Kubandika majina ya wasiotoa kikumi kanisani!!

majinaTumezungumza mara nyingi kuhusu uhalali wa kutoa kikumi, tukiwa bado hatujapa muafaka, hili bango limenifanya niibue swali hili, Je ni kibiblia kuweka hadharani majina ya wasiotoa kikumi? au kuwafuatilia kwanini hawatoi kikumi?

Advertisements

15 thoughts on “Kubandika majina ya wasiotoa kikumi kanisani!!

 1. Si sahihi kufanya hivyo kwani watu watakuwa wanalazimishwa kufanya hivyo wakati kila mtu anatakiwa kutoa kama alivyokusudia moyoni mwake na pia kulingana na agano lake na MUNGU.Pia mtu anaweza sasa akasema kwamba labda kipato changu ni 100,000 ili kwamba atoe kidogo,kumbe ni 350,000.Je,hapo si atatoa kutimiza matakwa ya mwanadamu na si MUNGU?,kwa nini , kwa sababu asipotoa atabandikwa jina.(2kor 9:6-8)
  6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
  7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
  8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
  MUNGU AWE NANYI MILELE,”AMEN”.

 2. wapendwa katika KRISTO,BWANA YESU ASIFIWE!,naomba mnipe maana ya neno KIKUMI,mi sijaelewa hilo swali,MBARIKIWE NA BWANA

 3. SHIKA NENO MLIOPEWA NEEMA KUBWA! Kiukweli dini na mahehebu wako mwilini tu hawana NENO la kuwafundisha waumini wao wakaelewa nini maana ya kutoa na kwanini wanatakiwa watoe. Isitoshe wachungaji wa dini na madhehebu huwa wanasema sadaka ya zaka ni ya mchungaji. kitu ambacho ni kinyume na NENO LA MUNGU. NENO linasema hivi, “TOENI ZAKA KAMILI ILI KIWEMO CHAKULA NYUMBANI MWA BWANA” Sasa wao wamebadilisha NENO wanasema toeni zaka kamili ili kiwemo chakula nyumbani mwa mchungaji. Ndio maana baada ya Mungu kuifunua kweli ya NENO kizazi hiki cha NNE,watu wamewashitukia ndio maana hawatoi kwakuwa wanajua hiyo zaka badala ya kufanya kazi za kulijenga kanisa zinafanya kazi za kujaza mfuko wa mchungaji.
  pia huwezi kumlazimisha mtu kutoa kwa kuwa ukimlazimisha kutoa hawezi kutoa kwa moyo wa furaha na kwakuwa hatatoa kwa moyo wa furaha hawezi kubarikiwa. Watu wanaona bora wasitoe kwakuwa hawazioni Baraka kama wangekuwa wanaziona Baraka waziwazi wasingelazimishwa kutoa.
  Jambo lingine la muhimu sana ni kwamba, Mungu ameagiza ktk kitabu cha Kumbukumbu la torati kwamba,” MAHALI AMBAPO MUNGU AMELIWEKA JINA LAKE NDIPO HAPO TUNATAKIWA TUELEKEZE MYOYO YETU NA NYUSO ZETU NA TUPELEKE HAPO ZAKA, MALIMBUKO NA DHABIHU ZETU ZOTE” UKITOA MAHALI AMBAPO MUNGU AMELIWEKA JINA LAKE LAZIMA UBARIKIWE. Kweye dini na madhehebu yote hakuna AGIZO LA MUNGU yaani MUNGU WA KWELI HAJALIWEKA JINA LAKE HAPO! Kwenye dini na madhehebu kuna maagizo ya watu waliojiita wenyewe au walioitwa na watu na sio MUNGU WA KWELI.

 4. shalom kubandika majina ya watu wasiotoa fungu la kumi kwenye mbao za matangazo ni kuwadhalilisha waumini au wana wa Mungu fungu la kumi ni agizo la Mungu kwa klia mtu halina cha askofu, mchungaji, mtume wala nabii kila mtu anapaswa kutoa tena kwa lazima na sii kwa hiari, tatizo lililopo leo wachungaji wengi wanawahimiza waumini kutoa fungu la kumi na wao wenyewe hawatoi, wanawatwisha watu mizigo ambayo wao imewashinda, kila mchungaji asiyetoa fungu la kumi na waumini wake hawatatoa, kubandika majina siyo mafundisho ya kuwafanya watu w2atoe ila ni kuwafukuza watu kanisani

 5. mkiijua kweli hiyo kweli itawaweka huru.
  mtazamo wangu ni kwamba ikiwa mwamini akifundishwa neno la kweli kweli itamweka huru katika maeneo yote. wahimizaji hawalazimika kutumia mbinu zozote kuwakumbusha watu juu ya wajibu wao kwa kristo. Ukiona kanisa limefikia hapo ni dalili kuwa mambo ya kiroho yanafanywa kimwili.

