ASKOFU MABOYA: JOSHUA AMEONDOKA, KALEB YUPO

Askofu mkuu wa makanisa ya Calvary, Dunstan Maboya akitoa salamu za rambirambi kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika salamu mbalimbali, viongozi wengi waliozungumza, wameonekana kuguswa aidha moja kwa moja na maisha ya hayati Kulola, ama watoto wake (yaani wale wa kiroho), ana watoto wengi – wengi sana, wale wa zizini na wale walio nje ya zizi, kama asemavyo Askofu Mkuu wa makanisa ya Calvary Assemblies of God, Maboya.

Nilipata taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa PCT (Askofu David Mwasota), nikaona lazima nije kushuhudia anapolala Jemedari. Aliishika injili na imani, sisemi kama kutumia maji na vitambaa ni mbaya, hapana – inachanganya, tunakuwa kama waganga.” Anasema askofu Maboya na kuongeza kuwa EAGT ni kanisa lenye misingi, ambalo bado kiongozi wa kuliendeleza yupo kwa kuwa halikuwa kanisa la mtu binafsi.

EAGT sio huduma ya mtu binafsi, ni kanisa lenye misingi, CAG (Calvary Assemblies of God) fuateni mtiririko. Kulola ni baba wa huduma CAG. Joshua ameondoka, Kaleb yupo.” anamaliza kusema Askofu Dunstan, ambaye alikuwa akishangiliwa vilivyo na umati wa watu uliojaza uwanja huo.

Wakati huo huo mahakama yatupilia mbali madai ya TAG kuweka pingamizi Askofu Dr Moses. Kulola asizikwe Kanisani Bugando. Wakidai kanisa la EAGT BUGANDO MWANZA NA EAGT TEMEKE DAR ES SALAAM ni Mali ya TAG.

–Gospel Kitaa, Mitandaoni

Advertisements

20 thoughts on “ASKOFU MABOYA: JOSHUA AMEONDOKA, KALEB YUPO

 1. Mungu siku zote atabaki kuwa Mungu. Viongozi wa TAG, jifunzeni kwa huyo mtumishi wa Mungu shujaa wa imani Kulola. Yawezekana kuna mengi hata yeye atakuwa alidhurumuiwa lakini mtumishi wa Mungu alikuwa shujaa wa kuachilia.

  Tafadhali tujifunze sio tu viongozi wa TAG bali hata viongozi wengine wenye mtazamo kama wa TAG.

 2. Ndugu zangu,

  Roho ya uasi ikishaingia ndo basi tena, hakuna jinsi! Imani iliyosimama kimwili ni DUDE linalo ning’inia tiyari kuanguka. Wenyemacho hawashangai wala hawawahurumii ‘VIPOFU’ ambao kilawakiwashauri kujiepusha na Dude lile, wao hujibu kwa dhihaka na kwa sauti kubwa wakisema, “Bwanaee, tunaona!” na kubaki wamesimama chini ya dude hilo huku wamekumbatiana kwa kicheko.

  Wakiambiwa, “tokeni katika dude hilo – tokeni kati yake” ni hatari! Lakini wao kama hawasikii kitu, wapo Kucheka tu! Harafu kama mazuzu wanasema, SISI NDO BASI TENA! Akili na mawazo katika roho zao zinataka mashamba, majumba, magari, pesa nk.

  Lakini Yesu ambaye ni UPENDO, hawanahaja naye, ukisimama na kuwasikiliza wasemavyo utashangaa, maana utawasikia wakisema, “SISI TUNATAKA TUFANANE NA YESU MIOYO YETU!”; Neno linasema, “ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE UOVU”! Mtu akilikataa Neno la Mungu NDIYO BASI TENA!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 3. Naamini kuwa jambo hili la AIBU kwa viongozi wa TAG kukimbilia mahakamani wakati kama huu bila kuona hata huruma ya kusababisha maumivu zaidi kwa wafiwa na kanisa kwa ujumla BWANA mwenye aliruhusu ili Roho iliyomo ndani mwao iwekwe wazi kwa watu wote ikiwa pamoja na washirika wao.
  Kwa namna hii pengine wataweza kumpa tena nafasi ROHO WA KWELI na kujitambua kuwa walishatoka nje ya mstari na yamkini WATUBU na KURUDIA ule UPENDO WA KWANZA WA KRISTO.Mungu wetu wa Kweli bado ana tawala na Neema bado iko!!!!

