Moses Kulola Amepumzika

moses

Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania (EAGT) Moses Kulola amefariki dunia leo tarehe 29/08/2013 katika hospital ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu ana watoto wengi wa kiroho nchini Tanzania, Kanisa  linahuzinishwa na habari hizi, Bwana awape faraja kwa kipindi hiki,  “Kuishi ni Kristo na kufa ni faida”

Mazishi yatafanyika Mwanza siku ya Jumatano Septemba 4 kwenye kanisa la EAGT Bugando.

Jina la Bwana libarikiwe.

….UPDATE KUTOKA IKULU

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Moses Kulola ambaye ameaga dunia , Alhamisi, Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 84.

Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulola.

“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Moses Kulola kutokana na maradhi yaliyomfanya wakati fulani apelekwe hadi India kupatiwa matibabu” amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Askofu Moses Kulola kwa miaka mingi wakati wa enzi za uhai wake, kama Mtumishi Hodari wa Kiroho aliyejitoa vilivyo katika kuwahudumia Waumini wa Kanisa lake ambapo mahubiri yake yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani za Waumini wake na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Aidha Rais Kikwete amesema kifo cha Askofu Mkuu, Moses Kulola kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa lake hapa nchini, bali pia miongoni mwa wapenda amani kote nchini na kwingineko duniani kwa vile enzi za uhai wake, Marehemu aliweza kufikisha ujumbe muhimu wa kiimani kupitia mahubiri yake kwa watu wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya  Bara la Afrika.

“Kwa niaba yangu mwenyewe na Serikali ninayoingoza, ninakutumia wewe Katibu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assembies of God Tanzania, Bwana Brown Mwakipesile na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu za Rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza Kiongozi muhimu wa Kiroho.  Ninawajulisha kuwa niko nanyi katika wakati huu mgumu kwa sababu msiba wenu ni msiba wetu pia. Sala na mioyo yetu iko nanyi wakati wa maombolezo ya kifo cha Kiongozi huyo shupavu wa dini. Nawaomba wote muwe wavumilivu na wenye subira kwani yote ni Mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.

“Vilevile kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola kwa kumpoteza Baba, Kiongozi Shupavu na Mhimili wa familia.  Natambua fika kwamba hiki ni kipindi kigumu sana kwao cha maombolezo.  Natambua machungu yenu wakati huu na naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke peponi roho ya Marehemu Moses Kulowa. Amina.”

Mazishi ya Marehemu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) yatafanyika mjini Mwanza Jumatano ijayo tarehe 4 Septemba, 2013.  Heshima za mwisho kwa mwili wa Kiongozi huyo zitatolewa siku ya Jumamosi tarehe 31 Agosti, 2013 katika Kanisa laEAGT karibu na Hospitali ya Temeke kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2013
Advertisements

38 thoughts on “Moses Kulola Amepumzika

 1. NDUGU yangu Obri,

  MUNGU aliye hai ameshasikia kilio chetu.Kilio kwamba UTUKUFU wake unatuacha
  kwasababu ya viongozi walio KATAA HEKIMA NA MAARIFA YA YESU katika nafasi
  zao(TAFAKARI-1 WAKORINTHO 6:1-20).Wameamua kuufanya wokovu kama TAMBALA LA KUPIGIA DEKI!Kumbe wao ndio wamekuwa MAJIVU JUU YA NCHI YA TANZANIA kama ilivyo
  roho inayowaongoza(TAFAKARI-EZEKIELI 28:16-19)

  Kuondoka kwa Baba yetu mpendwa SHUJAA WA IMANI,Mzee Moses Kulola ina maanisha TUMEINGIA MSIMU MPYA WA MAPAMBANO kati ya wateule wanaoipigania IMANI YA KRISTO kwa gharama yoyote inayompa Mungu utukufu na viongozi walioamua kushirikiana na MBWAMWITU kumtukuza shetani na kazi zake zote.

  Mungu anao MASHUJAA WAKE ambao alishawaandaa hata kabla ya kuwekwa
  misingi ya dunia!Na sasa ndiyo wanaingia KAZINI RASMI ILI KUHAKIKISHA MAONO
  MAKUBWA YA MUNGU JUU YA TAIFA LA TANZANIA YANATIMIA.WATEULE WOTE
  WALIOKUBALI KUISHI NDANI YA UNYENYEKEVU WA YESU(TAFAKARI-WAFILIPI 2:3-8) NI WATU HODARI NA WANATENDA MAMBO MAKUU KWA AJILI YA MUNGU WA TANZANIA(TAFAKARI-DANIELI 11:32).MBWAMWITU WANAENDELEA KUAIBIKA KILA KUKICHA(TAFAKARI-ISAYA 30:1-3).

  MWENYE MASIKIO NA ASIKIE UJUMBE HUU AMBAO ROHO WA MUNGU ALIYE HAI
  ANALIAMBIA KANISA LAKE LA TANZANIA.

 2. Ndg Orbi, Mabinza, Seleli, Haule & wapendwa,

  Nimekuwa nikitafakari michango yetu mingi iliyotolewa hapa na kusoma habari kwa kadiri zinavyoripotiwa ktk magazeti nk. kuhusu matukio ya karibuni yaliyo andamana na kulala kwa shujaa wa Injili, Askofu Kulola.

  Matukio ya kugombea ardhi yamemsikitisha kila mmoja wetu, na kwa sasa, ninaamini yamewasikitisha wooote, pamoja na vinara wa mgogoro huo, ambao wengi wa waumini wa madhehebu hayo mawili waliamini kwamba ulimalizika, bali ungali HAI!!

  Licha ya kwamba jambo la kumuomba Mungu atuletee UAMSHO leo tena ni jema na la kutia moyo, lakini , ni vizuri tukajifikisha katika uelewa sahihi wa sababu zilizopelekea kutokea kwa yote yaliyo tokea, na hali tete iliyopo sasa hivi, ndipo juu ya ufahamu huo, sasa tukamuomba Mungu lolote tulitakalo. Maana unapozungumzia UAMSHO, huo ambao dunia imeupitia kuanzia miaka ya 1950s hadi late 70s, kwa taifa la Tanzania, huwezi kuuongelea huo bila ya kumtaja Mwinjilisti Moses Kulola, huyu alikuwa ni sehemu ya huo UAMSHO! Ni jambo kubwa sana kwa mtu yeyote yule, kukirimiwa nafasi ya kuwa sehemu ya Huduma ya Mungu kwa kizazi!!

  Basi jambo ninalotaka mlitazame linahusu kanisa, hilo lililojengwa juu ya Msingi wa Uamsho, ambao twafahamu kwamba ni Sauti ya Mungu yenye kutuamsha tuliorudi nyuma na tulio dhambini, ambao kwa Sauti hiyo tuliamshwa na kuikimbilia Neema! Makanisa yote yaliyoupokea Uamsho huo, na hayo mapya yaliyoanzishwa chini ya miembe au vibarazani au upenuni mwa nyumba au kwenye madarasa ya shule nk, ndani yake yalikuwa na ile Nguvu ya Uamsho, hiyo ilikua ni chemchem iliyobubujisha furaha, upendo, utauwa, na utoshelevu uliojengeka katika Imani kwa Kristo, iliyozibeba na ishara na miujiza! Hiyo ndiyo Injili aliyoihubiri Ev. Kulola, na ilizalisha makusanyiko mengi sana!

  Sasa, ni vizuri kuelewa kuwa Uamsho huwa na wakati. Wakati wake ukiisha, dunia huanza kupoa kama maji ya bahari! Mzee Kulola katika kazi hiyo ya Uinjilisti wa Uamsho, Mungu alimbanza TAG!!! Kwahiyo utendaji wake ulikuwa ukiratibiwa na TAG kama Taasisi.

