Kanisa: Tumekosea Wapi?

kanisaa

Wapendwa,

Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu:

Hivi jinsi ambavyo tunaendesha makanisa yetu (staili, ibada, miundo ya uongozi, sadaka, nk) ndivyo Mungu alivyokusudia au tumebuni na/au tunafuata mapokeo ya wanadamu yaliyoingia hapa katikati?

Nikitafakari mambo yanayoendelea katika kanisa la leo duniani kote – jinsi watu wanavyotafuta kwa bidii madaraka na nafasi za uongozi (wakati mwingine ni kama utawala) makanisani (na inasemekana wengine huenda hadi kwa waganga wa kienyeji/wachawi); baadhi ya viongozi wa makanisa ambavyo hawako tayari kuhamishwa; jinsi mahubiri yanavyotolewa kulingana na yale ambayo waumini wanataka kusikia; jinsi watu wenye uwezo kipesa na hadhi katika jamii wanavyothaminiwa na kuenziwa makanisani; na jinsi ambavyo viongozi wengi wanavyotafuta kuwa karibu zaidi na wanasiasa na viongozi wa serikali za nchi husika hadi kufikia hatua ya kuwapa madhabahu wahubiri; nimejikuta nikiamini kuwa kuna mahali tumekosea – TENA TUMEKOSEA MNO kuliko Wakristo wengi wanavyoweza kufikiria au kuwa tayari kuamini.

Mara kwa mara hali ya kanisa inapozungumzwa, watu husema kuwa makanisa mengi yamegeuka kuwa miradi ya watu. Na hili sidiriki kulipinga. Ila ninaamini kuwa hiyo ni dalili (symptom) ya tatizo kubwa zaidi. JE TATIZO HILO NI LIPI HASA?

Ukiangalia jinsi viongozi wa baadhi (au mengi?) ya makanisa wanavyosisitiza watu kutoa – kuanzia zaka, sadaka za malimbuko, na aina nyingine za sadaka – huku baadhi ya viongozi hao wakiishi maisha ya anasa, na wakiwa hawako tayari kubainisha matumizi ya pesa hizo, wakati miongoni mwa washirika wao kuna watu hawajui hata watakula nini baada ya kutoka ibadani na hawafahamu watasaidiwa vipi – hakika maswali yanakuwa mengi kuliko majibu. Kwa anayesoma kitabu cha Matendo ya Mitume atagundua mara moja kuwa huo si mfano au kielelezo tulichoachiwa na kanisa la kwanza. Na kwa hakika huo sio upendo aliouzungumza Bwana Yesu Kristo ambao wanafunzi wake wanapaswa kuwa nao miongoni mwao, na ambao ulipelekea watu wengi katika enzi zile za kanisa la mwanzo, kuvutiwa na imani ya Kikristo.

Je umepata kujiuliza kwa mfano, kama hivi leo kungekuwa hakuna wachungaji wanaolipwa mshahara, bali kanisa la mahali pamoja (local church) lingekuwa linaongozwa na baraza la wazee (elders) ambao hawategemei sadaka za jumapili, bali wana shughuli zao za kiuchumi, na sadaka zinatumika kusaidia wenye uhitaji kanisani – wajane, yatima, wazee, na wasiojiweza wengine – hali ingekuwaje? Na kungekuwa na matokeo (impact) gani katika jamii inayolizunguka kanisa (local church) husika? Je, kungekuwa na hali ya baadhi ya wachungaji kung’ang’ania kanisa la mahali fulani na kuwa wakali pale habari ya uhamisho inapotajwa?

Ninafahamu wengine wanaweza kukwazwa na hiki nilichokiandika, lakini niseme tu kuwa, imenichukua muda mrefu kutafakari hayo, na sasa NIMELAZIMIKA KUFIKIRI KWA SAUTI, nisikie mawazo yako pia.

JWM

Advertisements

47 thoughts on “Kanisa: Tumekosea Wapi?

 1. Ndg Orbi,

  Nimefurahi sana kuyasoma hayo uliyoyaandika kutoka katika kilindi cha moyo wako, huko yalikojihifadhi, na sasa yakiletwa uweponi mwetu ili kutunururisha juu ya jambo hili kuu sana, ambalo linaishikilia hatma ya maisha yetu, HALI YA KANISA!

  Uimara wa Kanisa uko katika kuliishi Neno la Mungu. Nao uimara wa Kanisa hudhihirika ktk washirika wake, ule uimara wao ktk Njia, wakikikulia Kimo cha Kristo. Bali jambo hili lawezekana tu iwapo Kanisa litakaa katika nafasi yake kama alivyolikusudia Muasisi wake, Kristo, hapo alipozisimika ndani ya Kanisa hilo zile Huduma Tano ili kuwakamilisha Watakatifu wake. Lakini mambo haya leo ni ya kuyasoma tu katika Maandiko, huko uwanjani wanako dai kuwa kanisa liko imara hayako kabisa! Kilichoko huko ni injili ya supremacy tu, kila mmoja akijaribu kumshinda mwenzake, si ule Mwili mmoja tena bali ni vurugu tupu!

  Kwanza hata Biblia yenyewe wameiweka pembeni, ni miujiza kwa kwenda mbele! Nimesoma ktk mail, dada yangu ktk Kristo akiyashangaa mambo yanayoendelea, mtumishi anawapa watu upako wa kununua helikopta binafsi ili kukwepa foleni, na watu wanashangilia…, ‘kanisa imara’!!! ukiangalia kwa upesi unaweza kudhani ni suala la umasikini, bali si kweli, ni upako wa kuzimu ulio juu ya wahubiri na wahubiriwa!!! Yale mafundisho mbadala!!

  Ni kweli ndugu yangu, “.. inahitaji Mungu kutufungua ufahamu wa Kiroho kufahamu haya…….!”

  God bless u, brother!

 2. Wapendwa,

  Orbi & Tumaini Nelson,

  Asante sana, nimekueleweni vizuri sana. Bwana Yesu Kristo aendelee kukubarikini kiasi cha kufurika. Nimefurahi sana, kwani mmenifundisha jambo kuu kwangu!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 3. Ndugu Orbi,
  Nashukuru kwa mchango wako hasa ulivyomalizia. Kwa kifupi mimi ndiye nimeongelea changamoto ya umasikini kwa kanisa hasa la Tanzania miongoni mwa watumishi wengi. Kwa hiyo mchango wako unanihusu moja kwa moja.

  Ni kweli umasikini na utajiri vyote vinaweza kuwa changamoto, kwamba kwetu umasikini ni changamoto na huko Marekani na Ulaya utajiri ni changamoto.

  Kwa ujumla mimi nilikuwa najaribu kufupisha (summarize) kile ambacho mleta mada amekisema.

  Na hata mimi siwezi kujaribu kusema kuwa kanisa likiwa tajiri ndo changamoto zitaisha,la hasha, changamoto zitaibuka tu tena zingine na kwa namna nyingine.

  Lakini kwa sasa kusema kweli umasikini ni tatizo kubwa. Na hata hao wanaohubiri sadaka na utajiri, hata wakishazipata hizo pesa kinatokea kitu kinachoitwa ulimbukeni. Ndio huo ununuzi wa magari na vitu vya thamani wakati washirika wanalala njaa.

  Na hiyo hali inatokana na kile wazungu hukiita ”low self esteem”. Mtu kutoka kwenye umasikini wa kutupwa ,leo anakamata pesa,tena za bwelele, hutaka kila mtu ajue. Ukiangalia hii kitu inalisumbua sana kanisa la Afrika kwa ujumla,na ndio maana limeshindwa kuleta impact hata kwa serikali za Afrika kwa sababu waafrika karibu wote wanasumbuliwa na tatizo moja (low self esteem).

  Na ni kwa nini watu, hasa wakristo ni masikini pamoja na ahadi nyingi za mafanikio ambazo kimsingi ziko kwenye neno la Mungu?

  Hilo nalo ni swali la kujiuliza, maana wanaotoa hizo pesa za viongozi kununua magari aghali ni washirika ambao kimsingi ni hao masikini wa kutupwa.

  Wachungaji na maaskofu wengi wenye mali wala hawana miradi mingine zaidi ya matoleo ya washirika/waumini. Pesa/ mapato ya kanisa (local church) yanamilikiwa na mtu mmoja, na hakuna wa kumhoji

  Watu wengi wamefundishwa na kusomewa maandiko ya toa ili ubarikiwe. Lakini ni wachache sana ambao wanafundishwa kufanya kazi kwa bidii ili wawe na cha kutoa ili wabarikiwe, matokeo yake wanatoa hata kidogo walichinacho na wala hawabarikiwi na kingi maana kanuni imekosewa.

  Wameambiwa wapande mbegu, mbegu yenyewe mara zote huwa ni mali tu au fedha. Huwezi sikia wanaambiwa wapande mbegu ya matendo mema kuwa watabarikiwa, bali mbegu ni pesa tu na mali (materials).

  Watumishi kwa kutumia karama ambazo Mungu amewapa, wamegeuza uhitaji wa watu kuwa mtaji wao wa kiuchumi. Na watu kwa sababu wana shida zinawatesa huwafuata na kutimiza masharti wanayopewa na hao watumishi ili shida zao zikome.

  Watumishi hawa watakuwa na kesi ya kujibu mbele za Mungu kwa kuwakamua wana wa Mungu kwa karama ambazo wao wamepata bure.

  Walimu wasio na ujuzi wa neno la Mungu wameingia kuwafundisha waumini na kuwalisha matango mwitu. Ukiwauliza wanakwambia wanaongozwa na Roho mt., huku wakiyapotosha maandiko matakatifu kwa kujitungia tafsiri zao.

  Majengo yao yanazidi kujaa na Mungu bado anawatumia japokuwa wao wenyewe ni watu wa kukataliwa siku ile. Maana Paul anasema hata kama mtu atakuwa anachumia tumbo twende kazi almradi injili inahubiriwa

  Watu wamefundishwa mambo makubwa sana ya maarifa ya Mungu, huku wakiacha kufundishwa kwanza mambo ya msingi ya wokovu. Na matokeo yake tumejikuta tuko na watu wenye kunena mambo makubwa sana maneno ya Mungu ambayo wasingepaswa kunena maana hawana maarifa ya kweli ya mambo hayo, na matokeo yake huyapotosha.

  Lakini hii ni Afrika bwana, mwalimu ni mjinga na mwanafunzi ni mjinga,kwa hiyo mchezo huwa ni kama mazingaombwe vile. Mtu akifanya tu mauzauza fulani halafu akasema jamani njoni muone, utashangaa watu wanajaa wakubwa kwa wadogo.

  Afrika tunapenda magic na mauzauza/ au mazingaombwe, ndio maana hata makusanyiko ya walimu wajinga nayo yana wingi wa watu ambao nao ni wajinga villvile.

  Orbi wewe unajua kuwa kuna mafundisho yanafundishwa Afrika,amabayo USA hata dakika tano watu hawawezi kukaa wakiyasikiliza.

  Mungu siku zote ana watu!

 4. Mpendwa Orbi nimebarikiwa sana na namna unavyonyesha nia ya dhati kabisa kuelimishana!Ujuwe hakuna jambo zuri kama kukubali kujifunza au kupata jambo jipya kwa mwingine mimi binafc huwa cbarikiwi na ile hali ya baadhi ya cc wapendwa kuona kama mpendwa flani hawezi nipa jambo jipya na ndiyo maana mjadala unapokolea wapendwa wanatumia maneno magumu ambayo kwakweli binafc hayanibariki!Why 2celimishane kwa Upole?Maneno magumu yanatoka wapi wapendwa?Kuna cku nilishawahi uliza mfana coments hizi akisoma mtu acye mjua God je atajifunza nini?Hata kama ni hali ya kiinjilist bt inakuwa too much.Mimi camini kuwa kunamtaalamu saana wa neno kuliko Roho Mtakatifu.Je Mungu wetu ni wa kanuni moja?Mungu awabariki wote.

 5. Wapendwa……Lwembe. Mabinza…….Sungura na wachangiaji wengine…….

  Labda ni kweli tumeshindwa kumuelewa mtoa mada (JWM)….ambaye pengine hakutupa wigo wa majadiliano…

  Lakini nashangaa pia kwa mtazamo wa baadhi yetu kwamba Kanisa la Tanzania inawezekana linakosea kwa ajili ya “Changamoto za umaskini”…..!!!!!

  Eti ni changamoto za umaskini ndio zinafanya Viongozi wa Kanisa kukumbatia Wanasiasa…..! Kutaka madaraka chanzo chake ni umaskini……!!! Kujali na kupendelea wenye navyo chanzo chake ni umaskini……!!!

  Kwa mtazamo huu, ni kwamba Kanisa likiwa na fedha….likiwa tajiri…..litaacha kukumbatia wanasiasa……! Litaacha kugombania madaraka……! Je mtoa mada anasema haya kwa kuangalia maneno ya Mungu….? Ni kweli Kanisa la nyumbani Tanzania limeacha njia……kwa vile linakabaliwa na Changamoto za umaskini……?

  Kama baadhi tunadhani tukishinda changamoto za umaskini Kanisa litakua salama…..basi asome maneno haya ya Yesu mwenyewe kwa kanisa ambalo lilishinda changamoto za umaskini na kudhani limekuwa salama…….angalia Yesu anasema nini….! KWA KUWA UMESEMA WEWE MIMI TAJIRI, NIMEJITAJARISHA…..WALA SINA HAJA NA KITU, NAWE HUJUI YA KUWA WEWE NI MNYONGE, NA MWENYE MASHAKA….MASKINI, KIPOFU NA UCHI…..”

  Je Kanisa la Yerusalemu lilipokuwa maskini lilifanya nini…..? Hatukusikia lilianza kuwakumbatia Watawala wa Dola ya Rumi…..! Hatukusikia mitume wakigombania madaraka….! Hatukusikia wakisisitiza zaka…..panda mbegu na malimbuko…..!! Tunachoona Paulo analiambia Kanisa la Korintho wapitishe changizo …..na pia analishukuru Kanisa la Makedonia licha ya kuwa katika dhiki nyingi lilijitoa kwa hali na mali kusaidia Kanisa la Yerusalem!! Hili ndilo Kanisa lilivyoshinda changamoto ya Umaskini…!!!!!

  Angalia kanisa la nyumbani Tanzania……wengine ndani ya Kanisa hawana hakika na mlo wa Kesho……Kanisa linapitisha changizo kukunua Hummer, VX, LEXUS ya mtumishi…..! Wakati gari ya kwaida kabisa ingeliweza kutatua tatizo la usafiri la mtumishi…! Na mtumishi huyu anaona sawa tu! Watumishi wa namna hii kweli wamejawa na Roho Mtakatifu….au roho mtaka vitu…!

  Nataka kuwaambia ndugu zangu kanisa la nyumbani changamoto zake ni umaskini…….lakini (niko USA) kanisa la USA changamoto zake ni utajiri….! Kanisa la Kristo linatakiwa lishinde kila changamoto kwa kutumia maneno ya Mungu tu! Maneno ya Mungu tu! Maandiko aliyotuachia Yesu mwenyewe ndio yanaweza kulisimisha Kanisa kupita katika hali…..!! Hebu tuzirudie Biblia zetu……tuzisome tena na tena…na kuomboa Roho Mtakatifu atufunulie Maandiko…..!

  Mbarikiwe Wote.