 4. Ninavyofikiri,Pengine mpango ulikuwapo mapema mzee akiondoka tu,kesi zianze mahakamani,kitendo cha mzee kuomba kuzikwa kanisani ni uongozi wa roho wa Mungu ili mzee atakapolala kelele zisiwepo tena(it is the great miracle),Ujasiri wa kuzifungua kesi hizi baada ya tukio lile ni mdogo,maana aibu imekuwa kubwa.Tunachotakiwa kujua roho ya Mungu iliyokuwa na Mzee Kulola,ipo hai,kama walimwogopa Mzee Kulola akiwa hai badala ya Mungu,basi waliabudu mtu badala ya Mungu.Hili pia watumishi wa Mungu aliowaacha Mzee Kulola(EAGT) wajue Kulola ameondoka roho wa Mungu yupo,kama walimtii mzee Kulola ni kwasababu ya Roho wa Mungu aliyetumika pamoja naye,ambaye yeye bado yupo na ataendelea kuwapo.Mungu awabariki sana.

 5. Hii inaitwa nguvu ya dini ama “pepo la dini”. Tunahitaji rehema kwa Mungu ili kanisa liponywe.

  Kweli kama kanisa linachungwa na kuongozwa na wasiosamehe je Mungu amewasamehe?

  Wokovu ni zaidi ya kumpokea Yesu na kukiri kuwa umempokea Yesu.

  Mungu atusaidie.

 6. Mambo mengine bwana ukiyatafakari sana inashangaza!yaani utafirikiri yamefanywa na wapagani!Hii ndiyo tabu ya kufanya mambo kimwilimwili hata bila kuomba hekima ya Roho Mtakatifu!Mungu atusaidie kwakweli.

 7. Wenye dini zao bwana!

  Wanataka wakapigiwe magoti ndipo wakubali kusamehe kosa ambalo kimsingi halipo.
  Sijui nani wao atawasamehe makosa yao ikiwa wameshindwa kuwasamehe wengine makosa yao.

  Tena naomba mnisaidie kujua; Je walihudhuria hata hiyo harusi ya mwisho ya mtumishi wa Mungu au walikomea kuisherekea mahakamani tu?

 8. UPENDO WA WENGI UMEPOA!!
  Mkristo anapozaliwa mara ya pili, huyaanza “maisha mapya”, nao udhihirisho wa maisha hayo, ni kule kuishi kwake NDANI ya mipaka ya Neno la Mungu. Basi katika Efe 4:26-27 Neno linasema, “…jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.” Kwa matukio tuliyoyaona, yanadhihirisha kwamba, jua limetuchwea na uchungu wetu! Tena sijui majua mangapi yaliyotuchwea na uchungu wa MALI, ambao Ibilisi tuliyempa nafasi anaendelea kuikoleza tamaa hiyo ya Mali!

  “Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” UFU. 3:16-18

  Alipoonywa kuhusu “uvuguvugu” alionao, Hakusikia;
  Alipoonywa kuhusu “Utajiri anaojisikia”, hivyo vipawa na miujiza; Hakusikia,
  Aliposhauriwa kuhusu “Utajiri halisi”, Akampuuza Mshauri!!!

  Na sasa, AMETAPIKWA!!! Huyo hapo, ni Mnyonge, mwenye Mashaka, na Maskini; tena u Uchi, halafu ni kipofu!!! Huyo aliyejidhania ni MTAKATIFU, anagombea kipande cha ardhi, tena mchana kweupe, amekuwa ni WARAKA wa kusomwa na watu wooote, kwamba Kristo anagombea kipande cha ardhi; halafu, kwa ule upofu alionao, HAJUI hata kwamba dunia nzima inamtazama!!!!

  Kanisa, LIMEKOSEA WAPI???? Kipofu anaweza kurudi nyumbani kwa kujiongoza mwenyewe????

  Gbu all!

 9. Kusema kweli kitendo cha TAG kukimbilia mahakamani eti kuweka pingamizi kuhusu sehemu ya maziko ya mwili wa mtumishi wa Mungu,baba yetu wa kiroho na shujaa wa njili Askofu Moses Kulola ni AIBU tena ni Roho ya kigeni.Je,ni ushuhuda gani tutawaambia watoto wetu ambao tunataka wamjue Yesu na wawe na roho ya upendo na kusamehe???????
  Dr.Mtokambali hapo umepotoka.
  Hata kama kulikua na kutokuelewana huko nyuma msamaha uko wapi?
  Roho ambazo Yesu alizifia zinadhamani kuliko ardhi!!!
  Kweli TAG tumemuaibisha na kumhuzunisha Bwana Yesu katika hili.
  BWANA YESU ATUHURUMIE !

