Sababu ya Uchumba Kuvunjika!

mahusiano

Sababu/Matatizo 10 ya ”chumba” nyingi kuvunjika vunjika;

1. Kukosa uaminifu katika mahusiano ya uchumba.

mojawapo ya matatizo yanayosababisha chumba nyingi kuvunjika ni suala la kukosa uaminifu na hii hufungulia mlango wa shetani kuwashambulia na hatimaye uchumba kuvunjika na wakati mwingine utawakuta wachumba wakiwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengine na hii husababisha uchumba kuvunjika

2.Roho ya tamaa ya maisha makubwa nje ya uwezo wao.

hali ya kutamani maisha makubwa ambayo nje na uwezo husababisha uchumba kuvunjika na wakati mwingine akijitokeza mtu mwingine ambaye anaonyesha dalili fulani za kuwa na mali au pesa zaidi ya yule mchumba huchangia kuvunjika kwa uchumba hivyo ni vizuri kulidhika na mchumba wako na muanze pamoja na MUNGU atawabarikia mkiwa pamoja.

3.Kujihusisha na tendo la ndoa kabla ya ndoa.

Hili nadhani ni tatizo kubwa labda huenda kuliko haya mengine na hili ni sumu kubwa sana inayovunja chumba za watu wengi, kwanza huondoa imani kwa wale wachumba wenyewe, mtu anawaza huyu kakubali kufanya mapenzi na mimi ipo siku atanichoka na kufanya na mwingine pia kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa huweza kugundua baadhi ya madhaifu na mapungufu aliyonayo mmoja wa wachumba hao na kuamua ikiwa hiki ndicho nakitarajia wakati ndoa mbona nitakuwa nimejitwika tanzi? na hivyo huvunja uchumba na wakati mwingine kuwatangazia watu madhaifu ya mchumba wake.

4.Kuanza kusemasema na kutangaza mapema kabla ya wakati muafaka.

kutangaza juu ya uchumba wenu kabla ya hatua za awali kumesababisha baadhi ya chumba kuvunjika unakuta hatua za awali kabisa kanisa zima wanajua,kila mtaa wanajua yaani kila mtu anajua hii husababisha mmoja ya wachumba kuona kuwa huyu mwenzangu hana siri na hawezi kutunza mambo huenda hata tutakapooana hataweza kutunza siri hivyo anaweza kuvunja uchumba na wakati mwingine kusemasema kabla ya muda huwasababisha wale walio maadui zenu kuwazunguka kwa mbele na kupindua na ghafla unashangaa unakuta yule aliyekua rafiki yako wa karibu uliye kuwa unamshirikisha jambo hilo kakuzunguka na kukugeuzia kibao. Baada ya siku mbili tatu unaskia yuleyule mchumba wako anamvisha pete mchumba wako.

5.Kuwasikiliza watu wengine zaidi ya kumsikiliza MUNGU.

Hii inaweza kusababisha uchumba kuvunjika. ni vizuri kujifunza kumsikiliza MUNGU juu ya yule aliye kuongoza kwamba atafaa kuwa mwenzi wako wa ndoa badala ya kuwasikiliza watu wanasema nini juu ya wewe na mchumba wako. watu wanaweza kumtoa kasoro mfano mchumba mwenyewe hajasoma,ni mbaya,hana figa nzuri,mchafu,hamuendani, maskini na kasoro nyingi tu na hiyo husababisha uchumba kuvunjika

6.Kuchumbiana bila kumhusisha MUNGU.

Mlionana na kuvutiana pasipo kumhusisha MUNGU na kutangaza kwa watu na kuanza mipango ya kuoana ndipo mnakuja kugundua kumbe ilikuwa ni misisimko yenu tu wala MUNGU hakuhusika kabisa katika mchakato mzima wa uchumba wenu na matokeo yake uchumba wenu unavunjika na kuacha ukijiuliza maswali mengi.

7.kutumia muda mwingi katika uchumba kabla ya ndoa.

Kuna baadhi ya wachumba wanatumia muda mwingi sana kukaa katika mahusiano ya uchumba kwa malengo ya kusomana tabia au kuchunguzana au kusubiriana katika masomo nk. Hali hii hupelekea kuchokana katika mahusiano na kuwasababishia kuona kama huenda labda nilichagua mtu asiye sahihi. Baada ya kusoma na madhaifu mengi kwa muda mrefu mwisho uchumba huweza kuvunjika.
8.Roho ya haraka na kukosa uvumilivu.

