Balaa, Laana na mikosi ya kifamilia.

Na Mchungaji Josephat Gwajima

Mara nyingi unapoenda hospitali, daktari huwa anauliza kama kuna mtu katika ukoo wako, ana historia ya tatizo hilo na jibu lako humsaidia kujua tatizo lako kwa undani. Vivyo hivyo laana, mikosi na balaa vinaweza kufuata familia yako kama zilivyo baraka pia.

Ndio maana watoto wengi wa viongozi serikali huishia kuwa viongozi, na watoto wengi wa maskini hujikuta wanaishia kuwa katika umaskini zaidi, ni ukweli ulio dhahiri kuwa kilichotendwa na baba huwa kinashuka hadi kwa watoto wake. Ukisoma katika Mithali 13: 22 “Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.” Pia, Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.”

Adamu na Hawa walipotenda dhambi, hukumu kwa mwanamke ilikuwa hivi, Mwanzo 3:15, Mungu aliweka uadui kati ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka. Kwanini unafikiri Mungu aliweka uadui hata kwa watu ambao hawakuhusika? Jibu ni kuwa yaliyotendwa na wazazi au mababu wa ukoo yana matokeo sana katika maisha ya mtu ya leo. 2Timotheo 1:3-5 “…5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.” Kumbe kuna uwezekano wa tabia ya mtu kuunganishwa na familia au ukoo wake. Kama imani yaweza kusafiri kiukoo, vivyo hivyo na tabia ya kutokuamini au uovu mwingine waweza kusafiri kutoka kwa mtu kizazi kimoja hadi kingine.

Ndio maana inawezekana, mtu akajikuta anafanya tabia fulani, na ingawa haipendi lakini anaendelea kuifanya kumbe ni kwasababu ya ukoo wake. 1Petro 1:18-19 Waweza kuumkuta mtu mwongo, mwizi, mzinzi, mchoyo, mbisho kumbe ni kwasababu ya tabia za kurithi ambazo zinatokana na laana za familia. Kuna uwezekano mtu akajikuta hana ndoa ya kudumu, kumbe ni kutokana na laana iliyo katika ukoo.

Ni muhimu kumjua adui unayepambana naye, watu wengi sana wanajikuta wanapambana na adui wasiyemjua huku wakidhani wako sahihi, na mwisho hujikuta wana bidii yao haizai matunda, kumbe ni matokeo ya kupambana na adui usiyemjua. Huwezi kushindana na shetani bilankujua mbinu zake “watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.”

Jambo lingine la Muhimu, maamuzi yoyote unayoyafanya leo yana matokeo katika maisha yako na ya uzao wako. Ndio maana wana wa Israeli walipokuwa wanaingia katika nchi ya ahadi Yoshua aliwaambia, “chagueni hivi leo mtakaye mtumikia” uchaguzi unaoufanya leo una matokeo mazuri au mabaya katika maisha yako.

Biblia inasema kila andiko lenye pumzi ya Bwana lafaa kwa mafundisho, kwasababu hiyo tunaweza kujifunza kitu kutoka katika maisha ya baba wa Imani, Ibrahimu. Mwanzo (11:29-30), ibrahimu alikuwa hazai maana Sara alikuwa tasa, tunaona pia mwanaye Isaka naye akawa na tatizo hilohilo la kukosa mtoto kwa mkewe Rebeka (mwanzo 25:21); na jambo hilo halikuishia hapo kwani na Yakobo alipatwa na tatizo hilohilo.

Pia, kwa namna hiyihiyo ukifanya yaliyo mema mbele za Mungu, baraka zako hufuatana na uzao wako. Tunaona jambo hilo kuwa, baraka za Ibarahimu ziliweza kufuatana na uzao wake (Mwanzo 30:1-6; 13:15; 17:7-10) ahadi za Ibrahimu hazikuishia kwake tu bali zilipitiliza hadi kwa uzao wake. Kumbe baraka zaweza kusafiri kutoka kwa mababu hadi wabibi, vivyohivyo laana zaweza kusafiri kutoka kwa kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Ndio maana hata Yoabu alipomuua Abneri, ambaye alikuwa awali amesamehewa na Mfalme Daudi, ile laana ilifika hadi kwa uzao wake.

Utajifunza pia kwa habari ya Yesu, walipotaka kumuua, wayahudi walitamka wazi kuwa “25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.” Mathayo 27:24-26 wayahudi walijua ukweli huu kuwa laana zaweza pita kutoka uzao mboja wa uovu hadi mwingine, kwasababu hiyo inawezekana unaishi katika mateso leo kwasababu ya mambo yaliyopita huko nyuma.

Mungu hapendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha (Maombolezo 3:33). Lazima usimame kinyume na kila laana katika familia yako na katika maisha yako, jitenge na kila laana za kutoka kwa familia au ukoo wako. Balaa, laana na mikosi ya familia yako na ivunjike katika jina la Yesu Kristo.

Na Mchungaji Josephat Gwajima

Advertisements

28 thoughts on “Balaa, Laana na mikosi ya kifamilia.

 1. Mungu ambariki mch Gwajima, kwa fundisho hili. Nimefuatilia mafundisho yake mengi, nimegundua siri/hazina kubwa iliyomo ndani. Huduma yake ni ya kiuzoefu zaidi. Wengi huishia kunakikilisha maandiko bila kuyafanyia. Tukumbuke maneno ya mtume Paulo (maneno yangu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya wanadamu bali kwa dalili ya roho na nguvu). Watanzania Mungu atusaidie sana tunapenda sana argument badala ya vitendo. Mch Gwajima ni wa vitendo zaidi (sio kwamba namfagilia bali nasema kilichoko moyoni).

 2. Kama unadhani umeniambia jambo la muhimu sana na unawasi sitafanya, uje unisimamie live!

  Ila na wewe usisahau nilichokuambia kua si magonjwa yote ni devo eeeee…mengine ni kwa kua haupigi mswaki Sungura ivyo fizi zinajazia ukoko wa matobolwa na bacteria kwa uwezo waliopewa na Muumba, SI DEVO HATA KIDOGO, wananusia kwa mbaali na kukusaka maana umewatengenezea mana yao , wala iyo zege wakipita pita umo mjini ktk fizi zako uku wanajisaidia haja kubwa na ndogo wakiendelea kula nakufuraia upaji wa Muumba wao kisha unaumwa fizi, unakemea pepo, what imbalanced exaggeration of things is that?

  Press on

 3. Umecheka, safi sana.
  Cheka bwana, maana kucheka ni afya!
  Lakini usije ukawa umekomea kucheka tu bila kuelewa nilichomaanisha hapo.

  Aliyeniambia malaria fungu lako ni wewe mwenyewe, umesahau?

  See u!

 4. Sungura,

  Hahahahahaha, mwe! una milipuko na milopoko huna spare wewe kwa kweli! nimecheka mpaka machozi hahahahaha hii.yako hii..”So do u think that I’m being ghoulish? Basi nakushauri jambo hili: hata wewe nenda gym na upunguze kula maana unene utakuuwa mapema, koz kunenepa sana unajiumbia
  shinikizo la damu- labda kama umepungua maana sijakuona siku nyingi”’ Kwa toka kujadili sasa wewe umekua doktaaa? ati ujaniona siku nyingi, twih! such comedian aah!

  Sasa wewe kila kitu kwako , i mean kiiiiila ugonjwa ni devo hata kama haujafua nguo zako na unakua mchafu kisha wapata harahara wewe halafu wamsingiazi devo!!! hata kama devo ni mbaya, si kila kitu yeye bwanaaa, umesema let us be realistic, hii nayokwambia ndio reality, mengine unazidisha chumvi au ukiroho-fake sana wewe!

  Press on(aliyekuambia malaria fungu langu nani?) au okay Kaka!!!

 5. Seleli si kwamba sikuelewa ulichokisema katika hiyo Wakolosai.1:13, ishu ni kwamba sikukubaliana na msimamo wako hapo. Nikakwambia wokovu kwa ukamilifu wake ni process, si kila kitu lazima kitokee mara kwa kila mtu anapompkea Kristo.

  Na nikakuuliza unaposema baada ya mtu kuokoka unamaanisha kile kitendo cha mtu kuomba ile sala ya toba au nini?

  Leo hii mtu anaweza akasema hiyo sala hata kwa njia ya internet,au kitabu, unadhani hizo nguvu za giza kama atakuwa nazo zitaondoka mara?
  Let’s try to be realist Seleli, usilaumu tu kwamba kufikiria hivyo ni kufikiri kinyume na kazi ya Kalvary.

  Mara ngapi tumeona watu wanampokea Yesu na kesho yake wakija kwenye semina wanalipukwa na mapepo, au wewe hujawahi kuona hiyo?
  Huyo nyoka uliyemwona yawezekana hakutokea wakati mtu anaongozwa sala ya toba, bali wakati anafanyiwa maombi ya kufunguliwa. Na mimi nimeona mara nyingi tu mtu anakuja kufunguliwa hata mwezi baada ya kuwa amempokea Yesu.

  Ukweli ni kwamba mafunuo juu ya ya yale Mungu anweza kufanya haujafika mwisho na hayatafika mwisho, Yesu alisema tutafanya zaidi. Wazee wetu hao walitumiwa na Mungu kama alivyopenda,hata leo Mungu anawatumia waliopo kama anavyopenda. No limits.

  Lakini pia mafundisho ya ujanja ya wachumia tumbo hayo yapo tu siku zote hata wakati wa kanisa la kwanza.

  Ha ha haaa, you made me laugh Seleli. So do u think that I’m being ghoulish? Basi nakushauri jambo hili: hata wewe nenda gym na upunguze kula maana unene utakuuwa mapema, koz kunenepa sana unajiumbia shinikizo la damu- labda kama umepungua maana sijakuona siku nyingi.

  Kwamba Mungu alileta gharika, jaribu tu kurudi nyuma ujiulize kwa nini Mungu alishusha gharika, halafu utauona uhusika wa shetani.

  Mengi uliyoyasema( the so called biological factors), mwanadamu ni mtendwa au mtendewa, siyo source. Na kama na yenyewe yanaweza yakaondoka kwa neno la maombi basi haikuwa sawa yenyewe kuja katika mwili wa mwanadamu.

  Maana kama hayo ya kibaiolojia ni kazi ya Mungu basi tusingekuwa tunaweza kuyaharibu kwa jina la Yesu, maana yeye alidhihirishwa ili kuharibu kazi za shetani.

  Ukweli tu ni kwamba wengi wetu hatujaujua uwezo wa Mungu katika kupambana na haya mambo. Yesu hakuwahi kuugua pamoja na kulala kwake milimani akiomba,hata mitume sijaona kama waliwahi kuugua. Yule nyoka mikononi mwa Paulo hakuwa ametumwa kichawi, alikuja tu kama kiumbe na alikuja mahali ni lazima alikuwa amg’gate Paul, lakini yeye ndo akapelekwa un-natural.

  Seleli kama wewe unaona kwamba ni halali kwako kuugua malaria kwa kuwa ulisahau kuweka neti, ni halali kuugua tumbo kwa kuwa ulikunywa maji yasiyochemshwa, basi haina shida bila shaka unaona hilo fungu linakufaa.

  Asante!

 6. Sungura,

  Nimeshafafanua HASA nilikusudia nini katika surface outlook ya kile nilisema ambacho kilikutatiza lakini bado unakazia kama vile hakuna ufafanuzi! hii mambo ya kukiri/kupitiwa, halitatokea, cha msingi umepata hasa nilitaka kusema nini! ni maamuzi yako kuchukua kile kinachokusudiwa au kile kisichokusudiwa.

  Mchango wako wa mara hii, unanirudisha kule tulipoanzia na ndio maana mara nyingi nakusisitizia uwe una jibu maswali! Napenda ufahamu kua napouliza vitu, sikurupuki hata kidogo, naposoma mada humu kisha kwa ufahamu, kutafakari, uzoefu, maarifa ya Neno,ukweli halisia wa maisha haya, kuwaza kwa akili ya kawaida, nakua naona au nimeona mambo ya kuweka sawa, yatakayojili uko kwa aina ya mjadala/mada/somo na kwa kadiri mjadala utakavyo kwenda ndiposa naibua hoja/maswali kwa nia njema tu ili, mpaka tunafika uko, tumeshamaliza vema sana yanayojiri na hatimaye ni rahisi kuhitimisha kwa uzuri kabisa. Tatizo lako ni kudhani kila kitu hakina maana, kua yale unayosema wewe tu ndio yenye mashiko( kitu ambacho si kweli) na ivyo inakupelekea kutokua muungwana na mpevu wa dhati na ushirika ktk mijadala, sifa ambazo zingekuhubiria na kukukufanya uwajibike kwa yale unayoulizwa kama vile wewe unavyopenda wenzio wawajike kwa yale unayoibua na bila shaka wajijua pia kua uko mzuti wa kutaka sana yako yajibiwe! Fanya ivyo kwa wengine pia wanapokutaka ivyo, inasadia kumaliza mambo mapema na kwa uzuri.

  Kule mwanzo, niligusia aina/vyanzo vya magonjwa kwa kutumia lugha hii, ‘’yale ya ulozi/wanga/nguvu za giza/mizimu/ uchawi/pepo au shetani mwenyewe’’, nikasema hapo swala la magonjwa ya kibaolijia linakufa na nikatoa mfano kua unaweza kuta mtu ni mgonjwa kweli lakini wakipima Hostipitalini, hamna kitu lakini aumwa kwelikweli. Pia nikagusia ukweli huu kua Mtu anapookoka tu ILE YA KIKWELI-kuamua kwa dhati toka giza na kuja nuruni, yanang’olewa MARA MOJA magonjwa/ shida/ adha/ mateso/ makandamizi/ Nkutawaliwa/ laana/mikosi/mablaa na vurugu zote chafu za adui za aina ile pale juu dhidi ya Mtu na ndio maana ya andiko la Wakolosai.1:13…. …KUOKOLEWA toka NGUVU ZA GIZA kisha KUHAMISHWA NA KUINGIZWA nuruni.

