Mitume walibatiza ubatizo upi?

ubatizo

MATHAYO 28;19-20

Yesu anawaagiza wanafunzi wake kuwa waende ulimwenguni mwote wakawafanye mataifa kuwa wanafunzi na kuwabatiza kwa JINA LA BABA MWANA NA ROHO mtakatifu, na katika MATENDO 2;38 Petro anasema tubuni mkabatizwe kwa jina lake YESU KRISTO. Je ni kwanini mitume hawakubatiza ubatizo walioagizwa na Bwana wetu YESU Kristo?

–Emmanuel Charles

 

Advertisements

86 thoughts on “Mitume walibatiza ubatizo upi?

 1. Ubarikiwe ndg Lwembe.
  Ni ukweli usiopingika wanaowapinga Mitume wa Bwana Yesu ni wapinga Kristo.Kuwa Mpinga Kristo ni kuwa Mpinga Neno,na kuwa mpinga Neno ni kuwa mpinga YESU (Luka Mtakatifu 10:16)
  KAMA MTU YEYOTE ANAYEDAI KUWA NI MKRISTO HUJABATIZWA KWA JINA LA BWANAYESU KRISTO (MATENDO 2:38-39, 8:14-16, 10:48, 19:1-5) BADO NI MPAGANI

 2. @Brighton Jonathan

  1: Mdo 1:5
  “…ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.”

  1Kor 10:1-2
  “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari”

  Unauliza, Katika hiyo mistari ya Biblia maji yalitumikaje?
  JIBU:
  1: Maji ktk Mdo 1:5, ktk faida ya kiungu kwa kadiri ninavyofahamu, ni yenye kutakasa, ktk jambo hili, yanatakasa dhambi kulingana na Neno lililoliongoza jambo hilo. naye mjumbe aliyekuwa na Neno hilo ni Yohana, ndio maana Ubatizo huo unaitwa wa Yohana.

  2: Ubatizo ktk Maandiko tunauona kwanza kwa Yohana Mbatizaji, akiwa ndiye mjumbe wa jambo hilo hata jina lake kuongezewa huduma hiyo. Nayo tafsiri ya jambo hili kimatendo ndiko huko KUZAMISHWA majini, ambako RM anakufunua ktk nyaraka za Paulo hapo anapolileta jambo hilo la Ubatizo ktk maana kamili ya kufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Ndipo anaendelea kutuonesha umuhimu wa jambo hilo hapo anapoturudisha kwa Israeli ktk siku aliyowatoa Misri, kumbe hao pia aliwabatiza hapo alipowapitisha chini ya bahari akiwa amezisimamisha kuta za maji zenye nguvu ya kufisha ili awapitishe hapo kusanyiko lake lote ktk mkono wa mjumbe wake Musa, ndiko huko kubatizwa kuwa wa Musa, nayo maji hayo ya bahari yametumika ktk maana ile ile ya kuwasafisha!

  Basi ni katika maana hii hii ndio unauona Ubatizo ukibadilika kutoka wa Musa kuja wa Yohana na mwisho ndio huu wa Bwana Yesu Kristo unaofunuliwa ktk Mdo 2:38 ukituonesha kwamba huyo ndiye Mjumbe wetu!!

  Gbu!

 3. @ Brighton Geita,

  Shalom!

  Nitajaribu kuyajibu maswali yako, kulingana na ninavyofahamu, kwa ushahidi wa Maandiko kama hivi:

  1: YOHANA MBATIZAJI alibatizwa na nani?
  JIBU: Yohana Mbatizaji ni mjumbe wa ahadi, Mk 1:2 “… Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.” Suala la yeye kubatizwa halijaoneshwa ktk Maandiko. Pia tunapozungumzia yeye kubatizwa, itatufaa zaidi iwapo tutajiweka ktk ufahamu kamili kuhusu huduma yake, Mk1:4 “Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.”

  Kwahiyo kimsingi huo ubatizo uliandamana na kuondolewa kwa Dhambi. Lakini hapo hapo tunafahamishwa kwamba huyo mtoto alikulia huko nyikani mbali na makazi ya watu, (Luk 1:80 “Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.”) Basi ktk hili ni lazima Mungu awe amehusika na huko kumtenga na jamii yake ambayo ingeweza kumchafua hata asifae tena kuubeba huo Ujumbe uliokuwa na Umuhimu wa kipekee sana ktk Programu ya Mungu ya Wokovu, yaani ingemlazimu naye abatizwe akiisha kuziungama dhambi zake! Lakini tunaona akitokea huko nyikani na kuianza kazi moja kwa moja, ishara ya kwamba Mungu alikwisha kumtakasa hapo alipomtenga, kwani hakuna mchafu anayeweza kubeba Ujumbe wa Mungu, maana kubeba Ujumbe wa Mungu ni kumbeba Mungu!!

  2: Neno maji kibiblia lina maana gani?
  JIBU: ki Biblia, neno maji lina maana zaidi ya moja. ya kwanza ni maji ya kawaida kama inavyoonekana ktk Mwa 1:2 “… na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji”; ndio haya maji tunayoyatumia ktk kunywa, kusafisha, na kutunza uhai. pia neno maji hutumika katika semi kulingana na ule umuhimu wake kwa maisha ya viumbe, basi kutoka ufahamu huo kwamba pasipo na maji hakuna uhai, ndipo unamuona Kristo akilifunua zaidi jambo hilo kuhusu uzima ktk maana ya umuhimu kamili wa Neno la Mungu anapolifanananisha na chemchemi; Yn 4:14 ” walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.” Haya ndiyo Maji ya Uzima, yaani NENO la Mungu; Yn 7:37-39 “…Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.” Mstari wa 39 unalifafanua jambo hili: 39 “Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye …”

  Na maana ya tatu ya neno maji ni hii tunayoipata ktk kitabu cha Ufunuo. 17:1 inayataja maji, “… Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi” na ktk mstari wa 15 analifumbua fumbo hilo, ” Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” hii ndio maana ya tatu ya neno maji, ni watu!

  3: Mitume walibatizwa na ubatizo upi?
  JIBU: Ubatizo wa kwanza walioupitia mitume ni ule wa Yohana, uliowapa Ondeleo la Dhambi lililowastahilisha kumpokea Kristo. Maana kama nilivyokuambia huko juu, Mungu hawezi kushiriki uchafu, ndio maana wote wenye kumpokea hubidi kwanza awaondolee dhambi zao ndipo awe na ushirika nao. Wakiwa ni hao walio ondolewa dhambi zao, walimpokea Kristo na wakadumu ktk Kristo hata kustahili Ahadi waliyopewa na Yohana kuhusu Kristo, hiyo ya kuwabatiza kwa RM ktk Yn 1:33 “Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.” unaweza kuiona tena ahadi hiyo ktk Mdo 1:4-5 “Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.”

  Basi jambo hili liliwatimilia siku ya Pentekoste, waliupokea Ubatizo wa RM; Mdo 2:3-4 “Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu.” Huu ndio Ubatizo wao wa pili, wakiisha kuupokea huo wenye kuziondoa Dhambi zao, ule wa Yohana, ambao mkristo wa leo kabla ya kuupokea huu wa pili, naye anapaswa awe ameupitia ule wa kwanza ambao ndio huo unaooneshwa ktk kitabu cha Matendo ya mitume kuanzia siku hiyo ya Pentekoste walipotoka kuihubiri Habari Njema, Mdo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

  Kwa kiasi nimejaribu kuyajibu maswali yako kwa kadiri ya ufahamu wangu, ninaamini wapendwa wengine watapajaza palipoyapungukia maswali yako.

  Gbu!

 4. SHALOM. Hakuna mtu aitwaye Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu Duniani.Hilo lilikuwa fumbo (MATHAYO 13:34-35)Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni Bwana Yesu Kristo.Soma-MATENDO 2;36, 4;10-12,YOHANA MT,17;6,11-12WAFILIPI 2;10-11.Mitume ndio walioachiwa Maagizo na wengine wote wanaotaka kwenda Mbinguni hujenga kwenye Msingi huo,soma-1KOR 3;10-15, LUKA 10;16,WAEFESO 2;20.Mitume Waliokuw na Ufunuo Walibatiza KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO.Soma BIblia Yako vizuri-MATENDO 2;38, 8;12,16, 10;47-48, 19;4-5,WAKOLOSAI 3;17.Sasa kama HUJABTIZWA Kwa Jina La BWANA YESU KRISTO, UMELAANIWA( SOMA KWA MAKINI-WAGALATIA 1:8-9).AMEN

 5. Napenda kufahamu YOHANA MBATIZAJI alibatizwa na nani? Alafu neno maji kibiblia lina maana gani?na mitume walibatizwa na ubatizo upi?

 6. Lwembe,
  Unataka tuulizane maswali ya kitoto kiasi hicho!

  Labda na wewe nikuulize kwamba; kwa nini hakuwaagiza mitume wakabatize kwa jina lake, yaani ”nendenei mkawabatize kwa jina langu” kama alivyofanya wakati anawaagiza kwenda kutoa mapepo na kuponya magonjwa kwa jina lake?

  Au kwa nini hakuwaagiza wakatoe mapepo kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt.?

  Kwa nini akatofautisha agizo la ubatizo na agizo la kutoa pepo na kuponya magonjwa kwa habari ya matumizi ya jina? Au alikuwa anajifurahisha tu bila kuwa na maana yoyote ya msingi katika hizo tofauti?

  Je kinachofanyika katika kumtoa mtu pepo kina hadhi sawa na kinachofanyika katika kumbatiza huyo mtu?

  Ni rahisi sana kumwambia mwenzako ajikague ufahamu wake ikiwa tu utajiaminisha kuwa wewe unawaza sahihi sana.

  Kila wazo lina maana katika shule ya fikra.

  Usi-undermine wazo la mtu!!

 7. Sungura,

  Kubadilika kwa maelekezo ndio hivyo, mpaka uwe umeyaona, yaani umepata uelewa wake, vinginevyo utaishia kujiridhisha ktk tafsiri zako na zikakupa ahueni, maana ndicho unachokiona na kukielewa, huwezi kuvuka uendelee mbele ya ufahamu uliofungwa!

  Unaponiambia kuwa, “maana ya kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt, ndiyo hiyo ambayo mitume wanaiita ‘kubatiza kwa jina la Yesu’.” na kisha ukajilazimisha kubaki katika uelewa wa nyuma, inashangaza kidogo, kwanini usiungane nao mitume mkaendelea pamoja? Wenzako wanalo JINA wewe unayo “maana” ambayo haitambuliki na yeyote yule, Mungu amesema “Jina”! Hakuna mahali mitume walipoambiwa watafute “maana” wameambiwa JINA!!!!!

  Pia nilikuonesha kuwa KRISTO alikuwa nao mitume all the way, sijui kwanini unapenda kuwatenganisha! Amekaa nao siku Arobaini, kwanini wasimuulize “Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu” ndio lipi? Wewe unadhani kuwa wamejikurupukia tu??? Wanayo Kweli yote!!!

  Halafu jaribu kujikagua ufahamu wako, yawezekana katika kuukimbia kwako ukweli, umeishia kujichanganya! Hebu angalia hili unalong’ang’ana nalo licha ya kwamba linakuzidishia mkanganyiko kwa jambo lililowazi kabisa, nakunukuu:
  “”Na matumizi ya jina la Yesu kwa ajili ya ubatizo si sawa na matumizi ya jina la Yesu kwa ajili ya kutoa pepo, magonjwa, na vitu vya shetani.
Kumbuka nilisema kuwa Yesu aliwaambia watoe mapepo, na kuponya wagonjwa kwa jina lake.“”

  Kifungu kinachohusika hapo ni hiki hapa, Mk 16:17:
  “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; KWA JINA LANGU watatoa pepo…”

  Labda nikuulize, kwamba “Mwana” unasema ni jina, na Yesu pia ni jina; je, umetumia kigezo gani kubaini kwamba jina linalopaswa kutumika hapo ni Yesu na si Mwana? Au Yesu na Mwana ni personalities mbili tofauti?
  Na pia umefikaje kutumia jina la Yesu ilhali maelekezo yake ni “Kwa Jina langu” kwanini hutoi pepo “Kwa Jina langu” kama ulivyoelekezwa?

  Mungu hawezi kuruhusu “Kosa” lolote ktk Neno lake, wala hawezi kutuwekea jambo la kubahatisha humo. Neno liko kamili na ktk urahisi, na tuna hiyari ya kulifuata au kuyafuata Mapokeo tuliyoyazoea, vyote vinalipa katika wakati wake!!

  Ubarikiwe!!

 8. Mjoli Haule,

  Asante kwa tafakari!

  Kuhusu kughafilika, labda niseme hivi, ulipolisema hilo na kunipa hivi vifungu vinginevyo vinavyolihusu jambo hili la vyakula, imenisaidia sana katika kulitafakari jambo hili.

  Yaani niliporudi ktk ile Mk 7:18-19 nikaliona jambo hilo kwa uwazi zaidi, “Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? KWA KUSEMA HIVI ALIVITAKASA VYAKULA VYOTE.”!!! Ninaamini, kama ulivyosema, kwamba hapa ndipo Vyakula vyoooote VILITAKASWA; Kristo akiwa ndio MWISHO wa Sheria, ile Torati iliyovinajisisha, na sasa ikiletwa katika UKOMO!!!

  Katika msingi huu, inaonesha kwamba kwa Mdo 10:10, licha ya kwamba inashughulika na “kuchangamana” na Mataifa, lakini jibu la Petro katika jambo hilo, linaonesha kwamba naye kama mimi na Wasabato, aliikosa Mk 7:19, tazama jibu lake, “Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule. Lakini Petro akasema, HASHA, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.”!!! Unaona!

  Sasa, KALI zaidi ni kwamba kumbe nasi watu wa Mataifa tulikwa NAJISI, yaani kimsingi tuliwakilishwa ktk lile furushi; jamani, ni NEEMA kiasi gani tuliyokirimiwa!!!

  Basi hii 1Tim 4:4-5, kama pia ilivyo Mdo 10:10, imekuwa si ruksa tena bali ni msisitizo wa jambo lililokwisha amuliwa ktk hiyo Mk 7:19, sasa likisisitizwa na kuwekwa wazi zaidi, ili tutakapoyaona hayo tuyatambue ni nini: “Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.” Ingawa wewe umenukuu kuanzia kifungu cha 3, kifungu hiki hakiendani na msisitizo huo wa 4-5, bali wazo lake linafungamana na kifungu cha 1na 2 na kupumulia ktk hicho cha 3, kikilikamilisha Fundisho la kuzibaini “roho” za ukengeufu:
  “1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.”

  Hata ninaamini wengi wanaozuiliwa katika vyakula, wamefundishwa tafsiri za uongo za nyaraka za Paulo zinazohusu uhuru wa vyakula, ambazo roho hizo huzipindisha na kuwarudisha wafuasi wao ktk makatazo, nao waumini hao wakiwa wamekwisha kuondolewa ktk Kweli ya Mungu, basi huishia KUTOKIJUA kifungu hicho cha Mk 7:19 ambacho kingewatoa kifoni, maana zile roho zinakijua kuwa wengi hawakisomi kwa utulivu, na hata kwa mpindo wanaokuletea usingepata nafasi ya kukirudia kifungu hicho ili kikufungue macho yako ya kiroho yaliyopofushwa ktk tafsiri za kishetani!

  Yaani Mjoli Haule, NINAKUSHUKURU SANA KWA AJILI YA WOOOTE WALIO KTK UTUMWA wa MAFUNDISHO YA MASHETANI!!!!

  Ubarikiwe!

 9. Lwembe;

  Hiyo kauli yako kwamba maelekeo yalibadilika, ni kutaka kuleta mkanganyiko usio wa lazima na ambao haupo pia kimsingi.

  Mitume wasingebadilisha maelekezo katika yale maelekezo ya Yesu. Kama tunaweza leo kudhani kuwa walibadilisha, hiyo ni fikra tu inayotokana kushindwa kwetu kuutafsiri ukweli wa kilichofanyika.

  Agizo la Yesu kwa wanafunzi halikuwa kwenda kuwapa maelekezo mapya wale wanaowafanya kuwa wanafunzi wa Kristo, bali kuwafundisha kuyashika yale ambayo kristo aliagiza.
  (Mt 28: 20a and teaching them to obey everything I have commanded you)

  Ndio maana mimi wakati fulani nikawaambia kuwa maana ya kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt, ndiyo hiyo ambayo mitume wanaiita ‘kubatiza kwa jina la Yesu’.

  Bless u!

 10. Br Lwembe….
  Mwisho hapo umeghafilika kidogo
  Katazo la chakule linamalizwa na 1Tim4:3-5,Mk7:19 ,Andiko hili Mdo10:10-16 inamaliza utengano(kutochangamana) kati ya mataifa na Israel.

  Nina wasoma na Br Sungura

  Mbarikiwe

 11. Sungura,

  Si kwamba eti Yesu alitoa maelekezo yake na mitume nao wakatoa ya kwao, hapana, mitume hawajawahi kuwa na jambo lolote la kwao, yote waliyoyafanya yanaongozwa na Kristo ndani yao, Mt 28:20 “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Usipomuona Kristo ndani yao, ni hatari kubwa sana maana huduma yao ni ile ya Roho Mtakatifu, basi ukiwa na neno lolote juu yao, elewa kwamba una neno na RM!!! Hebu jiridhishe jambo hilo, itazame hii episode, Mdo 4:13 “Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.” Unaona, jambo fulani liliwaambia hawa walikuwa “Pamoja na Yesu” yaani saa hiyo, present!!!

  Kuhusu Maelekezo kubadilika, huwa inakuwa hivyo, yanaweza kubadilika kama tunavyoyaona haya ya Ubatizo. Katika hili huwa hatuulizi “kwanini?” bali tunatii moja kwa moja. Usipokuwa makini ni rahisi sana kuyakosa maelekezo na hivyo kuishia nje ya Ufalme! Hebu watazame Wasabato walivyoyakosa maelekezo ya vyakula na kuishia kung’ang’ana na maelekezo yaliyopitwa na wakati!!!

  Hebu yaangalie Maelekezo ya vyakula:

  Mwa 2:16-17 “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile…”

  Yaani kutoka Adamu mpaka Gharika, nyama ilikuwa hailiwi!!!
  Baada ya Gharika:
  Mwa 9:3 “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.”
  Vyoooote ruksa kuliwa!!!!

  Taifa la Israeli lilipozaliwa, baada ya kutolewa Misri, wakapewa katazo la vyakula:
  Law 11:2.. “Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. 3Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala. 4Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, …. lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.”
  Wasabato wamekwamia hapa, wamekosa “understanding” ya maelekezo yaliyofuata, which means they are not worthy of the Gospel!!!

  Hapa Katazo la vyakula LINAFUTWA:
  Mdo 10:10-16 “… akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi; ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani. Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule. Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi. Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.”

  Baraka tele ziwe kwako utakapofikia “kuyafurahia maisha”!!!

 12. Lwembe,

  Kwa hiyo unaniambia kuwa Yesu alitoa maelekezo yake na mitume nao wakatoa maelekezo yao?
  Kwamba yale ya Yesu ni maelekezo ya zamani na yale ya mitume ni maelekezo mapya?

  Asante!

 13. Sungura,

  Ah, sikuwa najipanga kujibu hoja hapana, bali wakati mwingine ndio hivyo mambo huwa mengi, na unaweza ukalisahau jambo, ni hivyo tu, otherwise majibu ya mambo ya Mungu yote yamo humo ktk Biblia, kwahiyo unayakopi tu humo!

  Kuna dhabihu ambayo hutolewa kwa ajili ya nafsi ambayo imetenda dhambi kwa ujinga, Mungu humsamehe huyo, Hes 15:28
  “Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi pasipo kujua, mbele za BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasemehewa.”
  Lakini kuna dhambi ambayo nafsi iitendayo ni lazima iuliwe, thereby denying the evil spirit a body to manifest itself in! Eze 18:20
  “The soul that sinneth, it shall die.”
  Kwahiyo, unaweza kuliangalia hilo unapoitafakari dhambi (Shetani) kwa jinsi anavyohusiana na nafsi.

  Kwahiyo, unapozungumzia dhambi, ni kuambatana na roho iliyo kinyume na Mungu, na kwa kuitumikia roho hiyo, ndipo Kristo kuhusu nafsi hiyo ambayo hushindana na Neno, anasema kwa kuwa nafsi hiyo inasema inalijua hilo inalolipindisha, basi dhambi yake inakaa! Yn 9:41 “Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.”

  Pia unasema,
  “Kwa kuwa utii huendana na kuelewa maelekezo au instructions, maelekezo kwa habari ya ubatizo yalitoka kwa Yesu. Alielekeza kubatiza kwa jina la Baba, Mwana , na Roho mt.”
  Hii ni kweli isiyopingika, hayo ndiyo maelekezo yaliyotolewa! Lakini kama utakumbuka nilikuambia kuwa usikivu, au umakini katika kuyasikiliza maelekezo ni muhimu sana maana kuna wakati hubadilika kama yalivyobadilika hapa ambayo wewe umeyakosa na kuendelea katika jambo lililo pitwa na wakati, Mdo 2:38
  ” Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
  Haya ndio Maelekezo mapya!!!

  Basi kwa kadiri ya mtazamo wako, vifungu hivi viwili (cha Mt 28:19 na hiki cha Mdo 2:38) vyote vinasimama kama Agizo. Tena ni Agizo hilohilo, bali sasa likiwekwa ktk namna ambayo inampa ibilisi nafsi ya kucheza na Maandiko, at least for a while, ili mavuno yanapokaribia, ile siku iliyo kuu na ya kuogofya, kama ilivyokuwa ktk siku za Nuhu, watu tena wakatae kuingia ktk Safina, kule kuondolewa dhambi zao!

  Tazama pia, iwapo umepewa Ukuhani, rudi kule AK, kaangalie ile manna iliyofichwa, basi zile siku arobaini walikuwa wanakula hiyo! Nawe kama u Kuhani utaitambua manna hiyo, ndio hili Neno la Kikuhani wanalo lihubiri kwa watu wa kikuhani! Ufu 2:17 “…Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa…”

  Waitwao ni wengi wateule ni wachache! Utaliongeleaje jambo hili, kwamba mlioitwa kwenye usaili mko elfu mbili, nafsi ziko mbili tu! Basi Mchujo wake utakuwaje, naye Mungu ndiye anayechuja!!! Utazame mchujo kwa Gidioni (Amu 7:1-7); halafu njoo hapa uuangalie mchujo wetu watu wa Mataifa, “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu. (RUM. 2:16). Basi Paulo alibatiza kulingana na hiyo Mdo 2:38, hii ndiyo Injili aliyoihubiri, ambayo ndicho kipimo cha Hukumu, basi ukija na ubatizo uliotofauti na huo, utapita kweli?!

  Tazama kivuli chetu, waliambiwa siku ya saba manna haitadondoshwa kwahiyo wakusanye ya kutosha siku ya sita ili waitumie na kesho yake. Hayo ndiyo maelekezo waliyopewa wayafuate. Lakini licha ya maelekezo hayo wako waliotoka kwenda kuokota manna ambayo waliambiwa HAITAKUWEPO!

  Basi hao ni kivuli tu, picha yenyewe ndio sisi. Tukimiss instructions, tunakuwa EJECTED, ndipo kule “kulia na kusaga meno” kunatutimilia!!!

  Bwana akubariki, ndg yangu Sungura, kwa Changamoto!

 14. Lwembe,
  Kumbe ulikuwa bado unajipanga kuijibu hii hoja? nilidhani kuwa tuliamua kukomea hapo!

  Lakini ona ulichosema hapa, wakati unaniambia kuwa nimekushangaza kama sijui kuwa dhambi ni pepo;

  ” Wazo lililo kinyume na Neno la Mungu huwa linatoka kwa nani? kwa RM? Adamu alipoanguka Dhambini, aliangukia ktk mikono ya nani? Au huelewi uhusiano uliopo kati ya mapepo na Shetani na Dhambi? Kama ambavyo malaika humzunguka mwaminio, mapepo pia humzunguka muasi, nayo mapepo yako dizaini nyingi sana, wewe zitazame dini halafu changanya na jini “Makata” na “Maimuna” !!!

  Lwembe, wazo lililo kinyume na mapenzi ya Mnugu hutoka kwa shetani (pepo), Adamu aliangukia katika mikono ya shetani (pepo), naelewa uhusiano uliopo kati ya mapepo na shetani na dhambi!

  Je mpaka hapo umegundua nini Lwembe, kwamba lile pepo au shetani ambaye huleta wazo lililo kinyume na mapenzi ya Mungu, mwenyewe ndiye dhambi au wazo aliloleta ndio dhambi?

  Au hivi, anayeleta wazo la dhambi ndiye dhambi au wazo lake lenyewe ndio dhambi?

  Kwa hiyo mpaka hapo jibu unalo mwenyewe, kama wazo la shetani ndilo dhambi au shetani mwenyewe ndiye dhambi. Hii ni rahisi saaaana!

  Kwa kuwa utii huendana na kuelewa maelekezo au instructions, maelekezo kwa habari ya ubatizo yalitoka kwa Yesu. Alielekeza kubatiza kwa jina la Baba, Mwana , na Roho mt.

  Kama wewe unadhani mitume hawakubatiza hivyo, basi wewe ndiye hujaelewa walivyotekeleza maelekezo ya Yesu. Na mimi naamini wasingekiuka hayo maelekezo.

  Ndio maana nikasema, hakuna sehemu ambapo tunalikuta tendo la mtu kubatizwa, huku anayembatiza akiwa anasema ‘nakubatiza kwa jina la Yesu’. Bali tunakuta tu taarifa kuwa walibatizwa kwa jina la Yesu. Na kwa vile tunaamini kuwa lazima walifuata maekezo, basi huko kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt. ndio huko kunaitwa kubatizwa kwa jina lake Yesu!

  Lakini kwenye kutumia jina la Yesu kuponya, kutoa pepo, kufufua, n.k angalao tunakuta Petro anamwambia kiwete ‘kwa jina la Yesu simama utembee’.

  Kwa hiyo maelekezo ya jinsi ya kubatiza na maelekezo ya jinsi ya kuponya, kufufua wafu, n.k, toka kwa Yesu yako tofauti si kwa bahati mbaya.

  Kwa ubatizo maelekezo yanasema kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt.

  Kwa kuponya wagonjwa, kutoa pepo, kufufua wafu, kutakasa wakoma, n.k maelekezo yanasema kwa jina la Yesu.

  Nawe nakutakia baraka Lwembe!

