Roho ya Kukataliwa

kukataliiwa

Roho ya kukataliwa inawasumbua watu wengi. Wengi wanaosumbuka na kukataliwa inawezekana walikuwa na wazazi wasiojali, wazazi walitengana, wamelelewa na mzazi wa kambo, hawakuwa vizuri darasani, n.k. Kukataliwa kunaumiza sana na kunaua kabisa hali ya kujiamini na shetani huitumia sana kuharibu maisha ya watu. Shetani anawafanya watu wasahau kabisa juu ya upendo wa Mungu na kuendelea kuumia na kuteseka.

EFE. 3:19 “na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.”

Kukataliwa kunaleta vidonda kwenye hisia na visipotibiwa hukua na kuwa vidonda vya kiroho kama kutokusamehe, wivu, chuki, uchungu na kumlaumu Mungu. Vidonda hivi hufungua milango kwa roho chafu kukuingilia kupitia milango hiyo. Shetani anafurahia moyo wako ukijaa mawazo mabaya juu ya watu wengine unaowaona kwamba hawajakutendea mema.

Kukataliwa kunamfanya mtu kuwa na tabia zifuatazo:
1. Uasi
2. Unafiki (ukiwa mbele za watu fulani unabadilika ili ukubalike)
3. Kukataa wengine
4. Kila wakati kujihisi kuwa unakataliwa
5. Kuhitaji sana kukubaliwa na kila mtu
6. Kujihurumia
7. Kutokuwa tayari kukosolewa au kusahihishwa
8. Kutokuweza kupokea wala kuonyesha upendo.
9. Kumlaumu Mungu kwa hali uliyonayo
10. Kiburi
11. Ukiwa hata ukizungukwa na watu.
12. Kujiona huna thamani, wala tumaini
13. Wivu, chuki na husuda.

Wengine wanahisi kukataliwa wakati si kweli. Roho hii ya kukataliwa inakufanya uone kama kila ambaye hajafanya jambo fulani kukusaidia au kukufurahia basi anakukataa. Biblia inasema aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Pia kuna wanaojikataa wenyewe na kupelekea kujichukia. Hali hii hutokana na kushindwa kujisamee kwa kosa fulani ukilotenda siku za nyuma na likakuletea madhara makubwa.

Unapoweka thamani yako kwa wanadamu ni lazima utaona kukataliwa na kujikuta unaruhisu roho za kukataliwa kuingia kwako. Lazima utambue kuwa thamani yako inatoka kwa Mungu na si wanadamu wanakuonaje. Haijalishi nani anasema nini bali tafuta Mungu anasema nini. Acha kumlaumu Mungu na kujilaumu unayopitia, biblia imasema mapito ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humlinda na hayo yote.

Usiruhusu chuki, uchungu, hasira na wivu vipate nafasi ndani ya moyo wako. Soma neno la Mungu lijae ndani yako na maombi kwa wingi. Kataa roho ya kukataliwa isipate kibali ndani yako kwa kuondoa milango ambayo ni kutokusamehe, chuki, wivu, uchungu na kumlaumu Mungu. Usiangalie yule aliyekutendea mabaya na kukukataa kama vile yeye ndiye mwenye hatima ya maisha yako bali muangalie Mungu aliyeahidi kuwa nawe siku zote.

EBR. 13:5b-6
“kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”

Mambo ya kufanya kushinda kukataliwa
1. Mruhusu Roho mtakatifu akuonyeshe umeumizwa wapi na kwa kiasi gani kwa kukataliwa.
2. Samehe wale waliokuumiza
3. Tupilia mbali matunda ya kukataliwa: chuki, hasira, uasi, uchungu n.k.
4. Kubali kuwa Mungu amekukubali kupitia Yesu Kristo.
5. Jikubali

ZAB. 71:5-7, 13 
“Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.    Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.    Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi, Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.    Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.”

Soma pia Ebrania 4:16 Zaburi 23 1 Samwel 53:4

–WomenofChrist Blog

Advertisements

11 thoughts on “Roho ya Kukataliwa

 1. Kaka Steve nilikuwa nafuatilia maelezo yako kuhusu hii roho ya kukataliwa ila kiukweli umenichanganya kabisa ulipoanza kulist vitu ambavyo ni dhambi , hapa kwenye KUTUMIA UTANDAWAZI(nisaidie kuelewa hapa, maana hata kuweza kuingia kwa mtandao huu na kuchangia ni mambo ya utandawazi, JE NI DHAMBI pia na mbona nawe upo humu wapata matunda ya utandawazi? ) pia uliposema MWANAMKE KUHUBIRI MADHABAHUNI , ungeongezea basi na maelezo kidogo maana vitu vingine si vya kutaja tu kirahisi rahisi hivyo, pia kuna maswali ya kaka Siyi hapo juu ungekuja uyajibu pia ili twende sawa.

