Sifa na kuabudu

praise1

Yule mwanamke akamwambia [Yesu], ‘Bwana, naona ya kuwa u nabii. Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.’ Yesu akamwambia, ‘Mama, unisadiki. Saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu wala kule Yerusalemu. … Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana, Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli’ (Yohana 4:19-24).

Maneno hayo kutoka kinywa cha Yesu yanaweka msingi wa sisi kuelewa juu ya mambo muhimu sana katika kuabudu. Yeye alizungumzia juu ya “waabuduo halisi” na kueleza sifa zao. Hii huonyeha kwamba wapo watu wanaoabudu, lakini si waabuduji wa kweli. Wanaweza kudhani kwamba wanamwabudu Mungu lakini ukweli si hivyo maana hawatimizi masharti Yake.

Yesu alitangaza alama za waabuduji wa kweli – wao huabudu “katika roho na kweli.” Basi, kinyume chake ni kwamba, waabuduji wasio wa kweli ni wale wenye kuabudu “katika mwili na uongo. Kimwili, waabuduji wasio wa kweli wanawea kufanya matendo yote ya kuabudu, lakini ni maonyesho tu maana hayatoki katika moyo unaompenda Mungu.

Ibada ya kweli kwa Mungu inatoka katika moyo unaompenda Mungu tu. Basi, kuabudu si kitu tunachofanya wakati tunapokutanika kanisani, bali ni kitu tunachofanya kila dakika ya maisha yetu, tunapotii amri za Kristo. Inashangaza kwamba yule mwanamke aliyekuwa anazungumza na Yesu alikuwa ameolewa mara tano, na wakati huo alikuwa anaishi na mwanamume, na bado alitaka kuhojiana na Yesu kuhusu mahali panapofaa kumwabudu Mungu! Yeye ni mfano wa watu wengi sana wenye dini, wanaohudhuria ibada huku wakiishi maisha yao kila siku katika kumwasi Mungu. Hao si waabuduji wa kweli.

Wakati fulani Yesu aliwakemea Mafarisayo na waandishi kwa sababu ya ibada yao ya uongo, isiyotoka moyoni.

Enyi wanafiki! Ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu’ (Mathayo 15:7-9. Maneno mepesi kukazia).

Ingawa Wayahudi na Wasamaria katika siku za Yesu walitilia mkazo sana kuhusu mahali pa watu kuabudia, Yesu alisema kwamba mahali hapakuwa na maana sana. Cha muhimu ni hali ya moyo wa kila mtu, na jinsi anavyomheshimu Mungu. Hayo ndiyo yanaamua jinsi ibada yake ilivyo.

“Ibada” nyingi katika makanisa siku hizi ni taratibu tu zilizokufa, zinazotendwa na waabuduji waliokufa pia. Watu wanarudia maneno ya mtu mwingine kuhusu Mungu, bila hata kuyafikiri, wanapoimba “nyimbo za kuabudu.” Kuabudu kwao ni bure, maana maisha yao yanaonyesha kilicho halisi katika mioyo yao.

Mungu angetamani hata kuambiwa “Nakupenda” rahisi tu itokayo moyoni kutoka kwa mtoto wake mmoja mtiifu, kuliko kuvumilia kelele zisizotoka moyoni za maelfu ya Wakristo wa Jumapili asubuhi, wakiimba “Jinsi Wewe Ulivyo Mkuu.”

Kuabudu Katika Roho

Kuna wanaosema kwamba kuabudu “katika Roho” ni kuomba na kuimba kwa lugha zingine. Hiyo ni tafsiri ngumu kukubali, ukitazama maneno ya Yesu. Yeye alsiema kwamba “saa inakuja, na sasa ipo, ambayo waabuduji wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli,” kuonyesha kwamba tayari walikuwepo watu waliotimiza masharti ya kuabudu “katika Roho” alipotoa tamko hilo. Ni kweli kwamba hakuna yeyote aliyenena kwa lugha mpaka Siku ya Pentekoste. Basi, aaminiye yeyote, awe ananena kwa lugha au hapana, anaweza kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Kuomba na kuimba kwa lugha zingine hakika huwa ni msaada kwa mwabuduji katika kuabudu kwake, lakini hata kunena kwa lugha kunaweza kuwa utaratibu usiotoka moyoni.

Picha ya kusisimua kuhusu ibada ya kanisa la kwanza inapatikmana katika Matendo 13:1, 2.

Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanya Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, ‘Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia’ (Maneno mepesi kukazia).

Ona fungu hili linavyosema: “walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada.” Basi tunajifunza hapo kwamba ibada ya kweli humhudumia Bwana. Ila, ni hivyo wakati Bwana anapokuwa ndiyo lengo la upendo wetu.

Njia Za Kuabudu

Kitabu cha Zaburi ambacho tunaweza kusema ni kitabu cha nyimbo cha Israeli, kinatushauri kumwabudu Mungu katika njia nyingi tofauti tofauti. Kwa mfano: Katika Zaburi ya 32 tunasoma hivi:

Pigeni vigelegele vya furaha; ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo (Zaburi 32:11b. Maneno mepesikukazia).

Japo kuabudu kimya, kwa utaratibu na heshima kuna nafasi yake, pia kuna nafasi ya kupiga kelele za shangwe.

Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni BWANA kwa kinubi, kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe (Zaburi 33:1-3. Maneno mepesi kukazia).

Tunapaswa kumwimbia Bwana katika kuabudu, lakini kuimba kwetu kuwa kwa furaha, ambalo ni onyesho lingine la nje kuhusu undani wa moyo wa mtu. Pia tunaweza kuimba kwa furaha tukitumia vyombo mbalimbali vya muziki. Ila, katika mikutano mingi ya kanisa, vyombo vya muziki vinakuwa na sauti ya juu kiasi cha kwamba vinafunika kabisa sauti ya uumbaji. Ni vizuri vipunguzwe sauti au vizimwe. Ukisoma zaburi, tatizo hilo halikuwepo!

Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai. Kwa jina Lako nitaiinua mikono yangu (Zaburi 63:4. Maneno mepesi kukazia).

Tunaweza kuinua mikono yetu juu kwa Mungu kama ishara ya kujitolea Kwake na kumheshimu.

Mpigie Mungu kelele za shangwe nchi yote; imbeni utukufu wa jina lake; tukuzeni sifa zake.Mwambieni Mungu, ‘Matendo Yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako. Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, naam, italiimbia jina lako’ (Zaburi 66:1-4. Maneno mepesi kukazia).

Tunatakiwa kumwambia Bwana jinsi alivyo mkuu na kumsifu kwa jinsi alivyo wa ajabu. Zaburi ni mahali pazuri sana pa kupa ta maneno yafaayo ya kumsifu Mungu. Tunahitaji kwenda zaidi ya kurudia rudia maneno haya: “Nakusifu, Bwana!” Kuna mengi sana ya kumwambia.

Njooni tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba (Zaburi 95:6).

Hata jinsi tulivyo ni onyesho la ibada: iwe ni kusimama, kupiga magoti au kusujudu.

Watauwa na waushangilie utukufu, waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao (Zaburi 149:5. Maneno mepesi kukazia).

Si lazima tuwe tumesimama au kupiga magoti ili kuabudu – tunaweza hata kuwa tumelala kitandani.

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni, lihimidini jina lake (Zaburi 100:4. Maneno mepesi kukazia).

Hakika, kushukuru kuwe sehemu ya kuabudu kwetu.

Na walisifu jina lake kwa kucheza (Zaburi 149:3. Maneno mepesi kukazia).

Tunaweza hata kumsifu Bwana kwa kucheza. Lakini kucheza kwenyewe kusiwe kwa kimwili, kwenye kuamsha ashiki, au kwa ajili ya kustarehesha watu.

Msifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi. Msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi. Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya (Zaburi 150:3-6).

Mungu ashukuriwe kwa walio na vipawa vya muziki. Vipawa vyao vinaweza kutumika kumtukuza Mungu kama watavipiga kwa moyo wa upendo.

Nyimbo Za Kiroho

Mwimbieni BWANA wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu (Zaburi 98:1a. Maneno mepesi kukazia).

Hakuna kosa lolote kuimba wimbo wa zamani, mpaka inapokuwa mazoea. Hapo ndipo tunahitaji wimbo mpya utokao mioyoni mwetu. Katika Agano Jipya, tunajifunza kwamba Roho Mtakatifu atatusaidia kutunga nyimbo mpya. Tunaambiwa hivi:

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu (Wakolosai 3:16).

Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo (Waefeso 5:18-20).

Paulo aliandika kwamba tunapaswa kuwa tunaimbiana “zaburi, na tenzi na nyimbo za rohoni”. Basi, hizo tatu zina tofauti. Uchunguzi wa lugha ya Kiyunani hautoi msaada wowote, ila pengine “zaburi” maana yake ni kuimba zaburi kama zilivyo katika Biblia, pamoja na vyombo. Pengine “tenzi” ni nyimbo mbalimbali za shukrani zilizokuwa zimetungwa na waamini katika makanisa. “Nyimbo za rohoni” labda zilikuwa nyimbo za papo kwa papo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ambazo ni sawa na ile karama ya unabii, ila, zenyewe ziliimbwa.

Kusifu na kuabudu vinapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku – si kitu fulani tunachofanya wakati wa kukutanika kanisani. Mchana kutwa tunaweza kumhudumia Bwana na kufanikiwa kujisikia ushirika wa karibu na Yeye.

Sifa Ni Imani Ikitenda Kazi

Kusifu na kuabudu ni madhihirisho ya kawaida kabisa ya imani yetu kwa Mungu. Kama kweli tunaamini ahadi za Neno la Mungu, basi tutakuwa watu wenye furaha, waliojaa sifa kwa Mungu. Yoshua na Waisraeli walitakiwa kupiga kelele kwanza, ndipo kuta zikaanguka. Biblia inatushauri hivi: “Furahini katika Bwana sikuzote” (Wafilipi 4:4), na “Shukuruni kwa kila jambo” (1Wathes. 5:18a).

Mfano mmoja wa hali ya juu sana kuhusu nguvu za sifa unapatikana katika 2Nyakati sura ya 20, wakati taifa la Yuda lilipovamiwa na majeshi ya Moabu na Amoni. Akijibu maombi ya Mfalme Yehoshafati, Mungu aliwaagiza Israeli hivi:

Msiogope wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili kwani vita si yenu bali ni ya Mungu. Kesho shukeni juu yao … Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu (2Nyakati 20:15b – 17).

Kisa kinaendelea, hivi:

Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama akasema, ‘Nisikieni enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.’ Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, BWANA akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka. Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana (2Nyakati 20:20-25. Manenomepesi kukazia).

Sifa iliyojaa imani huleta kulindwa na husababisha utoaji wa Mungu!

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hiyo ya nguvu za sifa, ona Wafilipi 4:6-7 (sifa huleta amani), 2Nyakati 5:1-14 (sifa huleta uwepo wa Mungu), Matendo 13:1, 2 (sifa hudhihirisha makusudi na mipango ya Mungu), na Matendo 16:22-26 (sifa huleta kuhifadhiwa na Mungu, na kufunguliwa kutoka gerezani).

––David Servant

Advertisements

21 thoughts on “Sifa na kuabudu

 1. Sungura,

  Nilichangia kweli mara ya kwanza( rejea juu) na kisha nikachangia tena kujibu maswali yako maana ulitualika wadau au guys( nami nimo ktk hao guys) na sasa tunawekana/kuweka sawa, YOTE NI MICHANGO iyo, haitoshi? hujaelwa wapi, usitie shaka, uliza tu na wadau au guys tupo na pia ROHO MTAKATIFU yuko tele kututumia.Kweli mimi si Roho Mtakatifu lakinI kwamba ninaye na ananitumia , kabisa, kabisa ni kweli tupu na asante kwake.

