Jinsi ya Kuifahamu Miujiza ya Mungu!!

miujiza
Ili kuifahamu na kuipambanua miujiza ya mashetani.itakuwa vema kujifunza alama zitakazotuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu.Tukiweza kufahamu namna ya kupambanua miujiza ya Mungu,itakuwa ni rahisi kufahamu kinyume chake,na kuifahamu miujiza ya mashetani.

ZIKO ALAMA KUMI (10) za kutuwezesha kuifahamu miujiza ya Mungu
.
Alama zote hizi,lazima zionekane katika huduma yoyote inayotumiwa na Mungu kufanya miujiza.Tukiziona alama zote hizi kumi katika huduma yoyote ya miujiza,tujue huduma hiyo niya Mungu,na hatupaswi kusema mtu huyo wa Mungu anatumia roho chafu au anatoa pepo kwa Beelzebuli,mkuu wa pepo.Alama hizi kumi ni hizi zifuatazo:-

1. .Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima mwenyewe awe ameamini na kuokolewa; akikiri mwenyewe wokovu ulio katika Kristo Yesu, na kuushuhudia ishara au miujiza ya Mungu, hufuatana nao WAAMINIO tu, au waliookolewa (MARKO 16:17).Mtu yeyote ambaye hajaokoka, hawezi kufanya miujiza inayotokana na Mungu.Miujiza anayoifanya mtu yeyote ambaye hajaokoka, ni miujiza ya shetani.

2. .Huduma yoyote ya miujiza ya Mungu, lazima iambatane na Biblia au Neno la Mungu, kwa kuwa Neno la Mungu ndiyo dawa ya ugonjwa na tena ndilo linalofanya miujiza(ZABURI 107:20; MITHALI 4:20-22; YOHANA 6:63). Mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, ataiamini Biblia na kuifanya kuwa msingi wa utendaji wake wote. Huduma yoyote ya miujiza isiyoambatana Biblia, inatokana na Shetani.

3. Huduma yoyote ya miujiza inayotokana na Mungu, LAZIMA iambatane na KUHUBIRI NA KUFUNDISHA Neno la Mungu. Mtu yeyote anayedai kwamba yeye hakupewa kuhubiri Neno, ila amepewa karama ya kutenda miujiza tu, huyo anatumiwa na Shetani (LUKA 4:18; 5:17; 9; 8:1-2; MATHAYO 10:7-8). Huduma yoyote ya miujiza ya Mungu, lazima iambatane kuhubiri kwamba watu watubu dhambi zao na kuziacha, na kuokolewa. Kinyume cha hapo, ni huduma ya Shetani (MARKO 4:6;12-13).

4. Miujiza yoyote ya Mungu, LAZIMA ifanyike kwa jina la YESU (LUKA 10:17; MATENDO 4:30; MARKO 16:17; MATENDO 3:6; 4:10; 3;13, 16, 16:18).

5. Miujiza yoyote ya Mungu, hutumika kuwaleta watu kwa Bwana Yesu na kuwafanya wawe wanafunzi wa Yesu, na kuwafundisha kudumu katika kanisa linalohubiri wokovu (MATENDO 5:12, 14; 2:41-43; 6:7-8; 8:5-8,12). Miujiza isiyo na lengo hili ni miujiza ya Shetani.

6. Mtu yeyote anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, lazima afanye huduma yake kwa kushirikiana na makanisa yanayohubiri wokovu, ili apate kutoa ripoti ya huduma yake inavyokwenda na kuwajibika (MATENDO 14:27; 21:17-19; 1WAKORINTHO 14:29).

7. Miujiza ya Mungu, hutusogeza katika kumtumikia Yesu Kristo na kushika maagizo yake, na kutufanya kuwa watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Miujiza yoyote inayoambatana na maagizo yoyote yaliyo kinyume na Neno la Mungu, kama kutumia sanamu za watakatifu, kufukiza uvumba, kutumia rozari au maji ya Baraka, kuzuru makaburi, kuwaomba wafu tuwaombee n.k; haitokani na Mungu (KUMBUKUMBU 13:1-4).Mafundisho ya mtu anayetumiwa kufanya miujiza ya Mungu, hutufundisha kuwa watakatifu, na kuwa mbali na mapenzi ya Mataifa. Wote waliotumiwa sana na Mungu kufanya miujiza kama Paulo, Petro, Yakobo na Yohana, walifundisha hivyo (WARUMI 12:1-2; 1YOHANA 2:15-17; 1 PETRO 1:14-16; 2:12; 4:2-3; YAKOBO 4:4; 1 WAKORINTHO 4:3-4).

