Nisaidieni kujua adhabu ya kutotoa kikumi…..

kikumi

Adhabu ya kutotoa/kuchelewa kulipa fungu la kumi ni zipi na kifungu kipi cha maandiko?

–Nico

Advertisements

73 thoughts on “Nisaidieni kujua adhabu ya kutotoa kikumi…..

 1. nimebarikiwa sana na michango ya wachangiaji karibu wote waliochangia ktk maada hii kwan wamechambua kwa mapana na marefu kwa kutumia neno la Mungu na imeonekana hakuna adhabu yoyote kwa asiyetoa kikumi. Lwembe,sungura na milinga hongereni sana kwa michango yenu. kwani imenibariki sana.

 2. Lwembe,

  No enjoying reading, no jazba, no kuzungusha mambo hapa, no what!!!!!!!! wacha nifanye kazi ya kuondoa mzaha wako umu na wewe kama Siyi na pia kuvunja mambo yako ya kuzungusha Watu kwa mambo clear but unataka kubandika ma-extremes and ma-imbalanced madude yako full of ”marasmasi” spiritually always!

  Nakuuliza,

  Kwa iyo Zaka in its strict sense ni fungu la Mia moja au ten?

  Na kama kuna 10%, kwa nini isiwepo % 1, 2,5, 50,60 ktk mahesabu ya ukadiliaji/upimaji wa vitu?

  Kwakua kuendelea kuwakomalia watu leo watoe strictly 10% tunarudi kwenye sheria na kwa kua tumekubaliana kulingania na kweli ya Maandiko si tu kukubaliana kijiwe cha kahawa deals kua Utoaji wowote Agano Jipya, hauna sheria, alimradi mtu ameamua na kupenda kwa uhuru kutoa basi ruksa kutoa % yoyote iwe 1, 10 au 100 au hata kutoa bila kipimo chochote eg sadaka kama alivyokomaaga Sungura na nikamuelewa, sasa wewe huelewi nini hapo kama si mzaha na upuuzi unaleta humu? eti mie nimeokoka, nina miaka ya kutosha ktk Bwana na Imani, unasema ati sikuwahi kuhubiriwa injili mie! ishiii! what! mie! upuuzi kweli huu uliovuka mipaka!

  Press on

 3. Seleli,

  Unajua unapozungumzia “CONTEXT”, usipende kuunganisha na vitu vingi vinavyopita kichwani mwako bila kuvichuja kwanza ili uvioanishe na jambo la Msingi!

  Mada inazungumzia “KIKUMI”, lakini angalia unachokiongelea wewe, hivyo mlivyokubaliana na Sungura,
  “…nika salute kua ni kweli kua atoaye kama ni % 10, 3, 6, 50 nk yote sawa as long as ni toka moyoni kwa furaha…”
  Sasa kupatana kwenu katika jambo la Uongo kunahusu nini Neno la Mungu? Ni nani aliyewaambieni kuwa %3 au 6 au 50 ni sawa na %10? Shule mlitoroka? Milinga alisema ulikuwa na akili sana huko shule kabla haujakimbilia shule za town, huku ndio wamekuambia kuwa “kikumi ni %50? Umejiona ulivyotoka nje ya mada na kung’ang’ania huko huko, nje ila unajiona unaongelea kikumi!!! Umemuona anaye “challenge kijinga”?

  Halafu naona ulijaa stimu, maelezo niliyomuandikia Sungura wewe umeyavaa na kujibebesha yasiyokuhusu, punguza jazba, soma pole pole, enjoy your reading!!!

  Sungura na Ziragora ndio waliokomaa kuwa KIINGILIO cha semina ni sawa na CHANGIZO alizokusanya Paulo, ila kama nawe unaona hili ni sawa, basi maelezo hayo nawe yanakuhusu, na kama mlikubaliana kuwa kila atoaye Zaka kuitimiza Mt 23:23, kuwa “atoaye kama ni % 10, 3, 6, 50 nk yote sawa…” basi mna umbali mrefu wa kujifunza kuyaelewa mambo katika Context yake badala ya kuongozwa na Hisia za dini; nitamuomba Amin aendelee na somo huenda huko mbele mkafunguka uelewa, Mungu atamlipa kumpoza machungu ya wanafunzi wabishi!

  Ila umenifurahisha sana kwa ule mfano wa yule mwanamke aliyemkosha Kristo kwa machozi, yule ktk Luke 7!!! Umeniambia,
  “”Wewe tokea lini toka nikufahamu umu ndani, uliwahi jua maana ya context ya andiko na ukaeleza vema inputs zako zaidi ya extremes/imbalanced and confusing doctrine kiiiiila mara ukigusa topic!”
  Hahahahaha!!! Sasa ngoje nije na li “extreme/imbalanced and confusing” dude jingine kuhusu huyo mwanamke, utafurahi saaaana, maana ni extreme kweli, kila siku nakuambiaga wewe hujawahi kuhubiriwa Injili, unaimbaga mapambio tu, Injili yenyewe hujawahi kuisikia!!!

  Gbu, my brother!

 4. Lwembe,

  Acha mzaha mbovu!

  Sungura alimjibu Mabinza kwa kusisitiza sana mambo ambayo tulisha-debate sana, tukakubaliana na yapo hatukukubalina, ya msingi kuliko yote on zaka debate ya mimi na huyu kiumbe wa Mungu Sungura tuliyokamata pamoja ni kua mambo yote na yafanyike kwa moyo wa kupenda na hakuna adhabu kwa asiye toa ila si vema kua na moyo wa kutotoa. Na pia akanichallenge na nika salute kua ni kweli kua atoaye kama ni % 10,3,6, 50 nk yote sawa as long as ni toka moyoni kwa furaha,so nilipoona Sungura amekomaa tena hapa,nikataka kujua, ana shida gani tena au kuna mtu amekataa tena hoja zake njema zilizopita za kutoa kwa moyo si sheria? Yeye amejibu, hakuna tabu ila wewe unaleta mzaha na upuuzi! Ati unani-challenge kijinga kua mi sijui context ya Neno! mimi kabisaaa? Nisikilize sasa nikwambie……

  Wewe tokea lini toka nikufahamu umu ndani, uliwahi jua maana ya context ya andiko na ukaeleza vema inputs zako zaidi ya extremes/imbalanced and confusing doctrine kiiiiila mara ukigusa topic!

  Nime-site mfano wa Yesu wa-Luka.7:36-50 wa Mtu anayesamehewa sana, atapenda sana na anayesamehewa kidogo, atapenda kidogo nikafanya application yake hata kwa swala la kumpenda Mungu sana kunapelekwa kujitoa sana kwakwe ivyo hata Utoaji wa Mtu anayependa sana, ni wa kufa Mtu kama si kupona Mtu-ndipo nikatumia flavour zangu za kuzimia au kuzimikia uko-kumaanisha kujiachia kwa BWANA bila chenji mpaka mwisho, why? umependa sana Mungu.

  Kila Andiko unaweza fanya good Bible Study methods namely Observations, Interpretations and Applicatios. Toka context ya andiko, unafanya applications freely as long as huvurugi context, sasa Kujitoa kwa Mwanamke yule ktk Luka.7 namely kumuosha Miguu Yesu na machozi yake, kumpangusa na nywele zake, kuibusa miguu na kuipaka na perfume ghali vile—yote hayo Yesu anakuja yasema yalitokana na kua MWANAMKE ALIPENDA SANA. From there nika-connect na swala la Kutoa kua UKIPENDA SANA-utafanya sana/utatoa sana/utazimia/zimikia uko ktk kutoa maana unapenda si mchezo. Hata hayo aliyoyafanya Mwanamke, ni aina ya Utoaji/Kujitoa pia-Yesu anasema, toka ameingia ile nyumba, Mwanamke amekua anaibusu miguu non-stop!

  Sasa kuniuliza kua Yesu alitoa zaka, mara nilichosema ni pasua skull, mara ngoja Sungura anizengue mie, mara nimesema kiingilio kwa semina sijui nini yaani ni upuuzi sana unamwagika humu na pia usimsingizie Sungura kwa kua hajanivuruga kwa hili na wala hawezi nivuruga mie kamwe labda tuvurugane! Iyo ya kiingilio kwa seminar niliisema vema sana kua ni njema kwa maana tu ya kusadia gharama as simple as that na kwamba hulazimishwi na pia kweli gharama zipo na pia ukienda ktk seminar iyo uliyolipia na ukakuta malipo yako yameendana na huduma za kimwili ukumbuni umo-msosi, Ac, Masomo ya seminar kupewa nk, kuna shida gani kuchangia seminar? Acha uzushi na utoto wa kuview mambo.

  Nadhani we ndio hujui misingi ya USOMAJI NENO NA NDIO MAANA KWA MENGI YA INPUT ZAKO, MIMI SIJAWAHI KUKUELEWA, waga nakuchukuliga tu kama confused brother in Christ who needs a big heart to engage with but hua napata shida sana na madude na manyangalagata yako to be honest, ni mara chache sana umefanya vema, umeongea vya kueleweka but 80% ya Stuff zako ni mambo ya unaenda Kinondoni but unaanzia Shanghai China iyo mzee kisha unakunja pale Dubai then unakula boda pale Entebe alafu una ramba bus via Kahama kisha unalala Ubungo bus then asub bodaboda to Mkwajuni Kinondoni!!!!!!!!!!!!! Inaboa sana stuff zako! Una hitaji brothers wanaokuchukulia kama mie na nadhani Sungura kusoma mambo yako.

  Press on.

 5. Seleli,

  Tatizo linalomsumbua Sungura ni jinsi milivyo miss the whole thing; typical of a people running away from the Truth!!! Mmelikonfuzi jambo zima kwa maelezo out of context, halafu mmekomaa nayo mpaka its a pity!

  ZAKA ni FUNGU LA KUMI!!!!!!!!!

  Angalia pasua kichwa hii:
  “”…bali kama ni zaka au la, yote ni kwa moyo wa kupenda na ktk moyo wa kupenda, tutatoa vingi mno ktk scale nyingi na kwa kweli unakumbuka mfano wa Yesu, yeye apendaye sana, amesamehewa mengi ivyo anaweza hata kuzimia kama si kuzimikia uko kwa kutoa sana kabisa””

  Haya Sungura, hao hapo wanakwambia eti “tutatoa vingi mno ktk scale nyingi na kwa kweli unakumbuka mfano wa Yesu”; hivi Yesu aliwahi kutoa ZAKA?

  Lakini, bora wakuzingue tu, wewe mwenyewe umewahi kung’ang’ana kuwa KIINGILIO kwenye Semina ni SAWA na CHANGIZO alizokusanya mtume Paulo; basi endelea nao mtaelewana tu, Zaka ni sawa na “Changizo la Jengo”: hahahahahaha!!!!!

 6. Seleli,

  I got no problem.

  Unaona tatizo lolote katika jibu langu kwa Mibinza?

  Mwenye matatizo alikuwa Mabinza, naye bila shaka mpaka hapo kesha elewa.

  Yesu oyeee!

 7. Sungura,

  Bado ”dude’ hili la zaka linakusumbua? shida yako nini? ni kweli hakuna adhabu kabisa na ni kweli hatupaswi kutoa kama sheria bali kama ni zaka au la, yote ni kwa moyo wa kupenda na ktk moyo wa kupenda, tutatoa vingi mno ktk scale nyingi na kwa kweli unakumbuka mfano wa Yesu, yeye apendaye sana, amesamehewa mengi ivyo anaweza hata kuzimia kama si kuzimikia uko kwa kutoa sana kabisa

  What is your problem todate ngosha and Nkoi oneee?

  Press on

 8. Mabinza,

  Ule ulikuwa ukuhani wa kilawi, na huu wa kwetu ni ukuhani wa kifalme, je unaiona tofauti iliyopo hapo?

  Hebu niambie wewe kwa ukuhani wako wa kifalme, unatumikia madhabahu ipi ambayo inakupa ulazima wa kula zaka?

  Ivi wewe unadhani kuwa zaka ktika agano la kale ilianza tu kutolewa bila sababu, au ni Mungu ndiye alikuwa anakula hiyo zaka?

  Na ni wakati gani Yesu kama kuhani mkuu wa madhabahu ya kimbingu, isiyofanywa kwa mikono ya kibinadamu,aliwahi kuhitaji zaka, au aliwahi kupewa zaka?

  Kwa nini mnakuwa wahanga wakubwa wa kutoelewa ‘transformation’ iliyopo kati ya agano jipya na la kale? what’s wrong with u guys?

  Na unaposema kuwa kutoa zaka ni kumrudishia Mungu vya kwake kwa kutumia mfano wa Yesu kuwa ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu, huoni kuwa unaingia chaka zaidi? Maana hizo zaka za pesa mnazotoa si za Mungu, bali ni za Nyerere, Kenyatta, Washington, n.k. au za serikali husika zenye kumiliki hizo pesa.

  Maana Yesu aliwauliza kuwa hiyo shekeli ina picha ya nani? ndipo wakasema ‘ya Kaisari.

  Lakini pia unanishangaza, kwamba tukitoa machangizo hapo unamtumikia Mungu kwa mali aliyotujalia, lakini tunapotoa zaka tunamrudishia Mungu kilicho chake.
  Je, hicho unachomtumikia nacho Mungu na hicho unachomrudishia Mungu kilicho chake, huoni kwamba vyote ni vyake? Unachomrudishia Mungu ni chake na unachomtumikia nacho Mungu ni chake pia, infact ukiwemo na wewe, ni wake pia.

  Mabinza, kama torati haitaondoka hata nukta moja, mbona kutahiriwa kumeondoka, yenyewe haikuwa torati au?

  Na Yesu hakukomea kusema kuwa torati haitaondoka hata nukta moja, bali aliendelea kusema mpaka yote yatimie.

  Kama hujui kkuwa yote yalitimia, muulize Yesu alimaanisha nini aliposema ‘imekwisha’ akiwa pale msalabani.

  Ati hapa unasema ” SHAURI HAPA SI NENO ZAKA, SHAURI NI KUTOA KWA MUNGU, KWA KUMRUDISHIA MALI ZAKE; HAKUNA NAMNA NYIGINE YA KUMRUDISHIA MUNGU MALI ZAKE ISIPOKUWA NI KWA NJIA YA ZAKA PEKEE! ”

  Ivi wewe ni mwanafunza mwenye hekima kweli au ni mwanafunzi mpumbavu?

  Ivi Mungu akitaka umrudishie kilicho chake wewe utabaki na nini? Hebu fikiri sawasawa. Na ni wapi ambapo Mungu aliwahi kusema kuwa tunapaswa tumrudishie vilivyo vyake, hebu nioneshe!

  Kwanza Yesu mwenyewe hakuwahi kutoa zaka, hata akina Petro hawakuwahi kutoa zaka. Nashangaa leo Mabinza huyu ambaye ni mzabibu wa kupandikizwa ndo anashadadia zaka!

  Au wewe uliwahi kumwona Yesu anatoa zaka, au Petro ,au Yohana?

  Ona na hapa unavyosema ”Kama Zaka isingekuwa kitu endelevu, Biblia isingemnukuu yesu alipokuwa akieleza juu ya toba ya kweli kwa mfano wa Yule Farisayo na mtoza ushuru katika ile, Lk. 18:12 kuwa, “12 Mimi…;…. hutoa zaka katika mapato yangu yote”

  Wewe ni kipofu wa ufahamu kweli, pamoja na msemao wako kuwa ufahamu ni chembe ya uhai.

  Hii nayo ni point ya kujaribu hata kusimamia kuonesha kuwa zaka inatakiwa kuendelea kutolewa,au hata hujui unachosema, ila unasema tu kwa vile umeona neno zaka kweli hivyo vifungu, basi hata hukutaka kuelewa maudhui yake yalikuwa nini?

  Halafu unamalizia hivi; ”Kama namwelewa Yesu sawa sawa hapa, ni kwamba, zaka ilipasa itolewe, KATIKA ADILI, NA REHEMA, NA IMANI, MAANA MAMBO HAYO NDIYO MAKUU KATIKA SHERIA! Kwa hiyo Zaka ni Sheria na Sheria ni Torati, na Yesu hakuja kuitangua Torati na tena Torati haitaondoka hata nukta moja”

  Kwa taarifa yako, jibu ni kwamba hukumwelewa Yesu sawasawa hapo. Hakuna kitu kinaitwa kutoa zaka kwa adili na rehema. Kamuulize tena mwalimu wako kuwa hapo Yesu alimaanisha nini!

  Mabinza unachotakiwa kufanya ni kutoa kwa moyo wa kupenda. Kama wewe unaona zaka ndo njia safi ya kumtolea kwako Mungu, fanya hivyo kwa moyo wa kupenda.

  Lakini kaa ukijua kuwa, hakuna adhabu yoyote kwa mtu kutokutoa zaka!

  Habari ndo hiyo!

 9. Sungura,

  Kwa maoni na mtazamo wako upo sawa, mimi binafsi hujanifundisha bado kwasababu nyingi tu, ila baadhi ni kama ifuatavyo:-

  Kwaza kabisa, Zaka kama zaka ni sehemu ya 10, au 10% ya mapato ya mwamini, utoaji wa zaka mwanzo na namna ulivyokuwa ukifanywa nilishaeleza kwa kirefu sana hapo juu. Lakini Zaka waliokuwa wakihusika nayo kwa mjibu wa Torati walikuwa Makuhani, ambao kwa kawaida walikuwa ni wa jamii ya Lawi, ambao wao hawakuwa na urithi katika Israeli. Makuhani walipoipokea hiyo zaka, nao walitoa fungu lao kwa Mungu. Kwa sasa sisi ndiyo makuhani wenyewe. Ndiyo maana tunajua kuwa moja ya kazi ya Kuhani ni kuratibu na kuifanya shughuli nzima ya mambo ya Zaka, na lazima ujue kuwa, huwezi kuitwa Kuhani bila kuwepo na Kazi za Kikuhuni! Biblia inasema “SISI NI MAKUHANI WA KIFALME” kwa hiyo lazima tufanye ukuhani wote, kama alivyoelekeza yesu katika Mt. 23:23.

  Zaka kwa mjibu wa Torati ilikuwa ikitolewa kwa Mungu, kwa sababu vya Mungu vilimpasa Mungu, Tazama, Mt.22:21 “21 Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya
  Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu” Kwa maana hiyo, Mungu anavitu vimpasavyo kurudishiwa japo vyote ni mali yake (Hag2:8). Hatuwezi kusema kuwa tunapotoa sadaka ama changizo mbalimbali mfano za ujenzi wa Kanisa, kupereka njili ama kuhudumia wajane tunamrudishia Mungu mali zake, bali pale tunamtumikia Mungu kwa kwa mali alizotujalia! Lakini tunapotoa Zaka, maana yake tunamrudishia Mungu Vyake. Na kutofanya hivyo ni wizi! Tazama Mal.3:8 inasema “8…!….?….. Lakini ninyi mnaniibia mimi……,….? Mmeniibia zaka…….” Umesema nahukumu (si mimi ni Neno), Biblia inasema Mtu asipotoa zaka ni Mwizi kwa hiyo amelaaniwa. Tazama tena Mal. 3:9 inasema kuwa, “9Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi,…,….”

  Kwa sababu Biblia ni Neno la Mungu, napaswa kuliamini lote, lakini pia najua kuwa Neno hili la Mungu ni toshelevu kwa nyakati zote, uliopo, ujao nauliopita; kwa maana hiyo lipo Neno la wakati, nadhani hapo ndipo uliposimama Sungura, kuwa Zaka ilikuwa ni maelekezo ya Mungu kwa watu kwa mjibu wa Torati, na kwa vile, sasa ni wakati wa Neema haiwapasi watu kutoa Zaka tena. Mimi nakubaliana nawewe katika upande mmoja tu kuwa, Zaka iliyokuwa ikitolewa kwa mjibu wa Torati ya Musa, haitupasi tena kuitekeleza kivile! Lakini zaka ya sasa ni ya kutoa chini ya sheria ya Neema ambayo ni upendo(Mt.23:23). Sioni popote panaposema waaminio wasitoe zaka (ila si zaka ya Torati kuwa ni lazima iwe-10%) ninachoweza kukiona ni kuwa yapo maelekezo ya kutoacha kutoa Zaka, ukiitazama ile, Kumb.14:22 inasema,
  “22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi ……..” Lakini jambo hili Bwana wetu Yesu Kristo aliligusia akiwaambia mafarisayo katika ile Mt. 23:2-3 kwamba, “2Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; 3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda;…….” Kwa hiyo lazima uelwe kwamba Torati haitaondoka wala Nukta moja, na Bwana Yesu alilithibitisha hilo, na hata pia akasema, “Mimi sikuja kuitangua Torati ila kuitimiliza” Cha msingi hapa ni kujua tu namna itupasayo kumrudishia Mungu vitu na mali zake, si kujiridhisha tu kwamba sasa tunaishi kwa Neema hivyo hakuna haja ya kumrudishia Mungu mali na vitu vyake, huku tukifarijika kwamba mitume hawakuitaja Zaka! SHAURI HAPA SI NENO ZAKA, SHAURI NI KUTOA KWA MUNGU, KWA KUMRUDISHIA MALI ZAKE; HAKUNA NAMNA NYIGINE YA KUMRUDISHIA MUNGU MALI ZAKE ISIPOKUWA NI KWA NJIA YA ZAKA PEKEE! Tunapotoa Sadaka ama matoleo mengine, ispokuwa Zaka ama Dhabihu, basi hapo tunamshukuru ama tuna mtumikia tu Mungu kwa mali zetu. Ndiyo maana usipotoa Sadaka huitwi mwizi, wala usipochanga kujenga kanisa huitwi mwizi pia, lakini usipotoa Zaka ama Dhabihu pale Maandiko yanasema mtu wa namna hiyo ni mwizi anamwibia Mungu. Mtu hawezi kuiba kitu chake, bali huiba mali ya mwingine; Kwa hiyo hakuna kitu au mali kwa jina jingine inayodaiwa na Mungu kuwa ni yake ila ni Zaka na Dhabihu!

  Kutotaka kutoa Zaka kwa kisingizio chochote kile si wizi tu, bali pia ni ubahiri na uchoyo wa kupita kiasi kuliko ule wa Paka, paka ukimgawia mnofu, kisha ukajaribu kumpokonya, ni lazima akukwangue na makucha yake marefu! 1Tm 6:8 inasema, “10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha;…….” Kama Zaka isingekuwa kitu endelevu, Biblia isingemnukuu yesu alipokuwa akieleza juu ya toba ya kweli kwa mfano wa Yule Farisayo na mtoza ushuru katika ile, Lk. 18:12 kuwa, “12 Mimi…;…. hutoa zaka katika mapato yangu yote.” Akiitaja kama moja ya vigezo mhimu vya uchaji Mungu! Vilevile hata alipokuwa akiongea na mafarisayo juu ya utoaji wa Zaka ulio bora na unaokubaliwa na Mungu, katika Mt.23:23 amsema,
  “23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. 24”

  Kama namwelewa Yesu sawa sawa hapa, ni kwamba, zaka ilipasa itolewe, KATIKA ADILI, NA REHEMA, NA IMANI, MAANA MAMBO HAYO NDIYO MAKUU KATIKA SHERIA! Kwa hiyo Zaka ni Sheria na Sheria ni Torati, na Yesu hakuja kuitangua Torati na tena Torati haitaondoka hata nukta moja! Sasa Sungura lipo wapi andiko LINALOSEMA HAITUPASI WAAMINIO KUTOA ZAKA KWA SASA?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 10. Mabinza asante kwa kufunguka.
  Ndio maana nilitaka sana uwe wazi maana nilijua kuwa kuna kitu umekificha moyoni mwako kuhusu swali la mleta mada.

  Kwa kifupi umesema Malaki 3:10 ni sawasawa na Luka 6:38.
  Na kilichokufanya useme hivyo ni matokeo yaliyosemwa katika hiyo mistari baada ya mtu kuwa ametoa.

  Lakini hukuona kitu kimoja,nacho ni kile kitu kinachotolewa. Katika Malaki kinachotolewa ni zaka, ambayo ilikuwa haipewi mtu bali Mungu. Na katika Luka kinachotolewa ni sadaka maana kinapewa mtu.

  Kwenye Malaki anasema(Mungu) atawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagia baraka mpaka pasitoshe.Lakini kwenye Luka Yesu( Mungu) anasema watu watawapimia kiasi cha kujaa, kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika.

  Kwa lugha nyingine, alichosema Yesu tuwape watu, zaka haihusiki. Kwa sababu hata katika torati zaka ilikuwa haiwezi kupewa mtu kwa ujumla kama vile Yesu anavyosema tuwape watu.

  Kwa hiyo Mabinza,katika hili suala la zaka nimekushangaa jinsi ambavyo umelihalalisha alhali mitume hawakusema hicho ulichokisema wewe. Na hakuna mahali biblia chini ya neema imesema asiyetoa zaka atalaaniwa na kufukuzwa katika ufalme wa Mungu. Huo ni uongo Mabinza!

  Kwa hiyo kama wewe unaweza kuhukumu hivi kitu ambacho mitume hata hawakukuagiza,wakati wewe unasisitiza kuwa tufanye tu yale mitume walifanya na waliagiza, basi unapingana kabisa na gizo la mitume hapa : Mdo 15:
  ambapo Petro anasema waaminio wa mataifa wasibebeshwe kongwa ambalo wao wenyewe akina Petro liliwashinda, na hata baba zao pia.

  Ni kongwa gani hilo kama si pamoja na zaka ambayo kwa mujibu wa hiyo Malaki 3: tunaona watu hao walikuwa wameshindwa kukitekeleza? Maana zaka ilikwa kundi moja na mambo ya tohara, miandamo ya mwezi, vyakula fulani,…..

  Hivyo basi, Mabinza umeyang’ang’aniza maadiko kukuhalalishia zaka katika hiki kipindi cha neema, lakini yamekukatalia. Umefanya hivyo kwa sababu nawe ni miongoni mwa wanaoitoa zaka kwa mujibu wa torati, lakini huku mkiihalifu sheria maana mnasema mtu anaweza kuizidisha lakini si kuipunguza. Nafsi yako imekulazimisha useme kuwa zaka ni wajibu mkristo leo aitoe, kwa sababu ungeikana nafsi ingekusuta ndani yako maana ni kitu ambacho nawe wakifanya.

  Kwa hiyo hata huhitaji kumshambulia Seleli,maana wewe ndio umeharibu zaidi katika kuhitimisa kwako juu ya suala la utoaji wa zaka, na adhabu ya asiyeitoa.

 11. Mpendwa Seleli, Sngura na wapendwa wote,

  Brother Seleli, Nimekupata vizuri, ila katika zile “Chembe zako 14 za uhai” ulizotoa hazina uhai hata kidogo ni Dead granule – Ufahamu wowote unaosababishwa na chembe mfu ni ufahamu mfu pia! Akili ni mwili, na matendo ya mwili husemwa katika Gal.5:17 kuwa, “17Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, nayo Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.”

  .
  . Biblia haijasema MSIZITUMIE AKILI bali imesema MSIZITUMAINIE AKILI ZENU! Kutumia akili ni kule Yesu alikosema “MUWE WELEVU KAMA NYOKA.” Na kutozitumainia akili ni kuwa “MPOLE KAMA HUA!” Huwezi kamwe kusema, eti kwa vile unazo Akili, basi uzitumie kwa kupambanua na kufundisha Neno la Mungu kwa kutumia akili zako, ukiamini na kufanya hivyo, unakuwa hujafika kwenye uelewa wenyewe! Kwani Paulo alisema,wenye kutegemea matendo ya mwili hawataurithi ufalme wa Mungu. Akili zinafaa kutumika katika mambo ya mwili duniani ambayo husimamiwa na seria tu, mambo yote yanayosimamiwa na Roho huwa si ya kisheria, bali ni ya kiimani tu!

  Mfano mzuri wa matumizi ya akili ni jinsi ya kuishi na mwanamke, bila akili huwezi kukaa naye, kwakuwa swala la kukaa na wanawake ni swala la sheria ndiyo maana linahitaji akili, akili husimama imara kwa sheria, kwa maana hiyo msingi wa kutumika kwa akili ni sheria, lakini tunajua kuwa huwezi kumpendeza Mungu kwa matendo ya sheria! Mpendwa wangu, akili hutumika ama kujidhihilisha tu palipo na ujinga, palipo na hekima huhitajika ufahamu; bali atumainiaye akili hutaka maarifa! Neno la Mungu ni HEKIMA hivyo linataka UFAHAMU, bali mwili ni AKILI na unahitaji MAARIFA; Lakini katika wingi wa maarifa kuna wingi wa majuto!! Unaona? Neno la Mungu hutegemea ufahamu, na kamwe halitegemei Akili.

  Biblia inasema Neno hili lilifunuliwa kwa watoto wadogo. Mtoto mdogo hufahamu tu kuwa huyu ni Baba yake hajiuliziulizi maswali, kwa mfano, mototo hajiulizi juu ya ukomo wa uwezo alionao baba yake! Humheshibu mzazi wake kwa hekima na wala hamtii mzaziwe kwa akili! Unapo kwenda shule kule unakwenda kutafuta MAARIFA na si kwamba unakwenda kuongeza Ufahamu ili uwe na Hekima! Chuo chochote, iwe cha sayansi ya jamii au ya ufundi, cha kijeshi ama cha Thiolojia vyote hivyo vinalengo moja tu, KUZALISHA MTU MWENYEUJUZI! Sipingi watu wasisome vyuo kama hivyo, lakini jiulize, Je, NENO LA MUNGU LINAFUNDISHWA NA WENYEUJUZI WA KUTOKA VYUONI? Kama ni Dini ndiyo! Iko siku moja watu wa vyuoni (wenye Dini yao) waliwahi kuhoji na kustajabia yale aliyokuwa akiyafafanua Yesu tokana na maandiko, ambayo wao walikuwa nayo kila siku na kwa miaka tele, lakini hawana UFAHAMU juu yake, wakisemezana wao kwa wao, “HIVI, HUYU ANATUFUNDISHA SISI ANAUJUZI TOKA WAPI, KASOMA WAPI?” wakidhani, vilevile kama Seleli kuwa Neno hili la Mungu hufundishwa na watu wasomi wa thiolojia wenye maarifa mengi yatokanayo na usomi, kumbe siyo, hili hufundishwa na Roho mtakatifu kwa ‘Elimu’ iitwayo HEKIMA. Mfalme mmoja mashuhuri wa zamani aliwahi kumshangaa Mungu jinsi ‘Elimu’ yake isivyotafasirika akasema, “Maarifa yako ni yaajabu yanishinda kujua, jinsi ulivyomuumba mwanadamu kwa namna ya ajabu ya kutisha”

  Watoto wa Mungu wanajua vitu bora hufanyika kwa hekima. Lakini wasomi hupima vitu vyao ubora kwa Viwango (standards) Kwa namna hiyo hiyo, wasomi na wanadini hudiliki pia hata kulipima Neno la Mungu kwa viwango, utawasikia ”Mimi ninaupako wa ajabu kuliko huyu, mimi nina kiroho sana kuliko huyu, mimi nalijua sana Neno kuliko huyu, Mimi nimeokoka sana kuliko huyu, mimi nimebarikiwa sana kuliko huyu, mimi nakubaliwa sana na Mungu kuliko huyu, Yesu yupo huku si kule….nk” huo ni ufarisayo mtupu, hamna lolote!

  Si mshangai seleli kuwaona mitume waliishi na kufanya mambo ya Mungu kimwili, japo maandiko yanasema, Yesu aliwaambia Mitume wake kuwa, “Msiondoke hapa, mpaka kwanza mpokee nguvu”….nitawatumia msaidizi….nitakuwa nanyi wakati wote hadi mwisho nk; Wasomi wa dini, utawasikia wakimkosoa sana Paulo, kwa vigezo vyao vya kisomi eti Paulo alijifanyia mambo mengine kwa mjibu wa mila, desturi , sheria, utaifa wake na kwa ubinafsi wake kama mwanadamu, wanalisahau Neno la Yesu mwenyewe ambalo litadumu kuwa hivyo hata milele kuwa “nitakuwa nanyi hadi ukamilifu wa dahari”

  Kwa ufahamu mwepesi tu ni kwamba, kila walilolifanya Mitume lilisimamiwa na Yesu mwenyewe, kwa sababu linamhusu, na kwakuwa yupo pamoja nasi hadi mwisho, hivyo hawezi kuacha lipotoshe aaibike! Yesu alikuwa na yungali makini wakati wote, akijua shetani yupo bize, utaliona hilo wakati shetani alipojiingiza kwa Petro, Yesu mara moja alimkemea na kumwambia “nenda nyuma yangu shetani” tunajua pia kuwa Yesu ni yeye Yule leo na hata milele, haingii akilini kuwaachia Mitume waingize ubinadamu wao, na kuacha mambo hayo yakarekodiwa kwenye “hansadi” kuwa Neno la Mungu, ndani ya Biblia! Seleli, nasema tena sikushangai kabisa jamaa yangu, kwa upole tu nakukumbusha kuwa, ni kawaida ya wenye maarifa na wanganga kuhoji kielimu mambo! Kama vipi rudisha kumbukumbu zako, Misri yakale na Musa, Babeli na Danieli, Manabii wa Baari na Nabii wa Mungu nk. Kwa hiyo, Thiolojia ni Dini na Dini ni Mwili na Mwili ni Dunia. Mungu hawezi kudhihilika ama kufahamika eti kwa sababu mwenye kuhubiri Injili ni mtu kapitia vyuo vya Thiolojia, kuwaza na kuamini vile ni ubinadamu tupu!

  Umegusia ubatizo ukimaanisha kuwa si lazima ubatizwe kwa Jina la Yesu na kwamba hiyo ni Imani inayotokana na mafundisho ya Jesus Only, ambaye kiongozi wake alimaliza kazi yake kwa upotofu. Ndugu yangu, mimi nakuhakikishia wazi kuwa simjui huyo mwanzilishi na pia hicho kikosi cha Jesus only, ‘Filosofi’ yake na hata mafundisho yake. Mimi najua kuwa ni lazima wote wanaomuamini Yesu Kristo kupitia Injili hii hii; TUBATIZWE kwa Jina la YESU kwa mjibu wa mafundisho ya Mitume ambao ndiyo waliotusikizisha Injili na tukaiamini, maana Mat 28:20 inasema, “20nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika Mimi niko pamoja nanyi sikuzote, hadi mwisho wa nyakati.’’ Amen.” Yesu, ambaye ndiye aliyewatuma hao mitume watufanye nasi kuwa wanafunzi (Mk. 16:15-16) ndiye aliyesema hivi, “Atakaye wapokea ninyi amenipokea mimi na atakaye wakataa ninyi amenikataa mimi” Baada ya Mitume kuamliwa na kuhakikishiwa hivyo na Bwana Yesu Kristo, Mitume walikuwa na hakika ndiyo maana wakasema, “Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo mtu na alaaniwe!” Utekelezaji wa matendo ya Mitume kuhusu ubatizo yanapaswa sasa kufanywa kwa mjibu wa mafundisho ya Mitume kama ilivyoelezwa katika Mdo 2:38! Katika hilo la Ubatizo si kwakuwa mimi ni “mjizazi onole” ila ni muumini wa mafundisho ya Mitume, na kwakweli asiyefundisha na kufanya kama Mitume anakuwa amelaaniwa, si mimi usinielewe vibaya ni maandiko!

  @ Sungura,

  umenitaka niweke wazi zaidi jibu kwa muulizaji, umesema sawa, pengine niliandika siku ile kwa harakaharaka na hivyo kutoeleweka vizuri, maana hata seleli anasema nirudie kusoma mwenyewe, katika hilo seleli alikuwa sawa! Sasa namjibu muulizaji na wengine wote pamoja nawe hivi:-

  Zaka ni shemu ya kumi ya mapato ya mwamini. Kwa kifupi kila matoleo yalikuwa na maana au sababu yake kama nitakavyojaribu kuainisha hapa chini kwa ufupi:-

  1. Zaka ni fungu la kumi la kila mapato ya mwamini (1Sa 8:15,17, Law 27:30, 27:32)

  2. Kwa ujuma matoleo ni desturi iliyowekwa kale, kama mpango wa kumjengea mwamini tabia ya kumtolea Mungu kupitia watumishi wake (Mw. 14:20; Ebr. 7:6)

  3. Ni kumrudishia Mungu shukrani kwa Baraka zake alizombaliki mwamini (Mw.28:22)

  4. Ni moja ya Sheria ya Mungu (Law. 27:30)

  5. Ni matoleo maalum (2Nyakati 31:6)

  6. Ilitolewa kwa ajili ya huduma ya Lawi (Hesabu 18:21,24; Ne 10:37)

  7. Walawi walipaswa kutoa nao katika vitu walivyopokea, ili iwe zaka ama matoleo maalumu ya kumuinua Mungu na kama fungu lao (Hesabu 18:26,2718:26, 28; 10:38)

  8. Ilitolewa Kama ongezeko la thamani kwa kila sehemu ya hamsini (Law 27:31)

  9. Ilitolewa kama Adhabu ya kubadili (Law 27:33)

  10.Ilitolewa ili Kufanya waamini kuwa na bidii na tabia ya utoaji,kama heshima na shukrani kwa Mungu (Hesabu13:10) nk.

  Zaka na matoleo mengine na sadaka zilisimamiwa na Makuhani. Mwanzoni ukuhani ulikuwa ni wa kila Mtu, mtu aliweza kutoa sadaka yake na matoleo mengine mbele ya Mungu yeye mwenyewe kama kuhani. Ni kweli kwamba Mitume hawajafundisha utoaji wa Zaka, wala kufafanua au kutoa mwongozo wowote juu ya hilo; Kwa sababu moja tu kwamba, Zaka na matoleo mengine na sadaka ni swala la kikuhani, biblia inasema sisi ni makuhani wa kifalme pamoja na Kristo. Mwanzoni ukuhani ulikuwa ni wa kila Mtu, mtu aliweza kutoa sadaka yake na matoleo mengine mbele ya Mungu yeye mwenyewe kama kuhani, baadaye ikawa kwa mkuu wa familia na hata ikawa swala la kitaifa, mpangilio huo tunauona katika wakati wa Nuhu (Mw. 8:20), Abraham (Mw. 12:7; 13:4), Isaka ( Mw.26:25), Yakobo (Mw.31:54), na Ayubu (Ayubu1:5). Lakini Neno hili ‘Kuhani’ kwa mara kwanza linaonekana kutumika kwa Melchizedek (Mw. 14:18).

  Chini ya mpangilio wa Kilawi katika ukuhani ulikuwa maalumu kwa kabila la lawi pekee na au mtu kutoka katika familia ya Haruni, kulikuwapo na sheria Fulani zilizotambua na kuziheshimu sifa za ukuhani kama ilivyoainishwa katika Law. 21:16-23. Sheria hizo za kale zilizingatia na kuainisha pia mavazi yampasayo Kuhani (Kut. 28:40-43) na kanuni zote za utakatifu katika ukuhani (Kut.29:1-37). Kazi zao nk, (Kut. 27:20, 21; 29:38-44; Law.6:12; 10:11; 24:8; Hes. 10:1-10; kumb. 17:8-13; 33:10; Mal.2:7). Kuhani aliwakirisha watu na kutoa sadaka mbele ya Mungu kwa mjibu wa Sheria za torati,

  katika wakati wa Mfalme Daudi Makuhani waligawanyika katika madaraja ishirini na nne (1 nyak. 24:7-18). Idadi hiyo ya makuhani ilizingatiwa sana, hata katika wakati wa uhamishoni walipokamatwa mateka (Ezra 2:36-39; Neh. 7:39-42). Makuhani hawakusambazwa nchi nzima, bali walikaa pamoja katika baadhi ya miji kwa idadi ya kama 48; ambapo 6 kati yao walikuwa katika miji kadhaa uhamishoni, ambao walipangiwa kazi zao kwa mjibu wa sheria za kikuhani. Kutoka na wajibu huo walikuwa wakienda na kufanya ibada katika hekaru kule Yerusalem ,lakini utekelezaji na usimamizi wa sheria na utaratibu mzima wa kidini uliwekwa mikononi mwa wakuu wa familia husika, mkuu wa familia alikuwa akiwajibika kwa asilimia zote katika maswala yote ya dini, hadi yalipoanzishwa Masinagogi, jambo ambalo halikuanza mara moja hadi taifa lilipo anza kutoka katika nchi za uteka (Uhamishoni). Sababu kubwa ya mpango huo ni Taifa kuwa huru, kukomesha na kuondoa kabisa ibada ya sanamu ambayo wayahudi kutokana na maelekezo ya Toirati ilikuwa dhambi kubwa! Kwa hiyo, mpango mzima wa ukuhani uliofanywa na wayahudi, ambapo pia ilikuwa ni kivuri cha jukumu la Bwana Yesu Kristo mwenyewe. Makuhani walimchagua kuhani mkuu, ambaye ndiye aliyekuwa akitoa sadaka mara moja kwa niaba ya watu wote mbele ya Mungu. (Ebr. 10:10, 12).