 15. Ndugu Lwembe, kama ndio hivi, tutapona kweli. Mungu atusaidie tuone kweli

  Bwana awabariki

 16. Mungu anaangalia utii wetu, kiwango cha utii wetu kwa Neno lake ndicho kinacho ithibitisha imani yetu. Utii huendana na kuyaelewa Maelekezo au Instructions. Usipokuwa makini katika kukielewa unachofundishwa katika hatua zake, ni rahisi sana kuishia porini, si lazima iwe kwa kupenda, bali hata kwa ujinga!

  Ubatizo ulioagizwa ktk Mt 28:19 unatafsirika katika kitabu cha Matendo, kama ulivyofanyika, kwa Jina la Bwana Yesu Kristo.

  Wengi hulikosa jambo hili kwa mazoea ya Mapokeo tu. Lakini jambo hili liko ktk urahisi kama linavyosomeka. Tena wengi hujiridhisha kwamba mitume huenda walikosea, jambo ambalo lingeifanya Biblia kuwa kitabu kisicho aminika! Lakini kama wangeupokea ukweli kwamba, baada ya kufufuka kwake, Kristo alikaa na mitume wake kwa siku 40, akiendelea kuwafunza, Mdo 1:3 “wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.” Aliwafunza nini, hayajaandikwa, bali wanafunzi wake ndio udhihirisho wa hayo waliyoendelea kufunzwa!

  Pia hata kwa akili ya kawaida tu, iwapo utajiachia ktk Uhuru, hiyo Mt 28:19 tunayong’ang’ana nayo kuwa ndilo agizo la Yesu, ni mitume hao hao ndio wanaotuambia kuwa Yesu akasema, basi kama ni watumishi wa kukosea kosea, huenda hata hili agizo limekosewa pia, maana halina support ya Andiko lolote lile zaidi ya lenyewe! Unaona mashaka yanavyoweza kukupeleka nje ya Ufalme?

  Bali hayo hayajakosewa, ni kipimo kizuri cha Utii ktk kuzifuata Instructions, unakwenda nazo kadiri ya beat inavyobadilika, kama umewahi kuimba kwaya utakielewa ninachosema; ukishindwa kuifuata beat, unapigwa chini, wokovu bye bye!!!!

  Mbarikiwe nyooote!!!

 17. Sungura,

  Umenishangaza sana uliposema Dhambi siyo pepo! Wazo lililokinyume na Neno la Mungu huwa linatoka kwa nani? kwa RM? Adamu alipoanguka Dhambini, aliangukia ktk mikono ya nani? Au huelewi uhusiano uliopo kati ya mapepo na Shetani na Dhambi? Kama ambavyo malaika humzunguka mwaminio, mapepo pia humzunguka muasi, nayo mapepo yako dizaini nyingi sana, wewe zitazame dini halafu changanya na jini “Makata” na “Maimuna” !!!

  Haujasoma ilipoandikwa kuwa pepo akimtoka mtu huenda kuzunguka zunguka kisha hurudi kuyatazama makazi alimotolewa, na akikuta yako tupu huenda na kuwachukua na wenzake saba waje kuishi humo? Ndipo kama atakuja nao wale wa kidini, ndio unasikiaga Sungura amelazwa hospitali alikuwa ktk mfungo wa siku arobaini, lakini tumemuwahi ktk siku yake ya nane!!!

  Kuhusu wewe kukuta taarifa tu ktk Biblia, sioni ni kwa nini unatatizika, maana Biblia nzima ni Taarifa tupu, bali zilizo HAI, maana zatoka kwa Mungu! Kwahiyo kutegemea kuliona tendo ndani ya Biblia, utakuwa umejichangaya kidogo, unalitafuta jambo usiloweza kuliona! Pia sijui kama hata wewe mwenyewe unakielewa hiki unachokisema:
  “”Ndio nikakwambia hakuna mahali mtu aliwahi kubatizwa kwa maji, akazamishwa huku mzamishaji anasema ”nakubatiza kwa jina la Yesu”. Tunakuta tu taarifa kuwa walibatizwa kwa jina lake Yesu. Sasa kama Yesu alishawaagiza namna ya kubatiza na huku tunawakuta wamebatiza, kwa nini tusiamini kuwa walibatiza vile tulivyoona Yeu anawaagiza (yaani kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt)?””

  Nakuona unapatwa na kigugumizi cha kuamini unayoyasoma, na unataka uyaamini mawazo yako, huoni kwamba utakosa wa kukutetea utakapofika Hukumuni? Kama umekuta Taarifa ya agizo la Yesu ukaiamini, amini na Taarifa ya utendaji wa jambo hilo unayoisoma!

  Haya maelezo uliyoyaleta sijui umetoka nayo wapi,
  “”Na pia si kweli kwamba wale wanafunzi waliojazwa Roho mt. siku ya pentekoste walibatizwa kwanza au walibatizwa tena, (maana walikuwa wamebatizwa ubatizo wa Yohana) ndipo wakajazwa. Hatusomi hiyo popote. Na hata akina Petro wenyewe hatuoni mahali wanabatizwa tena ili wajazwe Roho mt.””

  Mimi sijawahi kuyasema hayo hivyo, wewe utakuwa ni msahaulifu au haukuusoma mchango wangu wa 28/9 2013 katika thread hii, ngoja nikunukulie tena:
  “”Mitume na hao wote waliopokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste walikuwa wamebatizwa Ubatizo mmoja tu, ule wa Yohana, uliowatayarisha kumpokea Kristo, nao wakiisha kumpokea Kristo, wakatakaswa kwa Neno Yoh 17:17, ndipo wakastahili kumpokea RM kama alivyonena Yohana Mbatizaji, Mt 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu … yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.””

  Kama kuna kilichopungua ktk jibu hili nitafurahi kuliweka sawa, maana yote yamo humo humo ktk Biblia, iwapo utaiamini tu!

  Karibu sana, Sungura!

 18. Acha Lwembe,
  Dhambi siyo pepo,ni tendo au wazo lililo kinyume na mapenzi ya Mungu. Pepo ni kitu kingine kuhusiana na dhambi.

  Na matumizi ya jina la Yesu kwa ajili ya ubatizo si sawa na matumizi ya jina la Yesu kwa ajili ya kutoa pepo,magonjwa, na vitu vya shetani.
  Kumbuka nilisema kuwa Yesu aliwaambia watoe mapepo,na kuponya wagonjwa kwa jina lake.

  Lakini kwa habari ya kubatiza, akawaambia wabatize kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt.
  Ndio nikakwambia hakuna mahali mtu aliwahi kubatizwa kwa maji, akazamishwa huku mzamishaji anasema ”nakubatiza kwa jina la Yesu”. Tunakuta tu taarifa kuwa walibatizwa kwa jina lake Yesu. Sasa kama Yesu alishawaagiza namna ya kubatiza na huku tunawakuta wamebatiza, kwa nini tusiamini kuwa walibatiza vile tulivyoona Yeu anawaagiza(yaani kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt)?

  Na pia si kweli kwamba wale wanafunzi waliojazwa Roho mt. siku ya pentekoste walibatizwa kwanza au walibatizwa tena, (maana walikuwa wamebatizwa ubatizo wa Yohana) ndipo wakajazwa. Hatusomi hiyo popote. Na hata akina Petro wenyewe hatuoni mahali wanabatizwa tena ili wajazwe Roho mt.

  Na huko nyuma niliwahi kukuuliza kuhusu kauli ya Yohana,kuwa ‘mimi nawabatiza kwa maji,ajaye nyuma yangu…. yeye atawabatiza kwa Roho na kwa moto. Wala hakusema ajaye nyuma yangu atawabatiza kwa maji, na kwa Roho na kwa moto. Bali ni kauli inayoonesha kuwa kilicho kilikuwa kinakuja kuwa ‘substituted’ na kinachokuja. Hukutoa majibu yaliyo ya sawa katika hili pia.

  Asante.

 19. Sungura,

  Bravo!

  Umeiona Injili jinsi ilivyo rahisi, inajitafsiri yenyewe! Inashangaza jinsi wapendwa wanavyojikwaa! Dhambi ni pepo, na hakuna pepo anayetimuliwaga “kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu”, mapepo huwaga yanacheeeka!!!

  Hebu fikiria jambo jepesi wanavyoligeuza kuwa gumu mpaka wao wenyewe linawachanganya! Kama Mwana ni jina, basi Yesu ni nini? Au unaonaje kwamba Petro alimwambia yule kiwete “kwa jina la Mwana tembea” ila wakaandika tu kwa “kwa jina la Yesu”, Au pepo, kwanini huwa hawatolewagi “kwa jina la Mwana”? U see how funny it gets?

  Unajua nature ya binadamu aliyeanguka, ni ule wepesi wa kuupokea uongo na assumptions zake, kutokana na ile syndrome ya kuogopa ukweli! No wonder kauli yako sounds so sweet ktk masikio na mioyo iliyo ktk nature hiyo!

  Lakini, ili yeyote aungane na kundi la watakatifu walioingia siku ya Pentekoste, basi ni lazima aipite njia hiyo, abatizwe kama walivyobatizwa wote tunaowaona ktk Biblia, lile kanisa la kwanza, tofauti na hilo tunaishia katika lile kundi la wakristo “wannabes”!

  Down stream, the way of the world, is the easiest swim,
  & vultures don’t make eagles!!

  Gbu!

 20. Hahaaaa, Lwembe!
  Uko very funny!

  Umesema kitu ambacho kwenye biblia hakipo. Umesesma walikuzamisha kwa mara nyingine wakatamka “kwa Jina la Bwana Yesu Kristo”!

  Kwenye biblia niliwaambia kuwa hakuna sehemu hicho kitendo kimefanyika. Nikawapeni mfano wa Petro aliposema kwa yule kiwete wa mlango wa mzuri, ”kwa jina la Yesu tembea”

  Lakini ya kubatiza kwa jina la Yesu, tunakuta tu taarifa ikisema wakabatizwa/akabatizwa/nikabatizwa kwa jina lake Yesu. Ndiposa nikawaambia kuwa huko kubatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt. alikokusema Yesu ndiko mitume walikofanya, na ndio huko wanakuita kubatizwa kwa jina la Yesu.

  Aante kwa mchango wako mzuri.1

 21. Sungura,

  Umenichekesha saaana!!!

  Sikia, tangu wokovu ufike Afrika watu wamekuwa wakitoa Fungu la Kumi kwa Sheria, mpaka leo wanagombea kuendelea katika utoaji huo licha ya ukweli kwamba Mungu hana vitabu vinavyorekodi Zaka hiyo, labda madhehebu yetu na ndio maana wanatupa risiti! Lakini wako watu walioamka usingizini na wameyaacha mambo hayo yasiyo na faida kiungu. Pia Ubatizo ni hivyo hivyo!!!

  Mimi nilipoipokea kweli hiyo, nikazamishwa majini, badala ya kunilowesha kama walivyonifanyia hapo mwanzo waliponitumbukiza majini na suti yangu mpya wakanilowesha “kwa Jina la Baba na Mwana na RM” nikatoka yule yule, safari hii walinizamisha na wakanibatiza “kwa Jina la Bwana Yesu Kristo”; tangia nilipoibuka majini, ufahamu wangu kuhusu Neno la Mungu ULIBADILIKA. Sasa hivi ninao ujasiri wa kumdai Mungu Ahadi yoyote ile, na kumuomba samahani vile vile! He is a LOVING GOD!!!

  Basi, siku moja fulani tutakutana na Mungu uso kwa uso, and if you want to meet God smiling, toe the line, get rebaptised in the name of The Lord Jesus Christ, so that your sins may be remitted!!

  Hahahahahaha…!

  Ciao my good friend,
  Eagles Dare!!!
  Gbu.

 22. Siyi ndg yangu,

  Asante kwa note, zaidi sote tumshukuru Mungu kwa Upendo wake anaotukirimia kila leo licha ya mapungufu yetu, tukijiweka katika tumaini la kukifikia Kimo cha Kristo!

  Neno la Mungu ni challenge kwetu sote, kila wakati,
  BUT, Eagles Dare!!!

  Ubarikiwe!

 23. Hey Lwembe na wengine,
  Mbona mnahitimisha mjadala wakati tungali na mengi ya kunena?

  Basi mimi naomba tu ndugu yangu Lwembe na ndugu yangu Mabinza waniambie, wao walibatizwaje,maana ninavyojaribu kuona ni kama vile tangu wokovu ufike Africa watu wamekuwa wakibatizwa kama wanavyobatizwa leo.

  Nasubiri jamani!

 24. Ck Lwembe
  Hii ya kutofautiana na Mungu!! Noumerrr!!!
  Sijui itakuwaje?

  Bwana awabariki

 25. Lwembe,
  Hiki kitu umenena mjoli wa Bwana. Ni kweli kabisa jambo la msingi kuliko yote, Ni kuhakikisha tunaenenda sawasawa na Mungu, Sawasawa na neno lake. Sawasawa na maagizo yake kwa kuzingatia mambo haya mawili, NIA yetu ya kumtafuta Mungu na UTII wetu kwa neno lake.
  So ni jambo la kila mtu kujitathmini kuona kama anakubalika mbele za Mungu. Paulo anasema, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” 2 Timotheo 2:15
  Watu wanapaswa kufika mahali wakafikiri
  1. Je, ibada zao Mungu anazikubali?
  2. Mionekanao yao Mungu anaikubali?
  3. Matendo yao ambayo ni matokeo ya kilichomo ndani ya mioyo yao, Je, Mungu anayakubali?
  4. Je Sala zao si machukizo mbele za Mungu nk.
  Bwana atuasaidie sote.
  Ubarikiwe sana.
  Nimeipenda sana comment yako bro.

 26. Siyi,

  Asante kwa note, ni kweli tunazo tofauti nyingi, lakini bado ni vizuri kujihakikishia kwamba hatutofautiani na Mungu!!!

  Bwana akubariki!

 27. Seleli,
  “Enjoy the fellowship, learning what is learnable!”

  Gbu, my brother in Christ!

 28. Lwembe,
  Ubarikiwe kwa wito kaka.
  Tutajitahidi kufanya hivyo japo tafsiri zako na zetu kwa neno la Mungu zinatofautiana. Kikubwa tuombe Mungu atufunulie ili kulijua hili kwa undani wake.
  Ubarikiwe pia

 29. Mwisho, ndg zangu,

  Ninawashauri kwamba liangalieni jambo hili kwa uangalifu, maana si jambo dogo kama wengi wetu tunavyotaka kulifanya. Iwapo ulilazimika kubatizwa, kwa jinsi yoyote ile, basi jua kwamba umuhimu huo upo. Na kama Mungu ndiye aliyeuagiza, basi sioni ni kwa jinsi gani tutalikwepa jambo hilo, tena ni kipimo cha utii wetu kwa Neno lake.

  Nao ubatizo wa “kwa jina la Baba na Mwana na RM”, huu umetuingiza katika madhehebu yetu, tukazipitia zile hatua mbili za awali, Kuhesabiwa Haki na hatua yetu ya pili ni Utakaso. Nao Ubatizo huo naweza kuufananisha na ule wa Yohana, ambao umetutayarisha kutuingiza ktk Hatua ya Mwisho ambayo ni Ubatizo wa RM, ambao huikamilisha kazi ya Wokovu wetu, hapo Mungu anapokuja na kufanya makazi ndani yetu.

  Basi umuhimu wa kuondolewa dhambi zetu ni wa juu sana, tunapaswa kupiga hatua zaidi kwenda mbele kadiri ya Maelekezo ya Mungu yanavyojifunua kwetu. Basi kama leo hii Ubatizo umerejewa katika namna ya kuwekwa sawa kwa ajili ya hatua ifuatayo, basi kutokuupitia huo katika namna iliyoelekezwa ni Dhambi, au ni kuendelea ktk Dhambi tulizonazo ambazo hazijawahi kuondolewa, basi kuupitia Ubatizo wa “kwa jina la Bwana Yesu Kristo” utatupatia Ondoleo la Dhambi zetu kama Mitume walivyoagiza.

  Wengi wanajiridhisha kwamba mitume walikosea, lakini hilo si kweli, ni visingizio tu vya kulikataa Neno la Mungu, tukiidhihirisha Nguvu ya Dhambi inayotushikilia! Bali Kristo alisema hivi kuhusu sisi tunaosema kwamba mitume walikosea, ni neno gumu kidogo, lakini ukweli ndio huu:
  Lk 10:16 “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.”
  Mt 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.”
  Kwahiyo ndg zangu, jitahidini kuyapokea yaliyofundishwa na mitume kama yalivyo ili mlivuke Bonde la Uharibifu!

  Mbarikiwe saana!

 30. Lwembe,

  Nimesoma jibu lako kwa comment yangu kuhusu uyaandikayo humu blog, nimecheka kweli! brother I guess HAUKO NORMAL!!!!!!!!

  Embu nikuombe kirafiki jambo moja tu, Nisaidie kuniandikia hapa kwa sentence moja tu hata kama ni ndefu na yenye koma nyingi sitajali but iwe moja tu, yenye kueleza kitu gani hasa unasema/simamia ktk mada hii, ok? Alright, here we go, write it plz, very clearly and simple..your main idea/doctrine-let us make life simple, ayaa Karibu Kaka.

  Press on.

 31. Sungura,

  Sikiliza, unaposema kwamba huwa unashindwa kunielewa kuhusu uwezo wangu kiufahamu, well, napenda nikuamini kwamba usemacho ni kweli! Unajua, ufahamu unaambatana na mambo mengi, kubwa ni kule kujifunza katika uhuru, nadhani hiyo ndiyo barrier inayotutenganisha!!

  Ninachokiona kwako, ni restrictions, maana nimekuona unachomoka na wazo zuri kabisa, kitambo kidogo, tena umejifungia ndani ukiniachia hilo wazo huko nje!!

  Tazama niliposema kwamba Yesu, kwa kule kuja kwa jina la Baba yake, basi Babaye jina lake litakuwa ni hilo la Yesu; naona kwa maelezo haya umenishusha “uwezo” wangu kiufahamu mpaka Seleli amefurahia!! Unasema kwa ujasiri kabisa,
  “”“Sentensi ‘nimekuja kwa jina la Baba yangu’ huwezi kufikiri hata kidogo ati kuwa Baba ndio hilo jina. Kinachomaanishwa hapo ni kuwa nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu.(jina linasimama likiwa na maana ya mamlaka)””

  Na kuhusu Roho Mtakatifu unasema,
  “”Hapa napo umepotosha Lwembe. Sentensi ‘Baba atampeleka kwa jina langu, simply inamaanisha atampeleka kwa mamlaka iliyo katika jina langu. Mtu ukiwa unawaza sawasawa huwezi hata kidogo kusema ati hiyo sentensi ”Baba atampeleka kwa jina langu” Yesu alimaanisha kusema kuwa Baba atamwita Roho mtakatifu jina la Yesu.”

  Katika uwezo wangu mdogo kiufahamu, kama nimekuelewa vizuri, unalolisema hapa ni kwamba Jina la Yesu ndilo mamlaka ya Baba, naye Roho Mtakatifu ameletwa kwa mamlaka hiyo iliyo katika jina la Yesu ambalo ndilo mamlaka ya Baba. Yaani unapoliitia Jina la Yesu inakuwa ume ‘switch on’ Mamlaka ya Baba ambayo ndiyo inayofanya kazi kwa Yesu, yule aliyekuwa Mwili na pia kwa RM, yule aliyekuja kwa Ahadi ya Baba, na sasa kwa mkristo aliyezaliwa mara pili! Nimekupata sawa sawa au ndo kama kawaida yangu nimechomokea porini???

  Labda nikurudishe huko nyuma uliko ileta tafsiri ya kifasihi kuhusiana na hiyo Mt 28:19:
  “”Ukweli ni kwamba tafsiri ya hicho kifungu ”kwa jina la baba, na mwana, na Roho mtakatifu” kifasihi ni sawa na kusema kwa mamlaka ya Baba, na mamlaka ya Mwana, na mamlaka ya Roho mtakatifu.””

  Kutokana na maelezo haya ndipo tukakubaliana kwamba Jina la Yesu ndilo lenye mamlaka hayo yote kimaudhui, halafu tukalidhibitisha hilo kwa kifungu hiki ktk Mt 28:18, hapo Kristo anapowatangazia mitume wake kwamba, “… Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” Hili lathibitisha kwamba Kristo Yesu ndiye Mamlaka!!!

  Yaani saa zote ndg yangu Sungura umekuwa ukiliongea jambo hili, bali kwa ufahamu wa juuuu sana! Muda wote umekuwa ukisema “Jina la Yesu” ndilo Mamlaka ya “Baba na Mwana na Roho Mtakatifu”; Yaani unapotamka” kwa Jina la Yesu”, ktk sekunde hiyo Jeshi la malaika linashuka kukuhudumia!!! Angalia wewe mwenyewe unachokisema hapa,
  “”Maana kwa kuwa Mungu ndiye anayejidhihirisha kama Yesu, basi asemapo mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mt, maana yake ni kwamba mtu akisema:
-kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt., maana yake anakuwa amesema kwa jina la Yesu.
Sasa hapo tofauti ni nini kusema kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mt. na kusema kwa jina la Yesu?” Unaona? Unafika ktk pinacle ya jambo halafu unapaa zaidi katika ufahamu mpaka unakuwa huoni kitu! Shuka chini utulie hapo! Ngoja tuurudie ule mfano wako, bali tumtumie rais Kikwete tuone kama jambo hili litaeleweka kirahisi zaidi.
  Haya, Lango kuu la Ikulu linafunguka kwa kutamka code name. Ukifika hapo langoni unalitamka “jina la Mwenyekiti wa CCM, na la Amiri Jeshi Mkuu wa Tz, na la Rais wa Tz.” Sasa mfikirie Seleli atakapofika hapo Langoni, kifua mbele, anakwenda kuingia, akiisha iruka foleni kwa virisiti vyake vya Zaka, kapewa mic, “kwa jina la Mwenyekiti wa CCM, na la Amiri Jeshi Mkuu wa Tz, na la Rais wa Tz; lango funguka!!!” Kimyaaaa, askari wanakubeba na makelele yako wanakutupa huko nje! Basi kama ni Lango la Ufalme, je, …?

  Ukitamka “kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu”, kimyaaaaa, ni sauti isiyotambuliwa, Dhambi haziondoki, wala mapepo; hivi unajua kuwa Dhambi ndilo pepo kubwa linalowakalia watu??!! Baba, Mamlaka alikwisha ikabidhi kwa Kristo siku nyingi, kwahiyo akikusikia unamwita mwita anajua ndo wale wajeuri!

  Kuhusu kujifunua kwa Mungu, yule ambaye ni Roho (Yn 4:24), nilisema kwamba ameanza kujifunua katika Agano la Kale na AMEMALIZA kwa kujifunua ktk Kristo Yesu. Basi, jibu lake kwa Filipo, ndio hili hapa tena, Kol 1:9 “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”, unaona Sungura kwanini yeye alisema ukiniona mimi umemuona Baba? Yeye hakuwa Baba bali huo utimilifu wa Mungu katika Mwili, maana Mungu ni Roho! Ukisogea mbele kidogo inasema Kristo ndiye “…kichwa cha enzi yote na mamlaka”, yaani HAKUNA MAMLAKA zaidi ya Kristo Yesu!!!!

  Pia unasema, “”Na niliuliza, kwa nini Yesu kwenye suala la ubatizo anasema kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt., lakini kwa habari ya kutoa mapepo, kunena kwa lugha, kushika nyoka, na kula vitu vya kufisha, anasema ‘kwa jina langu? Tofauti ni nini?””

  Ninachokiona ni kwamba katika Ubatizo alikuwa anayaleta Mamlaka yaliyokuwa yanaonekan kujigawa gawa, sasa akiyakusanya yote katika Jina moja ambalo na la kwake, na akiisha kuliweka wazi jambo hilo, ndipo anaendelea nao mbele katika ufahamu huo mpya kwa wepesi, wakiwa tayari juu ya Msingi huo, ndio maana hatumuoni yeyote yule akihudumu katika namna hiyo ya ”Jina la Baba na Mwana na RM”. Halafu usisahau kwamba Biblia inasomwa na kila mtu bali yamo mambo mengi ambayo Mungu ameyafunga yasieleweke kwa kila mtu, bali kwa Kanisa lake tu!

  Jambo jingine unasema, “”Tunachobishania ni nini, kutowaona mitume wakibatiza kwa kutamka jina Baba, Mwana, na Roho?
Kwani biblia isemapo ‘wakabatizwa kwa jina lake Yesu’ maana yake ni kwamba aliyefanya hicho kitendo cha kuwabatiza hakutamka kinywani mwake maneno ‘kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mt.? au walichukua mtu wakamzamisha huku wakitamka ”nakubatiza kwa jina la Yesu”? How can u prove that?

  Mimi nachukulia kwamba mwisho wa maswali uliyoyauliza majibu yake umeyapata kwamba ktk ubatizo “walichukua mtu wakamzamisha huku wakitamka, ‘nakubatiza kwa jina la Yesu’” bali ninaamini walitamka, “nakubatiza kwa jina la Bwana Yesu Kristo”; ndipo unasema, “How can u prove that?”

  Proof ya ki Maandiko ndiyo hivyo vifungu vinavyotamka wazi, kama hicho cha Mdo 2:38, na hivyo ulivyovinukuu, maana sioni kulikuwa na ugumu gani wa kutamka “kwa Jina la Baba na Mwana na RM”, bali naona walihudumu katika FULL UNDERSTANDING ya jambo hilo, hence the smooth flow of the tongue!

  Vifungu vyote ulivyovinukuu havina tofauti ya kimaudhui, vyote vina denote Nguvu iliyomo ndani ya Jina la Yesu, ile Mamlaka, na sasa inakuwa applied to meet hitaji la hali iliyo mbele yao!

  Mitume na hao wote waliopokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste walikuwa wamebatizwa Ubatizo mmoja tu, ule wa Yohana, uliowatayarisha kumpokea Kristo, nao wakiisha kumpokea Kristo, wakatakaswa kwa Neno Yoh 17:17, ndipo wakastahili kumpokea RM kama alivyonena Yohana Mbatizaji, Mt 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu … yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.”

  Gbu brother, & all!

 32. Seleli,
  Yaani ishu yenyewe iko hivi, mfano wake:
  Wewe Seleli, na Sungura ni marafiki saana, kimsingi mmekuwa ndugu. Mimi Lwembe tunafahamiana na wewe Seleli. Basi siku moja nikakutana nanyi njiani, tukasimama kusalimiana, nawe ukanitambulisha kwa Sungura.

  Baada ya miezi sita tukaonana nawe Seleli, ndipo katika mazungumzo yetu, kwa furaha kabisa, nikakuuliza kama unamfahamu yule rafiki yangu anayeitwa Sungura??

  Unaionaje hali yangu hiyo? Kidogo nitakuwa fuzzy enhe??