Wengine wakichumbiana hupeleka mambo haraka haraka utadhani ni dharula, wengi huwa na hali ya kutokujiamini huenda kutokana na yaliyowapata siku za nyuma. labda walichumbiana na baada ya muda mfupi uchumba ukavunjika na kuacha majeraha makubwa hivyo hudhani hali hiyo itajirudia, katika kufanya mambo haraka huweza kusababisha hata huu uchumba kuvunjika.

9.Upinzani wa shetani ili ukose kilicho bora zaidi.

Kuvunjika kwa uchumba wakati mwingine kunaweza kusababishwa na ibilisi shetani ambaye ni mdau wa kwanza wa upinzani juu ya mafanikio ya wana wa MUNGU. Ndiyo maana tunahitaji sana kufunga na kuomba ili kuvunja na kuharibu kazi za shetani na mipango aanayotuwazia sisi katika maisha yetu.

10.Uchumba kuvunjika kwa sababu ya mapenzi ya MUNGU.

Sio kila kitu kinaweza kusababishwa na shetani, wakati mwingine MUNGU mwenyewe huingilia kati na kusababisha uchumba fulani kuvunjika kutokana na sababu za kimungu ambazo wakati mwingine kwetu sisi sio rahisi kuweza kuzijua kwa haraka mpaka wakati kamili wa MUNGU utimie au kusudi lake kujidhihirisha wazi. Ni vizuri kwetu sisi kama watu wa MUNGU kutafuta mapenzi ya MUNGU na kujua kwamba kuna wakati MUNGU mwanyewe anaweza kusababisha uchumba kuvunjika kwa ajili ya usalama wetu.

– kumbuka NDOA SAHIHI NI YA MKE MMOJA NA MME MMOJA {MWANZO 2:24}

– pia NI DHAMBI KWA WACHUMBA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA

– shetani ALIWADANGANYA ADAMU NA EVA KWA SABABU HAPENDI MAFANIKIO KWA WANA WA MUNGU na hata huwadanganya wachumba wengi ili watende dhambi kabla ya ndoa ili maisha yao ya ndoa yasiwe na baraka na pia ndoa hiyo haitakuwa na ulinzi wa MUNGU jambo ambalo ni hatari.
-MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kama hujampatia YESU KRISTO maisha yako unatakiwa ufanye hivyo leo maana pasipo yeye hakuna uzima wa milele (Yohana 14:6) na ukimshirikisha yeye hata kwenye uchumba wako yeye ni ngome imara na atakushindia yote.

-MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

Advertisements

16 thoughts on “Sababu ya Uchumba Kuvunjika!

 1. bwana yesu apewe sifa wapendwa mimi Nina swali kuhusiana n.a. mada hii
  mfano umependa mtu n.a. ukapata Amani ndani yako n.a. ukamshirikisha mungu akakujibu kuwa uliyempenda ni sahihi k wako lakini pale unapomwambia unamkuta yupo kwenye uchumba je mungu ni mwongo?
  2.lingine ni hili ‘unapomwomba mungu ni sahihi kumuomba rafiki (girl or boy friend)wa kuja kuishi naye kwenye ndoa au kumuomba mungu mke ndo sahihi?

 2. ni kweli ufunuo huu umegusa maisha ninayo pitia na hata sasa nimebaki bila mke,lakini hapa kati nimejifunza mambo makubwa kwa lugha nyingine nimepikwa hadi nimeiva.
  Kinacho nitia moyo namuona Mungu akiniandalia mke ,na ninaamini nikiwa naye nitasahau yaliyopita kwasababu itakuwa ni chaguo la Mungu.

 3. Mpendwa Sungura c kwamba tunatishana bt in reality hali ndiyo ipo hivyo!ckatai kuwa unahaki kabisa ya kuweka vigezo unavyotaka mfano mimi nilikuwa napenda wyf wangu awe mweupeee!acwe mfupi coz mimi ni mrefu wa cm185 then acwe mnene bt awe wa wastani so kwa vigezo hivyo nilijikuta nakutana na wengii wa type hiyo bt at the end of da day nakuta cwapendi kiviilee na kwakuwa nilikuwa cjaokoka nilijikuta natembea nao thn naona bado kwenye nafasi ya moyo wangu cjawashiba!nikawa najiuliza cfa nazotaka nazipata bt mbona coni hata mmoja anayekosha roho yangu?kama zali nikaja kumpata ninayempenda 100% bt c mrefu ila ana cm 156 mweupee na c mnene wala mwembamba!nikawa nampendaaa kuliko mwanamke yeyote niliyokuwa nimekutana naye ila hofu yangu ikawa je yeye ananipenda kama ninavyompenda?kama zali kweli nikaprove ananipenda the same way too!naita bahati coz nilikuwa cjaokoka thn kumbuka wale waliyotimiza vigezo nilivyovitaka na ni wengi bt ckuwapenda!huoni bahati nasibu hii ni wangapi wanaowezapata?Ujuwe mimi naprove.