  Hivyo basi makanisa yoote yaliyoanza katika Uamsho huo na hayo ya zamani yaliyoupokea Uamsho huo, yakiwa ndani ya Uasho huo, kwa ule mbubujiko wa ile Nguvu ya Mungu iliyomo ndani yao, yaliongozwa kwa hiyo mpaka kule kupoa kulipowafika, na hivyo mwishoni wakawa chini ya Taasisi ya TAG ambayo kimsingi si Kanisa bali ni Taasisi INAYOMILIKI na KUYAONGOZA makanisa hayo!!!

  Mgogoro ulipozuka katika Taasisi ya TAG, ulizalisha Taasisi nyingine ya EAGT, na ugomvi wa kuyamiliki makanisa ndio huu unaoendelea hata leo hii!!!

  Pia twapaswa kufamu kwamba Mungu hajawahi kuliacha Kanisa lake limilikiwe wala liongozwe na Taasisi yoyote ile. Mungu katika kila kusanyiko lake, “… ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, …” Hawa ndio Taasisi ya ki Mungu katika kuliongoza Kanisa chini ya Roho Mtakatifu!

  Ndipo mwaweza kuona kwamba Uongozi wa Taasisi zetu umeubadili ule wa ki Ungu unaopaswa kuliongoza Kanisa. Nayo misingi ya Taasisi zetu iko tofauti sana na ile ya ki Ungu. Taasisi zetu zimezaliwa kisheria, na uongozi wake wote unategemea sheria za nchi husika. Nao Umiliki na Uongozi wake wa makanisa, ni kisheria na si ki Ungu, maana katika mfumo wa ki Biblia, kila kusanyiko la mahali ni HURU, yaani sovereign, bali yote yanaongozwa na Roho Mtakatifu, huyu ndiye TAASISI!!

  Kwahiyo, mgogoro huu unazihusu Taasisi hizi mbili, ambazo si makanisa, bali zinagombea makanisa, na kwa vile Taasisi hizi ni za ki sheria, migogoro yao ni lazima itatuliwe kisheria, ndio maana wanalazimika kwenda mahakamani ili kupata haki, nayo makanisa HAYANA sauti!

  Ndipo Uamsho wa kwanza ni kuutambua ukweli huu kwamba TAG/EAGT si makanisa bali ni Taasisi, na waliyoyafanya ni haki yao kisheria. Tusisahau kwamba huko nyuma walipokuwa wakigawanyika, kuna maamuzi ya kisheria yaliyofikiwa, ambayo Taasisi zote mbili zilipaswa kuyatimiza. Kwahiyo kwa EAGT kulitumia eneo hilo kumzikia Askofu wao, yawezekana ilikuwa ni hila au provocation, kulingana na hukumu iliyokwisha kutolewa, na ambayo TAG wangali wakiisisitiza hata leo hii.

  Kwahiyo ndg Orbi, ili Mungu atuletee Uamsho, jambo la kwanza linaloyapasa makanisa yaliyo chini ya uongozi wa Taasisi hizo ni kujirudisha katika Uongozi wa Roho Mtakatifu, yatafanyaje kulifikia jambo hilo, hicho ndicho kitendawili!!! Ninakiona unachokiri hapa unaposema: “”Wengi tumechoka na tunayoyaona, kuyasikia na hata kuyashuhudia yanayotendeka ndani ya nyumba ya Mungu…..! Ni aibu……aibu mno….!”” Unauona mgogoro, ulivyowa suck in? Inawezekana mgogoro huo umehubiriwa sana makanisani, na sasa mahubiri hayo yamerudi tena, yakiendelea kupandikiza simanzi ndani ya mioyo ya waaminio!

  Ndipo najaribu kuwaza, hivi wanaposali ile sala aliyotufundisha Bwana, ile ya “Baba yetu uliye mbinguni…” basi wanapofika katika kile kipengele kinachoishikilia Sala nzima, pale tunapomuomba, “Utusamehe makosa yetu kama NASI TUNAVYO WASAMEHE WALIOTUKOSEA…” Basi kwa tamko letu wenyewe, kusamehewa kwetu kunategemea sisi tulivyowasamehe walio tukosea kwanza, ndipo iwapo hatujawahi kuwasamehe, ni kwamba nasi hatujawahi kusamehewa!!!

  Ni kweli, tunahitaji Uamsho wa Kweli, nao Uamsho ni revolutionary na si evolutional! Yaani Mapinduzi, hayo hupindua!!!!!!

  Mbarikiwe nyoote!!!

 3. Nimefuatilia mjadalaa huu tangu mwanzo sasa naona tunaelekea kupata ufumbuzi!mpendwa Orbi Mungu akubariki umenena vyema kwani tunapopatwa na jambo au tatizo cku zote kilio au kulia/lawama/kukimbia siyo suluhu ya tatizo bali nia kulikabili na kulipatia ufumbuza sana naanza kuona dira ya kuelekea kupata ufumbuzi.Mungu awabariki wote.

 4. Haule,
  Nawe ubarikiwe mno na Bwana……Kanisa litapita kipindi hiki……matumaini yangaliko kwa Kanisa….! Kama tu Kanisa litatambua liko mahali gani……Kama tu Watakatifu watamlilia Bwana na kumuomba atutembelee upya….! Hali tu ya Taifa letu la Tanzania ilivyo sasa hivi inaonekana tunahitaji sauti ambayo hata wasiomjua Mungu watatambua kwamba hii ni sauti ya Mungu…..hata kama hawataitii lakini wataigopa……!Na kuihofu….!

  Wakati taifa la Tanzania kwa ujumla linafikiria nani atatuongoza baada ya utawala huu kuondoka madarakani, Kanisa la Tanzania inabidi nalo limlilie Mungu na kusema tunataka kuisikia sauti yako Upya……! Tuandalie Watendakazi wenye nguvu ya kupambana na uozo ulioko katika jamii….! Hatuhitaji kiriba kipya tu…….tunahitaji na divai mpya!

  Sauti zilizopo sasa hivi Tanzania kutoka Kanisa la Mungu zimeishazoeleka kwa jamii…….hata watanzania hawazisikii tena……Tunahitaji sauti za akina Yohana Mbatizaji……ambaye atatokea kusikoeleweka…! Hatuji ni nyika ipi Bwana atakayomtoa mtenda kazi wake kuirudisha Tanzania kwa Mungu……Mtenda kazi aliyejaa nguvu……hekima…..ujasiri wa Roho Mtakatifu…..atakayeweza kukemea viongozi wa dini……nikiwa na maana dini zote….hata zile za Kilokole zilizojaa Bwana Asifiwe ya mdomoni tu…..!Kukemea viongozi wa siasa…..uovu katika taifa….na kuitangaza toba ya kweli ……inayozaa matunda ya kubadili jamii ya Kitanzania.

  Wengi tumechoka na tunayoyaona, kuyasikia na hata kuyashuhudia yanayotendeka ndani ya nyumba ya Mungu…..! Ni aibu……aibu mno….!Tunashindwa kujitetea mbele ya wasiomjua Mungu…..! La hivi karibuni kwa TAG kuonyesha upagani siku ya msiba limekuwa zito mno…..! Tunashindwa hata wapi tufiche sura zetu…! Ni wakati wa Mungu kujitetea mwenyewe….! Acha Mwenyewe Mungu wa Isreli aingie ulingoni kutetea Kanisa lake……Amefanya hivyo Karne na Karne…….Tunaamini atafanya tena…..Hiki ndio kilio cha Watakatifu……!

  UBARIKIWE.