  Sasa ifananishe na ya huyu ambaye mt. Paulo ndiye aliyemtambulisha kwa Kristo kwa maelezo yakinifu, baada ya miezi sita alipokutana na Paulo anamwambia ati yeye Kristo ndiye ‘Role Model wake’ na si Paulo, yaani hata Paulo akitaka kuwekwa sawa basi aje kwake yeye!!!!

  Basi mambo haya ndiyo nimeyarudia kuyasoma mara nyingi tu zaidi ya unavyoweza kufikiri, sijapata jibu la “hali iliyomkamata” mpendwa huyo, labda ndg yangu unalo jibu!

  Mjoli Haule aliwahi kusema, “Mbombo ngafu!”

  Gbu!

 33. Lwembe Lwembe Lwembe;

  Unavyojua kupangilia maneno yako katika sentensi huonekana uko vizuri sana kiuelewa, lakini linapofika suala la usahihi wa hicho ulichokielezea kwa mpangilio mzuri wa maneno mm hushindwa kukuelewa kuhusu uwezo wako wa kiufahamu.

  Ngoja nikuoneshe kitu hapa, nakunukuu:
  ”Katika Yn 5:43, Kristo anasema, ‘Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, …’ Ikiwa yeye amekuja kwa jina la Baba yake, na iwapo Baba ni jina basi Yesu alipaswa kuitwa ‘Baba’ jambo ambalo si sawa!”

  Sentensi ‘nimekuja kwa jina la Baba yangu’ huwezi kufikiri hata kidogo ati kuwa Baba ndio hilo jina. Kinachomaanishwa hapo ni kuwa nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu.(jina linasimama likiwa na maana ya mamlaka)

  Na hapa nakunukuu:
  ”Yn:14:26, Kristo anasema, ‘..Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampleka kwa jina langu…’, kwa hiyo kulingana na kifungu hiki, pia ni dhahiri Msaidizi huyo, Roho Mtakatifu, jina lake litakuwa YESU.”

  Hapa napo umepotosha Lwembe. Sentensi ‘Baba atampeleka kwa jina langu, simply inamaanisha atampeleka kwa mamlaka iliyo katika jina langu. Mtu ukiwa unawaza sawasawa huwezi hata kidogo kusema ati hiyo sentensi ”Baba atampeleka kwa jina langu” Yesu alimaanisha kusema kuwa Baba atamwita Roho mtakatifu jina la Yesu.

  Na uelewe Mungu hajajifunua kwa jina Yesu peke yake, kwa Musa alijifunua kwa jina la Niko ambaye niko.Na sidhani kama kuna mtu kwenye mada hii amesema kuwa Baba ni jina.
  Na kumbuka pia Yesu alipoombwa na Filipo kwamba ‘tuonyeshe Baba yatosha’, hakujibu akisema kuwa ‘mimi ndiye Baba’, bali alisema ukiniona mimi basi umemwona Baba.

  Fafanuzi nzuri ya Yesu kuwa ni Mungu ni ile ya Yohana 1

  Maana kwa kuwa Mungu ndiye anayejidhihirisha kama Yesu, basi asemapo mkiwabatiza kwa jina la Baba,Mwana, na Roho mt, maana yake ni kwamba mtu akisema:
  -kwa jina la Baba, Mwana,na Roho mt., maana yake anakuwa amesema kwa jina la Yesu
  Sasa hapo tofauti ni nini kusema kwa jina la Baba,Mwana,na Roho mt. na kusema kwa jina la Yesu?
  Tofauti ni nini kati ya anayesema mheshimiwa Obama, na mwingine akasema Raisi Obama, kiutekelezaji?

  Na niliuliza,kwa nini Yesu kwenye suala la ubatizo anasema kwa jina la Baba, Mwana,na Roho mt., lakini kwa habari ya kutoa mapepo, kunena kwa lugha, kushika nyoka, nakula vitu vya kufisha, anasema ‘kwa jina langu? Tofauti ni nini?

  Tunachobishania ni nini,kutowaona mitume wakibatiza kwa kutamka jina Baba,Mwana,na Roho?
  Kwani biblia isemapo ‘wakabatizwa kwa jina lake Yesu’ maana yake ni kwamba aliyefanya hicho kitendo cha kuwabatiza hakutamka kinywani mwake maneno ‘kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mt.? au walichukua mtu wakamzamisha huku wakitamka ”nakubatiza kwa jina la Yesu”? How can u prove that?

  Au mtu akishatamka ‘kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mt. basi haruhusiwi kutamka jina Yesu at the same time,au kutamka hizo sifa si kulitamka jina Yesu?

  Tofauti ya matumizi ya jina la Yesu katika haya matukio ni ipi?:

  ” Acts 10:48 And he commanded them to be baptized in the name of the Lord.
  ”Acts 19:5 they were baptized in the name of the Lord Jesus.
  ” Acts 3: Then Peter said, “Silver or gold I do not have, but what I do have I give you. In the name of Jesus Christ of Nazareth, walk.”

  Na swali jingine ni hili hapa:
  Ivi mitume(thenashara) pamoja na wale waliopokea Roho mt. siku ya Pentecoste walibatizwa tena(tofauti na ubatizo wa Yohana) ndipo wakapokea Toho mt.?

  Kwako Lwembe na wadau wote!

 34. Lwembe,

  Kuna nyakati niliwahi kukushauri kua- U PRINT COMMENTS ZAKO KWA MADA NYINGI HUMU KISHA AT HOME WHEN RESTING, PLZ SOMA KISHA JIULIZE, JE KUNA SUBSTANCES KWELI HUMO? Honestly jijibu but hulazimiki ku-share your reply here in public.

  Press on

 35. Tunapoendelea katika tafakari, hebu tulitazame Jina hili la YESU ili tuone asili yake, huenda tukapata mwanga zaidi juu yake, pia iwe fursa yetu ya kujisahihisha kwa kuuangalia tena ukweli huu ambao Mungu ameuweka hapo kwa ajili yetu:
  Katika Yn 5:43, Kristo anasema, ‘Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, …’ Ikiwa yeye amekuja kwa jina la Baba yake, na iwapo Baba ni jina basi Yesu alipaswa kuitwa ‘Baba’ jambo ambalo si sawa! Bali kama yeye Yesu amekuja kwa jina la Baba yake, basi jina alilonalo ndilo jina la Baba yake, kwa hiyo Baba yake atakuwa anaitwa YESU!

  Yn:14:26, Kristo anasema, ‘..Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampleka kwa jina langu…’, kwa hiyo kulingana na kifungu hiki, pia ni dhahiri Msaidizi huyo, Roho Mtakatifu, jina lake litakuwa YESU.

  Haya, Yesu alipozaliwa, jina hili alilopewa la Yesu halikutoka kwa Yusufu wala Mariam bali alikuja nalo Malaika Gabriel kutoka mbinguni ili apewe huyo mwana wa Mungu atakayezaliwa, Lk 1:31 ‘Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita YESU’!

  JINA la: bila shaka kama inavyosomeka Jina hilo litakuwa ni moja vinginevyo ingekuwa MAJINA YA, basi ni dhahiri kuwa “Jina” ni moja la “Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.” Ndipo iwapo ‘Jina la” ni jina moja na si majina mengi, basi hilo jina moja litakuwa ni “Baba na Mwana na Roho Mtakatifu” jambo ambalo kulingana na “Utatu Mtakatifu” unaojidhihirisha katika Nafsi tatu tofauti za Mungu; Nafsi ya Baba, Nafsi ya Mwana na Nafsi ya Roho Mtakatifu, nazo nafsi hizi tatu halisi ambazo si nafsi moja, ukizigeuza hizo nafsi kuwa jina utakuwa umeuvuruga mpangilio mzima wa jambo hilo, kwani tunafahamu kuwa Jina la Baba ni Jehova, na pia Maandiko yako wazi kuwa Jina la Mwana ni Yesu.

  Basi uelewa huu, kwa uchache watosha kutuhakikishia kuwa ‘Baba’ si jina bali ni cheo, maana jina lake twalijua toka huko Agano la Kale kuwa ni Jehova. Pia ‘Mwana’ si jina maana twalijua jina lake kuwa ni YESU. Ndio kusema vyeo vyote vitatu, cha Baba na cha Mwana na cha Roho Mtakatifu vinatumia ‘JINA MOJA’ ambalo kulingana na ushahidi wa kimaandiko tuliouona hapo awali, jina ambalo Nafsi hizo Tatu zilizolichagua kulitumia ni hilo la Yesu. Hata tungeweza kusema kwa mkristo wa leo kujifanya unaliitia Jina la Bwana kwa kuliitia jina la JEHOVA hilo laonesha hukuelewi unakokwenda wala ulikotoka! Mungu amekuwa akijifunua kwetu polepole toka Agano la Kale hata ametamatisha kujifunua kwake katika Agano Jipya kwa Kristo Yesu! Hata ungekuwa na shauku ya kuongea na ‘Baba’ katika siku za Kristo, basi ungeongea na Kristo, maana huyo alikuwa ndiye utimilifu wote wa Mungu katika jinsi ya Mwili (Kol 1:13)!

  Tena basi, katika kulikamilisha hilo tunaambiwa kuwa huyo Yesu, Mungu sasa amemfanya kuwa Bwana na Kristo (Mdo 2:36)! Neno ‘Bwana’ katika Biblia humaanisha Mungu au Baba, na Neno Kristo maana yake ni Upako wa Mungu au Roho Mtakatifu. Hivyo kuanzia hapo huyo Yesu sasa anaitwa Bwana Yesu Kristo!

  Basi Petro na mitume wakiwa ni wa rohoni, wao walijua wanachokifanya tofauti na makundi yetu ya mwilini.

  Gbu friends!

 36. Sungura,
  Comment yako hii kwa Mabinza kuhusu udhihirisho wa Mungu, imenichanganya kidogo, lakini ngoja nivute subira kidogo, niendelee na hili wazo la “Jina” katika Ubatizo, halafu tukijaaliwa basi utanifafanulia zaidi!

  Gbu, brother!

 37. Lwembe nimepitia hiyo makala yako uliyosema ueandika mengi.

  Ina mzaha mkubwa ndani yake, kwa hiyo sintaijibu.

  Nashukuru,

  Mungu akubariki brother

 38. Ndugu yangu Mabinza naendelea!

  Kwa hiyo katika hicho kisa cha uumbaji tunaona kuna mambo matatu.
  1. Kuna Mungu
  2. Kuna Roho wa Mungu
  3.Kuna Neno la Mungu

  Kumbuka nilikwambia ufikiri, wakati Roho wa Mungu anaatamia vilindi vya maji Mungu alikuwa wapi! Kwa hiyo Roho wa Mungu yeye ndiye aliyesimama juu ya vilindi vya maji kama neno linavyosema. Huyu ndiye baadae anakuja duniani kwa udhihirisho mwingie akiitwa Roho mtakatifu.
  Kwa hiyo hiki kitendo cha Roho wa Mungu kuatamia vilindi vya maji mimi naweza nikasema kwa lugha nyingine kuwa ni nguvu za Mungu zilitulia juu ya vilindi vya maji.
  Lakini huwezi kuuita huo udhihirisho kuwa Mungu na Roho wake ni Mungu wawili hao.
  Kwa hiyo hapo huwezi kumtenga Mungu na Roho wake ili upate vitu viwili ambavyo viko tofauti.

  Kisha kuna Mungu na Neno lake. Mungu aliposema kuwe nuru ina maana huyo Neno ndiye aliyekwenda kuitokeleza hiyo nuru, yeye fundi hodari wa hiyo kazi. Na huyo ndiye baadae alikuja akavaa mwili na kuweza kuonekana na watu akiwa kama mwanadamu. Na huyo alipotokea kwenye mwil alipewa jina maalum ambalo ni Yesu kulingana na kazi ya kile kilichomfanya avae mwili,yaani kazi ya uokozi. Na huyu ndiye katika udhihirisho wa kutumwa kwake Mungu akamwita pia mwana wake

  Hapa napo huwezi kumtenga Mungu na Neno lake ili upate vitu viwili tofauti.

  Anayejaribu kuutafsiri huu udhihirisho wa Mungukuwa ni Mungu watatu hao, ni wazi anapotosha maana ya huo udhihirisho au kujifunua kwa Mungu. Hakika huyu ni Mungu mmoja. Na pengine huwezi jua,anaweza akaamua kujidhihirisha kivingine tena.

  Huko kujidhihirisha kwake hakuna mtu anaweza kukuhoji na kujaribu kutafititafiti kuwa iliwezekanaje. Ndio mana yeye ni Mungu, na anadumu kuwa Mngu.

  Bila shaka yuele malaika katika kugombea mwili wa Musa angeweza kumkemea shetani kwa jina la Yesu ikiwa Mungu angeshajidhirisha na kujiwekea mamlaka yake katika hilo jina. Lakini kwa kuwa ilikuw bado malaika alisema ‘Bwana akukemee’.

  Kwa hiyo concept pia ya u-Baba na u-Mwana wa Mungu, au niseme u-Baba wa Mungu na u- Mwana wa Neno,inakuja kujidhihirika pale Mungu anapoamua kulivalisha / kumvalisha mwili Neno lake/wake.

  Huwezi kumtenganisha Mungu na Neno lake, na Nguvu yake pia.

  Hivyo basi, ukiondoa hizo dhihirisho za Mungu na kuamua kurudi kwenye square one, lugha inabaki ni moja tu,yaani Mungu mmoja.

  Ngoja nikomee hapo!

 39. Sungura, nimeandika majibu ya post yako ya nyuma kidogo nikiwa sijaziona hizi post zako mbili za leo mpaka niliporefresh! Kwahiyo, bila shaka waweza kuona mambo yanayojirudia, ambayo majibu yake umekwisha yatoa, basi tuyaoanishe katika ujumla wake na tuendelee kuanzia hapo!

  Thanx & Gbu!!

 40. Sungura,
  Nikiisha kuwa nimeuweka Msingi wa kwamba Biblia ndiyo Yakini yangu, in its entirety, nadhani sasa naweza kuyarejea maswali uliyoniuliza kwa wepesi zaidi.

  Kwanza umenifurahisha sana katika argument yako, kuhusu Ubatizo kwa jina la Yesu Kristo kuwa ni kwa ajili ya Ondoleo la dhambi na kuvipokea vipawa vya RM na hatimaye Ubatizo wa RM, kuhusu jambo hili unasema,
  “”Hii mimi siikubali. Zaidi sana inanifanya nikuulize swali jingine kuwa ubatizo wa Roho mt. maana yake ni nini?
Sikubali kuwa ubatizo wa maji ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi, maana hutokea watu wakajazwa na Roho mt hata kabla ya kubatizwa kwa maji.””

  Hili unalolieleza ni jambo lililotokea kweli, watu walijazwa RM kabla ya kubatizwa, ninaamini unalizungumzia hili lililotokea katika Mdo 10:44 “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno”, likiwa ndio msingi wa argument yako, nayo yanayoendana na jambo hilo ndio kama mfano wako mwenyewe, kwamba nawe ulijazwa RM kama Kornelio!

  Kabla ya kulifanya jambo hilo kuwa ni Fundisho, ulipaswa uyaelewe vizuri mazingira yaliyopelekea jambo hilo kuwa hivyo. Kornelio alikuwa ni Mmataifa, ambaye kimsingi hakuwemo katika Hesabu ya Wokovu, lakini alikuwa akimcha Mungu, kiasi kwamba Sala zake na sadaka zake zilifika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu! Pia mwaweza kuona utata uliomkabili Petro kuhusu jambo hilo, kulingana na desturi za Kiyahudi asingaliweza kwenda kumhudumia Mmataifa. Mambo hayo yakiwa katika jinsi hiyo, ndipo Mungu aliyatimiza yote kama tunavyoyasoma katika kisa cha Kornelio, yaani kama tutapata insight ya jambo hilo! Na kilichofuata ni Ubatizo wa maji kwa jina lake Yesu Kristo, ili kuitimiza Haki yote!

  Basi kama nanyi mazingira yaliyopelekea muupokea Ubatizo wa RM kabla ya Ubatizo wa maji yanashabihiana na ya hao, hilo pia ni jema maana ninyi wenyewe ndio mashahidi wa mambo hayo, bali mtakuwa mnatofautiana na Kornelio katika kuitimiza Haki yote kwa kubatizwa kwenu kwa jina la Baba na Mwana na RM; na kwa hilo hata “RM” mliyempokea ninyi atakuwa na ushuhuda tofauti na yule wa kwa Kornelio!

  Kwahiyo nashawishika kukuambia kuwa huyo unayedhani kuwa ni RM, hakuwa yeye, bali ulipokea ‘roho mpya’ tu kwa kule kudumu katika ukiri wako wa kumpokea Kristo, ambavyo wakristo wengi wameaminshwa na walimu wao kuwa huyo ni RM! Labda “walinena kwa lugha” zile ‘Asante Yesu’ x 666 na mambo mengine ya mwilini au vipawa hivyo visivyo na majuto nk. Lakini RM wa kweli hukuongoza kuliamini Neno lake, ndipo ungewaelewa kwa urahisi mitume katika hayo wanayoyafundisha, pamoja na hiyo jinsi ya Ubatizo, maana Roho anayewaongoza wao kuyafundisha hayo, ndiye anayekuongoza na wewe kuyapokea!!! Kwahiyo hata hao waliopokea RM katika Ubatizo wa kwa jina la Baba na Mwana na RM, kama tukio hilo halikuambatana na hizo “Asante Yesu” x 666, labda wakawa wamenena kwa lugha nanyi mkawasikia kwa lugha zenu, basi jua kwamba hao ni wacha Mungu kweli, naye Mungu anawajibika juu yao kulingana na Nuru waliyomo. Kama tulivyo muona Mungu akiwajibika kwa Kornelio, kwamba Sala na sadaka zake amezipokea kweli, lakini hawezi kumpokea Kornelio, sharti apitie kwa Kristo, nao Mwili wa Kristo ni akina Petro, huyo aliyekabidhiwa Funguo za Ufalme, ndio maana ilimlazimu aje amfungulie aingie!!!!

  Pia umeniuliza kwamba ninalielewaje Andiko la Mdo 1:5, hili lisemalo, “ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.” Maelezo haya mimi ninayaona ni kurejewa kwa neno alilolisema Yohana ktk Mt 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu … yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.” Na sasa akilithibitisha hilo kwao mitume tena, katika jinsi ya ile Ahadi kabla ya kulikamilisha kama tunavyoliona katika Mdo 2:3-4 “Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, …” Ninaamini hii ndiyo jinsi iliyo bora ya kuyafuata Maandiko kadiri yanavyojitafsiri yenyewe!!!

  Ukitafuta kujua “Kwanini tunabatizwa kwa maji”, kama utatafuta kulijua jambo hilo kulingana na Biblia, jibu lake mbona limo humo peupe, labda uwe ni mtu usiye tosheka tu kwa maumbile! Otherwise mbona hicho kifungu unachokirejea cha Mdo 2:38 kinatamka wazi kwamba ni kwa ajili ya Ondoleo la Dhambi, hata Ubatizo wa Yohana pia, Lk3:3, “Akafika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi,” ndio maana hao walioupitia ubatizo huo, kama hao mitume, wakiisha kutakaswa kwa Neno, wakaupokea Ubatizo wa RM. Hata hao aliowakuta Paulo ktk Mdo 19: 1-7, kwa kukaa katika Msingi wa Neno, waweza kuona kwamba hao waliupokea Ubatizo wa Yohana ambao manufaa yake ameyaweka wazi kuwa, “Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.” Ndipo wakalipokea Neno hilo lenye kuwatakasa kulingana na kuitimiza ile Yoh 17:20 “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao”, ndipo wakalitii hilo Neno likawatakasa, wakaupitia huo Ubatizo kama ulivyo amriwa, kisha wakajazwa RM!!! Ndio maana ninakushangaa ndg yangu kwamba ulipokeaje Ubatizo wa RM nawe ukiwa umelikataa Neno linalokutakasa na kukuleta ktk Utii na si “utafiti”?

  Pia unasema, “”Na sioni kama pia inamashiko kusema kuwa kama tulibatizwa kwa jina la Baba, na Mwana ,na Roho mtakatifu ina maana tofauti na kubatizwa kwa jina la Yesu””, kuhusu jambo hili na jinsi unavyoliona kwa hisia zako, ni vigumu mimi kukuelewa unachokisema, kwani hili jambo si langu mimi bali ni Mungu ndiye aliyeliagiza, kwahiyo kulibishia kwako kunakuunganisha na wabishi wengine waliokutangulia ambao nao walikuwa katika dini zao na hawakuwa na masikio ya kusikia chochote zaidi ya hicho walichokishikilia; Muangalie Paulo alivyojitahidi nao, Mdo 19:8-9 “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu. Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha.” Basi unadhani hali za hao wakaidi baada ya kuachwa zitakuwaje? They died without hope!!!!

  Unasema, ““Tunaangalia matokeo gani yaliyo katika hizo ‘application’ mbili ili tujiridhishe kuwa ziko tofauti?”” Labda nikuambie kuwa application ya Mt 28:19 haijawahi kutumika katika Biblia, sasa hayo matokeo yake utayapimia wapi?

  Na Mwisho unasema, ““Na kama Paul alijua kuwa ili mtu awe amesamehewa dhambi zake ni lazime afikie hatua ya kubatizwa kwa maji, kwa nini alikuwa hawabatizi watu baada ya kuwahubiria? Ina maana alikuwa anawaacha wakiwa na dhambi bado!!!!””

  HAKUNA jambo kama hilo! Paulo hajawahi kufundisha hilo! Wewe mwenyewe hushangai kwamba Paulo hakuwahi kuwa na Kristo katika mwili, hata hizo siku arobaini baada ya kufufuka kwake alizoendelea kuwa na mitume akiendelea kuwafundisha Paulo hakuwepo, lakini si unamuona Paulo akiurejea Ubatizo sawa sawa na hao? Mungu si mnafiki hata awe na jambo la NDIYO na HAPANA kwa suala moja! Tujitahidi kufuata Instructions, tusitegemee jambo liwe linarudiwa rudiwa maelezo yake each and every time, ndio maana Paulo anasema tukiyaacha mambo ya mabatizo na kuwekea mikono wagonjwa, hayo mafundisho ya kwanza ya Kristo, lets go for the deep things of God! Sasa kama hivi vitu vya msingi havieleweki, utaniambiaje kuwa ulijazwa RM? It’s joke, and a savage one for that matter because it involves your soul!

  Kwa hali uliyonayo, unapaswa urudi hapo katika Mafundisho ya kwanza ya Kristo, ubatizwe sawa sawa ndg yangu, halafu huyo RM utakaye jazwa safari hii mpeleke moja kwa moja kwenye Neno la Munguumpe WORD TEST. This time mpeleke pale kwenye kisa cha Sauli na yule mwanamke mchawi, akiitikia “Amina” kwamba yule aliyepandishwa alikuwa ni nabii Samweli, endelea mpeleke kule kwenye “Simpi ruhusa mwanamke…” akiitikia “Ameeeen!” nenda naye mpaka pale anapowataka wanawake wafunike vichwa vyao, akisema Amina, usiridhike upesi upesi usije nawe ukaanza kuwafunga vitambaa kwa haraka zako, muulize wafunikwe na nini? Akiumbia, “Wamepewa nywele zao ziwe kifuniko”, wewe sasa ndio ruuuka juuuu kwa AMEEEEEEEEEEN!!!!! Itakayoiamsha mbingu yote ikajua kuwa kuna mwenye dhambi mmoja ameokolewa!!!!!!

  Duh, nimeandika “mingi”!!!

  Gbu & all!

 41. Mabinza;
  Nakujibu kuhusu suala la utatu.

  Niliposoma tu jinsi ulivyoliongelea hilo suala, nilijikuta nasema moyoni mwangu kuwa wewe ni mjinga. Nikahisi nimekosea kuwaza hivyo, lakini baadae nikakumbuka kuwa ujinga si tusi, hata mimi ni mjinga kwenye mambo mengi tu.
  Kwa hiyo kwa suala hili wewe ni mjinga Mbinza.

  Sikia, nimekwambia Mungu ni mmoja, lakini KAJIDHIRISHA kwa wanadamu katika namna au phase tatu. Lakini wewe katika kutokuelewa kwako unadhani huko kujidhihirisha kwake kwa hizo namna maana yake wamejidhihirisha Mungu watatu.

  Kwani nini kinachomshinda Mungu kuwa Baba hapohapo akawa Mwana na hapohapo akawa Roho mtakatifu?

  Wewe unaposoma ule mstari wa pili wa hiyo Yohana unajifunza nini?
  Kama neno walikuwa pamoja na Mungu,kwa kiswahili cha kawaida tu Mabinza, inaonesha hapo kulikuwa na watu wawili au mmoja?

  Halafu Yesu anaposema muwe na umoja kama mimi na baba tulivyo na umoja alikuwa anamaanisha nini?

  Umejibu hovyo sana swali langu la kilichotokea baada ya Yesu kubatizwa, ambapo hilo jibu lako ni sawa na kusema hujajibu chochote.
  Ati unasema ilikuwa kwa ajili ya kuthibitisha yale Yohana alikuwa amesema! Ulichotakiwa kujibu Mabinza ni kueleza nini maana ya hicho unachokiita kuwa ni uthibitisho.

  Ulishawahi kujiuliza Mungu alijidhihirisha kwa Musa kama nani?(Baba,Mwana,au Roho)

  Na ulishawahi kujiuliza kwa nini kuwe na concept ya Baba, na Mwana?

  Unachotakiwa kusema kuwa hakimo kwenye biblia ni sentensi ”utatu mtakatifu”!

  Anyway, acha nikujibu swali lako hili la utatu:

  ” Labda nirudi kwako Sungura, iwapo Neno ndiye Mungu na huyo Neno ndiye Yesu, kama tulivyoona toka mistari hiyo michache iliyopo hapo juu, ikiwa utatu ni Mungu mmoja, niambie hapo Baba ni nani, na Mwana ni nani, na Roho mtakatifu ni nani?

  Let’s go back to Genesis:

  Wakati Mungu anaumba biblia inasema Roho wa Mungu alitulia juu ya uso wa maji;
  Think; Mungu ni nani hapo na Roho wa Mungu ni nani?Au wakati Roho ya Mungu anatulia juu ya vilindi vya maji Mungu yeye alikuwa wapi?

  Halafu akasema; na iwe nuru,nuru ikawa.
  Think;nani aliyeitokeza hiyo nuru, na wakati huo Mungu alikuwa wapi?

  Kesho ntaendelea Mabinza.

 42. Mabinza;

  Sikukwambia kwamba usijibu, bali nilisema sijakuuliza ili uyajibu, ila ukitaka unaweza kuyajibu. Umetaka kuyajibu ni vema.
  Pia kum-provoke mtu si kitu kibaya Mabinza, kwa hiyo hujanikosea, bali ulinifanya tu niseme zaidi.