 2. Shalom kaka Steve,
  Nimekusoma vizuri rafiki. Na nimekufuatilia vizuri kama ifuatavyo;
  1 Samuel 15:23-26, inazungumzia Sauli kuliasi neno la Mungu na hivyo kukataliwa na Bwana kuwa mfalme.
  2falme 17:20- Israel waliziasi sheria za Mungu, Mungu akawakataa.
  Yeremia 2:37, kadhalika Biblia inazungumzia uasi wa sheria/neno la Mungu kwa taifa la Israel-rejea mstari wa 29, na hivyo Mungu aliwakataa kweli.
  Ndg Steve, kwenye pachiko la tarehe 20/09/3013, ulielezea hali ya mtu kuwa na roho ya kukataliwa vizuri. Maelezo yako yalijikita zaidi kufafanua maana ya mtu kukataliwa na mtu/watuwengine. Pachiko lako hili la sasa, umeonesha mtu/watu kukataliwa na Mungu kwa kuvunja sheria zake/neno lake.
  Nimeshindwa kukuelewa hapa kidogo kaka. Una maanisha kuwa na Roho ya kukataliwa ni sawa na mtu aliyeliasi neno la Mungu na hivyo Mungu kumkataa mtu huyo? Au kuna mazingira gani tunaweza kuchora na kumtofautisha mtu mwenye roho ya kukataliwa na mwanadamu/wanadamu wenzake na yule anayekataliwa na Mungu yaani mdhambi? Please, naomba ufafanuzi hapa!!

 3. Kwenu nyote, hasa kwako Bwana M. J. N. Siyi
  Nimechelewa kujibu kwa mda kutokana na kukumbwa na majukumu makubwa ya kikazi
  Sasa naendelea kujibu swali lako linalouliza….
  swali na. 3
  ” Je!Kuna msingi wowote wa dhana hii ya ROHO YA KUKATALIWA ndani ya Biblia au mapokeo tu? ”

  Uthibitisho wa kibiblia upo na baadhi ni hii…
  1Samuel 15:23-26
  2 Wafalme 17:20
  Jeremia 2:37
  na mingine mingi

  NINGEPENDA KUKUFAHAMISHA KUWA SI KILA UOVU AU TABIA MBAYA NA ROHO MBAYA ZOTE ZIMEELEZEWA KINAGAUBAGA KWENYE BIBLIA
  ILA KUPITIA ROHO MTAKATIFU AMBAYE NDIYE MSAIDIZI WETU HUTUSAIDIA KUPATA KUJUA LIPI JEME NA LIPI BAYA KATIKA ULIMWENGU HUU ULIOJAA KILA AINA YA CHANGAMOTO KILA KUKICHA.

  Labda nikupe mifano michache tu ya aina ya dhambi ambazo zipo dhahiri lakini biblia haijazisemea imenyamaaza kimya…
  1. kuvuta sigara
  2. kunywa/kugusa pombe (na sio kuwa mlevi) swali ni kuwa wengi wanalewa hata bila ya kunywa
  3. mwanawake kuhubiri mdhabahuni
  4. Kutumia utandawazi
  5. kusoma elimu dunia inayosema mwanadamu katokana na sokwe huku ikikinzana na biblia
  6. Na mengine mengi mbayo ukiyalist hapa tutakesha

 4. Steve,
  Ubarikiwe kaka kwa jitihada ambazo kimsingi ni nzuri za kutuelmisha kwa hili. Binafsi nimeyabugia haya uliyoyaleta. Kwa sasa nayatafuna ili nione kama yanakubali kumezwa ama la!! Kimsingi nakushukuru sana, nasubiri kupokea zaidi kutoka kwako na kwa wadau wengine ndani ya blog hii kuhusiana na mada hii. Miongoni mwa maswali uliyoyajibu, naona ulipitiwa ukasahau swali moja. Naomba kukukumbusha swali hilo:
  3. Kuna msingi wowote wa dhana hii ya ROHO YA KUKATALIWA ndani ya Biblia au mapokeo tu?
  Ubarikiwe mjoli.

