Wanawake Katika Huduma

joy

Kwa kuwa ni kitu kinachojulikana kwamba wanawake ni zaidi ya nusu katika kanisa la Bwana Yesu Kristo, ni muhimu kuelewa nafasi yao waliyopewa na Mungu katika mwili wa kristo. Katika makanisa mengi na huduma, wanawake huonekana kama watenda kazi wa maana sana, kama ambavyo ni kawaida hata katika huduma ya jumla.

Lakini, si wote wanaokubaliana kuhusu nafasi zao. Wanawake mara nyingi wanazuiwa kufanya maeneo fulani ya huduma kanisani, yenye kuhusiana na kusema na uongozi. Makanisa mengine yanaruhusu wanawake wachungaji; mengi hayaruhusu. Mengine yanaruhusu wanawake kufundisha, na mengine hayaruhusu. Wengine wanawazuia wanawake wasiseme kabisa wakati wa ibada za kanisa.

Kutofautiana huko kwa sehemu kubwa kumejengwa kwenye tafsiri mbalimbali za maneno ya Paulo kuhusu nafasi za wanawake katika 1Wakor. 14:34-35 na 1Timo. 2:11 hadi 3:7. Maandiko hayo tutayatazama zaidi katika sura hii, hasa pale mwishoni.

Kuanza Mwanzo

Tunapoanza, hebu tutazame Maandiko yanadhihirisha nini kuhusu wanawake, tangu mwanzo kabisa. Sawa na wanaume, wanawake wameumbwa katika mfano wa Mungu.

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba (Mwanzo 1:27).

Bila shaka tunajua kwamba Mungu alimwumba Adamu kabla ya kumwumba Hawa, na hilo ni jambo lenye umuhimu wa kiroho kulingana na Paulo (ona 1Timo. 2:3). Baadaye tutatazama umuhimu wa mpango huo katika uumbaji kama unavyoelezwa na Paulo, lakini inatosha tu kwa sasa kusema kwamba hiyo haithibitishi ubora wa wanamume juu ya wanawake. Wote tunajua kwamba Mungu aliwaumba wanyama kabla ya binadamu (ona Mwanzo 1:24-28)[1]

Mwanamke aliumbwa awe msaidizi wa mumewe (ona Mwanzo 2:18). Hapa tena, huo si uthibitisho wa udogo wake bali huonyesha tu nafasi yake katika ndoa. Roho Mtakatifu ametolewa kuwa msaidizi wetu, lakini si wa hali ya chini kuliko sisi. Roho Mtakatifu yuko juu yetu! Na ni sahihi kabisa kusema kwamba Mungu alipomwumba mwanamke awe msaidizi wa mumewe inathibitisha kwamba wanaume wanahitaji msaada!Mungu ndiye aliyesema kwamba haikuwa vema kwa manamume kuwa peke yake (ona Mwanzo 2:18). Ukweli huo umethibitishwa mara nyingi sana katika historia, wakati wanaume wanapoachwa wenyewe bila wake wa kuwasaidia.

Mwisho – tunaona tangu kurasa za kwanza kabisa za Mwanzo kwamba mwanamke wa kwanza aliumbwa kutoka nyama ya mwanamume wa kwanza. Alichukuliwa kutoka kwake, kuonyesha kwamba kuna anachokosa pasipo yeye, na kwamba hao wawili walikuwa mmoja hapo kwanza. Zaidi ni kwamba, kile ambacho Mungu alikitenga kilikusudiwa kuunganika tena kwa njia ya mahusiano ya kushirikiana kimwili, jambo ambalo si la kuzaana na kuongezeka tu, bali la kuonyesha upendo na kufurahiana wote wawili, ambapo kila mmoja anamtegemea mwingine.

Kila kitu juu ya masomo haya kutoka uumbaji kinapingana na wazo la jinsia moja kuwa juu au bora kuliko nyingine, au moja kuwa na haki ya kutawala nyingine. Na kwa kuwa Mungu ameweka wajibu tofauti kwa wanawake au huduma haihusiani na usawa wao na wanaume ndani ya Kristo, ambako “hakuna mtu mume wala mtu mke” (Wagalatia 3:28, TLR).

Wanawake Katika Huduma – Agano La Kale

Baada ya kuweka msingi huo, hebu sasa tutazame baadhi ya wanawake ambao Mungu aliwatumia kutimiza makusudi Yake katika Agano la Kale. Ni dhahiri kwamba Mungu aliwaita wanaume kuingia katika huduma kama kazi katika kipindi cha Agano la Kale, kama alivyofanya katika kipindi cha Agano Jipya. Habari za wanaume kama vile Musa, haruni, Yoshua, Yusufu, Samweli na Daudi zimejaa katika kurasa za Agano la Kale.

Ila, kuna wanawake wengi tu wanaotokezea hapo kama ushahidi kwamba Mungu anaweza kumwita na kumtumia yeyote atakaye, na wanawake waliowezeshwa na Mungu wanatosha kufanya kazi yoyote atakayowaitia.

Kabla ya kutazama mwanamke mmoja, ni vizuri ijulikane kwamba kila mtu maarufu wa Mungu katika Agano la Kale alizaliwa na kulelewa na mwanamke. Asingekuwepo Musa bila ya mwanamke aliyeitwa Yokebedi (ona Kutoka 6:20). Wala wasingekuwepo watu wengine maarufu na wakuu wa Mungu kama si akina mama wa hao watu. Wanawake wamepewa na Mungu wajibu mzito na huduma yenye sifa kubwa ya kuwakuza watoto katika Bwana (ona 2Timo. 1:5).

Yokebedi hakuwa mama wa wanaume wawili walioitwa na Mungu tu – Mus ana Haruni – bali pia alimzaa mwanamke aliyeitwa na Mungu. Huyo ni Miriamu dada yao, nabii wa kike na kiongozi wa kuabudu (ona Kutoka 15:20). Katika Mika 6:4, Mungu anamweka Miriamu pamoja na Musa na Haruni, kama viongozi wa Israeli.

Kwa maana nalikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami naliwapeleka Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako (maneno mepesi kutilia mkazo).

Ni kweli kwamba nafasi ya Miriamu ya uongozi katika Israeli haikuwa kubwa sana kama Musa. Lakini, kama nabii wa kike, Miriamu alinena kwa niaba ya Mungu, nami nadhani kwamba ni salama kusema kwamba jumbe za Mungu kupitia kwake zililengwa kwa wanaume wa Israeli, si wanawake tu.

