Siri ya Kifo na Kaburi!

cross

Wapendwa,

 Shalom!

Katika siku za karibuni, nimeliona jambo moja ambalo huko nyuma sikuwahi kuliwazia sana, na katika namna linavyojitokeza, maelezo yake yamekuwa ni yenye kukanganya sana, KIFO na KABURI! Basi nimeonelea niwaletee maelezo machache ingawa ni marefu kidogo, lakini kwa hayo, hebu sote tujaribu kulitazama jambo hilo kama linavyojifunua katika Maandiko na ujuzi wa kisayansi uliopo, ili tuone kama tunaweza tukafika mahali ambapo tutaongezeka katika IMANI na hivyo tukapata UJASIRI, ndipo hata TUMAINI tunaloitiwa likawa halisi machoni petu!

Kwa namna fulani, isiyoelezeka, wengi wetu tungependa kufahamu au kujua kwa uhakika jibu la swali hili lilidumu karne zote:

 “Hivi ni nini ambacho hututokea hapo tunapofariki dunia au kufa?

Lakini, kabla hatujayaendea hayo mambo ya kufa, hebu tukiangalie kwanza hicho kilichomo katika uzima. Huyu hapa mtume Paulo, hebu na tulipate jambo hilo moja kwa moja kutoka kwake:

2Kor 12:2-4

“Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.”

Sasa, kwa kadiri ya maisha tunayoishi, tunafahamu ya kwamba tunaishi hapa katika jinsi tatu, yaani dimensions tatu. Nazo dimensions hizo ni Nuru au mwanga, Wakati na Mata au matter, yaani hayo ya mwilini yenye kushikika. Nasi kwa zile hisi tano, huzifikia hizo jinsi au dimensions; kwa kuona, kusikia, kugusa, kuonja (kwa ulimi) na kunusa. Hizi ndizo njia tuwezazo kwazo kuzifikia hizo jinsi tatu kupitia hizi hisi zetu tano kimawasiliano, katika hizo dimensions.

Lakini pia tunayo mawasiliano kupitia sayansi, ambayo hiyo ni Dimension ya Nne kama ilivyo. Kwani hata hapa tulipo sasa hivi, popote pale, kuna mambo mengi sana yanayopita hapo sasa hivi! Kuna picha zinapita hapo, sauti nyingi tu, za radio, picha za runinga nk ambavyo mambo yote hayo, zile hisi zetu tano haziwezi kuyakamata, lakini sayansi imetengeneza ving’amuzi vinavyoweza kuyadaka hayo na kuyadhihirisha. Basi, unaona, hapo katika jengo ulilomo sasa hivi, kuna matukio mengi ya watu yanayoendelea hewani, na sauti nyingi tu nk. Vyote hivyo vipo hapo. Tunafahamu hilo. Na huo ndio ukweli wa mambo. Kwa ving’amuzi, hayo hudakwa, nasi twafahamu, kupitia udhihirisho wa ving’amuzi hivyo, ya kwamba kuna hiyo jinsi au Dimension ya Nne, ndivyo inavyojitambulisha kwetu! Katika ulinganishi, unaweza kuliona jambo hili kwa uwazi kabisa ukiliangalia lile tukio pale Elisha alipokuwa amezingirwa na Wafilisti, naye msaidizi wake Gehazi akafa moyo baada ya kuuona wingi wa majeshi yale: 2Fal 6:17 “Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.” Basi unaona, ilimbidi Mungu amuingize huyo mtumishi wa Elisha, katika Dimension yaliyokuwako majeshi yake hayo ili  apate kuyaona!!!

Kisha kuna jinsi au Dimension ya Tano, ambayo ni Kuzimu, huko liliko “shimoni” (the deep”), huko ambako mdhambi, huyo asiyeamini, pindi anapokufa, huenda huko. Sasa, si katika mwili, huu wa duniani (1Kor 15:40), hapana, kwani mwili huu wa duniani hulazwa kaburini ili uoze, au huchomwa moto, kama zilivyo desturi za dini nyingine. Bali ni ile NAFSI ya mtu huyo, hiyo ndiyo tunayoizungumzia. Najua Siyi utaniletea zile hesabu zenu za: Mavumbi + Roho= Nafsi Hai!! Bali unapaswa uendelee kupokea maelezo kutoka kwa Muumbaji kwa kadiri anavyo kufunulia, maana katika kifungu cha 1Kor 15:40 tumepelekwa mbele zaidi katika ufahamu wa mambo hayo kiasi kwamba hiyo hesabu yenu kwa sasa imepitwa na wakati, tazama jambo hili jipya tunalo juzwa, “Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani”!!

Nimewaona wakristo wengi sana waliochanganyikiwa katika jambo hili. Labda ni kutokana na mafundisho waliyoyapitia, na inapofika katika ule wakati wa kulipambanua jambo hili, masikini hawajui kwa uhakika ni nini kinachomtokea mtu aliyekufa zaidi ya mazishi na vumi na umbeya unaoambatana na kifo! Na kupitia mafundisho hayo, wengine wanaamini kuwa kwa namna fulani wanaweza wakawasaidia wafu wao kwa maombi, na wengine hawaukubali ukweli wa kwamba yako makazi ambako wafu huenda, wakifikiri na kujiaminisha katika uongo wa kwamba mambo yote humalizikia hapo makaburini ambapo nafsi za wafu hao hubakia humo kaburini ulimolazwa huo mwili, na mambo ya jinsi hiyo. Lakini ukweli ni kwamba, hao huenda katika hayo makazi ambayo wakati mwingine hujulikana kama Sheol au Hades yaani Kuzimu, ambayo huko nyuma iligawanyika katika sehemu mbili, makazi ya waliookoka, Paradiso, na yale ya wadhambi. Hebu itazame Ahadi hii anayopewa yule mwizi pale msalabani, Lk 23:43

Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi

Basi tusemeje, kwamba Kristo hajui analolisema, au sisi ndio wagumu kuelewa?

Ndipo huku, katika hiyo Dimension ya Tano, wakiwako huku wao huendelea katika fahamu zao kamili, kumbukumbu na mambo yote yahusuyo fahamu. Nao wadhambi huendelea na ngwe zao za mateso! Dimension hii ya Tano ni ile tunayoweza kusema imejaa mateso, ni dimension ya kutisha saana! Huku ndiko Paradiso iliko kuweko, huku ambako Watakatifu wa Agano la Kale walizuiwa mpaka siku ilipotolewa ile Sadaka pale msalabani. Pia tulioneshwa kuwa makundi hayo mawili, Watakatifu na Wadhambi, yalitenganishwa kwa shimo refu sana.

Luka 16:22-23, 26

Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.”

Na kule kutenganishwa tunakuona katika kifungu cha 26:

Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.

Naye Samweli nabii, alipolala, aliungana na Watakatifu wengine waliomtangulia, huko Paradiso katika hii Dimension ya Tano. 1Samuel 28:11

Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.

Basi huyu mwanamke akiwa ni wakala wa Shetani, alikuwa na uwezo wa kuingia katika milki hii apendavyo, hii Dimension ya Tano. Kwani twafahamu pia kuwa ni katika dimension hii ambako pia ndimo yaliko makazi ya mapepo na kiti cha Shetani. Luka 8:30-31,

Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.