 5. Seleli, Lwembe, Haule, Joseph na wana blog wote kwa ujumla,

  Umezungumza mengi ndugu yangu Seleli, tena kwa uchungu mno, la msingi je viongozi wa dini ya TAG walitambua kwamba wamekosea? Kama hawajalitambua hilo kondoo watafanyaje? Kondoo ambao wanafungua midomo yao na kulishwa chochote toka mimbarini pasipo kutafakari? Ndio maana nasema kazi ipo!

  Lipi la kufanya katika haya yote? Kanisa la Mungu Tanzania, sio TAG tu, nikiwa na maana kanisa linalomkiri Kristo lina mambo mengi ya kufanya, kuondoka kwa Mzee Kulola kunatakiwa kulilazimisha Kanisa kuangalia kule lilikotoka na wapi linaenda.Kuondoka kwa Mzee Kulola kunatakiwa kufungue tafakari ya Kiroho kama kile kipindi Israel ilipokuwa mbali na Mungu, ilifanya taifa likumbuke nyakati ambazo Mungu alitembea nao, Mungu alikuwa karibu nao, na katika kipindi hicho taifa lilimwita Mungu na Mungu aliwainulia manabii ambao walizungumza Neno la Mungu kwa upya, sauti ya Mungu ikasikika tena. Hizo ndizo kazi walizofanya akina Yeremia, Isaya, Ezekiel Hagai na wengineo…..

  Kwa kifupi kwa macho ya Kiroho Tanzania inahitaji UAMSHO, uamsho ambao unatakiwa uanzie ndani ya nyumba ya Mungu kabla haujawafikia walio nje na nyumba ya Mungu. Tendo walilolifanya TAG linatakiwa liwe a WAKE UP CALL, Kuwa engine yetu ya kiroho inatakiwa iwe OVERHAULED….! Tunafanya hivyo tunapoona engine za magari yetu hazifanyi kazi, gari linaenda, linatoa moshi, ile nguvu yake haipo, japo gari hilo lina uwezo wa kwenda 160 km kwa saa, lakini lina sua sua! Kanisa la Tanzania lina sua sua, Kanisa linaenda mbele kwa shida mno! angalia mafundisho yanayatoka mimbarini! angalia impact yake kwa jamii! Angalia Kanisa linavyo behave siku ya msiba! dalili kuwa tunahitaji mguso mpya tumeziona, zimekuwa wazi mno!

  Jambo ambaloLinatia moyo katika haya yote ni kwamba, Mungu huwa anajisazia watu hata kiwe kipindi kigumu namna gani! Naamini Tanzania bado ina watu wenye macho ya Kiroho ambao wanaona, na wanatambua nini kifanyike.

  Wasomaji wa Historia ya Kanisa wanatambua wazi kuna nyakati kama hizi, ambalo kanisa linakuwa chini mno Kiroho na Mungu kwa Neema yake huwa anatuinulia watu, watu ambao watakuwa ni sauti kamili ya Mungu na kulirudisha Kanisa, kama ilivyokuwa kwa taifa la Mungu Israel ndivyo ilivyo kwa Kanisa, tumekuwa na watu kama akina Martin Luther, John Huss, John na Charles Wesley…..na wengi wengi wengi mno….na kwa nchi kama Tanzania akina Moses Kulola, Mungu kwa Neema yake alituletea Moses Kulola kipindi ambacho Tanzania ilikuwa imengia kipindi cha siasa za ujamaa, Na muasisi wa Taifa letu Nyerere japo alifanya kwa nia njema, alilazimisha kwa msaada wa serikali zianzishwe taasisi za dini ambazo zinasema na kuimba wimbo wa serikali tu kama TEC,CCT na BAKWATA, na Mungu kwa hekima yake na Neema yake kwa Tanzania akatuletea na kuwainua watu kama akina Kulola, sauti ya Mungu ambayo ilitokea mahali ambapo hata usingetarajia! Kwa kupitia mtu huyu Kulola WOKOVU ambao ndio INJILI ya Mungu ukasika katika Taifa letu!

  Tunamwomba Mungu tena atuletee sauti yake tena! Naamini kama alivyotuletea Kulola atatuletea kutoka kwa mtu ambaye hatutaitarajia! Wala pasipo kutegemea! Naamini kuna kina Gedion wengi ambao Bwana anao kwa taifa letu!

  Naamini kabisa Mungu atatuinulia Mtu/watu tena! Kwa watakatifu wa Mungu, ombi letu kuu kwa Bwana ni kumuomba BWANA AFANYE TENA……! NAAMINI ATASIKIA KILIO CHETU NA ATAFANYA TENA!

  MBARIKIWE

 6. Nadhani, mambo mengine ni marahisi sana na yanapaswa kubaki ktk urahisi wake huo huo, ku-complicate au kutwist ili yawe magumu wakati ni mepesi, si tu kwamba ni ushabiki usio na mashiko lakini pia ni aina fulani ya politics, destructive and corrupt ones.

  Ivi sincerely, Ukiulizwa kalamu ya raska inatumika kufanyia nini? u need NOT a big ‘sembe’ revelation na ma-annalysis ili utoe majibu mbalimbali kama ‘’ oooh kalamu inaweza tumika kuchomea mtu jicho ktk ugomvi, kuwashia moto maana zinayeyuka kama nailoni, zinatumika katika michezo ya watoto kutengeneza treni ndefu kwa kuunga-unga izo na kitu kinakua kirefu kwa udongo hapo kama treni ! What is that? Are we serious enough to speak/share tangible stuff for healthy brain and spirit to read and get the senses?

  Very clear and no black dot or doubt kua Kanisa lilikosea sana kuibua mambo haya wakati wa msiba tena aina ya msiba ambao hata wasiomcha Mungu kwa maana yetu ya Ki-kuokoka, walitiishwa/ feel/ sympathise/ regret/ mourn/ hudhuria hata wakuu na wenye mamlaka ya Nchi, wakawepo na kutamka mazito kuhusu Mtu wa Mungu mzuri, wa kutisha sana Mzee wetu huyo.

  Kwa vigezo vyote vya rohoni, akilini, maisha, common senses,elimu, ustaarabu, TULIKOSEA na CV yetu imeporomoka vibaya sana.

  Ikinikera kuliko, iliniuma sana, nilisikia aibu na mpaka sasa naposoma comments za Watu ktk social networks hata za secular kuhusu kitendo icho hata majirani zangu na marafiki wasiookoka kwa yale wayasemayo, nimeshushwa moyo, confidence ya kuwakomalia mambo kama nilivyokua nayo, ime-shrink kama ice cream kwa jua kali la Dar.

  Jambo hili limenifanya kupata ufunuo mpya kama ule wa Petro alipoona/shangaa kuona hata Mataifa wanapokea the same HSp kama wao spesheli people na akajikuta anatamka…’’Sasa NIMETAMBUA/ELEWA/FAHAMU kua…. Nimeelewa NENO la Mungu kwa upya kua, ili Mtu mpaka aokoke, ni KWELI, KWELI, KWELI TUPU, lazima avutwe na BABA kwanza akishakua convicted na RM.

  Kwa hali ilivyo na yaliyojiri, wale wote waliokuwepo msimbani na waliosikia tuliyomtendea Mzee,wataookoka kwa nguvu za Mungu mwenyewe wala si kwa kuhubiri kwetU, kuomba na kufunga au sijui kutema cheche au kugonga Injili! Utaongea nini sasa mbele yao? Utasema nini? si itakua ni mastori tu ya town ya clouds Fm! Jambo bovu kabisa tulifanya na inatia kasirani, jazba na hasira kali!

  Ilikuaje tuna akili za kutosha, hekima nyingi, tumejaa RM sana, twalijua NENO kweli kweli, Bwana yu pamoja nasi, RM anaongeaga tunasikia na kuelewa, ujuzi wa kutembea na Mungu tunao, utumishi wetu Mungu ameudhihirisha, tu mafundi na wenye uwezo mkubwa sana kutatua mambo na kusaidia wengine, halafu tuka shindwa kabisa kujitunza na ushuhuda na heshima yetu mbele za Wanadamu wanaotutegemea sana sisi kua mfano?!!!!!!