 6. Bwana asifiwe watumishi.Kwa upande wangu , fungu la kumi ni lazima kwa kila mtu.Hata hivyo sidhani kama ni halali kubandika majina ya watu wasiotoa fungu la kumi. Kanisa halipaswi kufanya hivyo kwa sadaka inategemeana na utayari wa mtug

 7. Kwamba majina ya wakristo wasiotoa Zaka yanabandikwa ktk mbao za matangazo hapo kanisani, jambo hili linadhihirisha kwamba hao wakusanyaji Zaka hiyo wanaidai ktk maudhui ya Sheria, Mt 23:23!

  Kwahiyo, kwa sababu wako ktk Sheria, ikifikia kwamba kuna wanaokacha kutoa hiyo Zaka, majina yao kubandikwa ktk mbao za matangazo hapo kanisani ni halali kwa sababu wamevunja Sheria! Tena ikiwezekana basi majina hayo, ya hao wahalifu, ni vizuri yaandikwe kwa font kubwa, labda point 48, ili mpaka vipofu wa Injili wayaone!!!

  Gbu all!

 8. Tukitaka kua wakweli kabisa wa nafsi zetu na mbele za Mungu na kama kweli ni Watu tunaotaka na kupenda kumcha Mungu kwa vile tulivyo na kwa kila tulichonacho na pia tukitumia Akili tuliyopewa na Mungu Baba kuwaza/ku-analyse mambo nauliza maswali haya ya kutafakarisha kuhusiana na maswali 2 ya mada na michango yetu ktk mada hii mpaka sasa kama ifuatavyo:(Mnaweza kuyajibu lakini pia hata yasipojibiwa, ni vema tu maana yanakusudia kutazamisha/tafakarisha baadhi ya kweli za ndani ya mioyo yetu)

  (a) Je ni kweli kabisa, kabisa Watu/Washirika wa zamani hapo kanisani hawajui Zaka KiBiblia Agano la Kale na Jipya?

  (b) Je tunahitaji mafundisho ya kiasi gani ili hatimaye Mtu atoe matoleo yote au mengi? Au Mtu afundisheje ndipo tutoe?

  (c) Je hata kama Mafundisho/Semina ni muhimu kwa ajili kuhimizana/kukumbushana/kuhamasishana mambo mema, mbona bado mwitikio unakuaga hafifu hata baada ya seminar kama za Utoaji wa aina zote au hata Maombi ya kawaida, ya Mfungo na Mikesha?

  (d) Je kwa kuzingatia ilo la (c), hamuoni tatizo si kukosa Mafundisho/Kukumbushwa/Kufundishwa au Watu hawamjui Mungu BALI NI MOYO NA NAFSI zetu zina tabu juu ya KUACHILIA/KUJIACHIA mbele za/kwa Mungu?

  (e) Na je Mbona inapokuja swala kufundishwa kuhusu mambo ya kupokea baraka kama Elimu, Scholarships, Visa, kupanda cheo, wachumba/Wenzi wa maisha, kuzaa watoto, kupata mpenyo ktk fedha, biashara nk, baada ya seminar/fandisho ilo TENA LA SIKU MOJA TU, SIO WIKI, Washirika hao hao, wawe wa zamani na wachanga, WANAELEWA VEMA SANA SEMINAR IYO NA KUTENDA HARAKA SANA KWA UTELE/RAHA/FURAHA tena kwa kujitolea mpaka kupitilizia?

  (f) Kwanini kwenye swala la sisi KUTOA iwe ishuu lakini kwa sisi KUPOKEA iwe si ishu?

  Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Embu tuwe wakweli jamani, ndio maana nilisema ktk mchango wangu wa kwanza hapo juu kua , kwa upande mmoja, si vema kubandika Watu hadharani namna ile LAKINI PIA si VEMA KATU, ‘’wabandikwaji’’ kuruhusu kwa sababu yoyote ile, wawe ktk kundi la aibu ilo kanisani na ktk Utumishi. Wao wakiondoa tatizo basi tatizo la kubandikwa, limekufa, ni kama vile ukifyeka majani yanayuzunguku nyumba yako, fukia mashimo na vidimbwi, lala ktk net basi no more Maralia.