Mwamuzi Mwanamke Juu Ya Israeli

Mwanamke mwingine ambaye Mungu alimwinua kuwa kiongozi katika Israeli ni Debora, aliyeishi wakati wa kipindi cha waamuzi wa Israeli. Yeye naye alikuwa nabii wa kike, na alikuwa mwamuzi juu ya Israeli sawa na akina Gidioni, Yefta na Samsoni wakati wao. Tunaambiwa kwamba “wana wa Israeli walimwendea awaamue” (Waamuzi 4:5, TLR). Basi, akatoa maamuzi kwa ajili ya wanaume, si wanawake tu. Angalia usikose hili: Mwanamke aliwaambia wanaume kitu cha kufanya, na Mungu alimtia mafuta afanye hivyo.

Kama wanawake wengi ambao Mungu huwaita katika uongozi, Debora alikabiliwa na mwanamume mmoja ambaye aliona taabu kupokea neno la Mungu kupitia chombo cha kike. Jina lake aliitwa Baraki, na kwa sababu alikuwa na mashaka kuhusu maagizo ya Dobora ya kinabii kwake kwamba akapigane vita na jemadari Mkanani aliyeitwa Sisera, Debora alimwambia kwamba heshima ya kumwua huyo Sisera ingemwendea mwanamke. Ndivyo ilvyokuwa, na mwanamke aitwaye Yaeli anakumbukwa katika Maandiko kwamba ndiye aliyemtoboa kichwa Sisera akiwa amelala, kwa kigingi cha hema (ona Waamuzi 4). Kisa hiki kinamalizika kwa Baraki akiimba wimbo wa kupokezana, na Debora! Baadhi ya mafungu yamejaa sifa kwa ajili ya Debora na Yaeli (ona Waamuzi 5), kwa hiyo, pengine Baraki alikuja kuamini “huduma ya wanawake” mwishowe!

Nabii Wa Tatu Mwanamke

Mwanamke wa tatu anayetajwa katika Agano la Kale kwamba ni nabii wa kuheshimika ni Hulda. Mungu alimtumia kutoa mtazamo unaoaminika wa kinabii na maagizo kwa mwanamume, mfalme aliyekuwa na wasiwasi sana, wa Yuda (ona 2Wafalme 22). Hapa tena tunaona mfano wa Mungu akimtumia mwanamke kumfundisha mwanamume. Bila shaka Hulda alitumiwa na Mungu kwa huduma kama hiyo mara kwa mara, vinginevyo Yosia asingekuwa na imani kubwa katika aliyomwambia.

Kwa nini Mungu alimwita Miriamu, Debora na Hulda kufanya kazi kama manabii wanawake? Mbona asiwaite wanaume?

Hakika Mungu angeweza kuwaita wanaume kufanya hayo hayo yaliyofanywa na wanawake watatu. Lakini hakuwaita. Na hakuna ajuaye sababu. Tunachotakiwa kujifunza kutokana na hili ni kwamba ni vizuri tujihadhari juu ya kumweka Mungu kwenye sanduku kwa habari ya anamwita nani kwenye huduma. Ingawa Mungu kawa kawaida alichagua wananume kufanya kazi wa uongozi katika Agano la Kale, wakati mwingine alichagua wanawake.

Mwisho – ijulikane kwamba hiyo mifano yote mitatu ya watumishi wanawake katika Agano la Kale walikuwa manabii. Zipo huduma zingine za Agano la Kale ambazo wanawake hawakuitwa kuzifanya. Kwa mfano: Hakuna wanawake walioitwa kuwa makuhani. Hivyo, yawezekana Mungu ametenga huduma fulani kwa ajili ya wanaume tu.

Wanawake Katika Huduma – Agano Jipya

Cha kushangaza ni kwamba tunamkuta mwanamke aliyeita na Mungu kuwa nabii mwanamke katika Agano Jipya. Yesu alipokuwa na umri wa siku chache tu, Ana alimtambua na kuanza kutangaza kwamba ndiye Masiya.

Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi. Alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake (Luka 2:36-38. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Ona kwamba Ana aliwaambia wote waliokuwa “wanautarajia wokovu wa Yerusalemu” habari za Yesu. Bila shaka walikuwemo na wanaume. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba Ana alikuwa anawafundisha wanaume habari za Kristo.

Kuna wanawake wengine katika Agano Jipya ambao Mungu aliwatumia kwa karama ya unabii. Mama yake Yesu – Mariamu – yuko katika fungu hilo (ona Luka 1:46-55). Kila mara maneno ya kinabii ya Mariamu yanaposomwa katika ibada ya kanisa, ni sawa kusema kwamba mwanamke analifundisha kanisa. (Na Mungu aliwaheshimu wanawake bila swali kwa kumtuma Mwana Wake duniani kwa njia ya mwanamke. Angeweza kufanya kwa njia zingine nyingi!)

Orodha hii inaendelea. Mungu alitabiri kwa kinywa cha nabii Yoeli kwamba wakati atakapomwaga Roho Wake, wana wa kiume na wa kike katika Israeli wangetabiri (ona Yoeli 2:28). Petro alithibitisha kwamba unabii wa Yoeli ulikuwa unafanya kazi katika kipindi cha agano jipya (ona Matendo 2:17).

Tunaambiwa katika Matendo 21:8-9 kwamba mwinjilisti Filipo alikuwa na binti wanne waliokuwa manabii.

Paulo aliandika kuhusu wanawake wakitoa unabii katika ibada za kanisa (ona 1Wakor. 11:5). Ni dhahiri kutokana na mantiki kwamba, wanaume walikuwepo.

Kwa mifano yote hiyo ya Maandiko kuhusu wanawake kutumiwa na Mungu kama manabii na kutoa unabii, kweli hatuna sababu nzuri ya kukataa wazo kwamba Mungu anaweza kuwatumia wanawake katika huduma hizo! Tena, hakuna kitu chochote kinachoweza kutupelekea sisi kufikiri kwamba wanawake hawawezi kuwatabiria wanaume kwa niaba ya Mungu.

Wanawake Kama Wachungaji?

