Kampeni Ya Mahusiano ya ndoa za jinsia Moja, Nani analengwa?

ushoga

Hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu la kampeni ya kutetea haki za mapenzi na ndoa za watu wa jinsia moja. Sababu zinatolewa ambazo ni udanganyifu wa ibilisi ambao kwa watu wasiomjua Mungu wanaona ni sahihi, kwa mfano eti mwanaume kuwa na homoni za kike. Niwaulize je Mungu anayeponya viwete ashindwa kuweka homoni za kiume? Kama si mpango mkakati wa shetani kutumia wasomi ni nini? Wengine wanasema wanatetea haki zao ili kuwapa elimu ya kujikinga na UKIMWI, niwaulize kwani hao hawajui njia za kujikinga na UKIMWI mpaka waruhusiwe mapenzi ya jinsia moja ndio wataelewa wanapofundishwa? Wengine wanadai walizoeshwa tangu wakiwa wadogo, kwani ni mambo mangapi tulizoeshwa utotoni lakini ukubwani tukasaidiwa au kukemewa na tukayaacha? Hivi ulimwengu unakumbuka dhambi zilizomuudhi Mungu na kuangamiza Sodoma na Gomora? Leo nataka niwaonyeshe kwa uwazi ni nani analengwa na janga hili, lakini kwanza tutambue kuwa kuna watu maarufu na program maarufu duniani kote ili wafanyike wasemaji wa kampeni hii ya uharibifu na kumchukiza Mungu.

Michael Jackson; huyu msanii Alikuwa maarufu duniani kote na alijibadilisha sura ili aonekane kama mwanamke. Katika jicho la rohoni huyu alikuwa anamaanisha mwanaume anaweza kuchukua nafasi ya mwanamke kwa hiyo naweza sema maana yake hata mwanaume anaweza kufanya mapenzi kama mwanamke bila kujali uwepo au kutokuwepo kwa viungo vya mwanamke. Kufanya kwake hivi kulichukuliwa kitu kigeni lakini baadaye watu wakamzoea na kumpenda.

Elton John; huyu pia ni mwanamuziki wa ulaya ambaye ameshatoa kauli nyingi chafu kwa wokovu. Alijitangaza wazi kuwa ni “shoga”. Kumbuka anafahamika na muziki wake kupendwa dunia nzima, muda mwingine huwa nashangaa kwa nini vijana wanapenda nyimbo za kidunia wakati hazimtukuzi Mungu?

Mike Tyson; huyu bondia maarufu duniani kote, bila shaka ulisikia fununu au uzushi kwamba alibadilisha sehemu zake za siri na kuweka nyeti za kike. Inawezekana hakufanya hayo lakini lengo la uzushi huo ni kuwakumbusha walimwengu kwamba hata mwanaume ana haki ya kuishi na kufanya mambo ya mwanamke. Kwa nini uzushi huo asitungiwe bondia wa Tanzania?hii ni kwa sababu kampeni hii ni yua dunia nzima.

Bunge la ufaransa limepitisha sheria kuruhusu uchafu huu. Nani asiyejua nguvu ya ufaransa kwa mataifa ya ulaya na mataifa yanayoendelea? Kwa hiyo ni wazi kwamba serikali nyingi zitalazimika taratibu kukubaliana na utaratibu huu.

Serikali ya uingereza na Marekani pia tumesikia wakitetea hata kwa sheria kutoka mahakama za juu kabisa. Kama wakubwa wa dunia wanafanya hayo je kuna pande ya dunia haijafikiwa na kampeni hii? Mashirika yao ambayo ndio yanaleta msaada Africa unafikiri hayataleta masharti magumu ya sisi kuona “ushoga” kama haki ya msingi ya raia?

Movie/maigizo  ya Hollywood za Marekani zimekuwa zinawafuasi wengi sana. Movie hizo nikiziangalia zina matukio mengi ya wanawake wakifanya usagaji au ishara za kuwa wapenzi wa jinsia moja, na kwa wanaume pia mambo hayohayo ya ushoga, lengo ni kuwafanya vijana waone jambo hilo kama jambo la kawaida tu. Katika tafiti zangu juu ya roho huyu wa uzinzi niligundua kuwa hata kufanya mapenzi kinyume na maumbile (anal sex), vijana wengi wamejifunza kupitia movie hizi za ulaya na majarida ya ajabu ajabu yaliyozagaa sana mitaani. Athari zake ni kubwa na mbaya sana. kwa wafugaji wanaweza kukubaliana nami kuwa hii ni tabia ya wanyama tena hata wanyama hufanya kwa bahati mbaya tu.

