Kuna haja ya kuombea uchumi wa Nchi?

pastor

“Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishauri hapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosema kama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanye maombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo? As a Theologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njia za ku-produce zaidi, we don’t pray for this, we don’t have to pray for this”

MCH PETER MSIGWA BUNGENI 19/6/12
Habari Kamili…..

“Matatizo hayawezi kutatuliwa kwa akili ile ile iliyotumika kuyasababisha”

Akichangia mjadala juu ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011/2012 pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2012/2013 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2012/2023 siku ya tarehe 19 Juni mwaka 2012; Mhe Mchungaji Msigwa alijenga hoja zifuatazo;

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuu ambayo naipenda sana inayosema:-

“Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result” yaani uwendawazimu ni kufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-

“Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them”. Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire (nawahusudu) sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason (tuna -dadisi), mahali ambapo tuna question (tunahoji) na mahali ambapo tunatoka na solutions (ufumbuzi) ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona is the opposite (ni kinyume kabisa), binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupo hapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika na mamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabara mbovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu za Watanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo ya khanga!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulaya karne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwa na fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofika karne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hii katika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamoto zinazotukabili kama taifa. Badala ya kukaa na kujiuliza kwa nini tupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongea ngonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga, kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamia ya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapa lakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. James Madison mwaka 1822 alisema, “knowledge forever will govern ignorance”. Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-govern knowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge, tunalipeleka wapi taifa? Akichangia professor hapa hana tofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtu mwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we taking this nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha za Watanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo ya msingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya? karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanza kudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi
wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi. Pia ninashangaa katika mapango wake wa bajeti taifa hili kama tunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma? Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maana yake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wako shuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sana kuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wa bajeti tulio nao hapa, there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa. Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wa kivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatua matatizo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume ni wengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini? Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ili tuwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto, ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusoma shule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya, hauzungumzi. Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifa limetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maana nimesema problems can not be solved by the same level of thinking that created them, you guys you are tired! Kwa sababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuweka kwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iweze kutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is the principle, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different results and this is what we are doing.

Tunafanya hayo hayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo. Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo ni matatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada ya mwaka ni matatizo yaleyale, why can’t we think a little bit more? We can’t stretch our brain a little bit more kama taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengine ambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoa ushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekana wanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoa maamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business as usual. Ndugu zangu, where are we going? Where are we heading?

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tena karibu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa, they can not think properly, they can not question, they can not ask. Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwe stretched ili uweze kuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapa duniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungeni tunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bunge la kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapa kwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja. Tuna mfumo na traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi na ulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwa kuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala ya kutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuri ili na wewe utimize wajibu wako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwaka linaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCM itaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo la Serikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kuna mmoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kama mtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya
Wachungaji vilevile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishauri hapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosema kama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanye maombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo? As a Theologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njia za ku-produce zaidi, we don’t pray for this, we don’t have to pray for this.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapa tumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki na wanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewa fedha bali wananchi wa Iringa wamenichangua, wananiamini na ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitaji kujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenye matatizo. We have to address this problems lakini siyo tunakuja hapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watu mnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba niachie hapo. Ahsante sana.

MCH. MSIGWA
Advertisements

18 thoughts on “Kuna haja ya kuombea uchumi wa Nchi?

 1. Paul;
  Ni kweli akili ya binadamu ina uwezo kamili wa kujisimamia katika mambo ya kimwili. Lakini kuna kitu kizuri umemalizia katika sentensi yako kuwa kama hakuna mwingilio wa kiroho.

  Kwa kiswahili kingine kukiwa na mwingilio wa kiroho akili ya mwanadamu hukwama.

  Kinachotusumbua sisi si kukosa akili lakini ni kukosa uadilifu. Kitengo cha uadilifu katika nchi yetu na Afrika kwa ujumla kimeingiliwa, na mwingilio huu ni wa kiroho maana hicho ni kitengo cha kiroho.