  Kwa sasa, hakuna tena mtu maalumu kuwa kuhani, ukuhani umerudishwa kwetu, kwa kila mmoja wetu, kama ilivyokuwa pale mwanzo, (tazama huduma ya Mitume wakati wote katika kitabu cha Waebrania). There is now no human priesthood. Kwa sasa Neno “KUHANI” linatumika kwa kila mwamini wa kweli wa Yesu kristo (1 Pet. 2:9 inavyosema kuwa, “9Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu.” Na ile Uf. 1:6 inasema kuwa, “6akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu Wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo vina Yeye milele na milele! Amen. “

  kwa sababu hii, inaonyesha kuwa hakuna tena huduma ya kutoa sadaka za kuchinja na ZAKA kwa mtindo wa kitorati. Labda ili nieleweke vizuri kwa Seleli ambaye anajua vizuri zaidi kimombo, sasa anivumilie maana nataka elewe, nitatumia kimombo kilekile lakini kwa kiwango change cha darasa langu la Saba, hebu nijidadafue, mpendwa kwakuungana na wale wanaokubali hivi, “All true believers are now kings and priests unto God. As priests they have free access into the holiest of all, and offer up the sacrifices of praise and thanksgiving, and the sacrifices of grateful service from day to day.”

  KWA HIYO KUTOA ZAKA KWA MWAMINI WA KWELI NI JUKUMU LA HAKI. Lakini mwamini hatuoi kwa kujionyesha kama vile kuorodhesha majina na kiasi cha matoleo katika mbao za matangazo, si kwa kila mwezi , mwaka au juma bali kwa MUDA WOTE KWA UPENDO FURAHA, AMANI NA HAKI KATIKA ROHO MTAKATIFU, maana sisi ni MAKUHANI wa KIFALME, na kwa hiyo tunatoa, tunasaidia, tunachangia na tunafanya kila lolote kwa watu na kwa Mungu KIFALME, maana tumo ndani ya huo ufalme ambao utumishi wake ni waajabu, maana unakubalika kote, kwa Mungu na kwa watu! Hebu tazama Rum.14:17-18 inavyosema, “17Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18Kwa sababu mtu ye yote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.” Labda nikubaliane na Neno la Mungu kwanza, kisha niwe pamoja na watu wanaosema pamoja nami hivi,
  do everything you can to understand God’s principles. The Bible says, “My people are destroyed for lack of knowledge” (Hosea 4:6). There are many Christians who have no concept whatsoever of the principles of God’s kingdom. They understand neither God’s laws dealing with material prosperity nor their own privileges as children of God. So, for lack of knowledge, they suffer.

  We need to understand a rule of God’s kingdom that I call the Law of Reciprocity. This is a law of cause and effect, of action and reaction. In the area of “Zaka nautoaji kwa wenyeuhitaji”, the law is simple: “Give, and it will be given to you: Good measure, pressed down, shaken together, and running over will be put into your bosom. For with the same measure that you use, it will be measured back to you” (Luke 6:38).

  When a person begins to give to God’s work and to the poor and less fortunate, God begins to give back to him. Regardless of the debt burden, a person should give a very minimum of 10 percent of his income to the Lord. Even if you are at a poverty-level income, you have something you can give to God. Start where you are. Reach out in compassion to those less fortunate than yourself. As a first priority, get into a position to give love, time, energy, and money to other people even if it is only a little bit.

  Labda, ni adhabu gani, kwa mtu asipotoa Zaka? Kabla ya kujibu hilo, wote tunajua kwamba, Zaka hutolewa kwa Mungu, lakini Neno ZAKA ni moja ya kumi, kama ndivyo, nilishasema tangu mwanzo kuwa, Zaka ya sasa si ya sheria, tunaitoa kwa upendo. Lakini ni vema tujiulize kuwa, kama Zaka ni toleo kwa Mungu, tunampampaje Mungu matoleo yetu hayo? Je, Mungu ameelekeza jinsi ya kumpa matoleo yetu katika kipindi hiki cha Yesu, ili kupata sawasawa na vile ilivyoelekezwa na Torati ya musa? Tunajua kuwa sasa hatutoi kwa sheria kwamba lazima iwe moja ya kumi, yaweza mtu akatoa zaidi ila kwa kumpenda Mungu. Biblia inasema, upendo wetu kwa Mungu, unadhihirika tunapo wapenda watu! Tunajua kuwa Neno halipingani, tunajua pia kuwa, kutoa ni sheria, lakini sheria ya torati ilikamilishwa na Yesu, na kuifanya mpya aliposema, katika Yh.11:34 akisema, “34‘‘Amri mpya nawapa: Mpendane kama Mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. 35Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi Wangu’’

  Kwakuwa matoleo yote ikiwemo Zaka ni kumtolea Mungu, Je, katika swala hilo la kumtolea mungu yeye kasemaje? Hebu tuiangalie ile Mt. 25:35-45, inasema, “35…………45“Naye atawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, kwa jinsi ambavyo hamkumtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’ Mtu mmoja atasema hapo alikuwa hazungumzii matoleo, ni sawa labda. Lakini Mtu alipotoa zaka alitegemea kupata nini kwa Mungu? Tuione Malaki 3:10 inasema, 10Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha……. ,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu.

  Sasa kama kutoa Zaka kulisababisha Baraka na kuongezeka kwa mapato kwa mtoaji; Je, Yesu anasemaje katika utoaji “Zaka” katika nyakati hizi za Neema? Hebu tuangalie Luka Luke 6:38, inasema, “38Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.” Basi ni kitu kilekile cha katika ile malaki 3:10 ni sawa tu na ile Luka 6:38! Hapo tunaona kuwa, hajasema toeni kwa wachungaji, maasikofu, mitume, manabii nk, ili nanyi mbarikiwe. Hii inamaanisha kuwa Baraka zilizokuwa zikiletwa na Mungu kupitia matoleo ya Zaka kwa sasa Baraka zilezile Mungu anazileta kwa kuitekeleza ile Lk 6:38, kwa kadri ile mtu anavyojariwa na Bwana.

  Kuhusu ADHABU mtu atakayopata kwa kutokutoa matoleo hayo ya “Zaka” ya sasa si kuishia kuwa fukra tu, bali pia na Kulaaniwa, unafukuzwa katika ufalme wa Mungu, unasagishwa meno nje! Kwakuwa Yesu mwenyewe amesema hivyo, hatakutambua, kama hutatambulika, basi, nikutolewa ‘lessi’ nje, maana hata malaika ambao anasema atakuwa ameambatana nao siku ile ya “kubagua mbuzi na kondoo” watakuwa hakutambui, watashindwa hata kujua umefikaje pale, utafurumshwa nje kama kitu kilichooza!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!

 12. Seleli,

  Haya hebu tuendelee, ‘mwalimu wangu’; swali (a) unaloniuliza kuhusu 1Kor 14:14-16, vifungu hivi vya Maandiko vinamalizia hivi “… Basi nawasihi mnifuate mimi.” Kwahiyo, hebu jaribu kuendelea kumfuata Paulo ili uone kama aliwahi kumwita mtu yeyote yule “Baba wa Kiroho au Anko wa Kiroho, ama Binamu wa Kiroho”, ukiliona jambo hilo basi jua ya kwamba Njia aliyoipita Paulo na wewe ndiyo unayoifuata, hivyo alipo Paulo nawe utapafika; la hulioni jambo hilo kwa huyo aliyekusihi umfuate, basi wewe endelea tu, huko mbele utamkuta “Baba yako wa Kiroho” anayekuongoza!

  Swali b naona zaidi unajiongelesha, hata hivyo, hebu nisaidie katika hili huenda tutafika mahali tutaelewana vizuri tukaondokana na ku “debate poorly”:
  Kristo anasema hivi,
  Mt 23:9 “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.”

  Naye Paulo anasema hivi,
  1Kor 4:15 “Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.”

  Nawe unawaita watu hapa duniani, “Baba zako wa Kiroho” katika urahisi wa ulimi, unawaita “Baba Askofu” au “Baba Mchungaji” au “Mama Askofu” au “Mama Mchungaji”, na unakiri kwamba unayafanya hayo katika context ya Paulo.

  Je, nini tofauti ya vifungu hivyo vya Maandiko, contextually? Kwamba Paulo alifundisha tofauti na Kristo, hata wewe ufikie kulihalifu Neno linalotukataza kumwita mtu yeyote yule “baba” kwa kisingizio kwamba Paulo ameruhusu??

  Paulo hajawahi kufundisha jambo hilo katika namna unayomsingizia. Huo ni uongo wako wa kinafiki unaotokana na kule kuligawa kwako Neno la Mungu! Na kwa kukosa Ufunuo, unatembea kama kipofu, mitego waliyowekewa wale wakupotea, imekukamata kisawa sawa! Kwamba unawaita watu hapa duniani “baba” inaonesha kuwa mishipa yako ya damu kwa yule “Seleli wa kiroho” imekauka, umebakia wewe wa mwilini unayepose wa rohoni, ndio maana tukifika kwenye issue za rohoni, dah, unatokaga kavu ile mbaya, hebu wazia kwamba leo hii, eti unataka kumwapisha mtu, hauko mbali sana, utayarudia matapishi yako, utampandisha “Baba Askofu” wako kuwa “Baba Mtakatifu” katika context ya Paulo hiyo hiyo; after all Bwana si ametufanya kuwa “Watakatifu”!!!

  Kuhusu Zaka ndg yangu, ili mradi umesema hauhitaji Ufunuo, sioni ni kwa jinsi gani utayaona ninayoyaona mimi; si unaoiona tofauti yetu, Mt 23:23 mimi nayaona Maandiko yakielekeza juu ya KULIPA zaka, ambavyo najua ni kulingana na Torati, na wewe unayaona yakikusisitiza wewe KUTOA zaka, jambo ambalo silioni ktk kifungu hicho, labda ni yale Mafunuo mnayooteshagwa, ambayo nayajua nguvu yake, zaidi ya Siloamu!!! Jaribu kujiangalia, Maandiko yanasema KULIPA lakini wewe umekomalia KUTOA, fuata utaratibu, bila ya Ufunuo utaishia kutoa kama Kaini tu!!!

  Gbu!

 13. Seleli,
  Kama aliyenihubiria habari njema nikaokoka ni baba yangu wa kiroho, je Mungu ni Baba yangu wa kinini sasa?

 14. Mabinza,

  Kwakua “Ufahamu ni chembe ya uhai!”, basi nifuatilie taratibu hapa ili upate chembe izo nimekupikia 14 haswaaa. Na kwakua umeongea mambo mengi mno kwa mara moja, basi nami namiminika ivyo ivyo hatua kwa hatua kwa urefu kweli, nikikufuatia. Ingawa mimi ni mtu nayependa kujikita NDANI na MBALI na mada ili kukidhi haja ya mengi, ila wewe umepitiliza sana rafiki, umekwenda MBALI MNO na mada mpaka kurudi umeshindwa kabisa. Nitajibu baadhi ya uliyosema na ivyo jibu langu nalo litakua huko huko mbali mno na mada kwa kuwa limepelekeshwa na post yako mchanganyiko mkubwa.

  Umesema….’’Watu wengi husimamia maelekezo ya kimapokeo tokana na walimu wa thiolojia ambao kwa kiasi kikubwa husimamia zaidi Dini zao, ambazo kwa kweli ni Taasisi za Kidunia tu!’’

  Response yangu: Elewa si kila Mapokeo ni dhambi au pepo au mbaya, ni yale tu yanayokwenda kinyume na Neno, mengine yote safi tu na hakuna mwandamu asiye na mapokeo hata baada ya kuookoka, tunayo tuliyotoka nayo uko yale yasiyo dhambi na yako mengine tunayazalisha hata leo. Yesu alisema, kwa nini mnaliharifu Neno la Mungu kwa sababu ya mapokeo yenu?-Mathayo.15:3. Kama mapokeo HAYAVUNJI NENO-hamna shida! Chembe ya uhai moja iyo, ikupe ufahamu wa kwanza!

  Umesema, ‘’Kwa sababu, ukilifuata Neno la Mungu kama lilivyo bila kuingizaingiza Tafsri za kithiolojia’’

  Response yangu: Thiolojia si pepo, ni kutoelewa tu. Thiolojia maana yake ni the ‘’Study about GOD’’, si yote ktk kozi hiyo ni hatari, mlidaganywa tu na baadhi ya wahubri wa kipentekoste , wavivu na wanaokimbia kwenda shule kwa visingizio vya kua wana upako na RM, na ivyo inatosha sana- ati kwa kua na RM na upako, wana vyote na kwamba hawahitaji kwenda shule kupata au kuongeza Elimu, Maarifa, Uelewa wa mambo na hata Ufahamu-Ujuzi! Hiyo si tu ni uwongo lakini pia imewafanya ktk huduma zao, uhubiri na kufundisha mambo mengine pumba kabisa na aibu kuyasikia au kumpeleka rafiki yako kusikia preacher wa ivyo. Kwa ivyo kupitia Thiolojia, tunapata Elimu muhimu sana na hata kutusaidia sana,sana, sana kabisa kupata uelewa na tafsiri sahihi ya dhana/mambo/vitu/matukio/maneno mengi sana ktk Maandiko. Usiponde kitu bila kua na ufahamu wa jambo, kisa tu umeiga au wengi wanapondaga au ulisikia mhubiri mmoja lazy hataki shule ameponda, ni kosa na kukosa ufahamu. Chembe ya uhai ya pili iyo, ikupe ufahamu wa pili.

  Umesema, ‘michango ya wapendwa iliyopo hapo juu, inathibitisha mgawanyiko mkubwa wa kweli ya Neno la Mungu na mafundisho ya uongo ya shetani’’

  Response yangu: Neno la Mungu haligawanyiki ila Watu na UFAHAMU WAO TENGE KTK NENO ndio wanagawanyika! Pia WATU NA MIOYO YAO MIGUMU KTK MAMBO YA MUNGU KWA SABABU YA NAFSI ZAO ZENYE KUKABA KOO YA ROHONI, NDIO WANAGAWANYIKA ILI KUYATETEA HAYO. Na watu wakigawanyika kwa msingi huo, ni sawa tu kabisa maana wanaotetea UKWELI NA MOYO WA MUNGU ktk maisha yetu wawe dhahiri na wale wanajidhani wanasimama na Mungu na Neno lakini kumbe ndani hamna lolote bali ni kutetea matwaka ya nafsi zao tu ili wale, wanywe, washibe wao kwanza kisha ya Mungu baadae, na wao wawe wazi. Kwa maana hiyo, si lazimia tue pamoja ktk hayo na kwa msingi huu, Ni vema na haki kabisa kutengana kwa amana iyo, maanaa upande moja SAHIHI hauwezi kubali kupelekwa shimo la ‘utafuteni KWANZA UFALME WA DUNIANI KISHA wa mbinguni baadaye au kesho au kwaheri. Chembe ya uhai ya tatu iyo, ikupe ufahamu wa tatu.

  Umesema..’’TAYARI KANISA HILO LILISHATAPIKWA’’

  Respone yangu: Acha kutumia sentence/maneno makubwa wakati huna uhakika nayo au ukibanwa huwezi thibitisha bila kuacha shaka! Wewe nani amekuambia kanisa linatapikwa? Umeitoa wapi iyo? ni ufahamu wako, ufunuo au mwinjilisti wako aliyekimbia shule ya Thiolojia ndio kawatishia? Chembe ya uhai ya nne iyo, ikupe ufahamu wa nne

  Umesema vema ivi, ‘’Kama mtu hataki kuiangalia na kuiamini ile kweli ili awekwe huru, basi kwisha!

  Response yangu: Kweli inaeleweka kwa njia nyingi mfano ni kusoma Thiolojia pia, si tu kitishwa na baadhi ya Wahubiri/Watumishi watoro wa shule na wavivu kusoma hata kozi fupi fupi za Bible ili aidha kunoa walichonacho au kupata mapya waliyokua hawana na wasingeyapata hata kwa kufunga na kuomba 40 kutaka upako na mafunuo au uelewa mkali/mkubwa kama wa aliyeende Chuo cha Biblia !!!!!!! Mungu wetu ni wa utaratibu, ameweka Elimu na Maarifa na kusisitiza MKAMATE/MTAFUTE SANA ELIMU. Kama hawataki basi wakae kimya au wasema mambo kwa tahadhari na si kufyatuka tu na confidence zote pori kumbe wako off ile mbaya na aibu tupu, wakishusha ‘P’ au ‘CV’ uku wakishangiliwa ‘’sema baba semaaaaa, aaaaaaaaiiiiimen! kumbe pumba kabisa! Waende shule full stop! Chembe ya uhai ya tano iyo, ikupe ufahamu wa tano

  Umesema vema ivi, ’’Neno la Mungu hufanyika CHENGA YA MWILI kwa kila atumiaye AKILI, kwakuwa akili ni mwili haziwezi kumtafsri Mungu na Hekima yake’’

  Response yangu: Ni kweli tunamuhitaji RM kulitafsiri Neno lakini kulingana na Mdo.26:25..Tunatumia pia akili kusema/kuelewa maneno ya Mungu ivyo sisi si roboti au matikitikimaji tusomapo Neno, vyote vya rohoni na kichwani, vinachacharika kulielewa Neno. Therefore, tumia akili ila si kuzitegemea. Tumia akili maana wewe siyo Chimpanzee ingawa naye anatumia na anayo akili sana, hata njiwa naye pia nyoka, wewe je Mwanadamu wa thamani ivyo? Ndio maana Yesu akitoa mifano mingi kama wa mpanzi-alitumia akili ya kawaida kuelemisha na Wanafunzi walieelewa mara moja mfano wa mpanzi kwa akili tu ya ugali wala hakuna mafunuo hapo wala nini, mstake kukuza mambo, kila kitu kukifanya kirohoooooo weeeee kumbe ulongo tu,hamna kitu. Chembe ya uhai ya sita iyo, ikupe ufahamu wa sita.

  Umesema kweli na ulongo ivi….’’Yesu alichagua mitume na kusema kuwa, “ATAKAYE WAKATAA NINYI AMENIKATAA MIMI” lakini kupitia hiyo michango ya wapendwa hapo juu, wapo wengi zaidi wanao WAKATAA MITUME na kusema kuwa, walifanya mambo yao wenyewe kwa kufuata au mila, desturi am utaifa wao, hivyo hawakufanya mambo yote kama walivyoelekezwa na Yesu’’

  Response yangu: Ni kweli Yesu aliwachangua lakini

  (a) Je aliwachangua Malaika au Watu?

  (b) Je wakati wanatumiwa na Mungu kuandika Bible, walikua mochwari au walikua wanadamu kamili?

  (c) Kama wakikua Wanadamu kamili, kwa nini ndani ya Bible kusiwepo sehemu ya kibinadamu kama desturi, mila, hisia zao, misimamo yao binafsi, maoni yao binafsi madhaifu yao, nk

  (d) Je ktk nyaraka zao maneno kama haya ni Mungu-RM au wao kama Watu mfano: SIMPI ruhusa Mwanamke, SINA amri ya Bwana bali nasema kama…., NILIMSIHI sana Appolo aje lakini hakua tayari….., Barua hii nimeandika kwa MKONO wangu mwenyewe, Vita NIMEvimaliza,Iman NIMEilinga, Bwana NITWAE roho yangu maana nimebaki mimi tu, Enyi waasi mwataka TUWAKOLEZEE maji kwa mwamba huu, NINGEPENDA wote muwe kama MIMI ila …., Utakapokuja UNILETEE nguo na vitabu nk? ni nani huyo/hao wanaongea hayo ktk Bible? Ni Mungu, Watu? Jibu hapo tafadhari!

  Chembe ya uhai ya saba iyo, ikupe ufahamu wa saba.

  Umesema, ‘’Kuhusu Ubatizo…Kwa Jina la Baba, Mwana na Roho au kwa jina la Yesu’’

  Response yangu: Hakuna hoja hapo ya maana kua watu wakikosa kuielewa wanakwenda jehanum, zaidi ni upotezaji wa muda na space humu, kusumbua watu na ya kutetea mapokeo ya Mkuu wa dini ya Jesus only! Hayo sasa ndio mapokea ya kuzimu kabisa. Acha mara moja.! JESUS only ni imani chafu, Kiongozi wake alikua fire Kiroho safi ila akamalizia kupotoka, hana tofuti na watu wazima kiroho na wanajua Bible imejaa Manabii wa kweli na wakutisha wa KIKE NA KIUME lakini bado wanamfuta kamdada ka M23 commandements! Chembe ya uhai ya nane iyo, ikupe ufahamu wa nane.

  Umesema Maandiko haya…’’Eva….. “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani. ’’BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu akamwambia, ‘‘Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani, 17lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.’’ Kisha ukafafamua ivi chini:

  Ukilinganisha maelezo ya Eva kwa Nyoka na Maagizo ya Mungu kwa Adamu, utaona kama yanatofautiana, Eva anasema wamezuiwa hata kukusa tu matunda yale wasije wakafa! Lakini tunaona maelekozo ya Mungu hajatamka Neno “Misguse” Je, unaweza kusemaje hapo? Eva alijitungia mwenyewe neno lile “msiguse”?

  SWALI:
  (a) Alilosema Eva hapo na Mungu, lipi ni Neno la Mungu na la Mtu? Tuchukue lipi na tuche lipi na kwa nini?

  Chembe ya uhai ya tisa iyo, ikupe ufahamu wa tisa.

  Kisha ukasema ivi..’’Lakini Biblia inatuambia kabla ya kula lile tunda Eva alikuwa hajawa mtenda dhambi, kwa hiyo hakudanganya wala kujitungia neno hilo ‘usiguse’!

  SWALI: Kwa iyo alilosema Eva ni sahihi? Je alilosema Mungu mwenyewe ni sahihi pia? So Which is which now? Chembe ya uhai ya kumi iyo, ikupe ufahamu wa kumi.

  Umesema vema ivi…..’’Neno la Mungu ni Roho, kama alivyo yeye kuwa ni Roho na wanaomwamini yeye humwamini katika Roho. Neno la kiroho heleweka na watu wa Rohoni tu.

  Response yangu: Kua mtu wa rohoni haimaanishi kutokua au kutotumia AKILI hii hii ya sembe kuyatafakari na kujifunza Neno…Paul alitumia sana akili-Mdo.26:25, Yesu alitumia sana akili ya kawaida kufafanua na kuelezea Kweli za Mungu mfano wa mpanzi, Kadhi katili, Bwana mwenye Shamba, Mimi ni mzabibu, ngano na magugu, ulishaji wa Mungu kwa ndege wa angani na maua ya kondeni na mengine mengi ya kawaida kabisa kuelewa. Usikuze na ku-complicate mambo ambayo RM alishaya simplfy. Chembe ya uhai ya 11 iyo, ikupe ufahamu wa 11

  Umesema ivi…’’Neno la Mungu mwenyewe na kwamba litabaki kuwa ni “chenga ya mwili” kila mwenye kujaribu kumtafsri Mungu kimwili!

  Response yangu: Acha ulongo! Tunaeelewa Mambo ya Mungu kwa kutumia kila tulichonacho namely roho, Roho, Mwili, akili, nafsi nk. Hakuna chenga wala mchanga hapa, msitishe Watu au kuspiritualize kila kitu 24/7, si kweli wapendwa, acheni mambo yenu hayo ya ajabu. Chembe ya uhai ya 12 iyo, ikupe ufahamu wa 12.

  Umesema, ‘’Ikiwa shetani mwenyewe hakumbishia Eva kuwa Mungu hakuelekeza “kutogusa” matunda ya mti ule wa katikati, na akaamini kuwa hilo neno “MSIGUSE” “ALILOLISEMA” Eva lilitokana na Mungu! Inakuwaje, kwa wapendwa wanaposema Baadhi ya Maneno au mafundisho ya Mitume ni yao wenyewe na kuwa hayatokani na Mungu (Yesu)?!

  Response yangu: Kwa hiyo uthibitisho wako wa kweli ya Neno, unautoa/pata kwa devo kukaa kimya? Na kwa iyo unaelekea kusema alichosema Eva ni sahihi na cha Mungu siyo? Mwe! Umenichekesha na umejiabisha kwa hoja hii ya porini kabisa! Chembe ya uhai ya 13 iyo, ikupe ufahamu wa 13.

  Mwisho umesisitiza haya…’’’ Mimi (si Mungu) nasema, Mtu anapowakataa ama kuwabishia au kuwa namashaka juu ya mafundisho ya Mitume ni “MBAYA” kuliko hata Dhambi yenyewe! Kwa sababu, dhambi ni KUTOAMINI Neno la Mungu, lakini Mtu asiyetunza Familia yake (Kuaminisha isiyo kweli vichwani mwa wana FAMILIA wa Mungu, ambayo mtu Fulani kapewa kuichunga iwe kama yake) ni Mbaya kuliko asiyea amini – yaani ni mbaya kuliko mtu mwenyedhambi, na mwenyedhambi ni SHETANI, maana Uzao wa nyoka ni nyoka, kwa hiyo ni MBAYA KULIKO SHETANI! Sheria imekamilishwa kwa njia ya Kristo Yesu, naye Kristo Yesu Neno linasema yupo pamoja na watu wake hapa duniani hadi mwisho, na kwamba yumo ndani ya watu wake akiwaongoza, kuwafundisha, kuwaelekeza, kuwalinda dhidi ya mwovu kwa jinsi ya Roho, sasa haingii akilini MATENDO YA MITUME!’’’

  Response yangu: Ivi umeandika manini hayo hapo brother?! Yasome tena! Khaaaa! Chembe ya uhai ya 14 iyo, ikupe ufahamu wa 14.

  Press on.

 15. Mabinza
  Ulivyoanza kuandika mchango wako nimlifurahia kweli kusoma, maana ulikuwa umefanya ‘summary’ nzuri kweli.

  Nimesikitika tu kwamba baada ya kumaliza kusoma nimejikuta sijaelewa umechangia nini hasa katika hii mada!

  Nilijua utajibu swali la mleta mada kwa ufupi na uwazi, lakini dah, hujafanya hivyo. Zaidi umetupia hapa mambo tuliyojadili katika mada ya ubatizo.

  Nitafurahi kama utachangia hii mada.

 16. Lwembe/Sungura,

  Kengele gani ilipiga Lwembe, mbona una mbwembwe! Unataka kumaanisha RM ndani yako ati amekupa signal siyo? Kwa lipi la maana? Lipi ilo lililokwenda tenge Kimaandiko ambalo mimi nimelileta halafu ‘roho’ wako akusitue? Mmmh! Watu bwana mna-illegal upako wa kuji-qualify kiroho ile mbaya, hamna tena mfano. Halafu bora ungekua unasimamia kitu cha ukweli lakini lo!

  Umerudia maandiko haya, ajabu na bila haya, unakiri kua hauoni kuna Mtu mwenye hadhi ya U-Baba wa Kiroho/imani kwa watu wake hapo! Hii ni ajabu kweli ufahamu wako!!!!!!!!!!!! Ngoja nie-expose aibu hii uliyofanya kwa namna hii.

  Imeandikwa ivi:

  1Kor 4:14-16 “Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. Basi, nawasihi mnifuate mimi.”

  Na………………….,

  1Tim 1:2 “…kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani.”

  Notice: Sentences izi toka maandiko hayo….. na maneno nimebold

  ‘mwanangu hasa katika imani’’ ,

  ‘kuwaonya kama watoto’’,

  ’walakini hamna baba wengi, maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili

  Swali: (a) Mtu anayekuita wewe ni Mwanae Kiimani, amekuzaa ktk Kristo, anakusisitizia kua hauna baba wengi( maana yake anasisitiza baba yako ni yeye tu), Je Mtu wa hadhi iyo kwako, wa aina iyo kwa maisha yako, UNAMUITA NANI, Anko au Binamu huyo?

  (b) A u kama kawaida yenu mnavyo debate poorly and illogically wakati mwimgine kua mpaka mkute ktk Neno live ivi kwa mfano… ‘’waalakini hamna baba wengi maana mimi ndimi BABA YENU WA KIROHO niliyewazaa ktk Kristo Yesu kwa njia ya injili! So ukikuta ivyo ndio ujue sasa tuwaite hao wenye hadhi izo kwetu Baba wa Kiroho/Kiimani?

  Unachojaribu kuonyesha Lwembe ni kwamba, uko makini kulinda Neno, kusiwepo kuongeza au kupunguza-which is excellent spirit brother BUT, YOU ARE DOING IT VERY POORLY! Huo sio umakini ktk Neno bali ni kutokua na uwezo wa kufafanua Neno na bado ukabaki ktk msingi wa Neno therefore, kwa mantiki izo za Paul kuwaita wale vile, ni sahihi ku-conclude kua alikua Baba yako kiroho/Kiimani na kusema ivyo bado ni Biblical(kina fall within the truths of the Book hata kama haijaandikwa live! Kitu kibaya ni kile hakijaandikwa live na kisha kiwe unbiblical-out of the Bible facts.

  Ivi kweli hamuelewi wewe na Sungura kwa hilo? Mbona simple tu!

  Ati umesema kuhusu Utoaji Zaka kwa sheria ya rohoni ni vema….’’umng’ang’anie Mungu mpaka akupe ufunuo wake, kuliko kujifanyia tu’’

  Jibu:! Don’t unnecessarily overspiritulize straight things! Kutoa, unatoa tu si kuomba tena mpaka Mungu akufunulie! Afunue nini tena! we vipi! Kila kitu kimeshafunuliwa kuhusu Utoaji ktk AJ, kanuni ni kwa kupenda, moyo uliyokusudia, kwa furaha na raha yako na Bwana hupelekea ivyo vyote na yote kua halali ilimradi kanuni iyo imezingatiwa, sasa unataka Ufunua gani tena? labda ufuniko ambao huo hakupi Baba wa Mbinguni bali ni ‘rijamaa’!

  Kwamba, ‘’Anayekimbia kulipa huhesabiwa kuwa Mwizi, lakini si anayekimbia Kutoa!
  SWALI: So anayekimbia/kataa Kutoa zaka anaitwaje? Mwekezaji au Fisadi la Kiroho?

  Press on.

 17. Sungura,

  Ulisisitiza kua, ‘’Umeniuliza kitu kidogo tu cha msingi kuwa, tuambie Adhabu ya kutotoa/kuchelewa kulipa fungu la kumi ni zipi na kifungu kipi cha maandiko’’

  Jibu: Usiwe unaniuliza mambo ambayo aidha nimeyajibu moja kwa moja au nimegusia ki- mantiki directly or indirectly ili mtu apate/ang’amue mwenyewe jibu. Hii inadhihirisha kua husomi comments zangu kwa wengine bali zangu kwa zako tu au unaposoma, hutaki kuelewa au huzingatii details au unasoma yale tu unayotaka kupinga au kupata ground ya kusema yako. Rudia kusoma comment zagu kisha kama hujaelewa/ridhiki, uliza tena, otherwise, sijibu tena ili ufanye assignment yako kabla hujanibambikiza tasks mimi.

  Hii fasihi ya Kitenesi’ na Mpira kwa maana ya hoja za mezani na vitini- nani ana ufinyu wa kuidaka iyo? afterall is not a big deal and am not interested either! Ungesema tu moja kwa moja kuliko kumaliza space tu hapa!

  Hii uliyosema ni ….hoja chipukizi ya kumwita mtu baba wa kiroho, SIHITAJI KUJIBU/FUNDISHA TENA, nayo nimeshaongea mengi, why unakua kama hauko hapa au umataka kupoteza muda/space tu kwa nyakati nyingine? Mimi nimeshasema vya kutosha tena vema sana Biblically kuhusu ilo, wewe kama unadhani una jipya sana au una kitu bora kunizidi, kiweke hadharani hapa ili tuki/nikione kweli kina uspesheli /ufahamu wowote wenye kilo au yale yale tu-porojo na kuzugisha mambo ambayo yako straight na mema tu! Kua na Baba wa Kiroho au wa Imani au Mtu Mungu aliyemtumia kukuzaa ktk Imani, ni jambo la kujadili weeee na kwamba ni ishu isiyoeleweka kweli Biblically?mambo mengine mepeeeeesi, ya ukweeeeeliii na yaki Bible yet mnaleta politics na Lwembe! Namna gani nyie!!!!!!!!!

  Press on.

 18. SAMAHANI,

  Katika kipengere cha mwisho, nilitaka kisomeke hivi ifuatavyo:-

  Sheria imekamilishwa kwa njia ya Kristo Yesu, naye Kristo Yesu Neno linasema yupo pamoja na watu wake hapa duniani hadi mwisho, na kwamba yumo ndani ya watu wake akiwaongoza, kuwafundisha, kuwaelekeza, kuwalinda dhidi ya mwovu kwa jinsi ya Roho, sasa haingii akilini Mtu anapoyatila shaka na kuto yaamini MATENDO YA MITUME!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 19. Wapendwa naamini hamjambo,

  nimeipitia michango yote kwa utulivu, kila mchangiaji amesema vizuri kwa upande wake. Wapo waliotaka kuonyesha umahili wao katika Neno la Mungu, na wapo walioonyesha wanachokijua moja kwa moja dhidi ya swali, na wengine walisimamia mafundisho ya wazazi wao wa Kiroho nk, Nilimwelewa Nico, alipouliza, “Adhabu ya kutotoa/kuchelewa kulipa fungu la kumi ni zipi na kifungu kipi cha maandiko? “NISAIDIENI KUJUA ADHABU YA KUTOTOA KIKUMI…..”

  Baadhi ya wachangiaji walisema kwa kifupi kama ifuatavyo:-,

  EDWIN SELELI 17/09/2013 at 12:29 AM, akakwepa kujibu kwa kumtega muulizaji ili ajijibu,
  “Nico…(a) Unadhani MUNGU anafurahia kuyafanya mambo yake yote kwa ujumla kwa ulegevu ilihali ya kwetu binafsi, tunafanya kwa bidii zote na kwa wakati?..”

  EDWIN SELELI siku ya tarehe 17/09/2013 at 4:25 PM, akaachana na Muuliza swali, akawageukia Amin na Wilson, kwa Maswali:(a) Kwa iyo, atoe au asitoe?……..”

  Boniface Evarist mnamo18/09/2013 at 9:24 AM, anamjibu Nico, kuwa Adhabu ya kutotoa Zaka ni KULAANIWA mhusika na MUNGU, alinukuu, MALAKI 3:7-11

  sungura tarehe 18/09/2013 saa 6:23pm, akiungana na muuliza swali, akasema na Evarist na kumtahadharisha kuwa, asiende faster kwenye kuainisha adhabu kwanza, bali ajipe nafasi kwa kuzipitia mada zilizotangulia kuhusu suala zima la zaka

  Naye Edwin Richard, 18/09/2013 saa 6:37pm, akilinganisha kitendo cha kutoa Zaka ni kumpenda Mungu, na kwamba sadaka ni kifanikishio cha kazi ya Mungu Duniani, akanukuu, Marko 12:30-”

  Sungura mnamo katika 18/09/2013 saa 7:24pm, akarudi tena, safari hii anamtaka Edwin Richard kuwa, “…..Sioni kama umejibu swali la mleta mada, lakini kwa maelezo yako hata wewe pia ningekushauri upitie mada ya zaka kama nilivyomshauri Evarist

  Naye EDWIN SELELI mnamo 18/09/2013 saa 7:36pm, akakubaliana na Edwin Richard, kwamba amemjibu Nico vema hata akasema kwamba, “Nakubaliana na wewe kabisa na labda ninaweza kukukaribisha ktk mada inaitwa ‘’Kutoa zaka kila mwezi au la! Ashukuriwe Roho Mtakatifu kwa kua kule tumejadili sana na nilifundisha somo zima kuhusu UTOAJI… Specifically Zaka….”.

  Amin Nguluma mnamo 17/09/2013 saa 0:26am, pamoja na mambo mengine, akasema;Hakuna adhabu yoyote ya kutotoa kikumi kwa Mkristo

  Wilson, mnamo 17/09/2013 muda wa 2:07pm, naye akasema kama Amin kwmba,Hakuna adhabu yoyote hivyo ni wazi kikumi hakina umuhimu kutoa ila kuna watu wanalazimisha sana kwa matakwa yao binafsi……………………”

  Naye Mpendwa wetu toka Ulaya aitwaye Rova Olombi siku ya 17/09/2013 saa 9:35pm, akaonyesha kutatanika, aamwamin nani kati ya “Wazazi wake wa kiroho wa uropa wa Afrika” na kuuliza kuwa,
  “…SWALI NI IYI MIMI NAISHI APA ULAYA EUROPA…… MIMI MOJA YANGU YA KUMI NIKIPATA NA TUMAKA AFRIKA . MWALIMU ANASEMA NI VIBAYA LAZIMA KULETA APA TU . SIO KUTUMA FASI ZINGINE . NA MIMI NATUMAKA KWA BABA YANGU YA IMANI . SIJUWE KAMA NAFANYAKA MAKOSA KUTUMA AFRIKA… .. NAOMBA USAIDI KWA SWALI IYI…….”

  Naye Mr. Milinga tarehe 01/10/2013 saa 4:22pm, akapongeza tu wachangiaji wote, na kuuliza maulizo manne na moja ya maulizo hayo ni “1. Kama Zaka ni sheria kwa wapendwa wa Agano Jipya ni kwa nini Mtume Paulo na Mitume wenzake hawakuwahi kutaja Zaka katika Mafundisho yao yote?….. ”, ambapo pamoja na mambo mengine, EDWIN SELELI mnamo, 02/10/2013 saa 6:11pm, alimjibu Mr. Milinga swali kwa swali, kwa kirefu na kwa uzuri.

  Tumaini Nelson katika,01/10/2013 mda wa 8:17 anampongeza Seleli kwa uvumilivu na ni mwalimu mzuri, anashangaa kwa nini watu wasikubariane tu na kutoa zaka!

  Sungura mnamo 02/10/2013 saa 12:17pm, anasema na Nelson Tumain,si lazima kuto moja ya kumi unaweza toa kiasi chochote tu na si kwa lazima!

  Ck Lwembe mnamo 02/10/2013 saa 4:52pm, akimgusia Milinga, anasema kuwa, “Nimeliona jambo moja la kusikitisha, kumbe watu wengine hawajui hata Zaka ni nini!….zaka, matoleo, sadaka, changizo na vyote… wamevirundika katika fungu moja!… Mungu si masikini na wala hana shida ya chochote kile, kwahiyo…. moja wapo ya matoleo yanayotufunza Wajibu ni toleo la Zaka, FUNGU LA KUMI……ukileta zaidi au pungufu, maana yake aidha hauijui Sheria inayoliongoza jambo hilo au ni mjinga wa kujitakia au mwizi!…,tunapaswa kuyasikiliza Maandiko….. Zaka inayotolewa kwa… Sheria, iliondoka na Sheria yake…. Jambo.. bora… manufaa zaidi iwapo litafanywa kulingana na misingi inayoliongoza!
  Wakristo wengi wanajaribu kuyavusha mambo yaliyokwisha, kutoka Agano la Kale, yale ya Torati, na kuyaleta katika Agano Jipya. Bali hilo ni kinyume…. Mungu alikwisha yafunga katika ujio wa Kristo, pamoja na Zaka,…Kristo ndiye MWISHO wa Sheria, nayo Zaka iliyo sehemu ya Sheria hiyo inapaswa ikome na Sheria yake iliyo izaa!…”

  Baada ya kunukuu michango michache hapo juu, naona nisiendelee kuiweka mifano mingine zaidi, kusudi langu katika kufuatilia mmoja baada ya mwingine katika wachangiaji, ninataka kuonyesha tu kwamba Watu wengi husimamia maelekezo ya kimapokeo tokana na walimu wa thiolojia ambao kwa kiasi kikubwa husimamia zaidi Dini zao, ambazo kwa kweli ni Taasisi za Kidunia tu!