Hivi karibuni tumesikia Askofu mkubwa Afrika akitetea jambo hilo kwa njia ya kusema eti anataka wapate nafasi ya kuelimishwa juu yaa kujikinga na UKIMWI. Hata kama angekuwa ni malaika wa mbinguni, alaaniwe Yule atakaye hubiri injili tofauti na ile itakayowaonya watu kuacha dhambi na kumrudia Mungu muumba wa vyote. Nathubutu kusema si huyo tu, viongozi wengi wa dini wamesema na wengine maarufu wataungana naye kwa sababu roho wa uongo anafanya kazi ndani yao, sibabaishwi na idadi ya wafuasi wake na ukongwe wake katika ukristo kiasi cha kukubali hoja zake zinazopeleka watu katika ziwa la moto.

Mifano ni mingi sana lakini nataka turudi kwa swali la nani analengwa? Kizazi kijacho ndicho kinacholengwa na uharibifu huu. Kasi ya kampeni ni kubwa, wanaounga mkono wengi wao si watendaji lakini watoto wanaozaliwa sasa watakua wakisikia kampeni inapewa msisitizo na wataona ni jambo la kawaida tu. Hebu fikiria mtoto amelelewa na baba na mama ambao wote ni “wanaume” je hata anzisha tabia hiyo kwa watoto wazuri waliolelewa na baba na mama ambao ni mwanamke na mwanaume? Hili jambo lazima tuliangalia kwa kujali kizazi kijacho na si tu kupigia debe kwa sababu tunajua sisi hatuwezi kuwa wasagaji au mashoga. Muda mwingine najiuliza vijana wa sasa hivi je tuwapo na watoto tunaendeleza utamaduni wa kuwasisitiza watoto kwenda kanisani japo kujifunza hata kipaimara? Tutatoa wapi ujasiri huo wakati kwetu jumapili ni siku za starehe? Watoto hawa tutawalea vipi wakaepuka roho hizi za uasherati wa jinsia moja? Je habari za wokovu watazisikia lini na kuziamini? Kizazi kijacho ndicho kinacholengwa, tusipotubu na kukemea uovu huu tutaipeleka dunia pabaya. Jambo kama ni baya litabaki kuwa baya tu, hata kama watu wazuri, maarufu, matajiri, wasomi, wanasiasa na viongozi wa dini watasema ni jambo zuri. Ni lazima kuomba ili Tanzania, Afrika na Dunia nzima ikamcha Mungu.

Na Mussa Kisoma.

Advertisements

6 thoughts on “Kampeni Ya Mahusiano ya ndoa za jinsia Moja, Nani analengwa?

 1. WALENGWA NI WASIOISIMIKA MIGUU YAO KATIKA MWAMBA/KRISTO /NENO AMBAYE NI CHANZO CHA HEKIMA NA KUFUATA HEKIMA ZAO. WARUMI 1:22

  “HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, HATA WANAWAKE WAKABADILI MATUMIZI YA ASILI KWA MATUMIZI YASIYO YA ASILI. WANAUME NAO VIVYO HIVYO WALIYAACHA MATUMIZI YA MKE, YA SILI, WAKAWAKIANA TAMAA, WANAUME WAKIYATENDA YASIYOPASA, WAKAPA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU WAO YALIYO HAKI”

  WARUMI 1:26,27

  WATU HAWA HULETA MIJADALA JUU YA KUKUBALI AU KUTOKUBALI MASHOGA KATIKA MAKANISA
  (EPUKA KUJADILI MAMBO AMBAYO MISINGI YAKE IMEKWISHAWEKWA-HUBIRI JUU YAKE TUU) HUWAANDAA WATU KATIKA MAKANISA NA PALE MNAPOFIKIA KUPIGA KURA UNAWEZA UKASHANGAA UMESHINDWA KUMBE MAMMLUKI WENZAKO WAMEPIGA KUKUBALI NDILO TATIZO LA MAKANISA YA MAREKANI NA SEHEMU NYINGINE HALAFU WATAKWAMBIA MIMI NIMEPIGA KURA YA HAPANA.

