Wokovu una nguvu kuliko Siasa – Askofu Kakobe

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospal Bible Fellowship, Zacharia Kakobe.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospal Bible Fellowship, Zacharia Kakobe ametoa ujumbe wa wazi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Terezya Huvisa kwa kuwaambia kuwa kama wanataka kwenda mbinguni hawana budi wajitangaze hadharani kuwa wameokoka.

Kiongozi huyo wa kiroho aliyasema hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kusikia kupitia kwenye redio kuwa Mangula aliimbisha pambio kwenye msiba wa Askofu Moses Kulola aliyefariki dunia Agosti 29 mwaka huu na kuzikwa Mwanza. “Nilishangaa sana kusikia mtu mzito kama Philip Mangula akitajwa kuwa aliimbisha pambio kwenye msiba wa Askofu Kulola, niwaambie pamoja na viongozi wengine wote kwamba mtu aliyeokoka akiogopa kujitangaza kwamba ameokoa hawezi kwenda peponi,” alisema Kakobe.

Alifafanua kwamba wokovu una nguvu kuliko siasa, hivyo akawataka viongozi wote wa chama na serikali kuokoka na kujitangaza bila woga. Akisimulia jinsi alivyookoka, Askofu Kakobe alisema alifanya hivyo mwaka 1973 akiwa anasoma Mkwawa Iringa lakini akaacha baada ya waliookoka kumsusia alipokuwa akiwasalimia kiimani “Bwana Yesu Afiwe” nao kumnyamazia.

“Nilikuja kuokoka tena baada ya miaka saba kupita na hapo nikawa mwokovu moja kwa moja hadi sasa,” alisema.

–Evan Stambuli

Advertisements

60 thoughts on “Wokovu una nguvu kuliko Siasa – Askofu Kakobe

 1. Marehemu Myles Munroe, alipokuwa anaongea na viongozi wa kanisa Diamond Jubilee alishauri na akahimiza akisema:

  Wahimizeni vijana wenu waingie kwenye siasa wakaangaze huko, wakawe chumvi huko, wakawe chachu huko.

  Ni kitu cha kusikitisha sana kulazimisha nuru ing’are nuruni, chachu(amira) ionyeshe u amira wake kwenye unga wa maandazi ulioumka tayari.

  Na ujinga huu ambao kimsingi ni uongo wa kuwaambia wenye haki wajiepushe na siasa, waovu ndo watawale hiyo siasa, tusipoamua kuuvua tutaota sugu magoti tukimwomba Mungu atupe viongozi wazuri watakaozuia mambo ya Epa, Escrow, Meremeta, nk.kutokea, na Mungu hatajibu hayo maombi.

  Mchongoma hauwezi kuzaa zabibu. Tusitegemee wafilisti wawe wenye kutenda haki wakati hakuna asili ya haki ndani yao.

  Walitudanganya kuwa hatutakiwi kuchanganya siasa na dini, wakati wanajua kabisa kuwa dini na siasa ni mtindo wa maisha ya kila siku ambao ni lazima tu mtu uuishi.

  Tumewaachia wakora watutawale na kutupeleka kama mungu wao (shetani)anavyotaka. Halafu wakituumiza sana tunaenda kusema kwa Mungu, wakati sisi wenyewe tuna nafasi ya kushika hizo nyadhifa na kuidhihirisha haki ya kristo.

  Sijui akina Daniel, akina Yusufu, akina Nehemia, wao kwa nini hawakuhesabiwa dhambi kujihusisha na mambo siasa huku wakiwa manabii!

  Kama tunaendelea kuona kuwa siasa ni dhambi basi tujue tunakiweka rehani kizazi chetu, na watakuja kutuhukumu kwa kutuhusu huu ujinga.

  Kazi yetu sisi ni kusubiri tu kusikia kuwa kuna hela za Escrow zimeibwa tuende kwrnye maombi kumwambia Mungu awashugulikie hao wezi. Na hajawahi kuwashugulikia kwa sababu haibugu maombi ya kijinga.

  Na kusubiri tu, kuna scandal za wizi wa mabilioni mengi kiliko Escrow zinakuja, tutaomba mpaka magoti yapinde.

  Sijui kinachotuogopesha kupeleka nuru ya kristo kwenye siasa ni nini.

  Maana sijawahi ona wapi biblia imesema kumtumikia Mungu kwenye siasa ni dhambi na ni marufuku.

  Acha sisi tupige injili na kwenye siasa tunaingia donge zima litakapochachuka najua nanyi mtafurahia matunda yake!

  Nuru hung’ara gizani siyo nuruni!

 2. Nuru na giza haviwezi katu kukaa pamoja, Yesu ni nuru shetani ni giza, kama kweli umekutana na Yesu na akakuokoa unawezaje kujizuia kujitangaza, maana ukimpokea Yesu umepokea nguvu ikuwezeshayo kufanya mambo yasiyo
  ya kawaida, kuna mifano ya watu wengi walio shindwa kujizuia kujitangaza walipokutana na Yesu, mfano mwanamke msamalia yoh 4:1…. mdo 2:1…. na yule mtu aliekuwa mtoza ushuru, Razalo. wokovu sio siri, Yesu kasema unawezaje kuwasha taa na kuiweka chini ya uvungu? Taa ikiwashwa inatakiwa iwekwe juu ya kiango ili iwaangazie wote. Mtu asietaka kujitangaza kama ameokoka, wakati huo anasema ameokoka ana ajenda yake, au mchanga kiroho.

 3. wapendwa HAkuna anaejua Mzigo alonao Kakobe katika kuhubiri injili tena ullimwenguni kote, na kwa bahati mbaya sana siku ya mwisho ndio tutajua ukweli wa mambo yote jaman vingine tuwe tunafanya utatifit kwanza ndio tuzungumze
  mfano dada Vai sidhani kama unaifuatilia hii kesi vizuri na hata historia ya kanisa hilo la Full Gospel Bible Fellowship, kwa faida ya wengi ile kesi ilifunguliwa na waliokua waumini na wakaasi zamani sana kwahiyo walipokwenda kufungua kesi ya madai walikua si waumini tayari, na la kushangaza ni wao wenyewe ndio walioomba kesi ifutwe lakini Kakobe akakataa kwa sababu moja tu kwamba iendelee ili ijulikane na watu wote kwamba ni kweli amekula fedha za kanisa au laa! hivyo ile kesi bado iko mahakamani dada vai,
  Lakin si kweli pia kuwa alisema kanisa ni la kwake na familia yake. jamani hebu tutumie akili kidogo tu kua siku zote kanisa ni taasisi na kama taasii kwa mujibu wa sheria lazima iwe na katiba yake na mfumo wa uongozi na hakuna kanisa lolote hapa nchini lililo chini ya mtu mmoja hivyo ukitaka kujua kanisa la Full Gospel Bible Fellowship ni la nani jaribu kutembelea website yao http://www.fgbfchurch.org. Kakobe ni askofu mkuu tu wa hilo kanisa na wala si kanisa lake kanisa ni la watakatifu wa Mungu walioko humo akiwemo Kakobe

 4. Sungura,

  Mawazo yetu yanakuwa na maana iwapo tu yatakuwa yamejengeka ktk Msingi wa Neno la Mungu! Uthibitisho unaoutaka nikupe, sidhani kama unalielewa unalolitaka!

  Pia nilikutegemea uje na mifano ya kimaandiko ya watumishi wa Mungu waliochanganya na siasa, badala yake unanipa mawazo yako tu, angalau John alijaribu!

  Lakini, iwapo kanisa litakuwa ni sehemu ya siasa, basi huko ni zaidi ya kushindwa! Hebu wazia kwamba Mungu angekuwa ni Mkomyunist, na Urusi ilivyosambaratika, naye si angeishia kuwa na stori kama zako! Au Mungu angekuwa ni Mjamaa, vipi leo na hali yetu ilipo, si atakuwa ameshindwa!!! Yesu alipojaribiwa aiache kazi aliyoijia awe mwanasiasa, aitawala miji yote mikubwa unayoijua, alikataa!
  Mt 4:8-9 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.”
  Umemuona anayezimiliki siasa? Huyo ndiye Prince wa ulimwengu, na lazima umsujudie kama nawe unataka uwe sehemu ya milki yake!

  Na kwa kuwa hayo ndiyo mnayoyaendea, basi mkiisha kumsujudia, subirini mtakapofikishwa kwenye pinacle ya siasa, hapo askofu wako akiwa ndiye mkuu wa mkoa pia, atakapolazimika kuwafungisha ndoa za kiserikali mashoga na wasagaji, na hakuna kukataa, sheria ikiisha kupitishwa!

  Kuhusu Mapenzi ya Mungu, kwa kifupi ni Instructions unazopewa, je, unazitii au unaanzisha mambo yako njiani kama Sauli? Yaani mlipoambiwa, “enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri Injili”, mlipaswa kubaki katika maelekezo hayo, lakini ninyi huko njiani mmeanzisha mambo yenu, mnataka na siasa!!!

  Hata hivyo, nakushukuru Sungura, kwa kubadilishana mawazo!

  Gbu!

 5. Lwembe,
  Mawazo yako yatabaki kuwa mawazo yako, na hakuna kosa kuwa na mawazo ya namna hiyo.
  Lakini kusema kweli umeshindwa kuyajengea hoja madhutbuti za kuyathibitisha kuwa hivyo unavyowaza ndivyo inavyotakiwa kuwa.

  Hakuna kosa lolote la kimaandiko la Kokobe kuambatana na wanasiasa, kinyume chake, kufanya hivyo ni kitu chema.

  Na hakuna msingi wowote wa kibiblia wa katazo kwa mtu aliye katika huduma zile tano kuwa kiongozi katika tasisi nyingine ya kijamii. Kwa yeyote mwenye uwezo wa ki karisma kufanya hivyo anaweza akafanya tu.

  Uchaguzi wa kambi za kutumikia uko katika njia mbili tu; au kumtumikia shetani ama kumtumikia Mungu. Hizi ndio njia mbili ambazo haziwezi kukaa pamoja.
  Na kumtumikia Mungu si kulihudumia neno tu, bali mtu anaweza alihudumia neno(huduma tano) na huku akaendelea kuwa mkuu wa chuo,mwalimu, waziri, MD, n.k. Sio dhambi.

  Kama watu huchukulia kila kauli za watumishi wa Mungu kama unabii, hayo ni makosa, na hatutakiwi kuyafanya mambo yawe hivyo, maana hayapaswi kuwa hivyo.

  Hata nabii kuna wakati ni baba/mama wa familia,kumna wakati ni mume/mke wa mtu, na kuna wakati ni mwanajamii wa jamii fulani anayepaswa kuhusika katika mambo fulani ya kijamii.Sasa kama kila kauli yake ni unabii,maisha yatakuwa magumu sana kwake na kwa wanaomzunguka.

  Sijui sana kauli ya mch. Kakobe ilikuwaje. Lakini najua kitu kimoja kuwa CCM mwaka 1995 kihalali walishindwa na Mrema. Walichakachua matokeo,haikutosha wakaamua kufuta kabisa matokeo ya mkoa wa Dar es Salaam.

  Ndio maana nilisema,mtu ukitaka kujua kama Mrema alishinda, basi ni vizuri kuwauliza viongozi wa ccm maana wanaujua vizuri ukweli wa kauli ya Kakobe!

