Kanisa la Kilutheri Marekani lapata Askofu Mkuu mwanamke!!

liz

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani (ELCA) tarehe 14/08/2013 limemchagua Bi. Elizabeth Eaton kushika nafasi ya uaskofu mkuu,  alipata kura 600 dhidi ya anayemaliza muda wake Askofu Mark Hanson, ambaye alipata 287.

Askofu Eaton, ambaye ni Askofu wa ELCA Cleveland, ni mama na mke wa Mchungaji Conrad Selnick. Mtumishi Eaton anaungana na Askofu  Jefferts Schori Katharine, ambaye mwaka 2006 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuliongoza kanisa la Anglikana duniani.

Eaton ataongoza kanisa kwa miaka sita (6) kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.

“Bwana analitoa Neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa” Zaburi 68:11

Advertisements

40 thoughts on “Kanisa la Kilutheri Marekani lapata Askofu Mkuu mwanamke!!

 1. Lwembe,
  Hakuna anayependa sifa kwa maana ya kuzisaka kwa udi na uvumba lakini ni ukweli pia anayestahili sifa/heshima basi apewe na ni ukweli pia zikija, sizikaushii maana ni tamu sana, tusidangaye hapa! Kutiwa moyo, kukubaliwa wewe na kazi yako, ni tamu sana, napenda sana maana mie kumung’uny’a mung’unya kitu fact/truth, siwezagi! Ili iweje kwanza nijikaushe! So what badala ya kujiachia na kufurahi ktk Bwana! Namna gani hapa!

  Kilichokosekana ktk post yangu kwako kwako ni kutokukuwekea page ya Vifupisho na Maana ya Maneno, right? so here we go
  Ibra = Ibrahimu( kutumia Ibra niliona inasaidia kwenda faster kuandika)
  Honey = Asali and maana ya post ni mpenzi wa moyo
  Nilitegemea msomaji wa mada hii na commentz zote, ungejua tu maana ya maneno hayo na vifupisho au umetaka tu tupige mastory yako ya town Jahazi ya kraaaaaudis efwe eme radio.

  Ukitaka kujua kuna u-honey kati ya Hajiri na Ibra, muulize Ibra ALIJISIKIAJE wakati Bi Mkubwa alivyocharuka na kufanya MAAMUZI MAGUMU? Na ili ikukolee vema, jiulize kwa nini MPAKA Mungu aingilie mtiti ule kwa kuongea na rafiki yake kirafiki!

  Sasa kunisisitizia Ibra alikua “Rafiki” yake Mungu?!! ndio unatisha au? Mbona yeye Ibra haja nitisha ivyo? halafu kama yeye ni rafiki wa Mungu, mimi je ni adui wa Mungu? hujui mie ni Mtoto kabisaa wa Mungu? namna gani hapa Lwembe!

  Kuhusu Laana, hakuna mzaha wala nini, Mimi nilisema toka mwanzo(husomagi na kumaliza kabla hujakurupuka kujibu), soma comments zangu,nilisema nini-kama kuna sehemu nilisema KWA MADA HII kua Mungu aliwalaani, weka hadharani hapa sasa ivi.Na Kama Siyi ndiye aliyepitiliza,nikamchallenge ajirudi na kuyasoma maandiko kisha akarekebisha na nikampongeza na ukaona wivu, why umenijumuisha ktk scandali iyo? HUO SASA NDIO MZAHA TENA WAKUTIA HASIRA KALI-usirudie tena, mwisho leo!!!!!!ole wako uniingize tena ktk kashfa kubwa kama hii ya kusema mimi nimesema Mungu akiwalaani Watu wake wakati nasoma neno vema tu na kuelewa.

  Kuhusu kufunguka macho, ati Siyi kanieleza vizuri tu kulingana na mtiririko wa tukio la kula tunda halafu bila haya umeni shauri ivi.. ‘’jaribu kuwa na moyo wa kujifunza kidogo!
  Jibu: Kwanza napenda kujifunza na kudaka vitu kwa kweli na ndio maana comment zangu za kwanza kwa Siyi, nilifurahi sana na kumbariki kwa baadhi ya points njema kabla hajayeyusha raha anayosikia kwa mimi kumu-appreciate, akanipangua kwa Kiswahili cha kamusi namely ‘Kongole’ sijui ‘kongolo!’ anajua mwenyewe(tatizo lako lilelile- husomi kwanza til mwisho kabla ya kujibu au in this case, tukishaendela sana ktk mada, unasahau tumetoka wapi-mi sisahau ivyo kunipa ushauri huo ati niwe na moyo wa kujifunza, ni usingiziaji tu(kwanza umeiga toka kwangu hilo shauri ilo nimekua nawaambia several time ktk mada ya Mafundisho Kuhusu Makatazo kwa Wanawake-unatakiwa ua-knowledge kwanza.

  Pia Nimewaambia kila mara kua Neno la Mungu ndio hatimaye ukata mashauri na kuamua mambo. Katika Mwanzo.3:1-13 imeandikwa ivi… 1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. 9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. 11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? 12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. 13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

  Mimi nikatoa maelezo haya…Inasema mstari wa 6…Mwanamke akala tunda na akampa mumewe naye akala-Notice: iko at the same verse! Halafu verse 7-imeandikwa.. NDIPO( Notice neno ‘Ndipo’-matokeo word…. Macho YAO-notice: ‘yao’ (sio ‘yake’), halafu Biblia inaendelea kusema…WOTE yakafunguliwa-Notice ni ‘wote’ sio Adamu kwanza! Halafu inasema- ‘WAKA’-siyo ‘aka’…fahamu kua ‘WAKO’-siyo ‘yuko’ uchi …nk na yote hayo ktk mstari the same.

  Kisha nilimuuliza hiki…, umefikiaje iyo conclusion KAMA INGEKUA KWELI anyway ya kusema Adamu ndiye alijitambua wa Kwanza u-uchi ivyo maana yake ndio inathibitisha ndiye PEKEE aliyepewa majukumu na Mungu? HOW IN HELL OR HEAVEN HAVE YOU COME TO THAT END

  We unasema hiki-‘’Kama Hawa ndiye aliyedanganywa na kula tunda hilo na kisha kumpelekea na mumewe, naye mume alipolila….( umeingiza hili neno…’’akampelekea’-kutaka kufitisha hisia zako kua Eva alikua somewhere na akala huko huko KISHA kumpelekea Husb, lakini Bible says ‘’akala na kumpa mumewe’’ WOTE- kwangu naona walikua wote hapo hapo na nyie mnatoa idea kua walikua mbali ndipo ile dhana kua Eva baada ya kula hakujitambua na eti ni mpaka alipokula Mwanaume!Yaani watu wako 2 mume na mkewe, mke anachukua tunda na kula na kumpa mumewe na kisha Bible inasema verse 7…macho YAO yakafunguka….unawezaje kusema Eva hakujijua mpaka Adamu alipokula? Hii mmeitoa wapi ?

  Huko pa kukutana J2, Siyi akupitie wewe, mkanieleze mmejuaje kua alikula kwanza na hakujitambua kana kwamba kulipita dk kadhaa?

  Press on.

 2. Siyi,

  Umesema mjadala unafikia mwisho! Ok tunamalizia ivi, kama ukiridhika, Amen, la bado hujaridhika au yeyote humu anapinga na asema sasa, nitafurahi kushughulika na issue izo za mengineyo au yaliyojiri.
  (a) Tumekubaliana kua Mungu hakuwahi kumlaani Mtu na kua wengi hua wanasoma haraka hapo kudhani Mungu aliwaalaani kumbe laana ilitamkwa/ilielekezwa kwa kitu kingine.

  (b) Tumekubaliana kua Kimajukumu/Nafasi na Jinsia, Mungu mwenyewe alitotofuatisha toka JUU

  (c) Natumai umeelewa kua tofauti izo, haimaanishi kamwe ziko ktk hali ya ubaya/unegative yaani mwanamke kua dangerous/risk au shetani saa yoyote yuko naye benet-benet

  (d) Kwamba kama ni swala la uwovu na dhambi au shetani kumtumia nani basi Wanadamu wote hawafai, wamepungukiwa na utukufu wa Mungu na ndiposa WOTE-hakuna cha Me/Ke walimuhitaji mmoja tu kuwafanya wakubalike kwa Mungu ivyo KAMWE hatupaswi kusonteana vidole na hata nikadokeza kua ktk Historia ya Mwanadamu, wanaume wamefanya na kuongoza maovu makubwa mno wakati Hawa alishapita siku nyingi na ndio maana kwa kua wote hawafai bila Adamu wa Pili, wakati Mungu anagawa adhabu, mbali na kusingiziana/kurushiana mpira, aliwachapa wote

  (e) Kwamba Mungu akishatutakasa wote kwa damu yake Mwanae, basi tuna sifa sawa kabisa kupata vya mbinguni na uko hawajali huyu ni Me/Ke na afterall, hatimaye tunakoenda uko uko hakuna cha Me/Ke. Ivyo basi ktk karama/huduma/vipawa, Yeye RM hutoa kwa YOYOTE kama apendavyo na kwa sababu iyo, wanaweza fanya mazito ya Bwana na huduma kama sisi kabisa maana in the first place yeye RM mwenyewe amewajaza na kuwapa vya JUU-nani au kiumbe gani athubutu kumpangia/bagulia RM kugawa vyake na kuwatumia, nani? na asema sasa hapa!

  (f) Kitaasisi ya Ki Mungu yaani Kanisa, hawaruhusiwi kua Viongozi wa JUU kuliongoza na kufanya huduma kwa nafasi ya juu kama kutoa miongozo,maelekezi,dira,maonyo,marekebisho nk,kutawala uko, mamlaka iyo, nafasi iyo, kapewa Mwanaume na iyo ni Biblia ILA maana yake si ktk tone chungu/negative kama ilivyokua inawekwa na washirika baadhi humu, mantiki yake ni ya KiMungu tu kutunza adili la Mungu na la Watu wa Mungu kua MWANAUME ni kichwa na asitawaliwe na Mwanamke

  (g) Kitaasisi za Kibinadamu kama madhehebu, dini, vikundi vya imani, uko ni bora liende na watajijua

  (h) Kwamba andiko hili-1Peter.3:7 linalosema Wanawake wanashabiana na hali gani, ningependa kushare mambo kadhaa hapa muhimu kwa ufahamu-swali hili nilikuuliza sana Siyi, sasa barikiwa kwa haya.

  • Mstari huo unasema ivi kwa Kiswahili…. ‘’ Kadharika ninyi Waume, Kaeni na Wake zenu kwa Akili na kumpa Mke heshima KAMA chombo kisicho na nguvu,….. Kiingereza inasema…’’ Husbands likewise, dwell with them with understanding, giving honor to Wife AS TO THE WeakER vessel….
  .
  • Mstari huo haukusema,..Mwanamke NI chombo dhaifu au A woman is weak vessel lakini imetumia KAMA/AS TO THE! Ukisema ivi.. ‘Jana ktk Mechi, Siyi ALIKUA simba na Lwembe kibogoyo, mantiki haitakua sawa na kusema.. ‘Jana ktk mechi, Siyi alikua KAMA simba na Lwembe kibogoyo.
  • Kwa andiko hili, linapotuambia tukae nao KAMA vyombo dhaifu, the idea hapa Peter ana rusha ktk akili na fahamu za moyoni kwa wanaume ni kua, KWA KULINGANISHA NA WAO WANAUME, wajua kua MWANAMKE is AS WEAK VESSEL-Ufahamu huo then utapelekea MWANAUME mwenye akili kua Mume bora sana kwa Mke yule. Hapo Peter wala hana mpango eti anafundisha au kutoa picha kua hao viumbe ni hatari kweli, anytime wanaleta uharibu au devo home.

  • Ndio maana NKJ version Kiingereza, ilo Neno ‘dhaifu’ au ‘chombo kisichokua na nguvu’, inaweka idea ya comparison yaani as weakER vessel ukilinganisha na Waume/Wanaume-ni ivyo tu wala si maudhaifu/manegetive/mahatari-hatari ambayo wanaume huwa fahamu zao zinawapeleka haraka kutafsiri ivyo na kusukumizia hisia zao wenyewe kabisa kwa ilo andiko kwamba linamaanisha ivyo

  • Neno ‘weaker’ au hata ‘weak’ , Bible nyingine inatumia neno ‘delicate’ na Ukiangalia maana ya maneno weak/delicate in connection sasa na Me kwa Ke wake, ni ajabu kweli kujua jinsi Mungu amewapa Wanaume/Waume jukumu kubwa sana. Baadhi ya maana za maneno hayo ni: easily breakable, can easily be hurt/ feel pain, ni sensitive, transparent, reflect things(mirror) nk…which all mean not that Mungu anatumbia/anatupa msg kua hawa viumbe ni wabovu kweli kweli bali hasa maana yake ni kua kama wako kama delicate/weaker vessel kwa maana zile baadhi juu, basi wanataka care, love, nice treatments, kupewa nafasi, kutiwa moyo, kulindwa,kutunzwa, kufahamiwa, kueleweka,kusifiwa,kufurahiwa nk

  (i) Tumekubaliana kua UN wana kazi njema sana kuhusu kutetea haki za Wawawake lakini pia tukasema ktk kufanya ivyo, wamepitiliza Bible kwa baadhi ya utafutaji na usimamiaji wa haki za Wanawake

  Press on kuwathamini Mama, Dada, Wake, Wachumba, Shangazi, Binadamu zetu wa Kike nk, Tukiwapa nafasi zote isipokua moja tu ya Utawala na Maongozi Ndani ya Kanisa, Familia.

 3. Seleli na Siyi,
  Msipende saaana sifa! Nawaona mnavyojiongelesha bila hata adabu kwa wakubwa zenu! Hivi nikikuuliza wewe Seleli, ni wapi katika Biblia iliposema kuwa Hajiri alikuwa “honey wake Ibra”? watoto wa kiswahili bwana, yanawatokaga tu, hiki sio kijiwe kaka!!! Angalia uliyoyaandika:
  “”Mstari 15 = Maji ya kunywa kumsaidia njiani aliyopewa na honey wake Ibra, yanakwisha akiwa na son wake na ni jangwani
  Mstari 16= Honey wa Ibra analia, hali tete jangwani…””
  Uwe na Heshima na Adabu kidogo unapowazungumzia wakubwa zako! Ninyi ndio wale mnaoingiaga na kokoko mkizigonga kwa bidii sehemu ambazo malaika wananyata!! Huyo unaye mwita “Ibra” na kumbambika “u honey” na binti wa kazi, wakati Sara anakusikia, sijui itakuwaje, si unajua kuwa huyo ni “Rafiki” yake Mungu?!!

  Katika mizaha yenu isiyo na staha, mmebandika LAANA binti wa Mungu Hawa, ambayo haipo. Ni wapi Mungu alimlaani Hawa?? angalieni ninyi wenyewe mnavyokubaliana hapa katika unafiki au ujinga ambao Mungu aweza kuhitaji muulipie, labda Kanisa la hapa SG liwaombee!:

  SIYI: Kuhusu laana kwa Adamu au Hawa; Kimsingi Ukisoma hapo kitabu cha mwanzo 3, huwezi kuona sehemu yoyote inasema kuwa Adamu anapewa laana kama Hawa.

  SELELI: Umesema vema hiki ivyo umekubali umeelewa nilichokuambia hiki…’’Kuhusu laana kwa Adamu au Hawa; huwezi kuona sehemu yoyote inasema kuwa Adamu anapewa laana kama Hawa’’ = safi sana na hongera kufahamu.