 5. dear all,
  Nashukuru kwa kunihitaji nichangie kwa kiwango nilivojaliwa kufahamu juu ya hii roho ya kukatalika.
  Somo hili ni refu kama nilivokwisha waeleza hivyo tutakuwa tunajifunza kwa hatua;

  ROHO YA KUKATALIKA:
  >>> Hii ni roho mbaya/chafu/balaa/nuksi inayomvaa mtu ili kumwondolea uso wa kupata kibali/baraka/neema mbele za mungu na hata kwa wanadamu.
  >>> Ni roho mbaya sana ambayo inamfwatilia mtu/familia/ukoo kuhakikisha haishi na wengine kwa mashirikino na umoja na amani- inamfanya aonekane mbaya tuuu bila hata ya sababu maalam. Na inapelekea asifanikiwe katika maisha yake na hata akifanikiwa ni kwa kiwango kidogo sana kulinganisha na juhudi anazowekeza. Kwa ufupi maisha yake yametawaliwa na NUKSI, BALAA na MIKOSI isiyo na misingi yoyote.
  >>> Pia inahakikisha kila alifanyalo halifanikiwi na halipati kibali popote pale, bila kujali anafanya kazi kwa juhudi kubwa kiasi gani.-na kama ni masomo anaweza asome sana ila anakosa usirikiano kutoka kwa wenzake na hata walimu, mwishowe anafeli – kama ni kama ni kazini basi wafanyakazi wenzake wanamtenga kikazi nahata promotion hapati, yaan anajikuta yupo peke yake mda mwingi na hana marafiki hata wawili na hata akiwa nao wanafanyika kero kwake maan wanakuwa wanamsema na kumwona mkosaji tu bila sababu ya msingi.

  ( KWA UTANGULIZI HUO NAFIKIRI MMEPATA PICHA FULANI JINSI ROHO YA KUKATALIKA ILIVYO MBAYA NA INAVOFANYA KAZI KWA MTU BILA YEYE KUJIJUA AU KWA KUJIJUA.
  NAOMBA MZINGATIE HILI ; MTU/FAMILIA/UKOO UNAOKATALIKA HAIJALISHI ANAFANYA KAZI BIDII GANI NA KWA KIWANGO GANI WALA ANAJITAHIDI KUWA MWEMA/MUUNGWANA KIASI GANI KWA MUNGU NA KWA WENZAKE – HII ROHO YA KUKATALIKA IKIKUINGIA YANI WEWE UTAONEKANA NI MBAYA TU EITHER UNA TABIA NZURI AU MBAYA, UNAFANYA KAZI KWA KUJITUMA/BIDII AU KWA ULEGEVU )

  Labda sasa nianze kuyajibu maswali yenu kwa uchache;

  Swali Na. 1
  ” hivi mtu anaposema roho ya kukataliwa, roho, ni pepo? Hali? Mzimu? Au ni nini? ”
  Ndio ni kweli kama ulivosema Roho zipo za aina mbili katika falme mbili tofauti
  Falme ya Mungu tuna Roho Mtakatifu (Holy Ghost/Spirity) na Falme ya Shetani tuna Roho Chafu/Mbaya ambayo nayo ndani yake imejigwanya katika makundi mbalimbali kutokana na kazi husika inayotaka kufanya na kwa wakati gani, kwa mfano tumeshasikia mapepo yanayotumwa kuleta magonjwa fulani fulani, mapepo ya wizi/ufisadi, mapepo ya uzinz/ukahaba, mappepo ya uchafu, uchawi na mambo kama hayo. Ni kwamba haya mapepo ni kama Wizara mbalimbli anazozitumia shetani kukamilisha kazi yake aliyoikusudia hapa dunia kuwa ahakikishe anampata watu wote ili aende nao jehanamu. sasa mojawapo ya Wizara ni hii ya UCHAWI /ULOZI ambao ndani mwake unakutna na idara ya PEPO LA ROHO YA KUKATALIKA linalohakikisha linakutesa basi tu umwone Mungu hafai na umuasi, huu mfano ni kama pepo linavoweza kukuletea ugonjwa, umaskini na balaa nyingine tu ilimradi uteseke na kuvurugikiwa na mwishowe kumuasi Mungu.
  -Roho kwa kingereza ni Spirity maana yake ni kuwa ni kitu/hali usichoweza kukiona kwa macho ya kawaida ya damu na nyama ila katika ulimwengu wa roho unakiona na kuhisi vyema kabisa.
  -Pepo ni vikaragosi vinavotumika na shetani kutumwa kwend kufany kazi ya mwovu shetani katika ulimwengu wa roho(invisible world)