  Ukiwa naye na una uhakika naye na kile alichokupa, unasema tu mara moja kwa kijiamini kabisa moja kwa moja bila kumungunya maneno kama wapendwa hawa walio jaaa Roho bila shaka na maisha ya kuabudu Mungu

  Mdo.2:14… = ‘’……Enyi watu wa Uyahudi na ninyi nyote mkaao Yerusalem, lijueni jambo hili, ‘’MKASIKILIZE MANENO YANGU’’ ( Notice: Mkasikilize maneno yangu! )

  Mdo. 2: 22 =… Enye Waume wa Israeli, SIKILIZENI MANENO HAYA….( Notice: ‘’Sikilizeni maneno haya’’ = ‘’maneno haya NAYASEMA, myasikilze’’)

  Mdo. 3:3-8=…Tutazame SISI…. NILICHO NACHO NAKUPA,……( notice: ‘’Sisi’’ ! Wangeweza sema Mtazame ‘’BWANA’’-to make it sound Kiroho na kujishusha ile tunavyodhaniaga mambo mengi na pia ‘’nilichonacho nakupa’’ = ‘’ninacho kitu’’ so chukua/pokea/chukua nakupa!

  Therefore, Seleli kusema.. ‘’Nisikilize/nifuatilie kwa makini hapa’’’ kwa nia tu njema kama ya rafiki zangu hapo juu yaani kuvutia usikivu/kuangalishia hoja na kufikirisha kwa undani na muhimu zaidi, kusababisha utulivu wa moyo na akili ili Roho Mtakatifu akuachilizie mambo kadhaa usomapo, haikua shida, ni Biblical na yapendaza sana.

  Press on kumsikiliza na ROHO anapohudumu humu na kuwasikiliza WAPENDWA hapa-Seleli nikiwemo sana kabisa bila woga, pale tunaposema na kushare ya JUU kwa Baba na hata wewe unasiklizwa unaposema ya JUU pia, usione wivu bali bariki na kufurahia unapopa mkate.Amen.

 2. Seleli hutakiwi kutuamuru tukusikilize, wewe si Roho Mtakatifu. Wewe changia mada, kuisoma au kutoisoma hoja yako hiyo ni hiari yetu!

  Acha utemi.

 3. Sungura,

  Ulisema tuache petty issues, sasa unarudi uko! basi karibu. Sidhani kama unajua itifaki na unyenyekevu wewe, una ujasiri kweli wa kunisahihisha mie? Hata ivyo wakati mwingi mtu uhudumiwa/pokelea kwa jinsi alivyokuja. Paul aliwahi dokeza iyo kua kwa walio hivi, aliJIFANYA vile ili kumechi/kupenyeza yake. Jinsi ulivyompokea mtoa mada mara ya kwanza-kutoana mema yake kwanza na kuyakubali-kubarikiwa, inatosha kuonyesha wewe mnyenyekevu na unaweza penda/taka jifunza toka kwa mwingine au la!

  Kama sikujadili kitu kikubwa sana-kitu ambacho si kweli(dalili nyingine ya kutonyenyekea iyo) basi hata hicho kidogo kinafaaa na umebarikiwa/umepata mwanga tu najua. Kwa upande mwingine yale yote uliyojadili pia mpaka sasa, ukubwa wake sijui uko wapi na sijui ilikuaje wewe tu ulishindwa kumuelewa David na somo lake zuri kama si tatizo binafsi!

  Kama nimeonyesha /changia tena kwa maandiko ambayo nadhani hata wewe hukuwahi kuyawazia kwamba toka humo, kunaweza patika dhahabu, yanayoonyesha namna( matendo, maneno, vitu,) walivyofanya watu na wanavyoweza fanya leo ili kwao ifahamike/au tujue wanaabudu Bwana badoukajiuliza swali hili kua kama nimejadili mada au la? Unahitaji kukubali tu unapobarikiwa kuliko kuwa tabia ya kudhani pia kua ni mpaka useme wewe na tena usema kila saa kwa kila kitu ndio kuwe kweli kumesemwa mambo, kumbe si lazima, wanaweza sema wengine yakawa bora na yenye kilo zaidi na actually ya kiNeno/Kiufunuo zaidi kuliko yako

  Press on.

 4. Seleli unatuamuru tukusikilize na tukufuatilie au umekosea kwa kusahau kuwa unatakiwa kutuomba tufanye hivyo?

  Au ndio huko kukosa unyenyekevu na kudhani kuwa wewe unaweza kuwa mwalimu wa kila mtu?

  Ni vema ukajua itifki za mambo kama haya ndugu yangu, hutakiwi kuamuru unatakiwa kuomba!

  Baada ya kuniamuru nikufuatilie kwa makini, nimefanya hivyo nikidhani kuwa umejadili kitu kikubwa sana.

  Lakini nimeishia kujiuliza tu swali kwamba; Kwa hiyo hapo ndio ulikuwa unajadili dhana ya Sifa na Kuabudu kama mada inavyosema?

 5. Sungura,

  You asked can I now go back to square one please! Yes I can as follows: Nisikilize/nifuatilie kwa makini hapa! Na Wasomaji wengine humu.