  Press on.

 9. too extreme and unbiblical, preach the word and the Faithful Holy Spirit will convict them for it. this is practically judging people, unabandika majina ili kuwaaibisha kama wezi. you have already judged them and we are taught kipimo upimacho ndicho utakachopimiwa. As a christian I dont accept this, naamini ni kazi ya roho mtakatifu kuwaconvict watu kwa kukosa utii, kazi yetu ni kumhubiri kristo, Just preach the true gospel and the rest will be taken care of by The Holy Spirit.

 10. Kubandika majina sio sahihi, ila tuwafundishe watu nao wakiijua kweli kutakuwa hakuna sababu ya kufuatana mpaka kubandikwa ukutani

 11. Mtu wa Mungu hahitaji kuhamasishwa wala kulazimishwa kutoa fungu la kumi au sadaka yoyote kanisani kwake au sehemu yeyote ambapo Mungu anaabudiwa, ila anatakiwa afundishwe neno la Mungu kuhusu utoaji pamoja na matumizi ya hayo matoleo, vilevile afundishwe neno la Mungu la kumsaidia kujua na kumfaham vizuri Mungu anayemtumikia ya kwamba ni Mungu wa Upendo na vyote vijazavyo including him or her ni mali yake, ili apate kumpenda Mungu sana akiwa na upendo na Mungu atatoa chochote kwa ajili ya kazi ya Mungu.
  nionavyo mimi mbarikiwe

 12. Huo uhimizaji ni katika mambo yote au fungu la kumi?
  Mimi nadhan tuwafundishe watu kuwa na mahusiano mazuri kati ya mtu na Mungu na hayo mengine yatakuja yenyewe bila kulazimishana.

 13. MASWALI LA MADA KUU HUSIKA Nimependa kuyagawa mara 2 nayo ni (a) Je ni KiBiblia kuweka hadharani majina ya wasiotoa kikumi? (b) Je ni KiBiblia kuwafuatilia kwanini hawatoi kikumi? na pia mada sindikizaji ni ( C) upo au haupo uhalali wa kutoa kikumi na ivyo kua au kusiwepo na Muafaka kuhusa zaka leo?

  MAJIBU:

  (a) SI KiBiblia kuweka majina hadharani ya wasiotoa kikumi maana ingawa lengo ni jema ( kuwakumbusha na kuwasukuma wale wazito na wasiojali mambo ya Mungu, kanisani kwao na shughuli na maisha ya Watumishi na watu wao hapo kanisani, lakini jambo lolote likifanyika nje ya Hekima na Upendo, linaharibika hata maana yake. Swali la Msingi kama Watu waendao mbinguni na wanaompenda Mungu kwa kila kitu ni hili..’’IMEKUAJE HAO WANAOWEKWA HADHARANI KURUHUSU WAWE KTK GROUP IYO? NANI ANA TATIZO KUBWA SANA LA ROHONI KATI YA WAWEKAJI MAJINA HADHARANI AU HAO WALIOWEKWA HADHARANI? Hahitaji Akili ya Chuo au Ufunuo spesheli kujua jibu hapo!!!!!!!!

  (b) NI Kibiblia kabisa kuwafuatilia kwa UPENDO si kijeshi! Neno la MUNGU limeongea mengi kuhusu kuchungana/ kujichunga/ kuhimizana/ kushaurinana/kuokoana kama kwa moto/kutomuacha ndugu ktk ubaya/uovu/uzembe/kurudi nyuma nk. Kuwafuatilia maaa yake hasa ni kuwakumbusha, hakuna jingine! Ivyo basi kwa njia mbali mbali tunaweza wafuatilia/kumbusha Watu mfano, kupitia mahubiri au fundisho maalum ktk seminar, Kuwa-appreciate publically si kwa majina bali general statement, wale wote wanaosimama na kanisa/Watumishi kwa kazi ya Bwana na ivyo, wale wasiotoa kama wana uhai bado ktk roho zao, watasikia aibu/hatia/vibaya/kua challenged na kutaka kumalizana na Mungu wao wenyewe. Pia wakati mwingine hata kuwaandikia kibinafsi kinote chao kwa hekima tu mfano ktk ki-note icho, kinaanza kwa kumbariki kwa yale ya nyuma aliyofanya vema na kisha kumualika/tia moyo kua asipoze bali aongeza gia ktk utumishi wake wa utoaji ili kazi isonge mbele.Mtu/Mpendwa mwenye Roho Mt na bado kule ndani networks zinakamata, kwa kanote ako kenye hekima/upendo na uangalifu mkubwa ktk maandishi na maneno yaliyotumia, ataguswa/kumbushwa ndani kwa nguvu sana, unless awe ndio ivyo, beyond repair siku nyingi.