  Hilo haukuelewa maana ktk michango yako, ulisema bado mtu akiookoka, anaweza kua na magonywa kwa maana ya aina izo za juu hapo na kwamba yanatufuata uko uko nuruni! na ndio kwa ufahamu huo, ‘tumechomekewa’ miaka hii ya 90 mwishoni mpaka leo fundisho kua hata kama tumeokoka, bado kuna ‘madude’ tunayo au yanatufuta-fuata au yanaishi nasi ivyo inabidi kupata huduma maalumu ya kuyaondoa! Ufahamu kama huu kwa Mtu wa Mungu dhidi ya kazi ya YESU Calvary, ni masikitiko na huzuni kubwa jinsi gani KWELI haijafahamika au imefahamika ila inapotoshwa ili baadhi ya Watu washibe kwakua wanaamika na wafuasi wao basi wameaminiwa kwa kila kitu hata kuliko Bible wakati mwingine kwa kila wakisemacho. Mambo haya ya miaka ya karibuni jambo ambalo ni ushahidi tosha kua kuna tatizo LEO kwani Wakati wa Wazee wetu wa Imani hii ya kipentecost Tz eg Mze Kulola, Emmanel Lazaro, Nshimba, Kapinga, David Kuselya na wengine shuhuda zao kuanzia miaka ile ya 40 kati mpaka ya-90 mwishoni, hakukuweko na wimbi ili la leo la mafundisho haya ya ‘man-made’’. Je ndio kusema sisi tuliozaliwa na wao Kiroho, ndio RM anatuonyesha sana mambo nini kuliko wazee wetu na kwamba leo tunaRM mkubwa sana kuliko wao? si wazi tu hapa kua kuna ujanja wa mijini na majijini umeingia maana hata uko ktk baadhi ya Wilaya na Mikoa bado kuko salama, man-made doctrines/skills ktk self-centred Word preachings, ni mdogo au hamna.

  Tokea hapo ndio nikaongea magonywa mengine ili kuyatofautisha na yale ambayo nimesisitiza ni ya moja kwa moja ya uwepo ana udhihirisho wa uonevu/utawala/umilikaji wa nguvu za giza/pepo/ulozi nk-mfano mtu kupima, hakuna ugonjwa lakini anaumwa, mimba ya miezi 9 kisha anazaa hewa au tumbo linauma kisha ktk maombi, anatapika kalamu za raska 7 au nyoka mrefu(imetokea live jangwani wakati ule wa Big Nov crusades na nikaona kwa macho yangu haya ya nyama si ya kuzama-zama rohoni). Haya ya kundi la pili, nikayataja kama magonjwa yanayosababishwa na Viumbe tu wa kawaida walioumbwa na Mungu then sisi Wanadamu kuwaingiza/karibisha ktk mazingira yetu ya nyumbani/mwilini ambamo hawaruhusiwi.

  Mfano: kuacha bila kuosha mwiko = kombamwiko/mende atakuja tu kula! anakuja pale kama kiumbe anayelishwa na Mungu maana Yeye huwahudumia wote kama alivyosema kuhusu ndege wa angani( na bundi yumo mpaka kunguru anayekunyakua samaki ukizubaa) na maua ya kondeni-Luka12:22-30.! Au ukila embe nje, Izi anakuja tu maana alikua angani au ktk manyasi na vimiti hapo anapunga hewa ya Muumba wake uku akisubiria kulishwa na Muumba huyo huyo, pia vivyo ivyo mnyoo,amoeba, ktk tunda na mboga mboga,mbu ktk nyumba za watu nk. Hawa wadudu na rafiki zao waliobeba(vimelea-viumbe wengine hao), wakihamishiwa toka sehemu moja na sisi wenyewe( kwa kunywa maji, tunda,acha vyombo au mwiko bila kuosha, kulia embe nje nk) na si lazima hata kidogo kua shetani anakua amemshawishi mtu ati sijui amempumbaza Mtu kula embe nje au kula bila kuosha mikono,(this is ghoulish and excessive accreditation of the devi, unrealistic and unbiblical spiritualizations indeed) because,wakati mwingine ni Mtu tu kama Mtu amechoka, anapuuza kuchesha maji kwa mfano au hazingatii tu, ni hulka halafu hatimaye kwa tabia izo zetu, tukajikuta tumewaingiza wadudu hao tumboni wasikostahili, matokea ni Ugonjwa( DISEASE )= an abnormal condition that affects the body of an organism. It is often construed as a medical condition associated with specific symptoms and signs, sorce-google! Ugonjwa kwa maana hii-nenda hata Hospitali kawaulize-maana yake ni viumbe wasiotakiwa kuwepo ktk eneno lisilotakiwa ivyo, wanauwawa kwa dawa na unapona, HAPO HAKUNA PEPO, WALA UGONJWA NGUVU ZA GIZA NA ULOZI BALI Ni chidudu eg ameoba nimekiweka tumboni, ndo maana nikikitoa kwa kula dawa eg conaz, mwisho wake umefika. Lakini magonywa yale ya juu, hata cozan ukimeza, amoeba-pepo/ulozi hafi, utaumwa tu!

  Au Magonjwa udhaifu wa mwili mfano kwa kua umechoka so kichwa kinauma au uzee, umepata ajali(si kila ajali ni devo-acheni uongo au kumpa credit sana, saa nyingine dereva mzembe tu au mkorofi, anaambiwa acha mwendo kasi hataki mpaka kumtishia trafiki au kumdunda na hatimaye atapunguza na hakutatokea ajali kamwe) au umekua subjected ktk hali fulani mbaya mfano huzuni, sononeko la moyo kisha unapata H or L pressure linalopelekea mengine au ulemavu wa viungo( kiwete, ngozi albino nk) yaani yale Magonjwa under group namely INFIRMITY = physical weakness or ailment, haya pia SI LAZIMA AWE DEVO! Ni human factor au human yeye mwenyewe.

  Kwa mantiki izo, bado nasisitiza, si kila kitu ni devo na si kila gonywa ni nguvu za giza au shetani bali na mengine ni ya kibailojia tu kama nilivyoeleza juu. Ni sawa na Mafuriko, ukisema hakukuweko na fungu la Mafuriko ktk plan ya Mungu ili wanadamu waishi bila dhahama yoyote, ni kweli lakini Mungu huyo huyo atasababisha mafuriko kuuwa watu( wakati wa gharika Mr. Nuhu-Mwanzo sura za 6,7,8,9) au Mwanadamu atakata miti ovyo, chimba madini ovyo, kukawa na mmomonyoka wa udongo, uoto wa asili ukaisha, yatakayotokea majanga kama ukame, mafuriko nk, all those will have COMPLETELY nothing to do with God or devo, ni geographical changes/factors engineered 100% by human. Tusipende kusema kila kitu shetani, SI KWELI! Najua tulikaririshwa wakati ule lakini kwani lazima tuendelee kukariri bila kuelewa sasa?

  Yupo Shetani na Mwanadamu basi Magonjwa yapo but yote SI devo!
  Press on

 7. Seleli acha maneno mengi ya kujikosha, ni bora ukasema ukasema ulipitiwa kama kukiri kuwa ulikosea ni kitu kigumu kwako.
  Ukweli ni kwamba mara ya kwanza ulisema si kila kitu huanzia ulimwengu wa roho, wala hukuwa umesema kwamba kila kitu huanzia ulimwengu wa roho lakini kuna human role. Ukatoa mfano wa maandishi kwenye yako laptop kwamba kudhani na yenyewe yanaanzi rohoni si sawa. Au nakusingizia?

  Ona hapa, ”TUNA YETU TUNAZALISHA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NA YENYEWE YANATOKA KTK ULIMWENGU WA ROHO,-Mfano ni kituko kusema napoandika sasa-haya maandishi kwa laptop, yalikuwepo/yaliumbwa ktk ulimwengu wa roho- eti yakoga uko” Haya ni maneno yako. Human role uliyosema hapa iko wapi Seleli?

  Mchango wako uliofuatia ukasema sasa hiyo human role, ”TUNA YETU TUNAZALISHA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NA YENYEWE YANATOKA KTK ULIMWENGU WA ROHO, ni simply kukuonyesha kua iko role ya Mtu mambo kutokea-ndicho nilichomaanisha na kama ulikimis ndicho icho. Ninaelewa concept/Ukweli huu wa Bible kua mambo uanzia ktk ulimwengu usio onekana kuja kwetu live, lakini ni ukweli pia, uko yatokako, hayajitoke tu! yanaumbwa kishwa undwa-idea ya laptop machine kisha kua kweli, ivyo tu. Na ilo ni gumu kufahamu au?” Ukamalizi kwa kuniuliza swali la dhihaka. Lakini hapa ulijaribu kukubali kijanja kuwa mambo yote huanzia ktk ulimwengu wa roho, tena kwa kujaribu kujificha kwenye ishu ya human role.

  Usijaribu kuona kuwa human role na source ya jambo ni kitu kimoja. Chanzo cha magonjwa hususani, na nafasi ya mwandamu kufanya hayo magonjwa yamuathiri ni vitu viwili tofauti

  Elewa kuwa human role haiondoi ukweli kwamba maandishi katika laptop yako yalikuweko tu siku zote katika ulimwengu wa roho, mwanadamu katumika kuyadhihirisha katika ulimwengu wa kuonekana.

  Kwa hiyo ulitakiwa ukubali kwanza ulichokuwa umekikataa kwamba mambo yote huanzia ktk ulimwengu wa roho, baadae ndo uje useme sasa kwamba lakini ili yadhihirike ktk ulimwengu wa mwili mwanadamu anaweza husika.

  Kama unakubali kwamba haikuwepo katika original plan ya Mungu wakati unajua kabisa kuwa hao viumbe walikuwepo ktk original plan ya Mungu, maana yake ni kwamba hawakuumbwa ili wasababishe magonjwa. Maana magonjwa yenyewe si toleo la Mungu,yaani kwamba Mungu hakuumba ugonjwa.

  Kwa kuwa ugonjwa si toleo la Mungu lakini tunaona leo upo, maana yake ni toleo la shetani. Mwanadamu anapata magonjwa kwa sababu ya hila za shetani, na shetani ndiye msababishaji wa hayo magonjwa wala si huyo mwanadamu ambaye anapatwa na hayo magonjwa.

  Mfano: Mpendwa/ mtu akila kipolo cha kande bila kukichemsha halafu akaharisha, ni rahisi sana kusema hapo si shetani ni huyo mtu. Lakini kamuulize akwambie ilivyokuwa mpaka akaamua kula. Tena kama ni mpendwa lazima shetani alimshawishi hata kwa maandiko; e.g mkila cha kufisha hakitawadhuru, nk. Lakini ukweli ni kwamba mchakato huo wote mpaka anaamua kula kipolo hicho kuna hila za shetani nyuma yake.

  Unasema namkuza shetani, siyo kweli. Ukweli ni kwamba shetani si mdogo kama unavyotaka tumwone. He is our arch- enemy. Yesu hakumpuuza shetani.
  Ni kwa sababu tu ya damu ya Yesu na kwa neno la Mungu tunamshinda.

  Hakuna shetani-hakuna magonjwa!

 8. Sungura, nimeshangaa kua unataka nithibitishe hapa hadharani, mambo yasiyofaa uko na kule ktk mada nyingine! uliyoteleza/pitiliza na kuongea vibaya, kimajigambo,kejeli na kusapoti mizaha iliyopindukia na kudharau wengine(mimi nikiwa mmojawapo wakati ulipokosea sana,sana kabisa, ukidhani mien aye ni rahisi kuvamiwa ovyo ovyo) You can’t be serious man.! Kweli? Una taka ni copy na kupaste hapa mambo yako yasiyo na tija? Come on, please try to be serious and let us avoid petty issues as very well recommended by you, however, if you think it is sweet thing to do, I SHALL speedily do it VERY WELL LEAVING NO ANY dot and you know very well I CAN.

  Hoja ya vitu kuanzia katika ulimwengu wa roho, pia umenishangaza! Mimi sijifichi na kama sijui nitasema ila kama najua, usinilazimishe niseme au nionekane sijui, nitakutalia mpaka kesho na kukuthibitishia najua. Ivi in an overall understanding, Mtu anayesoma Neno na kufahamu Biblical phrases kama ‘’viumbe visivyo na vinavyooneka’’ au ‘’ivi vionekanavyo vimeumbwa toka vile visionekana’’, unawezaje kudai kua huyo Msomaji hajui kua ‘vilivyopo, vimetoka uko kusikoshikika? That is a joke!

  Nimefafanua WHAT ACTUALLY I meant. Nadhani unajua kuna intended and surface meaning ktk maandishi au statement za mtu na inategemea mpokeaji na hata mtoaji, wamewasilishaje/wamewasilianaje ndio maana hata Rais, PM,MB,ASKOFU, nk wakitoa hotuba kisha akina MWANA HALISI WAKANUKUU baadhi ya waliyosema ambayo si hasa wali-intend watu wasikie, viongozi hao, hutoa Ufafanuzi-efforts za ku-clarify haswa walimaanisha nini ijapokua shape ya nje ya statement/maandishi yao(kama walitoa tamko kwa maandishi)-may appear or be wrongly swallowed wakati mwingine si lazima sana aliyewasilisha kakosea uwasilishaji bali wapokeaji tayari wanakua na wish/intentions/interests au crippled if not polluted pre-concived ideas. Besides, inategemewa Mhusika akishasema tena/fafanua hasa lilee alilokusudia, then akina MWANAHALISI(MAWIO) wachukue/shike ilo la mwisho KAMA WAKO MAKINI AND SI BIASED WAANDISHI. The worst conduct ni pale MWANAHALISI AKIENDELEA KUNG’ANGANA NA LILE LA KWANZA! hapo UNAJUA TU MARA MOJA, ANA LAKE JAMBO! Nimefafanua kua kusema si kila kitu LAZIMA kianzie ulimwengu wa roho, hasa si kukataa on serious note, kua- all are created/originate there lakini ni pia kuleta kweli nyingine kuna ROLE KUBWA SANA YA MTU ILI HAYO( at least SOME-yale yaliyo chini ya himaya yake) YATOKEE AU PIA YASITOKEE HATA KAMA YAPO UKO! Remove/place a man on earth, yanatokea au yanaweza yasitokee . Mtu si robot/box duniani ndio maana MWANZO.1:26-28- amepewa uwezo na mamlaka ya ajabu kweli na Yeye huyo mwenye yote-yaani ktk hayo yote ya Yeye mwenye yote, ame-delegate some kwa Mtu in full swing kuya-operate/sababisha/leta hivyo statement yako hii kua Mwanadamu ni ‘mtendwa au mtendewa’’, ongeza kua yeye pia ni ‘’Mtenda’’ kwa mantiki ya nilichosema juu na power iyo ktk Mwanzo aliyopewa. Nasisitiza, DONT MAKE HUMAN, A BOX, BOTTLE OF UHAI WATER OR TIKITIKIMAJI ON EARHT.