  Kanisa limekuwa NJE – NDANI bila kujua, na kutokana na kutokujua huko, kanisa hilo limeamini uongo na hata lenyewe limejua kuwa “KWAKWELI TUNAISHI BILA KULIKUBALI AMA KULIKATAA NENO LA MUNGU, LAKINI POTELEA MBALI!” Kwa sababu, ukilifuata Neno la Mungu kama lilivyo bila kuingizaingiza Tafsri za kithiolojia, litakuondoa na mkukutenga kabisa na wapendwa wako wa kishirika! Hapo ndipo, utaona kuwa Neno hili ni upanga wa ajabu unaoweza kukata kote na hata kutenganisha nafsi na chochote kile unachokipenda na kukitegemea sana! La kini, hasara ambayo inategemewa kwa asilimia zote kutokea kwa kanisa la namna hii, lililo NJE – NDANI kiimani, ni “KUTAPIKWA” na kwakuitazama michango ya wapendwa iliyopo hapo juu, inathibitisha mgawanyiko mkubwa wa kweli ya Neno la Mungu na mafundisho ya uongo ya shetani, kwa hiyo
  TAYARI KANISA HILO LILISHATAPIKWA, na mtapikaji anasema, yeye si kama Mbwa kwamba atayarudia matapishi yale! Na kama mtu hataki kuiangalia na kuiamini ile kweli ili awekwe huru, basi kwisha!

  Kama kweli tunakubaliana na Neno kwamba, Yesu ndiye Neno la Mungu (Uf ) basi haupo ubishi kwamba alichosema ndicho kifuatwe. Yesu alichagua mitume na kusema kuwa, “ATAKAYE WAKATAA NINYI AMENIKATAA MIMI” lakini kupitia hiyo michango ya wapendwa hapo juu, wapo wengi zaidi wanao WAKATAA MITUME na kusema kuwa, walifanya mambo yao wenyewe kwa kufuata au mila, desturi am utaifa wao, hivyo hawakufanya mambo yote kama walivyoelekezwa na Yesu! Maneno na mawazo kama hayo ndiyo yanayomtia KICHEFUCHEFU mwenye kutapika ili atapike! Kila siku Neno la Mungu hufanyika CHENGA YA MWILI kwa kila atumiaye AKILI, kwakuwa akili ni mwili haziwezi kumtafsri Mungu na Hekima yake. Kupagawa huku kwa kanisa hili kunaoneka wazi wazi kwa misimamo ya wanamadhehebu wanapopingana na Neno. Hebu ona, “Yesu akasema, wabatizeni wanaoami kwa Jina la Baba, la Mwana na la Roho mtakatifu” (Mark), Mitume nao wakasema “wabatizeni wanaoamini kwa Jina la Yesu ” (Mdo. 2:38) na waliokutwa wamebatizwa tofauti na fundisho la Petro walibatizwa upya! Jambo hili nimezusha mjadara na kusemwa kwa Bidii nyingi na wapendwa kuwa “MITUME WALIJIFANYIA JAMBO HILO KIVYAOVYAO, SI MAELEKEZO YA YESU!” Wamepingwa chenga ya mwili, unaona? Ukitumia akili lazima “Utie kichefuchefu tu” na sauti ya Neno, utaisikia kama sauti ya Muungurumo, Mungu ni Roho, huishi ndani ya mwamini kwa jinsi ya Roho, husema nakutenda kwa jinsi ya Roho, ukija kimwili lazima upigwe chenga tu huna jinsi. Hebu ona maongezi ya Eva (kabla hajaanguka) na Nyoka,, (Mw.3:2-3)

  ” 2Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani. ’’ pointi yangu ipo katika sentesi “‘….Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani.”Hebu ona alivyoagiza Mungu,(Mw.2:16-17) “16BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu akamwambia, ‘‘Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani, 17lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.’’ Ukilinganisha maelezo ya Eva kwa Nyoka na Maagizo ya Mungu kwa Adamu, utaona kama yanatofautiana, Eva anasema wamezuiwa hata kukusa tu matunda yale wasije wakafa! Lakini tunaona maelekozo ya Mungu hajatamka Neno “Misguse” Je, unaweza kusemaje hapo? Eva alijitungia mwenyewe neno lile “msiguse”? Lakini Biblia inatuambia kabla ya kula lile tunda Eva alikuwa hajawa mtenda dhambi, kwa hiyo hakudanganya wala kujitungia neno hilo ‘usiguse’! Neno la Mungu ni Roho, kama alivyo yeye kuwa ni Roho na wanaomwamini yeye humwamini katika Roho. Neno la kiroho heleweka na watu wa Rohoni tu. Kwa hiyo jambo kama hilo ndivyo lilivyo, litabaki hivyo, ni Neno la Mungu mwenyewe na kwamba litabaki kuwa ni “chenga ya mwili” kila mwenye kujaribu kumtafsri Mungu kimwili!

  Ikiwa shetani mwenyewe hakumbishia Eva kuwa Mungu hakuelekeza “kutogusa” matunda ya mti ule wa katikati, na akaamini kuwa hilo neno “MSIGUSE” “ALILOLISEMA” Eva lilitokana na Mungu! Inakuwaje, kwa wapendwa wanaposema Baadhi ya Maneno au mafundisho ya Mitume ni yao wenyewe na kuwa hayatokani na Mungu (Yesu)?! Mimi (si Mungu) nasema, Mtu anapowakataa ama kuwabishia au kuwa namashaka juu ya mafundisho ya Mitume ni “MBAYA” kuliko hata Dhambi yenyewe! Kwa sababu, dhambi ni KUTOAMINI Neno la Mungu, lakini Mtu asiyetunza Familia yake (Kuaminisha isiyo kweli vichwani mwa wana FAMILIA wa Mungu, ambayo mtu Fulani kapewa kuichunga iwe kama yake) ni Mbaya kuliko asiyea amini – yaani ni mbaya kuliko mtu mwenyedhambi, na mwenyedhambi ni SHETANI, maana Uzao wa nyoka ni nyoka, kwa hiyo ni MBAYA KULIKO SHETANI! Sheria imekamilishwa kwa njia ya Kristo Yesu, naye Kristo Yesu Neno linasema yupo pamoja na watu wake hapa duniani hadi mwisho, na kwamba yumo ndani ya watu wake akiwaongoza, kuwafundisha, kuwaelekeza, kuwalinda dhidi ya mwovu kwa jinsi ya Roho, sasa haingii akilini MATENDO YA MITUME!

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

 20. Seleli,
  Unanitishia nyau! Hahahahaha…!!!
  Unaniuliza, “A U SICK? Ni kweli I am sick, naumwa ugonjwa wa “Kuyapenda Maandiko” ndio maana flaw ndogo kama hiyo, kwangu ilipiga kengele kubwaa sana, nikakuona katika unafiki wako na nikakungojea ujidhihirishe zaidi kama ulivyofanya!

  Unaposema, ulisema “Baba yako Kiroho” ilikuwa ni katika context ya Paul, huo ni uongo tu vinginevyo ungenionesha na context ya Mt 23:9 ili tuijue tofauti ya hayo; maana Paul anaizungumzia nafasi yake kwa hao katika affection, hebu tazama hapa vizuri anachokisema:
  1Kor 4:14-16 “Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. Basi, nawasihi mnifuate mimi.”
  Na hapa tena:
  1Tim 1:2 “…kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani.”

  Hakuna sehemu yoyote ile katika vifungu hivi alipowafundisha hao anaowaandikia wamwite yeye “Baba wa Kiroho”, na wala yeye hajawahi kumwita mtu yeyote yule “Baba” katika jinsi ya roho! Kanisa la Kristo halina spirit ya kuitana “Baba wa Kiroho”! Tena hata capitalization unayoendelea nayo, ni kule kuendelea kujidanganya tu, maana nilikuambia kuwa “we both know it”, ndipo unapojifanya hujui unakuwa kichekesho! Ku capitalize kunachukua umakini zaidi kuliko lower cases, so its not accidental, “your actions are so loud I cannot hear your testimony!” Ulichokiandika kinatokana mazoea uliyonayo na kuyaishi, unapowa address “Baba Mchungaji” au “Baba Askofu” wako!!!!! Tena nilipokuuliza kuhusu hilo kuwa ni Neno la Mungu au maneno ya Paulo tu kwa wanae, nilitegemea utaniambia kuwa hayo mnayatumia, tena mmesogea mbele zaidi, kuliko alipowaacha Paulo, kwamba sasa hivi ninyi mnao mpaka akina “Mama Mchungaji” na “Mama Askofu”; badala yake unaniambia ,” Achana na mimi kama huna hoja! Aibu nyingine umevuna kuonyesaha uko shallow sana ktk Neno maana Paul hakua anamwandikia Timothy.”!!!! Kwahiyo, alikuandikia wewe Seleli?!!

  Asante kwa kunifundisha “sheria ya rohoni”:
  “Sheria ya Matoleo yote Leo AGANO JIPYA ni ile ya rohoni yaani Kutoa kwa hiari/moyo wa kupenda/kufurahi/kukusudia moyoni si kulazimishwa/kusukumwa na ufahamu wa rohoni wa Mtu mzima kiroho anayejua umuhimu wa kutoa kwa kazi ya Bwana/Watumishi na Watu wake”

  Je, huko KUTOA kwa hiari unakokufanya ukikutimiza KULIPA zaka kunakotakiwa ktk kifungu hicho cha Mt 23:23, huoni kuwa ni kujikanganya, na kulazimisha mambo nje ya Mpango anaoutaka Mungu? Mungu anapenda watu walio na Utii, ndio maana ni vizuri kulifuatilia jambo mpaka uwe na uhakika nalo, yaani umng’ang’anie Mungu mpaka akupe ufunuo wake, kuliko kujifanyia tu! It looks weird, but the whole thing abt God is weird!! Bali Kutoa na Kulipa si sawa, Mungu huyatumia maneno yake kwa ufasaha mkubwa sana!!! Anayekimbia kulipa huhesabiwa kuwa Mwizi, lakini si anayekimbia Kutoa!

  Utanisamehe kwa hili, lakini ukweli ndio huo, kwamba unapolazimisha kutoa bila ya Ufunuo, ni rahisi sana utoaji wako kuishia kuwa kama wa Kaini, which is a waste!!!

  Gbu my brother!

 21. Seleli;

  Nilikuuliza kitu kidogo tu cha msingi kuwa, tuambie Adhabu ya kutotoa/kuchelewa kulipa fungu la kumi ni zipi na kifungu kipi cha maandiko.

  Nashangaa umejifanya kama hujaona hicho kitu. Nipe jibu, maana hiyo ndiyo hoja ya msingi.

  Swala la kitenesi na mpira, ni ufinyu wako tu wa kuelewa fasihi. Nini hapo unachokiita taarabu? Simply ni msemo wa kifasihi wenye kumaanisha hoja ya msingi (mpira), na hoja zilizo nje ya hiyo hoja kuu( ndio kitenesi).

  Hoja ya msingi ni adhabu ya kutolipa zaka ni ipi, na hoja chipukizi ni kumwita mtu baba wa kiroho.

  Sasa sijui ni nini ulichokiita taarabu hapo.

  Tafadhali jibu kwanza swali hilo la adhabu ya kutolipa zaka ni ipi,kisha tuendelee na hilo la kumwita mtu baba wa kiroho.
  Maana naona unakwepa hilo swali la msingi na kuongea maneno mengiiii yasiyohusika sana hapa.

 22. Lwembe,

  Ati unasema…’’Nilijua utakikimbilia kifungu cha Paulo’’ …..khaa! A U SICK? Ulitegemea ninyanyuke na mistari ya Mtume Mohamed au Mtume alshababuibui? Huyu vipi uyu!

  Nimesema ivi kuonyesha alivyosema Yesu kua tusiite Mtu Baba duniani- Mt 23:9, context yake ni tofauti na h ii ya Paul…1Kor 4:15 “Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna Baba wengi…”

  Sasa wewe ukajibu kwa kuniambia nimeweka capilization kwa mimi kusema..’’Baba wa kiroho…kisha unasema ..’’we both know it acha janja! WHAT ARE YOU TALKING ABOUT boy? huyu vije jamani! we ukoje na ufahamu wako?

  Umeuliza hilo ktk 1Kor 4:15, ni Neno la Mungu au maneno ya Paulo tu kwa Timotheo na si “for past, present and future generations”?

  JIBU! Achana na mimi kama huna hoja! Aibu nyingine umevuna kuonyesaha uko shallow sana ktk Neno maana Paul hakua anamwandikia Timothy. Pia Kama kila mmoja wetu anapaswa kua na Baba yake ktk imani/aliyemzaa na kumlea kiroho basi Neno hilo lafaa kwa wote past,present and future.

  Kuhusu Ole ktk hili andiko- Mt 23:16-17 kama ina msg na kwetu pia, si Mafarisayo tu, umejibu pumba! Ivyo nahesabu umechemka ivyo, usinichezee mie ktk game hii, nina moto!!

  Nilikuuliza swali hili SERIOUS.. “Je, unatoa Zaka leo ktk sheria ya rohoni au hutoi?” Ukajibu pumba tena kua….’’Umeanza kujitungia mambo, hii ndio sheria gani ya zaka? Acha usanii!

  My response: Sheria ya Matoleo yote Leo AGANO JPYA ni ile ya rohoni yaani Kutoa kwa hiari/moyo wa kupenda/kufurahi/kukusudia moyoni si kulazimishwa/kusukumwa na ufahamu wa rohoni wa Mtu mzima kiroho anayejua umuhimu wa kutoa kwa kazi ya Bwana/Watumishi na Watu wake

  Sasa swali tena: JE WEWE UNATOA ZAKA kama moja wapo ya matoleo KWA SHERIA IYO AU HAUTOI AND WHY? Jibu hilo swali tafadhari, stop joking, mimi nipo kazini/hudumani hapa imara kabisa.

  Hakuna nachoweza toka kappa kwa chako chochote wala huna higher standards ambazo mimi naweza ona giza mbele zako/yake kutoelewa, huo ni uzushi na utani. Wewe unajua! ufurukuti na ukifurukuta, unatokota mbaya, nakubana mpaka unakua mwepesiii hadi unatia huruma maana unajikuta unashusha CV au ‘’P’’ .Kila ukinyanyuka, unashusha! Pole Kaka lakini ndio ivyo!

  Press on

 23. Sungura,

  Umeuliza: ‘’Seleli nini ‘context’ ya maneno ya Yesu kuwa msimwite mtu baba duniani?
  Jibu: Nini context ya maneno ya Mungu kuhusu kuwaheshimu BABA na MAMA yako… na ya Paul kua Wana waalimu wengi lakini hawana BABA wengi walio wazaa?

  Hii sentence ya mwisho, naona umeimba taarabu na mimi naimba pambio za kanisani so kindly drink it by yourself this thing…’’Hili swali ni kitenesi wala si mpira, kwa hiyo usilete maneno mengi sana. Mpira ni adhabu ya kutokulipa au kuchelewa kulipa zaka’’

  Press on

 24. Sungura,

  Unajua kuna wakati tunatakiwa tuyaamini Maandiko katika yanayotufundisha.

  Seleli alikwisha kiri kuhusika na Mt 23:23, kwahiyo hakuna namna ambayo ataweza kuyaruka Maandiko hayo, lazima ALIPE zaka yake ya “mnanaa na bizari na jira”; hawezi akatoa zaidi ya hayo, hizo kelele zake ni za Kifarisayo tu!

  Na kwa vile ni Mfarisayo wa leo, basi lazima achanganye mada kwa kutokuyaelewa Maandiko maana Mungu alisema hao ni vipofu!

  Lakini endelea kumpa “Eye salve” huenda atapona!!!

  Gbu!

 25. Hahahahahaha…..Seleli!

  Nilijua utakikimbilia kifungu cha Paulo, kwahiyo nilipokuandikia nilicheeeka sana nikikusubiri!!! Unajua, ukiishamjua mtu kuwa ni mnafiki, you can always tell their next move!!

  Katika Biblia Maandiko uliyoyanukuu yameandikwa kama hivi: 1Kor 4:15 “Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi…”
  Halafu Mt 23:9 “9 “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.”
  Sasa angalia ya kwako: “… and Baba yako Kiroho?” umeiona capitalization yako? it is not accidental, we both know it, acha “janja’! Pia nikuulize, hilo ktk 1Kor 4:15, ni Neno la Mungu au maneno ya Paulo tu kwa Timotheo na si “for past, present and future generations”?

  Kuhusu hayo mengine, ninaiamini kabisa kauli yako kwamba, “…YAANI NAKUAMBIA KWA UPENDO, NIMETOKA HEWA!” hii ni kweli tupu, maana hata mimi nimekuona ulivyo toka kapa! Hilo ndilo jambo linalonifanya NIISHANGAE sana Injili, hapo Maandiko yanapochukua mwili, na kuwa hai katikati yetu!

  Hebu nawe yatazame haya Maandiko uliyoyanukuu yanavyochukua “mwili” leo hii, si huko nyuma yaliponenwa, hapana, LEO HII! Mt 23:16-17
  “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga. Wapumbavu ninyi na vipofu…”

  Kuhusu Andiko hilo unasema: ““Swali/Maelezo: Akiwapa Ole hao, je sisi Ole hiyo haituhusu? Kama haituhusu kwa hiyo tuape kwa hekalu? Why not? kwa kua si hilo Neno anawaambia hao siyo sisi? YOU SEE MY POINT”” Yes sir, I see a blind man, exactly like the scriptures said, blind like a bat!

  Kama jibu lako lilivyo, ni kweli kwamba hayo yanakuhusu wewe na wenzio mlio katika ukiri huo, mimi nilikuambia kuwa hayawahusu Kanisa! nikakuambia kuwa kabla ya hotuba hiyo ktk Mt 23, Kanisa, wale wanafunzi WALIFUNDISHWA jambo hilo la kuapa kikamilifu nikakuwekea maelezo haya na nukuu zake, ngoja niyapaste tena, ingawa hayakuhusu na ndio maana unatoka kapa na kung’ang’aniza watu waape, ukiwaondolea ufunguo wa maarifa wasiingie: (MT. 5:1, 2, 33, 34, 37)
  “”Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, … Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; … Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.”

  Umeona sasa kwanini nakuambia kuwa hizo “Ole” na hayo mengine hayatuhusu? Sisi huyapata mafunzo yetu katika faragha, ninyi wa mikutano ya nje hamuwezi kuyajua mambo ya ndani, mnabaki na “NDIYO na HAPANA” zenu zinazo toka kwa yule mwovu all the way!!!””

  Kuhusu maswali niliyokuuliza, kwa wewe kukosa majibu ni sawa kabisa, mimi nimekuelewa vilivyo, maana utajibu nini kwa kitu ulichotoka kapa?

  Hata swali uliloniuliza limenifanya nicheke zaidi, “Je, unatoa Zaka leo ktk sheria ya rohoni au hutoi?” Umeanza kujitungia mambo, hii ndio sheria gani ya zaka? Acha usanii!

  Kuhusu ku “raise standard”, ukweli ni kwamba ninasita, maana hii ninayoitumia ni ile ya chini kabisa ya chekechea ambayo inakutoa kapa, sasa nikipiga mbawa kuinuka, si utanikimbia ukiyaona makucha!! Hebu tafuta “Eye salve” upone!!

  Gbu!

 26. Seleli nini ‘context’ ya maneno ya Yesu kuwa msimwite mtu baba duniani?

  Hili swali ni kitenesi wala si mpira, kwa hiyo usilete maneno mengi sana. Mpira ni adhabu ya kutokulipa au kuchelewa kulipa zaka.

 27. Sungura/Lwembe,

  Sungura, umechoka! I can c it. Hii game/flow imekueelemea. Tatizo una maneno na vijineno vyako vingi kuliko maneno yako yanayoshibishwa na Neno la Mungu au Maneno ya Mungu kabisa live….Umenipata statement iyo? nimeirudia sana. Ndio maana wewe kuprevail ktk mjadala huu na mimi wakati natumia ‘once for all truths and authority’’ yaani Neno la Mungu hai kwa halali na hekima yote, si rahisi! Huwezi kulishinda Neno na huwezi kunishinda mie mtumiaji wake, huna kitu kwangu to be honest. Mengi nimekucha mbali, nimekutupa mbali mno, kubali tu.

  Kuhusu Musa kua nimeandika mengi yasiyohitajika, SI KWELI. Wewe ulimponda Musa kua alikosea kuwaita wale WAASI na kwamba ndio ndio sababu ya yeye kutoingia Nchi ya ahadi! Nikachukua hatua ya kukupa lecture ya huduma ya Musa na changamoto zake na jinsi mara 2 zilizo nzito sana, aliwaombea kwa Mungu msamaha wakati Mungu alipotaka kuwafutilia mbali na kwamba japo walimchosha na Musa yet aliwabeba kama Baba na Mchungaji wa moyo kwelikweli. Kukuonyesha maisha na huduma yake kwa watu wale ambao Mungu Baba na Yesu wote walishadokeza kua kweli walikua na shingo ngumu, nilitaka nikusaidie ukisoma somo hilo na maneno ya MUNGU niliyokupa, UFUNGE KINYWA CHAKO CHA UROPOKAJI AGAINST MOSES KAMA ULIVYOFANYA KIENYEJI, Nilikusaidia uwe makini una-state nini maana mbele ya Neno na wala Neno kama mie, UTAPWAYA tu Sungura tena kila mara. Ulimuonea/kumvunjia heshima Musa, ilikua ni muhimu sana kukupa CV yake tamu ili utubu vema.

  Pia umetia aibu kubwa na imedhihirisha maneno yangu kua kweli una maneno na vijineno vyako kwa wingi si Neno na kua your Bible IN you is very small, uliposema Musa hakuingia Canaan kwa kua aliwaita Waasi watu wale Mungu aliowatoa utumwani! Ndipo pia nikakupa ukweli wa Neno-Hesabu.20:1-13 unaoonyesha wazi kwa nini Musa alikosa kuingia na kisha nikakupa shule nzito ya maneno yangu yaliyojazwa maarifa ya Neno la Mungu kua , usijifanye una huruma na rehema sana kwa Wana Israeli wale kumzidi Musa ambaye aliwahi hata kumwambia Mungu yeye afutwe toka kitabu chake ili Kondoo zake wapete na pia nikakuambia Mungu Baba mwenyewe alishataka kuwafuta mara 2 kisha aanzishe Taifa jipya kupitia Musa, kubwa na lenye nguvu kuzidi lile, yet Musa akadrop ile ofa na hata tena akawaombea msamaha mzito na jamaa wakasave. Navyokujua mpaka sasa ubinafsi na choyo uliyonayo ktk Utoaji naturally kama wewe kisha tatizo kubwa lako hilo la kiroho linakua worsen kwakua linatiwa moyo na roho kali iliyokupiga roba matata sana kukunyima fursa ya kupenda Utoaji, hiyo ofa ya wengine wafutike, ungeiramba Sungura, ili uukwae uanzilishi wa New Nation.

  Kuhusu Yesu kukataza msimuite yeyeto Baba duniani alivyochemsha Lwembe na sasa Wewe nilipomuuliza Sungura kama kweli yuko salama kwa Baba yake wa kiroho kwa kauli na tabia yake humu ndani, nimeshampa shule ya Neno Lwembe kua context ya andiko pale Yesu aliposma Tusiite Mtu Baba duniani, ni tofauti na context ya Paul kusema wana waalimu wengi but Baba ni mmoja au Mungu mwenyewe kusema ktk Kutoka 20:12..Waheshimu Baba na Mama yako…… soma post yangu kwa Lwembe, acheni kutia aibu humu ndani, kujishushaa ..’’p’’/ CV kijinga. Someni Neno, semeni Neno au semeni maneno yenu yet yanayoshibishwa na Neno. Pia kilichofanya mkosee tena Neno hilo la kudhani Yesu amekataa kwa wote na ktk yote kutoita Baba… ni kutozingatia hizi kanuni nayowafundisha kila mara MOJA, …2Timo.2:15c..’’KUTUMIA NENO kwa HALALI’’ na PILI, Col.3:16a..’’Neno kukaa kwa WINGI ktk HEKIMA YOTE’’……you see mnavyopwaya vijana?

  Kuhusu kujadili Utoaji wa Sadaka, sasa unaomba ruhusu ya nini kuanza kujadili? Tokea lini unaombaga ruhusu wewe kama si kuzidiwa na hoja na unapumulia mashine? Wewe mara ngapi unaongea lolote tena kwa vyovyote both majineno na vijineno bila hata kuwa-consult SG? Lini umekua na hekima iyo ya kujihoji kwanza na kuomba ruhusa? Usinidanganye hapa! UNA KITU KWANGU WALA NINI! Ndio maana nilisema kua kila mtu ana huduma/karama/namna yake ya kuhudumu na kufundisha Neno na Mungu ametupa neema tofauti, tukubaliane tu na kubariki ilo, tuache wivu mkali wa devo. Mmi Nikishaona mada, najua tu ktk kujadili, itafikia au kugusa mengi tu ndio maana mimi hupenda kotekote namely ktk mada but pia kuongelea mengine mengi yet muhimu ambayo in one way or the other, yana connect aidha directly au indirectly na mada husika.

  Nilichukua uamuzi wa kuleta soma la UTOAJI in general-ingawa liliombwa na mshiriki wa mjadala lakini pia nilijua kuweka msingi wa kitu kizima ni njema, inabaki tu tunapoendelea , kunyofoa na kujazilishia kama si kumodify. Nimekua natoa mfano huu kua Mwl efficient akiambiwa afundishe kuhusu ‘NGUVU YA DAMU YA YESU KWA MWAMINI’’, hatakaa hapo kwanza, atatrace/fundisha kwanza.. ‘’NGUVU YA DAMU YA MAFAHARI NA WANYAMA/VIUMBE WENGINE VILIVYOTUMIKA WAKATI WA AK KWA WATU WALE’’. Ni sawasawa na ‘’ZAKA’’ na ‘UTOAJI IN GENERAL. Therefore, ktk somo langu la Utoaji na later mijadala yetu kuhusu Zaka, tumeshajadili na kugusia Utoaji wa Sadaka.

  Labda niseme ivi, hata mkitaka kujadli kwa upya, endeleeni nami nitawanyemelea hatua kwa hatua ILA hamtavuka haya

  (A) Utoaji ni tabia kuu ya Mungu wetu ivyo na tuwe watoaji sisi wana wake na sisi vinginevyo

  (B) Utoaji wowote Agano Jipya namely zaka, malimbuko, changizo na sadaka nyingine nyingi ni halali na una baraka ili mradi si wa kulazimishwa au kwa matakwa ya sheria za kimwili bali kwa furaha/kusudio la moyo/maamuzi ya kiutu-uzima kiroho kujua umuhimu wa kutoa kwa kazi ya Bwana na umuhimu wa kujikatalia nafsi ili ya rohoni/ya Mungu yastawi

  (C) Kwakua Mungu amesisitiza ktk Neno lake kua heri kutoa, Yeye alimtoa Mwanae, Yesu mwenyewe alijitoa uhai wake then ingawa hatuna laana sisi tuliyo ndani ya Yesu lakini mwana wake yoyote akiacha kutii Neno hilo la utoaji au kua kama watakatifu wengie walivyokua watoaji na wakabarikiwa, basi atapata madhara ya tabia iyo kama vile ilivyo kweli kua mtoto wa Mungu ataathirika akipuuzia mengi ya Neno si hili tu la utoaji.

  (D) Mwamini yeyote anayetetea sana kutotoa na anayejali sana mambo yake binafsi, anayefikia hatua hata ya kutoa ushuhuda mbovu kwa Kanisa tena bila aibu kua hatoi matoleo fulani na kueneza moyo wake huo matata na wenye utata mwingi kwa wengine, nawahakikishia hatakua sawa maisha yake binafsi ya uchaji, kule Kanisani kwake si kondoo bali mbuzi na kwa Mchungaji wake na kazi ya MUNGU anapolelewa ni mwiba na majuto kwa Mtu wa MUNGU wake kusema ukweli

  Embu niambie baada ya hiyo shule, utakua na jipya kweli kuhusu somo la kutoa sadaka? Hamvuki hapo, huo ndio msingi, full stop, period.! Nasema tena wewe brother Sungura hamna kitu, umechoka! Una kitu kwangu, nimekuelelemea sana kwa hoja na teachings zangu za ukweli humu.

  Kwamba, nimeandika makala nyingi na ninakukopi wewe na kua labda ninakuogopa! Jibu ni kua ninapenda napo cover issue moja kwa mmoja, na najua mwigine anatatizo hilo hilo, basi nina mcc uko ili naye apone pia. Lakini pia kwa case yako, wewe ni almost beyond compare and repair, ivyo much attention kwako ni muhimu, ndio wanavyofanya madaktari kwa wagonjwa walio mauti-mauti maaana mahututi cha mtoto, wewe bro umecross iyo, Bwana akuhurumie tu.

  Kuhusu kuandika majina na kupewa lisiti baada ya kutoa Zaka, nilishasema sababu nzuri kwa nini baadhi ya makanisa wanafanya ivyo kwa nia/sababu njema kabisa namely Professionality ya Utunzaji fedha, Ku-meet mataka ya Banks kule zinapowekwa, kua reliable kukopa au kukopesha maana documentation matters there at financial institutions, kufanya biashara ili kuzalisha zaidi kwa kazi ya Bwana, demand ya wapendwa wenyewe kutaka kumbukumbu zao za Utoaji ili ktk maombi wanajua wanavyomung’ang’ania Bwana kwa reference Tangible not audible tu- eg maombi ya Hezekia ya Bwana Kumbuka hiki na kile-Isaya.38:1-3 au alipokufa Dorcas, wale waliokua wanalia, walikua wanaonyesha ushahidi tangible wa kazi yake-Mdo.9:36-43.

  KWA HIYO NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA NA BOLD KUA SI KWELI RISITI ZINATOLEWA KWA KUA NI NJIA YA KUTUWEKA JERA AU KULAZIMISHWA MAANA HAKUNA HATA MMOJA AMBAYE AKIACHA ,ATASHITAKIWA AU KULAZMISHWA, BADO INGAWA UTARATIBU HUO UPO, BADO WAPO WANATOA NA WENGINE HAWATOI NA HAWAFANYWI KITU, HATA WANAOTOA WENGINE HAWAFUTILII SANA KUPATA RISITI NA WENGIJE WANATAKA SANA…YOU SEE, SO YOTE YANAFANYIKA KWA UHURU NA NIA SAFI NA WATOAJI WAKO HURU…Mnapojaribu kuchora picha mbaya against ALL CHURCHES AND ALL WATUMISHI, ndio hapo hatuelewani na kwa kweli mtatoka jasho na mimi hata kama mko mia, nitawachambanga wote kabisa barabara kwa hoja za Neno, Maneno yangu ya maarifa toka Neno, ya akili, logic, realities, uzoefu, karama, huduma na God given grace mpaka muache uzushi na kibinadamu kibaya. Yaani hapa jamani mmefika na kumekucha ni mwanzo mwisho. Nampenda Yesu, kanitoa mbali, nampenda Mungu, kazi ya Bwana, kanisa langu, Mtumishi wa Mungu anayenilea na Watu wa Mungu na mwili wa Kristo in general . When it comes to God’s work, I love those are crazy yet clever.

  Kuhusu kuniponda na kunitukana kua nina akili ndogo kwa kuwang’ang’ania kua mtumie Neno la Mungu, ….acha kunitukana kua nina akili ndogo, si kweli, Bwana amenipa nyingi za mbinguni, Neno, mambo yake, ya huduma, Kanisa, Watumishi na za kichwani, aisee acha kabisa, wewe mwenyewe wajua, hutaki kukiri tu ila internally/privately jasho lakutoka na unakula kazi na kujuta kwa nini siku ya kwanza ulikosea step kunivamia kienyeji kwa kuniambia siko makini, ukidhani mie ni cheap chap kama wewe au hao unaowasumbuaga., Hapa ni break Kaka, mafuta iliyoko hapa juu yangu kwa neema ni mountaneous! Glory to God, kama wewe uko weak na mvivu kwa Neno basi kupitia mie, pata challenge na kuraise standards-ndio maana ya fellowship, umeona mwenzio na kitu kizuri, kuliko kuponda tu na kusaga kumbe unaumia na kuadmire, si ubariki tu kisha CUT or COPY and Past. Unanionea gele napoflow na kunukuu NENO pia najua kwa nini umeponda uwezo wangu Bwana amenipa huo mzuri…NI KWA KUA UNAABIKA MAANA KADRI NAVYOTUMIA NA KUTOA NENO KWA USAHIHI NA HALALI, UNAONEKANA MPAYUKAJI, HUNA NENO LA MUNGU bali majineno yako. Nitaendeleza moto huu mwanzo mwisho mpaka ujifunze kupunguza yako, usema ya Neno, hatuhitaji Taarabu Male Singera humu bali Men and Women of God with full Word and Holy Spirit to share HEAVENLY MANA.

  Nilisema ivi kua aidha TUMIENI/NUKUU KABISA NENO LIVE-Sura na Mistari au LITAMKENI bila sura na mistari AU tamkeni yenu but yaliyoshibishwa/ambukizwa/yenye elementS za Neno…ushauri mzuri sana huu nilitoa ili kupunguza maneno na vijineno vyenu kavu kavu au vitaarabu hasa wewe na Lwembe. Ilo nalo huelewi na kisha wanitusi kua nina akili ndogo! Mwe! Kweli umechoka bro.

  Yes it is about Qualirty not Quantity, nonetheless, when QUANTITY got QUALITY most of the time, its fantastic and blessings, oooh! alleluyah! Amen.

  Press on

 28. Lwembe,

  Kusema ukweli, nimejaribu kusoma kwa kurudia tene na tena makala uliyoandika, YAANI NAKUAMBIA KWA UPENDO,NIMETOKA HEWA! plz and plz and plz Lwembe nikuombe tena, yaani I am serious, rudia kusoma ulichoandika halafu kweli ukikuta kuna very serious substance, nita apologize! Yaani ni ajabu Brother you can spend such space kwa air!

  Kwakua sijaona kitu, usishangae ktk makala yako ndefu kweli, nimechomoka na vichache kama ifuatayo:

  Nakuuliza maswali machache tu ili unipate nilichosema kwamba Maneno ya Yesu hata kama akisema kuaddress makundi fulani, bado yanasababu nasi/ yanatuhusu kwa maana msg anayowaambia makundi fulani, msg iyo iyo ina msg pia kwetu. Mbona ni rahisi tu kuelewa.
  Mfano:
  “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; …Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake.” (MT. 23:16-22)

  Swali/Maelezo: Akiwapa Ole hao, je sisi Ole hiyo haituhusu? Kama haituhusu kwa hiyo tuape kwa hekalu? Why not? kwa kua si hilo Neno anawaambia hao siyo sisi? YOU SEE MY POINT
  Therefore, ukweli huo ndio unaweza kuapply hata ktk andiko la ZAKA la Mt.23:23 na mengine mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ambayo Yesu aliongea akiwa-address makundi fulani

  Ndio maana hata Yale yanayotuhusu sisi, pia makundi mengine yanawahusu, mfano: Anionaye Mimi amekwisha muona Baba au Mimi ndiye NJIA, KWELI NA UZIMA au Mfano wa Mpanzi na mengine mengiiiii alotuambia Sisi pia yana sababu/msg kwa wengine wote na as a matter of fact. yanawahusu WANADAMU WOTE past,present and future.

  Hivi kweli wewe na Sungura hamuelewi hayo nayowafundisha? BASI HAKUNA TUMAINI KWENU…MNAHITAJI MWL wa Neno toka sayari ya Jupiteri

  Haya maswali yako 3 chini, jijibu mwenyewe, ni minor and valueless ktk teaching yangu hapa, si kawaida yangu kuacha maswali maana mimi nawajibika hapa kwa dhati na siachagi jiwe juu ya jiwe lisiloondoshwa ILA kwa haya, nayacha, hayana/hamna kitu/tija brother.

  1: Kwamba ninyi mnakiri kuhusika ktk kifungu hiki ambacho kinazungumzia KULIPA zaka, nazo kauli zenu katika kulitimiza jambo hili zinazungumzia KUTOA zaka; Je, huu si unafiki mnaoendelea nao baada ya kuukiri?2: Je, mambo makuu ya Sheria, yale ambayo watangulizi wenu waliyaacha, ninyi leo mnayatimiza ilhali unafiki bado mnao?3: Upofu mlionao, umewatoka? Mkisema umewatoka, mmekosaje kuyaona haya?

  Kufuta maana ya maswali yako kuexist, nakuuliza swali moja tu hili tokana na hayo
  Je unatoa Zaka leo ktk sheria ya rohoni au hutoi?

  Kingine umenishangaza kweli nikasema sikukuonea kukuambia/challenge kua brother, you need to raise your standards ktk kuelewa Neno in order to make strong senses otherwise, unaleta vichekesho.

  Nimemuuliza Sungura kua kama kweli yuko sawa kwa Baba yake kiroho, ukaninukulia maandiko yanayosema..’’msimwite mtu yoyote Baba duniani! Jamani! UKO SAWA KWELI WEWE? context ya pale Yesu ALIPOKATAZA TUSIITE MTU BABA, ni sawasawa na context yangu? Yangu ni sawa na hii ya Paulo…1Wakor.4:15..Mnao Waalimu wengi lakini hamna BABA wengi maana mimi ndiye NILIYEWAZAA KTK KRISTO kupitia Injili

  Na kule nyuma AK mbona moja ya Amri ni ile ya Kuwaheshimi Baba na Mama yako ili siku zako zipate kua nyingi duniani-Kut.20:12

  Nadhani umeelimika sasa! Plz punguzeni maneno yenu tupu bali semeni maneno yenu but yenye Elimu/elemenets za Maneno ya Mungu au maneno ya Mungu kabisa live LAKINI PIA KUMBUKA GUIDANCE HII NASEMA KILA MARA-2Timo.2:15c-‘’’Kutumia Neno kwa halali’’’ na Col.3:16a-‘’Neno tunalotumia lazima liwemo kwa wingi ndani yetu lakini ktk HEKIMA YOTE’’.

  Press on.

 29. Haya Seleli,

  Tusiache mpira tukakimbilia kitenesi.
  Hii mada iko katika mfumo wa swali. Na mimi nimeweka bayana majibu yangu kuwa hakuna adhabu wala madhara yoyote ya kutokutoa, au kuchelesha kulipa fungu la kumi.

  Inavyoonekana wewe unaijua hiyo adhabu, hebu tuambie hapa wadau tuijue.

  Kumbuka swali linasema:
  ”Adhabu ya kutotoa/kuchelewa kulipa fungu la kumi ni zipi na kifungu kipi cha maandiko?”

  Haya tupe majibu mtaalamu wa kutoa zaka!

 30. Lwembe,

  Umejaribu tu kidogo kunyofoa vitu vichache sana kati ya vingi ambavyo Seleli hulopoka akidhani kuwa ni vya kibiblia, kumbe ni mapokeo ya dini yaliyo nje ya neno.
  Mfano wake ni huo wa kumwita mtu baba.

