina Elisha walikuwa wanakalishwa chuoni na kufundishwa (soma vizuri habari za wale vijana waliomtania Elisha wakimwambia paa wewe mwenye upaa).” Unauona Upofu uliowakamata? You are so blind that you don’t even know whom God placed to be your example! Kaka, vyuo hivyo vya manabii unavyovirejea katika siku hizo, ndivyo hivi unavyovipigia debe leo hii, they are one and the same, they serve the carnal church in its blindness! Unaniambia nisome habari za vijana wa mtaani waliomtania Elisha, hapana, mimi nataka tusome sote habari za manabii wako waliokuwa hapo chuoni, hao mnaofanana nao kwa leo. Hao hapo katika 2Fal 2 someni muwaone wanavyoweza kukamata mambo ya kiroho. Wanajua kuwa Eliya ataondoka, wanamdokezea Elisha, bali Elisha ayajua hayo! Hata Eliya alipoondoka walijua. Lakini hawakujua kenda wapi! Wakajitoa watu hamsini kwenda kumtafuta huko katika vilima na mabonde!!!

  Sasa hebu angalia mpambano! Mara zote Mungu hulifikisha jambo lake lililopindishwa katika mpambano, Yeye hufanya hilo! Alilifanya jambo hilo wakati wa Musa, wale Yanes na Yambre, zile roho; haya, huyu hapa tena akiwapambanisha manabii wa chuo na huyo aliyemfunza mwenyewe! Basi hao manabii wako wa vyuo, misosi ilipowaishia hapo chuoni, njaa ya kuua mtu ikawabana, (nadhani mlikaidi kupeleka mafungu ya kumi), wakaenda porini kuokoteza matango. Walipoyapika ili wayale, loh, kwa ule unabii walio nao wakakiona kifo ndani ya sufuria! Elisha akawakuta wanalia, wasipokula watakufa njaa, na wakila kitawaua, loh, ni ugumu kiasi gani wa maisha uliowapata hao manabii wa vyuo! Wanaweza kukiona kifo lakini hawana uwezo wa kukabiliana nacho, hao hapo wanalia! Wametumia “Kanuni zote za Kusoma na Kutafsiri Maandiko”, lakini kifo kimegoma kuondoka, si ndani ya sufuria wala matumboni mwao!

  Umeelewa Sungura, inamchukua nabii aliyesimikwa na Mungu, trained by God Himself, kama alivyofunzwa Elisha, kukabiliana na kifo, sio manabii uchwara wa vyuo wasiojua chochote kuhusu Mungu!!! No wonder unashangaa kuhusu mtazamo wangu, pamoja na hiyo sabato, maana kama kwa kuyasoma Maandiko, ukitumia hizo kanuni zenu, zikakuongoza kuwa Elisha aliwahi kusoma ktk chuo cha manabii, unaziona kanuni zako zilivyokutoa NJE na kukutupa huko kando ya NJIA, nawe hujui! Ndipo sijui hata nianzie wapi katika kukuelewesha kama hata haya mepesi unachemka!

  Ufafanuzi aliouleta Mathew ni mzuri sana katika kuzirejea hizo nukuu. Kama ni hayo maneno “Nashum” na “Isha” kwa kadiri ya tafsiri zake, binafsi nimejifunza hilo kutoka katika mchango huo. Bali siamini kwamba hao Nashum na Isha ni specie tofauti na hawa wanawake tunaowajua! Nimewaulizeni hivi, iwapo huyo asiyepewa ruhusa ya kufundisha ni mke (Isha), yaani kumfundisha mumewe, ndipo ninakuuliza nawe Sungura, Je, mke huyo anaweza kuwafundisha na kuwatawala wanaume wengine? Ndipo mke huyo akiwa ni mchungaji, je, mumewe anaruhusiwa kuwa sehemu ya kusanyiko hilo? Jibu la swali hili linaweza kukusaidia kuvielewa vizuri na hivyo vifungu vingine ulivyovinukuu, maana nakuona unahangaika na kucheza na maneno, sijui “toa teach”, halafu niongeze nini? Umeambiwa usitoe wala usiongeze, hamkufundishwa huko chuo? Mwalimu wako alikuwa profesa nani? mwambie she is fired, because she is just another Jezebel as far as the Bible is concerned!!!

  Mwisho, napenda nikueleze kuwa hao wanawake unaowasoma, hayo maelezo yanayowahusu, ni wanawake wanaolelewa katika familia za kikristo, hilo ndilo neno linalowatakasa, kwa neno hilo wao hutawaliwa na waume zao, nao mabinti wasioolewa huendelea kutawaliwa na baba zao hadi hapo watakapo olewa! Baba wa nyumba hiyo ndiye pastor wao. Nao wamama wazee, hao watakatifu, huendelea katika jukumu la kuwalea na kuwafundisha vijana wao wa kike katika yote yawapasayo katika ule mwenendo wa kitakatifu. Adabu huanza kufunzwa nyumbani na si kanisani! Nao watoto wa kiume hufunzwa na baba zao.

  Umeelewa ndg yangu Sungura? Wanawake huwa wanabaki kambini, hawaendi vitani! Hata huyo Debora mwamuzi, ilipofika saa ya vita alimuita Barak! Au haujasoma kuwa Uriah alimuacha mkewe nyumbani alipokwenda vitani? Au Ibrahim alipokwenda vitani kumkomboa Lutu, hao aliowakusanya wa nyumba yake, walikuwemo na wanawake? AU INJILI SIO VITA??? Msikilize Jemadari wa vita, kama anasema mwanamke abaki kambini, usijaribu kumsahihisha wewe ambye ni coporo!