  Kwa sababu iyo juu, NAPINGA SANA KABISA kusema source ya magonjwa YOTE ni adui. Mtu hawezi kaa bila kuoga siku mbili, akapata ugonjwa wa ngozi au uvivu tu wa kutofua mashuka, kisha akapata harahara halafu tuanze kukemea devo ati ni adui kaleta! Hayo maombi ni bora kwenda kupalilia karanga kwa matuta yangu Geita kuliko kuwa mjinga kiasi icho. Hizo washawasha au harahara kwa ngozi si devo hapo wala nini, bali ni Mtu ameunda mazingira kwa kujua au kutojua na viumbe vingine vya Mungu(si viumbe vya devo, maana devo naye pia ni kiumbe kilichokosa cha Mungu), vikapata nafasi ya kustawi, ni kama vile unakula embe hadharani bila kukinga, inzi akatua hapo akiwa kwa upendo kabisa amewapa lift vimelea wegine, huo ugonjwa utakaokupata, si devo wala nini, ni uzembe wako Mtu na huyo inzi na wenzake aliowapa lift, si devo wala pepo, ni viumbe vya Mungu vinatambaa angani, kufurahia maisha na kutafuta chakula hapa na pale,as simple and correct as that. Kusema KIIIILA kitu ni shetani au Mungu, ni kutaka ku-sound kiroho but hakuna maarifa/ufahamu-YOU CAN BE VERY SPRITUAL LAKINI KAMA HAKUNA MAARIFA/INFORMATION, UNAANGAMIZWA TU KAMA KAWAIDA- Hosea.4:6 THEN UTAJUA KIROHO CHAKO NI MECHANICAL/ARTIFICIAL OR REAL!

  Kwa maana iyo iyo ya juu, si KWELI ulivyosema Mtu akitukana, ongeza na basi na kuzini,kupiga wife, kufoka, kasirika,nuna, useme yote hayo ni devo! Mtu yuko wapi hapo? devo tu kila kitu? why do you make him so big? Izo ni tabia/hulka za Mtu AKIAMUA KWA UTASHI WAKE au KULAZIMISHWA ATAACHA AU KUENDELEA-MBONA JAMII NYINGINE, UKIIBA TU, UNAKATWA MKONO, NA IVYO STATISTICS ZA WIZI ZINAPUNGUA KAMA SI KWISHA KABISA? why? Simple!= Watu wanaogopa kukatwa mkono hence wanaamua kucha, iwe kwa hofu au raha but si kweli wameacha tu, sasa je! Kwa iyo ni kweli Yeye ni mtendwa tu au mtendewa BUT PIA MTENDA.

  Yes, Haikuwemo katika original plan ya Mungu wakati anaumba kwamba kuwe na ajira ya surua, majira ya mafua, majira ya malaria, n.k BUT HAO VIUMBE-strictly and get this in your mind-ni wa Mungu- WANAOSABABISHA HAYO MAGONJWA ni kwakua WANAWEZA kua wame KARIBISHWA NA MTU ivyo AKADHIRIKA-completely no devo hapo au devo akawatumia hao viumbe pia. Besides, bado Mtu akijiweka ktk mazingira safi, hata kama devo angetaka vipi kuwatumia, atashindwa tu-kuonyesha si kila gonjwa devo! Mfano akihakikisha Mtu hanywi maji yasiyochemshwa, hali matunda bila kuosha kwa maji moto, havai nguo za ndani mbichi, mashuka anafua, mbu wameuawa wote na ‘ekisipeli’, no devo wala gonjwa la devo au la kiumbe kuja sehemu isiyo yake. Hii mbona simple sana kuelewa Sungura au unatatizo gani lakini? Vitu vingine so clearly simple, logical, Biblically balanced, spiritually fine tuned yet you miss the WHOLE THING! Pole

  Press on( relax, I will keep flowing tutafika mahala kila fact/truth itakua well plated hapa)

 9. Seleli usiseme ninafahamika kwa tabia hiyo, sema wewe ndo unaniona nina tabia hiyo. Usiongee nadharia, jaribu kuthibitisha hiyo tabia yangu, michango yangu si ipo!

  Hoja ya vitu kuanzia katika ulimwengu wa roho ulivyoisema mwanzo na unavyojaribu kuisema kwa kujificha sasa hivi kwa kujificha usionekane kuwa ulikuwa hujui ni tofauti. Ngoja nikuoneshe.
  Nakunukuu ”-TUNA YETU TUNAZALISHA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NA YENYEWE YANATOKA KTK ULIMWENGU WA ROHO, hii itakua ni kulazimishia point ya ukweli hiyo kuiingiza kila sehemu ambako yaani waaaalaaa haihitajiki au hata ku-connect ili to make sense of out”

  Baada ya kusema hayo ulitoa mfano huu ”Mfano ni kituko kusema napoandika sasa-haya maandishi kwa laptop, yalikuwepo/yaliumbwa ktk ulimwengu wa roho- eti yakoga uko! Mmmhh! Mmmmmmh jamani, hii kulazimisha mambo yote yawe ya kiroho ili tuonekane siye wakiroho yanachekesha eee sometimes.”

  Hapa ulikataa kuwa maandishi katika laptop yako hayakuanzia ktk ulimwengu usioonekana, wala hukuwa unaoongelea role ya binadamu ktk kuyafanya hayo maandishi yaonekane.

  Lakini kwenye mchango wa mwisho umekubali kuwa mambo huanzia katika ulimwengu wa roho na baadae katika ulimwengu wa kuonekana. Na kwa hiyo tunakubaliana kuwa computer na hayo maandishi yanayotokea unapoachapa yalikuwepo tangu milelele ktk ulimwengu wa roho. Source yake si mwanadamu bali mwanadamu ametumiwa tu kuyadhihirisha katika ulimwengu wa kuonekana. Hiyo ndiyo human role katika hili.

  Kwa hiyo nikirudi kwenye swali lako, kwamba katika yote yanayompata mwanadamu yeye hana uhusika wake?

  Jibu ni kwamba mwanadamu ni mtendwa au mtendewa,lakini source ya hayo, magonjwa hususani, si yeye, bali ni adui.
  Ukimwona mtu anaondoka kwa miguu yake kwenda kuiba, ukimwona mtu anatukana, ukimwona mtu anakunywa sumu huku anajua kuwa hiyo ni sumu,kinachofanya kazi ndani yake si nguvu yake bali ni ya shetani. Yeye ni mtendwa tu au mtendewa.

  Ndio maana nikasema,source ya magaonjwa na mabaya yote ni shetani. Hata kama kwa kuonekana anaweza kuonekana bacteria fulani ndo anasababisha lakini chief engineer nyuma ya pazia ni shetani.

  Haikuwemo katika original plan ya Mungu wakati anaumba kwamba kuwe na ajira ya surua, majira ya mafua, majira ya malaria, n.k

  Namkomea hapa kwa leo.

 10. Sungura,

  Mtu akisoma tu hapa comments zako zilizopita hii uliyonijibu kuniambia nina majigambo na kujiinua na kuona najua sana, na asikusome comments zako ktk mada nyingi maeneo mengine, anaweza kudhania huna hatia kabisa na umeongea la kweli, lakini ushahidi wa nani hasa huwaambia wenziwe kua wasaidiwe, hawajui, huwaona wenzie hua hawako makini, hawakusema kitu, wana ufahamu mdogo wa Neno(uliwahi mwambia mmoja ivyo) na mara nyingi kwa yale wanayosema wengine, yanakua hajakamilika/fikishwa vema mpaka usema wewe, unafahamika kwa tabia iyo, ndipo sasa niliwahi kukushauri kua labda una miss vitu toka kwa posts za wengine kwa sababu ya attitude yako kwanza, iyo ikibadilishwa, utaweza ona mema ya wengine, fanya ivyo utaishi, na pengine ukifanya ivyo, utaniona ivi pia ulivyosema.
  Nikutoe wasi, hata mie sihitaji mwanafunzi aina yako, nitamfukuza mara moja darasani maana mwanafunzi anayeweza jiaminisha kua hata mwalimu wake, hawezi sema kitu kikapita mpaka yeye mwanafunzi akinyooshe, huyo ameshafuzu, hapaswi kufunzwa

  Mantiki ya nilichotaka kusema hapa… ”TUNA YETU TUNAZALISHA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NA YENYEWE YANATOKA KTK ULIMWENGU WA ROHO, ni simply kukuonyesha kua iko role ya Mtu mambo kutokea-ndicho nilichomaanisha na kama ulikimis ndicho icho. Ninaelewa concept/Ukweli huu wa Bible kua mambo uanzia ktk ulimwengu usio onekana kuja kwetu live, lakini ni ukweli pia, uko yatokako, hayajitoke tu! yanaumbwa kishwa undwa-idea ya laptop machine kisha kua kweli, ivyo tu. Na ilo ni gumu kufahamu au?

  Labda katika yote uliyosema, na niliyosema, niya summary kwa kukuuliza maswai haya ili niweze jua hasa tuko na uelewa tofauti kabisaaaa au mmoja maana inaweza kua unacheza na maneno tu kumbe unayosema na mimi ni yale yale kwa mantki ya ujumla
  (a) Kwa iyo ktk yote yanayomtokea na yatakayo mpata mwanadamu, YEYE HANA ROLE KABISA ya kuyasababisha yeye kama yeye 100% BALI NI AIDHA MUNGU AU SHETANI?-Bila shaka nikipata jibu, swali la nyongeza kwa hili litakua limekufa.

  (b) Narudia hili maana kuna baadhi ya maswali umepita mbaaali!!!!!!!!… Nilisema, Ukimuhamisha mdudu-kiumbe cha Mungu si devo aliyekiumba, toka eneo lake fano amoebe,myoo kikahamia tumboni kwa uzembe tu mfano kutochemsha maji kisha ukaugua kwa mantiki iyo tu tena ya kisayansi ya kiumbe kuwepo ktk eneo ambalo hakipaswi kua, huo ugonjwa mfano tumbo kuuma au kua na minyoo ni shetani huyo na amesabisha yeye au ni kosa la Mtu na ni kiumbe tu kimekaa kusiko kwake? au umeingia banda la kuku na kuanza usafi, ukasahau kuziba pua na mdomo kisha ukanza kupiga chafya mfururizo(wenye aleji wanalijua hili) mpaka kichwa kuuma-ugonjwa huo na kukohoa, kifua kubana-magonjwa hayo, ni shetani au vumbi ile au mtu kutofunika mdomo na pua kabla ya usafi? Au si wewe uliyeingia bandani lakini jirani uko anafanya usafi na vumbi yakufuateni mpaka kwenu, nani mhusika hapo wa magonjwa hayo?

  Ayo mengine ya niache kejeli na sijui nikijibu, najionyesha sijui, put pending, mimi si wewe na sitakua wewe, nina namna yangu ya kujadili na kuflow freely, don’t make me U, never, so ur advice is trashed. Kama sijui, jibu hoja zangu, leta majibu ya nayokuuliza, toa shule/somo then nitajua, la sivyo nitakuona unakwepa tu kuwajibika yanayokuhusu Sungura.

  Press on.

 11. ..inaendelea hapa Seleli….
  Mtu hufunguliwa toka katika kuonewa na shetani kulingana/ kwa kadiri ya nguvu ya Mungu inayofanya kazi ndani ya mtu anayemhudumia.

  Wanafunzi walishindwa kumtoa pepo, Yesu alipokuja pepo aliondoka mara moja.

  Lakini pia unaposema mambo kuondoka mara mtu anapookoka unamaanisha dakika mtu anapompokea kristo alimaarufu kama kuongozwa sakla ya toba?

  Na mimi nakwambia tena, kila weakness ya mwanadamu ni shetani. Role ya mwanadamu hapo ni kumpa nafasi shetani basi. Acha kumpa nafasi uone kama utakuwa na weakness yoyote.

  Kuna swali uliniuliza kama nina uhakika, nikakwambia nina uhakika, lakini umeongeza kuuliza almost kitu kilekile. Na chenyewe jibu lake ni ndiyo!

  Kama unadhani kuwa mwanajeshi (aliyeokoka- maana tunaongelea watu waliokoka) anaweza kuugua kwa sababu ya hali ya mazingira ya kazi yake kama ulivyolezea hapo kwenye mfano wako, basi hujaujua uweza wa Mungu Seleli.

  Ikiwa amesema hata wakila kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa, sembuse na kuvaa nguo mbichi tena kwa amri ya kamanda!!

  Naona unajaribu kuupima uwezo wa Mungu katika kipimo cha ‘common sense’ utapotea rafiki yangu.

  Infact, aliyeokoka akifikia ufahamu kamili wa uweza Mungu hatakiwi kuteswa na ugonjwa wowote, uwe wa kichawi au kibaiolojia, kijiografia, ki hali ya hewa, nk.

  Lakini pia kumbuka habari ya wana wa Israel katika nchi ya Misri ( Gosheni) jinsi kambi yao ilivyolindwa wakati Misri yote ikipigwa

  Yesu alikuwa mwanadamu, mbona hatumwoni akiugua kimazingira? Unadhani siku zote alikuwa anakunywa maji yaliyochemshwa, au chakula kilichopikwa vizuri sana, au alipokuwa amefunga siku arobaini alikuwa anapata maji ya kuoga ili asipatwe na fangasi?

  Hapa hata sikwambii kama hujui, lakini unatakiwa kujua kuwa hakuna kitu katika ulimwengu wa mwili ambacho hakikuanzia katika ulimwengu wa roho.
  Kwa kiswahili rahisi ni kwamba hakuna kitu chenye kuonekana ambacho hakikutoka kwenye kutokuonekana, hata gari ambalo amelifanya mwanadamu mwenyewe limetokea katiak kutokuonekana (ulimwengu wa roho).

  Kama hutaki prove hii sentensi yako ”TUNA YETU TUNAZALISHA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NA YENYEWE YANATOKA KTK ULIMWENGU WA ROHO” kipi ambacho mwanadamu kazalisha ambacho hakikutoka ulimwengu wa roho?

  Seleli punguza kejeli kwenye kuandika kwako brother, unajua kuna vitu unajaribu kuvijibu kwa kejeli kwa kudhani kuwa aliyeviandika hivyo hajui wewe ndo unajua, na kumbe wewe ndo huzidi kujionyesha kuwa hujui.

  Nani aliyekudanganya kuwa hayo maandishi yanayotokea kwenye laptop yako hayakutoka katika ulimwengu wa roho?

  Amina.

 12. Seleli kuna kitu kimoja ambacho unacho na sijui kama unajua kuwa unacho. Kinaitwa majigambo au kujiinua au kujiona kuwa unajua sana.