  Siyo kweli kwamba mikataba mibovu tuliyonayo imetokana na wataalamu/viongozi wetu kutojua kusoma mikataba, hapana. Hiyo mikataba wameiingia hivyo makusudi baada ya kupewa hongo na wengine kuwa moja ya wanahisa katika makampuni tuliyoingia nayo mikataba.

  Kinachosemwa ufisadi leo si tatizo la kiakili hilo, ni la kiroho.

  Nyerere kwa sababu alikuwa mwadilifu, alikubaliana ukweli wa kiakili kuwa madini yetu yasichimbwa hadi tutakapokuwa tumepata wataalam wetu wa mambo ya mdini hapo baadae.

  Lakini hawa jamaa waliokuja baada yake pamoja na wao kuufahamu huo ukweli wa kiakili kama Nyerere, mwingilio wa kiroho unaoitwa ufisadi uliwaamuru kuukataa huo ukweli na kufanya tunayoyaona leo.

  Ndio maana mimi nikasema hatuhitaji kuombea uchumi as uchumi bali watu wanaosimamia rasirimali zinazozaa uchumi, maana ni lazima wawe watu sahihi, kimaadili, kiutaalam, na kifikra, kama wewe ulivyo katika suala la kula vizuri kwamba humwagimwagi chakula.

  Asante.

 2. Ndg Sungura,

  Huwa ninapata taabu ni za kipagani tu, za waabudu miungu. Lakini linapokuja suala la UCHUMI wamefanikiwa mno. Na huwa siamini kama huwa wanaomba au wamefanikiwa hivyo kwa sababu ya maombi.

  Imani yangu ni kuwa akili ya Binadamu ina uwezo kamili wa kujisimamia katika mambo ya kimwili iwapo hakuna interference toka katika ulimwengu wa roho.

  Mimi sijawahi kuomba Mungu anisaidie niweze kuvaa nguo na viatu vizuri. Au kuomba Mungu niweze kula chakula vizuri pasipo kumwaga mwaga chakula. Akili inayotumika kutambua kuvaa viatu kilamilifu ndiyo hiyo hiyo inayofaa KUTUMIKA KATIKA KUTAMBUA KWAMBA RUSHWA NI ADUI WA HAKI. Akili hiyo hiyo inatosha kutumika kutambua kuwa BARABARA IKIJEGEWA CHINI YA KIWANGO HUHARIBIKA MAPEMA. Sasa tatizo ni KUTOKUZOEZWA TU KUTENDA SAWASAWA NA MIPANGO.

 3. Lakini kitu kingine cha msingi juu ya uchumi ni haki kutendeka kwa uwazi kwanza kanisani.

  Unajua mapato na matumizi ya makanisa mengi hasa yanayoitwa makanisa ya kiroho hayana uadilifu ndani yake. Kuna ufujaji mkubwa wa mapato katika kanisa,kiasi kwamba ni vigumu kwa wachungaji na maaskofu kuinyoshea kidole serikali kwa ubadhirifu wa mali za umma .

  Tunaona katika maknisa mengi jinsi mapato ya kanisa yasivyotumika sawasawa na neno la Mungu linavyoagiza.

  Mungu ni Mungu wa haki, haauwezi kutoa kibanzi kwa jicho la jirani wakati kwako kuna boriti. Kwamba hatuwezi kama kanisa tukamwomba Mungu ufisadi ukome na awashugulikie mafisadi ili uchumi ukue wakati ndani ya kanisa tunafanya yaleyale.

  Kuna wakati serikali iliwahi kutishia kuanza utaratibu wa kukagua mahesabu ya mapatao na matumizi ya taasisi za kidini. Aise wachungaji wengi walipiga kelele na wengine hata kutaka kuilaani serikali!

  Na mimi najiuliza, kwani kama matumizi ni ya haki na yako wazi,shida iko wapi wakaguzi wakija?

  Hela za makanisa wanakula wakubwa kwa sehemu kubwa kama tu ilivyo kwa serikali!

  Haki huinua taifa!