  Halafu kuhusu kufunguka macho, Siyi kakueleza vizuri tu kulingana na mtiririko wa tukio la kula tunda, jaribu kuwa na moyo wa kujifunza kidogo! Kama Hawa ndiye aliyedanganywa na kula tunda hilo na kisha kumpelekea na mumewe, naye mume alipolila , NDIPO MACHO YAO YAKAFUNGUKA, wakijiona wako uchi, sasa unabisha nini kuwa Hawa alipokula alijiona yuko sawa tu mpaka mumewe alipolila ndipo ikawa hivyo mambo ya kujiona hovyo!?

  Halafu ninyi inabidi nionane na wachungaji wenu ili wawaanzishe Sunday school, mkikomaa ndio mjage huku, maana mnajiandikia tu, yale ma confidence pori 400%!!!

  Haya tukutane Jumapili asubuhi sana, Siyi mpitie Seleli nikukute naye pale kanisani!!

  Gbu, friends!

 4. Seleli,
  Naona mjdala huu unaelekea mwisho sasa. Mengi tumeongea na kuelweshana mengi pia. Lakini mengine ya yale uliyoyauliza, nimekujibu individually. akili yangu ilituma kufanya hivyo.
  Ubarikiwe

 5. Siyi,

  Good on kongole now…. mwe!

  Umesema..’’Kelele za chura(I hope mi si chura wala mfananio wake anyway)—nilikuwa fahamu kabisa kuwa wanawake na wanaume tuna nyazifa tofauti pamoja na kwamba mbele za Mungu tuko sawa= Nili maanisha tuna NAFASI( not nyadhifa) tofauti na ndio nalieelewa sana hata kibailogia tu tuna tofauti sembuse ki-NAFASI! Nilichofanya mimi nilipochangia mara ya kwanza, niliuliza maswali tu kuhusu Wanawake wana matatizo gani mpaka muwa-negative ivyo na kisha nikasema kuhusu UN positive yake, basi ivyo tu, mlitakiwa kunijibu! sasa mkadhani kwa maswali hayo nina kataa fact ya kweli kuhusu Wamawake na Wanaume kutofautishwa na Mungu ktk NAFASI na MAJUKUMU..You see, you suffered your own assumptions on me which wrongly directed you to mis-interprete completely off, ndicho kilichotokea ktk fahamu zako uliposoma comments zangu za kwanza kabla sijafunguka..unaona sasa…bao la pili ilo la kisigino la kuingia mzima-mzima, tehe!

  Umesema umependa sana maelezo yangu on, “Kuhusu UN… na kunipa big up= asante, ni raha iyo and glory to Master and big down( not ups) to you bro tehe!Ila tena ghafla ukaharibu kwa kunisingizia ivi ….’Kwa upande wa kutokukubalina na UN, naona hukunielewa vizuri kakangu’’=NILIKUELEWE SANA TU, HAMNA GUMU HATA CHEMBE ULILOANDIKA ATI NISIELEWE! Ndio maana ukaendelea kusema kwa USAHIHI SANA KISHA UKACHAFUA KAMBI VIBAYA SANA-soma madude yako hapo chini:

  USAHIHI‘’’’’’Kidunia, UN wana kazi nzuri tu wanayoifanya kuhakikisha kuwa utu wa mwanamke unapatikana na unalindwa hasa kwa jamii zisizomjua Mungu’’ Maana kwa wanaomjua Mungu, kumnyanyasa mwanamke kwao ni dhambi inayofananishwa na mtu asiyeaminI’’

  UCHAFUZI WA KAMBI HUU HAPA…. ‘’kimbingu, UN hawana kazi nzuri hata kidogo’’

  SWALI: Umetoka kusema nini hapo juu? this is real very funny Siyi Nzala!!!!!!!!, ivi hua mna debateje wandugu? Sytematicness’/smooth flow, connectivity ya ideas zenu Wewe, Lwembe, Mabinza, na kwa mbaali Yusha, at least Sungura kwa hili namtoa but Amin Mguun du, wote ndani ya nyumba, hua mnafyatukae? Mwe! Linalokuja hilo hilo unaribwaga mezani siyo? Guys, raise the stds! Sasa ebu nijibu UN wakifanya kazi KIDUNIA kama ulivyodai ya kutetea utu kwa maana iyo ya juu ulosema mwenyewe tena ukasema Wanawake wapendwe maana ni upendo pia kuwajali utu wao, iyo siyo very sweet, holy, Godly, heavenic powefu job? Come on boy, think! Reason! Use even logic mnazogoma kuzitumia wakati nyie sio chimpa ambaye hata hivyo naye yuko smart pia upstairs

  Ona confidence pori hii ya 400%?…’’ Kibiblia au kimbingu, mtu au taasisi mbaya, haiwezi kutenda/kusema jambo jema, hali kadhalika na mtu/taasisi nzuri haiwezi kusema/kutenda jambo baya’’….mmh! aya ngoja uone why naziitaga ni confidence pori za kutishia watu but ukiziweka ktk mezani, unakuta ni mastori ya town. Aya let us test it kwa swali hapo, lijibu!

  SWALI: Serikali ni taasisi? Ikulu ni taasis? Wizara je? Si ni TAASISI NJEMA KABISA? Well, zinatendaje safi au ovyo? Ha ha ha kwisha habari yako, nyang’anga! Ndio maana kila mara nasemaga tumia sentence za kawaida but true aidha logically au Biblically, hii mambo ya kumiminika mastaments makubwa makubwa wakati una deal na jamaa wa upako wa nukta kwa nukta reading, utaaibika kila leo am telling you kijana wangu.

  Hapa ulitaka kusema nini hasa, Au ni yale yale ya kumwagiga tu lolote mradi la kiroho roho?….’’Nasema hivyo kwa sababu Mungu huangalia ile motive(nia, dhamira, lengo) inayomsukuma mtu kutenda/kusema jambo husika. Na kama motive yake ni mbaya, basi mtu au asasi hiyo hunajisika. Biblia inasema kimtokacho mtu(kile kibaya), ndicho kimtiacho unajisi’’

  Au ile ya juu ndio unaunga ni hii…’’Hivyo basi kama UN wanayafanya hayo kwa lengo la kuinganisha dunia pamoja, kutetea na maovu mengine yaonekane mema, bado asasi hii ni najisi mbele za Mungu’’ = but umesahau umesemaje kwa usahihi kule juu kuhusu kazi zao njema ambayo bila shaka ndio lengo lao! Namna gani Kijana mbona tennis ball sana mwanzo mwisho?

  Ili dai linajirudia rudia ni la uwongo…’’’Kuhusu Hajiri kufukuzwa, naona napo hukunielewa. Nakanusha, NIMEKUELEWA SANA, HAMNA GUMU UNAYOANDIKA NISIELEWE bwanaa, acha story. Ni bora umeomba radhi na kulia-lia ivi… ‘’maana na mimi ni mtu tu’’

  Kuhusu ili kua…’’Watu wa Humanism Association, wanadai kuwa, Mungu hakutenda haki/sawa kwa kumruhusu Ibrahimu kumfukuza Hajiri’’= ni wajinga na watoto, wakikua na kuelimika kiroho, wataacha, wewe wasiku-mis lead mpaka utu confuse hapa na kuzidisha manegative yako ili Mungu awe rude mbaya, afadhari umeomba radhi na radhi njema umepewa.

  Press on

 6. Seleli
  Ha ha ha ha ha!!! Kuhusu kongole, nakubaliana na wewe bro, nasema, GLORY TO GOD-AMIN. Ubarikiwe sana
  Nimeshangaaa saaana kuona kuwa kumbe na wewe pamoja na kelele za chura weeee, ulikuwa unafahamu kabisa kuwa wanawake na wanaume tuna nyazifa tofauti pamoja na kwamba mbele za Mungu tuko sawa. Nimependa maelezo yako haya, “Kuhusu UN…nilitaka nikubaliane na kutokukubaliana pia.Nakubaliana kua ktk agenda ya kutafuta haki kwa WANADAMU WOTE…wamepitiliza! Hilo halina ubishi na kwa Watu wa Mungu, tunakubali wote kua Me/Ke hatuwezi kua sawa kwa baadhi ya mantiki wanazosimamia UN! Kwa maana ya tuko sawa kwa kua wote ni wanadamu na tuna mahitaji basic sawa, iyo aina kwere lakini kwenye maswala ya Wajibu na Nafasi, tumetofautishwa na Mungu mwenyewe.” Maelezo matamu kweli kweli. Big up bro!!
  Kwa upande wa kutokukubalina na UN, naona hukunielewa vizuri kakangu. Kwana, kidunia, UN wana kazi nzuri tu wanayoifanya kuhakikisha kuwa utu wa mwanamke unapatikana na unalindwa hasa kwa jamii zisizomjua Mungu. Maana kwa wanaomjua Mungu, kumnyanyasa mwanamke kwao ni dhambi inayofananishwa na mtu asiyeamini. Wanaomjua Mungu, huongozwa na upendo wa Mungu ndani yao kuwapenda wake zao kadhalika na wake kuwatii waume zao. Hivyo basi sikumaanisha kuwa wanawake kwa vile hawapaswi kuwa na nyazifa za mamlaka, wanyanyaswe tu eti kwa vile wao ni dhaifu. Huo sio mpango wa Mungu. Mwanamke alitolewa ubavuni ili apendwe na siyo kumtendea unyama.
  Pili, kimbingu, UN hawana kazi nzuri hata kidogo. Kwa nini? Kibiblia au kimbingu, mtu au taasisi mbaya, haiwezi kutenda/kusema jambo jema, hali kadhalika na mtu/taasisi nzuri haiwezi kusema/kutenda jambo baya. Unaweza ukajiuliza how? Mbona tumewaona watu wabaya wanafanya mambo mazuri sometimes? Ndiyo, ni mambo mazuri kidunia/kibinadamu, lakini mbele za Mungu ni mabaya/dhambi. Nasema hivyo kwa sababu Mungu huangalia ile motive(nia, dhamira, lengo) inayomsukuma mtu kutenda/kusema jambo husika. Na kama motive yake ni mbaya, basi mtu au asasi hiyo hunajisika. Biblia inasema kimtokacho mtu(kile kibaya), ndicho kimtiacho unajisi. Hivyo basi kama UN wanayafanya hayo kwa lengo la kuinganisha dunia pamoja, kutetea na maovu mengine yaonekane mema, bado asasi hii ni najisi mbele za Mungu.
  Kuhusu Hajiri kufukuzwa, naona napo hukunielewa kama sikueleweka vibaya na hata kwa wengine. Lakini pia, huenda kweli nimeingiza hisia sana kwenye maelezo yangu hadi watu wakanielewa vinginenvyo. Na kama kweli imeonekana hivyo, basi mtambue kuwa sikukusudia wapendwa. Mniwie radhi maana na mimi ni mtu tu. Watu wa Humanism Association, wanadai kuwa, Mungu hakutenda haki/sawa kwa kumruhusu Ibrahimu kumfukuza Hajiri. Pamoja na kufahamu sote kuwa Mungu hakosei, na Mungu alikuwa na maana njema na nzuri sana kwa kuruhusu hayo yatokee kwa kijakazi Hajiri, Humanism Association wao huwa hawayaoni hayo kwa mtazamo chanya. Wamenukuu na kumchambua Mungu kama ni kiumbe mkatili na mwenye mfumo dume unaomkandamiza mwanamke, jambo ambalo kwa wanaomjua Mungu, sivyo!! Mungu wetu ni Mungu mwenye rehema mno, na mara nyingine huruhusu mambo yanayoonekana kutokuwa na maana kwetu, lakini mbele zake huwa na maana kubwa na nia njema sana. Na kama hatutaelewa kwa wakati huo, saa na wakati unakuja, tutaelewa kuwa Mungu alimaanisha nini kuyaruhusu haya yatutokee!! We are serving the very merceful God m/wapendwa.
  Ubarikiwe

 7. Siyi,
  Unapoulizwa maswali, ni vizuri ukajua kuwa huyo akuulizaye anataka kujifunza, kwahiyo nawe wapaswa kuyajibu maswali hayo kwa ukamilifu na si kumzungusha! Ngoja nilinukuu swali mojawapo uliloulizwa, nakisha ukatoa jibu lisiloendana na swali.
  3. Ni UNABII gani kwenye Biblia (nukuu ya maandiko inahitajika hapa) UNAOMTETEA/UNAOMTAMBULISHA Ellen G. White kuwa mwanamke nabii anayestahili kuongoza katika mambo ya Mungu TOFAUTI na mama Elizabeth Eaton ambaye ameteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Kaninsa la Kilutheri kule Marekani?

  Jibu,

  Unabii uko mwingi sana. Nikupe mfano mdogo tu usome unabii wa kitabu cha Daniel na Ufunuo, halafu chukua vitabu vyake kama vile Great Controversy, Testmonies to Ministers, Desire of Ages nk. Endapo utapata shida ya kiitikadi kuelewa, chukua vitabu vingine vya historia kama vile vya akina Uriah Smith(The 2300 Days and the Sanctuary), Andrews, John Nevins (The Commandment to Restore and to Build Jerusalem) nk

  Jibu ulilolitoa halina uhusiano wowote na swali! Ingawa umejitahidi kulijibu swali hilo, nikupongeze kwa jitihada hiyo, bali pia inadhihirisha kuwa ufahamu wako ktk mambo ya “manabii” kulingana na Maandiko ni mdogo sana, au huyajui kabisa! Yawezekana umeyakuta mambo hayo kwenye mkutano wa hadhara nawe ukayameza bila kipimo! Hata hivyo kwa vile nabii Ellen White ninamfahamu, kupitia kazi zake, nitakujibia hilo swali ili aliyeuliza awe ametendewa haki.

  JIBU:
  Hakuna Unabii wowote katika Maandiko unaomtambulisha nabii Ellen White kuwa ni sehemu ya Huduma itokayo kwa Mungu, si kwa ahadi wala kwa rejea, licha ya kwamba alikuwa ni nabii! Kwahiyo kumpokea nabii wa jinsi hii, ni sawa na kusombwa na mafuriko!!!

  Swali:
  Ina maana Bible Bila vitabu vya Ellen HAIJAKAMILIKA?
  JIBU:
  Hasha!!!! Bibia ni Neno la Mungu toshelevu kabisa.

  Pia jibu hili ulilolitoa, kama tutaliamini hivyo, basi unabii wa Ellen White utakuwa hauna nafasi ktk Maandiko, na si hivyo tu, bali hata faida ya kiungu kwa wanao upokea! Ndio kusema unakiri kwamba huyo hakuwa Nabii aliyetumwa na Mungu, na wala hayumo katika Programu ya Mungu!

  Swali jingine alikuuliza Sungura mara mbili:
  “Ivi Ellen G. White yeye hakuwa anasimama kwemye mimbari?”
  Jibu ulilompa ni la kumzungusha, “swali hili nililijibu vizuri sana hapo juu” hilo jibu la hapo juu ndio hili hapa:
  Ellen G. White alifanya kama walivyofanya manabii wengine wa kike wa agano la kale. Ellen G. White anakubalika kama nabii wa kweli kwa sababu unabii wake haupingani na manabii wote waliomtangulia ndani ya Biblia.