Vipi kuhusu wanawake kutumika kama wachungaji? Inaonekana dhahiri kwamba nafasi ya mchungaji au mzee au mwangalizi imekusudiwa na Mungu ishikiliwe na wanaume.

Ni neno la kuaminiwa: Mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja (1Timo. 3:1-2. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; ikiwa mtu hakushtakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja (Tito 1:5,6. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Paulo hasemi moja kwa moja kwamba wanawake wamekatazwa kushika wadhifa huo, kwa hiyo, tuwe makini tusitoe uamuzi wa mwisho. Inaonekana kwamba kuna wachungaji wengi wa kike, na wazee na waangalizi duniani kote siku hizi – hasa katika nchi zinazoendelea – ambao wanafanya vizuri sana. Ila, bado ndiyo wachache. Pengine Mungu mara moja moja anawaita wanawake kufanya kazi hiyo wakati ambapo katika hekima Yake, makusudi ya ufalme Wake yatatimizwa vizuri zaidi, au wakati kuanpokuwepo upungufu wa uongozi wa kiume wenye sifa zinazotakiwa. Pia yawezekana kwamba wachungaji wengi wa kike walio katika mwili wa kristo leo wana wito wa kushika nafasi zingine za huduma ambazo zinafaa KiBiblia kwao, kama vile nafasi ya nabii, ila, mfumo uliopo wa kanisa unawarhusu kufanya kazi kama wachungaji tu.

Kwa nini nafasi ya mchungaji au mzee au mwangalizi imetengwa kwa ajili ya wanaume tu? Kuelewa utendaji wa nafasi hiyo kutatusaidia. Sharti moja la Maandiko kuhusu mchungaji au mzee au mwangalizi ni kwamba,

[Awe] Mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) (1Timo. 3:4-5).

Sharti hili linaleta maana kabisa tunapotambua kwamba mzee wa Agano Jipya alisimamia kanisa dogo la nyumbani. Wajibu wake ulikuwa ni sawa na baba kusimamia familia yake. Hili linatusaidia kuelewa ni kwa nini nafasi ya mchungaji ishikwe na mwanamume – kwa sababu inafanana sana na mfumo wa familia, ambayo, kama inalingana na mpango wa Mungu, inatakiwa kuongozwa na mume, si mke. Tutasema zaidi juu ya hilo baadaye.

Wanawake Kama Mitume?

Tumegundua kwamba wanawake wanaweza kufanya kazi katika nafasi ya nabii (wakiitwa na Mungu). Vipi kuhusu aina zingine za huduma? Inasaidia kusoma salamu za Paulo katika Warumi 16, ambapo anawasifu baadhi ya wanawake waliofanya huduma kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Yawezekana hata mmoja akawa amepangwa kama mtume. Katika mafungu matatu yanayofuata, nimeandika majina ya wanawake wote kwa herufi nyepesi kama hizi.

Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea; kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamasaidie katika neno lolote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa mssaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia (Warumi 16:1, 2. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Amesifiwa kweli kweli! Hatujui Fibi alikuwa anafanya huduma gani, lakini Paulo anamwita “mtumishi wa kanisa la Kenkrea” na “msaidizi wa wengi” pamoja na yeye (TLR). Chochote alichokuwa anafanya kwa ajili ya Bwana kinaonekana kilikuwa kikubwa sana mpaka Paulo anamsifu kwa kanisa lote la Rumi.

Kisha tutasoma habari za Priska (au Priskila), ambaye, pamoja na Akila mume wake, walikuwa na huduma muhimu sana kiasi cha kwamba makanisa yote ya Mataifa yaliwafurahia.

Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu, waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia. Nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. Nisalimieni Mariamu,aliyejitaabisha sana kwa ajili yenu. Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu (Warumi 16:3-7. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Kwa habari ya Yunia – inaonekana kwamba mtu ambaye ni “maarufu miongoni mwa mitume” bila shaka naye ni mtume tu. Kwa mahesabu hayo, Yunia alikuwa mtume wa kike. Priska na Mariamu walikuwa watenda kazi kwa ajili ya Bwana.

Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana. Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu. Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo. Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana. Msalimieni Trifaina na Trifosa,wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana. Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliyae mama yangu pia. Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herman a ndugu walio pamoja nao. Nisalimieni Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao (Warumi 16:8-15. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Basi ni dhahiri kwamba wanawake wanaweza kuwa “watenda kazi” katika huduma.

Wanawake Kama Waalimu?

Vipi kuhusu waalimu wa kike? Agano Jipya halitaji hata mmoja. Wala Biblia haitaji wanaume wowote walioitwa kuwa waalimu. Priska (aliyetajwa hapo juu) mke wa Akila, alihusika katika kufundisha kwa sehemu ndogo. Kwa mfano: Wakati yeye na Akila walipomsikia Apolo akihubiri Injili yenye upungufu mwingi sana huko Efeso, “walimchukua na kumwelezea njia ya Mungu kwa usahihi zaidi” (Matendo 18:26, TLR). Hakuna awezaye kupinga kwamba Priska alimsaidia mume wake kumfundisha Apolo, aliyekuwa mwanamume. Tena, Paulo anawataja Priska na Akila mara mbili katika Maandiko, wakati anaposema juu ya “kanisa lililoko nyumbani mwao” (ona Warumi 16:3-5; 1Wakor. 16:19), na anawaita wote wawili “watenda kazi wenzangu katika Kristo” katika Warumi 16:3. Hapana shaka kwamba Priska alikuwa na nafasi tendaji katika huduma pamoja na mume wake.

Wakati Yesu Alipowaamuru Wanawake Wawafundishe Wanaume

Kabla hatujashughulikia maneno ya Paulo kuhusu wanawake kunyamaza kimya kanisani nay eye kuwakataza wanawake kufundisha wanaume, hebu tutazame andiko moja litakalotusaidia kulinganisha vizuri hayo.

Yesu alipofufuka, malaika aliwaagiza wanawake watatu kwenda kuwafundisha wanafunzi wa kiume wa Yesu. Hao wanawake waliamriwa kuwaambia wanafunzi kwamba Yesu amefufuka, na kwamba angewatokea huko Galilaya. Si hayo tu. Muda mfupi baadaye, Yesu Mwenyewe aliwatokea wanawake hao na kuwaamuru wakawaambie wanafunzi waende Galilaya (ona Mat hayo 28:1-10; Marko 16:1-7).