  Halafu ni wapi biblia imesema kuwa Theolijia ni hekima ya wanadamu?

  Nakunukuu; ”
  Kinachofanyika ni kwamba, Roho mtakatifu yupo kuhakikisha kuwa katika Biblia hakuongezewi Jambo jipya na wala hakupunguzwi Neno lolote toka humo na watoto wa nyoka!” Wewe hii umeitoa kwenye maandiko gani Mabinza?

  Na nyingine hii hapa ”‘Hard copy’ ipo katika ‘Soft copy’ kumpiga chenga shetani na wanae, kwakuwa kila mtoto wa Mungu ana uwezo wa kuwa nayo na wa kuitumia ‘Computer’! Computer niimaanishayo ni NGUVU ZA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU NDANI YA WATOTO WA MUNGU! Mtoto wa Mungu kila mmoja anawezo wa kumwelewa asemavyo na atakavyo Roho mtakatifu kipekee, kila mtu kwa Jina lake! Si wakati tena wa namna ile ya kwanza, sasa mwalimu ni Roho mtakatifu mwenyewe”

  Unaposema sasa mwalimu ni Roho mt. unamaanisha wakati wa kanisa la kwanza malimu alikuwa ni nani?

  Kwa hiyo wakati huo shetani alikuwa hawezi kupigwa chenga?

  Mabinza hapa umejiongelea tu ndugu yangu!!!

  Kama hujui maana ya theolojia, basi ndiyo hii uliyosema hapa, bahati mbaya tu ni kwamba ni theolojia mbovu. Unapenda sana kuiponda teholojia Mabinza bila kujua sana wewe inakuhusuje na unaitumiaje katika maisha yako ya kila siku.

  Mabinza acha kujadili ki-sunday school rafiki yangu kama ulivyofanya hapa;
  ”Hakuna hata mstari mmoja unaosema kuwa Mitume walifundisha MAKOSA! Biblia ambayo ndiyo Neno la Mungu inaniambia kuwa WALINENA NA KUANDIKA NA KUFUNDISHA KWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU! Kusema, upo wakati hawakufundisha ipasavyo maelekezo ya Yesu, NI KUMKUFURU YULE ROHO MTAKATIFU ANAYESEMWA NA BIBLIA KUWA ALIWATUMIA KUINJILISHA, AMBAYE NDIYE YESU MWENYEWE NA NDIYE MUNGU MWENYEWE” Huu ni utoto.

  Sikia, mtume au mtumishi wa Mungu kukosea maanayake si kwamba aliyekosea ni Roho mt. Kwa hiyo usijaribu kupindisha mambo kwa kujaribu kusema ati kwa kuwa tunadhani Petro alikosea, basi kwa kudhani kwetu/kwangu hivyo ni kumkufuru Roho mt. Najua maana ya kumkufuru Roho mt wala usijaribu kunitisha. Wewe tulia tuendelee na mdahalo.

  Hebu niambie kuhusu Petro, sera yake ya wayahudi kujitenga na wamataifa ilikuwa sawa, na kama haikuwa sawa kwa hiyo aliyekuwa amekosea si Petro bali ni Roho mt?

  Ngoja nikuoneshe sasa vile ambavyo haujui uhalisia wa unachokisema, na hivyo unaamua kupotosha. Ona hapa nakunukuu:

  ”Kinachotokea mtu akibatizwa kwa jina la Yesu, kimeelezwa katika Mdo. 2:38 ambayo inasema, “38……, “……. kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu. nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Na kile ambacho hakifanyiki mtu akibatizwa kwakutumia, Kwa Jina la Baba, na la mwana na Roho mtakatifu ni KUTOSAMEHEWA DHAMBi NA KUTOPOKEA VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU! Labda nikujibu kwa kifupi tu kwamba, kama ambavyo viwete, vipofu, tasa, wagonjwa na wengine wenye kuhitaji uponyaji, wasivyopokea uponyaji lisipotumiwa Jina la Yesu!”

  Unasema mtu asipobatizwa kwa jina la Yesu hawezi kusamehewa dhambi na hawezi kupokea Roho mt. Soma hapa nini kilitangulia kati ya watu kujazwa Roho mt. na kubatizwa kwa maji kwa juna la Yesu. (Acts 10:44 While Peter was still speaking these words, the Holy Spirit came on all who heard the message. 45 The circumcised believers who had come with Peter were astonished that the gift of the Holy Spirit had been poured out even on Gentiles. 46 For they heard them speaking in tongues[b] and praising God.

  Then Peter said, 47 “Surely no one can stand in the way of their being baptized with water. They have received the Holy Spirit just as we have.” 48 So he ordered that they be baptized in the name of Jesus Christ. Then they asked Peter to stay with them for a few days.)

  Umeona Mabinza, hawa watu walianza kujazwa Roho mt, baadae Petro nado akasema wabatizwe kwa maji.
  Unaona wewe jinsi ulivyosema uongo kwa sababu ya kukariri?!!!!

  Na kwa mujibu wa hii mistari na kile ulichokisema wewe ni kwamba mtu anaweza akajazwa Roho mt.akiwa mwenye dhambi maana umesema ubatizo wa maji unaondoa dhambi na hawa watu walijazwa Roho mt wakiwa hawajabatizwa kwa maji(yaani kwa tafsiri yako; wakiwa hawajaondolewa dhambi).

  Kingine, ati lisipotumika jina la Yesu mtu hapokei uponyaji; Vipi kivuli cha Petro na vitambaa vya mahema ya Paul kuponya, lilikuwa linatajwa jina la Yesu ndipo hivyo vitu vinaponya.

  Wapi umesoma mtu alitaka kuponya mtu bila kutumia jina la Yesu halafu uponyaji haukutokea? Wewe hujawahi ona unapita tu sehemu pepo linalipuka bila hata wewe kusema chochote?

  Hapa na penyewe inaonesha hujui maana ya kutumia jina la Yesu rafiki yangu.

  Ngoja nisichanganye suala la ubatizo na suala la utatu, ili suala la utatu uliliniuliza vitu fulani juu yake nilijibu separately.

  Tuendelee!

 43. Inaendele Lwembe:

  Lakini kuna jambo jingine ni kwamba biblia hii ambayo mimi na wewe tunasoma leo imepitia mahali kwingi sana. Kuna vitu vingi vilivyopunguzwa, tena na wanadamu wala si Mungu. Wewe Lwembe unajua vizuri kabisa kuwa leo kuna version nyingi tu za biblia. Kuna vitu vingi tu ukivifuatilia kwenye maandiko ya asili unakuta viko tofauti. Ndio maana Roho mt yupo nasi.

  Kuna kitu umesema hapa, nakunukuu: ” Ni vigumu sana kwa mtu aliyetolewa nje ya Njia kuweza kuyaelewa hayo, ndio maana siwashangai sana ninapowaona wanahangaika kuupindisha ukweli wa Injili kwa kujitafsiria Maandiko! Hata Biblia inaposema, “Maandiko yoote yamevuviwa na Mungu”, wanakataa na kujilisha upepo!”

  Hapo bila shaka ulikuwa unamwongelea pia Sungura na Orbi kuwa ni miongoni mwa waliotolewa nje ya njia. Anyway, si dhani kama tuko nje ya njia brother!

  Ukweli ni kwamba si maandiko yoote yamevuviwa na Mungu, kuna maandiko mengine ni mawazo tipical ya watu, na yako kwenye biblia kwa kusudi maalum la kujifunza kitu fulani kwayo. Hata Paul sehemu zingine anasema ‘hapo ni mimi si Bwana’.
  Ksema maandiko yoote yamevuviwa na Mungu ni tofauti na kusema kila andiko lenye pumzi ya Mungu….!
  Na kumbuka kuna tofauti ya kusema kuwa kuna watu walikosea kwenye biblia na kusema kuwa biblia ina makosa, au biblia imekosewa, ni vitu viwili tofauti.

  Tunajadili mambo ambayo yana historia yake Lwembe, hayajazuka tu. Kwa hiyo ni vizuri pia kurejea kwenye historia kujua kama kweli tunachoambiwa leo kiko sawasawa na kilicho kwenye historia ya mambo hayo.
  Na hili ni miongoni mwa mambo ambayo wakristo wengi huwa hawapendi kuyajifunza, kwa kudhani kuwa kuyajifunza ni kujaribu kum-doubt Mungu. Kitu ambacho si kweli. Biblia kufanyiwa hila hakujaanza leo. Kuna vitu vingi tu kwa mfano kwenye biblia ya kiswahili vinekosewa ama ki-semanatic, ki- lexical, au ki-syntactical.

  Ndio maana nimeuliza mara kadhaa kuwa kwa nini biblia ilikoma kuandikwa?
  Ni Roho mt aliyesema kuwa sasa ikome/imetosha au ni watu tu kwa hekima zao waliona kuwa imetosha?

  Kwa nini matendo makuu ya watu kama akina Moses Kulola, T.L. Osbon, O. Roberts, Catherine Kuhman, John Wisley n.k, hayakustahili kujumuishwa kwenye matendo ya mitume? Au aliyewatumia si Roho mt?

  Kwa nini kuna vitabu viliondolewa kwenye biblia, aliyekuwa ametaka viwekwe ni nani na aliyeviondoa ni nani?
  Mimi huwa najiuliza na kuuliza haya maswali na najua kuna siku Roho mt. atanipa jawabu yakinifu.

  Lakini kuna mambo niliuliza ndg Lwembe ambayo ningefurahi nikipata majibu yake.

  Ngoja niendlee kuuliza;

  Yohana mbatizaji ana maanisha nini kusema ‘mimi nawabatiza kwa maji, ajaye nyuma yangu yeye atawabatiza kwa Roho na kwa moto?
  Au alimaanisha kubatiza kwa Roho na kwa moto katika maji?

  Je ni sawa kuamini kuwa kubatizwa katika maji ndio huko kufa na kufufuka na kristo anakokusema Paul, na ndio kubatizwa katika kristo?

  Tuendelee kujifunza.

 44. Lwembe ndugu yangu;

  Kuna kitu kimoja nakukubali sana, nacho ni jinsi unavyojua kuandika na kufanya muunganiko mzuri wa kutetea kile unachokijengea hoja.

  Sasa basi ngoja niseme sawasawa na nilivyokuelewa;

  Kwanza mimi binafsi kwa kule kusema kwa nini Paul alikataa kubatiza ukiachilia mbali wale aliowabatiza tunaowasoma, hata sikuwa na wazo kwamba ubatizo si wa lazima kama ambavyo wewe umejaribu kutafsiri. Na suala la Paul kutobatiza nililigusia nikiwa nafuatilia kile ulichosema kuwa ubatizo wa maji ni kwa ajili ya msamaha wa dhambi.

  Nilichokisema hiki hapa ”Na kama Paul alijua kuwa ili mtu awe amesamehewa dhambi zake ni lazime afikie hatua ya kubatizwa kwa maji, kwa nini alikuwa hawabatizi watu baada ya kuwahubiria? Ina maana alikuwa anawaacha wakiwa na dhambi bado!!!!”

  Lakini pia matamshi ya Paul kwamba hakutumwa kubatiza si dhani kama alimaanisha kama ambavyo wewe umejaribu kufafanua. Na sidhani kama Paul alikuwa na watu ambao wao kazi yao ilikuwa ni kuwabatiza wale ambao Paul amewaambia habari za Kristo.
  ”For Christ sent me not to baptize, but to preach the gospel: not with wisdom of words, lest the cross of Christ should be made of none effect. ‘ – 1 Cor 1:17”
  Anayesema hayo maneno huko mwanzo wa huduma yake tunamwona anabatiza, je ni lini alitambua kuwa hakutumwa kubatiza basi? ina maana wakati anabatiza alikuwa hajatambua kuwa hakutumwa kubatiza.(ni mtazamo wangu brother, challenge me)

  Sasa tofauti ya ubatizo wa Yesu na wa Yohana ni nini ikiwa vyote ni kwa ajili ya msamaha/ ondoleo la dhambi? Maana wa Yohana nao ulikuwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi, na watu walizamishwa huku wakitubu dhambi zao.
  ”John did baptize in the wilderness, and preach the baptism of repentance for the remission of sins. And there went out unto him all the land of Judaea, and they of Jerusalem, and were all baptized of him in the river of Jordan, confessing their sins.” – Mark 1:4-5”

  Je na sisi tunapaswa kuzamishwa huku tukiziungama dhambi zetu?

  Au nikuulize swali la msingi Lwembe kwamba tofauti ya ubatizo wa Yohana na ubatizo wa Yesu ni ipi au ilitakiwa kuwa ipi?

  Tulichojikita kukijadili sana hapa ni lile agizo la Yesu la kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt, lakini katika kile tunachoweza kukiita utekelezaji wa hili agizo mitume wanabatiza kwa jina la Yesu tu. Kwa hiyo kuna swali linaibuka miongoni mwetu kuwa kwa nini mitume wanatekeleza tofauti na agizo, lakini wengine wetu tunaona kuwa hawakutekeleza tofauti bali hivyo ndivyo agizo lilitakiwa kutekelezwa.

  Basi kutokana na hali hiyo ndio limetokea suala la mitume kukosea.

  Lwembe ngoja nifafanue juu ya hilo kama ifuatavyo:

  Suala la mitume kukosea inawezekana lipo maana nao walikuwa wanadamu tu. Ambaye hakukukosea ni Yesu tu. Lakini kukosea kwao kama kupo hakuifanyi injili ya Kristo iwe pungufu, ndio maana Roho mt. yupo nasi mpaka leo.
  Wala tusidhani kuwa Roho mt. kwa mitume alikuwa ana nguvu tofauti na nguvu aliyonayo leo, la hasha ni yuleyule.

  Na mfano wa kwamba hata wao wanaweza kukosea ni kitendo cha Petro kujaribu kuwabagua wamataifa kwa kudhani kuwa hivyo ndivyo ilitakiwa kuendelea kuwa, kama ilivyokuwa wakati wa sheria.
  p.t.o

 45. A! Sungura,

  Umesema, nisijibu baadhi ya maulizo yako, eti kwakuwa hukuniuliza ili nijibu, uliniandikia kwa nini? Mimi nayajibu, ukisema nakuvunjia heshima basi bwana, Mimi inaniuma, kwanza, Maswali yako hayo yamezingatia theolojia zaidi ambayo Biblia inaisema ni HEKIMA za wanadamu!

  “‘U really provoked me big time’ kwenye mchango wako wa tarehe 20/09/2013. Badala ya kuandika yote hayo uliyoandika, ulitakiwa tu uniulize kwa maneno machache kuwa nilimaanisha nini kusema mitume nao walikuwa wanadamu!”
  I’m not a Provoker sir! Sina nia ya kuumiza wengine, napenda watu na hufurahi nikiona nao wana furahi, rudisha tu furaha yako kama nilikukwaza pahala nisamehe, si kwa nia ya makusudi, ila kwakweli mkiwa katika mpira KUKANYAGANA imo, But Sory Bro! Sungura, Mwalimu hamchagulii mwanafunzi swali na namna ya kuuliza, ulichotakiwa ni kujibu tu, lakini katika huo mchango wangu wa 20/09/ 2013, hukujibu, nami sikufuatilia kwani nilijua kuwa nawe umegundua kuwa ukinijibu ipasavyo tu, UTAUNGA MKONO KUWA MITUME HAWAKUKOSEA KWA HIYO UNGE ENDA NJE YA THIOLOJIA YA UTATU NA WANAWAKE KUHUBIRI NA KUBATIZWA KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU, UKAAMUA KUKAA KIMYA! Ulichangua fungu jema, maana mtu huchagua mzigo anaofikiri ni mwepesi kwake kuubeba!

  Kuhusu Tafsiri za Biblia, hiyo si mada, mada ni je Mitume walibatiza Kinyume na maelekezo ya Yesu? Kujadili Tafsri za Biblia, ni usomi wa Theology, ninachojua ni kimoja tu, kwamba NAAMINI Biblia kuwa ni Neno la Mungu! Nyaraka za Paulo kutoandikwa ama kuandikwa zote, hiyo kwangu si hoja, kilichoandikwa ndicho kile kile kinachonihusu mimi kama Kanisa na Bibi harusi wa Kristo. Kwakukuthibitishia hilo ni kwamba, hata shetani hutumia hichohicho kilichoandikwa, si kile ambacho hakikuandikwa, kama unao ushahidi ni wapi na lini shetani alitumia kulidanganya Kanisa kwa kile ambacho hakikuandikwa, nipe!

  Umeuliza,
  “Una uhakika gani kuwa kila kilicho kwenye biblia kina pumzi ya Mungu? By the way, the bible is not a book, it’s a library ( a collection of books)”

  Sungura, nimekwisha kukuambia kuwa, naamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu na katika 2Tim. 3:16 inasema, “16Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki” Mstari huo ndiyo unaonipa uhakika kuwa Neno la Mungu lina pumzi ya Mungu. Kama Biblia ni Library mimi sina ugomvi na hilo, maana hata Mdomo ni Library kwa mjibu wa wanafalsafawanafalsafa!

  Katika Phase 1, umemalizia kwa kuuliza hivi, “Na ulishawahi kujiuliza kwa nini biblia haiendelei kuandikwa , na nani aliyeamua kuwa isiendelee kuandikwa wakati kanisa lipo na Roho mt. yupo anafanya kazi ndani ya watu? Au watumishi waliopo leo hawana Roho mt. wa kutosha ukilinganisha na waliotangulia?”

  Sungura, mbona uko hivyo?! Nani aliyekwambia? Iandikweje na wapi tena? Kinachofanyika ni kwamba, Roho mtakatifu yupo kuhakikisha kuwa katika Biblia hakuongezewi Jambo jipya na wala hakupunguzwi Neno lolote toka humo na watoto wa nyoka! Kwa sasa Biblia haiandikwi katika ‘Hard copy’ ipo katika ‘Soft copy’ kumpiga chenga shetani na wanae, kwakuwa kila mtoto wa Mungu ana uwezo wa kuwa nayo na wa kuitumia ‘Computer’! Computer niimaanishayo ni NGUVU ZA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU NDANI YA WATOTO WA MUNGU! Mtoto wa Mungu kila mmoja anawezo wa kumwelewa asemavyo na atakavyo Roho mtakatifu kipekee, kila mtu kwa Jina lake! Si wakati tena wa namna ile ya kwanza, sasa mwalimu ni Roho mtakatifu mwenyewe. Labda, hapo utakuwa hujaelewa, ni hivi, Biblia inasema, katika Yer. 31:33 kwamba, 33“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya wakati ule,” asema BWANA. “Nitaweka sheria yangu ndani yao na kuiandika katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” Unaona Sungura? Sisi ndiyo nyumba ya Israeli kwa kupitia Yesu katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu. Biblia nzima tiyari “tulisha IMEMEZESHWA” ndani yetu, maandiko na tafsri zake zote pia. Haipo haja tena ya kupata maelekezo ya sheria ya Mungu kwa kumezeshwa Tafsiri za Ki- binadamu zilizojaa thiolojia ya kilimwengu!

  Nikisha kusema hayo, labda nimalizie kwa kusema tu hivi,
  Mimi kwanza nifurahi tu kwasababu nilichokwambia hakijachukua hata saa 24, kimetimia! Nilisema, “ni mawili tu, moja ndilo lisimame, aitha TUWAFUKUZE mitume ili UTATU usimame au TUWAKUBALI Mitume utatu na ushirika wake vivunjike vipande vipande!” Nimesema kuwa yametimia kwa sababu umechagua lile la KUUSIMAMISHA UTATU, na kuthibitisha mwenyewe kuwa MITUME MAMBO MENGINE WALIFUNDISHA KINYUME NA YESU! Kwa hiyo ni wazi UMEWAKATAA MITUME! Uliposema mwenyewe kuwa, “Nini cha ajabu mtume kukosea; Petro alikosea mara ngapi akiwa na Yesu(au ni kwa sababu hakuwa na Roho mt. bado)? Sungura, swali kama hilo huoni ni ‘Ubishi’?, nikikukubalia nawe katika hili ‘NITAKUWA NAJITENDEA KIBURI MWENYEWE!’ Hakuna hata mstari mmoja unaosema kuwa Mitume walifundisha MAKOSA! Biblia ambayo ndiyo Neno la Mungu inaniambia kuwa WALINENA NA KUANDIKA NA KUFUNDISHA KWA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU! Kusema, upo wakati hawakufundisha ipasavyo maelekezo ya Yesu, NI KUMKUFURU YULE ROHO MTAKATIFU ANAYESEMWA NA BIBLIA KUWA ALIWATUMIA KUINJILISHA, AMBAYE NDIYE YESU MWENYEWE NA NDIYE MUNGU MWENYEWE! Biblia katika 1Yh.5:20 inasema, “.20Nasi twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi akili ili tupate kumjua Yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani Yake Yeye aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele.” Kukubali uongo wako huo ni Ibada ya Sanamu, (2Yh.5: 20-21)

  Phase2, hujaongea kipya sana, karibu ni yaleyale tu, unatatizika kweli au unaogopa kuisema ile kweli? Sungura, Baba si jina, Mwana si jina na Roho mtakatifu si jina pia. Yesu anachosema, watu wabatizwe kwa Jina la Yule mwenyesifa hizo, naye ndiye Yesu! Umesema unataka kujua, “Nini kinachofanyika katika tendo la mtu kuwekwa kwenye maji kwa kutumia ”kwa jina la Yesu” ambacho hakifanyiki mtu akiwekwa kwenye maji kwa kutumia ‘ jina la Baba, Mwana, na Roho mt?

  Kinachotokea mtu akibatizwa kwa jina la Yesu, kimeelezwa katika Mdo. 2:38 ambayo inasema, “38……, “……. kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu. nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Na kile ambacho hakifanyiki mtu akibatizwa kwakutumia, Kwa Jina la Baba, na la mwana na Roho mtakatifu ni KUTOSAMEHEWA DHAMBi NA KUTOPOKEA VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU! Labda nikujibu kwa kifupi tu kwamba, kama ambavyo viwete, vipofu, tasa, wagonjwa na wengine wenye kuhitaji uponyaji, wasivyopokea uponyaji lisipotumiwa Jina la Yesu!

  Umeniuliza, “Lakini Mabinza unaposema kuwa Baba ndiye Yesu, Yesu ndiye Roho mt. na Roho mt. ndiye Baba, ni katika muktadha upi huo?
  Kwa sababu hicho kinachoitwa utatu ni namna za Mungu alivyojifunua kwa wanadamu, wala hakimaanishi ni Mungu watatu”

  Ni kwa mkutadha wa Biblia takatifu kama ifuatavyo:- Yh. 1:1-4 inasema, “Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
  3Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.” Katika Mistari hiyo, kumetajwa kuwa kulikuwepo na Neno, na huyo Neno alikuwa ndiye Mungu mwenyewe! Lakini katika Uf. 19:13, inasema kuwa Yesu ndiye hilo Neno la Mungu, na hilo Neno yohana 1:1 inasema, “Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. ” Labda nirudi kwako Sungura, iwapo Neno ndiye Mungu na huyo Neno ndiye Yesu, kama tulivyoona toka mistari hiyo michache iliyopo hapo juu, ikiwa utatu ni Mungu mmoja, niambie hapo Baba ni nani, na Mwana ni nani, na Roho mtakatifu ni nani?

  Umemalizia kwa kujiaminisha kuwa MUNGU ANA NAFSI TATU, Uliposema, “Mabinza utasemaje, kwamba wakati Yesu katoka kubatizwa akashukiwa na Roho kilikuwa ni nini hicho – kwamba alikuwa ni Yesu anajishukia mwenyewe(how?), au alikuwa ni Baba akimshukia Yesu(if so, na sauti iliyotoka ilikuwa ya nani basi?).
  Hapo Mungu alijidhihirisha katika u-baba, u-mwana, na u-Roho mt. Yaani ile sauti ni Baba, yule aliyeshukiwa ni Mwana, na yule njiwa ni Roho mt.”

  Usipotee mkubwa, sababu kuu ya tukio hilo ilikuwa si kwa ajiri ya kujidhihilisha kuwa Mungu ni utatu, bali jambo hilo lilikuwa kwa ajili ya ushahidi wayale alivyoambiwa Yohana kuwa Yesu atabatiza kwa Roho mtakatifu, wakati Yohana alipokuwa akitumwa kuja kuandaa ujio wa Kristo. Habari yenyewe Yohana anaithibitisa mwenyewe aliposema katika Yh.1:33 kuwa, “33Mimi nisingemtambua, lakini Yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu Yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.” Kwakuwa wewe ni msomi, fanya utafiti utaona jinsi jambo la utatu lisivyo fundisho la Yesu, ndiyo maana Mitume hawakubatiza hivyo na hata maombi ama maombezi hatuyafanyi kwa jina jingine ila la Yesu. Biblia iasema katika Filip.2:10 kuwa, “ 10ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 46. Sungura, Orbi and all,

  Kuna jambo moja ambalo limenifurahisha sana, zile “shools of thought” mlizo zileta kuhusu Ubatizo!!

  Ya kwanza, kwa kumnukuu Paulo, ”Maana Yesu hakunituma ili nibatize bali nihubiri habari njema” hii inajenga Msingi kwamba Ubatizo si lazima, bali kuipokea Habari Njema, kama yule mwizi wa msalabani…!

  Jambo hili si sahihi. Sote tunafahamu kwamba mtu aliyetumwa kubatiza ni Yohana Mbatizaji, huyu ndiye aliyekuwa na Huduma hiyo, kwahiyo kauli ya Paulo inayasahihisha makosa ya kujigawa; huyu wa Kefa, huyu wa Apolo nk na si Fundisho la Mitume! Na tena, katika vifungu hivyo vilivyonukuliwa, pia yako maelezo mengine anayokiri kuwabatiza watu. Na pia tunapaswa kujiweka katika Msingi tuliojengewa, Habari Njema anayoihubiri Paulo ni ile ile moja waliyokabidhiwa mitume wengine, ambayo Ubatizo ni sehemu yake! Kwahiyo kudhani kwamba Paulo hakubatiza, hilo laashiria Msingi mbovu! Hata nikiwaulizeni wapendwa mliobatizwa, Je, mlipompokea Kristo, Askofu wenu Mkuu ndiye aliyewabatiza? Hata Yohana Mbatizaji hakuwabatiza wote waliomjia, ndio maana imeandikwa na wanafunzi walikuwa wakiwabatiza watu!