8. Miujiza ya Mungu hutolewa bure, hainunuliwi (MATHAYO 10:8; 2 WAFALME 5:14-16; DANIELI 5:16-17; 1 WAFALME 13:6-8; MATENDO 8:18-20). Namna yoyote ya kuomba hela ili kununua muujiza ni kinyume na mpango wa Mungu .Hata kama tutaona wakiuza vitambaa,leso na sabuni zilizoombewa ili zitusaidie, hatuna budi kujua mapanzi ya Mungu kwa watumishi wake ni kutoa huduma ya maombezi bure. Huduma yoyote inayochangisha mchango au kiingilio kwa ajili ya semina ya Neno la Mungu hiyo siyo huduma ya kimungu, ni huduma ya Shetani. Mungu anataka injili iwafikie watu wote.Mfano 1 wa huduma ya shetani ni huduma ya babu wa Loliondo. Bila kutoa sh: 500 usingeweza kupata msaada.Pia miujiza ya Mungu inatokana na Neno la Mungu kama tulivyoona hapo juu. Miujiza ya Mungu inakuwa na lengo la kuwaleta watu kwa Yesu.Watu wanaokuja kutafuta msaada kwa Yesu sharti waongozwe kutubu dhambi zao
kwanza ili kuwapatanisha na Mungu kwa ajili ya kufungua mlango wa Miujiza yao.

9. Miujiza ya Mungu humtukuza mwana wa MUNGU yaani YESU KRISTO (YOHANA 11:4), wale wanaotumiwa na Mungu kufanya miujiza ya Mungu hubaki wanadamu na wao kukiri hivyo, na kumpa Mungu utukufu(MATENDO 14:8-18). Tunapomuona mtu akichukua utukufu kana kwa mba yeye ndiye anayetenda miujiza ndipo tunatambua kuwa huyo si mtumishi wa Mungu.

10. Maisha ya mtu anayetumiwa na Mungu kufanya miujiza yanapaswa kuwa sawasawa na Neno la Mungu. Watu wanaotumiwa na Shetani kufanya miujiza, huambatana na dhambi NNE zinazoonekana upesi-uzinzi au uasherati (1 WAKORINTHO 6:15-17), maneno ya kihuni (YAKOBO 3:10-12), maisha yaliyo sawa na mataifa katika kuvaa na kutenda (WARUMI 12:2; 1 PETRO 2:12; YAKOBO 4:4), maisha yasiyo na uaminifu katika masuala ya fedha na kusema uongo (NEHEMIA 7:2)

MUNGU akubariki sana

Ni mimi ndugu yako PETER MICHAEL MABULA

Advertisements

21 thoughts on “Jinsi ya Kuifahamu Miujiza ya Mungu!!

 1. Thank you Seleli…pls nitafutie nyumba nihame.

  ni mama mwenye nyumba wangu.mimi nimefundishwa kuheshimu wakubwa na wadogo.sheria za nyumba nazifuata pamoja na familia yangu.tuko wanne yani mume wangu,dada wa mtoto, na mtoto mdogo.
  mume wake hana shida kabisa…wanasali kanisa naliheshimu coz nilishawahi kufanya maombi pale zamani na wameokoka.naomba unisaidie maana nimefika mwisho. mpaka mumewe anamwambia mpaka tunasikia kuwa apunguze hasira coz ni mzizi wa dhambi na asipende kutusema bila sababu.anamuonea sana msichana wetu tusipokuwepo na ni mpole mno watu wengi wanamsifu. siku nyingine najificha ajue sipo namsikia anamsema bila sababu..nanyamaza maana pale sio kwangu.Juzi kanifukuzia watu wa jumuiya wasije kwangu.nikamuangalia nikamuacha.

  sio huyu tu nishakutana na wengi.nikiwambia watu wanasema kwani we huwajui walokole wanafanya ndivyo sivyo

  sorry kama niko nje ya mada
  bye

 2. Best,

  Pole kwa yote hata kushindwa kuwaelewa waliookoka, nami nilikua kama wewe na nadhani zaidi yako, sikuwahi kuwaelewa hawa watu wanaosema wameokoka wakati nikiwa ktk au na dini yangu ya RC na nikiwa ktk stage kubwa ya utumishi altareni na nikiwa nimefuzu mafunzo yote yanayompasa Mu-RC wa kweli na kubakiza sacraments 2 Za labda niwe Padri au nioe tu na kuishi kama waumini wengine ktk RC yetu. Lakini kuna kitu kilitokea, NIKAAMUA KUOKOKA. Tokea hapo, nilijua kweli nilikua na dini na imani lakini nilikua nimekufu ndani, ni mkavu, nimejaa taratibu na mazoea ya kufanya ibada na taratibu za madhehebu lakini ndani ya moyo, hamna kitu, hewa tu na kukariri wazungu walikufa zamani kua ndio watakatifu tu na Africa hamna wacha Mungu.