Kwanza, mimi nadhani ni kitu muhimu sana kwamba Yesu alichagua kuwatokea wanawake kwanza, kisha wanaume. Pili, kama kungekuwepo na kitu chochote kibaya kimsingi au kiadili, kuhusu wanawake kuwafundisha wanaume, ungetarajia kwamba Yesu asingewaambia wanawake wawafundishe wanaume kuhusu kufufuka Kwake – jambo ambalo si dogo – na ambalo Yeye Mwenyewe angeweza kuwafikishia (kama alivyofanya baadaye). Hakuna mtu awezaye kupinga hoja hii: Bwana Yesu aliwaagiza wanawake wafundishe kweli muhimu sana na kutoa maagizo fulani ya kiroho, kwa wanaume.

Maandiko Yenye Utata

Sasa kwa kuwa tunafahamu kidogo yale ambao Biblia inatuambia kuhusu nafasi za wanawake katika huduma, tutaweza kutafsiri vizuri yale “Maandiko yenye utata” katika nyaraka za Paulo. Hebu kwanza tutazame maneno yake kuhusu wanawake kunyamaza makanisani.

Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lolote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa (1Wakor. 14:34-35).

Kwanza – Kuna wenye swali kutokana na sababu nyingi, ikiwa hayo ni maagizo ya Paulo au anarudia kusema yale ambayo Wakorintho walikuwa wamemwandikia. Ni dhahiri kwamba katika sehemu yapili ya barua yake hiyo, Paulo alikuwa anajibu maswali ambayo Wakorintho walikuwa wamemwuliza kwa barua (ona 1Wakor. 7:1, 25; 8:1; 12:1; 16:1, 12).

Pili – katika mstari unaofuata, Paulo anaandika kitu kinachoweza kuhesabiwa kuwa ni itikio lake kwa desturi ya Wakorintho ya jumla ya kuwanyamazisha wanawake makanisani. Anaandika hivi:

Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? (1Wakor. 14:36).

Vyovyote vile, Paulo ni kama anayeuliza maswali mawili ambayo majibu yake ni dhahiri. Jibu kwa yote niHapana. Si Wakorintho waliotoa Neno la Mungu, wala Neno la Mungu halikutolewa kwao tu. Maswali ya Paulo basi ni kama makemeo, yanayoelekezwa kwenye viburi vyao. Kama ndiyo itikio lake kwa mistari hiyo miwili inayotangulia, inaonekana ni kama ifuatavyo: “Hivi, ninyi mnafikiri ni nani? Tangu lini mnatoa amri kuhusu Mungu amtumie nani kulisema Neno Lake? Mungu anaweza kuwatumia wanawake akitaka, nanyi ni wapumbavu kuwanyamazisha.”

Tafsiri hii inafaa kama tutafikiria kwamba Paulo – katika barua hii hii – tayari amekwisha andika juu ya njia inayofaa kwa wanawake kutoa unabii makanisani (ona 1Wakor. 11:5), kitu ambacho kinawataka wasinyamaze. Tena, mistari michaceh baada yah ii tunayochunguza, Paulo anawahimiza Wakorintho wote[2], ikiwa ni pamoja na wanawake, “watamani sana kutabiri” (1Wakor. 14:39, TLR). Basi itakuwa anajipinga mwenyewe kama kweli alikuwa anatoa amri ya jumla kwa wanawake kunyamaza katika ibada makanisani katika maandiko ya 14:34-35.

Mawazo Mengine

Lakini – hebu tuseme tu kwamba pengine hayo maneno ya 1Wakor. 14:34-35 ni maneno ya Paulo mwenyewe, naye anawaagiza wanawake wanyamaze. Tutafsirije maneno hayo?

Hapa tena, tutalazimika kushangaa ni kwa nini Paulo anatoa amri ya jumla namna hiyo kwa wanawake kunyamaza kabisa katika mikutano ya kanisa, wakati aliposema katika barua hiyo hiyo kwamba wanaweza kuomba hadharani na kutabiri – bila shaka katika mikutano ya kanisa.

Tena – Bila shaka Paulo aliijua mifano ile yote ambayo tumeitoa hapo mwanzoni kuhusu Mungu kuwatumia wanawake kulisema Neno Lake hadharani, hata kwa wanaume. Sasa – kwa nini awanyamazishe kabisa wale ambao Mungu amewahi kuwatia mafuta mara kwa mara ili waseme?

Kweli mawazo ya kawaida tu yanadai tukubali kwamba Paulo hakumaanisha kwamba wanawake wanyamaze kimya kabisa wakati wa ibada za kanisa. Kumbuka kwamba kanisa la kwanza walikutanikia majumbani na kula chakula pamoja. Kweli tufikiri kwamba wanawake hawakusema chochote tangu walipoingia nyumbani humo mpaka walipotoka? Kwamba hawakuzungumza chochote wakati wa kuandaa au kula chakula cha pamoja? Kwamba hawakusema chochote kwa watoto wao muda wote? Kufikiri hivyo ni ujinga.

Ikiwa mahali ambapo “wawili au watatu wamekusanyika” kwa jina la Yesu Yeye yuko katikati yao (ona Mathayo 18:20), na kama hiyo ni idadi halali ya mkutano wa kanisa, inakuwaje basi wakati wanawake wawili wanapokutanika pamoja katika jina la Yesu? Je, wasisemezane?

Hapana! Kama 1Wakorintho 14:34-35 kweli ni maagizo ya Paulo, basi alikuwa anashughulikia tatizo dogo la utaratibu katika makanisa. Kuna wanawake waliokuwa hawafuati utaratibu kwa namna fulani, kwa habari ya kuuliza maswali. Paulo hakumaanisha wanawake wanyamaze kimya kabisa kwa kipindi chote cha mkutano. Hata alipotoa maagizo yanayofanana na hayo mistari michache kabla ya hapo, yanayowahusu manabii, hakuwa na maana hiyo.

Lakini [nabii] mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze (1Wakor. 14:30, Maneno mepesi kutilia mkazo).

Hapa, maneno “anyamaze” maana yake “aache kusema kwa muda.”

Paulo pia aliwaagiza wale wanaonena kwa lugha kunyamaza kama hakuna mtafsiri kwenye kusanyiko.

Lakini asipokuwepo mwenye kufasiri, na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu (1Wakor. 14:28, Maneno mepesi kutilia mkazo).