  Ya pili inasema, “”Kwa maana kama ukiyangaalia Maandiko kwa lensi finyu na nyembamba, si hilo tu la ubatizo walilokiuka mitume kwa kulifanya kinyume cha Yesu”” Hii ina uondoa Ubatizo walioutimiza mitume, na unaisimika jinsi ya “Jina la Baba na Mwana na Roho Mt”.

  Wazo hili ndilo kiini cha kupotea kwa wengi! Kuna msemo wa kichina unaosema, “If you must play, decide upon three things at the start: the rules of the game, the stakes, and the quitting time!” Yaani katika kuliendea jambo lolote lile, kuna mambo matatu ambayo wapaswa kuyaangalia kwanza kabla ya kujiingiza katika hilo jambo, hata ikiwa ni jambo la wokovu! La kwanza ni Sheria zinazoliongoza jambo hilo, la pili ni Dau na la tatu wakati gani ujitoe.!

  Nao Ukristo ukiwa ni ‘Game of Life, ninachokiona hapa ni kwamba wakristo wengi wamejiingiza katika “Game of Life” bila ya kuyaangalia mambo hayo. Sheria inayouongoza Ukristo ni Biblia. Yaani katika safari yako ya kiroho unaanzia huko Mwanzo, kisha unapita humo mpaka unaibukia katika Ufunuo, basi kama ni somo wa Kaini au Habili, huku ndiko unalipokea Dau lako, aidha ‘Robe Nyeupe’ kama ni somo wa Habili au ‘Ziwa la Moto’ kama ni somo wa Kaini, nawe unayafikia hayo ghafla, hata kama ulipanga utajitoa sehemu fulani ukiisha fanikiwa , bali kama Esau unajikuta umeukosa Urithi!!!

  Basi unapofika katika kujiaminisha kwamba mitume “walikosea”, hili laonesha kwamba umejichanganya mahali fulani, yaani you have lost the Game!! Fikiria utaendelea katika direction gani kama si pembeni ya Njia! Kwako wewe Biblia si Neno la Mungu tena, wala si Sheria, bali ni mkusanyiko wa vitabu, kama anavyosema Sungura, au humo mna maneno ya watu, na Shetani na ya Mungu! Kwahiyo Biblia yako si Mwongozo wa kuaminika tena, unaweza kuikosoa sehemu nyingi sana, na ukiwa makini zaidi, hakuna hata cha kuaminika humo ndani, maana mambo yote yameandikwa na watu. Kama wameweza kukosea katika hayo yaliyo dhahiri uliyoyaona kwa leo, je una uhakika gani na hayo mengine unayoyaamini leo, kesho ukiambiwa na kuthibitishiwa kuwa Petro alikuwa Shetani?

  Ukiisha litilia shaka Neno la Mungu, ukaaminishwa kuwa ndani yake kuna makosa, au humo mna maneno ya watu na ya Shetani na ya Mungu; hiyo ni dalili tosha kwamba wamekupoteza, utabaki na dini tu, unaondolewa katika kweli ambayo ingekuingiza rohoni, hivyo kubaki mwilini. Kila unapokutana na Ujumbe ambao ungeweza kukubadilisha, wewe kwa kutozijua Sheria, unaukataa! Unapewa maelekezo, lakini kwa kule kudanganywa unasema huo ni “ushauri tu”, lakini Makanisa ya watakatifu, hao wenye kuuendea Utakatifu, jumbe hizo ndizo zinazo watengeneza ili wa conform na ile standard! Ni vigumu sana kwa mtu aliyetolewa nje ya Njia kuweza kuyaelewa hayo, ndio maana siwashangai sana ninapowaona wanahangaika kuupindisha ukweli wa Injili kwa kujitafsiria Maandiko! Hata Biblia inaposema, “Maandiko yoote yamevuviwa na Mungu”, wanakataa na kujilisha upepo! Ndugu zangu, ingieni ndani ya “Bible Land” msifanye ushabiki wa dini! Ni rahisi sana “Kumkufuru Roho Mtakatifu” kuliko mnavyojidhanisha, Huyo ndiye Mwandishi wa hayo yote unayoyaona yana MAPUNGUFU, yaani kwa maneno mengine kwa kujua au kutokujua unakiri kwamba Roho Mtakatifu si MKAMILIFU!!!

  Nayo mambo haya ni ya jinsi ya rohoni, ndio maana hayaeleweki kwa watu wa mwilini. Kwa yule wa rohoni, yeye kwa roho hurudi huko nyuma katika wakati na kuwa sehemu ya kusanyiko lililoletewa ujumbe huo, kwahiyo yeye huyapokea maonyo hayo moja kwa moja, akiyatii na kuyasimamia. Lakini yule wa mwilini huyasoma na kuyachambua akiyachukua yanayomfaa na kuyaacha mengine akiyaona hayamhusu kulingana na mila au desturi au utamaduni ambao ndio kipimo cha maendeleo alichomo, ile ‘injili mpya’!

  Ndio maana mt Paulo akilitambua jambo hili analiambia Kanisa, “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”! Sasa kwa watu waliodanganyika huishia kukariri vifungu hivi na kuvipa uhai hapo wanapokemea mapepo, hapo ndipo hujiona vitani kweli, lakini wanapopotoshwa kimaadili hawajui lolote!!!

  Basi, kupotoshwa kwa jambo hakuizuii Kweli ya Injili kupokelewa au kuhubiriwa, au kurejewa, ndipo nitakapoyatolea maelezo maswali machache ya Sungura, nategemea mtayapima katika kipimo cha mtu anayeiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu LISILO na MAKOSA, kama ambavyo nami nawapima katika kipimo cha watu wanaoamini kwamba Biblia INA MAKOSA!!!

  Mbarikiwe, tunapoendelea kujifunza!

 47. Mabinza inaendelea- – –

  Original manuscripts za mkiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana , na Roho mt. zinasomeka hivi: ”baptizing them IN the name of the Father THROUGH the Son WITH the Holy spirit”- Mkiwabatiza KTIKA jina la Baba KUPITIA Mwana KWA Roho mtakatifu.(herufi kubwa nimeziweka mimi,maana kisarufi hayo maneno ndio yamebeba maana ya sentensi) Mt.3:11

  Kama yaliyoandikwa ndo yangekuwa kila kitu basi, kusingekuwa na haja ya kuwepo Roho mt. leo. Na kanisa la leo linaamini sana kazi ambazo zimeandikwa Roho mt. alifanya kuliko anavyofanya leo, utadhani kuwa amepunguwa

  Si kila sehemu Yesu alipotaka jambo lifanyike kwa jina lake alisema kwa jina la Baba mwana na Roho mt. ili kumaanisha kwa jina la Yesu.e.g.katika Mark 16: 17.
  Kwa nini hapo tu kwenye suala la ubatizo ndio anasema Baba,Mwana, na Roho mt. akiwa anamaanisha kitu kilekile alichomaanisha hata kwenye hiyo Mark 16:17?(yaani kwa jina langu)
  Kwa hiyo tusirahisishe tu ile hali ya Yesu sehemu moja kusema Baba, Mwana ,na Roho mt, na sehemu nyingine akisema tu kwa jina lake.

  Nini kinachofanyika katika tendo la mtu kuwekwa kwenye maji kwa kutumia ”kwa jina la Yesu” ambacho hakifanyiki mtu akiwekwa kwenye maji kwa kutumia ‘ jina la Baba, Mwana, na Roho mt?

  Kama hizo title za ‘baba,mwana,na Roho mt maana yake ni jina la Yesu. Au kama ukitaja jina la Yesu sawasawa na kumtaja Baba, mwana, na Roh mt, kuna tofauti gani?

  Lakini Mabinza unaposema kuwa Baba ndiye Yesu, Yesu ndiye Roho mt. na Roho mt. ndiye Baba, ni katika muktadha upi huo?
  Kwa sababu hicho kinachoitwa utatu ni namna za Mungu alivyojifunua kwa wanadamu, wala hakimaanishi ni Mungu watatu.

  Mabinza utasemaje, kwamba wakati Yesu katoka kubatizwa akashukiwa na Roho kilikuwa ni nini hicho – kwamba alikuwa ni Yesu anajishukia mwenyewe(how?), au alikuwa ni Baba akimshukia Yesu(if so, na sauti iliyotoka ilikuwa ya nani basi?).

  Hapo Mungu alijidhihirisha katika u-baba, u-mwana, na u-Roho mt. Yaani ile sauti ni Baba, yule aliyeshukiwa ni Mwana, na yule njiwa ni Roho mt.

  Tuendelee..

 48. Mabinza:

  ‘U really provoked me big time’ kwenye mchango wako wa tarehe 20/09/2013.

  Badala ya kuandika yote hayo uliyoandika, ulitakiwa tu uniulize kwa maneno machache kuwa nilimaanisha nini kusema mitume nao walikuwa wanadamu!

  Labda nikwambie kitu kingine: unajua kuwa biblia ya Kiswahili imetafsiriwa kutoka biblia ya Kiingereza iitwayo ”King James”?
  Unajua King James alikuwa mfalme wa Uingereza, wala hakuwa mtume? Hiyo version yake ambayo watu wengi sana ndo hupenda kuitumia zaidi katika kuandikwa kwake aliamuru mwenyewe kipi kiwekwe na kipi kisiwekwe. Jiulize ni mangapi yaliachwa!

  Na je unajua kuwa nyaraka za Paul kwa wakorintho hazikuwa mbili tu,bali zilikuwa nne? Kwa nini ziliandikwa mbili tu na zingine zikaachwa?

  Una uhakika gani kuwa kila kilicho kwenye biblia kina pumzi ya Mungu? By the way, the bible is not a book, it’s a library ( a collection of books)

  Na ulishawahi kujiuliza kwa nini biblia haiendelei kuandikwa , na nani aliyeamua kuwa isiendelee kuandikwa wakati kanisa lipo na Roho mt. yupo anafanya kazi ndani ya watu? Au watumishi waliopo leo hawana Roho mt. wa kutosha ukilinganisha na waliotangulia?

  {Sijakuuliza hayo maswali ili uyajibu, ila ukitaka unaweza kuyajibu}

  Lakini hili nakuuliza ili unijibu:

  Petro alikuwa na Yesu, na ndiye alikuwa mtume kiongozi. Ivi alipokuwa anajitenga au kujibagua na watu wa mataifa waliomwamini Kristo, unaonaje alikuwa amemwelewa Yesu na kazi ya msalaba kweli katika hilo eneo? Na je kufanya hivyo lilikuwa ni kosa au siyo kosa?

  Nini cha ajabu mtume kukosea; Petro alikosea mara ngapi akiwa na Yesu(au ni kwa sababu hakuwa na Roho mt. bado)?

  Haya, katika suala la ubatizo; nabii Yohana(mbatizaji) aliweka wazi kuwa yeye alibatiza kwa maji, lakini ajaye nyuma yake (Yesu) yeye atabatiza kwa Roho na kwa moto.
  Kumbe ubatizo uko wa namna mbili, wa maji na wa Roho na moto.

  Je kwa kusema kwake hivyo Yohana, je alimaanisha kuwa ajaye nyuma yake atabatiza kwa maji, na kwa Roho na moto, au alimaanisha kuwa atabatiza kwa Roho na moto tu?

  Kwa nini Yesu hakubatiza, na kwa nini Paul hakuendelea hakubatiza?

  Na kama ubatizo wa maji ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi, je watu wanaweza kujazwa na Roho mt. kabla ya dhambi zao kuondolewa?

  Mabinza tusomeni na kufuatilia mambo kwa upana, maana sarufi na fasihi ya lugha tu nayo ni tatizo katika kuielewa biblia.
  p.t.o

 49. Sungura,

  Ni hakika sana maulizo yako hayo mawili uliyouliza, yakijibiwa kwa usahihi ndiyo itakuwa suruhisho na hitimisho la mada hii. Lakini ni kwa kiasi gani ukweli hukubaliwa na walimwengu? Wewe umeuliza hivi, nanukuu,

  “Sasa tuko katikati ya shule mbili za fikra hapa.
  Ya kwanza inasema; Je akina Petro walifanya tofauti na alichoagiza Yesu?
  Ya pili; Je kuna tofauti kimaana kati ya kusema kwa jina la Baba, Mwana,na Roho mt. na kutumia jina la Yesu pekee?” Mwisho wa kunukuu.

  Nilichokuja kukielewa katika ukrasa huu tuliopo, ni kwamba, mada zote zinazogusa Utatu, Ubatizo, utumishi ama mafungu ya kumi hazifikagi mwisho, ila huachwa vipolo na baadaye tena huibuka, aitha kwa namna ileile ama kwa namna na kwa muundo tofauti! Sababu za Mada kutofikia hitimisho, pamoja na sababu nyingine, ni kwa sababu ya ‘MAPOKEO’ yatokanayo na mafundisho ya Hekima za kibinadamu ambapo hekima hizo hukinzana kwa kiasi kikubwa na Neno halisi la Mungu.

  Lakini utofauti huo wa Neno la kweli la Mungu, na wa lile lisilo neno la kweli la Mungu hufanana sana, kiasi kwamba, ni wenyemacho na masiko tu ya kiroho ndiyo hugundua, kwakuwa wao ndiyo waliokusudiwa, na wengine hubakia katika utaji wa shetani katika nyuso zao na utando wa Nta nzito katika masikio yao, kiasi kwamba hawaoni chochote cha kweli ya Mungu, hawasikii kitu na hawaelewi kabisa. Hushikilia kuwa wanavyoelewa ndiyo kweli yenyewe, na si kwamba wanajifanyisha tu hivyo, ila hivyo ndivyo walivyo ili wasije wakaokoka wakaponywa!

  Baba wa mapokeo hayo ni shetani, nyoka Yule alipandikiza roho ya kutoliamini Neno la Mungu kupita kwa wazazi wetu tokea Edeni; Hadi sasa watoto wa nyoka huyo huendeleza kuimarisha MAPOKEO yaleyale kwa kuyaboresha ili yaendane na wakati, kwa hali hiyo roho hiyo hiyo ingali ikitenda kazi kwa usahihi (ef.2:1-2) kwasanabu shetani anajua vizuri kuwa, Neno la Mungu nalo lipo kwa kuzingatia wakati!

  Kwa hiyo, hata kama mtu akijibu kwa usahihi maswali yako hayo mawili yaliyopo hapo juu, mtu huyo HATAHITIMISHA mada hii, ila kitakachofanyika itabaki hewani ikining’inia! Kwakuwa, ni ngumu KUELEWEKA KILE KINACHOJUALIKANA!” Selemani katika Hekima zake anasema, “Mtu huishi kwa ufahamu, na huangamia kwa ujinga” Uki isoma kwa makini ile Mt.28:19-20, inasomeka wazi kuwa, “19Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 20nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.’’ Amen”

  Kwa mjibu wa Neno la Mungu mwenyewe ni kuwa, Baba, mwana na Roho mtakatifu ni sifa za mamlaka aliyonayo Mungu mmoja ambaye ndiye Yesu; tukilinganisha na ile Mdo, 2:38 ambayo inasema, “38Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu. nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” mmoja kasema kabatizeni kwa Jina la Yule “Mwenye mamlaka” ya Baba, ya Mwana nay a Roho mtakatifu (lakini mwenye mamlaka ya Baba ya mwana nay a Roho mtakatifu ndiye Yesu ), wa Pili akasema kabatizweni kwa Jina la Yesu, Je hapo ipo tofauti ya maana? Zaidi ya hapo, Mwenye kuelekeza jinsi ya kubatiza kasema nitakuwepo nanyi wakati wote (Mt. 28:20) nafasi ya kupotosha ilitoka wapi na Yesu aliiruhusuje kiasi kwamba wabaki kuwa Mitume wakati hawakushika yote waliyoamliwa wayashike?!

  Umesema kwamba, “Hizo shule mbili ndizo hasa msingi wa mjadala huu,tukishang’amua nini kimefichika ndani yake tutakuwa tumefika mahali pazuri pa kufikia hitimisho yakini la mada hii.”

  Sungura unahatari wewe?!!, Je, ni kweli unataka kuujua ukweli na umejiandaa kujua kilichojificha katika yote hayo? Nitakwambia kwa kifupi tu kwamba,

  Ikitokea kukubarika kwa majibu mazuri yatakayotokana na kile ulichouliza, BAADHI YA MADHEHEBU NA UPENTEKOSTE WOTE VITAVUNJIKAVUNJIKA VIPANDE! Hebu, tuende kwenye ukweli, fikilia kwamba; Jibu la kweli ni kuwa, Injili ya Yesu kristo ililetwa kwetu yote na Mitume na kwamba, Biblia ambayo ni Neno la Mungu, inasisitiza kwamba, tufuate mafundisho ya mitume na kinyume chake ni laana. Lakini Mitume wanafundisha kuwa, Ubatizo ufanywe, kwa JINA LA YESU (Mdo 2:38); Kwa maana hiyo wale wote, waliobatizwa KWA JINA LA BABA,NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU, itabidi wabatizwe upya kwa Jina la Yesu, Je, u-Pentekoste utasimama? Kwa hiyo,ili utatu usimame ukiwemo na upendekoste ni lazima Mitume wawe WALIKOSEA hawakumfuata Yesu kwa mambo yote, la sivyo, Utatu na washirika wa utatu wamekwisha!

  Sungura, Unajua, Kilichomo katika Biblia, iwe kimesemwa na Nabii, Yesu au Mitume hilo lote ndilo NENO la Mungu! Na tunaposema Neno la Mungu tuna maanisha kumtaja Yesu Uf. 19:13 inasema, “13….. na Jina lake ni ‘‘NENO LA MUNGU.’’” Mitume wenyewe wanashuhudia kuwa kile walichokuwa wakikisema, iwe mtume kama mtume au vinginevyo ilikuwa ni kwa mjibu wa Kristo mwenyewe, katika 2Yh. 1:9 -11 “9Mtu ye yote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo, bali akayaacha, yeye hana Mungu. Ye yote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. 10Msimpokee mtu ye yote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani kwenu. 11Ye yote amkaribishaye mtu wa namna hiyo anashiriki katika matendo maovu ya mtu huyo.” Unaliona ‘dude’ hilo?

  Tukisema, Mitume walikosea kutobatiza kwa Jina la Baba na la mwana na la Roho mtakatifu, basi MITUME TUSIWAKARIBISHE, sawa na Neno katika 2Yoh.1:10, la kama walikuwa sawa kubatiza kwa mjibu wa Mdo.2:38, UTATU NA WASHIRIKA WA HUO, KWISHA! Sawa na Neno katika Gal 1:8-9, ambayo inasema, “8Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo mtu na alaaniwe! 9Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
  10Je, sasa mi”Umeiona Dini hiyo?

  “Ufahamu ni chembe ya uzima!”

 50. Siyi,

  Ungebaki ktk mada kuliko kuchokoza au kuchokonoa vitu huviwezi! Tatizo unapenda blaah blaah! nayaweza yote! Ya mastori na ya serious stuff, changua ipi unataka! Ila kwenye serious stauff, Ukiongea jambo, hakikisha una back up ya Neno kwa UHALALI-2Tim.2:15c NA HEKIMA YOTE-Col.3:16. Kwa msingi huo, unapoyapinga kwa MAKUSUDI mambo nyeti, mazito, ya kweli tupu, hakuna kubembeleza wala kulembalemba mtu hapo, nikummenya kisawasawa. Huwezi sema kuokoka Si sasa bali siku ya mwisho akija Yesu, wakati unajua huo ni utani wa kuzimu! Hence, wewe hauhitaji neema/kuelimishwa sijui, kusaidiwa, kuonywa sijui BALI NI KUZIMWA KABISA hoja zako mbovu KWAKUTUMIA HOJA ZA KUTISHA SANA KUKUTHIBITISHIA KUOKOKA NI SASA, SASA,SASA IVI STRICTLY AND SERIOUSLY SPEAKING.

  IKIWA KWAKO BIBLIA NI KITABU CHENYE MANENO NA MATENDO YA MUNGU, then NAKUHAKIKISHIA UMO NDANI KUNA WALIOJUA KUMENYANA ZAIDI YANGU-sema namI nakaza mwendo.Watu wa Mungu wa kweli, WALIOOKOKA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU, walipokutana na wapinzani wa KAZI YA MSALABA, WALIWAMENYA KWELIKWELI hao WATU WA DINI BILA MUNGU. Mifano ya wamenyaji wa hatari hao ni Yesu mwenyewe, Paul, Petro, Stephano, Appolo. Leo nakupa Appolo-mpiga karate za kiroho za hatari.

  Mdo.18:23-28 imeandikwa…. 23 Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. 24 Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. 25 Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. 26 Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. 27 Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo. 28 Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko

  Umemuona huyo Mpiga karate/Mmenyaji hatati huyo? Usijifanye hujaona mstari wa 27? Huu hapo…. ‘’Kwa maana ALIWASHINDA Wayahudi KABISA MBELE ZA WATU WOTE , akionyesha kwa MANENO YA MAANDIKO ya kuwa Yesu ni Kristo( yaani Mwokozi)

  Narudia tena hii, ina nguvu sana ‘’ALIWASHINDA Wayahudi KABISA MBELE ZA WATU WOTE’’( Notice: Aliwashinda(si tu kushinda bali Kabisaaaaa), mbele ya Watu-(si watu tu bali WOTE!)

  Nakuhakikishia nitamenyana na wewe vilivyo kuhusu kuokoka ni sasa na NITAKUSHINDA KABISA MBELE ZA WATU WOTE, kama unabisha na una uwezo, anzisha mada na kama hubishi, MIMI ‘APPOLO’ NAKUAMBIA ,ACHA KUCHEZEA WOKOVU! ni sasa wala hata si kesho, achilia mbali hiyo ya ukooo Yesu kuja!

  Othewise, baki ktk mada hii ya Ubatizo, ukiende huko kupinga KUOKOKA, nitakua Appolo kwako hakika! nitakuteremkia kama mwewe kwa kifaranga with upako na maandiko/maneno ya Mungu aliye hai.

  Press on

 51. Sasa tuko katikati ya shule mbili za fikra hapa.

  Ya kwanza inasema; Je akina Petro walifanya tofauti na alichoagiza Yesu?

  Ya pili; Je kuna tofauti kimaana kati ya kusema kwa jina la Baba, Mwana,na Roho mt. na kutumia jina la Yesu pekee?

  Hizo shule mbili ndizo hasa msingi wa mjadala huu,tukishang’amua nini kimefichika ndani yake tutakuwa tumefika mahali pazuri pa kufikia hitimisho yakini la mada hii.

  Ni vema tukafanya uchambuzi zaidi wa kiuhalisia kuliko kujaribu sana kufikiri kuwa kila mtu hapa anasimamia mfumo wa dini yake.

  Hata hivyo kama kuna mtu atakayetuonesha msimamo mzuri/sahihi wa dini au dhehebu lake, mimi sioni shida kuufuata, maana nadhani dini hiyo yenye huo msimamo mzuri itakuwa ni miongoni mwa dini zilizo safi.

  Huwa kuna kanuni fulani ambayo si rasmi katika ulimwengu wa uimbaji ambayo mimi huitumia kutatua tatizo. Kuna sauti inaitwa soprano ambayo ndiyo ‘leading vocal’ ambayo sauti zingine zote hujifunzwa/hupangiliwa kutoka kwayo. Sasa huwa ukitokea mgongano wa sauti kwenye ku-harmonize mara nyingi ni sauti ya pili na tatu tu ndo huhisiwa kuwa zinakosewa, maana zenyeyewe hutakiwa kuifuata sauti ya kwanza (soprano).

  Ndipo siku moja baada ya shida hiyo kutokea, tuliamua kuchunguza kama hiyo sauti ya kwanza iko sawa, ndipo tukagundua yenyewe ndo inatoka kwenye mstari na kuziingilia alto na tenor,basi tukawa tumetatua tatizo.
  ( waimbaji wataelewa zaidi ninachosema hapa)

  Hivyo basi ni vema tukajaribu kuchunguza kila kitu katika mada hii,hata vile ambavyo tunadhani kabisa kwamba haviwezi kuwa vimekosewa, aidha kwa tafsiri zetu, uelewa wetu,na mapokeo yetu,unaweza kuta vyenyewe ndo vimekosewa.

  Tuzidi kujadili!

 52. Mpendwa Sungura,

  Umechoka kufundisha? Umeamua ujiongeleshe tu ali mladi? 2Tim. 3:16 inasema, “16Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki 17ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema.” Unataka kusemaje Sungura, Mitume hawakuwa watu wa Mungu? Au na huo mstari wa 17 hapo juu unaukataa kuwa hauna mashiko ya Yesu? Kama unasema Mitume walikoseakosea sana tu kwakuwa nao ni wanadamu, mimi sikubishii kwamba hawakuwa wanadamu, Biblia inasema kuwa, Mitume walijazwa Roho mtakatifu ili wakafundishe Injili ya Yesu Kristo, na Yesu mwenyewe alisema, ‘Mimi nitakuwa pamoja nayi hadi mwisho’ lakini pia Biblia inasema Yesu alikuja kama Binadamu lakini hakutenda dhambi, na ndiye aliyepo na mitume mda wote kama Roho mtakatifu. Paulo akasema kwa kujiamini kabisa katika ile Gal. 1:8-9 kuwa. “8Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo mtu na alaaniwe! 9Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele! ”

  Sungura umesimamia andiko gani linalokuambia kuwa Mitume yapo waliyoyatenda kinyume na Maelekezo ya Yesu ambaye ndiye Roho mtakatifu? Uwe makini Bro, usicheze na maandiko, maandiko huua (2Kor. 3:6.). Yesu alisema katika Yohana kuwa Neno ni Roho tena ni uzima lakini ukimkufuru….! Uwe serious kama a prudently person bwana! Upo hapa kufanya nini iwapo Neno la Mungu kwa maana ya Biblia huliamini lote? Utathubutuje kusema hivi kama ulivyosema hapa chini, hebu ona, (nakunukuu):-

  “Orbi umegusia kitu fulani ambacho ni kigumu zaidi hasa kwenye jukwaa hili. Nacho ni mambo waliokiuka mitume. Nasema ni gumu sana kwenye jukwaa hili kwa sababu ni wachache mno wanaoweza kuamini kuwa kuna vitu mitume nao kama wanadamu walikosea.”