  Inakera kwelikweli, inakasirisha, imetushusha moyo sisi tunaoongozwa kama kondoo, imeleta maswali mengi, imeharibu utisho juu yetu sisi kondoo kuwasikiliza wanaotuongoza na kutuhubiria! Nasema mbovu sana hii kitu, TUSIJIRIDHISHE NA KUJIPA MOYO KAMA VILE UPSTAIRS ZETU NGONJWA! WE GRAVELY AND MERCILESSILY MESSED UP NA MNAPOTETEA UBOVU HUU, MNATIA HASIRA SANA NASEMA KWELI WALA SINA HAJA YA KUWAONEA HAYA, KUSEMA MNATIA HASIRA KALI KULETA POLITICS KWA MAMBO MABOVU KWELI AMBAYO HATA WAPAGANI WAMETUSHA ‘P’, wametuona wote kama wasanii na tunafanya biashara tu ktk makundi ya madhehebu tuliyomo! Nasikia kukasiriiiiiiiiika sana, faulu wafanye wengine kisha wote tuwe ‘zerod’ down! mbovu sana! Kama kuna mtu ana hoja ya maana na aileta sasa, tuachane na la msiba, tuwekane sawa sisi kwa sisi maana kama kizazi chetu cha kati na kinachozaliwa sasa ktk BWANA, bado tunaendekeza kutosema kweli na kuleta mambo ya cdm/ccm, basi na tuponyane sasa ivi, tuurarue uwongo vibaya sana utupwe uko pembeni na ukweli ubaki kua tulichemka, twahitaji kurekebisha tena haraka sana, tusifanye kama tuna hati miliki ya mbingu na Mungu mjomba wetu saaaana kiasi ya kwamba tunaweza ende very clearly nje ya Neno kabisa kavu-kavu na live kisha tukabalansi-balansi! Namna gani hapa Wapendwa! Nasema, we did a horrible wrong thing, full stop and period!

  Way forward: Kutubu na kujitenga na yaliyopita hasa sisi wa juzi na leo na kesho.

  Angalizo: Wazee wetu Moses Kulola na Lazaro Emmanuel, walishawahi kupatanishwa/kupatana hadharani na wakatokea wamekumbatiana.Mnaofutilia mambo mtakumbuka tukio hilo ndani ya kanisa moja kubwa jijini. Kanda zipo, mkanunue.Kwa iyo, wahusika wakuu walishamalizana! Why? Walijua na kukiri walifanya mbovu kweli na kuaffect wengi, sasa kama kuna wadogo wao na wana wao wanapenda kuyaendeleza, aya wasongeni mbele, BABA ZETU HAO, WALISHA-CLEAR NA BABA MKUU, mtabaki na ‘’madude’’ kumbe wazazi wetu, walishashuka na kumalizana kisha kumalizana na BWANA.

  Press on.

 7. Joseph,

  Labda niongeze yangu machache kuunga mkono ulichosema. UTUKUFU WA MUNGU unaweza kabisa kuondoka kwa watu wa Mungu leo kama ulivyoondoka kwa taifa la Mungu Israel..! Ikumbukwe kwamba sisi ni mzeituni mwitu uliopandikizwa kati ya Mzeituni halisi (Israel) tukawa washirika wa taifa la Mungu, hivyo kama UTUKUFU WA MUNGU uliweza kuondoka katika Mzeituni halisi itashindikana kwa Kanisa la leo…?

  Makanisa mengi leo hasa yale yanayojiita ya “kiroho” yamebakia na taratibu za Ibada tu ! Ni taratibu za dini tu kama kile kipindi cha Kuhani Eli na wanawe. Si kwamba kipindi hicho taratibu za ibada zilisimama, la hasha! Sadaka zilitolewa lakini si kwa nia kwa kumwabudu Mungu, bali kuwalisha wana wa Kuhani Eli na wanawe! Uzinzi ulikuwepo ndani ya Hekalu kulimokuwepo Sanduku La Bwana! Na hakuna yeyote aliyeweza kukemea! Hata Eli aliwaonya wanawe kwa kuwabembeleza bembeleza tu…! Hata Israel ilipoenda vitani na kushindwa mara ya kwanza, uongozi mzima wa Israel, Eli akiwa kuhani na Wazee katika Israel, badala ya kumuuliza Mungu kwa nini wameshindwa vitani , waliamua kulichukua Sanduku La Bwana kama hirizi ya kushinda vita tu! Sio kitu cha kilichobeba UTUKUFU WA BWANA….KINACHOSTAHILI KUPEWA UTUKUFU…… Unajua kilichotokea…!

  Makanisa mengi ya leo , hasa yale yanayodai ni ya Kiroho yamebakia na majivuno tu ya kuwa na “proper doctrine” au “sisi ndio waanzilishi wa Injili” Lakini hakuna chochote ndani yake! Inatisha unapoona watumishi wengi kumtumikia Mungu sio wito bali ni profession….! Baraka za mali, sifa utajiri ndio unaowasukuma katika kumtumikia Mungu! Kwa wengi wamekuwa na ugonjwa wa kutaka kutambulikana kwa hata titles zao…..! Mara nina Phd….Degree hii au ile, bila kutaka kujulikana ni watenda kazi wa Bwana tu. Na kwa BAADHI YA WATUMISHI, tuhuma za uzinzi zimekuwa zikizungukazunguka katika huduma zao…….nachelea kusema UTUKUFU WA MUNGU UMENDOKA NDANI YA KANISA LA TAG!

  Yaliyotokea karibuni kwa Kanisa la TAG kipindi cha maombelezo kuanza kudai majengo na kuzuia mwili wa Marehemu Kulola usizikwe ni dalili ndogo tu kuonyesha dhehebu hilo liko wapi Kiroho! Huhitaji kuwa nabii au mtume kujiuliza Je uongozi wa Kanisa la TAG walikaa chini na kumuuliza Mungu kwa hilo! Au walikurupuka kama Israel kwenda kuchukua Sanduku la Agano..! Inashangaza wakati wa msiba Kanisa linakwenda kuchukua hukumu ya Jaji Chipeta na kwenda nayo msibani! Hukumu inayokumbusha kipindi cha giza katika kanisa, kipindi cha majonzi na maombelezo! Biblia inasema kimjazacho mtu ndicho kimtokacho! Je inawezekana Kanisa la TAG limejazwa roho ya kumiliki mali! Limejazwa na roho ya kutokuwa na msamaha!

  Kwa kifupi Kanisa la TAG inabidi lijichunguze kwa undani Kiroho! Limesimama wapi na Mungu! Linatembeaje katika kuisikia sauti ya Roho Mtakatifu.

  Kama Mungu alivyomwambia Kuhani Eli…….KWA SABABU HIYO, BWANA, MUNGU WA ISRAEL ASEMA, NALISEMA KANISA LA TAG LITAKWENDA MBELE ZANGU MILELE……LAKINI SASA BWANA ASEMA, JAMBO HILI NA LIWE MBALI NAMI, KWA MAANA WAO WANAONIHESHIMU NITAWAHESHIMU, NA WANAONIDHARAU WATAHESABIA KUWA KITU”

  Na vile vile kanisa la TAG linahitajika kwa sasa lichukue onyo la Kanisa la Laodikia……” KWA KUWA WASEMA, MIMI NI TAJIRI, NIMEJITAJIRISHA,WALA SINA HAJA YA KITU,HUJUI WEWE NI MNYONGE,NA MWENYE MASHAKA, NA MASKINI,NA KIPOFU NA UCHI……NAKUPA SHAURI UNUNUE DHAJABU ILIYOSAFISHWA KWA MOTO……UPATE KUVAA AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANA NA DAWA YA MACHO YAKO YAPATE KUONA…….BASI UWE NA BIDII UKATUBU……….”