  Sasa, nikulize ivi, JE UNAJUA NA UNAAMINI KUA BIBLIA INA MANENO YA MUNGU NA KWAMBA ALIYOSEMA HUMO MUNGU NDIO MAMLAKA YA MWISHO KWA MAISHA YAKO? Kama sivyo, je kwako MUONGOZO WA MAISHA YAKO NI UPI? na kama ni ndio, nitafurahi kujibu/kuchangia maoni kwa baadhi ya statements zako izi chini:

  …..Watu mnaojiita eti mmeokoka mimi huwa siwaelewi

  …….Idadi yenu inaongezeka na kujifanya eti mnalijua neno la Mungu

  …….Shetani nae anashindwa kuelewa.

  …….Acheni kuhukumu

  …….Hakuna hata mmoja aliye mtakatifu (Mhubili 7:20) tunangojea neema ya Mungu anayejua kusoma mioyo ya watu

  ………Hakimu wa haki.

  ……TUMECHOKA NA KASHFA ZENU!

  ……..MAOVU YAMEJAA AFRICA

  Karibu, uwe huru tu na kwa furaha kabisa, nijibu swali langu pale juu kuhusu Biblia kwako ni nini ndipo tuendelee. Usiseme kua hutaki zaidi!!!!!!!! sasa hapo tena ndugu yangu, itakua si sawa maana umeingia/umeleta mawazo yako ktk mada basi kila mtu-wewe na wengine tuna uhuru wa kushiriki na kutoa maoni.

  Karibu, nakusubiri kwa jibu lako, ili tuendelee kujifunza pamoja

  Press on.

 3. Anony,

  Excuse me, can I request you to come little clear and precisely! You might have the facts to be discussed, I will be glad to talk about them, however, first kindly see my opinions down here on what you said and you may wish to comment any, be free!

  Pole sana kwa kua na bahati mbaya ya kukaa na aina iyo ya Walokole(Waliookoka) uliyokaa nao kwamba wana wivu,hasira,chuki,wasusaji, wanafiki, wasengenyaji

  By the fact kwamba unaona tabia izo si za waliookoka, then unajua tabia safi za Watu wa Mungu. Nataka nikuhakikishie, wenye tabia njema wapo tena wengi sana, one day utakaa nao na mimi nakukaribisha ukae nami, utahakikisha kua tuna tabia njema sana, am serious, karibu tukae pamoja, na kama huna nyumba uko ukaapo, utakapotaka kupanga tena,nikutafutie huku kwetu ili uwe jirani yangu kabisa pua na mdomo

  Nonetheless, yafutayo ni muhimu kuelewa la sivyo unawezakuta unazidisha chumvi au kulaumu/critisize vitu ambavyo kumbe kama unauelewa navyo, utajua ni vya kawaida kabisa.

  Hasira= kila mwanadamu, ameokoka au la, hana hasira, In fact hata Mungu ana hasira kali tena ghadhabu nzito. Ivyo aliyeokoka kua na hasira, si issue bali baada ya kupata hasira, anafanya nini, ndio hapo hoja. Biblia yenyewe imesema tuwe na hasira au kwa maneno mengine, ni kwamba, hata tukiwa na hasira, tuchunge tusitende dhambi eg kupiga, tukuna, ua, vuruga mambo, unda kisasi,chongea, haribu nk.

  Wivu= Kila Mwanadamu ameokoka au la, ana wivu na as a matter of fact, Mungu naye amejisema ana wivu, so aliyeooka kua na wivu, si issue bali ni wivu wa aina gani na unampelekea kufanya nini, kubehave vipi, hapo ndio tunaweza ongea kua ‘mlokole’ yule mapepe!

  Chuki= Fafanua hapa maana mimi nimeooka na nachukia sana mazingira na hali za watu kunichafua,sababishia kutenda dhambi, maudhi, kutaka na kunilazimisha nishiriki mambo yao mabovu na kwa ivyo wananiona sina upendo na ushirikiano nao. Yesu alisema mwenyewe kua hakuja kuleta amani bali upanga kati ya ndugu, Baba, Mama, Kaka nk. Sasa kama ni ivyo, sina haja ya kujipendekeza au kucheka cheka nao, nitachukia yote mabaya na hali zote mbovu za kunivurugia maisha yangu ya uchaji wa Mungu na nitakua sawa kabisa KiBiblia, Siamini Mtu wa Mungu safi na amejazwa Roho Mtakatifu, from no where, atakua na chuki tu dhidi ya mambo au Watu. Ingawa tunatakiwa kuwapenda na kuwaombea adui lakini haimanishi nifurahie mambo yao na kushiriki! nitajitenga bila kusita na hata kuwaambia live kua sitaki hili au kile na I don’t care watanielewa au la, kwangu cha kwanza nimpendeze Mungu hata kama ikibidi familia, ukoo, marafiki, staff wenzangu wanichukue, I will not care at all maana wakati mwingine tunakua accused unnecessarily kua tuna chuki kumbe ni perceptions tu za Watu against sisi kutoshiriki au furahia mambi zao mbovu kabisa. Lakini kua ALIYEOKOKA KABISA KUCHUKIA TU kama vile ile chuki chungu ya kidini-islamu/Wakristo au kikabilia-Tusi/Hutu, chuki hiyo au ya aina izo, siamini kama mtu wa Mungu anayo….plz fafanua chuki gani unayosema, ni ipi na ya aina gani iyo anayokuwa nayo Mtu aliyeookoka?