Shimoni”! Je, yawezekana kwamba huko ni sehemu katika lile Shimo la Kuzimu (the Bottomless Pit)? Dalili zinaonesha ya kwamba itakuwa ni sehemu hiyo, ambako kutakuwa ni KIFUNGONI! Bali twafahamu kwamba Bwana Yesu Kristo alikwenda huko katika hiyo Dimension ya Tano, 1Petro 3:18-20

Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri, watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa

Pia twafahamu kwamba huko ndiko Shetani alinyang’anywa Funguo na kisha Watakatifu wa Agano la Kale kufunguliwa na kutolewa huko Kuzimu alikoshuka Kristo, maana kifo chake kilikuwa ni cha “Mdhambi” pale alipozibeba dhambi zangu na zako, ndipo ilimlazimu kushuka Kuzimu kama wenye dhambi wengine walivyoshuka huko Kuzimu! Zab 16:10

Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu

Haya ndiyo mambo tunayoweza kuyafahamu kuhusu Dimensions. Shetani anao uwezo wa kuzizungukia Dimensions zote tano na kucheza nazo apendavyo. Anaweza kufanya lolote apendalo, iwe ni kidini au kichawi; kama ni kuwalaghai au kuwatesa watu waliopo hapa duniani. Nao upana wa hizi dimensions tano ni mpaka Mbingu ya Pili, yaani galaxy, Mbingu ya Kwanza ikiwa ni hilo anga na na dunia yake.

Basi, hapo Kristo alipoimwaga Damu yake pale Kalvari, kama tulivyosoma 1Petro 3:18-20 hapo juu, pia, alipokuwa huko Kuzimu aliwafungulia huru Watakatifu wa AK na kisha kupaa nao mbinguni: Efeso 4:8-10

Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.

Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.

Ndipo, kuanzia hapo yale makazi ya Watakatifu, ile Paradiso, katika ile Dimension ya Tano, yalifungwa na kuhamishiwa katika Dimension ya Sita. Hii iko katika ile Mbingu ya Tatu, huko alikonyakuliwa mtume Paulo. Na ni katika Dimension hii ya Sita, ndiko ambako Watakatifu wa AK walipelekwa: Yoh 14:2

Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali

Basi, kutokea hapo makazi hayo yalipohamishwa, nao watakatifu wote wa Agano Jipya, kulingana na Ujumbe wa Siku yao, zile nyota saba za Ufu 1:20, hao hukusanyika katika makazi hayo yaliyogawanywa kulingana na Ujumbe walioupokea kutoka kwa nyota hizo saba, nayo makazi hayo yote yako Uweponi Mwake:

Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Kwani hao nyota kila mmoja alipewa Ujumbe kwa Kanisa lake, nayo makanisa hayo, mgawanyiko wake ni kutoka Kanisa la Efeso hadi Kanisa la Laodekia, yaani Wapentekoste, hilo Kanisa litakalo kuwepo katika wakati wa Unyakuo, yaani hali za kiroho za makanisa hayo kulingana na wakati.

Kwahiyo, mkristo anapolala, au anapokufa, akiisha kuuchukua ule mwili wake wa kimbinguni (celestial), huingia katika hiyo Dimension ya Sita, Paradiso; ambayo

kabla ya Kristo kutolewa Sadaka ilikuwa ndani ya ile Dimension ya Tano.

Naye Mungu yuko katika Dimension ya Saba; Yoh 3:13

Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.

Unaona hilo ndilo linatuthibitishia kuwa hata akina Henoko na Elia na hata Musa, hawakwenda katika Dimension hii aliko Mungu bali katika ile ya Sita.

Ndiposa, huyo mkristo aliyezaliwa mara ya pili, anapokufa, yeye hupelekwa hapo chini ya madhabahu ya Mungu, katika Uwepo wa Mungu. Naye hupumzika hapo, katika hiyo Dimension ya Sita, haleluyaaaaa! Mdo 7:56

Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu

Unaona, Stefano hakuzungumzia Kuzimu, kama Kristo na Watakatifu wengine wa Agano la Kale! Hakuna Mtakatifu yeyote yule wa Agano Jipya anayezungumzia Kuzimu katika namna ya mapito yanayomkabili, labda “watakatifu” wa Katoliki hao wanaopitia “Toharani” iliyoko huko Kuzimu kwa kadiri ya falsafa yao! Maana hao wamewahakikishia waumini wao kupitia huko Toharani, halafu ndio waje watolewe kwa maombi na sadaka za hawa waliobaki hai, angalia kamali ya roho wanayo chezeshwa; mwisho wa mchezo hakuna anayetolewa maana ukiingia huko ndio basi tena, unakuwa umefika!!!

Hivyo ndivyo hali ilivyo, mkristo ‘aliyezaliwa mara ya pili’, huyo hulala katika Kristo Yesu! Je, kuna mfu anayelala katika Ufufuo akawa mfu bado? Hiyo fimbo kavu ya Haruni aliyoisahau kule ndani, Patakatifu pa Patakatifu, yaani Uweponi, nayo aliporudi aliikuta imechipua, ule ufu na ukavu umeikimbia!!! Ndio maana katika kutuhakikishia jambo hili la kuwepo kwa hiyo Dimension ya Sita, hapo Uweponi Mwake, Mungu anatuambia, 1The 4:14 “… vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.” Sasa jambo hili lingetokea hapo katika Kuja kwa Bwana!

Miili hii tuliyoivaa leo hii, inakoma hapo tunapoiacha kaburini, ndipo sisi huivaa ile ya kimbinguni ambayo haihitaji chakula. Nimewasikia wahubiri wengi sana wakiwasisitizia wakristo kuhusu kwenda mbinguni katika namna ambayo yaonesha kuwa tukifika huko tutakaa huko milele yote, yaani eternity, bali hilo si sahihi. Sisi tumeumbwa ili tuitawale dunia. Ni sawa na mtu anayeanzisha mradi fulani ili mwanaye auendeshe, basi ikifikia mahali mtoto huyo akataka abakie kwa baba yake, hilo lingemhuzunisha babaye ambaye anategemea mwanaye kuumiliki mradi huo. Kumbukeni kwamba kuna Mbingu Mpya na Dunia Mpya! Basi hapo Mungu anapozungumzia kuwaleta pamoja naye Kristo, hao waliolala katika Kristo, huo ndio ule wakati ambao ile miili iliyolala mavumbini tutairudia, tena itabadilishwa kutoka hii iliyochakaa na kuwa ile iliyokuwa glorified, yaani iliyotukuzwa, kama ule mwili wa Kristo alipofufuka, ule usiozuiliwa na chochote, ule aliokula kwao samaki; kwa miili hiyo ndiyo tutaingia KARAMUNI!

Sasa katika kulikamilisha jambo hili, basi kwa yule mkristo ambaye hajazaliwa mara ya pili, yule asiyeongoka, lile kundi lililokataa kumkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wao; ni kama vile mtu anapopatwa na Jinamizi, si kwamba anakuwa amelala fofo, na wala si kwamba yuko macho, yeye huwa katikati ya usingizi na kuwa macho, hali yake huning’inia hapo, na ndiyo inayompelekea kutetemeka na kupiga makelele ya kutisha, kwa sababu yeye hajalala, na wala hayuko macho! Labda anadondokea kule katika lile Shimo lisilo na mwisho, tena ni giza totoro, naye anashuka kama jiwe lililoachiliwa, anategemea sekunde yoyote ile kwamba atajipiga hapo chini sijui kwenye mwamba, naye anawaza jinsi atakavyopasuka kama Yuda, ndipo makelele na kutetemeka kungeongezeka!!!