  Kuhusu aina za mapenzi ya Mungu nilizosema,hazihusiki tu na kutimia kwa unabii fulani. Hio mfano unabii kutimia niliutumia tu katika kufafanua.
  Lakini ukweli ni kuwa mapenzi yoyote ya Mungu kwa mwanadamu yako katika hizo aina mbili(Burumai & Tharema). Yaani yanayohitaji uhusika wa mtu, na yasiyohitaji uhusika wa mtu, ila Mungu peke yake, yawe yanahusu unabii au mambo mengine.

  -e.g, ni mapenzi ya Mungu mtu kupona, lakini lazima anayeponywa ahusike, hasa katika suala la kuamini (Tharema).
  – Yalikuwa ni mapenzi ya Mungu Yesu azaliwe kupitia mtu,lakini huyo mtu haikuwa lazima aamini ndipo hilo kusudi lifanyike (Burumai).

  Asante!

 6. Sungura,

  Mitaani, mtu akikuambia ‘utaona!’ jibu rahisi analopatiwa ni “Dua la kuku halimpati mwewe!” lakini mtumishi wa Mungu akikuambia “Utaona!” upesi watu watakushauri umuendee na kumuomba msamaha! Basi elewa kuwa kauli za watumishi huchukuliwa kipekee sana, na kama ni kuhusu mambo yajayo, basi huitwa “Unabii”!!! Pia unanitaka nikufahamishe kauli aliyoitoa, kwani wewe ulipokuwa ukijadili jambo hili, unataka kuniambia kuwa hata kauli yenyewe huijui?

  Katika jambo la Mapenzi ya Mungu, nimekuelewa vizuri sana, lakini kuna jambo moja dogo sana ambalo nahisi umelikosa. Haya Mapenzi ya Mungu uliyoyaelezea katika zile aina mbili, “Burumai” na “Tharema”, zaidi ninayaona ni UNABII, kule kutimia kwake, hizo jinsi mbili!

  Lakini Mapenzi ya Mungu ninayoyazungumzia mimi hayahusiani na kutimia kwa unabii, bali uhusiano wa Mungu na nabii wake. Mfano wa Balaamu nilioutumia kama ukiutazama kwa kituo unaweza kuliona jambo hilo kwa urahisi!

  Balaamu alipomuendea Mungu ili kuyajua Mapenzi yake kuhusu suala alilokuja nalo Balaki, Mapenzi Makamilifu ya Mungu kuhusu jambo hilo, yalikuwa ni lile jibu alilopewa “… USIENDE PAMOJA NAO; WALA USIWALAANI WATU HAWA, …” Nabii Balaamu alipaswa kubaki katika hayo Mapenzi Makamilifu ya Mungu aliyopewa!

  Lakini akiisha kupewa jibu hilo, aliporudiwa na ahadi za pesa na heshima, akajitoa akili akarudi tena kwa Mungu kwa suala lie lile alilokwisha kupewa jibu, na sasa akitaka kumlazimisha Mungu amkubalie! Mungu mwenye kuyasoma mawazo yetu, akamkubalia aende nao! Hii ndiyo PERMISSIVE WILL ya Mungu, kwa watumishi wanaolazimisha mambo! Hes 22:20 “Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao…” Na ili kutudhihirishia jambo hilo lisivyompendeza Mungu licha ya kuliruhusu, “, “22-Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda…”!!! Hata inawezekana kwamba kama si Kakobe kuongazana nao na kutoa unabii au utabiri au chochote alichokisema, huenda Mrema ANGESHINDA, lakini kwa kutopendezwa na mtumishi wake aliyeiacha madhabahu, akawapiga chini wote!

  Basi hayo ndiyo ninayoyazungumzia mimi, ni kuhusu Mungu na mtumishi wake anayejiingiza katika tamaa na kutafuta uhalali wa kuuacha wito wake, lile Neno alilopewa kwanza!

  Maswali uliyoniuliza labda nikujibu hivi:
  Kuhusu Kakobe kutangaza jumbe mbili, Mungu huwa hafanyi lolote bila kuwajulisha watumishi wake manabii kwanza, kwahiyo kama kuna mabadiliko, makusanyiko yetu yaliyo na vipawa vya unabii, yangetuhudumia majibu hayo!

  “”Je unamaanisha kuwa mchungaji, nabii, mtume, au mwinjilisti hawezi kuwa mwanasiasa huku anaendelea na huduma?””
  Jibu langu ni NDIO, ni lazima achague kambi ya kuitumikia, kwa sababu nafasi zote ni za kiuongozi, na kunaweza kukawa na conflict of interests ktk kuyatumikia makundi hayo mawili!

  Kuhusu, “Na je, kwani Kakobe aliacha/ameacha special duty yake na kukimbilia siasa? ”
  Tunachokiongelea hapa ni ushiriki wa askofu katika siasa, na si kuwaombea wagonjwa, ndio maana nilizungumzia kutembea katika opinions mbili, it breeds hypocrites, jambo ambalo si zuri kwa watumishi wa Mungu!

  Siasa ndg yangu zipo, na Mungu alikwisha kuyatenganisha makundi hayo mawili!

  Gbu!

 7. Lwembe,
  Kwa nini hujataka kunipa nukuu ya alichokisema Kakobe ili tujue kama ulikuwa unabii au la?

 8. Ndg John,

  Usinishangae sana, badala yake litafakari Neno la Mungu ili uujue Moyo wake!

  Huo mfano wa Daudi unaoniletea, naona ni kuyalazimisha mambo ambavyo mwisho wa siku utaishia kwenye mafundisho yasiyo na Hesabu mbele za Mungu! Unabii wa Daudi ni sawa na ukuhani tulionao sisi leo hii, pia ni kipawa, na pia ni kule Kutiwa Mafuta, yaani Kujazwa Roho Mtakatifu. Lakini Daudi alipokuwa mfalme, wapo manabii waliohusika katika kulihudumu Neno la Mungu:-

  1Sam 22:5 “Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, Usikae hapa ngomeni; ondoka, ukaende mpaka nchi ya Yuda. Ndipo Daudi akaondoka, akaenda zake, …”

  2Sam 7:1… “Ikawa usiku uo huo, neno la BWANA likamfikia Nathani kusema, Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, BWANA asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?”

  Umeelewa John? Hatumuwekei Mungu mipaka, bali tunayatazama Mapenzi yake! Jaribu kumuangalia Sauli pia akiisha Kutiwa Mafuta, 1Sam 10:10-11 “Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao. … Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?”Bali Nabii Samweli alikuwepo, Sauli alitiwa Mafuta kutawala kama Daudi!!

  Gbu!

 9. CK Lwembe unashangaza sana unapobishana na kukataa manabii wasijihusishe na siasa wala kuandamana na wanasiasa….unamfahamu mfalme Daudi??..kama ndio unatakuwa unajua hakika cheo alichokuwa nacho ni kama rais wa nchi kwa sasa….Je unajua kuwa rais Daudi alikuwa nabii??..ukisoma Matendo 2:29-30 ” Basi kwa kuwa Daudi ni nabii..”..

  ..Mungu anabaki kuwa Mungu huwezi kumwekea mipaka ya watumishi wake watumike maeneo gani.

  John

 10. Ndugu Vai,

  Vai na wewe jamani!!! Ukiongozwa unadhani umetukanwa!!! Vai, leta shukran kwa Mungu wakati wandugu wako tayari kukuombea! Kwa nini uendelee tu ndani ya njia ya upotevu?
  Vai, ningelipenda ubandike hapa jibu ya kuomba msaada wa maombi; itoke moyoni mwako.

  Bwana Yesu akusaidie.

 11. Vai kuna msemo usemao wajinga ndio waliwao. Huo msemo unakuhusu, fungua ufahamu wako upate kuelewa.
  Unapotea si kwa sababu ya kutokujua nini kimeandikwa kwenye biblia bali kwa kutokujua kilichoandikwa kina maana gani.

  Leo jina la Mungu halikai kwenye kiwanja, au eneo ,au jengo, au kwenye mlima. Kwa taarifa yako Mungu hayuko pool of Siloam church, huko hakai siku hizi. Kama hauko nae moyoni mwako jua imekula kwako mazima.

  Kuna siku moja utayakumbuka haya maneno tunayokwambia hapa, Mungu akusaidie tu isiwe too late!

  Pole sana.

 12. Furaha, Vai,

  Msimpe sifa Askofu au makanisa. Sifa ni za Bwana wetu Yesu Kristo. Hamjue kam hata “makanisa” za kishetani zinazo sifa? Muumini wa kanisa fulani akianza pinga filimbi akikuza jina la mchungaji wake, bah !!!!!! Au akikuza jina la kanisa(jengo) lake, hum!!!

  Jesus bless you!

 13. Ndugu Furaha,
  Mungu akupe Neema kubwa uweze kujua mahali sahihi Mungu alipoliweka jina lake ili uweze kumwabudu katika roho na kweli. Kwa Neema ya Mungu jinsi ilivyo kubwa itakuwezesha siku moja ndugu Furaha na wengine wenye mtazamamo kama wako kupajua mahali sahihi Mungu alipoliweka jina lake na akatuagiza kuwa wote tuelekeze nyuso zetu hapo ( Kumb 12:7)
  kwa hiyo mnatakiwa kufahamu kwamba si kila mahali pamechaguliwa na Bwana pengine pamechaguliwa na watu na wanadamu tu. MUNGU AMEPACHAGUA THE POOL OF SILOAM CHURCH! hata kama mkikataa, mkipinga, mkitukana, lakini mjue kwamba UKWELI ndio huo ktk Jina la YESU!

 14. Ukitaka kuona matunda ya Askofu Zachary Kakobe njoo kanisani juma pili au tembelea makanisa zaidi ya mia 400 ambayo Mungu ameyafungua kupitia Askofu Kakobe au ingia You tube search Bishop Zachary Kakobe angalia shuhuda za watu kutoka nchi mbalimbali kwenye mikutano nchi mbalimbali kama Korea DR Congo nk Mimi mwenyewe ni tunda moja wapo la Askofu Zachary Kakobe hapo mwanzo nilikua mtenda dhambi na sasa na sasa nipo ndani ya Kristo kupitia neno la Mungu aliloubiri Askofu Zachary Kakobe

 15. Shalom wana wa Mungu!

  Mungu ni wa ajabu. Ndiyo maana kumuelewa ni vigumu sana. Tunatakiwa kumtii na kumuogopa. Mungu hawezi jichanganya wala kuchanganyikiwa. Anapotumia chombo chake anakitumia jinsi atakavyo. Kuna wale manabii ambao aliwatumia mpaka kazi ikawaletea kifo, na wengine akawaepusha lile jambo, yote kwa utukufu wake na kwa faida yetu. Nafikiri munawafahamu vizuri munaposoma Biblia. Kwa akili zetu tunawezafikiri Mungu alijichanganya wakati ni jambo analoona ni halali kwa faida yetu. Nataka tujue kama unabii kutoka Mwenyezi Mungu ni lazma utimilike. Hii haimaanishe kam Mungu hawezi manage ujumbe jinsi atakavyo. Inafanyika wakati kuna Neno kubwa Mungu aliloahidi. Kwa mfano: tunajua kam “nafsi inayotenda dhambi itakufa” na vile tunajua kam “nafsi inayokiri na kutubu itaishi”. Hii yayiwezi badilika. Si kila ujumbe ni unabii. Mungu anapotuma ujumbe kuelekea nafsi ilio ktk dhambi, ni ujumbe wa kifo. Walakini kama baadaye ile nafsi inatubu sherti ipone. Sasa hapana kusema Mungu alijichanganya.
  Nabii ana kazi ya aina mbili: “kupeleka ujumbe” na “kutangaza msimamo kamilifu wa Mungu”. Kwa hii ya kwanza result inategemea yule aliepokea ujumbe ameipokeaje. Ya pili inategemea tu mda wa Bwana.

