Waimbaji Christina Shusho, Upendo Nkone na Upendo Kirahiro wako Marekani kihuduma.

Katika kipindi chetu wiki hiitumekuwa na habari za Mwimbaji Christina Shusho ambaye hatimaye harakati za wadau mbalimbali za kumpigia kampeni apate tuzo za Muziki za Kikristo zimezaa matunda baada ya Mwanamuziki huyo, Christina Shusho kufanikiwa Kutwaa Tuzo inayowahusu Wanamuziki wa Injili kutoka Africa ijulikanayo kama Africa Gospel Music Awards.

Itakuwa ni mara ya pili sasa kwa Christina Shusho kutwaa Tuzo kubwa ambapo mwanzoni mwa Mwezi July 2013 alipewa Tuzo nyingine nchini Kenya kwenye Tuzo za Groove Awards zinazofanyika nchini humo. Taarifa tulizozipata kutoka Uingereza zinasema Christina shusho amepata Tuzo hiyo akishindanishwa na Wanamuziki 6 Kutoka Kenya, Wawili Kutoka Uganda na Kutoka Tanzania alikuwapo Martha Mwaipaja, yeye kuibuka kidedea.

Kipindi cha Mwangaza kinampongeza sana Christina na pia tunaungana na Wadau mbalimbali waliompigia debe na hivyo kusaidia kumfikisha hapo alipo. Kila Lakheri Christina.

Aidha Tunazo Habari kwamba Waimbaji Upendo Nkone, Upendo Kirahilo na Christina Shusho wako nchini Marekani kufanya Tamasha kwa mwaliko wa Makanisa ya huko, na Mwangaza ilifanya mazungumzo na Christina kupitia mitandao  na haya ndio yalikuwa majibu ya Shusho nilipozungumza naye..

‘Ndio niko USA. Mimi na upendo kilahiro baada ya kumaliza tour yetu Canada ndio tumeingua hapa USA jana. Tukiwa hapa tunategemea kuhudumu zaidi ya state kumi ikuwemo Texas, California, Alabama, Ohio, Missouri, Washington D.C., new york city, n.k

Twaitaji msombi yenu’

 ITV

One thought on “Waimbaji Christina Shusho, Upendo Nkone na Upendo Kirahiro wako Marekani kihuduma.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s