 164. Niliposoma tu uchambuzi wa Mathew hapo juu nilijua kuwa Lwembe ninayemfahamu kama atakuja kujibu hoja hiiataongea blablaa. Na hicho ndicho Lwembe kafanya.

  Lwembe ndugu yangu kusema kweli hoja zako hazina mashiko. Ni vizuri kufika mahali mtu ukawa muungwana ukakubali ukweli ambao umetolewa kwa hoja za msingi, au ukatafuta muda wa kutosha kutafuta majibu ya uhakika.

  Ni vigumu sana kuzikataa ‘facts’ ambazo Mathew kazitoa hapo juu maana ziko na ‘substance’ kwenye neno la Mungu. Vinginevyo labda kama mtu unaamua kuwa mkorofi tu kwa kutokutaka kukubali kushindwa, japo hapa hatushindani.

  Hizo ni ‘facts’ ambazo mwenye kuzielewa kwa usahihi wake ni yule anayejua misingi ya kutafsiri maandiko, ”mburula” hawezi ona kitu hapo.

  Yaani ukifuatilia kwa umakini majibu ya Lwembe utagundua kwa uwazi kabisa kuwa ni ya kujikakamua tu.

  Mathew ubarikiwe, hili suala umelichambua vizuri sana.

 165. Wapendwa,

  Ninaomba Roho Mtakatifu atuongoze, zivyo tutafikia kusema Biblia inajipinga yenyewe.
  Sasa hii andiko nayo inamaanisha gani?
  “Wagalatia 3:27-28. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.”
  Nafikiri ni vizuri zaidi kuzingatia Biblia us Union Bible. Kama tunakuta maneno inayotupita akili inatubidi tusome tangu Mwanzo mpaka Ufunuo. Wenda tutajua kama andiko fulani lilipewa likilenga context ipi. Ninapojua kam DEBORAH alikuwa muamzi huko Israeli akiwekwa na Mungu mwenyewe, na tena ninaposoma hili shairi ya Wagalatia, na ginsi ni wanawake waliopasha habari njema ya ufufuko wa Yesu Kristo.
  Na ukisoma ile kitabu ya I Wakorintho 11, utaona mrorongo wa mashauri Paulo aliyoyapana, lakini inaonekana hata yeye hana uhakika kutoka kwa Mungu, bali neno la maonyo yake:
  Kwa ule wa 12 anapana ruhusa kwa watu kuhukumu wawo wenyewe, kwa ule wa 11 anatofautisha wanawake na wasichana(ina maana kama hapa anasema mambo ya kimwili) na kwa ule wa 18 anasema anasadiki kwa nusu, (hana uhakika).

  “12…….. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.
  11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.
  18 Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;”

  Yeye paulo nadhani alikuwa wazi kufwatana na context. Tutafute kwa bidii kumuelewa, si yeye atakaefika kutuelewa. Lakini tukiomba nguvu za Roho Mtakatifu tutaweza.

  Kufwatana na mambo haya madogo siwezi hakikisha kam ile Timotheo yatosha ili tuseme Mwanamke hastahili kufundisha kanisani. Please, tuangalie kwa makini.

  Mubarikiwe.

 166. Ndg Mathew na SG wote,
  Asante sana kwa maelezo mazuri na yaliyo wazi, Bwana akubariki kwa juhudi nzuri!

  Kuhusu wanawake kufungwa kamba, ni kweli huwa wanazikata, si wanawake tu, bali hata wanaume, maana sote tumefungiwa kamba hiyo katika ile Nanga, yaani Kristo, lile Neno, ndipo inapokuwa imekatika, basi mawimbi laini hutubeba pole pole na kutupeleka huko mbali na ile Nanga, na hata kutokomea huko ambako tunaweza kushurutishwa kuwa na miungu mingi, kama huyo “mungu wa Jinsia”!

  Kwamba umeyasoma maelezo yangu na unayaona ni yale yale niliyoyatoa nyakati za nyuma, hilo ni kweli, maana hivyo ndivyo ninavyoliona jambo hilo wakati wote, baada ya kuzitazama kwa kina angle nyingi za hoja hii ya kuwasimika wanawake na kuziona ni zenye chimbuko la hekima ya kibinadamu na logic zake, zikiishia katika siasa za dini. Kwahiyo, maelezo yangu ni kweli ndiyo hayo hayo, kama ambavyo yasivyobadilika hayo yaliyomo katika Biblia.

  Ufafanuzi ulioutoa kuhusu 1Kor 11:3, naona ‘umecheza’ na maneno zaidi kuliko kufafanua kama ulivyodai! Labda nirudie tena, kwamba wanawake katika ujumla wao, awe ameolewa au hajaolewa au ni binti, nilisema, hao chimbuko lao ni ndani ya familia zao, kwa hiyo kulingana na maadili ya kikristo, hao hutawaliwa na baba wa familia hiyo, baba wa familia hiyo ndiye pastor wa familia yake! Nayo Adabu huanza kufundishwa nyumbani na si kanisani. Ni katika msingi huu, ninaamini mafundisho ya mt. Paulo yamejikita, hata anaposema “kichwa cha mwanamke ni mwanamume”, mimi huelewa kuwa anamzungumzia mwanamke aliyelelewa katika nyumba iliyo katika muongozo huo. Kwamba mwanamke huyu akikutana na wanaume ambao si mumewe basi ana uhuru wa kuwapayukia? Hakuna jambo kama hilo! Ndio maana kila ninapojaribu kulitazama jambo hili kwa mtazamo wenu, naona limevuka hata mtazamo wa kawaida wa kimwili! Nimewahi kumuona mwanamke wa Kisukuma akimpelekea maji mgeni mwanaume, ambaye si mumewe, akapiga magoti kwa adabu na kumkabidhi ile glasi ya maji!!!