  Kwa comment yako hiyo ni kama kutuambia kuwa, Mafundisho ya Mitume baadhi hayafuati maelekezo ya Yesu hivyo ni makosa matupu kuyafuata! Huo naweza kuuita ni ujuzi uliopitiliza, huwezi kusema Mitume kunawakati HAWAKULIAMINI NENO LOTE! Kama ni hivyo, kumbe tunahangaikia nini? Tunyweni pombe tu basi! Katika 2Tim.1:11na ule mstari wa 13, Biblia inasema hivi, “11Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii….. 13Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. 14Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

  Unauona huo mstari wa 14? Timotheo ailinde ile amana aliyokabidhiwa na Roho mtakatifu akaaye ndani yao (MITUME)! Mtu ambaye Roho mtakatifu anaishi ndani yake, na tunajifunza kwamba Roho ndiye Mwalimu na hutufundisha kujua yote, sasa yawezekanaje Paulo afundishe kwa kumpotoa Roho Mtakatifu (yaani Yesu)? Roho Mtakatifu hadanganyiki wala huwezi kumsingizia, huwezi kujifanya maneno yako yawe ya Roho mtakatifu tazama Mdo. 5:1-10. Lakini si hivyo tu aliwajuvya mitume kuwa, zipo nyakati za ubishi usio na maana, ambapo watu watalikataa Neno la Mungu lililohalisi na kushikilia mafundisho ya kibinadamu, 2Tim 4:2-3, inasomeka hivi,

  “2Uhubiri Neno, uwe tayari wakati ufaao na wakati usiofaa, karipia, kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri.3Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima, badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia”

  Labda nikuulize hivi, wewe umemjulia wapi huyo Yesu, na maneno na maelekezo juu ya usahihi wa Injili yake? Amekuletea nani iwapo si kupitia Mitume? Biblia inaeleza wazi kuwa watu wameipata Injili ya Yesu kwa usahihi na kuiamini yote kupitia Mitume, Kwasababu katika 1Kor. 3:5 tunasoma hivi, “5Kwani, Apolo ni nani? Naye Paulo ni nani? Ni watumishi tu ambao kwa kupitia wao mliamini.”

  Mitume walichokifundisha si kwa akili yao bali waliongozwa na Mungu mwenyewe kwa jinsi ya Roho mtakatifu; 1Kor.2:10- inasema, “10Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa njia ya Roho Wake.
  Roho huchunguza kila kitu, hata mambo yandani sana ya Mungu. 11Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 12Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho yule atokaye kwa Mungu, ili tuwezekuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure. 13Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa wale watu wa kiroho. 14Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa jinsi ya rohoni. 15Mtu wa kiroho hutambua mambo yote, lakini yeye mwenyewe hatambuliwi na mtu ye yote. 16“Kwa maana ni nani aliyejua nia ya Bwana ili apate kumfundisha?” Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.”

  Ukikaa kimwilimwili ni lazima mambo ya Mungu yakupige chenga, maana huna lolote! Mtu anaweza kukataa kuwa hayupo kimwili, hakatazwi kujiaminisha kuwa yupo kiroho, ila “MTAWATAMBUA KWA MATENDO (MATUNDA) YAO!”Fikilia Mtu anapotetea na kusimamia kwa nguvu zote mafundisho ya dhehebu lake kuliko kuitetea Injili ya Kristo, akang’ang’ana na TAG, EAGT, AICT, ONENESS, CHURCH OF GOD, RC, ANGLIKANA, MOREVIAN, LUTHERAN, JEHOVA’S WITNESS, SEVENTHDAY ADVENTIST, KANISA LA MITUME, WAKRISTO WA SIKU ZA MWISHO, KANISA LA YESU KRISTO nk. Watu kama hao wapo mwilini kwakuwa hawajiulizi kwa nini hakuna umoja kama kweli mathehebu hayo yote ni ya Kikristo na yote yanaongozwa na Roho mtakatifu? Mathehebu si kitu kamwe cha kushikamana nacho mia kwa mia, kwasababu wamelikataa Neno, wakidai ‘MITUME WALIKOSEA HAPA’ Wakisema moyoni mwao, yote sawa lakini hili siyo! Hili la ubatizo au hili la wanawake kuhubiri halikumaanishwa hivyo ama hivi! Mitume hawakutii Neno lote kama alivyofundisha Kristo nk. Kila Dhehebu linajisifia na kusema Mungu yupo huku, sasa limeenda mbele zaidi katika ukengeufu hata udhehebu wao umehamia kwa viongozi wao ili kutimiliza Neno la Mungu.

  Kama upo Rohoni kikweli wala hutashangaa ukiwasikia wakijiita, sisi tu wa Mwingira, sisi wa TB Joshua, sisi wa Gamanywa, sisi wa Lwakatare, sisi wa Venandis, sisi wa Mzee wa upako, sisi wa Kakobe, sisi wa nanihii….nk. Sawasawa kabisana na zile nyakati za Paulo katika 1Kor.3:3-4 Paulo naye alikutana na Roho zilezile kama hizo, na akaziambia waziwazi kwamba, 3Kwa maana ninyi bado ni watu wa mwilini. Kwa kuwa bado kuna wivu na magombano miongoni mwenu, je, ninyi si watu wa mwilini, nanyi mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? 4Kwamaana mmoja anaposema, “Mimi ni wa Paulo,” mwingine, “Mimi ni wa Apolo”, je, ninyi si wanadamu wa kawaida?
  Kwa leo siendi zaidi ya hapa, ila nitaendelea kuiangalia kwa makini hii Comment yako niliyoianza kuijibu (19/09/2013 at 1:29).

  Elewa tu kwamba sikubaliani nawe mia kwa mia kama kweli ulimaanisha kama nilivyokuelewa! Maana najua kwamba, Kanisa ni Maminio wa Neno la Mungu, huyo ndiye Bibi harusi, iwapo mshenga akampotosha mchumba, hafai kuwa mshenga, ataharibiwa na anapaswa aadhibiwe vikali, sembuse Mtume ambaye ni Mshenga kwa Mchumba wa Kristo? Kamwe hawezekani mtu huyo kuendelea kuheshimiwa, kabisa haiwezekani, sababu Biblia inasema katika 1Kor.3:16-17 kuwa, 16Je, hamjui ya kwamba ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17Kama mtu ye yote akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamwangamiza mtu huyo, Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu,…..
  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 53. Seleli,
  Uelewe mara nyingine, hatuko hapa kwa ajili ya kumenyana au kulumbana kwa hoja ili nani aonekane mjuzi wa kutoa hoja!!Tunaelimishana tu, tena kwa upendo, nidhamu na pengine kukemeana kidogo lakini yote haya, yanafanyika kwa upendo kaka.
  Acha kufanya mazoezi ya kareti kwa ajili ya Siyi. Unajitaabisha bure. Ukitaka kusoma michango yyangu, isome kwa lengo la kujifunza. Ukiisoma kiitikadi na kwa pre-conceived ideads zako za udini, utaishia hewani tu!! Kaa utulie kaka!!
  Ubarikiwe

 54. Emmanule Charles,

  Maelezo safi mno na sahihi kwa swali lako, yameshatolewa ktk post aliyocopy na kupaste Kaka Siyi, hiyo ya Kiingereza yenye substances extremely very sweet, spiritual, Biblical and powerful for both IQ and spirit/heart, yakitofautisha ki-mantiki kati ya Agizo la Yesu na statement ya Petro, na ni rahisi kuelewa kabisa kwa yeyote mwenye akili kubwa, ndogo na ya kati au mwenye upako mwingi na mchache au mwenye experience kubwa ya kutumika na kutembea na Mungu na yule aliyeanza jana, au mwenye ujuzi mkubwa wa Neno na yule wa kati, na ni maoni yangu kua mada hii ilisha kwisha kirahisi kweli na kwa uzuri.

  Lakini kwa kua baadhi ya wachangiaji hupenda kuchelewesha mambo kwa mada/topic simple au kufanya issues zinazo-deserve wepesi, kua unnecessarily ngumu sana, nimeona nichangie kidogo tu kirahisi-rahisi tu ivi kama ifuatavyo:

  Katika akili ya kawaida tu, kama Rais amesema jambo na later akasema Mkuu wa Mkoa, unadhani nani haswa tunapaswa tumfuate? Na kama tunajua RC yule ni mtii mno kwa Rais na in fact hajawahi kua kinyume na matamshi ya Rais wake, je kama ametamka kitu kinachoonekana tofauti na cha Rais wakati ushahidi kua yeye hua ni mtiifu siku zote kwa Rais upo, unadhani maana yake nini? Yafutatayo yatakua sawa:

  (a) Kwa vyovyote vile RC akiulizwa ana maana gani kwa kauli yake, atafafanua na kuhitimisha kwa kuback up kauli ya Rais

  (b) Anaweza kua, kwa maana ya nje kama ilivyosikika/someka kwa Wasikilizaji( surface meaning), ile shape ya nje tu ikawa kama tofauti lakini intended meaning, ile hasa anayosimamia au ambayo hakuisema moja kwa moja kwa nje, well, labda akijua wanaosikia/watakaosoma wanajua na wata connect wenyewe concepts, ikawa ndio ile ile ya Boss wake.

  Hivyo ni wazi kabisa Petro asingekua na maana ya kiroho nyingine au namna nyingine ya kufanya mambo ya kiroho tofauti na Bwana wake na hivyo ni hekima sana na Biblically/Godly perfect and justified kujaribu kumu-adjust/analyse/shape/mould Peter’s statement ifit in ya Yesu na never Jesus’s fitting Peter! Or Paul mbaya na hatari sana! Na kwanza hata wao wakijua kuna mtu anawafanya wao kua final, watamtemea cheche hatari za moto.

  Pia mambo mengine ya Kiroho/Biblia, it is always safe kubaki na kuishi ktk basics/once and for all foundations ambazo mara nyingi ktk mijadala humu SG, mimi nimezipa jina la ‘’Neno/Jumbe/Kitu cha Ki-Mungu kwa vizazi vyote past,present and future’’ meaning, Mantiki ya Ki Mungu kuhusu kubatiza kwa Roho na kwa maji, ina-count more than kutetea doctrines za dini/madhehebu/movements/maono ya Viongozi wetu wa kiroho/kidini/waanzilishi wa beliefs husika ambazo nyingine ni imani mfu tu kwakua kiongozi huyo labda alikua ameokoka vema sana with sound doctrine kisha later akakengeuka na kuja na dini/doctrine mpya halafu baada ya karne kadhaa, wa Tz wakamezeshwa na kukumbwa nayo todate, .Poleni sana but there is hope for them/you-i.e. make a U turn now.! Or else keep and don’t spread it, however, any usambazaji utakutana na unyukwaji mzito ili kamwe usisimame/usiendelee tena.

  Tumaini Nelson,

  Asante kwa kutia moyo, kutoa aina fulani ya muongozo pia kutegemea mchango wangu, Glory to God, sikuchangia baada ya kusoma pachiko la Siyi, kazi njema ya kutokopia na kulibandika, nikadhani kweli mada imetendewa haki lakini sasa kwa kua yanajili mengi, basi na tumiminike sasa mwanzo mwisho,Amen.

  Boniface Evarist,

  Usiwe na wasi, relax, KAMA KWELI Siyi anadhani ana hoja za nguvu sana, upako mwingi, akili nyingi sana zilizobarikiwa, ana hoja zenye ujuzi mkubwa wa Neno la Mungu, ana uelewa mkubwa uliopakwa mafuta KUWEZA KUTHIBITISHA BILA KUACHA SHAKA KUA HAKUNA KUOKOKA SASA, na aseme sasa kwa sauti kubwa na kuanzisha debate iyo ktk mada tofauti pengine..Anakaribisha tena haraka sana kuanzisha mada iyo, nina hamu na moto kama nini kushiriki.

  Press on.

 55. Orbi umegusia kitu fulani ambacho ni kigumu zaidi hasa kwenye jukwaa hili. Nacho ni mambo waliokiuka mitume. Nasema ni gumu sana kwenye jukwaa hili kwa sababu ni wachache mno wanaoweza kuamini kuwa kuna vitu mitume nao kama wanadamu walikosea.

  Na jingine ni ukweli kwamba kama Yesu asingemleta Paul, kungekuwa na shida kubwa kwa kanisa. So, nakubaliana na wewe.
  – – – – – – – – –
  Lwembe umesema ubatizo wa Yesu ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi na kuvipokea vipawa vya RM na hatimaye Ubatizo wa RM!
  Hii mimi siikujbali. Zaidi sana inanifanya nikuulize swali jingine kuwa ubatizo wa Roho mt. maana yake ni nini?
  Sikubali kuwa ubatizo wa maji ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi, maana hutokea watu wakajazwa na Roho mt hata kabla ya kubatizwa kwa maji.

  Mimi mwenyewe nilijazwa Roho mt. wiki mbili tu baada ya kumpokea Yesu, ambayo ilikuwa ni siku nyingi tu kabla ya sijabatizwa katika maji.
  Lakini pia kuna watu wengi nimekuwa nikiwaona wanapokea ujazo wa Roho mt.wakiwa wanabatizwa hii hii ya kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt.

  Halafu wewe unayaelewaje maneno ya Mdo 1:5 ndugu Lwembe?

  Mimi nafikiri tunatakiwa kutafuta kujua kwa nini tunabatizwa kwa maji. Kama anavyosema Orbi tunatakiwa kutafuta kujua maana ya ubatizo wa maji kwa mtu aliyempokea Yesu, na unaashiria nini!

  Na sioni kama pia inamashiko kusema kuwa kama tulibatizwa kwa jina la Baba, na Mwana ,na Roho mtakatifu ina maana tofauti na kubatizwa kwa jina la Yesu.

  Tunaangalia matokeo gani yaliyo katika hizo ‘application’ mbili ili tujiridhishe kuwa ziko tofauti?

  Na kama Paul alijua kuwa ili mtu awe amesamehewa dhambi zake ni lazime afikie hatua ya kubatizwa kwa maji, kwa nini alikuwa hawabatizi watu baada ya kuwahubiria? Ina maana alikuwa anawaacha wakiwa na dhambi bado!!!!

  Tuzidi kujadili wapenzi!

 56. Mpendwa Sungura na Ndugu yangu Bonface,

  Niwaombe ladhi sanasana katika hilo, mimi nilikurupuka! Sikuelewa vema kuwa wewe na Boniface mnakubali kuwa Ikigundulika hatimaye kuwa ubatizo wa kwa jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu siyo, inabidi kubatizwa upya. Sawa sina neno katika hili, nisameheni bure ndugu zangu. Lakini kuhusu ile Mdo. 9:1-6 pia niliinukuu kimakosa, samahani sana kwa mkanganyiko huo.

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 57. Boniface & Sungura
  Mmesema mimi napotosha, sidhani kama ni kweli. Labda mkinieleza vilivyo marafiki. Mimi nikijuacho nitawaeleza, ili na ninyi muangalie wapi nimekosea/potosha then mnisaidie. Tuko hapa kwa ajili ya kujengana katika neno. Kumbuka tunapojengana, kuna wengine/wenzetu au mimi mwenyewe hapo awali nilikuwa nimeanishwa mapokeo, ninapopata ufafanuzi mpya na yakinifu wa kibiblia, inabidi nigutuke. Vinginevyo, nitaishia kupiga debe ya injili weee wasafiri wengine.. Fuatailieni uelewa wangu sasa…
  Maana ya kukoka!!
  Kwa maana halisi ya kikamusi, OKOA maana yake ni toa, epua, chopoa, ondoa kitu kwenye aghalabu mazingira ya hatari na weka kwenye mazingira salama. Mfano nyumba inapoungua moto, watu huokoa watu au bvitu vya ndani, Meli au feri inapozama, waokoaji hutumwa kwenda kutoa watu kwenye maeneo ya hatari/uangamivu na kuwaleta sehemu salama.
  Maana ya kumkiri/Kumwamini Yesu.
  Kifupi ni kumfanya Kristo kuwa kiongozi wa maisha yako badala ya shetani ambaye ni mtawala wa dunia hii. Kumkubali akuongoze katika kila hatua ya maisha yako. Mtu anapompokea Yesu, ya kale hufutwa na kisha huwa kiumbe kipya ndani ya Kristo. Safari mpya ya maisha ndani ya Kristo huanza-kuukulia wokovu. Safari hii huenda sambamba na mafundisho stahiki kuanzia ngazi ya awali hadi ya juu. Safari hii yaweza kuchukua muda mrefu au la, kutegemeana na bidii ya mtu kumtafuta Mungu.
  Wakati wa safari hii, muumini anaweza kujikwaa, akaanguka na hatimaye kuinuka tena. Kujikwaa huko kunaweza kuwa kwa muda tu, kwa kutokujua, au pengine kabisa kwa kukusudia tu eti atatubu baadaye. Ndiyo maana leo tuna waumini na hata viongozi wa dini wanaosafiri ktk safari ya imani, lakini, utawaona mienendo yao siyo ya utauwa! Kwa maana fupi, mtu huyo huwa bado hajaongoka-kufikia ukamilifu(dhambi haijakoma kuanzia mawazoni mwake ndiyo maana hujidhihirisha katika mwili wake). Kwa hiyo mtu huyo anaweza kuwa ni kiongozi au muumini wa kawaida, lakini nyendo zake zikawa zinatoa doa kwa kanisa la Mungu-mwili wa Kristo. Siku atakapoongoka-kufikia ukamilifu, ataacha dhambi (dhambi itakoma kuanzia kwenye kilindi cha akili na moyo wake). Hapo ndipo hufanyika mwana wa Mungu maana dhambi hukoma maishani mwa mtu huyo. Na kuna mifano michache ndani ya Biblia ya watu waliofikia hatua hii. Mf. Henoko, Eliya, Elisha, Daniel, Meshaki, mitume wa Yesu baada ya Yesu kuwa ameshapaa kwenda zake mbinguni na wengine wengi waliokuwa tayari kufa kwa ajili ya injili ya Kristo, mf Stefano nk.
  Tofauti yake ni nini sasa(kuokoka vs kumkiri Yesu)?
  Watu wengi badala ya kusema kwamba mimi ni mfuasi, muumini wa Kristo, husema nimeokoka. Mimi nafikiri huwa ni makosa ya matumizi ya maneno tu. Pale wanapopaswa kusema wamemwamini Yesu, wao husema wameokoka, jambo ambalo ni makosa. Maana hawawezi kusema wameokoka ilhali bado hawajatoka kwenye dunia hii ya mkuu wa giza-ibilisi. Mtu anapompokea Kristo hutangaza vita maradufu ya pale ambapo alikuwa hajaamini. Hivyo kusema umeokoka ilhali bado uko vitani, ni kushikilia mapokeo ya walimu wasiofahamu vyema neno la Mungu. Nasema hivyo kwa sababu moja kuu ifuatayo;
  Yesu alikuja kuokoa watu kutoka kwenye makucha ya Ibilisi, na ndiyo maana ya jina lake. Anawaokoa kutoka wapi kwenda wapi? Anawatoa duniani kuwapeleka mbinguni-sehemu salama isiyo na ibilisi tena. Mtu haokoki anapomwamini Yesu ila anabadilishwa tu, ya kale yanaisha na sasa yanaanza mapya akiwa bado yuko duniani-kwenye vita dhidi ya wema na uovu). Muumini huyo inabidi ajikabidhi kwa Kristo ili apate ushindi wa dhambi. Ndiyo maana hata mitume wa Yesu,, kabla Yesu hajafa, walikuwa hawajaokoka wala kuongoka!! Kwa nini? Wakati wa mateso ya Yesu, hakuna hata mmoja aliyeonekana katika eneo hilo. Imani yao ilikuwa wapi? Walikuwa hawajaokoka wala kuongoka/kufikia ukamilifu. Yesu alimwambia Petro mahali Fulani: “lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako” Luka 22:32. Kipindi chamvua ya RM kilipofika, mitume wote waliongoka, na walifanya matendo makuu ya Mungu.
  Watu wengi hufikiri mtu akiokoka(kwa maana ya kumwamini Yesu) hapohapo anakuwa mtoto wa Mungu- yaani mtu asiyetenda dhambi. Dhana hii siyo sahihi. Ukiangalia maisha ya mitume karibia wote, wakati wakiwa na Yesu, mara nyingine Yesu aliwaita baadhi yao Shetani, wenye imani haba nk!! Sasa swali la kujiuliza, mtu aliyeokoka aweza kuitwa shetani? Paulo katika utumishi wake, anapambana na vita dhidi ya wema na uovu, anasema, nilipendalo silitendi ila nilichukialo, ndilo nilitendalo… Rumi 7:15… Na mstari wa 20 anataja shida inayomsumbua kuwa ni uovu-dhambi iliyo ndani yake.
  Wapendwa mtu mwingine anaweza kufikiri kuwa Siyi anatetea dhambi. Hasha!! Ila naongea hali halisi ya maisha ya muumini tofauti na kile tukisiskiacho masikioni kutoka kwa walimu wetu hao. Maisha halisi ya mkristo huanza na Kumpokea Kristo →Msamaha wa dhambi→ Upendo wetu kwa Kristo → Utii wa Neno lake→ Uongofu/ukamilifu kamili. Katikati ya Msamaha na Uongofu ndipo kuna kuanguka na kuinuka kwa mkristo.
  Hivyo wapendwa, nijuavyo mimi, mtu anapompokea Yesu, anakuwa hajaokoka. Atakuja kuokolewa Yesu ataporudi kuwachukua wateule kuwapleka kwenye makao ya amani mbinguni. Ndiyo maana aya takribani nyingi za Biblia katika gano jipya, zinaporejea habari za Kuokoka, hurejelea njeo ya wakati ujao –TA-. Mf.
  Matendo ya Mitume 15:11 Bali twaamini kwamba tuTAokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

  Matendo ya Mitume 16:31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe uTAokoka pamoja na nyumba yako.

  Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, uTAokoka
  Marko 16:16 Aaminiye na kubatizwa aTAokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

  Yohana 10:9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, aTAokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

  Warumi 10:13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana aTAokoka.

  Warumi 11:26 Hivyo Israeli wote waTAokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

  NB: Katika habari za uzima wa milele, neno kuokoka liko future tense – kwa kiswahili alama yake ni –TA-. Katika sehemu nyingine za Biblia unaweza kukutana na neno kuokoka limetumika lakini si katika mukitadha wa mtu kupata uzima wa milele katika Kristo.
  Binafsi huwa nashngaa kuwaona watu wanatumia neno kuokoka kwa maana ya kumwamini Yesu, badala ya kutumia neno husika. Wokovu ni BAADAYE. Yesu atakaporudi na siyo sasa. Kwa sasa sisi tunaitwa wakristo, wafuasi wa Kristo, waumini wa Kristo, kondoo wa Kristo, tunaoendelea kukua katika YEYE. Tutakapokamilishwa kwa njia ya RM ndani yetu, Yesu atakuja kutuokoa… lini? BAADAYE!
  Huu ndiyo uelewa wangu ndg Boniface, Sungura na wengine wote. Kama ninyi nanyi mna uelewa tofauti, mwaweza kuuleta maadamu hatulumbani ila tunaeleweshana tu!! Bwana awabariki sana.

 58. Wapendwa,

  Hivi ubatizo unaashiria na kumaaninisha nini kwa Mkristo…? Au Maana ya ubatizo ni nini hasa….? Maana nimekutana na wapendwa wakimnukuu Paulo akisema…..”Maana Yesu hakunituma ili nibatize bali nihubiri habari njema” wala si kwa “hekima ya maneno” ili msalaba wa Kristo usije ukabatilika” Kwa wapendwa wanaomnukuu Paul, wanasema Ubatizo si kitu……bali kuipokea habari njema kama yule mwizi wa msalabani…! Na wasasema Paul anaonekana kupuuza agizo la Yesu…!

  Sipendi kuchangia kwa hili, maana ndugu Lwembe nadhani pia Mabinza anajua wapi ninasimama….tulishaipitia mada hii mara nyingi,maana imekuja kwa sura mbali mbali katika blog hii….! mimi licha ya heshima kubwa nayompa ndugu yangu Lwembe, kwa hili niliamua kutofautiana naye…! Wakristo tuna uhuru wa kutofautiana kwa vitu ambavyo havitukoseshe mbingu……! kwangu Baptism formula is one of them….!

  Nachotahadharisha tu ukiyaangalia Maandiko kwa mtazamo finyu na usipoyaweka Maandiko mahali pake……nini yanasema na kufundisha katika mpango kamili wa Wokovu….basi mtakesha hapa kwa hilo…..nawaambia wazi hamtapata ufumbuzi……..Kwa maana kama ukiyangaalia Maandiko kwa lensi finyu na nyembamba, si hilo tu la ubatizo walilokiuka mitume kwa kulifanya kinyume cha Yesu…..yako mengi mno……! Je utasemaje juu ya Paulo…? Kwani amefundisha mengi tena mengi mno ambayo Yesu hakusema wala kufundisha…? Na hata kutoa nukuu kwa kusema Yesu alisema…..na nukuu hizo hazimo katika Injili…..! Utasemaje kwa hilo…? Nampenda mno Paulo kwa sababu ufunuo wake wa Injili hakuupata kwa Mitume Yerusalem…..!Kama Paulo angecopy na kupaste kila walichofundisha na kufanya mitume Kanisa lisingefika lilipotakiwa lifike…! Ilichukua miaka kwa Mitume wa Yerusalem kufahamu na kuulewa Paulo anafundisha na kuhubiri nini hasa….! Ziangalieni Nyaraka za Paulo taratibu atawafungua kuhusu Baptism formula…!

  Nadhani mkikubaliana maana ya Ubatizo kwa mtu aliyempokea Yesu una maana gani……unaashiria nini…….hamtasumbuliwa na Baptism formula……! Lakini kama hamkulitanzua hilo mtakesha hapa…….!

  MBARIKIWE…..NAZIDI KUJIFUNZA TOKA KWENU…!

  Mbarikiwe

 59. Sungura & all,
  Ngoja nijaribu kuyajibu maswali uliyoyauliza, kukiwa na mapungufu basi utaniwia radhi, pia ndg wengine km akina Tumaini waweza kujazia!

  Ubatizo kwa mara ya kwanza tunauona kwa Yohana Zakaria, huyu ndiye mjumbe wa ubatizo, hata jina lake liliongezewa jambo hilo. Kwahiyo kimsingi unapozungumzia ubatizo, hauwezi ukaivuka tafsiri ya jambo hilo katika jinsi lilivyotimizwa, “Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.” (MT. 3:5, 6 SUV)

  Pia kati ya wanafunzi wa Yesu kuna waliokuwa wanafunzi wa Yohana, kwahiyo unapozungumzia ubatizo, wao wanaujua huo wa Yohana na ndio waliokuwa wakiendelea nao hata walipokuwa chini ya Yesu, kwa sababu halikuwa jambo la kujitungia bali ilikuwa ni Programu kamili ya Mungu ambayo Yesu alikuwa ni sehemu ya hiyo! Hivyo ni dhahiri kwamba ubatizo anaouagiza Yesu ni wa maji, huo wa Roho Mtakatifu yeye ndiye anayeutimiza, “Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” (MK. 1:7, 8 SUV) Katika hili nadhani sote tunafahamu kwamba huyo ajaye nyuma ya Yohana ni Yesu!