 10. Bwn apewe sifa?? Nimemsikia huyo mtumishi wa Mungu, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wadhamini TAG, Right Reverend, Archbishop, Daktari Mtokambali Barnabas, MKWEWE, Seniour & 1st Archbishop Assemblies of God Tz sijui na yy ni Daktari, au la, Emmanuel Lazaro( mjumbe wa bodi hiyohiyo), kupitia Radio WAPO International leo asubuhi, akitoa utetezi wake pasipo aibu, na hofu ya Mungu kbs, ya kuwa, walifanya hivyo, yaani, kule kwenda mahakamani kuzuia hayo mazishi yasifanyike ktk kile kiwanja cha kanisa la EAGT, Bugando, ati, kwa mujibu wa wao, lile eneo ni mali ya TAG, NA VIELELEZO vipo, yaani, ati walitaka court/judiciary redress regarding the ownership or the possession of the land, and the building (church)itself. Mimi nikaona huu ni utetezi tu baada ya kudhani mahakama ingalikuwa mkombozi wao wkt MZEE amepumzishwa kifuani mwa Ibrahim/Bwn Yesu.

  Ameendelea ktk huo utetezi wake ya kuwa, yeye binafsi amefurahishwa na kufarijika kbs ya kuwa, MZEE amepumzishwa mahala hapo, na ya kuwa, ati, AMERUDI kwao alikokuwa ametoka nyumbani kabla ya kwenda kuanzisha EAGT yake. Kitendo cha TAG kudai kuwa, lile eneo la Bugando, na EAGT Temeke vyote ni mali zao bado, ni km vile baada ya vyama vingi kuanzishwa nchini mwaka 1992, sheria ya au tume ya Jaji Nyalali, ILIHALALISHA ya kuwa, viwanja na mali zote zilizokuwa chini ya TANU/CCM kabla, baada ya vyama vingi kuanzishwa, ni MALI ZA UMMA, kwakuwa, kabla ya sheria hiyo kuanza, serikali iliyokuwako, ilikuwa na sheria ya kuwa, chama kimeshika hatamu, hivyo sasa, kuanzia mwaka 1992 kuendelea, ni mali ya UMMA, KWANI, NGnguvu ya umma ilitumika kuvijenga, NA SASA, HAOHAO umma UMEKUWA NI WATU WENYE IMANI TOTFAUTI ZA KIITIKADI.

  Hivyo, wao kuendelea kuving’ang’ania viwanja hivyo, ni makosa. Ndiposa, ht hao TAG kuendelea kudai ya kuwa, makanisa hayo ya Temeke na Bugando ni mali zao bado, ni ubabe tu km huo wa CCM kuendelea kuhodhi mali za umma, kwakuwa, zilikuwa ni mali za WASHIRIKA ambao walijenga kwa fedha zao. Nami ninafahamu kesi kadhaa ambazo, baadhi ya washirka na wachungaji makanisani, kwa upendo wa Mungu, walijitolea viwanja vyao kwa hiyari ya moyo mkunjufu, lkn, baada ya makanisa haya kupata hati za hivyo viwanja au usajili wa hayo makanisa yenyewe, leo hii itakuwa ni ajabu sana km haohao washirika ama wachungaji kuendelea kudai kuwa, hizo ni mali zao bado. Ht kanisa ninaloabudu miye, kiwanja kilikuwa, ni cha Mchungaji, lkn, baadaye alipokiuka maadili, alpotolewa kuwekwa pembeni, bado hakuilia ile hati ambayo hadi miaka ya 2000 hii toka 1990 amekuwa pembeni, na akakabidhi hati aliyoibadilisha mwenyewe Ardhi toka jina lake hd la kanisa ambalo yy tena halichungi kbs, anachunga sehemu nyengine kbs.