  Katika mijadala kama hii usijaribu hata kidogo kumwambia mwenzio kuwa ‘ngoja nikufundishe kitu’, wakati unachomwambia umfundishe kinachangamotoka tu.

  Haya ni maneno yako ya majigambo umeniambia ”NILITAKA SANA UPATE SHULE HII NZITO KUHUSU KAZI YA YESU KUBWA SANA, USIJE KWA KUTOELEWA, UKAHUBIRI/FUNDISHA MADUDU KWA WATU UKO/HAPA.”

  Shule unayosema umenifundisha hapo haipo Seleli’. Mimi siwezi kuwa mwanafunzi wako hata kidogo. Ukitokea umesema kitu sahihi na cha kweli waala sintaona shida kukwambia kuwa umesema kweli, na kama ulichosema nakiona sicho nitakwambia sicho, usijaribu kuwa mhadhiri wamgu brother, bado uko ‘so biased’.

  Wewe nawe ni mkristo tu mwenye ufahamu wa kawaida wa kweli ya Mungu, kun vitu vingi sana tena vya msingi unatakiwa kuendelea kujifunza.

  Kuna watu wamechanjwa chale za kichawi, je wanapompokea Yesu hizo chale hufutika?

  Sijawahi kuona biblia inasema kuwa kuna mabaya hutoka kwa mwanadamu kama mwanadamu, bali chanzo cha mabaya yote ni shetani.

  Kwa hiyo ni makusudi ya Mungu kwa kuwa ni msimu wa wadudu fulani kuzaliana wasababishe magonjwa kwetu?
  Kwamba Mungu alipowaumba hao viumbe alitaka ukifika muda wao wa kuzaliana watusababishie magonjwa?

  Seleli kujaribu kuona kuwa mambo ya kilozi,kichawi nk. ndiyo hasa yanatakiwa kuondoka mara na mengine ambayo unadhani si ya kichawi yanaweza yakabaki na kuondoka baadae si sawa.
  Nakuona tu uko sawa na mlokole anayedhani akifuatwa na mchawi atatumia mamlaka ya jina la Yesu, lakini akifuatwa na jambazi au kibaka kwa vile yeye anaonekana, basi itambidi apige simu polisi.

  Lakini ukweli ni kwamba mamlaka ya jina la Yesu inayotumika kumwondoa mchawi, inaweza vilevile kumwondoa jambazi. Cha msingi ni ufahamu tu. Mchawi na jambazi wote baba yao ni mmoja,ila majukumu tu ndo yako tofauti.

  Tofauti ya anaefanya kazi nyuma ya ishu ya uzinzi, ujambazi, ubwia unga, ulevi, utukananji, ushoga nk, na yule anayefanya kazi nyuma ya uchawi ni nini?
  Unadhani kuwa kuna shetani wawili tofauti nyuma ya hizo kazi?

  La hasha, huyo ni shetani mmoja, na hayo mambo ni mgawanyo wake tu wa kazi.

  Inaendelea….

 13. Sungura,

  Nianze na last statement yako kua umeandika sana kwa kua nimemuuliza mengi! PLZ BE FREE HAPA, alazimishwi mtu kusoma mambo humu, atayetaka na asome, kama per one sitting or after job au week-end au usiku, atajua mwenyewe apate muda lini na wapi, wewe tuchape kazi, hapa ni kazi/huduma tu basi, mengine should be considered by the ways or prematures stuff. So whatever lengthy or short inputs unaandika, naandika au yeyote, mi naRAMBA yote nukta kwa nukta, si niko kazini mimi bwanaa, hapana mchezo hapa, nikuchapa kazi tu basi ndicho nachosikiliza, mengine nayatowesha haraka na kuvunjinja mifupa na nguvu yake kwakua yanalenga kunitoa ktk focus ya kuchapa kazi tu 24/7.

  Ndiyo ni kweli Mbu, Bacteria,Virusi, Nzii, Mende/Komba Mwiko, Chawa,Kunguni, Mbung’o shetani anaweza kuwatumia hawa viumbe kutimiza mpango wake katika maisha ya mtu na NDICHO nililenga ukione kua ANAWEZA lakini wao kama viumbe wakingia sehemu isiyo takiwa mfano mwilini mwetu kwa UZEMBE wetu au wakati mwingine si uzembe lakini msimu tu wa wadudu wachafu kuzaliana-pia Wanaweza sababisha magonjwa sio kila kitu/gonjwa ni devo..si KWELI-ni unnecessarily over spiritulization of common facts which even if remained/understood as they are, haiendi contrary na Neno.Nasisitiza hapa hata kama devo ni mbaya kiasi gani bado HASABABISHI KILA KITU-yako mengine ni COMPLETELY AND 100% Human role na mengine ALTOGETHER RESULTS YA VIUMBE/UUMBAJI NA HALI YA HEWA AU GEOGRAFIA-kuna wadudu/magonywa mengine yanapatikana kirahisi sehemu fulani na Nchi nyingine hayapo, yalifutika kabisa.

  Umeshangaa ivi… mtu mpaka anakuwa mchafu kiasi hicho, injiniani nyuma ya hiyo hali ni Roho mtakatifu au?
  Jibu: Si RM bali
  (a) roho mchafu
  (b) yeye mwenyewe Mtu(roho mchafu hayupo kabisa, kabisaa)
  (c) Mazingira/Hali(yuko vitani-Mjeshi au anakimbia vita-mkimbizi, mafunzoni JKT/JWTZ, Uko vijijini serikali haijapeleka maji safi na kwa wingi
  (d) Hali ya hewa kubadikilika-msimu wa wadudu kuzaliana(hakuna devo hapo hata chembe, ni uumbaji wa Mungu hata mende/komba mwiko/mainzi unaowachukia a kuwararua na ‘ekisipel’’ wanapozaliana msimu fulani ktk mwaka

  Jibu hili kwa swali langu, umebabaisha tu/umezunguka-haukuface the pin haswa uso kwa uso..umesema/umekwepesha kwa kujibu…’’Biblia haijasema kuwa kila kitu huondoka tit for tat pale mtu anapompkea Yesu, ukatoa mfano wa Petro, alikuwa mtume lakini bado alikuwa na roho ya unafiki hadi Paul akamkemea.
  Maelezo: Nilitaka upate fahamu kwamba, yale mambo yakilozi/wanga/uchawi/mizimu ya kabila/maagano/mikosi/laana/mabalaa/makafara ya kidevo/kimakabila/magonjwa yaki nguvu za giza(hujawaona mtu anaumwa na anapima hakuna but anaumwa au ana tumbo kubwa la mimba na wanapima mtoto yumo, akizaa ana zaa hewa pyuuuuusshshshhs, au dunga ndugu haliponi au ana umwa na panya kisha kidonda kinatoa funza nk), so hayo makandimizi na maonevu na utawala dhahiri na athari zisizo na tashwishi za kidevo, HUNG’OLEWA MARA MOJA Mtu akiokoka, ndio maaana nzito ya Wakolosai 1: 13’’Naye alitu UOKOA toka nguvu za giza aka TUHAMISHA NA KUTUINGIZA ktk utawala mwigine namely wa nuru/ wake. NILITAKA SANA UPATE SHULE HII NZITO KUHUSU KAZI YA YESU KUBWA SANA, USIJE KWA KUTOELEWA, UKAHUBIRI/FUNDISHA MADUDU KWA WATU UKO/HAPA.

  Majibu yako kwa haya pia umechapia!…( a) Aliyeooka na amejwazwa Roho ya/wa Mungu, akiwa na unafiki, uongo, ni roho au tabia tu mbaya ya kawaida?
  Maeelezo: Nilitakua upate ufahamu kua iko role ya Mtu, Mungu na devo. Si kila tabia/weakness ya Mwanadamu ni devo-Again, unafanya dangerous un Biblical over- spiritualizations ya mambo ya kawaida KAWAIDA kweli(si yale ya kawaida kumbe si kawadi, kuna devo kweli)-nitategemea swali hapo kama utakua makini na nitalijibu tu vema sana.

  (b) Kwa hili umesema huelewi nje au ndani ninakokusema ni kupi na jibu la (c) unangoja majibu yangu kwa (b)
  Maelezo: Ni ndani ya moyo wake/utu wake amejaa Roho, Baba, Mwana wamefanya makao, kama kila kitu( magonjwa/tabia/weakeness ni roho wachafu ndio mantiki ya swali langu kua wanakaa wapi hao roho? Zaidi soma juu hapo maelezo kwa swali(a)

  Niliuliza ivi… Hata madhaifu tu ya Kimwili ni devo? Una uhakika? Ukajibu kwa kujiamini sana ivo..’’Jibu: Ndiyo ni shetani, nina uhakika! Du! Swali: Kua na hasira kila mara au kiurahisi, kusinzia-sinzia, kusoma Bible mbele za Watu kwa kukosea-kosea, kua na huruma kupita kawaida, ni devo au Mtu kama Mtu?

  Niliuliza ivi pia ‘ni yapi magonjwa hayo, ya nguvu za giza au ya kawaida kama utajibu kule juu maswali ya mwanzo? Ukajibu vema KIASI ivi-Jibu: Magonjwa yote hutokea kwenye giza, kwenye nuru hakuna magonjwa,ZAIDI ni kua yapo ya hali ya hewa, Geografia na Uumbaji wenyewe kwa maana Nzi akingia kwa chakula au amiba akingia kwa tumbo mahala si kwao-tumewaingiza/karibisha kwa uzembe wetu-tutaumwa tu-no devo hapo hata chembe! Ni kiumbe toka maji-alikoumbwa aishi kwa raha zake umo,nikamfuta mie mwenyewe kumuhamishia kwa tumbo kwa kunywa maji au vitu toka kwa watu wachafu walio na tabia mbaya/ udhaifu tu- no devo again hapo-wa kutojali wateja say matunda au juice ya kutengeneza hotelini au kwa mama ntilie.
  Na swali hili… la mwisho :Kwa kuzingatia maswali yale juu pale eg navaa nguO mbichi kisha fungus au ugonjwa wa ngozi unanivaa, ni devo ugonjwa huo au ni icho kiumbe-chichidudu( not kidudu-coz ni kidogo/kadogoo mno-my own word style anyway) tu, kazi/utendaji kazi wake kama kilivyoumbwa and not necessarily fully and purely devo?,Jibu lako nimecheka! Umebabaisha kweli-nadhani limekukaba vema ukasema..Jibu: Kama ulivaa nguo mbichi makusudi basi aliyekudanganya ni shetani, na kama hukua unajua shetani hufanya kazi vema zaidi pale penye giza (ujinga).

  Maelezo: Si kweli bwanaaa kama hujui kitu unasema upate msaada, hii umechemka! Si kila anayevaa nguo mbichi, devo anahusika au amemdangaya au yeye mjinga, sitakujibia ila jibu hili Swali: Na je zikiwa mbichi kwa kua uko safarini/jeshini/ukimbizini mnakimbia, na kisha uko mkanyeshewa mvua, hamna hata muda wa kuzivua na zikauke, mkavaa tu na hatimaye fungus, kunuka-devo yuko wapi hapo? Aaa bwanaaa, mbona unalazimishia mambo too appetitelessly mechanicall! havi-connect namna iyo Kakaaa.

  Hili ni kweli kabisa..’’Kitu hakiwezi kuonekana kwenye mwili (kibaiolojia) kabla hakijawa halisi kwanza katika ulimwengu wa roho, maana ulimwengu wa roho ni halisi kuliko wa mwili ILA haimaanishi KIIIIIIIIIIIIIILA kinachotokea kina side 2 tu..Mungu na Devo! Hapana! kuna ya Mwanadamu pia na ya kwake! Na ya viumbe wengine pia wana vyao. Besides, kwa kua vilivyokua ktk ulimwengu usioonekana ni viumbe-sisi, wadudu, wanyama, sasa kwa kua hatimaye tulidhihirika ktk ulimwengu wazi…kwa hapa ktk ulimwengu wa wazi tunaponekana wazi na kuishi wazi-TUNA YETU TUNAZALISHA AMBAYO SI LAZIMA YAWE NA YENYEWE YANATOKA KTK ULIMWENGU WA ROHO, hii itakua ni kulazimishia point ya ukweli hiyo kuiingiza kila sehemu ambako yaani waaaalaaa haihitajiki au hata ku-connect ili to make sense of out.Mfano ni kituko kusema napoandika sasa-haya maandishi kwa laptop, yalikuwepo/yaliumbwa ktk ulimwengu wa roho- eti yakoga uko! Mmmhh! Mmmmmmh jamani, hii kulazimisha mambo yote yawe ya kiroho ili tuonekane siye wakiroho yanachekesha eee sometimes.

  Press on

 14. Ok Seleli;

  Na mimi nakuuliza;
  Moja: Mbu, Bacteria,Virusi, Nzii, Mende/Komba Mwiko, Chawa,Kunguni, Mbung’o;

  -Jibu:Je shetani anaweza kuwatumia hawa viumbe kutimiza mpango wake katika maisha ya mtu?

  Mbili; Bacteria apohamia/ingia sehemu si yake( mwilini mwa Mtu) kwakua uko mwilini hawamuihitaji wala hawajawaji kua naye ndipo sasa kukaa kwake umo, anasababisha hali isiyotakiwa mwilini yaani Ugonjwa-hapo kuna pepo/shetani au kidudu/kuimbe kimerokea kukaa humo mwilini?

  -Jibu: Je shetani anaweza kuwatumia hawa bacteria kuleta ugonjwa?

  Tatu: Nisipooga nikawa mchafu, mdomo sipigi mswaki, nguo sifui, nikifua za ndani navaa bila kukauka vema, mazingira machafu,mitaro ya maji machafu haifukuliwa ivyo inakwamisha maji machafu na kupelekea watu kuvuta hewa chafu 24/7, kunywa maziwa na maji yasiyochemsha, kisha mambo yote hayo, yaka sababisha magonjwa = kwa maana ya viumbe wadudu wasioonekana na wanaoonekana wakaja/zaliwa/zalishwa, shetani/pepo iko/yuko wapi hapo?

  -Jibu: Ivi mtu mpaka anakuwa mchafu kiasi hicho, injiniani nyuma ya hiyo hali ni Roho mtakatifu au?

  Umeniuliza hivi:Je hili ndio nilikuuliza lipo/ni kweli ya Neno na kazi ya Yesu msalabani?

  Jibu; Biblia haijasema kuwa kila kitu huondoka tit for tat pale mtu anapompkea Yesu. Mfano ni Petro, alikuwa mtume lakini bado alikuwa na roho ya unafiki hadi Paul akamkemea.