  Tena inashangaza sana, hapo unapotamatisha kwamba, “Isipokuwa sio kila mwanamume ni kichwa cha kila mwanamke” Ukijaribu kumtoa mwanamke katika adabu impasayo na kumuachilia aelee bila Nanga! Mimi nafahamu kwa kufundishwa, kwamba wanawake ni aidha dada zangu au mama zangu katika namna ya heshima; na wanawake pia wamefunzwa hivyo kuhusu wanaume, au haujamsikia Sara akimuita Ibrahim, “bwana”, huyo mumewe?!!!

  Maelezo uliyoyaleta kuhusu isha na nashum hapo mwanzo na haya mapya, mimi nimeyaelewa kama yanavyojieleza, ninayaona yako sawa katika maana ya Fundisho kama yanavyojishuhudia, kwahiyo siwezi kuweka interpretation yangu juu ya hilo nililolielewa kama lilivyokusudiwa! Bali kuhusu maelezo kwamba wanawake wanapigaga kelele kanisani, kwa kweli niseme wazi, hilo ni jipya kabisa kwangu, ndio maana nimecheka saana nilipoisoma hii tafsiri ya OJB, ile “…for it is not permitted for them to blurt out”! Basi kichwani mwangu ukaanza kupita mkanda wa video, nikizirejea hali za ibada katika makanisa yetu tofauti!

  Sijui, labda utakuwa umejichanganya au unaweza ukawa uko sahihi kwa kiasi fulani kutokana na roho, kwamba roho iliyokuwa juu ya Wakorintho ndiyo hii iliyoko juu ya Wapentekoste leo hii katika kuzipiga hizo kelele, hapo kanisa zima linapolipuka katika unenaji wa lugha anaoukemea mt. Paulo! Lakini hata hivyo, hivi zile kelele za lugha huwa zinafundisha lolote kweli? Bali kwa suala la kelele, hebu ingia katika ibada ya Kikatoliki kwanza halafu jaribu kuyapima hayo maelezo yako, unaweza ukafika mahali fulani ukaiboresha hiyo tafsiri!

  Maelezo yako mengine bado yamejikita katika kupotosha Fundisho halali! Taratibu za ibada huendelea kama ilivyo desturi. Kama ni kuitikia “Ameen” wao huitikia kama ilivyo kawaida, yaani sauti itokayo hapo huwa ni moja tu ya yule Adamu wa Mwa 1:26, yule mme na mke!!! Kuwa silent, kama utakuwa unawazungumzia watu walio gulioni, utakuwa uko sahihi, lakini hapa mt. Paulo anazungumzia Kanisani, wawe kimya na submissive, maana Roho Mtakatifu huwepo hapo, yule mume!!!

  Kuhusu semina, kama mwanamke ndiye atakayeiongoza semina hiyo, nanyi wababa mkiwa mmeketishwa chini, hilo bado lina walakini kuhusu Roho anayeiongoza semina hiyo.

  Bali unapokuja katika jambo hili, “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu” hapa ndipo makanisa mengi yamejipachikia tafsiri yao wenyewe kwa kukosa uelewa wa utendaji wa vipawa katikati ya watakatifu! Wengi wenye mtazamo ulionao ndg Mathew, huamini kwamba kuwa na kipawa hukuhalalisha kuwa mchungaji au tuseme kufundisha! Basi tusemeje, wote wawe walimu au wachungaji au mashemasi nk? La hasha, Roho Mt ndiye azipangaye Huduma zote katika kusanyiko, na hayo yote unayoyasoma yanatimia hivyo na si kwa mapenzi ya mtu fulani bali ya Mungu mwenyewe aliye yaahidi hayo katika Hekima yake. Kwahiyo wanawake hutoa unabii katika kusanyiko walilomo, ambao hupimwa na uongozi wa kusanyiko, huo uliosimikwa na Roho Mt. Kutoa unabii sio kufundisha! Na pia ieleweke kuwa si kwamba utakatifu wa wanawake uko chini kuliko wa wanaume, si hivyo, sote tu sawa mbele ya Mungu iwapo kila mmoja atabaki katika majukumu aliyopangiwa!

  Deborah alikuwa ni nabii, na mwamuzi na mambo yake yako kama yalivyoandikwa. Kusudi la Mungu lilitimia kwa kadiri alivyolipanga katika kipindi hicho, bali si Fundisho. Hata Anna, alikuwa ni nabii, pia hakuondoka Hekaluni (sio katika makanisani yetu ya leo ambayo mafungu ya kumi maaskofu wanayapeleka majumbani kwao, angekufa njaa!), sasa si kwamba kwa kuwa kwake Hekaluni alikuwa Kuhani! Kila jambo huwa na utaratibu wake, hata unapoimba kwaya, unalazimika kuwa makini katika kufuata Instructions, using’ang’anie mambo yaliyopita at the expense ya new instructions!

  Umezungumzia kuhusu yaliyotokea kule Edeni, kwamba Mwanamke aliambiwa hivi “…..na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.” Nadhani katika hili utakuwa umeufikia mzizi wa mafundisho yako, yaani chimbuko lake. Mwanamke huyo anayeambiwa hayo, kwanza ni by-product ya Mwanaume, hakuwemo katika uumbaji wa mwanzo, zile siku sita, kwa hiyo ni dhaifu, ndiyo maana Shetani alimnyemelea huyo! Baada ya kula lile tunda ndipo alipoanza kuhubiri, mhubiri wa kwanza mwanamke, ni Hawa! Alimuhubiria Adamu injili mpya naye Adamu kwa makusudi akaipokea Injili hiyo huku akijua fika kuwa hilo ni kosa, ile iniquity, bali kasisi huyo wa kike yeye aliamini kabisa moyoni mwake kuwa hayo ni mapenzi ya Mungu! Huku ndiko hilo jambo mnalolipigia debe lilikoanzia, ule Ujuzi wa Mema na Mabaya! Basi, hata leo hii ningeisikia sauti ya Mungu tena ikituambia sisi tuliozisikiliza sauti za wanawake, tukayapuuza Maagizo ya Mungu kupitia mtumishi wake na mwalimu wetu Paulo, “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako…” sasa kinachofuatia hapo, kila mmoja wetu anayo nafasi ya kukitafakari, kama ni taji …!