  Mimi huwa navipuuza kwa kuogopa kutoka nje ya mada. Yaani yeye katika akili yake msisitizo wake mkubwa wa kutoa ni kwanza kumpa mchungaji wake, the so called baba wa kiroho.

  Ndio maana imefika wakati sasa nimemwambia tuingie kujadili mada ya sadaka, lakini yeye anaona kuwa wakati tunajadili zaka ati ndio tulikuwa tunajadili sadaka.

  Huku ni kuyachukua mambo kienyeji enyeji na kirahisi bila kuangalia kwa makini biblia inasemaje kuyahusu!

 31. Ha ha ha a a a, Seleli.

  Hebu sema ukweli, unajisikiaje moyoni unaposoma makala za Sungura na Lwembe? Kama vile najua jibu utakalotoa, maana kwa sehemu kubwa nimeshaujua moyo wako.

  Kilichonichekesha ni kule kuona makala nne ndefu zote za jana zikiwa zimeelekezwa kwa Sungura ambaye Seleli mwenye akili sana namwona kuwa ni mtu mwenye kuandika makala zisizo na ‘substance’ ndani yake.

  Seleli nikiri kitu kimoja kuwa unanizidi,ni kule kuandika maneno mengiii yenye wingi wa mipayuko na uzandiki wa kidini,lakini wewe mwenye kuyaandika ukiwa umevimbisha kifua na tumbo kuwa umeandiko mambo yenye mashiko sana. Hilo unanizidi.
  ‘Congratulations’.

  Umeongea mambo mengi sana non-sense,kwa hiyo hata sintayajibia hayo kwa maneno mengi .

  Kwa akili yako ndogo unadhani kujua neno ni kukariri mistari na kuinukuu. Umechelewa sana brother. Hakuna watu waliokuwa wamekariri maandiko kwenye vichwa vyao kama mafarisayo. lakini walikuwa wafu wakubwa,na walimuua Kristo.

  Umeongea maneno mengi sana juu ya Musa ambayo hata hivyo si ya maana sana hapa, ni kwa sababu tu upungufu wako katika kuelewa nini unachotakiwa kusema. Katika hayo yote, niambie tu kitu hiki kifupi:

  Ni kosa gani alifanya Musa akakosa kuingia Kanaani?

  Kitu kingine ni hiki:

  Umekuwa mtu usiyeelewa kwa ufasaha katika mada hii kwa sababu ulishindwa kutambua kuwa hatukuwa tunaongelea utoaji kwa ujumla, bali zaka. Kwa hiyo muda mwingi badala ya kuongelea zaka wewe umekuwa ukiongelea utoaji kwa ujumla wake, na hii kwa sehemu kubwa ni kutaka tu kuonesha kuwa wewe ni mtoaji au una moyo wa kutoa kuliko wengine.

  Na ndio maana umejikuta unapata nafasi kubwa sana ya kumkufuru Sungura kuwa ana matatizo, ni mchoyo,n.k. Kumbe ni kwa sababu Sungura hakuwa anajadili utoaji kwa ujumla wake, bali alikuwa anajadili zaka. Seleli sijaongelea utoaji wa sadaka katika hii mada ya zaka, kwa kuwa nimefundishwa nikajifunza kukaa kwenye mada husika unapofaqnya ‘presentation’!

  Siyo busara wala kibiblia kujaribu kuonyeshana kuwa nani ni mtoaji kuliko mwingine,lakini inawezekana kabisa kuwa wewe Seleli hata si mtoaji kutuzidi sisi akina Sungura . Ninahisi wewe ni mtu wa kujipendekeza sana ili uonekane, mtu mwenye kupiga panda ili kila mtu kwenye kusanyiko ajue umetoa ngapi.

  Uchaguzi ni wako, niite majina na kunisemea maneno yoyote unayotaka na kujisikia moyoni mwako,maana hayatanigharimu mimi chochote, bali ni wewe mwenyewe utayafanyia mahesabu.

  Seleli hiki kiswali usiendelee kukikwepa: KWA NINI UKITOA ZAKA HUWA UNAANDIKA JINA NA KUPEWA LISITI, LAKINI SADAKA HUANDIKI?

  Halafu, kwa nini umenijibu kwa makala nyingi kiasi hicho,kwani unaniogopa?

  It’s all about quality not quantity!

 32. Sungura,

  Namalizia ile yako ivi:

  Ulinionya kua kuhusu Zaka, niwe makini kutoleta Kongwa na kudharau kazi ya Bwana ya kutukomboa iliyompandisha Kristo mtini.

  JIBU! Kilichompandisha Kriso msalabani ni MOYO WA UTOAJI for your info. Mimi nakupa Bible kama ilivyo au pia maneno yangu ya fafanuzi na ufundishaji yaliyojaa Maarifa ya Neno, si wewe ya kikwako-kwako tuuu. Alisema mwenyewe ivi…Yoh.15:13- ‘’ Hakuna upendo Mkuu kuliko huu, wa Mtu KUUTOA uhai wake kwa ajili ya rafiki zake

  Nadhani in this case na in this topic, JESUS IS MORE INTERESTED WITH MY TEACHINGS AND HEART THAN YOURS ivyo usijipendekeza kwa Mtu Mtoaji kama huyu wakati unavunja moyo wa kutoa kwa Watu. He is interested with you on other issues but not this one I guess correctly!!!!!!!!!

  Umesema bila aibu kua…’’Zaka mimi nilishakwisha kukwambia kuwa huwa silipi na sina laana yoyote. Na hakuna mchungaji wala mtume wa kunilazimisha’’

  JIBU: Kwanza acha uzushi brother, husikii! Usikuze mambo kua Wachungaji au Mitume wanalazimisha kama vile ni kila sehemu .Tunao watumishi wa dhati wa Mungu na makanisa ya dhati kabisa na washirika wa dhati kabisa ambao hatuna noma yoyote Kutoa, ni mamluki tu ndio wanaoweza ingizia Watu mioyoni kitu iingine, ACHA HAYO, haufanyi kazi ya Bwana kwa maana iyo, una shida brother, mi nakwambia! utakua hauko ok kwa angle nyingine kiroho !!!!!!!!

  Pia tumekumaliza ubishi na ubinafsi wako wa kubania ela zako, TUMEKUBALIANA NA NI KWELI TUPU BIBLICALLY KUA ILIMRADI SHERIA YA ROHONI INAZINGATIWA namely kwa moyo wa kupenda/furaha/hiari/raha yako na Bwana, thamani unayoijua ya kazi ya Bwana, MATOLEO YOTE SAFI NA YANABARAKA. Sasa unalazimishwa na nani! NAONA HUNA HOJA, ushachoka bro, uko nyang’anyang’a!

  Kwamba….’’Ushuhuda wako wa kabla hujaokoka umenisaidia sana kuzidi kukujua u mtu wa namna gani Seleli na kwamba naweza kuzinyuka!’’ Kweli nyang’anyang’anya! Uzushi mtupu! Na pia elewa kila mtu ana flavour yake anavyoflow. Ni kweli nilitoa Ushuhuda kwa rahana furaha na udhani nilikua sijua kua mtanifahamu kwa undani nilivyokua! Ofcoz nilijua yet kwa joy nikamwaga vitu hadharani kwa raha zangu, mbona safi tu for His glory amen.

  Angalia pia husivyojua Neno bali maneno yako! Biblia inanijua kama kiumbe Kipya, ya Kale byebye…. But wewe unaashiria kua umenijua sasa jinsi nilivyo sasa kwa maana ya story ya nilivyokua Misri! Una maana hutambui Kazi ya Msalaba kwangu? Huyu vipi! Furu of your maneno not NENO.

  Umependekeza Tuongelee Utoaji wa Sadaka! Wa nini sasa? halafu kwani hajauongelea? TUMEONGEA SANA TU! Unadhani utakua na jipya Mtu mwenyewe ndio wewe? unataka upate room ya kuhalalisha ujanja wako kua unatoa Sadaka tu bali no Zaka, siyo? Nshakuona! Labda kama kuna muda wa kupoteza lakini tumeshaongea/gusia sana kua Zaka, sadaka mbalimbali, Changizo, Malimbuko..YOTE HAYA NI MATOLEO! Simple! Ni vitu vya KUTOA! Easy! Na vyote viko halali vikitoka kwa matakwa ya sheria ya rohoni! basi! Huna ujanja na hakuna jipya, tumeshayagusa na kwa kanuni ya rohoni, mambo yote safi kabisa.

  Press on.

 33. Sungura,

  Hata kwa Musa, bado umefanya kosa la uelewa wa Neno. umesema ivi…. ‘’Pole sana mwalimu kipofu wewe Seleli, mwenye kuchuja sisimizi na kumeza mende.
  Hujui kuwa hilo lilikuwa ksa kunbwa sana kwa Musa mbele za Mungu, na lilisababisha asiingie Kanani. Kuwaita waasi wale ambao Mungu amewatoa utumwani’’

  JIBU: Hujui Neno bali una maneno yako. Nisikilize upate ufahamu wa mambo ktkt Neno.

  Huwezi kumlaumu Musa kwakua aliwaita WAASI kama nyie mnavyoitwa na Biblia si Wachungaji kua ni WEZI, maana ndivyo walivyokua na ndivyo ulivyo wewe mwizi! Ni Mungu ndio kasema nyie WEZI-wala hakua na haja ya kuwabembeleza au kumung’unya maneno, yeye ni Mungu mwenye mbingu na uko hawakai wezi.

  Kauli yako hii against Musa kua… alikosea Kuwaita waasi wale ambao Mungu amewatoa utumwani’’, ni kama vile ya kiroho lakini kama navyokuambiaga kila mara, una maneno mengi si Neno la Mungu ivyo napoyapima unayosema na KWELI za Neno, nakuta pumba tupu Sungura.

  Huwezi kwa viwango vingi mno kumu-out-smart Musa na huduma yake, you are almost to non-existence tukilinganisha aliyoyafanya kwa BWANA na wewe Mtorokaji wa Zaka. Sasa angalia nakupa Neno na ujmbe wa Mungu kukuonyesha uliyosema kinyume na Musa ni vapour!

  Alichunga kundi ambalo hata Yesu mwenyewe anadokeza kua lilikua na shingo ngumu hadi kupelekea Musa kama kiongozi wa kiroho kuwatengenezea utaratibu (by-law) wa ku-handle mambo yao ya ndoa tofauti na original plan ya Mungu(main-law)-Marco.10:4-6.

  Ni kundi ambalo si tu Yesu alisema lilikua ni kazi kulichunga lakini Mungu Baba mwenyewe aliwahi kusema maneno ya uchungu kweli kuhusu ingia na toka yao mbele zake- Kut.32:9 Kut.33:33, Hesb.14:11,20-23,26-35. Biblia ya Kiingereza NKJ ilivyoweka ukweli huo ktk mstari wa 9 wa Kut.32, nimependa- inasema kuhusu hali ya kanisa lile la jangwani kwamba-‘’Nimewaona Watu hawa, KWAKWELI au KWA HAKIKA ni watu wenye shingo ngumu!!!-imagine mpaka Mungu achoke ivyo na kushangaa/kuumia hata kusema ‘’INDEED = truly/certainly/for sure/actually/ no doubt/ definitely/ ….’’these people are stiff-necked’’. Kuna nyakati walinungunika na kuongea maneno mabaya sana, Mungu hakuvumilia, akatuma nyoka wa moto kuwauma, wakafa wengi- Hesabu 21:4-9, wakati mmoja pia hasira ya Bwana iliwaka, moto ukawaka na kuwateketeza baadhi nje ya malango-Hesb.11:1-2. Pia waliwahi hata kutaka fanya mapinduzi, kumng’oa kihuni na kwa jabza Mchungaji wao Kiongozi Musa-Hesb.14:3-4 ili kusimika mwingine na kutaka KURUDI MISRI-(utumwani/dhambini/matesoni/kwa miungu ya kigeni kuitumikia!), yaani KUIFANYA PLAN YA MUNGU KUWATENGA=KUWAKOMBOA IWE NULL AND VOID!!!!!!!!!

  Si ivyo tu hata walishawahi kasirika mpaka Mchungaji wao kuona wazi wako karibu kumuua! (piga mawe) Kut.17:4, Hesb.14:10-( can you imagine that for a second? kwamba wapendwa wanaheuka kiasi hicho hata kuonekana wanaweza fanya kitu mbaya i.e. to KILL Mchungaji wao Kiongozi?!!!!!!)

  Mbaya kuliko yote ni wakati Mchungaji wao Musa amekawia toka ktk uweponi mwa Bwana mlimani, wao wakaona hamna haja ya kumngojea kupata maelekezo ya Bwana, wakaamua kujifanyia mungu kwa mikono yao wenyewe na hata kumu-infuence ‘Mchungaji Msaidizi’ kuingia ktk uasi na kufuru iliyovuka mipaka,akukubali kuwaongoza ktk mchakato wa kuumba ‘mungu ndama’ kisha kumuabudu, kumchezea na kumuimbia hata kumpa hadhi kubwa sana kua ndiye yeye aliyewatoa Misri wala si Mungu Yehova-Kut.32:1-6

  Kwa mwenendo wa Wapendwa hao mbele za Mungu na Mchungaji wao ,ulipelekea Mungu KUTAKA FANYA MAAMUZI MAGUMU dhidi yao -Kut.32:10= kuwafuta wote mara moja!! wana bahati/neema kua na aina ya Mchungaji ambaye kweli alikua ameitwa, mwenye mzigo na kazi ya Bwana ya Kuchunga watu wake na moyo wa kuwasaidia wafike Caanan( Mbinguni) ndio maana akawakingia kifua kwa kumuendea Mungu kihoja -Isaya.43:25-26- aka-mchallenge Mungu sana- Kut.32:11-14 mpaka ikamuingia/gusa na Yehova akaghairi kuwatenda kitu mbaya mno, mfano, ili kondoo wake wapone gadhabu ya Bwana wa majeshi, alimwambia Mungu kua yuko tayari yeye kufutwa toka kitabu chake Mungu-Kut.32:30-33.

  U-shingo ngumu wa wapendwa dhidi ya Mungu na Viongozi wao Kiroho- Mchungaji Kiongozi na Wasaidizi-Joshua na Haruni, uliendelea na ingawa kuna nyakati Mungu aliwasamehe walipoomba na kuombewa rehema na Musa, lakini wakati mwingine alisamehe na kuadhibu pia-mfano siku ile ile walipovuka mipaka ya uovu na kufanya kufuru ya kutengeneza mungu ndama, Mungu kupitia Musa aliamuru wana wa Walawi kuua ndugu, jirani na jamaa zao, wakafa watu alfu 3 mara moja!-Kut.32:26-28

  Wapendwa hawakuwahi kujirekebisha maana hata siku ile walipopata habari toka Wapelelezi 10 kuhusu Watu wanaoikaa Nchi wanayokwenda kuirithi kua ni ya majitu, wakaongea mbovu, Mungu akawapiga kwa tauni wakafa wale wapepelezi 10 walioleta habari na kusababisha kundi kulalamika-Hesb.14:36-37 na kisha akataka kwa mara nyingine kuwafuta wote kisha kupitia Musa, Mungu atengeneze-lizaliwe Taifa jipya kubwa na lenye nguvu zaidi. Ila Kama kawaida Mchungaji wa ukweli Musa, ingawa naye alikua anavurugwa na kuchoshwa na kondoo zake wale, bado ktk moyo wa ubaba/Uchungaji, alitoa hoja nzito mbele za Bwana kuwatetea Watu wake-Hesabu.14:11-20

  Bahati mbaya neno likatimia kua aonywaye mara nyingi akishupaza…..ivyo mwishowe Mungu akafanya sasa MAAMUZI MAGUMU!-Wale wote waliokua na vurugu safarini, waliomtesa Mchungaji wao, kumsumbua, kukufuru, kulalamika na kunung’unika , Mungu aka APA kwa nafsi yake kua, hawatairithi Nchi aliowahaidia na pia akasema atahakikisha wana wao ndio watarithi lakini wote kuanzia miaka 20 kuendelea isipokua Jushua na Kalebu, atahakikisha wanakufa wote jangwani, wana wao watazunguka jangwani miaka 40 wakati wakiwa wanachunga mifugo, wanapita uko na kule jangwani, watashuhudia maiti/mizoga ya Baba zao na watabeba uasherati wa wazazi wao walioufanya-Hesb.14:20-35.

  Ni Musa aliyesababisha Mungu kughairi kuwafuta WAASI hao ivyo wewe huwezi kua na huruma na kujali kuliko Musa mwenyewe na kali zaidi huwezi kua na rehema na huruma kuzidi Mungu mwenyewe aliyetaka kuwafutilia mbali vurugu mechi wale. THEREFORE YOUR STATEMENT AGAINST GREAT MAN OF GOD MOSES IS HEREBY MERCILESSILY DECLARED NULL AND VOID HENCE SACKED SINCE IT IS TYPICAL CARNAL- INSENSITIVE UTTERANCES AND COMPLETELY UNBIBLICAL.

  Pia umekosea kusema kilichomfanya hakose kuingia Canaan! Si kuwaita wale Waasi bali hiki hapa…uone tena jinsi gani uko shallow na Neno but furu maneno yako… ALIKOSEA KUSIKILIZA KWA MAKINI MAAGIZO ya Mungu ya namna ya kutatua tatizo la ukosefu wa maji wakati wana Israeli walipoanza tena kulalamika vibaya na kumkasirikia Musa walipopata kiu wakati hakuna maji-Hesb.20:1-12. Mungu alimwambia AUAMBIE mwamba MBELE YA MACHO YAO nao utatoa maji, lakini akiwa amekasirika( bila shaka kama mwanadamu-alichoshwa na aina ya kondoo wale wasiobadilika na kuwa wa baraka kwake yeye kama kiongozi, akatokea mbele zao baada ya kusikia toka kwa Bwana, akiwaambia…’’Sikieni sasa enyi Waasi(wajua mpaka uwaite-address watu ‘enyi waasi’-alikua amekasirika na kuchoshwa kwelikweli), Je TUWATOKEZEE MAJI ktk mwamba huu? Kisha akainua mkono wake na KUUPIGA(si kuu-ambia) ule mwamba mara mbili….maji yakatoka tena mengi licha ya kwamba alifanya TOFAUTI NA MAAGIZO YA MUNGU!!!!!!!!!

  Ndipo Mungu akasema, kwa kua Musa na Haruni HAWAKUMWANI NA KUMSTAHISHA/HESHIMISHA mbele za Wana Israeli, kwa kosa hilo na wao HATAWAINGIZA Nchi ya ahadi. Mwisho wa Mchungaji mzuri kama huyo, unakua ivyo kwa masikitiko makubwa, kisa? aina ya Wapendwa wale, toka, ingia na kaa-kaa yao mbele ya Mungu na Kiongozi wao wa kiroho, wamekua wanamtia pressure/misuko-suko mingi, muda mwingi vya kutosha hadi ikapelekea kutotenda ACCURATELY kama Mungu alivyoAGIZA

  Unaona sasa?, si umeongea kwanza uwongo against Moses, Bible! Nikikuita wewe mzushi unakataa! Ndio maana unasemelea mbovu makanisa na Watumishi wao kuhusu Zaka, si ajabu maana hata hapa umemyuka Musa vibaya ati alikosa Canaan kwa kuwaita Waasi! kumbe uwongo mkavu mkavu! Wewe una Chalinze Bible not Holy Bible aisee, aibu kweli kuongopa Mtu unaliyejifanya anajua zamani mambo kumbe…sasa anagundua alikua anatambia wengiene si sisi tuliyopakwa maana twakufanya kweli mwepesi sana kwenye Neno labda maneno na vijineno vyako vya kuropoka Sungura, hapo haujambo!

  Press on

 34. Sungura,

  Post yako iliyofuata, kusema kweli, hamna kitu, nijibu tu kitu kimoja kuhusiana na Bible, kukuthibitishia kua kweli una maneno yako mengi na si maneno ya Bible au kwa maneno mengine, indeed your Bible is not in you HUGELY as per this rules-2Timo.2:15c—‘’Kulitumia Neno kwa HALALI’’ na Col.3:16a—‘’Neno kujaa/kukaa kwa wingi ndani yetu KTK HEKIMA YOTE’’. Tuendelee kujadiliana then itakua wazi nani anatumia Maarifa tokana na Neno la Mungu na pia Neno la Mungu kama lilivyo na nani anajidhania kua ana Neno kumbe maneno yake.

  Nilisema kua Ibrahimu alitoa Zaka ile kwa moyo wa kumshukuru Mungu baada ya kushinda vita ile-Nikimaanisha kilichomsukuma kutoa Zaka kwa Mungu ni moyo huo wa shukrani kumaanisha alimu-acknoledge Mungu ndiye, alionyesha unyenyekevu kua kwa kweli hakushinda kwa nguvu yake pamoja na jeshi lake private kubwa , ni kicho chake kwa Mungu maana ni mtu mwenye Historia ya uchaji na moyo wa utaoji wa kutisha na ulikuja dhihirika wakati wa Isack, so ni rahisi kwa macho ya rohoni kumuona moyo wake huu past, present and future. Ajabu UMEKATAA UFAFANUZI HUU MURUA KABISA KIROHO,KIBIBLIA NA KIHISTORIA YA MIASHA NA TABIA za UCHAJI ZA IBRAHIMU….ukasema ivi….

  Hakutoa kwa sababu ya moyo wa kumshukuru Mungu BALI alitoa fungu la kumi kwa Melkizedki kwa sababu Melkizedki alimbariki Ibraham! unachosema wewe ni kua kilicho msukuma/motive behind ya Kutoa kwakwe ni tendo la kubarikiwa na Kuhani and yeye kama Ibrahimu mcha Mungu had nothing in himself juu ya huyo Mungu aliyemshindia vita. THIS IS NOT ONLY WRONG LAKINI NI UNSPIRITUAL UNDERTANDING YA IBRAHIMU HASA ALIKUA NANI NA YUKOJE NA MUNGU WAKE. Umeangalia jambo hili Kimwili-as it is/pale nilipo kama lilivyo but mimi nimeliangalia CORRECTLY Kiroho kwa maana ya Neno la Mungu kwa wingi rule-maeneo mengine kumuona Ibrahimiu ni Mtu gani hasa na alitembeaje na MUNGU ktk Utoaji-Climax yake ni Utoaji wa Isack. Mimi nanukuu pia mistari kadhaa kisha nitakutazamisha kitu.

  Mwanzo:14:14-24
  14 Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. 15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. 16 Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu. 17 Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote. 21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe. 22 Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi, 23 ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu; 24 isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao.

  Take notice kwa Mistari ifutayo! Fungua macho yako kiroho, usiwe kimwili sana kuhusu Zaka, umeipinga na kuipiga vita mpaka unakua kipofu kwa kila kitu chema, ndio maana una miss baadhi ya mambo na unayaendea au kuyatafsiri kimwili mno au literal.
  Haya maneno ktk mistali hii ni ya kuhani anapombariki Ibrahimu: Maneno hayo bila shaka Ibrahimu anayasikia Kuhani AKIKIRI WAZI KUA NI MUNGU ALIYEMSHINDIA VITA

  19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
  20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

  Sasa ndo maana wakati mwingi nasema tutumie akili tulizopewa kuelewa pia ya Mungu kwa kua ni halali-Paul alisema/alitumia maneno ya kweli na akili-Mdo.26:25. Ivyo nakuuliza kwa akili …kama Kuhani anaweza tamka maneno hayo ya SHUKRANI KWA MUNGU juu ya vita ambayo wala hakuipingana vipi Ibrahmi mchaji wa Mungu isiwe na tena zaidi?

  Lakin pia angalia kwa moyo wa ndani mistari hii inawakilisha hali gani ya undani wa Ibrahimu

  21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe.
  22 Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi,
  23 ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;
  24 isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao.

  Umeyazingatia majibu ya Ibrahimu kwa Mfalme wa Sodoma mstari wa 22? ‘’Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi’’ HANAKATAA/ANACHUKUA TAHADHARI MFALME ASIJEFANYA KOSA KUBWA KUYAHUSIANISHA MAFANIKIO YAKE NA WATU BALI MUNGU TU

  Je mpaka hapo ujaelewa somo wewe kwa yale niliyosema ni sahihi kuhusu Zaka yake ni Shukrani yake- kile kilichokuwemo kwanza ndani na si msukumo wa nje yaani Kuhani kumbariki? Yes I need to grow as you advised but U REAL NEED TO GROW DOUBLE IN THESE SPIRITUAL/ BIBLE MATTERS.
  Press on.

 35. Seleli,

  Hahahaha…!
  Nilikuambia mambo yako ya kuyapoozesha Maandiko kwa kuyafanya mila na desturi na mizimu, utaishia kuwa kaput, ukabisha saaaana!
  Haya, hebu angalia hapa unavyojidhirisha katika kukiri kwako kuhusika na Mt 23:1-39, kwamba nawe ni Mnafiki per se, ninainukuu kauli yako kama ulivyoiandika:
  “ARE u smooth Sungura in your life Kitumishi na Kiroho to your Church and Baba yako Kiroho? Kindly speak the truth-sijui nikwapishe au tutumie Ndio-Ndio na hapana-hapana rule?”

  Jitazame katika hicho kioo cha Mt 23:
  9 “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.” Mafarisayo ndio wenye kujiita “baba” juu ya watu wao, na kuitwa “baba”!
  16 “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu…” Jiangalie, “sijui nikwapishe …”!!

  “Baba yako Kiroho” ndio nani huyo tena? Nakuona umelivuka Neno si mchezo, Kristo anatuambia tusimwite mtu “baba” bali wewe unaye “Baba” hapa duniani, nini hiyo “baba”…! Unataka kumwapisha Sungura, bali Kristo anatuambia, “Lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa” ila kwa unafiki huwaga mnayakanyaga tu Maandiko!!!

  Duh, “Mbombo Ngafu”!!!

 36. Seleli,

  Pale mwanzo ulipokuwa unapiga kelele za kutumia akili na logic nk, nilidhani kweli, ila unaposhindwa kuyaelewa hata haya yaliyo wazi kabisa ktk hiyo Mt 23:1-39, umeniacha hoi, kwamba akili ime freeze au umenyang’anywa ufahamu?

  Haya ngoja nikuridhishe. niyarudie tena
  Mt 23:1 inasema hivi: “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,..” Umewaona wanaoambiwa hapo, ni makutano na wanafunzi wake. Akawaambia kuhusu nini? “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; …” (MT. 23:1-3)

  Agizo hilo la Yesu, linawataka makutano na wanafunzi wawasikilize na kuyashika wanayoambiwa na Waandishi na Mafarisayo, hao walioketi ktk kiti cha Musa. Umeelewa? Ukikosa kulielewa hili hutaelewa chochote kinachoendelea!!!

  Vifungu vinavyofuatia vinaendelea kuwachambua hao waandishi na Mafarisayo namna yao, zile tabia za kupenda masifa na kujisikia, mpaka kifungu cha 8 anapowatahadharisha makutano na wanafunzi kuto kuziiga tabia hizo za masifa na kujikweza, “Bali ninyi msiitwe Rabi, …” (MT. 23:8, 9, 11, 12)

  Haya maelezo ya vifungu hivi si main Ajenda bali ni yale yatokanayo na Ajenda, “Waandishi na Mafarisayo” na si wanafunzi wala makutano!

  Baada ya hapo Kristo anaendelea na Ajenda, akiisha kuziweka wazi tabia za hao waliokalia kiti cha Musa, sasa anatamatisha kwa kuwapigia “Ole” zinazohusiana na hayo wanayoyafanya, kama leo wanavyo wazuia watu wasiipate Kweli ya Mungu!!
  “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; …” (MT. 23:13) Ole hizo zinaendelea hadi kifungu cha 36.

  Labda kwa hapa nikukubalie kwamba kwavile unakiri kuwa yanakuhusu, basi umekwisha zipokea hizo “Ole” na upofu wake!!!! Sasa nina deal na kipofu mnafiki!

  Bali wanafunzi hawahusiki ktk unafiki na upofu wenu! Hebu itazame hii “Ole” ya kujiapia kwenu ovyo kwa unafiki wenu, ambayo kwa kuhusika nayo maana yake hukuweko katika ile faragha tulipofunzwa jambo hilo. Hebu jaribu kufananisha hii “Ole” unayoiona inawahusu na wanafunzi na lile somo walilopewa faraghani:

  “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; …Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake.” (MT. 23:16-22)

  Ukiisha yasoma hayo jaribu kuifikirisha akili yako hiyo ambayo iko raised katika standard, halafu uniambie ulichojifunza kutoka hayo, maana nawe kwa kuyasoma hayo ulikuwepo siku hiyo spiritually kama ambavyo nami nilikuwepo! Hauwezi kuja na jibu tofauti na hilo ulilolikiri huko nyuma na wakati wote, kwamba nawe yalikuhusu hayo yaliyo katika hiyo “Ole”!

  Ila mimi, licha ya kwamba nilikuwepo hapo ktk Mt 23:1-39, bali kabla ya kuja huko sisi tulifundishwa kuhusu jambo hilo kikamilifu: “Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, … Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; … Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.” (MT. 5:1, 2, 33, 34, 37)

  Umeona sasa kwanini nakuambia kuwa hizo “Ole” na hayo mengine hayatuhusu? Sisi huyapata mafunzo yetu katika faragha, ninyi wa mikutano ya nje hamuwezi kuyajua mambo ya ndani, mnabaki na “NDIYO na HAPANA” zenu zinazo toka kwa yule mwovu all the way!!!

  Haya, njoo ktk kifungu cha Zaka, hiki kinachokuhusu kwa kujing’ang’aniza kwako!
  “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. (MT. 23:23, 24)

  Haya, nafahamu kwa kukiri kwako, na wenzio wote mlio ktk ukiri wa kifungu hiki kuwahusu kwa kule kuwa kwenu ktk unafiki, basi niwaulize maswali machache, hata mkinipa majibu ya kinafiki, potelea kwa mbali!!!
  1: Kwamba ninyi mnakiri kuhusika ktk kifungu hiki ambacho kinazungumzia KULIPA zaka, nazo kauli zenu katika kulitimiza jambo hili zinazungumzia KUTOA zaka; Je, huu si unafiki mnaoendelea nao baada ya kuukiri?
  2: Je, mambo makuu ya Sheria, yale ambayo watangulizi wenu waliyaacha, ninyi leo mnayatimiza ilhali unafiki bado mnao?
  3: Upofu mlionao, umewatoka? Mkisema umewatoka, mmekosaje kuyaona haya?

  Nilipokuletea madhihirisho ya Hotuba ya Mt 23:1-39, naona imekuchanganya sana kuyaona mambo hayo katika uhalisi wake na nafasi yako katika hayo makundi, naona mpaka issue yenyewe imekupotea kichwani, uko Dar halafu unauliza njia ya kwenda Dar!! NINARUDIA TENA, kwa faida ya waliokufuata huko porini:
  Mt 23:1-3 “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda” (Nilikuambia usikose kulielewa hili)

  Hawa hapa Top cream ya uongozi, ambao wamekalia kiti cha Musa: Mdo 4:5-6
  “Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.”
  Unawaona hao? Basi hawa ndio aliowazungumzia Yesu, ni watu halisi kabisa na ukiwaamkua “Shikamoo” au “Tumsifu Yesu Kristu” wanakujibu, si hadithi wala ngonjera!

  Na hapa wanawapa Amri mitume, wanayopaswa kuitii kama Kristo alivyowaagiza, na sasa ndio wanaambiwa ya kuyatenda, Mdo 4:18 “Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.”
  Mitume wakawagomea! -“Petro na Yohana wakawajibu … sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.”
  Yaani maana yake ni kwamba, wanamwambia Kuhani Mkuu na uongozi wake wote kuwa, ‘wewe si Kuhani wetu tena!’ Hao wanaowakataa ndio wanaopokea Zaka, sasa utampelekea nani Zaka yako, nawe ukiwa umekwisha kupewa macho ya kiroho na kuliona jambo hilo la Ukuhani wa Haruni lilipoishia, kuna Ukuhani gani tena jamani na Pazia limeraruka? Mchezo UMEKWISHA!!!! Mwenye Hekalu lake kaondoka, wamebaki wahuni wa dini, wamelishona pazia na wanaendelea kutoza zaka! Iwapo vifungu hivyo vya Mt 23 vingaliwahusu, basi walipaswa kutii hiyo amri halali ya Kuhani Mkuu, lakini haviwahusu, kama una ufahamu!!!!

  Haya watazame wale wanaoendelea na dini yao huko Hekaluni kulikoshonwa pazia lililoraruka, walikuwa sehemu ya makutano, wakiongozwa na ile top cream waliyoambiwa na Kristo waitii: Mt 27:20 “Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.”
  … Jibu la makutano kwa ushawishi huo ndio hilo hapo katika hayo yanayoendelea kwa liwali: Mt 27:21-23
  “Basi liwali akajibu, akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi katika hawa wawili? Wakasema, Baraba. Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulibiwe. Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulibiwe.”

  Imedhihirika wazi kuwa huyo HANA kosa, lakini makutano kwa kuwatii hao walioketi ktk kiti cha Musa, wakaitii sauti ya viongozi wao wakamtoa Kristo asulubiwe! Sasa nikuulize Seleli, wanakosa gani hawa kulingana na maelekezo waliyopewa na Kristo? Si wameyatimiza kama nawe unavyoyatimiza maelekezo ya Zaka!!!

  Natumai sasa UTAILIPA zaka yako vizuri zaidi kuliko ulivyokuwa unadhania UNATOA. Ndivyo mambo yalivyo, najua haya yako juu yako kidogo lakini ndio hivyo, Ibrahimu wala Yakobo hawajawahi KULIPA zaka, Biblia huwa haikosei, ingawa ninyi hujidhanisha hivyo to your own detriment, bali iko SUPER, kundi moja la mwilini LINALIPA zaka, na kundi jingine la Rohoni LINATOA zaka; hii ndiyo distinction aliyoificha Mungu, ukiyakurupukia mambo, unaishia kwenye bin na mambo yako yaliyopitwa na wakati, maana Neno la Mungu linajitafsiri lenyewe, hakuna assumptions, mwisho mnaishia kum assume na Mungu!!!

  Naona hili la Mt 23:1-39 tumelimaliza, kama kuna ambalo hujalielewa, nitafurahi kulirudia tena mpaka uelewe, na kama ni shwari, basi nitayaendea hayo mengine ambayo nafahamu yako more spiritual kuliko hili tulilolimaliza!

  Gbu my “‘mingi-‘manga-manga’ syndromed” brother!!!

  “Kaka Mkubwa”!

 37. Sungura,

  Sio siri umechoka na umeishiwa sasa!

  Umeeanza kutaja/zusha majina ya madhahebu ya Wanamjadala na kujidai uko expert sana wa madhehebu ya Watu wanavyoendesha mambo uko! Umechoka Kaka.Kweli nimesoma comment yako ya sasa, nikasema huyu Bro sasa, off! Akalale au alete hoja nyingine, twende kazi.

  Tatizo una maneno yako mengi na si ya Mungu, Neno la Mungu ni final truth/authority, hukata mashauri, huamua kesi, huleta kweli, hubalansi hekima na akili zetu, huadjust hoja/comment zetu, hatimaye, kweli yake inakuja simama kisha mambo yetu, hutupwa hasa yale ya by the way kama yako mengi ndio maana sasa ulivyorudia swali ambalo comment na lecture yote niliyoitoa kwako, Milinga na Lwembe, this time, imeclear kila kitu tena baadhi ya hoja za Milinga, zime- correlate na zangu kuhusu kwamba…. Sasa UTOAJI WOWOTE NI HALALI NA BARAKA ikiwa tu utatolewa ktk moyo wa kupenda, furaha, uhuru, kusudio la moyo, kwa ufahamu wa kujali kazi na mambo ya Mungu na si kulazimishwa.

  Najua kwa point hii , UMEKWISHA na unapumulia mashine maana sasa si wewe tu bali kila mtu atatoa iwe Zaka, Malimbuko, Changizo, Sadaka za upendo ALIMRADI HALAZIMISHWI. Sasa TOA,acha usanii na ubinafsi uliokubuhu against your kanisa, Mchungaji wako, kazi zenu/zake za kiroho hapo kwenu na nje kwa Mwili wa Kristo kote but ANZIA NYUMBANI/wa nyumba kwa Mtu kwanza so says the Bible.

  Kwamba sijaweza tofautisha Zaka na Sadaka na ati waniuliza so called basic swali! Huu NI UTANI TU…umesema hili swali mara nyingi na nimesharijibu sana kule topic iliyokwisha na hii kwa lecture zangu kwenu wote, Pia niliwahi kukuliza/challenge kua kama nakosea/sijaweza, sema/onyesha tofauti iyo, hukufanya! Unagwaya! Sasa unaibukia hapa na iyo iyo eti this time unaiita basic question! UMECHOKA wewe, lete mada nyingine maana sasa kila mtu atatoa ilimradi kwa rana na moyo.Majibu ya swali lako, soma topic iliyokwisha na lecture zanga hapa kwa Milinga na Lwembe,acha uchovu Kaka..

  Aya basic question kwako pia-narudia TENA nililokuwaulizeni maaan najua na wewe unajua nguvu ya Kweli ya swali hili ndio maana una hali ngumu kihoja.Umefika mwisho wa kukwepa Zaka au hata ukikwepa, una ground Bibilcally bali kimwili/ubinafsi kabisa na choyo nzito.

  SWALI: JE LEO HII KTK AJ, MIMI NIKITOA AINA NYINGI YA MATOLEO KAMA ZAKA,MALIMBUKO, CHANGIZO NA SADAKA ZA UPENDO NYINGINE, BILA KULAZIMISHWA / KWA MOYO WA KUPENDA/RAHA ZANGU NA BWANA/ KWA KUPENDA KAZI YA MUNGU KANISANI KWANGU NA WATUMISHI WAKE, NI BIBLICAL OR NOT?

  By the way, plz acha uzushi/uwongo Kaka, tuelewene tafadhari! Nilisema na kweli nilikubali na ni KiBiblia si wewe uliyenifahamisha kwamba, HAKUNA LAANA kwa asiye toa Matoleo yoyote maana tayari tumo ndani ya Kristo, tumebarikiwa kwa maana hiyo ya kazi ya Bwana msalabani ILA KUNA MADHARA KWA MAISHA YA KIROHO NA KIMWILI KWA MAISHA YA MTU ASIYETOA! Unabisha? bisha sasa nikuone ulivyo na small Bible in your heart and severely disrupted God’s knowledge of His things by your uncultivated ego

  Hiyo misamiati teaching yako ni less interesting to me kwa sasa bali lete hoja, jibu maswali Kaka. Kwamba ktk baadhi ya makanisa wana handle vibaya mambo ya Zaka-kama kodi kwa kupiga kabari, pia nilishasema najua,ivyo usinizushie kua mi mnafiki,unaropoka tu,soma comment za nyuma ila nikasema..si yote na ivyo nikashauri, tuache maneno ya kienyeji dhidi ya kuchafua baadhi ya Madhehebu/,Kanisa la Mungu ambamo kuna Watu wanatoa Matoleo yote kwa furaha/upendo na kwa hiari, wakipenda kazi na Watumishi wanaowatumikia Wao na Mungu. Therefore, plz usitugombanishe na Watu wa Mungu wetu na usilete uzushi brother, si vema mtu mzima tena mwanaume na aliyeokoka na mwenye RM na mtumishi kama wewe kua mzushi/mpolitic against some true and real dedicated churches/Pastors and their members/kondoo…..unahuzunisha sana Sungura tabia yako hii ilhali umeookoka wewe. Nahisi kuna mambo kadhaa about your life kiroho/utumishi hayako sawa! Huwezi ukawa Mtu wa aina iyo, wa kauli izo against Kanisa/madhehebu na Watumishi wa kweli wa Mungu, ukasema angle nyingine zote uko sawa, atleast kwa uzoefu wangu wa Wapendwa wa aina yako, unakataa! ARE u smooth Sungura in your life Kitumishi na Kiroho to your Church and Baba yako Kiroho? Kindly speak the truth-sijui nikwapishe au tutumie Ndio-Ndio na hapana-hapana rule? Karibu.