  Naanza ivi, Neno la Mungu hukata/uamua mashauri/hutoa muongozo na kuonyesha njia/utoa akili na ufahamu wa mambo ikiwa likitumiwa/nukuliwa sawa sawa/gawiwa kwa usahihi/kihalali-2Timo.2:15c

  Kuhusu maisha ya kuabudu-Watu wengi ni rahisi kukumbuka na kutumia kila mara au siku zote story ya ukweli maarufu ya yule mama na Yesu Kisimani-Yohana.4:1-29 lakini Bible ni mgodi mtamu wenye dhahabu nyingi hazina kipimo hasa ukisoma chini ya uwepo/influence ya Roho Mtakatifu-utaONA/NG’AMUA/NURURISHWA/TAZAMISHWA/TAFAKARISHWA/DONDOSHEWA KTK MOYO NA HATA AKILI mambo ktk/toka Bible matamu na ya ajabu kweli ambayo mwingine anaweza asiyapate/ona tena ktk mistari, sura za story/mambo ya kawaida au yasiyo maarufu sana humo Bibliani

  Luka.2:36-38= Nabii Bibi Kizee wa miaka kama 84 HAKUONDOKA HEKALUNI,ALIKUA ANAMTUMIKIA/MHUDUMIA MUNGU KWA KUFUNGA NA MAOMBI USIKU NA MCHANA( notice: Maisha ya kumshia/kujitoa kila kitu kwa Mungu na mambo yake/hekaluni mwake- ni sehemu kubwa ya ku-define Kumwabudu Mungu)

  Embu tuchungulie na hili ktk influence ya RM=1Wakorinto.14: 23-26

  Mstari 25= siri za moyo wake huwa wazi ivyo ATAMWABUDU MUNGU AKIANGUKA KIFUDIFUDI NA KUKIRI KUA MUNGU YU KATI YENU BILA SHAKA( notice: hapa Paul mwenyewe ana-describe/point out Kuabudu kama tendo moja fulani Mtu AKIWA ndani ya Ibada- namely-ATAMWABUDU AKIANGUKA KIFUDIFUDI=kwa iyo ni sahihi kabisa, kabisa tukimuona Mtu anafanya tendo hilo kanisani-hata kabla ya kujua masaa mengine yote alifanya ivyo au la kwa maana ya Kuabudu ile kubwa-the totality of everything we do and say kwa Bwana, tukasema ANAMWABUDU MUNGU au AMETOKA KUABUDU, right? great.

  Mstari 26= Tunapokutanika mmoja ana Zaburi, mwingine fundisho, ufunuo, lugha, tafsiri( notice: TUNAPOKUTANIKA-kuabudu pia kunahusiana na kukutana/kua pamoja kwa ajili ya Mungu na ibada, Pia kuyafanya yote haya-kushare fundisho,ufunuo,kunena na kutafsiri na kuimba/sema Zaburi- ni part ya ibada/wakutanikapo hence ni sehemu ya kudefine pia nini maana ya muabuduji Mungu na hua anafanyaga nini.

  Conclusively then…Kuabudu kuna measure mambo na matendo ya kila siku kwa BWANA na pia BAADHI ya mambo na matendo-si lazima kila siku but yale YA/UKIWA SEHEMU FULANI NA-kanisani/nyumbani mmekutanika familia za wakristo-cell groups, mtu mmoja-mmoja

  Press on

 6. Ibada ya sifa katika makusanyiko mengi imekosa matokeo makubwa kwa sababu ipo tu ili kuandaa mazingira ya mhubiri kuja kutoa ujumbe. Kwa hiyo waimbaji hutangulizwa tu mbele ili kuwapunguzia watu mawzo na kuwaandaa wakae sawa kwa ajil ya mhubiri kuja.

  Halafu kudhani kwamba nyimbo za harakaharaka ni nyimbo za kuchangamsha ibada na ndio nyimbo za sifa, halafu nyimbo za polepole ndio nyimbo za kumfanya Mungu/nguvu za Mungu zitembee, nalo ni kosa kubwa sana.

  Mara nyingi ni watu wachache sana huandaa mioyo yao kuguswa na Mungu wakati wa nyimbo za harakaharaka hata kama zimbeba ujumbe mzito. Lakini wengi hukaaa mkao wa kukutana na Mungu wakati wa nyimbo za polepole ambazo ndo ati huitwa nyimbo za kuabudu. Lakini nimemwona Mungu akifanya maajabu wakati wa nyimbo za harakaharaka.

  Kitu kingine, watu huimba nyimbo bila kujali zina ujumbe gani lakini almradi ni wimbo wenye melidia nzuri. Ndio maana kuliwahi kuwa na nyimbo za kusifu kama ”vijana wengi wamemuasi Bwana, Shetani ninyan’ganye vyote niachie Yesu, n.k” na watu huimba wakidhani just wanamwimbia Mungu.

  Halafu kosa jingine ni wachungaji kudhani kuwa uwepo wa Mungu unapojidhihirisha katika kipindi cha sifa huwa ni nafasi ya wao kupanda mimbarini.

  Mara nyingi utaona wimbo unaendelea na wau wamezama ile mbaya, ghafla unasikia mchungaji kesha ingilia wakati muda wake wa kusimama ulikuwa bado.

  Ni vema watu wakajua kuwa uwepo wa Mungu unapojidhihirisha wakati wa uimbaji ni saa ya Mungu kufanya vitu vyake kupitia wimbo. Mchungaji asubiri kipindi chake maana na chenyewe kinapaswa kuwa na upako wake. Vinginevyo kama ni lazima kufanya hivyo.

  Tunaendelea!

 7. Sungura

  Surely, you said it perfect that the motion on discussion is not Sungura and Seleli, however, these two creatures and others, can help one another by in-putting more on what the other tabled, correcting and criticizing for good and also totally dismissing the other ones point by even stronger ones.

  This advice is tangible, hence it is swallowed in-‘Contribute what you know and believe in on the subject, as I will do the same.

  This is partly true..’’Some issues are too pet to waste time pondering on, while leaving the mega ones hanging’’….In the first place, you are the one who created petty things you know, how could you have missed a very visible an OSTRICH, so clearly presented by David and bulleted in a local CHICKEN!!!!! Not only that but also in your followed lengthy comments, saying almost THE SAME THING DAVID SAID-refer the the summary I did for u!

  Is it true that, After all, the quest was not for me, but I just zoomed in into it? YOUR MEMORY INDEED DOES NOT DO YOU A FAVOR! I thought you asked this SECOND question in Kiswahili under this post namely… ‘’Jamani WADAU, nimeuliza swali kuwa tunaongelea kuabudu na kusifu kupi, kule kwa kuimba au dhana nzima ya kuabudu?-Come on GUYS!! I am sure that am among the so called ‘WADAU’ and ‘GUYS’, right? and when David did not show up for your first question addressed specifically for him, his silence triggered you to ask the second one I have quoted here in Kiswahili-which this time was not for David only, I concluded that it is fair Sungura to get answers for we don’t know when Davd will come in from his temporary rapture dwellings!!!!!! I deserve blessings from you than blames since I did only respond to your call on us all here.