  Wasusaji= Mtu ana uhuru wa kukubali au kukataa kitu, ameokoka au la. Ana uchaguzi wa kushiriki jambo au la. Hata kama wewe ungemtaka sana au unategemea angekuwepo ktk jambo fulani, shughuli za kifamilia au kiofisi, bado si lazima wala sheria ashiriki. Unless ufafanue Ususiaji huu ni upi na uko ktk shape gani, otherwise, kususia kitu au jambo, ni right ya Mtu yoyote kama anapenda au hajafurahishwa na jambo. Mfano, mimi kama umenifanyia jambo baya siku moja kisha ukanifuata nikusaidie tena kwa lile au nishiriki jambo lako, sitakubali, nitalisusa tu na wala si dhambi maana si lazima na hata ivyo ushuhuda wako kwa yale yaliyotokea huku nyuma,yamenikatia hamu

  Wanafiki/Wasengenyaji= hii ni kupretend mambo na kuwasema watu wengine kwa nia mbaya. Haya hayakubaliki kwa yoyote awe ameokoka au la. Ila natahadharisha kua, jinsi wasiookoka wanavyo-behave na kuwadhania waliokoka, inalazimika waliookoka kuonekana wana-pretend au sengenya kwa baadhi ya vitu na mambo. Kwa mfano, kama najua fulani ni mshari na mgomvi, ana tabia chafu kazini, mwizi, anafoji, ni jirani tatizo kubwa, nikimwambia mwingine kwa nia kua awe na tahadhari na huyo mtu asiyeokoka,ni usengenyaji? Na pia kwa sababu ya ushari wake, akitokea nikajificha hisia zangu za kutomfurahia na matabia yake na kujitahidi kuonekana niko normal naye ili kuepusha ushari wake, je mie mnafiki? Kama unafiki ni huo basi kuna positive unafiki na tutaufanya tu ili kuepuka mabaya mengi ya watu wabaya wanaotuwinda au kututafutia visa visa.

  Kama ktk maoni yangu kwa hoja zako sijatenda haki au sijakuelewa, ndio mana ya hii forum, uko huru, so karibu ue-establish your position and hoja.

  Press on.

 4. Peter Mabula,

  Excellent message indeed, nimebarikiwa sana, sana kabisa, ni tamu sana hii mana brother, glory to God.Point zote powerful, napenda kuchochea upako kwa points numbers zifuatazo:

  2= NI NENO la MUNGU kwanza( si la binadamu na janja/blaah-blaah zake au akili tupu bila uhuwishaji wa KiiUng, ufundi/uzoefu), ilo linaanza/semwa/tamkwa kisha linaaminiwa halafu toka kwalo, yanazaliwa mengi mojawapo ni muujiza. Delete Neno la Mungu, no miracle toka kwa Mungu labda toka sehemu na kiumbe kingine!

  3= In fact Yesu alikataa kufanya miujiza kwa kua watu walikalia tu kutaka miujiza-ujiza ivi(ishara) badala ya kutilia maanani kusikia na kutii kwanza kile kinachoweza sababisha muujiza yaani Neno- Mathayo.12:38-40 na 16:1-4

  4= Ndio kabisa, miujiza ya Mungu LAZIMA YESU aaminiwe kwanza, si nabii, mtume au kiongozi yoyote wa dini/imani iwe past, present and future na kama Yesu aaminiwi, mbingu haina sababu wala nia ya kutenda makuu! kamwe hayatafanyika ingawa uwezo wa kuyafanya uko wa kutisha sana-Mathayo.13:53-58

  5=Sawa kabisa maana hatuna agenda nyingine eg show off, kujiinua, kutambiana, kukomeshana, kushindana, kuvutia watu kwetu bali ni kuteka kila roho kwa msaada ya Roho wa Mungu na kuzitambulisha kwa Bwana, full stop and period! nothing more, nothing less! Aiiiiiiiimeeeen.