  Tena umeniuliza:
  (a) Kufanyiwa kupi ni Udanganyifu na kupi na sahihi, (b) kule kufanyiwa kwa sahihi, anafayiwa mtu wa aina gani?

  Majibu: (a) (i)Ni kule kulazimisha kuwa kila aliyempokea Yesu anatakiwa kufanyiwa hayo maombi
  -a (ii) Kufanyiwa sahihi ni kule kufanyiwa pale kweli mtu anapokuwa na tatizo linalohitaji hiyo huduma.
  (b) Jibu la hapa nilishalisema kwenye swala la yupi anatakiwakufanyiwa deliverance kati ya aliyeokoka na asiyeokoka.

  Halafu ukauliza tena:ivyo vinavyowasumbua ingawa tayari wameokoka(Kuhamishwa kisha kuingizwa) ni associated na mambo ya kimwili tu ya kawaida kama kukosa tu maarifa, taarifa, Neno au nguvu za giza, ulozi,pepo, mizimu ya kabisa na maagano?

  Jibu; Vyote ulivyovitaja hapa vinaweza kuwa sababu. (Shetani anaweza kuitumia fursa ya mtu kukosa maarifa, tarifa, neno, kuweka cha kwake. Hufanya hivyo

  Ukauliza tena:(a) Aliyeooka na amejwazwa Roho ya/wa Mungu, akiwa na unafiki, uongo, ni roho au tabia tu mbaya ya kawaida?( b) Kama ni roho inamsumbua inakaa/tawala wapi/tawalaje Mtu huyo-tokea ndani mwake au nje?( c) kama ni tokea ndani, Roho Mtakatifu na iro riroho/maroho yanakaa pamoja?

  Majibu; (a) Tofauti ya roho na tabia ni sawa na tofauti ya nguvu ya Roho mtakatifu na Roho mtakatifu mwenyewe. Hakuwezi kukawa na tabia fulani bila kuwepo roho ya hiyo tabia nyumba ya pazia.
  (b) sielewi nje au ndani unakokusema ni kupi.
  (c) jibu linategemea ‘b’ ambayo inasubii malezo yako.

  Na hili nalo ukaniuliza: Hata madhaifu tu ya Kimwili ni devo? Una uhakika? Jibu kwa kuzingatia maswali yangu ya kwanza juu kule.

  Jibu: Ndiyo ni shetani, nina uhakika.

  Pia na hili: ni yapi magonjwa hayo, ya nguvu za giza au ya kawaida kama utajibu kule juu maswali ya mwanzo?

  Jibu: Magonjwa yote hutokea kwenye giza, kwenye nuru hakuna magonjwa.

  Na la mwisho hili hapa:Kwa kuzingatia maswali yale juu pale eg navaa nguO mbichi kisha fungus au ugonjwa wa ngozi unanivaa, ni devo ugonjwa huo au ni icho kiumbe-chichidudu( not kidudu-coz ni kidogo/kadogoo mno-my own word style anyway) tu, kazi/utendaji kazi wake kama kilivyoumbwa and not necessarily fully and purely devo?

  Jibu: Kama ulivaa nguo mbichi makusudi basi aliyekudanganya ni shetani, na kama hukua unajua shetani hufanya kazi vema zaidi pale penye giza (ujinga).
  Kitu hakiwezi kuonekana kwenye mwili (kibaiolojia) kabla hakijawa halisi kwanza katika ulimwengu wa roho, maana ulimwengu w a roho ni halisi kuliko wa mwili.

  NB: Nimeandika sana kwa sababu umeuliza vitu vingi sana.

  Asante.

 15. Sungura,

  Umeniuliza swali kama Kuna ugonjwa ambao asili yake si shetani? Na kama upo asili yake huwa ni nani? MAJIBU yake ni NI MASWALI YAFUATAYO-Ukiyajibu haya basi ndio majibu.
  Moja: Mbu, Bacteria,Virusi, Nzii, Mende/Komba Mwiko, Chawa,Kunguni, Mbungo wote hawa wanaleta/beba/sababisha magonjwa je ni pepo/shetani au viumbe tu hawa? Nani Muumba wake? Pepo/devo au?

  Mbili: Bacteria apohamia/ingia sehemu si yake( mwilini mwa Mtu) kwakua uko mwilini hawamuihitaji wala hawajawaji kua naye ndipo sasa kukaa kwake umo, anasababisha hali isiyotakiwa mwilini yaani Ugonjwa-hapo kuna pepo/shetani au kidudu/kuimbe kimerokea kukaa humo mwilini?

  Tatu: Nisipooga nikawa mchafu, mdomo sipigi mswaki, nguo sifui, nikifua za ndani navaa bila kukauka vema, mazingira machafu,mitaro ya maji machafu haifukuliwa ivyo inakwamisha maji machafu na kupelekea watu kuvuta hewa chafu 24/7, kunywa maziwa na maji yasiyochemsha, kisha mambo yote hayo, yaka sababisha magonjwa = kwa maana ya viumbe wadudu wasioonekana na wanaoonekana wakaja/zaliwa/zalishwa, shetani/pepo iko/yuko wapi hapo?

  Pia umeniuliza, ‘’Halafu unaposema magonjwa ya kimwili na ya kishetani una maanisha nini? upi ni ugonjwa wa kishetani au kiroho?
  JIBU: Nitajibu haya ukisha jibu maswali 3 pale juu, plz vumilia kidogoo, jibu kwanza yale, relax, polepole hamna shida.

  Pia umeniuliza kua nimekuuliza mtu anaweza kuokoka na kubaki chini ya nguvu ya uharibifu, ninamaanisha nini? au nguvu ya uharibifu unayoisema hapa ni nini? JIBU: Yaani anaokoka kisha anabaki na udhihirisho wa madhara negative ya utawala na utendaji wa shetani yaani kumilikiwa nae- kua AMEHAMISHWA-toka gizani KISHA KUINGIZWA-nuruni- Kol. 1:13 lakini BADO awe chini ya masaibu ya gizani- Je hili ndio nilikuuliza lipo/ni kweli ya Neno na kazi ya Yesu msalabani?

  Nikuulize ili..’’Si kila kufanyiwa maombi ya ukombozi ni udanganyifu: SWALI: (a) Kufanyiwa kupi ni Udanganyifu na kupi na sahihi, (b) kule kufanyiwa kwa sahihi, anafayiwa mtu wa aina gani?

  Nuliza na hili.. ‘’wako waliokoka ambao kuna vitu bado vinawasumbua wanatakiwa kufanyiwa deliverance (na deliverance si maombezi tu, inaweza kuwa ni ushauri’’ SWALI: ivyo vinavyowasumbua ingawa tayari wameokoka(Kuhamishwa kisha kuingizwa) ni associated na mambo ya kimwili tu ya kawaida kama kukosa tu maarifa, taarifa, Neno au nguvu za giza, ulozi,pepo, mizimu ya kabisa na maagano?

  Nauliza na hili..’’Mtu anaweza kuwa amempokea Yesu lakini akaendelea kusumbuliwa na roho ya unafiki au uongo. SWALI:(a) Aliyeooka na amejwazwa Roho ya/wa Mungu, akiwa na unafiki, uongo, ni roho au tabia tu mbaya ya kawaida?( b) Kama ni roho inamsumbua inakaa/tawala wapi/tawalaje Mtu huyo-tokea ndani mwake au nje?( c) kama ni tokea ndani, Roho Mtakatifu na iro riroho/maroho yanakaa pamoja?

  Nauliza hili pia..’’kwa kupigwa kwake tuliponywa, haimaanishi tulipona matatizo ya nguvu za giza tu bali ni pamoja na udhaifu wa kimwili ambao mimi najua asili yake ni huyohuyo mmoja shetani’’ SWALI: Hata madhaifu tu ya Kimwili ni devo? Una uhakika? Jibu kwa kuzingatia maswali yangu ya kwanza juu kule

  Nauliza na hapa, ‘’Lakini pamoja na kuwa tuliponywa kama inavyosema, leo magonjwa hayaogopi kutufuata ati kwa sababu tumeokoka na tumeponywa, yanakuja tu’’ SWALI: ni yapi magonjwa hayo, ya nguvu za giza au ya kawaida kama utajibu kule juu maswali ya mwanzo?

  Nipe uhakika wa hili..’’Mwasisi wa matatizo yote / magonjwa yote ni shetani, Yawe ya kiroho au kibaiolojia’’ SWALI:Kwa kuzingatia maswali yale juu pale eg navaa nguO mbichi kisha fungus au ugonjwa wa ngozi unanivaa, ni devo ugonjwa huo au ni icho kiumbe-chichidudu( not kidudu-coz ni kidogo/kadogoo mno-my own word style anyway) tu, kazi/utendaji kazi wake kama kilivyoumbwa and not necessarily fully and purely devo?

  Press on

 16. Seleli;

  Kuna ugonjwa ambao asili yake si shetani? Na kama upo asili yake huwa ni nani?
  Au je malaria engineer wake ni mbu au nani?

  Halafu unaposema magonjwa ya kimwili na ya kishetani una maanisha nini Seleli?
  Kwamba malaria ni ugonjwa wa kimwili, sawa, na upi ni ugonjwa wa kishetani au kiroho?

  Pia unapouuliza kama mtu anaweza kuokka na kubaki chini ya nguvu ya uharibifu, unamaanishani? au nguvu ya uharibifu unayoisema hapa ni nini?

  Niliposema habari ya nguvu aliyotumia Yesu kuwaondoa wale pepo region….
  nilimaanisha kuwa nguvu inayotumika kuondoa tatizo moja inaweza tofautiana na ngu itakayotumika kuondoa tatizo jingine. Hao niliowasema mwenye pepo region na mwenye pepo la kifafa wote walikutana na Yesu mwenyewe akawatoa hao pepo.

  Si kila kufanyiwa maombi ya ukombozi ni udanganyifu…!

  Nilichokimaanisha ni kwamba leo hii watu wanaofanya huduma za ukombozi (deliverance) wamekuwa wakisakamwa kuwa ni waongo. Ndo nikasema si kweli kwamba kila anayefanya hiyo huduma ni mdanganyifu.

  Nani anayefanyiwa maombi; wako waliokoka ambao kuna vitu bado vinawasumbua wanatakiwa kufanyiwa deliverance (na deliverance si maombezi tu, inaweza kuwa ni ushauri pia)

  Asiyeokoka deliverance inaweza kumhusu pale anapokuwa amemwamini Yesu kristo, hiyo inaweza kuwa ni mchakato wa yeye kwenda kumpokea Yesu.

  Aliyeamini anakombolewa kutoka kwenye nini? (umeuliza hivyo)

  Nafikiri nilisema kuwa wokovu ni mchakato,kwamba si kila kitu hutokea mara tu mtu anapompokea Kristo, kuna vitu hukamilika kulingana na mtu anavyozidi kujaza akili yake maarifa ya kwenli ya Mungu. Mtu anaweza kuwa amempokea Yesu lakini akaendelea kusumbuliwa na roho ya unafiki au uongo. Hili ni tatizo ambalo huyu mtu anatakiwa kukombolewa.

  Inaposema kwa kupigwa kwake tuliponywa, haimaanishi tulipona matatizo ya nguvu za giza tu bali ni pamoja na udhaifu wote ambao Seleli unausema ni wa kimwili, ambao mimi najua asili yake ni huyohuyo mmoja shetani. Lakini pamoja na kuwa tuliponywa kama inavyosema, leo magonjwa hayaogopi kutufuata ati kwa sababu tumeokoka na tumeponywa, yanakuja tu.

  Nini basi maana ya andiko kama hili: ni kwamba tumepewa mamlaka juu ya hayo magonjwa, kwa anayejifunza vizuri kabisa jinsi ya kuitumia hayo mamlaka hata ugonjwa unaweza usimsogelee kabisa. Lakini hata kwa asiyejua, ugonjwa ukimsogelea ana mamlaka na haki ya kuuondoa na ukatii.

  Kuhamishwa kutoka ufalme wa giza simply ni kutolewa kwenye kuishi kwa kufuata mfumo wa shetani(gizani) na kupelekwa kwenye kuishi kwa kufuata mfumo wa ki- Mungu (nuruni). Sasa magonjwa ( pamoja na mafua) na matatizo mengine hayaogopi kukufuata mpaka kwenye nuru uliko. Yatashindwa tu kukufikia ikiwa utakuwa umejua kuuishi mfumo wa nuru kiusahihi. Na kujua kuuishi kiusahihi ni mchakato, ndio maana kila leo tunajifunza neno la Mungu.

  Na kwa maana hiyo ndio maana nikasema si kila aliyeokoka anatakiwa kufanyiwa deliverance . Swali uliloniuliza ukitaka kujua yale yanayobaki kwa aliyeokoka ni yapi , nafikiri maelezo niliyotoa hapo juu yanatosha kujibu hilo pia.

  Mwasisi wa matatizo yote / magonjwa yote ni shetani.
  Yawe ya kiroho au kibaiolojia.

  Asante!

 17. Sungura,

  Mtu kua na matatizo YA KIMWILI HATA BAADA YA KUOKOKA ambayo yanatokana na familia/ukoo wake mfano magonjwa yale yasiyo ya nguvu za giza au ulozi, mashetani na majini/pepo, Ni kweli linawezekana na yametokea LAKINI mtu baada ya kuokoka kisha abaki na matatizo/magonjwa tokana na ulozi/mizimu/mashetani/majini/pepo na nguvu za giza ktk familia na ukoo, hili haliwezekani na sijawahi ona na kwanza KiBiblia kwa maana ya Kuokoka ile ya Kolosai.1:13 ya ulimwengu wa roho yaani Kuhamishwa toka ufalme wa giza na kuingizwa Ufalme wa Nuru, haiwezi tokea. Kukataa au kusita-sitia au kupata ukakasi towards KWELI iyo, ni kuifanya kazi ya UKOMBOZI NZIMA ile aliposema IMEKWISHA-kua zero na pia itayavuruga maandiko mengine mengi kuhusu kazi ya Yesu Mungu atendae kazi kamili. Mhubiri yoyote atayekuhubiri tofauti na kweli iyo ya yanayofanyika ktk Ulimwengu wa roho na jinsi Mtu anavyotengwa toka giza kuja nuruni, huyo ana taka pesa, ni tapeli na tutamtandika fimbo! Ni kitendo cha kudharau Kazi ya msalaba-Kumbuka nasisitizia ule upande wa Kiroho ambako Mungu 100% anahusika but uku kwa kimwili ndiko kuna kuja swala la sehemu ya mtu pia eg aamini ktk uponyaji na Neno la Yesu then anapona na kimwili toka magonjwa haya ya kimwili yasiyo na uhusiano na umilikaji/kukaliwa/agano na devo au mizimu.