  Press on.

 8. Seleli, I’ve got nothing to declare.

  And remember the motion on discussion is not Sungura and Seleli.

  Contribute what you know and believe in on the subject, as I will do the same.

  Some issues are too pet to waste time pondering on, while leaving the mega ones hanging.

  After all, the quest was not for you, but u just zoomed in into it!

  Thank u sir!

 9. Hiyo ni kweli, mimi humuona Sungura kama Asikari wa Kukodi, Asikari wa kukodi ukija na hela yako tu, anapigana upande wako,. Mwakani tena wakija na hela aliokuwa akiwapiga 2013, anawapigeni tena ninyi wa 2014!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 10. Sungura,

  Pengine kutokuelewa kwako kwa baadhi ya mambo kama ulivyokiri mwenyewe kuchanganywa na mada/somo ili la David, kunatoka na mkao-mkao wako wako( pre conceived/created status of your thoughts) unaposoma posts za wenzio. Kwa nini mimi nielewe kirahis kabia MAIN ISSUES, tena mara moja tu ujumbe huu na wengine kama navyosoma comment zao, wewe uchanganyikiwe?!!wakati mwingine chek youself, with which attitude unasoma nayo posts humu! Ndio maana nilishangaa na kukuliza umesoma post ya David NUKTA KWA NUKTA? hakuna ufundi nilifanya kukuuliza bali nilikua najaribu kukuleta ktk attitude fulani ili upate aliyoyaleta David. Sasa embu tuangalie swali lako na baadhi ya aliyosema David na kisha uliyochangia wewe kama kuna tofauti ya KIMSINGI kati yenu

  SWALI LAKO: ‘’tunaongelea kuabudu na kusifu kupi, kule kwa kuimba au dhana nzima ya kuabudu?

  KATI YA ALIYOSEMA DAVID( Angalia nimeweka baadhi ya statements zake ktk herufi kubwa)

  Waabuduji wasio wa kweli wanawea kufanya MATENDO YA KUABUDU, lakini ni maonyesho tu maana hayatoki katika MOYO UNAOMPENDA MUNGU

  Ibada ya kweli kwa Mungu inatoka katika moyo unaompenda Mungu tu. BASI KUABUDU SI KITU TUNACHOFANYA WAKATI TUNAPOKUTANIKA KANISANI BALI NI KITU TUNACHOFANYA KILA DAKIKA YA MAISHA YETU, TUNAPOTII AMRI ZA KRISTO

  Mungu angetamani hata kuambiwa “Nakupenda” rahisi tu itokayo moyoni kutoka kwa mtoto wake mmoja MTIIFU, kuliko kuvumilia KELELE ZISIZOTOKA MOYONI ZA MAELFU YA WAKRITSO WA JUMAPILI, wakiimba ….

  Matendo 13:1-2…..Basi hawa walipokuwa WAKIMFANYIA BWANA IBADA NA KUFUNGA, Roho Mtakatifu akasema, ‘Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia

  KATI YA ULIYOSEMA WEWE KTK MCHANGO WAKO WA MWISHO
  Lakini huku kusifu kote kuko ndani ya DHANA NZIMA YA KUABUDU ambapo KUABUDU ni pamoja na KUSALI,KUTOA SADAKA,KUFUNGA,KUSOMA NENO, KUSAIDIA, KUTEMBELEA WAGONJWA nk

  Yale aliyosema mleta mada/somo hapo juu ktk Herufi kubwa na uliyosema wewe ktk herufi kubwa apia, KUNA TOFAUTI YOYOTE YA MSINGI?

  Unaweza ona kwa nini nilikuuliza swali lako linakuje swali? Nadhani pia nisema kama unakua na mchango kama uliotoa sasa, basi na wewe nendaga moja kwa moja kwa mchango wako, uutoe kuliko kurusha/create wasiwasi kwa jambo ambali liko clear kabisa na lina bariki kama ilo la David maana umerudia kusema aliyosema yeye directly au kwa btn the lines reading. Tunaweza create query kama njia ya kuchajisha mambo,kumlete Mtu kwenye mstari ktk mada/mjadala/somo lakini si kwa mambo clear kama lengo KUU la somo hili la David.

  Press on.

 11. David pamoja na kwamba hujanipa fafanuzi niliokuomba, ninacho kitu cha kusema.

  Kwa maelezo yako yaliyo mengi, umejikita sana katika ibada ya kuimba. Japokuwa kuna maelezo na mistari mingine haijikiti sana kwenye ibada ya kuimba,ila kwenye ibada za namna zingine.

  Kwenye suala la kuimba sijui wazo la SIFA NA KUABUDU kwa maana ya kumwimbia Mungu lilianzaanzaje. Katika mtazamo wa asili yaani kuanzia agano la kale kuimba kuliitwa Kusifu, wala hakukuwa kunaunganishwa na hiki kipengele cha kuabudu.

  Kwa maneno mengine huwa hakuna kusifu na kuabudu kwa maana ya kuimba, ispokuwa kuimba kote ni Kusifu, ambako ni sehemu ya suala zima la kuabusu, ambapo kuabudu kumebeba almost kila kitu tunachofanya ktk maisha ya kila siku kama waamini.
  Kusifu (kwa kuimba) ndani yake pia kuna vipengele.
  eg;
  -kushukuru
  -kushangilia
  -kucheza
  -kupiga vyombo vya /ala za mziki
  -kupiga kelele
  -kupiga makofi
  n.k
  Haya mambo yote hufanyika ‘melodically’. Lakini huku kusifu kote kuko ndani ya dhana nzima ya kuabudu, ambapo kuabudu ni pamoja na kusali, kutoa sadaka, kufunga, kusoma neno,kusaidia na kutembelea wenye shida, n.k

  Kwa hiyo maelezo ya Yesu kwa mwanamke msamaria hayakuwa specific kwenye kuabudu kwa kuimba, bali kwenye dhana nzima ya kumfanyia Mungu ibada.