  6= Excellent on this tena maana hatujengi Kingdoms zetu wenyewe wala makanisa yetu wenyewe bali ni Ufalme wa Mungu na Kanisa ni moja tu la Yesu ivyo viungo ktk mwili mmoja kama ni sikio, jicho, mguu, mkono, kichwa, shingo, hakuna kutambiana, letu ni moja tu so kushirikiana ni lazima sio ombi au mjadala! hata ivyo kwa mfano sikio litamkataaje kichwa wakati wako kwa mwili mmoja?-1Wakorinto.12:12-27

  8= Sawa kabisa, nakwambia hata kama anayeuza hayo maji ya baraka/upako, vitambaa, sabuni, funguo nk ni mtu mkubwa sana ktk Utumishi huu unaosemekana ni wa Mungu, kwa kituko hiki tu pekee, sihitaji kufunga na kuomba ati nifunuliwe kama kuna shoti hapo au la. Hata kama kweli ktk huduma yake watu wanaokoka na nguvu za Mungu wakati mwingine ni ajabu tu, zinapita lakini ikumbukwe kua kunapokuwepo kuaminiwa kwa Mungu na agenda/kusudi la Mungu, Mungu anaweza tumia chochote na yeyote ili iwe faida kwa watu wake na utukufu kwake mfano mawe-Luka.19:40 au mnyama punda-Hesabu.22:23-31, mbweha-Waamuzi.15:4-5, Taya la punda kuua askari wengi mno-Waamuzi.15:15-17.

  9= Ndio kabisa, wakishatumiwa na Mungu, wale waliandika kuwahusu hao waliotumiwa au wao wenyewe waliotumiwa, WOTE wanafanya bidii ya dhati tena ya bila kumung’unya maneno na matendo hadharani, kukiri waziwazi kua wao ni watu tu na kua hawakutenda hayo basically kwa nguvu zao na kisha sifa na heshima zinaelekezwa kwa Mungu tu-Mdo.3:11-16, Mdo.10:24-27, Yakobo.5:17

  Press on.

 5. ila mimi nina bahati mbaya sijui!walokole wengi niliokaa nao wana wivu,hasira,chuki,kupenda kususa, wanafiki wanajitia wema ila ukiwasikiliza wakiwa hawakuoni wanakuwa wanasema watu vibaya..it is so disappointing.

  tatizo jingine ni mlipuko wa wachungaji/manabii na makanisa yao. wao pia wanasema walokole…Yesu nipe macho ya rohoni. otherwise kutangatanga makanisa kutakuwa ndio mtaji wangu

  hey its only God who can jugde. sijamuhukumu mtu nimetoa tu mfano wa watu ninaowafahamu.

 6. Mpendwa Sungura umenena vyema!Best unahitaji msaada wa kiroho ili uweze kutambua yanayozungumza!Naamini Mungu anamakusudi kabisa ya kukuokoa!Hongera kwakujitokeza na kueleza namna ambavyo inaonyesha wazi kabisa unahitaji kuponywa kiroho.Mungu akubariki.

 7. Huo ndio ukweli wenyewe Majo, wala hakuna anayekuhukumu,ispokuwa maneno ya kweli ya Mungu ndio yanayokuhukumu.

  Ni haki ipi ambayo waliookoka wamejihesabia, au kule kuwaambia muokoke nyie ambao hamjaokoka? Ukweli ni kwamba kama mtu hajaokoka hatakiwi kujiita mkristo. Au kwa lugha rahisi ni kwamba ukristo maana yake ni kuokoka.

  Ni lini wewe uliwasiliana na shetani mpaka akakwambia kuwa anashindwa kuelewa?

  Unasema tunangojea neema ya Mungu, lini sasa? Hujui kuwa tayari neema ya Mungu imekwisha kufunuliwa? (Titus- Tito 2:11-1211 For the grace of God has appeared that offers salvation to all people. 12 It teaches us to say “No” to ungodliness and worldly passions, and to live self-controlled, upright and godly lives in this present age,)

  Unauliza kuwa ”wewe u nani hata ulijue lipi ni la kweli”, Hujasoma biblia inasema mtawajua kwa matunda yao? Mbona hiyo ni rahisi kabisa.( Mathayo 7;16)

  Inaonekana kuna kitu kimesemwa ambacho kimekuchoma nawe hutaki kukubaliana na huo ukweli. Maana kama si hivyo sioni sababu ya wewe kukasirika na kunena mambo ambayo inaonekana hata undani wake huujui vema.

  Best mpe kristo maisha yako, utaijua kweli nayo itakuweka huru.

  Nimekupenda!

 8. Hongera kaka Sungura kwa kutokuwa mwanadamu wa kawaida. Ndiyo maana kumbe unao uwezo wa kuhukumu. Nimekuelewa na sitaki nyongeza.

