Sababu saba za kibiblia kwanini watu wanakufa mapema!

biblia

Bwana Yesu asifiwe sana wana wa Mungu, ni matumaini yangu na Imani yangu ya kwamba u mzima na ya kuwa unaendelea kuufurahia uzuri wa Yesu Kristo na kazi yake ya msalaba.

Leo ninataka kwa pamoja tuyachunguze maandiko na tuzipitie sababu hizi saba za Kibiblia ni kwa nini watu wengi wanakufa mapema…na sasa ongezeko la vifo vya mapema ni kubwa kuliko hata zamani. Kwa Tanzania wastani wa kiwango cha maisha ni miaka 45,Binafsi nauona umri huu kuwa ni mdogo sana kwa mtu wa rika hili kuondoka duniani kwani anakuwa na majukumu mengi ya kufanya na pia mchango wake unakuwa unahitajika kwenye familia, ukoo, wilaya, mkoa, taifa na hata duniani kwa ujumla.

Ni maombi yangu na dua yangu kwa Bwana ya kwamba umalizapo kusoma ujumbe huu, macho yako ya ndani yatafunguka na utaweza kuona swala hili kwa jicho la Rohoni…KARIBU SANA.

Zifuatazo ni sababu saba kwa mujibu wa Neno la Mungu ni kwanini watu wanakufa mapema(katika umri mdogo)

1.KUTOWAHESHIMU WAZAZI(BABA NA MAMA)

Biblia iko wazi sana na imesisitiza uhusiano mzuri na wa uhakika kati yetu na wazazi wetu…kinyume chake LAANA zitayaandama maisha yetu na maisha yetu hayatakuwa ya heri na marefu.

Ukisoma Waefeso 6:1-3 inasema, “Enyi watoto watiini WAZAZI wenu katika BWANA, maana hii ndiyo HAKI.Waheshimu baba na mama yako, amri hii ndiyo ya kwanza YENYE AHADI (za ustawi, baraka na wingi wa miaka), upate HERI, UKAE SIKU NYINGI( UISHI SIKU NYINGI) katika dunia”   pia katika Kumbukumbu la Torati 5:16 Biblia inasema, “Waheshimu BABA na MAMA yako; kama BWANA, Mungu wako alivyoamuru, SIKU ZAKO ZIPATE KUZIDI, nawe upate KUFANIKIWA katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako”

Kwa mujibu wa maneno ya Mungu hapo juu ni dhahiri kabisa ya kuwa watu wote wasiowaheshimu wazazi wao, ni ngumu kufanikiwa, Laana zinawafuatilia na zaidi ya yote wana muda mchache wa kuishi…WANAKUFA MAPEMA!

2.KUKOSA MAONO

  Kwa mujibu wa Biblia, mtu anayeishi ili mradi tu, asiyejua kwanini yupo duniani, asiyekuwa na kusudi na mpango katika maisha yake, na asiyeweza kupanga hata mipango ya ‘kesho nitafanya a, b, c nk’ yuko katika hatari kubwa ya kuondoka duniani kabla ya muda wake…Biblia inasema, “Pasipo MAONO watu huangamia”….Biblia ya kiingereza inasema, “Without VISION people PERISH”

Jitahidi kuwa na maono ya muda mfupi na ya muda mrefu, Mungu anashughulika na walio nacho, wasiokuwa nacho hata kile kidogo walichonacho hunyang’anywa.

3.KUTOKUMCHA MUNGU

Kumcha Mungu ni kuishi maisha yanayoongozwa na HOFU ya MUNGU (si woga dhidi ya Mungu)…Ni maisha ambayo moyo,mwili, nafsi na roho ya mtu inakuwa imejawa na kiu na njaa ya kumpendeza Mungu na kuyafanya maagizo yake yote-tena kwa furaha.

Mithali 10:27 inasema, “KUMCHA BWANA kwaongeza siku za mtu, Bali miaka yao WASIO HAKI itapunguzwa”  na pia Mhubiri 7:17 inasema, “Usiwe MWOVU kupita kiasi; wala usiwe mpumbavu; kwanini UFE KABLA YA WAKATI WAKO?”

Kwa mujibu wa ushahidi huu wa Neno la Mungu, ni dhahiri kuwa maisha yasiyo na uchaji na yasiyoongozwa na hofu ya Mungu, yanawafanya wengi wafe kabla ya muda wao waliokusudiwa kuishi.