  Hekima hiyo ndiyo inapaswa kutumiwa na TAG, lkn, nilivyomsikia Dr. Mtokambali radioni, wanachokitaka wao TAG ni kuona ati viongozi wa EAGT wanawapigia magoti kwanza, kwa sababu nimemsikia akitamka radioni kuwa, ‘or we can have out of court settlement’, yaani, maridhiano nje ya mahakama. Naam, mimi ningeliwashauri tu ya kuwa, wakae chini na bodi yao ya Wadhamini, hiyo ya kuyaachilia mambo ya kale, ndiyo iwe zawadi yao kwa KUMUENZI MZEE, DR. KULOLA MOSES (EAGT), kwakuwa, hata huko TAG, IDADI KUBWA YA WACHUNGAJI, MAASKOFU, na washirika wengi, ni WATOTO wa imani wa MZEE, DR. Kulola, wapende, wasipende, history can’t be turned down, km ile ya mmoja wa wana mapinduzi waliomng’oa sultani Zanzibar, yaani, John Okello (Mganda, ambaye, viongozi wa leo wanajaribu kuifuta, haiwezekani. Na si ajabu, ht hyo Mtokambali mwenyewe, yamkini ni matunda ya injili ya MZEE. Mungu awabariki.

 11. Dada Lily , Asante sana kwa maneno yako matakatifu, yaani ni aibu kubwa wanasema wameokoka lakini wanafanya vituko ambavyo hata katika dini tulizotoka watu wana hofu ya kutokuvifanya. Mtumishi wa Mungu wa thamani kiasi hiki eti unataka asizikwe! Hii inanikumbusha maneno ya Paulo alipokuwa anawaambia wakorintho kuwa kwao kuna zinaa mbaya ambayo haipo hata katika mataifa, mtu aliyeokoka akianza kurudi mwilini inatisha sana, ni afadhali hata mtu ambaye hajaokoka kabisa.

 12. Hii kali sana wapendwa, mi sijawahi ona namna hii kwa umri wangu wote wa almost 40 yrs. Niungane na wenzangu hapo juu kusikitika sana kwa kitendo hicho cha TAG. Tunakoenda huko wapendwa haya madhehebu yanakua dini kabisa kama tulikotoka ambako migogoro ni kitu cha kawaida na kwa kila jambo. Yaani mwilini kabisaaaaaaaaaa. Kweli ni aibu sina cha kusema haihitaji uwe na stashahada kujua kuwa kilichofanyika si sahihi. Du Mungu wangu utusaidie!!!!

 13. Kwani jamani kuzuia Kulola asizikwe Bugando kuna tija gani? Watu wa TAG mlitaka azikwe wapi? Maziko ya mtumishi huyu yanawakera nini? Mimi kweli siwaelewi na mjue kwamba kama amefanya kazi nzuri ameifanya tu na hata sisi ambao sio wafuasi wa EAGT tunajisikia 100% kuwa ni Askofu wetu kabisa na hata mngekataa niko tayari kutoa kiwanja changu cha eka 3 azikwe hapo. Acheni udunia na someni I Kor 6 na msifikiri haki ya mtumishi wa Mungu inapatikana mahakamani. Turudini kwenye wito wetu.

 14. Inapendeza mno watumishi kuitoa kauli taamu km hiz, na inabariki sana. Inasikitisha tu, ktk kizazi km hk cha karne hii nyengine kbs, ambacho hakikuwahi kuona mivutano ya ASSEMBLIES OF GOD TZ, leo hii baada ya kifo cha shujaa wa imani ktk taifa hili zuri, uongozi wa TAG wameona ni vyema, ati, kwa maono yao, wakayaleta mambo ya huko nyuma hadharani kwa kukimbilia mahakamani KUUZUIA MWILI WA NABII wa Bwm usipumzishwe. Tendo hilo la viongozi w TAG, tuwe wazi jamani ni la kishetani kbs, is UNHOLLY ACT in the midst of the believers. Kitendo hicho kinahitaji TOOOOBA YA DHATI KBS mbele za Mungu, kwani, walilenga kuzuia Upanga wa Bwn usitende haki, yaani, Malaika wa Bwn w ulinzi walioandaliwa kuupokea mwili huo na kuupa ulinzi kwa ni mwili w mtakatifu wake, kwa kwenda mahakamani, ili kuanze mashindano ya kimahakama kt ya TAG na EAGT, kiisha dunia itucheke. Ndg zangu, binafsi, nimeshushwa sana moyo, na nimewadharau mno viongozi madaktari wa TAG. MUBARIKIWE.