 4. Mpendwa Sungura nimekuelewa vizuri na leo ktk kusoma Biblia nikakutana na neno kutoka 2falme 2:19-22 Ktk kulitafakari Roho Mtakatifu akanifundisha kuwa kuna haja kabisa ya kuombea uchumi coz nchi inaweza kuwa nzuri ina madini na kila kitu bt ikawa inazaa mapooza hivyo kuna haja ya kuukombo uchumi ili tuweze kula mema ya nchi!Hata shetani alipomjaribu yesu alimtabishia kwa kumwonyesha milk yote ya dunian na kumtel kuwa akimsujudia atampa so kuna haja ya kuuteka mikononi mwa ibilisi ili wamiliki watu wanaomjua Mungu!nakubaliana nawewe pia kunahaja ya watu wanaomjua Mungu wakashika uchumi!coz hata tukiomba na nchi iczae mapooza bt ikikutana na Mafisadi Hali itaendelea kuwa mbaya so vyote vinahitajika kuombea yaan Uchumi ugeuke kuwa baraka na Viongozi wanaomjua God!Nitabarikiwa zaidi kama nitapata jipya la kujifunza kutoka kwako na kwa wapendwa wote.MUNGU AWABARIKI WOOTE!

 5. John Paul, salaam.

  Tukiamua tu kufuata kanuni tukaacha kuwaombea watu wanashika hizo nyadhifa, halafu kanuni/sheria ikasema mtu akikiuka auawe, believe me, tutawaua mno maana hakika hawataacha kukiuka hizo kanuni.

  Kwa ajili ya uchumi wetu kuwa sawa, ni lazima tumwombe Mungu watu sahihi wakae kwenye hizo nyadhifa.

  Mungu mwenyewe alinyosha mikono kwa wana wa Israel, maana pamoja na sheria kuwa kali lakini bado walizivunja.

  Asante.

 6. Tumaini nakupenda mjoli wa Bwana.

  Uchumi kama uchumi hauna tatizo, vyenye matatizo ni vile vitu ambavyo uchumi huvitegemea ili uweze kukuwa na kuwa bora. Na kiini ya hivyo vitu vyote ni mwanadamu.

  Tukipata watu sahihi wakasimamia rasirimali tulizonazo hakika uchumi qwetu utakuwa.

  Tunaposema watu sahihi ni watu wenye maadili sahihi, wenye kujua kuongoza, wenye maarifa sahihi, wachapa kazi, nk.

  Mfano mzuri ni mtu ambaye alitakiwa na Farao kwa ajili ya kuweza kukusanya chakula wakati wa miaka saba ya shibe amabacho kingetosha kuivuka miaka saba ya njaa.

  Farao hata hakupata shida, alijua moja kwa moja huyo mtu ni Yusufu. Sasa angalia uwezo wa Yusuf katika hizo nyanja/sifa nilizozisema. Yusuf ukiangalia jinsi alivyoifanya ile kazi utagundua uwezo wake haukuwa wa kawaida, maana hakupewa hiyo nafasi kiushabiki kama wengi wa viongozi wetu wanavyopewa nafasi walizonazo

  Asante.

 7. Kwa nchi kama Tanzania uchumi si wa kuombea. Tunao Tayari! Mbuga za Wanyama, Madini, Ardhi nzuri kwa kilimo, Milima mizuri, watu wa kutosha.

  Uchumi waTanzania UNATUMIKA VIBAYA. Pesa zinapelekwa mahali pasipostahili kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi.

  Na wala Viongozi siyo wa KUOMBEA bali KUFUATA TU KANUNI zilizowekwa kwamba mtu akigundulika amekula rushwa afanywe nini, akiwa ameiba afanywe nini, akizembea afanywe nini, akipotosha muelekeo wa fedha za maendeleo afanywe nini. Yakizingatiwa hayo TU uchumi utaelekea mahali sahihi na maisha ya watu yatabadilika!