4.KUMWEKEA MUNGU MIPAKA

Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi…kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni ‘DHARAU’ kwake… Zaburi 78:41 inasema, “Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel”

Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani.

Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya ‘Maziwa na Asali’…10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki…majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema…waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni ‘UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO’ wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim(Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi…WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO…Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-29)

Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako…ishi maisha ya IMANI…Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, “Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia” Isaya 55:8-11

5.KUTOKUMTUMIKIA MUNGU

Biblia inasema katika KUTOKA 23:25-26, ” Nanyi  mtamtumikia BWANA, Mungu wenu naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; NAMI nitakuondolea Ugonjwa kati yako…na hesabu ya SIKU zako nitaitimiza”

Huu ni ukweli ambao inabidi uufahamu na uweke kwenye matendo.Unataka kuishi muda mrefu hapa duniani? kazi ni rahisi…fanya sehemu yako, MTUMIKIE BWANA naye ATAITIMIZA hesabu ya siku zako…HAUTAKUFA KABLA YA WAKATI.

6.MAISHA YA DHAMBI

Dhambi ni mbaya…inakutenga mbali na Mungu( Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako…inakufanya ufe kabla ya muda wako…Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako…unafanya kazi ambayo mshahara uitwao ‘MAUTI’ utaupata.

Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, “Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI(KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”  pia Biblia inasema, “Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa”

Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi…Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?

Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!

7.KUKOSA BIDII KATIKA KUMPENDA MUNGU

Biblia iko wazi katika Zaburi ya 91:14-16, nayo inasema, “Kwakuwa AMEKAZA(Ameweka bidii katika) KUNIPENDA, Nitamwokoa; na kumweka palipo juu (NITAMWINUA) kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni. Nitamwokoa na kumtukuza; KWA SIKU NYINGI nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu”

Biblia inasema Atakayekaza/kuwa na bidii katika KUMPENDA MUNGU atashibishwa kwa WINGI WA SIKU.

Yesu ameweka wazi ni namna gani waweza kumpenda Yeye, Yohana 14:21 inasema, “Yeye aliye na AMRI  zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; Nami nitampenda na kujidhihirisha kwake”

Nayo Mithali 3:1-2 inasema, ” Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishikeAMRI zangu.Maana zitakuongezea WINGI WA SIKU, NA MIAKA YA UZIMA, NA AMANI

Unapozishika sheria na Amri alizozitoa Bwana maishani mwako…huo ndo udhihirisho wa Upendo wako kwa Mungu aliye hai…kila unapoongeza bidii ya kumtii na kumheshimu Mungu-ukakaza kumpenda, ANAKUSHIBISHA KWA SIKU NYINGI…Wewe ndiye unayeweza kumwambia Bwana, hii miaka 90 inatosha, nimekwisha shiba maisha…nataka kurudi nyumbani…au miaka 40 inatosha Bwana…nimeshiba siku nataka kurudi nikae na wewe…wewe ndo unayeamua wingi wa siku zako…tangu leo kaza kumpenda BWANA.

Ninaamini umejifunza kitu, na ya kuwa wewe nawe utayagusa maisha ya wengine kwa KWELI hizi ambazo Bwana amesema na wewe kupitia kwangu.Ubarikiwe

   Wako katika na Ndani ya Kristo,

Dickson Kabigumila.

15/12/2011

Advertisements

15 thoughts on “Sababu saba za kibiblia kwanini watu wanakufa mapema!

 1. Nimependa mahubiri Mungu akubariki 2tafanya kaz ya Mungu kwa nguvu zote. Ili 2ish muda mrefu na nina swali je. Kuna faida gani kukaa muda mrefu dunian? Mbona Yesu alikaa muda mfupi na henoko alitwaliwa?