  Ni kweli maana moja wapo ya laana ni nguvu unayokufanya ushindwe au usifanikiwe. Iwe kiafya, ki- maadili, ki-mafanikio ya uchumi, ki-utakatifu LAKINI pia ni nguvu SPESHELI ya uharibifu.Mtu anaweza shindwa/kutofanikiwa si kwa wakati wote ni kwa sabbu ana laana! hii itakua ni sentence too general! Kunaweza kua na factors nyingine kabisaa e.g. ujinga tu kwa kua Mtu hana Maarifa au amekosa Taarifa, basi, ivyo tu-info is power(nguvu!) Ila Laana ktk mantiki ya KiBiblia-Kumbu.28:15-68 ya kua ni nguvu spesheli ya uharibifu/ya kuadhibu hapo hata kama Mtu ana info, Elimu, Maarifa yote, pesa zote, familia, we mtoto wa Obama…ataharibiwa tu! why? kwa kua kuna nguvu specialy commsioned/allowed/released kum-deal huyo Mtu na mambo ayke yote-hana jinsi mpaka MWINGINE MWENYE NGUVU aje na akija-amekuja na shurti iyo nguu nyingine/ufalme huo na umilikaji/matakwa/uharibu wake ukatwe-ndio maana KUU ya kazi ya Msalaba na Yesu kwenda mpaka pande za chini-ndio maana nasema Mtu anayehubiri tofauti na kweli kama hii-Kazi ya Msalabu ktk part ya Mungu-Ulimwengu wa roho kwa kuchukulia yote tuliyonayo au kumbana nayo ktk ulimwengu wa mwili ni zao la uko nyuma kulikua hakuja kaa sawa, tutamchapa tena haraka na Paul alisema kwa ukali kabisa kua mhubiri wa hivyo na aangukiwe kama dhoruba na nguvu iyo iyo ya uharibifu-ie alaaniwe hata kama Preacher huyo anatoka mbinguni straight au hata Malaika Jibriri akakosea step-adhabu kwakwe ipo tu guranteed

  Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita-hii ni kweli kabisa lakini si lazima magonjwa ya kawaida haya e.g mafua, Malaria, asthma nk(si yale ya umilikaji wa kidevo,mizimu ya kikabila na maagano au ulozi), yatoke hapo hapo. Nimeona wengine hupona hapo hapo magonjwa YOTE-Spiritual and Bilogical diseases na wengine baadae kwa yale yaki mwili coz yale ya Kidevo hua yanang’oka on the SPOT wakati wa MWOKOZI ANASHUGHULIKA NA KUHAMISHA kisha KUINGIZA! Kwa iyo tafsiri sahihi ya Kua Kiumbe kipya ni hii ya Kolosai:1:13.

  Nauliza ivi kama Wokovu ni neno ‘sozo’ ni kuponywa magonjwa, kusamehewa dhambi, kukombolewa laana, kupata amani ya ki- Mungu nk na kisha unasema haya mambo siyo kweli kwamba kwa kila mtu hutokea kwa saa ile,pale mtu anapompokea Yesu- UNA MAANA MTU ANAWEZA MPOKEA YESU KISHA AKABAKI CHINI YA NGUVU YA UHARIBIFU? NA SWALA LA KUHAMISHA KISHA KUINGIZA LINAKUA LIMEFANYIKA AU LA?

  Hapa sijakupata vema Sungura..’’Nguvu aliyotumia Yesu kuwaondoa wale pepo ‘region’ mpaka wakawaingia nguruwe si sawa na ile kwa yule mtoto mwenye pepo kifafa’’, unamanisha nini ktk KWELI ya Neno hii ya ‘’Kuhamisha kisha Kuingiza’ au lina husina na yale magonjwa/matatiozo ya kawaida(si lazima mizimu na maagano ya kabila na koo?)

  ‘’ Unaweza fafanua hili pia?..’’Si kila kufanyiwa maombi ya ukombozi ni udanganyifu?’’ nani anafanyiwa maombi ya Ukombozi aliyeokoka tayari au mpagani anayetaka kuingia BAADA YA Kumwamini/kuliamini Neno? Na Maombi ya Ukomboz kutoka kitu gani labda-yale ya kawaida tu medically au yaki devo/ulozi/laana?

  Pia fafanua hapa… ‘maombi ya kukombolewa yanafanywa kwa mtu asiyeamini na pia aliyeamini’. Je Aliyeamini tayari, anakombolewa toka kwenye nini? je alipoamini, alihamishwa kisha kuingizwa au la?

  Nipe tena udadavuaji ktk hili’’Si kila aliyeokoka anatakiwa kufanyiwa ‘deliverance’, lakini pia si kila anayeokoka kila kitu kinaondoka mara’’ Kwa hayo yanayobaki yasioondoka mara kwa anayeamini-ni yale ya ulozi/laana/nguvu za giza/maagano/kukaliwa na Ufalme wa devo au yapi hayo?

  Press on

 18. Seleli nashukuru kwa majibu yako!

  Pengine niseme kwamba watu wengi wamelichukua hili swala kwa ujumla sana na kujaribu kumpinga Gwajima kwa kile alichosema kuwa mtu anaweza akawa na matatizo ambayo yanatokana na familia/ukoo wake.

  Laana kwa lugha nyepesi, ni nguvu unayokufanya ushindwe au usifanikiwe. Iwe kiafya, ki- maadili, ki-mafanikio ya uchumi, ki-utakatifu, n.k. Laana si kitu cha kuonekana,bali matokeo yake. Kama ilivyo barka, kwamba ni nguvu inayokuwezesha kushinda au kufanikiwa. Kuwa na afya njema, kuwa na familia nzuru n.k si baraka bali ni matokeo ya baraka

  Ni rahisi kuipinga hii kwa kusema mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita…., kwa maana ya kwamba kwa mfano mtu akiwa na ugonjwa wa kurithi siku tu akimpokea kristo huo ugonjwa nao unaondoka. Kitu ambacho si kwamba kiko hivyo kwa kila mtu.

  Maana ya wokovu kutoka kwenye neno ‘sozo’ ni kuponywa magonjwa, kusamehewa dhambi, kukombolewa laana, kupata amani ya ki- Mungu nk.Sasa haya mambo siyo kweli kwamba kwa kila mtu hutokea kwa saa ile,pale mtu anapompokea Yesu.

  Kumpokea Yesu ni mwanzo wa safari ya kuukulia wokovu, na hii safari haiivi siku moja wala mwezi mmoja. Inategemea na bidii ya mtu kama alivyosema Seleli. Pia inategemeana na nini mtu anapambana nacho.
  Kitendo cha mtu kumpokea Yesu siyo kweli kwamba ki-automatic magonjwa yote huondoka, umasikini wote huondoka,matokeo yote ya laana huondoka, hapana, hicho huwa ni kitendo cha kupata haki, mamlaka, nguvu na maarifa ya kuviondoa hivyo vitu kwa jina la Yesu.

  Ziko tabia watu wanapambana navyo kwa miezi na miaka ndo zinaondoka, na wengine zinaondoka kwa Muda mfupi tu.

  Kuokoka ninaweza kusema ni kitu kizuri cha kukuonesha adui unayepambana naye amekaaje, kwa nini yupo, ametokea wapi, n.k. Lakini kwa upande mwingine ni kitu kinachokupa maarifa, mamlaka na haki ya kumpiga huyo adui na kuweza kumwangamiza.
  Ndio maana Paul alisema anapigana…., na mwishoni anasema amevipiga vita vilivyo vizuri…

  Nguvu aliyotumia Yesu kuwaondoa wale pepo ‘region’ mpaka wakawaingia nguruwe si sawa na ile kwa yule mtoto mwenye pepo kifafa.

  Kwa kupigwa kwake Yesu sisi tuliponywa haina maana kuwa magonjwa hayatakuja. Yatakuja na yanakuja, lakini tuko na warantii ya kuyashugulikia na kuyaweza ikiwezekana hata kabla hayajajidhihirisha matokeo yake.

  Kuna watu wanampokea Yesu lakini wanaendelea kuwa na hasira, wanaendelea kutukana, n.k, mpaka baada ya muda fulani wa kumjifunza Kristo ndo hayo mambo yanakwisha.

  Kuna vitu baadhi Mabinza kamkosoa Gwajima. Kwa mfano Suala la Ibrahimu kutozaa. Ni kweli aliyekuwa tasa ni Sara, Ila hata Sara hakuwa tasa,hata Rebeka hakuwa tasa, hata Rahel hakuwa tasa, maana wote baadae walipata watoto.
  Cha msingi alichokuwa anaonesha Gwajima ni kwamba waliokuwa wanafuatiliwa na hilo tatizo si hao wanawake bali ni hawa wanaume ambao ni baba, mtoto na mjukuu. Hivyo Gwajima anatuonesha tatizo la kutopata watoto kwa hawa jamaa (ukoo),ambalo lilipitia tu kwa wake zao, lakini lilikuwa tatizo lao la kiukoo.

  Ni kweli pia ile laana alikuwa anaambiwa nyoka. Lakini Gwajima alikuwa hasa haongei habari za nani aliambiwa, bali alikuwa anajaribu kuonesha kuwa jambo linaanzia kwa baba linaweza kufika mpaka kwa mtoto na hata vitukuu.

  Kwa habari ya wayahudi kusema damu ya Yesu iwe juu yao na watoto wao, Gwajima haongelei jinsi gani wayahudi walijibariki au kujilaani kwa hiyo damu, bali anachoongea ni ile ”concept” kwamba suala linaweza kuanzia kwa baba likafika mpaka kwa mtoto ( swala hilo laweza kuwa baya au zuri, lakini hapa tunaongelea masuala yale mabaya–laana,balaa). Ndio maana wanasema laana ya damu ya Yesu iwe si kwao tu bali ipitilize hadi kwa watoto wao.

  Si kila kufanyiwa maombi ya ukombozi ni udanganyifu, bali kukombolewa kutoka laana ni sehemu ya wokovu. Na jambo hilo halifanyiwi mtu asiyeamini tu,bali aliyeamini pia.

  Si kila aliyeokoka anatakiwa kufanyiwa ‘deliverance’, lakini pia si kila anayeokoka kila kitu kinaondoka mara.

  Kimaudhui sioni kama kuna kosa katika alichokisema Gwajima.

 19. Sungura,

  Uliuliza Maswali 4, majibu yake ni kama ifuatavyo:

  SWALI-1. Kinachofanya mtu aliyeokoka asiguswe na pepo au roho chafu ni nini?

  JIBU: Ikiwa kwa neno ‘kutoguswa’ na pepo au roho chafu ulikusudia haya mambo mawili Moja: Kutopagawa/ kutotawaliwa/ kutokaliwa/kutomilikiwa na pepo na roho wa wachafu na Pili: Kutokuonewa/ kutonyanyaswa/kutosumbuliwa/ Kutohaharibiwa /kutoteswa /Kutoshambuliwa na pepo/roho wa chafu, basi yafuatayo ni majibu ya swali lako: (Zingatia pia kinyume cha maana ya ‘Kutoguswa’ na pepo/roho chafu yaani ‘Kuguswa’ nao, inatumika pia ktk majibu haya chini-

  Kwa swala la kwanza- hataguswa na pepo au roho chafu kwakua Mungu Baba,Bwana Yesu na Roho Mtakatifu wanakaa ndani yake.Kwakua kuokoka ni tukio la mara moja-Mungu ANAMVUTA Mtu kwa Yesu Yohana.6:44…. halafu kisha Mwokozi ANAMWOKOA mara moja (Bwana hua hamuokoi-okoi Mtu kila mara na kila wakati au haokoi nusu-nusu/robo-robo), ni kamilifu kwa upande wa Mungu la KUMUHAMISHA mtu toka ufalme wa shetani/giza( uchawi,wanga, ulozi, laana,mikosi, balaa, roho za kiukoo na familia, maagano ya kimila na desturi, nguvu na kifungo cha dhambi,kumilikiwa na pepo, nyamkera, majini,mizimu nk) Kisha Mtu huyo ANAINGIZWA ktk ufalme wa Mwana wa pendo lake yaani hakuna giza/shetani bali ni nuru (raha,furahu,uhuru,bubujiko la roho, kujazwa Roho ya/wa Mungu, vipawa, karama,baraka, mpenyo, mawasiliano na Mungu yenye uhai, kuandikishwa jina mbinguni, kua mrithi na mwana wa Mungu, kuhesabiwa haki bure, kukaliwa/kutawaliwa na MUNGU nk)- Wakolosai.1:13. Mtu wa aina iyo au akishafanyiwa hayo, anakua milki ya Mungu Baba na muhimu sana ni hii….MTU HUYO AKIDUMU ktk NURU iyo, HAIWEZEKANI KABISA kuguswa na pepo kwa maana ya kwanza na hata ikitokea kuguswa na pepo/roho chafu kwa maana ya pili, bado ushindi ni wake, ana nguvu za kumthihirishia shetani kwamba yeye( mtu huyo) hawezekaniki KWA KUA AMEDUMU NDANI YA NURU-Ayubu-sura zote 1 na 2, Mdo.4:1-33, Mdo.12:1-19, Mdo.16:22-26.

  Kwa swala la pili-Aliyeokoka anaweza kuguswa na pepo na roho wachafu kwa maana ZOTE mbili pale juu na yakamtokea yale niliyo orodhesha ikiwa tu ATAMUACHA/MKANA/KUONDOA UMILIKAJI WA BWANA JUU YAKE AU AKIWA NA BWANA BADO LAKINI AKATOA NAFASI KWA SHETANI-kwa hili ndio, yatamtokea yale ya maana ya pili ya kuguswa na shetani kwa kua bado ana BWANA ndani yake.Yesu aligusia uwezekano huo ktk Mathayo.12:43-46-‘’pepo amtokapo Mtu(bila shaka Mtu huyu atakua ameombewa na kufunguliwa hata kuamua kua mfuasi wa Yeye aliyemfungua-(Yesu)….akirudi na kukuta kuko kutupu, huchukua wengine wabaya zaidi na hali mwisho ya mtu inakua mbaya sana’’ pia, kwa kujua ilo, ndio maana tunashauriwa-Waefeso.4:27-‘Kutompa shetani nafsi’ na pia Yakobo.4:7b-‘Kumpinga shetani naye atakimbia’…

  SWALI 2. Ivi kiwango cha ujazo wa Roho Mt. kati ya mtu na mtu kinaweza kuwa kinatofautiana?

