Madawa ya Kulevya Tanzania!

Bwana Yesu asifiwe, Imekuwa ikisikika watu kujihusisha na madawa ya kulevya, wengine kufariki wakiwa airport, wengine wamekamatwa Afrika Kusini, Egypt, Hong Kong, China na nchi nyingine, wengine wafungwa au wanasubiri kunyonywa. Pamoja na Serikali kufuatilia suala hili, ningependa kuuliza kanisa, watumishi wa Mungu. Je tunawaza nini kuhusu vijana wetu? bado tuna kazi ya kufanya

Tomas Bagenda

Chini na maelezo ya historia ya mmoja aliyekamatwa China

Advertisements

7 thoughts on “Madawa ya Kulevya Tanzania!

 1. Wapendwa,

  Upo ushauri na maoni na pengine mshangao kwa nini ulevi unapendwa sana siku za hivi karibuni, kuliko wakati mwingine wowote? Takwimu za kidunia zinatisha ukizitazama, na kwa ubaya zaidi ulevi unawaathili sana hasa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya kila Taifa!

  Pengine kabla ya kuziangalia zile juhudi zinazofanywa na Mataifa kukomesha tatizo hili na kuonyesha kushindwa, tutazame kwanza Neno linasemaje juu ya ulevi huu, hasa kwa wakati wetu huu!
  Mtu anapolewa, huwa hajitambui kwa sababu ufahamu hupotoka! Biblia inasema Wanadhiri wa Mungu na Watawala ama wenyekuongoza watu haifai kunywa mvinyo. Sababu yake kubwa ni kuwa Mvinyo hupotoa ufahamu. Lakini mlevi hawezi kupambana na kujilinda, hawezi pia kujitetea na kujieleza kiufasaha, kwa kifupi mlevi ni kama mpumbavu, moyoni mwake hujiona na kujijua yeye ni yeye kwa maana hiyo hakuna mtawala akatawala kwa haki akiwa mlevi, Mkuu wa familia naye ni mtawala katika familia yake pia ni kuhani wa Nyumba yake, huyo naye haruhusiwi kulewa. Vile vile asikari mlevi hawezi kujilinda ama kupambana na adui, lakini pia mtumishi wa kinadhili wa Mungu hawezi kuzungumza na Roho mtakatifu wakati amelewa! Hivyo watu hawa wasilewe mvinyo!

  Biblia inasema, ili ufalme uangamie kwa urahisi “uleweshe!” Kwa nini sasa kuna ulevi wa kupindukia namna hii? Ukiisoma ile Yer. 25:15-16 inasema hivi, “15Maana BWANA, Mungu wa Israeli, aniambia hivi, Pokea kikombe cha divai ya ghadhabu hii mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote, ambao nitakupeleka kwao; 16nao watakunywa, na kulewalewa, na kufanya wazimu, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yao.”

  Mpaka hapo tunajifunza kuwa kama ulevi ukiwa mwingwi pahala popote basi maangamizi yapo mlangoni! Kulewa lewa kwa Dunia kama Isa. 24, inavyosema kunaashiria kuanguka kwa ulimwengu wote mzima kutokana na uovu wake! Kwa hiyo kabla ya kufikilia kuzuia urevi huu, lazima kwanza sisi kama wana wa Mungu tuangalie chanzo. Kuenea kwa shida hii ya ulevi, ni kwa mjibu wa Neno la Mungu, ni vema tukaangalia Neno kwanza ili tuone na kujiridhisha kuwa wanaoathiliwa na jambo hili ni Kanisa la Kristo? Kama si kanisa, basi sisi hatuwezi kuomba ili kuzuia wimbi na tufani hii ya ulevi, kwasababu lipo kwa ajili ya maangamizi ya wasio tii, swala hili limeukumba Dunia yote, na hata wenye nguvu za kiuchumi na hata za kijeshi, kwa pamoja wamejaribu kuzuia wamekwama. Kwanini wamekwama? Mpaka kusudi la Mungu litimie, waangamizwe wote! Utagundua hayo ukiiangalia tena Yer. 25: 17-26 kwani inasema hivi, “17Ndipo nikakipokea kikombe kile mkononi mwa BWANA, nikawanywesha mataifa yote, ambao BWANA alinipeleka kwao; 18yaani, Yerusalemu………. 26…… na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia;…….”