Basi unapoliangalia jambo hili, hilo lingekuonesha mtu huyo huenda wapi hapo anapokufa akiwa hajazaliwa mara ya pili (uncoverted). Unaona, yeye amemaliza muda wake wa kuishi, amekufa hapa duniani; naye hawezi kwenda Uweponi mwa Mungu, kwa sababu hastahili kufika hapo bila ya Damu. Ndipo hunasa hapo. Naye hawezi kurudi tena duniani, muda wake huku umekwisha. Yuko katika Jinamizi, ndipo yeye hubakia katika hali hiyo mpaka ile siku ya Hukumu. Ni jambo la kutisha sana hapo unapojikuta katika hali hiyo! Hali hiyo huendelea mpaka katika Hukumu ya mwisho ya waliopotea (2Petro 2:9), hapo wasiookoka wote, na Kuzimu nayo, vitakapotupwa katika ziwa la moto (Ufu 20:13-15)

Sasa, mtu awapo katika hii Dimension ya Tano, au Kuzimu, ni vizuri ieleweke wazi kwamba hakuna uwezekano wa chochote kile kufanyika kwa mtu aliyefika hapo, haiwezekani kubadilisha chochote kile baada ya kifo, jinsi ulivyokufa ndivyo utakavyoishia, hakuna fursa ya kubadili chochote wala kutubia chochote kile. “Baada ya kufa, hukumu”!!!

Kwahiyo ndugu zangu, kila tulilonalo katika upande huu, ambalo ni la asili, ni kivuli cha kile kilicho “Supernatural” au cha “Rohoni” au cha milele katika context ya “Eternal” kwa ule upande wa pili. Kwahiyo, ili mradi hapa duniani tunaye mkristo aliyezaliwa mara ya pili, na tuko katika miili kama hii tuliyonayo, basi jambo hili ni kioo dhahiri cha ile miili inayotusubiri upande ule wa pili, huko ambako hakuna kifo wala majonzi, 1Kor 15:40

Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.

Nalo jambo hili, ndilo linaloifanya mioyo yetu iyatamani hayo. Unaona, kuna jambo fulani ndani yetu ambalo hujiinua ili kuyafikia hayo. Kitu fulani hutuambia kuwa jambo hilo liko hapo katika uhalisi wake. Ndiyo maana iko katika mioyo yetu kuihubiri hii Habari Njema, kuwaeleza wapendwa kuwa kuna Mbingu ya kuipata na Jehanamu ya kuikimbia, na kwamba yuko Mungu anayetupenda, na Nguvu yake ya kutukomboa iko hapo tayari kutunyakua kutoka katika mzunguko wa kifo tuliomo, wakati wowote ule tutakapokuwa tayari kuipokea.

Unaona, wakati mwingine hali zetu hufikia kuwa kama ya yule mtu anayezama, au anaye kufa maji,  naye akiiona kamba inayoning’inia juu yake, ndipo angewaza, “Lah, hii hapa kamba, naweza nikajivuta nikatoka katika kifo hiki kinachonikabili, dah, lakini dhehebu langu haliamini katika kunena kwa lugha, wala uponyaji wa kiungu, hata ubatizo kwa Jina la Bwana Yesu Kristo kwa Ondoleo la Dhambi, oh, kamba hii inapaswa ije siku sabato, ule Muhuri wa Mungu!”

Bali kamba hiyo iliwekwa hapo kwa kusudi hilo, ili kwayo ujitoe katika mzunguko huo wa mauti za kidini. Hiyo ndiyo sababu Yesu Kristo aliutoa Uhai wake, kwa kusudi la kuwaokoa wenye dhambi. Naye akatuning’inizia kamba hiyo ya Uzima wa Milele (Eternal Life), ambayo leo hii inapita juu ya kila kichwa cha mwenye dhambi katika blogu hii, na duniani kote, ikiwa na ishara inayotukaribisha, “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo” Iwapo mngependa kuuitikia wito huo, matayarisho yamekwisha kufanywa, yabwageni hayo maroho ya dini yaliyowalemea, yaleteni Uweponi mwa Kristo, yatatimua kama yale ya Mgerasi!!!

Basi hadi hapo tutakapokutana tena huko katika Dimension ya Sita, katika lile pumziko, ile SABATO; yaani iwapo mtaipokea hiyo “kamba” leo hii, makabatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili muondolewe Dhambi zenu, mpate na kuzaliwa mara ya pili.

Mbarikiwe nyoote!

–Ck Lwembe

Advertisements

17 thoughts on “Siri ya Kifo na Kaburi!

 1. Siyi,
  Sikuyaona maswali yako mpaka leo hii nilipokuwa ninamjibu Lenda kuhusu jambo hili la kifo ktk thread nyingine, ndio hivyo tena, tuvumiliane!

  Ktk kuyajibu maswali yako:
  1. Damu ya kibinadamu (ya mwili wa Yesu wa kibinadamu) inaweza kumwokoa mwanadamu mwenzake?

  Jibu ni kwamba Damu iliyokuwamo katika mwili wa Yesu, ilkuwa ni Damu ya Mungu. kama ilivyo sheria ya uzazi, mbegu yenye uzima huwa ni ya baba, nao uzima hukaa ktk damu. Ndipo ili damu ya Yesu iwe ya kibinadamu, basi suala la Mariam kupata uja uzito kwa RM itabidi liwe la uongo, otherwise ile ilikuwa ni Damu ya Mungu, biologically, ndio maana inatakasa dhambi na kutuacha tulio safi na watakatifu, hata tunathubutu kumsogelea Mungu na kuongea naye!

  2. Mungu alipodhihirika ktk mwili alikuwa ni Masihi. Nalo kusudi la yeye kuwa Masihi ilikuwa ni kuwarejesha waliopotea, hao waliokuwa ktk Hukumu ya Kifo. Basi kazi hiyo haikuwa lele mama, nao unabii unayoihusu shughuli hiyo ndio huo unaousoma ktk hivyo vifungu vya Isaya kwa sehemu, nasi tunaunganishwa ktk unabii huo, kuupokea huo uzima na mema yake, iwapo tutaungana na Sadaka hiyo, ile Injili ya mitume, iliyotolewa kwa ajili yetu, ili kurejesha uhusiano wetu na Mungu ktk ile furaha aliyokuwa nayo Adamu kabla ya Anguko!!

  Asante, ndg yangu, likimbie hilo jinamizi linalokunyemelea!

 2. Lwembe,
  Nashukuru kaka kwa jibu lako la msingi.
  Kwa maelelzo yako, nimekuelewa kuwa, mwili wa kiubinadamu wa Kristo ndiyo uliouawa na siyo roho yake. Kwa maelezo mengine, ni ubindamu wa Yesu tu ndio uliokufa pale msalabani na siyo uungu wa Yesu (roho yake). Mimi nimepata swali lingine;
  1. Damu ya kibinadamu (ya mwili wa Yesu wa kibinadamu) inaweza kumwokoa mwanadamu mwenzake?
  2. Unaelewaje unaposoma Isaya 53:10?
  KJV: Yet it pleased the LORD to bruise him; he hath put him to grief: when thou shalt make his soul an offering for sin, he shall see his seed, he shall prolong his days, and the pleasure of the LORD shall prosper in his hand.
  SUV: Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake.

  Karibu kaka

 3. Siyi,
  Swali lako ni zuri sana. Yaani ukilisikiliza kutoka ndani ya moyo wako, ukaamini kwamba unahitaji kukijua kilichotendeka na namna yake katika siku ile pale Kalvari, hicho kilichosababisha Pazia la Hekalu linalopaziba Patakatifu pa Patakatifu kuraruka lenyewe, na maajabu yote yaliyotokea katika dakika zile za Kukata Roho Kwake; loh, unaweza kufika mbali zaidi ukilipokea jibu hilo kama Maandiko yanavyokwambia!