 6. Wapendwa,

  Sungura na Haule; Shida iliyopo kwa watu wajiitao ni kanjisa la Kristo, ni “UMWILI” mtu anapoijaza akili yake Umwili, mambo yote ya kiroho atakuwa anayajua tu lakini hayaelewi! Ni aibu mtu kutojua kabisa kuwa vita hivi vya Kanisa ni vya Kiroho. Inashangaza kusikia watu wajiitao kuwa ni wa Kanisa la Kristo, ati hawajui kuwa, kwakuwa Kristo analo kanisa na shetani naye lazima awe analo kanisa! Biblia inaliita, Kanisa ni ‘MWANAKE’. Tukirudi pale Mwanzo, tunaona Mungu ana weka uadui kati ya uzao wa Mwanamke na uzao wa nyoka. Kumbe, iwapo uzao wa mwanamke ni uzao katika kanisa la Kristo uzao wa nyoka si uzao katika kanisa la shetani? Kanisa la Kristo ni watu, vivyo hivyo kanisa la shetani ni watu.

  Kwa bahati mbaya sana, watu wa Mungu hupotea kwa kukosa tu maarifa yaani ujuzi wa kutosha katika Neno la Mungu, wengi hutegemea akili zao na ujuzi wao na maarifa yao, huku wakisoma bila kuelewa ile Yohana, inaoposema kuwa, “ bila mimi ninyi hamuwezi neno lolote”Kutotii Neno la Mungu, ni kutoamini; na huko kutoamini ndiyo dhambi na ndiyo uovu! Kwa hiyo, Kanisa lisilotubu na kuuacha uovu, hilo hupewa shetani, maana yeye ndiye aliyetenda dhambi, kwa hiyo wenye dhambi ni wa shetani, Sungura na Haule mnapokuwa hamtaki ukweli huo siwashangai, kwani kutoliamini neno kunatekelezwa na watu wajifanyao ni waamini!

  Siijui hiyo “Oneness”unayoisema kama ni kitu gani, hivyo siwezi kuisemea, ila ujue tu kwamba, ndani ya Kanisa ndimo alimo shetani, kwa hiyo unapoona kanisa usidhani kuwa liko moja, ni moja kimwili lakini kiroho ni mawili na hayo ndiyo yanayopambana. Kwa hiyo vita vya kanisa vimo ndani ya kanisa siyo nje ya kanisa. Kama ilivyokuwa huko mbinguni, mpango ni huo huo, Mungu habadiliki, ikiwa shetani alitupwa toka huko, maana yake ushetani wake ulianzia huko mbinguni akiwa pamoja na Mungu, vile vile alipokuwa akimkosesha Yule mwanamke wa kwanza, alikuwa pamoja naye katika lile shamba la Edeni. Siku moja Yesu alilithibitisha hilo kuwa, shetani yumo kanisani, alipotamka wazi wazi katika Yohana kuwa, “sikuwachagua ninyi theneshara na mmoja wenu ni shetani?”

  Kwa hiyo watu wasijidanganye, kiukweli shetani yumo humo humo kanisani, na ndiyo maana anapata nafasi kwa urahisi kulipotoa kanisa, maana ajenda zote huzisikia na pia hata huzishirikiswa. Lakini ieleweke tu kwamba shetani hana uwezo wa lolote kwa watoto wa Mungu ingawa anajihudhurisha pamoja nao, yeye anauwezo na watoto wake ambao nao wamo humo humo kanisani. kwakuwa wao ndiyo wengi, wakikosea huonekana kama kanisa LOTE limekosea, kitu ambacho si kweli, Kanisa la kweli haliwezi kuendela kukaa nje ya Neno likoseshwa na yule mwovu hurudi ndani ya Neno haraka, kwasababu ipo ile huduma ya UNABII!

  Kuhusu kusema kuwa, mimi sijiiti mmoja wa wanakanisa linalopatwa matatizo si kweli! Mimi ni mmoja wa kanisa linalosumbuliwa na shetani, lakini si mmoja wa kanisa ‘lililokosea pahala fulani’ Pengine hili niliweke wazi hivi, Kanisa hili lilikoseshwa na shetani ni la shetani kwakuwa halitaki kutubu, ndiyo maana mimi si kanisa langu, na wala simo humo katika kusikizishwa yale mafundisho yasiyokuwa Neno la Mungu! Kanisa lenye kujua ni wapi limekosea, likatubu na kuendelea vema kuwemo ndani ya Neno ingawa lina BUGUDHIWA na shetani hilo ndilo nilimo! Ieleweke kuwa mtu anapobeba jiwe anajua kuwa amebeba jiwe, na anapolitua chini pia anajua kuwa amatua jiwe chini; MTU HUYO ANAPOSEMA HAJABEBA JIWE, SI KWAMBA ANAJISIFU KWA WATU AMBAO WANGALI WAMEBEBA MAWE, HUO NDIYO UKWELI WA MTU HUYO KWAMBA, SI TENA BADO KABEBA JIWE!

  Labda nimalizie hapa kwakusema, Sungura na Haule msiwe wana wakaidi ambao kufaidi kwao ni mpaka inapofika idd, Lwembe na Orbi wamelielezea jambo hili kwa ujuzi mkuwa wa KIUUNGU mimi binafsi nimeridhika kabisa kuwa, hayo ndiyo majibu ya maswali yenu Haule na Sungura!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 7. Wadau pengine tunajadili kitu ambaho mleta mada hata hakikuwa hoja yake ya msingi, lakini kwa vile kimefanana na yale ambayo tunatamani sana tuyaseme.

  Mleta mada kaanza na mambo kama staili za ibada makanisani, miundo ya uomgozi, mambo ya sadaka n.k. Yaani vile makanisa yanavyoendeshwa kimfumo.

  Ameongelea watu kutaka madaraka kwa nguvu na wengine kwenda kwa waganga na wachawi kutafuta hayo madaraka ya uongozi kanisani. Mahubiri kutolewa sawasawa na matakwa ya waumini, na wachungaji wengine kutokuwa tayari kuhamishwa.

  Wenye pesa kuthaminiwa, viongozi wa kanisa kutaka kuwa karibu na wana siasa. Makanisa kugeuka kuwa miradi ya watu, watu kusisitizwa kutoa zaka,sadaka, malimbuko na sadaka nyingine ambazo wachungaji huzitumia kuishi maisha ya anasa.

  Na sehemu nyingine anaona kuwa wachungaji wasingelipwa mishahara ila makanisa yangekuwa chini ya wazee wa makanisa ili pesa hizo za sadaka zitumike kuwasaidia wahitaji, kama yatima ,wajane,wazee n.k

  Kwas kifupi hayo ndo mleta mada kayasema. Na mimi kwa mtazamo wangu nikasema kweli mambo hayo yapo, lakini kwa sehemu kubwa ni changamoto tu kwa kanisa.

  Hajaongelea mambo ya mafundisho potofu, mambo ya ushoga, mambo ya Loliondo

  Lakini nikadokeza kama kuna mtu anajiita mkristo na anakwenda kwa waganga wa kienyeji na kutumia uchawi ili kupata uongozi huyo si mkristo, tena hana tofauti na Simon mchawi.

  Na ninaongeza kusema, kama kuna wachungaji wanajiita wameokoka na wanahalalisha ushoga,hao wala si kanisa la kristo ni kitu kingine tu.

  Bila shaka nilisema tena kuwa mengi ya mambo ambayo mleta mada kayasema hapa chanzo chake kikubwa ukiangalia vizuri ni changamota ya umasikini.

  -Kusisitiza sana utoaji wa sadaka na zaka na malimbuko tatizo ni umasikini

  -Kutaka madaraka chanzo chake ni umasikini ambao unazaa tamaa ya mali na kutaka heshima

  -Kukataa kupewa uhamisho chanzo chake ni umasikini ambao humfanya mtu akatae kuacha vinono vya mahali alipo na kwenda kwingine.

  -Kuwa karibu na wanasiasa chanzo chake ni umasikini, maana kinachotafutwa kwa wanasiasa ni hela

  -Kupendelea na kujali sana wenye navyo/wenye pesa chanzo chake ni umasikini, ambapo mtu hutaka favor toka kwa huyo mwenye navyo

  Haya mambo yapo kweli na yalikuwepo hata kwa wanafunzi wa Yesu, bila shaka mnajua ishu ya kugombania ukubwa kati ya thenashara, na ishu ya mmoja kukaa mkono wa kuume na mwingine wa kushoto.

  Na mambo haya ndo mleta mada anataka tujiulize tumekosea wapi au chanzo chake ni nini? Na lengo lake la kuleta hii mada hapa ni kutaka tujibu hilo swali au tujue chanzo cha hayo mambo na ikiwezekana tutoe suluhisho.

  Sasa kama mnataka tuache kujadili haya ila tujadili mambo ya mafundisho potofu, mambo ya kuhalalisha ushoga, n.k, basi semeni twende huo mwelekeo.

  Lakini mambo haya yaliyoletwa na mtoa mada si mambo ya kusema ati kanisa liko uchi, kanisa limekuwa la shetani.

  Na kujadili hayo ya kuruhusu ushoga, hata kwenda kwa waganga kutafuta uongozi kanisani lazima tujiulize sana tunaongelea kanisa lipi. Maana hayo hayahitaji uamsho bali kuhubiriwa neno la msingi la wokovu. Wanaofanya hayo wala hawakusanyi pamoja na kristo na wala hawako upande wa kristo

  Asanteni

 8. Ndugu yangu Lwembe,

  Kila mtu ana miwani (lenses) yake anapoliangalia Kanisa la Kristo…! Kanisa la Kwanza lilianza na waumini 120 tu pale Yerusalam…….Je ilichukua muda gani kusambaa katika Dola ya Rumi…..angalia umbali tu….! Angalia Impact yake kwa jamii….! Angalia impact yake Ulaya……ilivyabadili Ulaya toka Upagani….na kufanya kuwa Ulaya nzima kuongoka….! Kila mtu anayesoma Historia awe mkristo au mpagani anashindwa kabisa kukimbia Ukweli Kanisa linaposimama IMARA NA KUWA NURU NA CHUMVI YA ULIMWENGUNI……!

  Angalia tena baada ya Kanisa kufikia kilele chake na kuangaza kuingiza mafundisho ya Kipagani….kishirikina…….kuji accomodate na Urumi…..Kanisa likamezwa na Kugubikwa na mapokeo makubwa…! Bila Mungu kuwainua kina John Hus…..Wycliffe…….ambayo waliishia kuchomwa moto kwa kutaka tu Biblia iweze kusomwa na kila mtu…..ni lile “linajiita Kanisa la Kristo” ambalo lilizuia maneno ya Kristo…..! Je Mungu asingesimamisha watu kama akina Martin Luther na angalau kuirudisha Biblia mahali pake Kanisa Lingekuwa wapi…..?

  Tuseme nini kuhusu hali ya kanisa kipindi cha Industrial Revolution….! Ilikuwa ni uozo….! Bila Mungu kumsimamisha John Wesley na ndugu na kuwasha moto mpya na kuleta uhai ambao ulivuka hadi America (USA) Marekani isingelifika hapa ilipo leo…..!

  Hebu angalia Yesu mwenyewe anatumia maneno gani kulionya Kanisa lake…..KUMBUKA UMEACHA WAPI UPENDO WAKO WA KWANZA…..! Kumbe kanisa linaweza kuacha njia….linaweza kuacha UPENDO WAKE WA KWANZA…..!Sehemu nyingine analionya Kanisa lake kwa kusema….”UNAO HUKO WASHIKAO MAFUNDISHO YA BALAMU…..YEYE ALIYEMFUNDISHA BALAKI ATIE KIKWAZO MBELE YA WAISRAEL ILI WAVILE VITU VILIVYOTOLEWA SADAKA KWA SANAMU NA KUZINI….” Kumbe kanisa linaweza kupokea mafundisho potofu……kumbe kanisa linaweza kupokea sadaka kwa sanamu……kumbe kanisa linaweza kufumbia macho uzinzi…..! Kwangu mimi inaonyesha wazi Kanisa linaweza kuacha njia! Haya ni Maneno ya Yesu Mwenyewe……! Yesu analiambia TUBU NA USIPOTUBU NAJA KWAKO UPESI…! Je kanisa likikataa kutubu halijaacha njia….?

  Ngugu yangu Lwembe kwa wengine Kanisa la nyumbani liko imara…! Unapoona Kanisa linawakaribisha watu wanaotuhumiwa na ufisadi kufungua makanisa….badala ya kuwakemea….huko sio kuacha njia…? Unapoona makanisa yanakuwa matupu ili kukimbilia Loliondo kunywa kikombe cha Babu hiyo sio ishara kanisa linafundisha mafundisho manyonge……! Unapoona waumini wanafurika kuondolewa laana ya mzaliwa wa kwanza……..laana ya mababu…. kuingizwa kwenye malango….kana kwamba Injili iokoayo imeshindwa kuondoa Laana…..Kana kwamba Lango la Kristo limeshindwa kuwakomboa….kama haya si mafundisho ya Baalamu ni nini hasa…! Unapoona watu wanafurika makanisa jumapili…lakini rushwa bandarini….mahakamani……ofisi za ardhi……Police…..inazidi kuongezeka kila leo….unashindwa kujiuliza Wakristo wako wako wapi…..! Unaposikia tuhuma mbali mbali za uzinzi kwa watumishi……lakini hakuna anayeshtuka…..je huko si kuacha njia…..? Unapoona Mitume…..Manabiii……Makuhani…..wanaota kama uyoga lakini impact yake kwa waumini ni sifuri……Je hujiulizi maswali…?

  Lwembe, ndugu yangu……inategemea umevaa miwani gani kuliangalia Kanisa…….Yesu alipokuwepo Ulimwenguni wale ambao ungelitegemea wafunguke macho na kumtambua walishindwa kabisa…..sababu walivaa miwani ya dini……! Yesu alisema…..KUSIKIA MTASIKIA, WALA HAMTAELEWA…..KUTAZAMA MTATAZAMA…..WALA HAMTAONA…..MAANA YA MIOYO YA WATU HAWA IMEKUWA MIZITO…..NA MACHO YAO WAMEYAFUMBA…..!

  Ubarikiwe….fanya kazi ya mtumishi wa Injili….!

 9. Lwembe,

  Nakubaliana na wewe kabisa kuwa inawezekana mada haina vigezo inajadili nini….au tumeshindwa kujua ni nini tunazungumzia kama mleta mada alivyozungumzia….!

  Kanisa la Kristo ndani ya Biblia…..na hata nje ya Biblia ukiangalia historia huwa linaacha njia ya Yule aliyelianzisha……Ndio maana Paulo aliandika Nyaraka za kuonya na kukumbusha nini Kanisa la Kristo linatakiwa lifanye! Huu ni ukweli usiokimbilika ulioko ndani ya Biblia.

  Kanisa la Kristo huwa linaweza kupotoka kwa mafundisho ambayo hayajajengwa Kabisa toka kwa Kristo…..Msomaji mzuri wa Agano Jipya ataona hilo, Kuanzia Paulo alipoanza safari yake zake tatu za kimissionari, Kila alipoanzisha Kusanyiko la waumini (Kanisa) hapo hapo kuna watu walikuja na kuleta mafundisho mengine mbadala…..Ndivyo ilivyokuwa kwa kanisa la Wakorintho….ndivyo ilivyokuwa kwa Kanisa la Epheso……ndivyo livyokuwa kwa Kanisa la Wagalatia……na Ndio maonyo Katika yale Makanisa Saba ya Asia……..Na ndivyo ilivyo leo….!