  Lakini jibu sahihi na la kweli na rahisi ni kwamba:
  Ellen White alisimama mimbarini! Na mwaka 1876 huko Groveland, Massachusetts aliwahubiria kusanyiko la wapatao watu 20,000!
  Ndipo ningali najaribu kulitafuta jambo hilo katika Biblia yangu ili niwaone hao manabii wa kike wa Agano la Kale wakihudumu hivyo! Hata hivyo nabii wa Agano la Kale katika Agano Jipya, mbona havieleweki!

  Katika Agano Jipya mwanamke haruhusiwi kuyafanya mambo hayo ambayo Ellen White na mama Eaton wanayafanya, na wote hawa wakiwa katika Agano Jipya, ndio kusema hawa nao na makusanyiko yao wamesimama kumpinga mt. Paulo, kwamba nao pia wanaye Roho Mtakatifu, kama walivyosimama akina Kora kumpinga Musa, Hes 16:1-3
  “Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; 2-nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; 3-nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, BWANA naye yu kati yao; n’nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa BWANA?”

  Sasa, kwa vyovyote utakavyolichukulia jambo hili, iwapo Mungu atawaachilia hawa ktk haya wanayoyafanya leo hii, basi itamlazimu awasamehe pia akina Kora. Lakini Mungu ni Mkamilifu katika Hukumu zake, ndipo ninapoliangalia jambo hili, ninamuona naye Paulo akisimama kama Musa, akimwita Bwana awe Mwamuzi wa Uasi huo, “Musa aliposikia maneno haya, akapomoka kifudifudi, …. Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao”! Basi kama Mungu hakuikubali sadaka ya hao ni dhahiri kwamba hata sadaka za haya makusanyiko ya jinsi hii zimekataliwa pia! Kinachofuata kwa makusanyiko hayo ni hiki, Hes 16:31-35:
  “Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi. Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.”

  Basi ni dhahiri kwamba makusanyiko hayo yote yamekufa kiroho!!!

 8. Ndugu Lwembe hapo ume nena,ubarikiwe kaka.«Awe mtu wa mke umoja nasi awe mke wa mume umoja»mafundi wa kuyageuza maandiko yageuzeni tu,ila ukweli unabaki tu ukweli.

 9. ‘Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, MUME WA MKE MMOJA, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha”
  (1Tim 3:1-2)

  Hivi ndivyo inavyopaswa kwa Makanisa ya Watakatifu, yaani hao waliolipokea Neno hilo ktk 1Tim 3:1-2!!!

  Basi unapoyaona mambo haya yaliyo kinyume na Neno, yakijiinua ktk nyumba zipaswazo kuwa za Mungu, jua kuwa wakati umepita saaana, Milango ya Rehema inaweza kuwa ndio inafungwa kama haijafungwa tayari!

 10. Siyi Nzala,

  Kauli za Mungu kabla ya vitendo vyake ktk sura ya Mwanzo 1 na 2,hazinisumbui hata kidogo, nadhani unatafuta credit tu mechanically badala ya kuacha ije automatically!!!!!!! Post yangu ya 3 hapa kuna passage hii, nainukuu kama ilivyo maana unakimbilia kujibu bila kumeza Mkate bila blueband ….. Ingawa pia ni kweli Adamu ndiye aliyepewa majukumu na Mungu lakini si KWELI HATA KIDOGO kua ni Adamu TU yaani yeye mmoja tu ndio alipewa. Labda kama unayo maana nyingine ya jukumu ili TU kwa adamu-sema, lakini ktk matamko ya Mungu kama anavyoya-report mwandishi kuelezea shughuli nzima ya uumbuaji wa WANADAMU WA KWANZA ilivyokua hapa-Mwanzo.1:26-28, usisahua hapa kuna MAJUKUMU MAKUBWA KABISA KWA WOTE SI MMOJA TU!!!!!!!! ALIEYEMZALIA WANA bwana ADAMU ni HAWA-jukumu la kuzaa kuongezekana na kutawala Nchi na viumbe vyote, lisingewezekana bila Hawa kuwepo! Adamu asigetimiza ilo kwa kutumia mawe, mwana selele-hawa, miti au pusi!!!.Majukumu mengine kama Kutunza sharti la Mungu, kuitunza/kulima bustani kunako reportiwa ktk Mwanzo.2:15-17 WOTE wanahusika ingawa Adam alihusika kwanza. Yeye kua wa kwanza kuhusika nayo, hakukumaanisha Hawa alikua exempted kwa hayo ndio maana walipokosea jukumu la Kutunza masharti ya Ukaaji bustanini, waliadhibiwa WOTE-Mwanzo.3:8-19( notice: mstari wa 13- baada ya Hawa kutenda kosa na Mungu kabla haja ajaadhibu, Anamuuliza Hawa SPECIFICALLY- ‘’Umefanya nini iki!!!!!!!!!!! Mungu si mjinga au unfair kumuuliza Hawa kama asingekua ana husika na Jukumu ndio maana adhabu naye pia alitandikwa!

  Sasa je toka juu pale, umeziona phrases kama izi namely…’’ lakini ktk matamko ya Mungu kama anavyoya-report mwandishi kuelezea shughuli nzima ya uumbuaji wa WANADAMU WA KWANZA ilivyokua hapa-Mwanzo.1:26-28, na je umeona hii…’’

  ‘’Ingawa pia ni kweli Adamu ndiye aliyepewa majukumu na Mungu lakini si KWELI HATA KIDOGO kua ni Adamu TU yaani yeye mmoja tu ndio alipewa,

  ‘’Mwanzo.1:26-28, usisahua hapa kuna MAJUKUMU MAKUBWA KABISA KWA WOTE SI MMOJA TU!!!!!!!! ALIEYEMZALIA WANA bwana ADAMU ni HAWA-jukumu la kuzaa kuongezekana na kutawala Nchi na viumbe vyote, lisingewezekana bila Hawa kuwepo! Adamu asigetimiza ilo kwa kutumia mawe, mwana selele-hawa, miti au pusi!!!.

  Sasa Mtu akishakuambia yote hayo juu na kipande hiki…. lakini ktk matamko ya Mungu kama anavyoya-report mwandishi kuelezea shughuli nzima ya uumbuaji wa WANADAMU WA KWANZA ilivyokua hapa, unawezaje kusema anachanganywa na aliyosema/panga MWANDISHI(mind you sio Mungu), akiuelezea Uumbaji ulikuaje in summary kwanza? Usifosi kusound the great teacher while mmmmh! mi sijui!

  Majibu ya maswali yangu, umeboronga: ukasema……
  (a) lazima tukumbuke kwamba Mungu alikuwa anatoa kauli ya hicho atakachokifanya kabla ya kukifanya- nauliza tena Swali: Aliyesema ivyo/anayetoa report iyo ni Mungu au mwandishi ndio amepanga ivyo?

  (b) Tena Iipi linalosimamia uendelezaji wa Uumbaji? Ukajibu-nafikiri ni kuzaa, japo Adamu na Hawa hawaonekani kuzaa katika mwanzo moja na mbili. Nauliza tena Swali:Kutowaona wakizaa Mwz 1,2 ndio una taka kuleta hoja gani sasa? kubali tu swali langu limekupa ufahamu hapo, acha maneno mengine ya by the way!

  (c) Na lipi lililosimama hadi leo maana bustani ya Eden haipo tena! Ukajibu kua ati
  Yote bado yanasimama hadi leo na kua Edeni haipo kweli lakini kuna mbadala wa Edeni-Ardhi. Nauliza tena Swali: Umefikije conclusion iyo kua Eden ni Ardhi leo?

  Hii naona kama unasema lolote linalokujia…’’Adamu asingeasi, angeendelea kuilima na kuitunza Edeni, lakini alipoasi, alipewa ardhi nayo ailime na kuitunza pia kwa ustawi wa maisha yake pia. Ndiyo maana leo mkristo anayeharibu mazingira, anavunja sheria za Mungu za asili’’

  Kuhusu nyaraka za Paulo na akina Petro kwamba zinaapply kwa nani na kwa nani haziapply!! Ati umenitia moyo nisome backgrounds za nyaraka hizo zote ili nielewe miktadha ya nyaraka hizo.Jibu: Kweli zisome kwa USAHIHI tena SOMA Kweli kisha unambie kama hakuna analysis inayoonyesha issue za culture na elements za an individual kama yeye alipokua anaandikia makanisa. Nimekuona umeongea kwa kujiamini hapa kua nisome backgrouds wakati kwa hoja zako, inaonyesha hujasoma chembe! Unadanganya wewe, hamna tena! mwe!

  Kwamba,’Watu hao waliandika hilo neno wakiongozwa na RM’’, Sasa kuna haja ya kusisitiza ilo? Unakuza mambo tu unnecessarily! LAKINI nimewafundisheni Wewe, Lwembe, Yusha na sasa nitangeukia na Mabinza kua HAO hawakua matikitiki maji wala mochwari hao bali Watu na tofauti zao, mfano..Mathayo.27:24-28 hasa mstari 28 ..Wakamvua Yesu nguo na kumvika vazi JEKUNDU (scarlet robe) lakini Marco.15:15-17 hasa mstari 17..Wakamvika vazi la rangi ya ZAMBARAU (purple).Hapa waandishi ni wawili tofauti ila tukio lilelile lakini limesemwa tofauti ie rangi ya nguo zile. Swali: Kwakua waliongozwa na RM na RM ni smart, nani aliongoza watoe report tofauti ya nguo zile kwa tukio hilo? Hahaha..sijui utajibuje! Nimeshakukaba mpaka koromeo hapo!

  Hadi akina Yohana(mwanaufunzi wa Yesu), nao walikuwa na msimamo huohuo wa majukumu ya kikuhani kwa wanaume tu: JIBU: Usikuze mambo, ktk swala la ndani ya Kanisa na position za ku-final say, nailewa Biblia sana tu na nimeshaweka sawa kua niliuliza hili kutaka kuweka sawa baadhi ya chumvi mlizozidisha kuhusu kuwafanya Wanawake wa MUNGU kama zero kwa kila kitu. Again, usitafute credit mechanicaly, itakuja automatically kama unatema pini za hatari,akili na Biblically balanced.

  Ati umejidai unanifahaaaamuu kwa kusema ivi…’’Natambua kuwa TAG kuna wachungaji wanawake wengi ndo maana hii dhana haikukai vizuri kichwani’’ Jibu: Umeanza mastori ya town-jahazi kraaadis efwe emee ya Lwembe ivyo si-pay attention kuuubwa kwa iyo ulosema unless unapenda tudance-dance kidogo tunapoendelea kudebate

  Nilikuuliza hii kauli yako ujajibu…’’kabla ya kumsubiri Mungu atamke kama alivyokuwa akitamka huko nyumba, leo watu wanajichagulia wao wenyewe viongozi wa kike. Swali: Anatamkaje leo ili ujue ametamka na ndipo wanawake wawe viongozi ktk mambo mengi mbali na kua FAINAL say/Preachers ndani ya Kanisa?

  Nilikiri kua Wanawake kua final say NDANI ya kanisa, si kwa sababu wewe ulisema, nalijua ilo toka Neno, nilichofanya mimi nilitaka nione kama mnaweza mkawa na ufahamu mpana kuweza kumulewa Paul anapowakataza Wanawake ni ktk mazingira( mila na desturi) gani na location ipi( NDANI ya Kanisa na ktk imani kwa ujumla eg ktk familia/Majumbani mwao) na SI kwa ulimwengu wote ktk kila sekta uko nje maana uko wala hawana habari iwe ya torati wala ya AJ. Again, usifosi kingi-kutaka credit hence huna haja ya kunipongeza ati nimekiri! Ni exeggerations zile zile tu basi-a common unhealthy trait of yours.

  Maswali yangu kuhusu wanawake sio wawe but TAYARI ni viongozi huko serikalini na sector nyingine NJE ya KANISA na IMANI yetu, si hoja dhaifu hata kidogo! Ni rahisi kusema neno dhaifu lakini yaingilie uone kazi na pia upate ufahamu unapoyajibu.Aya sasa jibu/respond PIA yangu napoyajibu yako kama ifuatavyo:
  Swali: Serikali za wanadamu duniani, zilitoka kwa nani? Kwa Mungu au Shetani?
  Jibu: Kwani mimi nilikufundishaje/nilisemaje na hata kunukuu maandiko haya -Warumi.13:1-5 na 1Timo.2:2? We vipi!

  Swali:Sheria za Mungu ambazo ni neno lake, zina exceptions kwa baadhi ya mifumo- kwa maana ya Serikalini na kanisani?
  Jibu: Kwa kanisa, baadhi ni Ndio mfano. Marko 10:1-9 =Zamani waliruhusiwa kuwatimua na kuwapa taraka, Leo Yesu ali/amekataa! Wow! hahaa mpaka nasikia upako mbichi, glory to God,amen! kwa jibu ilo nimekuba tena, over and out!
  Kwa serikalini: Jibu: ni swali: Nchi/Serikali inayoongwa na uislamu/Ubudha, NENO/Sheria gani inatawala? Hahaha meeen, glory to God, Amen! Kijana, umetibua maji na kuchokoza mafuta ya JUU-hahaa, aya unatokaje hapo tena? kazi kwako.

  Swali:Je, wanawake walioko nje ya kanisa, wao hawana ule udhaifu inaoutaja Biblia?
  Jibu: Niliwaulizeni Wanawake wana matatizo gani mpaka muwasemelee negative ivyo kuzidi hata fact ya kweli kuhusu weakness yao ktk uzuri kama Bible ilivyosema, hamkujibu,ulichekacheka tu!!!!!!! aya, jibu kwanza wewe, tenda haki, chapa kazi kwanza. Ila kwa kukusaidia, nimefundisha humu pia neno dhaifu lilotumika pale ni ‘in the concept ya comparisons with Men/husbands…NKJ and other versions, si zote-inatumia ‘weaker or delicate vessels! Plz usianze kuboa kama zamani kukurupuka na kukimbilia kujibu tu bila kusoma kwanza MPAKA MWISHO KISHA JIBU, TENA WITH ME—unasoma kila nukta ili ukijibu uwe connected/relevant au bora kuacha kujibu kabisa maswali ninayokupa na kuomba msaada ooho! aya huoni Yusha mwenzako anajidai kukaa kimya eti kahekima ako kumbe najua na yeye anajua why hajibu-hahaa au Lembe mwenzio bora liende ni ngoja afe na tai-hahaha uyu bwana ananichekesha kweli naposoma anavyojibu niliyomkaba! Usiingie kichwa na mabega yote, taratiibu na kwa makini

  Huyu mtu mzima Siyi ni KWELI alikwama kuhusu taasisi za kibinadamu kuzitofautisha na na ya kiMungu maana aliingia mzima-mzima na kusema TAG,EAGT, SDA,RC,Pentecost,Jumbo jet Ministry, helicopter winners chapeo/not chapel ati ni Kanisa/Makanisa yaani taasisi ya MUNGU! na rekodi ziko humu humu ktk post hii…kwa hiyo, na ajicheke yeye mwenyewe!?

  Kuthihirisha maswali mtego bado hayawezi, angalia swali hili la yeye anayejita mtu mzima…’’ Kama binadamu wote ni mali ya Mungu, je, kuna taasisi za kibinadamu ambazo siyo za Mungu? kisha anajijibu yeye mwenyewe hivi…’’ Labda kwa wale binadamu waliokubali kumfuata ibilisi. JIBU: ni swali-hao waliomfuta ibilisi, ni wanani? Aliyewaumba nani? Tehe tehe! umekwisha tena. Na kwaiyo ni kweli kuna taasisi za kibinadamu perce kwa kua kuna uwezekanao wakawa wameanzisha kumpendezesha devo eg madangulo camp, umoja wa mashoga duniani, mihandari sellers nk au walianzisha Ki-Mungu baade zika-turn to ubinafsi na udevilish aims sio? eg Jumbo jet 24/7 miracles tit for tat church! Under senior Pastor Dr. Apostle and Prophet, Professor of M23 AMRI, Honorable Siyi Nzala!