  1: Mk 15:37 “Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.”
  (“And Jesus cried with a loud voice, and gave up the ghost”) KJV

  2: 1Pet 3:18-19 “Mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri”
  “… but quickened by the Spirit: By which also he went and preached unto the spirits in prison.” KJV

  3: 2Pet 1:19 “We have also a more sure word of prophecy” KJV
  “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, …”

  Ukiweza kuyaamini haya, kwa kulipokea hilo neno la unabii kutoka kwa hao wanaokuambia Habari Njema hii, basi utakuwa umeuvuka mtihani wako wa kwanza katika safari yako ya “Kumfuata Kristo”; la ukishindwa, basi utabaki katika dini!!!

  Nakuombea usitindikiwe katika …

  Ubarikiwe!!!

 4. Lwembe,
  Inaonekana ulileta hoja za muda mrefu sana bila ya kuziona mapema.
  Kimsingi nimesoma maelezo yako ya umizimu. Najua wewe unaamini kuwa kuna roho za watu ambazo ni conscious kabisa hata kama hazina miili. Na miili nayo inajitegemea kwa namna fulani. Vinapoungana vitu hivi ndipo tunapata nafsi hai.
  Kwa mtazamo wangu na uelewa wangu wa kimaandiko, naomba nikuulize swali moja tu lenye viswali ndani yake, ili ukilijibu hilo, utata kuhusu umizimu ulio nao utakwisha.
  Swali,
  Biblia inatuambia kuwa Yesu ni Mungu. Ni Mungu aliyefanyika mwili-mwanadamu. Hivyo alikuwa ni Mungu lakini pia alikuwa ni mwanadamu wakati akiwa duniani.
  Je, ni nini kilichokufa msalabani? Ni mwili wa kibinadamu wa Kristo au ni Roho yake? Au vyote viwili vilikufa?.
  NB; Yeyote mwenye uelewa na mtazamo wa kimaandiko kama wa Lwembe, anaweza kujibu swali hili.
  Karibuni sana wanaSG.
  Shalom!
  siyi

 5. @ Mjoli wa Siyi

  “…..THOU SHALL SURELY DIE” ukiisoma Biblia yako kwa miwani ya dhehebu lako, hutakaa uielewe hata siku moja! Kifo maana yake ni KUTENGWA NA MUNGU! Ndio maana baada ya Kristo kuimwaga Damu yake sisi tulio wa Kristo tunao UZIMA WA MILELE. Uzima huu hatuupati baada ya KUFA, hapana tunaupata siku ile tunapozaliwa mara ya pili! Kwahiyo jaribu kuchangamsha akili yako, hebu liangalie jambo hili kwamba huyo aliyeupokea umilele leo hii, atakufaje kesho ilhali yuko ktk umilele? Mkristo anabadili makazi tu, Mjoli wa Siyi!

  Kuhusu wasioisikia Injili, kama unaweza kuyaamini Maandiko, yanasema hivi kuhusu hao wazee wetu: Rum 2:14-15
  “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15-Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea.”
  Naye Mungu huyafanya yote katika Mapenzi yake Makamilifu na si kulingana na hisia zetu za kidini au kibinadamu, kwahiyo suala la kuifananisha mahakama yako ya mtaani na Mahakama ya Mungu na kuikataa Haki ya Mungu, sioni unautofauti gani Shetani aliye asi!

  Kuhusu ule mfano wa Samweli, labda nikuulize kwanza kama wewe ni mkristo kweli au ni mfuasi wa dini tu? Maelezo yako unayoyatoa yanaonesha kwamba umetaharuki ulipoiona Kweli ya Biblia ambayo inauumbua uongo uliouzoelea na kuufundisha kama Nabii wa Uongo!

  Imenishangaza sana namna ambavyo huna hata chembe ya uoga hapo unapoyabishia Maandiko kavu kavu! Hebu itazame hii kauli yako:
  “”PIA SAMWELI MWNYEWE ANASEMA “Why have you disturbed me by bringing me up?SAMEL 28:15 ” SAMWELI ALIKUWA ANAFANYA MAMBO FULANI AKIWA HAI SASA MFALME KAMSUMBUA NA KUMRUDISHA MAANA YAKE MTU HUYU HAJAFA. PIA ANATAKA KUTUAMINISHA KUWA TUNAWEZA KUONGEA NA WATU WALIO KUFA KITU AMBACHO NI IMANI ZA KIMIZIMU.”
  Lakini Biblia ndiyo inayoyasema haya katika 1Sam 28 kilipo kisa hiki, hapo Sauli alipokwenda kwa yule mwanamke mchawi wa Endori:
  28:10-12 “Naye Sauli akamwapia kwa BWANA, akasema, Aishivyo BWANA, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu…”
  15 “Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha”

  Basi labda nikuulize Mjoli wa Siyi, ni wapi ambapo Biblia inasema kwamba hayo inayoyasema Biblia ni mambo ya mizimu? Ni wapi wewe umeyapata haya unayotuambia kuwa jambo hili Biblia inalotuambia ni Fundisho la Uongo linalotuaminisha kuwa tunaweza kuongea na watu waliokufa? Kwamba Biblia ina Mafundisho ya Uongo? Angalia unavyosimama kuyapinga Maandiko:
  “PIA MAFUNDISHO HAYA KIDANGANYIFU YA MTOA MADA YANAPISHANA MAANA SAMWELI (MAREHEMU) ANAONGEA NA SAULI MTU ALIYE MUASI MUNGU. PIA WANAONGELEA KWA WACHAWI WAKIWA KWENYE HIMAYA YA SHETANI.”!!!
  Labda kwa kauli zako hizi niseme kwamba HAUAMINI kwamba kitabu cha 1Sam kina UVUVIO wa Mungu, kwahiyo chatokana na Shetani kulingana na Fundisho hilo la Uongo linalojiwakilisha kama Neno la Mungu! Basi kama haya si mafundisho ya mashetani ni kitu gani? Shetani kaandika chapter 28 ya 1Sam!!!

  Kuhusu Lazaro kupiga stori, jaribu kutuliza munkari wa dini! Sikusema kwamba hao walikuwa katika Dimension ya Sita na ya Tano, nimesema katika wakati huo walikuwa ktk ile ya Tano iliyogawanyika kwa shimo reeeeeeeefu lisilovukika, kama ambavyo leo tena nasi tumetenganishwa hivyo, wewe unamuona Shetani ktk camouflage ktk maelezo ya 1Sam akileta mafundisho ya mizimu, na mimi namuona Mungu akinisimulia yaliyojiri katka nyakati hizo; halafu sote tunaamini kwamba tunaisikiliza na kuifuata Biblia!!! Kama ni kupotea sioni kupotea kunakozidi hali uliyonayo!

  Kuhusu hesabu zenu za Mavumbi + Roho= Nafsi Hai, unaonekana una piga makelele ya mlevi wa dini! Mimi sijawahi kuumba mtu, huyo aliyemuumba katika Hekima yake ndiye anayetujuza yote kwa kadiri anavyoyafunua, hatua kwa hatua kutoka Mwa 1:26 mpaka huko 1Kor 15 na kuendelea! Hata nikikuuliza, hiyo hesabu yenu, mnaweza kuithibitisha kwa Mwa 1:26 pekee? Acheni mafundisho yenu ya Uongo yenye kuipinga Injili!!!

  Unaponiuliza swali kama hili, “kama mtu akifa hakuna kilichobadilika mbona anatueleza kuwa yesu alienda kuhubiri kuzimu baada ya kufa msalabani?” Inaonesha kwamba uko mbali saaana na Kweli ya Injili! Mimi ndiye niliyekuambia kuwa Yesu alikwenda kuwahubiri walio kifungoni? Jamani, hili laonesha kuwa unafiki wako unakutesa wewe mwenyewe, 1Tim4:2 kwamba “kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe.”Hebu kaa kidogo na Siyi akupige brash halafu ndio uje tujadili mambo ya Mungu, maana hapa naona niko na mpagani per se anayepose ukristo!