  Press on.

 38. Seleli,

  Baada ya kukujibu chapisho lako ambalo angalao uliandika kwa busara,ngoja nikujibu hili ambalo umeliandika kipagani ukidhani unamtumikia Mungu kwa kuandika hivyo.

  Ngoja nikuoneshe sasa jinsi unavyotumia nguvu nyingi ya ugali kuliko kutumia maarifa yaliyo katika neno la Mungu. Remeber it’s not by power,nor by might….!
  Nguvu nyingi na hasira unayotumia inakufanya tu uonekane maamuma.

  Kwanza Ibrahim hakutoa zaka kwa sababu alikuwa anamshukuru Mungu kwa ushindi wa vita, bali alitoa fungu la kumi kwa Melkizedki kwa sababu Melkizedki alimbariki Ibraham.
  ( Mwa 14:18-20
 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”).

  Kama Ibra alitoa sadaka ya shukurani hapo basi tungemwona na sehemu zingine anafanya hivyo, maana hiyo haikuwa mara ya kwanza kwake kupigana vita na kushinda. Kumbuka alipomwokoa Luth ndugu yake. Kama unabisha,basi thibitisha kuwa hiyo ulikuwa sadaka ya shukurani.Tumia maarifa Seleli, si hasira, utaumia bure.

  Soma maneno yako hapa:
  ”Hard people needs sometimes harsh treatments (both words and deeds to level them), tatizo husomi Neno, umejaza mijineno yako tu, ona hii…Hesabu.20:10-Moses amekasirika kweli kwa vurugu za kila mara za akina ‘Sungura’ wa kipindi kile, anatokea mbele yao na kusema, ‘’Sikilizeni enyi WAASI, mwataka tuwatokezee maji toka mwamba huu? Aliwaita Waasi, wewe mwizi halafu unakataa nini? nani akupeti-peti kukuita malaika wewe wakati tabia na mwitikio wako wa mambo ya Mungu na ya Mtu wako wa Mungu anayekulea hapo ni wizi-wizi tu! kisanii-sanii tu na kelele nyingi za kugomesha watu Kutoa, kisa unajua sana kumzidi Pastor wako, eti umekomaa sana siku izi kiroho kuzidi Baba yako aliyewekwa na Mungu kukuleta ulipofika!”

  Umeniambia tatizo sisomi neno, nimejaza vijineno vyangu. Najua umeniandikia hii makala ya kipagani kwa sababu ya hasira ya kukupongeza kwa kukiri kwako kushindwa juu ya dhana ya ulazima wa kutoa zaka kwa kila mkristo.

  Kwa hiyo unajustify kuniita mimi nisiyetoa zaka kuwa ni mwizi kwa kunukuu kile ambacho Musa alikifanya kwa Israel. Kwa hiyo unakubaliana na hicho amabcho Musa alifanya.

  Pole sana mwalimu kipofu wewe mwenye kuchuja sisimizi na kumeza mende.
  Hujui kuwa hilo lilikuwa ksa kunbwa sana kwa Musa mbele za Mungu, na lilisababisha asiingie Kanani. Kuwaita waasi wale ambao Mungu amewatoa utumwani. Nawe wafanya hivyohivyo, kuwaita wezi wale ambao kristo kawafia.

  Hongera sana Seleli mwenye haki, hivyo kuwaona wasiotoa zaka kuwa ni wezi. Be careful anyway, usiikosee heshima kazi ya msalaba kwa kulazimisha kongwa amabalo lilimpandisha kristo mtini.

  In fact, unachotakiwa kujua ni kwamba zaka mimi nilishakwisha kukwambia kuwa huwa silipi na sina laana yoyote. Na hakuna mchungaji wala mtume wa kunilazimisha kuilipa, hata akishusha maneno yote makali unayoyajua. Nilishatoka kwenye huo ujinga na unyenyekevu kwa mambo manyonge yaliyopitwa na wakati.

  Ushuhuda wako wa kabla hujaokoka umenisaidia sana kuzidi kukujua u mtu wa namna gani Seleli. Nilikuwa sawa siku moja kukwambia kuwa hata ngumi wewe unaweza kurusha. Umekifanya kifua chako kuwa cha mpumbavu mwenye kuruhusu moyo wake ufure kwa hasira na kuamua kuongea maneno ya vivi hivi.

  Keep spilling all those junks Seleli,may be finally u will spill some useful relish!

  Kuna kitu kingine ulikidandia hapa bila kujua kwa nini nilikisema. Nakunukuu “NADHANI HULIPASWA KUONA AIBU WEWE MARA MIA KUULIZA SWALI HILO CHILDISH IN PUBLIC NA BADO UNASEMA UMEKOMAA KIROHO, UNAJUA UTUMISHI, WATUMISHI NA KAZI YA BWANA!”

  ulikuwa unajaribu kujibu swali langu la nani leo wananunua magari kati ya wachungaji na washirika.

  Hili swali nilikuuliza wakati majibu hoja yako kuwa umesema kuwa kwa nini washirika wananunua magari, plot, kulipa karo, n.k. lajini wakosa kuwatunza watumishi.

  Seleli, matoleo tunayotoa si kwa ajili ya wachungaji kujitosheleza na mahitaji yao. Au kwa lugha nyingine, sadaka si mali ya mchungaji. Kanisa lina vitu vingi sana vya kufanya, na watu wengi sana ambao linapaswa kuwahudumia. Mchungaji anatakiwa kupewa sehemu ya hayo matoleo, si yeye kuhodhi matoleo yote na kuyafanya ya kwake. Kufanya hivyo ni kinyume na biblia.

  Lakini leo wachungaji wengi wanahodhi kila kitu. Ndipo kanisa linapotukanwa sasa kwa wachungaji kuishi maisha ya anasa wakati kuna idadi kubwa ya watu katika makusanyiko yao wanateseka kwa kukosa basic needs.

  Yesu hakufanya hivyo,wala mitume hawakufanya hivyo, na wala ghalani mwa Bwana si nyumbani mwa mchungaji.

  Haya mambo si magumu kuelewa, just u are biased in yo attitude sir!

  U need to grow a bit!
  – – — — — – – — – — – – – – – – – – – – – – – – – – – – — – – – – – – — –

  Seleli, mimi nafikiri sasa tutumie hii nafasi kujadili utoaji wa sadaka, maana nakuona unachonga sana juu ya utoaji wa sadaka japokuwa mada ni zaka.
  Na umezidi sana kulonga maneno yasiyo na staha juu yangu kuhusiana na utoaji wa sadaka kana kwamba mada ilikuwa ni utoaji sadaka.

  Sasa naomba SG waruhusu tuujadili utoaji wa sadaka ndani ya hii mada ya zaka. Maana si mara moja au tatu kwa lugha tofauti umeniambia mimi sipendi kutoa, alhali nilishakwambia wazi nisichotoa mimi ni zaka.

  Sikuwa nimetaka kukujibu kwa ndani kuhusiana na dhana ya utoaji,ispokuwa dhana ya zaka. Na ukimya wangu hapo naona umeutumia kuchonga sana kuwa Sungura ana mkono wa birika, stinge, selfish, devilish, na mengine mengi.
  Sikuwa nataka kutoka nje ya mada.

  Karibu sasa tuongee huo utoaji,ili tuone kama utaendelea kujigamba kwamba wewe ndiye mtoaji kuliko akina sisi.

  Kribu Seleli!

 39. Seleli,

  Kuna unafiki fulani mkubwa unaufanya hapa, na ninajua kwa nini unaufanya.
  Unajifanya hujui maana ya kutoa zaka kwa lazima tunayoiongelea hapa. Na uhiari unaojificha kwao hapa, ni ule wa kukubali kuitii sheria ya zaka iliyoainishwa kwenye torai ya Musa, kama vile ambavyo pia Malaki nabii aliwataka waisrael waitii.

  Seleli, najua vizuri sana utaratibu wa dini yako ya TAG, kwamba zaka lazima kila mtu atoe, awe anapenda ama hapendi.Asipofanya hivyo hata kama huwa anakata nusu ya mshahara wake kuwapa wajane na yatima,huwa anaitwa mwizi. Lakini sadaka ni hiari kabisa wala huwa hawamfuatilii mtu kwa habari yake.

  Kama leo huko kwenye dini yenu mnatoa kwa sheria unayoiita ya roho, hebu niambie kwa nini mnaandika majina na kupewa kadi za zaka, lakini mnapotoa sadaka yenyewe hampewi kadi wala kuandika jina?

  Katika tafsiri ya zaka mnayotoa Seleli, kutokuitoa si unyimifu kama unavyosema, bali ni wizi, maana wafundishaji wa zaka husema hiyo si yako bali ni ya Mungu. Sasa huwezi kuitwa mnyimifu wakati hicho usichotaka kuk oa si chako bali cha huyo anayetaka ukitoe kwake, hapo jina lako zuri ni mdhulumaji, au mwizi.

  Unyimifu uko kwenye sadaka kama mtu hataki kutoa hiyo hapo ndipo anastahili kuitwa mnyimifu. Usichanganye misamiati tafadhali.

  Kuna kitu umeniomba nifafanue,hiki hapa:

  Ulikubali kuwa hakuna laana kwa mtu asipotoa zaka,lakini katika kufafanua hiyo hoja yako ukajikuta unaifafanua kwa maelezo ambayo si utoajiwa zaka bali sadaka.
  Ulichosema ni hiki hapa. “Ni kweli BUT-notice- it’s a big… ‘’BUT- yako madhara kwa Mkristo au mwana wa Mungu kutokua na tabia ya Kutoa-Imeandikwa.. Heri Kutoa kuliko kupokea na in this case au kwa nia ya wengine humu…’’ni heri kutoa kuliko kubania”

  Ukweli Seleli tangu tuanze kujadili suala la zaka hujaweza kabisa kutofautisha kimaudhui kati ya zaka na sadaka.

  Labda nikuulize leo swali basic:

  Unatofautishaje utoaji wa zaka na utoaji wa sadaka?

 40. Milinga,

  Notice to Lwembe/Sungura/Amin

  Reference to Tumain Nelson

  Yaa, thanks and bless u for a good attempt done kwa maswali yangu, hata ivyo nina maswali ya nyongeza kama ifuatavyo, lengo ni Kujifunza kama ulivyosema wakati wanitia moyo kusoma post yako ndefu ya zaka makala za nyuma na pia ni muhimu TO ESTABLISH THE TRUTH BEYOND ANY QUERY! Sasa, ili ku-keep the flow, kwa uchache ninanukuu tena statement zako kisha my previous responses/maswali,halafu majibu yako, hatimaye SWALI JIPYA LA NYONGEZA.

  1- Huwezi kubarikiwa kwa kutoa zaka (fungu la kumi) hata siku moja.

  My response ni Maswali:

  (a) Umefikiaje iyo conclusion?

  JIBU LAKO: Zaka ni mafundisho ya AG na yamepitwa na wakati, mambo ya kulazimishana na vitisho.

  SWALI NYONGEZA: Je nikiendelea kutoa -Zaka kwa sheria ya AJ-ya rohoni yaani kwa kupenda/kwa kukusudia moyoni si kwa kulazimishwa/kwa raha zangu na maamuzi yangu ya uhuru na furaha yangu na Bwana, nitabarikiwa au la?

  (b) Kwa nini umesema ivyo?
  JIBU LAKO: Soma maelezo hapo juu.
  SWALI NYONGEZA: Hayakukidhi haja, jibu sasa juu pale kwa swali(a) na hatimaye swali hili (b) litakua limejibiwa pia.

  (c) Kwa nini Mtu atoe kwa hiari, kwa moyo wa kupenda, kwa jinsi alivyokusudia/amua-pania moyoni mwake kisha kamwe ASIBARIKIWE? JIBU LAKO: Nadahani hapa ulisahau msimamo wangu. Soma tena maelezo hapo juu.
  SWALI NYONGEZA: Nilisahau Msimamo upi? useme sasa kwa kuzingatia maswali ya nyogeza ya (a) na (b)

  (d) Kuna dhambi gani kutoa fungu la Kumi kwa hiari ?
  JIBU LAKO: Dhambi ni kwamba utatakiwa kutoa kila mara 10% kwa kila pato. Na usipotoa unajikuta dhamiri inakuhukumu, unasikia sauti ikisema….. hujatoa 10%….., hujatoa 10%…..yaani kila uendako sauti hiyo itakufuata na kujikuta una dhambi ya kutotimiza NADHIRI yako ya kutoa 10% kila mara. Utakuta Mpendwa amepewa 10,000 na mpendwa ili aitumie kula LUNCH halafu anashindwa kula LUNCH ya Tshs 10,000 eti kwanza atoe 10%. Mpendwa amepewa Tshs 2,000 ya NAULI ya kwenda Gongolamboto anaanza kuwaza atoe 10% kwanza shs 200 ndipo atumie Shs 1800 kama nauli. HUU UNAKUWA KAMA UTUMWA FULANI.

  SWALI NYONGEZA: Maelezo yako naona yana kidhi Utoaji Zaka kwa sheria za AK-za mwilini ndio maana inakua ni dhambi na utumwa fulani ivi usipotimiza. Ulichojibu hakifit Zaka leo kwakua tunatoa kwa moyo wa kupenda, hakuna utumwa wala hatia, Je unakubali kua maelezo yako hayaelezei ubaya wa Zaka kwa njia ya leo ya rohoni?

  (e) Ili mtu abarikiwe kwa maana yako ya kubarikiwa/ atajirike materially, atoe Matoleo gani? Zaka, Malimbuko, Sadaka za Upendo, Changizo au Isack kabisa?
  JIBU LAKO: Msimamo wangu ni ule ule; UNAPOWAFUNDISHA WATU KUMTOLEA MUNGU EPUKA KUWAAMBIA KUWA WAKITOA KIASI FULANI CHA SEHEMU YA MAPATO YAO NDIPO WATABARIKIWA. Waache wenyewe watoe kwa kipimo chao kulingana na moyo wa kupenda. Zaka, Malimbuko, Sadaka za Upendo, Changizo kama vyatolewa si kama UTAMADUNI bali kwa moyo wa kupenda tena vitolewe kwa SIRI asijue mtu yeyote, HAPO NDIPO UTAAMBULIA BARAKA.

  SWALI NYONGEZA: Kwanini ulisema ktkt swali la kwanza kua hakuna baraka kutoa Zaka ilihali kwa maelezo yako haya, umeweka peupe kumbe wajua kuna baraka, alimradi yote yakitoka kwa sheria ya roho, yafaa sana? Ulikosea siyo? Unaweza kiri ivyo kwa unyeyekevu kisha kusahihisha?

  (f) Kwa jibu la juu hapo,NIHIBITISHIE KUA, UTAJIRI WALIONAO KWELI UMETOKANA na HICHO WALICHOTOA?
  JIBU LAKO: Utoaji uletao BARAKA ni ule tu wa kutoa kwa moyo wa kupenda kiasi chochote bila hofu wa shuruti.
  SWALI NYONGEZA: Kwa iyo alimradi kanuni ya sheria ya rohoni ie Kutoa kwa moyo wa kupenda imezingatiwa kama ulivyosema hapo basi tuko huru kutoa matoleo ya aina yote siyo?

  (g) Na toleo ilo walilotoa lina kanuni gani za KiMungu au likoje mbele za Mungu mpaka kwa hilo Mtu abarikiwe na kwa Zaka kamwe amepoteza muda, asibarikiwe na hata barikiwa?
  JIBU LAKO: Katika AJ mpendwa anayedhani atabarikiwa kifedha kwa kutoa ZAKA anajidanganya. Utoaji uletao BARAKA za kifedha limefafanuliwa vizuri sana na Mt. Paulo kwenye nyaraka zake sina haja ya kurudia hapa.
  MASWALI YA NYONGEZA-
  Kwanza: Nani kasema ktk Bible kua hatuwezi kubarikiwa kifedha kwa kutoa Zaka hata ktk msingi wa sheria ya rohoni ambayo wewe pia umeikubali?

  Pili-Je waweza sema/fundisha/dokeza baraka izo za kifedha alizofafanua Paul zinazotokana na Utoaji? Angalau taja maandiko machache maana kila mtu angependa kujua siri hizo na kukamata pesa nyingi tena haraka sana na wa kwanza wao ni mimi kabisa kabisa, nataka kumiliki pesa mingi-mingi sana Milinga ili nitoege hata 10%,20%,50%,100% kwa Bwana na Watu wake wote toka wa madhabahuni mpaka wa kwa bench( Wahitaji Wana wa Mungu)

  (h) How can you BE VERY SERIOUSLY SURE THAT IN THE WHOLE BODY OF CHRIST IN TZ, NEVER EVER HAPPENED THAT GOD BLESSED SOMEONE FOR HIS/HER TITHES GIVINGS?

  JIBU LAKO: Hapa Tanzania matajiri wakubwa waliopo ni Hawa wajiitao Mitume na Manabii na baadhi ya Maaskofu na wachungaji kadhaa. Ndani ya waumini sijui kama kuna muunini ni milionea au bilionea kama hawa wachungaji, Manabii, Mitume na Wazee wa Upako? Sijui. Wahubiri matajiri utawaona tu: Wanatembelea magari ya kifahari sana wakati waumini wao kibao wanaohimizwa kutoa zaka hawana hata ndala za kuvaa achilia mbali nyumba za kuishi. Seleli wewe mwenyewe utakuwa unawajua hao wahubiri matajiri, ila kumbuka wametajirishwa na zaka za waumini wanaoendelea kuwa maskini kila kukicha. Unamkumbuka Mhubiri mmoja alitoa rambirambi Tshs 15,000,000 kwenye msiba wa Dr. Moses Kulola? Je unamkumbuka Mwingine aliyetoa Tshs 10,000,000? Wahubiri kama hao ndio Mamilionea hapa Tanzania? Je, hizo pesa wamezipata wapi? Je, wanafanya biashara gani mpaka waweze kufika kwenye msiba wa Kulola wakiwa na magari ya kifahari ikiwemo HAMMER? VX, V8, nk?
  MASWALI YA NYONGEZA:

  Kwanza: Unadhani umejibu swali langu solidly kweli? Jipime tu kwa kurudia swali langu kulisoma!
  Pili: Je si kweli uliwaka-waka ‘kiinjilisti’ zaidi kutamka uliyotamka ktk statement yako ile kua hakuna aliyebarikiwa Tz na kwamba sasa ni wakati wako wa kuifuta kauli iyo maana tayari umeshakiri mwenyewe kua Utoaji wowote wenye baraka ni ule TU wa moyo wa kupenda? Na kwamba ktk TZ tupo wengi sana tunaotoa Zaka na mengine mengi hata Malimbuko kwa kupenda na kubarikiwa kiroho na kimwili ni lazima kama si jana, basi leo au kesho?
  Press on.

 41. Milinga,

  Notice to: Sungura/Lwembe/Amin.

  Cc to: Tumaini Nelson,

  Attention! Milinga, Response hii ni ndefu maana ina-cover yako ndefu sana ya yale uliyopost for me and Nelson mliyojadili mwaka juzi on Zaka.

  Nimesoma kila nukta ya Mafundisho yako kuhusu Zaka uliyowahi toa uko nyuma ambayo umeyapost hapa for me and Nelson. To be honest, ulifanya kazi kubwa sana, mimi pia napenda Ualimu, hence najua mpaka uweze toa hayo uliyokua unatoa, kuna sadaka ya kutosha ya muda, kula gombo haswa na vyanzo vingine vya kupata maarifa ya Mungu, gharama ya vocha kwa internet, masaibu ya kuproof read huge piece of writing kabla ya kutuma nk, so nakupa hongera ya dhati na kazi yako si bure hata kidogo as per this data base-Rev.20:12 in Jesus name,Amen.

  Ni kweli mimi na Nelson, hatukuwepo hapa SG kuchangia miaka iyo LAKINI napenda kukujulisha kua nimekuwepo ktk Biblia kuisoma na kuielewa subjects zake mbalimbali umo ikiwemo ya Zaka, kabla hata ya kuja hapa hence yaliyoko hapa na kwa kweli maandiko uliyotumia hapa, yamo ktk Bible yangu toka nijue from 1992 kwa hakika kua Bible ina Maneno na Matendo ya Mungu reccorded in it hence hamna jipya sana kiviiiiile chini ya jua la humu brother Milinga. Kwamba hatukuwepo ni kweli lakini ni dhahiri sana sasa Bwana ametuleta tuwepo na nahaidi kuwepo kanisa hili la kielekronika kwa uaminifu sana maana patamu sana hapa.

  Napenda kusemelea kidogo kisha kukuliza mambo kadhaa juu ya maandiko uliyosema yanatumiwa kuhimiza wapendwa wa Agano Jipya kutoa zaka.

  Waebrania 7:1-Ulisema..’’Andiko hilo linatuonesha kwamba Ibrahimu alitoa 10% kutoka kwenye nyara alizopata na wala siyo katika mapato ya mali zake’’

  Swali: Unataka kusema nini kuhusu ‘’alitoa Zaka toka nyara si mapato yake? Which doctrine or ufunuo so to speak, do u want us to pick from such msisitizo of yours? Nataka nikupate hapo vema sana kabla sija-respond kwa uzuri mno.

  Mwanzo 28:20- Ulisema…’’Wahubiri wote wanaorejea maandiko haya na kuyatumia kuhimiza kanisa la sasa limuige Yakobo’’

  Swali: Unadhani wanafanya vibaya/ kosea Biblical principle yoyote kuwahimiza/challenge Watu kuiga moyo huo mwema kabisa wa Mtu kujua na kushikilia ufahamu wa kiroho na kiMungu pia kiuchaji kua anapovuka kizingiti kizito, cha kwanza hasifikiri kwenda kula bata na makongoro au kuongeza mang’ombe zizini au sema to the extreme devilishly, kupata wife mwingine kama si gari ya 3, achilia mbali simu ya 4 kali ya ipod, bali ku-associate achievements/ survival/ escape/stepping up yake na neema/utendaji/usaidizi wa Mungu Baba ambaye Biblia inasema ktk yale yasimamayo against us kama mlima, yet si kwa uweza wala nguvu bali kwa Roho( Mungu)- tunavuka- Zak.4:6 na kwamba ingia, ishi yetu, lala yetu, amka yetu na toka yetu ni kwakua Yeye ametaka/ameridhia-Mdo.17:25-28, la sivyo, tutawajoin tena haraka sana jamaa zetu pale mochuri kabla ya kuwajoin for real kwa grave yard?

  Umesema hao wanaowahimiza Watu ivyo, ‘’wanapaswa kusoma tena vizuri neno kwa neno kabla ya kuweka mkazo katika maandiko haya kwa kua Yakobo hakutoa zaka kutoka katika mali zake bali mali za wengine alizowanyanganya’’

  Maelezo: Nikushauri kua wa kwanza anayepaswa kusoma si neno kwa neno andiko hili bali habari nzima ya Yakobo toka day 1 mpaka anaingia kaburini, ni wewe Milinga ili uje hapa na ushahidi kua ALITOA ZAKA NA tena ALITOA TOKA MALI ZA UNYANG’ANYI! La sivyo sema..’’sorry wana mjadala, niliteleza!

  By the way, just a common sense thought, unadhani Mungu alikubali Zaka za toka dhuluma maana unyang’anyi ni set, subset yake ni dhuluma! Notice: don’t make a mistake kufafanisha Mali kama nyara baada ya kuzinyuka vema na kushindiwa na MUNGU MTAKATIFU MWENYEWE Vs. kunyang’anya Watu kibedhuri/ kidhulumati!

  Umesema..’’Pia aliweka nadhiri kwa Mungu kwamba Mungu asipotekeleza matakwa yake hangetoa kabisa’’

  Swali: Ndicho alisema au ni your own interpretation of what he said? Better be fair kwakwe brother.

  Kwamba,..’’ hayo ni maombi ya kitoto kabisa’’
  Swali:

  (a) Ya kikubwa yakoje? Show sample hapa

  (b) Umetumia hints zipi kupima na ku-conclude kua such ni maombi ya kitoto?

  (c) Je huoni ndani ya maombi hayo moyo wa Mwanadamu kumtaka kweli Mungu na ni mtu mwenye akili na ufahamu wa kujua tumaini lake ni Mungu tu, hana jinsi na kwa kweli huyo Mungu amuelewe tu na tena amtendee na si vinginevyo? Huoni ivyo? huo ni utoto kweli? au ni ukomavu na ukweli kua uyo Mtu anatembea na anayetaka kutembea na kumuona Mungu, aliyefundishwa kuhusu habari za Yehova na Baba zake na anataka kua benet-benet na Mungu, kumfanya Yeye ni kimbilio lake tu na hakuna any other hope nje ya huyo Mungu wake? OPEN YOUR SECOND REAL EYES Brother AND SEE through.

  Ume-caution kua, ‘’Kama unamwomba Mungu akupe kazi au ajira ukaweka nadhiri kuwa ukipata ajira mshahara wako wote wa kwanza utamtolea Mungu na utamtolea 10% bila kusita, Jaribu kuwaza upya nadhiri hiyo’’

  Swali: What do you mean brother? Kuna tatizo gani? Nini UnBiblical act utakua umefanya na unakwenda kufanya? Any critically wrong or sinfull/unGodly thing done or to be done with/by that?

  Umesema sahihi kabisa on this kua…’’Ukifuatilia maandiko vizuri utaona kwamba Yakobo hakutoa hata hiyo nadhiri aliyoiweka’’

  Swali: Una harmonise vipi na yale uliyosema juu kuhusu Yakobo kutoa zaka?

  Umeongea kwa wasiwasi kua….’’Hata kama aliitimiza (kama kuna hilo andiko linalothibitisha) YAKOBO HAKUTOA ZAKA KILA MWEZI AU KILA MARA KAMA WANAVYOTAKA WAHUBIRI WA SASA’’

  Maelezo: Relax brother, hakuna hilo andiko na hakuna record ya yeye kutimiza yet he is justified kwa ule moyo mwema wa kupenda kutoa KAMA ISHARA MADHUBUTI YA KUMSHUKURU MUNGU- take note kua shukrani means many things, one of them is: it speaks of aknowlegment of God being everything and no. 1 in all your life matters.

  Swali: What is the problem nikiwa ktk sheria ya roho namely kwa moyo wa kukusudia, kufurahi, kupenda sana, uhuru, raha, kwa mapenzi na matashi yangu na Baba yangu,nikaamua kumtolea Zaka, acha kila mwezi but kila week?

  Walawi 27:30-34- Umesisitiza kua kwa andiko hili.. Zaka ni ya Vitu/Wanyama tu.

  Swali: Kama leo ktk sheria ya roho( refer juu hapo), nikaendelea kutoa Wanyama kama zaka au badala ya kubeba ng’ombe wangu walioko Geita kuwapeleka Dar kwa kua nimekusudia kutoa zaka kule kanisani Dar nakolishwa na kulelewa, sasa kuepuka usumbufu, nikauza ng’ombe hao kisha thamani sawa na ng’ombe hao, nikaitoa zaka, dhambi iko wapi kwa muktadha wa sheria ya rohoni?

  Hesabu 18:21-25, umesema….’’makuhani waliamuriwa kurithi zaka peke yake, hawakupaswa kuwa na mali yoyote zaidi ya kula zaka tu. Kwa kuwa kazi za kikuhani zilikwisha hasa zile za kusongeza sadaka za wanyama kwa ajili ya Mungu kuleta rehema kwa Waisraeli, hakuna tena kazi za kikuhani katika nyakati za leo. Kwa hiyo hakuna tena mwenye haki ya kurithi zaka kama walawi wa enzi za Musa’’

  Maswali:

  (a) Una uhakika leo hakuna kazi za kikuhani kweli? kwamba hatuna uhalisia wa kazi za hemani za leo, uhitaji wa watumishi kuwepo hapo kwa kudumu ili mambo yaende vema hapo kanisani kwa ajili ya Bwana na maisha yetu?

  (b) Umeshawahi fanya Bible study yako vema ktk RM kwa andiko hili..1Wakorinto.9:1-27?

  Mistari-1,2,3,4,5,6,8,12,15,16,17,18= Paul anasema kwakua yeye naye ni Mtume, anayo haki ya kuhudumiwa/kula vya injili/madhabahuni na haki nyingine kama kuoa/kutwaa mke ILA KWA UTASHI WAKE-si amri ya Bwana, AMEAMUA KUACHA IZO HAKI ZAKE

  Mistari-7,9,10,11,13,14= anasema, nani ( ofcoz Askari gani) huende vitani kwa gharama zake mwenyewe?, Nani apandaye mizabibu asiyekula matunda yake? au atunzaye kundi asiyekunywa maziwa yake? Kisha ananukuu andiko la AK kua… usimfungie maksai apulapo nafaka, then anamiminika kwa lecture kwamba….kama tumewapandia vitu vya rohoni, ni kitu cha ajabu tukivuna vya mwilini? anatema nondo kua… wale wanaohudumia mambo ya utakatifu hula vya hekaluni, wale wanaohudumia madhabahu hula vya madhabahuni na mstari ni 14 ni mtamu zaidi.. anasema..’’NA BWANA AMEAMURU-si ombi- KUA WALE WANAOHUBIRI INJILI WAISHI TOKANA NA INJILI! Oooh! Fantastic alleluyah! Therefore, Watumishi wanayo haki ya kutunzwa na Matoleo yote iwe Zaka, zaidi ya zaka, sadaka nyingine as long as yote yatoka kwa sheria ya roho. Tunazo kazi nyingi leo hemani kuliko zamani na niza kila mara na tunahitaji watu uko tena kwa kudumu, wachape mzigo for us na Bwana-simple and very good point, right?

  Umesema…’’Tunapaswa kuelewa hivyo kwa sababu maandiko haya hayawakatazi wachungaji kumiliki mali za aina mbalimbali kiasi kwamba wanapaswa kuishi kwa kutegemea zaka za Wakristo tena’’

  Maelezo: Embu tuwaze kwa upana kidogo ivi kama Watumishi wa Mungu, so kipi ni salama kwetu na kazi ya Bwana kati ya….

  ==== Kuwa na Wachungaji permanent, wakae na kutulia wakitenda kazi ya Bwana/ya madhabahuni/hekaluni tena kwa ajili ya Bwana na sisi, na kisha sisi tuwawezeshe kimaisha ILI WATULIE KWELI KWELI KUMSIKILIZA BWANA ANENAPO KISHA WAJE WANENE kwetu NA HATA WAVIKWE NGUVU ZA HUDUMA, Au

  ===Tuwe na Wachungaji wameajiriwa na serikali, NGO’s, Co Ltd, wajasiriamali 24hrs, Watafutaji madili ya tanzanites, plots za kuuza, Wauza supu asubuhi, Wanapiga misele mikoani wakati wa misimu ya kuvuna mazao na kuishi uko mwezi kukusanya magunia ili waje nayo Dar, wameteuliwa ktk tume ya HIV so inabidi waende TZ yote kwa kampeni, wako ktk tume ya Katiba mpya nk… na inabidi wafanye hayo ili aweze lipa kodi au kujenga nyumba, kulipa karo, kua na pesa wakiugua au mama Pastor akitaka kujifungua, kusaidia koo zao maana uko village pia wanawatengemea, kusaidia washirika maskini, wahitaji-yatima na wajane, kua na michango ya mitaani, serikalini, shuleni na harusi, kisha then wakati au wakishafanya hayo, wawe walipata muda kwa kumsikiliza RM kisha WAPANDE MIMBARINI WAKIWA NA WIRE IME-CONNECT JUU VEMA KULETA VITU CLEAN? Chagua brother, which Pastor would you like to be under on serious note?

  Cant you see walio ona ni vema Wachungaji wao wakae na kutulia huku wakiwezeshwa kwa matoleo ya upendo ya kila namna pamoja na zaka ili Watumishi hawa wawe na lao moja tu… kulihudumia Neno permanently Mdo.6:4?, walikua a hekima sana tu? waliona mbali ambako ninyi hamuoni ingawa sasa mwaona via mijadala hii, glory to God, the Holy Spirit is here?

  Umesema…’’Utaratibu huu wa kuwawezesha wa Zaka, umekoma pale tu sadaka za kuteketezwa zilipokoma kwa Kifo cha YESU’

  JIBU! Kwa maana ile ya zamani, yes, ni over and out, hatuna Walawi kama wale. Leo, wote sisi ni Makuhani lakini tokana na sisi sote tena Bwana anawa-appoint wengine kwa job/office-Waefeso.4:11-12- na kwakua job/ministry izo zina/ta..chukua maisha na muda wao mwingi, Wanahitaji kuwezeshwa kwa matoleo ya aina nyingi kabisa na hilo ni jema sana mbele za Bwana, linakibali and COMPLETELY BIBLICAL.

  Malaki 3:7- 12, Umesema…’’Wana Israeli walitoa ili Nchi ktk ghala zake kuwe na chakula hata leo, hakuna mtanzania asiyetoa kodi kwa njia ya VAT au Income Tax au Ushuru. Kwa sisi kutoa kodi serikali inapata uwezo kununua chakula toka kwa wakulima ili chakula kiwe kingi katika ghala la taifa na kuweza kuwasidia wale wanaokumbwa na maafa katika nchi’’

  Swali: Kama unakubali ili mambo yaende enzi zile AK na ili issue zikwenda hata ktk serikali Kodi itolewe, mbona ni rahisi sasa kuelewa kua ILI NA LEO mambo yaende vema, kodi but out of love, zitoke? tuko pamoja?

  Mathayo 10:9- 10 – Umesema….’Je watendakazi ikiwa ni pamoja na wahudumu, mashemasi, wazee wa kanisa, wachungaji, na wanakwaya, nk ndio wanaolipwa au ni mchungaji pekee anayelipwa?’’

  Swali: Kwani hao wengine wako hemani permanently? Got no any other job or assignment out there? Otherwise, wakimaliza huduma, si wanakwenda home na mishe-mishe? So wanataka noti za nini? washindwe mbaya!!!!!!!

  Hitimsho lako hili kua…’’Kuhusu zaka, changamoto zipo nyingi sana na kuna maswali mengi kuliko majibu yake’’-

  JIBU: Sidhani kama ni kweli tukiongelea zaka kwa maana ya sheria ya rohoni-kutoa kwa kupenda! Mambo yanakua raha na safi kabisa, yaani mbona peace tu! nyie ndio mna-complicate na kunegative badly mambo sweet and poa kabisa in Jesus name.

  Kwamba…’’Wapendwa wengi huyakwepa maswali hayo’’,

  JIBU: Hao wapendwa hawana Neno au? yapi maswali magumuau mengi hayo wanakwepa? YALETE HAPA HADHARANI TUYAONE kaka halafu tuone wakwepaji ni akina nani. Amen.

  Press on.

 42. Lwembe,

  Sungura/Milinga,Amini = you have your share here and may assist Lwembe kwa some serious stuff/questions to make senses hapa.

  Umeandika ma nini aya brother? Unaniachanga hoi kusema za ukweli! Katika yooote uliyoandika,nimepata vichache vyenye uzito wa kuvifafanua na kamoja tu ulichosema kenye substance, sorry brother, love u but that is the truth- hamna kitu kwa post yako bro kwa ujumla, ni extremely very insignificant!!!!!!!!

  Toka tumeanza mijadala hii ya zaka kwa topic ile iliyokwisha na sasa hii, hakuna hata sehemu moja, nilifundisha au kutoa maoni kua ni LAZIMA waitoe, ninasoma Neno mimi-nina maarifa ya kunitosha, siwezi fanya ivyo, pia sikuwahi hata siku moja kukataa Utoaji wa kwa kadri ya moyo wa kupenda/kufurahi/kusudio la moyo, KAMA NIMESHAWAHI KATAA UKWELI HUU WA BIBLE, comments zangu zote ziko humu, copy na kupaste hapa! Nilichopinga toka mwanzo kabisa ni uzushi wa kusema Makanisani tunapigwa kabali-meaning tunalazimishwa na kwamba Kutoa Zaka leo ni laana na kongwa. Niliwakatalia kua si Makanisa yote ivyo kuwachallenge kua na hekima na waangalifu na kauli zenu against Madhehebu ya Kanisa la Bwana na Watumishi wale walio wa kweli wa huko. Pia niliwakatalia kua Kutoa zaka Leo kwa moyo wa Mtu mwenyewe kupenda na hata kujiwekea nidhamu binafsi yake kama njia ya kuji-dicipline ktk uchaji wake na Mungu na mali zake kwa kua anatoa 10% ya mapato iwe kila saa/siku/ week/mwezi/ mwisho wa mwaka, ni kitu safi sana maana amefanya kwa kupenda, na yuko makini kudeal na nafsi yake maana hutuendesha sana tusifanye mapenzi ya Mungu bali yake, therefore, unaposema ivi….’’’Seleli eventually amelielewa somo la Zaka!! na kisha kutoa Hongera sana kwa Sungura na Amin, Millinga,….. I CALL THAT UZUSHI ANOINTING MINISTRY whose Apostle and Prophet are Lwembe and Sungura so far, more may wish to register in such close to confusion ‘ humanic church’.

  Kwakweli kwa jinsi ulivyojibu hoja yangu ya Math.23:1-39 nililokuuliza wewe na Sungura, Amin na hata Milinga, ni huzuni tu kiwango chako brother maana umenipa maandiko haya- Mdo.4:21, Mt 27:21-23 kama majibu yako- ni sawa na mtu amekuuliza unafahamu road ya kwenda Dar, unamtajia ya kwenda Dallas-USA! Mtu yeyote humu akisoma maandiko hayo na kuya-relate na andiko langu na maswali yake, kama hata cheka, atasikitika kwa kua kweli, U NEED TO RAISE YOUR STANDARDS brother. Niliwahi uliza uko nyuma topic ya zaka iliyopita, mkakwepa! Nilipowang’ang’ania jibuni maswali, mkajibu kwa kuchemka, wengine mkashindwa, ndipo nimeuliza hapa kwa sub-topic hii ya ile kule iliyokwisha, mkachemka, SASA NAULIZA TENA, PEUPE ZAIDI with MORE ELABORATIONS kwamba….

  (a) Ikiwa ktk mstari wa 1-Yesu anaongea na Wanafunzi na Makutano-Mstari-1, kisha akiendelea kuongea , anawagusa makundi yaleyale au mengine ktk audience namely Wanafunzi-2,3,4, 5,6,7 ,8,9, 10,11,12, kisha Waandishi na Mafarisayo-mistari-13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28,29,30,31,32,33,34,35,36, kisha Nchi/Mji mzima-mistari-37,38,39 anaongea haya in the same flow, kwa audience kubwa-Makutano na particular audience/groups namely Wanafunzi, Mafarisayo, Waandishi, Mji/Nchi then HOW CAN WE SAY KUA MANENO YA YESU MWENYEWE HAPO kuhusu zaka hayatuhusu na hatuna sababu nayo wala cha kufanya hapo kuhusu zaka?

  (b) Na kwanini mchambue Zaka tu hapo ndio si letu?

  (c) Na kama mengine aliyosema hapo, yanatuhusu, umefikaje conclusion iyo? na kwa nini zaka pia lisituhusu?

  (d) Unadhani, Wale wapendwa Waliokuwepo hapo wanamsikia Bwana, walichukua baadhi ya matamshi yake na mengine kuyaacha kua si yao?