  Kulingana na maelezo hayo hapo juu, ubatizo anaouitia Petro katika Mdo 2:38 ni wa maji ambao huziondoa dhambi zako na kukuweka katika hali ya kuweza kupokea vipawa vya Roho Mtakatifu, km kunena, nk (si Roho Mtakatifu).

  Kubatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama unaulizia mtindo ni kwamba, wanakuzamisha majini mpaka unakuwa huonekani kabisa hapa juu, ile ishara ya kufa na kuzikwa, nayo maneno yanayoambatana na tendo hilo ndiyo hayo aliyoyasema Petro na yale uliyomsoma Paulo, “Kwa jina la Yesu Kristo” dhambi zako zote, pamoja na mashtaka yote ya Seleli tunasamehewa, Mungu anayatupa katika kilindi cha usahaulifu, unapoibuka juu, uko safi kama mtoto aliyezaliwa leo! Kwahiyo unapokuta Biblia haijaorodhesha kila lililofanyika ni kwasababu inajua kuwa ilikwisha kukufundisha juu ya ubatizo kikamilifu na inajua kuwa unajua hivyo, kama umeingiwa na mashaka, basi wapo wahubiri waliowekwa kwa kazi hiyo.

  Ubatizo wa Yesu ni kwa ajili ya Ondoleo la Dhambi zako na kuvipokea vipawa vya RM na hatimaye Ubatizo wa RM!

  Pia ukisoma kuwa fulani kabatizwa, basi jua kuwa hilo limefanywa kulingana na tafsiri ya jambo hilo kama tunavyoiona ktk Biblia.

  Kwa kifupi Ubatizo wanaoagizwa mitume kutufanyia wakiisha kutuhubiria Injili, huo unaohusiana na wokovu ni ubatizo wa maji, kwa jina la Bwana Yesu Kristo, na kama hutakuwa na fursa ya kubatizwa labda unakabiliwa na kifo kama yule mwivi msalabani basi kukiri kwako kwatosha kama alivyoagiza Paulo ktk ile Rum 10:9-10

  Gbu!

 60. Wapendwa mwanzo nilisema tuchangie mjadala huu kwa kufuata kweli ya neno na c kuegemea kwenye misimamo ya mapokeo ya kimathehebu bt kadri mjadala unavyopamba moto ukisoma post ya kila mpendwa unaona anaegemea kwenye mapokeo ya dhehebu lake!wengine tunaelekea kuhukumiana badala ya kuendelea kusimamia neno!mfano ukicheki hili la wokovu tu jinc tunavyochangia unagundua tofauti za tafsiri za neno kimapokeo ya kimadhehebu!kama kweli tunaniya ya dhati ya kutaka kuponyana basi tusimame na neno thn tuombe hekima ya RM itawale ili tupate msosi sahihi bt tukiendelea kuleta maujuzi yetu na mahekima yetu ya kibinadamu nadhani hatutofika pale ambapo GOD mwenyewe analenga kutufikisha.wapendwa kunakuwa kama kuna kakikiburi kakujua neno hapo ndipo shetani anapitisha injili yake coz hatunana unyenyekevu ktk kulijua neno!binafc nahitaji kula msosi wenyewe bt c fake!MUNGU AWABARIKI WOTE.

 61. Mabinza;

  Umemshambulia Boniface bila sababu ya kweli.
  Alichompinga Siyi kwacho ndicho hichohicho nami nimempinga Siyi. Nacho ni kuokoka. Siyi kasema hakuna aliyeokoka kwa sasa ispokuwa mpaka Yesu atakaporudi .

  Na wewe umemshambulia Boniface kuhusiana na suala la ubatizo ambalo hata yeye hajampinga Siyi kwalo.
  Ukiangali vema kuhusiana na suala la ubatizo Siyi alijibu swali langu kuwa ikibainika tumebatizwa ubatizo usio sahihi itabidi tubatizwe tena.

  Siyi hayuko sahihi kuhusiana na suala la wokovu. Wokovu ni sasa wala si wakati Yesu atakapokuja. Wakati atakapokuja itakuwa ni hukumu.

  Halafu sijajua kwa nini Mabinza na Siyi mmenukuu Mdo 9:1-6
  – – – – – – – – – – –

  Mara nyingi mimi husema ni hekima pia kuangalia uhalisia wa mambo ulivyo ndip ujiulize je, ninavyoelewa andiko fulani ndivyo ilivyo?

  Hili suala tumelianzia juu kana kwamba halina mizizi yake.
  Hebu tujiulize, Yesu aliposema mkawabatize…, alimaanisha ubatizo gani,wa maji au wa Roho mt.?

  Na Petro aliposema tubuni mkabatizwe kwa jina lake Yesu alimaanisha ubatizo upi, wa maji au wa Roho mt.?

  Tunajua Yesu hakubatiza, ila wanafunzi wake.
  Na Yohana anasema ajaye nyuma yangu (yaani Yesu) atawabatiza kwa Roho mt. Mt 3:11, Mdo 1: 5

  Na kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho mt. kulikuwa ni kwa mtindo gani hasa? Maana namwona Philipo anambatiza towashi kwa maji lakini hakusema chochote ( hakusema kwa jina la Yesu wala kwa jina la Baba na …..)

  Ubatizo wa Yohana ulikuwa kwa ajili toba, je wa Yesu ulikuwa kwa ajili ya nini ikiwa Petro anasema tubuni, kisha anasema mkabatizwe kwa jina lake Yesu?(Mdo 2:38)

  Lakini hata Paul kwa wale waliokuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana, biblia inasema akawabatiza kwa jina lake Yesu, kisha inasema na akisha kuweka mikono juu yao wakapokea Roho mt.Mdo 19:4-6
  Hapa napo Biblia haikusema kama walipelekwa tena kwenye maji, kwa maana ya kwamba ndio maana ya kubatizwa kwa jina la Yesu.

  To paraphrase: Ninachojaribu kujenga hoja kwacho hapa, ni je ubatizo alioagiza Yesu ni ubatizo wa maji au wa roho mt.?

  Asanteni.

 62. Boniface Evarist
  Nukuu ulizotoa ni kweli ndivyo zinavyosomeka na ndivyo zinavyomaanisha. Tatizo ni kwamba ili uyapate hayo uliyoyanukuu, na kwamba ili mwenyewe (Mungu) akubari kukukilimia yale yaliyotajwa na mistari uliyoitaja, ni lazima uwe ndani ya Neno lake! Haiwezekani mwenye lile Neno lake akukubalie wakati wewe hutaki kulitii Neno lake lote, kwa madai kuwa unakubaliana na hiki lakini kile hutaki ati tu umesimama katika tafsri za mwilini na za kidini. Mungu hujificha katika yale manyonge, ni kawaida ya Mungu kuwapiga chenga ‘wajuwaji’ siku alipokuja kama mwana alizaliwa zizini, tena na binti toka familia masikini isiyo na jina la kikuhani! Si hivyo tu mpaka chini kabisa alishuka hata kifo cha msalaba, na hata kaburi hakuwa nalo! Unaona?

  Wasomi kupitia maandiko walijua Masia atazaliwa nchini mwao, lakini hawakumuona, walijua atakuja Eliya kwanza kabla yake, lakini hadi Eliya naye anakuja hawakumuona, waliambiwa huyo Masia atakufa msalabani, lakini mpaka anaangikwa pale msalabani hawakumjua wakamwambia “Jiponye nasi tutakuamini (yaani ndio tutakutambua kuwa wewe ndiye!)” Roho ni ile ile hadi mwisho! Wataambiwa Yesu tayari alisharudi, watasema atakujaje, mbona yule ELIYA aliyetajwa katika Malaki 4:5, hatujamuona akija?!! Kisha Yesu mwenyewe atawajibu, ELIYA ALISHAKUJA!

  Siyi alichosema ndicho hicho, kwa maoni yangu Siyi yupo sawa, aliposema kuwa, “………endapo hatima ya mada hii itaonekana kuwa wengi wetu tuliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana na RM tuliingizwa mkenge, inabidi tubatizwe upya. Maana hata Paulo, aliwahoji wanafunzi wake, je, mlipokea kipawa cha RM? Wakasema hapana!! Akawauliza tena, mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakajibu, ubatizo wa Yohana!!. Paulo alichofanya ni kuwabatiza upya.Mdo 9:1-6. Kwa hiyo ndg yangu Sungura, ikibainika kuwa tulibatizwa isivyopaswa, sharti tubatizwe upya. Ukikataa au kuona aibu au kulipima jambo hilo kama haliwezekani kwa macho ya kibinadamu, kwa Mungu linawezekana na lina maana kubwa sana.”

  Boniface, siyo wewe wa kwanza kusema unapotoshwa, na Siyi si wa kwanza kuambiwa anapotosha, Mafarisayo walisema tunapotoshwa na kumwambia Yesu anapotosha, Mitume nao waliambiwa wanapotosha, Roho hiyo hiyo iliyokuwepo wakati wa Yesu na mitume wake, ndiyo hiyo hiyo ipo mpaka leo! Utake usitake ukweli ndio huo, kama ulibatizwa kwa ubatizo usiofundishwa na mitume, nafasi yako ni moja tu, ni KUBATIZWA TENA, na si kubatizwa tena tu, bali ukabatizwe kwa jina la YESU sawasawa na ile Mdo 2:38, ili uondokewe kabisa na dhambi na upate vipawa vya Roho mtakatifu, kinyume na hilo unakuwa unakataa Neno la Mungu. Unajua ndugu yangu Mungu hayumo katika mawazo na akili za Kibinadamu, usipotii hutamuona! Sikia, Wataambiwa Yesu tayari alisharudi, watasema mbona yule ELIYA aliyetajwa katika Malaki 5, hatujamuona akija?!! Kisha Yesu mwenyewe atawajibu, ELIYA ALISHAKUJA! La hutaki ndo basi tena!

  “Ufahamu ni chembe ya uzima!”

 63. Siyi,
  Nakupinga kwa hali na mali kuhusu kuokoka, mimi nimeokoka na nimekuwa kiumbe kipya na nina nguvu ya Mungu kwa sasa.

  Warumi 10:9-10
  ‘Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.’

  Luka 16:15-16
  ‘ Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.’

  I Wakorintho 5:17
  ‘Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.’

  Waefeso 1:7
  ‘Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.’

  Acha kupotosha jamii iwaze tofauti na uhalisia sawa @Siyi?

 64. Siyi,
  Nimekataa kwa 100% hoja yako ya kuokoka. Maandiko hayajasema kama ambavyo wewe umesema. Hujawahi kusoma kuwa kanisa lilikuwa linaongezeka kwa wale waliokuwa wakiokolewa?
  Maana ya neno wokovu siyo hiyo kabisa Siyi uliyoisema, hapana!

  Tuendelee na hoja ya ubatizo, ambayo maelezo yako si mabaya,tukiendelea naona bila shaka tunaenda kuzuri.
  Asante.

 65. Sungura & all,

  Tunaporudi katika mada, napenda kuirejea kauli hii ya ndg Sungura,
  “Na chanzo au msingi wa mada hii ni kile kinachoonekana kama tofauti ya alichosema Yesu na namna mitume (Petro) walivyokitekeleza. Kwa hiyo hii ni ”Contextual conflict” katika kukamilisha ubatizo wa maji.”

  Jambo hili linapowekwa nuruni, ndipo hali hii yenye muonekano wa mkinzano wa kimaudhui hujitokeza. Lakini hapo awali usingeweza kuliona, yaani utakisoma hicho kifungu cha Mt 28:19 kama kilivyo, na ukifika katika ile Mdo 2:38 utaisoma pia kama ilivyo and yet hutaistukia tofauti, yaani ni kama ukifika hapo akili yako inafungwa! Ndio maana unaona wengi wetu leo hii tunashituka linapowekwa nuruni!

  Hata hivyo, ukweli wa jambo hili ni kwamba hakuna mkinzano wowote wa maudhui katika vifungu hivi vya Maandiko, vyote vinazungumzia jambo moja. Tukiirejea ile tafsiri ya kifasihi uliyoileta kuhusu agizo la Kristo katika Mt 28:19 “…kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu”, hili kifasihi likiwa sawa na “kwa Mamlaka ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu”, na ndipo tukatamatisha kwamba “kwa Jina la” maana yake ni “kwa Mamlaka ya”. Basi kwa ujumla neno “Mamlaka” kimsingi huwakilisha “Nguvu”. Kwa mfano serikali, ili mamlaka iliyonayo itambulike, ni lazima Nguvu yake iwe wazi. Askari ndio nguvu ya serikali inayoipa kuwa na mamlaka, ni kwamba hakuna mamlaka bila nguvu!

  Kwahiyo tunafahamu sasa kwamba Kristo aliwakabidhi mitume Mamlaka ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Lakini huwezi kukabidhi kitu ambacho huna, basi tukirudi juu kifungu cha 18, hapo twaweza kuona tamko linalohusu jambo hili la Mamlaka, “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” Basi kwamba hili likiwa liko hivyo, maelezo yanayofuatia yanakuwa na nguvu, maana amewapa kitu alichonacho!

  Kwahiyo, tukiwa katika uelewa huu sasa kwamba Mamlaka yote amepewa Kristo, tunaweza kutamatisha kwamba, Kristo ndiye Mamlaka! Ndipo tunapolitazama suala la Injili, katika maudhui ya huko kutumwa kwao kuihubiri hiyo Injili, yaani mitume, basi twafahamu kwamba ni Habari Njema ya KUSAMEHEWA kwetu DHAMBI kwa Mamlaka hiyo ambayo ni Kristo! Nao mtiririko wa kulifikia jambo hilo ndio huo hapo, kwamba unahubiriwa Injili, hiyo inayokufunulia hali yako ya kiroho ikikudhihirishia Dhambi uliyonayo na Hukumu inayokupasa, na Neema unayokirimiwa ili kuikimbia Hukumu hiyo. Moyo wako ukiipokea hiyo Neema, nawe ukajiweka chini ya Mamlaka hiyo, yaani Kristo, Ubatizo hulikamilisha jambo hilo. Sasa ndipo unaweza kuketishwa chini na kufunzwa zaidi kuhusu mambo yote yanayohusiana na Ukristo, na ukawa na urahisi wa kuyaelewa na kuyaamini maana Dhambi zako, hizo ambazo ndizo kizuizi kikuu zimekwisha kuondolewa!

  Basi jambo hili lina tafsrika vizuri zaidi tunapokiangalia kifungu hicho cha Mt 28:19 “Mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” nalo Jina likiwa ni Mamlaka, nasi Mamlaka hiyo twaijua kuwa ni Kristo, ndipo tukiwa katika ufahamu kamili wa jambo hili, bila kusita tungesema, “Mkiwabatiza kwa Jina la Bwana Yesu Kristo” kama alivyosema Petro na mitume wote! Maana pia tunao ufahamu zaidi wa jambo hili kutoka dondoo nyinginezo zinazotuweka sawa zaidi kimaudhui katika kulibainisha jambo hilo la Mamlaka iliyomo katika jina hilo la Yesu (ambaye sasa ni Bwana na Kristo, Mdo 2:36; kama sisi tunaitana Dr, Pastor nk, sembuse yeye!), Lk 24:47 “…na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.”

  Unaona! Injili haipingani, ni Neno la Mungu, halina mikinzano! Msamaha wa Dhambi unapatikana ndani ya Jina la Bwana Yesu Kristo, hili ndilo analolitangaza mtume Petro katika Mdo 2:38 “…Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Unaweza pia kuliona jambo hili ktk 1Yn 2:12 “Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.” Unauona Msamaha wa Dhambi unavyohusiana na Jina la Yesu? Ni Bwana Yesu Kristo pekee ndiye awezaye kutusamehe Dhambi zetu kwa Mamlaka aliyonayo, angalia watu wa dini walivyolikosa jambo hili, Mk 2:7-10 “Basi, wale Waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?” Maskini, hawakuijua Mamlaka yake, bali yeye akiwasoma mawazo yao, akawaambia, “Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi”

  Basi mwisho niseme hivi, kwa yeyote yule kuwa mkristo, haimaanishi kwamba huyo ni mtu mwema sana au ametukuka katika uchaji Mungu au chochote kile alichokifanya, yaani matendo. Tukipimwa katika hayo unaweza kushangaa kwamba tuko huko chini sana ya msururu! Wako watu wanaozishika dini zao katika kuyatimiza matakwa yake, sisi hatufai. Watazame Waisilamu, siku za Ijumaa utaona misururu ya omba omba wakiwasubiri nje ya misikiti yao, ila makanisani huwakuti, maana sisi hatuna shughuli nao kabisa!!! Lakini sisi tu BORA machoni pa Mungu kuliko yeyote yule, kwanini, ni kwa sababu ya Msamaha wa Dhambi tulioupata kwa Jina lake Kristo, ni huu peke unaotustahilisha Uzima wa Milele ambao wengine wataukosa licha ya jitihada zao, maana Dhambi zao zinabaki zikirundikana, “ … yeyote asiye mwamini Kristo, atafia dhambini” Yoh 8:24!!! Ndio maana kuna umuhimu wa kuipitia Njia hiyo, hilo Lango la Ufalme alilolifungua mtume Petro ktk Mdo 2:38, kwa ule Ufunguo aliokabidhiwa na Kristo!

  Bwana awabariki!

 66. Sungura, uliloliongea ni jambo zuri. Bali ni vizuri pia tukiwa wakweli kwa nafsi zetu, kwamba tunazo dini, na mafundisho yake yamekuwa ni sehemu ya maisha yetu, kwahiyo hata hapa tunapoyajadili haya, huwa ni fursa yetu ya kuyatazama mengi ya mafundisho hayo iwapo yanaendana na Maandiko. Ndio maana nilipoiona ile hesabu yako ya: Majina Matatu = Jina Moja; halafu na ile ya msomi wa Siyi ihusuyo nafsi:
  1 x 1 x 1 = 1, nikashindwa kuwaeleweni, nikawa najiuliza, nafsi utazi multiply kwa namna gani, labda kuzijumlisha, 1+1+1=3 unaona, hiki ndicho kisa kiliyoyafanya mawazo yangu yakimbilie kwenye dini, na si ku criticize, pole sana ndg yangu!

  Tukirudi katika mada, nikiyarejea uliyoyaandika, kwanza niseme kwamba tafsiri uliyoileta ya kifasihi ni nzuri na inaleta nuru katika hili tunalolitafakari, tena ni msingi mzuri katika maana ya kielelezo cha kuufikia ukweli wa jambo hili kwa urahisi. Unasema, “””kwa jina la baba, na mwana, na Roho mtakatifu” kifasihi ni sawa na kusema kwa mamlaka ya Baba, na mamlaka ya Mwana, na mamlaka ya Roho mtakatifu.”” yaani kama nimekuelewa vizuri, ni kwamba “kwa Jina la” maana yake ni “kwa mamlaka ya”, kwahiyo, ili kuwa sahihi zaidi, kulingana na kifungu hicho cha Maandiko, tafsiri hiyo inapaswa kuwa, “kwa Mamlaka ya Baba na ya Mwana na ya Roho Mtakatifu”. Hili ni jema na ninaamini tukili rejea hili laweza kutusogeza mbele

  Ninafikiri majibu aliyoyatoa Siyi yanajibu sehemu kubwa ya mashaka uliyokuwa nayo juu ya jinsi ya kukabiliana na changamoto hii ya Ubatizo. Binafsi naona hitimisho lake kwa jambo hili, kwa ushahidi wa Maandiko, limekaa vizuri sana!

  Basi naona , kabla sijaendelea na mada ya msingi labda nijaribu kuliangalia hili suala jingine ulilolileta kuhusu “wokovu” katika mjumuiko wa suala la Ubatizo.

  Kuhusu suala la “Wokovu”, kimsingi hiyo Mark 16:16 inayosema, aaminiye na kubatizwa ataokoka, na hii Rum 10: 9 inayozungumzia kumkiri Yesu, mimi sioni kama kuna tofauti ya kimaudhui. Sababu kubwa inayonileta katika uelewa huu ni kwamba, “kukiri” jambo si kukariri, au kufuatisha kama tulivyozoea katika ‘sala ya toba.’ Kukiri kunahusiana na jambo lililokutokea. Katika maudhui ya jambo hili, ni kwamba utakuwa umehubiriwa Injili kwanza, lile neno la Kristo likakujengea imani, ukamwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wako, basi ukiisha kukifikia kiwango hiki ndipo Ubatizo hufuata, kuidhihirisha imani hiyo uliyonayo. Kuna wengine wengi sana katika siku zile za mateso ya kanisa, ambao waliuawa pengine hawakuipata fursa ya kubatizwa, lakini kwa kumkiri kwao Kristo, walichukuliwa na kutupwa katika kundi la simba na wengine kuchomwa moto nk. Lakini wako wengine pia ambao waliupitia Ubatizo, bali walipobanwa na askari iwapo nao ni wakristo, walikana ili kuyaokoa maisha yao, na wengine hata siku hizi akiulizwa, wewe ni “mlokole”? kwa aibu wanajikanyaga! Kwahiyo unaweza kuupima umuhimu wa ukiri kimaudhui, katika jambo zima la wokovu, hilo ndilo linaloweza kukuongoza kwenda kubatizwa au kifoni kwa faida kamili ya kiungu, au kukutupa nje ya Ufalme wa Mungu kwa hasara yako!

  Pia ni vizuri tukajiweka katika ufahamu uliosahihi kuhusu jambo hili la Wokovu au KUOKOKA. Kuna mtazamo wa wakristo wengi wasio katika Upentekoste, kwamba kupiga kelele za “kuokoka” wakati ungali katika vita ni utoto au ufinyu wa uelewa! Unaweza kumuona Siyi akilizungumzia hilo, kiuwakilishi, “Sasa utasemaje umeokoka ilhali bado uko vitani?” Hii ni kweli tupu, ukiwa vitani chochote chaweza kukutokea, ndipo unaporudi kambini, hapo ndipo ungehesabiwa katika kundi la waliookoka!

  Lakini wokovu unaozungumziwa katika Biblia si huo, maana kama ni huo, basi mamilioni waliouawa kwa kumkiri Kristo, tutasemaje juu yao, kwamba waliokoka na upanga au simba? Haileti maana! Wokovu unaozungumziwa katika Biblia unahusiana na Hukumu, yaani usipofikia kumkiri Kristo, tafsiri yake ni kwamba hujaiamini Injili uliyohubiriwa, haijaugusa moyo wako, ndipo kwa jambo hilo, Injili hiyo usiyoiamini, kuhusu wewe inasema, “Asiyeamini, atahukumiwa”! unaliona jambo hilo? Tazama hapa lilivyo wazi zaidi, Yn 3:18 “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.” Huku ndiko Kuokoka Biblia inakokufundisha, haijalishi uko katika vita vya namna gani, ni Imani yako kwa Kristo, huyo uliyemkiri, ndiyo ikupayo wokovu, kule Kuhesabiwa Haki kwa Imani! Ambayo tamati yake ni kule kujazwa Roho Mtakatifu, kule Kupakwa Mafuta! Mtazame Sauli, alikuwa ni Mpakwa Mafuta. Ingawa alimkosea Mungu lakini hakupotea, Biblia inasema jioni ile aliyopigwa mshale alikwenda kuwa pamoja na nabii Samweli! Pia mfalme Daudi, alichukua mke wa mtu na akajitangazia mwenyewe hukumu ya kifo, lakini Mungu hakuitimiza juu yake! Naye Mkristo maana yake ni Mpakwa Mafuta!!!!

  Basi, kwamba siku hizi, “ukiangalia ‘applicability’ yake kwa wakati wetu huu, alichokisema Paul ndo kinafanyika zaidi kuliko alivyokisema Yesu” katika maana ya kwamba watu “Humkiri Kristo” yaani wanai recite hiyo Rum 9:10 na kupata “wokovu” na kuishia hapo, yaani kumkiri huko hakuwaongozi katika Ubatizo, hilo laonesha hawajawahi kumkiri Kristo, waliimba “shairi” tu, maana iwapo Kristo ni Bwana kweli katika maisha yao basi angewaongoza kuitimiza Haki yote!

  Basi ndg zangu, nadhani katika suala hili la wokovu, kama alivyolileta Sungura, nimejaribu kulijibu kwa kadiri ya uelewa wangu wa Maandiko, kwa vile nyote mnazo Biblia zenu, basi yakagueni hayo humo ili kuwa imara zaidi katika imani.

  Bwana awabariki sana!

 67. Sungura,
  Hoja nzuri na fikra pevu kwelikweli(kwa mtazamo wangu). Mimi nafikiri aliyeleta mada hii alikuwa na lengo jema. Hata wachangiaji nao wana malengo mema kadhalika.
  Kwanza, Kwa mawazo yangu mimi, endapo hatima ya mada hii itaonekana kuwa wengi wetu tuliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana na RM tuliingizwa mkenge, inabidi tubatizwe upya. Maana hata Paulo, aliwahoji wanafunzi wake, je, mlipokea kipawa cha RM? Wakasema hapana!! Akawauliza tena, mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakajibu, ubatizo wa Yohana!!. Paulo alichofanya ni kuwabatiza upya.Mdo 9:1-6. Kwa hiyo ndg yangu Sungura, ikibainika kuwa tulibatizwa isivyopaswa, sharti tubatizwe upya. Ukikataa au kuona aibu au kulipima jambo hilo kama haliwezekani kwa macho ya kibinadamu, kwa Mungu linawezekana na lina maana kubwa sana.

  Pili, kuhusu kupatikana kwa wokovu, wengi wetu huwa tunayakosea sana mafungu hayo ya Biblia kuyatafsiri. Wokovu haupatikani kwa mtu kumkiri Yesu na Kubatizwa, isipokuwa utapatikana kwa mtu kufanya hivyo. Tutaokolewa/Tutaokoka siku Yesu atakapokuja na siyo sasa kipindi ambacho hajaja bado. Kwa sasa, tunamwamini Yesu, tunabatizwa, na kisha kuendelea kukua ktk NEEMA(Yesu Kristo). Kwa maneno mengine, tunapomwamini/kumkiri Yesu, tunatangaza vita kati yetu na mamlaka za giza. Sasa utasemaje umeokoka ilhali bado uko vitani?
  Dhana sahihi ya kuokoka kwa mujibu wa biblia, tutaokoka siku Yesu atakapokuja. Hii ndiyo maana halisi ya jina la Yesu, mwokozi wa watu, kutoka kwenye ulimwengu-dunia ya dhambi kuwapeleka mahali pasipo na dhambi-mbinguni. Kwa hiyo sasa hivi hatuokoki, ila tunamwamini/tunamkiri Kristo tu. Mtu akisema ameokoka, tutamsikitikia tu maana haelewi maana ya kuokoka na kumwamni/kumkiri Yesu. Kaka Sungura, tutaokoka BAADAYE, Yesu akija.
  Barikiwa sana.