  Kanisa limeonyesha uchi wake mbele ya Watakatifu na wateule wa Mungu Tanzania. …Inabidi limrudie Bwana Upya na kuangalia ni wapi limesimama!

  Bwana Awabariki……ndimi mjoli wa Bwana Orbi

 8. ICHABOD

  The term “Ichabod” is found in two places in the Bible, 1 Samuel 14:3 and 4:21. Ichabod was the son of Phinehas and the grandson of Eli, the “priest of the LORD in Shiloh.” The sad story of Eli and his two wayward sons, Phinehas and Hophni, is found in 1 Samuel, chapters 2 and 4. Hophni and Phinehas died in battle with the Philistines who captured the Ark of the Covenant and took it away from Israel. Upon hearing this terrible news, Eli fell backward off his chair and broke his neck and died. Phinehas’s pregnant wife went into labor and bore a son.

  “And she named the child Ichabod, saying, ‘The glory has departed from Israel!’ because the ark of God had been captured and because of her father-in-law and her husband. And she said, ‘The glory has departed from Israel, for the ark of God has been captured’” (1Samuel 4:21-22). The word Ichabod means literally “inglorious” or “there is no glory,” and in her pain and despair, the woman (who is unnamed in Scripture) lamented over the loss of the glory of God from Israel.

  The glory of God is used to describe God’s favor and blessings towards His people. In the Old Testament, God’s glory is seen as a pillar of fire and cloud that followed the Israelites during the exodus from Egypt, guiding and guarding them (Exodus 13:21). Once the Ark of the Covenant was built and placed in the tabernacle in the wilderness, and later in the Temple in Jerusalem, God’s glory resided there as a symbol of His presence among His people. When the Ark was captured by the Philistines, the glory departed from the Israelites—Ichabod became a reality.

  Jesus later refers to the concept of the glory of God leaving Israel. In His last message to the populace of Israel, His final word to the religious leaders was, “O Jerusalem, Jerusalem, you who kill the prophets and stone those sent to you, how often I have longed to gather your children together, as a hen gathers her chicks under her wings, but you were not willing. Look, your house is left to you desolate” (Matthew 23:37-38). That was His final statement of judgment on Israel for the rejection of their Messiah. He has indicted them, indicted their leaders and by indicting the leaders, indicted all the people who followed the leaders. And now He says their house is left desolate—Ichabod, the glory is departing. God is moving away from Israel to another people.

  Notice that He says your house is desolate. Not My house, not My Father’s house, as He used to call it. Now it’s your house because God has left—Ichabod! God is no longer there, it’s not the Father’s house; it’s not My house; it’s your house. The Greek word translated “desolate,” means “abandoned to ruin.” This place is in abandonment. God has left. It’s cursed, devoted over to ruination. And they won’t see Jesus again till He comes in full Messianic glory (Matthew 23:39).

  IT IS TERRIBLE THING TO EXPERIENCE THE LOSS OF THE GLORY OF GOD. AND WHILE ISRAEL’S RUIN WAS TEMPORARY “UNTIL THE FULLNESS OF THE GENTILES” WOULD BE BROUGHT INTO THE KINGDOM OF GOD ON EARTH (ROMANS 11:25), ONE WONDERS HOW MANY CHURCHES TODAY HAVE LOST THE GLORY OF THE LORD, WHETHER WILLINGLY OR UNKNOWINGLY. THE SAME THINGS THAT CAUSED ICHABOD IN ISRAEL—SIN, DISOBEDIENCE, IDOLATRY—ARE PRESENT IN MANY OF TODAY’S CHURCHES. CHRISTIANS MUST NEVER TAKE THE GLORY OF GOD IN OUR MIDST FOR GRANTED, LEST WE WAKE UP ONE DAY AND FIND THAT ICHABOD HAS BECOME A REALITY AMONG US.

 9. ‘Mjoli’ Haule,

  Dah! Ndg yangu, naona kwa uchungu umenichanganyia mambo mengi katika namna ambayo ni vigumu kueleweka! Labda nikuache uchungu ukupungue kwanza, ninaamini utayaona tuliyoyaandika katika context yake, tofauti na ulivyoyaunga!

  Hata hivyo, Pole kwa yote, ndg yangu, Bwana na akuondolee Uchungu!

  Ubarikiwe,

  Kaka Mkubwa!

 10. Haule,

  Sijakuelewa hata kidogo…….kwenda mahakamani siku ya mazishi kudai mali yako huko sio kughafilika kama unavyofanya ionekane……!Kwangu mimi ni kiburi cha uzima tu…..! Ni Mashindano ya mwilini tu……!Hakuna uongozi wa Roho Mtakatifu hapo……Kila Andiko la Kristo na Mitume wake lilikiukwa……Na hata mila za Kitanzania tu za kumdai marehemu zilikiukwa………! Na kama kwako ndio ni umara wa kanisa……basi tumekwisha……! Hii ni dalili wazi TAG kunahitajika uamsho…….! Hivi Mahakama ikiruhusu TAG ichukue hayo makanisa mtafukua mwili wa Kulola….? Maanake inaonekana huko ndiko mnakoelekea….!

  Huko kutengana kwa Marko na Barnaba walikwenda kwa Mataifa kuamuliwa kesi hiyo…..? Hebu rudia Maandiko yako vizuri…..! Yaangalie Maandiko katika context yake…..! Kulikuwa kuna kung’angania mali kati ya Paulo na Marko….?

  TAG ina makanisa makubwa…..ina uwezo wa kifedha mkubwa…..lakini kwa hili inaonekana inatambaa kiroho…….! Mungu alisaidie dhehebu langu…..

 11. Bro Lwembe na Mabinza
  Ngoja niseme nanyi kama watu wa tabia za mwilini mnaonenenda kwa jinsi ya kibinadamu.

  Laumu yatoka wapi!

  Kanisa lenyewe marehemu TAG/EAGT kama mnavyowaita Wamebatizwa kwa Jina la Baba/Mwana/Roho Mtakatifu,Pia hao waamini wanawake hawajifuniki nguo wakiomba/kusali na tena wanahutubu hawakai kimya wakawaulize waume zao nyumbani.

  Bro Orbi
  Naomba kuku uliza
  Barnaba alipomchukuaa mjomba wake Marko na kutengana na Paulo kwenye kazi ya Baba,Kulikuwa na tamko la Mungu!? au kulipingwa ICHABOD

  Mimi ninacho ona kwako umeacha kupiga mbio ktk mashindano haya tangu pale ulipowabeba watu waliokwenda kwa babu Loliondo hutaki kuwasamehe, una uhakika kwamba hawajafanya matengenezo ,Mungu hajawarehemu.
  Angalia usije taka kujiua kama Yona.

  hivi kanisa toka lilipgawanyika miaka ya 80 limepingwa inchabod isipokuwa mlioenda tarshishi na Jesus only,au ndio unaleta utetezi wa Eliya kwa Bwana.kwamba umebaki peke yako.Angalia hayo maneno yako yasio na maana.

  Huku Nyumbani Kanisa linaendelea Yale makanisa uliyoyaacha madarasani ktk majengo ya shule baada ya maamuzi ya mahakama yalinunua viwanja na kumjenga nyumba za sala na maombi na mengine mapya yameanzishwa,Na bado yako yanayokodisha kumbi mbalimbali na Mzee amelala huku ameacha zaidi ya makanisa /kusanyiko 4000 hata miisho ya nchi na zaidi ya 80% ya waamin wake hawakuwepo wakati wa mgawanyiko wameacha maisha yao machafu ya uasi wamempa Bwana Yesu maisha yao

  Najua unaufahamu na Tunda la Roho
  lakini nataka nikukumbushe ni maandiko kukumbushana ili kujihakiki kama tunafanya mapenzi yake Bwana.