 2. Bwana Yesu Kristo Asifiwe Somo ni zuri na Mungu Akubariki, Nivema wanadamu wa jue ya kuwa ukristo siyo starehe bali ni kushindana tena mjue ya kuwa mauti na kuzimu si matukio bali vina personality yaani ni watu wenye akili ya kishetani kwa ajili ya kuharibu watu wa Mungu, Simpango wa Mungu watu wafe kabla ya wakati bali ni ukosefu wa maarifa Hosea 4:6, kimsingi tumepewa funguo za mauti na kuzimu alafu atuzitumii na pia inatupasa tusimpe ibilisi nafasi ukimpa ibilisi nafasi basi ujue nguzo zake kuu ni mauti na kuzimu, fahamu imeandikwa mauti na uzima u katika ulimi wako, imeandikwa nazishuhudiza mbingu na nchi ya kuwa nimeweka mbele yako uzima na mauti, Baraka na laana basi chagua uzima ili uwe hai…….. pia kuna mikataba inayopelekea mauti kabla ya wakati ama imefanywa na wewe au babu zako, sasa yakupasa kuivunja mikataba iliyofanywa na mababu na kuvunja laana KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETHI na kubomoa zote kwa DAMU YA MWANA KONDOO Hamu alikosea akalaaniwa kaanani, Yoabu alikosea wakalaaniwa watoto wake, Wefeso 6:11-18 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
  zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu, Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

 3. Ubarikiwe ubarikiwe, ukikaa vizuri unaweza andika kitabu kikawa msaada kwa wengi. KAPOLE

 4. Nimebarikiwa na somo,MUNGU AENDELEE KUKUTIA NGUVU NA KUENDELEA KUKUTUMIA KTK MASOMO MENGINE.

 5. Pia panua kuelezea kwa sababu nchi kama Japan na zingine zilizoendelea watu wanaishi maisha marefu? Je ni kwa sababu wanafuata kanuni hizo?

  Ni kweli…maisha ya dhambi…yanafanya…watu wafe…mapema…

  Mi nimeshaona…mtu..ni Professor..lakini..kutokana…na kupenda kulewa na wanawake…anakufa..kwenye miaka ya hamsini…wakati…kutokana..na…kipato..chake( angeweza kitumia..kwa mambo mazuri..yanayoboresha..maisha)…angegonga..hata.zaid..ya 70..

 6. Dickson,

  Asante kwa somo lako. Ni tamu na linaonyesha picha nzuri kabisa. Ila pengine Neno la Mungu likaenda mbali ya ile uliotamka na likalenga kiroho kuliko kimwili. Mungu anapoongea juu ya maisha hamaanishe tu maisha duniani, ila vile vile maisha mbinguni. Kwani kwenda mbinguni ni kuendelea kuishi na kwenda jehanum ni kufa.

  Mungu akubariki.

 7. NI HAKIKA UKIISHI MAISHA YA KUMPENDA MUNGU SIKU ZINAONGEZEKA ANGALIA VIJANA WENGI WANA KUFA KATI YA MIAKA 15-49 NI KWA SABABU YA UKIMWI , NA UGONJWA HUU SOURCE YAKE KUBWA NI UZINZI MUNGU AKUBARIKI NDUGU

 8. prays Lord,
  Nikweli somo limetulia ,ubarikiwe sana ,hakika tukizifuata hizi sheria ktk roho ,tutaishi na kuyaona maisha matamu.

 9. Kabigumila Dickson,

  Umesema unaamini, tu/nimejifunza kitu, NI KWELI KABISA nimejifunza na kubarikiwa sana brother na points zote kusema kweli hasa kwa kua zina kidhi vigezo muhimu ktk ufundishaji particularly utumiaji wa mamlaka ya Neno la Mungu. Nimependa na kuhuhishwa sana kipande cha point no.7 toka Zaburi 91 ulipokazia ivi-Atakayekaza/kuwa na bidii katika KUMPENDA MUNGU atashibishwa kwa WINGI WA SIKU. Iyo kukaza/tia bidii kumpenda Mungu ni tamu sana! Great discernment indeed, I love it, powerful to me, kipande icho kimesema nami kwa mafuta ya RM mabichi kabisa.

  Pia asante kwa point no.1 ya Wazazi! Ooh my God, nina/tunajisahau kweli hasa tukishatoka home kuja uku majijini na mijini na tukawa busy, ndio basi tena, miezi inapita KILA SIKU NEARLY, tunaramba supu na chapati zikisindikizwa na fanta baridi sana hatari, kila leo tunajaza vocha kwa simu na moderm ya internet, halafu hata kutuma alfu 10, 20, laki, mil, kwa mpesa kwa wazazi hamna!! Maana kuwaheshimu Wazazi inajumuisha pia kuwapenda na kuwajali. I like also no.5, nayo ina nguvu sana, ukiondoa iyo, hatuna sababu ya kuendelea kuishi baada ya kuokoka.