  (e) Ikiwa tutachambua ivyo ya Yesu mwenyewe, si ya Wanadamu wenzetu- Yak.5:17-akina Paul, Petro, na kwakua ni Watu kama sisi, si Mungu, then tuna uhuru wa kuwachambua waliyotenda na kunena- yapi ya Mungu kwa vizazi vyote na yapi kwa Utashi, kipindi na tamaduni zao, ni yao tu si lazima yawe yetu hadi leo kwakua hata wao ktk nyaraka zao, wamesema wazi maeneo kadhaa kua wasemayo ni wao si Bwana, itakuwaje kwa maneno mengine ya Yesu kwa subjects nyingine alipokua anaongea na audience kubwa Makutano na kisha akagusa kundi fulani la watu mfano wa maneno kama hayo ni mengi ktk Injili zote namely Math.12 nk, hamuoni kua mnaleta vurugu kubwa ktk maneno ya Master mwenyewe kwa kujitoa kwenu ktk maneno yake kisa kagusa Zaka? na kwa hakika hamuoni mtakua na hard time kujibu hoja hii ikiwa mtaidhinisha kujitoa kwenu ktk maneno ya Yesu kwa WATU WOTE kama ilivyoandikwa hapo? maana kwa maeneo mengine ktk Injili kwa subjects nyingine si hii ya zaka inayogusa noti zenu mnahaha, mtashindwa kujitoa.

  Plz jibu hayo maswali kwa ufasaha au wenzako wanaweza kukusaidia.

  Umesema kama Milinga kua, Ibrahim alitoa hilo fungu la kumi kwa imani! Why do you guys associate Utoaji wa Mtu wa Zaka kwa kuamua kutokana na furaha aliyonayo ya kushinda vita na kuteka nyara nyingi, anaona amshukuru Mungu kwa kutambua na kwa matetemeko akikiri kua kama si Mungu asingeshinda iyo vita? What do you mean kua alitoa kwa imani? Nyie watu vipi jamani analysis zenu?

  Ni kwa hili tu moja ndio umesema substance ivyo naunga mkono kua brother Milinga alikosea kusema Yakobo aliomba maombi ya uchanga.

  Ila hili kua..’’Yakobo, ameitoa hiyo Ahadi kwa uvuvio’’..again, ni zile porojo zako and Unbiblical utterances.

  Hii passage yote, umepoteza space!!!!! you should have gone for a coffee drink-soma tu mwenyewe ulifanya nini sasa!….’’Hapo anapokwenda kupambana na maisha, nyuma yake iko familia yake na hayuko kwa mjomba wake tena; anayo namna moja tu ya kukabiliana na yaliyo mbele yake, KUMTEGEMEA MUNGU!!! Yakobo alikuwa katika kiuno cha Ibrahim wakati alipomtolea lile fungu la kumi Melkizedeki, BAADA YA KUSHINDA, Yakobo yeye akalizunguka jambo hilo akamuahidi Mungu naye kumtimizia hilo kama babu yake, akipewa ushindi!!! Jamani tuutafuteni Utakatifu, ndani yake kuna Amani na Furaha tele itokanayo na kujitambua kwetu kuwa twahusika na Ufalme, kwamba tu sehemu Yake, Bwana akiwa upande wetu…; bali haya yote yawezekana tukiifikia ile hali tuliyoitiwa, prophetic!!!’’’’,….. ni dude gani ilo unajaribu kusema? Afterall, ungeliacha kuliandika, unadhani kuna kitu serious stuff kwa mind na roho tungekosa hapo/umo? Come on boy! wakati mwingine, just rest in peace brother.

  Look at this again, space killing game!!!!!….’’Yakobo alipomtolea Mungu Zaka, hatuna rekodi inayotuambia aliipeleka wapi’’, sooooo? Ehe? Namna gani Kaka Mkubwa, were you ok brother when dropping these?

  Again, check this out! burying space play as usual….’’Basi Zaka zetu zapaswa zitolewe kinabii katika Imani’’

  Ati kutoa zaka Kinabii/Kiimani ni kwa kuisikia sauti ya Mungu inayokuelekeza ilipo huduma yake ya Kikuhan’…… Well, sounds spiritual/Biblical yet useless! The practice is…Toa zaka kwa kutii Neno, don’t wait voice-voice! Its unnecessary spiritualizations of common things.

  This one, great statement yet irrelevant here….’’Ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kujazwa RM wa kweli ili atuongoze katika maisha safi ya Kikristo, nayo Zaka yetu ikiuleta mrejesho wa mabomba yaliyofunguliwa mbinguni pale tulipomuomba Mungu atufungulie hayo!’’

  Again, space elimination on this here again…..’’Mnaiona tofauti ya hizi Zaka? Zaka moja, ile ya Mt 23:23, inapotolewa, hii ndiyo huwa kisababishi cha mabomba ya mbinguni kufunguka, katika siku zake huko AK. Zaka aina ya pili ni hii ya Mwa 28:20 hii inatolewa baada ya mabomba ya mbinguni kufunguliwa, bali sharti uwe wa kinabii maana hii inawahusu hao tu’’…so what are u talking here?

  Kweli mpaka umejishangaa mwenyewe ivi..’’Duh! Nimeandika “mingi”…..Ni kweli ni ‘mingi’’ na yana ‘’manga-manga’’ kweli kweli hence, it is ‘mingi-‘manga-manga’ syndrome.

  Press on.

 43. Sungura,

  How do you know that you are not a boy anyway? do people age up in years or senses biologically and importantly, in our case,Spiritually? Do we fight to be Man? I simply advised not teaching you, you have the choice to take or drop it. Either way, you will have me in both shapes and flavour depending on how you take off and land, I am blessed in both I think! I also know and actually very well aware of SG cores, as a matter of fact, that is among the influencing factors crossed in my mind and pushed me to advise a reccomendable going this time, for this sub-topic of the former.…. you don’t need regularly to comment as if you speak on their behalf, may it stick joyfully and painfully in you that SG, is both ours and we are known to it, our work in here are also acknowledged by it and we both like to serve under its rooms. Be therefore admonished not to behave as if SG is yours, leading you to unhealthy practice of self-crediting or qualifying at its name.

  Sijaribu kujionyesha hapa kua mimi mtoaji bali NAJIONYESHA NA KUKUSHUHUDIA KUA MIMI MTOAJI….nikishakubaliwa na Mungu na mimi nikajifahamu kwa hakika na nikajikubali, ni ruksa toka mbinguni kujionyesha kua niko ivyo-2Timo.2:15a na ushuhuda wa mtu = kujisemelea yake ya kweli, una nguvu ya kutisha kuliko devo na ni Biblical again-Yoh.8:13-18 na kwakua pia, wako wengine wanaoshuhudia kwa ndani, ivyo siwezi ionea haya Injili hii nayohubiri ya Utoaji wa aina zote za matoleo kwa Bwana, zilizoandikwa au zilizowahi kuwepo na hata zile zisizokuwako live ktk Maandiko- za kufulumuka ndani ya moyo wa mtu akishajaa pendo kwa Baba na kuithamini kazi ya Mungu, Watumishi wake na watu wake Mungu in general, AS LONG AS MATOLEO YOTE NA UTOAJI WA KILA AINA uko ktk misingi Neno na hali ya moyoni ya kupenda/kufurahi/kuhiari/kusudia moyoni/raha ndani ya roho/ufahamu wa kujua kazi na mambo ya ufalme kwanza, yetu baadae nk. Na kwa sheria ya roho, uwezekano umepatikana wa yaliyokua batili, mabaya, mateso, laana,kongwa, mzigo mzito, nira ngumu, tazama yanakua mapya, matamu, uhuru, mzigo mwepesi na nira laini. Acha kukuza au ku-negative mambo extremly

  Mfano wako ni mzuri wa Baba kutoa pesa for his family kisha kujisifu Mtoaji,- a good thought again YET NI INAPPROPRIATE kwa sasa maana, leo AJ- hatuna WAJIBU KWA LAZIMA YA KIJESHI au kitisho, hofu ya adhabu/kupigwa hapo hapo na kufa bali tuna WAJIBU KWA HIARI-ndio sheria ya roho. Kua/Kuishi ktk sheria ya roho, hakutuachi huru kwa maana ile mbovu ya kutokua na duty ya kufanya, yaani tujiachie tu, kufanya au kutofanya, holela, kila mtu lwake, bali SHERIA YA ROHO INATU-TASK ZAIDI TENA KWA VIWANGO VIKUBWA YET KWA UPENDO na si kikabali au kupigwa roba, Elewa Kaka somo, usikuze mambo to harbour your unspiritual discharges.

  Wapo Wachungaji tena wengi tu pia naowafahamu mimi wanakemea ubahili, uchoyo, moyo kutu na kuntu, mkono wa bikira, ugumu wa mioyo, ubinafsi uliovuka mipaka kwa MATOLEO YOTE si zaka tu, acha uzushi au kukosa balance ktk kauli zako. Na kama hutoi then kwa mwenendo wako, ukiitwa wewe mwizi , mchoyo, hujali, mbinafsi, jambazi, mgumu wa moyo nk YOTE HAYO SAIZI YAKO NA HAWAJAKOSEA, MKOSAJI WEWE! Kama vipi, wacha tabia izo mbovu kisha angalia wachungaji wako kama watakua na sababu ya kushambulia Washirika tabu na wabinafsi kanisani kama wewe. Narudia tena kauli ya kikakamavu kwelikweli wala haina uchanga wowote kiroho, sema inauma kweli kweli kama msumari kwa aina yenu wakristo kwamba tunahitaji Wahubiri/Wachngaji ma-soja siku za leo, kudeal na Wana wa Mungu waliochukuliwa na anasa na masumbufu ya duniani hii, wakikabwa koo na matakwa hatari ya nafsi zao wanaopuuza kabisa ya maana ya JUU.

  Hard people needs sometimes harsh treatments (both words and deeds to level them), tatizo husomi Neno, umejaza mijineno yako tu, ona hii…Hesabu.20:10-Moses amekasirika kweli kwa vurugu za kila mara za akina ‘Sungura’ wa kipindi kile, anatokea mbele yao na kusema, ‘’Sikilizeni enyi WAASI, mwataka tuwatokezee maji toka mwamba huu? Aliwaita Waasi, wewe mwizi halafu unakataa nini? nani akupeti-peti kukuita malaika wewe wakati tabia na mwitikio wako wa mambo ya Mungu na ya Mtu wako wa Mungu anayekulea hapo ni wizi-wizi tu! kisanii-sanii tu na kelele nyingi za kugomesha watu Kutoa, kisa unajua sana kumzidi Pastor wako, eti umekomaa sana siku izi kiroho kuzidi Baba yako aliyewekwa na Mungu kukuleta ulipofika!

  Najua kinachoendelea kwa BAADHI ya Makanisa, si yote, acha uzushi tena. Don’t take one side problem to represent all. Pia hata kwa hayo yenye ukali kuhusu Matoleo TENA KWA SABABU YA TABIA MBOVU cronic za ubahili na kupuuza ya Mungu na shughuli za hemani mwao, Watu wao wa Mungu, sidhani wewe hunazidi smartness ya kumjua Mungu, kulea watu, kutembea na Mungu, utumishi na uzoefu na mambo ya Mungu na wanadamu- u need to be humble to appreciate their good job, acha majivuno au kujikweza kuona unajua sana au wewe ndio tbs ya Watumishi wa heshima hao ambao watu/kondoo wao wanawapenda na kuwaheshimu, otherwise, hao kondoo wangeondoka maana wako huru, acha kugombanisha Watu na Wachungaji wao, plz when will you stop to assist the devo’s terrible works against the Church and their men and women of God?

  The greatest fact than yours about Zaka ya Ibrahimu to me, si once for all thing/ doctrine yako or act unayo propagate rather, ule moyo wa why alitoa namely, kupenda kumshukuru Mungu kwa ushindi-which means alia-acknowledge kua bila Mungu asingeshinda, that is the spiritual big lesson we get from such story and it is applicable to date. Hii habari ya once for all alitoa zaka,… ehe so? So what seriously? Si ni humanic selfish tactic ya kukimbia utaoji tu unataka ku-resort on ! NimeKUONA! STOP!

  Kwamba nachemsha kuhusu ‘concept’ ya kivuli na kua wala haiongelei suala la kutoa nyingi au kidogo’’. ….Sincerely, sioni kwa dhati, ni kwa jambo/somo gani, utanipata ninachemka Biblically kama si maneno yako ya rejareja/ya kujidai tu patupu! ati nisifahamu mimi nini maana ya AK kua Kivuli na AJ kua halisi wakati the Bible ktk Ebran.10:1 na Wagal.3:24-26 iko so clear kwa ufafanuzi wake wa hapo hapo wala hauhitaji nyongeza? Nilichofanya mimi ni application ya KWELI iyo ya mambo kipindi kile kua kivuli, leo ni halisi….which could mean many things mfano, walitoa kwa lazima, leo kwa uhuru, walitoa Zaka kwa maana ya strictly 10%, leo kwa uhuru Zaka iyo iyo natoa, walienenda kisheria za mwili, twaenenda kwa sheria za rohoni! Simple like that, wewe upigweje lecture ya Neno na Kiroho upone wewe kiumbe?

  Hii…..’’Mtu anaweza akatoa nyingi ‘in terms of number’, na bado akazidiwa na aliyetoa kidogo kwa mujibu wa kanuni ya agano jipya (la rohoni) ya kutoa kwa moyo wa kupenda na kwa kukusudia toka moyoni mwake’’ NILISHAISEMA VENA ktk majibu yangu kwa Milinga, nilitumia terms mbili namely quantity Vs. quality…so huitaji kurudia hapa, unapoteza space, somaga na comment za/kwa wengine ili kupunguza mbwembwe zako au kurudia mambo unnecessarily.

  Wewe hujui kazi ya Mungu inayoweza kufanywa na zaka yangu/zetu? Look at you!

  Look at this devilish question of yours against, at least those true Pastors….’’Na ni nani anayenunua magari kati ya washirika na wachungaji,huna hata aibu ya kusema jambo hili public!’’ NADHANI HULIPASWA KUONA AIBU WEWE MARA MIA KUULIZA SWALI HILO CHILDISH IN PUBLIC NA BADO UNASEMA UMEKOMAA KIROHO, UNAJUA UTUMISHI, WATUMISHI NA KAZI YA BWANA! Again, this shows moyo wako ulivyo! U see…una shida kubwa rohoni! So unawaonea wivu Pastors ku-drive sio? Wapande donkey au bajaji ndio uone wako makini na zaka au sadaka zako! Halafu kama vipi, si uingie u-Pastor maana una nyongo chungu sana against them.

  Sina maumivu yoyote kukubali jambo la kweli. Kama Bible inasema, nipateje maumivi kukubali, acha matamshi ya kienyeji. Halafu usizushe nimekubali! Kwani nimepinga wapi, kwa lipi na lini kwa mambo ya kweli Biblically? Usifosi kupata credit by short cut, work for it and with me at the ring, work hardest man.

  Press on.

 44. Sasa, tukiwa ktk ufahamu kamili, kwamba Sheria ya Zaka iliyoamriwa katika Torati haipo tena, kwamba Ukuhani ulipobadilishwa na Sheria yake ilibadilishwa. Ndio kusema, na jinsi ya Zaka imebadilika! Israeli walitembea katika Sheria iliyoambatana na Utii. Bali Kanisa linapelekwa juu zaidi katika kiwango, likiunganishwa na Ibrahim aliye baba wa imani! Kanisa linarudishwa huko Mwanzo, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.” Hawa wote walikuwa ni wa kinabii! Nalo Neno la Mungu huenda kwa nabii! Ni bahati mbaya kwamba makusanyiko yetu hayana vipawa hivyo, lakini Mungu aliviweka ktk kila kusanyiko lake ili viwe njia ya mawasiliano ya kudumu na wanawe, kwa kukosekana kwake, makundi yetu yamebaki yakijibahatishia tu!!

  Kanisa, lililonunuliwa kwa Damu ya Kristo, ni kusanyiko la watakatifu. Hawa wakiisha kulipokea neno la unabii kutoka kwa mitume, wanakuwa ni wa kinabii,
  2 Pet 1:19 “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, …”! Kwahiyo wanayo mawasiliano na Bwana wao, kwao kila kitu kiko ktk uhalisi wake, hawafanyi mambo ya dini ya kubahatisha bahatisha. Kama ni sadaka wao wanajua hiyo ni nini, maana Roho anayeliangalia Kanisa na mahitaji yake ndiye huyo aliye ndani yao akiwaelekeza jinsi ya mambo yote, lile neno la unabii! Nayo Zaka kwao si kwa ajili ya kuhudumia kusanyiko kama ilivyokuwa ktk Torati, bali wao wanamtolea Mungu kulingana na hali na matarajio yao na shukurani na ibada na shangwe inayoambatana na ushindi!

  Ukizitazama hizi episode mbili za Zaka huko nyuma kwa Ibrahim na mjukuu wake, wote wakiwa ni wa kinabii, waweza kuliona vizuri jambo hili na likakufunza:
  IBRAHIM: Mwa 14:18-20
“Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”

  Kimsingi hapa Ibrahim alitoa hilo fungu la kumi kwa imani. Baraka zilimtangulia, nalo fungu hilo limetolewa katika ushindi alioupata akizijibu fadhila hizo kwa matoleo hayo. Imani ni mawasiliano ya siri kati ya Mungu na wanawe, ule unabii. Basi hawezi tu kujitolea anavyotaka bali kwa maelekezo kama ilivyokuwa kwa Habili. Mungu amelitaka FUNGU LA KUMI tu, naye mwanaye amelielewe hilo na amelitimiza kwa moyo safi wenye kutosheka! Utoaji huu unaishia hapo, haundelei na wala hauna Ahadi!

  YAKOBO: Mwa 28:20-22
“Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

  Kwa kiasi fulani sikubaliani na ndg Milinga hapo anapoyarejea Maandiko hayo akisema, “Kama wewe unasoma kwa makini kabisa utagundua kuwa Yakobo hakutoa zaka kutoka katika mali zake bali mali za wengine alizowanyanganya. Pia aliweka nadhiri kwa Mungu kwamba Mungu asipotekeleza matakwa yake hangetoa kabisa. Aidha, haya ni maombi ya kitoto kabisa.”
  Jambo hili si kweli, hakuna mali iliyonyang’anwa kwa yeyote yule, bali ni haki yake aliyotaka kudhulumiwa! Na pia maombi ya Yakobo hayakuwa ya kitoto kama anavyodai Milinga, bali yanaonesha Ukomavu!

  Yakobo alikuwa anajua kuhusu fungu la kumi alilolitoa babu yake na tukio zima. Hali tete iliyomkabili, ilimlazimu kumtafuta Mungu kwa bidii, ndipo akaiweka nadhiri hiyo, kwa imani akiamini Mungu atamtendea na yeye kuitimiza nadhiri hiyo katika mapenzi ya kukirimiwa na Mungu mafanikio hayo anayoyategemea. Linaonekana ni jambo la kitoto kumkaba Mungu akutimizie kwanza ndipo nawe uitimize nadhiri, yaani kumwekea Mungu nadhiri inayomtaka Mungu afanye kwanza, bali huo ndio UKOMAVU!!! Au haujawahi Milinga kumwambia baba yako kuwa akikununulia uniform mpya utajitahidi uwe wa kwanza darasani au jambo la namna hiyo? Milinga, ungeniambia kuwa Yakobo alikuwa anadeka ningekuelewa!!!

  Tofauti na hilo, ni kule kuwa kama mkristo unayejiendea tu kanisani, huna mpango wowote ule zaidi ya kuwa mwaminifu kwa sheria za kanisa, well, nadhani mishipa inayopeleka damu ya kiroho itakuwa imeziba kwa cholestrol, kwahiyo huna mpambano wowote ule wa kukusogeza karibu ya Mungu mpaka ukawa na jambo la kumuahidi! Tena itazame ahadi ya Yakobo, imeyakamata maisha yake yote , ahadi yake haiko kwa deal moja tu la nyumba unayoingojea ya Airtel huko Kigamboni city, hapana, maisha yake yote!

  Zaka ndg zangu inaonesha ukomavu, Yakobo, ameitoa hiyo Ahadi kwa uvuvio, hapo anapokwenda kupambana na maisha, nyuma yake iko familia yake na hayuko kwa mjomba wake tena; anayo namna moja tu ya kukabiliana na yaliyo mbele yake, KUMTEGEMEA MUNGU!!! Yakobo alikuwa katika kiuno cha Ibrahim wakati alipomtolea lile fungu la kumi Melkizedeki, BAADA YA KUSHINDA, Yakobo yeye akalizunguka jambo hilo akamuahidi Mungu naye kumtimizia hilo kama babu yake, akipewa ushindi!!! Jamani tuutafuteni Utakatifu, ndani yake kuna Amani na Furaha tele itokanayo na kujitambua kwetu kuwa twahusika na Ufalme, kwamba tu sehemu Yake, Bwana akiwa upande wetu…; bali haya yote yawezekana tukiifikia ile hali tuliyoitiwa, prophetic!!!

  Yakobo alipomtolea Mungu Zaka, hatuna rekodi inayotuambia aliipeleka wapi, lakini jambo hilo latufundisha zaidi kuutafuta Utakatifu ili kuondokana na kawaida tulizozilazimisha kuwa sheria, twafahamu kwamba Yakobo alikuwa nabii, nasi wakristo tumeitwa katika unabii, nao hutufikia hapo tunapolipokea Neno la Unabii ambalo walikabidhiwa mitume! Basi Zaka zetu zapaswa zitolewe kinabii, katika Imani, yaani kule kuisikia sauti ya Mungu inayokuelekeza ilipo huduma yake ya Kikuhani; ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kujazwa RM wa kweli ili atuongoze katika maisha safi ya Kikristo, nayo Zaka yetu ikiuleta mrejesho wa mabomba yaliyofunguliwa mbinguni pale tulipomuomba Mungu atufungulie hayo!

  Mnaiona tofauti ya hizi Zaka? Zaka moja, ile ya Mt 23:23, inapotolewa, hii ndiyo huwa kisababishi cha mabomba ya mbinguni kufunguka, katika siku zake huko AK. Hii kwa leo baada ya wakati wake kwisha, sasa inatolewa na yeyote yule hata wanafiki, Mungu hahusiki nayo tena kwa Kanisa lake, ndio maana inaambatana na baraka za kidhehebu kwa wanaoitimiza, na Laana zake kwa wasioitimiza! Zaka aina ya pili ni hii ya Mwa 28:20 hii inatolewa baada ya mabomba ya mbinguni kufunguliwa, bali sharti uwe wa kinabii maana hii inawahusu hao tu, na ni Baraka kwa kwenda mbele!!!!

  Duh! Nimeandika “mingi”

  Mbarikiwe wapendwa!

 45. Sungura,

  Maneno ya Mungu ktk Biblia ndio final truth and athourity ktk yote tunayoshirikishana iwe kufundishana, kubishana kwa hoja kwa nia njema si ilimradi-yale mabishano negative yenye intention devilish or unprofitable humanic yanayokatazwa na Neno pia.
  Kwakua Neno linahimiza mengi kuhusu Utoaji, kati ya hayo ni kama haya:
  Mathayo.6:19-21=Kutojiwekea kwa ajili yetu hazina hapa bali JUU (kuji-prioritize sana sisi at the expense ya mambo ya kudumu mbinguni)maana hazina zetu zilipo ndipo mioyo yetu itakapokua

  Mithali.3:9= Tumuheshimu Mungu kwa mali zetu

  Mathayo.23:1, 23= Yesu mwenyewe akiongea na WOTE- Makutano na Wanafunzi kisha kuwagusa Mafarisayo na Waandishi kuhusu namna walivyotoa Zaka( walivyokua wana –wrongly prioritize mambo), akiwasahihisha/fundisha namna BORA ya kutoa BILA kuacha Zaka-Neno ambalo najua mimi kama Mfuasi wa Yesu, nina sehemu ya kulifanya, la sivyo tukatae kila maneno mengine aliyosema Bwana kwa mambo mengine si Zaka tu kwa Makutano na Wanafunzi kisha akagusa group fulani in particular, jambo ambalo najua hutuwezi kulifanya.

  Na maneno mengine mengi yanayohimiza Kutoa na pia kuonyesha Watu wa Mungu zamani walivyotoa matoleoa mengi na ya aina nyingi na Mungu akafanya nini nao, HUWEZI SEMA KUA HAKUNA MADHARA KWA MKRISTO LEO AKIPUUZA JAMBO HILO. Na kama Zaka ni mojawapo ya aina ya UTOAJI na LEO itakua sahihi kuitoa kwa sheria ya rohoni kama tulivyoelewana, kwanini myimifu wa iyo asiwe na madhara kama vile atakavyokua Mkristo wa ajabu) mwenye madhara ya rohoni na mwilini), asiyetoa na matoleo mengine mengi iwe ya 20% au ya 2% au sadaka nyingine?

  Halafu kwa nini unazungusha jambo jepesi kuelewa? Kama na kwa kua ni kweli kua LEO NIKITOA TOLEO LOLOTE kwa sheria ya roho( uhuru/uhiari/maamuzi ya moyo wa kupenda na moyo wa mtu anayeelewa umuhimu wa kutoa kwa ajili ya kazi ya Bwana anayempenda/ wanapendana na Baba yake, akatoa bila kulazimishwa, kwa nini wewe unashambulia utoaji kwa mfuno wa 10%? Muhimu hapa si sheria ya rohoni na imetimizwa- kwa furaha mtu kaamua ivyo kwa Bwana wake, unaona soo gani?

  A u let me make my point this way? Je wakubali kua kutoa zaka kwa hiari ni sawa leo? Je wakubali kutoa matoleo mengine yote kwa hiari ni sawa leo? Je si kila matoleo yenye baraka leo ni kwa hiari na kusudio la moyo kwa kupenda? Sasa unadhani kwa kua tuna uhuru huo, ina maanisha kua tuna uhuru wa -nikitoa ni sawa na nisitoe yote sawa mbele za Bwana na nisipotoa bado nitakua sawa mbele za Bwana na Bwana ataendelea tu kunibariki sana na baraka zile zile zinazotokana na Mtu kutoa hata kama sitoi maana niko huru ktk AJ, nina hiari ya kutoa sawa, au nisipotoa fresh tu! Unasemaje kwa hili?

  Una maana gani kwa hili…. ‘’baada ya kusema kuwa hakuna madhara, amejikuta analielezea katika muktadha wa sadaka si zaka tena. Fafanua kidogo nikupate.

  Hili ulilosema ni akili njema sana Mdo.26:25- imebarikiwa na nimeipenda sana….’’Kumbe kama Mungu anajua kuwa mwingine uwezo wake ni 10% na mwingine ni 50%, basi Mungu anajua pia kuwa mwingine uwezo wake ni 2%’’-…….Excellent anointed thinking, therefore, WOTE WATOE kwa mifumo iyo ya asilimia au mingine isiyo ya kiasilimia, mimi ninatoa na kimfumo wa kiasilimia I opt/manage from 10% and above.

  Umesema..’’Mimi nilishamwelewa Seleli siku nyingi sana katika hili,kwamba si kwamba hajaelewa mantiki yetu kuhusu kutokutoa zaka. Anachokifanya ni kukwepa kukiri hadharani kuwa mkristo hawajibiki leo kutoa zaka’’

  JIBU: Hujanielewa na unafanya kosa kubwa! SIJAWAHI KUSEMA na kwakua nasoma Neno, siwezi fundisha KUA WATU WATOE ZAKA kwa lazima, sharti!-that is first class notorious uzushi! Ila pia ninyi kama hamtaki kutoa Zaka-kwa mfumo wa asilimia hata kwa sheria ya rohoni ambayo sisi sote tumeikubali-kwa hiari na maamuzi ya moyo wa kupenda, MIMI NATOA na waacheni wengine watoe maana hawalazimishwi na Mtu. Acha uzushi kijana! Hakuna anayekabwa kabari kufanya ivyo.

  Kua ‘’Umenipongeza Seleli kwa kujibu vizuri kuwa hakuna laana wala madhara yoyote. JIBU: Uzushi mwingine huu, SOMA TENA COMMENTS/TEACHING ZANGU- nilimaanisha hakuna laana maana tayari tumebarikiwa ktk Yesu but madhara kwa aliye mwana wa Mungu kutokua Mtoaji wa aina zote za matoleo kwa sharia ya rohoni na Zaka kwa sheria ya rohoni ikiwemo, yapo.

  Press on.

 46. Seleli,
  Kuna jambo moja ambalo limenifurahisha sana, kwamba Seleli eventually umelielewa somo la Zaka!!! Hongereni sana Sungura na Amin, na mwisho Millinga, kwa bidii inayoongozwa na Upendo mliyonayo; Mungu azidi kuwatia nguvu na ujasiri wa kuinena kweli yake. Ninaamini kisehemu kidogo kilichobaki kwa Seleli ni jinsi gani atawakwepa ‘makuhani’ wake; sasa hivi atakuwa anatafakari aitoeje hiyo zaka yake, akiitoa ki Ibrahim au ki Yakobo, “Kuhani” wake atamuelewa kweli? Au ndio utakuwa mwanzo wa kupigwa chini katika huduma na hata kwenye visemina!!! Lakini hayo ni madogo, ilimradi Kweli unayo, utaipata jinsi, kwanza ni mtaalam!

  Pia kuhusu Mt 23:1, 23, sijajua kwa nini unashindwa kuyakamata hayo kimantiki, maana nakujuaga kuwa una akili sana, au wamezimwagia barafu hizo akili? Hivi vifungu unavyoving’ang’ania ndg yangu, inashangaza sana kuwa hauvielewi maana yake licha ya kelele tunazokupigia. Unakuwa ni sawa na mtu ambaye kwa faida ya ubishi au kwa ujinga, unakwenda kujiunga na watu ambao wana kesi ya kuua kwa kukusudia, kila unavyoonywa husikii; basi Hakimu afanye nini nawe umekiri kwamba ulikuwa nao na yote yanakuhusu!!?

  Nilikuambia kuwa ujio wa Kristo uliligawa kundi lake kuwa makundi mawili, moja ndio hili Kanisa na jingine ni hilo linalojumuisha Mafarisayo nk ambao wangali wanaendelea katika Sheria, nayo maneno yaliyoko katika hiyo Mt 23:1-39 yanalihusu kundi hili la wanafiki ambao wewe ndio umejiunga nao upon your own confession!

  Haya kwa faida ya wengine wanaokufuata huko porini, ngoja tuyarejee yaliyojiri hapo ktk Mt 23:1-3 “Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda” Vema, hili ninalikubali kabisa kuwa sote tulikuwepo hapo na kuisikia hiyo kauli ya Yesu, Waandishi walikuwepo, na Mafarisayo pia, pamoja na wanafunzi wa Yesu na hao makutano.

  Sasa tuwatazame mitume (Kanisa) ilipofika saa yao ya kutimia kwa Andiko hilo. Hawa hapa Top cream ya uongozi, ambao wamekalia kiti cha Musa: Mdo 4:5-6
  “Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.”

  … Ile Amri waliyopewa mitume wanayopaswa kuitii: Mdo 4:18
  “Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.”

  … Jibu lao mitume kwa Amri hiyo:
  19-“Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.”
  Mambo yamebadilka, Utii wao si kwa Kuhani Mkuu wala yeyote kati ya hao walioketi ktk kiti cha Musa, wao sasa wako katika Mamlaka nyingine, wako katika Milki nyingine, Ufalme mwingine, Haleluyaaaa! Vinginevyo walipaswa kuwatii makuhani wao!!!

  Haya, liangalie kundi ulilojiunga: hii hapa tena ile Top cream inayokalia kiti cha Musa, … ile Amri kwa kundi la wanafiki: Mt 27:20
  “Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu.”

  … Jibu la wanafiki kwa Amri hiyo: Mt 27:21-23
  “Basi liwali akajibu, akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi katika hawa wawili? Wakasema, Baraba. Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulibiwe. Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulibiwe.”

  Hawa ndilo kundi la wanafiki unaojiunga nao hapo unapolikataa Neno lolote katika Biblia kwa ushawishi wa walimu wako, au kisingizio chochote kile; nakusikia Seleli sauti yako ilivyo juu, unapoulizwa tuwafungulie nani? “Tunataka wanawake wachungajiiiiii!!!” Basi utabarikiwaje katika unafiki???

  Gbu brother!

 47. Seleli,
  U are not talking to a boy,that u can teach him how to speak and behave. U are not here to lecture me how to do it, I know my duties, and I have my own way of doing it. So u better do your own home work brother.

  Kama unadhani niliandika matusi na yakawa publicised, ni vema ukamuuliza aliyekutafsiria ndani yako kuwa hayo yalikuwa ni matusi. Maana hapa SG hatuandiki matusi, na hata ukiyaandika hayawezi kuruhusiwa kusomwa.

  Thank u for understanding brother.
  ——————————————
  Baada ya kusema hayo,sasa narudi kwenye mada.

  Usijaribu kujionesha sana hapa kuwa wewe ni mtoaji, kutoa zaka siyo kipimo cha mtu kuwa mtoaji. Ni sawa na mzazi anayejisema kuwa yeye ni mtoaji pale anapotoa pesa kwa ajili ya kutimiza wajibu wake wa kisheria wa kuitunza familia yake.

  Hakuna mtu aliwahi kusifiwa kwenye biblia kwa sababu ya kutoa zaka. Yule mjane aliyesifiwa na Yesu hakuwa ametoa zaka, bali alitoa kutoka kwa kilichokuwa ridhiki yake ya kutegemewa. Na wale waliotoa nyingi walikuwa wametoa kidogo sana (mabaki) kutoka katika wingi wa mali walizokuwa nazo.

  Kama wachungaji wanachokifanya ni kuwakemea watu wenye roho ya ubahiri,kwa nn wanawakemea kwa habari ya zaka tu, kwani ubahiri wa mtu unapimwa kwa kutokutoa kwake zaka?
  Na sijawahi kumsikia mchungaji anakemea wasiotoa zaka kwa kuwaita mabahiri, bali huwa wanaitwa wezi,sijui wamemwibia hela yake mfukoni,duh!!!

  Seleli usijifanye kuwa hujui kinachoendelea huko kwenye dini kuhusu zaka,najua ni jinsi gani unatafuta mpenyo wa kukiunga mkono kimaandiko,lakini bahati mbaya sana huo mpenyo huwezi upata.

  Hebu ngoja nikupe fact nyingine Seleli unayesema unatoa kwa mujibu wa Ibrahim. Japokuwa ni bora tu ungesema kuwa wewe unatoa zaka kwa matakwa yako mwenyewe, kwamba hata kama Ibra asingetoa wewe ungetoa, na hivyo kuifanya zaka isiwe doctrine.

  Here is that fact:
  Ibrahim unayesema kuwa unatoa kwa mujibu wake, alitoa zaka kwa kuhani mkuu(Yesu kristo) kwa imani ‘once for all’. Hii ni kwa sababu kuhani mkuu mwenyewe alifanya duty yake ya hekaluni (ambayo kwayo alipswa kupewa zaka) once for all, hakurudia tena kuingia patakatifu pa patakatifu kufanya huduma ya kikuhani.

  Unasema utatoaje chini ya kumi, tungekuwa ‘live’ ningekuuliza ni nini hicho unachosema utakitoaje chini ya kumi.
  Lakini kama unayoongelea hapo ni zaka, elewa ukishaitoa zaidi au chini ya kumi hiyo si zaka tena, ni kitu kingine. Hata kama umeandika kuwa ni zaka,kwenye zile bahasha za majina ya watoa zaka mnazoandikaga.

  Halafu kitu kingine unachochemsha ni matumizi yako ya ‘concept’ ya kivuli.
  Agano la kale kuwa kivuli na jipya kuwa halisi, maana yake si kwamba kama la kale walitoa 10%,jipya ambalo ni halisi basi watoe zaidi ya 10%.

  Neno kivuli hapo linamaanisha agano la mwilini,na halisi mana yake ni rohoni. Kwamba agano la kale lilikuwa la mwilini na jipya ni la rohoni. Kwa maana ya kwamba ulimwengu wa roho ni halisi au dhahiri zaidi kuliko wa mwili. Kwa hiyo hapo wala haiongelei suala la kutoa nyingi au kidogo, kama unavyoshadadia.

  Mtu anaweza akatoa nyingi ‘in terms of number’, na bado akazidiwa na aliyetoa kidogo kwa mujibu wa kanuni ya agano jipya (la rohoni) ya kutoa kwa moyo wa kupenda na kwa kukusudia toka moyoni mwake.

  Ona maneno haya ya mtu mchanga kiroho na mwenye kuwaza kwa jinsi ya mwilini. Namnukuu; ”I am tellimg you, kwa nature ya wanadamu tulivyo, hasa akina SUNGURA kanisani, I love cruel and uncompromising speakers/preachers…wawatandike tu na maneno makali ya wezi nyie hata kama yako nje ya context maana hujui maneno ya Bible wewe ila maneno yako tu mengi!”
  Haya ni maneno ya mtu mchanga kiroho,hata hayahitaji majibu!

  Shame on you, ni kazi gani ya Mungu ambayo huwa inafanywa kwa zaka yako?
  Na ni nani anayenunua magari kati ya washirika na wachungaji,huna hata aibu ya kusema jambo hili public!

  Anyway, umeshaukubali ukweli kwamba hakuna madahara wala adhabu kwa mtu kutokutoa zaka. Maneno mengine mengi unayoongea ni kutaka tu kujipoza na maumivu uliyoyapata kwa kubanwa mpaka ukalazimika kuukiri ukweli.

  Japokuwa ni kwa maumivu na kisirisiri, Seleli ubarikiwe sana kwa ujasiri wako wa kuukubali ukweli.

  Asante.

 48. Mpendwa Tumaini Nelson,

  Nadhani kuna mambo hujayaelewa tangu umeokoka. Unapaswa kuendelea kukua kiimani, kimaandiko na kifikra katika roho. Nadhani unaposoma maelezo ya wapendwa wengi hutafakari kwa kina wayasemayo. HASARA ZA KUTOA ZAKA nimezieleza sana huko nyuma. Na wapendwa kama Sungura na Lwembe wameeleza sana. Tatizo wewe unasoma macho yakiwa juujuu. Yaaani unasoma ukiwa tayari umeshahitimisha hoja yaani unahitimisha hoja ya mtu kabla ya kutafakari au kumsikiliza.

  Hapa chini nimenukuu ulichoandika leo saa 7.26 mchana, Umesema ”
  Ujuwe nashangaa saaana coz kila aliyechangia na kutoa maandiko still cjaona hasara ya kutokutoa zaka zaidi zaidi ya faida tupu!kama mpendwa MILLINGA HUJABARIKIWA KWA KUTOA ZAKA UJUWE NI KWASABABU MOYO WAKO UNAHUZUNIKA SAANA NA UNAUMIA SAANA KWENYE KUTOA ZAKA NA MBAYA ZAIDI UNAIPINGA HIYO ZAKA KWA NGUVU ZAKO ZOOTE”

  Hapo wewe umeninukuu na kunihukumu kabla ya kuelewa hoja zangu na msimamo wangu katika mada hii ya ZAKA. Ukweli ni kwamba mimi tangu niokoke na kuyajua maandiko (ngaa kwa sehemu) sijawahi kutoa ZAKA. Na pia sitatoa ZAKA. Kama ni kubarikiwa na Mungu kifedha na kiafya na kifamilia nitabarikiwa kwa kumtolea Mungu kwa kufuata vigezo na maagizo ya mitume na Yesu mwenyewe kuhusu kutoa kwa moyo na hiari kiasi nitakacho mimi. Hivi wewe Nelson ukiwa umeshikilia Tshs 10,000 mkononi mwako ikiwa ni zaka ya Tshs 100,000 uliyoipata, halafu akaja mtu anauguliwa anakuomba umwazime Tshs 10,000 akatibiwe utampa au utakataa kuwa huna pesa kwa sababu tu unasubiri siku ya Jumapl ifike utoe zaka yako Kanisani? Au unatoka mjini kikazi unatembea barabarani unakutana na kiwete au mwenye ukoma, au yatima anaombaomba msaada wa ADA ya shule, je hiyo Tshs 10,000 utampa huyo yatima akasome shule au utatoa kanisani? N a kwa nini?