  Kuhusu Dimensions, wewe utakuwa umejichanganya, au uwezo wako wa kusoma na kuelewa mambo ni mdogo! Mwa 2:1, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.” Kwahiyo matumizi ya Dimensions hizo ndiyo niliyoyaelezea, na si hizo hadithi zako zilizojaa kufa kufa, ni kweli kwa kuipinga kwako Injili ni kwamba UMETENGWA na Mungu, ndio maana inawawia vigumu kuyakamata hata yaliyo rahisi!

  Kuhusu miili, iko kama nilivyoieleza, uoga wako wa kuzimu hauwezi kubadilisha chochote kile! Eliya na Musa walikuja ktk Mwili gani na walitoka wapi? Au uliwaona nao wakila samaki? Acheni upagani wenu huo, mnayabishia hata yaliyodhahiri halafu mnajifanya wakristo,!! Eleweni pia kuwa Hukumu ya kwanza inakukamata katika siku uliyoipinga au kuikataa Injili, Yn 3:18 “…asiyeamini amekwisha kuhukumiwa.” Hii ndiyo Hukumu inayoamua hatma yako, kama ni Dimension ya Tano, basi unaungana na waliokutangulia katika kulipindisha Neno la Mungu, mkiwa na miili na si roho maana twafahamu roho hazinywi maji! Halafu ndipo hiyo Hukumu mnayoizungumzia itawafikia, lile ziwa la moto huko Mwisho!!!

  Mwisho, kuhusu Yesu kuzihubiri roho zilizoko kifungoni, mimi nafahamu fika kuwa ninyi hamuliamini jambo hilo licha ya unafiki wenu wa kuyarejea Maandiko mara kwa mara na kuwadanganya waumini wenu mnaowashikilia. Si unajiona wewe mwenyewe ambavyo UMEYAKATAA kata kata maelezo ya Mungu katika 1 Sam 28, na sasa UNAYAKATAA, tena haya ya 1Petro 3:18-20, na pia hayo ya Luka 16:22-26, na tena haya ya Lk 23:43 “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” halafu …; loh the list is endless, hata siioni tofauti yenu na Yuda Iskariote, in short, ninyi ni hawa hapa katika 1Tim 4:1,3, as God Himself declares abt you:
  “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; … na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”

  Mjoli wa Siyi, Dimension ya Tano na ya Sita zote zipo na zinasubiri wateja, tafakari jambo hilo kwa unyenyekevu unaoihusisha roho yako na si ushabiki wa dini za kipagani!

  Bwana na akufungue moyo wako!

  Karibu sana!!

 6. 1: Tatizo lako Siyi ni moja, unayapima mambo kulingana na dini yako, jambo ambalo linakuletea ugumu kuyaamini hata Maandiko! Maandiko yanatufundisha wazi wazi kwamba “Baada ya kifo HUKUMU”, kwahiyo kudhani kwamba baada ya kufa unaweza kutenda dhambi ni makosa ya uelewa. Pia kauli yangu kwamba Kristo alikuwa katika Celestial form inatokana na Maandiko hapo yanaposema Kristo akahuishwa nasi twafahamu kuwa mwili wake ulibaki kaburini; bali hao waliohubiriwa zilikuwa ni roho, kwamba zilikuwa katika miili ya celestial, hilo sijui!

  Lakini pia ktk huko kuzihubiri roho hizo zilizoko kifungoni, unaweza kulipima jambo hilo iwapo utakirejea kile kifungu katika Ufu 22:11 “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” Basi wakati huu unapofika Milango ya Neema itakuwa imefungwa, nayo Injili ya kweli itaendelea kuhubiriwa, ikiendelea kuwachoma mioyo watu wa dini, wengine wakijaribu kuujia Wokovu walioudhihaki siku zile ambazo Uvumilivu wa Bwana ulikuwepo, na sasa wakijaribu kuikimbia Adhabu, maana Hukumu ilikwisha pita siku walipoidhihaki Injili ya Kweli wakiamua kuzifuata taratibu zao za dini! Ndipo roho za watu hao pia huendelea kuhubiriwa Kweli kwa USHUHUDA TU, kama ambavyo leo hii Huduma hiyo ya kuzihubiri roho hizi za leo ikiendelea, hizo roho ambazo hazitaokoka zaidi ya kujifariji kwa dini zao na wokovu wake!

  2: Kuhusu miili ya akina Henoko, Musa na Eliya, kwa Maandiko twafahamu kwamba Henoko na Eliya HAWAKUFA bali walinyakuliwa. Pia twafahamu kwamba Musa alikufa na mwili wake kugombewa, halafu twafahamu pia kuwa hao Musa na Eliya walikuja tena duniani katika miili hata wakaonekana kwa mitume. Basi ni katika majumuisho ya matukio kama haya, yanapofika katika tafakari ya vifungu kama hicho cha 1Kor 15:40, sisi huyaona hayo ambayo Mungu anatufungulia! Najua kuwa wewe Siyi kwa mafundisho yenu mnajua kwamba huyo Elia na Musa walikuwa ni mizimu, lakini hilo haliubadilishi ukweli wa Injili!

  3: Kazi za miili hiyo nilizianisha vizuri sana pale uliponiuliza kuhusu karamu, uwe unajifunza mambo Siyi, usiwe kama zezeta wa kiroho! Kuhusu kuangamizwa, vinaangamizwa vyote vilivyoupungukia utukufu wa Mungu, kama alivyoangamizwa Akani, Yoshua 7:24,26, “Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori … Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto…”!
  Naye Akani wa leo ni kiongozi wa familia inayojiwakilisha katika madhehebu yetu, ndipo ukifika wakati wake wa kupelekwa katika bonde la Akori, usidhani kwamba eti utakimbia Siyi!!!

  Hayo mafundisho ya Mathew unayoyasema, siyakumbuki, kwahiyo siwezi kukisemea kitu ambacho sikijui. Lakini kwa habari ya kuumbwa kwa Adamu, ninachokifahamu mimi kulingana na Maandiko ni kwamba Adamu aliumbwa kwanza katika roho, yule aliye mfano wa Mungu, Yoh 4:24 “ Mungu ni Roho…”, na mbele ilipoonekana hakuna wa kuilima ardhi, ndipo akapewa mwili na kuwa nafsi hai!

  Kuhusu 1Kor 15 ndg yangu, iko kama ilivyo na imekuwa hivyo kwa miaka 2000! Kwa vifungu hivyo wengine wameuona Ufalme wa Mungu na, wengine wameondoka na Laana kuelekea bonde la Akori!

  Asante sana Siyi kwa ukarimu wako!