  Kwani kutaka Kila katazo la Mungu kwa wanadamu liwe na aya ndani ya Biblia!! Kuna ubaya? Unashangaa nini sasa kama siyo kichekesho! Ati unacheka mimi kukutaka aya kuhusu Wanawake kukatazwa kuwa viongozi kwa huko nje ya kanisa! JIBU: Maliza kucheka kisha jibu, wacha danganya toto,kama hamna aya, toa maelezo ya kurithisha, fanya mchezo hapa tuko kazini!
  Anayesinzia na aliyechoka ni yule anayeshindwa kujibu na akijibu ni bora liende au yule anayejibu kwa uhakika na kuuliza ‘makabaji questions’’ ili watu wathibitishwe na kujithibitisha humu yale wanayasimamia na kutamka kwa mastatements makubwa-kubwa nama confidence mengiiiiiii ya pori?

  Kuvuta sigara au bangi hapana maana ktk NENO kwa MAPANA yake-angalia hapo narudia same phrase kila mara-‘’kwa mapana yake’ maana Lwembe, Yusha, Mabinza na Wewe kweli mnatatizo hapo, tuseme ukweli tu! so hutakuta statement ktk Bible..’’Sigara na Mirungi ni dhambi’’ ila kwa mapana yake..utadaka toka maneno kama..Miili yetu ni hekalu, atayeuharibu na Mwenyewe atamharibu’’ au ‘’si kila vyakula vifaavyo nk’’. Sasa Paul anakataa kutoa ruhusu kwa Ladies kunena KANISANI- very specific location a rule is stated tena with a reason why in the church, unataka kuihamishia kinyemela mpaka kwa serikali za mtaani ambako kuna wananchi wengi wa Maca na Madina tena ladies,hence wakamchagua Mwajuma kama Mwenyekitu wa serikali ya Mtaa!

  Hii umeniiga..’’Naona unaleta utani hapa’’ tafuta yako Kaka! nina reserved rights! Kwa hiyo acha utani, acha ku-cut na paste but you can copy and paste atleast

  Ati..’’Huwa unatubu moja kwa moja kwa kuhani mkuu Yesu Kristo na si kwa wachungaji wa kike kama mimi’’.Jibu: Mastori ya town hayo, kraaadis efwe eme ya Lwembe-aise mnaambukizana certain notorious spirits hamna tena, mwe!

  Ati, Hiyo ndiyo dhana ya Biblia, kuwa wanawake ni wadhaifu si kanisani tu, bali hata nje ya kanisa’’..Swali: Ni lile mpaka ulijibu, udhaifu gani Bible inamaanisha hapo?

  Ati umejiaminiiiiiii ivi…’’Hivyo hawapaswi kupewa wadhifa wowote ule wa kimamlaka. Swali: Kama wamepewa eg Mawaziri, Wabunge, Makatibu wa Wizara, akina Mwajuma stree uko, unafanyaje? Mbona unalipa kodi kama kawa? Mbona unanyenyekea kwa huyo Serikali ya Mtaa Mwajuma akupe clearance ili upate kibali cha polisi ufanye mkutano? Na izo mamlaka waliyopo sasa ni from devo or God? Hahaha, kwisha tena! maana kodi unalipa tena sana tu, kuomba kazi Wizarani-atakufanyia usaili mdada tena hajaolewa- mwenye cheo hiki-Principla HR Afsaa wa Wizara ya shule yako! Wewee! utakubali tu, chezea njaa wewe!unataka kasalary kaendelee kuflow!so Izi za kuwakataa wanawake kila pembe ya dunia kua leaders-ni story zako hapa mtandaoni tu.

  Halafu unatowaga wapi izi 400% pori confidence kuniuliza ivi…’’Umeelewa kaka Seleli? Jibu: can a new dog tech the old one new techiques? Yes, may be few but plenty of them, not all. Ati..’’Ubarikiwe sana! Na manini sasa? mastori haya bwana, unatiririka nayo mwanzo mwisho!mwe!

  Press on

 11. Siyi,

  Kongole or kongolo, nimeshasema acha pretendence, ni tamu na inatia moyo kua appreciated, unasema tu asante or Gbu and glory to God, siyo ucomedy mwingiiiii!

  Kuhusu UN…nilitaka nikubaliane na kutokukubaliana pia.Nakubaliana kua ktk agenda ya kutafuta haki kwa WANADAMU WOTE…wamepitiliza! Hilo halina ubishi na kwa Watu wa Mungu, tunakubali wote kua Me/Ke hatuwezi kua sawa kwa baadhi ya mantiki wanazosimamia UN! Kwa maana ya tuko sawa kwa kua wote ni wanadamu na tuna mahitaji basic sawa, iyo aina kwere lakini kwenye maswala ya Wajibu na Nafasi, tumetofautishwa na Mungu mwenyewe. Kwa upande wa pili, sikubaliani na wewe kwa maana tu kua pamoja na UN kupitiliza, yako mazuri sana wamesimama nayo kuhusu Utu wa Mtu kama Mwanadamu, awe Ke/Me. Wewe ungependa Wanawake wawe treated kama wakati wa Utawala wa talibani Afganistani au North Nigeria, Somali Alishabab dominated and most of Islamic socities?! Nilitaka uone side 2 ya UN siyo kuongea tu bila kuangalia kama uko off and on.

  Kuhusu Hajiri afukuzwe, pia una tatizo lile lile la kuzidisha chumvi/U-negativity kama ulivyosema viongozi Wanawake wanaingia na vimini mimbarini! Wakati ni kweli alifukuzwa, lakini usimuingizie ukatili/manegativity na majeure mbofu-mbofu YAKO BINAFSI ukambambikia Mungu kua ndivyo alivyo. Unajua kuna kitu unafanya kibaya sana ktk comments/inputs zako…YOU ARE SHIFTING TO GOD,YOUR OWN DISEASED PERCEPTIONS/FEELINGS/ AND COMPREHENSION OF THINGS ABOUT WOMEN/SOME PEOPLE IN THE BIBLE. Mungu ni Baba na ana care pia, ukisoma baada ya Hajiri kuondolewa, utafuta kauli yako au utaingoelea ktk tone ya kawaida kwa sababu Mungu hakua kama ivyo tone yako inakolozea/kandamizia ile mbaya! mwe! namna gani hapa unamfanya Mungu kama rude/injured buffalo, Osama or janjawid group! We vipi! Tusome hapa wote- Mwanzo.21:9-20

  Mstari 13= Mungu anasema, nitafanya Taifa toka kwa Son( Ishmael) kwa sababu ni uzao wako

  Mstari 15 = Maji ya kunywa kumsaidia njiani aliyopewa na honey wake Ibra, yanakwisha akiwa na son wake na ni jangwani

  Mstari 16= Honey wa Ibra analia, hali tete jangwani, hakuna maji, mtoto hoi, kwa uchungu analia na hataki kuona son wake akifa live mbele yake ivyo anajitenga naye
  Mstari 17 = Mungu anakua concerned na Malaika anamwita Hajiri na kumuuliza why kilio chake na kwamba Mungu amesikia kilio cha mtoto pia(kumbe mtoto naye alikua analia maskini)

  Mstari 18=Mungu anarudia ahadi aliyodokeza ktk mstari 13 na ahadi iyo inafanana na kwa sehemu na ile ya Ibra mwenyewe na Son Isack mwenyewe! Wow! hii tamu sana! Soma hapo uone kama Mungu ni kama wewe! unambambikia case tu. Tena ktk mstari 13 Mungu alisema kua nitafanya taifa kwa kua NAYE( Ishmael) ni UZAO WAKO-kwa maneno yangu ni sawa Mungu anaongea na rafiki yake kwa kua alitwa rafiki wa Mungu yule kwamba..’’Ibra, don’t worry man, relax, right? don’t panic nor become angry against your Wife’s Sarah decision, I know how to play the ball well, I will sort it out, relax big boy, your son( Ishmael deserves love/blessings too, he is your blood, chilly out meeeen! I will increase him too.

  Mistari 19-21= Mungua ana tenda MUUJIZA! AnaMFUNGUA macho kisha ANAONA kisima cha maji, wakaramba maji safi, halafu imeandikwa na ‘MUNGU alikua pamoja na mtoto’=HAYO MANENO NI MAKUBWA SANA wewe KAMA MSOMAJI WA BIBLIA, UNAJUA YALITAMKWA KWA WATOTO GANI TENA KTK AGANO JIPYA-utashangaa kweli-yatafute! Mwishowe Mungu akaendelea kua na dogo mpaka akawa an archer na hatimaye mkaka mkubwa na akapata kabinti toka kwa former Hosni Mubaraka land.

  Hicho ndio kilikua kiporo nilichosema nitamalizia, nilitaka kushare ufahamu huo maana unazidisha sana ‘uyumani’ wako na kumpachikia Mungu, ni bora uwe mkweli kama mie kwa kusema phrases kama..’’ ‘’kwa maneno yangu’’, ‘’nadhani’’, ‘labda’’, ‘’pengine’’ nk..siyo na maconfidence yoooote kama vile kweli! mwe!

  Press on( post yako mpya kwa majibu/posts zangu nitaipitia na kama kuna la maana, nitakubariki na mabovu, nitaendelea kuyakabili/kaba vibaya sana mpaka yataisha tu power yake, twende tu taratiiibuuu, tutaelewana/kitaeleweka tu.

 12. Seleli,
  Kimsingi nilikuwa sijaona posts zako hizi. Sasa nimefurahi tu kukuona umekuja na hoja zinazoelekea kuwa inaonekana tunasafiri pamoja ndani ya jahazi moja ktk hili pamoja na tofauti zako ndogondogo.
  Kongole ni nzuri, lakini zina hatari kwa kiasi Fulani kwa anayepewa hizo kongole. Mimi nimekopi kutoka kwa Mungu, halafu walimu-dunia (wasomaji), wakafurahishwa na makala hiyo, ni nani watampa hizo kongole? Yule source(Mungu) au yule(Siyi) aliyepaste? Jibu unalo!!
  Swali lako la kwanza unauliza nimefikiaje conclusion ya kusema kuwa Adamu kapewa kwanza majukumu. Kimsingi kaka Seleli, nilisoma tu kwenye Bible. Ninachokiona kukusumbua wewe, ni kauli za Mungu kabla ya vitendo vyake ktk sura ya Mwanzo 1 na 2. Mf. ukisoma mwanzo 1:26-30, Mungu anazungumza na Adamu na Hawa kwa pamoja japo alikuwa hajawaumba wote kwa pamoja. Hizi zilikuwa ni kauli za Mungu kabla ya vitendo kama ilivyokuwa kwa viumbe wengine wakati wa uumbaji. Ukifika mwanzo 2:15-20 utakuta Mungu kashamuumba Adamu na anamkabidhi majukumu akiwa Adamu peke yake. Mstari wa 21 na kuendelea katika sura hiyo ya pili, Utaona sasa Hawa naye ndo anaumbwa na Mungu haonekani kumpa Hawa majukumu kama alivyofanya kwa Adamu baada ya kumuumba. Hivyo, kusema kuwa Mungu alimpa majukumu Adamu na si mwanamke, ni rahisi tu kueleweka kama utaisoma Biblia katika urahisi wake huo bro.
  Pili, maswali yako ya mwanzo 1:27-30, nitayajibu kama ifuatavyo;
  (a) Kati ya kuilima na kutunza bustani na Kuzaa/kujaza kisha kuitawala/Kutiisha Dunia, lipi ni jukumu kuu?

  Jibu
  Nafikiri ukiisoma Biblia utapata jukumu lililo kubwa zaidi, japo hapa ni lazima tukumbuke kwamba Mungu alikuwa anatoa kauli ya hicho atakachokifanya kabla ya kukifanya. Na alitoa kauli kwa ujumla wake. Lakini mwanzo 2 amebainisha vyema mgawanyo wa majukumu hayo aliyoyatolea kauli katika mwanzo 1.
  (b) Tena Iipi linalosimamia uendelezaji wa Uumbaji?
  Kwa uelewa wangu, nafikiri ni kuzaa, japo Adamu na Hawa hawaonekani kuzaa katika mwanzo moja na mbili.
  (c) Na lipi lililosimama hadi leo maana bustani ya Eden haipo tena!
  Yote bado yanasimama hadi leo. Edeni haipo kweli lakini kuna mbadala wa Edeni-Ardhi. Adamu asingeasi, angeendelea kuilima na kuitunza Edeni, lakini alipoasi, alipewa ardhi nayo ailime na kuitunza pia kwa ustawi wa maisha yake pia. Ndiyo maana leo mkristo anayeharibu mazingira, anavunja sheria za Mungu za asili.
  Kuhusu nyaraka za Paulo na akina Petro kwamba zinaapply kwa nani na kwa nani haziapply!! Ukisema hivyo utatisha kijana. Nikutie moyo usome backgrounds the nyaraka hizo zote ili uelewe miktadha ya nyaraka hizo. Watu hao waliandika hilo neno wakiongozwa na RM. Hadi akina Yohana(mwanaufunzi wa Yesu), nao walikuwa na msimamo huohuo wa majukumu ya kikuhani kwa wanaume tu. Natambua kuwa TAG kuna wachungaji wanawake wengi ndo maana hii dhana haikukai vizuri kichwani. Lakini hii ndiyo hali halisi kaka. Kanisa limeingiliwa na watu kabla ya kumsubiri Mungu atamke kama alivyokuwa akitamka huko nyumba, leo watu wanajichagulia wao wenyewe viongozi wa kike. Mungu hapendi sana.
  Na katika post yako ya pili, Kwanza napenda nikupongeze kwa kukubali kuwa viongozi wa kike ndani ya kanisa, si mpango wa Mungu. Kwa kutambua hilo tu kwanza, basi unaonesha dalili za kufanikiwa huko mbele ktk imani na mahusiano yako na Mungu. Baada ya kukiri huko, bado ukaamka na hoja zako dhaifu za kutaka wanawake tena wawe viongozi huko serikalini. Sasa, naomba nikuulize maswali
  1. Serikali za wanadamu duniani, zilitoka kwa nani? Kwa Mungu au Shetani?
  2. Sheria za Mungu ambazo ni neno lake, zina exceptions kwa baadhi ya mifumo- kwa maana ya Serikalini na kanisani? Je, wanawake walioko nje ya kanisa, wao hawana ule udhaifu inaoutaja Biblia? Tafadhari na wewe nioneshe sasa!!!
  3. Unachekesha sana Seleli. Hivi maswali ya mtego kwa mtu mzima ndiyo hayo ya taasisi za kibinadamu na kiMungu? Kama binadamu wote ni mali ya Mungu, je, kuna taasisi za kibinadamu ambazo siyo za Mungu? Labda kwa wale binadamu waliokubali kumfuata ibilisi. Na kama ulimaanisha taasisi za namna hiyo yaani zinazofuata Luciferian policies. Be clear mwanaume!!
  Nasikitika maana nakuona unataka kila katazo la Mungu kwa wanadamu, unataka ni mpaka liwe na aya ndani ya Biblia!! Wanawake kukatazwa kuwa viongozi kwa huko nje ya kanisa, nako wataka aya ya Biblia? Ha ha ha ha !! Sasa umeonekana kuchoka bro. au ulijibu post hii ukiwa na usingizi… Sasa anza na kuvuta sigara maana Biblia haijasema popote kuwa usivute sigara au bangi… Kazana sasa, tuone kama utasalimika kijana. Naona unaleta utani hapa… Acha kuhalalisha uovu Seleli. Kama nbeno la Mungu limesema, tusimamie hapo tu na si vinginevyo bro. Acha kumdhihaki Mungu. Ni hatari mno.
  Hivi Seleli, kudai na kusema ni vitu viwili tofauti? Anyway, nikubali sasa yes, natumia Biblia imesema au imeandikwa. Na uzuri nikitaka kutubu, huwa natubu moja kwa moja kwa kuhani mkuu Yesu Kristo na si kwa wachungaji wa kike kama wewe. (Duuu, ngoja niseme polepole usalama wa taifa wasinisikie wakanikamata). Hiyo ndiyo dhana ya Biblia, kuwa wanawake ni wadhaifu si kanisani tu, bali hata nje ya kanisa. Hivyo hawapaswi kupewa wadhifa wowote ule wa kimamlaka.
  Umeelewa kaka Seleli?
  Ubarikiwe sana.