  Hafafu mimi nadhani wewe Nelson, bado unawaza kitoto sana!! Hebu angalia hapa unavyosema,” ……. .JUST IMAGINE TANGU NIJUE CRI HII YA UTOAJI ZAKA NA SADAKA NYINGINE KWA UAMINIFU NAONA KAPU LANGU LINAJAA KILA CKU IITWAPO LEO!THEN FAHAMU NIMEOKOKA MWAKA JANA TU NA BEFORE HAPO NILIKUWA NAPATA MPUNGA BT HAUELEWEKI UNAKWENDAJE BT NOW UKO TOO SECURED 100% Then Ujuwe Sir God C Muongo Ukifanya Kama Neno Lake Ni Full Neeema Yaan Mimvua Ya Baraka!……..”

  Ujue hapa unajidanganya kabisa. Baraka unazosema kwanza hukuzitaja ni zipi? Pili, unachanganya mada mbili yaani ZAKA na SADAKA NYINGINE. Ulipaswa useme ZAKA tu kwani ndiyo mada hapa. Tatu, hujasema kapu lako linajaa kila siku kutoka kiasi gani hadi kiasi gani? Je, una maana Mshahara wako unapanda kila siku? Je una maana Faida ya biashara zako inaongezeka kila siku? Una maana gani? Be specific bro. Ulitakiwa uniambie kwamba tangu umeokoka mwaka jana kipato chako baada ya kuwa mwaminifu kutoa zaka, sasa kimepanda kutoka Tshs 1,000,000 kwa mwezi hadi Tshs 6,000,000 kwa mwezi, n.k

  Unasema kabla ya kuokoa ulikuwa unapata mpunga na huelewi mpunga huo ulikuwa unaenda wapi? Siyo KWELI. Unapajua. J, utaka kusema ulikuwa unaibiwa bila wewe kujua au ulikuwa unalipia huduma na bidhaa usizojua? Siyo kweli.

  Halafu point zako kadhaa hata sijazielewa. Nanukuu, …….”Hivi Lipi Jema Kuto Kiten Au Kula Bata Bila Kutoa Kiten?Halafu Iwezekane Vipi Umkumjulie God Roho Kwa Kumtole Kiteni Thn Ule Kavu?Millinga Ur Not Serrious My Brother!B Crus MPENDWA!GOD BLESS U!”

  Hapo sijakuelewa kabisaaaaa. Na wewe nakuomba uwe serious. Eleza hoja kwa ufasaha na siyo kwa mbwembwe huku ukiwaacha wasikilizaji wako wakicheeeeeka wewe ukadhani wamekuelewa kumbe wanacheka jinsi usivyoeleza mambo kwa hoja mjarabu.

  Karibu sana.

 49. 1- Huwezi kubarikiwa kwa kutoa zaka (fungu la kumi) hata siku moja.
  My response ni Maswali:
  (a) Umefikiaje iyo conclusion? JIBU: Zaka ni mafundisho ya AG na yamepitwa na wakati. Kwa sasa kwenye AJ ni kutoa kwa hiari kiasi chochote apendacho Mpendwa mwenyewe, kiasi apendacho bila kulazimishwa kwa namna yoyote kama ilivyo makanisani leo eti mpaka uandikwe jina na upewe stakabadhi na usipotoa unatangazwa au kufukuzwa kanisani!!!!! MAJANGA. Utoaji wa kiasi chochote hata kama ni senti kumi ilimradi umeitoa kwa kutaka wewe mwenyewe si kwa sababu ya shinikizo la kiongozi wa Ibada au Mhubiri anayehubiri kwa kufoka, hapo ndipo UTABARIKIWA. Mimi sijawahi kutoa zaka tangu niokoke mwaka 1987 lakini huwa natoa tena sana lakini nisichokipenda ni mahubiri ya kusema kwamba kutoa fungu la kumi ni lazima mpaka wengine wanazidisha hofu kwa waumini eti kutotoa zaka ni UJAMBAZI, UFISADI, nk.

  (b) Kwa nini umesema ivyo? JIBU: Soma maelezo hapo juu.

  (c) Kwa nini Mtu atoe kwa hiari, kwa moyo wa kupenda, kwa jinsi alivyokusudia/amua-pania moyoni mwake kisha kamwe ASIBARIKIWE? JIBU: Nadahani hapa ulisahau msimamo wangu. Soma tena maelezo hapo juu.

  (d) Kuna dhambi gani kutoa fungu la Kumi kwa hiiri ?JIBU: Dhambi ni kwamba utatakiwa kutoa kila mara 10% kwa kila pato. Na usipotoa unajikuta dhamiri inakuhukumu, unasikia sauti ikisema….. hujatoa 10%….., hujatoa 10%…..yaani kila uendako sauti hiyo itakufuata na kujikuta una dhambi ya kutotimiza NADHIRI yako ya kutoa 10% kila mara. Utakuta Mpendwa amepewa 10,000 na mpendwa ili aitumie kula LUNCH halafu anashindwa kula LUNCH ya Tshs 10,000 eti kwanza atoe 10%. Mpendwa amepewa Tshs 2,000 ya NAULI ya kwenda Gongolamboto anaanza kuwaza atoe 10% kwanza shs 200 ndipo atumie Shs 1800 kama nauli. HUU UNAKUWA KAMA UTUMWA FULANI.

  (e) Ili mtu abarikiwe kwa maana yako ya kubarikiwa/ atajirike materially, atoe Matoleo gani? Zaka, Malimbuko, Sadaka za Upendo, Changizo au Isack kabisa?JIBU: Msimamo wangu ni ule ule; UNAPOWAFUNDISHA WATU KUMTOLEA MUNGU EPUKA KUWAAMBIA KUWA WAKITOA KIASI FULANI CHA SEHEMU YA MAPATO YAO NDIPO WATABARIKIWA. Waache wenyewe watoe kwa kipimo chao kulingana na moyo wa kupenda. Zaka, Malimbuko, Sadaka za Upendo, Changizo kama vyatolewa si kama UTAMADUNI bali kwa moyo wa kupenda tena vitolewe kwa SIRI asijue mtu yeyote, HAPO NDIPO UTAAMBULIA BARAKA.

  (f) Kwa jibu la juu hapo,NIHIBITISHIE KUA, UTAJIRI WALIONAO KWELI UMETOKANA na HICHO WALICHOTOA? JIBU: Utoajiuletao BARAKA ni ule tu wa kutoa kwa moyo wa kupenda kiasi chochote bila hofu wa shuruti.

  (g) Na toleo ilo walilotoa lina kanuni gani za KiMungu au likoje mbele za Mungu mpaka kwa hilo Mtu abarikiwe na kwa Zaka kamwe amepoteza muda, asibarikiwe na hata barikiwa? JIBU: Katika AJ mpendwa anayedhani atabarikiwa kifedha kwa kutoa ZAKA anajidanganya. Utoaji uletao BARAKA za kifedha limefafanuliwa vizuri sana na Mt. Paulo kwenye nyaraka zake sina haja ya kurudia hapa.

  (h) How can you BE VERY SERIOUSLY SURE THAT IN THE WHOLE BODY OF CHRIST IN TZ, NEVER EVER HAPPENED THAT GOD BLESSED SOMEONE FOR HIS/HER TITHES GIVINGS? JIBU: Hapa Tanzania matajiri wakubwa waliopo ni Hawa wajiitao Mitume na Manabii na baadhi ya Maaskofu na wachungaji kadhaa. Ndani ya waumini sijui kama kuna muunini ni milionea au bilionea kama hawa wachungaji, Manabii, Mitume na Wazee wa Upako? Sijui. Wahubiri matajiri utawaona tu: Wanatembelea magari ya kifahari sana wakati waumini wao kibao wanaohimizwa kutoa zaka hawana hata ndala za kuvaa achilia mbali nyumba za kuishi. Seleli wewe mwenyewe utakuwa unawajua hao wahubiri matajiri, ila kumbuka wametajirishwa na zaka za waumini wanaoendelea kuwa maskini kila kukicha. Unamkumbuka Mhubiri mmoja alitoa rambirambi Tshs 15,000,000 kwenye msiba wa Dr. Moses Kulola? Je unamkumbuka Mwingine aliyetoa Tshs 10,000,000? Wahubiri kama hao ndio Mamilionea hapa Tanzania? Je, hizo pesa wamezipata wapi? Je, wanafanya biashara gani mpaka waweze kufika kwenye msiba wa Kulola wakiwa na magari ya kifahari ikiwemo HAMMER? VX, V8, nk?

  Nadhani nimejibu maswali yako Seleli kama siyo yote ni kwa sababu ya ufinyu wa muda.

 50. Mpendwa Edwin Seleli na Tumaini Nelson,

  Huko nyuma nadhani mwaka jana kama siyo mwaka juzi 2011 mada hii tuliijadili sana hapa hapa SG. Seleli na Tumaini ninyi hamkuwepo kabisa wakati huo kwenye kuchangia mada hii. Hii mada imekuwa ikijirudia tena na tena kwa sura tofauti.

  Kabla sijacomment chochote kwa hoja zenu mlizotoa hapa naomba msome makala hii kwanza ingawa haya niliyaeleza mwaka mmoja uliopita wakati mada hii ya zaka imeletwa ila kwa faida ya Seleli na Nelson naomba nirudie hata kama wenzangu wameshayasema naomba usichoke Seleli, tunajifunza hapa:

  Hebu jaribu kutafakari kwa kina kuhusu maandiko haya yatumiwayo kuhimiza wapendwa wa Agano Jipya kutoa zaka.
  Kisha jiulize mafundisho hayo ni sahihi?

  Tuanze na Waebrania 7:1 Kwa maana Melikizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, na tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; 3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. 4 Basi angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, AMBAYE IBRAHIMU, BABA YENU MKUU, ALIMPA SEHEMU YA KUMI YA NYARA. 5 Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, WANA AMRI KUTWAA SEHEMU YA KUMI KWA WATU WAO, YAANI, NDUGU ZAO, KWA AGIZO NA SHERIA, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.

  Andiko hilo linatuonesha kwamba Ibrahimu alitoa 10% kutoka kwenye nyara alizopata na wala siyo katika mapato ya mali zake. Pia tunajifunza kuwa Walawi walipewa haki ya kula 10% kutoka kwa ndugu zao kwa maagizo ya sheria za Musa.

  Andiko lingine ni hili la Mwanzo 28:20. Inasema, ‘YAKOBO AKAWEKA NADHIRI AKISEMA, MUNGU AKIWA PAMOJA NAMI, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. 22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; NA KATIKA KILA UTAKALONIPA HAKIKA NITAKUTOLEA WEWE SEHEMU YA KUMI.

  Wahubiri wote wanaorejea maandiko haya na kuyatumia kuhimiza kanisa la sasa limuige Yakobo, wanapaswa kusoma tena vizuri neno kwa neno kabla ya kuweka mkazo katika maandiko haya.

  Kama wewe unasoma kwa makini kabisa utagundua kuwa Yakobo hakutoa zaka kutoka katika mali zake bali mali za wengine alizowanyanganya. Pia aliweka nadhiri kwa Mungu kwamba Mungu asipotekeleza matakwa yake hangetoa kabisa. Aidha, haya ni maombi ya kitoto kabisa.

  Kama unamwomba Mungu akupe kazi au ajira ukaweka nadhiri kuwa ukipata ajira mshahara wako wote wa kwanza utamtolea Mungu na utamtolea 10% bila kusita, Jaribu kuwaza upya nadhiri hiyo.

  Ukifuatilia maandiko vizuri utaona kwamba Yakobo hakutoa hata hiyo nadhiri aliyoiweka. Hata kama aliitimiza (kama kuna hilo andiko linalothibitisha) YAKOBO HAKUTOA ZAKA KILA MWEZI AU KILA MARA KAMA WANAVYOTAKA WAHUBIRI WA SASA.

  Andiko lingine ni Walawi 27:30-34. Inasema, ‘Tena zaka zote za nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA. 32 Tena zaka yote ya ng’ombe, au kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA. 34 Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwangiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.

  Hapa tunajifunza kuwa kama kuna mpendwa ana mifugo yoyote, kuku, mbuzi, ng’ombe, kondoo, bata, n.k anapaswa kutoa 10% ya mifugo hiyo. Kama una ng’ombe 50 watano wanapaswa kutolewa zaka, au kama una kuku 40 elewa kuwa kuku (hupaswi kuwauza ili ukatoe pesa) bali unapaswa kutoa kuku 4 kama zaka. Hilo ni kwa mifugo yote.
  Andiko lingine ni Hesabu 18:21-25, Inasema, ‘Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithiwao, badala ya huo utimishi wautumikao, maana, nihuo utumishi wa hema ya kukutania. 23 Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. 24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote. 25 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwa zaka mkononi mwa wana wa Israeli, niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongezayo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.

  Tunaona kuwa makuhani waliamuriwa kurithi zaka peke yake, hawakupaswa kuwa na mali yoyote zaidi ya kula zaka tu. Hata hivyo walipaswa kutoa zaka pia kutoka katika zaka iliyotolewa na waisraeli.

  Somo kubwa hapa ni kwamba kwa kuwa kazi za kikuhani zilikwisha hasa zile za kusongeza sadaka za wanyama kwa ajili ya Mungu kuleta rehema kwa Waisraeli, hakuna tena kazi za kikuhani katika nyakati za leo. Kwa hiyo hakuna tena mwenye haki ya kurithi zaka kama walawi wa enzi za Musa. Tunapaswa kuelewa hivyo kwa sababu maandiko haya hayawakatazi wachungaji kumiliki mali za aina mbalimbali kiasi kwamba wanapaswa kuishi kwa kutegemea zaka za Wakristo tena. Utaratibu huu umekoma pale tu sadaka za kuteketezwa zilipokoma kwa Kifo cha YESU.

  Andiko lingine linalotumiwa sana kutoza zaka ni Malaki 3:7- 12. Inasema , ‘Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gain? 8 Je! Mwanadamu atamuibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gain? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 NINYI MMELAANIWA KWA LAANA; MAANA MNANIIBIA MIMI, NAAM, TAIFA HILI LOTE. 10 LETENI ZAKA KAMILI GHALANI, ILI KIWEMO CHAKULA KATIKA NYUMBA YANGU, MKANIJARIBU KWA NJIA HIYO, ASEMA BWANA WA MAJESHI; MJUE KAMA SITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI, NA KUWAMWAGIENI BARAKA, HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA, AU LA. 11 NAMI KWA AJILI YENU NITAMKEMEA YEYE ALAYE, WALA HATAHARIBU MAZAO YA ARDHI YENU; WALA MZABIBU WENU HAUTAPUKUSHA MATUNDA YAKE KABLA YA WAKATI WAKE KATIKA MASHAMBA, ASEMA BWANA WA MAJESHI. 12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana watakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi

  Watumishi wengi hutumia andiko hili kuwahukumu watu ambao wanapata matatizo katika biashara zao, wanaopata hasara, wanaofukuzwa kazi, wanaougua magonjwa, wanaokosa kuzaa watoto-tasa/ugumba, wanaovamiwa na majambazi, wanaopata ajali barabarani, nk. Eti hayo yote hayangewapata kama wanatoa zaka.

  Mhubiri mmoja alisema kwamba kama tunatoa zaka hatutapungukiwa fedha kabisa. Kama tunatoa zaka kwa ukamilifu hatupata hasara katika biashara wala hatutaacha kupandishwa vyeo kazini kwa sababu tu tunatoa zaka.

  Watu wengi wamejaribu sana kutetea zaka kwa kusimamia andiko hilo na kuwaahidi watoaji wa zaka baraka tele sana na kwamba mataifa yote yatawaita wenye heri.

  Wapendwa tunapaswa kuelewa kwamba andiko hili lilikuwa linawahusu Waisrael pekee hadi leo hii. Andiko hili liliwataka waisrael watoe zaka ya mazao yao ili kwenye ghala kuu la Serikali kuwemo chakula cha kutosha kulisha watu maskini na yatima na wajane. Waisraeli walitoa zaka zao kama mataifa mengine yalivyotoa kodi kwa serikali.

  Hata leo tunapaswa kuelewa kwamba hakuna mtanzania asiyetoa kodi kwa njia ya VAT au Income Tax au Ushuru. Kwa sisi kutoa kodi serikali inapata uwezo kununua chakula toka kwa wakulima ili chakula kiwe kingi katika ghala la taifa na kuweza kuwasidia wale wanaokumbwa na maafa katika nchi. Hapa Tanzania wafanyakazi walioajiriwa ndio wanaoongoza kwa kutoa kodi iitwayo PAYE (Pay As You Earn) kila mwezi. Kodi hiyo ndiyo inayoendesha serikali na kuweza kutoa huduma za jamii.

  Kutotoa kodi huleta laana katika taifa lote. Kukwepa kodi za TRA ni kujiletea laana kwako na taifa lote. Ndiyo maana Yesu akasisitiza kuwa ‘YA MUNGU MPENI MUNGU NA YA KAISARI MPENI KAISARI’ kwa maana nyingine; Kila Mkristo anapaswa kulipa kodi kama wajibu wake lakini asiache kumtolea Mungu pia, au Usimtolee Mungu pekee ukaacha kutoa kodi za serikali.

  Zaka ilikuwa ndiyo kodi ya waisrael wote. Kutotoa zaka wakati ule ilikuwa ni kuleta laana katika taifa kwani lingeshindwa hata kulisha watu maskini pamoja na kulipa watumishi wa serikali ya Israeli ambao walikuwa makuhani.

  Katika mfumo wa serikali ambayo inaendeshwa kidini, zaka inakuwa ndiyo kodi ya serikali.

  Nabii Malaki alitumika kama vipaza sauti vya TRA mtaani vinavyopita kila mwisho wa mwaka kuwakumbusha wafanyabiashara wote kutoa kodi ya mapato kabla ya tarehe 30 Juni kila mwaka. Malaki naye alifanya kama TRA kuwakumbusha waisrael kutoa kodi ili maghala ya chakula yajazwe akiba za vyakula kwa ajili ya uendeshaji wa serikali ikiwemo makuhani waliopaswa kulipwa ujira kutokana na zaka.

  Andiko lingine ni Mathayo 10:9- 10: Inasema, ‘Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mshipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake.
  Wahubiri wengi wanahimiza kutoa zaka kwa hoja ya maandiko haya kwamba Mtendakazi amtumikiaye Mungu anastahili apewe ujira wake. Ikiwa yeye ni mtumishi wa kweli wa Mungu, anatakiwa asaidiwe na kwa njia ya zaka zetu.

  Wanasema ni amri iliyotolewa na Mungu mwenyewe kwamba tunapaswa tutoe zaka na kutoa sadaka ili kuisaidia Nyumba ya Mungu na watenda kazi wake.

  Haya yote yanatafsiriwa hivyo baada ya kuyageuza makanisa yetu kuwa kama makampuni ya biashara na mashirika ya kijamii yanayoajiri wafanyakazi na kuwalipa mishahara.

  Je kama ZAKA ni kwa ajili ya kulipa ujira watendakazi shambani mwa Mungu, ni Makanisa mengi hulipa mishahara watendakazi wake kutokana na zaka zitolewazo? Je watendakazi ikiwa ni pamoja na wahudumu, mashemasi, wazee wa kanisa, wachungaji, na wanakwaya, nk ndio wanaolipwa au ni mchungaji pekee anayelipwa? .

  Kuhusu zaka, changamoto zipo nyingi sana na kuna maswali mengi kuliko majibu yake. Wapendwa wengi huyakwepa maswali hayo.

  UBARIKIWE!!!!

 51. Lwembe,

  May be in love I should advise you, Don’t waste my/our/your time brother or complicate things!

  Mambo mengi so far ktk mada ile ya Zaka tuliyomaliza na hii sub-topic yake sasa ni clear yako tuliyokubaliana na yaliyo sawa na Neno, si kukubaliana tu kama Ccm/Cdm. HUITAJI KUSEMELEA MAMBO AS IF HAKUNA AGREED GROUND SO FAR!

  Nimeshasema tena na tena, Zaka nina/tunaijua kila mtu humu namely…

  (a) Kabla ya Sheria-Ibrahimu-Mwz.14:1-20, nia ya kuitoa-Mwz.28:15-22

  (b) Wakati wa Sheria-Musa-Hesb.18:1-32, na kunukuliwa vitabu vingine kama eg Neh.10:37-39

  (c) Wakati wa Neema-Sheria ya rohoni-Mathayo.23:1, 23 au kama iyo ya Math bado mnakana maneno hayo ya Bwana hayawahusu ingawa mlishindwa kabisa kujibu hoja kwa nini maneno mengine ya Yesu akiongelea mambo mengine si ZAKA na akawa-address groups za Watu wengine kama yanawahusu au la, basi njia/hekima ni hii… kwa maoni yangu, chukua yote ya wakati wa sheria, then leo yafanye yote kwa sheria ya rohoni yaani kwa hiari/kusudio la moyoni/furaha/raha/maamuzi ya utashi na pendo lako kwa Mungu, it will be fine with you and still Biblical and Godly.

  Therefore, usiunde hoja baseless kua hatuelewi au kua tunatoa zaka kwa sheria ya Musa, hii ulongo-ulongo tu. Maneno yenu punguzeni, speak substances, bring the Word, make senses here.

  Aya sasa una jipya lipi hapa? Una mtoka gani Kaka baada ya mimi kuweka sawa ivyo?

  Press on.

 52. Ninachofuatilia sana katika michango ya watu hapa.hasa wanaotoa zaka ni mtu atakayesema kuwa kuna madhara ya kutokutoa zaka.

  Seleli naye kakubali kuwa hakuna madhara, japokuwa ameingiza neno ‘but’ kwa harakaharaka.

  Hilo neno ‘lakini’ aliloliweka baada ya kusema kuwa hakuna madhara, amejikuta analielezea katika muktadha wa sadaka si zaka tena. Nami nakubaliana naye kuwa kuna madhara katika kutokumtolea Bwana au kutokuwa na moyo wa utoaji.

  Kumbe kama Mungu anajua kuwa mwingine uwezo wake ni 10% na mwingine ni 50%, basi Mungu anajua pia kuwa mwingine uwezo wake ni 2%.

  Lakini kitu cha ajabu kabisa ni kwamba Mungu hata haangalii uwezo wa mtu tu akakomea hapo,bali anaangalia zaidi hali ya moyo(attitude). Kama hali ya moyo ni mbaya unaweza ukatoa hata kila ulichonacho na isimguse Mungu.

  Mimi nilishamwelewa Seleli siku nyingi sana katika hili,kwamba si kwamba hajaelewa mantiki yetu kuhusu kutokutoa zaka. Anachokifanya ni kukwepa kukiri hadharani kuwa mkristo hawajibiki leo kutoa zaka. Hawezi kukiri kwa sababu anajua ni kwa kiasi gani kufanya hivyo ataonekana ni muasi katika dhehebu lake, maana huko asiyetoa zaka hata kama ametoa 40% ya mshahara wake kwenye sadaka au changizo, huyo huhesabika amemwibia Mungu. Huko ndiko wanaitwa vibaka,wale ambao hawatoi zaka.( hata mimi nimetokea huko, najua)

  Utasikia mtumishi anasema ‘ una uhuru wa kufanya chochote na pesa yako, lakini zaka hiyo usiiguse maana ni ya Bwana, vinginevyo unatafuta laana’. Very sad!!

  Sasa kwa kukwepa hicho ndio maana anajificha kwenye kichaka cha kutoa zaka kwa hiari,lakini anajua kabisa kanisani kwao inafundishwa kuwa zaka si hiari, bali ni lazima mtu atoe maana hiyo ni ya Mungu.
  Huwezi kumwekea mwanao sheria kuwa, ikifika saa kumi na mbili jioni lazima awe amesharudi nyumbani, halafu ukamwambia ati afanye hivyo kwa hiari.

  Kuna watu wao walishajiambia kuwa akiwa na sarafu hawezi kusimama kwenda kutoa katika kapu la sadaka, wengine walishasema kama kipato chake kwa wiki ni laki moja lazima kila J’pili atoe si chini ya elfu 40.
  Huo ni utaratibu mzuri sana,lakini hawatakiwi kuufanya kuwa fundisho (doctrine) kwamba kila mtu afanye hivyo, no!

  Nakupongeza Seleli kwa kujibu vizuri kuwa hakuna laana wala madhara yoyote.

  Bless u!

 53. Sungura,

  Sijakoma nini! Tunakomeshana kwani!

  PLZ UNAWEZA JTAHIDI KUA NA NIDHAMU AT LEAST KWA MADA HII ILI TUENDELEE KUJADILI VEMA MAANA MADA ILE ULIONGEA MENGI YA KIENYEJI NIKAMEZA! Natumaini umejifunza na this time, utakua makini,mtulivu, nidhamu, uangalifu ktk maneno yako, ondoa maneno na lugha za matusi,kashfa na mambo ya taarabu words ili twende vema. Mada ya kule nilikua vile sometimes kwa sabubu ya aina ya mjio/mtoko wako. Umeshajifunza tokana na makosa kua mimi si wa kuvamia ovyo or cheaply kama ambayo umekua ukifanya kwa kila mtu almost humu, usifanye kosa tena hilo. Kama hutakubaliana na na kuenendana na ushauri huu ili tujadiliane na kukosoana kwa dhati na ustaarabu, then I can be in all things/situation to fit all- you are welcome to provoke me to such moves. I SHALL JOIN you rockefully and more powerfully than you.

  Naamini na najua kwa maneno mengi au machache, natoa hoja nafundisha mengi na yenye tija, Biblical, thoughtfull, challenging, ideas bulding, truths and facts cementation and kuleta tafakari kubwa ktk mambo ya Mungu, maisha yetu ya utumishi na wokovu, ku-analyse nature ya mwanadamu inapokuja swala la kuchukua mambo yanayoigusa nk.. Unless unionyeshe/nikosoe kwa hoja ndipo nitajua nimekosea wapi, otherwise, utakua unapenda kuropoko tu, huna kitu kwangu. Pia natumia Neno la Mungu kusema/fundisha, si maneno tupu kama…….!!!!!

  Kuhusu Mitume kurudia kila kitu Yesu alifanya na kutenda=Try to be a BALANCED blessed thinker brother- nilitaka kupanua ufahamu kua, yako mambo Mitume walifanya ambayo Yesu hakuwahi kufanya mfano msisitizo wa Paul kuhusu nafasi ya Wanawake ktk kanisa, kwa iyo swala kua Mitume na Manabii hawakuwahi kusema kuhusu Zaka, to me, si hoja unless mjibu why pia walifanya mengine ambayo Master hakufanya. Kwaiyo nilitaka kusisitiza kua kama Yesu alidokeza kuhusu ZAKA, inatosha kwa mimi kutenda kwa kua Bwana final authority than Mitume na Manabii. To me what Jesus said/taught/touched comes first and carries much weight and Mitume/Manabii na Watumishi wengine past, present and future comes second.

  Kwamba umesema si lazima leo KILA mtu atoe kwa njia ya ZAKA, aliyebisha nani? toka tumeanza mpaka tumemaliza mada ile na sasa hii, si kila mmoja amebaki/atabaki na dizaini yake? So what is the problem? Ulikua umelala ukaibukia kuandika hapa au?

  Nitatoaje chini ya Kumi? Kwani Biblia inasemaje? Tatizo una maneno mengi yako bila angalau mara moja-moja kuya-TBS na Neno la Mungu. Ebrani.10:1-AK ni kivuli cha yajayo na Gal.3:23-26-AK lilikua Tutor…sasa kama uko kwa kivuli/tutor – basic scale ilikua 10% but kwa LAZIMA na at least iyo ndogo Mungu ndio aliona waitoe… leo nikipick from basic tutor/kivuli scale yet kwa HIARI/FURAHA/MAKUSUDI YA MOYO/RAHA YANGU NA BWANA nikafanya ICHO KIPIMO NA ZAIDI, kuna dhambi au laana/utumwa gani? Think big yet anointifully brother. Na kama kweli sasa nilivyookolewa, napendwa ivi, nimetendewa haya yote, nakwenda mbinguni, napenda kujiachia kwa Bwana, sina haja ya kukaa au kubani-bania niliyonayo, yote na vyote nilivyonavyo napenda viwe na agenda ya Mbinguni seriously, kwa nini kwa raha/uhuru/kusudio la moyo/hiari na akili ya utu uzima kiroho na kitumishi, NISIFIKIRIE KUONGEZA IYO SCALE YA 10% ya TUTOR WETU wa kale na kupaisha viwango kuanzia hapo ili kumpenda sana na kumfurahisha once and for all pure TUTOR WETU WA LEO AJ? Think again big Brother and desire to be spiritual not carnal when it comes to your shekel being called by heaven.

  Watu kulalamika kuhusu wao kukemewa kwa roho zao za choyo na kutanguliza kwanza yao na ya Mungu yalale, is none of my business! As a matter of fact, ningependa waandamwe zaidi ili wawe na akili ya JUU kwanza kisha ya Chini later. Why, kununua magari, kulipa kodi, karo, kwenda kwa supu, kununua pamba za X-mass, graduation, simu, kukamua vocha, kununua gifts za Wachumba/Mke/Mume, kununua pefume kali, simu, kwenda mechi kulipia game, kununua plot ni mambo ambayo wanalipa na kama hawana watakopa na kuuza walivyonavyo na wengine hata kuimba ilimradi kukidhi haja za mwili na nafsi izi, halafu Kanisani na kwa kazi ya Mungu, mbembelezwe/peti-petiwee/mletewe ice cream na kuimbiwa simama dede pipi Baba analeta, muombwe msamahaa, mtafutiwe taiming ya kuambiwa kuhusu changizo, zaka, ili kuwakumbusheni kutoa,? mpaka mlie-lie na kutishia kuhama kanisa! I am tellimg you, kwa nature ya wanadamu tulivyo, hasa akina SUNGURA kanisani, I love cruel and uncompromising speakers/preachers…wawatandike tu na maneno makali ya wezi nyie hata kama yako nje ya context maana hujui maneno ya Bible wewe ila maneno yako tu mengi! imeandikwa ..IWE KWA HILA AU BILA HILA, INJILI ITAHUBIRIWA!….Huna Bible au your Bible is small, hujui kuna ilo andiko! Au nikupe lile…Paul alisem..dizaini ya wengine, inaBIDI KUWAOKOA KAMA KWA MOTO! Na njia moja wapo ndio iyo, Watoe tu Zaka hata kwa maneno makali ili sisi tukahubiri Neno au hapo hemani mambo yakae sawa.

  Kwamba, Hakuna madhara yoyote ya kutokutoa zaka,hayapo!!!! Sasa unakomaa nini? tulia kwanza.Swali: Kuna madhara yoyote kwa Mkristo KUTOTOA Matoleo kwa Mungu? Mkristo asiyetoa, ana shida au hana?

  Press on.

 54. Milinga,

  Reference to Nico na Tumaini,

  Milinga Venrando, Kuna baadhi ya uliyosema hapa, Napata shida kukubali na hata kuyaelewa, nitaeleza na kukuuliza.

  1- Huwezi kubarikiwa kwa kutoa zaka (fungu la kumi) hata siku moja.
  My response ni Maswali:
  (a) Umefikiaje iyo conclusion?

  (b) Kwa nini umesema ivyo?

  (c) Kwa nini Mtu atoe kwa hiari, kwa moyo wa kupenda, kwa jinsi alivyokusudia/amua-pania moyoni mwake kisha kamwe ASIBARIKIWE?

  (d) Kuna dhambi gani kutoa fungu la Kumi kwa hiiri ?

  (e) Ili mtu abarikiwe kwa maana yako ya kubarikiwa/ atajirike materially, atoe Matoleo gani? Zaka, Malimbuko, Sadaka za Upendo, Changizo au Isack kabisa?

  (f) Kwa jibu la juu hapo,NIHIBITISHIE KUA, UTAJIRI WALIONAO KWELI UMETOKANA na HICHO WALICHOTOA?

  (g) Na toleo ilo walilotoa lina kanuni gani za KiMungu au likoje mbele za Mungu mpaka kwa hilo Mtu abarikiwe na kwa Zaka kamwe amepoteza muda, asibarikiwe na hata barikiwa?

  (h) How can you BE VERY SERIOUSLY SURE THAT IN THE WHOLE BODY OF CHRIST IN TZ, NEVER EVER HAPPENED THAT GOD BLESSED SOMEONE FOR HIS/HER TITHES GIVINGS?

  Otherwise, nitachukulia statement yako kama a SERIOUSLY WRONG AND UN-NECESSARY BOLD UTTERANCES AMBAYO ILIMUHITAJI MHUSIKA KUSITA KWANZA KABLA YA KUICHILIA FREELY AND THOUGHTLESSLY!

  2. Ibrahimu na Yakobo hawakutoa ZAKA kila mwezi wala kila mwaka, walitoa Zaka kwa imani siyo kama sheria.
  My response: Ni kweli kabisa na ulilosema ndiyo tumeshasema sana ktk mada iliyopita ya Zaka kila mwezi au kwa kipato!, kwa iyo, kwamba Ibrahimu alitoa kwa imani – na sahihi zaidi tusema, kwa hiari na furaha ya kumjua na kumpenda kumshukuru Mungu wake( maana kusema kutoa kwa imani is so weird to chew!), HAIHIHITAJI KURUDIA-RUDIA. Brother, You are late in here, U NEED TIME KUSOMA COMMENTS nyingi kama si zote za mada ilie ya Zaka ili uwe relevant, connected and updated kabla ya flow kwa kwa hii sub topic almost ya ile.

  TAKE EXTRA NOTE: Kuhusu Yakobo na Zaka, Tunachokiona kwa mara ya kwanza si kutoa zaka- HAKUTOA bali moyo wake wa UTAYARI kutoa Zaka wakati au kama BWANA akimfanyia mambo safi-Mwz.28:15-22

  3. Hakuna LAANA yoyote kwa Mkristo asiyetoa ZAKA. Wala hakuna adhabu yoyote
  My response: Ni kweli BUT-notice- it’s a big… ‘’BUT- yako madhara kwa Mkristo au mwana wa Mungu kutokua na tabia ya Kutoa-Imeandikwa.. Heri Kutoa kuliko kupokea na in this case au kwa nia ya wengine humu…’’ni heri kutoa kuliko kubania! Ni hekima na inalipa mbinguni kuwafundisha Watu kua ni kweli Mungu ni mwenye upendo, si lazima aoperate kama zamani za AK au AJ- kanisa la kwanza kwa kutandika/ua/piga hapo hapo, LAKINI kwakua tunampenda naye atatupenda na mtu umpendaye, utapenda umfurahishe na kufanya mambo yake/yenu, yasonge mbele, yastawi basi KUTOA MATOLEO YOTE, SI ZAKA tu, Ni njia bora ya kuyakuza na kusuma mbele mambo yenu wapenzi wawili

  4. Sheria ya kutoa ZAKA iligongomelewa MSALABANI sasa tuko HURU. Tunamwabudu Mungu na kumtolea sadaka na dhabihu za midomo na mali zetu si kwa vipimo tena vya mahesabu ya ten percent, zaka au fungu la kumi.
  My response: Ni kweli yet bado vipimo ivyo na kuzidi vikitumika kwa hiari, furaha na maamuzi ya Mtu mwenyewe kwa pendo lake kwa Mungu, hamna shida wala si dhambi na si kwenda kinyume na Bible.

  5. Kutoa ZAKA au FUNGU LA KUMI katika Agano Jipya ni kutojua NYAKATI NA MAJIRA tulizonazo na walizokuwanazo wenzetu wa Agano la Kale
  My response: Kutoa Zaka leo itakua tatizo tu kama ikitolewa ktk mfumo wa zamani-yaani lazima kutenda-ndio sheria but kama kwa furaha na moyo wa kukusudia na raha zako kwa Mungu, HAKUNA SHIDA KABISA NA KUISHI MAJIRA HAYA KWA MOYO HUO NA ZAIDI, INAMAANA ZAIDI

  6. Mtu Akipata Tshs 1,000,000 kisha akamega Tshs 500,000 akamtolea Mungu yaani akatoa fungu la HAMSINI au 50 percent na wewe ukang’ang’ania kutoa Fungu la Kumi au 10 percent ni nani ATAPATA BARAKA?

  My response: Nimependa point yako no.6 na nimenukuu hapo baadhi ya sehemu yake. Yote ni mema, mtu atoe kwa njia ya 10%, 20%, 50%, 70%,100%, the bottomline ni yote yanafanyika kwa sheria ya roho wa uzima yaani furaha, hiari, amani, utashi, kwa kupenda, kwa ufahamu wa siku zote kumtanguliza Mungu kwanza ktk tuliyonayo, moyo wa shukrani.
  Angalizo: Kipimo cha Mungu kubariki mtu hakiko ktk wingi au uchache wa yale tumetoa, kwa ivyo ni hatari na si sahihi kwakweli kuwafundisha watu kua anayetoa fungu la 50 huyo lazimi atabarikiwa sana kuliko wa fungu la 20, 30, 10! Najua ukweli kua Imeandikwa ‘’apandaye haba….na kwa wingi ata….. LAKINI UFAFANUIZI WAKE-that actually God intended/meant, ni my take kua… before kupanda haba/wingi..WHAT IS THE STATUES OF THE HEART? ITS MOTIVES/UKWELI WA DHATI WAKO KABLA YA KUPANDA HABA/WINGI-that counts a lot…Kama 10% ndio uwezo wake na Mungu anajua ivyo na yule 50% ndio level yake, scale ya Mungu hapo si quantity bali quality-Hao wote kwa Mungu wametoa sawa! Mfano wa mama wa kutoa shilingi na matajiri kumwaga mahela yakutisha, finalizes Godly what I have said…Luka.21:1-4

  Kuhusu point yako ya no.7, nilishajibu/toa maoni yangu kwa maswali uliyotuuliza wapendwa wote hapa. Kama una objection, Karibu.

  Press on.

 55. Seleli,
  Hujakoma tu kutulazimisha kudanganyika kwa maneno mengiii!?

  Sasa kama haikuwa lazima kwa mitume kurudia katika nyaraka zao yale aliyosema Yesu, wale watu wa mataifa ambao hata hawakuwahi kuijua wala kuishi kwa torati ya Munsa wangeyajuaje aliyosema Yesu baada ya kumwamni kama si kwa njia ya kuambiwa na mitume?

  Kwa nini unalazimisha sana kitu ambacho hakipo, kiasi kwamba hata hujulikani unasimamia nini?

  Mimi nilikwambia si lazima leo kila mtu amtolee Mungu kwa njia ya zaka. Na kama wewe unapenda kumtolea Mungu kwa mtindo wa % (asilimia) basi fanya hivyo,lakini ujue kuwa ukishaizidisha au kuipunguza hiyo si zaka tena, maana hakuna sheria ya zaka inayokuruhusu kuizidisha wala kuipunguza.

  Mara nyingi unapenda kusema unaweza toa hata zaidi ya 10%, lakini hakuna sehemu umejaribu kusema kuwa unaweza toa hata pungufu ya 10%.
  Najua huwezi kusema pungufu kwa sababu Malaki anasema habari za kuleta zaka kamili. Kwa hiyo bado uko chini ya hofu ya torati kuwa ukiwa unamtolea Mungu less ole iko juu yako. Seleli wewe bado ni mtumwa wa torati.

  Na kama huwa unatoa zaidi ya 10% na huku moyoni mwako ukiwa na concept kuwa hicho ulichokitoa ni zaka, umelaniwa Seleli, kwa mujibu wa sheria ya zaka.

  Get out of the ditch brother, just have a mindset of giving to God. Forget of the concept of tithing, u cant manage to practice the principle of tithing under the new testament. New wine into old wine-skins-impossible Seleli!

  Ulishasikia watu wangapi wanalalamika kuhusu kutoa sadaka, bila shaka ni wachache au hakuna kabisa. Lakini zaka imekuwa kongwa zito kwa sababu ya mashutumu wanayoambiwa watu na wachungaji, mara waitwe wezi, mara majina yabanbdikwe, mara waambiwe watapigiwa kelele ya ‘mwiziiiiii’ ati ili malaika wawakimbize kama wezi.

  Kwa nini pastors wanafanya hivyo?; Ni kwa sababu wameshika sheria kuwa mtu lazima atoe zaka, lakini sadaka ni hiari yake.

  Ndipo nikakuuliza ‘kwa nini zaka mpaka watu waandike majina????