 68. Lwembe nafikiri awamu hii tubadilishe style ya criticism ili ikiwezekana tufikie muafaka wa kukubaliana ikiwezekana.

  Sioni ishu ya udini unaoniambia hapo imetoka wapi. Anyway, ngoja nikubali kupoteza hii vita isiyo ya lazima ili tufike tunakotaka kufika.
  Asante Lwembe.
  — – – – – – – – – – – – – – – –
  Ukweli ni kwamba tafsiri ya hicho kifungu ”kwa jina la baba, na mwana ,na Roho mtakatifu” kifasihi ni sawa na kusema kwa mamlaka ya Baba, na mamlaka ya Mwana, na mamlaka ya Roho mtakatifu.

  Lakini kitu cha msingi pia lazima tujiulize, kwamba tunatafuta ku-achieve nini katika huu mjadala, halafu tukishakipata hicho kitu then iweje?

  Bila shaka wengi wetu tunaochangia hapa tumebatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho mtakatifu. Vipi tukishafikia muafaka kwamba ni makosa kubatizwa hivyo, je tutaenda kubatizwa upya?
  Au je kwa kubatizwa kwetu hivyo hatujabatizwa kwa ubatizo kamili?

  Na chanzo au msingi wa mada hii ni kile kinachoonekana kama tofauti ya alichosema Yesu na namna mitume (Pero) walivyokitekeleza. Kwa hiyo hii ni ”Contextual conflict” katika kukamilisha ubatizo wa maji.

  Ni vema tukaangalia mikinzano ya kimaudhui katika maeneo mengine pia ili tujue kama na yenyewe yana matatizo au la, ili yamkini tuweze kupata kitu chepesi cha kujifunza kuhusiana na huu mkinzano wa kimaudhui kuhusu ubatizo.

  Mfano katika suala la Wokovu kuna mkinzano pia.

  Yesu katika Mark 16:16a anasema aaminiye na kubatizwa ataokoka. Kwa hiyo wokovu hupatikana kwa mtu kuamini kisha kubatizwa.
  Lakini Paul katika Rum 10: 9 anasema ukimkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa ni Bwana na kuamini moyoni kuwa Mungu alimfufua toka kwa wafu utaokoka.
  Kwa hiyo Paul yeye anasema wokovu unapatikana kwa kukiri bila ubatizo.

  Je tusemeje hapa, kwamba Paul hapa alifundisha kinyume na Yesu? ”mkinzano wa kimaudhui”.
  Na ukiangali ‘applicability’ yake kwa wakati wetu huu,alichokisema Paul ndo kinafanyika zaidi kuliko alivyokisema Yesu.

  Ni muhimu kufikiri vema na kwa upana juu ya tunachokijadili hapa!

 69. Nelson,
  Ubarikiwe na Mungu ndg yangu. Ni kweli kama umegundua kwa sasa, mijadala ya hapa SG, hailalii wala kuegemea kwenye dhehebu la mtu. Kila mmoja anajitahidi kuiangalia Biblia kuona kama inaendana na hicho anachokiamini (mafundisho ya dhehebu lake). Na ukiona kuna utofauti, kuna haja ya kuhoji vizuri na kufuata Biblia. Mbinguni hatuendi kwa madhehebu yetu. Tutaokolewa kwa kuifuata Biblia tu na si vinginevyo. Hatua na taratibu za kumfikia Mungu, ibada kwa Mungu, nk zimo ndani ya Biblia. Karibu tujifunze pamoja.
  Bwana akubariki sana.

 70. Mimi binafc nabarikiwa saana na michango ya kila mmoja coz inanifanya nijifunze zaidi,bt all in all hapa kweli ndiyo inayohitajika na c swala la kiushabiki au ya kidhehebu!Mimi binafc cjui wenzangu ila mimi nitabarikiwa saana kama tutaelimishana kwa kweli tupu pasipo kuweka mambo binafc ili woote tupone.Tuwekane sawa kwa Upoole zaidi ingawa najuwa wengine ni wainjilist bt naamin tutakwenda sawa!Shule hii iko vizuri tunahitaji tuipate vizuri!Siyi,Lwembe,Mabinza,Sungura nawasoma vizuri na natarajia mazuri mengi kutoka kwenu!My Brothr Selel pia natarajia mazuri kutoka kwako! na wana S.G wote.Mungu awabariki wote.

 71. Sungura,
  Hahahaha…!
  Unasema: “Maana kumbe hayo majina matatu = na Jina moja!” X!!!

  Unakaribia sana kuipata Nuru ya jambo hili, only fungua macho yako zaidi, ondoa hiyo veil ya dini kwanza, halafu sasa soma tena hicho kifungu, hiyo equation yako itakaa sawa kulingana na hilo Andiko, maana Roho Mtakatifu hawezi akaja na hizo hesabu zako zisizoeleweka, sijui ni shule gani uliyosoma! Hesabu kamili hii hapa:
  Jina moja = Jina moja!!!
  Maana umeambiwa “kwa Jina” na si “kwa Majina”!!!

  Asante, brother!

 72. Siyi,
  Binafsi nimekuelewa vizuri sana ndg yangu!
  Unajua, katika jitihada yetu yooote ya ibada nk, shauku yetu kubwa ni kumjua Mungu ili tuwe na uhakika wa hayo yote tunayojitahidi na kuyafuata katika furaha ya kupokelewa katika mikono ya huyo aliyetuumba. Kwahiyo kuna umuhimu wa kipekee wa kulijua kwa UHAKIKA jambo hili kumhusu huyu Mungu, ili jitihada yetu isije ikawa ni “karata tatu”, kilio chake huwa hakinaga mbembelezaji, maana pesa ya mboga za nyumbani imeliwa yoote na wachezeshaji wameondoka, utambembeleza vipi huyo mpaka atulie, sana sana kama kuna kamba karibu, iondoe asije akajinyonga!

  Endelea “kudesuka” ndg yangu, jambo hili ni la kufa au kupona; akiwa ndiye Mungu, huyo Trinity, basi Uzima wa Milele unao!

  Akiwa siye, … duh, sipati picha!!!

 73. Lwembe,
  Ha ha ha !!! Shida yako iko kwenye neno TRINITY. Hapa ndiyo kuna shida kaka. Kama nilivyokuahidi, ngoja nidesuke kufa na kupona ili nijue kama kuna kitu kingine tofauti na TRINITY as persons of Godhead!!
  But kwa vile nina nuru hiyo ya TRINITY kwa sasa, acha nisimamie hapo kwanza. Nikipata kitu cha tofauti, nitabadilika tu.

 74. Siyi,
  Nimeipitia hii post yako, inatoa mwanga mzuri kuhusu inachokielezea, ingawa inaonesha iliwahusu haswa Wapentekoste wa kundi la Oneness, kuonesha udhaifu wao katika hicho wanachokiamini kuhusu Ubatizo kwamba wapaswa kufanywa kwa “Jina la Yesu pekee”. Ni kweli, Ubatizo wa kwa “Jina la Yesu pekee” si wa ki Biblia, ni wazo la mtu tu aliyelisimika na kuwaaminisha hivyo, lakini halina uhusiano wowote ule na Maandiko.

  Maelezo mengine katika passage hiyo ni yale yale ya kawaida yanayowapa tabu wasomi wengi katika kuoanisha kifungu cha Mt 28:19 na jambo la Utatu Mtakatifu. Unaweza kuona katika hayo maelezo uliyoyaleta, hapo huyo msomi wako anapojaribu kulielezea jambo hilo akikupa mfano wa “maji” ili kulithibitisha jambo hilo, lakini punde mbele anasema “Ni mfano mzuri, bali si kielelezo kamili cha Utatu Mtatakatifu” lakini tena anaendelea nao mfano huo sasa akiyapindisha mawazo ya wasomaji kumfuata huko anakotamatisha jambo hilo kinyume na uhalisi wa mfano huo ambao ungekuleta katika uelewa sahihi kwamba Mungu si Nafsi Tatu bali moja iliyojidhihirisha katika jinsi tatu kiutendaji.

  Hii hapa illustration iliyo sahihi na kamili kimfano, unaweza kumpelekea huyo msomi wako ili imsaidie zaidi anapoutumia mfano huo, badala ya kusita, “This is a good, albeit, not perfect illustration of the Trinity” sasa anaweza kusema, This is a good, and a perfect illustration of the Trinity”!

  H2O is the substance or chemical composition of water. And water can be in either Liquid or Vapor or Solid forms, but when in any of these forms, the chemical composition, H2O, does not change, what changes is the form ONLY! That is to say, the three different forms, Liquid, Vapor & Solid, are a manifestation of the same substance H2O and are not sharing the same substance! For in order to share, they would have to be distinctive in their substances to be able to derive a full meaning of “sharing”, contextually, otherwise you cannot share to yourself your own substance!

  So if we are to take this “substance” or this chemical composition H2O, to be God, who by the Bible definition is a Spirit, John 4:24 “God is a Spirit”. And if we are to take this to reflect the Trinity correctly, we’d say: The Father, The Son and The Holy Spirit, these being the three different forms, are the manifestation of the same God who is that Spirit, to meet the Demands of the Day or better said, The Three Dispensations, likened to liquid water to quench our thirst; water in vapor or steam form for the saunas and in solid form, the ice, for preservation of perishable foods etc.

  Therefore, the unchanging substance, that Personality, being God who is a Spirit, then The Trinity of God would only mean what it is, i.e. that same Spirit (God) manifesting Itself in those three different forms, The Father for the Fatherhood, The Son for the Son ship and The Holy Spirit for Church Leadership!

  Gbu & all!

 75. Mabinza, Sungura, Lwembe na the rest SGs
  Kimsingi tunapobatiza kwa jina la Yesu, maana yake tunabatiza kwa kuyatambua mamlaka ya Mungu Baba, Mwana pamoja na NGUVU yao – Roho Mtakatifu. Unapomzungumzia Mwana, unamzungumzia Baba, unapomzungumzia Baba, unamzungumzia Roho Mtakatifu(nguvu yake) ambayo ndiyo nguvu ya Kristo pia. Ndiyo maana Yesu akatoa fomula ya kubatiza kwa kuyatambua mamlaka ya utendaji kazi wa Mungu, yaani Kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hivyo Sungura, namwona yuko sahihi anapojenga hoja yake kwa msingi huo.
  Bwana awabariki, sana

 76. Kwamba kuhusu Ubatizo kwa huyo aliyehubiriwa Injili, Kristo anawaagiza mitume wake ktk Mt 28:19 kuwa,
  “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu”

  Lakini katika utekelezaji wa agizo hilo tunawaona mitume wakibatiza kama inavyoonekana katika kitabu chote cha Matendo, kuanzia siku ya Pentekoste, wakiisha kumpokea Roho Mtakatifu, mtume Petro anasimama na kutangaza, Mdo 2:38
  “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

  Kwa kadiri ya Maandiko yanavyojifunua, tunapaswa kuelewa kuwa jambo hili tunaloliona ktk kitabu cha Mdo, NDIYO Tafsiri halisi ya kiMaandiko ya kifungu hicho cha Mt 28:19, hilo ndilo Jina la Baba na la Mwana na la RM, iwapo tutayaacha Maandiko yajitafsiri yenyewe!

  Kwahiyo, kimsingi hiyo ndiyo jinsi sahihi ya kuutimiza Ubatizo kulingana na Maandiko, kwa Agizo na kwa Kutimizwa kwake. Pia hii ndio jinsi inayoendana na lile Agizo tulilopewa, hilo linalotuelekeza kwamba, “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” (KOL. 3:17)

  Basi, Ubatizo nao ukiwa ni tendo, wapaswa uwe hivyo kama walivyoutimiza mitume ili ile faida ya kiungu, lile Ondoleo la dhambi na Vipawa halisi vya RM, iwatimilie hao walioitwa wamjie Mungu wetu!

  Gbu!

 77. Niliwahi kuuliza kwamba:

  Ikiwa Jina la Baba, Mwana, na Roho mt. = Jina la Yesu.

  Tofauti ni nini basi kati ya anayebatiza Kwa jina la Baba, na Mwana na Roho mt na yule anayebatiza kwa jina la Yesu?

  Maana kumbe hayo majina matatu = na Jina moja!

  Thank u guys!

 78. Emmanuel Charles,
  Mtu anapokuwa haelewi au hujafika katika kuelewa jambo hilo, ni mjinga wa jambo husika, kwanini hataki kujifunza ili aelewe? Yapo mambo mawili na yote yanasababu moja, kwanza mtu huyo si “mbegu” ya Mungu na pili ni kiburi, kwa nini sasa? Ili apotee!
  Haiwezekani watu ambao waliishi chini ya mafundisho, uangalizi, na kwa maelekezo yaYesu mwenyewe , wafanye kimyume. Mwanafunzi hufanya anavyoelekezwa na mwalimu wake, ukiona mwanafunzi akifanya kinyume na maelekezo ya mwalimu wake huyo tayari kesha ‘Feli’ tayari, na aliyekuwa mwanafunzi ‘Feliya’ hawezi kuja kuwa mfundishaji, kwakuwa na wote watakofundishwa naye nao watakuwa ‘Feliya’ – wachungaji wake feliya na washirika wao nao feliya, sasa fikilia Kanisa la ma ‘Feliya’ litakavyoonekana!

  MAANA YA UBATIZO

  Yapo mambo kama matatu hivi yaliyojichanganya na kuwa kama Neno moja lenye maana moja kwa kuitazama ile mada iliyombele yetu, mambo hayo ni:-

  1. Maana ya kubatizwa:
  Ubatizo hufanywa ili kuthibitisha kuamini kwa mwamini, Mk 16:16 inasema, “16Ye yote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa.” Tunapaswa kuamini katika jina la Yesu, Mk. 16:17. Ubatizo ulianzia kwa wanaIsraeli wakati wa Musa 1Kor 10:1-2 inasema, “Zaidi ya hayo ndugu zangu, sitaki mkose kufahamu ukweli huu kwamba baba zetu walikuwa wote chini ya wingu na kwamba wote walipita katikati ya bahari. 2Wote wakabatizwa kuwa wa Musa ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari.”

  2. Jinsi ya kubatizwa
  Ubatizo ni wa maji mengi, mwenyekubatizwa lazima azamishwe, iwe ishara ya Kuzikwa na kufuka kwa Kristo, Kol. 2;12 inasema, “12mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa kuuamini uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu” mkazikwa pamoja naye katika ubatizo 1Kor. 10:2 inasema, “. 2Wote wakabatizwa kuwa wa Musa ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari.”

  3. Kubatizwa kwa jina gani
  Katika Mt.29;19, Yesu aliwaagiza wanafunzi wake kama ifuatavyo, “19Kwa sababu hii, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,”

  Kutokana na Yesu kusema hivyo, wasio watoto wake walitoka kapa! kwani walishindwa kumjua huyo Baba ni nani na huyo Mwana ni nani na pia huyo Roho mtakatifu ni nani, wanadhani kuwa Baba, Mwana na Roho mtakatifu ni watu watatu tofauti eti katika kimoja! Hapo ndipo mwovu alipopitishia mtego wake na kufanikiwa kuwanasa wengi. Neno la Mungu linasema, “atakayeamini ndiye atakaye Batizwa, na mwenye kubatizwa ataokolewa na mwenye kuamini huyo tu ndiye ataambatana na Ishara. (Mk. 16:16-17, na Mt. 29:19-20)” Imani ya wenyeishara wa kweli ni wale watakaokuwa wameamini katika Yesu Kristo, Mk. 16:17.

  Ukiitazama ile Mdo 2:38, inasema, “38Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu. nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Mtu anapokuwa katika kutokuufikia uelewa lakini nia ya moyo wake ni katika kutaka kumjua Kristo, utwajua hujifunza kwa unyenyekevu hadi anapofika katika kuelewa.

  Hainishangazi kuona kuwa Maelekezo ya Yesu juu ya kubatiza aliyowapa Mitume wake, yanawapiga chenga watu wa Dini wanapo soma ile Mt 29:19 na Mk. 16:16-17 wakilinganisha na ile Mdo. 2:38 na kuona ipo tofauti! Nikawaida ya Mungu kujificha kwa watu wanaotaka kujua kupitia akili na Elimu zao za Dini. Fikiria alivyojificha wakati ulipotimia ule wakati wa kuja kwake Duniani ili kuja kuwaokoa watu na dhambi zao. Isaya amesema jinsi mfalme huyo atakavyokuwa na sifa kuu, lakini watu wa Dini wakazitazama sifa zile kimwili, kielimuelimu na kiujuzijuzi wa kidini, yeye akaja na kujificha kwa Binti mdogo fukara na asiye toka katika ukoo wa makuhani, akazaliwa zizini katika mashonde ya wanyama na kulelewa na Yusufu fukara mchonga mbao! Unaona? Chenga hiyohiyo ipo hadi leo, kwa waendao pupa na u- boss boss wao!

  Mk. 15:16-18 inasema, “15Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16Ye yote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa. 17“Nazo ishara hizi zitafuatana na wale waaminio: Kwa Jina Langu watatoa pepo wachafu, watasema kwa lugha mpya, 18watashika nyoka kwa mikono yao na hata wakinywa kitu cho chote cha kuua, hakitawadhuru kamwe, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”

  Mdo 2:38 inasema, “38Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu. nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu na kwa wale wote walio mbali na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.” Je, katika mistari hiyo tofauti ni nini? Mtu mmoja atasema, mbona Yesu hakusema mkabatize kwa jina langu mimi Yesu? Anayejiuliza hivyo atanisamehe nikimwambia kuwa, yeye ni sawa na mtu anayesifia chakula kwa kuinusa halufu, bila kukionja!

  Kwanza ni wapi na wakati gani Yesu aliposema niiteni mimi kwa jina langu Yesu? Watu walimwita Yesu kwa sababu jina hilo alikuja nalo Malaika, na akasema mtoto huyo ambaye Isaya aliwatajia kuwa ni Emmanueli ataitwa Yesu, ataitwa na nani? Ataitwa na sisi watu tunaomwamini, Jina hilo ni kwaajiri yetu, tumepewa ili liwe siraha yetu dhidi ya mwovu, jina hilo si kwaajili ya yesu, ni letu! Ni mara zote Yesu alijiita ‘Mwana wa Adamu’ tu basi! Lakini hatufukuzi mapepo wala kuponya wagonjwa ama kutoa unabii kwa jina liitwalo Emanueli ama Mwana wa Adamu, hata mapepo wanajua hivyo, ukitaja tu Yesu utaiona shughuli yake’ ukitamka kwa nguvu Neno Yesu katika Kadamnasi, kila mmoja atageuka akutazame, na si kukutazama tu, ila anajiuliza kulikoni tena tunasikia YESU?!!!

  Hebu tuangalie, Mitume walibatiza na kufanya yote kwa maagizo ya Yesu? Ukisoma. mt.16:20 inasema “20nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.’’ Amen.” Sasa ukisema mitume walijifanyia tu mambo bila kuagizwa wakati Yesu mwenyewe ambaye ndiye yule mwenye kuwaelekeza cha kufanya yupo nao hapohapo unategemea nini?!!

  Biblia inasema Mungu alifanyika Mwili, Yesu ndiye Mungu tunaposoma Yh.1:1-5 inasema, “Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
  3Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 5Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda.”
  :, ikiwa waaminio utatu wanasema Mungu ana nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho mtakatifu na huyo ndiye Mungu, Kumbe inawawia ugumu gani kujua kuwa Yesu ndiye huyo baba na ndiye mwana na pia ndiye huyohuyo Roho mtakatifu? Wamefichwa, ili waamini uongo wapotee!

  Hata hivyo tunapata ushahidi wa moja kwa moja toka kwa Yule aliyeshuka kuja kulithibitisha hilo, hebu tazama tena Yh. 1:6-9 inasema “6Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia yeye watu wote waweze kuamini. 8Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. 9Nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni. Tatizo watu wanasikiliza toka kwa watu wasio mjua! Soma tena hiyo hiyo Yh. 1:10- “10Alikuwepo ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kwa Yeye, haukumtambua. 11Alikuja kwa walio Wake, lakini wao hawakumpokea.

  Wale wanaoliamini jina hilo la yesu ndiyo wana wa Mungu, wanajua anachosema na hata kujua mafumbo na semi ya Mungu, ndiyo maana wanaelewa alichokisema Petro katika ile Mdo 2:38, na wanaamini kuwa hadi sasa Yesu kwa namna ya Roho mtakatifu anaendelea kufundisha watoto wake! Yh 1:12 inasema, “12Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake.” UBATIZO NI KWA JINA LA YESU Mdo. 2:38!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 79. Shalom wapendwa, Kwa wanaoelewa kizungu kidogo, wanaweza pitia hii kidogo huenda itasaidia. Nimepachua na kupachika kutoka somewhere… Karibuni
  The phrase “in the name of Jesus” has been twisted by the Oneness sect to narrow the formula of baptism to certain words. It is true Peter said, “Repent and be baptized, every one of you, in the name of Jesus Christ for the forgiveness of your sins” (Acts 2:38). This sect claims that Peter gave the formula. But no person had the power to authorize the formula except the Son of God. The phrase “in the name of Jesus” meant “by the authority of Jesus” you should be baptized. In other words, Peter was declaring that Jesus commanded baptism; this is what is meant by the phrase “in Jesus name.”

  For example a police officer may command a thief who flees the scene of the crime, “Stop in the name of the Law!” He is not saying this is the formula to use in stopping criminals, but rather, the officer is authorize to stop thieves because the Law gave him authority. Peter was saying the same thing: be baptized because Jesus authorized us to baptize you. Peter was not giving the formula for baptism but his claim of authority.

  Who within the Godhead gave instruction to baptize? Jesus is the one who told us to baptize. The Father under the Old Covenant did not command it; it is a command given by Jesus in the Great Commission. So the question then is “how” did He tell us to baptize? Clearly in Matthew 28:19 Jesus says, “Therefore go and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father and of the Son and of the Holy Spirit.” This is the formula or manner of baptism. The formula or manner of baptism must come only from the One who authorized and commanded baptism—and that is Jesus. No one after Him can change the formula, and the book of Acts does not change the formula, but only clarifies Who authorized baptism.

  Some argue that the names Father and Son are “titles” and thus are not “names”. Those who argue the point miss the words of Jesus. He said to baptize in the “name” of the Father, Son and Spirit. He did not say in the “title” of the Father, Son and Spirit. The reason is simple; there is no distinction in ancient customs between a name and a title. They are one and the same. Consider this: most names come from titles. For example, the name “Johnson” means “son of John.” It is now shortened, however it is both a “name” and a “title”. Many names were originally titles: like Carpenter, Plumber, King, etc.

  What tells us more about a person, his “title” or his “given name”? I am Pastor Tom Brown. What says more about me, Tom or Brown or Pastor? I think you can see that the title Pastor says more about who I am and what I do than my given name. The same is with the Father. It describes more who God is than any other name.

  Bear in mind the baptismal formula—Father, Son and Spirit—this describes who God really is more than any other description. Jesus wanted to make sure that the foundation of our faith is the acknowledgment of the blessed Trinity—one God revealed in three persons. To deny this is to deny the foundation of our faith, and this is why Christians have rightfully declared heretical any teachings that deny the Trinity.

  The problem with the “Jesus Only” group is they insist unless you are baptized in the formula of “Jesus name” only, you will not be saved. That is pure rubbish. They are divisive and in error because they have denied the Trinity.

  They may argue that the term “Trinity” is not in the Bible, but so are other terms we take for granted like “rapture”, “sermon”, “incarnation”, “original sin” etc. But the doctrine of the Trinity is taught in the Bible. The baptismal formula in itself proves the doctrine of the Trinity. Everyone would agree that the Father is God, so if the name of the Son and the Spirit are also used in connection with the Father, they must both be equal to God because it would make no sense to include the names of lesser beings with God the Father.

  The Jesus only sect argues that the belief in the Trinity means people believe in three gods. This is simply not true. There is one God revealed in three persons. The three are eternally, existent and coequal. Someone may say, “But three persons equals three gods.” Not true. In math 1x1x1=1. You can have three numbers and still equal one. The “Jesus only” sect uses the wrong math formula to define the Trinity.

  Let me illustrate the Trinity this way: H20 is the substance of water, steam and ice. H20 makes up the prosperities of these three. Now water is not steam, and steam is not ice. These three are separate forms but they are all the same as far as substance. This is a good, albeit, not perfect illustration of the Trinity. The Father, Son and Holy Spirit share the same substance. The substance is God. Yet the Father is not the Son, nor is the Son the Holy Spirit. They are separate persons yet share the same substance. You cannot say water is steam, but you can say that both water and steam are H20. So you cannot say the Father is the Son or the Son is the Spirit, but you can say that the Father is God and the Son is God and the Holy Spirit is God. The Trinity coexist in the same way that water, steam and ice coexist. God is the substance of the Trinity.

  It is interesting to note that Jesus in His baptismal formula used the singular word “name” not plural “names” of the Father, Son and Spirit. The reason is obvious, there is only one God! The Jesus only group however says there is only one name to God and His name is Jesus! So they teach that Jesus is the Father and He is the Holy Ghost.

  This cannot be true, because when Jesus was baptized by John, the Father spoke from heaven and said, “This is my son in whom I am well pleased,” and the Holy Spirit descended on Him in the form of a dove. I often ask the “Jesus only” sect, Who spoke from heaven? They often try to evade the question, because they believe Jesus is the Father, so this would make Jesus testifying about Himself. Like a ventriloquist Jesus would be throwing His voice making it sound like He has a Father who testifies about Him. And then, like a magician, Jesus would turn into a dove and make it look like He descended on Himself. Can you see how ridiculous this view becomes? Jesus is not the Father, but the Son. The scriptures are quite clear on this. Precisely as the Trinity was involved in Jesus’ baptism, the Trinity should be involved in our baptism.

 80. Nichorous Shegwando!!
  Naomba unioneshe mtu mmoja tu aliye batizwa kwa Jina la baba na la mwana na Roho mtakatifu katika biblia?

 81. Nichorous Shegwando!!
  Naomba unioneshe mtu mmoja tu aliye batizwa kwa Jina la baba na la mwana na Roho mtakatifu?

 82. Ubatizo waliobatiza mitume ndio ubatizo unao tumika hata leo kwenye makanisa mengi ya kipente koste,unaweza ukaona nitofauti kwa sababu amesema mkawabatize kwa jina lake Yesu haina maana kwamba watu wa batizwe kwa jina la Yesu ila ina maanisha watu wabatizwe kwa maelekezo au maagizo ya Yesu,na maagizo ya yesu ni haya hapa>Mathayo 28 :19 mkawabatize kwa jina la baba na la mwana na la Roho mtakatifu,

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s