Je, Paulo alikuwa anawaagiza watu kama hao kunyamaza kabisa wakati wote wa mkutano? Hapana! Alikuwa anawaambia wanyamaze kwa habari ya kunena kwao kwa lugha wakati hakuna mfasiri. Ona kwamba Paulo anawaambia “wanyamaze katika kanisa,” ambayo ndiyo maagizo anayotoa kwa wanawake katika 1Wakor. 14:34-35. Basi, kwa nini tutafsiri maneno ya Paulo kwa wanawake kwamba wanyamaze kanisani kuwa maana yake ni “wanyamaze kwa kipindi chote cha ibada”, kisha tutafsiri maneno yake kwa wanaonena kwa lugha bila utaratibu kuwa maana yake ni “wasiseme katika kipindi fulani cha ibada”?

Mwisho ni vizuri tuone kwamba Paulo hakuwa anazungumzana wanawake wote katika fungu hilo. Maneno yake yanawahusu wanawake walio na ndoa tu, kwa sababu wanaagizwa “wakawaulize waume zao nyumbani” kama wana maswali.[3] Pengine sehemu ya tatizo au tatizo zima kwa ujumla ni kwamba wanawake wenye ndoa walikuwa wanawauliza wanaume wengine maswali, zaidi ya waume zao. Kama ni hivyo, hali hiyo si halali, na ingedhihirisha aina fulani ya kutokuheshimu na kutokutii waume zao wenyewe. Kama hilo ndilo tatizo analoshughulikia Paulo, ndiyo sababu anajenga hoja yake kwenye ukweli kwamba wanawake wanapaswa kuwa watiifu (kwa waume zao bila shaka!) kama Torati ilivyodhihirisha kwa namna nyingi katika kurasa za kwanza kabisa za kitabu cha Mwanzo (ona 1Wakor. 14:34).

Kwa kuhitimisha, ni hivi: Kama Paulo kweli anatoa maagizo kuhusu wanawake kunyamaza kimya katika 1Wakor. 14:34-35, basi anawaambia wanawake walio-olewa tu wanyamaze kwa habari ya kuuliza maswali kwa wakati usiofaa, au kwa namna ambayo ilionyesha kutowaheshimu waume zao. Vinginevyo, wanaweza kutabiri, kuomba na kusema.

Andiko Lingine Lenye Utata

Mwisho, tunafikia fungu la pili “lenye utata” linalopatikana katika barua ya kwanza ya Paulo kwa Timotheo.

Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa (1Timo. 2:11-14).

Hakika Paulo alijua kuhusu Miriamu, Debora, Hulda na Ana – manabii wanne wanawake waliosema kwa niaba ya Mungu na kuwaambia wanawake na wanaume maneno ya Mungu na kuwafundisha mapenzi ya Mungu. Hakika alifahamu kwamba Debora, mwamuzi wa Israeli, alikuwa na mamlaka kiasi fulani juu ya wanaume na wanawake. Hakika alijua kwamba Mungu alimimina Roho Wake siku ile ya Pentekoste, akitimiza kwa sehemu unabiiw a Yoeli kuhusu siku za mwisho wakati ambapo Mungu angemimina Roho Wake juu ya wote wenye mwili, ili wana na binti watabiri na kutangaza Neno la Mungu. Hakika alijua kwamba Yesu aliwaagiza wanawake fulani wapeleke ujumbe kutoka Kwake kwa mitume Wake wanaume. Bila shaka alijua maneno yake mwenyewe, ya kuunga mkono wanawake kuomba na kutoa unabii katika mikutano ya kanisa, aliyowaandikia Wakristo wa Korintho. Bila shaka alikumbuka kwamba aliwaambia Wakorintho kwamba yeyote kati yao anaweza kupokea fundisho la kuwaambia wengine kutoka kwa Roho Mtakatifu (ona 1Wakor. 14:26). Sasa, alitaka watu wapate nini alipoandika maneno haya kwa Timotheo?

Ona kwamba Paulo anajenga hoja yake kwenye kweli mbili zinazokubaliana kutoka Mwanzo, kwa ajili ya kufundisha: (1) Adamu aliumbwa kabla ya Hawa, na (2) Hawa ndiye alidanganywa, si Adamu, naye akaangukia katika kosa. Kweli ya kwanza inathibitisha mahusiano sahihi kati ya mume na mke. Kama uumbaji unavyofundisha, mume anatakiwa kuwa kichwa – jambo ambalo Paulo analifundisha mahali pengine (ona 1Wakor. 11:3; Waefeso 5:23-24).

Kweli ya pili anayotaja Paulo haikusudii kuonyesha kwamba wanawake ni rahisi zaidi kudanganywa kuliko wanaume. Si hivyo. Ukweli ni kwamba, kwa kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume katika mwili wa Kristo, hoja inaweza kutolewa kwamba wanaume ndiyo rahisi kudanganyika kuliko wanawake. Hata hivyo – kweli yapili inaonyeah kwamba wakati mpango uliokusudiwa wa Mungu katika familia unapopuuzwa, Shetani anaweza kuingia. Tatizo la binadamu lilianza bustanini, wakati mahusiano kati ya mume na mke wake yalipotoka kwenye utaratibu – mke wa Adamu hakumtii. Adamu lazima alimwambia mke wake agizo la Mungu kuhusu tunda lililokatazwa (ona Mwanzo 2:16-17; 3:2-3). Shida ni kwamba yeye hakufuata alichoambiwa na mumewe. Kuna jinsi alivyotumia mamlaka juu yake wakati alipompa tunda hilo ale (ona Mwanzo 3:6). Hapo, si Adamu aliyemwongoza Hawa, ni Hawa alimwongoza Adamu. Matokeo yakawa balaa.

Kanisa – Mfano Wa Familia

Utaratibu ambao Mungu amekusudia kwa ajili ya familia unapaswa kuonyeshwa na kanisa. Kama nilivyosema mapema, ni muhimu kukumbuka kwamba kwa miaka mia tatu ya kwanza ya historia ya kanisa, vikundi vya kanisa vilikuwa vidogo. Walikutania majumbani. Wachungaji na wazee na waangalizi walikuwa kama baba wa familia. Huo mpango wa kanisa wa KiMungu ulifanana sana na familia, na kwa kweli ulikuwa ni familia ya kiroho, kiasi cha kwamba uongozi wa kike juu yake ungepeleka ujumbe usio sahihi kwa familia za nje na hata ndani ya kanisa. Hebu fikiri mchungaji au mzee au mwangalizi wa kike akifundisha kila wakati katika kanisa la nyumbani, na mume wake ameketi kwa utii pale, akimsikiliza akifundisha na kutii mamlaka yake. Hiyo ingekwenda kinyume na utaratibu wa Mungu katika familia, na kuweka mfano usio sahihi.