  Tukiongea juu ya mada, Askofu Kakobe hakuleta ujumbe wala kutangaza msimamo wa Mungu. Inaonekana alihubiri tu , akaona aliehubiriwa hakutikisika kwa mda, baadaye akashangaa kusikia au kumuona akiimbisha pambio. Hapa Askofu Kakobe alipungukiwa kwani alidhani atapanda na aoteshe. Hii inaleta shida kwa wainjilisti wamoja, wakati wanapoita hawapati mtu wanawaza hawakutumika. Acheni Mungu aitwe Mungu!!!

  Mambo ya unabii wake ilijitokeza baadaye kulingana na jinsi wandugu manamfahamu. Lakini kwa kweli yeye hakusema ni nabii. Pengine ni mtumishi wa Mungu tu na vile vile anapenda siasa. Kitu anachokipenda atakiongelea tu. Na kam anategemea chama fulani atakitetea. Sasa shida ni kwamba watu wanaposikia Askofu amesema wanawaza alitumwa na Mungu. Mnadhani Askofu hana mafikara yake mwenyewe?

  Nadhani tuenende kwa mtazamo wa mada na sasa tuone kam alifanya vizuri/vibaya kuletea injili wana siasa. Au kam yeye binafsi kuwa mwana siasa haruhusiwe. Au method alioitumia ni je. Mambo ingine ya unabii nafikiri haikuletwa ndani ya mada, na hivi Askofu Kakobe ni mtumishi wa Mungu anewakilisha au kuongoza makanisa makubwa makubwa, lakini si nabii.

  Ahsante na mubarikiwe.

 16. Lwembe,
  Ungenisaidia sana kama ungenipa nukuu ya the so called unabii wa Kakobe.

  Kuhusu mapenzi ya Mungu,kuna lugha nyingi tofauti zimetumika.Wengine wameyaita Decretive/ Sovereign /Hidden will of God & Permissive/ Perfect will of God.
  Aina mbili ulizozisema wewe kimsingi ni aina moja tu ya mapenzi ya Mungu,ambayo kutokea kwake kunaweza kukawa kunahitaji au kusihitaji uhisika wako. Nitafafanua hapo chini.

  Kuna mapenzi ya Mungu yanayoitwa Burumai kwa kiebrania (naweza kuwa nimekosea spelling). Ndiyo hiyo aina ya mapenzi ya Mungu ambayo Mungu huyatimiza,bila kusubiri utashi wa mtu, hata kama Mungu anamtumia huyo mtu. Eg, Musa ilikuwa ni lazima arudi Misri kuwatoa Israel, Yona pia ilikuwa lazima aende ninawi, Yesu ilikuwa ni lazima azaliwe Bethlehem.

  Aina ya pili inaitwa Tharema kwa kiebrania (naweza kuwa nimekosea spelling), ni aina ya mapenzi ya Mungu ambayo hayawezi kutimia kama anayehusika hatashiriki kufanya sehemu yake. E.g, ni mapenzi ya Mungu mimi na wewe kuurithi uzima wa milele, lakini tusipofanya sehemu yetu hatuwezi kuurithi.
  Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu Batimayo kipofu, kuponywa upofu, lakini asingemwita Yesu, au angesema kitu tofauti na kupewa kuona, Yesu alipomuuliza wataka nikufanyie nini, basi asingepona upofu.

  Kwa habari ya unabii kwa Hezekiah, kama yangekuwa mapenzi ya Mungu- Burmai, lazima Hezekiah angekufa, . Lakini kumbe yalikuwa ni mapenzi ya Mungu-Tharema, ambapo kuishi au kufa kwa Hezekiah kulitegemeana na yeye angefanya nini baada ya kupewa unabii wa kwanza. Na tunaona alipofanya kitu ambacho kingemfanya aishi, Mungua alimtuma tena Isaya akamthibitishie kuwa ataishi.

  Hii sentensi “Sijui kama Mungu alijichanganya” siwezi kuwaza kwamba Mungu huwa anajichanganya. Katika hali ya kawaida ya kibinadamu, ili nieleza nilichota kueleza nilitumia hiyo lugha, nikjaribu kuonesha kuwa huu unabii ilikwa ni rahisi kuusema kuwa ulikuwa wa kujichanganya.
  Maana zimekwenda jumbe mbili zinazokinzana (kufa na kuishi), na zimepelekwa na mtu mmoja.
  Ujumbe wa kwanza unasema utakufa wala hutaishi. Na wa pili unasema utaishi miaka 15 zaidi.

  Lwembe, ivi kwa mfano Kakobe baada ya kusema kuwa Mrema atashinda, baadae kidogo siku chache kabisa kabla ya kura kupigwa angesimama tena na kusema ”sasa Mkapa ndiye atakuwa Rais, ungeamini kuwa hizo jumbe mbili zilitoka kwa Mungu?

  Ulisema hivi: ”Je mtu aliyeokoka ni dhambi kuwa mwanasiasa? Jibu langu ni kwamba anaweza kuwa mwanasiasa, tena akiwa ni yule mwenye hofu ya Mungu, ataisaidia sana nchi! Ila nabii au yeyote aliye na special duty ya Mungu huyo akiiacha kazi hiyo na kuikimbilia siasa, ana HASARA kubwa sana!!

  Nahitaji ufafanuzi hapa:

  Je unamaanisha kuwa mchungaji, nabii, mtume, au mwinjilisti hawezi kuwa mwanasiasa huku anaendelea na huduma?

  Au je unamaanisha kuwa mtu mwenye unayoiita ‘special duty’ akitaka kuwa mwanasiasa lazima aiacha hiyo special duty?

  Na je, kwani Kakobe aliacha/ameacha special duty yake na kukimbilia siasa?

  Ni hayo tu!

 17. Sungura,

  Nilichoona kama umechanganya mambo, ni kuhusiana na unabii, uliposema kutimia kwa kwake kunategemea aina mbili za mapenzi ya Mungu

  Ndipo aina hizo mbili za mapenzi ya Mungu ulizozisema, nikaelewa kuwa ziko ktk mifano yako hii miwili:
  1: “Miaka saba ya shibe na miaka saba ya njaa ilikuwa ni lazima itokee Misri ‘no matter what’.”
  2: Lakini mfalme Hezekia haikuwa ni lazima afe, japokuwa nabii Isaya alishatabiri na kuondoka. Sijui kama Mungu alijichanganya mpaka akamtuma Isaya mara mbilimbili kupeleka jumbe mbili zinazokinzana…”

  Unayaona maelezo yako, upande mmoja una acknowledge yaliyotendeka, halafu upande wa pili unajiingiza katika assumptions ambazo hazina msingi, “Sijui kama Mungu alijichanganya …”! Mungu hakujichanganya na HAWEZI KUJICHANGANYA! Wewe ndiye uliyejichanganya, maana umesoma yaliyotokea, umeyaelewa, halafu umetafuta kuya coin ktk fundisho la mapenzi ya Mungu aina hizo mbili ambazo hazipo! Unabii wote 1 na 2 uko sawa kulingana na hali. Na 1 umejitosheleza, balaa na remedy vyote vimekuja katika package moja, na 2 pia only huu ulikuwa na maombi ya kusitishwa na ndipo akapelekewa jibu!

  Mapenzi ya Mungu, ni kweli yako ya aina mbili, lakini si katika kuhusisha ushiriki wa watu kama ulivyosema. Kuna Mapenzi Makamilifu ya Mungu (Perfect Will of God) na Mapenzi ya Mungu yenye Kuruhusu (Permissive Will of God). Tukimtazama Balaamu nabii, tunaweza kuyaona hayo yote katika uhalisi wake.

  Perfect Will of God: (Hes 22)
  Mfalme Balaki alipoyaona makundi ya Israeli aliingiwa na hofu, kwahiyo akatafuta msaada wa kiungu ili awashide, ndipo akamuendea Balaamu nabii kwa jambo hilo:
  Hes 22:6 ““Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.”

  Naye Balaamu akiwa ni nabii, anafahamu ya kwamba ni LAZIMA apewe Neno na Mungu kuhusu hilo, “Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza.”

  Hii hapa ‘Perfect Will of God’. “Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.”
  Naye Balaamu akiisha kulipokea jibu, yale Mapenzi ya Mungu Makamilifu kuhusu jambo hilo, akawapelekea jibu hilo hao waliomfuata: “Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi.”
  Nalo jambo hili lilipaswa liishie hapo, ili liyatimize Mapenzi ya Mungu, hayo Makamilifu!

  Permissive Will of God
  Lakini baada ya Mungu kumpa Balaamu Mapenzi yake Makamilifu kuhusu jambo hilo la kuwalaani Israeli, mwanasiasa Balaki hakulikubali jibu aliloletewa, “15Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza.” Unawaona wanasiasa hao! Ziangalie ahadi zao, “16… wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lo lote lisikuzuie usinijie; maana nitakufanyizia heshima nyingi sana, na neno lo lote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa.”
  Usicheze na wanasiasa, nao wanao upako! Balaamu alifikiri hawezi kuupita mpaka wa Neno la Mungu, “18-Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.”
  Unaona, alikwisha ambiwa USIENDE, lakini kwa ahadi nzuri alizopewa, licha ya kujidai kwake hawezi kulivuka Neno la Bwana, huyu hapa akijitoa akili, “19Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua BWANA atakaloniambia zaidi.” Unamuona nabii mnafiki huyo, jibu la jambo hilo alikwisha kupewa huko nyuma, lakini huyo hapo tena, karudi kwa jambo lile lile!

  Hii hapa Permissive Will ya Mungu: “20-Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao…”
  Unaona, Mungu amemruhusu aende nao, ni baada ya nabii kumjia na “sintofahamu” ya kile alichoambiwa huko nyuma! Mungu huwa hapendezwi na watumishi wasiokaa ndani ya wito wao, mara nyingi Permissive Will yake huwa inaambatana na Hasira juu yao, “22-Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda…” Wanasiasa huivuruga kazi ya Mungu!!!

  Kwahiyo ndg yangu, kutoka maelezo haya kuhusiana na hizo Will za Mungu naweza kusema kwamba ufahamu wangu sasa umebadilika, ni kwamba yawezekana kabisa kuwa alioutoa Kakobe haukuwa unabii kutokana na kwamba yeye si nabii, ila ilikuwa ni jazba au munkari tu wa ule upako wa kichungaji , vinginevyo Mungu angelimkamata kinywa na angeishia kusema “BWANA ASEMA, Wapinzani mmeshindwa uchaguzi!!!” Pia sijawahi kumsikia akijitangaza kama nabii, ingekuwa ni hivyo, ndipo tungemjua kuwa ni Nabii wa Uongo, nadhani its more fair so!

  Kuhusu, “Je mtu aliyeokoka ni dhambi kuwa mwanasiasa? Jibu langu ni kwamba anaweza kuwa mwanasiasa, tena akiwa ni yule mwenye hofu ya Mungu, ataisaidia sana nchi! Ila nabii au yeyote aliye na special duty ya Mungu huyo akiiacha kazi hiyo na kuikimbilia siasa, ana HASARA kubwa sana!!

  Na kuhusu “Unabii wa Kakobe” jibu ndilo hilo kwamba haukuwa Unabii bali “Danganya Bwege” maana ingekuwa ni unabii angepindishwa mdomo!!

  Hata hivyo ninakushukuru Sungura kwa tafakari, imenisaidia sana kunisogeza mbele ktk ufahamu,

  May The Lord bless you!