  Hakuna madhara yoyote ya kutokutoa zaka,
  hayapo!!!!

 56. Ujuwe nashangaa saaana coz kila aliyechangia na kutoa maandiko still cjaona hasara ya kutokutoa zaka zaidi zaidi ya faida tupu!kama mpendwa MILLINGA HUJABARIKIWA KWA KUTOA ZAKA UJUWE NI KWASABABU MOYO WAKO UNAHUZUNIKA SAANA NA UNAUMIA SAANA KWENYE KUTOA ZAKA NA MBAYA ZAIDI UNAIPINGA HIYO ZAKA KWA NGUVU ZAKO ZOOTE .JUST IMAGINE TANGU NIJUE CRI HII YA UTOAJI ZAKA NA SADAKA NYINGINE KWA UAMINIFU NAONA KAPU LANGU LINAJAA KILA CKU IITWAPO LEO!THEN FAHAMU NIMEOKOKA MWAKA JANA TU NA BEFORE HAPO NILIKUWA NAPATA MPUNGA BT HAUELEWEKI UNAKWENDAJE BT NOW UKO TOO SECURED 100% Then Ujuwe Sir God C Muongo Ukifanya Kama Neno Lake Ni Full Neeema Yaan Mimvua Ya Baraka!Hivi Lipi Jema Kuto Kiten Au Kula Bata Bila Kutoa Kiten?Halafu Iwezekane Vipi Umkumjulie God Roho Kwa Kumtole Kiteni Thn Ule Kavu?Millinga Ur Not Serrious My Brother!B Crus MPENDWA!GOD BLESS U!

 57. Mpendwa NICO, SELELI na TUMAINI na wengineo,

  sikieni UKWELI NI HUU:

  1. Huwezi kubarikiwa kwa kutoa zaka (fungu la kumi) hata siku moja.Hakuna ushuhuda wa mtu yeyote aliyetajirika kwa sababu ya kutoa zaka. Kama unabisha nipatie watu wachache tu kanisani kwako waliotajirika yaani waliopanda kipato chao toka mamia kwenda mabilionea kwa sababu tu walikuwa waaminifu kwenye kutoa zaka kanisani.

  2. Ibrahimu na Yakobo hawakutoa ZAKA kila mwezi wala kila mwaka. Kama walitoa walifanya hivyo mara moja maishani mwao basi (They offered tenths once and for all in their lifetime). Halafu kama walitoa, basi ujue walitoa Zaka kwa imani siyo kama sheria.

  3. Hakuna LAANA yoyote kwa Mkristo asiyetoa ZAKA. Wala hakuna adhabu yoyote. Wanaonukuu Maandiko ya MALAKI 3 wanatafsiri nje ya maana halisi na huenda hawajui walengwa wake ni akina nani(They translate the text out of contextual meaning).

  4. Sheria ya kutoa ZAKA iligongomelewa MSALABANI sasa tuko HURU. Tunamwabudu Mungu na kumtolea sadaka na dhabihu za midomo na mali zetu si kwa vipimo tena vya mahesabu ya ten percent, zaka au fungu la kumi.

  5. Kutoa ZAKA au FUNGU LA KUMI katika Agano Jipya ni kutojua NYAKATI NA MAJIRA tulizonazo na walizokuwanazo wenzetu wa Agano la Kale

  6. Kutoa FUNGU LA KUMI yaani kumtolea Mungu shilingi moja kati ya kumi, au laki moja kati ya Milioni kumi, kwa kweli ni kukosa adabu mbele za Mungu atupaye vitu vyote. Haingii akilini kwa mtu mwenye Shilingi 1,000,000.00 kumtolea Mungu Shs 100,000 halafu ukaondoka madhabahuni ukijigamba eti hapo Mungu amepokea Sadaka zako, kwa kweli hapo ni uongo mtupu. Hebu tafakari kwa KINA. Wewe umefanya kazi umepata Tshs 1,000,000 kisha unachukua Tshs 100,000 unaenda kutoa Kanisani kisha unabaki na Tshs 900,000 hivi wewe na Mungu nani zaidi? Kwa nini watu wa nyakati hizi za Agano Jipya tunashindwa kuelewa UKUU wa Mungu? Hivi wewe na Mungu nani alistahili kubaki na Tshs 900,000? Kwa nini wahubiri wengi badala ya kuhubiri watu watoe SADAKA ZENYE KULETA BARAKA wanaendeleza mahubiri yenye kuleta LAANA. Je, Mtu akimtolea Mungu Tshs 900,000 akabaki na Tshs 100,000 mwingine akatoa kinyume chake kati ya hao wawili ni nai atakayepata BARAKA? Au mtu akipata Tshs 1,000,000 kisha akamega Tshs 500,000 akamtolea Mungu yaani akatoa fungu la HAMSINI au 50 percent na wewe ukang’ang’ania kutoa Fungu la Kumi au 10 percent ni nani ATAPATA BARAKA?

  7. UKWELI NI KWAMBA MITUME WOTE WA YESU HAWAKUWAHI KUTOA ZAKA WALA KUWAHI KUFUNDISHA SOMO LOLOTE LA ZAKA HATA KIDOGO KAMA ILIVYO KWA WAHUBIRI WA KANISA LA LEO. TAFAKARI.

 58. Milinga Venerando Juma and Tumain Nelson,

  Asanteni kwa Words of appreciations zenu and all glory goes back to our Father above. Amen and Amen kwa maneno yako ya inspiration Mr. Tumaini Nelson, uzidishwe nawe ktk Neno na moyo wa utoaji mwanzo mwisho…..give, give, give like crazy but clever!!!!!!!! give give, give like never before mwanzo mwisho mpaka ajapo Bwana then, ukishafika JUU, you WILL CLEARLY and JOYFULLY REALISE that DATA BASE YA HUKO HII.. Rev.20:12 ni tririons times smatter to capture your data than these cheap Bill Gates tools hence each dot and jot of your giving works/ministry is accurately recorded, thus, do more to fill the pages if not files and folders.

  TAFADHARI: Tunatofautiana njia/huduma/vipaji ktk KUFUNDISHA/ KUJADILIANA/ KUSHARE MKATE, ivyo tukubaliane kua kila mtu hana haja ya kua mwingine bali awe yeye original kwa jinsi Bwana alivyomfanya, kumpa na kumtumia- mfano, BINAFSI sipendagi kujibu kifupi-fupi hasa mwanzo wa kitu( maswali/mada/mjadala) na hasa zile mada/issues/maswali aidha tata au yenye ubishi mwingi au yenye ugumu kueleweka kwa wengi au yale yanayoweza kua twisted na sisi Wanadamu kwa faida zetu na si za Mungu na kazi yake, ndio maana naanza kwa lecture ndefu kwanza.

  Milinga,
  Umepata muda kweli wa kupitia mada yako ya KUTOA ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato tuliyojadili wengi pia ofcoz ‘kumenyana’ na Sungura kwa sana na hatimaye tumefikia mwisho, kila mmoja akichukua lwakwake-kwakwe kivyake vyake? Kama hujasoma comments zote au hukufuatilia kila mchango, well, sitashanga sana maana ni nyingi na bila shaka hatuwezi kuwemo humu blog 24/7 ilihali maisha mengine yanatudai, however, nilitaka kudokeza kama ingekua ulipitia kila comments, baadhi ya maswali yako, usinge yauliza au ungeyauliza kwa njia nyingine maana aidha yamejibiwa kabisa au yamegusiwa au yamepewa ground ya mtu mwenyewe kung’amua kweli/jibu ni lipi. Ukipata muda, pitia mada iyo iliyokwisha ila sasa ninagusia maswali yako kama ifuatavyo na si ajabu nikadondoa baadhi ya yale yale tuliyokwisha semezana na Sungura topic iliyopita maana maswali yako ndio yanatupelekea huko tena, hamna jinsi.

  Maswali yako ni both tricky and Biblical truths searching/confirmations, hence nitachangia ktk majibu na nadhani wengine watatoa inputs zao pia, ruksa kupinga/kukubali/kujazilishia hoja zangu, pia nami nitakua na uhuru huo huo kwa hoja zako au feedback yako. Karibu.

  SWALI 1. Kama Zaka ni sheria kwa wapendwa wa Agano Jipya ni kwa nini Mtume Paulo na Mitume wenzake hawakuwahi kutaja Zaka katika Mafundisho yao yote?
  JIBU/MAELEZO: Ktk Agano Jipya, hakuna SHERIA ZA KIMWILI kama ilivyokua Agano la Kale ila ni KWELI TUPU kua ktk AJ tuna SHERIA ZA ROHO.( Notice: Ni Sheria bado yet za Roho/rohoni. Kwa iyo, kwamba tuko huru kwa kua hatuko ktk sheria, si kweli, ni statement yenye mapungufu Biblically!!!!!!! tumeokolewa ili kuingizwa kwenye sheria za Roho ambazo moja ya tofauti yake kubwa na za Kimwili, ni kwamba izi za Kiroho tunazitenda kwa kua tunampenda Mungu, lile pendo ndani yetu, linatusukuma kwa raha na furahu KUMFURAHISHA MPENZI WETU.Zamani walitenda kwa hofu( hofu ni kinyume cha pure love and utulivu ndani ya Baba) maana wangekosea au wasingetenda, adhabu zilikua ni za kimwili na tena live wakati mwingi.

  Kwa sasa hatutendi mapenzi ya Mungu kuanzia nje kwenda ndani bali ndani kwenda nje, huo ndio UTIMILIFU WA SHERIA YA MWILI-TORATI kwa KUSIMIKA/ ESTABLISH/ ANZISHA SHERIA MPYA YA ROHONI- ALIKOKUSEMA NA KUMAANISHA YESU- Math.5:17- ndio maana mifano yake ya kutimiliza torati/uanzishaji wa sheria mpya ya rohoni ni kwamba si mpaka uzini( kuonekana nje live umevunja sheria ya Kimwili bali kule ndani ukishatamani, tayari umevunja sheria mpya yaani rohoni-

  Kwahiyo Zaka haiwezi kua sheria leo kama zamani(LAZIMA KUTEKELEZA KWA HOFU YA KUADHIBIWA) lakini yaweza kua sheria ya rohoni kama sheria nyingi tu tulizo nazo leo wa AJ kwa kutolewa ktk ktk moyo wa uhiari, shukrani, utayari wa kama Ibrahimu baada ya Bwana kumtendea makuu-Mwz.14:1-20 au pia yaweza tolewa kwa mujibu wa maneno ya Yesu kwa Makutano na Wanafunzi wake ktk Mathayo 23:1 alipogusia Zaka wakati-anawa-address Mafarisayo na Waandishi in particular ktk mstari wa 23 which also meant, yaliwahusu wote kwa kua, in the first place, ktk mstari wa 1, audience ni Makutano na Wanafunzi na hata ktk mistari mingine iliyofuata, alikua anawachanganya wote, mara anaongea kwa Mafarisayo mara Wanafunzi nk, hii ilikua kawaida yake tu( Kuongea na Wote lakini pia ktk maongezi yake, kugusa makundi kadhaa) hata ktk maneno mengine maeneo mengi kwa issues nyingine nyingi si hili la zaka tu-mfano Math.12 nk.

  Kwanini Mitume hawakuwahi kutaja zaka? Jibu sijui lakini Yatosha na NI MUHIMU/INA UZITO WA KIPAO MBELE ZAIDI Yesu AKIONGELEA JAMBO KULIKO MITUME,NABII AU MTAKATIFU YOYOTE MKUU/MAARUFU, kwa ivyo alitaja na kusisitizia ktk Mt.23:23 ivi…’’Bila ‘kuyaacha na hayo mengine’( yapi? Ya Zaka)

  Angalizo: Kwa wao kutotaja, kusifanyike assumption isiyo na mashiko kwamba WALIKATAZA! Au ILIKUA DHAMBI KUTOA ZAKA, Itakua rahisi sana kuindosha iyo assumption kwa hoja nyingine/ assumptions/ evidences nyingine direct and indirect za Scriptures zenye nguvu zaidi, maana bila shaka wasingeweza enda kinyume na comment ya boss wao ktk Math 23:23 maana wengi wao walikuwepo siku iyo na walimsikia na ndio maana wakaandika statement iyo ya Bwana wao kuhusu utoji zaka ktk namna bora ktk AJ.

  SWALI-2. Katika Mitume WOTE wa Yesu si Petro wala Paulo waliohimiza waumini wa nyakati za Kanisa la Kwanza watoe ZAKA, Kwa nini?
  JIBU: Soma maelezo/majibu kwa swali la kwanza, pia kwa kua Biblia iko kimya, nami sijui na hata tuwe makini kua-assume kwa kua hawakuitaja na sasa wasema hawakuihimiza then, tunataka kua–conclude nini? Nyongeza ni kwamba, tutafakari kua, ilikuaje Wanafunzi/Mitume walifanya baadhi ya Maneno na Matendo ambayo Yesu hakuwahi kuwaambia au kusisitiza? Una habari iyo? Unadhani walikosea kufanya ivyo? kwani ni lazima KILA WALICHOFANYA NA KUTENDA KIWE KILE YESU ALIFANYA? VILE VILE JE KAMA YESU ALIFANYA/SEMA KITU, NI LAZIMA WARUDIE KILA KITU KTK NYARAKA NA MATENDO YAO NDO TUJUE SASA KWAMBA, KWA KUA NA WAO WAMEKIFANYA/TENDA KAMA YESU ALIVYOFANYA NA KUTENDA BASI NA TUTENDE SASA!

  Si yatosha sana Yesu akitenda na kunena na pia si yatosha sana Mitume na Manabii wakitenda na kunena maana walipewa chance iyo-kutenda makuu zaidi ya …. na pia yapo walitenda na kunena kama Watu( ya kwao) na pia kama Neno kwa vizazi vyote. Cha msingi naanza kwa Yesu, natenda alichosema kisha natenda na yale ya Mitume na Manabi yaliyo ya vizazi vyote-si ya desturi na taratibu za mhusika kwa eneo fulani na maongozi yake kwa kundi alilopewa na Bwana kwa wakati huo ktk tamaduni iyo.

  SWALI-3. Kama ni ZAKA ni sheria inayoendelea mpaka vizazi vya Agano Jipya ili kuwawezesha Makuhani waweze kusimamia kazi ya Bwana hapa duniani, Je, KUHANI maana yake ni nini? Je, Kuhani wa Agano la Kale ni sawa na hawa wachungaji wa Agano Jipya?

  MAJIBU: Namna ya utoaji wa Zaka AK haundelei kama ulivyokua mpaka uku- yaani kuhama mzima-zima kama ulivyo AJ! Huku Utatoa zaka na hata zaidi ya zaka kwa msukumo na hasa MAAMUZI yanayotoka na kuzijua na kuzipenda sheria mpya ya rohoni namely out of raha, furaha, shangilio la moyo, uhiari, love bila hofu nk. Kutoka ktk Sheria za Mwili kuja za rohoni si KWAMBA KUNATU-EXCUSE MAMBO BALI NDIO KUNATU-TASK ZAIDI ILA KWA UPENDO NA FURAHA-ndio maana nyingine ya nira yangu ni laini( notice: bado ni nira) na mzigo wangu ni mwepesi( notice: bado ni mzigo!!!!- no wonder alisema…Kumfuata Yeye… kwanza kujikana kisha kubeba msalaba halafu kumfuta KILA SIKU!

  Kuhani wa Agano la Kale WAKATI WA MUSA-Sheria, alikua ni strictly toka kabila moja tu la Walawi-Hesb.18:1-32, lakini kuhani wakati wa Ibrahimu-kabla ya sheria, aliyepokea Zaka-Melkizedeki hakua hata ktk kabila la Walawi- Waebrania.7:1-24 ivyo Makuhani wale si sawa sawa na hawa wa leo kikabila( literally speaking), leo kwa mujibu wa AJ ni sisi sote TULIOOKOKA/ZALIWA MARA YA PILI-1Peter.2:9-10.

  Swali lako jingine kua Kuhani maana yake nini? JIBU: Ni jina la cheo/huduma! Na kama swali lako lingekua Kuhani ni nani? Jibu ni…. kwa AK ni Mtu toka kabisa la Walawi aliyefanya kazi/utumishi ktk hema ya kukutanikia/nyumba ya Mungu-Hesb.18:1-32 na Nehemia.10:36-37

  SWALI-4. Kama ZAKA ni sheria halali katika Agano Jipya (Maana kuna sheria nyingi za Agano la Kale zimefutwa na Yesu mf. ile ya kutokula kitimoto, sungura,kumbikumbi, kusali siku ya Jumamosi, nk), Je ni akina nani kanisani wanaopaswa kisheria kula ZAKA? Je, ni WACHUNGAJI, MAASKOFU, WALIMU, MANABII, WAINJILISTI, WANAKWAYA, WAZEE WA KANISA, WALINZI WA MALI ZA KANISA, WAJANE,YATIMA, MASIKINI?

  Jibu: Zamani zaka iliamriwa itolewe kwa Walawi kwa kua hawakua/ hawakuruhusiwa kua na ardhi-which should simply mean kwamba hawakua na permanent means to earn living which again meant( my own spiritual comprehension ya intention ya Mungu why afanye utaratibu huo kwao)-Nathani Mungu alitaka moyo, akili, mawazo na kila kitu chao kielekezwe ktk huduma maalumu na nyeti iyo bila kusumbukia tumbo na ndipo Mungu aliye fair, akafanya utaratibu wa kuwahakishia utulivu wa nafsi- si unajua tena mwanadamu akikosa shekeli, kunywa na kula, kufanya huduma kwa amani na moyo wakati mtoto kafukuzwa shule hakuna karo,kodi ya nyumba huna, nk, ni kazi. Pia Mungu akasema anawapa ruksa kupewa/kuchukua zaka ili iwe reward kwao kwa utumishi wao hemani-Heb.18:1-32

  Lakini pia walihudumia hata Wahitaji wengine kama wageni, wenye shida malangoni pao kwa zaka ila ukiniuliza mimi, kipi hasa kilikua ktk moyo wa MUNGU kufikiri/kuleta utaratibu huo, jibu ni Kuwahudumia Walawi kwa kua kupata watu permanent kuhudumu ktk hema ya kukutania, it is my take kua iyo kwa Mungu took first priority/weight-rather a pushing factor kwa utaratibu huo kuja.

  Leo nani ale kama sisi wote ni Makuhani? Nitajibu swali ilo Biblically na kwa reasoning/akili pia-which is also Biblical anyway as long as it doent not violate the Word-Mdo.26:25.

  Kwakua AK ni kivuli cha yajayo yaani AJ-Ebra.10:1 na kwa kua hata leo, tunayo hema za kukutanikia ambamo huku kuna Watu wanafanya utumishi muda mwingi kama si permanently kama Wachungaji,Wazee, Mashemasi, Wainjilist, Mitume, Waalimu, Wafanya usafi, Walinzi nk na kwakua pia tunao wahitaji kama Wajane, yatima, Wazee wakongwe, basi Watakula zaka hao. LAKINI kama vile navyoamimi intention ya Mungu hasa ya kwanza kipindi kile kuleta utaratibu huo wa zaka ilikua kuwawezesha na kuwatuliza Walawi wachape kazi bila pressure na kupoteza focus na concentration ya kazi yao nyeti, naamini na ni hekima Mchungaji au mwenye huduma yoyote ya kudumu but akiwa ktk nafsi ya kuchunga Watu hapo awe Mtume, Mzee wa Kanisa nk kwanza akawa ktk hali bora kisha wengine.

  Itakua ni tendo nzuri kusaidia kila mtu/mhitaji lakini litakua ni tendo pia LISILO NA HEKIMA ukimwacha Mlawi wako wa madhabahuni au kazi na maono yake ovyo kama si hoi. Unaweza fanya jambo zuri bila hekima bado likawa bovu tu-sawa na kutoa zaka yako ukaishia kumpa mlinzi kanisani na pale madhabuni kwa Mlawi hoi, nyumbani huko ni Mungu saidia. Lakini pia ikitokea Mlawi wangu ni Bakresa, bado nitaanza kwake kwa maana ya mimi na binafsi yangu kuziteka zile baraka za Kondoo kwa Mchungaji kisha nitatenda kwa wengine. Ila pia tukumbuke balance ya Yesu..’’Masikini/wahitaji tunao siku zote…which meant-First things( Priorities) first then second-Wahitaji walio nasi kila siku…nafasi ipo ya kuwabariki. To me, madhabuhuni pakitulia na anayehusika hapo akitulia, ALL SHALL BE WELL KWA WENGINE. Amen

  Press on.

 59. Nimeliona jambo moja la kusikitisha, kumbe watu wengine hawajui hata Zaka ni nini! Ninawaona wanavyoyachanganya mambo si kawaida, zaka, matoleo, sadaka, changizo na vyote wanavyovijua vinavyohusu kutoa, wamevirundika katika fungu moja! Hata wenzao wanapojaribu kuwafundisha, hawaelewi, sijui wanaogopa kusahihishwa!!!

  Kwanza ni vizuri tukajifikisha ktk ufahamu kwamba Mungu si masikini na wala hana shida ya chochote kile, kwahiyo huko kumtolea kwetu ni kulingana na Mapenzi yake yanayotufunza Wajibu! Na moja wapo ya matoleo yanayotufunza Wajibu ni toleo la Zaka, FUNGU LA KUMI la mapato yetu, hili ndilo linaitwa Zaka, ukileta zaidi au pungufu, maana yake aidha hauijui Sheria inayoliongoza jambo hilo au ni mjinga wa kujitakia au mwizi!

  Kwahiyo tunapolizungumzia jambo la Zaka, tunapaswa kuyasikiliza Maandiko. kwa kadiri yanavyotuongoza. Zaka inayotolewa kwa uongozi wa Sheria, iliondoka na Sheria yake. Mkristo yoyote anayeitoa Zaka kwa jinsi ya Sheria atakuwa amedanganywa, licha ya kwamba jambo hilo ni zuri, lakini linakuwa bora zaidi na lenye manufaa zaidi iwapo litafanywa kulingana na misingi inayoliongoza!

  Wakristo wengi wanajaribu kuyavusha mambo yaliyokwisha, kutoka Agano la Kale, yale ya Torati, na kuyaleta katika Agano Jipya. Bali hilo ni kinyume na linawagharimu kwa vile hakuna anayewajibika kwa hayo, maana Mungu alikwisha yafunga katika ujio wa Kristo, pamoja na Zaka, labda madhehebu yetu yanayoitoza hiyo!

  Kristo ndiye MWISHO wa Sheria, nayo Zaka iliyo sehemu ya Sheria hiyo inapaswa ikome na Sheria yake iliyo izaa!

  Kwahiyo faida na adhabu, vinavyoandamana na Sheria iliyokoma, HAVIPO maana vimekoma na Sheria yake!

  ….Nitaendelea, nijaribu kuyagusa aliyoyaleta Millinga

 60. Nelson Tumaini,
  Sijui kama unaelewa maana ya maneno yanayosema ‘bila sheria hakuna dhambi’.
  Unachotakiwa kujua ni kwamba tatizo si mtu kutoa moja kati ya kumi, maana hata kabla ya hiyo sheria watu walikuwa wanatoa hata zaidi ya moja kati ya kumi, au nje ya hiyo sheria watu wanaweza tu kutoa zaidi ya moja.

  Tatizo linaanza pale unapomwambia mtu kuwa ni lazima akipata kumi ahakikishe kuwa ile moja ameitoa pasipo kukosa. Hapo ndipo mwenye kupenyeza dhambi palipo na sheria(yaani shetani) anapopata nguvu ya kuhakikisha mtua ameivunja ile sheria ili nafsi yake iwe chini ya hukumu na ikose ujasiri mbele za Mungu.

  Na kwa sababu hiyo basi Mwana wa Mungu akaja kuitimiza kwa ukamilifu sheria iliyokuwepo (torati) ambayo kimsingi iliwashinda wanadamu wote. Na akisha kuitimiza/kuitenda kwa ukamilifu torati na matakwa yake yote, akaleta agano jipya ambalo linaiondoa ile lazima ya mtu kutoa moja kati ya kumi.

  Katika hilo agano jipya akisha kuondoa hiyo lazima,akaweka kitu kinachosema kuwa katika kumi toa chochote unachotaka wewe kutoa. Hakikisha tu unakitoa kwa moyo wa kupenda. Kwenye huu uhuru,yule mwenye kupenyeza dhambi palipo na sheria ana mwanya mdogo sana au hana kabisa wa kumfanya mtu atende dhambi,maana sheria ambayo ndiyo huwa nguvu ya mtu kutenda dhambi pale anapoivunja haipo tena.

  Ndipo unawakuta akina Paul wanasema kila mtu na afanye kama alivyokusudia moyoni mwake,si kwa kulazimishwa.

  Huku ndiko Yesu alikokuita ” Mwana akiwa weka huru mtakuwa huru kwelikweli”.
  Mitume kwa kujua siri hii,walikataa kuweka hili kongwa la sheria katika shingo za kanisa.

  Inashangaza sana mnapoyafuata jararani mambo amabayo muda wake wa matumizi (expiry date) umeisha na kulazimisha kuyatumia tena.

  Ama kweli mtu akizoea utumwa uhuru kwake huwa ni mzigo mzito kuliko ule utumwa wenyewe.
  Nelson yafahamuni haya ili mpate kujua raha na maana ya uhuru wa kristo kwa sisi tunaomwamini.

  Msidhani Agano la kale na Jipya kuwa pamoja kwenye biblia zenu maana yake ni vitu vinavyofanya kazi pamoja. Kuna tofauti kubwa mno kati ya haya maagano mawili. Agano jipya limegharimu damu ya Mwana wa Mungu.

  Ameni!

 61. Wapendwa kwakweli nimefuatilia mada ya kutoa zaka kila mwezi na hii hapa na nimefuatilia saana!mpendwa SELELI ameonyesha moyo wa dhati kabisa wa kufundisha kwa upendo na ameonekana kutochoka kabisa ingawa amekutana na challange nyingi bt GOOD ENOUGH ROHO MTAKATIFU AMEKUTUMIA VIZURI SANA!Mengi yamezungumzwa na mengine yanajirudia bt kikubwa ni kuomba kupata neema ya MOYO WA UTOAJI.Kwani kama wapendwa tungeipata hiyo tucngeumiza vichwa kiasi hiki kwa jambo ambalo ni very easy kwa mpendwa mwenye moyo wa kutoa!yaani tucngekuwa tunapiga chenga nyingi wakati game hii inataka watu tupige pass zinazonyoka kama za OZILI AMBAZO NI ZA USHINDI MWEPESI KULIKO TUNAVYOCHEZA GAME NGUMU KAMA YA TIMU FLANI HIVI HAWA WENYE POINT 7!HAWA MAN CJUI NANI!MPENDWA SELELI MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO ALIYOKUPA!

 62. Wapendwa,

  Swala la kutoa zaka na faida zake limekuwa likipata mjadala mpana sana na maelezo mengi hapa. Ila kwa sababu kuna wasomaji wapya ndiyo maana wakati mwingine mada huwa zinajirudia.

  Nawapongeza wote walioshiriki huko nyuma kutoa maelezo au mafundisho mengi na marefu na kwa wakati huu hapa pia hasa mpendwa Edwin Seleli.

  Hata hivyo, mimi kwa leo naomba nisieleze maelezo meeengi bali nitoe changamoto tu kuhusu zaka:

  1. Kama Zaka ni sheria kwa wapendwa wa Agano Jipya ni kwa nini Mtume Paulo na Mitume wenzake hawakuwahi kutaja Zaka katika Mafundisho yao yote?

  2. Katika Mitume WOTE wa Yesu si Petro wala Paulo waliohimiza waumini wa nyakati za Kanisa la Kwanza watoe ZAKA, Kwa nini?

  3. Kama ni ZAKA ni sheria inayoendelea mpaka vizazi vya Agano Jipya ili kuwawezesha Makuhani waweze kusimamia kazi ya Bwana hapa duniani, Je, KUHANI maana yake ni nini? Je, Kuhani wa Agano la Kale ni sawa na hawa wachungaji wa Agano Jipya?

  4. Kama ZAKA ni sheria halali katika Agano Jipya (Maana kuna sheria nyingi za Agano la Kale zimefutwa na Yesu mf. ile ya kutokula kitimoto, sungura,kumbikumbi, kusali siku ya Jumamosi, nk), Je ni akina nani kanisani wanaopaswa kisheria kula ZAKA? Je, ni WACHUNGAJI, MAASKOFU, WALIMU, MANABII, WAINJILISTI, WANAKWAYA, WAZEE WA KANISA, WALINZI WA MALI ZA KANISA, WAJANE,YATIMA, MASIKINI?

  Natamani kupata maelezo kwa wapendwa……

 63. Edwin Richard,

  Nakubaliana na wewe kabisa na labda ninaweza kukukaribisha ktk mada inaitwa ‘’Kutoa zaka kila mwezi au la! Ashukuriwe Roho Mtakatifu kwa kua kule tumejadili sana na nilifundisha somo zima kuhusu UTOAJI generally kisha Specifically Zaka. Uliyoyasema kuhusu Utoaji generally yaani tabia moja wapo ya Mungu iyo, imefafana kiasi kikubwa na niliyosema na pia ufahamu wako kuhusu kuwatunza na kuwawezesha watumishi(nia nzuri iyo ya KiMungu), ni sawa sawa na niliyosema, hence, RM anathibitisha hayo kupitia wewe hapa. Ubarikiwe na tafuta iyo mada pia usome uko, utabarikiwa sana.Amen

  Everist,

  Ni sawa yako madhara( hata tusiposema kuhusu adhabu) za kuwa na moyo sugu, mnyimivu, ubinafsi, choyo, kujipenda wenyewe kuliko Mungu, kufikia hatu ya kula kila kitu. Hata 1 kati yote 10, huna mpango, yote 10 unameza mwenyewe! Ukristo wa ivyo unasema mambo mengi mabovu juu ya maisha ya aina ya mpendwa wa ivyo, ni hatari na masikitiko kwa kazi na Waumishi wa MUNGU. Ukiwa na wapendwa wa software hiyo, ya wao kwanza na Mungu baadaye/pending kabisa au aachwe kabisa, hasa noti zao zikiguswa ni shida kanisani kusema kweli. Lakini waangalie watu hao hao wakishughulika na mambo ya maisha yao eg kupata magari, job, kuoa, kuolewa, kununua plots, kwenda beach,mbuga za wanyama, kununua nguo nk, watafikia hatua hata ya kukopa na kujinyima kabisa ili kujifurahisha kwa kua navyo wavitakavyo. Ni huzuini kweli.

  Rova Olombi,

  Nakupa hongera mpendwa kwa moyo wako wa KUPENDA KUTOA, Wewe huna shida au ugonjwa moyoni wa kukataa/kupuuzia kutoa au kuchukulia kutoa zaka kama ni ilimradi tu, ukitoa sawa, usitoe sawa! Wewe ni mtu wa Mungu unayejua na kutaka sana kumuheshimu Mungu kwa vile ulivyo navyo hata kujiwekea discipline kwa kupenda tu si kulazimishwa kua kwa kila 10 yako, 1 wampa BWANA halafu 9 furahia. Iyo ni training nzuri ya kuua nguvu ya nafsi na mwii na kusaidia matakwa ya rohoni yakue kwa kukandamiza ya mwili na nafsi.

  Nitachangia swali lako baadae, ngoja tutoe nafasi kwa watumishi na wapendwa wengine waendelee. Nilipenda niseme kidogo tu ivyo kwakua umenigusa na kunichallenge sana na huo moyo wako mzuri wa kupenda kutoa,Amen.

  Press on.

 64. Edwin Richard;

  Sioni kama umejibu swali la mleta mada, lakini kwa maelezo yako hata wewe pia ningekushauri upitie mada ya zaka kama nilivyomshauri Evarist. Zaka kama zaka tumeijadili sana na tunaendelea kumalizia kuijadili na akina Seleli.

  Ndio maana mtu aliyeshiriki katika hiyo mada anajibu hili swali kwa umakini mkubwa.

  Ubarikiwe!

 65. Marko 12:30-“Nawe Mpende Bwana Mungu wako kwa Moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa akili zako zote,na kwa Nguvu zako zote”-ukitafakari mistari hii utaona jinsi Tunavyofanya bidii katika maendeleo yetu ya kimwili, kwa Mungu inatakiwa zaidi.

  utaratibu ambao Mungu aliuweka ili kuitunza ofisi yake Duniani(Kanisa) ni watu wake kutoa Zaka na sadaka ili makuhani wake wafanye kazi katika mazingira mazuri ili wanapopeleka ibada kwa Mungu,ifike ikiwa safi bila kelele za Moyoni.

  Just imagine-Wachungaji wanavyoangaika kushughulikia familia zao,wakati wao waliitajika masaa 24 kulia madhabahuni siyo kwa ajili ya familia zao bali kwa ajili ya kanisa.Kwa namna hii hatuwezi kukaa na furaha ya Mungu.

  Ni kweli bado wengi tunamtazamo wa kuwa zaka ilikuwa ni kwa ajili ya agano la kale,lakini tujifunze yafuatayo kutoka kwa Bwana Yesu-Yohana 3:16-“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee..”-Pekee maana yake Mungu alitoa asilimia 100-akionesha upendo kwetu,basi nasisi tumrudushie Mungu upendo kwa kumtolea Mungu kwa Moyo wa upendo,Ni kwanini bado tunajiuliza maswali kuhusu kutoa-ni kwasababu bado hatutoi,wanaomtolea Mungu hawana Maswali ,wanafuraha tele.Ukweli ni kwamba shetani ametupofusha macho kuhusu kumtolea Mungu,inapotokea michango kanisani wengi wanalalamika na wakimtolea Mungu hata elfu kumi wanaona wamemtolea sana-hawatafakari kwenye harusi wanatoa 50elfu,na harusi zipo siku zote,mwingine anachangia send off pia harusi-halalamiki,ila kwenye kanisa-michango imezidi analalama kwa elfu kumi aliyeitoa kwa kuombwa sana pia hata kuwekewa mikono na mtumishi wa Mungu.

  Kwa hiyo ikiwezekana tutoe hata asilimia 100% kama alivyotupa kielelezo Mungu,Kumbuka Sadaka ya Ibrahim(Isaka-hakuwa na mtoto mwingine ),kumbuka mfano wa Mjane aliyetoa senti moja-hakuwa na chochote cha ziada-ndivyo vielelezo tulivyopewa na Mungu.Basi chagueni leo hii Mungu,mtakaye mtumikia(yoshua 24:15-Mungu aliyetupa wokovu ambao hatukuhustaili au Miungu inayotudanganya kumtumikia Bwana hakuna faida?-Malaki 3:13(Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu asema Bwana,Tumesema maneno yako juu yako kwa namna gani?-mmesema kumtumikia Mungu hakuna faida!-Musa akasema Kutoka 10:26″Makundi yetu pia yatakwenda pamoja nasi,hautasalia nyuma hata ukwato mmoja,kwa maana inampasa kutwaa katika hao tupate kumtumikia BWANA,Mungu wetu,nasi hatujui hata tutakapofika huko,ni kitu gani ambacho kwa hicho inatupasa kumtumikia BWANA”-kumbe mali tulizonazo ni talanta,inatupasa tumtumikie nazo BWANA ili zilete faida katika ufalme wa Mungu.

 66. Evarist;

  Kuna mada kuhusu suala zima la zaka{kutoa zaka kila mwezi..} tumeiongea sana na bado tunamalizia malizia kuiongea, hebu jaribu kuipitia pia kabla hujaenda mbali sana katika kuelezea adhabu ya kutotoa zaka.

  Barikiwa!

 67. Tazama MALAKI 3:7-11 “Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
  8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
  9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
  10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
  11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.”

  Kwa maneno hayo hapo Juu tunaona faida zifuatazo za Kutoa kikumi.
  1. Huwi chini ya laana.
  2. Nyumba ya Mungu inakuwa na chakula.
  3. Baraka zinamwagwa kwako maana madirisha ya Mbinguni yanafunguliwa.
  4. Alaye hukemewa, hawa ni wachawi, wezi, magonjwa, wadudu waharibifu n.k
  5. Ushirika mzuri na Mungu unakuwa nao hivyo anakuwa mtetezi wako sana.

  Hivyo adhabu za kutotoa kikumi ni:
  1. Unakuwa chini ya laana.
  2. Nyumba ya Mungu inakuwa haina chakula.
  3. Baraka hazinamwagwi kwako maana madirisha ya Mbinguni yanafungwa.
  4. Alaye hakemewi, hawa ni wachawi, wezi, magonjwa, wadudu waharibifu n.k
  5. Ushirika mbaya au uadui na Mungu unakuwa nao hivyo hawi tena mtetezi wako
  sana.

  Yapo majibu mengi nimeanza na hilo kwa kuwa nina haraka.

 68. BWANA ASIFIWE WAPENDWA
  NIME SHUKURU MUNGU TENA KUPATA MUDA KAMA IYI YA KUULIZA SWALI LANGU JUU YA SADAKA AMA MOJA YA KUMI KWAMAPATO YANGU .
  SWALI NI IYI MIMI NAISHI APA ULAYA EUROPA NIKO NA KANISA TUNASHIRIKI . NILISIKIYA MAFUNDISHO JUMA PILI TARIKI 15-09-2013 MWALIMU ALIFUNDISHA JUU YA MOJA YA KUMI . NA MIMI MOJA YANGU YA KUMI NIKIPATA NA TUMAKA AFRIKA . MWALIMU ANASEMA NI VIBAYA LAZIMA KULETA APA TU . SIO KUTUMA FASI ZINGINE . NA MIMI NATUMAKA KWA BABA YANGU YA IMANI . SIJUWE KAMA NAFANYAKA MAKOSA KUTUMA AFRIKA .ALILETA MUFANO YAKE IVI UWEZI KUKULA CHAKULA KWA KIBANDA IKI NA UKALIPE FASI ZINGINE . NAOMBA USAIDI KWA SWALI IYI

  MUBARIKIWE AMINA

 69. Amin na Wilson,

  Maswali:
  (a) Kwa iyo, atoe au asitoe? Kama adhabu ipo au la, mnamfundisha nini mleta mada? Neno gani la kweli na hakika Roho Mtakatifu anawahimiza kumwachia ndugu huyu kuhusu Zaka?

  (b) By the way, ni Watu ndio wameileta ishu ya zaka na wanalazimishia au imetoka kwa Mungu?

  (c) Na kama mahali kwingine hawalazimishii, je tukitoa kwa hiari, shukrani na upendo wetu kwa Mungu kama Ibrahimu- Mwz.14:1-20, kuna shida gani?

  Press on.

 70. Hakuna adhabu yoyote hivyo ni wazi kikumi hakina umuhimu kutoa ila kuna watu wanalazimisha sana kwa matakwa yao binafsi

 71. Nico,

  Kabla ya kuzungumzia adhabu ya kutotoa/kuchelewa kulipa fungu la kumi ni zipi na kifungu kipi cha maandiko? Je naweza kukuliza yafuatayo kama njia moja wapo ya kuchangia swali/haja yako nzuri ya kutaka kusaidiwa kujua? Niulize ivi:

  (a) Unadhani MUNGU anafurahia kuyafanya mambo yake yote kwa ujumla kwa ulegevu ilihali ya kwetu binafsi, tunafanya kwa bidii zote na kwa wakati?

  (b) Je kama hakuna adhabu yoyote kwa kuchelewa au kutolipa, utatoa kikumi?

  (c) Je Kama kuna adhabu, bado utachelewa au utaacha kutoa?

  (d) Kama hakuna adhabu na ukaacha kutoa au kuchelewa, unadhani kazi ya Mungu itakwama kabisa au la?

  (e) Kwa kuzingatia jibu la (d), unakubali kua mambo hayo Mungu ameyaweka ili kututengenezea njia ya Yeye kutusadia na kutushirikisha mambo yake na wala Yeye hayamu-affect vibaya kiviiiile maana amekuwepo kabla ya hayo yote?

  Press on.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s