Kusudi la Mungu kwenye maisha yangu!

kweli

Bwana Yesu asifiwe, Ninawezaje kujua kusudi la Mungu ndani yangu? Na ni wakati gani Mungu anataka nilitumikie kusudi hilo? tafadhali ninaomba majibu

–Frank

Advertisements

9 thoughts on “Kusudi la Mungu kwenye maisha yangu!

 1. Asante ndugu Frank kwa swali zuri, jibu la swali lako ni pana ila tajibu kwa sehemu. Kwanza ni vizuri ujue kwanza nini maana ya neno kusudi, neno kusudi ni sawa na kusema lengo. Ni rahisi sana kujua kusudi au lengo la Mungu kwako, labda tuangalie mifano hai; Kilichofanya Yesu aje ulimwenguni Biblia inasema…1 Yoh 3:8 kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa azivunje kazi za Ibilisi. Yesu alidhihirishwa ni ili azivunje kazi za Ibilisi na aliishi akijua amekuja duniani kuzivunja kazi za Ibilisi. Kwa hiyo kama Yesu angeishi bila kuzivunja kazi za Ibilisi na huku akijua anapaswa kuzivunja kazi za Ibilisi ingekuwa ni kosa kubwa ambalo lingefanya apigwe sana, Luk 12:47 imeandikwa, Mtumwa aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari wala kuyatenda mapenzi yake atapigwa sana. Ndugu Frank nataka ufahamu kwamba kusudi lile lile lililofanya Yesu aletwe duniani kaliachia kanisa(yaani watu waliookoka) kwa hiyo basi hata wewe unalo kusudi hilo hilo la kuzivunja kazi za Ibilisi. Hili ni kusudi la kijumla la kila aaminiye sasa naamini unazijua kazi za Ibilisi, wahubiri wanapohubiri wanazivunja kazi Ibilisi kwa kuwatoa wenye dhambi ktk utumwa wa dhambi, kuonewa na mapepo, magonjwa, umaskini. Asante kwa kuchangia kwa sehemu

 2. hongera kwanza unachotakiwa ni uchukue sadaka maalim kwa ajoli ya maombi ambayo utafanya halafu unaingia kwenye maombi
  coz mungu anasema kuwa anatujua kabla hatujatungwa mimba
  baada ya hapo unajenga madhabahu kupitia sadaka yako kwa kuwa neno linasrma “aapae kwa sadaka amejifunga”.
  baada ya kufanya yote hayo lazma ujibiwe na mungu

 3. Watu wengi wanapenda kufanya mapenzi ya Mungu, lakini inakuwa ngumu kwa sababu hawajui nini mapenzi ya Mungu kwenye maisha yao.

  Zifuatazo ni baadhi ya kanuni za Neno la Mungu ambazo zitasaidia kutambua nini mapenzi ya Mungu ni kwa ajili yako.

  Mungu ana mipango mikubwa kwa ajili ya maisha yako!
  Tuliumbwa na Mungu, kwa mfano wake, kwa kusudi. Tangu kabla hatujazaliwa (Isaya 49:1) na (Yeremia 1:5) na Paulo (Wagalatia 1:15) Mungu pia ana mpango maalum kwa ajili ya maisha yako.

  “Kwa maana najua mawazo ninayowawazia ninyi,’ asema Bwana, ‘Mawazo ya amani si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho” (Yeremia 29:11).

  Biblia inasema kwamba mapenzi ya Mungu ni “mazuri, kupendeza, na ukamilifu” (Warumi 12:2).

  Mapenzi ya Mungu, kwanza kabisa, ni kwamba tuwe na uhusiano naye kwa njia ya Mwana wake, Yesu Kristo.

  “Hili ni jema nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu, ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo ya kweli” (1 Timotheo 2:3-4).

  Tuwe wanafunzi wazuri wa Bwana Yesu
  Wapendwa hii ina maana kwamba tuwe na nia ya kufuata mapenzi ya Mungu kila siku, kwa gharama yoyote.

  “Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate” (Luka 9:23).

  Biblia itatusaidia kujua mapenzi ya Mungu.
  “Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu” (Zaburi 119:105).

  Wakati mwingine tunahitaji kumuomba Mungu atupe hekima kuyafahamu mapenzi yake. (Yakobo 1:05).