  MsomaJI wa Historia ya Kanisa….kutoka Kanisa la Kwanza Mpaka leo anaona pattern ni hiyo hiyo…! Kanisa linaweza kuwa mbali na Kristo aliyelianzisha na kuingiza au kukaribisha mafundisho ambayo sio Kristo aliyofundisha…! Na kuingiza kitu kingine Kabisa…..Na Kwa neema ya Kristo Mwenyewe huwa anainua Watumishi wake kulirudisha Kanisa kwenye Mstari unoatakiwa! Ndio Maana kuna UAMSHO ( REVIVAL)

  Ndugu yangu Lwembe, nashangaa mno wanaoukataa UKWELI huo ulioko ndani ya Biblia na Wa Kihistoria pia……….! Niko Marekani napoandika Waraka huu….Kila Mkristo aliye hai hapa Marekani anasema Mungu atutembelee upya….! Licha ya cheche ndogo za moto hapa na pale makanisa mengi ya Ameriika preaching ni Liberal! Ukiona Kanisa linamtawaza shoga kuwa Askofu….hiyo ni changamoto ndogo? Huko sio kuacha Njia…..? Waumini hata wanaojiita Wameokoka wanapoyumba hata kusema Ushoga ni dhambi….maana yake nini….? Ni Kanisa kuwa Imara kweli…?

  Labda nikipata nafasi nitaandikia kuhusu vipindi vya Kanisa kihistoria….ambapo kanisa la Kristo lilikuwa JUU MNO KIROHO NA KUUBADILI ULIMWENGU…! Na Ni nyakati gani Kanisa la Kristo lilimezwa na dunia na kukumbukwa na ideology au mafundisho ya mwanadamu kinyume kabisa na yale yaliyomo ndani ya Biblia…..Na Mungu kwa Neema yake akaleta UAMSHO…..! Kanisa lingekuwa wapi leo katika KARNE HII BILA BWANA KULITEMBELEA UPYA AZUSHA……baada ya miaka mingi ya ukavu wa kiroho na kukataa nguvu za Roho Mtakatifu….?

  Lwembe ndugu yangu….. inahitaji Mungu kufungua ufahamu wa Kiroho kufahamu haya…….!

 10. Sungura,
  Ingesaidia zaidi iwapo ungetuelimisha moja kwa moja kuhusu ‘Kanisa la Kristo ni kitu gani’ ili michango inayotolewa ipanuke zaidi, kuliko kuendelea kulalamika huku ukiuficha ukweli kama tunacheza karata vile!

  Kanisa kuwa ovu si jambo la ajabu kama mnavyotaka kulifanya. Uovu ni kuiacha Njia ya Bwana na kuzifuata akili za kibinadamu na hekima yake, ule Ujuzi wa Mema na Mabaya, ambavyo huishia katika mauti! Nalo kanisa linalo onywa ni hilo linalo zama katika uovu nalo halijui, hilo ndilo linalorejezwa, likikataa kurejezwa basi linakuwa ni sinagogi la Shetani! Ufu 2:9, “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.” Na pia ujumbe kwa Kanisa lililopo Filadefia, Ufu. 3:9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo.”

  Labda mkituelimisha kuhusu hilo “Kanisa la Kristo ni kitu gani” katika uhalisi wa mwenendo wa makundi yetu ya Kikristo leo hii, inaweza kusaidia kutuweka sawa ili tusije tukawa tunaongelea kitu ambacho hakipo, bali sisi pamoja na mleta mada, tukawa tunang’ang’aniza!

  Gbu!

 11. Tukisoma ktk Mathayo 16:18 tunaona Jesus akimtel Petro juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milangu ya kuzimu hautalishinda hii ni pale alipokiri kwa uhakika kuwa wewe ni Mwana wa Mungu!Yesu yule hajabadilika ni Yeye yule jana na hata milele na c kwamba nguvu zake zimepungua!Mpendwa Lwembe umeuliza tutalitambuaje kanisa imara? Just Simply kwa Matunda yao.Neno likikaa kwa wingi ndani yako hakuna ngurumo ya Ibilisi itakubabaisha.ukisoma pia Yohana 8:12 inaeleze Jesus ndiyo nuru ya Ulimwengu amfuataye yeye hatakwenda kamwe gizani bali atakuwa na nuru ya uzima na nuru cku zote ndiyo inayokimbiza giza so ramani inasomeka Yohana 12:46.Na aendae gizani hana ramani Yohana 12:35-36 so Lwembe kama umesimama na nuru utawatambua waliitalo jina hilo kisanii!Na huweze kuwatambua kama haupo ndani ya ramani soma filipi 2:9-11 so ukiwa ndani ya Ramani utakuwa imara.Mambo mengi ni changamoto tu!na ukijengwa ktk misingi ya Kristo lazima Uwe imara!Mungu akubariki mtoto wa Mungu Lwembe.

 12. Ndio maana kuna watu hapa nimewauliza,kama wanasema kanisa lina uovu, au ni la shetani, je na wao ni sehemu ya hilo kanisa ovu na la shetani? Au wao siyo kanisa? Na kama wao siyo kanisa wamepata wapi mamlaka ya kulisema kanisa ambalo haliwahusu?

  Wakati wa Paul kanisa la Korintho watu walifanya dhinaa isiyokuweko hata kwa mataifa (mtu kulala na mke wa baba yake), lakini hiyo bado haikulimaliza nguvu kanisa.

  Siyi namsubiri Mabinza ajibu swali ulilomuuliza ili nimkumbushe kitu.

  John Haule afadhali nawe umenena, wengine tukisema kuwa hizo ni changamoto tu,kanisa liko imara,tunaambiwa tumechanganyikiwa kiufahamu na ni ‘coward’.

  Sijui ni shetani yupi huyo anayeweza kulishinda kanisa hadi limekuwa ovu na likawa mali yake!

  Na wengi wa wanaosema kuwa kanisa limekosea, ukifuatilia sentensi zao utagundua kwamba wao wanajiweka pembeni.
  Huwezi kukuta wanasema ”kanisa tume….”, ispokuwa ”kanisa lime…”. Kwa maana ya kwamba wao hilo kanisa haliwahusu.

  Mabinza nilimuuliza kama yeye si wa imani ya Jesus only, aniambie alibatizwaje, lakini amekwepa kunijibu. Maana yeye kasema kubatizwa kwa jina la Baba, na la mwana, na la Roho mt. ni kulihalifu neno la Mungu.

  Mtu kuhubiri mafanikio hakuwezi kulifanya kanisa likawa halina Mungu ndani yake, watu kutetea wachungaji wao kama wapo wanaofanya hivyo hakuwezi kulifanya kanisa lisiwe na Mungu ndani yake. Hizo ni changamoto tu za kawaida.

  Upendo wa wengi kupoa hizo ni changamoto tu bado, kama ilivyokuwa changamoto ya ubaguzi wa wajane wa kiyunani kwa kanisa la kwanza, hakukulifanya kanisa lipoteze mwelekeo.

  Labda kama hatujui kanisa la kristo ni kitu gani.

 13. Wapendwa hizi tafsiri zenu za maandiko….hapana……kwa kweli ujuzi uleta majivuno na kuanza kujiesabia haki kwa haki yake yenyewe,

  Tangu lini Kanisa likawa la shetani…….Hizi changamoto zipo toka kanisa la kwanza lakini Kanisa sio shetani…. hakuna jipya yote yameandikwa kuwa yatakuwepo ……toka Mdo-Ufu

  kina Dema walikuwapo …..mitume/walimu/nabii wa uongo walikuwepo….wezi wa matoleo walikuwepo…..wachawi kwenye makusanyiko walikuwepo……..kondoo kumbe mbwa mwetu walikuwepo…..Yote yapo kama unabii wa mandiko ulivyo……

  Tunachopaswa kukiendea ni Toba na kushinda…
  Ufu2.16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu

  Hiyo hapo ndio zamu ya kusimama kwa ajili ya hao wengine ili nao waokolewe ktk hilo kusanyiko.

  Tuacheni kujitia wivu wa Mungu ambao sio…….unafiki …… laumu…..

  Moyo ufanywe imara kwa neema.

 14. Mabinza,
  Shalom kaka. Umesema kanisa lina UOVU. Watu waliokoka bado wanaweza kuwa na kitu kinachoitwa OUVU? Unaposema kanisa una maana gani? The whole entity as TAG, SABATO, RC, KKKT etc? Au muungano wa entities kama hizo tajwa, zaweza kuwa kanisa? Na kama ni ndiyo/hapana ni kwa namna gani?
  Ubarikiwe na Bwana

 15. Wapendwa,

  Kiukweli, kujikwaa kukubwa kwa Kanisa ni kule, KULIKATAA NENO LA MUNGU! Kanisa lipo uchi, lakini linakataa na kusema kuwa halipo uchi! Kwanini?

  Chanzo cha kila tatizo katika Kanisa ni “UOVU” kanisa lenye uovu ndani yake ni la shetani, kwa hiyo Mungu hashughuliki nalo! MWENYEKUPOTEA MARA ZOTE NI YULE ASIYEIJUA NJIA LAKINI HUJUA KUWA ANAIJUA!

  Meth.4:19 inasema, “19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae.” Tulitiini NENO LA MUNGU LOTE tupone!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 16. Mpendwa Tumaini,
  Unajua, shauku yetu kuu ni kuwa katika hilo KANISA LA KWELI, hilo ambalo ni IMARA, Sasa katika mkanganyiko huu wa makanisa zaidi ya elfu kumi, na yote yakijitangaza kuwa hapo ndipo alipo Kristo, hebu tusaidiane, inakuwaje hapo, unatumia kigezo gani kulibaini hilo Kanisa Imara?

  Gbu!

 17. Wapendwa watoto wa Mungu naamini mijadala hii ipo hapa kwa nia njema kabisa!Na itapendeza saana kama kila mmoja akathamini mchango wa mwenzake hata kama una hoja ya kukosoa basi tusiweke itikadi zetu just tutumie dira yetu Neno!Naamini kabisa kila mmoja anania njema kabisa ktk hili na c swala la Ushabiki!Maana dhumuni letu ni kujenga mwili wa Kristo!Naamini kabisa kwa wapendwa ambao wapo vizuri kiroho walio cmama na Neno ambao ndiyo uzima uimara lazima utakuwepo!Shida inakuja kwa wale wasanii wanaojiita kanisa huku hawana Nguvu ya Mungu ndiyo mambo hayo yapo!Mpendwa Sungura katoa mfano hivi mtu aliye vizuri kiroho atakwenda kwa mganga?Huoni hao ni wasanii?Cdhani ktk hili kunakupeana moyo au kuwa mnafiki!Maana Hakuna nguvu ipitayo nguvu ya Mungu!Haiwezekani ukamtumainia yeye 100% then ucwe imara!KANISA LA KWELI LIPO IMARA BT LA HAWA WASANII LINAKULA JOTO YA JIWE! Wapenda tucmame na Huyu Mungu wetu tuache michanganyo. Mungu awabariki wapendwa.

 18. Mpendwa JWM…..naendelea kuliangalia Kanisa la Leo…….

  KANISA LA LEO LINATOA NINI KWA JAMII YETU INAYOTUZUNGUZA?

  Petro akiwa na Yohana alimuuliza yule kiwete nje ya hekalu…” MIMI SINA FEDHA WALA DHAHABU…NILICHO NACHO NDICHO NIKUPACHO” Hii ni kanuni ya maisha, huwezi kutoa usicho nacho…..huweza kwenda Benki ukatoa zaidi ya pesa yako kumpa mwingine……

  Kanisa la leo katika jamii yetu unaona ni nini inachotoa kwa jamii yake….sana sana tumeipa jamii yetu mapambio…..! Na Bwana Asifiwe tu…! ndio hicho watu wanachotutambua nacho leo…! Waumini ni “hai” Jumapili…lakini waangalie kuanzia Jumatatu…mpaka Ijumaa…! Humuoni kabisa Kristo katika maisha yao…! Sio waaminifu katika biashara zao…….Ndoa zao hazina tofauti na wapagani wasiomjua Kristo…! Unaogopa kufanya biashara na mlokole! Angalia maisha ya utakatifu….yamekuwa bidhaa adimu kuanzia mimbarini hadi kiti cha nyuma makanisani…! Watumishi wana tuhuma za kutembea na waumini….Ni Nani atakayemfunga ngo’mbe Kengele? Tumesahau kabisa hukumu itaanza ndani ya Neno ya Nyumba ya Mungu!

  Petro na Yohana walimuuliza yule kiwete….”TUTAZAME SISI” Je kanisa la leo linaweza kuiambia jamii iliyotuzungka tutazame sisi….? Je jamii ikiyaangalia maisha ya sisi waumini nje ya kanisa inaweza kumuona Kristo…..? Inaweza kuona maisha yetu yakimtukuza Kristo…..? Sana sana watasikia mapambio ya “nibebe nibebe” “panda mbegu upate baraka” !

  Hatuwezi kabisa kuibadili jamii yetu kama watu watakapotuzama sisi na wasimwone Yesu….! Ni Yesu tu aliyejaa ndani ya maisha Yetu anayeweza kuleta uponyaji wa Kweli ndani ya magonjwa ya kila aina katika jamii….iwe maradhi ya mwilini…au rushwa….ufisadi….dhuluma na kadhalika….! Lakini kama watu wataliangalia Kanisa na kuona halina tofauti na wao….sana sana ni mapambio….. kesi za waumini mahakamani…..ndoa za wanaomkiri Kristo zivunjika……na huku tunaendelea na matamasha ya nyimbo …. basi tutakuwa tunatatwanga maji kwenye kinu….!

  Kanisa haliwezi kuibadili jamii kama haliimuhubiri Yesu wa Biblia! Yesu anayehubiriwa katika mimbari nyingi si yule wa ndani ya Maandiko…! Ni mwingine Kabisa……! Yesu wa kweli anabadili maisha na watu wanayaona….sio siku ya jumapili tu bali kila siku….! Huyu ndiye atakayebadili jamii yetu leo…..wala sio mapambio na Bwana asifiwe……

  Labda hata sisi mapepo wanatuuliza ….”Yesu tunamjua na watumishi wa Kweli wa Mungu tunajua wanahitajika kuhubiri nini …….je hawa watumishi wa leo wanamhubiri Yesu yupi.

  Kwa kifupi kanisa lilojaa utakatifu…..litahubiri Utakatifu….na kufanya waumini watembee katika utakatifu…..Kanisa lilojaa maombi….litawafundisha watu kuwa waombaji…….Kanisa lilojaa maneno ya Mungu litawafundisa watu kusimama katika maneno ya Mungu…… Kanisa litatoa kile lililonacho…..Je Kanisa la leo linatoa nini…..? Angalia jamii yetu….!!! Mungu na atusaidie na kuturehemu…..!

 19. Wapendwa,

  Hebu niendelee kidogo nilipokomea…….Kanisa lilipotea na kuacha njia…….