  JIBU: Roho Mtakatifu ni Roho ya/wa Mungu na kwakua sifa ya kua naye/kumpata ni kwanza/kukubali kua mfuasi/mwamini Yesu-Mdo.1:8,Mdo.2:1-4,Mdo.9:17,Mdo.10:1-48,Mdo.19:1-6 na kwa kua Mungu hana Roho nusu-nusu, ivyo awajazavyo Watu, huwajaza Roho nzima-nzima.Sasa ingawa wote tuna Roho wa Mungu mzima-mzima lakini kumbuka ktk mambo yote ya Kiroho/KiMungu/KiImani, iko sehemu ya Mungu ya kufanya na hakika iko sehemu ya binadamu na kwamba ni ukweli pia, binadamu asipofanya sehemu yake, Mungu hatamfanyia kamwe-mfano Mungu ametoa wokovu(Yesu) kwa watu wote-kashamaliza kazi kwa sehemu yake lakini wanaopaswa kuamini na kukubaliana na mpango kisha waoupokee ni Watu-iyo Mungu hafanyi, ni Mtu!Munguatamvuta/shawishi/hubiri/mnunurisha nuru lakini maamuzi ya kukubali hayo, ni Mtu ayafanye-ni sehemu yake mia asilimia.

  Kwa mantiki iyo, kiwango gani tunajibiidiisha/tunajitoa/tunajinyenyekeza/tunautafuta uso wake sisi Watu, Mungu hausiki kabisa na hilo wala kulazimisha, ndicho icho kitaamua MADHIHIRISHO YA VILE TULIVYONAVYO/WEKEWA/JAZWA NA MUNGU AMBAVYO TUNAVYO WOTE KWA KIWANGO KILE KILE KWA MAANA KUTOKA KWA MUNGU, WOKOVU, ROHO WAKE HUJA KWETU KAMILI/KIZIMA-ZIMA.Kwa iyo, yeye aonekanaye kua ‘amejaa sana’, ‘ana upako sana’, ‘amefurika sana’, haimaanishi kua ana Roho wa Mungu spesheli au Roho wa Mungu kwake alikujaga mzima-mzima na wengine alikujaga nusu na robo!!!!!!!! Kinachotokea ni kama vile wote ni Wanadamu wenye viungo sawa na wote tunaishi kijijini kweye mashamba na mvua ya kutosha lakini wengine wanacheza drafti na karata mwanzo mwisho na wengine wanakwenda mashambani kuchakarika na kiangazi wanalima bustani mabondeni.Madhihirisho tofauti yatakayoonekana ktk ya ustawi mzuri wa maisha kati ya makundi hayo mawili si kwa sabubu kundi moja lina miguu 6, macho 3, bongo 4,mikono 30 au lilipendelewa sana na serikali ya kijiji au ya mbinguni bali ni wachakarikaji-Yakobo.5:17-18.Mithali.8:17 Yeremiah.29:13 na wale wengine ni wavivu tu basi.

  3. Ivi nguvu inayotenda kazi ndani ya mwamini inaweza kutofautiana kati ya mwamini na mwamini?

  Jibu: Ndiyo kabisa, zingatia maelezo ya majibu ya swali no. 2 juu hapo. Nyongeza ni kua wote tunaweza kua tunafanya kazi BOT na tuna cheo na mshahara na tuko na haki sawa kama kusomeshwa,kusafiri, semina nk na tunapata wote sawa lakini ukitukuta baada ya miaka 5, tunatofautina maendeleo, tatizo ni Bank, Cheo, Boss, mshahara au sisi wenyewe staff na namna zetu tufanyazo na nguvu ya kutendea kazi-(Mshahara) ambao tunayo wote sawa kabisa?

  4. Je mtu akimaliza tu kumpokea Yesu kila kitu kilichokuwa kinamtesa huondoka au kuna vingine huondoka taratibu?

  Jibu: Swali hili lina changamoto zake ila kwanza tunaenenda na kanuni ya Neno inasemaje kisha tunaweza tumia uzoefu wa kihuduma na kutembea na Bwana kutoa majibu lakini bila kuvurugu kweli ya alichosema Mungu. Kanuni ziko nyingi ktk Neno ila kwa swali ili nachukua ili- 2Wakorinto.5:17-‘Mtu akiwa ndani ya Kristo ya KALE yamepita, sasa ni MAPYA. Kwa upande wa Mungu, afanyagi mambo nusu-nusu-kwa maana ya kutokamilisha kazi. Tafadhari tuelewane hapa Wapendwa- ni Kweli Mungu hutembea na Watu wake ‘hatua kwa hatua’ kama alivyowaambia wana Israeli kua atawamilikisha Nchi ya ahadi hatua kwa hatua lakini kwa upande wa Mungu, kutembea nasi hatua kwa hatua haimaanisha ndio ana kamilisha mambo kwa kua yalikua nusu na robo bali ina maana sana kua ANADHIHIRISHA HAYO ALIYOKWISHA KUYAMALIZA TOKEA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA DUNIA maana aliyajua hata kabla hayajatokea.

  Kati ya sifa nyingi za Ukuu wa Mungu ni pamoja na hii pia-Isaya.46:10 ‘kutamka(kufanya) mwisho tokea mwanzo’’. Ni sawa sawa na mzazi anayemwandikia Urithi mwanae wa cheki ya bil 1, nyumba 6, magari 10, mashamba 30 na migodi ya Geita gold 15-KWAKE BABA MZAZI, KAZI YA KURITHISHA IMEKWISHA NA KUKAMILIKA-ila ili Mtoto akue vema na kukamata huo Urithi, Mungu huyo huyo LAKINI KUTEGEMEANA NA mkao-mkao/mwenendo-mwenendo na MAAMUZI ya Mtoto, HUMSAIDIA Hatua kwa Hatua kurithi alichopewa tangu akiwa Mtoto au hata kabla hajazaliwa kwa kweli maana Baba yake anampenda na anamwazia mema siku zote kumpa tumaini na future-Yeremia.29:11.Hiyo ni sehemu ya Mungu, ni kamili mtu anapookoka. KUMBUKA KUSAIDIWA UKO tayari nako AMEKWISHA KUSEMA/KUUWEKA/TAMKA KTK NENO kwa iyo isije ikadhaniwa kua kutakuja kitu/mtu spesheli chenye/mwenye msaada nje ya Neno. YOTE ALISHAYASEMA KTK NENO-ukweli huu mzito unafutilia mbali maswala haya ya kisasa ya baadhi ya Wapendwa kudhani au kutangazwa kua wako spesheli na wana mambo spesheli toka kwa BABA ili kushughulikia ishu spesheli na namna ya ki-spesheli ambayo si lazima iwepo ktk NENO!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kwa upande wa Mtu, wakati au kwakua ameshasaidiwa MSAADA TOSHA NA KAMILIFU, ni swala la KUUAMINI NA KUUCHUKUA.Kwa iyo sasa kwa uzoefu wa huduma na kutembea na Mungu, ni kweli utakuta wengine wameooka lakini bado wanaumwa,hasira mbaya, mgomvi, mwizi wa mali za Mungu na Serikali,anafoji na kula rusha mwanzo-mwisho kule TRA, ana-trick vyeti vya kwenda Nje ya Nchi, anasema uwongo ktk Usaili nk..Tabia izi ni Mtu mwenyewe HAJAAMUA KUCHUKUA MSAADA AU KUENENDA SAWA NA MSAADA UNAVYOSEMA-NENO! Mungu hausiki hata kidogo-alishagamaliza!!!! Ndio maana ingawa ukweli huo hapo upo lakini vile vile kuna ukweli mwingine kwa wengine mara tu baada ya kuokoka, yote utoweka au huamua kama roketi kuyaacha yaliyo mabaya na kufuata matakwa ya Msaada ili Urithi uwe dhahiri ule uliokwisha kua dhahiri siku nyingi, tunarudia kule kule-sehemu ya Mungu kwisha kisha ifuate sehemu ya binadamu.

  Nimeona ktk uzoefu wa kihuduma, Watu wakishaokoka ile KIKWELII, kila nguvu za giza na wafayakazi wake(pepo, majini, mizimu nk na mateso/kazi za shetani percee eg-ulozi, magonjwa,kutupiwa ukichaa,mizimu kupinda mguu nk) hutoka mara(labda kama ni magonjwa ya hali ya halisi au hewa eg kipindu-pindu, mafua, chafya mfurulizo, kuwashwa kwa sababu tu mtu mchafu wakati sabuni deto/protex zipo za kumwaga na ya minyoo kufurahi kwa tumbo kwa sababu tu mpendwa mzembe anakula bila kunawa akitoka kwa toilet au shamba), kisha mabadiliko ya nje utegemea sana huyo na bidii yake kuyapenda/tafuta/kua na kiu ya mambo ya mbinguni-ndio maana utakuta aliyeooka-Mr.A anakua na bidii sana na ktk mwaka mmoja anamzidi kwa mbali Mr.B waliookoka siku na saa moja, wakiongozwa sala ya toba na Mwinjilisti mmoja tena kujazwa RM siku moja!!!!!!!Tena aibu yake, huyu aliyookoka juzi-juzi tu kwa bidii ya ajabu na Mungu, Urithi wa mambo ya Mungu ktk kiroho na kimwili chake toka kwa BABA yetu wote yanaanza kua wazi zaidi kuzidi wale waliookoka miaka 10 lakini wapo-wapo tu, wamezoena na BABA wa mbinguni.

  Kama kuna jambo hujaelewa vema Mr. Sungura na wengine au una swali na pia una jambo hukubaliani nalo ktk yote niliyosema/jibu, karibu kuuliza na kama yapo uliyoelewa vema sana pia karibu kwa mrejesho.

  Press on.

 20. Nimekapenda haka, katika hiyo kolosai 1:13 “….13Naye alituokoa katika nguvu za giza akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake…,”

  “Ufahamu ni chembe ya uhai”

 21. Wapendwa nina maswali:
  1. kinachofanya mtu aliyeokoka asiguswe na pepo au roho chafu ni nini?
  2. Ivi kiwango cha ujazo wa Roho mt. kati ya mtu na mtu kinaweza kuwa kinatofautiana?
  3. Ivi nguvu inayotenda kazi ndani ya mwamini inaweza kutofautiana kati ya mwamini na mwamini?
  4. Je mtu akimaliza tu kumpokea Yesu kila kitu kilichokuwa kinamtesa huondoka au kuna vingine huondoka taratibu?

  Nawashukuru sana!

 22. Wandugu,

  Mh! aya mambo bwana ya kua Tumeookoka lakini kuna ‘madude’ yalibaki-baki, yanatufuata-fuata, yako beneti-beneti nasi, kwa Wake/Waume zetu, Watoto wetu wenyewe wa kuzaaa, family na wakati saa nyingine familia yote ina Yesu, mnanayatowaga wapi jamani? Yeyeto, wa kimo na kina chochote, akikuambia wewe ULIYEOKOKA NA UNA ROHO MTAKATIFU (Roho ya Mungu wa mbinguni kabisaaaa ina/ana kaa ndani yako), ati una madude ndani yako na mengine yanakufutilia, mpe maandiko mengi bila kusahau hii ‘’fire brigade’’

  Wakolosai.1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake” Ukichunguza kwa makini maandiko haya utangundua kwamba mtu anapookolewa kwanza “ROHO YAKE HUZALIWA UPYA” na kisha “HUTOLEWA” kwa 100% kutoka katika ufalme wa shetani (kama vile wana wa Israeli walivyotolewa Misri) na “HUINGIZWA” kwa 100% katika ufalme wa Mungu (kama vile wana wa Israel walivyokuwa chini ya utawala wa Mungu walipokuwa wakiiendea nchi ya ahadi)!

  Kama utasahau maandiko/KWELI NYINGINE, HII KAMWE USISAHAU. Inamaliza kila kitu, kisha enende zako kwa amani nyumbani, full stop, over and out, period!!!!!!!!!!!!!

  Press on.

 23. Dada Jackline .Napenda nikujibu kama ifuatavyo na wengine wanaweza kuchangia na kuongezea wakitaka.
  Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya 2 wakolintho 5:17. neno pia linasema kuwa sisi tuliobatizwa ktk Kristo tumemvaa Kristo Garatia 3:27.Jiulize ndugu yangu uliyempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako , umemvaa Kristo hizo rahana na mikosi zipitie wapi kukukabiri? hazina njia maana uliyemvaa ana jina lipitayo majina yote Wafilipi 2:8-11. ana jina linalopita jina rahana, jina lake linapita jina mikosi , na magonjwa yote yanayojulikana kwa majina na hata yale yasiyokuwa na majina,Rahana zipo kweli lakini si kwetu sisi tulio ndani ya Yesu na kama kaka yetu Mabinza alivyosema kuwa zipo lakini siyo kweli sisi watoto wa Mungu , nahamini alikuwa anaongelea watoto wa Mungu kwa sisi tulio ktk wokovu. Ndiyo maana tunasema WOKOVU , na tunamhita Yesu BWANA NA mwokozi wetu maana alituokoa na rahana na mamikosi na mateso , maana Yesu mwenyewe alitununua kwa thamani 1 wakolintho 6:20. Sisi tuliookoka ni hekalu la Roho mtakatifu sisi si mali yetu wenyewe 1 wakolintho 6:19. Na Mungu anasema kuwa mtu akijaribu au akithubutu kuliharibu hekalu lake mtu yule ataharibiwa kabisa .1 wakolintho 3:16-17. Yesu mwenyewe alisema pale msalabani kwamba IMEKWISHA. yahani magonjwa, rahana, mikosi, na takataka zote alizimaliza pale msalabani, neno pia linasema kuwa Mwana wa Mungu Yesu alithiilishwa hili azivunje kazi za Ibilisi 1 Yohana 3:8. Hayo yote aliyotaja Gwajima yalishavunjwa kabisa, hizo ni kazi za ibilisi lakini ashukuliwe Mungu wetu aliyemtuma mwanae aje azivunje kazi zile rahana , magonjwa, mikosi n.k, kinachotakiwa na kuhamini neno linachosema na kusonga mbele. ifahamu kweli hili ikuweke huru. Yohana 8:31-36. Ukijua ukweli huu na kile alichofanya Yesu msalabani kwa ajiri yako ungepata ujasiri wa kutamka kama Paulo kuwa Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao Wagalatia 5:12. Dada uliyesema kuwa ufanyeje hili kuondokana na aliyotaja mch Gwajima kama umeokoka utafute maanadiko yanayoongelea jinsi Bwana Yesu alivyokukomboa, na wewe ni nani ndani ya Kristo , na pia ujue thamani uliyonayo mbele za Mungu kuwa wewe uliye ndani ya Yesu ni mboni ya jicho la Mungu pia baraka zote za Ibrahimu ni zetu . ndiyo kazi iliyomfanya Yesu afe msalabani akatukomboa ktk rahana ya Torati Wagalatia 3:13-14. Ikiwa Yesu hakufa na kufufuka basi imani yetu ni bure. 1 wakolintho 15:14,17. BWANA ASIFIWE SANA.Ninawapenda wana SG popote mlipo duniani. Mama K.