  kabisa kupendana kunakuja Automaticaly na ukiuliza sababu za msingi huzipati unajikuta kila ukimcheki ktk hali ya kawaida huoni kasoro thtswhy utackia watu wakisema Luv is blind na wengine wakisema da beuty of some1 is on da eye of beholder!na mkipendana kwa dhati bwana hata mgombane vipi hamhitaji mchungaji au mtu yeyote atatue ugomvi wenu yaani utakuta mambo yanajisolve automaticaly yani kila mmoja kasahau na kusonga mbele!je ni ndoa ngapi za wapendwa ambazo ugomvi wake hauishi hata waende kwa Askofu kusuluhisha?Huoni kama nyingi wameingia kwa kutumia maujuzi yao thn wakalamba garasa?ni wangapi ambao walikuwa wakiwa wachumba thn waka Do kabla ya ndoa na kwa akili zao wakaona hapa saafi sasa tuoane bt now ni majuto?Let me tel U ma Brothr Sungura!No one knws who iz the true lost rib except God!Coz yeye ndiye anayejua ubavu wako halic anaotakiwa kukurudishia ili ufit!Bila God wapendwa wataangukia pua!Muombe Mungu kwa uaminifu na atakupatia unayefanana naye!Hapa no janja!

  Ujuwe kanisa linachangamoto nyingi sana!mfano ndani ya kanisa kuna waongo,wambea,wanyaji pombe wa siri!wazinzi/washerati wa siri,wachoyo n.k.. bt mbona ktk orodha hii cjawahi ona majina yakibandikwa?kama lengo ni kuponya watu bt cdhani kama ni sahihi kutumia njia hii!Mimi naona neno pekee kama dira yetu ndiyo tulifuate!Coz hilo pekee ndiyo liletalo uponyaji!Bt sambamba na hilo neno bt kunawengine wanazidiwa mbinu na ibilisi kiasi kwamba mioyo yao inakuwa migumu!Hivyo inahitaji Mungu awarehemu na Kuwaponya!Mbona ukisimama imara na kuijua kweli itakuweka huru kiasi kwamba unaona furaha na amani kutoa bila kulazimishwa?Yaani unajua wajibu wako kama mwamini!Mambo mengine jamani utadhani huu wokovu tumelazimishwa?Wanaomwabudu Devil wanatushinda kwa utoaji!Hata hawambishii Devil wao!Akisema mtoe mama au mtoto wanatoa tena kwa furaha!Bt cc tuliookoka tunasumbuana wee mpaka majina yanabandikwa ubaoni!Mmmmh Kweli Mungu atusaidie!Mungu awabariki wote

 4. Tumaini;
  Umenishtua kidogo, kwamba unampenda mtu kwa dhati, yeye hajakupenda kwa dhati lakini ati anakubali kuolewa nawe ili atimize ndoto yake ya kuolewa!
  Ivi huyo binti anayefanya hivyo yuko timamu kabisa kiroho na kiakili?

  Tumaini Mungu anajua maana ya ‘beauty’ kuliko mimi na wewe.
  Kuweka vigezo vya mtu unayetaka siyo kosa kibiblia, ispokuwa uhalisia wake utategemeana na mtazamo (attitude) wako ndani. Yakobo anasema hampati kwa sababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa tamaa zenu wenyewe. Unataka mke/mume wa namna fulani ili iweje,uwarigishie washikaji zako au ili ujigamba unapotembea naye barabarani au ili watu wakufagilie kuwa una kifaa hatari?
  (ATTITUDE)

  Mungu hajisikii vibaya wewe ukisema nataka mwanamke mrefu, mwembamba, mfupi, mnene, mweupe/mweusi, mzungu/mhindi/mwafrika, n.k. Maana unataka kitu ambacho kitaufurahisha moyo wako, na Mungu anataka ufurahi. Cha msingi tu uwe na right attitude.

  Kasema ukiomba mkate hawezi kukupa jiwe,Mungu huwa hatuchagulii vitu, bali yeye yupo kwa ajili ya kutushauri na kutusaidia kujua hivyo vitu sahihi tunavyotaka viko wapi.