  Mwalimu mwingine, wa pili mwanamke alikuwa ni Sara. Alimuhubiria Ibrahimu akazaliwa Ishmaeli! Ibrahimu aliamua kumridhisha mkewe akaipokea injili hiyo, bali Sarah aliamini kabisa kuwa hayo ndiyo mapenzi ya Mungu! Hicho ninaamini ndicho kanisa linachofanya, limeisikiliza sauti nyingine!

  Nenda katika historia ya Kanisa hutamuona mwanamke mchungaji au shemasi, hao waliojitwalia nafsi hizo walikuwa ni wake za wachungaji, baada ya kuwashawishi waume zao, hao ndio walio set trend!! Basi kwa kadiri ya mwenendo wa kanisa, hapo linapozidi kutokomea katika hekima yake, iliyozingirwa katika fumbo za Shetani zilizo katika vilindi vyake, akiwainua wanawake, nalo kanisa likiliridhia jambo hilo, kama huko nyuma, lile kanisa tangulizi lilivyomridhia “yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza” Ufu 2:20, ni dhahiri kwamba WOKOVU wa Kweli unazidi kuadimika kama sio kuwa EXTINCT!!!

  Basi ndg zangu ni vizuri nasi tukakaa katika mafumbo ya Mungu, hayo aliyotufunulia, kutoka katika vilindi vyake, 1Kor 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.”

  Mbarikiwe nyote kadiri tunavyojifunza ili hatimaye tuweze kuufikia Ujuzi wa Kweli!

  Ck Lwembe

 167. Mpendwa Lwembe na SG wote.
  Ck, umenichekesha kweli kweli kuhusiana na kauli hii – Siamini kuwa Biblia inamzungumzia kahaba au mwanamke aliyekata kamba…..Yaani kumbe mwanamke kafungwa kamba!!!!

  Nimeyasoma maelezo yako uliyoyaandika nimeyaona kuwa hayana tofauti na yale uliyoyatoa nyakati za nyuma. Na kwa sababu maelezo uliyoyatoa sio maswali, nami sina kawaida ya kujadili hoja za mtu kwa kirefu, sitakuwa na maelezo mengi na ushauri wangu ni huu, Ni vema ukatafuta maana na chanzo cha jambo ili uwe katika mstari sahihi, usije ukaishia kuwa na Mungu wa JINSIA.

  Lakini umenukuu 1Kor 14:34-37 na 11:3. Kwa sababu umenukuu maandiko haya nina sababu ya kuyatolea ufafanuzi ufuatao. Nikianza na 1Kor 11:3 – ” ….kichwa cha KILA mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume,…….”. Ck, ukiangalia vizuri neno KILA nimetumika ktk uhusiano wa mtu na Kristo, lakini neno hilo halipo kwenye uhusiano wa mtu mme na mtu mke. Maana kama wewe ungekuwa kichwa cha kila mwanamke ingekuwaje? Haya ni mahusiano ya mme na mke na kwa hilo halina mjadala. Isipokuwa sio kila mwanamume ni kichwa cha kila mwanamke.

  1Kor 14:34-37 umenukuu hivi; ” “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii (sijui hawa ni Nashum au Isha!),kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
  Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.”

  Ndugu ya Lwembe umeuliza kuwa hawa ni Nashim au Isha. Kwenye mstari wa 34 na 35, katika tafasri ya OJB inasema hivi “Let the nashim in the kehillot be silent, for it is not permitted for them to blurt out, but let them become submissive, as it says in the Torah. And if the nashim wish to inquire about something, let them inquire of their own be’alim b’bayis, for it is a bushah (shame) for an isha to blurt out in the kehillah.” (bold added). Jibu la swali lako ni kuwa wote mwanamke na mke (Nashim na Isha). Kabla ya yote ieleweke kuwa maneno yaliyosema kuwa bali watii kama vile inenavyo torati nayo. Reference ya maneno haya ktk agano la kale ni Mwanzo 3:16 tukio la Adamu na Hawa (mme na mke). Ebu sasa linganisha na kipange hiki cha tafasri ya OJB – but let them become submissive, as it says in the Torah. Mwanamke aliambia hivi “…..na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”

  Halafu ukiangalia maneno niliyoya-bold (be silent, blurt out, inquire…) utaona kuwa kunachoongelewa hapo sio kufundisha!!! Kwa uelewa wangu hapa Mtume Paulo alikuwa anatibu tatizo lililopo kwa akina mama wengi la kujibishana pasipo utaratibu. Yaani mara huyu kasema kitu fulani mwingine kadaki na huku hivi, n.k. Kama kweli tafasri unayonayo (ndugu yangu Lwembe) ni sahihi… Tuseme Mtumishi akiwa anafundish/hubiri kanisani na anataka Kanisa wajibu/itikie neno fulani je akina mama wakiitia mfano – Ameen, kwao ni aibu? Maana Biblia imeandika …….. wanawake wanyameze katika kanisa …….maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au kuitika/kujibu swali kanisani sio kunena. Hebu fikiria Lwembe unafundisha semina ya akina mama halafu ndiyo una huo msimamo – wanawake hawatakiwi kusema ktk kanisa, Je hapo tena kutakuwa na semina kweli ndugu yangu, semina ya unayofundisha watu wakuangalia tu au tukubali kwamba tumekosa ufahamu sahihi?