  (USIKUBALI KUPIGA KURA JUU YA NENO LA BIBLIA NI KUTAKA HEKIMA YA KIBINADAMU ISHINDE).

  NDIO MAANA HATA KATIKA MIJADALA YETU UTAKUTA KUNA WATU AMBAO WANAJUA NENO
  LASEMA HIVYO LAKINI HUBISHA KWA KUJAZA KURASA KWA BUSARA ZAO/KWA HATA MANENO YALIYO WAZI KATIKA BIBLIA.

  SIMAMA NA YESU TU JUU YA JAMBO LA UZIMA.

  SOMA HABARI YA CHRISTIAN DEMOCRACY KUTOKA KWA RIVERA (JESUIT)

 2. Hizi ni nyakati za Mwisho kabisa!,Joka linakamata juu na kutia nguvu wakubwa wa dunia,halafu linashuka na kuwameza wote wakubwa kwa wadogo ambao hawadumu katika njia za Mungu na kushika imani ya Yesu kristo.Ni vizuri kila mmoja wetu akae ndani ya neno la Mungu, kwa kuwa hii ndio silaha pekee ya kutuwezesha kujua na kupinga hila na udanganyifu wa shetani.

 3. SHIKA NENO WANA WA MUNGU MLIOPEWA NEEMA KUBWA! NINASEMA KWA UJASIRI KABISA NA KWA UHAKIKA KWAMBA UCHAFU HUO WA USHOGA / USAGAJI HAUWEZI UKAINGIA NDANI YA TAIFA HILI LA GOSHENI (TANZANIA) MAHALI AMBAPO MUNGU AMETUINULIA NABII WA KWELI AMBAYE NI MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU! NI LAZIMA MUNGU WA KWELI AJULIKANE SASAHIVI NDANI YA TAIFA HILI NA UCHAFU HUU UMESHAFUTWA KWA DAMU YA HAKI, KWELI NA HUKUMU KATIKA JINA LA YESU AMBALO LIMEFUNULIWA KWA UPYA SASAHIVI. NA WOTE AMBAO WANAPIGA KAMPENI HIYO CHAFU HUKUMU YA MUNGU WA ELIYA KIZAZI CHA NNE IPO JUU YAO NA ITAWAANGAMIZA WOTE LA SIVYO LAZIMA WATUBU NA KUMFUATA MUNGU WA ELIYA ILI WAWE SALAMA KATIKA JINA LA YESU

 4. hakika haifai wala haitakiwi kusikika eti mwanaume na mwanaume mwanamke na mwanamke nasema uchafu ni kama mavi mtume paulo anayahesa yale mabaya ni kama mavi. acheni uchafu tubuni na kuokoka kwa jina la Yesu mpone jehanamu ya moto mspo tubu hzo dhambi ushoga usagaji uzinzi na dhambi nyingine hakuna haki kwa mabaya baadaye mtasema ni haki ya mtu kuua duuuu! hi ni sodoma na gomora waliangamizwa wasi nanyi mfanyao mambo ya jins tubuni s kwamba twafurahia kuangamia kwenu hapana twataka mpone na hukumu ya milele twawapenda ila twaomba ila twataka muacha hayo mabaya hakuna mbigu ya waovu jamani badilike enyi WAINJIRISTI WAALIMU MANABII WACHUNGAJI MITUME tulitangaze neno kwa usahihi si kwa mapato ya aibu itakuwa na faida gani ukawa na kanisa kubwa la watu 1000 ila watenda dhambi hiyo inatisha je wewe wadhani ile hukumu utaikosa kwa kujifariji na wingi wa watu wakati wapo njia ya upotofu hapana watumishi tueleze iukweli watu wapate kuoka na kuiona mbingu tukifanya hivyo una thawabu kubwa sana NAUMIA NINAPO ONA WATU WANAMKATAA KRISTO NA KUZIFUATA TAMAA ZA KIDUNIA TAMBUA DUNIA INAPITA ILA NENO LA MUNGU LADUMU HATA MILELE YEYE C KIGEUGE

  @EV& teacher PAULO B mw

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s