  Zaburi inasema hutupa sawasawa na desires za mioyo yetu. Biblia ya Kiswahili imesema mashauri ya mioyo yetu. Lakini desire si mashauri bali ni shauku au hamu ya kitu fulani.

  Hatuoni mifano ya watu kwenye biblia ambao waliwahi kufunga au kuomba ili Mungu awape wenzi (ukiacha story ya Rebeca ambayo tumeifafanua), bali tunachokiona ni watu kuweka vigezo fulani kama vile, awe wa jamaa yetu, awe mtu unayemfahamu vizuri na ameshuhudiwa wema, n.k. Lakini tunamwona pia Yakobo ambaye hakumpenda Leah kwa sababu ya kigezo fulani (macho yake). Ina maana Yakobo alipenda mwanamke mwenye macho maangavu, yasiyo kusinzia kama ya Leah.

  Suala la ndoa linaonekana kuwa lenye kutisha kwa sababu watu wanaingia bila kujua nini wanakitaka hasa (wengi wanakuwa na fantasy), kutishana juu ya ndoa kumekuwa ni kwingi zaidi kuliko kutiana moyo kuwa inawezekana kupatia, hofu ya kukosea ni kubwa ambayo imekuzwa na kigezo kwamba ukishaingia umeingia.

  Lakini pia watu hawafundishwi kanuni za kweli za jinsi ya kupata mke/mume- hasa kibiblia. Wengi wameambiwa tu kwamba ukitaka kuoa umtegemee au umwombe Mungu. Kwa namna gani? – hiyo hawajafundishwa.

  Kwa mfano umetaka sasa kupata mchumba ni kwa namna gani sasa unamtegemea au kumwomba Mungu?
  – Je unaomba kisha unakaa tu hutafuti
  -Je unasubiri Mungu akuambie kuwa mke/mume wako ni fulani?
  -Je unaomba halafu unafumba macho yako usitazame?
  Au inakuwaje?
  Unaona sasa suala la kusema tumtegemee Mungu lilivyoachwa kuwa tata?
  Kwani ukiwa unamwomba Mungu ili upate kazi huwa unaomba bila kutuma maombi ya kazi, au bila kuondoka kwenda kutafuta kazi? Je ndio maana yake kumtegemea Mungu huko?

  Ivi kweli inawezekana ukafika umri wa kuoa na huku hujui chochote kuhusu beauty ya mwanamke, ukawa huvutiwe na kitu chochote kwa mwanamke, kwamba kwako ni sawa tu yeyote almradi ni mwanamke, kwamba ukirefusha nywele au akinyoa kwako ni sawa tu, awe mtanashati au mwenye kujiachia ni sawa tu?

  Mimi najua maana ya kumtegemea Mungu katika suala la kuoa ni kumwomba aongoze hatua zako.

  Kama kunawatu wanaingia kwenye ndoa wakiwa hivi ndiyo maana matatizo ni mengi kwenye ndoa.

  Itaendelea..

 5. Nimekufuatilia vizuri mpendwa Sungura ila nataka nichangie kidogo!Mimi nadhani swala la Kupenda au kuchagua mchumba kwakutumia njia ya kimwili ni gumu sana!coz unaweza weka vigezo vyote unavyotaka kwa mchumba unayedhani anafaa kuwa wyf na ukampenda kwa dhati bt shida inakuja kwa huyo unayempenda unakuta yeye anakupenda kiasi!Na ktk swala zima la ndoa ili iweze kudumu lazima umpate unayempenda kwa dhati naye pia akupende kwa dhati!waweza sema binti huyu kwakweli nampenda na anasifa zote za kuwa wyf bt yeye akawa hakupendi kiviile!bt kwakuwa anataka kutimiza ndoto ya kuolewa anakubali ictoshe wenda type ya m.ume anayemhitaji hajawahi kutokea na umri unasonga!c anaona ni bora aolewe?unadhani ndoa hii hata ikifungwa c itakuwa balaa!thswhy binafsi naamini bila Mungu haiwezekani labda iwe bahati nzuri!Mungu utakapo mweleza nahitaji yule ninayefanana naye atakupatia kwa 100%.

