Mtu hawezi kuweka kiraka kipya kwenye vazi kuukuu!!

chombo

SHALOM WANA SG, NA KWA UPEKEE NDUGU EMMANUEL!!

YESU anaposema mtu hawezi kuweka mvinyo mpya katika chombo/kiriba cha zamani au mtu hawezi kuweka kiraka kipya kwenye vazi kuukuu alikuwa anamaanisha kwamba, mtu lazima ajifunze kufanya kitu kwa upya au kwa ukamilifu. Kwa mfano badala ya kuweka mvinyo mpya kwenya kiriba/balasi la zamani/chafu/chakavu ni bora kununua jipya. Unapoamua kuokoka si kumuweka Yesu ndani ya tabia zako za zamani bali kubadilisha moyo kwa Damu ya Yesu ili uwe kiumbe kipya yaani ukubali kuacha tabia za zamani na kuanza upya. Kwa mfano, Ndoa yako inayumba sababu wewe ni muongo, si mcha Mungu, mchafu, mchochezi, au msengenyaji, mlevi, si mwaminifu katika ndoa nk, suluhu si kununua zawadi na kumletea mwenzi wako, au kumtoa out, unachotakiwa ni kuondoa/kuacha kabisa ile tabia yote ili mvinyo mpya (tabia njema) uwe katika chombo kipya.

Unapoona huduma yako imepoa au imekosa mwelekeo, usianze kutafuta namna ya kuweka kiraka kwa kuleta mbwembwe au maigizo na utapeli wa maneno, kaa chini jipange upya kwa uongozi wa Roho mtakatifu. Vyeo au wasifu tulionao huisha kulingana na majira, kwa hiyo hata nguo iliyo mpya leo, siku moja itaitwa chakavu kwa mantiki hiyo basi Yesu alitaka tujue hilo na tuwe na akili ya kujiandaa ili lile vazi litakapokuwa limechakaa tuweze kupata vazi jipya badala ya kuweka viraka vya nguo mpya katika vazi la zamani. Hujawahi kusikia mtumishi anasema “Enzi za miaka ya 90 nilikuwa na upako sana!”.

Huo ni mfano wa kujaribu kuweka mvinyo mpya katika balasi la zamani,, historia haitusaidii, Mungu anajali sana jinsi tunavyomaliza, so badilisha upya mfumo wa maisha yako badala ya kutumia perfume wakati hujaoga na nguo hujafua. Mfano mwingine ni huu, Kuna watu wanaendelea kuabudu kwa kung’ang’ania dini zao hata kama hazina uwezo wa kumdhihirisha Mungu na kuwasaidia, tene wengine wanaokoka kwa vikundi vikundi ndani ya kanisa ambalo halikubali wokovu matokeo yake wanakuwa hawaeleweki vizuri kwa sababu jumapili wanarudi kuongozwa na walewale ambao hawakubaliani na suala la kuokoka, hiyo ndiyo staili ya kuweka kiraka kipya (wokovu) katika kiriba kilichochakaa (dini isiyotambua habari za kuokoka).

Kimsingi hiyo ndio maana yake kwa sababu ukitafuta maana ya vitu halisi kwa mfano mvinyo basi utakuta kila sehemu umetumika kwa maana nyingine.

Mussa Kissoma

Advertisements

3 thoughts on “Mtu hawezi kuweka kiraka kipya kwenye vazi kuukuu!!

  1. Haleluya              nimebarikia na maneno hayo. Zaidi ni kuyaeka ktk matendo.               Mbarikiwe

    ________________________________

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s