 9. Best,

  Wazo lako yawezekana ni zuri, lakini kwa sehemu kubwa umejaribu kujadili mambo usiyoyafahamu kabisa yanavyofanya kazi.
  Mawazo yako ni fikra tu za kawaida kabisa za mtu wa kawaida ambaye anafikiri kwa mfumo wa kawaida wa binadamu. Lakini unachokisema hapa kiko mbali sana na wewe kiasi kwamba badala ya kushauri ungehitaji kwanza wewe mwenyewe msaada wa kiroho, ili angalao upate mwanaga japo kidogo.
  Lakini asante kwa kujitokeza.

 10. Jamani nyie watu mnaojiita eti mmeokoka mimi huwa siwaelewi,idadi yenu inaongezeka na kujifanya eti mnalijua neno la Mungu,mbona ndiyo dunia mnaipeleka kubaya? angalieni kwa makini mambo ya karne hii na karne zilizopita wakati wanaojifanya wanalijua neno la Mungu kama nyinyi hawajajitokeza sana duniani. ni aibu, mpaka shetani nae anashindwa kuelewa. acheni kuhukumu hakuna hata mmoja aliye mtakatifu (Mhubili 7:20) tunangojea neema ya Mungu anayejua kusoma mioyo ya watu,mengine yote ni mbwembwe za wanadamu. kila mmoja anajiona ni bora zaidi ya mwenzake,kama makanisa mnayoyakashifu e.g RC yangekuwa na spidi na maneno mengi kama mliyonayo nyinyi mnaojihesabia haki, leo hii imani juu ya Yesu Kristu duniani isingekuwepo,wewe ni nani hata ulijue lipi ni la kweli(rozali,maji ya Baraka,watakatifu,wafu n.k.) mwachieni Mungu yeye ndiye Hakimu wa haki.TUMECHOKA NA KASHFA ZENU! NA KUJIFANYA MNA UJUZI USIOLETA MABADILIKO( Kuna mkanganyiko katika (IMANI ESPECIALLY AFRICA) .MAUAJI YA ALBINO,BABU LOLIONDO,WIZI,UBAKAJI,USHIRIKINA,UKOSEFU WA HAKI ,DHULUMA NA MAMBO KAMA HAYO YAMEJAA AFRICA. AMBAKO WATU WA BARA HILI WANAJIFANYA WANAMJUA MUNGU.

 11. Mpendwa Peter Michael Mabula,

  Fundisho lako ni jema, linaamsha upya hisia moyo za uchaji Mungu. Katika mafundisho yako hayo, umekazia zaidi watu waitambue aina ya Miujiza, aidha umeainisha tofauti zilizopo baina ya Muujiza wa Kweli utokao kwa Mungu na ule utokao kwa shetani. Hayo yote ni mambo mazuri, kwani waswahili husema, kujikinga ni bora zaidi kulikoni tiba.

  Muujiza ni tukio linalompata mtu lisilo la kanuni za kawaida za Sayansi ya Kimazingira, ya kifizikia ama ya kibaiolojia nk. Muujiza ni jawabu litokanalo na Imani juu ya Mungu dhidi ya hitaji la mhusika! Pamoja na mambo mengine Muujiza hutegemea IMANI YA MHUSIKA JUU YA MUNGU na MUUJIZA UNAOHITAJIKA IWAPO UMO NDANI YA NENO LA MUNGU.

  Watumishi wa sasa wamesimama zaidi katika kuitangaza miujiza hasa ya mafanikio, kwa uzito wa adha zinazosababiswa na ongezeko la maovu, watu wamepofuka na kushindwa kuujari ukweli wa Neno la Mungu. Kwa hali hiyo, kwa makusudi shetani naye hufanya miujiza inayofanana kama ni sawasawa na ile itokayo kwa Mungu, kwa sababu naye ana guvu kama hizo kupitia ‘IMANI’ yake ya kishetani, na kuicha bila subira Imani itokanayo na Mungu katika Neno lake! Lakini cha msingi hapa ni BORA MTU AKAJUA WANZI NABII NA MKRISTO WA KWELI NA MTUMISHI HALISI WA MUNGU KWANZA, ILI KUPATA KWA USAHIHI MUUJIZA ANAOUENDEA. Tatizo ni kwamba, wanaouendea muujiza si wote waaminio halisi, na huja hapo kwa pamoja kuomba kufunguliwa kutoka katika taabu zao ambazo kwa kweli walipewa na shetani.

  Na ikiwa kwa bahati mbaya muuombeaji ni wa upande wa shetani, shetani huwajalia wahusika haraharaka mahitaji yao, nao huondoka wakifurahi bila hata kujiuliza lolote! Sasa basi, kutokana na ukubwa wa hitaji, muda ambao hitaji lenyewe limekaa kwa mhusika na wahusika kutojua vema Neno la Mungu, wahusika huchoka kuka ndani ya tatizo husika na hivyo kwa uhakika wanaweza kukosa umakini wa kuichunguza miujiza yenyewe na aina ya waombeaji. Lakini la pili ni kwamba mtu hawezi kuchunguza jambo ambalo tayari linaushahidi – yeye alikuwa mgonjwa kwa mfano, na sasa amepona achunguze nini tena?!