 18. Lwembe ni wapi sasa nilipochanganya mambo, unaweza kunionesha?

  Hebu kuwa wazi zaidi hapa: Je mtu aliyeokoka ni dhambi kuwa mwanasiasa?

  Na ni wapi ambapo mimi nimesema habari za kukwezwa kwa Yusuf?

  Mimi nimesema Yusufu hakukomea kuambatana na wanasiasa tu, bali alifanyika kuwa mwanasiasa kabisa.

  Suala la alifika ikulu kwa kufanya kampeni au la, liko ndani ya mfumo uliokuwepo. Ule ulikuwa mfumo wa kifalme, tofauti na mifumo ya sasa ya demokrasia.

  Au unataka kusemaje,kwamba sasa hivi katika nchi kama Tanzania Mungu akimpa favour mtu fulani kuwa Raisi wa nchi,ili tujue kuwa ni Mungu inambidi huyo mtu asifanye kampeni au?

  Kumbuka pia kuna mifano nimeitumia nikiwa naelezea aina za mapenzi ya Mungu.

  Na mwisho, ni nini hasa huo unabii wa Kakobe ulisema? Naomba nukuu yake ili tujadili vema. Tujue kama ulikuwa ni unabii au ilikuwa kauli tu.

  Maana kama mtu akisema tu kesho itakuwa hivi au vile huo ni unabii, basi Nyerere naye alikuwa nabii mkubwa. Maana pale Mwanza mwaka walipomzomea alishuka jukwaani akawaambia ”mtake msitake mkapa ni raisi”.

 19. Vai 28/09/2013 at 11:20 AM
  Kwa ufahamu wa NENO lililofunuliwa tumefahamu kwamba peponi ni kwenye mbingu ya tatu au mahali yanapokaa maroho ya giza yote( Efeso 6:1-18).

  2 Wakorintho 12:2-4
  Namjua mtu mmoja katika Kristu, yapata sasa miaka kumi na nne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui, kwamba alikuwa ndani ya mwili sijui, Mungu ajua) MTU HUYO ALINYAKULIWA JUUUUU MPAKA MBINGU YA TATU! 4, YA KUWA ALINYAKULIWA MPAKA PEPONI (Huko katika mbingu ya tatu) aksikia maneno yasiyotamkika ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.
  Dada Vai siyo kila theolojia ni chakula kwa mkristu nyingine ni sumu, mtu anayesema kuwa hakuna peponi anaikataa hata hiyo kazi ya Bwana, kwa maana alitangaza Ufalme sio wa kidunia bali ni peponi aliposema Ufalme wa Mungu umetimia ndani yetu alimaanisha roho mt. ambaye ni kama upepo yaani humuoni kwa macho ya nyama bali hudhihirika kwa ishara kama hizo za Kakobe na walokole wengine (Marko 16:17) Huyo Mungu-Roho akiwa ndani yako hukupa wewe uliye nae neema ya kwenda peponi huko alikoenda Paulo saa yoyote ile mwili wa duniani unapofikia tamati yaani mpaka sasa kama kweli haumjapokea huyo Roho ufanye hima kubatizwa kwa maji na kwa roho (Yoh mt 3:5) wokovu hauuzwi,
  YESU anakuita NJOO! (Ufunuo 22:17)

 20. Being to much pessimistic doesnt mean that you know much, nawashangaa sana wakristu wenye negative attiude juu ya kila kazi ya Mungu halafu haohao baadae hukaa na kuanza kuwalaumu mafarisayo baada ya kuangalia filamu ya Yesu (kwa maana sidhani hata kama biblia huwa wanasoma) pasipo kujua kuwa wao ndio mafarisayo wa zama hizi,(math:23:29-34) eti mtu anamlaumu Kakobe kwamba hana matunda! binafsi nimeenda lindi na mtwara vijijini huko kusiko na makanisa bali machache tena ni waroma lakini cha kushangaza nimeyakuta matawi ya kanisa lake! kama yeye ni mchawi mwacheni aendelee nao ni vema, kwa sababu anawahubiri watu waje kwa Yesu. Mwacheni aendelee na hilo shetani linalomwambia awahubirie watu sheria za Yesu na kumkubali Yesu bila uoga. Naona shetani siku hizi anatumia mbinu ya kueneza injili ya Yesu ili kuwapeleka watu Jehanam! mh, hapo hata shetani atakukataa,(math12:24-25)
  Si ajab mtu anaweza kumshutumu mtu aliyeeneza makanisa ya wokovu nchi nzima huku yeye hajawahi kuhubiri hata uinjilisti! jamani tujihadhari na midomo yetu mnaweza mkajikuta mnaloga wakati hata uchawi hamuujui. Kuna mama mmoja alimsema nabii wa Mungu aliyekuwa akihubiri kupitia TV (mara nyingi watu wa Mungu hujaribiwa na shetani kupitia watu wasio na imani hasa katika mambo ya pesa(kwa sababu ni wabahili na wabinafsi) na ushirikina(kwa sababu hawaujui).) kwa ufupi huyo mama alipigwa utasa na Yahwe na alikuja kupona baada ya miaka kumi kwenye huduma ya nabii mwingine baada ya kuambiwa kuwa alimtukana nabiii wa Mungu kwa hivyo akamuombe msamaha Mungu na huyo nabii ili apone baada ya hayo akapata mtoto.
  Wateule tuwe macho
  (Marko 9:38-40)

 21. Sungura,

  Usichanganye mambo!
  Nakuona unavyoutafutia jinsi ya kuupendezesha machoni pa watu kwa kuupamba Unabii ulioshindwa!!

  Hakuna mambo ya unabii wa aina mbili, unabii uko wa aina moja tu, Mungu anakupa Neno lake unalisema kama alivyokupa, maana Roho wa unabii ni mmoja tu, Yesu Kristo! Balaamu alijaribu namna zako mbili hizo akashindwa, na mwisho akatumia maarifa, ambayo nanyi nawaona ndiyo mnayojaribu kuyatumia!

  CCM hawawezi kuwa na jibu la unabii ulioshindwa, unless unataka kutuambia kuwa wao wako more spiritual kuliko Askofu Kakobe, kwamba askofu alitoka bila kucheki Mafuta kama yamo!! Usijichanganye kaka!

  Mfano wa Yusufu uliouleta sioni unauoanisha vipi na unabii ulioshindwa, they just meet!

  Hata mfano wa Hezekia, labda utuambie kwamba askofu aliwatangazia mapema kuwa Mungu ameghairi kuwapa ushindi akina Mrema na amewapa tena ccm, au basi iwe kwamba aliwatangazia kuwa Mrema atashinda lakini ccm wataiba kura na kujitangaza washindi, ambavyo yote haya ni wishful thinking!

  Kukwezwa kwa Yusufu kutoka jela mpaka Ikulu, unakuona kama alikuwa na kampeni ya kisiasa? Why don’t you simply follow the story and get to understand the Mystery of God as It works Itself UP into Dominion? Yusufu mwenyewe amekuambia kuwa Mungu ilimbidi amtangulize Misri ili kui preserve familia yao, iliyo katika URITHI wake! Kwamba ndio unamfananisha na askofu? Mrema ndio Farao? Nayo miaka saba ya njaa ndio huko kuukosa ufalme? Na miaka saba ya neema ndio hii wanaitayarisha kwa katiba?

  Acheni kujichanganya, ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu!!

  Sungura, don’t only think wider, you could be running wild with your ideas, that prophecy didn’t materialize!

  Think harder now, and be sure you are anchored in Christ, for religious spirits are on the rampage!!

 22. Mpendwa Vai kwakeli unahitaji msaada wa haraka sana kwa wapendwa tena wapendwa kwa hili tulibebe kikamilifu!inaonekana ni jinc gani Vai alivyonyweshwa sumu nyingi ambazo zitampoteza,so kunahaja ya kumuombe mpendwa mwenzetu ili aingie kwenye the right truck!naamini tutamrejesha mwenzetu kwa upendo na upole zaidi.

 23. Bwana Yesu asifiwe,

  Shalom wana wa Mungu!

  Mimi sidhani Vai ni mukristo kwani ni vigumu kuelewa kama ni mchanga, amejidanganya, amechanganyikiwa, wala amefunzwa vibaya. Unapoona anayoandika ni rahisi kumtia kwenye list ya wa akina freemasons. Huyu akitaka inaomba afanyiwe delivrance.

  Asante.

 24. Kwa habari ya ukweli au uongo wa unabii wa Kakobe mwaka 1995 kuhusu Mrema kushinda uraisi, ninawashuri kwa faragha muende mkawaulize viongozi wa CCM swali hili ”je mwaka 1995 Mrema alishinda uraisi au hakushinda”?

  Hao ndio watawaambieni ukweli wa unabii wa Kakobe, maana wanaujua.

  Kutimia kwa unabii kunategemea aina ya mapenzi ya Mungu ambayo huo unabii umo. Kuna aina mbili za mapenzi ya Mungu.
  Ambazo ni mapenzi ya Mungu yanayohitaji ushiriki wa mtu, na mapenzi ya Mungu yasiyohitaji ushiriki wa mtu (kwamba haihitaji mtu afanye kitu fulani ndipo itokee).

  Miaka saba ya shibe na miaka saba ya njaa ilikuwa ni lazima itokee Misri ‘no matter what’.

  Lakini mfalme Hezekia haikuwa ni lazima afe, japokuwa nabii Isaya alishatabiri na kuondoka. Sijui kama Mungu alijichanganya mpaka akamtuma Isaya mara mbilimbili kupeleka jumbe mbili zinazokinzana. Ingetokea biblia haijasema alichofanya Hezekia baada ya kuambiwa atakufa, kuna wengine leo wangesema Isaya hapo hakutumwa na Mungu.

  Kama wachungaji wetu watakuwa watu wa kwenda tu ikulu kunywa chai na kupewa bahasha, na kuhubiri tu kwenye mimbari kuwa viongozi wa siasa wanatakiwa kutenda haki, tusahau ufisadi kuisha ktk taifa.

  Tunataka watu wengi wenye mfano wa Kakobe katika hii nchi.

  Hapa tunaongelea suala la kuambatana na wana siasa, Yusufu mtumishi wa Mungu yeye hakukomea kuambatana tu, bali alifanyika kuwa mwanasiasa kabisa, na wala hakuacha kumtumika Mungu.

  Let’s think more wider!

 25. Akina Vai wanatakiwa kuombewa,
  Hicho wanachokitumikia n kitu kingine. Nilipoona tu jinsi alivyojibu swali la Siyi la peponi ni wapi, nilipigwa na butwaa.

  Jamani mtu aidanganyika kumrejesha ni kazi ngumu kweli.
  Hebu tukumbuka habari za Kibwetele wa Uganda alichowafanyia watu waliomfuata!

  Nina wasiwasi sana na hawa akina Vai, dalili hizi siyo nzuri hata kidogo. Maana hata vitu ambavyo viko wazi wao wanavipindisha mpaka unashindwa kuelewa kama ni ujinga tu wa kawaida au ni giza la mkuu wa giza mwenyewe.