 7. Lwembe,
  Mengine haya hapa maoni ya mjoli mmoja kuhusu mada yako hii ya celestial na terestial bodies. Yapitie pia…
  FUNDISHO KUU NINALOLIPATA HAPA NI KUWA MTU HAFI BALI ANABADILISHWA KUTOKA KWENYE MWILI WA KIBINADAMU (TERESTRAIL) NA EITHER KWENDA MBINGU YA TANO AU YA SITA. MUNGU ALISEMA MWANADAMU ORIGINALLLY ‘’’’’’ …..THOU SHALL SURELY DIE GENESIS 2:17’’’’’ HIVYO BASI MTOA MADA ANAUNGANA NA KAULI YA SHETANI KUWA “YE SHALL NOT SURELY DIE GENESIS 3:4”
  —-dimension ya tano tunaelezwa wanaishi wasiomuamini yesu na wanateseka vibaya sana, je hawa wanaokufa Bila kusikia chochote kuhusu yesu wako katika dimension ya ngapi maana anatueleza wale wa kabla ya yesu aliwahubiri kule kuzimu je wa baada ya kufufUka aliwahubiri wapi (WAZEE WETU KABLA YA INJIRI), NA KAMA WAKO MBINGU YA TANO KWA MAELEZO YAKE HAONI KUWA MUNGU AMESHAANZA KUTEKELEZA HUKUMU KWA KUWAPA WATU MATESO KABLA YA SIKU AMBAYO AMEITENGA KWA AJILI YA HUKUMU. Hivyo basi tunafundishwa Mungu ni katili maana anaanza kuwatesa watu waliokufa hata kabla ya hukumu, hata kwa maHakama za kibinadamu hilo halikubaliki.
  MFANO UNAOTUMIKA KUTOKA KITABU CHA WAFALME KUHUSU SAMWELI
  ‘’’’’’’’ KWA MAANA ANAYOTUELEZA MTOA MADA HUMU NA KISA HIKI ANACHOKIHUSISHA SHETANI AU JINI LOLOTE AU MCHAWI ANAO UWEZO WA KUFUFUA MTU. MAANA ANATAKA KUTUSADIKISHA KUWA YULE MCHAWI ALIWEZA KUMFUFUA SAMWELI KISHA KUMRUDISHA KIFONI(KUUA KULINGANA NA DEFINITION YA MTOA MADA). PIA SAMWELI MWNYEWE ANASEMA “Why have you disturbed me by bringing me up?SAMEL 28:15 ” SAMWELI ALIKUWA ANAFANYA MAMBO FULANI AKIWA HAI SASA MFALME KAMSUMBUA NA KUMRUDISHA MAANA YAKE MTU HUYU HAJAFA.PIA ANATAKA KUTUAMINISHA KUWA TUNAWEZA KUONGEA NA WATU WALIO KUFA KITU AMBACHO NI IMANI ZA KIMIZIMU. PIA MAFUNDISHO HAYA KIDANGANYIFU YA MTOA MADA YANAPISHANA MAANA SAMWELI(MAREHEMU) ANAONGEA NA SAULI MTU ALIYE MUASI MUNGU. PIA WANAONGELEA KWA WACHAWI WAKIWA KWENYE HIMAYA YA SHETANI. WAKATI HUOHUO ANATUMIA MFANO WA RAZALO MASKINI NA TAJIRI INAONESHA KUWA WATU WA MBINGU YA TANO NA WATAKATIFU WAKE WA MBINGU YA SITA WANAUWEZO WA KUPIGA STORY NA KUBADILISHANA MAWAZO NA USHAURI. PIA INAONEKANA IBRAHIM NDIYE MKUU WA HIYO KAMBI.KUNA VITU VINGI SANA MTOA MADA ANATAKIWA KUELIMIKA NA BIBLIA TU NDIO INAYOWEZA KUSAIDIA.
  ‘’’’’’’Najua Siyi utaniletea zile hesabu zenu za: Mavumbi + Roho= Nafsi Hai!! Bali unapaswa uendelee kupokea maelezo kutoka kwa Muumbaji kwa kadiri anavyo kufunulia, maana katika kifungu cha 1Kor 15:40 tumepelekwa mbele zaidi katika ufahamu wa mambo hayo kiasi kwamba hiyo hesabu yenu kwa sasa imepitwa na wakati, tazama jambo hili jipya tunalo juzwa, “Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani”!!’’’’’’
  —–kutoka na hapo juu mtoa mada anapingana na kauli ya muumba. Huwezi kuzungumzia kufa kwa mtu bila kuelezea alianzaje kuwepo? Kwa nini ilibidi mtu afe?NA ALANZAANZAJE KUWEPO? Mtoa mada anataka kututaka tuazie fungu lake kuu la wakorintho la miili(wa mbinguni na wa duniani) bila kuwaeleza watu hutu mtu kaanzaje anzaje maana anakwepa direct answer kutoka kwa Mungu. Pia anatakiwa kujua kuwa KAULI ZA MUNGU HAZIPITWI NA WAKATI KAULI YAKE HIYO NI YA KIPOTOFU.
  UDANGANYFU NA UKANGANYIFU WA MTOA MADA KUHUSU SAMWEL NA MWANAMKE MCHAWI
  Rejea kauli ya mtoa Mada ‘’’’’’’’’’’’’

  ‘’’’’haiwezekani kubadilisha chochote kile baada ya kifo, jinsi ulivyokufa ndivyo utakavyoishia, hakuna fursa ya kubadili chochote wala kutubia chochote kile. “Baada ya kufa, hukumu”!!!’’’’’’
  —–kama mtu akifa hakuna kilichobadilika mbona anatueleza kuwa yesu alienda kuhubiri kuzimu baada ya kufa msalabani?

  —– —– pia kuhusu Maskini RAZALO na tajiri kwa Falsafa yake mtoa mada inadhibitisha kuwa haelewi anachokiamini kwani, tunajua yesu alitumia mfano wa ibrahimu kwenye kisa cha razaro maskini ili watu waelewe kuwa inabidi uwe mwema kabla ya kufa ili uokolewe. Lakini tuchukue muktadha wa mtoa mada kama ni hivyo (kulingana na anavyotaka kutuaminisha) mbona hayo makundi yanaonekana kutengwa hata kabla ya yesu kufa na kuhubiria hao wafu wake wa agano la kale. Maaana yesu alizungumzia wakati akiwa hajafa. Lakini kulingana na dimension ya sita na ya tano ya mtoa mada zilitokea baada ya yesu kufufuka. Mbona anajikanganya hapo??
  —–pia kuhusu miili ya mbinguni nay a duniani (carestrial and terrestrial bodies) watu wa mbingu ya saba (mbinguni kwa baba), sita (mahali Fulani pa kufikirika wanapokaa wafu waliookoka) na ya tano (bottomless pit wafu waliomkataa yesu wanamiili gani?) afafanue miili ya sehemu hizi zote. Anajichanganya maana amekwisha tueleza kuwa kule watu wanakuwa na roho na hawana miiili tena analeta habari za miili ya mbinguni. Pia alueleze maraika wanamiili ya wapi maana nao wana miili?

  WATUMISHI NINAMENGI ILA KWA SABABU NIMEIONA KWA HARAKA NIMEELEZA KWA MUHUTASARI NA KUMUULIZA BAADHI YA MASWALI YA MSINGI MTOA MADA AMBAYO MAJIBU YAKE INABIDI AYAPATE KWA WASABATO TU. SAMAHANI PIA SIJAPATA MUDA WA KUWEZA KUHARIRI KAZI HII.

 8. Lwembe,
  Ha ha ha ha. Tafadhari usinichoke kwa maswali ndg yangu. Maana kwa njia ya maswali, ndiko kujifunza kwangu zaidi huongezeka. Nashukuru kwa majibu yako.
  Kwa majibu yako mazuri ya swali la kwanza, nimekuelewa hivi, Yesu alienda kuzihubiri hizo roho kifungoni akiwa ktk celestial form. Na huenda hata hizo roho nazo zilizokuwa kifungoni, zilikuwa ktk hali ya celestial form. Celestial form ambayo ni miili ya mbinguni, inayokaa mbinguni.
  Swali:
  1. Celestial (wenye miili ya mbinguni) bado wanaweza kuwa na dhambi hadi wahitaji mhubiri? Mbinguni bado kuna dhambi?
  2. Akina Henoko, Eliya na Musa(wazee waliotutangulia mbinguni), nao walienda katika celestial au terestial forms?
  3. Ni mwili upi utakaongamizwa kati ya celestial au terestial au mbinguni tutakuwa na miili miwili? Maana huu terestial nao utafufuliwa!!!
  Majibu ya swali la pili siyaoni badala yake nakutana na swali tu. Na kwa mantiki ya swali hili, nimekuelewa kuwa, miili ya mbinguni mtoa pumzi ni huyohuyo-Mungu. Kwa hiyo unanirudisha kwenye fundisho la Mathew kuwa, Mungu aliwaumba akina Adamu wawili-visible(terestial) na invisible(celestial) Adams! Je, ukimwangalia vizuri msomi na mwanasheria maarufu mtume Paulo, unafikiri anamaanisha hivyo unaposoma sura nzima ya 1 Korinth 15? Hebu ipitie tena rafiki yangu.
  Mwisho, nakushukuru kwenye jibu la mwisho, umerejea kwenye maadiko vizuri kabisa. Ubarikiwe sana.
  Twende kazi…

 9. Swali na 1 uliloniuliza, ili uweze kulielewa vizuri jibu lake, utalazimika kujiachilia kutoka katika mafundisho ya dini yenu, angalau kwa muda mchache tu, ili Maandiko yapate fursa ya kukufunza katika Uhuru wake. Unajua, umechangamsha sana akili yako, ni jambo zuri na ni hatua yenye manufaa kiroho!