 13. Siyi,

  Hukuna nafasi ya Mapokea ktk Biblia = ni kweli kwa maana hii..ni Yale tu yatakayoPINGANA na NENO-Mark.7:13, otherwise sisi si pusi, ice cream au mafuta ya Vaseline kama siyo kerosine-Tuna Mila na Desturi safi kabisa na walio ktk Bible, walikua na mila na desturi safi tu, waliziacha zile tu na Yesu akaweka angalizo/kemea pale tu zili/takapowekwa JUU ya Neno la Mungu, ivyo tu so wacha maneno yako ya by the way!

  Kuhusu wanawake kuwa viongozi ama kwa taasisi za kibinadamu au ki-Mungu au kidunia kama vile serikali nk, umesema ivi- HUO SIYO MPANGO WA MUNGU

  Jibu: Nakubaliana na wewe kwa maana ya ndani ya Kanisa lakini uko nje hamna shida na maagizo/ushauri wa Mungu na Watu wake kuhusu hilo, ulikua na maana sana Ndani ya kanisa sio nje uko! Lakini SIKUBALIANI na wewe kuhusu nje uko mfano Ubungeni, Uspika, U = RC,DC,Jwtz, Uwazirini, Urais,Mashirika, Kampuni nk, ndio maana nimekazana sana kila mara kuwaambia phrases mbalimbli ktk mijadala humu moja ni hii-‘kulijua Neno la Mungu ktk Mapana yake na sasa naongeza na ktk hekima yote! Yako Maandiko/maneno mengine ya Mungu, kuyakomalia kama yalivyo pale pale ulipoyakuta-problem kubwa sana iyo ya Yusha na Lwembe! Utachafua kambi tu. Uko nje ambako hawataendena wala kujua system ya Mungu pia mila na desturi za Wanadamu kama wao au Torati, kinachoongoza uko ni amri moja tu hi-Warumi.13:1-5 na 1Timo.2:2-Notice ktk mistari hiyo kuna maneno kama ‘Hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, na ILE ILIYOPO IMEAMRIWA na Mungu, Mwenye mamlaka ni MTUMISHI WA MUNGU, ni LAZIMA kuwatii, dua na sala zifanyike kwa Wafalme na WOTE walio ktk mamlaka’’, so Ktk maneno yote hayo na hata maandiko menyewe hayajatenganisha kua hawa wenye mamlaka uko NJE ni LAZIMA wawe WANAUME!

  Hii ni clouds efwe eme mastori ya town…’’Huenda ndiyo maaana leo Mungu amekuwa hajibu baadhi ya maombi yetu kama nchi kwa sababu tumekiuka sheria zake,tumeweka viongozi wanawake, jambo ambalo Mungu hakuagiza’’. SWALI: Kwani wapi alikataa ktk maandiko hayo kwa uko nje? Au wapi Mungu aliagiza kwa Mambo ya Nje ya Kanisa kua Uongozi wa aina YOYOTE, kwa watu WOTE, mahali POPOTE na WAKATI WOTE, ni LAZIMA wawe WANAUME? Show me!

  Kwa mantiki iyo ya juu…Nje na Ndani ya Kanisa, ndio maana ya mimi kuuliza yale nilisema ni ‘maswali mtego mzuri’-namely ‘Taasisi za Kibinadamu( Madhehebu/Dini) na Taasisi ya Mungu-Kanisa! nilitaka uone iyo dhana kua uko nje si lazima kue kama ndani tufanyavyo! Nilijua tu kama kawaida ungeingia mzima-zima, sasa chomoka Kaka.

  Ati unatwaa confidence pori kuniuliza hiki ukidhani umeteme pini ya maana, ati..’’Umeelewa kaka? JIBU: Nielewe nini wakati mambo yako mengi yamepinda Kaka?

  Umesema, ‘’Unataka kujua kuna matatizo gani wanawake wakiwa viongozi? Kisha ukapiga mastoriiiii then Ati umehitimisha jibu lako ivi..’’kile alichokikataza Mungu, wewe ukikifanya tu, ni DHAMBI tayari.JIBU: Sasa hapo umejibu nini? wacha utani, Jibu, face it man.

  Kisha ukatapatapa ivi,..’’Lakini pia huenda Mungu hajawapa kwa sababu ya hali zao au kwa vile ni viumbe wadhaifu kama inavyodai biblia’’ JIBU: Kwanza tubu! Never say..’’ kama Bible inavyodai!!! Siku zote BIBLE INASEMA au IMEANDIKWA! Ila gazeti la Mwana Halisi(Mawio) ndio hua linadai kua Nzala Siyi na Lwembe, Amini Mgulumu, Kaswahili wakisaidiana na Sungura na Yusha, wamemteka Mchungaji na kumyang’anya zaka za mwezi mzima za washirika wake!’ na kisha kuzisigina amri za M23!! Pili, unahitaji skuli kaka-angalia ilo neno wadhaifu ktk Kiingereza Ni DELICATE au WEAKER-as compared to Man-Husband, so husilete maana chafu ya negativity na ubovu uliyopindukia unao-imply wewe.

  NB: Kile kiporo kuhusu Mama Ishamaeli afukuze na UN, chaja-lazima mjifunze kuwa makini na matamko yote mnayosema humu na kisha kuyasimamia kwa dhati na usahihi si ili ilimradi/by the ways games, ni lazima kukuwajibisha kuzoa kile umepollute kambini

  Press on

 14. Siyi,

  Asante kwa ushauri huu..’First Things First-God!!-lakini umesahau Biblia inasema nini kuhusu anayestahili sifa/heshima, je akaushiwe au apewe? na pia nadhani unafanya kujikausha tu najua ulisikia raha na ni tamu kweli kusoma maneno yangu ya ku-appreciate na kukutia moyo, mimi pia husikia raha, so hukua na haja ya kupangua kivileee kukubali kwangu BAADHI ya hoja zako njema sana, Don’t pretend brother, furahi tu, si dhambi maana utakumbuka kumpa utukufu Mwenyewe kivyako na kwa muda wako, some wapendwa/wana dini bwanaa, eti una act husikii rahaaa kua- appreciated! Ulongo ulogo tu.

  Umesema, ‘’Majukumu yalikuwa kwa Adamu tu na siyo Hawa na ati Adamu ndiye alikuwa the Initial &Final Point na ati iyo inadhihirishwa na Adamu kujitambua u uchi kabla na Hawa kutojitambua muda ule ule!-

  JIBU: Natamani ungekua karibu hapa nikunyuke fimbo za mgogoni! Plz wengine tuko kazini/hudumani hapa kwa moyo, bidii, nguvu na kujitoa sana kabisa, acheni utani na uwongo wa wazi. Mwanzo.3:1-13 Inasema mstari wa 6…Mwanamke akala tunda na akampa mumewe naye akala-Notice: iko at the same verse! Halafu verse 7-imeandikwa.. NDIPO( Notice neno ‘Ndipo’-matokeo word…. Macho YAO-notice: ‘yao’ (sio ‘yake’), halafu Biblia inaendelea kusema…WOTE yakafunguliwa-Notice ni ‘wote’ sio Adamu kwanza! Halafu inasema- ‘WAKA’-siyo ‘aka’…fahamu kua ‘WAKO’-siyo ‘yuko’ uchi …nk na yote hayo ktk mstari the same. Sasa una bahati mimi si fulani, ulistahili kufyatuliwa na maneno ya mtaani/ taarabu/radio clouds kwa uwongo wa wazi na zile naziitaga mie confidence 400% za porini za kuongeaga mambo makubwa au ya ovyo hadharani kisha kujifanya wa kiroho au uko na moyo wa Mungu. By the way, umefikiaje iyo conclusion KAMA INGEKUA KWELI anyway ya kusema Adamu ndiye alijitambua wa Kwanza u-uchi ivyo maana yake ndio inathibitisha ndiye PEKEE aliyepewa majukumu na Mungu? HOW IN HELL OR HEAVEN HAVE YOU COME TO THAT END? I need explanation na lazima uwajibike kwa hili- nakula sahani moja nawe maana mkiambiwa acheni ma-statements makubwa-makubwa haya yanayosemwa with confidence pori za 400% hamkomi! Na mikikabwa mya-justfy, mnahemea juu na kufoka hadi almost kutukana! Sasa hili sikuachi.

  Hili ni sawa..,Ukisoma Mwanzo. 2:15-20, utagundua kuwa, Adamu tu ndiye aliyepewa hayo majukumu’’ LAKINI, nilisema soma taarifa hii hapa-Mwanzo.1:27-28- ‘’zaeni, MKAongezeke, MKAijaze dunia na kuitiisha na kutawala kila kiumbe. Sasa ni maswali hayo kua,Mtu mwenye akili akiulizwa haya, ajajibuje?
  (a) Kati ya kuilima na kutunza bustani na Kuzaa/kujaza kisha kuitawala/Kutiisha Dunia, lipi ni jukumu kuu?

  (b) Tena Iipi linalosimamia uendelezaji wa Uumbaji?

  (c) Na lipi lililosimama hadi leo maana bustani ya Eden haipo tena!

  Siyi, si unaona hoja hii ilivyo na mashiko, sasa utaleta tena utani hapa! Namna gani hapa wapendwa/wana dini!

  Hiki ni mastori ya town…’’Suala la Hawa kuzaa, Biblia haijasema kuwa walikaa kwa muda gani wakiwa bustanini kabla ya kuanguka dhambini, wala haisemi kuwa, walikuwa wameshapata mtoto/watoto wakati wakiwa bustanini.

  Na hii ni fix za mjini…’’Wachambuzi wa Maandiko wengine wanadai kuwa, Hawa angepata katazo la kutokula tunda la mti wa Bustanini moja kwa moja kutoka kwa Mungu mwenyewe, huenda asingedanganyika kwa nyoka’’ unaleta fix za nini, lete nondo kaka!

  Umesema vema hiki ivyo umekubali umeelewa nilichokuambia hiki…’’Kuhusu laana kwa Adamu au Hawa; huwezi kuona sehemu yoyote inasema kuwa Adamu anapewa laana kama Hawa’’ = safi sana na hongera kufahamu.
  Ila hapa umechafua tena kambi, lazima uzoe hii takataka…’’Kwa sababu Hawa alikuwa ni sehemu ya Adamu(mwili wa Adamu), laana ilimpata na Adamu indirectly’’,

  Na haya ni mastory ya jahazi Clouds efwe eme!…’’ndiyo maana leo, hawafi wanawake peke yao, wala hawapati machungu ya kuzaa peke yao(ushahidi wa kidaktari unaonesha hivyo).

  Hapa kama umelewa vile na kama bado vile…’’Athari zilimkumba Adamu pamoja na familia, na uzao wake’’

  Hii ni kali mwe!…’’Wewe mwanaume huwezi kukinywea kikombe kama wanachokinywea akina mama = angalia Lwembe atakwambia una udhaifu wa Adamu kwa wanawake ohoo! Aya, mi simo.

  Kuhusu uwezo wa Mungu leo kusema mwamamke fulani awe kiongozi, kuwa upo au haupo!!= asante kwa kukubali kua upo

  Umeuliza ivi, ‘’ni kwa kiasi gani tunaweza kuchora mstari kuwa haya yalikuwa ya kipindi cha Paulo na akina Petro? JIBU: soma posts zangu zote kwa Lwembe/Yusha kwenye post ya ‘’Mafundisho dhidi ya Wanawake yalitafsiliwa vibaya na kama unadhani utakua umetoka kapa, sema nitarudia kama kawaida, hamna tabu.

  Umeuliza, ‘’ Je, kuna maandiko ya Mungu yanayoapply kwa baadhi ya watu na tamaduni zao na kwa wengine hayaapply? JIBU: Yale ya MUNGU kweli yaani Neno/Ujumbe/Fundisho/ Kitu cha KiMungu, basi Ni kwa vizazi vyote ivyo ni JUU YA TAMADUNI ZOTE na yale yaliyo rekodiwa ktk Bible ya Wakati, Majira, Agano fulani, Watu, Mtu kwa jamii, eneo, mila desturi zao, haya-apply kwa wote kwa kua SI Neno/Ujumbe/Fundisho/ Kitu cha KiMungu kwa vizazi vyote.

  Hii statement yako ni kitisho cheap tu hiki ’’Ukipata majibu thabiti ya maswali hayo’’= unaonaje wewe hayo majibu yangu sasa, ni thabiti, kizibiti au dhabiti?

  Press on.

 15. Ndg Paul,
  Naomba kujibu tena hivi swali lako hili:
  Ina maana Bible Bila vitabu vya Ellen HAIJAKAMILIKA?

  Jibu
  Hasha!!!! Bibia ni Neno la Mungu toshelevu kabisa. Ukiamua kulisoma vizuri, litakuongoza kwenye njia sahihi mno, dini sahihi ya Biblia na si mapokeo ya wanadamu.
  Ubarikiwe sana

 16. Sungura,
  Ubarikiwe na Bwana kwa maswali mazuri. Nimejaribu kidogo tu kudondoa kukupatia majibu yake. Karibu sana.

  1. Aliyetoaga unabii wa kurudi kwa Yesu tarehe fulani, na wasabato wakakusanyika milimani wakimgojea na matokeo yake hajarudi mpaka leo alikuwa nabii nani?
  Jibu
  Watu wengi sana hufkiri kuwa huyo alikuwa ni Ellen G. White. Kipindi hicho unachikibashiri ndg Sungura, kilikuwa ni kati ya mwaka 1843 na 1844. Ukiangalia maisha ya mwanadada huyu kwa kipindi kile, alikuwa na umri wa miaka 17. Ndiyo, Mungu alianza kumtumia akiwa na umri mdogo huo, lakini njozi au maono yake ya kwanza, yalimtokea baada ya mwaka 1844, nanukuu maelezo yake “It was not long after the passing of the time, in 1844, that my first vision was given me” (Life Sketches of Ellen G. White, Page 64).
  Sasa kama ni hivyo, nani basi aliyetabiri ujio wa Yesu kwenye miaka hiyo? Jibu; Hawa walikuwa ni wanamatengenezo kama vile William Miller, watu waliokokotoa vibaya tu unabii wa Daniel na ufunuo na kudhani kuwa Yesu angekuja kipindi hicho, na kama wangekokotoa vizuri na kwa usahihi, wangebaini kuwa, kipindi hicho hakikuwa cha Yesu kuja na badala yake Yesu alikuwa anaingia patakatifu pa patakatifu mno. Sehemu alipo hata sasa akituombea mimi, Sungura, Paul John, na SG wote ili kwa pamoja tumjue YEYE na tufikie ukamilifu
  .
  2. Na Ellen alikuwaga anasimama wapi anapofikisha ujumbe wake,ikiwa wanawake hawakutakiwa kusimama kwenye mimbari
  Ndg Sungura, kama ulipitia kwa makini majibu yangu ya kwanza kwa maswali yako,, swali hili nililijibu vizuri sana hapo juu.Jaribu tena kurejea sehemu hiyo hapo juu.
  Mungu akubariki ndg yangu.,
  Asante.