 26. Ndg Vai,

  Kweli mko salama huko? Sidhani kama mko salama, dalili zinaonesha kuwa mnatumikishwa nje ya utu wenu! Hebu yasome haya uliyoyaandika ujionee mwenyewe kuhusu “PEPONI”:

  “”Kiukweli dini zote walikuwa wakitufundisha kuwa peponi ni mahali pa Mungu wa kweli au Mbinguni. Lakini huo ni uongo! Peponi ni mahali pa mapepo na maroho yote machafu kwa jina lingine panaitwa toharani, hapa ndipo mahali panapoitwa ulimwengu wa roho. Japo walokole huwa wanajua kuwa kwenye ulimwengu wa roho ndipo mahali Mungu anakaa. Kwakweli wamedanganyika na wamewadanganya wengi.
  Kwa ufahamu wa NENO lililofunuliwa tumefahamu kwamba peponi ni kwenye mbingu ya tatu au mahali yanapokaa maroho ya giza yote (Efeso 6:1-18). Mungu wa kweli ameliweka kanisa/watakatifu katika UUMBAJI WA WATAKATIFU ULIOFUNULIWA ROHONI. Hapa ni mahali ambapo maroho yoyote ya giza yanayokaa ktk ulimwengu wa roho hayawezi kupafikia.
SHIKA NENO MLIOPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA NDANI YA TAIFA TAKATIFU LA MUNGU GOSHENI KIZAZI CHA NNE!””

  Hiyo Efeso 6:1-18 haina uhusiano wowote na hayo uliyoyaandika, na wala hayo yote uliyoyaandika hayana uhusiano wowote ule na Neno la Mungu, ndio maana yawezekana umeshindwa kumjibu ndg Ziragora alipokuuliza:
  “”Unaweza tuambia tofauti ilipo kati ya “peponi” unoyosema na peponi inayotajwa na Yesu hapa”Luka 23:43. Yesu akamwambia, Amini, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami PEPONI.”? Hivi Yesu alimualika huyu mutu amkute mahali pa mapepo?!!””

  Hii ni dalili tosha kuwa Shetani amekwisha zitwaa nafsi zenu na kuzifungia huko Gizani!

  Hata pole haitawafaa kitu!!

 27. Joe,
  Kuhusu Yona, kumuomba Mungu afe, nimekujibu labda utakuwa hujayatafakari tu niliyoyaandika.

  Mtumishi wa Mungu anapopewa Ujumbe kwa kanisa, yeye huwa sehemu ya Ujmbe huo, na huuamini kikamilifu na kuyategemea yote yalimo katika Ujumbe huo, akiwa katika Upako wa kuuhubiri Ujumbe huo! Kwahiyo yeye Yona aliyategemea yatokee hayo aliyoyahubiri, pia unapaswa uelewe kwanini Yona alikacha kwenda huko, basi alipolazimika na alipouuhubiri Ujumbe wa Ninawi asingalitegemea jambo tofauti! Halafu nikakuambia kuwa kupewa Ujumbe si lazima uwe ndio Nia ya Mungu, wakati mwingine Unabii huletwa kuwa Onyo!

  Kwahiyo mtu anapolalamikiana na Baba yake haiwi issue kubwa, ndio maana unamuona Mungu akimpoza mwanawe, yeye mwenyewe Yona anaijua Neema iliyomponya huko chini ya bahari!

  Upako wa kazi maalumu unapoondoka, watumishi huhangaika kidogo mpaka Mungu mwenyewe aingilie kati. Mtazame Eliya, ujasiri aliokuwa nao wa kuwaua manabii 850 wa Yezebeli, halafu Upako ulimuondoka akaanza kumkimbia Yezebeli.; au Yohana Mbatizaji, akiwa jela, ghafla tena anawatuma wanafunzi wake wakamuulize Kristo kama “Ndiye” wakati yeye ndiye aliyemtambulisha kwa watu! Kwahiyo usimshangae sana Yona!!

  Kuhusu njia ya kupeleka Ujumbe, kama madhabahu uliyopewa haitoshi, bado nadhani ni vema kumsubiri mwenye kazi yake kuliko kuandamana na makundi hayo ambayo in principal yanakutumia wewe bila kujua, haushangai kwanini wanasiasa wanasaidia sana makanisa siku hizi? Hiyo ni “LONG SHOT” ndg yangu!

  Mwisho niseme hivi, kuhusu kuandika “mingi”, inatokana na kujibu maswali, jaribu nawe kulitazama swali hili, “Mungu ni nani?” Jibu lake unaweza kuchukua zaidi ya mwaka ukiandika kila siku na usifikie kulijibu!!

  Asante, Gbu!

 28. Joe,
  Kuhusu unabii kuchakachuliwa, unapotaka kulilinganisha jambo hilo na kutumwa kwa Musa, bado naona utakuwa unalazimisha mambo tu. Musa alipotumwa kwenda kuwatoa Israeli, hakukurupuka tu kwenda, kwanza alijiridhisha kwamba Mungu ndiye anayemtuma, akiisha kujiridhisha hivyo aliondoka katika imani thabiti na kuyaendea hayo aliyotumwa kuyatimiza, tena alitumwa mara moja tu na si mara sita, bali alirejea mara sita kwa Farao in the course of duty!

  Kwani Musa alipoitupa ile fimbo yake chini ikageuka nyoka, wale wachawi walipozitupa fimbo zao pia na zikawa nyoka, kuna mahali ambapo umesoma Mungu kumwambia Neno lolote Musa kuhusu hao nyoka wa wachawi? Au wale wachawi walipozitupa chini fimbo zao, walitegemea kuwe na mpambano wa nyoka?

  Mungu akiwako uwanjani mambo huwa tofauti, na kwa wanao mtegemea Mungu huwa hawafadhaiki, wao hukingojea kiwango kitakachoinuliwa kuyakabili hayo yaliyozuka, ndio maana Musa alitulia tuli; hakuanza kutoa visingizio, akiwategemeza watu katika saikologia za siasa, ili mwaka watakao anguka CCM ajiinue na kudai kutimia kwa unabii alioutoa miaka hiyoooo! Ndio maana tunaandika haya ili kuiondoa aibu katika kambi, kubahatisha bahatisha si jambo zuri kwa mtumishi wa Mungu! Angalia unabii unasemaje kuhusu siku za mwisho, itabidi zikatishwe vinginevyo hakuna kitakacho okolewa! Mapepo yanateka kila kitu, kuanzia siasa, makanisa na kila kitu! Wauza unga wataanzisha makanisa au kuyateka kwa tamaa za umashughuri za viongozi, kama unavyowaona mashoga wanavyoyakamata makanisa, kupitia siasa; kaeni ktk sehemu zenu jamani, kuna wenzenu waliziacha sehemu zao za kazi wamefungiwa huko gizani mpaka leo!!!

  HAKUNA anayeweza kuupindisha unabii usitimie, Joe, soma Biblia yako vizuri, kufanywa moyo mgumu si kuupindisha unabii! Soma pole pole ukielewe Mungu alichokifanya. Lengo halikuwa Farao bali wana wa Israeli ambao Mungu wao, huyo Mungu wa baba zao, wamemsikia tu kwa kuhadithiwa. Wao wanaijua vizuri miungu ya Farao, hata Musa anaijua hiyo! Si unaona mapigo ya mwanzo yaliwakumba woote, nchi nzima, lakini baadae wakatengwa katika mapigo hayakuwafika; walikuwa ktk “TUITION” ya kumjua Mungu wao kabla ya climax ya kuondoka! Farao wakati wake wa kulipwa ulifika, ndio huo moyo mgumu na mapigo yooote!!

  Basi Joe, usijidanganye katika yaliyo peupe, utasubiri saana usafiri uliokwisha kukupita wakati umefumba macho!

  Asante & Gbu!

 29. Joe,

  Hivi uliisoma hiyo chapter ya 15 yote mpaka ukakifikia hicho kifungu cha 31 au ulilitafuta kwenye itifaki neno “kuandamana” ndipo ukalibandika? Maana nina uhakika kama ungeusoma mlango huo ungeona jinsi Sauli alivyofanana na Kakobe ktk jinsi tunayoizungumzia kimaudhui!

  Huko kuandamana na Sauli unakokusema, ni nje ya maudhui tunayoyazungumzia. Sauli alipewa Maagizo na Mungu ambayo alipofika katika utendaji aliyakiuka, Mungu hakupendezewa naye. Ndipo kwa Neno la Mungu, Samweli aliinuka kwenda kumfuata Sauli na kumpasha hasira ya Mungu juu yake. Lakini kama kawaida yetu, alianza kujitetea na kuwasukumia watu mizigo, na visingizio vya kila aina; sijui wameiba kura, mara Mungu ameghairi, mara unabii unaendelea, mpaka alipobanwa, 1 Sam 15:22-23
  “Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
  Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,
  Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.”
  Hii ndio Hukumu iliyopitishwa juu yake, sasa tukisoma zaidi hapa tutakuona huko “kuandamana” ulikokunukuu, 24-31
  “Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA. Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute. Akasema, Nimekosa; LAKINI UNIHESHIMU SASA, NAKUOMBA, MBELE YA WAZEE WA WATU WANGU, NA MBELE YA ISRAELI, RUDI PAMOJA NAMI, nimwabudu BWANA, Mungu wako. 31Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.” Umekuona “kuandamana” huko, unaweza ukakufananisha na huko kwa Kakobe na wanasiasa? Ni TOFAUTI kabisa, Roho wa Mungu hawezi kuruhusu wala kushiriki!!

  Unaniuliza kinachonitatiza ni nini? Ni ile stubbornness ya kuutafutia visingizio unabii ulioshindwa, na matokeo yake ni huku kuendelea katika njia hiyo, ukijaribisha hili na lile kama kwenye bahati nasibu ya kutimia, huku nyuma yako ukiwa na kusanyiko kubwa linaloongozana nawe katika safari hiyo, wakiamini kuwa Mungu amewatangulia, kwamba ni mapenzi ya Mungu kuwakemea wanasiasa walio madarakani kwa kuungana na wanasiasa wanaowania madaraka, kwa visingizio vya Yohana na Herode!!! Kwani Shetani alimuonesha nini Kristo alipotaka amsujudie? Si alimuonesha “milki yake” na akamuahidi kumpa akimsujudia! Ni viongozi wangapi leo wanaogombea kwenda kuwasujudia wanasiasa? Joe usijichanganye ndg yangu, hivi kwa mawazo yako, Mungu kajiunga vyama vya upinzani? Mnarudi kule kule, ili mradi mlijidanganya kuwa “Mungu ameghairi”, HAMUWEZI KUEPUKA kuendelea katika uongo huo, yaani you willfully blinded yourselves after you rejected plain Bible truth, what can God do abt it!?

  Mnaziri wa Bwana ni yule aliye wekwa wakfu kumtumikia Mungu, mitume, wachungaji, manabii, wainjilisti na walimu; hawa wanahudumu ktk makusanyiko ya Bwana, wametengwa kwa ajili hiyo, they don’t flirt with the world! Ukiwaona wanavizia mikutano ya siasa, basi jua kuwa wameshindwa, upako wa Mungu umewaondoka, maana Yona hakwenda kwa mfalme ili amkusanyie watu wa kuwahubiri!

  Pia usijichanganye sana ndg yangu na maombi, kuna saa ya maombi na kuna saa ya kuyadhihirisha kwamba umeyapokea uliyoyaomba! Nao watumishi wa Mungu, kwa hayo unayosema ni maombi, wao huwasiliana na aliyewatuma kazi, huyo Mwenye kazi yake, kisha hupewa maelekezo ya nini wafanye, sio kujikoki tu na kumsingizia Mungu kama Sauli! SUBIRI MAELEKEZO, kama kweli Mungu alikuita!!!

  Gbu!