 15. imefika wakati,watumishi wa Mungu inabidi wawe watu wa rohoni.Kwa walio rohoni ni wakati wao wa kuyatafakari matendo makuu ya Mungu na kumshukuru Mungu kwa ajili ya mtumishi wake.Watumishi wa Mungu TAG kitendo cha kufungua kesi ni jambo la kuhaibisha sana.Tulitegemea kuona ukomavu wa kiroho kwa kanisa hilo mama hapa Tanzania.Wapendwa kwa wanaofuatilia habari za mashujaa wa Imani,Mwaka Juzi amefariki mtumishi wa Mungu Rud lack(Mwandishi wa kitabu “sitaogopa kupeleka injili katika nchi za kikomunist”,na mashujaa wengine wengi.Tumwombe Mungu atupe neema na sisi ya kuitimilza huduma zetu na wala siyo wakati wa kufunguliana kesi,ni nyakati za kusameheana na siyo kiuhukumiana.Mtumishi wa Mungu Moses amelala “inuka wewe Joshua badala ya Musa”,Inuka wewe Elisha badala ya Eliya”-Ebrania 11-“wameorodheshwa mashujaa wengi wa imani…..Askofu Moses ameungana nao,Je mimi na wewe?Kwa neema ya Mungu tutaweza.Bwana ametoa,Bwana ametoa,Jina lake libarikiwe.Amen

 16. daa! MUNGU WANGU HAYA MAMBO YATAISHA LINI JAMANI! KTK msimba mkubwa kama huu mpaka wasio mjua Mungu wametetemeka, tunafanya ivi!, nimesiktika kweli na kulegea kila kitu.

 17. PINGAMIZI LA T.A.G KUZUIA ASKOFU KULOLA KUZIKWA EAGT BUGANDO LASHINDIKANA

  Katika hali isiyotarajiwa hapo jana bodi ya wadhamini wa kanisa la Tanzania Assemblies of God nchini jijini Mwanza iliamua kwenda mahakamani kuwasilisha pingamizi la kutoruhusu mwili wa aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa la E.A.G.T marehemu Dkt. Moses Kulola kuzikwa katika viwanja vya kanisa hilo lililopo maeneo ya Bugando jijini Mwanza wakidai ni mali yao jambo ambalo hata hivyo haikuwezekana na mwili huo utazikwa kama ilivyopangwa mapema hii leo.

  Akizungumza na WAPO Radio Fm kupitia kipindi cha habari Yaliyotokea askofu Lameck Mkumba wa E.A.G.T amesema ameshangazwa na uamuzi huo kwakuwa waumini wa kanisa la E.A.G.T wamekuwa wakilitumia kanisa hilo la Bugando kwa muda mrefu sasa bila kuwapo matatizo yeyote hadi kuibuka kwa suala hili ambalo hawakutarajia” Mimi mwenyewe nina miaka zaidi ya 15 nikiwa muumini na niliokoka ndani ya kanisa hili la Bugando E.A.G.T” amesema askofu Mkumba

  Aidha askofu huyo amesema baada ya kuona wenzao wametumia taratibu za kisheria kwakutumia bodi ya wadhamini wao mahakamani ikabidi nao pia kutafuta uwakilishi wa kisheria ambao uliwasimamia vyema kwakuwasilisha vielelezo na maelezo ya msingi ambayo mahakama iliridhika nayo nakuamua kuwapa kibali cha kuendelea na maziko ya askofu Kulola katika viwanja hivyo.

  Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la E.A.G.T City centre la jijini Dar es salaam Florian Katunzi amesema licha ya changamoto zote za kibinaadamu zilizojitokeza bado askofu Moses Kulola ataendelea kuwa shujaa wa imani nchini kutokana na kufahamika kwake vyema katika suala la injili na kulitaka kanisa kwa ujumla kukaa tayari kwakuwa Yesu anakuja na kuwataka kuachana na migongano ambayo haisaidii kanisa kusonga mbele.

  Wakati huo huo askofu mkuu wa kanisa la T.A.G Barnabas Mtokambali anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake saa nne asubuhi leo kwaajili ya kutolea ufafanuzi baadhi ya mambo baada ya kuulizwa na mtangazaji wa WAPO Radio FM Beatrice Kamanga kupitia kipindi cha Yaliyotokea akitaka kujua amepokeaje hali iliyojitokeza huko Mwanza hapo jana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s