Natamani huduma ya Mwl Mwakasege ifike mikoani!!

mwl

Bwana Yesu Asifiwe Wapendwa ktk Bwana? Mimi naipenda huduma ya Mwakasege, ninaomba mnisaidie juu ya hili, Je Huduma hii inalenga Dar, Arusha, Moshi. Dodoma, Mwanza na USA pekee? Binafsi natamani nisikie Mwalimu Christopher Mwakasege amefika Mtwara, Lindi au Sumbawanga ama sehemu zenye uhitaji wa Neno la Mungu. Lakini mikoa niliyotaja anairudia mara kadhaa kwa mwaka. Naomba ujumbe huu ufike.

Emanuel Samweli

 

 

Advertisements

11 thoughts on “Natamani huduma ya Mwl Mwakasege ifike mikoani!!

 1. Bwana Yesu asifiwe,

  Nampenda sana Mwl Mwakasege. Anajitahidi afikishe habari njema popote. Ndio maana anarikodi mafundsho yake na vituo vya ma radio vinapeperusha. Mwl Mwakasege hatafika kimwili popote, lakini fungua radio yako ndogo umufwate. Baraka waliopata wale waliomwona na macho nawe ukimwona kwa macho ya roho na kumsikiliza utazipata, ukijua kam hizo baraka zinatoka kwa Mungu. Tena niwape pole wakazi wa vijijini. Kam Mwl Mwakasege hafike pale, fwateni walimu munao, nao ni wazuri. Mnakumbuka ule tajiri akiwa motoni aliomba Ibrahimu atume Lazaro duniani kufundisha watu wa jamaa yake, lakini jibu ni kwamba wasikilize wale manabii wanao.

  Wokovu ni wa kipekee: Mathayo 11:12-13 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni HUPATIKANA KWA NGUVU, NAO WENYE NGUVU WAUTEKA. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.”

  Kwa mafanikio kipesa, unapofwata Mwl Mwakasege, anabandika kwanza shurti:”Amini kwanza Yesu Kristo na tii maagizo yake”, ndipo utabarikiwa.

  Si kwamba Mwl Mwakasege hapendi kufika huko vijijini, lakini pamoja na ile itambidi mafundisho yake irekodiwe, wafanyakazi pamoja naye wawe wamemsindikiza, nk. Na hii inaomba garhama kubwa. Sasa kama huna pato, mfwate kwenye radio na kam una tolea ndogo tuma kwenye M-Pesa au Tigo Pesa, ukiwa na imani atakuombea na Mungu atakubariki.

  Tangu zamani injili iliomba garhama. Tunaposema ni kwa bure ina maana haina bei, kwani unawezakuwa umetoa mingi unabarikiwa sawasawa na yule alietowa kidogo. Mungu anaona moyo, wala si kiwango ya pesa:

  “1 Wakorintho 16:2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;”
  Hivi inatakiwa mkutano wa injili kama ule ufikiwe michango ikiwa tayari.

  Asante.

 2. Jamani mbona Mwalimu Mwakasege utembelea mikoa mbalimbali, alikuwa hapa Morogoro siku za karibuni na huduma yake ilikuwa nzuri sana, watu wengi walipata uponyaji na Mungu alionekana siku zote Mtumishi alizokuwa hapa Morogoro!

 3. Wapendwa wote mliotoa mawazo,Yote ni kulenga kupata huduma lkn nikirudi kwa Daniel J. (Rumi 10: 14-15) Hapo kuna haki na wajibu mimi nipo Ngara Kagera, Nimfuatiliaji wa karibu wa Mwl Mwakasege, kitu alichokifanya cha muhimu ameanzisha utaratibu wa kuwepo kamati za huduma ya Mana Ministry mikoani na wilayani, huu ni utayari wake wa kuona huduma inawafikia kote mliko.
  Ni kweli hawawezi kuamini bila kusikia, Vipindi vya mwl vipo kwenye vyombo vya habari ikiwa nipamoja na intenet. Kama mlifuatilia vizuri mwezi wa saba kulikuwa na kongamano la maombi Dodoma ambapo kila mkoa na wilaya ilitakiwa kupeleka wawakilishi na wao wawapelekee wengine.
  Kwa hiyo wapendwa tutumie fursa ya kuboresha uongozi wetu kiwilaya na kimkoa baba huyu anapatikana na yupo tayari kwa kazi ya MUNGU,
  Ni kweli Uchumi anathiri ijili ya kweli, Lakini pia Inijili inatutaka tufanikiwe kiuchumi na nyanja nyingine pia.(mwanzo 1:18). ukisoma na kutafakari vizuri jambo kubwa aliloahidiwa Ibrahimu na Mungu ni kubarikiwa yeye kuitwa baba wa mataifa si hilo tu na kuwa na mali nyingi na uzao kama mchanga.Kwa hiyo Mungu wetu ni wa baraka na hili ndilo kusudi la kwanza ‘ kuwa wafalme na makuhani PAMOJA na kumiliki na kutawala’ Ufunuo 5:9-10,Mwanzo 1;18.
  Nimalize kwa kusema tuwaombee watumishi wetu,na sisi tufanye bidii kuwapeleka huko wanakotakiwa kupeleka injili.
  Amina.