  Katika Wafilipi 4:6, Mungu anatuambia kwamba tunaweza kuomba lolote.

  Mungu ametupa Roho Mtakatifu kutuongoza.
  “… Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote …” (Yohana 16:13 a).

  Tunapaswa kusikiliza ushauri wa watumishi wa Mungu ambao Mungu amewaweka katika maisha yetu.

  “Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe, Bali yeye aliye na hekima husikiliza ushauri” (Mithali 12:15).

  “Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibitika” (Mithali 15:22).

  Biblia inasema kwamba tukijifurahisha kwa Bwana yeye atatupa haja za mioyo yetu.
  Kuna mambo mengi umewaza lakini kimoja ambacho unasikia amani ya Kristo ndani hicho ndio chako

  “Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki itakuwa ni utulivu na matumaini daima” (Isaya 32:17).

  Tunapaswa kumwamini Mungu kwamba mapenzi yake yatatimizwa kwenye maisha yetu.

  “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako” (Mithali 3:5-6).

  “Nami niliaminilo ndio hili , ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema ndani yenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu” (Wafilipi 1:6).

  Mungu ametoa vipawa na karama mbali mbali kwa kila mmoja wetu pia ametupa uwezo wa kuvitumia kwa ajili ya utukufu wake.

  SIku zote Mungu amepandikiza vitu ambavyo ametupa tuvifanye, Kama wewe haina vipawa katika eneo fulani, pengine Mungu amekuita kwenye huduma fulani. (SomaWarumi 12:6-8, 1 Wakorintho 12:1-11 na Waefeso 4:11-13 kujua kuhusu karama na vipawa.)

  Kumbuka kwamba mpango wa Mungu kwa ajili yetu sisi sote ni yeye Atukuzwe (1 Wakorintho 10:31) na kuuinua ufalme wa Mungu (Mwanzo 50:20 na Wafilipi 1:12).

 4. Kaka Moses asante kwa ushauri ulitoa kwa mpendwa kuhusu kusudi la Mungu ktk maisha yake. Ni ushauri mzuri sana maana na mimi nimefaidika sana sana na ushauri huo hasa kipengere cha Mungu anavyoweza kutumia ndoto ukiwa usingizini kukuonyesha kusudi lake, hii imekuwa ikinitokea sana mimi na kwa wewe kusema hilo inanitia nguvu kuzidi kujua kuwa kweli ndoto zile ni Mungu ananionyesha kusudi lake na anayotaka kufanya kupitia mimi Ubarikiwe sana kaka. Ombi langu kwako kaka Moses ningeomba utumie lugha ya Kiswahili kama aliyotumia aliyeomba ushauri, ni kweli sote tunapenda lugha ya Kiingereza lakini siyo wote tunaoweza kuongea lugha hiyo na kuiandika, ninajua kuwa wewe kaka unafahamu lugha ya Kiswahili vizuri kwa jinsi ulivyotoa ushauri wako ktk lugha ya kiingereza lakini sijui kama yule uliyemshauri anajua lugha ya kiingereza, hata kama na yeye anaijua lugha hiyo ningependa tutumie lugha ya Kiswahili kwa manufaa ya wengine ambao lugha ya Kiingereza ni tatizo hili sote tuweze kufaidika. Asante sana kaka .Kila kusudi uthibitika kwa kushauriana Mithali 20:18. Mama K.

 5. Thanks for your good question

  This is how God reveals the future : calling / purpose
  1) strong inner desire in your heart . What’s your inner most desire ? What’s that you wanna do for the people ie God that’s burning deep within you
  2)dream . God can use dreams at night when you are sleeping to show you the purpose and calling
  3) inspiration . Who in the world inspires you and you wish you could do or be like them ? A preacher . A business man , a singer etc
  4) divine visitation eg Jesus appearing to you etc an angel etc
  5)Divine Guidance eg through mentorship. God can use your mentor to reveal to you your future

  Please know that it’s not that God is just hiding your future from you .. For no reasons .. The reason is God wants to hide it from the devil lest he distract it

 6. Bwana Yesu asifiwe! Napenda kutoa ushauri kwa admn kuwa ni vyema Post mpya mpya au maswali na majibu mapya yawe ya kwanza au juu kuonekana na siyo Post za zamani za 2008, Post mpya au swali na majibu yake mapya viwe mwanzo/juu ya zingine za zamani. Amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s