  Kuabudu kwa melodia ambako watu wengi humaanisha kuimba nyimbo za taratibu, ambako ndio haswa kumeleta dhana ya ”Sifa na Kuabudu” kunatakiwa tu kuitwa kusifu.

  There is no such a thing like Praise & Worship when it comes to singing, but there is only Praise. Therefore, the so called praise & Worship is all together Praise. Praising God is part of worshiping Him.

  Lakini David kwa kuwa maelezo yako mengi yamejikita kwenye kumwimbia Mungu, nami ngoja sasa nichangie katika huo mwelekeo.

  Mimi kwa mtazamo wangu, kuimba katika roho ni kuimba wimbo bila kujali ni wa zamani au mpya au wa saa hiyohiyo, ispokuwa uwe ni wimbo wa muunganiko wa kiungu (divinely connected). Roho mtakatifu anaweza kukupa wimbo au melody ya zamani sana,lakini huo ndio ukawa wimbo wa majira yake na ukafanya watu wafunguliwe. Au akakupa wimbo wa papo kwa papo vilevile

  Au Roho mtakatifu anaweza kukwambia kufanya kama moja ya vitu ambavyo nimevisema hapo juu kuwa ni vipengele vya Kusifu, na katika kufanya hivyo ukaona uwepo wa Mungu ukijidhihirisha.

  Kama wimbo mpya ungekuwa na maana ya wimbo wenye melodia mpya na maneno mapya basi tusingeona ujumbe wa Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema kwa maana fadhili zake ni za milele ukijitokeza tena na tena katika historia ya Israel kumsifu Mungu.

  Nitaendelea kuchangia.

 12. Unajua Seleli ndio maana mimi na wewe katika mada nyingi tunavutana sana, kwa sababu unajaribu mno kuwa mwanafalsafa.

  Wa kwanza kuchangia hii mada alikuwa Yusha, wa Pili Siyi, wa tatu Sungura.

  Sasa hebu angalia kwenye mchango wa Sungura ambao ni namba tatu uone kama sikumuuliza hilo swali David mleta mada.

  Kuna wakati unatakiwa ujibu tu kilichoulizwa kama hutaki unaacha, kuliko kujaribu kuweka ufundi ambao hauna umuhimu wowote.

  Ilikuwa rahisi kujibu kuliko kuuliza swali juu ya swali!!

 13. Sungura,

  Umeuliza swali na unatarajia jibu, ivyo ni haki upate jibu na njia ziko nyingi za kuleta majibu

  MAJIBU:

  1-Umesoma post yote nukta kwa nukta?

  2-Ktk kuisoma yote, hukuona humo points/issues/tips /clues ambazo zinasema moja kwa moja na nyingine by implication ni aina gani ya Kuabudu alikosemelea David?

  3- Sasa ili swali lako tunaongelea kuabudu na kusifu kupi, kule kwa kuimba au dhana nzima ya kuabudu? Linakuaje swali?

  Jibu maswali hayo kisha utapata jibu lako au la, kama ulivyoomba wadau, sema tena kama kwa kujibu maswali hayo yenye jibu lako, yatakua hayajakupa jibu, then tutakupa majibu au bwana David mwenye somo ukimtaka/taja specifically, basi atawajibika I hope.

  Press on.

 14. Jamani wadau, nimeuliza swali kuwa tunaongelea kuabudu na kusifu kupi, kule kwa kuimba au dhana nzima ya kuabudu?

  Come on guys!!

 15. David,
  Bwana akubariki sana kwa somo zuri na lenye kufunza kunakotanguliwa na maonyo kama haya uliyoyaleta!

  Binafsi, nimebarikiwa sana na uwazi wa hali zote kama ulivyozirejea, naona yote ni yenye kutia moyo na kuigeuza mioyo yetu kutoka katika Mazoea na kutuingiza katika Uhalisia wa ibada na kuabudu.

  Ndipo katika tafakari ya ‘kuabudu’, nimevutwa zaidi na ile rejea uliyoitumia ya yule mwanamke wa Kisamaria, hivyo napenda kutoka mfano huo nami niuunge katika hili ulilolisema kwamba, “”“Ibada” nyingi katika makanisa siku hizi ni taratibu tu zilizokufa, zinazotendwa na waabuduji waliokufa pia””; bali kwa mtazamo tofauti kidogo.

  Katika siku hizo ambazo ibada ilikuwa ikifanyika Yerusalemu kulingana na taratibu zilizokuwepo, twafahamu kwamba mji huo ulikuwa ndio Makao Makuu ya dini ya Kiyahudi katika maana ya mfumo mzima wa Torati na Sheria na Manabii. Naye Msimamizi wa mambo hayo yoote yahusuyo Ibada alikuwa ni Kuhani Mkuu. Kwa hiyo Mungu alijidhihirisha kupitia Mfumo huo aliouweka. Ndipo macho na masikio ya watu wote yalielekezwa Yerusalemu ili kupata maono ya wakati kwa kadiri Mungu anavyoyaleta. Yaani Yerusalemu ndipo mahali pa kuabudia Mungu alipopachagua, kama alivyokiri huyu mwanamke wa Kisamaria!