  – KANISA LA KRISTO LINAPOKUWA NI MALI AU HIMAYA YA MTU……

  Sina haja ya kunukuu ndani ya Maandiko kuonyesha Kanisa au kusanyiko la watu wa Mungu ni mali ya Kristo! Yeye ndiye aliyewanunua waamini na kuwafia…ni yeye aliyewajaza Roho Mtakatifu……na ni Yeye anayewatuma waende ulimwenguni kutangaza ujumbe wake….!

  Angalia Paulo alivyosema Kwa Kanisa alilolianzisha mwenyewe aliposikia kuna baadhi ya waumini wanasema mimi ni wa Paulo….! “Basi Paulo ni nani”? ……Yeye ni Muhudumu tu…..! Ukweli ni kwamba ni Paulo ndiye aliyeanzisha kanisa la Korintho…Lakini hakutaka Kanisa litambulikane kama mali yake! Au kama himaya yake…! Kama Kampuni yake…..! Kama Biashara yake….! Paulo aliuliza mashabiki wake “Je ni Paulo aliyewafia…? Ni Paulo aliyewaokoa?

  Turudi kwenye Kanisa la leo nyumbani…..Kanisa limekuwa na “washabiki” kuliko wa Simba na Yanga! Kuliko Chadema na CCM! “Mimi wa Ndegi” “Mimi wa Mwingira” “Mimi wa Kakobe” ” Mimi wa Upako Na Ngurumo” ….Waumini wengi ni “damu damu” na “Mtumishi” wanaweza kumtetea “Nabii” , “mtume” au “mwalimu” kwa ushabiki mkubwa kuliko Yesu aliyewafia msabalani! Wanaweza kutetea mafundisho ya “mtumishi” kwa hamasa kubwa huku mate yakiwatoka na kujaa mdomoni Kuliko Neno la Mungu! Na jambo la kusikitisha “Watumishi, Manabii, na Wachungaji na Mitume wa leo” Hawakemei jambo hili! Waumini wengi wako tayari kumfia “mtumishi” kuliko kumfia Kristo na Neno lake!

  Kwa kifupi mpaka watumishi watakapofunguka na kutambua wao ni watumwa tu wa Kristo…wao ni sehemu tu ya mwili wa Kristo….wao ni viungo tu…..! Watakapokataa kukweza…..kuabudiwa…..Na waumini nao pia watakapofunguka macho na kutambua kwamba mtumishi ni mtenda kazi tu katika mwili wa Kristo….ni chombo tu ambacho Mungu amependa kukitumia, kinaweza kukataliwa pia, watumishi ni vyombo dhaifu tu kama vyombo vingine, vinahitaki kusaidiwa na kuombewa tutaendelea na huu ugonjwa wa “bongostar” “ma- celebrities” katika kanisa…..!

  Ni nani atakaye weza kutuondoa katika “INJILI HII YA USHABIKI KWA WATUMISHI” Isipokuwa watumishi wenyewe? Mpaka wao wenyewe wakapo sema “Mwingira ni nani? Kakobe ni nani? Mchungaji ni nani! …..”MAANA SISI TU WAFANYA KAZI PAMOJA NA MUNGU……NINYI NI SHAMBA LA MUNGU…….! BASI MTU YEYOTE ASIJIFIE WANADAMU……KWAMBA NI WA PAULO AU APOLO AU KEFA…..NANYI NI WA KRISTO NA KRISTO NI WA MUNGU (1 Cor 3)

 20. Ndugu yangu JWM na wengine mliochangia hoja hii, hebu na mimi ninene machache,

  Kwanza nashukuru kwamba kuna baadhi ya waumini ambao wanaona kuna kitu ambacho hakiko sawa katika Kanisa la Mungu leo na labda hapa kwetu nyumbani Tanzania ( Naamini hazungumzii kuhusu dhehebu fulani au kundi fulani- Bali Kanisa la Mungu kwa ujumla tukimaanisha waumini ambao wameitwa na Bwana na kuwa hai kiroho na ambayo wametawanyika katika madhehebu mbali mbali)

  Huitaji kuwa na karama ya unabii unapoliangalia kanisa leo na kulilinganisha na maneno ya aliyeilianzisha Kanisa hasa aliposema ” NINYI NI NURU YA ULIMWENGU…..NINYI NI CHUMVI YA DUNIA” na alipoendelea kusema ” NURU YENU NA IANGAZE MBELE YA WATU” ! Huoni NURU ya Kristo ikiangaza leo….si kwamba NURU hiyo imezimika kabisa, kwani haiwezi kufa kabisa kwa ahadi ya Aliyelianzisha! Ila hali halisi inaonyesha wazi NURU ya Kanisa imefifia mno! tena sana! Imekuwa kama Kibatari katika giza nene…! Huwezi kuamini hili ndilo lile kanisa kipindi chake cha mwanzoni ilitikisa dola ya Kirumi na lilipoingia Amfipoli na Apolonia hadi Thesalonike watu walisema ” WATU HAWA WALIOUPIUNDUA ULIMWENGU WAMEFIKA HUKO NAKO” ( Matendo 17)

  Ukiliangalia kanisa la leo hasa kwetu nyumbani Tanzania, ni kwamba badala ya Kanisa kuubadili ulimwengu, ni ulimwengu na jamii inayotuzunguka ndio inalibadili Kanisa! Tena kwa haraka mno! Kuanzia mimbarini hadi kwa waumini tunaangalia jamii inataka nini na ndicho hicho hicho tuchachokihubiri na kufundisha,,,,! Hebu angalia vigezo vifuatavyo;

  – INJILI YA MAFANIKIO: Jamii ya leo sifa na thamani ya mtu ni wingi wa mali aliyo nayo……”hapendwi mtu wala huheshimiwi katika jamii, bali inapendwa pochi yako tu, na sifa yako katika jamii itatokana na ukubwa wa pochi yako” Na kanisa la leo limeamua kutumia kigezo hicho! Kanisa limepindisha Maandiko na kulazimisha mafanikio ya mali na vitu kuwa kama ndicho au jambo la msingi ambalo Kristo aliitia kanisa! Maandiko yanapindishwa na kulazimisha kusema ambacho jamii inataka kusikia! Unashindwa kabisa kuona Injili ya Mafanikio kwa Yesu mwenyewe na hata katika Nyaraka za Paulo! Si kwamba Mungu hataki waumini wake wafanikiwe kwa mali na utajiri, la hasha…ukitanguliza Injili ya mafanikio….ni kama kutanguliza mkokoteni mbele na kumfunga Punda nyuma……hutafikisha mzigo wako! Kanisa la leo linafanya makosa hayo! Kwa kifupi baadhi ya watu wengi leo wanamfuata Yesu kutafuta muujiza wa kula makate na samaki tu kama ilivyokuwa huko nyuma! Na Yesu alipoona kundi linazidi kufuata mkate na samaki alisema ” MSIKITENDEE KAZI CHAKULA CHENYE KUHARIBIKA…BALI CHAKULA KIDUMUCHO AMBACHO MWANA WA ADAMU ATAWAPA (Soma Yohana sita sura yote)
  Hivyo watumishi wengi hawako kumtumikia Yesu wa Biblia….bali matumbo yao tu! Unapoona Mtumishi anaendesha Hummer katika nchi kama Tanzania yenye lindi la umaskini, gari hiyo hata Marekani imeacha kutengenezwa kwa gharama ya uendeshaji unaona wazi ni upofu wa Kiroho….hasa unapoangalia waumini wengi hata mlo wa kila siku ni tendo la muujiza! Kwa mimi huku ni kukejeli baraka za Mungu…

  Kwa kifupi huwezi kupigwa mawe kwa kuhubiri Injli ya mafaniko! Hata kidogo! Ila utavuta magugu na makapi mengi ndani ya Kanisa…..

  – INJILI NYINGINE- MAFUNDISHO POTOFU! YENYE MFANO WA NURU! Kanisa la leo limejaa mafundisho mengi tena meng mno ambayo ambayo yamejengwa katika sensationalism/ emotionalism lakini hayako kabisa ya ndani Biblia kabisa! Hebu angalia hofu ya Freemason ndani ya kanisa! Hofu ya kulogwa ndani ya Kanisa! Kuchukulia “nyota ya bahatI” ,”malango” “mzaliwa wa Kwanza” ” shetani ameisha kufa” makanisa mengine yamejaa “misukule” badala ya waumini waliiokoka wakitembea katika utakatifu na kumuishia Yesu! Watu wanataka kuona “msukule” aliyerudi kuzimu kuliko Yesu anayeokoa!
  Hebu angalia BABU wa Loiliondo alivyovuta wengi ndani ya Makanisa! Usingetegemea kabisa imani ya wengi ni kama rangi ya chokaa iliyopakwa leo! Mvua kidogo za rasha rasha zilifichua rangi halisi wa waumini wengi! Wako ndani ya kanisa si kumfuata Yesu…..bali Miujiza! Je Yesu alisemaje kwa wale waliofuta miujiza tu? Hebu Tusoma Biblia kwa mtazamo mpana jamani! Paulo alisema “NASTAAJABU KWA KUWA MNAMWACHA UPESI ALIYEWAITA NA KUIGEUKIA INJILI NYINGINE……WALA SI NYINGINE LAKINI WAPO WATU WAWATABISHAO NA KUTAKA KUIGEUZA INJILI YA KRISTO, LAKINI IJAPOKUWA SISI AU MALAIKA WA MBINGUNI ATAWAHUBIRIA INJLI YOYOTE ISIPOKUWA ILE TULIYOWAHUBIRIWA NA ALANIWE”
  Kama kanisa linahubiri ambacho si Yesu wala mitume walichohubiri unategemea nini? Utaona matokeo tofauti kabisa na yale yanayoletwa na INJILI YA KRISTO………..

  Kwa leo nitakomea hapa…..nitaendelea kukuletea nini cha kufanya Kanisa la Mungu linapokwama…….Sisi si wa kwanza kupita tunapopapita leo! MBARIKIWE…

 21. Wapendwa,
  Kwamba Kanisa, kuna mahali limekosea, hiyo ni kweli isiyopingika, hivyo kwamba, KANISA: TUMEKOSEA WAPI? hii ni changamoto ambayo inatuhitaji kuukusanya ujasiri tulionao ili kuweza kulitazama jambo hili katika kuutafuta Ukweli wa hali ya Kanisa ili kuona iwapo inawiana na hicho kipimo, kama tunacho, au la!

  Ishara ya kwanza inayomdhihirisha mtu aliyekosea ni kutokujitambua. Hata kama mtu huyo hatajitambua kuwa amekosea, bado kwa kule kukosea kwake atakuwa ametofautiana na mazingira yanayomzunguka licha ya kuyalazimisha kwake, ndio atakuwa anazidi kuyaharibu kama si kuharibikiwa mwenyewe!

  Kauli za Sungura na Tumaini Nelson, kwamba “Kanisa liko Imara”, ni kauli zenye kutia moyo lakini si halisi. Naye mtu anayejiridhisha kwa jambo ambalo si HALISI, huyo anawakilisha mtu anayeuogopa ukweli (a coward) na aliyechanganyikiwa kiufahamu, ndipo huyo huwa ni sehemu ya huko KUKOSEA, kwa hilo Kanisa!

  Lakini tunapozungumzia ‘KUKOSEA’, iwapo tutachukua muda kulitafakari jambo hili la kukosea, hata tukajiuliza, inachukua nini hata mtu awe amaekosea? Jibu rahisi na lisilobadilika ni kwamba Kukosea ni Kufanya tofauti na Maelekezo, aidha kwa makusudi ama kwa kudanganywa na ama kwa ujinga!

  Ndipo ili yeyote aweze kubaini KUKOSEWA kwa chochote kile, ni lazima awe na kipimo kwanza, ambacho katika hili tutasema awe na hayo Maelekezo au INSTRUCTIONS. Basi tunapolitazama Kanisa katika hali yake, ni lazima tulipime mwenendo wake kwa kipimo cha Biblia, inalielekeza litembeeje?

  Kwa mfano, ukiwauliza akina Tumaini na Sungura, hilo kanisa mnalosema liko imara na linasonga mbele li wapi leo hii? Kama ni wakweli kwa nafsi zao, basi kanisa hilo ni lazima liwe ni hilo kusanyiko lao, hilo ndilo Mwili wa Kristo, vinginevyo walipaswa waondoke humo kama si wanafiki! Pia madhehebu mengine, nayo huamini hivyo kuhusu makusanyiko yao! Au ndugu Lenda unasemaje kuhusu jambo hili, Je, Wasabato si Mwili wa Kristo? Na iwapo katika Mwili huo kiungo kimojawapo kikawa ni Katoliki, je, Mwili huo hautaumwa kweli? Ndipo tukiyatazama madhehebu yetu, idadi yake yaweza vuka laki moja duniani kote, na kila moja hujihesabu kwamba ndilo Kanisa, ule Mwili wa Kristo; huu ndio ukweli lakini ni ukweli usio KWELI! Hauwezi ukawa na makundi hayo yaliyo tofauti katika mienendo yao, na yote yakikiri kufuata Maelekezo ya Biblia, na yote hayo yakawa yako sahihi katika tofauti zao. Aidha huyo anayefanya tathmini ya jambo hilo atakuwa hajui anachokifanya au ni Muongo tu wa kawaida ya waongo! Basi tunda la KUKOSEA kwetu ndiyo haya madhehebu yetu.

  Kutoka katika tunda hilo la ‘madhehebu’, humo ndimo twaweza kuipata ‘mbegu’ inayoyazalisha hayo, ile ‘mbegu ya hitilafu’! Mbegu hii ni pando la Ibilisi ambalo kazi yake ni kuleta hitilafu katika makusanyiko kwa kuyatafsiri Maelekezo aliyoyatoa Mungu kwa Kanisa lake, akishawishi kutukuzwa kwa ujuzi binafsi ndani ya waaminio, akili zao, na hivyo kundi kuishia nje ya Maelekezo yaliyokusudiwa.

  Mungu katika Mithali 3:5 analiambia Kanisa lake, “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe”; hapa ndipo kilipo kiini cha matatizo yanayolikumba Kanisa. Wakristo wengi wamenasa katika “utukufu” wa kutumia akili zao. Unapowaambia usitumie akili zako katika mambo ya Mungu, wao hukuona kuwa wewe ni mjinga usiyejua lolote! Ndipo mwingine ungemsikia akifoka, “kwani sisi ni chimpanzee? Mungu amesema Usizitegemee akili zako hakusema usizitumie!” Akijaribu kulazimisha jambo la kutumia akili kinyume na agizo la Mungu!! Unapolitazama jambo hilo huonekana ni lenye busara sana, nadhani ndio maana hawaishi kutoa mifano ya jinsi hiyo kulingana na hekima yao inavyowaongoza. Lakini kabla ya kuyashabikia hayo walipaswa waichukue hiyo mifano yao na kuipima ktk Neno la Mungu ili wajihakikishie usahihi wake kwanza, ndipo waitumie au waiachilie mbali. Bali uongozi wa mwili hauna uwezo huo, akili za kawaida hazina uwezo wa kuyapambanua hayo; na utashangaa kwamba huyo chimpanzee wanayemtolea mfano, ana “akili” kuwashinda wao! Mtazame chimp huyo ktk siku za Nuhu, aliingia ndani ya Safina, na hao waliojidhania ni wenye akili, wangapi waliangamia? Hata leo hii, Je, umewahi kusikia au kumuona chimp ambaye ni ‘shoga’? Lakini ni makanisa mangapi kwa kutumia akili yanawakumbatia mashoga? Mengi tu, na kwa kutumia akili hiyo hiyo, yooote yatawakubali! Maana Maandiko yanasema katika ujio wa Kristo, hali itakuwa kama ilivyokuwa Sodoma na Gomora, sasa wengi kwa kutumia akili, huidhania hali hiyo kuwa itakuwa huko nje, bali ni makosa, hali hiyo itakuwa ndani ya kanisa, Sodoma na Gomora itakuwa ndani ya kanisa, kama mnavyoiona ikiingia kwa kasi!!!

