Tegemeo langu ni Yesu tu!

maombi

Bwana Yesu asifiwe.

Nawasalimu katika jina la Bwana.

Naitwa Vicky nipo Dar es salaam Tanzania. naomba niwashirikishe hitaji langu mnisaidie kuomba.  Nyumba yangu imekuwa chungu kila siku machozi yananitoka kwa kukosa amani. Mume wangu ni mlevi ana kauli zinazo umiza za kejeli na dharau kubwa, tangu amejiunga kwenye Siasa nyumba yangu imekuwa haina amani tena. Anapenda kunywa sana, amekuwa mtu wa wanawake, hajali kama ana mke salamu kwake ni nadra sipaswi kuuliza chochote kutoka kwake nitaambulia maneno ya masimango na dharau. Tena anasema hata nimuombe vipi Mungu yeye hawezi kubadilika atabadilika atakapo sijisikia.

Wapendwa naumia sana. Naishi kama mtumwa, nimekata tamaa.  Mume wangu hafanyi kitu chochote bila kwenda kwa waganga wa kienyeji hata leo hii asubuhi nimekuta kwenye nguo zake dawa za kienyeji aina tatu, amezifungia kwenye suruali yake. Watu wa Mungu nisaidieni katika maombi,  nitanyanyasika na kudharaulika mpaka lini. Mimi tegemeo langu ni Mungu tu sina wa kunisaidia wala wakunisikiliza.

Mungu awabariki.

Advertisements

13 thoughts on “Tegemeo langu ni Yesu tu!

 1. Hallow Vick.waweza kutujuza maendeleo tangu utushirikishe maombi? Ili tuanze kushukru kwa ajili ya matendo yake makuu na kama bado ningependa kujua ili tukaze uzi hadi huyo ibilisi akashindwe mmbomoa ndoa za watu.
  Barikiwa Vick

 2. Pole sana dada!
  Nakushauri usikate tamaa Mungu atakupigania utashinda.Hivyo, endelea kumwomba Mungu nasi tunakuombea kwani hilo ni jaribu la muda na ninaamini Mungu atafanya mlango wa kutokea. Amina!!

 3. pole sana dada mpenzi majaribu yanamlango wa kupitia na kuingilia pokea ukombozi wa damu ya Yesu Kristo kwa ndoa yako,usiogope wacha usimangwe maana mwangaza unakuja kati ka ndoa yako na MUNGU ANAKWENDA KUKUTANA NA MUME WAKO KWA MUDA SIO MLEFU NA UTASHANGILIA UTUKUFU WA BWANA

 4. Dada Vicky unajua Mungu anasema tuombe lolote kwa jina lake naye atatupa wakati wa kuomba embu mkumbushe Mungu ahadi zake kwetu kupitia neno lake utaona muujiza mpendwa. Mungu akutetee

 5. omba Mungu dada Vicky utashinda tu Mungu atafanya njia muda na wakati usiozania

 6. Shalom! pole sana dada vick, najua ni jinsi gani moyo wako unaumia kuhusu mateso unayopata kupitia ndoa yako, ila amini kuwa Mungu yuko pamoja nawe, na Yesu ni mfariji wako na atayabadilisha machozi yako kuwa furaha cha msingiweka tumaini lako kwa Mungu, wote waliomkimbilia Bwana wamekuwa salama. niko pamoja nawe katika maombi.

 7. Pole dada najua ni jinsi gani unafeel< lakini wacha nikutie moyo huyo atabadilika hadi utashangaa hayo si maneno yake ni maneno ya shetani anataka kukufadhaisha usikasirike wala usiumie omba sana hasa pale anapolewa san muwekee mikono mkumbushe Mungu ahadi zake juu ya ndoa, mweleze Mungu vile unavyojisikia usiombe kwa kunun'gunika omba kwa ujasiri shetani ataona aibu na kumwachia huru Mume wako.

 8. oooooh! pole sana dada mtegemee YESU mana hufanya njia pasipo na njia, omba bila kuchoka uyashinde majaribu hayo.

 9. Pole sana dada Vick,shaka ondoa mumeo atafinyangwa na JESUS Mpaka utashangaa!Ngoja nikupe haka kaushuhuda..Ujuwe kabla cjaokoka nilikuwa naona isue ya kuokoka kama ni usanii na mtu alikuwa akinitel ameokokoka nilikuwa naona kama ameishiwa na mbinu za maisha!Mbaya zaidi nilikuwa nakunywa pombe monday 2 sunday,jan 2 dec!ukija swala la warembo ndiyo usiseme kiasi kwamba hata marafiki zangu walikuwa wananiogopa!Bahati nzuri wyf alikuwa ameokoka kila alikuwa akinitel habari za wokovu ndiyo naona kama ananitukana!kutokana ikitokea nimesafiri na wyf kikazi nilikuwa namtel mamaa achana na mambo ya wokovu twende zetu club tukale maisha na kwakuwa alikuwa ananipenda ilibidi twende so anakaa akiniangalia nikicheza mziki!kwa mambo yote hakukata tamaa coz aliamini 1day nitachange na alizidi kupiga maombi!

  cku1 alinitel mch anaomba umtembelee kunajambo anataka kukushirikisha!Nikamjibu niko busy sana!ikabidi awe mpole bt baadaye nikamtel twende!Nilivyofika 2kaongea mambo ya kawaida baadaye akaniuliza huna jambo lolote la kukuombea?4rom no where nikamtel niombe kazi yangu,akasema jingine!nikamjibu natamani kuokoka ila cjui itakuwaje pastor coz napend sana pombe akasema ucjali ngoja kwanza nikuongoze sala ya toba then nitakuombe!baada ya mambo yote kukamilika akanitel ukinywa pombe ucnifiche njoo uniambie nikasema sawa pastor lakini nataka nikwambie tangu cku ile nilivyokiri kiu ya pombe ikakata thn macho yangu yalikuwa yakiona warembo tena weupe nilikuwa napagawa bt 4rom tht day ile hali ikafutika!Nataka nikwambie dada Vicky uckate tamaa hata kidogo keep on praying nakwambia ipo cku Mungu atafuta machozi yako yote!Mtumainiye yeye tu coz ndiye anaweza yote!Hizo cheche za shetani atazizima zote!Mungu akubariki dada Vick.

 10. Pole sana Vick kwa majaribu unayopitia kwasasa naomba kukutia moyo na kukuhakikishia kua utayapita hayo mapito na utapata amani, kikubwa ni kusimama hapo uliposimama yaani kwenye maombi hivi naungana nawe kwenye maombi. Anayeyafanya hayo ni shetani na sio mume wako hvyo kwa maombi ya pamoja utapata faraja na mume wako atafunguliwa.

 11. Pole sana dada,nakuomba usikate tama hata kama mazingira yanayokuzunguka unaona hauwezi Mungu yu upande wake hatakuacha soma Isaya 59:1,Dumu katika kuomba Mungu wetu si mwanadamu hata aseme Uongo kila analosema atalifanya.Kumbuka ahadi yenu ya ndoa pale kanisani simama nayo mwombe Mungu akusaidie Mume wako atageuka hata we mwenyewe utashangaa,pia kumbuka neno hili Waefeso: 6:12 Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho,ina maana usipambane na mume wako pambana na kila falme za giza na pepo wabaya katika ufalme w giza ili kumkomboa huko pia mwombe Roho mtakatifu akupe na kibali cha kufunga maana mambo mengine hayawezekani ila kwa kuomba na kufunga.kumbuka mwanamke atamlinda mume wake,usimwache apotee simama kwenye nafasi yako kama mwanamke Mungu akutetee.Amen

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s