  Kwa upande mwingine, wewe kama Mwalimu, utakubaliana nami kua somo hili pamoja na utamu/uzuri na nguvu yake, lina- delicateness kwelikweli kwa baadhi ya points ili kueleweka moja kwa moja, tafadhari karibu Mwl. Dickson ufafanue zaidi kupitia facts izi zifuatazo:

  Kwakua ni kweli pia KUTOKUMCHA MUNGU kunafupisha siku, tunafundishaje/jibuje challenges izi za ukweli kabisa mfano siku unafanya seminar na kufundisha somo hili na ukatoa nafasi kwa Wanafunzi/wasikilizaji wako kuuliza maswali.

  (a) Vipi Watoto wadogo au wachanga wanaokufa! lini wameanza kutomcha Mungu ili kupelekea siku zao zikatwe? mfano statistics Wizara ya Afya kwa Watoto wanaokufa kabla kufika miaka 5 zinatisha sana, wewe wasemaje Mwalimu kwa hilo?

  (b)
  Nina Bibi yangu kabisa mzaa Baba anaitwa Mwanampuni, ana miaka sasa zaidi ya 115, ameishi kwa kufuata mizimu ya kinyamwezi na mila kwa miaka yote mpaka alipokuja kuokoka akiwa na akili timamu na kufanya maamuzi akielewa kabisa Injili maana ana ufahamu wa kawaida kabisa, ana nguvu, anatembea mwenyewe kwa kafimbo tu, anapika, kupepeta mchele, anasigina karanga ili kutupikia mlenda na kisamvu safi, anaona macho mpaka sasa na hajawai tumia miwani kamwe, huyu naye wasemaje? Au aina ya watu waovu sana duniani eg wachawi, wanga uko vijijini, madikiteta, wote hao, wapo wameishi miaka mingi na wengine mpaka leo wapo, hawakufa mapema, why?

  (c) Ninafahamu Watumishi wa Mungu kwelikweli na wapendwa wanamcha Mungu na utumishi mwanzo-mwisho lakini ghafla wakafa ktk ajali ya ndege, magari-mfano costa iliwahi kuuwa kwaya nzima na mchungaji wao wakiwa njiani kwenda kuhubiri, Mv.BK iliua ndugu zangu 22 na Mama yangu Mzazi kwa mara moja, unasemaje kwa hayo pia?

  Angalizo: Hii ya ‘’KUKOSA MAONO, Watu wanaangamia, ktk NIV Bible, imeandikwa ivi….’’Where there is no revelation, people cast off restraint;
  but blessed is the one who heeds wisdom’s instruction. Nadhani kwa jinsi ulivyoelezea hoja iyo ya Kua na Maono ni tofauti na context ya andiko husika, hapo inaongelea KUKOSA MAONO KWA MAANA YA KUTOKUA NA MAELEKEZO/NENO/MAAGIZO/SHERIA ZA MUNGU na si maono kama ulivyoeleza ya kua na jambo/ndoto/kitu unachotaka kua nacho/ua-accomplish au Bwana anakufanikishe kukitwaa/fikia kabla ya kuondoka duniani au hata ukiondoka, kibaki kinafikiwa na hatimaye kusaidia wengine. Plz cross-check and come again brother.

  Press on.

 10. Dickson,
  Mungu akaubariki kaka kwa meseji nzuri. Ni kweli kabisa, Mungu hakutuumba kama wanyama. Alituumba kwa mfano wake. Mungu ni Mungu wa njozi, unabii, nk. Kadhalika na watoto wake, sharti wawe wa namna hiyo.

 11. Amen,ubarikiwe mpendwa;ila Nina swali;je hawa wote wanao kufa huwa wanakosea moja wapo wa sababu hizi?pili nasikia watumishi wanasemaka eti Mungu aliwezaka kukadirisha Maisha ya watu je ni kweli?

 12. shaloom mtu wa Mungu, Nashukuru sana kwa kuniongezea mengi zaid ya kumjua Bwana Mungu wa Majeshi Zaidi ni Kuongeza bidii kuyatenda yale yote yaliyo mema toka Bwana wetu na kuyashika na kuayaelewa vyema sawasawa na mapenzi yake. ubarikiwe. Siaka Nyanchiwa

  ________________________________

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s