  Katika hayo makundi yetu yanayovuka laki moja kwa idadi, hayo yanawakilisha TAFSIRI LAKI MOJA tofauti za jambo moja, Neno la Mungu! Yaani kila mmoja akitumia akili zake!!! Unaona, Biblia inapokuambia usizitegemee akili zako, ina maana kwamba inajua kuwa unazo akili, ndio maana inakuambia usizitegemee hizo. Sasa wewe unapotafuta kuchomwa sindano ya kukutoa hizo akili ili uwe kichaa ili ujipeleka katika hali ya utaahira, ni dhahiri kwamba utakuwa na utaahira wa kiroho kama unavyokiri wewe mwenyewe, au sijui wewe ni tikiti maji au chimpanzee nk ilimradi unayakiri mambo hayo na kuyadhihirisha hapo unapokuja na mafundisho yaliyo kinyume na Mungu anayolifundisha Kanisa lake, basi hiyo ndiyo hali iliyokukamata baada kuukimbilia utukufu aliokuning’inizia Ibilisi machoni pako!!

  Lakini Maelekezo ya Mungu yako wazi. Na ni kwa uwazi huo ndio kazi za Ibilisi zinadhihirika. Neno la Mungu linajitafsiri lenyewe, halimuhitaji mtu yeyote yule kulitafsiri. Mungu anaposema Kanisa lake limejengwa juu ya Msingi wa Mitume na Manabii, hilo huonesha wazi kwamba mitume ndio wanaotangulia katika ujenzi wa Kanisa na kisha hao ndio hutuleta kwa manabii. Basi tunapowatazama mitume, twapaswa kutambua kuwa hao ndio Mwili wa Kristo uliodhihirika kwanza, na kama nasi leo hii tutasimamisha dai la kuwa nasi tu Mwili wa Kristo, udhihirisho wa jambo hilo ungekuwa hayo Mafundisho yetu, yangekuwa sawa sawa na hayo ya Mitume, maana Roho anayetuongoza ni mmoja. Lakini si hivyo, Mafundisho yetu yanatofautiana sana tu kulingana na tafsiri zetu, yakidhihirisha roho tofauti!

  Kufuata Maelekezo kama yanavyojitafsiri katika Mwongozo ni muhimu sana. Kwa mfano Maandiko yanaposema Kanisa limepewa wengine kuwa wachungaji na wengine mitume, na wengine walimu, wengine wainjilisti na wengine manabii. Huu ndio utaratibu mpya kwa Kanisa. Sasa unawakuta watu wanang’ang’aniza cheo cha Ukuhani, “huyu ndiye kuhani wetu” akimtambulisha mchungaji wake au askofu wake, halafu huyo anayepewa cheo hicho naye anakiridhia, jamani, hilo si kundi la maamuma kweli!? Makusanyiko yetu hayana ndani yake hizo Huduma Tano, ambazo ndizo tulizowekewa ili kutukamilisha, kutufikisha katika kimo cha Kristo, kwahiyo yamebaki kuwa yatima wa Neno wakiingizwa utumwani bila kujijua!

  Kwahiyo unapomkuta mkristo anabishana na Maandiko, kama ninavyomuona Sungura akijaribu kumkana Petro na mitume kuhusu Ubatizo unaompasa Mkristo, huo ambao umerekodiwa katika kitabu chote cha Mtendo ya Mitume, hao Mwili wa Kristo, hilo laonesha kwamba Sungura ni ‘Mwili wa Dhehebu’ lake, yaani kanisa pia, lile tawi pori, lililopandikizwa kwenye Shina la ule Mzabibu, ambaye ni Kristo. Nalo tawi la asili la Mzabibu huo, likichomoza litakuwa ni muendelezo wa Huduma iliyorekodiwa katika kitabu cha Matendo na nyaraka zote kama zinavyojifunua katika Agano Jipya bila hitilafu!

  Kwa kifupi kanisa, kama Samson, limeondoka katika nadhiri yake ya Utakatifu kwa kucheza na ulimwengu, limeishia kunyolewa nywele zake na kupofuliwa macho yake ya kiroho baada ya kushawishika kutumia akili, LINAPASWA KURUDI ktk INJILI waliyoihubiri mitume na kufuata maagizo yooote wanayopewa wayatimize.

  Gbu all, friends!

 22. Mabinza;

  Hii ni kauli yako ” kanisa lenye uovu ndani yake ni la shetani, kwa hiyo Mungu hashughuliki nalo!”

  Yale makanisa saba yaliyo katika ufunuo yalionekana kuwa na matatizo, kama Mungu hashuguliki na kanisa lenye uovu, mbona hayo alishugulika nayo? Huu nao ni uongo mwingine ambao sehemu kauli zako.

  Hata Israel wakati wowote walipokuwa na matatizo au walipokuwa na uovu bado Mungu alishugulika nao. Halafu wewe unasema kanisa likiwa na uovu Mungu hashuguliki nalo. Sasa uovu wa kanisa ukiwwepo huondolewa na nani kama si Mungu?

  Na unaosema ni waovu hapa ni akina nani Mabinza? Au sisi ambao tunasema kanisa la kristo halina matatizo ispokuwa ni changamoto? Wewe ulitaka wote tuwe na mtazamo kama wako ndipo uone kwamba nasi ni wenye haki?
  Ok, kwa kuwa haki haitoki kwa Mabinza bali kwa Mungu,haina shida hata kama utaona wewe ndo mwenye haki wengine ni waovu, cha msingi tuoneshe hayo matatizo ya kanisa la kristo yako wapi.

  Ati kanisa limeacha neno la Mungu(ubatizo). Hii nayo ni ajabu sana.
  Yale ambayo mleta mada kasema ni matatizo yalianza lini katika kanisa Mabinza?
  Na huo ubatizo ulioachwa uliachwa lini, na nini uhusiano wa huo ubatizo na watu kuhubiri mafanikio, kwa mfano?

  Yaani unataka kusema kwamba mtu asipobatizwa kwa jina la Yesu moja ya matatizo atakayokuwa nayo ni kuhubiri sana mafanikio, au kupenda kuwa karibu na watu wenye fedha?
  Come on Mabinza, get serious!!!!

  Kwani ubatizo ulianza kufundishwa na mtume Petro, au ulianza kufundishwa na Yesu?

  Kuna kanuni ambayo umeilazimisha, kwamba aliposema kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho mt, alimaanisha kwa Jina la Yesu pekee.

  Mimi nimekwambia kanisa halina matatizo, mbona unanilazimisha kusema kwamba lina matatizo? Na jana nilikuuliza je wewe ni sehemu ya hilo kanisa, kwa hiyo na wewe una matatizo? Mbona hujibu unaleta wingi wa maneno yako tu?

  Basi labda kanisa la kwenu ndio lina matatizo, usitake kulazimisha kuwa kanisa kristo lina matatizo.

  Na unadhani anayeongea na wewe peke yako hapa ni nani? wote tunaoongea hapa tunaongea na watu wengi sio tunaojibizana nao tu.

  Nilikushauri ujichome sindano kwa sababu umeng’ang’ana sana kusema kuwa sisi tunatumia akili kufasiri neno la Mungu.
  Nikakuuliza wewe ni mjinga? Na kama si mjinga una akili, basi kajichome ile sindano ili ujaribu huko kutokuwa na akili jinsi kulivyo.

  Malalamiko yako ktk paragrafu yako ya mwisho ni maneno mazuri ambayo lakini hayana msingi wowote katika mada hii. Hakuna aliyekutukana, na kama kungekuwa na tusi moderators wa SG wasingeiruhusu comment yenye tusi kuwa hewani.

  Nilikujibu tu sawasawa na ulichokiandika na jinsi ulivyokiandika, kwa kujaribu kutuonesha kwamba wewe peke yako ndo unasema kilicho sahihi wengine tunatumia akili kufasiri maandiko, ndo nikataka kujua kam wewe una akili au hauna hapo ulipo.

  Kuna maswali nilikuuliza Mabinza ingependeza ukiyajibu hayo,pamoja na niliyokuuliza katika chapisho hili.

  Kabla mtu hujaanza kujadili kitu lazima uangalie kwanza ukweli na usahihi wa ukijadilicho.

  Kumbuka si kila kusanyiko la wajiitao wakristo ni kanisa.

  Asante.

 23. Sungura,

  Mith. 4:19 inasema, “19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene, hawajui kinachowafanya wajikwae.”

  Chanzo cha kila tatizo katika Kanisa ni “UOVU” kanisa lenye uovu ndani yake ni la shetani, kwa hiyo Mungu hashughuliki nalo! Ingekuwa vizuri kama ungekuwa na NIA ya kufundishana, ungekaa na kutafakali, ili uone kama Kanisa likiacha Neno la Mungu litakuwa na Matatizo ama la! Ukiangalia Agano la kale, kuna ushahidi wa Kutosha tu kwamba, matatizo yalipokuwa yakiwapata wana wa Mungu, walimkimbilia Mungu na kumuuliza, “Wapi tumekosea?”

  Mleta mada naye kwa Roho yuleyule, kasema “Mbona kanisa linamatatizo mengi, limekosea wapi?” Swali kama hili mimi naamini kabisa kwamba, linatoka kwa Mungu, ili watu wajihoji wapi wamekosea ili wapate kutengeneza! Lakini waovu wapo Gizani, hawataki hata kujua wapi wamejikwaa, ni wakali,wakiambiwa sababu, wanasema siyo kweli, lakini utajua kuwa wapo gizani kwa sababu hawaisemi sababu wanayodhani ama kuiona katika maandiko kuwa ni ndicho chanzo cha Matatizo ya kanisa!

  Mimi nimekwambia, Kanisa limeacha Neno la Mungu, moja wapo ya Neno lililoachwa ni ubatizo, naam ubatizo uliofundisha na Mtume Petro katika Mdo. 2:38, nilidhani utajiuliza kuwa, kweli ubatizo huo ni Neno la Mungu? Na kani Neno la Mungu, mimi nilipo nimelitekeleza hilo? Na kama mimi bado, vipi kusanyiko langu? Badala yake wewe unasema ubatizo hauwezi kuwa sababu ya Kanisa la leo kupata matatizo! Lakini hausemi kuwa huo ubatizo ni Neno la Mungu ama la! Na utueleze kwa Neno la Biblia kuwa, kama ni Neno la Mungu, kuachwa huko kwa Neno hilo la Mungu siyo chanzo cha mataizo ya kanisa, kumbe ni nini? Tueleze basi ndugu yetu ili tujue kanisa kwa nini linamatatizo, limekosea wapi kwa mjibu wa Neno sungura?

  Yote uliyoniambia, mimi siyaoni kama tatizo, maadamu najua ninayeongea naye ni mtu wa namna gani, vile vile hapa siongei na Sungura peke yake, wapo wengi wanaojua yupi ni yupi, na hivyo wanajifunza ile kweli! kwa sababu hata nikijaribu kuchoma hiyo sindano ya ukichaa (ambayo haipo!) haitanifanya nithibitishe vinginevyo. NIJUACHO NI KWAMBA, KANISA LINAPOACHA NENO LA MUNGU LAZIMA LIPATE MATATIZO, BILA KUJALI KWAMBA NENO HILO NI UBATIZO AMA LA!

  Moja ya sifa za Mwalimu asiye na ujuzi mkubwa wa kufundisha huendekeza matusi na fimbo! Na kwakuwa hajijui udhaifu wake huo, hujikuta HAELEWEKI kwa wanafunzi wake. Ipo haja ya mtu kuelewa kuwa Kanisani si pahali pa malumbano na ugomvi ama maneno machafu, hapa tupo kanisani, tukijaribu kuujenga mwili wa Kristo pamoja. Inapotokea tofauti ya kimaoni, hiyo ndiyo hasa inayotufanya tujifunze zaidi, tutachunguza Neno mstari kwa msitari ili tuijue kweli. Lakini kama wote tutakubaliana KINAFIKI kamwe hatutajifunza na maana ya Blog hii itakuwa Zero!

  Mjadala huleta suruhu, mjadala hukuza ufahamu! Haiko sababu ya Mtu kutukana, kudhalau, ama kukashifu wenzie eti kwa kuwa huko aliko anaitwa Pasto, mama pasto, mwinjilisti ama shemasi lazima ukija mahali kama hapa ujue kuwa kukosolewa kupo, Biblia inasema, “hasira haitendi haki ya Mungu” na ukisona ile Mith. 4:24 inasema, “24Epusha kinywa chako na ukaidi, weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako.” Kumbuka kuwa wewe ni Kanisa, unapo acha kuishi katika Neno lazima upate matatizo, kwa matatizo yako kama mtu mmoja kisha kuna uwezekano wa kusanyiko zima kuingia matatizoni kwa ‘UCHAFU’ hata wa kimatamshi wa mshirika mmoja! Kwa nini kuutaka umaarufu na sifa kwa kuuendekeza ubaya, songa mbele mwana wa Mungu, usiku umeenda sana! Mith.4:25-27 inasema, “25Macho yako na yatazame mbele, kaza macho yako moja kwa moja mbele yako. 26Sawazisha mapito ya miguu yako
  na njia zako zote ziwe zimethibitika.27Usigeuke kulia wala kushoto, epusha mguu wako na ubaya”.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 24. Ndugu nikukate kauli sadaka ni agizo la Mungu,ila wanaoipokea wamepoteza makusudio ya Mungu,maana ni kwa ajili ya kupeleka Injili mbele lakini utakuta kubwa hapa da lina waamini hata elfu tatu lakin hata tawi halina mmmh inatisha atupelek mbele ila tumbon,wanaogombea madaraka kwenye makanisa hao ni waasi,namalizia sikia sauti ya Roho Mtakatifu kisha utoe sadaka.Amen

 25. Mabinza:

  Uhakika wa kwamba kuna mbinguni haina maana kuwa mada ya biblia ni kwenda mbinguni.

  Je na wewe ni miongoni mwa hao wenye hayo matatizo unaosema wamekataa kulitii neno au wewe uko nje?

  Mabinza hapa siyo kweli pia: kwamba HAKI ni IMANI. Haki ni haki na imani ni imani. Labda kama ungesema kwamba haki ya Mungu hupatikana kwa imani.

  Unaniuliza mimi naonaje; Mimi naona ubatizo siyo chanzo cha kile kinachoitwa tatizo la kanisa, wewe wasemaje, mbona unamung’unya maneno?

  Nakuona tu unasema ukweli ndio huo, upi huo Mabinza?

  Nani unayejaribu kumwambia kuwa ameondoa ukweli wa neno? Ukweli upi huo
  Tatizo ni ujinga wa kuyafasiri maandiko kama unavyofikiri au kama ulivyofundishwa na mwalimu ambaye naye ni maamuma tu.

  Nimekuuliza tangu mwanzo ni ubatizo gani huo;wa maji au wa Roho mtakatifu mbona hunijibu, badala yake unaongea maneno ya kwako tu mengine.