  Kwa hiyo, muujiza unapofanywa kupitia muuombeaji na kumpata mhusika, mhusika kamwe hawezi kuurudisha muujiza ambao tayari ulishakwisha fanyika eti kwakuwa amegundua kuwa kumbe , muujiza huu alioupata haukutoka kwa Mungu, itakuwa ‘too late’ shetani atakuwa tayari amekwisha vuna! Cha msingi KINGA iwe Bora kulikoni TIBA.

  Biblia inasema, “watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” kumbe utaona kwamba, cha kwanza ili mtu asiangamie ni kuwa na Maarifa. Mtu anapongojea muujiza ufanywe na mtu asiyemjua ki ukweli utumishi wake hujipoteza mwenyewe, kwakuwa kujua namna muujiza utakavyo ombwa na muombeaji, itabidi mwenye kuhitaji muujiza akae hadi mhubri anapofikia hatua ya kuwaombea watu, muombewaji ni lazima ayasikilize yale maombi hayo hadi mwisho, jambo ambalo tayari litamfanya aiingizwe katika himaya ya mapepo kama mhubiri ni wa kishetani! Neno la Mungu linasema, “ondokeni kati yao”. Kwa andiko hilo, mimi najifunza kwamba, inafaa kumsikiliza Roho wa Mungu kwanza, kabla ya kumwendea mtumishi muombeaji!

  Biblia inasema, “WATAKUWEPO MANABII NA MAKRISTO WA UONGO” kwakuwa Neno linasema hivyo, nakubaliana nawe kabisa kwamba, upo pia muujiza wa kishetani! Kwa hiyo iko haja sana ya kuwajua manabii na makristo hao wa uongo kwanza, KULIKONI KUJUA TOFAUTI YA MUUJIZA UTOKAO KWA MUNGU NA ULE UTOKAO KWA SHETANI!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 12. PS Clara,
  Kabla hujasaidiwa juu ya sifa unazoziita za kununua jitafutie kwanza wewe msaada kwa kujibu swali hili:

  Vipi kuhusu biblia ya kununua ambayo imeokoa na kubadilisha maisha ya maelfu ya watu duniani?

  Ubarikiwe.

 13. Mpendwa Mabula,

  Ulichokieleza kimenifurahisha sana. Wanadamu kutokana na taabu zinazoletwa na shetani, imekuwa ni vigumu sana kusema wazi kama watu huzingatia uchunguzi kupitia Neno la Mungu juu ya miujiza inayohubiriwa ama kufanywa na watumishi mbalimbali hapa Duniani kwa sasa. Sababu kubwa ni kwamba watu wengi wafatao miujiza wamegawanyika katika sehemu kuu mbili, wamo waliookoka na wamo wasiookoka pia, lakini wote hao ni wale waliochoshwa na taabu na shida ambazo shetani amewapa na kwamba wamekosa njia ya kawaida inayoweza kumtoa mtu katika shida husika! kwa hiyo, kwakusikia ama kwa kujua hufikia uamzi wa kuifuata miujiza husika kule inakodhaniwa iko ili mladi tu, mhusika akaondokane na tatizo lake lililomchosha! Lakini magrupu yote hayo mawili mara nyingi hayajipi nafasi kubwa katika kuutafuta ukweli wa kutosha juu ya nani ni mtumishi wa kumwendea ili akajipatie huo muujiza unaohitajika; kutokana na kutumia akli, ama uwezo wa kimwili juu ya kutafuta ufumbuzi, hamu kubwa ya kujinasua na tatizo, kuchoka tokana na kiwango cha tatizo alilonalo na muda alionao ndani ya tatizo tajwa; hupoteza uwezo wa ‘KUSUBIRI’ unaotokana tu na kuyauliza maandiko ambayo ndiyo Neno la Mungu ili kutokeza jawabu mwanana.

  Shetani yumo ndani ya Kanisa, naye hutumia maandiko yayohayo, Biblia inasema, “shetani alitumia maandiko (Neno la Mungu) kumjaribu Yesu”! Vilevile shetani hujificha kwa mwamvuri uleule wa ‘IMANI’ lakini kwa kuyapotosha Maandiko kama lisemavyo Neno la Mungu, sawa na hilo Biblia inasema, “shetani huamini kwa kiwango cha kutetemeka” utaona kuwa shetani pia anayo imani, kwa sababu hiyo naye anakuwa na uwezo wa kufanya miujiza mikubwa na midogo! Biblia inasema, “anaweza kufanya hata moto ukashuka toka mbinguni”!