  Kwa kumalizia niulize hili; Je, mtu anaweza KUTABIRI bila kusema? Ngoja tusome maandiko haya “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. – YOEL 2:28-29. Petro yeye amesema….. wana wenu na binti zenu watatabiri….. Mdo 2:17. (SUV msisitizo added). Ck, kama bado unaendelea kushikilia msimamo wako unawataka wanawake wasitabiri kanisani kwenu? Kwenu watakaotoa unabii watakuwa wanaume tu!!! Lakini wako manabii wa kike (Debora aliongoza Israel na Hulda alitoa maelekezo ya Bwana kwa wafalme na Israel), Je Nabii wa kike Ana aliyewatolea Israel habari za mtoto Yesu kuwa ni mwokozi hekaluni (LUKA 2:36-37) ingekuwa ni nyakati hizi, mhh???

  Huyo Mungu wa Jinsia jamani !!! Bwana aturehemu, halafu yake sisi wanaume tuwaache wanawake wafanye kazi ya Mungu zikiwemo za kufundisha na kuongoza pasipo kuwawekea mipaka ya kijinsia na SG wote bila kujali jinsia waseme Ameeeeen ya nguvu.
  Keep on digging,
  Mathew.

 168. Jiulize kwa nini Yesu kwenye suala la ndoa anasema hao wawili si wawili tena bali ni mwili mmoja! Ni mwili mmoja kwa vipi wakati kila mtu ana mwili wake? Kama huwa unaielewa logic ya Yesu hapo, basi hata hii utaielewa.

  Ninashangaa kwa nini umerudia kuniuliza swali lilelile Yusha wakati nimekuibu nikakuonesha ni katika mtazamo gani wote tu wanawake mbele za Mungu.

  Na uelewe kuwa jinsia zetu zipo tu kwa ajili ya suala la uzazi tukiwa katika hii miili, lakini tukishatoka katika miili hii wala haziwi na maana yoyote.
  Ndio maana Yesu akawaambia masadukayo kuwa mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa, hivyo wote huwa kama malaika.

  Yusha usijisikie vibaya wewe kuwa bibi harusi ndugu yangu, mwanaume ni mmoja tu Yesu kristo.

  Asante.

 169. @Sungura yaani mwanamke na mwanaume wote mbele za Mungu ni wanawake?ikawa je kuumba watu wawili?

 170. Yusha usichanganyikiwe ndugu yangu, ni kitu rahisi sana kelewa.

  Kwa kuwa unajua kuwa wewe ni sehemu ya kanisa na wewe mwenyewe ni kanisa, basi kumbuka tu kwamba kanisa ni bibi harusi na kristo ni bwana harusi, na bibi harusi bila huwa ni mwanamke.

  Kwa hiyo mimi na wewe kama tu bibi harusi wa Kristo, basi sisi ni wanawake mbele za kristo kwa muktadha huo.

  Bariiwa Yusha

 171. Mathew kafafanua vile ambavyo inatakiwa kufafanuliwa. Kuna mambo mengi sana hapa duniani ambayo yana kanuni zake, lakini kwa sababu ya watu kupuuza hizo kanuni wamejikuta wanaingia kwenye upofu mkubwa.

  Ukiangalia mchango wa Mabinza ule wa kwanza kabisa hapo juu utagundua kuwa hata baada ya kufafanuliwa vizuri kabisa na Mathew yeye (Mabinza) ameendelea kutumia kanuni za kutafsiri maandiko anazozijua mwenyewe, yaani bila kujali kuwa neno mwanamke kwa mfano, ni neno la jumla (inclusive) ambalo ndani yake kuna msichana, binti, mwanamke asiyeolewa, mwanamke aliyeolewa, mwanamwali (bikira)

  Wao akina Mabinza huona hata kwenda chuo kujifunza haya mambo ni kupoteza muda, maana wao huwa wanasema Roho mtakatifu atosha. Lakini hawakumbuki hata manabii enzi za akina Elisha walikuwa wanakalishwa chuoni na kufundishwa (soma vizuri habari za wale vijina waliomtania Elisha wakimwambia paa wewe mwenye upaa). Hata biblia wanazosoma hazikuwekwa mikononi mwao na Roho mtakatifu, bali na wataalam wa mambo ya uandishi kutafsiri maandiko, ambayo kwa ujumla wake ndo yanatengeneza ”Theolojia”

  Ndio maana mimi huwa najiuliza sana kwamba kama mtazamo wa akina Lwembe uko hivi, huwa wanapata wapi tafsiri za kukataa kutunza sabato kama wasabato wanavyoitunza katika mwili kabisa!!? Maana ili pia kujua tafsiri nzuri za mambo ya sabato lazima ujue kanuni hizi za kutafsiri maandiko kama alivyofafanua Mathew. Bila kujua hizo kanuni kukwepa kutunza Jumamosi (huo ni mfano)

  Lwembe kwa nini unajilazimisha kuchanganywa na fafanuzi ya Mathew wakati iko wazi kabisa kuhusu “nashim na nashi”, kama si makusudi tu?

  Ametofautisha vizuri kabisa kati ya mwanamke na mke, kwa hiyo ni wajibu wa msomaji kila unapokutana na neno linaloongelea jinsia ya kike kwenye biblia, kurudi kwenye lugha ya asili kujua kama anayeongelewa ni mke (isha) au mwanamke (nashim).