 30. CK lwembe naona unazungukazunguka na kutaka ku-politicize main issue ya hii topic.

  Mbona hujajibu kuhusu nabii Yona kumuomba Mungu afe kuliko kuishi baada ya unabii aliotoa kutotimia??..unasema “Ninawi kupewa nafasi ya kuzitubia dhambi zao na neema waliyokuwa nayo”..ni sahihi kabisa….Je umeweza kuchunguza na kujua hakika kuwa ccm (wanachama) haikupewa neema hii na Mungu hata kumfanya aghairi yamkini maneno aliyomtuma mtumishi wake Kakobe juu yao?

  vp kuhusu kujibu hoja ya njia sahihi unayoiona wewe kwa watumishi wa Mungu kupeleka sauti ya Mungu kwa viongozi na wa-tz?maana njia ya kuambatana nao uliikataa hapo awali..!

  CK lwembe ni vizuri zaidi kujibu hoja direct na si kuandka maneno mengi yaliyo nje ya hoja.

 31. Mimi si muumini wa dhehebu la Kakobe( notice: sijasema ‘Kanisa’ la Kakobe!!!!!-maana hakuna mwanadamu mwenye kanisa bali Yesu), lakini mambo mengine ni mepesi tu kuelewa na kila kitu kinakua cha baraka. Ni kweli ukimfuatilia Mtumishi Kakobe kama ilivyokwa Watumishi wengine wakubwa wa zamani TZ( hence Kakobe should not be the big issue) na wa kileo wale wa kweli tu acha wale walio out kabisa kwa vigezo vingi tu, toka alipooanza, kumekua na mambo mengi ya ukweli na ulongo na ni ukweli pia kwa hakika amerekebisha mengi. Ni vema nikaweka msingi kua hata ktk huduma/utumishi, Wanadamu hukua! Kama vile tunavyoukulia wokovu vivyo ivyo ktk huduma au majukumu ya Bwana TULIYOPEWA AU KUJIPA kwa utukufu wake. Hence, si ajabu kumuona Mtumishi leo ana mapungufu haya, kashindwa yale, kafanya vibaya kwa hili lakini kesho akawa chombo madhubuti kabisa ktk mambo ya ufalme, ni uelewa tu ktk kweli za Mungu, utaweza ng’amua na kujawa na hekima na maarifa ya Ki- Mungu/KiNeno kabla ya kuhukumu BILA HAKI-maana tunaambiwa tusihukumu….ili pia tunaruhusiwa kutoa hukumu ya haki.

  Mdo.18:23-27= Mstari wa 25= Appolo ana hubiri motomoto lakini hajui baadhi ya vitu, wapendwa wakampa shule nyingine ili kumuweka sawa.

  1Nyakati.22: 5-18 : Mstari wa 5, Daudi anakiri wazi kua mwanae bado mchanga/Kijana mno, hana uzoefu bado kwa jukumu la kiMungu kubwa analopewa na Mungu la kujenga Nyumba ya Bwana lakini mstari wa 17 wanaamuriwa Wakuu=Watu wazima, Wenye uzoefu kumsaidia ktk jukumu ilo. Kwa maneno mengine, asiposaidiwa hataweza au atakosea kazi ingawa ni kweli kabisaa, ni Mungu alimpa ilo jukumu huku akijua bado jamaa yu mchanga na hana uzoefu.

  Gal.2:10-13 Paul anamkemea Petro hadharani kwa kukosea ktk mwenendo unaopaswa

  Mathayo.17:14-21…Wanafunzi wa Yesu wanashindwa kutoa pepo, kisha wakiwa faragha wanauliza kwa nini hawakuweza, Yesu anatoa shule-ndio kukua uko, later waangalie baada ya kukua ktk imani na utumishi ktk kitabu cha Matendo.

  Kwakua ktk kuukulia Wokovu, Imani, Utumishi,Wapendwa hao juu wapo waliokosea, wengine walikua na madhaifu au kutokua na sifa, SI AJABU KWA Bishop Kakobe kufanya makosa ktk kuendeleea kwake na nia yake njema ya kumtumikia Mungu na kujitoa wazi wazi bila woga kukemea mambo, Kuwa-challenge Watu wenye mamlaka ktk Nchi hii.

  Kuna Watumishi ktk Nchi hii, ukiwaangalia kwa vigezo kadhaa mfano ukawasikiliza wanavyo gawa mkate, ukiwafutilia misimamo yao imani, Utakatifu, kuhubiri Injili, wametoka wapi, walikuaje na sasa wakoje, ukiwa hakimu muungwana, utakubali Bishop Kakobe kwa miaka mingi sasa ya karibuni, is far better and SAFE to hear than many famous church and TV preachers.

  By the way, I would like us to think this way, ktk ibada zetu makanisani, wahubiri wetu kanisani, je si ni kwei hua wanakosea baadhi ya vitu kutamka/kuhubiri? au wapendwa ktk kujazwa Roho na labda ni wachanga na karama hua hazingonjagi ati Mtu akomae sana ndio zije, je huyu anaponena na kutoa unabii, si waga wanakosea pia sometimes au kusema mambo ndivyo sivyo? DOES THAT SHARPLY group them kua ni wapendwa fake, satanic agents, manabii wa uwongo? If that is the case and fact to be held, then si tu Kakobe bali hata baadhi yenu ninyi humu, Wachungaji wenu, Manabii wenu, Wahubiri wenu, Wapendwa ktk ibada, wote ninyi ni manabii wa uwongo na devilish workers!-Something which is not only un healthy manner to hang on when analysing things but also it is an extreme comprehension of simple things sending them unnecessarily into profitless complexities for the body of Christ.

  Press on.

 32. Ndg Joe,

  Kuhusu Biblia ninayoitumia, nami kama wewe, natumia KJV.

  Kwamba Yona alitoa unabii wa kuangamizwa kwa Ninawi, hilo halina shaka kabisa, tena haukuwa unabii wa ki cosmetic, bali ulikuwa ni wa kishindo cha kuitikisa mioyo, Maandiko yanalishuhudia jambo hilo, Yon 3:5 “Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.” Huu ukiwa ni udhihirisho wa Nguvu iliyokuwamo katika mahubiri hayo, Yona alipewa Ujumbe wa kuwapelekea Ninawi lakini hakuijua Nia ya Mungu!

  Kuhusu Ninawi kupewa nafasi ya kuzitubia dhambi zao, naona hujaliona hili, lakini lipo hapo hapo katika Maandiko, iwapo utakisoma kisa hicho si kwa kutafuta vifungu vya kunikabili, bali kujaribu kuona Mungu alikuwa akifanya nini huko? Yon 3:4 “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, BAADA YA SIKU AROBAINI NINAWI UTAANGAMIZWA.”

  Kwamba Ninawi walipewa siku arobaini, basi hilo lingekuonesha Neema waliyokuwa nayo katika jambo hilo, kama nasi tuliyopewa, hapo tunapohubiriwa Injili, “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”; Au tu kwamba watu wa Ninawi waliupokea Ujumbe huo na kuufanyia kazi katika jinsi wanayoijua, hilo lingekuthibitishia kuwa hao walikuwa wanawe Mungu! Au hebu utazame unabii alioletewa mfalme Hezekia ktk 2 Fal 20:1-6 “…Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA akasema, Nakusihi, BWANA, … Hezekia akalia sana sana. Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la BWANA likamjia, kusema, Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA. Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano…” Mimi naona unabii wa Ninawi na huu wa Hezekia vina shabihiana, naona katika package hiyo, Neema imeambatanishwa, ambayo ndilo kusudi la Mungu kwa hao!

  Kinyume na huo hebu utazame unabii huu halafu ulinganishe:
  Kuuhusu mji wa Capernaum: Lk 10:15 “And thou, Capernaum, which art exalted to heaven, shalt be thrust down to hell.”
  Au kumhusu Yezebeli: 2Fal 9:10 “10-Na mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli, wala hapatakuwa na mtu wa kumzika. Akaufungua mlango, akakimbia”
  Au kumhusu mfalme Ahazia: 2Fal 1:4 “Basi sasa, BWANA asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.”
  Unabii huu mimi ninauona ni Hukumu iliyopitishwa na si itakayopitishwa; na hayo yote yaliwatimilia!

  Ingawa inapendeza na kutia moyo hapo Unabii usiotimia unaposogezwa na kufungwa katika fungu la Unabii alio ughairi Mungu, lakini sote twafahamu kwamba jambo hilo ni kujilisha upepo, maana hakuna aliyejitokeza na kututangazia “kughairi” kwa Mungu kuhusu unabii huo. Hata haya unayoyaongea Joe, wewe mwenyewe unajua kuwa ni speculations!!

  Gbu!

 33. Ndugu Vai, Joe

  Ndg Vai,
  Unaweza tuambia tofauti ilipo kati ya “peponi” unoyosema na peponi inayotajwa na Yesu hapa”Luka 23:43. Yesu akamwambia, Amini, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami PEPONI.”? Hivi Yesu alimualika huyu mutu amkute mahali pa mapepo?

  Ndg Joe,
  Tusipotazama utimilifu wa unabii, tutambuaje manabii wa wongo?

  Asante.

 34. ndugu CK lwembe katika hoja ya unabii wa Mungu kuchakachuliwa na wanadamu waovu nadhani usome tena na kwa taratibu jibu langu la kuchakachuliwa ndio utaweza elewa vizuri…hoja unayosema ” Mungu alipokuwa anatoa tamko hilo hakujua kuwa wataiba kura? Kama hakujua basi hata sifa ya Uungu ameipoteza!!!”..naomba nikuulize Je Mungu alipomtuma Musa kwenda kwa Farao kwa mara zote zile sita hakujua kuwa Farao atagoma kuwaachia waisraeli?jibu ni kuwa ALIJUA lakini BADO ALIMTUMA Musa kwenda mara hizo zote!

  nadhani CK lwembe ungekuwa kipindi cha Musa ungesema Mungu wa Musa amepoteza sifa ya uungu maana kwann amtume Musa na yasitimie kwa mara ya kwanza. Nataka uelewe ya kuwa yule Mungu aliyemtuma Musa mara zote zile kwa farao akijua kuwa farao hatakubali ndie Mungu huyo huyo awezaye kumtuma mtumishi yoyote wa sasa huku akijua wanadamu watakavyofanya. Na ndio maana nilikwambia kama vile farao alivyopindisha unabii usitimie mara ya kwanza na mapigo yakaja kuwa mazito huko mbeleni ni vivyo hivyo itakuwa kama kuna waliopindisha na unabii wa ccm kutotimia!

  Lakini yote kama ulikuwa unabii wa kweli ama la Bwana atayaweka peupe tusubiri.

  Joe

 35. CK lwembe ulisema “Sijaona mahali popote pale ambapo Kuhani au Mtume aliyekuwa akiongozana na wanasiasa, maana hata majuzi tu alikuwa na kundi la wanasiasa viwanja vya jangwani “wakihubiri” katiba mpya!”…vipi kuhusu 1Samweli 15:31 “Basi samweli akarudi na kuandamana na Sauli”…

  Je kinachokutatiza ni mtumishi Kakobe kuandamana na wanasiasa viwanja vya jangwani au kufanya siasa za kichama??kwa tafsiri yako ya kuongozana/kuandamana basi mtumishi kakobe yupo sahihi..maana yeye pia alikwenda kuhubiri hiyo katiba mpya kama mwakilishi wa Mungu na kukemea kama Yohana mbatizaji alivyokemea wakati wa Herode.

  sijui hiyo separation unayoisema inalenga nini hasa..maana mtumishi Kakobe sijui kama ni kiongozi wa chama cha siasa chochote kwa mantiki ya kuchanganya wito wake na siasa. Au unataka watumishi wa Mungu watumie njia gani kupeleka sauti ya Mungu kwa viongozi na wananchi wa tz?kwa kujifungia makanisani na kuomba tu?kwa kutoka na kusema kweupe kama kina yohana mbatizaji,samweli,etc, au njia gani hasa unayoiona ni sahihi???

