Maana yake nini?

ndoto

Bwana Yesu Asifiwe! Naomba kujua tafsiri ya ndoto hii nimeota mama yangu kaweka ndoo mbili ndefu kama diaba akaweka juice na viungo vingine ndani yake akajaza juice na akaweka nyoka warefu ndani yake maana yake anatengeneza pilipili basi wale nyoka wakafurumia na kutoka wakazagaa ndani ya nyumba ikatokea nkashika mmoja na kumweka mapajani akatulia kuna kipindi nlimwachia nae alitoa maji mengi hadi nyumba ikawa imejaa maji kote nkajitahidi nkamshika tena nkapata na mwingine wa rangi ya njano nkawashika wote ikatokea siku ile kuna sherehe wale nyoka wakapotea nkawaona kwenye sherehe wapo kwenye nyavu vichwa vyao visifunikwe na kulikua kuna mwanamke kama kiongozi akawa anaongea kama kifaransa nilikua nmekaa karibu na rafiki yangu wa kike nae ni muislamu namwambia nakumbuka hayo maneno nliwahi kuyaongea japo siyakumbuki,hayo ndo nayokumbuka je, maana yake nini?

–Doris Charles

8 thoughts on “Maana yake nini?

 1. NI kwelI kabsa kwamba nyoka nI shetan, kwa upande wa mama yAke co lazIma awe anafUga mAjinI ila kuna kitu ambacho si cha kmungu ana kitumikia aidha kwa kujua au kutokujua, maana yake ni kurithishwa.

 2. dada Doris wewe umeokoka? na kama umeokoka bado unaendelea kufunguliwa, una vifungo vya nguvu za giza havijaisha unahitaji kufunguliwa zaidi natamani ningewasiliana nawe kwa karibu kwa mahojiano zaidi ili nijue nitakusaidiaje

 3. Dada Doris Charles na kanisa la kielektronikali la SG, nawasalimu kwa Jina la Yesu! Binafsi ndoto yako imenishtua kidogo na nadhani ulipoamka japo hukusema uliogopa sana! Kama hukuogopa hiyo nayo ina tafsiri nyingine ama inakamilisha tafsiri hiyo. Kifupi ki Biblia shetani/mapepo hufananishwa na nyoka. Kwa jinsi hiyo mama anaweza kuwa ni mfuga majini ama mruka na ungo… Kwa wewe kupakatia nyoka hio ni dalili ya kurithishwa kazi

 4. Amina. Kwa kawaida inavyosemekana na watahalamu wa ndoto
  1.ukiwa umezoea kuota ndoto nyingi kilasiku alafu ukiamuka asubuhi unakuta umezisahau uwezi kumuhadisia mtu ikatokea siku ukaota ndoto ukahamuka asubuhi unaikumbua vizuri basi hiyo ndoto usiipuuzie inakuwa na maana mungu anakua ameamua kukuo,nyesha kitu.
  2.ukiota ndoto ya aina yeyote ukashituka usingizini ukajikuta moyo unaenda mbio na umejawa na woga ;kemea hapohapo unpo amuka inakua haina maana nzuri.
  Kwahiyo kati ya vitu vilivyo husishwa kwenye ndoto yako ukaunganisha na haya jibu litakuja taratibu.
  Mungu akulinde

 5. Nyoka huashiria, uadui, umbea, mafarakano, uongo au kuzushiwa. Au kutokea mtafaruku fulani, tusikie na wengine

 6. Hiyo ndoto imeniogopesha kidogo..ila nashindwa kupata maana yake.Lakini pia wanasemaga nyoka anaashiria shetani..so moja kwa moja kuna mashambulizi fulani kutoka kwa muovu shetani.Tususbiri wengine watuletee tafsiri ya hii ndoto.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s