  Ati ina hapa unachoniambia: ”SHIDA ni halali yenu Sungura! Ukifia kisimani kwa kiu…..”

  Nina shida gani mimi Mabinza, au umeamua kusema neno lolote kwa kutekewa?

  Mimi sina shida na wala kanisa la Kristo halina shida.

  Kama wewe si mshirika wa JESUS ONLY ni wa makanisa ya kipentekoste, au Kataoliki au Rutherani, hebu niambie mchungaji wako alikubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt, au kwa jina la Yesu?

  Mabinza mbona mwapenda kuongea kwa pupa,au kwa sababu tunaongea kwenye mtandao?

  Mabinza ni kweli kwamba wewe huna akili?

  Na kama unazo, umejaribu lile zoezi la kujichoma sindano ya kichaa ili uonje ile hali ya kutokuwa na akili?

 26. JOHN HAULE,

  Mimi sijambo, hofu na mashaka ni juu yako!
  Unapoona unashangiliwa kwa kelele usivimbe kichwa, humo ndani kuna wazomeeaji! Ushabiki si uanachama, kuna wapenzi na washabiki wa Yesu, lakini si wanachama wa Imani yake. Kufahamu hili mpaka umejaliwa.

  Si kila asemaye Yesu Yesu analo hilo jina, wengine hulitaja bure pia! Kipo kipindi ambaco ndicho hiki, wenyeufahamu watauacha “Ushabiki” wa Neno la Mungu. Wataijua kweli kisha watakuwa Huru kwelikweli!

  Hata ushabikie kwa maelezo ama madai ya upenzi wa ‘Mchungaji wangu ama Kanisa langu’ ukweli utabakia uleule, NENO LITASIMAMA MILELE!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 27. Sungura,
  Ninachojua ni Neno moja tu, Neno la Mungu, si mtazamo ama maoni ya Sungura ambayo anayatoa pasipo kusema kayapata wapi! Kama mpango wake si kutupeleka mbinguni mimi hilo sijui, kwakuwa hakuna aliyekwenda huko, yupo aliyetoka huko, na ndiye Neno linamnena kuwa; Alikufa, alifufua na akapaa mbinguni na amekaa kuume kwa Mungu, na kwa kinywa chake alisema “naenda kuwaandalia makao ili mimi nilipo nanyi muwepo, nyumbni mwa Baba kunamakao mengi kama sivyo nisingaliwaambia”. Upo ushahidi wa kutosha tu kuwa kipo kitu kinachoitwa Mbinguni, pia inasemwa na Biblia kuwa, mitume walikaza macho mbinguni wakimuona Yesu akielea mawinguni akienda zake mbinguni. Na huko ndiko alikoweka Mungu kiti chake cha Enzi. Inajulikana wazi kuwa palipo na kiti ndipo mtu anapokaa. Na ikiwa Yesu yupo kuume Kwa Mungu, na ikiwa alisema, alipo nami nitakuwepo nijihangaishie nini kujua Kuwa mpango wake si kunipeleka mbinguni? Mimi ni mtoto, atakosema Baba tukaishi tutakwenda, nitajua ndiko huko mbinguni, maana alipaa mbinguni kwenda kutuandalia pa kukaa. Kama mpango wake si huo, wewe jua tu, inatosha! Kwanza sina haja ya kujua wengine Mungu anapongo wa kuwapeleka wapi! Shida yangu ni moja tu kwamba, kusaidia kazi shambani mwa Bwana ili walioandaliwa kuwa “Mbegu” wajitambue na wajibague kutoka katika mazao yaliyopo kwa ajili ya kuliwa!

  Hoja yako nyingine ambayo nayo haipo katika mada nikuwa “Najigamba”! Sungura, ukiwa katika mwili, utayaona mambo Kama ulivyo na si kama yalivyo!

  Kuhusu matatizo yaliyomo katika kanisa lililosemwa na mleta mada, yanatokana na KULIKATAA NENO KIMYAKIMYA kunakofanywa na hao wajiitao kuwa wameokoka, huku hawajui ama wanajua kama wanakataa Neno la Mungu. Unapokataa ubatizo uliosemwa na Mitume na kujifanya unamjua sana Yesu, wakati upo ushahidi wa kutosha kuwa Mitume ndiyo walioachiwa watuelekeze Neno kwa usahihi. Kwanza kumbuka kuwa waliambiwa wasubiri kabla ya kuhubili wapokee kwanza ‘NGUVU’, nguvu hiyo tunajua ni Roho mtakatifu ambaye ndiye Yesu mwenyewe. Unapokataa kuwasikiliza mitume kwanini usiwe na laana? Taabu na shida za Kanisa linalosemwa na mleta mada ni kutokuwa watii katika Neno la Mungu tu basi. Biblia inasema, “kama mtatii…..” utaona kuwa, utii katika Neno ndipo hutokeza msaada wa Mungu, Mungu anapokuwa upande wa Kanisa, hakuna nguvu itakayosimama kinyume na kanisa itashinda!

  Tatizo la hilo Kanisa nikukosa ‘KWELI’ ndani yake. Unajua Neno linasema “Mkiijua kweli nayo kweli itawaweka huru”! Kweli ni nini? Kweli ni NENO la Mungu. Kama mtu anayafuta baadhi ya Maneno ya Mungu na kuwanafikia wenzi wake kuwa ameokoka, na kupaza sauti ya kuutaka msaada wa Mungu, eti anamuomba Mungu, ayaondoe matatizo yake, huoni kuwa maombi kama hayo ni upuuzi? Mtu mmoja atauliza kwanini ni upuuzi? Neno litajibu hivi:-

  Kwanza uwe HURU, ndipo uombe “HAKI” yako! Uhuru hutokana na kuijua KWELI ambayo ni Neno la Mungu, lakini haki ni IMANI. Biblia inasema, “mkiomba, ombeni katika mapenzi yake”, utaona kuwa mapenzi yake ndiyo Neno lake, mtu anapoomba nje ya Neno la Mungu, hukosa HAKI ya kupata sawasawa na hitaji lake, maana ASIYE HURU HANA HAKI! Kwa msemo mwingine, ukiacha Neno hata liwe moja, basi haupo huru, mtu asiye huru “AMEKUFA” katika ufu mtu, hana maamzi, hawezi kusema lolote. Biblia inasema, “Mfu hana neno lolote” Biblia pia inasema katika Uf. 22: 19 kuwa, “19Kama mtu ye yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

  Mungu analiheshimu sana Neno lake, acha watu warukeruke wapendavyo, lakini UKWELI ndio huo. Umekataa ile Mdo 2:38 umekataa Neno la Mungu, hujatekeleza hiyo Mdo. 2:38, hujatekeleza Neno la Mungu, hakuna zaidi! Sasa eti unasema bila hata aibu “Tuseme ubatizo huo ndiyo chanzo cha matatizo ya Kanisa?” Utasema najigamba labda, nikikujibu kwa swali kuwa “WEWE UNAONAJE?” Mwenye macho haambiwi tazama, mstari wa ufunuo 22:18-19, huo hapo!. Kama kanisa halina Sehemu katika ‘UHAI’ na halina shemu katika ‘MAKAO’ Si SHETANi hilo? Maana Biblia inasema, shetani hana makao mbinguni! Sasa Ikiwa Kanisa hilo ni SHETANI linamuomba Mungu wa Mbinguni aliondolee matatizo, siyo DRAMA hiyo? Mtakesha!

  Neno halijaishia hapo, mtu akizidisha Neno japo nukta moja, Bibli katika Uf. 22:18 inasema,
  “18Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu ye yote akiongeza cho chote, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.”

  Unaona? Siyo majigambo yangu mimi, labda anajigamba Yesu, maana ukweli ndiyo huo. Haijalishi Mtu anakanisa Kubwa kiasi gani, ni maarufu kiasi gani, mnyonge, muungwana, mwenyekuyajua maandiko ama mbumbu kiasi gani, habari ndiyo hiyo ukiongezea tu kitu, “Ishu” ndiyo hiyo!

  Mtu anasema Ubatizo ni kitu kidogo sana, au kilichosemwa na Petro mtume katika Mdo 2:38, si ubatizo ulioagizwa na Yesu, au eti anasema, Yesu hakuagiza ubatizo huo, hata useme,watu wanatafsri kimakosa sawa tu, ila jua kuwa umeuondoa ukweli wa Neno. Na wote watakaokuwa wamekuamini nae kwa ujinga huo anakuwa anashiriki katika kuondoa ukweli wa mstari huo, kwa hiyo mfundishaji na mwamini wake inawapasa kuongezewa Mapigo yaliyosemwa katika Neno la Mungu!.

  Wasilalame eti, oooo Kanisa linamatatizo sana, wakati wanaongezea na kuondoa “MANENO” ya Mungu kila kukicha, bila kurekebisha, munaendekeza ubishi na ujuzi wenu wa kiakili, ukiambiwa hiki, unadandia kile, SHIDA ni halali yenu Sungura! Ukifia kisimani kwa kiu, kwa maelezo kuwa hunywi maji ambayo hayajachemswa, wenyeufahamu watashindwa kukuelwe!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 28. Inapendeza sana kuona wapendwa wakiwa busy sana kujadili mambo ya Mungu!Humu ndani naona kuna wapendwa wainjilist wengine waalimu wengine wachungaji!naona huduma nyingi bt all in all twendeni kwa nia njema ya kujifunza!kufundisha bt vilevile tukae ktk namna ya kupeana maneno ya Hekima na Busara!Yote tufanye kwa utukufu wa Mungu.Dira yetu tunayo neno la Mungu litumike kuelimishana,kukosoana!bt kwa hali ya kipendwa isiwe kama ni vita!Kuna wapendwa mnavipawa humu hebu vitumieni ili Mungu apate Utukufu!Sungura nakuelewa sana Mungu akubariki.Edwin say somthng man of God!I believe u’ve somthng God 2share wth Us!God Bless U All.

 29. Kanisa ni wale washikao amri za Mungu, Ushuhuda na Imani ya Yesu,wenye

  kusubiri marejeo wahubirio kuwa amani na Haki yao kuwa ni Kristo.

  Yanayojiita makanisa ya leo yanatafuta haki kwa wafalme wa dunia hii na fedha zao zenye sifa ya ufisadi.

  Kanisa linalotaka kutembea katika njia sahihi lazima litembee katika mstari wa
  utakatifu/bikra lisilochafuliwa na mafundisho Babeli.

  Ufunuo 12:17

  Ufunuo 14:12

 30. Hello Seleli;

  Kuna umuhimu kwanza wa kuelewa kanisa ni nini.
  Ni rahisi sana kuchanganya kati ya kanisa,dini,na dhehebu. Tunaweza kuanza kujadili matatizo tunayodhani ni ya kanisa kumbe ni ya dini,au dhehebu fulani tu na wala si ya kanisa.

  Au tukaanza kujadili matatizo ya wajiitao wakristo tukidhani tunajadili matatizo ya kanisa.

  Lakini pia kuna vitu ambavyo ni changamoto wala si matatizo au makosa vinavyoendelea katika mwili wa kristo, tusipoangalia tunaweza tukaanza kuvijadili tukidhani kuwa ni matatizo au makosa.

  Vitu vya namna hii hata kwa kanisa la kwanza vilikuwepo, lakini kanisa halikuacha mwelekeo.

  Kwa kifupi, kanisa ni mwili wa kristo, kwa maana ya mtu mmoja aliyempokea Yesu kristo au kusanyiko la watu wa namna hiyo, ambao wanaenenda sawasawa na msingi wa imani ya Yesu Kristo. Hapa maana ya kanisa kama jengo siiweki.

  Si kila kusanyiko la wanaojiita wakristo ni kanisa.

  Ukiangalia mambo mengi ambayo mleta mada ameyasema kama matatizo yako katika eneo la fedha. Na hii kwangu ni changamoto tu ya umasikini ambayo inalitesa kanisa, wala tatizo.

  Yako mabo machache ya kimaadili ambayo mleta mada ameyasema pia kuwa ni mataizo ya kanisa. Lakini mimi nikiyaangalia nagundua kuwa hayo si matatizo ya kanisa bali ya dini na madhehebu. Kwa mfano tatizo la viongozi kwenda kwa waganga kutafuta uongozi, tatizo la viongozi kuwapa madhahabu wanasiasa mafisadi (maana si kila mwanasiasa hastahili kupewa madhabahu, kuna wana siasa ambao ni wana wa Mungu)

  Ivi kweli Seleli mtu ambaye ni kanisa na Roho mtakatifu yuko ndani yake aende kwa mganga kutafuta ”ndagu” ya uongozi, hiyo kweli inawezekana?

  Kwa hiyo kuna changamoto zaidi kuliko matatizo kwa mujibu wa mleta mada.

  Asante

 31. Mabinza ndugu,nashukuru

  Kwanza nakataa kuwa mada ya biblia ni kuwafikisha watoto wa Mungu mbinguni. Hatuokoki au kumwamini Mungu ili tufike mbinguni. Au lengo la Mungu kuleta neno lake kwetu si ili tufike mbinguni. Hata Yesu hakusema kwamba tunamwamin ili tufike mbinguni. Haya ni maneno ya ya kimapokeo yaliyozoeleka tu vinywani mwa wapendwa. Si mpango wa Mungu mwanadamu akaishi mbinguni, soma vizuri biblia yako juu ya hilo.

  Halafu kama unadhani neno la Mungu halihusiki na akili tuliyopewa na Mungu, jaribu tu siku moja kujiondoa akili kwa kujichoma sindano ya ukichaa, kisha soma neno la Mungu halafu utuambie kama umekielewa kilichoandikwa hapo.
  Hii nayo ni kauli ambayo mnaitumia sana watu wengi lakini haiko sahihi, badala yake mnatakiwa kusema jinsi akili inavyohusika katika neno la Mungu.
  Mabinza sijui kama aunajua ukijiondoa akili unakuwa kitu gani.

  Roho mtakatifu halifundishi neno kwa taahila, bali analifundisha kwa mtu mwenye akili timamu zenye nia ya kristo. Hujasoma Paul anaposema nitaimba kwa roho na kwa akili pia? Au mnaidharau kazi ya uumbaji wa Mungu alivyomuumba mwanadamu na kumpa akili ya ajabu!

  Mabinza mnarukia kunena mambo magumu ambayo hata hamyajui mapana yake.
  Jihadhari sana na kusema vitu vikubwa ambavyo huna elimu navyo just kwa sababu umeona andiko kwenye biblia, mtajitafutia hukumu isiyo na sababu.
  Kama unadhani mwili hauna maana yoyote kuhusiana na maisha ya imani, kwa nin Yesu alikuja katika mwili, si angebaki tu rohoni ?

  Wakati sauti inatoka mbiguni ikisema ”huyu ni mwanangu mpendwa….” ialiyekuwa anaongea ni nani na aliyekuwa anaambiwa ni nani?

  Sijui kama unaielewa kiunagaubaga concept ya Baba, Mwana na Roho, naona tu kama unarukia jambo usilo na uwezo nalo kwa kutuona wengine hatuelewi wewe ndiye unayeelewa. Lakini ki ukweli hata huelewi, ni majigambo tu. Swala hili nadhani lilijadiliwa vema kwenye mada ya utatu.