  Joe

 36. ndugu Vai umesema “habari ya unabii aliopewa Yona kuhusu Ninawi ni kwamba nia ya Mungu ilikuwa wale watu wa Ninawi wasikie na watubu wamgeukie Mungu”..vyema kwa mtazamo wako….BUT je haikuwa nia ya Mungu kumtumia mtumishi wake Kakobe kutoa huo unabii na usitimie kwa sababu kama uliyoitoa ya NIA ya Mungu ilikuwa kuwabadilisha viongozi wa CCM kwa faida ya wa-tz???kama uliweza kuiona NIA ya Mungu kipindi cha Yona je huwezi kuiona NIA ya Mungu kipindi cha Kakobe??

  Vai ni muhimu kusoma biblia taratibu sana&kuielewa na si vinginevyo!

  Joe

 37. ndugu ck lwembe sina uhakika unasoma biblia ipi…ila biblia ya king james version ipo clear kuwa Yona alikwenda kutoa unabii wa kuangamizwa kwa ninawi na si kuwapa option ya kuchagua kuangamizwa au la (Yona 3:4; Yona 4:10)..na ndio maana Mungu alipoamua kama Mungu kutokuuangamiza Ninawi hali hiyo ilimtia hasira sana (na pengine aibu kubwa)nabii Yona akamuomba Mungu afe kuliko kuendelea kuishi “Ee Bwana nakuomba uniondolee uhai wangu maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi (Yona 4: 3). Na ndio maana Mungu anabaki kuwa Mungu mwenye rehema tele awezaye kughairi hata katika unabii.

  CK lwembe soma biblia taratibu ili kuilewa vizuri.

 38. Ndugu yangu Joe, naomba usome kitabu cha Neno ( Bibilia) Kumb kumbu la torati 18: 21-22, Mungu amesema mwenyewe kuwa nabii yeyote atakayetabili jambo lisipotokea huyo hajatumwa na Mungu. Hapa Neno limeweka wazi kabisa. kwahiyo kakobe hapo alijituma mwenyewe na wala sio Mungu. Pia umesema unabii unaweza kuchakachuliwa. Neno la Mungu alilolinena mwenyewe hata watu na wanadamu wakijifanya kulichakachua Mungu atalitimiza tu na kwa habari ya unabii aliopewa Yona kuhusu Ninawi ni kwamba nia ya Mungu ilikuwa wale watu wa Ninawi wasikie na watubu wamgeukie Mungu.
  tunaona wale watu baada ya kusika ule unabii walichomwa mioyo yao wakatubu wakamgeukia Bwana na Bwana akawasamehe akaghairi kuwaangamiza (Yona 3: 1-10) kwakuwa tunapokubali na kutubu uovu, uasi na dhambi na kuuacha Mungu anatusamehe na hukumu zote ambazo zilikuwa ziwe juu yetu Mungu anazifuta na anatuhesabia haki mbele zake (Rumi 8: 1-2).SHIKA NENO WANA WA MUNGU Mbarikiwe na Mungu.

 39. Ndg Joe,

  Sina uhakika iwapo “kuongozana” nilikokusema mimi ndiko nawe unakokusema kutokana na mifano uliyonitolea. Ninachokifahamu ni kwamba Samweli ndiye aliyekuwa mtawala wa Israeli akimuwakilisha Mungu mpaka alipokataliwa na Israeli na Mungu akawapa Sauli. Na kuanzia hapo mamlaka zikatenganishwa, Ofisi ya Mungu iliendelea kusimamiwa na nabii Samweli na serikali ikawa chini ya Sauli. Samweli alikuwa ni Sauti ya Mungu kwa Israeli ambayo Sauli alipaswa kuisikiliza. Nabii Samweli hakuwahi kuondoka ktk nafasi yake aongozane na Sauli katika kampeni zake, ndio maana mambo yalipomfika shingoni Sauli, alimtafuta Samweli tena kwa nia ya kujiwakilisha kwa Mungu na akatolewa unabii uliomtimilia, akauliwa!

  Hata Yohana Mbatizaji hakuwahi kuongozana na Herode, bali alimkemea katika nyendo zake!

  Kuhusu Unabii, sijui kama unaifahamu maana yake haswa! Unabii unawakilisha Sauti ya Mungu, ni LAZIMA utimie au Mungu awe muongo! Mfano wa Yona uliouleta hauendani kimaudhui na jambo la unabii usio timia, maana Yona alitumwa kuwapelekea Ujumbe ambao uliwapa fursa ya kuchagua, aidha kuangamia wasipouitii au kupona wakiuitii, nao wakachagua kutii, wakapona!

  Jambo la kuuchakachua unabii pia si kweli, ni kule kujiridhisha tu kusiko na faida yoyote kiungu! Ukiona mtu anaweza kuuchakachua Unabii, basi jua hata huyo Mungu mwenyewe kachakachuliwa, jambo ambalo ni hatari kwa Wokovu!!! Mimi ningekushauri uwe mkomavu, kama unabii haujatiamia, AMINI hivyo tu, kuwa Mungu hakulisema hilo!!! Hata ukisema eti waliiba kura, labda nikuulize, Mungu alipokuwa anatoa tamko hilo hakujua kuwa wataiba kura? Kama hakujua basi hata sifa ya Uungu ameipoteza!!!

  Halafu, watumishi wa Mungu, yeye Mwenyewe huwaweka Wakfu kumtumikia. Jambo la kwanza, He separates them from the world, they become Nazarites unto the Lord! Watazame akina Samson walipojichanganya na dunia waliishia ktk matatizo!

  Shida nyingine ni kwa hao masikini wanasiasa, hawajui chochote kile zaidi ya kuwatumia hawa viongozi wa dini wanaoziacha nafasi zao walizokabidhiwa, nao wanasiasa wakijihakikishia makusanyiko hayo kuongozwa kuwapigia kura, lakini licha ya wanasiasa hao kuzipata hizo kura huishia kupigwa ukoma wa kiroho kama Uzia, maana makusanyiko hayo wamekabidhiwa for that vote time while, kinyume na mapenzi ya Mungu, nayo damu yao itadaiwa kutoka mikono ya hao watumishi waliowauzia makusanyiko hayo!

  Hata mimi nakubaliana na nia yako, kwani hata mimi nia yangu si kumshusha mtumishi wa Mungu bali tunaivinjari Kweli ya Neno la Mungu inayouongoza Utumishi!

  Gbu!

 40. Sungura,

  Sina vendetta na Askofu, ni ndg yangu, wala hayo mengi unayosema nimeyaandika nje ya mada, sidhani kama uko sahihi, maana kinachozungumziwa hapa in principal ni “Wokovu.” Ndipo ninaamini nawe unafahamu kwamba ndani ya Wokovu kuna mambo mengi tu, sasa kama utauongelea huo kwa jinsi ya mwenendo wa wanasiasa, nilidhani pia tunaweza kuuongelea huo kwa jinsi ya mwenendo wa watumishi wa Mungu, ndipo to break even!

  Kwamba wapi niliona mitume wamekatazwa kuongozana na wanasiasa, naona umekwisha izoelea tabia iliyokomaa siku hizi ya kuwaalika viongozi wa siasa kwenye madhabahu za Mungu ili kuwaomba hela! Wengine huwaga wanahubiri kabisa, wanawafungulisha waumini Biblia zao na kuwahubiria! Mfalme Uzia alikuwa rafiki wa Isaya, akayazoelea mambo ya Mungu, 2Nya 26: 16 “… aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia. Azaria kuhani akaingia nyuma yake, na pamoja naye makuhani themanini wa BWANA, mashujaa; wakamzuia Uzia mfalme, wakamwambia, Si haki yako, Uzia, kumfukizia BWANA uvumba, ila ni haki ya makuhani wana wa Haruni, waliofanywa wakfu, ili wafukize uvumba…” aliishia kupigwa ukoma, Mungu awasamehe wanasiasa wetu!

  Kukujibu zaidi, siasa si dhambi na ni kwa wote, waliookoka, ambao ni bora zaidi, na pia kwa wapagani. Ila ukimuona Askofu anajiingiza katika siasa basi jua kuwa, hakuwahi kuitwa na Mungu amtumikie, atakuwa ameingia katika utumishi kwa akili zake tu, labda emotions nk, au kazi tu, kwa sababu its an equal opportunity employer, the church!

  Macho yangu ya kiroho ndg yangu nazidi kuyatumbua nione sawa sawa, ndio maana nipo hapa nikijifunza zaidi katika freedom!

  Gbu!

 41. Pia Ck Lwembe issue ya mtumishi wa Mungu kutoa unabii usiotimia inategemea mambo mengi kama:

  1. Mungu aliyempa mtumishi unabii wa jambo fulani na akalisema bado Mungu anaweza akaamua kughairi na hilo jambo lisitokee maana Yeye Bwana Mungu anabaki kuwa Mungu regardless of anything. mfano nabii Yona alitumwa na Mungu kutoa unabii wa kuangamia kwa mji wa Ninawi na bado Mungu akaamua kughairi na unabii ule haukutimia.

  2. Mwanadamu pia anaweza akauchakachua unabii wa Mungu na Mungu akaja kushusha ghadhabu yake kwake in very harsh ways…hakuna anayejua kwa uhakika kama unabii aliotoa kakobe ulichakachuliwa kwenye matokeo ya kura au la…hakuna anaejua bila kuwa na mashaka yoyote kama matokeo ya ule uchaguzi aliotabiri kama chama kilichoshinda kilishinda kwa haki bila wizi wa kura ama la..!.hakuna anaejua kama mateso wanayopitia wa-tz na baadhi ya waliohusika maybe ni matokeo ya uchakachuaji wa ule unabii au la…But rest assured kuna siku moja kila kitu tulichofanya hapa duniani kitawekwa peupe!

  Nia yangu si kumtetea Kakobe au kumpinga…nia yangu ni kukuonyesha usahihi wa biblia ndugu Ck Lwembe

 42. Ck Lwembe

  kauli yako kuwa “Sijaona mahali popote pale ambapo Kuhani au Mtume aliyekuwa akiongozana na wanasiasa” inaonyesha unahitaji kusoma vizuri biblia kuelewa. Ni hivi toka enzi za mfalme Sauli (ambaye kwa tafsiri ya sasa ni kama rais wa nchi) makuhani/mitume/manabii/etc waliongozana nao kwa kukubaliana au kutokukubaliana…mfano kuhani Samweli enzi za utawala wa Sauli,yhana mbatizaji enzi za utawala wa Herode, etc etc

  Joe

 43. HERI YA SIKU YA NNE WANA WA MUNGU MLIOFUNULIWA KWA NENO NA KWA ROHO TAKATIFU YA MUNGU!
  Sungura na Siyi:
  Sungura nitakujibu swali uliloniuliza, siri ya dini ya kakobe imefichuka kama ifuatavyo: Neno la Mungu linasema wazi kuwa kanisa ni mali ya YESU/ MUNGU mwenyewe . Kama umekuwa ukifuatilia habari za dhehebu la kakobe utakunbuka kwamba kuna wakati alifunguliwa kesi na waumini wake kwamba amekula fedha ya kanisa lakini yeye alisema hili kanisa langu na nimelisajiri kwa jina langu na familia yangu na kutokana na majibu hayo akashinda kesi, kwahiye dhehebu la kakobe sio la Mungu ili ni la kwake kwa mantiki hiyo Mungu wa kweli hana sehemu kwenye dhehebu lake. Pia siri nyingine madhabahu anayoitumia ni ya marehemu shetani.
  Ndugu Siyi umeuliza kuhusu peponi ni wapi? Kiukweli dini zote walikuwa wakitufundisha kuwa peponi ni mahali pa Mungu wa kweli au Mbinguni. Lakini huo ni uongo! Peponi ni mahali pa mapepo na maroho yote machafu kwa jina lingine panaitwa toharani, hapa ndipo mahali panapoitwa ulimwengu wa roho. Japo walokole huwa wanajua kuwa kwenye ulimwengu wa roho ndipo mahali Mungu anakaa. Kwakweli wamedanganyika na wamewadanganya wengi.