  coz isue ya wfy c mchezo kama utaweka michanganyo!thswhy unakuta ndoa nyingi hata za wapendwa ni za uigizaji coz hawakuwa na msingi wa hawakuwa na msingi wa kiMungu!swala na uchumba linatakiwa wote mpendani 100% na tena Automatical tena icwe sababu za kimwonekano mfano,sura,shape,rangi,mwendo wengine sauti n.k ktk haya je akijapata matatizo itakuwaje may B ajali au kwa wakinamama akizaa huwa Maumbile yanabadilika!Huoni ni balaa tupu.Nani anayeweza fanya wote mpendane Automaticaly kama c Mungu?Wapendwa inatakiwe tumtegeme God 100% coz he knows wht we desire & deserve!Ujuwe haya mambo mtu ukijichanganya ni balaa!Kuna ndoa za wapendwa wengine ni majuto unakuta kila mtu anakabarafu kake ka moyo pembeni kanakomfanya ajione bora!unadhani kwa staili hii c balaa!je kuna Mbingu kweli?wapendwa hapo hakuna janja ni kumtumainia Mungu pekee!MUNGU AWABARIKI WOTE..

 6. Mabula hata mimi nakuunga mkono mtumishi.

  Kuna jambo moja tu ambalo limebeba sababu namba 5 na 6. Nalo ni kumsikiliza/kumshirikisha/kumhusisha Mungu.

  Huu ni msamiati mwepesi kweli kuusema kwa vinywa vyetu, utasikia watu wanasema ‘muulize Mungu au msikilize Mungu- Roho mtakatifu.
  Lakini ukilileta kwenye uhalisia utakuta watu wengi hata hawajui wanamshirikisha vipi Mungu. Kuna waty wengi walidhani aliyekuwa anawaambia ni Mungu, lakini baadae wanakuja kugundua si yeye.

  Suala la kuoa liko 100% kiroho na 100% kimwili.
  Kwa nini hil neno ‘msikilize Bwana lipo sana kwenye suala la kuoa/kuolewa/
  Ni kwa sababu kanuni ya kiroho inayoliongoza inamwanya mdogo sana kwa mtu kupata nafasi ya pili (second chance) baada ya kukosea. Ambayo kwanza ni kifo, lakini pia ni suala zima la uasherati/uzinzi.

  Kwa hiyo kuna hofu kubwa ya watu kukosea maana mlango wa kutoka ni mfinyu sana kwa mujibu wa kanuni ya ndoa kiroho/kibiblia.

  Lakini ukweli ni kwamba mwenye kupanga aina ya mwenzi anayetaka kitabia, kimuonekano, kijiografia (anakotoka), kielimu, n.k ni muoaji au muolewa, wala si Mungu. Mungu hata siku moja hatulazimishi kuoa au kuolewa na watu ambao tusingependa kuwa nao.

  Yakobo hakuambiwa na Mungu amuoe Raheli, ila ni yeye alimpenda Rahel kwa jinsi alivyokuwa, ki muonekano na tabia.

  Hakuna dhambi yoyote kumpenda mtu, kisha ukamwomba Mungu juu ya huyo mtu. Kumbuka kupenda si tendo la hiari, inaweza ikatokea tu ukamwona mtu ukampenda ( u fall for her). Ikisha kuwa hivyo wala usimwombe Mungu kwa kumwambia akuoneshe mtu, bali mwambie kuwa moyo wako umempenda fulani, akuhakikishie tu kama huyo mtu mtatimiza hatima ya ki -Mungu pamoja nae.

  Kama Isaka angeenda mwenyewe pale kisimani,asingehitaji kuweka ishara ambayo mtumishi wa Ibrahim aliiweka ili kujua kama Rebeca ndiye. Isaka angemwona tu Rebeca angejua kuwa ndiye maana yeye ndiye haswa alikuwa anajua aina ya mke anayetaka. Yule mtumishi aliweka ishara bila shaka kwa sababu hakuwa anajua aina ya mke ambye Isaka angetaka.

  Mara nyingi tunaambizana tumuulize au tumshirikisha Mungu, na watu wengi wanaposikia hii misamiati huamini kuwa maana yake ni kwenda kuomba tu. Lakini si kweli. Kumshirikisha Mungu ni nini?

  Kwanza tunatakiwa kama waamini kujua kanuni za ki- Mungu juu ya ndoa. Hii ni hatua ya kwanza ya kumhusisha Mungu.

  Pili sisi wenyewe kujua tunachotaka ndani ya hizo kanuni za Mungu. kwamba je, tunachotaka kiko ndani ya hizo kanuni? Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, jawabu la ulimi hutoka kwa Mungu. Tusitaka Mungu atuandalie na atutolee majibu, si yeye anayeoa/olewa bali ni sisi.