  Kwa maana hiyo swala hili ni la Dunia yote kwa kwa watu wote wakaao juu ya uso wa dunia, hakuna wa kulizuia jambo hili hata mmoja, mpaka yote yatimie! Jambo hili limekusudiwa kuwaangamiza wote WASIOAMINI, halipo kwa ajili ya Kanisa tiifu la Mungu wetu. Kwa maana hiyo hakuna hofu wala mshangao kwetu, lipo, limesemwa na halituhusu! Waliokusudiwa watalewa chakali kiasi cha kutojitambua, ili waangamie. Hayo nayo yameelezwa vizuri katika hiyo Yer.25:27 ona inavyosema, “27Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu.”

  Biblia haijaishia hapo, inasema pia, “wale watakaojifanya kukataa kunywa ‘KILEVI’ kile watalazimishwa kunywa hadi walewe!” Na hata wanajifanya walokole kumbe siyo, wakijikatalisha kunywa kwa hiari yao kinafiki, kwa maelezo kuwa wameokaka na ni watoto wa Nyumba ya Mungu, huku kiukweli hawako ‘Fiti’ wajue hakuna kuongopa, “WaTAKUNYWA KWA LAZIMA ILI WAANGAMIE!” tazama tena Yer. 25:28-29 inasma, . “28Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa. 29Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe?” Kwa hiyo hakuna juhudi yoyote itakayofanikiwa kuzuia ‘ULEVI’ huu mbaya ulioikumba Dunia, hadi kusudi la kuangamizwa kwa waliokusudiwa litimie!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”.

 2. Sungura,

  Ubarikiwe…..! Madawa ya kulevya ni kama uovu mwingine wowote ule, hakuna mikakati ya kibinadamu inayoweza kufanyika kuzuia uovu usitendeke! Si kwamba nasema serikali isifanye chochote. Angalia China na baadhi ya nchi za Asia ambako adhabu ya kifo hutolewa kwa watumiaji na wafanya ya biashara hiyo, mbona licha ya adhabu hiyo bado watu huko huko wanajitosa kuifanya! Ndio maana vijana wetu wametumwa huko!

  Marekani ina kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya chenye nguvu mno na vifaa vya kila namna…..lakini unaona wazi wanapigana vita vya kushindwa.

  Kwa kifupi nguvu na msukumo wa kufanya uovu unaweza kusukumwa na mengi, kwa wengine umaskini (kama) kwetu Tanzania unaweza kufanya mtu akafanya lolote, lakini si umaskini tu, tamaa ya fedha na utajiri wa haraka haraka unaweza kuwasukuma wengine wakafanya hivyo biashara hiyo. Biashara hii yenye pesa nyingi za haraka haraka ni kichecheo cha wenye pesa na wasio na pesa, hivyo hata usema tatizo ni ajira kwa vijana hilo sio suluhisho, He ni ajira gani inayoweza kukupa pesa za haraka haraka!
  Na hata watumiaji wa madawa haya…..si maskini tu ! Mtu yoyote ambaye amepoteza mwelekeo wa maisha naweza kujiingiza katika utumiaji wa madawa haya! Angalia Hollywood kwenye macelebrities wa pesa za kutupwa, angalia baadhi ya yao walivyoathiriwa na madawa haya! Maisha yakiisha poteza mwelekeo tu, na kupoteza maana ya kuishi, haijalishi una pesa au la unaweza kunaswa!

  Kama ulivyosema Sungura, dawa ni Revival- Uamsho au uhai wa Kiroho unaletwa na Injili ya Kristo kwa mtu anayemkubali. Injili ikiweza kuwafikia Vijana wetu au mtu yoyote yule ina uwezo wa kuyapa maisha maana na kubadili mwelekeo wake!
  Maisha haya bila kujua kwa nini nipo dunia, ni rahisi mno kuingia katika mtego wa kudhani maisha ni kuwa na pesa nyingi, vitu vingi, kupata “furaha” nyingi….nk! Hakuna kitu kinachoweza kuvunja kiu na matamanio ya mwanadamu, human soul is yearning for something…..we will be always restless and craving for a thing which we think will give life meaning.