  Tunda la Roho(umoja)linabeba Matunda ya Roho ktk hayo tisa(9)likipungua moja ilo sio Tunda la Roho,

  Uwezi kuwa na upendo au amani wakati huohuo una chuki/husuda/wivu …..

  Tusijisifu bure Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

  Tukae ktk zamu zetu tuwarehemu na kuwaombea ndg zetu wa TAG hao wenye mamlaka ambao wamewekwa na Roho Mtakatifu, ambao Bwana aliwapa waongoze kanisa lake alilolinunua kwa damu yake, ili Bwana awatie nuru ktk mioyo yao.

  Mpendwa akighafilika katika kosa lo lote, sisii tulio wa Roho tumrejeze….Tuchukuliane mizigo ili kuitimiza hiyo sheria ya Kristo.

  Acha laumu inafanya unaonekana mtoto mchanga baada ya miaka yote hiyo ya wokovu,mtoto hapewi urithi…..enenenda ktk kimo cha Kristo yaani ufukie kuwa mwana.

  Yeye apandaye kwa mwili wake…….

  Mjoli wenu

  Haule

 12. Lwembe + Mabinza na wengineo……..

  Sina la kuongeza……kwa kifupi kile kitendo tu cha TAG nzima wakati ule kupelekana kwa Jaji Chipeta ambaye alichukua kisu na kuipasua TAG na kuianzisha EAGT kwa tamko lake tu…….Wala sio tamko la Mungu……wala chini ya kwa uongozi wa Roho Mtakatifu….kunasema mengi….! Tena mengi mno…! Ni kweli kabisa kilianza kipindi cha ICHABOD…….utukufu ulishaondoka….!! Inawezekana zilibakia kelele za dini tu Israel……..Tunapoona leo Kanisa TAG INARUDI KWA Jaji “Chipeta” mwingine ili kuzidi kushinikiza kile kilichofanyika miaka ya themanini unajua wazi bado kuwa ” NENO LA MUNGU BADO ADIMU” Japo La msingi ni lini UTUKUFU utarudi tena Israel…….. nyumba ya Mzee Eli na watoto wake imeisha kataliwa…..Ni lini Mungu atatuinulia Samweli….?

 13. Ndg Orbi, Mabinza,

  Ninawaona ndg zangu mmeanzisha msiba siku ya memorial!!!
  Kama nimewaelewa, msiba mlikwisha ulia siku marehemu TAG alipojitenga na Neno la Mungu pale Tabora mbele ya jaji Chipeta, mkalia! Kilio ni ishara ya kupotelewa na kitu kizuri na cha kutegemewa. Siwapeni pole, bali ninawashauri wapendwa mjue jinsi ya kulipokea Neno la Mungu, mkiyafungua macho yenu ya kiroho zaidi ili kuzisoma nyakati.

  Kama mtairejea kauli ya mtume Dunstan Maboya, huyu ambaye ni Askofu Mkuu, nafasi hiyo kiulinganishi, ni sawa na Kuhani Mkuu, ambavyo ofisi hiyo hubeba pia unabii, basi kauli yake kwamba “Joshua ameondoka, Kaleb yupo” hebu ichukulieni katika uzito unaostahili ili kuibaini hali ya kanisa!

  Katika kuitafakari kauli ya Askofu Maboya, nafasi ya Mzee Kulola katika kanisa haiwezi kuwa ni ile ya Joshua, kwa sababu ya maudhui ya hali ya kanisa liliyoipitia, kwa maana ni katika uongozi wa mzee Kulola ndipo mgogoro huu ulipozaliwa. Tukirudi kuiangalia hali ya kanisa katika siku za Musa, inashabihiana na hali hiyo, kanisa huko jangwani lilikuwa na migogoro mingi. Kwahiyo mzee Moses Kulola, kimaudhui ya uongozi wake unashabihiana na wa Musa kule jangwani, kile kivuli! Ni katika kulitazama jambo hili katika uhalisi wake, ndipo unapojitokeza umuhimu wa kuitafakari kauli ya Askofu Maboya, maana kauli hii imetoka, yaani imekuwa uttered katika kipindi ambacho kanisa hilo limeirudia kikamilifu hali iliyolikumba siku ile lilipoliacha Neno la Mungu, kule kupatana anakokuzungumzia ndg Orbi, na kuingia katika MKANGANYIKO, ambao limeurejea tena leo hii!!! Ndio maana nikasema ni “Memorial Service” ya TAG katika ujumla wake (TAG & EAGT), likiirejea ile ibada ya msiba iliyoongozwa na jaji Chipeta, na sasa ibada ya kumbukumbu hiyo ikifanyika katika mahakama ya Mwanza chini ya jaji mwingine!

  Kwamba “Joshua ameondoka”, jambo hili ni kweli na ni la kinabii. Joshua, huduma yake, hapo alipolichukua Kanisa, ilikuwa ni sawa na Roho Mtakatifu. Israeli wote walishikamana kama familia moja, wenye nia na kusudi moja. Ukienda kinyume na maagizo ya Joshua, basi kwa hakika kifo kilikuwa kinakukabili, kama ambavyo kwenda kinyume na RM pia ni kifo cha kiroho! Basi kwamba “Joshua ameondoka”, kwa tamko hilo tunaambiwa kuwa Roho Mtakatifu katika “nyumba” hiyo ya TAG alikwisha kuondoka siku nyingi, tangu huko walipoinua miguu yao kwenda kwa jaji Chipeta, wakamuacha na Neno lake, yaani ICHABOD!!! Naye Kaleb, yule mwaminio, ni kweli yupo, huyo ndiye aliyebaki! Basi tumuombe Mungu kwa ajili yake ili Neema ikiwepo, basi Mungu amwinulie tena Joshua mwingine, alikusanye kusanyiko lote pamoja na kulirudisha katika Njia, ili liweze kumfanyia Mungu Ibada iliyo safi na liwe baraka kwa jamii inayolizunguka!

  Bwana awabariki sana!

 14. Mabinza,

  Nilijizua mno nisiandike kuhusu pingamizi la Kanisa la TAG kwa mazishi ya Mtumishi wa Mungu Mzee Kulola. Lakini angalau kwa leo nitaandika kidogo kwa hilo.
  Kwa kifupi tu, kitendo cha Kanisa la TAG kuweka pingamizi ya Mzee Kulola kuzikwa Bugando kimefichuwa wazi hali ya Kiroho ya ndani ya Kanisa la TAG, na Kanisa la Mungu kwa ujumla Tanzania. Kama wiki chache zilizopita kulitokea mada ndani ya Blog isemayo (mimi na- paraphrase) ” KANISA LA TANZANIA WAPI LIMEACHA NJIA NA KIPI KIFANYIKE) Baadhi ya wana blog waling’ang’ana kusema Kanisa la Tanzania ni Imara kabisa, lakini kwa kilichotokea majuzi sidhani kabisa wana ujasiri huo!

  Kuna mengi ya kujifunza katika hilo, kwa leo nitabainisha moja tu.