 8. Mpendwa Sungur nakupata vizuri bt Tunaweza sema tuna madin,mbuga za wanyama,bandari na n.k.lakin hivi ili vifanyike kuwa uchumi si lazima vihusiane na watu ili viwe uchumi mbaya au mzuri?Nilipo toa mfano wa Kilimo nilikuwa nikimaanisha nacho kinatumika kuinua uchumi wa nchi!Ndiyo maana nikasema bila mvua kilimo kitakwama!hata watu wajitume vip!Nachukulia Mvua ni kama madin ambayo ndiyo uchumi wetu!Isiponyesha ni kama vile madini hajatumika vizuri kuleta matokeo ya uchumi!Je kwa mahusiano hayo c bado Mungu anahitajika kuombea Uchumi ambao unawa inlude watu na madini,Mvua n.k?Wewe unaonaje Sungura?Itapendeza tunapoelimishana coz naamini wote tunapenda kujifunza!God Bless u.

 9. Nafarijika kuchukua nafasi hii kusema UCHUMI SIYO TATIZO ila tatizo ni nafasi na maono watu hawatambui. Nchii hii hatustahili kuwa kama tulivyo sasa yaani hatukustahili kuwa maskini hivi ukiangalia fursa zote zinapatikana hapa, ukianziaa anga, nchi kavu na majini kote fursa.
  Kwa nature ya nchi yetu hatuna sababu ya kulalamikia UCHUMI tunachotakiwa kulalamikia ni VIONGOZI kwa sababu wameshindwa kusimamia yale mambo ya msingi waliotakiwa kusimammia zaidi ya kwenda kusimamia utashi binafsi wa mambo yao ndiyo maana sasa tunalalamika uchumi mbaya.
  Binafsi ninasema kuomba ni muhimu; kama kweli tunaitaji nchi nzuri yenye uchumi na mipango mizuri kwa pamoja embu tuombe kuanzia sasa kwa ajili ya 2015 Mungu atupatie viongozi watakaokwenda kusimamia MAONO na siyo NAFASI. Tuombe kwa Mungu tupate viongozi bora na siyo bora viongozi tukiwapata hao viongozi bora hakika uchumi utabadilika na kukuwa kwa kuwa itawekwa mikakati bora ya kukuza uchumi na hawatakuwa na utashi binafsi kwa kuwa wataweka maslahi ya wengi kwanza.
  Mungu atubariki na kutulinda na atupatie viongozi bora kwenye changuzi zote kuanzia sasa na wote wale wanaoteuliwa wasimamie kusudi la Mungu

 10. Nelson, ni kweli tunatakiwa kufanya maombi.
  Lakini maombi tunayofanya si kuombea uchumi bali viongozi ambao uchumi ni matokea ya wao kuwa na mipango bora na yenye tija.

  Kwa mifano uliyotoa hapo juu ukiangalia tu unagundua kuwa kwa ule mfano wa zile fedha za kujenga zahanati kuliwa, cha kuombea hapo si hizo fedha bali watu waliokula hizo fedha, tena si hao watu bali ni ile roho inayofanya kazi ndani yao.

  Na kama uchumi haukuwi kwa sababu labda hakuna mvua,ca kuombea hap si uchumi, angalao ni mvua ili inyeshe.

  Tunahitaji viongozi wenye maadili, wachapa kazi, wenye kujua kupanga vipao mbele vya taifa, wenye kusimamia sheria n.k.

  Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake Alfonso aliwahi kutuambia sisi kama taifa tunatakiwa tukae chini tuangalie upya vipaombele vyetu (yaani nini kifanyike kwa wakati gani).

  Hayo yakishakaa sawa,kinachobaki ni sisi tu kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kumcha na kumshukuru Mungu.

  Asante.

 11. Mungu ametupatia mengi.
  MALI ZIPO ZA KUTOSHA SHIDA NI ULAFI NA UFISADI.

  WAACHENI WENYE INJILI YA PANDA UVUNE LABDA NDIYO AGENDA ZAO ZA KUOMBEA MIFUKO NA MATUMBO YAO YAJAE.

  OLE MLAO KUVIMBISHA MATUMBO YASIYO SHIBA HUKU MKIMNYANGANYA MASIKINI KWA RUSHWA NA DHULUMA.