 4. du poleni kwa wsiofikiwa na huduma ya mwl Mwakasege, inahitaji maombi ya nguvu ili akumbuke na maeneo hayo, nema ya Mungu yatosha.

 5. AMEEEN..!

  Warumi 10: 14 – 15.

  14. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
  15. Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!

 6. BWANA ASIFIWE WATANZANIA

  SASA MIMI NIKO NA SWALI UYU MUNGU TUKO NA MUTAJA AO ENYE NINYI MUKONA MUTAJA SIO MUNGU WAUPENDO ? KWA NINI MUNAJUWA TU ULAYA NA U.S.A. LAKINI SISI JERANI YENU WAKONGOMANI WANDUGU WETU WAKO NAMALIZIKA NA VITA ENYE WATU YA DUNIA IYI WATUTAFUTIYA KWA INCHI YETU YA CONGO ATA KUTUWEKA AMA KUOMBA AMANI IFIKE KWENYE INCHI YETU NA NENO LA MUNGU IUBIRIWE POPOTE AKUNA ?LAKINI KAMA NIMESEMA MUBAYA MUNISAMEHE JUU NINYI MUNAJUWA TU INCHI YENU GINSI TUNAPOSIKIYA ATA KWA MAOMBI YENU ,,,,,,,,NAOMBA MUTUSAIDIYE JUU YA INCHI YETU YA CONGO

 7. Wapendwa,

  Mikutano kama hiyo aifanyayo mwakasege, ni mikutano inayopendwa na wengi sana. Lakini zipo sababu kadhaa ninazoziona kama “kikwazo” kwa mikutano hiyo kufika kote ndani na nje ya nchi katika maeneo yanayoitwa ya pembezoni!

  Sababu mojawapo ni kwamba mikutano hiyo inagharimu kwa kiasi kikubwa cha fedha, hivyo maandalizi huhitaji ujitoaji mkubwa sana wa washirika, waamini na wadau mbali mbali wa Injili husika.

  Lakini sababu ya pili, ni mlengo wa mhubiri mwenyewe, wahubiri husema wanaelekezwa na Roho mtakatifu juu ya nini wafanye, ingawa mara nyingi hutumia hilo kama utetezi wao binafsi ili wapate kutekeleza utashi wao. Watumishi wengi hulenga Fedha, jambo hilo hulipa kipau mbele kulikoni hata ule umhimu wa Injili yenyewe, waandaaji huaangalia kama gharama watakazozitumia kuandaa mkutano zitarudi ama la, kulikoni kutaka sana kujua ni kiasi gani cha watu wataokolewa na Injili itakayopelekwa sehemu hiyo ya mtwara, Lindi, Magu, mara na kwingineko!

  Ukitaka kujua nisemacho ni kweli, angalia na ujiulize, kwanini vijijini Injili haipelekwi huko na akina Bonke, Billgraham, Big november nk? Waandaaji huona huko hakulipi kifedha, kutokana na gharama kubwa zinazotumika katika kuandaa na kuwahudumia wahubiri wakubwa na maarufu kama wale, vilevile kuleta wahubiri wakubwa kama wale na au kuandaa mikutano mikubwa kama ile ni ‘BIASHARA!’ kilichotolewa kirudi na ziada ipatikane, hiyo tayari utaona imekuwa ni biashara!

  Pamoja na kwamba zipo sababu nyingi, lakini nimalizie na hii ya tatu kuwa, AINA ya Injili inayotangazwa katika nyakati zetu hizi, ni ya ‘UTAJIRISHO NA MAFANIKIO’. Ujue mjini kikubwa PESA lakini vijijini kikubwa UTU. Maisha ya mjini hutegemea Pesa, heshima na utu wa mjini ni Pesa, ukiwa duni kipesa mjini hutatambuliwa na pia inawezekana ukawa huna hata haki ya kusema ama kushauri lolote, wakati Vijijini maisha hutegeme utu zaidi na fedha huchukuliwa kama nguvu ya kuendeshea maisha yaliyobebwa na utu, heshima ya kijijni hutegemea utu zaidi wa mhusika! Waweza kuniambia ni mhubiri gani aliye mjini ni maarufu sana lakini anaishi kama Yesu? Wahubiri huhubiri mafanikio kuliko kuutangaza zaidi wokovu kwa sababu, watakaohudhuria ni wachache, maana wengi hupenda pesa, na hicho ndicho huwajaza makanisani, lakini si Neno la uzima!