  Nasi twafahamu kwamba Neno la Mungu ndiyo Mbegu ya asili. Ndipo Ibada zetu zinawakilisha yule Mpanzi, kwamba Neno linapohubiriwa, hilo hupandwa mioyoni mwetu. Basi niseme kwamba kwa kadiri yule mwanake alivyohudhuria zile ibada, Neno la Mungu lilipata kuhifadhika moyoni mwake, ile Mbegu. Ndani yake kukawa na Tumaini la Masihi! Yawezekana maisha yalikuwa yamembana, labda alikumbana na wanaume waongo, ambao walimlaghai na kumtumia na kisha kumuacha, kama ambavyo wengi wetu tunavyotumiwa na makanisa yenye hizi taratibu zilizokufa, hata ile kiu ya Kweli ingetuhamisha kutoka kwa mfu huyu kwenda kwa yule! Ukiyarejea mazungumzo yao pale kisimani, unaweza kuona kwamba yalikuwa ni yenye kupenya hata kukifikia kilindi cha moyo wa mwanamke huyo, ile Nuru!!!

  Nuru hupenya ardhini na kuifikia Mbegu iliyolala huko chini na kui germinate! Huyu mwanamke alikuwa na wanaume watano huko nyuma na hata huyu wa sita naye ndo wale wale, wamejaa taratibu mfu! Bali maongezi yake na huyu mwanaume wa Saba, yalikuwa na jambo fulani ambalo halielezeki, ni Nuru tamu yenye kusisimua! Akajikuta anajieleza siri yake!! Neno linasema, “…vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake…” Ebr 4:13. Ndipo akaelezwa siri zilizofichika moyoni mwake! Yn 4:25 “Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.” Ile Mbegu ime sprout out! Mwanamke wa mitaani amemtambua Masihi ndani ya takribani dakika 10/15 za maongezi yao, Nuru imemfikia, akaiacha na ndoo yake ya maji hapo hapo kwa furaha iliyomjaa, akakimbia mjini na kuwatangazia wote Habari Njema, iliyosubiriwa kwa mamia ya miaka na sasa yeye ambaye aliye wa chini katika jamii, maana hata hapo kisimani hakuruhusiwa kwenda kuteka maji asubuhi muda wa mabikira, ilimbidi aende muda huo wa mchana ili asiwaharibu hao mabikira! Bali ndio muda wa Masihi, “Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?” Mwanamke yule amepapata mahali papya pa kuabudia, KRISTO, Hapa ndipo mahali Mungu alipopachagua, katika KRISTO, Haleluyaaaaa!!!

  Haya hebu tumtazame Kuhani Mkuu na baraza lake, wanasemaje kuhusu Masihi? Yn 7:45-49 “Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa.”

  Nayo Torati yao iliwafunza kuwa katika ujio wa Masihi, “Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba;” Isa 35:5-6. Nayo mambo haya hayajawahi kufanyika huko nyuma, lakini yote yametimia machoni pao, wao ni mashahidi wa kutimia huko, lakini wamechagua kifo badala ya uzima, maana kwa kauli yao wenyewe wamejitoa ufahamu wa Torati na hivyo ile laana waliyotaka kuwaangushia makutano kuwarudia wao wenyewe!

  Hii ndiyo hali ya kanisa lililokufa, hujilaani lenyewe kwa kuyakataa na kuyagawa Maandiko!!!

  Mbarikiwe nyote!

 16. Barikiwa sana David binafsi nimebarikiwa sana na somo na nimejifunza mambo mengi sana bt hv kama ninamsifu na kumwabu Mungu wangu kwa upendo wa kweli moyo safi kuna mipaka?Coz mfalme Daudi alijiachia kwa God hadi nguo zikaanguka!Je kwa kizazi cha leo tunamipaka?Kama watu wa dunia wanajiachia na Devil wao!!why cc nac tucjimwage kwa God wetu?Wapendwa napenda kujifunza mengi kuhusu Mungu wetu.God Bless U All.

 17. David Servant,

  Jamani, it is so sweet! ni msg ndefu kwa wengine lakini soma tu na utagundua-THIS IS AMAZING AND GREAT MESSAGE kuhusu Sifa na Kuabudu am telling you. Mimi kama Mwandishi pia, sikuwahi kuwaza na si Waalimu wengi hu-take time kuandaaa somo kuhusu Sifa na Kuabudu, at least kwa uzoefu wangu, ni rare case, si common thing kukutana nalo ktk social networks au majadiliano. Roho Mtakatu amekusukuma na kukuvuvia kusema kitu very huge in a very sweet analysis, Mungu wa mbinguni akutumie tena na tena. Nimeshindwa kujizuia kusoma tu na kuondoka nikaona ili nikate kiu yangu na kusikia utamu zaidi rohoni, nidondoe kati ya vitu vya ajabu sana na vyema ambavyo kwangu ni precious stones zilizonibariki na na kunipa ufahamu wa ajbu sana, we mtu wa Mungu, ubarikiwe na kutunzwa siku zote ili utumike hapa na kule zaidi na zaidi,Amen.

  DONDOO toka Somo lako Nzuri sana:( pengine itasadia na wale wasioweza soma maandishi yote mstari kwa mstari/somo lote)

  …..Umetumia Andiko Msingi MOJA na ku-support kwa maandiko mengine 17= hapa kuna upendo/kujitoa kwa wengine, sadaka ya muda na upenzi wa kulisoma Neno-(hongera sana brother).

  ….Maandiko yanayonyesha nguvu ya Sifa na Kuabudu ni matamu sana yakiongozwa na kisa chema mno cha Yeshoshafati

  ….Wapo watu wanaoabudu, lakini si waabuduji wa kweli, Wanaweza kudhani kwamba wanamwabudu Mungu lakini ukweli si hivyo maana hawatimizi masharti Yake.