Hicho ndicho Paulo anashughulikia. Ona kwamba maneno hayo yako karibu tu na maelezo kuhusu masharti ya mtu kuwa mzee (ona 1Timo. 3:1-7). Shartri moja ni kwamba awe mwanamume. Pia ijulikane kwamba wazee walipaswa kufundisha mara kwa mara kanisani (ona 1Timo. 5:17). Maneno ya Paulo kuhusu wanawake kupokea mafundisho kwa utulivu na kutoruhusiwa kufundisha au kutawala wanaume bila shaka yanahusiana na utaratibu sahihi wa kanisa. Anachosema kwamba si sahihi ni mwanamke – kwa sehemu au kikamilifu kabisa – kutimiza kazi ya mzee au mchungaji au mwangalizi.

Hii si kusema kwamba mwanamke au mke hawezi kuomba, kutabiri, kupokea fundisho fupi la kuwaambia washirika, au kusema kwa ujumla katika mkutano wa kanisa – akiwa chini ya mamlaka ya mume wake. Hayo yote anaweza kufanya kanisani bila ya kuharibu utaratibu wa Mungu, kama ambavyo anaweza kufanya hayo yote nyumbani bila kuwa amekiuka mpango wa Mungu. Alichokatazwa kufanya kanisani ni sawa na alichokatazwa kufanya nyumbani – kumtawala mume wake, au kuwa na mamlaka juu ya mume wake.

Kutokana na mistari ya baadaye tunaona kwamba wanawake wangeweza kufanya kazi kama shemasi, sawa na wanaume (ona 1Timo. 3:12). Kuhudumu kanisani kama shemasi au mtumishi (ambayo ndiyo maana ya neno lenyewe) hakudai kuvunjwa kwa utaratibu wa Mungu kati ya mume na mke.

Hii ndiyo njia pekee ya kulinganisha maneno ya Paulo katika 1Timo. 2:11-14 na mengine yote yanayofundishwa na Maandiko. Katika kila mfano wa Maandiko tuliotazama wa Mungu kuwatumia wanawake, hakuna uliokuwa mfano wa familia kama kanisa lilivyo, na kwa hali hiyo, hakuna unaovunja utaratibu wa Mungu. Hatupati popote mfano wa wanawake wakiwa na mamlaka juu ya waume zao katika familia. Kumbuka tena kusanyiko dogo la familia kadhaa katika nyumba, na mke ndiye anasimamia kundi hilo: akifundisha na kulisimamia wakati mume wake ameketi tu na kutii uongozi wake. Mungu hataki hayo, maana ni kinyume na utaratibu Wake kwa ajili ya familia.

Ila – kwa Debora kuwa mwamuzi wa Israeli, Ana kuwaambia wanaume habari za kristo, na Mariamu na rafiki zake kuwaambia mitume kuhusu ufufuo wa Kristo – hakuna ujumbe wowote mbaya unaopelekwa au kwa njia yoyote ile kuonyesha isivyostahili utaratibu wa Mungu katika familia. Kusanyiko la kila mara la kanisa ni nyeti, ambapo ipo hatari kwa ujumbe usiostahili kutumwa ikiwa wanawake au wake watakuwa na mamlaka na kuwafundisha wanaume au waume kila mara.

Kumalizia

Kama tukijiuliza tu hivi: “Ni kitu gani kinachoweza kuwa kosa kimsingi kwa wanawake kufanya huduma, wakiwatumikia wengine kwa moyo wa huruma na kutumia vipawa vyao walivyopewa na Mungu? Kuna kanuni gani ya kiadili inayovunjwa?” Ndipo baadaye tunatambua kwamba kuvunjwa kwa kanuni ni kama huduma ya mwanamke kwa namna moja au nyingine ingehalifu utaratibu wa Mungu kwa habari ya mahusiano kati ya wanaume na wanawake, kati ya waume na wake zao. Katika mafungu yote mawili “yenye utata” tuliyotazama, Paulo anataja utaratibu wa Mungu katika ndoa kama sababu yake ya kusema anachosema.

Basi, tunatambua kwamba wanawake wamezuiliwa kufanya huduma kwa sehemu ndogo sana. Kwa njia zingine nyingi tena kubwa, Mungu anataka kuwatumia wanawake kwa ajili ya utukufu Wake, Naye amekuwa akifanya hivyo kwa maelfu ya miaka. Maandiko yanazungumza kuhusu michango mingi inayofaa ambayo wanawake wameitoa kwa ufalme wa Mungu – na tumekwisha tazama baadhi yake. Tusije kusahau kwamba baadhi ya marafiki wa Yesu wa karibu sana walikuwa wanawake (ona Yohana 11:5), na kwamba wanawake walisaidia huduma Yake kifedha (ona Luka 8:1-3). Hakuna mwanamume anayetajwa kuwa alifanya hivyo. Yule mwanamke kisimani Samaria aliwaambia wanaume habari za Kristo kijijini kwake, na wengi walimwamini Yesu (ona Yohana 4:28-30, 39). Mwanafunzi mwanamke aitwaye Tabitha anasemekana kuwa “alizidi katika matendo ya wema na fadhili aliyofanya daima” (Matendo 9:36, TLR). Mwanamke ndiye alimtia Yesu mafuta kwa ajili ya maziko Yake, na alimsifu kwa hilo wakati wanaume wengine wlaipolalamika (ona Marko 14:3-9). Mwisho, Biblia inaandika kwamba wanawake ndiyo waliomwombolezea Yesu alipobeba msalaba Wake katika mitaa ya Yerusalemu. Hakuna mwanamume anayetajwa katika hilo. Hii mifano na mingi kama hiyo inapaswa kuwatia moyo wanawake kuinuka na kutimiza huduma zao walizopewa na Mungu. Tunawahitaji wote!