  1. Ugomvi wa TAG na EAGT japo ulisulihishwa na mahakama na kuonekana kama umepata ufumbuzi, lakini ufumbuzi wa kweli wa Kiroho haukupatatikana! Huwezi ukaivunja Kanuni ya Mungu ya Kimaandiko ukabakia salama! Kanuni hii iliyovunjwa bado itaitesa TAG NA EAGT: ” BALI MWASHTAKIANA NDUGU KWA NDUGU TENa MBELE YA WASIOAMINI , BASI IMEKUWA UPUNGUFU KWENU KABISA, KWAMBA MNASHTAKIANA NINYI KWA NINYI KWA NINYI MAANA SI AFADHALI KUDHULUMIWA? MAANA SI AFADHALI KUNYANG’ANYWA MALI ZENU….? JE MTU WA KWENA AKIWA NA KESI JUU YA MWENZAKE ATHUBUTUJE KUSHTAKI MBELE YA WASIO HAKI WALI SI MBELE YA WATAKATIFU…? HAMJUI WATAKATIFU WATAUHUKUMU ULIMWENGU?…..HAMJUI TUTAHUKUMU MALAIKA…?

  Kwa kifupi mimi nilikuwepo Mahakamani nikumuona Askofu Lazaro akiumbuana na Mzee Kulola mbele ya Jaji Chipeta……! Wakiongozwa na wanasheria wasio wacha Mungu! Mzee Kulola akiongozwa na Advocate Kikwima muislamu mwenye siasa kali…..na Na Lazaro akiogozwa na Advocate wake jina simkumbuki…..lakini hata kwa macho ya dunia tu ungeona alivyo mbali na Mungu! Machozi yalinitoka nililia mno nikiwa mahakamani Tabora….! Nilijua Kanisa hilo halitakuwa tena lilivyo……na ni kweli kanisa halijawa hivyo tena Kiroho…ingawa kwa macho ya mwilini haionekani hivyo……!

  Miaka imepita Kanuni ya Mungu iliyovunjwa ya kwenda kwa wasio watakatifu kuamua mambo ya waliosafishwa na damu ya Kristo bado inaitesa kanisa pande zote, si TAG tu bali EAGT…..na kinachosikitisha zaidi ungelidhani baada ya miaka mingi kupita viongozi waliopo leo wangetumia kanuni ya Mungu kutatua tatizo hilo, yaani kanuni ya msamaha, kusameheana na kutubu kwa yaliyotokea, Kukubali kwamba kanisa wakati huo lilikikuka Neno la Mungu, na kukimbliana ushabiki tu juu wanadamu……lakini huoni hivyo! Bali tunaona leo hii viongozi hao wanazidi kulikwangua kovu ambalo linaonekana kama limekauka kumbe bado! Bado bichi kabisa……Kwa kumalizilia leo, neno langu kwa EAGT NA TAG Wasiporudi nyuma nakuliangalia tatizo hili kwa mtazamo wa Neno la Mungu safari bado iko ndefu……kwani Mungu hadhihakiwi…..kila alichopanda mtu ndicho avunanacho….! Lazima Kanisa la EAGT NA TAG waifukue mbegu waliyoipanda mbele ja Jaji Chipeta miaka ya themanini…..ama sivyo itaendelea kuwatesa…….

  Tuonane siku nyingine……hasa kujifunza kwa hili….MBARIKIWE…

 15. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pazuri poleni xana na msiba huu kwa wanafamiliya na watu wote walio jitokeza kwenye msiba wa askofu

 16. Wapendwa,

  Mzee Kulola ataendelea kuenziwa na kila mmoja apendaye neno la Mungu, Mimi nilimjua kama mmoja wa wana uamsho wakuu katika Tanzania, Afrika na hata Duniani.

  Ni kweli mzee wetu Kulola amemaliza kazi yake, ni vema sasa waliobaki katika kiti chke na wote wanaojiita watoto ama wajukuu wake wa Imani, wajiulize kama wataweza kwenda katika njia yake, kwa kujitazama katika kioo cha mwenendo wa Kanisa hilo (TAG na EAGT kwa mfano wa TAG ya kale) Kinachonisikitisha ni namna inavyoonesha kama tiyari TAG na EAGT imeanguka mwanguko wa mende yaani chali! waamini wapo katika mparaganyiko uliojaa unafiki vibaya sana. Waamini wa Madhehebu ya TAG na EAGT yamejigawa na kuubeba ubinafsi na kuliacha Neno kwa mbali kiasi cha kutisha! Madhehebu hayo mawili yamejaa umagharibi na ukasikazini kwa namna ya Kimwili kabisa katika Tanzania! Bila kificho utaona tamaa za maungio ya yule mwovu zimelijaa kanisa hilo, kuliko nilvyokuwa nalijua miaka 1980.

  Sasa kunakugombania mali na kudharauliana kwa washirika. Kwa kifupi, mimi nauona msingi wa kanisa la TAG na EAGT haupo na dira yao imepotea! Kwa sababu wakati watu wengine na wasiokoka wakimheshimu na kuukubari utendaji wa Mzee kulola, wengine katika hao wajiitao wameokoka washirika wa Maghehebu hayo, wanamdhalilisha! Haiwezekani Watu wa Mungu, kugombania Ardhi kama wafanyavyo mataifa, kanisa humwabudu Mungu, sasa kwanini kugombania Ardhi? Hutaki kulola azikwe katika sehemu yako, ni wazimu! Tunasoma Neno la Mungu na linatuambia kwamba, Yesu hakuwa na Kaburi la yeye kuzikwa baada ya kifo chake, lakini kwa heshima na utukufu na kwa kazi yake iliyotukuka, mtu mmoja aitwaye Yusufu alitoa bure Kaburi lake ili Yesu apate kuzikwa kwa heshima! Binafsi nikipasoma hapo, Naweza kulifananisha kanisa hili lilikuwa TAG halipo tofauti na ile SEHEMU YA NYAYO YA SANAMU ALIYEIOTA MFALME WA BABELI, amayo ilikuja KUSAGILIWA mbali na lile JIWE lisilofanya kwa mikono. Kuliona kanisa hili linafanya mambo ‘Mafu’ si hoja, hoja ni kujua kama kweli lipo hai ama lilisha kufa!

  Silihukumu kanisa hilo lililo julikana kama TAG, na sasa limegawanyika na Kujiita TAG na EAGT kutokana na kutokuelewana kwa viongozi wake wakuu wawili yaani, Mzee kulola na Mzee Lazaro. Baada ya Tafaruku ile kuu ya pale Dodoma kupoa, ambayo ilipelekea “KUCHANIKA” kwa TAG, wote wawili na washirika wao walisema eti wamesameheana, kama alivyomnafiki, wakaanza hata kuonyesha kama wapo pamoja, kumbe waongo! Uongo wao huo wa KINAFIKI umeonekana waziwazi alipofariki Kulola, Baadhi ya Viongozi waandamizi wa TAG hawakuwepo hata katika mazishi wakidai kuwa wametingwa na Ugeni, kama haitoshi UONGOZI wa TAG ukazuia mzee yule asihifadhiwe katika Enelo la Kanisa la Bugando ambalo wana EAGT wanalitumia kwa Ibada hadi sasa, kwa madai kuwa Eneo hilo ni la TAG na kwamba eti TAG wamewachia EAGT wasalie hapo kwa kiroho safi, ila EAGT waelewe tu kuwa, TAG wanasubiri tu “KUPOE” waanze tena libeneke kudai wakabidhiwe Eneo hilo na lile la Temeke! Huo ndiyo UNAFIKI kwa kisingizio cha ucha MUNGU kumbe “TUPU HUMO!”