 17. Ndg Siyi,
  Naomba kuuliza tena hivi:
  Ina maana Bible Bila vitabu vya Ellen HAIJAKAMILIKA?

 18. Siyi,
  Aliyetoaga unabii wa kurudi kwa Yesu tarehe fulani, na wasabato wakakusanyika milimani wakimgojea na matokeo yake hajarudi mpaka leo alikuwa nabii nani?

  Na Ellen alikuwaga anasimama wapi anapofikisha ujumbe wake,ikiwa wanawake hawakutakiwa kusimama kwenye mimbari
  Asante.

 19. Paul John,
  Ubarikiwe na Mungu. Mimi napenda nidokoeze majibu kama watakavyofanya na wengine hapa SG ili kukidhi haja yako ya kujua kama ulivyoomba.
  Maswali:
  1. Ellen G. White, KWA KUFANYA KAMA WALIVYOFANYA MANABII WENGINE WA KIKE WA AGANO LA KALE, Je hiyo haimfanyi yeye kuwa NABII wa Agano la Kale?

  Jibu
  Ukiangalia historia ya kuandikwa kwa Biblia, utaona kuwa, Biblia iliandikwa kuanzia mwaka 1400’s BC hadi 400’s BC (Agano la kale) na Mwaka 40’s hadi 90’s AD (Agano Jipya). Ellen G. White alizaliwa 1827 hadi 1915 AD. Ukisoma vitabu vya manabi wa Agano la Kale, Jipya(Biblia nzima) na Maandishi(unabii) ya Ellen G. White, vyote vinashabihiana vizuri. Matukio aliyoyatabiri Ellen G. White yalishatokea na mengine yanaendelea kutokea. Ukisema kuwa Ellen G. White anafaa kuwa nabii wa Agano la Kale, mimi siwezi kukubishia maana aliyoyaandika yamo kwenye agano pia. Ukisema Ellen G. White ni wa Agano Jipya, napo ni sahihi tu maana kazaliwa kipindi cha agano jipya na maandishi yake, yanaendana na maandishi(vitabu) vya manabii wa agano Jipya. Ndiyo maana, Wasabato wanaamini kuwa, nabii Ellen G. White, ni nabii kama manabii wengine walioandika Biblia katika maagano yote mawili.

  2. Ellen G. White anakubalika WAPI/NA AKINA NANI kama nabii wa kweli wa kike?

  Jibu.
  Ellen G. White anakubalika sehemu yoyote na kwa watu wote kama nabii wa kike kwa wale wote wanaoisoma Biblia yote kisha kuilinganisha na maaandishi yake. Kwa wale wasiosoma Biblia na maandishi yake, hawawezi kuelewa maana hawaelewi.

  3. Ni UNABII gani kwenye Biblia (nukuu ya maandiko inahitajika hapa) UNAOMTETEA/UNAOMTAMBULISHA Ellen G. White kuwa mwanamke nabii anayestahili kuongoza katika mambo ya Mungu TOFAUTI na mama Elizabeth Eaton ambaye ameteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Kaninsa la Kilutheri kule Marekani?

  Jibu,
  Unabii uko mwingi sana. Nikupe mfano mdogo tu usome unabii wa kitabu cha Daniel na Ufunuo, halafu chukua vitabu vyake kama vile Great Controversy, Testmonies to Ministers, Desire of Ages nk. Endapo utapata shida ya kiitikadi kuelewa, chukua vitabu vingine vya historia kama vile vya akina Uriah Smith(The 2300 Days and the Sanctuary), Andrews, John Nevins (The Commandment to Restore and to Build Jerusalem) nk

  4. a). Kuna tofauti gani kati ya kile anachotakiw kukifanya mama Eaton na kile wanachofanya Mama Rwakatare, Joyce Mayor, Paula, na akina mama wengi ambao wanaendesha utumishi wao katika kuhudumia watu kiroho na kuwakutanisha watu na nguvu za Mungu?
  b). Au kina mama wote hao, wayafanyayo ni machukizo mbele za Mungu?

  Jibu.
  @a na b. Hawa wote uliowataja kimsingi siyo manabii wala waamuzi na wala Mungu hajawatuma kufanya hayo wanayoyafanya hivi sasa. Nasema hivyo kwa sababu, ukiwapima kama wanaendana na manabii au waamuzi, maaskofu wa zamani ndani ya Biblia, huwezi kukuta hata aya moja ya Biblia inayoshabihiana na nyadhifa zao. Ukiwapima kwa vigezo vya kibiblia, wanapwaya kiasi kikubwa mno. Wangekuwa wametumwa na Mungu, wasingepingana na wale waliotumwa na Mungu kwanza. Hivyo wayafanyao ni machukizo mbele za Mungu na wanapaswa kutubu, vinginevyo watakiona cha mtema kuni maana wanaongoza wengi mno katika upotovu, damu za hao watu zitadadiwa mikononi, mwao. Watasalimikaje ndg Paul?

  Bwana akubariki.
  Karibu sana

 20. Amani iwe nanyi wapendwa!

  Samahani, yawezekana nisipate muda kwa haraka kufuatilia majibu ya swali ninalotaka kuuliza hapa. Ila nitaomba kama kuna mtu atakuwa ana wazo kama la kwangu anaweza kuendeleza hiki nitakachokuwa nimekiuliza!

  Nitanukuu kwanza toka kwa ndugu MJ,N,Siyi halafu maswali yatafuata:

  “Hivyo basi, Ellen G. White alifanya kama walivyofanya manabii wengine wa kike wa agano la kale. Ellen G. White anakubalika kama nabii wa kweli kwa sababu unabii wake haupingani na manabii wote waliomtangulia ndani ya Biblia. Na kama atatokea nabii mwingine wa kike au kiume, tutampima kama unabii wake unafanana na manabii wengine ndani ya Biblia.”

  Maswali:

  1. Ellen G. White, KWA KUFANYA KAMA WALIVYOFANYA MANABII WENGINE WA KIKE WA AGANO LA KALE, Je hiyo haimfanyi yeye kuwa NABII wa Agano la Kale?

  2. Ellen G. White anakubalika WAPI/NA AKINA NANI kama nabii wa kweli wa kike?

  3. Ni UNABII gani kwenye Biblia (nukuu ya maandiko inahitajika hapa) UNAOMTETEA/UNAOMTAMBULISHA Ellen G. White kuwa mwanamke nabii anayestahili kuongoza katika mambo ya Mungu TOFAUTI na mama Elizabeth Eaton ambaye ameteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Kaninsa la Kilutheri kule Marekani?

  4. a). Kuna tofauti gani kati ya kile anachotakiw kukifanya mama Eaton na kile wanachofanya Mama Rwakatare, Joyce Mayor, Paula, na akina mama wengi ambao wanaendesha utumishi wao katika kuhudumia watu kiroho na kuwakutanisha watu na nguvu za Mungu?
  b). Au kina mama wote hao, wayafanyayo ni machukizo mbele za Mungu?

 21. Seleli,
  Ha ha ha ha , Una maswali ya mtego kaka. Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili, hukata kwa mhubiri na mhubiriwa!! Sidhani kama kuna kitu inachokiita Biblia mapokeo, bado kina nafasi katika mafundisho ya wateule wa Mungu. Kama kipo, nitaomba na mimi nijifunze kwako.
  Kuhusu wanawake kuwa viongozi ama kwa taasisi za kibinadamu au ki-Mungu au kidunia kama vile serikali nk, HUO SIYO MPANGO WA MUNGU. Kwa wale walio upande wa Mungu, wawe ni serilaki, taasisi, chama, dhehebu nk, kusimamisha kiongozi mwanamke, NI MACHUKIZO MBELE ZA MUNGU. Huenda ndiyo maaana leo Mungu amekuwa hajibu baadhi ya maombi yetu kama nchi kwa sababu tumekiuka SHEria zake. Tumeweka viongozi wanawake, jambo ambalo Mungu hakuagiza. Umeelewa kaka?
  Unataka kujua kuna matatizo gani wanawake wakiwa viongozi? Nakuona unajiuliza maswali kama ya Usa kuhusu kugusa Sanduku la Bwana. Kaini kutoa sadaka ya maembe, ndizi, mapapai nk badala ya mnyama. Lakini pia nakuona unahoji kama Hawa kutoruhusiwa kula tunda, what will happen if I eat?? Do you know what happened?? Mimi sina jibu la moja kwa moja. Ila napenda kukwambia kuwa kile alichokikataza Mungu, wewe ukikifanya tu, ni DHAMBI tayari. Maana neno la Bwana-Biblia ni SHERIA. Na dhambi ni uvunjaji wa sheria ya Mungu. Lakini pia huenda Mungu hajawapa kwa sababu ya hali zao au kwa vile ni viumbe wadhaifu kama inavyodai biblia.
  Barikiwa sana.

 22. Seleli,
  Ubarikiwe kaka na M/Mungu kwa tafakuri yako nzuri kuhusu posts/michango yangu kwa mada husika. Ingekuwa vyema zaidi kumshukuru Mungu pale unapoguswa/kubarikiwa na michango yangu badala ya kumpatia Siyi kongole(shukrani/pongezi)nyiiiingi, huku Mungu ukimpa nafasi ya mwisho kwazo!! First Things First-God!!
  Kuhusu suala la majukumu kuwa yalikuwa kwa Adamu tu na siyo Hawa, umesema siyo kweli, ni kweli siyo kweli kama utangalia kwa haraka. Lakini ukiangalia vizuri utagundua kuwa, Adamu ndiye alikuwa the Initial &Final Point. Ndiyo maana hata Hawa alipokula tunda, hakujitambua kuwa yu uchi muda uleule. Walijitambua kuwa wa uchi baada ya mfalme-Adamu kula na yeye. Hata hivyo ukisoma Mwanzo 2:15-20, utagundua kuwa, Adamu tu ndiye aliyepewa hayo majukumu. Suala la Hawa kuzaa, Biblia haijasema kuwa walikaa kwa muda gani wakiwa bustanini kabla ya kuanguka dhambini, wala haisemi kuwa, walikuwa wameshapata mtoto/watoto wakati wakiwa bustanini. Inachojaribu kutumbia biblia, ni kwamba, Adamu na Hawa wanapata mtoto/watoto baada ya kuwa walishafukuzwa bustanini kwa sababu ya dhambi. Hata ukiangalia Sura ya tatu mstari 2-3, Hawa anatoa ripoti ya kauli taarifa kwa nyoka aliyokuwa ameipata kutoka kwa mumewe Adamu kuhusu kukatazwa kula matunda ya mti wa katikati. Hawa hakuwepo wakati huo. Hii inaonekana kuwa, Adamu alipewa peke yake majukumu ya kuilima, kuitunza bustani, kuita wanyama majina nk. Hawa alipoumbwa, majukumu mengine aliyakuta tu Adamu kashayafanya tayari na hivyo kumwelekeza kuhusu maelekezo ya Mungu kwao. Wachambuzi wa Maandiko wengine wanadai kuwa, Hawa angepata katazo la kutokula tunda la mti wa Bustanini moja kwa moja kutoka kwa Mungu mwenyewe, huenda asingedanganyika kwa nyoka. Anyway, hizi ni assumptions ambazo hatuwezi kuzisimamia sana. Kile alichoagizwa Adamu na Mungu, kilimhusu Adamu, familia yake na uzao wake wote.
  Kuhusu laana kwa Adamu au Hawa; Kimsingi Ukisoma hapo kitabu cha mwanzo 3, huwezi kuona sehemu yoyote inasema kuwa Adamu anapewa laana kama Hawa. Kwa sababu Hawa alikuwa ni sehemu ya Adamu(mwili wa Adamu), laana ilimpata na Adamu indirectly, ndiyo maana leo, hawafi wanawake peke yao, wala hawapati machungu ya kuzaa peke yao(ushahidi wa kidaktari unaonesha hivyo). Athari zilimkumba Adamu pamoja na familia, na uzao wake pamoja na kwamba, wewe mwanaume huwezi kukinywea kikombe kama wanachokinywea akina mama.
  Kuhusu wanawake viongozi na ving’ani vyao kuingia patakatifu, kama nilionekana kuponda sana, basi nikiri tu kuwa, huenda kweli nilipitiliza kusema saaana. Nilipaswa kusema tu positively!! Oooh, tafadhari, mnisamehe wanawake mliokwazika kwa maelezo hayo, japo hamkujitokeza kusema. Nilisema kwa nia njema tu ya kuonesha mipaka ya mamlaka kimajukumu aliyotupatia Mungu kati ya wanaume na wanawake.
  Kuhusu uwezo wa Mungu leo kusema mwamamke fulani awe kiongozi, kuwa upo au haupo!!! Binafsi, niseme tu kuwa, Mungu hajabadilika. Nguvu na uwezo wake haujabadilika. Mungu ni yuleyule jana, leo na hata milele. Anaweza kusema tena bila tatizo lolote kama ataamua kufanya hivyo.
  Kuhusu kauli ya Paulo kwa wanawake kuwaambia wakae kimya kanisani kuwa alimaanisha mamlaka au kutosema/hubiri kabisa ndani ya kanisa? Mimi napenda kukuuliza, kuwa, ni kwa kiasi gani tunaweza kuchora mstari kuwa haya yalikuwa ya kipindi cha Paulo na akina Petro? Habari gani Paulo angekuwa ktk agano la kale? Je, kuna maandiko ya Mungu yanayoapply kwa baadhi ya watu na tamaduni zao na kwa wengine hayaapply? Ukipata majibu thabiti ya maswali haya, nina imani utakuwa umepata majibu ndg na kaka yangu kipenzi.
  Wasalaamu
  Karibu tena kwa kiporo ulichobakiza.

 23. Siyi,

  Sijakuelewa hapa kidogo kuhusu..’’tumezoea mazoea/mapokeo mabaya sana ambayo yamekuwa ni kawaida makanisani kwetu, Lakini mbele za Mungu, ni hatari na machukizo tupu’’. Si kwamba sijakupata kua ulikichosema ni KWELI tupu lakini nina maana hii..Kulingana na niliyosema ktk jibu langu la kwanza kwa post yako kama alivyojibu pia Nelson kuhusu mapokeo, nimedokeza kua SI KILA POKEA NI CHUKIZO! Sasa response yako hii ya sasa, inakusudia kujibu hili? Kua UMEKATAA NA KWAMBA KILA MAPOKEA KIIMANI NI CHUKIZO-msisitiozo ni neno ‘KILA’- tafadhari fafanua kidogo tu hapo, kidogo tu sana mantiki ya kujibu uliyojibu au tu ulisapoti my part one ya jibu niliposema YAKO MAPOKEO AMBAYO NI CHUKIZO NA TUYAFYATULIE MBALI TENA HARAKA SANA KABISA?