  Haya, ninairejea tena ile 1Pet 3:18-20, ya KJV, kwani tafsiri ya kiswahili haiko sawa sana katika kipengele cha “Roho” ndio maana katika jibu langu nilikurejesha katika KJV ili tupate kwenda sambamba.
  “For Christ also hath once suffered for sins, the just for the unjust, that he might bring us to God, being put to death in the flesh, but quickened by the Spirit: By which also he went and preached unto the spirits in prison”

  Ndipo kifungu hiki kinaanza kwa kumuongelea Kristo, kinasema “huyo akauawa katika mwili, bali Roho AKAMHUISHA: na kwa huyo pia alikwenda na kuzihubiri roho zilizoko kifungoni.” Mwili wake ule terrestrial ulibaki kaburini kama Maandiko yanavyosema, Mt 12:40 “Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.” Kwahiyo kwa kifungu hiki twajua kuwa mwili wake ulikuwa kaburini ule terrestrial, ndipo kule kuhuishwa kwake tungekufahamu katika namna ya huo mwili Celestial hapo unapoipokea ile Roho yake na kuendelea kuyatimiza majukumu yampasayo, kama huko kuzihubiri hizo roho zilizoko kifungoni. Kufufuka kwake kulikuwa ni ule mwili, Terrestrial, ule uliokuwa umelala mavumbini, huo ndio uliofufuka kulingana na kazi yake, ile glory tofauti ya miili, kama ANAYOTUFUNDISHA mt. Paulo katika 1Kor 15:40
  “… lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.”!

  Swali na 2 ni gumu kidogo, kutokana na maudhui yake kujengeka katika kulitilia shaka Neno la Mungu, yaani KUTOKUAMINI. 1Kor 15:40 inatufundisha kuhusu mambo ambayo yako nje ya upeo wetu katika zile hisi tano, ni mambo ambayo yako katika Dimension nyingine. Lakini, mkristo ameongezewa Hisi ya Sita ambayo nilikuambia inaitwa Faith, yaani Imani. Kwahiyo, ili ufike katika kulielewa jambo hili ni lazima Hisi hii ya Sita iwe active, ndipo yanapokuja maelezo kama haya, katika uwazi kama huu, “Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali”, kwako itakuwa rahisi kuyapokea na kuyahifadhi moyoni mwako kwamba ni yale uliyofunuliwa uyajue!

  Kwahiyo unaponiuliza, Je, kuna miili aliyoiumba Mungu ambayo haina roho (celestial) na hivyo inasubiri roho kutoka kwa terestial? Labda nikuulize nawe, pale Mungu alipoufinyanga ule udongo, je, aliufinyanga na roho yake?

  b. Miili hii ya kimbinguni inakaa wapi? Jibu rahisi ninaloliona ni kuyafuata Maandiko yanavyosema, “miili ya kimbinguni” lazima itakuwa huko mbinguni kama ambavyo ya ile ya duniani iko duniani!

  c. i. Miili ya terrestrial ndiyo inayoupitia UFUFUO.

  ii. Ushahidi wa kimaandiko kuwa sisi tuliumbwa kabla ya misingi ya dunia. Sisi kuumbwa kabla ya misingi ya dunia, hapana, bali kuchaguliwa kabla ya misingi ya ulimwengu sawa! Efe 1:4 “…kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu”

  Haya Siyi, majibu ndiyo hayo katika urahisi huo, kama tulivyowekewa tuyajue hayo katika urahisi huo!

  Ubarikiwe!

 10. Lwembe,
  Nakushukuru sana kwa majibu yako ndg yangu.
  1. Kimsingi, leo sipendi kuwa na maneno mengi. Naenda kwenye hoja zako moja kwa moja. Kuhusu majibu yako ya 1 Petro 3:18-20, umesema kuwa roho ya Kristo haikuhuishwa, bali Roho alimhuisha Kristo…nanukuu “bali Roho alimhuisha Kristo, na kwa huyo Roho akazihubiri roho zilizoko kifungoni!” Naona bado umenichanganya kaka. Hivi wakati RM anamhuisha Kristo, Kristo alikuwa katika roho au katika ule mwili wa Celestial? Na kama ni roho yake ndiyo iliyohuishwa kwa nini unakana tena? Na kama ni mwili(terestial) wake, uliohuishwa, ni kusema kwamba RM alimfufua akaenda kuzihubiri zile roho then RM ukamrudisha tena kaburini ili siku ya tatu afufuke? Hili ndiyo fundisho lenu?
  2. Majibu ya swali ya pili yanaleta new theology kweli. Nanukuu, “Miili, nilikuambia kulingana na Maandiko iko ya aina mbili kwa kila mmoja wetu, hii ya duniani, Terrestrial na ile ya kimbinguni, Celestial, kwahiyo roho inapotoka katika huo mwili wa duniani, yaani hapo unapokufa, hiyo huuvaa ule mwili wa kimbinguni na hivyo huendelea kuwa nafsi hai, hiyo yenye ufahamu wote!”
  Maswali;
  a. Je, kuna miili aliyoiumba Mungu ambayo haina roho(celestial) na hivyo inasubiri roho kutoka kwa terestial?
  b. Miili hii(celestial) inakaa wapi, mbinguni, kuzimu au hapa duniani?
  c. Rejea maelezo yako ya majibu ya swali langu la nne. Nanukuu, “hapo ndipo miili hii iliyolala mavumbini, ile ya kidunia hiyo yenye kupenda kula, hiyo ambayo aliipa kula miti yote kule Edeni, hiyo ndiyo itakayokuwa Glorified kama ule Mwili wa Kristo alipofufuka”
  Maswali;
  i. Miili itakayoenda mbinguni pindi Yesu atakapowafufua waliolala-kufa ni ile Terestial(itakayokuwa glorified ) au Celetial(all knowing ones)?
  ii. Una ushahidi wa kimaandiko kuwa sisi tuliumbwa kabla ya misingi ya dunia?

  NB; Naomba majibu yako yajengwe kwenye misingi ya neno na siyo porojo za kithiolojia yenu!!!
  Kazi kwako.

 11. Siyi, maswali uliyoyauliza nimejaribu kuyajibu, nategemea yatakupa mwanga zaidi katika hayo yaliyokutatiza.

  1: Kuhusu hiyo 1Petro 3:18-20, hebu itazame hii ya KJV, imekaa vizuri zaidi kueleweka RM anachotueleza:
  “…being put to death in the flesh, but quickened by the Spirit: By which also he went and preached unto the spirits in prison”
  Unaona si kwamba roho yake ilihuishwa, bali Roho alimhuisha Kristo, na kwa huyo Roho akazihubiri roho zilizoko kifungoni! Ninaamini hivi ndivyo yapaswa iwe kwa tafsiri nyepesi kulingana na kifungu hicho kilivyo, kama nilivyokunukulia ktk KJV. Basi nadhani hata maswali yako yaliyojitokeza kutokana na hili yatakuwa yamepata majibu!