  Pia ni muhimu kuwafahamu tunaochumbiana nao kabla ya kuamua kuwa wachumba( Isaka alioa kwa ndugu zake). Tusianze kwanza uchumba ndo tuanze kufahamiana.

  Watu wengi ambao walikimbilia kwenye maombi kumwomba Mungu awape wenzi, walijikuta wanajuta baadae, kwa kuwa waligundua kuwa hao wenzi wala hawakutoka kwa Mungu kama walivyodhani. Huku ni kule kupata mke kwa kutegemea ufunuo wa Mungu.

  Kuujua ufunuo wa Mungu si jambo jepesi ki hivyo, linahitaji kumjifunza Mungu na kupata uzoefu. Si kutaka tu ufunuo wakati unataka mke/mume.

  Ni muhimu pia kusimamia machaguo yetu, si leo wa hivi, kesho ukiona wa vile unabadilisha chaguo tena.

  Nitaendelea……

 7. Mungu atusaidie vijana swala la uchumba linahitaji nguvu ya MUNGU, mana kuumizwa kujeruhiwa ndo kama maigizo Mungu aonekane mke/mme mwema atoka kwa Bwana.bla Mungu mapenzi ya dhati hayapo kabsa.

 8. Mada ni nzuri sana. kama kuna jambo lenye changamoto ktk maisha ni hili hasa kwa wapendwa. sijui nini kimetuloga wapendwa tunafuata sana matakwa yetu na matakwa ya watu badala ya kumthibitisha Mungu kwanza. tusome mwanzo 24 tuone yule mtumishi aliyetumwa na ibrahim akamtafutie isaka mke alivoweka mkakati na Mungu akamthibitishia.Baadhi ya vijana wengi tunaanza kumuomba Mungu tukiwa tayari tumeshajiwekea vigezo vyetu vingi tena vya kimwili wal si kiroho ikitokea Mungu akakuelekeza tofauti na vigezo vyako basi tunaona huyo sio Mungu. mfano unakutana na kijana kwa mara ya kwanza akiwa anataka kukuomba uchumba lakini maswali anayokuuliza mpaka unachoka. Mungu atusaidie tukumbuke ni wapi tulipoanguka

 9. nimezikubali hoja hizi,, ubarikiwe sana , na endelea kuchambua kuna sababu nyingine kibao za uchmba kuvunjika, sababu nyingine NI KUWA NA MCHUMBA ZAIDI YA MMOJA-HAPA LAZIMA MMOJA AACHWE TU.

 10. Relationshp World is so comfusing in either way, but let pursue trustng in God…!
  Mengi uliyozungumza ni amin na kwel

 11. Hoja nzuriiiiii!!
  Nyingine ni kudanganyana eti mmoja kaoneshwa na Mungu kumbe ni tamaa za mtu tu. Vijana wengi wamekuwa wakiwakama mabinti na wavulana hivhivi kumbe sivyo…. Mungu atusaidie sana. Ubarikiwe Peter

 12. Mtumishi wa Mungu Mabula nimekupata vizuri sana ila na mimi nichangie kidogo!Kuna baadhi ya vipengele ambavyo umesema mfano wachumba kuwa na tamaa,kuanza mapenzi kabla ya ndoa,kutangaza uchumba kabla mambo haya!Mimi siamini kama Wapendwa waliyosimama vizuri kiroho na ambao wanamahusiano mazuri na Mungu kama mambo haya yanawahusu!Coz unawezaje fanya hayo wakati bible inasema mke mwema hutoka kwa Bwana!Na ni lazima Apatikane kwa kumtel God mwenyewe coz God knws who is ur true lostrib!sasa iwezekane vp umwombe God then akupe Garasa?

  Mimi nadhani baadhi ya hivi vipengele vinawahusu hawa wapendwa vuguvugu!Mimi namkubali sana Sir God coz C Muongo wala mbabaishaji!Neno lake ni kweli na amini!Shida yetu cc wapendwa tunaleta usanii thtswhy kuna mambo kama hayo yanatokea!Maana hayo mambo ni ya watu wa Ulimwengu!Haiwekani umwombe God then akupe usichofanana nacho kianze usumbufu mara nionjeshe!Mara Ooh iwe siri!mara watu wanasema huna mvuto!haya c ya Ulimwengu!Ngoja niishie hapa kwanza.

 13. ndugu yangu umejitahidi sn kwa kutoa mawaiza hii ni sahii kabisa mpaka sasa hv mimi cina mpango wa kuoa maana yalinikuta

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s