  Na ukiangalia kiusahihi kwa jicho la mwalimu tafsiri ya KJV utagundua kitu ambacho mtu asiyejua kanuni ya uandishi hawezi kukiona kwa urahisi.
  Inasomeka hivi: Bid the older women …….. they are to teach what is good and so train the young women. Toa teach what what is good ni kitu kimoja, and so train the young women ni kitu kingine. Wameambiwa wafundishe mema bila kubagua kuwa wamfundishe nani hayo mema, kisha wawafunze mabinti…..
  Kwa hiyo mtu akiamua kusema kuwa wanawake wazee wameambiwa wawafundishe mabinti, yaani kwamba wawafundishe manbiti peke yao, basi huyo ni mtu asiyejua kanuni za uandishi na kutafsiri maandiko.

  New International Version (NIV) yenyewe imesema hivi: (Titus 2:3-5)
  3 Likewise, teach the older women to be reverent in the way they live, not to be slanderers or addicted to much wine, but to teach what is good. 4 Then they can urge the younger women to love their husbands and children, 5 to be self-controlled and pure, to be busy at home, to be kind, and to be subject to their husbands, so that no one will malign the word of God.

  Kutofautiana ndio msingi wa kujifunza, tuendelee!!

 172. Wapendwa,
  Binafsi nimefurahishwa sana na mchango wa ndg Mathew kuhusu Fundisho la kuwazuia Wanawake kuwa Viongozi na Kufundisha, akiliweka Fundisho hili katika UPOTOFU! Kuhusu watumishi hao wanaowazuia wanawake kuwa hivyo, anasema, “Wanayatumia maandiko hayo bila kuzingatia kanuni za kusoma na kupata tafsiri sahihi ya Maandiko.” Kwa jambo hili la “kanuni za kusoma na tafsiri” ninakubaliana naye kwa mapana na marefu, iwapo tutaichukulia Biblia kuwa ni kitabu cha tamthilia na tamaduni zake, intellectually! Huu ni upande mmoja.

  Lakini, upande wa pili ni mgumu kidogo, maana upande huu Biblia hujulikana kuwa ni Neno la Mungu, tena anasema amelihakiki mara saba, ndipo ameliwekwa hapo, hiyo Biblia. Basi ni katika kuzioanisha pande hizi mbili ndipo mitafaruku hutokea, kwani ule upande intellectual, wao hufika mahali wakawaona watu walioandika hivyo vitabu vilivyomo humo, ndipo katika namna ya kuyagawa Maandiko hayo, ili kuyafisha, basi wangekuambia kuwa hilo lilikuwa ni wazo lake tu, kila wanapolifikia jambo ambalo hawataki kuliafiki. Kuna kundi linalokuambia kuwa kuna Sheria za Musa na kuna Sheria za Mungu alizoziandika kwa kidole chake. Sasa unapowauliza zi wapi hizo alizoziandika Mungu kwa kidole chake, mnayo hiyo original copy? Hawana, wanayo hadithi yake tu! Ni sawa kabisa na swali hili analoliuliza ndg Mathew, hapo anaposema, “SIMPI …… ni nani huyo ambaye hatoi ruhusa?” Mwisho wake Biblia hugeuka kuwa “Fable”!!!

  Lakini kwa upande wa pili, sisi twafahamu kuwa humo katika Biblia, HAKUNA neno la mtu yeyote yule, yote yaliyomo humo ndiyo yanayolifanya na kulikamilisha hilo Neno. Tena tunapolifikia Agano Jipya, sisi twafahamu kwamba Efeso, Korintho, Galatia nk, zote hizo ni roho, na kwahiyo hazifungwi katika wakati, kwamba eti zimezeeka, hapana, ndio maana unaweza kuziona leo hii tena zikiendelea katika shughuli ile ile waliyoikemea mitume huko nyuma!

  Nikija katika tafsiri anazozifundisha ndg yangu Mathew, bado ninaziona zina mapungufu makubwa kwa kadiri ya Injili inavyofundisha. 1 Tito 2:3-4 “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji ….., bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili,…….” katika namna yoyote ile utakavyolichukua agizo hili, sioni ni kwa namna ipi unaweza kuliunganisha na hilo linalo mkataza mwanamke kufundisha. Maandiko yako wazi kuwa wanawake wazee wawafundishe wanawake vijana, tena wanawake hao wazee ni hao wenye mwenendo wa utakatifu. Ninaamini huo ndio utaratibu anaotuwekea ili kuyaongoza maisha yetu katika utakatifu. Kuna mambo yawahusuyo wanawake, ndipo vijana wa kike hufunzwa hayo na akina mama hao wazee, waliokomaa katika Kristo. Sina uhakika kama ndg yangu Mathew atakomea hapo alipofika tu, inawezekana kabisa kwa andiko hili akawapa USHEMASI na UASKOFU hao wanawake wenye “mke mmoja”!

  Pia hii 1Timothy 2:9-13, katika namna alivyoileta hii tafsiri ya Kiebrania, ni jambo la kupendeza tena linalotia moyo, ile kiu ya kuijua zaidi tafakari ya Neno la Mungu. Isipokuwa, ninapojaribu kuioanisha tafsiri hii ya Kiebrania ili kulipata Fundisho la kuwasimika wanawake kuwa wachungaji, bado naona litakuwa ni jambo la kulazimisha! Labda ndg Mathew arudi tena katika hiyo tafsiri, kisha aje na upambanuzi zaidi ili tuelewe anachotaka kufundisha ni nini haswa. Nashim=wanawake, ndipo kuhusu mavazi ya kujisitiri inaeleweka. Isha=mke, basi katazo la kufundisha na kumtawala mwanamume, kulingana na Mathew, linamuhusu mwanamke aliyeolewa, huyo ndiye anayekatazwa kumfundisha mumewe na kumtawala, bali nashim, yaani wanawake, sijui ni wale wasioolewa au wasichana au …, hawa katazo hilo haliwahusu! Ndipo huyo Isha anaweza kuwa mchungaji wa kanisa, lakini ili katazo hilo liheshimiwe basi mumewe anapaswa asikusanyike hapo au la itamlazimu afundishwe na kutawaliwa na huyo Isha!