  Kwa ufahamu wa NENO lililofunuliwa tumefahamu kwamba peponi ni kwenye mbingu ya tatu au mahali yanapokaa maroho ya giza yote( Efeso 6:1-18). Mungu wa kweli ameliweka kanisa/watakatifu katika UUMBAJI WA WATAKATIFU ULIOFUNULIWA ROHONI. Hapa ni mahali ambapo maroho yoyote ya giza yanayokaa ktk ulimwengu wa roho hayawezi kupafikia.
  SHIKA NENO MLIOPEWA NEEMA KUBWA NA BWANA NDANI YA TAIFA TAKATIFU LA MUNGU GOSHENI KIZAZI CHA NNE!

 44. Nyakati hizi watumishi wenye ujasiri wa kusema maneno kama ya Kakobe ni wachache sana. KAKOBE NI MTUMISHI WA mUNGU, tunajuaje huenda kama mtumishi wa Mungu yeye anawafahamu watu hawa kuwa ni wanafiki tu. Maneno tunayoyaandika hapa ya kuwatetea viongozi hawa wa kisiasa walitakiwa wao ndio walalamike kuwa kwa nini wanashutumiwa juu ya wokovu walioupokea tayari!

  Mimi nataka niwaulize jambo moja kutoka kwenu mnaomlaumu Kakobe kwa kauli yake njema ya kuwahamasisha viongozi hawa wakae katika kweli. Labda mnafahamu lolote kuhusu hawa viongozi wa siasa kwamba wanaabudu wapi katika wokovu wao? Ninavyofahamu mimi huwezi kusema kuwa umeokoka halafu ukawa unasali msikitini!.

 45. Mheshimiwa Askofu Kakobe,

  Kama una neno la uzima ya kuwapa wanasiasa, hebu wakute huko ofisini mwao , uwahubiri, uwaonye, nk . After this nyamazeni kimya. Kama utakuwa umefaulu, utukufu si wako bali ni wa Mungu.

  Ubarikiwe.

 46. Lwembe kwa namna fulani uko sahihi,

  Lakin pia na wewe inaonekana una ‘ personal vendetta’ na Kakobe, maana umeongea mengi saaana hata yasiyohusika na tamko lake ambalo ndio haswa watu wanalijadili hapa.

  Kama wewe hujawahi kuona kwenye biblia kuhani au mitume wakiambatana na wanasiasa, wapi umeona kwenye biblia mitume wakikatazwa kuwa/kuambatana na wanasiasa?

  Kwani siasa ni ya wasiookoka tu? au siasa ni dhambi?

  What is the role of politics in a society, jamii ambayo na waliookoka ni wanajamii wake?

  Au u miongoni mwa watu wanawazuia wakristo kuwa wanasiasa, halafu nchi ikishachukuliwa na waovu na mambo kuanza kwenda vibaya mnaanza tena kutuambia tufunge na kuomba maana waovu wanaipeleka nchi kubaya?

  Hata wewe unatakiwa kufungua macho yako ya kiroho Lwembe!

 47. Kauli kwamba “Wokovu una nguvu kuliko siasa” ni ya kisiasa zaidi kuliko Injili! Labda wapendwa mnifafanulie jambo hilo ili nijue mmezipimia wapi “nguvu” hizo hata kuzilinganisha!

  Bali mimi naiona kauli hiyo kutoka kwa Askofu kuwa ni moja ya zile kauli ambazo huwatoka wote ambao wana maono mawili mawili! Sijaona mahali popote pale ambapo Kuhani au Mtume aliyekuwa akiongozana na wanasiasa, maana hata majuzi tu alikuwa na kundi la wanasiasa viwanja vya jangwani “wakihubiri” katiba mpya!

  Pia sijapaona popote ktk Injili ambapo panasema ukiokoka sharti “Utangaze”, bali ninachojua ni kwamba ukiokoka unakuwa waraka wa kusomwa na watu wote, jambo ambalo ndilo lililosomwa kwa Mangula mpaka Askofu Kakobe akashangaa, “Nilishangaa sana kusikia mtu mzito kama Philip Mangula akitajwa kuwa aliimbisha pambio kwenye msiba wa Askofu Kulola”!!! Our actions speak louder than words, your actions are so loud, we can’t hear your testimony!

  Tatizo la kujiingiza katika siasa ni kule kujiingiza ktk unafiki. Kakobe ana siasa za kuichukia CCM kama Munishi, kwahiyo hata ukiitazama kauli yake hiyo utaiona ina maudhui ya vendetta kwa viongozi wa ccm, its a veiled onslaught, otherwise why coin Wokovu wa mtu na mambo ya kujitangaza kuwa ndio kipimo cha kwenda peponi?

  Ni vizuri kwa viongozi wa dini Kuchagua Upande wa kutumika, kama ni kulisimamia Kusanyiko la Bwana au kama ni Siasa badala ya kujaribu kutembea njia zote mbili! Askofu alikuwa na ushirika gani na hivyo vyama ambavyo vimewaongoza watu wengi vikiwaingiza ktk huzuni mbali mbali, wengine kifo, ulemavu na umasikini ktk familia zao kwa hekima yao ya kupambana na askari wenye silaha, na kurushiana mawe wao kwa wao wakitoana ngeu kwa siasa za ushindi, huyo Askofu anafanya nini katikati ya makundi hayo? Mungu hashiriki Utukufu wake na yeyote yule, ukijichanganya anakuacha!!!

  Tatizo letu kubwa ni kule kupofushwa kwa mafanikio, watu wengi huamua kuvutwa na hayo wakiiacha Kweli ya Mungu iliyofunuliwa iwaongoze katika maamuzi yao.

  Hivi hamkumbuki kwamba aliwahi kusimama hadharani kwa nafasi yake aliyonayo katika Huduma ya Mungu, akatoa unabii ambao haukutimia? Je, hamjui inampasa nini nabii wa uongo?

  Hivi ninyi mlio hapa Dar, hamkuwaona washirika wake waliokuwa wakililinda eneo lao la kanisa usiku na mchana wakipeana zamu, ili kuwazuia Tanesco kupitisha nyaya za umeme?

  Au hamuwaoni wanawake wa kanisa hilo wanavyofungishwa vitambaa vichwa vyao kinyume na Neno la Mungu?

  Yafungueni macho yenu ya kiroho muipokee Kweli ili mpate kuwekwa Huru badala ya kuwa watumwa wa dini!

  Gbu!

 48. Mhhh,
  Peponi!!! Kwani mtu akifa, anaenda peponi? Ni wapi huko peponi?? Help me Biblically please!!!

 49. mtumishi wa Mungu bishop Kakobe upo juu usisikilize kelele za chura wewe tiabidii songa mbele usiangalie nyuma najuaa unavita na mwovushetani shetani anauwezo wa kukuijia live anachofanya anapitia watu kamaao wanaokusema mabaya natena yasiyo kuapo kwako tena atawakujui sasa niivi mtumishi wa Mungu usikae kimya kwalolote utakaloona lipokinyume unakemea bila woga usisikie sauti za shetani alafu mtumishi wa Mungu kuna roho zawengi zinapotea na kunawengi wana danganya watu mtumishi wa Bwana wamajeshi tunakuomba utufikilie japo kwa TV hata ya hapa Tanzania unakua unalusha vipindi vya mafundisho naamini itakua balaka sana….@

 50. Vai na Michael Alphonce, nina maswali kwenu:

  Vai unaweza kuniambia matunda ya Kakobe yaliyokufa kama ulivyosema kwenye comment yako? Na ni siri gani ya dini unayoiita ya Kakobe ambayo umesema imefichuliwa na Mungu?

  Michael kwa nini unataka Kakobe aachane na mambo ya siasa, amefanya kosa gani kusimama kwenye jukwa la siasa?

  Ni hayo tu!

 51. Wapendwa mbona Bishop kanena vyema?wawezaje ona haya kuwatel watu umeokoka?ukiona mpendwa wa namna hiyo basi msanii!huwa nashangaa utakuta umekutana na mpendwa kwenye daladala au kwenye umati wa watu thn ukamtel BWANA YESU ASIFIWE utaona anazuga mara unasiki powa au mimi mzima jamani si usanii huo?Mbona JESUS kaweka wazi ktk hili?MUNGU AWABARIKI WOTE.

 52. Tafadhari mzee, tunakusihi uachane na mambo ya siasa ya kutupiana maneno, muhubiri KRISTO.

 53. Brethren,

  1Cor. 2:15 says, “15But he that is spiritual judgeth all things, yet he himself is judged of no man.”

  But WISELY says, A man hath joy by the answer of his mouth; and a word spoken in due season, how good is it! He that keepeth his mouth keepeth his life; but he that openeth wide his lips shall have destruction.

  “Prudence, life granule!”

 54. Mmh! Wapendwa,

  Mantiki ya alichosema Bishop Kakobe, hamuiona kweli au ni ku-criticise tu? by the way, pamoja na kurekebisha mengi sana toka miaka ilee alivyoanza na alivyokua kwa wale mnaojua ilikuwaje uko nyuma, bado mnamdauti Mtumishi huyu? Aaaa jamani, let us be fair.

  Press on.

 55. Atakayenionea haya mimi na maneno yangu nami nitamwonea haya siku ile ya mwisho hayo ni maneno ya Bwana Yesu. Kutokuwaambia watu kuwa umeokoka no kuionea haya Injili na kumuonea haya Bwana Yesu. Na kwa maneno yake Mwenyewe, mtu wa namna hiyo hataiona mbingu. Kwa Ndugu Paul acha kupotosha watu.

 56. Kutokana na NENO tunajifunza kwamba aliyeokoka kweli anatakiwa ajitangaze kupitia kazi na matunda anayozaa kwamba ni mazuri au mabaya. wala si lazima aanze kujitangaza kwa maneno tu hiyo sio maana yake. Kakobe naomba hata yeye pia atuonyeshe matunda mema aliyozaa na kazi njema aliyoifanya kama bado inadumu mpaka sasa tangu mwaka anaosema aliokoka 1973. kwa mtazamo wangu kwa sasa naona matunda yote aliyokuwa ameyazaa sasa yamekufa wala hayapo tena japo hapo nyuma alivuma sana wakati ule kabla siri ya dini yake haijafichuliwa na Mungu. Naomba Askofu kakobe atuambie AGIZO alilopewa na Mungu ili tulijue jamani.

 57. Wao askofu mkuu, kwa upande wangu nafurahi kusikia umerudi Tz maana niliogopa sana baada ya kusikia umeregister ministry na umehamia US. Kanisa linakuhitaji askofu uwepo na usilikimbie tafadhari. Huduma ina majaribu mengi lakini simama mtumishi na uendelee kumtumikia Mungu kwa uaminifu, utavuna kwa wakati wake.

 58. Hapo kakobe anachosema sikubaliani naye. kuna mwanasheria aliyemfata Yesu usiku kwanini?unajua kujitangaza au kutojitangaza mnh!God looks inside deep down.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s