  “HAYA BASI ENYI MATAJIRI! LIENI, MKAPIGE YOWE KWA SABABU YA MASHAKA YENU YANAYOWAJIA. MALI ZENU ZIMEOZA, NA MAVAZI YENU YAMELIWA NA NONDO. DHAHABU YENU NA FEDHA YENU ZIMEINGIA KUTU, NA KUTU YAKE ITAWASHUHUDIA, NAYO ITAKULA MIILI YENU KAMA MOTO. MMEJIWEKEA AKIBA KATIKA SIKU ZA MWISHO. ANGALIENI, UJIRA WA WAKULIMA WALIOVUNA VIMEINGIA MASIKIONI MWA BWANA WA MAJESHI. MMEFANYA ANASA KATIKA DUNIA, NA KUJIFURAHISHA KWA TAMAA; MMEJILISHA MIOYO YENU KAMA SIKU YA MACHINJO. MMEHUKUMU MWENYE HAKI MKAMWUA; WALA HASHINDANI NANYI. “
  YAKOBO 5:1-6

 12. huo uchumi gani tunaouombea? hata ukienda kumuomba Mungu mfano unaomba,”mungu naomba unipe hela” Mungu hawezi kukunyeshea mvua ya hela bali atakupa wazo au mbinu (ambalo)ukilitumia vzr unapata hela uliyokuwa unaomba! tz Mungu ametupa rasilimali nyingi mno ambazo wataalam wanakwambia hata tungeamua kuitumia sekta ya madini tu vzr tungetoka. achana na bahari ambako unapata bandari na shughuli za uvuvi,kuna gesi kuna maliasili hapa nazungumzia mbuga za wanyama na vivutio ambavyo nchi nyingine hazina. kuombea uchumi ni sawa na kuendelea kuombea jambo ambalo tayari umeshajibiwa. nchi yetu imekosa siasa safi na siasa safi haiwezi kupatikana mpaka watu wamemcha Mungu. na kama watu watamcha mungu utapata siasa safi namaanisha hakutakuwepo na mikataba ya kifisadi ambayo inadidimiza uchumi ambao tayari Mungu ameshatupa, kama watu watamcha Mungu huwezi kukuta kiongozi anafanya vile anavyotaka bali atafanya kama Mungu anavyotaka hata ikibidi afe lakini atafanya kile anachotaka Mungu! na kama mnataka kukubali kuwa hii nchi ina utajiri mkubwa mno angalia mataifa makubwa yalivyotoa macho huku kwetu! kwa nini? kuna kitu wameona ambacho sisi hatujui jinsi gani ya kutumia na wao wanajua jinsi ya kutumia so wankuja wanachuma wanazidi kutajirika! mi sijasema tusiombe ila tunaombea nini? na tunaombaje? kuna vitu vingine tusipofanya kwa upande wetu hata tukiomba namna gani hatutaona matokeo! kwangu mimi kuombea uchumi ni sawa na mtu anyefunga na kuomba Mungu ampe imani wakati tayari Mungu alishasema “imani chanzo chake ni kusikia kunakokuja au kunakotokana na neno la Kristo”. kwa maana nyingine ili uwe na imani ni lazima uwe msomaji sana wa Neno la Mungu na pia uwe unapenda kusikia au kujifunza kutoka kwa watumishi wake aliowaita! sasa tujiulize kama mungu ametupa madini ardhini na yapo kwetu na kuna wengine hawana na wanhitaji kutoka kwetu na tukiwauzia tunapata fedha zinazokuza uchumi wetu halafu sisi kwa kutokumcha kwetu Mungu tuaingia mikataba ambayo haitunufaishi bali inawanufaisha wanaokuja kununua,baada ya hapo tunarudi kwa mungu eti tunaombea uchumi ukue kweli mungu anatuelewa? tunatoa misamaha ya kodi kwa makampuni labda unaisamehe kampuni kulipa kodi kwa miaka mitano ikiisha unataka ilipe kodi unakuta wanabadili tu jina wanasema biashara si nzuri wanakwambia wameiuza hiyo kampuni kumbe ni walewale isipokuwa kinachofanyika ni kukwepa kodi tu halafu tunataka kuomba uchumi ukue? Wengine watasema nimeingia kwenye siasa lkn kama tunataka kuona mabadiliko ktk uchumi wetu tunahitaji siasa safi na siasa safi haiwezi kupatikana kama watu hawamchi Mungu! “HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOTE”