  Maisha yanapata maana tu pale yanaporudishwa kwa muumba wake! Na Injili ya Kristo inafanya hivyo! Inampa uwezo wa kufanyika Kiumbe Kipya!

  Sasa tutafanyaje Kuleta REVIVAL katika jamii yetu! Je tunajua kwamba tuna silaha kali inayoweza kuleta mabadiliko katika jamii yetu! Tufanyaje kuifikia jamii yetu? Hili ndilo swala linatakiwa kutukosesha usingizi sisi tulioguswa na Kristo ……Ubarikiwe ndugu Sungura.

 3. Inawezekana jumuiya ya wauza unga ina nguvu si tu ya kifedha, bali na ya kijeshi kuliko mkuu wa nchi. Huwa najiuliza sana kwa nini hata yeye kashindwa kuwataja hawa magangwe wakati alisema majina yao anayo!!!

  Kama tunataka kukomesha hiyo kitu kwa mlengo wa kanisa, inabidi jambo fulani lifanyike ili ishuke ‘revival’ ambayo huweza hata kuwafanya majambazi waje kanisani kutubu wao wenyewe!

 4. Swala hili sio la kuliacha hivihivi, ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuomba maombi ya Esta, sipati picha nikifikiri wakubwa na watoto wao ndio wafanyabiashara wakubwa, halafu watumiaji ndo watoto wetu, kizazi cha miaka 50 ijayo kitakuwaje? nachelea kufikiria kwamba hapo baadae nchi hii inaweza kufanana na Samaria enzi za mfalme Ahabu. Tuunganishe nguvu tuombe kwa nguvu, hata manabii/wachungaji watatiwa nguvu kusema kitu na viongozi wa nchi, nahisi nguvu yetu bado ni hafifu ndio maana hata mchungaji alipojaribu kuwahubiri mateja akatishiwa ,naye akaacha kwa hofu, tukiwa na maombi ya dhati hakuna kitakachosimama mbele na kushindana na MUNGU.Hatuna haja ya kujua majina yote ROHO MTAKATIFU anawajua na atatufunulia.

 5. Huyu muuza unga kama anajuta kweli angetoa list yote ya wahusika, kwa nini ametaja majina machache eti mengine ya wakubwa. Rabbish!!! hao ndio wamemfikisha hapo wenyewe wanatanua huku. Taja wote usiogope la sivyo tunakuona mnafiki wewe.

 6. Vita hii akisimama mtu mmoja ni lazima atapigwa vita lakini tukisimama kwa umoja wetu, watanzania wanaoitakia mema nchi tunaweza kufanikiwa.

  Lakini jambo la kushangaza ni kuwa nchi ina Rais ambaye ndiye mwenye kauli ya MWISHO KATIKA NCHI. Sasa inapotokea rais hana mamlaka ya kufanya chochote hapo inakuwa ni hatari.
  Lakini naamini watu wema wote tukiunganisha nguvu VITA HII TUNAWEZA KUISHINDA.

 7. Kwa namna hii kutokomeza madawa ya kulevya ni kazi ngumu, labda Mungu aingilie kati mwenyewe. Hebu fikiri jinsi mtandao ulivyo mpana na unahusisha watu wa aina mbalimbali yaani watu wa serikalini na wafanya biashara. Na mtu ukuamua kufuatilia kwa kupambana nao ujue maisha yako yapo hatarini. Wapo wengi wameshapoteza maisha kwa kujaribu kuwafuatilia hawa watu na mfano mzuri ni Amina Chifupa. Nilishakutana na mchungaji mmoja ambaye alinipa story jinsi alivyoandamwa na watu asiowajua kutokana na maono yake ya kuwahubiri injili mateja ili wamjue Yesu. Alipata vitisho vingi na kupewa onyo kali na kuambia iwapo ataendelea kuwafuatilia basi uhai wake upo mashakani. Kwakweli tunamhitaji sana Mungu katika eneo hili kwa maana huu mtandao ni mpana sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s