 24. Mchungaji Gwajima,

  Somo lako ni zuri tena ni zuri sana. Ila tu baba mchungaji nimeona kama kuna mambo machache sijayaelewa labda uniweke sawa, naamini utafanya hivyo kwa kuwa nia yako nikufundisha, kwa sababu katika kanisa letu hili SG tupo huru kuuliza na kuulizwa, kukosoa na kukosolewa na hata kuonywa! Nichukue nafasi hii kwa heshima kukukosoa na kunakoambatana na kukuuliza kwa uchache; Sababu kubwa sijakuelewa. Binafsi naona kama, umechanganya vitu viwili na kuvifanya kuwa kimoja!

  Kusema kweli umeanza Vizuri uliponukuu habari ya Wazazi wetu wa mwanzo, yaani Adamu na Eva maana “hapo ndipo mwanzo”, ingawa pia sina hakika kama ule ‘AUDUI’ uliowekwa na Mungu baina ya uzao wa Mwanamke na wa Nyoka, ilikuwa ni “hukumu” kwa Eva kama (ulivyosema hapo nilikuelewa kuwa Eva alihukumiwa “Alilaaniwa”) – kwa maana kwamba Biblia katika Mw. 3:14, inaonesha kuwa aliyekuwa akipewa maelezo ya uadui ule namna utakavyo piganwa alikuwa Nyoka, na hukumu hiyo ilikuwa laana kwa Nyoka! Hebu ona mstari huo – Mw. 3:14;
  14Hivyo BWANA Mungu akamwambia nyoka, ‘‘kwa kuwa umefanya hili, ‘‘Umelaaniwa kuliko wanyama wote wa kufugwa na wa porini! Utatambaa kwa tumbo lako na kula mavumbi siku zote za maisha yako. 15Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino.’’

  Lakini siri ya ushindi katika vita vitakavyoletwa na uadui ule alipewa Mwanake! Hadi hapo, aliyekuwa akipewa hukumu kwa Neno la “uadui” alikuwa Nyoka na watoto wake, siyo yule mwanamke. Ndiyo maana ile siri ya ushindi katika vita vitakayoletwa na uadui huo, walipewa Watoto wa Mwanake! Tazama Mw.4:4 inasema, “4Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka katika baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. BWANA akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake!

  Lakini watoto wa Nyoka walifichwa wasiijue ili “WAANGAMIE” Ona Mw. 4:4 “4…..5lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni. Mungu hakuishia hapo tu, akamuwekea na mlango wa kutokea huyo Mwanamke, soma hii Uf.12:15 inasema, “15Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. 16Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake.”

  KWA HIYO KAMA ILIKUWA NI HUKUMU KWA MWANAMKE ALIPASWA KUITUMIKIA HADI MWISHO, kama ambavyo tunavyoendelea kumbamiza Nyoka kwa Neno la Msalaba na kwa Damu ya mwanakondoo ili, aendelee kuitekeleza hukumu yake huyo ALIYEKWISHA KUHUKUMIWA yaani Nyoka na watoto wake!

  Lakini kwa habari ya wenye ‘Laana’ na wenye ‘Neema –Baraka za kiuungu’ ili kuiweka sawa habari hiyo naomba nami nianzie hapohapo ulipopagusia wewe. Tukisoma ile Mw. 4:1 inasema, “Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa BWANA nimemzaa mwanaume.” Ukiendelea katika Mw. 5:3 inabainisha hivi, “3Adamu alipokuwa ameishi miaka 130 alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.” KJV inasomeka hivi, “And Adam lived an hundred and thirty years, and begat a son in his own likeness, after his image; and called his name Seth:” Hapo ndiyo chanzo cha hayo mambo uyasemayo, hizi ni koo mbili tofauti, ingawa inaonekana kama kwamba Kaini na Sethi, wote hao ni watoto wa Baba na Mama mmoja!

  Ukimwangalia Kaini mara tu alipozaliwa, Adamu hakushughulika hata kumtafutia jina, jina alipewa na Mama yake, na tena Biblia haisemi kama alifanana na nani! Lakini tunapomtazama Seth, tunaona anazaliwa na kuitwa Jina na Baba yake, na tena Biblia inasema alifanana na Baba yake, na wale wa kiume na wakike waliofuata baada ya Seth, walifanana na Adamu baba yao!

  Kwa hiyo, nakubaliana nawe uliposema kuwa, “Waweza kuumkuta mtu mwongo, mwizi, mzinzi, mchoyo, mbishi kumbe ni kwasababu ya tabia za kurithi ambazo zinatokana na laana za familia. Kuna uwezekano mtu akajikuta hana ndoa ya kudumu, kumbe ni kutokana na laana iliyo katika ukoo.” Maana “ALIVYO BABA NDIVYO ALIVYO MWANA” Lakini ieleweke kuwa Mungu kamwe hakuwalaani Adamu wala Eva, kwa sababu Adamu ni mwanaye naye Eva ni mwili katika mwili wa Adamu, Mungu hana tabia ya kuwalaani watoto wake! Mwanadamu aliingia katika laana kwa sababu ya Torati, na Yesu alipokuja alikuja kuondoa hiyo laana ya Torati. Ni watoto wa Nyoka tu ndiyo wenye laana hadi leo! Lakini waliokombolewa na Yesu Kristo, kamwe hawawezi kufuatiliwa na laana, kwa sababu Yesu ndiye alifanyika laana ili wao wasiwe na laana. Wokovu unapofanyika mfungwa wa dhambi, hufunguliwa kikamilifu, hafunguliwi nusunusu, eti kaoshwa dhambi lakini bado anafuatiliwa na laana za mababu na mabibi. Ukiona mtu anasema kaokolewa lakini bado anakwenda kutaka maombi ya kuodolewa laana, huyo kwa vyovyote atakuwa hajafika katika kuelewa ama ni mwana wa Kaini, maana hata kaini alifanya Ibaada pamoja na Abeli. Zabibu mbichi akila baba mwana hawezi kupatwa na kiwi ya meno, labda kwa kipindi kile cha sheria!

  Mtu akisema kuwa analaana na anakwenda kuombewa, ili andolewe hiyo laana na aende tu kuombewa kama alivyo chagua, maana ukichagua kuamini uongo unapewa huo. Kwakuwa laana ni Sheria, mtu akichagua kubaki katika sheria, hawezi kuwa katika hii neema ya Kristo – huwezi kuwa huku na huku, hukumu hutokana na kile ulichoamini, maana utatenda imani yako!

  Jambo lingine ninaloona halipo sawa ni pale ulipoeleza hivi,
  “kwasababu hiyo tunaweza kujifunza kitu kutoka katika maisha ya baba wa Imani, Ibrahimu. Mwanzo (11:29-30),ibrahimu alikuwa hazai maana Sara alikuwa tasa, tunaona pia mwanaye Isaka naye akawa na tatizo hilohilo la kukosa mtoto kwa mkewe Rebeka (mwanzo 25:21); na jambo hilo halikuishia hapo kwani na Yakobo alipatwa na tatizo hilohilo”

  Mtumishi, Biblia inasema kuwa Sara ndiye aliyekuwa Tasa, nawe umekili hivyo, sasa mke akiwa tasa mme anakuwa hazai kwa nini? Umenichanganya sana uliposema, “na……jambo hilo halikuishia hapo kwani na Yakobo alipatwa na tatizo hilohilo”

  Ndugu yangu, tunajua kupitia mwanzo kuwa Yakobo ndiye Baba wa wote kumi na wawaili ndiyo hao wana wa Israeli! Pengine unataka kuchanganya kati ya mtu kuchelewa kupata Mtoto na kule mtu kuwa tasa ukaona ni kitu kimoja. Hebu isome hii mw. 30:1-2 inasema, “Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea ndugu yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, ‘‘Nipe watoto, la sivyo nitakufa!’’
  2Yakobo akamkasirikia akamwambia, ‘‘Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia usizae watoto?’’ Hapo wewe unaona Yakobo ndiye hazai? Mbona unamsingizia Baba wa watu ugumba?

  Biblia inasema Yakobo ndiye alikuwa chaguo la Mungu mwenyewe, na ndiye aliyetakiwa kuja kuikamilisha ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu. Mungu alipomchagua mwanamme fulani na kumkutanisha na mwanamke fulani na kuzaliwa Mabinza, sababu kubwa ni kwamba, Mungu alimtaka “MABINZA”, azaliwe kwa kwa kusudi alilolipanga na kuona kuwa kusudi hilo ni la Mabinza kama Mabinza si la Mtu mwingine. Kumbuka kwamba, hakuna mtu yeyote anayeweza kumjua mabinza, hata wale wazazi wake nao hawamjui, kwani HAWAJAWAHI kumuona kabisa! Lakini mwenyekuweza kuzungumza na Mabinza, na hata kumpa majukumu ni Mungu tu pekeyake, kwa sababu huyo ndiye anayemjua na kumuona Mabinza halisi. Kwa hiyo ili ampate Mabinza amtakaye aliye “FITI” kwa jukumu husika, atatafuta Mwanamume na Mwanamke ambalo atawaunganisha ili wawe wazazi wa huyu mabinza ambaye tunadhani kuwa tunamjua kwa sababu ya mwili wake.
  wazazi tofauti ya wale leo waliomzaa Mabinza, angezaliwa si Mabinza na asingefaa kwa kusudio la Mabinza.

  Raheli kama mwanamke yeyote alijua kuwa yeye alibeba tu mayai, hivyo mwenye watoto ni Baba, ndiyo maana akasema apatiwe mtoto la sivyo atakufa! Lakini Yakobo ambaye yeye kama Mwanamme atakiwavyo kuwa kuhani wa Nyumba yake, kwanza alijua kuwa mkewe anamayai, (haikutajwa kuwa alikuwa tasa, kama ilivyotajwa kwa Sara.) hivyo Yakobo alimjulisha mkewe kuwa, “Mimi siwezi kuwa mbadala wa Mungu, ambaye AMEKUZUILIA watoto” lakini kwanini Mungu alimzuilia Raheli watoto? Ni kwa sababu ya “WAKATI” Mungu alijua kuwa kuunganika kwa Yakobo na Raheli kutatokeza, Yusufu wa namna ileile ya kusudio la Mungu, na ulipofika wakati, hakuna maombi wala nini, akazaliwa Yusufu! Ili uzao wa Ibrahimu ukawe utumwani miaka 400, kazi ile kwa kushirikiana na mdogo wake Benjamini waliifanya kazi ile, kama ilivyokusudiwa. Na toka hapo Yakobo na Raheli walimaliza kazi yao kwa Mungu, Yakobo kupitia Raheli hakuzaa tena!.

  Labda nimalizie na kipengele hiki, umesema,
  “Utajifunza pia kwa habari ya Yesu, walipotaka kumuua, wayahudi walitamka wazi kuwa “25 Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.” Mathayo 27:24-26 wayahudi walijua ukweli huu kuwa laana zaweza pita kutoka uzao mboja wa uovu hadi mwingine, kwasababu hiyo inawezekana unaishi katika mateso leo kwasababu ya mambo yaliyopita huko nyuma”

  habari ya wayahudi kujitakia laana ile, wao walikuwa sawa. Kwanza yohani kwa roho ya unabii alikwisha waona na kuwaita kwa jina la baba yao kuwa “enye uzao wa Nyoka”! Yesu naye alilitimiliza hilo alipowaambia, “Jililieni ninyi na watoto wenu” nao wakakubari wakasema “Damu yake iwe juu yetu na kwa watoto wetu”, basi ilikwisha kuwa! Lakini kwa ule mstari uliomaliza na hapa kuwa “kwasababu hiyo inawezekana unaishi katika mateso leo kwasababu ya mambo yaliyopita huko nyuma” hiyo si kweli kwa wana wa Mungu, Mtu akipata neema ya kuokolewa, anaokalewa wokovu kamili, hakuna cha kubakia tena unavuta tela la kitu kinachoitwa laana. Na ukimwona mtu anaamini hilo ujue anashida mbili, moja, atakuwa hajaelewa Neno na hivyo halimo kwake ndiyo maana hayupo huru, na pili, mtu wa aina hiyo anadai kuwa kaokoka lakini yumo katika laana iwe ya Babu au bibi au yake mwenyewe, lazima huyo atakuwa ni mmoja wa wana wa Nyoka.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai”

 25. nashukuru sana kwa ujumbe mzuri,je ukisha okoka unatakiwa kufanya nini ili kuwa mbali na laana?na je ntaokoaje kizazi changu kisiingia kwenye laana?

 26. Mama k
  safi sana kwa imani sisi. Sisi tulio okolewa na Bwana wetu Yesu alitusamehe dhambi hata zile za mababu. Damu ya yesu huwa inatakasa kabisa maovu yetu huwa haibakishi kitu ila usipo ijua kweli utabaki na malaana wakati Yesu alitutakasa kwa damu ya thamani

 27. Ninamshukru sana Bwana Yesu aliyenikomboa ktk laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajiti yetu,maana imeandikwa , amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti , Hili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie maaifa ktk Yesu Kristo tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani, Wagalatia 3:13-14. Pia ktk 1Petro 1:18-19 Imeandikwa pia kuwa Nanyi mfahamu kuwa mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhaabu mpate kutoka ktk mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu, Bali kwa damu ya thamani , kama ya mwana kondoo asiye na hila , asiye na waa, Yaani ya Kristo.

  Tukitembea ktk ukweli huu tutazidi kuwekwa huru, maana laana zipo kweli na mikosi na mabalaa yote , lakini tukiifahamu kweli hii ya kile kilichofanyika pale msalabani, kweli hii itatuweka huru kwa sisi ambao tumo ndani ya Yesu, na kwa kuwa tumo ndani ya Yesu tunaweza pia kuitumia damu ya Yesu tukaitangaza ktk maisha ya ndugu zetu ambao hawajamjua Bwana vilevile tukaona matokeo. Bwana alisema kuwa nanyi mtaifahamu kweli nayo itawaweka huru. Yohana 8:31-32. Ninawapenda.mama .K.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s