———————————–

– Ijulikane kwamba kila mwanamume mwingine tangu Adamu ameumbwa na Mungu baada ya Mungu kuwaumba wanawake ambao walimzaa. Kila mwanamume baada ya Adamu ametoka kwa mwanamke, kama Paulo anavyotukumbusha katika 1Wakor. 11:11-12. Sidhani kama kuna yeyote ambaye atatoa hoja kwamba huo utaratibu wa KiMungu unathibitisha kwamba wanaume ni wadogo ukilinganisha na mama zao.

– Ushauri wa Paulo ni kwa “ndugu” – neno analotumia mara 27 katika barua hii, na ambalo linawahusu Wakristo wote katika Korintho, si wanaume tu.

-Ni vizuri kujua kwamba katika lugha ya asili ya Kiyunani, hakuna maneno tofauti kwa wanawake na mke,au mwanamume na mume. Hivyo inabidi kutambua kutoka mantiki ikiwa mwandishi anazungumza juu ya wanaume na wanawake, au waume na wake. Katika fungu tunalotazama, Paulo anazungumza na wake, kwa sababu wao ndiyo wangeweza kuwauliza waume zao chochote wakiwa nyumbani.

—David Servant

Advertisements

13 thoughts on “Wanawake Katika Huduma

 1. Wapendwa;
  Madhehebu bado wanaabudu damu za wanawake kama kipindi cha nyuma alivyokuwa akiabudiwa mungu mke aitwaye DIANA.
  Ukiliacha Neno la Mungu utaamini chochote.Madhehebu wanamini mungu mwenye nafsi tatu,wanabatiza kwa vyeo Baba Mwana na Roho Mtakatifu badala ya kubatiza KWA JINA NA YESU KRISTO ( MATENDO 2:38, 8: 14-17, 10: 48, 19:1-7) na wengine wanabatiza watoto,wanaruhusu wanawake kushika huduma mbalimbali kama vile wachungaji,wainjilisti,mashemasi,….nk.
  Madhehebu Wamechanganyisha MBEGU, wamechanganya SIASA na DINI na wamepata Dini CHOTARA (Hybrid Religion).Ndio maana Kila mwenye roho ya kidhehebu hana budi kutetea Wahubiri Wanawake ( MA-YEZEBELI).
  Huu ni wakati wa roho ya yule mwanamke YEZEBELI.Hiki ni kizazi cha LAODIKIA yaani kizazi cha HAKI ZA WATU, hivyo lazima MADHEHEBU wadai haki za wanawake,haki za Dini na Siasa.
  Hebu soma hali ya kizazi hiki kilicho katika kipindi cha LAODIKIA na USHAURI wa MUNGU kwenye UFUNUO 3:14-22.
  >>>MUNGU NDIYE MKWELI PEKE YAKE<<>>Mwanamke ni Mchungaji wa WATOTO ( Ni mlezi wa watoto ) 1 TIMOTHEO 2:15 “15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.” <<<
  TAHADHARI.
  WAGALATIA 1:8-9 " 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
  9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe."
  *** NA WATU WOTE WOTE WASEME AMINA.****

 2. Wapendwa;
  Madhehebu bado wanaabudu damu za wanawake kama kipindi cha nyuma alivyokuwa akiabudiwa mungu mke aitwaye DIANA.
  Ukiliacha Neno la Mungu utaamini chochote.Madhehebu wanamini mungu mwenye nafsi tatu,wanabatiza kwa vyeo Baba Mwana na Roho Mtakatifu badala ya kubatiza KWA JINA NA YESU KRISTO ( MATENDO 2:38, 8: 14-17, 10: 48, 19:1-7) na wengine wanabatiza watoto,wanaruhusu wanawake kushika huduma mbalimbali kama vile wachungaji,wainjilisti,mashemasi,….nk.
  Madhehebu Wamechanganyisha MBEGU, wamechanganya SIASA na DINI na wamepata Dini CHOTARA (Hybrid Religion).Ndio maana Kila mwenye roho ya kidhehebu hana budi kutetea Wahubiri Wanawake ( MA-YEZEBELI).
  Huu ni wakati wa roho ya yule mwanamke YEZEBELI.Hiki ni kizazi cha LAODIKIA yaani kizazi cha HAKI ZA WATU, hivyo lazima MADHEHEBU wadai haki za wanawake,haki za Dini na Siasa.
  Hebu soma hali ya kizazi hiki kilicho katika kipindi cha LAODIKIA na USHAURI wa MUNGU kwenye UFUNUO 3:14-22 “14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
  16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
  19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
  20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
  21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
  22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”
  >>>MUNGU NDIYE MKWELI PEKE YAKE<<>>Mwanamke ni Mchungaji wa WATOTO ( Ni mlezi wa watoto ) 1 TIMOTHEO 2:15 “15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.” <<<
  TAHADHARI.
  WAGALATIA 1:8-9 " 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
  9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe."
  *** NA WATU WOTE WOTE WASEME AMINA.****

 3. Wapendwa;
  Madhehebu bado wanaabudu damu za wanawake kama kipindi cha nyuma alivyokuwa akiabudiwa mungu mke aitwaye DIANA.
  Ukiliacha Neno la Mungu utaamini chochote.Madhehebu wanamini mungu mwenye nafsi tatu,wanabatiza kwa vyeo Baba Mwana na Roho Mtakatifu badala ya kubatiza KWA JINA NA YESU KRISTO ( MATENDO 2:38, 8: 14-17, 10: 48, 19:1-7) na wengine wanabatiza watoto,wanaruhusu wanawake kushika huduma mbalimbali kama vile wachungaji,wainjilisti,mashemasi,….nk.
  Madhehebu Wamechanganyisha MBEGU, wamechanganya SIASA na DINI na wamepata Dini CHOTARA (Hybrid Religion)
  Ndio maana Kila mwenye roho ya kidhehebu hana budi kutetea Wahubiri Wanawake ( MA-YEZEBELI).
  Huu ni wakati wa roho ya yule mwanamke YEZEBELI.
  Hiki ni kizazi cha LAODIKIA yaani kizazi cha HAKI ZA WATU, hivyo lazima MADHEHEBU wadai haki za wanawake,haki za Dini na Siasa.
  Hebu soma hali ya kizazi hiki kilicho katika kipindi cha LAODIKIA na USHAURI wa MUNGU kwenye UFUNUO 3:14-22 “14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
  15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
  16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
  17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
  18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
  19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
  20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
  21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
  22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”
  >>>MUNGU NDIYE MKWELI PEKE YAKE<<>>Mwanamke ni Mchungaji wa WATOTO ( Ni mlezi wa watoto ) 1 TIMOTHEO 2:15 “15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.” <<<
  TAHADHARI.
  WAGALATIA 1:8-9 " 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
  9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe."
  *** NA WATU WOTE WOTE WASEME AMINA.****