  Kwahiyo unaposema mtu ana Roho ya Kukatalika una maanisha kuwa anamilikiwa na roho mchafu katika ulimwengu wa roho, yaani badala ya roho mtakatifu kumjaa na kumuhuisha mtu inakuwa ni kinyume chake. Hili pepo likishatumwa kwa mtu/familia basi linawavaa na kuwabadilisha sura na tabia ya heri mliyonayo na kuwavisha roho mbaya ya kukatalika (ambayo unaweza ita ni mzimu wa kutokubalika kwa chochote kile ) ktk ulimwengu wa roho , mtu akikuangalia hakuoni wewe kama John/Daudi/Edson/Eva/Anna tunayemjua ila unaonekana ni wewe kwa sura ila kiroho unakuta watu wanakuchukia bila sababu na pia wanakutenga katika mambo mbaimbali bila sababu na hufanikiwi katika mambo yako.

  =kwa kumalizia ni kuwa pepo anapotumwa kuja kumvaa mtu ili kumharibu anamjaza roho chafu ya nuksi na balaa ambayo unawez iita ni kama mzimu wa aina yake ila haumfanyi mtu akapoteza personalty yake kwa kuwa kichaa au mwendawazimu. yote hiyo ipo kwenye kapu la ulimwengu wa roho ambao wewe huwezi uona hadi uingie rohoni, basi mwisho wake ndo hiyo uakayoiita ni Hali ya kitabia katika ulimwengu wa roho inavofanya kazi ktika kuwatesa watu wa Mungu.

  Swali Na. 2
  ” Je, kuna roho ya kukubalika? Na kama ipo, je tunawezaje kutofautisha roho hii na jinsi Mungu anavyowainua watu wake? ”

  Roho ya Kukubalika ipo na kwa jina lingine inaitwa hata kwenye bibia imetajwa sana kama “KUPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU” ukipata kibali mbele za mungu maana yake unakuwa umejawa na mungu kukupenda/kukubariki kwa namna nyingi/kukulinda/kukupa amani/kufanikiwa katika mambo yako, na zaidi ya yote KUKUPA USHINDI – KUKUSHINDANIA KATIKA MAGUMU YOTE.

  Kuhusu kulinganisha na jinsi mungu anavowainua watu wake nadhani ni vigumu maana hata kutambua huyu ni mtakatifu kweli na huyu sio ni kazi sna kwasababu sisi sio mahakimu bali ni watumishi wa mungu tu. Anayejua ni Mungu pekee.
  ++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
  UKWELI NI KWAMBA YAPO MAFANIKIO YANAYOTOKANA NA MUNGU KWA MTU KUJIBIDISH NA KUMTEGEMEA MUNGU NA PIA YAPO YANAYOTOKANA NA MWOVU HAYA YAPO WAZI NA HAYANA UBISHI.
  SHIDA YA KIPINDI HICHI TUNACHOISHI NI KWAMBA KUNA MCHANGANYIKO MKUBWA KATI YA UOVU NA UDINI NA ELIMU/MARIFA MEGI HIVYO MATOKEO YAKE TUNASHINDWA KUM-JUDGE MTU MOJA KWA MOJA MAANA MTU ANAKWAMBIA NIEOKOKA NA ANAPATA MAFANIKIO MAKUBWA LAKINI UKIWANGALIA VIZURI ANA MICHANGANYO MINGI AMBAYO MINGINE SI YA HAKI NA KWELI YA MUNGU. KWA HIYO MHUKUMU ABAKI KUWA MUNGU PEKEE.
  +++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
  {NI KWELI KWA HARAKA HARAKA UNAWEZA ONA MBONA NI MAMBO YA KAWAIDA KATIKA MAISHA YA BINADAMU ILA KIUKWELI MTU ANAYEKATALIKA NDIE ATAKAYE KUAMBIA SIO KAWAIDA KAMA UNAVOHISI.
  Hapa chini ni sifa kuu muhimu za MTU anayekatalika…….mwenye ROHO YA KUKATALIKA
  1. Lazima yeye mwenyewe atajihisi kuwa ana matatizo either kwa kuonewa au kwa kujitakia
  2. Atakuwa anahisi kutengwa na jamii/marafiki/watu wa karibu nae bila sababu maalum
  3. Atakuwa mwenye huzuni mda mwingi na MPWEKE
  4. Atakuwa anahisi watu wanamchukia yeye peke yake hivyo atajawa hasira
  5.Atajawa ubishi na ushindani kwa kuhisi watu hawamkubali kwa lolote analosema
  haya ni baadhi ukijumlisha na yaliyotajwa hapo juu kwenye kichwa cha mada hii utapata picha huyu anayezungumzwa ni mtu wa aina gani.