  Na kama kumbe mnajua kuwa Yesu kristo yuko ndani ya kanisa, kwa nini mnajaribu kusema kanisa halina nguvu, lina matatizo, kwamba limekosea mahali?

  Ndio maana nimekuuliza swali la msingi kuwa kutobatizwa kwa jina la Yesu unakosema ndio chanzo cha matatizo ya kanisa? hujajibu umeleta blablaa.
  Kumbuka hatujadili ubatizo bali tunajadili matatizo ya kanisa na kujaribu kujua mahali lilipokosea.

  Tena nikakuuliza na huo ubatizo ni upi, wa maji au wa Roho mtakatifu,au wa moto?

  ”Mwenye dhambi hana pa kuuweka mzigo wake?? what is this here?”

  Yesu anapowaita watu akisema njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha…, alikuwa anawaita watu gani Mabinza, wenye haki au?

  Mabinza, be careful brother, unaongea Heresy!!!

 32. Sungura,

  Post yako ya kwanza hapa, ulisema..’’Kanisa liko imara’’
  SWALI: Kulingana na mleta mada na contents ya mada, yeye ameona kuna shida tena si ndogo ktk Kanisa, wewe unasema ni Imara! Una maana huoni kua somewhere something ia wrong/missing sincerely speaking? Kweli kila kitu ni super?

  Press on

 33. Ndugu yangu Sungura,

  Kwakuwa umechelea kuwa tutakuwa nje ya mada, basi tuendelee nakile unachodhani kuwa kimo ndani ya mada. Ila Biblia ni Neno la Mungu, mada yake ni moja tu kwafikisha watoto wa Mungu mbinguni salama! Na kitu chochote cha Dini, kinapoanzishwa kuwa ni Mada kinakwenda weeeeee………hadi kinakwenda kugota kwenye “UTATU”. Na ngoma inapogonga hapo tu, inarudi tena mwanzo kama mwangwi; na inashindikana kushikamana inapolazimishwa kuwa……..Baba, Mwana na Roho mtakatifu ni majina ya kubatizia kwa ‘force’ kwamba, mwana ni Yesu, lakini Baba si Yesu na Roho mtakatifu si Yesu!

  Tuachane nahayo, umesema,” Nilishawahi kuuliza siku moja wakati tunajadili suala la ubatizo, kwamba jina la Mwana tunalijua, jina la Baba alilosema Yesu ni lipi, na jina la Roho mtakatifu ni lipi?” Mwisho wa kunukuu.

  Sungura, swali lako lililopo hapo juu linamaanisha kwamba, wewe unaujua ule “Mwili” wa Yesu uliozaliwa na Mariamu, huku ukibaki kapa juu ya hasa kilichokuwa ndani ya Yesu ni nini!

  Mimi najua kuwa Yesu ndiye huyo huyo Baba, mwana na ndiye Roho mtakatifu, Ukitaka kujua Majina ya Baba, Mwana na Roho mtakatifu, nipe ruhusa tutoke nje ya Mada kama kweli upo Serious vya kutosha. Bila hivyo, ni lazima ‘uipite’ ile Mdo 2:38 bila kuikubali kimya kimya, maana mtu akiikataa kwa sauti kuwa ‘SIIKUBALI’, kila mwenyekulikubali Neno la Mungu lote, atajua waziwazi kuwa mtu Yule tayari keshalaaniwa kwa mjibu wa Paulo katika Gal. 1:8. Cha msingi ni kukataa kimyakimya, hata hivyo mtu kama huyo mbele za Mungu atakuwa kama atembeaye gizani huku kafumba mcho ama sawa na Mtu atembeaye porini mara – hamadi! uso kwa uso na simba, kisha mtu Yule akafumba macho kwa kuelewa kuwa, kwavile hamuoni Simba na simba naye hamuoni pia, na kudhani kuwa Simba naye atakuwa kafumba macho!

  Jambo jingine ulilouliza ni kuwa, “Ni mhimu sana kufikiri kwa kina kwamba kwa nini Yesu hakusema mkawabatize kwa jina langu (yaani la Yesu)?…..” Mwisho wa kunukuu;

  Sungura, Neno la Mungu halitumii akili za mtu, ati kwamba afikiri, Roho ndiye mwenyekulitafsiri na kulifundisha. Mtu ajapo kwa kufikirifikiri kwake lazima atabaki nje ya Neno, maana Neno ni Roho, tena ni uzima, lakini akili ni mwili tena ni mauti! Ni wewe tu utakayekuwa huelewi, Je,umepaona pahala popote katika Biblia, Mitume wengine wakimbishia Petro kuwa fundisho lako la ile Mdo 2:38 linapishana na maelekezo ya Yesu? Mmoja katika mitume aliuliza kwa uelewa kama ulio nao wewe juu ya Yesu kuwa, “Bwana tuonyeshe Baba” Yesu alimjibuje mtu Yule? “Aliyeniona mimi amemuona Baba”. Zaidi ya hilo, Yesu alisema kuwa yeye alikuja kwa jina la Baba, pia akasema kwajina langu nitamtuma msaidizi (wote tunajua msaidizi ni Roho mtakatifu) Kama kumuona Yesu ndiyo kumuona Baba, baba ni Yesu. Na kama Yesu alikuja kwa Jina la Baba, Baba huyo naye jina lake ni Yesu. Na vilevile kama Roho mtakatifu alikuja kwa jina la Yesu, basi Roho mtakatifu anaitwa ni Yesu. Kama pia huelewi hapo, Yesu alisema nitakuwa pamoja nanyi hadi ukamilifu wa dahari, tunajua wote kuwa Roho mtakatifu ndiye yupo hapa hadi mwisho, kwa maana hiyo Yesu yupo hapa kwa NAMNA ya Roho mtakatifu.

  Wewe unakiri kuwa Yesu ni Mwana, lakini hujataja ni mwana wa Nani! Au unataka kusema ni mwana wa Mungu? Ni sawa, lakini Mungu hana jina? Watoto wote wa Mungu wanajua kuwa Mungu ni Baba yao, lakini pia wanajua kuwa lazima analo jina. Ndiyo maana Musa alimuuliza katika kile kichaka cha Moto kuwa, “…nikawaambie kuwa nimetumwa na nani?”

  Biblia inaeleza wazi wazi kuwa Mungu wakati wa Agano la kale alijitambulisha kwa “SIFA” kulingana na kile anachokwenda kufanya. Na hata Isaya alijua hivyo, maana aliambiwa atakayezaliwa ni ‘Mungu pamoja na watu/ Mungu katikati ya watu – ataitwa Emanueli’. Lakini katika Agano jipya Jina la huyo Emanueli, lilikuja na malaika toka mbinguni na kutambulishwa wazi kuwa “Mtoto huyo wa kiume ataitwa YESU” ni jina tu, naam ni jina kuu,lililokuzwa sana, halijapata kutajwa kabla na halitatajwa jingine tofauti baadaye, watoto wote wa Mungu na mashetani wote wanajua jina hilo! Siku moja mapepo yalithibitisha na kuwaambia wenyekujifanya waamini kuwa, “Yesu tunamjua na Paulo tunamjua ninyi ni akina nani?” Kama mapepo na magonjwa na dhambi na umasini na Adha zote zinakimbia na kutoweka kwa jina la Yesu, inakuwaje ubatizo usiwe kwa jina la Yesu? Jina hilo ndilo Jibu la kila kitu, utakuwa tu hujaelewa Sungura!

  Umesema pia kuwa, “Anyway, kwa hiyo ni akina nani hao Mabinza ambao unawataka sasa wakabatizwe kwa Jina Yesu?”

  Mimi kama mimi sina ubavu wa kuwataka wakabatizwe kwa jina la Yesu, maana siwajui wanaopaswa kubatizwa katika jina hilo. Mtu yeyote tu anaweza kujifanya kuwa anakubaliana na ubatizo huo, lakini aliyewaambia Mitume wawabatize watu kwa jina Yesu, ni Yesu mwenyewe, huyo ndiye atakuwa anawataka watu aliokwisha wakubali na kuwachagua ili wakabatizwe kwa jina lake, kama ambavyo yeye yupo kwa jina lake na watoto wake nao wakamilishwe na kuitwa kwa jina lake.

  Kisha ukamalizia na Swali linalo ihusu mada, uliposema, kwamba kutokubatizwa kwa jina la Yesu ndo kunasababisha kanisa liwe na matatizo ambayo mleta mada amejaribu kuyasema? Mwisho wa kunukuu;

  AAaaah, Sungura, Sasa bila jina la Yesu mapepo yatatokaje? Na vipawa vya Roho mtakatifu vinawezaje kukaa kwa mtu mwenyedhambi? Biblia inasema “Mwenyedhambi” ndiye mwenye matatizo maana hana pakuuweka ‘MZIGO’ wake. Akija nao hapo kanisani anauweka mlangoni, na akitoka anaupitia tena, mfano wa mtu anayeingia Msikitini kuswali, huvua viatu vyake na kuviacha nje mlangoni ama nje kwa mlinzi na akimaliza kuswali hupitia nakuvaa viatu vyake na kwenda navyo kama ambavyo alikuja navyo kuswali, na hurudia hivyo hivyo hadi Dhuhuri, na kitendo hicho huwa endelevu bila hata kuchosha, vua viatu, pitia vaa, vua viatu tena, pitia vyaa…..hadi akienda ‘peponi’ kwake!

  “Ufahamu ni chembe ya neema”

  Mabinza LS.

 34. Nachelea sana kukujibu kwa mujibu wa ulichokiandika Mabinza maana tutatoka mbali sana kwenye mada, lakini ndani yake kuna ”Heresy” ya kutosha tu.

  Nilishawahi kuuliza siku moja wakati tunajadili suala la ubatizo, kwamba jina la Mwana tunalijua, jina la Baba alilosema Yesu ni lipi, na jina la Roho mtakatifu ni lipi?

  Ni muhimu sana kufikiri kwa kina kwamba kwa nin Yesu hakusema ”mkawabatize kwa jina langu (yaani la Yesu)? Hiki si kitu cha kurahisisha namna hiyo katika kukitafsiri Mabinza.

  Kwanza hapo Yesu alikuwa anaongelea ubatizo gani; wa maji au wa Roho mtakatifu (moto)?

  Anyway, kwa hiyo ni akina nani hao Mabinza ambao unawataka sasa wakabatizwe kwa jina Yesu?

  Kwamba kutokubatizwa kwa jina la Yesu ndo kunasababisha kanisa liwe na matatizo ambayo mleta mada amejaribu kuyasema?

  Mimi sioni kama kanisa limepungua nguvu!

 35. Sungura,

  Sikumaanisha mimi lolote tofauti na ilivyoandikwa, na maandiko ndiyo yanayosema hivyo! Yanasema lipo jina moja tu tulilopewa ambalo kwa hilo kila kitu kifanyike! Vilevile ndugu yangu kwa kila mwenyekufikiri vizuri anajua kuwa, Baba, Mwana au Roho mtakatifu Si jina na wala si majina ila ni Sifa za mtu mmoja tu ambaye ni Yesu. Na kwa kifupi sana, hakuna pahala popote palipoandikwa kuwa tutapona kwa kuzitaja sifa za Mungu au kwa kuita baba au mwana au roho mtakatifu bali tuite katika Jina la YESU pekee!

  Zaidi sana, Neno linasema, tulichopaswa kujifunza na kukiamini ni kile kilichojengwa kwa misingi ya Mitume na Manabii, mjengaji akiwa Yesu mwenyewe. Kama ndivyo, Gal. 1:8 inasema, 8Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo mtu na alaaniwe! Hebu chukua huo mstari kisha njoo nao uufikishe katika ile Mdo. 2:38 utaikuta inasema hivi, 38Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu. nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Sasa Paulo na Petro si ndiyo Mitume? Je, hiyo injili ya Ubatizo wa kwajina la Baba la mwana la roho mtakatifu ni Mtume nani alihubiri? Kwa mjibu wa hiyo Gal. 1:8, mafundisho yoyote yasiyo simama kwa mafundisho ya Mitume ni laana! Mtu mmoja atasema, mbona Yesu mwenyewe ndiye aliyehubiri kuwa, “…enendeni…..mkawabatize kwa jina la Baba na la Mwan na la Roho mtakatifu”, sasa nani mkubwa kati ya Yesu na Mitume? Jibu ni YESU.

  Mkubwa ni Yesu, na Mitumea walichaguliwa na Yesu ili watuletee sisi Maneno ya Yesu. Kwa hiyo aliyemwambia Petro abatize kwa Jina la Yesu ni Yesu na kwakuwa Neno la Mungu halipingani, wenye macho na masikio wanaona Maandiko ya Biblia na kusika Neno la Mungu likimtambulisha Yesu kwetu kuwa, YESU ni Mungu mwenyewe (Yh. 1:1…) lakini pia Yesu ndiye Baba amesema hivyo Yesu mwenyewe “Aliyeniona mimi amemuona Baba” ! Si hivyo tu, hata waliokuwa wakimshitaki walimwambia “Hatukupigi kwa maneno yako mazuri ila kwakuwa unajiita/ unajifanya/ unajifananisha wewe mwenyewe na Mungu” alipo ambiwa hivyo Yesu hakupinga kuwa Yeye siyo Mungu. Lakini pia Yesu alisema “……Maneno niwaambiayo ni Roho tena ni Uzima” lakini pia kitabu cha ufunuo kinasema “ ….na Jina lake anaitwa ni Neno la Mungu…”

  Kwakifupi sana, Baba, Mwana au Roho mtakatifu ni SIFA za Yesu, si Jina! Yesu alipokuwa akisema Kabatizeni kwa jina la Baba, la mwana na la Roho mtakatifu, ni kama alimaanisha tu kwamba wakabatize kwa Jina la mwenye Sifa ya Ubaba Umwana na Uroho mtakatifu ambaye ni mimi Yesu, basi!

  Mtu mmoja hakubaliani na hilo, aikubali ile Mdo 2:38, kama haikubali hiyo basi, yeye ni mtu ASIYE AMINI, na asiyeamini ni yule ASIYEFUTIWA DHAMBI zake na asiyefutiwa Dhambi zake ni Yule ASIYEOKOKA na yule asiye okoka ni yule BADO MWENYE DHAMBI, na Yule mwenye dhambi Biblia inasema MUNGU HAMSIKILIZI MWENYE DHAMBI, na kama mwenye dhambi yumo Kanisani na analazimisha kuwa ameokoka wakati haiamini Injili ya mitume, kumbe humo kanisani anafanya nini? Mtu asiyeamini NENO KAMA LILIVYOFUNDISWA NA MITUME ANAKUWA AMELAANIWA! Na kama Kalaaniwa, Kalaaniwa na nani? Kama kalaaniwa atakuwa KALANIWA NA YESU, ambaye ndiye aliyewatuma Mitume kuhubiri! Na kama kalaaniwa na Yesu, humo Kanisani kaenda kufanya nini? Kama kalaaniwa na Mungu naye yumo kanisani, atakuwa kaenda KUJIHUDHURISHA kama baba yake alivyofanya kwa wana wa Ayubu, maana mtoto hafanyi isipokuwa kamuona baba yake akifanya! Sungura umeelewa?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai”

  Mabinza LS.

 36. Tafadhali Mabinza, hapa ulimaanisha nini?

  ”WOTE MLIOBATIZWA KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU, HUJABATIZWA! KABATIZWENI KWA JINA LA YESU ILI DHAMBI ZENU ZIONDOLEWE NA MPATE VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU, MPATE KUTAJIRIKA, ILI MKANUNUE MAVAZI NA DAWA YA MACHO MPATE KUUONA UKWELI MPONE!”
  Asante.