  Kwa mantiki hii basi, utaona ni kwa jinsi gani mikutano hii mikubwa inayofanywa na watumishi mbali mbali inavyoweza kuwavuta watu wengi, nao wakajiingiza humo bila hata ufahamu wa mhubiri na mfanyaji miujiza ile ni nani hasa! Biblia inasema, “Dhambi hutokana na tama ya mtu mwenyewe” kwa hali hiyo, tamaa ya kupona, kupata mchumba, kupata mali, kufunguliwa katika laana zinazoitwa za ukoo, kupata kazi na maisha mazuri, kupanda vyeo, kupata umaarufu nk, yote hayo utaona ndiyo yanayohubiriwa sana kuwa ndiyo muujiza wa maana, lakini ukiyaangalia mambo yote hayo ni ya MWILI tu, na katika mwili ndimo mna tama za kila aina; Mtu akishafika hapo, hana haja ya kumuuliza Roho mtakatifu (kwa wanasema wameokoka) bali, hutumia akili na kuzingatia wanachokisikia toka kwa watu, napengine hukubari kusikizishwa toka hata kwa wasiookoka!

  Miujiza imekuwa mtego nambari moja anaoutumia shetani kuwanasa watu yu mkini hata wateule siku zisigepunguzwa wangepotezwa! Kitu cha msingi, kinachotakiwa ni Neno la Mungu, Miujiza yote ipimwe kupitia Neno la Mungu, lakini, umakini wa Kiroho unahitajika zaidi ili kutambua tu kwamba, Muujiza ukifanywa kwa mjibu wa Neno la Mungu lakini Mhubiri si mtumishi sahihi wa Mungu muujiza unaweza kutokea! Muujiza ni karama na karama haina majuto.

  Muujiza hutegemea mambo makuu mawili, kwanza hutegemea Neno la Mungu kuhusiana na muujiza wenyewe na pili ni kiwango cha Imani alichonacho mhusika mwenyekuuhitaji muujiza ule. Tofauti tu ni kwamba, muujiza unaotokana na Mungu huwa ni ‘HALISI’ na muujiza unaotokana na shetani huwa ’SI HALISI’ kwa maana ya matokeo ya kimwili nayale ya kiroho! Kwa maoni yangu cha kuangalia na kuchunga sana hapo, SI MUUJIZA kama muujiza bali, MHUBIRI anayeombea watu wapate muujiza wenyewe! Watumishi wote ni watumishi tu, lakini wapo watumishi wa Mungu na watumishi wa shetani, lakini wote hawa wamo ndani ya kanisa.

  Kwakuwa Biblia haipo kabisa kwa ajiri ya watu walionje ya kanisa, ni vigumu shetani kufanikiwa katika misheni yake ya kulipotosha kanisa kama hatatumia neno kama Neno la Mungu katika kulishghlikia kanisa. Ni uongozi pekee wa Roho mtakatifu unaweza kututoa katika kudanganywa huko, maana hatuna ujanja wowote dhidi ya ujanja wa shenani, Biblia inasena, “PASIPO MIMI NINYI HAMUWEZI NENO LOLOTE” kwa hiyo, kuwafahamu watumishi wa kweli wa upande wa Kristo ndicho kitu cha maana zaidi, kuliko kuweka akili zetu katika kuichunguza miijiza na aina zake; kujua hilo kutatufanya “TUSILE CHA KUFISHA!” maana mleta chakula ndiye mhimu zaidi kuliko chakula chenyewe!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 14. Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu, nimejifunza kitu kikubwa sana. Hivi wale wanaotuuzia nyimbo za injili huduma yao tuiweke mazingira gani? Kwani ninafahamu Kwamba Mungu anakaa katika sifa na anapendezwa sana na sifa na pia anaweza kutenda miujiza mikubwa kupitia sifa. Tunaona muujiza mkubwa uliofanyika kwa Jeshi la Yehoshafati wakati anaingia vitani (NYKT 2:20 – 30). Angalia mstari wa 22 ”Wakati walipoanza kuimba na kusifu, Mwenyezi-Mungu aliwavuruga akili wanajeshi wa Amoni, Moabu na wa Mlima Seiri waliokuja kupigana na Yuda. Na wanajeshi hao wakashindwa”. Sasa sijui tusemeje juu ya sifa za kununua. Nisaidieni – Asante

 15. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu nimebarikiwa sana na Somo.MUNGU AKUTIE NGUVU KTK HUDUMA.

 16. asante sana kwa ufafanuzi huu umenifundisha kitu katika kujua huduma yenye uwepo wa Mungu wa kweli,Be blessed na utufundishe mengne pia

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s