  Ndiyo maana utaweza kukuta makanisa mazuri mazuri na makubwa yapo mjini! Wahubiri, wenye umaarufu wapo mjini, na hata wale waliyopo kijijini wanaoonekana kuuendea umaarufu, hufikiria na kuamua kuhamia mjini ili huko wakafanikiwe, utawasikia wakisema “….huduma yangu nahitaji ipanuke, hivyo nimepata maono nahamia Dar, Mwanza, Arusha mjini nk….!” Mtumishi anapoiona Injili kama ni MUDUMA YAKE ujue huyo tayari, maana Injili si huduma ya mhubiri, bali ni huduma ya Kristo! Kwa maelezo hayo machache, mikutano ya wahubiri waliomaarufu ni kitendo cha bahati na sibu!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 8. wapendwa ni hivi! kila mahali unapoona mwl. Mwakasege anafanya semina ujue kuna kamati ya maandalizi ya semina zake sasa hii inategemea na uwezo wa kifedha wa hizo kamati namaanisha kua gharama ambazo zinatumika kuandaa semina hizi ambazo huandaiwa na kamati ya maandalizi ya mkoa husika, kama zikiweza zinamwita anakuja na kufanya huduma ndo maana utaona tofauti ipo kwa siku anazohudumu ktk mikoa mf. anaweza kuhudumu Dar mara 2 mapka 3 kwa mwaka lkn mwanza akahudumu mara1 kwa mwaka tena kunatofauti hata ya siku anazohudumu. kama mnafuatilia ratiba za semina utaona kwa mfano alipokuwa mza alihudumu siku 8 akaja shy akahudumu siku 5 tbr nadhani kama sijakosea ni siku 3 na kigoma ni 3 pia. hii inatokana na nguvu na uwezo wa kipesa wa kamati za maandalizi kwa kila mkoa husika. so wale wa mikoa ambayo hajafika iwe ni changamoto ya kuomba na pia kushirkisha kwa wachungaji wenu maana semina za mwal. mwakasege mara nyingi zinaandaliwa na umoja wa makanisa na hii ndo tofauti kubwa aliyonayo mt. huyu. akiwezeshwa naamini atafika tu, kuna wtz wanaoishi ulaya mara nyingi nao wanajikusanya wanaandaa na mt. anakwenda. mi nadhani kikubwa zaidi kuna haja ya kuomba mungu ainue waalimu wengi zaidi wa mfano wake ili kazi ya mungu isambae kote. cha mwisho ni hiki kila mahali mt. anapofanya semina siku ya mwisho huwa zinatolewa kadi za kuchangia maandalizi ya semina inayokuja mwakani na huu mi naona ni utaratibu mzuri maana kwa mwaka mzima sidhani kama watu watakosa fedha ya kuwezesha semina ijayo. wale wanaokumbuka miaka ya tisini na 9 mpaka 2000 tulikuwa tunalipa kiingilio pale diamond jubilee ili kuweza kuhudhuria semina ya mwal.Mwakasege itu amabacho kilikuwa kinawanyima wengi haki ya kupata Neno kwa hiyo mi naona kadiri miaka inavyokwenda mambo ynabadilika tuzidi kumuombea mt. wa Mungu ili aishi miaka mingi lkn pia tuombe Mungu ainue waalimu wa mfano wake nchini mwetu!

 9. Shalom, niwe wa kwanza kuunga mkono, nimekuwa mdau wa kusikiliza mafundisho ya mtumishi, Mwakasege kupitia radio wavuti , kwa kweli nami nimekuwa nikijiuliza ni vipi tufanye ili mwl huyu aje huku Lindi nasi tule MANA.
  MBARIKIWE MARY JOSHUA

 10. Ni kweli.. Ni moja ya mikutano ambayo hutupatia mafundisho mazuri..Natumaini ipo siku atafika..Mbeya,Iringa umeisahau Mbona huwa anakuja pia? Pamoja na hayo Nimesikia juzi alikuwa Tabora pia.. Natumaini siku moja atafika maeneo uliyoyataja.. Ki ukweli Mikoa uliyoitaja ikiwepo Ruvuma naona watumishi wengi wameisahau sana.. Tuwaombee watumishi wote ili siku moja waweze kufika maeneo hayo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s