  Ktk kifungu cha 14, mtume Paulo anatamatisha Fundisho lake hilo pale RM anapomrudisha Edeni kuitazama hali ilivyokuwa, ndipo analifunga Fundisho hilo kwa kutuambia, “Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” Hiyo ndiyo sababu Mungu amemkataza mwanamke Kufundisha! Labda katika ile tafsiri twaweza kupata maana iliyo bora zaidi ili tumpe mwanamke (nashum) nafasi ya kufundisha, kwamba labda tuseme aliyedanganywa ni Isha! Lakini Hawa aliumbwa akiwa Isha, nayo Biblia yangu (KJV) inaniambia mwanamke, sasa sijui ndiyo huyo Nashum au Isha! Unaziona “kanuni za kusoma na tafsiri” zinakoishia, kwenye mkanganyiko, bali Neno la Mungu hufikiwa kwa Imani!!!

  Labda katika kutamatisha maelezo yangu niseme hivi, kuwa hilo andiko ktk Timotheo, si andiko linaloning’inia hewani, bali ni Fundisho kamili linalosimama kulingana na Injili aliyokabidhiwa mtume Paulo kuja kutufundisha sisi watu wa Mataifa; 1Tim 2:7 “Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.” Basi, ktk 1Kor 11:3 anatufundisha, akitusisitizia kuwa, ““Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.” Huo ndio utaratibu na nafasi zilivyopangwa! Ukimkuta mwanamke kawa kichwa, naye mwanaume kawa “gigolo”, basi jua kuwa hapo kuna tatizo. Wote wawili, mwanaume aliyegeuka kuwa kiwiliwili na huyo mwanamke aligeuka kuwa kichwa wametoka katika nafasi zao na wanapaswa kufungiwa kama wale wa Yuda 1:6!!

  Pia waweza kupata ushahidi zaidi wa jambo hili ktk 1Kor 14:34-37, “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii (sijui hawa ni Nashum au Isha!), kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
  Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.”
  Kwa kauli yake hiyo ya mwisho, ni dhahiri kuwa mtume Paulo ameliona Fundisho la kusimika wanawake litakavyo sambaa, ndipo ametamatisha hivyo kuwa “..mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.” Yaani ni ruksa kuendelea katika ujinga maana yote yamekwisha kuwekwa wazi!

  Pia ni vema mkafahamu kwamba, Nashum na Isha, hawa wote hupatikana ndani ya familia, naye kiongozi wa familia ya kikristo ni mume, ndipo wote wawili, mke na binti, hutawaliwa na baba wa nyumba, binti huondoka katika utawala wa babaye hapo anapo olewa. Biblia inawazungumzia hao katika utaratibu huo. Siamini kuwa Biblia inamzungumzia kahaba au mwanamke aliyekata kamba, bali hao walio katika utakatifu; nayo mafundisho yanayoweza kuwaleta katika utakatifu ndiyo haya mtume Paulo anayoyawekea Msingi!

  Mbarikiwe nyote!

 173. Mwanamke ni mwanamke tu,hata watu wafanye je na wayadeuze maandiko lakini hawata geuza umbile lake;wanao kubali mwanamke kutawala na watuonye mu biblia wapi aliwezaka kutawala ao mwanamke aliye wahi kuwa mtume.

 174. Kaka Sungura, muna nichanganya sasa munasema sote ni wanawake mbele za Kristo“1wakorintho 11:7,Mwanamume ni utukufu wa Mungu na mwanamke ni utukufu wa mwanamume”.na kutuonyesha kama tukiwa mbele za Kristo lazima mume asifunike kichwa na mke afunike kichwa.swali:kwanini Mungu kutia utofauti hapo huku sote ni wanawake mbele zake?

 175. Acha tuvumiliane tu Mabinza,lakini uelewa wako ni mdogo juu ya elimu ya Mungu.

  Yes, mume ni kichwa si kwa kanisa bali kwa mkewe, kichwa cha kanisa ni kristo. Ndo maani nilikwambia cc sote waamini(kanisa) ni wanawake,mwanaume ni mmoja tu Kristo- kichwa cha kanisa.

  Mabinza wapi biblia imesema kuwa kanisani kuna aina tatu za washirika? na kama hakuna mahali pasemapo hivyo wewe umeitoa wapi hiyo?(jibu hili swali ni muhimu plz)

  Niko serious kuwa mm ni mwanamke mbele ya kristo, haya nifundishe.

 176. Mpendwa Sungura,

  Nimeisoma tena 1Tim. 2;12 (UV- 1952); Swali lako inalijibu hivi:-
  12Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Bali awe katika utulivu. Hivyo ndivyo ANDIKO hilo linavyosomeka na ndivyo linamaanisha hivyohivyo, Mimi naona hapo, hapana ugumu wowote wa kimsamiati, kiasi kwamba Sungura ushindwe kuelewa sentesi kuwa “Mwanamke atulie, asifundishe , asimtawale mwanaume!” hivyo ndivyo inavyomaanisha hakuna nyongeza, nyongeza yoyote au punguzo lolote katika hopo; Ikiwepo, basi, hiyo itakuwa “yatoka kwa yule mwovu”

  Nakubaliana na wewe kwamba huo ni ukweli usiopigika kama ulivyosema kuwa, “Uhalisia niliosema ni kwamba leo kuna wanawake wengi ni viongozi na wachungaji na wanaongoza kwa mafanikio hata kuliko wenye ndevu..”