  Sasa hii la pili naona kidogo, umefanya haraka…NAKUHAKIKISHIA NAWEZAFANYA MAKOSA YA KIUANDISHI kama kukosea herufi, kuruka neno nk LAKINI SI LA KI- MANTIKI/MAUDHUI!

  Niliposema ‘’Taasisi ya Kibinadamu’’-nikataja mifano yake, umesema nimetoa mfano wa Kanisa!!!!! du! Labda nikiiweka ivi then nipe jibu..Mfano wa ‘Taasisi za Kibinadamu(ya mambo ya dini/imani) ni RC,Shiha, Suni, Yehova Witness, aya narudia na yale ya kwanza kama Jumbo Jet Ministry, Helicopter fellowship, Assemblies, Menonite, Lutheran, labda nikolezee kwa kuweka pia Anglican, na nimalizie kabisa kwa kuongeza na CDA-Sabato nk, JE HAYO NI MAKANISA? Maana umesema nimetoa mfano wa Kanisa!!!!!!!!!! Lakina pia kwa upande wa pili, nilisema ‘’Taasisi ya Ki-Mungu’’ nikasema mfano KANISA-sikutaja kitu zaidi ya ‘’Kanisa’’!!!!!!!!…NIULIZE UMENIPATA?

  Lakini pia kuna swali la msingi hapa nimeuliza ivi KUNA TATIZO GANI WAO WAKIWA….napenda kujua hayo MATATIZO as per your akili,maarifa, ujuzi, uzoefu, tafiti, uhalisia, mawazo ya Watu na juu ya yote as per the BIBLE? JE KUNA MATATIZO YOYOTE VERY CRITICAL MUNGU ALISHA TAMKA KWA VIZAZI VYOTE ILI KUA MAKINI SANA NA HAWA VIUMBE ‘KE’ KUHAKIKISHA KAMWE KATU, WASIWE WAKUU KWA SABABU YA HATARI LABDA WANAZOBEBA/WALIZONAZO AU WATAKAZOSABISHA? au ni sisi tu Wanadamu na UANAUME NA MISIMAMO YETU? –mmh! mi nauliza tu wajameni!

  Press on

 24. Siyi,

  Swali lako kua ‘Ninyi hamsomi Biblia- nikutoe wasiwasi kua ninajitahidi kuisoma, so don’t worry, relax, Amen?.Nimesoma kila nukta ya post yako na nimebarikiwa sana na ukweli mzito uliosema kuhusu ili-NAFASI YA MUME NA MKE au viumbe vya Kike na vya Kiume. Uliyoyasema ktk hoja iyo, BAADHI ni sawa kabisa Ki-Mungu na KiBiblia-nakubaliana na wewe 100% and great is your Godly/Biblical lecture brother. Hata dunia ipumue, izime, iinuke, ikae, system ya Mungu kwa Wanadamu kulingana na jinsi zao itabakia nasi tulio wake tutasimama kwa ilo.(Angalizo: System ( wenye ndani yake wishes/ rules/ Neno/matakwa/Will) ya Mungu inayoweza hakikishwa na thibitishwa kwa kweli nyingi ktk Bible na ivyo iyo kua KWELI kwa vizazi vyote past,present and future-utanielewa tu kwanini nimesema ivi kadri hii mada itakavyofunguka na kupanuliwa na washiriki na kupelekea/lazimu ili lifafanulike). Pamoja na kubarikiwa sana na KWELI TUPU kuhusu System ya Mungu ulivyoeleza vema sana, yako baadhi ya mambo hapa, mengine nitapenda kukuuliza maswali na mengine nitakosoa na mengine nitachangia ufahamu wa mambo kama ifutavyo:

  Ni kweli Mungu hakumuumba Hawa ila Adamu kwanza lakini ni UKWELI PIA kua at last au nzuri/yenye upako zaidi , at best- Hawa nae alitokea/aliumbwa. Ingawa pia ni kweli Adamu ndiye aliyepewa majukumu na Mungu lakini si KWELI HATA KIDOGO kua ni Adamu TU yaani yeye mmoja tu ndio alipewa. Labda kama unayo maana nyingine ya jukumu ili TU kwa adamu-sema, lakini ktk matamko ya Mungu kama anavyoya-report mwandishi kuelezea shughuli nzima ya uumbuaji wa WANADAMU WA KWANZA ilivyokua hapa-Mwanzo.1:26-28, usisahua hapa kuna MAJUKUMU MAKUBWA KABISA KWA WOTE SI MMOJA TU!!!!!!!! ALIEYEMZALIA WANA bwana ADAMU ni HAWA-jukumu la kuzaa kuongezekana na kutawala Nchi na viumbe vyote, lisingewezekana bila Hawa kuwepo! Adamu asigetimiza ilo kwa kutumia mawe, mwana selele-hawa, miti au pusi!!!.Majukumu mengine kama Kutunza sharti la Mungu, kuitunza/kulima bustani kunako reportiwa ktk Mwanzo.2:15-17 WOTE wanahusika ingawa Adam alihusika kwanza. Yeye kua wa kwanza kuhusika nayo, hakukumaanisha Hawa alikua exempted kwa hayo ndio maana walipokosea jukumu la Kutunza masharti ya Ukaaji bustanini, waliadhibiwa WOTE-Mwanzo.3:8-19( notice: mstari wa 13- baada ya Hawa kutenda kosa na Mungu kabla haja ajaadhibu, Anamuuliza Hawa SPECIFICALLY- ‘’Umefanya nini iki!!!!!!!!!!! Mungu si mjinga au unfair kumuuliza Hawa kama asingekua ana husika na Jukumu ndio maana adhabu naye pia alitandikwa!

  Kuhusu mwanamke peke yake alilaaniwa na siyo Adamu na Laana ya mwanamke, anaibeba mwenyewe, tafadhari naomba usome maandiko haya ya wakati Mungu anatoa adhabu..Mwanzo.3:14-19 kisha niambie KAMA KWELI MUNGU ALIMLAANI HAWA, ADAM! Tafadhari nijie kwa jibu ukisha soma maandiko hayo pole pole. Pia niambie kitu gani hasa kiliilaniwa so clearly hapo

  Hili la mwanamke kuingia na (skin tight) kwenye shughuli za kikuhani-hekaluni, ni kweli halikuruhusiwa na halitakiwa kamwe na sidhani hata leo kwa Viongozi Wanawake mfano huyo pichani, atakwenda na skin tight acha tu mimbarini bali hata benchi la nyuma kanisani kwakwe, Nadhani hapo, umeponde kiinjilisti kifire-fire kilichopitilizia rafiki, taratibu kamanda wa Bwana, upendo kwanza kisha hukuma,Amen?

  Kwa wanawake waliokuwa manabii na waamuzi kua walipata MADARAKA HAYO kwakua NI MPAKA MUNGU MWENYEWE ALISEMA, Nauliza tu kua KWA IYO UWEZEKANO HUO WA MUNGU KUSEMA LEO ILI KIONGOZI WA KIKE KUPATIKANA UPO HAUPO?-mi nauliza tu wajameni, nisaidieni!!!!!!!!!

  Kuhusu Paulo kusisitiza kua wanawake kutokuwa na mamlaka makubwa ya kikuhani ndani ya kanisa, badala yake, wakae kimya wakijifunza kwa unyekekevu unaowapasa wanawake watakatifu, naomba niulize, Paul alisemelea kusisitizia Wanawake kutokua na mamlaka ya ukuhani kweli ktk maandiko hayo au ya kufundisha mbele ya Wanaume tu basi tena kwa makanisa ya wakati wake na ya chini yake kama mwanzilishi na Baba yao Kiroho lakini pia na kwa mengine ktk tamaduni zile za wanawake hata kutohesabiwa hata ktk mikutano ya Yesu mwenyewe?

  Press on( nitamalizia maoni yangu kuhusu uliyosema on UN, HAKI SAWA NA HAJIRI-MAMA ISHMAILI ati AFUKUZWE!

 25. Seleli,
  Ni Kweli leo tumezoea mazoea/mapokeo mabaya sana ambayo yamekuwa ni kawaida makanisani kwetu. Lakini mbele za Mungu, ni hatari na machukizo tupu. Kimsingi maswali yako, nayaona kama ni swali moja tu. Taasisi za kibinadamu halafu ukatoa mifano ya kanisa…na taaisisi za ki-Mungu ukataja makanisa,…noana ni kama swali moja ndani ya mawili. Sema lile la kwanza sidhani kama makanisa ni taasisi za ki-binadamu kama ulivyosema. Nijuavyo mimi, kanisa ni la Mungu. Anyway, utatueleza ulikuwa na maana gani.
  Kwa vile hujasoma posts zangu, naomba nisianze kurudia rudia kusema kitu kilekile. Soma kwanza, halafu kama utakuwa na swali au utata utakuja tena.
  Ubarikiwe sana

 26. Siyi na Nelson,

  Siyi, Nilitegemea uyaone kwanza maswali yangu 2 niliyoweka wazi tu kwa MAANA nzuri tu lakini pia kimtego-mwema!!!!!!!!!!! Nimetumia neno Taasisi ya ‘’Kibinadamu’’ na ya ‘KiMungu’. Labda niyaboreshe maswali hayo hayo tena chini hapa kisha nipitie post yako maana umeniita kwa jina niangalie yaliyojiri kwa uliyoleta. Maboresho au niliyokusudia ktk maswali ya mwanzo ni kama ivi: (Notice: Maneno yenye misisitizo e.g kama ‘bold, capital letters au underline’)

  MOJA: Kuna tatizo gani Mwanamke akiwa Kiongozi MKUU wa Taasisi ya KIBINADAMU mfano dini au dhehebu namely Lutheran, Sabato, Assemblies, Pentecost, Menonite, Methodist, Baptist, Jesus Only, Full Gospel, Helicopter Ministry, Jumbo Jet fellowship nk?

  PILI:Kuna tatizo gani Mwanamke akiwa Kiongozi MKUU wa Taasisi ya KI-MUNGU yaani Kanisa Kusanyiko la Waliokombolewa na Damu ya Yesu/waliozaliwa mara ya pili, Waliojazwa na Roho Mtakatifu, dalili na ishara za kua wao wameokoka zinajidhirisha waziwazi wamuabudupo Mungu, wafanyapo huduma na kulihubiri Neno, waishipo ktk uso wa Nchi?

  Siyi naomba majibu kwanza kwa hayo na pia bwana Nelson Tumaini kama umenipata pia karibu, jisikie huru kabisa kuflow ndugu yangu, uwe na amani and free over 500%, relax brother, go for them.

  Nakubaliana nawe Mtumishi wa Mungu Nelson Tumaini kua nia na madhumuni ya mijadala hii ni kupeana kweli kwa kufuta msingi sahihi wa neno la Mungu ili wapendwa tupone na mwisho wa siku tukutane wote mbinguni kwa baba na kua Itakuwa c vyema na haki tukasimamia mapokeo ya kibinadamu ila nadhani ili nalo ni FACT-kua SI MAPOKEO YOTE YA KIBINADAMU MABAYA NA KILA KITU CHA WANADAMU WALICHOKUA NACHO- KABLA YA YESU KUJA, YOTE YALIKUA OVYO, KUZIMU NA HATARI TUPU, ningependa kuliweka ilo sawa kwanza-Yanakua mabaya tu pale yatakaposababisha kitu hiki Yesu alisema/dokeza ivi Marko.7:13-Kwa Kiswahili imesema.. MKILITANGUA neno la Mungu, Kiingereza napenda zaidi na pia najua unapenda/unabarikiwa na lugha hii ya Wanadamu nzuri tu yakutumia, inasema..’’Making the Word of God OF NO EFFECT by holding onto your traditions received… Kwa hiyo ni pale tu Neno la Mungu au kwa ujumla Kanuni za Mungu ZITAKAPOKUA ZINAKOSA EFFECTS/MASHIKO/NGUVU/MAMLAKA/FINAL SAY KWA SABABU TU YA SISI KUKOMALIA MAMBO YETU( Utamaduni kwa maana pana-totality of life-toka Kiuchumi,Kisiasa,Kijamii(mambo ya imani yapo hapa)ndipo hapo TWAPASWA BILA HAYA WALA HILA AU KUMUNG’UNYA MANENO NA HATUA, kuyafyatulia mbali kabisa, ikibidi kupingana na system nzima ya familia, Kijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa…Taifa mpaka Bara. Otherwise kama Tamaduni eg Traditions zetu hazi haribu neno la Mungu basi ni baraka, ni mapokeo safi kabisa, hamna shida hapa duniani mpaka mbinguni, na pia ikumbukwe, sisi ni wanadamu, tumezaliwa duniani, hajutaremka toka Juu kama Bwana! as a matter of fact, hata BWANA wetu ingawa alikuwapo kabla ya Ibrahimu uko JUU yet alipoteremka ilibidi naye azaliwe na kisha kuishi kwa taratibu alizozikuta bila shaka zile tu zilizokua hazifanya Neno kua OF NO EFFECTS!

  Napenda pia nisema ku Wakati ule tulipookoka, kwa ule moto na hamu, furaha ya kumjua Yesu na hata pia kwa Ufahamu mdogo wa Neno na mambo ya Mungu tuliyolelewa kwayo, ilitufanya tufikiri/chukulia kila mila na desturi ni PEPO au KUZIMU na ivyo kukataa kila kitu na kujitenga nao kwa kila kitu almost ndugu zetu ktk Ukoo na Familia na hata kusababisha mahusiano na ndugu zetu KUHARIBIKA vibaya sana unnecessarily BEYOND repair todate- si kwa kua ilikua ni mapenzi ya Mungu na tulikua kweli tunamtetea Bwana wa Majeshi na kuisimamia Imani yetu thabiti kithabiti bali simply ilikua ni… WATU WANGU WANAANGAMIZWA( sio wana ANGAMIA-iliyozoeleka na wengi) na in this case WANAJIANGAMIZA( kusababisha makwazo, vurugu,huzuni, chuki, vita, kukatika mahasiano na familia,Koo, jirani, hata Ndoa nk) kwa KUKOSA MAARIFA-Hosea.4:6-(knowledge is always power iwe Kiroho au Kimwili, ina-apply kote)

  Niishie hapa kwa sasa, huku yasiwe marefu sana kama topic ya kule! Nitarudi kwa ajili ya Post ya Kaka Siyi specifically. Amen.

  Press on.