  ( C) Katika yote tuyafanyayo, kutenda, kunena, kufanya maamuzi nk, tuko huru wakati tunaeleza mawazo yetu kutumia njia nyingi kadhaa mfano elimu za darasani, uzoefu wa kawaida kabisa wa maisha haya au kutembea na Mungu,Akili hi hi ya kawadia, ustadi tuliojipatia ktk huduma, kwa kuambiwa au kufundishwa mambo, kujisomea mwenyewe vyanzo kadhaa kama vitabu vya kiroho na wana Dini/Theolojia, Historia ya mambo ya imani, dini, Kanisa nk LAKINI vi vema sana na kwa kweli iwe ndio siku zote mtindo wetu ktk majadiliano kwamba tukishasema yote ktk njia zote, hatimaye NENO la MUNGU linasemaje kama mamlaka ya mwisho kwetu LAKINI tukilitumia NENO kwa UHALALI(usawa/usahihi/ukweli/kimsingi/kitakatifu/ki-nia njema nk) =2Timotheo.2:15c NA KTK HEKIMA YOTE( kiuelewa mpana wa maneno ya Mungu kwa ujumla/kiufahamu wa Mungu hasa Neno/ujumbe wake ni upi ktk vizazi vyote/ ktk akili yote ya Mungu ili kubebe Neno fulani ndio hasa letu leo kwa leo/kiufahamu mkubwa kujua wapi na namna gani nina-appy neno hili na lile/kimpangilio wa KiMungu bila kupindisha kweli au kugoganisha kweli nyingine nk= Kolosai.3:16

  Kwa mantiki iyo hapo juu, naamini ktk haya ni kweli na yanajibu kwa nini tutoe zaka leo, ivyo kwangu,muafaka upo maana Neno la Mungu hukata mashauri/huamua mambo,husema sasa la ukweli ni hili na mengine yaachwe. Hoja ni hizi kama ifuatavyo:

  Mwanzo.14:1-20: Kabla ya Sheria, Ibrahimiu rafiki wa Mungu, kwa kupenda kwake,moyo wake wa shukrani, furaha yake kwa Muumba , kicho chake kwa Mungu na ufahamu wake wa rohoni kutambua kua vita ile kama si Bwana, isingezekana, ANATOA ZAKA kwa Melkizedeki aliyekua Mfalme na Kuhani ambaye hakutokana na kabila la Lawi kwa utaratibu uliokuja kuwekwa na MUNGU baadaye wakati wa Musa.( Notice: Zaka inatolewa wa kuhani Melkizediki-mfano wa Kuhuni Yesu Kristo- Waebrania.7:1-28 na 8:1-3,. Kwa kua Agano la Kale( Torati) ni kivuli- Waebrania.10:1, si picha halisi yaani lilikua linaashiria/elekezea Agano jingine(picha halisi/jambo lenyewe haswa- na ingawa hapa Paul anasema Agano la Kale kwa maana ya wakati wa Sheria lakini ni ukweli pia ametoa mifano ya Ibrahimu na Melkizedeki ambayo ni kabla ya Sheria kwa sura zilizotangulia za 7 na 8, basi kwa uhalisi wa Agano la leo ambapo tunafanya mambo kwa utashi/uhiyari WENYE KUSUKUMWA NA UELEWA WA KUJUA UMUHIMU NA WENYE MAAMUZI YA MAKUSUDI KUTAKA MAMBO YA MUNGU YAFANIKIWE NAKUSONGA MBELE NA PIA IBADA ZETU ZIWE NA SEHEMU KUBWA YA SHUKRANI SI YA MANENO TU BALI NA MATENDO PIA kama vile ‘kutoa’ kama Ibrahimu, basi tunaweza kutoa sana matoleo mbalimbali mfano zaka na zaidi ya zaka(Isack), kwa kwakua Agano letu la leo ni bora zaidi na nila-kimahusiano ya karibu na mazito sana na Mungu wetu kiasi kwamba hatuwezi jisaza inapokuja swala la kujitoa kwetu si maisha tu bali na kila tulivyonayo.