 4. Seleli,
  Hoja yako hii nilikuwa sijaiona tangu mwaka jana!! Pole sana, umepotea sana na wewe!!!
  Kama ulivyoona nimemuuliza Stella, nilimaanisha hivyo!! Wewe kama una hoja kuhusu utawala wa wanawake ndani ya kanisa, lete hoja!! Usiniletee hisia hapa za kinyamwezi!! Leta hoja!! Sawa bro!!
  Kazi kwako
  Siyi

 5. Lwembe,

  Raise your standards Brother, What are u talking meeeeeen? So kama Walikua na Mila ndio iidhinishwe kua tenga/under-estimate/zero down Wanawake wenye RM kama na sisi? We vipi Kaka mbona unaongea vitu chekechea hapa! Acha bwana mambo hayo, unashusha ‘’P’’

  Siyi,

  What do you mean jibu lako kwa Stele! Fafanua ili nikunyake vema! Amekosea nini kwani! Weka peupe fasta ili twende kazi, naomba kazi iyo tema haraka. Simply she meant, with Roho wa Bwana upon all…men or women. Every task including kutawala mengi si Mume wake tu, mengine na wengine….possible kabisa kwa uwezeshwaji wa RM.

  Press on.

 6. Oguda,

  Hahahaha…!Mtume Paulo atakuwa amekupigia “thumbs up” kwa kulisimamia Neno la Mungu! Umemuona David anavyotumia akili? Wako wengi wa staili yake, na mwisho, kwao Biblia huwa ni “Kijiwe”!!!

  Hebu mfikirie mtu wa jinsi hii ambaye anadai kuwa yeye ni mkristo, halafu anapokushuhudia kuhusu Neno la Mungu anakuambia, “Maandiko yenye Utata”! Kama si utani ni nini? Neno la Mungu lina Utata?

  Wanajiandikiaga tu mambo ambayo hawayajui? Kufundisha kwamba kuna Utata ndani ya Biblia, ni dalili ya kwamba hata jambo lenyewe hulijui! Na kwa kukosa ufahamu, ndio hao hufikia kuamini kwamba mitume walikuwa wakifundisha na mila!

  Maandiko yooote kama yalivyo, ndio Mila mpya ya Mkristo, mkiiona ni ngumu kuifuata, basi rudini kwenye mizimu yenu, msiwahayawanishe mabinti za Mungu!!!

 7. Stelle,
  Jitahidi ulielewe neno dada!! Kwani nani alikwambia kuwa kutabiri na kutawala ni kitu kimoja?

 8. “Naan itakuwa siku za mwisho nitamwagia roho yangu watumishi wangu wanawake na wanaume nao watatabiri matendo ya mitume 2:18
  roho amemwagwa hivyo ni wewe kujiachia ili umpokee.
  amen,stella

 9. David,

  Asante kwa somo, ni zuri kweli, lime summarize vema yale yote tumejadili, kuelimishana, kuchallenjiana na kuhojiana sana ktk mada mbili humu, moja inaendelea namely-‘’Mafundisho kuhusu wanawake yanatafsiriwa vibaya!! na nyingine imekwisha almost inaitwa, Kanisa la Kilutheri Marekani lapata Askofu Mkuu mwanamke!! Limemaliza vema somo hili kuonyesha, WANAWAKE WANAYO NAFASI KUBWA ktk UTUMISHI NDANI NA NJE YA KANISA, IMEDHIHIRIKA IVYO PAST,PRESENT AND SHALL BE IN THE FUTURE, anything less than that, ni kibinadamu kidume tu, as simply as that! Sijui kama unasomaga mada humu kabla ya kupost, ungeyaona hayo yote uko tulipojadili kweli kweli, unaweza pitia kupata pia upako mwingine, ila mada ya Wanawake, unahitaji muda maana ni kubwa sana, so far ina comments-134!

  Oguda,

  Plz don’t simply sweep the statement kukataa bila base yenye mashiko somo lake! SOMO HILI LA DAVID-aliloprove beyond doubts kuhusu Wanawake na huduma, kwa Maandiko kihalali-2Timo.2:15d. na kwa ukaaji wa Neno la Mungu kwa hekima yote-Col.3:16, halina tashwishi hata kidogo, if you wish, somo pia my comments katika mada zile 2 juu. Unless ulete hoja mahususi kupinga na kweli kupinga kwa uhalali na sahihi, mimi sioni kama una jambo serious la kukataa alichosema. Plz re-read kwa utulivu alichofundisha na zile mada 2, ili usije anza kujibu/comment mambo kumbe kila kitu kimeshaweka wazi kwa hoja za nguvu mno kitambo.Plz prove kua ulichosema ni sahihi bila kuacha shaka na alichosema David na siye wengine ktk mada zile ni off the Bible, off the truth, bila ivyo, you are overpowered my brother kwa hoja in this topic.

  Press on.

 10. Hayo mafundisho ndg yangu D. Servant, sehemu kubwa nimegundua, ni , ACTIVIZM/ UHANAHARAKATI. Or, call it Gender Sensitivity. However, its very bad luck that, watu wa Mungu wameamua kuwa wana harakati kbs. Tafasiri nyingi humo nimezisoma, huna kitu, naye Mungu akusaidie tu, ninakuonea huruma saana. Poole.

 11. Asante sana mtumishi nimejifunza tusiadharau wanawake katika utumishi. Wanaobisha wote baba yao ni Ibilisi hawatoki kwa Mungu aliyetumba asiye na upendeleo.

 12. Jambo la msingi ni kwamba tumeacha upendo kwani mtu ni mtu haijalishi jinsia yake, watu wanao wabagua wanawake wameathilika kisaikolojia na wamepungiwa na upendo alio tuagiza Yesu kupendana kama tunavyo ji penda nafsi zetu hapa haijalishi jinsia ya mtu. b blessd by Mabuga Emmanuel

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s