 27. Sungura,
  Nakushukuru kwa swali zuri.
  Kama ulipitia mchango wangu wa awali kikamilifu, nina imani ulipitia sehemu niliyogusia habari za manabii na waamuzi kama kama Debora, Miriamu, Hulda, nk ambao Biblia inawataja kwa wadhifa huo. Lakini ukiangalia ndani ya neno ya Neno, Mungu alisema ndipo wakawa na wadhifa huo.
  Hali kadhalika na kwa Ellen G. White, Mungu alisema awe nabii na ikawa hivyo japo yeye mwenyewe (Ellen G. White) hakujiita nabii kama walivyo manabii wa leo. Hivyo basi, Ellen G. White alifanya kama walivyofanya manabii wengine wa kike wa agano la kale. Ellen G. White anakubalika kama nabii wa kweli kwa sababu unabii wake haupingani na manabii wote waliomtangulia ndani ya Biblia. Na kama atatokea nabii mwingine wa kike au kiume, tutampima kama unabii wake unafanana na manabii wengine ndani ya Biblia. Tofauti na hapo, watakuwa ni wajasiliamali tu!!
  Wasalaamu

 28. John Haule.
  Nakushukuru kwa maswali yako mazuri. Mimi nitajaribu tu kukujibu na nina imani na wadau wengine hapa SG, watajitokeza kukujibu ndg yangu. Bwana akubariki sana.
  Maswali 1&2 . Nani anatakiwa kuwa KUHANI ktk agano jipya!!?kwa mfano Mtume,Nabii,Mchungaji, Munjilisti, Mwalimu. Wazee nk. Hivi kwenye AGANO JIPYA kuna KUHANI au KUHANI MKUU!!?
  Majibu
  KUHANI ni nani? Kuhani Kiingereza Priest na Kiebrania Kohen, katika agano la kale, lilitumika kumaanisha mwanaume aliyekuwa amepambwa sana kwa mavazi marefu ya kitani safi kwa ajili ya huduma takatifu. Ili kumfahamu mtu anayepaswa kuwa KUHANI katika agano jipya, ni vyema tukafahamu majukumu ya KUHANI katika agano la kale. Miongoni mwa majukumu ya KUHANI katika agano la kale yalikuwa ni pamoja na:
  a. Kutoa huduma sehemu pa patakatifu, sehemu ambayo wakati wana wa Israel wakiwa Jangwani, ilikuwa ni MADHABAHU, na pindi taifa la Israel walipokuwa taifa kkt nchi yao-Kaanani, sehemu ya patakatifu ilikuwa ni HEKALUNI.
  b. Kufundisha Sheria za Mungu(yaani Neno la Mungu).
  c. Kufanya maombi kwa ajili ya taifa la Israel (au mtu mmojammoja, familia au ukoo).
  Sifa za Makuhani wa Agano la kale(Jitahidi uzisome Walawi 21).
  Kwa makuhani hawa, alikuwepo pia KUHANI MKUU. Huyu alikuwa akiingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa mwaka mzima kwa ajili ya kazi ya upatanishi wa dhambi za taifa zima (kutoka 30:10, Walawi 16:34, Waebrani 9:7 nk).
  Hoja ya msingi, ni nani anapaswa kuwa kuhani leo?
  KUHANI Mkuu kwa leo tunaye mmoja tu. Yesu Kristo 1 Timoth 2:5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu Waebrania 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu. 1 Yohana 2:2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. 1 Yohana 4:10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 1 Yohana 2:1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.

  Makuhani wengine (wadogo), ni hawa viongozi wetu wanaowekwa wakfu kwa kazi ya Bwana, ambao kimsingi sharti na wao wawe WANAUME- REJEA walawi 21. Yesu alipokuja, alichukua nafasi ya Kuhani mkuu, na akawapa mamlaka ya ukuhani mitume wake(wanaume tu), pamoja na kwamba, wanafunzi wa Yesu wanawake walikuwepo.
  Katika 1 Petro 2, Kiufupi, Wakristo wanaitwa makuhani na Wafalme kama uthibitisho wa haki yao kuwa warithi wa Ufalme wa Mungu na Mwanakondoo. Kwa mantiki hiyo, kwa vile wanaitwa kuwa ni makuhani, Kwanza, hakuna mtu duniani ambaye anaweza kuwa mpatanishi kati ya mtu/watu na Mungu badala yake, mtu/watu wenyewe wanaweza kuomba moja kwa moja kwa Mungu kupitia kuhani mkuu Yesu Kristo. Na Pili, Wakristo wanaitwa makuhani kwa maana ya kutakiwa kumtumikia Mungu kwa dhamira/mioyo yao yote. Tunapaswa kumsifu na kumfanyia Bwana kazi YEYE aliyetutoa gizani na kutuleta katika nuru yake ya ajabu. Suala la mamlaka hapa halipo. Jaribu kupitia na Bible commentary kwa ajili ya maelezo zaidi.

  Pamoja na kupewa majukumu haya ya kufanya uinjilisti kwa pamoja, bado kuna sifa za viongozi wa kanisa, sifa ambazo Biblia imeziweka wazi kuwa ni kwa ajili ya viongozi tu wa kanisa hapa duniani. PITIA HIZI AYA ZOTE. (Hesabu 11:16-17, Mdo 6:1-6, Mdo 13:1-3, Mdo 14:23, 1Timoth 3:1-12 na Tito 1:5-9 ).

  Hakuna hata aya moja inayosema kuwa kiongozi/kuhani awe ni mwanamke. Wote waliotajwa hapo, ni WANAUME tu. Kama Yesu mwenyewe alichagua wanaume tu katika kuifanya kazi yake kwa ngazi ya mamlaka, na kanisa la mitume nao walifuata nyayo zilezile za Yesu, sisi leo ni akina nani hadi tunaweka hoja lukuki za kuhalalisha dhambi hii kubwa??
  Biblia haisemi kwamba wanawake wasifanye chochote ndani ya kanisa. Mifano ipo ndani ya biblia ya wanawake waliokuwa na huduma njema na kubalifu tu mbele za Mungu. Mf. Mariamu ndguye Lazaro, Susana, Dorica, Prisila na wengine wengi, huduma zao za uinjilisti kwa jamii Biblia/Mungu anazitambua. Wanawake wanaweza kufanya kazi nyingine yoyote ndani ya kanisa, lakini siyo kazi za Kikuhani, kazi za kuwekewa mikono, kazi zenye mamlaka. Hizi ni kwa ajili ya wanaume tu. Tofauti na hapo ni machukizo mbele za Mungu. Ni kuingiza Luciferian policy ndani ya kanisa. Tukumbukeni kuwa, kuna Ole imewekwa kwa watu wanaohalalisha uovu wa namna hii!
  Wasalaamu.
  Karibu tena.

 29. Binafsi nazidi kubarikiwa sana na michango mbalimbali coz inanifanya nijifunze mengi sana Mpendwa Siyi ubarikiwe kwa kujaribu kuweka mambo wazi kwa ushahidi wa kimaandiko so inakuwa ni rahisi kuomba Muongozo wa Roho Mtakatifu na kujifunza zaidi!Mpendwa Seleli na Sungura kuna jambo mnalifahamu kuhusu hili bt hamtaki kusema!Ningebarikiwa sana kama mgesema kimaandiko!Naamini nia na madhumuni ya mijadala hii ni kupeana kweli kwa kufuta msingi sahihi wa neno la Mungu ili wapendwa tupone na mwisho wa siku tukutane wote mbinguni kwa baba.Itakuwa c vyema na haki tukasimamia mapokeo ya kibinadamu ambayo itatupeleka motoni!Mbarikiwe wapendwa.

 30. Siyi, naona umechachamaa kwelikweli!

  Ivi Ellen G. White yeye hakuwa anasimama kwemye mimbari?

  Asante.

 31. Shalom SG,
  Neema izidi sana kwenu,

  Nami namshukuru Mungu kwa hii fursa kupitia hapa nami nichangie kwa sehemu.
  sina muda kwa sasa ila nitarejea kwa mapenzi ya Bwana.

  Bro Siyi na SG naomba kuuliza

  1.Nani anatakiwa kuwa KUHANI ktk agano jipya!!?kwa mfano
  Mtume,Nabii,Mchungaji,Munjilisti,Mwalimu.Wazee nk.

  2.Hivi kwenye AGANO JIPYA kuna KUHANI au KUHANI MKUU!!?

  Ninavyofahamu watu wote walio pata wokovu ni makuhani watakatifu

  1Pet2:5 Ninyi pia, kama mawe hai mjengwe kuwa nyumba ya kiroho, mpate kuwa makuhani watakatifu, mkitoa sadaka za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo

  9 Lakini ninyi ni uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa takatifu, watu pekee wa Mungu mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu.-SNT(Bibblegate)
  .

  Naomba msaada wenu wapendwa

  Maandiko P/se

  Mjoli Haule

 32. Hivi nikwli wanawake hawaruhusiwi kuhubiri anayefaham juu ya hili anifafanulie jamani

 33. Seleli na Kombe,
  Ninyi hamuisomi biblia? Mungu hakumuumba Hawa ila Adamu kwanza. Baada ya uumbaji, Adamu tu ndiye aliyepewa majukumu na Mungu na siyo Hawa au wote. Alipewa mmoja tu-Adamu. Baada ya dhambi kuingia duniani, mwanamke peke yake alilaaniwa na siyo Adamu. Laana ya Adamu ambaye alikuwa ni mtawala tangu mwanzo, inawaangukia watawaliwa wote wa Adamu, wanyama, viumbe wengine pamoja na ardhi. Laana ya mwanamke, anaibeba mwenyewe. Mwanzo 1:16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
  Kwa ujumla katika agano la kale, hata wakati wa Waisarel jangwani na katika nchi ya Kaanani, Hakuna mwanamke aliyekuwa akiingia na king’ani chake(skin tight) kwenye shughuli za kikuhani-hekaluni. Kuna baadhi ya wale wanawake waliokuwa manabii na waamuzi, HAWA UKIFUATILIA HISTORIA ZAO ZA KUPATA MADARAKA HAYO, UTAKUJA KUONA KUWA, NI MPAKA MUNGU MWENYEWE ALISEMA. Kulikuwa na watumishi wa Mungu enzi zile kama vile makuhani, lakini Mungu hakuwatumia kuwachagua wanawake kuwa viongozi-manabii na waamuzi. Mungu mwenyewe alichagua, teua, ALISEMA. Swali la kujiuliza, leo hawa wanaokuwa viongozi, Mungu kasemaaaa au tunawachagua sisi wenyewe tu? Je, tuna reference yoyote ndani ya Biblia inayotupa mamlaka hayo ya kuwachagua wanawake kuwa viongozi wakubwa kanisani? Chunguzeni na ninyi, acheni kushangaa tu!!
  Na katika agano jipya, Mungu anawaonesha wanawake wakishiriki katika huduma mbalimbali za uinjilisti tu lakini siyo kuwa na mamlaka makubwa yenye hadhi ya kikuhani ndani ya kanisa. Wanawake wanapaswa kuhubiri injili sana tu lakini siyo kwenye mimbari ya kanisa, ambayo ni sehemu ya makuhani pekee. Kristo kama kielelezo chetu, alikabidhi majukumu makubwa yooote kwa mitume/wanafunzi wake wa kiume tu japo wanafunzi wa kike walikuwepo. Paulo naye kalisisita hilo la wanawake kutokuwa na mamlaka makubwa ya kikuhani ndani ya kanisa, badala yake, wakae kimya wakijifunza kwa unyekekevu unaowapasa wanawake watakatifu.
  Vuguvugu la HAKI SAWA, 50 KWA 50(democrasia), siyo mpango wa Mungu. Ni mpango wa Ibilisi wa kumkosoa Mungu kuwa Mungu ana upendelelo, kampendelea sana mwanaume kuliko mwanamke. Vuguvugu hili lilianzishwa na Shetani mwenyewe kupitia asasi maalumu sana ya mpinga Kristo- UN. Kwa mf, wanamkosoa Mungu wakidai hivi, Mungu amekuwa akimpendelea sana mwanamke kuliko mwanaume. Hajiri hakujitakia kuzaa mtoto-Ishmail. Lakini Sara alipopata wa kwake, akamwambia Ibrahim amfukuze Hajiri na mtoto pale nyumbani wasije wakapata nafasi ya Ishamil kuwa mrithi. Ukiendelea kusoma kisa hicho, Ibrahimu alionekana kusita kumfukuza Hajiri na mwanae, lakini Mungu anaingilia kati na kumwambia Ibrahimu aisikilize sauti ya mkewe-Sarai yaani Hajiri afukuzwe. Kwa mf, ktk muktadha huu, UN wanadai kuwa, je, Mungu alifanya vyema hapa? Kama siyo upendeleo ni nini? Ndiyo maana leo UN, wamefanikiwa sana kulipigia debe hili suala la 50 kwa 50 na limeingia hadi ndani ya kanisa la Mungu. Na sasa wamepitiliza hadi ushoga wanaupigia kampeni na ushakubalika na unaungwa mkono hadi na viongozi wa dini!! Wapendwa, sina muda wa kuyasema yote, lakini Ibilisi anafanya mambo mengi sana ya kuwapumbaza wanawake na wanaume na kujiona kuwa wako sahihi ilahali wamepotoka kwelikweli. Ndani ya Serikali zetu leo, ukionekana una mtazamo hasi kwa wanawake kuwa viongozi, utaonekana MPUMBAVU kama siyo kuchukuliwa hatua za kisheria kabisa. Na hata jamii nzima itakushangaa sana. Hata baadhi ya Wakristo nao watakushakungaa sana. Na wanaonekana kulipinga hili, wanaonekana kuwa ni watu washamba sana na waliopitwa na wakati hapa duniani. Je, swali la kujiuliza, kipi kinalipa? Kuwa washamba wa Mungu ili tuwe wastaarabu kwa serikali za dunia? Au tuwe washamba wa dunia ili kuwa wastaarabu wa Yesu/Mungu(tufuate neno)? Ushauri wangu ni huu, inalipa sana kuwa mshamba wa Yesu!!
  Ni wakati wa wanawake kuisikiliza sauti ya Mungu tu na si UN. Mungu ana mfumo wake wa kifalme. Hakuna democrasia kwa Mungu. Majukumu ya Baba ni ya Baba tu, majukumu ya Mwana ni ya Mwana tu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kazi ya Roho Mtakatifu tu. Majukumu ya Gabriel, ni majukumu yake tu, maserafi na makerubi nao wana majukumu yao tofauti na wala hawaingiliani katika kazi zao. Je, sisi leo tumepata wapi ujasiri wa kuutangua mpango wa Mungu? Wapendwa, kwa vile Mungu ni mwenye rehema na upendo mwingi sana, ndiyo maana bado yu atuvumilia ili tutubu na kurudi kwenye mapito ya zamani. Mungu analalamika sana; Yeremia 18:15 Maana watu wangu wamenisahau, wameufukizia ubatili uvumba; nao wamewakaza katika njia zao, katika mapito ya zamani, ili wapite katika njia za kando, katika njia isiyotengenezwa.
  Na anazidi kuwasihi watu wake warudi, warejee kwa Mungu wao… Yeremia 6:16 Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
  Wale watakaoisikia sauti yake watapona lakini kwa wale watakaokaidi, kuna ole imewekwa kwao. Mungu atusadie sote.
  Wakatabahu!!

 34. Yusha/Siyi/Kombe

  Kuna tatizo gani Mwanamke kua Kiongozi wa Taasisi ya KIBINADAMU -Kidini/dhehebu eg Lutheran, Sabato, Assemblies, Pentecost, Menonite, Methodist, Baptist, Jesus Only, Full Gospel, Helicopter Ministry, Jumbo Jet fellowship nk? kisha nisaidieni kuna tatizo gani wakiwa Viongozi pia wa Taasisi ya Ki Mungu yaani Kanisa?

  Press on.

 35. Mungu ni mwema.Hongera MAMA NGU ASKOFU!MFUMO DUME SIYO UASI TU NIMEKOSA JINA ZURI!

 36. Mwanamke kuwa kiongozi tena wa ngazi ya juu hivyo, huo ni UASI. Mwanamke kuwa na authority ni uasi mbele za Mungu. Na hii ni ajli kubwa sana maana imekumba makanisa yetu yalo mengi. Mungu atusaidie sana

 37. Hapo analitangaza ao analiongoza kanisa?jambo ambalo halikuwezaka fanyika kwa wakati wa manabii ao mitume;njama za ibilisi hizo mpingeni huyu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s