 6. Seleli,
  Ha ha haha a!! Utukufu kwa Bwana mjoli wa Bwana. Nimefurahi kukuona japo ulipotea kitambo hivi!! Tumekosa michango yako makini!! Karibu sana kamanda wa jeshi la Bwana.

 7. Siyi,

  Good questions indeed, I like them! Great appearance of yours on this topic man! Safi sana. Your questions, if well answered, will help us all a lot since, are well brain-cooked, nicely Biblical provoking, spiritually welcoming and Godly truths searching. Mimi pia nangoja kwa hamu fafanuzi au mwendelezo kwa mapana yake kama alivyodokeza Steve na pia naweza changia baada ya mwendelezo au ushuhuda binafsi wa Steve ukifanyika kwanza maana itakua kama muongozo.

  Press on

 8. Steve,
  Nashukuru kwa mwitiko wako ndg yangu. Ningependa nikuombe wewe mwenyewe maadamu unalifahamu somo hilo vizuri, tafadhari leta somo hilo kwa uzuri wake ili litujenge na akina Siyi. Maana mimi nashindwa kuelewa, hivi mtu anaposema roho ya kukataliwa, roho, ni pepo? Hali? Mzimu? Au ni nini? Je, kuna roho ya kukubalika? Na kama ipo, je tunawezaje kutofautisha roho hii na jinsi Mungu anavyowainua watu wake?

 9. Ndugu, MJ<N<Siyi kwa kukuhakikishia ni kuwa hii roho ipo na mimi binafsi nimekwisha ipitia na nafahamu utofauti uliopo kati ya MAJARIBU YA KAWAIDA na ROHO YA KUKATALIKA.
  Unajua Ndugu hii roho kama maelezo ya mada yanavyojieleza ni roho mbaya sana ambayo inakuwa na sifa kama zilivoainishwa hapo juu. Ninachotaka kusema ni kuwa anayekatalika anakuwa ankuwa ana degree za juu sana za utofauti na yule anayepitia majaribu ya kawaida.

  Ndomana nikasema hili somo inatakiwa liandikwe kwa urefu sana ili liweze kueleweka vizuri hasa kwa wale wasiofahamu juu ya hii roho. Maana bila hivo ni rahisi mtu wa kawaida kuchanganya na kutokuelewa kabisa.
  Kwa ufupi inatakiwa lifundishwe kwa hatua ya kwanza ya pili na ya tatu ndo mtu ataelewa vyema.

 10. Maswali
  1. Roho ya kukataliwa ni nini? Ni pepo linalomkumba mtu au hisia tu?
  2. Tunawezaje kukubaini na kisha kukutofautisha kati ya KUWA NA ROHO YA KUKATALIWA na TESTS ANAZOZIRUHUSU MUNGU ZITUPATE MAISHAINI MWETU KWA KWA AJILI YA KUIMARISHA IMANI?
  3. Kuna msingi wowote wa dhana hii ya ROHO YA KUKATALIWA ndani ya Biblia au mapokeo tu?

 11. Tunashukuru sana kwa mafundisho yako hapo juu pamoja na comments ulizoweka kwa msaada wa mtu anayesumbuliwa na roho ya kukatalika, nafikiri kwa namna moja ama nyingine itasaidia wengi.
  Ila mimi kwa kiasi ninachofahamu kuhusu roho ya kukatalika ni somo pana sana na kama kweli una nia ya kumsaidia mtu anaesumbuliwa na hii roho kuna mengi sana hujayagusia. Kiufupi hili somo linahitaji maelezo mapana sana na ya kiunagaubaga ili kumsaidia mtu anaekatalika.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s