  2: Ni kipi baada ya kufa huwa na ufahamu bado? Ni mwili au roho? Kwa namna gani huwa na ufahamu?
  Miili, nilikuambia kulingana na Maandiko iko ya aina mbili kwa kila mmoja wetu, hii ya duniani, Terrestrial na ile ya kimbinguni, Celestial, kwahiyo roho inapotoka katika huo mwili wa duniani, yaani hapo unapokufa, hiyo huuvaa ule mwili wa kimbinguni na hivyo huendelea kuwa nafsi hai, hiyo yenye ufahamu wote!

  3: Naomba unifafanulie (nipe sifa zao) kuwa kanisa la Laodikia ni wapentekoste!!!
  Upentekoste ndio Kanisa la mwisho, hilo linaloungojea unyakuo! Hakuna tena Kanisa litakalozaliwa au kuinuka juu ya hilo katika wito wa Mungu maana hilo ndilo kipeo. Nazo sifa zake za kiroho, ndizo hizo zinazoainishwa katika ujumbe wanaopewa: Ufu 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”

  Basi jaribu kuchunguza, ni kanisa gani ambalo watu ni matajiri na wametajirika kwa Neno la Mungu? Pia jaribu kuangalia, ni rahisi kumuonesha mkatoliki ukweli wa Biblia, kuliko Mpentekoste, maana yeye anao utajiri wa vipawa, yeye hunena kwa lugha kiashirio ambacho amekifanya kuwa ni kujazwa RM, sasa utamwambia nini ili akuelewe? Na hili ndilo Kanisa linalojiwa na Kristo, kama unavyomuona mwenyewe akisema yuko mlangoni, ili alinyakue, maana hili ndilo linalowakilisha ule ukamilifu wa Wokovu katika hatua zake, ya Kwanza, kule Kuhesabiwa Haki kwa Imani, hapo Kanisa lilipofufuliwa kutoka katika mauti ya Kikatoliki, ule wito wa Kiluteri, kama alivyoitwa Lazaro kutoka kaburini, kisha kupitia hatua ya Pili ya Utakaso, ambayo nanyi Wasabato mlizaliwa humo, lakini kwa bahati mbaya mkapinda kona na kupotelea porini na kuota miiba, yaani mkawa Cult. Lakini walio endelea, hao Wamethodist wakaifikia ile hatua ya Tatu ujazo wa Roho Mtakatifu, Mungu akivirejesha vipawa ndani ya Kanisa lake, lakini nao hawakufika mbali wakaanza kuvitukuza vipawa badala ya Bwana wa vipawa, ndio maana wanaambiwa WATUBU! Ngoja nikomee hapa kwa leo!

  4: Karamu hii, ni karamu ya namna gani isiyohuishsa kula? Je, kula ni matokeo ya dhambi?
  Ufu 19:9 “Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo.” Kuhusu hili haukuliangalia vizuri tu, nilisema Mungu atakapowaleta hao waliolala katika Kristo pamoja naye, hapo ndipo miili hii iliyolala mavumbini, ile ya kidunia hiyo yenye kupenda kula, hiyo ambayo aliipa kula miti yote kule Edeni, hiyo ndiyo itakayokuwa Glorified kama ule Mwili wa Kristo alipofufuka na kula samaki na mwenye kuweza kupita ukutani! Nadhani umeliona pia jambo la kula kwamba hakutokani na dhambi, bali ndivyo Mungu alivyotuumba sisi wakazi wa duniani!

  Mwisho, ingawa jambo hili sikuliweka katika huo mtiririko wa mada, unajua wakati mwingine flow ya wazo yaweza kuwa interrupted, lakini hili hapa ambalo ndilo Ufunguo wa hayo yote niliyojaribu kuyaandika.

  HISI ya SITA baada ya zile hisi tano tulizonazo, yaani, kuona, kusikia, kugusa, kuonja (kwa ulimi) na kunusa, tunayo hisi ya sita inayoitwa Imani (Faith). Nasi kwa hisi hii huzifikia Dimensions zote Saba! Mungu huongea nasi kupitia hisi hii. Hapo ndipo kuna umuhimu mkubwa wa kuifikia hiyo ili shughuli zoote za kumtafuta Mungu zikome, na kwa hiyo sisi huingizwa katika Pumziko kamili, ile Sabato ya Bwana, yaani umilele au kwa lugha nyepesi, sisi huondoka katika wakati na kurudi katika Eternity, huko tulikokuwa kwa Mungu, kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa, bali tukingali hapa duniani, hiyo ndiyo Siri ya utauwa!

  Nakushukuru sana Siyi, karibu katika Pumziko!

 12. Emmanuel na Daniel,
  Ninawashukuru nyote kwa michango yenu yenye kujieleza kwa ujasiri, basi sote tumshukuru Mungu kwa kutufunulia mambo yaliyo Siri!

  Mbarikiwe!!

 13. Ubarikiwe sana haya ndio mafundisho yanayo hitajika kwa watu wa Mungu kwani bila mafundisho ya kweli watamini uongo na kupotea.

 14. Shukrani kaka kwa somo lako lenye changamoto… Aidha, nikupongeze tu kwa kukiri kuwa kuna pumziko la Sabato mbinguni. Hii ni habari njema kwa wote wanaopanga kwenda huko. Maandalizi ya pumziko hilo yanaanza sasa. Huwezi ukaenda kupumzika sabato mbinguni, ilhali haupumziki sasa hivi hapa duniani.
  Kimsingi, unajitahidi sana kufundisha. Sijui kwa wafundishwa wenzangu kama na wao wameelewa. Mimi naomba kukuuliza mto mada maswali machache tu ili unielimishe zaidi. Karibu sana…
  1. 1Petro 3:18-20 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri, watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa”
  Swali: Unaelewa maana ya neno KUHUISHA? Kwani roho nayo hufa? Na kama hufa, Kristo alipokufa, alikufa mwili, roho au vyote viwili?

  2. Kwa maelezo yako, kuzimu ni shimoni ambako roho za wafu huenda. Kaburi ni shimoni ambako miili ya wafu huenda.
  Swali, Ni kipi baada ya kufa huwa na ufahamu bado? Ni mwili au roho? Kwa namna gani huwa na ufahamu?

  3. Naomba unifafanulie(nipe sifa zao) kuwa kanisa la Laodikia ni wapentekoste!!!

  4. Nukuu na tafsiri yako ya 1 Korinth 15:40, umesema kuwa kuna miili ya mbinguni na duniani. Katika maelezo yako ukasema kuwa mbinguni hatutakuwa na miili yenye hali ya kula ikashiba. Lakini tena kwenye maelezo yako ukasema tutakaribishwa KARAMUNI!!!
  Swali; Karamu hii, ni karamu ya namna gani isiyohuishsa kula? Je, kula ni matokeo ya dhambi?

  Maswali ni mengi, lakini acha nikomee hapo, niwaachie na wengine. Naomba majibu. Usiingie mitini tafadhari…
  Ubarikiwe na wewe/wengine pia…

 15. Umefafanua vizuri sana .. Ila inabidi nirudie Mara nyingi kusoma ili niweze kukaa kichwani mwangu Moja kwa Moja Holy Ghost I pray that you assist me to understand what is written in this article in the might name of Jesus amen!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s