 37. Wapendwa,

  Nimefurahi sana kuuona ujumbe huu, Biblia inasema, “Anayeuchukia uovu ni Mcha mungu”. Shetani anasifa tatu kuu; Kiburi, uongo na Uuaji. Ieleweke pia kwamba moja ya kazi mashuhuri ya shetani ni “kujihuzurisha kanisani” . Lakini ukitaka kujua “KOSA” la Kanisa ni nini, ama ni wapi kanisa limekosea, jibu liko wazi katika Ufunuo, Mungu anasema, “Kanisa lipo uchi, tena ni kipofu, tena ni masikini!” na kwa upendo na upole wa Mungu kanisa limepewa ushauri kuwa, “pata dawa ya macho upate kuona, pata Dhahabu iliyosafishwa kwa moto, ukauze upate kuwa Tajiri, ununue mavazi ufiche uchi wako”; Lakini, Kanisa kwa “Kiburi” limekataa linasema lenyewe ni Tajiri sana. Na kwa “Uongo” linasema “Tunampenda Yesu” huku kwa tabia ya “Muuaji” hawahubiri sheria ya Yesu Bwana, wanaye dai kuwa ni Bwana wao, kabisa hawataji wala kuufanya ama kuuhubiri UPENDO ambayo ndiyo kanuni na sheria ya Mungu! Kwanini? Kwa sababu “Aliyejihudhurisha” kwao ndiye anawatawala, wanamwamini huyo…..Maana wanasema ni wacha Mungu huku wakizikana nguvu zake! Wameliacha Neno la ‘MSALABA’…….”Kwa maana, Kwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanaye wa pekee…” Amri mpya nawapa MPENDANE…, Hakuna upendo uliomkuu kuliko huu wa MTU KUUTOA UHAI WAKE KWA AJIRI YA RAFIKI ZAKE! Kumbe, maslaba ni UPENDO. Asiyehubiri na kuufanya UPENDO najasirika kusema kuwa HUYO SI WA KRISTO!

  Ukiona jambo kama hilo linafanyika, iwe kwa mtu mmojammoja ama ndani ya kusanyiko jua kuwa hilo ni “DUDE” ambalo litalipuka hivi karibuni, kimbia sana kasimame mbali palipo salama, ‘tokeni kati yao’. Mtu mmoja atauliza, kama hali ni hii wapi pako salama? Mahali salama pako, ni Vipofu peke yao ndiyo hawapaoni, na kwa bahati mbaya, wamewafuata vipofu wenzao ili wawaongoze, kwa maombi na mafundisho ya utajijrisho, kuvunjiwa laana, wanawake wahubiri, Zaka ndani ya Neema nk. Sasa wote wametumbukia shimoni. Katika shimo walilolichimba wenyewe kisha wameshindwa kutoka!.MAHALI PEKEE PALIPO SALAMA PA KUKIMBILIA NI “NENO” unapaswa kuliamini na kulishika lote, likikataa hiki, ukiache hicho, likikubali hiki ukifanye, uwe ‘Mtoto’ usiingize ujuzi na udadisi wako. Batizweni kwa Jina la Yesu Kristo mpate ONDOLEO la DHAMBI na VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU (Mdo 2:38)

  Bila kuondolewa Dhambi na bila kuwa na vipawa vya Roho mtakatifu, wewe ni kipofu, masikini, mnyonge na upo uchi. Kwa hali hiyo, wewe ni “Mwana sesele” wa shetani! Kama unavyoona sasa, Mwanamke yupo karibu uchi na anatembea barabarani huku akifurahi na kwa raha zake bila hata aibu ama wasiwasi, usimtazame huyo kama mwanamke wa kawaida, jua kua, ‘HILO NDILO KANISA LA SASA’ Roho ni ile ile iliyokuwa Edeni! Kwakifupi, siogopi kukuambia ukweli kuwa, WOTE MLIOBATIZWA KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU, HUJABATIZWA! KABATIZWENI KWA JINA LA YESU ILI DHAMBI ZENU ZIONDOLEWE NA MPATE VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU, MPATE KUTAJIRIKA, ILI MKANUNUE MAVAZI NA DAWA YA MACHO MPATE KUUONA UKWELI MPONE! Kweli ndiyo itakayomuweka mtu kuwa huru. Ukiukataa UKWELI unapewa kuuamini UONGO, hiki ndicho kinacholitesa kanisa!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”
  Mabinza LS.

 38. Wapendwa inatupasa kila mmoja asimame ktk nafasi yake kiroho!Cdhani kama kunashida coz Neno la Mungu tunalo ambalo ndiyo msingi wetu na Jambo zuri zaidi tunaye Roho Mtakatifu ambaye ndiyo Msaidizi wetu!Hatupo yatima kiasi kwamba tupate tabu!Mbona JESUS aliisha tutel kila jambo?Kama mpendwa ukiwa mkristo jina yaani Hujaokoka basi utaburuzwa tu coz huna nguvu ya Mungu!SO KANISA LA KWELI LIPO IMARA NA LINAZIDI KUSONGA MBELE!

 39. Kwa nini tunapata shida jamani,si ni lazima mambo ya namna hii yatokee!
  Hata kanisa la kwanza lilikuwa na changamoto pengine ngumu kuliko hizi, sema tu hazijaandikwa zote.

  Liko jambo moja tu dogo, kwamba Mungu awajua walio wake, na hakuna nguvu inaweza kulishinda kanisa au kulipoteza.

  Kama kuna watu hapa bado mmesimama imara kuinena na kuisimamia misingi ya kanisa, baisi dunia kote kuna watu wengi kama ninyi.

  Kanisa liko imara.

 40. Kanisa la nia msingi wa roho ya ushuhuda lilibeba sifa za kazi ya kitume, unyenyekevu,utii upendo, kutoa kwa ajili ya Kristo sio Kupanda kusubiri uvune (ubinafsi) ndio lisilofungamana na dunia ndio njia salama.

  Matendo 4:32. Matendo 2:4,8,111

 41. Makanisa yalizaliwa katika misingi ya wanamatengezo, hasa miaka ya kuanzia 1500, na wengine kabla ya hapo.

  Kupoteza msingi wa wanamatengenezo ambao ni kutumia Neno la Biblia kama njia ya kufikia uzima

  wakasahau msingi wa Kujiandaa kwa marejeo watu wakageukia injili ya
  1. Tunaondoa mikosi, nuksi,
  2. Panda uvune
  3. Utasa
  4. Unataka kuolewa
  5. unataka kazi
  6. Unateswa na majini
  7. Unataka kubarikiwa katika biashara yako
  8. Je unapigana na wachawi usiku

  Mbao za matangazo ya Biashara ya makanisa ya kisasa.

  Hizi zote ni kauli mbiu za waganga wa kienyeji Walioamua kufuata wateja wao waliowakimbia wanaosema tumeokoka, wachungaji hawa wanapotosha roho za watu wa Mungu, Ole maana wakati u karibu kila lililo la giza kuwekwa hadharani. Kiu Ya YESU haitaisha japo mtu aimbe kwa sauti, apige gitaa, acheze kiduku, upande Mbegu (Doctrini ya wa Evengeliko) sadaka (Utii wa injili ni bora kuliko sadaka) maana hawakutii injili bali maneno yaliyotungwa kwa ustadi wa ushawishi yakichangannywa na Neno la Mungu kuleta mvuto.

  ADUI ANENAPO KAMA JOKA, NI NENO NA NENO TU TEGEMEO LA MSAFIRI WA MBINGUNI, ANENAYE KINYUME NA NENO NI NABII WA UONGO.

  VIJANA ACHENI KUHUDHURIA MIKUTANO YA INJILI NA KUKOPI MANENO YA WATU YASIYO NA MISINGI YA BIBLIA, NAKUANZA KUWAFUNDISHA WATU MSIJE MKAINGIA HUKUMUNI KWA KUWAPOTEZA WATU, SOMENI BIBLIA TIINI INJILI YA YESU WA NAZARETI, MWEPUKENI ROHO YA MATREYA YA MAKANISA YA KISASA. AMBAYO DHUMUNI LAKE NI KUKUSANYA WATU KATIKA MATITA MATITA NA KUWARUDISHA KWA MAMA YAO BABELI. AMBAYE AMEKAA KIMYA KAMA HAHUSIKI LAKINI LAKINI ANAFURAHI WATOTO WAKIKUSANYWA KATIKA MATITA MATITA NA KURUDI KUNYONYA KWA MAMA YAO WA KALE (ECUMENICAL MOVEMENT/OIKUMENE)

  Makanisa yanashindana kufikisha watu 50,000 ili wakidhi vigezo vya katiba ya WCC na kupata faida kutoka shirika hilo linaloshabikia dunia yenye amani,haki (moto: PEACE, JUSTICE, GOD OF LIFE)-wananena kama kondoo lakini mmh! Ilimradi Dunia itawalike na kuasi kama Babeli na falme 3 zilivyotawala dunia nzima (babeli,wagiriki,wamedi, Warumi). si mioyo iliyo tayari kumlaki Kristo ambaye ni Haki na Amani ya Wasafiri wa mbinguni. (Shetani ameamua kutumia kitu hicho hicho wanachoamini watu ili kuwa tawala Uongo+Ukweli)

  Patakapotokea Amani ya Dini za upagani na Ukristo ndipo uasi mkuu ulipo mana WEMA na UOVU Havichanganywi. Maana kanisa la kwanza lilipata mateso kwa sababu Ulimwengu ulilipinga. Leo hii Makanisa yanajiweka chini ya WCC (ulimwengu) hapa ndipo yalipoo machafuko Uongo+Ukweli= Uvuguvugu=kutapikwa

  Uponyaji wa Roho ungeweza kuleta mabadiliko juu ya shida zote hapo juu. Yesu hapendi watu wamwendea kwa kutaka faida za kimwili. Bali Upendo kwake si faida ya mali ambayo imekuwa ni wimbo.

  Laiti Petro angetumia nafasi kama wachungaji wa leo kujilisha mpaka matumbo kuvimba,dhahabu shingoni,magari ya anasa huku waumini wakiwa mifupa mitupu wasioopona roho, asingekuwa asingekuwa mvuvi wa samaki (Yohana 21:6) angekuwa amejilimbikizia, watu hawa utamu wa maisha yao ilikuwa kuhubiri si heshima na mali kama wachungaji wa leo. Kuwabebesha watu habari za mali kabla hawajampenda Yesu ni kuwapoteza wakatumikia mali injili ambayo Yesu hakuhubiri bali aliwaonya matajiri.

  Hata wakihubiri na kutabiri amani agenda ambayo wachangaji wote, mashehe,wabudha, wayahudi ya WCC na NEW WORLD ORDER majukwaa Yote hawatapata jibu. Uasi ndio unazidi na utazidi kila siku. Tafuta amani ya moyo wako.

  “NABII ATABIRIYE HABARI ZA AMANI, NENO LA NABII YULE LITAKAPOTOKEA, NDIPO NABII YULE ATAKAPOJULIKANA, KUWA BWANA AMEMTUMA KWELI KWELI.” YEREMIA 28:9

  “NIKAONA ROHO TATU ZA UCHAFU ZILIZOFANANA NA VYURA, ZIKITOKA KATIKA KINYWA CHA YULE JOKA, NA KATIKA KINYWA CHA YULE MNYAMA, NA KATIKA KINYWA CHA YULE NABII WA UONGO. (UFUNUO 16:13)

 42. Hili ni suala ambalo ni muhimu. Lakini sisi kama wana wa Mungu ni jukumu letu kusoma biblia na kupata maelekezo ya Mungu. Maana siku ya mwisho kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe hao wachungaji wanaopotosha kondoo wa Mungu, Yesu ndiye anajua atawafanyaje lakini kwetu sisi tunatakiwa tumtafute Mungu kwa moyo wetu wote na hata sadaka tukitoa tutowe kwa moyo mmoja kwa kuwa inasaidia kazi ya Mungu kama watumishi wa Mungu watatumia sadaka vibaya, Mungu anajua.

 43. Kazi kwa kwel ipo, Ila mi nadhani suala la kwenda mbingun ni jambo la mtu binafsi

 44. Mungu akubariki kaka JWM umeongea ukweli ambao umekuwa mgumu kwetu wengi kuongea waziwazi.

  Siku hz hali imebadilika sana, tumeanza kuwekeza sana mwilini. J2 mtumishi mmoja huko kanisani anawaita waumini mabilionea na anawapa upako wa kununua helikopta binafsi sababu magari foleni zimezidi. Hao watu wanaoshangilia Mhh Mungu anajua.

  Hatukatai Mungu hachukii sisi kufurahia baraka za dunia LAKINI hilo siyo lengo letu kuu katika safari yetu.
  Mathayo 6:33
  ‘TAFUTENI KWANZA UFALME WAE NA HAKI YAKE ‘ na hayo mengine mtazidishiwa.

  Mungu akitujalia mafanikio, baraka, (ambazo lazima zipatikane kwa njia halali) tunamshukuru kwa ajili ya utukufu wake LAKINI hata kama hatupati basi tusipende kujifananisha na watu, tuwe na moyo wa kuridhika na tumshukuru kwa yote na anajua kipi sahihi kwetu na kwa wakati upi..

  Mithali 30;7
  Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime matatu kabla sijafa. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.

  Mara nyingi mahubiri ya mafanikio yamekuwa yanasisitiziwa sana kuliko utakatifu hapo ndipo shida ilipo. Duniani tunaishi muda mfupi ukilinganisha na kule tutakapoishi baada ya kufa. (Mbinguni au Jehanamu). Matokeo yake maisha yetu yamejaa manung’uniko na malalamiko, hatuna tena furaha wala kuridhika. Kila siku tunatafuta laana zilipo, wachawi tuwauwe na watu wa kuwalaumu. MUNGU ATUSAIDIE tujifunze kutoka kwa waanzilishi wa imani yetu akina Paul na wengine.

  Dada Imani Kapinga

 45. Ndugu JWM yaani hapo ume nena,kwa maoni yangu mimi,mambo kama hayo ninayashika kama biashara za watu ndizo zinafanyika nasi kazi ya Mungu sababu tukisoma story ya kanisa la kale ni tofauti kabisa na makanisa ya leo,Na tulipo kosea nafikiri ni hapa Waefeso 2:20(kanisa lazima lijengwe juu ya mafundisho ya manabii na mitume,huku Yesu akiwa mwalimu mkuu)kwa leo kanisa nyingi zina jengwa juu ya mafundisho ya watu.naishia kwanza hapa.

 46. Mimi nakusapoti kabisa, kwa sababu siku hizi wahubiri wana hubiri kuhusu sadaka tuu, baraka na kwenda mbinguni, sasa fikiri ndugu yangu, tutawezaje kwenda mbinguni kama myononi mwetu tuna dhambi, aw baraka tupata vipi kama uhusiano wetu na mungu hauko sawa, hizi ni siku za mwisho inaumiza sana kuona wachungaji wakihubiri tuu kuhusu baraka instead of repentance, Jesus is near let focus on bringing people to the Lord so they can recieve salvation rather than, preaching what people want to hear. Let not mislead people because God will Judge us if we Mislead people

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s