  Mithali.3:9: Kumuheshimu Bwana KWA MALI ZETU NA MALIMBUKO ya kila ongezeko pia inawaweza kua ni Neno la Mungu la Agano la Kale lenye ukweli unao hama moja kwa moja mpaka Agano Jipya, si laana kua-apply baadhi ya kweli za Agano la Kale ZISIZOPINGANA AU VURUGWA KWELI ZA AGANO JIPYA. Na ni maoni yangu kua njia moja wapo bora sana kwa Mwanadamu kujizoeza uchaji kumfikiria na kumkumbuka/mtambua Mungu kila mara ktk maisha yake( maana tuna nature ya kusahau tukisha shiba-Kumbu.8:10-14 au tu nafsi zetu zinapenda tupendelee kwanza maisha yetu kisha ya Mungu baadae au kuyafuta kabisa wakati mwingine-Mathayo.16:24-26 Vs.Mathayo.6:33, ivyo basi ni vema, haki na akili njema sana na salama kwa mcha Mungu kujiwekea kwa furaha tu na uhuru wote kua, nitatenga 1 tu kwa Bwana kama namna nzuri ya kuji-train/discipline nafsi kulainika ktk kumuheshimu/mwachilia Bwana mali zetu, kisha mengine yote 9 ruksa, kula mwenyewe au labda na wengine.

  Mathayo.22:37: Mwanadamu akipenda kitu/Mtu, unaweza fahamu anafanyaga nini yaliyo ndani na hata NJE ya uwezo wake kumfurahisha tu huyo mpezi wake au kipenzi kitu chake anachokipenda kwa moyo, akili,nafsi, nguvu nk. Kwa kua tuna nature hiyo wanadamu wote tukishapenda, basi Yesu anadai zaidi sana tufanye kwa Mungu. Ndiposa kumtolea Mungu zaka, malimbuko,matolea mengine yote, mali, muda,akili, vipaji,karama na mengine yote, yanawezekana leo mpaka kesho
  .
  Mathayo.23:1, 23: Ktk mstari wa 1, imeandikwa ..’’Yesu akaongea na mkutano na WANAFUNZI WAKE akisema, …halafu mbele uko mstari 23-Anawasahihisha/challenge Mafarisayo na Waandishi kua wanajali sana kulipa ZAKA za…. wakiacha mambo ya haki,imani na rehema, kisha anasema, yafanywe kwanza hayo( ya rehema/imani/haki) BILA KUACHA na hayo MENGINE kutofanywa!- ya Zaka! Ni wazi hapa na rahisi kabisa kuelewa kua Yesu hakufuta zaka bali aliweka sawa yapi yaanze/yakamate mioyo yote ili tukishayajaza/fanya hayo( rehema/imani/haki) NDIPO tufanye na mengine BILA KUYACHA! ( Notice: Huyu ni Yesu mwenyewe anaongea/weka sawa/reccomend ivyo kuhusu ZAKA)

  Kwa hoja hizo, TUMTOELEE BWANA AINA ZOTE ZA MATOLEO KABISA NA ZAKA IKIWAPO.

  Press on.

 14. si sahihi lakini kwa upande mwingine ni sawa tu hasa kama walengwa ni washiriki wa kanisa tajwa(si wageni). Nijuavyo kikumi si wingi wa utoaji bali ni aslilimia mfano kama ukisema wewe kipato chako kwa mwezi ni elfu kumi utatoa elfu moja kama kikumi.

  Unajua injili kiukweli ni gharama sana..hv usipotoa sadaka je umeme, maji, ulinzi wa kanisa, mishahara ya watumishi wa kanisa (ambao wanakaa siku nzima kukusikiliza shida zako na kuku-consel&kuombea), ukarabati wa jengo, upambaji wa madhabahu&jengo, urushaji wa vipindi redioni ili watu wengi wampokee Bwana (wenye prgm za kurusha mahubiri), usafi wa kanisa, manunuzi ya stationeries za kanisa, etc etc etc vitafanywa kwa kutumia pesa kutoka wapi???au unavyokuja kanisani na kukuta kila kitu kimeandaliwa na wewe kuketi sehemu nzuri huku ukipepewa na feni unadhani ni nani ameingia gharama zote hizi au vimetokea tu??

  Me binafsi nilikuwa mpinzani wa utoaji lakini nilipoitwa kwenye kamati ya kuandaa mkutano wa injili ndipo nilipoona aibu kubwa kwa msimamo niliokuwa nao. Tutoe tu hata kama ni kwa kusukumana ila tuweke imani kwa Mungu na si watu,

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s