 13. Mpendwa Sungura nimejaribu kutoa kasample ka hao wanaoweza kusimamia uchumi coz uchumi unamhusu kila mtu, mfano Kama mimi ni mtumishi wa serkali za mitaa Labda idara ya Mipango yaa Afiss Mipango na kuna Fedha za ruzuku zimeletwa kujenga
  Zahanati,Madarasa,Nyumba za Walimu au Mradi wa Maji Kwenye Kijiji flan!Then akakaa Mkurugenz,Afisa Mipango na Mweka Hazina wakazichakachua fedha kiasi na Miradi iliyokusudiwa haijakamilika je Hiki c kizuizi cha uchumi?

  Au wakulima wamelima mazao kwa wakati na wamepanda kwa wakati ghafla mvua zikanza kusumbua na wakati wa mavuno badala ya ekari moja ya mahindi kupata gunia kumi unapata mbili!

  Je kweli hapo hatuhitaji maombi?Au unaonaje mpendwa Sungura?

 14. Ukitaka watu waokoke unawaombea au unawahubiri injili?

  Ukipata jibu la hapo ndipo utajua kama dawa ya kukuza uchumi wa nchi ni kuuombea au…

  Nelson ukisoma tena mchango wako utagundua ulichosema tukiombee si uchumi, bali viongozi wa kisiasa ambao uchumi ni matokeo ya utashi wao!
  Maana umesema ”tunapoombea uchumi naamini tunataka Viongozi wa nchi wasimame kwenye nafasi zao…”

  Sasa hapo umeombea uchumi au umeombea viongozi?

  Asante!

 15. Hivi tunapoomba nadhani kuna Mambo mengi ya kuombea!mfano haja zetu binafsi,ndugu na jamaa zetu,watumishi wa Mungu,Viongozi mbalimbali,Amani ya nchi pamoja na huo uchumi wa nchi ambao Postor haoni haja ya kuuombea!Pamoja na theory zote lakini Mungu pekee ndiyo Master Planer!Na tunapoombea uchumi naamini tunataka Viongozi wa nchi wasimame kwenye nafasi zao na wawe wazalendo ambao hawawezi kuingia Mikataba yenye kuwanufaisha wao!Hivi kweli kuna mwananchi anayekaa tu akisubiri neema imshukie?Bt kuna mafisadi wachache wanaoila nchi hao ambao ndiyo yapasa kumweleza God ahusike nao!Unakuta mafisadi wengi ndiyo wakwanza kupinga ufisadi wakati wao ndiyo Mafisadip!Kweli Postor huoni sababu ya kumtel God aingilie kati?Unahitaji maombi Pastor! 4real u need prayers!Ngoja niishie hapa kwanza!God Bless U!

 16. Mambo hayajileti yenyewe mambo yanasabishwa kutokea! kama watu hawataki kufanya kazi wasitegemee uchumi kukua kwa hiyo hata wachungaji wakifunga na kuomba eti kuombea uchumi kama watu kwa “upande” wao hawatafanya wajibu wao uchumi hauwezi kukua mchungaji yupo sawa! dada Mary naomba kama inawezekana lirudie kulipost lile somo mambo hayajileti yenyewe mambo yanasababishwa kutokea. haya ndo yale ya mwanafunzi ameokoka hataki kusoma halafu anajifariji eti Mungu amesema tutakuwa vichwa wala siyo mikia, halafu mtihani ukija anafeli anaaanza kumlaumu Mungu!

 17. i thnk ths pastor should assess himself and realz that the bible says u should ask for everthng God never do in suo motto,u must speak tht why it said the words of your mouth may create or condem

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s