  NDIYO mzee nakubali, yule ‘mwenyendevu’ tu kama ulivyosema lazima azidiwe, aongozwe, afundishwe na atawaliwe na awaweke WANAWAKE kuwa wachungaji, maasikofu na mashemasi, maana sifa si kuwa na ndevu, bali SIFA nikuwa, mhusika awe kweli MWANAUME! Lakini MWANAMME hasa anayesemwa katika Maandiko, ambaye ni mfano wa Kristo, kamwe hazidiwi na hatazidiwa katika kila ‘Kiwanja’, wala hatakuwa Nyuma ya Mwanamke, maana Mwanaume ni KICHWA, si mimi ninayesema hilo ni MUNGU!

  Watu wengi wa ‘Makanisani’ hujikuta wakihaha na kuukataa ukweli wa Neno kwa kisingizimo chochote ili kulinda mapokeo na mafundisho ya Kithiolojia, ambayo ni Elimu za Kibinadamu tu, wao hulazimisha Neno la Mungu likubaliane na matakwa yao! Lakini jua kwamba, UKIAMINI UONGO, UNAPEWA HUO. Ndiyo maana unaona wale unaowaita wewe kuwa, “ni wanawake waliofanikiwa!” wanaonekana mbele ya ‘WENZAO’ kuwa wamebarikiwa sana, bila kujiuliza kuwa, hizo ‘BARAKA’ ni nani katoa, iwapo aliyesema, usizini ndiye huyohuyo aliyesema Wanawake wasifundishe ?!
  Mstari mmoja wa Neno la Mungu, watosha kukuponya ama kukuua kabisa! Neno ni upanga wenye makali kuwili. Ndani ya Kanisa Sungura, wapo washirika wa aina tatu;

  Wa kwanza ni yule asiyeamini Neno kabisa, yeye kila siku hukubali kila kitu, akitoka tu mbele ya hao wanaosema, anakataa yote na kutenda mambo yote kinyume na lile Neno la Mungu, wala hajuti moyoni mwake, maana hana matunda yapasayo toba; Wiki ijayo yupo tena, lakini pia haoni hasara kuondoka zake na kuliacha Neno wakati wowote.

  Wa pili ni mwenyekujifanya tu kuwa ni mwamini, huyu huyakumali maandiko lakini hukataa sehemu moja ya hayo. Maana hulitafakali Neno lile kwa akili, maarifa na hekima zake mwenyewe, hivyo akili yake ikiambiwa jambo lolote linalotokana Mungu lakini likapingana na ufahamu wake, hilo kwa vyovyote hatakubaliana nalo, anaweza kusema ‘nakubaliana na Biblia yote lakini, Andiko hili halimaanishi hivyo!’ Huyo jua kwamba, ni mwamini wa KUJIFANYA TU!

  Watatu, yeye huliamini Neno lote, bila kusitasita popote katika hilo, mfano wa Mtoto mdogo, huyu ndiye mwamini wa kweli na ndiye mbegu ya Kristo imo ndani yake!

  Umeendelea kusema pia kwamba, “Kumbuka, mbele ya Kristo sote cc ni wanawake tu,hata kama tuna ndevu nyingiii kuliko bin Laden!”

  Nikweli, mbele ya Kristo, nyinyi wote, mnakuwa Wanawake! Kama unalosema unamaanisha kweli; Basi ya kupasa ukae kimya kwa utulivu, tukufundishe sisi ambao ni wanaume katika Kristo, maana ndivyo Neno linavyoelekeza, na ujue pia kuwa, hupaswi kututawala sasa na baadaye, maana mwamamke ndiye aliyedanganywa na shetani! Kama kweli wewe ni wakiume lakini kumbe, ni ‘Mwanamke’ katika Kristo, usikasilike, nielewe kwa makini nilivyomaanisha!

  ANGALIZO:-

  (Mtu asinikoti vibaya hapa, nasemea juu ya Baraka zitokanazo na kazi zilizokatazwa kufanywa na wanawake katika kanisa)

 177. Mabinza,ukiona unapingana na uhalisia kwa sababu ya andiko fulani,basi kaa chini ulijifunze vizuri hilo andiko maana utakuwa umepotosha maana yake.

  Hebu soma tena hiyo 1Tim 2:12 halaf utujibu hili swali,kwamba mwanamke anakatazwa kumfundisha na kumtawala nani na wapi?

  Uhalisia niliosema ni kwamba leo kuna wanawake wengi ni viongozi na wachungaji na wanaongoza kwa mafanikio hata kuliko wenye ndevu.

  Kumbuka, mbele ya Kristo sote cc ni wanawake tu,hata kama tuna ndevu nyingiii kuliko bin Laden!

 178. kama namwelewa vizuri Paulo katika fundisho lake kwa wagalatia sura ya kwanza Wgal. (1:8); Basi Ukikataa, Yesu atakutia hatiani kwa lile fundisho alilolitoa kupitia Mtumishi wake mwaminifu Paulo, ambaye alifundisha hivi, “8Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo mtu na alaaniwe! 9Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!” Maana kama Paulo unamwamini kuwa ni Mtume wa Bwana Yesu Kristo, na pia kama unaiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu lisilogoshiwa. Basi Paulo alisema hivi katika ile, 1Tim. 2:11-13, “11Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utii wote. 12Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. 13Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. 14Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji.”

  Mabinza LS.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s