  Kiongozi mmoja akizungumza na vyombo vya Habari kufuatia pingamizi la TAG mahakamani, kuzuia Mwili wa Mzee kulola usilazwe hapo Bugando alisema, “NIMEFURAHI SANA KUONA MZEE KULOLA, KUZIKWA KATIKA ENEO HILI LA BUGANDO, KWA SABABU KARUDI NYUMBANI”! Unafiki, unafiki mkubwa; Jiulize, kama si unafiki ni nini? Ulifurahia tukio liwe liwezekane, kwa nini ulienda mahakamani kuzuia tukio lisifanyike????!!! Eti Jibu lake lilikuwa, “UNAJUA MTANGAZAJI, MAHALI MTU ANAPOZIKWA NDIPO HUWA PAKE! TULIFANYA HIVYO ILI KULIWEKA WAZI JAMBO HILO, WATU WAJUE KUWA ENEO HILO NI LA TAG NA KWAMBA TUMELIACHA MIKONONI MWA EAGT KWA NIA NJEMA, WASALIE TU HAPO, BAADAYE TUTALITWAA, KWA HIYO MTU ASIJEKUJIDANGANYA KUWA HAPO NI PA EAGT!” Unauona huo ubinafsi wa kanisa la sasa? Najua wanadamu hawachelewi kusema wamehukumiwa!

  ‘Ufahamu ni chembe ya Uhai!’

 17. Heri wafu wafao katika Bwana, maana wanao uzima. Kazi kwetu sisi tuliosalia kuyaenzi kwa vitendo aliyotuachia Mzee wetu.

 18. Tukimaliza kazi tuta pokea taji,baba amemaliza vizuri.
  Amepiga vita vilivyo vizuri,mwendo ameumaliza,imani ameilinda,baada ya hayo amewekewa taji ya haki ambayo bwana mhukumu mwenye haki,atamupa siku ile, wala si yeye tu bali na sisi wote pia kama tumemsikiliza na kupenda kufunuliwa kwake Bwana 2 thimoteo 4:7-8
  amani kwa jamaa lote la kiroho na la kimwili
  Bwana awafariji.

 19. Hakika yote ni mapenzi yake Mungu,Maana Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa,Jina la Bwana Libarikiwe.Ni habari za kuhuzunisha na kusikitisha lakini jambo kubwa la faraja ni kwamba Amemaliza vizuri mwendo na amevipiga vizuri vita vya Imani,Roho wa Mungu azidi kutuhudumia katika kipindi hiki kigumu.Pole kwa familia ya Kiongozi wetu mpendwa na wakristo wote duniani

  Ameeen.

 20. A servant of The Most High, he fought the fight of Faith gallantly, and now gloriously gathered with his people, behind the Curtain of Time!

  For a Christian can’t die, there is not one scripture in the Bible that says a Christian dies; they don’t die, because they have Everlasting Life! We just change habitations!
  What a Promise we have in Christ, soldier on Christian soldiers!!!

  God bless u all!

 21. Oooh!ma God!kwakweli tumepoteza chombo!cc tulimpenda sana bt God kampenda zaidi.Bwana alitoa Bwana ametwaa jina Bwana libarikiwe.

 22. Apumzike kwa amani AMEVIPGA VITA VILIVYO VIZURI NA MWENDO AMEUMALIZA, Bwana alitoa na ametwaa jina lake ni kuu, sote tu mavumbi na mavumbini tutarejea sku moja hivo tujiweke tayari kwa kutubu na kuiamini injili.

 23. Du very sad indeed, babu yetu na askofu aliyemtumikia Mungu kwa uaminifu kwa kipindi chote akiweka maisha yake na mali pembeni. Nimesikitika sana kwa taarifa hii. Mungu mwema aipumzishe roho yake mahali pema peponi. Amfariji Mama K, watoto wake na ndg wote pamoja na kanisa zima. Tunayo mengi sana ya kujifunza kutoka kwa babu yetu, sijaona kwa kweli namna ya mzee!!!!.
  Lily Sam, Europe

 24. Pole kwa wanafamilia, pole kwa wanajumuia ya mzee Kulola. Bwana atutie nguvu sote kwa pamoja.
  Naye yu angoja ufufuo, wa uzima au mauti!! Hili Mungu ajua peke yake!!

 25. Bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.Rest in peace my holly father

 26. Mzee kamaliza kazi sasa anakwenda kupumzika,eish mzee aliyekua na mshimamo kwa injili iliyo halisi.RIP father.

 27. Hii ni changamoto ya moto wa injili kwa vijana wa Tanzania kumtumikia Mungu toka ujana hadi uzee, kama ilivyokuwa kwake. Alianza akiwa kijana na hata sasa ameondoka akiwa mzee, ameacha mbegu idumuyo hata uzima wa milele. Mimi na Wewe Je? Kwa hali ya kibinadamu ni msiba lakini kwa Mungu wetu ni ushindi ili tuushike tena usukani huu ambao mzee ametuachia. mimi nalia lakini ni machozi ya furaha jinsi mbingu ilivyojawa na shangwe. Jina la Bwana libarikiwe. Mzee wetu amevipiga vita vile vizuri vya Imani, kazi ameimaliza, anastahili kupumzika kwa Baba.

 28. Ooh My God, my heart is greatly shocked/touched! This Great man of God is NO MORE! I love (d) so much, this great Evangelist of our times kwa kweli Toka niko shule ya msingi mpaka maisha baada ya shule namsikia na kuona anafanya huduma, bila shaka CV/taji yake yatisha kama nini mbinguni natiwa wivu kutumika zaidi, ni challenge nzito kwangu/kwetu , such generational land mark indeed in our TZ. Mungu nisaidie nifanye kazi yako in a non-stop pace manner kama Mzee the loving Moses. Poleni wote Mama, Wana, Ndugu na Ukoo mzima wa kimwili na kiroho Tz na East Africa and Central, Europe nk kote huko Bwana alipompeleka kusema Neno la Uzima. Hata ktk hili japo lauma na linasimanzi bado tunanyanyua mikoni na mioyo kusema, Ee Mungu ubarikiwe kwa kumtuza ktk majaribu mabaya na mazito ya huduma aliyopitia, asante kwa kumpa miaka mingi ya kuishi, ubarikiwe Baba kumrehemu kwa utumishi uliotukuka kweli kweli, wenye kicho na maisha yasiyo na tashwishi , mahubiri yenye jumbe za INJILI ORIGINAL/basic kabisa, isiyo na mambo mengine mengine!!!!!Najifunza mengi na kupata somo kubwa niyasomapo aina ya maisha alliyoishi na kutathimini Utumishi wa Mze na Mtu wa Mungu huyu, Mose Kulola. Nitamisi sana kabisa zile anointed live ‘’yooo’’ unapeeenda nikwambie, ni Yesu Kristo tu! funika macho, funika macho (kwa sauti kubwa la besi na mafuta ya ajabu ya Roho Mtakatifu) jamani! Amen and blessed be the name of God for everything.

  Press on NA INJILI ,AMETUACHIA KIJITI

 29. Asante sana kwa taarifa, kwa kweli ni pigo kubwa kwa kanisa la Mungu na kwa familia ya Mzee Moses na wa kristo kwa ujumla hapa Tanzania. Bwana ametoa, Bwana Ametwaa , Jina la Bwana libarikiwe. Asante , pole sana kwa ndugu jamaa na marafikia kwa msiba huu mzito.

 30. Najifunza mengi kwa huyu mtumishi ,anayo mengi ya kukumbukwa ,wewe na mimi tutakumbukwa kwa yapi ?,

 31. Dah, kuna mengi yamenivutia katika historia ya BABU ASKOFU KULOLA…lakini kubwa kuliko hili hapa “Inasemekana hajawahi kunyoa kwa takribani miaka 47, alitumia imani kumwomba Mungu urefu wa nywele zake usiongezeke wala kupungua.. na ikawa hivyo. Kwakweli imani yangu imeongezeka

 32. Kwakweli huyu baba alikuwa mtume haswa, kazi yake inaonyesha. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi aliyokuwa ametupa watanzania. Jina lake na litukuzwe

 33. Tutamkosa mhubiri maarufu na kiongozi wa kanisa hapa tanzania. Mungu ampunzishe maana ni kwa mapenzi yake alimleta hapa duniani na sasa amemtwaa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s