  …..Wale wenye kuabudu “katika mwili na uongo”(hii spiritual creativity imenibariki na kunichekesha kweli-asante)

  ….Kuabudu si kitu tunachofanya wakati tunapokutanika kanisani, bali ni kitu tunachofanya kila dakika ya maisha yetu, tunapotii amri za Kristo= (Great understanding of HSp ndani yako)

  ….Inashangaza kwamba yule mwanamke aliyekuwa anazungumza na Yesu alikuwa ameolewa mara tano, na wakati huo alikuwa anaishi na mwanamume, na bado alitaka kuhojiana na Yesu kuhusu mahali panapofaa kumwabudu Mungu! Yeye ni mfano wa watu wengi sana wenye dini, wanaohudhuria ibada huku wakiishi maisha yao kila siku katika kumwasi Mungu. Hao si waabuduji wa kweli.( amazing insipired observation/revelation-Glory to Jesus, Amen)

  …..Yesu alisema kwamba mahali hapakuwa na maana sana. Cha muhimu ni hali ya moyo wa kila mtu, na jinsi anavyomheshimu Mungu. Hayo ndiyo yanaamua jinsi ibada yake ilivyo (fantastic fact, blessed be the name of Jesus in you)

  …….“Ibada” nyingi katika makanisa siku hizi ni taratibu tu zilizokufa, zinazotendwa na waabuduji waliokufa pia. Watu wanarudia maneno ya mtu mwingine kuhusu Mungu, bila hata kuyafikiri( straight, a red and yellow bold statement..nipenda ujasiri huu,Mungu nisaidie nisiwe mmoja wao)

  …..Mungu angetamani hata kuambiwa “Nakupenda” rahisi tu itokayo moyoni kutoka kwa mtoto wake mmoja mtiifu, kuliko kuvumilia kelele zisizotoka moyoni za maelfu ya Wakristo wa Jumapili asubuhi, wakiimba “Jinsi Wewe Ulivyo Mkuu.”( nimeshangaa sana hii, wow! one more qualified than many thousands!!!!!!!!! aisee! lovely and am proud to be saved,Amen)

  …..Kuna wanaosema kwamba kuabudu “katika Roho” ni kuomba na kuimba kwa lugha zingine. Hiyo ni tafsiri ngumu kukubali, ukitazama maneno ya Yesu. Yeye alsiema kwamba “saa inakuja, na sasa ipo, ambayo waabuduji wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli,” kuonyesha kwamba tayari walikuwepo watu waliotimiza masharti ya kuabudu “katika Roho” alipotoa tamko hilo. Ni kweli kwamba hakuna yeyote aliyenena kwa lugha mpaka Siku ya Pentekoste. Basi, aaminiye yeyote, awe ananena kwa lugha au hapana, anaweza kumwabudu Mungu katika roho na kweli.( such Biblical great understanding, you are blessed)

  …..Tunaweza hata kumsifu Bwana kwa kucheza. Lakini kucheza kwenyewe kusiwe kwa kimwili, kwenye kuamsha ashiki, au kwa ajili ya kustarehesha watu.( nimependa hii-kiinjilisti/kiangalizo zaidi…kumbe tunacheza yet si kuamsha ashiki-tehe! nimecheka ilo neno, ok..noted vema sana)

  …Pia maandiko yanayonyesha kupiga vyomb vya muziki, kupiga kelele, kumbe hata tuwe tumelala, tumekaa, kusimama vyote tunaweza tu tukamsifu na kumwabudu(nimependa hii, inatuweka huru mbali na taratibu kadhaa tulizo kariri e.g. kua mpaka uwe umesimama tu ndio unabudu au sifu vema)

  Ubarikiwe sana David, Bwana aendelee kukujaza vitu toka JUU ili uvilete hapa na ktk yote, naku-appreciate na hapo hapo sifa na utukufu twampa BWANA WA MAJESHI, Amen.

  Press on,

 18. David mimi naona umenichanganya kidogo!
  Unaongelea kusifu na kuabudu katika muktadha upi?
  Maana kuabudu ni zaidi ya kuimba na kusifu halikadhalika, kwa maana ya kusifu na kuabudu melodically .
  Maana ukisema kuabudu ni kitu tunachokifanya kila dakika ya maisha yetu ni wazi kuwa huongelei kuimba (yaani melody), maana huwa hatuwi tunaimba kila dakika ya maisha yetu.

  Nahitaji ufafanuzi!

 19. Ubarikiwe sana David.
  Mimi naomba kuchangia kwenye mambo mawili tu-kumwabudu Mungu katika 1. Roho na 2. Kweli.
  1. Kumwabudu Mungu katika Roho.
  Ni kweli kabisa ulivyosema kuwa, ibada ya kweli ni ile itokayo moyoni. Ibada ya kujitoa kikamilifu mbele za Bwana. Ibada ya kuumimina moyo kwa Bwana. Na kwa maneno mengine, ni ibada iliyojengwa kwenye misingi ya upendo wetu kwa Mungu. Hivyo kumwabudu Mungu katika roho, sharti kujengwe kwenye msingi wa upendo. Upendo hukaa moyoni na matendo yake hujidhihirisha kwa nje-yaani vitendo vya kuonesha upendo huo.
  Mungu alipotuumba, alitupatia tabia yake ndani yetu ili nasi tuishi kwa kumpenda kama YEYE alivyo Pendo. Tunapomwabudu ktk roho na kweli, sharti tuakisi tabia ya Mungu-upendo.
  2. Kumwabudu Mungu katika Kweli.
  Neno la Mungu ndilo kweli-Yohana 17:17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kwe. Tunapomwabudu Mungu, sharti tufuate Biblia inavyoelekeza jinsi na namna ya kumwabudu Mungu. Kumwabudu katika kweli, ni kuyafanya yote aliyoyaagiza ndani ya neno lake ili yafuatwe na watu wake. Huwezi kusema unamwabudu Mungu kama huenendi sawasawa na Mungu alivyoagiza.
  Kwa kuhitimisha, kumwabudu Mungu katika roho na kweli ni pande mbili za shilingi moja. Huwezi kusema unamwabudu Mungu rohoni huku unavunja maagizo yake. Kadhalika, huwezi kumwabudu Mungu katika kweli-neno huku moyoni huna upendo kwake. Mtawatambua kwa matunda yao, kilichomo ndani, hujidhihirisha kwa nje. Tunapotii neno la Mungu rohoni, sharti lionekane katika mwili-matendo. Kutii sharti kuanzie rohoni-moyoni ndipo kuonekane kwa nje. Na hiyo ndiyo imani iliyo hai.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s